mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii kupitia ...shn.cloudapp.net/shared...
TRANSCRIPT
-
Mwongozo wa kufundisha afyakatika shule na jamii kupitia
wafanyakazi wa afya
-
Hati zifuatazo zimeandikwa kwa ushirikiano kati ya Partnership for child
Development (PCD) yani Ushirikiano wa Maendeleo ya Mtoto, na Serikali ya
Kenya, Taasisi ya Utafiti ya Kenya ya magonjwa (KEMRI) na International Rescue
Committee, Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na Shirika la
Chakula Duniani (WFP).
Maudhui imeanzishwa kushughulikia changamoto za afya na maarifa, mitazamo na
mazoea ya jamii la Turkana na kambi la Kakuma zinazohusiana na; tabia ya Kula,
viini vya ungojwa na maambukizi, Trachoma, Usafi wa Maji na Mazingira. Taarifa
zilikusanywa kupitia utafiti wa shule za msingi nafasihi ya mapitio ya data sekondari ili
kuhakikisha ujumbe pia kuti maanani umuhimu wa mazingiramaalum na utamaduni.
Picha ni hati miliki ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Watoto(PCD), Imperial College London.
Maelezo [email protected]
-
3
Mathumuni ya kijitabu hiki ni kupatia wafanyakazi wa afya wa kambi ya wakimbizi kakuma na
habari kuwasaidia kufundisha na kuwasiliana kuhusu madhara ya kutokula chakula bora
magonjwa yanayo wadhuru siku hizi kambini na maeneo jirani. Kijitabu hiki ni mojawapo ya
maelekezo ya kuchangia kuhusu afya ya jamii pamoja na mazingira bora ya afya, maelezo ya
lishe bora kwa madhumuni ya kuboresha afya ya jamii kambini na maeneo jirani. Kulingana na
habari zilizopatikana baada ya kukadiria mahitaji, kijitabu hiki kinapeana habari muhimu
ambayo wenyeji wanaweza kutumia kujikinga pamoja na familia zao magonjwa pamoja na
vyakula wanavyo tumia kwa lishe bora.
Kitabu hiki kita patiana elimu na hoja pia habari kuhusu uzuiaji wa magonjwa, ulaji wa lishe
bora na wakati wa kutafuta matibabu ya magonjwa yanayo wakabili. Lishe bora ina umuhimu
mkubwa kwa afya ya mama na watoto, inachangia pakubwa ukuaji wa mtoto, ukomavu wa
akili na pia kuzuia uambukizi wa magonjwa. Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu
kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji wa magonjwa tofauti tofauti.
Mwisho, itachangia kwa habari kuhusu magonjwa na uzuiaji na pia wakati wa kuhitaji
matibabu ambayo itasaidia jamii kushughulikia afya na kuwapa nafasi nzuri kuishi kwenye
mazingira ya afya na maisha mazuri.
Kitangulizi
-
4
Kitabu hiki kina ujumbe kwa mambo manne
ambayo yanaweza kusaidia wafanya kazi wa
afya kupeana ujumbe wa afya na lishe bora
kwa wananchi wa kakuma. Kila sehemu
inaelekeza kiini cha habari, ikieleza hali ya
afya na magonjwa na njia mwafaka za
kujizuia pamoja na jamii na familia wasipate
Marathi na pia kusambaza magonjwa.
Sehemu ya mwisho inazungumzia mamboa
yote yanayoweza kusaidia uzuiaji wa
magonjwa katha na Marathi mengineyo.
Kiini cha habari zifuatazo hapa chini zinaweza
kusaidia kujumuisha jamii na kusaidia
uelewaji wa hatari za magonjwa na pia
wanacho takiwa kufanya kujizuia na lishe
isiyo faa.
Ishara na Muundo
Elimu ya lishe – Umuhimu wa lishe bora una zungumziwa kwa ufasaha,
ambapo kula chakula chenye madini yote na vyenye aina tofauti za
vyakula pamoja na kuzidisha madini bora ya afya ya watu Kaunti ya
Turkana.
Kuepuka ugonjwa wa macho – Sehemu hii inzungumzia zaidi ugonjwa
wa macho unaosababishwa na viini ambavyo vinapatikana sana ndani ya
kambi ya Kakuma. Mbinu zinaelezwa jinsi ya kuzuia ugonjwa wa macho
kutumia tahathari – SAFE (upasuaji, madawa, kuosha uso, kuboresha
mazingira).
Malaria – Ni ugonjwa mbaya ambao unsambazwa na mbu. Sehemu hii
inatujuza kuhusu vimelea (vidudu) na kueleza vile vinavyo smbazwa kwa
wanadamu, dalili na jinsi ya kutibu na pia njiwa za kujikinga kuambikizwa
na ugonjwa wa malaria.
Zuia Minyoo! – Sehemu hii inahusika na minyoo ya tumbo, vile
wafanyavyo mwilini, vile zina sambazwa jinsi ya kujizuia kupata minyoo na
la kufanya ukiwa umeambukizwa.
Maji, mazingira na usafio (WASH) – Sehemu hii inazungumzia
umuhimu wa kuosha mikono mara kwa mara na pia uso kuzuia magonjwa
kwa jamii. Inatufunza kitakacho tokes kukiwa hakuna maji, mazingira bora
ama usafi na pia la kufanya kutahathari na la kufanya ukiwa mgonjwa. Ina
sisitiza sana umuhimu wa kutumia choo na kuosha mikono baada ya
kutoka chooni na pia wakati wa kupika chakula.
Ishara:
1.
2.
3.
4.
5.
-
Lishe hafifu inatokea wakayi watu hawapati
chakula chenye nguvu, protein, mafuta,
vitamin na madini muhimu kutoka kwa
chakula wanacho kula. Haya madini
yanahitajika kwenye mwili ili kufanikisha,
hasa lishe duni inasababishi motto kutokuwa
inavyo hitajika na huweza pia kusababisha
unyonge na umbilikimo, pia iki tatiza uwezo
wa mtoto kusoma vizuri. Baathi ya lishe duni
zinapotokea (chini ya miaka mitano) ni
vigumu sana kurekebika. Ndio maana kuna
umuhimu wa kutengneza chakula kizuri kwa
jamii na watoto wadogo na pia kuhakikisha
watoto wanakula chakula cha kutosho.
Pamoja na hivyo, hata kama chakula ni kizuri,
kama mtu ana njaa siku yeyote ile ni vigumu
kuzingatia na kufanya mambo magumu, ni
vizuri kila familia kula chakula bora na chenye
madini muhimu.
Vyakula viwe na vitu muhimu kama vile GO,
GROW and GLOW – ‘ G Tatu. Hizi aina tatu
za vyakula vinaelezwa hapa.
Kuendelesha jamii elimu juu ya vyakula
vinavyo faa kula ina changia sana kubadilisha
tabia zao za kubadili tabia zao wale vyakula
vya kujenga miili yao
1. Ni nini lishe bora? Kwanini ni muhimu?
Lishe bora ni chakula chenye anina tatu
za vyakula; chakula cha kujenga mwili,
vyakula vya kupatia mwili nguvu,
vyakula vya kuzuia magonja.
Hizi aina tatu za vyakula vinakumbukwa kama
GO, GROW and GLOW vyakula – ‘ Gs’Tatu.
• Vyakula vya GO vyakula vyenye
kupatiana nguvu (carbohydrates kama
vile nafaka na vyakula kama mihogo, viazi
5
1: Elimu ya lishe
Baraza la kufundisha 1: Vyakula vyenye Afya
Umuhimu wa kula vyakula
vyenye afya: ‘GLOW GROW na
GO’ Ujumbe na aina tofaiti za
vyakula
Tunawezaje kuongeza uzuri
wa chakula chetu?
Uduni wa madini muhimu
Micronutrient deficiencies
Vyakula vilivyo jaza madini
muhimu wa kuvijua.
Ishara:
1.
2.
3.
4.
-
6
tamu, karoti na mafuta). Vinatupa nguvu
ya kuendelea na kazi ngumu na kwa mda
mrefu, Tusipokula vyakula vya kuongeza
nguvu mara nyingi tutakuwa na uchovu
na huwezi kufanya shughuli za kila siku.
• Vyakula vya kukua – GROW ni vya
kujenga mwili (kama nyama,
maharagwe and maziwa), Vinatu fanya
kukuwa, omekana na nguvu na wenye
afya. Usipokula vyakula vya kujenga
mwili, watoto wanaweza kuwa na mwili
mdogo sana dhidi ya umri wao.
• Vyakula vya GLOW ni vyakula vya
kukinga mwilivikiwa vime jaa vitamin
na nadini (matunda na mboga za
majani). (Vina saidia kukuza akili
(ubongo) na kufanya mwili kuwa na
nguvu na kukuwa vizuri. Vinatusaidia
kukinga magonjwa na pia husaidia baada
ya kupona ugonjwa. Tusipokula vyakula
vyakuzuia kwa wingi tunaweza kuugua
nmara kwa marana tuta pona pole pole
sana.
2. Tunaweza je kuboresha vyakula vyetu
na vitu tunavyo kula?
Ili kuwa na afya bora na pia kusaidia familia
kuwa na afya jamii wanahimizwa kutengeneza
vyakula vya nyumbani hivi:
• Tengeneza aina tofauti za vyakula kutoka
kwa vikundi vya GO, GROW and GLOW
• Ongeza ukulaji wa vitamin na madini kwa
kula matunda safi, mboga za majani. ma.
Machungwa, matunda ya njano na
mboga za majani mabichi zina lishe bora.
• Lima shamba dogo la mboga pamoja na
matunda ili yaliwe yangali mazuri.
• Himiza mama kunyonyesha watoto wao
hadi miezi sita’ Maziwa ya mama yana
lishe zote mototo ana hitaji ili kukua na
mguvu na pia kuzuia maambukizi ya
magonjwa. Kusitisha unyonyeshaji wa
motto yaweza kusababisha kukua kwa
shida na kusababisha motto apate
magonjwa katha.
• Kula vyakula kama nyama za ngombe,
mbuzi, samaki na kuku ambavyo vina
madini muhimu yanayoweza kuzuia
ukosefu wa damu. Ukiwa huna damu ya
kutosha, kuna kuwa na ukosefu wa hewa
mwilini. Hii husababisha uchovu,
usumbufu, kukosa hewa na huweza
kuzimia.
• Usipike mboga zaidi, hii ina sababisha
madini muhimu kupotea ndanin ya maji
hivyo kuharibu. Pika kidogo tuu ndio
upate madini ya sawa.
3. Kuongeza madini, kwa chakula
Madini ya aina Fulani yana hitajika kwa mwili
kwa asili mia kidogo kidogo. Ukosefu wa hayo
madini husababisha mwili kukosa vitu vya
muhimu na huwa sana kwa watoto. Kwenye
sehemu hii madini muhimu ya afya ya jamii
yana zungumziwa hapa, yanapopatikana, na
muhimu wake kwa mwili, ukosefu na jinsi ya
kuzungumzia kupitia kuongeza madini
kwenye vyakula.
4. Kutambua madini, kazi zinazofanya,
na shida zinazoletwa kwa upungufu
wake.
Madini ndani ya vyakula yana hitajika
mwilini na vitu vilivyo hai kwa maisha
yao yote. Madini hutumika kwa mambo
mengi kwa maish ya wanadamu. Madini
huchangia sehemu nyingi za maisha. Madini
inayo maslahi katika wizara ya afya ni
Vitamin A, Iodine, Zinki na iron. Ukosefu wa
haya madini kwa maisha ya kila siku yana
julikana kama Ukosefu. Ukosefu wa haya
madini husababishwa na:
• Mchanga mahali Fulani una kosa madini
Fulani.
• Vyakula vya jamii Fulani havina madini
muhimu.
• Magonjwa ya aina Fulani yana sababisha
ukosefu wa madini Fulani.
-
7
Vitamini A
Madini yaIodini
Madini yachuma
Madini yaZinc
Maziwa, mayai,
maini, mboga za majani
kama vile spinachi,
sukuma wiki na
machungwa, matunda,
karoti, malenge, viazi
tamuna papayu
Chumvi iliyo na iodini,
maziwa ya ngombe na
mayai
Nyama, samaki,
maini, spinachi,
mayai, mboga za
majani
Nyama, kuku, samaki,
maziwa, nafaka na
njugu
• Ni muhimu kwa afya ya macho na kuona
vizuri. Pia inafanya ngozi kuwa nadhifu na
yenye afya. Ina zuia kuhara, ukambe,
utapiamulo.
• Ukosefu a vitamini A husababisha kuto
ona vizuri na pia upofu wa usiku.
• Inasadia mwili katika kupumua na kukua kwa
misuli. Ni muhimu sana kwa kukua na
kuongeza nguvu ya ubongo na neva.
• Iodini hupatikana kwenye vyakula vinavyo
pandwa mchngani wenye hayo madini kwa
wingi. Mchanga usio namadini ya iodine
unapatikana sehemu za milimani.
• Ukosefu wa iodini leads husababisha ugonjwa
wa goita (uvimbe kwenye shingo).
• Inweza kuwa hali mbaya sana hasa kwa
mama wajawazito kusababisha kuzaa
watoto wenye uzani mdogo, uavia mimba na
watoto walemavu.
• Husaidia damu kuwa na afya nzuri. Kama
huli vya kutosha inasababisha ukosefu wa
damu, uchovu, uvuvu, kizunguzungu na
kuumwa na kichwa.
• Husaidi kufanya mwili kuwa na afya na
kuendeleza ukuaji wa mototo na baru baru.
• Ukosefu wa madini ya zinc ina sababisha
kutokua na magonjwa kama vile kuhara.
Baathi ya mathara yanaelezwa hapa:
Ukosefu wa madini yeyote ni vigumu san kutambua. Kuzuia ni kujaribu kula vyakula vyenye
hayo madini na chakula cha muhimu.
Aina ya madini yanapotoka Kazi yake mwilini
-
8
5. Mazungumzo juu ya kuongeza madini
kwa chakula
Ili kuzuia ukosefu wa madini kwa jamii,
vyakula Fulani vya weza kuongezewa madini
ambapo vitaminni, na madini vinachanganywa
kuongeza lishe za muhimu.
Waulize jamii kama wanajua hivi vyakula
ambavyo vimeongezwa madini.
6. Kuhakikisha umekula vyakula vilivyo
ongezwa madini muhimu
Serikali ya Kenya imesema kuna aina Fulani
ya vyakula vya vinavyo weza kuongezewa
madini:
• Unga wa ngano – umeongezwa Zinc and
chuma
• Unga wa mahindi – umeongezwa Zinc
and chuma
• Chumvi – imeongezwa Iodini
• Mafuta ya kupikia – yameongezwa
vitamini A
Kanuni: Zungumzia kuhusu ana nyingi
za vyakula ambavyo wako navyo hapo
nyumbani na uliza kama kuna vyakula
vilivyo ongezewa madini ama vyaweza
kuongezewa madini.
Eleza kwamba ni vizuri kununua vyakula ambavyo vimeongezwa madini na vitamin kila wakati
iwezekanavyo ili kuwa na afya nzuri. Pia tuangalie vile vyakula vinavyo fungwa, kama vile
chumvi, sukari, ma futa ili kuwa na afya bora nyumbani.
Eleza vyakula vyote vilivyo ongezwa
madini Kenya vina alama ya kuthihirisha.
Onyesha hiyo alama. Uliza kama
nyumbani wana chakula chenye hiyo alama
-
9
Taswira
Trachoma ni ungonjwa unaosabishwa na
vimelea na hatimaye kusababisha upofu na
huambukizwa na mikono michafu, nguo na nzi
ambao hubeba vimelea hivyo. Mapema kabla
ya maambukizi, trachoma huwa haina dalili,
lakinimaambukizi husababisha muwasho,
macho mekundu na kutoa usaa. Dalili zingine
ni kuwashwa kwa macho na kuathiriwa na
mwangaza mkali kwa macho. Vimelea
husambazwa sana na kati ya watoto wadogo
na hatimaye kusababisha upofu wa macho.
Trachomahuathiri jamii maskini, na wanaoshi
katika misongamano na pia wanaoishi bila
maji safi. Jamii zinazoishi maeneo kame na
kavu pia huathirika pakubwa. Uzuiaji wa
maambukizi huhusishwa sana na uoshaji wa
uso (ambao hupunguza uvujaji wa macho
ambayo husababisha maambukizi na pia nzi),
mazingira safi na uwepo wa maji safi
piahupunguza maambukizi.
Upofu wa macho unaweza kuzuiwa, wakati
haswa ubora wa mazingira safi umetiliwa
maanani na jamii zote. Pia unaweza kuzuiwa
kwa kutumia maji safi, kunawa nyuso na
sabuni na pia mikono. Utafiti unaonyesha
kuwa, kupunguza kunya mahali ambapo
hakuna vyoo ni muhimu katika kupunguza
maambukizi haya ya trachoma na
kipindupindu. Mikakati ya WHO ni kuangamiza
ugonjwa wa trachoma hapo mwaka wa 2020
wakitumia mikakati inayofahamika kama
SAFE (Surgery, Antibiotics, Facial cleanliness
and Envirnmental improvement).
Ni muhimu kwa jamii zinazokabiliwa na
maambukizi kufahamu jinsi ya kujikinga
kutokana na maambukizi haya sas na pia kwa
siku zijazo na lipi la kufanya iwapo
wataambukizwa. Ni muhimu pia kuzitia moyo
jamii zilizoathirika kutafuta huduma za
matibabu kwa nja ya madawa ama upasuaji
kabla ya kupofuka macho.
Maudhui
Maelezo yafuatayo yananuiwa kusaidia jamii
na elimu ya kuikinga dhidi ya trachoma.
Sehemu ifuatayo imepeana vipengele muhimu
vya afya kuhusu tabia zitakazosaidia kuzuia
maambukizi hayo.
1. Trachoma ni nini?
Trachoma ni ugonjwa wa maambukizi
ya macho unaosababishwa na uchafu
(vimelea). Hatimaye, husababisha upofu wa
macho kwani husababishakubambuka kwa
kope za macho – kwanza ugonjwa huu ndio
kiini kikuu kinachosababisha upofu ambao
hatimaye unaweza kuzuiwa.
2: SAFE from Trachoma
Trachoma ni nini?
Husambazwaje?
Tutawezaje kusitisha
ugonjwa huu?
Hutibiwa vipi ugonjwa huu?
Vipengele:
1.
2.
3.
4.
-
10
2. Trachoma husambazwaje?
Trachoma husababishwa na uchafu na
vimelea, pia trachoma inaeza ambukizwa
kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia
uhusiano wa karibu hususani kwa vitu
vilivyoathirika kutokana na ugonjwa huo.
Trachoma huambukizwa haswa wakati kitu
kimegusa jicho lililoathirika na baadaye
kugusa jicho ambalo halija athirika, kwa
mfano:
• Taweli, vitambaa vya mkono na
karatasi ya chooni
• Vidole
• Nzi
3. Tutawezaje sitisha/komesha
trachoma?
Usambazaji wa Trachoma unaweza
komeshwa kupitia aina tofauti za
utendakazi.Tunafahamu SAFE.
S is for Surgery: Baadhi ya watuwalioambukizwa trachoma kwa muda mrefu
wanaweza fanyiwa upasuaji ili kurekebisha
macho yao.
A is for Antibiotics: Baadhi ya watuwalioambukizwa na vimelea hivyo wapate
madawa ili kuuwa viini hivyo.
F is for Facial cleanliness: Kuweka usokuwa msafi ili kuzuia nzi kubeba viini hivyo
kwa macho.
E is for Environmental improvement:Kwa kuimarisha usafi wa shule na nyumba,
na matumizi ya vyoo, unaeweza punguza
nzi karibu na wewe na hatimaye kupunguza
uwezekano wa kupata viini
vinavyosababisha trachoma.
Upasuaji na madawa yanahitajika kwa visa muhimu, lakini tunaweza kuhusika kwa sasa ili
kuzuia ogonjwa wa trachoma. Kuweka uso na pia uimarishaji wa usafi wa shuleni na nymbani
utaweza kupunguza nafasi za uambukizaji wa trachoma.
Shughuli: Katika kiwango cha boma na pia kila mhusika ama wahusika wa boma, angalia
vitu ama shughuli ambazo zinaweza changia sana katika maambukizi ya trachoma na pia
vitu vinavyoweza kuzuia usambazaji huo.
Baadhi ya vitu hivyo ni: Nyumba safi, jiko. Matumizi ya choo ama ufukiaji wa kinyesi.
Uoshaji wa uso na usaidizi wa watoto wa changa kunawa mikono.
Unapotembea katika kila boma, angalia vitu vizuri na vibaya kwa wanajamii. Elezea athari
zilizoko,(kwa mfano uwepo wa nzi kwa nyuso za watoto) na jinsi ya kuzizuia (mfano kwa
kunawa uso na kuweka mazingara safi).
-
11
3: Malaria
Utangulizi
Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na mbu.
Huathiri mamilioni ya watu ulimwenguni
mzima na pia husababisha ugonjwa kwa
watoto na wamama waja wazito. Viini
vyenyewe hutambulikana kama Plasmodium
ambavyo huishi kwa damu. Mbu zilizoathirika
na viini hivyo husababisha ugonjwa huo
kupitia kuuma wakati inapofyonza damu.
Walioambukizwa malaria huwa wagonjwa
sana, wakiwa na homa kali, kuhara, kutapika,
kuumwa na kichwa au kuhisi baridi mwilini.
Huhisi kuchoka kwa sababu ya upungufu wa
damu mwilini kwani viini hivyo vya
plasmodium huzaana na kuongezeka mwilini.
Kwa watoto, na pia wamama waja wazito,
malaria yaweza kuwaathiri zaidi. Tiba ya
haraka ni kumeza tembe za malaria ili
kupunguza ueneaji wa viini hivyo. Watu pia
wanaweza kujikinga kwa kulala ndani ya
vyandarua kwani mbu zinazosababisha
malaria huuma usiku. Matumizi ya vyandarua
ama unyunyiziaji wa dawa kwa manyumba pia
husaidia kuuwa mbu kabla ikuume na
kusababisha madhara.
Maudhui
Agenda zifuatazo zinanuiwa kuhamasisha
jamii kuhusu athari za malaria, utoaji wa
mafunzo ya kujizuia wao na familia zao
kutokana na malaria na kugundua dalili za
malaria ili kutoa matibabu mapema.
1. Malaria ni nini?
Malaria ni ugonjwa unaosababisha kifo.
Hufanya watu kuwa wanyonge na kushindwa
na kufanya kazi ama pia kusoma vizuri, na
husababishwa na mbu. Unaposhikwa na
malaria, mtu huhisi uchovu, homa, kuumwa
na kichwa ama pia kuendesha is a killer
disease. Viini vya malaria hujulikana kama
Plasmodium na vidogo sana zaidi ya mbu.
Vinapokuwa ndani ya mwili, huongezeka na
mwishowe kumaliza chembechembe za damu
hivyo kusababisha ukosefu wa damu mwilini.
2. Huambukizwaje?
Malaria huambukizwa kupitia mbu.
Mbu aina ya Anopheles ndo huhusika sana.
Huishi katika kila nchi ote ulimwenguni
ambapo viwango vya joto ni shwari.
Wakati mwengine inaweza maanisha malaria
ni ugonjwa wa msimu. Huwa wakati wa mvua
pekee. Mbu ya kike huitaji maji kulea mayai.
Ni muhimu basi kupunguza maji
yaliyosimama karibu na nyumba na kufunika
vyombo vya maji karibu na maeneo yenu ili
kupunguza hali hii. Mbu ambayo haijaathirkia
huathirika inapouma mtu aliyeathirika.
3. Nani yuko hatarini?
Kila mtu aliyeumwa na mbu aliyeathirika
yumo hatarni, lakini watoto wachanga na
wamama waliowjswszito wamo hatarini zaidi
na wanaweza kuaga kfuatia ugonjwa huo. Ni
muhimu basi endapo mtu wa jamii yuko na
malaria umsaidie apate matibabu.
Wengine huibuwa kinga sababu ya kukaa na
viini hivyo kwa muda mrefu, hii ndio sababu
watoto na waliokuja karibuni wamo katika
hatari ya kuuguwa na malaria.
4. Hutibiwaje?
Iwapo unashuku ama unajua mtu
aliyeathirika na ugonjwa huu, ni muhimu
kupata usaidizi wa kimatibabu katika kituo
cha afya. Tiba ni kupeana dawa za malaria.
Ikiwa hali hii itasalia kama haijatibiwa,
huenda ikasababisha kifo.
Malaria ni nini?
Huambukizwaje?
Nani yuko hatarini?
Hutibiwaje?
Uzuizi wa dawa za malaria
dhidi ya kinga ni nini?
Tunawezaje kuzuia maambukizi
ya malaria?
Vipengele:
1.
2.
3.
4.
5.
6.
-
12
5. Uzuizi wa dawa za malaria dhidi ya
kinga ni nini?
Huu ni ule wakati viini vya malaria, kwa muda
hushindwa kuhisi makali ya dawa na hivyo
kuwa sugu katika kukabiliana na viini hivyo.
Mgonjwa hushindwa kupata afueni hata baada
ya kumeza tembe hizo. Hii ni hatari kwa
sababu matibabu watakayopokea
hayatawasaidia. Tukio hili linatendeka sana
ulimwenguni na sana ni kwa sababu ya dawa
duni ama kutomaliza dawa zote unapopewa
kwa matibabu. Ni muhimu kuhakikisha dawa
ni za kiwango kizuri. Ni muhimu pia
kuhakikisha na anameza kiwango sawa cha
dawa hizo alizopewa mpaka apate nafuu.
Ni muhimu pia kuhakikisha dawa zinazofanya
kazi zafanya!
6. Unaweza kujizuiaje na wengine kupata
malaria?
Kulala chini ya chandarua huzuia mbu kuuma
kwani mbu za malaria huuma usiku. Hii ni
muhimu kwa watoto wachanga katika jamii
na vile vile wamama wajawazito. Ni muhimu
pia kulala chini ya chandarua ikiwa
umeambukizwa malaria kwani huzuia mbu
kutoathirika. Vyandarua vinafaa kufunika
mwenye amelala na kuchomekezwa chini ya
godoro Mashimo ama alama zilizobuniwa kwa
chandarua hicho zafaa kurekebishwa haraka
ili kuzuia mbu. Kuvaa nguo zinazofunika
mkono na miguuwakati wa usiku pia husaidia.
Ni muhimu kuzuia watoto wachanga kwa
kutumia njia hii.
Dawa ya kufukiza ni kemikali inayoweza
kuuwa mbu au kupunguza maisha ya mbu a
hivyo kuuma watu wachache. Vyandarua na
kunyunyuzia vyumba na dawa hizi mwishowe
husaidia kuzuia mbu kutouma. Dawa hizi za
kemikalli zinafaa kunyunyiziwa kila baada ya
miezi 6 hadi mwaka mmoja.
Ikiwa una chandarua cha kudumu. kinafaa
kubadilishwa bssds ys miaka 3.
Mbu aina ya Anopheles hupenda kuishi kwa
maji, ziwa, kidimbwi, na pia mosquitoes like
to breed in water, lakes, ponds and even little
pools of water made in potholes and ditches.
Ikiwezekana hakikisha ya kuwa hakuna maji
yaliyotulia karibu na nyumba.
Shughuli : Uliza mwenye nyumba kama wana vyandarua vya mbu?Uliza
kuonyeshwa. Elezea tofautikati ya LLIN na chandarua kinachostahili kutibiwa kila
baada ya mwaka.
Ikiwa kuna mashimo kwa chandarua elezea sababu ya mashimo hayo na jinsi
yanaweza kurekebishwa.
Onyesha njia nzuri na mwafaka ya kulala kwa chandarua hicho. (completely covered
and with the edges of the net tucked into the mattress).
Uliza mwenye nyumba walichokuwa wakifanya kwa kitanda usiku uliopita? Elezea
umuhimu wa kujifunika usiku, kuwa kwa nyumba na kuzuia kuumwa na mbu wakati
wa msimu.
-
Taswira
Soil-transmitted helminths (STH) ni minyoo
ambazo huishi kwa tumbo na husambazwa
kupitia mchanga, mikono, na wakati
mwenginekupitia kwa chakula ambacho
hakijapikwa vizuri ama kusafishwa vizuri na
huwa na mayai ya Minyoo. Maambukizi
husababisha uchovu, kuumwa na tumbo na
kufura kitambi. Baada ya muda Minyoo hizo
huchangia kutohudhuria shule na matokeo
duni na pia kiwango cha chini cha lishe kwa
ukuaji na maendeleo. Kwa watu wazima, kuna
shida ukuaji na uwezo wa kufanya kazi na
kubidika katika utendaji majukumu ya siku
kwa siku kwani Minyoo huishi kwa tumbo na
hula chakula kilichonuiwa hivyo basi kudorora
kiafya na kutokuwa vyema.
Maudhui
Zifuatazo ni ajenda za mafunzo kwa lengo la
kuwafahamisha wanachama wa jumuiya
hatari ya maambukizi ya vimelea minyoo, na
njia ambazo wanaweza kujilinda na kulinda
familia kupitia tabia ya usafi na jinsi ya
kuvunja mzunguko wa kuambukizwa. Lengo
la ujumbe wa afya ni muhimu kusaidia
kuzingatia kuwa natabia ya usafi.
1. Minyoo ni nini?
Elezea wanajamii kwamaba Minyoo huishi
kwa tumbo na kuzuia chakula na madini
kufika katika sehemu zinazostahili za miili
ya watot. Maambukizi na Minyoo
huwafanya kuchoka, kuumwa na tumbo na
kuwafanya kuhisi wanyonge. Kwa watoto.
maambukizi huzuia ukuaji na pia
huzuia kutohudhuria shule na hatimaye
kupata matokeo duni. Kwa watu wazima,
na pia watoto, mambukizi husababisha
ugumu wa kufanya kazi vyema za siku
baada ya siku. Kuna aina tatu ya
maambukizi ya STH: hookworm,
roundworm, and whipworm.
13
4: ZUIA minyoo!
Minyoo ni nini?
Huambukizwaje?
Tunawezaje kusitisha tatizo
hili la minyoo?
Maana ya Echinococcus jinnsi
ya kuizuia
Vipengele:
1.
2.
3.
4.
-
14
2. Huambukizwaje?
Elezea kwamba Minyoo hutaga mayai
ambayo hutoka kwa tumbo kupitia kinnyesi
na kuambukiza watu wengine kupitia ngozi,
chakula na mikono ambayo haikusafishwa
vizuri baada ya kugusa mayai yaliyo kwa
kinyesi.
Mayai ya Hookworm huanguliwa kwa kinyesi
na kutmbea mahali mtu alitupa kinyesi kupitia
kwa miguu.
Mayai ya Roundworm na whipworm huganda
kwa mikono na chakula kutoka nje. Kula
kutumia mikono chafu ama kuweka mikono
michafu husababisha maambukizi.
3. Tunawezaje kusitisha tatizo hili la
minyoo?
Minyoo zinaweza kuzuiwa kwa njia tofauti:
1. Kutumia choo kila mara
2. Kunawa mikono baada ya kutumia
choo, kuosha motto na baada ya kula.
3. Kuvaa viatu.
4. Kupokea matibabu ya Minyoo mara
moja kila mwaka.
Elezea kuwa utumizi wa choo huzuia watu
wengine kukanyaga kinyes na hatimaye
kuambukizwa hookworm, na pia hueka
kinyesi mbali na watu wengine na mikono.
Mayai ya wadudu wengine hukaa kwa muda
mrefu katika mazingira, hii inamaanisha
yanaweza kuchukuliwa kwa urahisi bila
ufahamu wa kujua umegusa kinyesi
Eleza umuhimu wa kunawa mikono:kunawa
mikono na sabuni baada ya kuenda choo
huangua mayai ya wadudu hawa endapo
yataganda kwa mikono na hivyo kuifanya
mikono kuwa salama kucheza na marafiki
ama kula. Minyoo yengine huishi kwa
mchanga, kwa hivyo ni vizuri kunawa mikono
baada ya kucheza na mchanga ama kutoka
shambani.
Kuvaa viatu pia huzuia maambukizi ya
hookworm ambazo huishi kwa mchangana
karibu na nyumba pia. Zinaweza kuganda
kwa ngozi na kutambaa ndani, kabla ziingie
kwa tumbo.
Kupokea matibabu mara moja kila mwaka
huangamiza minyookatika mwili na hatimaye
kupunguza idadi ya Minyoo. Madawa haya ni
salama na unahitaji tu tembe moja! Tembelea
kituo chako cha afya upate matibabu.
4. Echinococcus na jinsi ya kuizuia
Echinococcus ni aina nyingine ya Minyoo
ambayo kwa kawaida haishi kwa binadamu,
bali huishi kwa mbwa na ng’ombe, kondoo na
mbuzi pia huwa na Minyoo hizi. Kwa kawaida,
njia ya maambukizi huwa ni kati ya mbwa na
wanyama wanaofugwa, wakiambukiza kupitia
nyama ya ng’ombe ama mbuzi (kupitia kwa
mbwa) na kutokakwa kinyesi cha mbwa
ikirudi kwa ng’ombe. Wakati mwengine, watu
huambukizwa kwa kula kinyesi cha mbwa ka
bahati mbaya na hatimaye kusababisha
ugonjwa wa hydatid. Hii hutokea kutokana na
uchafu, mikono michafu ama kunywa maji
kutoka kwa kidimbwi kilichowachwa wazi.
Ugonjwa huu ni vigumu kupata matibabu kwa
hiyo ni vyema mtu kujikinga kwa mara ya
kwanza. Njia za kuzuia maambukizi haya ni
kama ifuatavyo:
• Kunawa mikono kabla ya kugusa chakula
kila mara
• Kutibu maji yaliyochotwa kutokakwa
kidimbwi kilichowachwa wazi kabla ya
kunywa.
-
Taswira
Uhaba wa maji na usafi duni wa kiafya yote
haya yamesababisha maambukizi kupitia
uchafu kama vile kinyesi. WASH yaani Water,
Sanitation and Hygiene ni muhimu katika
kuzuia magonjwa kwa hali kama vile
kuharisha trachoma na maambukizi ya
wadudu. Kwa muktasari, maji safi huzuia
usambazaji wa magonjwa yanayohusiana na
maji kama vile kuharisha na kipindupindu.
Kuharisha ni baadhi ya magonjwa matatu
ambayo husababisha vifo kwa watoto.
Vile vile, usafi wa maji huzuia usambazaji wa
magonjwa kama vile trachoma na magonjwa
mengine yanayosababishwa na wadudu.
Maambukizi ya
magonjwa haya
yanaweza kutokea
kupitia hali duni za
kiafya kwa sababu ya
uhaba wa maji safi ya
kuosha.
Mbinu za usafi, kama vile kuongeza
matumizi ya vyoo inaweza kusaidia kuweka
kinyesi na vitu vingine vinavyosababisha
maambukizi mbali na watu na hivyo kuzuia
nzi kuzaa. Kinyesi kwa mara nyingi huweka
mayai ya wadudu na pia uchafu. Hookworm
kwa mfano hupatikana kwa kinyesi na
inaweza kusambazwa kupitia kutembea kwa
kinyesi na kutonawa mikono kabla ya kula na
kutayarisha chakula.
Mabadiliko kuhusu
huduma za WASH ni
lazima ziambatane na
mabadiliko ya
mapendekezo kuhusu
afya, ambayo ndo
maana elimu ya afya na
habari ni muhimu.
Unawaji wa kawaida wa mikono baada ya
kutumia choo na kabla ya kutayarisha chakula
unaweza kupuguza mizigo mingi ya
magonjwa na athari zake.
Maudhui
Agenda za mafunzo zifuatazo zimelenga
kuhamasisha wahusika wa jamii kuhus njia
ambazo wanaweza kujikinga wao pamoja na
jamii zao kutokana na vimelea na viini
vinavyosababisha maambukizi. Kiini kikuu cha
ujumbe wa afya ni vipi maambukizi ya
vimelea na viini vinaweza kuafikiwa kupitia
uoshaji wa mikono, matumizi ya vyoo safi na
uvaaji wa viatu.
1. Kwa nini uwekaji wa mikono na nyuso
ni muhimu?
Magonjwa mengi husababishwa na uchafu
ama viini ambavyo husambaa kupitia kwa
mikono michafu na mazingira machafu.
Magonjwa haya ni Minyoo, trachoma na
kipindupindu.
Elezea jamii na wenye nyumbas: Viini vingi
huwa kwa kinyesi na inaweza kukupea
ugonjwa iwapo utakula ama kunywa kwa
bahati mbaya. Huwa ni vidogo mno, kwa hiyo
hatuwezi kuviona na ni muhimu mtu kuwa
muangalifu.
Kwa nini uwekaji safi wa
mikono na nyuso ni muhimu?
Kuharisha ni nini na ni vipi
inaweza kutibiwa?
Ni vipi tunaweza kudumisha
usafi wa mikono nyuso?
Wakati muhimu wa
kutekeleza uoashaji a mikono
Jua lini na vile utaweza
kutibu maji kabla ya kunywa.
Vipengele:
1.
2.
3.
4.
5.
15
5: Maji na Usafi wa Mazingira and wa mwili
-
16
Viini i vinaweza kukusababisha ukawa
mgonjwa na kufanya tumbo kuwa na shida na
hatimaye kuharisha. Viini hivi ni vimelea na
Minyoo ambavyo ni vidogo mno. Huanza
kidogokwa kimo na hatimaye kukuwa kwa
urefu wa zaidi 35cm
E lezea jamii kwa vile viini viko kwa mchanga
ni muhimu kuepuka yafuatayo:
• Matumizi ya choo kumaanisha watu
hawatagusa kinyesi
• Kunawa mikono kumaanisha hutashika
viini au hata kula na mikono chafu.
• Kuweka choo kuwa kisafi kumaanisha
hutabeba uchafu unapoenda choo
• Kutoenda choo ama kunya karibu na maji
husambaza viini kupitia kwa maji.
• Kuvaa viatu.
Hatua hizi pia ni muhimu kwa kuzuia
trachoma: kujiweka msafi na nyumba yako
na shule itaondoa nzi ambazo husababisha
kuenea kwa trachoma.
2. Kuharisha ni nini na ni vipi kunaweza
kutibiwa?
Uliza mwenye jamii jinsi anavyoeza kuelezea
ya kwamba kuna kuharisha ?
Eleza kwamba: DKuharisha hutokana na
kula chakula ama maji machafuyaliyo na viini
hivyo. Kunaweza sababishwa na kutumia
mikono chafu.
Dalili za kuendesha ni kama kunya damu,
ama kutoa choo laini kwa siku kwa muda wa
siku tatu.
Husababisha kuishiwa na maji mwilini. Watoto
wachanga wanaweza poteza uhai sababu ya
kuishiwa na maji mwilini.
Lipi la kufanya ikiwa kuna mtu katika jamii
ambaye anaharisha?
Eleza kwamba: Ni muhimu kuhakikisha
kwamba mgonjwa anakunywa maji mengi na
kula chakula kilicho na madini ili kustiri
upotevu wa maji mwilini. Kwa
kawaidakikombe kimoja (250ml) cha maji
kwa kila kipindi.
Oral Rehydration Therapy pia husaidia na
endapo atakuwa mgonjwa sana, ORS pia
husaidi mwili.
Eleza njia ya kutengeza ORS nyumbani
ukitumia yafuatayo:
• Vijiko 6 vya sukari.
• Kijiko ½ teaspoon chumvi.
• Litre moja ya maji masafi yaliyotibiwa.
Elezea pia ni muhimu kuhakikisha ya kwamba
vipimo ni kamili.
-
17
3. Jinsi ya kuweka uso na mikono yako
kuwa safi
Eleza jinsi ya kunawa mikonos:
1. Loa mikono yako na maji safi
2. Weka sabuni kwa mikono yote
3. Sunza mikono ukitumia maji safi
Ikiwa sabuni haipo, tumia jivu Kunawa uso
fanya hivyo pia.
4. Ni wakati gani unafaa kunawa mikono
na uso?
• Wahusika wote wa jamii wanapaswa
kunawa nyuso zao kila siku kupunguza
athari za kupta trachoma.
• Unafaa kunawa mikono na sabuni ama
jivu baada ya kuenda chooni ili kupunguza
viini.
• Unafaa kunawa mikono kabala ya kula
chakula ama kutayarisha chakula kuzuia
maambukizi.
• Mikono inafaa kusafishwa baada ya
kubadiliisha mtoto.
• Mikono inafaa kusafishwa kabla ya
kunyonyesha.
5. Kunywa maji masafi
Maji yaliyochotwa kutoka kwa mto ama
kidimbwi kilichowazi yanafaa kutibiwa kabla
ya matumizi ili kupunguza viini na uchafu na
hatimaye kuifanya kuwa salama. Kwa mfano:
• Kuchemsha maji: maji yanafaa kuwa
yakichemka kwa muda wa dakika 10.
• Kutibu na aquatabs, PUR.
• Kutumia chlorine: 1/8 yakijiko kidogo
cha unga huo kwa lita 10 za maji. Unga
huo unafaa kuwa mkavu na kuhifadhiwa
kwa mkebe uliofunikwa. Maji na Chlorine
yanafaa yatulie kwa muda wa dakika 30.
• Kuua vini vya ungojwa vilivyomo
ndani ya maji kwa kutumia nguvu za
miali ya jua: Jua hua na miyale ambayo
pia huaribu viini vinavyosababisha
maradhi. Acha maji yatulie kwa chupa
kwa muda masaa matano.
-
18
Maelezo
-
Maelezo
19
-
Partnership for Child Development
Imperial College London
School of Public Health
Norfolk Place
London
W2 1PG
www.schoolsandhealth.org
@schoolshealth