jarida la nishati na madini
DESCRIPTION
JARIDA LA NISHATI NA MADINITRANSCRIPT
-
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]
Simbachawene: TANESCO sogezeni huduma vijijini ... Uk 8
HABARI ZA NISHATI &MADINI
Toleo No. 67 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 15-21 Mei, 2015
BulletinBulletinBulletinBulletinNews
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]
http://www.mem.go.tz
HABARI ZA NISHATI &MADINI
Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015
JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini Stephen Masele
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga
Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba
Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya
Wabunge Soma habari Uk. 2
Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2
Uuzaji madini ya Bati wasainiwa
Wachimbaji wadogo Kyerwa kunufaika Wanunuzi haramu waonywa
Mkataba
Soma habari Uk. 2
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO Mhandisi Edwin Ngonyani
-
2 BulletinBulleBulleNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
Mkataba madini ya Bati Na Issa Mtuwa -
STAMICO
Imeelezwa kuwa, kusainiwa Mkataba wa ununuzi wa madini ya Bati (Tin) baina ya KYERWA TIN COM-PANY LTD ambayo ni
kampuni tanzu ya Shirika la Ma-dini la Taifa (STAMICO) na DAR GOLD DMCC LTD ya Dubai ni moja ya mkataba wenye manufaa na maslahi si tu kwa STAMICO bali ni neema kwa wachimbaji wa-dogo wa madini hayo ya bati ya wilaya ya Kyerwa, mkoani Kag-era.
Akizungumza mara baada ya kutiliana saini mkataba huo ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandi-si Edwin Ngonyani, alisema kuwa, wameingia mkataba huo kwa kuzingatia maslahi ya Taifa kwani Wachimbaji wadogo wa madini ya Bati watanufaika kwa kupata soko la uhakika na bei nzuri.
Aidha, Ngonyani aliongeza kuwa, bei ya kununulia kutoka kwa wachimbaji wadogo itakuwa inabadilika kwa kadri bei ya kuuzia katika soko la metali la Uingereza (LME) itakavyobadi-lika, ambapo muda wote STAM-ICO itabakiwa na faida isiyozidi asilimia 5-10.
STAMICO haikusudii kupata faida kubwa katika biashara hii kwa sababu lengo mahsusi la Shirika ni kuwasaidia wachimbaji wadogo wainuke na sio kupata faida, alieleza Ngonyani.
Mhandisi Ngonyani alisema kuwa, katika mkataba huo masu-ala kadhaa yamezingatiwa husu-san suala la bei. Kusainiwa kwa mkataba huo kunaleta uhakika wa soko la kuaminika la madini ya bati jambo ambalo kwa muda mrefu lilikuwa ni tatizo,alisema Mhandisi Ngonyani.
Alisema moja ya makubaliano waliyofikia ni kuwa, uuzwaji wa madini hayo utakuwa unazin-gatia bei ya soko la dunia jambo ambalo linaondoa mjadala wa kujadili bei ya kuuzia.
Aliongeza kuwa, hivi sasa uhakika wa kununua madini hayo kutoka kwa wachimbaji wadogo upo kwa kipindi chote bila kusimama kwa kuwa uhakika wa soko upo, tofauti na awali ambapo tatizo la soko lilikuwa ni kikwazo. Hivyo, amewaonya wanunuzi haramu wanaotoro-sha madini hayo nje ya nchi bila kulipa kodi stahiki wafunge virago warudi walikotoka maana kuanzia sasa hawatapata nafasi ya kununua, na Serikali itakuwa
Vijiji, Halmashauri washauriwa kuomba leseni madini ya ujenziNa Greyson Mwase, Dodoma
Waziri wa Ni-shati na Ma-dini George Simbachawene amesema kuwa
kwa leseni za uchimbaji wa madini ya ujenzi ipaumbele kiwe kwa vijiji na Halmashauri badala ya kumi-likiwa na watu binafsi ili kuongeza kipato kwa wananchi wa eneo husika
Simbachawene aliyasema hayo wilayani Kibakwe mkoani Dodoma wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya umeme vijijini inayosi-mamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) pamoja na kuzungumza na wananchi.
Alisema kuwa leseni za uchim-baji wa mchanga na mawe zina-pomilikiwa na watu binafsi wenye kuhodhi maeneo makubwa, kijiji hukosa mapato yake stahiki.
Ndugu zangu napenda ifikie mahali leseni za uchimbaji wa mchanga na mawe zimilikiwe na kijiji ili kuongeza pato la kijiji badala ya kuwapa watu binafsi ambao hunufaika zaidi, alisema Simbachawene.
Akielezea mikakati ya ku-wawezesha wachimbaji wadogo, Simbachawene alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikitoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo wenye vigezo na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo kwa kuunda vikundi vidogo vidogo na kuomba ruzuku.
Alitaja vigezo vinavyotumika wakati wa kutoa ruzuku kuwa ni pamoja na kuwa na leseni ya uchimbaji madini na kuwa na eneo lililofanyiwa utafiti.
macho kulinda maslahi yake. Kwa upande wake mratibu
wa mradi huo Raymond Rwe-
humbiza alisema kuwa, mkataba ulioingiwa una maslahi na Shirika halitapata hasara kutokana na jinsi mradi huo utakavyoendesh-wa, kutokana na kwamba, awali
tatizo la soko lilikuwa ni kikwazo kikubwa cha mradi.
Rwehumbiza alieleza kuwa, kuanzia kwa Shirika litaanza kumuuzia mteja wao huyo mpya jumla ya tani 40 za madini ya Bati zilizopo Kayanga wilayani kyerwa kwa kuzingatia makubaliano ya mfumo wa bei ya dunia siku ya kuuza.
Kuhusu bei ya kununulia kutoka kwa wachimbaji wadogo Rwehumbiza alisema wachimbaji wadogo watanufaika kwanza na uhakika wa kununuliwa madini yao muda wote watakapoyapata lakini pili ni ununuzi utakaozin-gatia hali ya bei ya soko la dunia kwa kipindi husika. Kwa kuwa STAMICO lengo letu ni kubore-sha na kuinua hali na vipato vya wachimbaji wadogo ni dhamira ya Shirika kununua kwa bei nzuri, aliongeza Rwehumbiza.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) akisaini moja ya mikataba ambayo STAMICO imewahi kuingia na wadau mbalimbali. Kushoto ni Mwanasheria wa STAMICO, Mudrikat Kiobya. (Picha na Maktaba)
Alisema moja ya
makubaliano waliyofikia ni kuwa, uuzwaji wa ma-dini hayo utakuwa unazin-gatia bei ya soko la dunia jambo ambalo linaondoa mjadala wa kujadili bei ya kuuzia.
K
George Simbachawene
-
3BulletinBulleBulleNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
TahaririMEM
Na Badra Masoud
FIVE PILLARS OF REFORMS
KWA HABARI PIGA SIMU KITENGO CHA MAWASILIANO
BODI YA UHARIRI MHARIRI MKUU: Badra Masoud
MSANIFU: Essy OgundeWAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James
na Nuru Mwasampeta
INCREASE EFFICIENCYQUALITY DELIVERY
OF GOODS/SERVICESATISFACTION OF
THE CLIENTSATISFACTION OF
BUSINESS PARTNERS
SATISFACTION OF SHAREHOLDERS
TEL-2110490FAX-2110389
MOB-0732999263
Habari kubwa katika jarida la leo ni kusainiwa kwa Mkataba wa ununuzi wa madini ya Bati (Tin) baina ya kampuni ya KYERWA TIN LTD ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na DAR GOLD DMCC LTD ya nchini Dubai.
Tumeelezwa kuwa huu ni moja ya mkataba wenye manufaa na maslahi makubwa sio tu kwa STAMICO bali ni neema kwa wachim-baji wadogo wa madini ya bati nchini hasa katika wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera ambapo madini hayo yanapatikana kwa wingi.
Akizungumza mara baada ya kutiliana saini mkataba huo ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Kaimu Mkurugenzi Mtend-aji wa STAMICO Mhandisi Edwin Ngonyani, alisema kuwa, STA-MICO imeingia mkataba huo kwa kuzingatia maslahi ya Taifa kwani Wachimbaji wadogo wa madini ya Bati watanufaika kwa kupata soko la uhakika na bei nzuri.
Ngonyani alisema kuwa STAMICO haikusudii kupata faida kub-wa katika biashara hii kwa sababu lengo mahsusi la Shirika hilo ni kuwasaidia wachimbaji wadogo wainuke na sio kupata faida.
Kusainiwa kwa mkataba kunathibitisha uhakika wa kuwepo kwa soko la kuaminika la madini ya bati jambo ambalo kwa muda mrefu lilikuwa ni changamoto kwa wachimbaji wa madini husika.
Jambo la kutia moyo ni kuwa pande hizo mbili zimekubaliana kuwa uuzwaji wa madini hayo utakuwa unazingatia bei ya soko la du-nia jambo ambalo linaondoa mijadala mirefu ya kujadili bei ya kuuzia. Hii ni kusema kuwa suala la kuwadhulumu wachimbaji wa madini haya sasa limefikia tamati.
Vilevile wachimbaji wetu sasa wana uhakika wa kuuza madini hayo kwa kipindi chote bila kusimama kwa kuwa uhakika wa soko upo, tofauti na awali ambapo tatizo la soko lilikuwa ni kikwazo.
Baada ya kusaini mkataba huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi Edwin Ngonyani alitoa onyo kwa wanunuzi haramu wanaotorosha madini hayo nje ya nchi bila kulipa kodi stahiki wafunge virago warudi walikotoka maana kuanzia sasa hawatapata nafasi ya kununua, na Serikali itakuwa macho kulinda maslahi yake.Hili linawezekana kwa kuwa sasa wachimbaji wadogo wanajua wapi pa kupeleka madini yao na si kuwauzia wafanyabashara haramu.
Ili kuonyesha kuwa suala hili si bla bla, Kwa kuanzia STAMICO itaanza kumuuzia mteja wao huyo mpya jumla ya tani 40 za madini ya Bati zilizopo katika eneo la Kayanga wilayani Kyerwa kwa kuzingatia makubaliano ya mfumo wa bei ya dunia siku ya kuuza.
Heko STAMICO chini ya Kaimu Mkurugenzi, kwa kuwa mnaonesha kwa vitendo jinsi mnavyoendelea kuwasimamia vyema wachimbaji wetu wadogo nchini katika masuala mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu kuhusu Sekta ya Madini na kuwatafutia masoko ya madini yao.
Tunawatakia kila la heri STAMICO kwa kufungua njia kwa wachimbaji wadogo ikiwemo hao wa Kyerwa na wengine ambao wa-nahitaji kuwezeshwa.
TEL-2110490FAX-2110389
MOB-0732999263
Kupatikana kwa soko la madini ya Bati, fursa muhimu kwa wachimbaji wadogo
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa sita kutoka kushoto, mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme vijijini, Awamu ya pili katika kanda hiyo, mara baada ya kumaliza kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa miradi husika. Kulia kwa Naibu Waziri ni Meneja Mwandamizi wa Tanesco Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Salome Nkondola na kushoto kwa Naibu Waziri ni Kaimu Meneja wa Tanesco katika mkoa wa Mbeya, Magwila Mbalamwezi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa pili kushoto) akiangalia nguzo zinazotumika kusambaza umeme vijijini katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kabla ya kuzindua mradi wa umeme ambao umewezesha vijiji sita katika kata hiyo kuunganishwa na huduma ya umeme. Vijiji hivyo ni Kapyo, Ilongo, Ilaji, Igalako, Mchongole na Igalako. Wengine katika picha ni Kaimu Meneja wa Tanesco katika mkoa wa Mbeya, Magwila Mbalamwezi (kulia kwa Naibu Waziri) na Afisa Miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Emmanuel Yesaya (kushoto kwa Naibu Waziri).
George Simbachawene
-
4 BulletinBulleBulleNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
TanzaniaKushirikiana na Japan Sekta ya Nishati
Na Veronica Sim-ba, Dar es Salaam
Wizara ya Nishati na Madini ina-panga kushiriki-ana na Kampuni ya Mitsubishi
Hitachi Power System ya Japan katika kuendeleza Sekta ya Nishati nchini.
Kamishna Msaidizi wa Umeme wa Wizara, Mhandisi Innocent Luoga aliyasema hayo hivi karibu-ni baada ya kukutana na uongozi wa juu wa kampuni hiyo, Makao
Makuu ya Wizara jijini Dar es Sa-laam.
Mhandisi Luoga alisema katika kikao hicho, Ujumbe wa kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power Sys-tems Ltd uliwasilisha mapendek-ezo ya matumizi ya teknolojia ya kisasa ya kufua umeme kutokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo makaa ya mawe, Jotoardhi na Gesi.
Sisi kama Serikali, kupitia taasisi zetu tumeona ni vema tush-irikiane na Kampuni hii ambayo inajishughulisha na kutengeneza mitambo ya kufua umeme wa Gesi, Makaa ya Mawe na Jotoardhi kwa kutumia teknojia ya kisasa. Hii ni kutokana na vyanzo vipya
vya umeme tulivyonavyo hususan makaa ya mawe na jotoardhi, am-bavyo hatujaanza rasmi kuvitumia kuzalisha umeme, alisema Kam-ishna Luoga.
Aliongeza kuwa, lengo la Seri-kali ni kuhakikisha umeme wa ku-tosha, wa uhakika na wa bei nafuu unazalishwa na kusambazwa nchi-ni ili kuwaletea wananchi maen-deleo na hivyo kuinua pato la Taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa, Kampuni hiyo ilishafanya majadiliano kuhusu ushirikiano katika Sekta ya Nishati na taasisi zilizo chini ya Wizara am-bazo ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) pamoja na Shirika la Ma-dini la Taifa (STAMICO).
Akizungumzia kuhusu faida za matumizi ya teknolojia hiyo ya kisasa inayotumika kufua umeme, Kamishna Luoga alizitaja kuwa ni pamoja na kuwa rafiki wa mazin-gira, kuwezesha uhakika wa kufua umeme kwa bei nafuu pamoja na kufua umeme kwa ufanisi mkub-wa.
Awali, katika kikao hicho baina ya Wizara na Kampuni hiyo, Rais wa Kampuni, Takato Nishizawa alisema kampuni yake iko tayari kutoa mafunzo ya namna ya ku-
tumia mitambo yao inayotumia teknolojia hiyo ya kisasa kwa Wa-handisi wa kitanzania.
Aidha, Nishizawa alitoa mwa-liko kwa wataalamu hao kutoka Tanzania, kutembelea mitambo hiyo nchini Japan kwa lengo la ku-jifunza zaidi.
Katika hatua nyingine, iliele-zwa kuwa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd, tayari imeingia mkataba na Kampuni ya Sumitomo ambayo inatekeleza Mradi wa Kufua Umeme wa gesi wa Kinyerezi II unaofikia kiasi cha Megawati 240, kwa kazi ya kufunga mitambo ya kufua umeme (gas turbines) aina ya Hitachi.
Makamu Rais wa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd, Satoshi Uchida (Kulia), akifafanua jambo kwa Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini, wakati wa kikao baina yao kilichojadili ush-irikiano katika sekta ya nishati. Kikao kilifanyika Mei 12, 2015 Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Makamu Rais wa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd, Satoshi Uchida (Kulia), akifafanua jambo kwa Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini, wakati wa kikao baina yao kilichojadili ush-irikiano katika sekta ya nishati. Kikao kilifanyika Mei 12, 2015 Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Rais wa Kampuni ya Mitsubishi Hitachi Power System Ltd, Takato Ni-shizawa (Kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Umeme wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Innocent Luoga (Kulia) (Walioshikana mikono), wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa kutoka Kampuni hiyo na Wataalamu wa Wizara, mara baada ya kikao baina yao kilicho-jadili ushirikiano katika sekta ya nishati nchini. Kikao kilifanyika Mei 12, 2015 Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam.
02
01
031
2
3
-
5BulletinBulleBulleNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI GEORGE SIMBACHAWENE KATIKA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA UMEME YA REA MKOA WA DODOMA
Baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati, Sosthenes Masolla (wa nne kutoka kulia) wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (hayupo pichani) katika kijiji cha Chinyanghuku wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kushoto) akikabidhi mfano wa zawadi ya jezi kwa mmoja wa wasanii wa kikundi cha sanaa kijulikanacho kama Neema Group, Ackley Mwaluka katika kijiji cha Chaludewa kilichopo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Sehemu ya wakazi wa Kata ya Mulunduzi wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (hayupo pichani)
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akisalimiana na Diwani wa Kata ya Mulunduzi Hitler Chambilu (kushoto) mara baada ya kuwasili katika kata hiyo iliyopo katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia chini) akiangalia mafundi kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) waliokuwa wakiendelea na kazi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika Kata ya Mulunduzi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kushoto) akikabidhi zawadi ya jezi na mpira wa miguu kwa mmoja wa wanamichezo wa timu ya mpira wa miguu ya Chaludewa wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
-
6 BulletinBulleBulleNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
Na Greyson Mwase, Dodoma
Waziri wa Nishati na Madini, George Sim-bachawene ameliagiza Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kutoa mafunzo pamoja na vibali kwa mafundi umeme nchini kote watakaofanya kazi ya kuweka mifumo ya umeme kwenye nyumba kabla ya kuunganishwa kwenye miundombinu ya umeme inayojengwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Tanesco.
Simbachawene alitoa agizo hilo katika ziara yake ali-yoifanya katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma ya kukagua miradi ya umeme vijijini ili kujionea maendeleo yake, pamoja na kuzungumza na wananchi. Miradi hiyo iliyopo chini ya Awamu ya Pili ya REA inatarajiwa kuka-milika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.
Alisema katika kujiandaa na huduma ya umeme, wa-nanchi wanatakiwa kuwekewa mifumo ya umeme (wir-ing) katika nyumba zao na wataalamu waliothibitishwa na Tanesco na kupewa leseni pamoja na mafunzo ili kuondo-kana na majanga ya moto yanayosababishwa na ufungaji holela wa mifumo ya umeme.
Alieleza kuwa katika utekelezaji wa miradi ya REA kumekuwepo na mafundi wasiotambulika na Tanesco wanaojulikana kama vishoka ambao wamekuwa wakiji-tokeza kwenye makazi ya watu na kudai kuwa ni mafun-di kutoka Tanesco na kuwawekea mifumo mibovu ya umeme hali inayopelekea hasara kubwa ya kuunguliwa na nyumba baadaye.
Alisisitiza kuwa ili kukabiliana na mafundi ambao ni vishoka Tanesco inatakiwa kuchagua makampuni na mafundi binafsi ambao ni wataalamu wenye leseni na ku-tambuliwa na shirika hilo na kuwapa mafunzo kabla ya kuanza zoezi la kuweka mifumo ya umeme kwenye nyum-ba za wananchi wanaotarajiwa kufungiwa umeme chini ya mradi wa REA awamu ya pili.
Aliongeza kuwa mara baada ya mafundi hao kupatiwa mafunzo na Tanesco, watapewa barua maalum za utam-bulisho au hati maalum zitakazotumika wakati wa uende-shaji wa zoezi hilo
Simbachawene alisema kuwa hatua hiyo inatokana na mikakati ya serikali katika kuwapunguzia wananchi gharama na muda wa kufuatilia huduma za kufungiwa mifumo ya umeme katika nyumba zao mijini.
Aliendelea kusema kuwa mbali na kuwapunguzia wa-nanchi gharama na muda wa ufuatiliaji wa kufungiwa mi-fumo ya umeme katika nyumba zao, mpango huo utaleta ushindani wa gharama kati ya makampuni na mafundi binafsi wenye leseni zinazotambuliwa na Tanesco.
Akielezea hali ya uunganishaji wa umeme nchini Simbachawene alisema mwaka 2005 wakati Serikali ya Awamu ya Nne inaingia madarakani, ni asilimia 10 tu ya wananchi walikuwa na umeme lakini hadi kufikia mwaka 2015, asilimia 36 ya wananchi wana umeme na kusisitiza kuwa mara baada ya miaka mitano asilimia ya wananchi wenye umeme itakuwa ni 45 na kuifanya Tanzania kuwa nchi inayoongoza Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa ku-waunganishia umeme wananchi waishio vijijini.
Hii ni hatua kubwa ambayo tumepiga kama Serikali na bado tutaendelea kuhakikisha kuwa wananchi wote hasa waishio vijijini wanapata umeme wa uhakika in-gawa tutafanya kwa awamu tofauti tofauti, alisema Sim-bachawene.
Simbachawene alifafanua kuwa ingawa sio rahisi ku-weka umeme katika vijiji vyote kwa pamoja nchi nzima, miradi ya REA itatekelezwa kwa awamu tofauti tofauti.
Simbachawene aliwataka wananchi kushirikiana na Tanesco pamoja na REA katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme kwa kutoa sehemu ndogo ya mashamba yao ili ziweze kuwekwa nguzo za umeme ili waanze kunufaika na umeme huo mara moja.
Wakati huo huo Afisa Uhusiano - Huduma kwa Wate-ja wa Tanesco mkoa wa Dodoma Innocent Lupenza alise-ma kuwa kwa wananchi wenye nyumba zenye vyumba viwili hawatahitaji kufungiwa mifumo ya umeme, badala yake watawekewa kifaa maalumu kujulikanacho kwa jina la UMETA yaani Umeme Tayari.
Akielezea kifaa hicho, Lupenza alisema kuwa kifaa hi-cho kitamwezesha mtumiaji kuwasha taa mbili pamoja na matumizi mengine madogo kama pasi na kuongeza kuwa kifaa hicho kitauzwa kwa shilingi 42, 480
Akielezea taratibu za kufungiwa umeme kwenye ny-umba Lupenza alisema wananchi waliopo umbali wa mita 30 toka ilipo miundombinu ya umeme watalipia shilingi 27,000.
Alisema katika hatua za awali wananchi watatakiwa kulipia fomu kwa shilingi 5900 na baada ya hapo mkandar-asi atafanya ukaguzi wa mifumo ya umeme iliyowekwa ka-tika nyumba husika kabla ya kuiunganisha nyumba hiyo na miundombinu ya umeme.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kushoto) akitoa maelekezo kwa Afisa Uhusiano - Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) mkoa wa Dodoma, Innocent Lupenza (kulia) mara baada ya kuwasili katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme vijijini. Waziri Simbachawene aliyekuwa mkoani Dodoma kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili na Tanesco pamoja na kuzungumza na wananchi. Katikati ni Katibu wa Waziri Simbachawene Mhandisi Joseph Kumburu.
Tanesco yaagizwa kutoa vibali kwa mafundi umemeWananchi epukeni matapeli wa madini Na Greyson Mwase, Dodoma
Wananchi wametakiwa kuepuka matapeli katika biashara ya madini kwa kuwasili-sha mawe wanayohisi kuwa yana madini kwenye ofisi za madini ili kuweza kubaini thamani yake.
Wito huo ulitolewa na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati, Sosttenes Masolla wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene aliyoifanya ka-tika mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na kuzungumza na wananchi.
Akitoa ufafanuzi katika moja ya mikutano hiyo, Masolla alisema kuwa imekuwa ni kawaida ya wananchi, kupeleka mawe wanayohisi kuwa yana madini kwa watu wasio wataal-am wa madini ambao ni matapeli na hivyo kupata hasara kubwa.
Akieleza hatua za kufuata baada ya kupata mawe wanay-ohisi kuwa yana madini, Masolla alisema kuwa mwananchi anapoona jiwe hilo anatakiwa kufika nalo katika ofisi za madini na kukabidhi kwa wataalam wa madini ambalo wa-takagua jiwe hilo ili kubaini aina na kiwango cha madini kili-chopo.
Alisema mara baada ya kubainika kwa kiwango cha madi-ni katika jiwe, wataalam wa madini watampatia mwananchi fomu ya maombi ya leseni ya uchimbaji madini baada ya kubaini eneo kama liko wazi.
Baada ya kufanikiwa kupata leseni, mwananchi atakuwa huru kufanya shughuli za uchimbaji wa madini na kulipa kodi kama mchimbaji mwingine yeyote, alisema Masolla.
Masolla aliongeza kuwa ofisi pia inaweza kusaidia ku-muunganisha mchimbaji wa madini na wanunuzi wa madini wenye leseni kupitia Wizara ya Nishati na Madini.
Masolla alisema kuwa mara nyingi wananchi wanapowa-patia matapeli mawe wanayohisi kuwa yana madini, matape-li hao huchukua mawe yao na kuwazunguka kwa kuomba leseni na kumilikishwa maeneo bila ya wao kuwa na taarifa hali inayopelekea kuwepo kwa migogoro.
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati, Sosthenes Masolla akitoa ufafanuzi wa jinsi ya kupata leseni za madini mbele ya wananchi wa kijiji cha Ikuyu huko Kibakwe mkoani Dodoma.
-
7BulletinBulleBulleNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
http://www.mem.go.tz
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI, CHARLES MWIJAGE KANDA YA KUSINI
ZIARA YA MWIJAGE
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (kushoto) akizungumza na wananchi katika katika kijiji cha Lilondo, wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma, mara baada ya kuzindua mradi wa umeme wa kiasi cha kilowati 40 uliobuniwa na wananchi hao ambao umeshanufaisha nyumba 100.
. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro (wa pili kushoto) akimwonyesha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa kwanza kushoto, ramani ya mkoa wa Mbeya ambayo pia inaonyesha kilipo chanzo cha jotoardhi mkoani humo ambacho kikiendelezwa kitazalisha nishati ya umeme. Naibu Waziri alifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kabla kufanya kikao na Mameneja Tanesco wa mikoa na wilaya katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ya usambazaji umeme vijijini, Awamu ya pili katika kanda hiyo
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa tatu kulia) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama (katikati) ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Peramiho, wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa mradi wa umeme wa kiasi cha kilowati 40 uliobuniwa na wananchi katika kijiji cha Lilondo, wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mwenye suti ya kaki) akilakiwa na wananchi katika kijiji cha Kanga wilayani Chunya wakati alipofika kijijini hapo ili kukagua utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini Awamu ya Pili inayotekelezwa na TANESCO kwa kushirikiana na REA.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mwenye shati la mistari) akiangalia jinsi wateja wanavyohudumiwa katika ofisi za Tanesco, Makambako, mkoani Njombe. Naibu Waziri alitembelea ofisi hizo akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa katika Kanda ya Kusini pamoja na kuzindua kituo cha kufua umeme mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa tatu kutoka kushoto) akiangalia nyaya zinazotumika kusambaza umeme mkubwa wa 33/11KV na umeme mdogo wa 400/230V katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kabla ya kuzindua mradi wa umeme ambao umewezesha vijiji sita vya Kapyo, Ilongo, Ilaji, Igalako, Mchongole na Igalako kuunganishwa na huduma ya umeme.
-
8 BulletinBulleBulleNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya Nishati na Madini Karibu tuhabarishane na
tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINITANZANIA GEMOLOGICAL CENTRE
MAOMBI YA UDAHILI NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2015/2016
Kituo cha Tanzania Gemological Centre(TGC) kinakaribisha maombi ya kujiunga ngazi ya cheti kwa kozi zifuatazo, zitakazoanza 15 Juni 2015 1.Ukataji na usanifu wa madini ya vito (Lapidary) 2.Uchongaji wa Vinyago vya Mawe (Stone Carving)Muda wa kozi ni miezi sita (6)
SIFA ZA MUOMBAJIMuombaji anatakiwa awe amehitimu kidato cha nne na kufaulu kwa kiwango cha daraja D katika masomo ya Kiingereza na Hisabati na masomo mawili kati ya masomo yafuatayo; Kemia, Fizikia, Jiografia, Biashara, Bookkeeping, na Accounts au Uchumi
JINSI YA KUOMBAFomu za maombi zinapatikana kituoni (TGC), ofisi za madini kanda na ofisi za maafi-sa madini wakazi nchi nzima. Ada ya maombi kiasi cha shilingi 10,000/= ilipwe kupitia benki: National Microfinance Bank (NMB), Jina la Akaunti: Tanzania Gemological Cen-tre, Namba ya Akaunti: 40801000074. Fomu ya kuweka fedha benki iwasilishwe kituoni kama ushahidi wa malipo. Kituo hakipokei fedha taslimu. Mwisho wa kupokea maombi ni 22/05/2015Maombi yatapokelewa na kufanyiwa kazi yakiwa na fomu ya kuweka fedha benki, maelezo binafsi ya muombaji yaliojitosheleza na historia ya elimu yake pamoja na vivuli vya vyeti vya elimu ya kidato cha nne na cheti /ushahidi unaodhibitisha sifa za muombaji pamoja na cheti cha kuzaliwa.Maombi yaambatanishwe na vivuli vya vyeti vya elimu yatumwe kwa;
Mratibu, Tanzania Gemological Centre, P. O. Box 119, ARUSHA.
Na Greyson Mwase, Dodoma
Waziri wa Nishati na Madini, George Sim-bachawene amelitaka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kusogeza huduma ya kuwaunganishia umeme wananchi vijijini badala ya wananchi kufunga safari mji-ni kwa ajili ya kufuata huduma ya kuunganishiwa umeme kwenye nyumba zao.
Simbachawene alitoa agizo hilo akiwa Kibakwe mkoani Do-doma alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya umeme vi-jijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili kwa kushirikiana na Shiri-ka la Umeme Nchini (TANESCO) pamoja na kuzungumza na wa-
nanchi ili kutatua kero zao.Alisema ili kuwarahisishia
wananchi maombi ya kuungan-ishiwa umeme, ni vyema Tanesco ikapanga siku maalum na kwenda katika kijiji husika na kuwasaidia wananchi kujaza fomu, pamoja na kulipia badala ya wananchi kufunga safari hadi mjini kufuata fomu, kujaza na kuzirejesha.
Mfano fomu ya maombi ya kuunganishiwa umeme ni shilingi 5,900 sasa mwananchi anapo-tumia zaidi ya shilingi 20,000 kama gharama ya nauli kwenda kufuata fomu halafu ajaze na kurudisha inakuwa ni kazi nzito yenye ghara-ma kubwa na kupoteza muda wa mwombaji, hii inapelekea zoezi kusuasua, hivyo basi wanachi wasogezewe huduma karibu, ali-sisitiza Simbachawene.
Alisema kwa kutambua umuhimu wa umeme katika uku-aji wa uchumi wa nchi, serikali imekuwa ikiweka mikakati mbal-imbali ya kusambaza umeme hu-susan maeneo ya vijijini pamoja na kuwakaribisha wawekezaji ku-toka ndani na nje ya nchi.
Vilevile alitoa angalizo kuwa, wananchi wanatakiwa ku-changamkia fursa zinazowekwa na serikali kwa kujipatia kipato na hivyo kuwa na maisha bora bada-la ya kulalamika. Aliendelea kuse-ma kuwa ile kauli ya Maisha bora kwa kila mtanzania haikumaani-sha serikali kumfanyia mwa-nanchi kila kitu bali mkakati wa serikali ni kuwawezesha wananchi kwa kuwapa fursa za kiuchumi ikiwa ni pamoja na umeme.
TANESCO Sogezeni huduma vijijini Simbachawene TANESCO