fataawa za sharh-us-sunnah ya barbahaariy - ´allaamah al-fawzaan
DESCRIPTION
Fataawa Za Sharh-Us-Sunnah Ya Barbahaariy - ´Allaamah al-FawzaanTRANSCRIPT
1
Mkusanyiko Wa Fataawa Za
Sharh-us-Sunnah Lil-Barbahaariy
Abu Muhammad bin ´Aliy bin
Khalaf al-Barbahaariy
´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
©
2
Dibaji
Bismillaah, Alhamdulillaah. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu
Muhammad na ahli zake na Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum
ajma´iyn) mpaka siku ya mwisho. Amma ba´ad:
Himidi zote ni Zake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Aliyeniwezesha
kukusanya Fataawa hizi. Hizi ni Fataawa zilizokusanywa baada ya Duruus
zote alizotoa Shaykh al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) akisherehesha kitabu
cha Imaam al-Barbahaariy (Rahimahullaah) mmoja wa wanachuoni wakubwa
maarufu, kitabu ni cha ´Aqiydah kinaitwa “Sharh-us-Sunnah Lil
Barbahaariy.”
Fataawa nyingi ni kuhusiana na masuala ya ´Aqiydah kwani kitabu chenyewe
ni cha ´Aqiydah. Kuna baadhi ya Fataawa pia kuhusiana na ´Aqiydah na
masuala ya Fiqh na mengineyo ila si nyingi.
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kijitabu hichi kilichokusanya
Fataawa muhimu ziweze kutunufaisha sisi na nyinyi na kuleta faida kubwa
katika Ummah wetu wa Kiislamu. Tunamuomba Allaah Atuwafikishe sote
kwa Ayapendayo na Kuyaridhia.
Tanbihi: Fataawa zote hizi tumezifasiri kwa njia ya Video na zinapatikana
Youtube waweza kusoma na huku wasikiliza. Kwa mwenye kutaka hizo
Fataawa za Video aende Alhidaaya au Youtube kwa juu sehemu ya kutafuta
aandike au kukopi kichwa cha habari cha Fatwa (kama ilivyo hapo chini kwa
kila Fatwa ina kichwa chake cha habari) na atafute itajitokeza In Shaa Allaah.
Jazaakumu Allaahu Khayra
Swalla Allaahu ´alaa Muhammad, wa ´alaa aalihi wa Aswhaabihi wa sallam.
3
Fataawa zilizomo: 1. Masuala Ya ´Amali Ni Katika Imani Yana Khilafu? 2. Tofauti Ya ´Arshi Na Kursiyy 3. Aadam (´alayhis-Salaam) Ni Mtume Au Nabii? 4. Kafanya Zinaa Na Aliwahi Kuoa, Apigwe Mawe Au Fimbo? 5. Mwenye Kusema Ya Kwamba Aadam Alifanya Makosa Mawili 6. Suufiyyah Wanaochukulia Anashiyd Ni Kumdhukuru Allaah 7. Bid´ah Ya Kilugha 8. Dalili Ipi Ya Kwamba Maneno Ya Allaah Ni Kwa Herufi Na Sauti? 9. Du´aa Na Kuunga Udugu Kunarudisha Qadar? 10. Fitina Ya Shubuha Na Fitina Ya Kufuata Matamanio 11. Msingi Wa ´Aqiydah Ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah Kwa Maswahabah 12. Hadiyth "Allaah Kamuumba Aadam Kwa Sura Yake" 13. Ni Watu Gani Hawa? 14. Si Sharti Kwa Mlinganiaji Awe Hana Makosa 15. Hukumu Ya Aliyekufa Kabla Ya Kuja Mtume Muhammad (´alayhis-Salaam) 16. Hukumu Ya Kufa Na Mtu Hakumpa Mkono Wa Utiifu Kiongozi Wa Kiislamu 17. Kutamani Mtu Laiti Angelikuwa Pamoja Na Maswahabah 18. Hukumu Ya Mtu Ambaye Anategemea Qur-aan Tu Na Kupinga Sunnah 19. Mwenye Kumtukana Abu Bakr, ´Umar Na´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhum) 20. Hukumu Ya Wendawazimu Aakhirah 21. Ibaadhi (Maibaadhi) Wasemao Kuwa Qur-aan Imeumbwa 22. Watu Wanaotahadharisha Madhehebu Ya Salaf 23. Baadhi Ya Fadhila Za Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anhu) 24. Imani Kwa Mujibu Wa Jahmiyyah 25. Imani Ya Kwamba Qur-aan Imeumbwa Ni Ukafiri 26. Jahmiyyah Wapo Leo? 27. Nani Kasema Kwamba Kutofautiana Ni Rahmah? 28. Kusoma Elimu Ya Falsafa, Mantiki, Na Mfano Wa Hizo 29. Mtume Na Imaam Ahmad Kumuona Allaah Usingizi 30. Kwenda Kaburini Kumzuru Maiti Wako Ila Hujui Mahali Alipo 31. Kafiri Akinipa Salaam Kamili, Je Nami Nimpe Kamili? 32. Madu´aat Wanaodai Wanalingania Katika Haki Za Mwanamke 33. Kuwalea Watoto Kwa Filamu Za Katuni 34. Kauli Inayosema Jahannam (Moto) Utaisha 35. Kazi Hii Ni Maalum Kwa Wanachuoni 36. Kipi Kilichoumbwa Kabla, ´Arshi Au Kalamu? 37. Shaykh Fawzaan Kuhusu Kitabu Cha Ibn-ul-Qayyim "ar-Ruuh" 38. Kuashiria Kwa Mkono Wakati Wa Kutaja Sifa Za Allaah (´Azza wa Jalla) 39. Kuchukua Elimu Kwa Watu Wanaokhalifu Manhaj Ya Salaf 40. Kuwa Na Nia Nzuri Haitakasi Kosa La Mtu 41. Maulidi Yana Bid´ah Na Shirki 42. Mwenye Kuifanyia Mzaha Sunnah Ya Mtume (´alayhis-Salaam) Ni Kafiri 43. Kumfuata Mwanachuoni Katika Kitu Kipya Cha Fiqh 44. Kumkufurisha Mshirikina Kwa Kitendo Chake Cha Dhahiri 45. Kukataza Uovu Kwa Kumpa Mtu Mkanda 46. Mume Anaweza Kumrejea Mke Wake Bila Ya Mashahidi? 47. Kufuru Ndogo Ya Kumwingilia Mke Kwa Nyuma 48. Kumvalisha Hijaab Binti Wa Miaka Saba
4 49. Inajuzu Kunyoa Kipara? 50. Inajuzu Kuoa Wasichana Wa Nje Ya Ndoa? 51. Kuomba "Ee Allaah Usinikadirie Kadha Na Kadha" 52. Kwanini Ahl-us-Sunnah Wanawakufurisha Jahmiyyah? 53. Ni Kweli Watu Wa Makaburini Hutembeleana Kila Siku Ya Ijumaa? 54. Watoto Wa Shaykh Katika Kitabu "ad-Durur as-Sania" 55. Makafiri Wanaposilimu Watoto Wao Huzingatiwa Kuwa Ni Wa Zinaa? 56. Dalili Ya Mafungu Matatu Ya Tawhiyd Katika Qur-aan 57. Watu Wa Mantiki, Wanafalsafa Na Wanatheolojia 58. Wanaosema Watawala Ni Ma´ulamaa Na Sio Viongozi Waasi Na Madhalimu 59. Tafsiri Ya Neno "adh-Dhikra", Katika Suurat 16; Aayah Ya 44 60. Radd Kwa Mwenye Kutatiza Watu Na Kitabu Na "Sharh as-Sunnah” Cha al-Barbahaariy 61. Bid´ah Zinazoenezwa Na Kuchukua Elimu Kwa Njia Ya Simu 62. Mtu Yuko Huru Katika Uislamu Katika Mipaka Ya Kishari´ah 63. Sifa Ya Kundi Lililookoka 64. Ahl-ul-Takfiyr Ni Katika Ahl-ul-Bid´ah Wabaya Zaidi 65. Kuwatakia Swalah Na Salaam Kwa Wasiokuwa Mitume 66. Kumuuliza Muislamu Katika Mji Wa Kiislamu "Wewe Ni Muumini"? 67. Kumkuta Imamu Katika Takbiyrah Ya Tatu Katika Swalah Ya Janaza 68. Mwanaume Kuswali Na Suruwali 69. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) Waliwahi Kumuona Masiyh ad-Dajjaal? 70. Mtu Akimuona Allaah Usingizini Kamuona Kweli? 71. Je, Sunnah Inaweza Kufuta Qur-aan? 72. Sisi Tunalingania Katika Umoja Wa Waislamu 73. Kufuata Kauli Za Wanachuoni Kwa Matamanio 74. Kuna Tofauti Kati Ya Mashia Na Raafidhwah? 75. Kuoa Kwa Nia Ya Talaka Ni Kumhadaa Mwanamke 76. Salaf Walikuwa Hawajui ´Ilm-ul-Kalaam 77. Sababu Ya Khawaarij Kupigwa Vita 78. Roho Hukutana Na Kuongea Ndani Ya Kaburi? 80. Qur-aan Lazima Iendane Sambamba Na Sunnah 81. ´Adhaab Na Qiswaas 82. Nishikamane Na Jamaa´ah Ipi Katika Miji Ya Kikafiri? 83. Kisichokuwa Na Asli Katika Dini Ndio Bid´ah 84. Sababu 4 Za Kukufanya Upate Unyenyekevu Wakati Wa Kusoma Qur-aan 85. Waliopewa Mtihani Wa Kupenda Picha 86. Mtu Anamtii Mtawala Ambaye Yuko Chini Ya Uongozi Wake 87. Ninapoulizwa Swali Ilihali Najua Jibu, Naweza Kulijibia? 88. Lini Mji Unakuwa Wa Kiislamu Na WaKikafiri? 89. Nini Maana Ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah? 90. Ipi Dini Sahihi Kabla Ya Mtume (´alayhis-Salaam) Kuja Na Uislamu? 91. Hadiyth "Kutofautiana Kwa Ummah Wangu Ni Rahmah" Ni Dhaifu 92. Nani Bora Zaidi; "Mu´aawiyah" Au "´Umar bin ´Abdil-´Aziyz"? 93. Uwajibu Wa Msomi Kuthibitisha Sifa Za Allaah 94. Kumtanguliza ´Aliy Juu Ya ´Uthmaan Kwa Fadhila Au Uongozi 95. Ipi Hukumu Ya Mwenye Kusema Uhuru Ni Bora Kuliko Shari´ah? 96. Je, Kutukana Maswahabah Ni Kumtukana Mtume (´alayhis-Salaam)? 97. Mwenye Kumtukana Mtume (´alayhis-Salaam) Ana Tawbah? 98. Mtu Anayemponda Mu´aawiyah Na ´Amr bin ´Aasw 99. "Hatutegemi Sunnah, Qur-aan Yatosha" 100. Anayekufa Kwa Saratani Na Kuunguwa Kwa Moto, Wamekufa Mashahidi?
5 101. Anayeacha Swalah Akianza Ni Wajibu Kukoga Na Kutoa Shahaadah Upya? 102. Mwenye Deni Lake Kafa, Pesa Hizi Nizifanye Nini? 103. Kuacha Swalah Ya Witr Na Sunnah YaKabla Ya Fajr Daima 104. Mwanachuoni Kuwa Na Baadhi Ya Makosa Katika Masuala Ya ´Aqiydah 105. "al-Mustwafah" Ni Jina La Mtume(´alayhis-Salaam)? 106. Jahmiyyah Ndio Pote Baya Zaidi Katika Murji-ah 107. Inajuzu Kwangu Kuhudhuria Na Kusimamia Jeneza Na Mzazi Wangu Kafiri? 108. Mu´tazilah, Ashaa´irah Na Maaturidiyyah Ni Wanafunzi Wa Jahmiyyah 109. Mtume Ana Orodha Ya Majina Ya WatuWa Peponi Na Motoni? 110. Usiku Wa Mi´raaj, Mtume Alisikia Maneno Ya Allaah Moja Kwa Moja? 111. Msimamo Wa Imaam al-Bukhaariy Juu Ya Qur-aan 112. Wanaokufa Kwa Ajali Ya Ndege Hupatwa Na Maumivu Ya Kutokwa Na Roho? 113. Watu Wa Sasa Walioathirika Na Suufiyyah Na Qubuuriyyah 114. Chuo Kikuu Cha Mchanganyiko Wa Wanaume Na Wanawake 115. Majini Pia Watamuona Allaah Aakhirah Peponi? 116. Mwenye Kusema Mikono Miwili Ya Allaah Katika Qur-aan Ni Majaaz 117. Maiti Naweza Kumwambia Khabari Za Familia Yake? 118. Suufiyyah Ni Wajinga 119. Maana Ya "Hayaat al-Barzakhiyyah" 120. Tafsiri Ya Kauli Ya Allaah "Hapana Kulazimisha Katika Dini" 121. Mtu Kama Huyu Ndie Mwenye Udhuru 122. Kwanini Raafidhwah WanawatukanaMaswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) 123. Kuziwekea Hadiyth Sahihi Majaaz 124. Mwenye Kuwatukana Wake Wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) 125. Kuwasikiliza Wapiga Visa 126. Kuanza Kuwalingania Ma´ulamaa Wapotofu Ni Bora Zaidi Kuliko Kuanza Na `Awwaam Wao 127. Kuuliza Daraja Ya Hadiyth 128. Asiyemuombea Du´aa Mtawala Wa Waislamu Ni Mtu Wa Bid´ah 129. Kutoka Siku 40 Ni Katika Bid´ah Za Suufiyyah 130. Hadiyth Hii Inajuzisha Kutoka Na Jamaa´at-ut-Tabliygh? 131. Kwenda Na Jamaa´at-ut-Tabliygh KufanyaDa´wah Katika Miji Ya Makafiri 132. Nikiingia Nyumba Na Hakuna Mtu Nitoe Salaam? 133. Radd Kwa Madu´aat Wanaojuzisha Kutibu Uchawi Kwa Uchawi 134. Kuswali Nyuma Ya Qubuuriyyuun 135. Kusoma Siyrah Ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) 136. Kusikiliza Visa Vya Tofauti Za Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) 137. "Shikamaneni Na ´Atiyq, Na Tahadharini Na Mambo Ya Kuzua" 138. Kusema Neno "Sayyidna" Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anhu) Inajuzu? 139. Kushahidilia Swahabah Fulani Kuwa Peponi Pasina Ushahidi 140. Kusema Kuwa Pepo Au Moto Utaisha 141. Kusema Kafiri Fulani Kafa Katika Ukafiri Na Ni Wa Motoni 142. Kusema Fulani Kafa Shahidi 143. Ashaa´irah Ni Katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah? 144. Tunapenda Haki Zaidi Kuliko Fulani 145. Kuridhia Qadhwaa Na Qadar Ni Wajibu 146. Uwajibu Wa Kujirejea Unapokosea 147. Kuongea Ni Katika Sifa Ya Allaah Ya Kimatendo 148. Madu´aat Wasiolingania Katika Tawhiyd Wala Hawaonyi Dhidi Ya Mubtadi´ah Na Bid´ah
6
بسم اهلل الرحمن الرحيم 1. Masuala Ya ´Amali Ni Katika Imani Yana Khilafu?
Swali:
Imeenea katika mji wetu wanaosema ya kwamba yule mwenye kuacha ´amali
za mwili ni masuala yana khilafu baina ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Je,
kauli hii ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Muongo huyu. Hakuna khilafu baina ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ya
kwamba ´amali ni katika Imani. Wala haisihi Imani bila ya ´amali, kama jinsi
haisihi ´amali bila ya Imani. Ni mambo mawili yanayoenda sambamba. Hii
ndio kauli ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ya kwamba Imani ni:
"Kauli kwa ulimi, na kuamini moyoni na ´amali za mwili. Inazidi kwa utiifu
na kupungua kwa maasi."
Na lau ikikadiriwa ya kwamba kuna khilafu kwa baadhi ya Ahl-us-Sunnah,
ibra ni kwa yale yaliyosimama juu ya dalili na Jamhuri ya Ahl-us-Sunnah. Na
huchukuliwa hii ni kauli mbovu inayokhalifu isiyotegemewa.
2. Tofauti Ya ´Arshi Na Kursiyy
Swali:
Ipi tofauti kati ya ´Arshi na Kursiyy?
´Allaamah al-Fawzaan:
7
´Arshi sio Kursiyy. ´Arshi ndio kiumbe kilicho juu kabisa katika viumbe, na
ndio [kiumbe] kikubwa katika viumbe. Na Allaah (Subhaanahu) Kastawaa1
juu yake. Ama Kursiyy iko chini ya ´Arshi. Imethibiti katika Hadiyth ya
kwamba ndio mahali pa Miguu [ya Allaah]. Iko chini ya ´Arshi, na ni ndogo
kuliko ´Arshi na ni kubwa kuliko mbingu na ardhi.
3. Aadam (´alayhis-Salaam) Ni Mtume Au Nabii?
Swali:
Aadam alikuwa ni Nabii au Mtume?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni Nabii. Ni Nabii Aliyeongeleshwa kama ilivyo katika Hadiyth.
Aliongeleshwa na Allaah.
4. Kafanya Zinaa Na Aliwahi Kuoa, Apigwe Mawe Au Fimbo?
Swali:
Kuna mtu alioa kisha akataliki na hakuoa tena, kisha akaanguka kwa
mwanamke ambaye si Halali kwake. Katika hali hii, je apewe adhabu ya
kupigwa mawe?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Maadamu hilo limetokea baada ya kufanya ndoa sahihi, hata kama
[alioa] katika miaka ya mwanzoni na akazini katika [miaka] ya mwishoni,
apigwe mawe. Kwa kuwa katangulia kufanya ndoa iliyokuwa ya sahihi.
1 Kalingana sawa
8
5. Mwenye Kusema Ya Kwamba Aadam Alifanya Makosa Mawili
Swali:
Imethibiti katika baadhi ya Hadiyth ya kwamba Aadam (´alayhis-Salaam)
alifanya makosa mawili. Kosa la kwanza aliomba...
´Allaamah al-Fawzaan:
Ewe ndugu! Msimseme vibaya Aadam. Aadam ni Nabii katika Manabii wa
Allaah. Ni Nabii Aliyeongeleshwa. Isitoshe, ni baba yenu. Hata baba yenu
mwamsema hivyo? Acheni maneno kama haya.
6. Suufiyyah Wanaochukulia Anashiyd Ni Kumdhukuru Allaah
Swali:
Tumekusikia ukisema ya kwamba anayesikiliza Anashiyd2 za Kiislamu ni
katika Suufiyyah3 na ni katika Hawaa. Je, tutahadharishe kukaa na watu
wake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Wapi mmesikia maneno haya ya kwamba anayezisikiliza ni katika Suufiyyah?
Mimi sikumbuki kama nilisema hivyo. Lakini mimi nilisema hizi Anashid
ambazo wanaziita ni za Kiislamu, ni Anashiyd za Suufiyyah. Kwa kuwa
Suufiyyah wanachukulia ya kwamba Anashidy ni Dhikr liLlaah kumdhukuru
Allaah. Wanachukulia ni za Kiislamu. Kumdhukuru Allaah. Hivi ndio
nilisema. Ama kusema ya kwamba mwenye kuzisikiliza anakuwa Suufiy, si
sahihi. 2 Qaswiydah 3 Masufi
9
7. Bid´ah Ya Kilugha
Swali:
Ni yapi makusudio ya Bid´ah al-Lughawiyyah Bid´ah ya kilugha?
´Allaamah al-Fawzaan:
Bid´ah ya kilugha ni kwa mfano wa hii gari yako. Gari yako hii ni Bid´ah
lakini ni Bid´ah ya kilugha. Kwa kuwa ni kitu kipya ambacho hakikuwepo,
mwanzoni watu walikuwa wakipanda punda na mipando mingine. Kukaja
badala yavyo gari n.k. Hii ndio Bid´ah ya kilugha.
8. Dalili Ipi Ya Kwamba Maneno Ya Allaah Ni Kwa Herufi Na Sauti?
Swali:
Tunajua ya kwamba katika Itikadi ya Ahl-us-Sunnah ni kuwa Maneno ya
Allaah ni kwa herufi na sauti. Ipi dalili ya kwamba ni kwa herufi na kwa
sauti?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kwa kuwa ni Maneno yanayosikika na ni wito. "Akamnadi Mola Wake",
"Tukamnadi". Na wito lazima uwe kwa herufi na sauti.
9. Du´aa Na Kuunga Udugu Kunarudisha Qadar?
Swali:
10
Je Du´aa, na kuunga udugu na kuwatendea wema kunarudisha Qadar?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni sababu. Havirudishi Qadar, kwa kuwa Allaah Kakadiria ya kwamba
utaunga udugu. Ni Qadar. Kakadiria ya kwamba utaswali, utatoa Swadaaqah.
Ni katika Qadar ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
10. Fitina Ya Shubuha Na Fitina Ya Kufuata Matamanio
Swali:
Mtu ambaye katumbukia katika kitu katika maasi huzingatiwa ni katika Ahl-
ul-Ahwaa? Na ni ipi tofauti baina yake na baina ya Swaahib-ul-Hawaa
Mubtadi´?4
´Allaamah al-Fawzaan:
Sivyo hivyo. Sio kila mwenye kutumbukia katika maasi anakuwa ni katika
Ahl-ul-Ahwaa. Huyu ni katika Ahl-ul-Shahawaat5. Kwa kuwa fitina
imegawanyika sehemu mbili:
1. Fitina ya kufuata matamanio; kama Zinaa, kuiba, kunywa pombe na kula
Ribaa.
2. Na fitina ya shubuha - na Allaah Atukinge nayo. Hii ndio baya zaidi. Nayo
ni ile inayokuwa katika ´Aqiydah. Na hii ndio fitina ya Ahl-ul-Ahwaa. Fitina
ya Ahl-ul-Ahwaa inakuwa katika shubuha. Hii ndio baya zaidi.
11. Msingi Wa ´Aqiydah Ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah Kwa Maswahabah
4 Mtu wa Bid´ah 5 Wanaofuata mtamanio yao
11
Swali:
Yapi maoni yako kwa mwenye kusema:
"Yule ambaye alisimama katika fitina iliyotokea baina ya ´Aliy na Mu´aawiyah
(Radhiya Allaahu ´anhumaa) ni bora kuliko yule ambaye alishiriki katikafitina
hii."?
´Allaamah al-Fawzaan:
Sisi tuko na "Qaa´iydah" msingi, nao ni kwamba hatuingilii yaliyopitika baina
ya Maswahabah, na wala hatusemi kamwe yeyote katika wao alikosea.
Hatuingilii yaliyopitika baina yao. Bali tunawatakia radhi na kuwachukuliwa
ni katika karne bora. Huu ndio msingi na ni katika Usuul (msingi) wa
´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
12. Hadiyth "Allaah Kamuumba Aadam Kwa Sura Yake"
Swali:
Wamesema baadhi ya wanachuoni kuhusu Hadiyth:
"Kwa hakika Allaah Kamuumba Aadam kwa sura Yake."
Wakasema ya kwamba dhamiri inamrudilia Aadam. Je, ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hadiyth itakuwa na faida gani? Ikifasiriwa ya kwamba dhamiri inamrudilia
Aadam Hadiyth itakuwa haina faida.
"Kwa hakika Allaah Kamuumba Aadam kwa sura Yake."
Hili halina shaka. Hili ni jambo la kwanza. Jambo la pili ni kwamba, imekuja
katika Riwaayah nyingine inayofasiri hii:
12
"... kwa sura ya Ar-Rahmaan."
Namna hii. Wala isikutatize [Hadiyth] hii. Kwa kuwa baadhi ya watu
wameingiza akili zao ndani ya masuala haya. Allaah Hakukukalifisha hili.
Thibitisha yaliyokuja na kuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam), kama yalivyokuja. Ikiwa hukubainikiwa na kitu, tawaqqaf
(usiseme kitu) kwa hili na waulize wanachuoni. Ama kuyaingilia sana ndani,
haijuzu.
13. Ni Watu Gani Hawa?
Swali:
Imethiti katika Hadiyth ya kwamba kuna watu watakaozuiwa [kunywa]
katika hodhi, aseme Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Ni watu
wangu, ni watu wangu." Aambiwe: "Wewe hujui waliozusha baada yako." Ni
watu gani hawa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Watu hawa ni wale walioritadi na wanafiki waliodhihirisha Uislamu nao
wako juu ya unafiki.
14. Si Sharti Kwa Mlinganiaji Awe Hana Makosa
Swali:
Je, Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anaweza kujaalia Uongofu wa kuonesha na
kuelekeza kupitia mikono ya muumini mwenye Imani pungufu?
´Allaamah al-Fawzaan:
13
Ndio. Mwenye kulingania kwa Allaah anaongoza. Anaongoza kwa Allaah,
kwa maana ya kwamba anabainisha na kuelekeza. "Hidaayat ad-Dalaalah"
maana yake ni kwamba anabainisha na kuelekeza. Na hili hupitika kwa kila
mlinganiaji. Na wala si sharti kwa mlinganiaji awe mkamilifu, si sharti kwa
mlinganiaji awe mkamilifu asiwe na makosa. Yanayoshurutishwa kwake ni
yeye kuwa na Imani, elimu na ´Aqiydah sahihi na Manhaj safi hata kama
atakuwa na baadhi ya vijikosa khafifu.
15. Hukumu Ya Aliyekufa Kabla Ya Kuja Mtume Muhammad (´alayhis-Salaam)
Swali:
Aliyekufa kabla ya kutumwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Je,
ataitwa Muislamu au kafiri?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ataitwa ni katika Ahl-ul-Fatrah. Na hukumu yake ni kwa Allaah (Subhaanahu
wa Ta´ala).
16. Hukumu Ya Kufa Na Mtu Hakumpa Mkono Wa Utiifu Kiongozi Wa Kiislamu
Swali:
Kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa aliyekufa na
hakumpa mkono wa utiifu kiongozi(mtawala) yeyote ya kwamba kafa kifo
cha ki-Jaahiliyyah. Atakuwa kafanya dhambi kubwa katika madhambi
makubwa akawa ni Faasiq au katika katika Uislamu?
´Allaamah al-Fawzaan:
14
Atakuwa ni Faasiq. Na kafanya dhambi kubwa katika madhambi makubwa.
Lakini hatoki katika Uislam.
17. Kutamani Mtu Laiti Angelikuwa Pamoja Na Maswahabah
Swali:
Tunaposoma fadhila za Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), kupigana
kwao Jihaad na Zuhd yao na nguvu ya Imani yao tunasema "laiti tungelikuwa
nao au laiti tungelipigana Jihaad pamoja nao tukiwa na Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam)." Je, kauli hii ni sahihi na kutamani huku
kunajuzu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haifai kufanya hivi, haifai kwako kutamani ungekuwa nao. Kwa kuwa
waweza kuwa nao na ukakosa kustahamili, hujui huenda usingelistahamili.
Kuna watu hawakustahamili, walikuwa pamoja nao na hawakuweza
kustahamili, wakapoteana kufanya unafiki - Allaah Atukinge. Hujui.
Yatosheleza kwako wewe kuwapenda, kuwatakia radhi, kuwaombea
msamaha, uwafuate na utetee heshima zao. Haya yanatosheleza kwako katika
haki yao.
18. Hukumu Ya Mtu Ambaye Anategemea Qur-aan Tu Na Kupinga Sunnah
Swali:
Nilimuona mtu ambaye kwa uinje anaonekana ni mwema na kahifadhi Qur-
aan, na pindi nilipomueleza Sunnah na Hadiyth akanambia mimi ni mtu wa
Qur-aaniy na anategemea Aayah za Qur-aan tu. Je, huyu ni katika watu
waliopinda ambao hawategemi Sunnah?
15
´Allaamah al-Fawzaan:
Huyu ni baina ya mambo mawili, ima ni mjinga kapandikizwa fikra hizi
kutoka kwa wengine akidhani ya kwamba ni sahihi. Huyu anapewa udhuru
mpaka abainishiwe. Akiendelea anahukumiwa kuwa ni kafiri, kwa kuwa
anamkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Au kakusudia
kitu hichi, kakusudia kusema hivi na anajua ya kwamba ni upotofu na
kwamba ni makosa, huyu anakufuru bila ya shaka. Kwa kuwa kakusudia
kuziponda Hadiyth za Mtume na kumkadhibisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam).
19. Mwenye Kumtukana Abu Bakr, ´Umar Na´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhum)
Swali:
Mwenye kumtukana Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan (Radhiya Allaahu
´anhum) na kuwaponda na wala hakubali ukhalifa wao. Je, mtu anaweza
kusema ya kwamba ni Waislamu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Ikiwa anajua dalili ya hilo na akazikataa, huyu anakufuru. Ama
ikiwa anafuata kichwa mchunga au ni mjinga, huyu anapewa udhuru mpaka
abainishiwe haki. Akiendelea [baada ya kubainishiwa haki], anahukumiwa
kuwa ni kafiri.
20. Hukumu Ya Wendawazimu Aakhirah
Swali:
Hukumu ya wendawazimu siku ya Qiyaamah yaani mafikio yao?
16
´Allaamah al-Fawzaan:
Mafikio yao ni kwa Allaah ambaye Kawaumba. Mimi sijui.
21. Ibaadhi (Maibaadhi) Wasemao Kuwa Qur-aan Imeumbwa
Swali:
Ni kipote kipi cha tatu ambacho kinasema ya kwamba Qur-aan imeumbwa
mbali na Jahmiyyah na Mu´tazilah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Nimewaambia ya kwamba ni Ashaa´irah, ndio wanasema kuwa maana
haikuumbwa, ama lafdhi imeumbwa. Wanasema hii ambayo imeandikwa
katika sahifu imeumbwa, kwa kuwa ni lafdhi na herufi.
Muulizaji:
Vipi kuhusu Ibaadhi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Ibaadhi ni pamoja na Jahmiyyah. Nao wanasema kwamba
imeumbwa.
22. Watu Wanaotahadharisha Madhehebu Ya Salaf
Swali:
17
Ni watu gani ambao wanalingania katika kutahadharisha madhehebu ya Salaf
ambao uliwataja?
´Allaamah al-Fawzaan:
Wako wengi ewe ndugu katika waandishi leo. Wanasema sio lazima kwetu
kuwarejelea Salaf na kurejelea kauli za wanachuoni, ambao wanasema hili ni
Haramu na hili ni Halali.
23. Baadhi Ya Fadhila Za Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anhu)
Swali:
Je, yamethibiti matamshi haya kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam):
"Mfalme bora ni Mu´aawiyah."?
´Allaamah al-Fawzaan:
Allaah Anajua zaidi. Sujui. Mu´aawiyah yatosheleza ya kwamba ni Swahaabiy
katika Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Na ni shemeji ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Dada yake
Ummu Habiybah ni mke wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam), na ni mwandishi wa Wahyi pia. Anamwandikia Wahyi Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na ana fadhila kubwa (Radhiya Allaahu
´anhu).
24. Imani Kwa Mujibu Wa Jahmiyyah
Swali:
18
Ni ipi Imani kwa Jahmiyyah? Na yapi madhehebu yao kwa Imani katika
Swalah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Nimeshakariri hili mara nyingi na kusema ya kwamba madhehebu katika
Imani ni maarifa (ujuzu) tu moyoni, hata kama mtu hakufanya ´amali yoyote,
hata kama mtu hakutamka Shahadatayn huchukuliwa ni muumini kwao. Kwa
kuwa anajua moyoni mwake.
25. Imani Ya Kwamba Qur-aan Imeumbwa Ni Ukafiri
Swali:
Umesema ya kwamba Jahmiyyah wamekufuru kwa mambo yote haya
wanayoamini. Je, tufahamu kwa hili ya kwamba hakufuru katika wao
isipokuwa yule ambaye yamemkusanyikia mambo yote haya?
´Allaamah al-Fawzaan:
Akiwa na baadhi yake, haambiwi kuwa ni Jahmiy, anaambiwa yuko na kitu
katika Tajahhum na Jahmiyyah. Ikiwa kitu hichi anachokiamini kinakufurisha,
anakufurishwa hata kama ni baadhi yake. Ni kama mfano wa Imani ya
kwamba Qur-aan imeumbwa, hii ni kufuru. Maneno ya Jahmiyyah kuko
ambayo ni kufuru ya wazi na kuko ambayo ni chini ya kufuru. Hivyo si kila
ambaye ana kitu katika madhehebu ya Jahmiyyah anakuwa kafiri, isipokuwa
tu ikiwa kitu hicho alichonacho kinakufurisha. Hapo ndipo anakufurishwa.
Lakini ambaye imemkusanyikiwa Imani yote ya Jahmiyyah, huyu hakuna
shaka ya kufuru yake.
26. Jahmiyyah Wapo Leo?
19
Swali:
Wanasema baadhi ya watu ya kwamba madhehebu ya Jahmiyyah yamepotea
na hakupatikani katika zama hizi hata mmoja. Je, kauli hii ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Anajuaje kama Jahmiyyah wamepotea? Je, yeye anajua Jahmiyyah na anajua
madhehebu yao mpaka aseme kuwa yamepotea? Jahmiyyah wapo na vitabu
vyao vipo na wafuasi wake wapo.
27. Nani Kasema Kwamba Kutofautiana Ni Rahmah?
Swali:
Je, kutofautiana ni Rahmah kama tunavyosikia?
´Allaamah al-Fawzaan:
Nani kasema kuwa ni Rahmah?Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema:
حم ربك ول يزالون مختلفينإلا من را
"Na hawatoacha kukhitilafiana. Isipokuwa yule Aliyemrehemu Mola wako."
(11:118-119)
Kamtofautisha Aliyerehemu Mola wako katika waliyotofautiana. Ni dalili
ioneshayo ya kwamba Rahmah ni katika Umoja. Rahmah inapatikan katika
Umoja na si kutofautiana.
حم ربك ول يزالون مختلفينإلا من را
"Na hawatoacha kukhitilafiana. Isipokuwa yule Aliyemrehemu Mola wako."
(11:118-119)
28. Kusoma Elimu Ya Falsafa, Mantiki, Na Mfano Wa Hizo
20
Swali:
Je, inajuzu kusoma elimu ya mantiki? Na ni ipi tofauti kati ya elimu ya
mantiki na elimu ya falsafa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Falsafa sio katika mantiki, inaingia mantiki na nyinginezo. Allaah
Katutosheleza kwa Kitabu na Sunnah. Soma Kitabu na Sunnah, na
usijishughulishe na mantiki na falsafa.
29. Mtume Na Imaam Ahmad Kumuona Allaah Usingizi
Swali:
Je, imethibiti kwa Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ya kwamba alimuona
Allaah usingizini? Na je, inawezekana kumuona Allaah duniani katika
usingizi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, yasemekana hili ya kwamba Imaam Ahmad alimuona Allaah usingizini.
Yasemekana na Allaah Anajua zaidi. Kumuona Allaah usingizini ni jambo
linawezekana bila ya shaka. Alimuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam) usingizini.
30. Kwenda Kaburini Kumzuru Maiti Wako Ila Hujui Mahali Alipo
Swali:
21
Nikienda kaburini kumzuru maiti mmoja na wala sijui mahali kaburi lake
lilipo, nikamtolea Salaam. Je, hujua kama nimeenda kumtembelea?
´Allaamah al-Fawzaan:
Allaah Anajua zaidi. Mimi sijui. Haya ni mambo yasiyojua yeyote ila Allaah
(Subhaanahu wa Ta´ala). Wewe watolee Salaam maiti na muombee maiti
wako. Na Allaah Hapotekewi na kitu (Subhaanahu wa Ta´ala).
31. Kafiri Akinipa Salaam Kamili, Je Nami Nimpe Kamili?
Swali:
Kafiri akikupa Salaam ya sahihi ya wazi kwa kusema: "as-Salaam ´alaykum
war-Rahmatullaahi wa Barakatuh", je nimrudishie kwa mfano wake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Mrudishie kwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Wanapokusalimieni Ahl-ul-Kitaab waambieni "wa ´alaykum" (Nanyi pia)."
Usizidishie zaidi ya "wa ´alaykum". Hii inakuwa inaendana na Kauli Yake
(Ta´ala):
وها وا بأحسن منها أو رد ة فحي يتم بتحيا إذا حي
"Na mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo bora kuliko
hayo au yarudisheni hayo hayo (kama mlivyoamkiwa)." (04:86)
Hadiyth inaendana sawa na Aayah.
32. Madu´aat Wanaodai Wanalingania Katika Haki Za Mwanamke
22
Swali:
Tunasikia na kusoma siku hizi watu wengi ambao wanalingania katika yale
yanayoitwa "haki za mwanamke" na wanaita katika kujuzisha mchanganyiko
sokoni, [mwanamke] kuendesha gari na mengineyo. Upi wajibu wetu kwa
hilo? Na je, hawa ndio wale walinganiaji wanaolingania katika milango ya
Motoni tutahadhari nao?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni kama nilivyosema hivi karibu, ikiwa wewe uko na elimu kwa makosa ya
watu hawa wapige Radd, ni juu yako uwatwange Radd sawa sawa kwa fikra
zao. Katika Khutbah za Ijumaa, mihadhara na makala zinazoandikwa na
kusambazwa, na katika kitabu ikiwa uko na uwezo. Ama ikiwa huna elimu, ni
juu yako uwafikishie wanachuoni wanayoyasema.
33. Kuwalea Watoto Kwa Filamu Za Katuni
Swali:
Umeongelea kuhusu uumbaji na picha. Ni nini hukumu ya filamu za katuni
ambazo wanadai kuwa zinawalea watoto?
´Allaamah al-Fawzaan:
Picha zote [ni Haramu], sawa ikiwa ni filamu za katuni au nyinginezo. Ni
picha. Kila utachoona kuwa ni picha. Bali hizi ni aina baya zaidi ya picha, kwa
kuwa zinafanya harakati, zinasema, zinacheka n.k. Hizi ni baya zaidi kuliko
picha za kutundikwa, picha za kichwa tu na mwili usiofanya harakati. Ni baya
zaidi. Na wala tusiwalee watoto wetu katika maasi ya picha. Hili ndio
wanataka kwetu makafiri. Wanataka tuwalee watoto wetu kwa kwenda
kinyume na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
23
34. Kauli Inayosema Jahannam (Moto) Utaisha
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kusema ya kwamba Moto utaisha? Na je, achukuliwe
kuwa ni mpotofu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Achukuliwe kuwa kakosea kwa hilo. Wananasibisha hili kwa Shaykh-ul-
Islaam bin Taymiyyah, lakini halikuthibiti kutoka kwake uthibitisho wa wazi.
Na lau imethibiti ni kosa.
35. Kazi Hii Ni Maalum Kwa Wanachuoni
Swali:
Ni nani mwenye haki ya kutafsiki watu na kuwakufurisha?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hili ni kwa wanachuoni na watu wa Baswiyrah wajuao ni nani anayestahiki
Kufuru, Fisq na Bid´ah. Hili ni maalum kwa wanachuoni.
36. Kipi Kilichoumbwa Kabla, ´Arshi Au Kalamu?
Swali:
Tofauti ya kipi kilichoumbwa kwanza, ni ´Arshi au ni kalamu. Hii ni tofauti
iliotokea baina ya Salaf au ni baina ya waliokuja mwisho?
24
´Allaamah al-Fawzaan:
Hili kalisema Ibn-ul-Qayyim kwa waliokuwa kabla yake, lilitokea wakati wa
Salaf kwa kuchukua nususi. Kipi kinachotangulizwa, ´Arshi ndio iliumbwa
kabla au kalamu? Sahihi ni kwamba ´Arshi ndio iliumbwa kabla kama
inavyoonesha dalili Hadiyth. Na jambo hili ni sahali. Mwenye kusema kalamu
ndio ya kwanza au ´Arshi ndio ya kwanza, ni jambo la sahali halina utatizi.
37. Shaykh Fawzaan Kuhusu Kitabu Cha Ibn-ul-Qayyim "ar-Ruuh"
Swali:
Mtu huyu anauliza kuhusu Kitaab "ar-Ruuh cha Ibn-ul-Qayyim na kama kuna
makosa na anayeanza hafai kukisoma?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Kina faida kubwa na utafiti. Na pia kina mambo ambayo yanatakiwa
kutazamwa. Mwanafunzi anayeanza asikisome. Ambaye anaweza kukisoma
ni yule aliye thabiti na achukue ya faida humo na aache ambayo yanatakiwa
kutazawa. Yasemekana ya kwamba ndio kitabu cha kwanza alichoandika Ibn-
ul-Qayyim kabla ya kukutana na Shaykh wake [Ibn Taymiyyah]. Yasemwa
hivi na Allaah Anajua zaidi.
38. Kuashiria Kwa Mkono Wakati Wa Kutaja Sifa Za Allaah (´Azza wa Jalla)
Swali:
Inajuzu kuashiria kwa mkono wakati wa kutaja Hadiyth za Sifa za Allaah
(´Azza wa Jalla)?
25
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Usiashirie kwa mkono.
39. Kuchukua Elimu Kwa Watu Wanaokhalifu Manhaj Ya Salaf
Swali:
Ni upi msimamo wetu kwa Madu´aat6 wanaokwenda kinyume na Manhaj ya
Salaf? Je, ichukuliwe elimu yao au iachwe? Na je, inajuzu kusoma baadhi ya
vitabu vyao vya faida?
´Allaamah al-Fawzaan:
Allaah Amewatajirisha (tosheleza) kwa watu hawa. Chukueni elimu kwa
watu wake waliyonyooka na vitabu vyenye manufaa vya faida. Na hakuna
haja ya vitabu vya watu hawa.
40. Kuwa Na Nia Nzuri Haitakasi Kosa La Mtu
Swali:
Baadhi ya watu wanafanya maasi na mambo ya Haramu na
tunapowabainishia wanasema "nia yangu ni nzuri, na mimi nataka kheri na
napenda kheri na watu wake, lakini mimi nachukia maasi haya." Vipi kumpa
nasaha mtu kama huyu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haya ni maneno yasiyofidisha. Anasema "mimi nia yangu ni nzuri",
kinachoongelewa si nia yako bali ni kitendo chako. Maadamu kitendo chako
6 Walinganiaji, wahubiri
26
ni cha makosa, ni wajibu kwako kuleta Tawbah na kujirejea. Na nia nzuri
haitakasi kosa kamwe, kama tulivyosema. Ni juu ya aliyekosea arudi katika
usawa na hana udhuru ya kusema "nia yangu ni nzuri na akaendelea kwenye
kosa." Haijuzu kwake hili. Itapobainika kwake usawa ajirudi.
41. Maulidi Yana Bid´ah Na Shirki
Swali:
Je, Bid´ah ya kusherehekea Maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam) ni Bid´ah khafifu inayotujuzishia kukaa na wanayoifanya au hapana?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kusherehekea Maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Bid´ah
bila ya shaka. Kwa kuwa ni kitendo ambacho hakikufanya Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam), Khalifah wake waongofu wala karne bora. Wala
hayakuzushwa isipokuwa baada ya karne ya nne, wakati utawala wa
Faatwimiyyuun, ambao ni Mashia wanaotoka magharibi. Wao ndio walikuja
na Bid´ah ya Maulidi. Hivyo ni Bid´ah bila ya shaka. Isitoshe, yanaingia kitu
katika Shirki, nayo ni kumuomba msaada Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam), kuomba atatue haja na kumshtakia kwa mambo yaliowasibu
Waislamu. Wanamshtakia Mtume na wala hawamshtakii Allaah (Jalla ´Alaa).
Na wala hawamuombi msaada Allaah, wanamuomba msaada Mtume katika
mnasaba huu. Na wao wanajua ya kwamba hutokea kitu katika haya. Hivyo
yamejumuisha baina ya Bid´ah na baina ya Shirki.
42. Mwenye Kuifanyia Mzaha Sunnah Ya Mtume (´alayhis-Salaam) Ni Kafiri
Swali:
27
Kumedhihiri zama hizi wanaoifanyia mzaha Sunnah ya Mtume wa Allaah
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Je, kuifanyia mzaha Sunnah ni katika
Kufuru?
´Allaamah al-Fawzaan:
Una shaka juu ya hili? Mwenye kuifanyia mzaha Sunnah ya Mtume, hakuna
shaka ya ukafiriwake. Kwa kuwa anamkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) na kumponda.
43. Kumfuata Mwanachuoni Katika Kitu Kipya Cha Fiqh
Swali:
Akijitahidi mwanachuoni na kusema katika masuala ya Fiqh jambo ambalo
halikusema yeyote katika Salaf. Je, inajuzu kumfuata kipofu kwa hilo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kwa kiasi cha dalili. Ikiwa yuko na dalili, ndio inachukuliwa kauli yake. Ama
ikiwa hana dalili hapana. Hata Salaf, ikiwa mtu hana dalili inaachwa kauli
yake. Sisi tunafuata dalili.
44. Kumkufurisha Mshirikina Kwa Kitendo Chake Cha Dhahiri
Swali:
Je, tumkufurishe anayesujudia sanamu au kuchinjia sanamu au tusubiri
mpaka kwanza tumsimamishie hoja?
´Allaamah al-Fawzaan:
28
Yeye anakufuru kwa hili. Unaweza kuhukumu kitendo chake kuwa ni kufuru
na ukamkufurisha kwa dhahiri [wa uliyoyaona]. Kisha baada ya hapo
ukamnasihi. Akitubu [sawa], la sivyo anachukuliwa kuwa ni kafiri kwa
dhahiri na kwa ndani.
45. Kukataza Uovu Kwa Kumpa Mtu Mkanda
Swali:
Mwenye kuona maovu akampa aliyeyafanya mkanda. Je, huchukuliwa huku
ni katika kukataza maovu kwa ulimi? Na dhimma itakuwa imenitoka kwa
kufanya hivi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Huenda asijui ni mkanda gani. Ni lazima umbainishie. Umwambie ewe
ndugu unaona kuwa huku ni kwenda kinyume na hivyo nakupa mkanda
usikilize ili ustafidi. Ama kumpa mkanda na kunyama, huenda akauunguza
mkanda au asifaidiki nao au asiupe umuhimu. Lakini ukimbainishia pale
unapompa na mkanda ili astafidi kutoka kwenye mkanda huo, ni jambo zuri
hili.
46. Mume Anaweza Kumrejea Mke Wake Bila Ya Mashahidi?
Swali:
Je, ni wajibu kushahidisha katika kumrejea mke?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hili ni jambo limependekezwa na sio la wajibu. Lau atamrejea bila ya
mashahidi ni sahihi.
29
47. Kufuru Ndogo Ya Kumwingilia Mke Kwa Nyuma
Swali:
Ni aina ipi ya kufuru iliokuja katika kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam):
"Mwenye kumwendea mke wake kwa nyuma amekufuru."?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hii ni kufuru ndogo. Haimtoi mtu katika Uislamu. Ni kama mfano wa [kauli
yake Mtume]:
"Kumtusi muumini ni ufasiki, na kumuua ni kufuru."
Yaani ni kufuru chini ya kufuru [kubwa]. Hii ni katika kufuru ndogo. Hatoki
katika Uislamu yule ambaye kamwendea mke wake nyuma. Bali anakuwa
kafanya dhambi kubwa katika madhambi makubwa. Imesifiwa kuwa ni
kufuru kwa ajili ya watu waigope.
48. Kumvalisha Hijaab Binti Wa Miaka Saba
Swali:
Binti mwenye miaka saba avikwe Hijaab?
´Allaamah al-Fawzaan:
Azoweshwe Hijaab. Kama jinsi anavyozoweshwa Swalah, Wudhuu, Swawm.
Azoweshwe hili na kukuzwa juu ya hilo.
30
49. Inajuzu Kunyoa Kipara?
Swali:
Ipi hukumu ya kunyoa kichwa bila ya sababu? Je, ni kujifananisha na
Khawaarij?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hakuna neno. Kunyoa kichwa hakuna neno na wala hakuna neno kukiacha.
Ni wajibu kunyoa au kupunguza wakati wa Hajj na ´Umrah, nje ya hapo
wewe ni mwenye khiyari. Ukitaka utakinyoa na ukitaka utakiacha. Lakini mtu
akiamini kuwa kukinyoa ni katika Dini na kadhalika, utakuwa ni katika
Khawaarij. Akiamini ya kwamba kukinyoa ni mubaha [imeruhusiwa] na wala
haina neno, hakuna ubaya kufanya hivyo.
50. Inajuzu Kuoa Wasichana Wa Nje Ya Ndoa?
Swali:
Inajuzu kuoa watoto wa Zinaa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Wakiwa ni wema, makatazo yako wapi? Wakiwa ni wema, hakuna makatazo.
Lakini bora mtu kujiepusha, pengine akawa na kitu katika tabia ya mama yake
au wamama zake. Pengine wakawa wamerithi. Mtu ajiepushe. Ama kusihi
inasihi. Wakiwa ni wema inasihi.
51. Kuomba "Ee Allaah Usinikadirie Kadha Na Kadha"
31
Swali:
Je, inajuzu kusema:
"Ee Allaah Usinikadirie wala usiniandikie kadha na kadha."?
´Allaamah al-Fawzaan:
Sema badala yake "Ee Allaah usinikadirie! Ee Allaah nakuomba upole,
Rahmah na urahisi!, na mfano wa haya."
52. Kwanini Ahl-us-Sunnah Wanawakufurisha Jahmiyyah?
Swali:
Vipi Jahmiyyah wanakufurishwa na Ahl-us-Sunnah pamoja na kwamba
Jahmiyyah wanamjua Allaah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Tunasema makusudio sio kumjua tu kwani hata Iblisi anamjua Allaah.
قال رب بما أغويتني
"(Ibliys) Akasema: “Mola wangu! Kwa vile Umenitia makosani." (15:39)
Iblisi anamjua Allaah, Fir´awn anamjua Allaah. Hakutoshelezi kujua tu.
"Imani ni kutamka kwa ulimi, kuamini moyoni na matendo ya viungo; inazidi
kwa utiifu na kupungua kwa maasi." Hii ndio Imani.
53. Ni Kweli Watu Wa Makaburini Hutembeleana Kila Siku Ya Ijumaa?
Swali:
32
Je, ni sahihi watu wa makaburini wanatembeleana makaburini mwao yao kila
siku ya Ijumaa na khaswa waumini?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kwa kweli hatujui, haya ni mambo ya Aakhirah hatuthibitishi kitu isipokuwa
kwa dalili. Anayesema kwamba wanatembeleana atuletee dalili ya kwamba
wanatembeleana. Ama maneno ya watu ni mengi, lakini kinachozingatiwa ni
dalili. Iko wapi dalili? Kuna mwenye kuwaona wakitembeleana,
akawashuhudia mwenyewe wakikusanyika na kadhalika? Kuna dalili katika
Shari´ah mpaka aseme dalili ni namna hii? Hana dalili.
54. Watoto Wa Shaykh Katika Kitabu "ad-Durur as-Sania"
Swali:
Katika Kitaab "al-Durur as-Sania" wakati mwingine kunasemwa: "Waliulizwa
watoto wa Shaykh". Ni yapi makusudio watoto wa Shaykh?
´Allaamah al-Fawzaan:
Watoto wa Shaykh ni Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab; ´Abdullaah, ´Aliy,
Ibraahiym, Hasan na Husayn. Na mkubwa wao ni ´Aliy kwa kuwa anaitwa
Abu ´Aliy. Hawa ndio watoto wa Shaykh.
55. Makafiri Wanaposilimu Watoto Wao Huzingatiwa Kuwa Ni Wa Zinaa?
Swali:
Je, watoto wa makafiri huzingatiwa ni watoto wa Zinaa kwa vile wazazi wao
hawakufunga ndoa sahihi?
33
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Adhabu huchukuliwa ni ya kwao [wa zazi] na watoto wao ni wa
Kishari´ah. Na kwa sababu hii ndio maana mwenye kusilimu katika makafiri,
hakuwaamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kufunga ndoa
upya na wala hakuwanyanganya watoto wao kutoka kwao.
56. Dalili Ya Mafungu Matatu Ya Tawhiyd Katika Qur-aan
Swali:
Ipi hukumu kwa mwenye kupinga kugawa Tawhiyd mafungu matatu;
Rubuubiyyah, Uluuhiyyah na al-Asmaa´ was-Swifaat na anasema haya ni
katika mambo yaliyozushwa ambayo hayakuwepo wakati wa Mtume
(´alayhis-Salaam)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mimi nimekwishawaambia ya kwamba watu hawa wanajaribu
kuiharibu´Aqiydah. Mara utawasikia wanasema hakuna neno "´Aqiydah"
wala "at-Tawhiyd" katika Qur-aan na Sunnah. Na mara wanasema kuigawa
Tawhiyd mafungu matatu ni Bid´ah. Wanataka kutatiza watu katika jambo
hili. Neno ´Aqiydah lipo katika Qur-aan na Sunnah, bali ni jina lililotolewa
katika Qur-aan na Sunnah, jina la ´Aqiydah na Tawhiyd. Hata kama si kwa
andiko la moja kwa moja, lakini lipo kimaana. Ama mafungu ya Tawhiyd ni
jambo lipo katika Qur-aan. Bali Qur-aan yote ni Tawhiyd kama alivyosema
hilo Ibn-ul-Qayyim. Yanayozungumzia Rubuubiyyah (Ubwana) wa Allaah,
Ufalme Wake, Uwezo Wake na Matakwa Yake; haya ni katika Tawhiyd
Rubuubiyyah. Yanayozungumzia Majina na Sifa za Allaah ni katika Tawhiyd
al-Asmaa´ was-Swifaat. Yanayozungumzia kumuabudu Allaah Mmoja
Asiyekuwa na mshirika na kuacha ´Ibaadah (kuabudu) asiyekuwa Yeye, ni
katika Taawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Yote yanapatikana katika Qur-aan. Mafungu
ya Tawhiyd matatu yanapatikana kuanzia Suurat ya kwanza al-Faatihah.
34
ه رب العالمين الحمد للـا
"Alhamduli-Llaah (Himdi zote) Anastahiki Allaah Mola wa walimwengu."
Hii ni Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. "Mola wa walimwengu."
ين حيم مالك يوم الد ن الرا ـ حم الرا
"Ar-Rahmaanir-Rahiym (Mwingi wa Rahmah-Mwenye Kurehemu). Maalik
(Mfalme) wa siku ya malipo."
Hii ni Tawhiyd al-Asmaa´ was-Swifaat.
اك نستعين اك نعبد وإيا إيا
"Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada."
Hii ni Tawhiyd ipi? Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah.
Katika Suurat ya mwisho ya Qur-aan; Suurat "an-Naas".
قل أعوذ برب النااس
"Sema: “Najikinga na Mola wa watu."
Hii ni Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah.
"Ilaah wa watu." Hii ni Tawhiyd ipi? Tawhiyd-u-Uluuhiyyah.
ملك النااس
“Maliki (Mfalme) wa watu."
Hii ni Tawhiyd ipi? al-Asmaa´ was-Swifaat.
Lakini watu hawa ima ni wajinga wasiojua chochote. Na asiyejua vipi atataka
naye kukataza asiyoyajua? Au ima ni wapotofu wanaotaka kuiharibu
´Aqiydah na mara nyingi huwa hivi kwao.
57. Watu Wa Mantiki, Wanafalsafa Na Wanatheolojia
Swali:
35
Ipi tofauti kati ya al-Manaatwiqah (watu wa mantiki), al-Falaasifah
(wanafalsafa) na Ahl-ul-Kalaam (wanatheolojia)?
´Allaamah al-Fawzaan:
al-Manaatwiqah ndio Ahl-ul-Kalaam. Ama Falaasifah ni wale wanaodai wana
hekima na mara nyingi huwa katika makafiri. Ama ´ulamaa al-Kalaam na
´ulamaa al-Mantwiq ni katika vipote vya Kiislamu; kama Mu´tazilah na
waliofuata elimu yao ya mantiki na akategemea dalili yao au hoja yao katika
´Aqiydah. Watu hawa ni vipote katika vipote vya Waislamu. Lakini miongoni
mwao kuko ambao wametoka katika Uislamu na miongoni mwao kuko
ambao wamepotea na hawakutoka katika Uislamu kiasi cha daraja yao. Ama
Falaasifah wengi wao huwa makafiri.
58. Wanaosema Watawala Ni Ma´ulamaa Na Sio Viongozi Waasi Na Madhalimu
Swali:
Katika zama zetu hizi kuna Waislamu wanaosema ya kwamba watawala ni
wanachuoni na sio raisi wa dola kutokana na kasoro alizonazo. Ipi hukumu ya
kauli hii na ipi nasaha yako?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haya ni madhehebu ya Khawaarij na Allaah Atukinge. Katika Maswahabah
kulikuwepo wanachuoni na walikuwa wakimtii Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan
na ´Aliy na wala hawakusema Imaam [kiongozi] wetu ni mwanachuoni fulani.
Na wala hakuna Muislamu yeyote aliyesema kwamba mtawala wetu ni
mwanachuoni fulani. Wanasema ni kiongozi wetu katika elimu, ama kusema
ni kiongozi wetu katika usikivu na utiifu hakuna hata mmoja aliyesema hivi
katika Waislamu. Hakuna asemae hivi isipokuwa mtu ambaye ni mpumbavu
asiyekuwa na akili au asiyekuwa na Dini kabisa.
36
59. Tafsiri Ya Neno "adh-Dhikra", Katika Suurat 16; Aayah Ya 44
Swali:
كر رون وأنزلنا إليك الذ ل إليهم ولعلاهم يتفكا لتبين للنااس ما نز
"Na Tumekuteremshia Adh-Dhikra (Qur-aan ee Muhammad عليه وآله صلى هللا
ili uwabainishie watu (kwa Sunnah) yaliyotere-mshwa kwao na huenda (وسلم
wakapata kutafakari.” (16:44)
Je, ni Qur-aan au Sunnah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni vyote viwili. Lakini asli ni Qur-aan, na kunaingia humo Sunnah.
60. Radd Kwa Mwenye Kutatiza Watu Na Kitabu Na "Sharh as-Sunnah” Cha al-Barbahaariy
Swali:
Kuna mtu kanitatiza kwa kitabu hichi "Sharh as-Sunnah" cha Imaam al-
Barbahaariy na kwamba hakikuthibiti kwake kihistoria. Je, maneno yake ni
sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Lipi ajualo kuhusiana na historia? Huyu ni mjinga asiyejijua. Yaani yeye
haamini wanachuoni ambao wamekithibitisha kitabu hichi? Na wala
hamuamini Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah ambaye kanukuu kutoka katika
Risaalah hii [ya Barbahaariy] katika Fataawa zake? Yaani tukadhibishe
wanachuoni na tumsadikishe yeye? Lipi ajualo katika historia na maisha ya
wanachuoni? Huyu ni mjinga asiyejijua. Na pengine kaguswa katika nafsi
yake na kitu kwa ´Aqiydah hii, hivyo anataka kutatiza watu kwacho. Watu
37
wamesema hata kuwa Qur-aan sio Maneno ya Allaah. Mnastaajabu? Je,
hakuna watu ambao wanasema Qur-aan sio Maneno ya Allaah? Ajitokeze mtu
aseme Risaalah hii sio maneno ya al-Barbahaariy. Hili halistaajabishi.
61. Bid´ah Zinazoenezwa Na Kuchukua Elimu Kwa Njia Ya Simu
Swali:
Tunasikia siku hizi ya kwamba kuna mtu katolewa katika kaburi lake na uso
wake umeungua na haya yameenea kwa njia za simu. Je, tusadikishe khabari
hizi au ni katika mambo ya Ghayb?
´Allaamah al-Fawzaan:
Msisadikishe simu kamwe katika mambo haya. Kwa kuwa nyuma ya siku
hizo kuna watu wapotofu ambao wanataka kueneza Bid´ah na kuharibu
´Aqiydah za Waislamu. Hivyo tahadharini sana. Wala msichukue elimu
kwenye simu.
62. Mtu Yuko Huru Katika Uislamu Katika Mipaka Ya Kishari´ah
Swali:
Anayesema katika al-Mufakkiruun ya kwamba yeye ni ´Ilmaaniy au
Libraaliy...
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni nini maana ya Libraaliy? Uhuru? Uhuru wa kinyama au uhuru wa
Kishari´ah? Ikiwa ni uhuru wa kinyama ni kufuru, ama ikiwa anamaanisha
yuko huru kwa mipaka ya Kishari´ah, haina neno. Watu wako huru -
Alhamdulillaah - katika mambo yao katika mipaka ya Kishari´ah. Wako huru
38
katika mali zao, katika mipaka ya Kishari´ah. Uhuru sio moja kwa moja,
uhuru umedhibitiwa kwa dhawabiti za Kishari´ah.
63. Sifa Ya Kundi Lililookoka
Swali:
Je, kuna tofauti kati ya at-Twaaifah al-Mansuurah kundi lililonusuriwa na al-
Firqah an-Naajiyah pote lililookoka?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haliwezi kunusuriwa isipokuwa ni lazima liwe lililookoka, na haliwezi kuwa
ni lililookoka isipokuwa ni lazima liwe ni lililonusuriwa. Sifa zote hizi ni za
kundi hili. Ni pote lililonusuriwa, lililookoka, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
Sifa zote hizi ni zake. Anayetofautisha baina ya hayo, huyu hana dalili ya
kufanya kwake hivi.
64. Ahl-ul-Takfiyr Ni Katika Ahl-ul-Bid´ah Wabaya Zaidi
Swali:
Ahl-ul-Takfiyr wanaowakufurisha Waislamu ni katika Ahl-ul-Bid´ah?7 Na
nikikaa nao kwa makusudio ya kuwabadili ikiwa wako katika makosa, je
itakuwa kikao hichi ni chenye kulaumiwa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ahl-ul-Takfiyr ni katika Ahl-ul-Bid´ah wabaya zaidi. Wanaowakufurisha
Waislamu ni katika Bid´ah baya zaidi. Ama kukaa nao, ni kama tulivyosema
mwanzo. Ikiwa uko na uwezo wa kukaa nao na kujadiliana nao na kuradi 7 Watu wa Bid´ah
39
shubuha zao, hili ni jambo la wajibu. Kwa kuwa hili ni katika kulingania kwa
Allaah.
"Lau Allaah Atamuongoza mtu mmoja kupitia mikono yako, ni kheri kwako
kuliko zizi la minyama."
65. Kuwatakia Swalah Na Salaam Kwa Wasiokuwa Mitume
Swali:
Kulipokuja jina la Mahdiy ulisema (´alayhis-Salaam). Je, anazingatiwa ni
katika manzilah ya Mitume au huku ni kwa ajili ya heshima tu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Inajuzu kuwatakia Salaam kwa wasiokuwa Mitume na kusema "Swalah na
salaam ziwe juu yao." Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:
"Allaahumma swalliy ´alaa Aali Abiy ´Awfah (اللهم صل على آل أبي عوفة)". Inajuzu
kuwatakia Swalah na Salaam kwa wasiokuwa Mitume, lakini mtu asidumu
kwa kufanya hivyo kama mtu anavyodumu kuwatakia Swalah na Salaam
Mitume. Ikisemwa baadhi ya nyakati hakuna neno.
66. Kumuuliza Muislamu Katika Mji Wa Kiislamu "Wewe Ni Muumini"?
Swali:
Akiniuliza mtu: "Je, wewe ni muumini?" Je, naweza kusema: "Ndio, mimi ni
muumini na ninakusudia namwamini Allaah, Malaika Wake, vitabu Vyake na
Mitume Wake, siku ya Mwisho na Qadar; kheri na shari yake?".
´Allaamah al-Fawzaan:
40
Yaani wewe uko katika mji wa kikafiri na hajui ya kwamba wewe ni muumini
muislamu mpaka akuulize? Kusema "mimi ni muislamu hakuna neno".
Usiseme "mimi ni muumini", sema "mimi ni muislamu" ikiwa uko katika mji
wa kikafiri. Ama ukiwa katika mji wa Kiislamu, hakuna haja ya maswali kama
haya.
67. Kumkuta Imamu Katika Takbiyrah Ya Tatu Katika Swalah Ya Janaza
Swali:
Nikiingia katika Swalah ya Janaza katika Takbiyrah ya tatu. Vipi ntatimiza
Swalah yangu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kabiri na Imamu zilizobaki, na pindi Imamu atapotoa Salaam kamilisha
Takbiyrah zilizobaki. Ni kama uliyepitwa katika Swalah ya faradhi, sawa
sawa. Kamilisha na toa Salaam baada ya kukamilisha.
68. Mwanaume Kuswali Na Suruwali
Swali:
Kuna mnasaba upi wa kutajwa suruwali katika kitabu hichi (Sharh as-Sunnah
lil-Barbahaariy) pamoja na kuwa ni kitabu cha ´Aqiydah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kama nilivyowaambia, kunatajwa masuala ya Fiqh wakati fulani ili
kuwakhalifu Mubtadi´ah.8 Kwa kuwa kuko wanaopinga kuswali na suruwali.
Suruwali ikisitiri ´Awrah, mtu anaswali nayo. Muhimu ni kusitiri ´Awrah, hii 8 Watu wa Bid´ah
41
ni sharti moja wapo ya kusihi kwa Swalah. Kusitiri ´Awrah. Kwa nisba ya
mwanaume ni baina ya kitovu mpaka kwenye magoti. Kwa nisba ya
mwanamke, mwili wake wote ni ´Awrah ndani ya Swalah.
69. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) Waliwahi Kumuona Masiyh ad-Dajjaal? Swali:
Je, Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walimuona Masiyh ad-Dajjaal na
mnyama?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hakukuthibiti kitu katika hili. Yasemekana ni Ibn Sayyaad ndio Masiyh ad-
Dajjaal. Lakini haikuthibiti ya kwamba ndio Dajjaal. Ibn Sayyaad alikuwepo,
lakini haikuthibiti ya kwamba yeye ndio Dajjaal.
70. Mtu Akimuona Allaah Usingizini Kamuona Kweli?
Swali:
Mtu akimuona Mola Wake usingizini. Sura ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) ni ya
uhakika kama atavyomuona mwenye kuota usingizini?
´Allaamah al-Fawzaan:
Enyi ndugu! Mimi siingii ndani ya jambo hili. Ni nani ana uwezo wa kusema
namjua Allaah ukweli wa kumjua na nimemuona Allaah kwa Sura Yake ya
hakika (Subhaanahu wa Ta´ala)? Unaweza kujiwa na Shaytwaan na kusema
"mimi ndio Allaah au mimi ndio mola wako" au akasema "mimi ndio Mtume
wa Allaah." Utamuona mtu anaingia katika jambo na pengine asitoke humo.
42
Aache jambo hili. Kumuona Allaah usingizini kunahitajia nguvu ya Imani na
mtu awe anamjua Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na nguvu ya elimu.
71. Je, Sunnah Inaweza Kufuta Qur-aan?
Swali:
Tumejua ya kwamba Sunnah inafasiri Qur-aan. Je, Sunnah inaweza kufuta
kitu katika Qur-aan?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, inawezekana. Usuuliyyuun wanasema kwamba Qur-aan inafuta
Sunnah na Sunnah inafuta Qur-aan. Na Qur-aan inafuta Qur-aan na Sunnah
inafuta Sunnah.
72. Sisi Tunalingania Katika Umoja Wa Waislamu
Swali:
Yapi maoni yako kwa mwenye kusema:
"Msiwafarikanishe Waislamu na wala msitahadharishe Raafidhwah kwa
kuwa ni Waislamu"?
´Allaamah al-Fawzaan:
Sisi hatuwafarikanishi Waislamu, bali tunalingania katika Umoja wa
Waislamu. Lakini Waislamu wasiokuwa na moja ya jambo katika mambo
yanayovunja Uislamu wa mtu, Waislamu sahihi sisi tunalingania wawe na
Umoja. Ama mwenye moja katika mambo yanayomtoa mtu katika Uislamu,
hawa sio Waislamu.
43
73. Kufuata Kauli Za Wanachuoni Kwa Matamanio
Swali:
Ipi maana ya kauli ya Salaf (Rahimahumu Allaah):
"Anayefuata [mambo ya] rukhusa amefanya Uzanaadiqah."?
Ina maana anakuwa mnafiki?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, kwa kuwa anafuata hawaa (matamanio) yake. Huyu ni mbaya kuliko
mnafiki. Kwa kuwa mtu huyu anatoka katika Dini. Itafikia awe ni mwenye
kuchukua kila rukhusa iliyosema mwanachuoni na akaacha kauli sahihi
[yenye nguvu] mpaka anakuwa mnafiki.
74. Kuna Tofauti Kati Ya Mashia Na Raafidhwah?
Swali:
Ipi tofauti kati ya Mashia na Raafidhwah? Na ni zipi aina zao?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mashia wako aina mbali mbali, sio kundi moja. Kuna Mashia khafifu, Mashia
wenye kuchupa mipaka, Mashia al-Baatwiniyyah na kadhalika. Mashia wako
makundi mengi. Raafidhwah ni kundi katika Mashia; Zayniyyah,
Raafidhwah, al-Baatwiniyyah n.k. Yote haya ni katika makundi ya Mashia.
44
75. Kuoa Kwa Nia Ya Talaka Ni Kumhadaa Mwanamke
Swali:
Ipi hukumu ya kuoa kwa nia ya Talaka. Na je, ni kama Mut´ah?9
´Allaamah al-Fawzaan:
Kuoa kwa nia ya Talaka sio kama Mut´ah, kuna tofauti. Lakini kauli ya sahihi
ni kwamba haijuzu. Kwa kuwa ni kumhadaa mwanamke, [haikukatazwa]
kwa sababu ni kama Mut´ah ila ni kwa sababu ni kumhadaa mwanamke na
walii wake. Kwa kuwa umemuoa kwa nia ya kubaki naye na wewe unaficha
ndani ya nafsi yako nia ya [... sauti imepotea... ]. Ni Mut´ah ndogo na sio
Mut´ah [...]. [...] kwa nisba ya mwenye kunuia [...], mke, walii. Hii haiitwi
Mut´ah ya kihakika.
76. Salaf Walikuwa Hawajui ´Ilm-ul-Kalaam
Swali:
Imesihi kwa mmoja katika wanachuoni wa Salaf ya kwamba aliita elimu ya
´Aqiydah ´Ilm-ul-Kalaam (elimu ya kimantiki)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Salaf hapakupatikana katika wakati wao ´Ilm-ul-Kalaam, ilipatikana katika
zama za mwisho baada ya karne bora. Ikaenea baada ya karne bora.
Walikuwa hawajui ´Ilm-ul-Kalaam.
77. Sababu Ya Khawaarij Kupigwa Vita
9 Ndoa ya muda; ambayo hukumu yake ni haramu
45
Swali:
Katika wanachuoni kuko waliowakufurisha Khawaarij na kutumia dalili ya
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Nitawaua kama walivyouawa kina ´Aad."
Na kuna ambao hawakuwakufurisha kwa kutumia dalili ya ´Aliy (Radhiya
Allaahu ´anhu) alipoulizwa kama wao ni makafiri:
"Hapana. Wameikimbia kufuru."
Ipi kauli yenye nguvu katika kauli hizi mbili?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Wametofautiana wanachuoni katika kuwakufurisha Khawaarij, na
wengi wao wanaona kuwa sio makafiri bali ni wapotofu. Kule ´Aliy (Radhiya
Allaahu ´anhu) kuwaua na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
kaamrisha kuwapiga vita, sio kwa sababu ya kufuru yao. Yule ambaye
anawafarakanisha Waislamu na kuhalalisha damu ya Waislamu anapigwa
vita hata kama ni Muislamu. Kupigwa vita haina maana kwamba ni makafiri.
Kila anayejiingiza kwa Waislamu na anataka kuwafarakanisha au kuhalalisha
damu yao, apigwe vita hata kama ni Muislamu.
78. Roho Hukutana Na Kuongea Ndani Ya Kaburi?
Swali:
Roho ndani ya kaburi zinaonana na kuongea?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ewe ndugu hatujui yaliyomo ndani ya kaburi. Haya ni katika mambo ya
Ghayb. Hakuongelewi khabari ya makaburini isipokuwa kwa dalili. Sisi
hatuingii katika mambo haya.
46
79. Sauti Ni Ya Msomaji, Maneno Ni YaAllaah
Swali:
Kauli hii ilithibiti kutoka kwa Salaf:
"Maneno ya ni Maneno ya Al-Baariy (Allaah) na sauti ni sauti ya msomaji?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, yamesihi. Maneno ni Maneno ya Al-Baariy na sauti pindi mtu
anaposoma [Qur-aan] ni maneno ya msomaji. Hii ndio maana ya kauli ya Ahl-
us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Yanayosomwa ni Maneno ya Allaah, na lafdhi hichi
ni kitendo cha kiumbe.
80. Qur-aan Lazima Iendane Sambamba Na Sunnah
Swali:
Je, ni sahihi kusema "Qur-aan inaihitajia Sunnah zaidi kuliko jinsi Sunnah
inavyoihitajia Qur-aan"?.
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Qur-aan pamoja na Sunnah. Haitoshelezi moja wapo yenyewe
isipokuwa pamoja na nyenzake. Ikichukuliwa Qur-aan pasina Sunnah, itabaki
Qur-aan bila ya Tafsiyr sehemu kubwa na bila ya bayana.
81. ´Adhaab Na Qiswaas
47
Swali:
Ipi tofauti baina ya Qiswaas10 na baina ya ´Adhaab?
´Allaamah al-Fawzaan:
´Adhaab ni natija ya Qiswaas.
82. Nishikamane Na Jamaa´ah Ipi Katika Miji Ya Kikafiri?
Swali:
Tumejua uwajibu wa kushikamana na Jamaa´ah na mimi niko katika mji moja
wapo ambayo inahukumu kinyume na Shari´ah ya Allaah. Ni Jamaa´ah ipi
ambayo ni wajibu kwangu kujiunga nayo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ambao wako katika madhehebu ya haki; katika ´Aqiydah, ´Ibaadah,
wamesalimika na Shirki na Bid´ah na wako madhubuti katika kushikamana
na dalili. Hawa ndio Jamaa´ah.
83. Kisichokuwa Na Asli Katika Dini Ndio Bid´ah
Swali:
Tumesikia baadhi ya wanachuoni wakisema : "Hii ni Bid´ah", na wakati
mwingine wanasema: "Jambo hili halina asli". Vipi kujumuisha baina ya lafdhi
hizi mbili?
10 Kisasi
48
´Allaamah al-Fawzaan:
Haya yanagongana. Jambo lisilokuwa na asli yaani ni Bid´ah. Kwa kuwa
Bid´ah ni yasiyokuwa na asli katika Kitabu na Sunnah. Hii ndio Bid´ah.
84. Sababu 4 Za Kukufanya Upate Unyenyekevu Wakati Wa Kusoma Qur-aan
Swali:
Mimi nina matatizo, nayo ni wakati ninaposoma Qur-aan siogopi na wala
sifahamu chochote kana kuwa sisomi maneno ya kiarabu. Bali wakati
mwingine nafikiria kitu na huku nasoma Qur-aan kwa masikitiko makubwa.
Ipi sababu ya hili kwa vile mwanzoni nilikuwa tofauti na hivi ninaposoma
Qur-aan?
´Allaamah al-Fawzaan:
Pengine uko na mukhalafaat na maasi na umeshikamana na dunia. Ni juu
yako uihesabu nafsi yako juu ya jambo hili. Na unyenyekevu ni kitu kinatoka
kwa Allaah (Subhaanahu Ta´ala), lakini wewe fanya sababu za kukufanya
upateunyenyekevu.
Na katika sababu za kukufanya uwe na unyenyekevu: a) Omba kinga kwa
Allaah kutokana na Shaytwaan aliyelaaniwa mwanzoni mwa kisomo, b)
usome kwa moyo uliyohudhuria, c) uzingatie Aayah unazosoma kwa
kuzifikiri na maana yake na d) na usome katika wakati mzuri usiokuwa na
vishawishi. Hizi ni sababu.
85. Waliopewa Mtihani Wa Kupenda Picha
Swali:
49
Nimepewa mtihani wa kupenda picha na ninazitundika [... sauti imepotea... ]
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni juu yako kutubu kwa Allaah na kujiweka mbali na jambo hilo.
86. Mtu Anamtii Mtawala Ambaye Yuko Chini Ya Uongozi Wake
Swali:
Mimi naishi katika mji huu Saudi Arabia lakini si mtu mwenye asli ya hapa.
Ni mtawala gani ambaye ni wajibu kwangu kumtii na ambaye juu ya shingo
langu kuna bay´ah, ni mtawala wa mji huu au mtawala wa mji wangu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni mtawala ambaye wewe uko chini ya uongozi wake. Wewe uko katika mji
huu, ni wajibu kwako kumtii mtawala wa mji huu. Na utapoenda katika mji
wako, wewe utambay´ah mtawala wa mji huo.
87. Ninapoulizwa Swali Ilihali Najua Jibu, Naweza Kulijibia?
Swali:
Ataponiuliza mtu usahihi wa Hadiyth au udhaifu wake, je nijibu ikiwa najua
jibu?
´Allaamah al-Fawzaan:
50
Ikiwa unajua jibu kutoka kwenye kitabu kiaminifu, mjibu. Mwambie: "kasema
fulani kadha na kadha, kuhusiana na Hadiyth hii", muelekezo katika
maregeleo ikiwa ni kitabu cha kuaminika. Ama ikiwa kitabu hakiaminiki au
mwandishi wake hajulikani, wewe nyamaza na kusema: "mimi sijui kitu
kuhusiana na hili. Waulize wanachuoni na wenye fani ya Hadiyth."
88. Lini Mji Unakuwa Wa Kiislamu Na WaKikafiri?
Swali:
Lini mji unahukumiwa ya kuwa ni mji wa Kiislamu au mji wa kufuru?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa unahukumu kwa Uislamu, ni mji wa Kiislamu. Na ikiwa unahukumu
kwa kufuru, basi ni mji wa kikafiri. Kinachotazamwa ni inavyohukumu.
89. Nini Maana Ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?
Swali:
Ni nini maana ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na lini Muislamu anakuwa
katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Yaa Subhaana Allaah! Hili tumelirudi mara nyingi katika darsa. Ahl-us-
Sunnah ni wale walioshikamana kwa yale aliyokuwemo Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake. Makusudio ya "as-Sunnah"
ni njia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndio Sunnah. "al-
Jamaa´ah" ni wale waliomo juu ya haki hata kama watakuwa wadogo. Yule
51
ambaye atakuwa juu ya haki, hata kama atakuwa mmoja au wadogo basi yeye
ni "al-Jamaa´ah".
90. Ipi Dini Sahihi Kabla Ya Mtume (´alayhis-Salaam) Kuja Na Uislamu?
Swali:
Je, Dini sahihi kabla ya kutumwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam) ni Haniyfiyyah Mila (Dini) ya Ibraahiym au ni Shari´ah ya ´Iysa
(´alayhis-Salaam)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kwa nisba ya waarabu Aal Ismaa´iyl, Dini waliokuwemo ni Dini ya
Ibraahiym. Dini ya baba yake na Ismaa´iyl ni Dini ya Ibraahiym (´alayhis-
Salaam). Ama kwa nisba ya mayahudi na manaswara walikuwa katika Dini ya
Muusa na ´Iysa (´alayhimus-Salaam). Na kuko katika waarabu walioathirika
na uyahudi na unaswara, na wakaacha Dini ya Ibraahiym.
91. Hadiyth "Kutofautiana Kwa Ummah Wangu Ni Rahmah" Ni Dhaifu
Swali:
Kuna ambao wanatumia kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Kutofautiana kwa Ummah wangu ni Rahmah." katika masuala ya tofauti,
ni halali au haramu. Hili ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Hili ni kosa. Yaani akisema hivyo, kinachofahamika ni kwamba
wakiwa wamoja ni adhabu? Ikiwa kutofautiana kwao ni Rahmah
kinachofahamika ni kwamba wakiwa wamoja itakuwa ni adhabu. Na hili
52
hakuna aliyelisema. Bali ni kinyume chake. Kuwa kwao wamoja ndio Rahmah
na kutofautiana kwao ni adhabu. Hili ndo sahihi bali ndo sawa. Kasema
Allaah (Ta´ala):
حم ربك ول يزالون مختلفينإلا من را
"Na hawatoacha kukhitilafiana. Isipokuwa yule Aliyemrehemu Mola wako."
(11:118-119)
Kawatoa katika waliotofautiana wale Aliowarehemu Allaah.
Hawakutofautiana. Na Hadiyth isemayo:
"Kutofautiana kwa Ummah wangu ni Rahmah."
Haikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
92. Nani Bora Zaidi; "Mu´aawiyah" Au "´Umar bin ´Abdil-´Aziyz"?
Swali:
Inajuzu kumfadhilisha ´Umar bin ´Abdul-´Aziyz juu ya Mu´aawiyah (Radhiya
Allaahu ´anhu)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Halijuzu hili. Hakuna yeyote anayefadhilishwa juu ya Swahabah
kamwe. Hili halijuzu. Si ´Umar bin ´Abdul-´Aziyz wala mwengine yeyote.
´Umar bin ´Abdul-´Aziyz (Radhiya Allaahu ´anhu) ana fadhila zake, manzilah
yake, elimu na ni katika Mujaddidiyn katika Uislamu. Lakini hawekwi sawa
wala kuwekwa karibu na mmoja katika Maswahabah, si Mu´aawiyah wala
mwengine yeyote.
93. Uwajibu Wa Msomi Kuthibitisha Sifa Za Allaah
Swali:
53
Ipi hukumu ya mwenye kuulizwa baadhi ya Sifa za Allaah anasema "sijui".
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa hajajifunza kweli, aseme "sijui". Ama ikiwa ni mjuzi na amesoma
´Aqiydah, ni wajibu kubainisha elimu aliyonayo.
94. Kumtanguliza ´Aliy Juu Ya ´Uthmaan Kwa Fadhila Au Uongozi
Swali:
Anayemfadhilisha ´Aliy juu ya ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhumaa), je
huchukuliwa ni Raafidhwiy au Shi´iy?11
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Hachukuliwi ni Raafidhwiy wala Shi´iy. Kufadhilishwa ´Aliy juu ya
´Uthmaan ni masuala yana tofauti kwa baadhi ya Maswahabah na
wanachuoni. Hatozingatiwa mtu huyu kuwa na kitu katika ushia. Isipokuwa
tu, yule ambaye anamtanguliza ´Aliy juu ya ´Uthmaan katika uongozi, au juu
ya Abu Bakr na ´Umar huyo ndo atakuwa ni Raafidhwiy. Uongozi ni tofauti
na fadhila.
95. Ipi Hukumu Ya Mwenye Kusema Uhuru Ni Bora Kuliko Shari´ah?
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kusema ya kwamba uhuru ni bora kuliko Shari´ah?
´Allaamah al-Fawzaan: 11 Mshia
54
Huyu mna shaka ya kwamba ni kafiri? Anasema kwamba uhuru ni bora
kuliko Shari´ah, huyu ni kafiri mwenye ukafiri mbaya. Allaah Atukinge.
96. Je, Kutukana Maswahabah Ni Kumtukana Mtume (´alayhis-Salaam)?
Swali:
Anayewatukana Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) anakuwa
kamtukana Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hili halina shaka. Kwa kuwa ni Mtume ndo kawafanya kuwa waadilifu,
kawasifia na kakataza kuwatukana. Kwa hivyo, yule anayewatukana
Maswahabah anakuwa kamtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam). Kwa kuwa ni Mtume ndo kawafanya kuwa waadilifu, na huyu
anawakadhibisha. Huyu anakwenda kinyume na Mtume na anapingana na
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuona kwake kuwa Maswahabah
ni waadiliifu.
97. Mwenye Kumtukana Mtume (´alayhis-Salaam) Ana Tawbah?
Swali:
Katika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah ni kwamba hakuna dhambi ila mja yuko
na Tawbah, je huingia humo mwenye kutubia kwa kumtukana Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?
´Allaamah al-Fawzaan:
55
Ndio. Kila mwenye kutubia. Lakini anayemtukana Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) hatoacha kupewa adhabu, ama Tawbah - ikiwa ni mkweli
baina yeye na Allaah - Allaah Atamkubalia. Lakini hatoacha kupewa adhabu.
98. Mtu Anayemponda Mu´aawiyah Na ´Amr bin ´Aasw
Swali:
Ipi hukumu ya anayewaponda Maswahabah kama mfano waMu´aawiyah na
Amr bin ´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa) katika baadhi ya waandishi na
al-Mufakkiriyn?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hawa ni Maswahabah watukufu. Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anhu) ni
Swahabah mtukufu na ni mwandishi wa Wahyi. Ni katika waandishi wa
Wahyi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ni
kiongozi wa Waislamu baada ya ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Allaah
Aliwakusanya Waislamu na akawafanya kuwa na Umoja kupitia mikono
yake. Ana fadhila nyingi (Radhiya Allaahu ´anhu). ´Amr bin ´Aasw pia ana
fadhila nyingi na ni Mujaahid katika njia ya Allaah (Radhiya Allaahu ´anhu).
Ana manzilah katika Uislamu. Hakuna anayewaponda isipokuwa ima ni
mjinga au ni mdanganyifu au kaathirika na Itikadi ya Shi´ah ambao
wanamtukana Mu´aawiyah, ´Amr bin ´Aasw na al-Mughiyrah bin Shu´bah.
99. "Hatutegemi Sunnah, Qur-aan Yatosha"
Swali:
Kauli ya mwandishi [al-Barbahaariy] (Rahimahu Allaah):
"Na utaposikia mtu hataki Athaar (Sunnah) na badala yake anataka Qur-aan
tu, basi usishuku ya kwamba ni mtu yuko na Zandaqah."
56
Je, ina maana ni kafiri?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Ni kafiri. Akikataa Sunnah, kuna nini ikiwa hii sio kufuru? Hii ni
kufuru ya wazi. Akisema "hatutegemei Sunnah kamwe, bali tunategemea
Qur-aan tu", hii ni kufuru.
100. Anayekufa Kwa Saratani Na Kuunguwa Kwa Moto, Wamekufa Mashahidi?
Swali:
Anayekufa kwa kuunguwa au kwa saratani, je wanaitwa kuwa ni mashahidi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kutokana na Hadiyth, wanaitwa ni mashahidi. Lakini ni mashahidi Aakhirah
na si duniani. Shahidi wa duniani ni yule wa vitani. Ama shahidi wa Aakhirah
ni shahidi ambaye si wa vitani; kama kuunguwa kwa moto, kuuawa kwa
dhuluma na kadhalika, hawa wanatarajiwa Shahaadah.
101. Anayeacha Swalah Akianza Ni Wajibu Kukoga Na Kutoa Shahaadah Upya?
Swali:
Ni jambo lenye kujulikana ya kwamba mwenye kuacha Swalah kwa uvivu na
kuzembea anakuwa kafiri. Akiacha Swalah kama Swalah ya Dhuhr kwa
kukusudia mpaka ukatoka wakati wake, je ni wajibu akoge kisha atoe
Shahaadah upya kwa kuwa nitakuwa nimetoka katika Uislamu na kuwa
kafiri?
57
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, ukikusudia hili ni juu yako Tawbah na kuingia katika Uislamu upya.
Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:
"Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao [makafiri] ni Swalah, atakayeiacha basi
amekufuru."
"Baina ya mja na kufuru, ni kuacha Swalah."
Kuna [ushahidi] ulio wazi zaidi kuliko huu?
Hali kadhalika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kaamrisha kulipa
Swalah kwa yule mwenye kupitikiwa na usingizi au kusahau, ni dalili
ioneshayo ya kwamba mwenye kukusudia si sahihi na haimfai kwake kulipa.
102. Mwenye Deni Lake Kafa, Pesa Hizi Nizifanye Nini?
Swali:
Mtu ambaye alikuwa na deni la mtu na wala hawezi kumrudishia kwa sababu
ya kukosekana mwenye deni lake, lipi la wajibu juu yake katika hali hii?
´Allaamah al-Fawzaan:
Warithi wake. Akifa mtu wa deni, ana warithi. Awape warithi wake.
103. Kuacha Swalah Ya Witr Na Sunnah YaKabla Ya Fajr Daima
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kuacha Swalah ya Witr na kadumu kwa kuacha
Sunnah ya Swalah ya Subh?
58
´Allaamah al-Fawzaan:
Huyu kapindukia. Bali Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) imepokelewa
kutoka kwake ya kwamba kasema:
"Mwenye kudumu kwa kuacha Witr, usikubaliwe ushahidi wake, kwa kuwa
ni mtu muovu."
Na Imaam Abu Haniyfah anaonelea ya kwamba Witr ni wajibu na si Sunnah,
bali ni wajibu kwa Abu Haniyfah. Witr imesisitizwa.
Ama Rakaa mbili za kabla ya Fajr, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
alikuwa haziachi sawa akiwa mkazi au msafiri. Ni dalili ioneshayo ya
kwamba ni Sunnah iliyosisitizwa. Haijuzu, au haitakikani kwa mtu kuziacha
kwa kuwa ni Sunnah zilizosisitizwa. Akiziacha basi ni mwenye mapungufu
na kapindukia.
104. Mwanachuoni Kuwa Na Baadhi Ya Makosa Katika Masuala Ya ´Aqiydah
Swali:
Kauli ya al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah):
"Haambiwi mtu kuwa ni "Swaahibu as-Sunnah" (mtu wa Sunnah) mpaka
Sunnah yote imkusanyikie."
Mwenye kukosea katika wanachuoni katika baadhi ya masuala ya ´Aqiydah
kwa Ijtihaad, kama mwenye kuharibu sifa moja au mbili na mengine yote
anaafikiana na Ahl-us-Sunnah, je huzingatiwa ni katika Ahl-us-Sunnah au
aitweje?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, huzingatiwa ni katika Ahl-us-Sunnah kwa mengi yanayoonekana
kwake. Ama kukosea kosa moja mbili au kitu kidogo, hii huchukuliwa ni
59
kasoro kwake lakini haimtoi katika Ahl-us-Sunnah. Ama makosa yakiwa
mengi, anatoka katika Ahl-us-Sunnah.
105. "al-Mustwafah" Ni Jina La Mtume(´alayhis-Salaam)?
Swali:
Katika majina ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni pamoja na "al-
Mustwafaa" (aliyechaguliwa) au hii ni sifa yake tu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni jina na sifa. Ambaye anataka kujizidishia [elimu] kuhusiana na masuala
haya, arejelee [kitabu] "Jalaail al-Afhaam was-Swalaat was-Salaam ´alaa
khayr-il-Anaam" cha Imaam Ibn-ul-Qayyim. Kataja majina ya Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) na kasherehekesha kila jina.
106. Jahmiyyah Ndio Pote Baya Zaidi Katika Murji-ah
Swali:
Je, Murji-ah wanaingia katika Jahmiyyah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Jahmiyyah ni pote katika Murji-ah. Lakini ndio baya zaidi, baya zaidi katika
mapote ya Murji-ah ni Jahmiyyah.
107. Inajuzu Kwangu Kuhudhuria Na Kusimamia Jeneza Na Mzazi Wangu Kafiri?
60
Swali:
Je, inajuzu kwa Muislamu kuhudhuria jeneza la wazazi wake wawili na wote
wawili sio Waislamu kwa kuwa kutohudhuria kwake kutasababisha matatizo
baina yake yeye na ndugu na jamaa zake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Kafiri anasimamiwa na makafiri, na Muislamu hasimamii jeneza la
kafiri hata kama itakuwa ni katika watoto wake. Isipokuwa tu ikiwa hakuna
wakumzika, hivyo atamzika. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam) alimuamrisha ´Aliy kumzika Abu Twaalib, amfukie. Kwa hivyo,
kukiwa hakuna yeyote atakayemsimamia katika makafiri, Waislamu
hawatomuacha juu ya ardhi, bali watamzika. Lakini hawatomzika katika
makaburi ya Waislamu.
108. Mu´tazilah, Ashaa´irah Na Maaturidiyyah Ni Wanafunzi Wa Jahmiyyah
Swali:
Je, Mu´tazilah ni Jahmiyyah katika Majina na Sifa za Allaah, Khawaarij katika
Imani na uongozi na Qadariyyah katika Qadar?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kwa kiasi wa waliyo nayo. Wako na Tajahhum, Qadar n.k. Kwa kiasi wa
waliyo nayo. Ni katika wanafunzi wa Jahmiyyah, Mu´tazilah ni katika
wanafunzi wa Jahmiyyah. Hali kadhalika, Ashaa´irah na Maaturidiyyah wako
na kitu katika madhehebu ya Jahmiyyah, sawa kiwe ni kidogo au kikubwa.
Lakini asli katika upotofu ni madhehebu ya Jahmiyyah. Wamerithi mambo
haya.
61
109. Mtume Ana Orodha Ya Majina Ya Watu Wa Peponi Na Motoni?
Swali:
Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anajua majina ya watu wa
Peponi na majina ya watu wa Motoni?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mtume hajui isipokuwa yale Aliyomfunza Allaah (´Azza wa Jalla) na wala
hajui majina ya watu wa Peponi na majina ya watu wa Motoni. Hajui hili.
Yeye hajui isipokuwa yale Aliyomfunza Allaah (´Azza wa Jalla).
110. Usiku Wa Mi´raaj, Mtume Alisikia Maneno Ya Allaah Moja Kwa Moja?
Swali:
Je, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisikia Maneno ya Allaah
(´Azza wa Jalla) moja kwa moja usiku wa Mi´raaj au alisikia kwa mkaakati?
´Allaamah al-Fawzaan:
Alisikia moja kwa moja bila ya mkaakati. Alisikia Maneno ya Allaah bila ya
mkaakati. Ni katika usiku huu tu. Ama siku zingine zote, Wahyi ulikuwa
ukimteremkia kwa kuletewa na Jibriyl (´alayhis-Salaam).
111. Msimamo Wa Imaam al-Bukhaariy Juu Ya Qur-aan
Swali:
62
Upi usahihi wa maneno ya mwenye kusema "kwa hakika al-Bukhaariy
(Rahimahu Allaah) alichagua kunyamaza katika masuala ya kusema kuwa
Qur-aan imeumbwa."?
´Allaamah al-Fawzaan:
Huu ni uongo. al-Bukhaariy alipewa mtihani katika jambo hili, pindi
aliposema kama alivyosema Imaam Ahmad [ya kwamba Qur-aan ni Maneno
ya Allaah na Hayakuumbwa] alipewa mtihani baadhi ya watu wa wakati
wake na wakamhama. Alifikwa na yakufikwa. Kama inavyojulikana katika
Historia na Siyrah yake (Rahimahu Allaah).
112. Wanaokufa Kwa Ajali Ya Ndege Hupatwa Na Maumivu Ya Kutokwa Na Roho?
Swali:
Vipi kujumuisha baina ya maumivu ya kutokwa na roho [wakati wa mauti] na
baina ya wanaokufa kwa ajali ya ndege katika makafiri na Waislamu na wala
hawapati maumivu ya mauti?
´Allaamah al-Fawzaan:
Wewe umejuaje kuwa hawahisi maumivu ya mauti? Hakuna yeyote
anayekufa bila ya kuhisi maumivu ya mauti. Huku ni kupinga bila ya dalili.
113. Watu Wa Sasa Walioathirika Na Suufiyyah Na Qubuuriyyah
Swali:
Kunapatikana katika baadhi ya vitabu vya madhehebu manne baadhi ya
mambo ya ´Aqiydah yanayokwenda kinyume na waliyokuwemo Salaf; kama
63
Tawassul kwa viumbe, Du´aa kwa jaha n.k. Je, mwenye kuyachukua na
kuyaeneza katika duruus akatazwe au hapana?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haya sio katika maneno ya Salaf. Haya ni katika vitabu vya waliokuja
baadaye, walioathirika na Suufiyyah na Qubuuriyyah. Ni katika vitabu vya
waliokujabaadaye. Ama vitabu vya Salaf, maimamu wanne, na waliokuwa
kabla yao, katikati yao na zama zao huwezi kukuta mambo kama haya,
vimesalimika na mambo haya. Na mimi nimewaambia, wananasibishiwa
maimamu wanne wa Fiqh mambo ya ´Aqiydah yasiyokuwa katika
madhehebu yao.
114. Chuo Kikuu Cha Mchanganyiko Wa Wanaume Na Wanawake
Swali:
Ipi hukumu ya kusoma katika chuo kikuu cha mchanganyiko, sawa ikiwa ni
kwa wanaume au wanawake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haijuzu kusoma katika chuo kikuu cha mchanganyiko, kutokana na maovu
yanayopatikana na fitina. Ama kusoma, atapata masomo yasiyokuwa na
mchanganyiko na asome.
115. Majini Pia Watamuona Allaah Aakhirah Peponi?
Swali:
Je, Allaah Ataonekana Peponi hususan na wanaadabu au pamoja na Majini
pia?
64
´Allaamah al-Fawzaan:
Haya hatuyajui ewe ndugu. Ambayo hatukujiwa na dalili yake hatuyatafuti.
116. Mwenye Kusema Mikono Miwili Ya Allaah Katika Qur-aan Ni Majaaz
Swali:
Ipi Radd kwa mwenye kusema:
"Mikono miwili iliotajwa ya Allaah (´Azza wa Jalla) katika Qur-aan ya
kwamba ni majaaz."?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hili ni batili. Yaani sio ya ukweli, majaaz maana yake ni kwamba sio Mikono
miwili ya uhakika. Haya ndio madhehebu ya Jahmiyyah. Allaah Atukinge.
117. Maiti Naweza Kumwambia Khabari Za Familia Yake?
Swali:
Inaruhusiwa kumueleza maiti hali za familia yake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Nini? Nani kakwambia haya ya kumueleza maiti hali ya familia yake? Je,
wewe unaweza ukawafikia ili uweze kuwafikishia khabari hizo? Maneno yote
haya ni ya kipuuzi. Msalimie maiti na umuombee kisha uondoke.
65
118. Suufiyyah Ni Wajinga
Swali:
Suufiyyah wamechukua ´Aqiydah yao kutoka kwa Jahmiyyah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Suufiyyah wamechukua ´Aqiydah yao... Asli ni kwamba Taswawwuf
maana yake ni kujitahidi katika ´Ibaadah, na Tashaddud [kukazia] katika
´Ibaadah. Ilianza namna hii. Kisha ikakua, kukaingia humo Malaahidah
mpaka ikafikiakatika Wahdat-ul-Wujuud. Na sababu ya hili ni ujinga, ya
kwamba ni wajinga. Kwa kuwa Suufiyyah kama mnavyojua, hawaonelei mtu
kutafuta elimu. Wanasema msisome kwa kuwa kutafuta elimu
kutawashughulisha na ´Ibaadah na kumdhukuru Allaah. Fanyeni ´Ibaadah na
Dhikr, elimu itawajia kutoka kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Shaytwaan ndio
anawaambia hivi. Ndio maana wanatumbukia katika waliyotumbukia.
119. Maana Ya "Hayaat al-Barzakhiyyah"
Swali:
Nini makusudio ya uhai wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
kaburini mwake ni "Hayaat al-Barzakhiyyah"?12
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni kama mashahidi wengine. Hayaat al-Barzakhiyyah maana yake ni kwamba
ni katika mambo ya Aakhirah na sio kama uhai wake wa duniani. Na kwa ajili
hiyo, Maswahabah hawakuwa wakienda katika kaburi lake na kusema Mtume
yuko hai, wakimuuliza na kumuomba. Hawakuwa wakifanya hivi. Japokuwa
12 Maisha ya ndani ya kaburi
66
yuko hai, lakini ni "Hayaat al-Barzakhiyyah", ni uhai hususan wa Aakhirah.
Mfano wa uhai wake huu sio kama uhai wake wa duniani. Kuna tofauti.
120. Tafsiri Ya Kauli Ya Allaah "Hapana Kulazimisha Katika Dini"
Swali:
Kauli ya Allaah Ta´ala:
ين ل إكراه في الد
"Hapana kulazimisha katika Dini (kuingiza iymaan katika moyo wa mtu)"
(02:256)
Kuna ambao wanaitumia kama dalili na kusema ya kwamba mtu ana uhuru
wa moja kwa moja katika Dini yake. Maneno haya ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Lau yangekuwa ni sahihi kusingelikuwa na haja ya kutuma Mitume na
kuteremsha vitabu na kuwekwa Jihaad katika njia ya Allaah. Kila mmoja
angelikuwa huru na kila mmoja anaabudu atakacho. Na wala kusingelikuwa
haja ya kitu. Haya maneno ni batili. "Hapana kulazimisha katika Dini" hakuna
yeyote awezae kuiingiza Dini kwenye moyo wa yeyote au kumfanya mtu
akaipenda Dini isipokuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Hakuna yeyote anayemiliki
moyoni na kuiendesha. Hii ndio maana ya:
"Hapana kulazimisha katika Dini."
121. Mtu Kama Huyu Ndie Mwenye Udhuru
Swali:
Lini hupewa mjinga udhuru kwa ujinga wake katika masuala ya ´Aqiydah?
67
´Allaamah al-Fawzaan:
Atapokuwa hana mtu yeyote wa kumfunza. Hapati mtu wa kumfunza,
kumuuliza, atapewa udhuru mpaka atapopata wa kumfunza na kumuelekeza.
Na je, leo masuala ya ´Aqiydah yamefichikana ilihali yanafunzwa na
kuenezwa? Katika vyombo vya khabari mashariki na magharibi na yanasikia
watu wote. Allaah (Jalla wa ´Alaa) kutokana na Hekima Yake Kaweka vitu
hivi ili kufikisha Dini hii. Ilipokuwa Dini hii imetumilizwa kwa wanaadamu
wote, Akaweka vya kuifikisha, kwanza kwa Jihaad. Ilipokuwa Jihaad
haiwezekani, kukaja vyombo vya khabari hivi vinavyowafikishia Dini watu
wote sawa wa mashariki na magharibi. Alhamduli Allaah. Hakuna yeyote
mwenye udhuru leo.
122. Kwanini Raafidhwah Wanawatukana Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum)
Swali:
Ipi sababu ya Raafidhwah13 kuwatukana Maswahabah (Radhiya Allaahu
´anhum)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mmesikia. Ni kwa sababu wanachukia Uislamu, na Maswahabah wao ndio
waliosimamisha Uislamu. Waliusimamisha katika uhai wa Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) na baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam). Kwa ajili hiyo, ndio maana wakawa wenye kuwaponda
wapokezi na wabebaji wake. Walioufikisha katika Ummah. Hawakuwatukana
kwa jengine ila ni kwa sababu hii. Ni kwa ajili ya nini? Isipokuwa ni kwa
sababu ni wao ndio waliisimamisha Dini hii na kuifikisha.
13 Raafidhwah au Rawaafidhw ni kundi katika Mashia, na ndio kundi ovu zaidi.
68
123. Kuziwekea Hadiyth Sahihi Majaaz
Swali:
Mwenye kuziwekea Hadiyth zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) majaaz14 kwa ajili ya taawili ya kiakili, huzingatiwa ni
katika Ahl-ul-Ahwaa15?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Ikiwa anaziwekea majaaz ili kubadili maana yake ya sahihi, ni katika
Ahl-ul-Ahwaa.
124. Mwenye Kuwatukana Wake Wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
Swali:
Anayewaponda wake wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa
kuwatukana na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum),anakufuru na kwa
nini?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Kwa kuwa anaewatukana wake wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam) anamtukana Allaah (´Azza wa Jalla). Kwa kuwa Allaah ndio ambaye
Kamchagulia wake hawa Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
14 Kuziwekea mafumbo; yaani kwa mfano badala ya kuthibitisha Sifa Tukufu za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kama ya Mikoni, Mguu na nyinginezo wao watu wa Bid´ah wanasema “neema”, “amri Yake” na taawili kama hizo. 15 Watu wanaofuata matamanio; yaani watu wa Bid´ah
69
Na vipi Allaah Atamchagulia Mtume Wake wake wenye kutukanywa? Hali
kadhalika anamtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vipi
atakuwa mke wa Mtume ambaye ni mama wa waumini juu yao kuna aibu au
kasoro? Na anakuwa katukana Ijmaa´ ya Ummah ambayo imekubaliana
fadhila za mama wa waumini, na kwamba wao ndio mama wa waumini, na
wake zake ni mama zao - hili lipo katika Qur-aan. Je, hivi kweli wewe
unaridhia mtu kumtukana mama yako? Mama yako wa nasaba huwezi
kuridhia mtu kumtukana, tusemeje mama yako katika Dini ambaye ni wake
wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Vipi utaridhie mtu
kumtukana? Mama yako wa Dini ni mkubwa kuliko mama yako wa nasaba na
hili halina shaka. Hakuna shaka ya kuwa, mwenye kukusudia kuwatukana
wake wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) - mwenye kukusudia hili
- basi huyo ni kafiri.
Hali kadhalika Maswahabah, mwenye kukusudia kuwaponda huyo ni kafiri.
Kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema:
ليغيظ بهم الكفاار
"Ili liwaghadhibishe makafiri." (48:29)
125. Kuwasikiliza Wapiga Visa
Swali:
Ipi hukumu ya kusikiliza wapiga visa kwa ajili ya kutengenemaa kwa kuwa
mimi siwezi kukaa kwenye duruus za elimu kwa Wanachuoni. Sifahamu
mustwalaha wa kielimu ya Kishari´ah ambao wanausema?
´Allaamah al-Fawzaan:
Usikae na wapiga visa. Salaf walikuwa wakihadhari dhidi ya wapiga visa
ambao wanajishughulisha sana na hadithi hata kama itakuwa ni uongo. Na
wanatumia nguvu nyingi kwa kupiga visa ambavyo wanadai vinaathiri watu.
Wala hawatumii nguvu zao katika Qur-aan na Sunnah. Msingi wao
umejengeka juu ya kupiga visa na hadithi. Salaf walikuwa wakihadhari watu
70
kama hawa na kuwasikiliza.
126. Kuanza Kuwalingania Ma´ulamaa Wapotofu Ni Bora Zaidi Kuliko Kuanza Na `Awwaam Wao
Swali:
Je, wanalinganiwa ma´ulamaa wapotofu kama wanavyolinganiwa
´Awwaam16 wao katika Rawaafidhw na Qubuuriyyuun?
´Allaamah al-Fawzaan:
Bila shaka. Da´wah ni wajibu sawa kwa ma´ulamaa wao na ´Awwaam wao.
Da´wah ni wajibu. Na lau wataongoka ma´ulamaa wao pia ´Awwaam wao
wataongoka, huenda wakatubu baadhi yao ikawa ni sababu ya kuongoka
wengi katika wafuasi wao. Kuanza kwa ma´ulamaa wao, bila ya shaka hili ni
bora kuliko kuanza kwa ´Awwaam wao.
127. Kuuliza Daraja Ya Hadiyth
Swali:
Mwenye kuuliza usahihi wa Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam) huchuliwa ni mwenye shaka na Hadiyth yake (´alayhis-Salaam)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Anayeuliza daraja ya Hadiyth, huyu ni kwa ajili anataka
kuhakikisha. Na hili ni wajibu kwake kuuliza na kujua usahihi wa Hadiyth
kama ni dhaifu, au ni maudhu´ah n.k. Huku ni kuhakikisha na si kuwekea
16 Watu wa kawaida wasiokuwa na elimu
71
shaka. Kuwekea shaka ni pale ambapo Hadiyth itasihi kisha akawa na shaka
maana yake na kuifanyia kazi. Akasema haifai Hadiyth hii katika wakati huu,
huyu ndiye mwenye kuwekea shaka na mpotofu. Allaah Atukinge. Ama
kutafuta daraja ya Hadiyth ili ahakikishe, hakuna ubaya wa hilo.
128. Asiyemuombea Du´aa Mtawala Wa Waislamu Ni Mtu Wa Bid´ah
Swali:
Je, ni sahihi yaliyosemwa na baadhi ya wanachuoni ya kwamba:
"Asiyemuombea Du´aa mtawala, hakika huyo ni mtu wa Bid´ah"?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Hili limethibiti kutoka kwa Salaf. Wamesema ukimuona mtu
hamuombei Du´aa mtawala, basi mtuhumu katika Dini yake. Nadhani hata
katika kitabu hichi [Sharh-us-Sunnah Lil-Barbahaariy] yamo tutayapitia.
129. Kutoka Siku 40 Ni Katika Bid´ah Za Suufiyyah
Swali:
Je, kuwalazimisha watu kutoka kwa ajili ya Da´wah siku 40, mwezi na miezi
40 ni katika kujikalifisha kunakolaumiwa au ni katika juhudi katika kheri?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hili ni katika Bid´ah. Haliwezi kuitwa kuwa ni kujikalifisha kunakolaumiwa
tu, bali tendo hili huitwa kuwa ni Bid´ah. Hizi ni katika Bid´ah za Suufiyyah.
Na hakuna katika Da´wah kutoka masiku, miezi 40 au kadha na kadha. Yote
haya ni katika Bid´ah ambayo Allaah Hakuteremsha chochote kuhusiana na
hilo.
72
130. Hadiyth Hii Inajuzisha Kutoka Na Jamaa´at-ut-Tabliygh?
Swali:
Wanatumia baadhi yao [Jamaa´at-ut-Tabliygh] kwa Hadiyth Swahiyh
isemayo:
"Kwa hakika huu ni mji muovu, akaenda katika mji mwingine ambapo
Anatiiwa Allaah"
Kujuzisha kutoka na Jamaa´at-ut-Tabliygh. Dalili hii ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mashaa Allaah!! Hadiyth hii iko wapi na Jamaa´at-ut-Tabliygh? Hii ni katika
Hijrah, hii ni safari ya Hijrah ewe ndugu. Na sio safari ya [... sauti haiko wazi...
], hii ni safari ya Hijrah. Katoka kama Muhaajir.
131. Kwenda Na Jamaa´at-ut-Tabliygh KufanyaDa´wah Katika Miji Ya Makafiri
Swali:
Ipi hukumu ya kutoka na Jamaa´at-ud-Da´wah17 kwenda kulingania katika
miji ya makafiri?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mwenye kutaka kufanya Da´wah atapata nafasi na alinganie kwa Allaah
sehemu yoyote bila yayeye kujiunga na kundi au chama. Ikiwa yuko na elimu,
alinganie kwa Allaah yeye mwenyewe bila ya kujiunga na makundi na
vyama, kwa kuwa mambo haya ndani yake kunaingia baadhi ya vitu, baadhi
ya mifumo - kama mnavyojua - alinganie kwa Allaah na wala asiwe
17 Jamaa´at-ut-Tabliygh
73
amejiunga na yeyote. Na wala hahitajii kutoka wala kuingia. Alinganie kwa
Allaah sehemu yoyote atapopata fursa.
132. Nikiingia Nyumba Na Hakuna Mtu Nitoe Salaam?
Swali:
Muislamu atoe Salaam atapoingia nyumba isiyokuwa na mtu hata mmoja?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, toa Salaam.
فإذا دخلتم بيوتا فسلموا على أنفسكم
"Mtakapoingia majumbani toleaneni salamu." (24:61)
Hii ni kwa jumla. Na nyumba haikosi Malaika, majini Waislamu n.k.
133. Radd Kwa Madu´aat Wanaojuzisha Kutibu Uchawi Kwa Uchawi
Swali:
Nataka bayana na kuwekewa wazi katika masuala ya hukumu ya kutibu
uchawi kwa kutumia uchawi mfano wake, kwa kuwa tumesikia baadhi ya
wanaodai wana elimu wakisema ya kwamba hilo linajuzu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kutibu uchawi kwa kutumia uchawi mfano wake haijuzu. Na ni kufuru. Kwa
kuwa uchawi ni kufuru sawa kujifunza nao na kuufunza na kuutumia. Sawa
autumia ili kutibu uchawi au kautumia ili kuwadhuru watu. Anasema
(Ta´ala):
74
حر وما أنزل على الملكين ببابل هاروت ياطين كفروا يعلمون النااس الس كنا الشا ـ ن من أحد وماروت وما يعلماول
ما نحن فتنة فل تكفر ى يقول إنا حتا
"Lakini shayaatwiyn ndio waliokufuru; wanafundisha watu uchawi na
yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili (katika mji wa) Baabil Haaruwt na
Maaruwt. Na (hao Malaika wawili) hawamfundishi yeyote mpaka
wamueleze: “Hakika sisi ni fitnah (mtihani), basi usikufuru (kufanya
uchawi)".” (02:102)
Yaani msijifunze uchawi. Ni dalili ioneshayo ya kwamba uchawi ni kufuru.
Mwisho wa Aayah Anasema:
من خلق اشتراه ما له في الخرة ولقد علموا لمن
"Na kwa hakika walielewa kwamba atakayenunua (atayefanya biashara ya
uchawi) hatopata katika Aakhirah fungu lolote." (02:102)
Yaani hana katika Pepo fungu. Na hili haliwi isipokuwa kwa kafiri. Allaah
Atukinge. Vipi atajitokeza mwenye kusema ya kwamba inajuzu kutumia
uchawi? Yaani mtu ajitibu kwa kufuru?
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:
"Msijitibu kwa haramu."
Na uchawi ni haramu kubwa.
Na Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) anasema - kama ilivyo katika
Swahiyh al-Bukhaariy:
"Kwa hakika Allaah Hakufanya dawa yenu katika yale Aliyowaharamishia."
Na uchawi ni haramu kwetu.
"Allaah Hakuteremsha ugonjwa ila Kateremsha dawa yake."
Uchawi una dawa isiyokuwa kufuru na uchawi. Maneno haya hafikirii [uzito
ulionayo] mwenye nayo, na lau angelifikiria sidhani kama angelijuzisha kwa
kukimbilia kutoa Fatwa kama hii. Tunamuomba kwa Allaah uongofu, al-
Baswiyrah, kurejea katika haki. Isitoshe, tukifungua mlango kujuzisha
wachawi kuwatibu watu tutabaki nao katika mji na uchawi ukaenea katika mji
kwa hoja ya kwamba mtu huyu anawatibu watu. Yaa Subhaana Allaah!
75
Hafikirii huyu matukio yake? Hivi kweli hamuogopi na kumcha Allaah
(Ta´aal) kwa kuwadanganya kwake watu kwa udanganyifu kama huu?
134. Kuswali Nyuma Ya Qubuuriyyuun18
Swali:
Inasihi kuswali nyuma ya waabudu wa makaburi kwa kuwa wanasema "Laa
ilaaha illa Allaah, Muhammad Rasuulu Allaah"?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haisihi. Kwa kuwa kuabudu kwao makaburi kunavunja kauli yao "Laa ilaaha
illa Allaah, Muhammad Rasuulu Allaah." Hivyo, si kila mwenye kusema Laa
ilaaha illa Allaah Muhammad Rasuulu Allaah anakuwa Muislamu isipokuwa
mpaka aifanyie kazi na ajitenge na yanayoivunja.
135. Kusoma Siyrah19 Ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum)
Swali:
Kusoma Siyrah ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na kujua
walivyokuwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) huchukuliwa ni
katika ukaribisho unaomkurubisha mtu kwa Allaah (´Azza wa Jalla)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Ni katika kujikurubisha na ni katika ´Aqiydah pia. Hili ni katika
´Aqiydah kwa kuwa katika misingi ya ´Aqiydah ni kuwapenda Maswahabah
18 Waabudu makaburi 19 Historia
76
wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na huwezi kujua
fadhilah zao na manzilah yao isipokuwa ukisoma Siyrah yao na hali zao.
136. Kusikiliza Visa Vya Tofauti Za Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum)
Swali:
Ipi hukumu ya kusikiliza visa kwa yaliyopitika baina ya Maswahabah
(Radhiya Allaahu ´anhum)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Usisikilize, kwa kuwa huenda ukaingiwa katika nafsi yako [na shubuha].
Usisikilize mikanda hii au ukasoma vitabu hivi. Jiweke navyo mbali. Ila tu
kwa yule mwenye elimu ya sawa sawa na anataka kuvipiga Radd, atavipitia
kwa dharurah au akasikiliza [mikanda] hiyo kwa dharurah ili aipige Radd.
137. "Shikamaneni Na ´Atiyq, Na Tahadharini Na Mambo Ya Kuzua"
Swali:
Yapi maoni yako kwa andiko hili:
"Shikamaneni na ´Atiyq, na tahadharini na mambo ya kuzusha."?
´Allaamah al-Fawzaan:
´Atiyq yaani waliokuwemo Salaf. Maana yake ni sahihi. ´Atiyq yaani ya
zamani waliokuwemo Salaf-us-Swaalih.
77
138. Kusema Neno "Sayyidna" Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anhu) Inajuzu?
Swali:
Kusema "Sayyidna" (bwana wetu) kwa Abu Bakr na Maswahabah wengine
waliobaki (Radhiya Allaahu ´anhum) inajuzu? Na je, kumekuja Hadiyth
kutokakwa Mtume (´alayhis-Salaam) inayosema: "Msiniite bwana katika
Swalah"?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ama kuhusiana na Hadiyth hiyo, mimi sijui. Ama kusema Sayyidna Abu
Hurayrah, Sayyidna Abu Bakr na kadhalika huku ni kuwatukuza na
kuwaheshimu. Halina ubaya In Shaa Allaah.
139. Kushahidilia Swahabah Fulani Kuwa Peponi Pasina Ushahidi
Swali:
Ikiwa tunashahidilia Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wote wako
Peponi, wamekufa waumini, Allaah Kawaridhia nao wamemridhia, kwa nini
tusimshahidilie mmoja wao binafsi ya kuwa yuko Peponi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hatushahidilii ila kwa dalili. Lakini tunasema kwa ujumla ya kwamba
Maswahabah wote wako Peponi, kwa ushahidi wa Allaah na Mtume Wake
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ambaye kafa katika Uislamu, ama
aliyeritadi ni katika watu wa Motoni.
140. Kusema Kuwa Pepo Au Moto Utaisha
78
Swali:
Anakufuru anayesema Pepo na Moto vitakwisha, au Pepo tu au Moto tu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Enyi ndugu! Mimi ninawanasihi kutoingia katika masuala haya. Ikiwa kuna
mwanachuoni yeyote aliyekosea na akaingia humo, usifuate jambo hili. Sisi
tunaamini Pepo na Moto, na kwamba vimeumbwa, na kwamba Pepo ni
nyumba ya wachaji Allaah na Moto ni nyumba ya makafiri. Ipi faida ya
kwamba vitaisha au havitosha? Hatuingii katika hili na wala hakuna faida
nyuma ya hili. Ikiwa kuna yeyote katika wanachuoni aliyekosea, sisi
tunamtakia Rahmah, kumuombea maghfirah na tunaacha maudhui haya na
wala hatuyaenezi kwa watu.
141. Kusema Kafiri Fulani Kafa Katika Ukafiri Na Ni Wa Motoni
Swali:
Swali hili limekariri. Akifa mtu na tunajua ya kwamba kafa kafiri, tushahidilie
kwa binafsi yake ya kwamba ni katika watu wa Motoni?
´Allaamah al-Fawzaan:
Unajuaje kuwa kafa kafiri? Unajua Ghayb? Pengine katubu na wewe hujui?
Unatakiwa kusema, yadhihirika kwangu ya kwamba kafa katika ukafiri,
yadhihirika kwangu kadha na ninakhofia kuwa kafa kafiri. Ama kuhusisha
kwa kusema kafa katika ukafiri, huku ni katika kudai kujua elimu ya Ghayb.
142. Kusema Fulani Kafa Shahidi
Swali:
79
Ipi kauli sahihi kwa kusema kwetu ya kwamba fulani ni shahidi? Kumekithiri
siku hizi kusema neno hili.
´Allaamah al-Fawzaan:
Hali kadhalika, hatuhukumu ya kwamba fulani ni shahidi ila yenye kuonesha
dalili. Ama wengine, sisi tunatarajia kwao Shahaadah. Tunatarajia na wala
hatusemi "ni shahidi", bali tunasema tunatarajia kwake Shahaadah. Kwa kuwa
kuhukumu ya kwamba ni shahidi, hili linahitajia kujua makusudio yake [ya
moyoni]. Je, anapigana kulinua Neno la Allaah? Vita hivi vinajuzu au hapana?
Si kila mwenye kupigana anaambiwa kuwa ni shahidi.
143. Ashaa´irah Ni Katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?
Swali:
Je, al-Ashaa´irah na Maaturidiyyah ni katika Ahl-us-Sunnah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mwenye kwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah sio katika wao. Na al-
Ashaa´irah wanategemea ´Ilm-ul-Mantwiq na ´Ilm-ul-Kalaam katika
´Aqiydah. Wanachukua ´Aqiydah yao katika ´Ilm-ul-Mantwiq, vipi watakuwa
ni katika Ahl-us-Sunnah? Upokeaji (utegemezi) wao sio kama Ahl-us-Sunnah.
144. Tunapenda Haki Zaidi Kuliko Fulani
Swali:
80
Je, inatakikana kwa wanafunzi kusambaza Radd ya mwanachuoni kwa yule
aliyemradi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa hili lina maslahi, ndio. Ikiwa kuisambaza hiyo Radd kuna maslahi ya
kutahadharisha madhehebu haya, au kauli hii, hilo halina shaka. Tunaipenda
haki zaidi kuliko fulani. Hatumlindi fulani au karama za fulani, kama
wanavyosema na kuiacha haki.
145. Kuridhia Qadhwaa20 Na Qadar21 Ni Wajibu
Swali:
Kuridhia Qadhwaa na Qadar ni wajibu au amustahaba22?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni wajibu. Kuridhia Qadhwaa na Qadar, ina maana kuviamini na kuviitakidi.
Ama kuridhia maradhi na kadhalika, hili si lazima ya wewe kuridhia maradhi.
Lakini unalazimika kusubiria hilo, ama kuridhia hilo hili halikulazimi. Lakini
subiria hilo na usikasirike na kulalamika.
146. Uwajibu Wa Kujirejea Unapokosea
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kufasiri kitu kwa kutegemea dalili kisha ikambainikia
ya kwamba tafsiri yake ni ya makosa. Lipi lililo la wajibu kwake?
20 Aliyopanga Allaah 21 Aliyokadiria Allaah 22 Jambo linalopendekezwa
81
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni wajibu kwake kurejea kosa lake. Na ikiwa kosa hili lilienea kwa watu,
inampasa kuwabainishia hili watu na kwamba amejirejea.
147. Kuongea Ni Katika Sifa Ya Allaah Ya Kimatendo
Swali:
Sifa ya kuongea kwa Allaah ni ya kidhati au kimatendo au ni yote mawili?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni kujikalifisha kulikoje huku? Inatosha kwako kusema, Maneno ya Allaah
(Subhaanahu wa Ta´ala) ni katika Sifa za matendo yake. Maneno ni katika Sifa
za matendo, aifanyayo wakati Atakapo (Subhaanahu wa Ta´ala) na kwa
namna Atakayo. Na wala hatuingii katika kupindukia kama huku.
148. Madu´aat Wasiolingania Katika Tawhiyd Wala Hawaonyi Dhidi Ya
Mubtadi´ah Na Bid´ah
Swali:
Muulizaji anauliza, jee dhawabiti hii ni sahihi:
"Yule ambaye halinganii katika Tawhiyd na wala haonyi dhidi ya Shirki,
Bid´ah na Ahl-ul-Bid´ah, (mtu huyo) ni Mubtadiy´23 na yule asiyembadiy´24 na
yeye ni Mubtadiy´ kama yeye"?
23 Mtu wa Bid´ah 24 Asiyemtia katika Bid´ah
82
´Allaamah al-Fawzaan:
Mtu huyu ikiwa anajinasibisha na Da´wah katika Dini ya Allaah na wala hajali
Tawhiydi na wala hajali Shirki na haonyi dhidi yake na kuhamasisha
kushikamana na Sunnah, huyu anakwenda kinyume na Manhaj ya Mitume
(´alayhis-Swalaat was-Salaam). Ni mbaya zaidi kuliko hata Mubtadiy´. Huyu
anakwenda kinyume na Manhaj ya Mitume (´alayhimus-Salaam). Kwa kuwa
Mitume walikuwa wakiijali ´Aqiydah na wakiibainisha na kuonya dhidi ya
Shirki. Wakabainisha hukumu za Kishari´ah na kuziweka wazi. Hii ndio
Manhaj ya Mitume na wafuasi wa Mitume (´alayhimus-Salaam).
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroos?tid_1=164
Swalla Allaahu ´alaa Muhammad, wa ´alaa aalihi wa Aswhaabihi wa sallam.