mkuhumi ni nini? - tanzania natural resource forum (tnrf) · sheria ya misitu (2002) inaelezea kuwa...

12

Upload: others

Post on 04-Feb-2020

51 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: MKUHUMI ni nini? - Tanzania Natural Resource Forum (TNRF) · Sheria ya Misitu (2002) Inaelezea kuwa kamati za vijiji za ardhi ya misitu zinapaswa kuzingatia uwiano wa jinsia Programu
Page 2: MKUHUMI ni nini? - Tanzania Natural Resource Forum (TNRF) · Sheria ya Misitu (2002) Inaelezea kuwa kamati za vijiji za ardhi ya misitu zinapaswa kuzingatia uwiano wa jinsia Programu

2 | Wanawake na misi tu Tanzania

Wanawake ni miongoni mwa mamia ya mamilioni ya watu wanaotegemea misitu kwa maisha yao. Majukumu ya kijinsia yaliyopo katika jamii nyingi mara nyingi yanaonekana kwa namna mbalimbali wanawake na wanaume wanavyotumia rasilimali za misitu. Katika nchi ya Tanzania na nchi zingine nyingi,, maisha ya wanawake na majukumu yao katika jamii yanategemea moja kwa moja rasilimali za misitu ili kukidhi mahitaji ya lishe, afya, na ya kiutamaduni kwa ajili ya familia na jamii yao. Wanakusanyaa mazao ya misitu kama vile nishati ya kuni, chakula kwa ajili ya familia, malisho na dawa za mitishamba.

MKUHUMI ni nini? MKUHUMI ni Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji na uharibifu wa Misitu (MKUHUMI). Ni mpango unaowezesha nchi zinazoendelea kusaidia/kutoa motisha ya kifedha kwa jamii ambazo zinasimamia misitu yao kwa njia endelevu. Uharibifu wa misitu ni tatizo la kidunia. Madhara yake si tu kwa mazingira na uhaianuwai inayotegemea mazingira hayo bali pia kwa sehemu kubwa huchangia katika mabadiliko ya tabia nchi. Mabadiliko haya ni tishio kwa maeneo kama Tanzania ambako idadi kubwa ya watu hutegemea mazingira yanayowazunguka. Mabadiliko ya tabia nchi huleta madhara mengi ikiwa ni pamoja na mafuriko ya mara kwa mara na ukame wa muda mrefu, mvua zisizotarajiwa, mlipuko wa magonjwa yatokanayo na hali ya hewa, na hata kusababisha kutoweka kwa mazingira asilia tuliyonayo leo. Kutokana na hatari hizi, jamii ya kimataifa inaangalia njia mbalimbali za kupunguza matatizo haya, na njia mojawapo ni Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji miti na uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) Ifuatayo ni hadithi ya msichana aitwaye REDDA anayehofia kutoweka kwa misitu ambayo ipo kwenye mji wake, na anataka kupata njia ya kuhakikisha kuwa kuna ustawi wa misitu kwa manufaa ya kizazi kilichopo na vizazi vijavyo.

Jinsia humaanisha majukumu na mahusiano kati ya wanawake na wanaume.

Page 3: MKUHUMI ni nini? - Tanzania Natural Resource Forum (TNRF) · Sheria ya Misitu (2002) Inaelezea kuwa kamati za vijiji za ardhi ya misitu zinapaswa kuzingatia uwiano wa jinsia Programu

Wanawake na misi tu Tanzania | 3

Kwa nini wanawake wahusishwe katika MKUHUMI?

Wanaume/wanawake wataathiriwa na MKUHUMI kwa namna tofauti kutokana na tofauti ya mamlaka, majukumu, wajibu, haki na majukumu ya wanaume na wanawake katika utawala wa misitu na nyanja nyingine. Wanawake wanapaswa kuhusishwa zaidi katika MKUHUMI kwa kuwa wana uwelewa maalumu katika usimamizi wa misitu na usimamizi wa maji unaowafanya wawe muhimu katika kuzuia ukataji ovyo misitu. Pia wanayo mengi ya kupoteza linapokuja suala la kusimamia misitu hivyo na wanapaswa kuwa na sauti katika hili. Ushiriki wa jinsia unapaswa kuangaliwa kwa kuwa wanawake kwa ujumla wana yafuatayo:

Page 4: MKUHUMI ni nini? - Tanzania Natural Resource Forum (TNRF) · Sheria ya Misitu (2002) Inaelezea kuwa kamati za vijiji za ardhi ya misitu zinapaswa kuzingatia uwiano wa jinsia Programu

4 | Wanawake na misi tu Tanzania

• Mamlakarasminayasiyorasmimadogonaushirikikatikamifumoya utawala wa misitu ni mdogo;

• Uwezekanomdogowakupatahaki,masokonamitaji,elimurasmi,ajira, na rasilimali zingine;

• Majukumumakubwazaidikwaajiliyauzalishajiwamazaoyachakula, utayarishaji wa chakula, na uokotaji kuni, vyakula vya porini, dawa, maji, na maliasili nyingine;

• Wajibumdogokatikausimamiziwamisitu,pamojanauwelewana umuhimu na ustadi waliyonao katika misitu;

• Kukosahakinaumilikiwaardhi,maranyingikutokananaufahamu mdogo na kutoheshimu haki za kisheria; na

• Hatariyaunyanyasajiwakijinsia.

Mara nyingi wanawake wanakabiliwa na ubaguzi mwingi, na kwa hiyo wanakuwa na hatari zaidi ya kubeba gharama za MKUHUMI na kupoteza kabisa faida zake. Hata hivyo, kuna sababu nyingi za kutaka usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake katika MKUHUMI, ikiwa ni pamoja na wajibu wa kisheria na kimaadili katika kuheshimu haki za wanawake, ukijumuisha na uhuru wa kutobaguliwa. Sheria, sera na mikakati mingi ya kimataifa na kitaifa, pamoja na wafadhili, wawekezaji na wengineo wanaojishughulisha na MKUHUMI, wamekuwa wakizidi kuunga mkono kanuni za haki za kijinsia. Kwa kuongezea, kuwashirikisha wanawake kunaweza kuongeza ufanisi na manufaa ya MKUHUMI. Ni ukweli kwamba, usawa wa kijinsia katika MKUHUMI unaweza kuleta manufaa mapana ya kijamii kwa kuwa wanawake wanachangia zaidi katika ustawi wa familia na jamii.

Page 5: MKUHUMI ni nini? - Tanzania Natural Resource Forum (TNRF) · Sheria ya Misitu (2002) Inaelezea kuwa kamati za vijiji za ardhi ya misitu zinapaswa kuzingatia uwiano wa jinsia Programu

Wanawake na misi tu Tanzania | 5Wanawake na misi tu Tanzania | 5

Je, tutarajie changamoto zipi? Ni wazi kuwa kuna faida nyingi za kuhusisha usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake katika MKUHUMI; hata hivyo, kuna changamoto nyingi ambazo inabidi zishughulikiwe ili hili litokee:

• Masualayakijinsianimagumu,namaranyingihayalengiMKUHUMItu. Watetezi wa MKUHUMI wanapaswa kuelewa namna ya kushughulikia masuala ya jinsia katika muktadha mpana kihistoria, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, na kiikolojia, na kutambua tofauti mbalimbali miongoni mwa wanawake ndani na nje ya jamii.

• Kuhakikishausawawajinsianauwezeshajiwawanawakemwishowe unamaanisha kubadili mahusiano ya kimadaraka na kitaasisi; na hili huchukua muda na kujituma, hasa mahali ambapo imani za kibaguzi zinadumishwa kwa nguvu.

Page 6: MKUHUMI ni nini? - Tanzania Natural Resource Forum (TNRF) · Sheria ya Misitu (2002) Inaelezea kuwa kamati za vijiji za ardhi ya misitu zinapaswa kuzingatia uwiano wa jinsia Programu

6 | Wanawake na misi tu Tanzania

• Kubadilimahusianoyakijinsiawakatimwinginekunawezakuongezahatari kwa wanawake, mathalani kuongezewa mzigo zaidi wa kazi.

• Madhaifukatikautashiwakisiasa,mwamko,taarifanauwezoinabidi kukabiliana nayo.

• Kujumuishajinsiayamkinikunahitajirasilimalizaidi—muda,fedha,watuna utaalam.

Ni bahati kwamba masuala mengi ya kijinsia katika MKUHUMI si “mapya”. Kuna utajiri mkubwa wa elimu na rasilimali zinazoweza kusaidia kujumuisha jinsia. Hakuna haja ya kuanza upya.

Je, ni mikakati ipi ya kuhusisha usawa wa jinsia na kuwawezesha wanawake na MKUHUMI?

Masuala mengi ya kijinsia katika MKUHUMI si “mapya.” Badala yake, tunaweza kujifunza kutoka uzoefu wa nyuma na kutumia rasilimali zilizopo. Japo ni kidogo, rasilimali katika jinsia kwenye usimamizi wa maliasili ya jamii, usimamizi shirikishi wa misitu na MKUHUMI zinajitokeza. Washiriki wa MKUHUMI wanaweza pia kuzifikia rasilimali zingine zilizopo, kama vile wahusika wa jinsia katika serikali, wataalamu na asasi za kiraia zinazojihusisha na masuala ya jinsia. Wadau wa MKUHUMI wanaweza kuchangia katika kujifunza zaidi kupitia, mfano, mitandao ya mawasiliano inayowezesha sera.

Kuwa mbunifu na kutumia njia mbalimbali za kuleta mabadiliko. Kubadili vitendo vinavyohusiana na wajibu wa kijinsia kunaweza kubadili mawazo... na vinginevyo! Saidia wanawake na wanaume kwa kujifunza kwa vitendo katika majukumu mapya, na kuwahusisha katika mijadala yenye kuheshimu na kuongelea masuala yenye changamoto zinazohusiana na jinsia.

Chagua njia itakayowezesha uhusishwaji wa jinsia yenyewe, ikiwa ni pamoja na kujengea kwenye ujuzi na uwezo wa wanawake, kanuni na mifumo.

Page 7: MKUHUMI ni nini? - Tanzania Natural Resource Forum (TNRF) · Sheria ya Misitu (2002) Inaelezea kuwa kamati za vijiji za ardhi ya misitu zinapaswa kuzingatia uwiano wa jinsia Programu

Wanawake na misi tu Tanzania | 7

Kuongeza zaidi ushiriki, uwakilishi mzuri wa wanawake na uliokamilika, na upashanaji wa taarifa ngazi zote. Hii inaweza kujumuisha Uundaji wa taratibu za kushughulikia maslahi na mahitaji ya wanawake: fanya mikutano katika nyakati na mahali ambapo panawafaa wanawake, tumia njia za mawasiliano zinazofaa, buni fursa za wanawake kuchangia (si kupokea tu) taarifa, na tambua tofauti zilizopo miongoni mwa wanawake. Pia saidia wanawake kuwa kwenye uongozi, menejimenti, na nafasi zingine ambazo ni zaidi ya “kiti na meza”.

Pia wahusishe wanaume! Baadhi ya mawazo ni pamoja na kusaidia uwezo wa wanaume kushika majukumu mapya ya kijinsia, kushirikisha visa vya mfano, na kuandaa matukio ya kuwaleta wanaume pamoja katika kujadili masuala ya jinsia.

Kuongeza uwezo wa wanawake na wadau wengine na rasilimali kwa ya kujumuisha masuala ya jinsia. kuimarisha uwezo na fursa ya wanawake katika kujihusisha na MKUHUMI, na kudai haki na faida, mfano, kutoa huduma za kisheria. Mafunzo ya jinsia pia ni muhimu kwa wadau wote.

Kuendeleza usawa wa kijinsia katika usimamizi na ugawaji wa malipo ya MKUHUMI, kwa mfano, kunganisha shughuli za misitu ya jamii na taasisi za fedha za wanawake, na kutoa mwiongozo kwa ajili ya matumizi ya fedha za pamoja zinazogusa jinsia.

Hakikisha kuwa haki za wanawake zinaheshimiwa, na usawa katika kugawana gharama na faida, katika usimamizi na hifadhi ya misitu. Kwa mfano, saidia wanawake kupata hati za kumiliki ardhi; hakikisha kuongezeka kwa kazi kwa wanawake ni kwa hiari na kunafidiwa kikamilifu; tambua uelewa, maarifa na uwezo wa wanawake; wahusishe wanawake katika majukumu mbalimbali, ikiwa pamoja na yale yanayoonekana ni ya “wanaume”, na unganisha kukabiliana, kilimo endelevu na MKUHUMI kwa njia zinazojali jinsia.

Shirikisha jinsia katika kutathmini, kufanya ufuatiliaji, na kutoa taarifa kupitia njia za uwezeshaji. Aidha, katika kupata takwimu zilizotawanyika, inaweza kuwa ni kuhakikisha ushirikishwaji uliokamilika na wenye ufanisi, na kuzingatia haki na maslahi ya wanawake.

Page 8: MKUHUMI ni nini? - Tanzania Natural Resource Forum (TNRF) · Sheria ya Misitu (2002) Inaelezea kuwa kamati za vijiji za ardhi ya misitu zinapaswa kuzingatia uwiano wa jinsia Programu

8 | Wanawake na misi tu Tanzania

Fanya ushawishi (na saidia kuimarisha!) masuala ya jinsia katika sheria na sera za kimataifa na kitaifa, kwa mfano, kuendeleza utekelezaji wa vipengele vilivyopo, na kutetea vipengele vya jinsia vyenye nguvu zaidi katika Mkakati wa Taifa wa MKUHUMI, Programu ya Taifa ya Misitu, nk.

Chukulia ushirikishaji wa jinsia kama mchakato – wa kufanyiwa kazi wakati wote – kuliko kuchukulia kama tukio la mara moja.

Fanya unayosema! Hakikisha kuwa kuna usawa na uwezeshaji wa jinsia katika kazi yako mwenyewe.

Je, jinsia inashughulikiwaje katika nyanja ya kitaifa na kimataifa?Matatizo ya kijinsia hayajashughulikiwa vizuri katika mijadala ya kimataifa ya mabadiliko ya tabia nchi, kama vile Mkataba wa Umoja wa Mataifa Juu ya Tabia Nchi (UNFCCC). Hata hivyo, wanawake wengi wamekuwa wakishiriki kama wajumbe kwenye mikutano, na maamuzi ya makongamano yanaonesha matatizo ya kijinsia. Kinga na viwango vingi vya kimataifa vya MKUHUMI hushughulikia a jinsia kwa udhaifu. Hata hivyo, kwa kuwa kinga zinazidi kuendelezwa, udhaifu huu unaweza kushughulikiwa.

Rasimu iliyopo ya Mkakati wa Taifa wa MKUHUMI (Desemba 2010) haina nguvu sana katika kuhakikisha kuwa kuna usawa na uwezeshaji wa kijinsia. Wakati ambapo hatua zilizopendekezwa katika masuala ya usalama wa miliki, kufaidika pamoja, na kufanya tathmini kungejumuisha kipengele cha jinsia, marejeo maalum ya jinsia yanabaki kuwa finyu. Pengo hili linaweza kushughulikiwa katika rasimu za mkakati zitakazofuata. Aidha, sheria, sera na mikakati mingine ya kitaifa inatambua matatizo ya kijinsia, inalinda haki za wanawake, na kuendeleza usawa na uwezeshaji. Haya yanaweza kusaidia kuelezea Mkakati wa Taifa wa MKUHUMI. ’Baadhi ya sera na sheria zilizoko hapa chini ni baadhi ya mifano michache inayosaidia kulinda haki za wanawake:

Page 9: MKUHUMI ni nini? - Tanzania Natural Resource Forum (TNRF) · Sheria ya Misitu (2002) Inaelezea kuwa kamati za vijiji za ardhi ya misitu zinapaswa kuzingatia uwiano wa jinsia Programu

Wanawake na misi tu Tanzania | 9

Vyombo vya maliasili na mazingiraSera ya Misitu (1998) Inataja jinsia katika matamko mawili

ya sera:

1) huduma za msitu wa jamii

zitazingatia jinsia (Tamko la Sera7);

2) haki za kumiliki msitu, ardhi na

miti zitaanzishwa kwa ajili ya jamii…

pamoja na wanawake (Tamko la Sera

39)

Sera ya Misitu (1999) Zanzibar Inaelezea kuwa wanawake na

wanaume watasaidiwa katika

kuotesha miti, na inataka sera ya jinsia

ianzishwe kwa ajili ya maendeleo ya

sekta ya mistu.

Sheria ya Misitu (2002) Inaelezea kuwa kamati za vijiji za

ardhi ya misitu zinapaswa kuzingatia

uwiano wa jinsia

Programu ya Misitu (2001 – 2010) Inaendeleza ushirikishaji jinsia

na kutambua hitaji la uwiano wa

‘ushirikishwaji wa jinsia katika jamii .

Katiba ya Tanzania Inapiga marufuku ubaguzi wa kijinsia

Sera ya Maendeleo ya Wanawake na

Jinsia (2000)

Inasisitiza ushirikishaji wa kijinsia

katika sekta zote

Sera ya Kulinda Jinsia na Maendeleo

ya Wanawake (2010) - Zanzibar

Inalenga kulinda haki za wanawake,

kutambua usawa jinsia katika fursa,

na kushirikisha jinsia katika mifumo ya

kitaifa.

Page 10: MKUHUMI ni nini? - Tanzania Natural Resource Forum (TNRF) · Sheria ya Misitu (2002) Inaelezea kuwa kamati za vijiji za ardhi ya misitu zinapaswa kuzingatia uwiano wa jinsia Programu

10 | Wanawake na misi tu Tanzania

Pamoja na hayo, kuna mapango mengi

katika kushughulikia jinsia katika mfumo

wa kisheria wa taifa. Mathalani, Sheria

ya Usimamizi wa Mazingira (2004)]

na kanuni za Tathmini na Ukaguzi wa

Mazingira (2005), zina vipengele dhaifu

vya jinsia. Aidha, kuna mgongano kati ya

sheria za kimila na za kitaifa kuhusiana na

umiliki na urithi wa ardhi kwa wanawake.

Na kwa kuongezea, vipengele vingi vya

sheria havitekelezwi au havifanyiwi kazi

kikamilifu.

Page 11: MKUHUMI ni nini? - Tanzania Natural Resource Forum (TNRF) · Sheria ya Misitu (2002) Inaelezea kuwa kamati za vijiji za ardhi ya misitu zinapaswa kuzingatia uwiano wa jinsia Programu
Page 12: MKUHUMI ni nini? - Tanzania Natural Resource Forum (TNRF) · Sheria ya Misitu (2002) Inaelezea kuwa kamati za vijiji za ardhi ya misitu zinapaswa kuzingatia uwiano wa jinsia Programu

12 | Wanawake na misi tu Tanzania

Michoro imefanywa na Adam Lutta

Tafsiri imefanywa na Gwandumi Mwakatobe Atufwene

Muhtasari huu ni msingi wa “Jinsia na REDD” taarifa fupi, kilichotungwa na

Jessica Campese

© Copyright Jumuiko la Maliasili Tanzania 2011