bunge la tanzania majadiliano ya...

179
1 6 JUNI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Arobaini na Nne - Tarehe 6 Juni, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYA SALUM): Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka 2013/2014. MHE. SAID MUSSA ZUBEIR (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

Upload: others

Post on 28-Oct-2019

0 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

1

6 JUNI, 2013

BUNGE LA TANZANIA

________________

MAJADILIANO YA BUNGE

________________

MKUTANO WA KUMI NA MOJA

Kikao cha Arobaini na Nne - Tarehe 6 Juni, 2013

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYASALUM):

Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka2013/2014.

MHE. SAID MUSSA ZUBEIR (K.n.y. MWENYEKITI WAKAMATI YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA):

Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi,Viwanda na Biashara Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu yaWizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 pamojana Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

Page 2: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

2

6 JUNI, 2013

MHE. DAVID E. SILINDE (MSEMAJI MKUU WA UPINZANIKWA WIZARA YA FEDHA):

Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani waWizara ya Fedha Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumiziya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

MASWALI NA MAJIBU

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaanza na swalila Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na atakayeulizaswali letu la kwanza ni Mheshimiwa Omar Rashid Nundu.

Na. 351

Wananchi Kuuawa kwa Tuhuma za Wizi Mdogo Mdogo

MHE. OMAR R. NUNDU aliuliza:-

Kumezuka hulka mbaya kwa baadhi ya watukuchukua sheria mkononi mwao kwa kuwaua wenzaokutokana na tuhuma za wizi mdogo mdogo kama wa simuza mkononi na kadhalika:-

(a) Je, ni Wananchi wangapi wameuawa katikamazingira haya?

(b) Je, Serikali inachukua hatua gani kukomeshavitendo hivyo?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Omari Rashid Nundu, Mbunge wa Tanga Mjini,kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha kuanziaJanuari, 2012 hadi Aprili, 2013 jumla ya watu 1,666 waliuawakwa kupigwa na Wananchi waliojichukulia Sheria mkononi.

Page 3: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

3

6 JUNI, 2013

(b) Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Jeshi la Polisiimekuwa ikichukua hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja nakuwakamata watuhumiwa wote wanaohusika na matukioya aina hiyo na kuwafikisha Mahakamani. Aidha, Jeshi laPolisi chini ya dhana ya utii wa sheria bila shuruti, hutoamafunzo kupitia vyombo vya habari il i kuwaelimishaWananchi umuhimu wa kufuata Sheria, pia kuwashirikishaViongozi wa Dini kuwataka waumini wao kuacha ukatili.Serikali inalaani vikali tabia ya Wananchi kujichukulia sheriamkononi na inawataka Wananchi kufuata sheria za nchi.

MHE. OMAR R. NUNDU: Mheshimiwa Spika, ahsante.Pamoja na majibu ya ufasaha lakini ya kusitusha kutokanana idadi kubwa ya watu ambao wameuwa kwa kipindikifupi na ukichukulia kuwa uhai wa binadamu ni tuzonadhimu ambayo Mwenyezi Mungu ametupatia:-

(i) Je, ni kesi ngapi za mauaji ya aina hiizimekwishatolewa hukumu na hukumu hizo ni za aina gani?

(ii) Kwa kuwa Vituo vya Polisi vikiwa karibu nasehemu ambazo zimejificha husaidia kujua uhalifuunaotokea; na kwa kuwa kuna vitu vingi ambavyovimejengwa kwa muda mrefu ambavyo mpaka leo havinaPolisi kama kile ambacho kipo kwa Munduwangu, Kijiji chaMwambani kule Tanga kilichojengwa takribani miakamitano iliyopita na kinaota nyasi tu lakini hakuna polisi. Sasani hatua gani Serikali inachukua kuhakikisha kuwa Polisi wakokaribu na sehemu ambayo matukio kama haya yanawezakutokea ili kuyazuia?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: MheshimiwaSpika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,napenda kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, kuhusu kesi ngapi. Kesinyingi ambazo zimetokea katika suala hili bado ziko kwenyeupelelezi, kwa sababu hii ni mob justice na siyo rahisi kupatamsaada wa Wananchi katika kuwaonesha wahusika.

Page 4: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

4

6 JUNI, 2013

Pamoja na hivyo, bado upelelezi unaendelea kwenye kesinyingi za namna hii na nyingine zimefikia hatua karibukuzipeleka mahakamani.

Mheshimiwa Spika, la pili kuhusu vituo vya polisi;naomba niseme kwamba, Vituo vya Polisi kuwa kwenyemaeneo mengi ni faida, lakini siyo Vituo vya Polisi ambavyovitatufanya tusiuane kiholela. Hili ni suala la elimu, kuthaminimaisha na kutaka kila mtu, kila raia, akubali kutii sheria bilashuruti, lakini pia kwa yule ambaye anamwona mwenzakebado analegalega, amsaidie kumuweka sawa.

Mheshimiwa Spika, suala muhimu pamoja naWananchi wenyewe kukataa kuuana, kuna doria ambazotunazifanya katika maeneo mengi; hizi ndizo ambazozinaweza zikasaidia kuliko kusema kila litakapotokea tukiopawe na kituo. Pamoja na hayo, vituo ambavyovimeshajengwa na bado havijawekewa askari, hil itunalifanyia kazi lakini mara nyingi kuna standards aumambo ambayo yanakuwa hayajatimia, ndiyo maanainakuwa tabu kupeleka askari. Namwomba MheshimiwaMbunge, kama ana specific issue au kituo, tutalizungumzana tutalifanyia kazi kama tutakavyokubaliana.

SPIKA: Ahsante. Sikuona wengine walioomba,tunaenda swali linalofuata; Mheshimiwa Khalifa SuleimanKhalifa!

Na. 352

Raia wa Kigeni Kuhesabiwa na KujipatiaVitambulisho vya Taifa

MHE. KHALIFA SULEIMAN KHALIFA aliuliza:-

Zoezi la uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifalinaendelea katika nchi yetu ambayo inazungukwa na nchinyingine zenye migogoro:-

Page 5: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

5

6 JUNI, 2013

(a) Je, raia wa nchi nyingine hawawezi kujipatiavitambulisho hivyo?

(b) Je, zoezi la kuhesabu watu (sensa)halikuwagusa raia wa nchi nyingine?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Khalifa Suleiman Khalifa, Mbunge wa Gando,lenye sehemu (a) na (b), kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa nchi yetuimezungukwa na nchi zenye migogoro; hivyo, kutoa viashiriovya kuweza kuandikisha watu wasiostahili. Kwa kulitambuahilo, NIDA inaendesha zoezi hili kwa umakini na kwakushirikiana na taasisi mbalimbali kama vile TAMISEMI, RITAna Uhamiaji ili kuthibitisha makazi ya mwombaji, kutambuaumri wa mwombaji na kupata uthibitisho wa uraia wamwombaji kabla ya kutoa kitambulisho.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwahatuandikishi watu wasiohusika, Serikali imepelekaMadaftari ya Wakazi yanayoratibiwa na Serikali za Mitaa,ambayo lengo lake kubwa ni kuandikisha wakazi wote wakila kaya zilizo katika kijiji au shehia na kuzihifadhi taarifahizo. Taarifa zilizoko kwenye Madaftari ya Wakazi ndizozitakazotumika kumwandikisha mwombaji wa kitambulishocha Taifa kama kigezo kikuu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kujaza fomu yamaombi, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kijiji au Shehia,ikijumuisha Wajumbe wa Vitongoji, itachambua maombihayo na kubainisha watu ambao siyo Raia wa Tanzania.Hatua hii itazuia raia wa nchi nyingine kuweza kujipatiaVitambulisho vya Mtanzania.

Mheshimiwa Spika, zoezi la kuhesabu watu lina lengola kujua idadi ya watu waliopo nchini. Katika kutekelezazoezi hilo, kila mtu anayehesabiwa hutakiwa kutoa taarifa

Page 6: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6

6 JUNI, 2013

ya uraia wake. Lengo la kufanya hivyo ni kuiwezesha Serikalikutambua nani ni raia na nani siyo raia.

SPIKA: Mheshimiwa Khalifa swali la nyongeza,naomba kidogo msimame ninyi mlioomba.

MHE. KHALIFA SULEIMAN KHALIFA: MheshimiwaSpika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya MheshimiwaNaibu Waziri, nina maswali mawili madogo ya kumwulizakama ifuatavyo:-

(i) Sote tunaelewa kuwa zoezi la sensa lililopita,lilikumbwa na matatizo kiasi kwamba wako baadhi yaWatanzania wenzetu hawakutaka kujiandikisha auhawakuandikishwa na wao pia wanayo haki ya kupatavitambulisho. Katika mazingira hayo ambayo mtuhakuandikishwa kwenye sensa, lakini anataka kitambulishocha Utanzania na anayo haki ya kupata; inakuwaje katikasuala hilo?

(ii) Kielelezo cha msingi cha mtu kuandikishwakuwa raia au kupata haki za uraia ni cheti chenyewe chakuzaliwa na tunaielewa nchi yetu kwa sasa kuwa maranyingi fedha zinakufanya upate kitu hata kama siyo hakiyako. Inapotokea watu wamepewa vyeti vya kuzaliwa kwakununua halafu wakapewa Vitambulisho vya Taifaambavyo vitawafanya wawe Watanzania wa kudumu.Katika mazingira hayo Serikali inatoa tamko gani na hivivitu siyo vigeni kwa sababu kuna watu hivi sasa tunaelewawapo Tanzania Bara lakini wanakuja Zanzibar wanapigakura, wako watu wa nchi nyingine wanapiga kura hapana tunajua hilo. Je, unatoa kauli gani?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: MheshimiwaSpika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza yaMheshimiwa Khalifa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, kulitokeamatatizo katika uandikishaji wa watu kwenye sensa iliyopita,lakini naomba niseme kwamba, utaratibu wa kuandikisha

Page 7: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

7

6 JUNI, 2013

na kutoa vitambulisho hauendani moja kwa moja na sensailiyopita. Vina uhusiano, lakini usajili wa watu unafanywakivyake na hilo ndiyo muhimu kwamba, madaftaritumeyatoa na watu wanafuatwa kwenye kaya zaokuandikishwa. Hapo ndipo ambapo mtu ambayehakuandikisha anaweza akapata tatizo, lakini siyo lazimamtu aliyeandikishwa sensa ndiyo apate kitambulisho; hilohaliko sawa kwa sababu siku ya sensa wengine hawakulalanchini. Kwa hiyo, wote hao watapata vitambulisho ikiwamchakato huu wa vitambulisho utafuatwa na kukamilikailivyo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu vyeti vya kuzaliwa nauraia na Vitambulisho vya Kitaifa. Kama nilivyosema awalini kwamba, nguvu kubwa ya kuamua na kuhakiki nani niMtanzania wa kuzaliwa ni kijijini alikotoka. Sasa nguvutunaziweka huko ili ile Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kijijindiyo ambayo inajua nani kamzaa nani na nani mjukuu wanani. Kwa hiyo, kwa kutumia daftari ambalo tumelipeleka,tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sotetutakuwa wawazi na kutaka kuilinda hii nchi, hakuna raiawa nje mwenye cheti atakayepata Kitambulisho cha Taifa.

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, nashukurusana. Kwa kuwa zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vipyalimekuwa likiendelea lakini mpaka hivi sasa ni Viongozipekee ndiyo ambao wamekuwa wakipata. Sasaningependa tupate kauli ya Serikali kwa sababu tunatarajiavitambulisho hivi vinaweza vikaenda mpaka kupigia kurakatika uchaguzi ujao. Je, ni lini sasa Serikali itamaliza zoezihili la kuandikisha Wananchi wote na kupata vitambulishohivi?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: MheshimiwaSpika, napenda kujibu swali la nyongeza la MheshimiwaSilinde, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, speed ambayoinakwenda zoezi hili siyo tuliyoitegemea. Mpaka sasawalioandikishwa zaidi ni Wafanyakazi wa Serikali wa Bara

Page 8: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

8

6 JUNI, 2013

na Zanzibar, wameandikishwa pia watu wa Kilombero kwasababu kulikuwa na majaribio na watu wengine wakawaida Dar es Salaam. Jumla ya watu kama 2,700,000wameshaandikishwa. Hata hivyo, lengo hasa la zoezi hilina lini limalizike, tulikuwa tumepanga limalizike mwakaunaokuja. Mwaka 2014 tuwe tumelimaliza na vitambulishohivi viwe ni sehemu katika mchakato wetu wa kupiga kurana kwa matumizi mengine.

Mheshimiwa Spika, niseme kwamba, kweli kunatatizo na tatizo hasa lipo kwenye bajeti. Mahitaji ya NIDAkwa ajil i ya shughuli hii hayafikiwi kwenye bajeti natunaishukuru Serikali, mwaka huu imepiga hatua kulikoilivyofanya mwaka jana, lakini tuna gap ya hatua na fedhahasa kwenye vifaa vya kuchukulia alama za vidole pamojana picha za waandikishwaji. Tunategemea kwamba,pengine mwaka huu tunaweza tukaongezewa fedha kwautetezi wetu sisi lakini pia na Waheshimiwa Wabunge. Piamwakani tukifanikiwa kuiziba hiyo gap, speed itaongezekana tunaweza tukakamilisha kwa wakati unaotakiwa.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Spika,nashukuru. Kwa kuwa zoezi hili la uandikishaji kupataVitambulisho vya Taifa ni muhimu hasa kwenye suala lakuhamasisha Watanzania kuweza kulipa kodi kwa ajili yamaendeleo ya Taifa na ni mradi mkubwa; na kwa kuwakuna Project ya Big Results Now; Serikali haioni kuna umuhimuwa kuwekeza kwenye mradi huu kwa haraka ili ukamilikekwa wakati ambayo itasaidia pia kwenye kura ya maoni,kwenye Katiba na Uchaguzi Mkuu ujao, badala ya kusuasuaambayo inaweza ikasababisha vurugu katika chaguzi namambo ya kuongeza Pato la Taifa? (Makofi)

SPIKA: Unajua maswali mengine yana-repeatthemselves, lakini naomba ujibu Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: MheshimiwaSpika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbatia, kamaifuatavyo:-

Page 9: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

9

6 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, katika mazungumzo ya Serikali nilipi liingie kwenye labs vitambulisho havikuingia. Vitambulishovilichukuliwa kama ni kipaumbele cha Taifa na Serikaliinatambua umuhimu wa vitambulisho. Lazima tushukurukwamba tulivyotoka mwaka jana ambapo tulipata bilionikumi kwa ajili ya shughuli hii na mwaka huu kupata 251, nihatua tayari ya Serikali. Pamoja na hivyo, nafikiri nipooptimistic kwamba, mwakani tutamaliza zoezi hili na Serikaliipo conscious kwenye hilo na umuhimu wake.

MHE. MUHAMMAD IBRAHIM SANYA: MheshimiwaSpika, kwa kuwa vitambulisho hivi mchakato wakeumeanza muda mrefu sana huko nyuma na ulisuasuakutokana na sababu mbalimbali na leo tunapewa sababukwamba, kuna upungufu wa fedha na hatujajua kamafedha hizi zitatengwa au zitapatikana mwakani. Je, Serikalisasa pamoja na sisi Wabunge tunajiandaaje ili hizi fedhazipatikane kwa wakati mwafaka na vipande hivivipatikane kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015?

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, suala lakutenga fedha kwa ajil i ya kumaliza utayarishaji waVitambulisho vya Taifa litakamilika. Kwa hiyo, msiwe nawasiwasi, mpango wa fedha umekamilika na tuna uhakikatutamaliza.

SPIKA: Maswali ya nyongeza saba haiwezekani,isipokuwa Wabunge mkafanye uhamasisho kwa watuwajitokeze kupata vitambulisho. Nadhani ndiyo kubwa lakufanya. Tunaendelea na Wizara ya Kilimo, Chakula naUshirika, Mheshimiwa Martha Mlata, atauliza swali hilo.

Na. 353

Ruzuku ya Mbolea na Pembejeo za Kilimo

MHE. MARTHA M. MLATA aliuliza:-

Serikali imeendelea kutoa ruzuku ya mbolea napembejeo za kilimo kwa ajili ya mazao ya chakula na

Page 10: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

10

6 JUNI, 2013

biashara kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao,kuongeza Pato la Taifa na la mkulima:-

Je, Serikali inatambua kwamba kuna baadhi yamazao ambayo ni chakula na pia yanatumika kama zaola biashara hivyo ione jinsi ya kuyapa kipaumbele zaidi kwaruzuku hizo?

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Martha M. Mlata, Mbunge wa Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa, baadhi ya mazaoambayo ni ya chakula pia yanatumika kama mazao yabiashara katika sehemu mbalimbali hapa nchini. Mfano,mazao ya mahindi na mpunga, ambayo Serikali imekuwaikiyapa ruzuku ya mbolea pamoja na mbegu bora kwamiaka mitano mfululizo.

Katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Serikali ilitoaruzuku ya tani 126,117 za mbolea ambapo kaya 940,783zilinufaika na tani 8,278 za mbegu bora za mahindi na tani1,694 za mbegu bora za mpunga ili kuboresha uzalishaji wamazao hayo na kuhakikisha wakulima wanapata chakulacha kutosha na kuwaongezea kipato.

Mheshimiwa Spika, kuanzia mwaka 2013/2014 hadi2015/2016, Wizara kupitia Mfumo wa Matokeo MakubwaSasa (Big Results Now), imejiwekea malengo ya kuongezauzalishaji kwa kiasi cha mahidi tani 100,000 na mchele tani290,000 katika mashamba mapya ya wakulima wakubwana wadogo. Kwa wakulima wadogo, katika mwaka wa2013/2014, Serikali itatumia shilingi bilioni 91.5 kugharimiaruzuku ya pembejeo za mazao zikiwemo mbolea, mbegu,miche na viatil ifu. Aidha, lengo la Wizara yangu nikuwawezesha wakulima kuzalisha chakula kwa wingi nakuwaruhusu kuuza ziada ya mazao ndani na nje ya nchibila vikwazo vyovyote.

Page 11: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

11

6 JUNI, 2013

SPIKA: Mheshimiwa Mlata, swali la nyongeza.Naomba msimame kidogo; Mheshimiwa Mlata endelea,lakini ninyi wengine simameni kidogo.

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Spika,ahsante. Nashukuru kwa majibu mazuri ambayo amenipatiaMheshimiwa Waziri.

(i) Ni kweli katika tani alizozitaja, tani kumi zamtama ndizo zilizokuja kwenye Mkoa wa Singida, lakini alizetizilikuwa tani nane tu na mbolea ya Minjingu ilikuwa tani 63.Hatukuweza kupata ruzuku kwenye mazao ya mahindi,ambayo mahindi ni zao la biashara la pili katika Mkoa waSingida na Zao la Mpunga ambalo linalimwa kwa wingi sanakule Mgungira. Sasa napenda kujua kama Serikaliinatambua kwamba, kuna kituo ambacho kinazalishambegu bora ambacho kipo Mpambaa Mtinko ili wawezekukiingiza katika utaratibu wa kutoa ruzuku na Mkoa waSingida uweze kupata ruzuku ya mahindi?

(ii) Kwa nini Serikali inakataza mazao mengineyasilimwe katika Mkoa wa Singida na hali mazao mengineyakiwa yanalimwa; kwa mfano mahindi; kwa nini isiachemahindi pia yakalimwa kama zao la biashara? Ahsante.

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili yaMheshimiwa Mlata, kama, ifuatavyo:-

Kwanza, kama nilivyosema, mazao yote haya,mahindi na mpunga, yanaweza yakawa ya chakula nawakati huo huo yakawa ya biashara mradi tu uzalishe ziadana yauzwe nje. Sasa kuhusu kwa nini mazao fulanihayaruhusiwi na mengine yanaruhusiwa. Katika nchi hiitunakwenda na agro-ecological zones. Mikoa ya Kati,mvua zake siyo nzuri, lakini hata hivyo, katika Mikoa hii nahususan Mikoa wa Singida, yapo maeneo mengineyanayopakana na Mkoa wa Singida, ambayo mvua zakeniyo nzuri. Sisi tunachokifanya ni kuangalia pale ambapomvua siyo nzuri, basi tunasema walime mazao ambayo

Page 12: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

12

6 JUNI, 2013

yanaweza kustahimili ukame. Ninakubaliana na MheshimiwaMlata kwamba, yapo maeneo katika Mkoa wa Singida,ambayo mvua zake ni nzuri na kwa kweli hatuna sababu yakusema kama mvua ni nzuri katika maeneo fulani basituwazuie kabisa. Kuhusu hicho kituo, nitatuma wataalamuwatakwenda pale watakitazama, kwa sababu vituo vyoteviko chini.

Mheshimiwa Spika, labda nimalizie tu kwa kusemakwamba, Mkoa wa Singida ni mmoja wa mikoa ambayohaikupatwa na kashfa yoyote ile katika ubadhirifu wapembejeo. Kwa hiyo, namshukuru sana Mheshimiwa Mlata,kwa kufuatilia suala hili.

SPIKA: Ahsante, Mheshimiwa Kayombo!

MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Kwa kuwa takwimu zinaonesha kwamba,mara Serikali ilipoanza kutoa ruzuku kwenye mazao haya,uzalishaji katika mazao haya umeongezeka sana na kwahiyo, wakulima hasa wa Mkoa wa Ruvuma kwenye Zao laMahindi wanapata matatizo ya soko.

Je, Serikali haioni kwamba wakati sasa umefika wakufikiria kutoa ruzuku kwa ajili ya kununua mashine zakukoboa na kusaga haya mahindi ili wale wakulima wawezekuuza unga badala ya kuuza mahindi?

SPIKA: Hakulielewa swali naomba urudie!

MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO: Kwa kuwa huumfumo wa ruzuku umeonesha matokeo mazuri kwa maanaya ongezeko la mazao hasa ya mahindi:-

Je, Serikali haioni kwamba, wakati umefika sasa wakutoa ruzuku ya fedha kwa wakulima hawa hasa wa kuleMbinga, Songea na Namtumbo, kwa ajili ya kununuamashine za kukoboa na kusaga hayo mahindi ili wawezekuuza unga badala ya kuuza mahindi? (Makofi)

Page 13: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

13

6 JUNI, 2013

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la MheshimiwaKayombo, kama ifuatavyo:-

Kwa sasa tunatoa ruzuku kwa ajili ya pembejeo,hata ruzuku yenyewe ya pembejeo haijawatosha wakulimaambao tunawalenga. Sasa tukiingia kwenye kutoa ruzukuya fedha kununulia mashine, bado muda huo utakuwahaujafika. Ninachoweza kusema tu ni kwamba, tunautaratibu mzuri tu wa kuwasaidia wakulima ili kujipatiamashine kama hizi anazozisema Mheshimiwa Kayombo.Tunao Mfuko wa Pembejeo ambao unakopesha wakulimafedha kwa riba nafuu, kiasi cha asilimia saba kwa mwaka,unaweza kujipatia fedha hizo ukanunua mashine zakukoboa mahindi au kukamua mafuta ya alizeti. Kwa hiyo,namshauri Mheshimiwa Kayombo na Wabunge wote,tutumie fursa hii, uko Mfuko huu, iko pia Benki ya TIB, zotezinatoa fursa hizi za kukopesha wakulima kujipatia fedhakwa ajili ya usindikaji wa mazao.

MHE. KURUTHUM J. MCHUCHULI: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Katika Mwaka wa Fedha wa 2013/14, Serikaliimekuja na utaratibu mpya wa kukopesha pembejeokwenye vikundi hususan kwa vijana; na kwa kuwa tunajuahali ya hewa wakati mwingine inaweza ikawa mbaya, vijanawakalima lakini hawapati mafanikio. Wakati huo huowanakuwa wanadaiwa ule mkopo. Sasa; je, Serikali inamkakati gani au imeandaa utaratibu gani kama vile kuwana bima kwa vijana hawa wanaokopa mkopo kupita CRDBili wasije wakapata matatizo badala ya kuinuliwa kiuchumi?

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la MheshimiwaMchuchuli, kama ifuatavyo:-

Kwanza, utaratibu huu mpya wa mikopo, tumesemanao bado haujawa sahihi kabisa, kwa sababu vikundivyenyewe havijulikani kwa uhakika katika nchi nzima. Katikamaeneo vipo, kwa hiyo, tumesema tuaanza na maeneoyale tu ambayo vikundi vinajulikana kwa uhakika na

Page 14: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

14

6 JUNI, 2013

vinakopesheka. Sasa kuhusu kinga kwamba, imetokeadharura kama hiyo; nadhani hilo ni suala zuri na ndiyo maanahata kwa upande wa mazao tumesema tutakuja nautaratibu wa price stabilisation fund yanapotokeamatatizo kama hayo. Jambo hili nadhani ni zuri, miminalichukua, tunatakiwa kulijadili pamoja na vyombovinavyohusika, kuweka kinga kama hizo, bima ya mazao.Nadhani ndungu zangu linajadilika hili, ni wazo zuri.

MH. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja lanyongeza. Katika msimu wa kilimo uliopita Wananchi waMkoa wa Manyara walilazimishwa kusainishwa vocha yambolea, ukiachilia mbali ya mbegu. Wao walihitaji Mbegulakini mawakala wakawalazimisha wasaini ya mboleaambayo hawahitaji. Walitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilayana hakuna hatua zilizochukuliwa. Naomba nifahamu kutokakwa Waziri; je, ni azma ya Serikali kushirikiana na mawakalakuwaibia Wananchi hawa?

SPIKA: Wewe Gekul kwani waliwaibia? (Kicheko)

Mheshimiwa Waziri majibu!

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la MheshimiwaGekul, kama ifuatavyo:-

Ni kweli zoezi la kutoa pembejeo kupitia vochalimekuwa na changamoto nyingi. Wapo wajanja wengi,wala siyo mawakala tu, hata baadhi ya watendaji ambaowalishiriki katika mazoezi hayo. Ninachoweza kusema nikwamba, hao ni wezi na ni waharifu kama waharifu wenginena Serikali haijashirikiana nao. Sasa niseme nimelichukua hilo.Sisi tunafanya zoezi la kuwabaini watu wote hawatuwafikishe mahakamani. Kwa hiyo, hata huko kwakoMheshimiwa nitakuja, nitawatuma na watakapobainikawatakamtwa tu wafikishwe Mahakamani.

SPIKA: Ahsante, tunaendelea na swali linalofuata,

Page 15: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

15

6 JUNI, 2013

Mheshimiwa Suleiman Nchambi Suleiman, alitakiwa kuulizalakini kwa niaba yake Mheshimiwa Mansoor!

Na. 354

Uchimbaji wa Mabwawa kwa Ajili ya Kilimo Kishapu

MHE. MANSOOR S. HIRAN (K.n.y. MHE. SULEIMAN N.SULEIMAN) aliuliza:-

Jimbo la Kishapu lina ukosefu wa mvua kwakiwango kikubwa hivyo kusababisha kilimo Jimboni humokuwa duni:-

Je, ni lini Serikali itachimba mabwawa kwa ajili yakilimo cha umwagiliaji kwa kuwa tunayo mito mikubwa?

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Suleiman N. Suleiman, Mbunge wa Kishapu,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, natambua changamotoinayowakabili Wananchi wa Jimbo la Kishapu, ukizingatiakwamba Kishapu ni moja ya maeneo ambayo yanaathiriwana ukame wa mara kwa mara unaosababisha uhaba wachakula na hivyo, Serikali kulazimika kuwapelekea chakulacha msaada. Kwa upande mwingine, Wilaya ya Kishapuinazo fursa za kuendeleza kilimo cha umwagiliaji hususankwa kuvuna maji ya mvua katika mabonde yaliyopo.

Mheshimiwa Spika, Mbunge wa Kishapu,Mheshimiwa Suleiman Nchambi, amekuwa akifuatiliauanzishaji wa Miradi ya Umwagiliaji yeye mwenyewe binafsi.Nampongeza sana kwa jitihada hiyo. Kinachotakiwa sasani kuibua miradi ya ujenzi wa mabwawa na miundombinumingine ya umwagiliaji na kuiweka katika mipango yamaendeleo ya Kilimo ya Wilaya ya Kishapu ili iweze kujadiliwa,kupitishwa na kuombewa fedha za utekelezaji.

Page 16: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

16

6 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, tayari hatua zimeanzakuchukuliwa, ambapo wataalam wa umwagiliaji kutokaOfisi ya Kanda ya Ziwa kwa kushirikiana na Wataalam waHalmashauri ya Wilaya ya Kishapu, wamekamilisha usanifuwa mabanio mawili ya Ngeme na Nyenze hekta 267, kwaajili ya utekelezaji kupitia Mradi wa DASIP (Mradi waNyenze). Aidha, natumia fursa hii kumuahidi MheshimiwaMbunge kwamba, Wataalam wa Umwagiliaji wataendeleakufanya uchunguzi wa maeneo yote yanayofaa kwakujenga mabwawa katika Halmashauri ya Wilaya yaKishapu na kufanya usanifu wa miradi hiyo ili itafutiwe fedhaza utekelezaji kutoka Serikali na katika vyanzo vingine vyafedha.

MHE. MANSOOR S. HIRAN: Mheshimiwa Spika,nashukuru. Wilaya ya Kwimba ni jirani na Wilaya ya Kishapu.Kwenye Wilaya ya Kwimba tuna Mradi wa Umwagiliaji waMahiga ambao uko chini ya Serikali Kuu. Leo una miakamitatu, huo Mradi unasuasua haueleweki unaisha lini.Naomba Waziri au Serikali itoe tamko kwamba huo Mradiutaisha lini, nauliza swali hilo kwa sababu hata Halmashauriya Wilaya haifahamu Mradi utaisha lini? Ahsante.

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la MheshimiwaMansoor, kama ifuatavyo:-

Naomba nimfahamishe kwamba, nimepata taarifaya huu Mradi wa Mahiga na kwamba unasuasua. Sasaninamuahidi kwamba, nitaufuatilia kuanzia leo hii. Nitatumawataalam wafuatilie ni nini kinausibu Mradi huu maana niwa siku nyingi, ulishapata fedha tangu miaka ya nyuma.Kwa hiyo, tuna kila sababu ya kuhakikisha kwamba, Mradihuu unakarabatiwa. Ninamhakikishia kwamba, nitafuatilia.

SPIKA: Shida yangu mmesimama wengi, wotewatasema miradi ya kwao itawezekana kweli? MheshimiwaChibulunje na Mheshimiwa Lembeli mtauliza maswali hayo.Kwanza, Mheshimiwa Chibulunje!

Page 17: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

17

6 JUNI, 2013

MHE. HEZEKIAH N. CHIBULUNJE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo lanyongeza. Kwa kuwa yapo mabwawa ya zamaniyaliyochimbwa katika baadhi ya maeneo kame hapa nchinina sasa hivi yanahitaji ukarabati. Nataka Mheshimiwa Wazirianifahamishe wana mpango gani wa kuyakarabatimabwawa haya ya zamani ili yaweze kuwa na uwezo waumwagiliji, yakiwemo Mabwawa ya Ikowa na Dabalo katikaJimbo langu la Chilonwa?

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika Ukanda huu, CentralPlateau, Mikoa ya Kati ambayo mvua zake ni za shida shida,lengo letu ni kuhakikisha kwamba, tunajikita kwenye uvunajiwa maji ya mvua kwa kujenga mabwawa. Bwawa la Ikowani mojawapo ya Mabwawa ambayo yamekuwa yanafanyakazi vizuri, lakini yanahitaji kukarabatiwa na hasa yanahitajikuongezewa tuta. Wengi wanadhani suala ni kwendakuchimbua udongo ulioko mle ndani. Kitaalam, kuondoaudongo katika bwawa lililojaa mara nyingi ni gharama kulikokutafuta eneo lingine. Kuna uwezekano pia wa kuongezatuta ili tuweze kulikarabati.

Mheshimiwa Naibu Waziri ametembelea bwawa hiliwiki iliyopita nadhani na ameliona. Kwa hiyo, nakuahidiMheshimiwa Chibulunje kwamba, Wizara yangu itafuatiliamabwawa yote haya, tuangalie uwezekano wakuyakarabati.

MHE. JAMES D. LEMBELI: Mheshimiwa Spika, kwa kuwahali ya hewa ya Wilaya ya Kishapu inafanana kabisa katikamaeneo mengi ya Kanda ya Ziwa, yakiwemo ya Wilaya yaKahama; na kwa kuwa tayari eneo la Kata ya Nyandekwakatika Jimbo la Kahama, lilishaanishwa kwamba linafaa kwakilimo cha umwagiliaji lakini Serikali bado haijaanzautekelezaji katika hilo:-

Page 18: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

18

6 JUNI, 2013

Je, ni lini Serikali itatekeleza hilo ili kuweza kuwasaidiaWananchi katika eneo hilo? Ahsante.

SPIKA: Naona mtaenda kwenu kila mtu, lakiniMheshimiwa Waziri hakujiandaa huko; Mheshimiwa Wazirilakini unajua yote, haya!

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, labda nitoe siri tu kwamba,Mheshimiwa Lembeli tumekubaliana kabisa naamenikaribisha Kahama. Sasa labda kwa faida ya watuwake ni kwamba, tutakwenda kutembelea Kahamakuangalia mabwawa na siyo bwawa tu, tunakwenda piakuangalia tatizo la tumbaku kule Kahama. Kwa hiyo,Mheshimiwa Lembeli ahadi yangu bado iko pale pale.

MHE. DAVID Z. KAFULILA: Mheshimiwa Spika,Tanzania kwa mujibu wa Economist Report ya mwaka 2011.

SPIKA: Usije ukatuhutubia, kwanza haiendi hivyo,endelea! Tunasema usituhutubie!

MHE. DAVID Z. KAFULILA: Mheshimiwa Spika,ahsante, ni swali tu. Kwa mujibu wa Ripoti ya Economist yamwaka 2011, Tanzania ni nchi ya 11 kwa mito mingi Duniani;na kwa taarifa ya hali ya maji Duniani, Tanzania ina majiyanayofaa kwa umwagiliaji kwa maana ya fresh water,zaidi ya asilimia 17 ya maji yote yanayopatikana Duniani.Hata hivyo, Tanzania ina eneo la takribani hekta milioni29,400,000 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Hizi zote nipotentials ambazo zinalifanya Taifa hili liwe mzalishajimkubwa wa kuuza nje. Ni bahati mbaya kwamba mpakasasa Tanzania inaagiza mchele kutoka nje. Naombakuiuliza Serikali; inaona aibu kiasi gani kuwa Taifa la uagizajichakula nje wakati ina fursa zote hizi?

SPIKA: Yale yale, Mheshimiwa Waziri majibu!(Kicheko)

Page 19: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

19

6 JUNI, 2013

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, akihutubia na mimi inabidi nimhutubie.

SPIKA: Mimi nitakuzuia!

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naomba kumfahamisha MheshimiwaKafulila kwamba, kwanza, naomba nimsaidie kwamba, sisiwenyewe wala siyo taarifa za economist, tumefanya utafitiwenyewe; eneo linalofaa kumwagilia katika nchi hii ni hizo29.3 million hekta, hizo ni jumla. Katika hizo, hekta milioni 2.3zinafaa sana kuliko maeneo mengine. Hekta milioni 4.8zinafaa kwa kiwango cha kati na zilizobaki 22.3 zinabakikwa kiwango cha chini. Sasa kinachotusibu hapa siyo sualala kuona aibu, ni kwamba, kujenga miradi ya umwagiliajikunahitaji fedha, miradi midogo inahitaji kwa wastani kitukama dola 2000 kwa hekta. mikubwa zaidi inakwendampaka 10,000 kwa hekta. Kwa hiyo, suala hilo ndiyolinalotuletea shida.

Tukija kwenye suala la uagizaji wa mchele, sisihatujaagiza chakula kwa muda mrefu. Mwaka huu ndiyotumeagiza mahindi Zambia na mchele. Hata hivyo,tumeagiza baada ya kuona hali ya hewa ilikuwa mbaya,tukawa na wasiwasi tusije tukajikuta Wananchi wanapatatabu kwa ajili ya mfumko wa bei. Kwa hiyo, tumefanya hivyotu kwa ajili ya kujikita kupambana na mfumko wa beiunaoweza kujitokeza. Kwa miaka mitatu, mine, mfululizo,Tanzania ilikuwa haiagizi kabisa chakula.

SPIKA: Swali la mwisho, Mheshimiwa Cheyo!

MHE. JOHN M. CHEYO: Mheshimiwa Spika, ahsantesana kwa kuniona. Kwa kuwa tuna mabwawa mbalimbali;kwa mfano, Nkoma tuna Bwawa na tuna Ziwa Victoriaambalo linatumika sana Misri na ndugu yangu kule nayeanajenga Bwawa la Kasori; ni lini tutapelekewa Wataalamwa kuweza kupima Miradi ya Umwagiliaji kwa kutumia majiya mabwawa na Ziwa Victoria?

Page 20: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

20

6 JUNI, 2013

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la MheshimiwaCheyo, kama ifuatavyo:-

Wataalam katika Kanda ya Ziwa; tumegawanyanchi hii katika Kanda za Umwagiliaji, Kanda ya Ziwainahudumiwa na Ofisi ya Umwagiliaji ya Kanda ya Ziwa,ambayo Makao Makuu yako pale Mwanza nawanaendelea kufanya upembuzi na utafiti kuangaliamabwawa na mito iko wapi, lakini kwa kushirikiana naHalmashauri za Wilaya.

Miradi lazima iibuliwe na Halmashauri, lakini natakatu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Wataalamhao wataendelea kufanya zoezi hili na hivi sasa wako katikautaratibu wa kuangalia namna bora ya kutumia maji yaZiwa kwa kutumia nishati mbadala, kwa sababu yaleunaweza ukayachukua kwa kutumia solar energy, windenergy, halafu ukamwagilia maeneo ambayo yako pembenimwa Ziwa. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge, hili tunaendeleakulifanyia kazi.

SPIKA: Tuendelee na swali la mwisho.

Na. 355

Uzalishaji Duni Katika Kilimo

MHE. RASHID ALI ABDALLAH (K.n.y. MHE. RUKIAKASSIM AHMED) aliuliza:-

Licha ya kuwa na ardhi kubwa na yenye rutubanchini, wakulima wengi huzalisha magunia manane kwaekari moja, wakati kihalisia ekari moja huzalisha magunia80:-

Je, Serikali inafanya maandalizi gani kwa wakulimaili waweze kuzalisha kwa tija na hivyo kuondokana naumaskini uliokithiri?

Page 21: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

21

6 JUNI, 2013

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Waziri, leo umepatikana.(Kicheko)

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali laMheshimiwa Rukia Kassim Ahmed, naomba nisahihishekidogo, kwa faida yake tu kwamba, figures zile alizowekaza magunia 80 kwa ekari, mimi pamoja na utaalam wangu,kwa miaka yangu yote, nikipiga hesabu inakuja kwenyeuzalishaji wa tani 17 mpaka 20 kwa hekta, sidhani kamaziko mahala popote.

Baada ya kusema hayo, naomba kujibu swali laMheshimiwa Rukia Kassim Ahmed, Mbunge wa Viti Maalum,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwakuwapongeza wakulima kwa jitihada kubwa wanayofanya,kuzalisha chakula tunachokula katika nchi hii. Ni kwelikwamba, bado kuna haja ya kuongeza tija na uzalishajiwa mazao ya kilimo ili kufikia Mapinduzi ya Kijani. Ili kufikialengo hilo, kazi zinazotekelezwa ni pamoja na kupanuakilimo cha umwagiliaji, kuhamasisha matumizi ya pembejeobora, kuongeza uzalishaji wa mbegu bora, kuimarisha utafitina huduma za ugani, ukaguzi wa madawa ya kilimo nambegu, kutoa mafunzo kwa wakulima, kuhamasishamatumizi ya zana za kilimo na kuimarisha udhibiti wavisumbufu vya mimea.

Mheshimiwa Spika, utaratibu wa Serikali wa kutoapembejeo zenye ruzuku umeanza kuonesha mafanikiomazuri, ambapo uzalishaji wa mazao umeanza kuongezeka.Kwa mfano, uzalishaji wa mahindi kwa miaka mitatu iliyopitaumeongezeka kutoka wastani wa tani 1.2 kwa hekta haditani 4.5 kwa hekta, wakati mpunga umechupa kutokawastani wa tani 1.8 kwa hekta hadi zaidi ya tani 4.5 kwahekta.

Pamoja na mafanikio hayo, Serikali inafanya juhudi

Page 22: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

22

6 JUNI, 2013

kuhakikisha kwamba, matumizi ya pembejeo hususanmbolea, yanaongezeka kwa sababu takwimu tulizonazozinaonesha kwamba, matumizi yetu ya mbolea bado yakochini; ni takribani kilo kumi tu kwa hekta, ikilinganishwa nakilo 21 kwa hekta katika nchi ya Malawi, kilo 51 kwa hektakatika nchi ya Afrika Kusini na nchi nyingine kama Hollandimefikia mpaka zaidi ya kilo 500 kwa hekta. Jitihadazinazofanywa ni pamoja na kuhamasisha sekta binafsikuzalisha na kuingiza mbolea nchini pamoja na kuanzishaviwanda vya kuzalisha mbolea.

MHE. RASHID ALI ABDALLAH: Mheshimiwa Spika,pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, naombakuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

(i) Wakulima wanalalamika sana kwamba,pembejeo hazifiki kwa wakati na hili ndilo linalofanyakupungua kwa uzalishaji. Je, Serikali iko tayari kutoa kaulisasa kuhakikisha kwamba mbolea zinafika kwa wakati kwawakulima?

(ii) Kwa mujibu wa takwimu alizotupa ni kwambaTanzania sasa inatumia kilo kumi kwa hekta na hiiinapunguza sana uzalishaji, wakati nchi za wenzetu zimezidizaidi ya kilo 50 kwa hekta. Mheshimwia Waziri haonikwamba kufanya hivyo ni kudhoofisha ile dhana nzima yaKILIMO KWANZA?

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Kwanza, kuhusu suala la pembejeo kutofika kwawakati, tumekuwa tunajibu hatua tunazozichukua ilikuhakikisha pembejeo zinafika. Moja ya changamototulizokuwa tunazipata huko nyuma, ni utaratibu wa Bajetiya Serikali (Budget Cycle). Tulikuwa tunamaliza msimu aubajeti mwezi wa nane, ndipo fedha zianze kutoka. Kwahiyo, tatizo la uchapishaji wa vocha, uagizaji wa mbolea,

Page 23: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

23

6 JUNI, 2013

lilikuwa pia linatuathiri katika mfumo mzima wa mtiririko wapembejeo. Sasa huu utaratibu wa budget cycle tuliouanza,tunamaliza June, come July, tunaamini kwamba, sasatutakuwa tunapata fedha mapema; na imani yangu nikwamba, kutakuwa na mabadiliko katika ufikishwaji wapembejeo kwa wakulima.

Mheshimiwa Spika, kuhusu matumizi madogo yavirutubisho, kilo kumi kwa hekta; ni kweli nimeziweka hizifigures makusudi kwa sababu huko nyuma tulikuwatunatumia kilo nane tu. Sasa baada ya kuweka taratibuhizi za ruzuku ndiyo tumepanda mpaka kumi na ndiyomaana tumeweka utaratibu huu sasa wa kwamba,tuhakikishe tunazalisha mbolea kwa wingi, tutumie rasilimalizetu, Minjingu Rock Phosphate, Gesi iliyopo, viwandavihamasishwe vijengwe, tupate mbolea nyingi ili tuwafikiehao wenzetu na kwa kweli wamefikia kwenye greenrevolution kwa matumizi makubwa ya mbolea. Kwa hiyo,lengo siyo kudhoofisha, lengo ni kwenda huko ambakowenzetu wamefika.

MHE. JENISTA J. MHAGAMA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru, nina swali dogo la nyongeza. Kwa kuwaSerikali ilitangaza kuwa msimu huu itabadilisha mfumo wakutoa pembejeo na baadaye wakasema kwamba,haitabadilisha mfumo utabaki uleule wa mwaka jana; nakwa kuwa Wananchi wameanza kulalamika, hawaelewisasa ni mfumo gani utatumika kwa mwaka huu wa kilimo,yaani wa 2013/14; je, ni kupitia mawakala ama kupitiavikundi:-

Sasa Serikali inatoa tamko gani kwa wakulima iliwaweze kujiandaa vizuri kama ni kwa vikundi wajiwekekwenye vikundi, kama ni kwa mawakala wawatafutemawakala ambao ni waaminifu ili tusijichanganye msimuwa kilimo utakapofika? (Makofi)

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza laMheshimiwa Jenista Mhagama, kama ifuatavyo:-

Page 24: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

24

6 JUNI, 2013

Tarehe 28 na 29, tulikuwa na Semina hapa Dodoma,ambayo ilikuwa inajadili mfumo wa usambazaji wa ruzukuya pembejeo, walihudhuria Wakuu wa Mikoa, Wakuu waWilaya na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge.Tulichokubaliana ni kwamba, tukisema mfumo wa kutumiavikundi ndiyo tu utumike, bado kuna wengine wataathirika,kwa sababu kuna mahali pengine vikundi hivyo havipo.Kuna mahali pengine ukisema vikundi, ndiyo vinaibuka sikuhiyo hiyo na mfumo wa vikundi pia unahitaji mabenki nayoyavitambue, mabenki yanataka vikundi vyenye taratibuvinavyoweza kulipa vyenye bank statements.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tulichokubaliana kwakifupi ni kwamba, mifumo yote itatumika, yale maeneoambayo utaratibu wa vocha uligubikwa na changamotonyingi za wizi na nini, hao tutawaangalia kivyao. Waleambao walifanya vizuri zaidi nao tutawaangalia kivyao.

Mheshimiwa Spika, kwa kifupi tu ni kwamba, wiki hiitutatoa maelezo kwamba, ni Mikoa ipi itatumia utaratibuwa vocha, kulingana na mfumo uliotumika mwaka jana.Pia tuna sababu ya kurejea utaratibu wa vocha kwasababu tunazo fedha za World Bank, takribani shilingi bilioni19, fedha hizi zinatakiwa zitumike kwa utaratibu wa vochamaana ndiyo masharti yao. Kwa hiyo, kwa maeneo ambayoyalifanya vizuri, tutatumia utaratibu wa vocha.

Wale ambao vikundi vipo imara, kama kule kwaMheshimiwa Jenista Mhagama, ninaamini tutakwenda nautaratibu wa mikopo kwa vikundi. Kwa hiyo, mifumo yoteitakwenda sambamba. (Makofi)

MHE. DUNSTAN L. KTANDULA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa furasa hii. Kwa kuwa matumizi boraya rasilimali ardhi ni msingi muhimu katika mapinduzi ya kilimo;na kwa kuwa Sekta ya Ufugaji wa Samaki imeonekana ndiyosekta inayokua zaidi kuliko sekta yoyote ya uzalishaji wachakula. Je, Wizara ya Kilimo ipo tayari sasa kutoa agizokwamba pale tutakapoanzisha skimu yoyote ya umwagiliajiiende sambamba na ufugaji wa samaki? (Makofi)

Page 25: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

25

6 JUNI, 2013

SPIKA: Mheshimiwa Waziri, swali zuri hilo.

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali zuri sana hilokwamba, kwa kweli hiyo sasa ndiyo integrateddevelopment katika kilimo na wala siyo jambo geni.Mahala pengine ukienda Mikoa kama ya Kilimanjaroambako nimefanya kazi sana, tulikwishaanza kufanyautaratibu huo, ambapo Miradi yote ya Umwagiliaji,inawekewa pia mabwawa ya samaki pembeni na siyosamaki tu, samaki na juu wanaweka chanja za kufugiamifugo mingine kama bata. Kwa hiyo, inawiana; batawanatoa kinyesi kinasaidia samaki wanakula, maji yaumwagiliaji yanakwenda kwenye samaki, kwa hiyo, inakuwamlishano.

Mimi nakubaliana naye, ni suala ambalo tunatakiwakulifanyia kazi kwa kushirikiana kwa karibu na Wizara yaMifugo na Uvuvi na Halmashauri za Wilaya, tunapoibuaMiradi yote hii; na kwa njia nyingine itatupunguzia gharamakwamba kila mradi utenge fedha zake, maana mvuviatenge fedha za uvuvi, kumbe maji ya umwagiliaji yakohapo hapo. Mimi nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge,hili ni wazo zuri sana.

SPIKA: Mheshimwa Leticia Nyerere, swali la mwisho.

MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Ukosefu wa chakula nchini husababishwaama kwa sababu ya ukosefu wa mvua, yaani ukame aukwa sababu ya ongezeko kubwa la mvua za kupindukiakama iliovyotokea kule Wilayani kwetu Kwimba. Je, Serikaliinatoa elimu kwa kiwango gani kuhusu tabia nchi, yaaniclimate change ili tuweze kuepukana na njaa za mara kwamara nchini?

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la MheshimiwaLeticia Nyerere, kama ifuatavyo:-

Page 26: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

26

6 JUNI, 2013

Elimu kwa wakulima kuhusu tabia nchi ni sehemumojawapo ambayo tumeijenga katika Miradi yetu. Sasahivi kila Mradi unaoanzishwa, una kipengele cha mamboya mazingira na hilo ni suala mojawapo na hakuna hatamradi mkubwa sasa hivi unaoweza ukauanzisha bilakwanza kupitia masuala mtambuka haya ya mazingira. Kwasababu hiyo, ndani ya Serikali, katika Ofisi ya Makamu waRais, chini ya Mheshimiwa Huvisa, kipo Kitengo Maalum chaMasuala ya Mazingira na mojawapo ni kutoa elimu yamasuala kama hayo. Ndani ya Wizara yangu pia kunaKitengo cha Mazingira, kwa hiyo, labda tu tuseme tuachesuala hili liendelee kupata hamasa kubwa ili Wananchiwapate uelewa huu.

SPIKA: Ahsante. Waheshimiwa uhuru mlionao huusiyo wa kawaida, kwa hiyo, kinachotakiwa ni kuuliza maswalimafupi na wanaojibu wajibu kwa kifupi, kusudi tuwe nawachangiaji wengi, lakini hatuwezi kuendelea tu. (Makofi)

Nina matangazo mawili tu. Kwanza kabisa, Katibuwa Wabuge wa CHADEMA, Mheshimiwa David ErnestSilinde, anaomba niwatangazie Wabunge wa CHADEMAkuwa, leo baada ya kusitisha shughuli za Bunge saa saba,watakuwa na kikao chao katika Ofisi ya Kiongozi waUpinzani. Hii ni baada ya kuahirisha kikao humu ndani, saasaba.

Ofisi pia inawatangazia Waheshimiwa Wabungekwamba, kwenye Viwanja vya Maonesho vya Bunge, kunaMaonesho ya Meza za Maabara ya Shule, yaani ScienceKit and Mobile Laboratory Science Table, yanaoneshwana Kampuni ya Worldwide Education Care. Maonesho hayayataanza leo tarehe sita na hivyo Wabunge wapite nakuona ili wapate fursa ya kuzisaidia shule zao kwa kupataushauri juu ya matumizi ya vifaa hivyo muhimu. Mpite tumkaangalie hayo mambo ya kisayansi yako pale.

Baada ya kusema hayo, Waheshimwia Wabunge,tunaendelea.

Page 27: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

27

6 JUNI, 2013

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2013/2014Wizara ya Fedha

SPIKA: Kabla hatujaendelea, nina tangazo; wenginewanaleta vikaratasi bila kuchapwa ndiyo maana Spikaanasahau. Nimeombwa na Katibu wa Wabunge wa CCMkwamba, niwatangazie Waheshimwa Wabunge wa CCMleo saa saba mchana kutafanyika Kikao cha Chama katikaUkumbi wa Pius Msekwa.

Mheshimiwa mtoa hoja!

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika naWaheshimiwa Wabunge wote, kufuatia taarifailiyowasilishwa hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati yaKudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara,naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu likubalikupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba nichukuefursa hii kutoa pongezi zangu za dhati kwako pamoja naNaibu Spika, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai (Mbunge waKongwa), Waheshimiwa Wenyeviti; Jenista JoakimMhagama (Mbunge wa Peramiho), Mussa Azzan Zungu(Mbunge wa Ilala) na Muhammed Seif Khatib (Mbungewa Uzini), kwa kuongoza vyema majadiliano ya Bunge laBajeti.

Mheshimiwa Spika, naomba nitumie nafasi hiikuishukuru kwa namna ya pekee, Kamati ya Kudumu yaUchumi, Viwanda na Biashara chini ya Mwenyekiti wake,Mheshimiwa Mahmoud Hassan Mgimwa (Mbunge waMufindi Kaskazini) na Makamu wake, Mheshimiwa DunstanLuka Kitandula (Mbunge wa Mkinga), kwa maoni, ushaurina mapendekezo waliyoyatoa kwa Wizara wakati wakuchambua mapendekezo ya Bajeti ya Wizara ya Fedha.Aidha, nachukua nafasi hii kumshukuru Mwenyekiti wa

Page 28: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

28

6 JUNI, 2013

Kamati ya Kudumu ya Bajeti, Mheshimiwa Mtemi Andrew JohnChenge, Mbunge wa Bariadi Mashariki, pamoja na Kamatinzima kwa ushauri wao makini. Katika uandaaji wa Hotubahii, Wizara imezingatia ushauri na mapendekezo ya Kamatihizo pamoja na ushauri na maoni ya hoja mbalimbalizilizotolewa wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara kwamwaka 2012/2013.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kutumia fursa hiikuwashukuru Naibu Mawaziri; Mheshimiwa Saada MkuyaSalum (Mb) na Mheshimiwa Janeth Zebedayo Mbene (Mb).Aidha, napenda kutoa shukrani za dhati kwa Wakuu waIdara na Vitengo, Wafanyakazi wa Wizara ya Fedhawakiongozwa na Katibu Mkuu, Ndugu Ramadhan M. Khijjahna Naibu Makatibu Wakuu; Dkt. Servacius B. Likwelile,Ndugu Elizabeth J. Nyambibo na aliyekuwa Katibu MkuuMsaidizi, Ndugu Laston T. Msongole aliyestaafu hivi karibuni,kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kusimamia utekelezaji wamajukumu ya Wizara. Vilevile, napenda kuwashukuruProfesa Benno Ndulu, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,Ndugu Harry Kitilya, Kamishna Mkuu wa Mamlaka yaMapato Tanzania (TRA), Dkt. Albina Chuwa, MkurugenziMkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu pamoja na Wakuu waTaasisi na Wakala wa Serikali chini ya Wizara kwa michangoyao katika kuboresha utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

Mheshimiwa Spika, mapitio ya utekelezaji wampango na bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha wa2012/2013 na malengo ya mwaka 2013/2014. Uandaaji,utekelezaji na usimamizi wa Mpango na Bajeti ya Wizara,unazingatia mambo yafuatayo: Malengo ya Maendeleoya Milenia 2015; Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka2025; Awamu ya Pili ya Mkakati wa Kukuza Uchumi naKupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA II); Vipaumbelevilivyoainishwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifawa Miaka Mitano wa mwaka 2011/2012 - 2015/2016; Ilaniya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010; Mkakati wa Pamojawa Misaada Tanzania (MPAMITA); Mwongozo wa Mpangona Bajeti wa mwaka 2013/2014 - 2015/2016; pamoja na

Page 29: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

29

6 JUNI, 2013

Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma -Public Finance Management Reform Programme (PFMRP).

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2012/2013, Wizara iliandaa mpango unaolenga kutekelezayafuatayo: Kuongeza mapato ya ndani kufikia uwiano waPato la Taifa wa asil imia 18 kwa mwaka 2012/2013ikilinganishwa na asilimia 16.9 kwa mwaka 2011/2012;kufanya mapitio ya Mkakati wa Pamoja wa MisaadaTanzania (MPAMITA); kuandaa Mwongozo wa Mpango naBajeti; kufuatilia matumizi ya fedha za Serikali; kufanyauchambuzi wa mawasilisho ya Bajeti za Wizara, Idarazinazojitegemea, Taasisi, Wakala, Mikoa na Mamlaka zaSerikali za Mitaa; kutoa Kitabu cha Bajeti Toleo la Wananchi- Citizen’s Budget; kujenga uwezo wa uandaaji na usimamiziwa Bajeti ya Muda wa Kati pamoja na utoaji wa taarifa zautekelezaji kwa wakati; kusimamia na kuimarisha uendeshajina uunganishaji wa Mfumo wa Malipo wa Serikali -Intergrated Financial Management System (IFMS);kuimarisha usimamizi na utoaji wa taarifa mbalimbali zafedha; kuendelea na ukaguzi wa miradi ya maendeleo nakutoa ushauri wa kitaalam kwa watekelezaji wa miradi hiyo;na kuhakikisha sheria za ununuzi wa umma na fedha zaumma zinazingatiwa katika utekelezaji wa Bajeti ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, Wizara piailipanga kuratibu utekelezaji wa MKUKUTA Awamu ya Pili;kuimarisha utaratibu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma naBinafsi - Public Private Partinership (PPP) ili kupanua fursaza kuchangia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo;kuendelea kusimamia utendaji wa Mashirika ya Umma naTaasisi za Serikali; kuendeleza kada za Uhasibu, Ukaguzi waNdani, Ugavi, Uchumi, Uhakiki Mali, Watakwimu, Usimamiziwa Fedha na Wataalamu wa TEHAMA; kuendelea kuhuishaDaftari la Mali ya Serikali; kuongeza upatikanaji wa hudumaza kifedha; na kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradichini ya Mpango wa Millenium Challenge AccountTanzania (MCA-T). Pamoja na hayo, Wizara pia ilipangakutathmini mzunguko wa Bajeti (Budget Cycle) nakuwasilisha Serikalini mapendekezo yake.

Page 30: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

30

6 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012, Pato la Taifaliliendelea kuimarika na kufikia ukuaji wa asilimia 6.9ikilinganishwa na asilimia 6.4 mwaka 2011, ikiwa ni zaidi yalengo la asilimia 6.8 mwaka 2012. Sekta ya Fedha ambayoinasimamiwa na Wizara ya Fedha ilichangia katika shughuliza kiuchumi na kukuza Pato la Taifa. Katika mwaka 2012,Sekta hii ya Fedha ilichangia asilimia 1.8 ya Pato la Taifa,ikilinganishwa na asilimia 1.7 ya mwaka 2011. Ongezeko hilila ukuaji lilitokana na utekelezaji madhubuti wa Programuya Maboresho ya Sekta ya Fedha.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho cha mapitio,Wizara pia ilitekeleza Sera ya Fedha na bajeti kwa lengo lakupunguza ukwasi na mfumuko wa bei ambapo Benki Kuuya Tanzania iliongeza mauzo ya fedha za kigeni katika Sokola Fedha kama njia mojawapo ya kudhibiti mfumuko wabei. Aidha, Benki Kuu ya Tanzania ilipandisha kiwango chachini cha akiba ya amana za Serikali katika mabenki kutokaasilimia 30 hadi asilimia 40 pamoja na kupunguza kiwangocha kuhodhi fedha za kigeni kulingana na mitaji yao kwamabenki kutoka asilimia 10 hadi asilimia 7.5 kuanziaDesemba, 2012. Hatua hizo zilisaidia kupunguza kiwangocha mfumuko wa bei kutoka asilimia 18.7 mwezi Aprili, 2012hadi asilimia 9.4 mwezi Aprili, 2013 pamoja na kusaidiakuimarika kwa kiwango cha ubadilishaji wa shilingi dhidi yaDola ya Kimarekani. Aidha, katika kuimarisha usimamizi namaendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara imerekebishamuundo wake (Organisational Structure), kwa kuanzishaIdara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha – Financial SectorDevelopment Division ambayo itasimamia Sera za Sektaya Fedha na taasisi ndogo za fedha kama SACCOS naVICCOBA.

Mheshimiwa Spika, Wizara iliendelea kusimamiauandaaji na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya Matumizi yaKawaida na Miradi ya Maendeleo. Wizara imeratibumaboresho ya uandaaji wa bajeti ya 2013/2014 kwakuzingatia mzunguko mpya wa bajeti (New Budget Cycle).Aidha, Mwongozo wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka waFedha wa 2013/2014, uliandaliwa kwa kushirikisha wadau

Page 31: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

31

6 JUNI, 2013

mbalimbali na kusambazwa kwa wakati. Vilevile, Wizaraimeandaa na kusambaza nyaraka muhimu za bajetiambazo ni pamoja na Vitabu vya Bajeti ya Serikali (VolumeI, II, III na IV kwa mwaka 2012/2013) kama vilivyopitishwa naBunge lako Tukufu na kitabu kinachotoa maelezo ya Bajetiya Serikali katika kipindi cha muda wa kati kwa mwaka2012/2013 - 2014/2015. Kitabu hiki kinasaidia kuwajulishaWananchi na wadau wengine kuhusu matokeo yautekelezaji wa bajeti ya mwaka uliopita pamoja namwelekeo wa bajeti ijayo kwa kipindi cha muda wa kati.Kadhalika, katika kuboresha uelewa wa Bajeti ya Serikalikwa Wananchi, Kitabu cha Bajeti Toleo la Wananchi kwamwaka 2012/2013 kimeandaliwa na kusambazwa kwawakati na kuwekwa kwenye tovuti ya Wizara. Kitabu hikikimesaidia kueleza bajeti kwa Wananchi wa kawaida kwalugha rahisi na hivyo kuongeza uwazi katika kutoa taarifamuhimu za kibajeti.

Mheshimiwa Spika, katika kujenga uwezo wakuandaa mipango na bajeti kwa Wizara, Idarazinazojitegemea, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa,Wizara ilitekeleza mambo yafuatayo: Kufanya tathmini yamchakato wa bajeti ya 2012/2013 kuhusu namna bajetiilivyoandaliwa, changamoto zinazojitokeza na jinsi yakuzitatua; kuwajengea uwezo Maofisa wa Bajeti wa Wizara,Idara, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaakuhusu kuandaa bajeti ya 2013/2014, maboreshoyaliyofanywa kwenye Mfumo wa Kugawa Fedha za Bajeti -Strategic Budget Allocation System (SBAS) na kuandaabajeti inayozingatia utendaji - Performance BasedBudgeting; na kuhuisha Mwongozo wa kuandaa mipangona bajeti, ambao umezingatia mzunguko mpya wa bajeti.Wizara imeendelea kuandaa na kusimamia malipo yamishahara ya kila mwezi kwa aji l i ya Wizara, IdaraZinazojitegemea, Taasisi na Wakala wa Serikali, Mikoa naMamlaka za Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Wizara inatarajia kutekeleza yafuatayo:Kuendelea kusimamia na kufuatilia uandaaji na utekelezaji

Page 32: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

32

6 JUNI, 2013

wa Bajeti ya Serikali; kupitia mifumo na taratibu zinazotumikakatika uandaaji wa mpango na bajeti pamoja na ufuatiliajiwa utendaji i l i kuongeza ufanisi katika uandaaji nautekelezaji wa bajeti; na kuziwezesha Wizara, Mikoa naMamlaka za Serikali za Mitaa kuandaa mipango na bajetizake zinazoendana na miongozo ya mipango na bajeti yataifa. Aidha, Wizara itaanza kutekeleza mkakati wakuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi zaSerikali kutoa taarifa za kila mwezi za malipo ya mishaharakwa Watumishi wa Serikali katika vituo vyao vya kazi.

Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuboreshausimamizi wa misaada na mikopo ili kupata matokeotarajiwa. Mafunzo ya mfumo wa kutunza takwimu nakumbukumbu zingine za misaada na mikopo yalitolewa kwaMaafisa kutoka Wizara 21 na Washirika wa Maendeleowapatao 20. Aidha, mapitio ya utekelezaji wa Mkakati waPamoja wa Misaada Tanzania (MPAMITA), 2006 – 2011wenye lengo la kuimarisha usimamizi wa misaada,yalifanyika.

Mheshimiwa Spika, Wizara ilifanikisha kusainiwa kwamikataba mbalimbali ya misaada na mikopo nafuu kutokakwa Washirika wa Maendeleo na mikopo ya kibiasharakutoka katika mabenki kwa ajili ya miradi mbalimbali yamaendeleo ikiwemo ujenzi wa vinu viwili vya kusafisha gesiasilia Mtwara na Songosongo; ujenzi wa bomba kubwa lagesi kutoka Mtwara kupitia Somanga - Fungu mpaka Dares Salaam; upembuzi yakinifu kwa ajili ya ukarabati wa Reliya Tanzania Zambia (TAZARA); na fedha kwa ajili yakutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Kilimo.

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha usimamizi wamisaada na mikopo ya kibajeti, Wizara iliandaa mkutanowa Mwaka wa Mapitio ya Misaada na Mikopo ya Kibajeti- General Budget Support Annual Review uliofanyika mweziNovemba, 2012. Matokeo yaliyotokana na Mkutano huoni Washirika wa Maendeleo kuipatia Serikali misaada yakibajeti yenye thamani ya shilingi bilioni 1,163.13, fedhaambayo imepangwa kutumika katika bajeti ya 2013/2014.

Page 33: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

33

6 JUNI, 2013

Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo(Development Partners), imeimarisha Mfumo wa Mapitioya Matumizi ya Umma - Public Expenditure Review (PER)kwa kuanzisha sekretarieti ya pamoja yenye wajumbe waupande wa Serikali na upande wa Washirika waMaendeleo pamoja na kuandaa Mpango Kazi wa mwaka.

Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014, Wizara inatarajia kukamilisha Mfumo mpya waUshirikiano wa Kimaendeleo - Development CooperationFramework kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo.Mfumo huu ndiyo utakaoongoza usimamizi wa Misaada naMikopo ya Kibajeti katika kutekeleza mipango na programuza kitaifa za kukuza uchumi, kupunguza umaskini na kuletamaendeleo. Aidha, Wizara itaendelea kutoa mafunzo yaMfumo wa Kutunza Kumbukumbu za Misaada na Mikopo(Aid Management Platform) kwa Wizara, Idara, Taasisi zaSerikali na Asasi za Kiraia. Vilevile, Wizara itaendelea nautaratibu wa kuandaa mkutano wa Mapitio ya mwaka yaMisaada na Mikopo ya Kibajeti pamoja na Mapitio yaMatumizi ya Umma.

Mheshimiwa Spika, Deni la Taifa linajumuisha mikopoya nje na mikopo ya ndani. Wizara iliendelea kusimamiaulipaji wa deni la Taifa ambapo katika kipindi cha Julai,2012 hadi Aprili, 2013 malipo yalifikia shilingi bilioni 1,666.77.Kati ya hayo malipo ya deni la nje ni shilingi bilioni 213.57 namalipo ya deni la ndani ni shilingi bilioni 1,453.20. Aidha,katika kuboresha usimamizi wa Deni la Taifa, Wizarainakamilisha uanzishwaji wa Idara ya Usimamizi wa Madeniambayo itaanza kazi mwaka ujao wa fedha, pamoja namambo mengine itakuwa na jukumu la kujenga uwezo wakufanya upembuzi yakinifu na kuhakikisha kuwa uwezo wausimamizi madhubuti wa Deni la Taifa unajengwa nakuimarishwa.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2012/2013, Wizara ilitekeleza yafuatayo: Kuboresha Mfumowa Malipo Serikalini – Integrated Financial ManagementSystem (IFMS) kutoka mfumo wa toleo la EPICOR 7.3.5

Page 34: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

34

6 JUNI, 2013

kwenda toleo la EPICOR 9.05 kwa lengo la kuongeza ufanisikatika usimamizi wa fedha za umma; kukamilisha zoezi lakutoa mafunzo ya kufanya malipo moja kwa moja benkikwa njia ya kielektroniki - Tanzania Inter-Bank SettlementSystem (TISS) kwa Watumishi wa Hazina ndogo zote, Bunge,Mikoa, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI na Idara ya Ushirika,ikiwa ni maandalizi ya kuunganisha Taasisi hizo kwenyemtandao wa TISS ili kuboresha usimamizi wa fedha za umma.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, Wahasibu200 kutoka mikoa 25 walipata mafunzo juu ya usimamizi wafedha za umma; Wahasibu 425 kutoka Wizara mbalimbalina Sekretarieti za Mikoa walipata mafunzo juu ya Viwangovya Kimataifa vya kihasibu vya kuandaa Hesabu za Serikali– International Public Sector Accounting Standards (IPSAS)na watumishi 120 kutoka katika Wizara na Taasisi walipatamafunzo ya kusimamia Mabadiliko na Kuandaa MipangoMkakati - Change Management and Strategic Planningkwa lengo la kujenga uwezo wa Idara za Bajeti naMipango katika kutekeleza maboresho ya usimamizi wafedha za umma.

Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuboreshausimamizi wa fedha za umma kwa kuendelea kutekelezaProgramu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma– Public Finance Management Reform Programme (PFMRP),ambapo Awamu ya Nne ya Programu ilianza kutekelezwaJulai, 2012 na itakamilika Juni, 2017. Programu ya PFMRPpamoja na mambo mengine, imewezesha Mamlaka zaSerikali za Mitaa kuanza kutumia akaunti sita za benkibadala ya akaunti nyingi zil izokuwepo kwa lengo lakuendelea kuboresha usimamizi wa fedha za Umma. Aidha,Programu ilitoa fedha za kuwezesha Serikali ya MapinduziZanzibar kuandaa Mpango Mkakati wake wa Programuya Usimamizi wa Fedha za Umma. Vilevile, matokeo yatathmini ya utekelezaji wa programu yalifanywa kamasehemu ya mapitio ya mwaka ya Misaada na Mikopo yaKibajeti yaliyofanyika mwezi Novemba, 2012 yalioneshakuwa utekelezaji wa Programu ulikuwa wa kuridhisha na

Page 35: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

35

6 JUNI, 2013

ulizingatia Sheria ya Ununuzi wa Umma katika kufanyaununuzi ulifikia asilimia 74.

Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea kutekelezampango kazi wa miaka mitano wa kuiwezesha Serikali Kuukuandaa hesabu kwa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu– International Public Sector Accounting Standards (IPSAS)accrual basis. Kwa mara ya kwanza, hesabu za Wizara,Idara za Serikali zinazojitegemea na Sekretarieti za Mikoakwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2013zitaandaliwa kwa kutumia viwango hivyo vya Kimataifa.Aidha, Wizara imeandaa miongozo mbalimbali na kufanyamikutano elekezi ili kuwajengea uwezo na uelewa wahasibuna wadau mbalimbali. Katika kuimarisha usimamizi wamapato na matumizi ya Serikali pamoja na utoaji wa taarifazenye ubora na uwazi, Wizara imeendelea kusimamia nakuimarisha mtandao wa malipo ya Serikali katika Wizara,Sekretarieti za Mikoa, Hazina Ndogo pamoja na Vikosi vyaJeshi.

Mheshimiwa Spika, ili kudhibiti na kusimamia mapatona matumizi, Wizara ilitoa mafunzo ya matumizi bora yamashine za kutolea VISA kwa Wahasibu waambata waBalozi zetu zote 32. Aidha, mashine hizo zil ifanyiwamatengenezo na mashine nyingine mpya ziliwekwa. Vilevile,watumishi 263 wa kada za Uhasibu, Ukaguzi wa Ndani,TEHAMA na Ugavi kutoka Wizara, Idara za Serikali,Sekretarieti za Mikoa na Serikali za Mitaa walipata udhaminikatika mafunzo ya shahada na stashahada katika vyuombalimbali vya hapa nchini ili kuendelea kujenga uwezowao katika eneo la usimamizi wa fedha.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Wizara itaendelea kusimamia, kuimarisha nakudhibiti mapato na matumizi ya fedha za Serikali kwakuboresha mtandao wa malipo wa Serikali. Aidha, Wizaraitatoa ushauri wa kitaalamu na kuunganisha Hazina Ndogona Sekretarieti za Mikoa ili kuziwezesha kufanya malipo kwanjia ya kielektroniki kupitia Benki Kuu ya Tanzania (TISS).Vilevile, Wizara itaendelea kutoa mafunzo ya muda mfupi

Page 36: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

36

6 JUNI, 2013

na mrefu kwa wahasibu wa Wizara, Mikoa na Idara za Serikaliya kuandaa hesabu katika viwango vya kimataifa – IPSASAccrual Basis na kuongeza uelewa wa matumizi ya mtandaowa EPICOR 9.05.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Wizara itaendelea kusimamia utekelezaji waAwamu ya Nne ya Programu ya Maboresho ya Usimamiziwa Fedha za Umma kwa kufanya yafuatayo: Kuandaamkakati wa utekelezaji wa kubadilisha mfumo wa IPSASCash kwenda IPSAS Accrual; kuufanyia marekebishomwongozo wa uandaaji wa Mipango na Bajeti za mudawa Kati; kuwajengea uwezo watumishi kwa kuwapamafunzo katika kada za fedha, ununuzi, ukaguzi wa ndanina usimamizi wa mali ya Serikali katika Wizara, Idarazinazojitegemea na Mamlaka za Serikali za Mitaa katikakusimamia fedha na mali ya umma; kufanya mapitio yamifumo ya fedha za Serikali kwa ajili ya kuhuisha nakuwianisha; kuandaa Mkakati wa Kudhibiti Uanzishwaji waMifumo ya Fedha inayojitegemea; kuandaa Sera yaUsimamizi wa Madeni; na kuandaa Mpango wa Mafunzokwa ajili ya kuwajengea uwezo Watumishi wa Umma kwenyemaeneo ya uandaaji wa mipango, utekelezaji pamoja nakumudu mabadiliko yanayojitokeza katika Usimamizi waFedha za Umma.

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Programu yaMaboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu yaNne, itaendelea kusambaza mfumo wa kompyuta waukaguzi wa ndani kwa Wizara na Idara zinazojitegemea 15pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa 15. Aidha, mkakatiwa utekelezaji wa mapendekezo ya utafiti juu ya vyanzovya mapato kwa ajili ya Mamlaka za Serikali za Mitaautaandaliwa pamoja na kuhuisha mfumo wa ugawaji wafedha kwenda kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.Vilevile, Mpango Mkakati wa Programu ya Maboresho yaUsimamizi wa Fedha za Umma kwa upande wa Zanzibarutaandaliwa na kusambazwa.

Mheshimiwa Spika, katika eneo la Sera ya Ununuzi

Page 37: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

37

6 JUNI, 2013

wa Umma, Wizara imetekeleza yafuatayo: KukamilishaRasimu ya Sera ya Taifa ya Ununuzi wa Umma; kukamilisharasimu ya Kanuni za Ununuzi wa Umma; kuendelea kuhuishataarifa za Maofisa Ununuzi na Ugavi katika daftari ambapojumla ya Maofisa 989 wameingizwa katika daftari hilo.Aidha, Wizara imeendelea na taratibu za kuanzisha kadaya Ununuzi Serikalini pamoja na kusimamia na kuendelezakada ya Ugavi nchini.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Wizara imepanga kufanya yafuatayo: Kuanzautekelezaji wa Sera ya Taifa ya Ununuzi wa Umma; kufuatiliana kufanya tathmini ya mfumo wa Ununuzi wa Umma; nakuendelea kuhakiki Daftari la Taifa la Taarifa za MaafisaUnunuzi na Ugavi Serikalini.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumuyake ya kudhibiti shughuli za ununuzi nchini, Mamlaka yaUdhibiti wa Ununuzi wa Umma - PPRA ilifanya yafuatayo:Kaguzi za ununuzi katika miradi 137 ya ujenzi inayotekelezwana Halmashauri mbalimbali za Wilaya; kaguzi za ununuzikatika Taasisi za Umma 121; chunguzi sita za ukiukwaji waSheria ya Ununuzi zimefanyika na hatua zinazotakiwakuchukuliwa zimependekezwa; kuchapisha jarida laTanzania Procurement Journal ili kutoa matangazo ya zabunina taarifa nyingine zinazohusu ununuzi wa umma; nakusambaza Mfumo wa Upokeaji na Usimamizi wa Taarifaza Ununuzi nchini - Procurement Management InformationSystem (PMIS) kwa Taasisi 299 na kutoa mafunzo juu yamfumo huo. Aidha, PPRA ilitoa mafunzo ya ununuzi waumma kwa watumishi 735 kutoka Taasisi za Umma 41.Vilevile, PPRA iliandaa Mkutano wa Commonwealth PublicProcurement Network (CPPN), uliofanyika Dar es Salaammwezi Oktoba, 2012 na washiriki wapatao 111 kutoka nchimbalimbali Duniani walihudhuria ili kubadilishana uzoefukatika fani ya ununuzi.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, PPRA imejiandaa kufanya ukaguzi katika Taasisiza Umma 115 pamoja na miradi ya ujenzi 200 kwa ununuzi

Page 38: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

38

6 JUNI, 2013

uliofanywa na taasisi hizo. Aidha, Ofisi za Kanda Dodomana Mbeya zinatarajiwa kufunguliwa ili kusogeza karibu zaidishughuli zake kwa Halmashauri na Manispaa na kuandaaMpango Kazi wa utekelezaji wa kuanzisha Mfumo waUnunuzi kwa njia ya Mtandao wa kielektroniki - e-procurement system, ambao pamoja na mambo mengine,unatarajia kupunguza upungufu wa ufanisi wa ununuziunaotokana na kuweka taarifa kwenye makaratasi.

Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Rufaa za Zabuni –PPAA imeendelea kushughulikia rufaa za zabuni za umma.Hadi kufikia mwisho wa mwezi Aprili, 2013, Mamlaka ilipokeajumla ya mashauri 24 ambapo mashauri 21 yalifanyiwamapitio na maamuzi kutolewa. Katika mapitio hayo,mashauri 15 walalamikaji walishinda na Taasisi za Ununuzikuagizwa kufanya marekebisho kwa kuzingatia sheria.Mashauri mawili yalikataliwa baada ya kuletwa nje yamuda uliowekwa kisheria na pia Mamlaka kutokuwa nauwezo wa kuyajadili - lack of powers of jurisdiction. Aidha,mashauri matatu walalamikaji walishindwa na shauri mojalilifutwa na mlalamikaji mwenyewe.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Mamlaka itaendelea kusikiliza na kutoleamaamuzi migogoro katika Ununuzi wa Umma na kuelimishaumma na wadau juu ya Sheria ya Ununuzi wa Umma yamwaka 2011.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2012/2013, Wizara kupitia Wakala wa Huduma ya UnunuziSerikalini – Goverment Procurement Services Agency (GPSA)imetekeleza yafuatayo: Ofisi za kutoa huduma ya uuzaji wamafuta na vifaa kwenye Mikoa mipya ya Njombe, Katavi,Geita na Simiyu zimefunguliwa na zimeanza kufanya kazi;Mafunzo kuhusu mfumo wa vifaa na huduma mtambukayalifanyika kwenye vituo vinane ambavyo ni Arusha,Morogoro, Mbeya, Dodoma, Dar es Salaam, Tanga, Kigomana Mtwara ambapo jumla ya washiriki 498 walihudhuria ilikuwajengea uwezo wa huduma ya ununuzi Serikalini; nakuandaa utaratibu wa kununua kwa pamoja vifaa na

Page 39: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

39

6 JUNI, 2013

huduma mtambuka kwa kutangaza zabuni 31 ambapowaombaji 9,256 wamejitokeza. Aidha, ukarabati wa ofisikatika Mikoa ya Lindi, Tabora na Shinyanga umekamilikana ukarabati wa ofisi katika Mkoa wa Mtwara na ujenziwa ofisi, ghala na kisima cha mafuta katika Mkoa waManyara unaendelea kwa lengo la kuimarisha huduma zaununuzi Serikalini.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Wizara kupitia GPSA imepanga kutekelezayafuatayo: Kukamilisha ujenzi wa ofisi, ghala na kisima chamafuta katika Mkoa wa Manyara; kufanya upembuziyakinifu kwa ajili ya ujenzi wa ghala na kisima cha mafutakatika Mikoa ya Njombe, Katavi, Geita na Simiyu; kufanyaukarabati wa majengo ya ofisi za Mikoa ya Dodoma,Manyara, Dar es Salaam, Mtwara, Kagera na Morogoro;kuongeza wigo wa vifaa (stock range) kutoka 86 iliyoposasa hadi kufikia 100; na kuanza kutekeleza mkakati wakununua vifaa vya kuuza kutoka kwa watengenezaji namawakala wakubwa.

Mheshimiwa Spika, ununuzi wa magari ni moja yaeneo ambalo linatumia fedha nyingi za Umma na kutokanana hilo, Serikali imeona kuwa kuna umuhimu wa kuwekautaratibu bora utakaowezesha kupata thamani ya fedhakatika ununuzi pamoja na matumizi ya magari yake. Ununuziwa magari kwa sasa umekuwa ukifanywa na kila Wizara,Idara zinazojitegemea, Taasisi za Serikali, Halmashauri naOfisi za Mikoa kwa kila moja kuandaa mchakato wa ununuziwake. Utaratibu huu umesababisha kuwepo kwa ununuziwa aina nyingi za magari na kwa bei zinazotofautiana bainaya Taasisi moja na nyingine. Wizara imeandaa rasimu yautaratibu wa mfumo wa ununuzi wa magari kwa pamojaambapo GPSA itahusika na jukumu hili. Utaratibu huuutaanza kutumika mara baada ya kupitishwa na Mamlakazinazohusika.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2012/2013, Wizara imeanza kuandaa Sera ya Taifa ya Maliya Serikali. Wizara pia iliendelea kuhakiki Mali ya Serikali

Page 40: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

40

6 JUNI, 2013

iliyopo katika Wizara, Idara zinazojitegemea na kutoa ushauriwa kuhakikisha kuwa mali ya Serikali inatunzwa na kutumikakwa malengo yaliyokusudiwa. Aidha, Wizara iliendelea nazoezi la kuondosha mali chakavu katika Wizara na Idara zaSerikali, ambapo jumla ya shilingi milioni 401.14 zilipatikanakutokana na mauzo ya magari 98, mitambo 57 na vifaavingine chakavu.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Wizara itaendelea na zoezi la kuthamini mali;kuhakiki na kuhuisha Daftari la Mali ya Serikali kwa ajili yakufanya usuluhishi kwa njia ya mtandao, kufuta nakuondosha vifaa chakavu zikiwemo samani, magari,mitambo na madawa yaliyokwisha muda wake na vifaavingine katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala waSerikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali zaMitaa. Aidha, Wizara itaendelea na hatua mbalimbalizinazohusika katika kukamilisha Sera ya Taifa ya Mali zaSerikali ili kuweza kuwa na usimamizi bora wa mali za Serikali.

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mpango waMillenium Challenge Account – Tanzania (MCA-T),imeendelea kusimamia utekelezaji wa miradi inayofadhiliwana Serikali ya Marekani kupitia Shirika la MillenniumChallenge Corporation (MCC). Utekelezaji wa miradiinayohusika umeendelea vizuri licha ya changamotoambazo zimeathiri kasi ya utekelezaji kama vile mvua nyingikwa Mikoa ya Ruvuma na Rukwa na matatizo ya kiufundi.Ujenzi wa Barabara ya Tanga - Horohoro ulikamilika kwakiwango cha lami na kukabidhiwa kwa Serikali mweziOktoba, 2012; ujenzi wa barabara za Ukanda wa Mtwara,yaani Songea – Namtumbo na Peramiho – Mbinga na ujenziwa Kiwanja cha Ndege cha Kisiwa cha Mafia naounaendelea vizuri. Aidha, kazi ya kuweka lami katikabarabara tano za Pemba Kaskazini imeanza na ujenzi waBarabara ya Tunduma – Sumbawanga ambaoumegawanywa katika sehemu tatu; Tunduma – Ikana,Ikana – Laela na Laela – Sumbawanga unaendelea.

Mheshimiwa Spika, Miradi ya kupeleka umeme

Page 41: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

41

6 JUNI, 2013

Zanzibar kupitia chini ya bahari na ule wa ukarabati wamtandao wa umeme kwa Mkoa wa Dodoma sasaumekamilika kupitia akaunti hii ya Millenium Challenge.Utekelezaji wa miradi mingine ya ukarabati wa vituo vyakupoozea umeme, ukarabati wa mtandao wa umeme kwaMikoa ya Tanga, Morogoro, Iringa, Mbeya, Mwanza naKigoma, ikiwa ni pamoja na Mradi wa Umeme wa Juakalipale Kigoma, inaendelea. Aidha, miradi ya upanuzi wamtambo wa maji Ruvu chini na ukarabati wa mfumo wamaji kwa Manispaa ya Morogoro nayo pia inaendelea kwakutumia Mfuko huu wa Msaada kutoka Marekani.

Mheshimiwa Spika, kutokana na utekelezaji wakuridhisha wa miradi, katika kikao cha Bodi ya MCCkilichofanyika mwezi Desemba, 2012, kiliamua kuikubaliaTanzania kuidhinisha maandalizi ya Mpango wa Pili waMiradi ya MCC (MCC Compact II). Serikali imeshaanzamaandalizi hayo baada ya kuunda Sekretarieti ya uratibu.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2012/2013, Wizara imeandaa na kutoa miongozo yausimamizi wa vihatarishi katika Sekta ya Umma pamoja naMwongozo wa Uhakiki wa Ubora wa Ukaguzi wa Ndani.Miongozo hii ilizinduliwa mwezi Machi, 2013. Aidha, Wizaraimetayarisha Mwongozo wa Ukaguzi wa Ndani kwakuzingatia viwango vya kimataifa vya ukaguzi wa ndanina unategemea kuanza kutumika rasmi mwezi Julai, 2013.Kadhalika, Wizara imekamilisha Mkataba wa Makubalianokati ya Wakaguzi wa Ndani na Wateja wake na pia kutoakanuni za maadili ya wakaguzi wa ndani. Miongozo hiyoina lengo la kuboresha utendaji kazi wa ukaguzi wa ndani.

Mheshimiwa Spika, Wizara pia imefanya kaguzi nakutoa ushauri wa kitaalamu kwa wahusika katika miradisita ya ujenzi. Miradi hiyo ni skimu za kilimo cha umwagiliajiMorogoro; Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma; Hospitali yaMkoa wa Dodoma; Barabara ya Tunduma - Sumbawanga;Barabara ya Gairo – Dodoma – Kintinku; na Barabara yaMorogoro – Gairo. Aidha, Wizara ilitoa mafunzo kuhusuukaguzi wa ndani kwa kufuata viwango vya kimataifa vya

Page 42: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

42

6 JUNI, 2013

ukaguzi wa ndani kwa wakaguzi wa ndani 364 wa Wizara,Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti zaMikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Vilevile, mafunzoyanayohusu mfumo wa malipo wa EPICOR yametolewa kwawakaguzi wa ndani 80 kutoka Wizara tisa na Wakala waSerikali moja.

Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kusimamia nakuimarisha ukaguzi wa ndani katika Mwaka wa Fedha wa2013/20 14 Wizara itatoa miongozo ya ukaguzi wa ununuzi;ukaguzi wa mfumo wa malipo ya mishahara; ukaguzi wabajeti; udhibiti wa ndani pamoja na ukaguzi wa kiufundikwa wakaguzi wa ndani wa Wizara, Idara Zinazojitegemeana Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, Wizara itatoamafunzo kwa Wakaguzi wa ndani na Wajumbe wa Kamatiza Ukaguzi kwenye Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakalawa Serikali na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu matumizina uzingatiaji wa nyaraka za ukaguzi na miongozoiliyotolewa. Vilevile, Wizara itafanya mikutano elekezi kwawakaguzi wa ndani wa Wizara, Idara zinazojitegemea naMamlaka za Serikali za Mitaa kwa lengo la kujadili kwapamoja changamoto na kuweka mikakati ya kuboreshaukaguzi wa ndani Serikalini.

Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kujengauwezo kwa Maafisa Masuuli na timu zao za menejimentijuu ya sheria, kanuni na taratibu za fedha na ununuzi kwalengo la kuwawezesha kufanya kazi zao vizuri na hivyokufanikisha kupata Hati Safi za Ukaguzi. Aidha, mafunzohaya yataboresha uandaaji wa vitabu vya hesabuambavyo ndiyo msingi wa ukaguzi wa Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali ili viandaliwe kwa mujibu waviwango vya kimataifa.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2012/2013, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi iliendelea kutekelezayafuatayo: Kufanya ukaguzi wa hesabu za mafungu yoteya Wizara na Idara za Serikali, Mikoa ya Tanzania Bara,Halmashauri, Mashirika ya Umma, Balozi na Wakala waSerikali; kukamilisha ripoti tano za ukaguzi wa ufanisi -Value

Page 43: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

43

6 JUNI, 2013

for Money Audit ambapo taarifa zote hizi zimewasilishwahapa Bungeni tarehe 11 Aprili, 2013; ukaguzi wa Mashirika50 ulikuwa unaendelea katika hatua mbalimbali za ukaguzi;Ofisi imeendelea kukiimarisha Kitengo cha Ukaguzi naUfanisi kwa kutoa mafunzo kwa watumishi saba nakukipatia vitendea kazi zaidi. Aidha, ofisi iliendelea kulipiamafunzo ya muda mrefu kwa watumishi 53 waliopo katikavyuo mbalimbali na kugharamia mafunzo ya muda mfupikwa watumishi 400. Vilevile, ujenzi wa ofisi unaendelea katikaMikoa ya Dodoma na Rukwa na unatarajiwa kukamilikamwanzoni mwa mwaka 2014.

Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014, Ofisi itatekeleza shughuli zifuatazo: Kuendeleakutekeleza mkakati wa kuwaondoa wakaguzi katika ofisiza wakaguliwa ambapo kwa kuanzia, ofisi inatarajiakupanga ofisi Dar es Salaam, Mwanza, Tanga, Tabora,Iringa na Kagera; kuanza ukaguzi wa mapato na matumiziya vyama vyote vya siasa nchini ili kukidhi matakwa yasheria ya vyama vya siasa na kuendelea kufanyamazungumzo na Msajili wa Vyama vya Siasa namna yakutekeleza Sheria ya Gharama za Uchaguzi; na kuziimarishaKamati za Bunge za Hesabu za Serikali – Public AccountsCommittee (PAC) na Local Authorities AccountsCommittee (LAAC), Kamati ya Bajeti na Kamati ya Uchumi,Viwanda na Biashara kwa kuzijengea uwezo kwa njia yamafunzo, tafiti na ushauri kwa kuzingatia mahitaji – Basedon Training Needs Assessment (TNA).

Mheshimiwa Spika, shughuli nyinginezitakazotekelezwa ni pamoja na kuhakiki matumizi ya fedhaza Halmashauri zinazopelekwa vijijini, pamoja na kufuatiliasalio la fedha ifikapo mwisho wa mwaka wa fedha; kushirikikikamilifu katika zoezi la ukaguzi wa mali katika Halmashaurizote, Mikoa, Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali ilikuhakikisha kumbukumbu za mali na fedha zinaingizwakwenye vitabu; kushiriki kikamilifu katika jukumu jipya lakukagua Taasisi za Umoja wa Mataifa ambapo ofisi inaingiamwaka wa pili wa kuwepo kwenye Bodi ya Ukaguzi yaUmoja wa Mataifa -UN Board of Auditors; kufanya kaguzi

Page 44: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

44

6 JUNI, 2013

sita za thamani ya fedha na kupanua wigo wa ukaguzi wafedha (Regularity Audit); kuendelea na uunganishaji wa Ofisiza Ukaguzi zilizoko mikoani na makao makuu kwa kutumiaMtandao Mpana - Wide Area Network (WAN); kuimarishaukaguzi wa kiutambuzi - Forensic Audit; na kuongeza idadiya watumishi kwa kuajiri watumishi wapya 141.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa MKUKUTAhuratibiwa na Wizara kupitia Mpango wa Ufuatiliaji natathmini ya MKUKUTA Awamu ya Pili - MKUKUTA II MonitoringMaster Plan. Mpango huu umeainisha viashiria vya kupimautekelezaji wa Malengo ya MKUKUTA II, Malengo yaMaendeleo ya Milenia 2015 na Dira ya Taifa ya Maendeleo2025. Katika kipindi cha mwaka 2012/2013, Wizara iliandaana kusambaza ripoti zifuatazo: Ripoti ya Mwaka yaUtekelezaji wa MKUKUTA - MKUKUTA AnnualImplementation Report (MAIR 2011/12); Ripoti ya Hali yaUmaskini na Maendeleo ya Watu – Poverty and HumanDevelopment Reports (PHDRs 2011); na Ripoti ya Maoni yaWatu - Views of the People Report 2012 kuhusu jitihada zakupunguza umaskini. Ripoti hizi zinachambua kwa kinamwenendo wa viashiria katika kila lengo la MKUKUTA kwakuainisha mafanikio, changamoto na hatua za kuchukua.

Mheshimiwa Spika, ili kufanikisha kufikiwa kwamalengo ya MKUKUTA II, Wizara imeendelea kusimamiautekelezaji wa Mradi wa Small Enterprenuer Loan Facility(SELF), ambao jukumu lake kuu ni kujenga uwezo wa asasindogo za fedha kwa kuzipatia mikopo na mafunzo yautaalamu wa fedha, ili ziweze kuwafikia wajasiriamaliwadogo na kati hususan katika maeneo yenye uhaba wahuduma za fedha. Asasi hizo ni pamoja na Vyama vya Akibana Mikopo (SACCOS), Benki za Wananchi Vijijini (VICOBA)na Mashirika yasiyo ya Kiserikali. Hadi kufikia mwishoni mwaMwezi Aprili, 2013, Mradi wa self umetoa mikopo ya shilingibilioni 8.32 kupitia asasi ndogo za fedha zipatazo 66 kwawalengwa 5,198. Aidha, Mradi wa SELF umetoa mafunzokwa wajasiriamali wapatao 1,330; watendaji 289 wa asasiwakiwemo Maofisa Mikopo, Wajumbe wa Kamati za

Page 45: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

45

6 JUNI, 2013

Mikopo, Watunza Vitabu vya Hesabu na Wajumbe wa Bodi;na Maofisa Ushirika 113 kutoka Wilaya mbalimbali nchini.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Wizara itaendelea kusimamia utekelezaji waMKUKUTA II; kufanya tafiti na uchambuzi wa kitaalamukuhusu mwenendo wa umaskini na kutoa elimu juu yautekelezaji wa MKUKUTA; Kuandaa Ripoti ya Mwaka yaUtekelezaji wa MKUKUTA II; Ripoti ya Hali ya Umaskini Nchini;Kuhamasisha wadau ngazi zote kuhusu masuala yaMKUKUTA na Malengo ya Maendeleo ya Milenia. Aidha,Wizara itakamilisha utafiti wa kutambua programu za kingaya jamii na fursa za maendeleo kwa makundi tete(Vulnerable Groups) ili kuboresha utekelezaji na ufahamukwa walengwa.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Mradi wa SELF utaendelea kutoa huduma zamikopo kwa wajasiriamali wadogo na kujenga uwezo waasasi ndogo za fedha hususan katika maeneo ambayohayajafikiwa. Aidha, ili shughuli za mradi kuwa endelevu,Mradi wa SELF utafanyiwa maboresho ya kimuundo nakuufanya kuwa Kampuni inayojitegemea chini ya Udhaminiwa Serikali ambapo mapendekezo hayo yapo katika hatuaya Rasimu ya Waraka wa Baraza la Mawaziri.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2012/2013, Wizara iliendelea kuzifanyia marekebisho sheriambalimbali ili kuweka usimamizi mzuri wa kodi na fedha zaumma. Baadhi ya sheria zilizofanyiwa marekebisho ni sheriambalimbali za kodi ambazo zilipitishwa kupitia Sheria yaFedha ya mwaka 2012 (The Finance Act, 2012) na Sheria yaUdhibiti wa Fedha Haramu iliyofanyiwa marekebisho kupitiaSheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali iliyopitishwana Mkutano wa Bunge wa mwezi Februari, 2013. Aidha,marekebisho ya Mkataba wa Cotonou unaohusu ushirikianobaina ya nchi za Jumuiya ya Ulaya, Afrika na Visiwa vyaCaribbean ambapo Tanzania ni mwanachama,yalipitishwa na Bunge lako Tukufu kupitia Azimio la Bungekatika Mkutano wa mwezi Novemba, 2012.

Page 46: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

46

6 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, Wizara pia iliandaa kanunimbalimbali ili kuwezesha usimamizi na utekelezaji wa Sheriaza Kifedha. Baadhi ya kanuni zilizotolewa ni zile za kuanzishaCredit Reference Databank ya Utunzaji wa Taarifa zaWateja wa Benki na Taasisi za Kifedha, pamoja na CreditReference System; Matumizi ya Vifaa vya Kielektroniki katikaUkusanyaji wa Kodi ya Mapato; Usimamizi wa Marejeshoya Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa abiria wa ndegeambao siyo Raia wa Tanzania; Kanuni za Sheria ya Udhibitiwa Fedha Haramu; na Kanuni za Sheria za Uwekaji Stempukwenye kazi za Wasanii.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Wizara itaendelea kukamilisha maandalizi yakuwezesha kutungwa kwa Sheria mpya ya Kodi yaOngezeko la Thamani – Value Added Tax (VAT), Sheria yaUtawala wa Kodi - Tax Administration Act, Sheria ya Hoteli- Hotels Tax Act, Sheria ya Takwimu, Sheria ya Msajili waHazina na Sheria ya Mfuko wa Akiba ya WafanyakaziSerikalini - Government Employees Provident Fund (GEPF);zote hizi zitashughulikiwa. Aidha, Wizara inatarajiakuwasilisha Bungeni mapendekezo ya marekebisho kwenyeSheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma, pamoja na Sheriaya Mikopo, Dhamana na Misaada ili kuihuisha kulinganana mazingira ya sasa ya uchumi. Vilevile, Wizara itaandaakanuni mbalimbali zitokanazo na sheria hizi ili kuwezeshautekelezaji wake uwe mzuri.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2012/2013, Wizara imetoa mafunzo kuhusu dhana ya Ubiakwa watumishi 33 wa Serikali na wa Sekta Binafsi. Aidha,watumishi 60 wa Serikali na wa Sekta Binafsi wamepatamafunzo ya kina kuhusu kutathmini Andiko la Awali la Miradiya PPP. Vilevile, Wizara inakamilisha kuandaa kanuni za PPP(PPP Finance Regulations) zitakazotumika kutathmini Miradiya Ubia. Kadhalika, Wizara imepokea maandiko (FeasibilityStudies) na kufanya uchambuzi wa awali na kutoa ushaurikatika Miradi ya Bandari ya Mtwara, Bandari ya Mwambani- Tanga, Bandari ya Kasanga Kigoma na Barabara ya Dares Salaam - Chalinze.

Page 47: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

47

6 JUNI, 2013

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2013/2014, Serikali inatarajia kupitia upya muundo wa vitengo vyaPPP na kufanya mapitio ya Sheria na Kanuni za Ubia;kuhamasisha watu kuhusu dhana ya biashara ya ubia; nakutoa mafunzo ya ubia kwa wadau. Aidha, Serikali itaanzishaMfuko wa kuwezesha utekelezaji wa Miradi ya Ubia (PPPFacilitation Fund). Lengo la Mfuko huu ni kugharamiaupembuzi yakinifu wa miradi inayoanzishwa kwa mfumo waPPP.

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Kitengo chaUdhibiti wa Fedha Haramu imeendelea kusimamiautekelezaji wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu. KatikaMwaka wa Fedha wa 2012/2013, Kitengo kimeendeleakupokea na kuchambua taarifa za miamala shuku(Suspicious Transaction Reports), ambapo taarifa 29zilipokelewa na kuchambuliwa, kati ya hizo matokeo yauchambuzi wa taarifa kumi ziliwasilishwa katika vyombovinavyosimamia utekelezaji wa sheria (Law EnforcementAgencies). Aidha, Kitengo kimefanya ukaguzi wa watoataarifa na kuimarisha mifumo ya kushirikiana na wadau wandani na nje ya nchi. Vilevile, Kitengo kimetoa mafunzo kwamakundi 357 ya wadau ikiwemo kutoka Sekta ya Benki naTaasisi nyingine za Kifedha, Sekta ya Ujenzi, Asasi zisizo zaKiserikali, Wanasheria wa Kujitegemea, Wahasibu naWakaguzi wa Kujitegemea, Kampuni za Bima, Michezo yaKasino na taasisi zinazojihusisha na Masoko ya Mitaji naDhamana.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Wizara kupitia Kitengo cha Udhibiti wa FedhaHaramu imepanga kutekeleza yafuatayo: Kupokea nakuchambua taarifa za miamala shuku na kuwasilishamatokeo ya uchambuzi kwenye vyombo vinavyosimamiautekelezaji wa sheria; kuandaa miongozo ya ukaguzi(Inspection Manuals) kwa sekta mbalimbali za watoataarifa; kutoa mafunzo kwa Watumishi wa Kitengo nawadau wengine katika nyanja mbalimbali za udhibiti wafedha haramu; kuandaa na kuhuisha miongozo yautekelezaji wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu kwa

Page 48: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

48

6 JUNI, 2013

watoa taarifa wa taasisi mbalimbali; na kufanya tathminiya viashiria hatarishi vya fedha haramu na ufadhili wa ugaidi.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2012/2013, Tume ya Pamoja ya Fedha imewasilisha katikangazi zinazohusika mapendekezo na matokeo ya tafiti yaUsimamizi wa Deni la Taifa baina ya pande mbili zaMuungano. Tume pia inaendelea na Tafiti za Mfumo Borawa Kodi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha,Tume imefanya Tafiti ya Uhusiano wa Mwenendo wa Uchumina Mapato ya Muungano kwa lengo la kubaini hali yamapato kutokana na ukuaji wa uchumi na kushauri njiabora ya kuimarisha mapato hayo.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Tume inatarajia kukamilisha Ripoti za Tafiti yaMfumo Bora wa Kodi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania na Tafiti ya Uhusiano wa Mwenendo wa Uchumina Mapato ya Muungano na kuwasilisha mapendekezoyatokanayo na tafiti hizo kwenye ngazi husika. Aidha, Tumeinakusudia kufanya tafiti kuhusu uwekezaji kwa lengo lakubaini na kushauri njia bora za kuimarisha uwekezaji.

Mheshimiwa Spika, Habari, Elimu na Mawasilianokwa Umma. Wizara imeendelea kusimamia na kuboreshamawasiliano kati yake na wadau kwa kutoa taarifa sahihina kwa wakati. Katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013,Wizara imetoa elimu kwa umma kuelezea majukumu,mafanikio na changamoto za Wizara kupitia maoneshoikiwa ni pamoja na Saba Saba, Nane Nane, Maadhimishoya Kumbukumbu ya Uhuru wa Tanzania Bara; makalamaalumu ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne;machapisho; vyombo vya habari vikiwemo Magazeti,Redio, Tovuti, Televisheni na Vipeperushi.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Wizara itaendelea kuandaa vipindi vya rediona televisheni, kuandaa machapisho na makongamanombalimbali na kushiriki katika maonesho ya kitaifa kwa ajiliya kuelezea majukumu na utekelezaji wa shughuli za Wizara.

Page 49: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

49

6 JUNI, 2013

Aidha, Wizara itakamilisha uandaaji wa Mkakati waMawasiliano wa Wizara.

Mheshimiwa Spika, Wizara ina jumla ya Watumishi1,313. Kati ya hao, Watumishi 819 ni Wanaume na Watumishi494 ni Wanawake. Katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013,Wizara imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kujengauwezo wa watumishi wake ili iweze kutekeleza majukumuyake kwa ufanisi. Hatua hizo ni pamoja na kupelekawatumishi 365 katika mafunzo ya muda mfupi na watumishi57 katika mafunzo ya muda mrefu, kuthibitisha watumishi11 kazini, kupandisha vyeo watumishi 404, kuboreshamazingira ya kazi kwa kukarabati baadhi ya ofisi na kununuavifaa vya ofisi. Aidha, Wizara imeendelea kutoa hudumastahiki kwa Watumishi wa Wizara wanaoishi na Virusi vyaUKIMWI.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Wizara inatarajia kuajiri watumishi 115 wa kadambalimbali; kupandisha vyeo watumishi 614; na kuthibitishawatumishi kazini waliomaliza muda wao wa majaribio.Aidha, Wizara inatarajia kuwapatia watumishi 200 mafunzombalimbali ya kuwajengea uwezo katika kutekelezamajukumu yao, kutoa elimu kuhusu magonjwa sugu nakuwapatia lishe walioathirika na UKIMWI.

Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamiautendaji wa Mashirika ya Umma pamoja na Taasisi zake.Majukumu yaliyotekelezwa kwa kushirikiana naConsolidated Holdings Corporation (CHC) ni pamoja nakuendelea na zoezi la urekebishaji wa mashirika yaliyo namatatizo katika Sekta za Usafirishaji, Madini, Mawasiliano,Utalii na Fedha.

Mheshimiwa Spika, Taarifa za Hesabu za Mashirikaya Umma 103 zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali zilichambuliwa na mapendekezokutolewa kwa Bodi za Wakurugenzi, Watendaji Wakuu waTaasisi na Wizara husika kwa lengo la kuboresha utendajina uangalizi wa mali ya umma. Aidha, uchambuzi wa

Page 50: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

50

6 JUNI, 2013

Miongozo ya Kiutendaji ya Taasisi na Mashirika ya Ummaambayo ni Kanuni za Fedha 25, Miundo ya Utumishi 27,Kanuni za Utumishi 21 na Miundo ya Taasisi sita ulifanyikana vibali vilitolewa. Vilevile, Muundo na majukumu ya Ofisiya Msajili wa Hazina umeidhinishwa na umeanza kutumika.Kadhalika, Ofisi ya Msajili wa Hazina imepata ofisi katikaJengo la CHC Mtaa wa Samora na tayari watumishiwamehamia katika ofisi hiyo.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina inatarajiakutekeleza yafuatayo: Kusimamia utendaji wa Bodi zaWakurugenzi wa Mashirika na Taasisi za Umma na kuboreshaUtawala Bora kwa kuingia Mikataba ya Utendaji(Performance Contracts) na Bodi za Mashirika ya Umma;kusimamia mikakati ya kurekebisha Mashirika ya Umma nauperembaji (Monitoring and Evaluation) wa Mashirika yaUmma yaliyobinafsishwa; na kuimarisha usimamizi waMashirika na Taasisi za Umma ili kuongeza mapato yaSerikali.

Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kuimarishautendaji kazi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kukamilishataratibu za kutunga sheria mpya na kuwajengea uwezoWatumishi. Aidha, taratibu za kujaza nafasi mbalimbalikulingana na muundo zinaendelea na zinatarajiwakukamilika katika nusu ya kwanza ya mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, hadi Desemba, 2012, CHCilifuatilia na kuyafanyia tathmini mashirika 170; kati ya hayo,mashirika 42 yalibainika kufanya kazi kwa faida, mashirika70 yanafanya kazi kwa hasara na mashirika 58 hayafanyikazi. Zoezi la tathmini juu ya utendaji wa mashirika hayo ilikuainisha kiini cha matatizo na kupendekeza hatua zakuchukua linaendelea. Aidha, mapato ya CHC katikakipindi hicho yalikuwa shilingi bilioni 7.68 ikilinganishwa nashilingi bilioni 6.3 zilizopatikana katika kipindi kilichoishiaDesemba, 2011. Kuongezeka kwa mapato kumetokana najuhudi za ukusanyaji wa madeni na ufuatiliaji wa ukusanyajiwa madeni chechefu ya iliyokuwa Benki ya Taifa ya

Page 51: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

51

6 JUNI, 2013

Biashara. Katika mwaka 2013, CHC ilipanga kubinafsisha aukurekebisha mashirika 27. Vilevile, CHC inatarajia kukusanyajumla ya shilingi bilioni 11.35 ikiwa ni mapato kutokana naukusanyaji wa madeni chechefu, uuzaji wa viwanja namajengo, ufilisi wa makampuni, ukusanyaji wa madeniyanayotokana na ubinafsishaji na riba.

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha huduma zapensheni, Wizara imeanza utaratibu wa kulipa Pensheni kwavipindi vya miezi mitatu mitatu badala ya vipindi vya miezisita sita kuanzia Januari, 2012. Katika utaratibu huu,Wastaafu wanalipwa pensheni ya miezi miwili mapema (inadvance), badala ya miezi mitano iliyokuwa inalipwa katikautaratibu wa awali. Pensheni inalipwa mwishoni mwa mieziya Julai, Oktoba, Januari na April i. Aidha, Wizaraimeendelea na kazi ya kuweka kumbukumbu za Wastaafuwaliopo kwenye Daftari la Pensheni la Hazina kwenyeMfumo wa Kompyuta ujulikanao kwa jina la SAPERION kwalengo la kurahisisha upatikanaji wa taarifa zao. Hadi kufikiamwezi Aprili, 2013, kumbukumbu za Wastaafu 106,030ziliwekwa kwenye mfumo wa kompyuta yetu. Zoezi hililitaendelea kufanyika katika mwaka 2013/2014 ili kukamilishauhifadhi wa kumbukumbu za Wastaafu wote wanaolipwakupitia Wizara ya Fedha (Hazina).

Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamiana kuratibu shughuli za Mifuko ya Pensheni iliyo chini yaWizara ya Fedha. Mifuko hiyo ni Mfuko wa Pensheni kwaWatumishi wa Umma (PSPF), Mfuko wa Pensheni waMashirika ya Umma (PPF) na Mfuko wa Akiba yaWafanyakazi Serikalini (GEPF).

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2013 Mfuko waPensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), ul isaji l iwanachama 332,067. Katika kipindi hicho, Mfuko piaulikusanya jumla ya shilingi bilioni 446.12. Kati ya makusanyohayo, michango ya wanachama ni shilingi bilioni 374.76 namapato yatokanayo na vitega uchumi ni shilingi bilioni 71.36.Matarajio ni kukusanya jumla ya shilingi bilioni 749.10 ifikapomwisho wa Mwaka wa Fedha wa 2012/2013. Aidha, thamani

Page 52: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

52

6 JUNI, 2013

ya Mfuko hadi tarehe 30 Aprili, 2013 ilifikia shilingi bilioni 1,112.24na unatarajiwa kufikia shilingi bilioni 1,226.59 mwezi Juni, 2013.Jumla ya shilingi bilioni 422.16 zilitumika kulipa mafao ikiwani pamoja na mafao ya kiinua mgongo na pensheni za kilamwezi, sawa na asilimia 93.21 ya lengo la mwaka. Vilevile,ili kuongeza wigo wa wanachama, Mfuko umeanzishampango maalum wa kuchangia kwa hiyari kwa watumishiwa sekta rasmi na isiyo rasmi.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Mfuko unatarajia kukusanya jumla ya shilingi bilioni680.55. Kati ya makusanyo hayo, michango ya wanachamani shilingi bilioni 539.18, na mapato yatokanayo na vitegauchumi ni shilingi bilioni 141.37. Aidha, thamani ya Mfukoinatarajiwa kufikia shilingi bilioni 1,522.01. Mfuko unatarajiakulipa kiasi cha shilingi bilioni 522.32 kwa ajili ya mafaombalimbali ikiwa ni pamoja na kiinua mgongo na pensheniza kila mwezi, ambapo jumla ya wanachama wapatao7,647 wanatarajiwa kustaafu kwa mujibu wa sheria. Vilevile,Mfuko unatarajia kuwekeza kiasi cha shilingi bilioni 1,211.39kwenye maeneo mbalimbali ya vitega uchumi hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Akiba ya WafanyakaziSerikalini (GEPF) hadi kufikia Machi, 2013 umesajili jumla yawanachama 6,755, wakiwemo Wananchi waliojiajir iwenyewe katika sekta isiyo rasmi. Katika kipindi hicho,michango ya wanachama ilifikia kiasi cha shilingi bilioni 22.74sawa na asilimia 64.60 ya malengo ya mwaka mzima.Mapato yatokanayo na vitega uchumi yamefikia shilingibilioni 11.64, ambayo ni sawa na asilimia 72.75 ya malengoya mwaka mzima na thamani ya Mfuko imeongezeka nakufikia shilingi bilioni 190.0 Machi, 2013. Aidha, Mfuko umelipamafao ya shilingi bilioni 7.13 hadi kufikia Machi, 2013 nakufungua ofisi katika Manispaa za Temeke, Kinondoni naIlala kwa lengo la kusogeza huduma karibu na Wananchi.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Mfuko utaendelea na jitihada zake za kuboreshahuduma kwa wanachama, kutanua wigo wa wanachama,kukuza mapato yatokanayo na uwekezaji na kusajili

Page 53: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

53

6 JUNI, 2013

wanachama wengi zaidi kupitia Mpango wa Hiari wakujiwekea akiba ya uzeeni na wa lazima. Aidha, Mfukounatarajia kusajili jumla ya wanachama 16,500 na kukusanyamichango yenye thamani ya shilingi bilioni 40.50. Vilevile,mapato ya vitega uchumi yataongezeka hadi kufikia shilingibilioni 19.24 na thamani ya Mfuko huu inatarajiwa kufikiashilingi bilioni 227.

Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Pensheni wa Mashirikaya Umma (PPF), katika mwaka 2012, ulikusanya shilingi bilioni229.1 kutokana na michango ya wanachama, ikiwa ni sawana ongezeko la asilimia 21.7 ikilinganishwa na shilingi bilioni188.1 zilizokusanywa mwaka 2011. Ongezeko hili lilitokanana waajiri kuzingatia sheria kwa kuleta michango kwawakati na uandikishaji wa wanachama wapya. Aidha, idadiya wanachama imeongezeka kutoka 180,049 mwaka 2011hadi 203,981 mwaka 2012. Mfuko pia ulilipa mafao ya jumlaya shilingi bilioni 99.4. Mafao hayo ya PPF yalijumuisha namafao ya elimu ambayo hulipwa kwa ajili ya kusomeshawatoto wasiozidi wanne wa mwanachama aliyefariki akiwakazini. Mwaka 2012 Mfuko ulisomesha watoto 1,333 kwagharama ya shilingi milioni 683, ikilinganishwa na watoto 1,392waliosomeshwa mwaka 2011 kwa gharama ya shilingi milioni573. Watoto hawa husomeshwa kuanzia elimu yachekechea hadi kidato cha nne.

Mheshimiwa Spika, mapato yatokanayo nauwekezaji yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 91.4 mwaka2011 hadi kufikia shilingi bilioni 105.5 kwa mwaka 2012, ikiwani ongezeko la asilimia 15.4. Aidha, thamani ya Mfuko huukufikia Desemba, 2012, ilikuwa imeongezeka kufikia shilingibilioni 1,089.8 ikiwa ni ongezeko la asilimia 21.8 ikilinganishwana thamani ya Mfuko ya shilingi bilioni 894.5 iliyokuwepoDesemba, 2011.

Mheshimiwa Spika, Mfuko unatarajia kukusanyajumla ya shilingi bilioni 281.7, kuandikisha wanachamawapya 72,000 kutoka sekta ya umma na binafsi nakukusanya shilingi bilioni 125.6 kutokana na uwekezaji ifikapo

Page 54: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

54

6 JUNI, 2013

Desemba, 2013. Aidha, thamani ya Mfuko inatarajiwa kufikiashilingi bilioni 1,302.68.

Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na changamotokadhaa katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ikiwemoWanachama kulalamikia kiwango kidogo cha mafaokitolewacho na baadhi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii palewanapostaafu. Vilevile, kuna suala la malimbikizo yamadeni yanayotokana na Mifuko kugharimia utekelezaji waMiradi ya Serikali. Aidha, katika kutafuta ufumbuzi wachangamoto hizo, Serikali kupitia Mamlaka ya KusimamiaSekta ya Hifadhi ya Jamii, imepanga kutathmini uwezo waMifuko yote ya Hifadhi ya Jamii na kupendekeza viwangovya mafao na kuhakikisha kwamba, Mifuko hiyo inakuwaendelevu. Vilevile, Serikali inaendelea kulipa madeni yaMifuko ya Jamii kwa awamu na pia imeunda kamati yakuchambua na kuhakiki madeni mengine ya baadhi yaMifuko hiyo ili kupendekeza njia endelevu ya kulipa mafaostahiki.

Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), imeendelea kutekeleza Mpango wa Tatu waMaboresho wa mwaka 2008/2009 - 2012/2013 ambaoumekuwa msingi wa kuongezeka kwa ukusanyaji wamapato mwaka hadi mwaka. Katika jitihada za kuongezamapato ya ndani, Wizara kupitia TRA imetekelezayafuatayo: Kuanzisha mfumo wa kimtandao wa kuwasilishatax returns; kufanya tathmini maeneo hatarishi katikaUtawala wa Sekta za Umma; kuweka mfumo wa taarifawa RADDEX 2 na kutoa mafunzo kwa watumiaji; kusambazaMfumo wa Ki-elektroniki wa Kufuatilia Usafirishaji Mizigo(Electronic Cargo Tracking System); na kuboresha mfumowa utunzaji kumbukumbu na Taarifa za Magari. Aidha, TRAimekamilisha uandaaji wa Awamu ya Nne ya Mpango waMaboresho (2013/2014 - 2017/2018) unaotarajiwa kuanzakutekelezwa katika Mwaka wa Fedha wa 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2013/2014, Wizara kwa kushirikiana na TRA itaendelea naazma yake ya kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani

Page 55: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

55

6 JUNI, 2013

kwa kupanua wigo wa makusanyo na kuchukua hatuambalimbali za kisera na kiutawala katika maeneo yamapato yatokanayo na kodi. Serikali itaendelea kuwamakini kuhakikisha kwamba, kodi inalipwa na inalipwa kamainavyostahiki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2012/2013, Bodi ya Rufani za Kodi (TRAB), imepokea jumlaya rufani 127 na kusikiliza na kutolea maamuzi rufani 95. Bodipia imetoa elimu kwa walipa kodi kuhusu taratibu za kukatarufaa za kodi na sheria za kodi katika Mikoa ya Tabora,Singida na Shinyanga. Aidha, Bodi imeandaa Tanzania TaxLaw Reports kwa rufaa zote zilizoamuliwa mwaka 2009 -2010 ambapo kwa sasa ripoti hizo zipo katika hatua yamwisho ya uchapishaji vitabu. Kwa upande wa Baraza laRufani za Kodi (TRAT), jumla ya rufani 31 zimepokelewa, katiya hizo rufani 29 zimesikilizwa na kutolewa maamuzi. Barazapia limetoa elimu kwa walipa kodi kuhusu taratibu zakukata rufaa za kodi na sheria za kodi katika Mkoa waMwanza. Katika Mwaka wa Fedha wa 2013/2014, Wizarakupitia Bodi ya Rufani na Baraza la Rufani za Kodi itaendeleakutoa elimu kwa walipa kodi juu ya taratibu za kukata rufaaza kodi na kutoa mafunzo kwa Wajumbe wa Bodi na Barazajuu ya taratibu za kutatua migogoro ya kodi itokanayo naSheria za Kodi zinazosimamiwa na Mamlaka ya MapatoTanzania. Aidha, Bodi ya Rufani inatarajia kuchapishaTanzania Tax Law Reports za mwaka 2011 – 2012 kwa ajiliya rejea kwa wadau wake.

Katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013, Wizara kwakupitia Benki Kuu imeendelea kutekeleza mabadilikochanya katika Sekta ya Fedha ili kuhakikisha kuwa, sektahiyo inachochea maendeleo ya jamii na ukuaji wa uchumi.Mabadiliko ya Sekta ya Fedha yamesababisha utendajimzuri wa Taasisi za Fedha, ikiwa ni pamoja na kuongezekakwa idadi ya mabenki kutoka benki 49 mwezi Februari, 2012mpaka benki 51 mwisho wa mwezi Februari, 2013. Aidha,rasilimali za mabenki zimeimarika zaidi na kufikia shilingi trilioni17.3 mwezi Februari ambapo mikopo iliyotolewa kwa sektabinafsi imefikia shilingi trilioni 8.8.

Page 56: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

56

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Benki Kuu yaTanzania imetoa Mwongozo wa Huduma za Kibenki kwakutumia Wakala wa 2013 (Guidelines on Agent Banking forBanking Institutions, 2013), ambao ulianza kutumika mweziFebruari, 2013.

Mheshimiwa Spika, kutolewa kwa mwongozo huu nisehemu ya mpango wa kuweka mazingira yatakayowezeshakupanua wigo wa huduma za kibenki na kuhakikisha usalamawa benki mbalimbali zitakazojihusisha na mfumo wa utoajihuduma za kibenki kwa kutumia Mawakala. Mfumo huuutarahisisha upatikanaji wa huduma bora na nafuu za kibenki.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha kupitia Benki Kuuimeunda Kamati ya Kitaifa ya Udhibiti wa Mfumo wa Fedha(Tanzania Financial Stability Forum) ili kusaidia kuimarishaushirikianona kubadilishana taarifa kati ya wadhibiti wa sektaya fedha, kama msingi imara kwa ajili ya kuhakikisha uthabitiwa mfumo wa fedha nchini na kupanua wigo wa usimamizikatika mfumo wa fedha kutoka usimamizi unaolenga taasisimoja kwenda usimamizi wa mfumo wa fedha unaolengasekta nzima ya fedha kwa ujumla wake. Aidha, taarifainaonesha hali halisi ya udhibiti wa sekta ya fedha inatolewakila baada ya miezi sita.

Mheshimiwa Spika, Benki Kuu za Afrika Masharikizilikubaliana kutengeneza mfumo wa malipo utakaorahisishamalipo kwa kutumia sarafu za nchi husika. Mfumo huuutakaojulikana kama East African Cross Border PaymentSystem (EAPS) umefikia hatua ya majaribio kupitia mifumoya malipo makubwa (Real Time Gross Settlement System –RTGS) ya nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Mheshimiwa Spika, mategemeo ni mfumo huu kuanzakutumika kwa nchi hizi tatu ikiwa taratibu zote za kujiunganana mfumo huu zitakuwa zimekamilika mwezi Julai mwaka huu.Aidha, nchi za Rwanda na Burundi zitakapokuwa tayarizitajiunga na mfumo huu. Kuanza kwa mfumo huu wa malipokutarahisisha malipo katika Jumuiya na kukuza shughuli zakibiashara hapa nchini.

Page 57: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

57

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2013/2014, Wizara kwa kushirikiana na Benki Kuu itaandaamapendekezo ya kutunga Sheria ya kusimamia mifumo yamalipo nchini (National Payment Systems Act). Aidha, BenkiKuu itaendelea kuandaa sera za kifedha na kusimamiautekelezaji wake.

Mheshimiwa Spika, vile vile, Wizara kwa kushirikianana Benki Kuu itafanya tathmini ya mpango wa utekelezajiwa Awamu ya Pili ya Mpango wa Maboresho ya Sekta yaFedha unaoishia Juni, 2013 na kuandaa mpango wautekelezaji wa awamu ya tatu.

Mheshimiwa Spika, kadhalika, Benki Kuu itahakikishaMwongozo wa Kitaifa kuhusu elimu ya masuala ya fedha(Financial Education Framework) unazingatiwa. Mwongozohuu unalenga kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wakuweka akiba na kutumia huduma za fedha katika shughulizao za kila siku.

Mheshimiwa Spika, Benki ya Maendeleo TanzaniaInvestment Bank - TIB Development Bank; katika kipindi chamwaka 2012/2013, Benki ilifungua tawi Mkoani Mbeya naofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, hii inafanya benkikuwa na jumla ya matawi matano na ofisi tatu za kanda.Aidha, hadi kufikia Desemba, 2012, Benki ilitoa mikopo yenyethamani ya shilingi bilioni 242.9 ikilinganishwa na mikopo yashilingi bilioni 181.7 Desemba, 2011, sawa na ongezeko laasilimia 74.8.

Mheshimiwa Spika, mikopo mingi ilitolewa kwenyesekta ya kilimo na usindikaji wa mazao ya kilimo (mikopo hiini tofauti na ile ya Dirisha la kilimo). Benki ilipata faida kablaya kodi ya shilingi bilioni 8.6 ikiwa ni ongezeko la asilimia 48toka shilingi bilioni 5.8 zilizopatikana mwaka ulioishia Desemba,2011.

Mheshimiwa Spika, Dirisha la Kilimo katika Benki yaMaendeleo TIB liliendelea kutoa mikopo kwa wakopajimbalimbali kwa riba nafuu. Tangu kuanza kwa dirisha mwaka

Page 58: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

58

2010 hadi kufikia Desemba, 2012, maombi yenye thamani yashilingi bilioni 40.1 yaliidhinishwa ambapo shilingi bilioni 20.0(asilimia 49.9) zilikopeshwa kwa makampuni; shilingi bilioni 5.7(asilimia 14.2) kwa taasisi ndogo za fedha zinazokopeshawakopaji wadogo; na shilingi bilioni 14.4 (asilimia 35.9) kwavikundi vya kuweka na kukopa (SACCOS) ambavyo piavinafaidisha wakopaji wadogo.

Mheshimiwa Spika, hii inamaanisha asilimia 50.1 yamikopo imetolewa kwa wajasiriamali wadogo. Aidha, kuanziaJulai, 2013 Dirisha la Kilimo lililopo TIB litahamishiwa katika Benkiya Maendeleo ya Kilimo Tanzania.

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Desemba, 2013,mikopo inayotolewa na Benki ya Maendeleo TIB katika sektambalimbali inatarajiwa kufikia shilingi bilioni 379.2 na faidakabla ya kodi inatarajiwa kufikia shilingi bilioni 16.6.

Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na mpangowake wa kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania– TADB. Lengo la kuanzisha benki hiyo ni kutoa mikopo yamuda mfupi, wa kati na mrefu katika sekta ya kilimoinayojumuisha uvuvi na mifugo. Aidha, muundo wa benki yakilimo na majukumu ya wafanyakazi katika nafasi mbalimbaliumeandaliwa. Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi yaWakurugenzi wameteuliwa na ajira za maafisa waandamiziwa benki hiyo inatarajiwa kukamilika hivi karibuni. Katikamwaka 2013/2014, shilingi bilioni 10 zimetengwa ili kukamilishalengo la mtaji wa kuanzia wa shilingi bilioni 100.

Mheshimiwa Spika, Twiga Bancorp, katika kipindikinachoishia Desemba, 2012 Taasisi iliendelea kupanuashughuli zake kwa kufungua tawi moja Mkoani Dodoma nakuifanya taasisi kuwa na matawi matano. Katika kipindi hicho,amana za wateja zilifikia shilingi bilioni 58.41 ikilinganishwana shilingi bilioni 54.2 Desemba, 2011 sawa na ongezeko laasilimia 7.8.

Mheshimiwa Spika, aidha, mikopo iliyotolewa ilifikiashilingi bilioni 39.43 ikilinganishwa na shilingi bilioni 35.9 kwa

Page 59: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

59

mwaka ulioishia Desemba, 2011 sawa na ongezeko la asilimia9.8. Vile vile, Taasisi iliwekeza shilingi bilioni 4.7 kwenyeDhamana za Serikali na Amana katika Benki zingineikilinganishwa na shilingi bilioni 19.0 zilizowekezwa katikakipindi kama hicho mwaka 2011.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka unaoishiaDesemba, 2013, amana za wateja zinatarajiwa kufikia shilingibilioni 73.25 kutoka shilingi bilioni 58.41 za Desemba, 2012;mapato kutokana na shughuli mbalimbali za kibiasharayanatarajia kufikia shilingi bilioni 12.66 ikilinganishwa na shilingibilioni 9.56 zilizokusanywa Desemba, 2012; na mtaji ghafi waBenki (Owners’ Equity) unatarajiwa kukua kutoka shilingi bilioni5.81 hadi shilingi bilioni 7.24 ifikapo Desemba 2013.

Mheshimiwa Spika, aidha, thamani ya mikopo kwawateja inatarajia kufikia shilingi bilioni 49.10 na uwekezajikatika Dhamana za Serikali na Amana za Muda Maalumkwenye mabenki unatarajia kufikia shilingi bilioni 16.80. Vilevile, Taasisi inatarajia kupata faida kabla ya kodi ya shilingibilioni 0.48.

Mheshimiwa Spika, Benki ya Posta (Tanzania PostalBank); katika kipindi cha mwaka 2012 Benki ilianzisha hudumampya ya Platinum Account inayowalenga vijana walio katikaVyuo Vikuu na Taasisi nyingine za elimu ya juu. Manufaa yahuduma hii ni kuwawezesha vijana kujiwekea akiba nakupitishia mikopo ya elimu. Aidha, Benki iliendelea kupanuamtandao wake kwa kufungua matawi madogo katika ngaziya Wilaya katika vituo vya Shirika la Posta.

Mheshimiwa Spika, vile vile, Benki ilianzisha hudumaya POPOTE Quick Account, inayomwezesha mteja kupatahuduma za benki mahali popote kupitia simu ya mkononi kwalengo la kuwafikia wananchi walio wengi wanaoishi vijijini.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012, amana zawateja zimeongezeka kutoka shilingi bilioni 120.92 mwaka2011 hadi kufikia shilingi bilioni 144.56 ikiwa ni ongezeko laasilimia 19.4. Aidha, benki ilitoa mikopo yenye thamani ya

Page 60: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

60

shilingi bilioni 103.34 ikilinganishwa na shilingi bilioni 66.75mwaka 2011 ikiwa ni ongezeko la asilimia 54.83. Vile vile,uwekezaji katika vitega uchumi vya Benki ya Postaumeongezeka kutoka shilingi bilioni 117.67 mwaka 2011 hadikufikia shilingi bilioni 146.96, ikiwa ni ongezeko la asilimia 24.9.

Mheshimiwa Spika, kadhalika, Benki imepata faidabaada ya kodi ya shilingi bilioni 3.59 ikilinganishwa na shilingibilioni 2.58 mwaka 2011 ikiwa ni ongezeko la asilimia 39.4.Katika mwaka 2012/2013, Serikali iliiongezea Benki ya Postamtaji wa shilingi bilioni 1.5 na kufanya mtaji wa benki kuwajumla ya shilingi bilioni 16.82.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013, benkiitaendelea na mkakati wake wa kuimarisha hudumazitolewazo kupitia Shirika la Posta kwa kukarabati nakuunganisha katika mtandao wa benki vituo 10 vya Postavilivyoko Temeke, Tunduma, Kahama, Geita, Masasi,Peramiho, Njombe, Kyela, Simiyu na Kasulu hivyo kuvipauwezo wa kutoa huduma za haraka. Vituo hivi vitakuwa nimatawi madogo na hivyo kufanya benki kufikisha jumla yamatawi 23. Aidha, benki itafunga vifaa vya kielektroniki katikavituo vya mauzo.

Mheshimiwa Spika, vile vile, Benki inatarajia kupanuawigo wa mikopo kwa kuingia mikataba na Sekretarieti zaMkoa na Jeshi la Kujenga Taifa na kuongeza kipindi chamarejesho kutoka miaka mitatu hadi minne. Kadhalika, Benkiinatarajia kupata faida baada ya kodi ya shilingi bilioni 5.11ikiwa ni ongezeko la asilimia 25.5 ikilinganishwa na faida yashilingi bilioni 4.07 iliyopatikana mwaka 2012.

Mheshimiwa Spika, huduma za bima; katika mwaka2012, Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima imeendeleana mchakato wa kuanzisha Baraza la Usuluhishi la Bima(Insurance Ombudsman) ambapo kwa sasa Mamlakaimekamilisha uandaaji wa Kanuni zitakazoongoza utendajiwa Baraza hilo na kusambaza kwa wadau mbalimbali kwaajili ya kutoa maoni yao.

Page 61: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

61

Mheshimiwa Spika, Mamlaka imefungua ofisi katikaJiji la Mbeya kwa ajili ya kutoa huduma katika Mikoa yaKanda ya Nyanda za Juu Kusini. Hii inafanya idadi ya Ofisi zaKanda zilizofunguliwa hadi sasa kufikia tatu ikijumuisha ofisizilizopo Kanda ya Kaskazini katika Jiji la Arusha na Kanda yaZiwa katika Jiji la Mwanza. Aidha, Mamlaka inaendelea namaandalizi ya kufungua ofisi nyingine za kanda katika mikoaya Dodoma (Kanda ya Kati) na Mtwara (Kanda ya Kusini).

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2013/2014, Mamlaka inatarajia kuendelea na taratibu za kuoanishasheria na kanuni za soko la bima katika eneo la AfrikaMashariki na nchi za SADC; kuendelea kushirikiana na VyuoVikuu vya hapa nchini na nje ya nchi kwa ajili ya kurahisishautolewaji wa elimu ya juu ili kupatikane wataalam wengi wafani ya bima; na kukamilisha tafiti za bima ya kilimo na mifugo,bima ya watu wa kipato cha chini (micro-insurance) nanamna bora ya kuanzisha bima inayofuata Sheria za Kiislam- Takaful. Aidha, Mamlaka inatarajia kuanzisha vipindi vyautoaji wa elimu ya bima katika vyombo vya habari, vyuonina mashuleni.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2012/2013, Shirika la Bima la Taifa limeendelea na utekelezaji wamkakati wa kuligawa Shirika katika kampuni mbili tofauti, mojaya bima za maisha na nyingine ya bima za kawaida. Shirikalimeanza kutenganisha hesabu za biashara hizi mbili lengolikiwa kujua uwezo wa kila kampuni kujiendesha kibiashara.Aidha, katika kipindi cha mwaka 2012, Shirika lililipa madaiya shilingi bilioni 6.79 kwa wateja wake.

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2012, mapato yabima yalikuwa shilingi bilioni 27.87, mapato ya Shirikakutokana na bima za mtawanyo (reinsurance income)yalifikia shilingi bilioni 2.08 na mapato kutokana na vitegauchumi yalifikia shilingi bilioni 5.17. Aidha, kwa mwaka wafedha 2013/2014, NIC itaendelea na utekelezaji wa mkakatiwa kuligawa Shirika katika kampuni mbili kwa mujibu waSheria ya Bima ya mwaka 2009.

Page 62: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

62

Mheshimiwa Spika, masoko ya mitaji na dhamana;katika mwaka wa fedha 2012/2013, Mamlaka ya Masoko yaMitaji na Dhamana imekamilisha uanzishwaji wa soko laujasiriamali (Enterprise Growth Market) ikiwemo kutoa lesenina Mafunzo kwa wataalam washauri (Nominated Advisors)watakaoshauri kampuni zinazotaka kujiorodhesha kwenyesoko la kampuni za ujasiriamali.

Mheshimiwa Spika, soko la kukuza ujasiriamali likotayari kwa kampuni kujiorodhesha na Mamlaka inaendeleakutoa elimu juu ya fursa zilizopo kwenye Soko hilo. Aidha,Mamlaka imeandaa Mpango Mkakati wa miaka mitano2013/2014 - 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, Mamlaka imekamilisha utafitikuhusu mfumo wa kisheria na uendeshaji wa soko laHatifungani za Manispaa (Municipal Bond). Aidha, Mamlakainafanya maandalizi ya kuanzisha soko mbadala lahatifungani ikiwa ni pamoja na kuandaa taratibu za soko hilo.Maandalizi yote muhimu yanatarajiwa kukamilika ndani yamwaka wa fedha 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, vile vile, Mamlaka imefanya tafitinyingine tatu ambazo zinahusu Mfumo wa Kisheria naUsimamizi wa Soko la Bidhaa; muundo wa soko la bidhaa; nauhusiano kati ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani na Soko laBidhaa. Tafiti hizi zitasaidia kuweka mazingirayatakayowezesha uanzishwaji wa Soko la Bidhaa nchini.

Mamlaka pia imetayarisha Mpango Kazi juu yauanzishwaji wa Soko la Bidhaa ambao unatarajiwakutekelezwa kuanzia mwaka 2013/2014. Kadhalika, katikamwaka wa fedha 2013/2014, Wizara kwa kushirikiana naMamlaka imepanga kuandaa sera na mpango wa Kitaifawa maendeleo ya masoko ya mitaji na dhamana.

Mheshimiwa Spika, soko la Hisa Dar es Salaam (DSE);hadi kufikia Aprili 2013, hisa zilizoorodheshwa kwenye soko nihisa milioni 35.4 za ziada na upendeleo za DCB CommercialBank. Kwa upande wa uuzaji na ununuzi wa dhamana, hisa

Page 63: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

63

zenye thamani ya shilingi bilioni 49.25 ziliuzwa. Vile vile,hatifungani za Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni 379.61ziliuzwa.

Mheshimiwa Spika, DSE iliendelea na mipango yamaandalizi ya uzinduzi wa Soko la Ujasiriamali (EnterpriseGrowth Market- EGM) kwa kupitia upya kanuni za soko nakufuatilia kwa Mamlaka hatua za upatikanaji leseni kwakampuni za udhamini. Rasimu ya kanuni mpya za sokoimewekwa katika tovuti ya DSE (www.dse.co.tz) ili kupatamaoni kutoka kwa wadau. Aidha, utafiti kuhusu kubadilishaSoko kuwa kampuni inayojiendesha kibiashara umefanyikana DSE wataandaa mpango kazi wa utekelezaji wamapendekezo yaliyotolewa.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2013/2014, DSE inatarajia kuweka mazingira yatakayowezeshakampuni za sekta muhimu kama madini na mawasiliano yasimu kuorodheshwa sokoni; kupanua wigo wa huduma zasoko na kuimarisha muundo wa Soko kuendana na mahitajiya ukuaji wake.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, UTTimeanzisha Mfuko mpya wa uwekezaji wa pamoja unaolengakuwekeza katika masoko ya fedha na dhamana ujulikanaokama Liquid Fund. Mfuko huu unatoa njia mbadala kwaWawekezaji wanaotaka kuweka fedha zao katika kipindi chamuda mfupi na katika kiwango kilichopo kwenye ushindani.Aidha, kuanzia mwezi Aprili, 2013, UTT imeanza kutoa mikopoili kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, UTTinatarajia kuanzisha Mfuko mmoja wa uwekezaji wa pamojaujulikanao kwa jina Dollar Fund. Mfuko huu uliahirishwakuanzishwa mwaka wa huu wa fedha ili kutoa muda zaidiwa kutathmini mazingira ya uendeshaji wa Mfuko kwakuzingatia vigezo mbalimbali vya fedha za kigeni nchini.Aidha, UTT itaendelea kuhamasisha uelewa juu ya dhana yauwekezaji kupitia elimu kwa umma kwa njia mbalimbali.

Page 64: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

64

Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Kitaalam na Hudumanyinginezo Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS); katika mwaka wafedha 2012/2013, Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeendesha zoezila Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012. Matokeo yaawali yanaonesha kuwa Tanzania ina idadi ya watu44,928,923 ambapo Tanzania Bara kuna watu 43,625,354 naTanzania Zanzibar kuna watu 1,303,569. Serikaliimekwishasambaza matokeo ya Sensa ya Watu na Makaziya mwaka 2012.

Mheshimiwa Spika, pamoja na shughuli ya sensa, NBSilitayarisha na kusambaza Takwimu za Msingi (Core Statistics)ambazo zilihusisha ukokotoaji wa Pato la Taifa. Aidha, NBSilifanya tafiti za kijamii na kiuchumi na kusambaza viashiriavilivyotokana na tafiti hizo kwa wadau wote.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2013/2014, Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendelea kutekeleza jukumulake la kukusanya, kuchambua na kusambaza takwimu rasmikwa wadau wote nchini kama ilivyoainishwa katika Sheriaya Takwimu, Sura 351. Vile vile, NBS itaendelea na kazi yauchambuzi na uchapishaji wa makala ya takwimu za Sensaya Watu na Makazi ya mwaka 2012.

Mheshimiwa Spika, Bodi ya Taifa ya Wahasibu naWakaguzi (NBAA); hadi kufikia Desemba, 2012, idadi yaWahasibu waliosajiliwa ilikuwa 4,281, kati ya hao: watunzavitabu ni 208; Wahasibu wahitimu 2,254; Wahasibuwaliosajiliwa ngazi ya CPA 1,185; Wahasibu waliosajiliwa kamaWakaguzi Hesabu katika ngazi ya CPA-PP 452; Kampuni zaUkaguzi Hesabu zilizosajiliwa 166; na Kampuni za Uhasibuzilizosajiliwa 16.

Mheshimiwa Spika, aidha, NBAA imekamilisha kuharirimitaala na silabi za taaluma ya uhasibu ambapo mitihani yakwanza chini ya silabi mpya inatarajiwa kufanyika katikamwaka wa fedha 2013/2014. Vile vile, Bodi inaendelea naawamu ya pili ya ujenzi wa Kituo cha Taaluma ya Uhasibueneo la Bunju - Dar es Salaam unaotarajiwa kukamilikamwaka 2013/2014.

Page 65: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

65

Mheshimiwa Spika, Bodi ya Wataalam wa Ununuzi naUgavi (PSPTB), katika mwaka 2012/2013, Bodi imetahiniwanataaluma 1,971 ambapo wanataaluma 744 sawa naasilimia 37.7 walifaulu hivyo kufanya idadi ya wahitimu kufikia20,610 ikijumuisha wahitimu wa Bodi ya Taifa ya Usimamizi waVifaa. Aidha, Bodi ilitoa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu25 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya juu kwa lengo lakuwajengea uzoefu wa kazi ili waweze kujiajiri.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2013/2014, Bodi inatarajia kutekeleza yafuatayo: kutoa mafunzoendelevu kwa wataalam ili kuboresha uwezo wa utendaji;kuongeza idadi ya watahiniwa wa mitihani na usajili kwawanataaluma na kuboresha mazingira ya kujifunzia.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2012/2013, hadi kufikia Aprili 2013, Bodi imekusanya kodi ya shilingibilioni 9.58 sawa na asilimia 85.23 ya lengo la shilingi bilioni11.24. Aidha, mapato ya Bodi yalifikia shilingi bilioni 4.29 sawana asilimia 81.01 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 5.37.Katika mwaka 2013/14, Jumla ya shilingi bilioni 15.16zinatarajiwa kukusanywa na Bodi, ikiwa ni kodi itokanayo namichezo ya kubahatisha. Aidha, mapato ya Bodiyanatarajiwa kufikia 6.68 na ongezeko la asilimia 24.39.

Mheshimiwa Spika, Taasisi za Mafunzo, katika mwaka2012/2013, Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA) imeendelea kutoamafunzo ya muda mrefu na mfupi katika ngazi za stashahadaya juu na uzamili ambapo jumla ya wanafunzi 3,303walidahiliwa. Aidha, Wanafunzi 1,708 walihitimu katika mwakawa masomo 2011/2012, katika ngazi na fani mbalimbali hivyokuifanya IAA kufikisha jumla ya wahitimu 8,010 toka mwaka1999.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, IAAinakusudia kuanzisha Kituo cha Elimu kwa Njia ya Mtandao(e-Learning Centre); kuanzisha Kitengo cha Masomo ya Jionina kuanzisha Kampasi ya masomo katika Mji wa Babati,Mkoani Manyara.

Page 66: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

66

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM), katika mwaka 2012/2013, Chuo kilifanya maandalizi yakuanzisha kozi mpya nne za Shahada ya Uzamili za: Uhasibuna Fedha, Fedha na uwekezaji, Menejimenti ya RasilimaliWatu na Biashara (MBA) ambayo itaendeshwa kwaushirikiano na Chuo cha IIFT (Indian Institute of Foreign Trade)cha India. Aidha, Chuo kilidahili wanafunzi 9,500 katika kozina fani mbalimbali, ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 1,500 sawana asilimia 18.75 kulinganisha na mwaka 2011/2012.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, chuokitatekeleza yafuatayo: kuanza maandalizi ya ujenzi waKampasi ya Msata yenye uwezo wa kuchukua zaidi yawanafunzi 15,000; kuboresha ufanisi wa chuo katika utafiti,machapisho na majarida; kuboresha mlingano wa kijinsia;kuboresha mifumo ya habari na utoaji huduma; nakukitangaza chuo ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA);katika mwaka 2012/2013, TIA ilidahili wanafunzi 8,379. Aidha,Taasisi imefungua tawi jipya katika Jiji la Mwanza. Vile vile,Taasisi imeendelea na mipango ya kuanzisha tawi katika Mjiwa Kigoma ili kuhudumia Mikoa ya Kigoma, Tabora na Rukwana hivyo kusogeza huduma zake karibu na wananchi.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, TIAinatarajia kuanza maandalizi kwa ajili ya kutoa mafunzo yaShahada ya Uzamili kwa kushirikiana na vyuo vya nje ya nchi.Matarajio kwa mwaka ujao wa fedha ni kufikia Wanachuo8,800.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/2013, Chuocha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) kilifanya udahili kwawanafunzi 2,394 na kufanya jumla ya wanafunzi kufikia 4,600.Katika kipindi hicho, wanafunzi 1,490 walihitimu katika kozimbalimbali. Aidha, Chuo kilikamilisha uandaaji wa mitaalana kuanzisha Programu tano (5) mpya kwa ajili ya Shahadaya kwanza na Shahada ya Uzamili.

Mheshimiwa Spika, Programu hizo mpya ni Shahada

Page 67: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

67

ya Mipango na Usimamizi wa Rasilimali Watu; Shahada yaUchumi wa Maendeleo; Shahada ya Mipango Miji naUsimamizi wa Mazingira; Shahada ya Uzamili katika Uchumiwa Maendeleo; na Shahada ya Uzamili katika Mipango naUsimamizi wa Mazingira.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Chuokinatarajia kukamilisha mradi wa ujenzi wa jengo la pili laTaaluma Kampasi ya Dodoma. Kukamilika kwa mradi huukutasaidia kuongeza udahili wa wanafunzi na kuwa namazingira bora katika kutimiza majukumu ya kitaaluma.

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Takwimu Mashariki mwaAfrika – EASTC, katika mwaka 2012/2013, Chuo kilidahiliwanafunzi 177 katika fani ya Takwimu kwa ngazi ya Cheti,Stashahada na Shahada. Chuo pia kiliendesha mafunzo yaTakwimu za Kilimo chini ya ufadhili wa Benki ya Maendeleoya Afrika kwa kushirikiana na Chuo cha NASA kilichopo India.Mafunzo hayo yalitolewa kwa Maofisa 30 kutoka Wizara naTaasisi mbalimbali. Chuo pia kilitoa mafunzo ya muda mfupiya uchambuzi wa takwimu kwa watumishi wa Ofisi ya Taifaya Takwimu.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/2014, Chuokitaendesha mafunzo ya muda mfupi kwa nchi zinazotumiahuduma ya Chuo ili kuzijengea uwezo na kuongeza idadi yawatumishi wenye uelewa na weledi wa kukusanya nakuchambua takwimu. Aidha, Chuo kinatarajia kuongezaidadi ya kozi kufikia nane. Kozi mpya zinazotarajiwa kuanzakufundishwa ni Shahada ya Takwimu katika Kompyuta,Stashahada za Uzamili katika Takwimu Rasmi na Takwimu zaKilimo na kozi ya Uzamili katika Takwimu za Kilimo.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu yake,Wizara ilikabiliwa na changamoto zifuatazo:-

(i) Kudhibiti matumizi ya fedha za ummasambamba na kuongeza mapato ya Serikali;

(ii) Kuzingatia kanuni na taratibu zilizoainishwa

Page 68: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

68

kwenye Mkakati wa Pamoja wa Misaada Tanzania(MPAMITA) na upatikanaji wa fedha kutoka kwa wafadhiliwa nje;

(iii) Kuwa na Sera ya Mali ya Serikali;

(iv) Kufikiwa kwa malengo ya ukusanyaji wamapato yasiyo ya kodi;

(v) Kuwepo kwa mahitaji makubwa ya fedha njeya bajeti;

(vi) Kuwepo kwa mchakato mrefu wa upatikanajiwa fedha za kugharamia Miradi ya Maendeleo hasa mikopoya kibiashara (non-conscessional borrowing); na

(vii) Kuongezeka kwa malimbikizo ya madeni yandani katika mafungu mbalimbali ambayo yameshindwakuingizwa kwenye viwango vya bajeti.

Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana nachangamoto hizo, Wizara itachukua hatua kupitia mipangona bajeti zake ili kuhakikisha kuwa changamoto hizizinapatiwa ufumbuzi katika mwaka 2013/2014 na kuendelea.Ufumbuzi wa changamoto hizi utaelezwa katika hotuba yabajeti ya Serikali itakayowasilishwa tarehe13 Juni, 2013.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2012/2013, majukumu ya Wizara yalitekelezwa katika mafungu sitaya kibajeti. Mafungu hayo ni Fungu 50 - Wizara ya Fedha;Fungu 23 - Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali; Fungu 22 -Deni la Taifa; Fungu 21 – HAZINA; Fungu 13 - Kitengo chaUdhibiti wa Fedha Haramu; na Fungu 10 – Tume ya Pamojaya Fedha. Aidha, Fungu 45 - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ambayoinajitegemea linaombewa fedha Bungeni na Waziri wa Fedhakwa mujibu wa Sheria.

Mheshimiwa Spika, Fungu 50 - Wizara ya Fedha,Wizara ilitarajia kupata shilingi bilioni 124.42 kutoka vyanzombalimbali vya mapato yasiyo ya kodi kupitia Fungu 50.

Page 69: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

69

Vyanzo hivyo ni pamoja na mauzo ya mali, uuzaji wa nyarakaza zabuni na mapato kutoka katika Mashirika ya Umma naTaasisi za Serikali (Gawio, Michango na Marejesho ya mikopo).

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Aprili, 2013,makusanyo yalifikia shilingi bilioni 37.27 sawa na asilimia 29.95ya lengo. Makusanyo zaidi yanatarajiwa katika robo ya nneya mwaka wa fedha baada ya Mashirika mengi kuandaahesabu za mwaka na ukaguzi wa hesabu hizo kukamilishwa.

Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya Fungu50 kwa mwaka 2012/2013 yalikuwa shilingi bilioni 98.41 kwaajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 546.51 kwa ajiliya matumizi ya maendeleo. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2013,matumizi ya kawaida yalifikia shilingi bilioni 70.32 sawa naasilimia 71.46 ya makadirio na matumizi ya maendeleoyalifikia shilingi bilioni 311.28 sawa na asilimia 56.96 yamakadirio.

Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya Fungu23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali; kwa mwaka 2012/2013 yalikuwa shilingi bilioni 75.12 kwa ajili ya matumizi yakawaida na shilingi bilioni 6.12 kwa ajili ya matumizi yamaendeleo. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2013, matumizi yakawaida yalifikia shilingi bilioni 49.34 sawa na asilimia 65.68ya makadirio na matumizi ya maendeleo yalifikia shilingi bilioni1.29 sawa na asilimia 21.08 ya makadirio.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2012/2013, makadirio ya matumizi ya Fungu 22 – Deni la Taifa,yalikuwa shilingi bilioni 2,735.91. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2013matumizi ya fungu hili yalifikia shilingi bilioni 2,226.70 sawa naasilimia 81.39 ya makadirio.

Mheshimiwa Spika, Fungu 21 – Hazina; katika mwakawa fedha 2012/2013, Wizara kupitia Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA) ilikadiria kukusanya mapato ya shilingi bilioni8,070. Hadi kufikia Aprili, 2013, TRA ilikusanya shilingi bilioni 6,580sawa na asilimia 97.84 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni6,725 katika kipindi hicho.

Page 70: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

70

Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya Fungu21 kwa mwaka 2012/2013 yalikuwa shilingi bilioni 725.57 kwaajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 101.95 kwa ajiliya matumizi ya maendeleo. Aidha, kiasi cha Shilingi bilioni50.66 kilifanyiwa uhamisho kuongezea katika zoezi la Sensaya Watu na Makazi na kufanya makadirio ya matumizi yamaendeleo kwa mwaka 2012/2013 kuwa shilingi bilioni 152.61.Hadi kufikia mwezi Aprili, 2013, matumizi ya kawaida yalifikiashilingi bilioni 516.61 sawa na asilimia 71.2 ya makadirio namatumizi ya maendeleo yalifikia shilingi bilioni 131.95 sawana asilimia 86.46 ya makadirio.

Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya Fungu13 – Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu kwa mwaka2012/2013, yalikuwa shilingi bilioni 2.16 kwa ajili ya matumiziya kawaida na shilingi bilioni 0.26 kwa ajili ya matumizi yamaendeleo. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2013, matumizi yakawaida yalifikia shilingi bilioni 1.01 sawa na asilimia 46.76 yamakadirio, na matumizi ya maendeleo yalifikia shilingi bilioni0.04 sawa na asilimia 15.38 ya makadirio.

Mheshimiwa Spika, Fungu 10 – Tume ya Pamoja yaFedha, makadirio ya matumizi ya kawaida kwa Fungu hiliyalikuwa shillingi bilioni 1.99, hadi kufikia Aprili, 2013 matumiziyalifikia shilingi bilioni 1.33 sawa na asilimia 66.83 ya makadirio.

Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya Fungu45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa mwaka 2012/2013 yalikuwashilingi bilioni 55.02 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingibilioni 9.62 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadi kufikiamwezi Aprili, 2013, matumizi ya kawaida yalifikia shilingi bilioni39.51 sawa na asilimia 71.81 ya makadirio na matumizi yamaendeleo yalifikia shilingi bilioni 3.18 sawa na asilimia 33.06ya makadirio.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2013/2014, Wizara ya Fedha inakadiria kukusanya mapato yasiyoya kodi yapatayo shilingi 2,718,102,000 (bilioni 2.72) kupitiaFungu 50 - Wizara ya Fedha na shilingi 124,013,512,000 (bilioni124.01) kupitia Fungu (7)- Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Page 71: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

71

Mheshimiwa Spika, maombi ya fedha, baada yakueleza kwa kina utekelezaji wa majukumu na kazi za Wizarakwa mwaka 2012/2013, changamoto na hatuazilizochukuliwa na mpango na malengo ya bajeti kwa mwaka2013/2014, nawasilisha rasmi mapendekezo ya maombi yafedha kwa mwaka 2013/2014 kwa ajili ya matumizi ya Fungu50, 23, 22, 21, 13, 10, (7) na 45 kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Fungu 50 – Wizara ya Fedha, katikafungu hili kwa mwaka wa fedha 2013/14, Wizara inaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-

(a) Matumizi ya kawaida Sh. 53,011,091,000 (bilioni53.01). Kati ya hizo mishahara ni sh. 4,564,609,000 (bilioni 4.56)na matumizi mengineyo sh. 48,446,482,000 (bilioni 48.45).

(b) Miradi ya Maendeleo Sh. 233,669,169,000(bilioni 233.67). Kati ya hizo:

(i) Fedha za Ndani – Sh. 10,200,000,000 (bilioni10.20).

(ii) Fedha za Nje – Sh. 223,469,169,000 (bilioni223.47).

Mheshimiwa Spika, Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuuwa Serikali: Katika fungu hili kwa mwaka wa fedha 2013/2014, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kamaifuatavyo:-

(a) Matumizi ya kawaida – Sh. 80,831,672,000(bilioni 80.83). Kati ya hizo mishahara sh. 4,434,410,000 (bilioni4.43) na matumizi mengineyo sh. 76,397,262,000 (bilioni 76.40).

(b) Miradi ya Maendeleo – Sh. 4,755,547,000(bilioni 4.76) Kati ya hizo:

(i) Fedha za Ndani –Sh. 400,000,000 (bilioni 0.40).

(ii) Fedha za Nje -Sh. 4,355,547,000 (bilioni 4.36).

Page 72: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

72

Mheshimiwa Spika, Fungu 22 – Deni la Taifa, katikafungu hili kwa mwaka wa fedha 2013/14, Wizara inaombakuidhinishiwa kiasi cha Sh. 3,319,017,772,000 (bilioni 3,319.02).Kati ya hizo mishahara ni sh. 6,311,772,000 (bilioni 6.31) namatumizi mengineyo ni sh. 3,312,706,000,000 (bilioni 3,312.71).

Mheshimiwa Spika, Fungu 21 – Hazina, katika funguhili kwa mwaka wa fedha 2013/2014, Wizara inaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-

(a) Matumizi ya kawaida Sh. 1,378,142,566,000(bilioni 1,378.14). Kati ya hizo mishahara ni sh. 2,632,424,000(bilioni 2.63) na matumizi mengineyo sh. 1,375,510,142,000(bilioni 1,375.51) ambazo ni kwa ajili ya matumizi ya Idara naTaasisi zilizo chini ya Fungu hili, nyongeza ya mishahara yaWatumishi wa Serikali na matumizi maalum.

(b) Miradi ya maendeleo ni sh. 38,190,162,000(bilioni 38.19). Kati ya hizo:

(i) Fedha za Ndani- Sh. 7,893,000,000 (bilioni 7.89).

(ii) Fedha za Nje- Sh. 30,297,162,000 (bilioni 30.30).

Mheshimiwa Spika, Fungu 13 – Kitengo cha Udhibitiwa Fedha Haramu: Katika Fungu hili kwa mwaka wa fedha2013/2014, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedhakama ifuatavyo:-

(a) Matumizi ya kawaida – Sh. 1,944,790,000(bilioni 1.94).

(b) Miradi ya Maendeleo, fedha za nje Sh.399,985,000 (bilioni 0.39).

Mheshimiwa Spika, Fungu 10 – Tume ya Pamoja yaFedha: Katika fungu hili kwa mwaka wa fedha 2013/2014,Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha Sh. 2,064,424,000(bilioni 2.06) kwa matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo,

Page 73: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

73

sh. 362,771,000 (bilioni 0.36) ni kwa ajili ya mishahara na sh.1,701,653,000 (bilioni 1.70) ni matumizi mengineyo.

Mheshimiwa Spika, Fungu (7) – Ofisi ya Msajili waHazina: Katika fungu hili kwa mwaka wa fedha 2013/2014,Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kamaifuatavyo:-

(a) Matumizi ya kawaida – Sh. 38,088,142,000(bilioni 38.08). Kati ya hizo sh. 303,192,000 (bilioni 0.30) ni kwaajili ya mishahara na sh. 37,784,950,000 (bilioni 37.78) nimatumizi mengineyo.

(b) Miradi ya Maendeleo – Sh. 1,665,300,000(bilioni 1.67). Kati ya hizo:

(i) Fedha za Ndani –Sh. 600,000,000 (bilioni 0.60).

(ii) Fedha za Nje -Sh. 1,065,300,000 (bilioni 1.07).

Mheshimiwa Spika, fungu 45- Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi:Katika fungu hili kwa mwaka wa fedha 2013/2014, Wizarainaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-

(a) Matumizi ya kawaida sh. 57,406,414,000 (bilioni57.40). Kati ya hizo mishahara ni sh. 6,692,935,000 (bilioni 6.69)na matumizi mengineyo sh. 50,713,479,000 (bilioni 50.71).

(b) Miradi ya maendeleo sh. 21,449,100,000 (bilioni21.45). Kati ya hizo:

(i) Fedha za ndani sh. 15,250,000,000 (bilioni15.25).

(ii) Fedha za nje sh. 6,199,100,000 (bilioni 6.20).

Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuruWaheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. Hotuba hii piainapatikana katika tovuti ya Wizara (www.mof.go.tz).

Page 74: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

74

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika,naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

SPIKA: Ahsante, hoja imeungwa mkono sasanitamwita Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Viwanda naBiashara Mheshimiwa Mahmoud Mgimwa.

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA – MWENYEKITI WAKAMATI YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA: MheshimiwaSpika, kwa mujibu wa kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumuza Bunge, Toleo la 2013, naomba kuwasilisha Taarifa yaKamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda naBiashara kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Fedhakwa mwaka wa Fedha 2012/2013 na Makadirio ya Mapatona Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2013/2014:Fungu 50 – Wizara ya Fedha, Fungu 21- Hazina, Fungu 22 –Deni la Taifa, Fungu 23 – Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali,Fungu 10 -Tume ya Pamoja ya Fedha, Fungu 13 – Kitengocha Kudhibiti Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi na Fungu07-Msajili wa Hazina.

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Uchumi, Viwanda naBiashara ilikutana na Wizara ya Fedha kwa nyakati tofautina kupokea maelezo ya muhtasari wa Bajeti ya Wizara yaFedha kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014; pamoja na kupokeaTaarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara hiyo namafungu yake kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013.

Mheshimiwa Spika, aidha, Waziri wa Fedha alitoamaelezo kuhusu utekelezaji wa maoni na ushauri wa Kamatikwa Wizara kwa mwaka wa Fedha 2012/2013, changamotoza utekelezaji wa kipindi cha mwaka 2012/2013; na malengona maeneo ya vipaumbele pamoja na makadirio ya Mapatona matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa Majukumu ya

Page 75: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

75

Wizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013; Kamatiinaipongeza Wizara ya Fedha kwa kutekeleza vyemamalengo yake kwa mwaka uliotangulia ikiwa ni pamoja namipango mizuri waliyojiwekea kwa Mwaka huu wa Fedha iliiweze kufikia malengo yake.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, Kamati imeendeleakutoa maoni, ushauri na maelekezo ambayo Wizara ya Fedhaimeendelea kuyazingatia katika kuboresha utekelezaji wamajukumu yake ya msingi ambayo ni; kubuni na kusimamiautekelezaji wa sera za uchumi jumla; kusimamia ukusanyajiwa mapato ya ndani na nje pamoja na matumizi ya Serikali;kufuatilia mipango ya kupunguza umaskini; kusimamia denila Taifa; upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya miradi yaubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi; kusimamia Sheria, Kanunina taratibu za uhasibu, ukaguzi wa ndani wa Serikali, ununuziwa umma na usimamizi wa mali za Serikali pamoja nakushirikiana na Tume ya Mipango katika kutekeleza mipangoya maendeleo iliyoainishwa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikioyaliyopatikana katika Kipindi cha mwaka 2012/2013, badoWizara inakabiliwa na changamoto zifuatazo:-

(i) Matumizi makubwa ya Serikali pamoja nakuwepo kwa mahitaji makubwa ya Serikali nje ya Bajeti;

(ii) Kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za ummasambamba na kuongeza mapato ya Serikali;

(iii) Kuongezeka kwa malimbikizo ya madeni yandani katika mafungu mbalimbali ambayo yameshindwakuingizwa kwenye viwango vya bajeti;

(iv) Kupunguza na kudhibiti Mfumuko wa Bei iliurudi kwenye viwango vya tarakimu moja;

(v) Upungufu katika Sheria ya Msajili wa Hazinana Sheria zilizoanzisha Asasi na Mashirika mbalimbali yaumma;

Page 76: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

76

(vi) Kuwepo kwa mchakato wa muda mrefu waupatikanaji wa fedha za kugharamia Miradi ya Maendeleohasa mikopo ya kibiashara (non-conscessional borrowing);

(vii) Matumizi ya fedha nje ya bajeti iliyoidhinishwana Bunge;

(viii) Kutozingatiwa ipasavyo kwa Sheria ya Ununuziwa Umma; na

(ix) Kutokuwa na Sera ya Mali za Serikali.

Mheshimiwa Spika, pamoja na changamoto hiziWizara imejitahidi kuchukua hatua mbalimbali kukabiliananazo ikiwa ni pamoja na kupitia mipango na bajeti zake ilikuhakikisha kuwa changamoto hizo zinapatiwa ufumbuzikatika mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa maoni na ushauriwa Kamati kwa mwaka wa fedha 2012/2013, pamoja nachangamoto katika kutekeleza Mpango na Bajeti ya Mwakawa Fedha wa 2013/2014; Kamati Uchumi, Viwanda naBiashara ilitoa maoni na ushauri juu ya utekelezaji katikamaeneo mbalimbali ya kukuza Uchumi, hasa kwenyemaeneo yaliyohusu Matumizi na Mapato ya Serikali; Deni laTaifa Misamaha ya Kodi; Ubia kati ya Sekta ya Umma na SektaBinafsi (Public Private Partnership); Manunuzi ya Umma;Urasimu uliopo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleopamoja na vikwazo katika maeneo ya uwekezaji na ufanyajiwa biashara.

Mheshimiwa Spika, Kamati iliridhika na utekelezaji wabaadhi ya ushauri iliyoutoa kwa Wizara na hivyo kuliombaBunge lako Tukufu lipitishe makadirio ya Wizara hii. Hata hivyo,bado yapo maeneo yanayohitaji kuangaliwa ili kuendelezaufanisi na tija katika utekelezaji wa kuinua uchumi wa nchipamoja na nidhamu ya matumizi ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, sekta ya fedha imeendeleakuimarika kufuatia usimamizi thabiti wa Benki Kuu na hivyo

Page 77: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

77

kuwa na jumla ya benki na taasisi za fedha 51 zenye matawi559 nchini kote. Rasil imali katika sekta ya mabenkiimeendelea kukua na kufikia kiasi cha trilioni 17.9 mwezi Machi2013 kutoka trilioni 14.7 mwezi Machi 2012, hii inaonesha kuwamabenki yote nchini yana mitaji ya kutosha (capitaladequate ratio) ni salama na yanaweza kuhimili misukosukoya kifedha.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuongezeka kwa idadiya benki hapa nchini, huduma za kifedha hazijawezakuwafikia wananchi wa kawaida wakiwemo wakulima nawafanyabiashara wadogo wadogo. Mfumo wa kibenkitulionao unalenga zaidi kuhudumia wafanyabiasharawakubwa, makampuni makubwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, aidha, mabenki na taasisi nyingiza fedha zimeendelea kutoa huduma za kibenki na kifedhamijini na hivyo kuwafanya Watanzania wengi ambaowanaishi vijijini kutofikiwa na huduma hizo kwa urahisi, haliambayo inaufanya uchumi wetu kuwa ‘cash based’. Tafitizinaonyesha ni asilimia 8 tu ya Watanzania kati ya 100wanatumia huduma za kibenki na asilimia nne ya watanzaniahutumia huduma za asasi ndogondogo za fedha (MFIs).

Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kwamba, mwaka1998 Serikali iliruhusu kuwepo kwa Benki za Wananchi hatuahiyo ilipelekea kuanzishwa kwa benki za wananchi za Mufindi,Mwanga, Mbinga na kadhalika na hadi sasa kuna benki zaaina hiyo 11. Benki za wananchi, pamoja na uchache wakezimeweza kutoa mchango mkubwa katika kutoa hudumaza kibenki kwa Watanzania wa kawaida.

Mheshimiwa Spika, aidha SACCOS ambazo zilikuwani mkombozi wa watu wa vijijini, zimedumaa au kufilisikakutokana na kukosekana kwa usimamizi thabiti kama yalivyomabenki; hali inayopelekea kuwepo kwa uzalishaji duni katikakilimo - wakulima (kukosekana mitaji), wajasiriamali wadogokushindwa kukuza biashara zao, kuwepo kwa huduma zakifedha haramu kama DECI, wakulima kuuza mazao yako

Page 78: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

78

kwa bei ya chini kwa wakopeshaji binafsi na pia hali yauwekaji akiba Kitaifa kuwa chini ya kiwango cha Sub SaharanAfrica cha asilimia 30.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia haya, Kamatiinapendekeza yafuatayo:-

(a) Kuwepo na sheria ya huduma za kifedha kwawatu wa kipato cha chini (The Microfinance Act). Asasi nyingizinazotoa huduma za kifedha kwa watu wa chinihazijasajiliwa na kupewa leseni ya kutoa huduma za kifedha.Asasi hizo zimesajiliwa kwa sheria mbalimbali zikiwepo Sheriaya NGO’s (2002), Sheria ya Makampuni (2002), RITA nakadhalika. Pamoja na usajili huo lakini hazina leseni ya kutoahuduma za kifedha.

(b) Benki Kuu iandae taratibu na kanuni maalumza kusimamia benki za wananchi kama ilivyo kwenye nchinyingine zenye benki za aina hiyo. Benki nyingi za Wananchizinatoa huduma za kifedha vijijini tofauti na Mabenkimakubwa ya Kitaifa au Kimataifa.

(c) Serikali ianzishe Sheria ya SACCOS sambambana uanzishwaji wa mamlaka itakayosimamia SACCOS hizokama ilivyo kwa nchi ya Kenya. Tanzania haina sheria yaSACCOS au Financial Cooperatives, kwa sasa sheriainayotumika ni ile ya Ushirika. SACCOS ni asasi za kifedha hivyozina kanuni na unyeti tofauti na ushirika wa aina nyingine.

(d) Serikali isaidie kurasimisha asasi zisizo rasmi.Kumekuwepo na huduma za akiba na mikopo zinazotolewana asasi zisizo rasmi kama vile Upatu/vibati (Rotating andSavings Associations-ROSCAS), Vikundi vya akiba na mikopo(Accumulated Savings and Credit Associations-ASCAS),VICOBA na Vyama vya Kufa na Kuzikana. Asasi hizo zimekuwamaarufu sana hapa nchini na zinatoa fursa ya kujenga tasniaendelevu ya fedha lakini havijapewa uzito unaostahili.

(e) Serikali ianzishe Sera ya Maendeleo yaHuduma za Kibenki (Banking Sector Development Policy) ili

Page 79: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

79

kujenga mfumo wa huduma za kibenki unaolingana na hatuaya maendeleo na mazingira ya nchi husika pamoja na kutoahuduma ya kibenki kulingana na sekta inayohudumia.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2007/2008 - 2012/2013, takwimu zinaonesha kuwa, kiasi cha asilimia3.1 ya Pato la Taifa lilitolewa kwenye mapato ya Serikaliyakiwa kama misamaha ya kodi kwenye VAT na Ushuru waForodha. Kamati inaona bado kiwango cha misamaha yakodi kipo juu kwa kiasi kikubwa na hivyo vinaathiri ujazo wamapato yatokanayo na kodi. Mfano takribani ya asilimia 64ya wastani wa kodi zote zilizosamehewa katika kipindi cha2008/2009 - 2011/2012 zilikuwa ni misamaha ya VAT, kupitiajedwali la Tatu la Sheria ya VAT ambalo hapo awali mwaka1997, wakati linaanzishwa lilikuwa na vitu vitano tu na sasalina vitu 27.

Mheshimiwa Spika, zoezi la kupitia upya Sheria ya VATna kuondoa nusu ya misamaha ya kodi, litapunguzamisamaha kwa asilimia 33 na hivyo kuweza kuchangia zaidiya asilimia sita kwenye Pato la Taifa. Aidha, Serikali iendeleena mazungumzo na Makampuni ya Madini ili kuweza kutozakodi za mafuta na ushuru wa forodha.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Serikali kwakuweza kusimamia vizuri utekelezaji wa Miradi inayofadhiliwana Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Millenium ChallengeCorporation (MCC). Pamoja na changamoto mbalimbalizilizojitokeza wakati wa utekelezaji, kukamilika kwa miradi hiikwa wakati kama vile Miradi ya barabara, Miradi ya Umemena Miradi ya Upanuzi wa Mtambo wa Maji Ruvu-Chini itasaidiakuleta maendeleo haraka kwenye maeneo husika na nchikwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, Kamati inatoa angalizokuwa, pamoja ya kwamba MCC iliamua kuikubalia Serikaliya Tanzania kuanza kuandaa Mpango wa Pili wa Miradi yaMCC, upo upungufu uliojitokeza katika utekelezaji wa awamuya kwanza ya Miradi ya MCC hasa ile ya upande wa Miradi

Page 80: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

80

ya ujenzi wa barabara. Serikali iyafanyie tathmini nakurekebisha upungufu huo ili awamu hii ya pili ikamilike kwawakati kama ilivyopangwa.

Mheshimiwa Spika, Kamati inapenda kuipongeza Bodiya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Board of Tanzania) kwakuweza kutekeleza majukumu na hivyo kuchangiamaendeleo ya nchi kiuchumi kupitia kodi inayokusanywakutokana na michezo ya kubahatisha nchini.

Mheshimiwa Spika, Bodi hii ilianza kuchangia mapatoSerikalini hata kabla ya kutungwa kwa Sheria ya Fedhainayohitaji Taasisi za Umma zichangie Serikalini asilimia 10 yamapato yake. Aidha, takwimu zinaonyesha kuwa kodiimekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, mathalani,mwaka 2006/2007 makusanyo yalikuwa shilingi bilioni 2.83,mwaka 2007/08 yalikuwa bilioni 3.9 na kwa kipindi cha kufikiaJuni 2012/2013 makusanyo yanatarajiwa kufikia shilingi bilioni11.24.

Mheshimiwa Spika, hii imetokana na utaratibu mzuriwa bodi iliyojiwekea katika ukusanyaji wa mapato pamojana kufunga mfumo wa mtandao wa kieletroniki katikamaeneo ya michezo ambao unaratibu mzunguko wa fedhana hivyo kupunguza tatizo la udanganyifu. Kamati inashaurikuwa fedha zinazopatikana kwenye michezo ya kubahatishazitengenezewe Mfuko maalum ambao utatumika kuhudumiajamaii katika sekta ya elimu au afya.

Mheshimiwa Spika, Kamati inatambua kuwa Serikaliinakopa ndani na nje ya nchi ili kugharamia miradi yamaendeleo ambayo ina mahitaji makubwa ya fedhaukilinganisha na mapato ya ndani. Malipo kwenye Deni laTaifa ambalo linahusisha mikopo ya nje na mikopo ya ndanikwa kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka yalifikia shilingibilioni 1146.41, hii ni sawa na ongezeko la asilimia 29.

Mheshimiwa Spika, angalizo la Kamati ni kwamba,ongezeko la Deni la Taifa haliendani na kasi ya ukuaji wauchumi wa nchi yetu pamoja na ukusanyaji wa mapato yetu.

Page 81: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

81

Uchumi wa nchi yetu (GDP growth rate) tangu 2008/2009 hadi2011/2012 umeongezeka kwa wastani wa asilimia 6.5 tu,wakati Deni la Taifa limeongezeka kwa asilimia 15.4.

Mheshimiwa Spika, hali hii isipodhibitiwa upouwezekano mkubwa wa Deni hilo kutokuwa himilivu kwa sikuza usoni. Ni muhimu Serikali ikachukua hatua ili kudhibiti kasikubwa ya madeni yanayotokana na dhamana za Serikali,kuwa na sera nzuri za kibajeti ikiwemo kupunguza mikopo yakibajeti, pamoja na kuendelea kupanua wigo wa makusanyokatika maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, bado kuna tatizo kubwa lamatumizi makubwa kwa upande wa Serikali pamoja namatumizi nje ya bajeti iliyopangwa na kuidhinishwa na Bungekwenye mafungu ya kila Wizara. Kamati inaendelea kuishauriSerikali juu ya umuhimu wa kudhibiti na kusimamia matumiziya Serikali pamoja na nidhamu ya matumizi kadriyalivyoidhinishwa kwenye vifungu husika.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kurekebisha haya,Serikali inahitajika kuendelea kuimarisha sera za mapato namatumizi na maboresho mbalimbali katika sekta ya Umma;kuendelea kuangalia eneo la sera na uendeshaji wa taratibuza kukusanya kodi pamoja na kupanua wigo wa ukusanyajiwa kodi; kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara;kuimarisha uzalishaji na ubora wa bidhaa za ndani na kuwezakuuza nje ya nchi ili kuongeza fedha za kigeni; pamoja nakupitia upya utaratibu wa kutoa misamaha ya kodi kwamadhumuni ya kushusha misamaha hiyo angalau iwe asilimiamoja ya Pato la Taifa kama Kamati ilivyopendekeza hukonyuma.

Mheshimiwa Spika, Sekta isiyo rasmi ni sekta ngumukutozwa kodi kwa kuwa haina mfumo rasmi wa ufanyaji wabiashara pamoja na kutunza kumbukumbu za biashara zake.Katika utafiti uliofanywa kwenye nchi 110 duniani, Tanzaniainakadiriwa kuwa na sekta isiyo rasmi kiasi cha asilimia 60.2ya Pato la Taifa, ikiwa ni kiwango kikubwa kuliko kwa nchi

Page 82: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

82

zote za Afrika isipokuwa Zimbabwe, kwa upande wa Kenyani asilimia 34.3, Malawi ni asilimia 40.3 na Zambia ni asilimia48.9.

Mheshimiwa Spika, hii ni changamoto kubwa kwaSerikali katika kuhakikisha inatafuta namna au mfumoutakaotumika kuwezesha sekta isiyo rasmi kulipa kodi na hivyokuongeza mapato makubwa kwa Serikali. Utoaji wavitambulisho vya Taifa utawezesha kudhibiti shughuli za kilamlipa kodi katika biashara zake na hivyo kuweza kupelekaTRA return ya kodi ya mapato kama ilivyo kwa nchi za Kenyana Afrika ya Kusini.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2011, Bunge lilipitishaAzimio la kuongeza muda wa uhai wa mpito wa Shirika Hodhila Mali za Mashirika ya Umma (CHC) kwa kipindi cha miakamitatu kuanzia tarehe 1 Julai, 2011 hadi 30 Juni, 2014.

Mheshimiwa Spika, lengo la Azimio hilo lilikuwa kutoafursa kwa CHC kukamilisha taratibu za kiutendaji na za kisheriapamoja na kuhamisha kazi zitazokuwa zimebaki kwenda Ofisiya Msajili wa Hazina pindi kipindi cha mpito kitakapofikiaukomo pamoja na kukamilisha marekebisho ya kimuundo nakisheria ya Ofisi ya Msajili wa Hazina ambayo itakabidhiwamajukumu ya CHC.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio iliyoyapataCHC katika utendaji wake bado inakabiliwa na changamotokubwa kuweza kukamilisha kazi zake kulingana na mudauliopo. Baadhi ya changamoto kubwa zinazoikabili CHC niuwepo wa mashauri 330 dhidi ya Shirika kwenye Mahakamambalimbali nchini; ukusanyaji sugu wa madeni ya wateja suguwa iliyokuwa NBC ambayo Shirika limerithi; uwezo wa Shirikakuwa mdogo kwa upande wa rasilimali watu, fedha namfumo wa utendaji ukilinganisha na majukumu waliyopewa.

Mheshimiwa Spika, Kamati inatoa angalizo kuwa,Serikali ihakikishe inaweka mipango na mikakati kuhakikishakuwa, shughuli zilizobaki za ubinafsishaji zinakamilika ifikapotarehe 30 Juni, 2014 kama ilivyotarajia. Pia, Serikali lazima

Page 83: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

83

iandae utaratibu wa utekelezaji wa shughuli zitakazobakibaada ya uhai wa CHC kufikia kikomo. Maamuzi ya sualahili yanahitaji umakini mkubwa ili kuhakikisha kuwa Serikalihaikosi mapato yake toka kwa makampuni yaliyobinafsishwa.

Mheshimiwa Spika, bado kuna tatizo kubwa laukwepaji kodi linalofanywa na wafanyabiashara wasiowaaminifu wanaoshirikiana na watendaji wa TRA pamoja nawatendaji wengine wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, udanganyifu huu unatumia mbinumbalimbali zisizo za halali ili kuhakikisha wanalipa kodipungufu kuliko wanavyostahili au kutolipa kabisa; mbinu hizizinahusisha kuficha mauzo halisi, kutotoa risiti kwa mauzo,kuwa na vitabu zaidi ya kimoja, kuwa na mihuri bandia,kudanganya aina ya bidhaa inayoingizwa nchini na kuingizasokoni bidhaa zilizokusudiwa kwenda nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, mfano mzuri ni hivi karibuni TRAilifanya ukaguzi wa dharura na kugundua zaidi ya makontenamengi yenye bidhaa mbalimbali ambayo yanasemekanahayajalipiwa ushuru halali kulingana na bidhaa iliyopo ndaniau yamedanganya aina ya bidhaa iliyomo ndani na hivyokulipa ushuru mdogo isivyo halali.

Mheshimiwa Spika, ukwepaji wa ulipaji wa Mapatoya Nchi ni Uhujumu Uchumi na unawanyonya na kutoa kerokubwa kwa wafanyabiashara waadilifu na pia wananchi.Bunge limekuwa likijadili kila siku na kuibana Serikali wapiitapata mapato yake ili iweze kusaidia kugharamikia kutoahuduma kwa wananchi wa Tanzania, kumbe kuna watuwachache (wafanyabiashara, mawakala wa mizigo nawatendaji) wasio na huruma na nchi hii, wanaendeleakuikosesha mapato Serikali bila woga na hivyo kuathiri uchumiwa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, vitendo kama hivi vya ukwepajiwa kulipa kodi ni dhahiri vinahusisha mtiririko mkubwa (chain)wa wafanyabiashara, Mawakala wa kutoa mizigo na

Page 84: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

84

watendaji wa Serikali wasio waaminifu. Hapa Kamati inaiulizaSerikali ipo wapi, ilikuwa wapi na inafanya nini mpaka sasa?

Mheshimiwa Spika, ni dhahiri suala kama hili likitokeakwa nchi kama ya China mnajua nini kitakachofuata kwawahusika na mali zao zitafanywa nini. Tumekuwa tukiimbawimbo bora kila siku wa uadilifu na utawala bora, haya leoyametokea ni vema Serikali ikatoa kauli juu ya suala hili nahatua stahili ilizozichukua. Kamati inaiagiza Serikali ifanyeuchunguzi wa kina juu ya suala hili na hatua za kisheriazichukuliwe dhidi ya watakaobainika na ukwepaji wa kodihizo.

Mheshimiwa Spika, Kamati inashauri kuwa, sasaimefikia wakati mashirika yaliyobinafsishwa yaorodheshwekwenye soko la mitaji ili kuongeza ufanisi wa kodi.

Mheshimiwa Spika, mwisho, Kamati inaendeleakuikumbusha Wizara ya Fedha kuwa yenyewe ndio kitovu chaWizara zote. Kushindwa kuwajibika vyema kwa Wizara hii,mwisho wa siku kutapelekea kushindwa kufikia malengo kwaWizara nyingine.

Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hiikumshukuru Mheshimiwa Dunstan Kitandula, MakamuMwenyekiti wa Kamati kwa kunisaidia kuiongoza Kamati;Mheshimiwa Dkt. William Mgimwa, Waziri wa Fedha naManaibu wake Mheshimiwa Janet Mbene na MheshimiwaSaada Mkuya Salum. Naomba niwashukuru WatendajiWakuu wa Wizara, Benki Kuu, Mashirika, Taasisi na Asasi zilizochini ya Wizara ya Fedha kwa kuandaa Taarifa ya Utekelezajiwa Majukumu ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha2012/2013 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwakawa Fedha 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisa,napenda kuwashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Bungeya Uchumi, Viwanda na Biashara ambao wameweza kutoamaoni na michango ya mawazo yao mbalimbali katikakuboresha makadirio haya ili hatimaye yaletwe mbele ya

Page 85: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

85

Bunge hili Tukufu. Naomba nitumie nafasi hii kuwatambuawajumbe wote kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mahmoud H. Mgimwa, Mwenyekiti;Mheshimiwa Dunstan L. Kitandula, Makamu Mwenyekiti;Mheshimiwa Margaret Agness Mkanga, Mjumbe;Mheshimiwa Haji Khatib Kai, Mjumbe; Mheshimiwa EsterLukago Minza Midimu, Mjumbe; Mheshimiwa Hussein NassorAmar, Mjumbe; Mheshimiwa Ahmed Juma Ngwali, Mjumbe;Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina, Mjumbe; MheshimiwaDkt. Titus Mlengeya Kamani, Mjumbe na Mheshimiwa JoyceJohn Mukya, Mjumbe.

Mheshimiwa Spika, wengine ni Mheshimiwa DavidZakaria Kafulila, Mjumbe; Mheshimiwa Shawana BukhetHassan, Mjumbe; Mheshimiwa Said Mussa Zubeir, Mjumbe;Mheshimiwa Vicky Pascal Kamata, Mjumbe; MheshimiwaNaomi Ami Mwakyoma Kaihula, Mjumbe; MheshimiwaKhatibu Said Haji, Mjumbe; Mheshimiwa Freeman AikaelMbowe, Mjumbe; Mheshimiwa Amina Mohamed Mwidau,Mjumbe; Mheshimiwa Josephine Jonson Genzabuke,Mjumbe; Mheshimiwa Engineer Habib Juma Mnyaa, Mjumbe;Mheshimiwa Mohamed Hamis Misanga, Mjumbe;

Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru sana wewemwenyewe binafsi na Mheshimiwa Naibu Spika kwakutupatia maelekezo mbalimbali kwa Kamati yetu ambayowakati wote yamefanikisha kazi za Kamati. Aidha, napendapia kumshukuru na kumpongeza Katibu wa Bunge Dkt.Thomas D. Kashililah; Katibu wa Kamati ya Uchumi, Viwandana Biashara, Ndugu Michael Kadebe kwa kuratibu shughuliza Kamati hadi taarifa hii kukamilika.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, sasanaliomba Bunge lako Tukufu likubali kuidhinisha Makadirio yaMapato na Matumizi ya Wizara Fedha, kama alivyowasilishamtoa hoja muda mfupi uliopita.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naungamkono hoja. (Makofi)

Page 86: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

86

MHE. DAVID E. SILINDE (K.n.y. MHE. KABWE Z. ZITTO -MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KWA WIZARAYA FEDHA): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Msemaji Mkuuwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuhusiana na Wizaraya Fedha, naomba kuwasilisha hotuba ya makadirio yamapato na matumizi ya Wizara husika kwa mwaka wa fedha2013/2014.

Mheshimiwa Spika, Dira kuu ya Wizara ya fedha nikuhakikisha kuwa uchumi unakua kwa kiwango cha juu namatokeo yake kuwanufaisha wananchi wote na kuhakikishausimamizi thabiti na uwajibikaji wa fedha za umma. KambiRasmi ya Upinzani inaikumbusha tena Wizara ya Fedha katikakutimiza wajibu wake ikumbuke kwamba “Maslahi ya Taifani zaidi ya Vyama vya Siasa, mahali tunapotoka au dinitunazoziamini. Maslahi ya Taifa ni kwa ajili ya Watazania nahasa Watanzania milioni 30 (The Bottom 30M) ambao badowanaishi katika ufukara mkubwa sana wakikosa hudumamuhimu za jamii na wanaoishi vijijini ambapo hakuna umeme,barabara hazipitiki na wanahangaika kutwa kutafuta majisafi na salama.

Mheshimiwa Spika, maslahi ya Taifa sio faida yawachache wenye kuishi mijini au wanasiasa wanaotafutaushawishi kwa umma bila kujali matakwa ya umma.Watanzania wanyonge wa vijijini wanajua maslahi yao ninini”. Hivyo, ni vema Wizara ya Fedha itimize majukumu yakekwa kuzingatia maslahi ya wananchi walio wengi.

Mheshimiwa Spika, katika kutimiza majukumu hayoWizara imegawanyika katika idara mbalimbali zenyemafungu yafuatayo: –

- Fungu 50 - Wizara ya Fedha.

- Fungu 21 - Hazina.

- Fungu 22 - Deni la Taifa.

- Fungu 23 - Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali.

Page 87: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

87

- Fungu 10 - Tume ya Pamoja ya Fedha.

- Fungu 13 - Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi.

- Fungu jipya ni 7 - Msajili wa Hazina.

Mheshimiwa Spika, tija katika ukuaji wa uchumi ndichokipimajoto cha afya ya uchumi wa nchi, hivyo uelewa borawa hali ya uchumi wa Tanzania utaonekana ni kwa vipiuchumi au rasil imali za nchi zinavyotumika katikakuwanufaisha Watanzania na uzalishaji wa ajira mpya katikasekta mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaWizara ya Fedha kutafakari kwa kina ni kwa nini ukuaji wauchumi wa Tanzania haupunguzi umaskini. Nchi nyinginekatika bara la Afrika zenye kasi ya ukuaji wa uchumi kamanchi yetu, Ethiopia na Uganda, wameweza kuwaondoa zaidiya asilimia 30 ya wananchi wao katika dimbwi la umaskinikatika kipindi cha muongo mmoja (2000 – 2010). Wizara yaFedha kama msimamizi mkuu wa sera za uchumi imeshindwakabisa kutafsiri ukuaji wa uchumi wa Tanzania kutoka takwimukwenda kwenye maisha ya watu wa chini.

Mheshimiwa Spika, hoja za Kambi ya Rasmi yaUpinzani ambao hazijatekelezwa; kwa mwaka wa fedha2012/2013 tuliitaka Serikali kufanya yafuatayo ili kuongezawigo wa utendaji na udhibiti wa mianya ya upotevu wamapato ya Taifa na pia kutoa mwelekeo mpya wa kuongezaajira:-

(i) Tulisema kwamba TRA wanao uwezo wakukusanya mpaka shilingi trilioni moja kwa Mwezi iwapotutadhibiti misamaha ya kodi, tutakusanya kodi stahili katikaSekta ya Madini na tutasimama kidete kuzuia ukwepaji kodiwa Makampuni ya Kimataifa. Wizara haijatoa maelezokuhusu utekelezaji wa ushauri huu.

(ii) Kambi Rasmi ya Upinzani iliitaka Mamlaka ya

Page 88: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

88

Manunuzi ya Umma (PPRA) kufanya uchunguzi wa kina kuhusumanunuzi ya mafuta ya kuzalisha Umeme, Wizara ndio yenyekusimamia uchumi wa nchi kwa ujumla ituletee BungeniTaarifa ya Uchunguzi utakaofanywa na PPRA kuhusumanunuzi shilingi 1.4 bilioni kila siku ya mafuta kuendeshamitambo ya kuzalisha Umeme. Kwa masikitiko makubwaukaguzi maalum bado haujafanyika.

(iii) Wizi kwenye mabenki ni moja ya sifa mbayasana ya mfumo wetu wa fedha na hivyo kusababisha Benkikuweka riba kubwa sana ili kufidia risk kama hizi za watu‘kupiga’ amana za wateja kwenye mabenki. Kambi Rasmiya upinzani iliitaka Wizara ya Fedha kupitia Kitengo chaUdhibiti wa Fedha haramu kudhibiti wizi kwenye Benki za hapanchini.

Fedha bado zinaibiwa na hivyo kufanya ribakuendelea kupanda na wananchi kushindwa kufanyabiashara yenye tija kwa maendeleo yao. Tunataka majibukuhusu suala hili ambalo linaharibu sifa ya sekta yetu ya Benki.

(iv) Taifa linavyoibiwa kupitia kesi mbalimbaliambazo Serikali imeshtaki au kushtakiwa kwenye Mahakamaza Kimataifa. Tulipenda kufahamu ni kwa nini mpango wakumaliza kesi hii nje ya Mahakama hautekelezwi na vile vilempango wa kugeuza Mtambo wa kufua umeme wa IPTLkuwa wa gesi kwa nini hautekelezwi?

(v) Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kupatamajibu kuhusu fedha zilizoko kwenye Escrow Akaunti, BenkiKuu za IPTL (Tegeta escrow) zimefikia kiasi gani mpaka sasana usalama wa fedha hizo ukoje?

(vi) Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniiliitaka Serikali kuunda Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta Ndogoya Fedha (Tanzania Microfinance Regulatory Authority).Kwani mamlaka italinda Haki za wanyonge dhidi ya loansharks na wajibu wa wanyonge wenye kuchukua mikopo.

(vii) Katika kuleta uwazi na uwajibikaji wa Mifuko

Page 89: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

89

ya Hifadhi za Jamii, Kambi Rasmi ya Upinzani, ilitaka kamailivyo kwa Mabenki, taarifa za mahesabu za robo mwaka zaMifuko ya Hifadhi ya Jamii ziwe zinatangazwa kwenyemagazeti yanayosomwa zaidi nchini ili wananchi na hasawanachama wa Mifuko waone namna Mifuko yaoinavyofanya kazi. Hili nalo bado halijafanyika.

(viii) “Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzaniilipendekeza kwa Mifuko ya PSPF na PPF kuangalia namnaya kuwekeza katika maeneo yanayochochea ukuaji wauchumi na hivyo kuzalisha ajira na kupata wanachama zaidi.Maeneo kama uwekezaji kwenye Bandari na Reli yanapaswakuangaliwa.

(ix) Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani piailipendekeza kwamba fao la Elimu ambalo Mfuko wa PPFunatoa kwanza Fao hili liwe fao la lazima kwa Mifuko yotenchini, lakini pia lipanuliwe hadi kufikia elimu ya Chuo Kikuu.

(x) Mheshimiwa Spika, Kambi ya UpinzaniBungeni bado ilisisitiza kwamba Mifuko yote ya Hifadhi yaJamii ihamishiwe Wizara ya Kazi na Ajira kama Wizarainayohusika na social security.

(xi) Aidha, Mifuko ipunguzwe na kubakia naMifuko miwili tu, mmoja wa wafanyakazi walio katika sektabinafsi na sekta isiyo rasmi na mwingine kwa wafanyakaziwa sekta ya umma. Kwamba Mifuko ya NSSF na PPFiunganishwe kuwa Mfuko mmoja kwa ajili ya sekta binafsi nasekta isiyo rasmi na Mifuko ya PSPF, LAPF na GEPF iunganishwekuwa Mfuko mmoja kwa ajili ya kushughulika na wafanyakaziwa Sekta ya Umma”.

(xii) Kambi ya Upinzani ilitaka kupata maelezo yakina ni kwa nini Msajili wa Hazina anaendelea kuwa mjumbewa vikao vya Bodi za Mashirika ya Umma kinyume na sheria?

(xiii) Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani ilitakakupata maelezo ya Serikali kuhusu uuzwaji wa hisa za Shirikala UDA umefikia wapi?

Page 90: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

90

Mheshimiwa Spika, Fungu 50 - Wizara ya Fedha nataasisi zake; Benki Kuu ya Tanzania na udhibiti wa fedha nasera ya fedha. Benki Kuu ya Tanzania ni chombo cha Kitaifakinachosimamia masuala ya kibenki na kifedha. Sheria yaBenki ya Tanzania ilifanyiwa marejeo mwaka 2006 na kuipabenki hii jukumu la kusimamia Sera ya Fedha nchini (monetarypolicy).

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Benki Kuu imeipa uhuruBenki kuendesha shughuli zake bila kuingiliwa na Serikali.Lengo la msingi la Benki Kuu ya Tanzania ni kudhibiti mfumukowa bei, kwa sababu lengo hili ndilo litakalohakikisha kuwepokwa utengamavu wa uchumi mpana utakaosaidia ukuajiendelevu wa uchumi. Aidha, Benki Kuu ya Taifa lolote ndiotaasisi pekee yenye takwimu zote nyeti na za uhakikazinazohusu uchumi wa Taifa hilo.

Mheshimiwa Spika, Taarifa ya ukaguzi wa hesabu zaBOT ya mwaka 2011/2012; Mnamo mwezi April 2013 Benki Kuuya Tanzania (BOT) ilitoa taarifa yake ya ukaguzi wa hesabuza mwaka wa fedha 2011/2012, miongoni mwa mamboambayo yaliweza kuainishwa katika ripoti hiyo ni pamoja nataarifa ambayo ni ya kustua kwani Benki Kuu imepata hasarakubwa katika mwaka huo wa fedha ya kiasi cha shilingi bilioni52.431 ikilinganisha na mwaka uliotangulia 2010/2011 ambaoBOT walipata faida kubwa ya kiasi cha shilingi bilioni 727.793.

Mheshimiwa Spika, aidha, katika taarifa hiyo yaukaguzi ya BOT yapo mambo mbalimbali ambayoyaliainishwa kama vile uwepo wa fedha za EPA, Mikopomikubwa ya wakurugenzi na wafanyakazi wa Benki Kuu,fedha za IPTL katika Tegeta Escrow account ya BOT,kufungwa/kufilisiwa kwa kampuni ya ubia ya MwananchiCompany Limited na mengineyo mengi.

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni,inataka kupata majibu ya kina kuhusiana na masualayafuatayo yaliyoibuliwa na ripoti hiyo ya ukaguzi:-

(i) Ni utaratibu gani unatumika katika

Page 91: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

91

kuwakopesha wafanyakazi fedha kwa ajili ya nyumba nakununulia magari binafsi na kukokotoa riba ya mikopo kwawafanyakazi na viongozi wakuu wa BOT kwani mpaka tarehe30 Juni, 2012 walikuwa tayari wamejikopesha shilingi bilioni55.668, ikilinganishwa na shilingi bilioni 38.965 mwaka 2011.

Mheshimiwa Spika, aidha, tunataka kujua kamafedha hizi ni tofauti na kile kinachoitwa staff Housing Fundambao ni mkopo kwa wafanyakazi unaotokana na faida yakila mwaka inayopatikana kutokana na shughuli mbalimbaliza BOT, 2012 Mfuko ulikuwa na kiasi cha shilingi bilioni 34.170kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa BOT kwa ajiliya nyumba.

(ii) Mfuko wa Elimu wa Mwalimu Nyerere(Mwalimu Nyerere Scholarship Fund), mnamo mwaka 2009,BOT ilianzisha Mfuko huo kwa ajili ya kuwapa udhaminiwasichana kusoma shahada ya kwanza kwa wale ambaowatafaulu vizuri masomo ya Sayansi na Hisabati na hadimwezi Juni 2011 Mfuko ulikuwa na kiasi cha shilingi bilioni 1.715.Aidha, katika mwaka wa fedha 2012, mpaka tarehe 30 Juni,Mfuko ulikuwa na shilingi sifuri. Je, ni utaratibu gani huwaunatumika katika kupata fedha hizi na ni wanafunzi wangapimpaka mwaka huu wa fedha wamesomeshwa na Mfuko huuna wanasoma vyuo gani?

(iii) Akaunti ya malipo ya nje (EPA), Mpaka tarehe30.06. 2012 kwa mujibu wa ripoti hiyo akaunti hii ilikuwa nakiasi cha shilingi bilioni 205.743, jeb fedha hizi zina usalamagani mpaka sasa na je, hazitachotwa kama ilivyofanyikamwaka 2005?

Mheshimiwa Spika, aidha, mpaka sasa ni akina nani(orodha ya majina ya watu waliorejesha fedha) na ni kiasigani cha fedha kimerejeshwa kutokana na ufisadi wa shilingibilioni 133 uliofanyika katika kipindi cha mwaka 2005?Maamuzi ya Serikali ilikuwa ni kuondoa kabisa akaunti hii yaEPA kutoka Benki Kuu. Kwa nini bado akaunti hii ipo BenkiKuu?

Page 92: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

92

(iv) Kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi wa hesabuza BOT, katika mwaka wa fedha 2011/2012, ni kuwa BOTilipata hasara ya shilingi bilioni 52.431 ikilinganishwa na faidaya shilingi bilioni 727.793 iliyopatikana mwaka 2011. Tunatakamajibu ya kina kuhusiana na hasara hii kwani haiwezekanitaasisi nyeti kama hii ipate hasara na Taifa lisiweze kupewataarifa za kina kuhusiana na chanzo cha hasara hii na nihatua gani zimechukuliwa mpaka sasa katika kukabiliana nahasara hii.

Mheshimiwa Spika, dhamana za Serikali kwa Mashirikana Taasisi; katika taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali ya mwaka 2012, Serikali inakiri na kuafiki mapendekezoya ukaguzi juu ya kutokuwa na viwango vya dhamanakinyume na Sheria ya Mikopo ya Dhamana na Ruzuku, sheriaya mwaka 1974 kama ilivyorekebishwa mwaka 2004.

Mheshimiwa Spika, kutokana na upungufu huo wausimamizi wa dhamana za Serikali uamuzi wa kusimamishautoaji wa dhamana kwa Wizara ambayo imepelekeakuwepo kwa athari katika uendelevu wa madeni, pia ni vipiSerikali inatoa uhakiki wa utendaji kwa Mifuko ya Hifadhi zaJamii ambayo ndio itakuwa imeaathirika na usimamizi huumbovu wa dhamana za Serikali?

Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishiwa Umma (PSPF); taarifa ya POAC ya Aprili, 2011 ilioneshaPSPF ilikuwa ikilipa mafao ya pensheni kwa watumishiwaliostaafu kabla ya mwaka 1999 kwa maelewano na Serikalikuwa Serikali itarejesha kiasi kilichotumiwa na PSPF. Lakini hadikufikia tarehe 30/06/2010, jumla ya Sh. 716.6 bilioni zilikwishakutumiwa na PSPF kulipa wastaafu na kiasi hicho kilipaswakurejeshwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, katika taarifa ya Kamati ilioneshakuwa, Serikali ilikiri kudaiwa na kuahidi kuanza kulipa. Kishawakalipa shilingi bilioni 30, kumbe baadaye hawakulipa tenana uchambuzi wa acturials umeonesha ukubwa wa denikaribu mara mbili ya ilivyokuwa mwaka 2010. Kutokana nabarua ya Wizara kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF ya

Page 93: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

93

tarehe 25 Machi, 2011, Wizara ilisema itairejeshea fedha PSPFndani ya miaka 10 kwa kutenga kwenye bajeti kiasi cha Sh.71 bilioni kila mwaka kuanzia mwaka wa fedha wa 2011/2012.

Mheshimiwa Spika, kutokana na taarifa ya Mkaguzina Mdhibiti Mkuu wa Serikali iligundua kuwa: Kwanza, Wizaraya fedha haikutenga kiasi cha Sh. 71 bilioni katika bajeti yamwaka 2011/2012. Kiasi kilichorejeshwa PSPF cha Sh. 20 bilionindani ya mwaka unaokaguliwa sasa kimelipwa kutoka Mfukowa Tahadhari (Contingency Fund) badala ya kutoka kwenyemafungu yaliyotengwa kila mwaka kama ilivyokusudiwahapo mwanzo.

Mheshimiwa Spika, pili, kiasi kilichorejeshwa PSPFmwaka 2011/2012 cha Sh. 20 bilioni kilikuwa kidogo kuliko kiasikilichokusudiwa cha Sh. 71 bilioni (asilimia 28 tu ya kiasikilichokubaliwa kwa mwaka cha Sh. 71 bilioni) hali ambayoitaathiri uwezo wa kifedha wa PSPF.

Mheshimiwa Spika, kama tulivyosema katika hotubayetu ya Ujenzi kwamba, Serikali ya CCM hawatembei kwenyemaneno yao, kwani wanatoa ahadi lakini wanashindwakutimiza. Hivyo basi, Kambi Rasmi yya Upinzani inasema sasani muda muafaka wa CHADEMA kupata ridhaa za wananchikuongoza nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati akifunga Wiki ya HifadhiMei 17, 2013 kwenye Uwanja wa Nyerere Square MjiniDodoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Jakaya Kikwete alisema: “Rasilimali ya Mifukoya Hifadhi ya Jamii imeongezeka kutoka Sh. trilioni 3.7 mwaka2010 na kufikia trilioni 5.3 mwezi Desemba, 2012. tathmini hiiimefuta dhana ya watu wachache waliokuwa wanaenezauvumi kuwa baadhi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ipo katikahali mbaya kifedha.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Mfuko wa Pensheni yaWatumishi wa Umma (PSPF) unaidai Serikali mabilioni yafedha, jambo ambalo Rais Kikwete amesema ni kweli nakufafanua historia ya deni hilo akisema kuwa lilizaliwa Julai,

Page 94: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

94

mwaka 1999 wakati watumishi wote wa Serikali walipoingizwakatika Mfuko wa Hifadhi ambako watumishi hao walitakiwakulipiwa mchango kiasi fulani na Serikali.

Mheshimiwa Spika, aliendelea kusema, awali deni hilihalikujulikana. Lakini maadamu limejulikana litalipwa na kwakuanzia mwakani Serikali italipa kiasi cha sh. bilioni 50 ikiwa nisehemu ya kulipa deni hilo. Lengo letu ni kuona kuwa hakunamfanyakazi atakayekosa mafao yake kwa sababu ya Serikali,yaani mwajiri wake. Hatuwezi kufanya kamari na mafao yawafanyakazi.”

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni,inapenda kulijulisha Bunge kuwa Wizara ya Fedha haikumpataarifa za kweli Mheshimiwa Rais. Kwanza ahadi ya kisheriani kulipa shilingi 71 bilioni kila mwaka kutoka kwenye Bajetikuanzia mwaka 2011/2012 ambapo toka wakati huozimelipwa shilingi bilioni 30 tu. Hivyo kumpa Rais taarifa zakwamba zimetengwa shilingi bilioni 50 katika bajeti ya mwakahuu bila kuzingatia miadi ya kisheria ya miaka ya nyuma yashilingi 110 bilioni ni kumchonganisha Rais na wanachamazaidi ya 300,000 wa PSPF waliozagaa nchi nzima.

Mheshimiwa Spika, Serikali ieleze shilingi bilioni 110ambazo hazikulipwa miaka miwili iliyopita na shilingi bilioni70 za mwaka wa fedha 2013/2014 zitalipwa lini? Serikaliikumbuke kuwa fedha hizi sio hisani bali ni malipo halali yawastaafu ambao wameitumikia nchi yetu kwa uwezo waowote.

Mheshimiwa Spika, mbali na tatizo hilo la Serikalikukataa kulipa deni inalodaiwa na PSPF bado kuna tatizo lamsingi la kutokuwepo kwa mtendaji mkuu, kwani aliyepoanakaimu kwa takribani miaka mitatu sasa. Huu ni uzembeambao unasababisha maamuzi makubwa ya kiutendajiyanashindwa kufanyika. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kumthibitisha au kuendesha mchakato wa kumpataMkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo haraka iwezekanavyo.

Mheshimiwa Spika, mafao, pensheni, mirathi na

Page 95: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

95

mapunjo; kumekuwepo na malalamiko mengi sanakuhusiana na pensheni kwa wastaafu waliokuwa ni watumishiwa Serikali katika taasisi mbalimbali, pia kucheleweshwakutolewa kwa fedha za mirathi kwa familia za marehemuambao walikuwa ni watumishi wa Serikali. Aidha, malalamikoya mapunjo kwa watumishi wa taasisi mbalimbali kwa hiariyao waliamua kustaafu kutokana na ahadi walizopewa nataasisi husika.

Mheshimiwa Spika, ubaguzi wa malipo ya penshenikwa wastaafu katika jeshi la ulinzi, kati ya wale waliostaafuchini ya mwaka 2006 na wale waliostaafu juu ya mwaka 2006.Mfano mzuri ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu, JeneraliMirisho Sarakikya kwa mujibu wa gazeti la Mwananchianalipwa shilingi 50,000 kama pensheni kwa mwezi, hii ni aibukwa nchi na udhalilishaji kwa makanda wastaafu. Wakatiwenye cheo kama chake waliostaafu kuanzia mwaka 2006kuja juu wanalipwa pensheni ya 80% ya mshahara waliokuwawanapokea wakiwa kazini.

Mheshimiwa Spika, vivyo hivyo, ni kuwa hata wastaafuwa vyeo vya Brigedia na Makanali chini ya mwaka 2006,pensheni yao kwa mwezi umezidiwa na wastaafu wa vyeovya chini wa kuanzia mwaka 2006 kupanda juu.

Mheshimiwa Spika, suala hili la pensheni hasa kwawanajeshi linaleta sononeko kubwa kwa wazee wetu ambaowalijitolea maisha yao katika kuhakikisha Tanzania inakuwasalama. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kurekebishaharaka iwezekanavyo viwango vya ulipwaji wa pensheni kwawanajeshi waliostaafu miaka ya 2006 kushuka chini.

Mheshimiwa Spika, kuhusu madai ya mapunjo kwawatumishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliostaafishwamwaka 2006, waliamua kuunda Kamati ya Kufuatilia Mapunjoyao, Kamati ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wao NduguRashid H. Mohamed, Makamu Mwenyekiti wao NduguBathromeo S. Milanzi na Katibu wao Ndugu Hassan A. Hassanni kwamba hazina imekuwa ikiwapiga chenga wakati madaiyao kwa mujibu wa barua ya tarehe 1 Agosti, 2011 yenye

Page 96: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

96

kumb. Na. J/C.60/4/32/74/19, toka Ofisi ya Mwanasheria Mkuuwa Serikali kwenda kwa Katibu Mkuu wa Hazina iko wazi, ninihasa wanadai wastaafishwa hao wapatao 638 waliokuwawafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, kwa ushauri wa Ofisi ya AGkwamba, hakuna haja ya kuunda Kamati ndogo ya kuhakikimadai hayo kama ilvyopendekezwa na kikao cha tarehe 28Desemba, basi wastaafu hao walipwe madai yao kamawalivyoomba na mgogoro huu ufungwe.”

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali izingatie ushauri uliotolewa na Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali wa kuwalipa wazee hawa ambao walifanyakazi kubwa na kwa uadilifu mkubwa katika kulitumikia Taifalao ila leo wanaendelea kulia kutokana na Serikali kutokulipamafao yao.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani(Internal Auditor General); Bunge lilipitisha sheria inayoitwaThe Local Government Service ACT, 1982 na sheria hii iliunda“Tume ya Usajili katika Serikali za Mitaa” kwa lengo kuu lakuwa ndicho kingekuwa chombo kikuu chenye mamlaka yakutoa ajira katika ngazi hiyo ya Serikali. Aidha, kwa sasa kunachombo kingine kinaitwa “Sekretarieti ya Ajira katika Utumishiwa Umma” ambacho kinatoa ajira hadi za watendaji katikangazi za vijiji.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali iwaeleze Watanzania, hii sheria iliyotungwa na Bungeya The Local Government Service Act, 1982 imefutwa aumajukumu yake yameingizwa kwenye Sheria ya Civil ServiceAct, 1989? Kama bado ipo utendaji kazi wa sheria hiyo ukoje?

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inatakamaelezo hayo, kutokana na ukweli kwamba katika kufanyausimamizi wa fedha za walipa kodi, vyombo vya Serikalivinavyotakiwa kufanya kazi hiyo ni Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa

Page 97: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

97

Ndani (Internal Auditor General) na Ofisi ya Mkaguzi naMdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and AuditorGeneral).

Mheshimiwa Spika, hawa wote mmoja hana nguvukisheria ya kuhamisha watendaji wanaofanya kazi kwa niabayake, naye ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani kwani katikaHalmashauri mamlaka ya ajira kwa Wakaguzi wa Ndani sioofisi yake bali wako Ofisi ya TAMISEMI chini ya Mkurugenzi waHalmashauri.

Mheshimiwa Spika, kwa hoja hiyo ni kwamba, hatahao Wakaguzi wa Ndani wa Halmashauri wanakuwa nisehemu ya utawala badala ya kuwa washauri, jambo hililinatengeneza mazingira ya kifisadi yanayofanywa katikakatika ngazi hiyo kutokana na mahusiano yanayojengwa naMkaguzi Mkuu wa Ndani anakosa mamlaka ya kufanyauamisho ila kwa ridhaa ya Waziri mwenye dhamana naTAMISEMI.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kuzifanyia marekebisho sheria husika ili Mkaguzi Mkuuwa Ndani awe na mamlaka ya kuwahamisha Wakaguzi waNdani kwa kadri atakavyoona inafaa kama ilivyo kwaMkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mheshimiwa Spika, Fungu 22 - Deni la Taifa; KambiRasmi ya Upinzani Bungeni tunatambua kuwa nchi nyingiduniani kama sio zote zinakopa ili kuboresha huduma na kwaajili ya miradi mbalimbali ya kimaendeleo na hutumia fedhaza walipa kodi katika kuendesha shughuli za Serikali.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Deni la Taifa liliongezekakwa asilimia 38 kutoka Shilingi trilioni 7.6 mwaka 2008 mpakashilingi trilioni 10.5 mwaka 2009/2010.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2010/2011, deni hiloliliendelea kuongezeka kutoka shilingi trilioni 10.5 na kufikiakiasi cha shilingi trilioni 14.441. Katika mwaka wa fedha 2011/

Page 98: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

98

2012, Deni la Taifa liliendelea kuongezeka kutoka shilingi trilioni14.441 na kufikia kiasi cha shilingi trilioni 16.975 mwakauliofuatia.

Mheshimiwa Spika, katika hali isiyokuwa ya kawaida,Deni la Taifa limeongezeka kwa kasi sana na hadi Disemba,2012 lilikuwa limefikia kiasi cha shilingi trilioni 21.028 kutokakiasi cha shilingi trilioni 18.258 Disemba, mwaka 2011 na katiya hizo asilimia 75.97 zilikuwa ni deni la nje.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,ina taarifa kwamba takwimu hizi za Deni la Taifa hazihusishidhamana ambazo Serikali imezitoa kwa Mashirika ya Ummana Kampuni binafsi. Aidha, ni lazima dhamana katika siku zausoni ziwe ni sehemu ya Deni la Taifa maana tumeshuhudiasasa ambapo Kampuni nyingi binafsi zimeshindwa kulipamikopo iliyodhaminiwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, mfano ni malipo ya deni lenyethamani ya shilingi bilioni 60 la kukodisha ndege ya Airbuskwa Shirika la ATCL kutoka kampuni ya Wallis Traders yaLebanon na Deni lililochukuliwa na Kampuni ya Kiwira Coaland Power limited ambayo Mbia wake alishindwa kuendeshamradi wa Makaa ya Mawe Kiwira licha ya kudhaminiwa naSerikali Mkopo kutoka kwenye taasisi za Fedha hapa nchiniambapo sasa Serikali imelipa shilingi bilioni 40 katika Bajetiya mwaka 2012/2013.

Mheshimiwa Spika, aidha, tunatambua kuwa Serikaliina madeni ambayo hayajajumuishwa kwenye deni la Taifana hiyo inalipelekea Deni la Taifa kuwa kubwa kulikolinalooneshwa kwenye taarifa mbalimbali za Serikali na ileya CAG , kwa mfano kuna madai ya PSPF ya sh.716,600,000,000 kati ya madai ya shilingi trilioni 6.5 ambayoSerikali inadaiwa na imekubali kuyalipa madeni hayo.

Mheshimiwa Spika, vile vile kuna madeni ya Shirika laNdege la Afrika ya Kusini na Citi Bank kiasi cha dola4,129,298.38 na dola 1,460,000 sawa na shilingi bilioni 8.8 kwaujumla wake ambazo hazijajumlishwa kwenye Deni la Taifa

Page 99: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

99

wakati zitalipwa na Serikali. Aidha, kuna dhamanambalimbali zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Idara, Wizarana Mashirika ya Umma zinazofikia shilingi trilioni 1.250. Chanzoni ripoti ya CAG.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani hainatatizo na uhimilivu wa Deni la Taifa (Debt sustainability) kwanitunajua kuwa Mataifa makubwa yanakopa sana na yanauwiano mkubwa wa Deni kwa GDP kuliko sisi. Tatizo letu ninamna ambavyo fedha za mikopo zinatumika. Matumizi yamikopo tunayochukua sio endelevu maana sehemu yamikopo hiyo hutumika kwa matumizi ya kawaida badala yamatumizi ya uzalishaji au kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha.

Mheshimiwa Spika, pamoja na umuhimu wa kukopakama ambavyo Mataifa mengine hufanya hivyo, kwetu sisihii ni kasi kubwa mno ukilinganisha na ukuaji wa uchumi wanchi yetu kwa sababu ukopaji unategemea uwezo wa kulipapia.

Mheshimiwa Spika, hii itasababisha mzigo huu wamadeni kubebwa na kizazi cha sasa na kijacho. Ukilinganishana nchi nyingine za Afrika Mashariki, Tanzania bado inaviwango vidogo vya mikopo kama sehemu ya Pato la Taifa(debt/GDP ratio).

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, wakati wenzetuwanakopa ili kuongeza uzalishaji (capital investments), sisitunakopa kwa matumizi ya kawaida. Kambi ya Upinzaniinapendekeza kuwepo kwa namna bora zaidi ya kuamuakuhusu mikopo ambayo Taifa linaingia ili kuhakikishainaelekezwa katika uzalishaji mali.

Mheshimiwa Spika, katika taarifa ya CAG ya mwaka2012, kuna jumla ya shilingi bilioni 619 ambazo zipo kwenyeDeni la Taifa, lakini hazina vithibitisho. Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali ameandika “Uhakiki wamchanganuo wa madeni ya Taifa kama ulivyokuwa tarehe

Page 100: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

100

30 Juni, 2012 ulibaini kuwepo kwa marekebisho ya Deni yashilingi 619.8 bilioni ambao uongozi haukuweza kutoamaelezo ya kuridhisha” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeniimeshtushwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha deniambalo halina vielelezo. Tunataka maelezo ya kina sana nasahihi kuhusu taarifa hii kwa haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Dhamana za Serikali kwa ajili yamakampuni yanayouza bidhaa nje (Export GuaranteeSchemes) zilianzishwa ili kuwezesha makampuni yetu kumudukuuza bidhaa nje na kuingizia Taifa mapato ya Fedha zaKigeni.

Mheshimiwa Spika hata hivyo katika mpango huu,Serikali inaelekea kupoteza jumla ya shilingi bilioni 300kutokana na makampuni yaliyopewa dhamana kutolipamikopo yao kwenye mabenki. Hii inaongeza deni la Taifa kwakiwango hicho cha fedha.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzaniinaendeleza wito wake wa kutaka Fungu 22 la Deni la Taifalifanyiwe Ukaguzi Maalum (Special Audit) na Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili tuweze kujua mikopohii tunayochukua kila wakati inatumika kufanyia nini na miradiiliyotekelezwa kama ni miradi ya kipaumbele kwa mujibu waMpango wa Taifa wa Maendeleo. Aidha, ukaguzi huumaalum utatuwezesha kama Taifa kujua kiwango halisi chaDeni la Taifa ambalo tunadaiwa.

Mheshimiwa Spika, malipo ya riba na Deni la Taifa;kwa miaka mingi mfululizo tumekuwa tukitenga fedha kwaajili ya kulipia deni la Taifa pamoja na riba mbalimbalizitokanazo na deni hilo la Taifa .Kwa mujibu wa ripoti yaukaguzi ya CAG iliyoishia Juni, 2012 ni kuwa, tumekuwa tukilipariba ya deni la Taifa kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2007hadi 2012 jumla ya kiasi cha shilingi trilioni 1.523, (tazamajedwali namba moja)

Page 101: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

101

Jedwali 1: Malipo ya riba kwa miaka mitano iliyopita (tarakimukatika bilioni):

Wadeni 2007/08 2008/09 2009/10 2010/11 2011/12

Multilateral 20.29 26.75 26.32 51.41 2.58Bilateral 8.07 4.06 1.47 11.07 2.61Commercial/Exp - 5.09 0.81 2.58 20.42Jumla ndogo 28.36 35.90 28.60 65.06 85.61Domestic 241.64 208.35 229.39 271.64 328.75Jumla kuu 270.00 244.25 257.99 336.70 414.36

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014, Fungu 22 programme 10 utawala, kasma 100,1 kifungukidogo 820300, inaonesha kuwa jumla ya sh. 357,304,000,000zimetengwa kwa ajili ya kulipia deni halisi la Taifa (Principal).

Mheshimiwa Spika, vilevile katika kifungu 250500 kwamwaka huu wa fedha zimetengwa jumla ya sh.425,700,000,000 kwa ajili ya kulipia riba ya madeni ya mudamrefu (Interest payments on long-term debt to other GeneralGovernment).

Mheshimiwa Spika, aidha, katika kifungu 250100,fedha zilizotengwa kwa ajili ya kulipia riba itokanayo na Denila Taifa ni kiasi cha sh. 323,154,880,000 na katika kifungu250600, fedha zilizotengwa kwa ajili ya kulipia riba ya Deni laTaifa la ndani other domestic interest payments not elsewhereclassified kiasi cha sh. 3,087,837,000.

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla ni kuwa, fedhailiyotengwa kwa ajili ya kulipia deni halisi la Taifa (loanspayment principal, Kifungu 820300) kwa mwaka huu wafedha ni sh. 357,304,000,000 wakati fedha iliyotengwa kwaajili ya kulipia riba itokanayo na Deni la Taifa la nje na ndanikasma 22, (Fungu 250100, 250300, 250400, 250500 na 250600)kwa mwaka huu wa fedha ni sh. 1,021,942,717,000.00.

Mheshimiwa Spika, kutokana na hali hii ya kutenga

Page 102: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

102

trilioni za fedha kwa ajili ya kulipia riba za Deni la Taifa, KambiRasmi ya Upinzani inasisitiza kuwa kuna haja ya kufanyika kwaukaguzi maalum (special audit) ili Taifa liweze kujua kamamikataba ya madeni haya inafuata utaratibu mzuri wakiwango cha riba ambayo tunatozwa kila mwaka.

Mheshimiwa Spika, tunasisitiza ukaguzi maalumkufanyika kutokana na ukweli kuwa, mpaka sasa Serikali hainakitengo maalum kwa ajili ya deni la Taifa na hii inathibitishwana taarifa ya Waziri wa Fedha ya tarehe 25 Machi, 2013;Maelezo ya Waziri wa Fedha kwa Bunge la Jamhuri yaMuungano wa Tanzania akiwasilisha Mwongozo, matazamiona Upeo wa Bajeti ya 2013/2014, ukurasa wa Nne (4), aya yapili alisema, nanukuu:

“Serikali iko katika mchakato wa kuanzisha Idara yaMadeni ambayo pamoja na mambo mengine itakuwa najukumu la kujenga uwezo wa kufanya upembuzi yakinifu nakuhakikisha usimamizi madhubuti wa Deni la Taifa.”

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni,haiwezi kuendelea kukubaliana na utaratibu huu wa kukopabila hata kuwepo kwa idara inayofanya uchambuzi yakinifuwa deni hilo na riba husika kama mkopo unazingatia thamanihalisi ya fedha value for money ya mradi unaokopewa fedhahizo, hatuwezi kuendelea kulipia deni ambalo hatujuilimewekezwa kwenye mradi gani wa maendeleo namanufaa ya mradi husika kwa Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, Fungu 13 - Idara ya Udhibiti waFedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi; Dira ya Idara hii nikuimarisha na kudumisha mfumo wa udhibiti wa fedhaharamu wenye hadhi ya Kimataifa utakaoimarisha mfumowa fedha na kudumisha haki kwa jamii, kuleta utulivu wakisiasa na ukuaji wa uchumi endelevu.

Mheshimiwa Spika, dhahiri kuwa fedha nyingi zaWatanzania zilizowekwa kwenye mabenki ya nje kwa kiasikikubwa ni fedha ambazo hazikupatika kwa njia za halali nakwamba kuna uwezekano wa ukwepaji mkubwa wa kodi.

Page 103: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

103

Aidha, nchi yetu imekuwa katika matatizo makubwa yafedha za kigeni, jambo ambalo limepelekea kushushathamani ya shilingi ili kukabiliana na gharama za manunuziya bidhaa nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaonakuwa, dira hii inashindwa kutekelezeka kwani bado fedhanyingi za nchi hii zinahamishwa na kufichwa kwenye mabenkiya nje na fedha hizo kunufaisha zaidi wenzetu wakatiWatanzania wakiachwa hoi bin taaban na hivyo kupelekeauchumi wetu kukosa utulivu na uendelevu kama dira ya Idarainavyosema.

Mheshimiwa Spika, bajeti ya matumizi ya kawaidakwa idara hii kwa mwaka wa fedha 2012/2013, ilitengewashilingi milioni 1,944.79 lakini hadi kufikia februari, 2013, fedhazilizotolewa ni shilingi milioni 653.65 tu ambazo ni sawa naasilimia 33.6 ya makadirio. Kwa upande wa matumizi yamaendeleo bajeti ilikuwa ni sh. 267,800,000 lakini hadi februari,2013, hakuna fedha yoyote iliyokuwa imetolewa kwa ajili yashughuli za maendeleo za idara hii.

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014, fedha za matumizi ya kawaida zimetengwa shilingimilioni 1,944.79 kama ilivyokuwa mwaka 2012/2013 na kwamwaka 2013/2014 fedha za maendeleo zimetengwa jumlaya sh. 399,685,000.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaulizakama fedha zinazotengwa hazitolewi kwa utoshelezi napengine hazitolewi kabisa, je, ni kwa vipi idara hii itafanyakazi zake? Vita dhidi ya fedha haramu sasa ni vita yaKimataifa. Wizara ya Fedha ni lazima iimarishe kitengo hiki ilikuendana na changamoto iliyopo.

Mheshimiwa Spika, Fungu (7) - Msajili wa Hazina; Ofisiya Msajili wa Hazina ndiyo ambayo imepewa majukumu yakusimamia shughuli za uendeshaji wa Mashirika ya Umma,Taasisi na Wakala za Serikali. Majukumu hayo ni kwa mujibuwa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali.

Page 104: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

104

Mheshimiwa Spika, miongoni mwake ni pamoja na:Sheria ya Msajili wa Hazina (The Treasury Registrar’s OrdinanceCap 418 na marekebisho yake); Sheria ya Mashirika ya Ummaya mwaka 1992 na marekebisho yake; Tangazo la Serikali Na.23 la mwaka 1993 la kuvunjwa Kamati ya Rais ya Mashirikaya Umma (SCOPO) na mgawanyo wa majukumu yakeyaliyokuwa yanatekelezwa na Kamati hiyo kufanywa naMsajili wa Hazina; na pia kupitia Nyaraka mbalimbalizinazotolewa na Msajili wa Hazina. Mwisho, ni ofisi hiikusimamia uandaaji wa ikama na bajeti ya mishahara katikaTaasisi na Wakala wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, katika zoezi la ubinafsishaji wamitaji ya kiuchumi lililofanywa na nchi nyingi za Kiafrikakwenye miaka ya 60 limechangia kuua uchumi wa ndani wanchi nyingi barani Afrika. Ubinafsishaji huo ulitikisa misingi yakiuchumi na matokeo yake hadi leo nchi nyingi badozinahangaika na kukuza uchumi ambao utaendeshwa nasekta binafsi (Private Sector Led Economy).

Mheshimiwa Spika, suala la utaifishaji njia kuu zakiuchumi limechangia kuzorotesha uchumi wa nchi nyingi zaAfrika, ni lazima tujiulize ni kwa nini wenzetu wa Ulaya na Asiawanasonga mbele wakati sisi bado tunabaki nyuma” (Kwamujibu wa Yoweli Kaguta Museveni – Mkutano wa Utekelezajimalengo ya Milenia, Serena Hotel Kampala, tarehe 4 Oktoba,2010).

Mheshimiwa Spika, Mwaka jana tulizungumzia sualahili katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi,Kambi Rasmi ya Upinzani ilitaka kupata msimamo wa Serikalikatika suala la ubinafsishaji wa mashirika ya umma, Shirika laCHC linasimamia sera ya ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma.

Mheshimiwa Spika, Sera ya ubinafsishaji iliyoanzakutekelezwa mwanzoni mwa miaka ya tisini pamoja na kuletabaadhi ya manufaa imekuwa ikilalamikiwa sana siku hadi sikuna wananchi. Malalamiko mengi ni kwamba nchi yetuimetekeleza zoezi la ubinafsishaji vibaya, liligubikwa na rushwa

Page 105: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

105

(briberization as termed by Joseph Stiglitz) na uuzaji holelawa mali za yaliyokuwa mashirika ya Umma kama majengona kadhalika.

Mheshimiwa Spika, Kampuni nyingi zinapoteza kiasikikubwa cha fedha na zimeshindwa kutoa ushindani. Nyingizimeendelea kuwepo kutokana na sababu za kisiasa nauwezo wa Serikali wa kuzifanya ziwepo unatokana nakuungwa mkono na fedha za wahisani. Mfano unaooneshakuwa Serikali inatumia kampuni hizo kwa maslahi ya kisiasani usimamizi wa miundombinu ya umeme nchini.

Mheshimiwa Spika, umeme wa Tanzania ni wa mgao,wananchi na wenye viwanda wana fursa nzuri ya kutokatiwaumeme mwaka wa uchaguzi, lakini baada ya uchaguzi,kukosekana kwa umeme kunaendelea. Wahisaniwanaufanya mfumo wa kisiasa uliopo kuwa endelevu,wanaunga mkono miundombinu inayoanguka kulikokuangalia ujenzi wa biashara zinazofikiwa na kusimamiwavizuri, zikiwa na utumiaji na usimamizi wa fedha ambao nimzuri.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa Serikaliinapata stahili zake kutokana na ubinafsishaji wa mashirikayake yanayobinafsishwa iliunda Shirika Hodhi la yaliyokuwaMashirika ya Umma (CHC) kwa lengo la kuhakikisha mikatabaya ubinafsishaji inalinda. Aidha, ni jukumu la msingi la Msajiliwa Hazina kulinda hisa za Serikali katika ubia wa Serikali namashirika hayo.

Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa, Ofisi yaMsajili wa Hazina (TR-Treasury Registrar) imekuwa dhaifu mnokatika kusimamia mali za Serikali katika Mashirika. Mifano yanamna hisa za Serikali zilivyouzwa itasaidia kuonesha hali hii.

Mheshimiwa Spika, kwanza Kampuni ya Oryx ilikuwainamilikiwa na Serikali kwa asilimia hamsini mpaka mwaka2004. Mwaka 2004, kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR),Serikali iliuza hisa zake ambazo ni asilimia 50 kwa bei ya kutupakwa thamani ya dola 2.5 milioni.

Page 106: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

106

Mheshimiwa Spika, pili, hisa asilimia 25 zilizokuwa zaSerikali katika Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kuuzwa kwawamiliki wa Kiwanda kwa utaratibu usio wa wazi. Jambo hililimeonesha pia udhaifu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Mheshimiwa Spika, katika kuthibitisha udhaifu huoMkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali alitoa ushauri:“Serikali itapaswa kuangalia uwezekano wa kuanzishaMamlaka ya Usimamizi itakayokuwa na jukumu la kudhibitina kusimamia uendeshaji wa Mashirika na Taasisi Nyinginezoza Umma 176 zenye hisa/mtaji ya jumla ya Shilingi trilioni 12.2katika kukuza uwajibikaji na uwazi katika kutoa huduma nzurikwa Umma” (Kwa mujibu wa Taarifa ya Mdhibiti na MkaguziMkuu wa Hesabu za Serikali, Ripoti ya Mashirika ya Umma2011/2012 Ukurasa wa 18).

Mheshimiwa Spika, utendaji mbovu wa Msajili waHazina kwa njia moja au nyingine unatokana na uzembe waSerikali wa kutowathibitisha watendaji au Mkurugenzi badalayake amekuwa akikaimu nafasi hiyo ya juu kwa kipindi chotejambo linalopelekea ashindwe kutoa maamuzi.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitakaSerikali kufanya uteuzi au mchakato ambao utajaza nafasizote muhimu zinazokaimiwa ili kuondokana na tatizo la utoajiwa maamuzi kwa taasisi zetu.

Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Uwekezaji ya (NICOL);Mwaka 2001 ilianzishwa kampuni ya Wazalendo ya uwekezajiiliyokusanya mtaji wake kwa kuuza hisa kwa wananchitakribani Wilaya zote za Tanzania Bara na ikafikisha mtaji wakiasi cha shilingi bilioni 8.4 kutoka kwa wanahisa waketakribani 48,000.

Mheshimiwa Spika, pamoja na ukweli kuwa hii nikampuni ambayo imekusanya fedha kutoka kwa wananchimaskini baada ya kuwauzia hisa pamoja kwamba imekuwahaifanyi vizuri siku za hivi karibuni kutokana na migogoroambayo imeikumba kampuni hii ikiwemo mgogoro wake naMamlaka ya Mitaji na Dhamana (CMSA), jambo ambalo

Page 107: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

107

lilipelekea kufungwa kwa akaunti zote za kampuni hii katikaBenki mbalimbali na hivyo kushindwa kutoa taarifa zake zafedha kwa mwaka 2010, 2011 na 2012, jambo lililopelekeakuondolewa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,inaitaka Serikali kuwaeleza Watanzania hasa wanahisakuhusiana na mambo yafuatayo:-

(i) Ni nini hatima ya fedha za wanahisa wakampuni hii ambao ni Watanzania maskini waliohamasishwakununua hisa, je, fedha zao ziko salama?

(ii) Serikali inatoa tamko gani kuhusiana naWatanzania kuendelea kununua hisa na kuwekeza kwenyemakampuni mbalimbali hapa nchini hasa baada ya uzoefuhuu wa NICOL na TOL.

(iii) Nini athari za mgogoro huu wa NICOL kwenyeumiliki wa Benki ya NMB kwa hisa milioni 33 ambazo ni sawana asilimia 6.6 ya hisa zote za Benki hiyo?

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, kwaniaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, naomba kuwasilisha nayale yote ambayo sijayasoma yaingie katika Hansard.Ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante, ni kama umeni-time kabisa.Waheshimiwa Wabunge sasa naomba niwataje wafuataoambao watachangia; Mheshimiwa Zakhia Meghji,Mheshimiwa Omari Nundu, Mheshimiwa Joseph Selasini,Mheshimiwa Said Mussa Zubeir, Mheshimiwa David Kafulila,Mheshimiwa Kombo Khamis Kombo, Mheshimiwa MansoorShanif Hiran na Mheshimiwa Devotha Likokola. MheshimiwaZakhia Meghji!

MHE. ZAKHIA H. MEGHJI: Mheshimiwa Spika, kwanzakabisa nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuwezakuchangia Wizara ya Fedha. Napenda kumpongezaMheshimiwa Waziri na timu yake yote.

Page 108: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

108

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha ndiyo Wizaraambayo inapanga, inayopendekeza na pia kusimamiautekelezaji wa Sera zote ambazo zinahusu fedha.

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo kama vyanzo vyamapato ni vidogo, kama riba katika mabenki ni kubwa, sualala utendaji wa pensheni, schemes, sheria zinazohusu fedhana mikopo pamoja na uwekezaji na pia kudhibiti deni la Taifasote tunanyoosha kidole kwa Wizara ya Fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo, sera zinazotokaWizara ya Fedha ni sera muhimu sana na kwa maana hiyo,katika mchango wangu huu nitajikita zaidi katika serazinazohusu masuala ya fedha.

Mheshimiwa Spika, kama muda utaniruhusuningependa kuzungumzia maeneo matatu. Kwanza kabisa,sera inayohusu mikopo ya nyumba yaani Mortage Financing;pili, sera inayohusu retention yaani makusanyo ya fedhayanayobaki pale pale ambapo kunakusanywa, kama katikaWizara au katika Idara, na tatu, mikopo midogo midogo kwawananchi wa hali ya chini yaani micro-financing.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa ningependakuzungumzia juu ya mikopo ya nyumba au mortagefinancing. Wizara ya Fedha ilileta Sera na Sheria ya Mikopoya Nyumba ili kuweza kuhakikisha kwamba wananchiwanaweza kujenga nyumba na kuweza kuishi pia kwenyenyumba bora kwa kuchukua mikopo kutoka benki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini ni budi tujiulize je, utekelezajiwake upo vipi na unasaidia vipi sehemu kubwa ya jamiiambao ni wananchi wa hali ya chini. Kwa maana hiyo, nilazima tuangalie riba inayotozwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivi sasa riba ya mikopo yanyumba inayotozwa Tanzania tunaweza kusema kwambani kubwa sana. Riba ya juu nafikiri ni kama asilimi 19 na ribaya chini ni asilimia 15. Kwa maana hiyo wastani wa riba

Page 109: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

109

inayotozwa ni kama asilimia 17 ambayo mtu analipa kwamuda wa miaka 20 mpaka 25. Hii ni riba kubwa sana.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mikopo ya nyumba ili iwezekusaidia wananchi na waweze kulipa, wasiweze kufikakatikati halafu nyumba zao zikauzwa, ni lazima riba hii iwena tarakimu moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati nchi kama Australia kwamfano, riba ni kama asilimia tano tu, kwa maana hiyo unalipamkopo wako kama vile unalipa kodi yako, badala ya kumlipamwenye nyumba ile kodi unalipa ile kodi kwenye benkimpaka unaweza kumaliza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo, kuna hajakubwa ya kuangalia sera hii ya riba ya mikopo ya nyumba.Kuna wakati mmoja ambapo hata Gavana wa Benki Kuu,Profesa Ndulu, alishangaa kwamba, iweje mabenki yachajiriba kubwa wakati taasisi ya Mortage Refinancing Companyambayo inapitisha mikopo yake kwa wateja kwa kupitiabenki zilizoungana ilipata mkopo kwa kuanzia kutoka Benkiya Dunia kwa riba ya asilimia nane(8).

Mheshimiwa Spika, sasa hapa wamepata riba yaasilimia nane, lakini wao wanachaji riba ya asilimia 19. Hatakama tutazungumzia masuala ya administration cost nakadhalika, nafikiri hii ni riba kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo, kwa mfano, mtuakikopa labda milioni 25 kujenga nyumba, kwa asilimia hiyokumi na tano au kumi na tisa, kwa muda miaka 25 kwa ribahiyo utalipa karibu shilingi milioni 60 mpaka 70, hii ni ngumusana kwa wananchi kuweza kulipa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mara nyingi sana tunaambiwakwamba Tanzania ingekuwa ina vitambulisho vya Taifa, labdariba ingeweza kupungua, lakini tujiulize kwa sababuwanasema kwamba hawajui mahali watu wanakaa nakadhalika, tujiulize Wabunge hapa ambao wanajulikana

Page 110: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

110

wanaishi wapi, wanafanya wapi, wanapata mshahara ganiasilimia ngapi ambayo wanalipa? Ni asilimia kubwa ambayowanalipa, asilimia 15 mpaka 90. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hivyo, jibu la kusema kwambakwa sababu tu hakuna vitambulisho vya Taifa nafikiri siyo jibusahihi, kuna haja ya Wizara ya Fedha ilichukue jambo hili naiangalie ni jinsi gani ambavyo mikopo au riba ya fedhaitaweza kupungua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa haraka haraka naonakengele ya kwanza imelia, napenda kuzungumzia juu yakuwashirikisha wananchi wa kipato cha chini kupata mikopomidogo midogo. Ukurasa wa tisa wa Ilani ya Uchaguzi yaChama cha Mapinduzi ya mwaka 2010, inazungumzia juu yakuhamasisha uanzishaji wa ushirika wa kuweka na kukopayaani SACCOS na VICOBA ili wananchi wengi zaidi wa haliya chini waweze kujihusisha katika uzalishaji mali, katika kilimo,uvuvi, ufugaji na kadhalika. Kwa maana hiyo, hivi sasawananchi wengi sana wameitikia wito huo kupitia VICOBA.

Mheshimiwa Spika, tunaambiwa kwamba amana yaVICOBA inachukua karibu bilioni 300 ukichukua kwa TanzaniaBara na Tanzania Zanzibar. Lakini tatizo kubwa limekuwahakuna sera ya microfinance.

SPIKA: Mheshimiwa ahsante.

MHE. ZAKHIA H. MEGHJI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa nitamwita Mheshimiwa OmarNundu na Mheshimiwa Joseph Selasini ajiandae.

MHE. OMAR R. NUNDU: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana. Awali ya yote niisifu Serikali na Bunge zimakwa kuja na huu mfumo mpya wa bajeti wa kuangalia Wizarazote tumeona kipi kinahitaji na mwisho wa siku tunakuwahatuna matatizo ya kubishana pale tunapohitimisha.

Page 111: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

111

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, bajeti ya trilioni kumina saba na nusu kwa nchi kama ya Tanzania, tunakwendakwenda tu, lakini siyo bajeti ambayo itatupeleka mbele zaidi.Sasa kama pesa hizo hazikuweza kupatikana, ikawa businessas usual, mwisho wa mwaka tukakuta kuna Wizara kadhawa kadha ambazo hazikupatiwa pesa hizo. Matatizoyatakuwa ni makubwa zaidi.

Mheshimiwa Spika, hapa ndipo ambapo nakwendasasa kwenye Wizara husika ambayo hoja yake tunai-discussleo. Pamoja na kuwasifu kwa kutoa hotuba nzuri na mikakatimingi, lakini kikubwa mwisho wa siku ni kuwa, Wizara na Taasisizake zote kwa jumla zijitahidi kile ambacho kinatakiwakikusanywe, kikusanywe na kipelekwe kule kunakohitajikakwa wakati.

Mheshimiwa Spika, Wizara hii ina jukumu kubwa sanala kutumia rasilimali yetu ya asili tuliyo nayo ambayo nibinadamu wenyewe na tunao wengi, tuko karibu milioni 45sasa hivi. Nchi yoyote haiwezi kuendelea kama rasilimali yakehiyo haitumiki na tuna bahati kwa Tanzania. Watanzania kwaumaskini wao wanajitahidi kwa kila njia kutafuta njia yakujipeleka mbele kimaendeleo, lakini uhusiano uliopo kati yaTaasisi ya Wizara hii na Wizara yenyewe pamoja nawafanyabiashara hawa ambao wengi ni wadogo wadogo,naomba uangaliwe vizuri.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana hapa tuliangaliasuala la boda boda ambao walikuwa wanapata unafuu wakodi kwa kufikiria kuwa wanakusanya milioni tatu. Tukasemawakikusanya milioni nne, ndiyo unafuu wa kodi uanzie hapo.

Mheshimiwa Spika, ukweli ni kuwa boda bodamapato yao ni milioni tano na laki sita, siyo milioni nne. Kwahiyo, kukurupuka hatuna kusema kuwa milioni nne ndiyowasilipe kodi, naona halikuwa jambo sahihi. Wataalamwalioko kwenye Wizara hii naomba wasifanye uvivu,waangalie mapato na matumizi ya wafanyabiasharawadogo wadogo. Tusiangalie tu kuwa wanalipa kodikutokana na mapato tuangalie na matumizi yao.

Page 112: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

112

Mheshimiwa Spika, nimesema kuwa kipato cha bodaboda na nilifanya mkakati hapa wa kuona gharama zao nivipi. Ni milioni tano na laki sita kwa mwaka, lakini matumiziyao ukiyafuata ni milioni saba laki moja na kumi na nane elfu.

Mheshimiwa Spika, boda boda hizi zinapata hasaraya zaidi ya milioni moja na si kwamba, ukiwa na boda bodanyingi basi faida inakuwa kubwa kwa sababu kila boda bodamoja ni kitengo kinachojitegemea. Mtu hata ukiwa na bodaboda tano, hasara ile ya kila boda boda moja utairudia katikaboda boda nyingine zote.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ukiwa na nyingi ndiyounazidi kupata hasara. Sasa tunaposema anayekuwa naboda boda mbili aanze kulipa kodi, tunawaua,tunawamaliza. Wanachofanya kukwepa hili ni kuwalipa walemadereva mshahara ambao hauendani na hali ya maishahapa na kufanya hivyo boda boda zao zinamalizika upesisana.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Meghji ameliongeleasuala la riba na huku linajitokeza. Hatuwategemei hawawawe na hela zao mfukoni, wanakwenda Benki kukopa pesa,riba kule ni asilimia 20. Ukikopa milioni moja na laki saba nahamsini elfu, unaishia kulipa zaidi ya milioni mbili na ukisemauzilipe kwa miaka mitatu inabidi utenge laki saba nathemanini elfu, halafu kama hiyo haitoshi boda bodainatozwa shilingi elfu kumi kwa fire extinguisher, boda bodagani inayobeba fire extinguisher. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hebu hii elfu kwanza itoeni kabisa,kesho mtasema abebe matairi halafu pia muwa-charge,halafu inaambiwa fire extinguisher inachajiwa siyo kwasababu wanapewa, kwa sababu wanatakiwa watu wa firewafanye inspection. Hakuna fire yeyote anayefanyainspection yoyote kwa boda boda. Hii elfu kumi naombaMheshimiwa Waziri uitoe kabisa, usipoitoa nashika shilingihapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vijana wetu wadogo wadogo na

Page 113: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

113

Tanga ninao wengi wanatoka Lushoto na sehemu nyingine,wanauza njugu kuweza kujikimu. Akinunua kilo tatu za njuguyule anapata kwa mwaka makusanyo karibu milioni tano nalaki moja. Ukienda kwa kile Kitengo cha milioni nne, yuleanavunja sheria anapata milioni tano na laki moja lakini halipikodi.

Mheshimiwa Spika, lakini mwangalie gharama zakeza kuuza njugu zile anatumia karibu milioni sita laki sita natisini na saba. Sasa ukimwambia alipe kodi ni matatizo. Hebujamani fanyeni kazi, Accountants wapo hapa, ndugu yanguKatagira nilikuwa naye Glasgow kule anasomea hilo, labdammwambie mambo haya.

Mheshimiwa Spika, hakuna mtu ambaye anaanzakutoza kodi kwa mapato wakati hajajua mtu ametengenezahasara au vipi? Kama mnaona uvivu kufanya hivyo, basimuweke kiwango ambacho napendekeza mpaka milionisaba mtu asitoe kodi na mtu hata akiwa na boda boda kumizile ni hasara tupu, asitoe kodi. Ndiyo hapo tutawezakuwapata wafanyabiashara ambao watakuwa katikamazingira ya kuzoea kulipa kodi. Maana wakianza kukwepakodi huku nyuma, huko mbele ndiyo matatizo hataanapokuwa mfanyabiashara mkubwa hapa nchini, lazimatuwaanzishie huku chini waendelee zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa pesa zitatoka wapi?Sheraton Hotels inapokuja kuanzisha biashara Tanzania, ilehaitegemei itengeneze faida siku ya kwanza hapa. Lile nijikampuni kubwa, wanafanya cross subsidization. Sasa nimaajabu sisi tunapojipeleka kichwa mbele na kuwapamsamaha. Halafu siyo msamaha wa miaka mitano tu, miakamitano ikiisha tunawapa msamaha tena. Tunataka kijana waboda boda alipe kodi, lakini huyu wa Sheraton apatemsamaha, apate msamaha apate msamaha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama akina Sheraton hawajihapa, wanakuja watu wanaokuja kujaribu kufanya biasharahapa, ndiyo wanaohitaji msamaha. Tusiwakaribishe,tusiwakaribishe watu wanaokuja kujaribu kufanya biashara,

Page 114: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

114

halafu anakuja anakopa kwenye mabenki yetu haya.Wanaondoa nafasi za vijana hapa wanaotaka kujiendeleza,wanakopa pesa wao halafu tunawasamehe.

Mheshimiwa Spika, ukiingia hoteli za akina Sheratonhizi chupa ya maji ya shilingi mia tatu wakati ule nje, kuleunauziwa kwa elfu tatu. Halafu mtu huyu anapewamsamaha wa kodi, inakuwaje? Lazima tutoke huko.Nimesema nchi yoyote watu wake ndiyo wanakwendambele kwa Tanzania hii, kitu kikubwa ni biashara na watuwetu wanaojituma.

Mheshimiwa Spika, wanaanzia chini kabisa nawanaendelea na mifano iko mingi. Uingereza pale kulikuwana mtu anaitwa Allan Michael Sugar, yeye alikuwa anauzamaandazi Liverpool Street. Akapewa unafuu na nchi yake.Yule mtu alikuja mwaka 1986 akaanzisha televisheni ambayoina na video pamoja, inaitwa ARMSTRAD ile ARMSTRAD Brandni Allan Michael Sugar amekuwa millionaire. Akina Fred Lakehivyo hivyo. Wenzetu wanaenzi hawa wafanya biasharawadogo wadogo. Sisi tusiwadhalilishe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Meghji amegusiasuala la riba. Riba hapa jamani, inaathiri kweli. Ukitakakukopa, kwanza kukopa kwenyewe kwa Mtanzaniautazungushwa weee, kinachotakiwa hakijulikani pale. CRDBilikufa hapa na mnajua kwa nini ilikufa mpaka ikaanzakufufuka upya, ilikwenda kabisa ikafilisika kutokana na watuwanavyohangaishwa mpaka kupata pesa.

Mheshimiwa Spika, juzi nilikuwa naongea na Menejawa CRDB, akaniambia Tanga yako hapa, ile mikopo ilifikabilioni 52, watu wakashindwa kulipa. Mtu wa Tanga ganialiyekopa bilioni 52 ashindwe kulipa pale. Kama si hao haowenyewe maofisini wanayapitisha pitisha tu huko.

Mheshimiwa Spika, sasa tumekwenda tumechukuamabenki yote tumewakabidhi watu binafsi. Lazima tuwetunaangalia, kuna vyombo vingine huwezi ukakabidhi vyotekwa watu binafsi. Kwa nini isianzishwe benki ambayo itasaidia

Page 115: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

115

wananchi? Mabilioni ya Rais Kikwete ukiyauliziayamekwenda wapi na akina nani wamepata, vurugu tupu.Watu hawakupata. Kwa nini tusirudi nyuma. Kuna Taasisiambazo nchi haiwezi kukosa kuwa na Taasisi hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukienda Canada wana NationalBank of Canada pale, pamoja na mapesa waliyonayo. Ileni benki ya nchi, inatoa riba nafuu na Serikali yenyeweinatafuta njia ya ku-absolve hiyo, lazima tuanzishe Taasisikama hiyo.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante.

MHE. OMAR R. NUNDU: Mheshimiwa Spika, nitaungamkono hoja kwanza zile elfu kumi zitakapotolewa pale.Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa naendelea, sasa namwitaMheshimiwa Joseph Selasini, atafuatiwa na Mheshimiwa SaidMussa Zubeir.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia hoja iliyo mbeleyetu. Kabla sijachangia nami nikupongeze kwa kusimamiahuu mfumo mpya wa kujadili Bajeti ya Serikali ambaounaendelea sasa hivi. Vile vile nikupongeze pia kwa sababuya kuunda ile Kamati ya Bajeti ambayo kwa kiasi kikubwaitasaidia sana katika kupunguza mivutano kati ya Serikali naWabunge.

Mheshimiwa Spika, nataka kuchangia katika mamboyafuatayo:- Karibu asilimia 70 ya fedha ambazo tunajadilihapa zinaelekezwa katika Halmashauri zetu. Katika miakamiwili iliyopita nilikuwa Mjumbe katika Kamati ya Kudumu yaHesabu za Serikali za Mitaa. Nilichokiona na kinachoendeleakufanyika sasa hivi ni kwamba ndani ya Halmashauri zetu

Page 116: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

116

kuna ufisadi uliokithiri. Karibu nusu ya fedha hizi zinazopelekwakatika Halmashauri zinaishia kwenye mifuko ya watendaji.Sisemi wote, lakini baadhi yao.

Mheshimiwa Spika, fedha hizi zinaishia kwenye mifukoya watendaji kwa sababu mbili. Sababu ya kwanza nikwamba, sheria tuliyonayo ya manunuzi, bado ina mianyamingi sana, inahitaji kufanyiwa mabadiliko makubwa sana.

Mheshimiwa Spika, utashangaa, kitu kinachouzwadukani shilingi elfu tano, kikiingizwa katika mfumo wa tenda,basi yule mkandarasi atadai shilingi laki tano. Hii siyo siri nijambo linaloendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa kama sisi Wabunge tunadhamira ya fedha zile ziwafikie wananchi kwa ajili ya miradiyao lazima tuhakikishe Sheria hii inatazamwa ili tuweze kuzibahii mianya. Napendekeza ikiwezekana baadhi ya bidhaaSerikali itoe bei elekezi kwa baadhi ya bidhaa. Kwa mfanokaratasi, bunda moja la karatasi kila mtu anafahamu, dukanini sh. 10,000/=, lakini mkandarasi akiipeleka Halmashauri nish. 40,000/=. Hivi kweli ni sahihi tunaangalia tu hivi? Zile fedhani fedha ambazo zingekwenda kwa ajili ya huduma kwawananchi wetu.

Mheshimiwa Spika, fedha hizi zinapotea kwa namnanyingine tena kupitia kwa Wakaguzi wa Ndani. Baadhi yaWakaguzi wa Ndani nadhani wana ubia na Wakurugenzi.Kwa sababu haiwezekani Mkaguzi hana gari, hana Komputa,hana kitendea kazi chochote, anakwenda kuchukua palekwa Mkurugenzi halafu amkague Mkurugenzi na kugunduakwamba ameiba au ametumia fedha vibaya, halafu huyuMkaguzi wa Ndani atoe maelezo yanayotoshelezahaiwezekani.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ni lazima tuitenganisheIdara ya Mkaguzi wa Ndani na Mkurugenzi Mtendaji. Ili hiiIdara ijitegemee na ripoti za hii Idara zisiende kwa Mkurugenzi

Page 117: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

117

Mtendaji, ziende katika utaratibu kama utaratibu wa CAG.Kwa jinsi hiyo tutadhibiti wizi mkubwa sana ambao unatokeandani ya Halmashauri.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambaloningependa kuchangia ni kuhusu kucheleweshwa kwa fedhaza maendeleo kwenye Halmashauri. Fedha zotetunazoidhinisha hapa, mwisho wa siku lazima Wizara izipelekekwenye Halmashauri kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, lakini kwa kiasi kikubwa sanafedha hizi huwa zinachelewa na zikichelewa miradiinachelewa kukamilika. Zinakwenda kwenye robo ya mwishoya mwaka. Sasa Sheria ya Manunuzi inapoanza kutumika, nikwamba fedha zile zinashindwa kutumika na matokeo yakezinarudi Hazina na miradi mingi sana inachelewa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo naiomba Serikali kamakweli dhamira ni kusukuma maendeleo ya wananchi wetu,basi ni vema sana fedha hizi zikaenda kwenye Halmashaurikwa wakati.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambaloningependa kuchangia, ni Sera ya Microfinance. Wananchiwengi sana vijijini mpaka leo hii fedha zao ziko mchagoni naziko mchagoni kwa sababu benki kubwa ziko mijini tu, hizibenki za biashara, NBC, NMB, CRDB ni benki za mijini.Wananchi wetu kule vijijini hawana utaalam, hawana ujuzi,hawana mazoea ya kutumia mabenki.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naishauri Serikali, kamakweli tunataka kuendeleza watu wetu. Hakunamfanyabiashara anayefanya biashara kwa pesa zakemfukoni hayupo. Wafanyabiashara wote tunaowafahamuwakubwa na wanaofahamika, wanafanya biashara kwakutumia fedha za mzunguko kwenye mabenki. Sasa tunatakawananchi wetu waendelee wataendelea kwa pesa kutokawapi?

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naishauri Serikali

Page 118: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

118

ikamilishe Sheria na Sera ya Microfinance ili wananchi wetuwapate nafasi ya kuanzisha benki zao ndogo ndogo vijijini.SACCOS tulizoanzisha zigeuzwe kuwa banks, VICOBA nakadhalika vya Mama Likokola, watu waweze kukusanywa,waweze kufundishwa namna ya kukopa.

Mheshimiwa Spika, katika hili nataka niendeleze palealipofikia Mheshimiwa Nundu, kwamba, watu wetuwanajitahidi sana, mama zetu vijijini wanajitahidi sana, lakiniwanakwamishwa kwa sababu ya sera na taratibu ambazotunaziweka sisi wenyewe za kuwahujumu. Amezungumzasuala la boda boda ni kweli. Boda boda wanazungushwa,wanahangaishwa kila Wilaya, hakuna Jimbo ambalo matesohaya boda boda hayapatikani.

Mheshimiwa Spika, kule kwangu Rombo sasa hakunamradi mzuri wa Watendaji wa aina mbalimbali, baadhi yaPolisi na baadhi ya watu TRA kama kukimbizana na vijanawa boda boda na hili ni lalamiko kubwa, kila mahalitunalizungumza, lakini halisikilizwi.

Mheshimiwa Spika, kwa kusema hivyo, sitaki nisemekwamba eti utengenezwe utaratibu wa kukwepa kodi, lakiniziwekwe kodi za kueleweka ili walipa kodi wawe rafiki kwaSerikali.

Mheshimiwa Spika, katika hili ningependa pianiwazungumze wafanya biashara wakubwa. Ni lazima sasahivi Watanzania tupunguze au tuondoe kabisa fikra za kufikirikwamba kila mfanyabiashara mkubwa ni mwizi, kilamfanyabiashara mkubwa ni fisadi, hapana, hii si kweli. Wakowafanyabiashara wakubwa waaminifu sana, wanalipa kodina kodi hii ndiyo inayotusaidia. Lakini wako wafanyabiasharaau baadhi ya wafanyabiashara wakubwa ambao piawanakwenda utaratibu wa kodi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niseme, naipongeza TRA,imeleta mabadiliko makubwa sana katika mfumo wa kodikatika nchi yetu na imefanya kazi kubwa pamoja na kwamba

Page 119: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

119

tunaitaka ifanye zaidi. Ukiangalia ulipaji wa kodi kwa miaka10 iliyopita na sasa hivi kuna tofauti kubwa kabisa. Sasa miminaiomba TRA itengeneze urafiki na wafanyabiashara...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana. Sasa nitamwita MheshimiwaSaid Mussa Zubeir, atafuatiwa na Mheshimiwa David Kafulilana Mheshimiwa Kombo Khamis Kombo ajiandae.

MHE. SAID MUSSA ZUBEIR: Mheshimiwa Spika, ahsante.Nashukuru kwanza kwa kupata nafasi hii nikiwa na wingi waafya. Niipongeze Wizara ya Fedha kwa hotuba yake nzuri nayenye mwelekeo na naunga mkono asilimia mia moja.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,ninachotaka kuwaelewesha Watanzania ni kwamba,umefika wakati tunatakiwa lazima tukubali kidogotulichonacho, halafu tutafute mbinu za kusonga mbele.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, tusipofanya hivi siku zotehatutaweza kuendelea mbele. Yaani tukikataa ukweli aukama utakuwa unakimbia kivuli chako ambacho unacho,basi huwezi ukafikia popote. Nazungumza haya nikiwa namaana halisi kuna baadhi ya watu nafikiria kwenye Taasisizetu na Wizara zetu wameligundua hilo, lakini bado kunakuganda ganda na kusita sita.

Mheshimiwa Spika, kuna mradi mzima wa PEMANDUambao huu tuliuhisi kwamba pengine ungekuwa ni farajana ni mkombozi wa Tanzania, lakini naona kwenye bajeti hiibado tunasuasua na tulikwishafikia hatua nzuri. Niliona niwakati muafaka umefika kuanza kufanya hili suala ilitukaenda nalo.

Mheshimiwa Spika, kati ya yaliyozungumzwa humokwenye huo mradi wa PEMANDU, kwanza Serikali ilikula

Page 120: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

120

hasara sana, ilipeleka watu kule Malaysia kwenda kusoma,watu wameitwa wamekuja huku; ndio pale Tanzaniatunaposifika kwa kuhifadhi makabrasha yenye thamani,wakaja watu kwa maelezo yetu tu, wakayachukua yalemaelezo, note ndogo wakaenda wakafanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, kuna nguzo tano za BFR hii Big FastResults. Kwanza ni Uongozi Thabiti uliodhamiria kuletamabadiliko na kuipeleka nchi mbele, kutekeleza vipaumbelevichache kwa nguvu na kuelekeza rasilimali nyingi zaidi katikavipaumbele hivyo; haya mambo jumla yako matano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa ningeishauri Serikali. Serikali,ilianza hili suala vizuri, lakini bado iliweka vipaumbele karibusita; sasa ndio pale ninaposema jamani tunatakiwa tukubalihali tuliyokuwanayo. Naona kama kweli kwa mwaka tunauwezo wa kukusanya trilioni 17 na katika hizi karibuni trilionisaba zinakwenda labda kwenye mishahara, basi naona hatahivi vipaumbele tuvipunguze, twende na kama kimoja amaviwili na si aibu kwa sababu, ndio fedha yetu ya ndanitunayoweza kukusanya. Kutegemea Wahisani na watu wanje, tusitegemee kama tutafika mahali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapoweka miradi mikubwakama hii ya kutaka ku-generate nchi, kuitoa hapa ilipokwenda sehemu nyingine, halafu ndani yake tukaweka naasilimia ya kutegemea Wahisani, kwa kweli tunakuwa hatufikimahali.

Mheshimiwa Spika, Wahisani hawa hawapendelei sisituendelee kabisa na watakuwa wako tayari kutusaidiakwenye miradi kama ya vyura Kihansi, ambayo inatupotezeamuda au kuileta ile mifupa ya mjusi mkubwa, haya mambohayatuendelezi; huku wataleta fedha nyingi, lakinitutakapowapa miradi kama tunawaambia tuna shida yaumeme au tuna masuala ambayo, kama wakijua kwamba,hili likifanikiwa tutakuwa tumekwenda hatua mbili mbele,hawawezi wakatusaidia mia kwa mia. Kazi yetu itakuwatunakwenda na kurudi. (Makofi)

Page 121: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

121

Mheshimiwa Spika, ni afadhali tukategemea fedhazetu ndogo za ndani tukaamua kama ni mradi mmoja au nimiwili basi, tukafanya huo ukakamilika, ukaisha. HawaWazungu wanasema if you want to please all, you pleasenone, kama unataka kufurahisha wote, hutafurahisha hatammoja. Ni lazima kwa wengine kutakuwa kuna manung’unikona vilio, lakini tukisema kwamba, hebu tupeni mradi mmojaambao tukiufanya utakuja kusaidia baada ya miaka mitatumbele, basi tufanyeni hivyo.

Mheshimiwa Spika, hao watakaokabidhiwa hizidhamana za kufanya hivyo, wajijue wana kitanzi kwa sababu,wamezuia fedha za walipa kodi wa Tanzania nzima kwasababu, tunaweza tuka-dump fedha nyingi pale kwamategemeo ya kwamba, pale ndipo patakapokujakutusaidia kutukwamua kutoka hapa kwenda mbele.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa huyo atakayekuwa nadhamana hiyo itatakiwa atoe time frame, awe na uhakikawa muda kwamba, kwa mradi huu mtakaonipa na fedhahizi mtakazonipa, basi ndani ya miaka mitatu tutakuwatumeondoka hapa na kuelekea safari nyingine. Baada yamiaka mitatu, hakuna lililotokea, ajijue yeye ana kitanzihakuna kitu kingine; ndio tutaweza kuendelea, kinyume chahapo hatuwezi kufika, tunatakiwa kwanza tuwe na imani yakutaka kujisaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, unapotaka kufanya jambo, kamani Waziri au ni nani, jambo la kwanza ujiulize, hivi I am doingthis for the sake of what? Unajiuliza kwamba, hiki ninachotakakufanya nataka kufanya kwa maslahi ya nini au ya kitu gani?Jibu, hana haja ya kukaa kwenye vyombo vya habari,akijiuliza tu mwenyewe, basi jibu atalipata tu, kama ni kwamaslahi yake mwenyewe binafsi ama kweli anataka kulisaidiaTaifa. Sasa akifikia hatua hii, hapa tutakwenda tu kwa sababuhata majanga na matatizo na Mungu naye atamwangalia.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika maelezo ya hawa watu wa

Page 122: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

122

PEMANDU waliokuja hapa, wameeleza. Kwanza tuwe namikakati, tuwe na ujasiri, tuwe wakweli na mwisho Mungu nayeye vile vile anasaidia kwa ile nia uliyokuwa nayo, lakinikama nia yenyewe ni mtu kutafuta nafasi, akipata aanzekuvutia upande wake ukweli hatutafika. Ndipo haponiliposema kwamba, ni vizuri tufikie hatua basi, mtu aweanajiuliza na ajijue kwamba, ana kitanzi kwa sababu,amechukua fedha za mwaka mzima za walipa kodi waTanzania tumepeleka upande mmoja, wengine wanasikitika,nafikiri, tunaweza tukafika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine nisije nikasahau, kuna sualala NMB kule Zanzibar, inafanya kazi vizuri sana, lakininingemwomba Waziri, basi awaambie hawa watuwatuongezee matawi, angalau tupate mawili au matatu kwapale Unguja. Kwa sababu, ukweli, hili lilipigiwa kelele sanalimeshajaa watu pale. Unguja nzima ni eneo moja tu naukitazama Benki nyingine kama Barclays wapo mpakaMwanakwerekwe na maeneo mengine kule, wanafanya kaziza vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna suala la mini tiger. Hili sualalilikuwepo kwenye bajeti iliyopita na kuna fedha kidogozilitolewa karibu bilioni 10 na point na hazijakwisha zile fedha.Sasa ninachoshangaa tumemaliza na tunaingia kwenyemuhula mwingine hakuna chochote, yaani kuko silence nandio yale ya kugawagawa fedha, ndio yale niliyoyasemakwamba, unapotaka kuwafurahisha wote, huwezikumfurahisha hata mmoja.

Mheshimiwa Spika, kuna bilioni 10 zilishaanza kutolewakwenye bilioni 50.2, bado fedha nyingine zinahitajika.Zimetoka hizo 10, sasa hizi nyingine safari hii hazimo tena,yaani zile ndio zitakuwa zimetoka na huku tunakokwendahatujui huu mradi utakwisha vipi na mradi huu ungewezakutoa ajira kwa vijana wengi sana na kuweza kukusanya hizokodi ambazo tunazitarajia kwa huko mbele tunakokwenda.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba Mheshimiwa Waziriatakapohitimisha, aeleze hili suala kama ndio halipo tena

Page 123: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

123

na zile fedha zetu za Tanzania bilioni 10.9 ndio zimeshakwendaharijojo kwa masuala haya ambayo tunakwendanayo kamahivyo nilivyosema huko nyuma.

Mheshimiwa Spika, lingine kulikuwa kuna suala laupande ule wa Zanzibar. Kulikuwa kuna watu walizuiliwa kulenanihii zao, lakini hili lilikuwa ni tatizo la TRA, hata Wizara yaFedha, hili suala watakuwa wanalijua. Kuna watu walizuiliwalicence zao, lakini imegundulika kwamba, matatizo hayayametokana na watu wa TRA kuvujisha zile password.

Mheshimiwa Spika, kuna magari kwa ufupiyamezuiliwa yako pale Dar-es-Salaam, yanatakiwa yalipiweushuru. Kuna viroja vimefanyika, wakishirikiana na watu waTRA, lakini ukweli huyu mhusika ambaye yeye ndio kazuiliwahii license yake ya Clearing and Forward, yeye hakuwa namatatizo hayo na hili wameligundua. Sasa naomba basiwafanye utaratibu huyu mtu aweze kuendelea na ile kazi...(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana. Sasa nimwite Mheshimiwa DavidKafulila, atafuatiwa na Mheshimiwa Kombo.

MHE. DAVID Z. KAFULILA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipatia nafasi ya kujadili Wizara muhimukabisa, pengine kuliko Wizara zote ambazo tunazijadili katikaBunge la Bajeti. Unapojadili Wizara ya Fedha, maana yakeunajadili, kwa kiasi kikubwa, namna gani tunaweza tukajengauwezo wa kujitegemea kama Taifa.

Mheshimiwa Spika, ni bahati mbaya sana kwamba,Taifa letu lina uwezo mkubwa sana wa mipango kulikoMataifa mengi duniani, kuliko Mataifa mengi katika Afrika,lakini tuna uwezo mdogo sana; tuna Serikali, yenye uwezomdogo sana katikia kusimamia mipango hiyo.

Mheshimiwa Spika, tatizo kubwa ambalo linakabili

Page 124: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

124

Taifa hili kwa sasa, ni namna gani tunaweza tukakusanyamapato ya kutosha kuweza ku-finance budget, kuwezakutoa huduma za afya, kuweza kutoa huduma za elimu.Kiwango kikubwa sana cha umaskini wa leo, kinatokana nauwezo mdogo wa Serikali, kukusanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja ziko wazi. Mwaka 2010miongoni mwa maeneo ambayo tunakabiliwa na tatizo hilini kwenye eneo la madini. Mwaka 2010 ikapitishwa Sheriahapa kwamba, TRA sasa ianze kukusanya fedha kutokanana migodi hii ya madini kama kodi, lakini uwezo wa TRAkukusanya kodi kwenye migodi ya madini ni mdogo mno. Siomdogo kwa bahati mbaya, ni mdogo kwa makusudi kwasababu, kuna watu wanafaidika na huo udhaifu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Makampuni ya Madiniyanapandisha gharama za uzalishaji kila kukicha, bei yadhahabu ikiongezeka na wao wanaongeza bei ya uzalishaji,ili kupunguza kodi. Wakati bei ya dhahabu ni dola 300, waowanasema gharama ya uzalishaji kwa gramu 30, yaani ounceni 200. Wakati bei ya dhahabu inapanda mpaka 1,800/=, waowanaongeza gharama ya uzalishaji kwa gramu 31 ni dola1,200; yaani wanaongeza bei, wanaongeza gharama yauzalishaji kadiri bei ya dhahabu inavyoongezeka, kupunguzasehemu ya faida ili kuweza kukwepa kodi.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi vitu viko wazi, lakini bahatimbaya sana ni kwamba, waliopewa dhamana ya kufanyahivyo, hawafanyi na hawafanyi kwa makusudi. IlitakiwaKanuni ziandaliwe kwa ajili ya utekelezaji wa Sheria hiyo,tangu mwaka 2010 mpaka leo Serikali imeshindwa kuandaaKanuni kwa ajili ya kuratibu jambo hilo, sababu ni nini?

Mheshimiwa Spika, mwaka 2010 kwenye Sheria hiyohiyo, kilipitishwa Kipengele ambacho kinaruhusu Makampunihaya ya madini kwa sababu, yanakwepa kodi kutokana nakuficha takwimu zao, kutokana na kuficha mapato yao,yawe listed kwenye soko la mitaji pale DSE, (Dar-es-SalaamStock of Exchange), lakini mpaka leo yamegoma.

Page 125: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

125

Mheshimiwa Spika, Sheria ipo, lakini Wizaraimeshindwa kuandaa Kanuni, ili kusudi haya Makampuniyawe listed pale. Yakiwa listed pale ni kwamba, mtajua sasatransactions zote ambazo zinahusiana na mgodi, kwa hiyo,governance ya mgodi itakuwa wazi, lakini pia faidaitapatikana.

Mheshimiwa Spika, leo TBL Serikali, ina 4% tu, lakini TBLinaingiza kwenye Serikali fedha nyingi kuliko Airtel ambakoAirtel tuna 40%. Hizi ni hesabu za darasa la pili tu kwamba,inawezekanaje Kampuni ambayo tuna hisa 4% iingizie Serikalizaidi kuliko kampuni ambayo tuna 40%? Ni kwa sababu, TBLimekuwa listed pale DSE, imekuwa listed kwenye StockMarket, lakini Airtel tangu mwaka juzi, tangu mwaka janampaka leo Serikali, mmekataa ku-list hisa zenu, sio zote hata10% tu; lengo hapa mki-list pale kwenye Soko la Mitaji nikwamba, hesabu zote za Kampuni zitafahamika, mnagomanini? Sasa watu wakichachamaa, mnasema kwamba, hawawatu wana matatizo, sio kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ambalo duniani kote,hata vinchi kama vya Sri-Lanka, ambavyo kimsingi vimekaana vita muda mrefu, eneo la benki bado ni tatizo katika nchihii. Nchi kama Sri-Lanka, wao benki zao zote, yaani financialinstitutions zote, benki na taasisi nyingine za fedha kamainsurance zote zinakuwa listed kwenye Stock Market, lengoni kuhakikisha kwamba, yale mabenki yanafanya majukumuambayo yalikusudiwa.

Mheshimiwa Spika, Tanzania leo ni nchi ambayo inabenki nyingi kuliko nchi zote za SADC, tuna benki 51, lakinihuduma za kibenki ziko chini sana kwa sababu, mabenkimengi hayafanyi kazi za kibenki yanafanya ma-deal yamoney laundering; wanasafirisha fedha tu hawa, ndio maanabenki zinaongezeka, lakini huduma za kibenki zinashuka.Namna mojawapo ya ku-control hiyo hali, haya mabenki yotemoja ya condition yawe listed kwenye Stock Market pale, ilikusudi tu-own, tumiliki hata 10% tu, hesabu zao zotezitafahamika. (Makofi)

Page 126: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

126

Mheshimiwa Spika, Wizara hii ya Fedha inahusika piana masuala ya ubinafsishaji. Hii nazungumza kwa maranyingine tena kwamba, kama kuna maeneo tulifanyamakosa na tunaendelea kufanya makosa na Serikali,inaendelea kufanya mikakati ya kuficha hayo makosa nikwenye eneo la ubinafsishaji.

Mheshimiwa Spika, wakati tunabinafsisha, moja yamalengo ya kuanzisha lile soko la hisa, ilikuwa ni kwamba,mashirika yote yatakayobinafsishwa yaweze kuwa listed palehata kwa asilimia ndogondogo kwa lengo la ku-manage sokohuria.

Mheshimiwa Spika, lakini mpaka leo, tumebinafsishamashirika takribani 320, lakini mashirika pekee ambayoyamekuwa listed pale ni mashirika saba tu, mashirika mengineyote yamegoma, yameigomea Serikali. Yamegoma kwalengo la kuficha taarifa zao, ndio maana tunashindwakufaidika na ubinafsishaji kwa sababu, haya mashirikayangekuwa listed pale, tungekuwa na mtaji mkubwa.Kwenye uchumi, Stock Market ndio barometer ya uchumi kwasababu, watu wengi watashiriki pale. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine inahusiana na Benkiya NBC, kwenye Kamati tulijadiliana pale. Benki ya NBC kunamadeni ambayo mpaka leo wanasema ni madenikichefuchefu, takribani bilioni 60. Wakati wa utaratibu wakutoa mikopo ile, watu wamekopeshwa kwa dhamanaambazo haziendani na mkopo aliochukua.

Mheshimiwa Spika, matokeo yake CHC imeshindwakurudisha madeni yale kwa sababu, mtu amekopa mkopowa bilioni 10, ameweka dhamana ya milioni 10. Kwa hiyo,hata ukichukua dhamana yake haina maana yoyote ile.

Mheshimiwa Spika, tunataka majina ya watu wotewaliokopa NBC yaletwe Bungeni, kama ni Kampuni, Kampunina wamiliki waletwe Bungeni hapa tujue. Maana kunawengine ni matajiri wako mtaani, lakini kwa sababu mlikosea

Page 127: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

127

wakati wa mchakato mzima wa utoaji wa mikopo, mpakaleo tunashindwa kuwakamata; bilioni 60 is a lot, nchiinashindwa kutengeneza madawati miaka 50, lakini kunawatu wanamiliki bilioni 60, haiwezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine naomba kuishauriSerikali na Wizara hii. Bado kuna mashirika kadhaa takribani40 ambayo bado hayajabinafsishwa, nawashauri ingawajehamshauriki, haya mashirika yawe listed pale hata kwaasilimia kwenye Stock Market. Mnagoma nini? Mnafaidikanini? Haya ni maeneo muhimu sana ya ku-manage mapatoya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kabla muda wangu haujaniishia,naomba nigusie jambo la Bandari. Katika maeneo ambayokuna udhaifu mkubwa wa Serikali hii ni kwenye ku-managemapato pale Bandarini. Kwanza kuna watu ambaowanapandishiwa bei, lakini pili, kuna watu ambao hawalipikabisa; yaani kila kitu matatizo, wengine hawalipi na wenginewanapandishiwa bei. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye Kamati tumezungumzapale kwamba, Serikali, ifanye uchunguzi madhubuti.Walifanya uchunguzi wa takribani wiki mbili tu, Serikali,imepoteza takribani milioni 900 kwa wiki mbili tu, sasa kwamuda mrefu, mpaka leo ni kiasi gani ambacho kimepotea,kama ni miaka mitano, wiki mbili milioni 900, miaka mitanoinakuwaje?

SPIKA: Ahsante. Ulikuwa unasema mambo mazurimpaka nimesahau saa. (Makofi/Kicheko)

Sasa nimwite Mheshimiwa Kombo Khamisi Kombo,atafuatiwa na Mheshimiwa Mansoor Hiran.

MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO: Mheshimiwa Spika,nishukuru kwa kupata nafasi. Nianze kwa kusema ukitakakujua tabasamu la mtoto, basi mtilie kitu chenye ladha tamu

Page 128: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

128

ndani ya kinywa chake. Lakini ukitaka uone uchungu wamtoto, basi vile vile mtilie kitu kinachoitwa shubiri ndani yakinywa chake. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, niseme kwamba, kwa miaka 50Watanzania sote tumemeza shubiri. Ni kwa sababu zifuatazo:Tanzania tuna madini ya dhahabu, almasi, uranium,tanzanite, lakini mapato tunayopata ni madogo zaidi kulikomapato ambayo wanayapata wageni wale ambaowanamiliki migodi ile. Kwa hivyo, hii ni njia moja ambayoWatanzania tumelishwa shubiri kiasi ambacho Serikali yetuinakosa mapato ya kuweza kuendesha nchi yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini la pili ni suala zima la bandari.Niungane na wenzangu, pale Bandarini pana karibu ma-container 600; ma-container haya 600 bado menginehayajalipiwa ushuru na wengine wanatafuta njia yakuyahamisha kupeleka Uganda au Kenya kwa sababu,wameshindwa kulipia ushuru pale.

Mheshimiwa Spika, sasa ni lazima tuwe na mfumorafiki, utakaowezesha wafanyabiashara wakubwa pamojana wafanyakazi wa TRA, waweze kushirikiana ili biashara zetuziweze kwenda kwa uaminifu na kwa uadilifu.

Mheshimiwa Spika, jambo moja ambalo linaturudishanyuma ni ushuru. Biashara inayochukuliwa nje ikaletwaTanzania, ushuru unaotakiwa kulipia pale ni mkubwa zaidikuliko malipo unayolipia nje. Gharama unayochukulia nje nindogo zaidi kuliko ushuru unaotakiwa ulipie pale. Kwa hiyo,ni lazima Serikali, ilifikirie hili ili iweze kuingiza mapato.

Page 129: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

129

Mheshimiwa Spika, la pili niseme kwamba TanzaniaMwenyezi Mungu katujalia kuwa na vyanzo vingi vya mapatolakini bado tunashindwa kuvitumia. Tunayo bahari kuu, baharikuu Tanzania bado haijatumika kwa manufaa yaWatanzania. Wanaokuja kuitumia bahari kuu ni watu kutokanchi nyingine. Wanaingia na vyombo vyao, wanachukuasamaki, wanapeleka kwao, Tanzania haiingizi chochote.Wakati miaka kumi nyuma iliyopita, Chama cha WananchiCUF kiliwahi kuishauri Serikali kwamba ijenge viwanda vyakusindika samaki na vilevile iweke kituo cha mafuta ambapomeli kubwa kutoka nje zitakapofika pale zitaingiza mafutapale na vilevile itajulikana wamevua samaki wa kiasi gani,wana thamani gani na kitakachopatikana pale kitaingiaSerikalini lakini mpaka leo hili halijafanyika. Hivyo basi,naomba ushauri utakaoonekana kwamba unamaana nautaleta tija kwa nchi, usiangaliwe kwamba unatokana nachama gani au unatokana na nani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile niseme kwamba ni kwelikaribu 50% ya fedha za maendeleo zinazokwenda kwenyeHalmashauri haziendi kwenye miradi ambayo imekusudiwa.Sasa basi, nasema hili kwa sababu haya yanatokana nabaadhi ya Madiwani wetu na hata Wakurugenzi wao, baadhiyao hawana uelewa wa masuala ya fedha. Naomba kwanguvu zote kwamba suala hili lifuatiliwe ili liweze kupatiwaufumbuzi unaofaa ili fedha za wananchi zisipotee ovyo.

Mheshimiwa Spika, lingine ni Serikali kutumia zaidifedha kuliko kuzalisha. Hili la kutumia fedha zaidi kulikokuzalisha ndilo linalopelekea Serikali yetu kutegemea zaidiwafadhili na wahisani kuliko fedha za ndani. Naiomba Serikaliyetu tamko lake ililolitoa mwaka jana kwamba watapunguzamatumizi l itekelezwe kwa sababu kama tamko li lehalikufuatwa na leo tukasema kama fedha hizi tunazipelekakwenye OC, bado tutakuwa tunarudi kulekule nyumaambako tuliisema kama fedha hizi hazitatumika.

Mheshimiwa Spika, la mwisho, niseme kila mfanyakaziajue kuwa ni mstaafu mtarajiwa na kama kila mfanyakazi nimstaafu mtarajiwa, sote humu miongoni mwetu baadaye

Page 130: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

130

tutakuwa wastaafu. Kuna baadhi ya Wabunge au wotewanapostaafu, akitimiza miezi mitatu utafikiria ni mzee wamiaka mia moja na hamsini. (Kicheko)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Haya ahsante. (Kicheko)

MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO: Mheshimiwa Spika,sikumaliza lakini nitapeleka kwa maandishi.

SPIKA: Ahsante. Nil ikuwa nashangaa Mbungeanakuwa mstaafu au ameanguka sasa ndio na mwenyeweanaitwa mstaafu? Mheshimiwa Devotha Likokola atafutiwana Mheshimiwa Mansoor.

MHE. DEVOTHA M. LIKOKOLA: Mheshimiwa Spika,ahsante. Niungane na Wabunge wenzangu kumpongezaWaziri na Watendaji wa Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, tumeona Wizara hii imeendeleakujitahidi katika kutekeleza majukumu yake na hasahasakutuletea sera za kuangalia uchumi wetu lakini vilevile seraza kuangalia sekta ya fedha.

Mheshimiwa Spika, katika kuangalia masuala mazimaya uchumi wetu, naomba kuishauri Serikali na kuisisitizakwamba bado wananchi hawajaridhika na hali halisi yauchumi. Wananchi wetu bado wana hali ngumu ya uchumina kwa maana hii Serikali inatakiwa iangalie ni kwa niniwananchi hawa wanahangaika katika kukuza uchumi wao.Hali ya umaskini bado ipo na kwa maana hiyo, ni lazimaSerikali ionyeshe dhamira ya dhati ya kuondoa umaskini wawananchi wake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nampongeza Waziri ametuambiakwamba katika kuangalia masuala mazima ya sekta yafedha, tutakuwa na idara ya kuendeleza sekta ya fedhanchini lakini ahadi hii Mheshimiwa Waziri alishaitoa tangu

Page 131: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

131

mwaka jana. Tungependa kusikia leo, utekelezaji wakeumefikia wapi, Idara hiyo imeshaundwa, Mkuu wa Idara hiyoni nani na nini kimefanyika kwenye hiyo Idara? Haiwezekanitukaendelea na ahadi mwaka hadi mwaka.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana tuliishauri Serikaliishirikiane sana na taasisi ya TAMFI katika kuendeleza sekyaya fedha. Napenda kujua, wameshirikiana katika maeneogani na kumekuwa na mafanikio gani katika kuendelezasekta ya fedha. Pia napenda kujua Mheshimiwa Waziri naWizara hii ina dhamira gani ya kuwatoa wananchi ambaowanatumia huduma rasmi za kifedha kutoka asilimia ngapikwenda asilimia ngapi kwa mwaka huu ili tuendane natakwimu na tuweze kuhoji kiukamilifu.

Mheshimiwa Spika, bado tunamwomba Waziri,mwaka jana aliahidi mwaka huu angeleta Sheria yaMicrofinance lakini hajaleta bado. Tunaomba afanye haraka.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna suala zima la communitybank, nashindwa kuelewa, Serikali haizipendi communitybank au wananchi hawapendi community bank kwa sababugani wananchi wamehangaika. Ukiangalia humu ndaniWabunge ndiyo wamekuwa ma-promoter wa communitybank, Wabunge ndiyo wanahamasisha SACCOS, Wabungendiyo wanahamasisha vikundi vya kuweka na kukopa, hii nikazi ya Wabunge? Ni nini role ya Serikali katika ku-promotecommunity bank na ime-promote community bank ngapikipindi cha mwaka jana mpaka mwaka huu. Hii ni aibu.Haiwezekani Waheshimiwa Wabunge wanahangaikakwenda kutafuta vibali vya community bank na katika hayaninayosema nina ushahidi. Waheshimiwa Wabungewamekuwa wakihangaika na wananchi wao katikakuwatengenezea mifumo ya fedha, haiwezekani, naombaSerikali mchukue jukumu lenu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nizungumzie benki zabiashara, nashukuru zimetoa mikopo kwa wafanyabiasharawakubwa, wamefanya kazi nzuri lakini bado kuna

Page 132: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

132

changamoto. Masharti ya kufungua akaunti katika beni hizini magumu sana na wananchi wanahangaika sana lakinibado kuna foleni kubwa sana kwenye benki hizi! Hivi ni ninikifanyike ili wananchi waweze kupata huduma kwa urahisikatika benki hizi? Inapofika mwisho wa mwezi kwenye Wilayazetu ukienda kwenye benki utaona huruma, haiwezekanijamani! Hawa wananchi wa Tanzania tayari wana miakahamsini ya uhuru, hawawezi wakakaa kwenye foleni kamamiaka ya zamani lazima tuendane na sayansi na teknolojia.

Mheshimiwa Spika, naomba nizungumzie benki yaTwiga. Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri mwaka janaaliisaidia benki hii lakini tunataka aongeze msaada wake kwasababu benki hii sasa imekuwa ni mkombozi mkubwa sanana imesaidia sana vikundi na wananchi wa ngazi ya chini.Tunaomba benki hii ifanye huduma zake kama benkinyingine. Ni benki ambayo inaweza kusaidia sana kwasababu kwanza ni benki ya Serikali na ili ionyeshe mfanowapeni nguvu. Ukienda kwenye benki i le na miminawahamasisha hata Wabunge waende kwenye benki ilehuduma ni nzuri sana lakini bado hawana nguvu ya kutosha.Aidha, nafurahi kwamba Serikali pia imeangalia benki yaPosta na naomba mipango hiyo iendelee.

Mheshimiwa Spika, bado naomba kuzungumzia sualala rural financial strategy. Mimi sielewi strategy hii iko wapi nanani anai-hold maana yake siku zote tunaambiwa kunamkakati wa kuendeleza masuala ya fedha kwa wananchihususan vijijini, huo mkakati mbona hauonekani, mbonahautekelezeki? Tunaomba kwa kweli tujitahidi.

Mheshimiwa Spika, BOT. Pamoja na kwambaukimwangalia Mheshimiwa Gavana Ndulu, ana nia ya dhatiya kuendeleza masuala ya housing microfinance, masualaya financial literacy lakini speed imekuwa ndogo. NaombaBenki Kuu iongeze speed yake kwa sababu huduma za fedhabado ni tatizo kubwa nchini.

Mheshimiwa Spika, tuna suala zima la TRA, wanafanyakazi nzuri lakini bado kwa kipindi hiki kumekuwa na

Page 133: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

133

malalamiko makubwa sana hasa kwa wananchi wanaotoamizigo yao bandarini. Kumekuwa na tatizo la system, maramtandao, mara nini na wananchi wengi mizigo imebakibandarini na kwa maana hiyo ukienda madukani sasa hivibei zimepanda na mbaya zaidi wafanyabiashara wetuwamechanganyikiwa. Wale wafanyabiashara wanafanyazile biashara kwa kuchukua mikopo na kwa maana hiyoukiwacheleweshea muda wao wa kutoa mizigo bandarini,wanaongezewa riba, charges mbalimbali, kwa hiyo,tunawachanganya wafanyabiashara wetu.Wafanyabiashara wa nchi hii wakichanganyikiwa, kodihaitapatikana, pesa haitapatikana na Serikali itakujakuchanganyikiwa, haiwezekani, ni lazima wafanyabiasharawetu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wamzungumzaji)

MHE. DEVOTHA M. LIKOKOLA: Mheshimiwa Spika…

SPIKA: Ahsante.

MHE. DEVOTHA M. LIKOKOLA: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Mansoor.

MHE. MANSOOR S. HIRAN: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi na mimi nichangie hoja hii.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, naombanimpongeze Waziri na Manaibu wake kwa kazi nzuriwanayofanya na watendaji wake wote. Pia nichukue nafasihii kumpongeza Kamishna wa TRA kwa kazi nzuri anayofanyana timu yake.

Mheshimiwa Spika, nitazungumzia mambomachache yafuatayo. Kwanza, ni deni la Taifa. Nimeonakwenye kitabu cha Wizara, wamelenga sana kulipa madeniya nje tu, madeni ya ndani naona kama hawayatambui

Page 134: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

134

kabisa. Madeni ya ndani ni mengi, yako ya Walimu, wazeewastaafu, Halmashauri zinadaiwa madeni makubwa,naomba wajipange kuyalipa madeni hayo. Naombaniikumbushe Wizara kwamba hawa watu wa ndaniwanaotudai ndiyo watu waliotupa kura za kuja huku. Kwahiyo, naomba hizo kura tusiziharibu, tunataka kurudi tena.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nijielekeze tena kwenyeSheria ya Manunuzi. Sheria hii inapandisha bei ya bidhaazinazonunuliwa na Halmashauri zetu kwa kiasi kikubwa. Miminashauri Wizara itoe bei elekezi ya vifaa muhimu ambavyovinanunuliwa na Halmashauri zote kwa mfano simenti, nondona kadhalika. EWURA wanatoa bei elekezi ya mafuta, naowangeanzisha kitu kama hicho, itatusaidia kupunguzagharama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, TANESCO. Wizara hii imetoa ruzukuya mabilioni ya fedha kwa ajili ya kuendesha mitambo yaTANESCO na kununua mafuta mazito. Naomba Wizara itoetaarifa rasmi Bungeni, imetumia shilingi ngapi nje ya bajetiiliyopitishwa na Bunge hili mwaka huu? Pia nimeona kwenyebajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ya mwaka kesho, fedhawalizoziomba hazitoshi, kwa hiyo, mwaka kesho piawamepanga kutumia fedha nje ya taratibu ya kupitishwana Bunge. Naomba Waziri atupe maelezo kuhusu masualahaya.

Mheshimiwa Spika, manunuzi ya magari. Kila Wizara,Idara na Taasisi hununua magari kivyake bila kuwa na centralsystem ya kulinganisha bei. Pia kwenye manunuzi ya magariwanaingia kwenye mtego wa kupata warranty ya miakamitatu mpaka mitano, sasa wale wauzaji wa magariwanapata faida kwenye vipuli vya kuuza kwa miaka mitatumpaka mitano. Unaweza ukanunua gari kwa Sh.200,000,000/= lakini matunzo ya gari lile kwa miaka mitano inakuwaSh.600,000,000/= mpaka Sh.800,000,000/= kwa sababu miakaile mitano ya warranty wale watu hawana masharti, wanauzavipuli kwa bei wanayotaka wao. Mimi nashauri Serikaliinaponunua magari pia iongee na wale wauzaji wa magari

Page 135: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

135

watoe orodha ya vipuli vitakavyohitajika kwenye miakamitatu ya warranty na bei zake, washindaniwe pia kwenyebei zile za vipuli ili ujue gari lile moja litakugharimia shilingingapi kwenye miaka minne ijayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, China Tanzania Logistic Centre,huu mradi ulioletwa na Wizara ya Viwanda na Biasharaandiko tumelipata kutoka kwa EPZ ambalo linazungumziamambo mazuri sana. Mimi nashauri Wizara ya Fedha, ifanyeuchambuzi wa kina kuhakikisha kwamba hiyo China TanzaniaLogistic Centre haitaathiri viwanda vyetu vya ndani nahaitaathiri mapato ya nchi. Pia kuna sentensi mojawameweka kwenye hilo andiko ambayo mimi sielewi vizuriningeomba Wizara inieleweshe, wanasema kwamba huomradi utatoa ajira ya moja kwa moja ya zaidi ya watu 25,000.Sasa mimi nashangaa kwenye hekari 60, ajira ya watu 25,000zitatoka wapi, naomba andiko la kina liletwe ili tuwezekufahamu vizuri.

Mheshimiwa Spika, naunga hoja, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Nashukuru kwa kuniokolea muda ili niwezekutangaza yafuatayo:-

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwandana Biashara, Mheshimiwa Mahmoud Mgimwa, anaombaniwatangazie wajumbe wa Kamati yake kwamba mchanahuu watakuwa na kikao katika ukumbi namba 227.

Tangazo lingine, nadhani watalitawanya maanawengi wameondoka, kwa miaka mingi tumekuwa nautaratibu wa kutembelewa na Wabunge wa Mabungemengine na sisi pia tuna utaratibu wa kutembelea Mabungeya wenzetu. Wabunge wachache wanaweza wakajiwekapamoja wakawa rafiki wa Bunge lingine lakini utaratibuhaujawekwa vizuri, tunaendelea kuratibu hilo.

Tuna urafiki kati ya Wabunge wa Bunge la Uingereza,The House of Commons na sisi na kwa utaratibu ule ndiyoiliyosaidia hata kufuatilia zile fedha za rada. Mhimizo ulitokana

Page 136: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

136

na Wabunge wanachama hapa na Wabunge waWanachama House of Commons. Kwa hiyo, walewakaishinikiza Serikali yao mpaka tukarudishiwa zile fedha.

Juzi mimi nilipata mwaliko wa kwenda kushiriki kwenyeBunge la Oman, kwa sababu nilikuwa na shughuli nyingineakaenda Naibu Spika na mwisho wa mwezi huu, Spika waOman anakuja hapa. Moja ya kitu ambacho walikubalianaalipokuwa kule, kuundwe urafiki wa Wabunge wa Bunge laTanzania na wale wenzetu wa Oman. Kwa hiyo, wale ambaowangependa kuwa katika kikundi hicho cha urafiki naWabunge wa Oman, leo hii kutakuwa na kikao, nafikiri ukumbiwa Msekwa, ukumbi wa Msekwa inaelekea kuna mikutanomingi, mtajua huko huko, naomba mkitoka hapa muendekule ambapo huko mtaelekezwa mambo mengi zaidi.Tutaorodhesha na nchi nyingine ambazo zinatafuta urafikihuo ili na sisi tuwe na vikundi vya namna hiyo.

Hivyo hivyo kuna vyama vingi vya Wabungevinaanzishwa hapa, hivi sasa kuna Chama kinginewanaanzisha karibuni, hakija-take root, kinaitwa Chama chaWabunge wenye Kupambana na Magonjwa yaKuambukizwa, watatoa maelezo yao. Vyama hivivinatambulika katika Mabunge yote, ni vyama visivyo vyaSerikali, ni kama NGO’s lakini za Bunge.

Kwa leo, naomba wale wanaotaka kuwa na urafikina Wabunge wa Oman waende katika ukumbi wa Msekwa,watawakuta wataalam pale watawaelekeza.

Sina matangazo ya ziada, nasitisha shughuli za Bungempaka saa kumi na moja.

(Saa 7.00 Mchana Bunge lilisitishwa mpaka Saa 11.00 Jioni)

(Saa 11.00 Jioni Bunge lilirudia)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, wale wote ambaowalikuwa wanastahil i kupata nafasi ya kuchangia,walimalizika asubuhi. Kwa hiyo, kwa sasa nitaanza kuwaita

Page 137: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

137

wasaidizi wa mtoa hoja. Nitaanza na Naibu Waziri, ni revenueor what, ni dakika ishirini ishirini, Waziri ni dakika arobaini.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYA SALUM):Mheshimiwa Spika, ahsante. Nakushukuru kwa kunipa fursahii. Aidha, naomba kuchukua fursa hii kumshukuru MwenyeziMungu, Subhanah Wataala ambaye ametuwezesha jioni hiiya leo kukutana tena katika kukamilisha ungwe yetu hii.

Mheshimiwa Spika, kabla sijasema chochote,naomba kuunga mkono hoja iliyotolewa hapa na Waziri waFedha na vilevile naomba kuwashukuru Wabunge woteambao wamechangia hoja hii. Napenda kuwataarifukwamba kutokana na muda, sote kwa pamoja hatutawezakujibu hoja zote ambazo zimetolewa lakini tutajitahidi kujibukadri inavyowezekana na nyingine tutajibu kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kujibu hojaambazo zilitolewa na Mheshimiwa Devotha Likokola. Hojazake zote zilikuwa za msingi sana na kama mwanamkemwenzangu, nampongeza sana kwa kuweza kuteteawanawake kujiwezesha kiuchumi, kupitia VICOBA. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza lilikuwa, ni vipiSerikali inashirikiana TAMFI. Kwanza napenda kumwambia,kama tulivyokuwa tumetoa miadi katika Bunge lililopitakwamba Wizara ya Fedha itaanzisha Idara ya Microfinanceambayo pamoja na mambo mengine sasa itaanzakushughulikia hivi vikundi vidogovidogo mfano SACCOSpamoja na VICOBA, vyenyewe kwa mfano kama VICOBAvinajiona havina mahali pa kukaa particularly, lakinitunasema sisi Wizara ya Fedha sasa tunaanzisha hiyo Idarana muundo upo katika hatua za mwisho kukamilika. Kwa hiyo,ni taratibu tu ambazo tunakamilisha na mwanzoni mwamwaka wa fedha 2013/2014, Idara hii itakuwa iko tayari paleWizara ya Fedha. Kwa hiyo, tuwataarifu tu akina mamaambao wako kwenye VICOBA, mama yao atakuwepo palena sisi sote tutakuwa tunashirikiana katika kuhakikishakwamba kuna mazingira mazuri ya VICOBA kuwezakuendelea. (Makofi)

Page 138: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

138

Mheshimiwa Spika, alikuja na swali lingine kuhusutakwimu za watumiaji fedha nchini. Sisi kama Serikalitunaelewa na tunapata machungu sana kuona kwambakwa jitihada ambazo tunaweka, maana kama tunawekapolicies nzuri, tunaweka sheria nzuri kushajihisha communitybanks, commercial banks ziweze ku-enshrine nchi yetu, targethasa ni yule mwananchi wa kawaida. Hata hivyo, kutokanana mazingira yenyewe ya kibiashara, kutokana nacomplicated system za finances, bado kabisa jamii kubwaya Watanzania haikuweza kuwa captured katika formalfinancial system. Kutokana na ripoti ya FINCOP inatuambiakwamba, only 12% ndiyo wapo kwanza katika mfumo rasmiwa kibenki. This is real very small amount lakini 4.3% ndiyoambao wako kwenye hizi microfinance ambazo ziko rasmiparticularly lakini 27% only ndiyo wako katika asasi ambazoziko rasmi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, utaona jamii iliyo maskiniambayo inataka kujikwamua kutoka katika umaskini, asilimia56% haina access na hizi financial institutions. This is realdepressing ukilinganisha na jitihada nyingi sana ambazozimefanyika, tunaweka mikakati madhubuti kuhakikishakwamba wananchi wanakuwa na hizi huduma za kibenki.Tunakotaka twende sasa, coming 2015, tunaweka sasamikakati madhubuti kwa kushirikiana na wewe MheshimiwaMbunge na Waheshimiwa Wabunge wote, target yetu sisikama Serikali tufikie 50%. Kwa hiyo, tushirikiane sote kwapamoja maana hii siyo kazi ya Serikali, Serikali ni structure,lakini sisi sote tunajukumu hili la kusajihisha sasa watu wawewanapata hizi financial access, lengo, waweze kujikwamuakiuchumi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Likokola, tunakwendakwenye 50% by 2015 na hii inakwenda sambamba nakuwawezesha wanawake, maana inategemea na hudumanzuri za kijamii. Kama hujajenga barabara nzuri, mwanamkeakatoka akafanya biashara yake, we can not reach there.Kama hujaweka miundombinu mizuri ya maji, mwanamkeawe na access na clean and safe water ili muda wakemwingine aweze kufanya vitu vingine, we can not reachthere. Kwa hiyo, hii yote inategemea sana na kuimarishwa

Page 139: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

139

kwa sekta nyingine lakini hiyo ni ndio Sera ya Serikali hiiambayo inaongozwa na CCM. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aidha, kuna issue ya communitybanks, zipo lakini bado, hii ndio sasa tunaweza tuka-link naile small percentage ya watu bado hawajawa na access yafinance. Ni role ya Serikali in one part lakini MheshimiwaMbunge, Waheshimiwa Wabunge, tusaidiane kwa pamoja,ku-promote community banks, whatever it takes, Serikalitumeweka miundombinu lakini tusaidiane sote kwa pamojasasa kuhakikisha kwamba community banks zinafanya kazi.Ni role ya Serikali kuweka policies, kuweka sheria, kuwezeshacommunity banks ku-enshrine. Vilevile hili jambo sasa la ku-promote community banks, ni letu sote sisi kama Serikali lakinipamoja na Waheshimiwa Wabunge. Nakuomba MheshimiwaLikokola, kwa vile umekuwa mstari wa mbele, maana mpakaunajulikana kama mama VICOBA, kama vile tunavyokuitamama VICOBA, basi ushirikiane na sisi kuhakikisha kwambatuna-promote community banks. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ilikuwa ni benki zabiashara, kweli hili limejitokeza, benki za biashara ziko mbalisana na mwananchi wa kawaida. Hili tunaliona na kwa vilehuko tunakokwenda tunataka kila mtu aingie, basitutahakikisha kwamba benki za biasahara nazo zinafanyaliwezekanalo kuhakikisha kwamba mwananchi wa kawaidaanapata mkopo, tena kwa masharti ya kawaida. Nalo hilitutashirikiana na sekta nyingine, kwa sababu benki yabiashara, kwa sababu na wao wanafanyabiashara, kamaunakwenda huna zile credible documents, kidogo wanaanzakuingia wasiwasi, anahangaika, mwananchi mwinginemwenyewe anahangaika, simply kwa sababu kuna vituvingine ambavyo vinakosekana. Tuwashajihishe wananchiwajitokeze kupata vitambulisho kwa sababu kina advantagenyingi including hii ya kupata fedha. Kwa hiyo, hili haliji pekeyake, tunaweza tukaweka miundombinu, pengine interestrates zikashuka, lakini kwa sababu kama mwananchimwenyewe hana details, hana identity, hii benki ya biasharakama inavyoitwa inakuwa haina confidence ya kuweza

Page 140: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

140

kumkopesha huyu mwananchi. Hili nalo liwe linafanyiwa kazina ninyi Wabunge pamoja na sekta nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mambo yalikuwa mengi, labdaniondoke hapo, niende kwenye hoja ya Mheshimiwa Rajab.Yeye alileta kwa maandishi lakini bado hoja zake zilikuwazina msingi na amenitishia hapa kwamba anaweza akazuiamshahara wa Waziri. Kwa upande wake yeye aliona kwambaPemba ASYCUDA++ haifanyi kazi, I do know for how long,lakini takwimu nilizokuwa nazo mimi ASYCUDA++ Pembainafanya kazi. Tatizo lipo na siyo kwa Pemba tu, tatizo lipokwa mfumo huu wa ASYCUDA++ kutokana na network.Sometimes inawezekana biashara inakwenda lakini networkiko chini sana. Kwa hiyo, hilo lipo, inawezekana Mheshimiwawakati unatembeatembea, wakati uko huko Jimboni nakwingineko, timing ilikuwa ndiyo hiyo. Hapa ninazo dataambazo tumefanya transaction kule Pemba, kwa Machi 2013,kulikuwa na transactions tano na hizi zote zimefanyika kwakutumia hii ASYCUDA++ lakini Aprili kulikuwa na transactionnne, ofcourse kutokana na mfumo mzima wa biasharaPemba hauko active kuliko Unguja au kulinganisha na Dares salaam. Hata Juni hii, sasa hivi tumeweza kufanyatransaction moja kwa kutumia ASYCUDA++. Kwa hiyo, natakanikupe confidence Mheshimiwa Mbunge kwambaASYCUDA++ inafanya kazi Pemba isipokuwa kuna matatizoya mtandao. Hili tunalirekebisha kwa sababu tunachotakasisi wafanya biashara wawe wanapata access kwaniultimately ndiyo Serikali anapata mapato, kwa hiyo, tunatakakila kitu kiende sawa lakini sisi tutalichukua na tutalifanyia kazi.Kimsingi linafanyika, ni techinichal problems. Tunachokifanyasasa kupitia TRA wameagiza ku- increase ile bandwithambayo pengine tu sometimes transactions zinakuwa kubwana zile system haziwezi kubeba.

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine na ambayoimetolewa na wengi ni kuhusiana na shughuli za CHC. Kamasote tunavyojua Azimio la kukamilisha shughuliza za CHC niAzimio la Bunge, ni mpaka Juni 2014. Baada ya hapo, Ofisiya Msajili wa Hazina, itachukua kazi ambazo zitakuwazimebakia. Hata hivyo, nalo hili lilikuwa linakwenda pamoja

Page 141: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

141

na kuimarishwa kwa Ofisi ya Msajili wa Hazina. Naombakuchukua fursa hii, kuwafahamisha kwamba Msajili wa Hazinaili aweze kufanya kazi zake kwa nafasi, kwanza,tumerekebisha Sheria mwaka 2010, lakini lingine ni kwambatumemtoa katika lile jengo letu la Wizara na tumempelekakatika jengo la CHC na awe anafanya kazi zake kule comingJuly first. Hiyo itategemea Waheshimiwa Wabunge pia,tupitishe bajeti hii ili kumwezesha sasa Msajiri wa Hazina awezekufanya kazi zake kama zinavyostahiki.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, organization structurepia tayari imeshakamilika chini ya mamlaka husika (PIC) lakinimuundo nao vilevile umewekwa kwa ajili ya kuhudumiamasuala ya urekebishaji na ubinafsishaji wa mashirika yaumma, kazi ambayo imekuwa ikifanywa na CHC lakinimuundo sasa wa TR umewekwa in such a way kuwezakufanya kazi hizo. Vilevile katika TR ndani yake kuna kitengohicho cha kushughulikia uperembaji wa mashirika ambayoyamebinafsishwa, uperembaji maana yake ni monitoring andevaluation. Tumepata jengo hilo kama nilivyokuarifuni, Wizarasasa inakamilisha zile taratibu za kuchukua baadhi yawatumishi na kuwapeleka kule. Kwa hiyo, hivi ndivyoambavyo Serikali imeweza ku-strengthen capacity ya TR kwasasa hivi, kuweza kufanya kazi zake kama ambavyo inatakiwalakini vilevile kujitayarisha kwa ajili ya kuchukua kazi ambazozitakuwa zimeachwa na CHC wakati muda wakeutakapokuwa umekamilika. Kwa hiyo, tunajitahidi,nawaomba tu Waheshimiwa Wabunge kwamba mtupitishiebajeti yetu hii ili sasa kuweza kufanya kazi zetu kamainavyotakiwa.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa kuna suala jingine,ambalo limetolewa na Mheshimiwa Said Mussa Zuber. Yeyekwa maoni yake, anasema kwamba hii speed ya Big ResultNow, aliita PEMANDU, initiative yetu sisi kama Tanzaniatumesema Big Result Now (BRN), hakuna kusuasua. Natakakumhakikishia kwamba tumeji-commit, tuna-determine,tutafanya kazi. Big Result Now kuna initiative nyingi, kunainnovation nyingi kule zimetokea katika sekta ambazotumezipa priority mfano kilimo, elimu, maji hata resource

Page 142: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

142

mobilization. Kwa hiyo, Big Results Now haijaja tu yenyewekimyakimya, labda kama ndiyo sawasawa na mikakatimingine, imekuja pamoja na kuangalia mapato zaidi, wapitutapata kwa ajili ya kutekeleza yale ambayo tunayawekakule. Siyo hivyo tu, uzuri wa Big Result Now, inaanishaimplementation time frame, nani atafanya hii kazi na mwakagani itakuwa imekamilika. Kwa hiyo, hii ni initiative nzuri, tui-support na kuna baadhi ya Mawaziri hapa tayaritumeshasaini hata zile performance contract na kila Waziriameshaji-commit kwamba hiki ndicho ambacho kitafikiwakwa muda ambao umewekwa kutokana na ile mipango kazi.

Mheshimiwa Spika, kuna issue nyingine yaMheshimiwa Zuber kuhusiana na tawi la NMB Zanzibar, hilitumeliona. Mimi mwenyewe at one point in time nilikuwa NMBpale, hali ilikuwa mbaya yaani utaweza ukafananisha paleNMB Zanzibar kama uko Muhimbili, watu wamelala chini, watuwengine wapo mpaka saa saba usiku wanakuambiawanasubiri kuchukua mishahara yao. Nataka kumhakikishiaMheshimiwa Zuber pamoja na Waheshimiwa Wabungetutalifuatilia kwa sababu mimi mwenyewe nimeliona,tutahakikisha kwamba kunafunguliwa matawi mengine paleZanzibar, hali ni mbaya. Mimi binafsi nimekwenda, nimetokamachozi kuona mtu anasubiri pesa yake mwenyewe lakiniunam-intimidate kiasi gani? It was real very bad, that scenewas very bad, kwa hiyo, hili tutalifuatilia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna issue ya hawa ambaowamefungiwa leseni, kesi zimekuja kwetu sisi na ukiwasikilizaTRA they have a point, ukisikiliza na hawa wengine, they havea point, lakini kikubwa hapa mimi nachotaka kuwaambiahawa watu wa clearing and forwarding agents kwambahukumu zilizotolewa za kufungiwa kama wana maelezo zaidina kutokana na wengine ambao tumezungumza nao wanamaelezo zaidi, basi wafanye appeal katika hii Tax AppealBoard, sisi kama Wizara ya Fedha tutawafahamisha hao TRAor whoever wakitaka maelezo zaidi lakini waende waka-appeal. Kama itaonekana kwamba hawana makosa, ninaimani kwamba hizi kazi zao zitafunguliwa maana TRAwanataka mapato, tunabanwa hapa ndani tunataka

Page 143: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

143

mapato. Kwa hiyo, the only thing ni hao watu kufanyabiashara lakini niwahakikishie kwamba hata wakufungulia,kutakuwa na tight management kuhakikisha hata hizobiashara wanazozifanya zitakuwa zinafanywa katika uangalizimkubwa.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na Sheria na Sera zaMicrofinance, wengi wameelezea hapa, bado hazijawatayari. Tunawahakikishia Waheshimiwa Wabunge kwambaSera ya Microfinance iko katika hatua za kukamilika chini yaBOT na hii tutaifanya agency kwa sababu microfinanceinstitution nyingi ndipo wananchi wengi wa kawaidawanapoponea. Tukienda kwenye commercial bank, hatuingiihapo, kwa hiyo, nadhani hili ni jambo ambalo tutalifanyaharaka kuangalia hasa wananchi nao wanapata financialinclusion.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa kuna suala linginekuhusiana na wananchi wa kawaida kutoelewa faida yaCapital Market and Security Authority ama Dar es SalaamStock Exchange, wengi hawaelewi, ni kweli hatukatai, lakinisisi hili tunalichukua kama Wizara ya Fedha kuhakikishakwamba elimu inatolewa kupitia vyombo vya habari tenakwa lugha nyepesi kabisa ambapo mwananchi anawezaakaelewa kwa sababu wako wananchi wana pesa lakinihawajui…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYA SALUM):Mheshimiwa Spika, kutokana na muda, naomba kuungamkono hoja na nashukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Nimwite sasa Mheshimiwa NaibuWaziri mwingine, nikisema aliyemaliza wa kwanza weweutakuwa wa pili, sasa niseme mwingine tu, karibu. (Kicheko)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. JANET Z. MBENE):Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda kukushukuru kwa

Page 144: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

144

kunipa nafasi hii kuchangia hoja iliyowasilishwa na Waziri waFedha, Mheshimiwa Dkt. William Mgimwa, napenda kuungamkono hoja hii kwa asilimia 100. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kabla sijaanza kuchangia,napenda na mimi vilevile kutoa shukrani zangu kwaWaheshimiwa Wabunge, kwa maoni yao, nasaha namaelekezo waliyotupatia wakati wa kuchangia. Napendavilevile kuwashukuru kwa miongozo mingi ambayo imetolewana kwa kweli tumeiona kuwa itakuja kutusaidia katikakuboresha shughuli zote zinazoendana na Wizara yetu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hivyo, napendakuchangia maeneo machache kwa sababu mudahautaruhusu, nitaomba yale ambayo tutashindwa kuyajibusasa hivi, tutayajibu kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, nianze vilevile na mimi kwa sualazima la mashirika yaliyobinafsishwa/ kuorodheshwa katikasoko la mitaji. Mashirika yaliyobinafsishwa/kuorodheshwakwenye soko la mitaji ili kuongeza ufanisi wa kodi na masualamengine yote yanayoendana na uwekezaji wa aina hii, nikweli yapo mashirika mengi ambayo mpaka sasa hivi tayariyameshaorodheshwa katika soko la mitaji. Kuna yale ambayobado na ambayo Serikali ina hisa zake, uamuzi wetu ni kuwasisi kama Serikali kwanza, tutamalizia kanuni zinazohitajika kwaajili kuwezesha zoezi hili kufanyika halafu sisi tutatoa mfanokwa kupeleka zile hisa zetu sisi Serikalini kwenye soko la mitaji.Naamini hiyo itachochea na wengine kufanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja ya kuwa kwa nini uchumi waTanzania haupunguzi umaskini pamoja na kuwa unakuwa,jibu lake kwa kweli, ni kuwa uchumi wa Tanzania umekuwaukikua kwa wastani, lakini pamoja na hayo inaonekana kuwakiwango cha umaskini hakijashuka vya kutosha, japokinashuka. Tathmini zinaonyesha kuwa tatizo kubwa liko katikavijiji na sehemu ambazo wako watu wengi ambao ndiyotunategemea umaskini huu uondolewe kwa haraka zaidi. Hiiyote ni kutokana na miundombinu na taasisi nyingi badohatujaweza kuzifikisha kule. Hii haina maana kuwa Serikali

Page 145: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

145

haijataka kufanya hivyo kwa sababu tunaelewa wazi maananzima ya kuondoa umaskini kwa Watanzania wengi ambaowako vijijini na hii itakuwa ndiyo njia pekee ya kufanya nchiyetu ifikie lengo la kuwa nchi ya mapato ya wastani mwaka2025. Suala lingine ni kuhakikisha kuwa elimu ya kujitegemeakatika masuala ya ujasiriamali, ufundi ambavyo vitawezeshawananchi wengi zaidi kujitegemea kwa kujiajiri katika sektambalimbali hasa kilimo, zitaendelea kutolewa kwa bidii zaidiikiambatana na uwezeshwaji wa mitaji ambayo tumetokakulizunguza sasa hivi, ikiambatana na utoaji wa pembejeombalimbali na vitu mbalimbali vitakavyowezesha wananchiwengi zaidi kujiajiri.

Mheshimiwa Spika, suala la mifuko sikutaka kuliingiliasana kwa sababu Mheshimiwa Saada amelizungumzia lakinilabda nije kwenye suala lingine lililozungumzwa kuhusianana masuala ya Mifuko ya Hifadhi kuwa kwa nini na yenyewehaijiorodheshi au haitangazi kwenye magazeti na vyombovya habari taarifa za uendeshaji wao. Nilitaka kuwafahamishaWaheshimiwa Wabunge kuwa mfumo wa Mifuko ya Hifadhini tofauti na mabenki, kwani Mifuko haitengenezi faida baliinatengeneza ziada ya kulipa mafao ya wanachama wao.Hivyo bila kuwa na mfumo wianifu katika Mifuko yote,hatutaweza kuwawekea taratibu za kutangaza kwa sababukwanza inaweza ikapeleka message tofauti kwa wananchiwasipoweza kuelewa kwa nini Mfuko huu unaoneysha hivina mwingine unaonyesha hivi. Vilevile sheria iliyotengnezaMifuko hii, haiwawajibishi Mifuko kutoa taarifa kama mabenkiyafanyavyo kwa kila quarter. Kwa sababu gani? Mfuko hataungeweza kutoa taarifa kwa kila quarter, isingekuwa tofautikubwa sana, kwa sababu Mifuko inaenda kwa umri wawachangiaji, sasa quarter moja na quarter nyingine badomwaka ni uleule. Kwa hiyo, bado taarifa utakazozipata palehazitasaidia sana kuonyesha tofauti.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa kuna hoja kwamba kwanini Mifuko ya PSPF na PPF isiwekeze katika maeneo ambayoyanazalisha ajira kama vile reli na bandari. Kuwekeza katikareli na bandari kwa Mifuko inawezekana au isiwezekanekufuatana na jinsi gani uwekezaji huo utaleta faida kwa

Page 146: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

146

Mifuko. Ikumbukwe kuwa Mifuko ni fedha ambayoimewekwa pale kwa ajili ya kuja kulipa mafao. Uwekezajikatika reli na bandari, inaweza ikachukua muda mrefu sanakiasi kwamba ikaathiri ulipwaji wa mafao. Hata hivyo, hiihaizuii kwa Mifuko kama vile PSPF na PPF, kuangalia nakutathmini kama inawezekana kuwekeza katika sekta hizo.Vilevile kama mnavyojua kuwa Mifuko hii tayari inawekezakatika sekta nyingine nyingi ambazo zinazalisha ajira,zinazalisha faida ambayo inawezesha kulipa mafao kwawanachama wao.

Mheshimiwa Spika, nataka kulifahamisha Bunge lakoTukufu kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi yaJamii yaani SSRA, kwa kushirikiana na Benki ya Tanzania, tayariimetoa miongozo ya uwekezaji tangu mwaka 2012, ambayoimezingatia maeneo yenye tija kwa wanachama wake kwamanufaa ya kiuchumi na hii ikiwa ni pamoja na kutengenezaajira. Kwa hiyo, kuna miongozo maalum ambayo inawasaidiahata wao wenye Mifuko kutambua ni maeneo gani ambayoni salama zaidi kwao kuwekeza.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa kuna suala vilevilekwamba fao la elimu liwe katika Mifuko yote kama lilivyo PPF.Vilevile kulikuwa kuna suala lililofuatana na hilo, juu ya fedhaza wanahisa wa NICOL, je, ziko salama? Napenda kujibu hilikuwa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya Dhamana imechukuahatua mbalimbali kulinda maslahi ya wawakezaji waKampuni ya NICOL, ikiwa ni pamoja na kuzuia kuuza hisaambazo Kampuni ya NICOL imewekeza NMB baada yakubaini kuwa fedha ambazo zingepatikana zingewekezwakatika maeneo ambayo yanayohatarisha maslahi yawanahisa. Kwa hali hii, tayari inaonyesha kuwa fedha hizi zikosalama. Mali ya wanahisa katika Kampuni ya NICOL, zikosalama na kwa hisa za NMB peke yake thamani ya hisaimekua kutoka shilingi bilioni 4.6 tangu mwaka 2005 na kuwashilingi bilioni 52 kufikia Juni, 2013. Hili ni ongezeko kubwaambalo linaonyesha wazi kuwa amana hizo ziko salama.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa pia kuna hoja kuwaSerikali inatoa tamko gani kuhusiana na Watanzania

Page 147: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

147

kuendelea kununua hisa na kuwekeza kwenye makampunimbalimbali hapa nchini hasa baada ya uzoefu huu wa NICOLna TOL. Napenda kulifahamisha Bunge lako kuwa Serikaliingependa kuwahakikishia wawekezaji na wananchi kwaujumla kuwa hali ya Masoko ya Mitaji ni shwari na hatua stahikiza kulinda maslahi ya wawekezaji, hususan katika NICOL,zimechuliwa na Serikali kupitia Capital Market and SecuritiesAuthority. Soko la Hisa limekuwa likionyesha kuboreka kwavigezo muhimu vya kupima ufanisi wa soko, hususan thamaniya hisa zote, yaani market capitalization, zilizoorodheshwa.Wastani wa bei umekuwa ukipanda kila mwaka. Kampuniya TOL, imekuwa ikiimarika na wameanza kupata faida,shilingi milioni 119 tangu 2011. Vilevile kuna kampunizinazofanya vizuri kama vile Kampuni ya Bia, Kampuni yaSigara, Kampuni ya Swisport, Kampuni za Saruji za Tanga naTwiga, Benki za CRDB, NMB na Benki ya Wananchi wa Dar esSalaam.

Mheshimiwa Spika, vilevile kulikuwa kuna hojaambayo ilitolewa kuwa kumekuwa na wimbi kubwa lakampuni za kigeni kufanya huduma za Uwakala wa Forodha.Kwa mujibu wa Sheria za Forodha za Afrika ya Mashariki,taratibu za kutoa leseni za Uwakala wa Forodha haubaguiaina ya kampuni au wamiliki wake. Utaratibu uliopo sasaunawataka wanaoomba leseni kufanya mtihani wa Uwakalawa Forodha. Waliofuzu hupewa leseni baada ya kukidhimahitaji mengine ya Forodha pamoja na kuwa na ofisi yauhakika. Hata hivyo, tumezingatia ushauri na tutaangaliakatika Jumuiya ya Afrika Mashariki usajili wa makampuni hayoili kulinda maslahi ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, hil i la TRA, nitamwachiaMheshimiwa Waziri mwenyewe atakapokuja kuzungumzaatalijibu.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa vilevile na suala la Sheriaya Manunuzi ya Umma. Rasimu ya Kanuni za Ununuzi waUmma imekamilika. Hata hivyo, utekelezaji wa Kanuni hizo,unasubiri kukamilika kwa marekebisho ya baadhi ya Sera naSheria za sekta nyingine ili kuwa na uwiano katika utekelezaji

Page 148: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

148

wake. Maeneo ambayo yanapaswa hufanyiwa marekebishoni pamoja na Sera ya Sheria ya PPP, hususan katikaushughulikiaji wa zabuni zenye maombi (unsolicited bids), yalemaombi ambayo yanakuja yenyewe tu, watu wanajitoa tukuwa wanataka kuja kuwekeza nchini, kwa hiyo, wanaletamaombi yao. Sasa inabidi nayo pia yasimamiwe ili kuhakikishakuwa hawa wanaoleta maombi kama haya, je, wao ndiyoambao watakidhi ubora na usalama wa uwekezaji nchinikote kama vile ambavyo wangekuwa wengi wameombakuwekeza katika nchi yetu. Eneo lingine ni Sheria ya Ununuziwa Umma ya Mwaka 2011, kuhusu uteuzi wa wajumbeMamlaka ya Rufaa za Zabuni na masuala yahusuyomwingiliano wa maslahi kati ya wahusika wa zabuni. Hivyo,Serikali imeona umuhimu wa kufanya marekebisho hayokwanza ndipo utekelezaji wa Kanuni mpya za Ununuzi uanze.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa kuna hoja ambayoimechangiwa na Waheshimiwa Wabunge wengi kiasi, juu yahali ya kifedha ya Mfuko wa PSPF. Katika kuhakikisha kwambasuala la madeni ya Mfuko wa PSPF linapatiwa ufumbuzi,Serikali imeunda Kamati inayochambua mapendekezombalimbali yaliyopo na kushauri hatua sahihi ya kulipa denihilo. Mapendekezo yaliyopo hadi sasa baina ya PSPF naSerikali ni kama ifuatavyo:-

(i) Serikali ilipe deni la mchango ya awali lashilingi bilioni 716 kwa awamu kwa kipindi cha miaka 10.

(ii) Serikali iongeze kiwango cha michango kufikiaasilimia 25 ili kuendelea kupunguza nakisi ya Mfuko.

(iii) Serikali itoe hati fungani maalum (special longterm interests bond) ili kuweza kufikia nakisi iliyopo.

(iv) Serikali kulipa michango ya kabla ya 1999 kwawatumishi wastaafu katika miaka mitano.

(v) Serikali ihamishe baadhi ya hisa zakembalimbali ili kufidia nakisi ya PSPF.

Page 149: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

149

(vi) Serikali ihamishe baadhi ya umiliki wa majengokwa Mfuko wa PSPF ili waweze kuutumia kwa ajili ya kuzalishamapato.

(vii) PSPF kubadili fomula ya ukokotoaji wa makato.

Mheshimiwa Spika, hayo ni mambo ambayoyamependekezwa lakini bado hayajapitishwa kwa sababulazima yafanyiwe kazi kuona jinsi gani yatafaa kutumika.Nataka kuonyesha tu kuwa tayari hatua zinachukuliwa katikakushughulikia hili suala la kifedha la PSPF.

Vilevile kulikuwa kuna masuala ya kuangalia jinsi ganiambavyo PSPF watawekeza katika miradi inayozalisha kwamuda mfupi badala ya ile ya muda mrefu ambayo inazuiafedha muda mrefu katika sehemu moja.

Mheshimiwa Spika, Kamati hii iliyoundwa imeanza kaziyake na imeandaa hadidu za rejea na kikosi kazi kinajumuishawajumbe kutoka Wizara ya Fedha, Kazi, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina,Msimamizi wa Mifuko (SSRA) na Benki Kuu ya Tanzania. Kamatihii itaangalia pia madeni ya Serikali yanayohusu mikopoiliyotolewa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa ajili miradi yamaendeleo ya Serikali ili kuangalia usalama wake na jinsi ganiambavyo itaendelea kusimamiwa vizuri. Aidha, Serikaliinatekeleza hatua za kulipa madeni ya PSPF na hadi sasashilingi bilioni 30 zilizokasimiwa katika bajeti ya mwaka 2012/13 zipo katika mchakato wa kulipwa na vilevile malipoyaliyoahidiwa kwa mwaka ujao wa fedha shilingi bilioni 50na zenyewe pia zitaendelea kutolewa kila mwaka.

Mheshimiwa Spika, naomba niendelee katika sualahilohilo kwa masuala ya wastaafu. Kulikuwa kuna suala lamafao ya wastaafu na maswali kuhusu wafanyakaziwanaostaafu na kulipwa mafao ya kustaafu na Wizara yaFedha. Wanaolipwa mafao hayo na Wizara ya Fedha ni walewote waliostaafu kabla ya tarehe 1 Julai, 2004, tareheambayo Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma PSPFulianza kulipa; Wanajeshi na Usalama wa Taifa

Page 150: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

150

wanaoendelea kulipwa mafao ya kustaafu na Wizara yaFedha kwa sababu wao siyo wanachama wa Mfuko wowotewa Hifadhi ya Jamii; watumishi wenye mamlaka mbili za ajirayaani walioajiriwa Serikali Kuu na kuhamia Serikali za Mitaaau Mashirika ya Umma na sehemu za ajira ya Serikali Kuu;wenye ajira za mikataba; viongozi wa Kitaifa Wastaafu;Marais; Makamu wa Rais; Mawaziri Wakuu; Viongozi waKisiasa; Wabunge; Wakuu wa Mikoa na Wilaya; Maafisa waSerikali ambao pensheni yao ni asilimia 80 ya mshahara wamaafisa wa ngazi zao walioko madarakani na ambao niwanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii na hulipia iletofauti ya pensheni kati ya inayolipwa na Mfuko husika naasilimia 80 ya mashahara wa walioko madarakani.

Mheshimiwa Spika, Maafisa wanaolipwa pensheni yaasilimia 80 ya maafisa wa ngazi zao walioko madarakaniviongozi wa kitaifa wastaafu; Majaji wastaafu kuanzia Julai,1999, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za SerikaliMstaafu (CAG); Inspector General wa Polisi Mstaafu;Kamishna Mkuu wa Magereza Mstaafu na Katibu MkuuKiongozi Mstaafu. Wastaafu wanaolipwa na Mfuko waPensheni wa Watumishi wa Umma, ni watumishi wenye ajiraya kudumu na malipo ya uzeeni katika mamlaka ya ajira yaSerikali Kuu waliostaafu kuanzia tarehe 1 Julai, 2004 nakuendelea.

Mheshimiwa Spika, sambamba na suala hilo,kulikuwa pia kuna suala la kima cha chini cha pensheni chaSh.50,114 kinacholipwa kuwa ni kidogo na kuwa hakikidhimahitaji muhimu ya mstaafu. Serikali imekuwa ikiboresha kimacha chini cha pensheni kila hali ya uchumi ilipokuwa ikiruhusuna itaendelea kuboresha kima cha chini cha pensheni.Serikali itaboresha kima cha chini cha pensheni katika mwakahuu wa fedha 2013/2014 kwa kuzingatia uwezo ulipo sasa.Kama Mheshimiwa Waziri alivyoeleza katika hotuba yake,pensheni kwa wastaafu inalipwa kwa vipindi vya miezi mitatu,mitatu, ambapo pensheni ya miezi miwili hulipwa mapemakatika kila kipindi kwa lengo la kuhakikisha wastaafuhawapati shida.

Page 151: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

151

Mheshimiwa Spika, vilevile kulikuwa na masuala yaSheria ya Ununuzi wa Umma na upungufu wake kuwa beizimekuwa zikipandishwa sana wakati tenda zikitumika nakushauri kuwa Serikali iweke bei elekezi. Napenda kujibuharaka haraka kuwa, Serikali imechukua hatua kadhaa katikakuimarisha ununuzi wa umma, lengo ni kuzidi kudhibiti na piakuwezesha kufanyika kwa ununuzi wenye tija kwa taifa. KatikaBunge la Novemba, 2011, Sheria mpya ya Ununuzi ilipitishwana utekelezaji wa Sheria hiyo utapunguza sana mapungufuambayo yamejitokeza katika Sheria ya Ununuzi ya 2004. Mojaya hatua ambazo zimechukuliwa na ambazo zimesisitizwana Sheria mpya, ni matumizi ya mikataba inayosimamiaununuzi wa bidhaa na huduma mtambuka (a common useditems). Katika utaratibu huo, bidhaa zote zilizoorodheshwakama bidhaa mtambuka, huwekewa bei elekezi. I l ikufanikisha hilo, Serikali imeanzisha Wakala wa Huduma yaUnunuzi Serikalini (GPSA) ambapo moja ya majukumu yakeni kusimamia mikataba ya bidhaa na huduma mtambuka.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. JANET Z. MBENE):Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa nimwite Mheshimiwa mtoa hoja,una dakika 40. (Makofi)

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa,nachukua nafasi hii kuwashukuru Naibu Mawaziri wangu kwamajibu yao mazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, nachukua nafasi hii,kuwashukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Fedha,Kambi ya Upinzani kwa mawazo yao na mwisho nawashukuruWaheshimiwa Wabunge wote kwa kushiriki mjadala huuambao umetusaidia sisi Wizara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kuwashukuru hao,nichukue nafasi hii vilevile kuwashukuru Waheshimiwa

Page 152: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

152

Wabunge wote waliopata nafasi ya kuzungumza ambaowalikuwa 10. Hii ni kujumuisha pamoja na Mwenyekiti waKamati ya Uchumi, pamoja na muwasilishaji wa hoja yaUpinzani. Vile vile nachukua nafasi hii kuwashukuru wale wotewaliowasilisha maoni yao kwa njia ya maandishi.

Mheshimiwa Spika, nitaanza na Mwenyekiti waKamati ya Uchumi na Viwanda. Katika mapendekezo yakeyote, kuna pendekezo moja zito ambalo nafikiri lipewe nafasiya kulisemea. Ametaka Serikali tueleze kwa kifupi autunavyofahamu tatizo la makontena lilivyo bandarini, kwasababu limeathiri mapato ya Serikali kama Kamati ilivyoeleza.Kwa sababu ya uzito wa hoja, nami nachukua nafasi hiikupitia Bunge hili na vivyo hivyo kufikisha ujumbe huu kitaifakueleza nini Serikali imekifanya baada ya kusikia tatizo hilona hali ikoje. Ni kweli, kuanzia tarehe 8 Aprili mpaka 31Mei,TRA walifanya kazi ya ukaguzi wa makontena, baada yakuwa na taarifa za ukiukaji wa kodi. Mpaka dakika hii kontenaambazo zimekuwa profiled ni 522 na ambazo zimechekiwani 498 na zilizoonyesha kuwa na mizigo tofauti na declarationni 188. Hizi kontena 188 zimekusanywa kodi yaSh.1,249,672,076/=, ni kodi ya ziada tuliyoikusanya baada yaku-check hizo kontena. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa exercise hii,inaonyesha kwamba, kuna ukweli wa aina hii kwambakumekuwa na ukwepaji wa kodi kwa kipindi fulani lakini TRAwameifanya hiyo kazi na kupatikana kodi hiyo ambayoingepotea kwa ukwepaji.

Mheshimiwa Spika, sasa katika kukagua makontena,criteria ambazo zinatumika ziko tano, ya kwanza,wanaangalia aina ya mzigo ulivyoelezwa kwenyedeclaration. La pili wanaangalia nchi ambako mzigo huounatoka (country of origin). Tatu, mhusika mwenye mzigo.Nne, nani anafanya ile clearing agent, identity ya clearingagent halafu tano, wanalinganisha na historia ya mwingizajiwa mizigo. Hizi criteria tano zinasaidia kubaini uharaka waku-screen container.

Page 153: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

153

Mheshimiwa Spika, lakini matatizo ambayoyamejitokeza yamelega katika maeneno manne. Makontenahaya ambayo nimesema ni 188 yaliyobainika kwambayalikuwa na mizigo ambayo il ikuwa si sahihi kamailivyoandiwa, hoja moja ni kwamba kulikuwa na hitilafu katikadeclaration, ilikuwa ni tofauti na hali halisi ya mzigo iliyokuwandani ya kontena. Pili, makontena mingine yalikuwa na mizigoya ziada. Tatu makontena mengine yalikuwa na aina tofutina mzigo ulivyojazwa kwenye makaratasi na nne, wajazajiwengine wali-declare thamani ndogo ya mzigo kuliko halihalisi ya mzigo wenyewe.

Mheshimiwa Spika, pia, napenda kulijulisha Bunge hilikwamba ni aina gani ya mali zilizokithiri katika makontenayaliyobainika yamekiuka taratibu. Aina ya mizigo ni kama,kwanza, CPU yaani computers, kinakuwa declared kitu tofautindani unakwenda kuzikuta computer. Pili, mosquito netsambazo zinakuwa zimeandikwa kwamba huu ni mzigo wamosquito nets kumbe ni mzigo mwingine ndani ni kwa sababumosquito nets hazichajiwi. Tatu, ni monitor za computers. Nne,ni nguo mbalimbali. Tano, ni solar panel. Sita, ni aina ya mizigoya alminium. Hii ndiyo historia iliyojitokeza katika kukaguamakontena hayo.

Mheshimiwa Spika, Serikali imechukua hatua gani?Serikali baada ya kufanya kazi tumegundua la ziada kwambakuna udanganyifu mwingine unatumia mtandao yaani fakedocuments kwa ajili ya kufanya declaration na clearingagents wengine sio wema.

Mheshimiwa Spika, karatasi hii ninayoionyesha kamamfano ni aina ya mihuri mbalimbali ambayo imebainikakuthibitisha kwamba wamefanya clearing. Sasa documentsza namna hii zikiwasilishwa, nyingine ni fake. Kwa hiyo, ninasampuli za ofisi mbalimbali zinazoonyesha mihuri yaoinayotumika kwa ajili ya kufanya kazi ya udanganyifu. Serikalitumechukua hatua ya kufuatilia na kubaini ofisi hizi na chanzocha matatizo haya.

Page 154: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

154

Mheshimiwa Spika, pia katika hili Serikali tunaelekezakwamba utaratibu wa direct release ya mizigo usimamishwe.Watu wote wanaoagiza mizigo tunataka wakaguliwe iliSerikali ipate kitu kinachostahili. Serikali haitaki mtu aonewelakini inataka kila mtu alipe anachostahili kulipa kwa kodi yakisheria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimeona niliseme hilo kwa kirefukwa sababu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Viwandana Biashara ameielekeza Serikali itoe maelezo na haya ndiyomaelezo.

Mheshimiwa Spika, baada ya hayo kuna hoja zaKambi ya Upinzani. Namshukuru Mheshimiwa Sil indeameorodhesha vitu vingi na Serikali tumechukua nafasi yakuvifanyia kazi na kuja na majibu. La kwanza, ametaka Serikaliitoe ufafanuzi kwa kiwango gani takwimu za uchumi wakitaifa zinaonyesha kwamba uchumi unakwenda vizuri lakiniumaskini unapungua kidogo sana au inaonekana hakunaimpact. Hoja hii ni sahihi. Takwimu za ukukaji wa uchumi yaanikwa GDP average kutoka 2000 mpaka 2012, GDPimeongezeka kwa wastani wa kati ya 6.9% mpaka 7%, nigrowth rate lakini umaskini kwa wastani toka 2000 mpaka 2012umepungua kwa 2.1% tu. Kwa hiyo, ukiangalia hilo,utagundua kwamba kweli notion hii, hakuna uwiano ulio namsukumo unaofanana katika ukuaji wa uchumi na upunguzajiwa umaskini. Tunahitaji sisi kama Serikali kuja na sera namikakati mipya kusaidia namna ya kupunguza umaskini. Hiini hoja ya ukweli na Serikali tumeifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa tumefanya nini? Serikalitumekuja na kitu tunasema financial inclusion, maana yaketunaweka mikakati ya kuangalia walio wengi ambao ni 75%ya wananchi wa Tanzania wako vijij ini, hawa ndiyohawaguswi na ukuaji mkubwa wa uchumi na ukuaji mkubwawa uchumi umeonyesha kwamba upo katika transport sector,construction na financial sector lakini sector hizi zinaajiri watuwachache ukilinganisha na sekta inayoajiri walio wengi, sektainayoajiri walio wengi ni sekta ya kilimo na kwa wastani katikamiaka 10, sekta ya kilimo imeongezeka kwa 4.3%. Kwa hiyo,

Page 155: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

155

growth rate ya kilimo imekuwa ndogo ukilinganisha na growthrate ya sekta nyingine na ndiyo maana walio wengi wakawawameachwa kidogo nje ya mfumo wa ukuaji wa haraka.

Mheshimiwa Spika, sasa Serikali tumeangalia natumechukua majukumu ya kuangalia kwamba tuboreshesekta ya vijijini. Tunaangalia namna gani tutapelekapembejeo za kilimo kwa kuboresha na kuimarisha utengajiwa mafungu katika bajeti ili shughuli hii iweze kuwa na impactkwa wananchi walio wengi. Tunaangalia namna yakuboresha barabara vijijini, tunaangalia uwekaji wa umemeili usambae haraka na tunaangalia namna tutakavyosaidiaupatikanaji wa maji vijijini. Wananchi wetu wakiwa na vituambavyo ni vya muhimu katika maisha na kuwasaidiawaweze kuendelea kiuchumi basi kilimo kitapanda. Kwa hiyo,kwa kuchukua hatua hizo, tuna hakika tatizo hili litatatuliwa.Kwa hiyo, Mheshimiwa Silinde alichosema ni sahihi na sisi hayondiyo majibu ya Serikali kwamba tunalifanyia kazi suala hili.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, mzungumzaji wa Kambi yaUpinzani, Mheshimiwa Silinde amesema kwamba kwa halituliyonayo TRA inavyokusanya fedha kwa kusema kwelikulingana na hali halisi kama misamaha ya kodiingeondolewa au ingepunguzwa, makusanyo ya kila mweziwalau yangefikia one trillion, hapa pana changamotokidogo. Mimi sipingani sana na hoja hii, nasema kunachangamoto kwa maana mbili. Kwanza, sasa hivi,tunachokusanya kwa wastani kwa kila mwezi kinaelekea katiya shilingi bilioni 750 mpaka 800, hayo ni makusanyo ya TRA.Kwa hiyo, anachosema Mheshimiwa Silinde kwambatungeweza tukafikisha one trillion inawezekana tukitatuachangamoto, kwa mfano, changamoto hii tuliyosema yamakontena bandarini.

Mheshimiwa Spika, changamoto nyingine nimisahama ya kodi kama alivyosema Mheshimiwa Silindelakini changamoto ni kwamba Waziri wa Fedha kwa kawaidahana mamlaka mwenyewe kusamehe kodi, kodianazozisamehe Waziri wa Fedha ni zile mlizoidhisha ninyi

Page 156: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

156

Waheshimiwa Wabunge kwa kupitia Sheria. Waziri wa Fedhaanachokifanya ni kuitazama sheria inamruhusu asamehe kitugani alichoidhinishiwa na Bunge kwa mujibu wa sheria iliyopo.Kwa hiyo, sisi Serikali tumefanya maamuzi ya ku-review ilesheria na italetwa hapa Bungeni ili Waheshimiwa Wabungemuamue ni maeneo gani yapunguzwe ili Waziri wa Fedhaasiwe na mamlaka ya kuitumia sheria ile apendavyo. Kwahiyo, mpunguze madaraka ninyi Waheshimiwa Wabungemliyonipa kwenye sheria. Kwa hiyo, hil i nasema nichangamoto lakini tutashirikiana wote kwa pamojakuangalia maeneo ya kupunguza ili tuweze kuwa namisamaha mingi isiyotuletea tija katika uchumi, sheriayenyewe tunairekebisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine, msemaji wa Kambiya Upinzani anasema kwamba tuliagizwa sisi Serikali kuiagizaPPRA ifanye ukaguzi wa manunuzi ya mafuta ambayo kwamaelezo yake ni kwamba Serikali inatumia 1.4 billion kwa sikukwa ajili ya kulipia mafuta kuendesha umeme. Hoja ya Kambiya Upinzani ni kwamba tupeleke PPRA wakakaguewathibitishe kitu gani kinatokea kule. Serikali tumeshaagizana PPRA kwa taarifa niliyonayo wanafanya ukaguzi sasa.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine kutoka Kambi yaUpinzani ilikuwa inasema kwamba mfumo wa mabenkiTanzania umekithiri wizi yaani kinachotokea katika mabenkini wizi na kwamba wizi unaotokea katika mabenki unatokanana mfumo mbovu wa banking system. Tumelichunguza sualahili na kwa taarifa tuliyonayo ni kwamba mifumo ya benki yautendaji iko imara. Mimi mwenyewe nimefanya kazi katikabanking system kwa miaka mingi kwa hiyo ninasema kileninachokifahamu na nilichopata mpaka leo lakini wiziunatokea katika mabenki, umekuwa unapitia katika ATM.Benki Kuu hivi ninavyozungumza tayari wameshachukuahatua kwa ajili ya kwenda kwenye version nyingine ya EuroSystem ATMs ambazo zipo imara, reliable zinazowezazikapunguza wizi wa kutumia ATM. Kwa hiyo, nawaombakwa pamoja tuwe na subira wakati Benki Kuu inalifanyia kazihili kwa ATMs zilizoonyesha zina hitilafu.

Page 157: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

157

Mheshimiwa Spika, suala lingine la Kambi ya Upinzaniambalo wametushauri vizuri ni kwamba tutazame namna yakuondoa kesi nyingi za Serikali ambazo ziko Mahakamaniambazo zinatuletea gharama kubwa tuka-settle out ofCourts. Hoja ina both ways yaani ina merits na demerits. Meritsni kwamba ikiwa Serikali ina weak point basi ni vizuri tuka-settle out of Court kwa sababu kuendelea ndani yaMahakama kunakuwa na hasara kwa sababu hakunaprospect ya Serikali kushinda lakini pale tunapokuwa nastrong points kama Serikali ,tukiondoa tuka settle out of Court,inakuwa ni hasara kwa Serikali na kwa wananchi wanaoi-finance Serikali iwepo. Kwa hiyo, ni case to case, kama tunahoja kubwa au hatuna hoja ushauri huo unakuwa mzuri.

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine kutoka Kambi yaUpinzani imehoji kwamba ni muda sasa microfinanceinstitutions hazina regulatory framework, ni kweli mpakadakika hii tulitarajiwa kuwa tungekuwa tumefikia hatuakubwa lakini hivi ninavyozungumza Benki Kuu wanaendeleakutengeneza sera itakayoongoza utayarishaji wa kanuni ilikanuni za microfinance ziweze kutolewa. Kwa hiyo, hili ndiyojibu lake.

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine iliyoletwa naWabunge wa Upinzani ni kwamba wanaona kuna umuhimuwa Mifuko ya Jamii iweze kutoa report kila quarter kama vileinavyofanywa na mabenki ili wananchi waweze kuwa naupeo na kuelewa hali ya usalama wa fedha zilizokuwa katikahizo hifadhi za jamii. Kwa kusema kweli na mimi naona kunastrong point lakini tatizo tulilonalo kwa dakika hii ni kwambamabenki tuliyonayo yanatumia mifumo tofauti kwa hiyofrequency ile ya kutoa publications, hatuwezi tukatumiasheria ile ambayo inalazimisha mabenki ya-publich onquartely basis tukaitumia kwa ajili ya Mifuko hiyo mpaka Sheriailiyoanzisha Mifuko hiyo iweze kusema hivyo. Lingine nikwamba actuarial valuation, nazo zinafanyika na zile ndiyohuwa zinatupa indicator ya hali halisi ya risk au hapana katikaMifuko hiyo. Pia lingine ni kwamba kulingana na Sheria yaMifuko, audit report zinafanyika mara moja kwa mwaka.

Page 158: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

158

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na maswali mengineambayo kwa muda uliopo na kwa umuhimu wa kuwa majibuambayo yanakidhi matakwa ya Waheshimiwa Wabungetumeyaweka kimaandishi ambapo yatakapokuwayamemalizika, tutaomba tuwasilishe kwa WaheshimiwaWabunge. Kuna hoja nzuri na kuna maswali mengi namengine ndiyo kama hivi yamebaki lakini tunaoneleakwamba ni hekima tuyaweke kimaandishi ili WaheshimiwaWabunge baadaye waweze kuwa na kitu kilichokamilika.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombanichukue nafasi kuwaomba Waheshimiwa Wabungemuiunge mkono bajeti hii ili ipite, nikae vizuri kutengenezafedha niwape ili muweze mkanufaika na bajeti. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naombamniunge mkono kuidhinisha bajeti hii na ninaomba kutoahoja. (Makofi)

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

SPIKA: Hoja hiyo imeungwa mkono na umetuachiadakika ishirini na tano. Tunaendelea na hatua inayofuata.

KAMATI YA MATUMIZI

MATUMIZI YA KAWAIDA

Fungu 7 - Ofisi ya Msajili wa Hazina

Kif. 1001 Administration and HumanResource Management … ……Tshs. 38,088,142,000/=

(Kifungu Kilichotajwa Hapo Juu Kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila Mabadiliko Yoyote)

Page 159: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

159

Fungu 23 - Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali

Kif. 3001 Public Debt Management … … .Tshs. 350,000,000/=Kif. 3002 Expenditure Management ... Tshs. 25,400,000,000/=Kif. 3003 Financial Management … …. Tshs. 45,905,681,200/=Kif. 3004 Financial System … … … … ......Tshs. 4,757,360,800/=Kif. 3005 Sub Treasury Arusha … … …........Tshs. 170,000,000/=Kif. 3006 Sub Treasury Coast … … … …......Tshs. 149,000,000/=Kif. 3007 Sub Treasury Dodoma … … …... Tshs. 339,000,000/=Kifl. 3008 Sub Treasury Iringa… … … …......Tshs. 160,880,000/=Kif. 3009 Sub Treasury Kagera… … … ….... Tshs.151,000,000/=Kif. 3010 Sub Treasury Kigoma … … …......Tshs. 160,000,000/=Kif 3011 Sub Treasury Kilimanjaro … … …....Tshs.167,000,000/=Kif. 3012 Sub Treasury Lindi …… … … …......Tshs.156,000,000/=Kif.3013 Sub Treasury Mara…… … … ......…Tshs.152,000,000/=Kif 3014 Sub Treasury Mbeya… … … ….......Tshs.154,000,000/=Kif 3015 Sub Treasury Morogoro … … ….....Tshs.205,400,000/=Kif. 3016 Sub Treasury Mtwara … … ….........Tshs.177,100,000/=Kif 3017 Sub Treasury Mwanza … … ….......Tshs.160,000,000/=Kif. 3018 Sub Treasury Rukwa … … … ….....Tshs. 159,000,000/=

(Vifungu Vilivyotajwa Hapo Juu Vilipitishwa na Kamati yaMatumizi Bila Mabadiliko Yoyote)

Kif. 3019 Sub Treasury Ruvuma … … …Tshs.150,000,000/=

MHE. JENISTA J. MHAGAMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Hapa tupo Sub Treasury Ruvuma, kuna kilekifungu 220900 Training Foreign, naona mwaka janahawakutengewa fedha za training nje ya nchi na mwakahuu pia hawajatengewa fedha lakini maeneo menginenaona wametengewa. Ni kwa nini watumishi wa Sub TreasuryRuvuma hawapewi fedha na wao kwenda kujifunza mambohuko nje?

MWENYEKITI: Kifungu gani?

MHE. JENISTA J. MHAGAMA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ni kifungu 220900, Training Foreign.

Page 160: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

160

MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu!

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA SALUM MKUYA):Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ruvuma bado tunawafanyakazi ambao ni wapya na kama unavyoonatunaanza kwanza kuwa-training domestically kablahatujaenda kuwa-train outside ili wawe na capacity kwanzaya kufanya kazi za pale ndani.

(Kifungu Kilichotajwa Hapo Juu Kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila Mabadiliko Yoyote)

MWENYEKITI: Naomba msiniandikie barua, mimi nipokazini hapa. Tunaendelea. (Kicheko)

Kif. 3020 Sub Treasury Shinyanga …........…Tshs. 149,000,000/=Kif. 3021 Sub Treasury Singida … …......... …Tshs.150,000,000/=Kif. 3022 Sub Treasury Tabora… … … ......…Tshs.152,000,000/=Kif. 3023 Sub Treasury Tanga… … … …......Tshs.151,000,000/=Kif. 3024 Sub Treasury Manyara… … … … .Tshs.151,000,000/=Kif. 4001 Local Government Finances ........Tshs.426,000,000/=Kif.7001 Pension and Gratuity … … .........…Tshs.629,250,000/=

(Vifungu Vilivyotajwa Hapo Juu Vilipitishwa na Kamati yaMatumizi Bila Mabadiliko Yoyote)

Fungu 50 - Wizara ya Fedha

Kif. 1001 Administration and HR Management …Tshs.7,898,819,000/=

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, sasa nimshahara wa Waziri. Wizara hii ina mafungu mengi hivyo basinitawapeleka kwenye Kanuni ya 101(4) ambapo vyamavinavyohusika vimependekeza majina yao ambao niMheshimiwa Zungu, Mheshimiwa Betty E. Machangu,Mheshimiwa Masoud Omar, Mheshimiwa Jitu Soni,Mheshimiwa Tundu Lissu na Mheshimiwa Rajab MbaroukMohamed. Mheshimiwa Tundu Lissu!

Page 161: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

161

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nipate ufafanuzi wa Mheshimiwa Waziri lakini nianzekwa kusema kwamba Mheshimiwa Waziri amejibu maswaliyake vizuri sana, ingekuwa ni vizuri na Mawaziri wenginewakajifunza kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. Mgimwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti…

MWENYEKITI: Akili ni nywele kila mtu ana zake, hee!(Kicheko)

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nitajikita tu kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri na jamboambalo nataka ufafanuzi kutoka kwake ni suala la deni laTaifa. Katika aya ya 17 ya hotuba yake, Mheshimiwa Waziriamesema kwamba malipo ya deni la Taifa hadi kufikia mweziAprili mwaka huu yalikuwa shilingi trilioni 1.666 ambapo katiya hizo shilingi bilioni 214 zilikuwa ni kwa ajili ya deni la nje nashilingi trilioni 1.453 zilikuwa ni deni la ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hotuba hiyohiyokwenye paragraph ya 127, Mheshimiwa Waziri anazungumziatena deni la Taifa na hapa anatuambia kwamba matumizikatika deni la Taifa hadi kufikia Aprili 2013 yalikuwa shilingitrilioni 2.227 kati ya makadirio ya shilingi trilioni 2.736. Kwa hiyo,tuna maneno mawili, tuna ndimi mbili nilizozizungumza jana,tuna shilingi trilioni 1.666 matumizi ya deni la Taifa na tunashilingi trilioni 2.227 matumizi ya deni la Taifa. Sasa tumetumiashilingi ngapi kulipa deni la Taifa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili ni muhimu sanakwa sababu katika hotuba nzima ya Mheshimiwa Waziri waFedha hajatwambia hivi tunadaiwa shilingi ngapi kama nchi?Haya malipo ya matrilioni haya, hizi ni fedha nyingi sana,tunahitaji Mheshimiwa Waziri atwambie kwanza, kati hizindimbi mbili, tufuate ulimi upi? Tufuate ulimi wa kushoto shilingitrilioni 1.66 au tufuate ulimi wa kulia shilingi trilioni 2.227?

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, Mheshimiwa Waziri nimuhimu alieleze Bunge hili Tukufu hivi haya madeni makubwa

Page 162: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

162

yametokana na mikopo ipi? Bunge hili lipate a completebreakdown ya wanaotudai ili tuweze kujua hivi tumewakopavitu gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na nitaondoashil ingi kama Waziri atageuka na kuleta majibu yaajabuajabu. (Kicheko)

MWENYEKITI: Kwa hiyo, unayo majibu tayari.Waheshimiwa Mawaziri m-note wanayozungumza nainawapeni nafasi kujiandaa vizuri. Mheshimiwa Zungu.

MHE. MUSSA Z. AZZAN: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kila Taifa linapokaribisha wawekezaji linakuwana lengo kunyanyua uchumi katika Taifa lake.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge sisi hatukusikii vizurilabda uhame.

MHE. MUSSA Z. AZZAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifalinapokaribisha wawekezaji lina lengo la kutaka wawekezajiwawekeze lakini Taifa nalo lifanikiwe. Kuna Sheria za stockexchange ya nchi yetu na makampuni haya ya simuyalitakiwa yote yasajiliwe ili sasa uchumi upenyezwe kwawananchi wetu lakini sheria hii toka ianzishwe badohaijafanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa mfano mdogo tu kwanchi jirani ya Kenya na Kampuni ya Safaricom ambayo sasahivi imetangaza namna walivyopata faida kwa wananchikumiliki kampuni ile na namna Serikali ilivyopata faidakuwemo kwenye kampuni ile. Nataka kujua tu, ni lini sasaMheshimiwa Waziri ata-implement sheria hii na kuhakikishamakampuni yote haya ya simu yanaingizwa kwenye stockexchange ili sasa wananchi na wao waweze kununua hisakatika makampuni haya na baadhi ya pesa hizi badala yakusafirishwa kwenda nje zitumike kwa wananchi kamawalivyofanya nchi nyingine. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Betty Machangu.

Page 163: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

163

MHE. BETTY E. MACHANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti,Serikali ilibinafsisha Mashirika ya Umma na mengi yao yalikuwani viwanda na mashirika haya yaliwekwa kwenye ShirikaHodhi la Consolidated Holding Corporation na tumekuwatunaambiwa hapa na Serikali ki la leo kwamba kwamakampuni yale ambayo hayakuendeleza vile viwanda,Serikali ita-revoked title ya vile viwanda lakini mpaka leohakuna kinachofanyika na badala yake Serikali inatuelezakuhusu Consolidated Holding Corporation kumaliza mudawake mwaka kesho na Hazina kuchukua kazi zake.Tunachohitaji sisi ni ajira kwa vijana wetu, kwa nini inakuwavigumu kwa Serikali ku-revoked titles ili watu wenginewaanzishe hivyo viwanda vijana wetu waweze kupata ajira.Naomba Serikali ieleze Taifa kwa nini hizo title za hawa watuwaliochukua viwanda ambavyo hawaviendelezi hawazi-revoke, kuna matatizo gani? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Rajab MbaroukMohamed.

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Serikali iliamua kwa dhamira nzuri tukuondoa suala la ukusanyaji kodi ya majengo kutoka katikaHalmashauri na kuzipeleka TRA kwa lengo moja la kuwezakupata ufanisi. Kutokana na hali ilivyo sasa hivi, Halmashaurizetu nyingi kwa kweli zimepungukiwa na mapato yakeyanayotokana na hii property tax na ufanisi unaonekanakulegalega chini ya TRA. Naomba kujua kipindi cha mpitocha TRA kukusanya hizi tax kitamalizika lini? Naomba Wazirianipe ufafanuzi, wamejipangaje kurejesha mfumo huu katikaHalmashauri zetu ili ziendelee kupata mapato yake katikanjia nzuri?

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Nassib Omar.

MHE. NASSIB SULEIMAN OMAR: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Katika mchango wangu wa maandishi,nilimweleza Mheshimiwa Waziri kuhusiana na wizi ambaounafanyika TRA kwa Kampuni ya za Forwarding and Clearing.Wafanyakazi wa TRA hutumia password za makampuni haya

Page 164: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

164

na kuwapa watu binafsi na kuweza kuingiza magari ndaniya nchi bila kulipa ushuru. Mfano halisi ni Kampuni ya KisiwaniEnterprise ambayo imefungiwa toka mwaka 2009.Wafanyakazi wa TRAwaliohusika badala ya kuachishwa kaziwalitawanywa na bado waendelea na kazi. Vilevile kesi hiiipo Polisi na Mheshimiwa Waziri kwa kweli hakulitoleaufafanuzi mzuri. Kwa hiyo, namtaka Mheshimiwa Wazirianieleze lini kesi hii itamalizika kwa sababu sasa hivi ni zaidiya miaka minne na bado wanapigwa danadana huku nahuku. Nyaraka na vielelezo vyote wameshapewa Wizara naTRA lakini bado halijapatiwa ufumbuzi. Kwa hiyo, naombanipate ufafanuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikiwa suala hili sikupewamaelezo mazuri itabidi nizuie shilingi, ahsante.

MWENYEKITI: Unazuia, unatoa? Haya twende kwaMheshimiwa David Kafulila.

MHE. DAVID Z. KAFULILA: Mheshimiwa Mwenyekiti,katika mchango wangu nilihoji kwa nini Serikali isichukuehatua za ziada kufuatia wanaodaiwa na benki ya NBC kiasicha takribani shilingi bilioni 60 ambazo kwa mujibu wa taarifaya CHC iliyopewa dhamana ya kukusanya madeni hayo nikwamba deni hilo halilipiki limewekwa kwenye orodha yamadeni chefuchefu. Sasa kiasi cha shilingi bilioni 60 ni kiasikikubwa sana. CHC wanasema kwamba watu hawa ambaowanadaiwa tatizo ni kwamba dhamana walizoziweka wakatikuchukua mikopo ni kidogo ukilinganisha na mkopowaliouchukua kwamba mtu amechukua mkopo wa shilingibilioni 10 wakati dhamana iliyotumika ni shilingi bilioni moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kupata kauli yaSerikali, moja imechukua hatua gani kuhusu hao ambaowalikopa na ni matajiri wangeweza kufilisiwa katika namnanyingine. Pili, kwa watumishi waliokuwa NBC kwa sababu nijinai, wamechukua hatua gani kwa watumishi ambao walitoamikopo kiholela kiasi hicho na kuliingizia Taifa hasara?

Page 165: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

165

MHE. JITU V. SONI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.Mimi naomba kuuliza Serikali pamoja na kazi nzuriinayofanywa na Serikali kwa kupitia TRA kukusanya mapatona kukusanya kodi mbalimbali, ni lini sasa Serikali itakaa nawadau, lakini pia kubadilisha sheria na kuiangalia upya Sheriaya Manunuzi ambayo inadidimiza uchumi wa nchi hii? Katikasheria ile kuna masuala mawili. Moja, ni ile short list ya walewazabuni, wale wachache wanaobaki ambaowanaruhusiwa kuhudumia Halmashauri zetu au Serikali huwawanaungana na wanaweka bei maalum. Pia katika bei zahuduma wanazotoa na bidhaa ambazo wanaleta Serikaliniunakuta zile bei ni mara mbili au mara tatu au zaidi ya ile beiambayo ipo sokoni. Sasa tungekuwa na Sheria ambayoitalinganisha bei za sokoni na ile bei ya huduma inayotolewa,tutaweza kuwa na akiba kubwa ya fedha na ile kasi yamakusanyo na matumizi tukiibana vizuri uchumi wetu utakuasana. Sehemu kubwa tunayopoteza uchumi wetu ni kwenyehiyo sekta ya manunuzi. Ni lini sasa Serikali itakaa na wadaumbalimbali pamoja na Wabunge na kuiangalia upya Sheriahiyo ya Manunuzi ili tuweze kubana matumizi?

MWENYEKITI: Ahsante. Naomba nipate uhakikaMheshimiwa Nassib Omar, unaposema kuna kesi iko wapi,TRA, Mahakamani au wapi?

MHE. NASSIB SULEIMAN OMAR: MheshimiwaMwenyekiti, hii kesi bado wanayo Polisi haijaendaMahakamani.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri maelezo. Naombamtajibu kwa kutaja majina yao.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA SALUM MKUYA):Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza, nami nijikitehapohapo kwa suala la Mheshimiwa Nassib. Tulipotoka hapatumekwenda kulifuatilia hili suala ambalo amelieleza…

MWENYEKITI: Sauti haitoki.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA SALUM MKUYA):Mheshimiwa Mwenyekiti, tulipotoka hapa, tulikwenda

Page 166: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

166

kulifuatilia suala hili na tumeona kwamba hawa KisiwaniEnterprises, kweli walifungiwa na katika maelezo yao kulikuwana maelezo ya kwa nini walifungiwa na wao wenyewewameweza kujitetea kwa kiasi kikubwa sana. Huko nyumawalikwenda Polisi, lakini final decision ilikuwa ni kwa TRAkuwafungia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala nilijibu mimi, kwasababu Bodi tayari imeshafanya maamuzi yake, hatuainayofuata ni kwa Kisiwani Enterprises kwenda kwa TaxRevenue Appeal Board, waka-appeal, waka-revoked hiyodecision ya TRA, hapo sasa ndipo TRA wataweza kukaa nakuanza kuliangalia suala hili. Kwa hiyo, tunaomba wafuatehuo utaratibu uliopo kwa ajili ya suala lao kutazamwa upya.Namwomba Mheshimiwa Nassib Omar awasiliane na haowatu kwamba waanze maandalizi ya kwenda Tax RevenueAppeal Board.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na suala lingine laMheshimiwa Rajab kuhusu kodi ya majengo, kweli muda waTRA kwa ajili ya kufanya kazi hii umemalizika na kweli capacityilikuwa ndogo kutoka na complexity ya Taasisi hizi. Katikampango wetu wa Big Result Now, tunaandaa system yakuweza ku-strengthening capacity ya Halmashauri zenyeweziwe zinaweza kukusanya kodi i le kwa sababu hatatukiirejesha, itarudi kwa sababu mwezi Juni ndiyo mwisho wamkataba wa TRA kukusanya kodi hii lakini bado hii itakwendasambamba na kuweza ku-strengthening capacity yaHalmashauri kuweza sasa kukusanya zile kodi kamainavyostahiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MWENYEKITI: Muendelee.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. JANET Z. MBENE):Mheshimiwa Mwenyekiti, nijibu kwa niaba ya Waziri wa Fedhaswali alilouliza Mheshimiwa Zungu kuhusiana lini sasamakampuni ya simu yataingia kwenye stock exchange kamavile ambavyo nchi jirani zinazofanya.

Page 167: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

167

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumfahamishaMheshimiwa Mbunge pamoja na Bunge lako kuwa sasa hiviCapital Market and Securities Authority wameshakamilishakanuni zitakazowezesha makampuni ya migodi ya madinipamoja na makampuni ya simu kuingia katika soko la hisa.Wao wamependekeza kuwa ubia huu kwa mfano kamaSerikali itaingia katika ubia huu, basi tutakuwa na asilimia 30ya hisa katika makampuni ya migodi. Vilevile inapendekezakuwa katika makampuni ya simu Serikali iwe na ubia waasilimia 25 na kuwe kuna conditions ambazo zitawekwa kwaajili ya kuhakikisha kuwa aidha iwe ni asilimia 25 au nambaya wanunuaji wa hizo shares au utaratibu mwingine ambaounaenda sambamba na usimamizi huo. Kwa sasa hivi Serikaliimeamua kuwa hili suala inalifuatilia kwa karibu na litafanyikakwa sababu inaonekana kuwa wao wenyewe wakiachiwahawana shauku sana kuingia katika soko la hisa lakini sisikama wadau wakubwa Serikali tunahitaji ifanyike ili tuwe nacontrol zaidi katika makampuni haya.

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, sualalililoletwa na rafiki yangu Tundu Lissu, ni suala zuri hata miminingeuliza. Nitoe tu ufafanuzi kiujumla, ni kwamba matumiziya shilingi trilioni 1.6 ni deni ambalo limeshalipwa yaani nifedha zilizolipwa na shilingi trilioni 2.227 ni matumizi ya Fungu22 ya deni la Taifa. Kama kuna maandishi yalienda vibayabasi tunaomba radhi lakini ndiyo ufafanuzi wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yake ya pili, alikuwaanataka kujua orodha ya madeni haya tunakowekeza. Kwakuwa imeulizwa orodha, naomba angetupa nafasitukaitayarishe ili mbele ya safari iweze kuwasilishwa.

MWENYEKITI: Nilimhurumia tu akauliza maswali mawiliinatakiwa moja lakini kutoa orodha baadaye si vibaya.Endelea bado kuna swali lingine.

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mheshimiwa Zungu ameeleza umuhimu wa makampuni yasimu kujiunga na stock exchange ili watakaonunua hisawaweze kunufaika. Ni hoja nzuri, lakini nitoe ufafanuzi tu

Page 168: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

168

kwamba sasa hivi tunavyozungumza CMSA wameshapelekaShirika husika TCRA ili badaye zichambuliwe kwa ajili yakufanikisha ombi alilosema. Kampuni ambazo CMSAwameshapeleka mapendekezo kwa ajili ya listing ni kampuniza madini pamoja Telecom companies kama alivyosemaMheshimimwa Zungu.

MWENYEKITI: Suala la Mheshimiwa David Kafulilahamjajibu.

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mheshimiwa Betty Machangu ametaka tufafanue kwa ninibasi mashirika yale ambayo yalibinafishwa lakini hayatumiinafasi zile kwa mujibu wa Mkataba yasiwe revoked nakwamba CHC inafanya nini katika kazi yake ya kuangaliamashirika hayo. Napenda kufafanua kwamba dakika hiitunapozungumza, CHC wameshatayarisha tathmini yamakampuni yote na ipo tayari kwa ajili ya kuifanyiwa kazi.

MWENYEKITI: Bado kuna swali la Mheshimiwa Soni naMheshimiwa David Kafulila hamjajibu.

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mheshimiwa Kafulila ameuliza swali kwamba NBC wapokwenye ile credit portfolio list, kuna mikopo inayofikia shilingibilioni 60, benki wakati huo ilikopesha watu ambao sasa hivihawalipi. Aliuliza kwa nini basi wale waliokopesha naowasichukuliwe hatua kwamba walikopesha watu wasio nauwezo wa kulipa au walikopesha bila kuangalia effectivinessya matokeo ya kukopesha na kupoteza fedha. Katika halihalisi ya ukopeshaji, kuna njia tatu ambazo lazima ziangaliwe.Kwanza, je, wale waliokuwa wanakopesha ni kweliwalikopesha nje ya taratibu za ukopeshaji au yulealiyekopeshwa alikuja akajiweka akawa mwovu mwenyewebadala ya kurudisha pesa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara nyingi watu wanakujakukopa katika mabenki wakionyesha kila dalili iliyo njema,mara wanapopata fedha kwa kupata misukosuko au kwatabia zao kubadilika basi hilo ndilo linakuwa tokeo. Wakati

Page 169: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

169

mwingine si sababu ya mkopeshaji lakini pale inapobainikakwamba na mkopeshaji alikiuka kanuni za ukopeshaji akawasehemu ya tatizo la kukopesha mtu asiyeweza kulipa, taratibuza mabenki yenyewe zipo wazi kuwachukulia hatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hali hiyo, Serikali hainataarifa kwamba wale waliokuwa wanakopesha mpaka sasahivi benki i le inadai shil ingi bil ioni 60 kutoka kwawaliokopeshwa ambao hawajarudisha na kama walikuwanao sehemu ya tatizo lakini hiyo ndiyo hali halisi ya kazi zaukopeshaji. Kama kweli ikibainika mkopeshaji alikuwa sehemuya tatizo ni lazima system itamchukulia hatua na systemwenyewe ni mabenki yenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, taratibu za benkizenyewe ikiwa deni lile litaonekana limeshindikana, wanataratibu kwanza ya restructuring, wanamhusisha mkopajiajieleze ana tatizo gani, kama bado kuna viability propositionsambazo zinaonyesha kwamba tatizo lililosababisha asilipelinaweza likaangaliwa kwa mapana mengine, benki huwazinasikiliza na kuangalia namna ya kumsaidia mkopaji. Pili,ikiwa market conditions na viability position ya Shirika haipo,benki yenyewe lazima ikubali kuchukua hasara kwa niabaya mkopeshaji. Proposition ya tatu ni kwamba kama mkopajibado yupo, mali zipo na security iliyochukuliwa kwa mkopoule basi inategemea benki ile ilichukua mkopo ule na kuwekarehani ya security ya aina gani. Kama ni legal mortgage auother securites kama guarantees, wana-reinforce securitiesili ziwe-realised na mkopo urejeshwe. Inaweza ikatokeakwamba pale wanapojaribu kuchukua hatua au security zilehazipo au hazikuchukuliwa, kwa hiyo, hapo ndipolinapogeuka kuwa tatizo la benki kuwa na mkopo usiowezakuwa-recovered. Sasa itategemea hali halisi iliyokuwepo nakama alivyozungumza Mheshimiwa Mbunge mwenyewekwamba ulikuwa mkopo wa shilingi bilioni moja, mimi kamaupande wa Serikali sina uhakika kama kweli ulikuwa mkopowa shilingi bilioni moja sasa kwa sababu ya riba ikafikia shilingibilioni 60, hili ni suala ambalo linatakiwa lifanyiwe tathminikatika hali halisi ya kilichotokea.

Page 170: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

170

MWENYEKITI: Bado swali moja la Mheshimiwa Soni.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. JANET Z. MBENE):Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la MheshimiwaJitu Soni kuhusiana na Sheria ya Manunuzi kuwa itapitiwa lini?Naamini labda alikuwa hayupo wakati tunajibu, sasa hivi tupokatika utaratibu wa kuainisha zile sheria ambazozinashabiana, Sheria ya PPP na Sheria ya Manunuzi ya mwaka2011 ili kuondoa mgongano wote ambao utajitokeza kablaya kuanza sasa kupitia ile Sheria yenyewe ya Manunuzi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tundu Lissu.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Kwa vile sijaridhika na majibu ya MheshimiwaWaziri, naomba kutoa hoja ya kuondoa shilingi katikamshahara wa Waziri ili hili suala lijadiliwe na Kamati yako yaBunge Zima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, kunakauli mbili hapa za Serikali na Waziri hajazitolea ufafanuzi.Kauli ya hotuba yake kwamba tumetumia shilingi trilioni 1.666kulipa deni, hiyo ni ya kwanza na kauli ya pili, tumetumiashilingi trilioni 2.227 kwa matumizi ya Fungu 22. Fungu 22 ni ladeni la Taifa, matumizi ya Fungu 22 hayawezi yakawamengine zaidi ya kulipa deni la Taifa. Kwa hiyo, atwambieMheshimiwa Waziri na nimemsikia akisema kwamba kunamakosa mahali fulani hajayaeleza ni makosa gani, kamaWizara ya Fedha ambayo ndiyo imekabidhiwa jukumu lakusimamia hazina ya Taifa hili inaleta kauli mbili zisizoeleweka,fedha zetu zipo salama kiasi gani? Tutashangaa kwelitunaposikia wizi kama wa miaka iliyopita wa mabilioni ya EPAya madeni hayahaya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tafadhali,Mheshimiwa Waziri atueleza katika hizi kauli mbili, ipi ipo sahihi.Tumetumia shilingi trilioni 1.666 au tumetumia shilingi trilioni2.227 kulipa deni la Taifa na kama kuna kosa Waziri afafanueni kosa lipi lililofanywa na Wizara, wataalam mamia wa Wizarahawakuliona mpaka limeletwa Bungeni hapa anakuja kukiri

Page 171: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

171

kwamba kuna makosa. Majibu haya rahisirahisi hayahayatatosheleza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba WaheshimiwaWabunge waniunge mkono, hili suala la deni la Taifa nimsalaba mkubwa kwa Taifa. Mimi nilikuwa naangalia kwenyekitabu hiki. Kwenye kitabu hiki, Fungu 22, fedhatunazoambiwa tuidhinishe mwaka huu kwa ajili ya kulipa ribatu ya deni la Taifa, ni shilingi trilioni 1.29, ni mapesa mengikweli kwa interest payments alone, zipo kwenye kitabu hiki.Sasa kama hatupewi majibu yanayotosheleza ni kipikinalipwa kwa kweli tunaweza tukawa tunapitisha fedhahapa zinakwenda kwenye mifuko binafsi, nchi yetu inazidikuagamia kwa sababu ya malipo ya aina hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba WaheshimiwaWabunge waniunge mkono, suala hili lijadiliwe, suala hili nikubwa, ni zito, niungeni mkono tupate majibu sahihi kutokaSerikalini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Unajua, tatizo hata mimi ni Mhasibu,unajua mahesabu hayana lugha mbili, mimi nakuambiawengine watakaounga mkono hapa, watatupigia kelele tuhapa sisi laiti ungekuwa umeandaa watu na kuwafundishahaya matrilioni, sasa Waziri tujibu tena, hata Naibu unawezakujibu.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA SALUM MKUYA):Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Mheshimiwa Waziri,Mheshimiwa Tundu Lissu alikuwa rafiki yake, mie kaka yangunaomba...

MWENYEKITI: Naomba mzungumze kwa taratibumpaka sisi wote ituingie vizuri.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA SALUM MKUYA):Sawa.

Page 172: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

172

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipengele cha kwanza cha17 na kama utaangalia vizuri title yake ni usimamizi wa denila Taifa ambapo hapo kuna malipo ya madeni ambayoyamefikia shilingi trilioni 1.6. Nachotaka kuelezea ni kwambakifungu hiki kingine cha 127, ni deni la Taifa. Kweli kwa mtuambaye hayupo katika mahesabu inaleta confusion. Ndipopale ambapo Mheshimiwa Waziri alipoona kwamba penginekama kutakuwa kuna makosa kwa sababu yeye alisomasummary, lakini kitabu hiki kipo. Deni la Taifa ni vote nzimayaani ile vote 22 inajulikana ni deni la Taifa lakini ndani yakemna hilo deni, mikopo tuliyokuwa tumekopa ndani, lakinivilevile kuna vitu vingine vingi. Kwa mfano, vote ya deni laTaifa, vote 22 ndani yake mna hilo deni la Taifa ambayo nishilingi trilioni 1.6, lakini ndani yake kuna fedha ambazozimewekwa kwa ajili ya michango ya kulipia katika Mifukoya Hifadhi ya Jamii yaani michango ya wafanyakazi woteimo katika hiyo vote 22. Vilevile kuna michango ya kulipiaBima ya Afya inayotokana na mishahara, kwa hiyo, inalipiwakule. Pia ndani ya vote hiyohiyo 22 ambayo inajulikana kamadeni la Taifa ndani yake kuna stahili za Maafisa wa Serikaliambao wanalipwa malipo yao kupitia deni la Taifa, kwamfano, Makamishna hawa wa Tume ya Kurekebisha Sheria,mishahara yao na mafao yao yote yamo humo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nachotakakuelezea hapa ni kwamba deni la Taifa ni title kubwa, ni vote,lakini ndani yake kuna vipengele vingi. Kuna hilo deni la Taifa,kuna matumizi kama hayo ya kulipia wafanyakazi ambaowanastahili kulipwa kutokana Fungu hili, kuna matumizi yakulipia Bima za Afya, kuna matumizi ya kulipia Mifuko yaPensheni na ndiyo hii yote sasa kwa umoja wake ndiyoimewekwa katika hicho kipengele cha 127 ile ya kule 17 nikile ki-component kidogo tu cha kulipia yale madeniyenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mtoa hoja.

Page 173: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

173

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,haya majibu kwa kweli hayatoshelezi kabisa. Haiwezekani,kama haya anayoyasema Mheshimiwa Naibu Waziri ni yakweli yangesemwa katika hotuba yao kwambatunapozungumzia Fungu 22 – Deni la Taifa tunazungumziana mishahara, posho, zote hizo ambazo anazisema sasa hivi.Ukiliacha hivi, ukasema kwamba matumizi ya Deni la Taifamatrilioni yote haya, nani atakayeelewa kwamba kwenyeposho mmelipa kiasi gani, kwenye michango ya Mifuko yaJamii mmelipa kiasi gani, haiwezi kuwa hivi, hii ni ya jumla,haiwawezeshi Waheshimiwa Wabunge kupata ufahamu wanamna hizo fedha zimefikia idadi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naona watuwanagunaguna, hili suala sio dogo kama Serikali inaletamahesabu ya jumlajumla na kama alivyosema Waziri kunamakosa yamefanyika, ni ukosefu wa umakini. Huwezi ukaletafigure ambazo hazielezeki. Tukiuliza ndio unaanza ooohunajua, haiwezekani tunataka tuletewe taarifa ambazozinaelezeka. Mtu ukimweleza kwamba hii figure ya shilingitrilioni 2.227 inatokana na vitu hivihivi inajieleza yenyewekatika hotuba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda kwa siku nyingine,kwa kesho na kesho kutwa Mheshimiwa Waziri na watu wakomlete Bungeni vitu vilivyopikika vikaiva. Hivi vitu half cooked,havitakubalika siku zingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Waziri kuna maelezo mengine labda uki-clearile ya kusema ulisema kuna makosa.

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, sikusemakuna makosa. Nimesema kama maelezo hayakueleweka,hakuna makosa. Vote 22 iko wazi na mimi nikaruhusu NaibuWaziri ili tutumie mdomo mwingine lakini hakuna makosayoyote, I have all the details here, kwa hiyo hakunakubabaisha hapa, kila kitu kiko-clear. (Makofi)

Page 174: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

174

MWENYEKITI: Unajua kila mtu na fani yake, miminimeelewa kabisa. (Makofi/Kicheko)

(Kifungu Kilichotajwa Hapo Juu Kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila Mabadiliko Yoyote)

Kif. 1002 - Finance and Accounts…….....Tshs. 1,287,129,000/=Kif. 1003 - Policy and Planning................Tshs. 29,311,935,000/=Kif. 1004 - Legal Services…………….............Tshs. 842,046,000/=Kif. 1005 - Government Comm. Unit.........Tshs. 1,092,517,000/=Kif. 1006 - Internal Audit Unit ………….......Tshs. 377,886,000/=Kif. 1007 - MCC Tanzania…………….............Tshs. 500,000,000/=Kif. 1008 - Procurement Mgt. Unit…...............Tshs.617,381,000/=Kif. 3001 - Internal Auditor General………Tshs.3,610,951,000/=Kif.5001-Government Asset

Management Div…........................Tshs.4,520,908,000/=Kif. 6001 - Financial Mgt. Inform.

Systems Division….....................Tshs. 2,951,519,000/=

(Vifungu Vilivyotajwa Hapo Juu Vilipitishwa na Kamati yaMatumizi Bila Mabadiliko Yoyote)

Fungu la 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha

Kif.1001 - Administration and HR Management…......................Tshs.1,610,389,000/=

Kif. 1002 - Internal Audit Unit …......................Tshs.71,090,000/=Kif. 2001 - Technical Department…..............Tshs.269,360,000/=Kif. 2002 - Zanzibar Office…...........................Tshs.113,585,000/=

(Vifungu Vilivyotajwa Hapo Juu Vilipitishwa na Kamati yaMatumizi Bila Mabadiliko Yoyote)

Fungu la 13 – Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu

Kif. 1001 - Administration and HR Management…...................Tshs. 1,132,777,000/=

Kif. 1002 - Finance and Accounts Unit...........Tshs. 62,290,000/=Kif. 1003 - Internal Audit Unit….........................Tshs.32,753,000/=Kif. 1004 - Monitoring Unit….......................…Tshs.344,810,000/=

Page 175: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

175

Kif. 1005 - Inspection Unit………...............…Tshs.123,150,000/=Kif. 1006 - Procurement Mgt. Unit...................Tshs. 14,570,000/=Kif. 1007 - Legal Service Unit…...................….Tshs. 19,420,000/=Kif. 1008 - Management Information

Systems Unit….................................Tshs.215,020,000/=

(Vifungu Vilivyotajwa Hapo Juu Vilipitishwa na Kamati yaMatumizi Bila Mabadiliko Yoyote)

Fungu la 21 – Hazina

Kif. 1009 - Public Procurement Policy Unit (PPU) ……….....................Tshs.1,142,312,000/=

Kif. 2001 - Government Budget Division…...............Tshs.1,170,668,174,000/=

Kif. 2002 - Policy Analysis Division……...Tshs.196,226,540,000/=Kif. 4001 - External Finance Division….......Tshs.6,535,158,000/=Kif. 4002 - Public Private Partnership

Unit..............................................Tshs.1,032,400,000/=Kif. 7001- Poverty Eradication an

Empowerment……....................Tshs.2,537,982,000/=

(Vifungu Vilivyotajwa Hapo Juu Vilipitishwa na Kamati yaMatumizi Bila Mabadiliko Yoyote)

Fungu 22 – Deni la Taifa

Kif. 1001 – Administration ande HR Management…................Tshs. 3,319,017,772,000/=

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nipate ufafanuzi wa kasma 250500 - InterestPayments on Long-term Debt to Other General GovernmentUnits ambayo imeongezeka kutoka shilingi bilioni 311 zamwaka jana mpaka shilingi bilioni 424.7 za mwaka huu.Naomba nipate ufafanuzi haya malipo ya ribayameongezeka kwa kiasi kikubwa hiki kwa sababu gani kwazaidi ya shilingi bilioni 114, ni sababu zipo ambazo zinafanyamalipo ya riba tu yaongezeke kwa kiasi kikubwa hivi katikakasma hiyo?

Page 176: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

176

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu, si umeionakasma anayoizungumzia?

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti,inazungumzwa interest payments, hii ni cost of borrowing. Hiini gharama ya ku-service mikopo ambayo ilikopwa mudamrefu. Tuko katika kipindi cha convergence, tuna mikopomingi tuliyokopa miaka ya 20, 30, 40 sasa ina-mature. Hukonyuma tumekuwa na moratorium period ya muda mrefu sasamaturities zimeingia. Sasa kadri maturities zina-converge,volume ya ulipaji nayo inakuwa kubwa. Kwa hivyo, riba nimkusanyiko wa madeni ambayo tulikopa kwa muda mrefuhuko nyuma lakini si kwamba riba ya mikopo tuliyochukualeo au juzi.

(Kifungu Kilichotajwa Hapo Juu Kilipitishwa na Kamati yaMatumizi bila Mabadiliko Yoyote)

Fungu la 45 – Ofisi Taifa ya Ukaguzi

Kif. 1001 - Administration and HR Management…........Tshs.25,095,005,300/=Kif. 1002 - Finance and Accounts Unit...Tshs. 2,259,605,600/=Kif. 1003 - Internal Audit Unit….......................Tshs.574,033,400/=Kif. 1004 - Ministerial Audit Division….........Tshs. 7,702,036,600/=Kif. 1005 - Regional and Local Govt Audit Division…..................... Tshs.11,781,903,800/=Kif. 1006 - Value For Money Audit Div.......Tshs.2,260,942,000/=Kif. 1007 - Treasury Audit Division…...........Tshs. 3,076,793,000/=Kif. 1008 - Techn. Support, Research

and Consultancy …...............Tshs. 4,656,094,300/=

(Vifungu Vilivyotajwa Hapo Juu Vilipitishwa na Kamati yaMatumizi Bila Mabadiliko Yoyote)

Page 177: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

177

MIPANGO YA MAENDELEO

Fungu 7 – Ofisi ya Msajili wa Hazina

Kif. 1001 - Administration and HR Management….............Tshs.1,665,300,000/=

(Kifungu Kilichotajwa Hapo Juu Kilipitishwa na Kamati yaMatumizi Bila Mabadiliko Yoyote)

Fungu la 13 – Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu

Kif. 1001 - Administration and HR Management…................Tshs.399,685,000/=

(Kifungu Kilichotajwa Hapo Juu Kilipitishwa na Kamati yaMatumizi Bila ya Mabadiliko Yoyote)

Fungu 21 – Hazina

Kif. 1009 - Public Procurement Policy Unit (PPU)…........................Tshs. 876,000,000/=

Kif. 2001 - Government Budget Div.....….Tshs. 3,748,000,000/=Kif. 2002 - Policy Analysis Division….........Tshs.22,458,234,000/=Kif. 4001 - External Finance Division….......Tshs. 9,217,928,000/=Kif. 7001 - Poverty Eradication

and Empowerment.........…..Tshs. 1,890,000,000/=

(Vifungu Vilivyotajwa Hapo Juu Vilipitishwa na Kamati yaMatumizi Bila ya Mabadiliko Yoyote)

Fungu 23 - Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali

Kif. 3003 - Financial Management…........Tshs. 2,590,147,000/=Kif. 3004 - Financial Systems ........….......Tshs. 1,646,400,000/=Kif. 4001 - Local Government Finances…..Tshs.519,000,000/=

(Vifungu Vilivyotajwa Hapo Juu Vilipitishwa na Kamati yaMatumizi Bila ya Mabadiliko Yoyote)

Page 178: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

178

Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

Kif. 1001 - Administration and HR Management….....................Tshs. 7,500,000,000/=

Kif. 1002 - Finance and Accounts Unit.................................................Tshs. 6,199,100,000/=

(Vifungu Vilivyotajwa Hapo Juu Vilipitishwa na Kamati yaMatumizi Bila ya Mabadiliko Yoyote)

Fungu 50 – Wizara ya Fedha

Kif. 1001 - Administration and HR Management…..................... Tshs. 407,000,000/=

Kif. 1003 - Policy and Planning…. ............ Tshs.11,183,488,000/=Kif. 1005 - Government

Communication Unit....................Tshs. 623,500,000/=Kif. 1007 - MCC Tanzania…................... Tshs. 213,612,181,000/=Kif. 3001 - Internal Auditor General….........Tshs.2,639,000,000/=Kif. 5001 - Government Asset Mgt. Div…. Tshs. 2,510,000,000/=Kif. 6001 - Financial Mgt.

Inform System Division…............Tshs.2,694,000,000/=

(Vifungu Vilivyotajwa Hapo Juu Vilipitishwa na Kamati yaMatumizi Bila ya Mabadiliko Yoyote)

(Bunge lilirudia)

T A A R I F A

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kutoataarifa kwamba Kamati ya Matumizi imeyapitia Makadirioya Matumizi ya Wizara ya Fedha na Ofisi ya Mkaguzi Mkuuwa Serikali kwa mwaka wa fedha 2013/2014, kifungu kwakifungu na kuyapitisha pamoja na mabadiliko yake. Hivyo,naomba kutoa hoja kwamba sasa Bunge lako Tukufuliyakubali makadirio haya.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

Page 179: BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGEparliament.go.tz/polis/uploads/documents/1462185249-HS-11-44-2013.pdf · tuna hakika kwamba, mtu ambaye amefoji cheti kama sote tutakuwa wawazi

6 JUNI, 2013

179

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Makadirio ya Matumizi kwa Wizara ya Fedha kwa Mwaka2013/2014 yalipitishwa na Bunge)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kwanza kabisa,napenda nichukue nafasi ya pekee kumpongezaMheshimiwa Waziri na Manaibu wake, Mawaziri akina mama,kwa kazi nzuri kabisa waliyoifanya mpaka tumeshindwa kuwana maswali mazito. (Makofi)

Pia ni kwa sababu ya kazi nzuri ambayo Hazina nawasaidizi wao wamefanya lakini kama walivyosemawachangiaji, leo michango ya Wizara yenu ilikuwa one ofthe best, wachangiaji waliochangia leo walichangia vizurimpaka tunasahau kugonga kengele. Message ambayowaliileta katika michango yao, tuimarishe ukusanyaji wamapato. Nadhani ndio message iliyokuwepo na kuwezakuziba mianya mbalimbali ambayo inaweza kuwa ni sababuya kuondoka matumizi kwa sababu kuomba tu fedha bilaya kutumia zile tulizonazo vizuri na kutafuta nyingine kwa kwelitutashindana humu ndani. Kwa hiyo, tunawapongezenimuendelee kufanya kazi iliyo njema na tunawasubiri tenatarehe 13, nadhani mtaelewana na budget committeeyangu.

Waheshimiwa Wabunge, kesho tutakuwa na maswaliasubuhi halafu tutakuwa na Uchaguzi wa nafasizilizotangazwa juzi, naomba wote mhudhurie.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayo,nawatakieni jioni njema, naahirisha kikao cha Bunge mpakakesho saa tatu asubuhi.

(Saa 1.6 Usiku Bunge liliahirishwa Mpaka Siku ya Ijumaa,Tarehe 7 Juni, 2013, Saa Tatu Asubuhi)