operesheni vipaji mwaka 2018/2019 - bcic.wapo.or.tz · viashiria vya operesheni vipaji katika...
Post on 10-Sep-2019
3 Views
Preview:
TRANSCRIPT
Operesheni Vipaji Mwaka 2018/2019
OPERESHENI VIPAJI
Ni kampeni ya kitaifa ya kutekeleza ‘’dhima’’ ya WMI. Katika kampeni hii, kutafanyika uhamasishaji, uelimishaji na usisitizaji wa kurejesha maadili mema ya kitabia kwa mtu mmoja-mmoja, familia, jumuia, jamii na Taifa kwa ujumla. Pia kutia msukumo wa umilikaji uchumi endelevu kwa jamii na hasa vijana.
MALENGO MAHUSUSI YA OPERESHENI VIPAJI
1. Kuhamasisha, kuelimisha vijana wa kizazi kipya katika utambuzi na
unoaji vipaji wenye kuambatana na urejesho wa maadili mema kama msingi wa uchumi endelevu kwa maendeleo ya kijami
2. Kupata, kumiliki na kuendeleza ardhi kwa kushughulika na Kilimo cha kisasa na uanzishwaji wa viwanda vidogo-vidogo.
3. Kupitia kampeni ya Operesheni Vipaji, urejeshaji wa maadili mema ya kitabia umejengwa kwenye falsafa ya ukombozi wa kimwili, kiakili na kiroho katika kukabiliana na maadui wakuu watatu ambao ni:
Ø Mmomonyoko wa maadili Ø Kukithiri kwa umaskini wa kipato Ø Afya duni
4. Mkazo wa ujumbe wa kampeni ni kuhimiza vijana walioko mashuleni, vyuo vya kati na vyuo vikuu kubadilika kitabia, kutunza afya zao, kunoa vipaji vyao na kumiliki uchumi halali na endelevu kwa wote wao wakiwa ndio nguvu kazi ya Taifa.
5. Matarajio ni kufanikisha lengo kuu la kuleta watu MILIONI MOJA kwa Yesu katika mwaka 2018. Kampeni ya Opereseheni Vipaji ilizinduliwa Dar es Salaam makao makuu ya WMI kuanzia 27 Januari, 2018 na itaendelea mpaka tarehe 30/12/2019
VIASHIRIA VYA OPERESHENI VIPAJI
Katika kutimiza malengo makuu mahususi ya Operesheni Vipaji, inatarajiwa mabadiliko makubwa ya kitabia kutokea wakati yafuatayo yatakapofanyika: 1. Kurejeshwa hofu ya Mungu katika mioyo ya watu kwa kuwaelimisha jinsi ya kutumia nguvu za utashi binafsi wa kujizuia kushiriki vitendo viovu. 2. Kurejeshwa nidhamu, utu, staha, ubinadamu, uungwana na utamaduni wa kuheshimu serikali iliyoko madarakani pamoja na mamlaka zilizowekwa na kutii sheria za nchi kwa hiari 3. Kurejeshwa kwa moyo na ari ya kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia vipaji vya asili ili kujikwamua katika umaskini wa kipato 4. Raia kuhamasika kimtazamo katika kulinda amani na utulivu katika jamii kwa kujiepusha na vishawishi vinavyohamasisha uasi, migomo, maandamano yasiyo na tija, na badala yake watu wajikite kwenye uzalishaji wenye tija kwa manufaa ya taifa
NGAZI ZA UTEKELEAJI WA KAMPENI YA OPERESHENI VIPAJI
KITAIFA Ø Kupitia mtandao wa multisite live kufanya makongamano na midahalo
ya utambuzi wa vipaji vya asili; sanjari na kurejesha maadili mema ya kitabia kwa watu zaidi milioni 1 waliomo katika miji mikuu ya wilaya 50 ya kikanda kila mwaka
Ø Lengo ni kurusha mubashara makongamano makubwa ya kunoa vipaji siku 5 kila mwisho wa mwezi ili kuleta watu 350 Yesu kwa kila mji katika miji mikuu ya wilaya 50.
WILAYA Kuanzisha na kuendesha vituo vya ushauri wa kibibilia na maombezi (BCIC) kwa kusudi la kuona na kulea vipaji kwa vijana watakaoitikia kampeni ya kubadilika kimaadili kwenye miji mikuu 50 ya Wilaya
FALSAFA
YA
KUNOA VIPAJI
1 UTAMBUZI WA VIPAJI
2 UTAKASO WA VIPAJI
3 URATIBU WA
VIPAJI
4 MAFUNZO YA VIPAJI
5 TUZO ZA VIPAJI
HATUA 5 ZA MCHAKATO WA KUNOA VIPAJI
UTAMBUZI UTAKASO URATIBU MAFUNZO TUZO u Makongamano ya
utambuzi wa vipaji
q Maombezi ya Toba na ubatizo kwa ajili ya wokovu
Ø Kuandaa na kusimamia mwongozo wa kunoa vipaji vya waamini wapya
² Kutoa ushauri kuhusu mahali pa kupata masomo yanayolingana na vipaji mama vya wahusika
ü Kuandaa mazingira na miundombinu ya mazoezi ya kunoa vipaji mama
u Warsha za majadiliano ya vikundi
q Maombezi ya kufunguliwa kutoka vifungo vya pepo wachafu
Ø Kuunda na kuwezesha mtandao wa vikundi vya vipaji mama
² Kuendesha midahalo na vipindi vya mafunzo ya vipaji kupitia media
ü Kudhamini matamasha na maonesho ya vipaji bora
u Ujazaji wa fomu za utambuzi wa vipaji
q Maombezi ya Ujazo wa Roho Mtakatifu kwa ajili ya utakaso wa vipaji
Ø Kuwasajili wana-vipaji kwenye mtandao wa vipaji mama
u Uchambuzi wa fomu za utambuzi wa vipaji
q Mafunzo ya awali ya kibiblia
UCHAMBUZI WA MAJUKUMU YA HATUA ZA 5 ZA KUNOA VIPAJI
NA ENEO LA KIKANDA
WALENGWA ENEO LA KONGAMANO
1. DaresSalaamnaPwani Wanafunziwavyuonamashuleni
BCICMbeziBeach
2. TanganaMtwara WanafunziwavyuonaMashuleni
KumbizaVyuo
3. Mwanza,KagerashinyanganaKigoma
Wanafunziwavyuonamashuleni
Ukumbiunaotosheleza
4. Dodoma,MorogoronaTabora Wanafunziwavyuonamashuleni
UkumbiwaUDOM
5. Mbeya,IringaTunduma Wanafunziwavyuonamashuleni
UkumbiwaUhasibuMbeya
6. Arusha,ManyaranaMoshi Wanafunziwavyuonamashuleni
UkumbiwaAICC
MTANDAO WA KAMPENI ZA VIPAJI KATIKA MIJI YA KIKANDA
UBUNIFU
Uongozi wa kimaono
Uanzishaji wa makampuni
mapya
Uanzisha wa taasisi mpya za unasihi wa
kijamii
MUZIKI
Kipaji cha sauti
Kipaji cha kutunga nyimbo
Kipaji cha upigaji vyombo
Ustadi wa kuzalisha
muziki
UHUSIANO
Uongozi wa kisiasa
Uongozi wa kikanisa
Uongozi wa kijamii-vikundi
vya kijamii
Mawasiliano ya kimasoko na
kijamii
MICHEZO
Michezo ya vikundi mf mpira nk
Michezo ya riadha
Michezo ya sarakasi
Michezo ya kuigiza
HESABU
Ujasiriamali
Utaalamu wa kihasibu na ukaguzi wa
hesabu
Utaalamu wa michanganuo
ya miradi
MASOMO NA MAZOEZI YANAYOHITAJI KWA VIPAJI MAMA 5 VINAVYOONGOZA
MIKAKATI YA KUFANIKISHA KAMPENI
① WAPO MEDIA kutokea Mbezi Beach Dar es Salaam kukamilisha miundombinu ya kurusha matangazo ya moja kwa moja kupitia mfumo wa video conference ili kuwahutubia wakazi watakaoitikia mialiko ya mikutano ya kampeni ya kunoa vipaji kwenye miji 50 ya kikanda
② Kuunda mtandao mpya wa kunoa vipaji vya vijana waliokubali kubadilika kitabia kuwawezesha kupata mafunzo maalum ya kunoa vipaji vyao ambavyo vitaweza kuwainua kiuchumi.
③ Kuanzisha na kuendesha chuo cha vipaji na uongozi wa kimaadili
(TMLC) kwa ajili ya kutoa mafunzo na mazoezi ya vipaji kwenye ngazi za miji ya wilaya
④ Kuanzisha na kusimamia taasisi ya mikopo kwa ajili ya miradi ya vikundi vya Mtandao wa kunoa vipaji katika ngazi za miji ya wilaya
top related