mradi wa maji kibamba - kisarawe: dawasa yatekeleza … · baada ya serikali kufuta lililokuwa...

24
Toleo Na. 01 www.dawasa.go.tz Tanzania Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja DAWASA YATEKELEZA AGIZO LA MHE. RAIS MAGUFULI Habari kamili Uk...4 MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE:

Upload: others

Post on 13-Aug-2020

28 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

Toleo Na. 01 www.dawasa.go.tz Tanzania

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

DAWASA YATEKELEZA AGIZO LA MHE. RAIS MAGUFULI

Habari kamili Uk...4

MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE:

Page 2: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

2 | DAWASA YETU: TOLEO NA. 01

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

Neno kutoka kwaAfisa Mtendaji Mkuu

DAWASA mpya ilizinduliwa Deptemba 8, 2018 baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake na DAWASA.

Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji yalik-wenda vizuri na bila kuwepo changamoto za kiu-tendaji kwani Menejimenti yangu, chini ya usima-mizi wa Bodi ya Wakurugenzi inayoongozwa na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange iliwekeza katika kujenga timu yenye kujiamini, yenye kuzin-gatia ubunifu, weledi na uchapa kazi.

Ni katika kipindi kifupi tu DAWASA iliweza kurekodi mafanikio mengi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa wateja kutoka wateja 289,668 iliyokuwa nao mwezi Septemba 2018 hadi wateja 308,301 tunapoelekea kufunga mwaka wa fedha 2019/20, hii ikiwa ni asilimia 88 ya upatikanaji wa maji. Lengo ni kufikia asilimia 95 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2020 kama yalivyo malengo ya Serikali na Malengo Endelevu ya Dunia (SDGs).

Kiwango cha maji yanayozalishwa kwa siku ki-meendelea kufikiwa kwa kadiri ya uwezo wa vyan-zo vya Mamlaka ambavyo ni Mitambo ya Mtoni, Ruvu Juu na Ruvu Chini pamoja na visima virefu. Hii imewezesha upatikanaji wa maji safi na sala-ma na ya kutosha katika maeneo mengi ambayo yanahudumiwa na DAWASA.

Katika kipindi hiki kifupi, kiasi cha maji yan-ayopelekwa kwa walaji kimeongezeka baada ya kutekeleza miradi midogo 119 ambayo imeweza kusogeza huduma kwa wananchi. Kupitia mira-di hii maeneo mengi kama vile Saranga, Mbezi Muhimbili, Mbezi Manyema, Mbezi Mtoni, Kwa ndambi, Kontena Mbuyuni, Baraza la Mitihani,

Goba, Mbezi Juu, Mikocheni Mabwepande, Malo-lo, Mabwe, Salasala, Kilimahewa, nk yameweza kufikiwa na kumaliza kabisa tatizo la maji katika maeneo hayo.

Mabadiliko haya yamewezesha mapato ya kila mwezi ya Mamlaka kuongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 9.3 kwa mwezi mwaka 2018 hadi kufikia wastani wa shilingi bilioni 12 kwa mwezi mwaka huu 2020.

Mamlaka pia imewekeza katika kuleta maba-diliko ya mfumo wa huduma za majitaka kwa ku-wekeza katika kukarabati mfumo mzima kuanzia katika mabwawa ya kusafisha majitaka hadi ka-tika vituo vya kusukuma majitaka sambamba na mabomba ya kukusanya na kusafirisha majitaka.

Ni katika muktadha huo basi, DAWASA il-iamua kwa makusudi kuwekeza asilimia 35 ya mapato yake katika miradi ya maendeleo ili ku-weza kuongeza wigo wa utoaji huduma ndani ya eneo lake la huduma.

Katika toleo hili la jarida la DAWASA YETU, tunawaletea habari za miradi mbalimbali inayote-kelewa katika jiji la Dar es Salaam na miji ya Mkoa wa Pwani, ambayo sasa inahudumiwa na DAWA-SA.

Ni matarajio yetu kuwa baada ya kusoma jarida hili, utafahamu mengi zaidi kuhusu DAWA-SA na zaidi utaungana na Mamlaka katika ute-kelezaji wa programu zake za maendeleo kwani mwelekeo wetu sasa ni dhahiri na matokeo cha-nya yanaonekana.

Mhandisi Cyprian LuhemejaAfisa Mtendaji Mkuu Dawasa

Page 3: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

DAWASA YETU: TOLEO NA. 01 | 3

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

TUNADIRIKI kusema ni ‘Mapambazuko ya Awamu Mpya’…’The Down of a New Era’… katika sekta ya maji Dar es Salaam na baadhi ya miji ya Mkoa wa Pwani. Kazi ambayo imefanyika katika kipindi kifupi imeandika ukurasa mpya wa mafan-ikio lukuki katika uboreshaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira ndani ya eneo la huduma la DAWASA.

Mafanikio haya ambayo tunayaeleza kwa kina ndani ya toleo hili la Jarida la “DAWASA YETU” ni sehemu tu ya kazi kubwa, ambayo inafanywa na Mamlaka ili kuboresha huduma zake kwa wanan-chi, wenye viwanda, biashara na taasisi mbalimbali zinazopata huduma kutoka DAWASA.

Mamlaka hii kubwa kuliko zote nchini Tanza-nia, inatambua umuhimu wa upatikanaji wa hudu-ma kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi hasa kwa sababu eneo lake la huduma ni Dar es Salaam ambalo ndilo jiji la kibiashara lenye kutoa mchango mkubwa katika pato la taifa.

DAWASA pia inahudumia miji ya Kibaha, Mlandizi, Bagamoyo, Mkuranga, Kisarawe na Chalinze Mkoani Pwani, ambao nao ni kitovu cha viwanda nchini.

Hivyo DAWASA inatambua mchango wake katika kulifikisha Taifa katika uchumi wa kati na ndiyo maana tangu kuanzishwa kwake, imekuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha mabadiliko yanaonekana ndani ya taasisi na zaidi kwa WA-HESHIMIWA WATEJA WETU.

Aidha, ni matarajio yetu kuwa kwa ku-soma jarida letu na kuona jitihada zilizo-

fanyika, wadau wetu wataendelea ku-unga mkono jitihada zinazoendelea.

Hivyo tunakusihi mpenzi mso-maji, usome Makala moja hadi nyingine ili uweze kuifahamu vizuri Mamalaka yako ya DA-WASA.

Neli MsuyaMkurugenzi wa

Mawasiliano na Jamii

Kazi kubwa kwa muda mfupi imeandika

ukurasa mpya wa mafanikio Dawasa

TAHARIRI

Pwani yaridhishwa na utendaji kazi wa DAWASA Uk >11

DAWASA yajivunia kuboresha huduma ya maji kwa wananchi jijini Dar Uk >13

DAWASA yakamilisha Mradi wa Majiwa Jamii Zingiziwa Uk >16

Maji Gairo: Kutoka karahahadi raha Uk >22

Jarida hili Hutolewa na DAWASASimu: 0800110064 (Bure) au *152*00#

baruapepe: [email protected]: www.dawasa.go.tz

HABARI

MAKALA

MAJI NA JAMII

MAKALA YA MGENIBODI YA UHARIRI

Mwenyekiti: Mhandisi Cyprian Luhemeja

Mhariri Mkuu:Neli MsuyaWajumbe:

Everlasting Lyaro David NkulilaJamir Bakari

Neema MbalamweziJoseph Mkonyi

Page 4: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Magu-fuli ameisifu Mamlaka ya Majisafi na Us-afi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWA-SA), kwa kutekeleza Mradi mkubwa wa Maji wa Kibamba hadi Kisarawe wenye thamani ya Sh.bilioni 10.6.

Mradi huo unaotoa huduma katika eneo la Kisarawe, una mtandao wa kilo-mita 15.65 na umejengwa kwa fedha za ndani za Mamlaka.

Akihutubia wananchi katika sherehe za uzinduzi wa mradi huo, Rais Magufuli aliipongeza Wizara ya Maji na DAWASA kwa kushughulikia changamoto mbalim-bali, ikiwemo kutatua kero ya maji kwa Watanzania na wakazi wa Jiji la Dar es

Salaam na miji ya Mkoa wa Pwani. Alise-ma kuwa mradi huo ni kielelezo tosha cha juhudi hizo.

Aidha, Rais alipongeza jitihada za ukusanyaji wa mapato na mipango mizuri ya upanuzi wa mtandao wa maji, inayoendelea kutekelezwa na DAWASA. Aliitaka Wizara ya Maji pamoja na Mene-jimenti ya DAWASA, kuboresha maslahi ya wafanyakazi wake ili waweze kupam-bana na kasi ya kusambaza huduma ya maji

Pia aliipongeza Wizara ya Maji kwa utekelezaji wa miradi ya maji nchini, am-bapo katika kipindi cha miaka mitano jumla ya miradi 1,423 imetekelezwa nchi-ni kwa gharama ya Sh.trilioni 3. Alisema

kutokana na juhudi hizo, hali ya upatika-naji wa maji nchini imeboreshwa kutoka wastani wa asilimia 47 hadi 70.1 (Vijijini) na kutoka wastani wa asilimia 74 hadi 84 (Mijini).

Ufanisi wa DAWASAAwali, Katibu Mkuu wa Wizara ya

Maji, Profesa Kitila Mkumbo alisema, DAWASA kwa sasa ndiyo Mamlaka kub-wa kuliko zote nchini kwa wingi wa maji yanayozalishwa, idadi ya wakazi inayo-hudumia na kiwango cha makusanyo kwa mwezi.

“Kwa sasa nchi nzima tuna maun-ganisho ya wateja wa mamlaka za maji 859,179, kati ya maunganisho haya,

Rais Magufuli azinduamradi mkubwa wa

maji Kisarawe, aipa heko DAWASA

Inatoka Ukurasa wa Kwanza

HABARIKUU - UTEKELEZAJI>>

4 | DAWASA YETU: TOLEO NA. 01

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

Page 5: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

maunganisho 310,000 yako Dar es Salaam na Pwani ambayo ni asilimia 35,” alisema Profesa Mkumbo.

“Kwa mwezi tunakusanya mapato Shilingi bilioni 22 na kati ya fedha hizo, DAWASA inakusanya takribani wastani wa Shilingi bilioni 10 ambazo ni sawa na asili-mia 45,” alisema.

Aliongeza pia kuwa kiasi cha maji yan-ayozalishwa nchini kwa siku ni lita milioni 835, ambapo kati ya hizo DAWASA inazal-isha lita milioni 509 (baada ya kuiunganisha na iliyokuwa Mamlaka ya Maji Chalinze ya CHALIWASA). Hii ni sawa na asilimia 56 ya maji yote yanayozalishwa kwa siku nchini. “Hivyo kwa viwango vyovyote vya ulin-ganifu, DAWASA ni Mamlaka kubwa ku-liko nyingine zote nchini” alisema Profesa Mkumbo.

Malengo kufikia 2025Akitoa taarifa ya Mamlaka, Afisa

Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema mradi huo wa Kisarawe una mtandao wa kilometa 15.65 za bomba kuu, kilometa 48 za mabomba

ya usambazaji, tanki la Maji lenye ujazo wa lita milioni 6 na pampu mbili. Alisema mradi huo umejengwa kwa gharama ya Sh.bilioni 10.6, zote zikiwa ni makusanyo ya ndani ya DAWASA.

Alisema Mradi huo umetekelezwa kwa kipindi cha miezi 14 na unawanufaisha wa-nanchi wa Kata za Kisarawe, Chang’ombe A, Chang’ombe B, Masaki, Kazimzumbwi, Masali, Kibuta, Kiluvya, Kwembe, Kisopwa na Mloganzila.

Luhemeja pia alieleza kuwa baada ya Mradi wa Kibamba – Kisarawe kukamilika, DAWASA walijiongeza na kupanua mra-di huo kwa awamu ya pili wa Kisarawe – Pugu utakaogharimu Sh.bilioni 7.3.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa tanki la maji Pugu lenye ujazo wa lita milioni 2 na ujenzi wa mtandao wa urefu wa kilomi-ta 68. Mradi huo utahudumia wananchi wa maeneo ya Pugu, Gongolamboto, Kitun-da na Ukonga, Airwing, Banana, Mongo-landege, Kinyerezi, Chanika, Mwanagati na Segerea na utawezesha kuunganisha mtandao wa maji kutoka mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini.

Mhandisi Luhemeja alisema upati-kanaji wa maji kwa jiji la Dar es Salaam wakati Rais Magufuli anaingia madarakani mwaka 2015, ulikuwa asilimia 68 lakini kwa sasa umefikia asilimia 88.

“Wakati unaingia madarakani hali ya maji haikuwa nzuri, DAWASA ilikuwa inazalisha maji lita milioni 300 kwa siku wakati mahitaji yalikuwa lita milioni 450 na huduma kwa wateja haikuwa nzuri, ku-tokana na mwingiliano wa madaraka kati ya Mamlaka na Serikali za Mitaa,” alisema Luhemeja.

“Miaka mitano baadaye Serikali ime-fanikiwa kupanua mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini na kuongeza uzalishaji kutoka lita milioni 300 hadi kufikia lita milioni 502 kwa siku,” alisema

Alisema mwaka 2015 wakati Rais Magufuli anaingia madarakani, maun-ganisho ya maji yalikuwa kwa wateja 121,000 ulioleta makusanyo ya Sh. bilioni 2.8 kwa mwezi, lakini kwa sasa maungan-isho yamefikia wateja 310,00 na mapato yamefikia Sh.bilioni 12.3 kwa takwimu za mwezi Machi 2020.

DAWASA YETU: TOLEO NA. 01 | 5

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

Page 6: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

6 | DAWASA YETU: TOLEO NA. 01

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

JUMUIYA ZA MAJI ZAJIPANGAKUKABILIANA NA MAAMBUKIZI

Kunawa mikono kwa maji safi yan-ayotiririka na sabuni ni moja kati ya njia muhimu zinazosisitizwa na Serikali katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona nchini.

Ikiwa hiyo ndiyo njia rahisi ambayo kila mtu anaweza kuimudu mbali na utumiaji wa vitakasa mikono, basi Serikali kupitia wataalamu katika sekta ya afya ilisisitiza kila nyumba na katika kila eneo la biasha-ra, kuwepo na maeneo maalum ya kuna-wa mikono.

Agizo hilo lilijumuisha ofisi zote za umma na binafsi, maduka, hospitali na vituo vya afya, katika vituo vya mabasi, pikipiki na hata teksi na katika magenge na masoko.

Ili kufika katika maeneo ya pembezoni mwa jiji, wito huo ulitolewa kwa wasi-mamizi wa visima vya umma na binafsi wenye kutoa huduma kwa jamii. Ilikuwa jambo la faraja kuona mwitikio mzuri kutoka kwa watoa huduma za maji am-bao kimsingi ndio walio katika mstari wa mbele katika vita ya kinga ya kuenea kwa virusi vya Covid 19.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) in-ahudumia Jiji la Dar es Salaam na miji ya Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kisarawe na Chalinze Mkoani Pwani. DAWASA pia ni msimamizi wa miradi ya umma ambayo inaendeshwa na jamii kupitia Jumuiya za Watumia Maji ama Kamati za Maji. Aidha inaendelea na mpango wa kusajili watoa huduma za majisafi binafsi, ambao wame-kidhi vigezo ambayo ni pamoja na kupata kibali cha matumizi ya maji ardhini kutoka Bonde la Wami Ruvu na ubora wa maji.

DAWASA imepewa mamlaka hayo kufuatiwa kupitishwa kwa sheria mpya ya Maji na Usafi wa Mazingira Namba 5 ya Mwaka 2019 (The Water Supply and San-itation Act.2019) ambayo inaipa DAWASA jukumu la kusimamia huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira (sanitation) katika Jiji la Dar es salaam.

Katika mapambano dhidi ya maam-bukizi ya ugonjwa wa Corona, watoa huduma za maji walialikwa katika ofi-si za Dawasa na kuhamasishwa kuunga

mkono jitihda za serikali za kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo ndani ya maeneo wanayohudumia na yenye uhita-ji. Walitakiwa pia kuhakikisha kuwa sabuni na hatua muhimu za unawaji wa mikono ili nao waweze kufundisha wateja na wana-nchi wanaowahudumia. Mwitikio ulikuwa nzuri na wa kuridhisha.

Katika Jiji la Dar es salaam lenye wakazi zaidi ya milion tano, jumla ya wa-toa huduma za maji hamsini na nne (54) wameweza kuweka vifaa kinga vinavyo-jumuisha ndoo za maji za kunawa mikono pamoja na sabuni kwenye maeneo 241 yenye mikusanyiko ya watu kama vile kwenye ofisi za umma za kihuduma, sten-di za basi, maeneo ya waendesha bodabo-da na bajaji katika maeneo ya kuchotea maji. Kazi hii ni endelevu.

Mwenyekiti wa moja ya jumuiya ya maji ya Mamboleo iliyopo wilayani Teme-ke, Ndugu Ally Saidi anasema kumekuwa na mwitikio mkubwa wa jamii katika suala zima la kunawa mikono na kujikinga na maambukizi ya Corona.

“Kwakweli baada ya maelekezo ya ser-ikali kuhusu kuweka vifaa kinga kwenye

maeneo muhimu ya kihuduma wananchi wengi wamepokea hili jambo kwa haraka zaidi na kwa muamko mkubwa sana. DA-WASA pia walipita kutuelimisha namna bora ya kujikinga kwa kupitia huduma ya majisafi ambayo sisi tunaisimamia chini ya Mamlaka” alisema ndugu Saidi.

Said ameongeza kuwa kwa sasa kila kituo kilichopo chini ya mradi wa maji kimewekea ndoo na sabuni kwa ajili ya kuwawezesha wahitaji wa huduma ya maji, kunawa mikono yao kabla ya kushi-ka bomba.

Kiongozi huyo wa Mradi wa Kijamii wa Maji eneo la Mamboleo A, anasema hatua ya uwekaji wa ndoo na sabuni, haikushia katika huduma za maji, bali wameziweka katika maeneo mbalimbali yenye mku-sanyiko wa watu.

Kwa upande wa Jumuiya ya Watumia Maji Moringe iliyopo Mbagala Kizuiani, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ndugu Yu-sufu Chilala anasema wameweka utarati-bu wa kuhakikisha kila mtu anayefika kwa ajili ya kupatiwa huduma ya maji katika vizimba vyetu vya maji, ananawa mikono kwa sabuni katika ndoo iliyowekwa pem-

Mapambano Dhidi ya Corona>>

6 | DAWASA YETU: TOLEO NA. 01

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

Page 7: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

DAWASA YETU: TOLEO NA. 01 | 7

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

beni , vinginevyo ya hivyo hatapata hudu-ma hapa.

“Sasa hivi ujanja ni kunawa mikono na sabuni ndipo upate huduma , huwezi ku-shika koki ya kwenye vizimba bila kunawa mikono yako na sabuni, usipofanya hivyo huwezi kupata maji. Tunaishukuru Dawasa wametukabidhi vitendea kazi vya namna ya kujikinga na corona ikiwemo ndoo na sabuni na elimu sahihi ya kutumia pia.” al-isema Chilala.

“Dawasa haijaishia hapo wameturuhu-su pia kuunganisha maji kwa wananchi ili kuhakikisha wanapata huduma hii ya kun-awa mikono kwa maji safi tiririka. Ndoo hizi pia tumeziweka hadi katika mkusan-yiko wa watu,” anasema.

Kwa mujibu wa Chilala, hatua ya Da-wasa kuwapa vifaa hivyo imewaongezea nguvu katika utekelezaji wa majukumu yao kwa ufanisi katika suala zima la kutoa huduma lakini kwa kuzingatia tahadhari zote dhidi ya kujikinga na corona.

Kwa upande wa mmoja wa mwanan-chi anayehudumiwa na jumuiya ya maji, Bi Rukia Simba ameshukuru hatua zilizo-fanywa na jumuiya hizo za kuhakikisha upatikanaji wa maji unakuwa mkubwa hu-susani kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa Corona na kutoa wito wa jumuiya hizo

kuchukua hatua kali kwa wale ambao wat-akiuka taratibu zilizowekwa.

“Hatua hii ni nzuri sana kwetu ambao hatuna maji ya mtandao wa Dawasa na ambao tunahudumiwa na jumuiya hizi za maji, ugonjwa huu ni hatari sana na bila uhakika wa upatikanaji wa maji basi hali ingekuwa mbaya zaidi. Kwa sasa huwezi kupata huduma ya maji kama hujana-wa mikono yako na sabuni ukifika katika vizimba vya kuchotea maji. Kwa kweli ni utaratibu mzuri kwa sababu unawakinga wananchi dhidi ya corona kama Serikali ilivyoagiza.

“Kama unataka kuteka maji lazima un-awa mikono yako na sabuni kisha upate huduma. Tunaishukuru Dawasa imerahi-sisha mchakato huu kwa kutoa na sabuni ndoo zaidi ya 20 eneo letu la Kigamboni” anasema Rukia.

Kwa upande wa DAWASA, Mkurugen-zi wa Mawasilinao na Jamii, Neli Msuya anasema jumuiya za maji zimekuwa msaa-da sana kwenye kutoa huduma ya maji kwenye maeneo ambayo hayana mtand-ao wa DAWASA, huku zikisimamiwa kwa karibu na Mamlaka katika uendeshaji wa shughuli zake za kila siku.

“Kwa kipindi hiki cha mapambano dhidi ya virusi vya corona na ugonjwa wa

Covid-19, tumejizatiti kuhakikisha jumuiya hizi za maji zinakuwa mstari wa mbele ka-tika kujikinga dhidi ya maambukizi na vile-vile kuwakinga watumiaji wa huduma zao wanaopata maji kupitia vizimba vilivyowe-kwa.

Tumewapa vifaa kinga ambavyo ni ndoo za kunawa pamoja na sabuni pamoja na elimu juu ya usahihi wa kunawa miko-no na tahadhari nyingine kwa kipindi hiki” anaongezea Neli

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) in-ahudumia Jiji la Dar es salaam na miji ya Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kisarawe na Chalinze Mkoani Pwani. Licha ya ku-toa huduma ya majisafi, pia DAWASA inasimamia miradi ya jamii iliyokuwa in-aendeshwa na Manispaa na iliyokuwa iki-simamiwa na kamati za maji za wananchi katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Sa-laam takribani Jumuiya 321.

DAWASA imepewa mamlaka hayo ku-fuatiwa kupitishwa kwa Sheria mpya ya Maji na Usafi wa Mazingira Namba 5 ya Mwaka 2019 (The Water Supply and San-itation Act.2019) ambayo inaipa DAWASA pekee jukumu la kusimamia huduma ya maji na usafi wa mazingira katika Jiji la Dar es salaam.

Mapambano Dhidi ya Corona>>

DAWASA YETU: TOLEO NA. 01 | 7

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

Page 8: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

8 | DAWASA YETU: TOLEO NA. 01

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

MRADI wa usambazaji maji kutoka matanki ya Chou Kikuu cha Dar es Salaam hadi Mji wa Bagamoyo Mkoani Pwani unatekelez-wa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) chini ya mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia kwa gharama ya Sh 65,423,284,210.

Mradi huu unatarajiwa kuhudumia wakazi zaidi ya 750,000 na kuunganisha wateja wa-pya 60,000 watakaopata huduma ya majisafi kwenye maeneo ya Changanyikeni, Mbezi Beach, Vikawe, Goba, Bunju, Wazo, Ocean Bay Zone, Salasala na Bagamoyo.

Kazi zinazoendelea katika Mradi huuMradi huu unahusisha ujenzi wa matan-

ki matatu ya kuhifadhi maji yatakayojengwa maeneo ya Tegeta A, Oceanic Bay (Bunju) na

Mradi wa Usambazaji maji kutoka Makongo Juu hadi Bagamoyo

Utekelezaji Miradi ya Maji>>Mhandisi Mshauri (WAPCOS) na usanifu kuka-milika Agosti 2014. Mradi huu ni mwendelezo wa mradi wa usambazaji maji awamu ya kwan-za, ambao tayari umekamilika chini ya mkan-darasi Jain Irrigation.

Kazi zilizotekelezwa katika awamu ya kwan-za ya mradi huo zilihusisha:1. Ujenzi wa matanki matano ya kuhifadhi

maji yaliyojengwa maeneo ya • Tanki la Maji Makongo lita milioni tano• Tanki la Maji Salasala lita milioni sita• Tanki la Maji Wazo lita milioni sita• Tanki la Maji Mabwepande lita milioni

sita• Tanki la Maji Bagamoyo lita milioni sita

2. Ujenzi wa vituo vya kusukuma maji (buster stations) kwenye maeneo ya Bunju,

Salasala, Changanyikeni, Wazo na Bunju.3. Ulazaji wa bomba kwa umbali wa Kilomita

za mraba 429

KUKAMILIKA KWA MRADI• Mategemeo ya kumalizika kwa mradi

huu ni Novemba 2021.

Vikawe (Bagamoyo) yenye ukubwa wa cubic meter (6000–5000), ujenzi wa vituo viwili vya kusukuma maji vitakavyojengwa eneo la Goba na Vikawe, ulazaji wa mabomba makubwa ya maji kuanzia kipenyo cha mm 400 hadi mm 90 kwa umbali wa Kilomita 1,500.

Kazi hii inatekelezwa na Mkandarasi Chengdu Industrial Equipment Installation ikishirikiana na Hainan International Limited.

Awali mradi huu ulifanyiwa usanifu na

750,000Idadi ya wakazi watakaoweza

kupata huduma ya majisafi baa-da ya Mradi huu unaotarajiwa

kukamilika mwaka 2021

Page 9: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

DAWASA YETU: TOLEO NA. 01 | 9

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

MRADI wa Majitaka Vingunguti unaoendesh-wa na kusimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa), umeweze-sha ujenzi wa vyoo takribani 200 kwa wananchi wa-naoishi maeneo ya karibu na mabwawa ya kuchaka-ta majitaka yaliyopo Vingunguti na kusaidia kwa kiasi kikubwa kubadilisha hali ya Maisha ya wakazi wengi wa eneo hilo.

Hiyo si faida pekee, bali pia umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza magonjwa ya mlipuko, ikiwe-mo kuhara, matumbo na kipindupindu.

Mradi huo wa kuwajengea vyoo wananchi, kupitia mfumo wake unaruhusu mtu anapokitumia, maji hayabaki pale bali yanaenda moja kwa moja mpaka kwenye mabwawa ya Dawasa ya kumwaga majitaka na hilo limesaidia sana kuondokana na ma-gonjwa ya mlipuko

Kudra Khamis anasema awali kabla hawaja-sogezewa huduma hizo na Dawasa, eneo lao lili-kuwa na hali mbaya kutokana na kukosekana kwa mifumo ya majitaka na pia vyoo salama.

Anasema harufu na magonjwa ya mara kwa mara, ni baadhi ya kero zilizowafanya waishi ka-tika wakati mgumu, licha ya kushindwa kuyaha-ma makazi yao kwa kuwa hawakuwa na makazi mengine wala gharama za pango.

“Ukiosha vyombo au kufua nguo hakukuwa na sehemu ya kumwaga yale maji na kwa kuwa vyoo vyetu vilikuwa vya shimo, hata kuoga ilikuwa mtihani lazima utumie maji kidogo ili choo kisijae mapema.”Kudra anasema.

Anasema vyoo vilijaa mapema na hivyo waka-wa wanashindwa pa kumwaga maji. “Zamani hata ukiosha vyombo unatafuta wapi ukamwage maji ukimwaga yanaenda kwa mtu mwingine, linakuwa ni kosa.”alisema

Jafari Hamis mkazi wa mtaa wa Mji Mpya, Kata ya Mnyamani anasema uwepo wa mfumo huo ume-

miezi miwili, kwa kuwa vilijaa. Anasema ilifikia hatua mwenye choo fedha

ya kunyonya hana, anasubiri usiku watu wamelala anazibua ili angalau kesho choo kipumue aendelee kujisaidia apate sehemu ya kujisitiri.

Hata hivyo, anasema kufuatia tabia hiyo, watu walikuwa wanakamatwa na kupigwa faini, lakini baada ya kupata hivyo vyoo, hali ilibadilika kwani mfumo wake hauhifadhi kinyesi, kwani ni choo am-bacho ukijisaidia ukamwaga maji, hakuna choo kin-achobaki kikielea au kuonekana.

“Kwa sasa hata mtu akipata magonjwa, inate-gemea na utumiaji wake wa choo, kwa kuwa ukijisa-idia na kumwaga maji hakuna kitu kinatuama pale. Kama utatumia maji ya kutosha hakuwezi kuwa na nzi wala shida yoyote.” anasema Kisambi.

Haikuwa rahisi kushawishiKisambi ambaye ni balozi wa mradi huo, anase-

ma tangu kuanza kwa mradi amekuwa akihudhuria vikao mbalimbali na wakaguzi walifika eneo lake, kuhakikisha namna mradi utakavyokuwa.

Anasema haikuwa rahisi kushawishi watu, kwani wengi hawakuwa na uelewa na walishazoea maisha yale na harufu iliyokuwepo.

“Nilikuwa nafuatilia vikao vyote vilivyofanyika kipindi hicho tunafanya vikao Dawasco Mwananya-mala. Nilikuwa mtu wa kwanza wazungu wanakuja hapa tunakwenda vikao. Tukirudi watu wakaanza kuninyooshea vidole kwamba ninataka kuuza mtaa.

“Walisema unatembea sana na wazungu na hao Dawasco, unafanya mipango eneo hili liuzwe. Nikawaambia nipo kwenye mipango ya kuwasaid-ia, wote wakawa wanasema hapana hatutaki ni-kasema nitakuwa wa kwanza kukubali hiki choo.” anasema

Kisambi anasema alitoa elimu kwamba iwapo watu wameamua kuwasaidia kuondokana na hali hiyo, ni vema wakubali ili kuondoa magonjwa na ha-rufu, ambayo ni kero kwao.

Kisambi anasema licha ya kuwa alianza kwa changamoto hiyo kubwa, hivi sasa mambo yame-badilika.

“Sasa wananchi wanakuja kama nyuki, tuna-taka vyoo! Tunataka vyoo! Kwa sasa wamejenga wameondoka kila mtu anakuja akihitaji kujengewa wanaona harufu ipo kwao na hata mlipuko ukitokea unatokea kwao ambao wapo eneo hatarishi.”anase-ma

Kwa upande wa DAWASA, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii, Neli Msuya anasema mradi huu umelenga kunufaisha wananchi wa kipato cha chini ili kuwaondolea kero ya utiririshaji majitaka na kuboresha makazi yao.

“Mradi huu wa ujenzi wa mtandao wa majitaka katika eneo la Vingunguti ni awamu ya pili, ambao unahusisha ujenzi wa chemba ndogo ndogo mia mbili arobaini tano (245) na nyumba zaidi ya mia mbili sabini na tisa (279) zimekwishaunganishwa ka-tika mtandao huo” alisema Msuya.

“Tumetoa mkopo wa gharama nafuu wa hadi kufikia shilingi 700,000 kwa choo na mnufaika anaruhusiwa kulipia hata kwa miaka minne kulinga-na na uwezo wake.” aliongeza Msuya.

Mradi wa majitaka ulivyoboresha makazi, kuondoa magonjwa ya mlipuko vingunguti

Usafi wa mazingira>>

Kabla ya maboresho. Baada ya maboresho.

saidia kwa kiasi kikubwa kuondoa kero zilizokuwepo lakini changamoto iliyobaki kwa sasa ni kukosekana kwa mfumo wa majisafi.

“Hivi vyoo vinahitaji uwe na maji mengi ili uweze kusafirisha mzigo, lakini kwa bahati mbaya chan-gamoto tunayokutana nayo huku hatuna mfumo wa maji safi na tunayoyatumia ni yale ya kuchimba kwenye visima, haya ni ghali kidogo ukilinganisha na hali zetu kiuchumi,” anasema Jafari.

Anasema ndoo moja ya maji kubwa, wana-nunua kwa Sh100 na ndogo kwa Sh50, ambayo hata hivyo yanapatikana umbali mrefu, “Ili usukume mzi-go choo kinahitaji angalau ndoo ndogo iliyojaa maji, lakini kutokana na hali ya kiuchumi inakuwa ngumu kumudu, hivyo tukiletewa mfumo wa maji safi ita-saidia kuondoa hii changamoto.”alisema

Balozi wa eneo hili kwa miaka kumi na mbili na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Mariam Kisambi anasema vyoo vimebadilisha hali ya makazi ya Vin-gunguti na maisha ya wakaazi kwa ujumla.

Kisambi anasema kipindi cha nyuma, mvua ikinyesha kidogo tu, hawakuweza kukaa maeneo yao na hata kula ilikuwa ni shida.

“Utakula wakati maji yanatiririka yanakwen-da bondeni, tena machafu ya kijani yaani yale ya chooni lakini tangu tumepatiwa hivi vyoo hii, hali haipo tena.

“Hata mvua ikinyesha husikii kuna harufu. Kwa kuwa hakuna kinachozibuliwa na hata kipindupin-du kikianza, mtaa wetu ndiyo ulikuwa wa kwanza mpaka tukawa tunashangaza wengine Vingunguti wana nini mbona kila kipindupindu kikianza ni wao.” anasema

Kisambi anasema zamani hakukuwa na vyoo na vichache vilivyopo vilikuwa vya shimo.

Anasema asilimia kubwa vilikuwa duni, am-bavyo ni chakavu. Hata hivyo kumiliki maji ilikuwa changamoto na iliwalazimu kunyonya kila baada ya

Page 10: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

10 | DAWASA YETU: TOLEO NA. 01

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

GHARAMA YA MRADI Mradi huu unatekelezwa kwa kutumia fedha za ndani za DAWASA ambapo gharama zote ni kama ifuatavyo;a. Ujenzi/ulazaji wa bomba (59km) ni TZS 3.4

Bilioni bila VAT,b. Ununuzi wa mabomba ni TZS 9.68 Bilioni

bila VAT

Mradi wa Maji Mji wa Chalinze - Mboga

TAARIFA>>

KATIKA jitihada za kuboresha huduma kwenye maeneo mbalimbali yenye chan-gamoto ya upatikanaji wa maji, DAWASA iliingia mkataba wa ujenzi wa mradi wa bomba kuu la kusafirisha maji lenye kipenyo cha inchi 16(DN 400) umbali wa Km 59 kutoka Mlandizi (Mitambo ya Ruvu Juu) hadi Kijiji cha Mboga (Mlandizi). Mradi huu wa bomba kuu unatara-jiwa kusafirisha kiasi cha lita za ujazo milioni tisa na laki tatu (9,300,000) kwa siku amba-zo zitawezesha kuhudumia wakazi wapatao 120,00. Maunganisho mapya ya wateja zaidi ya 18,000 yatafanyika mara baada ya kukamilika kwa mradii huu.

KAZI ZINAZOTEKELEZWAMradi huu unahusisha kazi zifuatazo:

1.0) Ujenzi wa bomba kuu la chuma la kusafirisha maji lenye kipenyo cha inchi 16 (DN400 MS pumping main) -59km kutoka Mlandizi hadi Mboga.

2.0) Ujenzi wa maunganisho maalum (Offtakes) katika maeneo ya Mlandizi, Ruvu (Milo), Vigwaza, Eneo la Mizani, Chamakweza, Pingo, Pera, Chalinze, Msoga, Mboga Sayona na Mboga Matenki ya Maji

3.0) Ujenzi wa matenki ya kuhifadhi maji (Sump) zenye ujazo wa lita 675,000 (675m3) kila moja katika maeneo ya Chamakweza na Msoga

4.0) Ujenzi wa vituo viwili vya kusukuma maji (Booster Pumping Stations) katika mae-neo ya Chamakweza na Msoga

5.0) Ufungaji wa pampu za kusukuma maji na vifaa vya umeme katika vituo vya kusu-kuma maji maeneo ya Chamakweza na Msoga.

c. Ununuzi wa viungo maalum (Special fit-tings) ni USD 464,148.32 (sawa na TZS 1,057,209,194.40) bila VATAidha, vituo viwili vya kusukuma maji

(Boosting pump stations) vinatarajiwa kujeng-wa ikiwa ni pamoja na ununuzi na ufungaji wa pampu za kusukuma maji katika maeneo ya Chamakweza na Msoga.

9,300,000

18,000

Kiasi cha lita za ujazo ambazo Mradi huu wa bomba kuu

unatarajiwa kusafirisha kwa siku. Kiasi hiki kitawezesha kuhudumia wakazi zaidi ya

laki moja

Idadi ya maunganisho ma-pya ya wateja yatafanyika mara baada ya kukamilika

kwa mradii huu.

Page 11: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

DAWASA YETU: TOLEO NA. 01 | 11

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

SERIKALI Mkoani Pwani, imeridhishwa na utekelezaji wa miradi iliyo chini ya DAWA-SA ,pamoja na mkakati wake wa kufikisha majisafi na salama maeneo ya viwanda ikiwe-mo Mradi wa Maji Chalinze - Mboga, utakao-tumia Sh.bilioni 17.1 pamoja na Mradi wa Soga kuelekea Kiwanda cha Nyama TANCHOICE utakaogharimu Sh.bilioni 1.1 .

Licha ya kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi huo, imemuelekeza mkandarasi Shanxi Co. Ltd wa Mradi wa Maji Chalinze - Mboga hadi Msoga, kuhakikisha anamaliza ujenzi huo kwa wakati ifikapo mwezi Juni mwaka huu ili kuondoa kilio cha wanaChalinze ambacho ki-medumu kwa miaka mingi.

Akitoa rai hiyo, wakati wa kutembelea mi-radi hiyo, Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandi-si Evarist Ndikilo alisema mradi huo chanzo chake ni kutoka mtambo wa Ruvu Juu na sasa umefikia asilimia 52, hivyo kasi iongezwe ili ukamilike kwa wakati lengwa.

Pamoja na hilo,alitembelea eneo la viwan-da unapotekelezwa Mradi wa Maji Zegereni, ambapo imeidhinishwa kiasi cha Sh.bilioni 2.3 ambapo unatarajiwa kuanza mwezi Juni hivyo aliiomba DAWASA kuuchukulia uzito ili fedha ikitoka mradi uanze mara moja.

Alisema, mradi huo utanufaisha viwan-da takriban 25 kwenye eneo hilo, kwani Hal-mashauri ya Mji wa Kibaha imetenga eneo hilo kwa ajili ya viwanda.

“Nikuombe Mtendaji Mkuu DAWASA, mradi huu wa Zegereni ni muhimu sana, mkoa wa Pwani ni ukanda wa uwekezaji na viwanda hususan eneo hili, hivyo basi enda-

uzalishaji utaanza wakati wowote. Aliitaka ta-asisi hiyo kumalizia hatua za mwisho za Mradi wa Soga eneo la Kongowe ili mwekezaji aanze uzalishaji.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja al-isema wamejikita kutatua kero ya maji kwenye viwanda kwa kufikisha huduma hiyo kupitia miradi yake, ambayo pia inakwenda kujibu kil-io cha wananchi.

Alifafanua kuwa serikali imejipanga kuinua sekta ya viwanda na uwekezaji na DAWASA in-aunga mkono juhudi hizo kwa kusogeza hudu-ma ya maji kwa wawekezaji hao.

Luhemeja alibainisha kuwa, Mradi wa Soga umekamilika na kuongeza kuwa Kiwanda cha TANCHOICE kijipange kwa kuwa mteja mzuri wa DAWASA.

Ofisa Miradi wa TANCHOICE, Boniventure Mtei alisema maji yamefika kiwandani hapo, kilichobakia ni kuweka mita na kuanza uzal-ishaji. Aliushukuru uongozi wa mkoa na DA-WASA Kibaha kwa ushirikiano wao na kusema wanatarajia kutoa ajira kwa wazawa na kusaid-ia wafugaji kupata soko la uhakika.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete aliipongeza Ser-ikali ya Awamu ya Tano kwa kutatua kero ya maji katika jimbo lake kwani sasa hata akisima-ma katika mikutano, maswali ya kero ya maji yamepungua.

Ridhiwani alielezea kuwa, Chalinze kilio chao kikubwa ni maji lakini kutokana na Mradi wa Chalinze - Mboga na Chaliwasa chini ya DA-WASA, kero ya maji inakwenda kuwa historia.

Pwani yaridhishwa na utendaji kazi wa DAWASAinavyojibu hoja ya maji viwandani

HABARI>>

Mkuu wa Mkoa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akipata maelezo ya uboreshwaji wa huduma ya maji mkoa wa Pwani kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Pwani hivi karibuni.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani (sasa amestaafu) Theresia Mbando wakiangalia moja ya pampu katika kituo cha kusukuma maji cha Kibamba, akiwa ameambatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa ziara yake ya kutem-belea Mradi wa Kisarawe.

po taasisi wezeshi mtashirikiana kikamilifu na wawekezaji kuondoa changamoto ya ma-ji,umeme na kuboresha barabara, kwa haki-ka viwanda vitanufaika na kuzalisha hatimae kuingiza pato kwa serikali.

“Taasisi wezeshi ndio nguzo ,kama kuna kuwa na vikwazo ,wawekezaji hawa hawawezi kuanzisha uwekezaji na kuzalisha kwani nao wanahitaji faida na manufaa,” alisema.

Alieleza kuwa, Kiwanda cha TANCHOICE ni kikubwa kwa Afrika Mashariki na Kati na

Page 12: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

KONA YA SHERIA>>

SHERIA MPYA YA HUDUMA ZA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA NA.5/2019

Sheria mpya ya huduma za maji na usafi wa mazingira imesainiwa na Mhe. Rais wa Jamhu-ri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli na kuanza kutumika rasmi tarehe 01/07/2019. Ni sheria inayoweka mfumo endelevu wa usimamizi, uendeshaji na udhibiti wa huduma za maji na usafi wa mazingira. Ili kufikia malengo, sheria imeainisha majukumu ya watekelezaji mbalimbali ambao ni:

a) WAZIRI WA MAJI• Kuratibu masuala ya kiufundi na fedha• Kuratibu mipango na utafutaji wa fedha ku-

toka kwa wadau (wafadhili, NGOs)• Kupendekezwa kutungwa kwa Sera, Sheria

na Mikakati• Kusimamia utekelezaji wa utoaji wa huduma

za maji na usafi wa mazingira.

b) WAZIRI WA TAMISEMI: • Kuweka mazingira mazuri ya ushiriki wa

jamii na sekta binafsi, mamlaka za maji, RUWASA kutekeleza majukumu yake.

c) SEKRETARIATI YA MIKOA: • Kuweka mazingira mazuri kuhakikisha

mamlaka za Maji, RUWASA, na jamii kute-keleza majukumu yao katika mkoa.

d) MAJUKUMU YA SERIKALI ZA MITAA • Kuratibu mipango na mamlaka za maji• Kuhamasisha jamii kusimamia uendeshaji

miradi ya maji• Kuhamasisha uwepo wa miundombinu ya

usafi wa mazingira

Ijue sheria mpya ya huduma za Maji na Usafi wa Mazingira

SHERIA MPYA NA. 5/2019MAKOSA YA JINAI NA ADHABU

KOSA

Kuharibu miundo mbinu ya majisafi na majitaka au mali

Kuchukua maji au kuchepu-sha maji kutoka kwenye miundo mbinu ya maji

Kutumia maji vibaya

Kuchezea dira za maji ili ku-fanya udanganyifu wa maji aliy-oomba

Kutumia maji kinyume na matumizi yaliyoidhinishwa

Kuosha, kutupa, kusababisha au kuruhusu kitu kuingia kwenye miundombinu ya Maji

Kufunga au kufungua koki za miundombinu ya maji au mifu-niko

Kuchafua Maji

Kujenga juu ya miundombinu ya maji

Kuzuia uchafuzi

Na

1

2

3

4

5

6

7

8

9

10

ADHABU

• Faini: Sh.500,000 hadi Sh.Milioni 50• Kifungo: Miaka 2 hadi miaka 5

• Faini: Sh. 500,000 hadi Sh. 50,000,000• Kifungo mwaka 1 hadi miaka 6

• Faini: Sh.500,000 hadi Sh.Milioni 10• Kifungo: Miezi 6 hadi miaka 2

• Faini: Sh.500,000 hadi Sh.Milioni 10• Kifungo: Miezi 6 hadi miaka 2• Endapo kosa litajirudia; faini Sh.Milioni 10 hadi Sh.Milioni 20• Kifungo: Miaka 2 hadi miaka 5

• Faini: Hadi Sh.Milioni 5• Kifungo: Mwezi 1 hadi miezi 6

• Faini: Sh.50,000 hadi Sh.Milioni 1• Kifungo: Mwezi 1 hadi miezi 3

• Faini: Sh.50,000 hadi Sh.Milioni 1• Kifungo: Mwezi 1 hadi Miezi 3

• Faini: Sh.Milioni 1 hadi Sh.Milioni 5• Kifungo: Mwaka 1 hadi miaka 3

• Faini: Sh.Milion 1 hadi Sh.Milioni 10• Kifungo: Miezi 6 hadi Miaka 2

• Faini: Sh.Milion 1 hadi Sh.Milioni 3• Kifungo: Miezi 6 hadi miaka 2

12 | DAWASA YETU: TOLEO NA. 01

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

Page 13: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

MAKALA: UTEKELEZAJI>>

DAWASA yajivunia kuboresha huduma ya maji kwa Wananchi Jijini Dar

Miaka Mitano ya Uongozi wa Serikali ya Rais Dkt. Mhe. John Pombe Magufuli

- Yatenga asilimia 35 yamapato yake ya ndani kwenye utekelezaji Miradi- Maeneo mapya 119 yapata Maji

UONGOZI wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tan-zania, Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli inakwenda sambasamba na mafanikio makub-wa katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika sekta muhimu ya maji.

Ni awamu ya uongozi iliyojikita katika ku-leta majibu ya haraka ya changamoto halisi za wananchi, zinazogusa maisha yao ya kila siku. Katika hilo, Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA) yenye dhamana ya kutoa huduma ya majisafi imed-hamiria kufikisha huduma ya maji eneo lake la kihuduma ambapo ni Jiji la Dar es Salaam na baadhi ya miji ya Pwani huku ikijinasibu na ma-fanikio mengi yaliyopatikana.

Kama ambavyo Mhe. Rais Magufuli ame-kuwa akisisitiza kuhusu umuhimu wa wana-nchi kusogezewa huduma za maji safi karibu na makazi yao, ndivyo ambavyo DAWASA imekuwa ikihakikisha inatekeleza azma hiyo kwa wakazi wa Dar es Salaam na katika miji ya Pwani kwa vitendo.

Mafanikio hayo yamechochewa na kuwe-po kwa mazingira bora ya kiutumishi yanayo-chochea ubunifu na matumizi ya teknolojia yaliyopelekea kuongezeka kwa kasi ya ute-kelezaji wa majukumu ya Mamlaka na hivyo kuchochea mabadiliko makubwa katika utoaji wa huduma.

Miradi ya Majisafi yatekelezwa kwa kasiBaada ya DAWASA kukamilisha miradi

mikubwa ya upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu

Mkazi wa Goba Kibululu, Khamis Mabali akifurahia huduma ya majisafi kwa mara ya kwanza baada ya Mam-laka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kukamilisha mradi wa maji katika eneo hilo. Mradi wa Maji Goba utanufaisha wananchi wa zaidi ya 300 wa maeneo ya Kibululu, Lastanza na Goba Centre.

DAWASA YETU: TOLEO NA. 01 | 13

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

Inaendelea Uk. 14

Page 14: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

14 | DAWASA YETU: TOLEO NA. 01

Tunatekeleza usimamizi wa mbolea kwa kilimo bora na kwa Maendeleo Endelevu

na Ruvu Chini, kazi kubwa ambavyo imekuwa ikiendelea sasa ni kuboresha mfumo wa us-ambazaji maji na kupanua mtandao ili kufiki-sha maji yaliyoongezeka kwa wananchi wengi zaidi. Hadi sasa miradi mikubwa na midogo ipatayo 18 inaendelea kutekelezwa na miradi midogo midogo 199 imekamilika ili kuongeza wigo wa huduma ikiwa ni pamoja na kufikisha maji katika maeneo mengi ambayo hapo awali hayakuwa na huduma.

Mafanikio haya yamefikiwa baada ya DA-WASA kuamua kutenga asilimia 35 ya mapato yake na kuyaelekeza kwenye utekelezaji wa miradi na hivyo kuwezesha miradi kutekelez-wa kwa wakati na kwa ubora.

Mafanikio ya uboreshaji huduma ya majisafiMwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi

wa DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwa-munyange anabainisha wazi kuwa siri ya ma-fanikio yaliyopatikana chini ya uongozi ya Ser-ikali ya Awamu ya Tano ni uimara na malengo ya menejimenti na watumishi kufikisha hudu-ma zaidi kwa wananchi katika kutoa huduma bora ya majisafi na majitaka kwa wakazi wana-ohudumiwa.

“Katika yote tunajivunia ni utayari wa Serikali yetu inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kusimamia uboresha-ji wa huduma kwa wananchi wake ikiwemo huduma na utayari wa watumishi wetu katika kutekeleza kwa vitendo maagizo ya viongozi na mikakati shirikishi inayopangwa” anasema Jenerali Davis Mwamunyange

Mkuu huyo wa Majeshi mstaafu anase-ma, “Miaka minne ndani ya kipindi cha kwan-za cha Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli kwangu mimi kama Mwenyekiti wa Bodi na wajumbe wengi inatupa faraja ya kuona Mamlaka tunayoisimamia inafanya kazi nzuri inayoonekana na umma wa Watanzania husu-sani wakazi wa Dar es Salaam na miji ya Mkoa wa Pwani unafurahia huduma.”

Hali ya upatikanaji MajiAfisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA,

Mhandisi Cyprian Luhemeja, anasema awa-li mwaka 2015 Jiji la Dar es Salaam lilikuwa linapata maji kwa asilimia 68 na jumla ya maunganisho ilikuwa 123,000. “Leo hii hali ya upatikanaji maji jijini Dar es Salaam imepanda hadi asilimia 88 na maunganisho ya maji yame-ongezeka kutoka 123,000 hadi kufika 326,000”, anasema Mhandisi Luhemeja.

Huduma kwa MtejaMhandisi Luhemeja anatabanahisha kuwa

huduma kwa mteja ni nguzo muhimu na ni uti wa mgongo wa Mamlaka, hivyo DAWASA imeendelea kuboresha njia za ulipaji wa anka-ra. “Wateja wetu sasa wanalipia kutumia mtan-dao, hiyo imewarahisishia badala ya kupoteza muda mwingi kulipia kwa fedha katika ofisi za DAWASA ama mabenki,” anasema.

Mhandisi Luhemeja anasema DAWASA inaendelea na mpango wake wa kuunganisha wateja kwa mkopo, ambapo wengi sasa wana-jitokeza.

“Pia nitumie fursa hii kuwakumbusha wa-nanchi kwamba maunganisho ya maji kwa

MAKALA: UTEKELEZAJI>>

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

mara ya kwanza inatolewa kwa mkopo. Kwa hiyo yeyote anayekuja kutoza fedha kwa ajili ya ada ya kuunganisha, huyo atakuwa tapeli, wananchi wamripoti kwenye vyombo vya dola haraka”, anasema Mhandisi Luhemeja.

Anataja maeneo ambayo awali hayakuwa na huduma ya maji na sasa yana huduma. Mae-neo hayo ni Majengo, Tatedo, Mbezi Manyema, Mbezi Mtoni, Kwa Ndambi, Kontena Mbuyuni, Baraza la Mitihani, Kwa Abarikiwe, Usukumani, Kwa Mtenga, Gold star, Kwa Santa, Kwa Power Nyati , Mito Miwili na maeneo jirani haya yote yapo mkoa kazi wa DAWASA -Kawe.

Vile vile kwa eneo la Tegeta, maeneo ma-pya yanayopata huduma ya maji sasa ni Miko-cheni Mabwepande, Malolo, Mabwe, Salasala, Kilimahewa, Kitunda Street, Bunju Beach, Mu-ungano, Goba, Majengo na Majengo Goba.

Wilaya ya Ubungo nayo kwa muda mrefu maeneo mengi yalikuwa na changamoto za upatikanaji wa huduma ya maji, ila kwa sasa maeneo yafuatayo yanapata huduma ya maji ni Kimara kwa Mtoro, Msuguli - Mji Mpya, Go-lani, Saranga - Upendo, Saranga – Ukombozi, Msingwa, Kwa msuguki, Mbezi – Magari Saba, Malamba, Mbezi - Makabe, Luguluni Lapaz, Mdidimua, Kibamba - Kibwegere.

Mradi wa Maji Mkuranga upo katika hatua za utekelezaji, ambapo unahusisha ulazaji wa mtandao wa maji kwa umbali wa kilomita 63.5, ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji lenye uwezo wa kuhifadhi maji kiasi cha lita milioni moja na nusu, ambapo mradi unategemea kukamilika Juni, 2020. Mradi huu vile vile unatekelezwa kwa kutumia fedha za ndani za Mamlaka.

Mradi huu unategemea kuhudumia wakazi takribani elfu ishirini na tano ambao wako ka-tika Kata za Mkuranga, Kiparang’anda, Mwa-nambaya na Vikindu kwa awamu ya kwanza baada ya kuanza.

Mradi wa Maji Chalinze -Mboga ambao un-ahusisha ujenzi wa bomba la kusafirisha maji lenye kipenyo cha inchi 16 kwa umbali wa Ki-lomita 59 kutoka Mlandizi ( Mitambo ya Ruvu Juu) hadi Kijiji cha Mboga (Mlandizi) ni mwen-delezo wa jitihada za Mamlaka za kuboresha huduma ya maji katika Mji wa Chalinze.

Mradi wa Chalinze unatarajiwa kusafiri-sha kiasi cha maji cha lita za ujazo milioni tisa na laki tatu (9,300,000) na kuhudumia wakazi wapatao laki moja na ishirini kwa siku. Maun-ganisho zaidi ya elfu kumi na nane yatafanyika baada ya kukamilika kwa mradi.

Mradi huu unatekelezwa kwa kutumia mapato ya DAWASA yatokanayo na makusan-yo ya kila mwezi.

Miradi yote hii ya kimkakati inayotekelez-wa na DAWASA, kwa mwaka 2019/2020, ina-lenga kukidhi agizo la Serikali la kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka huu 2020, upatikanaji wa huduma ya maji inafikia asilimia 85 kwa mae-neo ya vijijini na asilimia 95 kwa maeneo ya mijini.

Miaka Mitano ya Uongozi wa Serikali ya Rais Dkt. Mhe. John Pombe Magufuli

DAWASA yajivunia kuboresha huduma ya maji kwa Wananchi Jijini Dar es Salaam

Miaka minne ndani ya kipindi cha kwanza cha serikali ya Rais John

Magufuli kwangu mimi kama Mwenyekiti wa Bodi na wajumbe

wengi inatupa faraja ya kuona Mamlaka tunayoisimamia inafa-nya kazi nzuri inayoonekana na umma wa Watanzania hususani

wakazi wa Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange

Inatoka Uk. 13

Page 15: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

MAKALA: UTEKELEZAJI>>

DAWASA YETU: TOLEO NA. 01 | 15

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

KATIKA kuimarisha huduma ya majita-ka na usafi wa mazingira jijini Dar es Salaam, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeeleza faida za uwepo wa mabwawa ya kutunza, kuchakata na kusa-firisha majitaka kuwa ni moja ya chanzo cha ubora na usafi wa mazingira katika Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na “DAWASA Yetu”, Mkuru-genzi wa Usimamizi wa Huduma za Majitaka, Mhandisi Lydia Ndibalema amesema uwepo wa mabwawa ya majitaka ni muhimu kwa mai-sha ya binadamu na baadhi ya viumbe hai, am-bao hutegemea katika uzalishaji na mmeng’en-yo wa majitaka.

Alisema Dawasa ina jumla ya mabwawa tisa ya majitaka yanayohudumia Jiji la Dar yali-yopo maeneo ya Lugalo, Mabibo, Mikocheni, Chuo Kikuu, Vingunguti, Kurasini, Airwing, Ukonga na Buguruni na huwekwa katika utara-tibu wa kuyasafisha mara kwa mara ili kupun-guza kiwango cha hewa chafu kwa jamii inayoi-shi jirani na mabwawa hayo.

“Mabwawa haya yamejengwa ili kucho-chea usafi wa mazingira kwa jiji la Dar es Sa-laam na yamewekwa katika utaratibu rafiki ambao unasaidia kuboresha usafi wa mazin-

gira kwenye kila eneo ambalo mabwawa haya yapo” alisema Mhandisi Lydia

Amesema mabwawa ya majitaka yana-hudumia wananchi wa namna mbili, wale waliounganishwa moja kwa moja kwenye mfu-mo wa Dawasa na wale wanaohifadhi kwenye chemba na kusubiri huduma ya kuja kuyamwa-ga kupitia njia ya magari.

“Kuna baadhi ya wananchi walioungan-ishwa moja kwa moja katika mfumo wa maji-taka ambapo hawalazimiki kuhifadhi majitaka katika makaro au chemba, bali yanakwenda moja kwa moja kwenye mfumo wetu, na kuna wale ambao wamehifadhi majitaka kwenye chemba maarufu kama “Septic” ambapo yaki-jaa hutumia huduma ya gari kumwaga katika mabwawa” aliongeza mhandisi Lydia

Aidha mhandisi Lydia amewasihi wananchi kulinda na kutunza miundombinu na mifumo ya majitaka ili yaweze kusaidia vizazi vya sasa na vijavyo.

“Wananchi wafuate sheria mbalimbali iki-wa ni pamoja na kutojenga karibu na mabwa-wa ya majitaka, kutotupa taka ngumu katika mashimo ya majitaka, kutoharibu au kuhujumu miundombinu ya majitaka ili tuweke Jiji letu safi na salama” alimalizia mhandisi Lydia.

Mabwawa ya Majitaka nikichochezi cha Usafi wa Mazingira

- Mhandisi NdibalemaKatika kuhakikisha inasogeza

huduma kwa wananchi, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imefungua ofisi mpya nne za kihuduma ambayo ni Ki-gamboni, Ukonga, Mkuranga na Kis-arawe.

Kuanzishwa kwa mikoa ya Kis-arawe na Mkuranga ni kutekeleza mabadiliko ya sheria ya kuongezeka kwa eneo la kihuduma kwa DAWASA lililotolewa na Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa.

Lengo la kuanzisha mikoa hiyo ni kuwafikia wanachi wengi waishio pembezoni mwa mji katika kutekele-za adhima ya kumtua mama ndoo kichwani chini ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jonh Pombe Magufuli.

Akizungumza na Dawasa Yetu, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja, amese-ma kuanzishwa kwa mikoa mipya ya kihuduma ni sehemu ya jitihada za ku-hakikisha Mamlaka inasogeza hudu-ma ya maji safi kwa wananchi wengi hasa wale wanaoishi pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam.

“Maeneo ambayo ofisi ya mkoa kazi wa Ukonga utakuwa ukitoa hudu-ma zake ni eneo la Pugu Matangini na ofisi ya Kigamboni itakuwa eneo la Gezaulole bustanini ikiwa ni hatua za kuboresha hali ya huduma ya maji kwa wananchi” amesema Mhandisi Luhemeja.

Ametoa wito kwa wananchi wa maeneo hayo kutembelea ofisi hizo ili kupata huduma ya maji na kufahamu mipango ya utekelezaji wa miradi ka-tika maeneo hayo.

DAWASA YAONGEZA MIKOA YA KIHUDUMA

DAR NA PWANI Mhandisi Luhemeja abainisha

mikakati ya utekelezaji

Moja ya mabwawa ya kuchakata majitaka lililopo Lugalo Jeshini, linalohudumia Kambi ya Lugalo.DAWASA ina jumla ya mabwawa saba ya majitaka katika Jiji la Dar es Salaam.

Page 16: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

16 | DAWASA YETU: TOLEO NA. 01

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

MRADI wa Maji wa Zingiziwa ni mradi uliosimamiwa na kutekelezwa na Mamla-ka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) katika Kata ya Chanika, Wilaya ya Ilala.

Chanzo cha maji kwa mradi huu ni kisi-ma kirefu cha maji safi chenye urefu wa mita 90 na kinachotoa maji ujazo wa lita 31,000 kwa saa. Mradi huu umehusisha uchimbaji na ulazaji wa bomba za usambazaji maji ze-nye ukubwa wa inchi moja na nusu (1.5) hadi inchi tatu (3). Mtandao wa mradi huu ni Kilo-mita 5.2 (mita 5243) uliolazwa katika mitaa ya Zingiziwa na Ngobedi.

Mradi huu umehusisha ujenzi wa vituo nane (8) vya kuchotea maji vilivyopo mae-neo mbalimbali kama vile Shule za Msingi na Sekondari Zingiziwa na ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Ngobedi. Vituo vingine vime-jengwa maeneo ya pembezoni mwa mitaa ya Zingiziwa ili kunufaisha watu wengi Zaidi.

Mradi wa Maji Zingiziwa unategemea kunufaisha wakazi takribani elfu nne (4,000) na kuhudumia mitaa ya Zingiziwa na Ngobe-di.

Kabla Dawasa haijakarabati mradi huu, eneo la Zingiziwa halikuwa na chanzo cha uhakika wa huduma ya Maji.

Huduma ya maji ilitegemea zaidi visima vifupi vya watu binafsi vilivyokuwa na urefu wa kati ya mita ishirini (20) na visima hivi ha-vikuwa na maji salama kwa matumizi.

Mradi wa maji Zingiziwa wakamilika

Maji na Jamii>>

Page 17: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

DAWASA YETU: TOLEO NA. 01 | 17

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

Utekelezaji wa Mradi wa maji Jeti - Buza

Mradi wa Maji Pugu - Kisarawe

MRADI wa Jeti - Buza ni mradi un-aotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWA-SA) katika Wilaya ya Ilala.

Mradi huu huu unahusisha uchimbaji na ulazaji wa mabomba ya maji ya inchi 4 na Inchi 2 kwa urefu wa mita 7,500. Hadi sasa mabomba yenye urefu wa Kilomita 6.6 eneo la Jeti hadi Buza

Mradi utahudumia Kata za Vituka, Buza, Makangarawe, Mwanagati na seh-emu kidogo ya Kata ya Kiwalani

Mradi wa Jeti hadi Buza utahudumia wakazi wa maeneo ya Yombo, Vituka, Buza, Makangarawe, Machimbo, Sigara, Mji Mpya, Kivule, Mwanagati na Mashine namba 5 ya Maji.

Mradi wa maji wa Jeti - Buza unatege-mea kunufaisha wakazi takribani 173,810.

MRADI wa Pugu – Kisarawe ni mradi unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisa-fi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana kampuni ya ukandarasi kutoka China – China Henan International Cooperation Group Co Lim-ited katika Wilaya ya Ilala.

Mradi huu unahusisha ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji la ujazo wa lita milioni 2 pamoja na ulazaji wa mabomba ya in-chi 16 kwa urefu wa kilomita 13.5 kutoka Kisarawe kuelekea Pugu hadi Gongo la Mboto.

Kazi ya ujenzi wa tanki hilo umeanza ambapo linajengwa katika eneo la Pugu na utanufaisha wakazi wa maeneo ya Kis-arawe, Pugu, Gongo la Mboto, Airwing, Ukonga, Kigogo Fresh na Majohe.

Mradi wa maji Pugu - Kisarawe utagharimu kiasi cha Shilingi Sh 8.5 Bilioni hadi kukamilika kwake.

Miradi ya Maji>>

Maandalizi ya eneo kwa ajili ya ujenzi wa tanki la Maji litakalokuwa na uwezo wa kuhifadhi lita Milioni Mbili ukiendelea eneo la Pugu.

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

Page 18: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

Mradi wa Usambazaji Majikutoka Kiluvya hadi Mbezi - Makabe

Mradi wa Maji Nia Njema

MRADI wa maji wa usambazaji maji un-atekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Serikali ya India kupitia kam-puni ya Contractor Jain Irrigation System lim-ited katika Wilaya za Ubungo, Kinondoni na Bagamoyo.

Mradi huu unahusisha ujenzi wa matan-ki, pampu za kusukuma maji na ulazaji wa mabomba ya maji ya inchi 3”, 6”, 8”, 10”, 12”, 16” na 20” kwa urefu wa kilomita 906.5 katika wilaya za Ubungo, Kinondoni na Bagamoyo.

Hadi sasa mabomba yenye urefu wa Kilo-mita 312.46 yameshalazwa kutoka eneo la Ki-luvya hadi Mbezi Makabe.

Mradi wa usambazaji maji utahudumia Wilaya za Ubungo, Kinondoni na Bagamoyo.

Maeneo ambayo tayari yamenufaika na mradi huu ni Msakuzi, Kwembe, Malamba Mawili, Kwa Msuguli, Njeteni, Kibamba kwa Mangi, Kibamba Matembezi, Kibamba Cha-ma, Kibamba Shule, Kiluvya Madukani, Kilu-vya Kwa Komba, Gogoni, Kibamba Kwa Mwan-gi, Kibamba Hospital, Shule, Luguruni, Mbezi Makabe, Mbezi Mpakani, Goba.

Jumla ya wateja 9,900 wa Kiluvya hadi Mbezi Makabe tayari wameshanufaika na mradi.

MRADI wa Maji wa Nianjema ni mradi un-aotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) katika wilaya ya Bagamoyo.

Mradi huu unahusisha uchimbaji na ulazaji wa mabomba ya maji ya inchi 4 na Inchi 2 kwa urefu wa Kilomita 10. Hadi sasa mabomba yenye urefu wa Kilomita 6.6 yameshalazwa hadi eneo la Nianjema A hadi Nianjema C.

Mradi utahudumia Kata za Nianjema A, Nianjema C na Kimara Chang’ombe.

Tanki la Maji la Bagamoyo lenye ujazo wa lita milioni sita (6,000,000) litahudumia waka-zi wa Nia Njema hadi Kimara Chang’ombe. Kumalizika kwa Mradi huu kutanufaisha kaya takriban 1000.

18 | DAWASA YETU: TOLEO NA. 01

Tenki jipya la Kimbamba lililo na uwezowa kuhifadhi lita milioni 10 za maji

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

Miradi ya Maji>>

Page 19: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

DAWASA YETU: TOLEO NA. 01 | 19

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

Fuata njia hizikufanya malipoya huduma ya maji kwa simu

TTCL-PESA1. Piga *150*71#2. Chagua namba 4 Lipa Bili3. Chagua namaba 5 Malipo ya Serikali4. Weka namba ya malipo inayoanza

na 99104…..5. Ingiza kiasi cha Pesa6. Ingiza namba ya Siri7. Thibitisha Kiasi kwa malipo ya

Serikali 001001AIRTEL MONEY1. Piga: *150*60#2. Chagua namba 5 Lipa Bili3. Chagua namba 5 Malipo ya Serikali4. Ingiza namba 1 namba ya Malipo5. Weka namba ya malipo inayoanza

na 99104…….6. Ingiza kiasi cha pesa 7. Ingiza namba ya Siri8. Thibitisha Kiasi kwa malipo ya

Serikali 001001

TIGO PESA1. Piga *150*01#2. Chagua namba 4 lipa bili3. Chagua namba 5 malipo ya serikali4. Weka namba ya malipo inayo 991045. Ingiza kiasi cha pesa6. Ingiza namba ya siri7. Bonyeza moja kuthibithisha malipo

ya serikali

M-PESA1. PIGA *150*00#2. Chagua namba 4 Lipa kwa M-pesa3. Chagua namba 5 Malipo ya Serikali4. Ingiza namba 1 namba ya malipo5. Weka namba ya malipo inayoanza

na 99104…..6. Ingiza Kiasi cha Pesa7. Ingiza namba ya Siri8. Thibitisha kiasi kwa malipo ya

Serikali 001001 HALO PESA1. Piga *150*88#2. Chagua namba 5 Lipa kwa Halo pesa3. Chagua namba 7 Malipo ya serikali4. Weka namba ya malipo inayoanza

na 99104…..5. Ingiza kiasi cha malipo6. Ingiza namba ya siri kukamilisha

malipo7. Thibitisha kiasi kwa malipo ya

Serikali 001001

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

Page 20: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

20 | DAWASA YETU: TOLEO NA. 01

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

GAWIO:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Sh.bilioni 1.3 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA, Jenerali Davis Mwamunyange (wa pili kulia) katika Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma. Wana-oshuhudia ni Waziri wa Fedha, Spika wa Bunge na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja.

UTIAJI SAINI:Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akitia saini mkataba wa makubaliano wa uendelezwaji wa ujenzi wa Mradi wa Usambazaji Maji Kimbiji.

BONANZA: Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo akipata maelezo ya huduma ya maji kutoka kwa Meneja Mawasilia-no DAWASA, Everlasting Lyaro wakati wa tamasha la “Mama Lishe Kisarawe 2020” lililodhaminiwa na taasisi mbalimbali za serikali ikiwemo DAWASA.

HABARIPICHANAMATUKIO>>

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI: Sehemu ya wanawake watumishi wa DAWASA walioshiriki mchakato wa kuzalisha maji katika Mtambo wa Ruvu Chini wakati wa maadhimisho hayo.

Page 21: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

DAWASA YETU: TOLEO NA. 01 | 21

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

DAWASA imeendelea kutekeleza agizo la Serikali la kuhimiza un-awaji mikono kwa sabuni kwa maji tiririka. Ofisi zote za kihuduma za Mamlaka zimeweka utaratibu wa kunawa kwa wateja na watumishi pindi wanapoingia katika majengo.

Moja ya beseni la kisasa lililobuniwa na DAWASA kwa ajili ya wananchi kunawa mikono ili kujikinga na ugon-jwa wa corona.

Mwananchi wa eneo la Kipunguni A Wilaya ya Ilala akinawa mikono kama tahadhari ya maambukizi ya ugonjwa wa corona. Vifaa kinga (ddoo na sabuni) vimetolewa katika Jumuiya za Maji takriban 74 zinazosimamiwa na DAWASA.

Jumbe za tahadhari na namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona zinaendelea kutolewa na DAWASA kwa njia mbalimbali. Stika za tahadhari zimebandikwa kwenye vyombo vya moto vya Mamlaka ili kufikisha ujumbe kwa watu wengi zaidi.

MAPAMBANO DHIDI YA CORONA>>

Page 22: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

22 | DAWASA YETU: TOLEO NA. 01

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

HUDUMA ya majisafi kwa wakazi wa mji-ni Gairo katika mkoa Morogoro hivi sasa ni ya uhakika na inapatikana wakati wote. Haya ni matokeo ya kazi iliyofanywa na serikali kwa kununua mtambo wa kuchuja maji ili wanan-chi wapate huduma ya majisafi, salama na ya uhakika. Hatua hiyo imechukuliwa ili kuimar-isha huduma ya maji kwa wananchi baada ya idadi ya wakazi kuongezeka na mahitaji kuwa makubwa.

Awali, kabla ya hatua hii iliyochukuliwa, wakazi wa eneo hili walipata adha ya huduma ya majisafi, tatizo kubwa likiwa chumvi katika maji hivyo kushindwa kuyatumia kwa ma-tumizi mbalimbali ya nyumbani na shughuli nyingine za maendeleo. Hali ilivyokuwa ni dha-hiri kwamba upatikanaji wa majisafi na salama kwa wakazi wa mjini Gairo ilikuwa ni ya kutati-za na kuwa kilio cha muda mrefu.

Wenyeji wa eneo hili wanasema kuwa ili-wabidi kuacha shughuli nyingine za kuwain-gizia kipato hadi wapate maji. Ili kufanikisha hilo iliwalazimu kuamka saa nane usiku kuwahi foleni katika Maji ya Ubalozi”, ambayo yaliy-otolewa kwa utaratibu wa mgao ili kila mwa-nanchi apate kiasi kwa matumizi ya nyumbani.

Huduma hiyo ya maji maarufu kwa jina la “Maji ya Ubalozi ilitolewa kwa kufuata mzun-guko wa mabalozi, ambapo kila balozi alipata

Makala ya Mgeni>>

ikwamisha wananchi kuleta mabadiliko katika shughuli za maendeleo kama vile kilimo. Moja ya kazi muhimu katika eneo hili ni kilimo cha mazao ya biashara hususan mahindi, viazi vit-amu, maharage, mihogo na mazao mengine. Muda mwingi uliishia katika kutafuta maji.

Kuhusu jambo hili, Mkuu wa Wilaya ya Gai-ro, Bi. Siriel Shahidi Mchembe, anasimulia hilo kwa kusema shida ya maji mjini Gairo ilikuwa kubwa.

“Tatizo la maji lilileta mtafaruku kwa baadhi ya wanandoa, pia kuzorota kwa shu-ghuli mbalimbali za kiuchumi na maendeleo kwa wananchi. Wakazi wa hapa walitumia muda mrefu kutafuta huduma ya majisafi na salama” Mkuu wa Wilaya, Bi. Siriel anasema.

Anaongeza kuwa suala la maji hapa nchi-ni na mahali pengine ni mtambuka, kwa kuwa maji ni kichocheo kikubwa cha uchumi na maji huboresha afya za wananchi kwa matumizi ya kila siku.

Hata hivyo, kukamilika kwa mradi wa maji wa Gairo mjini, kwa kufunga mtambo wa kuondoa chumvi katika maji Gairo, hali ime-badilika kabisa na maisha ya wakazi wa Gairo kwa ujumla yamekuwa kama mapya. Huduma ya majisafi na salama ya uhakika imekuwa mkombozi kwa wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Bi. Siriel anase-

mara moja katika eneo lake na kila mwananchi mwenye makazi, alitakiwa kuchota ndoo tano au sita, ambazo kutokana na idadi ya watu na mahitaji bado zilikuwa hazitoshi. Pamoja na hilo, maji hayo yalitoka kwa muda mfupi kati ya saa mbili hadi tatu na yanapokatika ilibidi kusubiri mzunguko mwingine.

Maji hayo hayakuwa ya uhakika. Kaya moja iliweza kupata wastani wa ndoo tatu za maji katika mzunguko mmoja wa mgao.

Kero ya maji mjini Gairo, kwa wakati huo il-

Sh.50Gharama ya sasa ya ndoo ya

maji mpaka inafika nyumbani, wakati kabla ya mradi ilikuwa shilingi 500 hadi 1,000 kutege-

mea na umbali na muda...Sisi wakazi wa Gairo mjini,

hususan wakina mama tunapen-da kuipongeza na kuishukuru

sana serikali kwa kutubadilishia hali ya maisha, sasa tunaona

kama tumezaliwa upya baada ya kupata majisafi na salama, awali tulipata shida

kubwa ya majisafi...

Mtambo wa kuchuja maji wilayani Gairo. Hivi sasa huduma ya maji sio tatizo na kero ya maji chumvi imekwisha. Majisafi na salama yanapatikana muda wote. Pichani Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) akikagua namna ambavyo mtambo huo unavyofanya kazi hivi karibuni akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji mkoani Morogoro.

Upatikanaji Maji Mji wa Gairo sasa ni wa UHAKIKA

Page 23: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

DAWASA YETU: TOLEO NA. 01 | 23

Jarida la Habari, Taarifa na Utekelezaji wa Miradi kwa Wanachi na Wateja

Mwanzoni kabla ya mradi, maji yalikuwa ya mgao, hivyo hos-pitali ilikuwa inakosa maji kwa

siku mbili au tatu jambo ambalo lilikuwa ni changamoto katika utunzaji wa vifaa vya hospi-

tali na maabara, pia hata maji yalipopatikana, chumvi ilifanya vifaa kuharibika mapema au ku-fanyiwa matengezo kila wakati.

- Mganga Mkuu Dkt. Mfugale

ma serikali imemtua mama ndoo ya maji kichwani na kumuondolea ile adha ya kutafu-ta maji ambayo awali ilisababisha migogoro katika baadhi ya ndoa. Aidha, bajeti ya maji ya familia ambayo ilikua kubwa, sasa haipo. Awali majisafi mjini Gairo yaliuzwa kwa dumu moja la lita 20 kwa Sh.1,500/= hivyo kufanya maji kuwa kama anasa badala ya hitaji la msingi kwa kila mwananchi.

Hivi sasa huduma ya maji inapatikana kwa uhakika, na gharama ya dumu la lita 20 haizidi shilingi 50. Wananchi na wakazi wa mjini Gairo wanaona fahari baada ya Serikali kuondoa shi-da ya maji katika eneo lao. Ile adha waliyoku-wa wakiipata sasa haipo na imekuwa jambo la kusimulia.

Mohamedi Haji, mkazi wa Magoyeko Mamboya, ambaye anafanya kazi ya kuuza maji kwa kutumia mkokoteni, anasema kabla ya mradi, hali haikuwa nzuri na kwa wafanya-biashara wa maji kama yeye biashara ilikuwa ngumu. Hata hivyo, Mradi wa Maji wa Gairo mjini baada ya kukamilika, Haji anasema kuwa sio tu biashara imekua rahisi, pia ameweza kuingiza kipato na kununua kiwanja.

Naye wakala wa kuuza maji wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Gairo, Bw. Musa Elias anase-ma mwanzoni kulikuwa na changamoto kub-wa ya makusanyo ya pesa za huduma ya maji. “Baada ya mradi kukumilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi, makusanyo yame-ongezeka kutoka wastani wa siku wa shilingi 7,000 hadi shilingi 35,000” Elias anasema.

Aneth Moses, mkazi wa Gairo mjini, anase-ma kabla ya mradi wa maji mjini Gairo, ilikua adha sana kwa sababu gharama za ziada zilitu-mika kupata majisafi yakutosha.

“Unaamka saa nane usiku na unapata ndoo tano au sita tu za ubalozi, hivyo tulilazi-mika kutumia maji ya visima vilivyochimbwa kwa mikono, na havikuwa salama,” Aneth anasema na kuongeza kuwa maji hayo yalitu-mika kwa kufulia nguo, kuoga, na matumizi mengine ya nyumbani kama usafi wa vifaa na nyumba. Anashukuru kwa mradi kukamilika kwa sababu gharama zimepungua, ambapo sasa hivi ndoo ya maji inafikishwa nyumbani kwa shilingi 50 wakati kabla ya mradi ilikuwa shilingi 500 hadi 1,000 kutegemea na umbali na muda.

“Sisi wakazi wa Gairo mjini, hususan wakina mama tunapenda kuipongeza na kui-shukuru sana serikali kwa kutubadilishia hali ya maisha, sasa tunaona kama tumezaliwa upya baada ya kupata majisafi na salama tena yasiy-okuwa na ladha ya chumvi, awali tulipata shida kubwa ya majisafi,” Aneth Moses anasema.

Hilo linaungwa mkono na Afisa Mtendaji wa Kata ya Gairo, Bwana. Shanta Mwingira ambaye anasema hali ya maji kwa wakazi wa Gairo ilikuwa ni gumzo na kilio cha kila siku ila kwa sasa ni ukurasa uliofungwa. Mwingira ana-sisitiza kuwa huduma ya maji imeimarika na

Dkt. Mfugale anasema hivi sasa huduma ya maji imeboreka na inaridhisha, mazingira ya hospitali yameboreka kwa sababu maji yana-patikana wakati wote katika wodi na wagon-jwa hawapati usumbufu wa kufikiria kuhusu upatikanaji wa maji kwa kusafisha nguo au kuoga. Pia, nyumba za watumishi wa hospitali zina maji ya kutosha, hivyo kuwapa morali ya kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.

Mjini Gairo serikali imetumia kiasi cha shilingi bilioni 2.3 kununua mtambo wa kuchu-ja chumvi katika maji (Reverse Osmosis). Kazi ya kufunga mtambo katika mradi huu, ilifany-wa na Wakandarasi wa Kampuni ya Protecno Srl kutoka nchini Italia.

Mradi wa maji wa Gairo kukamilika kwake, kumeondoa adha ya huduma ya majisafi na salama kwa wakazi wa eneo hilo na maeneo jirani. Mradi umebadilisha maisha ya wana-nchi kwa kiasi kikubwa kama walivyoeleza wenyewe, na hilo ndilo lengo kuu la serikali kuwaletea wananchi maendeelo na wananchi kutumia fursa mbalimbali, kwa kufanya kazi za kujiingizia kipato.

Ni jambo muhimu kuelewa kuwa maji ni msingi wa maendeleo.

wananchi wanapata majisafi na salama na shu-ghuli za kiuchumi sasa hivi zinafanyika vizuri na kwa wakati.

Naye, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospi-tali ya Gairo, Dkt. Ezekiel Mfugale anasema mwanzoni kabla ya mradi, maji yalikuwa ya mgao, hivyo hospitali ilikuwa inakosa maji kwa siku mbili au tatu, jambo ambalo lilikuwa ni changamoto katika utunzaji wa vifaa vya hos-pitali na maabara, na hata maji yalipopatikana, chumvi ilifanya vifaa kuharibika mapema au kufanyiwa matengezo kila wakati.

Utekelezaji Miradi ya Maji>>

Page 24: MRADI WA MAJI KIBAMBA - KISARAWE: DAWASA YATEKELEZA … · baada ya serikali kufuta lililokuwa Shirika la Majis-afi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) na ku-unganisha shughuli zake

TUNAJIZATITI KUBORESHA HUDUMA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA DAR ES SALAAM NA PWANI