jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya makamu wa...

125
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA MAKAMU WA RAIS TAARIFA YA KIKOSI KAZI CHA KITAIFA CHA KUOKOA MFUMO-IKOLOJIA WA BONDE LA MTO RUAHA MKUU MEI, 2017

Upload: others

Post on 05-Feb-2020

13 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MAKAMU WA RAIS

TAARIFA YA KIKOSI KAZI

CHA KITAIFA CHA KUOKOA MFUMO-IKOLOJIA WA BONDE LA MTO RUAHA MKUU

MEI, 2017

ii

MUHTASARI

Taarifa hii imeandaliwa na Kikosi Kazi cha Kitaifa kilichozinduliwa rasmi na

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu

Hassan tarehe 11/4/2017 kwa lengo la kuokoa Ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha

Mkuu wenye umuhimu wa kipekee hapa nchini na duniani. Umuhimu wa hatua za

haraka za kuokoa Mfumo Ikolojia wa Bonde la Mto huo umetokana na upungufu

mkubwa wa maji na athari zinazojitokeza ndani ya Bonde la mto huo

unaosababishwa na ongezeko la shughuli za kiuchumi na kijamii.

Aidha, athari hizo zimejitokeza kwa watumiaji wa maji chini ya Bonde (downstream

users) katika Wilaya ya Kilombero ambako kilimo cha miwa na mpunga hutegemea

maji ya mto huo na katika Wilaya ya Rufiji hususan eneo la delta lenye misitu ya

mikoko ya asili. Kilimo cha mpunga katika Bonde la Mto Rufiji hutegemea pia maji

yanayotoka katika Bonde hili. Aidha, kupungua kwa maji katika bonde hili

kumesababisha athari kwa uchumi wa nchi kwa ujumla katika maeneo ya kilimo,

utalii na nishati.

Ili kuwa na maendeleo endelevu, shughuli za kiuchumi na kijamii nchini ni lazima

zifanyike kwa kuzingatia misingi ya Katiba yetu na kuhakikisha kizazi hiki

kinatumia kwa makini utajiri wa maliasili tulionao ili tuweze kurithisha maliasili

hizi kwa kizazi kijacho katika hali iliyo endelevu kama haki yao ya msingi. Katiba ya

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 katika ibara ya 27 (1) na (2)

inatamka kuhusu wajibu wa kulinda mali ya umma. Katika ibara ya 27(1) Katiba

inatamka kuwa “Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Jamhuri ya

Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na

wananchi, na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine”. Aidha, ibara ya 27(2)

inatamka “Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya

nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na

kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali

ya baadaye ya taifa lao”. Kwa upande mwingine, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha

Mapinduzi 2015-2010 Ibara 152 (d) nayo inasisitiza kuhusu umuhimu wa kutunza

iii

vyanzo vya maji, kuwa: “kuendelea kufanya tathmini ya vyanzo vya maji

vilivyohifadhiwa, kuongeza vyanzo vipya na kufufua vilivyopotea ama

kuharibika ili kuwa na uhakika wa kuwa na maji safi na salama”. Maelekezo haya

pia yanaenda sambamba na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia

ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Kimataifa wa Ardhi Oevu (Ramsar Convention)

wa mwaka 1971 na Mkataba wa Kimataifa wa Bioanuai wa mwaka 1992.

Kwa kutambua hali ya uharibifu wa Mazingira na Ikolojia ya Bondel la Mto Ruaha

Mkuu, Mhe. January Y. Makamba (Mb.), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu ya Rais,

Muungano na Mazingira, alifanya ziara mnamo mwezi Oktoba, 2016 ili kutafuta

ufumbuzi wa kudumu wa kushughulikia uharibifu huu. Matokeo ya ziara hiyo

yalipelekea Serikali kuona umuhimu wa kuunda Kikosi Kazi cha Kitaifa ili

kunusuru mfumo- ikolojia wa Bonde hilo. Madhumuni ya Kikosi Kazi cha Kitaifa ni

pamoja na:

(i) Kuchambua kwa kina tafiti na matokeo ya miradi mbalimbali ya serikali na

wafadhili ambayo imeshafanywa katika mfumo–ikolojia wa Mto Ruaha Mkuu na

Ardhioevu (Wetland) ya Bonde la Usangu na kubainisha hatua mpya na za haraka

za kudhibiti kupungua kwa maji kwenye Mto Ruaha Mkuu; (ii) Kukusanya maoni

na mapendekezo ya wadau wote, ikiwemo wananchi waishio katika bonde la Mto

Ruaha Mkuu, kuhusu hatua za hifadhi ya mazingira katika bonde hilo; (iii) Kutumia

mamlaka ya sheria mbalimbali husika kuchukua hatua za haraka za kudhibiti

uharibifu wa mazingira na kurekebisha madhara ya uharibifu wa mazingira

yaliyojitokeza; (iv) Kuandaa rasimu ya mpango wa Kitaifa wa Hifadhi ya Mazingira

ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu; na (v) Kutoa ushauri wowote wa kisera au kiutendaji

wenye lengo la kuokoa mfumo–ikolojia wa Bonde la Mto Ruaha Mkuu.

Taarifa hii imegawanyika katika Sura Tano. Sura ya Kwanza ni Utangulizi, ambayo inaelezea historia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu, mifumo ya ikolojia yake na hali ya mabadiliko ya viwango vya maji.

Sura hii pia imeonesha umuhimu wa bonde hili kiuchumi, kijamii na kiikolojia na baadhi ya changamoto za uharibifu wa mazingira zinazolikabili bonde la mto Ruaha Mkuu.

iv

Sura ya Pili inaeleza mbinu zilizotumika na Kikosi-Kazi katika uchaguzi wa wadau waliohojiwa, ukusanyaji, uchakataji, uchambuzi na uwasilishaji wa takwimu na taarifa.

Sura ya Tatu inaeleza hali halisi ya mazingira katika bonde hili, maumbile ya nchi, hali ya hewa, shughuli mbalimbali za kiuchumi na mwenendo wa viwango vya maji. Aidha, matatizo makuu yanayolikabili bonde hili na juhudi mbalimbali za kunusuru ikolojia.

Sura ya Nne imeainisha uchambuzi wa takwimu na taarifa ya mambo yaliyojiri uwandani. Mambo yaliyojionesha katika sura hii ni pamoja na sababu za tatizo la kupungua kwa maji katika bonde, madhara ya kiuchumi na kiikolojia.

Sura ya Tano inaeleza hitimisho na kutoa mapendekezo ya utekelezaji ili kuokoa ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu.

Taarifa hii inahusu eneo lote la Bonde la Mto Ruaha Mkuu ambapo baadhi ya maeneo yaliyotembelewa yameainishwa kwa kutumia vigezo vifuatavyo: (i) Maeneo ya vyanzo vya maji (water towers/catchment areas) yaliyopo katika wilaya za Makete, Wanging’ombe, Mbeya, Mufindi, Iringa, Kilolo na Chunya; (ii) Maeneo yenye matumizi makubwa ya maji yanayozunguka Eneo Oevu la Ihefu yaliyopo katika Wilaya ya Mbarali; na (iii) Maeneo yanayopokea maji kutoka kwenye Eneo Oevu la Ihefu ikihusisha Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Bwawa la Mtera na baadhi ya maeneo katika Wilaya ya Iringa. Taarifa ilihusisha sampuli ya jumla ya wahojiwa 570 kutoka katika makundi mbalimbali.

Tathmini ya uwandani inaonesha kuwa Bonde la Mto Ruaha Mkuu linakabiliwa na changamoto zinazosababishwa na shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na matumizi ya maji yasiyoendelevu katika kilimo cha umwagiliaji, miundombinu duni ya umwagiliaji, uchepushaji wa maji bila vibali, kilimo katika maeneo ya miteremko na ukataji wa miti, kilimo cha mabondeni (vinyungu), kilimo (upandaji) wa miti kibiashara, kukosekana kwa uratibu stahiki wa usimamizi wa jitihada mbalimbali, kilimo kisichotunza maji, udongo na bioanuai, uchomaji moto holela, upandaji miti isiyo rafiki kwa mazingira katika vyanzo vya maji, uingizaji wa mifugo na uchimbaji madini katika kingo za mito katika bonde bila kuzingatia taratibu na mipango ya matumizi ya ardhi.

Baada ya kikosi kazi kufanya ziara katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu, kupitia taarifa mbalimbali, tafiti na miradi iliyowahi kufanyika kwa lengo la kuokoa ikolojia ya Mto na pia kufanya mahojiano na viongozi wa kitaifa, katika mkoa, wilaya na wananchi wanaoishi katika Bonde hilo; Kikosi Kazi kimejiridhisha kwamba Bonde la Mto Ruaha Mkuu linakabiliwa na changamoto ya upungufu mkubwa wa mtiririko

v

wa maji. Upungufu huo katika miaka ya karibuni umesababisha kuongezeka kwa muda wa maji kuacha kabisa kutiririka kutoka wastani wa kipindi kisichozidi miezi miwili (2) katika miaka ya 1960 hadi kufikia miezi sita (6) katika miaka ya 2000. Sababu kubwa zinazochangia hali hiyo ni kuongezeka kwa kasi kwa shughuli za binadamu hususan, kilimo kisicho hifadhi ikolojia, kilimo cha umwagiliaji, ufugaji holela, upandaji mkubwa wa miti kibishara na kuondolewa kwa uoto wa asili. Aidha, eneo la Bonde hukabiliwa na mabadiliko ya tabianchi hususan, ongezeko la hali ya joto kunachangia kuongeza kasi ya upotevu wa maji katika Bonde.

Kutokana na changamoto hizo kikosi kazi kimependekeza hatua za kuchukua ili kunusuru ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu. Mapendekezo yamejikita katika maeneo ya kisera, kisheria, kimkakati na kiutendaji. Mapendekezo ya kisera na kisheria yanajumuisha maeneo yafuatayo:-

(i) Sheria zote zisimamiwe na kutekelezwa ipasavyo kwa ukamilifu;

(ii) Serikali iunde Taasisi au Mamlaka Maalum kisheria itakayokuwa na majukumu ya kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali zilizopo katika Bonde la Mto Ruaha. Pamoja na mamlaka hiyo uundwe Mfuko Maalum wa Wakfu (Trust Fund) ambao utachangiwa na wote wanaonufaika na rasilimali za Bonde na wadau wengine na usimamiwe kwa pamoja na wadau hao (Serikali, sekta binafsi na wabia wa Bonde la Mto Rufiji). Taasisi hiyo iwe chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais;

Aidha, ili kutekeleza pendekezo hilo mpango uhusishe hatua mbili kuu: (a) kwa hatua ya awali Mamlaka hiyo ianzishwe kwa kutumia Sheria ya Mazingira Na. 20 ya Mwaka 2004 kwa maana ya Eneo Lindwa (Enviromentally Protected Area); (b) na hatua ya kudumu itungwe sheria maalum ya kuunda Mamlaka, Mfuko na utaratibu wa kuuchangia na kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za Bonde. Kikosi Kazi kinatambua zipo mamlaka mbalimbali ambazo zimeundwa katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu/Rufiji, hivyo, ufanyike mpango wa kurazinisha mipaka na majukumu ya mamlaka hizo ili ziweze kutekeleza majukumu yake chini ya Mamlaka Maalum na Mfuko;

(iii) Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya

Makazi, na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, wahakikishe Wilaya na Vijiji vyote vilivyopo ndani ya Bonde vinaandaa, kutekeleza na kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi. Aidha, mipango iliyopo ipitiwe na kuhuishwa;

(iv) Ili kuhakikisha wamiliki wa ardhi wanatumia rasilimali hiyo kwa uendelevu na kuchangia utunzaji wa ikolojia ya Bonde, Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ziharakishe uwekaji wa

vi

ukomo wa kiwango cha juu cha ardhi ambacho kinaweza kumilikiwa na kutumiwa kwa kilimo, misitu, ufugaji, viwanda na matumizi mengine kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Na. 4 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya Mwaka 1999;

(v) Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Ofisi ya Makamu wa Rais, na Wizara ya Maji na Umwagiliaji ziharakishe kubaini maeneo maalum yanayotoa mchango mkubwa wa upatikanaji wa maji (vyanzo vya maji) katika Bonde (mfano katika milima na misitu ya asili) na kudhibiti shughuli za kibinadamu. Aidha, vyanzo vyote vya maji ndani ya Bonde vibainishwe, vipimwe, viwekewe mipaka kwa kutumia alama na kumilikishwa kwa mamlaka husika. Mfano mzuri upo katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika kuweka mipaka ya maeneo ya barabara;

(vi) Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waharakishe utekelezaji wa Tangazo la Serikali Na. 28 la mwaka 2008 kwa kuzingatia sheria na taratibu;

(vii) Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ihakikishe uzalishaji wa mazao, mifugo na uvuvi unafanyika kwa kutumia mbinu bora za uzalishaji (Good Agricultural Practices – GAP). Uzalishaji wa mazao ya kilimo uzingatie kilimo hifadhi katika maeneo yanayotegemea mvua na kilimo shadidi katika maeneo ya umwagiliaji; ufugaji uzingatie uwezo wa maeneo ya malisho (Carrying Capacity) na uboreshaji na utunzaji wa nyanda za malisho. Aidha, uendelezaji wa uvuvi na ufugaji wa samaki kwenye mito na mabwawa na maeneo oevu usimamiwe ili ufanyike katika taratibu endelevu. Kazi hii iendane ya utengaji wa maeneo ya uwekezaji wa miundombinu ya kuongeza thamani na masoko ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi;

(viii) Ofisi ya Makamu wa Rais isimamie uandaaji wa Tathmini ya Mazingira Kimkakati (Strategic Environmental Assessment - SEA) katika Bonde. Katika kuandaa “SEA” hiyo, wadau wote washirikishwe. Aidha, Sera na Sheria ya Mazingira pamoja na sera na sheria nyingine zinazohusika katika eneo hilo zitazamwe upya ili kuendana na mabadiliko ya mazingira ya sasa;

(ix) Kutokana na umuhimu wa misitu ya biashara kwa ustawi wa wananchi

katika maeneo ya Bonde, taasisi za utafiti wa mbegu za misitu zizalishe mbegu za miti ya biashara isiyotumia maji kwa wingi; na

(x) Kwa kuwa rasilimali maji ni muhimu sana kwa uhai na ina wadau wengi,

upo umuhimu wa kuanzishwa kwa “Water Resource Regulatory Authority” ambayo itadhibiti matumizi ya maji nchini. Wizara ya Maji na Umwagiliaji wamepewa majukumu ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata maji safi na

vii

salama ya kunywa; Sekta ya Kilimo inahitaji maji kwa ajili ya umwagiliaji (irrigation); Sekta ya Mifugo inahitaji maji kwa ajili ya mifugo; Uvuvi vile vile inahitaji maji kwa ajili ya uvuvi na kila sekta inahitaji maji kwa ajili ya matumizi mbali mbali. Hivyo Wizara ya Maji na Umwagiliaji ni mdau mmojawapo na hawezi kuwa sehemu ya mtoa vibali vya kutumia maji kwa sekta nyingine.

Katika eneo la kimkakati, Kikosi Kazi kimependekeza mambo yafuatayo:-

(i) Ofisi ya Makamu wa Rais ihakikishe Tathmini ya Mazingira Kimkakati

(Strategic Environmental Assessment - SEA) inafanyika kwa Sera, Sheria, Mikakati na Programuu zote zinazohusiana na matumizi na usimamizi wa rasilimali zilizopo ndani ya Bonde. Aidha, miradi yote inayotekelezwa ndani ya Bonde ambayo haijafanyiwa Tathmini ya Athari za Mazingira (Environmental Impact Assessment - EIA) ifanyiwe;

(ii) Mamlaka inayopendekezwa ihakikishe mipango na shughuli za sekta

mbalimbali ndani ya Bonde vinaratibiwa ili kuhakikisha inatekelezwa kwa utaratibu endelevu na inachangia katika maslahi mapana ya maendeleo ya Bonde na Taifa badala ya kuwa na kila taasisi na mipango yake;

(iii) Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na

Uvuvi iharakishe kukamilisha kazi inayoendelea ya utambuzi na uwekaji alama mifugo yote. Kazi hii iendane na kazi inayoendelea ya utengaji wa maeneo ya malisho na uwekaji wa miundombinu ya mifugo (majosho, njia za mifugo, mabirika ya kunyweshea mifugo, minada, viwanda vya vyakula vya mifugo na kuchakata mazao ya mifugo); na

(iv) Ofisi ya Makamu wa Rais, ihakikishe taasisi zote zinazosimamia utekelezaji

wa shughuli za kiuchumi katika Bonde zinatoa elimu kuhusu mbinu za kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Katika eneo la kiutendaji, Kikosi Kazi kimependekeza mambo yafuatayo:-

(i) Ili kuhakikisha usimamizi wa sera na sheria katika utekelezaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii katika Bonde, Mamlaka inayopendekezwa ipewe uwezo wa kuhakikisha kazi zote zinazotekelezwa katika Bonde zinazingatia sera na sheria zilizopo za uhifadhi wa mazingira na ikolojia ya Bonde;

(ii) Ili kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali maji katika eneo la

Bonde yanakidhi mahitaji ya wadau wote, Mamlaka inayopendekezwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, ihakikishe kilimo cha umwagiliaji kinafanyika kulingana na sheria na taratibu zilizopo. Aidha, ifanyike tathmini ya kiasi cha maji katika kila

viii

chanzo, mahitaji katika skimu za umwagiliaji zilizopo kwa sasa na kulinganishwa na vibali vilivyotolewa. Teknolojia za kisasa zitumike katika kuongeza ufanisi katika miradi ya umwagiliaji;

(iii) Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na

Utalii ifanye tathmini ya kina kwa ajili ya kutambua maeneo yanayopaswa kubakizwa katika uoto wa asili na misitu ya asili na yale yanayoweza kutumika kwa upandaji wa miti isiyo ya asili kibiashara bila kuathiri ikolojia na upatikanaji wa maji. Pale ambapo tathmini itabaini miti isiyo ya asili inaathiri mazingira, miti hiyo iondolewe. Aidha, tathmini hiyo ielekeze upandaji wa miti kibiashara ufanyike kwa kuzingatia mipango ya matumizi ya ardhi;

(iv) Ofisi ya Rais - TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo

na Uvuvi ihakikishe kilimo katika maeneo yenye miteremko iliyo na mwinamo mkali yanajengewa makinga maji, kubakiza uoto wa asili, kuzingatia kilimo hifadhi na kutumia mbinu nyingine za kuzuia mmomonyoko wa udongo. Aidha, tathmini ifanyike kubaini maeneo yasiyofaa kwa kilimo kutokana na mwinamo mkali, ili maeneo hayo yazuiliwe kutumika kwa kilimo na makazi;

(v) Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji

ihakikishe uwekaji wa vipimo unafanyika katika mabanio na matupio ya maji ili kujua kiasi cha maji kinachotumika na kinachorudishwa mtoni kulingana na kibali cha maji kilichotolewa. Watumiaji wa skimu zote za umwagiliaji ambazo hazina vipimo waweke vipimo vya kujua kiasi cha maji kinachochukuliwa na kurudishwa mtoni. Aidha, wamiliki wa mashamba ya umwagiliaji ambao hawajafunga vipimo hivyo wasitishiwe vibali;

(vi) Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Maliasili na Utalii na

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zifanye tathmini kwa ajili ya kujenga mabwawa ya kuvuna maji ya mvua ili yasaidie kuwepo na mtiririko wa maji kwa mwaka mzima na kutumika kwa shughuli za kiuchumi na kijamii. Mabwawa makubwa yaliyopendekezwa ya uvunaji wa maji ya mvua ya Ndembera na Usalimwani yajengwe na Bwawa la Lwanyo ujenzi ukamilike;

(vii) Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za

Mitaa zihakikishe kuwa kilimo kisichozingatia kilimo hifadhi na kilimo shadidi kisitishwe katika eneo la Bonde la Mto Ruaha Mkuu. Aidha, kutokana na ukubwa wa kazi hiyo utolewe muda wa kutoa Elimu kwa Watendaji ili watumike kuelimisha wakulima juu ya utekelezaji wa kilimo hicho;

(viii) Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo

ix

ya Makazi na Wizara ya Maji na Umwagiliaji zifanye uhakiki wa milki zote zilizotolewa katika ardhi oevu na vyanzo vya maji ili zibatilishwe;

(ix) Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Nishati na Madini, na Baraza la

Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira zifanye tathmini ya maeneo ya uchimbaji wa madini katika bonde kwa lengo la kutambua uchimbaji unaofanyika katika vyanzo vya maji na maeneo oevu na kusitisha. Aidha, Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Bonde zitunge Sheria Ndogo zinazowataka wachimbaji wa madini ya aina zote katika maeneo ya Bonde kupata kibali cha uchimbaji. Aidha, Wizara ya Nishati na Madini isitoe leseni za uchimbaji wa madini katika Bonde bila kuzishirikisha Halmashauri husika;

(x) Ofisi ya Rais - TAMISEMI ikishirikiana na wadau isimamie utatuzi wa

migogoro ya matumizi ya ardhi iliyopo katika Bonde kwa kuzingatia mapendekezo na mpango kazi wa Kamati ya Kisekta ya Utatuzi wa Migogoro ya Matumizi ya Ardhi iliyoundwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Serikali itoe kipaumbele kwa utekelezaji wa mpango wa Kupanga-Kupima-Kumilikisha (K3) eneo lote la ardhi katika Bonde;

(xi) Ofisi ya Makamu wa Rais na Wizara ya Maji na Umwagiliaji ziimarishe

huduma za Ukaguzi, Ufuatiliaji na Tathmini zinazotolewa na: Ofisi za Kanda za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC); Tume ya Taifa ya Umwagiliaji; na Bodi ya Maji ya Bonde;

(xii) Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya

Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na wadau wengine watekeleze mipango maalum ya kuwawezesha wakazi wa Bonde kuanzisha na kutekeleza shughuli mbadala za kiuchumi ambazo ni rafiki kwa mazingira. Shughuli hizo ni pamoja na ufugaji wa nyuki na samaki, wanyama wadogo na kuku, na kilimo cha mazao ya bustani kwa kutumia matone;

(xiii) Wizara ya Maji na Umwagiliaji ifanye tathmini ya maeneo ambayo

mito imepoteza muelekeo na kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mpango wa kurejesha mito hiyo katika mikondo yake. Aidha, Wizara hiyo isimamie ukamilishaji wa kazi iliyoanza katika baadhi ya mito ya Ndembera, Mswiswi, Mkoji na Kioga.

(xiv) Tume ya Taifa ya Matumizi Bora ya Ardhi kwa kushirikiana na Ofisi

ya Rais – TAMISEMI na wadau wengine wa maendeleo kuendelea kuandaa na kuhuisha mipango ya matumizi ya ardhi katika maeneo yote ya ngazi za Halmashauri na Vijiji vilivyopo ndani ya Bonde ili kuainisha maeneo maalum yenye Miundombinu stahiki kwa ajili ya

x

ufugaji kwa kuzingatia utaratibu shirikishi. Vile vile kuondoa mifugo katika maeneo ya Hifadhi za Taifa, Hifadhi za Akiba na maeneo mengine yaliyoainishwa kwa shughuli zisizo za ufugaji;

(xv) Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Wakala wa

Mbegu za Miti Tanzania (Tanzania Tree Seed Agency – TTSA) na taasisi za utafiti wazalishe mbegu za miti ya biashara isiyotumia maji mengi kwa kuwa ni muhimu kwa uchumi wa wananchi;

(xvi) Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,

Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wahakikishe kuwa elimu inatolewa ili kudhibiti ongezeko la watu kwa kuzingatia uwiano wa rasilimali za asili zilizopo na idadi ya wakazi katika Bonde; na

(xvii) Badala ya kuendelea kuongeza maeneo ya kilimo katika Bonde, kilimo

kinachozingatia uzalishaji endelevu kizingatiwe na wakulima wote ili kuongeza tija (productivity).

Pamoja na taarifa hii, Kikosi Kazi pia kimeandaa rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Hifadhi ya Mazingira ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu. Katika mpango huo mambo ya msingi yanayopendekezwa ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi yameoneshwa kwa muhtasari katika jedwali lifuatalo:

xi

Jedwali: Mpango Kazi wa mambo yanayotakiwa kutekelezwa

Changamoto Suluhisho Mhusika Muda Upungufu wa maji

1. Kuharakisha utekelezaji wa Tangazo la Serikali Namba 28 la tarehe 14 Machi 2008 linalohusu upanuzi wa mipaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

OR TAMISEMI,MAU, AG, MLHHSD, TANAPA, WFU

Juni 2017 –Machi 2018

2. Kutathmini hali ya skimu zote za umwagiliaji kuona upotevu wa maji na kuudhibiti.

WMU, OMR, OR TAMISEMI, NEMC,

Juni – Septemba 2017

3. Kuanisha vyanzo vya maji, kuviwekea mipaka na kuvilinda kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.

MLHHSD, OR TAMISEMI

Juni – Desemba 2017

4. Kubainisha na kuondoa miti yote isiyo rafiki na maji na kupanda miti rafiki na maji kwenye vyanzo vyote vya maji (mfano: Mivengi (Mizambarau), na Mikuyu pori (Misombe).

WMU, WMU,OR TAMISEMI

Juni 2017 – Julai 2018

5. Kuondoa waliovamia maeneo ya hifadhi. OMR, OR TAMISEMI, NEMC

Juni – Septemba 2017

6. Kuhakiki hati za hakimiliki zote zilizotolewa kwenye ardhi oevu na kuzibatilisha.

WAMM, OR TAMISEMI, WMU

Juni – Septemba 2017

7. Kuainisha maeneo tekechu (Environmentally Sensitive Areas ) na kuyatangaza kama maeneo lindwa.

OMR, OR TAMISEMI, NEMC

Juni 2017 –Machi 2018

8. Kurejesha mito iliyopoteza mikondo. WMU, OMR, OR TAMISEMI, NEMC

Juni 2017 – Julai 2019

Changamoto Suluhisho Mhusika Muda

xii

Matumizi yasiyo endelevu

1. Kufukia mifereji yote isiyo rasmi kwenye skimu za umwagiliaji. OMR, OR TAMISEMI, NEMC, WMU

Juni – Septemba 2017

2. Kusafisha na kusakafia mifereji mikuu, midogo na ya kati katika skimu na miradi yote ya umwagiliaji.

OR TAMISEMI, NEMC, WMU

Juni – Desemba 2017

3. Kusitisha shughuli za kibanadamu ndani ya mita 60 kutoka kwenye kingo za mito na vyanzo vya maji.

OMR, OR TAMISEMI, NEMC, WMU

Juni – Desemba 2017

4. Kujenga mabanio imara ya kudhibiti na kuweka vipima maji (flow meter) kwenye mifereji wa maingizio na matoleo.

OR TAMISEMI, NEMC, WMU

Juni 2017 –Machi 2018

5. Kujenga mifereji ya kutolea maji mashambani na kurudisha mtoni OR TAMISEMI, WMU

Juni 2017 –Machi 2018

6. Kupitia vibali vyote vya watumia majina kufuta visivyo halali na kuhakiki kama vinalingana na upatikani wa maji (uhalali, uzingatiaji wa masharti, uhitaji wa maji).

OR TAMISEMI, NEMC, WMU

Juni 2017 –Machi 2018

7. Kuhamasisha kilimo shadidi kwa wakulima wa umwagiliaji. OR TAMISEMI, NEMC, WMU, WKMU

Juni 2017 –Machi 2018

8. Kuhamasisha kilimo hifadhi katika Bonde la Mto Ruaha ili kuongeza tija na kupunguza matumizi ya maji na ardhi.

OR TAMISEMI, NEMC, WMU, WKMU, WAMM

Juni 2017 –Machi 2018

Changamoto Suluhisho Mhusika Muda

1. Utekelezaji wa sheria za mazingira kwa kutoza faini wanaoiba maji kwa kuchepusha ili kutoa funzo kwa watumiaji wabaya wa maji.

OMR, OR- TAMISEMI, NEMC

Juni – Desemba 2017

xiii

Usimamizi usio endelevu wa rasilimali maji

2. Kuandaa Tathimini ya Mazingira Kimkakati (SEA) ya Bonde. OMR, NEMC Juni – Desemba

3. Wilaya na vijiji vyote ndani ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu viwezeshwe kuandaa, kutekeleza na kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi.

WAMM, OR- TAMISEMI,

Juni 2017 – Julai 2019

4. Kufanya sensa ya mifugo katika bonde la Mto Ruaha Mkuu na kuweka alama ili kudhibiti idadi ya mifugo katika Bonde (idadi, alama, nakuanzisha kanzidata).

WKMU OR- TAMISEMI

Juni 2017 –Machi 2018

5. Kuunda kamati wezeshi ya usimamizi wa pamoja wa bonde la Mto Ruaha Mkuu.

OMR, WMU, WAMM, OR- TAMISEMI, NEMC

Juni 2017 –Machi 2018

6. Kuhakiki miradi yote inayotekelezwa katika mabonde ili kuona kama imezingatia Tathamini ya Athari za Mazingira (EIA).

NEMC, OMR, Juni – Desemba 2017

7. Kuweka ukomo wa matumizi ya ardhi inayopaswa kumilikiwa na kutumiwa kwa shughuli zote za kibinadamu.

WAMM, OR- TAMISEMI

Juni 2017 –Machi 2018

8. Kuanzisha mamlaka ya wadau ya kusimamia na kuratibu rasilimali zote ndani ya bonde. Pia, kuanzisha mfuko wa wakfu (Trust Fund) kwa ajili ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu.

OMR, WMU, WAMM, OR- TAMISEMI, NEMC

Juni 2017 – Julai 2019

9. Kufanya utafiti wa miti inayosadia utunzaji wa maji. NEMC, Wizara ya Maliasili & Utalii, WKMU

Juni 2017 – Julai 2019

xiv

Jedwali: Orodha ya Wajumbe wa Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Kuokoa Mfumo-Ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu.

Na JINA CHEO OFISI

1. Dkt. ANDREW M. KOMBA

Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu.

Ofisi ya Rais - TAMISEMI

Dkt. STEPHEN J. NINDI

Mkurugenzi Mkuu.

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Dkt. VEDAST MAKOTA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu. Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)

Bi. MARY G. MAKONDO

Kamishna wa Ardhi.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi

2. Bw. RICHARD S. MUYUNGI

Mkurugenzi wa Mazingira.

Ofisi ya Makamu wa Rais, Idara ya Mazingira

ENG. SETH LUSWEMA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu.

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Wizara ya Maji na Umwagiliaji

3 Bi. MARIAM A. MTUNGUJA

Katibu Tawala wa Mkoa. Mkoa wa Mbeya

4 Bi. WAMOJA D. AYUBU

Katibu Tawala wa Mkoa. Mkoa wa Iringa

5 Bw. JACKSON L. SAITABAU

Katibu Tawala wa Mkoa. Mkoa wa Njombe

xv

6 Bw. ALLAN KIJAZI Mkurugenzi Mkuu. Hifadhi za Taifa (TANAPA)

7 Bw. MZEE A.H. KANDORO

Mdau wa Mazingira Iringa. Mkoa wa Iringa

11. Bw. TITO E. MWINUKA

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji. Shirika la Umeme la Taifa (TANESCO)

13. Bw. GEOFFREY KIRENGA

Mtendaji Mkuu.

Taasisi ya Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania

14. Bw. IDRIS A. MSUYA

Afisa wa Maji, Bonde la Rufiji Wizara ya Maji na Umwagiliaji

15. Bw. ISMAIL A. MANJOTI

Wakili wa Serikali Mkuu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu

xvi

Orodha ya Vifupisho

ASDP Agricultural Sector Development Programume

BMU Beach Management Unit

BRN Big Results Now

CBFM Community Based Forest Management

CCM Chama cha Mapinduzi

CITES Convention on International Trade in Endangered Species

DANIDA Danish International Development Agency

DC District Council

DFID Department for International Development

EIA Environmental Impact Assessment

EMEDO Environmental Management and Economic Development Organization

HIMA Hifadhi ya Mazingira

IWRMDP Integrated Water Resources Management and Development Plan

JFM Joint Forest Management

JUWAMA Jumuiya ya Watumia Maji Matamba

KUU Kamati ya Ulinzi na Usalama

MAMCOS Madibira Marketing and Cooperative Society

MEMA Matumizi Endelevu ya Maliasili

NOSC Njombe Outgrowers Services Company

xvii

PFP Private Forest Programume

RBMSIIP River Basin Management and Small Irrigation Improvement Project

RBWB Rufiji Basin Water Board

RCC Regional Consultative Committee

RUBADA Rufiji Basin Development Authority

RUNAPA Ruaha National Park

SAGCOT Southern Agriculture Growth Corridor of Tanzania

SMUWC Sustainable Management of Usangu Wetland and its Catchment

SPANEST Strengthening the Protected Area Network in Southern Tanzania

SRI System of Rice Intensification

SSIDP Small Scale Irrigation Development Project

STEP Southern Tanzania Elephant Programume

SUA Sokoine University of Agriculture

SEA Strategic Environmental Assessment

TAMISEMI Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

TANAPA Tanzania National Parks

TANESCO Tanzania Electric Supply Company

TANWAT Tanganyika Wattle Company

TAWA Tanzania Wildlife Authority

TC Town Council

TFP Tanzania Forest Programume

TFS Tanzania Forest Services

xviii

USM Usimamizi Shirikishi wa Misitu

WSDP Water Sector Development Programume

WWF World Wide Fund for Nature

WRG-Tz Water Resources Group - Tanzania

xix

Tafsiri ya Maneno

Ardhioevu: Ni maeneo ya bwawa la tope, mbuga ya kinamasi, ardhi ya mboji au maji, yawe ya asili au ya kutengenezwa na binadamu, ya kudumu au ya muda, yenye maji yaliyotuama au yanayotiririka ya maji baridi, ya chumvi ikiwa ni pamoja na maeneo ya maji ya bahari ambayo kina chake katika maji kupwa hakizidi mita sita.

Bonde la Mto Ruaha Mkuu: Ni mfumo wa mtiririko wa maji kutoka kwenye chemichemi, vijito na mito ambayo huingiza maji kwenye mto Ruaha Mkuu ulio kwenye mikoa ya Iringa, Mbeya, Njombe na Morogoro.

Bwawa: Ni umbo au miundombinu iliyojengwa ili iweze kukinga na kuhifadhi maji ya mto au mito, maji ya mvua yanayotiririka ardhini au yanayoingia moja kwa moja kwa lengo la kudhibiti mtiririko wake na kuyatumia wakati wa uhaba wa maji.

Eneo linalofaa kwa umwagiliaji: Ni eneo linalofaa kiutaalamu, kiuchumi, kijamii na kimazingira kwa kilimo cha umwagiliaji kwa kuzingatia uwepo wa ardhi inayofaa kwa kilimo, upatikanaji wa maji na hali ya kukubalika kiuchumi na kijamii.

Hifadhi: Ni eneo la mbuga na misitu.

Ihefu: Ni eneo lenye maji (ardhi oevu) wakati wote wa mwaka na lipo mashariki ya tambarare za Usangu.

Jumuiya ya watumia maji: Ni chombo ambacho kinajumuisha watumia maji wa aina tofauti kama vile matumizi ya nyumbani, umwagiliaji, matumizi ya mifugo, uvuvi (ufugaji wa samaki), ujenzi wa nyumba, kutengeneza nishati na wanyamapori.

Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Kuokoa Ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu: Ni kamati iliyoteuliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kuokoa mfumo ikolojia wa Bonde la Mto Ruaha Mkuu.

Kilimo hifadhi: Kilimo kinachozingatia hifadhi ya mazingira kwa kutumia mbinu na mifumo, Pembejeo na kemikali sahihi za kilimo.

Kilimo shadidi: Kilimo cha mpunga kinachotumia teknolojia ya kiwango kidogo cha maji huku kikiongeza tija.

Kurasimisha: Mfumo unaowezesha mabadiliko katika kumiliki mali na kufanya biashara katika sekta isiyo rasmi kwenda katika mfumo wa sekta rasmi ya uchumi wa kisheria.

xx

Mabanio: Ni maumbo yaliyojengwa kihandisi katika maeneo ya kuchepushia maji kutoka kwenye vyanzo kwa ajili ya umwagiliaji. Haya huweza kujumuisha maumbo katika mkondo wa maji, na pampu za kusukuma maji kutoka mtoni au bwawani.

Mazingira: Ni vitu vyote vinavyotuzunguka vyenye uhai na visivyo na uhai, vikiwemo pamoja na ardhi, sauti, hewa, maji, mimea, maisha ya binadamu na wanyama na vipengele mbalimbali vinavyohusu uchumi, utamaduni na maisha ya jamii.

Mbuga: Ni eneo lenye nyasi ambalo hufurika maji wakati wa masika.

Mfumo-ikolojia: Ni namna ya maisha katika maeneo ambapo viumbe wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanyama na mimea hutegemeana, aidha kwa chakula ama hifadhi au vyote kwa pamoja.

Skimu kubwa za umwagiliaji: Ni mashamba makubwa ya umwagiliaji ambayo eneo lake lina ukubwa wa zaidi ya hekta 2,000.

Skimu za umwagiliaji za ukubwa wa kati: Ni mashamba ya umwagiliaji ambalo eneo lake ni zaidi ya hekta 500 na halizidi hekta 2,000.

Skimu ndogo za umwagiliaji: Ni mashamba ya umwagiliaji yenye eneo lisilozidi hekta 500.

Skimu ya umwagiliaji iliyoboreshwa: Ni mashamba ya umwagiliaji ambayo yamefanyiwa kazi za kuboresha miundombinu ya umwagiliaji na ufanisi wake.

Skimu ya umwagiliaji iliyoendelezwa: Ni mashamba ya umwagiliaji ambayo yamejengewa au kuwekewa miundombinu ya umwagiliaji kitaalam.

Skimu ya umwagiliaji: Ni eneo ambalo linastawishwa mazao kwa aina yoyote ya umwagiliaji uwe wa matone au kunyunyuzia au wa wazi ikiwa ni pamoja na mifumo inayotumia maji yanayotiririka kwa nguvu ya mvutano wa ardhi au kusukumwa kwa pampu kuingia kwenye mifereji au mabomba kutoka kwenye chanzo wazi au chini ya ardhi au maji ya mvua yaliyovunwa.

Uhifadhi: Ni tendo la kulinda na kudumisha matumizi ya bioanuwai.

Umoja wa watumiaji maji: Ni muungano wa vyama mbalimbali vya watumiaji maji wanaotumia maji kwenye chanzo kinachowahusu wote.

Umwagiliaji: Ni matumizi ya kiasi cha maji katika eneo maalumu ili kukidhi mahitaji ya kuota na ustawi wa mimea katika eneo husika kwa kiwango kinachostahili kulingana na hatua ambayo mmea umefikia katika ukuaji wake.

xxi

Ushoroba: Ni maeneo yanayotumiwa na wanyama wakati wa kuhama kutoka sehemu moja ya mfumo wa ikolojia kwenda nyingine kila siku, kwa wiki, kwa mwezi, kwa msimu kwa mwaka katika kutafuta mahitaji ya msingi kama vile maji, chakula, nafasi na makazi. Vinyungu: Ni maeneo chepechepe ambayo udongo wake umefunikwa na maji au maji yapo kina kifupi kutoka ardhini hivyo hutengeneza mashamba kwa kunyanyua udongo na kustawisha mazao.

Vyama vya umwagiliaji: Mkusanyiko wa wakulima wenye nia moja ya kuendeleza na kuendesha kilimo cha umwagiliaji katika skimu kwa lengo la kuongeza tija na uzalishaji wa mazao kwa kuzingatia usimamizi wa matumizi bora ya maji, kufanya usimamizi, uendeshaji na matunzo katika skimu yao.

Vyanzo vya maji: Ni eneo lenye chemichemi, mtiririko, bwawa, mto au ziwa.

Wakulima wadogo: Ni wakulima wanaomiliki au waliogawiwa maeneo yenye ukubwa usiozidi hekta 5 kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji katika skimu.

xxii

YALIYOMO

MUHTASARI .......................................................................................................................... ii

Orodha ya Vifupisho ............................................................................................................xvi

Tafsiri ya Maneno ................................................................................................................. xix

SURA YA KWANZA.............................................................................................................. 1

1.0 UTANGULIZI .............................................................................................................. 1

1.1 Historia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu ......................................................................... 2

1.1.1 Sera na Sheria zilizotumika .................................................................................... 4

1.1.2 Tafiti zilizofanyika katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu ......................................... 5

1.1.3 Programuu na Miradi iliyotekelezwa katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu .......... 8

SURA YA PILI....................................................................................................................... 11

2.0 MBINU ZA UKUSANYAJI, UCHAKATAJI, UCHAMBUZI NA UWASILISHAJI WA TAKWIMU NA TAARIFA ........................................................................................... 11

2.1 Eneo husika.................................................................................................................... 11

2.2 Wadau Waliohojiwa (Wigo wa Sampuli) .................................................................... 12

2.3 Ukusanyaji wa Takwimu na Taarifa ............................................................................ 13

2.3.1 Takwimu za Awali/Msingi .................................................................................. 13

2.3.2 Takwimu za Upili .................................................................................................. 14

2.4 Uchakataji, Uchambuzi na Uwasilishaji wa Taarifa ................................................... 15

2.5 Muundo wa Taarifa ...................................................................................................... 15

SURA YA TATU ................................................................................................................... 17

3.0 HALI HALISI YA MAZINGIRA NA JITIHADA ZILIZOFANYIKA KUOKOA IKOLOJIA YA BONDE LA MTO RUAHA MKUU............................................................ 17

3.1 Hali ya Ikolojia na Mazingira ....................................................................................... 17

3.1.1 Maumbile ya Nchi ................................................................................................. 17

3.1.2 Hali ya Hewa ......................................................................................................... 18

3.2 Shughuli za Kiuchumi .................................................................................................. 18

xxiii

3.2.1 Kilimo ..................................................................................................................... 19

3.2.2 Ufugaji .................................................................................................................... 19

3.2.3 Misitu ...................................................................................................................... 20

3.2.4 Uvuvi ...................................................................................................................... 21

3.2.5 Uchimbaji madini .................................................................................................. 22

3.2.6 Wanyamapori na Bioanuai Nyingine .................................................................. 22

3.3 Tatizo Kuu katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu ........................................................... 23

3.4 Juhudi za Kunusuru Ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu .................................................... 25

3.4.1 Sera na Sheria ......................................................................................................... 26

3.4.1 Uchambuzi wa Miradi na Tafiti Mbalimbali zilizofanyika katika Eneo la Bonde la Mto Ruaha Mkuu .............................................................................................................. 58

3.4.2 Juhudi za ziada za Serikali na wadau katika kuokoa Ikolojia ya Bonde ........... 65

3.4.3 Maagizo ya Viongozi wa Ngazi za Juu ................................................................ 68

SURA YA NNE ..................................................................................................................... 70

4.0 UCHAMBUZI NA TATHMINI YA MAMBO YALIYOJIRI UWANDANI .......... 70

4.1 Kilimo Kisicho Endelevu Katika Bonde ...................................................................... 70

4.1.1 Matumizi ya maji yasiyo endelevu katika kilimo cha umwagiliaji ................... 71

4.1.2 Miundombinu duni ya umwagiliaji ..................................................................... 74

4.1.3 Uchepushaji wa Maji Usio na Vibali vya Umwagiliaji ....................................... 75

4.1.4 Miradi Inayotekelezwa na Serikali ....................................................................... 75

4.1.5 Kilimo katika maeneo ya miteremko na ukataji wa miti .................................... 76

4.1.6 Kilimo cha Vinyungu ............................................................................................ 77

4.1.7 Kilimo cha Miti ya Biashara .................................................................................. 78

4.1.8 Kilimo Kisicho tunza Maji, Udongo na Bioanuai ................................................ 80

4.2 Madhara ya Uchungaji Usio Endelevu ........................................................................ 83

4.3 Madhara ya Mabadiliko ya Tabianchi ......................................................................... 86

4.4 Madhara ya Kutofanyika Tathmini ya Athari kwa Mazingira .................................. 89

xxiv

4.5 Madhara Katika Maeneo Yanayopokea Maji Kutoka Ardhi Oevu ya Ihefu ............ 90

4.5.1 Madhara yaliyosababishwa na upungufu wa Maji katika Hifadhi ya Taifa Ruaha 90

4.6 Matatizo ya Upungufu wa Kina cha Maji kwenye Bwawa la Mtera katika Ufuaji wa Umeme kwenye Vituo vya Mtera na Kidatu ...................................................................... 92

4.6.1 Kiuchumi ................................................................................................................ 93

4.6.2 Kijamii .................................................................................................................... 94

SURA YA TANO .................................................................................................................. 95

5.0 HITIMISHO NA MAPENDEKEZO ......................................................................... 95

5.1 Hitimisho ....................................................................................................................... 95

5.2 Mapendekezo ................................................................................................................ 96

1

SURA YA KWANZA

1.0 UTANGULIZI

Uandaaji Mkakati thabiti wa usimamizi wa Bonde la Mto Ruaha Mkuu ni

muhimu kutokana na mchango wa eneo hili kimazingira, kiuchumi na

kijamii kwa wananchi wanaoishi katika Bonde na taifa kwa ujumla.

Bonde hili limekuwa likitumiwa na wadau mbalimbali kwa matumizi

tofauti na malengo tofauti. Pamoja na kuwepo Mamlaka za kusimamia

eneo hili, uratibu na usimamizi wa eneo hili umekuwa dhaifu na

kusababisha migongano ya uhitaji wa matumizi ya maji, na kwa kiasi

kikubwa matumizi yasiyo endelevu. Uharibifu wa mazingira na

matumizi yasiyo endelevu ya maji kwenye vyanzo vya maji na maeneo

ya mabonde muhimu yamesababisha kiwango cha maji kupungua

mwaka hadi mwaka, na kuathiri mtiririko wa maji kwa shughuli za

uhifadhi, utalii, uzalishaji umeme, uvuvi, kilimo na ufugaji kwenye

maeneo yaliyoko maeneo ya bondeni. Jitihada mbalimbali zimekuwa

zikifanyika kulinda ikolojia ya bonde hili kwa kufanya utafiti, na

kuanzisha miradi mbalimbali ambayo imetekelezwa kwa ngazi tofauti.

Pamoja na taarifa za kiutafiti kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu njia bora

za kutunza mazingira ya bonde hili na matumizi endelevu ya maji, na

baadhi ya mapendekezo hayo kutekelezwa kwa kupitia miradi na

Programuu mbalimbali, changamoto zimeendelea kuwepo, na hivyo

kusababisha uhitaji wa kuongeza nguvu ya usimamizi. Ili kuweza

kufanikisha azma hii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, iliunda Kikosi Kazi cha Kitaifa

ambacho kimepewa jukumu la kufanya tathmini ya kina ya hali ya

ikolojia ya Bonde hili, na kushauri namna bora ya kuboresha mfumo wa

usimamizi wa ikolojia ya eneo kwa lengo la kuhakikisha mtiririko wa

maji wa kutosha kwa kipindi chote cha mwaka kwenye Mto Ruaha

2

Mkuu. Taarifa hii inalenga kutoa hali halisi ya eneo na mapendekezo ya

hatua za kuchukua.

1.1 Historia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu

Bonde la Mto Ruaha Mkuu ni moja kati ya mabonde manne yanayounda

Bonde la Rufiji ambapo mabonde mengine ni Kilombero, Luwegu na

Rufiji Chini. Eneo la Bonde la Mto Ruaha Mkuu lina ukubwa wa kilometa

za mraba 85,554 ambazo ni sawa na asilimia 47 ya eneo lote la Bonde la

Rufiji. Bonde hili linajumuisha mikoa saba ambayo ni Iringa, Njombe,

Mbeya, Morogoro, Dodoma, Singida na Tabora. Bonde la Mto Ruaha

Mkuu linaundwa na Mito mikubwa ya Mbarali, Ruaha, Kimani, Kizigo,

Lukosi, Ruaha Mdogo, Ndembela na Chimala. Pia Mitomidogo ya

Umrobo, Mkoji, Lunwa, Mlomboji, Ipatagwa, Mambi, Iyovi, Mwega na

Mswiswi nayo huingiza maji katika Bonde hilo. Aidha, Bonde la Mto

Ruaha Mkuu linahusisha eneo la ardhi oevu ya Usangu lenye ukubwa

wa kilomita za mraba 10,026 ambalo hupokea maji kutoka katika mito

mikubwa ya Mbarali, Ruaha, Kimani, Ndembela na Chimala pamoja na

mito midogo ya Mkoji, Lunwa, Ipatagwa, Mambina na Mswiswi.

Mto Ruaha Mkuu una urefu wa kilomita 475 kutoka milima ya Kipengere

hadi unapoingia Mto Rufiji katika eneo la Maporomoko ya Shughuli

(Shughuli Falls) Mkoa wa Morogoro. Vyanzo vya Mto Ruaha Mkuu,

vinaanzia katika safu za milima ya Livingstone, Kipengele na Uporoto.

Aidha, Mto Kisigo unaoanzia Wilayani Manyoni na Mto Ruaha Mdogo

unaoanzia katika Wilaya za Kilolo na Mufindi pia humwaga maji katika

Mto Ruaha Mkuu. Mto Ruaha Mkuu unapita katika Hifadhi ya Taifa ya

Ruaha yenye ukubwa wa kilometa za mraba 20,226 na huingiza maji yake

katika bwawa la Mtera na baadaye bwawa la Kidatu.

Katika hali ya kawaida, maji ya Mto Ruaha Mkuu huchangia takriban

asilimia 56 ya maji yote yanayoingia katika Bwawa la Mtera. Vilevile Mto

3

Ruaha Mdogo unaoungana na Mto Ruaha Mkuu eneo la kijiji cha

Makuka, unakadiriwa kuchangia takriban asilimia 18 na Mto Kisigo

unakadiriwa kuchangia asilimia 26 ya maji yanayoingia katika Bwawa la

Mtera. Bonde la Mto Ruaha Mkuu ni maarufu kwa shughuli mbalimbali

za kiuchumi kama kilimo, ufugaji, uvuvi, uchimbaji mdogo wa madini,

viwanda vidogo, uhifadhi na utalii kama inavyoonekana kwenye

Kielelezo Na. 1. Kwa upande wa shughuli za kilimo, maji ya Bonde la

Mto Ruaha Mkuu hutumiwa na zaidi ya wakulima 45,626 kwa kilimo cha

umwagiliaji katika eneo la hekta 77,187 kati ya hekta 126,816 zinazofaa

kwa kilimo hicho. Vilevile maji hayo hutumika kwa uzalishaji wa umeme

katika mabwawa ya Mtera na Kidatu ambapo Bwawa la Kidatu huzalisha

megawati 204 wakati Bwawa la Mtera huzalisha megawati 80. Kwa

upande wa shughuli za uhifadhi wa mazingira, maji ya bonde hili

hutumika kama chanzo kikuu katika ustawi wa ikiolojia ya Hifadhi ya

Taifa ya Ruaha. Shughuli nyingine muhimu za kiuchumi zinazofanyika

ndani ya bonde hili ni pamoja na uvuvi na ufugaji. Aidha, kwa upande

wa shughuli za kijamii, maji ya Mto Ruaha Mkuu hutumika kukidhi

mahitaji ya majumbani kwa wakazi wanaoishi katika bonde hilo.

4

Kielelezo Na, 1: Shughuli za kiuchumi katika Bonde la Mto Ruaha

Mkuu

Kuanzia miaka ya 1990, Bonde la Mto Ruaha Mkuu limekuwa

likikabiliwa na changamoto mbalimbali za uharibifu wa mazingira na

hivyo kuathiri mfumo-ikolojia wake. Kutokana na changamoto hiyo,

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikichukua

hatua zinazoendana na utekelezaji wa Sera na Sheria mbalimbali ili

kuokoa ikolojia ya Bonde hili.

1.1.1 Sera na Sheria zilizotumika

Baadhi ya sera na sheria zinazohusika katika utekelezaji wa usimamizi

wa Bonde hili ni pamoja na:- Sera ya Taifa ya Mazingira (1997), Sera ya

5

Taifa ya Umwagiliaji (2010), Sera ya Maji (2002), Sera Taifa ya Kilimo

(2013), Sera ya Taifa ya Wanyama Pori (2007), Sera ya Taifa ya Ardhi

(1995) na Sera ya Taifa ya Mifugo (2006). Aidha, utekelezaji wa Sera hizo

unafanywa kupitia sheria zifuatazo;- Sheria ya Usimamizi wa Mazingira

Na. 20 ya mwaka 2004, Sheria ya Uhifadhi wa Wanyama Pori Na. 5 ya

mwaka 2009, Sheria ya Misitu Na. 14 ya mwaka 2002, Sheria ya Utalii Na.

29 ya mwaka 2008, Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya

mwaka 2009, Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji Na. 5 ya mwaka 2013, Sheria

ya Ardhi ya Malisho ya Mifugo Na. 13 ya mwaka 2010, Sheria ya Ardhi

Na. 4 ya mwaka 1999, Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999,

Sheria ya Matumizi ya Ardhi Na. 6 ya mwaka 2007, Sheria ya Utwaaji wa

Ardhi Na. 47 ya mwaka 1967, Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 na

Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (Wilaya) Na. 8 ya mwaka 1982.

1.1.2 Tafiti zilizofanyika katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu

Tafiti mbalimbali zimefanyika katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu ili

kubaini hali halisi ya ikolojia yake, mabadiliko mbalimbali ya kimazingira

na athari zake kwenye mtiririko wa maji katika Mto Ruaha Mkuu,

migogoro baina ya watumia maji na changamoto zinazolikabili Bonde hili

pamoja na njia mbalimbali za utatuzi wake. Baadhi ya tafiti hizo ni:

Uchambuzi wa Mifumo ya Rasilimali za Maji kwenye Tambarare za

Usangu na Mabonde yake Madogo (Water resources system analysis for the

Usangu Plains and its sub basins, Tanzania). Utafiti huu uliofanywa na Dr.

Y. C. Ethan Yang, Dr. Sungwook Wi and Dr. Rikard Liden, 2015;

Tathimini ya Mtiririko wa Maji kwa Ajili ya Mazingira ya Mto Ruaha

Mkuu na Ardhi Oevu ya Ihefu, Tanzania na Mibadala ya Kuhuisha

Mtiririko wa Maji Wakati wa Kiangazi (Environmental Flow Assessment:

The Great Ruaha River and Ihefu Wetlands, Tanzania, and options for the

restoration of dry season flows). Utafiti huo uliofanywa na WWF, Julai 2010;

na Migogoro ya Matumizi ya Rasilimali Katika Tambarare za Usangu,

6

Wilaya ya Mbarali (Resource Use Conflicts in Usangu Plains, Mbarali

District). Utafiti huo uliofanywa na G.C. Kajembe, A. J. Mbwilo, R.S

Kidunda and J. Nduwamanga, 2009.

Tafiti nyingine ni pamoja na;- Mazingira Endelevu na Upatikanaji wa

Maji: Uchambuzi wa Uhaba wa Maji na Nafasi za Maboresho Katika

Tambarare za Usangu (Environmental sustainability and water availability:

Analyses of the scarcity and improvement opportunities in the Usangu plains).

Utafiti huo uliofanywa na Z. J. U. Malley, 2008; Kuelekea Kurudishwa

kwa Ikolojia ya Maji ya Ardhi Oevu ya Usangu na Mto Ruaha Mkuu

(Towards an Ecohydrology-based Restoration of the Usangu Wetlands and the

Great Ruaha River, Tanzania). Utafiti huo uliofanywa na M. G. G. Mtahiko,

E. Gereta, A. R. Kajuni, E. A. T. Chiombola, G. Z. Ng’umbi, P. Coppolillo

and E. Wolanski, 2007; Mabadiliko ya Kimazingira na Udhaifu katika

Tambarare za Usangu, Kusini-Magharibi mwa Tanzania: Muonekano

kwa Maendeleo Endelevu (Environmental Change and Vulnerability in the

Usangu Plain, Southwest Tanzania: Implication for Sustainable Development).

Utafiti huo uliofanywa na Malley, Zacharia J. U na Takeya, Hiroyuki,

2007; na Mgao wa Mtiririko wa Kimazingira katika Mabonde ya Mito:

Kutafiti Changamoto za Mgawanyo na Mibadala Katika Kidakio cha Mto

Ruaha Mkuu, Tanzania (Environmental Flows Allocation in River Basins:

Exploring Allocation Challenges and Options in the Great Ruaha River

Catchment in Tanzania). Utafiti huo uliofanywa na Japhet J. Kashaigili,

Reuben M.J. Kadigi, Bruce A. Lankford, Henry F. Mahoo, Damus A. &

Mashauri C, 2005.

Tafiti nyingine zimeangalia Mgogoro wa Matumizi ya Maji kati ya

Mitambo ya Kufua Umeme na Umwagiliaji katika Tanzania: Mjumuisho

wa Taratibu za Sera za Kisekta katika Maendeleo ya Rasilimali za Maji

(Conflict of Water Use Between Hydropower and Irrigation in Tanzania: the

Conundrum of Sectoral Policy Approaches to Water Resources Development).

7

Utafiti huo uliofanywa na Makarius V. Mdemu na Machibya D.

Magayane, 2005; Ardhi Oevu ya Mabondeni inaweza Kuokoa Bioanuai na

Kuboresha Maisha ya Wananchi (Valley Bottom Wetlands Can Serve for Both

Biodiversity Conservation and Local Livelihoods Improvements). Utafiti huo

uliofanywa na Pantaleo K.T. Munishi, Nice N. Wilfred, James S. Nshare,

Stein R. Moe, Deo D. Shirima na Halima H. Kilungu; Sababu za Kiuchumi

na Kijamii za Upotevu wa Bioanuai Katika Kidakio cha Maji cha Eneo la

Ruaha (Socio-Economic Root Causes of the Loss of Biodiversity in the Ruaha

Catchment Area). Utafiti huo uliofanywa na H. Sosovele & J.J. Ngwale,

2002; Usimamizi wa Mazingira na Uhifadhi wa Bioanuai ya Misitu ya

Nyika na Ardhi Oevu ya Delta ya Mto Rufiji na Uwanda wa Mafurikio

(Environmental Management and Biodiversity Conservation of Forests

Woodlands and Wetlands of the Rufiji Delta and Floodplain: Rufiji River Basin

Upstream-Downstream Linkages). Utafiti huo uliofanywa na Rufiji

Environmental Management Project, 2001; Uchambuzi wa Usimamizi wa

Bonde la Mto: Mitizano ya Watumiaji Mbalimbali na Ushindani katika

Matumizi ya Rasilimali za Maji katika Mto wa Ruaha Mkuu (Analysis of

existing river basin management frameworks, Multi-user Perspectives and

Competition for Water resources in the Great Ruaha River Basin, Tanzania.

Critical Analysis of River Basin Management in the Great Ruaha: An Analysis

of SMUWC and RIPARWIN). Utafiti huo ulifanywa na Bruce Lankford,

Nuhu Hatibu, Henry Mahoo, Barbara van Koppen na Hervé Levite, 2002;

Sababu za Kushuka kwa Kina cha Maji ya Mto Ruaha Mkuu, Tanzania

(The Root Causes of the Declining levels of Water in the Great Ruaha River,

Tanzania). Utafiti huo uliofanywa na Hussein Sosovele, 2007; na Muundo

Kuelekea Uwiano: Uhimili wa Muundo kwa ajili ya Usimamizi wa Bonde

la Mto katika Nchi zinazoendelea (From Integrated to Expedient: An

Adaptive Framework for River Basin Management in Developing Countries).

Utafiti huo uliofanywa na Bruce A. Lankford, Douglas J. Merrey, Julien

Cour and Nick Hepworth, 2007.

8

1.1.3 Programuu na Miradi iliyotekelezwa katika Bonde la Mto Ruaha

Mkuu

Jitihada nyingine zimehusisha utekelezaji wa Programu na miradi

mbalimbali. Baadhi ya miradi iliyotekelezwa ni pamoja na Mradi wa

Usimamizi wa Mabonde ya Mito na Uboreshaji wa Umwagiliaji (RBMSII

Poject) mwaka 1996–2003, Usimamizi Endelevu wa Ardhi Oevu ya

Usangu na Eneo Lake (SMUWC Project) mwaka 1998– 001, Mradi wa

Usimamizi wa Mazingira Rufiji (REM Project) mwaka 1998–2003, Mradi

wa Kuimarisha Uzalishaji katika Umwagiliaji na Mradi wa Uhifadhi wa

Maji kwa Ajili ya Mahitaji ya Kisekta (RIPARWIN Project) mwaka 2002–

2005. Vilevile serikali kwa kushirikiana na wahisani imetekeleza

Programu ya Maji Ruaha (Awamu ya Kwanza) – chini ya WWF 2003–

2010, Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP I) mwaka 2006-

2014, Programu ya Maji Ruaha (Awamu ya Pili) – Chini ya WWF mwaka

2011–2016 na Programu ya Shirikisho la Usimamizi wa Rasilimali za Maji

Tanzania (2030 WRG-Tz) mwaka 2013.

Pamoja na kuwepo kwa sera, sheria na utekelezaji wa tafiti, Programu na

miradi mbalimbali, ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu imeendelea

kuathirika. Baadhi ya sababu zinazochangia kuathirika kwa ikolojia hii ni

pamoja na kukosekana kwa usimamizi thabiti wa utekelezaji wa sheria

zinazosimamia rasilimali zilizopo ndani ya bonde, kupanda miti isiyo

rafiki wa mazingira katika vyanzo vya maji, ongezeko la shughuli za

kilimo na ufugaji bila kufuata sheria, mabadiliko ya tabianchi,

kukosekana kwa mpango wa matumizi bora ya ardhi, ukosefu wa uratibu

wa jumla wa shughuli zinazotekelezwa ndani ya bonde, ukosefu wa

elimu ya matumizi endelevu ya maliasili, kuwepo kwa matamko na

maagizo ya viongozi wa kisiasa yanayokinzana na mikakati na mipango

iliyokubalika hivyo kuchangia kuzorota kwa juhudi za Serikali na wadau

katika kuokoa ikolojia ya Bonde hili. Kuharibika kwa ikolojia ya Bonde

9

hili kumeleta madhara ya kimazingira, kiuchumi na kijamii kwa wakazi

na wadau waliopo katika bonde hili na Taifa kwa ujumla.

Baada ya tafakari ya kina ya hali hii na kwa kuzingatia umuhimu wa

Bonde la Mto Ruaha Mkuu, Serikali kwa kushirikiana na wadau imeona

kuna haja ya kuwa na mtazamo mpya wa namna ya kukabiliana na

changamoto za Bonde la Mto Ruaha Mkuu kwa ufanisi zaidi. Kwa

muktadha huo, Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa mujibu wa Sheria ya

Mazingira ya Mwaka 2014, imeunda Kikosi Kazi cha Kitaifa cha

kunusuru mfumo ikolojia wa Bonde la Mto Ruaha Mkuu

kinachojumuisha viongozi, watendaji na wataalam katika sekta muhimu,

kilichopewa jukumu la kuandaa “mtazamo mpya” wa kukabiliana na

changamoto hizo, ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za haraka na za

dharura na pia kubuni mikakati, mipango na mbinu bora (innovative

strategies) zaidi za kukabiliana na changamoto hizo. Kikosi Kazi hicho

kilizinduliwa rasmi na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais

wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 11 Aprili, 2017, mjini

Iringa katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo. Majina ya wajumbe wa Kikosi

Kazi yameoneshwa katika kiambatisho husika.

Kielelezo Na. 2: Wajumbe wa Kikosi Kazi katika picha ya pamoja na Makamu

10

wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

siku ya uzinduzi, Iringa, Tanzania (Tarehe 11 April 2017)

Madhumuni ya kuundwa kwa Kikosi Kazi ni kama ifuatavyo:-

i) Kuchambua kwa kina tafiti na matokeo ya miradi mbalimbali ya

serikali na wafadhili ambayo imeshafanywa katika mfumo–ikolojia

wa Mto Ruaha Mkuu na Ardhi Oevu (Wetland) ya Bonde la

Usangu na kubainisha hatua mpya na za haraka za kudhibiti

kupungua kwa maji kwenye Mto Ruaha Mkuu;

ii) Kukusanya maoni na mapendekezo ya wadau wote, ikiwemo

wananchi waishio katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu, kuhusu

hatua za hifadhi ya mazingira katika bonde hilo;

iii) Kutumia mamlaka na sheria mbalimbali husika kuchukua hatua za

haraka za kudhibiti uharibifu wa mazingira na kurekebisha

madhara ya uharibifu wa mazingira yaliyojitokeza;

iv) Kuandaa rasimu ya mpango wa Kitaifa wa Hifadhi ya Mazingira

ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu; na

v) Kutoa ushauri wa kisera au kiutendaji wenye lengo la kuokoa

mfumo–ikolojia wa Bonde la Mto Ruaha Mkuu.

Pamoja na madhumuni hayo, Kikosi Kazi kilitakiwa kukamilisha kazi

zifuatazo:-

i) Kupendekeza mfumo mpya utakaoimarisha uratibu wa pamoja wa

juhudi za usimamizi wa rasilimali za Mto Ruaha Mkuu;

ii) Kuweka muundo wa kitaasisi kwa ajili ya uratibu wa pamoja;

iii) Kubainisha utaratibu bora wa usimamizi wa maeneo ya bonde

pamoja na rasilimali zake; na

iv) Kuainisha utaratibu madhubuti wa kuhakikisha tathmini ya

kimkakati ya mazingira kwenye Bonde la Mto Ruaha Mkuu

inafanyika.

11

SURA YA PILI

2.0 MBINU ZA UKUSANYAJI, UCHAKATAJI, UCHAMBUZI NA

UWASILISHAJI WA TAKWIMU NA TAARIFA

2.1 Eneo husika

Maeneo yaliyotembelewa yalihusisha sehemu kubwa ya Bonde la Mto

Ruaha Mkuu kama yanavyoonekana katika Kielelezo Na.2 na orodha ya

maeneo yaliyotembelewa yameambatishwa katika Kiambatisho Na. 2.

Maeneo hayo yaliainishwa kwa kutumia vigezo vifuatavyo: (i) Maeneo ya

vyanzo vya maji (water towers/catchment areas) yaliyopo katika wilaya

za Makete, Wanging’ombe, Mbeya, Mufindi, Iringa, Kilolo na Chunya. (ii)

Maeneo yenye matumizi makubwa ya maji yanayozunguka Eneo Oevu la

Ihefu yaliyopo katika Wilaya ya Mbarali. (iii) Maeneo yanayopokea maji

kutoka kwenye Eneo Oevu la Ihefu ikihusisha Hifadhi ya Taifa ya Ruaha,

Bwawa la Mtera na baadhi ya maeneo katika Wilaya ya Iringa.

12

Kielelezo Na. 3: Ramani ya Mikoa iliyotembelewa na Kikosi Kazi

2.2 Wadau Waliohojiwa (Wigo wa Sampuli)

Katika kupata maoni ya wadau, mbinu mbalimbali za kuchagua sampuli

wakilishi zilitumika. Mbinu ya sampuli ya ulazima (purposive sampling)

zilitumika kuchagua mikoa mitatu (Iringa, Mbeya na Njombe) inayounda

sehemu kubwa ya eneo la Bonde la Mto Ruaha Mkuu. Vilevile mbinu hii

ilitumika kuchagua viongozi mbalimbali hususan Mawaziri, Wakuu wa

Mikoa, Wabunge, Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti na Wakurugenzi wa

Halmashauri, Watendaji wa Kata na Vijiji vilivyopo katika Bonde la Mto

Ruaha Mkuu. Mbinu ya uchaguzi wa makundi wakilishi yaani Cluster

Sampling ilitumika kuchagua makundi yaliyohojiwa. Zoezi hili lilihusisha

jumla ya wahojiwa 570 kutoka katika makundi mbalimbali. Majina ya

wadau waliohojiwa na vigezo vilivyotumika vimeoneshwa katika

Kiambatisho Na. 3.

13

2.3 Ukusanyaji wa Takwimu na Taarifa

2.3.1 Takwimu za Awali/Msingi

Ukusanyaji wa takwimu za msingi ulihusisha mahojiano na makundi

mbalimbali, mikutano na mahojiano ya mtu mmoja mmoja. Wahusika

katika mahojiano hayo ni pamoja na viongozi wa Serikali, Mawaziri,

Wabunge, Madiwani, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya,

Kamati za Mazingira, na Wadau wa Maendeleo (mfano: Benki ya Dunia).

Wengine waliohojiwa ni pamoja na: wawekezaji wa mashamba

makubwa, Mashirika na Taasisi za Serikali (TAWA, TANAPA, RUBADA,

TFS, SAGCOT, Shamba la Mifugo Kitulo na TANESCO), washiriki toka

Programuu mbalimbali zilizotekelezwa katika bonde hili kama vile

Tanzania Forest Programume (TFP), Asasi za Kiraia na mashirika yasiyo

ya kiserikali (STEPS, PFP, SPANEST, WWF, EMEDO, na NOSC). Aidha,

Shirika la TNC liliwakilisha mashirika ya CARE INTERNATIONAL,

IUCN, SHAHIDI WA MAJI, 2030 WRG na WWF kupitia mahojiano.

Viongozi wa Vyama vya Siasa, Watendaji wa Serikali, Viongozi wa Dini,

Jumuiya za Watumia maji, Wamwagiliaji (wakubwa na wadogo),

Wafugaji, Watu Maarufu na Wananchi nao pia walishiriki katika

mahojiano.

14

Kielelezo Na. 4: Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kutoa maoni, Kijiji cha Madibira, Wilaya ya Mbarali (Tarehe 20 Aprili, 2017)

2.3.2 Takwimu za Upili

Uchambuzi wa takwimu za upili ulihusisha mapitio ya sera, sheria, taarifa, Programu, miradi, tafiti na matamko mbalimbali ya viongozi. Sera zilizopitiwa ni pamoja na;- Sera ya Taifa ya Mazingira (1997), Sera ya Taifa ya Umwagiliaji (2010), Sera ya Taifa ya Maji (2002), Sera ya Taifa ya Kilimo (2013), Sera ya Taifa ya Wanyama Pori (2007), Sera ya Taifa ya Ardhi (1995) na Sera ya Mifugo (2006). Vilevile, sheria zilizopitiwa ni pamoja na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004, Sheria ya Uhifadhi wa Wanyama Pori Na. 5 ya mwaka 2009, Sheria ya Misitu Na. 14 ya 2002, Sheria ya Utalii Na. 29 ya mwaka 2008, Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya mwaka 2009, Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji Na. 5 ya mwaka 2013, Sheria ya Ardhi ya Malisho ya Mifugo Na. 13 ya mwaka 2010, Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999, Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999, Sheria ya Matumizi ya Ardhi Na. 6 ya mwaka 2007, Sheria ya Utwaaji wa Ardhi Na. 47 ya mwaka 1967, Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 pamoja na Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (Wilaya) Na. 8 ya mwaka 1982.

Ripoti zilizopitiwa kwa kina ni pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kuandaa Programu ya Kuendeleza Bonde la Mto Ruaha Mkuu ya mwaka 2002, Taarifa ya Kamati ya Waziri Mkuu ya mwaka 2012, Mpango wa

15

Usimamizi wa Pamoja wa Rasilimali za Maji katika Bonde la Rufiji wa mwaka 2015, Tangazo la Serikali Na. 28 la mwaka 2008, Mpango wa Taifa wa Umwagiliaji wa mwaka 2002 na Mwongozo wa Uendelezaji wa Miradi ya Umwagiliaji wa mwaka 2010.

2.4 Uchakataji, Uchambuzi na Uwasilishaji wa Taarifa

Zoezi la uchakataji wa takwimu lilihusisha hatua mbalimbali zikiwemo kupitia takwimu zilizokusanywa na kuziweka katika muundo wa taarifa uliokubaliwa. Aidha, uchambuzi wa takwimu uliwasilishwa kupitia nyenzo rahisi kama vile asilimia, wastani na viwango. Uwasilishaji wa taarifa umefanyika kwa kutumia majedwali, grafu, ramani na picha.

Uchambuzi na tathmini umefanywa kwa kuzingatia taarifa zilizopatikana kutokana na maoni, uchambuzi wa tafiti na miradi mbalimbali kama ilivyooneshwa katika sehemu 2.3 kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:- vyanzo vya maji yaliyopo katika wilaya za Makete, Wanging’ombe, Mbeya, Mufindi, Iringa, Kilolo na Chunya; maeneo yenye matumizi makubwa ya maji yanayozunguka eneo la ardhi oevu ya Ihefu, ambalo lilihusisha Wilaya ya Mbarali pekee; na maeneo yanayopokea maji kutoka kwenye eneo la ardhi oevu ya Ihefu ikihusisha Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Bwawa la Mtera na baadhi ya maeneo katika Wilaya ya Iringa.

2.5 Muundo wa Taarifa

Taarifa hii imegawanyika katika Sura Tano. Sura ya Kwanza ni Utangulizi, ambayo inaelezea historia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu, mifumo ya ikolojia yake na hali ya mabadiliko ya viwango vya maji. Sura hii pia imeonesha umuhimu wa bonde hili kiuchumi, kijamii na kiikolojia na baadhi ya changamoto za uharibifu wa mazingira zinazoikabili bonde la mto Ruaha Mkuu. Sera na Sheria mbalimbali zinazoweza kutumika kunusuru ikolojia ya bonde hili pamoja na madhumuni ya Kikosi Kazi hiki pia zimetajwa katika sura hii.

Sura ya Pili inaeleza mbinu za uchaguzi wa wahojiwa, ukusanyaji, uchakataji, uchambuzi na uwasilishaji wa takwimu na taarifa. Maeneo yaliyotembelewa, wigo wa sampuli ukianisha aina za wadau waliohojiwa pamoja na vigezo vya uchaguzi wa sampuli yameainishwa. Sura hii pia inaonesha jinsi ukusanyaji wa takwimu na taarifa za awali/msingi na za upili ulivyofanyika na pia jinsi uchakataji, uchambuzi na uwasilishaji wa taarifa ulivyofikiwa.

16

Sura ya Tatu inaeleza hali halisi ya mazingira katika bonde hilo, maumbile ya nchi, hali ya hewa, shughuli mbalimbali za kiuchumi na mwenendo wa viwango vya maji. Shughuli za kilimo, ufugaji, uvunaji wa mazao ya misitu, uvuvi, uchimbaji madini, wanyamapori na bionuwai katika bonde hilo navyo vimeainishwa katika sura hii. Matatizo makuu yanayolikabili bonde hili na juhudi mbalimbali za kunusuru ikolojia.

Sura ya Nne imeainisha uchambuzi wa takwimu na taarifa ya mambo yaliyojiri Uwandani. Mambo yaliyojionesha katika sura hii ni pamoja na sababu za tatizo la kupungua kwa maji katika bonde, madhara ya kiuchumi na kiikolojia.

Sura ya Tano inaeleza hitimisho na kutoa mapendekezo ya utekelezaji ili kuokoa ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu. Aidha, kuna sehemu ya rejea inayofuatiwa na viambatisho. Viambatisho hivyo ni pamoja na Rasimu ya Mpango wa Kuokoa Ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu.

17

SURA YA TATU

3.0 HALI HALISI YA MAZINGIRA NA JITIHADA ZILIZOFANYIKA KUOKOA IKOLOJIA YA BONDE LA MTO RUAHA MKUU

3.1 Hali ya Ikolojia na Mazingira

Bonde la Mto Ruaha Mkuu lina maumbile na hali ya hewa inayofaa kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji, uvuvi, uzalishaji wa nishati, uhifadhi wa wanyama pori na utalii. Kwa upande wa shughuli za kijamii, bonde hili limekuwa ni sehemu ya makazi na uoto wake wa asili unatumika kwa shughuli za ibada na mambo mengine ya kijamii. Maelezo ya kina kuhusiana na maumbile, hali ya hewa, hali ya mvua, uoto wa asili katika bonde hilo yametolewa katika sehemu zifuatazo:-

3.1.1 Maumbile ya Nchi

Maumbile ya nchi ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu yanatawaliwa na miinuko na milima. Upande wa kusini-mashariki na kusini-magharibi kuna miinuko ya wastani wa mita 1,100 mpaka mita 3,000 kutoka usawa wa bahari. Upande wa kusini na kusini-mashariki kuna nyanda za juu za milima ya Rungwe, Uporoto na Kipengere pamoja na nyanda za juu za Kitulo naGofio. Miinuko ya Mafinga (Mafinga escarpment) huambaa upande wa mashariki mpaka Iringa na kuunda sehemu ya nyanda za juu za kusini na sehemu za kingo za Bonde la Ufa. Upande wa magharibi kuna miinuko ya Chunya ikiwa ni pamoja na safu za miinuko ya Mbeya.

Milima mingi katika bonde hili imeundwa na miamba yenye asili ya “granite” pamoja na Volkano, hususan maeneo ya Rungwe. Kuwepo kwa matukio ya Volkano kumesababisha miamba hiyo ya granite kubadilishwa kuwa udongo laini wenye asili ya tindikali. Maeneo ya Usangu ambayo ni tambarare yana udongo wa “alluvial” na mfinyanzi ambao hupatikana sehemu zenye miinuko ya mita 1,000-1,100 kutoka usawa wa bahari na hupungua kadri mto unavyoelekea katika Bwawa la Mtera.

18

Kielelezo Na. 5: Ramani ya Maumbile ya Nchi ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu

3.1.2 Hali ya Hewa

Viwango vya mvua katika Bonde vinatofautiana na vinategemea maumbile ya nchi. Mvua nyingi hunyesha katika nyanda za juu au kwenye miinuko ambapo kiwango cha juu nimilimita 2,600 na kiwango cha chini ni milimita 1,000 kwa mwaka. Nyanda za chini hasa upande wa Kaskazini na Mashariki mwa Bonde hupata wastani wa mvua wa milimita 500 kwa mwaka. Kwa ujumla msimu wa mvua katika Bonde hili huanza mwezi Novemba mpaka mwezi Mei na hupata mvua mara moja kwa msimu (unimodal rainfall pattern).

3.2 Shughuli za Kiuchumi

Bonde la Mto Ruaha Mkuu ni kitovu cha shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo kilimo, ufugaji, uvuvi, uzalishaji nishati, uchimbaji madini na shughuli mbalimbali zinazoendana na uhifadhi wa wanyamapori.

19

3.2.1 Kilimo

Kwa kiasi kikubwa uchumi wa bonde hili hutegemea kilimo cha mvua na Umwagiliaji. Uzalishaji wa mchele katika mwaka 2015/2016 ulikuwa tani 2,229,071 ambapo kati ya tani hizo, Bonde la Mto Ruaha Mkuu lilizalisha tani 253,636 ambazo ni sawa na asilimia 11.4 za mchele wote uliozalishwa nchini. Aidha, shughuli za kilimo zimeajiri takriban asilimia 90 ya wakazi wanaoishi katika Bonde hilo.

Kilimo cha umwagiliaji katika Bonde hili kinafanyika katika skimu ndogo, skimu za kati na skimu kubwa za umwagiliaji kama inavyoonekana katika Kiambatisho Na. 4. Skimu kubwa zinazomilikiwa na wawekezaji zipo 11 na zina ukubwa wa hekta 12,425 zinazomwagiliwa. Skimu kubwa zinazomilikiwa na umoja wa wakulima zina ukubwa wa hekta 50,704 zinazofaa kumwagiliwa zenye jumla ya hekta 29,533 zinazomwagiliwa kwa sasa na jumla ya wamwagiliaji 7,855. Skimu za kati katika Bonde hilo zina ukubwa wa hekta 44,634 zinazofaa kumwagiliwa zenye jumla ya hekta 24,501 zinazomwagiliwa kwa sasa na jumla ya wamwagiliaji 20,594. Vilevile, Skimu ndogo katika Bonde hili zina ukubwa wa hekta 19,053 zinazofaa kumwagiliwa zenye jumla ya hekta 10,728 zinazomwagiliwa kwa sasa na jumla ya wamwagiliaji 8,175.

Changamoto za kilimo cha umwagiliaji katika Bonde hilo ni pamoja na matumizi ya maji yasiyo endelevu, miundombinu ya umwagiliaji isiyoboreshwa, usimamizi mbovu wa matumizi ya maji mashambani na matumizi madogo ya teknolojia zinazotumia maji kwa ufanisi.

3.2.2 Ufugaji

Ufugaji ni moja kati ya shughuli muhimu za kiuchumi zilizopo katika

Bonde la Mto Ruaha Mkuu. Aina kuu za mifugo inayopatikana katika

eneo hili ning’ombe, mbuzi, kondoo na kuku. Kwa wastani inakadiriwa

eneo hili kuwa na ng’ombe 623,160, mbuzi 452,250, kondoo 110,880 na

kuku 2,500,000. Kulingana na viwango vya mipango ya matumizi bora ya

ardhi, idadi hii ya mifugo inahitaji eneo la ardhi la kilomita za mraba

11,660 kwa mifugo isiyozidi uzito wa kilo 200 kwa mfugo mmoja,

ambapo mfugo mmoja (Livestock Unit- LU) unahitaji hekta 2 za malisho

20

kwa mwaka. Eneo hilo ni sawa na asilimia 16.2 ya eneo lote la Bonde la

Mto Ruaha Mkuu. Hata hivyo, kumekuwepo na wingi wa mifugo

uliokithiri katika bonde hili ambao umesababisha uharibifu mkubwa wa

vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla. Mfano, Wilaya Mbarali ina

uwezo wa jumla ya mifugo (Livestock Unit) 65,000 wakati mifugo iliyopo

ya wakazi halali ni zaidi ya 200,000 (Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, 2017 –

mawasiliano binafsi). Pamoja na idadi hiyo ya mifugo ya wakazi halali,

bado kuna idadi kubwa ya mifugo ambayo huingizwa na wafugaji wa

kuhamahama na kusababisha uharibifu mkubwa wa ikolojia.

Kielelezo Na. 6: Shughuli za Kilimo na Mifugo zikifanyika kwenye eneo chepechepe katika kata ya Inyala, Wilaya ya Mbeya (Tarehe 24 April 2017)

3.2.3 Misitu

Upandaji na uvunaji wa mazao ya misitu hasa mbao ni miongoni mwa

shughuli muhimu za kiuchumi katika eneo hili, hususan katika wilaya za

Kilolo, Wanging’ombe, Mufindi na Makete. Mbao hupatikana kutoka

katika miti aina ya misindano (Pines) na mikaratusi (Eucalyptus) ambayo

inapatikana katika maeneo ya miinuko na mabonde yaliyomo ndani ya

Bonde la Mto Ruaha Mkuu. Upandaji wa miti unafanywa na wawekezaji

wakubwa, wakulima wadogo, taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za

21

kiserikali. Mojawapo ya taasisi na makampuni yanayojihusisha na

upandaji wa miti ya mbao ni:- Sao Hill Forestry Plantations, Programu za

MEMA, CONCERN, Forest Escarpment na Hifadhi Mazingira (HIMA)

Mkoani Iringa. Aina nyingine za miti inayopandwa kwa wingi ni ile

isiyokuwa ya asili kama vile; Grevillea robusta, Leucaena leucocephala,

Jacaranda mimosifolia na Syzygium cuminii. Aidha, jamii imekuwa

ikihamasishwa kupanda miti ya asili kama vile Erythrina abysinica,

Syzygium cordatum, Cordia Africana, Croton macrostrachys na Hakea

abbysinica ili kuimarisha bioanuai. Kupanuka kwa shughuli

zinazohusiana na ujenzi kumesababisha kuongezeka kwa uvunaji wa

misitu hasa katika miji ya Makete na Mufindi ambayo ndiyo kilipo

chanzo cha Mto Ruaha Mkuu na kusababisha uharibifu wa mazingira

kama vile mmomonyoko wa udongo, kupotea kwa uoto wa asili pamoja

na kuongezeka kwa tabaka la udongo (siltation) katika mto Ruaha Mkuu.

3.2.4 Uvuvi

Shughuli za uvuvi hufanyika zaidi katika Bwawa la Mtera na katika mito

mbalimbali. Uvuvi katika Bwawa la Mtera una umuhimu mkubwa

kiuchumi na kijamii ambapo zaidi ya watu laki mbili kutoka maeneo

mbalimbali ya nchi hutegemea uvuvi katika bwawa hilo. Samaki wengi

hupatikana kipindi cha mvua za mwanzo na wakati wa kupungua kwa

kiwango cha maji mtoni. Kuna zaidi ya aina 38 za samaki ambao

wametambulika kuwepo katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu ambapo,

asilimia 40 ya samaki hao hawapatikani mahala popote duniani kama vile

Oreochromis urolepis (tilapia), Labeo ulangenis, Alestes stuhlmanii, na

Hydrocynus tanzaniae (tiger fish). Wananchi pia hujihusisha na ufugaji wa

samaki kwenye mabwawa ya kuchimba ambao umeanza kuongezeka

kwa kasi. Kupungua kwa kiwango cha maji katika Bwawa la Mtera

kumeathiri kwa kiwango kikubwa shughuli za uvuvi na kusababisha

22

kutoweka kwa baadhi ya aina za samaki.

3.2.5 Uchimbaji madini

Uchimbaji wa madini ni mojawapo ya shughuli inayofanyika katika

Bonde la Mto Ruaha Mkuu. Shughuli za uchimbaji zinzhusisha hasa

uchimbaji wa mawe katika maeneo ya Inyala Wilaya ya Mbeya na

dhahabu katika maeneo ya pembezoni mwa safu za Milima ya Mpanga-

Kipengere na katika maeneo mengi ya Wilaya ya Chunya. Aidha,

uchimbaji wa udongo na mchanga kwa ajili ya kutengeza matofali

unafanyika katika maeneo yaliyo kandokando ya mito inayoingia katika

Bonde la Mto wa Ruaha Mkuu. Uchomaji wa matofali hayo hutumia

kuni, magogo na pumba za mpunga. Matumizi ya kuni na magogo

kutoka katika uoto wa asili huchangia uharibifu wa mazingira. Uchimbaji

wa madini hayo ni mojawapo ya shughuli za kibinadamu

zinazosababisha uharibifu wa vyanzo vya maji na mazingira katika

Bonde hilo.

3.2.6 Wanyamapori na Bioanuai Nyingine

Bonde la Mto Ruaha Mkuu linaungana na Hifadhi za Taifa za Ruaha

pamoja na Kitulo ambazo zinahifadhi aina mbalimbali za wanyamapori,

mimea (maua) pamoja na aina tofauti za ndege takriban 570 wakiwemo

ndege wanaohama. Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ina ukubwa wa Kilometa

za mraba 20,226 na ni ya pili kwa ukubwa katika AfrikaMashariki.

Hifadhi ya Taifa ya Kitulo ina ukubwa wa kilomita za mraba 413.

Vilevile, kuna Hifadhi ya Akiba la Mpanga-Kipengere yenye kilomita za

mraba 1,574. Maeneo mengine yenye wanyamapori ni pamoja na Hifadhi

ya Taifa ya Mikumi na Milima ya Udzungwa; Hifadhi za Akiba za

Rungwa, Kizigo na Muhezi; Hifadhi Tengefu la Lunda/Mkwambi na

Lihongosa; pamoja na maeneo ya wazi. Pia kuna takriban aina 1,650 za

23

mimea ya asili ikiwemo maua ya Kitulo na Viazi Pori (Calanthe syvatica)

maarufu kama “chikanda”. Mmea wa chikanda ambao hutumika kama

chakula na dawa upo katika hatari ya kutoweka, hivyo umewekwa katika

orodha ya mimea iliyopo katika Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia

Biashara ya Viumbe na Mimea ilivyo hatarini Kutoweka “CITES”. Aidha,

baadhi ya wanyama wanaopatikana katika hifadhi hizo ni pamoja na

simba, tembo, twiga, mamba, viboko, nyati, pundamilia na tandala

wakubwa na wadogo. Katika hifadhi hizo pia kuna aina 38 za samaki wa

asili.

3.3 Tatizo Kuu katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu

Usimamizi na uratibu duni wa shughuli za kiuchumi na kijamii katika

Bonde la Mto Ruaha Mkuu umesababisha uharibifu mkubwa wa

mazingira. Uharibifu huo umejidhihirisha katika maeneo mbalimbali

ikiwemo upungufu mkubwa wa maji na mara nyingine kukauka kwa

mito mbalimbali inayochangia maji kwenye Mto Ruaha Mkuu, ikiwemo

kukauka kwa muda mrefu kwa Mto Ruaha Mkuu.

Historia inaonesha kwamba kabla ya miaka ya 1980 mtiririko wa maji

katika Mto Ruaha Mkuu wakati wa kiangazi ulikuwa kati ya mita za

ujazo 0.5 na 1.0 kwa sekunde. Uharibifu wa mazingira na kuongezeka

kwa shughuli za kibinadamu, hasa kilimo cha umwagiliaji kisicho

endelevu, ufugaji, upandaji wa miti ya kibiashara na uvunaji wa misitu

usio endelevu na shughuli nyingine za kibinadamu zimesababisha

mtiririko wa maji katika mito na vijito kupungua na kukauka kwa muda

mrefu kuliko ilivyokuwa hapo awali. Maeneo ya umwagiliaji hususan

katika eneo la Usangu yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka

kutoka hekta 14,000 mwaka 1980 mpaka hekta 24,000 mwaka 1990 na

kufikia hekta za mraba 115,000 mwaka 2015 kama inavyooneshwa katika

Kielelezo Na. 7. Hali hii imekuwa ikichangia kupungua kwa mtiririko wa

maji katika Mto Ruaha Mkuu kutoka mwaka hadi mwaka.

24

Kielelezo Na. 7: Ongezeko la eneo la Umwagiliaji

Chanzo: Rufiji Basin IWRMD Plan, 2015

Kwa mujibu wa Mpango Shirikishi wa Uendelezaji na Usimamizi wa

Rasilimali za Maji wa Bonde la Rufiji (IWRMDP), kuanzia mwanzoni

mwa miaka ya 1990 mto umekuwa ukikauka nyakati za kiangazi na idadi

ya siku za kukauka imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka

(Angalia Jedwali Na. 1). Hali hii imesababisha ukubwa wa ardhi Oevu ya

Ihefu kupungua kutoka kilometa za mraba 180 kabla ya mwaka 1990 hadi

120 mwaka 2015.

Jedwali Na. 1: Idadi ya siku za kukauka Mto Ruaha Mkuu - Kituo cha Msembe

ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha

14,000 ha 24,000 ha

115,000 ha

+500%

25

Mwaka Kuanza

Kukauka Mwanzo wa Mtiririko

Idadi ya Siku za Kukauka

1994 17-Novemba 15-Desemba 28

1995 19-Oktoba 23- Desemba 65

1996 17-Oktoba 16- Desemba 60

1997 20-Septemba 22-Novemba 63

1998 18-Novemba 9- Machi 87

1999 21-Septemba 20- Desemba 90

2000 17-Septemba 22- Novemba 66

2001 12-Novemba 23- Desemba 41

2002 2-Novemba 24- Desemba 52

2003 21-Septemba 16- Januari 104

2004 3-Novemba 4-Desemba 31

2005 26-Oktoba 31- Januari 98

2010 3-Oktoba 20-Machi 169

2011 23- Oktoba 10- Desemba 48

2012 21- Novemba 11 – Desemba 19

2013 3- Novemba 28 - Novemba 25

2016 23 Oktoba 30 Januari 100

Chanzo: RUNAPA, 2016

3.4 Juhudi za Kunusuru Ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu

Kufuatia ongezeko la vipindi virefu vya kukauka kwa Mto Ruaha Mkuu,

Serikali pamoja na wadau walianzisha na kutekeleza jitihada mbalimbali

26

kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo. Utekelezaji wa jitihada hizo

ulianza kabla ya mwaka 1990 na unaendelea hadi sasa, kupitia Sera,

Sheria na Kanuni zilizopo. Serikali na wadau wametekeleza Programu,

miradi na tafiti mbalimbali ili kubaini na kuchukua hatua za kupunguza

au kumaliza changamoto ya kupungua au kukauka kwa maji ya Mto

Ruaha Mkuu. Yafuatayo ni maelezo ya baadhi ya jitihada

zilizochukuliwa:-

3.4.1 Sera na Sheria

Katika kushughulikia urejeshwaji wa ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha

Mkuu, Kikosi Kazi kilibaini sheria mbalimbali ambazo zinazotumika

katika kusimamia urejeshwaji wa ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu.

Kikosi Kazi kimebaini kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau katika

kusimamia na kutekeleza sera na sheria hizo, yapo mapungufu

mbalimbali kama inavyonesha katika maeneo yafuatayo:-

i. Kukosekana kwa uratibu wa pamoja katika utekelezaji wa sera,

sheria na kanuni;

ii. Kutofanyika kwa marejeo au mapitio ya mara kwa mara ya sera na

sheria ili kuona kama sera, sheria na kanuni hizo zinakidhi

vipaumbele na matakwa ya wakati uliopo;

iii. Uchelewaji wa kutungwa sheria kwa ajili ya utekelezaji wa sera

husika; na

iv. Kutokuwepo kwa mikakati ya utekelezaji wa sera zilizotungwa au

kutokuwepo kabisa kwa sheria ambazo sera zake zipo ni

mojawapo ya sababu zinazokwamisha juhudi za kurejesha ikolojia

ya Mto Ruaha Mkuu.

Baadhi ya sera na sheria zilizobainishwa na Kikosi Kazi zimeainishwa

katika Jedwali Na. 2.

27

28

Jedwali Na.2: Uchambuzi wa Sera na Sheria muhimu kwenye eneo la Bonde Mto Ruaha Mkuu

NA. SERA MATAMKO CHANGAMOTO USHAURI 1. Sera ya Taifa ya

Ardhi ya mwaka 1995

Sera imetamka katika Kifungu cha 4.1 (iii) kuwa Serikali za Vijiji zitasimamia na kuendesha masuala ya ardhi katika vijiji vyao na madaraka yao yatakuwa na ukomo utakaotamkwa wazi wazi katika taratibu na Sheria.

Usimamizi na ugawaji wa ardhi ya vijiji hauzingatiwi kwani halmashauri za vijiji zimekuwa zikikiuka sheria na taratibu za ugawaji na usimamizi wa ardhi ya kijiji kwa kugawa au kuruhusu/kutokuzuia shughuli za kibinadamu katika ardhi ya hifadhi hasa katika maeneo ya hifadhi za misitu, ardhi oevu, vyanzo vya maji na maeneo mengine ya hifadhi.

Sera ihuishwe ili kudhibiti mamlaka ya ugawaji na usimamizi wa ardhi ya vijiji.

Sera katika Kifungu cha 3.4.1.1 inatoa utaratibu wa kuandaa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Kijiji kwa lengo la kuharakisha utekelezaji wake. Aidha, Mipango ya Matumizi Ardhi ya kijiji itatoa msingi utakaoongoza huduma za ugani ikiwa ni pamoja na mbinu za kilimo, ufugaji, usimamizi wa misitu, wanyamapori, uvuvi na hifadhi ya mazingira.

Vijiji vingi havina Mipango ya Matumizi ya Ardhi. Hali hii imesababisha mwingiliano uisiowiana wa matumizi ya ardhi na wakati mwingine kusababisha migogoro ya ardhi kati ya watumiaji mbalimbali wa ardhi (Mfano Wakulima na wafugaji).

Kipaumbele kitolewe kwa ajili ya kuandaa Mipango ya matumizi ya ardhi katika maeneo yenye umuhimu wa pekee kwa Taifa.

Aidha, Sera imetamka kwenye kifungu cha 6.10 kuwa mipango ya matumizi ya ardhi vijijini itaandaliwa na kutekelezwa na Halmashauri za Wilaya kwa kushirikiana

Aidha kutokuwepo kwa Mpango wa Matumizi ya ardhi kumesababisha kuwepo kwa shughuli za kibinadamu katika ardhi za hifadhi, vyanzo vya maji na

Ugawaji wa maeneo makubwa ya ardhi na ardhi kwa ajili ya uwekezaji visifanyike mpaka uandaliwe Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Kijiji ili kabla

29

NA. SERA MATAMKO CHANGAMOTO USHAURI na Serikali za Vijiji.

ardhi oevu.

ya ugawaji huo, kijiji na mamlaka nyingine zinazohusika zijiridhishe kuwa ardhi ya ziada na kwa ajili ya uwekezaji ipo.

Sera katika Vifungu 7.3.0-7.3.3 imetamka kuwa ufugaji wa kutangatanga umesababisha migogoro katika umiliki na matumizi ya ardhi katika jamii zilizo na makazi ya kudumu. Kukosekana kwa udhibiti wa nyendo za mifugo kumesababisha uharibifu wa mazingira katika maeneo wanayopita. Sera inatamka kuwa: Kilimo na ufugaji wa kutangatanga vitazuiwa; kutakuwa na vivutio kwa ajili ya ufugaji bora ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya maji na majosho na njia za kisasa za ufugaji zitaimarishwa; nyendo za za mifugo zitadhibitiwa kuwa na mipango iliyoratibiwa na kuanishwa kwa mapito ya mifugo na mbinu nyingine mbalimbali. Wafugaji na wakulima wataelimishwa juu ya usimamizi bora wa ardhi na matumizi.

Ufugaji wa kutangatanga bado upo katika maeneo mbalimbali nchini. Hali hii imeendelea kusababisha migogoro kati ya wakulima na wafugaji, mifugo kuharibu ardhi ya Hifadhi, ardhi oevu, vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla.

Kutokana na umuhimu wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi Vijijini, Serikali kuu na Halmashauri za Wilaya zitenge fedha ya kutosha katika bajeti za kila mwaka ili kuharakisha Uandaaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi vijijini.

Kifungu cha 4.2.1 cha sera kimetamka kuwa ukomo wa kiasi cha umiliki wa ardhi kitawekwa na serikali kwa kuzingatia misingi ya matumizi, eneo ardhi ilipo, upembuzi yakinifu na uthibitisho wa uwezo

Katika maeneo mengi nchini bado hakuna utaratibu uliowekwa wa ukomo wa kiasi cha ardhi kinachoweza kumilikiwa na mtu mmoja.

Msisitizo uendelee kuwekwa katika kusimamia na kudhibiti nyendo za mifugo. Ufugaji wa kuhamahama uendelee

30

NA. SERA MATAMKO CHANGAMOTO USHAURI wa mwombaji kuiendeleza ardhi husika. kupigwa marufuku na suala hili

lisimamiwe ipasavyo na mamlaka zinazohusika. Mifugo ipigwe chapa ili kurahisisha utambuzi na udhibiti wa nyendo zake. Ufugaji bora uendelee kusisitizwa na kusimamiwa; hii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya maji, majosho na elimu ya ufugaji wa kisasa kwa wafugaji. Serikali iandae na kusimamia upembuzi yakinifu utakaowezesha uandaaji wa ukomo wa umiliki wa ardhi katika maeneo yote nchini

Sera ya Taifa ya Umwagiliaji ya Mwaka 2010.

Sera katika kifungu 2.4.1.1 (a) inaeleza kuhusu skimu za umwagiliaji ambazo hazijaboreshwa na hivyo kusababisha ufanisi mdogo katika umwagiliaji. Hali hii huchangia kwa kiasi kikubwa katika upotevu wa maji.

Bado Skimu nyingi za umwagiliaji wa asili hazijaboreshwa; zina miundombinu mibovu na hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa maji.

Msisitizo mkubwa unatakiwa katika kuboresha miundombinu ya skimu za umwagiliaji wa asili.

2. Madhumuni ya sera ni kuimarisha miundombinu na taratibu zote zinazohusu mifumo ya umwagiliaji wa asili ili kukidhi upatikanaji wa uhakika wa maji ya

Aidha, kuna haja ya kuweka msisitizo katika kutoa mafunzo kwa wakulima na wataalamu kuhusu mbinu za umwagiliaji na hasa katika teknolojia ya

31

NA. SERA MATAMKO CHANGAMOTO USHAURI umwagiliaji na kuongeza ufanisi katika matumizi yake. Ili kufanikisha madhumuni ya sera katika jambo hili, sera inatamka kuwa yafuatayo yatatekelezwa: i. Kuendelea kuwezesha uboreshaji wa

miundombinu ya umwagiliaji na taratibu zake katika skimu za umwagiliaji za asili;

ii. Kuivutia sekta binafsi, asasi zisizokuwa za kiserikali, asasi za kijamii, asasi za kidini na wadau wengine, kuwezesha uboreshaji wa miundombinu ya umwagiliaji na taratibu zake;

iii. Kujenga uelewa wa walengwa kuhusu umuhimu wa kuchangia gharama za uboreshaji wa miundombinu ya umwagiliaji ya skimu zao na

iv. Kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu mbinu za umwagiliaji katika nyanja za usimamizi wa maji ya umwagiliaji na kuwawezesha wataalamu ngazi ya wilaya kuhakikisha ubora wa shughuli za kilimo.

Sera katika kifungu cha 2.4.1.2 imeeleza juu ya skimu za umwagiliaji za kukinga maji ya

umwagiliaji inayotumia maji kidogo; mfano Kilimo Shadidi (System of Rice Intensification).

32

NA. SERA MATAMKO CHANGAMOTO USHAURI mvua. Madhumuni ya sera ni kuhakikisha upatikanaji wa maji wenye uhakika kwa ajili ya skimu za umwagiliaji za kukinga maji ya mvua. Ili kufanikisha madhumuni haya, sera inatamka kufanya yafuatayo: i. Kusaidia uboreshaji wa miundombinu

ya asili ya kukinga maji ya mvua pamoja na taratibu zote zinazohusika;

ii. Kuwezesha ujenzi wa mabwawa madogo, ya kati na makubwa ya kimkakati na kuyahamisha maji kutoka bonde moja hadi lingine kwa ajili umwagiliaji katika hali yenye ufanisi kiuchumi, yenye kukubalika kijamii na kimazingira; na

iii. Kuongeza uelewa wa walengwa kuhusu uchangiaji katika uboreshaji wa miundombinu ya skimu zao za umwagiliaji za kukinga maji ya mvua.

Sera katika kifungu cha 2.4.10.1 imeeleza juu ya umwagiliaji unaozingatia hifadhi ya mazingira. Madhumuni ya sera ni kuwa na mifumo ya umwagiliaji ambayo inakubalika kiuchumi na kijamii na inayojali mazingira. Ili kufanikisha madhumuni haya, pamoja na mambo

Bado maeneo mengi nchini, skimu nyingi za umwagiliaji zinatumia maji ya mito. Na hata zile chache zinazotumia umwagiliaji wa kukinga maji ya mvua bado hazijaboreshwa na zinatumia teknolojia za asili kutiririsha maji shambani jambo ambalo halileti ufanisi wa umwagiliaji kutokana na upotevu mkubwa wa maji Suala la kurejesha baada ya kutumika katika umwagiliaji bado ni tatizo kwani kwenye skimu nyinigi, mifereji ya

Msisitizo zaidi uwekwe katika umwagiliaji wa uvunaji maji ya mvua kwa kuzingatia Sheria. Jambo hili liende sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya skimu ambazo tayari zinatumia maji ya mvua yaliyokingwa ili kuongeza ufanisi wa umwagiliaji; na pia mafunzo yatolewe kwa wakulima juu ya teknolojia sahihi ya umwagiliaji wa kutumia maji ya mvua. Kuhakikisha kuwa skimu mpya zinazojengwa zizingatie uwepo wa miundombinu ya kurejesha maji kwenye mkondo yake.

33

NA. SERA MATAMKO CHANGAMOTO USHAURI mengine; sera imetamka katika kifungu cha 2.4.10.2 (i)-(ii)

i. Kuhakikisha kuwa masuala ya mazingira yanazingatiwa katika uendelezaji wa umwagiliaji kulingana na sheria ya mazingira ya mwaka 2004.

ii. Kuhakikisha kuwa mipango ya uendelezaji wa skimu za umwagiliaji unazingatia suala la kurudisha maji kwenye mkondo wake.

kurejesha maji katika mitohaijajengwa kitaalam na haisafishwi hivyo kusabahisha upotevu mkubwa wa maji. Aidha, skimu nyingine hasa zile za kiasili hazina kabisa miundombinu ya kurejesha maji katika mikondo.

Aidha, kwa skimu ambazo zipo, iwe ni sharti la lazima kuhakikisha kuwa zinapewa muda maalumu kuhakikisha kuwa zinakuwa na miundombinu sahihi ya kurejesha maji katika mikondo yake.

3. Sera ya Taifa ya Misitu ya Mwaka 1998

Sera hii katika mafungu 1-4 inalenga kuwa na usimamizi madhubuti katika maeneo ya misitu nchini kwa kuhakikisha kuwa kunakuwepo na upatikanaji endelevu wa mazao na huduma za misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho kwa kulinda misitu na mipaka yake. Aidha, sera inatamka jinsi ya kusimamia misitu ya hifadhi na mashamba ya miti.

Maeneo mengi ya misitu yamekuwa yakivamiwa kwa kutokulindwa au kusimamiwa ipasavyo.

Halmashauri nyingi za vijiji zimeshindwa kuilinda misitu ya asili dhidi ya uvamizi na uharibifu.

Sera inahitaji kuhuishwa. Maeneo yote ya misitu ya hifadhi yatambuliwe, yatangazwe na kupimwa na kuwekewa alama za mipaka zinazoonekana kwa urahisi ili kurahisisha usimamizi wake.

4. Sera ya Taifa ya Mifugo ya mwaka 2006

Sera katika Kifungu 3.23.3 inaeleza kuhusu Hifadhi ya Mazingira. Mazingira hujumuisha hewa, ardhi, maji, mimea, maisha ya binadamu na wanyama; na vipengele mbalimbali vinavyohusu uchumi, utamaduni na maisha ya jamii. Ufugaji endelevu na shughuli nyingine

Katika maeneo mengi nchini kumekuwa na tatizo la ufugaji wa kuhamahama na usiozingatia mbinu za ufugaji wa kisasa. Hali hii imesababisha uharibifu wa mazingira unaosababishwa na kuhamahama kwa mifugo, migogoro kati ya wakulima na wafugaji, uvamizi wa maeneo ya hifadhi na uharibifu wa vyanzo

Kuwepo na idadi maalum ya mifugo inayostahili kumilikiwa na kila mtu kulingana na uwezo wa ardhi ya malisho iliyopo katika eneo hilo. Yatengwe maeneo maalum ya malisho ya mifugo ili kudhibiti ufugaji huria usio na tija.

34

NA. SERA MATAMKO CHANGAMOTO USHAURI zinazohusiana nao zinahitaji matumizi sahihi na utunzaji wa mazingira. Aidha, ongezeko la mifugo na shughuli za kibinadamu zinazohusiana na uzalishaji wa mifugo katika baadhi ya maeneo nchini umesababisha matumizi makubwa ya maliasili. Hali hii imesababisha uchungaji uliokithiri, mmomonyoko wa ardhi, kutoweka kwa misitu na uharibifu wa vyanzo vya maji na mazingira. Hifadhi ya mazingira katika uzalishaji wa mifugo inaathiriwa na uelewa mdogo wa wadau, kutopewa kipaumbele katika utengaji wa maeneo ya mifugo, upungufu wa wataalamu na udhaifu katika uratibu baina ya sekta mbali mbali. Madhumuni ya sera ni kuhakikisha mazingira yanahifadhiwa kwa ajili ya ufugaji endelevu. Hivyo basi sera inatamka: (i) Serikali itaimarisha utoaji wa huduma za kitaalam juu ya masuala ya mazingira. (ii) Jitihada zitafanyika kuhimiza upangaji sahihi wa matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya uzalishaji wa mifugo. (iii) Jitihada zitafanyika kuimarisha uratibu

vya maji na ardhi oevu. Aidha, katika maeneo mengi nchini, hakuna maeneo yaliyotengwa maalumu kwa ajili ya malisho; na hii inatokana na kutokuwepo kwa Mipango ya Matumizi ya Ardhi katika vijiji vingi nchini.

Vianzishwe viwanda vikubwa, vya kati na vidogo kwa ajili ya kuongezea thamani mazao ya kilimo kwa ajili ya lishe ya mifugo. Aidha, Serikali iondoe kodi kwenye vyakula vya mifugo. Vianzishwe viwanda vikubwa, vya kati na vidogo kwa ajili ya kuongezea thamani mazao ya mifugo kwa ajili kuongeza upatikanaji wa masoko Kuwepo kwa soko la uhakika kwa ajili ya bidhaa za mifugo. Uandaliwe utaratibu wa kutoza kodi mifugo ili mapato hayo yachangie uboreshaji wa sekta mifugo hususan miundombinu na nyanda za malisho pamoja na udhibiti wa uhamishaji wa mifugo kutoka eneo moja hadi jingine Msisitizo uendelee kuwekwa hasa katika kutoa elimu ya ufugaji bora kwa wafugaji.

35

NA. SERA MATAMKO CHANGAMOTO USHAURI baina ya sekta mbali mbali kuhusu masuala ya mazingira.

Aidha, katika kifungu cha 3.7, sera inaeleza kuhusu uwiano wa mifugo na malisho, Sera inaeleza kuwa mojawapo ya kanuni muhimu za ufugaji endelevu ni kuzingatia uwiano wa mifugo na malisho. Hata hivyo, mila na desturi kwa baadhi ya wafugaji ni kuwa na idadi kubwa ya mifugo kama ufahari na uhakika wa kuendelea kuwa na akiba ya mifugo. Hali hii husababisha kuwa na mifugo mingi kuliko uwezo wa ardhi na malisho. Sababu ya pili ya kufuga bila kuzingatia uwiano huu ni uhamaji unaofanywa na wafugaji kutoka sehemu moja hadi nyingine kutokana na ukame wa mara kwa mara. Aidha, upanuzi wa kilimo na shughuli za wanyamapori, kuwepo kwa mbung’o, pia huchangia kupungua kwa maeneo ya malisho. Aidha, Uwiano wa mifugo na malisho unaathiriwa na utumiaji mdogo wa mbinu bora za ufugaji, malisho ya asili duni, ukosefu wa ujasiriamali, ukosefu wa mfumo wa utoaji tahadhari ya majanga, sehemu chache za kunywea maji, tija ndogo ya mifugo ya asili, ukosefu wa

36

NA. SERA MATAMKO CHANGAMOTO USHAURI vitega uchumi mbadala sehemu za vijijini na uhaba wa miundombinu ya masoko.

Madhumuni ya sera ni kuhimiza ufugaji unaozingatia uwiano wa mifugo na malisho kwa ajili ya uzalishaji endelevu. Katika kutekeleza haya, sera inatamka:

(i) Serikali kwa kushirikiana na wadau, itahimiza ufugaji kulingana na uwezo wa ardhi na malisho. (ii) Jitihada zitafanyika kuhimiza uboreshaji wa nyanda za malisho. (iii) Serikali itaimarisha utoaji huduma za kitaalam kuhusu uwiano wa mifugo na malisho. (iv) Serikali kwa kushirikiana na wadau, itahimiza uendelezaji wa vyanzo vya maji kwa mifugo. (v) Serikali itahimiza uboreshaji wa kosaafu za mifugo ya asili. (vi) Serikali itaimarisha ufuatiliaji na udhibiti katika kuhamisha mifugo. i. Serikali kwa kushirikiana na wadau,

itahimiza ufugaji kulingana na uwezo wa ardhi na malisho;

ii. Jitihada zitafanyika kuhimiza

37

NA. SERA MATAMKO CHANGAMOTO USHAURI uboreshaji wa nyanda za malisho;

iii. Serikali itaimarisha utoaji huduma za kitaalamu kuhusu uwiano wa mifugo na malisho;

iv. Serikali kwa kushirikiana na wadau, itahimiza uendelezaji wa vyanzo vya maji kwa mifugo;

v. Serikali itahimiza uboreshaji wa kosaafu za mifugo ya asili;

vi. Serikali itaimarisha ufuatiliaji na udhibiti katika kuhamisha mifugo.

5

Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 1997

Sera katika Kifungu cha 46 inaeleza juu ya Kilimo. Lengo la sera katika kifungu hiki ni kuhakikisha usalama wa chakula na kuondoa umaskini vijijini kwa kuhamasisha mifumo ya uzalishaji, teknolojia na mbinu rafiki kwa mazingira. Sera imeeleza malengo mahususi yafuatayo: i. Kuboresha hifadhi ya ardhi kwa

kudhibiti mmomonyoko wa udongo na kuboresha rutuba ya udongo;

ii. Kupanua wigo wa uzalishaji wa mazao ya kilimo;

iii. Kupunguza uvamizi wa ardhi ya umma ikiwa ni pamoja na misitu, nyika, ardhi oevu na malisho;

iv. Kuimarisha matumizi, ufuatiliaji, usajili

Kilimo katika vyanzo vya maji kimeendelea kuathiri hifadhi ya mazingira na kusababisha upungufu wa maji katika mito. Aidha, kilimo katika miinuko na vilima kimeendelea kusababisha uharibifu wa mazingira hasa kwa kusababisha mmonyoko wa ardhi unaosababisha mito na vijito kujaa michanga.

Sera ihuishwe ili kuzingatia haja ya usimamizi wa mazingira kulingana na fursa na changamoto za sasa na baadaye. Usimamizi wa sheria zinazohusiana na hifadhi ya mazingira usisitizwe na uweke utaratibu wa kuwahusisha wadau katika utekelezaji wake katika ngazi zote. Uratibu katika utoaji wa huduma za kitaalamu za mazingira kwa ngazi zote uimarishwe. Msisitizo uwekwe katika utoaji wa elimu ya mazingira katika jamii na ngazi zote

38

NA. SERA MATAMKO CHANGAMOTO USHAURI na usimamizi wa kemikali za kilimo kwenye maji yaliyopo juu na chini ya ardhi;

v. Kuhamasisha kilimo mchanganyiko ili kuinua mifumo ya kibaolojia katika mashamba kupitia kilimo mseto na mazao mchanganyiko, kilimo mzunguko na kilimo cha mazao ya misitu;

vi. Kuongeza ufanisi wa umwagiliaji ikiwa ni pamoja na kuzuia kutuama kwa maji na maji kuwa na chumvi;

vii. Kupanua wigo wa Programuu za uhifadhi wa Vinasaba vya asili vya mimea; na

viii. Kuhamasisha njia shirikishi kupitia mipango ya matumizi ya ardhi na usimamizi.

Sera katika Kifungu cha 47 inaeleza ukuzaji wa sekta ya mifugo nchini kwa kuzingatia hifadhi ya mazingira. Pamoja na mambo mengine, sera inalenga kuweka mifumo ya utatuzi wa migogoro miongoni mwa maslahi mbalimbali ya ardhi kama vile uhifadhi wa wanyamapori, misitu, ufugaji na kilimo.

za elimu.

39

NA. SERA MATAMKO CHANGAMOTO USHAURI Aidha sera inalenga pia kurejesha na kulinda ardhi ya malisho na kuhamasisha malisho ya mzunguko, usimamizi na udhibiti wa uhamaji wa mifugo. Katika Kifungu cha 48, sera imeeleza pamoja na mambo mengine ni kupanga na kutekeleza Programuu za raslimali za maji na Programuu nyingine za maendeleo kwa njia shirikishi kwa lengo la kulinda vyanzo vya maji na uoto wa asili . Aidha, sera ina lengo la kuboresha usimamizi na hifadhi ya ardhi oevu.

40

NA. SERA MATAMKO CHANGAMOTO USHAURI 6 Sera ya Maji ya

Mwaka 2002 i.Kuweka utaratibu wa haki ya kuyafikia maji na ugawaji wa rasilimali ii.kuhakikisha kuwa shughuli za huduma za jamii na sekta za uzalishaji, na mazingira zinapata mgao wake kulingana na mahitaji. iii.Kuhakikisha kuwa maji yanatumika kikamilifu na kwa mahitaji. iv.Kuweka msukumo katika usimamizi wa ubora na hifadhi za rasilimali za maji. v.kuboresha usimamizi na hifadhi ya mifumo ya ikolojia na maeneo oevu. vi.Kuweka msukumo katika kupanga na kusimamia raslimali za maji kwa pamoja

Vii.Kuhamasisha wananchi na kupanua wigo wa ushirikishaji wa wadau katika kupanga na kuendeleza rasilimali za maji.

vii.Kuhakikisha kuwa vyombo vya kusimamia maji kimabonde vinatekeleza majukumu yake na panakuwepo uhuru wa kufanya maamuzi yake na kujiendesha vyenyewe kimapato

ix.Kuendeleza ushirikiano wa kimataifa katika kupanga na kusimamia rasilimali za maji

X.Kuweka msingi wa kuandaa mfumo wa usimamizi wakitaasisi na kisheria kwa ajili ya rasilimali zamaji.

Bado katika maeneo mengi nchini kuna matumizi ya raslimali za maji yasiyoendelevu. Hii ni pamoja na matumizi ya maji yasiyo na vibali, matumizi ya maji yasiyoendana na kiasi halisi cha maji kinachohitajika kwa matumizi husika.

Sera ya Maji 2002 ihuishwe; Taasisi, mamlaka na wadau wanaosimamia raslimali za maji wajengewe uwezo kwa kupewa raslimali watu, uwezeshaji na vitendea kazi; Msisitizo uwekwe katika usimamizi wa sheria za raslimali za maji. Vyombo vya kusimamia maji viangalie raslimali maji kwa upana wake ikiwemo usimamizi wa matumizi na mipango ya maeneo yanayopokea mvua ili maji yanayotokana na mvua hizo yaingie kwenye mzunguko wa maji (hydrological cycle) . Maeneo oevu yaainishwe na kuwekewa mipaka, na waziri mwenye dhamana ya mazingira ayakabidhi kwa mamlaka itakayohusika kwa ajili ya kuyalinda. Iundwe mamlaka ya kudhibiti matumizi ya maji kwa kuwa mfumo wa kiasasi wa sasa unaruhusu mgongano wa kimaslahi kati ya watumiaji maji kutoweza kujidhibiti wenyewe.

41

NA. SERA MATAMKO CHANGAMOTO USHAURI 7. Sera ya Taifa ya

Umwagiliaji ya Mwaka 2010

i. Kuongeza kasi ya sekta ya umma na sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya umwagiliaji;

ii. Kuhakikisha kuwa mfuko wa kuendelza umwagiliaji unaanzishwa;

iii. Kuhamasisha matumizi bora ya maji katika mifumo ya umwagiliaji;

iv. Kuzingatia usimamizi wa pamoja wa rasilimali za maji katika uendelezaji wa umwagiliaji;

v. Uendelezaji na umwagiliaji unakidhi matakwa ya kitaalamu, kiuchumi, kijamii na ambao ni endelevu kimazingira;

vi. Kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa uwiano sahihi katika matumizi yake kwa lengo la kuwa na tija na utaratibu mpana katika uzalishaji wa mazao ya kilimo pamoja na malisho ya mifugo na kilimo cha majini na

vii. Kuwajengea uwezo wafaidika katika ngazi zote ili waweze kushiriki kikamilifu katika kupanga, kutekeleza na kusimamia ipasavyo mifumo ya umwagiliaji.

Pamoja na sera kuwa na madhumuni mazuri kama yalivyoainishwa, kiwango cha utekelezaji wa madhumuni hayo bado ni mdogo kutokana na uwekezaji mdogo kwenye miundombinu ya umwagiliaji. Mfuko wa Kuendeleza Umwagiliaji – pamoja na kwamba umeanzishwa kisheria lakini bado haujaanza kufanya kazi.

Kuhuisha sera Wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na Wizara ya Fedha na Mipango ziharakishe taratibu za kuhakikisha Mfuko huo unafanya kazi. Aidha, vyanzo vya uhakika vya fedha vianishwe ili kuhakikisha Mfuko huo unakua endelevu. Kwa kuwa rasilimali maji ni muhimu sana, utaratibu wa kutoza kiasi cha maji kinachotumika uwekwe ili kushawishi wakulima kutumia teknolojia za kutumia maji kidogo na kuyaachia mengine yaendelee kutumika kwa ajili ya watumiaji wa uwanda wa maji.

42

Jedwali Na.3: Sheria

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI 1. Sheria ya Utwaaji

Ardhi, Na. 47/1967

Sheria hii katika Kifungu cha 3 inaweka bayana kuwa ardhi ni mali ya umma ambayo iko chini ya udhamini wa Rais. Wananchi wamepewa haki ya kumiliki, kukalia na kutumia ardhi kwa matumizi mbalimbali pale watakapopewa umiliki. Aidha, pale ambapo ardhi hiyo itahitajika kwa ajili ya matumizi ya umma, kifungu cha 10-14 vinatoa utaratibu wa kuitwaa na kulipa fidia kwa wananchi wanaokalia na kutumia ardhi hiyo.

Baadhi ya wananchi katika baadhi ya maeneno ya nchi wamekuwa wakitwaa ardhí na kujimilikisha pasipo kupewa na mamlaka zinazohusika katika ugawaji wa ardhí. Utwaaji huo holela umepelekea kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya watumiaji mbalimbali wa ardhi.

Sheria hii inapaswa kuzingatiwa katika kuondoa migogoro ya ardhi, hivyo, mamlaka zilizopewa jukumu la kusimamia ugawaji wa ardhi zinapaswa kuzingatia jukumu hilo.

2. Sheria ya Ardhi, Na.04/1999

Sheria inaainisha usimamizi wa ardhi isipokuwa ardhi ya kijiji pamoja na utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Kifungu cha 4(1) kinaweka bayana

Sheria haijatekelezwa kutokana na uwezo mdogo wa mamlaka zilizopewa jukumu la kusimamia sheria za ardhi.

Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Fedha zishirikiane kubuni utaratibu wa kupatikana fedha ili

43

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI kuwa ardhi yote ya Tanzania ni mali ya umma na kuwa Rais ndiye mwenye kushika dhamana ya ardhi.

Kifungu cha 4(4) kimegawa ardhi katika aina tatu ambazo ni ardhi ya kijiji, ardhi ya jumla na ardhi ya hifadhi. Kifungu cha 21(1) kinazitaka mamlaka za halmashauri za wilaya na miji kuwa na mpango wa matumizi ya Ardhi mpango ambao utakuwa na skimu ya ukomo wa ardhi katika maeneo yao. Kifungu cha 6(1) kimeanisha ardhi ya hifadhi inajumuisha ardhi kama ilivyotajwa katika sheria za:- Misitu(Sura ya 323), Hifadhi za Taifa (Sura ya 282), Wanyamapori (Sura ya 283), na Utwaaji wa Ardhi (Sura ya 118). Pia, maeneo ambayo yako ndani ya

Viongozi wa kisiasa kuingilia utekelezaji wa sheria. Kukosekana kwa rasilimali fedha kwa ajili ya kuwawezesha wasimamizi wa sheria kuweza kufika maeneo muhimu ya nchi kwa ajili ya kutekeleza sheria

kuwezesha usimamizi na utekelezaji wa sheria. Fedha hizo ziwekewe utaratibu wa fedha inayolindwa (ring-fenced)

44

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI mfumo wa asili wa mabonde ya maji.

3. Sheria ya Ardhi ya Vijiji, Na.05/ 1999

Sheria inasimamia utawala na usimamizi wa ardhi ya vijiji. Kifungu cha 3(1) (a) kinaweka wazi kuwa ardhi yote ya Tanzania ni ya umma na kuwa Rais ndiye mwenye kushika dhamana ya ardhi. Mabadiliko ya matumizi ya ardhi ya kijiji kuwa ya hifadhi au ya kawaida ni budi yapate ridhaa ya Rais. Kifungu cha 9(1) kinaipa Halmashauri ya Wilaya jukumu la kusimamia vijiji vilivyo chini yake katika masuala ya ardhi. Kifungu cha 75 kinaweka hitaji la kuwa ukomo wa ardhi ya kumiliki na matumizi.

Sheria haijatekelezwa ipasavyo kwani kumekuwa na utwaaji na ugawaji holela wa ardhi hususan vijijini. Aidha, vijiji vingi havijaweka ukomo wa ardhi inayopasa kumilikiwa na kila mtu na kwa kila shughuli ya kiuchumi. Halmashauri za wilaya hazitekelezi jukumu lake la kusimamia mipango ya ardhi ya vijiji kama ilivyoanishwa katika Kifungu cha 9(1) cha sheria hii hivyo kusababisha uholela wa mipango na matumizi ya ardhi ya vijiji.

Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Fedha zishirikiane kubuni utaratibu wa kupatikana fedha ili kuwezesha usimamizi na utekelezaji wa sheria.

4. Sheria za Serikali Kifungu cha 30(2) cha Sheria ya Taratibu na vigezo Uanzishwaji wa mamlaka

45

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 na (Mamlaka za Miji) Sura 288 toleo la 2002

Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287, na Kifungu cha 16(1) cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura 288, Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ana mamlaka ya kugawa eneo la Halmashauri ya Wilaya au la Mji katika Kata kwa idadi atakavyoona inafaa, baada ya kushauriana na Rais.

vilivyowekwa katika kuanzishwa Mamlaka za Serikali za Mitaa hazizingatiwi, hivyo kusababisha kasoro na changamoto mbalimbali kama ifuatavyo: Baadhi ya maeneo kuanzishwa bila kuzingatia vigezo, (a) Mamlaka kuanzishwa katika maeneoyasiyotakiwa ikiwemo maeneo ya hifadhi, ranchi za mifugo na maeneo hatarishi, (b) Kutozingatia Sera na Miongozo ya kisekta, ukuaji holela wa Miji (Miji Midogo, Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji).

mbali mbali za miji na vijiji uzingatie sheria na mahitaji halisi kuliko matakwa ya kisiasa. Sera na miongozo ya kisekta izingatiwe. Uanzishaji wa mamlaka za miji ushirikishe mamlaka zote zinazohusika ili kupata ushauri husika.

5. Sheria ya Misitu, Na.14/ 2002

Kifungu Na. 26 cha sheria hiyo kinatoa makatazo juu ya kufanyika kwa shughuli za binadamu ndani ya

Adhabu za faini zilizowekwa kwenye sheria hiyo ni ndogo mno,

Kuna haja ya kufanya mapitio ya sheria hii hususan katika viwango vya adhabu

46

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI misitu ya hifadhi. Aidha, vifungu vya 84-93 vinaanisha makosa mbalimbali na adhabu za kifungo kuanzia miezi sita na kisichozidi miaka miwili, au faini kuanzia shilingi 30,000 na isiyozidi shilingi 1,000,000 au vyote faini na kifungo endapo sheria itakiukwa.

hii inatoa mwanya kwa wakosaji kuendelea kutenda makosa.

zilizowekwa kwa makosa mbalimbali.

6 Sheria ya Hifadhi za Taifa, Sura ya 282

Sheria hii ilitungwa kwa ajili ya kudhibiti na kusimamia uhifadhi wa Hifadhi za Taifa.

Kifungu cha 21(1) kinadhibiti uingiaji katika Hifadhi za Taifa. Pia kinatoa adhabu ya faini isiyozidi shilingi 500,000 au kifungo kisichozidi mwaka mmoja kwa mtu binafsi na kwa kampuni au taasisi faini isiyozidi shilingi 1,000,000 endapo atakiuka sheria hii.

Kifungu cha 25(1) (d) na (e) kinadhibiti uingizaji wa mifugo,

Adhabu zilizowekwa katika sheria hii ni ndogo hivyo haziwezi kuzuia wakosaji kurudia kutenda makosa

Mapitio ya sheria yanahitaji kufanyika ili kurekebisha viwango vya adhabu zilizowekwa pamoja na mengineyo.

47

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI ukataji wa miti na kilimo ndani ya hifadhi za Taifa.

48

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI 7. Sheria ya

Usimamizi wa Mazingira, Na. 20/2004

Sheria ya Mazingira ilitungwa ili kuweka masharti ya muundo wa kisheria na kiasasi ya usimamizi endelevu wamazingira, kuweka misingi ya usimamizi, tathmini na kuchukua hadhari kuhusu madhara ya mazingira, kinga na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira, usimamizi wa taka, ubora wa viwango vya mazingira, ushirikishwaji Umma, utekelezaji sheria; kuweka misingi ya utekelezaji wa misingi ya kimataifa.

Kifungu cha 57(1) kinaweka katazo la kufanya shughuli za kibinadamu zinazoweza kuwa na madhara, ndani ya mita 60 kutoka kwenye kingo za mito, bwawa au miambo ya asili ya ziwa.

Kifungu cha 60(1) kinaagiza Mamlaka zinazotoa Vibali vya Kutumia Maji chini ya sheria husika

Miradi mingi ikiwemo ya kilimo cha umwagiliaji haijafanyiwa tathmini ya athari kwa mazingira kabla ya uanzishwaji wake.

Aidha, miradi hiyo haina vibali vya matumizi ya maji.

Pia kuna baadhi ya miradi hiyo haijawekewa miundombinu inayowezesha kurudishwa kwa maji toka katika vyanzo vyake baada ya kutumika. Vilevile miradi mingine ya umwagiliaji pamoja na shughuli nyingine za kibinadamu zimeanzishwa ndani ya eneo la mita 60 ambalo kisheria limekatazwa.

Kuwekwa mkazo katika usimamizi wa sheria. Baraza la Mazingira liwezeshwe kwa kupatiwa watumishi wa kutosha ili liweze kufanya kazi zake za usimamizi wa mazingira katika ngazi zote. Kuwepo na ushirikishwaji wa umma katika masuala ya uhifadhi wa mazingira. Elimu itolewe kwa ajili ya uhifadhi kwenye ngazi zote.

49

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI zinazotawala usimamizi wa rasilimali maji, kuwataka waombaji kutoa tamko la kuhusu uwezekano wa athari kwa Mazingira zitakazotokana na matumizi ya maji yaliyoombwa.

Aidha, Kifungu cha 60(2)(a)na(b) kinaweka wajibu kwa mtumiaji kurejesha maji kwenye chanzo yalikochukuliwa baada ya kuyatumia na yakiwa hayajachafuliwa.

Pia Kifungu cha 60(3) kinaelekeza vibali vya maji vianishe masharti ya wajibu kwa muombaji kurudisha maji kutoka kwenye chanzo yalikochukuliwa baada ya kuyatumia; aidha, mtumiaji kuhakikisha atarejesha maji yakiwa safi na kuhakisha hatasababisha mrundikano wa takataka zozote

Ushirikishwaji Umma katika uhifadhi wa mazingira ni wa kiwango cha chini.

50

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI zitakazozuia maji kutiririka.

Kifungu cha 81 kinaweka wajibu wa kufanya tathmini ya athari kwa mazingira kabla ya uanzishaji wa mradi, kwa miradi kadhaa ambayo imeainishwa kwenye Sheria. Miradi hio inajumuisha: Kilimo, ufugaji, misitu, mabwawa na uwekezaji unaohusisha rasilimali za maji.

Kifungu cha 196 kinaipa mamlaka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira kutoa amri ya kizuizi kwenye shughuli zenye madhara makubwa kwa mazingira.

51

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI 8. Sheria ya

Wanyamapori, Na.5/2009

Sheria hii imetungwa mahsusi kuleta maelekezo mazuri kwa ajili ya usimamizi, utunzaji na matumizi endelevu ya Wanyamapori na mazao ya Wanyamapori. Madhumuni ya sheria hii yametanabaishwa vizuri kwenye vifungu vinavyoanzisha mapori ya akiba, hifadhi ya maeneo oevu na mapori tengefu ya wanyama na kuweka vizuizi vya kuingia kwenye maeneo hayo, pia kuzuia shughuli zisizokubalika kisheria kufanyika ndani ya hifadhi ikiwemo uingizaji wa mifugo kama inavyoainishwa katika vifungu vya 14, 15, 17 na 21.

Kwa upande mwingine Kifungu cha 3 cha sheria kinadhibiti uwindaji wa wanyamapori kwa kuanzisha vibali vya uwindaji na kudhibiti silaha na uwindaji usiofuata taratibu za

Shughuli za kibinadamu kama vile ulishaji wa mifugo, uvuvi, uwindaji haramu na uvunaji wa mazao ya misitu bado zinaendelea kufanyika ndani ya mbuga za hifadhi ya wanyamapori. Mipaka ya hifadhi haijawekewa alama za kuweza kutambuliwa kiurahisi.

Mipaka ya hifadhi iwekewe alama za kudumu zinazoonekana ili kuzuia uingiaji ovyo ndani ya hifadhi kwa kigezo cha kutokuona mipaka. Wavunjaji wa sheria kwa makusudi wapewe adhabu kali.

52

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI uwindaji.

9. Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji, Na.11/2009

Sheria hii imeanzishwa kwa madhumuni yafuatayo:-

Kuweka utaratibu wa haki ya kuyafikia maji kama hitaji la msingi,

Vyanzo vingi vya maji havijatambuliwa, havijawekewa alama zinazooneka kwa urahisi

Hatua zichukuliwe katika kuvibaini, kuorodhesha, kuviwekea alama zinazoonekana kwa urahisi na

53

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama, kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali maji, kuwezesha shughuli za kijamii, ushirikishwaji wa wadau katika ngazi zote za usimamizi wa rasilimali za maji na kuboresha usimamizi na hifadhi ya mifumo ya ikolojia na bayoanuai.

Sheria hii inaelekeza vyanzo vya Maji vitambuliwe, viwekewe alama na kusimamiwa ipasavyo.

Sheria hii ikisomwa pamoja na Kifungu cha 60 cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya 2004,kinataka kibali cha maji kuweka masharti kwa muombaji/mtumiaji wajibu wa kurudisha maji kwenye chanzo yakiwa safi.

na havina usimamizi wa kutosha. Kuna matumizi makubwa ya maji katika kilimo cha umwagiliaji ambayo hayana kibali hali inayopelekea kuwa na matumizi mabaya yasiyo endelevu ya maji. Sheria inatoa viwango vidogo vya adhabu.

kuvisimamia ipasavyo vyanzo vya maji kama sheria inavyoelekeza. Hatua hizo ziende sambamba na maboresho ya usimamizi wa jumla wa hifadhi za ikolojia na bayoanuai.

Viwango vya adhabu viongezwe ili kwenda na hali halisi.

54

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI 10. Sheria ya

Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo, Na.12/ 2010.

Kuwepo kwa Mfumo wa Kitaifa wa utambuzi wa mifugo na wafugaji. Kuwepo kwa mfumo wa kitaifa wa usajili wa mifugo, wafugaji na mashamba ya mifugo. Kuwepo mfumo wa kitaifa wa kumbukumbu na udhibiti wa usafirishaji wa mifugo. Kuwepo kwa maafisa ugani kwa ajili ya utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Kuwepo kwa maeneo mahsusi kwa ajili ya usajili wa mifugo.

Hakuna ufanisi katika mfumo wa Taifa wa utambuzi na uwekaji wa kumbukumbu za mifugo, hivyo mifugo mingi haijatambuliwa na haijasajiliwa na wala haijawekewa alama za utambuzi. Sheria za skta ya mifugo zimekuwa nyingi na hivyo kuwa tatizo katika usimamizi.

Kuna haja ya kufanya marekebisho ya sheria. Masuala yote ya mifugo na mtambuka yaanishwe katika sheria. Kanzidata ya mifugo nchini ianzishwe kwa kuhusisha ngazi zote inayohuishwa mara kwa mara. Ipo haja ya kurazinisha sheria za mifugo.

11. Sheria ya Maeneo ya Malisho na Vyakula vya Mifugo, Na.13/2010

Kuanisha ardhi ya malisho ya mifugo katika mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji. Waziri mwenye dhamana ya Mifugo kuteua mkaguzi atakayesimamia

Hakuna kifungu kinachotoa jukumu lolote kwa wafugaji kutunza ardhi ya malisho. Muda wa ukomo kwa

Sheria iweke wajibu kwa wafugaji kutunza maeneo ya malisho. Muda wa ukomo kwa wafugaji kuhamisha mifugo iliyozidi

55

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI uendelezaji wa maeneo ya malisho. Mkaguzi ana mamlaka ya kutoa muda wa miaka mitatu kwa wafugaji ili kuondoa mifugo iliyozidi katika eneo la malisho.

wafugaji kuhamisha mifugo iliyozidi ni mrefu mno.

ufanyiwe marejeo.

12. Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji Na.5/2013

Sheria hii imeanzishwa mahsusi kwa ajili ya kuanzisha Tume ya Taifa ya Umwagiliji, kuleta maendeleo, utendaji, urekebishaji wa mifumo ya umwagiliaji na kuweka utekelezaji madhubuti wa Sera ya Taifa ya Umwagiliaji na Mpango wa Taifa wa Umwagiliaji.

Kifungu cha 20 kinaweka utaratibu wa kujenga miundombinu ya umwagiliaji, utaratibu ambao unataka tathmini ya athari za mazingira ufanywe kabla ya kuomba leseni ya kujenga miundombinu ya umwagiliaji.

Kumekuwa na ujenzi holela wa miundombinu ya maji, pia kumekuwepo na uanzishwaji wa miradi ya umwagiliaji pasipo kufanya tathmini ya athari za mazingira. Kumekuwa na matumizi holela ya maji pasipo kuwa na vibali vya matumizi. Kumekuwa na matumizi ya maji yanayozidi viwango vilivyowekwa katika vibali.

Kunahitajika kuwa na mfumo thabiti wa kufuatilia uanzishwaji na usimamizi wa miradi ya umwagiliaji. Wadau wapatiwe elimu ya sheria ili waweze kufahamu na kutekeleza matakwa yake.

56

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI Kanuni ya 50 ya Kanuni za Taifa za Umwagiliaji, 2015 za sheria hii, inatambua umuhimu wa rasilimali maji katika shughuli za umwagiliaji hivyo inahamasisha kutekeleza mpango wa maendeleo wa rasilimali za maji katika maeneo ambayo tayari kuna mifumo ya umwagiliaji na maeneo yanayotarajiwa kujengwa mifumo hiyo na pia kuvitambua na kuviwekea mipaka vyanzo vya maji kwa ajili ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali. Hakuna maombi ya skimu yanayoweza kupata kibali cha ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji bila ya kuwa na kibali cha maji.

Kanuni ya 53 (2) inasisitiza matumizi ya maji kwa ajili ya umwagiliaji yafuate masharti yaliyoainishwa kwenye Kibali cha Maji.

57

NA. SHERIA MATAKWA CHANGAMOTO USHAURI Kanuni ya 28 ya Kanuni za Taifa za Umwagiliaji, 2015 zinamtaka Mkaguzi wa Umwagiliaji anapoona Skimu haina kipimo cha kupima maji yanayotoka kwenye Skimu ahahakikishe anaweka vipimo hivyo. Kifungu cha 38 kinampatia Mkurugenzi wa Tume ya Umwagiliaji mamlaka ya kutwaa miundombinu ya umwagiliaji kwa ajili ya matengenezo na usimamizi.

58

Katika kuzichambua Sera na Sheria mbalimbali zinazohusiana na usimamizi wa uhifadhi wa mazingira, imebainika kuwa kuna baadhi ya Sera na Sheria ambazo zinahitaji kuhuishwa ili kuendana na mazingira na mahitaji ya sasa kwani baadhi ya Sera na Sheria hizo ni za muda mrefu, na mahitaji na mazingira yaliyokuwepo wakati sheria hizo zinatungwa yamebadilika na hivyo sera na sheria hizo hazikidhi mahitaji ya sasa ya jamii. Aidha, upo umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa wadau wote ili wawe na uelewa mpana zaidi ya ilivyo sasa juu ya umuhimu wa mchango wao katika utunzaji wa mazingira.

3.4.1 Uchambuzi wa Miradi na Tafiti Mbalimbali zilizofanyika katika Eneo la Bonde la Mto Ruaha Mkuu

3.4.1.1 Mradi wa Usimamizi wa Mabonde ya Mito na Uboreshaji wa Umwagiliaji (RBMSIIP): 1996–2003

Mradi huu ulikuwa na lengo la kuimarisha uwezo wa Serikali katika kusimamia Rasilimali za Maji na kuelekeza rasilimali fedha na nyinginezo kwa ajili ya kuhifadhi mazingira katika ngazi ya kitaifa na mabonde na kuongeza ufanisi katika skimu Umwagiliaji. Mradi uliboresha skimu 7 katika wilaya za Mbarali na Iringa pamoja na uanzishaji wa taasisi za usimamizi wa rasilimali za maji. Aidha, Mradi huu ulisaidia uanzishaji wa Jumuiya za Watumia Maji na timu za wawezeshaji za Wilaya.

Maoni ya Kikosi Kazi Pamoja na juhudi hizo mradi haukuweza kufikia malengo yake kutokana walengwa na eneo la mradi kuwa dogo ukilinganisha na mahitaji halisi ya Bonde. Hivyo inapendekezwa kuwa miradi ya usimamizi wa mabonde ilenge kuwafikia wamwagiliaji walio wengi ili kumaliza tatizo lililopo. Pia, Serikali iweke taratibu za kuhakikisha matokeo ya miradi yanakuwa endelevu hata baada ya kukamilika kwa miradi husika.

3.4.1.2 Usimamizi Endelevu wa Ardhi Oevu ya Usangu na Vyanzo Vyake (SMUWC): 1998–2001

Mradi huu ulihusu utafiti juu ya Usimamizi Endelevu wa Ardhi Oevu ya Bonde la Usangu na maeneo yanayolizunguka. Utafiti huu ulifanywa na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha East Anglia, Uingereza, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID). Matokeo ya utafiti yalionesha kwamba tatizo la upungufu wa maji katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu haukutokana na uharibifu

59

wa mazingira wala mabadiliko ya tabianchi bali ulisababishwa na matumizi makubwa ya maji katika kilimo cha umwagiliaji. Utafiti pia ulionesha kuwa uwezo wa ardhi kuhimili (Carrying Capacity) idadi ya mifugo iliyokuwepo wakati ule ulikuwa umefikia ukomo. Hali hii ilisababisha kupungua kwa maji na ukubwa wa eneo la ardhi oevu la Usangu na hivyo kuathiri mtiririko wa maji wa Mto Ruaha Mkuu. Utafiti ulipendekeza kuongeza ufanisi katika Umwagiliaji kwa kuboresha miundombinu ya umwagiliaji na kuondoa mifugo katika eneo la Usangu.

Maoni ya Kikosi Kazi

Tathmini ya kikosi kazi kuhusu mradi huu na utafiti husika inakubaliana na sababu ya matumizi makubwa ya maji ya Mto Ruaha Mkuu kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta upungufu wa maji. Hata hivyo mradi ulishindwa kubaini sababu nyingine ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa maji katika Mto Ruaha Mkuu zikiwemo: kilimo kisichozingatia kanuni za kilimo endelevu, ufugaji usiozingatia kanuni za ufugaji endelevu, uharibifu wa uoto wa asili kutokana na upandaji miti kibiashara, uchomaji wa mkaa, uchimbaji madini, uchomaji moto holela na mabadiliko ya tabianchi. Hivyo, inapendekezwa Serikali ishirikiane na wadau katika kufanya tafiti za kina zitakazoweza kubaini, kupimana kutoa mapendekezo stahiki yatakayowezesha kutoa suluhisho la kudumu la kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu.

3.4.1.3 WWF Awamu ya Kwanza (2003 – 2010) na Awamu ya Pili (2011-2016)

WWF ilitekeleza Programuu ya Maji katika Bonde Ruaha Mkuu ambayo ililenga kurejesha mtiririko wa maji kwa mwaka mzima katika Mto Ruaha Mkuu. Mradi ulisaidia uanzishwaji wa jumuiya za watumia maji ambapo jumla ya jumuiya za watumia maji 10 zilianzishwa na timu 11 za uwezeshaji katika ngazi ya Wilaya, hususan zilizoko katika eneo bonde la Mto Ruaha Mkuu ziliundwa. Mradi pia ulisaidia kujenga uelewa wa wananchi juu ya usimamizi wa pamoja wa rasilimali za maji. Maoni ya Kikosi Kazi Tathmini ya Kikosi Kazi imeonesha kwamba mradi (awamu ya kwanza na pili) husika ulifanikiwa kuanzisha jumuiya za watumia maji katika wilaya husika pamoja na kujenga uelewa kwa viongozi na wananchi wa namna ya kusimamia rasilimali za maji. Hata hivyo, utaratibu wa kutoa elimu pekee bila kusaidia ujenzi wa miundombinu ulichangia mradi kutofikia malengo yake. Kwa msingi

60

huu inapendekezwa miradi ya namna hiyo kuhusisha kusaidia ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na mifugo katika eneo la Bonde.

3.4.1.4 Programu ya Uendelezaji wa Sekta ya Maji –Awamu ya Kwanza WSDP I (2007-2014) na Awamu ya Pili II (2014-2019)

Programu ya Uendelezaji wa Sekta ya Maji (Awamu ya Kwanza na ya Pili) ililenga mambo kadhaa ikiwemo usimamizi wa Rasilimali za maji kwa kuimarisha taasisi husika kama vile Bodi za maji za mabonde, Kamati za Maji za Vidakio (Catchment Committees) na Jumuiya za Watumia Maji. Pia ilihusisha uandaaji wa Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Rasilimali za maji. Progamu ilisaidia kuimarisha Bodi ya Maji Bonde la Rufiji kwa kuipatia watumishi na vitendea kazi, ujenzi wa vituo vya kukusanya takwimu za maji mtoni na hali ya hewa. Aidha, Awamu ya Pili ya Programu inayoendelea imelenga katika kuendeleza malengo yaliyoainishwa katika Awamu ya Kwanza. Maoni ya Kikosi Kazi Kazi ya kuimarisha Bodi ya Maji imesaidia katika kuiwezesha Bodi kumudu majukumu yake ya kusimamia rasilimali za maji ndani ya bonde. Hata hivyo, uundaji wa taasisi za kusimamia rasilimali za maji bado haujakamilika. Wakati huo huo kazi ya kujenga uwezo wa taasisi hizo haijakamilika kama ilivyokusudiwa. Hivyo, inapendekezwa kuwa Programu hii imalize kazi ya kujenga uwezo wa taasisi husika ikiwa ni pamoja na kuangalia maeneo ya kipaumbele ya sasa ikiwemo ujenzi wa miundombinu inayosaidia kuleta matumizi endelevu ya maji katika bonde. Pia inapendekezwa kuwa Serikali iangalie kwa mapana zaidi changamoto zilizopo katika bonde hilo, kwa kuweka mfumo mpana utakaowashirikisha wadau wote katika kugharamia na kutekelezashughuli za uhifadhi wa ikolojia ya Bonde.

3.4.1.5 Kuweka Mipaka kwenye Vyanzo vya Maji na Kufukua Mito Iliyopoteza Mikondo yake ya Asili (2013-2016)

Mradi huu ulilenga katika kurejesha hali ya mtiririko wa maji katika mito inayochangia maji katika Mto Ruaha Mkuu. Mradi huu ulitekelezwa na Bodi ya Maji Bonde la Rufiji kwa kushirikiana na wadau kwa lengo la kuhifadhi vyanzo vya maji na kurejesha mtiririko wa maji katika baadhi ya mito iliyopoteza mikondo yake ya asili. Utekelezaji wa mradi huu umesaidia kurejesha mtiririko wa maji katika baadhi ya mito kama Ndembela, Kioga, Mswiswi na Mkoji iliyokuwa imepoteza mikondo yake. Juhudi hizo ziliweza kuweka mipaka katika

61

baadhi ya vyanzo kwenye Bonde la Mto Ruaha Mkuu.

Maoni na Mapendekezo ya Kikosi Kazi Utekelezaji wa mradi huu haukukamilisha kazi iliyokuwa imekusudiwa hivyo kuacha idadi kubwa ya mito ikiendelea kupoteza maji nje ya mikondo yake. Hivyo, inapendekezwa Serikali ikamilishe kazi ya kurudisha mikondo ya mito. Ili kudhibiti michanga inayoingia katika mito husika ni muhimu shughuli za kilimo na ufugaji kwenye vyanzo vya maji na mito husika zidhibitiwe kikamilifu. Ili kutekeleza mapendekezo haya, taasisi na wizara za kisekta, Bodi ya Bonde la Rufiji, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na wadau wengine kama vile wadau wa maendeleo, Asasi Zisizo za Kiserikali, Sekta Binafsi na watumia maji zihusishwe kikamilifu katika utatuzi wa tatizo hilo.

3.4.1.6 Mradi wa Hifadhi ya Mazingira (HIMA), Iringa na Njombe 1990-2002 Mradi huu ulilenga kuhifadhi mazingira kwa ujumla katika mikoa ya Iringa na Njombe (kwa sasa) kwa ufadhili wa Serikali ya Denmark. Mradi ulifanikiwa katika utoaji elimu kwa wananchi juu ya Hifadhi ya mazingira na vyanzo vya maji, uanzishaji wa vitalu vya miti, upandaji miti, kilimo hifadhi (makinga maji na matumizi ya mbolea ya samadi), matunda na mbogamboga, uhifadhi wa misitu ya asili ya vijiji kwa njia shirikishi jamii (CBFM, JFM), ufugaji wa samaki kwenye mabwawa, ufugaji bora wa mifugo kama mbuzi wa maziwa, ng’ombe wa kisasa na wanyama wadogo mfano sungura. Pia mradi ulifanikiwa kuazisha misitu ya hifadhi ya vijiji ambayo ni vyanzo vya maji mfano misitu ya Udzungwa na West Kilombero ambayo kwa sasa ni Hifadhi Asilia (Forest Nature Reserves). Vilevile, mradi uliweza kuanzisha misitu hifadhi yenye vyanzo vya maji vinavyopeleka maji yake Mto Ruaha Mkuu katika tarafa za Wanging’ombe, Matamba, na Mdandu katika Wilaya ya Njombe kwa wakati huo.

Maoni na Mapendekezo ya Kikosi Kazi

Mradi wa HIMA ulifanikiwa kuleta uhifadhi katika maeneo yaliyokusudiwa kwa kuongeza hali ya uhifadhi na kuboresha ikolojia ya maeneo husika. Hata hivyo tatizo kubwa lilibaki katika kuendeleza mafanikio yake kwa wananchi baada ya Programu kufikia ukomo. Hali hii imesababisha jitihada zilizofikiwa kutoendelezwa na baadhi ya maeneo kupoteza hadhi ya uhifadhi iliyokuwa

62

imefikiwa na Programu.

Kwa upande mwingine Programu ya HIMA ilihamasisha kilimo cha miti ya biashara kwa wakulima ambayo imesababisha idadi kubwa ya wakulima kuacha shughuli za kilimo cha mazao mengine na kubakia katika kilimo cha miti kinachochukua sehemu kubwa ya ardhi. Hali hii imesababisha kuongezeka kwa mahitaji ya ardhi kwa ajili ya kilimo cha miti ya biashara kuelekezwa katika maeneo ya vyanzo vya maji, maeneo ya hifadhi na maeneo yaliyotengwa kwa kilimo na ufugaji. Hivyo, inapendekezwa, Serikali kuendelea kutekeleza mafanikio ya Mradi wa HIMA kwa kuziwezesha Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwawezesha wananchi kupanda miti ya asili, na kutumia kanuni endelevu za kilimo na ufugaji. Pamoja na kupunguza miti ya kibiashara ikiwa ni pamoja na kuing’oa ile iliyopandwa katika maeneo ya vyanzo vya maji.

3.4.1.7 Mradi wa Matumizi Endelevu ya Maliasili (MEMA) 2001-2003

Mradi huu ulitekelezwa katika maeneo ya Kilolo na Iringa Vijijini kwa ufadhili wa Serikali ya Denmark (DANIDA) ukiwa na lengo la kuendeleza uhifadhi wa misitu ya Miombo na vyanzo vya maji. Mafanikio ya mradi huu ni kuanzishwa kwa misitu ya hifadhi ya Kitapilimwa na Nyang’oro (Iringa Vijijini) ambayo ina uoto wa misitu ya Miombo. Upande wa Wilaya ya Kilolo Mradi ulifanya kazi ya kuhifadhi misitu ya New Dabaga Ulongambi, Kitemele, Kilanzi Kitunguru, Kawemba, na Udzungwa Scarp ambayo sasa ni Hifadhi Asilia ya Kilombero (Kilombero Nature Reserve).

Maoni na Mapendekezo ya Kikosi Kazi Tathmini ya Kikosi Kazi inaonesha kuwa Mradi wa MEMA ulifanikiwa kusaidia uhifadhi katika maeneo husika. Mradi huu ulitekelezwa katika maeneo machache hivyo kupunguza uwezo wake katika kuleta mabadiliko yanayotakiwa katika maeneo yote yenye mahitaji husika.

3.4.1.8 Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu (USM) 2004-2014

Mradi huu wa usimamizi shirikishi wa misitu (Participatory Forest Management –PFM) ulikuwa na lengo la kushirikisha jamii katika masuala yote ya kusimamia misitu katika maeneo yao. Mradi huu ulikuwa chini ya ufadhili wa Serikali ya Denmark na uliwezesha jamii kushirikiana na Serikali kuu au Halmashauri husika katika kusimamia misitu (Joint Forest Management – JFM) au jamii

63

kumiliki na kusimamia msitu yao (Community Based Forest Management – CBFM) kwa mujibu wa Sera ya Misitu ya mwaka 1998 na mwongozo wa usimamizi shirikishi wa jamii wa misitu wa mwaka 2007. Mradi ulifanikisha kuanzishwa kwa misitu ya jamii (CBFM) 61 na misitu shirikishi (JFM) 9 katika Mkoa wa Iringa na CBFM 44 na JFM 5 kwa Mkoa wa Njombe. Jitihada hizi zilitekelezwa pia katika Mkoa wa Mbeya.

Maoni na Mapendekezo ya Kikosi Kazi Pamoja na mafanikio ya kuanzishwa kwa misitu ya jamii na misitu shirikishi, mingi ya misitu hiyo ilikuwa ni ya miti ya kigeni ambayo ilipandwa katika maeneo ambayo awali yalikuwa na misitu ya asili na nyika na hivyo kusababisha mabadiliko makubwa ya aina ya uoto na kuleta aina ya miti ambayo sio rafiki kwa mazingira. Serikali kwa kushirikiana na wadau, ifanye tathmini ya kutambua kiwango cha uoto wa asili kinachohitajika (minimum requirement for maintainance of ecosystem) kulingana na ukubwa wa ardhi ya eneo husikana kuandaa mpango wa kurejesha na kuulinda uoto huo kwa kuzishirikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa katika maeneo husika. Aidha, mamlaka za serikali za mitaa kwa kushirikiana na vijiji husika waondoe mara moja miti isiyo rafiki ambayo imepandwa kupitia Programu hii katika maeneo ya vyanzo vya maji.

3.4.1.9 Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Ardhi Oevu - Sustainable Wetland Management (2006-2013)

Mradi huu ulitekelezwa katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe ukiwa na lengo la kuhifadhi maeneo yenye ardhi oevu. Mradi ulitekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Denmark. Katika Mkoa wa Njombe mradi uliweza kuhifadhi maeneo oevu tisa (9) na katika Mkoa wa Iringa maeneo matano yameanzishwa kwa ajili ya shughuli mbadala kama vile ufugaji wa nyuki na upandaji miti rafiki na maji kwa jamii zinazozunguka maeneo oevu. Mradi ulifanikiwa pia kuanzisha vikundi vya kijamii vya kusimamia maeneo ya mialo katika bwawa la Mtera na Ziwa Nyasa eneo la Manda (Beach Management Units – BMUs).

Maoni na mapendekezo ya Kikosi Kazi Kulingana na tathmini iliyofanyika, mradi huu haukufanikiwa kuwaondoa wananchi kulima katika maeneo oevu (vinyungu). Hali hii ilisababishwa na wananchi kupanda miti ya kibiashara katika maeneo ya kilimo cha mazao na

64

hivyo kukosa maeneo mbadala ya kilimo, hali iliyofanya kuongezeka kwa kilimo cha mazao ya chakula katika maeneo ya ardhi oevu. Serikali kupitia wizara na taasisi husika (Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi), Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zishirikiane na wadau wengine kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi. Aidha, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ziendelee na zoezi la kuwaondoa wakulima na wafugaji waliopo katika ardhi oevu.

3.4.1.10 Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo – ASDP I (2006-2014)

Pamoja na malengo mengine, ASDP I ililenga kuendeleza kilimo cha umwagiliaji kwa kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji na pia kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu Kilimo Shadidi cha Mpunga. Aidha, chini ya programu hiyo jumla ya skimu za umwagiliaji 34 za wakulima wadogozilitekelezwa katika wilaya za Mbarali, Iringa, Kilolo na Makete. Vilevile, mafunzo ya uendeshaji na utunzaji wa miundombinu ya skimu za umwagiliaji katika Mikoa ya Mbeya na Iringa yalitolewa.

Maoni na mapendekezo ya Kikosi Kazi

ASDP I ilifanikiwa kujenga uwezo wa mamlaka za serikali za mitaa na wakulima katika kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya umwagiliaji katika maeneo yao. Aidha, Programu hii ilikarabati miundombinu katika skimu za umwagiliaji zilizokuwa zimeharibika. Maeneo mapya ya skimu za umwagiliaji yalianishwa na kujengwa. Hata hivyo, Programu hii ilishindwa kukamilisha miradi mingi ya umwagiliaji iliyoanzishwa na hivyo kusababisha miradi hiyo kupoteza maji na kuwa na tija ndogo katika uzalishaji wa mazao na uhifadhi wa mazingira. Madhara hayo yamechangia katika kutofikiwa kwa malengo ya Programu ambapo mpaka kiasi cha eneo linalomwagiliwa ni asilimia moja (1%) ya eneo lote la Bonde la Mto Ruaha Mkuu. Pia, imebainika kwamba changamoto kubwa ya Programu hii ilikuwa ni kukosekana kwa usanifu stahiki wa miradi iliyobuniwa. Kutokana na hali hii, inapendekezwa kwamba wakati ambapo serikali ikijiandaa na utekelezaji wa Programuu ya ASDP II, mapungufu yaliyojitokeza katika ASDP I yafanyiwe kazi.

65

3.4.2 Juhudi za ziada za Serikali na wadau katika kuokoa Ikolojia ya Bonde 3.4.2.1 Udhibiti wa matumizi ya maji na ukaguzi wa miundombinu

Kila mwaka wakati wa kiangazi, Bodi ya Maji ya Bonde la Rufiji huendesha operesheni za kudhibiti matumizi ya maji yasiyokuwa na vibali. Operesheni hizo huhusisha ufungaji wa mifereji na hatua za kisheria dhidi ya wanaotumia maji kinyume na taratibu za kisheria. Maoni na Mapendekezo ya Kikosi Kazi Operesheni hizo zimesaidia kuongeza ufanisi katika kuzingatia sheria katika maeneo mengi yenye skimu za umwagiliaji. Hata hivyo, operesheni hizo hazikufanikiwa kumaliza tatizo kutokana na hali duni ya miundombinu, kutokuwepo na vifaa vya kupima viwango vya maji na uchache wa wakaguzi. Hivyo, Kikosi Kazi kinapendekeza miundombinu iboreshwe na kuzijengea uwezo wa mamlaka na bodi husika zikiwepo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira. Aidha, juhudi za kutoa elimu na kuwajengea uwezo watumia maji katika skimu ziendelezwe.

3.4.2.2 Juhudi za Kupandisha Hadhi Hifadhi ya Akiba ya Usangu na Ardhi Oevu ya Ihefu

(i) Kuanzishwa kwa Pori la Akiba la Usangu (Usangu Game Reserve) Hifadhi hiyo ilianzishwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 436a la mwaka 1998 kwa lengo la kunusuru uharibifu wa mazingira kutokana na kuongezeka kwa mifugo na kilimo holela cha umwagiliaji katika Bonde la Usangu. Juhudi hizi za Serikali hazikuweza kufanikiwa kuwaondoa wafugaji na wakulima waliokuwa wamevamia eneo hilo kwa sababu ya kukosekana kwa fedha, vitendea kazi na nguvu kazi ya watendaji wa Hifadhi ya Akiba ya Usangu. (ii) Zoezi la Kuondoa Mifugo katika Eneo la Ihefu 2006 Zoezi hili lililenga kuondoa mifugo iliyokuwa imezidi katika eneo la Ihefu na kuipeleka katika Mikoa ya Lindi na Pwani. Kulingana na takwimu za kitaalam za mwaka 2001 zilizoainishwa na Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Ardhi Oevu ya Usangu na vyanzo vya maji (SMUWC), kiasi cha mifugo iliyoondolewa ni 138,732 sawa na asilimia 37 ya mifugo yote iliyokuwepo ndani ya eneo hilo. Zoezi hili lilisaidia kwa kiwango kikubwa kurejea kwa uoto wa asili katika eneo

66

oevu la Ihefu na kuboresha mtiririko wa maji wa Mto Ruaha Mkuu kama inavyoonekana katika Kielelezo Na. 8.

Kielelezo. 8: Kurejea kwa uoto wa asili na maji katika eneo oevu la Ihefu baada ya mifugo kuondolewa (Tarehe 26 April 2017).

(iii) Kupandisha Hadhi Hifadhi ya Akiba ya Usangu na Eneo la Ardhi Oevu ya Ihefu kuwa Sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha2008

Mpango wa kupandishwa kwa hadhi Hifadhi ya Akiba ya Usangu pamoja na eneo la ardhi oevu ya Ihefu kuwa sehemu ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha ulilenga kuhifadhi mazingira ya ardhi oevu ya Usangu kwa kuzuia shughuli zote za kibinadamu katika maeneo hayo. Ombi la serikali la kupandisha hadhi maeneo haya kuwa hifadhi ya Taifa kwa kuunganishwa katika Hifadhi ya Taifa Ruaha lilipitishwa na kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya (RCC) tarehe 14/07/2006. Serikali ilikubali pendekezo la kupanua mipaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa kujumuisha Hifadhi ya Akiba ya Usangu na ardhi oevu ya Ihefu kuwa sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa Tangazo la Serikali Na. 28 la mwaka 2008. Hata hivyo, upanuzi wa mipaka ulipingwa mahakamani na wananchi wa maeneo husika na kusababisha utekelezaji wa tangazo la serikali Na 28/2008 kukwama. Aidha, baadhi ya wananchi wa Vijiji saba na Vitongoji vitatu walikubali kupokea fidia na kutoka kwenye maeneo hayo. Vijiji hivyo ni Ikoga, Upagama, Msangaji, Ukwaheri, Sololwambo, Kiwale na Idunda; na

67

vitongoji niKapunga (Kijiji cha Vikae), Taganu (Kijiji cha Ikanutwa) na Isimikwe (Kijiji cha Mapogoro).

(iv) Kikosi Kazi cha Kupitia Upya Mipaka ya Hifadhi katika Eneo Lililojumuishwa 2009

Kikosi Kazi kiliundwa na Mh. Waziri wa Maliasili na Utalii mwaka 2009 kwa lengo la kupitia mipaka katika eneo lililojumuishwa na kutoa mapendekezo kwa Waziri juu ya njia nzuri ya kutekeleza Tangazo la Serikali Na. 28 la mwaka 2008. Kikosi Kazi kilipendekeza kubadili mipaka ya hifadhi kwenye baadhi ya maeneo ili baadhi ya vijiji ambavyo awali vilionekana kuwa ndani ya hifadhi, viwe nje ya hifadhi kwa vile kwa kufanya hivyo kusingekuwa na athari kubwa kwenye malengo ya hifadhi pamoja na kuvihamisha vijiji vilivyokuwa ndani ya hifadhi.

(v) Kamati ya Waziri Mkuu 2012

Kamati hii iliundwa na Waziri Mkuu ikijumuisha wataalam kutoka Wizara za Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maji, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, TAMISEMI na Maliasili na Utalii kwa ajili ya kupitia upya tatizo la mipaka ili hatimaye kutoa mapendekezo ya ufumbuzi wa mgogoro huu. Mapendekezo ya kamati hii yalikuwa ni kuwahamisha wananchi katika eneo la ardhi oevu ili kunusuru mtiririko wa maji wa Mto Ruaha Mkuu na kutoa elimu kwa wakazi wa Mbarali juu ya umuhimu wa eneo hilo kwa uhifadhi.

Maoni na mapendekezo ya Kikosi Kazi

Jitihada hizi zililenga kuhifadhi mazingira ya Ardhi Oevu ya Usangu kwa kupandisha hadhi ya Hifadhi ya Akiba ya Usangu na eneo oevu la ihefu kuwa sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ili kuzuia uharibifu uliokuwa ukisababishwa na shughuli za binadamu katika maeneo hayo. Hata hivyo kumeendelea kuwepo na changamoto zilizosababishwa na baadhi ya wananchi kugomea zoezi hilo ambapo vijiji 36 vinahusika. Ili kumaliza mgogoro uliopo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ameunda Kikosi Kazi ambacho kimepewa jukumu la kupitia upya Tangazo la Serikali Na. 28 la mwaka 2008. Kikosi Kazi kinapendekeza Mkoa kukamilisha kazi hiyo haraka iwezekanavyo na kuwasilisha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa hatua zaidi za maamuzi.

68

3.4.3 Maagizo ya Viongozi wa Ngazi za Juu

Viongozi mbalimbali wamekuwa wakitoa maagizo kadhaa katika nyakati tofauti ili kuokoa ikolojia ya Bonde. Baadhi ya maagizo hayo ni kama ifuatavyo:-

(i) Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiwaapisha Wakuu wa Mikoa wapya wa Serikali ya Awamu ya Tano mwezi Machi 2016, aliwataka wakuu wa mikoa minne iliyo katika Mto Ruaha Mkuu washirikiane na wadau wengine kuhakikisha mtiririko wa maji katika mto huu unarejea katika kiwango chake cha kawaida;

(ii) Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliagiza Halmashuri zote nchini kuhakikisha zinachukua hatua madhubuti katika kulinda vyanzo vya maji. Waziri Mkuu alitoa maagizo haya wakati akifanya uzinduzi wa Mradi wa Maji Madaba Songea mwezi Januari 2017. Nukuu “Naomba niwasihi, na kila mmoja achukulie hii kama kauli kamili inayohitaji kusimamiwa. Kama kule kwenye vyanzo tunakata miti yote, basi haya maji yatakauka - mradi huu hautakuwa na maana na lawama zitaelekezwa kwa serikali. Usiende kulima, kupeleka mifugo wala kukata kuni kwenye vyanzo vya maji. Naziagiza Halmashauri zote kutambua na kuvitunza vyanzo vyote vya maji nchini”;

(iii) Mwezi Desemba 2005, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa

Serikali ya Awamu ya Nne, aliagiza Serikali katika ngazi zote zibebe dhamana ya kudhibiti uharibifu wa Mto Ruaha Mkuu ili kurejesha mto kwenye hali yake ya awali. Nukuu “Maeneo machache yanahitaji hatua za haraka kulinda mazingira kwa sababu hali ni mbaya kiasi kwamba inaathiri sekta nyingine. Moja ya maeneo hayo ni Bonde la Mto Ruaha, ambalo linaunganisha mito muhimu nchini. Tumeshuhudia huduma za Bwawa la Mtera zikidhoofika. Mto Ruaha Mkuu si Mkuu tena na karibu umekauka wote katika baadhi ya maeneo. Serikali katika ngazi zote ni lazima iingilie kati na iwe tayari kubeba dhamana ya hali halisi. Uharibifu huu lazima udhibitiwe na hali irejeshwe ilivyokuwa.” na

(iv) Mwezi Machi mwaka 2012 Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akizindua Wiki ya Maji nchini, aliziagiza wizara za Maji, Maliasili na Mazingira pamoja na Mikoa ya Mbeya, Iringa, Singida, Dodoma, kuchukua hatua ili kudhibiti hali ya kukauka kwa Mto Ruaha Mkuu. Nukuu “Ni ukweli ulio wazi kwamba maji yanapungua kwa kasi. Ninyi wa Iringa ni mashahidi. Nani kati yenu alifikiria mto

69

mkubwa kama Ruaha ungeweza kukauka? Sasa si jambo la kufikirika tena. Tujiulize kwa nini? Tujiulize je, inawezekana ukarudi katika hali yake ya zamani? Kama ndiyo kwa vipi? Tuhifadhi mazingira toka unakoanzia na kote unakopita. Nawataka, Wizara za Maji, Maliasili na Mazingira pamoja na Mikoa ya Mbeya, Iringa, Dodoma na Singida kulipa kipaumbele suala hili”;

70

SURA YA NNE

4.0 UCHAMBUZI NA TATHMINI YA MAMBO YALIYOJIRI UWANDANI

Tathmini ya uwandani inaonesha kuwa Bonde la Mto Ruaha Mkuu linakabiliwa na changamoto zinazosababishwa na shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na kutokuwepo na kutotekelezwa kwa mipango ya matumizi ya ardhi, usimamizi duni wa sheria, uchepushaji wa maji kinyume na taratibu na uchungaji holela wa mifugo. Nyingine ni udhibiti hafifu wa shughuli za umwagiliaji mashambani, kuwepo kwa migogoro inayoanzishwa kwa makusudi ya kudhoofisha usimamizi wa ardhi, muingiliano wa kisiasa katika usimamizi na utekelezaji wa maamuzi ya kitaalamu. Aidha, ongezeko la watu ikiwa ni pamoja na wahamiaji kunaongeza ukubwa wa tatizo.

Pia kutokuwepo kwa elimu ya kutosha kuhusu usimamizi wa mazingira, kukosekana kwa teknolojia stahiki katika uzalishaji, uwekezaji mdogo katika miundombinu ya umwagiliaji, kukosekana kwa uratibu stahiki wa usimamizi wa jitihada mbalimbali, utekelezaji na endeshaji wa shughuli za kilimo cha umwagiliaji bila usimamizi thabiti, upandaji wa miti ya kibiashara katika maeneo ya kilimo, uchomaji moto holela, uchimbaji madini katika kingo za mito, upandaji miti isiyo rafiki kwa mazingira katika vyanzo vya maji na uingizaji wa mifugo katika bonde bila kuzingatia taratibu na mipango ya matumizi ya ardhi.

Sababu hizo kwa pamoja zinachangia hali inayojitokeza kila mwaka ya upungufu wa maji, kukauka kwa mito na vijito, mmomonyoko wa udongo, kuhama kwa mito, kupungua na hata kupotea kwa baadhi ya bionuai ya asili, kuwepo kwa migogoro ya ardhi pamoja na kutofikiwakwa ukuaji endelevu katika sekta za nishati, kilimo, ufugaji na uvuvi. Kwa ujumla, shughuli zisizo endelevu zinazochangiwa na usimamizi duni wa sheria, kanuni na taratibu zinasababisha uharibifu unaoendelea katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu. Uchambuzi na tathmini ya mambo yaliyojiri uwandani wakati wa ziara iliyofanywa na Kikosi Kazi ulibaini changamoto mbalimbali katika maeneo yafuatayo:

4.1 Kilimo Kisicho Endelevu Katika Bonde

Bonde la Mto Ruaha Mkuu lina mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa na

71

usalama wa chakula nchini. Kwa mfano, utafiti ufuatao kuhusu “Hali ya uchumi katika mashamba ya umwagiliaji mpunga ndani ya Bonde la Usangu, Tanzania: Tija katika matumizi ya maji, kipato na viashiria vya maisha” uliofanywa na Reuben M.J. Kadigi na wenzake mwaka 2004, umeonesha athari zitakazotokana na kusitishwa kwa kilimo cha Mpunga kwa sababu ya kukosekana kwa maji katika mashamba ya umwagiliaji ndani ya Bonde la Usangu kama ifuatavyo:-

Upungufu wa mpunga ndani na nje ya nchi kwa takriban tani 105,000 sawa na tani 66,000 za mchele, kiasi ambacho ni sawa na asilimia 14.4 ya mpunga unaozalishwa nchini Tanzania kwa mwaka;

Kusababisha hasara kwa wakulima wa mpunga wa eneo la Bonde la Usangu kwa takriban dola za Marekani milioni 530 kwa mwaka; na

Kuathiri urari wa malipo “Balance of Payment” kwa nchi kwa wastani wa dola za Marekani milioni 15.9 kwa mwaka kutokana na kupungua kwa kiasi cha mchele kitakachouzwa nje ya nchi kwa mwaka au kiasi kitakachoingizwa toka nje ya nchi kutegemeana na ugavi na mahitaji.

4.1.1 Matumizi ya maji yasiyo endelevu katika kilimo cha umwagiliaji

Kikosi Kazi kimebaini kuwa kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu kwa sehemu kubwa kinafanywa bila kuwepo kwa miundombinu ya umwagiliaji iliyoendelezwa au kutokuwepo kwa matunzo ya kuridhisha ya miundombinu iliyoendelezwa. Hali hiyo inasababishwa na uongozi mbovu, ujuzi mdogo kwa upande wa wakulima kuhusu usimamizi wa skimu na matumizi ya maji usiozingatia utaratibu ukiwemo wa kurudisha maji mtoni. Aidha, baadhi ya skimu kubwa za umwagiliaji na nyingi ya zile zinazomilikiwa na wakulima wadogo hazina kiwango cha kuridhisha cha utunzaji wa miundombinu ya umwagiliaji. Hali hiyo inasababishwa na ukosefu wa matunzo ya miundombinu ikiwa ni pamoja na uchafu wa mifereji ya umwagiliaji na matupio. Kwa skimu kubwa ambazo zinamilikiwa na wakulima wadogo, imebainika ukubwa wa skimu, kiwango kidogo cha utaalamu pamoja na usimamizi hafifu wa sheria ndogo unachangia katika matumizi ya maji yasiyoendelevu. Changamoto hizi zilidhihirika wakati Kikosi Kazi kilipotembelea Skimu ya Mwendamtitu, Madibira, Mbarali, Ukombozi na Kapunga katika Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya. Skimu za Ukombozi naPawaga-Mlenge katika Mkoa wa Iringa nazo zinakabiliwa na changamoto hizo.

72

Kielelezo Na.9: Skimu ambayo haijaendelezwa -Skimu ya Mkombozi, Wilaya ya Iringa. Tarehe 21 Aprili, 2017

Tathmini imeonesha kuwa ufanisi wa skimu za umwagiliaji katika matumizi ya maji kwa watumiaji wakubwa ni asilimia 40 na kwa watumiaji wa kati na wadogo ni chini ya asilimia 20 kwa kutumia umwagiliaji kwa njia ya mtiririko. Hali hii husababisha zaidi ya asilimia 70 ya maji yanayotumika kwa umwagiliaji kupotea. Aidha, skimu nyingi za wakulima wadogo na wakati hazina miundombinu ya kurudisha maji mtoni.

73

Kielelezo Na. 10: Mgawanyo wa ufanisi wa matumizi ya maji kwa watumiaji Wakubwa, Wakati na Wadogo kwa mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya mtiririko

Chanzo: Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, 2017

Hata hivyo, tathmini imebaini uwepo wa mifumo yenye ufanisi mkubwa wa matumizi ya maji ndani ya Bonde inayofikia kiasi cha asilimia 80 hadi 85. Orodha ya skimu za umwagiliaji kwa makundi husika imeambatishwa

Kielelezo Na. 11: Umwagiliaji kwa kutumia mifumo yenye ufanisi katika Shamba la Silverlands, Wilaya ya Iringa. Tahere 19 Aprili, 2017

74

4.1.2 Miundombinu duni ya umwagiliaji

Eneo linalofaa kwa umwagiliaji katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu ni sawa na hekta 132,898 sawa na asilimia 1.6 ya eneo lote la Bonde. Hivi sasa, eneo linalotumika kwa umwagiliaji ni hekta 79,978 sawa na asilimia 60 ya eneo linalofaa kwa umwagiliaji katika Bonde. Jedwali Na. 4: Linaonesha mchanganuo wa skimu za umwagiliaji katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu.

Jedwali Na. 4: Muhtasari wa Skimu za Umwagiliaji kulingana na ukubwa wa eneo linalohudumiwa

MUHTASARI WA SKIMU ZA UMWAGILIAJI- BONDE LA MTO RUAHA MKUU

Aina ya Skimu Idadi ya Skimu

Ukubwa (Ha)

Eneo linalomwagiliwa

(Ha)

IdadiyaWamwagiliaji

Skimu Ndogo (Chini ya hekta 500) 111 21,548 12,233 8,753 Skimu za Kati (Kati ya hekta 500 hadi 2000) 55 48,221 25,787 22,106

Skimu Kubwa (Zaidi ya hekta 2000) 15 63,129 41,958 16,656

181 132,898 79,978 47,515 Chanzo: Tume ya Taifa ya Umwagiliaji 2017

Katika Bonde zima zipo skimu 181, kati ya hizo, skimu 35 zina miundombinu iliyoboreshwa. Skimu zilizobaki 146 hazina miundombinu iliyoboreshwa hivyo kusababisha ufanisi wa utumiaji maji kuwa chini ya asilimia 20. Hali hiyo huchangia kwa kiasi kikubwa kupotea na kupungua kwa maji katika mito hivyo kusababisha madhara makubwa katika ikolojia ya Bonde. Kikosi Kazi kilibaini na kushuhudia skimu za umwagilaiji za wakulima wadogo za Madibira, Mwendamtitu, Igomelo, Pawaga-Mlenge na Mkombozi na zile za mashamba makubwa ya Mbarali na Kapunga zikiwa na idadi kubwa ya mifereji mikuu na ile ya upili ambayo haijaboreshwa na hivyo hupoteza maji kwa wingi.

Wakati wa ziara ya Kikosi Kazi, wakulima wakubwa watatu katika skimu za Madibira, Mbarari Estate na Kapunga walitozwa faini ya jumla ya Shilingi 111,100,000.00/-. Aidha, wakulima wadogo katika Skimu za Nguvukazi-

75

Mwanavala, Kapunga Smallholder, Mwashikamile na Mwendamtitu walitozwa faini ya jumla ya Shilingi 113,390,000/-.Hivyo jumla ya adhabu zilizotolewa ni Shilingi 224,490,000/-.

Kikosi Kazi kimebaini kuwa miundombinu ya umwagiliaji: ya asili, isiyokamilika, iliyochakaa, kiwango kidogo cha utaalamu pamoja na uelewa mdogo wa masuala ya umwagiliaji ni miongoni mwa sababu zinazochangia upungufu wa maji katika Bonde la Ruaha Mkuu.Jedwali Na. 4 linaonyesha maoni ya wadau kuhusiana na maeneo yanayochangia upotevu wa maji katika tasnia ya umwagiliaji.

Jedwali Na. 4: Maoni ya wadau kuhusiana na maeneo yanayochangia upotevu wa maji katika tasnia ya umwagiliaji

Miundombinu isiyoboreshwa Daraja Miundombinu ya Asili 1 Miundombinu Isiyokamilika 2 Elimu duni 5 Teknolojia duni 4 Uchakavu wa Miundombinu ya Mashamba Makubwa 3 Matumizi ya Pampu 6 Ufunguo: Daraja 1=sababu inayopoteza maji kwa wingi na Daraja 6=sababu inayopoteza maji kidogo katika kilimo cha umwagiliaji.

4.1.3 Uchepushaji wa Maji Usio na Vibali vya Umwagiliaji

Kikosi Kazi kilibaini kuwa kuna ongezeko la shughuli za umwagiliaji nje ya skimu za umwagiliaji zilizosanifiwa unaofanyika kupitia uchepushaji wa maji kutoka katika mito na skimu za umwagiliaji. Uchepushaji mwingi hufanyika bila vibali na mara baada ya maji hayo kutumika huwa hayarudishwi mtoni na hivyo kuwa chanzo cha upotevu wa maji. Maeneo yaliyodhihirika kufanya uchepushaji ni pamoja na mito ya Mbarali, Ruaha, Ndembela, Kimani na Chimala iliyopo Wilaya ya Mbarali. Pia, uchepushaji wa maji katika Mto Mlowo uliopo Wilaya ya Mbeya umekuwa ukifanyika katika maeneo ya Mbarali na Mbeya Vijijini. Inakadiriwa kuwa vitendo vya uchepushaji wa maji vinachangia upotevu wa maji kwa kiasi kikubwa katika eneo la bonde.

4.1.4 Miradi Inayotekelezwa na Serikali

Kikosi Kazi kimebaini kuwepo kwa miradi inayotekelezwa na Serikali katika

76

eneo la bonde kupitia Agriculture Sector Development Programume (ASDP) na The Big Results Now (BRN). Miradi hii ni sehemu ya jitihada za Serikali za kukabiliana na upotevu wa maji; hata hivyo mingi ya miradi hii haijakamilika na hivyo kuwa chanzo cha upotevu mkubwa wa maji. Aidha, kwa sehemu kubwa juhudi hizi hazikufikia malengo yaliyotarajiwa hasa kutokana na kukosekana kwa rasilimali fedha za kutekeleza malengo yaliyokusudiwa.

4.1.5 Kilimo katika maeneo ya miteremko na ukataji wa miti

Tathmini iliyofanywa na Kikosi Kazi baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya za Makete, Wanging’ombe, Kilolo, Mufindi na Mbeya imebaini kuwepo kwa shughuli za kilimo kisicho endelevu katika maeneo ya miteremko.Kilimo katika miteremko kisicho na makinga maji na matuta kinachangia uharibifu wa vyanzo vya maji kupitia mmomonyoko wa udongo na uharibifu wa uoto wa asili. Pia, ukataji miti katika maeneo ya wilaya zilizotajwa pamoja na Wilaya ya Chunya vimekuwa vikichangia katika kuleta mmomonyoko wa udongo na upotevu wa maji. Aidha, kilimo hicho husababisha kujaa kwa mchanga katika mito na wakati mwingine kusababisha baadhi ya mito kupoteza mwelekeo. Mito ambayo imekumbwa na tatizo la kupoteza mwelekeo ni pamoja na Mto Ndembela na Mto Kioga katika maeneo ya Wilaya ya Mbarali.

Kielelezo Na. 12: Kilimo Katika Maeneo ya Miteremko, Wilaya ya Mbeya, Tarehe

77

25 Aprili, 2017.

Kutokana na upotevu mkubwa wa maji, Serikali na wananchi wamekuwa wakifanya jitihada za kurudisha mito kwenye mikondo yake (river training). Mito iliyorudishwa katika mikondo yakeni pamoja na Mto Ndembela kwa kilomita nne na Mto Kioga ambapo zaidi ya kilomita saba zilihusika. Pamoja na jitihada hizo, bado kazi ya kurejesha mito hiyo katika mikondo yake haikukamilika kutokana na upungufu wa fedha na hivyo tatizo la mito kupoteza mwelekeo limeendelea kuwepo na kusababisha upotevu mkubwa wa maji katika mito husika.

4.1.6 Kilimo cha Vinyungu

Kikosi Kazi kilishuhudia shughuli za kilimo cha vinyungu kikifanyika katika vyanzo vya maji. Mazao yanayozalishwa ni pamoja na mahindi, viazi, mbogamboga, vitunguu na nyanya. Maeneo yaliyobainika kujihusisha na kilimo cha vinyungu ni pamoja na Wilaya za Wanging’ombe, Mbeya, Mufindi na Kilolo. Kilimo hiki kimeendelea kuleta madhara makubwa katika mazingira kwa kuwa maeneo yanayolimwa huathirika na mmonyoko wa udongo na kukauka kwa vyanzo vya maji na udongo kujaa kwenye mito. Mahojiano ya viongozi na wananchi yameonesha kwamba sehemu kubwa ya wananchi wanajihusisha na kilimo hicho cha vinyungu na kwamba kilimo hicho kinafanyika zaidi wakati wa kiangazi. Ili kudhibiti kilimo cha vinyungu, Serikali katika ngazi ya mikoa na wilaya zimekuwa zikitoa elimu na matamko mbalimbali ya kusitisha kilimo hicho. Hata hivyo, jitihada hizo hazijaweza kuleta mafanikio katika kukomesha kilimo hicho.

78

Kielelezo Na. 13: Kilimo cha Vinyungu katika Wilaya ya Wanging’ombe, Tarehe 20 Aprili, 2017

4.1.7 Kilimo cha Miti ya Biashara

Kikosi Kazi kilibaini kuwa kilimo cha miti ya biashara kimekuwa kikiongezeka na hivyo kutumia sehemu kubwa ya ardhi katika Wilaya za Makete, Wanging’ombe, Mufindi na Kilolo. Tathmini iliyofanyika imebaini kuwepo kwa ongezeko kubwa la ardhi inayotumika kwa kilimo cha miti katika wilaya hizo. Hali hiyo imesababisha kubadilishwa kwa matumizi ya ardhi ya kilimo cha mazao ya chakula, ardhi ya akiba na mifugo. Aidha, baadhi ya vyanzo vya maji vimegeuzwa kuwa sehemu ya mashamba ya miti ya biashara. Kielelezo Na. 14 kinaonesha kilimo cha miti iliyopandwa katika eneo la vyanzo vya maji.

79

Kielelezo Na. 14: Kilimo cha miti ya kibiashara kwenye vyanzo vya maji, Dabaga, Wilaya Kilolo, Mkoa wa Iringa, Tarehe 24 Aprili, 2017

Kupungua kwa maeneo ya kilimo na ufugaji yanayosababishwa na kilimo cha miti ya kibiashara, imesababisha wakulima na wafugaji kuvamia maeneo yasiyoruhusiwa kwa kilimo ikiwemo maeneo tengefu, hifadhi za kitaifa, hifadhi za akiba, maeneo ya vyanzo vya maji, na maeneo ya miteremko na hivyo kusababisha migogoro na madhara makubwa katika maeneo yaliyotajwa. Aidha, kumekuwepo uharibifu mkubwa unaotokana na kubadilishwa kwa ardhi ambayo awali ilikuwa na uoto wa asili na badala yake kutumika kwa upandaji wa miti isiyo ya asili kwa ajili ya biashara.

Ongezeko la eneo lililopandwa miti ya kibiashara linatishia uoto na uendelevu wa ikolojia ya maeneo husika. Zipo juhudi zilizoanza kuchukuliwa na Serikali pamoja na wadau kudhibiti hali hiyo. Hatua hizo ni pamoja na kukata au kuzuia upandaji wa miti isiyo ya asili, kung’oa miti isiyo rafiki katika maeneo ya vyanzo vya maji, kuzuia kilimo cha miti ya biashara jamii ya misindano, mikaratusi na miwati katika vyanzo vya maji. Hata hivyo bado hatua zilizochukuliwa hazijafanikiwa kuleta suluhisho la kudumu ili kunusuru uoto wa asili na ikolojia

80

katika maeneo yaliyoathirika. Ili kudhibiti changamoto hiyo, kuna umuhimu wa kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi na kuanisha miti rafiki kwa ajili ya kupandwa katika vyanzo vya maji sambamba na kuzuia shughuli za uondoaji wa uoto wa asili ikiwa ni pamoja na ukataji holela wa miti ya asili katika maeneo husika.

Kielelezo Na. 15 kinaonesha eneo la mita 60 lililong’olewa miti isiyo rafiki na vyanzo vya maji katika maeneo ya chanzo cha maji katika msitu wa miwati inayomilikwa na Kampuni ya Miwati katika kijiji cha Nyumbanyitu, Wilaya ya Wanging’ombe.

Kielelezo Na. 15: Utunzaji wa chanzo cha maji katika Kijiji cha Nyumbanitu, Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoa wa Iringa, Tarehe 20 Aprili, 2017

4.1.8 Kilimo Kisicho tunza Maji, Udongo na Bioanuai

Kikosi Kazi kilibaini kuwa moja ya changamoto ni aina duni za kilimo kinacho sababisha upotevu mkubwa wa maji na unyevunyevu, kuharibu udongo na bioanuai. Aina hizo zinahusisha kilimo cha kukwatua na kuchoma moto; aina nyingine za uharibifuwa uoto wa asili ni uondoaji mabaki ya mimea baada ya mavuno au kuingiza wanyama mashambani kwa ajili ya malisho. Aina hii ya ufugaji huchangia kuharibu udongo, kuleta mmomonyoko na hivyo kuchangia katika upotevu wa maji na unyevunyevu, rutuba na bioanuai. Tathmini imeonesha kuwa takriban zaidi ya asilimia 90 ya wakulima na wafugaji katika Bonde waliotembelewa hawazingatii mbinu bora za uzalishaji wa mazao na mifugo. Mbinu hizo ni pamoja na kilimo shadidi, kilimo hifadhi na ufugaji unaozingatia uwezo wa ardhi kutunza wanyama. Kilimo na ufugaji huo

81

usiozingatia kanuni za kilimo bora tayari umeleta madhara makubwa katika mazingira ikiwemo kuchangia kwa sehemu kubwa kwa kukauka kwa vijito na mito inayofanya Mto Ruaha Mkuu. Baadhi ya madhara hayo ni pamoja na upotevu mkubwa wa maji kupitia uvukizo (evaporation) unaosababishwa na ardhi ya joto isiyofunikwa na mimea au mabaki ya mazao. Aidha udongo huo usiofunikwa huharibika kwa urahisi kupitia mmomonyoko, na kupotea kwa muundo asili wa udongo na rutuba.

Tathmini ya Kikosi Kazi imebaini kuwepo kwa jitihada mbalimbali za kudhibiti hali hii. Jitiahada hizo ni pamoja na tafiti mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika ikiwa ni pamoja na zinazofanywa na serikali kupitia Kituo cha Utafiti wa Kilimo Uyole na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine. Aidha, viongozi na wakulima kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe wamekuwa wakijifunza namna ya kuzingatia kilimo hifadhi kwenye mashamba ya wawekezaji ya Clinton Foundation na Rutuba Farm yaliyopo mkoani Iringa. Hadi sasa, wakulima wapatao 6,000 wa mikoa ya Iringa na Mbeya wamekwisha pata mafunzo hayo. Pia, Halmashauri zikishirikiana na wadau wengine wa maendeleo zikiwemo SAGCOT, USAID, DFID, FAO, WWF na CDI wameendelea kushirikisha wadau wa kilimo kwa kuwaelimisha wakulima wadogo kuzingatia kilimo hifadhi katika maeneo ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu. Tathmini pia imeonesha kuwepo kwa uratibu mdogo katika utekelezaji wa juhudi hizo.

Pamoja na juhudi hizo, tathmini imeonesha kuwa kilimo kisichokuwa cha hifadhi kimeendelea kuwa miongoni mwa sababu zenye kuleta madhara makubwa ya upotevu wa maji na udongo na hivyo kuchangiakupungua kwa ufanisi wa uzalishaji katika maeneo ya Bonde. Ili kudhibiti hali hiyo, kuna umuhimu wa kuchukua hatua za haraka kwa lengo la kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu za kilimo na ufugaji endelevu unaofanyika katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu.

Kikosi Kazi kilibaini kwamba tija kubwa inapatikana kutokana na matumizi ya kilimo shadidi kwenye zao la mpunga ambapo tija huongezeka wakati ambapo matumizi ya maji hupungua kwa takriban asilimia 50. Jedwali Na. 5 linaainisha kiwango cha tija na mbinu za kilimo bora cha zao la mpunga katika skimu zinazotumia mbinu za kilimo shadidi katika mikoa ya Mbeya na Iringa.

82

Jedwali Na. 5: Uzalishaji wa zao la mpunga kwa kilimo shadidi (SRI)

S/N

Mkoa

Wilaya

Jina la Skimu

Uzalishaji (t/ha)

2011/12 2012/13 2013/14

1 Mbeya Mbarali Ipatagwa 3.25 3.03 8.80 2 Mbeya Mbarali Uturo 3.60 3.53 9.00 3 Mbeya Mbarali Mbuyuni 4.00 3.90 13.8

0 4 Mbeya Mbarali Madibira 4.50 5.40 9.20 5 Iringa Iringa Magozi 2.58 4.10 6.00 6 Iringa Iringa Pawaga 2.80 4.40 10.5

0 Wastani (t/ha) 3.46 4.06 9.55 Wastani wa uzalishaji wa mpunga kwa SRI (t/ha) 6.00

Uzoefu kutoka maeneo ya Wilaya za Babati, Iringa na Mbeya umeonesha kuwa matumizi ya kilimo hifadhi yameleta tija kubwa katika uzalishaji na uhifadhi wa mazingira. Njia zinazotumika ni pamoja na; kutokuondoa mabaki ya mimea baada ya mavuno, kupunguza hadi kuacha ukatuaji wa ardhi wakati wa maandalizi ya mashamba (minimum to zero tillage), kuzingatia kilimo cha mzunguko na kuweka makinga-maji kwenye maeneo ya miteremko.

Kikosi Kazi kilibaini kwamba tija kubwa inapatikana kutokana na matumizi endelevu ya pembejeo ambapo mbolea ya chokaa huwekwa kulingana na mahitaji ya udongo baada ya kupima kiwango cha mahitaji halisi. Jedwali Na. 6 linaainisha kiwango cha tija na mbinu za kilimo bora cha zao la mahindi katika mashamba yanayotumia kilimo hifadhi na yale yasiyotumia kilimo hicho.

Jedwali Na. 6: Kiwango cha Ufanisi wa Aina za Kilimo cha Mahindi

Aina ya Kilimo Uzalishaji (Tani/Ha)

Shughuli zinazohitajika

Kilimo hifadhi Zaidi ya tani 10.0 Kuandaa shamba bila kulima au kutumia tindo

Kupanda na kuweka pembejeo zinazohitajika (mbolea, viua magugu kwenye mashimo)

Kuvuna na kuacha mabaki shambani

83

Kilimo kisicho hifadhi

Tani 1.3 – 4.0 Kulima, kuchoma moto, kutokuweka makinga maji kwenye miteremko

Kupanda na mbolea Kupalilia Mbolea ya kukuzia Kuvuna Kuhifadhi mazao

Kielelezo Na. 16: Matokeo kati ya kilimo hifadhi na kilimo cha kawaida. Eneo la karibu limelimwa kwa kutumia kilimo hifadhi. Eneo la mbali (upande wa juu ya picha limelimwa bila kilimo hifadhi na hakuna mazao). Rutuba Farm, Wilaya ya Kilolo, Iringa, Tarehe 14 Februari, 2017

4.2 Madhara ya Uchungaji Usio Endelevu

Ufugaji ni mojawapo ya shughuli muhimu za kiuchumi katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu. Hata hivyo, tathmini ya Kikosi Kazi imebaini kuwa sehemu kubwa ya ufugaji unafanyika kwa kutumia mbinu zisizo endelevu na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira hususan, uoto wa asili, maumbile ya udongo, mmomonyoko wa udongo na vyanzo vya maji. Ufugaji wa ainahii huchangia kupungua kwa rutuba, kuwa na malisho duni na pia

84

kuruhusu maji mengi kupotea (evaporation and surface runoff).

Aidha, Kikosi Kazi kimebaini kuwa mbinu duni za ufugaji huhitaji matumizi makubwa ya maji. Baadhi ya mbinu hizo ni pamoja na uchepushaji wa maji kwa kutumia miundombinu duni kwa ajili ya kunyweshea mifugo na pia utaratibu wa kuyaacha maji yatiririke mbugani kwa ajili ya kuotesha malisho ya mifugo hasa wakati wa kiangazi. Utaratibu huu unafanywa bila kuzingatia urejeshaji wa maji mtoni na hivyo kupoteza kiasi kikubwa cha maji hayo. Tatizo hili limedhihirika katika maeneo ya Madibira na Iyala yaliyopo Wilaya ya Mbarali.

Aidha, ufugaji umekuwa ukihusika katika kuharibu vyanzo vya maji ambapo makundi makubwa ya mifugo yamekuwa yakiingizwa kwenye vyanzo hivyo bila kuangalia athari zake. Katika maeneo hayo imebainika kuwa kuna idadi kubwa ya mifugo kwenye maeneo ya vyanzo vya maji hali inayochangia uharibifu mkubwa wa vyanzo hivyo. Kwa mfano, uwezo wa malisho katika Wilaya ya Mbarali ni mifugo 65,000 wakati mifugo iliyopo kwa sasa ni zaidi ya 200,000. Aidha, kumekuwa na ongezeko la ufugaji wa kiholela katika baadhi ya maeneo ya Bonde hili unaosababisha madhara makubwa katika mazingira ikiwemo kuchangia kuongezeka kwa migogoro ya matumizi ya ardhi. Kwa kutumia ndege maalum, wajumbe wa Kikosi Kazi waliweza kujionea makundi 27 ya mifugo yakichungwa ndani ya maeneo ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Pia shughuli za uchungaji zimeshuhudiwa zikiendelea katika maeneo ya Misitu ya Hifadhi, Hifadhi za Akiba na vyanzo vya maji katika maeneo ya Inyala, Wilaya ya Mbeya na Bitimanyanga katika Wilaya ya Chunya. Aidha, Kikosi Kazi kimebaini kwamba maeneo mengi ya wafugaji hayana miundombinu ya malambo na hivyo kusababisha mifugo kupelekwa katika vyanzo vya maji. Katika maeneo yaliyotembelewa na Kikosi Kazi, wafugaji walionesha utayari wa kuchangia katika ujenzi wa miundombinu hiyo.

85

Kielelezo Na. 17: Mifugo iliyoonekana katika Pori la Akiba Rukwa-Lukwati, Wilaya ya Chunya, 29 Aprili, 2017

Pamoja na changamoto za ufugaji zilizotajwa, kumekuwepo na ukataji wa miti unaoambatana na uchomaji moto wa uoto wa asili, uchomaji mkaa, ufugaji na kilimo ndani ya Misitu ya Hifadhi na Hifadhi za Akiba, kama ilivyoshuhudiwa katika Hifadhi ya Akiba ya Lukwati katika Wilaya ya Chunya na Lundamkwabi iliyopo Pawaga katika Wilaya ya Iringa. Pia, tatizo la ufugaji huria limedhihirika katika Wilaya ya Makete ambapo mifugo huachwa ikijichunga yenyewe na hivyo kuingia katika maeneo ya hifadhi za vijiji vikiwemo vyanzo vya maji.

Kikosi Kazi kimebaini kwamba katika kukabiliana na hali hiyo, Serikali katika ngazi za mikoa, wilaya na vijiji zimekua zikichukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupanga matumizi ya ardhi ambapo jumla ya vijiji 247 kati ya vijiji 843 vilivyopo katika Bonde vimekamilisha zoezi la kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi. Jitihada hizi zinahusisha pia ujenzi wa miundombinu ya mifugo, kutoa elimu ya ufugaji bora unaozingatia hifadhi ya mazingira, na kufanya operesheni mbalimbali za kuwaondoa wafugaji wavamizi katika maeneo ya hifadhi. Pia, zoezi la utambuzi wa mifugo na kuwawekea alama linaendelea katika maeneo hayo. Jedwali Na. 7 linaonesha hali ya vijiji kuhusu mipango ya matumizi ya ardhi katika eneo la Bonde.

86

Jedwali Na. 7: Upangaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi

Wilaya Idadi ya Vijiji

Vijiji vyenye

Mipango

Vijiji visivyo na mipango

Asilimia ya vijiji vyenye

mipango Chunya 42 14 28 33.3 Mbarali 102 29 73 28.4 Mbeya 152 10 142 6.6 Makete 91 30 61 33 Wanging’ombe 108 22 86 20.3 Iringa 133 61 72 45.9 Mufindi 121 43 78 35.6 Kilolo 94 38 56 40.4

Pamoja na jitihada hizo, shughuli za ufugaji zimekuwa zikiendelea kuathiri mazingira ya bonde kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo utekelezaji duni wa mipango ya matumizi ya ardhi, uwezo mdogo wa kifedha wa kugharamia uwekaji wa mipaka, kutotengwa kwa maeneo yanayo tosheleza kwa ajili ya ufugaji na kutokidhi sifa za kuwa maeneo ya malisho kwa maeneo mengi yaliyotengwa.

4.3 Madhara ya Mabadiliko ya Tabianchi

Kikosi Kazi kimebaini kuwa pamoja na kwamba mabadiliko ya tabianchi yanachangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa maji katika maeneo mengi nchini, upatikanaji wa mvua katika Bonde kwa miaka 45 iliyopita umeendelea kuwa wa wastani na hivyo upungufu wa mvua kutokuwa sababu ya msingi ya kupungua kwa maji katika Bonde. Kielelezo Na 18 kinaonesha mwenendo wa mvua katika kituo cha Matamba kilichopo maeneo ya miinuko katika Wilaya ya Makete kwa kipindi cha miaka ipatayo 45 kuanzaia mwaka 1971 hadi 2016. Takwimu hizo zinaashiria kupungua kwa maji katika Mto Ruaha Mkuu huenda kunachangiwa na mambo mengine ikiwemo shughuli za kibinadamu na kuvukizwa kwa maji kutokana na ongezeko la joto na kuondolewa kwa uoto wa asili.

87

Kielelezo Na. 18. Mwenendo wa Mvua Kituo cha Matamba, Iringa

Kielelezo Na. 19: Mwenendo wa joto katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuanziamwaka 1985 hadi 2014

HALI YA NYUZI JOTO 1995 - 2014

HALI YA NYUZI JOTO 1985 - 1995

Sentigredi

88

Kielelezo Na. 20: Kupungua kwa eneo oevu la Ihefu kati ya mwaka 1991 na 2006

Matatizo ya kupungua kwa maji katika maeneo ya Bonde, yamesababisha madhara mbalimbali ikiwemo vifo vya wanyamapori na mimea katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, kuathirika kwa shughuli za kilimo, uvuvi katika mito na mabwawa, uzalishaji wa nishati ya umeme katika vyanzo vya Mtera na Kidatu, na kupungua kwa ukubwa wa eneo oevu la Ihefu kutoka kilomita za mraba 322 mwaka wa 1991 hadi kilomita za mraba 153 mwaka wa 2000 na kufika kilometa za mraba 84 mwaka 2006. Kielelezo Na. 20 kinaonesha kupungua kwa eneo oevu la Ihefu kati ya mwaka 1991 na 2006.

Kikosi Kazi kimebaini kuwepo kwa jitihada mbalimbali za kukabiliana na madhara

(Chanzo: LANDSAT Enhanced Thematic Mapper ETM+, Path 169 Row 066, MODIS 500m spectral reflectance, composite 2-9Feb 2006; Wildlife Conservation Society Landscape Ecology and Geographic Analysis Programu).

22 Agosti 1991 322 km

2

21 Julai 2000 153 km

2

2-9 Feb 2006 84 km

2

(Awamu 3)

Hifadhi ya Akiba ya Usangu ENE

0

10

20

30

40

199

199

200

200 MWAK

Km

89

yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi, Serikali na wadau wengine wa maendeleo wamekuwa wakitekeleza sera, sheria, mikakati na mipango mbalimbali. Jitihada hizo zinajumuisha kampeni za upandaji miti, uanzishwaji wa kamati za mazingira katika vijiji, kata na wilaya. Jitihada nyingine zinahusisha utungaji wa sheria ndogo za mazingira katika ngazi za vijiji na halmashauri, kuanzisha shughuli mbadala zikiwemo upandaji wa miti ya matunda na kuni, ufugaji wa nyuki na utunzaji wa misitu, na matumizi ya nishati mbadala ikiwemo gesi inayotokana na samadi (biogas). Aina nyingine ya nishati mbadala ambazo wananchi wanazitumia ni joto linalo tokana na uchomaji wa pumba za mpunga, maranda na unga wa mbao unaotokana utengenezaji wa mbao. Wananchi pia wame elimishwa na kuhamasishwa matumizi ya majiko banifu.

Pamoja na jitihada hizo, Kikosi Kazi kimebaini hali ya upungufu wa maji katika Mto Ruaha Mkuu ambayo inaathiri shughuli za kiuchumi na kijamii katika Bonde. Hii ni kutokana na kuwepo kwa vikwazo mbalimbali vikiwemo; maelekezo ya kiutendaji na mipango ya sekta mbalimbali isiyoratibiwa. Pia kumekuwa na ufinyu wa rasilimali fedha za kutekeleza mipango ya uhifadhi wa maji. Hali hii inalazimisha umuhimu wa kuchukua hatua za haraka kuokoa ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu.

4.4 Madhara ya Kutofanyika Tathmini ya Athari kwa Mazingira

Kikosi Kazi pia kimebaini kuwa masuala mengine zaidi yanayochangia upungufu wa maji katika Mto Ruaha Mkuu ni pamoja na kutofanyika na kutozingatiwa kwa matokeo ya utafiti na tathmini za athari kwa mazingira zinazofanywa (EIA) kwa miradi mbalimbali. Aidha, Tathmini ya Mazingira Kimkakati (SEA) kwa Bonde haijafanywa na hivyo kukosekana kwa ufahamu mpana wa matokeo ya shughuli za kibinadamu na pamoja na kukosekana kwa uratibu. Kwa mfano, mapungufu haya yanajidhirisha katika upandaji wa miti isio asili usioratibiwa, kuendelea kufanyika kwa kilimo ambacho hakizingatii uhifadhi wa ardhi na mazingira na ufugaji holela pamoja na ujenzi wa makazi usiozingatia mipango endelevu. Aidha, hali ya ongezeko la migogoro kati ya mipaka ya hifadhi na wananchi katika Hifadhi ya Akiba ya Mpanga Kipengele, Hifadhi ya Taifa ya Kitulo na Shamba la Mifugo Kitulo. Kwa ujumla kukosekanakwa SEA kunaiweka Serikali katika hali ya kutokuwa na utayari (reactive) badala ya kuwa katikahali ya utayari (pro-active).

Aidha, Kikosi Kazi kimebaini kuwepo kwa changamoto ya watendaji kushinikizwa kutekeleza maagizo yanayokinzana na ushauri wa kitaalam kinyume na mipango

90

na maelekezo ya kitaalam. Changamoto nyingine zinahusisha kuongezeka kwa wahamiaji katika bonde, kukosekana kwa uratibu stahiki wa usimamizi wa jitihada mbalimbali na uchomaji moto holela.

4.5 Madhara Katika Maeneo Yanayopokea Maji Kutoka Ardhi Oevu ya Ihefu

Uharibifu wa mazingira katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu umesababisha madhara makubwa katika maeneo yanayopokea maji ya Mto Ruaha Mkuu. Maeneo makuu yanayopokea maji kutoka katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu ni: (i) Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, (ii) Bwawa la Mtera na (iii) Bwawa la Kidatu. Uharibifu wa mazingira yaliyotajwa hapo juu unajidhihirisha kupitia upungufu mkubwa wa maji yanayoingia katika maeneo hayo. Kielelezo Na: 21 kinaonesha mwenendo wa kiasi cha maji yanayoingia katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ikilinganishwa na ongezeko la eneo la umwagiliaji.

Kielelezo Na. 91: Kinaonesha mwenendo wa kiasi cha maji yanayoingia katikaHifadhi ya Taifa ya Ruaha ikilinganishwa na ongezeko la eneo la umwagiliaji.

4.5.1 Madhara yaliyosababishwa na upungufu wa Maji katika Hifadhi ya Taifa Ruaha

Bonde la Mto Ruaha Mkuu hutiririsha maji yanayonufaisha maeneo ya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa Ruaha, Hifadhi ya Taifa ya Kitulo, Hifadhi ya Taifa ya

91

Udzungwa, Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Hifadhi ya Akiba la Selous na maeneo mengine yenye umuhimu kiutalii. Kupungua kwa mtiririko wa maji katika Mto Ruaha Mkuu kutaharibu ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu. Hali hiyo itasababisha athari katika utalii kwa kupoteza Watalii na hivyo kupunguza kiasi kinachochangiwa na Sekta ya Utalii katika pato la Taifa. Katika taarifa za Programu ya Mtandao waMaeneo Lindwa Kusini mwa Tanzania (SPANEST), maeneo ya vivutio vya utalii na vitalu vya uwindaji yaliyomo katika eneo la Bonde la Mto Ruaha Mkuu yalichangia kiasi cha takriban Shilingi Bilioni 22.3 kwa mwaka.

Kikosi Kazi kimebaini kwamba upungufu wa maji katika Mto Ruaha Mkuu umeathiri ubora wa hifadhi na hivyo kusababisha madhara ya kimazingira, kiuchumi na kijamii kama ifuatavyo:

4.5.1.1 Kiuchumi

i. Kupungua kwa mvuto wa hifadhi kwa watalii na kuhatarisha kupungua kwa idadi yao siku za usoni;

ii. Kukosekana ajira kutoka kwenye shughuli za utalii; na iii. Wanyama kutoka nje ya hifadhi na kuleta mwingiliano hatarishi kwa

wanyama (ujangili) na wanadamu (kiusalama na uharibifu wa mazao).

4.5.1.2 Kijamii

i. Uharibifu wa mazalia ya samaki yaliyopo ndani ya hifadhi na kusababisha kupungua kwa samaki katika mito na Bwawa la Mtera;

ii. Kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa baina ya mifugo na wanyamapori; na

iii. Kuongezeka kwa migogoro kati ya wanyamapori na wananchi.

4.5.1.3 Kimazingira

i. Kupungua kwa viumbe wa majini hususan samaki; ii. Kupungua uwezo wa eneo oevu kusafisha maji, kuhifadhi mtiririko wa maji,

kutunza bioanuai na mvuto; iii. Kutoweka kwa bioanuai; na iv. Kuongezeka kwa mmomonyoko wa udongo.

92

4.6 Matatizo ya Upungufu wa Kina cha Maji kwenye Bwawa la Mtera katika Ufuaji wa Umeme kwenye Vituo vya Mtera na Kidatu

Mitambo ya kufua umeme katika vituo vya Mtera na Kidatu, ina uwezo wa kuzalisha asilimia 41 ya umeme wote nchini. Mto Ruaha Mkuu huchangia asilimia 56 ya maji yanayozalisha umeme Megawati 204 sawa na 1,429 Gigawati kwa saa (GWh), wenye thamani ya Shilingi trillion 3.5. Kukauka kwa maji katika Mto wa Ruaha Mkuu kutasababisha hasara ya asilimia 41 ya umeme na kupunguza uzalishaji viwandani nchi nzima. Utafiti uliofanywa na TANESCO mwaka 2016 kuhusu hali ya baadaye ya uzalishaji wa umeme, inaonesha kuwa kilimo cha umwagiliaji kinasababisha upungufu wa uzalishaji wa umeme kwa kiwango cha 400GWh kwa mwaka katika vituo vya Kidatu na Mtera. Kama hali ya mvua katika Nyanda za Juu Kusini haitakuwa nzuri katika miezi 41 mfululizo kuanzia 2016 kuna uwezekano wavituo hivi kushindwa kuzalisha umeme.

Upungufu wa kina cha maji katika Bwawa la Mtera ambao husababishwa na kukosekana au kupungua kwa mtiririko wa maji katika Mto Ruaha Mkuu husababisha upungufu wa ufuaji wa umeme katika Vituo vya Mtera na Kidatu.

Kielelezo Na. 22: Kina cha Maji katika Bwawa la Mtera kuanzia mwaka 2005 hadi

93

2016

Pia upungufu wa kina cha maji husababisha uzalishaji wa umeme kufanyika chini ya kiwango na kusababisha athari zifuatazo:

4.6.1 Kiuchumi

i. Kupungua kwa ufanisi katika mitambo ya kufua umeme husababisha uharibifu wa mitambo na ongezeko la gharama za matengenezo;

ii. Kusimamishwa mara kwa mara uzalishaji wa umeme katika Bwawa la Mtera na hivyo kuondoa megawati 80 kwenye gridi ya Taifa na kuathiri mikoa ya Kaskazini na Magharibi;

iii. Kusimamishwa mara kwa mara uzalishaji wa umeme katika Bwawa la Kidatu na hivyo kuondoa megawati 204 kwenye gridi ya Taifa; na

iv. Kusimamishwa kwa mitambo ya kufua umeme wa maji huilazimisha TANESCO kufua umeme kwa gharama kubwa kwa kutumia gesi na mafuta.

94

Kielelezo Na.23: Ufuaji wa Umeme Katika Bwawa la Mtera (Mwaka 2005 hadi 2016)

4.6.2 Kijamii

i. Kukosekana kwa maji karibu na makazi ya wananchi huwafanya kufuata maji na samaki katika maeneo hatarishi ndani ya eneo la hifadhi ya Bwawa hivyo kuhatarisha maisha yao na mitambo ya TANESCO;

95

SURA YA TANO

5.0 HITIMISHO NA MAPENDEKEZO 5.1 Hitimisho

Baada ya kufanya ziara katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu, kupitia taarifa mbalimbali na tafiti na miradi iliyowahi kufanyika kwa lengo la kuokoa ikolojia ya Mto na pia kufanya mahojiano na viongozi wa kitaifa, katika mkoa, wilaya na wananchi wanaoishi katika Bonde hilo; Kikosi Kazi kimejiridhisha kwamba Bonde la Mto Ruaha Mkuu linakabiliwa na changamoto ya upungufu mkubwa wa mtiririko wa maji. Upungufu huo katika miaka ya karibuni umesababisha kuongezeka kwa muda wa maji kuacha kabisa kutiririka kutoka wastani wa kipindi kisichozidi miezi miwili katika miaka ya 1960 hadi kufikia miezi 6 katika miaka ya 2000. Sababu kubwa zinazochangia hali hiyo ni kuongezeka kwa kasi kwa shughuli za kibinadamu hususan, kilimo kisicho hifadhi, kilimo cha umwagiliaji, ufugaji holela, upandaji mkubwa wa miti kibiashara, na kuondolewa kwa uoto wa asili. Aidha, mabadiliko ya tabianchi hususan ongezeko la hali ya joto kunachangia kuongeza kasi ya upotevu wa maji katika Bonde.

Kikosi Kazi kimebaini kwamba pamoja na juhudi nyingi zilizofanywa na zinazoendelea kufanyika bado hazijafanikiwa kama ilivyotegemewa kutokana na sababu mbalimbali. Sababu hizo ni pamoja na kukosekana kwa Tathmini ya Mazingira Kimkakati (SEA) ya Bonde ambayo ingeelekeza mipango muafaka ya maendeleo na uwekezaji katika Bonde pamoja na kuratibu miradi ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira. Kwa mfano, ilibainika kwamba sera, sheria na mipango mbalimbali ya kisekta iliyotekelezwa na inayotekelezwa katika Bonde imekuwa ikitekelezwa bila uratibu na usimamizi wa jumla. Hali hii inatokana na kutokuwepo kwa chombo ambacho kimepewa majukumu mtambuka kwa ajili ya kufanya uratibu na ufuatiliaji wa utekelezaji.

Aidha, pamoja na kuongezeka kwa ufahamu juu ya mbinu za matumizi endelevu ya rasilimali za uzalishaji, sehemu kubwa ya mbinu hizo hazijawafikia wadau ili zitumike katika juhudi za kuokoa ikolojia ya Bonde. Shughuli zote za kiuchumi na kijamii katika Bonde zimekuwa zikifanyika hususan kilimo na ufugaji bila kuwepo mipango ya matumizi bora ya ardhi. Pia katika nyakati na maeneo tofauti kumekuwepo na matamko yanayokinzana na maelekezo ya kitaalamu hali ambayo imechangia kudhoofisha juhudi za kuokoa ikolojia ya Bonde. Katika miaka ya karibuni ukubwa wa changamoto hizi zote umekuwa ukiongezeka kutokana na

96

ongezeko la idadi ya watu katika eneo la Bonde kutokana na kuzaliana na uhamiaji.

Baada ya tathmini hii, Kikosi Kazi kinapendekeza yafuatayo yatekelezwe ili kuleta mtazamo na taratibu mpya kwa ajili ya kurejesha ikolojia na mazingira ya Mto Ruaha Mkuu:-

5.2 Mapendekezo

Yafuatayo ni mapendekezo ya Kikosi Kazi yanayozingatia masuala ya kisera na kisheria, kimkakati na kiutendaji: Mapendekezo ya kisera na kisheria yanajumuisha maeneo yafuatayo:-

(i) Sheria zote zisimamiwe na kutekelezwa ipasavyo kwa ukamilifu;

(ii) Serikali iunde Taasisi au Mamlaka Maalum kisheria itakayokuwa na majukumu ya kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali zilizopo katika Bonde la Mto Ruaha. Pamoja na mamlaka hiyo uundwe Mfuko Maalum wa Wakfu (Trust Fund) ambao utachangiwa na wote wanaonufaika na rasilimali za Bonde na wadau wengine na usimamiwe kwa pamoja na wadau hao (Serikali, sekta binafsi na wabia wa Bonde la Mto Rufiji). Taasisi hiyo iwe chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais;

Aidha, ili kutekeleza pendekezo hilo mpango uhusishe hatua mbili kuu: (a) kwa hatua ya awali Mamlaka hiyo ianzishwe kwa kutumia Sheria ya Mazingira Na. 20 ya Mwaka 2004 kwa maana ya Eneo Lindwa(Enviromentally Protected Area);(b) na hatua ya kudumu itungwe sheria maalum ya kuunda Mamlaka, Mfuko na utaratibu wa kuuchangia na kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za Bonde.Kikosi Kazi kinatambua zipo mamlaka mbalimbali ambazo zimeundwa katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu/Rufiji, hivyo, ufanyike mpango wa kurazinisha mipaka na majukumu ya mamlaka hizo ili ziweze kutekeleza majukumu yake chini ya Mamlaka Maalum na Mfuko;

(iii) Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, wahakikishe Wilaya na Vijiji vyote vilivyopo ndani ya Bonde vinaandaa, kutekeleza na kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi. Aidha, mipango iliyopo ipitiwe na kuhuishwa;

(iv) Ili kuhakikisha wamiliki wa ardhi wanatumia rasilimali hiyo kwa

uendelevu na kuchangia utunzaji wa ikolojia ya Bonde, Ofisi ya Rais -

97

TAMISEMI na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ziharakishe uwekaji wa ukomo wa kiwango cha juu cha ardhi ambacho kinaweza kumilikiwa na kutumiwa kwa kilimo, misitu, ufugaji, viwanda na matumizi mengine kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Na. 4 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya Mwaka 1999;

(v) Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Ofisi ya Makamu wa Rais, na Wizara ya Maji

na Umwagiliaji ziharakishe kubaini maeneo maalum yanayotoa mchango mkubwa wa upatikanaji wa maji (vyanzo vya maji) katika Bonde (mfano katika milima na misitu ya asili) na kudhibiti shughuli za kibinadamu. Aidha, vyanzo vyote vya maji ndani ya Bonde vibainishwe, vipimwe, viwekewe mipaka kwa kutumia alama na kumilikishwa kwa mamlaka husika. Mfano mzuri upo katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika kuweka mipaka ya maeneo ya barabara;

(vi) Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Fedha

na Mipango, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waharakishe utekelezaji wa Tangazo la Serikali Na. 28 la mwaka 2008 kwa kuzingatia sheria na taratibu,

(vii) Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ihakikishe uzalishaji wa mazao,

mifugo na uvuvi unafanyika kwa kutumia mbinu bora za uzalishaji (Good Agricultural Practices – GAP). Uzalishaji wa mazao ya kilimo uzingatie kilimo hifadhi katika maeneo yanayotegemea mvua na kilimo shadidi katika maeneo ya umwagiliaji; ufugaji uzingatie uwezo wa maeneo ya malisho (Carrying Capacity) na uboreshaji na utunzaji wa nyanda za malisho. Aidha, uendelezaji wauvuvi na ufugaji wa samaki kwenye mito na mabwawa na maeneo oevu usimamiwe ili ufanyike katika taratibu endelevu. Kazi hii iendane ya utengaji wa maeneo ya uwekezaji wa miundombinu ya kuongeza thamani na masoko ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi;

(viii) Ofisi ya Makamu wa Rais isimamie uandaaji wa Tathmini ya Mazingira Kimkakati (Strategic Environmental Assessment - SEA) katika Bonde. Katika kuandaa “SEA” hiyo, wadau wote washirikishwe. Aidha, Sera na Sheria ya Mazingira pamoja na sera na sheria nyingine zinazohusika katika eneo hilo zitazamwe upya.

(ix) Kutokana na umuhimu wa misitu ya biashara kwa ustawi wa wanannchi

katika maeneo ya Bonde, taasisi za utafiti wa mbegu za misitu zizalishe mbegu za miti ya biashara isiyotumia maji kwa wingi; na

98

(x) Kwa kuwa rasilimali maji ni muhimu sana kwa uhai na ina wadau wengi, upo umuhimu wa kuanzishwa kwa “Water Resource Regulatory Authority” ambayo itadhibiti matumizi ya maji nchini. Wizara ya Maji na Umwagiliaji wamepewa majukumu ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata maji safi na salama ya kunywa; Sekta ya Kilimo inahitaji maji kwa ajili ya umwagiliaji (irrigation); Sekta ya Mifugo inahitaji maji kwa ajili ya mifugo; Uvuvi vile vile inahitaji maji kwa ajili ya uvuvi na kila sekta inahitaji maji kwa ajili ya matumizi mbali mbali. Hivyo Wizara ya Maji na Umwagiliaji ni mdau mmojawapo na hawezi kuwa sehemu ya mtoa vibali vya kutumia maji kwa sekta nyingine.

Katika eneo la kimkakati, Kikosi Kazi kimependekeza mambo yafuatayo:-

(i) Ofisi ya Makamu wa Rais ihakikishe Tathmini ya Kimkakati ya Mazingira

(Strategic Environmental Assessment - SEA) inafanyika kwa Sera, Sheria, Mikakati na Programuu zote zinazohusiana na matumizi na usimamizi wa rasilimali zilizopo ndani ya Bonde. Aidha, miradi yote inayotekelezwa ndani ya Bonde ambayo haijafanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Environmental Impact Assessment - EIA) ifanyiwe;

(ii) Mamlaka inayopendekezwa ihakikishe mipango na shughuli za sekta mbalimbali ndani ya Bonde vinaratibiwa ili kuhakikisha inatekelezwa kwa utaratibu endelevu na inachangia katika maslahi mapana ya maendeleo ya Bonde na Taifa badala ya kuwa na kila taasisi na mipango yake;

(iii) Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo Mifugo

na Uvuvi iharakishe kukamilisha kazi inayoendelea ya utambuzi na uwekaji alama mifugo yote. Kazi hii iendane na kazi inayoendelea ya utengaji wa maeneo ya malisho na uwekaji wa miundombinu ya mifugo (majosho, njia za mifugo, mabirika ya kunyweshea mifugo, minada, viwanda vya vyakula vya mifugo na kuchakata mazao ya mifugo); na

(iv) Ofisi ya Makamu wa Rais, ihakikishe taasisi zote zinazosimamia

utekelezaji wa shughuli za kiuchumi katika Bonde zinatoa elimu kuhusu mbinu za kuhimili nakukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Katika eneo la kiutendaji Kikosi Kazi kimependekeza mambo yafuatayo:-

(i) Ili kuhakikisha usimamizi wa sera na sheria katika utekelezaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii katika Bonde, Mamlaka inayopendekezwa ipewe uwezo wa kuhakikisha kazi zote

99

zinazotekelezwa katika Bonde zinazingatia sera na sheria zilizopo za uhifadhi wa mazingira na ikolojia ya Bonde;

(ii) Ili kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali maji katika eneo la Bonde yanakidhi mahitaji ya wadau wote, Mamlaka inayopendekezwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, ihakikishe kilimo cha umwagiliaji kinafanyika kulingana na sheria na taratibu zilizopo. Aidha, ifanyike tathmini ya kiasi cha maji katika kila chanzo, mahitaji katika skimu za umwagiliaji zilizopo kwa sasa na kulinganishwa na vibali vilivyotolewa. Teknolojia za kisasa zitumike katika kuongeza ufanisi katika miradi ya umwagiliaji;

(iii) Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na

Utalii ifanye tathmini ya kina kwa ajili ya kutambua maeneo yanayopaswa kubakizwa katika uoto wa asili na misitu ya asili na yale yanayoweza kutumika kwa upandaji wa miti isiyo ya asili kibiashara bila kuathiri ikolojia na upatikanaji wa maji. Pale ambapo tathmini itabaini miti isiyo ya asili inaathiri mazingira, miti hiyo iondolewe. Aidha, tathmini hiyo ielekeze upandaji wa miti kibiashara ufanyike kwa kuzingatia mipango ya matumizi ya ardhi;

(iv) Ofisi ya Rais TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo

na Uvuvi ihakikishe kilimo katika maeneo yenye miteremko iliyo na mwinamo mkali yanajengewa makinga maji, kubakiza uoto wa asili, kuzingatia kilimo hifadhi na kutumia mbinu nyingine za kuzuia mmomonyoko wa udongo. Aidha, tathmini ifanyike kubaini maeneo yasiyofaa kwa kilimo kutokana na mwinamo mkali, ili maeneo hayo yazuiliwe kutumika kwa kilimo na makazi;

(v) Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji

ihakikishe uwekaji wa vipimo unafanyika katika mabanio na matupio ya maji ili kujua kiasi cha maji kinachotumika na kinachorudishwa mtoni kulingana na kibali cha maji kilichotolewa. Watumiaji wa skimu zote za umwagiliaji ambazo hazina vipimo waweke vipimo vya kujua kiasi cha maji kinachochukuliwa na kurudishwa mtoni. Aidha, wamiliki wa mashamba ya umwagiliajiambao hawajafunga vipimo hivyo wasitishiwe vibali;

(vi) Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Maliasili na Utalii na

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zifanye tathmini kwa ajili ya kujenga mabwawa ya kuvuna maji ya mvua ili yasaidie kuwepo na

100

mtiririko wa maji kwa mwaka mzima na kutumika kwa shughuli za kiuchumi na kijamii. Mabwawa makubwa yaliyopendekezwa ya uvunaji wa maji ya mvua ya Ndembera na Usalimwani yajengwe na Bwawa la Lwanyo ujenzi ukamilike;

(vii) Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali

za Mitaa zihakikishe kuwa kilimo kisichozingatia kilimo hifadhi na kilimo shadidi kisitishwe katika eneo la Bonde la Mto Ruaha Mkuu. Aidha, kutokana na ukubwa wa kazi hiyo utolewe muda wa kutoa Elimu kwa Watendaji ili watumike kuelimisha wakulima juu ya utekelezaji wa kilimo hicho;

(viii) Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo

ya Makazi na Wizara ya Maji na Umwagiliaji zifanye uhakiki wa milki zote zilizotolewa katika ardhi oevu na vyanzo vya maji ili zibatilishwe;

(ix) Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Nishati na Madini, na Baraza la

Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira zifanye tathmini ya maeneo ya uchimbaji wa madini katika bonde kwa lengo la kutambua uchimbaji unaofanyika katika vyanzo vya maji na maeneo oevu na kusitisha. Aidha, Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Bonde zitunge Sheria Ndogo zinazowataka wachimbaji wa madini ya aina zote katika maeneo ya Bonde kupata kibali cha uchimbaji. Aidha, Wizara ya Nishati na Madini isitoe leseni za uchimbaji wa madini katika Bonde bila kuzishirikisha Halmashauri husika;

(x) Ofisi ya Rais - TAMISEMI ikishirikiana na wadau isimamie utatuzi

wa migogoro ya matumizi ya ardhi iliyopo katika Bonde kwa kuzingatia mapendekezo na mpango kazi wa Kamati ya Kisekta ya Utatuzi wa Migogoro ya Matumizi ya Ardhi iliyoundwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Serikali itoe kipaumbele kwa utekelezaji wa mpango wa Kupanga-Kupima-Kumilikisha (K3) eneo lote la ardhi katika Bonde;

(xi) Ofisi ya Makamu wa Rais na Wizara ya Maji na Umwagiliaji

ziimarishe huduma za Ukaguzi, Ufuatiliaji na Tathmini zinazotolewa na Ofisi za Kanda za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Bodi ya Maji ya Bonde;

(xii) Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya

101

Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na wadau wengine watekeleze mipango maalum ya kuwawezesha wakazi wa Bonde kuanzisha na kutekeleza shughuli mbadala za kiuchumi ambazo ni rafiki kwa mazingira. Shughuli hizo ni pamoja na ufugaji wa nyuki na samaki, wanyama wadogo na kuku, na kilimo cha mazao ya bustani kwa kutumia matone;

(xiii) Wizara ya Maji na Umwagiliaji ifanye tathmini ya maeneo ambayo

mito imepoteza muelekeo na kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mpango wa kurejesha mito hiyo katika mikondo yake. Aidha, Wizara hiyo isimamie ukamilishaji wa kazi iliyoanza katika baadhi ya mito ya Ndembera, Mswiswi, Mkoji na Kioga;

(xiv) Tume ya Taifa ya Matumizi Bora ya Ardhi kwa kushirikiana na Ofisi

ya Rais – TAMISEMI na wadau wengine wa maendeleo kuendelea kuandaa na kuhuisha mipango ya matumizi ya ardhi katika maeneo yote ya ngazi za Halmashauri na Vijiji vilivyopo ndani ya Bonde ili kuainisha maeneo maalum yenye Miundombinu stahiki kwa ajili ya ufugaji kwa kuzingatia utaratibu shirikishi. Vile vile kuondoa mifugo katika maeneo ya Hifadhi za Taifa, Hifadhi za Akiba na maeneo mengine yaliyoainishwa kwa shughuli zisizo za ufugaji;

(xv) Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Wakala wa

Mbegu za Miti Tanzania (Tanzania Tree Seed Agency – TTSA) na taasisi za utafiti wazalishe mbegu za miti ya biashara isiyotumia maji mengi kwa kuwa ni muhimu kwa uchumi wa wananchi;

(xvi) Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,

Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wahakikishe kuwa elimu inatolewa ili kudhibiti ongezeko la watu kwa kuzingatia uwiano wa rasilimali za asili zilizopo na idadi ya wakazi katika Bonde; na

(xvii) Badala ya kuendelea kuongeza maeneo ya kilimo katika Bonde,

kilimo kinachozingatia uzalishaji endelevu kizingatiwe na wakulima wote ili kuongeza tija (productivity).