impressum kimechapishwa na pori la akiba la selous/idara ya

24
Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya Wanyamapori na Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiufundi la Ujerumani (GTZ) Dar Es Salaam 2005 GTZ, S. L. P. 1519 Dar Es Salaam, Tanzania Picha: Rolf D. Baldus, Vernon Booth, Rod East, Rudi Hahn, Doug Macdonald, Spike Williamson Mhariri: Dr. Rolf D. Baldus Tafsiri: David Kaggi ©Baldus/Siege Email: [email protected] Simu: 22-2866065 www.wildlife-programme.gtz.de/wildlife

Upload: tranliem

Post on 08-Jan-2017

539 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

ImpressumKimechapishwa na Pori la Akibala Selous/Idara ya Wanyamaporina Shirika la Ushirikiano waMaendeleo ya Kiufundi laUjerumani (GTZ) Dar Es Salaam 2005GTZ, S. L. P. 1519 Dar Es Salaam, Tanzania

Picha: Rolf D. Baldus,Vernon Booth, Rod East,Rudi Hahn, Doug Macdonald,Spike Williamson

Mhariri: Dr. Rolf D. BaldusTafsiri: David Kaggi©Baldus/Siege

Email: [email protected]: 22-2866065www.wildlife-programme.gtz.de/wildlife

Page 2: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Pori la Akiba la SelousRolf Baldus na Ludwig Siege

Page 3: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

2

Page 4: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

3

Page 5: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Mpaka sasa, kijitabu cha Mwongozo wa usafiricha Selous kimekuwa kikipatikana kwenye lughaya Kiingereza pekee. Toleo la kwanza lilichapish-wa mwaka 1989 na kufuatiwa na matoleo yaliy-ofuata baada ya kupitiwa kikamilifu yalichapish-wa mwaka 1999 na 2002.Makala hizi zimekuwa zikilenga soko la kitalii lanje ya nchi hali kadhalika wageni wataalamwalioko hapa nchini Tanzania. Nakala zipatazo15,000 zimekwisha chapishwa hadi kufikiawakati huu, na toleo la kijitabu kipya cha muon-gozo wa safari liko kwenye maandalizi. Lakinimpaka sasa hakuna mwongozo kwa lugha yaKiswahili. Kijitabu hiki kinaziba pengo hili nakutosheleza mahitaji ya wageni wanaozungumzaKiswahili ambao hutembelea Selous hasa vijana.Tunadhani kwamba hiki kitakuwa kijitabu chakwanza cha mwongozo cha usafiri katika lughaya Kiswahili kwa maeneo yanayohifadhiwa kis-heria nchini Tanzania.

Imekuwa ni nia kubwa ya menejimenti ya Pori laAkiba la Selous ikishirikiana na Mpango waKuhifadhi Pori la Akiba la Selous (SCP), kuinuahali ya soko la utalii wa ndani kwa wananchinchini Tanzania. Kwa bahati mbaya , watanzaniawengi wanashindwa kusafiri kwenda Selous kwasababu gharama za usafiri ni za juu mno kiasicha kufanya watanzania kushindwa kuzimuduingawaje viingilio wanavyotozwa Watanzania nividogo mno kulinganishwa na vile wanavyotoz-wa watalii toka nchi za nje..

Kwa muda usiopungua miaka kumi hadi leo,uongozi wa Selous umekuwa ukiwakaribisha nakuwapa fursa wananchi na hasa wanafunzi washule na taasisi mbalimbali kulitembelea eneohilo. Majengo na huduma mbalimbali za kukidhimahitaji ya wageni zimewekwa huko Matambweambako ndiyo makao makuu ya Selous.

Serikali ya Ujerumani imekuwa ikisaidia uhifadhiwa Pori la Akiba la Selous, kupitia shirika lake laUshirikiano wa Maendeleo ya kiufundi (GTZ)kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitiamradi wa Mpango wa Uhifadhi wa Selous.Utoaji wa kijitabu hiki cha mwongozo umewe-zekana kwa msaada wakifedha kutoka GTZ.Tunawashukuru R.H.Hall, G.Mnjeja, P.M.Ngoti naH. Ramadhani kwa kupitia kijitabu hiki.Kijitabu hiki kimetunukiwa kwa askari wa wanyama pori wa pori la Akiba la Selous na askariwa wanyamapori wa vijiji vya Eneo la Jumuiya laHifadhi ya Wanyamapori (WMA) nje ya pori laAkiba la Selous.Rolf D. Baldus (GTZ), Benson Kibonde (Muhifadhimkuu Pori la Akiba la Selous) na Ludwig Siege(GTZ).

Dibaji

4

Page 6: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Likiwa na eneo lipatalo kilometa za mraba48,000 au asilimia tano ya eneo la nchi kavu yaTanzania, pori la akiba la Selous ni moja ya mae-neo makubwa yaliyohifadhiwa hapa ulimweng-uni.Ni pori kubwa kuliko yote hapa Afrika na lenyemaji ya kutosha kiasi kwamba uwezekano wamakazi ya binadamu ungekuwepo.Ukweli huu unalifanya pori hili kutofautiana namaeneo mengine makubwa yaliyohifadhiwahapa Afrika kama vile Namib-Naukluft lililokoNamibia ambalo sehemu yake kubwa ni jangwa.Ukubwa wa eneo unastaajabisha, ni kubwa kuli-ko nchi ya Switzerland au Denmark, hakunamakazi ya watu, na mwingiliano au mguso wawanadamu ni kidogo sana.Wageni wanaolitembelea pori hili hujisikia kuwakwenye nyika asilia mbali na maeneo yaliyozoeamapito ya kitalii. Wanyamapori waliopo hapo niwakushangaza, makundi ya wanyama (nyati,tembo, viboko, mbwa mwitu na mamba) nimakubwa kuliko yote hapa Africa. Mfumo wamito na maziwa ni wa kipekee hapa Afrika yaMashariki.

Hakuna mahali pengine ambapo mtu anawezaakafanya safari za mashua (mitumbwi) kupitiamkusanyiko wa wanyamapori wa kushangazakama ilivyo ndani ya pori hili. Ndani ya Selouskuna aina 440 za ndege hivyo kufanya eneo hilikuwa sehemu maaalum kwa wapenzi wa kuan-galia ndege.Pori lina maeneo aina kwa aina yakiwemo mae-neo wazi yenye nyasi fupi, misitu ya miombo,hali kadhalika misitu kando kando ya mito.Mabwawa ni sehemu muhimu kwa maisha yamimea ya ardhi oevu, jamii ya mijusi namakazi ya ndege wanaohama hama. Likiwa naeneo kubwa la misitu ya miombo kunalifanyapori la Selous kuwa eneo kubwa la misituiliyohifadhiwa. Umoja wa Mataifa ulilipa Pori laSelous hadhi ya kuwa eneo la Urithi waUlimwengu (World Heritage Site) kwa sababulina ikolojia ya kipekee.Pori la Selous ndilo pekee hapa Africa lililobakiakatika hali halisi ya asilia. Kutokuwepo kwashughuli kubwa za Utalii kunachangia kuwepokwa hali ya nyika. Ili kuhifadhi mazingira hayona vile vile kuzuia utalii mkubwa, ni utaliimdogo unaodhibitiwa ndio unaoruhusiwa.

Kwa nini pori la akiba la Selous ni eneo maalum?

5

Page 7: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Maelezo ya mfumo waikolojia

Sehemu kubwa ya eneo la kanda ya kaskazini yaSelous imetengwa kwa matumizi ya utalii wapicha. Ni moja ya maeneo mazuri na yenyewanyama wengi kupita maeneo mengine yamfumo mzima wa ikolojia. Kanda hii imepakanana reli ya TAZARA kwa upande wa kaskazini,mashariki ni mpaka wa pori lenyewe na kwaupande wa magharibi ni Stiegler's Gorge pamojana barabara iendayo Matambwe na kwa upandewa kusini mpaka ni mto Rufiji. Eneo hili ndilolinaloelezewa ndani ya kitabu hiki cha maelezo.Maeneo mengine ya upande wa kusini wa mtoRufiji na Ruaha hayajaendelezwa kwa shughuliza utalii wa picha. Robo tatu ya pori la Selous nimisitu ya miombo iliyojaa miti aina ya mitundu,muwa, mininga na milama. Magharibi mwa porini mbuga za nyasi pamoja na miti ya mitagalala,nyasi fupi na tambarare zinazopata mafurikokwa nyakati za mvua - sehemu hizi hujulikanakama "mbuga" au udongo wa mfinyanzi - sehe-mu ngumu kwa waendao kwa magari nyakati zamvua. Uoto huu (savannah) huwa ni malishomazuri kwa wanyama aina nyingi hasa nyumbu.Makundi mbali mbali ya wanyama huonekanakwenye maeneo haya mara kwa mara .Misitu ya mabondeni na vichaka visivyoingilikavya Pori la Selous huwa maficho mazuri yawanyama.Mto mpana wa Rufiji na muelekeo wake wakuzunguka zunguka hali ambayo inafanya kuwana maeneo mengi ya ardhi oevu za maziwa namabwawa na vijito/makorongo, ni moja yamfumo wa ikolojia wa ajabu katika eneo lote lamashariki mwa Afrika.

Mikoche yenye urefu hadi mita 25 hukua kandokando ya mto Rufiji, aina hii ya mimea huhitajimaji mengi na hufa kama maji yanapungua sanaardhini. Uoto huu wa Rufiji ni makazi ya ainambali mbali za wanyama kama tembo, viboko,mamba, wanyama wenye kwato na ndege.Miombo ina uwezo wa kuhimili ardhi isiyo narutuba na mvua chache. Wastani wa mvua nikati ya millimita 750 kwa upande wa masharikihadi millimita 1300 upande wa magharibi. Mvuazinanyesha tokea mwishoni mwa Novemba hadiDesemba na kufuatiwa na kipindi cha jua(ukame) miezi ya Januari na Februari na kuende-lea tena hadi Mei. Miombo ni misitu iliyoreke-bishwa kwa karne nyingi na mioto inayotokeakila mwaka au inayoanzishwa na wavuna asaliau wawindaji. Nyakati za ukame kuna hali kamavile pori zima la Selous linaungua. Maeneoyanayochomwa mapema huota majani na nyasichanga na wanyama hupata malisho. Maeneoyanayochelewa kuungua huota nyasi nyakati zamvua tu. Mioto hii ya kila mwaka huzuia ukuajiwa miti, lakini miti mingi ya miombo haifi kwamoto. Kuna ubishani tofauti kuhusu mioto hiikwa vile inaonekana kudhuru mimea na viumbewadogo, hivyo kudhani kwamba ni lazima kujari-bu hatua za kuzima mioto hii. Wengine husisitizakwamba mioto hii ni lazima kutokea na ni sehe-mu ya mfumo wa ikolojia. Kwa sababu hii miotohuanzishwa na (menejimenti) utawala wenyewekwa vile inafikiriwa kwamba ni vema kuchomamoto mapema ili usidhuru zaidi uoto kamamioto inayotokea nyakati za ukame ambaponyasi zote ni kavu na ni wakati wa joto kali.

6

Page 8: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Wanyama wenye ngozi neneMkazi muhimu wa misitu ya miombo ni mbung'oambaye ingawaje hana madhara kwa wanyamapori lakini ni muuaji wa ng'ombe. Mbung'oamezuia au kukatisha tamaa makazi ya binada-mu na mifugo ndani ya Selous.Wahifadhi wengine husema mbung'o ni mlinzibora wa wanyamapori.

Pori la akiba la Selous linajulikana sana kwakuwa na tembo wengi. Kwa bahati mbayakutokana na mfululizo wa ujangili wa biasharaya meno, hadi ilipofikia mwanzoni mwa miakaya tisini (1990), hesabu ya tembo ilipunguakutoka 110,000 ilivyokuwa mwaka wa 1976 nakufikia chini ya tembo 30,000 ilipofikia 1989.Mafanikio ya hatua za ulinzi wa uhifadhi kuto-kea mwaka 1989 yamewezesha ongezeko latembo kufika 55,000 ilipofika mwaka wa 1998.Zaidi ya asilimia hamsini ya tembo wote waTanzania wapo Selous. Ni wapi pengine tembowangeweza kuishi kama siyo hapa?Sio mara nyingi tembo kuonekana wakiwa kwe-nye makundi makubwa sana ndani ya Selous,bali tembo huonekana wakitembea kwa vikundividogo vidogo vinavyoongozwa na kiongozi.Madume ya tembo hupendelea kukaa ndani yavichaka lakini hujiunga na makundi ya kike mara kwa mara.Ujangili uliokithiri mnamo miaka ya themaniniumesababisha kuwepo kwa tembo wachachewenye meno makubwa, makundi machache yamadume na tofauti kubwa ya mfumo wa marika.

Tembo wa rika ya miaka 30 ni wachache.Madume wenye meno ya uzito wa ratili 80 na zaidi wanaongezeka kidogo kidogo na hawa-patikani sana. Tembo wanatengeneza mazingiraya mahali wanapoishi. Misitu ya miombo huwana wanyama wachache lakini wapitapo tembohuvunja matawi na miti na kuwezesha kuwepokwa nafasi wazi. Uwazi huu huwezesha nyasi naaina nyingi za mimea ambayo hufanya uwezek-ano wa mchanganyiko wa malisho ya aina mbalimbali za wanyama, hivyo kuleta ongezeko lawanyama aina mbali mbali. Kwa hiyo kilekinachoonekana kwamba ni tabia ya tembo yauharibifu wa mazingira ndicho kinachojengahatua na tofauti mbali mbali za uoto wa mimea.Tembo ni mtengenezaji wa uoto wa miombo namaeneo ya uwazi (savannah) ya Selous hivyobasi kama mnyama huyu atatoweka si ajabuuoto utabadilika na aina nyigine ya mimea itaa-thirika. Ingawaje tembo ni wanyama wa pole nilazima watu wawe waangalifu na wasi wakari-bie karibu.Kama dume mdogo wa tembo au kiongozi ana-chezesha masikio yake, anasimamisha mkonga na anasonga mbele, kwa kawaida ana-jifanya kutishia ila kama kuna adui. Yatakamoyo kukutana na tembo anayetishia. Askariwanyamapori wenye uzoefu ndio wanaowezakutambua kama tembo anatishia tu au amekasi-rika. Inashauriwa kuwa mwangalifu.Vifaru weusi ndio walioathiriwa na ujangili zaidiya aina nyingine zote za wanyamapori waSelous.

7

Page 9: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Wanyama wenye ngozi nene

Jina faru mweusi linapotosha sana kwa sababusiyo mweusi kuliko faru mweupe anavyoitwamweupe. Faru mweusi ana mdomo wa juu uliopinda kama ndoano unaomuwezesha kulamajani ya miti. Faru mweupe ana mdomo wamraba hula nyasi na hapatikani hapa Tanzania.Faru jike ni mzito kuliko dume, uzito wake unafikia kilo 1,300. Faru weusi hutembea mmojammoja siyo kama faru weupe wanaotembeawawili wawili au kwa makundi.Kinachoonekana kuwa pembe, siyo pembe halisiila ni nywele nyingi zilizosukana na kugandamanabila kuwa na kiini cha pembe.Ikitokea kuvunjika inakua tena. Ushauri wakuwakata faru pembe iwe njia ya kuwa kingadhidi ya ujangili uliwahi kutolewa. Kilicho sabab-isha ujangili wa faru ni biashara kubwa ya vipu-sa.Huko Asia kuna mahitaji makubwa ya vipusaambavyo hutumika kwenye dawa za kiasili zina-zotumiwa kuponyesha magonjwa mbali mbali yahoma na hata yale ya moyo. Ni mara chachesana vipusa vinatumika kwa dawa zakuongeza nguvu za kiume kama wengi wanavy-odhania. Soko kubwa la vipusa liko Yemen yakaskazini ambako hutumiwa kwa kutengenezeamipini ya majambia kitu ambacho humfanya mtumwenye jambia la namna hiyo aonekane kuwatajiri na mwenye uwezo.Biashara ya aina yo yote inayotokana na mazaoya faru ilifungiwa toka mwaka 1973 kwa mujibuwa mabadiliko ya biashara ya kimataifa ya viumbe na mimea iliyo hatarini kutoweka (CITES).Kufungwa kwa biashara ya vipusa hakukusaidiakuokoa maisha ya faru kwa vile majangili

walilipwa fedha nyingi sana kwa vipusa, kitu ambacho kiliwafanya waongeze juhudi zao zakuua faru. Mwanzoni mwa miaka ya themaniniidadi ya faru waliokuwemo ndani ya Selouspamoja na maeneo yanayolizunguka pori,ilikadiriwa kuwa faru 3,000. Idadi hii ilikuwandiyo kubwa zaidi kuliko idadi ya faru waliokuweko kwenye maeneo mengine hapaAfrika. Faru hawa wasioona mbali na mara nyingiwenye hasira, walikuwa wanaonekana kwaurahisi karibuni kwenye maeneo yote ya Selous.Sasa hivi wamebaki wachache sana na wanajifichakwenye maeneo yenye vichaka vinene. Juhudi zapamoja za utawala wa Selous, GTZ, WWF wakishirikiana na mwekezaji wa hoteli ya kitalii,zimeleta ongezeko la faru ingawaje ni kwa haliya pole pole.Sasa hivi kuna uwezekano wa kuona faru kwenyemaeneo ya utalii. Faru anapoonekana pahalipopote ni lazima taarifa itolewe na ikiwezekanaipigwe picha. Picha zinasaidia kutambua farummoja mmoja na kuwezesha utawala wa Selouskuweka hesabu ya ongezeko na idadi ya faru.Faru hutambulika kwa kuangalia tofauti yaumbile la vipusa vyao na mkato wa masikioambayo kila faru ana namna ya pekee. Njia nyingine ya kuwatambua ni kutumia DNA kwakupima kinyesi. Kwa kawaida kinyesi kina masa-lia ya malisho ambayo yana alama za jini (gene-tic finger prints) ambazo huwezesha kumtambuafaru anayehusika na kinyesi hicho. Ujangili wafaru ulikoma mwaka 1990. Faru kidogo walisaliaambao kwa hivi sasa wameanza kujitokeza kwenye maeneo ya wazi nyakati za mchana.

8

Page 10: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Wanyama wenye ngozi neneFaru wadogo na wa makamu wanaonekana,nyakati nyingine vidume vidogo vimeonekanavikitembea kutafuta malisho kwenye maeneo yambali kutoka maeneo yao ya makazi. Matokeoyote hayo yanatutia tumaini kwamba faruwataendelea kuishi ndani ya Selous. Mnyamamwigine mwenye uzito mkubwa ni kiboko.Kiboko hupatikana kwa wingi ndani ya mito namaziwa ya Selous. Kwa hivi sasa kuna vibokowapatao 40,000 ndani ya Selous. Idadi hii hufiki-riwa kuwa kubwa kuliko uwezo wa makazi yakendani ya Selous hivyo kupelekea kuweko kwavifo vingi nyakati za mwisho wa vipindi vyaukame, kwa sababu ya kukosa malisho. Vibokohupendelea kukaa ndani ya maji nyakati zamchana lakini usiku hutoka na kutembea nchikavu kutafuta chakula. Viboko huonekana waki-wa kwenye vijito vidogo na hata kwenyemadimbwi yaliyoko mbali na mito. Viboko wana-weza kuzama ndani ya maji zaidi ya dakika tano.Kundi la viboko huweza kuwa na fujo ndani yamaji, lakini hata wanapoelekea kusogeleamtumbwi, huwa ni vitisho tu. Ikiwa wanatakakushambulia hasa, huzama na kufanya masham-bulizi chini ya mtumbwi kwa kuusukuma juu.Madume hushambuliana sana na ni kawaidakuona dume akiwa na makovu na hata madondamabaya .

9

Page 11: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Meno na makucha - Wanyamawalao nyama

Pori la akiba la Selous lina idadi kubwa ya simbawapatao 3,000 hadi 4,000. Hawa huwa wapokaribuni kila mahali katika maeneo ya kanda yakaskazini mwa Selous kwenye eneo la utalii wapicha, hasa kando kando ya maziwa na eneo laBeho Beho. Kutokana na hali ya uoto wa misituna vichaka vilivyopo, inakuwa siyo rahisi simbahawa kuonekana kama ilivyo kwa simba waNgorongoro na Serengeti. Utafiti umeonyeshakwamba kuna makundi 11 yenye simba wakub-wa 80 na watoto 20 wanaoishi kando kando yamto Rufiji.Ngurumo za simba zinazosikika hata kwa umbaliwa kilometa 8 huwa ni jambo la kawaida nyakatiza usiku, zinatisha kwa mtu ambaye yuko ndaniya hema anaposikia simba anakaribia. Tofauti naimani iliyopo kwamba simba huogopa moto,ukweli ni kwamba simba hawaogopi moto nainashauriwa kwamba mtu anapopiga kambiporini, asitoke na kutembea tembea nyakati zagiza. Hema lililofungwa ni salama sana hatakama kundi la simba litaamua kukaa mbele yahema.Wanyama wengine kama vile nyoka na mambawanahusishwa na imani mbaya, lakini simbahuhusishwa na alama ya ukuu - mfalme wawanyama wote, mkuu wa himaya ya wanyama.Simba wana tabia ya simba na siyo kama watuwanavyowadhania. Kama wakipewa nafasiwataiba windo (mzoga) la mnyama mwinginemla nyama kuliko kuwinda wao wenyewe. Jikendiye anayefanya uwindaji lakini dume anakuwawa kwanza kula na halafu anafuata jike. Watotondio wanaokuwa wa mwisho kula.

Ikitokea kwamba kuna uhaba wa mawindo,watoto wanaweza kubaki na njaa kwa sababusimba wakubwa wakiwemo mama zao hawawa-bakishii chochote. Watoto wanaweza kufa kutok-ana na kutelekezwa na mama zao au kuuawa namadume mageni yanayohodhi mama zao.Kwa kawaida simba hawana adui zaidi ya wana-damu ingawaje mara chache fisi anaweza akalawatoto wa simba. Simba hufanikiwa katikauwindaji wake, huwinda wanyama kutokeaswala hadi nyati. Inapotokea kwamba simbaamepata mnyama mkubwa, humvuta chini mny-ama, hung'ata shingo na kuinyonga. Kundi lasimba hujumuisha majike na watoto wao, madu-me hujiunga nao kwa miezi au miaka kadhaahadi inapotokea kwamba dume wageni wana-waingilia na kuwafukuza. Ugomvi wa madumeni jambo la kawaida nyakati nyigine vifo huto-kea kwa wale wanaoshindwa.Simba hawapendwi na watu wanaoishi kandok-ando ya Selous kama vile wanavyopendwa nawatalii. Miaka mingine wanavijiji wapatao 40huuawa na simba kwenye maeneo ya karibu napori la akiba ukiachilia vifo vinavyotokana namamba, viboko na tembo. Kwa ujumla nchinzima ya Tanzania hupata vifo vya watu wapa-tao 200-300 kila mwaka kutokana na wanyamawakali, huu ni ushahidi mwingine unaodhihirishakiasi cha nchi inavyojitoa mhanga kwa ajili yauhifadhi. Kwa bahati nzuri hakuna maafa yaliyo-wapata watalii waliotembelea Selous hadi sasa,lakini ushauri wa kuwa waangalifu hasa kwawatalii waendao kwa miguu unasisitizwa.

10

Page 12: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Meno na makucha - Wanyama walao nyamaChui hawaonekani mara kwa mara kwa sababuhawa ni wanyama wanaotembea usiku na hud-haniwa kwamba chui ni wachache sana. Hivisivyo ilivyo ndani ya Selous, ukweli ni kwambani wengi kuzidi simba.Chui hawatembei au kukaa kwa vikundi hivyo nibahati kuona chui kwa vile hujificha mmojammoja. Fasheni ya uvaaji wa makoti ya ngozi zachui imekwisha kwa hiyo chui hawa hawauwawisana kama ilivyokuwa zamani, kwa sababu hiichui hawapo katika fungu la wanyama waliomohatarini kutoweka.Chui wana uwezo wa kuishi kwenye aina zoteza mazingira ya Selous lakini wanapendeleakukaa kwenye uoto mnene na vichaka.Wanaweza kuishi karibu sana na makazi yawatu. Mara kwa mara inatokea kwamba wanakamata kuku ndani ya kambi ya Matambwe.Chui ni mwindaji hodari na anaweza kukamatamnyama ye yote wa ukubwa kufikia pongo.Ingawaje chui wanapenda pia kula samaki,wadudu na ndege, nyani/kima ni chakulawanachopenda sana. Mara nyingi chui hupan-disha mizoga ya mawindo yao hadi juu kwenyepanda za matawi ya miti na baadae kurudi kula.Ukiona mikwaruzo ya kucha kwenye magambaya mti basi ujue chui wapo maeneo hayo.Duma nao huonekana kwenye maeneo ya kandaya kaskazini mwa Selous. Duma ni adimu lakiniwamepata kuonekana mara nyingi miaka ya hivikaribuni. Huenda ikawa misitu ya miombo siyomakazi mazuri ya duma na labda wameathirikakutokana na kuwepo kwa ushindani kutoka kwawanyama wengine walao nyama.

Hii inaweza kuwa sababu mojawapo ya kutoku-wepo wingi wa mbweha wa miraba mirabaambao hawaonekani kwa makundi makubwa.Mbwa mwitu wa Afrika wanatoweka japo nijamii inayolindwa kwa mujibu wa sheria yaCITES. Inakadiriwa kwamba ni mbwa mwituwapatao 2,000 hadi 4,000 tu ndio waliosalia.Makazi yao ya asili yanaharibiwa na wakulimana wafugaji.Kwa hivi sasa wametoweka huko Serengeti pen-gine ni kwa sababu ya ushindani kutoka kwa fisiwa madoa madoa na simba ambao ni wengi nakwa sababu ya magonjwa yanayoambukizwa nambwa wanaofugwa na wachungaji wa mifugo.Kwa upande mwingine mbwa mwitu wa Selouswanaendelea kuishi na kuongezeka. Idadi iliyo-tokana na mtafiti aliyefanya utafiti kwa mudawa miaka mitano inaonyesha kwamba kunambwa mwitu wapatao 1,300 pamoja na watoto.Mbwa mwitu 900 kati ya mbwa 1,300 niwakubwa. Hata hivyo kuna mbwa mwitu wengi-ne wanaoishi katika maeneo mengi ya mfumowa uoto huu, kwa mfano kuna mbwa mwituwapatao 140 ndani ya Hifadhi ya Mikumi naidadi nyingine isiyojulikana kwenye maeneoyanayohifadhiwa na wanavijiji (WMA). Idadi hiiya mbwa mwitu ndiyo iliyo kubwa na ya umuhi-mu sana hapa barani Afrika na Selous ndipomahali pekee mgeni anapoweza kupata nafasiya kuwaona mbwa mwitu. Wanapoonekanahuwa hawaogopi watu na hivyo huwa jambo laurahisi kuchunguza undani wa maisha yao kija-mii kwa karibu zaidi.Katika maeneo ya utalii, wingi wa mbwa mwituni 1 kwa kila kilometa za mraba 17 (ni pamoja

11

Page 13: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Meno na makucha - Wanyamawalao nyama

na watoto) au mbwa mkubwa 1 kwa kila kilo-meta za mraba 25. Hii ni idadi iliyo kubwa kulikopahali pengine popote hapa Afrika. Sehemunyingine za Selous ambako uwiano wa wanyamakwa chakula ni wachache na hali ya mazingirahairuhusu kuona mbali, wingi wao ni mbwa 1kwa kila kilometa za mraba 56. Kwa kawaidambwa mwitu hukaa kwenye makundi ya mbwawapatao 20. Kundi kubwa sana lililowahi kuo-nekana lilikuwa na mbwa mwitu 56.Mbwa mwitu ni wawindaji hodari na hupatamawindo yao kikamilifu, hali hii ukichanganyana ukweli kwamba hawadhuriwi na wanadamundio maana wanaishi vizuri.Mbwa mwitu walioko Selous wanajilinda vema,hawazembei, pia hawapotezi chakula kingi, ilakiasi cha 2% kinacholiwa na fisi madoa, si kamambwa mwitu wa hifadhi nyingine.Mbwa mwitu wa Serengeti hupoteza 86% yachakula chao kwa fisi.Mbwa mwitu hutegemea sana macho yao kuonambali na huwinda nyakati za mchana tu.Mawindo hutanguliwa na vitendo vya kulamba-na hadi midadi ipande na ukisikia kubweka basiujue tayari kazi ya kuwinda iko tayari.Mbwa mwitu wana uwezo wa kukamata mnya-ma mkubwa kama vile pundamilia. Mbwammoja au wawili wanamzingira mnyama nakumuuma mnyama huyo puani na kushikilia,huku mbwa wengine wanashambulia kwa kupa-sua tumbo na kutoa matumbo. Mbwa mwitu niwadogo na hawana uwezo wa kuua mnyamamkubwa kwa kung'ata mara moja, hivyowanaua kwa kumuuma mnyama mara nyingisana.

Kwa tabia yao hiyo watu wanaona kwamba nimauaji ya kikatili, hivyo huwaonea na kuwas-hambulia kila walipokuwa wanawaona. Hadimiaka ya themanini hata wahifadhi maarufuwalikuwa wanawaua mbwa mwitu kila wanapo-waona ndani ya hifadhi kwa kuwachukuliakwamba ni waharibifu na adui wa wanyamawengine. Kwa ukweli ni kwamba mbwa mwituni wachache sana ukilinganisha na wanyamawengine walao wanyama kama vile simba, chuina fisi hivyo wasingekuwa na madhara makub-wa hata kama mawindo yangekuwa machache.Mawindo hayawi machache kwa kuuawa nawanyama walao nyama, ila huathiriwa na ukose-fu wa malisho yao. Huwa ni mbwa jike mmoja tukatika kundi anayezaa na huzaa kiasi cha wato-to 12. Kundi zima hushirikiana kulea watoto,mbwa mmoja hubaki kwenye pango na kulindawatoto wakati mbwa wengine huenda kuwinda,wanaporudi kutoka mawindoni hutapika chakulana kuwalisha watoto.Fisi madoa hutembea usiku tu lakini mtu mwe-nye macho makini anaweza kuwaona fisi nyakatiza mchana wakiwa wamepumzika vichakani aukwenye shimo.Si kweli kwamba fisi hula mizoga tu au mabakiyaliyoachwa na simba. Fisi ni wawindaji hodaripia na mara nyingi simba hula mabaki yamawindo ya fisi. Fisi wana mbio kiasi cha kilo-meta 60 kwa saa na wanaweza kufuatia windolao kwa mwendo mrefu sana.Kutokea enzi za mwana falsafa Aristotle iliamini-ka kwamba fisi huwa mnyama mwenye jinsiambili yaani kiume na kike. Viungo vyao vya uzazihufanana ingawaje kwa majike ni vikubwa na

12

Page 14: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Wanyama wenya kwato

kwa madume ni vidogo lakini ni vigumu kuto-fautisha kati yao wanapokuwa mbali. Wanaishikwenye koo kubwa na majike huwa wengi.Majike hutafuta chakula hadi umbali wa kilome-ta 100 na wanaweza kurudia watoto wao baadaya siku 2 hadi 3. Fisi anaweza kuonekana akiwapeke yake lakini bado ni sehemu ya ukoo fulanina huwasiliana kwa kuitana.Wito wao unaoanzia kwa sauti ya chini nakumalizikia kwa sauti kali ya juu ni milio yakawaida nyakati za usiku hapa Afrika. Wageniwanatishika sana. Fisi ni wengi ndani ya Selousna wingi wao unazidi wingi wa simba kwa eneo.

Pori la akiba la Selous ni makazi ya idadi kubwaya nyati hapa Afrika. Sensa ya 1998 inaonyeshakwamba kuna kiasi cha nyati zaidi ya 110,000.Kuona kundi kubwa la mamia ya nyati likijakunywa maji kwenye mto Rufiji nyakati za jionini jambo lisiloweza kusahaulika. Makundi kamahaya huonekana kama vurugu lakini kwa kwelihuwa yana mshikamano wa mfumo wa kijamii.Nyati wakubwa na wenye nguvu au majikeyenye watoto huwa mbele ya kundi, hivyo kupa-ta malisho mazuri siku zote. Wanyama waliokonyuma ya kundi ni wale walio na hali ya unyon-ge. Jike anayelea anaweza kuwa kiongozi lakiniinampasa arudi nyuma baada ya kumalizamalezi (unyonyeshaji). Kundi kubwa linakuwakinga nzuri dhidi ya wanyama wengine walaonyama kama vile simba, mbwamwitu, n.k.Vikundi vidogovidogo vinakuwa hatarini kus-hambuliwa na simba kwa urahisi.

Kwa kawaida madume wakubwa huchanganana kukaa pamoja na majike kwa muda wakatiwa kulea kwa vile huwa wanapoteza nguvunyingi wakati wa kupanda na ugomvi na madu-me wengine. Wanajitenga na kundi la majike ilikupata afya na nguvu kabla ya kurudi na kuji-unga tena na majike hao. Nyati wa jinsia zotewana pembe, ila zinatofautiana kwani pembe zamadume huwa pana kuliko za majike. Pembe zamajike ni nyembamba na mashina yao siyomakubwa, ni rahisi kutofautisha kati ya madumena majike.Nyati ni walaji wa nyasi lakini matumbo yaoyana uwezo mkubwa wa kusaga malisho kulikowanyama wengine wasiokula nyama hapaAfrika ya Mashariki, wanao uwezo wa kula hatamimea yenye vitawi na majani madogomadogo(fibrous plants) ambayo wanyama wenginehawana uwezo wa kusaga. Simba ndio maaduiwakubwa wa nyati.Kabla ya karne hii, nyati walikufa kwa wingikutokana na mlipuko wa kimeta kilichoambukiz-wa na ng'ombe walioletwa na wataliani hukoEritrea kwa ajili ya kampeni yao ya Ethiopia.Mlipuko wa ugonjwa huo ulitanda bara zima laAfrika kutoka kaskazini hadi kusini na kuuanyati wengi na wanyama wengine wenye kwato.Nyumbu wa Selous ambao hujulikana pia kamanyumbu wa Nyasa huwa wana rangi ya kijivu-manjano na videvu na mikia myeusi. Jina hilolinatokana na ukweli kwamba hapo zamaniwalikuwa wanapatikana huko Nyasalandambayo sasa ni Malawi hadi Msumbiji na kusinimwa Tanzania. Kwa sasa hivi aina hii ya nyumbuwapo kwenye pori la akiba la Selous.

13

Page 15: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Wanyama wenye kwato

Wanatofautiana sana na nyumbu wa aina nyin-gine kwa rangi na ukubwa wa mwili. Wanautepe mweupe puani. Jambo la kushangaza nikwamba nyumbu wote waliopo kusini mwa mtoRufiji wana alama hii, ambapo nyumbu wa kas-kazini mwa mto eneo la utalii wa picha niwachache tu au asilimia 1 ndio wenye alama hii.Kongoni wanapendelea kuishi kwenye misitu yamiombo lakini huwa wanaonekana mbuganikando kando mwa barabara iendayo Kinyanguru.Pembe zao zinawatofautisha na Kongoni ainanyingine wa hapa nchini. Pembe hizi zina nchakali na zina umbo la herufi "S" na ni nene nafupi zikilinganishwa na pembe za Kongoni wen-gine. Kongoni wa aina hii hupendelea kutembeakatika makundi yasiyozidi wanyama 15.Mnyama mwingine anayeonekana kwa wingi niswala, ni mzuri wa umbile na ana ukubwa wakawaida. Huonekana wakiwa kwenye makundiya madume tu au makundi ya majike yanayoleaakiwemo dume mmoja. Ni jambo lisiloaminikakwamba kwenye maeneo ya uhifadhi kijamiiyaliyoko kaskazini mwa mto Mgeta, swala wana-onekana wakiwa kwenye makundi ambayokundi moja la madume linakuwa na zaidi yaswala 1,000 hii hutokea nyakati za kukaribiakuanza kwa majira ya mvua.Swala ni watembezi nyakati za mchana na niwarukaji wazuri hasa itokeapo kwamba wame-tishiwa . Swala wana uwezo wa kula nyasi,majani na kutumia aina nyingi za makazi, hatamaeneo yenye ukame yanaweza kuwahifadhi nakuwa na malisho ya swala wengi.Kundi la swala likitishiwa , madume hutoa mliokabla ya kuruka na kutimua mbio.

Mchanganyiko wa swala, pundamilia na nyumbuni jambo la kawaida. Uwezo wa hisia za wanya-ma hawa zinasaidiana na huwa salama wanapo-kuwa pamoja.Tandala wakubwa ni wanyama walio wachachesana, hawaonekani kwa wingi kama wanyamawengine ndani ya pori hili. Hawa ni wakubwakuliko aina nyingine za swala, wana masikiomarefu, mabega yaliyojaa na miraba myeupeipatayo nane hadi kumi mwilini. Tandala huonek-ana wakiwa kwenye vikundi vikundi vyenyewanyama wachache lakini madume wakubwahupendelea kutembea mmoja mmoja, hawawana pembe ndefu zilizojinyonga nyonga. Huwawanajificha vema kwani wanafanana na mazin-gira ya pahali wanapojificha, hivyo inahitajimacho makali kumuona Tandala aliyetulia chiniya kivuli cha kichaka akijikinga na jua kali najoto. Unaweza kuwaona kwenye maeneo yavichaka kati ya Mtemere na Mbuyu hasa sehemuambapo barabara inapita kando kando ya ZiwaNzerekela au sehemu ya kwanza ya barabaraielekeayo Kinyanguru.Pori la Selous ndilo lililobakia kama eneo pekeelenye Mbarapi, kuna kiasi cha mbarapi 4,000 nainasadikiwa kwamba kuna kiasi kingine chambarapi wapatao 6,000 au zaidi kwenye mae-neo ya kingo yaliyoko kusini na kaskazini mag-haribi mwa pori hili. Hata hivyo wanyama hawani wachache katika maeneo ya utalii unawezakubahatika kuwaona kati ya Kisaki naMatambwe pia na eneo la barabara ielekeayoStiegler's Gorge toka Matambwe.Mbarapi walioko Selous ni wadogo kwa mwili nawenye rangi nyepesi ya weupe kulinganisha na

14

Page 16: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Wanyama wenye kwato

mbarapi wa maeneo mengine ya Tanzania napia pembe zao ni fupi. Idara ya Wanyamaporiikishirikiana na Mpango wa Uhifadhi (SCP) imef-anya utafiti na kugundua kwamba Mbarapihawa ni aina ya Roosevelti iliyokuwa imedhani-wa kwamba imo hatarini kutoweka kwani ilika-diriwa kwamba kulikuwa na Mbarapi aina hiyo100 tu waliobakia huko kwenye hifadhi ya mili-ma ya Shimba iliyoko nchini Kenya. Mbarapiaina ya Roosevelt ni tofauti na Mbarapi waliokokatikati na magharibi mwa Tanzania pamoja nawale waliopo huko Afrika ya Kusini. Pofu naowanapatikana ndani ya pori hili, hawa ni wanya-ma wakubwa katika jamii yote ya Swala , Pofudume anafikia uzito wa kilo 700. Pamoja nauzito wote huo, pofu anaweza kuruka kiasi chazaidi ya mita mbili kwenda juu hata kama akiwaamesimama na siyo kwenye mbio. Mara nyingiwanatembea kimakundi na kundi moja lawezakuwa na Pofu zaidi ya mia moja.Madume wana rangi ya kijivu zaidi hasa wana-pokomaa/zeeka wanaonekana zaidi kwenyemaeneo ya wazi ya Kinyanguru na idadi yaoimeongezeka sana hivi karibuni. Madume waPofu walioko Selous wanajulikana sana kutok-ana na kuwa na pembe zilizo kubwa kuliko Pofuwengine walioko hapa Afrika ya mashariki.Tohe nao wapo kwenye maeneo haya. Hawa niwadogo kimaumbile kulinganisha na Swala nani wekundu kwa rangi. Ni madume tu ndiowenye pembe zililizojikunja kwa kuelekeambele. Wanapendelea makazi yenye magugukaribu na mabwawa au maeneo tepe tepe.

Mgeni mwenye macho yanayoona sana anawe-za akaona Pongo. Ni wengi kwa kawaida lakiniwao hutembea sana usiku. Mchana hujifichakwenye vichaka/misitu minene kandokando yamito na maziwa. Rangi yao ni nyekundu kaha-wia na miraba mstatili, na madoa meupe kwanyuma mkiani. Wanaposhituliwa wanatoa mliomkali mithili ya kubweka. Pongo hupendeleakuwa mmoja mmoja isipokuwa majike yakiwana watoto huwa kwenye vikundi vidogo auwawili wawili. Kama utaona mnyama jamii yaSwala anaruka kwa ghafla toka kichakani namara hiyo hiyo akatokomea basi ujue kwa haki-ka anaweza kuwa ni Pongo.Kuro wanapatikana kwa wingi kando kando yaMto Rufiji na maeneo ya maziwa. Wana utepemweupe wa mviringo matakoni, na rangi yakahawia na ni mkubwa kiasi. Majike hawanapembe na wanafanana na jamii ya "Deer"wekundu wa Ulaya.Pundamilia nao wanaonekana kila mahali, lakiniTwiga wapo kwenye maeneo ya kaskazini yaSelous tu, na Mto Rufiji ndio unaokuwa kamampaka kwani ndiyo sehemu ya mwisho mtuanapoweza kuona Twiga hapa Afrika yaMashariki.Taarifa za Bwana Nicholson aliyekuwa mhifadhikiongozi zinaeleza kwamba Twiga wameongeze-ka sana katika miaka ya sabini.Twiga ni nembo/alama ya Taifa hawawindwipopote hapa Tanzania. Hata hivyo ni wenye aibuna hupenda kukaa mbali na wageni.Ngiri hutembea na kujificha nyakati za mchana,mara nyingi wanaonekana wakikimbia hukumikia ikiwa imesimama au wakiwa wamepiga

15

Page 17: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Wanyamapori wengine

magoti miguu ya mbele wakila minyoo, mizizi aumatunda. Watu huwa wanasema ngiri wana surambaya, kiasi kwamba wanaweza kuitwa wenyesura nzuri. Macho yao hayaoni mbali ndiyomaana huwa kama mtu anawasogelea huwawanamfuata karibu lakini wana wepesi wakunusa harufu na kusikia sauti au mshindo.Wanapenda maji sana ndiyo maana hawakaimbali na sehemu zenye maji. Usiku wanajifichakwenye mashimo ya mchanga. Inachukua uzoefukidogo kutambua kati ya dume na jike, kwanijike ana chuchu nne na dume ana mbili tu.Madume yaliyo makubwa / wazee yana menomakubwa yanayotumika kama silaha kujihamizidi ya simba, chui na mbwa mwitu. Maeneo yaKinyanguru yana ngiri wengi kwa eneo kulikopengine popote hapa Afrika.Nguruwe kwa upande mwingine wanaonekanakwa shida kwa vile wao hutembea usiku na hupumzika mchana kwenye vichaka karibu namaji. Nguruwe anaweza kuwa na uzito wa kilo80. Mtu anaweza kubahatika kuona Nguruwekama atakuwa anatembea karibu na Mto Rufijisaa za alfajiri. Kama walivyo Nguruwe wote,hula chochote wanachopata, mizizi, matundapori, mayai, wadudu au nyama.

Nyani, Tumbili na Kima wanaonekana kila mahali. Mbega wanaovutia kwa rangi zao nyeusina nyeupe wanaonekana kwenye misitu iliyokokando kando ya mito.Kuna aina nyingine ya Kima ambao hujulikanakama kima wekundu wa Uhehe. Hawawanapatikana kwenye msitu wa Magomberakusini mwa kambi ya Msolwa ambapo reli yaTAZARA inapita eneo la magharibi lapori la Selous. Inakadiriwa kwamba aina hii yakima wako kiasi cha 400 ndani ya pori hili.Mamba nao wapo kwa wingi sana kwenye mitona maziwa ya pori la Selous na maeneo yanayolizunguka pori hili. Mamba wanakulasamaki kama chakula chao kikuu lakini hula wanyama wengine pia. Wanakamata wanyamahao wanapokuwa wanasogelea maji. Mambawanapenda na kujali sana uzazi wao. Mambaakishataga na kufukia mayai jike anachungaeneo hilo hadi atakapototoa, halafu anabebavitoto akitumia mdomo wake, bila kuwadhuruhadi mtoni ambapo atawachunga kwa muda wamiezi mitatu.Nyoka wapo kila mahali. Mmoja wa mababa waPori la Selous Constantine Ionides alipachikwajina la utani - "Bwana Nyoka" kwa sababuya kupenda kwake kukamata nyoka wenye sumuna kuwafuga. Nyoka wengi hawana sumu nawanakimbia watu. Si mara nyingi watukung`atwa na nyoka.

16

Page 18: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Vyombo vilivyotengenezwa kwa mawe na watuwakati tusioujua vimeonekana. Maeneo hayayalijulikana kwa kuwa mapito makubwa yamisafara ya watumwa na pembe za ndovu tokabara kuelekea pwani. Kijiji cha Kisaki ambachosasa kiko mpakani mwa pori la Selous kilikuwani kiungo cha njia kuu mbili za biashara.Misafara mikubwa yenye watu maelfu ilikuwaikipita mara kwa mara hasa nyakati za kiangazi.Wavumbuzi kama Burton na Speke (1857) naJohnson na Thomson (1879) walipita maeneohaya na Johnson alifia Beho Beho na alizikwahapo. Wasafiri hawa waliona vijiji vichache,walitoa taarifa kwamba wanyama walikuwa wachache nyakati hizo.Mwaka 1905 Wilhelm Kuhnert aliyezaliwa (1865 - 1926) aliyekuwa mmoja wa wazunguwa kwanza wanasanaa kuangalia na kuchorawanyama pori wa Afrika maporini, alivuka mtoMgeta na kuingia eneo ambalo sasa ndilo porila Selous. Alisifia sana eneo la Beho Beho kwauzuri wake (mandhari yake mazuri) pamoja naziwa Tagalala.Miaka mitatu baada ya kuja kwa bwana Kuhnert,Mjerumani mwingine aitwaye Hans Schomburgkalifanya uwindaji katika maeneo ya kaskazini yaSelous na vitabu vyake vingi vinaonyesha pichaza wanyamapori kandokando ya mto Rufiji.Mwaka 1905 vita vya Maji Maji kuupingaukoloni wa kijerumani vilipamba moto na kupig-anwa katika eneo la kusini mwa nchi. Eneoambalo maji hayo yaliyoaminika kuwa na nguvuza kiganga yalipatikana toka eneo moja karibuna Mto Rufiji na sehemu nyingine yalipotoka nikwenye kijiji cha Ngarambe kinachopakana na

pori la Selous kwa upande wa Mashariki.Mapigano mengine yalirudi Selous wakati wavita kuu ya pili ya Dunia. Manowari/meli ya kivita iitwayo "Konigsberg" ilipata mafichondani ya mdomo wa mto Rufiji umbali wa kilo-meta 100 mashariki mwa Mtemere.Ilipozamishwa na wanamaji wa kiingereza,askari wa kijerumani walifanikiwa kuondoamizinga 10 yenye vipenyo vya inchi 4.1, wakai-pakia juu ya magurudumu na kusafiri nayo mae-neo yote ya Afrika ya Mashariki wakati wa kam-peni zao za kivita. Mwaka 1917 askari wawajerumani wakiongozwa na General vonLettow Vorbeck walipigana na askari wa kiinge-reza karibu na eneo la Beho Beho mahali ambapo mvumbuzi/mpelelezi maarufu wa kiingereza Frederick Courteney Selous alifikwa na maafawakati wa mapigano. Rafiki yake J. G. Millais,alitoa maelezo ya tukio hilo kama ifuatavyo:Majeshi yetu yalisonga mbele kutoka Kisakialfajiri ya tarehe 4.1.1917 kwa lengo la kushambulia na kuzingira kiasi kikubwa chaaskari wa wajerumani waliokuwa wamepigakambi chini ya vilima mashariki mwaBeho Beho (Milima ya sukari) kaskazini mashariki mwa barabara inayoelekea Kisakikusini mashariki mwa Mto Rufiji umbali ulikuwakiasi cha maili 13 kati yetu na maadui. Vilimavifupi ambavyo ndipo askari wa wajerumani walipojificha, vilikuwa na vichaka vinene vyenye miiba hivyo ilikuwa ni vigumu kuonaupande uelekeao magharibi. Hata hivyowalitambua mara moja hatari iliyo karibu naokwani waliona mzunguko wa

Tuangalie historia fupi ya eneo hili

17

Page 19: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Tuangalie historia fupi ya eneo hili

yaliyokuwa yakiongozwa na General von LettowVorbeck kuelekea kusini mwa Tanzania.Inasemekana kwamba Selous hakutumia usafiriwa aina ye yote bali alitembea kwa miguupamoja na askari wake wakihimili shida nataabu za mazingira magumu ya hali ya hewa namagonjwa. Hata ilipofika mwishoni mwa mwaka1916 walifanikiwa kuwafukuzia mbali askari wawajerumani kutoka kwenye ngome yao kuu yaKisaki na wakati huo alibakiwa na askari 60 tukutoka askari 1166 aliokuwa nao awali. Nyakatiza jioni wakati askari wake wakiwa wamechokana kupumzika kwenye mahandaki, yeye alikuwaakikamata vipepeo na kuwinda. Hadi leo familiayake iliyoko Uingereza inatunza nyara ambayo nifuvu/pembe za mnyama Kudu aliyemuua hukoKisaki.Mwaka 1896 Gavana wa Kijerumani alifungauwindaji eneo kati ya mto Mgeta na Rufiji nakulitangaza kuwa Pori la Akiba. Sehemu ambayokwa sasa imekuwa kivutio kikubwa kwa utaliiwa picha eneo la kanda ya kaskazini ya pori laSelous na imekuwa ndiyo ya kwanza hapa Afrikakutangazwa kuwa pori la akiba miaka miwilikabla ya Hifadhi ya Krueger ya Afrika ya Kusini.Baadaye eneo kati ya Ruaha-Kilombero na mtoUlanga upande wa magharibi pamoja na mae-neo mengine mawili upande wa mashariki karibu na Liwale yalitangazwa na wajerumanikuwa mapori ya Akiba. Sheria ya kuhifadhi ilitungwa na kuanza kutumika. Nyarakazilizopatikana hivi karibuni zinaonyesha kwambampiga picha na muandishi aitwaye Carl GeorgSchillings (1865-1921) aliandika sera ya

18

sehemu ya kikosi cha 25 cha wapiganaji wakifalme ambacho kimeagizwa kuwazuia askariwa wajerumani katika barabara ielekeayo kusinimashariki, barabara pekee iliyokuwepo ambayowangeitumia kurudi nyuma. Inaonyesha wazikwamba askari wa wajerumani waliamua kurudinyuma mapema kwa sababu kikosi cha askariwa Waingereza wakiongozwa na Captain Selouswalifika sehemu hiyo wakati huo huo kama wao.Mapigano makali yalizuka kati ya pande hizombili na Selous aliamrisha askari wake kuwas-hambulia Wajerumani ambao walikuwa ni wengina waliwazidi Waingereza na kuwafukuziavichakani. Ilikuwa ni wakati huu ambapo aliuliwakwa risasi iliyompiga kichwani.Frederick Courteney Selous (anayetamkwa Seloona "s" ya mwisho iliyofichika) alizaliwa 1851akiwa mtoto wa kiume wa mwenyekiti waLondon Stock Exchange. Alipenda sana kufuatanyayo za jasiri wa tangu utoto wake Dr. DavidLivingstone kuja Afrika, kitu ambacho alifanikiwamwaka 1871. Aliwinda na kupeleleza nchi yaMatabele huku akiwa mtangulizi kumwezeshaCecil Rhodes kufungua Zimbabwe kwa ajili yawalowezi wa kizungu. Muwindaji hodari na nimuhifadhi wa kwanza, aliandika vitabu vingivinavyohusu safari zake na historia asilia, vitabuvyake vingi vilikuwa miongoni mwa vile vilivyouzwa kwa wingi sana enzi za utawala waMalkia Victoria wa Uingereza. Shujaa huyu alipojiunga tena na jeshi alikuwa na umri wamiaka 64 wakati wa vita kuu ya pili ya duniailipoanza. Alijiunga na kikosi cha 25 cha wapiganaji wa miguu wa kifalme huko Nairobina akasaidia kuyafukuza majeshi ya wajerumani

Page 20: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Tuangalie historia fupi ya eneo hiliwanyamapori ikijumuisha kuhifadhi na matumiziendelevu ya wanyamapori jambo ambalo ndilolinalojumuishwa kwenye sera ya wakati huu.Hadi hi vi leo pori la akiba la Selous hujulikana kwa jina la shamba la bibi nainasemekana chanzo kilitokana na mtawala waujerumani Kaiser Wilhelm II, ambaye alimzawa-dia mke wake pori hilo kama zawadi ya kumbukumbu ya kuzaliwa ingawa hatukupata ushuhuda wa maandishi kuhusu swala hili.Baada ya vita Tanganyika ikawa chini ya uanga-lizi wa Waingereza na pori la akiba likapanuliwa na kupewa jina la Selous hapo mwaka 1922kwa kumkumbuka mvumbizi/mpelezi shujaaaliyefia humo mwaka 1917.Mnamo miaka ya 1930 na 1940, utawala wa Tanganyika ulihamisha wananchi waliokuwawanaishi kwenye maeneo yenye mbung'o ilikuwaepusha na ugonjwa wa malale. Njia iliyotumika kuwazuia watu wasiyarudie makaziyao ya zamani ilikuwa ni kuyatangaza kwambani sehemu ya pori la akiba na kuongeza eneolililokwisha hifadhiwa tangu awali.Zaidi ya Tembo elfu tatu waliuawa kila mwakanje ya maeneo yaliyotengwa/hifadhiwa ili kuzuiauharibifu wa mazao. Sera ya wakati huo ilikuwani kulinda wanyama walio ndani ya maeneo yaliyotengwa na kuua wanyama wote waharibifu wa mazao na maisha ya watu.Constatine Ionides muingereza mwindaji maarufu aliyekuwa kwenye kituo cha Liwalepamoja na askari wachache ndio waliokuwa najukumu la kuwadhibiti wanyamapori ndani yaeneo la maelfu ya kilometa za mraba ikiwa nipamoja na sehemu kubwa ya pori la Selous.

Asingefanikisha kazi hii nzito bila usaidizi wamaofisa wa kitanzania miongoni mwao akiwaMzee Madogo ambaye tulimwajiri baadayeakiwa na umri wa zaidi ya miaka sitini ili awa-fundishe askari na bahati mbaya Mzee Madogoakafariki dunia akiwa ndani ya "shamba la bibi"alilolipenda sana. Brian Nicholson, muhifadhi wakizungu wa mwisho alitenda kazi nzuri kuibadiliSelous kuwa namba moja ya mapori yote yaakiba. Nicholson alianzisha uwindaji wa kitaliindani ya Selous ambalo lilikuwa halitumiki kwakuwa alihitaji fedha za kujengea vituo, barabarapamoja na shughuli za kuzuia ujangili ndani yaeneo kubwa la pori. Eneo la mwisho kuunganishwa na pori la Selous ni lile lililopokusini mwa kingo za mto Rufiji wakati wa kampeni za vijiji vya ujamaa mwaka 1974. Hadiwakati huo kulikuwepo na usafiri wa basi hadikingo za kusini ya mto mkabala na Kibambawe.

Wakazi wa maeneo hayo walipatiwa makazimengine kando kando ya barabara ya Mloka -Mkongo. Wananchi hawa waliondolewa kutokakwenye ardhi nzuri yenye rutuba na maji yenyeuvuvi mzuri kwa hiyo ujangili umekuwa ni kikwazo kikubwa na kazi ngumu kwa utawalawa pori tangu wakati huo.

19

Page 21: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Janga latokea

Wanyamapori imeweza kubadili hali ya Selous.Kwa sasa pori la Selous ni moja ya mapori yanayotambulikana kimataifa kama moja linaloendeshwa kiustadi na kuhifadhiwa vemahapa Afrika. Idadi ya wanyamapori wakiwepoTembo inaongezeka na ujangili ndani ya pori nikidogo sana.Hakuna mahali po pote duniani ambapo maeneoyaliyotengwa na kuhifadhiwa yanaepuka vitishovya nje. Sasa hivi kuna mawazo ya kufanyauchimbaji wa madini ya Uranium ndani ya Selous.Cha kutisha zaidi ni mipango iliyokuwepo yakuchimba bwawa kwenye Mto Ruvu karibu nampaka wa kaskazini. Bwawa hili lingeleta mafuriko kwenye eneo la sehemu ya kanda yakaskazini ya Selous lakini cha muhimu zaidi nimaeneo nyeti ya malisho nyakati za ukame njeya maeneo yaliyohifadhiwa ambayoyangeharibiwa.

20

Serikali ilipofunga uwindaji wa kitalii mwaka1975, mapato kutokana na uwindaji yakawasifuri, wataalamu wa uwindaji wakaondoka porini na kuliacha pori wazi kwa majangili.Uharibifu ukaanza na hadhi ya pori ikaporomokaikazidi kuongezeka kutokana na uchumi duni wanchi. Juhudi za kuchimba bwawa kubwa kwaajili ya umeme zilileta wafanyakazi wapatao2,000 huko Stiegler's Gorge.Faru wengi waliokuwepo kwenye maeneo hayowaliuawa. Mwanzoni mwa miaka ya themanini,shughuli za utafiti wa kutafuta mafuta ulifanyika,hivyo barabara/njia nyingi zlizonyooka zilitengenezwa ndani ya pori, na kufungua vichaka na misitu minene. Njia hizi zimevutiamajangili kwani zimewawezesha kuingia nakupitia maeneo mengi, makundi makubwa yamajangili mara nyingi yenye watu kiasi cha sitinikwa kundi yamekuwa ya kiingia kufanya uhalifu.Mwaka 1982 wakati pori la Selous linapewahadhi ya kuwa urithi wa ulimwengu, mauajimakubwa ya Tembo yalikwishaanza na kupunguza Tembo kutoka 110,000 waliokuwepomwaka 1976 hadi kufikia Tembo wachache chiniya 30,000 hapo mwaka 1991.Inakadiriwa kwamba Tembo 20 walikuwa wanauawa kwa mtutu wa bunduki kila siku.Katikati ya miaka ya themanini, vijana wenyedhamira nzuri walipewa uongozi wa Selous.Pamoja na misaada ya mashirika ya uhifadhikama Frankfurt Zoological Society, Mfuko waUhifadhi Duniani hali kadhalika Shirika laMisaada ya Maendeleo ya Kifundi la Ujerumani(GTZ) pamoja na sera nzuri za Serikali, Idara ya

Page 22: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Mpango wa kuhifadhi pori la SelousKutokea mwaka wa 1987 pori la Selous limepatamsaada mkubwa chini ya makubaliano yaSerikali ya Ujerumani - Tanzania mpango wakuhifadhi Selous (SCP) kupitia Shirika la Misaadaya Maendeleo ya kuhifadhi la Ujerumani (GTZ).Vikosi vya askari vimepatiwa nyenzo na vitendeakazi, mawasiliano yameimarishwa na mpangowa menejimenti umetengenezwa na ndiounaoongoza shughuli za pori.Sehemu kubwa ya mpango huu ni ile ya ubakishaji wa sehemu ya mapato (fedha) amba-po Selous inaruhusiwa kubakisha nusu ya fedhazote zilizozalishwa humo. Mapato kwa mwakani kiasi cha dola za kimarekani zaidi ya millionitatu.Sehemu ya pili ya mpango huo ni ile inayoshug-hulika na ushirikishwaji wa jamii katika uhifadhiwa maliasili.Kati ya matatizo mengi ni pamoja na tatizo lauharibifu wa mazao na upotevu wa maisha yawatu kutokana na wanyama. Pamoja na sheriaza kudhibiti uwindaji mahitaji ya nyama vijijinina biashara nzuri mijini na Dar es Salaam yanasababisha uwindaji haramu usiodhibitiwakwa ajili ya biashara na yote hayo yalizidi kuletamfarakano kati ya wanavijiji na utawala waSelous.Ni filosofia ya SCP kwamba ni vigumu kudumis-ha uhifadhi kwenye maeneo yaliyotengwa kamahakuna kuwapatia faida wananchi wanaoishikando kando mwa maeneo hayo. Ili kufanikisha,uhifadhi ni lazima ufanyike - pamoja kwa kupitiakwa watu na siyo kinyume chake.

Vijiji vya kwanza vilijiunga na mpango huu hapomwaka 1989 na hadi sasa kuna vijiji 57 vinavyoendesha uhifadhi kwa jamii. Wanavijiji wanatenga sehemu ya eneo la ardhi yao kwashughuli za uhifadhi - kilimo kinazuiwa na uhifadhi wa Mali Asili unaruhusiwa. Hivyo wanavijiji wanaruhusiwa kuwinda kwa mgao maalumkwa ajili ya matumizi yao. Wanachagua askariwao kwa kazi ya doria. Mfumo huu umejumuishwa kwenye sera mpya ya Idara yaWanyamapori Tanzania na itatumika nchi nzima.Wanavijiji wataweza kujipatia fedha kutokanana biashara ya utalii wa picha na uwindaji kwe-nye maeneo ya ardhi yao.Kuna ukweli kwamba ujangili umepungua sanakwenye maeneo ya kinga na hata yale ambayoyana wanyama wengi na kwamba wanyamawanaongezeka na wanarudi hata kwenye yalemaeneo ambamo walitoweka kwa miaka mingi.Idara ya wanyamapori ndani ya Wizara ya MaliAsili na Utalii ndiyo inayotawala na kusimamiaPori la Akiba la Selous. Ofisi/Kituo kikuu chapori hili kiko Matambwe kanda ya kaskazini.Jumla ya watumishi 350 wakiwemo askari,mafundi na utawala (sawa na kila askari mmojakulinda kilometa za mraba 140) wanafanya kazindani ya Selous.Kazi zao kubwa ni kufanya doria, kuzuia ujangilina pia wanafuatilia idadi ya wanyama, nakufungua barabara, kuzitunza pamoja na njiazote za mawasiliano, viwanja vya ndege,nyumba za watumishi n.k. shughuli zote hizozinalipiwa na fedha iliyobaki kutokana na asilimia hamsini ya mapato ya Selous.

21

Page 23: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya

Mpango wa kuhifadhi pori la Selous

Mapato ya Selous yanatokana na vyanzo viwili (I)Mapato kidogo kutoka utalii wa picha (II)Asilimia 80 kutoka uwindaji wa kitalii. Kiasi chawawindaji wageni wapatao 400 hutembelea porihili kila mwaka kati ya Julai na Desemba kiasicha wanyama 3,000 wanauawa kila mwaka.Uwindaji huu ni endelevu kwani mgao wa wanyama wa kuwindwa unatolewa kufuatanana matokeo ya ufuatialiaji wa ikolojia na nisehemu ndogo tu ya idadi ya wanyama inayotolewa. Wale wasiopenda uwindaji waelewekwamba bila pato la fedha kutoka uwindaji, kaziya kuwalinda wanyama na kutunza poriisingewezekana na mapori yangetoweka.Mpango wa menejimenti ya Selous unawekabayana sera na vizuizi/vizingiti kwa pori laSelous.Nia ni kuhakikisha kwamba shughuli za wanadamu zinakua za kiasi kidogo sana. Hii nipamoja na utalii. Kwa sasa pori lina watalii zaidiya 6,000 kwa mwaka. Watalii ni lazima wapatena wafurahie hali ya kipekee na mazingiraambayo hayajaharibiwa.Utalii wa picha unapanuka pole pole ili ifikapomwaka 2001 kuwepo kambi/hoteli sita zinazo-hudumia kwenye kanda ya kaskazini ya Selous.Kuna mpango wa kufungua kambi mpya kusinimwa Mto Rufiji.Mpango wa utalii umetengenezwa kwa kuangalia wakati wa usoni/mbele uwezekanokwamba utalii unaweza kuwa wa vurugu namkubwa kando kando ya maziwa .

22

Mradi wa mpango wa kuhifadhi Pori la Selous(SCP) umefikia mwisho wake hapo mwishonimwa mwaka 2003. Shughuli zote zinazo husuvijiji zinaendelea chini ya mradi wa ushirikishwajiwa jamii katika uhifadhi uliokita (CBC) unaoen-deshwa na GTZ kwa ushirikiano na Idara yaWanyamapori.

Page 24: Impressum Kimechapishwa na Pori la Akiba la Selous/Idara ya