fataawa za ad-dur an-nadhwiyd fiy ikhlaasw kalimaat at-tawhiyd - ´allaamah al-fawzaan
DESCRIPTION
Fataawa Za ad-Dur an-Nadhwiyd Fiy Ikhlaasw Kalimaat at-Tawhiyd - ´Allaamah al-FawzaanTRANSCRIPT
1
Mkusanyiko Wa Fataawa
ad-Dur an-Nadhwiyd Fiy
Ikhlaasw Kalimaat
at-Tawhiyd
Imaam Muhammad bin ´Aliy
ash-Shawkaaniy (Rahimahu Allaah)
´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
(Hafidhwahu Allaah)
Imefasiriwa Na:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
©
2
Dibaji
Bismillaah, Alhamdulillaah. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu
Muhammad na ahli zake na Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum)
mpaka siku ya mwisho. Amma ba´ad:
Himidi zote ni Zake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Aliyeniwezesha kufanya
kazi hii. Hizi ni Fataawa zilizokusanywa baada ya Duruus zote zilizotolewa
na Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) akisherehesha kitabu cha Imaam
ash-Shawkaaniy (Rahimahu Allaah) cha Tawhiyd kiitwacho “ad-Dur an-
Nadhwiyd Fiy Ikhlaasw Kalimaat at-Tawhiyd.”
Fataawa nyingi ni kuhusiana na masuala ya Tawhiyd na ´Aqiydah kwani
kitabu chenyewe ni cha Tawhiyd. Kuna baadhi ya Fataawa ni masuala ya Fiqh
na mengine ila si nyingi.
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kijitabu hichi kilichokusanya
Fataawa muhimu ziweze kutunufaisha sisi na nyinyi na kuleta faida kubwa
katika Ummah wetu wa Kiislamu. Tunamuomba Allaah Atuwafikishe sote
kwa Ayapendayo na Kuyaridhia.
Tanbihi: Fataawa zote hizi tumezifasiri kwa njia ya Video na zinapatikana
Youtube waweza kusoma na huku wasikiliza. Kwa mwenye kutaka hizo
Fataawa za Video aende Alhidaaya au Youtube kwa juu sehemu ya kutafuta
aandike au kukopi kichwa cha habari cha Fatwa (kama ilivyo hapo chini kwa
kila Fatwa ina kichwa chake cha habari) na atafute itajitokeza In Shaa Allaah.
Jazaakumu Allaahu Khayra.
Swalla Allaahu ´alaa Muhammad, wa ´alaa aalihi wa Aswhaabihi wa sallam
3
Fataawa zilizomo ni hizi zifuatazo:
01) Mwenye Maradhi Ya Kutokwa Na Ugonjwa Kuongoza Kuwa Imaam
02) Witr kabla Ya Swalah Ya Alfajiri Kwa Nusu Saa
03) Kuswalia Jeneza Mbili Bila Ya Kujua
04) Masikini Anafanya Shirki Kwa Ajili Ya Maisha Bila Ya Kuitakidi
Anachofanya
05) Kuna Tawassul Inayojuzu Kwa Mtume (´alayhis-Salaam) Baada Ya
Kufa?
06) Hukumu Ya Kutoka Msikitini Wakati Muadhini Anaadhini
07) Hekima Ya Kuwalingania Makafiri Kazini Kwake
08) Vipi Mtu Atawalingania Waabudu Makaburi?
09) Hekima Wakati Wa Kuwalingania Waabudu Makaburi
10) Kumpa Mtu Pesa Akuombee Du´aa
11) Hukumu Ya Kuwatolea Salaam Mashia Ismaa´iliyyah
12) Hukumu Ya Kunyama Makosa Ya Madu´aat Wanaokhalifu Sunnah
13) Makatazo Ya Kuwanasibishia Wanachuoni Na Mambo Yasiokuwa
Na Ushahidi
14) Lini Unaanza Huhesabu Muda Wa Kupangusa Juu Ya Soki?
15) Madu´aat Wa Ushirikina Katika Chaneli
16) Wanaodai Ni Wafasiri Wa Ndogo Katika Vyombo Vya Habari
17) Je, Maji Ya Zamzam Yakitoka Nje Ya Makkah Baraka Yake Bado
Yabaki?
18) Kurukuu Kabla Ya Kufika Katika Safu Kwa Ajili Ya Kudiriki Rakaa
19) ´Amali Za Kuweza Kumfanyia Maiti Zikamnufaisha
20) Je, Kila Maradhi Yasioweza Kutibiwa Na Madaktari Inakuwa Na
Uchawi, Kijicho Au Hasadi?
21) Kujuta Tu Baada Ya Kosa Yatosha Kuwa Ni Tawbah?
22) Je, ´Iysa (´alayhis-Salaam) Alipewa Utume Alipofikisha Miaka
Arubaini?
23) Kafiri Wanatana Kumsimamishia Hadd Akamtaka Shahaadah, Je
Atasaliwa?
24) Mzee Kakatwa Mguu Na Ana Maradhi Ya Kutokwa Na Akili, Mwaka
Mzima Haswali
4
25) Nifanye Hijrah Kuhama Kutoka Europe Na Wakati Nadhihirisha
Dini?
26) Hafidh Wa Qur-aan Ambaye Si Mwarabu Anatumbukia Katika
Shirki, Je, Ana Udhuru?
27) Watu Watapewa Udhuru Katika Shirki Mpaka Lini?
28) Huyo Si Mke Hakufai, Tafuta Mwengine!
29) Mke Mkaidi Anafanya Ya Haramu Na Kusema Nisimwingilie Katika
Uhuru Wake
30) Kijana Ameoa Mnaswara, Mke Anataka Waende Nae Kanisani
31) Je Inajuzu Kuweka Mlio Wa Simu Sauti Ya Adhaana au Aayah
Tukufu?
32) Muislamu Katumbukia Katika Shirki Kubwa, Je Atoe Shahaadah
Upya?
33) Kuswali Kwenye Msikiti Uitwao Masjid Sayyid al-Badawiy Usio Na
Kaburi
34) Je, Kijusi Kikitoka Tumboni Hufanyiwa ´Aqiyqah?
35) Hukumu Ya Mtu Anaedai Kuwa Ni Muislamu Ila Haswali
36) Muislamu Ambaye Anafanya ´Ibaadah Zake Zote Kwa Kukhalifu
Sunnah
37) Hukumu Ya Muislamu Asietoka Zakaah
38) Hukumu Ya Mwanaume Mwenye Kulipa Swawm Ya Dhwihaar
Akamjamii Mke Wake Kabla Hajamaliza Swawm Yake
39) Mwanafunzi Anaehofia Mas-ala Ya Qadhwaa Na Qadar
40) Mwanamke Mjamzito Kafa Na Mtoto Tumboni, Mtoto Atolewe Na
Kuzikwa Mwenyewe?
41) Mwanamke Kafa Baba Yake Mdogo Kafiri
42) Mwanamke Mgonjwa Kafa Naye Hakufunga Ramadhaan
43) Hukumu Ya Kuzuia Mimba Moja Kwa Moja
44) Mwanamke Kwenda Sokoni Bila Mahram
45) Mwanamke Ambaye Yuko Katika Familia Yake Kutoka Bila Ya
Ruhusa Ya Mumewe
46) Inajuzu Kuwatolea Wanawake Salaam?
47) Mwenye Kuanguka Katika Bid´ah Moja Tu Ya Kiitikadi Anakuwa
Mubtadi´ah?
48) Daa´iy Anaetoa Fatwa Kujuzisha Ndoa Ya Mut´ah Kwa Vijana
49) Miongoni Mwa Masharti Ya Laa Ilaaha Illa Allaah
50) Je, Fuqahaa´ Murji-ah Ni Mubtadi´ah?
5
51) Radd Kwa Mwenye Kusema Mzazi Kumchunguza Mtoto Wake Ni
Ujasusi
52) Waalimu Wasiofunza Tawhiyd Katika Madrasa
53) Nasaha Kwa Wanafunzi Wanaopondana Wao Kwa Wao
54) Wake Zangu Wawili Wameingia Katika Uislamu, Je Ni Wajibu Kwao
Kurudi Upya Ndoa Zao?
55) Ufafanuzi Kuhusu Kufuru Ya ´Amali (Ya Kimatendo)
56) Wajibu Wa Kumkata Ndugu Ambaye Anachukia Sunnah Na Watu
Wa Sunnah
57) Kufanya Jamaa´ah Nyingine Wakati Jamaa´ah Ya Kwanza Inapokuwa
Katika Tashahhud Ya Mwisho
58) Wafanyao Barnamiji Za Video Kwenye TV
59) Je Kutahadharisha Watu Dhidi Ya Maulamaa Wa Ahl-ul-Bid´ah Ni
Katika Kusengenya Na Kueneza Uvumi?
60) Radd Kwa Mwenye Kusema Kaburi La Mtume Liko Ndani Ya
Msikiti
61) Wanayomba Makaburi Kwa Hoja Eti ´Umar Alimuomba Abbaas
(Radhiyallaahu ´anhum)
62) Ribaa Ni Dhambi Ya Pili Baada Ya Dhambi Ya Ushirikina
63) Mwenye Kula Ribaa Pamoja Na Kujua Kuwa Ni Haramu
64) Risaalah Ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab Kwa Watu Wa
Europe
65) Jinsi Ya Kumtibu Aliemsibu Ndugu Yake Kwa Kijicho
66) Tawassul Na Sharti Zake
67) Sijdah at-Tilaawah Ndani Ya Gari
68) Sisi Tunawaua Washirikina Tu Na Hatuwaui Waislamu
69) Sunnah Ya Kuangalia Kidole Cha Shahaadah Wakati Wa Tashahhud
70) Sifa Ya Swalah Ya Istisqaa Ni Kama Swalah Ya `iyd
71) Aina Mbali Mbali Za Tawassul Na Hukumu Zake
72) Nyote Ni Wakoseaji Na Mbora Ni Yule Mwenye Kutubia
73) Tawhiyd-il-Ilaahiyyah Na Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah
74) Tawhiyd-ul-Khaaliqiyyah, Tawhiyd-ul-Raaziqiyyah Na Tawhiyd-ul-
Haakimiyyah
75) Tofauti Baina Ya Sanamu Na Wathan
76) Tofauti Ya Ujinga Na Upotevu
77) Usikae Na Mvuta Sigara!
78) ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Madu´aat Wanaohudhuria Katika
Maulidi
6
79) Kuomba Kwa Nuru Ya Uso Wa Allaah Mambo Ya Kidunia Na
Aakhirah
80) Kuswalishwa Na Imaam Wa Kisufi Ambaye Msimamo Wake
Haujabainika
81) Shubuha Za Waabudu Makaburi
82) Waabudu Makaburi Lazima Wasimamishiwe Hoja!
83) Kila Aliye Fikiwa Na Qur-aan Hoja Imemsimamia
84) Qur-aan Yatosheleza Kuwa Hoja Kwa Kila Mtu!
85) Kufasiri Kwa Ajili Ya Taazia (Kutoa Ole Kwa Wafiwa)
86) Wanafunzi Wanaotoka Katika Miji Ya Kikafiri Na Kwenda Kusoma
Saudi Arabia Kisha Wanabaki Huko
87) Utata Wa Waabudu Makaburi
88) Wanaolilia Umoja Wa Uislamu Bila Kujali ´Aqiydah
89) Ni Kweli Kwamba Kuna Wenye Kuomba Kwenye Kaburi La Mtume?
90) Hukumu Ya Kuapa “Wallaahi Kwa Nyumba Aliyojenga Allaah”
91) Vipi Ntamlingania Baba Yangu Aingie Katika Uislamu?
92) Vipi Muislamu Kafiri Asieswali Atatubia?
93) Vipi Kumsimamishia Mtu Hoja?
94) Vipi Mtu Atamjua Mwanachuoni?
95) Jinsi Ya Kutangamana Na Makafiri Kazini
96) Wanafunzi Kupiga Radd Makundi Potevu Katika Miji Yao
97) ´Uzayr Ni Nani?
98) Aina Mbali Mbali Za Tawassul Na Hukumu Zake
99) Mzee ambaye Muusa Alikutana Naye Madyaan Ni Mtume Shu´ayb
(´alayhis-Salaam)?
100) Kuswali Nyuma Ya Mshirikina Kwa Kusoma Msikiti Wa Sunnah
101) Asiyeweza Kulipa Kafara Ya Yamini Kwa Kulisha Anafunga
102) Shaykh Muhammad ibn ´Abdil-Wahhaab Si Bora Kuliko
Wanavyuoni Wa Madhehebu Manne
103) Kupita Mbele Ya Mwenye Kuswali Kwa Nguvu
104) ´allaamah al-Fawzaan Kuhusu Answaar-us-Sunnah
105) Kuacha ´Amali Kwa Kukhofia Riyaa
106) Kumwita Mtu Bwana
107) Kumuambia Kafiri Ni Rafiki
108) Hukumu Unaposhtushwa Na Kitu Kuita “Ewe Mtume”
109) Hukumu Ya Kusema Mimi Ni Kwa Allaah Na Kwako
110) Anaepinga Hadiyth Ya Shafaa´ah Anakuwa Kafiri?
111) Hukumu Ya Kuapa Kwa Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
7
112) Anataka Kumpa Alieingia Katika Uislamu Tafsiri Ya Qur-aan
113) Kumuomba Kafiri Msaada Kwa Ayawezayo
114) Kuomba Msaada Kwa Majini
115) Je, Kufuru Ya Kimatendo Yaweza Kuwa Kubwa?
116) Haijuzu Kuomba Maiti Kwa Kuwa Hana Anachokiweza
117) Sote Tuwaite Washirikina Kuwa Ni Washirikina
118) Je, Ni Kweli Kuwa Wengi Wa Washirikina Wa Leo Wanafanya Shirki
Kwa Kutokujua?
119) Nina Miaka 17 Wazazi Wangu Hawaswali Alfajiri, Unaninasihi Vipi?
120) Kulipa Swalah Za Rawaatib Kinyume Na Wakati Wake
121) Baada Ya Siku Tatu Ndo Kajua Kuwa Aliswahi Kinyume Na Qiblah,
Alipe?
122) Kuomba Viumbe Waliyo Hai Wakuombee Du´aa Ni Makosa Na
Udhaifu?
123) Hukumu Ya Kuambizana “Ijumaa Yenye Baraka” Siku Ya Ijumaa
124) Hukumu Ya Kutawassul Kwa Jaha Ya Mtume (´alayhhis-Salaam)
125) Hukumu Ya Kuwaombea Du´aa Watu Wa Bid´ah
126) Je, Kutamka Shahaadah Tu Bila ´Amali Inatosha?
127) Hukumu Ya Anaesema Laa Ilaaha Illa Allaah Ila Hakufuru
Vinavyoabudiwa Kinyume Na Allaah
128) Wana Ada Wakiona Maiti Usingizi Wanamchinjia Na Kualika Watu
Walimani
129) Kumuomba Allaah Kwa Kusem “Ewe Wa Allaah”
130) Hukumu Ya Mtoto Kushtushwa Na Kusema “Ewe Mama”
131) Watu Wataotoka Motoni Bila Ya Kufanya Kheri Yoyote
132) Hukumu Ya Wazazi Wasiofahamu Kiarabu Wanaita “Ewe Mtume Wa
Allaah!”
133) Mume Anamlingania Mke Wake Katika ´Aqiydah Ya Ash´ariyyah,
Mke Amtii?
134) Hukumu Mwanamke Kusoma Qur-aan Kwa Mashaykh Wanaume
135) Acheni Falsafa, Mwenye Kufanya Shirki Ni Mshirikina!
136) Hukumu Ya Kuweka Nadhiri Kwa Asiyekuwa Allaah
137) Hukumu Ya Kuitamidi Kwa Allaah Kisha Kwa Kiumbe
138) Hukumu Ya Kutosoma Kwa Tajwiyd
139) Kumuomba Mtu Ni Vibaya?
140) Nilikuwa Na Deni La Mtu Simjui Ama Sasa Nimejua, Nimpe Au
Nitoe Swadaqah?
141) Tahadhari Na Kundi La Qur-aaniyyah Linalopinga Sunnah!
8
142) Makataza Ya Wanafunzi Kuwapa Zawadi Waalimu Zao
143) Imaam ash-Shawkaaniy Ni Imaam Wa Ahl-us-Sunnah
144) Ni nani ´Abdul-Qadir al-Jaylaaniy?
145) Waabudu Makaburi Wanaotumia Hoja Aayah Katika Suurat-ul-Kahf
146) Inajuzu Kusema Allaah Na Mtume Wake Ndio Wanajua?
147) Aliechelewa Swalah Ya Istisqaa Upi Wajibu Wake?
148) Nasaha Kwa Anaekhofia Riyaa
149) Imaam Kukariri Aayah Fulani Anaposalisha Jamaa´ah
150) Anamtangulia Kumsalia Maiti Kabla Ya Imaam Kusalisha
151) Kuelekea Kaburi La Mtume (´alayhis-Salaam) Msikitini Na
Kumuomba
152) Mgonjwa Anaepata Tabu Kutia Wudhuu Afanye Nini?
153) Msafiri Anaejua Lini Atarudi Kwao Hachukui Hukumu Za Msafiri
154) Anaemwendea Mpiga Ramli Kisha Akatubia Swalah Zake
Zitakubaliwa?
155) Lini Mtu Anaweza Kuingia Peponi Bila Ya ´Amali?
156) Je, Athari Ya Mtume (´alayhis-Salaam) Inapatikana Mpaka Hivi Leo?
157) Ni Sahihi Muadhini Kusema Haqqan Laa ilaaha illa Allaah?
158) Mgonjwa Anaruhusiwa Kujumuisha Swalah Na Haruhusiwi
Kuzifupisha
159) ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Tijaaniyyun Na Burda
160) Qaswiydah Ya Burda Ina Shirki Na Ghuluu
161) Kulingania Katika Tawhiyd Inatosha Kukataza Tu Kuabudu
Makaburi?
162) Tofauti Baina Ya Du´aa Ya Masuala Na Du´aa Ya ´Ibaadah
163) Eda Ya Mwanamke Aliyezaa Baada Ya Kufa Mumewe Kwa Saa Au
Dakika Kadhaa
164) Wanafunzi Wanadai Kwamba Kusoma “Suurat-ul-Ikhlaas Baada Ya
Kila Swalah Ni Bid´ah
165) Ghurabaa Ni Watu Gani?
166) Hukumu Ya Mafukara Wanaotumbukia Katika Shirki Kwa Ajili Ya
Kutafuta Riziki
167) Anadai Watu Hawana Haja Ya Kusoma Elimu Imejaa Kwenye
Internet Na Kwenye Mikanda
168) Hukumu Ya Kusema Washirikina Ni Ndugu Zetu
169) Anataka Kuacha Kupiga Punyeto Anashindwa, Ipi Nasaha Yako?
170) Haijuzu Kuomba Shafaa´ah (Uombezi) Kwa Maiti Sawa Mtume Au
Mwengine Yeyote
9
171) Kuvaa Nguo Za Makafiri Za Kumalizia Masomo
172) Hukumu Ya Anaeacha Kufunga Ramadhaan Ila Hapingi Uwajibu
Wake
173) Anaetetea Ushirikina Sawa Hakimu Au Yeyote Yule Ni Mshirikina
174) Mwanaume Si Sawa Na Mwanaume
175) Daa´iy Mpotofu Anaewaponda Maswahaba (radhiya Allaahu
´anhum)
176) Anaejuzisha Kujengea Misikiti Makaburi Ni Mshirikina
177) Imaam Kujumuisha Maghrib Na ´Ishaa Wakati Wa Mvua Na Baridi
Kali
178) Ahl-ul-Kitaab Wa Zama Hizi Inajuzu Kuwaoa
179) Wazazi Haijuzu Kuwapeleka Watoto Katika Madrasah Ya Ahl-ul-
Bid´ah Kama Masufi
180) Itikafi Potofu Ya Kuogopa Kijicho Kwa Kutupa Kipande Cha
Chakula Chini
181) Allaah (Ta´ala) Ana Sifa Ya Nafsi
182) Allaah Yuko Kwenye Jiha Ya Juu
183) Je Al-Muhaasib Ni Jina La Allaah (Ta´aal)?
184) Khatari Ya Kumkufurisha Mtu Binafsi?
185) Maulamaa Waliopinda Wasiojua Tawhiyd
186) Maiti Hata Wakisikia Hawawezi Kukunufaisha Kwa Kitu
187) Picha Ni Haramu Sawa Za Digital Au Za Aina Yoyote
188) Usingizi Hauwajibishi Kustanji, Kinachowajibisha Ni Kutokwa Na
Kitu Tupuni
189) Kila Kivazi Cha Mwanaume Chenye Kuvuka Kongo Mbili Za Miguu
Ni Motoni
190) Tawassul Ni ´Ibaadah?
191) Kulisha Watu Watano Mara Mbili Ili Ihesabike Kalipa Kafara Ya
Yamini Kwa Watu Kumi
192) Aliyeuawa Na Usaamah Bin Zayd Ni Katika Maswahaba?
193) Kaweka Nadhiri Kuamka Kuswali Fajr La Sivyo Ataswali Rakaa
Kumi
194) Kufunga Safari Kwenda Kwenye Kaburi Ya Mtume Au Mwengine
Yoyote
195) Kila Jina La Allaah Linajenga Sifa Kinyume Na Matendo
196) Hukumu Ya Swalah Ambayo Wudhuu Haukushika Kidogo Cha
Mguuni
10
197) Aliopigana Nao Abu Bakr (radhiya Allaahu ´anhu) Ilikuwa Ni Kwa
Ajili Ya Kufuru Yao
198) Kazi Ya Kuamrisha Mema Na Kukataza Mabaya Ni Ya Nani?
199) Mtazamo Wa Kwanza Kuiangalia Ka´abah Mtu Hukubaliwa Du´aa?
200) Hukumu Ya Kuapa Kwa Ahadi Ya Allaah
201) Kuchinja Kwa Ajili Ya Allaah Kwenye Kaburi La Walii Fulani
202) Kuchukua Mkopo Benki Kwa Ajili Ya Kuoa
203) Kufanya Mzaha (Maskhara) Na Hadiyth Za Mtume
204) Ruqyah Kwenye Maji Ya Zamzam Na Mti Wa Mzaituni
205) Tofauti Ya Kufuru Na Shirki
206) Kufanya Mjadala Na Ahl-ul-Bid´ah
207) Kuacha Nyumba Inasoma Qur-aan Na Hakuna Wakuisikiliza
208) Waitao “Ewe Yuma” Wanaposhtuliwa Na Kitu
209) Haijuzu Kuwanunulia Wanawake Simu Za Khatari Za Kisasa
210) Ni Haramu Kumpa Mwanamke Mwanamke Ajinabi
211) Kumpigia Simu Aliehai Na Kumuomba Akuombea Du´aa
212) Kuomba Rahma Na Kinga Ndani Ya Swalah
213) Kauli Sahihi Kuhusiana Na Thawabu Kumfikia Maiti
214) Haijuzu Kuomba Kwa Uso Wa Allaah Mambo Ya Kidunia
215) Kumwambia Mtu Unaefanya Kazi Kwake “Bwana Wangu”
216) Kuosha Mikono Mtu Anapoamka Kutoka Usingizini
217) Kutokataza Shirki Kwa Kukithiri Kwa Jambo Lile Kwa Watu
218) Nikiona mtu mwenye kumshirikisha Allaah na nisimbainishie
219) Kumsalia Mtume (´alayhis-Salaam) Ni Katika Sababu Za
Kukubaliwa Du´aa
220) Kutawassul Kwa Allaah Kwa Kukusanyika Msikitini Na Kufanya
Dhikr
221) Kutenga Siku Maalumu Kwa Ajili Ya Taazia
222) Tofauti Ya Kusimama Kwa Kumuadhimisha Mtu Na Kumpokea
Mgeni
223) Haijuzu Kuleta Adhkaar Maalumu Baada Ya Swalah Ambazo
Hazikuthibiti
224) Hakuna Haja Ya Kuchukua Elimu Kwa Mtu Mwenye Baadhi Ya
Bid´ah
225) Kuswali Nyuma Ya Imaam Anaevaa Herizi
226) Kunyunyizia Maji Ya Kisomo Kwenye Kuta Za Nyumbani Kuzuia
Madhara
227) Kuswali Na Nguo Yenye Damu
11
��م ا�ر�ن ا�ر��م
01) Mwenye Maradhi Ya Kutokwa Na Ugonjwa Kuongoza Kuwa Imaam
Swali:
Ipi hukumu ya kwenye tatizo la kutokwa na mkojo wakati anapowaongoza
watu katika swalah - yaani anakuwa imaam, je inajuzu kwake kuwa imaam
ikiwa hawakupata mwengine awazae kuwasalisha?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mwenye tatizo la kutokwa na mkojo haijuzu kumuongoza mtu ila yule
nwenye tatizo kama yeye. Ama mtu salama [asiye na ugonjwa huu] haijuzu
kuswali nyuma yake. Kwa kuwa mtu kama huyu hata akitokwa na mkojo
[anaendelea] kuswali na swalah yake ni sahihi. Lakini haisihi swalah ya mtu
salama nyuma yake. Anaweza tu kumuongoza mwenye tatizo kama yeye,
mwenye hadathi daima [kama yeye].
02) Witr kabla Ya Swalah Ya Alfajiri Kwa Nusu Saa
Swali:
Mimi naswali witr kabla ya swalah ya alfajiri kwa nusu saa. Je kitendo changu
hichi ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
12
Umesali usiku hakuna ubaya. Witr inasaliwa usiku mzima ni sawa. Sawa ni
mwanzo wa usiku au mwisho wake.
03) Kuswalia Jeneza Mbili Bila Ya Kujua
Swali:
Tukiswalia jeneza msikitini, na wakati wakufika makaburini kukaletwa
jeneza. Sijui kama ni katika jeneza tuliyoiswalia [msikitini] au hapana.
´Allaamah al-Fawzaan:
Mswalie. Hata swalah ikikariri kwa maiti ni kheri kwake. Kwa kuwa du´aa ni
jambo jema kwake yeye na wewe pia. Mswalie!
04) Masikini Anafanya Shirki Kwa Ajili Ya Maisha Bila Ya Kuitakidi
Anachofanya
Swali:
Mwenye kulingania watu katika kuabudu makaburi ya watu wema kwa ajili
ya kupata riziki, naye anajua kuwa hii ni shirki na wala haamini kuwa
waliomo ndani ya kaburi wananufaisha au kudhuru...
13
´Allaamah al-Fawzaan:
Huyu kakhasirika duniani na akhera - Allaah Atukinge. Riziki iko mikononi
mwa Allaah na si kwenye makaburi. Ikiwa ni mkweli katika kazi yake aombe
riziki kutoka kwa Allaah. Na si kwenye makaburi.
05) Kuna Tawassul Inayojuzu Kwa Mtume (´alayhis-Salaam) Baada Ya
Kufa?
Swali:
Je kuna masharti ya kujuzisha kutawassul kwa Mtume (swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam) baada ya kufa kwake katika du´aa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Tawassul kwa kumfuata na kumpenda (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Kwa kuwa haya ni matendo mema. Kumfuata na kumpenda haya ni matendo
mema. Tawassul kwavyo. Ama kutawassul kwa dhati ya Mtume, haijuzu
kutawassul kwake. Wala kutawassul kwa jaha yake.
06) Hukumu Ya Kutoka Msikitini Wakati Muadhini Anaadhini
Swali:
14
Ipi hukumu ya mwenye kutoka msikitini na muadhini anaadhini?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa ni kwa dharurah na atarejea, hakuna ubaya. Kama kutawadha, kuongea
na mtu halafu atarejea, hakuna ubaya. Ama ikiwa hatorejea, hili ndo sehemu
ya kutazamwa. Anasema mmoja katika Maswahaba ´Umar bin Yaasir.
"Anaetoka msikitini baada ya adhaana, kamuasi Abal Qaasim [Mtume]
(swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)."
Alitoka mtu baada ya adhaana, akasema ama huyu kamuasi Abal Qaasim
(swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kutoka bila ya udhuru haijuzu. Ama kwa
udhuru hakuna neno.
07) Hekima Ya Kuwalingania Makafiri Kazini Kwake
Swali:
Ipi njia nzuri tunayotakiwa kuifuata katika kuwalingania makafiri ambao
wako pamoja nami kazini? Je naweza pia kula pamoja naona kuwapa
swadaqah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, hakuna neno. Waweza kula nao na wao wakala nawe katika [chakula]
mubaha. Kuwapa swadaqah ya zakaah haijuzu. Ama [swadaqah] ya kujitolea
15
[ya kawaida] hakuna ubaya kwa hilo. Khasa ikiwa kwa hili walenga
kuwaingiza katika Uislamu.
08) Vipi Mtu Atawalingania Waabudu Makaburi?
Swali:
Je waabudu makaburi tuwawie wagumu na wanadiwe kabisa kwa kuambiwa
ewe fulani na fulani? Au tuwanasihi kwa uzuri [upole] na tuwalinganie kwa
uzuri?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mwenye kukubali nasaha, tunamnasihi kwa uzuri upole. Ama kwa yule
asiyekubali nasaha, huyu mtu awe mgumu kwake.
��ھد ا�����ر وا�������ن وا��ظ ���م ��� �� ا��� � �� أ�
“Ewe Nabii! Pambana na makafiri na wanaafiki, na kuwa mgumu kwao!”
(66:09)
Kuwa mgumu! Ikiwa hawakubali, hakuna njia ingine ila kuwa mgumu kwao.
Upole ni kwa yule mwenye kukubali [nasaha].
09) Hekima Wakati Wa Kuwalingania Waabudu Makaburi
16
Swali:
Katika mji wangu kuna waabudu makaburi. Je ni lazima kwangu kuwawekea
wazi kuwa ni makafiri? Au badala ya hili niwalinganie?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, wabainishie kwa hekima na uzuri. Huenda wakakubali. Usiwaambie
nyinyi ni makafiri nyinyi ni washirikina. Watakukimbia na... Lakini waambie
Qur-aan Allaah Kasema kadha na Mtume Wake kasema kadha.Wabainishie
kwa uzuri na hekima.
10) Kumpa Mtu Pesa Akuombee Du´aa
Swali:
Mwenye kuwapa watoto wadogo pesa ili wamuombee du´aa. Je kitendo hichi
kinajuzu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, mtu hapewi ujira kwa ajili ya kumuombea mwengine. Akiomba kwa
ajili ya [kupewa] ujira haitokubaliwa du´aa yake. Kwa kuwa du´aa ni
´ibaadah, haichukuliwi ujira.
17
11) Hukumu Ya Kuwatolea Salaam Mashia Ismaa´iliyyah
Swali:
Mimi nina ndugu katika Ismaa´iliyyah [kundi katika Mashia] na nafanya
juhudi kuwalingania waingie katika Uislamu. Je niwatolee salaam wakati
naenda kuwazuru kwenye manyumba yao kwa kusema "as-salaam
´alaykum"? Na ikiwa kufanya hivyo haijuzu, je ntakuwa mwenye kupata
madhambi nikiwatolea salaam hivi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hii salaam ni ya Kiislamu. Haitolewi kwa watu kama hawa. Lakini waweza
kuwaambia "as-Salaam ´alaa mani taba´al hudaa." Hili ndio alilolifanya
Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
12) Hukumu Ya Kunyama Makosa Ya Madu´aat Wanaokhalifu Sunnah
Swali:
Je wale wanyamazao na wala hawabainishi baadhi ya makosa ya wafuasi
wanaofuata mifumo, ambao wanafuata mifumo kinyume na mfumo wa
Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Je mwenye kunyamazia hilo
anaingia katika wale wenye kuficha aliyoteremsha Allaah [waliolaaniwa]?
18
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Lazima abainishe kwa kila mkosaji. Sawa makosa yake ikiwa ni ya
shirki au kinyume na shirki au maasi au... Lazima abainishie watu. Wenye
kukaa kimya naye ana uwezo wa kubainisha, atakuwa ni mwenye kuficha
elimu. Au mtu mwenye makosa katika manhaj.
13) Makatazo Ya Kuwanasibishia Wanachuoni Na Mambo Yasiokuwa Na
Ushahidi
Swali:
Ni jambo lenye kujulikana kuwa Shaykh ibn Baaz alijibu kuwa wanachuoni
ambao wanawapata waabudu makaburi udhuru kwa ajili ya ujinga
wanafanya taawili na ni wajibu kuwawekea wazi. Lakini ikiwa wanachuoni
hawa watawapa udhuru watu hawa baada ya kuwawekea wazi hoja....
´Allaamah al-Fawzaan:
Ewe ndugu tuletee maneno hayo ya Shaykh ibn Baaz. Leta dalili tuisome hapa
halafu ndo tutaangalia maneno yako haya. Wanachuoni wana nafasi zao,
msiwanasibishie kitu ila kwa [kuleta] vyanzo kutoka katika maneno yao. Ili
uthibitishe ukisemacho. Ama kujisemea tu fulani kasema hivi kuhusu Shaykh,
au alisema fulani - ananukuu kutoka kwa Shaykh kuwa kasema kadha, hili
halijuzu.
19
14) Lini Unaanza Huhesabu Muda Wa Kupangusa Juu Ya Soki?
Swali:
Lini unaanza kuhesabu muda wa kupangusa juu ya soki?
´Allaamah al-Fawzaan:
Unaanza unapopata hadathi baada ya kuzivaa. Utapotenguka wudhuu wako
uliouvaa juu yake, wudhuu wako unaanza muda ule [mpako wa kwanza]
ulioanza kupangusa. Ulipopata hadathi [ukapangusa] baada tu ya kuzivaa.
15) Madu´aat Wa Ushirikina Katika Chaneli
Swali:
Katoa Fatwa mmoja katika wale wanaodhiri katika chaneli mbovu kwamba
tawassul na kuomba au kutafuta kinga kwa mawalii na watu wema waliokufa
ni jambo linajuzu, bali ni jambo lina ujira mwingi. Je inajuzu kuchukua kutoka
kwake...
´Allaamah al-Fawzaan:
Huyu ni katika wao. Huyu ni katika wao waabudu makaburi. Anaejuzisha
mambo haya ni katika wao, usidanganyike kuwa anadhihiri katika wao
20
mmoja wao katika madu´aat [walinganizi] wa makaburi. Lisikudanganye hili.
Hakuna mwanachuoni awazae kusema hili anamuogopa Allaah na kumcha.
16) Wanaodai Ni Wafasiri Wa Ndogo Katika Vyombo Vya Habari
Swali:
Katika siku zimezopita kumekithiri wafasiri wa ndoto, na imekuwa
wanajitokeza hata kwenye chaneli mbovu...
´Allaamah al-Fawzaan:
Wanatafuta pesa hao, wanatafuta pesa hao. Leo jambo hili imekuwa ni kama
biashara. Watu hawa wasifatwe na wala wasiangaliwe [kwenye hivyo
vyombo vyao vya habari].
17) Je, Maji Ya Zamzam Yakitoka Nje Ya Makkah Baraka Yake Bado
Yabaki?
Swali:
Yakipelekwa maji ya zamzam katika mji wowote, yatabaki kuwa na baraka
inayojulikana au yatapungua?
21
´Allaamah al-Fawzaan:
Kwanini [ipungue baraka]? Maji ya zamzam yana baraka sehemu yoyote
yawapo.
18) Kurukuu Kabla Ya Kufika Katika Safu Kwa Ajili Ya Kudiriki Rakaa
Swali:
Kuna mtu ameingia msikitini na imaam amerukuu, kwa ajili ya kutaka kudiri
rakaa akarukuu kabla ya kufika katika safu. Na baada ya kufika kwenye
rukuu akawa anatembea [kwa kusutama] kwa kupiga hatua kama kumi hivi
au zaidi ili afike kwenye safu. Ipi hukumu ya swalah yake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hili kalikataza Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alilifanya Abu
Bakr (radhiya Allaahu ´anhu) na akamkataza.
Alimwambia:
"Allaah Akuzidishie juhudi, na wala usirudi. Halifanywi hili wala halijuzu.
Tembea taratibu kama alivyosema Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Mtazowahi swalini na zitazowapita timizeni au lipeni."
19) ´Amali Za Kuweza Kumfanyia Maiti Zikamnufaisha
22
Swali:
Kuna mtu kafa ndugu yake. Ipi amali bora awezayo kumfanyia imnufaishe
kwayo huyo maiti?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kumtolea swadaqah, kumuombea du´aa, amhijie na amfanyie ´Umrah. Yote
haya imethibiti dalili zake.
20) Je, Kila Maradhi Yasioweza Kutibiwa Na Madaktari Inakuwa Na
Uchawi, Kijicho Au Hasadi?
Swali:
Je ni kila maradhi ambayo matabibu hawakuweza kuyatibu inakuwa ni
uchawi, au kijicho au hasadi? Na nini unaninasihi mimi ni mtu nimepatwa na
mfano wa maradhi haya, kwa kuwa watu wengi wananambia ni uchawi, na
hili [kuambiwa hivi] limenizidishia] pia maradhi.
[Mtume anasema]:
"Allaah Hakuteremsha ugonjwa ila Kateremsha dawa yake, mwenye kujua
amejua na asiyekuwa hakujua."
Kama hawakuyajua baadhi ya matabibu, kuna matatibu wengine wayajuayo
[maradhi hayo]. Usiishie kwa matatibu wawili watatu, maadamu unaweza
kupata wengine. Waulize huenda Allaah Akajaalia kupitia katika mikono yao
ponyo. Ama uchawi unatibiwa kwa Qur-aan au kwa du´aa mubaha. Hakuna
23
makatazo ukatibiwa kwa Qur-aan na ukatibiwa kwa du´aa mubaha. Ama
kutibiwa kwa wachawi, hili halijuzu.
21) Kujuta Tu Baada Ya Kosa Yatosha Kuwa Ni Tawbah?
Swali:
Je kujuta baada ya kufanya maasi moja kwa moja inachukuliwa kuwa ni
[kama kufanya] tawbah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haitoshelezi kujuta tu. Lazima mtu aache dhambi hio na aazimie kuwa
hatorudi. Halafu ndo ajute kwa dhambi. Masharti matatu [ya tawbah].
22) Je, ´Iysa (´alayhis-Salaam) Alipewa Utume Alipofikisha Miaka
Arubaini?
Swali:
Je imethibiti kuwa Iysa (´alayhis-Salaam) kuwa alipewa Utume kabla ya
kufikisha miaka arubaini?
´Allaamah al-Fawzaan:
24
Allaah Ndiye Ajuae zaidi.
Swali La Pili:
Na je imethibiti kuwa katika mwisho wa dunia atapoteremka kwamba ataoa
na kuzaa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Litapodhihiri hilo tutawafunza, [msijali!]. Kuna mmoja alimuuliza Taabi´iyn,
akasema: "Iblisi ana watoto, nani mke wake?"
Akamwambia: "Halikudhihiri hili."
Kwanini maswali kama haya ya pumba, kwanini mnayauliza??!!
23) Kafiri Wanatana Kumsimamishia Hadd Akamtaka Shahaadah, Je
Atasaliwa?
Swali:
Je mwenye kusimamishiwa hadd (adhabu) kwa kuwa ni mchawi au mwenye
kuritadi akasema Laa ilaaha illa Allaah kabla ya kusimamishiwa hadd, je
atasaliwa na kuzikwa katika makaburi ya Waislamu?
25
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, atafanyiwa anayofanyiwa alieritadi. Lakini ni baina yake yeye na
Allaah ikiwa tawbah yake ni sahihi - Allaah Ndiye Aijuae zaidi. Tunamwachia
hilo Allaah. Ama sisi tunamsimamishia hadd na tunamfanyia anayofanyiwa
alieritadi.
24) Mzee Kakatwa Mguu Na Ana Maradhi Ya Kutokwa Na Akili, Mwaka
Mzima Haswali
Swali:
Baba yangu ni mgonjwa sasa miaka 30, wakati fulani anakuwa bado yu na
akili na wakati mwingine haiwi hivyo. Mwaka ulopita alikatwa mguu wake
na wala hawezi kufanya kitu ila kwa msaada wa watoto, na mwaka mzima
haswali. Swali ni vipi ataswali baba yangu? Na je tumlipie swalah zake
zilizompita mwaka mzima au miwili?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa akili zake bado zimebaki anaswali kwa kiasi cha hali yake.
�� ا$!ط"!م ��!��وا %�
”Basi mcheni Allaah kama mwezavyo.” (64:16)
26
Aswali kwa wudhuu au kwa kutayamamu. Aswali hali ya kuwa amesimama
au amekaa au kwa ubavu nk - kadiri na atavyoweza.
�� ا$!ط"!م ��!��وا %�
”Basi mcheni Allaah kama mwezavyo.” (64:16)
Ama ikiwa akili zake zimeenda na hajui kitu kinachoendelea, hana juu yake
swalah.
25) Nifanye Hijrah Kuhama Kutoka Europe Na Wakati Nadhihirisha Dini?
Swali:
Mimi niko katika mji wa Europe, je ni wajibu kwangu kufanya Hijrah
[kuhama] pamoja na kuzingatia ya kwamba ninadhihirisha swawm, swalah
na adhaana?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ukiweza kufanya Hijrah hama - ukiweza. Na ikiwa huwezi wewe utakuwa
mwenye kupewa udhuru [ila] pamoja na kushikamana [bara bara] na dini
yako. Na huko si kudhihirisha dini. Kufunga kwako, kuswali nk na hawasemi
kitu [makafiri]. Sivyo hivyo kudhihirisha dini. Kudhihirisha dini ni kulingania
kwa Allaah, kulingania katika Tawhiyd, na katika kumuabudu Allaah na
katika dini ya Kiislamu. Huku ndo kudhihirisha dini.
27
26) Hafidh Wa Qur-aan Ambaye Si Mwarabu Anatumbukia Katika Shirki,
Je, Ana Udhuru?
Swali:
Ikiwa mfanya shirki kahifidhi Qur-aan lakini sio mwarabu na wala hafahamu
maana ya Aayaat, je inaweza hili kuwa udhuru kwake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haitoshi kwake kuhifadhi tu Qur-aan. Lazima aulize maana yake na tafsiri.
Hili halitoshi, ni mpuuzaji. Kwanini asiulize?! Ila tu ikiwa hakuwa na uwezo
na wala hakupata wakati, huyu atapewa udhuru. Lakini ikiwa ni mwenye
kuweza kusomakiarabu na kufahamu Qur-aan, huyu hapewi udhuru. Kwa
kuwa ni mpuuzaji.
27) Watu Watapewa Udhuru Katika Shirki Mpaka Lini?
Swali:
Masuala ya kupewa udhuru kwa ajili ya ujinga yanachukuliwa ni katika
masuala naazilah hayaongelewi na yeyote ila wanachuoni wakubwa tu?
´Allaamah al-Fawzaan:
28
Kupewa udhuru kwa ajili ya ujinga - kwa hakika leo, udhuru kwa kila
anaetumbukia katika shirki na anatumbukia katika kufuru wanasema huyu ni
mjinga, pamoja na kuwa Qur-aan inasomwa usiku na mchana. Katika idhaa
zao wanasikia. Mpaka lini ujinga?
28) Huyo Si Mke Hakufai, Tafuta Mwengine!
Swali:
Kuna mtu Kamneemesha Allaah kwa kumpa msimamo naye kaoa lakini mke
wake hataki ajidhihirishe kama Salafiy - kama kufuga ndevu na kufupisha
nguo. Na wakatianapomuamrisha kuachana na mambo ya mchanganyiko
[wanaume na wanawake] na kwenda kwenye hafla za muziki anakataa.
Nimemsubiria na kumnasihi. Ipi nasaha yako kwa hilo kwa kuwa sina watoto
nae?
´Allaamah al-Fawzaan:
Alhamdulillaah huna nae watoto. Huyu ikiwa hasikii tengana nae na tafuta
mke mwengine.
29) Mke Mkaidi Anafanya Ya Haramu Na Kusema Nisimwingilie Katika
Uhuru Wake
Swali:
29
Mke wangu anafupisha nywele zake na hajali katika kufupisha kwake.
Nimemnasihi kwa hilo na kuwa ni wajibu anitii ananijibu kuwa "Huu ni
uhuru wangu, na eti namwingilia katika mambo yake". Ipi nasaha yako
kwangu na kwake kwa hilo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, qadhia hii imeenewa kwa watu. Nayo ni kuhusu udhuru - uhuru wa
maoni, uhuru wa kutabiri, uhuru wa tabia. Nini maana ya uhuru? Uhuru ni
katika mipaka ya Shari´ah, uhuru ni katika mipaka ya Shari´ah. Ama uhuru
unaovuka mipaka ya Shari´ah umekatazwa na ni upotofu. Sisi ni waja wa
Allaah Waislamu. Tunatekeleza amri za Allaah (´Azza wa Jalla).
30) Kijana Ameoa Mnaswara, Mke Anataka Waende Nae Kanisani
Swali:
Mimi ni kijana nimemuoa mnaswara na anahudhuru pamoja nami ijumaa na
sikukuu kwa kutaka aongoke [awe mwislamu], lakini anataka nende nae
kanisani ili "Qissiysu" [mchungaji] aibariki ndoa yetu...
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Hapana! Hapana! Haijuzu kwenda nae. Wala hatokubariki huyo
Qissiysu. Ni Shaytwaan na si Qissiysu. Hana baraka. Baraka zinatoka kwa
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Usende nae! Na ichukie dini yake. Ichukie
dini yake chuki kubwa kweli kweli.
30
31) Je Inajuzu Kuweka Mlio Wa Simu Sauti Ya Adhaana au Aayah Tukufu?
Swali:
Je inajuzu kuweka mlio wa simu sauti ya adhaana au Aayah tukufu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Zisitumiwe adhkaar katika simu kwa ajili ya tanbihi ya maongezi.
Huu ni mtihani kwa dhikr - mtihani kwa Qur-aan.Weka mlio usiokuwa na ala
wala muziki wala... kwa jili tu ya kukushtua [kuwa kuna mtu anapiga].
32) Muislamu Katumbukia Katika Shirki Kubwa, Je Atoe Shahaadah Upya?
Swali:
Ukiona mtu anafanya kitendo cha shirki kisha nikambainishia kuwa hii ni
shirki akatubia. Je ni juu yake kutamka shahaadah [upya]?
´Allaamah al-Fawzaan:
Akiwa ni Muislamu naye anafanya shirki atatamka shahaadah. Ama ikiwa sio
Muislamu na ukambainishia huyu anaingia katika Uislamu upya, si kwamba
karitadi kisha akatubu.
31
33) Kuswali Kwenye Msikiti Uitwao Masjid Sayyid al-Badawiy Usio Na
Kaburi
Swali:
Katika mji wetu nje ya mji huu [Saudia] kuna Suufiy kajenga msikiti na
akaupa jina "Masjid Sayyid al-Badawiy [msikiti wa bwana al-Badawiy]." Je
inajuzu kuswali katika msikiti huu kwa kuwa hauna kaburi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Jina litolewe na mtu aswali maadamu hakuna kaburi, mtu aswali na jina
litolewe. Wamnasihi kutoa jina.
34) Je, Kijusi Kikitoka Tumboni Hufanyiwa ´Aqiyqah?
Swali:
Je kijusi [mtoto mbichi sana tumboni] hufanyiwa ´aqiyqah au huchinjiwa
´aqiyqah?
´Allaamah al-Fawzaan:
32
Ndio, akifikisha siku arubaini anachukua hukumu za mtoto [wa kawaida].
Anaoshwa, anakafiniwa, anaswaliwa. Anazikwa kwenye makaburi ya
Waislamu na anapewa jina.
35) Hukumu Ya Mtu Anaedai Kuwa Ni Muislamu Ila Haswali
Swali:
Mtu ambae anajinasibisha na Uislamu lakini haswali...
´Allaamah al-Fawzaan:
Uislamu wake uko wapi? Asiyeswali sio Muislamu. Uislamu wa bila swalah?!
Muulizaji:
Je inajuzu kula katika kichinjo chake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Hapana haijuzu kula katika kichinjo chake. Ikiwa anaacha swalah
kwa kukusudia, huyu sio Muislamu wala sio halali kichinjo chake.
33
36) Muislamu Ambaye Anafanya ´Ibaadah Zake Zote Kwa Kukhalifu
Sunnah
Swali:
Mwenye kusema Laa ilaaha illa Allaah, lakini haswali swalah ya Waislamu,
hafungi swawm yao na wala hatoa zakaah yao bali anatekeleza ´ibaadah zote
hizi kwa mfumo unaokhalifu Sunnah.
´Allaamah al-Fawzaan:
Sio Muislamu huyu. Mwenye kukhalifu sifa ya swalah na zakaah ya
Kishari´ah na anazileta kwa sura tu, huyu sio Muislamu.
37) Hukumu Ya Muislamu Asietoka Zakaah
Swali:
Kuna wanaotamka Laa ilaaha illa Allaah na wanaswali, lakini hawatoi zakaah
iliyofaradhishwa. Je mtu huyu, mtu atasema ni Muislamu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Anaweza kuwa amekataa kwa ajili ya ubakhili na hapingi. Huyu anasihiwe na
ichukuliwe kutoka kwake hata kama itakuwa kwa kutumia mabavu na
mtawala wa Waislamu. Wala hahukumiwi ukafiri, bali huyu ni bakhili.
34
38) Hukumu Ya Mwanaume Mwenye Kulipa Swawm Ya Dhwihaar
Akamjamii Mke Wake Kabla Hajamaliza Swawm Yake
Swali:
Ipi hukumu lau mwanaume kafanya dhwihaar kwa mke wake, akamjamii
katikati ya swawm ya kafara. Je ataanza swawm upya au atajengea juu yayo
[ataendelea]?
´Allaamah al-Fawzaan:
Bila shaka ataanza, kwa kuwa kabatilisha swawm yake. Kwa kuwa Allaah
Kasema. [Kwa mwanaume aliyefanya dhwihaar]afunge miezi miwili
mfululizo. Na huyu kaikata. Ataanza upya [mwanzo].
39) Mwanafunzi Anaehofia Mas-ala Ya Qadhwaa Na Qadar
Swali:
Mimi ni katika watafutaji elimu, lakini ninakhofia kusoma maudhui ya
Qadhwaa [yaliyopangwa na Allaah] na Qadar. Ipi nasaha yako kwangu?
´Allaamah al-Fawzaan:
35
Amini Qadhwaa na Qadar. Ni lazima kuamini Qadhwaa na Qadar. Ama
kuingia katika hayo na kukithirisha kuyauliza, hili kuliacha ni bora kwako na
litakuweka mbali na mashaka. Amini Qadhwaa na Qadar na muachie mambo
haya Allaah (´Azza wa Jalla). Allaah Hakukukalifisha kwa haya.
40) Mwanamke Mjamzito Kafa Na Mtoto Tumboni, Mtoto Atolewe Na
Kuzikwa Mwenyewe?
Swali:
Mwanamke kafa na tumboni mwake kuna mtoto, je apasuliwe kutolewa
mtoto na kuzikwa sehemu yake kwa hoja akibaki mtoto tumboni mwake
atazikwa kwa kutokielekea Qiblah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana ataachwa mtoto tumboni mwake.Azikwe yeye na [mtoto] yu tumboni
mwake. Haifai kumpasua. Qiblah cha mtoto tumboni ndio Qiblah cha mama
yake. Maadamu mama yake kaelekea Qiblah anamfuata.
41) Mwanamke Kafa Baba Yake Mdogo Kafiri
Swali:
36
Kuna baba mdogo wa mwanamke kafa ambaye alikuwa ni kafiri. Je inajuzu
kwa mwanamke kuhudhuria janaza yake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, watahudhuria makafiri! Watamsimamia makafiri na si Waislamu.
Lakini kukiwa hakuna mtu katika makafiri, anaweza kumsimamia - yaani
akamuosha akamkafini na akamzika mahala pa mbali na si katika makaburi
ya Waislamu. Haifai kumuosha kwa kuwa kuosha ni ´ibaadah na haifai kwa
kafiri. Mzingire kwenye kitu na amzike mahala mbali na njia [manyumba].
42) Mwanamke Mgonjwa Kafa Naye Hakufunga Ramadhaan
Swali:
Mwanamke kasibiwa na maradhi akafa naye hakufunga Ramadhaan na wala
hakulipa, je alipiwe?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa aliacha kufunga kwa ajili ya maradhi na akafa kwayo, hana juu yake
kitu.
43) Hukumu Ya Kuzuia Mimba Moja Kwa Moja
Swali:
37
Dada kutoka Holland anasema, ipi hukumu ya mwanamke kuzuia mimba
kabisa ikiwa kuna matatizo baina ya wanandoa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Asizuie mimba ila kwa maradhi, wakithibitisha hilo matatibu kuwa hafai
kushika mimba kwa ajili inaweza kumuua au itamfanya mgonjwa. Hivyo
ataakhirisha na si kukata uzazi moja kwa moja, bali ataakhirisha. Haijuzu
kwake kuzuia uzazi.
44) Mwanamke Kwenda Sokoni Bila Mahram
Swali:
Inajuzu kwa mwanamke kuingia sokoni bila mahram?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mahram ni katika safari, ama mjini mwake hahitajii mahram. Akiwa ni
mwenye kujiheshimu, kavaa Hijaab na hatochanganyika na wanaume na
akaenda sokoni kwa haja [dharurah]; hana haja ya mahram. Mahram ni
wakati wa safari.
38
45) Mwanamke Ambaye Yuko Katika Familia Yake Kutoka Bila Ya Ruhusa
Ya Mumewe
Swali:
Je inajuzu kwa mwanamke ikiwa kakaa katika familia yake, inajuzu kwake
kutoka na familia yake bila kumuomba ruhusa mume wake na bila kujerea
kwake [kuomba ruhusa]?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mume wake ndiyo kamruhusu kwenda kuwazuru. Ataenda nao kwa kuwa
hili pia [kuwafuata] linaingia katika ruhusa.
46) Inajuzu Kuwatolea Wanawake Salaam?
Swali:
Ipi hukumu ya kuwatolea salaam wanawake, mwanaume kuwatolea salaam
wanawake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hakuna neno. Wasalimie wanawake kwa maneno na si kwa kupeana mikono.
39
47) Mwenye Kuanguka Katika Bid´ah Moja Tu Ya Kiitikadi Anakuwa
Mubtadi´ah?
Swali:
Anayetumbukia katika bid´ah ya Kiitikadi (´Aqiydah) huku alikuwa
akijulikana ni mwenye kushikamana na mfumo wa Ahl-ul-Sunnah katika kila
kitu lakini katumbukia tu katika bid´ah hii, anachukuliwa ni mubtadi´ah au
kuangaliwe mfumo wake wote?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, huchukuliwa ni mubtadi´ah. Ikiwa hatotubia na kuacha bid´ah ni
mubtadi´ah hata kama bid´ah yake ni moja tu.
48) Daa´iy Anaetoa Fatwa Kujuzisha Ndoa Ya Mut´ah Kwa Vijana
Swali:
Baadhi ya wanaojiita maulamaa wanadhihiri sana katika TV wanawapa vijana
Fatwa za kujuzisha [ndoa ya] mut´ah na kuwa ni afadhali kuliko kuzini...
´Allaamah al-Fawzaan:
40
Jitu hili ni shia. Isichukuliwe Fatwa yake. Wanachuoni wamekubaliana wote
uharamu wa ndoa ya mut´ah, baada ya kufutwa wamekubaliana uharamu
wake. Mwenye kuiruhusu ni kafiri.
49) Miongoni Mwa Masharti Ya Laa Ilaaha Illa Allaah
Swali:
Mwenye kusema laa ilaaha illa Allaah na asifanye mambo mengine, si swalah
wala swawm. Lakini anakiri nguzo zote za Uislamu lakini hayafanyii kazi. Je
itamfaa [laa ilaaha illa Allaah]?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Akiacha amali naye ni muweza; haswali, hatoi zakaah, hafungi na
wala hahiji na yeye ni muweza. Haitomfaa laa ilaaha illa Allaah. Kwa kuwa
hakuifanyia kazi muqtadhwa yake, hakuifanyia kazi haki yake. Ama lau
ataisema kwa ikhlaasw kisha akafariki kwa hali moja au nyingine au akauawa
na hakuweza kufanya amali, huyu itamfaa kwa idhini ya Allaah. Mithili
Hadiyth ya bitwaaqah, yule aliyesilimu kisha akauawa akaingia Peponi.
Mithili kijana wa kiyahudi aliyekuwa mgonjwa akamzuru Mtume (´alayhis-
Salaam) akamlingania katika Uislamu akasilimu, akaingia Peponi. Hawa
hawakuweza kufanya amali. Ama kwa mtu aliyeweza kufanya amali akaacha
bila ya udhuru wa Kishari´ah huyu si muumini na wala haimtomfaa kitu laa
ilaaha illa Allaah.
Kulisemwa kwa Wahbiy bin Munabeh (rahimahu Allaah):
"Je laa ilaaha illa Allaah si ndiyo funguo ya Pepo?" Akasema "ndiyo!", ila
hakuna funguo ila huwa na meno. Ukija na funguo ya meno utafunguliwa, la
sivyo hutofunguliwa”.
41
Laa ilaaha illa Allaah ndio funguo ya Pepo sahihi, lakini ina meno. Na meno
yake ni amali [matendo]. Ukija na laa ilaaha illa Allaah na amali utafunguliwa
Pepo. La sivyo hutofunguliwa Pepo.
50) Je, Fuqahaa´ Murji-ah Ni Mubtadi´ah?
Swali:
Yapi maoni yako kwa mwenye kusema Fuqahaa´ Murji-ah ni mubtadi´ah, na
mwenye kusema ni katika Ahl-ul-Sunnah kauli yake ni upotofu. Je mtu
huyu...
´Allaamah al-Fawzaan:
Kwa kuwa hajui mubtadi´ah na wala hajui upotofu. Huyu ni masikini.
Anataka kusema Hanafiyyah ni mubtadi´ah? Hakuna waliyo katika Ahl-ul-
Sunnah? Nani awezae kusema Hanafiyyah si katika Ahl-ul-Sunnah?! Haya ni
maneno ya mjinga.
51) Radd Kwa Mwenye Kusema Mzazi Kumchunguza Mtoto Wake Ni
Ujasusi
Swali:
42
Kuna baadhi ya watu wasemao kitendo hichi cha baba [kuwachunguza
watoto] ni katika ujasusi uliokatazwa, vipi kauli hii?
´Allaamah al-Fawzaan:
Maneno haya ni maneno batili. Mzazi kaamrishwa kuwalea watoto wake,
kuwaangalia na kuwakemea, hili ni wajibu kwake. Na si ujasusi, bali hili ni
kusimama na la wajibu aliyomuwajibishia Allaah juu yake. Lakini leo watu
wamekuwa na fikra mbovu wanasema "msiwapeleleze watoto wenu wala
wake zenu na wala mabanati zenu, waacheni wafanye wapendalo ni uhuru
wao msiwaingilie." Wanataka pasiwe yeyote atayesimama na la wajibu
kwake, na kila mmoja afanye akipendacho.
52) Waalimu Wasiofunza Tawhiyd Katika Madrasa
Swali:
Baadhi ya ndugu wanaosomesha katika madrasah hawafunzi Tawhiyd, bali
wanafunza Fiqh, Tafsiri na Hadiyth. Je una nasaha katika hili?
´Allaamah al-Fawzaan:
Nasaha haitowafaa kitu, watu hawa wafikishiwe wasimamizi wao.
Wasiwaweke wakafunza Tawhiyd, wawatoe na waweke waalimu wenye
kupenda Tawhiyd na wanaifunza kwa sura itakikanayo.
53) Nasaha Kwa Wanafunzi Wanaopondana Wao Kwa Wao
43
Swali:
Muulizaji kutoka Europe anasema, ipi nasaha yako kwa watafutaji elimu na
madu´aat ambao wanasusana wao kwa wao na wanapigana radd wao kwa
wao bila ya hoja wala dalili?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hili halijuzu. Maadamu wao ni madu´aat na ni watafutaji elimu haijuzu
kusasana wao kwa wao. Watu hawawakubali, isitoshe wao kwa wao waanze
tena kujengeana uadui na kukatana wao kwa wao?! Ni lazima ndugu
wasaidizana na wawe kitu kimoja. Na watanabahishane makosa baina yao,
wapeane nasaha. Na wala wasidhihirishe ikhtilaf mbele ya makafiri. Kwa
kuwa makafiri watawatawanyisha na wala hawatokubali da´wah yao.
54) Wake Zangu Wawili Wameingia Katika Uislamu, Je Ni Wajibu Kwao
Kurudi Upya Ndoa Zao?
Swali:
Wake zangu wawili wameingia katika Uislamu, je ni wajibu kwao kurudi
upya ndoa zao?
´Allaamah al-Fawzaan:
44
Kama wameingia katika Uislamu wote, hapana [kufanya ndoa upya]!
Watabaki katika ndoa yao. Washirikina walikuwa wakisilimu wakati wa
Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wala hawaamrishi kurudi
kufunga ndoa zao upya. Lakini lau mwanamume atasilimu na akachelewa
mwanamke kuingia katika Uislamu mpaka akatoka katika eda, ni lazima
kufunga ndoa upya. Ama lau atasilimu mmoja wao na akasilimu mwengine
ndani ya eda pia ndoa inabaki na haina haja kufunga ndoa upya.
55) Ufafanuzi Kuhusu Kufuru Ya ´Amali (Ya Kimatendo)
Swali:
Ni ipi kufuru ya amali? Na je, inamtoa mtu katika Uislamu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kufuru ya amali ni ile iliyoitwa kufuru na haijafika katika kiwango cha shirki
kubwa. "Kama kumtukana Muislamu ni ufaasiq, na kumuua ni kufuru."
Kumuua Muislamu ni dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa na
ni kufuru, lakini ni kufuru ndogo. Na dalili ya hilo ni katika Qur-aan:
وإن ط�)�!�ن �ن ا��ؤ���ن ا&!!�وا
”Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana.” (49:09)
Angalia kawaita waumini na wao wanapigana.
45
إ*داھ�� 3� ا12رى ������ �/ن �.ت وإن ط�)�!�ن �ن ا��ؤ���ن ا&!!�وا �,+�*وا
”Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni.
Na likiwa moja la hao linamdhulu mumwenzie.” (49:09)
Mpaka Aliposema:
�� ا��ؤ��ون إ1وة �,+�*وا ��ن أ1و��م إ��
”Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu.” (49:10)
Ni dalili ya kuwa kumuua Muislamu ni dhambi kubwa na kufuru ndogo,
haifiki katika kiwango cha kufuru kubwa.
56) Wajibu Wa Kumkata Ndugu Ambaye Anachukia Sunnah Na Watu Wa
Sunnah
Swali:
Niko na ndugu anachukia Sunnah na watu wa Sunnah, mpaka rafiki zangu
wanamwita adui wa Sunnah na mimi nimemkata na simuongeleshi na wala
simsalimii kiasi cha miaka mitano. Je mimi nina haki katika amri hii?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio! Wewe wafanya sawa na uko katika haki. Na kumkata ni wajibu mpaka
atubu kwa Allaah (´Azza wa Jalla).
46
57) Kufanya Jamaa´ah Nyingine Wakati Jamaa´ah Ya Kwanza Inapokuwa
Katika Tashahhud Ya Mwisho
Swali:
Ninapoingia katika swalah na imaam kakaa katika tashahhud ya mwisho,
naona watu wananiita wafanye jamaa´ah nyingine. Sahihi ni kujiunga nao au
niingie na imaam?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kutokana na kauli sahihi kuwa jamaa´ah haipatikana ila kwa rakaa moja.
Hivyo akitoa salaam imaam salini. Msisali na imaam hajatoa salaam. Akitoa
salaam salini jamaa´ah.
58) Wafanyao Barnamiji Za Video Kwenye TV
Swali:
Barnamiji za dini mubashara kwa sauti na picha kwenye TV zinazorushwa
baada ya kuziremba, je zinajuzu au nazo ni katika picha ambazo ni haramu?
´Allaamah al-Fawzaan:
47
Hili liko katika dhima ya wafanyao hivyo. Liko katika dhima yao.
59) Je Kutahadharisha Watu Dhidi Ya Maulamaa Wa Ahl-ul-Bid´ah Ni
Katika Kusengenya Na Kueneza Uvumi?
Swali:
Utahadharisho dhidi ya maulamaa potofu na watu wenye fikra potofu na Ahl-
ul-Ahwaa, huchukuliwa ni katika usengenyaji na kueneza uvumi? Na ipi
dhwaabit ya hilo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Utahadharisho - ikiwa uko na elimu na baswiyrah katika Kitabu na Sunnah,
na una ujuzi wa kosa hilo na upi usawa na upotofu, na una uwezo wa
kubainisha ni lazima kubainisha na hili si katika usengenyaji na kueneza
uvumi; hili ni katika [kupeana] nasaha. Lakini ukaanza kuwajeruhi watu na
kuwaponda, fulani hana khayr na fulani ni hivi - hili halijuzu na halileti khayr
hili. Hili linazidisha shari juu ya shari. Hili haliwi ila kwa wanachuoni na
wenye baswirah wanaokataza kwa njia sahihi na kupiga radd. Si kwa kila
mtu.
60) Radd Kwa Mwenye Kusema Kaburi La Mtume Liko Ndani Ya Msikiti
Swali:
48
Vipi kumpiga radd shubuha za mwenye kusema kaburi la Mtume (swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) liko ndani ya msikiti wa Mtume na anashikamana
na hili?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haipo ndani ya msikiti, ipo ndani ya chumba cha ´Aaishah na si ndani ya
msikiti. Na ilikuwa nje ya msikiti katika uongozi wa makhalifah waongofu, na
uongozi wa Mu´aawiyah na uongozi wa ´Abdul-Maalik bin Marwaan.
Alipokuja Waliyd ibn ´Abdil-Maalik baada ya baba yake ´Abdul-Maalik na
wakaupanua msikiti, hivyo wakawa wameingiza chumba cha Mtume ndani,
kwa rai yake yeye na hakushauriana na maulamaa. Maulamaa
hawakukubaliana na hili. Lakini mtu hawezi kusema kaburi la Mtume liko
ndani ya msikiti, iko ndani ya chumba. Na chumba kimeingizwa msikitini.
61) Wanayomba Makaburi Kwa Hoja Eti ´Umar Alimuomba Abbaas
(Radhiyallaahu ´anhum)
Swali:
Tukiwakumbusha washirikiana katika mji wetu kuwa kuyaomba makaburi ni
shirki, wanaturadi na kusema ´Umar alikuwa akimuomba ´Abbaas.
´Allaamah al-Fawzaan:
´Abbaas alikuwa hai na hakuwa maiti. Na ´Umar alimuomba ´Abbaas
[amuombee] du´aa. Inajuzu kuomba mtu aliyehai akuombee du´aa. Wala
49
hakumuomba, tamko hili "aliomba" hapana! Kilichothibiti ni kuwa alitaka
kutoka kwa ´Abbaas amuombe Allaah Awanyeshelezee mvua.
62) Ribaa Ni Dhambi Ya Pili Baada Ya Dhambi Ya Ushirikina
Swali:
Ulisema katika khutbah ya ijumaa iliopita kuwa kula ribaa ni dhambi kubwa
baada ya kumshirikisha Allaah, je kula ribaa ni dhambi kubwa kuliko kuuwa
mtu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Allaah Katoa makemeo makali kwa mla riba makemeo ambayo hajatoa
kwa mwengine. Makemeo makali sana. Ni dhambi kubwa.
63) Mwenye Kula Ribaa Pamoja Na Kujua Kuwa Ni Haramu
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kusema mimi najua kuwa ribaa ni haramu, lakini
pamoja na hivyo nitakula na nitaifanyia kazi. Je mtu huyu anachukuliwa
kaihalalisha?
50
´Allaamah al-Fawzaan:
Huyu hakuhalalisha lakini hatoacha kula ribaa. Huyu anakula ribaa na anajua
kuwa ni haramu.
�� 6 ��و�ون إ �ط�ن �ن ا��س7 �6 ��� ��وم ا��ذي �!1��ط9 ا��ذ�ن �,��ون ا�ر7 ا�>�
“Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliyezugwa na
shaytwaan kwa kumgusa.” (02:275)
Siku ya Qiyaamah aliyekuwa akila ribaa duniani litavimba tumbo lake kwa
ribaa, hatoweza kusimama na watu watapotoka kwenye makaburi yao na
kutaka kwenda kwenye uwanja wa hesabu atakuwa akitaka kusimama
anaanguka. Kwa kuwa tumbo lake linamtia uzito - Allaah Atukinge. Itakuwa
ni fedheha kuwa kwake mbele ya umati. Haijuzu kula ribaa.
64) Risaalah Ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab Kwa Watu Wa
Europe
Swali:
Je Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab ana risaalah (ujumbe) kwa watu
wa magharibi na Qairawaan akiwalingania katika Tawhiyd?
´Allaamah al-Fawzaan:
51
Ndiyo. Ana risalah aliwatumia watu wa magharibi. Inapatikana katika risalah
zake.
65) Jinsi Ya Kumtibu Aliemsibu Ndugu Yake Kwa Kijicho
Swali:
Vipi atajiosha mwenye kudhani kuwa kamsibu ndugu yake kwa kijicho? Je
atatawadha au atajiosha ndani ya...
´Allaamah al-Fawzaan:
Yote ni sawa. Anaweza kumtawadhia, akamuoshea nguo yake, akamsomea.
Yote ni sawa inshaa Allaah.
66) Tawassul Na Sharti Zake
Swali:
Sura ya pili uliyotaja katika sura za tawassul imenitatiza kwa kuwa tulisoma
kwako katika kitabu cha "Tawassul" kuwa kutawassul kwa mtu mwema kwa
kusema kwa mfano "ewe fulani niombee kwa Allaah anisamehe" kuwa ni...
´Allaamah al-Fawzaan:
52
Hili ni sahihi ila ni katika uhai wake. Katika uhai wake unaweza kumwambia
mtu mwema niombee kwa Allaah anisamehe. Ama kuliendea kaburi na kudai
eti ni mtu mwema - Allaah ndiye Mwenye Kujua [wema wake], na
kumwambia "ewe fulani maiti niombee kwa Allaah", hili halijuzu. Kuna
tofauti baina ya aliyehai na maiti. Na kuna tofauti baina ya aliyehudhuria na
asiyeonekana. Hata aliyehai ikiwa haonekani, [haifai] kumuomba kitu.
Utamuomba tu aliyehai na kahudhuria. Sharti ya tatu pia ni kuwa uwe
unamuomba kitu akiwezacho. Sharti tatu. Sharti ya kwanza awe hai, ya pili
kahudhuria na sharti ya tatu awe ni muweza wa unachomuomba.
67) Sijdah at-Tilaawah Ndani Ya Gari
Swali:
Nikiwa ndani ya gari na mimi niko nasoma Qur-aan kisha nikakutana na
Aayah yasajdah, je naweza kusujudu sehemu ya kiti kilichoko mbele yangu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hakuna ubaya ukasujudu sehemu ya kiti, au ikiwa unaweza kusujudu katika
ardhi kwenye gari fanya hivyo.
68) Sisi Tunawaua Washirikina Tu Na Hatuwaui Waislamu
Swali:
53
Tunapowanasihi waabudu makaburi wanasema "nyinyi ni Makhawaarij",
mnawaua Waislamu na mnawaacha waabudu masanamu.
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndiyo, wangelikuwa ni Waislamu tusingeliwaua. Thibitisheni kama kweli ni
Waislamu?! Ilihali mnaabudu asiyekuwa Allaah, mnachinja kwa asiyekuwa
Allaah na mnatazamia kwa asiyekuwa Allaah. Nyinyi sio katika Waislamu.
Kutokana na dalili sahihi mutawaatir. Ama sisi tunajikinga kwa Allaah
kuwaua Waislamu. Sisi si kama Makhawaarij. Sisi tunamuua yule ambaye
imewajibika kumuua, waliyouawa na Maswahaba na Abu Bakr Asw-
Swiddiyq. Tunawaua!
69) Sunnah Ya Kuangalia Kidole Cha Shahaadah Wakati Wa Tashahhud
Swali:
Je ni katika Sunnah kuangalia mwenye kuswali kidole cha shahaadah katika
tashahhud ya mwisho na tashahhud ya kwanza?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, hili limepokelewa kuwa ataangalia katika kidole cha shahaadah.
54
70) Sifa Ya Swalah Ya Istisqaa Ni Kama Swalah Ya `iyd
Swali:
Je kuna dalili ya kuwa swalah ya istisqaa wakati wake ni pale jua
linachomozapo, au inaswaliwa wakati wowote?
´Allaamah al-Fawzaan:
Imepokelewa kuwa ni kama swalah ya ´Iyd, inavyofanywa ni kama swalah ya
´Iyd - mahala pake sifa yake. Inachukua akhaam kama swalah ya ´Iyd.
71) Aina Mbali Mbali Za Tawassul Na Hukumu Zake
Swali:
Je tawassul bila ya kumfanyia chochote katika ´ibaadah [unayemfanyia
tawassul] ni shirki ndogo au ni bid´ah au?
´Allaamah al-Fawzaan:
Nimeshawaambia hili, nilisema tawassul ni aina mbili. Tawassul iliyokatazwa
ni aina mbili:
Aina ya kwanza ni afanye kitu katika ´ibaadah kwa yule anayemfanyia
tawassul, hii ni shirki kubwa. Na hichi ni kitendo cha Ahl-ul-Jaahiliyyah.
55
ھم و6 ���"�م و��و�ون �ھـؤ6ء >�"�ؤ�� �د % و�"�دون �ن دون % �� 6 �=ر
"Nao, badala ya Allaah, wanaabudu wasio wadhuru wala kuwanufaisha, na
wanasema: Hawa ndiowaombezi wetu kwa Allaah!" (10:18)
Aina ya pili ni kumfanya unayemfanyia tawasssul mkaakati (mpatanishi) tu
baina yako wewe na Allaah. Unadai kuwa anakukurubisha kwa Allaah tu, na
kuwa Allaah Atakuitikia kwa upatanishi wake, hii ni bid´ah na ni njia
inayopelekea katika shirki; Ikiwa hukumfanyia kitu katika ´ibaadah.
72) Nyote Ni Wakoseaji Na Mbora Ni Yule Mwenye Kutubia
Swali:
Ikiwa mtu ni Muwahhid anahifadhi nguzo za Uislamu, lakini ana madhambi
mengi kukiwemo makubwa na madogo. Je anachukuliwa ni katika wapotofu
na kuwa hakuna kinachomzuia kurudi katika haki?
´Allaamah al-Fawzaan:
[Mtume anasema]: "Nyote ni wakoseaji, na mbora wa kukosea ni wenye
kutubu. "Atubu kwa Allaah (´Azza wa Jalla) kwa madhambi na Allaah
Humsamehe mwenye kutubu. Na wala asiseme mimi ni katika wapotofu
akamtia wasiwasi shaytwaan. Aache fikra hizi na atubu kwa Allaah.
56
73) Tawhiyd-il-Ilaahiyyah Na Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah
Swali:
Je kuna tofauti baina ya Tawhiyd-il-Ilaahiyyah na Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, zote maana yake ni moja. Tawhiyd-il-Ilaahiyyah na Tawhiyd-ul-
Uluuhiyyah. Tawhiy-il-´Ibaadah. Yote ni maana moja.
74) Tawhiyd-ul-Khaaliqiyyah, Tawhiyd-ul-Raaziqiyyah Na Tawhiyd-ul-
Haakimiyyah
Swali:
Je kunapatikana katika ´Aqiydah sahihi kitu kiitwacho Tawhiyd-ul-
Khaaliqiyyah, Tawhiyd-ul-Raaziqiyyah na Tawhiyd-ul-Haakimiyyah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ndio inayoitwa Tawhiyd-ul-Khaaliqiyyah,
Tawhiyd-ul-Raaziqiyyah; yaani ndio Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Tawhiyd-ul-
Haakimiyyah inaingia katika Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Isitengwe!
57
75) Tofauti Baina Ya Sanamu Na Wathan
Swali:
Kuna tofauti baina ya sanamu na wathan?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndiyo. Sanamu ni ile yenye sura ya mnyama. Tofauti ni ya kilugha tu, hakuna
tofauti Kishari´ah. Lakini kilugha [sanamu] ni ile yenye sura ima ya mtu au
mnyama. Na wathan ni ile isiyokuwa na sura, kama [mwenye kuabudu]
kaburi, mti na jiwe.
76) Tofauti Ya Ujinga Na Upotevu
Swali:
Je kuna tofauti ya ujinga na upotevu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ujinga ni kwa yule asiyejua haki, huyu ni mjinga. Ama upotevu ni kwa yule
mwenye kujua haki na akaicha, au akamuabudu Allaah pasina elimu kama
manaswara na Masufi. Wameisusa elimu.
58
77) Usikae Na Mvuta Sigara!
Swali:
Kuna baadhi ya maasi yameenea sana kwa Waislamu na wamekuwa hawajali
kila mahala, kama kuvuta sigara. Je kwa mtu mmoja anaweza kukataza uovu
kama huu au aache kwa kukithiri kwake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, akataze kiasi atavyoweza. Akumbushe na kubainisha madhara ya
sigara na athari yake mbaya, awawekee wazi hili. Na ikiwa hawatokubali,
asikae nao. Jiweke nao mbali usikae nao.
78) ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Madu´aat Wanaohudhuria Katika
Maulidi
Swali:
Baadhi ya watu wa bid´ah Masufi na khasa Tijaaniyyah katika mji wetu wana
harakati mbali mbali kwa mnasaba wa kusherehekea Maulidi. Kunakuja
baadhi ya madu´aat na wanahudhuria nao na wanawaombea mwishoni siha
na afya na du´aa nyinginezo katika Mashaykh wa Kisuufiy walioandaa
mambo haya. Ipi hukumu ya mambo kama haya na kuhudhuria madu´aat
hao?
59
´Allaamah al-Fawzaan:
Huyu anaafikiana nao na kuwasifia. Halijuzu hili, halijuzu hili. Isipokuwa tu
wakati tu pale unapohudhuria unawakataza na kuwabainishia kuwa hili
halijuzu na wasifanye mambo haya na si sawa. Walinganie kwa Allaah kabla
na la sivyo jendee zako waache. Usikae nao, unaafikiana, ukala nao chakula
ukapiga nao vicheko. Ukadai ni kuwalingania [Da´wah]! Hapana katu hii si
Da´wah.
79) Kuomba Kwa Nuru Ya Uso Wa Allaah Mambo Ya Kidunia Na Aakhirah
Swali:
Ulisema katika darsa iliopita kuwa haijuzu kuomba kwa Uso wa Allaah
[mambo] ya dunia. Vipi ikiwa nitamuomba Allaah kwa Nuru ya Uso Wake
jambo la dunia na Aakhirah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ukimuomba Allaah jambo katika mambo ya dunia na Aakhirah hakuna
ubaya. Kilichokatazwa ni kuomba cha dunia tu. Hilo ndo halijuzu.
80) Kuswalishwa Na Imaam Wa Kisufi Ambaye Msimamo Wake
Haujabainika
60
Swali:
Kuna watu watatu, na aliyehifadhi Kitabu cha Allaah ndiye anaewasalisha. Ni
sahihi kwa kuwa kuna wanaosema ana taswawwuf pamoja na kuwa
hadhihirishi wazi katika ´Aqiydah ya Kisuufiy. Je tuswali nyuma yake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa hamjabainikiwa na kitu, swalini nyuma yake. Ama mkibainikiwa na
kitu ni katika Masufi na mubtadi´ah, msiswali nyuma yake. Thibitisheni hilo.
81) Shubuha Za Waabudu Makaburi
Swali:
Katika utata wanaotaja waabudu makaburi wanasema sisi ni wapungufu,
wafanya madhambi na tunasikia haya kumuomba Allaah. Tunaomba kupitia
walii [kipenzi cha Allaah] kwa kuwa ana jaha na hadhi, vipi kuwapiga radd?
´Allaamah al-Fawzaan:
Waambie, je Allaah Kawaamrisha hili?! Leteni dalili kuwa Allaah
Kawaamrisha hili?! Hii ni sheria asiyoiruhusu Allaah. Ni bid´ah na wala
haijuzu. Allaah Kawaamrisha kumuomba moja kwa moja bila ya mkaakati.
61
��م ادو� �أ$!�ب ��م و&�ل ر�
"Na Mola Wenu Anasema: Niombeni nitakuitikieni." (40:60)
Hakusema niombeni kwa kupitia kwa fulani. Wewe ni mwenye madhambi
kisha wewe unasikia haya?! Msikilie haya Allaah na umuombe Allaah
msamaha na utubu kwa Allaah na Allaah yu karibu Mwenye kujibu.
Ghafuuru Ar-Rahiym.
82) Waabudu Makaburi Lazima Wasimamishiwe Hoja!
Swali:
Baadhi ya mubtadi´ah na waabudu makaburi wanakataa ushirikina
unaofanywa kwenye makaburi; kama yafanywayo kwa al-Badawiy na
Karbala na sehemu zingine. Je nikiona video kwenye internet yenye mambo
kama hayo ya kishirki ili nimkinaishe na asadikishehilo, je nina makosa kwa
hilo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa atakinaika - Alhamdulillaah, lakini dhahiri ni kuwa hakinaiki. Lakini
wewe wajibu wako ni kumsimamishia hoja tu, aghlabu hawakinaiki ila -
Allaah Anajua zaidi, ni nadra sana.
62
83) Kila Aliye Fikiwa Na Qur-aan Hoja Imemsimamia
Swali:
Kuna wanaosema ni lazima kuwasimamishia hoja waabudu makaburi, na
wala hawaisimamishi....
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndiyo, ni lazima [kwanza] kusimamisha hoja. Lakini hoja imesimamishwa
kwa Qur-aan Tukufu inayosomwa, wameiihifadhi, kuirudu na wanaisikiliza.
La sivyo, ipi faida ya Qur-aan?! Ingekuwa haisimamishi hoja. Ipi faida yake
baina ya watu?! Inasimamisha hoja.
C�� 9 و�ن�ھذا ا��رآن 2�ذر�م �� وأو*� إ�
“Na nimefunuliwa Qur-aan hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila
inayomfikia.” (06:19)
Aliye fikiwa na Qur-aan naye ni mwarabu, hoja imekwishamsimamia. Ama
akiwa siyo mwarabu, atarjumiwe maana ya Qur-aan mpaka imsimamikie hoja
na afahamu.
84) Qur-aan Yatosheleza Kuwa Hoja Kwa Kila Mtu!
Swali:
63
Waabudu makaburi hawasimamishiwi hoja na mtu ni mtu, bali ni lazima awe
ni mwanachuoni na si kila mwanachuoni, bali ni lazima mjinga [huyo]
amsadikishe na amwamini. Je maneno haya ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hoja imekwishawasimamia - wa lillaahil hamd. Tangu iteremshwe Qur-aan
hoja imekwishasimama.
Muulizaji:
Na si mtu ni mtu atawasimamishia hoja, bali ni lazima awe ni mwanachuoni,
na si kila mwanachuoni.
´Allaamah al-Fawzaan:
Inatosheleza Qur-aan, inatosheleza Qur-aan. Yeye anasoma Qur-aan na ni
mwarabu, anafahamu maana ya lugha ya kiarabu; Anafahamu maana ya
kufuru, maana ya shirki. Anafahamu haya. Hoja imekwishawasimamia kwa
kufikiwa na Qur-aan, kwa lugha yake.
85) Kufasiri Kwa Ajili Ya Taazia (Kutoa Ole Kwa Wafiwa)
´Allaamah al-Fawzaan:
64
Safari kwa ajili ya kutoa pole, jambo hili halina asili. Mtoa pole hana haja ya
kusafiri, mtoa pole anaweza kuchukua simu na kumuongelesha kama
kwamba amehudhuria nao. Hakuna haja ya safari. Lakini akijikalifisha akenda
safari, huyu ni mgeni - huu ni ugeni na si utoaji pole. Huu ni ugeni kwa
walokuja.
86) Wanafunzi Wanaotoka Katika Miji Ya Kikafiri Na Kwenda Kusoma
Saudi Arabia Kisha Wanabaki Huko
Swali:
Baadhi ya wanafunzi wanakuja kutoka katika miji ya kikafiri na wanatafuta
elimu ya Kishari´ah kisha hawataki kurudi katika miji yao kwa ajili ya
Da´wah. Ipi nasaha zako kwa watu hawa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa wanaweza kuishi na kubaki hii ni Hijrah. Wamefanya Hijrah [kuhama].
Hili ni jambo zuri.
87) Utata Wa Waabudu Makaburi
Swali:
Wanapokumbushwa washirikina kuomba maiti, wanaturadi kuwa hakuna
tofauti kuomba maiti na aliye hai. Wanasema ni sababu katika sababu...
65
´Allaamah al-Fawzaan:
Waulize, je kuna tofauti baina ya aliye hai na maiti au hapana? Je wanaweza
kweli kusema hakuna tofauti baina ya aliye hai na maiti?! Hawawezi kusema
hili. Waambie hivi. Je aliye hai na maiti ni sawa? Akisema ndiyo, atakuwa ni
mwenye kiburi. Akisema hawako sawa, aambiwe kuomba aliye hai si kama
kumuomba maiti. Kwa kuwa aliye hai anaweza kuombwa, na ama maiti
hawezi kuombwa. Hawezi hata kujiombea mwenyewe!!
88) Wanaolilia Umoja Wa Uislamu Bila Kujali ´Aqiydah
Swali:
Ipi hukumu ya kukimbiza watu kunako Da´wah katika Tawhiyd na kuali
"Watu wengi wanakubali kuwa hanapa mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila
Allaah."
´Allaamah al-Fawzaan:
Huku ni kukimbiza watu katika njia ya Allaah. Anakimbiza katika Da´wah ya
Allaah (Jalla wa ´Alaa). Haya ni mapote yamejitokeza [siku za] nyuma,
wanataka kuwafanya watu wawe wamoja bila ya kuangalia ´Aqiydah (itikadi)
zao. Na hili haliwezekani kamwe. Hawawezi watu kuwa wamoja ila kunako
´Aqiydah. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa):
�م &وم �6 �"��ون !*$��م ���"� و&�و��م >!�3 ذ�ك �,��
66
”Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni
kwa kuwa wao ni watu wasio na akili.” (59:14)
Hakuna kinachowafanya watu kuwa wamoja ila ´Aqiydah iliowajumuisha
Maswahaba, ikajumuisha mashariki na magharibi na ikajumuisha waarabu na
wasiyo kuwa waarabu. Chini ya Laa ilaaha illa Allaah. Haliwezekani hili. Kila
mmoja akibaki katika ´Aqiydah yake potofu, watafarakana hata wakiwa
pamoja kwa miili yao.
�م &وم �6 �"��ون !*$��م ���"� و&�و��م >!�3 ذ�ك �,��
”Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni
kwa kuwa wao ni watu wasio na akili.” (59:14)
89) Ni Kweli Kwamba Kuna Wenye Kuomba Kwenye Kaburi La Mtume?
Swali:
Mtu anaweza kuchukua kutoka katika kauli ya Mtume (swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam) "Ee Allaah! Usiijalie kaburi yangu wathanan yenye kuabudiwa",
tunayoona leo wenye kuomba kwenye kaburi lake. Je, mtu anaweza kusema
kuwa wamemfanya wathanan...
´Allaamah al-Fawzaan:
Siyo kwenye kaburi lake, wanaofanya haya ni katika msikiti na si kwenye
kaburi lake Mtume. Kaburi la Mtume liko mbali nao kabisa limezuia na kuta
hawamuoni na wala hawajui alipo. Hili linafanywa msikitini.
67
90) Hukumu Ya Kuapa “Wallaahi Kwa Nyumba Aliyojenga Allaah”
Swali:
Baadhi ya watu wanasema katika viapo vyao "Wallaahi, na nyumba
Aliyojenga Allaah." Je kauli hii ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haijuzu kuapa hivi. Asiape kwa nyumba. Siyo Allaah aliejenga nyumba!
Ilijenga Ibraahiym (´alayhis-Salaam) na waliokuja baada yake.
91) Vipi Ntamlingania Baba Yangu Aingie Katika Uislamu?
Swali:
Vipi ntamlingania baba yangu katika Uislamu, kwa kuwa hakubali nasaha
wala wito wa yeyote katika sisi?
´Allaamah al-Fawzaan:
68
Mchukue kwa urafiki, hekima na mawaidha yaliokuwa mazuri pole pole.
Huenda Allaah Akamuongoza. Usikatike moyo kwa kuongoka kwake. Jitahidi
kadiri na utavyoweza.
92) Vipi Muislamu Kafiri Asieswali Atatubia?
Swali:
Ikiwa mwenye kuacha swalah iliofaradhishwa kwa kukusudia inachukuliwa
ni ukafiri, vipi mwenye kufanya kitendo hichi atatubu kwa ukafiri huu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Asimamishe swalah. Atubu kwa Allaah na asimame kwa swalah katika
mustaqbal, ahifadhi swalah katika mustaqbal.
93) Vipi Kumsimamishia Mtu Hoja?
Swali:
Upi ufahamu wa kumsimamishia mtu hoja?
´Allaamah al-Fawzaan:
69
Kusimamisha hoja ni kufikisha dalili kwa ufahamu wake, ikiwa ni katika wale
wenye kufahamu. Au kumtarjumia ikiwa hafamu kwa lugha yake.
94) Vipi Mtu Atamjua Mwanachuoni?
Swali:
Ulisema kuwa mtu aulize [dini yake] wanachuoni wanaojulikana
rabbaniyyuun na siyo wanachuoni wapotevu, vipi mtu atajua [kupambanua]
hawa na hawa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Watu wanawajua, elimu yao hujidhihirisha.Maneno yao, vitabu vyao,
hudhihiri hili. Pia mtu atajua kwa aliesoma kwake na kutakharaj kupitia
mikono yake, litajulikana hili. Hili lina msingi [chanzo] chake.
Muulizaji:
Je kule kuchaguliwa na kudhihiri, ni dalili [tosha] ya kuwa ni mwanachuoni
rabbaniy...
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Tunasema ni lazima kwanza ijulikane ni kwa nani alichukua elimu?
Wapi alisoma? Nani mashaykh wake? Pia tujue njia apitayo baada ya hapo. Je,
70
anawafuata watu wa haki? Au ni mbabaishaji tu mwenye fikra mbovu? Ni
laziam tujue haya.
95) Jinsi Ya Kutangamana Na Makafiri Kazini
Swali:
Vipi ntatangamana na makafiri? Kwa kuwa wanachanganyika nami kazini
kila siku.
´Allaamah al-Fawzaan:
Ukipata kazi nyingine mbali nao ndio bora. La sivyo, fanya kazi yako na
waache katika kazi yao. Kila mmoja afanye kazi yake.
96) Wanafunzi Kupiga Radd Makundi Potevu Katika Miji Yao
Swali:
Mimi karibu nitaenda katika mji wakiarabu kumekithiri Masufi, je kuna
vitabu unaninasihi kuvisoma na kwenda navyo katika mji huo?
´Allaamah al-Fawzaan:
71
Chukua vya mukhtasari ambavyo vina radd kwa Masufi. Utavipata kwenye
maofisi.
97) ´Uzayr Ni Nani?
Swali:
Je ´Uzayr ni Mtume katika Mitume wa Banu Israaiyl, na kwa nini Mayahudi
walimuhusisha tu yeye kumtaja na hapana mwengine?
´Allaamah al-Fawzaan:
´Uzayr wametofautiana [wanachuoni] kuwa ni Mtume au ni katika watu
wema tu, kuna kauli mbili. Kauli yenye nguvu - Allaah Anajua zaidi - ni kuwa
si Mtume bali ni katika watu wema wa Banu Israaiyl. Alijishughulisha na
swalah na elimu mpaka wakampandisha. Bali yasemekana kuwa alikuwa
kahifadhi Tawrat ilihali Tawrat haiwezekani kuihifadhi. Lakini yeye Allaah
Alimpa uwezo na akaihifadhi.
98) Aina Mbali Mbali Za Tawassul Na Hukumu Zake
Swali:
Shaykh-ul-Islaam (rahimahu Allaah) katika kitabu chake "Tawassul wal-
Wasiylah" kataja katika maudhi kuwa tawasuli ni bid´ah, na katika maudhui
mengine kasema kuwa ni njia katika shirki na katika maudhui ya tatu kasema
kuwa ni shirki. Je hizi kauli zote ni zake?
72
´Allaamah al-Fawzaan:
Mimi niliwawekea wazi hili. Niliwaambia kuwa mwenye kutawasali
ikimfanyia ´Ibaadah anaemtawasalia - kama kumchinjia, kumuwekea nadhiri
na kumuomba, hii ni shirki. Hii ni tawasuli ya shirki. Ama tawasuli isiyokuwa
na ´Ibaadah kwa huyo mwenye kumfanyia hio tawasuli, hii inachukuliwa ni
bid´ah. Na ni njia katika shirki.
99) Mzee ambaye Muusa Alikutana Naye Madyaan Ni Mtume Shu´ayb
(´alayhis-Salaam)?
Swali:
Mzee ambaye Muusa alienda kwake huko Madyaan ni Shu´ayb (´alayhis-
Salaam)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haijulikani - Allaah Ndiye Anajua zaidi. Baadhi ya watu wanasema kuwa
alikuwa ni Shu´ayb, lakini haikuwekwa wazi na sidhani kama ilikuwa ni
Shu´ayb. Allaah Hakusema kuwa ilikuwa ni Shu´ayb, bali ilikuwa ni mzee
mkubwa wakafanya na Muusa waliokubaliana. Ni mtu mwema katika watu
wa Madyaan.
100) Kuswali Nyuma Ya Mshirikina Kwa Kusoma Msikiti Wa Sunnah
Swali:
73
Kwetu kumekithiri ushirikina wa sampuli mbalimbali na bid´ah na usomaji
wa burda misikitini na wanafunza wanafunzi, na tunapoongea nao
wanapinga. Ipi hukumu ya kuswali nyuma ya watu hawa kwa kuzingatia ya
kwamba hakuna msikiti wa Ahl-us-Sunnah mahala hapa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Usiswali nyuma yao. Usiswali nyuma ya mshirikina anaeabudu mawalii,
watu wema na Mtume usiswali nyuma yake. Swalah yako ni batili. Swali peke
yako nyumbani kwako au sehemu ingine. Na kama uko na ndugu zako
wengine au watu wa kawaida tafuteni mswalah mswali.
101) Asiyeweza Kulipa Kafara Ya Yamini Kwa Kulisha Anafunga
Swali:
Nina deni la kafara ya yamini, na nina baadhi ya mali ila niko nazo haja na
siwezi kuzitolea kafara. Je naweza kufunga au ni wajibu kwangu...
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio funga. Ikiwa huna kitu cha kutosheleza haja - kulisha, funga.
��� �� ��� ����م ��� أ��م
“Na asiyepata, afunge siku tatu.” (02:196)
74
Na wewe hukupata kitu cha kutosheleza haja zako.
102) Shaykh Muhammad ibn ´Abdil-Wahhaab Si Bora Kuliko Wanavyuoni
Wa Madhehebu Manne
Swali:
Je ni sahihi kuwa watu wa Najdiy na Hijaaz wanamuadhimisha Imaam
Muhammad ibn ´Abdil-Wahhaab (rahimahu Allaah) zaidi kuliko
wanavyowaadhimisha maimamu wanne na wengineo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Nani kasema haya? Mwenyewe alikuwa akiwafuata maimamu wanne na ni
katika wafuasi wao. Na anawasifia, kuwaombea na kuwaiga. Yeye si bora
kuliko maimamu wanne.
103) Kupita Mbele Ya Mwenye Kuswali Kwa Nguvu
Swali:
Mtu anaswali mbele yake kukapita mwanaume akamzuia lakini akapita, je
swalah yake inabatilika kwa hilo?
75
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, swalah yake haibatiliki. Lakini aliepita anapata dhambi kubwa. Na
mwenye kuswali hana juu yake kitu kwa kuwa alimzuia lakini akapita.
Dhambi ni za yule aliepita.
[Anasema Mtume]:
"Angelijua yule mwenye kupita mbele ya mwenye kuswali ana nini juu yake,
ingekuwa bora kwake kusimama arubaini kuliko kupita mbele yake."
Swali La Pili:
Akipita mwanamke mbele ya mwanaume katika swalah yake, je swalah yake
inabatilika kwa hilo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kauli sahihi ni kuwa swalah yake haibatiliki; sawa akipita mwanamke, mbwa
wala punda isipokuwa makusudio hapa ni kupungua thawabu na si
kubatilika. Madhehebu ya Imaam Ahmad ndio inabatilika kwa kupita vitu
hivi vitatu; mwanamke, mbwa mweusi na punda. Lakini jumhuri - na ni moja
ya upokezi wa Ahmad, kuwa makusudio kubatilika hapa ni kupungua
thawabu. Bali madhehebu ya Ahmad wanaona kuwa swalah inabatilika kwa
kupita mbwa mweusi tu. Haibatiliki kwa kupita mwanamke na punda, bali ni
mbwa mweusi tu.
104) ´allaamah al-Fawzaan Kuhusu Answaar-us-Sunnah
Swali:
Kusifia kwako Jamaa´at Answaar-us-Sunnah wa Misr na Sudan ni sifa ya
watu maalumu au ni kwa yale wayafanyayo kwa sifa ya ujumla?
76
´Allaamah al-Fawzaan:
Mimi sikutaja watu maalumu. Mimi nilisema Answaar-us-Sunnah. Answaar-
us-Sunnah wa mahala popote, sawa ikiwa ni Egypt au sehemu zingine.
Mwenye kuinusuru Sunnah sisi tunamsifia. Na watu hawa wamesimama kwa
Da´wah ya Tawhiyd na kukataza shirki katika mji ambapo kuna shirki.
Allaah Awajaze kheri. Wana juhudi. Mimi sikutaja watu bali nilitaja kundi tu.
105) Kuacha ´Amali Kwa Kukhofia Riyaa
Swali:
Mimi nakhofia riyaa kwa daraja ambayo siwezi hata kuswali kwa mtu.
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana ewe ndugu. Haijuzu kuacha amali na kusema mimi nakhofia riyaa.
Hili linatokana na Shaytwaan. Fanya amali na yatakase kwa Allaah (´Azza wa
Jalla). Usiache amali kwa kukhofia riyaa. Hili ndo alitakalo Shaytwaan
anakudanganya na kukwambia usiswali watu watadhani kuwaunajionyesha
kwao, usisimame usiku kwa kwa kuwa ni kujionyesha. Muombe Allaah kinga
kwa riyaa na shirki na endelea kufanya amali njema.
106) Kumwita Mtu Bwana
77
Swali:
Watu wengi wanapotaka kumwita mtu wanamwambia "Ewe bwana!".
Inajuzu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kujuzu inajuzu, lakini kuacha [kusema hivo] ni bora zaidi.
107) Kumuambia Kafiri Ni Rafiki
Swali:
Ipi hukmu ya neno “rafiki” kumwambia kafiri?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haijuzu. Haijuzu kumwambia kafiri rafiki. Rafiki maana yake ni kipenzi.
Haijuzu hili.
108) Hukumu Unaposhtushwa Na Kitu Kuita “Ewe Mtume”
Swaali:
78
Baadhi ya watu wakistaajabishwa na kitu wanasema “Ewe swalah ya
Mtume!”. Ipi hukumu ya kusema hivi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haijuzu hili. Kwanini ewe swalah ya Mtume? Hii ni du´aa na wito. Haijuzu.
Kwanini hasemi Ewe Allaa! Na anasema ewe swalah ya Mtume? Haijuzu
kusema ewe Mtume! Anamuomba Mtume. Haijuzu hili. Vipi ataomba ewe
swalah ya Mtume, anamuoba.
109) Hukumu Ya Kusema Mimi Ni Kwa Allaah Na Kwako
Swali:
Katika mji wetu kuna neno linasemwa kwenye ndimi nyingi za watu, nalo ni
“Mimi ni kwa Allaah na kwako”. Inajuzu kusema hivi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Haijuzu kwa "na" - haijuzu. Aseme kwa Allaah kisha/halafu kwako,
anaweza kusema hivi. Kwa kuwa kaweka neno "kisha", na neno kisha halileti
maana ya ushirikiano bali linaleta maana ya mpangilio.
110) Anaepinga Hadiyth Ya Shafaa´ah Anakuwa Kafiri?
79
Swali:
Tunaweza kusema kwa mwenye kupinga Hadiyth ya Shafaa´ah [maombezi]
kuwa ni kafiri?
´Allaamah al-Fawzaan:
Tunasema kuwa kapotea. Ikiwa anajua kuwa maombezi ni haki na kuwa
yamethibiti [katika hadiyth] kisha akakataa, anakufuru kwa hilo. Ama
akidhani kuwa haikuthibiti au akafahamu vibaya, huyu ni mpotofu wala
hakufurishwi.
111) Hukumu Ya Kuapa Kwa Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
Swali:
Baadhi ya watu wanapotaka kutoka kwa mtu mwengine kitu wanamwambia:
“Naapa kwa Mtume fanya hivi”, katika kauli hii kuna kitu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, huku ni kuapa kwa asiyekuwa Allaah. Naapa kwa Mtume huku ni
kuapa kwa asiyekuwa Allaah. Lakini yawezekana kakulia katika hili na wala
hakusudiii kuapa bali ni mazowea ya ulimi. Lakini kwa vyovyote ni wajibu
kujiepusha na kusema hivi na kumkataza anaesema hivo. Wanaosema hivi
wengi ni watu wa Egypt, naapa kwa Mtume, naapa kwa Mtume. Na kuna
mmoja anasema "Naapa mimi ni Muwahhid!".
80
Swali La Pili:
Je nimkataze anaesema hivi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, mbainishie mfunze. Ikiwa ni mjinga hajui mbainishie hili. Huenda
kaona watu katika mji wake wanasema akaishi katika hilo akadhani kuwa
inajuzu.
112) Anataka Kumpa Alieingia Katika Uislamu Tafsiri Ya Qur-aan
Swali:
Siku moja nilimfanyia da´wah asiyekuwa mwarabu kuingia katika Uislamu
akakubali. Akaniomba kumpa tafsiri ya Qur-aan Tukufu kwa lugha yake,
inajuzu kwangu kumpa tafsiri hii ambayo iko katika lugha yake? Au nimpe
kitabu kingine chenye mafunzo ya Uislamu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mpe tarjum ya maana ya Qur-aan Tukufu na itume kwa madu´aat wa nje
wampe ili afahamu maana ya Qur-aan. Ama Qur-aan yenyewe haifasiriwi
wala haijuzu na wala haiwezekani. Lakini kutarjum maana yake tafsiri hakuna
neno. Mpe tarjum ya tafsiri. Hii huitwa tarjum ya maana ya Qur-aan Tukufu,
wala hakusemwi tarjum ya Qur-aan Tukufu.
81
113) Kumuomba Kafiri Msaada Kwa Ayawezayo
Swali:
Inajuzu kuwaomba makafiri msaada kwa ayawezayo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Wakati wa haja na dharurah hakuna ubaya. Unapokuwa katika safari na
wewe unahitajia msaada huwezi kumwambia nisaidie? Hili ni jambo linajuzu.
Hili ni jambo mubaha.
114) Kuomba Msaada Kwa Majini
Swali:
Inajuzu kuomba msaada kwa majini?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Visivyoonekana na waliokufa na majini haijuzu kuwaomba msaada.
Haijuzu kuomba kinga wala kuomba msaada kwa visivyoonekana na
waliokufa. Hili ni kwa haki ya mtu aliehai kahudhuria.
115) Je, Kufuru Ya Kimatendo Yaweza Kuwa Kubwa?
82
Swali:
Je yaweza kuwa baadhi ya kufuru ya amali [matendo] kufuru kubwa kama
kusujudia sanamu na kumchinjia asiyekuwa Allaah?
´Allaamah al-Fawzaan:
A´udhubi Allaah. Hii ni shirki ndogo? Kusujudia sanamu ni shirki ndogo?
Kumchinjia asiyekuwa Allaah ni shirki ndogo? Hii ni shirki kubwa. Hizi ni
kufuru kubwa. Ni za matendo lakini
ni kufuru kubwa. Si kila kufuru ya matendo inakuwa ndogo. Baadhi yazo ni
kubwa.
116) Haijuzu Kuomba Maiti Kwa Kuwa Hana Anachokiweza
Swali:
Katika kauli ya Imaam Shawkaaniy (rahimahu Allaah), kasema inajuzu
kuwaomba msaada viumbe kwa yale mambo wayawezayo. Je haingii aliye hai
na maiti katika neno viumbe?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa maiti anaweza! Nani anadai kuwa maiti anaweza? Maiti hawezi kitu ni
maiti. Amesagika tena ni udongo!
83
�����ا ��� � �5�+ون �4+!�� و& �3,01 �/. -,�+ إن )�#�ھ� & �%���ا د#�ء!� و�� ����ا �� ا�و��م ا6���
“Mkiwaomba hawasikii maombi yenu; na hata wakisikia hawakujibuni. Na
Siku ya Qiyaamah watakataa ushirikina wenu. Na hapana atakayekupa
khabari vilivyo kama Yeye Mwenye khabari.” (35:14)
Maiti ni udongo hawezi... Hata akisia du´aa yako hawezi kukujibu kwa kuwa
si muweza. Unamuomba maiti?! Subhaana Allaah! Wewe ni hai unamuomba
maiti. Huu ni upumbavu!
117) Sote Tuwaite Washirikina Kuwa Ni Washirikina
Swali:
Hukumu kwa mtu kuwa ni mshirikina ni kwa wanachuoni tu au hata kwa
wasiyokuwa wanachuoni watapomuona anaetumbukia katika shirki
wamwambie kuwa ni kafiri mshirikina?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mwenye kudhihirisha shirki ni mshirikina. Mwenye kuomba asiyekuwa
Allaah, akachinja kwa asiyekuwa Allaah na akaweka nadhiri kwa asiyekuwa
Allaah huyu ni mshirikina. Kwa watu wa kawaida na wanachuoni. Mwenye
kusema ewe ´Aliy, ewe Husayn n.k huyu ni mshirikina. Kila mtu anajua kuwa
ni mshirikina.
Swali La Pili:
Mmoja katika wanafunzi anasema kuwa mwenye kutumbukia katika shirki
84
anakuwa kafiri, lakini akasema mwenye kuhukumiwa kuwa ni mshirikina na
karitadi si kwa kila mtu hata wanachuoni bali hili ni kwa Qaadhi tu kwa
kuwa...
´Allaamah al-Fawzaan:
Hii sio hukumu. Hukumu ya kuritadi inakuwa kwa Qaadhi kwa kuwa
anaweza kuuawa. Lakini kusema hii ni shirki hili kila mmoja analisema. Kila
mwenye imani anasema hii ni shirki na haihitajii Qaadhi tu.
118) Je, Ni Kweli Kuwa Wengi Wa Washirikina Wa Leo Wanafanya Shirki
Kwa Kutokujua?
Swali:
Watu wanajua kuwa shirki ni haramu, lakini hawajui kuwa wayafanyayo ni
shirki na hilo inatokana na ujinga wao.
´Allaamah al-Fawzaan:
Shirki iko wazi. Hakuna chakutokujua shirki. Shirki ni kumuomba asiyekuwa
Allaah. Kuchinja kwa asiyekuwa Allaah, kuweka nadhiri kwa asiyekuwa
Allaah, kumuomba du´aa asiyekuwa Allaah na kuwachinjia maiti, Haya yako
wazi. Kila mmoja anayajua haya.
Muulizaji:
85
Na baadhi yao ni watu wa kawaida na wazee...
´Allaamah al-Fawzaan:
Watu wa kawaida na wazee wamesikia kuwa hii ni shirki kwa walinganizi,
katika vitabu, katika vyombo vya habari. Wamesikia hili. Lakini hawataki
kuachana nayo. Watu hawa imekwishawasimamikia hoja. Wewe wataka
kuwasimamishia hoja vipi, uiingize imani katika nyoyo zao?? Hapana! Hoja ni
wewe kuwafikishia. Wamekwishasimamishiwa hoja, lakini wamekataa.
Tuwafanye nini?
119) Nina Miaka 17 Wazazi Wangu Hawaswali Alfajiri, Unaninasihi Vipi?
Swali:
Mimi nina miaka kumi na saba na sina ndugu wakubwa kuliko mimi na
wazazi wangu hawaswali swalah ya alfajiri ila mara chache tu na wanaiswali
kabla ya kwenda kazini, na sina mtu ataeniamsha katika swalah ya alfajiri. Ipi
nasaha yako kwangu na kwa wazazi wangu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Nasaha yangu kwao watubie kwa Allaah na wamuombe msamaha Allaah na
waswali swalah ya alfajiri. Hawana isipokuwa Allaah. Watakuwa wamebaki
na nini wakiacha swalah? Watakuwa wamebaki na nini katika dini?
Watakuwa hawakubaki na kitu. Wasaidie na uwakumbushe. Ama wewe swali
na jamaa´ah, swali uamke. Na ninakunasihi ikiwa utaweza kuhama na kuishi
nje yao ni wajibu kwako kuishi nje yao ikiwa hawatokubali nasaha.
86
120) Kulipa Swalah Za Rawaatib Kinyume Na Wakati Wake
Swali:
Leo nilikuwa Hospitali na baba yangu alikuwa mgonjwa nami, nikaswali
dhuhr Hospitali na wala sikuswali Rawaatib [sunnah] si ya kablia wala baadia
kwa kushughulishwa na maradhi ya baba yangu. Je inajuzu kuzilipa hivi sasa
kwa kuwa mimi nimekuwa mwenye kuhifadhi sunnah hizi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Umekufutu wakati wake. Hizi ni naafilah na zimekufutu wakati wake.
Usizilipe.
121) Baada Ya Siku Tatu Ndo Kajua Kuwa Aliswahi Kinyume Na Qiblah,
Alipe?
Swali:
Kuna mtu kaswali kinyume na qiblah na kajua hilo baada ya kupita siku tatu,
je alipe swalah hizo?
´Allaamah al-Fawzaan:
87
Ikiwa yuko katika bari na wala hajui kilipo qiblah akajitahidi akaswali swalah
yake ni sahihi. Ama kama yuko katika mji na kuna misikiti na kuna watu
wakuuliza akaswali kinyume na qiblah alipuuza ni lazima azirudi [kuziswali].
122) Kuomba Viumbe Waliyo Hai Wakuombee Du´aa Ni Makosa Na
Udhaifu?
Swali:
Kuna mtu anaesema kuwa kuwaomba viumbe wakuombee du´aa ni udhaifu
wa kumtegemea Allaah na si katika ukamilifu wa kumtegemea na kuegemea
Kwake. Je kauli hii ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Yaani ´Umar (radhiya Allaahu ´anhu) ana udhaifu wa kumtegemea Allaah
alipomuomba ´Abbaas amuombee du´aa? Maswahaba (radhiya Allaahu
´ahum) walipomuomba Mtume awawaombee wana udhaifu wa kumtegemea?
Hapana! Hili ni kutokana na uwezeko mkubwa wa kujibiwa, kwa sababu
du´aa ya mja mwema kuna uwezekano mkubwa wa kujibiwa. Na si kuwa
unamtegemea yeye, bali ni kutokana tu na uwezekano mkubwa wa kujibiwa.
123) Hukumu Ya Kuambizana “Ijumaa Yenye Baraka” Siku Ya Ijumaa
Swali:
88
Inajuzu kwa mtu kumwambia mwengine siku ya ijumaa kumwambia:
"Ijumaa yenye baraka"?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, hili halikuthibiti kupeana hongera siku ya ijumaa. Wasipeane
pongezi siku ya ijumaa, halikuthibiti. Hata siku ya Idi hapakuthibiti chochote,
lakini ni kitu kimezoeleka tu na watu. Na imaam Ahmad anasema mimi sianzi
kwa kutoa hongera lakini kwa ataeanza kunipa nitamrudishia.
124) Hukumu Ya Kutawassul Kwa Jaha Ya Mtume (´alayhhis-Salaam)
Swali:
Je inajuzu kutawasuli kwa Allaah kwa jaha ya Mtume (swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hili halikuthibiti ni bid´ah. Hii ni Hadiyth ya uongo kama mlivyoona katika
[kitabu] "Tawassul wal-Wasiylah" cha Shaykh-ul-Islaam ibn Taymiyyah.
Kutawasuli kwa jaha yake ni jambo halina dalili. Ni bid´ah.
125) Hukumu Ya Kuwaombea Du´aa Watu Wa Bid´ah
89
Swali:
Je inajuzu kuwaombea du´aa watu wa bid´ah kwa rahmah, msamaha na
Pepo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa ni Waislamu na bid´ah zao hazikuwatoa katika Uislamu; wanasihiwe,
walinganiwe waache bid´ah na waombewe pamoja na Waislamu kwa ujumla
na watu wa Tawhiyd. Ama zikiwa bid´ah zao zimechanganyika na bid´ah na
shirki zinawatoa katika Uislamu, hapana [wasiombewe]. Kwa mfano du´aa
badala ya Allaah, kuabudu makaburi hizi ni bid´ah za shirki. Kujengea
makaburi kwa ajili ya kuyaabudu na kuyaadhimisha.
126) Je, Kutamka Shahaadah Tu Bila ´Amali Inatosha?
Swali:
Vipi kumradi ambae anatumia hoja Hadiyth ya Mtume (swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) nayo ni:
"Atakayesema Laa ilaaha illa Allaah [ataingia Peponi]"
Anasema muhimu ni kutamka tu na si matendo yanayostahiki.
´Allaamah al-Fawzaan:
90
Mtume (´alayhis-Salaam) hakusema Laa ilaaha illa Allaah akanyamaza.
"Atakayesema Laa ilaaha illa Allaah akiwa mkweli ndani ya moyo wake."
"Atakayesema Laa ilaaha illa Allaah na akakufuru kwa vinavyoabudiwa
kinyume ya Allaah."
"Allaah Kamharamishia Moto atakayesema Laa ilaaha illa Allaah akitafuta
kwa hilo Uso wa Allaah."
Vipi wewe ndugu utachukua Hadiyth moja na uache Hadiyth zingine zote?
127) Hukumu Ya Anaesema Laa Ilaaha Illa Allaah Ila Hakufuru
Vinavyoabudiwa Kinyume Na Allaah
Swali:
Katika kauli ya Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Atakayesema Laa ilaaha illa Allaah na akakufuru vinavyoabudiwa kinyume
na Allaah imeharamika kwake mali yake na damu yake."
Ina maana ya kwamba atakayesema Laa ilaaha illa Allaah na asikufuru
vinavyoabudiwa badala ya Allaah, mtu huyo haiharamiki kwake mali yake na
damu yake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, liko wazi hili ni maneno ya Mtume. Kuwa atayesema Laa ilaaha illa
Allaah na wala asikufuru kwa vinavyoabudiwa badala ya Allaah, huyu
hakutoka katika shirki. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema:
91
8�� �� ��� �5�+ ���>�;�ت و�9
“Basi anayemkufuru Shaytwaan na akamuamini Allaah.” (02:256)
Katanguliza kwanza kuyakufuru matwaghuut [mashaytwaan] kabla ya
kumuamini Allaah. Kwa kuwa imani ya kumaumini Allaah haisihi ila kwa
sharti mpaka uanze kukufuru mashaytwaan. Ni kama Laa ilaaha illa Allaah,
ni kukanusha na kuthibitisha.
128) Wana Ada Wakiona Maiti Usingizi Wanamchinjia Na Kualika Watu
Walimani
Swali:
Katika kabila yetu kuna ada nayo ni anapoona mmoja wetu ambae yu hai mtu
maiti usingizini, basi humchinjia maiti huyu na kuwaalika watu katika
waliymah huu kisha wanamuombea [du´aa] maiti. Ipi hukumu ya kitendo
hichi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hili halijuzu, hili halijuzu. Na ndoto isizushiwe ahkam za Kishari´ah za
kuchinja, hii ni hukumu ya Kishari´ah. Haijuzu kuchinja kwa mujibu wa
ndoto au kwa yanayofanana na hayo. Haijuzu. Lakini kama kamuona maiti
[usingizini] na akakwambia kuwa ana deni la fulani na akamnasihi na umlipie
deni lake, hakuna ubaya. Au akakunasihi umuombee, hakuna ubaya. Ama
anakuomba umchinjie, hili halijuzu.
92
129) Kumuomba Allaah Kwa Kusem “Ewe Wa Allaah”
Swali:
Ipi hukumu kauli baadhi ya watu "Ewe Uso wa Allaah!" Inajuzu kusema hivo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haijuzu kumuomba kwa Sifa. "Ewe rehema za Allaah!, ewe Uso wa Allaah!."
Inatakikana kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ewe Allaah, na mtu
anatawasuli Kwake kwa Sifa au Jina Lake.
130) Hukumu Ya Mtoto Kushtushwa Na Kusema “Ewe Mama”
Swali:
Baadhi ya watu na khasa watoto wadogo wanapoona kitu kinachowatia khofu
wanamwita mama yao [Ee mama!] wala hakusudii hilo bali ni kitu
kinachomtoka tu kwenye ulimi na mama yake anaweza kuwa hayupo, je
huchukuliwa hii ni katika kuomba badala ya Allaah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Huyu ni mtoto asikalifishwe. Na wala hamuoni mwengine anayeweza
kumwangalia kwa mambo mbalimbali zaidi ya mama yake. Haya ndio
makusudio yake.
93
131) Watu Wataotoka Motoni Bila Ya Kufanya Kheri Yoyote
Swali:
Vipi kumpiga radd anaetumia hoja Hadiyth ya Shafaa´ah [maombezi] "Na
atatoka Motoni ambae hakufanya kheri yoyote."
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio ni katika watu wa Tawhiyd na kafa hakuweza kufanya amali. Alisema
Laa ilaaha illa Allaah akauawa au akafa kabla ya kuweza kufanya amali.
Huyu ni katika watu wa Tawhiyd na ni mwenye udhuru kwa kuacha amali
kwa kuwa hakuweza kufanya. Ama kwa yule aliyeweza kuishi miaka mia
haswali wala hafungi, kisha basi anasema tu Laa ilaaha illa Allaah. Kisha
wasema huyu ni katika watu wa Peponi? Na huyu eti atapata maombezi [ya
Mtume]? Nani anaedai hivi? Kama niwaambiavyo kila siku enyi ndugu
msichukue Hadiyth moja na mkaacha Hadiyth zingine zote. Lazima
zijumuishwe Hadiyth na zipeane nguvu. Huku ni kurejea [dalili] zisizo wazi
na kuacha zilizo wazi. Ama kuchukua Hadiyth moja isiyo wazi na ukaacha
Hadiyth zilizo wazi, huu ni mtindo wa watu wapotevu.
� ا�=� �>� ?3� ?��4( ���,��ن �� A�ز �C��DE F� �
“Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano
[zisizo wazi].” (03:07)
Mpaka Aliposema:
94
� #3� ر�3� � .! ?� �3�ا��Jن �F ا��D� �6���ن آ وا�+
“Na wale waliobobea katika ilimu husema: Sisi tumeziamini ZOTE.” (03:07)
Zilizo wazi na zisizo wazi.
� #3� ر�3� � .!
“ZOTE zimetoka kwa Mola Wetu.” (03:07)
Vipi utachukua upande huu na uache upande mwingine? Kama huku
sikufuata matamanio ni nini? Na huu ndo mtindo wa watu wapotofu, Allaah
Atukinge. Hadiyth ni lazima zioanishwe na zinapeana nguvu na zinaweza
kufutwa kwa kuoanishwa hivyo. Ni lazima kufanya hivyo na hii ndio njia ya
wanachuoni waliobobea katika elimu. Ama wenye kujifunza hawajui mambo
kama haya.
� #3� ر�3� � .! ?� �3�ا��Jن �F ا��D� �6���ن آ وا�+
“Na wale waliobobea katika ilimu husema: Sisi tumeziamini ZOTE.” (03:07)
Lakini mwenye kujifunza hajui mambo haya masikini. Hali kadhalika kwa
yule mwenye matamanio hufuata yale yanayoafikiana na matamanio yake tu
na huacha yale yanayoenda kinyume na matamanio yake.
132) Hukumu Ya Wazazi Wasiofahamu Kiarabu Wanaita “Ewe Mtume Wa
Allaah!”
95
Swali:
Wazazi wangu wanatoka Pakistan na wala hawafahamu lugha ya kiarabu na
mara nyingi wanasema "Ewe Mtume wa Allaah!". Je niwape udhuru kwa hili
au nifanye nao nini?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haijuzu kuwapa udhuru kwa hili. Wabainishie kwa lugha yao. Kama
unafahamu lugha yao wabainishie kuwa hili halijuzu.
133) Mume Anamlingania Mke Wake Katika ´Aqiydah Ya Ash´ariyyah, Mke
Amtii?
Swali:
Ikiwa mume anamwita mke wake katika ´Aqiydah ya Ash´ariyyah na
anafanya siri kwa hilo. Upi wajibu wa mke na anakhofia ´Aqiydah yake na...
´Allaamah al-Fawzaan:
Wajibu kwake ni kumuasi. Ni wajibu kwake kwanza kumbainishia kuwa hili
ni kosa na kuwa Ashaa´irah wako katika makosa. Akikubali sawa la sivyo
usimtii kwa hilo. Baki katika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
96
134) Hukumu Mwanamke Kusoma Qur-aan Kwa Mashaykh Wanaume
Swali:
Je mwanamke anaweza kusoma Qur-aan kwa Shaykh mpaka afikie kiwango
cha kuweza kusoma?
´Allaamah al-Fawzaan:
Leo - Alhamduli Allaah, wanawake mahafidhi wanaojua kusoma ni wengi.
Asome kwa mwanamke.
135) Acheni Falsafa, Mwenye Kufanya Shirki Ni Mshirikina!
Swali:
Wanasema wanachuoni "sisi tunamhukumu mtu kwa uinje wake", vipi
tutajumuisha hili na mwenye kusema "mwenye kutafuta baraka udongoni
kwenye kaburi ni shirki kubwa akikusudia [akiamini] kuwa udongo huyo
unanufaisha la sivyo itakuwa ni shirki ndogo.
´Allaamah al-Fawzan:
Hizi ni falsafa. Mwenye kudhihirisha shirki tutamhukumu kwa hilo bila
falsafa kama hizi. Eti akiamini, akisema nadkhalika. Nani mwenye kudai hivi?
97
136) Hukumu Ya Kuweka Nadhiri Kwa Asiyekuwa Allaah
Swali:
Mwenye kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah anakuwa mshirikina kwa
kauli yake hiyo au kwa kitendo chake hicho?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kwa yote mawili, kwa kauli yake na kwa kitendo chake. Kwa kuwa nadhiri ni
´Ibaadah na haiwekewi mtu mwengine ila Allaah (´Azza wa Jalla).
137) Hukumu Ya Kuitamidi Kwa Allaah Kisha Kwa Kiumbe
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kusema "mimi naitamidi kwa Allaah kisha kwako"?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hakuna ubaya. Naitamidi kwa Allaah kisha kwako, umemfanya ni
wakufuatia na hukumfanya akawa ni mshirika wa Allaah (´Azza wa Jalla).
98
138) Hukumu Ya Kutosoma Kwa Tajwiyd
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kutochunga ahkaam za kisomo na Tajwiyd kama yule
asiyeleta muduud, inajuzu kuswali nyuma yake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ewe ndugu kinachotakikana ni Tajwiyd ya nahwu, asilete kisomo ambacho
kitaenda kinyume na nahwu. Ama zaidi ya hapo ni katika kule kukamilisha tu
na hakudhuru. Ukikhalifu haidhuru. Muhimu ni kuchunga nahwu kwa lugha
ya Qur-aan iliotemreka kwayo. Achunge sehemu kama ya marfuu´, ahifadhi
majruur, manswuub na majzuum. Hili ndo muhimu. Hii ndio Tajwiyd
inayohitajika. Ama Tajwiyd kama ya Idghaam, Ghunnah na mduud hizi ni
kwa kukamilisha tu na si lazima.
139) Kumuomba Mtu Ni Vibaya?
Swali:
Nilikuwa nikimuomba mmoja katika watu, vipi nitubie kwa hilo?
´Allaamah al-Fawzaan:
99
Swali haliko wazi. Ikiwa anakusudia kuwa alikuwa anamuomba kwa mambo
ambayo anayaweza hakuna ubaya kwa hilo. Ama ikiwa alikuwa anamuomba
mambo ambayo hayawezi mwengine isipokuwa Allaah hili halijuzu. Ni juu
yake kufanya tawbah kwa Allaah na kuacha kitu hichi.
140) Nilikuwa Na Deni La Mtu Simjui Ama Sasa Nimejua, Nimpe Au
Nitoe Swadaqah?
Swali:
Baba yangu alikuwa na deni na wala sikuwa namjua mwenye deni hilo, kwa
sasa nimemjua. Nitoe swadaqah kwa mwenye deni hilo au nifanye nini?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kama umemjua sasa mkabidhi kama yu hai. Na kama kishafariki, wape
warithi wake na usizitoe swadaqah. Isipokuwa tu kama hukumpata yeye na
hukupata mrithi wake, hapo utazitoa swadaqah.
141) Tahadhari Na Kundi La Qur-aaniyyah Linalopinga Sunnah!
Swali:
100
Je yawezekana Qur-aan na Sunnah vikatofautiana na akasema mtu "Sichukui
kinachoenda kinyume na Qur-aan"? Je vipi kauli hii ni kufuru?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mwenye kusema hivi hayuko mbali na kufuru. Kwa kuwa anampinga Mtume
(swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kukataa Hadiyth zake. Na kuna pote
maarufu linaitwa Qur-aaniyyah wanakataa Sunnah. Na wakwanza wao
ilikuwa ni Makhawaarij, Makhawaarij wanapinga kuifanyia Sunnah kazi. Hili
halijuzu. Sunnah ya Mtume ni hoja baada ya Qur-aan. Anasema Allaah (Jalla
wa ´Alaa):
�C�اK�� ?3# �!�CK ����ل �J=وه و و�� آ)�!� ا�+
“ Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni
nacho.” (59:07)
�C�D# 3�كD���ل �6� أط�ع هللا و�� )O�� ��� أر � �>S ا�+ ��U�5V
“Mwenye kumtii Mtume basi ndio amemtii Allaah. Na anayekengeuka, basi
Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao.” (04:80)
��ل �� أC�� ا�=�� آ�3�ا أط���ا هللا وأط���ا ا�+
“Enyi mlioamini! Mtiini Allaah, na mtiini Mtume.” (04:59)
��واC( ه��وإن )>�
“Na mkimtii yeye mtaongoka.” (24:54)
��ل ��V+( ��D��ن وأط���ا هللا وا�+
101
“Na mtiini Allaah na Mtume ili mpate kurehemewa.” (03:132)
Ni lazima kumtii Mtume na kuzifanyia kazi Hadiyth zake sahihi baada ya
Qur-aan Tukufu. Na Hadiyth za Mtume ndo zinaifasiri Qur-aan, zinaiweka
wazi na zinaitolea dalili. Zenyewe ndo zinaibainisha Qur-aan. Kwa kuwa
Allaah Kasema:
�C��ل إ XK ���,�� �3D�س � +! وأ3�XK� إ0�� ا�=
“Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo
teremshwa kwao.” (16:44)
Atabainisha kwa nini?
Atabainisha kwa Sunnah, Sunnah za Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam). Wapi tumetoa kuwa swalah ya dhuhr na ´asr ni raka nne na maghrib
ni tatu na fajr ni mbili, wapi tumetoa haya? Je ni katika Qur-aan?
Ni katika Sunnah. Wapi tumetoa kipimo na kiwango cha zakaah na mali
ambazo ni wajibu kutoa zakaah?
Tumetoa katika Sunnah. Qur-aan iko kwa jumla na inabaishwa na Sunnah.
Huyu anaesema maneno haya haifanyii hata Qur-aan kazi. Angekuwa
anaifanyia Qur-aan kazi, angechukua Kauli ya Allaah:
�C�اK�� ?3# �!�CK ����ل �J=وه و و�� آ)�!� ا�+
“Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho.”
(59:07)
Kasema Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Ee tambueni! Mimi nimepewa Qur-aan na mfano wake pamoja." Na Allaah
(Jalla wa ´Alaa) Kasema:
102
OV�� FV�ى إن ھ� إ& وC�3>] #� ا� �� و
“Wala hatamki kwa matamanio. Hayakuwa haya ila ni ufunuo [wahyi] ulio
funuliwa.” (53:03)
Sunnah ni wahyi [utemremsho] kutoka kwa Allaah. Je unakadhibidha wahyi?
Jambo hili ni hatari sana.
142) Makataza Ya Wanafunzi Kuwapa Zawadi Waalimu Zao
Swali:
Kuna dada anauliza. Je inajuzu kwa wanafunzi wanawake kumpa zawadi
mwalimu baada ya kumaliza mwaka wa masomo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Wanafunzi wanawake wasimpe zawadi mwalimu. Kwa kuwa hili
lina tuhuma kwa mwalimu akikubali zawadi ina maana kutakuwepo
upendeleo fulani kwao. Hii ni katika rushwa, hili linangia katika rushwa.
143) Imaam ash-Shawkaaniy Ni Imaam Wa Ahl-us-Sunnah
Swali:
103
Ipi sababu ya Zaydiyyah kumchukua imaam Shawkaaniy na kujinasibisha
kuwa ni katika wanachuoni wao?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana si katika maimamu wao. Ni katika wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah. Ni
katika wanachuoni wa Ahl-ul-Hadiyth.
144) Ni nani ´Abdul-Qadir al-Jaylaaniy?
Swali:
Ni nani ´Abdul-Qadir al-Jaylaaniy?
´Allaamah al-Fawzaan:
´Abdul-Qadir al-Jaylaaniy ni imamu miongoni mwa maimamu wa Ki-
Hanbaliy, ni mtu mwema mcha Mungu. Lakini wanamdanganyia na
kumsingizia mambo ambayo alikuwa nayo mbali kabisa.
Swali La Pili:
Na ni nani al-Badawiy?
104
´Allaamah al-Fawzaan:
Al-Badawiy kilicho dhahiri ni kuwa ni mtu wa Makkah alienda Egypt.
Inasemekana kwa alibaki muda mrefu msikitini siku ya ijumaa bila ya
kuchoshwa hivyo akawa walii, kwa kuwa mawalii ndo hawapati machovu
bila kujali wanachokifanya. Hivyo watu wakamuabudu badala ya Allaah.
145) Waabudu Makaburi Wanaotumia Hoja Aayah Katika Suurat-ul-Kahf
Swali:
Katika suurat-ul-Kahf Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Hakuwakataza
waliofanya makaburi kuwa misikiti. Vipi tutaradi shubuha [utata] huu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Subhaana Allaah! Hakukataza?
&�ل ا��ذ�ن ���وا 3� أ�ر
“Wakasema walioshinda katika shauri yao.” (18:21)
Haya ni makatazo, "walioshinda katika shauri yao". Wametumia nguvu zao
bila ya dalili wala hoja. Ni kushinda tu [kwa jeuri].
�دا&�ل $ 1ذن� ���م �� ا��ذ�ن ���وا 3� أ�رھم ��!�
105
“Wakasema walioshinda katika shauri yao: "Bila ya shaka tutawajengea
msikiti juu yao." (18:21)
Wewe husomi tafsiri ya Qur-aan na wala hujui kitu.
146) Inajuzu Kusema Allaah Na Mtume Wake Ndio Wanajua?
Swali:
Akiulizwa mtu kitu fulani anasema "Allaah na Mtume Wake ndo wanajua."
Inajuzu kusema hivi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Kusema hivi ilikuwa wakati Mtume alikuwa bado yu hai (swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam), kulikuwa kukisemwa "Allaah na Mtume Wake
ndo wanajua. Ama baada ya kufa Mtume, kunasemwa "Allaah ndo Anajua
zaidi." Yatosha!
147) Aliechelewa Swalah Ya Istisqaa Upi Wajibu Wake?
Swali:
106
Nikiingia kwenye mswallah [aina ya msikiti mdogo] na watu
wamekwishaswali swalah ya Istisqaa [ya kuomba mvua] na imaam anatoa
khutbah, nawajibika kufanya nini?
´Allaamah al-Fawzaan:
Utakaa na kusikiliza khutbah. Yakutosheleza kufanya hivi Inshaa Allaah.
148) Nasaha Kwa Anaekhofia Riyaa
Swali:
Mimi mara nyingi nakhofia riyaa na huwa na shaka kunako amali zangu, ipi
nasaha zako kwangu kwa hilo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Wasiwasi huu unatokana na shaytwaan. Fanya amali zako na itakase nia yako
kwa Allaah na wala usijali wasiwasi wa shaytwaan.
149) Imaam Kukariri Aayah Fulani Anaposalisha Jamaa´ah
Swali:
107
Imaam msikitini kwetu anaposoma suurat-ul-Maa´uun, afikapo kwenye Kauli
ya Allaah (Ta´ala):
�و�ل �7��+��7ن
“Basi, ole wao wanaosali.” (107:04)
Anaikariri mara mbili, mara ya kwanza anasimama mwisho wake na mara ya
pili anafuatisha na aayah ya kufuata. Anafanya hivyo kila siku. Jambo hili
linafaa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Jambo hili halifai. Asome suurah bila ya kukariri.
150) Anamtangulia Kumsalia Maiti Kabla Ya Imaam Kusalisha
Swali:
Ipi hukumu ya kusimama baadhi ya watu kuwasalia maiti kabla hata imaam
hajasimama na kuanza kusalisha?
´Allaamah al-Fawzaan:
108
Hizi ni katika tabia mbaya. Haraka hizi hazifai. Haifai kwake kuja msikitini na
kumtangulia imaam akaanza kumsalia maiti, haifai. Amekuja msikitini
amfuate imaam. Subiri ndugu yangu, subiri! Mpaka atapokuja imaam uswali
nae.
151) Kuelekea Kaburi La Mtume (´alayhis-Salaam) Msikitini Na Kumuomba
Swali:
Nimeona mmoja wa waabudu makaburi anaomba kwenye kaburi la Mtume
(swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nikamkataza akasema "mimi namuomba
Allaah msikitini, nyumbani kwangu na kwenye kaburi la Mtume (´alayhis-
Salaam) na kila mahala.
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Kwenye kaburi la Mtume hapana usimuombe Allaah. Kaa msikitini
wa Mtume elekea Qiblah na umuombe Allaah (´Azza wa Jalla), hakuna
anaekukataza. Ama kuelekea kaburi na kuomba hili halijuzu. Ikiwa
unamuomba Mtume hii ni shirki, ikiwa unamuomba Allaah kwenye kaburi la
Mtume hii ni bid´ah na ni njia inayopelekea katika shirki.
152) Mgonjwa Anaepata Tabu Kutia Wudhuu Afanye Nini?
Swali:
109
Mgonjwa mwenye maradhi awezae kuweka kutawadha na kujipangusa baada
ya kutia wudhuu lakini kwa kufanya hivyo anapata tabu, je anaweza
kutayamamu?
´Allaamah al-Fawzaa:
Ikiwa kuna ambaye anaweza kumsaidia ni wajibu kufanya hivyo, kwa kuwa
atamsaidia kutia wudhuu. Ama ikiwa hana wa kumsaidia na hawezi
kutawadha kwa maji, atayamamu.
153) Msafiri Anaejua Lini Atarudi Kwao Hachukui Hukumu Za Msafiri
Swali:
Mtu mwenye kuja Saudi Arabia kufanya kazi ana hukumu sawa na msafiri
kwa kuzingatia ya kuwa kazi yake imewekea muda mwaka mmoja?
´Allaamah al-Fawzaan:
Huyu si msafiri. Ni msafiri njiani - anapotoka na kule anapokwenda. Ama
muda wake wa kubaki Saudi Arabia kwa ajili ya kazi mwaka au zaidi huyu ni
mkazi na si msafiri. Atatimiza swalah, atafunga Ramadhaan. Ahkam zake zote
ni kama za wakazi.
110
154) Anaemwendea Mpiga Ramli Kisha Akatubia Swalah Zake
Zitakubaliwa?
Swali:
Hadiyth ya Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mwenye kumwendea mpiga bao (mpiga ramli) akamuuliza kuhusu jambo
lolote, kisha akamsadiki aliyoyasema, hazikubaliwi Swalah zake kwa siku
arubaini” [Muslim]
Je vipi mtu akitubia Allaah Atakubali swalah zake hizi au hukumu itabaki
kama ilivyo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Allaah Ndiye Mwenye kujua zaidi. Tunaichukulia Hadiyth kama ilivyokuja.
155) Lini Mtu Anaweza Kuingia Peponi Bila Ya ´Amali?
Swali:
Hadiyth ya al-Batwaaqah. Hii si dalili ya kuwa mwenye kusema Laa ilaaha
illa Allaah ataingia Peponi hata kama hakufanya amali yoyote njema?
´Allaamah al-Fawzaan:
111
Ikiwa hakuweza kufanya amali. Akiisema kwa kuiamini na mwenye yakini na
hakuweza kufanya amali, kauawa au akafa kabla ya kupata fursa ya kufanya
amali ataingia Peponi. Ama akiacha amali kwa khiari yake na hakufanya
chochote, huyu si muumini. Kwa kuwa Laa ilaaha illa Allaah si kutamka tu
kwa ulimi, ina masharti yake na maana yake sahihi. Enyi ndugu! Msichukue
dalili moja ya jumla na mkaacha dalili zilizofafanua, za wazi na nyinginezo
zilizokuja kwenye Hadiyth nyingine, msifanya hivyo. Hadiyth kama hizi
lazima zirejelewe Hadiyth zilizoweka wazi suala hili. Ama kuchukua tu
Hadiyth moja na ukaacha Hadiyth zingine, hii ni njia ya watu wapotevu.
Ambao wanafuata [dalili] zisizowazi.
156) Je, Athari Ya Mtume (´alayhis-Salaam) Inapatikana Mpaka Hivi Leo?
Swali:
Athari ya Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) je, ipo mpaka hivi leo
kama nguo zake na nywele zake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Wametoa wapi? Nani awezae kuthibitisha kuwa kweli ni nguo za Mtume na
nywele za Mtume nk? Nani awezae kuthibitisha hili? Huu ni ukhurafi
usiokuwa na asli.
157) Ni Sahihi Muadhini Kusema Haqqan Laa ilaaha illa Allaah?
112
Swali:
Muda si mwingi nimesikia kwenye idhaa moja muadhini alipomaliza kutoa
adhaana akasema "Haqqan Laa ilaaha illa Allaah" [ni haki, hapana mungu
apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah]. Je kauli yake hii si makosa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana si makosa. Hapana mungu apasaye kuabidiwa kwa haki ila Allaah, ni
haki.
158) Mgonjwa Anaruhusiwa Kujumuisha Swalah Na Haruhusiwi
Kuzifupisha
Swali:
Baba yangu ana maradhi mazito hivyo anashindwa kuweka wudhuu katika
kila swalah, je anaweza kujumuisha swalah na kufupisha?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kufupisha hapana, hakuna kufupisha [swalah] ila katika safari tu. Ama
kujumuisha akihitajia hilo mgonjwa anaweza kufanya hivyo.
113
159) ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Tijaaniyyun Na Burda
Swali:
Katika mji wetu Tijaniyyuun [kipote cha mashia na masufi] wanamrehemu
Busiri [Gogo la Suufiy aliyetunga kaswiydah ya Burda, kaburi lake liko ndani
ya msikiti Misri] na wanamtakasa.
´Allaamah al-Fawzaan:
Si katika mji wenu tu, ni kila mahala. Baadhi yao wanasema Burda ni bora
kuliko hata Qur-aan. Hivyo ndo maana hawaipi umuhimu Qur-aan. Wanaipa
umuhimu Burda, wanaihifadhi, wanaiimba kila wakati. Huu ni upotevu -
A´udhubi Allaah. Huu ni mtihani khasa ukizingatia Burda ina baadhi ya
maneno maalumu, ya kupambia, kuimbika vizuri. Hii ni fitina - Allaah
Atukinge.
160) Qaswiydah Ya Burda Ina Shirki Na Ghuluu
Swali:
Ulisema katika darsa Burda ya Ahmad Shawqiy, je ndo ile Burda yenye
shirki?
´Allaamah al-Fawzaan:
114
Ndio, ni kama ile ya Busiri. Zote ni moja tu. Zina ghuluu nakadhalika.
161) Kulingania Katika Tawhiyd Inatosha Kukataza Tu Kuabudu
Makaburi?
Swali:
Je kulingania watu katika Tawhiyd na kubainisha mfumo wa Mitume katika
Tawhiyd inatosheleza kukataza wanaoabudu makaburi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Awabainishie watu ´Aqiydah [itikadi] na kumkataza anaekwenda kinyume
nayo. [Waislamu wa leo] ukitaka kuwafunza Tawhiyd wanasema sisi
tunampwekesha Allaah na hatwendi kinyume na Tawhiyd. Lazima
uwabainishie na uwalinganie.
162) Tofauti Baina Ya Du´aa Ya Masuala Na Du´aa Ya ´Ibaadah
Swali:
Je kuna tofauti baina ya du´aa ya masuala na du´aa ya ´ibaadah?
´Allaamah al-Fawzaan:
115
Du´aa ya masuala ni haja yako wewe. na du´aa ya ´ibaadah ni
kumuadhimisha Allaah (´Azza wa Jalla).
�ك �$!"�ن �ك �"�د وإ�� إ��
“Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.” (01:05)
Unaposema:
راط ا��$!��م اھد�� ا�+7
“Tuongoze katika njia iliyonyooka.” (01:06)
Haya ni masuala.
9 رب7 ا�"����ن ﴿ *�م ﴿٢ا�*�د ��ـ� ن ا�ر� ـ �* �ن ﴿ ﴾ ���ك �وم ٣﴾ ا�ر� ﴾٤ا�د7
“Sifa Njema zote Anastahiki Allaah Mola wa al-‘Aalamiyn (walimwengu)
wote. Ar-Rahmaanir-Rahiym (Mwingi wa Rehma-Mwenye Kurehemu
Daima). Maalik (Mfalme) wa Siku ya Malipo.” (01:02-04)
Hii ni ´ibaadah. Ni kumsifia na kumuadhimisha Allaah (Jalla wa ´Alaa).
�ك �"�د إ��
“Wewe Pekee tunakuabudu.” (01:05)
Hii ni du´aa ya ´ibaadah.
116
�ك �$!"�ن وإ��
“Na Wewe Pekee tunakuomba msaada.” (01:05)
Mpaka mwisho wa suurah, hii ni du´aa ya masuala. Na ndio maana Allaah
Kasema nimeigawa suurah hii baina Yangu Mimi na mja Wangu. Kuanzia
Kauli Yake:
9 رب7 ا�"����ن ا�*�د ��ـ�
“Sifa Njema zote Anastahiki Allaah Mola wa al-‘Aalamiyn (walimwengu)
wote.
(Mpaka):
�ك �$!"�ن �ك �"�د وإ�� إ��
“Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.” (01:02-05)
Hii ni ya Allaah (Jalla wa ´Alaa).
(Akisema):
�ك �$!"�ن وإ��
“Na Wewe Pekee tunakuomba msaada.” (01:05)
Mpaka mwisho wa suurah, hii ni du´aa ya masuala. Hii ni du´aa ya mja.
117
163) Eda Ya Mwanamke Aliyezaa Baada Ya Kufa Mumewe Kwa Saa Au
Dakika Kadhaa
Swali:
Mwanamke mjamzito kafa mume wake, mimba ikatoka baada ya kufa mume
wake kwa saa moja. Vipi eda yake imekwisha?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Ikitoka baada ya kufa mume wake katoka kwenye eda hata ikiwa kwa
saa moja au dakika.
���ن� أن �="ن *���ن� وأو6ت ا2*��ل أ
“Na wenye mimba eda yao mpaka watakapo zaa.” (65:04)
164) Wanafunzi Wanadai Kwamba Kusoma “Suurat-ul-Ikhlaas Baada Ya
Kila Swalah Ni Bid´ah
Swali:
Baadhi ya watafutaji elimu wanasema "Kusoma suurat-ul-Ikhlaas baada ya
kila swalah ni bid´ah. Wanasema eti ni Fatwa ya Shaykh ibn Baaz?
´Allaamah al-Fawzaan:
118
Yeye ndiye mubtadi´ah [mtu wa bid´ah], mwenye kusema hivi yeye ndiye
mubtadi´ah. Yaani yeye kila asichokijua anakikataa na kusema ni bid´ah?
Haijuzu. Je karejea Fatwa ya Shaykh vizuri au ni dhana zake tu? Namna ndo
wanavyokuwa baadhi ya wanafunzi, na wenye haraka. Shaykh ibn Baaz ni
imaam Jaliyl na hasemi ila yale alionayo yakini yana dalili.
165) Ghurabaa Ni Watu Gani?
Swali:
Yapi makusudio ya Ghurabaa ambao kasema Mtume (swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam) kuhusu wao "Bishara nje kwa Ghurabaa [wageni]."
´Allaamah al-Fawzaan:
Kawabainisha Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). [Maswahaba]
walimuuliza "Ni kina nani Ghurabaa?” Akasema "Ni wale watengenezao
wanapoharibu watu." Katika riwaayah nyingine "Ni wale wenye kutengeneza
walioharibu watu." Hawa ndo Ghurabaa.
166) Hukumu Ya Mafukara Wanaotumbukia Katika Shirki Kwa Ajili Ya
Kutafuta Riziki
Swali:
119
Sisi katika mji wetu Eritrea kuna makaburi watu wanayazuru.
´Allaamah al-Fawzaan:
Kila mahala siku hizi kuna makaburi.
Muulizaji:
Baadhi ya watu hawa [wanaozuru] ni mafukara na wanaenda wawasaidie
matumizi na njaa walonayo ili wale katika vichinjo hivi vinavyochinjwa huko.
Inajuzu kufanya hivyo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Yaani milango mingine yote ya riziki imefungwa mpaka aende makaburini
tu? Tafuta riziki kwa Allaah Allaah (´Azza wa Jala). Na Allaah yu Karibu
Mwenye kujibu. Na njia za kutafuta riziki ni nyingi na usende makaburini na
kula katika vichinjo vyao ni haramu kwa kuwa ni maiti hiyo mizoga. Kuchinja
kwenye makaburi ni shirki, vimechinjwa kwa asiyekuwa Allaah.
� �م �ذ�ر ا$م % �9� و6 !,��وا ���
“Wala msile katika wale wasio somewa jina la Allaah.” (06:121)
م ���م �� *ر� م و�*م ا�1�ز�ر و�� أھل� �9 �.�ر إ�� % ا���!N وا�د�
“Yeye Amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyamaya nguruwe na
kilicho tajiwa - katika kuchinjwa kwake jina la asiyekuwa Allaah.” (02:173)
120
Zimechinjwa kwa asiyekuwa Allaah, hivyo ni haramu kwenu.
167) Anadai Watu Hawana Haja Ya Kusoma Elimu Imejaa Kwenye Internet
Na Kwenye Mikanda
Swali:
Lipi jibu kwa anaesema leo watu hawana haja ya kwenda kwa mashaykh
misikitini, wanaweza kutosheka na elimu ya kwenye Internet na kusikiliza
mikanda na kusoma vitabu.
´Allaamah al-Fawzaan:
Huyu ni mpotevu, ni kama yule niliewaambia anasema msiwalinganie watu
katika Tawhiyd. Elimu haichukuliwi ila kwa wanachuoni. Si katika vitabu
wala mikanda. Inachukuliwa kwa wanachuoni. Kwanza nani aliyevifanya,
nani mwenye kuongea? Utamjuaje muongeaji? Utaijuaje ´Aqiydah yake?
Hujui ikuwa ni mwanachuoni au si mwanachuoni. Baadhi ya watu
wanayapamba maongezi, maneno yao lakini hawana elimu. Mtu kuongelea
kuwa na usulubu mzuri na tabia nzuri, si elimu. Ni kuiongelea elimu na Fiqh.
Fiqh imekuwa ndogo sana kwa watu leo. Wasomaji wamekuwa wengi na
wanachuoni wamekuwa wadogo kama alivyosema Mtume (swalla Allaahu
´alayhi wa sallam). Tunachoongelea ni Fiqh na si kusoma tu. Elimu
haichukuliwi kwenye vitabu. Vitabu vina haki na batili, vina upotevu, makosa
na kupatia. Na wala hakuna awezae kupambanua haya ila wanachuoni. Wewe
unajisomea tu na hujui kitu, utachukulia [kitabu] kama kilivyo. Na huenda
ukaitakidi upotevu na wewe hujui. Hili halijuzu katu. Na aliesema maneno
haya ima ni mjinga wakutupia au ni mpotevu. Anataka kuwakimbiza watu na
kutafuta elimu na kuchukua elimu kwa wanachuoni.
121
168) Hukumu Ya Kusema Washirikina Ni Ndugu Zetu
Swali:
Je mwenye kumuomba Hasan na Husayn (radhi za Allaah ziwe juu yao) au
akatafuta baraka katika makaburi yao. Je mtu anaweza kusema kuwa ni
Waislamu au kusema ni ndugu zetu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Si ndugu zetu. Tunajiweka mbali na Allaah na mtu huyu na dini
yake. Naye ni mshirikina adui wa Allaah na ni adui wa Waislamu.
ون �ن *�د� %� � وا��وم ا1Oر �واد �P�� د &و�� �ؤ��ون�و ���وا آ��ءھم أو أ���ءھم أو إ1وا��م أو ور$و9� و� ا ! >�ر!�م
“Huwakuti watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa
wanawapenda wanao mpinga Allaah Mtume Wake, hata wakiwa ni baba zao,
au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao.” (58:22)
Hakuna mapenzi baina yetu sisi na baina ya washirikina na makafiri. Katu!
169) Anataka Kuacha Kupiga Punyeto Anashindwa, Ipi Nasaha Yako?
122
Swali:
Kuna mtu Allaah Kampa mtihani wa kupiga punyeto, na mara nyingi anataka
kuacha lakini anashindwa. Anasema ipi nasaha yako kwake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hakushindwa isipokuwa tu hana azima. Ana udhaifu wa azima. Aazimie,
awe na nia nzuri, amuombe Allaah Amsaidie na aache jambo hili. Kuna watu
wameacha mambo makubwa kuliko haya, wameyaacha nao wanayapenda
lakini wameyaacha kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jalla) na Allaah Kawasaidia
kuyaacha. Kuwa na nia nzuri kwa Allaah na azimia kuacha. Jambo lingine
jiweke mbali na watu wake wasije kukudanganya au kukuweka katika
mkumbo huo, jiweke nao mbali. Ikaa na watu wena na wenye msimamo.
170) Haijuzu Kuomba Shafaa´ah (Uombezi) Kwa Maiti Sawa Mtume Au
Mwengine Yeyote
Swali:
Ipi rai yako kwa mwenye kusema "Ewe bwana wangu niponye!", akikusudia
Mtume wa Allaah (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mtume kwa sasa haombwi shafaa´ah, ataombwa siku ya Qiyaamah
atapokuwa hai. Shafaa´ inaombwa kwa aliehai. Shafaa´ah inaombwa kwa
123
aliehai. Kwa maana anamuomba Allaah. Inajuzu kuomba du´aa kwa aliehai.
Ama maiti haombwi shafaa´ah wala du´aa wala chochote.
171) Kuvaa Nguo Za Makafiri Za Kumalizia Masomo
Swali:
Sisi ni mjumuiko wa wanafunzi tunaenda thanawiy na karibu madrasah yetu
yatafanya hafla ya kumaliza madrasah na wametuomba kuvaa nguo za
kumaliza madrasah. Ni nguo zinazovaa watu wa magharibi wamalizapo
masomo. Je inajuzu kwangu kuvaa nguo hizi katika hafla hii?
´Allaamah al-Fawzaan:
Vaa nguo katika nguo za Waislamu na usivae nguo za makafiri. Vaa nguo za
Waislamu zenye kusitiri nzuri na usivae katika nguo za makafiri. Usiwaige
makafiri.
172) Hukumu Ya Anaeacha Kufunga Ramadhaan Ila Hapingi Uwajibu
Wake
Swali:
Mwenye kuacha swawm ya Ramadhaan lakini hapingi wajibu wake,
anakufuru kwa hilo?
124
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Vipi ataacha kufunga naye hapingi? Vipi ataacha swawm ya
Ramadhaan naye hana udhuru wa Kishari´ah ikiwa kweli hapingi? Ameacha
kwa kuwa anaona si wajibu.
173) Anaetetea Ushirikina Sawa Hakimu Au Yeyote Yule Ni Mshirikina
Swali:
Hakimu anaetetea ´ibaadah ya makaburi, anayahami na kukataza kuyaharibu.
Ipi hukumu ya hilo na hukumu yake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mnajua wenyewe hukumu ya mwenye kutetea shirki kuwa ni mshirikina na
karitadi akiwa anadai eti ni Muislamu.
174) Mwanaume Si Sawa Na Mwanaume
Swali:
125
Kuna daa´iy [mfanya da´wah] kajitokeza na kusema kuwa hakuna tofauti
baina ya wanaume na wanawake isipokuwa tu wanaume...
´Allaamah al-Fawzaan:
Wanaume kama yeye hawana tofauti baina yao wao na wanawake. Ama
wanaume wakihakika si kama wanawake.
3Q�2�� �ر و��س ا�ذ�
“Na mwanamume si sawa na mwanamke.” (03:36)
175) Daa´iy Mpotofu Anaewaponda Maswahaba (radhiya Allaahu ´anhum)
Swali:
Baadhi ya watu wanasema kuwa haitupasi kwetu kuwasifia Maswahaba
(radhiya Allaahu ´anhum) wote, kwa kuwa kati yao kuna wanafiki na sisi
hatujui...
´Allaamah al-Fawzaan:
Huku ni kuwatia ila Maswahaba, huyu anataka kuwatia shubuha kwa
Maswahaba wa Mtume wa Allaah ( 9 و$�م��3 % �+ ). Huyu ni daa´iy mpotofu,
puuzeni maneno yake.
126
176) Anaejuzisha Kujengea Misikiti Makaburi Ni Mshirikina
Swali:
Mwenye kujuzisha kutawassul kwa Mtume ( 9 و$�م��3 % �+ ) baada ya kufa
kwake na akapinga adhabu ya kaburi na akajuzisha kujengwa misikiti kwenye
makaburi. Je anakufuru kwa hayo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Bila shaka, akijuzisha kujenga misikiti kwenye makaburi naye anajua mwenye
kufanya hivyo kalaaniwa - haya yapo katika Hadiyth swahiyh. Mwenye
kujenga msikiti katika kaburi kalaaniwa na pia ni katika watu waovu sana
mbele ya Allaah (´Azza wa Jalla) kama ilivyo katika Hadiyth swahiyh. Ikiwa
anajua hilo basi anakufuru.
177) Imaam Kujumuisha Maghrib Na ´Ishaa Wakati Wa Mvua Na Baridi
Kali
Swali:
Je ni lazima kwa imaam anapotaka kujumuisha maghrib na ´ishaa kwa ajili ya
mvua atoke nje na kuangalia kama mvua bado yaendelea au yatosha
kuangalia waliotangulia waliopo msikiti [waliokuja wakati mvua ilikuwa
yanyesha]?
127
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa wanaingia msikiti na mvua yanyesha na kuna matope na ni wakati wa
baridi, udhuru bado upo [wa kujumuisha]. Ama ikiwa ni mvua ni hafifu au
hajui kama bado kunaendelea kunyesha au hapana, ni lazima awe na uhakika.
178) Ahl-ul-Kitaab Wa Zama Hizi Inajuzu Kuwaoa
Swali:
Inajuzu kuoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab [mayahudi na manaswara] katika
zama zetu hizi baada ya wao kutumbukia katika kumshirikisha Allaah
(Subhaanahu wa Ta´ala)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mpaka Qiyaamah inajuzu kuoa mwanamke mnaswara kwa sharti
[mwanamke huyo] awe si mzinifu, yaani awe mwema.
وا��*+��ت �ن ا��ذ�ن أو!وا ا��!�ب
“Na wanawake wema miongoni mwa walio pewa Kitabu.” (05:05)
Yaani ambaye si mzinifu. Allaah Anawajua vizuri manaswara tangu wakati
wa Mtume Qur-aan ilipokuwa ikiteremka, ila pamoja na hilo Akaruhusu hilo.
Hakuna yeyote awezae kupinga Aliloruhusu Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
128
179) Wazazi Haijuzu Kuwapeleka Watoto Katika Madrasah Ya Ahl-ul-
Bid´ah Kama Masufi
Swali:
Je niwasomeshe watoto wangu katika madrasah ya Masufi kwa kuwa hatuna
madrasah mengine katika mji wetu. Wanawafunza huku ya kwamba Allaah
Yuko kila mahala - Ametakasika Allaah na hilo. Na mimi nilisoma katika
madrasah haya na nnajua yaliomo. Je inajuzu kuwaingiza katika madrasah
haya?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Haijuzu kuwaingiza katika madrasah ya shirki na bid´ah na Itikadi
potofu. Wafunze wewe ukijuacho na inatosha hilo. Lau katika mji ulipo kuna
kundi la Waislamu wengine mnaweza kufungua madrasah ya kwenu kwa
watoto wenu tu. Huu ndo wajibu kwenu.
180) Itikafi Potofu Ya Kuogopa Kijicho Kwa Kutupa Kipande Cha Chakula
Chini
Swali:
Wanapotaka baadhi ya watu kula wanatupa [wanaweka] kwanza kipande
kidogo cha chakula chini, na wanasema wanakhofia kupatwa na kijicho?
129
´Allaamah al-Fawzaan:
A´udhubi Allaah - hizi ni Itikadi potofu wala haijuzu kutupa chakula.Bali
Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:
"Kitapoanguka [kipande] cha chakula cha mmoja wenu, akichukue [akiokote]
na akitoe maudhi [uchafu] uliokipata na akile naasimuachie nacho
shaytwaan."
181) Allaah (Ta´ala) Ana Sifa Ya Nafsi
Swali:
Kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Iysa aliposema:
� و6 أ�م �� �� ��$ك $�� � !"�م �� �
“Wewe Unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo
katika Nafsi Yako.” (05:116)
Hii ina maana Allaah Anathibitishiwa Sifa ya kuwa na Nafsi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio bila shaka. Kuna uthibitisho wa Allaah kuwa na Nafsi.
ر�م % 9$�� و�*ذ7
130
“Na Allaah Anakutahadharisheni Nafsi Yake.” (03:28)
Kasema hivyo mara mbili katika suurat-ul-´Imraan.
182) Allaah Yuko Kwenye Jiha Juu
´Allaamah al-Fawzaan:
Je wewe unaamini kuwa Allaah yuko katika kila jiha? Lazima uamini kuwa
Allaah Yupo katika jiha ya Juu. Kasema Mwenyewe kuwa Yuko katika Jiha ya
Juu.
183) Je Al-Muhaasib Ni Jina La Allaah (Ta´aal)?
Swali:
Je imethibiti kuwa katika Majina ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ni al-
Muhaasib?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Sikumbuki kitu kuhusiana na hili. al-Muhaasib?!
131
184) Khatari Ya Kumkufurisha Mtu Binafsi?
Swali:
Ipi hukumu ya kumlaani mtu binafsi, kama kusema "Laana ya Allaah iwe juu
ya fulani"?
´Allaamah al-Fawzaan:
Yule ambaye laana yake imethibiti katika Qur-aan au Sunnah analaaniwa.
Ama yule ambaye laana yake haikuthibiti katika Qur-aan wala Sunnah hapa
ndo kuna khilaaf. Kauli yenye nguvu - na Allaah ndo Anajua zaidi - ni kuwa
asilaaniwe kwa kuwa hujui mwisho wake utakuwa vipi.
185) Maulamaa Waliopinda Wasiojua Tawhiyd
Swali:
Je kuna maulamaa wasioijua Tawhiyd?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni wengi. Maulamaa wengi hawaijui Tawhiyd. Wamebobea kunako lugha,
Fiqh, huenda pia Hadiyth. Lakini ´Aqiydah hakusoma. Unakuta yuko katika
132
madhehebu ya Ashaa´irah au madhehebu ya wale wasiokataza ´ibaadah ya
wenye kuabudu makaburi.
186) Maiti Hata Wakisikia Hawawezi Kukunufaisha Kwa Kitu
Swali:
Lipi jibu la dalili ithibitishayo kuwa maiti anasikia? Na wameishikilia kweli
kweli waaburu makaburi.
´Allaamah al-Fawzaan:
Hata akisia ndo iweje!!. Allaah Kasema:
�$�"وا د�ء�م و�و $�"وا �� ا$!���وا ��م إن !دوھم 6
“Mkiwaomba hawasikii maombi yenu; na hata wakisikia HAWAKUJIBUNI.”
(03:14)
Hivyo hakuna faida ya kuwaomba nao HAWAKUJIBUNI. Lakini watu hawa
huchukia sehemu ya Aayah au katika Hadiyth na wanaacha... Wanachukua
yale ya kwao na wanaacha yale yaendao dhidi yao. Na hii ndio tabia ya watu
wapotevu. Kama Alivyosema Allaah (Jalla wa ´Alaa):
�"ون �� !>��9 9�� ا�!.�ء ا��!N� وا�!.�ء !,و�9� �!�� C��م ز��و& �� ا��ذ�ن � ��,�
“Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotevu, hufuata zile
zilizoshabihiana kutafuta fitnah na kutafuta tafsiri zake.” (03:07)
133
Wanachukua yanayoenda sawa na madai yao na wanaacha yanayokwenda
kinyume nao. Na wanaacha yanayoweka wazi [kuponda] yake waliochukua
katika mujmal au zilizoshabihiana. Hii ndio njia ya watu wapotevu.
187) Picha Ni Haramu Sawa Za Digital Au Za Aina Yoyote
Swali:
Ninawanasihi wale wanaopiga picha kwa kutumia ala ya digital camera,
wananirudi kwa kusema "masuala haya wanachuoni wametofautiana". Ipi
dalili yenye nguvu katika masuala haya ya khilaaf?
´Allaaamah al-Fawzaan:
Waambie sisi hatujali eti wanachuoni wametofautiana. Sisi tunaangalia dalili.
Yule mwenye [kukhalif] kupinga kama yuko na dalili sahihi tunachukua. Ama
ikiwa hana dalili anapuuzwa. Hii ndio kanuni yetu katika masuala yote na si
picha tu.
188) Usingizi Hauwajibishi Kustanji, Kinachowajibisha Ni Kutokwa Na
Kitu Tupuni
Swali:
134
Kuna mtu kalala usiku kisha akaamka, je ni wajibu kwake kustanji [kuosha
ima tupu ya mbele au ya nyuma]? Na akiswali kwa kutawadha tu bila ya
kustanji swalah yake ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Usingizi hauwajibishi kustanji, kinachowajibisha kustanji ni kutokwa na kitu
nje. Akitokwa na kitu atastanji au atastijmaar [kujisafisha kwa kutumia kama
mawe, karatasi nk]. Ama kulala tu hili haliwajibishi kustanji.
189) Kila Kivazi Cha Mwanaume Chenye Kuvuka Kongo Mbili Za Miguu
Ni Motoni
Swali:
Hadiyth ya Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Kilichoko chini ya kongo mbili za miguu katika izaar [nguo ya chini] ni
Motoni."
Je inaingia katika hukumu hii suruwali?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni chochote chenye kuvuka kongo mbili za miguu, ni jumla. Suruwali, izaar
vyote ni Motoni.
135
190) Tawassul Ni ´Ibaadah?
Swali:
Tulisoma katika darsa iliopita kwamba kutawassul kwa maiti ni aina mbili.
Moja wapo mtu akitawassul bila ya kumfanyia ´ibaadah yoyote ni bid´ah,
kwani vipi tawassul sio ´ibaadah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Tawassul ni kuomba du´aa kutoka kwa maiti. Ikiwa hakumfanyia
aina yoyote ya ´ibaadah ni bid´ah na njia inayopelekea katika shirki.
191) Kulisha Watu Watano Mara Mbili Ili Ihesabike Kalipa Kafara Ya
Yamini Kwa Watu Kumi
Swali:
Mtu akiwa na deni la kafara ya yamini na akapata masikini watano, je
anawajibika kuwalisha mara mbili ili ihesabike kama kawalisha watu kumi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Hata ungelisha watu tano mara elfu, hukulisha ila watu watano na
kunabaki juu yako kulisha watu watano wengine.
136
192) Aliyeuawa Na Usaamah Bin Zayd Ni Katika Maswahaba?
Swali:
Yule mtu aliyeuawa na Usaamah bin Zayd (radhiya Allaahu ´anhu) je, mtu
anaweza kusema ni katika Maswahaba wakamtakia radhi kwa kuwa kafa
baada ya kusema Laa ilaaha illa Allaah moja kwa moja?
´Allaamah al-Fawzaan:
Achana nalo, mtu huyu hakukutana na Mtume ( 9 و$�م��3 % �+ ). Swahaba ni
mtu ambaye alikutana na Mtume ( �+9�� % 3 akamuamini. Alikutana ( و$�م
naye akamuamini na akafa kwa hilo kwa sharti hizi. Ama aliekutana naye
ilihali si muumini huyu si katika Maswahaba. Abu Jahl alikutana nae na Abu
Lahab wala hawakuwa katika Maswahaba. Aliekutana nae akamuamini. Kwa
sharti hizi. Ama aliyemuamini na hakukutana naye si Swahaba kwa kuwa
hakukutana na Mtume ( 9 و$�م��3 % �+ ). Hata kama ni muumini. an-Najaashiy
(rahimahu Allaah) alimuamini Mtume lakini hakukutana nae na haihesabiki
ni mmoja katika Maswahaba bali ni Taabi´iyn. [Sharti ya pili] akafa juu ya
imani yake. Ama aliyekutana na Mtume ( 9�� % 3�+ و$�م ) akamuamini kisha
akaritadi, huyu si katika Maswahaba.
193) Kaweka Nadhiri Kuamka Kuswali Fajr La Sivyo Ataswali Rakaa Kumi
Swali:
137
Kuna mtu kalala usiku na akaweka nadhiri kabla ya kulala ikiwa hatoamka
swalaat-ul-Fajr ataswali rakaa kumi siku hio hio, hakuamka na akasahau
kutekeleza nadhiri yake, kumeshapita mwezi au zaidi. Anawajibika nini?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni juu yake kulipa kafara ya yamini. Kwa kuwa hakukusudia kujikurubisha
kwa Allaah kwa kuweka nadhiri hii, alichokusudia ilikuwa ni kuamka
mwenyewe. Alipe kafara ya yamini.
194) Kufunga Safari Kwenda Kwenye Kaburi Ya Mtume Au Mwengine
Yoyote
Swali:
Wanatumia hoja wale wanaofunga safari kuzuru kaburi ya Mtume ( 9�� % 3�+
?ni kama wale wanaofunga safari kwenda kutafuta elimu, vipi tujibie hili ( و$�م
´Allaamah al-Fawzaan:
Kufunga safari kwenda kutafuta elimu hili lakubalika.
�ن ��و6 ��ر �ن ��م طN�(R �7�!����وا �� ا�د7 7� N&�ل7 �ر
“Lakini kwanini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao,
wakajifunze vyema Diyn.” (09:122)
138
Kufunga safari kwenda kwenye kaburi ya Mtume si kutafuta elimu. Ni njia
inayopelekea katika shirki. Kuna tofauti baina ya kufunga safari kwenda
kwenye kaburi ya Mtume au nyingine yoyote na baina ya kufunga safari
kwenda kutafuta elimu.
195) Kila Jina La Allaah Linajenga Sifa Kinyume Na Matendo
Swali:
Je mtu anaweza kuchukua Majina ya Allaah (´Azza wa Jalla) ni katika
matendo Yake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana! Kila Jina Lake linajenga Sifa ama matendo Yake hayachukuliwi Jina.
Usichukue Jina katika matendo Yake. Kwa mfano "Kaandika Allaah", je
utasema kuwa Allaah ni "Mwandishi"? Ukamwita "Mwandishi"? Hapana, si
kila kitendo [Chake] huchukuliwa Jina wala Sifa.
����ن ��"N� % 3� ا�ظ�
“Laana ya Allaah iwapate walio dhulumu.” (07:44)
Je waweza kusema Allaah Anaitwa "Mwenye kulaani"? Hapana.
139
196) Hukumu Ya Swalah Ambayo Wudhuu Haukushika Kidogo Cha
Mguuni
Swali:
Kuna mtu mmoja kidole mguuni kilikuwa hakipati maji, na alifanya siku tatu
alikuwa akitawadha bila ya kuosha kidogo hichi kwa ujinga, je ana nini juu
yake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni juu yake kurudi kuziswali kwa kuwa sehemu katika mwili haikupata maji,
ina maana arudi kutawadha na arudi kuswali. Mtume ( 9 و$�م��3 % �+ )
alimuona mtu katika mguu wake kuliku sehemu ndogo imekosa maji,
akamuamrisha kurudi.
197) Aliopigana Nao Abu Bakr (radhiya Allaahu ´anhu) Ilikuwa Ni Kwa
Ajili Ya Kufuru Yao
Swali:
Je yaweza kufahamika kwa Abu Bakr asw-Swiddiyq (radhiya Allaahu ‘anhu)
kwa waliokataa kutoa zakaah kuwa aliwakufurisha na aliwaua kwa kufuru
yao?
140
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, walisema hatutokupa ila Mtume tu Mtume wa Allaah ( 9 و$�م��3 % �+ ),
ina maana walipinga. Na Mwenye kupinga kutoa zakaah anakufuru. Ama
mwenye kukataa kwa ubakhili, huyu alazimishwe kutoa hata ikiwa ni kwa
kutumia nguvu.
198) Kazi Ya Kuamrisha Mema Na Kukataza Mabaya Ni Ya Nani?
Swali:
Kuna ambao wanasema kuwa kuamrisha mema na kukataza mabaya ni kazi
khasa ya wanaume [wanachuoni] wa al-Lajnah [ad-Daa´imah] na hairuhusiwi
kwa wengine, je kauli hii ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kuamrisha mwema na kukataza kwa kutumia nguvu ni khasa kwa wanaume
wa al-Lajnah. Ama kukataza kwa ulimi na kubainisha na kutoa nasaha na
kuwafikishia wasimamizi hili ni wajibu kwa kila mmoja awezae.
"Mwenye kuona munkari auondoshe kwa mkono wake."
"... na akiwa hawezi basi afanye hivyo kwa ulimi wake; na akiwa hawezi basi
afanye kwa moyo wake na huo ni udhaifu wa Imani." [Muslim]
Ni lazima kuondosha munkari hata ikiwa ni kwa moyo, lazima kuuondosha
munkari hata ikiwa ni kwa moyo ktiu cha mwisho.
141
199) Mtazamo Wa Kwanza Kuiangalia Ka´abah Mtu Hukubaliwa Du´aa?
Swali:
Je imethibiti mtazamo wa kwanza kuiangalia al-Ka´abah, hukubaliwa du´aa
[ya mwenye kuomba]?
´Allaamah al-Fawzaan:
Sijui kitu kuhusiana na hili.
200) Hukumu Ya Kuapa Kwa Ahadi Ya Allaah
Swali:
Ipi hukumu ya kuapa kwa kusema: "[Naapa] kwa ahadi ya Allaah"?
´Allaamah al-Fawzaan:
Halina asli hili. Mtu anaruhusiwa kuapa kwa Jina la Allaah au Sifa miongoni
mwa Sifa Zake.
Swali La Pili:
142
Vipi pia kuapa kwa kusema "Naapa kwa dini"?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hakuna kuapa kwa dini, wala amaanah nk. "Mwenye kuapa aape kwa Allaah
au anyamaze."
201) Kuchinja Kwa Ajili Ya Allaah Kwenye Kaburi La Walii Fulani
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kuchinja kwa ajili ya Allaah kwenye kaburi la walii
miongoni mwa mawalii kwa kuamini baraka ya sehemu hio?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hii ni njia inayopelekea kunako shirki. Hii ni bid´ah. Kwa kuwa sehemu hii si
sehemu ya kuchinja. Na ni njia inayopeleka katika shirki.
202) Kuchukua Mkopo Benki Kwa Ajili Ya Kuoa
143
Swali:
Ipi hukumu ya kuchukua sehemu [mkopo] katika benki kwa ajili ya kuoa au
kwa ajili ya kununua gari?
´Allaamah al-Fawzaan:
Unaweza kuchua maadamu ni mubaha [mkopo] hauna ribaa, chukua.
Wakikupa bila ya faida na bila ya kitu - sehemu nzuri, hakuna ubaya sawa
ikiwa kwa ajili ya kuoa au mengine. Ama kuchukua sehemu na faida juu hii
ni ribaa, haijuzu. Sawa ikiwa kwa ajili ya kuoa wala mengine.
203) Kufanya Mzaha (Maskhara) Na Hadiyth Za Mtume
Swali:
Ipi hukumu kwa mwenye kufanya mzaha na Hadiyth kisha anasema mwisho
wake "Hadiyth imepokelewa na Muslim." Anakusudia mzaha na hoja yake
anasema...
´Allaamah al-Fawzaan:
A´udhubi Allaah - tunamuomba Allaah kinga. Kasema Mtume ( 9 و$�م��3 % �+
): "Ataenisemea uongo kwa kukusudia, ajiandalie sehemu Motoni."Haijuzu
144
mzaha kwa Hadiyth, Qur-aan au mengine ya dini. Haijuzu mzaha kwa haya.
Hii ni tabia ya wanafiki.
204) Ruqyah Kwenye Maji Ya Zamzam Na Mti Wa Mzaituni
Swali:
Ipi hukumu ya kusoma Qur-aan kwenye maji ya zamzam au mti wa mzaituni,
jambo hili lina asli?
´Allaamah al-Fawzaan:
Maji ya zamzam ni maji yenye baraka. Ikikusanyika ruqyah na maji ya
zamzam yenye baraka kunatarajiwa ponyo kwa idhini ya Allaah. Na mti wa
mzaituni pia ni mzuri. Mtu akitaka kufanya ruqyah kwa kuutimia baraka
inazidi kwa idhini ya Allaah (´Azza wa Jalla).
205) Tofauti Ya Kufuru Na Shirki
Swali:
Ipi tofauti kati ya kufuru na shirki? Na je kila kufuru ni shirki?
´Allaamah al-Fawzaan:
145
Kufuru ni jumla. Mtu anaweza kuwa kafiri kwa kupinga kuwepo kwa Allaah,
mulhid. Hamuamini Allaah. Ama mshirikina yeye anaamini kuwepo kwa
Allaah. Anakubali Tawhiyd Rubuubiyyah lakini anamshirikisha Allaah katika
Tawhiyd Uluuhiyyah. Ama kafiri yeye haamini si hili wala hili.
206) Kufanya Mjadala Na Ahl-ul-Bid´ah
Swali:
Je ni katika njia ya Salaf na uongofu wao kufanya mjadala na Ahl-ul-Bid´ah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa mtu yuko na elimu na uwezo, bila shaka hii ni njia ya kufikisha haki na
kuiangamiza batili. Na haki haiwezi kuenezwa ila kwa njia hio. Lakini awe ni
mtu mwenye uwezo - uwezo wa elimu na kujua kujadili.
207) Kuacha Nyumba Inasoma Qur-aan Na Hakuna Wakuisikiliza
Swali:
Vipi kwa mwenye kuiacha Qur-aan inasoma wakati wa safari yake ili
aihifadhi nyumba?
146
´Allaamah al-Fawzaan:
Isitumiwe Qur-aan namna hii. Aweke mlinzi nyumbani au afunge milango
vizuri nakadhalika. Ama kuiacha Qur-aan inasoma kwa ajili ya ulinzi, hii ni
katika kuiweka Qur-aan mtihanini.
208) Waitao “Ewe Yuma” Wanaposhtuliwa Na Kitu
Swali:
Ni jambo limeenea kwenye ndimi nyingi za watu, wakifikwa na jambo lenye
kushtua wanaita na kusema "Ee mama au yuma!" na wala hawakusidii hilo. Je
hili ni katika shirki?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hakuna mkubwa asemae hivi, hakuna anaesema hivi ila mtoto. Si dhani kama
kuna mkubwa asemae "Ee Yuma!"
209) Haijuzu Kuwanunulia Wanawake Simu Za Khatari Za Kisasa
Swali:
147
Nimruhusu mke wangu kushiriki na kaka zake kununua simu ya kaka yao
anaesoma darsa la pili, simu iitwayo blackberry. Je nimruhusu hilo na
kutumia simu hii?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, simu ambayo ni khatari kwa mtu isinunuliwe. Mtu anunue simu ya
maongezi tu, isiwe na ya zaidi ya kuongea. Simu zenye vitu vya haramu na
vitu vya khatari haijuzu kuziuza wala kuzinunua.
210) Ni Haramu Kumpa Mwanamke Mwanamke Ajinabi
Swali:
Ipi hukumu ya kumpa mkono mwanamke ajinabi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haijuzu kumpa mkono mwanamke ambae si mahram. Mtume ( 9 و$�م��3 % �+
) hakuwahi kumpa mkono wake katu mwanamke yeyote ambae si halali
kwake, bali alikuwa akiwabaay´ wanawake kwa maneno. Haijuzu kumgusa
au kumpa mkono mwanamke yeyote. Isipokuwa tu katika mahram zake.
211) Kumpigia Simu Aliehai Na Kumuomba Akuombea Du´aa
148
Swali:
Inajuzu kumuomba aliehai akuombee du´aa ambae yuko nje ya mji nikimpigia
simu na kumuomba du´aa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hakuna ubaya wa hilo kwa kuwa ukimpigia simu sio [kama kumuomba]
ghayb [jambo ambalo ni shirki].
212) Kuomba Rahma Na Kinga Ndani Ya Swalah
Swali:
Imaam akisoma Aayah yenye istighfaar, tasbiyh au takbiyr. Maamuma
anaweza akakabir, kuomba istighfaar au kusabihi?
´Allaamah al-Fawzaa:
Jambo lililothibiti ni kuwa Mtume ( % 3�+ 9 و$�م�� ) - tena ilikuwa ni katika
swalah ya usiku. Akifika katika Aayah ya Rahma, anamuomba Allaah
Amrehemu. Na akifika katika Aayah ya adhabu anamuomba Allaah kinga.
Hili ndo lililothibiti kwa Mtume ( 9 و$�م��3 % �+ ). Tunatosheka na haya.
149
213) Kauli Sahihi Kuhusiana Na Thawabu Kumfikia Maiti
Swali:
Ipi kauli yenye nguvu katika masuala ya kumtumia thawabu maiti? Kuna
wanaosema inajuzu kumtumia thawabu aina yoyote ya ´ibaadah, na kuna
wanaoiwekea mpaka kwa yale yenye dalili tu katika ´ibaadah. Kauli yenye
nguvu katika hili?
´Allaamah al-Fawzaan:
Sema kauli sahihi hapana kauli yenye nguvu. Kauli sahihi ni kuwa amali za
Muislamu ni zake mwenyewe tu, ispokuwa yale ambayo shari´ah imeruhusu
katika kumuombea du´aa, swadaqah ya kuendelea aliofanya au mtoto
anaemuombea baada ya kufa kwake. Du´aa yake [zao watoto] humfikia,
swadaqah wamtoleayo. Alipomuuliza mwanamke [Mtume], na alipomuuliza
Sa´ad bin ´Ubayd kumtolea swadaqah mama yake maiti. Kauli ya Allaah
(Ta´ala):
�$�ن إ�6 �� $"3 T� وأن ���س
“Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe?” (53:39)
Yanabagua [tenga] yaliokuja katika dalili tu. Na waliobaki thawabu zao
hazimfikii maiti, kwa kuwa ni matendo ya mtu mwenyewe.
214) Haijuzu Kuomba Kwa Uso Wa Allaah Mambo Ya Kidunia
150
Swali:
Ipi hukumu kwa mwenye kuomba kwa Uso wa Allaah na anasema
"nakuomba kwa Uso wa Allaah ufanye hivi na hivi."?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haijuzu hili kabisa. Hadiyth "Hakuombwi kwa Uso wa Allaah isipokuwa
Pepo tu." Wala hakuombwi kwa Uso wa Allaah mambo ya kidunia.
Hakuombwi kwa Uso wa Allaah ispokuwa Pepo au yanayomfikisha mtu
Peponi. Wala mtu haombwi mambo ya kidunia.
215) Kumwambia Mtu Unaefanya Kazi Kwake “Bwana Wangu”
Swali:
Ikiwa nafanya kazi kwa mtu na nikamwambia "Ewe bwana wangu!". Hili
linajuzu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa ni bwana wako hakuna neno. Wewe ni mtumwa wake? Ikiwa
anakumiliki waweza kusema "Ewe bwana wangu!".
151
216) Kuosha Mikono Mtu Anapoamka Kutoka Usingizini
Swali:
Kuosha mikono miwili kwa mwenye kuamka kutoka katika usingizi wa usiku
ni khasa wakati mtu anataka kutia wudhuu tu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Hata wakati wa kula, kunywa nk. Lakini imewekewa nguvu wakati
wa kutia wudhuu.
217) Kutokataza Shirki Kwa Kukithiri Kwa Jambo Lile Kwa Watu
Swali:
Yule mwenye kusikia matamshi ya shirki kama kuapia kwa asiyekuwa Allaah
na asikataze jambo hilo kutokana na kukithiri kwa jambo hili, atakuwa mtu
huyu ni katika wale wenye kuificha elimu [waliolaaniwa na Allaah]?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kila afichae kitu katika wanayohitajia watu katike elimu basi ni mfichaji. Na
hili linatofautiana itategemea kaficha nini. Ila tu ikiwa hawezi, ikiwa hawezi
hilo atakuwa ni mwenye kupewa udhuru.
152
218) Nikiona mtu mwenye kumshirikisha Allaah na nisimbainishie
Swali:
Nikiona mtu mwenye kumshirikisha Allaah na nisimbainishie kuwa
akifanyacho ni shirki, kwa kuwa katika mji wetu mwenye kufanya hivyo
anahukumiwa na serikali inayohukumu katika mji wetu nayo ni ya serikali ya
kinaswara. Ipi hukumu ya kunyamazia hili?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kubainisha kuna daraja nyingi. Mbainishie baina yako wewe na yeye,
mbainishe siri, mpe nasaha siri kadiri na uwezavyo kwa kutumia njia
uwezazo. Serikali inaweza kuwa haikatazi ila jambo lililo dhahiri tu, ama
mambo yakujificha serikali haiyajui. Wewe fanya uwezavyo.
219) Kumsalia Mtume (´alayhis-Salaam) Ni Katika Sababu Za Kukubaliwa
Du´aa
Swali:
Je ni sahihi kuwa mtu akimuomba Allaah na asimalizie du´aa yake kwa
kumsalia Mtume ( 9 و$�م��3 % �+ ) kwamba du´aa yake haikubaliwi wala
kupandishwa?
153
´Allaamah al-Fawzaan:
Imethibiti kuwa du´aa yake huzuiwa mpaka amsalie Mtume ( 9 و$�م��3 % �+ ).
Kwa kuwa kumsalia Mtume ni miongoni mwa sababu za kujibiwa [du´aa].
220) Kutawassul Kwa Allaah Kwa Kukusanyika Msikitini Na Kufanya
Dhikr
Swali:
Tukikubaliana katika mji wetu kukusanyika watu msikitini siku ya Ijumaa na
kusoma Qur-aan na kumuomba Allaah Atuteremshie mvua kwa hoja ya
kutawassul kwa Allaah kwa matendo mema walioyafanya, je kitendo hichi
kinajuzu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, hii ni bid´ah. Wanakusanyika na kusoma Qur-aan kwa ajili ya
kuomba mvua hili ni jambo la bid´ah. Kilichothibiti ni kuwa wanaswali
swalah ya istisqaa na imaam anakhutubu baada ya swalah na anaomba du´aa.
Kama alivyokuwa Mtume ( 9 و$�م��3 % �+ ) akifanya. Haikuthibiti kuwa
[watu] walikuwa wanakusanyika wanasoma Qur-aan kisha wanamuomba
Allaah mvua. Haikuthibiti.
221) Kutenga Siku Maalumu Kwa Ajili Ya Taazia
154
Swali:
Ipi hukumu ya kutenga siku khasa kwa ajili ya kutoa pole [kwa wafiwa]?
Kama kukusanyika watu kwenye nyumba hivi na kukaletwa vyakula na
vinywaji hapo?’
´Allaamah al-Fawzaan:
Hakuna dalili ya hilo. Bali hili ni jambo limezushwa na lina kujikalifisha na
kupoteza wakati na kupoteza mali na watu kukosa kufanya kazi. Mambo yote
haya hayajuzu. Watoa pole wasiwe ni wenye kukaa [hapo wakakusanyika],
unapokutana na ndugu yako [mfiwa] unampa pole au unaweza kumpigia
simu. Hakuna cha kujikalifisha.
222) Tofauti Ya Kusimama Kwa Kumuadhimisha Mtu Na Kumpokea Mgeni
Swali:
Wamezowea watu kumsimamia mgeni wakati wa kumpokea, ipi hukumu ya
kusimama kwa kuzingatia ya kwamba Mtume ( 9�� % 3�+ و$�م ) alikataza hilo
na alikuwa analichukia. Na je ni katika kumpandisha mtu?
´Allaamah al-Fawzaan:
155
Ewe ndugu yangu si hivyo. Kusimama kumsalimia na kumpokea mgeni
hakuna ubaya. Mtume ( 9 و$�م��3 % �+ ) aliwaambia Answaar "Simameni kwa
ajili ya bwana wenu", yaani Sa´ad bin Mu´aadh. Kumpokea mgeni na
kumsalimia hakuna ubaya. Alichokataza Mtume ni kusimama kwa ajili yake
nawe umekaa. Mtu anakuwa katika hali ya kukaa na watu wakamsimamia.
Hili halijuzu. Hivi ndivyo alivyokuwa akifanya Faaris wa Rome. Isipokuwa tu
ikiwa anahitajia ulinzi, ikiwa mtawala anahitajia ulinzi hakuna neno. Ama
kumsimamia yeye kwa ajili ya kumuadhimisha hili halijuzu.
223) Haijuzu Kuleta Adhkaar Maalumu Baada Ya Swalah Ambazo
Hazikuthibiti
Swali:
Inajuzu baada ya kumaliza kusoma adkhaar za swalah maarufu, je inajuzu
kuleta dhikr maalumu? Kama kuleta istighfaar mara mia na akadumu kwa
kufanya hivyo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni juu yako ewe ndugu yangu kurejea kunako adhkaar zilizothibiti katika
usahihi wake na idadi yake. Fanya hizo.
224) Hakuna Haja Ya Kuchukua Elimu Kwa Mtu Mwenye Baadhi Ya Bid´ah
Swali:
156
Ipi hukumu ya kuchukua elimu kwa mtu ambae ana baadhi ya bid´ah katika
matendo, amali na si katika ´Aqiydah? Inajuzu kusoma katika mikono yake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ewe ndugu maulamaa - Alhamdulillaah ni wengi. Na huna haja ya mtu wa
bid´ah ukachukua elimu kwake. Haijuzu kukaa na mtu wa bid´ah, vipi
kuchukua elimu kwake?!
225) Kuswali Nyuma Ya Imaam Anaevaa Herizi
Swali:
Je mtu mwenye kuandika katika karatasi suurah miongoni mwa suurah za
Qur-aan au Aayah na akajitundikia nayo na akategemea Aayah hii kuwa
inazuia madhara. Je inajuzu kuswali nyuma yake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Abainishiwe kuwa hili halijuzu. Hii ni herizi. Haijuzu kwake hili. Anasihiwe.
Ikiwa hatoivua, ikiwa wako na uwezo kubadilisha na kuweka imaam
mwengine, ni wajibu kwao kufanya hivyo.
157
226) Kunyunyizia Maji Ya Kisomo Kwenye Kuta Za Nyumbani Kuzuia
Madhara
Swali:
Je imethibiti kwa Mtume ( % 3�+9 و$�م�� ) kunyunyizia nguzo na kuta za
nyumbani kwa maji alioyasomea ili azuie kupatwa na kijicho na uchawi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kamwe! Hili halijuzu. Kunyunyizia kuta za nyumbani kwa Ruqyah. Baadhi ya
wengine wananyunyizia kwa [... sikufahamu neno alotumia Shaykh]. Yote
haya ni ukhurafi. Allaah Hakuteremsha chochote kuhusiana na hayo.
227) Kuswali Na Nguo Yenye Damu
Swali:
Ipi hukumu ya kuswali na nguo yenye damu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Aoshe damu na aiondoshe na mashaka. Aoshe kabla ya swalah. Na akiswali
nayo kwa kusahau au hakuona swalah yake ni sahihi, lakini baadae aioshe.
158
Swali La Pili:
Anauliza tena, ikiwa ataiosha lakini rangi bado imebaki. Hilo laathiri?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haliathiri. Akiiosha na... akishindwa kuondosha rangi haliathiri. Na kwa hili
Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomuamrisha mwanamke
kuosha damu ya hedhi kwenye nguo, akamwambia "wala haidhuru athari
yake."
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroos?tid_1=252
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, na Aali zake na
Maswahaba wake (Radhiya Allaahu ´anhum) na watakaowafuata kwa
wema mpaka hiyo siku ya Qiyaamah.