jamhuri ya muungano wa tanzania - tzonline · 2005. 9. 9. · 3 4.8 watumishi wa sekta ya afya na...

112
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA RIPOTI YA HUDUMA ZA AFYA TANZANIA BARA 2004 Imetayarishwa na: Idara ya Tiba Afya Makao Makuu P.O. Box 9083, DAR ES SALAAM June 2005

Upload: others

Post on 25-Jan-2021

6 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    WIZARA YA AFYA

    RIPOTI YA HUDUMA ZA AFYA TANZANIA BARA 2004 Imetayarishwa na: Idara ya Tiba Afya Makao Makuu P.O. Box 9083, DAR ES SALAAM June 2005

  • 2

    Yaliyomo Ukurasa Vifupisho 4 Utanguli 5 1.1 Ripotiya Huduma za Aya Makao Makuu 2004/2005 6 1.2 Dira/Mwelekeo (Vision ya Wizara) 6 1.3 Majukumu ya Wizara ya Afya 6 1.4 Azma (Mission) ya Wizara ya Afya 6 1.5 Malengo ya Wizara ya Afya 6 1.6 Maeneo yaliyopewa Kipaumbele 2004/2005 7 1.7 Muhtasari wa kazi zilizopangwa kutekelezwa na Wizara ya Afya 2004/2005 8 2.0 Utekelezaji wa Majukumu Afya Makao Makuu 2004/2005 9 2.1 Mipango ya Maendeleo 9 2.2 Sera na Mipango 10 2.2.1 Mabadiliko katika Sekta ya Afya 10 2.2.2 Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya 11 2..2.3 Mfumo wa Taarifa za Uendeshaji wa Huduma za Afya 13 2.3. Huduma za Kinga 14 2.3.1 Udhibiti wa wa Magonjwa ya Kuambukiza 14 2.3.2 Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria 15 2.3.3 Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma 16 2.3.4 Mpango wa Taifa wa Kuzuia Upofu na Kudhibti Ugonjwa wa Usubi 18 2.3.5 Huduma ya Elimu ya Afya kwa Umma 19 2.3.6 Huduma ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto 19 2.3.7 Mkakati wa Kutibu Magonjwa ya Watoto kwa Uwiano 20 2.3.8 Mpango wa Taifa wa Chanjo 21 2.3.9 Huduma ya Afya Shuleni 21 2.3.10 Afya ya Mazingira 21 2.3.11 Huduma za Afya Mipakani 22 2.3.12 Afya katika Sehemu za Kazi 23 2.3.13 Huduma za Afya Wilayani (District Health Services) 23 2.3.14 UKIMWI 24 2.3.15 Mradi wa Uimarishaji wa Huduma Muhimu za Afya 25 2.4 Huduma za Tiba 26 2.4.1 Huduma za Uchunguzi wa Magonjwa 26 2.4.2 Huduma za Tiba Asili 27 2.4.3 Hudma za Afya ya Kinywa 28 2.4.4 Huduma za Afya ya Akili na Vita Dhidi ya Dawa za Kulevya 28 2.4.5 Huduma za hospitali za Mshirika ya Kujitolea na Watu Binafsi 29 2.4.6 Huduma ya Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba 29 2.4.7 Huduma za Kuzuia Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto 30 2.4.8 Huduma ya Matibabu ya Nje ya Nchi 30 2.5 Hudma ya Utawala na Utawala na Utumishi 31 2.5.1 Idara ya Utawala 31 2.6 Huduma ya Mafunzo ya Watumishi 32 2.7 Ofisi ya Mganga Mkuu Kiongozi 34 2.7.1 Huduma za Dharura na Maafa 34 2.7.2 Ukaguzi wa Huduma za Afya 35 2.7.3 Huduma za Uuguzi na Ukunga 35 2.8 Uhasibu na Fedha 36 2.8.1 Ukusanyaji wa Mapato 36 2.8.2 Matumizi ya Fedha za kawaida 37 2.8.3 Matumizi ya Fedha za Miradi ya Maendeleo 37 3.0 Taasisi na Mamlaka zilizo chini ya Wizara ya Afya 39 3.1 Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) 39 3.2 Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali 40 3.3 Mamlaka ya Chakula na Dawa 42 3.4 Taasisi yaTaifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu 43 3.5 Matatizo na changamoto 45 3.6 Maeneo yaliyopewa kipaumbele mwaka 2005/2006 46 4.0 Ripoti ya huduma za Afya Mikoa 48 4.1 Utangulizi 48 4.2 Mchanganuo wa Watu katika 48 4.3 Mchanganuo wa hali ya Vifo vya Watoto na Mama wajawazito katika Mikoa 48 4.4 Mchanganuo wa Maeneo ya kiutawala katika Mikoa 50 4.5a Uwiano wa Wataalam wa Afya na Idadi ya Watu 50 4.5b Uwiano wa Wataalam wa Afya ya Kinywa (Dental) na Idadi ya Watu 53 4.6 Idadi ya Vituo vya kutolea Tiba na Umiliki wake 53 4.7 Idadi ya vitanda vya kulaza wagonjwa kwa kufuata miliki ya Vituo vya kutolea tiba 56

  • 3

    4.8 Watumishi wa Sekta ya Afya na Sehemu za Kazi 58 4.9a Magari na Pikipiki 58 4.9b Hadubini 59 4.9c Mashine za X-ray 59 4.9d Vifaa vya Utakasaji 60 4.9e Vifaa vya Tiba ya Meno 60 4.10 Magonjwa yanayotolewa Taarifa 61 4.11 Magonjwa yaliyojitokeza kwa Wagonjwa wa Nje 64 4.12 Magonjwa yaliyojitokeza kwa Wagonjwa Waliolazwa 66 4.13 Taarifa ya Huduma Maalum 68 4.14 Aina za X-ray zilizopigwa 69 4.15 Huduma za Maabara 69 4.16 Matokeo ya Vipimo vya Maabara 70 4.17 Huduma za kliniki ya Meno 70 4.18 Mahudhurio ya kliniki kwa Mama Wajawazito 71 4.19 Mama wajawazito kujifungua 71 4.20 Huduma kwa Mama waliojifungua 72 4.21 Matatizo ya akinamama wakati wa kujifungua 72 4.22 Sababu za Vifo vya Mama wajawazito 73 4.23a Taarifa ya watoto waliozaliwa mmojammoja 74 4.23b Taarifa ya Watoto waliozaliwa zaidi ya mmoja 74 4.24 Idadi ya watoto chini ya mwaka mmoja waliopata chanjo 75 4.25 Chanjo ya TT2+ kwa akinamama wajawazito 77 4.26 Wateja wa uzazi wa mpango wanaoendelea na Huduma 77 4.27 Watoto waliopata matone ya Vitamin A 78 4.28 Kiwango cha Watoto wenye Utapiamlo Mkali 80 4.29 Kiwango cha Kaya zenye vyoo vinavyokubalika na maji toka vyanzo salama 80 4.30 Mapato na vyanzo vyake 81 4.31 Fedha zilizotumika 82 5.0 Ripoti ya Hospitali za Rufaa 84 5.1 Utangulizi 84 5.2 Ripoti ya huduma zilizotolewa 88 5.2.1 Mahudhurio ya Nje 88 5.2.2 Wagonjwa waliolazwa 89 5.2.3 Magonjwa yaliyojitokeza kwa mahudhurio ya nje 89 5.2.4 Magonjwa Kumi yaliyoongoza kwa Mahudhurio ya Nje 90 5.2.5 Magonjwa yaliyojitokeza kwa Wagonjwa wa Ndani 91 5.2.6 Magonjwa yaliyojitokeza kwa Wagonjwa waliolazwa Idara ya “Internal Medicine” 92 5.2.7 Magonjwa yaliyojitokeza kwa Wagonjwa waliolazwa Wodi ya Upasuaji 92 5.2.8 Huduma za Upasuaji 92 5.2.9 Magonjwa ya Akinamama (Ggynaecology) 94 5.2.10 Sababu za kulazwa Mama wajawazito 94 5.2.11 Kujifungua Mama Wajawazito 95 5.2.12 Aina ya kujifungua Mama Wajawazito 95 5.2.13 Matokeo ya kujifungua Mama Wajawazito 96 5.2.14 Sababu ya Vifo vya Mama Wajawazito 96 5.2.15 Sababu za kulazwa na vifo wodi za watoto 97 5.2.16 Sababu ya Vifo vya watoto wa umri chini ya mwaka mmoja 97 5.2.17 Magonjwa ya Macho kwa waliolazwa 98 5.2.18 Magonjwa ya Akili kwa waliolazwa 98 5.2.19 Magonjwa ya Kinywa 99 5.2.20 Idara ya Vipimo vya Maabara 99 5.2.21 Takwamu za Damu Salama 100 5.2.22 Takwimu za X-ray zilizopigwa 101 5.2.23 Takwimu za kipimo cha Ultrasound 101 5.2.24 Takwimu za kipimo cha CT Scan 102 5.2.25 Takwimu za Watumishi 103 5.2.26 Takwimu za Madaktari Bingwa 103 5.2.27 Taarifa ya Fedha za Kuendesha Huduma 104 5.3 Mafanikio na Matatizo katika Hospitali za Rufaa 105 6.0 Ripoti za Hospitali za Huduma Maalum 107 6.1 Hospitali ya Kibongoto 107 6.2 Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa MOI 107 6.3 Hospitali ya Mirembe na Taasisi ya Mirembe 108 6.4 Taasisi ya Saratani Ocean Road 109 7.0 Ushirikiano na Nchi za Nje 110 8.0 Shukrani 111

  • 4

    VIFUPISHO ADB African Development Bank ADDO Accredited Drug Dispensing Outlets ARVs Anti Retro Viral Drugs BADEA Bangue Arabe pour Development Economique en Afrique BF Basket Funds CCHP Comprehensive Council Health Plans CHSB Council Health Services Board CDC Centre for Disease Control and Prevention CEDHA Centre for Education in Health Development Arusha CHF Community Health Fund (Mfuko wa Afya ya Jamii) CLP Central Pathology Laboratory CUAMM International College for Health Cooperation in Developing Countries DANIDA Danish International Development Agency DDH Designated District Hospital DFID United Kingdom Department for International Development DOTS Directly Observed Treatment Short Course EEG Electro Encephalogram EOP Emergency Operational Plan EPI Expanded Programme of Immunization EU European Union HFGC Health Facility Governing Committee GAVI Globed Fund for Vaccine Initiative GTZ Gesellschaft fuer Technische Zusammenarbeit ICU Intensive Care Unit IDRC International Development Research Centre of Canada IMCI Integrated Management of Childhood Illnesses ITI International Trachoma Initiate JICA Japan International Cooperation Agency KCMC Kilimanjaro Christian Medical Centre KfW German Bank for Development MDRTB Multi Drug Resistant TB MDT Multi Drugs Therapy MKUKUTA Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania MOI Muhimbili Orthopedic Institute MoU Memorandum of Understanding MSF Medicine Sans Frontieres MTUHA Mfumo wa Taarifa za Uendeshaji wa Huduma za Afya MUHUMA Mradi wa Uimarishaji wa Huduma za Afya NACTE National Council for Technical Education NEPHI National Essential Package of Health Interventions NIMR Institute for Medical Research OC Other Charges OPD Out Patient Department ORCI Ocean Road Cancer Institute OREC Organization of Petroleum Producing Countries OPET Overseas Related Export Trade PHCI Primary Health Care Institute PMTCT Prevention of Mother to Child Transmission DOTS Directly Observed Treatment Short Course PPM Planned Preventive Maintenance RHMT Regional Health Management Team SAFI Sawazisha Kope, Anza Matibabu Mapema, Fanya Usafi wa Uso na Mwili Imarisha Mazingira SAREC Swedish Agency for Research Cooperation in Leading Countries SDC Swiss Agency for Development and Cooperation SIDA Swedish International Development Authority SP Sulphurdoxine Pyrimethemine STI Sexually Transmitted Infections SWAP Sector Wide Approach Programme TAMISEMI Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa TALGWU Tanzania Local Government Workers Union TFDA Tanzania Food and Drug Authority TFNC Tanzania Food and Nutrition Centre TIKA Tiba kwa Kadi TUGHE Tanzania Union for Government Health Employees UKIMWI Ukosefu wa Kinga Mwilini UNHCR United Nations High Commission for Refugees UNDP United Nations Development Programme UNFPA United Nations Fund for Population Activities UNICEF United Nations Children Fund USAID United States Agency for International Development VAs Voluntary Agencies VCT Voluntary Councelling and Testing VVF Vesicle Vaganal Fistula WB World Bank WHO Word Health Organization ZBTC Zonal Blood Transfusion Centres

  • 5

    Utangulizi Katika kipindi cha mwaka 2004/05, Huduma za Afya nchini ziliendelea kuimarika. Malengo yaliyowekwa katika kipindi hicho yalitekelezwa kwa ufanisi na vipaumbele vya Wizara pia vilifikiwa. Pamoja na mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi hicho kulikuwa na tatizo la takwimu kutokamilika katika Sekta ya Afya. Kwa ujumla wake bado limeendelea kujitokeza katika uandikaji wa taarifa za mwaka za hospitali za Rufaa na Mikoa. Kutokana na hali hiyo bado ipo haja ya kuzingatia umakini katika kupata takwimu sahihi za utendaji kwani ndizo zitakazosaidia kutoa takwimu sahihi ya hali ya magonjwa na hali halisi ya Huduma za Afya Nchini. Matatizo yaliyojitokeza katika taarifa zetu za utendaji za mwaka yanatoa changamoto kwetu sisi watendaji tujipange upya katika kutekeleza majukumu yetu katika Sekta ya Afya. Aidha, takwimu zimeonyesha kushuka kwa viashiria vingi vya hali ya Afya katika taarifa za mwaka za Mikoa na Hospitali za Rufaa. Iwapo hapatakuwa na juhudi za kutosha za kurekebisha hali hiyo ni wazi kwamba hali ya Huduma ya Afya itazidi kushuka na hivyo kuathiri afya za wananchi. Kutokana na hali hiyo zinahitajika jitihada za kutosha za kujifunza kwa Mikoa/Hospitali iliyofanya vizuri ili kasoro zilizojitokeza ziweze kurekebishwa. Changamoto la tatizo la UKIMWI linataka kujipanga upya ili kutekeleza wajibu wetu katika kutoa huduma za afya kwa Watanzania.

  • 6

    1.0 RIPOTI YA HUDUMA ZA AFYA MAKAO MAKUU 2004/2005 1.1 Utangulizi

    Kwa mwaka 2004/2005 huduma za afya nchini ziliendelea kutolewa kwa kuzingatia sera, miongozo, mipango na mikakati mbalimbali iliyowekwa na Wizara ya Afya. Kazi zilizopangwa kufanyika katika kipind hiki zililenga dira, malengo na majukumu yaliyopewa kipaumbele. Vyote hivi ni mwendelezo wa utekelezaji wa mipango na mikakati iliyowekwa katika mwaka 2003/2004.

    1.2 Dira/Mwelekeo (Vision) ya Wizara

    Dira ya Wizara ya Afya ni “ Kutoa huduma za afya zenye ubora wa hali ya juu zinazofaa na zinazofikiwa na kutumiwa na wananchi wote kulingana na mahitaji yao kupitia mfumo wa afya ulio imara na endelevu”.

    1.3 Majukumu ya Wizara

    Ili kuiwezesha Wizara kufikia dira yake inatakiwa kutekeleza majukumu yafuatayo:- • Kusimamia Sera na kutayarisha miongozo ya Afya ya huduma za Kinga na Tiba • Kudhibiti kemikali na kuendesha uchunguzi wa kisayansi wa sababu za vifo • Kusimamia na kudhibiti ubora wa dawa, vifaa tiba, vipodozi na vyakula • Kuendeleza huduma za Tiba ya Asili • Kusimamia Mpango wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto • Ukaguzi wa huduma za afya • Kuandaa na kusimamia programu za mafunzo ya wataalamu wa afya na kuwaendeleza

    kitaaluma watumishi wa sekta ya afya • Kuinua kiwango cha ushirikiano kati ya Wizara, mashirika ya umma na dini, sekta

    binafsi, idara na miradi mbalimbali ya afya katika kuongeza na kuimarisha ubora wa huduma za afya

    • Kutafuta rasilimali na vyanzo vya kutosha vya fedha na kuhakikisha matumizi bora ya watumishi wa afya, fedha na vifaa

    • Kuongoza na kusimamia wakala za Serikali, taasisi na mashirika ya umma yaliyo chini ya Wizara ya Afya

    • Kushirikiana na jumuia za kimataifa katika kuimarisha huduma za Afya. 1.4 Azma (Mission) ya Wizara ya Afya

    Azma ya Wizara ya Afya ni kutoa huduma za afya kulingana na mahitaji, kusimamia sera na kutayarisha miongozo sahihi inayowezesha upatikanaji wa wataalamu wa afya wenye ari na hamasa ili kuboresha afya hasa ya wale walio katika hatari ya kuugua zaidi.

    1.5 Malengo ya Wizara ya Afya

    • Kupunguza magonjwa na idadi ya vifo kwa makundi yanayoathirika zaidi hasa watoto wachanga, na walio chini ya miaka mitano, chipukizi ambao hawajafikisha umri wa kwenda shule na walio shuleni, vijana, watu wenye ulemavu, wazee na wanawake walio katika umri wa uzazi na kuongeza umri wa kuishi

  • 7

    • Kuhakikisha kuwa huduma muhimu na za msingi za afya zinasaidiwa na kusimamiwa kwa utaratibu sahihi wa huduma za rufaa, utafiti, takwimu zenye mgawanyo wa kijinsia na kuwahusisha kikamilifu wananchi

    • Kufanya tathmini na kudhibiti usalama na ubora wa vyakula, dawa, kemikali na vipodozi ili kulinda afya ya wananchi wote na mazingira kwa ujumla

    • Kuzuia na kudhibiti magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza yakiwemo Malaria, Kifua Kikuu, Utapiamlo na yale mengine yanaohusiana na afya ya mazingira, afya kazini, matumizi ya kemikali

    • Kupanga mafunzo ya watumishi na kujitosheleza kwa wataalam wa afya wenye uwezo na ujuzi katika kada mbali mbali kwa kuzingatia uwiano wa kijinsia katika kutoa huduma za afya katika ngazi zote

    • Kuainisha mahitaji na kukarabati miundo mbinu ya afya kwa kuzingatia huduma zinazotolewa kwa watu wenye ulemavu na kuweka mfumo wa matengenezo ya majengo ya afya, mitambo na vifaa

    • Kufanya mapitio, kutayarisha, kuhamasisha, kueneza, kufuatilia na kutathmini sera ya afya, mipango na bajeti, miongozo, sheria za afya za viwango mbali mbali vya huduma, kanuni na taratibu zinazohakikisha huduma za afya zinatolewa kwa ubora unaotakiwa

    • Kuweka mazingira mazuri ya kazi na vitendea kazi kwa ajili ya kutoa huduma bora na muhimu za kiutendaji na utawala zenye kuzingatia jinsia.

    1.6 Maeneo yaliyopewa kipaumbele 2004/2005

    Maeneo yaliyopewa kipaumbele ni yale yaliyolenga katika kupunguza umasikini, magonjwa na vifo kwa wananchi wote, kuongeza umri wa kuishi na ubora wa maisha. Maeneo hayo yaliainishwa kama yafuatayo:-

    • Kuzipatia hospitali, vituo vya afya na zahanati dawa muhimu na vifaa vya hospitali • Kuimarisha huduma za hospitali za rufaa kwa kuzipatia vifaa vya hospitali, vifaa vya

    uchunguzi na dawa za maabara. Vifaa hivi huwawezesha waganga kugundua tatizo mapema na kutoa tiba sahihi

    • Udhibiti na uzuiaji wa Malaria • Kutoa mafunzo ya kitaalamu ya watarajali (pre-service) ya wataalam wa afya na ya

    kujiendeleza kwa kada zote za afya • Kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto, kwa kusambaza dawa za uzazi

    wa mpango, vifaa vya uzazi na kutoa mafunzo kwa waganga na wauguzi jinsi ya kutambua, kuainisha na kutoa tiba sahihi kwa magonjwa ya watoto kwa kupitia mpango wa uwiano wa kutibu magonjwa ya watoto (IMCI)

    • Kuimarisha huduma za chanjo kwa kununua dawa za chanjo, vifaa na vipuli kwa ajili ya mnyororo baridi

    • Udhibiti na uzuiaji wa kuenea kwa Kifua Kikuu na Ukoma • Kuboresha hali ya elimu ya lishe nchini • Kuimarisha afya na usafi wa mazingira nchini kote • Kuzipatia fedha hospitali Teule (DDH) na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) ili

    kuongeza uwezo wa kutoa huduma kwa wananchi katika sehemu zisizo na vituo vya afya vya Serikali

    • Kutekeleza majukumu ya sekta ya afya katika kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI • Kutumia matokeo ya utafiti yanayotolewa na taasisi mbalimbali za utafiti katika kutoa

    mapendekezo ya sera, miongozo na mipango mbali mbali ya afya • Kutoa mchango wa Serikali katika miradi yote inayopewa fedha na wahisani mbali

    mbali

  • 8

    • Kufanya ukarabati wa majengo ya afya yaliyo katika hali mbaya na vifaa vya tiba na kuweka utaratibu wa kufanya matengenezo ya kinga (Planned Preventive Maintainance PPM)

    • Kufanya uchunguzi wa vyakula, dawa na kemikali, kutoa ushauri wa kitaalam na kutambua vyanzo vya vifo kwa kufanya uchunguzi wa kisayansi

    • Kusimamia na kudhibiti kemikali za viwandani na majumbani, utakaotekelezwa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

    1.7 Muhtasari wa kazi zilizopangwa kutekelezwa na Wizara ya Afya 2004/2005

    Katika kipindi hiki kazi zilizopangwa kutekelezwa na Wizara ya Afya kwa kutumia fedha za matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo, imefuata vipaumbele vilivyoanishwa hapo juu. Kazi hizo ni kama zifuatavyo:-

    • Kutoa dawa na vifaa vya hospitali kwa zahanati, vituo vya afya na hospitali katika ngazi zote ili kuiwezesha Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kutoa huduma muhimu za afya kwa wananchi

    • Kutoa ruzuku kwa hospitali za mashirika ya dini • Kusimamia, kufuatilia na kutathmini huduma za afya zitolewazo na Serikali za Mitaa,

    Mikoa, hospitali za Rufaa na Taifa • Kuimarisha huduma za chanjo, kuendeleza ubadilishaji wa mfumo wa uendeshaji wa

    majokofu ya chanjo kutoka matumizi ya mafuta ya taa kwenda katika matumizi ya gesi. Shughuli za chanjo zitaendelea kuimarishwa kote nchini

    • Kutekeleza mpango wa ukarabati na matengenezo ya hospitali za Mikoa na za Rufaa. Karakana Kuu za Kanda za vifaa na za ukarabati zitatumika kusaidia hospitali za Mikoa na Serikali za Mitaa kuanzisha uhakikimali na kuweka viwango kamili vya vifaa vya kutolea huduma za afya vinavyotumiwa na vituo vinavyotoa huduma za afya

    • Kufuatilia na kusimamia ubora na usalama wa chakula, dawa na vipodozi utakaotekelezwa na Mamlaka ya Taifa ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kutoa huduma za ukaguzi, usajili wa uzalishaji, majaribio na uchunguzi wa kimaabara wa sampuli ili kuhakikisha kuwa wazalishaji, wasafirishaji nje, waagizaji, wasambazaji na wauzaji wanazingatia ubora, viwango, taratibu na matendo ya utunzaji yanayokubalika

    • Kuzuia magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza hasa Malaria, UKIMWI, Kifua Kikuu na Utapiamlo. Hatua zitakazochukuliwa zitajumuisha uimarishaji na kuinua elimu ya afya na usimamizi wa kemikali

    • Kuweka kipaumbele katika utekelezaji wa mkakati mpya wa sekta ya afya wa kupambana na UKIMWI kwa kuhakikisha mpango huu unatekelezwa na kila idara umeingizwa katika mpango wa afya wa mwaka wa kila Halmashauri ya Wilaya.

    • Kutoa huduma za tiba kwa wagonjwa wa UKIMWI na magonjwa yanayoambatana nayo, kutoa ushauri nasaha na kupunguza unyanyapaa kwa walioathirika

    • Kutoa mafunzo kwa wataalamu mbalimbali wa afya juu ya tiba sahihi ya Malaria katika Wilaya zote nchini, uhamasishaji juu ya utumiaji wa vyandarua vyenye viuatilifu, utafiti wa usugu wa vimelea vya Malaria na tiba mseto

    • Kuhakikisha usalama wa damu, kuzuia maambukizi ya UKIMWI kwa mtoto toka kwa mama, kuhamasisha uzuiaji wa kuenea kwa UKIMWI kupitia ngono, uaminifu kwa mpenzi mmoja na matumizi ya kondom

    • Kuchukua hatua ambazo zitaongeza upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI kwa kushirikiana na wahisani na mifuko mbali mbali kama vile “Global Fund, The Bill and Melinda Gates Foundation”, “Clinton Foundation” na “President G. W. Bush Initiatives”

  • 9

    • Kutekeleza mikakati ya pamoja ya kudhibiti maambukizi ya Kifua Kikuu na UKIMWI, kutoa dawa za Kifua Kikuu na Ukoma katika vituo vyote vya matibabu. Kufanya utafiti wa kitaifa wa Kifua Kikuu na kampeni za kutokomeza Ukoma

    • Kuendelea kutoa kipaumbele kwa magonjwa mengine kwa kutekeleza mipango na kazi zinazolenga utoaji wa huduma muhimu za afya kwa jamii, huduma za afya ngazi ya Wilaya na katika hospitali za Mikoa na Rufaa

    • Kuimarisha mipango ya mafunzo ya wataalamu na kuboresha mafunzo katika vyuo vyake ili kuhakikisha elimu inayotolewa na vyuo hivyo inakuwa bora zaidi. Kuweka mkazo zaidi katika mafunzo ya kujiendeleza ili kuwaongezea ujuzi na utaalamu wafanyakazi wa afya katika ngazi zote. Kuandaa mipango ya mafunzo endelevu ya wafanyakazi ambayo itatengenezwa kulingana na mahitaji ya kazi

    • Kukarabati majengo na vifaa vya kutolea huduma za afya na kukamilisha uchunguzi utakaosaidia uandaaji wa mpango wa maendeleo wa miaka 10 wa huduma za hospitali

    • Kukamilisha mapitio ya Sera ya Taifa ya Afya kwa kujumuisha maoni yaliyotolewa na wadau wengine wa afya

    • Kuwasilisha muswada wa sheria ya Afya ya Jamii katika Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba ili ukamilishwe na uwasilishwe bungeni

    • Kuimarisha ushirikiano na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa • Kutoa mafunzo ya huduma za dharura kwa wazazi kwa kufundisha waalimu 12 wa

    kitaifa na 80 kutoka Mikoani.

    2.0 UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU AFYA MAKAO MAKUU 2004/2005 2.1 Mipango ya Maendeleo

    Mwaka 2004/05 Wizara ya Afya ilitengewa kiasi cha shilingi 91,215,753,600/= kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Kati ya kiasi hicho, jumla ya shilingi 3,552,448,200/= zilitolewa na Serikali ya Tanzania na kiasi cha shilingi 87, 663, 305,400/= zilitoka kwa wahisani mbalimbali, wakiwemo wahisani wanaochangia Mfuko wa Pamoja wa Afya (Health Basket Fund). Fedha hizo zimetumika kutekeleza miradi ifuatayo: -

    • Ukarabati wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Wizara iliendelea kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ili kukamilisha ukarabati mkubwa unaoendelea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Ukarabati huu unaenda sambamba na ununuzi na ufungaji wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya Hospitali ya Taifa Muhimbili na hospitali za Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni

    • Kuendeleza ujenzi wa wodi ya watoto (Paediatric Ward Complex) • Kuimarisha Hospitali Maalum na za Rufaa

    o Ukarabati wa majengo ya huduma ya wagonjwa wa nje, upasuaji, mfumo wa maji taka katika hospitali ya Meta mjini Mbeya, pamoja na ukarabati wa kijiji cha wagonjwa wa akili Isanga

    o Kutayarisha michoro kwa ajili ya ujenzi wa hosteli ya madaktari wanafunzi (Intern Doctors) na kukamilisha ujenzi wa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa Mbeya

    o Ununuzi wa vifaa vya tiba kwa ajili ya hospitali za rufaa na maalum o Serikali imeweza kutoa mchango wake wote kama ilivyopangwa katika Taasisi

    ya Mifupa Muhimbili (MOI) o Serikali iliweza kukarabati majengo ya vyuo vya mafunzo ya afya nchini o Serikali imeweza kumalizia kutoa mchango wake wote (counterpart fund) ili

    kununua vifaa vya Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili – MOI o Udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza

  • 10

    o Kukamilisha ujenzi wa jengo la ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu (NIMR) Tukuyu

    o Kufanya ukarabati wa mifumo ya njia za umeme kwenye jengo la ofisi za Huduma za Mama na Mtoto Dar es Salaam

    o Kufanya ukarabati wa ofisi, mabweni na madarasa katika vyuo 33 vya afya vilivyo chini ya Wizara

    o Kuvipatia vituo vyote vya afya dawa na vifaa kwa ajili ya kukinga na kutibu magonjwa ya zinaa – STIs

    o Kukomboa na kusambaza dawa za ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma. Serikali imetoa mchango wake (counterpart funds) kwenye mradi kwa ajili ya kudhibiti magonjwa haya

    o Kutayarisha na kusambaza vitabu vya Mfumo wa Taarifa za Uendeshaji Huduma za Afya (MTUHA) nchi nzima.

    2.2 Sera na Mipango 2.2.1 Mabadiliko katika Sekta ya Afya (Health Sector Reforms)

    Wizara kwa mwaka 2004/2005 ilifanikiwa kuhamasisha na kutoa mafunzo kwa Halmashauri za Wilaya 92 Tanzania Bara na kuziwezesha kuandaa na kupitisha Sheria ndogo ya kuanzisha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF). Halmashauri hizo hazijumuishi Halmashauri kwa Wilaya 8 ambazo ni mpya kwa kuwa Wizara bado inasubiri zipate mabaraza ya Madiwani, October 2005. Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) unaendelea kuwa mkombozi kwa wananchi wenye kipato cha chini kwa kutoa unafuu wa matibabu kwa wale wanaojiunga na mfuko huo kwa kuwahakikishia upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vifaa muhimu. Wilaya za Mbinga, Igunga, Singida, Iramba, Songea na Iringa zimeendelea kuwa mfano. Wizara kwa kushirikiana na TAMISEMI na Halmashauri imeweza kuandaa na kusaini Mikataba ya CHF inayolenga kuwa na mwongozo wa matumizi bora ya fedha za CHF. Wizara itatumia mikataba ya CHF kulipia tele kwa tele kwa Halmashauri 30 zilizochanga kwa awamu mbili, yaani mwezi Oktoba 2004 Wizara ililipa shilingi millioni 400 na Juni 2005 ililipa shilingi millioni 100. Wizara pia imehamasisha Halmashauri za Miji ya Moshi, Iringa, Mtwara na Jiji la Mwanza juu ya utaratibu wa kuchangia huduma za afya kabla ya kuugua kwa sekta isiyo rasmi katika maeneo ya mijini. Utaratibu huu unajulikana kwa jina la TIBA KWA KADI (TIKA). Mpango huu wa TIKA unafanana na CHF ya Halmashauri ya Wilaya na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambapo kaya au watumishi wanachangia kabla ya kuugua na kupata matibabu ya mwaka mzima kwa kutumia KADI ya matibabu na hivyo kuzuia kutoa fedha taslimu ambazo zinaashiria mianya ya rushwa. Matarajio ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Mwaka 2005/2006 Mwaka 2005/06 Wizara inatarajia kutekeleza yafuatayo:

    • Kutoa mafunzo ya njia bora za kufanya makisio ya makusanyo • Kuhamasisha kwa ufasaha na ufanisi • Utunzaji na matumizi bora ya fedha za CHF

  • 11

    • Kujenga msingi wa kudumu katika ngazi ya Kanda na Mikoa kwa kuvitumia vyuo vya kanda na kushauri Mikoa yote kuteua waratibu wa CHF wa Mikoa chini ya Kamati za uendeshaji huduma za afya za Mikoa, RHMT ili wawe kiungo kati ya Wizara, Kanda na Halmashauri

    • Kushauri Halmashari nazo ziwe na waratibu wa CHF.

    Pia, Wizara imepanga kuhamasisha na kuziwezesha Halmashauri zote za Miji/Manispaa/Jiji kuanzisha mpango wa Tiba kwa Kadi (TIKA) kwa kutunga sheria ndogo za TIKA na kuidhinishwa katika ngazi ya Halmashauri.

    2.2.2 Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya

    Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeendelea kuimarisha shughuli zake na kuboresha huduma kwa wanachama wake. Mfuko huu sasa upo katika mwaka wake wa nne wa utekelezaji na sote tu mashahidi kuwa matatizo mengi ya awali yaliyotokana na uchanga wa Mfuko huu yamekuwa yakipatiwa ufumbuzi na kazi ya kuuboresha Mfuko huu inaendelea.

    Mwaka 2004/2005 Mfuko ulitekeleza yafuatayo:-

    • Ulisajili wanachama wapya 6,321 na hivyo kuufanya Mfuko kufikisha jumla ya wanachama 248,829 ikilinganishwa na wanachama 242,508 waliokuwepo kipindi cha 2003/2004. Kati ya hao asilimia 56 ni wanaume na asilimia 44 ni wanawake. Juhudi zaidi za kusajili wanachama wapya zinaendelea kupitia ofisi za kanda pamoja na Makao Makuu ya Mfuko ili Watanzania wengi zaidi waendelee kunufaika na Mfuko huu

    • Idadi ya wanaonufaika na mpango huu imeongezeka kutoka 1,115,537 kipindi cha mwaka 2003/2004 hadi kufikia 1,144,614 katika mwaka 2004/2005. Hii ni sawa na asilimia nne (4%) ya Watanzania wote. Kundi la wazee nalo lipo ambapo wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 walioandikishwa na watoto wao kama wategemezi ni 468,148. Mfuko huu utaendelea kuangalia namna bora ya kuwajumuisha wazee wengi hasa kundi la wastaafu chini ya utaratibu huu

    • Umetengeneza jumla ya vitambulisho 949,153 kutokana na fomu zilizopokelewa. Hii ni asilimia 83.1 ya lengo la kutengeneza vitambulisho 1,142,378

    • Mahudhurio katika vituo vya matibabu yameongezeka kutoka wastani wa wanachama 64,917 kwa mwezi katika mwaka 2003/2004 hadi kufikia wastani wa wanachama 98,825 kwa mwezi katika mwaka 2004/2005. Jumla ya mahudhurio (Total attendance) tangu mwaka 2001 hadi Januari 2005 ilikuwa 1,991,977. Kati ya waliotibiwa asilimia 62.5% ni walimu na asilimia 37% ni kundi la wanawake na watoto

    • Aidha, jumla ya shilingi bilioni 7.35 zimekwishalipwa kwa watoa huduma wa Serikali na wale wa asasi zisizo za Serikali tangu utaratibu huu ulipoanza kutumika miaka minne iliyopita, ikiwa ni marejesho kwa huduma walizotoa kwa wanachama

    • Jumla ya vituo 3,558 vya matibabu vilisajiliwa na Mfuko ili kuhudumia wanachama, ambapo asilimia 70 ya vituo hivi vipo vijijini. Kati ya vituo hivi vituo 519 vinamilikiwa na madhehebu ya dini na asasi zisizo za Serikali na maduka ya dawa ni 36 yanamilikiwa na wamiliki binafsi

    • Umeweza kufanya tathmini ya uhai wa shughuli zake kwa kutumia wataalamu wake. Kwa upande wake Shirika la Kazi Duniani (ILO) limeipitia tathmini hiyo na kuridhika nayo. Utekelezaji wa tathmini hiyo utauwezesha uongozi wa mfuko kuboresha mafao mbalimbali pamoja na wigo wake, ikiwemo orodha ya madawa

  • 12

    • Umekwishakamilisha mpango wake wa miaka 5 wa “Strategic Corporate Plan” unaoanza utekelezaji wake katika mwaka ujao wa fedha wa 2005/06. Mfuko utaweka kipaumbele vijijini katika mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa mpango huo makini

    • Umetoa elimu kwa wadau 96,414 wakiwemo viongozi wa vyama vya wafanyakazi, watoa huduma na vilevile kwa vyombo vya habari

    • Umeimarisha ofisi zake saba za kanda kwa kuzipatia nyenzo, vifaa na madaraka zaidi. Katika kipindi hicho jumla ya watumishi 37 waliajiriwa katika Ofisi za Kanda, wengi wao wakiwa ni wakaguzi na hivyo kufanya Mfuko kuwa na watumishi 121 nchi nzima

    • Ulifanya zoezi la sensa kwa wanachama wake pamoja na ukaguzi wa vituo vya matibabu. Zoezi hili lilifanyika katika kanda ya mashariki na kanda ya ziwa na linaendelea katika kanda nyingine. Lengo kuu la zoezi hili, ni kuhakiki taarifa muhimu za wanachama hususan upande wa vitambulisho na upatikanaji wa huduma za matibabu hasa vijijini. Tathmini imeonyesha mafanikio makubwa katika kulipatia ufumbuzi tatizo la vitambulisho, kuimarisha na kuboresha zaidi huduma kwa wanachama

    • Umeweza kuimarisha shughuli zake kupitia teknolojia ya habari na mawasiliano ambapo shughuli nyingi sasa zinafanyika kupitia mfumo huo. Hii ni pamoja na kuziunganisha ofisi zote saba za kanda na Makao Makuu, kurahisisha uandaaji wa malipo kwa watoa huduma na mawasiliano ya haraka na wateja.

    Matarajio ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mwaka 2005/2006

    Mkakati utawekwa wa kutumia mbinu za soko ili kusajili waajiri wote wanaotakiwa kusajiliwa kisheria (k.m, Mashirika ya Umma na Taasisi za Umma) ikiwa ni katika kusajili wanachama wengi zaidi.

    Mfuko utaendelea na zoezi la sensa ya wanachama wake ili kutambua idadi yao, maeneo waishio na upatikanaji wa huduma za Afya katika maeneo husika. Zoezi hili pia linahusisha ujazaji wa fomu za uanachama kwa wanachama ambao walikuwa bado hawajajaza fomu za kujiandikisha na hivyo kutokuwa na vitambulisho. Zoezi hili limebaini kwamba asilimia kubwa ya wanachama wanaolalamikia kutokuwa na vitambulisho ukweli ni kuwa hawajajaza fomu za uanachama wala kuwasilisha picha.

    Mfuko umekwishaanza zoezi la ukaguzi wa watoa huduma wote kwa lengo la kuangalia huduma zitolewazo kwa wanachama, mazingira ya vituo, idadi ya wafanyakazi katika vituo, hali ya vifaa vya vipimo, tiba na vitendea kazi, majengo ya vituo, pamoja na mpangilio wa jinsi wagonjwa wa Mfuko wanavyohudumiwa. Lengo la zoezi la ukaguzi ni kuhakiki na kuboresha huduma za afya zitolewazo.

    Mfuko utaendelea na programu ya uelimishaji kwa kutumia mabango ambayo yanasambazwa katika maeneo ya vijijini ambako njia za mawasiliano ni hafifu. Mabango hayo yatachapisha ujumbe mbalimbali muhimu kuhusu Mfuko, kwa mfano, mafao yatolewayo na Mfuko, namna ya ujazaji wa fomu za uanachama, ujazaji wa fomu za madai, haki na wajibu wa Wanachama na Wadau wengine wa Mfuko.

    Programu maalum ya mafunzo kwa watoa huduma wa ngazi za vituo vya afya na zahanati ambako wanachama wengi wa Mfuko wanatibiwa itaendelea katika kipindi cha mwaka ujao wa fedha ili kujenga uwezo zaidi wa watoa huduma.

  • 13

    Mfuko unatarajia kuingia katika awamu ya mwisho ya zoezi la kufunga mitambo ya mfumo wa kompyuta na mifumo habari katika ofisi zote za Mfuko. Mifumo na mtandao huu wa teknolojia ya habari (TEKNOHAMA) unatarajiwa kuongeza uwezo wa kufanya mawasiliano na watoa huduma na kurahisha taratibu na mchakato wa ulipaji madai na hivyo kupunguza ucheleweshaji na kero zilizokuwepo hapo awali.

    Mfuko unatarajia kuwekeza zaidi katika eneo la utoaji wa huduma za Mfuko katika ofisi za kanda kwa vile uzoefu wa uendeshaji wa ofisi za kanda uliokwishapatikana katika kipindi cha miaka miwili iliyopita umebaini mahitaji zaidi ya watumishi na vitendea kazi.

    Mfuko umekusudia kuandaa na kuanza kutekeleza Mkakati maalum wa miaka mitano (2005 - 2009). Mkakati huu utaweka bayana na kuainisha maeneo ya msingi ambayo Mfuko utayapa kipaumbele katika kuhakikisha kuwa dira, dhamira na mipango ya Mfuko inatekelezwa kama ilivyopangwa.

    Mfuko unatarajia kufanya mapitio ya sera ya uwekezaji ya Mfuko, ili kuweza kuanzisha maeneo zaidi ya uwekezaji, mkakati unaolenga kuleta faida zaidi, pasipo kuwa na uwezekano mkubwa wa kupoteza fedha za wanachama.

    Ongezeko la akiba (Reserve) litauwezesha Mfuko kupanua uwigo wa mafao vikiwemo vipimo zaidi, miwani na muda mrefu zaidi wa kuhudumia wastaafu, ambavyo vitahitaji marekebisho ya sheria.

    Mfuko unakusudia kufanya marekebisho katika baadhi ya maeneo mfano, suala la mafao ambayo hayamo katika kitita cha mafao, (exclusions), wigo wa wanachama na uboreshaji wa mafao, ambavyo vinapendekezwa kuhamishiwa kutoka kwenye Sheria mama na kuwekwa katika Kanuni na Taratibu (Regulations), ili pindi vikihitaji kubadilishwa visiwe vinakuwa na mlolongo mrefu kama kurejeshwa Bungeni ambako huchukua muda mrefu.

    Lengo la marekebisho yote hayo ni kurekebisha mfumo wa utekelezaji na hivyo kuondoa kero mbalimbali zinazowasibu wanachama kwa vile baadhi ya malalamiko ya wanachama ni ya kweli lakini pamoja na dhamira ya Mfuko ya kuyashughulikia malalamiko hayo, sheria ya Mfuko bado hairuhusu maeneo hayo kujumuishwa.

    Lengo la baadaye la Mfuko ni kupanua uanachama ili kujumuisha wananchi wengi zaidi wakiwemo walio katika sekta ya ajira isiyo rasmi, ili kuboresha upatikanaji wa huduma bora ya Afya kwa wananchi wote.

    2.2.3 Mfumo wa Taarifa za Uendeshaji wa Huduma za Afya (MTUHA)

    Wizara imeendelea kutoa kipaumbele kwa upatikanaji wa takwimu katika sekta ya afya. Kumekuwapo na mikakati ya makusudi ili kuhakikisha kuwa takwimu zinazohitajika zinapatikana kwa ajili ya mipango, kutoa tathmini ya utoaji wa huduma za afya, kufuatilia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kisekta na kuboresha sera na miongozo mbalimbali ili kuhakikisha kwamba huduma zinatolewa katika ubora unaostahili.

  • 14

    Katika kufanikisha mipango ya upatikanaji wa takwimu mikakati ifuatayo imetekelezwa katika mifumo inayotumika kupata takwimu:-

    • Mfumo wa Taarifa za Uendeshaji wa Huduma za Afya (MTUHA) umeendelea kuboreshwa katika ngazi ya Wilaya. Hii ni baada ya kuweka kompyuta na programu ya kuchambua takwimu hizo. Hii imesaidia kuongeza kasi ya upatiakanaji wa takwimu katika ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa

    • Takwimu zinazopatikana kupitia mfumo wa kufanya tafiti mbalimbali nao umeimarishwa zaidi. Mafunzo yametolewa kwa viongozi waliomo kwenye Kamati za Afya za uendeshaji wa huduma Wilayani na Mikoani. Lengo kuu la mafunzo hayo lililikuwa kuwapa uwezo wa kimbinu wa kuandaa miswada ya kukusanya takwimu zilizo sahihi, kufanya utafiti, kuchambua takwimu zitokananzo na tafiti na kutumia matokeo ya fafiti ili kuboresha huduma ngazi ya Wilaya na Jamii kwa ujumla

    • Wizara imeendelea kuimarisha kitengo kinachoratibu takwimu za jamii ambazo zinakusanywa katika maeneo maalum hapa nchini. Takwimu hizi ndizo zinazotoa makadirio yanayoonyesha uzito wa matatizo ya magonjwa yanayoisibu jamii yetu

    • Mfumo wa mawasiliano ya kompyuta katika Makao Makuu ya Wizara yamekamilika. Hii itaboresha upatikanaji wa takwimu katika idara, sehemu na vitengo mbalimbali kuwa na kasi zaidi. Mtandao wa kompyuta kupitia mfumo huo umeanza kufanya kazi na huduma nyinginezo zitaongezwa kulingana na mahitaji.

    Matarajio ya Mfuko wa Taarifa za Uendeshaji wa Huduma za Afya mwaka 2005/2006

    Katika mwaka 2005/2006, Wizara inatarajia kuunganisha mfumo wa kompyuta uliopo makao Makuu ya Wizara na mifumo iliyopo mikoani na katika hospitali za mikoa na za rufaa. Lengo kuu ni kurahisisha ubadilishanaji wa taarifa mbalimbali zikiwemo takwimu za afya. Pia Wizara ipo mbioni kuanzisha tovuti yake kwa lengo la kuwapatia wananchi taarifa muhimu zinazohusu sekta ya afya.

    Pia, Wizara ipo mbioni kubadilisha nyenzo za kukusanya takwimu za afya za siku hadi siku. Mabadiliko hayo yanalenga kuhakikisha kuwa takwimu zinazokusanywa kutoka vituo vya kutolea tiba vinaingizwa kwenye kompyuta moja kwa moja badala ya kuandaa ripoti maalum inayopelekwa Wilayani kwa ajjili ya kuingizwa kwenye kompyuta

    Umuhimu wa takwimu kutoka katika jamii unazidi kuongezeka siku hadi siku. Kwa sababu hiyo mwaka 2005/2006 Wizara itaboresha huu mfumo ili vigezo vitakavyopatikana vitoe takwimu ya nchi nzima na sehemu muhimu za jamii. Lengo ni kupanua wigo wa maeneo ya kukusanya takwimu za aina hii.

    2.3 Huduma za Kinga Utekelezaji wa Majukumu mwaka 2004/2005 2.3.1 Udhibiti wa Magonjwa ya Kuambukiza

    Pamoja na juhudi kubwa zinazochukuliwa za kupambana na magonjwa, tatizo la magonjwa ya kuambukiza limeendelea kuwepo nchini. Katika kipindi cha Juni 2004 hadi Aprili 2005 kulikuwa na wagonjwa 3,462 wa kipindupindu na kati yao 93 walifariki ikilinganishwa na kipindi kama hicho 2003/2004 ambapo kulikuwa na wagonjwa 12,397 na vifo 217. Mikoa iliyoathirika zaidi na tatizo hili ni Dar es salaam, Morogoro, Tanga, Kigoma, Mbeya, Kagera, Arusha na Kilimanjaro. Ipo haja ya kuzingatia kanuni za afya bora ili kuondokana na ugonjwa huu unaotokana na uchafu.

  • 15

    Tatizo la watu kuumwa na mbwa au wanyama wanaohisiwa kuwa na kichaa cha mbwa limekuwa likiongezeka kila mwaka. Mwaka 2004 watu 15,528 waliumwa na mbwa au wanyama wanaohisiwa kuwa na kichaa cha mbwa na kati yao watu 98 waliugua ambapo 78 walifariki ikilinganishwa na mwaka 2003 ambapo watu 12,120 waliumwa na kati yao 56 waliugua ambapo 47 walifariki. Wizara inashughulikia kinga ya kichaa cha mbwa, pia iliendelea kuwasiliana na Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuandaa mkakati wa kukabiliana na tatizo la watu kuumwa na wanyama wanaohisiwa kuwa na ugonjwa wa kichaa cha mbwa. Kutokana na kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wananchi wa nchi zetu tatu wamekuwa na uhuru zaidi wa kutembeleana, kwa hiyo Wizara inashirikiana na Wizara husika za Kenya na Uganda katika kupanua wigo wa ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ya milipuko hasa sehemu za mipakani. Udhibiti wa Magonjwa yanayoenezwa na Wadudu (Vectors and Vector Borne Diseases) Katika kipindi cha mwaka 2004/2005 Wizara ikishirikiana na Taasisi ya Viuatilifu ya Arusha (TPRI) imefanya utafiti ili kupata viuatilifu (acaricides) vinavyofaa kuangamiza papasi wanaoleta homa ya papasi na matokeo ya utafiti huu yatakapokamilika yatatolewa kwa wadau. Aidha, wananchi katika mikoa husika wameendelea kuhamasishwa juu ya ujenzi wa nyumba bora na usafi wa mazingira ikiwa ni pamoja na matumizi ya vitanda ili kujiweka mbali na mazalio ya papasi.

    Matarajio ya Udhibiti wa Magonjwa ya Kuambukiza mwaka 2005/2006 Ili kudhibiti magonjwa ya kuambukiza Wizara itaendelea kutoa mafunzo juu ya ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa kwa wataalam katika Wilaya 30. Wizara itaendelea na mapambano dhidi ya magonjwa yanayoenezwa na wadudu wanaoruka, wasioruka pamoja na wanyama (Vectors and vector borne diseases) kwa kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa shughuli za udhibiti wa magonjwa hayo katika Wilaya 20.

    2.3.2 Mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria

    Ugonjwa wa malaria bado ni tatizo kubwa hapa nchini na linahitaji jitihada za pamoja katika kukabiliana nalo. Katika kipindi cha 2004/2005, Wizara ilitekeleza majukumu mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa wa Malaria. Utekelezaji huo ulihusu:-

    • kutoa mafunzo kwa wataalam mbalimbali wa afya kuhusu tiba sahihi, • uhamasishaji juu ya utumiaji wa vyandarua vyenye viuatilifu hasa kwa mama

    wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka 5 • utafiti wa usugu wa vimelea vya malaria • utafiti juu ya tiba ya mseto • utoaji wa tiba ya tahadhari kwa vipindi kwa mama wajawazito • tahadhari za kudhibiti milipuko ya malaria katika wilaya zenye milipuko ya malaria

    na uimarishaji wa udhibiti wa malaria ngazi ya jamii.

    Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea na uhamasishaji wa jamii katika kutumia vyandarua vyenye viuatilifu.

  • 16

    Wizara pia ilizindua Mpango wa Taifa wa Hati Punguzo tarehe 22 Oktoba mwaka 2004, mpango ambao unawawezesha mama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kupata vyandarua vyenye viuatilifu kwa bei nafuu. Kwa hivi sasa, mpango wa Taifa wa Hati Punguzo unatekelezwa katika mikoa ya Dar-es-salaam, Dodoma, Morogoro, Tanga, Pwani, Kilimanjaro na Arusha. Mpango huu utajumuisha mikoa yote ya Tanzania Bara ifikapo mwishoni mwa mwaka 2005. Kufikia mwezi Mei mwaka 2005, mpango huu umeonyesha mafanikio makubwa katika utekelezaji kwani mama wajawazito wapatao 100,000 wametumia Hati Punguzo kununulia vyandarua.

    Matarajio ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria mwaka 2005/2006 Mwaka huu Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali iliadhimisha Siku ya Malaria Afrika iliyofanyika Kitaifa tarehe 25 Aprili, 2005 mkoani Singida. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa “Tushirikiane kwa pamoja tushinde Malaria”. Kauli mbiu hii inakumbusha na kusisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wadau wote katika Afya kupiga vita Malaria, hii ikiwa ni pamoja na jamii, Serikali kuu, Serikali za mitaa, wahisani mbalimbali, mashirika ya dini, watu binafsi nk. Pamoja na jitihada kubwa zinazofanyika ili kudhibiti ugonjwa wa Malaria nchini, kuna Wilaya 25 ambazo zipo katika hatari ya kupata milipuko ya ugonjwa wa malaria. Kwa hali hiyo, Wizara katika mwaka huu wa fedha imeandaa mikakati ya kuziweka wilaya zenye uwezekano wa kupata milipuko ya Malaria katika hali ya tahadhari ya kuweza kutabiri na kudhibiti milipuko hiyo. Wizara imeanza maandalizi ya kubadilisha matibabu ya Malaria kutoka dawa ya SP kwenda dawa ya mseto ya Artemether /Lumefantrine (ALU/Coartem). Maandalizi ya kubadili mwongozo wa matibabu, kuendesha mafunzo kwa watoa huduma za afya kuhusu tiba mpya na kuelimisha jamii yatafanyika. Matarajio ni kuanza kutumia dawa mseto ifikapo mwezi wa 8, mwaka 2006.

    2.3.3 Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma

    Mwaka 2004 kumekuwa na ongezeko la usajili wa wagonjwa wa Kifua Kikuu toka 64,665 mwaka 2003 hadi 65,644 mwaka 2004. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 1.5. Aidha, uponaji wa wagonjwa wa Kifua Kikuu pia umeongezeka kutoka asilimia 80.2 mwaka 2002 hadi asilimia 82.5 mwaka 2003. Ongezeko hili ni la asilimia 2.8. Vilevile, idadi ya wagonjwa wa Kifua Kikuu wasiomaliza matibabu kama ilivyoelekezwa na wahudumu imepungua kwa asilimia 0.5. Kwa upande wa ugonjwa wa Ukoma, wagonjwa wamepungua kutoka 5,771 mwaka 2003 hadi wagonjwa 5,602 mwaka 2004 ambalo ni punguzo la asilimia 3. Mafanikio haya yametokana na utekelezaji wa mikakati ya kudhibiti maradhi haya kwa kushirikisha jamii ambayo ni kuwatafuta, kuwatambua mapema na kutoa tiba kamilifu kwa wagonjwa chini ya usimamizi maalum unaoitwa ‘Directly Observed Treatment Short Course (DOTS)’ kwa ajili ya Kifua Kikuu na Multi -Drug Therapy (MDT) kwa ajili ya Ukoma.

  • 17

    Katika kipindi cha Julai 2004 mpaka Juni 2005, Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma ulifanya ufuatiliaji wa watoto wa shule 1,048 waliobainika kuwa na uambukizo wa ugonjwa wa Kifua Kikuu katika mikoa ya Singida, Iringa, Mbeya, Kigoma na Kagera.

    Asilimia 48 ya watoto hao walipata uambukizo ndani ya kaya zao na jumla ya watoto 75 yaani asilimia 3 walikuwa tayari na ugonjwa wa Kifua Kikuu (active TB) na walipewa dawa za matibabu. Kampeni za kutokomeza ugonjwa wa Ukoma Duniani zilifanyika katika mikoa ya Kagera, Rukwa na Tabora ambako jumla ya wagonjwa wapya 836 waligunduliwa na kuanzishiwa tiba. Aidha, katika juhudi za kurekebisha ulemavu (prevention and rehabilitation of disabilities) unaotokana na Ukoma, watu walioathirika na Ukoma wenye ulemavu 175 walifanyiwa upasuaji wa aina mbalimbali na wengine 5,811 walipewa viatu maalum na watu 37 walipewa miguu bandia. Vile vile, madaktari bingwa wa upasuaji 5 walipewa mafunzo rejea juu ya upasuaji wa wagonjwa waliopata ulemavu kutokana na Ukoma. Katika kipindi cha 2004/2005, jamii iliendelea kuelimishwa kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa matangazo kwa kutumia vyombo vya habari, kusambaza vipeperushi na mabango yenye ujumbe wa jinsi ya kutambua dalili, kujikinga na matibabu ya Kifua Kikuu na Ukoma. Aidha, dawa za kutosha za Kifua Kikuu na Ukoma ziliendelea kusambazwa katika mikoa, wilaya na vituo vyote vya matibabu. Dawa hizo zilitolewa kwa wagonjwa wote bila malipo. Matarajio ya Mpango wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma mwaka 2005/2006 Katika kipindi cha 2005/06 Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma utaendeleza kampeni za kutokomeza Ukoma katika mikoa ya Ruvuma, Morogoro na Tanga. Aidha, shughuli za kurekebisha rejesta za wagonjwa wa Ukoma zitaendelea sambamba na kampeni za kutokomeza Ukoma ili kufikia lengo la kimataifa ifikapo Desemba mwaka 2005. Mpango utaendelea kuimarisha huduma za pamoja za kudhibiti Kifua Kikuu na UKIMWI na zile za kudhibiti Kifua Kikuu sugu ili kisienee nchini. Aidha, uagizaji na usambazaji wa dawa za kutosha za Kifua Kikuu na Ukoma katika vituo vyote vya matibabu nchini utafanywa. Sambamba na hili, Mpango utaendelea kuelimisha jamii kwa kutumia vipeperushi, mabango na kutoa habari kwa njia ya luninga na radio jinsi ya kujikinga na maambukizi, kutambua mapema na taratibu za kufuata wakati wa matibabu ya magonjwa ya Kifua Kikuu na Ukoma. Wizara inategemea kuanzisha huduma kwa wagonjwa wenye Kifua Kikuu sugu (Multi Drug TB) katika hospitali ya Kibong’oto iliyopo Wilayani Hai na kuanzisha mpango wa kutumia dawa za mseto zilizochanganywa pamoja (4 Fixed Dose Combinations) kutibu Kifua Kikuu katika Wilaya 6 za mwanzo za majaribio. Aidha, Wizara itaendelea na utekelezaji wa mpango wa pamoja wa kudhibiti uambukizo wa Kifua Kikuu na UKIMWI katika wilaya za Temeke, Korogwe na Iringa mjini. Bado jitihada za pamoja zinahitajika katika kuelimisha jamii kutambua dalili za Kifua Kikuu na Ukoma, kujitokeza kufanya uchunguzi na kuanza matibabu mapema ambayo hutolewa bila malipo katika vituo vya kutolea huduma za afya.

  • 18

    2.3.4 Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho na Kudhibiti Ugonjwa wa Usubi

    Katika kipindi cha mwaka 2004/2005 Wizara imetekeleza azimio la kimataifa la kutokomeza upofu unaozuilika duniani ifikapo mwaka 2020 (Vision 2020”) kwa kukamilisha na kuuzindua rasmi Mpango/Mkakati wa miaka mitano (2004-2008) wa Huduma za Macho Kitaifa. Mpango/Mkakati huu unatoa dira na mwelekeo wa Huduma za Macho katika jitihada za kudhibiti upofu ambao vyanzo vyake vikuu ni mtoto wa jicho, ukungu wa kioo cha jicho unaosababishwa na Trachoma, upungufu wa Vitamin A na Surua, presha ya macho, matatizo ya kuona yanayorekebishwa na lensi za miwani pamoja na Kisukari. Tanzania ni mojawapo ya mataifa ya kwanza kabisa kukamilisha Mpango Mkakati huu wa Kitaifa. Vilevile, katika kipindi hiki Wizara imeweza kutoa tiba ya ugonjwa wa Trachoma kwa kutumia dawa ya Zithromax kwa mtindo mpya unaoitwa “District Wide Approach” katika Wilaya 6 za Sikonge, Handeni, Dodoma vijijini, Tunduru, Magu na Ruangwa ambapo watu 1,186,913 walitibiwa ikiwa ni juhudi za kutokomeza ugonjwa wa Trachoma ulimwenguni ifikapo mwaka 2020. Wizara pia imeandaa Mpango Mkakati wa miaka mitano (2004-2008) wa kudhibiti Ugonjwa wa Trachoma ambao unatoa dira na mwelekeo wa kuzuia upofu unaosababishwa na ugonjwa wa Trachoma, ugonjwa ambao unakadiriwa kuathiri takriban wilaya 50 hapa nchini. Ili kuharakisha utokomezaji wa upofu utokanao na Trachoma, Shirika la Afya Duniani limetoa mwongozo mpya wa utoaji wa dawa ya Zithromax inayotumika kutibu na kuzuia Trachoma, dawa inayotolewa kwa msaada na kampuni ya Pfizer kupitia Shirika la Kimataifa la kudhibiti Trachoma (International Trachoma Initiative). Mwongozo huu ulipelekea kufanyika kwa utafiti wa awali ili kuweza kujua kiwango cha ugonjwa huu katika ngazi ya wilaya. Wizara kwa msaada wa shirika la Kimataifa la kudhibiti Trachoma imefanikiwa kukamilisha utafiti huo katika Wilaya thelathini zenye ugonjwa huu. Utafiti huu bado unaendelea katika Wilaya 20 zilizobakia. Tanzania ni nchi ya kwanza kufanya utafiti huu kulingana na mwongozo mpya na inachukuliwa kama nchi ya mfano kwa nchi nyingine ambazo zina tatizo la ugonjwa huu kulingana na mafanikio yaliyojitokeza. Matokeo ya awali ya utafiti huu yameonyesha kuwa wilaya 26 kati ya 30 zina ugonjwa huu kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 10. Mpango wa Taifa wa kudhibiti ugonjwa wa Usubi uliweza kugawa dawa ya Mectizan katika vijiji 650 vilivyopo katika Wilaya 14 ambazo ni Ulanga, Kilombero, Kilosa, Songea, Mbinga, Tunduru, Ludewa, Rungwe, Kyela, Muheza, Mvomero, Morogoro, Korogwe, na Lushoto. Jumla ya wananchi 2,948,862 walipatiwa dawa hii katika kipindi cha mwaka 2004/2005. Wizara inatarajia kugawa dawa ya Mectizan kwa wananchi wapatao 3,000,000 katika kipindi hiki. Malengo ya Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho na Kudhibiti ugonjwa wa Usubi mwaka 2005/2006 Katika kipindi cha 2005/2006 Wizara inatarajia kuongeza Wilaya 10 zaidi katika mpango wa kudhibiti ugonjwa wa Trachoma nchini kwa kutumia mtindo mpya wa “District Wide-Approach”. Jumla ya Wilaya 8 kati ya hizo zinatarajiwa kutolewa dawa ya Zithromax kwa wananchi wake.

  • 19

    Wilaya zitakazojumuishwa katika mpango huo ni Kongwa, Kilosa, Meatu, Iramba, Singida vijijini, Igunga, Simanjiro na Mkuranga ambapo watu wapatao 2,300,000 wanatarajiwa kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa Trachoma. Wizara inatarajia pia kugawa dawa ya “Mectizan” kwa ajili ya tiba ya ugonjwa wa Usubi (mass treatment) kwa wananchi wapatao 3,000,000 katika vijiji 690 vilivyoko katika Wilaya 15 za Ulanga, Kilombero, Kilosa, Songea, Mbinga, Tunduru, Ludewa, Rungwe, Kyela, Muheza, Mvomero, Morogoro vijijini, Korogwe, Lushoto na Tunduru.

    23.5 Huduma ya Elimu ya Afya Kwa Umma

    Kwa mwaka 2004/2005, kazi ya kuelimisha na kuhamasisha jamii ishiriki katika kutambua na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya ki-afya yanayoisibu iliendelezwa. Aidha, Wizara inaendelea kukuza uwezo wa Kamati na Bodi za Afya za Wilaya ili ziweze kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini huduma za Elimu ya Afya katika Jamii. Hii ni pamoja na kuwezesha Kamati na Bodi za Afya kubuni mikakati ya mawasiliano ya afya na kuandaa vielelezo vya afya vyenye uwezo wa kuleta mabadiliko yanayohitajika katika kuboresha afya ya jamii.

    Matarajio ya Huduma ya Elimu ya Afya kwa Umma mwaka 2005/2006 Katika kipindi cha 2005/2006, Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma kitaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali kuelimisha wananchi mbinu za kubadili tabia na mitindo ya maisha inayohatarisha afya zao. Aidha, Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma kitaimarisha uratibu na kupanua wigo wa shughuli za utoaji Elimu ya Afya kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari vilivyopo katika jamii yetu, ikiwa ni pamoja na sanaa kwa maendeleo, ili kuweza kufikisha ujumbe wa afya kwa wananchi wengi.

    2.3.6 Huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto

    Katika kipindi cha 2004/2005, huduma maalum kwa wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano ziliendelea kutolewa bila malipo katika vituo vyote vya kutolea huduma vya Serikali. Huduma hizo ni pamoja na huduma kwa wanawake wajawazito, huduma za kujifungua, chanjo, matibabu kwa watoto wagonjwa wenye umri chini ya miaka 5 na uzazi wa mpango. Aidha, Wizara ilihakikisha upatikanaji na usambazaji wa dawa mbali mbali za uzazi wa mpango unafanyika nchini kwa kushirikiana na wahisani mbalimbali. Tathmini ya kina ya kutambua hali halisi ya uwezo wa vituo vyetu katika kukabiliana na dharura ya uzazi pamoja na rufaa imefanyika. Taarifa kamili itakuwa tayari Mwezi Julai 2005. Matokeo yatatumika katika kuimarisha mikakati iliyopo ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ambapo wilaya zitakuwa ni watekelezaji wakuu. Aidha, tathimini ya kitaifa kuhusu hali halisi ya Afya ya Uzazi na Mtoto hapa nchini imefanyika (Tanzania Demographic Health Survey) kwa kushirikiana na National Bureau of Statistics. Matokeo ya awali yatapatikana mwezi Septemba 2005. Tathmini hii itatupatia takwimu ya hali halisi ya sasa ya vifo vya wanawake vinavyotokana na uzazi kitaifa.

  • 20

    Katika kipindi cha 2004/2005, watoa huduma na wakufunzi 130 walipata mafunzo rejea kuhusu uzazi wa mpango kutoka mikoa ya Dodoma, Kilimanjaro, Morogoro, Tanga, Lindi, Mbeya, Pwani na Mwanza. Pia, watoa huduma 100 kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Dodoma, Tanga, Mtwara, Morogoro, Lindi, Mbeya, Mwanza na Pwani walipata mafunzo rejea ya utoaji huduma za wajawazito ikijumuisha matibabu ya tahadhari na kutoa kinga kwa wajawazito dhidi ya Malaria na upimaji wa ugonjwa wa Kaswende. Matarajio ya Huduma ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto mwaka 2005/2006 Wizara ya Afya itaendelea kuboresha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto bila malipo ikiwa ni huduma za matibabu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, chanjo, uzazi wa mpango, huduma kwa wanawake wajawazito ambao watahudhuria kliniki na kujifungua katika vituo vya kutolea huduma vya Serikali. Aidha, Wizara itaendelea kununua na kusambaza dawa za uzazi wa mpango nchi nzima kwa kushirikiana na wahisani. Wizara imetenga fedha kiasi cha shilingi billion 6.8 kwa ajili ya manunuzi hayo na usambazaji. Wizara imepanga kutoa mafunzo mbalimbali katika maeneo ya uzazi wa mpango (100), uzazi salama (80), Afya ya uzazi kwa vijana (40) kutoka katika mikoa ya Kilimanjaro, Dodoma, Tanga, Mtwara, Morogoro, Lindi, Mbeya, Mwanza na Pwani. Ufuatiliaji na usimamizi wa masuala ya afya ya uzazi, mama na mtoto utafanyika katika mikoa saba hapa nchini. Uhakiki wa utumiaji wa dawa za uzazi wa mpango katika maghala ya MSD makao makuu na Kanda (6), pamoja na zile za baadhi ya Wilaya katika Kanda zote saba za Afya ya Uzazi na Mtoto utafanyika ili kuboresha utunzaji wa dawa husika.

    2.3.7 Mkakati wa Kutibu Magonjwa ya Watoto kwa Uwiano (Intergrated Management of

    Childhood Illness-IMCI)

    Wizara ikishirikiana na wahisani iliendelea kutekeleza mkakati wa Udhibiti wa Magonjwa ya Watoto kwa Uwiano unaolenga kupunguza vifo vya watoto hasa vinavyotokana na Malaria, Kuharisha, Pneumonia, Surua na Utapiamlo. Katika kipindi cha 2004/2005, Wilaya 87 zimetekeleza mkakati wa IMCI. Jumla ya Wahudumu wa Afya 300 wamepata mafunzo kuhusu stadi za kumtibu mtoto. Wahudumu 40 kutoka hospitali 7 wamepata mafunzo juu ya huduma ya dharura na kuboresha huduma kwa mtoto aliyezidiwa. Aidha, jamii imeendelea kuelimishwa juu ya mienendo inayoboresha afya ya mtoto. Mienendo hii inakazia lishe kwa mtoto, Makuzi ya Mwili na Akili, pamoja na Uzuiaji wa Magonjwa ya Watoto. Mafunzo haya yametolewa hadi ngazi ya kaya katika Wilaya 13. Matarajio ya Udhibiti wa Magonjwa ya Watoto kwa Uwiano (IMCI) mwaka 2005/2006 Huduma za Afya na matibabu kwa watoto chini ya miaka mitano zitaendelea kuboreshwa katika ngazi zote. Wizara inatarajia kutoa mafunzo ya stadi za kutibu watoto kwa wahudumu wa afya na wakurufunzi 160. Mafunzo ya huduma ya dharura kwa wahudumu wa afya yatafanyika kwa wahudumu 30 na mafunzo ya wakurufunzi ngazi ya Taifa 50 na ngazi ya Wilaya 200 watapata mafunzo ya mienendo inayoboresha Afya ya Mtoto.

  • 21

    2.3.8 Mpango wa Taifa wa Chanjo

    Huduma za chanjo zimeendelea kutolewa nchi nzima kwa watoto wanaostahili kupata chanjo hizo kama juhudi za serikali za kupunguza vifo na magonjwa ya watoto yanayozuilika kwa chanjo. Magonjwa hayo ni Kifua Kikuu, Dondakoo, Kifaduro, Pepopunda, Polio, Surua na Homa ya ini. Viwango vya chanjo vimeendelea kuongezeka vikilinganishwa na viwango vya mwaka uliopita DPT HB3 kutoka 89% hadi 91%, Measles toka 90% hadi 93% Polio toka 92% hadi 93%, Kifua Kikuu kutoka 94% hadi 95%. Mafanikio haya yametokana na juhudi za serikali, jamii wadau mbalimbali pamoja na GAVI.

    Matarajio ya Mpango wa Taifa wa Chanjo mwaka 2005/2006 Katika kipindi cha mwaka 2005/2006, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na mikoa itaendelea kusimamia huduma za chanjo katika ngazi za Wilaya na itaendelea kutoa vitendea kazi na chanjo ili kuhakikisha watoto wote wanaostahili chanjo wanapata chanjo. Aidha, juhudi zitafanywa ili kutokomeza polio, kupunguza magonjwa ya surua, kufuta pepopunda kwa watoto wachanga na kupunguza vifo zitaendelea kuimarishwa. Wizara pia itaendelea kufanya tathmini ya magonjwa mengine yanayozuilika kwa chanjo ambazo hazijaanza kutumika hapa nchini.

    2.3.9 Huduma za Afya Shuleni

    Katika mwaka 2004/2005 Wizara ilisambaza Kadi za kupimia Afya za wanafunzi katika Manispaa za IIala, Temeke na Kinondoni. Waratibu wapatao 150 kutoka ngazi ya mkoa na wilaya walipatiwa mafunzo juu ya Udhibiti wa Magonjwa ya Kichocho na Minyoo mingine. Aidha, utafiti kuhusu ugonjwa wa Kichocho katika shule za msingi umefanyika katika Wilaya zote nchini.

    Matarajio ya Huduma za Afya Shuleni mwaka 2005/2006 Katika mwaka 2005/2006, Wizara ya Afya inategemea kutoa mafunzo ya Huduma ya kwanza kwa Waratibu wa Afya Shuleni ngazi ya Wilaya, kuhamasisha Wilaya kuchangia katika kuchapisha kadi ya kupima afya za wanafunzi kwa shule za awali hadi sekondari. Utoaji wa dawa za Kichocho /Minyoo kwa wanafunzi pia utatekelezwa katika maeneo yaliyoathirika.

    2.3.10 Afya ya Mazingira

    Katika mwaka 2004/2005, Wizara imeimarisha udhibiti wa taka za hospitali (Health care Waste Management) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuendesha mafunzo juu ya udhibiti taka za hospitali na ujenzi wa matanuru katika hospitali za Wilaya za Kilosa na Mahenge, Hospitali ya Ocean Road na Hospitali ya Rufaa ya Kibongoto. Aidha, Wizara imeboresha na kuinua hali ya Afya na Usafi wa Mazingira kwa kuendesha mashindano ya Afya na Usafi wa Mazingira nchini. Mashindano haya yalishirikisha Halmashauiri za Jiji la Mwanza, Manisipaa 12, Halmashauri za Miji 9 na Halmashauri 114 za Wilaya nchini.

    Ili kuinua kiwango cha usafi na ubora wa vyoo, kalibu (Moulds) za kutengenezea mabamba (slab) 560 zilitengenezwa na kusambazwa katika Wilaya za Rungwe, Bagamoyo, Kisarawe, Monduli na Mufindi pamoja na Mkoa wa Kigoma ili zitumike kujengea vyoo bora.

  • 22

    Aidha, Wizara iliandaa na kusambaza miongozo ya utekelezaji wa huduma za Afya ya Mazingira nchini Miongozo na mikakati iliyoandaliwa ni pamoja na:-.

    • Mwongozo wa Mafunzo ya Mbinu Shirikishi Jamii katika kuboresha tabia za Afya na Usafi wa Mazingira

    • Mwongozo wa Udhibiti wa Taka (Waste Management Policy Guideline) • Mkakati wa Kitaifa wa Afya na Usafi wa Mazingira (National Environmental Health,

    Hygiene and Sanitation Strategy) mkakati huu unazingatia malengo ya kuondoa umaskini nchini pamoja na Malengo ya Maendeleo ya Milenia (Millenium Development Goals).

    Matarajio ya Afya ya Mazingira mwaka 2005/2006 Katika kipindi cha 2005/2006, Wizara ya Afya inakusudia kuanzisha Vijiji bora kwa kila Mkoa ambavyo vitakidhi mahitaji yote ya kiafya. Tunatarajia kuanza na Wilaya tano kwa kuchagua Kijiji kimoja kila Wilaya. Aidha, Wizara itaendelea kushirikiana na Wizara mbali mbali, jumuia za kimataifa, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs) na jamii katika upangaji mipango mbinu shirikishi jamii ili kuboresha hali ya afya na usafi wa mazingira katika mikoa yote. Aidha, Wizara itaanza kutekeleza Mpango maalum wa Kudhibiti Taka za Hospitali (Health Care Waste Management) ili kudhibiti hali ya uambukizi wa maradhi kwa watoa huduma, wateja na jamii kwa jumla kwa vile mara nyingi taka zitokanazo na huduma za afya nchini zimekuwa zikionekana zikizagaa ovyo mahali zisipotakikana. Mpango huu utatekelezwa kwa muda wa miaka mitano 2005/06 – 2009/2010 katika mikoa yote. Mpango huu utaanza kwa kuzihusisha hospitali za Halmashauri zote za Wilaya, hospitali za mikoa na hospitali za rufaa nchini. Vilevile, itaratibu mapitio ya sheria ya ‘Drainage and Sewerage Ordinance Cap 259’ ya mwaka 1955 inayosimamia udhibiti wa maji taka nchini. Sheria hii ni ya zamani sana na imepitwa na wakati itapitiwa na kufanyiwa marekedisho yanayokidhi haja ya hali ilivyo kwa wakati huu. Katika kupima maendeleo ya Afya ya Mazingira Wizara itaendeleza mashindano ya Afya na Usafi wa Mazingira nchini, ambayo yataendelea kujumuisha halmashauri zote nchini (Jiji, Manisipaa, Mji na Wilaya). Lengo kuu la mashindano haya ni kushirikisha wananchi, sekta binafsi katika kuboresha hali ya usafi wa mazingira katika maeneo yao

    2.3.11 Huduma za Afya Mipakani

    Katika kuhakikisha kuwa udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza kutoka nje ya nchi unaimarika, Wizara imeboresha huduma za Afya Mipakani ambapo maafisa wa Afya wamepata mafunzo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kupambana na majanga. Pia, vituo vimeimarishwa kwa kuongeza vitendea kazi na kuajiri wataalam wa afya katika vituo vya Afya. Katika mwaka huu wa fedha, zaidi ya tani 5,470,000 za vyakula zilikaguliwa ambapo tani 40,800 ziliharibiwa baada ya kuthibitika kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.

  • 23

    Matarajio ya Huduma za Afya Mipakani mwaka 2005/2006 Wizara itaendelea kuhakikisha kuwa magonjwa ya kuambukiza ya kimataifa yanadhibitiwa kwa kufuata sheria za Afya za Kimataifa. Vituo vya mipakani vitapatiwa nyenzo na vitendea kazi vya kisasa ikiwemo usafiri. Pia, udhibiti wa uingizwaji wa vyakula, dawa na vipodozi visivyokidhi viwango vya Afya utaimarishwa kwa kushirikiana na wadau wengine kwa Halmashauri zote nchini 113.

    2.3.12 Afya katika Sehemu za Kazi

    Kwa kuzingatia umuhimu wa Afya ya Wafanyakazi hususan maeneo ya viwanda, ujenzi na mashamba, Wizara imefanya uhamasishaji wa kamati za Halmashauri za Wilaya 48 juu ya uainishaji wa huduma za afya sehemu za kazi na huduma za afya ya msingi. Shughuli za usimamizi na ufuatiliaji wa afya sehemu za kazi zimefanyika katika Halmashauri 12. Aidha, mafunzo kwa wachimbaji wadogo wadogo 70 wa madini katika Mikoa ya Arusha na Mwanza yamefanyika. Matarajio ya Afya katika Sehemu za Kazi mwaka 2005/2006 Kwa kutambua umuhimu wa afya ya wafanyakazi mahali pa kazi, Wizara imeweka mikakati ya kuwafikia na kuwahamasisha wafanyakazi wote juu ya madhara yatokanayo na kazi ifikapo 2015. Aidha Wizara imeweka mikakati endelevu inayotilia mkazo juu ya uzuiaji wa maambukizi ya UKIMWI mahali pa kazi. Ili kufikia azma hii madaktari 118 wa Halmashauri za Wilaya watapatiwa mafunzo juu ya uboreshaji wa afya ya wafanyakazi sehemu za kazi.

    2.3.13 Huduma za Afya Wilayani (District Health Services)

    Utekelezaji wa mabadiliko ya Sekta ya Afya ngazi ya Wilaya yalianza kutekelezwa kwa awamu tatu tofauti. Awamu ya kwanza ilikuwa kwa Halmashauri 37 kwa mwaka 2000, awamu ya pili 2002 Halmashauri 45 na awamu ya mwisho Halmashauri 31 na kufanya jumla ya Halmashauri za Wilaya, Jiji, Miji na Manispaa 113. Utekelezaji ulianza kwa kufundisha Halmashauri zote namna ya kuandaa Mipango Kambambe ya Afya ya Halmashauri (Comprehensive Council Health Plan) na kutayarisha taarifa za robo mwaka za utekelezaji zikihusu fedha na kazi halisi zilizotekelezwa (quarterly progress implementation reports – technical and financial). Mpaka sasa Halmashauri zote zinaandaa, kutekeleza na kutoa taarifa ya utekelezaji wa mipango hii kama ilivyopangwa.

    Mabadiliko yamekwenda sambamba na uundaji wa taasisi na miundo ya kuwezesha jamii kushiriki katika uendeshaji, umiliki na usimamizi wa huduma za afya. Vyombo hivyo ni Bodi za Huduma za Afya za Halmashauri na Kamati za Vituo vya Tiba. (Council Health Service Boards and Health Facility Governing Committees). Aidha, mpaka sasa Halmashauri zote 113 zimehamasishwa na kuridhia uundaji wa Bodi za afya na Kamati za Vituo vya Tiba. Hati Rasmi pamoja na Sheria Ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii zipo katika ngazi ya utekelezaji kwa kuwa zikitoka Wilayani zinapelekwa mikoani ili kupitiwa na kuandikiwa barua na kupelekwa kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa. Mwisho Katiba na Sheria kuandikwa kama Sheria na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.

  • 24

    Mpaka sasa kati ya Halmashauri 113 zilizohamasishwa ni Halmashauri 70 tu ambazo zimezindua Bodi za Huduma za afya na Kamati za vituo vya Tiba na zinafanyakazi. Wizara pia kwa mwaka jana ilibadilisha magari mapya 24 kwenye Halmshauri kwa ajili ya ufuatiliaji na usambazaji wa dawa na vifaa tiba na kinga kwenye vituo vya kutolea huduma. Matarajio ya Huduma za Afya Wilayani (District Health Services) mwaka 2005/2006 Mwaka 2005/06 Wizara itakamilisha uzinduzi wa Bodi za Afya katika Halmashauri 63 zilizobakia mara Sheria zao zitakapotangazwa kwenye Gazeti la Serikali. Sambamba na uzinduzi na uhamasishaji wa Bodi na Kamati za vituo vya Tiba, pia Halmashauri zitaendelea kuhamasishwa ili kuanzisha Mfuko wa Afya wa Jamii (Community Health Fund). Kwa vile hadi sasa Halmashauri za Wilaya 40 kati ya 113 zinatekeleza Mfuko wa Afya wa Jamii. Kwa kuwa Mfuko wa Afya wa Jamii unaendana na uzinduzi wa Bodi za Afya za Halmashauri inategemewa kwa mwaka wa 2005/06 kusaidia Halmashauri 73 zilizobakia ziwe zinatekeleza Mfuko huu. Wizara kwa mwaka 2005/06 itaendelea kutoa usimamizi wa kitaalam kwa Halmashauri juu ya uendeshaji wa huduma za afya katika ngazi ya Wilaya ili kuboresha huduma na kuendelea kubadilisha na kupeleka magari mapya 10 kwenye Halmashauri kwa ajili ya ufuatiliaji na usambazaji wa dawa na vifaa muhimu vya afya. Wizara itatoa mafunzo juu ya uainishaji wa MKUKUTA (NSGPR), Kitita cha Huduma Muhimu za Afya (NEPHI), Mpango wa Mabadiliko ya Afya wa miaka mitano (HSSP) na Mipango Kabambe ya Halmashauri CCHP). Aidha, mafunzo yatatolewa kwa timu za uandaaji Mipango ya Afya ya Halmashauri jinsi ya kutumia teknolojia ya kisasa ya kukotoa hesabu za bajeti za mipango ya Halmashauri (CCHP) kwa kulinganisha na mzigo wa magonjwa (Burden of Disease).

    2.3.14 UKIMWI

    Katika kukabiliana na janga hili la UKIMWI nchini, Wizara ilitekeleza Mkakati wa Sekta ya Afya wa Kudhibiti UKIMWI 2003-2006, ambao ni pamoja na Huduma ya Damu Salama, kutoa Ushauri Nasaha, Kufuatilia Mwenendo wa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI katika Jamii, pamoja na Huduma ya Magonjwa ya Ngono (Sexually Transmitted Infections – STI). Mwaka 2004/05, kulikuwa na azma ya serikali ya kuanzisha mpango wa kitaifa wa kutoa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI. Mpango huu uliweza kununua dawa kwa kutumia fedha zilizotengwa na Serikali. Hadi sasa wagonjwa wapatao 4,200 wameanzishiwa dawa hizo katika vituo hivyo 32. Aidha, dawa zaidi zimeagizwa na zinategemewa kupokelewa hapa nchini kuanzia mwishoni wa mwezi April 2005. Dawa hizo zitatosha kuwaanzishia wagonjwa waliokusudiwa dawa wapatao 44,000.

    Aidha, katika kujenga uwezo wa hospitali wa kupima wagonjwa wa UKIMWI na kutambua hatua ya ugonjwa kwa lengo la kuanzisha matibabu, machine za Facs Count zinazopima viwango vya chembechembe za CD4 zipatazo 20 zimenunliwa na kusambazwa katika hospitali zote za rufaa na baadhi ya hospitali za mikoa. Mashine nyingine nane (8) zimeagizwa kwa ajili ya hospitali za mikoa iliyobakia.

  • 25

    Aidha, mafunzo kwa wataalam wa afya ambao watatoa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI kwa wagonjwa yametolewa kwa wataalam mbalimbali wa afya wapatao 492 kutoka vituo 96 vya kutolea huduma za Afya. Vituo hivyo 96 vinajumuisha hospitali zote za rufaa na mikoa, baadhi ya hospitali za Wilaya, hospitali za Mashirika ya dini na Watu Binafsi. Huduma za kutoa madawa ya kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI zitaendelezwa kwa awamu kulingana na uwezo wa kifedha wa Serikali. Nchi yetu ina idadi kubwa ya watu wanaaohitaji dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI. Idadi hiyo ambayo inakisiwa kufikia watu 500,000 ni kubwa sana kulinganisha na uwezo. Serikali itaendelea kuongeza idadi ya wagonjwa wanaopata huduma hii kwa awamu mpaka wote wafikiwe. Matarajio ya Mpango wa kukabiliana na Ugonjwa wa UKIMWI mwaka 2005/2006 Katika kuendelea kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI na kutoa huduma kwa wale walioathirika na ugonjwa huu, Wizara mwaka 2005/2006 itaendelea kufuatilia mwenendo wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI katika jamii kwa kufuatilia wajawazito katika kliniki 93 zilizopo kwenye mikoa 15 ya Tanzania Bara. Matokeo ya ufuatiliaji huu yatatoa picha kuhusu kuenea kwa virusi vya UKIMWI katika jamii na matokeo ya mikakati inayoendelea ya kudhibiti UKIMWI. Katika kipindi hiki, Wizara itakamilisha kuandaa utafiti wa kufuatilia usugu wa virusi vya UKIMWI kwa madawa yanayotumika hivi sasa kupunguza makali ya UKIMWI. Hivyo, ufuatiliaji wa usugu wa madawa ya kupunguza makali ya UKIMWI (HIV drug resistance threshold surveys) utaanzishwa katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo dawa za kupunguza makali ya UKIMWI yalianza kutumika miaka kadhaa kabla ya serikali kuanza mpango wa kutoa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI kwa wagonjwa wa UKIMWI. Matokeo yake yatasaidia katika kugundua dawa ambazo tayari Virusi vya UKIMWI vimekwisha kuwa sugu nazo kiasi kwamba haziwezi kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI na hivyo kusaidia wataalam kutoa maelekezo ya dawa zinazofaa. Wizara itanunua na kusambaza dawa za kupunguza makali ya UKIMWI katika vituo 180 vilivyoteuliwa kutoa huduma hiyo kote nchini ili kuwafikia wagonjwa wapya 56,000 ili kufikia lengo jipya lililowekwa la kuwafikia wagonjwa 100,000 nchini kote ifikapo Juni 2006. Vituo vipya vitakavyohusishwa katika mpango huu ni pamoja na hospitali zote za Wilaya na hospitali za binafsi ziliopo kwenye mikoa ya pembezoni na mikoa iliyo na viwango vya maamukizi ya UKIMWI zaidi ya asilimia saba. Huduma za ushauri nasaha na upimaji wa hiari zitaendelea kutolewa katika vituo 521 vinavyotoa huduma ili kuweza kutoa ushauri nashaha kwa wagonjwa wote 100,000 watakaokuwa kwenye tiba ya dawa za UKIMWI. Aidha, tutahakikisha mafunzo kwa wataalam wa kutoa huduma za dawa za kupunguza makali ya UKIMWI katika kila kituo yatatolewa na angalau watalam wanne ambao wameshapatiwa mafunzo wanakuwepo katika vituo vya huduma. Wizara itaendelea kutoa huduma za Magonjwa ya Zinaa katika mikoa yote 21 pamoja na kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa wa UKIMWI hususan kuacha kuwanyanyapaa wagonjwa wa UKIMWI na kuzingatia matumizi sahihi ya dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI.

  • 26

    2.3.15 Mradi wa Uimarishaji Huduma Muhimu za Afya (MUHUMA) TEHIP

    Mradi wa Uimarishaji Huduma Muhimu za Afya (MUHUMA) umekuwa ukitekelezwa katika Wilaya mbili za Morogoro vijijini na Rufiji toka Mwaka 1997 mpaka mwaka 2004 ulipofikia kikomo kama mradi. Utafiti umeonyesha kuwa kasi ya vifo imepungua katika Wilaya zote mbili kwa asilimia zaidi ya 55% kwa watoto chini ya miaka mitano na asilimia 18% kwa watu wazima. Kupungua huku kumeziweka Wilaya hizo mbili kwenye matumaini ya kufikia moja ya malengo ya milenia ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza kasi ya vifo miongoni mwa watoto chini ya miaka mitano kwa theluthi mbili ifikapo mwaka 2015.

    Kufuatana na matokeo haya, Wizara ya Afya ikishirikiana na wadau wengine imeanza mikakati ya kupata fedha za kueneza mbinu na nyenzo zilizobuniwa na kufanyiwa kazi katika Wilaya hizo mbili katika Wilaya zote nchini. Dhana ni kuwa endapo nchi nzima itatekeleza yaliyofanywa Morogoro na Rufiji basi kasi ya vifo vya watoto wadogo na wakubwa itapungua na hivyo Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kutekeleza mpango huo.

    2.4 Idara za Tiba Utekelezaji wa Majukumu mwaka 2004/2005

    2.4. 1 Huduma za Uchunguzi wa Magonjwa

    Mradi wa uimarishaji wa huduma za X-ray na Ultrasound ulikabidhiwa kwa Serikali kutoka kampuni ya “Philips Medical Systems” ya nchi ya Uholanzi ili tuweze kuuendeleza wenyewe. Makabidhiano hayo yalifanyika Jijini Mwanza katika hospitali ya Bugando tarehe 22 Februari 2005, ambapo Mheshimiwa Rais alikabidhiwa mashine kubwa na maalum ya Ultrasound kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni hiyo yenye thamani ya takriban fedha ya kitanzania shilingi milioni 88. Mashine nyingine ilipelekwa Zanzibar katika hospitali ya Mnazi mmoja tarehe 14 Machi, 2005. Aidha, Wizara iliagizwa kusimamia ukarabati na kinga ya matengenezo ya mashine hizo baada ya mradi kwisha ifikapo mwishoni mwa mwaka 2005. Vilevile, Wizara imekamilisha taratibu zote za kupeleka Bungeni muswada wa sheria inayohusu usajili wa wanataaluma ya mionzi ili kuboresha huduma za mionzi. Kuhusu usimamizi na utekelezaji wa huduma za karakana zetu za Kanda, Wizara imeendelea kuziimarisha kwa kuzipatia vipuli, vifaa na nyenzo za utekelezaji wa matengenezo ya mashine hizo za kutolea huduma za Afya. Kuhusu uimarishaji wa maabara za hospitali ili ziweze kufuatilia wagonjwa wanaopatiwa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI, Wizara imekwishaweka mashine 20 za kupima CD4 katika hospitali zote za rufaa na mikoa 16. Mashine nyingine 8 za CD4 na dawa zake zimeshawasili kwa ajili ya mikoa iliyobaki na hospitali za manispaa za Dar es Salaam. Vilevile, mashine kwa ajili ya vipimo vingine (Clinical Chemistry and Haematology) kwa ajili ya hospitlai 10 za mikoa na 13 za Wilaya zimegizwa. Vipimo hivyo ni kwa ajili ya kufuatilia athari za ARV (Toxicity follow up) kwa wagonjwa wanaotumia. Kuhusu huduma ya damu salama, ujenzi wa vituo vya kanda vya upatikanaji wa damu (Zonal Blood Transfusion Centres- ZBTC) umekamilika katika Kanda za Ziwa, Kasikazini na Nyanda za juu Kusini. Kwa upande wa Kanda ya Mashariki, ujenzi umeshaanza Dar es Salaam na kanda ya Kusini ujenzi haujaanza. Mwongozo wa huduma za damu salama umekamilika.

  • 27

    Matarajio ya Huduma za Uchunguzi wa Magonjwa mwaka 2005/2006 Wizara itaingia mkataba na Kampuni ya Philips Medical Systems katika kuhakikisha kuwa, mashine za X-ray, Ultrasound na vifaa vingine chini ya mradi wa kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa nchini zinadumu kwa miaka mingi. Katika mkataba huo mafunzo maalum hasa yale ya mashine zenye teknolojia ya hali ya juu hususan X-ray na Ultrasound yatatolewa kwa watumiaji, makandarasi na mafundi wetu waliopo kwenye karakana za Kanda. Mkataba huu utakuwa wa miaka 5 kuanzia Januari 2006 hadi Desemba 2010. Wizara pia itaendelea kuvifanyia matengenezo ya mara kwa mara vifaa tiba kupitia karakana za kanda kwa maeneo yote yanayotoa huduma ya afya kuanzia zahanati hadi hospitali za rufaa, kwa utaratibu utakaopangwa kwa ajili ya utekelezaji wake kufuatana na mwongozo wa Wizara juu ya uboreshaji na matengenezo ya vifaa tiba vya hospitali nchini. Wizara inakusudia kupeleka Bungeni muswada wa sheria inayohusu taaluma ya mionzi nchini katika mwaka 2005/06. Pia Tanzania imepewa heshima na nchi za Afrika ya kuwa mwenyeji wa kongamano la wanataaluma ya Radiologia kutoka Afrika mnamo mwezi Septemba, 2005. Wizara itaendelea kuimarisha huduma za maabara kwa kuagiza mashine nyingine, na vifaa vya maabara kwa ajili ya kufuatilia wagonjwa wanaopatiwa dawa za kusaidia kupunguza makali ya UKIMWI. Aidha, baadhi ya maabara zitaboreshwa kwa kufanyiwa ukarabati ili kukidhi mahitaji ya utoaji wa huduma hizo. Kuhusu huduma ya damu salama, Wizara itakamilisha ujenzi wa Kanda ya Mashariki pamoja na kuanza mipango ya ujenzi wa Kanda za Kusini (Mtwara) na Kati (Dodoma). Wakati huo Kanda za Ziwa, Nyanda za Juu Kusini na Kaskazini zitaanza kazi ya ukusanyaji wa damu salama katika hospitali zetu kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania.

    2.4.2 Huduma za Tiba Asili

    Mwaka 2002/2003 muswada wa Sheria ya Dawa, Tiba Asili na Tiba Mbadala, ulipitishwa na Bunge. Utekelezaji wa Sheria Namba 23 ya mwaka 2002 utaanza July 2005. Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala tayari limekwisha teuliwa na mamlaka husika kwa mujibu wa Sheria hiyo. Wizara ya Afya imeandaa Kanuni na Miongozo ya usajili wa Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala. Usajili wa vituo vya kutolea huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala; nidhamu na maadili kwa Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala; usimamizi na usajili wa bidhaa nyinginezo za Asili zinazotumika kwa ajili ya afya ya binadamu. Matarajio ya Huduma za Tiba Asili mwaka 2005/2006 Wizara itaendelea kuwaelimisha Waganga wa jadi na Wadau wa Tiba Asili na tiba mbadala ili kuielewa sheria ya tiba asili na tiba mbadala. Aidha, Wizara itaendelea na ufuatiliaji wa tiba asili na tiba mbadala likiwemo suala la utafiti.

  • 28

    2.4.3 Huduma za Afya ya Kinywa

    Katika mwaka 2004/2005, Wizara ya Afya imefunga vifaa vya Tiba ya Meno (Dental Units) katika Halmashauri za Wilaya zifuatazo: Mbarali, Karatu, Ngorongoro, Simanjiro, Kiomboi, Morogoro Vijijini, Morogoro Manispaa, Mbozi, Hanang, Sikonge, Mpanda, Mvomero, Bariadi, Bukombe, Kilombero, Liwale, Njombe, Ludewa, Sengerema, Geita, Ukerewe, Misungwi, Newala, Mwanga na Kwimba. Pia, vifaa vilifungwa katika hospitali zifuatazo: Iringa, Bombo, Mawenzi, Mt. Meru na KCMC. Aidha dawa na vifaa muhimu vya tiba ya meno vilinunuliwa kwa ajili ya matumizi ya hospitali za mikoa na kwa ajili ya mafunzo vyuoni.

    Matarajio ya Huduma za Afya ya Kinywa mwaka 2005/2006

    Katika mwaka wa fedha 2005/2006 awamu ya pili ya ufungaji vifaa kwa kuzipatia kliniki za meno za Wilaya na Halmashauri viti (Dental Chairs), taa maalum (operating lights) na viti vya kukalia madaktari wa meno wanapofanya kazi (Operating Stools) utaanza. Wilaya/Halmashauri zitakazopatiwa vifaa hivyo ni:- Muheza, Korogwe, Chunya, Ileje, Mbeya Vijijini, Mbeya Manispaa, Mbarali, Rungwe, Kyela, Karatu, Ngorongoro, Simanjiro, Iramba, Morogoro Vijijini, Morogoro Manispaa, Mbozi, Hannang, Singida, Tabora, Sikonge, Mpanda, Musoma, Kigoma, Kilombero, Mvomero, Bariadi, Bukombe, Kishapu, Liwale, Njombe, Ludewa, Bukoba, Karagwe, Sengerema, Geita, Ukerewe, Misungwi, Newala, Mwanga, Kwimba, Dodoma Manispaa, Tarime, Bunda, Biharamulo, Tabora Manispaa, na Mbinga. Pia hospitali zifuatazo zitapatiwa vifaa hivyo; Kibosho, Mbeya Rufaa, Mawenzi, Mt. Meru, Bombo, Iringa, Dodoma, Mbeya Mkoa, Mirembe, Kilema, Bugando, Dareda, Ligula, Maweni, Singida na Bukoba.

    2.4.4 Huduma za Afya ya Akili na Vita dhidi ya Dawa za Kulevya

    Mwaka 2004/2005, Wizara imeendelea kusimamia uboreshaji wa huduma za afya ya akili ngazi ya msingi. Shughuli hizo zinaendelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Manyara, Mtwara na Mwanza. Toleo rasmi la kwanza la vitabu vya Huduma ya Afya ya Akili ngazi ya Msingi vimechapishwa nakala 4,500 na kusambazwa kulingana na utaratibu wa kutoa mafunzo katika kila Mkoa. Matarajio ya Huduma za Afya ya Akili mwaka 2005/2006 Kitengo kitaendelea na mipango ya kueneza huduma ya afya ya akili ngazi ya msingi kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje katika Mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Mwanza kwa kushirikiana na MEHATA na CORDAID na Mkoani Mtwara kwa kushirikiana na shirika la Basic Needs. Mpango wa kutoa Mafunzo kwa watoa huduma ngazi ya msingi utaendelea katika Mikoa ya Dar es Salaam na Manyara. Pia, Wizara inategemea kukamilisha uchapishaji wa mwongozo wa Sera ya Afya ya Akili.

  • 29

    2.4.5 Huduma za Hospitali za Mashirika ya kujitolea, Makampuni na Watu Binafsi

    Katika mwaka 2004/2005, Hospitali mbili za Mashirika ya Dini (Karatu na Mugana) ziliombwa na Halmashauri za Wilaya ya Karatu na Bukoba Vijijini zitumike kama Hospitali Teule. Hospitali hizo tayari zimeanza kutumika kama hospitali Teule za Wilaya hizo. Ruzuku ilibakia kuwa TShs 30,000/= kwa kitanda kwa mwaka. Kulikuwa na ongezeko la vitanda 174 kwa ajili ya kupewa Ruzuku. Jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya vilivyosajiliwa mwaka 2004/2005 ni 53 ambavyo ni 73% kati ya 73 vilivyoombewa usajili.

    Matarajio ya Huduma za Hospitali za Mashirika ya kujitolea, Makampuni na Watu Binafsi mwaka 2005/2006

    Wizara itaanza kutumia “Service Agreement” katika kufanya makubaliano kati ya Halmashauri za Wilaya na wamiliki wa hospitali za mashirika ya dini. Vile vile, Wizara itajadili maombi ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuhusu kutumia hospitali ya Tosamaganga kama hospitali Teule ya Wilaya hiyo.

    2.4.6 Huduma ya Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba

    Mwaka 2004/05, kiasi cha Tshs. 35,175,356,000 zilitumika kununua dawa, vifaa na vifaa tiba kwa matumizi ya hospitali, Zahanati na Vituo vya Afya. Aidha, hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa ziliendelea na utekelezaji wa uchangiaji wa gharama za dawa chini ya mfumo wa ‘Capitalization of Hospital Pharmacies’ ambapo wananchi wanalipa nusu ya bei halisi ya dawa. Fedha kutokana na mauzo ya dawa ziliingizwa kwenye mfuko wa dawa (Drug Revolving Fund) kuwezesha hospitali hizo kununua dawa nyingine zilizohitajika. Mwaka 2004/2005, Zahanati mpya 526 na Vituo vya Aya 36 vilivyojengwa na Halmashauri na kwa nguvu za wananchi vilipewa masanduku ya dawa. Aidha, Zahanati 716 na vituo vya afya 88 katika Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza na Shinyanga vilianza kuagiza dawa na vifaa kwa kutumia mfumo wa Indent. Ili kurahisisha utoaji wa dawa na vifaa kwa mfumo huu, sehemu maalum imejengwa katika Bohari ya Mwanza kwa ajili ya kuhudumia Zahanati na Vituo vya Afya hivyo. Kutokana na hatua hiyo, Bohari ya Mwanza sasa imeondokana na mfumo wa usambazaji wa masanduku ya dawa. Wizara pia ilitoa mafunzo ya utekelezaji wa mfumo wa Indent kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati za Uendeshaji wa Huduma za Afya katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga. Wajumbe hawa watatoa mafunzo kwa watumishi katika Zahanati na Vituo vya Afya katika mikoa yao ili kuwezesha uagizaji wa dawa na vifaa kulingana na mahitaji na kwa kuzingatia mgao wa fedha na maradhi katika sehemu zao. Bohari ya Dawa iliendelea na usambazaji wa dawa na vifaa vya miradi misonge (vertical programmes) na vya misaada. Katika kipindi hicho, Bohari ya Dawa ilisambaza chanjo, dawa za kutibu Kifua Kikuu na Ukoma, Usubi, Uzazi wa Mpango, Matende, Ngirimaji na magonjwa ya mtegesheo kwa watu waishio na UKIMWI.

  • 30

    Matarajio ya Huduma ya Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba mwaka 2005/2006

    Katika mwaka wa fedha 2005/06, Wizara ya Afya imetengewa jumla ya Tshs. 32,320,996,556 kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa na vifaa tiba kwa matumizi ya Zahanati, Vituo vya Afya na hospitali za Serikali na hospitali Teule kwa matumizi ya kawaida. Pia Serikali imetenga Tshs. 20,000,000,000 kwa ajili ya ununuzi na usambazaji wa dawa na vifaa tiba vya kupunguza makali ya UKIMWI. Wizara ya Afya kupitia Bohari ya Madawa, itasambaza dawa na vifaa katika Zahanati 3,500 na Vituo vya Afya 400. Kati ya hivyo, Zahanati 175 na Vituo vya Afya 25 vitakuwa vipya vilivyojengwa na Halmashauri na nguvu za wananchi. Aidha, katika kuboresha usambazaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba, Wizara ya Afya itaendesha majaribio ya mfumo ujulikanao kama Integrated Logistics System katika mikoa ya Dodoma na Iringa. Mfumo huu utawezesha Zahanati, Vituo vya Afya na hospitali kuagiza dawa na vifaa vya kawaida na vile vya miradi na misaada chini ya mfumo mmoja. Mfumo huu unatarajiwa kuiwezesha Wizara kukusanya takwimu za mahitaji na matumizi halisi ya dawa, vifaa na vifaa tiba.

    2.4.7 Huduma za kuzuia Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto

    Katika mwaka 2004/2005 wizara imesambaza huduma ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mototo katika mikoa 9 zaidi ya Tanzania bara na kufanya huduma hii kupatikana katika hospitali zote za mikoa na 82 za Wilaya. Mikoa hiyo ni Lindi, Dodoma, Ruvuma, Rukwa, Kigoma, Mara, Shinyanga, Tanga na Singida.

    Vilevile, wizara inashirikiana na wadau mbalimbali ilikuweza kusambaza hudma hii katika hospitali na vituo vya kutolea huduma vinavyomilikiwa na mashirika ya dini.

    Wizara imeendelea na mpango wa kutoa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI kwa akinamama wajawazito, wazazi wenzao na watoto wao. Mpango huu ambao unaitwa “MTCT –Plus” unaenda sambamba na mpango wa Taifa wa kutoa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ART programe) na hivyo umeanza kutekelezwa katika vituo 96 vilivyo katika mpango wa ART.

    Matarijio ya Huduma za kuzuia Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto mwaka 2005/2006 Katika mwaka 2005/2006 Wizara ya Afya imepanga kupanua huduma ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) katika wilaya 20 zaidi ambazo hazina huduma hiyo na kufanya jumla ya wilaya 102 kuwa na huduma hii. Vile vile, Wizara itaendelea kuimarisha huduma ya “MTCT – Plus” ambayo imeanza kutolewa katika vituo vile 96 vilivyo katika mpango wa “ART Programme”. Lengo ni kuhakikisha akinamama wajawazito walioathirika na VVU na wenye vigezo vya kupata “ART” wapate huduma hiyo na wale ambao hawana vigezo wakisha jifungua waendelee kufuatiliwa na pindi watakapobainika kuwa wana vigezo wapatiwe huduma ya ART.

  • 31

    2.4.8 Huduma ya Matibabu Nje ya Nchi

    Wizara imefanya mazungumzo na wahisani kutoka nje ya nchi ili kuanzisha hapa nchini huduma ya tiba ya magonjwa ambayo kwa sasa yanatibiwa nje ya nchi. Wahisani hao ni Serikali ya Japan na Serikali ya Watu wa China. Mipango hii imelenga kulipunguzia Taifa gharama za tiba nje ya nchi pamoja na kuwapunguzia wagonjwa maumivu wakati wakingojea kwa muda mrefu kwenda kutibiwa nje ya nchi kutokana na upungufu wa fedha. Matarajio ya Huduma ya Matibabu Nje ya Nchi mwaka 2005/2006 Bajeti itaongezwa ili kuwezesha wagonjwa wengi zaidi kupelekwa kutibiwa nje ya nchi na kuendelea kutoa msaada kwa matibabu ya wagonjwa ambao badala ya kupelekwa kutibiwa nje ya nchi watatibiwa hapa nchini kwa vile wanashindwa kumudu gharama za matibabu hayo.

    Wizara itaendelea kushirikiana na mashirika na hospitali zinazoanzisha utoaji wa matibabu ambayo kwa sasa yanapatikana nje ya nchi, pamoja na Serikali ambazo zina mpango wa kusaidia nchi kuweza kutoa matibabu kama hayo.

    2.5 Huduma ya Utawala na Watumishi 2.5.1 Idara ya Utawala Utekelezaji wa Majukumu mwaka 2004/2005

    Mwaka wa 2004/2005, Wizara ya Afya imeendelea kutekeleza Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya Mwaka 1999, kwa kuajiri jumla ya Watumishi 148 wa kada mbalimbali za Afya. Aidha, katika kushughulikia maslahi na maendeleo ya watumishi ili kuimarisha utendaji kazi Wizara imewapandisha vyeo watumishi 6,587. Hili ni ongezeko la asilimia 65 ya lengo lililokuwa limewekwa la kuwapandisha vyeo watumishi 4,000. Watumishi wapatao 110 wa kada na ngazi tofauti walifanyiwa upekuzi (vetting) kwa madhumuni ya kuwawezesha kuelewa na kuzingatia misingi ya maadili mema katika utumishi wa Umma kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu zilizopo. Msisitizo mkubwa uliowekwa katika mafunzo hayo ulihusu suala zima la matumizi sahihi ya taarifa za Serikali na utii kwa Serikali. Aidha, Wizara iliendelea kutoa mafunzo ya jinsia kwa watumishi ili kuendelea kudumisha Utawala Bora ambapo jumla ya watumishi 744 walipatiwa mafunzo hayo. Pia Wizara ilitoa mafunzo kwa maafisa waandamizi na wa ngazi ya kati kuhusu misingi ya Utawala Bora na mapambano dhidi ya rushwa ili kuzuia matukio ya rushwa na kuziba mianya ya rushwa. Mafunzo haya yaliwahusisha Wakurugenzi wa Wizara ya Afya, Waganga Wakuu wa Mikoa, Waganga Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Vyuo vyote vya Afya nchini na Maafisa wengine. Jumla ya watumishi 1,169 walipatiwa mafunzo hayo. Sambamba na mapambano dhidi ya rushwa, Wizara ilichapisha vijarida 850 vya Mkataba wa Huduma kwa Mteja na kuvisambaza kwa wadau. Lengo lilikuwa kuwafahamisha wateja wetu kuhusu mahusiano yetu na majukumu yetu kwao pamoja na haki na wajibu wao. Mkataba huu unaelekeza pia namna mteja anavyoweza kutuma malalamiko/maoni kuhusu huduma zetu.

  • 32

    Matarajio ya Huduma za Utawala na Watumishi mwaka 2005/2006 Wizara ya Afya itaendelea kutoa kipaumbele katika kuimarisha na kuboresha maslahi, maendeleo na utendaji kazi (Capacity building) kwa watumishi wake ili kuimarisha na kuongeza utoaji wa huduma za afya kwa wananchi watakaohitaji huduma hiyo muhimu. Malengo haya yatafikiwa kwa kuajiri watumishi wapya ili kuziba mapengo yaliyopo na kuwapandisha vyeo watumishi waliopo kwa kuzingatia sifa, vigezo na ikama iliyoidhinishwa. Ili kwenda sambamba na mabadiliko yanayoendelea kufanyika katika Sekta ya Afya, Wizara imejiwekea mpango wa kutoa mafunzo ya Huduma kwa Mteja kwa watumishi wake wote (customer care and Public ethics).Mafunzo haya yatawahusisha watumishi wapatao 3,336 kutoka Makao Makuu ya wizara, Hospitali tatu za Rufaa, Vyuo vya Afya 108 pamoja na Kanda 6 za mafunzo. Mafunzo hayo yataendeshwa kwa awamu tatu. Aidha, Wizara imejipangia kuanzisha teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Information Communication Technology) ili kuimarisha na kuongeza utoaji wa huduma bora ya upatikanaji na upashanaji wa habari kwa haraka zaidi. Wizara tayari imeanza utoaji wa mafunzo kwa watumishi wake na itaendelea na mafunzo hayo ili kuwawezesha kumudu matumizi ya teknolojia hiyo. Kwa kutambua umuhimu wa mashirikiano na M