covid-19 mabadiliko mct · kutoka jiji la china la wuhan mwezi desemba, janga hilo linaleta balaa...

17
Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikisha viwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji Jarida la Baraza la Habari Tanzania Toleo la 152, April, 2020 ISSN 0856-874X Mwito wa kuwaaachia huru waandishi Hofu ya IPI yathibitishwa Matangazo yakwaza vyombo vya habari Uk 7 Uk 17 Uk 10 Covid-19 yalazimisha mabadiliko MCT Mwongozo kutoka MCT: Uandishi wa Habari za Janga la Korona NDANI

Upload: others

Post on 14-Oct-2020

4 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikishaviwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji

Jarida la Baraza la Habari TanzaniaToleo la 152, April, 2020ISSN 0856-874X

Mwito wa kuwaaachia huru waandishi

Hofu ya IPI yathibitishwa

Matangazo yakwaza vyombo vya habari

Uk 7 Uk 17Uk 10

Covid-19 yalazimisha

mabadiliko MCT

Mwongozo kutoka MCT: Uandishi wa Habari za

Janga la KoronaNDANI

Page 2: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

BODI YA UHARIRI:Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji – MCTDavid Mbulumi Meneja ProgramuHamis Mzee Mhariri

MAWASILIANOKwa Maoni na Malalamiko:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzani (MCT)S.L.P. 10160, Dar es SalaamSimu: +255 22 27775728, 22 2771947Simu ya Kiganjani: +255 784 314880Fax: + +255 22 2700370Baruapepe: [email protected]: www.mct.or.tzFacebook:- www.facebook.com/mediacounciltanzania Twiter:- www.twitter.com/mctanzania

2

TAHARIRIJarida la Baraza la Habari Tanzania

Vyombo vya habari viachwe vifanyekazi kwa umakini na uhuru Ni ukweli unaouma kwamba mlipuko wa janga la

virusi vya corona umeikumba duniani inahaha bila kutegemea. Ni wa aina yake, na kwamba hakuna kitu cha aina yake kimewahi kutokea katika miaka

ya karibuni. Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga

hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri, wenye nguvu , wanataaluma na hata wanasiasa pia.

Kimsingi dunia inahaha huku wanasayansi wanafanyakazi ya ziada kutafuta chanjo ya kukabiliana na janga hili.

Hali ilivyo sasa kwa vyombo vya habari kuripoti janga hili ni eneo jipya kabisa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kitaifa limetoa mwongozo wa jinsi vyombo vya habari vitakavyo ripoti janga la virusi vya corona.

Virusi hivyo vimeathiri jamii kwa kiasi kikubwa. Ni tatizo la afya, lakini tatizo la kiuchumi, kitamaduni na hata michezo na kuathiri shughuli zote za kibinadamu na taifa.

Kwa vyombo vya habari licha ya mwongozo uliotolewa na MCT, jinsi ya kuandika habari za janga hili imekuwa mtihani kama ilivyotokea kuwa baadhi ya vyombo vya habari tayari vimeteleza.

Ni bahati mbaya baadhi ya vyombo vya udhibiti vimevipa adhabu kali baadhi ya vyombo vinavyodaiwa kuwa vimekosea, hali ambayo inaweza kuwatisha wanahabari kuandika kwa ukamilifu habari za ugonjwa huo.

Vyombo kadhaa vya habari vimetozwa faini kubwa na kuamriwa kuomba radhi na pamoja na hayo chombo kimoja na mwanahabari mmoja wamesimamishwa kwa miezi sita.

Katika jitihada za kuepusha adhabu kali, MCT imewakumbusha wanahabari kusoma na kuelewa muongozo iliyotoa kuhusu kuandika habari za virusi vya corona, na pia kuwataka wenye mamlaka kuzingatia hali halisi kuwa vyombo vya habari vinapitia katika mazingira mageni kabisa.

Baraza linaamini kwamba kinachotakiwa sasa ni kuelimishana na siyo kukimbilia kutoa adhabu.

Ni muhimu kwa wakati huu kuwezesha vyombo vya habari kufanyakazi kwa umakini, uwajibikaji na uhuru.

MCT, MSHINDI WA TUZO YA IPI 2003

FREE MEDIA PIONEER

Mtumishi wa Serikali, Humphrey Tillya (kulia) akiwa na Mkuu wa Maudhui wa kampuni ya MCL ambaye pia ni Kaimu Mhariri wa gazeti la Mwananchi,Angetille Osiah walipofika mbele ya Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) ambapo malalamiko ya Tillya dhidi ya gazeti hilo yalisikilizwa. Habari Uk. 7.

Page 3: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

3

Habari

Toleo la 152, April, 2020

Na Mwandishi wa Barazani

Kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19 uliosambaa duniani kote, Baraza la Habari Tanzania(MCT)

limelazimika kurekebisha uendeshaji na utendaji wa kazi na majukumu yake.

Katika barua iliyosambazwa na Baraza kwa wadau na washirika wake Katibu Mtendaji, Kajubi Mukajanga amesema “hizi ni nyakati ngumu kwetu sote, na ni muhimu tukashikamana na kutiana nguvu huku tukihimizana kutenda yale yatakayosaidia kuliondosha janga hili mapema nchini mwetu na duniani kote”.

Alisema kuwa Baraza limedhamiria kuendelea kutoa huduma kwa wadau wake kwa kadri inavyowezekana, lakini pia limelazimika kufanya marekebisho katika namna linavyoendesha programu zake na jinsi litakavyofanya kazi na wadau na washirika wake.

Baraza limeeleza katika barua hiyo kuwa limeamua kwamba kwa kiasi kikubwa wafanyakazi wake watafanyia kazi majumbani kwao. Uendaji ofisini utakuwa pale tu ambapo italazimu.

Mawasiliano na wadau na washirika yanaendelea kwa njia za simu, barua pepe, barua na mikutano ya kidijitali kupitia teleconference, Skype au Zoom, imeeleza barua hiyo iliyosainiwa na Mukajanga.

Baraza pia limeeleza kuwa limechukua hatua ya kuweka vifaa vya kujikinga kwa wafanyakazi wake na wageni watakaokuja katika ofisi zake. Pia limeweka mashine za vieuzi ofisini kwake, pamoja na vitakasa, barakoa na glavu, na kuweka matangazo ya kuhimiza watu kunawa mikono na sabuni kila mara wawapo ofisini na kwingineko.

Wafanyakazi wa Baraza wamepewa mafunzo kuhusu kujikinga na virusi vya corona wawapo kazini, nyumbani na kwingineko.

Barua ya Baraza imeeleza kuwa katika uendeshaji programu zake kumekuwa na mabadiliko kadhaa

Janga la COVID 19 lasababishaMCT kufanya marekebisho

Mtumishi wa Baraza wa Habari Tanzania, Elizabeth Munisi, akitumia kitakasa mikono ikiwa ni hatua mojawapo ya Baraza dhidi ya virusi vya corona.

Page 4: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

4

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

ambapo kwa upande wa uragbishi na mafunzo, shughuli zote zinazohitaji mikusanyiko ya watu zimeahirishwa hadi hali itakaporuhusu.

“Hii imeathiri shughuli zetu nyingi za mafunzo na mikutano mikubwa, ikiwamo pia EJAT 2019”, imeeleza barua hiyo ya Bazara kwa washirika wake na wadau.

Kuhusu EJAT, barua hiyo imeeleza kuwa Baraza linawasiliana na washirika wake na muda utakapowadia litawatangazia hatima yake. Pia linawasiliana kuhusu uwezekano na usahihi wa kuongeza kipengele cha uandishi wa habari za janga la corona katika EJAT 2020 ambayo itaadhimishwa mwakani.

Katika kukabiliana na janga la Covid 19, Baraza limetoa na kusambaza Mwongozo wa Uandishi wa Habari za Corona na linawahimiza wanahabari kuusoma na kuuzingatia ili kuhakikisha weledi

na umakini katika kuripoti janga hili.

Kuhusu usuluhishi wa malalamiko, Baraza litaendelea na shughuli hii zaidi kwa njia ya mawasiliano.

Baruahiyo imeeleza kuwa itakapolazimu watu kukutana, basi wataruhusiwa watu wawili tu kutoka upande wa mlalamikaji na wawili tu kutoka upande wa mlalamikiwa lakini waandishi wa habari hawataalikwa, na badala yake watajulishwa matokeo ya shauri kwa njia ya taarifa ambayo itatumwa kwa barua pepe.

Shughuli za utetezi wa haki ya habari zitaendelea bila kuwa na semina na makangomano, Baraza limesema na kuongeza kuwa linawaasa watoa habari rasmi wasiwakwaze wanahabari kwa kuwanyima taarifa.

Baraza linatambua uwapo wa vikomo vya kitaaluma na kitabibu katika kutoa habari zinazohusu wagonjwa, lakini linavitaka vyanzo kutoa habari zisizokuwa na makatazo

bila kuzichelewesha, imeelza barua hiyo. Kuhusu kesi zinazohusu utetezi wa haki za habari zilizoko mahakamani, Baraza limeeleza katika barua hiyo kuwa zitaendelea kadri mahakama zitakavyoamua, na wadau wanashauriwa kufuatilia kwa karibu. Baraza litawajulisha kila mara taarifa na maamuzi yatakapotolewa.

Ufuatiliaji wa vyombo vya habari, utaendelea ambapo wanafunzi wa vyuo vya uandishi ambavyo vilishaanzisha utaratibu huo wanashauriwa kuendelea kukusanya taarifa hata wawapo majumbani.

Pia Baraza litaendelea kuwasiliana na wahariri Iakini ziara za Kamati ya Maadili ya MCT katika vyuo na vyombo vya habari zimesitishwa hadi hali itakapokuwa nzuri. “Baraza linakaribisha ushauri wowote kutoka kwa wadau na washirika wake kuhusu jinsi ya kuboresha huduma zake katika kipindi hiki kigumu, na litaendelea kuwasiliana kila kutakapokuwa na haja.

Janga la COVID 19 lasababishaMCT kufanya marekebishoInatoka Ukurasa wa 3

Ofisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania, Paul Mallimbo achambua magazeti akiwa amevalia barakoa na glavu.

Page 5: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Kutokana na kuendelea kusam-baa kwa janga la virus co-rona, mashirika ya uhuru wa vyombo vya habari na haki za

binadamu yametoa mwito kwa wakuu wanchi 10 za Afrika kuwataka wawaachie huru waandishi wa habari kutoka magerezani na kuwaambia kuwa uandishi wa habari usibebe ad-habu ya kifo.

Wanahabari waliofungwa hawana uwezo wa kudhibiti mazingira yao, hawawezi kuamua kujitenga na mara nyingi wananyimwa huduma ya afya, mashirikia 81 likiwamo Baraza la Habari Tanzania yameeleza katika barua yao kwa wakuu hao wa nchi.

Kwa waandishi waliofungwa katika nchi zilizokubwa na janga la corona, uhuru sasa ni suala la kufa na kupona imeeleza barua hiyo kwa Marais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria, Patrice Talon wa Benin, Pierre Nkurunziza wa Burundi , Paul Biya wa Cameroon, Idriss Deby wa Chad, Abdel Fattah el-Sisi (Misri), Isaias Afwerki wa Eritrea, Paul Kagame wa Rwanda na Mawaziri Wakuu - Abiy Ahmed Ali wa Ethiopia na Saad-Eddine ElOthmani wa Morocco.

Wengi wa waandishi hawa wameshikiliwa kizuizini bila mashtaka kwa vipindi virefu na wanakabiliwa na hali mbaya kiafya kutokana na hali mbaya ya magereza yaliyofurika ambapo wamepata malaria, kifua kikuu na magonjwa mengine.

Mashirika yaliyoandika barua hiyo ikiwemo Kamati ya Kutetea Waandishi (CPJ) yamesisitiza kwa wakuu hao wa nchi kuwa achia kila mwandishi aliyefungwa na kulinda

vyombo huru vya habari na mtiririko wa habari katika kipindi hiki muhimu.

Hatua hii inafuatia barua ya wazi iliyoandikwa na CPJ kwa viongozi duniani kuwataka kuwaachia wanahabari wote waliofungwa kutokana na kazi zao.

Kutokana na idadi kubwa ya wanahabari waliofungwa katika magereza Barani Afrika, mashirika hayo ya uhuru wa habari na haki za binadamu yamesisistiza mwito huo kwa nchi husika katika kipindi hiki kigumu .

Kulingana na utafiti wa CPJ wa karibuni uliofanyika Desemba 1,2019 kulikuwa na waandishi waliofungwa wapatao 73 Afrika ikiwemo Misri (26), Eritrea (16) Cameroon (7), wanne kila nchi Burundi, Rwanda na Morocco na mmoja kila nchi -Algeria, Benin, Nigeria, Chad, Tanzania, Ethiopia, Somalia, Comoros, Jamhuri ya

Kidemokrasi ya Congo na Sudan Kusini.

Ilipofika Machi 31,waandishi 11 wametoka gerezani kutoka Somalia, Ethiopia, Tanzania, Nigeria, DRC, Algeria, Comoros, Sudan Kusini na Misri, kulingana na utafiti wa CPJ.

Hata hivyo waandishi wengine sita wamefungwa tangu Desemba 1 na wapo gerezani hadi sasa wakiwemo wanne wa Ethiopia na mmoja mmoja Cameroon na Algeria.

Barua hiyo iliyoandikwa kwa lugha za Kiingereza na Kifaransa imenakiliwa kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Afrika Kusini Matamela Cyril Ramaphosa, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Moussa Faki, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus.

5

Habari

Toleo la 152, April, 2020

Waachieni wanahabari waliofungwa, Wakuu wa Afrika waambiwa

Baadhi ya wakuu wa nchi za Afrika ambao wametakiwa kuwaachia huru waandishi wa habari waliofungwa kutokana na kuenea kwa virusi vya corona Juu kutoka kushoto ni Marais Pierre Nkurunziza wa Burundi, Abdel Fattah el-Sisi wa Misri na Paul Kagame wa Rwanda. Chini kutoka kushoto ni Marais Paul Biya wa Cameroon, Isaias Afwerki wa Eritrea na waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed Ali.

COVID – 19

Page 6: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

6

Fursa

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Page 7: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) imevi-agiza vyombo vya habari kuz-ingatia kanuni za maadili ya

uandishi wa habari hasa kwa suala la ulinganifu.

Kamati imesema lengo la kanuni ya ulinganifu ni kupata maoni au mtizamo wa upande wa pili.

“Daima, habari zenye mgogoro zifanyiwe ulinganifu kwa lengo la kupata pande zote mbili na sio kutafuta mshindi”, Kamati hiyo ilisema katika uamuzi wake kuhusu shauri la lalamiko la wakazi wa Mtaa wa Pwani-Tegeta, Dar es Salaam, dhidi ya Radio Clouds FM kuhusiana na habari iliyotangazwa katika kipindi cha Power Breakfast kuhusu mgogoro wa mpaka uliopo katika mtaa wao.

Kamati hiyo, iliyokaa Aprili 29, 2020, ilisikiliza mashauri mawili ambapo shauri la pili liliwasilishwa na Mtumishi wa Serikali, Bw. Humphrey Tillya, akilalamikia habari iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi la tarehe 24 Februari, 2020. Bi. Rosemary Mwakitwange aliwakilisha wakazi wa Mtaa wa Pwani-Tegeta ambapo Afisa Uhusiano Simon Simalenga na mtangazaji Redemptus Siza waliwakilisha Clouds FM.

Katika uamuzi wake wa shauri hilo, Kamati iliviasa vyombo vya habari kuandika habari za mahakamani kwa kufuata kanuni za uandishi wa habari wa mahakama.

Aidha, Kamati iliipongeza Clouds FM kwa kusitisha kurusha habari hiyo yenye mgogoro mara baada ya kuelezwa kwamba mgogoro huo una kesi mahakamani.

Kamati imeishauri Clouds FM kufuatilia habari hiyo kama itakavyoendelea mahakamani na kuiripoti kwa usahihi mwenendo

wake. “Vyombo vya habari vikianza kuandika kesi basi viripoti na matokeo ya kesi,” Kamati iliagiza.

Kamati pia iliwapongeza walalamikaji kwa kuleta malalamiko yao Baraza la Habari Tanzania (MCT), kwa usuluhishi.

Katika shauri la pili, Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania ikiwa chini ya Mwenyekiti wake, Jaji Juxon Mlay, pia imelikuta na hatia gazeti la Mwananchi ya kuandika habari ya upande mmoja bila kuzingatia kanuni za ulinganifu katika habari hasa zinazohusiana na tuhuma.

Katika shauri hilo, Mtumishi wa Serikali, Bw. Tillya, alilalamikia habari iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi la tarehe 24 Februari, 2020. Alisema kuwa habari hiyo imemshushia heshima yake, kuhatarisha ajira yake na kumdharaulisha mbele ya wana jamii wa Wilaya ya Pangani.

Baada ya kuwasikiliza Tillya na Mkuu wa Maudhui wa MCL ambaye pia ni Kaimu Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Angetile Osiah, Kamati hiyo pia imeona kulikuwa na tatizo la

usahihi na utimilifu katika habari husika.

Aidha Kamati hiyo imebaini kuwa mlalamikaji hakutendewa haki na mwandishi aliyeandika habari hiyo kwa kushindwa kumpa nafasi ya kueleza utetezi wake dhidi ya tuhuma dhidi yake.

Kamati imeviagiza vyombo vya habari nchini kuweka mifumo mizuri ya kufuatilia waandishi wao wa mikoani, na pia imewakumbusha wananchi wasioridhika na jambo katika vyombo vya habari kutumia huduma za Usuluhishi za Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Pamoja na maamuzi hayo, Kamati imempongeza mlalamikaji kwa kuleta malalamiko yake Baraza la Habari Tanzania (MCT), lakini pia Kamati imempongeza Mkuu wa Maudhui wa MCL na Kaimu Mhariri wa gazeti la Mwananchi kwa kuitikia mwito na kufika katika kikao cha usuluhishi.

Kamati hiyo, inaundwa na Mwenyekiti wake, Jaji Juxon Mlay, Bibi. Edda Sanga ambaye ni Makamu Mwenyekiti, na wajumbe ni Bi. Anna Henga, Bw. Wallace Mauggo na Bi. Benardina Chahali.

7

Habari

Toleo la 152, April, 2020

Habari lazima ziwe na ulinganifu, Kamati ya Maadili yaagiza

Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania ikiendelea na kikao cha usuluhishi.

Page 8: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

8

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Mwananchi mtandaoni yafungiwa miezi sita

Na Mwandishi wa Barazani

Toleo la mtandaoni la gazeti la Mwananchi limesimamishwa kwa miezi sita na Kamati

ya Maudhui ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Tanzania (TCRA).

Kampuni ya MCL inayochapisha toleo hilo imepigwa faini ya Tsh. milioni tano kwa kukiuka kanuni za mawasiliano ya kieletroniki na posta ya mwaka 2018.

Kulingana na taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkurugenzi wa TCRA, ilidhihirishwa kuwa Aprili 13, 2020 katika kurasa zake toleo hilo la mtandaoni lilichaopisha habari zisizo za kweli zilizosababisha taharuki kinyume na kanuni namba 5(1) na 12(1) ya mawasiliano ya kieletroniki na posta.

Imeelezwa kuwa maofisa wa gazeti hilo walipofika mbele ya Kamati ya Maudhui Aprili 15, 2020 walikiri kuwa walikiuka kanuni hizo.

Katika hatua nyingine mwandishi wa habari wa Zanzibar anayeandikia gazeti la Tanzania Daima amesimamishwa kwa miezi sita kufanyakazi ya kuandika habari kuanzia Aprili 20,

2020 kwa kile ambacho idara ya habari visiwani imedai kukiuka maadili ya uandishi.

Talib Ussi Hamad anadaiwa kutoa taarifa kuhusu mgonjwa wa virusi vya corona bila idhini ya mgonjwa huyo jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya kitibabu.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Idara ya Habari ya Zanzibar, Dk. Juma Mohamed Salum akikariri vifungu 41, 42(a) na (b) vya Sheria ya Magazeti, Vitabu na Wakala wa Taarifa Namba 5 ya 1988 na marekebisho yake Namba 8 ya 1997, mwandishi Talib Ussi Hamad haruhusiwi kukusanya, kusambaza na kufanya shughuli yoyote ya uandishi wa habari kwa miezi sita.

Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International limepinga hatua ya kusimamishwa mwandishi huyo, toleo la mtandaoni la Mwananchi na vyombo vingine vitatu vya habari - Star Media Tanzania Ltd, Multichoice Tanzania Ltd na Azam Digital Broadcast Ltd – ambavyo Aprili 2 kila kimoja kilitozwa faini ya milioni tano na kutakiwa kuomba radhi kwa kutangaza habari

ya kupotosha kuhusu jinsi nchi inavyoshughulikia janga la virusi vya corona.

Katika taarifa, Deprose Muchena, Mkurugenzi wa Amnesty International kwa Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika ametaka mamlaka kuondoa mara moja amri ya kumfungia mwandishi na vyombo vya habari ambavyo amesema vimechukuliwa hatua kwa kufanya kazi zao.

“Kupata taarifa ni muhimu katika mapambano dhidi ya covid-19, lakini serikali ya Tanzania inachagua kubinya wanahabari na vyombo vya habari vinavyoripoti kuhusu ugonjwa huo. Hatua hizi za karibuni ni za wazi kuwa ni za kisiasa na kwamba msimamo wa serikali ya Tanzania kupinga kukoselewa ndiyo unaosababisha kubinywa haki za wanahabari na kuathiri vipato vyayo”, alisema Muchena.

Vyombo vya habari vina wajibu muhimu katika kuwahabarisha wananchi kuhusu hali halisi na hatua zinazochukuliwa na serikali dhidi ya covid-19.Uwezo wa kufanyakazi kwa uhuru usikwazwe, Mkurugenzi huyo wa Amnesty International amesema.

l Mwandishi wa Zanzibar anayeandikia Tanzania Daima afungiwa

l Shirika la kimataifa la haki za binadamu Amnesty International lataka kuachwa mara moja kufungiwa mwandishi na vyombo vya habari

Page 9: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

9

Toleo la 152, April, 2020

Habari

Na Mwandishi wa Barazani

Baraza la Habari Tanzania(MCT) limetaka mamlaka za udhibiti kutokimbilia kuadhibu

vyombo vya habari vinapokosea kuripoti kuhusu janga la ugonjwa wa covid-19.

Katika barua ya kuwafahamisha wadau na washirika wake kuhusu hatua iliyochukua kufanya marekebisho ya shughuli zake kutokana na janga hilo, Baraza limeomba mamlaka hizo kuzingatia hali halisi na mazingira ya janga hili.

Kinachotakiwa sasa ni kuelimishana badala ya kufungiana, Baraza limeeleza katika barua yake bila shaka ni kutokana na wimbi la amri za kufungia na kuvitoza faini vyombo vya habari kwa madai ya

kukiuka taratibu za kuripoti virusi vya corona.

Licha ya kuvitaka vyombo vya habari kuzingatia mwongozo ambao Baraza limetoa kuhusu kuripoti virusi vya corona, Baraza limesisitiza kuwa ni muhimu wenye mamlaka wakazingatia hali halisi.

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Tanzania (TCRA) imesimamisha Mwananchi mtandaoni kwa miezi sita na kutoza faini ya sh. milioni tano kwa madai ya kukiuka kanuni za mawasiliano ya kieletroniki na posta za mwaka 2018.

Imedaiwa kuwa Mwananchi mtandaoni Aprili 13, 2020 ilichapisha habari zinazodaia kusababisha hofu kinyume na kanuni namba 5(1) na 12(1) ya mawasiliano ya kieletroniki na posta.

Kamati hiyo pia Aprili 2, 2020

ilitoza faini vyombo vingine vitatu vya habari - Star Media Tanzania Ltd, Multichoice Tanzania Ltd na Azam Digital Broadcast Ltd na kuviamuru kuomba radhi kwa kutangaza taarifa zisizo za kweli kuhusu namna taifa linavyoshughulikia na kusimamia COVID-19

Katika hatua nyingine mwandishi wa Zanzibar anayeandikia gazeti la Tanzania Daima amesimamishwa kwa miezi sita kuandika habari kuanzia Aprili 20, 2020 Kwa kile idara ya habari visiwani ilichoeleza kukiuka maadili ya taaluma.

Talib Ussi Hamad anadaiwa kutoa habari za mgonjwa wa virusi vya corona bila ridhaa ya mgonjwa huyo kinyume na maadili ya kitabibu. Amri hiyo ya kumsimamisha mwandishi huyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Visiwani.

Msikimbilie kuadhibu vyombo vya habari, MCT yasema

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, Kajubi Mukajanga.

Page 10: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

10

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Na Mwandishi wa Barazani

Hofu kuhusu vyombo vya habari kubanwa wakati huu wa janga la virusi vya corona iliyoelezwa na

Shirika la Kimataifa la Habari (IPI) imethibitishwa kufuatia kutozwa faini ya sh. milioni tano – Shirika la Utangazaji la Azam, Star Media na Multi Choice kila kimoja na ktakiwa kulipa ndani ya siku 30.

Vyombo hivyo vimetakiwa kuomba radhi mara saba kwa kile Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imedai kwa kurusha habari zisizo za kweli kuhusu hali ya virusi vya corona Tanzania. Taarifa kuhusu janga la corona zinadhibitiwa na zinatolewa na maofisa wa serikali tu – Waziri Mkuu au Waziri wa Afya.

Mfumo uliopo ni kwamba vyombo vya habari haviwezi kuandika habari za corona kwa kutumia vyanzo huru. Kwa msingi huo mawazo huru yanabanwa.

Baraza la Habari Tanzania kwa kuzingatia janga hilo limetoa mwongozo kwa vyombo vya habari jinsi ya kuuripoti na imevitaka vyombo vya habari kuwa waangalifu kwa kuwa kuna habari nyingi zinafurika kwa sasa lakini

ukweli wake hauna uhakika, Wakati huo huo Baraza

limewataka wenye mamlaka kutoa habari kwa wanahabri bila vikwazo na kutoa ushirikiano.

Katika taarifa iliyotolewa Machi, IPI yenye makao yake Vienna imezitaka serikali duniani kote kutambua wajibu mkubwa wa vyombo vya habari huru katika kukabiliana na janga la corona na kwamba hatua za dharura za kupambana na ugonjwa huo hazitumiki kama kisingizio cha kubinya habari zote pamoja na za mitandaoni ama kutekeleza kanuni mbaya dhidi ya vyombo hivyo.

“Awali ya yote tunatambua kuwa COVID-19 ni tishio kwa afya duniani na kwamba serikali zinalazimika kuchukua hatua za dharura kulinda afya za raia

wake”, Mkurugenzi Mtendaji wa IPI Barbara Trionfi ameeleza katika taarifa yake iliyotolewa Machi 19, 2020.

“Utoaji huru wa habari ni muhimu zaidi katika hali ya sasa, katika kuwahabarisha wananchi na pia kuwa na mjadala kuhusu ubora wa hatua zinazochukuliwa ambayo ni mambo muhimu kuweza kupata imani ya wananchi.”

Aliongeza: “Katika zama hizi za upotoshaji habari, umma unahitaji kupata habari za kuaminika. Ni muhimu katika hatua hii kwamba serikali iunge mkono vyombo vya habari binafsi ambavyo ni washirika muhimu katika mapambano dhidi ya COVID-19.”

Wakati huo huo, Trionfi alieleza wasiwasi kuhusu uwezekano wa mamlaka kutumia janga hili kuweka sheria mbaya kubinya haki, ikiwa pamoja na uhuru wa kujieleza hatua ambazo zitaendelezwa hata baada ya janga hili kupita. .

Trionfi alisema IPI inatoa mwito kwa serikali zote kufanyakazi na vyombo vya habari na kuhakikisha wanahabari wanawezeshwa kufanyakazi zao vizuri katika kuripoti janga hili la afya.

Hofu ya IPI yathibitishwa

Page 11: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

11

Habari

Toleo la 152, April, 2020

Na Mwandishi wa Barazani

Mwandishi wa habari na mtetezi wa haki za binadamu Albert George Sengo amefunguliwa

mashitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mwanza kwa kutoa habari za mtandaoni bila kuwa na leseni halali kinyume na kanuni 14 (1 & 2) na 18 ya Mawasiliano ya eletroniki na posta ya mwaka 2018.

Kulingana na Umoja wa watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Sengo alifikishwa mahakamani Aprili 23,2020 akituhumiwa kuwa Machi 24, 2020, katika mji na mkoa wa Mwanza, kinyume cha sheria alitoa habari za mtandaoni kwa kupitia runinga ya mtandaoni iitwayo GSENGO TV bila kuwa na leseni inayotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA).

THRDC imempatia wakili na ameachiwa kwa dhamana kupitia wakili huyo Hans Edwin na Edwin Soko, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi ya Mwanza.

Machi 31, 2020, Sengo alipokea simu kutoka Polisi ikimtaka aripoti kituo cha Kati cha Mwanza, aliripoti Aprili 1 na akakamatwa mara moja, akawekwa ndani na kuhojiwa kuhusu kutangaza habari kupitia runinga ya mtandaoni ya GSENGO bila kuwa na leseni halali ya TCRA.

Baada ya kushikiliwa na kuhojiwa kwa muda mrefu bila kuwepo wakili wake, aliachiwa kwa dhamana ya polisi. Alitakiwa kuripoti katika kituo hicho kwa tarehe mbalimbali na hatimaye kufikishwa mahakamani.

Kesi yake inafuatia kukamatwa kwa watetezi watatu wa haki za binadamu – waandishi wa habari wawili na mtu mmoja anayemiliki akautni ya YouTube Moshi, mkoani Kilimanjaro Aprili 5, 2020 kwa kumiliki blogi na akaunti ya YouTube bila leseni kutoka TCRA.

Machi 4, 2020,Watetezi wanne wa haki za binadamu - waandishi watatu

na mmiliki mmoja wa akaunti ya YouTube walifunguliwa mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Njombe kwa kutoa maudhui ya mtandaoni bila kuwa na leseni ya TCRA. Kutoka Januari 2020 hadi sasa, waandishi wa habari 13 na watetezi wengine wa haki za binadamu wameshitakiwa kwa kutoa maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni kutoka TCRA. Miongoni mwao wawili walitiwa hatiani na kutozwa faini nzito.

THRDC, inaamini kwamba mitandao na majukwaa mengine ya mtandaoni ni kwa ajili ya matumizi huru kwa mtu yoyote duniani. Mwanzilishi wa YouTube kwa mfano hadai malipo yoyote kwa watumiaji wake. THRDC inawataka watetezi wote wa binadamu, vyombo vya habari mitandaoni na watumiaji wa mitandao, watunga sheria kuendelea kupinga kanuni hizi kwa vile ziko kinyume na haki za uhuru wa kujieleza.

Mwanahabari ashitakiwa kwa kurusha habari mtandaoni bila leseni

Mwandishi wa Habari na Mtetezi wa Haki za Binadamu Albert George Sengo.

Page 12: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Na Gervas Moshiro

Saluti nyingi na kubwa sana kwa wanahabari wote walio mstari wa mbele wakati huu mgumu dunia nzima inapokabiliana kivita dhidi ya janga ambalo

halijawahi kutokea. Kama ilivyokuwa kwa jamaa zake huko nyuma, gonjwa hili – corona limekuja na litapita. Amina.

Kama kuna aliyekuwa ana shaka juu ya uwezo wa vyombo vya habari, huu ni wakati mwafaka wa kuona manufaa yake. Wakati wa vita kama huu, habari ndiyo silaha kuu na ni kazi ya vyombo vya habari kutoa mwelekeo na elimu hitajika ili kushinda.

Mara baada ya Rais Dk. John Pombe Magufuli alipolieleza taifa nia ya kupambana kivita na ugonjwa huo na kutaja umuhimu wa vyombo vya habari katika vita hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari (MCT) Kajubi Mukajanga alikutana na sehemu ya wanahabari, kwa niaba ya wenzao katika tasnia, ili kuhakikisha dhima na wajibu waliopewa wanaitekeleza kikamilifu ilivyo matarajio ya wananchi na kwa heshima ya taaluma ya habari, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na MCT.

Yawezekana baadhi ya wanahabari hawajui tofauti ya uandishi wa habari wakati wa vita na mwingine. Hii ndiyo sababu Mukajanga aliwaita wanahabari hao kuhakikisha wanafahamu vyema utaratibu unaohusika .

Alizungumzia vipengele muhimu katika kuripoti vita hiyo: kuzingatia kikamilifu usahihi wa taarifa na data za kweli, kutotoa taarifa za mihemko na kuwa makini kwani ni wakati kama huu taarifa nyingi za uongo na za kupotosha hutolewa. Vyanzo rasmi ndio kinga pekee dhidi ya tuhuma za uongo.

Mukajanga aliwatahadharisha wanachama kutotumia janga hilo kwa manufaa binafsi kwa kupotosha wafuasi au watumiaji wa habari kwa vichwa vya habari vyenye kuvutia kinyume na maelezo halisi ya taarifa. Kadhalika vyombo vya habari visisababishe hofu kwenye jamii. Sina nia ya kurejelea yote aliyosema gwiji huyo, lakini iwe ni kifungua kurasa cha magumu yanayokuja. Nawapongeza tena walioitikia wito wa Mukajanga. Mwendelee bila kuchoka.

Baada ya maelezo hayo, nirudi sasa kwenye ninayotaka kuandika katika makala haya. Mengi ni maoni na hisia zangu kutokana na uzoefu na uelewa wa taaluma ya habari kwa karibu nusu karne. Yapinge kama una udhibitisho wa data.

Mwenendo katika baadhi ya vyombo vya habari unanisababishia mfadhaiko wa saikolojia kiasi cha kunifanya nipoteze mwelekeo wa taaluma ninayoipenda na ambayo imenilea kwa miongo mingi. Kupoteza mwelekeo huenda isiwe kwa usahihi ndivyo ninavyojisikia lakini itoshe kusema

kuwa napata mfadhaiko ninapolinganisha yanayotokea na kufanywa na baadhi ya vyombo vya habari na nilivyofunzwa na kuzoea kufanya.

‘Mfadhaiko tambuzi’ ni wakati ambapo, kwa mujibu wa kamusi ya Wikipedia, ‘mtu anapokuwa na imani mbili zinazopingana, mawazo au anaposhiriki kitendo kinachoenda kinyume na hayo na kupata hisia ya kufadhaika kiakili kutokana na hilo’. Lengo la makala haya ni kuonesha kwa nini nadai nimefadhaika.

Naweza kusema bila shaka yoyote kuwa mimi ni kati ya wanataaluma wa habari waliojaliwa kuishi kwenye vipindi vingi vya maendeleo ya vyombo vya habari - kutoka ukoloni, vyombo huru baada ya uhuru, vyombo vya kijamaa, vyombo huru tena baada ya jamii kukumbatia vyama vingi vya siasa, na sasa, kuanzia miaka ya hivi karibuni kipindi ambacho nashindwa kukipa jina kutokana na mkanganyiko uliopo wa kukosa itikadi iliyo wazi.

Kipindi hiki kinashuhudia mchanganyiko wa udhibiti wa serikali, kutukuza mamlaka, kujikomba, kujinufaisha binafsi na kukosekana kwa itikadi. Sio ajabu kwa hiyo kuwa leo, miaka sitini baada ya uhuru, wanasiasa wanadiriki kuwahutubia wanahabari juu ya uzalendo na wajbu wao, kitu ninachoona kuwa maajabu, labda kama wanahabari hao sio weledi wa taaluma yao. Iweje tumepoteza uanataaluma? Nini kimetokea?

Vyombo vya habari vimekuwa ni vyombo vya kusaidia kuleta maendeleo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa jamii husika kulingana na itikadi inayoyaongoza. Ni wajibu wa msingi. Kwa kuwa ni vyombo,vinasimamiwa na wamiliki kwa malengo ya kijamii na kibinafsi na ndio sababu uwepo wa itikadi ni muhimu. Itikadi huongoza vyombo vya habari kujali maendeleo ya nchi rika zijazo na sio uchaguzi ujao wafanyavyo wanasiasa.

Sio kwamba Tanzania haina mwelekeo wa kiitikadi au kujua inachotaka, ila ni kwamba ufuatiliaji wa dhati kama ilivyokuwa wakati wa Ujamaa haupo, na hakuna juhudi nyingine za kuainisha itikadi ya nchi kiimani, kimawazo, kanuni za kuongoza uhusiano na vitendo vyetu kisiasa, kijamii na kiuchumi. Kuna jitihada za kutumia katiba ya nchi inapokuwa masuala ya tunu za taifa na njozi lakini hizi haziwezi kuchukua nafasi ya itikadi iliyo wazi ili hata katiba iweze kufuata matakwa ya itikadi ya nchi.

Uzuri wa kuwa na itikadi ya taifa ni kwamba mifumo mingine – iwe ya kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa, kidini, kihabari na mingine inakuwa na dhima mahususi na taasisi ambazo ni huru kutekeleza majukumu yake bila kuingiliwa na wanasiasa.

Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere ni mashuhuri kwa mambo mengi ikiwemo falsafa yake ya nafasi ya vyombo vya habari katika jamii. Wakati wa utawala wake wa kijamaa aliwahi

kutoa sera ya habari ambayo, si tu ilipambanua wajibu wa habari katika jamii ya Kijamaa lakini pia ulinzi kwa niaba ya jamii bila kujali mwelekeo wa kiitikadi.

Mwaka 1973, Mwl Nyerere alihutubia mkutano wa wanahabari huko Arusha na kuweka bayana sera ya habari ya nchi. Pamoja na hayo Mwalimu alisisitiza zaidi umuhimu wa uweledi wa taaluma kwa kuzingatia ukweli, usahihi, uhakika na ukamilifu wa taarifa, bila kusahau uzalendo.Wakati ule vyombo vyote vya habari vilikuwa vinamilikiwa na serikali na washirika wake na asasi za kidini.

Hata hivyo sekta ya habari ilikuwa na uchangamfu mkubwa na uhuru wa aina fulani ulioendana na ufuasi wa itikadi ya nchi. Katika ulinzi wa maslahi ya wananchi, itakumbukwa vipindi vya redio kama Mikingamo, Mazungumzo Baada ya Habari na Mahoka; vibonzo katika gazeti la Uhuru vya Chakubanga, habari za uchunguzi kuhusiana na ufisadi kama vile kashfa ya Gapex, ‘Loliondogate’ na nyingine zilizoripotiwa katika vyombo vya umma. Kwa jumla vyombo vya habari vya umma vilifanya kazi nzuri sana ya kuwa kioo na mlinzi wa jamii, na hasa katika kufichua kashfa za ufisadi kabla ya ujio wa vyombo binafsi miaka ya tisini.

Vyombo vya habari binafsi vilishamiri baada ya kuwa na mfumo wa siasa za vyama vingi na kuwezesha wananchi kutoa maoni yao katika vyombo anuwai vya habari inavyoruhusiwa kikatiba kwa matarajio kuwa, kama alivyosema kiongozi wa Uchina zamani Mao Zedong mwaka 1957: “Let a hundred flowers bloom, let a hundred schools of thought contend,” akiwa na maana ya kuachia njia mia za mawazo kushindana kama sera ya kukuza maendeleo katika sanaa na sayansi na kushamiri utamaduni wa kijamaa nchini humo. Katika ushindani, wazo bora litaonekana na ndilo litakaloshinda.

Hadi 2015, uchangamfu na msisimko katika vyombo vya habari ilikuwa kitu cha kusaidia nchi kupambana dhidi ya ufisadi na mienendo kinzani ya utawala bora. Vyombo vya habari vilikua kwa kasi kwa idadi na ubora katika taaluma iliyoshaajishwa na jitihada mbalimbali za Baraza la Habari Tanzania na kuthibitisha kuwa kweli vyombo hivyo ni muhimu katika maendeleo, na hasa utawala bora.

Kwa muda serikali na vyombo vya habari vilishirikiana kutunga sera ya habari na japo ule uhusiano wa chuki-upendo ulikuwepo hapa na pale, haikuzuia sekta hizi kutambuana kama ni muhimu kwa maendeleo ya pande zote. Baraza la Habari Tanzania lilijitahidi kuleta utangamano kwa kuhusisha watendaji wa umma katika shughuli za kihabari na pia kuwa na makubaliano ya ushirikiano kitaasisi kama vile Polisi na Mahakama. Mfumo wa Usuluhishi wa Baraza ulikuwa unatumiwa na baadhi ya viongozi wakuu wa nchi, ishara ya kukubalika katika jamii. Kama ulivyo msemo wa Kiswahili: Tunajenga nyumba moja, kwa nini tugombee fito? Na isitoshe kuwa pamoja na serikali sio dhambi.

Vyombo vya habari vilijinoa zaidi kwa kujijengea uwezo wa habari za uchunguzi kwa kusaidiwa na jitihada za asasi ya Tanzania Media

12

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Maoni

Muhimu kuepuka mfadhaiko wa habari

Endelea Ukurasa wa 14

Page 13: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

13

Toleo la 152, April, 2020

Uchambuzi

Na Saidi Nguba.

Baadhi ya wasomaji wa magazeti, wasikilizaji wa redio na watazamaji televisheni na hata baadhi ya wanahabari wenyewe, huwa

wanazipuuza sana barua za wasomaji zinazopelekwa kwa mhariri kwa ajili ya uchapishaji au utangazaji.

Baadhi ya watu hao huwa hata hawasomi kurasa za barua hizo. Na kwa upande wa vyombo vya kieletroniki – radio na televisheni hufunga vyombo hivyo wakati wa vipindi vinavyohusu barua hizo.

Lakini ukweli ni kwamba barua za wasomaji ni muhimu sana na kwa kukariri maneno ya mhariri mmoja wa Kimrekani ambaye ni mdau mkubwa wa barua hizo, ni kipimo cha kujua kwa kiwango gani vyombo vya habari vinakubaliwa na wasomaji wa magazeti, wasikilizaji wa redio na watazamaji wa televisheni.

Ronald D. Clark wa gazeti la Pioneer Press la St. Paul, ambalo ni shirikishi katika Umoja wa Kitaifa wa Waandishi wa Tahariri (National Conference of Editorial Writers - NCEW) nchini Marekani aliandika kijarida cha umoja huo “…chukulia kuwa barua za wasomaji kuwa ni kipimo cha kiasi gani unakubalika na wasomaji, wasikilizaji na watazamaji. Kadri unavyozipata kwa wingi ndivyo hivyo unavyokuwa na mawasiliano mazuri nao. Ukipata chache basi ujue kuwa ni dalili tosha kuwa unaufanya umma ulale usingizi…”

Kwa ujumla, barua za wasomaji ni zile zinazotumwa kwenda kwa wahariri wa magazeti na vyombo vya kielektroniki zikiwa ni mawasiliano kwenda kwa wahariri kutoka kwa umma. Waandishi wa barua hizo huwa wanatoa maoni yao au wanajibu mambo mbalimbali yaliyojitokeza kwenye vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na habari zenyewe, tahriri, makala mbalimbali na hata barua nyingine za wasomaji.

Barua hizo wakati mwingine zinaweza zikazusha jambo jipya kabisa kwa madhumuni ya kutaka umma ulijue jambo hilo. Pia zinaweza ama kuunga mkono ama kupinga msimamo wa chombo cha habari au msimamo wa watoa maoni wengine. Barua pia zinaweza zikajikita katika masuala ya eneo mwandishi aliko au masuala ya kitaifa ama hata ya kimataifa. Kama ada, barua hizo madhumuni yake zichapishwe kwenye magazeti au majarida au kutangawa kwenye redio na televisheni au kutolewa kwenye vyombo vya habari vipya vya kijamii – mitandao ya intaneti tovuti na blogu.

Katika baadhi ya magazeti na vyombo vya kieletroniki nilivyobahatika kufanya kazi, nilishuhudia umuhimu wa barua za wasomaji. Kikiwa kinapendwa na kuaminika, kunakuwa na mshikamano na wasomaji na wasikilizaji wake, kwa kupitia barua hizo. Utaona barua zinamiminika kwa wingi kutoa maoni, pengine ya kupongeza au kulaumu au kutoa habari mpya kuhusu nini kimejiri katika vyombo hivyo. Na kama kuna ukame wa barua hizo, nimebaini baadhi ya wahariri wakijishusha chini kabisa na kutengeneza wenyewe barua hizo zikielezea mambo ya kijamii yakidaiwa kuwa yametolewa na wasomaji. Na hiyo ni dalili mbaya. Kama chombo cha habari hakipati barua kutoka kwa wasomaji na wasikilizaji ili kujua wana maoni gani, kinakuwa mbali na watu hao. Ufumbuzi siyo kuchonga barua bali ni lazima chombo hicho kijitafakari na kufanya marekebisho yanayohitajika ili kuwa karibu na watu.

Wahariri mara nyingi huwa na mashaka sana na barua za wasomaji ambazo mwandishi wake anaficha jina na anuani. Na wasiwasi huo umetokana na matukio yaliyojitokeza huko nyuma. Imeelezwa kuwa nchini Canada mwaka 1999, mwanasiasa mmoja Paul Reitsma alituma barua kwenye magazeti kwa kutumia jina la bandia “Warren Betanko”, akijisifu mwenyewe na kuwashambulia vikali wapinzani wake wa kisiasa. Lakini baada ya muda ilikuja bainika kuwa Warren Betanko ni Paul Reitsma na kulifanya gazeti moja kati ya aliyokuwa anayatumia barua hizo, kuchapisha habari kubwa ya ukurasa wa kwanza iliyosema “…Reitsma ni mwongo na tunao ushahidi wa jambo hilo…” na kusababisha akome kabisa kujishughulisha na siasa. Huko Israel nako, mwaka 1966, kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia, barua katika magazeti mashuhuri zilizokuwa zinamshambulia aliyekuwa kiongozi wa upinzani wakati huo, Menachem Begin, zilithibitika kuwa zilikuwa zinaandikwa na hasimu wake wa kisiasa katika kugombea uongozi wa chama cha Herut, kwa kutumia majina bandia. Baada ya kugundulika, hasimu hiyo akaumbuliwa na akafukuzwa kutoka katika chama hicho jambo lililomsaidia Begin kuinua hadhi yake ya kisiasa na kiuongozi na kumfanya ashinde uchaguzi mkuu wa mwaka 1977 na kuwa Waziri Mkuu wa Israel. Katika vyombo vingi vya habari, barua zisizokuwa na majina au zenye majina bandia, hukataliwa moja kwa moja kuchapishwa. Ingawa huwa kuna mazingira mwandishi wa barua kumuomba Mhariri ahifadhi jina lake na asilichapishe, kwa sababu fulani za msingi lakini jina kamili

na anuani huwa anabakinayo Mhariri kwa kuwa huenda akahitaji kuwasiliana na mwandishi huyo baadaye. Uhitaji wa hovyo wa kuficha jina unatokana na mtindo wa mwandishi wa barua kutoa maoni yasiyokuwa ya msingi na kuwashambulia watu wengine bila ya kuwa na hofu ya nini kitatokea kwa vile atakuwa hajulikani. Kwa kawaida barua huchapishwa kadri zinavyokuja lakini wahariri husisitiza kuwa itabidi zihaririwe kupunguza maneno, kupata nafasi nzuri na zieleweke vizuri kwa ufasaha. Lakini barua zenye harufu ya kukashifu watu, usingiziaji wa makusudi, mashambulio kwa watu wengine na lugha za matusi, hukataliwa ili zisitoke kwa umma.

Kwa mujibu wa historia, mambo mengi yaliyokuwa yanapelekwa kuchapishwa katika magazeti ya zamani, yalikuwa ni barua za wasomaji kwenda kwa mhariri. Mtu anaweza akaona jambo fulani zuri na anafikiri umma ulijue, ataandika barua kwa mhariri. Utaratibu huo ndio ulikuwa wa kawaida na waandishi wa habari waliokuwa wameajiriwa moja kwa moja na magazeti walikuwa wachache mno. Na hii ndiyo sababu ya msingi kwa nini magazeti ya zamani yalikuwa yanawategemea waandishi walioko mbali na wa kujitegemea ambao ndiyo hukusanya taarifa mbalimbali na kuzituma kwenye magazeti na vyombo vya habari vingine. Lakini hata leo katika ujio huu wa vyombo vya habari vya kijamii – intaneti, tovuti na blogu, barua zina nafasi kubwa. Taarifa nyingi zinazotumwa huko, kwa mfano, ni barua tu kwa wenye blogu na wahariri, siyo hata habari kamili kwa uhalisia wake ila ni maoni na taarifa mbali mbali kutoka kwa umma.

Hata hivyo, barua za wasomaji kwa mhariri, lazima ziwe fupi, zinazoeleza jambo bila ya utata, zinazoeleweka kwa urahisi na siyo za kuzungukazunguka. Licha ya kutoa maoni kuhusu kilichoelezwa katika chombo cha habari, mtu anaweza kuandika barua kwa mhariri kuonyesha kukarishwa na jambo fulani na kutaka watu wengine wajue. Unaweza pia kuliona jambo fulani kuwa ni muhimu na inabidi ulielezee vizuri watu walijue au unataka kuushawishi umma ukubaliane na mtazamo fulani au unataka kuwatahadharisha watunga sera, ni sababu pia za kuandika barua kwa mhariri. Kwa hiyo, barua za wasomaji kwa mhariri zina jukumu pana kwa jamii.

Mwandishi wa makala hii ni mwandishi wa habari na mhariri mkongwe nchini

Tanzania. Anapatikana kwa Barua-pepe: [email protected] na Simu ya

Mdomo: 0754-388418.

Barua za Wasomaji: Ni kipimo cha chombo cha habari kukubalika

Page 14: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

14

Maoni

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Fund ambayo sasa ni Wakfu kwa zaidi ya miaka kumi.

Hili ni eneo jingine la mfadhaiko: habari za uchunguzi kutoweka kwenye vyombo vya habari nchini, ina maana kuwa uzoefu na mamilioni ya shilingi yaliyotumika yameenda jalalani?

Sina hakika kama vyombo vya habari vya umma vinaweza kudiriki kutoa habari za uchunguzi kama ilivyokuwa miaka ya 70 na 80 na viongozi wake wakabaki salama. Sakata la Tido Mhando na TBC – ni mfano mmojawapo. Hakuongezwa muda wa mkataba wake, lakini kwa kipindi kifupi cha uongozi wake tuliweza kuona manufaa ya utangazaji wa umma. Wengi wetu tukimuunga mkono Tido ili aweze kugeuza mwenendo wa shirika hilo kuwa wa umma badala ya idara ya serikali. Hakujua kuwa huko nyuma, miaka ya 90, wazo la kugeuza TBC kuwa chombo cha umma kinachosimamiwa na wananchi kupitia kamati ya Bunge lilikwisha kataliwa.

Uamuzi huo umeendelea kunifadhaisha kwa sababu wananchi ndio wanaolipia huduma hiyo, hata vile vilivyopo katika halmashauri za wilaya na miji zinazotakiwa kuwa za kijamii, bado ni vyaa kiserikali. Wananchi hawana chombo cha kusemea bila mawazo yao kupitia kwanza uhariri wa serikali. Pale penye vyombo binafsi, uhariri umekuwa wa tahadhari mno kiasi cha kuogopa kuruhusu chochote kinachoonekana kuwa hakitafurahisha mamlaka fulani. Nani sasa aliyebaki kulinda maslahi ya jamii katika kudhibiti mamlaka za utawala?

Matumizi na ueneaji wa vyombo vya habari nchini unahitajika kufahamika, kazi ambayo watafiti na miradi ya kitaaluma ya wanachuo ingesaidia sana kutoa data. Huu ni mfadhaiko mwingine: wanataaluma na akademia za wanahabari kutojihusisha na utafiti; au labda wanafanya lakini hazichapishwi.

Mfadhaiko mkubwa zaidi unasababishwa na matumizi ya vyombo vya habari vya kidijiti kupitia simu na kompyuta. Vingi, kama sio vyote, ya vyombo vya mfumo wa zamani – redio na runinga – navyo hutumia mtandao kama njia ya ziada ya kuwasilisha maudhui kwa umma. Ni vizuri kunyakua furksa za maendeleo ya teknolojia ili kuenenda na wakati.

Hivi karibuni iliwekwa klipu ya video kuhusu mtu mmoja aliyefariki kwenye mtaa mmoja huko Kariakoo Dar es Salaam iliyoniacha nikijiuliza kama aliyeweka hiyo video amejifunza chochote kutoka maelekezo ya serikali na ushauri aliotoa Katibu Mtendaji wa MCT kuhusiana na kuripoti yanayohusu ugonjwa wa corona.

Video hiyo ilionesha mtu mmoja aliyefariki akiwa kwenye kibanda chake cha biashara na wananchi wakimweleza mwandishi kuwa mtu yule alikufa kutokana na corona – walifahamuje kuwa ni corona, sijui. Wananchi hao walishutumu sana Polisi kuwa hawakuja mapema walipopigiwa simu, kana kwamba hiyo ingemfufua. Kifo hicho kilichodaiwa kutokana na corona kilifanya watu

wawe na hofu kubwa na kufunga biashara zao kwa tahadhari wasijeambukizwa. Mtaa ulitelekezwa!

Ilikuwa inasemwa wazi kuwa ni corona. Nani kampa mwandishi yule mamlaka ya kutambua na kutangaza kuwa mtu yule kafa kutokana na corona wakati mamlaka za nchi zilishakataza taarifa za aina hiyo kutotolewa na mtu mwingine yeyote isipokuwa zenyewe? Taarifa za mitandao husambaa haraka, na nina hakika madhara kwa biashara na mfadhaiko kwa wananchi wengi ulikuwa mkubwa.

Data iliyo kwenye tovuti ya TCRA yenyewe ina fadhaisha, ni ya mwaka 2018 ambayo nayo itakuwa imepitwa na wakati. Natamani taasisi za umma zingefahamu umuhimu wa kuhuisha data kuendana na wakati. Wananchi wanazitegemea sana kujua hali ilivyo kwa sasa na sio historia. Mwishoni mwa 2018 TCRA ilikuwa imetoa leseni za maudhui ya kidijiti, ukiondoa wale walio na leseni za kawaida ambao nao wanatumia mtandao, redio 6 na runinga 91. Wale wa blogu walikuwa 90.

Kuna haja ya kufahamu manufaa ya mamia ya vyombo hivi, kwani kwa kupewa leseni vimekubali kuwa ni huduma ya jamii na sio kwa manufaa binafsi.

Ni fedheha zaidi tunapotumia wingi wa vyombo hivi na kudai kuwa nchi ina demokrasia na uhuru wa habari. Kinachojalisha ni wingi na uhuru wa kutoa mawazo na sio wingi wa vyombo. Hapa napo watafiti wangetusaidia kujua uanuai wa maudhui kama unaendana na tambo zetu.

Napata mfadhaiko ninapoona machapisho ninayopenda na muhimu ya habari yakikosa matangazo lakini vyombo vya mirengo fulani fulani vikisheheni matangazo hayo. Kwa mujibu wa Kanuni za Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari, usambazaji wa matangazo kutoka taasisi za umma ni jukumu la Idara ya Habari. Nafadhaika kuona kuwa huenda vyombo vya mrengo fulani hupendelewa zaidi, kitu ambacho hakikutajwa kwenye sheria. Ninachojua ni kwamba ili mradi vyombo hivyo vimesajiliwa rasmi na vina majukumu sawa, vinastahili kupata mgao. Ni muhimu suala hili likatafutiwa ufumbuzi wa kisheria kuondoa dhana ya upendeleo. Vigezo vya nani apewe yabidi viainishwe wazi.

Hakuna shaka kuwa mitandao ya kijamii imekuwa ni vyanzo muhimu sana vya habari na taarifa na pia kuwezesha wanajamii kuwasiliana na watu kujumuika japo wako mbalimbali. Ni vigumu kukosoa mitandao hii kwani haina mpaka wa maudhui. Ni juu ya watumiaji wenyewe kujidhibiti. Hata hivyo katika nchi nyingi, Tanzania ikiwemo, maudhui yanayowekwa kwenye mitandao yanazidi kudhibitiwa kwa sheria ili yaendane na vyombo vya habari asilia.

Inasikitisha hata hivyo kuona wanahabari wengine wamepoteza kazi zao kutokana na maudhui waliyochapisha kwenye mitandao mingine ambayo hayakuwafurahisha viongozi wao. Ni kejeli kwa sababu vyombo vya habari hapa nchini vimekuwa vikilaumu sana watendaji wa serikali kwa kuwakandamiza kutokana na maudhui ya vyombo hivyo kuhatarisha maslahi ya

wakubwa hao, ama ya kisiasa, kijamii au kiuchumi.

Kwa chombo cha habari kutumia kigezo kile kile cha kupenda au kutopenda maudhui yaliyowekwa mtandaoni kumwadhibu mfanyakazi, haielezeki; pengine kuna sababu nyingine ambazo kama zingewekwa bayana, tungeelewa, ila kutokana na uhaba wa maelezo ya matukio hayo, najisikia kufadhaika kwa vile waathirika ni watu waandamizi katika taaluma; kadhalika vyombo vyao vinaheshimika mno.

Wiki chache zilizopita mchekeshaji maarufu nchini anayemiliki runinga mtandaoni alihoji baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma kutafuta uelewa wao wa ugonjwa wa corona au COVID 19. Hiyo namba inaonesha mwaka gonjwa hilo lilipoibuka na kuanza kudhuru binadamu. Tunaambiwa kuwa virusi vinavyosababisha ugonjwa huo kwa kawaida huishi ndani ya miili ya wanyama wa porini au msituni. Hakika haijawekwa wazi nadharia hii kwani bado kuna watu wanaoamini kuwa virusi hivyo ni vya kutengeneza kwenye maabara.

Mchekeshaji huyo alitumia neno COVID 19 katika kuuliza maswali yake bila kutaja corona na hakuna aliyeoanisha COVID 19 na corona. Wengi walijibu kuwa wangependa kuona COVID nyingi zaidi au serikali ijitahidi kuwaongezea msaada wa COVID 19 hata kama zitafikia milioni mbili.

Ama hakika hakuna aliyejua COVID 19 ni nini. Walizoea neno corona. Nani alaumiwe – vyombo vya habari au Wizara ya Afya au wote wawili?

Mchekeshaji huyo alitimiza lengo lake la kutufanya tucheke ujinga wa waliokuwa wanaomba wapewe COVID 19 zaidi wakidhani ni kitu kizuri kumiliki. Pamoja na kucheka kwangu nilifadhaika baadaye nilipotafakari hali ile. Tulio kwenye vyombo vya habari hudhani wakati mwingine kuwa watumiaji wa h uduma zetu wana uelewa sawa na wetu, kumbe wakati mwingine sivyo. Inabidi kuwa makini sana tunapotumia misamiati na hasa istilahi kwani elimu na uzoefu huenda visifanane na wale tunaowalenga.

Suala la elimu ni muhimu sana katika jitihada zozote za maendeleo. Umma ndio askari katika vita hii ya corona hivyo hatuna budi kuhakikisha wanamfahamu vyema adui wao. Sekta inayohusika yabidi iwekeze katika elimu na mawasiliano kama kiambajengo muhimu. Serikali isitegemee wenye vyombo vya habari kutumia rasilimali zao kutoa elimu hiyo bila mwafaka fulani kama hali si ya dharura. Wakati huu wa vita dhidi ya virusi vya corona ni wa dharura hivyo ni mwafaka kila mdau – serikali na wananchi kutumia kila nyenzo inayowezekana kutoa elimu na vile vile kutafuta hiyo elimu. Kamati zilizoundwa kushughulikia mpambano huu yabidi itenge fungu kufadhili mawasiliano ya elimu, ikiwezekana kwa kuwezesha vyombo vya habari ili kuhakikisha serikali na wananchi wako pamoja.

Kaa salama na kama una mfadhaiko na niliyoandika katika makala haya, yaseme hapa katika matoleo yajayo. Kumbuka Corona – COVID 19 inaua. Chukua tahadhari.

Muhimu kuepuka mfadhaiko wa habari Inatoka Ukurasa wa 12

Page 15: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

15

Muongozo wa kuripoti COVID19

Toleo la 152, April, 2020

Utangulizi

Ni jukumu la mwanahabari kutoa taarifa sahihi na kuwa makini katika kuiarifu jamii. Wakati wa kipindi hiki kigumu mitaarafu ya afya ya binadamu ambapo tunapambana na ugonjwa wa COVID-19 (ambao pia unajulikana kama ugonjwa mpya wa homa ya mapafu—novel Coronavirus au “Korona” kwa kifupi) jukumu hili la wanahabari linapata umuhimu mkubwa zaidi. Kirusi cha COVID-19 kimeshatinga Tanzania tayari, kwa mujibu wa uthibitisho uliotangazwa na Wizara ya Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Baraza la Habari Tanzania (MCT), pamoja na mambo mengine, linawajibika kuhakikisha kwamba wanahabari nchini wanazingatia viwango vya juu kabisa vya kitaaluma na kimaadili. Ili kuhakikisha vyombo vya habari nchini vinafanya kazi za kuarifu umma kwa usahihi katika kipindi cha majanga kama hiki tunachopitia sasa, MCT imetayarisha Mwongozo ufuatao kwa ajili ya wanahabari.

Mwongozo• Pamoja na kwamba hutegemewi kupuuzia uzito wa

janga lililo mbele yetu kwa sasa, unapaswa kuchangia katika kupunguza hofu na taharuki miongoni mwa jamii.

• Jitahidi kuelewa mipango na mikakati ambayo inatekelezwa katika juhudi za kupambana na janga la Korona na athari zake kijamii na kiuchumi.

• Ongea na kuhoji watu wengi iwezekanavyo na wa tabaka mbalimbali. Jaribu kupata mitazamo anuwai ya watu wanaopitia kipindi cha tukio la janga hili ili uweze kupata mrejesho utakaowezesha uongozi wa nchi kuwa na mipango sahihi ya kupambana na janga lililopo.

• Zingatia kwa makini taratibu za kitaaluma, huku ukihakikisha unatumia vyanzo vya habari vya kuaminika kama vile Wizara ya Afya na Shirika la Afya Duniani (WHO).

• Jihadhari na taarifa potofu! Fanya juhudi ya kuthibitisha ukweli wa taarifa ulizopata ili usiwe sehemu ya mtandao wa kuzambaza habari zizizo za kweli.

• Waheshimu waathirika wa Korona na jali haki yao ya faragha. Punguza mahojiano nao na waathirika wasipigwe picha na majina yao yasitajwe katika habari zinazowahusu, labda pale tu ambapo wangependa kutajwa ili kueleza uzoefu wao ili jamii ijue bayana juu ya kadhia iliyowasibu.

• Kuripoti janga la COVID-19 kwa njia ya picha kuna umuhimu mkubwa, lakini panatakiwa umakini katika utumiaji wa njia hii ya kuripoti. Wanahabari wanapaswa kuhakikisha picha au vielelezo wanavyotumia katika taarifa zao ni sahihi na vinaakisi hali halisi iliyopo.

• Jikite katika kuripoti na si kufanya uchambuzi, labda tu pale uchambuzi wako unapokuwa umegezwa katika maoni uliyopata kwa wataalamu.

• Wahariri wawe makini katika uandishi wa vichwa vya habari. Kutokana na uwepo wa utitiri mkubwa wa taarifa, ikiwa ni pamoja na uharaka wa usambaaji habari kupitia mitandao ya kijamii, watu wengi wanatosheka na kile wanachokiona kwenye vichwa ya habari na kuchukulia kwamba hizo ndizo habari zenyewe.

• Tumia takwimu na vielelezo kwa umakini na usahihi kulingana na muktadha husika ili kuepusha hofu miongoni mwa jamii.

• Epuka matumizi ya viashiria vya ubaguzi wa rangi—usihamasishe mitazamo finyu ya kibaguzi au kutoa habari kwa namna ambayo inaweza kusababisha wengine kushadidia ubaguzi.

• Chunguza kwa makini aina ya tukio ambalo umepanga kuhudhuria, ukizingatia kwamba pana amri ya Serikali inayokataza mikusanyiko ya idadi fulani ya watu.

• Kuwa mwangalifu, ukijua kwamba pana uwezekano wa wewe kukwamishwa kwenye karantini ndani ya eneo lililozuiliwa kutokana na Korona.

• Tafakari juu ya athari za kisaikolojia zitakazokutinga pale ambapo utakuwa umelazimika kuripoti ukiwa ndani ya eneo ambalo limeathiriwa na Korona, hasa pale ambapo utakuwa ukiripotia chombo chako cha habari huku ukiwa ndani na kituo cha afya, eneo lililotengwa au eneo lililo chini ya karantini.

Mwongozo kutoka MCT:Uandishi wa Habari za Janga la Korona

Page 16: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

16

Jarida la Baraza la Habari Tanzania Muongozo wa kuripoti COVID19

• Hakikisha umejipanga vizuri kwa ajili ya dharura, ukizingatia kwamba kuna uwezekano wa maeneo fulani, wilaya, mikoa na hata nchi nzima kutengwa kwa njia ya karantini au kufungwa kwa mipaka baada ya kutolewa taarifa ya muda mfupi au bila kutolewa tahadhari yoyote.

• Epuka kukaa karibu na mtu yeyote mwenye kuonyesha dalili za kuwa na ugonjwa wa njia za hewa, kama vile kikohozi na kupiga chafya. Hakikisha unafunika mdomo na pua unapokohoa au kupiga chafya.

• Nawa mikono yako mara kwa mara kwa kutumia maji moto na sabuni. Tumia jeli au vifutio vya kuua vijidudu iwapo hakuna maji moto na sabuni, lakini hakikisha kwamba baadaye, unanawa kwa maji moto na sabuni.

• Usikaribiane sana na mtu unayemhoji iwapo anaonyesha dalili za kuumwa Korona. Umbali unaoshauriwa ni mita moja hadi mbili.

• Kuwa mwangalifu na aina ya usafiri unaotumia wakati wa kwenda kukusanya habari na kurejea ofisini. Epuka kutumia usafiri wa umma (daladala) nyakati ambazo vyombo hivi vinakuwa vimejaza abiria mpaka pomoni; na hakikisha unatumia jeli yenye viua-vijidudu wakati unashuka kwenye daladala.

• Tumia maikrofoni ya kushikilia (directional mic) ukiwa umeishika kwa mbali iwezekanavyo, badala ya kutumia maikrofoni inayoshikizwa kwenye mavazi (clip mic).

• Tumia glavu ukiwa, ama unafanya kazi, unazuru eneo lenye maambukizi ya korona kama vile kwenye kituo, au ukiwa kwenye eneo la kutolea matibabu. Yawezekana pia ukahitaji mavazi ya kujikinga kiafya kama vile suti ya kitabibu (bodysuit) na barakoa inayofunika uso gubigubi (full face mask).

• Vifaa vya kazi kama vile kamera, vinasa sauti na maikrofoni ambavyo vinatumiwa kwa kushirikiana, ni lazima vifutwe kwa vieuzi (sanitisers) vyenye uwezo wa kuondoa vijidudu kwa haraka kabla na baada ya kutumika, na watumiaji wa vyombo hivi wavae glavu.

• Kwa muda wote, hakikisha unanawa mikono vizuri ukitumia maji moto na sabuni kabla ya kuingia eneo lililoathirika, uwapo kwenye eneo hilo, na baada ya kuondoka.

• Iwapo utapatwa na dalili za maambukizo ya virusi vya Korona, hasa homa inayoambatana na shida

wakati wa kupumua, wahi kumwona daktari. Zingatia kwamba, kama upo ndani ya eneo lililoathirika kwa kiwango kikubwa, unakuwa hatarini kukutana na wagonjwa wa COVID-19 kwenye vituo vya matibabu, na hivyo kuongeza uwezekano wa wewe kuambukizwa.

• Zingatia miongozo na maelekezo ya wataalamu wa afya wa eneo unaloishi.

• Shirila la Afya Duniani (WHO) na Wizara ya Afya Tanzania wanakubaliana kwamba si lazima kwa watu wasio na dalili za Korona kuvaa barakoa, labda tu pale utapoamriwa kufanya hivyo na mamlaka ya eneo ulipo, au kama upo katika eneo hatarishi kama vile hospitalini au pale ambapo wewe ni mwangalizi wa mtu ambaye anashukiwa ana maambukizi ya COVID-19.

• Yawezekana wanahabari ambao wamekuwa wakiripoti kutoka kwenye maeneo yenye maambukizi yaliyoshamiri kutakiwa watengwe na wenzao maofisini, au wakatazwe kuchanganyika na vyanzo vya habari, familia zao au watu wengine, kwa kipindi cha siku 14.

• Vipindi vinavyohusisha wageni studioni vyapasa kuepukwa. Kama ni lazima kuwa na washiriki ndani ya studio, basi pawe na umbali wa angalao mita moja kati ya mshiriki mmoja na mwingine. Waendesha vipindi sharti wanawe mikono kabla na baada ya kipindi na waepuke kugusa nyuso zao wakati wowote.

• Vieuzi sharti viwekwe sehemu zote za kuingilia vyumba vya habari, msisitizo ukiwekwa zaidi kwenye milango ya kuingia studio. Waendesha vipindi na wageni wa studio sharti wanawe mikono kabla ya kuingia studioni. Wasaidizi wa vipindi sharti wanawe kwa maji na sabuni kabla na baada ya shughuli nzima ya kurusha kipindi na pale itakapoonekana ni lazima, wavae barakoa na glavu, na

• Meza za kufanyia uhariri, kompyuta, vichanganyio (mixers) na vifaa vingine vya kazi lazima vifutwe na vitakasa kila baada ya kipindi au shughuli ya uhariri.

Vipengele hivi vya mwongozo vimetokana na vianzo mbalimbali vya hapa nchini, vya kikanda na vya kimataifa vinavyohusu utendaji bora na salama kwa wanahabari ndani ya mazingira hatarishi.

Dar es Salaam, Machi 20, 2020

Page 17: Covid-19 mabadiliko MCT · Kutoka Jiji la China la Wuhan mwezi Desemba, janga hilo linaleta balaa na kuua watu wengi bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii – maskini, matajiri,

17

Habari

Toleo la 152, April, 2020

Na Mwandishi wa Barazani

Kabla ya kupitishwa kwa she-ria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016, matangazo ya serikali katika vyombo vya

habari hayakuwa yakiratibiwa na kud-hibitiwa.

Kila idara kutegemea uwezo wa fedha katika bajeti zao, walitangaza kwenye vyombo vya habari walivyopenda.

Sasa hali haikuwa hivyo. Chini ya sheria hiyo mpya, mkurugenzi wa Idara ya habari anaratibu na kuamua vyombo vinavyostahili kupewa

matangazo ya serikali. Maofisa katika idara na hata mashirika ambao wapo katika nafasi za kutoa matangazo wamejawa na wasiwasi, kilieleza chanzo kimoja katika vyombo vya habari.

Ofisa wa serikali anaweza kuahidi kutoa tangazo kwa chombo cha habari lakini baadaye akakwepa kabisa kuwa na mawasiliano na chombo hicho, chanzo hicho kimeeleza.

Hatua hii imesababisha kutokuwepo uwiano katika utoaji wa matangazo kwa vyombo vya habari hasa vya binafsi. Kwa vyombo vingi, havina uhakika wa kutafuta matangazo siyo tu vile vyombo vinavyoandika habari kwa

mtazamo unaonekana hasi na wenye mamlaka lakini kwa vyombo vingine pia. Ni vyombo vichache viteule kama vya chama tawala na serikali na vyombo vya mtazamo mpya wa kimkakati ndivyo vinavyopata zaidi matangazo.

Kutokana na mwelekeo huo, wahariri wengi hawana matumaini kwa kuwa vyombo vyao vinakwazwa kiuchumi na wanalazimika kutafiuta mbinu mbadala kuweza kuendelea kuwepo.

Kwa kuwa serikali ndiyo mtangazaji mkubwa, fursa ni chache.

Katika majadiliano ya karibuni mtandaoni ambayo Barazani iliyanasa, mhariri mmoja alisema kuwa vyombo vya habari tayari vimo kwenye shimo vikisubiri kuzikwa akielezea hali hiyo mbaya inatokana na aina ya habari zinazoandikwa na kuchapishwa na kutangazwa.

Kulingana na mhariri huyo, wasikilizaji ama wasomaji hawahitaji gazeti ama taarifa za habari hata vipindi kwa kuwa habari zenyewe ziko upande mmoja.

Hakuna mtu anayeweza kuweka tangazo katika vyombo vya habari vya aina hii na bila shaka inasababisha vyombo hivyo kuwa na matatizo kifedha.

Janga la virusi vya corona, alisema ni sawa na kuweka chumvi katika kidonda kilichokosa tiba.

Ingawa katika majadiliano hayo hakukutolewa ufumbuzi, ni wazi kuwa uamuzi wa kuratibu matangazo na kuwepo kwa vifungu hasi katika sheria hiyo mpya, kumechangia hali ambayo vyombo vya habari vimejikuta vipo sasa. Wahariri katika majadiliano yao hawakuzungumzia mahitaji hayo ya sheria mpya, lakini wamelalama kuhusu ukata kutokana na kushuka kwa mauzo na kukosa matangazo.

Mkongwe mmoja katika vyombo vya habari, anayekerwa na hali ya sasa inayokabili vyombo vya habari alisema kuwa uwepo wa vyombo vya habari unategemea zaidi matangazo na kuvinyima vyombo hivyo matangazo ni sawa na kukata uhai!

Kuhusu utoaji wa matangazo kwa upendeleo, alisema, wanaotoa hayo matangazo wana uhakika gani kuwa vyombo vinavyopewa matangazo vinapendwa na wananchi? Kama siyo hivyo, kuvipa matangazo ni upotezaji wa raslimali na kwamba wananchi hawatapata ujumbe uliolengwa kuwafikia.

Kupunguzwa watumishi na hata kufukuzwa kazi wahariri ni mambo yanayojiri katika baadhi ya vyombo vya habari kutokana na matatizo ya mapato na pia katika kujaribu kutekeleza matakwa ya wenye mamlaka.

Vyombo vya habari vyayumba kwa kukosa matangazo