jifunze ukue kiroho - wordpress.com · 2016-09-24 · kumbe ni mpango mungu mimi na wewe kukua na...

31
JIFUNZE UKUE KIROHO "Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako………." (Mhubiri 12:1, [SUV]) Mwl. Daudi, JL VIJANA NA UTUMISHI.

Upload: others

Post on 08-Mar-2020

24 views

Category:

Documents


8 download

TRANSCRIPT

Page 1: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE

UKUE

KIROHO

"Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako………." (Mhubiri 12:1, [SUV])

Mwl. Daudi, JL

VIJANA NA UTUMISHI.

Page 2: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

Uk. | i

JIFUNZE UKUE KIROHO

Mwl. Daudi, JL

© 2016 VIJANA NA UTUMISHI

baruapepe; [email protected]

simu: +255(0) 764 771 298

blogu: vijananautumishi.wordpress.com

HAKI ZIMEHIFADHIWA.

e-kitabu hii ni bure na unaweza kutumia masomo yake kufundisha

katika semina, makongamano, n.k ukipata ruhusa kwa mwandishi

husika na si vinginevyo!.

Page 3: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

Uk. | ii

e-kitabu hii ni kwa heshima ya Mungu aliyenipa WAZO la

kuandika na kuunganisha masomo mbalimbali ya watumishi

wa Mungu.

Page 4: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

Uk. | iii

SHUKRANI

Kwanza kabisa, Napenda kumshukuru Bwana Yesu aliyenipa WAZO hili la kuandika e-kitabu itakayounganisha masomo yote ya watumishi mbalimbali yalisomwa kwenye blog ya VIJANA NA UTUMISHI kwa mwaka 2015. Sikuishia kuwa na WAZO tu bali nilipiga hatua ya kuanza kuandika baada ya kuwashirikisha baadhi ya watumishi wa Mungu kuwa masomo yao yatakuwepo kwenye e-kitabu. Mpaka kufikia hatua ya kumaliza kuunganisha masomo yote na kukamilika kwa kazi hii, SIFA na UTUKUFU ni kwa Mungu wa Mbinguni.

Pia niwashukuru watumishi wote wa Mungu kutoa ridhaa ya kuchukua masomo yao. Mungu akubariki sana Raphael, JL Founder wa YKM, Mwl. Conrad Conwell wa Neema Ya Kristo, Peter M Mabula wa Maisha ya Ushindi, Hosea G Paul Mission Leader wa COTOJEMI, Mwinjilisti Seth Nyenzi na Godfrey Miyonjo.

Namshukuru kipekee mchungaji Elly Chilewa wa EAGT-BUIGIRI mkoani Dodoma kwa kunilea kiroho tangu nimempokea Yesu Kristo katika maisha yangu. Pia shukrani zangu za dhati ziwaendee Mchungaji Godwin Shilla wa EAGT-MWENGE, Mchungaji Elly Boto wa PAG-KAWE na wengine wote ambao kwa namna moja au jingine wamehusika kujengana katika safari ya kwenda mbinguni.

-Mwl. Daudi, JL.

Page 5: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

Uk. | iv

YALIYOMO

SHUKRANI……………………………………………………………………………………...…iii

WALIOGUNDUA UTAJIRI WA HII SIRI WAMEPONA…………………………………………….1

HOFU YA MUNGU………………………………………………………………………….……..5

NGUZO ZA MIPAKA NA HUKU UNAFURAHIA UHURU USIO NA MIPAKA……………………..7

KUKUWA, KUSTAWI, KUCHANUA KIROHO……………………………………………………11

NINI MAANA YA UPENDO………………………………………………………………………13

SABABU SABA (7) ZITAKAZO KUFANYA KUWA MSHINDI DUNIANI………………………….15

VIZUIZI KUMI (10) VINAVYOZUIA MAOMBI YAKO USIPOKEE ULICHOOMBA KUTOKA KWA MUNGU………………………………………………………………………………………….18

Page 6: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

Uk. | v

Utakapomaliza safari ya kusoma masomo mbalimbali yaliyo ndani ya e-kitabu hii, maisha yako ya kiroho hayatabaki kama yalivyokuwa. JIFUNZE UKUE KIROHO kama ilivyo jina la e-kitabu baada ya kujifunza tegemea ongezeko la maisha yako ya kiroho hata kiwango chako cha kumtumikia Mungu kitapanda juu. Safari huanza na hatua ya kwanza mpaka kufika mwisho, katika ebook usiishie njiani fika mpaka mwisho. Mungu akubariki, twende pamoja sasa!............

Page 7: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 1

WALIOGUNDUA UTAJIRI WA HII SIRI WAMEPONA

Na: Mwl. Daudi, JL.

“Kwa ufupi, Mwl. Daudi, JL ni mwalimu wa Neno la Mungu na amekuwa akihubiri na kufanya semina sehemu mbalimbali Tanzania. Amewahi kufanya kazi pamoja na huduma ya vijana mashuleni inayoitwa CASFETA-TAYOMI. Pia ameshiriki pamoja na CASFETA-TAYOMI kufanya huduma ya kufikia maeneo yasiyofikiwa na injili hasa vijijini ijulikanayo kama OUTREACH MISSION.Pia Mwl Lubeleje ameshiriki sana makongamano ya PASAKA yanayoandaliwa na wanafunzi mashuleni. Amehitimu shahada ya ualimu katika masomo ya Hesabu na Uchumi katika chuo kikuu cha Mzumbe Tanzania. VIJANA NA UTUMISHI ilianza Januari, 2015 mbebaji MAONO akiwa ni Mwl. Daudi, JL ikiwa na lengo la kutengeneza “UWANJA” au PLATFORM maalumu kwa vijana ili kutambua fursa zao za kumtumikia Mungu. Sasa twende pamoja katika somo hili”.

UTANGULIZI

Kabla sijaendelea nikumegee neno moja kuwa “Usipoelewa kitu Mungu anakupa Adui huja na kuondoa ili usije ukaelewa na kupona na kupokea muujiza wako”. Ukisoma mathayo 13:19 inasema “19 Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake……….”. Kinachomfanya mwovu aje kunyakua/kuiba/kuondoa neno la ufalme lililopandwa moyoni mwa msikiaji ni “….wasije wakaamini na kuokoka” (Luka 8:12, SUV). Unaona!!! Wengi wetu tunaibiwa bila sisi kujua. Unaposoma somo hili naomba kwa jina la Yesu siri iliyoko ndani yake ubaki nayo na uanze kukua kwenda viwango vya juu.

Katika-kati ya miezi ya 8 hadi 9 mwaka 2014 Nilikuwa nafundisha shule moja iliyoko mkoa wa Dar-es-salaam. Nakumbuka jioni moja baada ya kutoka shule nilipata msukumo wa kusoma kitabu cha wakolosai. Wakati nasoma ndipo nilipopata siri hii ambayo binafsi imebadilisha maisha yangu, najua na wewe hutabaki ulipo.

Siri hii kubwa inaitwa “KUZIDI KATIKA MAARIFA YA MUNGU” ambayo mtume Paulo anaifunua na kuiweka wazi katika mstari wa 10 wa kitabu cha wakolosai sura/aya ya kwanza. Maandiko yanasema “10 Mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa

Page 8: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 2

matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;”. Nataka uone tena Mtume Paulo anachosema kwa wazi kuwa “….na kuzidi katika maarifa ya Mungu”. Waliogundua siri hii wengi WAMEPONA!!!. Sasa nataka tuone siri hii kwa undani wake ilivyo na namna ambavyo viwango vyetu vya kiroho na kumjua Bwana vinaweza vitaongezeka.

MAARIFA YA MUNGU NI NINI?

Maarifa hujulikana kama Knowlegde. Neno maarifa lina maana nyingi kulingana na watu mbalimbali wanavyofafanua na kuelewa. Ziko maana kadhaa ambazo nimetafuta na kukuandikia kama ifuatavyo;

Maarifa ni Elimu uliyoipokea Pia maarifa ni taarifa na ujuzi uliopatikana kupitia uzoefu au mafunzo fulani

(information and skills acquired through experience or education)

Hivyo taarifa, ujuzi au elimu ambayo imepatikana kupitia kujifunza darasani au uzoefu wa kufanya jambo kwa muda mrefu kwa ujumla wake inaitwa maarifa.

Maarifa ya Mungu ni taarifa na ujuzi au elimu inayopatikana kupitia kujifunza mambo ya Mungu. Kwa namna nyingine tunaweza sema kuwa Maarifa ya Mungu ni kuwa na taarifa (information) kamili za mambo ya Mungu. Sasa najua mpaka hapo utakuwa umepata vizuri maana ya neno maarifa ya Mungu. Hebu daka pointi hii hapo chini;

POINTI: Kama maarifa ya Mungu kupatikana kwa kujifunza mambo ya Mungu, Hatuwezi kwepa kusoma Neno la Mungu maana ndilo limejenga msingi wa kujifunza kwetu. Kujifunza kwetu hufanya Neno la Mungu lijae kwa wingi ndani yetu na kufanya hivo ni kupata maarifa ya Mungu.

Kumbuka tulisoma wakolosai 1:9 ambayo inasema “10 Mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;” Mstari huu pia unaweza kusomeka kama ifuatavyo;

“…….and steadily growing and increasing in and by the knowledge of God (Amplified Bible)

Page 9: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 3

“…….and increasing in the knowledge of God (ESV)

“………….growing in the knowledge of God (NIV)

Tunaweza ona sasa kuwa neno KUZIDI ni INCREASING au GROWING kwa lugha ya kingereza. Tafsiri ya neno increasing ni KUKUA, KUPANUKA au KUONGEZEKA. Hivyo kwa tafsiri pana ya mstari wa 10 tunaweza sema;

“…..na kuzidi au kukua au kupanuka au kuongezeka katika maarifa ya Mungu”

Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Hebu daka pointi hii;

POINTI: Kuzidi katika maarifa ya Mungu ni kuongezeka, kukua na kupanuka katika ile hali ya kuwa na taarifa, elimu au ujuzi uliopatikana kupitia kujifunza mambo ya Mungu.

Ukitaka kukua na kuzidi katika maarifa ya Mungu uwe mwenye kufundishika pale Roho Mtakatifu anapoachilia maarifa ya Ki-Mungu ndani yako, uwe tayari kuwa mwanafunzi mwa Yesu Kristo unayepokea cha Bwana. Tusome mstari ufuatayo na utaona na gundua kilichopo hapo;

“……akiwatokea muda wa siku arobaini na KUYANENA MAMBO YALIYOUHUSU UFALME WA MUNGU” (Matendo ya Mitume 1:3). Hapa akina Petro, Yohana walikuwa darasani na Kristo alikuwa akishusha somo la “Mambo ya ufalme wa Mungu”. Katika hali utegemee kuona kwamba hawa wanafunzi WALIZIDI NA KUONGEZEKA KATIKA MAARIFA YA MUNGU.

CHANZO CHA MAARIFA.

Kuna vyanzo vitatu vya maarifa;

1. Mungu 2. Shetani

Page 10: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 4

3. Mwanadamu

Kulingana na somo letu tutaona chanzo kimoja ambacho ni Mungu. Tunazidi tunakua tunaongezeka katika maarifa ya Mungu. Chanzo cha maarifa ya Mungu ni Mungu mwenyewe. Hebu tuone kwenye maandiko.

Neno la Mungu katika Mithali 1:7 linasema “ Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa………”. Katika biblia ya English Standard Version (ESV) inasema “The fear of the Lord is the beginning of knowledge……”. Maandiko yanasema kuwa KUMCHA BWANA NI CHANZO CHA MAARIFA. Hapo hakuna ujanja kabisa kwamba unataka maarifa ya Mungu basi anza kumcha Mungu. Hebu tuone tafsiri ya neno KUMCHA BWANA kama tunavyoona ndio msingi wa maarifa ya Mungu. Neno kumcha Bwana kwa tafsiri ya kiingereza ni fear of the Lord ambayo humaanisha HOFU YA MUNGU. Sasa HOFU YA MUNGU ni KUMPA MUNGU HESHIMA YOTE, ni KUMWESHIMU, KUMTUKUZA na KUMPA SIFA ZOTE MUNGU. Sasa unaweza kujiuliza kwamba nikimcha Mungu hayo maarifa yanakujaje?. Haleluya!!! Jibu lake ni hili. Tusome katika Mithali 2:6 imasema “Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;”. Narudia tena kuwa “Kinywani mwake (Mungu) hutoka maarifa”. Kinywa kazi yake ni kusema, kwahiyo Mungu anachokuwa anasema kinakuwa kimebeba UJUZI/ELIMU/TAARIFA kwa ajili yako ambayo ukiyapata ni MAARIFA tosha ya kukusaidia au kukuvusha mahali unapita. Sasa ile hofu ya Mungu inakufanya kuwa na tabia ya KUSIKILIZA cha Mungu. Hebu daka pointi ifuatayo;

POINTI: Tukimcha Mungu, tutasikiliza anachosema maana kinywani mwake hutoka maarifa na hivyo chanzo cha maarifa ya Mungu ni Mungu mwenyewe.

Tusome tena katika Mithali 12:1 na Neno la Mungu linasema “Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa…….”. Nataka uone siri hii wewe ambaye umekuwa hupendi kufundishwa kwamba “Ukipenda mafundisho umependa maarifa” kwanini? Jibu ni kuwa Ndani ya mafundisho kuna huo ujuzi na elimu ya kuachilia maarifa ndani yako. Ila kumbuka hayo mafundisho hutoka ndani ya kinywa cha Mungu. Soma tena katika Ayubu 22:22 inasema “Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, na maneno yake yaweke moyoni

Page 11: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 5

mwako”. Sasa utakuwa umeona siri iliyopo hapo kuwa Kumcha Bwana kunapelekea kupokea cha Mungu na baada ya kupokea tegemea kuona kuna maarifa ya Ki-Mungu yanakuwa yameachiliwa ndani yako.

FAIDA ZA KUZIDI KATIKA MAARIFA YA MUNGU.

Sasa hebu tuone faida za kuzidi katika maarifa ya Mungu. Ziko faida nyingi kwa kadiri unavyozidi kusoma neno utaona Bwana anazidi kukufunulia zaidi. Hapa nimeandika faida tano (5) ambazo sisi watoto wa Mungu tutapata

1. Hatuwezi kuangamizwa kwa kukosa maarifa. Hosea 4:6 inasema “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa……”. Tunapojaa maarifa ya Mungu ndani yetu tunatoka kwenye kundi la kuangamizwa.

2. Hatuwezi kuchukuliwa mateka kwa kukosa kuwa na maarifa. Isaya 5:13 inasema “ Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa…..”.

3. Maarifa ya Mungu hutufanya tuzidi kukua katika kumjua Mungu. 2 petro 3:18 4. Tunazidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Waefeso 6:10 5. Tunajazwa na maarifa ya mapenzi ya Mungu katika hekima yote na ufahamu wa rohoni.

Wakolosai 1:9

HOFU YA MUNGU

Na: GODFREY MIYONJO

“Kwa ufupi, Godfrey Miyonjo ni mtumishi wa Mungu ambae Mungu amempa Neema ya kuandika masomo mbalimbali ya Neno la Mungu. Anatarajia kuhitimu masomo yake katika chuo cha Mount Meru. Somo hili la Hofu ya Mungu amefafanua vitu vingi vya msingi, karibu!”

“Ibrahim akasema , kwa sababu naliona, Yamkini hapana HOFU YA MUNGU mahala hapa, nao wataniua kwasababu ya mke wangu” MWANZO 20:11.

Watu wengi hudhani kuwa, kuwa na HOFU YA MUNGU ni kuhubiri, kuimba kwaya, kushuhudia nyumba kwa nyumba, kutoa sadaka, kukemea mapepo, kuhudhuria ibadani, N.K,

Page 12: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 6

kitu ambacho siyo kweli. Kutokana na dhana walizonazo watu wengi katika vichwa vyao huwapelekea kufanya vitu ambavyo kimsingi havina faida yoyote kwao. Unakuta mtu anahubiri, anafunga, anaomba, anaimba kwaya, anatoa sadaka, N.K, lakini ndani ya moyo wake anashuhudiwa kabisa kuwa yeye ni mpagani/haishi sawasawa na Neno la Mungu.

Kutokana na kutokuwa na HOFU YA MUNGU na kujiepusha na uovu mtu huyo anafanya kazi ya bure (kazi isiyo na faida), Imeandikwa “Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali name, Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu” MATHAYO 15:8-9.

Hofu ya Mungu ni hali ya utii na unyenyekevu aliyonayo mtu ndani ya moyo wake. Hali hiyo humpelekea mtu kuishi sawasawa na Maagizo ya Mungu/Neno la Mungu. Yaani HOFU YA MUNGU humfanya mtu kuyajua yale yampasayo kutenda na yasiyompasa kutenda. HOFU YA MUNGU humfanya mtu kuishi MAISHA HALISI, Yaani kutokuishi maisha ya maigizo. Mtu aliye na HOFU YA MUNGU kila jambo analolifanya ni halisi kwake, ikiwa ni kutumika mbele za Mungu ni kiuhalisia, anapofanya ibada mbele za Mungu ni ibada halisi. YOHANA 4:23-24. Hafanyi jambo kwa kufuata mkumbo tu, kama wasio na HOFU YA MUNGU wafanyavyo, Kwa maana Wasio na HOFU YA MUNGU hufuata mkumbo, huwa hawaishi MAISHA HALISI, huwa anaigiza daima, humkiri Mungu kwa midomo tu, ila ndani ya mioyo yao huwa hawana mapatano kabisa na Mungu/Wamefarakana na Mungu.

Mtu asiye na HOFU YA MUNGU hufanya jambo kutokana na hofu ya wanadamu, hali au mazingira. Hata kama anafanya ibada, anaimba, anatoa sadaka, anahubiri, N.K ni kutokana na mazingira tu, Yaani anafanya ili aonekane na watu kuwa nay eye anafanya. Ndani ya moyo wake huwa na mambo haya: “nisipofanya hivi flani atanionaje?” “nisipofanya hivi nitatengwa na jamii”, “nisipofanya hivi nitafukuzwa kazi”, “nisipofanya hivi watoto wangu watakufa na njaa” “nisipofanya hivi sitaoa/sitaolewa”, N.K. Mtu hajiulizi kuwa Mungu atanionaje, anajiuliza juu ya watu na mazingira. Mungu huchukizwa sana na watu wa jinsi hii, wasio na HOFU YA MUNGU badala yake wanakuwa na hofu ya wanadamu, ndiyo maana anasema:“Mimi, naam, mimi ndimi niwafarijiye; wewe u nani hata ukamwogopa mtu atakayekufa, na mwanadamu atakayeffanywa kuwa kama majani?” ISAYA 51:12.

Page 13: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 7

Yaani imezoeleka mitaani kuona wachawi wakiogopwa kuliko Mungu, Imezoeleka kuona kiongozi wa dini/siasa anaogopwa kuliko Mungu. Mtu yupo tayari kunyenyekea chini ya mkono wa mwnadamu kuliko knyenyekeza chini ya mkono wa Mungu.Yupo tayari kutekeleza maagizo ya mwanadamu (kiongozi wa dini/siasa, mganga) kuliko maagizo ya Mungu. Hayo yote huwa hivi kwasababu watu wengi wamekataa ndani ya mioyo yao kuwa na Mungu, watu hawataki kufungua mioyo yao ili wapate kujifunza habari za UFALME WA MBINGUNI. Wamekataa kuwa na ufahamu ndani ya mioyo yao, wameamua kujilisha vitu visivyofaa,

Imeandikwa: “Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa; Bali kinywa cha wapumbavu hula upumbavu” MITHALI 15:14.Je! Wewe nawe u miongoni mwao? Ninasema! Ni heri uamue kutubu leo, kwa maana siku ile ya ajabu na ya kutisha imekaribia sana, kumbuka kuwa imeandikwa: “Naye aliye mwenye moyo mkuu miongoni mwa mashujaa Atakimbia uchi siku ile asema BWANA” AMOSI 2:16.

NGUZO ZA MIPAKA NA HUKU UNAFURAHIA UHURU USIO NA MIPAKA

Na: Raphael, JL. THE YOUTH KINGDOM MINISTRIES [YKM] FOUNDER.

“Kwa ufupi, Mwaka 2003 nilipata maono ya kuwatumikia vijana kwani niliona GAP au NAFASI au FURSA iliyokuwa imefungwa ndani ya ufahamu wa vijana. Nikahudhuria mikutano mingi ya vijana ndani na nje ya nchi na kuzidi kuona aina ya vijana wanaoandaliwa kuwa viongozi, napo nikazidi kuona GAP. Mwaka 2007, nikaanza kutuma jumbe kwa simu kwa vijana 24, kwa wakati ule nilikuwa na huduma ikiitwa INTELLECTUAL PRAYER WORRIERS NETWORK (IPWN) ambayo iliniwezesha kutuma jumbe fupi kwa njia ya simu zilizoitwa WEEKLY SCRIPTURE PRAYER POINTS (WSPP) kwa lengo la kuwahamasisha vijana kuomba kwa kutumia neno la Mungu. Mwaka wote wa 2007 nilifanikiwa kuwa natuma jumbe fupi za namna hiyo kwa vijana ambao walikuwa wakipatikana katika baadhi ya vyuo vikuu kama Mzumbe, Dar es salaam na Tumaini Iringa ambayo sasa ni chuo kikuu cha Iringa.

Shauku yangu ilikuwa ni kuwasaidia vijana kuweza kuona uwezekano wa kuomba kwa kutumia neno la Mungu kwa kupata jumbe fupi kwenye simu zao. Niliamini simu zinaweza kutumika

Page 14: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 8

vizuri kama madhabahu ya kupeleka ujumbe wa kuwasaidia vijana. Mafanikia yalikuwepo na yalionekana.

Mwaka 2008, niliendelea kutuma msg na kipindi hiki kwa kufichua jina la Mindset Upgrade, ambalo lilinisaidia kuendelea kupeleka jumbe mbalimbali za neno la Mungu kwa vijana kwa njia ya simu zao. Niliendelea kutuma na kufanya hivi ikiwa ni pamoja na kutoa maombi kwa vijana kwa njia ya simu zao mpaka YKM ilipozaliwa mwisho wa mwaka 2011 na kuwekwa wakfu rasmi mwaka 2012 na mpaka sasa. Tokea wakti huo YKM imekuwa ikiwafikia vijana Tanzania na nje, nchi kama China, Afrika ya Kusini, India, Uingereza nk (Raphael, JL. YKM Founder)”.

UTANGULIZI

Hizi ni changamoto. Zipo nyingi. Nisipofanikiwa kuzisema zote, wewe unaepitia kama mimi nilivyopita unaweza ukaongeza kwa kuweka comment zako hapo chini ili watumishi wengi zaidi wafunguliwe na ili vinaja wengi zaidi pia waelewe hali halisi katikati ya utumishi huu. Ni muhimu tukaelewa kuwa kuishi ndani ya mipaka ni jambo gumu sana kwenye ulimwengu unaokutaka uwaze nje ya box au uondoe mipaka na vikwazo vinavyokufanya uwaze kama mfungwa. Ni muhimu sana kuweka mipaka.

NGUZO ZA MIPAKA NA HUKU UNAFURAHIA UHURU USIO NA MIPAKA

Narudi tena, mipaka ni muhimu katika huduma yoyote na hasa ya vijana. Zipo sababu nyingi sana za kuweka mipaka kwani kwa bahati mbaya sana yapo mambo tunayoyafurahia wakati tunajitajidi kuyawekea mipaka. Yaani unaweka mpaka kwenye jambo baya unalopenda kulifanya, ni sawa kabisa na Eva alipokula tunda alilokatazwa na Mungu pale Mwanzo 3:6, kuna sababu zimfanya ale tu ambazo ni; alipoona ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa basi alitwaa lile tunda na akala na akampa na mume wake naye akala. Naomba nieleweke. Eva hakula tunda kwakuwa alikuwa hajui alichokuwa anatakiwa kufanya au alikuwa hana maono. Kibaya zaidi yeye hakula kama Esau. Yaani hakula kwakuwa alikuwa na njaa, hapana. Na katika sababu zilizoandikwa njaa haipo. Ndo hapo nasema najitahidi kujiwekea mipaka katika mambo mabaya ninayoyapenda. Mambo gani hayo ninayoyapenda yaliyonipelekea kujifunza haya mambo kwa maumivu haya:

1. Tamaa in nguvu ya ajabu. Mtumishi kijana kama mimi na umbile zuri la mwili alilonipa Mungu lina kusudi lake lakini nawezaje kumtumikia Mungu kwa vijana ambao wana

Page 15: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 9

mvuto nana ni warembo. Hata hapa simaanishi ni changamoto kubwa kwa mtumishi mkaka kuwatumikia wadada au kinyume chake maana siku hizi kuna mambo ya ushoga na usagaji, nadhani naeleweka hapa. Mungu alinivusha viunzi vya ushoga nikiwa mwaka wa pili chuo kikuu toka kwa mtu ambaye nae ni mtumishi. Asante Yesu. Tamaa mbaya biblia inasema ndio kuabudu sanamu. Tamaa ya mali, tamaa ya wanawake, tamaa ya wanaume, tamaa ya umaarufu, tamaa ya kutaka kuonekana najua kila kitu, ipo inakula ndani kwa ndani. Wakati natoa ushauri na hasa kwa jinsi tofauti, kwa ndani kabisa ya mtima wangu kuna kitu kinapiga kelele kikiibua hisia za tamaa. Tamaa iliyojificha katika huruma za kibinadamu. Tamaa iliyojificha katika udhaifu wa anaetamaniwa. Tamaa iliyojificha ndani kabisa ya kutaka huyo unaemshauri akuone hakuna mwingine anaeweza kumwelewa au kumsaidia zaidi ya wewe.

2. NAJISIKIA VIZURI KUSIFIWA KULIKO HERODE. Kiukweli nataka nifanye huduma, nimshauri na kumsaidia huku moyoni mwangu nikitarajia pamoja na mambo mengine kusifiwa kwa maneno anayostahili kupewa Mungu. Nitaumia na kukwazika zisipokuja sifa kwa njia moja au nyingine. Nakuwa natamani sana moyoni mwangu kuitwa majina mazuri. Kuitwa baba. Kuitwa dady. Kuitwa mentor. Kuitwa majina ambayo yataonyesha utegemezi wa kudumu wa anaeniita. Kumbuka Eva hakula tunda kama Esau,liweke hili moyoni. Nataka niweke mipaka ili nisisifiwe lakini napenda sifa nan i ukweli kuwa nina maono. Natokaje. Najiona bado nipo paple. Hili la kusifiwa kwakuwa ndani yake lina hila na ubinafsi basi linanisukuma mpaka kuanza kuchokonoa hadi mambo nisiyotakiwa. Yaani navuka mipaka ya vigezo vilivyopo. Nilitakiwa niishie hapa mimi nataka niende mpaka kule na wakati naenda kule kuna watu nawakanyaga vichwa vyao ili tu niendelee kuoneka ni mtu mweye hekima na ufahamu wa juu sana kuliko wengi wa rika langu. Hata hili nimejifunza kwa maumivu. Sifa zinaua. Sifa zinalewesha. Sifa zinapofusha. Ni vigumu sana kumsikia Mungu katika mazingira haya. Kwakuwa Herode aliposifiwa na kulewa aliliwa na change, ole wangu mimi na wewe. Hatuliwi na change aonekanae bali angalia huduma zetu zinavyolaumiwa. Angalia muda wetu tunaotumia kuomba. Angalia tunavyoendenenda kibabe. Angalia familia zetu. Angalia uchumi wetu. Angalia mwenendo wetu. Ni heri Herode aliyepunguziwa kuendelea kukosea kwa kuuwawa, Mungu nisaidie nisiendelee kukosea kwa kuwa bado naishi na kwahiyo uwezekano wa kukosea ni mkubwa. Kwa kupenda sifa iliyojificha ndani ya maneno ya upole kuna watu lazima wakanyagwe vichwa vyao. Nimewakanyaga wengi. Mungu niasaidie na umsaidie anaepitia mambo haya sasa.

Page 16: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 10

3. KUNA AJENDA ZENYE NGUVU. Hakuna anaebisha kuwa kati ya ajenda ngumu zinazowakabili vijana ni MAHUSIANO YA KIMAPENZI. Ni kweli vijana wanataka umaarufu na pesa na mali na ndani yao kuna kiburi lakini mambo ya nitaoa au kuolewa na nani ni mwiba kwa wengi. Napo natakiwa nishauri na kuombea na tena natakiwa nishauri na kuombea bila kujali kama mimi mwenyewe nilikosea au la na kama nilishauriwa au la. Natakiwa nishauri kana kwamba mimi ni KAMUSI YA MAHUSIANO na kwakweli kwakuwa ajenda yenyewe ina nguvu ya ushawishi wa kuzungumza basi tena. Kushauri juu ya mahusiano sio jambo bay ahata kidogo ila nataka nikuonyesha UPELE UNAOELEKEA KWENYE JIPU ili uone kama utajikuna kama mimi au utasubiriwa ukunwe au mpaka jipu lenyewe lipasuke. Hapa nimekosea sana. Naweza hata kulaumiwa lakini Musa hakulaumiwa kwa kuua kama alijifunza maana lawama ijapo na nisijifunze toka kwenye laumu hiyo basi hakika nitattmbuliwa jipu. Hapa najifunza sana. Huduma yangu na yako HAITAKIWI KULAUMIWA KWA MAMBO TUNAYOSABABISHA WENYEWE KWA UJINGA NA ULIMBUKENI NA TAMAA ZETU nje na yale tuliyoandikiwa yatokanayo na kusudi letu. Unaposhauri kijana wa jinsi tofauti na wewe unajikuta unataka sana kujua ALIKOSEAJE na ilikuwaje mpaka akakosea na katika kukosea ALIFANYAJEFANYAJE katika kulifanya kosa liwe na nguvu na maana. Alifanya uasherati, okay, alifanyajefanyaje. Ipo ladha ya kusikia story ya uasherati na ngono bila kujua inaweza ikawa inakuchafua na kukunajisi na zaidi kukuharibia stamina yako ya ndani. Ni vizuri na muhimu kujua historia ya jambo. Mipaka. Mipaka. Mipaka. Utasikia mpaka wapi. Utasikia nini. Utauliza mpaka wapi. Utauliza nini. Na kwa nini uyajue hayo yote. Yesu akiniuliza ntasemaje. Jambo hili usipoangalia litakuzidishia tamaa za ngono. Zitakuhamisha toka kwenye kuwa na hisia na mkeo au mumeo na kukupeleka kwa kondoo unawahudumia na utakapofumbua macho utajikuta umeangukia aibu ya ajabu sana. Kuna ziadi ya hili. Mipaka. Labda unashauri mpaka wapi na kwanini. Nilikosea. Nikawa kila nikishauri najikuta nimeamua na kumsaidia kuamua ninaemshauri kwakuwa nataka nimtawale na kummiliki kimaamuzi nay eye asiwe na maamuzi yake binafsi bila mimi kujua au kukubali baada ya kujua na nikijua ameamua bila kunambia nakwazika sana maana mimi ni remote yake. Ni rahisi sana kusahau kuwa huyo sio mtoto. Huyo sio mdoli wala robot. Unaendelea kushauri na kuamua na kisha unaamini umefanya jambo la hekima na wala hutajua kama ni hekima mpaka umeona uharibifu mlangoni. Mungu nisaidie. Nikakumbushwa na rafiki yangu Chavala hapa majuzi kuwa wewe shauri tu na umwache anaeshauriwa afanye maamuzi mwenyewe maana hayo maamuzi ni yak wake nan i maisha yake. Kumbe ukishiriki kwenye maamuzi ya maisha

Page 17: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 11

ya mtu kwa kujificha kwenye ushauri ni rahisi sana kukosea na ukaishia kulaumiwa na hata kusingiziwa kwa mambo usiyofanya. Lakini pia utajikuta unaongea hata mambo ya watu wengine, hata kama ni ya kweli lakini hayakuwa muhimu uyaseme au uyatolee mfano bila kujua kuwa watu huambiana. Utaingilia maisha ya watu walikubaliana kupatia au kukosea na utajikuta unawakosesha waliopatia wakosee na walikosea wazidi kukosea. Ni mbaya. Mungu nisaidie. na YKM FOUNDER RAPHAEL JL.

KUKUWA, KUSTAWI, KUCHANUA KIROHO

Na: Seth Nyenzi

“Kwa ufupi, Seth Nyenzi ni mtumishi wa Mungu ambae nimebahatika kuwa karibu nae na nikaweza kuona vitu vingi vya thamani ambavyo Mungu ameweka ndani yake. Mtumishi wa Mungu huyu ni mwinjilisti anayevuna roho za watu wengi kwa Yesu, nakumbuka tulikuwa kwenye huduma inayoitwa OUTREACH MISSION katika kijiji cha Makuyu mkoani Morogoro na Mungu alipata watu wengi waliookoka kupitia mtumishi wa Mungu Seth Nyenzi. Amehitimu masomo yake chuo kikuu Mzumbe mkoani Morogoro.

UTANGULIZI

KUKUA ni kuongezeka katika kimo, maarifa,umbile kwa maana ya biological factor nk Kustawi ni hali ya kuendelea kimafanikio katika nyanja zote muhimu za kimaisha na Kuchanua ni kuendelea kupendeza katika Bwana,

Katika kitabu cha Yeremia 17:5-9 Biblia inasema amebarikiwa mtu yule amtegemeaye Bwana, maana atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya maji, hautaona ukame wakati wa hali ujapo…………..”

KANUNI KUU TANO ZINAZOZINGIRA UKUAJI NA USTAWI KIROHO.

1.Ni lazima uzaliwe mara ya pili( Born again). Yule Nkodem alimwendea Yesu akamwuliza eti nifanye nini ili niweze kuurithi ufalme wa Mungu?Yesu akamwambia mtu hana budi kuzaliwa mara ya pili, (Yohana 3:1-5). Kuzaliwa mara ya pili kunamfanya huyu mtu kuondokana na maisha ya kale, maisha ya umauti uti, maisha ya dhambi, na kumbuka maisha ya dhambi ndiyo yanyomharibu mtu, uchunguzi au utafiti umeonyesha kuwa watu wasiookoka wanazeeka

Page 18: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 12

mapema zaidi kuliko watu ambao hawajaokoka, na pia wanakufa mapema zaidi kuliko wale ambao wameokoka.

FAIDA ZA KUZALIWA MARA YA PILI.

Unasamehewa dhambi zako zote. Baada tu ya kuzaliwa mara ya pili dhambi zako zoote zinafutwa, na kumbuka dhambi zoote ulizonazo ndiyo sababu ya uso wako kukunjamana (Mwanzo 4:1-7) Pia Isaya 1:6-18 anazungumzia kwa habari ya msamaha wa dhambi unaotolewa pindi mtu anapokuwa ameokoka na mpendwa ni vyema ukakumbuka kuwa msamaha wa dhambi unakuweka huru kabisa, unathibitika katika maisha yako mwenyewe na unakupa uhakika, msamaha wa dhambi unakuondolea hati ya mashitaka hivyo unakuwa huru kwelikweli.

Unaingizwa katika pendo la mwana wa Mungu pekee. Mtu unapokuwa umezaliwa mara ya pili unaingizwa katika pendo la mwana wa Mungu, Unapendwa na Mungu, unapendwa na Yesu mwenyewe unapendwa na Malaika unapendwa na wanadamu pia, pendo la Mungu linakufanya wewe uitwe mwana wa Mungu, pendo la Mungu linakufanya upate kibali katika kila mahali unapoenda, Pendo la Mungu linakufanya uogelee katika uwepo wake siku zote, pendo la Mungu linakufanya upatanishwe na ndg zako, Pendo la Mungu linakufanya uwe na kibali na upate hofu ya kimungu daima.

Unaingizwa katika familiya ya Kimungu.(divine principle). Mtume Paul katika waraka wa waefeso 2;18-21 anasema tangu sasa ninyi si wageni tena bali ni wenyeji pamoja na watakatifu, mmejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii, na Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.Pia katika kitabu cha mambo ya walawi 20:7 anasema mtakuwa watakatifu kama mimi nilivyo mtakatifu.Hivyo baada ya kuokoka mtu anakuwa sehemu ya watakatifu nyumbani mwake Mungu nk nk

2. Ni lazima ujazwe Roho mtakatifu. Roho mtakatifu ni Mungu katika utatu mtakatifu, kazi ya Roho mtakatifu ni kuhuisha, kufufua, kurejesha nk.Roho mtakatifu ni kama mafuta, mtu anapokuwa amejazwa Roho mtakatifu hupelekea mambo yafuatayo;

Kumwabudu Mungu katika Roho na kweli, na Mungu akiabudiwa katika Roho na kweli hupelekea Mungu kufanya mambo makubwa ambayo yatakushangaza

Page 19: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 13

Somo hili bado linaendelea..!

NINI MAANA YA UPENDO

Na: Hosea G. Paul.

“Kwa ufupi, Hosea G. Paul ni Mission Leader katika huduma inayoitwa Come To Jesus Mission[COTOJEMI]. Somo hili limegusa maisha ya vijana hasa kujibu baadhi ya maswali magumu katika eneo la mahusiano, Hivyo karibu na wewe pia uweze kufaidi siri zilizo ndani ya somo hili!”

Napenda tukajifunze maana halisi ya neno upendo. Sisi vijana tunatumia sana neno upendo. Love….

I LOVE YOU!

Biblia katika kitabu cha Marko12:29-31 inasema upendo ni “amri ya kwanza”. Katika kitabu cha Mathayo 22:36-40 biblia inasema upendo ni “amri kuu”. Tunaona upendo ni kitu cha msingi sana katika maisha yetu ya ukristo.

UPENDO?

Biblia inasema “upendo ni Mungu” 1Yoh.4:8b; 16. Biblia inaendelea kusema katika upendo Mungu anakaa ndani yetu nasi ndani yake. Mungu anakaa ndani yetu katika Roho mtakatifu (1Yoh.3:24).

Point: Kuwa na upendo ndani yako ni kuwa na Mungu ndani yako.

Mungu ni mtakatifu; hivyo aliye na Mungu ndani yake naye ni mtakatifu. Upendo hutuongoza katika mema yote.

Neno la Mungu linasema; 1Yoh.3:18 tusipende kwa ulimi wala kwa neno, bali kwa tendo na kweli. Tusipende kwa midomo; kwamba unamtangazia mtu kuwa unampenda; unatongoza! bali mwenye upendo wa dhati anaonesha katika matendo.

Vijana wengi wamepotea kwa kudhania kitofauti matendo yanayoashiria upendo. Wengine wamedhania uzinzi; lakini hapo wameangukia katika kifo au dhambi. Biblia inasema tena,

Page 20: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 14

2Petro2:13-14 kuna watu ambao wasiokoma kutenda dhambi, wenye macho yajaayo uzinzi, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani… wana wa laana!

Kumbe wapo ambao wanadhani wanapenda kumbe wanatamani tu; wana wa laana! hao ni hatari kwa karamu yenu ya upendo. Wanatamani zinaa na anasa zote; hawakufai kwa kuwa hao watakutenganisha na Mungu wako, yaani watauondoa upendo ndani yako. Haleluya!

Upendo ni kutenda matendo mema. Biblia inasema tupatapo nafasi tuwatendee mema watu wote, Galatia 6:9-10. Tena Neno la Mungu linasema, utawezaje kumpenda Mungu usiyemwona wakati unamchukia ndugu yako unayeishi naye?

Biblia inasema Marko12:31 mpende Bwana Mungu wako;

1. kwa moyo wako wote, 2. kwa akili zako zote 3. kwa nguvu zako zote.

Sehemu ingine Yesu anasema nilipokuwa mgonjwa hamkuja kuniona; nilipokuwa na kiu hamkuninyesha maji; nilipokuwa na njaa hamkunilisha… Mlivyokuwa mnawatendea wale ndugu ndivyo mlinitendea.

Point: ili kumpenda Mungu; kwa moyo wote, kwa akili zote na kwa nguvu zote hatuna budi kufanya hivyo kwa ndugu zetu tunaoishi nao.

Luk10:30-37 tunakuta mfano alioutoa Bwana Yesu; mtu mmoja aliyekuwa akisafiri kutoka Yeriko kwenda Yerusalem aliangukia mikononi mwa wanyang’anyi, vibaka, majambazi… Wakamnyanganya kila kitu hata nguo; walimpiga sana wakamtupa akiwa mahututi karibu kufa.

Alipita kuhani, akamwangalia akampuuza; akafuata mlawi akamwona akampuuza lakini alipita msamaria akamwona akamhurumia. Akamsaidia kwa moyo wake wote, kwa akili zake zote na kwa nguvu sake zote. Msamaria huyo alikuwa na upendo ndani yake; alikuwa na Mungu ndani yake, alikuwa na roho mtakatifu.

Tujitahidi wapendwa kuwa na upendo ndani yetu, kuwa na Mungu ili tuishi katika misingi imara ya wokovu. Mungu awabariki sana.

Page 21: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 15

SABABU SABA (7) ZITAKAZO KUFANYA KUWA MSHINDI DUNIANI

Na: Mwl. Conrad Conwell

“Kwa ufupi, Mwalimu Conrad Conwell,Ameokoka 2003,Ni Mwalimu wa Neno la MUNGU,Kwa Sasa yupo Mkoani Morogoro,Mwalimu Conrad Pia ni Mwinjilisti anafanya Huduma katika Mikoa isiyofikiwa na Injili,Pia Ni Katibu wa TAYOMI,Mkoa wa Morogoro,ana SHAHADA. YA UALIMU. Anaabudu THE BODY OF CHRIST MINISTRY Mkoani Morogoro”

UTANGULIZI

Glory to GOD watu wa MUNGU, nataka nizungumze na wewe Sababu saba zitakazokufanya kuwa Mshindi Duniani…Zifuatazo ni Sababu hizo..

1. NENO LA MUNGU LIWE KWA WINGI NDANI YAKO..

Neno la MUNGU likiwa kwa wingi ndani yako ni Dhahili utakuwa Mshindi lakini ndano yako kukiwa na Maneno mengine kinyume na Neno la MUNGU unaweza ukatikiswa na adui na kujikuta umeanguka.ndio Maana Mfalme Daudi akasema “Moyoni Mwangu nimeliweka Nno lako nisikutende dhambi” Zaburi 119:11, Je! moyoni mwako wewe umeweka neon la namna gani?

2. MAOMBI/KUOMBA

Daniel, Eliya, Mussa, Bwana YESU ,nk Hawa wote walihakikisha wanaishi katika Maombi,Wakati Mwingine kwa kufunga,Bwana Yesu kuna sehemu aliwaambia wanafunzi wake hamkuweza kukesha name hata saa moja. Mathayo 26:40 Akawaendea wale wanafunzi, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, “Ndiyo kusema hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? 41 Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho i tayari lakini mwili ni dhaifu.”

3. MAONO.

Hakikisha katika maisha yako Duniani unakuwa na maono,(Yaani mtazamo wa Mbeleni) hata kama wenzako hawajafika wewe unasema nitafika,usiishi bila maono,ukiwa na maono mipango yako inakuwa inaenda vizuri pasipo na shida. Bila ya kuwa na maono ya wapi unaelekea ni rahisi kuchukuliwa na upepo na kupelekwa usikokutazamia. Maono yatakufanya ujue ni nini

Page 22: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 16

ufanye kwa ajili ya Mungu na maisha yako kwa ujumla. Mithali 29: 18 Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.

4. .KUTOKUWA NA TAMAA YA VITU VISIVYOFAA

Kuna watu wanatamani vitu visivyofaa ambavyo ni kinyume na agizo la MUNGU,Ndiyo maana MUNGU hakasema usitamani mke wa jirani yako,wengine wanatamani mali za wengine bila kujua chanzo chake na wengi wamepotea kwa namna hiyo. Zaburi 119:37 Unigeuze macho yangu nisitazame yasiyofaa, unihuishe katika njia yako.

5. AMBATANA NA MARAFIKI WEMA.

(Mithali 27:17) Chuma hunoa chuma. ni dhahili chuma hakiwezi kunoa embe angalia marafiki zako wanakunoa au? angalia mtazamo wao,kuwaza kwao,nk..Wao waliokutana na Marafiki wabaya, ambao wamesababisha mpaka maono yao kufa na kurudi nyuma kwa kumuacha YESU KRISTO..Wapo waliokutana na marafiki wabaya waliokuwa na lugha chafu na kusabadilisha..Je una marafiki wa aina gani?

6. .KUTOMWEKEA MUNGU MIPAKA

Hii ni hali ya mwanadamu kuamini kuwa Mungu anaweza hili na hili hawezi…kitendo hiki Mungu anakiita kuwa ni ‘DHARAU’ kwake. Zaburi 78:41 inasema, “Wakarudi nyuma wakamjaribu MUNGU; Wakamwekea MPAKA Mtakatifu wa Israel” Mstari huu wa Zaburi unaelezea maisha ya wana wa Israel njiani toka Misri kwenda nchi ya Maziwa na Asali-Kanaani.Biblia inaeleza jinsi Musa alivyowatuma wapelelezi 12 kwenda kuipeleleza nchi ya ahadi waone kama kama kweli ni nchi ya ‘Maziwa na Asali’ 10 kati yao Waliporudi walirudisha ripoti ya kuwa kweli ile nchi ni ya maziwa na asali, ila inakaliwa na Wanefili-wana wa Anaki…majitu na ya kwamba wao ni kama panzi tu na hawawezi kwenda na kuimiliki. Joshua na Kalebu walileta habari njema…waliona kwa macho lakini wakazungumza kile ambacho ni ‘UHAKIKA WA MAMBO YATARAJIWAYO’ wakamwamini Mungu kuwa aweza kuwapa ile nchi kuwa milki yao sawa na alivyomwapia Ibrahim(Hesabu sura ya 13 na ya 14) na wote waliomwekea Mungu mpaka walikufa huko jangwani, hawakuingia nchi ya ahadi…WALIFUPISHA MAISHA YAO KWA KUTOKUAMINI KWAO…Ila Kalebu aliishi muda mrefu sana, alikuwa na nguvu kama za mtu wa miaka 40 hata alipokuwa na miaka 85( soma Joshua 14:6-14) na inaeleza pia ya kuwa Joshua alikuwa MZEE SANA, alikufa akiwa na miaka 110 lakini alikuwa na nguvu zake kamili mpaka pale BWANA alipompumzisha(Joshua24:1-

Page 23: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 17

29)Kama unataka kuwa na maisha marefu, na unataka kuziongeza siku zako…ishi maisha ya IMANI…Usimwekee Mungu mipaka, kumbuka, “Njia zake zi juu mno na fahamu zake pia” Isaya 55:8-11

7. KUACHA DHAMBI

Dhambi ni mbaya…inakutenga mbali na Mungu( Isaya 59:1-2) lakini kibaya zaidi inapunguza maisha yako…inakufanya ufe kabla ya muda wako…Unafurahia kuishi maisha ya dhambi? ni mzinzi, mwongo, msengenyaji, usiyesamehe,mwenye kinyongo, kisasi nk? Unajipeleka kaburini kabla ya wakati wako…unafanya kazi ambayo mshahara uitwao ‘MAUTI’ utaupata.Katika Warumi 6:23 Biblia inasema, “Kwa maana mshahara wa DHAMBI ni MAUTI (KIFO), bali karama ya Mungu ni uzima wa Milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” pia Biblia inasema, “Roho itendayo DHAMBI ndiyo itakayokufa” Maisha ya dhambi yanakata muda wa mtu wa kuishi…Ni wangapi waliokufa wakiwa vijana wadogo kwa sababu ya UKIMWI kwa kutoikwepa dhambi ya Uzinzi? au ni Wezi wangapi wamekufa wakiwa katika harakati za kuiba?Dhambi ni adui mkubwa kwangu na kwako!

VIZUIZI KUMI (10) VINAVYOZUIA MAOMBI YAKO USIPOKEE ULICHOOMBA KUTOKA KWA MUNGU

Na: PETER M MABULA.

“Kwa ufupi, Nilifahamiana na Mtumishi wa Mungu Peter M Mabula mwaka 2013 nilipoabudu kwa mara ya kwanza kanisa la Kawe Pentecostal Chuch [KPC]. Kwa Neema ya Mungu, Mtumishi wa Mungu Peter M Mabula ana hazina nyingi za thamani ndani yake, Masomo yake yamekuwa yakigusa maisha ya wengi. Katika somo hili yako mambo mengi utajifunza, tafadhali soma mpaka mwisho (Mwl. Daudi, JL)”

UTANGULIZI

Watu wengi hupenda sana kuombewa na hata kuomba pia. Hutamani wapokee kile walichoomba lakini muda mwingine hawapokei, Tatizo sio la MUNGU bali tatizo ni la wewe unayeomba. Nimekuandalia vizuizi 10 vya maombi ambavyo ukivitendea kazi maombi yako yatakuwa na matokeo mazuri sana,

Page 24: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 18

”Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.-1 Yohana 5:14-15.”

Kumbe lazima kwanza tuombe sawa sawa na mapenzi au matakwa yake MUNGU. Hayo matakwa yake ni yapi?. Hebu ndugu ona vizuizi hivi kumi vya maombi yako ndipo utajua matakwa au mapenzi ya MUNGU hata akajibu maombi yako.

VIZUIZI KUMI(10) VYA MAOMBI.

1. UCHUNGU NA KUTOKUSAMEHE:

Mathayo 5:22-24 ”Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto. Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako”.

Uchungu maana yake ni kukaa na jambo moyoni. Moyo ni kwa ajili ya ROHO MTAKATIFU na sio vinginevyo. Sadaka sio bora kuliko msamaha, samehe kwanza ndipo na utoaji wako utakuletea baraka kuu. Usikubali kuwa na hasira kwa ajili ya watu. Mathayo 6:14-15 ”Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na BABA yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala BABA yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. ”. MUNGU hatakupa hicho ulichomuomba hadi usamehe kwanza.MUNGU ana kanuni zake lazima tuzifuate ndipo tutapokea baraka zetu baada ya maombi. Umelala na uchungu na umeamka na uchungu hiyo haina faida kwako hata moja hivyo achilia kwanza na MUNGU atakujibu hitaji lako. Kuna watu mioyoni mwao hakuna ROHO MTAKATIFU ila kuna watu tu waliowaweka moyoni ambao waliwaudhi. Ndugu ondoa watu moyoni mwako na muweke ROHO wa MUNGU.

2. DHAMBI ZA MAKUSUDI ZISIZOUNGAMWA:

Zaburi 66:18 ”Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, BWANA asingesikia”. Kama unakusudia mabaya maana yake ni dhambi na hakika MUNGU hatakusikia maombi yako. Tubu kwanza dhambi yako. Kama hujaungama MUNGU hatasikia maombi yako na hutapokea ulichoomba kwake. Ukichagua kumkimbia MUNGU kwa kufanya dhambi utakuwa umejitenga

Page 25: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 19

na MUNGU na kwa kujitenga na MUNGU hakika hutajibiwa hitaji lako. Tukiwaza maovu mioyoni mwetu MUNGU hatasikia maombi yetu.

3. MIZOZO ISIYOTATULIWA NA MAOMBO YA NYUMBANI:

1 Petro 3:7 ” Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe”. Mizozo ya kwenye familia yako inaweza kuzuia maombi yako. Hata kama ni muombaji kiasi gani lakini kama kila siku mnapigana au kutukanana na mwenzi wako wa ndoa hiyo inaweza kuzuia maombi yako. Tafuta wapi ulipoangukia ukatubu. Unaweza ukasema mbona mwaka unaisha MUNGU hata hajajibu ombi langu la mtoto kumbe tatizo ni mizozo isiyoisha kwenye familia yako.

4. DHAMIRI MBAYA:

Wagalatia 6:3-4 ” Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake”. Unaweza ukajiona ni kitu kumbe si kitu kwa sababu ya dhamiri yako mbaya. kila saa unawaza mabaya. Ndugu waza mema maana kuwaza mabaya kunaweza kukunajisi wewe. Usijifananishe na watu wengine. BWANA YESU alisema neno hili kati ya mtu mwenye dhamiri mbaya na asiye na dhamiri mbaya. Luka 18:10-14 ” Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee MUNGU, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee MUNGU, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa”. Dhamiri yako kama ni mbaya hakika hutajibiwa maombi yako.

5. KUTOKUMPA MUNGU NAFASI YA KWANZA:

Malaki 1:6-10 ”Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni BABA yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni BWANA wenu, kicho changu ki wapi? BWANA wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani? Mnatoa chakula kilichotiwa unajisi juu ya

Page 26: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 20

madhabahu yangu Nanyi mwasema, Sisi tumekutia unajisi kwa jinsi gani? Kwa sababu mwasema, Meza ya BWANA ni kitu cha kudharauliwa. Tena mtoapo sadaka aliye kipofu, si vibaya? Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya? Haya! Mtolee liwali wako; je! Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema BWANA wa majeshi. Na sasa, nawasihi, ombeni fadhili za MUNGU, ili atupe neema; ikiwa jambo hili limetoka katika mikono yenu; je! Atawakubali nafsi zenu? Asema BWANA wa majeshi. Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yo yote mikononi mwenu”

Watu wengi leo MUNGU ni ziada tu kwao. Watu wengi maombi kwao pia ni ziada tu, hutaka tu kuombewa. Ndugu zangu, MUNGU anataka atuongoze yeye na sio sisi tumuongoze MUNGU jambo ambalo halitawezekana. Ndugu, najua umekuwa makini sana kwenye mambo yako ya kidunia, ndugu maombi yako yanaweza kutokujibiwa kwa sababu MUNGU umemfanya kuwa ziada tu kwako. Watu wengi ukiwauliza kwanza ” kitu cha kwanza na cha muhimu maishani mwako watasema ni MUNGU lakini matendo yao hata hayaonyeshi kwamba MUNGU ni wa kwanza katika maisha yao.”. Kuna watu wengi tumewaombea lakini walipopokea tu uponyaji wao hata BWANA wakamsahau na hiyo inaonyesha kabisa kwamba wao hawakumhitaji MUNGU ila walihitaji tu uponyaji na baraka zake. MUNGU lazima awe nafasi ya kwanza maishani mwetu.

Luka 14:26 ” Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”. Ndugu zangu BWANA hana maana kwamba tuwachukie wazazi au wake/waume zetu au watu wengine wowote bali MUNGU wetu anataka apewe kwanza yeye nafasi ya kwanza maana ndio nafasi yake milele yote. Maana kama baba yako atakukataza kuokoka na wewe ukakubali maana yake umemtii baba yako kuliko MUNGU lakini ukimtii MUNGU kwa kuokoka utamchukiza baba yako lakini kwa MUNGU wewe utaitwa heri maana umemtii mwenye uzima wako wa milele. Tukishindwa kumpa MUNGU nafasi ya kwanza ni madhara kwetu maana tutakuwa mbali naye tu.

Ufunuo 3:16 ”Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.” MUNGU hawahitaji watu ambao wako uvuguvugu yaani nusu wako kwake MUNGU na nusu wako kwa shetani. Ndugu zangu kama kuna jambo la kwanza katika maisha yetu basi MUNGU aliyetuumba awe wa kwanza. MUNGU akikuacha utaenda kwa

Page 27: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 21

nani?. Leo watu wengi ni vuguvugu kitu ambacho ni hatari sana. Ndugu, BWANA MUNGU anahitaji zaidi muda wako na hapo ndipo utakuwa na sifa za kuomba na kujibiwa.

6. KUTOKUOMBA IPASAVYO:

Yakobo 4:2 “Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi! '' -Kuna watu hata hawana muda wa kuomba lakini hutaka na kutamani sana MUNGU awape mahitaji yao. Kutokuomba ipasavyo ni moja ya kizuizi cha kupokea baraka kutoka kwa MUNGU.

7. KUTOKUWA WASIKIVU:

Isaya 28:23 ''Tegeni masikio, sikieni sauti yangu, sikilizeni mkasikie neno langu”. Watu wengi humuomba MUNGU kuhusu baraka fulani na BWANA nae kabla ya kuwapa husema nao ili watengeneze vitu fulani katika maisha yao hata kuruhusu baraka iwajie lakini watu walio wengi huwa si wasikivu na kupelekea kutokua watii na hayo yakitokea hupelekea kutokujibiwa maombi yao. -Hebu mfano wewe jigeuze yule mama wa Salepta wakati wa Nabii Eliya ambaye alitaka BWANA ambariki chakula, lakini jibu la MUNGU likawa yule mama ampe Eliya Chakula, alipotii alibarikiwa hata isiwepo sehemu ya kubaki. Leo ni wangapi ambao wangemuomba MUNGU harafu MUNGU akasema nao neno gumu kama hilo la mama wa Salepta lakini bado wao wakatii? Huo ni mfano tu lakini MUNGU husema na sisi waombaji kwa namna nyingi, ni vizuri kuwa wasikivu na watii. Kumb 28:1-7 '' Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, MUNGU wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, MUNGU wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, MUNGU wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba'' .Baraka hizi zitakuja kwa sababu ya kuitii sauti ya MUNGU. -Kuitii sauti ya MUNGU ni muhimu sana. -Kama huitii sauti ya MUNGU hata ungeombaje huwezi kupokea.

8. UBAYA NA UDHALIMU:

Page 28: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 22

Mika 3:4 '' Ndipo watakapomwomba BWANA, asiwaitikie; naam, atawaficha uso wake wakati huo, kwa kadiri walivyotenda mabaya kwa matendo yao''. Mitindo ya maisha inaweza kusababisha mtu asijibiwe maombi yake. Matendo na usemi mbaya unaweza kuwa kikwazo cha kupokea kutoka kwa MUNGU hata kama unaomba sana maana maovu hayo yatauficha uso wa MUNGU. Zaburi 34:15-16 ''Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao. Uso wa BWANA ni juu ya watenda mabaya, Aliondoe kumbukumbu lao duniani''

9. KUOMBA VIBAYA:

Yakobo 4:3 '' Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu''. Kuomba vibaya ina maana nyingi sana. Kuna watu huomba kwa lengo la kushindana na watu wengine. Wengine hawaombi bali wanalalamika tu mbele za MUNGU, Mfano wanandoa wengi huwalaumu wenzi wao kwa kuwaona kwamba wao ndio chanzo cha kila aina ya tatizo kwenye ndoa kumbe tatizo wakati mwingine linaweza likawa la mlalamikaji. Wengi hufikia hata kuomba sasa kumbe hapo ni kulalamika tu kwa MUNGU maana tatizo ni la muombaji. Unaweza ukasema '' BABA wa mbinguni finyanga moyo wa mke/mme wangu '' kumbe alitakiwa aombe kwanza yeye atengenezwe moyo wake maana yeye ndio tatizo. Wengine huomba kwa kutaka kubalikiwa kama mtu fulani ambaye wanamfahamu. Ndugu fulani ni fulani na wewe ni wewe, omba uwe kama wewe sio kama alivyomtu fulani. Kuomba vibaya ina maana nyingi sana.

10. KUTOKUOMBA KWA IMANI:

Waebrania 11:6 ''Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao'' .Usimwendee MUNGU kwa kujaribu. Hata kama unaumwa kiasi gani na ugonjwa gani kama umeamua kumwomba MUNGU basi omba kwa imani. Wengi huenda kwa YESU kwa kujaribu tu ndio maana hata hawapokei walichokiomba. Naamini umejifunza kitu kizuri. Warumi 8:26-27 ''Kadhalika ROHO naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini ROHO mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyoMungu”.

Page 29: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 23

MWISHO.

Page 30: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 24

Kwa shuhuda na maoni yako, unaweza kuwasiliana kwa namba +255(0) 764 771 298 au kwa baruapepe [email protected]. Pia tembelea blog ya VIJANA NA UTUMISHI kupitia vijananautumishi.wordpress.com.

Kama unataka kufanya kazi pamoja na VIJANA NA UTUMISHI, una masomo yako yawekwe mtandaoni au kuchapishwa kwenye e-kitabu karibu pia, tumia mawasiliano hapo juu.

Page 31: JIFUNZE UKUE KIROHO - WordPress.com · 2016-09-24 · Kumbe ni mpango Mungu mimi na wewe kukua na kuongezeka na kupanuka na kuzidi sana katika maarifa ya Mungu ambayo Tujifunza chini

JIFUNZE UKUE KIROHO

VIJANA NA UTUMISHI #Sema_Nafanya_Navuna2016.

Uk. | 25

JIPATIE an article titled “MAMBO MUHIMU UNAPOANDAA SOMO/UJUMBE WA KUFUNDISHA” ujifunze kuandaa somo lako vizuri Mungu alilokupa!.

Kupata this article tembelea blogu ya VIJANA NA UTUMISHI na uweze kukipakua. Mungu akubariki sana.