utafiti unaohusu usimamizi wa misitu na vyanzo vya maji ......wanachama wa kimothon wakijadiliana...

4
Wanachama wa Kimothon wakijadiliana mnamo. February 2018 Utafiti unaohusu usimamizi wa misitu na vyanzo vya maji katika msitu wa Kimothon eneo la Mlima Elgon Mradi wa Minara ya Maji Lengo Kuthibitisha ikiwa na jinsi mashirika ya jamii yanayohifadhi misitu na mashirika ya wanaotumia maji yanavyoshirikiana kusimamia msitu na maji. Kuhusu msitu mdogo wa Kimothon Msitu wa Kimothon unapatikana katika Msitu wa Mlima Elgon, kwenye mpaka wa Kenya na Uganda. Msitu wa Kimothon unasimamiwa na Shirika la Huduma za Misitu la Kenya (KFS) na Shirika la Msitu wa Jamii ya Kimothon (CFA) lenya wanachama wapatao 1000. Makundi hutumia kulisha mifugo, kupata kuni, kupanda miche katika nasari, kufuga nyuki na kwa Mradi wa kubuni mashamba makubwa na kuboresha maisha ya wakazi (Plantation Establishment and Livelihood Improvement Scheme; PELIS). Hakuna chama cha Wanaotumia Maji (Water Resource User Association; WRUA) eneo la Kimothon.

Upload: others

Post on 21-Feb-2021

16 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Utafiti unaohusu usimamizi wa misitu na vyanzo vya maji ......Wanachama wa Kimothon wakijadiliana mnamo. February 2018 Utafiti unaohusu usimamizi wa misitu na vyanzo vya maji katika

Wanachama wa Kimothon wakijadiliana mnamo. February 2018

Utafiti unaohusu usimamizi wa misitu na vyanzo vya maji katika msitu wa Kimothon eneo la Mlima Elgon

Mradi wa Minara ya Maji

LengoKuthibitisha ikiwa na jinsi mashirika ya jamii yanayohifadhi misitu na mashirika ya wanaotumia maji yanavyoshirikiana kusimamia msitu na maji.

Kuhusu msitu mdogo wa KimothonMsitu wa Kimothon unapatikana katika Msitu wa Mlima Elgon, kwenye mpaka wa Kenya na Uganda. Msitu wa Kimothon unasimamiwa na Shirika la Huduma za Misitu la Kenya (KFS) na Shirika la Msitu wa Jamii ya Kimothon (CFA) lenya

wanachama wapatao 1000. Makundi hutumia kulisha mifugo, kupata kuni, kupanda miche katika nasari, kufuga nyuki na kwa Mradi wa kubuni mashamba makubwa na kuboresha maisha ya wakazi (Plantation Establishment and Livelihood Improvement Scheme; PELIS). Hakuna chama cha Wanaotumia Maji (Water Resource User Association; WRUA) eneo la Kimothon.

Page 2: Utafiti unaohusu usimamizi wa misitu na vyanzo vya maji ......Wanachama wa Kimothon wakijadiliana mnamo. February 2018 Utafiti unaohusu usimamizi wa misitu na vyanzo vya maji katika

UongoziUongozi wa CFA una vyeo vitano; mwenyekiti, mwenyekiti msaidizi, katibu, katibu msaidizi na mwekahazina. Kuna mwanamke mmoja (mwekahazina) katika uongozi. Kati ya makundi manne yaliyohusika, kuna mwanamke mmoja (1) mwenyekiti, mwanamke mmoja (1) mwenyekiti msaidizi, wanawake wawili (2) walio wawekahazina na mmoja aliye katibu.

Kawaida, wanawake hushiriki katika shughuli zote za makundi, tofauti na viongozi wanaume wanaochagua shughuli za kushiriki. Wanawake wanasambaza taarifa haraka na wanaaminika kuwa wanyenyekevu kuliko wanaume wanaochukuliwa kuwa wajasiri wanaopata watakalo. Wanawake wana uwezo wa kujadili maswala yanayoathiri wanawake na wanaume.

Kutokana na desturi za kimila na kijamii zinazoimarisha umiliki wa ardhi, wanaume wanaaminika kuwa na mamlaka zaidi, hivyo wanasikilizwa zaidi. Inakuwa rahisi kwao kubuni na kushinikiza masharti. Wanawake huchaguliwa kuwa wawekahazina kwa wakazi wanashikilia ni wawazi, wawajibikaji, hivyo waaminifu.

Uchaguzi wa viongozi wa CFA hufanyika kila baada ya miaka mitatu. Wanachama wa CFA wa Kimothon wamefanya uchaguzi mara mbili tangu wabuni shirika. Makundi maalumu yanayotumia msitu kama vile PELIS yana wanawake wachache katika uongozi kutokana na desturi za kimila na kijamii ambapo wanaume pekee ndio wanaweza kumiliki ardhi.

Shughuli kati ya CFA na WRUAHakuna shughuli zinazofanywa kati ya CFA na WRUA kwani hakuna WRUA katika eneo la Kimothon. Isitoshe, wanachama wa CFA waliohojiwa walisema hawana habari kuhusu WRUA katika eneo hilo.

Mchoro 1. Jinsia na umri wa waliohojiwa katika makundi ya majadiliano

Mchoro 2. Idadi ya makundi ya majadiliano katika kila kundi la watumiaji msitu wa Kimothon

Utaratibu wa utafitiTulichagua makundi manne ya CFA yanayotumia msitu ambayo ni walishaji mifugo, wapataji kuni, wanaopanda miche, wafugaji nyuki na wenye mashamba makubwa na wanaowasaidia wakazi kuboresha maisha (PELIS). Tuliandaa mikutano 16 na wanachama wa makundi hayo, viongozi wa makundi hayo na wakazi wasio wanachama wa CFA. Tena, tuliwahoji, mara tatu, viongozi wa CFA. Kwa jumla, tulizungumza na washirika 149 (wanaume 87 na wanawake 62), wenye umri tofauti kama mchoro 1 unavyoonyesha.

2

3

4

0

10.5

1.5

2.5

3.5

4.5

Ufugaji

Nasari y

a mich

e

Kuni

Wasio

wanach

amaViongozi

wa makundi

ya watu

miajiPELIS

20%

24%14%

18%

8%

16%Wanawake wachanga (18-35)

Wanawake wazee (Zaidi ya 35)

Wanaume wachanga (18-35)

Wanawake wazee (Zaidi ya 35)

Wanawake wachanga na wazee

Wanaume wachanga na wazee

Page 3: Utafiti unaohusu usimamizi wa misitu na vyanzo vya maji ......Wanachama wa Kimothon wakijadiliana mnamo. February 2018 Utafiti unaohusu usimamizi wa misitu na vyanzo vya maji katika

Jinsi CFA na WRUA yanavyoweza kushirikianaIngawa hakuna WRUA katika eneo hilo, wanachama wa CFA walisema ni muhimu WRUA kubuniwa na kupendekeza shughuli ambazo wanaweza kushirikiana kutekeleza. Baadhi ya shughuli walizopendekeza ni: • Kulinda vyanzo vya maji, kulinda sehemu zinazopakana

na mito, visima, kuhakikisha wenye ardhi wanalinda eneo la mita 30 kutoka mto, kulingana na sheria.

• Kupanda nasari za miche na kupanda miti ikiwemo miti inayohifadhi maji kama vile bamboo, Msemwa, Sosiondet na Lamaiywet.

• Kujenga mitaro kuzuia mmonyoko wa udongo.• Kuwafunza na kuwahamasisha wakazi kuhusu umuhimu

wa kulinda misitu na maji.

Kushiriki katika mikutano na shughuli za CFAHakuna WRUA eneo la Kimothon hivyo hakuna mikutano kati ya WRUA na CFA. Kawaida, wanachama wa CFA huandaa mikutano 3-5 kila mwaka, ukiwemo mkutano mmoja mkuu (AGM) kila mwisho wa mwaka, ingawa wakati mwingine huandaa mikutano baada ya miezi mitatu. Huandaa mikutano ya dharura maafisa wakuu wa serikali ama wageni wakiwatembelea.

Asili mia 70% ya wanachama wa Kimothon huhudhuriwa na kushiriki katika mikutano ya CFA. Katika mikutano, wanachama hutoa maoni kuhusu maswala mbalimbali yakiwemo ya wanachama wote kupata ardhi ya kulima na kushiriki katika maamuzi kama vile kubuni sheria na kuchagua viongozi. Wanachama walitoa sababu tofauti za kutohudhuria mikutano. Walisema baadhi yao hukosa mikutano kwa sababu hawaambiwi mapema, wengine hawaridhishwi na viongozi. Wengine wanadai majukumu ya familia yanawanyima nafasi ilhali wengine wanasema CFA huwabagua maskini na wasiojiweza.

Wanachama walipendekeza wajulishwe mapema tarehe ya mikutano ili waweze kuhudhuria. Pia walisema wanaokosa kuhudhuria mikutano bila kutoa sababu ama kukosa kushiriki watozwe faini.

MwishoWanachama wa CFA wanasema msitu asili imepungua katika miaka 10 iliyopita kutokana na kuongezeka kwa mashamba na makao ya watu. Kadhalika, walisema sababu nyingine ambazo zimeathiri eneo la msitu ni maji kupunguka katika mito, matope kuongezeka katika mito na mmonyoko wa udongo. Baadhi ya mambo yanayowazuia wanachama kushiriki katika mikutano na shughuli za CFA ni kukosa kujulishwa kuhusu mikutano mapema. Kuna wanawake wachache katika nafasi za uongozi. Kati ya vyeo 5 katika usimamizi wa CFA, kuna mwanamke tu mmoja (1) ambaye ni mwekahazina. Katika makundi ya watumiaji misitu, kuna mwanamke mmoja (1) mwenyekiti, wanawake mara nyingi huwa wawekahazina katika makundi ya watumiaji misitu. Hakuna shirika la WRUA katika eneo la Kimothon. Hii ni nafasi bora ya CFA kubuni WRUA ili kupanua miradi ya usimamizi wa misitu na maji.

Mapendekezo• Kuwafunza na kuwahamasisha wanachama wa CFA ili

wafahamu zaidi majukumu yao katika kuhifadhi msitu na maji.

• Kuwafunza na kuwahamasisha wanachama wa CFA kuhusu majukumu ya wanachama wote na umuhimu wa kuwahusisha wanawake zaidi katika uongozi wa CFA na wa makundi.

Kufunza na kuhamasisha jamii kuhusu kubuni WRUA, haswa kuhimiza pande hizo mbili kuungana katika usimamizi wa msitu na maji, ajenda kuu ikiwa kuongeza kiwango cha maji na ubora yake.

Page 4: Utafiti unaohusu usimamizi wa misitu na vyanzo vya maji ......Wanachama wa Kimothon wakijadiliana mnamo. February 2018 Utafiti unaohusu usimamizi wa misitu na vyanzo vya maji katika

cifor.org/water-towers forestsnews.cifor.org

Center for International Forestry Research (CIFOR)CIFOR advances human well-being, equity and environmental integrity by conducting innovative research, developing partners’ capacity, and actively engaging in dialogue with all stakeholders to inform policies and practices that affect forests and people. CIFOR is a CGIAR Research Center, and leads the CGIAR Research Program on Forests, Trees and Agroforestry(FTA). Our headquarters are in Bogor, Indonesia, with offices in Nairobi, Kenya; Yaounde, Cameroon and Lima, Peru.

The CGIAR Research Program on Forests, Trees and Agroforestry (FTA) is the world’s largest research for development program to enhance the role of forests, trees and agroforestry in sustainable development and food security and to address climate change. CIFOR leads FTA in partnership with Bioversity International, CATIE, CIRAD, ICRAF, INBAR and TBI.

FTA’s work is supported by the CGIAR Trust Fund.