maagano mawili aliyetafsiri ni, daniel wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ......

66
1

Upload: others

Post on 10-Mar-2021

11 views

Category:

Documents


5 download

TRANSCRIPT

Page 1: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

1

Page 2: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

2

MAAGANO MAWILI

Aliyetafsiri ni,

Daniel Wikama.

@2019

Page 3: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

3

YALIYOMO

UTANGULIZI .....................................................................................4

AHADI KWA IBRAHIMU (E.J.WAGGONER).................................8

MAAGANO MAWILI........................................................................15

MAISHA YA IBRAHIMU.................................................................16

HAJIRI NA SARA..............................................................................20

JE UPO AGANO GANI?....................................................................25

LITUPE MBALI AGANO LA KALE ................................................30

MWANZO WA “IKIWA” NA “NDIPO”...........................................34

AGANO LA KALE LIMETETA JIPYA............................................38

TOFAUTI YA MAAGANO ...............................................................43

NAFSI AU KRISTO...........................................................................48

KUKAMILIKA KWA AGANO LA MILELE....................................56

Page 4: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

4

UTANGULIZI.

Somo la maagano mawili ni somo ambalo wengi hawana uelewa mzuri.

Lakini japokuwa wengi hawana uelewa mzuri kuhusu maagano mawili,

wapo wengi ambao hawafahamu kama hawana uelewa mzuri kuhusu

maagano mawili. Lakini kwa rehema za Mungu, mwaka 1888 Mungu

aliwatumia vijana wawili E.J.Waggoner na A.T.Jones kufunua ukweli

uliopo katika maagano mawili. Ellen White baadae alifunuliwa kuwa

ukweli ambao umefunuliwa na watu hawa wawili ulikuwa ni kweli na

ni muhimu kwa watu wote waufahamu kabla ya ujio wa Yesu Kristo

mara ya pili. Akasema,

Bwana katika rehema yake, ametuma ujumbe wake wa kipekee kupitia

Wazee Waggoner na Jones. Ujumbe huu unatakiwa utolewe

ulimwenguni kote kuhusu mwokozi aliyeinuliwa, aliyekafara kwaajili

ya dhambi za ulimwengu. Umewasilisha kuhesabiwa haki kwa imani

kwa hakika, na unawaalika watu wapokee haki ya Yesu Kristo, ambayo

inadhihirishwa katika kutii amri zote za Mungu. (Ellen White,

Testimonies to Ministers 91,92 1895).

Lakini cha kusikitisha ni kwamba ujumbe huu ulikataliwa na viongozi

wa kanisa la waadventista wasabato. Ni muhimu kila mmoja ajue nini

maana ya agano, na nini kilicho ndani ya agano ili iwe rahisi sana kwa

msomaji aweze kuelewa yale ambayo yanaelezwa na mwandishi. Nini

maana ya agano? E.J.Waggoner alisema,

“Agano na ahadi ni kitu kimoja na vyote ni sawa na inaonekana wazi

katika wagalatia 3:17, ambapo inaonekana kuwa kubatilisha agano ni

kubatilisha ahadi. Katika mwanzo 17 tunasoma kwamba Mungu

alifanya agano na Ibrahimu kumpa nchi ya kaanani—na kwahilo ni

dunia nzima—kwa ajili ya urithi wa milele, lakini wagalatia 3:18

inasema kuwa Mungu alimpa kwa njia ya ahadi. Agano la Mungu kwa

wanadamu haiwezi kuwa kitu kingine ila ahadi zake kwao. “Au ni nani

aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena? Kwa kuwa vitu vyote

vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu

una yeye milele. Amina” (Warumi 11:35-36). Ni nadra sana kwa watu

ufanya jambo bila kutegemea malipo, ndio maana wanateolojia

wamechukulia ndivyo hivyo hivyo kwa Mungu. Ndio maana wameanza

maandiko yao kuhusu agano la Mungu wakiwa na kauli kuwa “ni

Page 5: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

5

makubaliano kati watu wawili au zaidi, kwaajili ya kufanya au

kutokufanya jambo fulani” Lakini Mungu hafanyi makubaliano na

wanadamu,kwasababu anajua kuwa hawawezi kutimiza sehemu yao.

Baada ya gharika, Mungu alifanya agano na kila kiumbe chenye uhai,

lakini wanyama wala ndege hawakurejesha ahadi yoyote (Mwanzo 9:9-

16). Walipokea upendeleo kutoka katika mkono wa Mungu. Hilo ndilo

tunalotakiwa kulifanya. Mungu ameahidi kila kitu tunachohitaji, zaidi

ya tunavyoweza kusema au kufikiri kama zawadi. Sisi tunampa nafsi

zetu, ambayo haina kitu, na yeye anatupa yeye mwenyewe ambaye ni

kila kitu. Kitu kinachosababisha tatizo, hata pale wanadamu

wanapomtambua Mungu, wanataka kufanya makubaliano naye.

Wanataka iwe ni mahusiano ya pande mbili—wabadilishane ili wajione

wapo katika makubaliano na Mungu. Lakini yoyote anayetaka

makubaliano na Mungu lazima ajihusishe naye kwa mujibu wa vigezo

vyake, kwamba katika uhalisia—hatuna kitu na sisi si kitu na yeye

anakila kitu na yeye ni kila kitu na anatoa kila kitu” (Glad tidings 70-

71)

Hivyo tunagundua kuwa Agano ni ahadi ile ambayo Mungu ameitoa.

Kama jinsi waggoner alivyosema, kuwa agano na ahadi ni jambo moja

na ni kitu kimoja, ni muhimu kuelewa kuwa Mungu anapoahidi jambo

ni sawa na kuwa ameweka agano. Kama jinsi alipoahidi kuwa

hatoangamiza dunia kwa gharika, ni sawa na kusema kuwa Mungu

aliweka agano kuwa hatoangamiza dunia kwa gharika.

Mwanzo 9

9 Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu

10 tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa,

na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina,

hata kila kilicho hai katika nchi. 11 Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila

chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika,

baada ya hayo, kuiharibu nchi

Ahadi kuwa “Kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika

wala hakutakuwa tena gharika” hili ndilo agano la Mungu. Na hakuna

kiumbe chochote kilichoahidi chochote kwa Mungu, ni Mungu ndiye

anayeweka agano kwa maana yeye ndiye anayeweza kutimiza agano

lake. Japokuwa Mungu alitamka agano lake kwa viumbe wote kuwa

hatoangamiza tena dunia kwa gharika, agano hili halikuwa agano la

Page 6: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

6

wokovu na la Kumhesabia haki mwanadamu lakini lilikuwa tu kuwa

hatoangamiza dunia kwa gharika sio zaidi ya hapo.

Lakini kuna agano ambalo Mungu aliahidi kumhesabia haki mdhambi.

Hili ni agano la milele ambalo haki inapatikana kwa kumuamini Kristo.

Na hili agano lilikuwa katika akili ya Mungu hata kabla dhambi

haijaingia. Ellen White anasema,

Mpango wa wokovu wetu haukuanza baadae, kwamba mpango

ulianzishwa baada ya anguko la Adamu. Ulikuwa ni ufunuo wa “ile siri

iliyositirika tangu zamani za milele” (Warumi 16:25). Ulikuwa ni

mafunuo ya kanuni ambazo tangu zamani za milele zilikuwa ni msingi

wa kiti cha enzi cha Mungu. Tangu mwanzo, Mungu na Kristo walijua

uasi wa Shetani, na kuhusu anguko la mwanadamu kupitia nguvu ya

muasi. Mungu hakutaka dhambi iwepo, lakini aliona ujio wake, na

akafanya maandalizi kwaajili ya kukabiliana na dharura hiyo ya

kutisha. Upendo wake ulikuwa mkubwa sana kwa ulimwengu, kiasi cha

kuweka agano kumtoa mwanae wa pekee “ili kila mtu amwaminiye

asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16) (Desire of Ages,

22)

Agano ambalo Mungu aliweka hata kabla dhambi haijaingia

ulimwenguni ni agano la kumtoa mwanae wa pekee. Hili ni agano

ambalo kwa Lugha nyingine tunaweza kuliita agano jipya. Kuna jambo

ambalo tunagundua hapa, ya kuwa agano jipya ndio agano la milele

lililowekwa hata kabla ya dhambi haingia ulimwenguni. Hili ni agano

la wokovu, kwamba haki inahesabiwa kupitia Yesu Kristo. Agano jipya

ndio agano la wokovu kwa mwanadamu, hili ndilo lilikuwa agano la

kwanza Mungu kulitoa hata kabla ulimwengu haujawa na dhambi.

Ellen White anasema,

“Japokuwa hili agano jipya lilifanywa na Adamu na kurudiwa kwa

Ibrahimu, halikuweza kuthibitishwa mpaka kifo cha Kristo. Lilikuwepo

kwa ahadi ya Mungu tangu mpango wa wokovu ulipotolewa kwa mara

ya kwanza, lilikubaliwa kwa imani, lakini lilipothibitishwa na Kristo,

liliitwa agano jipya. Sheria ya Mungu ilikuwa ndio msingi wa hili

agano, ambalo lilikuwa ni mpango wa kuwaleta wanadamu tena katika

amani na mapenzi ya Mungu, na kuwaweka sehemu ambayo wanaweza

kutii sheria ya Mungu. Jambo jingine linalotajwa katika Maandiko ni

Page 7: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

7

“Agano la Kale” lililofanywa kati ya Mungu na Israel pale sinai,

ambalo lilithibitishwa kwa damu ya kafara. Agano la Ibrahimu

lilithibitishwa kwa damu ya Kristo, na ndilo lilipoitwa agano la “pili”

au “Jipya”,kwasababu muhuri wa damu iliyomwagwa baada ya damu

ya agano la kwanza. Kwamba agano jipya lilikuwa ni thabiti katika siku

za Ibrahimu ni wazi kutokana na kuwa lilithibitishwa kwa ahadi na

kiapo cha Mungu—“vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika

hivyo Mungu hawezi kusema uongo” Waebrania 6:18 (Partriach and

Prophets 370-371)

Wapo wengi wanaodhani kuwa Agano la sinai ndio lilikuwa la kwanza

kufanywa. Na kwamba pale lilipovunjwa ndio la pili lililetwa kupitia

Yesu Kristo. Lakini ukweli ni kwamba kati ya haya maagano mawili,

agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza

kufanywa na Mungu na lilikuwa halisi kutokana na kiapo cha Mungu,

lakini japokuwa lilikuwa la kwanza kufanywa, agano hili lilikuwa

linasubiri damu ya Kristo ambaye ndiye mzao wa agano Hilo. Agano

hili lilikuwa linasubiri msalaba wa Yesu. Wakati agano la pale sinai

lilipofanywa, damu ya kafara ilitumika kuthibitisha agano hilo.

Kwahiyo agano la sinai ni la kwanza kwasababu ndilo lililokuwa la

kwanza kuthibitishwa kwa damu, wakati lile la Ibrahimu lilikuwa

linasubiri damu ya Yesu Kristo, na damu ya Yesu ilipomwagwa agano

hilo japokuwa ndio lilikuwa la kwanza kufanywa likawa agano la Pili.

Katika kitabu hiki A.T.Jones anaeleza kwa undani zaidi kuhusu

maagano mawili na kwa nini agano la sinai lilifanywa wakati tayari

kulikuwa na agano tayari –agano la Ibrahimu? Ubarikiwe.

Daniel Wikama.

Page 8: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

8

AHADI KWA IBRAHIMU.

Na,

E.J.WAGGONER.

Tunaposoma ahadi, sehemu mbili katika maandiko zinatakiwa

ziwekwe katika akili. Ya kwanza ipo katika maneno ya Yesu

Yohana 5

39 Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima

wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia 46 Kwa maana kama

mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari

zangu. 47 Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?

Maandiko pekee katika kipindi cha Kristo yalikuwa ni vitabu

vinavyojulikana kama ni agano la kale: haya ndio yanayomshuhudia.

Yalitolewa si kwa dhumuni jingine. Yalikuwa yanaweza

kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu

(2 Timotheo 3:15) na miongoni mwa hayo maandiko ni vitabu vya

Musa, kama jinsi vilivyotajwa na Bwana vilikuwa vinamdhihirisha.

Yoyote anayesoma vitabu vya Musa na agano la kale lote bila

kutegemea kumpata Kristo na njia ya uzima kupitia yeye atajikuta

anashindwa kuvielewa. Na kusoma kwake kutakuwa ni bure.

Andiko lingine ni,

2Wakorintho 1

19 Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu, aliyehubiriwa katikati yenu na sisi,

yaani, mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni

Ndiyo. 1.20 Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa

hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.

Hakuna ahadi ya Mungu iliyotolewa kwa mwanadamu isipokuwa

kupitia Kristo. Kuwa na imani katika Kristo ni kitu kimoja muhimu ili

kupata chochote kile ambacho Mungu ameahidi, Mungu hawaheshimu

wanadamu: Anatoa utajiri wake kwa kila mtu: lakini hakuna mtu

yoyote anaweza kuwa na sehemu katika hayo bila kumpokea Kristo.

Page 9: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

9

Hii ni sawa kabisa, kwa maana kristo ametolewa kwa wote kama

wanataka wanaweza kuwa naye.

Kwa kuwa na hizi kanuni kichwani, tunasoma sehemu ya kwanza ya

ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu,

Mwanzo 12

1 Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na

nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; 2 nami nitakufanya

wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; 3

nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa

zote za dunia watabarikiwa.

Kwa kuanza kabisa tunaweza kuona kuwa ahadi hii kwa Ibrahimu

ilikuwa ni ahadi katika Kristo.

Wagalatia 3

8 Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki

Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika

wewe Mataifa yote watabarikiwa. 9 Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja

na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani

Katika hili tunajifunza kuwa katika Ibrahimu familia zote za dunia

zitabarikiwa, alikuwa anamuhubiria Injili. Baraka ambazo zilikuwa zije

kwa watu wa dunia kupitia yeye zitafurahiwa tu kupitia Imani.

Kuhubiri injili ni msalaba wa Kristo.Ndio maana mtume Paulo anasema

kuwa alitumwa ili ahubiri injili sio kwa hekima ya maneno, ili kwamba

msalaba wa kristo usiwe na manufaa yoyote. Na akaongeza kuwa

kuhubiri msalaba ni nguvu kwa wote waliookolewa (Angalia 1Kor

1:17,18). Hii ni njia nyingine ya kusema kuwa ni injili, kwa maana injili

ni nguvu ya Mungu kwaajili ya wokovu.

Hivyo kwa vile kuhubiri injili ni kuhubiri msalaba wa Kristo ( na

hakuna wokovu kwa namna yoyote ile) na Mungu alihubiri injili kwa

Ibrahimu pale aliposema “katika wewe jamaa zote za dunia

watabarikiwa.” Ni wazi kuwa katika ahadi hiyo, msalaba wa kristo

ulifunuliwa wazi kwa Ibrahimu, na ahadi iliyotolewa ilikuwa inaweza

kupatikana kupitia msalaba wa Yesu pekee.

Hili limewekwa wazi sana katika sura ya tatu ya kitabu cha wagalatia.

Baada ya kauli kuwa ahadi ya baraka ni kwa watu wote wa dunia

Page 10: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

10

kupitia Ibrahimu na kwamba wote waliokatika imani wanabarikiwa

pamoja na Ibrahimu, maneno,

Wagalatia 3

13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili

yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; 14 ili

kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea

ahadi ya Roho kwa njia ya imani.

Haya yanaeleza kwa uwazi kabisa kuwa baraka za Ibrahimu, ambazo

zinakuja kwa familia zote za dunia, zitakuja tu kupitia msalaba wa

Kristo.

Hili ni jambo ambalo linatakiwa liwe katika akili zetu mwanzoni

kabisa. Kushindwa kuelewa kote kuhusu ahadi za Mungu kwa Ibrahimu

na mzao wake zimesababisha kushindwa kuona injili ya msalaba ndani

yake. Kama itaendelea kukumbukwa kuwa ahadi zote za Mungu ni

katika Kristo, ili zifurahiwe kupitia msalaba wake pekee, na kwamba

ni za kiroho na za milele katika asili yake, hakutakuwa na ugumu na

somo la ahadi kwa mababa litakuwa ni la furaha na baraka.

Tunasoma kuwa Ibrahimu kwa kuitii sauti ya Mungu, alijitenga na

nyumba ya baba yake, na kutoka katika nchi yake ya asili.

Mwanzo 12

5 Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao

vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka

ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani. 6 Abramu

akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa

More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo. 7 Bwana akamtokea

Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea

madhabahu Bwana aliyemtokea. 8 Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima

ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli

upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea Bwana madhabahu

huko, akaliitia jina la Bwana.

Ni muhimu tuweze kuelewa maana halisi ya ahadi za Mungu na

alivyokuwa anajihusisha na Ibrahimu tokea mwanzo na ndipo somo

letu litakuwa rahisi kwasababu litakuwa linatumia hizo kanuni. Katika

mstari wa mwisho kuna vitu vimeletwa ambavyo vinachukua uzito

mkubwa katika somo hili, na hivyo tutaviainisha hapa, Kwanza

Page 11: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

11

MZAO

Bwana alimwambia Ibrahimu, alipofika katika nchi ya kaanani

Wagalatia 3

16 Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao,

kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani,

Kristo

Hili linaweza milele kuweka sawa swala hili,ili kwamba kusiwe na

mkanganyiko wowote kuhusu hilo. Mzao wa Ibrahimu, ambaye ahadi

zilinenwa ni Kristo. Yeye ndiye mrithi.

Lakini sisi pia ni warithi sawa na Kristo.

Wagalatia 3

27 Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.28 Hapana

Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu

mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. 29 Na kama ninyi

ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Isisahaulike kuwa kuna maelfu wengi wanajumuishwa katika mzao,

kuna mzao mmoja, kwa maana wote ni wamoja katika Kristo, ambaye

ndiye mzao.

Wote waliobatizwa katika Kristo wapo ndani ya Kristo, na hivyo ni

wamoja katika yeye. Hivyo inaposemwa kuwa Kristo ni mzao wa

Ibrahimu, ambaye ahadi zilinenwa, wote waliondani ya Kristo

wanajumuishwa. Kusema kwamba urithi ulioahidiwa kwa mzao wa

Ibrahimu utaweza kupatikana kwa njia yoyote isipokuwa wale

waliokatika Kristo kupitia Imani ni kuipuuzia Injili, na kukataa neno la

Mungu. Kama mtu yoyote aliyendani ya Kristo ni kiumbe kipya. Hivyo

kwa vile ahadi kuhusu nchi ilikuwa ni kwa Ibrahimu na mzao wake,

ambaye ni Kristo na wote waliondani yake kupitia ubatizo na hivyo ni

viumbe wapya inamaana kuwa ahadi za nchi ilikuwa ni kwa wote

walioviumbe wapya katika kristo—Wana wa Mungu kupitia imani kwa

Kristo Yesu.

Hii ni ushahidi wa ziada ahadi zote za Mungu ni katika kristo, na ahadi

zote za Mungu zinaweza kupatikana kupitia msalaba wa Kristo. Kanuni

Page 12: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

12

hii isisahaulike katika kusoma kuhusu Ibrahimu na ahadi kwake na

mzao wake—Kwamba mzao ni Kristo na wote waliondani yake.

NCHI

Ibrahimu alikuwa katika nchi ya kaanani wakati Mungu

alipomwambia, “Kwa mzao wako nitampa nchi hii” Turudi kwa

maneno ya mfia dini stefano, akiwa amejazwa na roho mtakatifu na

sura yake ikiwa ikin’gaa kama malaika aliwaambia wale wanaomtesa

Matendo 7

2 Naye akasema, Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni: Mungu wa utukufu

alimtokea baba yetu Ibrahimu, alipokuwa katika Mesopotamia, kabla hajakaa

Harani, 3 akamwambia, Toka katika nchi yako na katika jamaa zako, ukaende hata

nchi nitakayokuonyesha. 4 Ndipo alipotoka katika nchi ya Wakaldayo, akakaa

Harani, akatoka huko baada ya kufa babaye, Mungu akamhamisha mpaka nchi hii

mnayokaa ninyi sasa

Haya ni marudio ya yale tuliokwisha soma katika sura ya kumi na mbili

ya Mwanzo. Sasa soma mstari unaofata

5 Wala hakumpa urithi humu hata kiasi cha kuweka mguu; akaahidi kwamba

atampa, iwe milki yake, na ya uzao wake baadaye alipokuwa hana mtoto.

Tunajifunza hapa kuwa japokuwa wakati mwingine ni nadra sana

kusema “Kwa mzao wako nitakupa nchi hii” Ibrahimu mwenyewe

alijumuishwa katika ahadi hiyo. Hii ni wazi kabisa katika marudio

yanayofata katika kitabu cha mwanzo.

Lakini tunajifunza zaidi kuwa Ibrahimu hakupata urithi wowote wa

nchi. Hakuwa na hata sehemu kiasi cha kuweka mguu wake, lakini bado

Mungu alimuahidi kwake na mzao wake baada yake. Je tutasemaje

kuhusu hili?—kwamba ahadi ya Mungu ilishindikana?—hapana.

Mungu hawezi “kudaganganya” “Yeye ni mwaminifu.” Ibrahimu

alikufa bila kupokea ahadi ya urithi, lakini bado alikufa akiwa na imani.

Tunatakiwa kujifunza katika hili somo ambalo Roho mtakatifu alitaka

wayahudi wajifunze, kwamba ahadi ya urithi itapokelewa kupitia Yesu

na ufufuo. Hili pia liliwekwa wazi kabisa kupitia maneno ya mtume

Petro

Page 13: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

13

Matendo 3

25 Ninyi mmekuwa watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu

aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za

ulimwengu zitabarikiwa. 26 Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu,

alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia

Ahadi za Ibrahimu kama jinsi tulivyojifunza, zinawafikia watu wa

mataifa na familia zote za dunia, kupitia Yesu kristo na msalaba, lakini

baraka za Ibrahimu zinaambatana na ahadi ya nchi ya kaanani. Ambayo

ilikuwa ipokelewe kupitia Kristo na ufufuo. Kama ingekuwa ni

kinyume, Ibrahimu angekuwa amekwazwa, badala ya kufa akiwa na

imani tele kuhusu ahadi. Lakini hili nalo litakuwa wazi zaidi

tutakapoendelea.

Page 14: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

14

Page 15: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

15

1. MAAGANO MAWILI.

Wagalatia 4

21 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22 Kwa maana

imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja

kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana

kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano

mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri

ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa

anatumika pamoja na watoto. 26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye

mama yetu sisi. 27 Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti,

ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa

huyo aliye na mume. 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. 29 Lakini

kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho,

ndivyo ilivyo na sasa. 30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa

maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. 31

Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye

mwungwana.

“Haya ni maagano mawili.” maagano mawili ni yapi?—Hawa

wanawake wawili, kwa vile agano la pale sinai linawakilishwa na

Hajiri, Hivyo agano jingine linawakilishwa na Sara. Tafsiri nyingine ya

mstari wa 24 unasomeka “Kwa maana hawa ni maagano wawili”

Hawa wanawake wawili ni mama wa watoto wawili wa Ibrahimu.

Mwana mmoja alizaliwa na mtumwa, mwingine kwa Mwanamke huru

(Mwungwana): Sara alikuwa ni mwanamke Huru. Wana wawili wa

hawa wanawake wawili wanawakilisha watoto wa maagano mawili.

“Hawa ndio maagano mawili” yoyote basi anayesome kuhusu

maagano mawili lazima asome kuhusu hawa.

“Hawa ndio maagano mawili” Kila somo basi kuhusu maagano mawili,

kama sio somo kuhusu hawa basi hilo sio somo kuhusu maagano

mawili.

“Hawa ndio maagano mawili” Kwa kupitia hawa basi somo la maagano

mawili linaanza na yoyote anayesoma kuhusu maagano mawili lazima

aanze pale ambapo somo linaanza. Hivyo hapa ndipo tunapoanzia somo

la maagano mawili. Na ili tuweze anza kwa manufaa yetu ni lazima pia

tusome Mwanzo 15, 16, 17, na 21: 1-21- angalau mara saba.

Page 16: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

16

2. MAISHA YA IBRAHIMU.

Wagalatia

21 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22

Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa

mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa

mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;

kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo

kwa utumwa, ambalo ni Hajiri

Hivyo maagano mawili yalikuwa katika familia ya Ibrahimu. Kwa

maana “Hawa ndio maagano mawili” mstari wa 24

Kwa nini maagano mawili yaliingia katika familia ya Ibrahimu, na moja

kati ya hayo ni agano la sinai? “kwa maana Hawa ndio maagano mawili

moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri”

Kwa vile Hajiri ni moja kati ya maagano mawili—la Kutoka sinai, na

ambalo linalozaa utumwa,—hadithi ya Hajiri katika familia ya

Ibrahimu ni hadithi ya agano kutoka sinai.

Lakini Mungu alifanya agano na Ibrahimu mwenyewe, kabla hata

Hajiri hajasikika. Na hili agano lilithibitishwa katika Kristo, kabla hata

Hajiri hajatajwa.

Agano hili lilikuwa ni agano la ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu na kwa

mzao wake—sio “wazao kama vile ni wengi: lakini kama vile ni

mmoja, na kwa mzao wake yani Kristo” Hili ni agano la Haki ya

Mungu—haki ya Mungu kwa imani—kwa maana Mungu alipofanya

agano na Ibrahimu, Ibrahimu alimwamini Bwana na alimuhesabia

kuwa ni haki” (Mwanzo 15:6)

Hii ahadi ilikuwa kwa Ibrahimu, kwamba kwa kupitia yeye Familia

zote za dunia zibarikiwe—Kwa kupitia mzao wake atampa Nchi ya

ahadi, ambayo ndio ulimwengu ujao, na kwamba mzao wake atakuwa

kama nyota za mbinguni.

Mzao huyu, ambaye kwa yeye ahadi ilifanywa, ndiye Kristo, agano hili

lilifanywa kupitia Kristo, na pale ambapo Ibrahimu alipomwamini

Mungu, ilihesabiwa kwake kuwa haki, agano hili lilithibitishwa katika

Page 17: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

17

Kristo. Hili ndilo agano la milele, Jerusalem ya juu, kwa maana katika

agano hilo, kwasababu ya ahadi ile, Ibrahimu “akiutazamia mji wenye

misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu” (Waebrania

11:10).

Haya yote yalikuja kwa Ibrahimu kipindi hana mtoto na ahadi lazima

ingetimizwa kupitia mzao wake. Miaka mingi ilipita tokea Bwana wa

Mzao wa Ibrahimu aongelee hilo kwa mara ya kwanza kipindi hana

mtoto. Ibrahimu alikuwa tayari mzee wakati alipoambiwa kwa mara ya

kwanza jambo hilo kuhusu mzao wake, na alikuwa anaendelea kuzeeka

bila hata kuona mzao yeyote. Hivyo alisema,

Mwanzo 15

2 Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina

mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski? 3 Abramu

akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye

mrithi wangu. 4 Nalo neno la Bwana likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali

atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi. 5 Akamleta nje, akasema,

Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu.

Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. 6 Akamwamini Bwana, naye

akamhesabia jambo hili kuwa haki. 7 Kisha akamwambia, Mimi ni Bwana,

niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi.

Na pale ambapo Ibrahimu alipouliza “Mungu, nitajuaje kama kweli

nitairithi?” Bwana “Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu,

na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na

hua, na mwana njiwa. 10 Akampatia hao wote, akawapasua vipande

viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege

hakuwapasua.” Ndipo Bwana kwa kupita katikati ya vile vipande

“akafanya agano na Abramu” agano la damu, ambalo linahitaji

kutimizwa kwa kila ahadi ambayo iliahidiwa kwa Ibrahimu. (Mwanzo

15:8-10, 18)

Hapa ndilo, Agano lake mwenyewe la kimbingu la Mungu, agano la

milele lilipofanywa na kuthibitishwa kwa Ibrahimu, Kwa ahadi yake

mwenyewe Mungu kuwa kila kitu kilichoahidiwa lazima kitimizwe, ili

kwamba chochote kilichoahidiwa kikishindwa kutimizwa basi Mungu

ataacha kuwepo.

Page 18: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

18

Lakini bado muda unaenda, na hakuna mtoto anayeonekana, kwa

maana “Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana.” Lakini Sara

“alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri” na Sara akamwambia

Abramu, Basi sasa, Bwana amenifunga tumbo nisizae, umwingilie

mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye” (Mwanzo 16:1,2). Hapo

ndipo Hajiri anapokuja katika tukio, na kuletwa katika hii hadithi.

Lakini kwa namna gani Hajiri analetwa katika hadithi hii? Je ilikuwa

kwa kuamini ahadi ya Mungu? –Hapana. Imeletwa kwasababu ya

kutokuwa na imani. Je ilikuwa kwasababu ya Imani?-Hapana. Ilikuwa

ni kwasababu kutokuwa na imani. Hii inathibitishwa kutokana na jinsi

huu mpango ulivyofanywa, ni lazima mzao aje kupitia Sara yeye

mwenyewe na “Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa

kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa

alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu” (Waebrania 11:11)

Kama hilo ndilo lilivyokuwa mwisho, kwanini hapo mwanzo “Sara

mke wa Abramu hakumzalia mwana”?-Ilikuwa ni kwasababu ya

kutokuwa na imani kwake na yeye kushindwa “kumhesabu yeye

aliyeahidi kuwa mwaminifu”

Ndipo kwa kutokuwa na imani na Mungu, kwa kutokuwa na imani

huku, Sarai alifanya mpango uliomleta Hajiri. Huu mpango ulifanywa

kwasababu ya kutokuwa na imani na Mungu, ulikuwa ni mpango wa

akili ya asili—ulioletwa na mwili—ilikutimiza ahadi ya Mungu.

Kitu cha muhimu zaidi cha kuzingatia kutoka katika mpango huu ni

kwamba ulikuwa upo kwaajili ya kutimiza ahadi ya Mungu. Sio tu

walidhani kuwa Mungu hajatimiza ahadi yake, lakini pia alikataa

kutimiza. Kwa maana Sarai alisema wazi “Bwana amenifunga tumbo

nisizae.” Hii ni tuhuma ya wazi kabisa ya kutokuwa na imani na upande

wa Bwana, kwa vile aliamini kuwa Bwana ameshindwa kutimiza ahadi

yake, wakahitimisha kuwa walitakiwa wao wenyewe kutimiza kwa

kuleta mpango wao wenyewe ambao uliotokana na kutokuwa na imani

na Mungu.

Hata Abram alitolewa kutoka katika Imani yake kwa Mungu, kutoka

katika Imani kwa Bwana na ahadi yake. Abram akaanguka katika

Page 19: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

19

mpango huu wa kutokuwa na imani, ulioletwa na mwili “Abramu

akaisikiliza sauti ya Sarai”

“Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada

ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu

mumewe, awe mkewe. Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba.

Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni

machoni pake.... Hajiri akamzalia Abramu mwana wa kiume; Abramu

akamwita jina lake Ishmaeli, yule mwanawe, ambaye Hajiri alimzaa”.

(Mwanzo 16:4,15)

“Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili,” Kwanini hakuzaliwa

kwa njia nyingine yoyote? Mpango wote, ambao umemfanya mpaka

amezaliwa, wote ulikuwa ni akili ya asili, Katika Kutokuwa na imani

na Mungu—ulioletwa na mwili.

“Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama

maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa,

ambalo ni Hajiri. Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni”

(Wagalatia 4:24,25)

Hivyo Agano ambalo Hajiri anasimama—agano kutoka sinai—ni

agano ambalo watu walikuwa hawana Imani na Mungu na kutoamini

ahadi zake, wakijua tu akili ya asili na kuzaliwa katika mwili na kuunda

mipango yao wenyewe, na juhudi zao wenyewe kupata haki ya Mungu

na urithi ambao unaambatana na haki.

Lakini Haki ya Mungu ikiambatana na urithi katika ukamilifu wake ni

zawadi ya Bure.

Page 20: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

20

3. HAJIRI NA SARA

Wagalatia 4

21 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22

Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa

mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa

mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;

kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo

kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko

Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na

watoto

Hajiri anawakilisha agano kutoka sinai. Hajiri alikuwa ni mtumwa na

mmisri. Hivyo na mwana wake alikuwa ni mtumwa. Alikuwa ni

mtumwa kwa namna yoyote ile. Kwasababu mama yake alikuwa ni

mtumwa. Kama jinsi tulivyoona kuwa mwana wa Hajiri alizaliwa

kwasababu ya kukosa imani na Mungu na kutokuwa na imani katika

ahadi yake—ulikuwa ni mpango wa mwili, kwa hiyo “yule wa mjakazi

alizaliwa kwa mwili” Lakini

Warumi 8

“.7...ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu,

wala haiwezi kuitii. 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu”

Hivyo hivyo agano ambalo Hajiri anasimama—agano kutoka mlima

sinai—ni agano ambalo watu wanajua tu mtu wa asili na kuzaliwa kwa

mwili, wakitafuta kwa mafumbuzi yao wenyewe na kwa juhudi zao

wenyewe kupata haki ya Mungu, na urithi unaoambatana na haki hiyo.

Hili, kama jinsi tulivyokwisha ona, Sara na Abram walikuwa na ahadi

ya Mungu kwa ukamilifu, na haki yake, katika agano la Mungu

lililothibishwa kupitia Kristo, kabla hata mpango unaomleta Hajiri

haujaundwa. Na mpango huu uliundwa na ungeundwa, kwa kuweka

mbali ahadi na agano. Na kutelekeza ahadi na agano ni kuwa na imani

katika mwili.

Je watu pale Sinai walikuwa na ahadi yoyote kutoka kwa Mungu, au

agano ambalo wangeweza kuwa na imani kwake, kabla hata

hawajaingia katika agano la sinai?—Walikuwa nalo. Walikuwa na

Page 21: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

21

agano la Ibrahimu, kama jinsi Abramu na Sarai kabla hawajaingia

katika mpango wa kumleta Hajiri.

Si tu walikuwa na hili agano la Ibrahimu, kwa kulinganisha umbali wa

muda kati ya Ibrahimu na wao, lakini lilirudiwa kwao, moja kwa moja

na Bwana, na kufanya nao kama jinsi ilivyokuwa kwa Ibrahimu kabla

hata hawajaondoka Misri.

Kutoka 6

2 Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; 3 nami

nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina

langu YEHOVA sikujulikana kwao. 4 Tena nimelithibitisha agano langu nao, la

kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya kukaa kwao hali ya ugeni.5 Na zaidi ya hayo,

nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami

nimelikumbuka agano langu. 6 Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA,

nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na

utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu

kubwa; 7 nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi

mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya

mizigo ya Wamisri. 8 Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo naliinua mkono

wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni

YEHOVA.

Hapa tunaona lilitolewa kwa wana wa Israel huko Misri pia lilitolewa

kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Agano hilo hilo alilo “fanya na

Ibrahimu na kuapa kwa Isaka” na “lililothibitishwa” kwa Yakobo,

lilifanywa na Israel, wakati bado wapo Misri, wakati Mungu anashuka

ilikuwaokoa kutoka Misri.

Sasa kwa nini tena wana wa Israel waliingia katika agano la pale

Sinai?—Kama jinsi mpango uliomhusu Hajiri ulivyoletwa. Kwa nini

agano jingie lililetwa?—Ni kama vile Hajiri alivyoletwa—yote ni

kwasababu ya kukosa imani katika agano la Mungu, yote ni kwasababu

ni kutokuwa na imani kuhusu ahadi ya Mungu iliyothibitishwa kwa

Kiapo chake. Kwa maana kama wangeamini katika ahadi za Mungu

alizozitoa kwao huko Misri, wangepata yote ambayo Ibrahimu au mtu

mwingine yoyote angeyapata, wangepata haki ya Mungu, wokovu

wake wa milele, na urithi ulioahidiwa kwa Ibrahimu na yote haya yapo

katika Kristo; Hii ndio jinsi Ibrahimu alivyopata.

Page 22: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

22

Ni kweli waliimba nyimbo za ushindi katika Bahari ya shamu, baada

ya kuvuka, na kama wangeendelea katika imani hiyo, wangeendelea

katika agano la milele la Mungu alilowapa wakiwa huko Misri:

kusingekuwepo na agano lingine pale sinai.

Lakini hawakuendelea katika Imani; kwa maana muda mfupi tu

baadaye katika safari walipofika Marah, wakaanza kulalamika dhidi ya

Mungu. Na Mungu alipowaokoa kutoka katika hofu zao, walifikapo

katika nyika ya dhambi na “Makusanyiko yote walianza kulalamika”

tena.

Kutoka 17

3 Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung'unikia Musa, wakasema, Mbona

umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa

kiu?

Na baada Mungu kuwaondolea hafu zao katika muda huo na wakaipita

nyika ya dhambi, wakafika Rephidimu, tena wakaanza kunun’gunika

na kusema

Kutoka 17

3 .................Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na

wanyama wetu kwa kiu? 4 Musa akamlilia Bwana, akisema, Niwatendee nini watu

hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe.

Haya yote wanathibitisha kutokuwa na imani na kukosa imani kwake,

kwa upande wa Israel. Kukosa imani huku na kutokuwa na imani huku

ulizuia baraka na nguvu iliyotolewa katika agano la Ibrahimu, ambalo

Mungu aliwapa kipindi wapo huko Misri.

Hawakumuamini Mungu kwa urithi ambao ulikuwa unakuja, wala kwa

haki, ambayo pekee ndio ungewapatia urithi. Hili walifikiri wao

wenyewe wanaweza kulipata, na ili waone kwa jinsi gani wasingeweza

kuipata, Bwana aliwapa fursa pana sana ya kujaribu. Alisema,

Kutoka 19

4 Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya

mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi. 5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu

kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu

kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, 6 nanyi

Page 23: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

23

mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno

utakayowaambia wana wa Israeli

Lakini bado hawakusikia sauti yake, lakini walipoisikia, Amri kumi

zilipotamkwa, wakakubali kutii amri kumi. Na hata waliposikia sauti

na utukufu wake na wakaogopa na “wakajiondoa na kukaa mbali”

walisema

Kutoka 24

7.............. Hayo yote aliyoyanena Bwana tutayatenda, nasi tutatii.

Na wakafanana na mwana wa Hajiri mtumwa, ambaye “alizaliwa kwa

mwili.” Walijua tu kuzaliwa kwa Mwili na ndipo akili ya mwili pekee

ambayo ni

Warumi 8

7 .......uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.

Na hawakuweza kuitii sheria kama Ishmael, mwana wa mwilini katika

familia ya Ibrahimu, asingeweza kutimiza ahadi kwa Ibrahimu. Katika

hali kama hii wasingeweza kushika agano la Mungu kama mpango wa

Sarai katika kumleta Hajiri ndivyo katika kushika agano hilo.

Kwanini agano hilo lililetwa? Kwanini waliingia katika agano hilo?

“Walikuwa hawana uelewa kuhusu utakatifu wa Mungu, na kuhusu uovu wa mioyo

yao na kutojiweza kwao kutoa utii wa sheria za Mungu na uhitaji wao wa mwokozi.

Haya yote ni lazima wafundishwe....... Watu hao hawakugundua uovu wa mioyo

yao na kwamba bila Kristo ilikuwa haiwezekani wao kutii sheria ya Mungu

wakaingia mara moja katika agano na Mungu. Walihisi kuwa wanaweza kuanzisha

haki yao wenyewe, wakasema “Yote aliyosema Bwana tutafanya na kutii” (Ellen

White Wazee na manabii uk. 371,372)

Walikuwa tayari katika kifungo cha dhambi na kujihesabia haki; na

katika kifungo hicho kwa “akili zisizotii sheria ya Mungu” na

zisizoweza kufanya hilo, waliahidi kutii sheria za Mungu. Lakini kwa

hali waliyokuwepo ilikuwa ni wazi kuwa wangevunja ahadi yao.

Ilikuwa haiwezekani kwao kufanya hilo. Hivyo katika agano hilo,

walikuwa ni wavunjaji wa Sheria na wavunjifu wa ahadi yao ya

kutovunja sheria ya Mungu.

Page 24: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

24

Na hili ndilo lilikuwa katika agano hilo, au kwa mujibu wa chochote

katika agano hilo. Hivyo katika Agano hilo KAMA HAJIRI, alizaa

utumwa pekee. Na hii ni kwasababu ya kutokuwa na imani na kukosa

imani na Mungu katika ahadi zake kama jinsi zinavyooneshwa katika

agano la Ibrahimu, ambalo lilitolewa kwao moja kwa moja, kabla hata

hawajaanza kutoa Misri.

“maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai,

lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. Maana Hajiri ni kama mlima

Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa

anatumika pamoja na watoto. Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana,

naye ndiye mama yetu sisi. Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe

uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana

watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na

mume. Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi”

Page 25: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

25

4. JE UPO AGANO GANI?

Wagalatia 4

21 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22

Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa

mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa

mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;

kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo

kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko

Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na

watoto.

Ishmael alikuwa ni mwana wa Ibrahimu aliyezaliwa mwilini. Je

alikuwa mtu wa aina gani? Kabla ya kuzaliwa Bwana alieleza kuwa

“Atakuwa ni kama punda pori.” Tafsiri ya marudio (Revised Version)

inatafsiri “Atakuwa kama punda poro kati ya wanadamu.” “Mkono

wake utakuwa kwa watu wote na mkono wa kila mtu kwake”.

Kumbuka kuwa mtoto huyu wa Hajiri, huyu mwana aliyezaliwa katika

mwili, huyu “punda pori kati wa wanadamu” alikuwa ni matunda ya

mpango wa Sarai, uliokuja baada ya kutokuwa na imani na Mungu, na

kukosa imani katika ahadi yake kuwa atampa mwana. Pia weka akilini

kuwa mtoto huyu alidhamiriwa na Sarai kuwa ndiye atakaye timiza

ahadi za Mungu. Ilidhamiriwa na Sarai, hata na Ibrahimu kuwa huyu

mwana wa mwilini, huyu mtu pori, akubaliwe na Mungu kuwa ndiye

mwana aliyemmaanisha katika ahadi zake, na kwamba ahadi ya

Ibrahimu itekelezwe ndani yake. Hii ni wazi kabisa pale Bwana

alipomwaambia Ibrahimu kwamba atampa mwana kwa kupitia Sarai,

Ibrahimu alijibu, “lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele

yako.”(Mwanzo 17:18)

Sasa kumbuka kuwa Hajiri, mama wa huyu “Punda pori” anawakilisha

agano kutoka sinai, na mtoto wake alizaliwa katika mwili—Huyu mtu

pori—anawakilisha wana wa agano la sinai. Na kama vile ule mpango

uliomleta Ishmael, ulifikiriwa kutimiza ahadi ya Mungu, na kwamba

agano la Mungu kwa Ibrahimu litimizwe katika yeye, ndivyo kwa wana

wa hilo agano la sinai, kama Ishmael, walizaliwa katika mwili, na

walifikiri watamiza Ahadi ya Mungu kupitia wao, hivyo kupitia mwili.

Page 26: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

26

Lakini Ibrahimu alishika amri za Mungu. Haki ya Mungu ndio kitu cha

kwanza cha muhimu katika agano na Ibrahimu, kwa maana bila hiyo

hakuna anayeweza kupata urithi aliopewa Ibrahimu katika Agano.

Lakini Je Ishmael atazaliwaje katika mwili, kisha akashika amri za

Mungu, wakati akili ya mwili ni uadui kwa Mungu na wala haiwezi

nyenyekea sheria za Mungu? Je inawezekanaje kwa huyo Punda pori

kushika amri za Mungu, wakati mkono wake upo kwa kila mtu, hali

moja kati vitu viwili katika sheria yote ya Mungu ni “Mpende jirani

yako kama nafsi yako”?

Huyu mtoto wa Hajiri aliyemtumwa anafanana na watoto wa agano lile

la Sinai, lililozaa utumwa. Kama Ishmael, walikuwa wanajua tu

kuzaliwa kwa mwili,na “akili ya mwili pekee” ambayo ni uadui dhidi

ya Mungu, na wala haitii sheria ya Mungu, na wala haiwezi kuwa,

waliahidi kuwa watatunza sheria ya Mungu “Ni kweli”

Lakini Ishmael alikuwa sio mtoto aliyedhamiriwa na Bwana,

hawezitimiza ahadi ya Mungu, wala ahadi ya Mungu haiwezi

kutimizwa katika yeye. Kwa jinsi ahadi na Agano la Ibrahimu lilivyo,

Kuzaliwa kwa Ishmael ilikuwa ni kama vile hajazaliwa kabisa.

Hivyo pale Ibrahimu alipomwambia Bwana “ Oh Ishmael angeishi

mbele yako” Mungu alisema

Mwanzo 17

“19 Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake

Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya

uzao wake baada yake. 20 Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki,

nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili,

nami nitamfanya awe taifa kuu. 21 Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka,

ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao”

Katika wakati huu Sarai alikuwa tayari ameamini katika ahadi ya

Mungu na kumuamini Mungu pekee na Mungu akambadili Jina kuwa

Sarah. Na hivyo “Kwa imani “hata Sara mwenyewe alipokea uwezo

wa kuwa na mimba” na kwa mujibu wa ahadi Isaka akazaliwa.

Sasa Isaka alikuwa ni mtu wa aina gani? Mienendo yake inaoneshwa

katika kipindi cha Ibrahimu pale alipokuwa anatakiwa atolewe kama

Kafara. Alinyenyekea kama mwanakondoo aliyetakiwa kutolewa. Na

inaoneshwa zaidi katika mwanzo 26 Baada ya Ibrahimu Kufa na isaka

Page 27: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

27

akawa ndio mrithi wa agano, aliishi katika sehemu ambayo wafilisti

nao walikuwepo

Mwanzo 26

15 Na vile visima vyote walivyochimba watumwa wa baba yake, siku za Ibrahimu

babaye, Wafilisti walikuwa wamevifukia, wakavijaza kifusi. 16 Abimeleki

akamwambia Isaka, Utoke kwetu, maana wewe una nguvu sana kuliko sisi. 17 Basi

Isaka akatoka huko akapiga kambi katika bonde la Gerari, akakaa huko. 18 Isaka

akarudi akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu

babaye; maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake

Ibrahimu; naye akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye. 19 Watumwa

wa Isaka wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika.

Hivi visima bila pingamizi ni kwa Isaka. Ibrahimu alivichimba, na

hivyo ni mali ya Ibrahimu. Na pale Isaka alipokuwa ni mrithi wa

Ibrahimu, visima hivi vikawa ni mali yake kwa urithi. Na sasa

anavichimba tena, ambavyo ni kama anavichimba tena upya. Hivyo

bila pingamizi vilikuwa ni vyake. Lakini japokuwa vilikuwa ni vyake

kwasababu ya wafilisti pale visima vilivyofunguliwa, kutoka katika

kuwa vimejazwa na kifusi, ni wazi inaonesha kuwa hawakuwa

wanavitaka hata kidogo.

Lakini wafilisti wakaja kwa Isaka na kuvitaka visima ambavyo

vimefunguliwa ambavyo kwa haki kabisa ni vyake. “Maji ni yetu”

(Mwanzo 26:20). Isaka aliwaachia wawe navyo. Lakini ishmael

angefanyaje? Je wewe ungefanyaje? Kati ya wana wawili wa Ibrahimu

wewe upo upande upi? “Haya ni maagano mawili” Je wewe upo agano

gani?

Isaka “alichimba tena kisima kingine” na wafilisti tena “wakakitaka

tena na hicho.” Lakini Isaka badala ya kushindana nao ambacho kwa

kiwango kikubwa sana kilikuwa ni haki yake, alijiondoa kutoka kwao

na “akachimba kisima kingine” Lakini Ishmael angefanyaje? Wewe

ungefanyaje? Kati ya wana wawili wa Ibrahimu wewe ni yupi? “Haya

ni maagano mawili” je agano lipi upo?

Isaka alipochimba kisima cha mwisho, wafilisti hawakukitaka, ndipo

akakiita Rohoboth na akasema,

Page 28: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

28

Mwanzo 26

22 Kwa kuwa sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi

Lakini Bwana alimuwekeaje nafasi?—Ni kwasababu alikataa

kugombana na wafilisti, kwa kuwakubalia yote ambayo wao

waliyataka, japokuwa ilikuwa ni haki yake. Lakini Je Mungu

angeweka nafasi kwaajili ya Ishmael na wafilisti? Je Mungu anaweka

nafasi kwaajili yako na wanaokupinga? Wewe ni yupi kati ya hawa

wana wawili wa Ibrahimu? “Haya ni maagano mawili” Je upo agano

gani?

Mwanzo 26

23 Akapanda kutoka hapo mpaka Beer-sheba. 24 Bwana akamtokea usiku uleule,

akasema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako, usiogope, maana mimi ni

pamoja nawe, nami nitakubarikia, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Ibrahimu

mtumishi wangu. 25 Akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Akapiga

hema yake huko, na watumwa wa Isaka wakachimba kisima huko26 Ndipo

Abimeleki akamwendea kutoka Gerari, pamoja na Ahuzathi rafiki yake, na Fikoli,

jemadari wa jeshi lake. 27 Isaka akawauliza, Mbona mwanijia, nanyi

mmenichukia, mkanifukuza kwenu? 28 Wakasema, Hakika tuliona ya kwamba

Bwana alikuwa pamoja nawe; nasi tukasema, Na tuapiane, sisi na wewe, na kufanya

mapatano nawe 29 ya kuwa hutatutenda mabaya, iwapo sisi hatukukugusa wewe,

wala hatukukutendea ila mema, tukakuacha uende zako kwa amani; nawe sasa u

mbarikiwa wa Bwana.

Lakini ilikuwa ni kwasababu ya unyenyekevu endelevu wa Isaka ndiyo

kilichowafanya waone kuwa Bwana alikuwa ndani yake na kwamba

alikuwa ni mbarikiwa wa Bwana. Lakini Ishmael angefanya nini? Je

wewe ungefanya nini? Wewe unafanya nini? Wewe ni yupi kati ya

wana wawili wa Ibrahimu? “Haya ndio maagano mawili” je wewe upo

agano gani?

Na ndivyo

Wagalatia 4

Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa

mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa

mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;

kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo

kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko

Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na

Page 29: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

29

watoto. 26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. 27

Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe

usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo

aliye na mume. 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi.

Wewe upo wapi?

Page 30: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

30

5. LITUPE MBALI AGANO LA KALE.

Wagalatia 4

Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22 Kwa

maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa

mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa

mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;

kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo

kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko

Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na

watoto. 26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. 27

Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe

usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo

aliye na mume. 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. 29

Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule

aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa. 30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze

mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na

mwana wa mwungwana. 31 Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali

tu watoto wa huyo aliye mwungwana.

Mpango ulioanzishwa na Sarai na kukubaliwa na Abram, uliomleta

Ishmael mwana wa mtumwa, ambaye alizaliwa kwa mwili, ulionesha

kuwa haukuwa wa kuridhisha kwa wote kuanzia hatua ya kwanza ya

kuanza kwake.

Mwanzo 16

3 Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa

Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe

mkewe. 4 Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya

kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake.

Japokuwa kama kumbukumbu zinavyonesha kuwa Sarai ndiyo wa

kwanza kutoa mpango huo kwamba “Sarai mkewe Abramu akamtwaa

Hajiri Mmisri mjakazi wake”...... “Akampa Abramu mumewe, awe

mkewe” lakini mara tu alipojua kuwa Hajiri anamuona duni, hii ni

kwasababu ya mafanikio ya mpango wa Sarai, anamgeukia Abramu

na kusema

Page 31: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

31

Mwanzo 16

5 Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako,

naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake.

Bwana na ahukumu kati ya mimi na wewe 6 Naye Abramu akamwambia Sarai,

Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako.

Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake

Japokuwa Bwana alimwambia Hajiri

Mwanzo 16

.... 9 Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake.

Ni wazi kuwa hakukuwa na amani katika maisha yaliyofata. Tunaona

kuwa baada Ishmael kuzaliwa. Abram alimwambia Bwana “Ishmael

angeishi mbele yako” hakusikilizwa, lakini Ishmael aliwekwa pembeni,

na Abram akamwambia Sarai mke wake kuwa atamzalia mwana, na

atamwita jina lake Isaka “Nami nitafanya agano langu imara kwake

kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake” (Mwanzo

17:19).

Mwanzo 21

2 Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake,

kwa muhula alioambiwa na Mungu..... 8 Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya;

Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya. 9 Sara

akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya

dhihaka. 10 Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na

mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka. 11

Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe. 12

Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya

huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa

maana katika Isaka uzao wako utaitwa

Lakini bado rekodi haijawa wazi. Ibrahimu alitoka katika ahadi

zilizowazi za Mungu na kuweka tegemeo katika mwili. Na sio tu

mtumwa na mwana wake wafukuzwe, na pia kila kitu kilichoshikiri

katika mpango kilichomleta mtumwa na mwana wake lazima

vitelekezwe. Hivyo Mungu akamwambia Ibrahimu,

Page 32: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

32

Mwanzo 22

2 Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako

mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima

mmojawapo nitakaokuambia

Isaka alikuwa ni mwana wa ahadi, hakukuwa na mwana mwingine wa

ahadi, hakukuwa na ahadi nyingine na hakukuwa na mwana mwingine

kwa ahadi nyingine. Na sasa kwa Ibrahimu kumtoa Isaka kama kafara

ilikuwa ni zaidi ya kudhania kuchukua yote ambayo Mungu aliahidi.

Lakini Ibrahimu alipoangalia, aliangalia mbali zaidi, hata katika

chimbuko la ahadi ya Mungu na akaamini na kutegemea atakapomtoa

Isaka, Mungu anatimiza ahadi yake kwa kumfufua kutoka katika wafu-

kwa kumrudisha kutoka katika majivu baada ya kuwa ameunguzwa na

moto wa kafara.

Muito huu wa Bwana kwa Ibrahimu kumtoa Isaka kama sadaka ya

kuteketezwa, ulimrudisha Ibrahimu katika usiku wa ahadi halisi,

wakati Mungu aliposema,

Mwanzo 15

5 Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza

kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. 6 Akamwamini

Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.

Hivyo Ibrahimu alirudishwa kuamini katika ahadi ya Mungu iliyowazi

pekee, na yote ambayo ahadi imejumuisha. Na kama Ibrahimu

angesimama na kukataa pendekezo la Sarai kuhusu Hajiri,

kusingekuwa na matatizo ya kifamilia yaliyokuja kati ya Sarai na

Hajiri, Ishmael asingezaliwa na Ibrahimu asingeambiwa amtoe Isaka

sadaka. Kama tokea mara ya kwanza asinge “sita kwa kutokuamini”

(Warumi 4:20) lakini angekuwa ni imara katika imani akimpa Mungu

utukufu, akiamini kile kilichoahidiwa kukifanya, angepewa haki siku

zote.

“Haya ni maagano mawili moja kutoka katika mlima sinai, linalozaa

utumwa ambalo ni Hajiri” Agano la sinai ni matunda ya mwili, wa

kutokuwa na imani na kutoamini katika Mungu. Kama jinsi ule mpango

uliomleta Hajiri na uliomleta Ishmael. Kama jinsi Hajiri na Ishmael

mtumwa na mwana wake, walivyofukuzwa na mpango wote ulioletwa

Page 33: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

33

ulivyowekwa pembeni, ndivyo agano la sinai linavyotakiwa lifukuzwe,

na yote yaliyofanya kuwepo kwa hilo agano yanatakiwa yawekwe

pembeni.

“Kwa kuwatoa Misri Mungu alikuwa anataka kuwaonesha nguvu yake na huruma

yake, ili kwamba wamwamini na wampende. Aliwaleta mpaka bahari ya shamu—

hali wakiwa wanafukuzwa na wamisri, na kutoroka ilikuwa ni ngumu—ili waone

hali yao kuwa hawajiwezi, na kuhitaji msaada wa Mungu, ndipo alipowaokoa.

Ndipo walipojawa na upendo na shukurani kwa Mungu na wakiwa na ujasiri katika

nguvu ya Mungu aliwachukua kama ndiye mwokozi katika utumwa.

Lakini kulikuwa na ukweli mwingine mkubwa kwaajili ya kushangaza akili zao,

hali wakiishi katikati ya sanamu na uovu, walikuwa hawana uelewa kuhusu

utakatifu wa Mungu, na kuhusu uovu wa mioyo yao na kutojiweza kwao kutoa utii

wa sheria za Mungu na uhitaji wao wa mwokozi. Haya yote ni lazima wafundishwe.

Mungu aliwaleta Sinai aliwadhihirishia ukuu wake, aliwapa sheria zake, akitoa

ahadi ya mibaraka kama watatii “Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli,

na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila

yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, nanyi mtakuwa kwangu ufalme

wa makuhani, na taifa takatifu” (Kutoka 19:5,6).Watu hao hawakugundua uovu wa

mioyoyao na kwamba bila Kristo ilikuwa haiwezekani wao kutii sheria ya Mungu

wakaingia mara moja katika agano na Mungu. Walihisi kuwa wanaweza kuanzisha

haki yao wenyewe, wakasema “Yote aliyosema Bwana tutafanya na kutii” (Kutoka

24:7)

Walishuhudia kutolewa kwa sheria katika ukuu unaotisha, na waliogopa na

kutetemeka mbele ya mlima, lakini baada ya wiki chache walivunja agano lao na

Mungu, na walisujudia sanamu. Hawakuwa na tumaini tena kuwa katika upendeleo

wa Mungu kwa kupitia agano, ambalo wamelivunja SASA kwa kuona dhambi yao

na haja yao kwa kusamehewa, walipelekwa kuona hitaji lao la kuwa na mwokozi

aliyefunuliwa katika agano la Ibrahimu aliyekivuli katika kafara. SASA kwa imani

na upendo walimshikilia Mungu kama ndiye mkombozi kutoka katika vifungo vya

dhambi. SASA walikuwa katika hali ya kukubali baraka zilizokuwa katika

AGANO JIPYA’ (Ellen White, Wazee na manabii uk. 371,372)

Page 34: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

34

6. MWANZO WA “IKIWA” NA “NDIPO”

Wagalatia 4

21 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22

Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa

mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa

mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;

kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo

kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.

Agano la sinai ni agano ambalo Mungu alifanya na wana wa Israel

alipowachukua kutoka Misri. Agano hilo lilikuwa na makosa,

Waebrania 8

7 Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa

kwa lile la pili.

Agano hilo lilikuwa na makosa katika ahadi zake kwa maana agano la

pili ni bora zaidi kuliko hilo kuwa “lililoamriwa juu ya ahadi zilizo

bora” (Waebrania 8:6)

kosa katika agano hilo lilikuwa ni kwa upande wa watu,

Waebrania 8

8 Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami

nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya

Hivyo kwasababu kosa la agano hilo lipo katika ahadi zake, kosa

lilikuwa kwa watu wenyewe, maana yake ahadi zilizotumika kuanzisha

agano hilo zilikuwa ni ahadi za watu.

Sasa je hizo ahadi zilikuwa ni ahadi zipi?—zilikuwa katika agano,

lililofanywa na wao walipotoka Misri na hilo ndilo agano.

Kutoka 19

4 Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya

mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi. 5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu

kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu

kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, 6 nanyi

mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno

utakayowaambia wana wa Israeli.....8 Watu wote wakaitika pamoja wakisema,

Page 35: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

35

Hayo yote aliyoyasema Bwana tutayatenda. Naye Musa akamwambia Bwana

maneno ya hao watu.

Katika haya makubaliano watu wote waliahidi kusikia sauti ya Bwana.

Hawakusikia hata sauti ambayo angeiongea. Lakini katika sura ya

ishirini walisikia hiyo sauti likiongea maneno ya amri kumi,ambazo

Bwana alizinena na “Hakuongeza chochote.” Na waliposikia haya,

walirudia ahadi yao “Yote aliyosema Bwana tutafanya na kutii”

Hili ndilo agano ambalo Bwana alifanya na wao alipowashika mkono

kutoka Misri, na linaoneshwa wazi katika maneno yafuatayo

Yeremia 7

22 Maana sikusema na baba zenu, wala sikuwaamuru kwa habari za sadaka za

kuteketezwa na dhabihu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri; 23 lakini

naliwaamuru neno hili, nikisema, Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu

wenu nanyi mtakuwa watu wangu; mkaende katika njia ile yote nitakayowaamuru

mpate kufanikiwa.

Na haya yanathibitishwa na maneno haya

Yeremia 11

3 ukawaambie, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Na alaaniwe mtu

asiyeyasikia maneno ya maagano haya, 4 niliyowaamuru baba zenu, siku ile

nilipowatoa katika nchi ya Misri, katika tanuru ya chuma, nikisema, Itiini sauti

yangu, mkafanye sawasawa na yote niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa

watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu;

Kuwa makini kwa kila kauli ya agano hili nakuona mfululizo wa ahadi.

Ya kwanza inaanza kwa upande wa Mungu “IKIWA mtaisikia sauti

yangu na kushika agano langu, NDIPO..............nanyi mtakuwa kwangu

ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno

utakayowaambia wana wa Israeli” n.k Katika hili tunaona kuwa ahadi

ya Mungu itakuja pale watakapotimiza ahadi yao, kwa maana agano

limeanza na “ikiwa” “IKIWA utafanya hili na hili, NDIPO hili na hili.

Huu pia ni mpangilio katika kauli ya pili, “Tiini sauti yangu NA

nitakuwa Mungu wenu, NA mtakuwa watu wangu”. Kwa mujibu wa

haya makubaliano, hawezi kuwa Mungu wao au wao kuwa watu wake,

mpaka wafanye kile walichoahidi, mpaka watakapo sikia sauti yake

kama walivyoahidi.

Page 36: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

36

Kauli ya tatu nayo inasema hivyo hivyo “Itiini sauti yangu, mkafanye

sawasawa na yote niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa watu

wangu.” Hii inaweka wazi sio tu kwanza hakuna chochote kutoka kwa

upande wa Mungu kinaweza kuja, ni mpaka wao watimize kile

ambacho wameahidi. Upande wa Mungu utakuja kwa kufanya kile

ambacho wameahidi “Tiini sauti yangu” na “mkafanye” Hivyo [Kwa

jinsi hiyo na kwamtindo huo] mtakuwa watu wangu na nitakuwa

Mungu wenu”

Kwa vile katika agano hili sehemu ya Bwana, kile ambacho Bwana

angekifanya, kile ambacho ameahidi, kinaweza kuja baada ya watu

kufanya kile ambacho wameahidi, hii ni wazi kabisa kuwa ndio

msimamo wa agano, lilivyofanywa, ni kwa ahadi za watu pekee.

Nini thamani ya ahadi za watu? Nini walichoahidi? Waliahidi kutii

sauti ya Bwana kabisa. Waliahidi kutii sheria zake-kushika amri kumi

kabisa.

Lakini walikuwa katika hali gani wakati wanatoa ahadi hiyo?—

inafanana na hali ya ishmael katika familia ya Ibrahimu. Walifanana

na Ishmael: walikuwa wamezaliwa mwilini na walijua tu kuzaliwa

mwilini, hivyo walikuwa na akili ya mwilini. Lakini “Akili ya mwilini

ni uadui dhidi ya Mungu kwa maana hainyenyekei sheria ya Mungu

wala haiwezi kuitii” “Waliomwilini hawawezi kumpendeza Mungu”

Kama hii ndio ilikuwa ndio hali zao, kulikuwa na maana gani kutoa

ahadi kwamba watashika amri za Mungu kabisa?—ahadi yoyote au

zote zilikuwa ni sawa na hakuna kitu kabisa.

Katika agano watu walikuwa wanaahidi kufanya kitu ambacho

hawaizekani wao kukifanya. Na kwavile Bwana pamoja na ahadi zake,

asingefanya chochote katika agano hilo, mpaka watimize ahadi zao,

mpaka wafanye kile ambacho wamekubaliana, ilikuwa ni kwamba

katika uhalisia kile ambacho watu walikigundua au walichokibuni, hilo

agano halikuwa na maana yoyote, kwa maana ahadi ambayo ilikuwa

imesimamishwa nalo zilikuwa hazina maana yoyote.

Kwa asili ya vitu lile agano lilikuwa linazaa utumwa, kwasababu watu

ambao walikuwa wametoa ahadi walikuwa katika utumwa wa mwili,

utumwa wa dhambi, na badala ya kutunza amri za Mungu kweli kweli,

Page 37: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

37

walikuwa wanazivunja. Na sio tu walikuwa wanavunja amri, ambazo

waliahidi kutozivunja, lakini walikuwa wanavunja ahadi yao ambayo

waliitoa kuwa hawatovunja amri. Hii ni kwasababu walikuwa katika

hali ya kutotii sheria za Mungu na hawawezi kutii.

Na hili limeelezwa haraka. Kwa maana Musa alipoenda kwenye mlima

kupokea Nakala ya sheria, ambayo waliahidi kuitii, alitoweka kwa

muda wa siku arobaini waliposema

Kutoka 32

1............Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa

huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.

Na wakajifanyia ndama wa dhahabu-mungu wa misri- na

wakamwabudu, kwa mtindo wa kimisri, hii inaonesha katika mioyo yao

walikuwa bado katika utumwa wa kimisri na walikuwa kama Ishmael,

mwana wa Hajiri mmisri “Aliyezaliwa katika mwili”

Japokuwa haya yote yameandikwa kwaajili watu wote watakaokuja

baadae, na kwaajili yetu “Kwa ambao miisho ya ulimwengu itakuja” ni

wazi kabisa hata leo wapo wengi ambao wanajua tu kuzaliwa katika

mwili, ambao hawajazaliwa tena, ambao hawajui kuzaliwa katika roho,

na bado wataingia katika agano kama hilo na watataka kutii amri zote

za Mungu. Lakini tatizo la hawa ni kama tatizo la watu wa sinai, na

kama ilivyotatizo la watu wa sinai, “Walikuwa hawana uelewa kuhusu

utakatifu wa Mungu, na kuhusu uovu wa mioyo yao...............Walihisi

kuwa walikuwa wanaweza kuanzisha haki yao wenyewe na wanasema

“Yote aliyosema Bwana tutafanya na kutii|”

Swali linakuja hapa, kwanini waliruhusiwa waingie katika agano kama

hilo? Kwanini Mungu alifanya nao agano kama hilo?

Page 38: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

38

7. AGANO LA KALE LIMELETA JIPYA

Wagalatia 4

Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22 Kwa

maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa

mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa

mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;

kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo

kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko

Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na

watoto. 26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. 27

Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe

usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo

aliye na mume. 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. 29

Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule

aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa. 30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze

mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na

mwana wa mwungwana. 31 Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali

tu watoto wa huyo aliye mwungwana.

Agano la kwanza lilikuwa na makosa. Lilikuwa na makosa kwasababu

lilitegemea ahadi za watu ambapo watu waliahidi kitu ambacho

ilikuwa haiwezekani kukitimiza.

Kwanini sasa waliruhusiwa waingie katika agano hilo? Je hakujua

kuwa watu wasingeweza kutimiza kile walichoahidi? Kwa uhakika

alijua.

Lakini watu ndio ambao hawakugundua. “hali wakiishi katikati ya

sanamu na mauovu, walikuwa hawana uelewa kuhusu utakatifu wa

Mungu, na kuhusu uovu wa mioyo yao na kutojiweza kwao kutoa utii

wa sheria za Mungu na uhitaji wao wa mwokozi. Haya yote ni lazima

wafundishwe. Mungu aliwaleta Sinai aliwadhihirishia ukuu wake,

aliwapa sheria zake, akitoa ahadi ya baraka kama watatii “Sasa basi

ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo

ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana

dunia yote pia ni mali yangu, nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa

makuhani, na taifa takatifu” (Kutoka 19:5,6).Watu hao hawakugundua

uovu wa mioyoyao na kwamba bila Kristo ilikuwa haiwezekani wao

Page 39: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

39

kutii sheria ya Mungu wakaingia mara moja katika agano na Mungu.

Walihisi kuwa wanaweza kuanzisha haki yao wenyewe, wakasema

“Yote aliyosema Bwana tutafanya na kutii”

Kwa vile watu hawakugundua vitu vya msingi kuhusu wao-

kutokuweza kwao n.k—kwavile hawakuamini katika Mungu ili

waweze kujua –na kwavile kila kitu wanatakiwa wafundishwe—njia

pekee ambayo inaweza kuwafanya wajifunze hiki ambacho hawakuwa

wanajua ni kuwafanya wajaribu na kushindwa ili wajifunze kutokana

na hayo kwamba wao wenyewe hawawezi kuanzisha haki yao

wenyewe kama ni haki ya Mungu. Ndipo wanaweza kukubali kwa

imani haki ya Mungu, ambayo imejengwa na Imani. Haya yote yapo

wazi katika mambo hayo.

Kama jinsi tulivyoona katika somo lililopita, kabla ya kuondoka Misri

Bwana alisema

Kutoka 6

“7 nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua

ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya

Wamisri

Ilikuwa wazi sana kama wangeamini tayari, wangejua kuwa tayari

alikuwa ni Bwana Mungu wao na wasingeingia katika makubaliano ili

Mungu awe Mungu wao na wao kuwa watu wake.

Kama wangeamini neno lake, kwamba siku zote alikuwa ni Mungu

wao,na kwamba wao tayari walikuwa ni watu wake,na kama

wangeelewa kuwa tayari alikuwa ni Bwana Mungu wao, je wangeitaji

kuahidi kuwa wataitii sheria yake “kwelikweli” ili kwamba wawe watu

wake, na yeye awe Mungu wao? Ni wazi kabisa, hapana.

Kama wangeamini kuwa Bwana angewapa wao urithi aliyoahidi kwa

Ibrahimu kuwa atampa, na kwa Isaka, na kwa Yakobo (Kutoka 6:8),

je kungekuwa na sehemu yoyote ambayo kuna makubaliano ambayo

wangeingia?, na kwamujibu wa waliyofanya, je kwa matendo,

wangeweza kupata urithi huo? Ni wazi hapana.

Kwa maneno mengine, kama wangempokea Mungu kwa imani katika

vitu hivi, alivyowaahidi kabla hata hawajatoka Misri, je wangejaribu

Page 40: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

40

kutafuta njia ya ushindi dhidi yake katika vitu hivyo, kwa matendo yao?

Ni wazi hapana.

Kwa maneno mengine, kama wangemjua na wangekuwa ndani ya

agano ambalo Mungu alifanya na Ibrahimu, agano la milele, je

wangehitaji kumjua na kuingia katika agano hili la sinai, ambalo

lilianzishwa na wao, kwasababu lilitegemea ahadi zao wenyewe? Ni

wazi hapana.

Tukifatilia mtiririko wa mawazo na kurudi katika mwanzo wake, katika

mistari hii ya wagalatia swali ni Kama Sarai na Abram wangeamini

ahadi ya Mungu na wangeishikilia , je ishmael angeonekana katika

familia ya Ibrahimu? Je wana wawili wa Ibrahimu wangezaliwa na

Ibrahimu? Ni wazi hapana.

Ni wazi kuwa, hakukuwa na haja yoyote ya Ibrahimu kuwa na mwana

zaidi ya mmoja—zaidi ya mwana ambaye Bwana alimuahidi. Lakini

“haya ni maagano mawili” Moja kutoka Sinai, linalozaa utumwa,

ambalo ni Hajiri.

Na kama jinsi ilivyokuwa hakukuwa na haya Ibrahimu kuwa na wana

wawili ila mmoja—mwana ambaye Mungu ameahidi—Hivyo

hakukuwa na haya Israel kuwa na maagano mawili ila agano moja—

Agano la Mungu na Ibrahimu—agano la milele.

Kama jinsi ilivyokuwa hakukuwa na haya ya wana wawili, hakukuwa

na haja ya maagano mawili.

Kutokana na kutoamini na kukosa imani na Mungu, Hajiri na Ishmael

waliingia kama vile kutokana na kutokuwa na imani na Mungu, agano

la Sinai liliingia.

Na kama vile Hajiri na Ishmael hawakuwa wanatambuliwa kwa namna

yoyote ile katika ahadi ambayo Mungu alimuahidi Ibrahimu kuhusu

mwana, ndivyo ilivyo kwa agano la sinai halikuwa linatambuliwa kwa

namna yoyote ile katika ahadi za Mungu kuhusu wokovu kwa

Wanadamu.

Kama jinsi Hajiri na Ishmael walikuwa wafukuzwe na yote

yaliyowaleta yalitakiwa yawekwe pembeni, ili kwamba mwana

aliyeahidiwa na Mungu awe na nafasi anayostahili, ndivyo ilivyo kwa

Page 41: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

41

agano la Sinai lazima lifukuzwe na yote ambayo yaliyoleta agano hilo

lazima yawekwe pembeni, kwa upande wa watu, ambapo ndio ahadi za

agano hilo lilipoelemea, ili kwamba agano halisi—agano la Ibrahimu—

agano la milele liwe na nafasi linalostahili, katika maisha na wokovu

wa watu.

Lakini kama kulivyokuwa na matatizo na kushindwa kwa Sarai na

Ibrahimu katika mpango uliowaleta Hajiri na Ishmael, ilikuwa ni

chombo ya kuwaleta katika sehemu ambayo wangeweza kumwamini

Mungu pekee, ndivyo hivyo matatizo na kushindwa kwa wana wa Israel

katika agano la kwanza liliwaleta katika sehemu ambayo walikubali na

waliamini katika, agano halisi la Mungu—agano la Ibrahimu—agano

lake la Milele—ambalo alilitoa kabla hawajatoka Misri.

Hivyo tumeona Israel walivunja sheria ya Mungu na agano lao kuwa

hawatoivunja. Na Musa aliposhuka kutoka katika mlima, akiwa katika

mkono wake mbao za Sheria, walizoahidi kuwa hawatozivunja,

alipoona walichokifanya “akazitupa zile mbao mikononi mwake,

akazivunja chini ya mlima” (Kutoka 32:19)

“Ikiwakilisha kuwa walikuwa wamevunja agano lao na Mungu, hivyo

Mungu amevunja agano lake na wao” (Ellen White, Wazee na manabii

uk, 320)

Hivyo wakajikuta hawana la kufanya na wasio na msaada, wakiwa

wamechoka. Kwa maana “Hawakuwa na tumaini tena kuwa katika

upendeleo wa Mungu kwa kupitia agano, ambalo wamelivunja SASA

kwa kuona dhambi yao na haja yao kwa kusamehewa, walipelekwa

kuona hitaji lao la kuwa na mwokozi aliyefunuliwa katika agano la

Ibrahimu aliyekivuli katika kafara. SASA kwa imani na upendo

walimshikilia Mungu kama ndiye mkombozi kutoka katika vifungo vya

dhambi. SASA walikuwa katika hali kukubali baraka zilizokuwa katika

AGANO JIPYA” (uk. 372)

Hivyo agano la Sinai lilileta Agano la Ibrahimu. Agano la kwanza

lilileta la agano la pili. Agano la kale lilileta agano jipya. Hivyo sheria

ambayo ndio msingi wa agano hilo—sheria iliyovunjwa—ilikuwa ni

kiongozi kuwaleta kwa kristo ili wahesabiwe haki kwa imani.

Page 42: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

42

Page 43: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

43

8. TOFAUTI YA MAAGANO

Wagalatia 4

21 Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22

Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa

mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa

mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;

kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo

kwa utumwa, ambalo ni Hajiri......... 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu

watoto wa ahadi.

Kama Ishmael alizaliwa katika mwili, bila ahadi yoyote ya Mungu,

lakini kutokana na Kutokuwa na imani na Mungu na kukosa kuamini

ahadi zake, ndivyo ilivyokuwa kuhusu agano la kwanza—agano la

sinai.

Na kama ilivyokuwa kwa Isaka alivyozaliwa kwa ahadi ya Mungu,

kwa kutegemea ahadi za Mungu, ndivyo ilivyokuwa kwa agano jipya—

agano la milele.

Agano la kwanza lilitegemea ahadi za watu, na lilitegemea kabisa

juhudi za watu. Agano la pili linategemea kabisa ahadi ya Mungu, na

linategemea katika nguvu na kazi ya Mungu.

Agano la kwanza linamtindo “Ikiwa mtafanya” hili na hili. Agano jipya

halina “ikiwa” wala mtu kufanya jambo, lakini ni kufanya katika

Bwana. Angalia jinsi yalisimama pamoja.

Agano la Kale

Kutoka 19

5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo

ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote

pia ni mali yangu, 6 nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu.

Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli. (Kutoka 19:5,6 Jeremia

7:23, 11:4)

Agano Jipya

Waebrania 8

10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile,

asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao

Page 44: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

44

nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu. 11 Nao

hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema,

Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao.

12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena.

Tuanze kusoma agano jipya, tukianza na neno “ikiwa mtafanya” n.k

“Ikiwa mtaweka sheria zangu katika akili zenu, na kuandika katika

mioyo yenu, ndipo nitakuwa Mungu wenu na mtakuwa watu wangu”

weka sheria zangu katika akili zenu na ziandike katika mioyo yenu, ili

kwamba niwe Mungu wenu na nyie muwe watu wangu”

Kama agano jipya linasomeka hivyo, ni watu wangapi wangeweza

kuwa watu wa Mungu? Na yeye angekuwa ni Mungu wa watu

wangapi?—hakuna hata mmoja; kwasababu hakuna mtu yoyote

anayeweza kuandika sheria ya Mungu katika moyo wake; hakuna mtu

anayeweza kuweka sheria ya Mungu katika akili yake. Kwa maana akili

ya asili ni uadui dhidi ya Mungu haiwezi nyenyekea sheria ya Mungu

na wala haiwezi itii.”Hakuna chochote kilichopungukiwa na nguvu ya

Mungu pekee, kupitia roho wa milele, anaweza kuweka sheria ya

Mungu katika akili ya mtu yoyote au kuandika katika moyo wake.

Lakini kufanya haya yote, ndio ambayo wana wa israel walikubali

kufanya pale Sinai, katika agano la kale. Kwa maana walikubali

kushika sheria za Mungu “kabisa” ambayo hakuna mtu anaweza

kufanya hilo kama sheria haijawekwa katika akili yake. Na kuandikwa

katika moyo wake. Walikubali kushika sheria ya Mungu “kabisa” ili

kwamba wawe watu wake na yeye awe Mungu wao. Makubaliano yao,

yalikuwa ni wazi kwamba wao wenyewe waweke sheria za Mungu

katika akili zao na kuandika katika mioyo yao wakati bado walikuwa

wanachojua ni kuzaliwa katika mwili, wakati bado walikuwa wana akili

ya asili, ambayo ni uadui dhidi ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya

Mungu na wala haiwezi kutii.

Hivyo ilikuwa ni juhudi zao wenyewe kwamba wawe wenye haki, na

kwa haki hii wajiweke kuwa ni watu wake. Na kushinda ili awe Mungu

wao.

Hivyo agano hilo lilikuwa ni la matendo, la haki kwa matendo, la

kushindania upendeleo wa Mungu kwa matendo, la wokovu kwa

matendo.

Page 45: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

45

Ilikuwa ni agano ambalo kwasababu ya matendo, zawadi haikuwa ni

kama neema, lakini ni kama deni.

Ilikuwa ni agano halikuwa na kitu kama kusahemewa dhambi; ilikuwa

ni kifungo, na kuzaliwa kwa utumwa.

Ndio maana agano hili limeletwa katika waraka huu wa wagalatia.

Wagalatia walikuwa wanatafuta haki kwa matendo, kwa juhudi zao

wenyewe. Walikuwa wanatafuta kuwa “wakamilifu katika mwili.”

Lakini mkristo yoyote akitafuta haki au kuwa mkamilifu, kwa njia hii,

ameanguka nje ya neema. Atakuwa ameiacha neema; kwasababu

Warumi 4

4 Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa

ni deni

Na,

Warumi 11

6 Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa

neema

Hii ndio ilikuwa ni nafasi na hali za “mafalisayo waliyoamini” ambao

ndio waliowafanya wagalatia waende nje ya njia. Katika mfumo wa

kuhesabiwa haki kwa matendo, na kujaribu kuwa wakamilifu katika

mwili, mafalisayo walioamini walibadili kila kitu ambacho alichowapa

kuwaokoa kutoka katika utumwa wa kujihesabia haki na matendo ya

mwili na wangeweza kuharibu kwa huo uongo kila injili ya Kristo

mwenyewe.

Kwa upande mwingine, agano jipya lote ni la neema,na la matendo ya

Mungu kwa neema.

Ni agano ambalo kazi yote ni kazi ya Mungu na haki ni haki ya Mungu.

Ni agano ambalo kila mmoja anayendani yake amezaliwa katika roho

na kila mmoja anayepokea akili mpya na Moyo mpya, katika akili hiyo

sheria ya Mungu inawekwa, na katika moyo huo sheria inaandikwa kwa

roho wa Mungu aliyehai.

Ni agano ambalo kwa nguvu ya ubunifu ya Mungu, kila mmoja

anayekubali ile ahadi anafanywa kuwa mwana na Mungu.

Page 46: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

46

Waefeso 2

10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema,

ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

Ni agano ambalo ni kwasababu ya Huruma ya Mungu, na kwa ahadi

yake, kuna kusamehewa dhambi, zote na Bure; dhambi na uovu

havitakumbukwa tena.

Ni agano ambalo kweli msamaha lazima upatikane kwaajili ya dhambi

za watu waliokuwa katika agano la kwanza. Kwamaana,

Waebrania 9

15 Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa

kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee

ahadi ya urithi wa milele.

Kumbuka tena, katika agano jipya hakujatajwa kokote kuhusu kazi ya

watu. Kazi yote ni ya Mungu

Waebrania 8

10.......... Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika

12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena.

Katika agano jipya ni Mungu pekee ndiye anayefanya kazi.

Wafilipi 2

13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda

kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema

Ni kwa kupitia “damu ya agano la milele” ndipo “Mungu wa amani”

anawafanya kuwa “wakamilifu katika kila tendo jema, mpate

kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele

zake, kwa Yesu Kristo” ambaye ndiye hakika kwa “agano lililo bora”

(Waebrania 13:20,21;7:22)

Njia pekee ya mtu kuja katika agano hili ni kwa unyenyekevu, ni lazima

wajinyenyekeze katika haki ya Mungu. (Warumi 10:3). Wamkubali

Mungu na miili yao “viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za

haki.”(Warumi 6;13)

Page 47: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

47

Hivyo yoyote ambaye yupo katika agano hili kwa namna yoyote ile,

yupo kikamilifu katika ahadi za Mungu, na kuwa “Kama isaka” mwana

wa ahadi.

Hakuna njia nyingine kuwa mshiriki wa agano jipya bila ahadi ya

Mungu kwa maana hakuna chochote katika agano ila ahadi za Mungu

zilizowazi. Hakuna njia nyingine ya kuwa mwana wa Mungu, ila kwa

kupitia ahadi ya Mungu. Ahadi iliyopokelewa kwa imani. Dhambi zetu

zimesamehewa na kutokuwa na haki kwetu kumesamehewa,

kwasababu Mungu amesema hilo, na kwa neno hilo la ahadi tunalijua.

Yoyote anayepokea na kutegemea katika ahadi za Mungu pekee ni

moja kati ya watu wa Mungu kwasababu Mungu amesema. Mungu

ndiye Mungu wake, kwasababu Mungu amesema hilo. Sheria ya

Mungu ipo katika akili yake na imeandikwa katika moyo wake,

kwasababu Mungu ameahidi kuwa ataweka katika akili yake na

kuandika katika moyo wake na yeye amejinyenyekeza mbele za Mungu

na kuacha Mungu afanye kazi. Na baada ya kujinyenyekeza katika haki

ya Mungu, anapata pumziko na ulinzi katika ahadi ya Mungu katika

Kristo, ambaye ndiye mpatanishi na hakika ya agano jipya. Na

Yohana 6

29 Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye

Agano la kale linaahadi na matendo ya watu ambao wanajua tu

kuzaliwa na mwili na akili ya mwili. Agano jipya lina ahadi na matendo

ya haki ya Mungu kwa wale wanaojua kuzaliwa kwa Roho katika ahadi

ya Mungu.

Page 48: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

48

9. NAFSI AU KRISTO?

Wagalatia 4

Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je! Hamwisikii sheria? 22 Kwa maana

imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja

kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana

kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano

mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri

ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa

anatumika pamoja na watoto. 26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye

mama yetu sisi. 27 Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti,

ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa

huyo aliye na mume. 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. 29 Lakini

kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho,

ndivyo ilivyo na sasa. 30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa

maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. 31

Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye

mwungwana.

Agano la kwanza lilitegemea ahadi za watu, ambao walikuwa wanajua

tu kuzaliwa katika mwili. Na ahadi hiyo ilikuwa ni kutunza amri kumi

za Mungu kikamilifu. Lakini kwa vile walikuwa wanajua tu kuzaliwa

katika mwili, katika muda huo walikuwa ni wavunjifu wa sheria ya

Mungu, na hivyo walikuwa katika kifungo cha dhambi. Na kwakujua

tu kuzaliwa kwa mwili na kwa kuwa tu na akili ya mwilini, ahadi yao

ya kushika sheria ya Mungu kikamilifu ilikuwa haina maana,

kwasababu

Warumi 8

7 ........nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu,

wala haiwezi kuitii”

Hata kama wasingeahidi chochote kuhusu kuitii sheria ya Mungu, bado

wangeivunja, kwasababu walikuwa wanajua tu kuzaliwa kwa mwili,

“na walio mwilini hawawezi kumpendeza Mungu”. Hivyo, bila ahadi

yoyote kushika sheria ya Mungu, bila kuzaliwa upya, wangeendelea

kuwa katika utumwa wa dhambi. Na walipoahidi kushika sheria, na

kisha wakavunja ahadi yao (ambayo, kwa kuwa na akili ya mwilini

ilikuwa ni lazima kuwa wangefanya hivyo), hili liliwafanya waingie

katika utumwa wenye kina kikubwa, kwasababu

Page 49: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

49

Kumbukumbu 23

21 Utakapoweka nadhiri kwa Bwana, Mungu wako, usiwe mlegevu katika

kuiondoa; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi

itakuwa dhambi kwako

Hivyo, agano hilo lililetwa na watu ambao walikuwa tayari wapo katika

utumwa, na ni agano ambalo, kwa jinsi lilivyo, lilizaa utumwa, lilikuwa

ni agano la utumwa—agano ambalo linategemea juhudi zao kujitoa

katika utumwa ambao tayari wamo, liliwafanya wawe katika utumwa

mkubwa zaidi, utumwa wa dhambi, utumwa wa matendo yao wenyewe

na ahadi zilizovunjika, ambazo ni dhambi tu.

Yote yaliyoonekana au yangeonekana, katika agano la kwanza ilikuwa

ni kuvunjwa kwa sheria. Na hii itakuwa ni wazi milele kiasi cha

kwamba hakuna ambaye atashindwa kuona pale Musa aliposhuka

kutoka katika mlima na akaona sanamu zao, japokuwa alikuwa na mbao

za mawe zenye sheria ya Mungu,

Kutoka 32

19 .......... akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima.

Wao ndio waliokuwa wa kwanza kuvunja sheria. Waliahidi kutovunja

sheria. Lakini sasa walivunja vyote sheria na ahadi yao ya kutovunja

sheria. Na kwa hiyo, kwasababu hii, Musa alizitupa zile mbao za mawe

zenye sheria ya Mungu na kuzivunja, hii ni ili kuwapa watu wote somo

milele lenye mfano, kwamba katika agano la kwanza, katika juhudi zote

za kujihesabia haki, na katika ahadi zao zote za kutovunja sheria ya

Mungu, hakuna mtu yoyote anayeweza kuona chochote isipokuwa

KUVUNJWA KWA SHERIA.

Lakini lilikuwepo na hata sasa lipo agano la Ibrahimu, agano la imani,

agano la milele la Mungu, kuwaokoa kutoka katika vifungo vya

dhambi, ambao juu yao kwasababu ya agano la matendo, la kutokuwa

na imani,ambalo walikuwa wameingia, “Hawa kuwa na tumaini lolote

la upendeleo wa Mungu kupitia agano ambalo walikuwa

wamelivunja”—kupitia agano ambalo hakuna chochote kinachoweza

kuonekana isipokuwa sheria iliyovunjwa. “sasa kwa kuona dhambi yao

na haja yao ya kusamehewa, walipelekwa kuona hitaji lao la kuwa na

Page 50: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

50

mwokozi aliyefunuliwa katika agano la Ibrahimu aliyekivuli katika

kafara”

Ilikuwa ni agano kupitia Ibrahimu, Isaka na Yakobo ambalo Musa

alimsihi Mungu, rehema kwa watu waliokuwa wanaabudu sanamu ya

dhahabu ya ndama chini ya mlima, wakati bado akiwa mlimani, kabla

bado hajashuka kwa mara ya kwanza. Angalizo: Kutoka 32:1-6

imeonesha watu wakiwa wanatengeneza ndama wa dhahabu na

kumuabudu, katika mstari wa saba,

Kutoka 32

7 Bwana akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa

katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao, 8 wamepotoka upesi kuiacha ile njia

niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea

dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya

Misri. 9 Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama,

ni watu wenye shingo ngumu 10 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao,

niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.

Kutoka 32

11 Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira

zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu,

na kwa mkono wenye nguvu? 12 Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa

kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso

wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu

wako. 13 Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao

uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota

za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi

milele. 14 Na Bwana akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu

wake.

Hili lilikuwa ni agano la Ibrahimu, agano la milele la Mungu ndilo

lililowaokoa watu kutoka katika vifungo na laana ya dhambi zao, katika

agano la kwanza. Na ndivyo ilivyokuwa. (Waebrania 9:15)

Ndipo aliposhuka kutoka mlimani, akiwa na mbao za sheria ya Mungu

katika mikono yake, na akazitupa zile mbao za sheria ya Mungu, na

akazivunja,

“Ikiwakilisha kuwa walikuwa wamevunja agano lao na Mungu, hivyo

Mungu amevunja agano lake na wao,” na inawakilisha kuwa katika

agano hilo hakuna chochote isipokuwa sheria iliyovunjwa, na kwamba

Page 51: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

51

“Hawa kuwa na tumaini lolote la upendeleo wa Mungu kupitia agano

ambalo walikuwa wamelivunja” na “sasa kwa kuona dhambi yao na

haja yao kwa kusamehewa, walipelekwa kuona hitaji lao la kuwa na

mwokozi aliyefunuliwa katika agano la Ibrahimu aliyekivuli katika

kafara. Sasa kwa imani na upendo walimshikilia Mungu kama ndiye

mkombozi kutoka katika vifungo vya dhambi. Sasa walikuwa katika

hali kukubali baraka zilizokuwa katika agano jipya” (Wazee na manabii

p.373).

Hivyo agano la Sinai liliwaleta katika agano la Ibrahimu. Agano la

kwanza liliwaletea la pili. Agano la kale liliwaletea agano jipya. Na sasa

sheria ambayo ndio msingi wa agano—sheria iliyovunjwa—ilikuwa ni

kiongozi kuwa leta kwa Kristo, ili wahesabiwe haki kwa imani.

Ndipo,

Kutoka 34

1 Kisha Bwana akamwambia Musa, Chonga mbao mbili za mawe mfano wa zile

za kwanza; nami nitaandika juu ya mbao hizo maneno hayo yaliyokuwa juu ya

mbao za kwanza, hizo ulizozivunja

Na Musa akasema,

Kumbukumbu 10

3 Basi nikafanya sanduku la mti wa mshita, nikachonga mbao mbili za mawe mfano

wa zile za kwanza, nikakwea mle mlimani, na zile mbao mbili mkononi mwangu.

4 Naye akaandika juu ya mbao mfano wa maandiko ya kwanza, zile amri kumi,

alizowaambia Bwana huko mlimani toka kati ya moto siku ya mkutano; Bwana

akanipa. 5 Basi nikageuka nikashuka kutoka mlimani, nikazitia mbao ndani ya

sanduku nililofanya; nazo zimo humo kama alivyoniamuru Bwana.

Na kukaanzishwa kati ya watu huduma ya Hekalu, na mwokozi akiwa

ni kivuli cha “kafara” na Kristo “mjumbe wa agano jipya” na

mpatanishi pekee kati ya Mungu na mwanadamu” akiwakilishwa na

kuhani mkuu katika huduma ya Hekaluni. Katika hekalu hilo walileta

kwa imani na unyenyekevu sadaka zao na kutubu dhambi zao. Damu

ya sadaka zao ilichukuliwa na kuhani mkuu katika hekalu, na

upatanisho ulifanyika kwaajili yao, na dhambi ilisamehewa. Katika

sikukuu ya upatanisho damu ya kafara kwa watu wote ilinyunyuziwa

Page 52: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

52

katika kiti cha rehema na mbele ya kiti cha rehema, kilichokuwa juu ya

sanduku , juu ya zile mbao za mawe.

Hivyo kati ya mdhambi na sheria kulikuwa na kafara, ikiwakilisha

Kristo, ( na ambaye kwa imani alikuwa ni Kristo, hakika ya agano

lililobora), ambaye kwa yeye alimletea mdhambi msamaha wa dhambi,

na haki ya Mungu, ambayo inatosheleza matakwa yote ya sheria. Na

hivyo kupitia imani kwa Kristo, katika agano hili ambalo Kristo

alikuwa ni mpatanishi, na ambaye yeye ni hakika, kinachoonekana ni

sheria isiyokuwa imevunjwa.

Hivyo ndio jinsi na ndivyo ilivyo maana halisi ya utaratibu mpya pale

sinai, baada ya kuvunja mbao za mawe, na baada ya kuliacha kabisa

agano la kwanza. Ilikuwa ni kupitia imani, kupitia haki ya Mungu

iliyokatika imani ya Yesu Kristo kwa wote wanaoamii (Warumi 3:22)

Lakini tazama katika kutoamini kwao, baadaye Israel waligeukia

mfumo wa matendo, kama ilivyokuwa katika agano la kwanza. Na

kafara na sadaka, na ibada iliyokuwa inaambatana nazo, zilitolewa na

Mungu iwe kielelezo cha imani. Lakini Israel katika kukosa kwao

imani, walipoteza yote haya, na wakafanya kuwa mfumo wa matendo,

na wakimatambiko. Badala ya haki kuja kupitia imani, na sadaka na

kafara kuwa kama kielelezo cha imani, walitegemea haki kupitia kafara

yenyewe, na kwa matendo yao mema kwa kutoa kafara.

Ndivyo ilikuwa kipindi cha Yesu hapa duniani, na kipindi cha Paulo na

wagalatia. Ndivyo ilivyokuwa kwa “mafalisayo walioamini”

(Mafalisayo waliodai kuamini injili) waliowachanganya wagalatia na

kuwaendesha kurudi nyuma kutoka haki kwa imani kwenda kwenye

haki kwa matendo na matambiko. Na hivyo Paulo angeandika na

aliandika,

Wagalatia 4

Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa

mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa

mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano;

kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo

kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 4.25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko

Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na

watoto.

Page 53: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

53

Hivyo njia ambayo Mungu aliitoa kuwaokoa kutoka katika utumwa wa

agano la kale, kwasababu ya kutoamini kwao, waligeukia mfumo wa

utumwa, uliokuwa unafanana kabisa na utumwa wa agano la Kale.

Waliharibu agano jipya kama jinsi ilivyokuwa limeelezwa kwenda

katika kanuni za agano la kale—haki kwa matendo. Kile ambacho injili

imeleezea kupitia kafara, sadaka na huduma ya kipindi hicho,

walibadili kuwa utumwa wa haki kwa matendo na matambiko, vile vile

kama ilivyokuwa “mafalisayo walioamini” walikuwa wanabadilisha

injili iliyokuwa inaelezwa kupitia kafara na huduma ya Kristo

mwenyewe.

Na kama jinsi Hajiri na Ishmael walivyofukuzwa, ili kwamba agano la

Mungu pamoja na Ibrahimu lifurahiwe kikamilifu, na kama jinsi

lilivyowekwa pembeni na kutupwa ili kwamba baraka za agano la

Ibrahimu, agano jipya, ziweze kufurahiwa, Kristo alipokuja kwa

kupitia sadaka na kafara yake mwenyewe, na kwa huduma yake

mwenyewe alileta ukamilifu wa injili—ilikwamba hili liweze

kufurahiwa kikamilifu, lazima mfumo wa ibada na matambiko uwekwe

pembeni, mfumo wa haki kwa matendo ambao Israeli walibadilisha

ambao hapo awali ulikuwa ni kielelezo cha injili ya kweli, wa haki kwa

imani. “Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na

watoto.”.......... “Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na

mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na

mwana wa mwungwana” “Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana,

naye ndiye mama yetu sisi.”........... “Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi

tu watoto wa ahadi”

Na ndipo kanuni za matambiko ziliachwa milele—kanuni ambazo

zilikuwa ni utumwa wa haki kwa matendo katika mtindo wowote ule

utakaojidhihirisha, na kukaanzishwa katika nafasi yake kanuni za

kimbingu za uhuru, katika haki kwa imani.

Wagalatia 5

1 Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe

tena chini ya kongwa la utumwa.

Agano la kale, agano la sinai, linaweza kuhitimishwa kwa neno

“NAFSI.” Agano jipya, agano la milele, linaweza kuhitimishwa kwa

neno “KRISTO”

Page 54: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

54

Agano la kale ni nafsi na haki yake. Agano jipya ni Kristo na haki ya

Mungu. Agano la kale ni nafsi na utumwa wa dhambi na matendo ya

sheria. Agano jipya ni Kristo na uhuru wa haki, ambao ni imani.

Agano la kale—nafsi—lazima ziachwe na liwekwe pembeni, ili

kwamba agano jipya—Kristo—awezekuchukua nafasi yake na

kudhihirisha nguvu yake ya wokovu, kwa maana mwana wa mjakazi

hawezi kuwa mrithi pamoja na mwana wa mungwana.

Page 55: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

55

UFUPI WA SOMO LINALOFATA.

Nimeona niweke na sura hii inayofata katika kitabu hiki ilikutoa

maelezo ya kina zaidi kuhusu agano jipya kutoka kwa E.J.Waggoner.

Sura hii ni sura ya mwisho kwenye kitabu chake cha Agano la milele

(Everlasting Covenant). Katika sura hii waggoner anajaribu kutanua

uelewa wetu kuhusu agano jipya kwa kueleza kuwa, agano la sinai sio

tu lilikuwa ni agano la kwanza kuthibitishwa kwa damu, na Agano la

Ibrahimu japokuwa lilikuwa la kwanza kuanzishwa likawa agano la pili

kwasababu lilikuwa linasubiri damu ya Yesu pale msalabani, lakini pia

Agano la sinai ndio pia lilikuwa ni agano la kwanza kufanywa na

nyumba yote ya Israeli.

Waggoner anaamini kuwa kama jinsi Mungu alivyokusanya Israeli ya

kale ndivyo atakavyokusanya Israeli ijayo. Mungu atakusanya watu

wake ambao ndio Israeli kama jinsi ilivyoelezwa katika ufunuo wa

yohana sura ya 7. Na baada ya kuwakusanya watu wake ambao ndio

taifa lake Israeli katika siku ya ufufuo na pale ambapo waovu

watakapoangamizwa, Katika siku ambayo Mungu atafanya kila kitu

kipya, ndipo Mungu atafanya agano na Israeli, taifa lake, taifa la wote

waliomkubali Kristo kama ni Bwana wao, agano Jipya. Waggoner

anaamini kuwa agano jipya bado halijafanywa kwa maana bado Israeli

ijayo haijakusanywa pamoja kama taifa, lakini agano la Ibrahimu halina

tofauti na agano jipya kwa maana halina chochote zaidi ya agano jipya.

Hivyo japokuwa agano jipya halijafanywa bado katika uhalisia wake,

yoyote aliyekatika agano la Ibrahimu, ni kama yupo katika agano jipya,

kwa maana atakuwa miongoni wa watu ambao Mungu atafanya nao

agano jipya. Kwa maelezo zaidi endelea kusoma Sura inayofata.

Page 56: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

56

KUKAMILIKA KWA AGANO LA MILELE

Na,

E.J.WAGGONER

Matendo 15

18 Asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele

Matendo 3

20 bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na

uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu. 21 Kwa maana tangu

zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji

husomwa kila sabato katika masinagogi

Matendo 10

43 Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila

amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.

Kazi ya mwisho ya kukusanya watu wa Mungu na kusimama kwao

katika dunia mpya, imekuwa ndio somo la manabii tokea anguko na

wote wamekuwa mashahidi kuwa wote walio ndani ya Kristo watapata

ondoleo la dhambi, kwa vile ni kwa kupitia tu ondoleo la dhambi ndipo

kukusanywa na marejesho yanaweza kufanyika. Tuangalie vitu

vichache katika unabii unaozungumzia vitu hivi, na vitasimama kama

viwakilishi kwa vitu vingine. Tuangalie kwanza sura ya kumi na moja

ya kitabu cha Isaya

Isaya 11

1 Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka

katika mizizi yake litazaa matunda. 2 Na roho ya Bwana atakaa juu

yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya

maarifa na ya kumcha Bwana; 3 na furaha yake itakuwa katika

kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa

Page 57: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

57

macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio

yake; 4 bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya

wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya

kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya. 5 Na

haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia.

(Linganisha na 2Thess.2:8)

6 Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala

pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono

watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. 7 Ng'ombe na dubu

watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula

majani kama ng'ombe. 8 Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la

nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira.

9 Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote

mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji

yanavyoifunika bahari.

Hapa tunamchanganuo wa historia ya injili, ikiwamo na kuondolewa

kwa dhambi na wadhambi na kusimamishwa kwa watakatifu katika

dunia iliyoumbwa upya, wakati ambapo “wenye upole watairithi nchi,

Watajifurahisha kwa wingi wa amani” (Zaburi 37:11)

Kama vile alivyotupa simulizi, ambayo tayari tumekwisha isoma, nabii

anaendelea mbele kutupa ujumbe zaidi. Tukirudi pale alipoanzia,

anaendelea—

Isaya 11

10 Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara

kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na

mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu. 11 Na itakuwa katika

siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu

wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka

Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na

kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari. 12 Naye atawatwekea

mataifa bendera, atawakutanisha watu wa Israeli waliotupwa,

atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyika, kutoka ncha nne za

dunia.

Page 58: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

58

Kwa kuwakusanya watakatifu kutoka pande nne za dunia, tunasoma pia

katika Mathayo 24:31. Nguvu ambayo itakayotumika kukusanya huku

itakuwa ni sawa na ile ambayo Bwana aliitumia kukusanya katika

mkono watu wake kwa mara ya kwanza, Tunasoma:

Isaya 11

16 Itakuwako njia kuu kwa mabaki ya watu wake watakaobaki,

watokao Ashuru, kama vile ilivyokuwako kwa Israeli, katika siku ile

waliyotoka katika nchi ya Misri

Kuhusu kukusanya, mwanzo na mwisho tunasoma pia katika sura ya

arobaini ya isaya. Kuhubiri injili inahusu pia kusamehewa dhambi,

kumtoa msaidizi, Roho mtakatifu, kumuweka Mungu kama ndio nguvu

pekee katika ulimwengu, Muumbaji na mtetezi, na kutangaza kuhusu

ujio wa Bwana katika utukufu, yote yanapatiana humo. Hivyo ujumbe

ni

Isaya 40

10 Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake

ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na ijara

yake i mbele zake. 11 Atalilisha kundi lake kama mchungaji,

Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani

mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.

Hapo mwanzo tulisoma kuhusu kukusanya kondoo waliopotea wa

nyumba ya Israeli katika zizi moja ili kuwe na “Zizi moja na Mchungaji

mmoja” hapa tunaona kukusanya kunaanza na kuhubiri injili, na

inakamilika pale ambapo Bwana anakuja katika utukufu, akiwa na

malaika zake, na zaidi ni kwamba nguvu na utukufu ya ujio wa Bwana

ni sawa nguvu iliyopo katika kuhubiri injili.

Katika mistari inayofata tunasoma hali ya kondoo waliopotea wa

nyumba ya israel, na jinsi wachungaji wasiokuwa waaminifu

walivyowatawanya badala ya kuwakusanya—

Ezekieli 34

2 Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli, toa unabii,

uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole

wao wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasi

Page 59: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

59

wachungaji kuwalisha kondoo? 3 Mnawala walionona, mnajivika

manyoya, mnawachinja walionona; lakini hamwalishi kondoo. 4

Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi,

wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha

waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na

kwa ukali mmewatawala. 5 Nao wakatawanyika, kwa sababu

hapakuwa na mchungaji; wakawa chakula cha wanyama- mwitu,

wakatawanyika. 6 Kondoo zangu walitanga-tanga katika milima yote,

na juu ya kila kilima kirefu; naam, kondoo zangu walitawanyika juu ya

uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu aliyewaulizia, wala

kuwatafuta. 7 Basi, enyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana; 8 Kama

mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, kwa sababu kondoo zangu

walikuwa mateka, kondoo zangu wakawa chakula cha wanyama-mwitu

wote, kwa sababu hapakuwa na mchungaji, wala wachungaji wangu

hawakutafuta kondoo zangu, bali wachungaji walijilisha wenyewe

wala hawakuwalisha kondoo zangu; 9 kwa sababu hiyo, enyi

wachungaji, lisikieni neno la Bwana; 10 Bwana MUNGU asema hivi;

Tazama, mimi ni juu ya wachungaji; nami nitawataka kondoo zangu

mikononi mwao, nami nitawaachisha hiyo kazi ya kuwalisha kondoo;

nao wachungaji hawatajilisha wenyewe tena; nami nitawaokoa kondoo

zangu vinywani mwao, wasiwe tena chakula chao. 11 Maana, Bwana

MUNGU asema hivi; Tazama, mimi mwenyewe, naam, mimi,

nitawatafuta kondoo zangu, na kuwaulizia. 12 Kama vile mchungaji

atafutavyo kondoo zake, siku ile anapokuwa kati ya kondoo zake

waliotawanyika; ndivyo nitakavyowatafuta kondoo zangu; nami

nitawaokoa katika mahali pote walipotawanyika, katika siku ya

mawingu na giza. 13 Nami nitawatoa katika watu wa mataifa, na

kuwakusanya katika nchi zote, nami nitawarudisha katika nchi yao

wenyewe; nami nitawalisha juu ya milima ya Israeli, kando ya mifereji

ya maji; na katika mahali pote pa nchi panapokaliwa na watu.

“23 Nami nitaweka mchungaji mmoja juu yao, naye atawalisha, naam,

mtumishi wangu, Daudi; yeye atawalisha, naye atakuwa mchungaji

wao. 24 Na mimi, Bwana, nitakuwa Mungu wao, na mtumishi wangu,

Daudi, atakuwa mkuu kati yao; mimi, Bwana, nimesema haya. 25 Nami

nitafanya agano la amani nao, nami nitawakomesha wanyama wakali

kati yao; nao watakaa salama jangwani, na kulala misituni. 26 Nami

Page 60: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

60

nitawafanya wao, na mahali palipo pande zote za mlima wangu, kuwa

baraka, nami nitaleta manyunyu kwa wakati wake; yatakuwako

manyunyu ya baraka. 27 Na mti wa kondeni utazaa matunda yake,

nayo ardhi itatoa mazao yake, nao watakuwa salama katika nchi yao;

nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapovunja vifungo vya

kongwa lao, na kuwaokoa katika mikono ya watu wale

waliowatumikisha. 28 Hawatakuwa mateka ya makafiri tena, wala

mnyama wa nchi hatawala; bali watakaa salama salimini, wala hapana

mtu atakayewatia hofu.

Jinsi kazi ya kukusanya itakavyofanyika tunaambiwa vizuri katika sura

ya 37

Ezekieli 37

1 Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika

roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa

mifupa; 2 akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa

na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu

sana. 3 Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami

nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe. 4 Akaniambia tena, Toa

unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno

la Bwana. 5 Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya;

Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. 6 Nami nitatia

mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika

ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa

mimi ndimi Bwana. 7 Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata

nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama,

tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa

mwenziwe. 8 Nikatazama, kumbe! Kulikuwa na mishipa juu yake,

nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika juu yake; lakini haikuwamo

pumzi ndani yake. 9 Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo,

mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo,

kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa,

wapate kuishi. 10 Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi

ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno.

11 Kisha akaniambia, Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya

Israeli; tazama, wao husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini yetu

Page 61: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

61

yametupotea; tumekatiliwa mbali kabisa. 12 Basi tabiri, uwaambie,

Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi yenu, na

kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami

nitawaingizeni katika nchi ya Israeli. 13 Nanyi mtajua ya kuwa mimi

ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa ninyi

katika makaburi yenu, enyi watu wangu. 14 Nami nitatia roho yangu

ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi

mtajua ya kuwa mimi, Bwana, nimesema hayo, na kuyatimiza, asema

Bwana.

Hivyo tunaona kuwa ahadi ya Bwana kwa Daudi ni kwamba ataandaa

mahali kwaajili ya watu wake Israeli, na kuwaweka ili kwamba wakae

katika sehemu zao wenyewe na wasiondoke tena na wasiteseke tena

(2sam.7:10), litatimia katika ufufuo wa wafu. Kukusanya Israeli, watu

pekee walioahidiwa, inajumuisha watu wote wa zama zote, kwa maana

Bwana anaponena, “Wote walio katika makaburi watasikia sauti yake

na kutoka”

Tunaona kuwa kukusanya huku ni kwa “nyumba nzima ya Israeli”

mstari unaofuata unaonesha kuwa katika muda huo hakutakuwa na

mgawanyo wa falme, bali “zizi moja na mchungaji mmoja”

Ezekieli 37

15 Neno la Bwana likanijia tena, kusema, 16 Na wewe mwanadamu,

twaa kijiti kimoja; ukaandike juu yake, Kwa Yuda, na kwa wana wa

Israeli wenzake; kisha, twaa kijiti cha pili; ukaandike juu yake, Kwa

Yusufu, kijiti cha Efraimu, na kwa nyumba yote ya Israeli wenzake; 17

ukaviunge pamoja kwa ajili yako hiki na hiki viwe kijiti kimoja, viwe

kimoja katika mkono wako. 18 Na wana wa watu wangu

watakapokuambia, wakisema, Je! Hutatuonyesha maana ya mambo

hayo utendayo? 19 Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama,

nitakitwaa kijiti cha Yusufu, kilicho mkononi mwa Efraimu, na kabila

za Israeli wenzake, nami nitawaweka pamoja nacho, yaani, pamoja na

kijiti cha Yuda, na kuvifanya kuwa kijiti kimoja; navyo vitakuwa kimoja

mkononi mwangu. 20 Navyo vijiti, ambavyo uliandika juu yake,

vitakuwa mkononi mwako mbele ya macho yao. 21 Ukawaambie,

Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitawatwaa wana wa Israeli toka

kati ya mataifa walikokwenda, nami nitawakusanya pande zote, na

Page 62: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

62

kuwaleta katika nchi yao wenyewe; 22 nami nitawafanya kuwa taifa

moja katika nchi hiyo, juu ya milima ya Israeli; na mfalme mmoja

atakuwa mfalme wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa mawili,

wala hawatagawanyikana kuwa falme mbili tena, hata milele. 23 Wala

hawatajitia uchafu tena kwa vinyago vyao, wala kwa vitu vyao

vichukizavyo, wala kwa makosa yao mojawapo; lakini nitawaokoa, na

kuwatoa katika makao yao yote, ambayo wamefanya dhambi ndani

yake, nami nitawatakasa; basi watakuwa watu wangu, nami nitakuwa

Mungu wao. 24 Na mtumishi wangu, Daudi, atakuwa mfalme juu yao,

nao wote watakuwa na mchungaji mmoja; nao wataenenda katika

hukumu zangu, na kuzishika amri zangu, na kuzitenda. 25 Nao watakaa

katika nchi niliyompa Yakobo, mtumishi wangu, walimokaa baba zenu;

nao watakaa humo, wao na watoto wao, na watoto wa watoto wao,

milele; na Daudi, mtumishi wangu, atakuwa mkuu wao milele.

Sasa angalia kile kinachofuata

26 Tena nitafanya agano la amani pamoja nao; litakuwa agano la

milele pamoja nao; nami nitawaweka na kuwazidisha, na patakatifu

pangu nitapaweka katikati yao milele. 27 Tena maskani yangu itakuwa

pamoja nao; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

28 Na mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, mimi niwatakasaye

Israeli, patakatifu pangu patakapokuwa katikati yao milele

Ni pale ambapo mji mtakatifu utakaposhuka kutoka kwa Mungu kutoka

mbinguni, ndipo sauti ikasikika ikisema “ Maskani ya Mungu ni

pamoja na wanadamu na ataishi kati yao na Mungu mwenyewe

atakuwapamoja nao na kuwa Mungu wao” (Ufunuo 21:2,9)

..............

Katika uhusianisho huu, hatuwezi kuwa katika hali ya kusita kuwa ni

wakati gani ambao unamaanishwa hapa, ni wakati wa kuadhibiwa kwa

waovu na kupewa ujira wale waliowanyenyekevu; muda ambao watu

wa Mungu wataokolewa milele kutoka katika uovu na katika

manyanyaso, na kusimamishwa katika nchi, na kuitawala katika zama

zote katika amani na katika haki. Wakati tukiongelea kuhusu muda huo,

unabii unaendelea,

Page 63: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

63

Yeremia 31

Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na

nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. 32 Si kwa mfano wa agano lile

nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili

kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja,

ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana. 33 Bali agano hili ndilo

nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana;

Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami

nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 34 Wala

hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake,

wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye

mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema

Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka

tena. 35 Bwana asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati

wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku,

aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; Bwana wa majeshi,

ndilo jina lake; 36 Amri hizi zikiondoka, zisiwe mbele zangu, asema

Bwana, ndipo wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele zangu

milele. 37 Bwana asema hivi, Kama mbingu zikiweza kupimwa, na

misingi ya dunia ikiweza kugunduliwa huko chini, ndipo wazao wa

Israeli pia nitawatupilia mbali, kwa ajili ya hayo yote waliyoyatenda,

asema Bwana

Hili ni hitimisho la kila kitu. Kwa kufanya agano jipya, siku za

uhamishoni na mateka yote yameisha, na watu wa Mungu wanaishi

katika uwepo wake usioisha milele. Agano hilo linasubiri lifanywe,

lakini kwa imani iliyohai baraka zake zinafurahiwa hata sasa, hata

nguvu ya ufufuo, ambayo katika hiyo watu wa Mungu

watasimamishwa katika nchi yao, ni nguvu ambayo iliwaandaa kwaajili

ya siku hiyo yenye utukufu.

Katika somo hili la ahadi kwa Israeli tumeona kwanini na kwa

mazingira yapi agano la kale lilifanywa, pale Israeli waliposimama

chini ya Mlima sinai.Hili linaitwa agano la “kwanza” au “agano la

kale”, sio kwamba kulikuwa hakuna agano kabla yake, lakini ni

kwasababu lilikuwa ni agano la kwanza “lililofanywa na nyumba ya

Israeli na nyumba ya yuda”—Lilifanywa na nyumba yote ya Israeli.

Page 64: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

64

Agano la Ibrahimu lilikuwepo zaidi ya miaka mia nne kabla, na

lilikuwa na kila kitu ambacho Mungu angeweza kumpa mtu. Ni kwa

kupitia hilo agano la Ibrahimu, lililothibitishwa na kiapo cha Mungu,

ndipo sasa tunakuja kwa kujiamini katika kiti cha rehema na kupata

upatanisho wa makosa yetu (Waebrania 6:13-20). Watu wote wenye

imani ni watoto wa Ibrahimu.

Lakini Israeli ya kale walikuwa sio waaminifu na walisahau au

walipuuzia agano la milele lilifanywa na Ibrahimu. Walitaka kutembea

kwa kuona na sio kwa imani. Walijiamini wao wenyewe badala ya

Mungu. Na katika jaribio, ambapo Mungu aliwakumbusha agano lake

na Ibrahimu kama msaada ili waamini katika nguvu ya ahadi yake,

aliwakumbusha yale ambayo alikwisha kuwafanyia lakini walichukua

jukumu kuhusu wokovu wao wenyewe, na wakaingia katika agano

ambalo halikuwa lingine lolote ila utumwa na kifo kikifuata. Mungu

ambaye ni mwaminifu, japokuwa wanadamu hawamuamini, alitumia

hili kama mfano wa kijifunzia. Katika kivuli wajifunze uhalisia, hata

utumwa wao ulikuwa na unabii na ahadi ya uhuru.

Mungu hawezi kuwaacha watu wake sehemu ambayo ujinga wao ndio

uliowapeleka. Hivyo akaahidi agano jipya. Sio kwamba kuna kitu

chochote kinacho pungua katika agano alilofanya na Ibrahimu, lakini

kwamba afanye agano hilo hilo na nyumba yote ya Israeli, kama taifa.

Hii ahadi ya agano jipya bado inauzuri, kwa maana kwa kiapo cha

Mungu na kwa kafara yake Yesu alifanywa kuwa ni “uhakika wa agano

bora” Angalia neno “hakika.” Wanadamu hawahitaji kuwa na uhakika

wa vitu ambavyo tayari wanavimiliki. Kwa vile kristo ni “Hakika ya

agano bora” inaonesha kuwa agano hilo litakuja. Sisi ni watoto wa

Mungu kwa imani katika Kristo Yesu, na kama niwa kristo, hivyo sisi

ni mzao wa Ibrahimu, na warithi wa ahadi. Tunaenda kwa Yesu

kwasababu ya agano alilofanya na Ibrahimu. Hilo ndio tegemeo letu

kubwa la kukimbilia kwa Yesu kwaajili ya hifadhi. Hakuna mtu

“aliyekatika agano jipya”, kwa maana hilo bado halijafanywa, lakini

kila mtu anayetunza agano la Mungu na Ibrahimu atakuwa miongoni

mwa hao ambao agano litafanywa. Kwa yoyote ambaye atakuwa

mkristo kama Ibrahimu alivyokuwa, atakuwa na uhakika kuwepo

katika agano jipya kama vile tayari amefufuliwa kutoka katika wafu,

Israeli yote itakusanywa na agano jipya, agano la milele litafanywa

Page 65: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

65

pamoja nao—taifa takatifu linaloshika ukweli. Agano halitafanywa na

mwingine yoyote isipokuwa Israeli, lakini mtu yoyote asiachwe, yoyote

anayetaka anaweza kuja.

Pale ambapo agano la kwanza lilipofanywa na Israeli. Mungu alikuja

na malaika zake wote; na tarumbeta za Mungu zilipigwa, na sauti yake

ilitikisa dunia wakati Sheria inatamkwa. Hivyo agano Jipya

litakapofanywa, Israeli yote itakuwepo—hakutakuwa na yoyote

ambaye hatakusanywa—na “Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza”

(zaburi 50:3) “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka

mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda

ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza”( 1Thess

4:16) katika utukufu wa Baba yake “pamoja na malaika zake”

(Mathayo 24:27) Sauti yake itaitikisa dunia lakini katika muda huu

hautaitikisa Dunia pekee lakini hata Mbingu pia. Kwa hiyo, ulimwengu

mzima utahusika, na Israeli itaungana na “familia yote ya Mbinguni”

kwa msalaba wa Yesu, “Damu ya agano la milele” kwa hii, kiti cha

ufalme cha Mungu kimethibitishwa, na kile kilichowaokoa waliopotea

wa duniani ndio kinga ya milele ya viumbe ambao hakuanguka. Wakati

agano la kwanza linafanywa na Israeli, sheria ilitangazwa. “Sheria ya

kutisha” ilikuwa mbele yao.Hivyo wakati Mungu anakuja na malaika

zake wote, kufanya agano jipya na nyumba yote ya Israeli, “mbingu

zitatangaza haki yake” (Zaburi 50:6). “Moto hutangulia mbele zake,

Nao huwateketeza watesi wake pande zote.Umeme wake uliuangaza

ulimwengu, Nchi ikaona ikatetemeka. Milima iliyeyuka kama nta

mbele za Bwana, Mbele za Bwana wa dunia yote.Mbingu zimetangaza

haki yake, Na watu wote wameuona utukufu wake.” (Zaburi 97:3-6)

Somo moja ambalo linaweza kutolewa tunapomaliza ni kwamba agano

jipya halileti chochote kipya, isipokuwa dunia mpya, na hiyo ndivyo

ilivyokuwa mwanzo. Watu ambao agano limefanywa tayari watakuwa

wamefanywa upya katika Kristo. Utawala wa kwanza utarudishwa.

Mtu yoyote asitoe kisingizio cha kutoshika amri za Mungu kwa kusema

kuwa yupo chini ya agano jipya. Kama yupo ndani ya Kristo, basi yupo

katika (sio chini) agano la Ibrahimu, na kama mtoto wa Ibrahimu, ni

mrithi pamoja na Kristo, atatumaini katika agano jipya ambalo Kristo

ni mjumbe. Yoyote ambaye hakubali kuwa yupo katika kizazi cha

Ibrahimu, Isaka, na Yakobo na katika ushirika na Musa, Daudi na

Page 66: MAAGANO MAWILI Aliyetafsiri ni, Daniel Wikama. · 2019. 8. 1. · dunia nzima —kwa ajili ya ... agano linaloitwa agano jipya au la pili ndilo lililokuwa la kwanza kufanywa na Mungu

66

manabii, hawana sehemu katika tumaini la agano Jipya. Na yoyote

anayefurahi katika ahadi za agano jipya, baraka ambazo hata sasa Roho

mtakatifu anafanya ziwe halisi, inabidi akumbuke kuwa ni kwa kupitia

agano jipya, sheria za Mungu zinawekwa katika mioyo yetu. Agano la

Kale halikumleta mtu yoyote katika kuitii sheria hiyo, lakini agano

jipya inaifanya iwe ya ulimwengu, ili kwamba dunia ijae maarifa ya

Bwana, kama jinsi maji yanavyojaza bahari.

Ndipo “Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo

Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja” (Zak.14:9). Na watu

“yatauona Yerusalemu umekuwa kao la raha; hema isiyotanga-tanga;

vigingi vyake havitang'olewa, wala kamba zake hazitakatika” (Isaya

33:20)

Agano la amani litaondoa wanyama waovu katika nchi, kwa maana

simba atakula majani kama n’gombe, na mbweha atacheza na ndama

mtoto na “nao watakaa salama jangwani, na kulala misituni” (Eze.

34:25) kwa maana “Ndipo hukumu itakaa katika jangwa, na haki itakaa

katika shamba lizaalo sana. Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao

ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima” (Isaya 32: 16-17) Na

zaidi ya yote, tutakuwa na Bwana na tutamuona uso.Hivyo sasa na

hata milele, Shukrani ziende kwa Mungu, kwa zawadi yake

isiyoelezeka. Katika yeye na kupitia yeye na kwa yeye vitu vyote

vimtukuze milele. Amen.