jarida la wiki la nishati na madini, toleo la 117

Upload: ahmad-issa-michuzi

Post on 06-Jul-2018

354 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • 8/17/2019 JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI, TOLEO LA 117

    1/12

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali

    kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizar a ya Nishati na MadiniWasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263

    au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM)

    HABARI ZA

    NISHATI &MADINI

    Toleo No. 117 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Aprili 28 - Mei 4, 2016Bulletinews

     

    http://www.mem.go.tz

     

    Prof. Sospeter Muhongo

    Ni Rasmi

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akipunga mkono mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndegewa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini Uganda ambapo ilitangazwa Bomba la mafuta litajengwa kutoka Hoima nchini Ugandahadi Bandari ya Tanga. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa aliyeambatana na Waziri nchiniUganda. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, nyuma kutoka kushotoni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe, Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Maendeleo yaNishati, James Andilile na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio.

    n  Bomba la Mafutakupita Tanzania

    n  Reli, Barabara, Usalama vyachangia ushindi >>SOMA UK. 2

  • 8/17/2019 JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI, TOLEO LA 117

    2/12

    BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    2

    Na Asteria Muhozya, DSM

    Waziri wa Nishati naMadini, ProfesaSospeter Muhongoamesema kuwa,

     bomba la kusafirishamafuta ghafi kutoka Hoima ZiwaAlbert nchini Uganda litapita nchini

     baada ya hoja za Tanzania kupitisha bomba hilo nchini kukubaliwa naUganda.

    Profesa Muhongo aliyasema hayomwishoni mwa wiki, mara tu baadaya kuwasili katika Uwanja wa Ndegewa Kimataifa wa Mwalimu Julius

    Nyerere (JNIA), akitokea nchiniUganda, ambapo pia aliambatana naKatibu Mkuu wa Wizara ya Nishatina Madini, Profesa Justin Ntalikwana Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikala Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC), Dkt. James Mataragio.

    Kauli ya Profesa Muhongo inakuja baada ya Rais wa Uganda YoweriMuseveni kutangaza hivi karibuniwakati wa Mkutano wa 13 waUshoroba wa Kaskazini kuwa, bombahilo la mafuta ghafi kutoka Hoima,Ziwa Albert nchini Uganda litapitakatika ardhi ya Tanzania kwendaBandari ya Tanga.

    Akieleza kuhusu siri ya ushindi

    wa Tanzania, Prof. Muhongoalisema kuwa, zipo sababu kadhaazilizochangia ushindi huo ikiwemokina kirefu cha maji katika bandari

    ya Tanga ukilinganisha na bandariya Lamu nchini Kenya, na kuongezakuwa, bandari ya Tanga ina kina chafuti 25 kwenda chini jambo ambalolitawezesha shughuli za kupakiamafuta hayo kuwa rahisi, na kuongezakuwa, bandari hiyo ina uwezo wakufanya kazi kwa kipindi cha mwakamzima.

    Vilevile, Prof. Muhongo aliitajamiunganiko ya njia ya reli ya Tangahadi reli ya Kati kuwa ni sababunyingine iliyochangia Tanzaniakushinda, ambapo alimsifu Rais JohnPombe Magufuli kwa kusimamia vemamasuala ya ujenzi wa barabara nchini

    wakati alipokuwa Waziri wa Ujenzina kusema kuwa, miundombinu ya barabara imechangia katika ushindi waTanzania.

    “Kwa kweli ninampongeza sanaRais Magufuli kwa kusimamia vemaujenzi wa miundombinu ya barabarawakati akiwa Waziri wa Ujenzi.Uwepo wa barabara nyingi ilikuwanafasi nyingine kwa Tanzania kushindakwa sababu miundombinu kama hiyohaipo kaskazini mwa Kenya. Magufuliasingesimamia vema suala hili,tusingepata sifa hizi,” alisisitiza Prof.Muhongo.

    Mbali na sifa hizo, Prof. Muhongopia aliitaja sababu nyingine kuwani usalama na uzoefu wa Tanzania

    katika ujenzi wa mabomba na kuyatajamabomba ambayo tayari yamejengwanchini kuwa ni pamoja na bomba lakusafirisha mafuta kutoka Tanzania

    hadi nchini Zambia la (TAZAMA), bomba la gesi la kutoka Kisiwa chaSongosongo mpaka Ubungo, Dar esSalaam na bomba la Gesi la

    “Uzoefu wetu katika ujenzi wamabomba mbalimbali nayo ni sababuiliyochangia ushindi wetu pamoja nausalama. Tunataka kujenga bombahili haraka sana mpango ni kukamilika

    ifikapo Juni, 2020,” alisema Prof.Muhongo.Akizungumzia gharama za mradi

    huo, alisema kuwa utagharimu kiasi cha

    Dola za Marekani Bilioni 4 na kuutajakuwa ni mradi mwingine mkubwa wakihistoria, ambapo kukamilika kwakekutawezesha kusafirisha jumla yamapipa ya mafuta Laki mbili (200,000)kwa siku, ikiwemo kutoa ajira rasmi nazisizo rasmi.

    Nje ya matumizi ya mafuta, Prof.Muhongo alisema kuwa, bomba hilo

    pia litatumika kwa ajili ya matumiziya kupitisha gesi asilia kwenda katikamikoa ya Kaskazini.

    “Watanzania tujiamini, tunaweza,wazazi wasaidieni vijana wasomemasomo ya sayansi. Bado tunahitajiwataalam wana sayansi. Lakini mbalina hilo, bomba hili ni fursa ya ajira.Wafanyabiashara na watanzaniamjitayarishe kuchangamkia fursazitakazotokana na ujenzi wa bombahili,” alisema Prof. Muhongo.

    Kuhusu watumiaji wengine wa bomba hilo nje ya Tanzania, alizitajanchi za Burundi, Sudan na Kongo nakueleza kuwa, kwa miaka ijayo nchihizo pia zitatumia bomba hilo.

    Ili kuanza utekelezaji wa ujenzi

    wa bomba hilo, Prof. Muhongoalisema kuwa, Aprili 29, 2016, Wazirianayeshughulikia masuala ya Mafutawa Uganda pamoja na kampunizitakazojenga bomba hilo za TotalE&P ya Ufaransa, Tullow Oil yaUingereza, China National OffshoreOil Corporation (CNOOC) naMamlaka zinazohusika na masuala yamafuta za Tanzania watakutana jijiniDar es Saalam ili kuweka mpango kaziwa utekelezaji wa mradi huo.

    Tanzania ilikuwa ikishindanana nchi ya Kenya kupata nafasi yamradi wa bomba hilo wenye kilomitazipatazo 1,403 kutoka Hoima –Uganda hadi bandari ya Tanga. Bombahilo linatarajiwa kupita katika mikoa

    kadhaa nchini, ikiwemo ya Kagera,Geita, Tabora, Shinyanga, Dodoma naTanga.

    Bomba la Mafuta

    kupita Tanzania

    Mmiliki wa Blogu ya Michuzi na Mwandishi wa habari Mwandamizi waMagazeti ya Serikali, Issa Michuzi (kulia) akiongea na Waziri wa Nishatina Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati). Kushoto ni NaibuKatibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt. Mhandisi JulianaPallangyo , Nyuma ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Profesa Justin Ntalikwa.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akiwaonesha waandishi wa habari ramaniya mahali litakapopita bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini.

  • 8/17/2019 JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI, TOLEO LA 117

    3/12

    3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    FIVEPILLARS OFREFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMUKITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI

    MSANIFU: Lucas Gordon

    WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, GreysonMwase, Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,

    Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

    INCREASE EFFICIENCY 

    QUALITY DELIVERYOF GOODS/SERVICE

    SATISFACTION OFTHE CLIENT

    SATISFACTION OFBUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OFSHAREHOLDERS

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Bomba la Mafuta kupitaTanzania, watanzania

    tuchangamkie fursa

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Makamishna wa Madinikukutana Morogoro

    Tarehe 24 April, 2016, Viongozi wa Wizara ya Nishati naMadini wakiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini, ProfesaSospeter Muhongo walitua kwa ushujaa katika Uwanja waNdege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyererewakitokea nchini Uganda katika Mkutano wa 13 wa Ushorobawa Kaskazini ambapo Rais wa Uganda, Yoweri Musevenialitangaza kuwa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima, ZiwaAlbert nchini Uganda litapita Tanzania badala ya bandari yaLamu nchini Kenya.

    Mara baada ya kuwasili katika Uwanja huo akiwa ameambatana Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa JustinNtalikwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleoya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio, ProfesaMuhongo alisema kuwa bomba hilo litapita Tanzania baada yasababu za kupitisha bomba hilo nchini zilizotolewa na wataalamwa Tanzania, kukubalika na nchi ya Uganda.

    Akieleza kuhusu siri ya ushindi wa Tanzania, Prof. Muhongoalisema kuwa, zipo sababu kadhaa zilizochangia ushindihuo ikiwemo kina kirefu cha maji katika bandari ya Tangaukilinganisha na bandari ya Lamu nchini Kenya.

    Alisema kuwa bandari ya Tanga ina kina cha futi 25 kwendachini jambo ambalo litawezesha shughuli za kupakia mafutahayo kuwa rahisi, na kuongeza kuwa, bandari hiyo ina uwezo wa

    kufanya kazi kwa kipindi cha mwaka mzima.Vilevile, Prof. Muhongo aliitaja miunganiko ya njia ya reliya Tanga hadi reli ya Kati kuwa ni sababu nyingine iliyochangiaTanzania kushinda, ambapo alimsifu Rais John Pombe Magufulikwa kusimamia vema masuala ya ujenzi wa barabara nchini wakatialipokuwa Waziri wa Ujenzi na kusema kuwa, miundombinu ya

     barabara imechangia katika ushindi wa Tanzania kwani itakuwarahisi kwa usafirishaji ikiwemo wa mizigo kama mabomba.

    Ili kuanza utekelezaji wa ujenzi wa bomba hilo, Prof. Muhongoalisema kuwa, Aprili 29, 2016, Waziri anayeshughulikia masualaya Mafuta wa Uganda pamoja na kampuni zitakazojenga bombahilo za Total E&P ya Ufaransa, Tullow Oil ya Uingereza, ChinaNational Offshore Oil Corporation (CNOOC) na Mamlakazinazohusika na masuala ya mafuta za Tanzania watakutana

     jijini Dar es Saalam ili kuweka mpango kazi wa utekelezaji wamradi huo.

    Hizi ni habari njema kwa nchi yetu kwani mradi huounakuja na fursa mbalimbali ambazo watanzania sasa inabidituzichangamkie ili kuona manufaa ya mradi huo.

    Baadhi ya fursa zitakazopatikana mara baada ya kuanzakwa utekelezaji wa mradi huo ni pamoja na kufanya hudumaya Tathmini za ulipaji fidia, Huduma za magreda/makatapila,Huduma za kunyanyua vitu vizito, Usanifu/michoro, Hudumaza usafirishaji, Uchimbaji visima vya maji, Ukodishaji wa ndegena helikopta na huduma za kihasibu na ukaguzi wa mahesabu.

    Huduma nyingine ni Ujenzi wa kambi za ujenzi, Majengoya kuhifadhia vifaa mbali mbali vya ujenzi, Huduma za vyakulana malazi kwenye kambi za ujenzi , Huduma za uuzaji mafuta,Karakana za ukarabati wa mashine mbali mbali na magari,Huduma za sheria, Huduma za Mawasiliano, Kandarasi zakusamba vifaa vya ujenzi, Huduma za ulinzi wakati wa ujenzi napia mradi utakapokamilika.

    Hima hima watanzania, tujiandae ili mara fursa hizozitakapotangazwa kuanza rasmi, tujitokeze na hivyo kuleta faidakwa Taifa letu na mwananchi mmoja mmoja.

    Na Greyson Mwase,Dar es Salaam

    Makamishna Wasaidizi waMadini kutoka MakaoMakuu ya Wizara yaNishati na Madini pamojana Kanda zake, na Maafisa

    Madini Wakaazi nchini wanatarajia kufanyakikao kazi chenye lengo la kujadili shughulizinazotekelezwa na Mradi wa UsimamiziEndelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP)pamoja na Sekta ya Madini kwa ujumla.

    Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizaraya Nishati na Madini iliyotolewa hivikaribuni jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa

    kikao hicho cha siku mbili kitakutanishaMakamishna wasaidizi wa Madini waliokoMakao Makuu ya Wizara, MakamishnaWasaidizi wa Madini wa Kanda, MaafisaMadini Wakaazi na Katibu Mkuu waWizara Prof. Justin Ntalikwa lengo likiwa nikujadili maendeleo ya utekelezaji wa miradiinayosimamiwa na SMMRP na Sekta ya

    Madini kwa ujumla.Taarifa hiyo ilieleza kuwa katika

    kikao hicho na Katibu Mkuu wa Wizaraya Nishati na Madini Prof. Ntalikwa,Makamishna Wasaidizi na Maafisa Madinihao kutoka katika ofisi zote za madininchini, watatakiwa kuwasilisha changamotowanazokabiliana nazo wakati wa utendajiwa kazi zao ili kuangalia njia bora zakutatua.

    Aidha, kikao hicho kitajadili jinsi yakutekeleza Awamu ya Pili ya Mradi waUsimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini(SMMRP) hususan uanzishwaji wa senta

     bora za mfano kwa ajili ya wachimbajiwadogo.

    Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwatimu ya Mradi itawasilisha utekelezajiwa shughuli za mradi na kujadiliwa nawataalam kama mwongozo wa utekelezajiwa mradi unavyotaka ambapo sehemu yauchimbaji mdogo itawasilisha mafanikio nachangamoto zilizojitokeza wakati wa utoajiwa ruzuku ya Awamu ya Pili.

    Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA),Mhandisi Dominic Rwekaza (kushoto) akiwa na Meneja Mradi wa UsimamiziEndelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), Mhandisi Idrisa Yahaya na Kiongoziwa Mradi wa SMMRP wa Benki ya Dunia, Mamadou Barry, wakizungumzamara baada ya kuhudhuria Semina ya Mafunzo kutoka Chuo cha Jemolojiacha Madagascar iliyotolewa wakati wa Maonesho ya Tano ya Kimataifa yaVito – Arusha, yaliyofanyika jijini Arusha tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016.

    TAHARIRI

  • 8/17/2019 JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI, TOLEO LA 117

    4/12

    4   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Mnada wa Madini waiingizia

    Serikali Bilioni 1.6Teresia Mhagama na Asteria Muhozya, Arusha

    Serikali imepata jumla yashilingi bilioni 1.6 ikiwa nimapato yaliyopatikana katikamnada wa madini uliofanyikawakati wa Maonesho ya Tano

    ya Kimataifa ya Vito yaliyofanyika jijini Arusha katika Hoteli ya Mt.Merukuanzia tarehe 19 hadi 21, Aprilimwaka huu.

    Hayo yameelezwa hivi karibuni jijiniArusha na Mkurugenzi wa Kitengo

    cha Uthaminishaji Madini ya Almasina Vito (TANSORT) katika Wizara yaNishati na Madini, Archard Kalugendo,wakati akitangaza matokeo ya mnadahuo.

    Katika maonesho hayo, kulikuwana Tenda Tatu; Tenda ya Kwanzailikuwa ya Serikali ikihusisha madinimbalimbali yaliyokuwa yakishikiliwana Kamishna wa Madini ambapo

     jumla ya shilingi za kitanzania bilioni1.3 zilipatikana kutokana na mauzo yamadini hayo.

    Tenda ya pili ilikuwa ni madiniya Tanzanite ghafi yaliyozalishwa namgodi wa TanzaniteOne unaomilikiwakwa ubia kati ya kampuni ya SkyAssociates na Shirika la Madini la Taifa

    (STAMICO).“Napenda kushukuru mgodi waTanzaniteOne kwani wametuleteamadini ya Tanzanite ambayo ni ghafiyenye thamani kubwa ambapo madini

    yote kutoka mgodi huu yamenunuliwakwa thamani ya shilingi za KitanzaniaBilioni Tano (5),” alisema Kalugendo.

    Kalugendo alisema kuwa tendaya tatu ya mnada huo ilikuwa yakampuni ya El-Hilal inayochimbamadini ya Almas nchini. Alifafanuakuwa, kampuni mbili zilizojitokezakatika tenda hiyo hazikufikia kiwangocha chini cha bei iliyowekwa naSerikali hivyo kupelekea madini hayokutokuuzwa katika mnada huo.

    “ Hii ni kusema kwamba madini yoteya Tanzanite yaliyoletwa na mgodi waTanzaniteOne na Tanzanite iliyoletwa

    na Serikali katika kifurushi cha kwanzapamoja na dhahabu yote iliyokuwakatika kifurushi hicho yameuzwa,”alisema Kalugendo.

    Aliongeza kuwa, fedha yoteiliyopatikana kutokana na mauzo yamadini yaliyokuwa yakishikiliwa naKamishna wa Madini, inaingizwa katikamfuko wa Serikali na kwamba madinighafi yaliyouzwa kutoka TanzaniteOneyatalipiwa mrabaha serikalini washilingi milioni 245,686,000 ili madinihayo yaweze kusafirishwa popote.

    Aidha, Kalugendo alisisitiza kuwamapato hayo ni ya mnada tu hivyomauzo ya jumla ya maonesho hayoyatatangazwa baada ya kujumuishamatokeo ya mauzo yote yaliyofanyika

    katika Maonesho husika.Pia, Mkurugenzi wa Uthamini waMadini na Huduma za Kimaabarakutoka Wakala wa Ukaguzi wa

    Madini Tanzania (TMAA), MhandisiGilay Shamika, akiwa katikaMnada wa Madini yaliyo chini yaKamishna wa Madini, alitoa witokwa wafanyabiashara kufuata sheria,taratibu na kanuni za biashara yaMadini ili kutotaifishiwa Madini yaomara wanapokamatwa bila kuwa navibali husika.

    ‘Madini haya unayoyaonayakipigwa mnada, yalikamatwa nakutaifishwa pindi yakitoroshwa nje ya

    nchi bila wahusika kuwa na vibali vyausafirishaji. Ni vema wafanyabiasharakufuata taratibu kwa mujibu wa Sheriaya Madini ya mwaka 2010,’’ AlisemaShamika.

    Naye kamishna Msaidizi wa Madinianayeshughulikia Uchumi na Biashara,Salim Salim aliwashukuru wadau wotewalioshiriki na kudhamini maoneshohayo ambayo ni muhimu katikauendelezaji wa Sekta ya Madini nchini.

    Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Almas na Vito,katika Wizara ya Nishati na Madini, Archard Kalugendo akiangaliamaombi ya ahadi za bei ya madini yaliyopigwa mnada katika Maoneshoya Tano ya Kimataifa ya Vito yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe19 hadi 21, Aprili, 2016. Wanaoshuhudia ni Kamishna Msaidizi waMadini, Uchumi na Biashara, Salim Salim (Wa Pili kushoto), Wa Pili

    kulia ni Mkurugenzi wa Uthamini wa Madini na Huduma za Kimaabarakatika Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi GilayShamika na wa kwanza kulia ni Mthamini Almas wa Serikali, EdwardRweyemamu.

    Wadau mbalimbali wakishuhudia, Mkurugenzi wa Kitengo chaUthaminishaji Madini ya Almas na Vito, katika Wizara ya Nishati naMadini, Archard Kalugendo akifungua masanduku yenye bahasha zaahadi ya bei za madini yaliyopigwa mnada katika Maonesho ya Tano yaKimataifa ya Vito yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 19 hadi 21,Aprili, 2016.

    Wadau mbalimbali walioshiriki Maonesho ya Tano ya Kimataifa yaVito yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 19 hadi 21 wakimsikilizaMkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Almas na Vito,

    katika Wizara ya Nishati na Madini, Archard Kalugendo (hayupopichani) wakati akitangaza matokeo ya mnada wa madini uliofanyikakatika Maonesho hayo.

  • 8/17/2019 JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI, TOLEO LA 117

    5/12

    5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Teresia Mhagama, Arusha

    Imeelezwa kuwa Maabara yaMadini ya Wakala wa Ukaguziwa Madini Tanzania (TMAA)mbali na kupima ubora waSampuli za Madini kutoka katika

    Migodi mikubwa, Kati na Midogokwa ajili ya Serikali kupata Mapatokulingana na ubora wa Madini husikapia inatoa elimu kwa wananchi iliwaweze kutumia maabara hiyokutambua aina na thamani ya Madiniya Vito pamoja na Madini ya Metali.

    Hayo yalisemwa na Mkurugenzi waUthamini wa Madini na Huduma zaMaabara kutoka Wakala wa Ukaguziwa Madini (TMAA), Mhandisi GilayShamika katika Maonesho ya Tano yaKimataifa ya Vito yaliyofanyika jijiniArusha hivi karibuni.

    Alisema kuwa TMAA imeamuakutumia maonesho hayo kutoa Elimuhiyo ya kupima ubora wa sampuli zamadini kwa wananchi kwa kuwa watuwengi hawafahamu aina za Madinihayo na hivyo kuyauza au kununuakwa bei isiyo halali.

    “Mfano, Watu wengi wamekuwawakitapeliwa Madini ya Rubiwanapopeleka sokoni kuyauza nakuambiwa kuwa siyo Rubi bali niGarnert nyekundu. Hali kadhalikawatu huuziwa Iolite kwa kuambiwakuwa ni Tanzanite kwa sababuzinafanana rangi,” alisema MhandisiShamika

    Pia kwa upande wa dhahabu,alieleza kuwa kuna wimbi la watukuuziwa Madini ya shaba badala yadhahabu kwani Dhahabu kidogohuwekwa juu ya shaba na kuuzwakama dhahabu halisi.

    Ili kuondokana na utata wote huowa kutapeliwa, Mhandisi Shamikaalitumia Maonesho hayo kuwaasawananchi kutumia maabara yaTMAA iliyopo katika Makao Makuu

    ya Wakala huo, Barabara ya Chole jijiniDar es Salaam, Capripoint Mwanza,Mafao House Arusha na Uhindini

    Mbeya.Alisema kuwa Maabara ya Wakalawa Ukaguzi wa Madini Tanzania inaubora wa kimataifa yaani ISO 17025,ikimaanisha kuwa huduma zakezinatambulika na kukubalika ndani nanje ya nchi.

    Kwa upande wa Madini ya

    Metali kama dhahabu,shaba, fedhana chuma, Maabara ya TMAA inauwezo wa kutambua aina na asilimia

    za Madini zilizopo katika miamba (rocks) na udongo (soil), pia kupimaubora wa Madini kwa kuainisha kiasicha asilimia za Madini kwa kutumiaAAS Machine, XRF Machine, Fireassay na njia nyingine.

    Aidha kwa Madini ya Vito,Maabara ya Wakala ina uwezo wa

    kutambua aina ya Madini ya Vitopamoja na kupanga ubora wa hayo naHuduma nyingine muambata.

    Kuhusu Mawasiliano, MhandisiShamika alisema kuwa, tovuti yaWakala ambayo ni www.tmaa.go.tzinaonesha Mawasiliano ya Maabarazote za Wakala zilizopo katika OfisiKuu na Ofisi za Kanda za Wakala.Mawasiliano ya Makao Makuu ni+255-22- 2601819

    Meneja wa Maabara ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi Mvunilwa Mwarabuakionesha mashine ya kupima kiwango cha madini inayoitwa Atomic Absorption Spectroscopy (AAS).

    Wananchi waelimishwa kuhusu

    Maabara ya Madini ya TMAA

    Mkemia kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA),

    Alfred Aloyce akionesha sampuli ya dhahabu iliyotayarishwa kwa ajiliya kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara ili kubaini kiasi cha madini yadhahabu na fedha.

    Mashine ya kuyeyusha sampuli za madini (fusion and cupellationfurnaces) inayotumika kwenye Maabara ya Wakala wa Ukaguzi waMadini Tanzania (TMAA).

  • 8/17/2019 JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI, TOLEO LA 117

    6/12

    6   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    TPDC YASAIDIA MADAWATI

    KINYEREZI – DAR ES SALAAMMkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kulia)akipokea mfano wa hundi ya Shilingi milioni 7,440,000kwa ajili ya kununulia Madawati katika Shule ya MsingiZimbili, Kinyerezi kutoka kwa Meneja Mawasiliano waShirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), MarieMsellemu (Kushoto) kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendajiwa TPDC.

    Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akioneshahundi ya Shilingi milioni 7,440,000 iliyotolewa na Shirikala Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa ajili yaununuzi wa Madawati kwa Shule ya Msingi ZimbiliKinyerezi jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wahabari.

    Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (mwenye nguonyeupe) akiwa na wafanyakazi wa TPDC katika haafupi ya kukabidhi hundi ya Shilingi milioni 7,440,000 kwaajili ya kununulia Madawati ya Shule ya Msingi Zimbili,Kinyerezi Jijini Dar es Salaam.

    Meneja Mawasiliano – TPDC, MarieMsellemu akizungumza katika haa fupiya kukabidhi hundi ya Shilingi milioni7,440,000 kwa ajili ya kununulia Madawatiya Shule ya Msingi Zimbili, Kinyerezi JijiniDar es Salaam hivi karibuni, wengine niMkuu wa Wilaya ya Ilala,. Raymond Mushi

    (wa pili kulia) na Diwani wa Kinyerezi,Greyson Selestine (kushoto).

  • 8/17/2019 JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI, TOLEO LA 117

    7/12

    7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Zuena Msuya, DSM

    Waziri wa Nishatina Madini ProfesaSospeter Muhongoamesaini kibali chakuhamisha leseni ya

    uchimbaji wa kati wa madini kutokaampuni ya uchimbaji wa madini yaChina ya Henan AfroAsia Geo-Engeneering (Tanzania) kwendaKampuni ya uchimbaji wa DhahabuZEM Tanzania Limited.

    Akizungumza mara baada ya

    kusaini kibali hicho hivi karibuni, jijini Dar es salaam,Profesa Muhongoalisema kampuni hiyo itaanzashughuli za uchimbaji mwanzonimwa mwezi Desemba mwaka huu,katika kijiji cha Nyasirori wilayaniButiama Mkoani Mara.

    Alifafanua kuwa kusaini kibalihicho kunatoa fursa kwa kampuniya China ya uchimbaji wa madini yaZEM, ambayo iliingia makubalianaoya kufanya kazi na kampuni yaHenan AfroAsia Geo- Engeneering(Tanzania) mwezi Desemba mwaka2015. Gharama za mradi huozinakadiriwa kufikia kiasi cha dola zaMarekani mlioni43.3.

    Aidha Profesa Muhongo alisemakuwa kampuni za China kuendeleakuwekeza katika miradi mikubwa yamaendeleo ni kuendelea kuimarishaushirikiano kati ya nchi hizo mbiliTanzania na china ulioanzishwa naMwasisi Baba wa Taifa Mwalimu

    Julius Nyerere.Kwa upande wake Naibu Katibu

    Mkuu wa Wizara ya Nishati naMadini anayeshughulikia MadiniProfesa James Mdoe aliisisitizakampuni hiyo kutekeleza masharti

    katika leseni za uchimbaji wa madiniili kuweza kufanya kazi kwa ufanisimkubwa.

    Vilevile aliwataka wawekezaji haokutekeleza mradi huo katika mudawalioahidi ili kuondoa usumbufuna dhana ya kutokuwa na imani naKampuni hiyo.

    Aliongeza kuwa, mradi huoumepokelewa vyema na wakazipamoja na wachimbaji wadogo waeneo hilo kwani hakuna malalamikoyoyote yaliyojitokeza hadi kufikiahatua ya kuanza uchimbaji. NayeKansela wa ubalozi wa China nchiniTanzania, Gou Haodong aliwatakawawekezaji hao kujenga mahusiano

    mazuri kati yao na wakazi wa vijijivinavyozunguka mgodi huo kwakuwawekea huduma za kijamii.

    Haodong alitaja miradi hiyo kuwani pamoja na kujenga visima vyamaji safi na salama karibu na makaziya watu kwani wanavijiji wengiwamekuwa wakitembea umbalimrefu kwenda kufuata huduma yamaji. Sambamba na hilo alieleza kuwakampuni hiyo ya uchimbaji inatakiwakutoa huduma ya afya kwa wananchiwa maeneo hayo kwa kuwajengeazahanati na kuwezesha upatikani wahuduma za dawa na madaktari.

    Kansela huyo wa Ubalozi waChina nchini, alisisita kuhusu suala la

    elimu ambalo alisema kuwa ni vyemakampuni za uchimbaji wa madinizikaweka mazingira mazuri ya elimu

     bora kwa jamii zinazowazunguka ilikuunga mkono Serikali ya Tanzaniaya kutoa elimu bora kwa kilamtanzania.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (wapili kulia) Kansela wa Ubalozi wa China nchini, Gou Haodong(wa pili kushoto) na Maneja wa Kampuni ya Uchimbaji Madiniya Henan AfroAsia Zhang Jiangbo kwa pamoja wakionesha kibalicha kuhamisha leseni ya uchimbaji wa kati wa madini kutokaKampuni ya uchimbaji Madini ya China ya Henan AfroAsia Geo-Engeneering (Tanzania) kwenda Kampuni ya uchimbaji wa DhahabuZEM Tanzania Limited, uchimbaji wa madini hayo utafanyika katikakijiji cha Nyasirori Wilayani Butiama Mkoani Mara kuanzia mweziDesemba mwaka 2016.

    Profesa Muhongo asaini

    kibali cha kuhamisha leseni

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (katikati)akiwa na ujumbe kutoka Ubalozi wa China ukiongozwa na KanselaGou Haodong (kulia kwa Waziri) pamoja na watendaji wa Wizarawakiwa katika kikao cha pamoja kabla ya kusainiwa kwa kibali chakuhamisha leseni ya uchimbaji wa kati wa madini kutoka Kampuniya uchimbaji wa madini ya China ya Henan AfroAsia Geo-Engeneering (Tanzania) kwenda Kampuni ya uchimbaji wa DhahabuEM Tanzania Limited.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akisainikibali cha kuhamisha leseni ya uchimbaji wa kati wa madini kutokaKampuni ya uchimbaji Madini ya China ya Henan AfroAsiaGeo- Engeneering (Tanzania) kwenda Kampuni ya uchimbaji waDhahabu ZEM Tanzania Limited. Tukio lilifanyika katika Ukumbiwa Mikutano wa Wizara ya Nishati na Madini.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (kulia)akibadilishana mawazo na Kansela wa Ubalozi wa China, GouHaodong (wa pili kushoto) katika Osi ya Waziri wa Nishati naMadini baada ya kumaliza kusaini kibali cha kuhamisha leseni ya

    Uchimbaji Madini katika Kijiji cha Nyasirori wilayani Butiamautakaoanza mwezi Desemba mwaka huu. Kulia ni Meneja waKampuni ya uchimbaji madini ya Henan AfroAsia Zhang Jiangbo.

  • 8/17/2019 JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI, TOLEO LA 117

    8/12

    8   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

     Viongozi  wakipokele wa  JNIA

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikiaMadini, Profesa James Mdoe (wa kwanza kulia) akizungumza jambona baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakatiwakisubiri kuwasili kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa

    Sospeter Muhongo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji waShirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. JamesMataragio, Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikiaMaendeleo ya Nishati, James Andilile, Naibu Katibu Mkuuanayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt. Mhandisi JulianaPallangyo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Profesa Justin Ntalikwa.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC), Dkt. James Mataragio (kushoto) akipongezwa na baadhi yawatumishi kutoka Idara ya Mawasiliano wa shirika hilo mara baadaya kuwasili kutoka nchini Uganda.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa SospeterMuhongo akipongezwa na Madereva wa Taxi waUwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere kufuatiaushindi wa Tanzania wa kupitisha bomba la mafutanchini. Wengine wanaofuatilia ni baadhi ya watendajiwa Wizara walioka uwanjani hapo kumpokea nabaadhi ya wananchi waliokuwa uwanjani hapo.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika laMaendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio(kulia) akiongea jambo na baadhi ya watendaji wakuu wa Wizaraya Nishati na Madini wakati wakisubiri kuwasili kwa Waziri waNishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Kutoka kushotoni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Nishati,Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa, Kamishna Msaidizi

    wa Nishati anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, JamesAndilile na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madinianayeshughulikia Madini , Profesa James Mdoe.

    BOMBA LA MAFUTA KUTOKA UGANDA...

  • 8/17/2019 JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI, TOLEO LA 117

    9/12

    9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Madini ya shilingi Bilioni 3.2 yaokolewa na TMAANa Teresia Mhagama,

     Arusha

    Imeelezwa kuwa katika kipindicha Julai 2015 hadi Januari 2016,Wakala wa Ukaguzi wa MadiniTanzania (TMAA) umewezeshamadini yenye thamani ya shilingi

     bilioni 3.2 kukamatwa yakitakakutoroshwa nje ya nchi bila kuwa navibali katika matukio 16.

    Hayo yameelezwa na MhandisiGilay Shamika wakati wa Maoneshoya Kimataifa ya Vito ya Arushayaliyofanyika jijini humo kuanziatarehe 19 hadi 21, Aprili mwaka huu.

    Mhandisi Shamika alisema kuwamadini hayo yalikamatwa kufuatiaukaguzi uliofanyika kupitia madawatimaalum yaliyopo katika Viwanja vya

    Ndege vya Mwl.Julius Nyerere (Dares Salaam), Kilimanjaro, Mwanza,Songwe (Mbeya) na Arusha.

    Aliongeza kuwa watoroshajihao wa madini walikamatwa kwaushirikiano wa Jeshi la Polisi, Mamlakaya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka

    ya Viwanja vya Ndege (TAA), Idara yaMadini na Usalama wa Taifa.

    Mhandisi Shamika alisema kuwa,

    ili kudhibiti hali hiyo ya utoroshajimadini, TMAA imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ikiwemo kutoaelimu kwa umma kuhusu sheria nataratibu za kuingiza na kusafirishamadini nje ya nchi, kuimarishaushirikiano na vyombo vingine vyaSerikali na kuchukua hatua za kisheriakwa kuwafikisha watuhumiwamahakamani ambapo hupewa adhabuya kulipa faini na madini kutaifishwa.

    Aidha Mhandisi Shamika alielezakuwa madini hayo yanayotaifishwahuuzwa katika mnada wa madiniunaofanyika katika Maonesho yaKimataifa ya Vito ya Arusha ambapokatika Maonesho ya Tano ya Vitoyaliyomalizika hivi karibuni, Serikali

    ilipata jumla ya shilingi za kitanzaniaBilioni 1.3.

    Mbali na kutoa wito kwa wadauwa madini kufuata sheria na kanunizinazoongoza Sekta ya Madini nchini,Mhandisi Shamika alieleza kuwaWakala huo umetumia Maonesho

    hayo ya Vito kutoa elimu kwa wadauwa ndani na nje ya nchi kuhusuumuhimu wa kuwa na vibali vyote

    vinavyohitajika katika usafirishaji wamadini yaliyokuwa yakiuzwa katikamaonesho hayo.

    Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA),Mhandisi Dominic Rwekaza

    Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Vito Arusha (AGF),Peter Pereira (Wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Chama chaWafanyabiashara wa Madini (TAMIDA), Sammy Mollel wakiwakaribishaWashiriki wa Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Vito ya Arusha.

    Vijana wa Kitanzaniawakiwa wamevaamadini ya ainambalimbali ya Vitoyaliyokatwa nakunakshiwa nchiniTanzania.

    Madini hayo ya Vitovilivyonakshiwapamoja na ghaikiwemo Tanzaniteyanayopatikana nchiniTanzania yalikuwayakiuzwa wakati waMaonesho ya Tanoya Kimataifa ya Vito

    yaliyofanyika JijiniArusha kuanzia tarehe19-21 Aprili, 2016.

    MAONESHO YA 5 YA VITO - ARUSHAAPRILI 19 - 21, 2016

  • 8/17/2019 JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI, TOLEO LA 117

    10/12

    10   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    MAKALA

    Na Veronica Simba

    “Madini ya Graphiteyanatumika kwenye betri zasimu zote ambazo ni smartphones; kwenye betri zamagari yanayotumia umeme

    na pia kutengeneza Penseli ambazozamani waliziita za risasi. Ukweli hiyosiyo risasi bali ni Graphite.”

    Hivyo ndivyo Kamishna Msaidiziwa Madini Kanda ya Kusini, MhandisiBenjamin Mchwampaka alivyoanzakunieleza kuhusu maendeleo yashughuli za Mradi wa Nachu wakuchimba madini ya Graphite, hukowilayani Ruangwa, Mkoani Lindi.

    Mhandisi Mchwampaka anaelezakuwa, Mradi huo unaendelezwana Kampuni ya Uranex Tanzania

    Limited ambayo inamilikiwa nakuendeshwa na Kampuni Mamaya Magnis Resources iliyopo nchiniAustralia.

    Kutokana na umuhimu wa Mradihusika kwa nchi yetu, kama ilivyokwa miradi mingine mbalimbalinchini, yenye lengo la kuinua uchumiwa nchi yetu, Makala hii inaangaziamaendeleo ya Mradi huo ikiwemokazi iliyofanyika mpaka sasa, manufaayanayotarajiwa kwa Taifa pamoja nachangamoto zilizopo.

    Maelezo yaliyo katika Makalahii yanatokana na mazungumzoniliyofanya na KamishnaMchwampaka pamoja na Taarifailiyoandaliwa na Kampuni ya Uranex.

    Mradi wa kuchimba Graphite waNachu

    Inaelezwa kuwa Serikali yaTanzania ni Mbia wa Mradi waNachu unaohusika na kuchimbamadini ya Graphite. Hii inatokana naSerikali kumiliki hisa asilimia Tano(5). Hata hivyo, inaelezwa kuwa, upouwezekano wa hisa za Serikali kufikiaasilimia 15.

    Kuanzishwa kwa Mradi huo

    kunatokana na kubaini kuwa yapomashapo ya kutosha ya madiniya Graphite ambayo yanawezakuchimbwa kwa faida. Uthibitishohuo unatokana na shughuli zautafutaji wa madini husika WilayaniRuangwa uliofanywa na Kampuni yaUranex tangu mwaka 2013 kwa leseniya utafutaji Namba PL 9076/2013.Baadaye, mwaka 2015, Serikali kupitiaWizara ya Nishati na Madini, ilitoaleseni kubwa ya uchimbaji wa madinihayo, yenye Namba SML 550/2015kwa ajili ya ujenzi wa Mgodi.

    Kazi iliyofanyika Pamoja na shughuli za utafutaji

    wa madini katika Wilaya ya Ruangwazilizoanza mwaka 2013, Kampuniya Uranex pia imetayarisha taarifa yaUpembuzi Yakinifu ya awali kuhusuMradi.

    Mpaka sasa, mashapoyaliyogunduliwa ni takriban tanimilioni 156, ambapo madini yagraphite yaliyomo kwenye mashapohayo yanafikia zaidi ya tani milioniNane (8). Aidha, inaelezwa kuwa,kiwango hicho kipo katika eneo dogotu la leseni husika ya utafutaji, hivyoinamaanisha kuwa mashapo ambayohayajagunduliwa ni mengi zaidi ya

    kiasi kilizhogunduliwa hadi sasa.Vilevile, inaelezwa kuwa, kutokanana ubora wa madini ya Graphitekutoka mgodi huo, Kampuni yaSINOMA kutoka China imesainimkataba wa kutoa mkopo wa kujengamgodi wenye thamani ya Dola zaKimarekani milioni 150, ambazoni sawa na asilimia 90 ya fedha zotezinazohitajika kuanza uzalishaji.

    Manufaa yanayotarajiwa Manufaa kadhaa yanatajwa

    kuwa yatapatikana na kuwanufaishawananchi wa Wilaya ya Ruangwa naTaifa zima kwa ujumla, kutokana naMradi wa Nachu wa kuchimba madiniya Graphite. Baadhi ya manufaa

    yanayoelezwa kuwa yataletwa naMradi huo ni ajira kwa Watanzania,malipo ya kodi na manufaa mengineyanayotokana na kuongezeka kwa

    shughuli za kiuchumi.Kwa mujibu wa taarifa ya Uranex,

    Kampuni hiyo imeandaa mpango waAjira na Mafunzo kwa Watanzaniaambapo kipaumbele kitakuwa ni ajirakwa Watanzania wenye sifa kwanzakabla ya kuajiri wataalam kutokanje. “Watanzania wengi zaidi ya 800wataajiriwa wakati wa ujenzi wamgodi, lakini idadi itapungua hadikufikia wastani wa 360 wakati wauzalishaji.”

    Aidha, inatarajiwa kuwa mradiwa kuchimba Graphite utakapoanza,utakuwa ndiyo Mgodi mkubwa wa

    kuzalisha madini hayo duniani. Kwasasa Mgodi mkubwa wa Graphite ukoChina na unazalisha tani 150,000 zaGraphite kwa mwaka.

    Vilevile, imeelezwa kuwa,Kampuni haijaweka msamaha wakodi wa aina yoyote, hivyo kodizote zinazostahili kulipwa zitalipwa.Uzalishaji unatarajiwa kufikia kiwangocha tani 250,000 baada ya mwaka wapili wa kuanza uzalishaji.

    Pia, imeelezwa kuwa Mgodiumepanga kununua bidhaazipatikanazo hapa nchini na kamazitakosekana ndipo zitaagizwa nje.Aidha, huduma nyingi zitakazohitajikamgodini zitatolewa na Kampuni zahapa nchini.

    Fidia kwa watakaopitiwa na MradiKwa mujibu wa Kamishna

    Mchwampaka, hatua iliyofikiwakwa sasa ni uthamini wa mali zawatu ambao wanatakiwa kupishaeneo ambapo mgodi utafunguliwana tayari kazi ya uthamini kwa maliyaani mazao, nyumba na ardhi tupulilikamilika mwishoni mwa mweziFebruari, 2016 na hatua itakayofuatani kuanza kuwalipa wahusika kwamujibu wa taratibu za nchi.

    Ni jambo la fahari kwa Watanzaniakuwa na wingi wa rasilimali za madiniya aina mbalimbali. Ili madini yaGraphite yalinufaishe Taifa ipasavyo,wananchi wa Ruangwa hawana budi

    kutoa ushirikiano pale inapotakiwapamoja na kuchangamkia fursambalimbali zinakuja sambamba nauwekezaji huo.

    Madini ya Graphite

    Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Mhandisi BenjaminMchwampaka

    Hivi ndivyo Tanzaniainavyonufaika na

    Madini ya GraphiteMradi huo unaendelezwa naKampuni ya Uranex TanzaniaLimited ambayo inamilikiwana kuendeshwa na KampuniMama ya Magnis Resourcesiliyopo nchini Australia.

  • 8/17/2019 JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI, TOLEO LA 117

    11/12

    11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

     Zuena Msuya naGodwin Masabala DSM

    Mpango wa UhamasishajiUwazi katika mapatoya madini, gesi asiliana mafuta( TEITI)umezindua ripoti ya 5

    na 6 ya Mapato ya Serikali kwa mwaka2012/2013 na 2013/2014 kutoka katikauchimbaji wa madini,mafuta na gesiasilia.

    Akizindua Ripoti hiyo jijini Dares salaam, aliyekuwa Mkaguzi Mkuuna Mdhibiti wa Hesabu za Serikali,Ludovock Utouh pamoja na mambomengine alisema ripoti ya TEITIimeongeza uwazi wa mapato ya Serikaliyatokanayo na Madini, Mafuta pamojana Gesi Asilia.

    Alisema Ripoti hiyo itawarahisishiawananchi kufahamu matumizi namapato yatokanayo na rasilimali hizo nakuondoa dhana iliyojengeka kwa jamiiuu ya upotevu wa mapato yatokanayo

    na madini, mafuta na gesi asilia katikashughuli za utafutaji na uchimbaji wamadini,mafuta na gesi asilia nchini.

    Alifafanua kuwa, matokeo ya Ripotiya Tano ya TEITI mwaka 2012/2013imeonesha kuwa Serikali ilipata mapatoya shilingi bilioni 956 kutokana nakampuni 46 za madini na kampuni 19za mafuta na gesi asilia.

    Aidha, matokeo ya ripoti ya ya SitaTEITI ya mwaka 2013/2014 imeoneshakuwa Serikali imepata mapato ya shilingibilioni 1,221 kutokana na kampuni 38 zamadini na kampuni 21 za mafuta na gesiasilia katika shughuli za uchimbaji nautafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini.

    Alisisitiza kuwa baada ya kuundwa

    kwa taasisi hiyo, hivi sasa taarifa sahihiza malipo na mapato ya Serikaliinayopokea kutoka katika makampuniya tasnia ya uziduaji inafahamika wazi.

    Aidha, Utouh aliishauri TEITIkuongeza kasi katika ufanisi wa kazizake ili kila mtanzania aweze kupatataarifa za mapato ya Serikali kuhusuuchimbaji wa madini, mafuta na gesiasilia na kuondoa maswali yaliyojengekamiongoni mwa jamii.

    Sambamba na hilo alivitaka vyombovya habari kuchambua kwa kina ripotina kutoa taarifa sahihi kwa wananchi

    ili waweze kuelewa kwa undanikinachofanywa na Serikali katika sektaya madini,mafuta na gesi asilia.

    Kwa upande wake, Mwenyekitiwa Kamati ya TEITI, Jaji MarkBomani ambaye anamaliza mudawake, alisema kuwa kwa mujibu waripoti hizo mbili mapato ya Serikalikutokana na uchimbaji pamoja nautafutaji wa madini, mafuta na gesi asiliayameongezeka kutoka shilingi ya zaidiya shilingi bilioni mia moja na ishirinihadi kufikia zaidi ya shilingi bilioni elfumoja na mia mbili na ishirini ongezekola takribani mara kumi ya makusanyo.

    Hata hivyo, ameshauri kuwa masualaya mauzo ya asilimia 60 ya kampuni za

    madini na kwenye mikataba maalumyazidi kufikiriwa zaidi ili kuongezamapato kwa kuzingatia kuwa ni asilimia20 tu ya madini yaliyogunduliwa nchinindio yanayochimbwa hadi leo hukuasilimia 80 zikiwa bado hazijaguswakabisa.

    Vilevile, aliongeza kuwa bado Sektaya Madini inakabiliwa na changamotonyingi ikiwamo kutanua wigo wawachimbaji madini wa kati ili na wao

    wachangie katika pato la Serikali kwanimpaka sasa kampuni kubwa pekee ndiozimekuwa zikihusika.

    Jaji Mark Bomani alitumia uzinduzi

    wa ripoti hizo kuwaaga rasmi wajumbewa Kamati Elekelezi ya TEITI

    iliyoundwa mwaka 2008 iliyopewa jukumu la kuingalia Sekta ya Madini,Mafuta na Gesi Asilia kwa undani nakutoa mapendekezo ya kuiboresha

     baada ya kutumikia nafasi ya Uenyekitikwa miaka 7.

    Akiyekuwa Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali LudovickUtouh (wa pili kulia) akikata utepe, ikiwa ni uzinduzi wa Ripoti za TEITIya Mapato ya Serikali yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta

    Gesi na Madini ya mwaka 2012/2013 na 2013/2014. Wa pili kushotoni Mwenyekiti wa kamati ya TEITI anayemaliza muda wake, Jaji MarkBomani na Katibu Mtendaji wa TEITI Mhandisi Benedick Mushingwe (wakwanza kulia)

    Katibu Mtendaji wa TEITI, Mhandisi Benedict Mushingwe (kushoto) na

    baadhi ya watendaji wa TEITI (kulia) wakifuatilia taarifa ya Uzinduzi waRipoti za TEITI za mapato ya Serikali kutokana na Uchimbaji na Utafutajiwa Madini, Mafuta na Gesi Asilia kuanzia 2012-2014.

    TEITI yazindua ripoti ya 5 na 6 ya Mapato ya Serikali

    Mwenyekiti wa kamati ya TEITI anayemaliza muda wake, Jaji MarkBomani (kushoto) na aliyekuwa Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu zaSerikali, Ludovick Utouh (kulia) wakizungumza wakati wa uzinduziwa ripoti ya TEITI ya mapato ya Serikali yatokanayo na uchimbaji nautafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia.

    Baadhi ya washiriki wakifuatilia uzinduzi wa ripoti ya TEITI ya mapato yaSerikali yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Madini, Mafuta na gesiAsilia za mwaka 2012-2014 uliofanyika jijini Dar es salaam.

    n  Mapato ya Madini, Mafuta,

    Gesi Asilia yaongezeka

  • 8/17/2019 JARIDA LA WIKI LA NISHATI NA MADINI, TOLEO LA 117

    12/12

    12   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Urusi yaalikwa kuwekeza kwenye umeme

    Na Greyson Mwase,Dar es Salaam

    Imeelezwa kuwa Tanzania inavyanzo mbalimbali vya kutoshakwa ajili ya kuzalisha umeme wauhakika utakaochangia katikaukuaji wa uchumi wa nchi.

    Hayo yalielezwa na KamishnaMsaidizi wa Nishati anayeshughulikiaNishati Mbadala MhandisiEdward Ishengoma katika jukwaalinalokutanisha wataalam nawawekezaji kutoka Urusi naTanzania lijulikanalo kama Russian-

     African Forum, 2016.Masuala yaliyojadiliwa katika

     jukwaa hilo kwa siku mbili ni pamojana Miundombinu, Kilimo, fursaza uwekezaji na Nishati. KatikaJukwaa linalojadili Sekta ya Nishatiwataalam na wawekezaji katika nchiza Tanzania na Urusi walipata fursaya kubadilishana uzoefu wa jinsi yakuboresha sekta ya nishati.

    Akizungumza katika jukwaahilo kwa niaba ya Naibu KatibuMkuu wa Wizara ya Nishati na

    Madini anayeshughulikia NishatiMhandisi Juliana Pallangyo,Kamishna Msaidizi wa Nishati

    anayeshughulikia Nishati Mbadala,Mhandisi Edward Ishengomaalisema kuwa Tanzania ina vyanzovya kutosha kwa ajili ya uzalishajiwa umeme na hivyo inawaalikawawekezaji kutoka Urusi wenyeuwezo katika uwekezaji huo ilikuwezesha Tanzania kupata umemewa uhakika.

    Alifafanua kuwa Tanzania inavyanzo mbalimbali vya umemekama vile Makaa ya Mawe, Upepo,Umeme Jua, Jotoardhi, Gesi naMaji na kuyataka makampuni yenyeuwezo kwenye uzalishaji wa umemekujitokeza na kuwekeza.

    Alisisitiza kuwa vyanzo hivi

    vinahitaji kuendelezwa ili kuhakikishampango wa kuzalisha umeme

    wa kutosha kwa ajili ya matumiziya majumbani na viwandaniunafanikiwa.

    “Tanzania ina mpango wakuwekeza kwenye viwanda,kwa kutambua umuhimuwa nishati katika viwanda,tunakaribisha wawekezaji wenyeuzoefu ili kuzalisha umemeutakaokidhi mahitaji ya viwandavitakavyochangia katika ukuaji wauchumi wa nchi kupitia ajira nakuuza bidhaa nyingine nje ya nchi,”alisisitiza Mhandisi Ishengoma.

    Urusi ni nchi inayoongozaduniani kwa uuzaji wa gesi nje yanchi huku ikiwa ni nchi ya nne katika

    uzalishaji wa umeme duniani baadaya Marekani, China na Japan.

    Wajumbe wa jukwaa kwa ajili ya kujadili Sekta za Nishati na Madinikati ya nchi ya Tanzania na Urusi wakiendelea na majadiliano katikamkutano ujulikanao kama Russian-African Forum 2016 uliofanyika

     jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

    Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Nishati Mbadala,

    Mhandisi Edward Ishengoma kutoka Wizara ya Nishati na Madini,akifafanua jambo katika jukwaa hilo.

    Wajumbe wa jukwaa linalowakutanisha wataalam kutoka Tanzaniana Urusi lijulikanalo kama Russian African Forum 2016 wakifuatiliahotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara waUrusi, Denis Manturov (hayupo pichani).

    Waziri wa Viwanda na Biashara kutoka Urusi, Denis Manturovakisoma hotuba ya ufunguzi wa jukwaa linalowakutanisha wataalamkutoka Tanzania na Urusi lijulikanalo kama Russian African Forum2016 lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.