maelezo kuhusu hakijamii. · nchini kenya halijatokana na ukosefu wa sheria za ardhi pekee. sababu...

12
MWONGOZO WA HALI HALISIA TARATIBU ZA KUFURUSHA WATU KUAMBATANA NA SHERIA ZA ARDHI 2016

Upload: others

Post on 30-Aug-2019

9 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Maelezo Kuhusu Hakijamii. · nchini Kenya halijatokana na ukosefu wa sheria za ardhi pekee. Sababu tatu za kimsingi za watu kuhamishwa nchini Kenya zinajumuisha: (1) Migogoro dhidi

MWONGOZO WA HALI HALISIA

TARATIBU ZA KUFURUSHA WATUKUAMBATANA NA SHERIA ZA ARDHI 2016

Maelezo Kuhusu Hakijamii.

Kuhusu Haki jamii

Hakii jamaii ni shirika lisilo la kiserikali linalotetea haki za binadamu na lililoasisiwa mwaka wa 2004. Hakii Jamii hushugulikia jamii zilizotengwa kutetea haki zao za uchumi na jamii ili kuimarisha uwezo wao wa kukidhi maisha yao. Dhamira yetu ni kuhakikisha ulinzi na uimarishaji wa haki za kila mtu.

Shirika hili lililosajiliwa kama shirika lisilo la kiserikali na chini ya sheria ya ya kushirikisha mashirika yasio ya kiserikali; linaongozwa na mkurugenzi ambaye husimamiwa na bodi ya wakurugeni. With a secretariat in Nairobi, Hakijamii has strategic community partners in Nairobi, Kisumu, Kitale, Eldoret, Garissa, Kakamega, Kisii, Migori, Homa Bay, Turkana, Lamu and Mombasa

Economic and Social Rights Centre (Hakijamii)53 Park Building, Along Ring Rd, off Ngong Rd

Sanduku la Posta: 11356 - 00100, Nairobi, KenyaSimu ya Rununu: +254 726 527876 +254 020 528 3496

Barua Pepe: [email protected] | Tovuti: www.hakijamii.com

© 2017. Haki zote zimehifadhiwa

Page 2: Maelezo Kuhusu Hakijamii. · nchini Kenya halijatokana na ukosefu wa sheria za ardhi pekee. Sababu tatu za kimsingi za watu kuhamishwa nchini Kenya zinajumuisha: (1) Migogoro dhidi

MWONGOZO WA HALI HALISIA

TARATIBU ZA KUFURUSHA WATU KUAMBATANA NA SHERIA ZA ARDHI 2016

Page 3: Maelezo Kuhusu Hakijamii. · nchini Kenya halijatokana na ukosefu wa sheria za ardhi pekee. Sababu tatu za kimsingi za watu kuhamishwa nchini Kenya zinajumuisha: (1) Migogoro dhidi

Economic and Social Rights Centre (Hakijamii)53 Park Building, Along Ring Rd, off Ngong Rd

Sanduku la Posta 11356 - 00100, Nairobi Kenya Simu ya Rununu: +254 726 527876 +254 020 528 3496;

Barua Pepe: [email protected] | Tovuti: www.hakijamii.com

© 2017, Haki zote zimehifadhiwa.

Wachapishaji watakubali ombi la kuchapisha sehemu ya mwongozo huu kwa nia ya kuhakikisha nakala hii imesambazwa kwa wale wanaohitaji.

Ili kuwasilisha ombi hilo wasiliana na:

MkurugenziEconomic and Social Rights Centre (Hakijamii)53 Park Building, Along Ring Rd, off Ngong Rd

P.O. Box 11356 – 00100, Nairobi Kenya

Designed & Printed By: Myner Logistics Ltd

Tel: +254 722 210 260 | 0722 917 290Email: [email protected]

Page 4: Maelezo Kuhusu Hakijamii. · nchini Kenya halijatokana na ukosefu wa sheria za ardhi pekee. Sababu tatu za kimsingi za watu kuhamishwa nchini Kenya zinajumuisha: (1) Migogoro dhidi

Mwongozo wa hali halisia iii

Yaliomo

Utangulizi 1

Historia ya kikatiba kuhusu taratibu za uhamisho katika

mabadiliko ya sheria za ardhi 2016 1

Taratibu za lazima wakati wa kufurusha watu 2

Uhamisho katika ardhi ya umma 3

Uhamisho katika ardhi ya jamii 4

Ardhi ya umma ni ipi? 4

Taratibu za kuhamisha watu katika ardhi isiyo sajiliwa 5

Taratibu za kuhamisha watu katika ardhi iliyosajiliwa 5

Taratibu za kuhamisha watu katika ardhi ya kibinafsi 5

Jinsi ya kushughulikia mali iliyosalia baada ya watu kufurushwa 6

Hitimisho 6

Page 5: Maelezo Kuhusu Hakijamii. · nchini Kenya halijatokana na ukosefu wa sheria za ardhi pekee. Sababu tatu za kimsingi za watu kuhamishwa nchini Kenya zinajumuisha: (1) Migogoro dhidi

Mwongozo wa hali halisia 1

Historia

Madhumuni makuu ya kurekebisha sheria za ardhi 2016 kati ya sheria nyengine,ni kutoa mwongozo wa kufurusha watu. Mabadiliko ya sheria za ardhi yaliegemea zaidi mswada wa tarataibu za kufurusha watu 2013 ambao hatimaye ulisalia kuwa sheria kamilifu kuhusu kufurusha watu. Sheria hizi zimebuniwa katika wakati mwafaka hasa ikifahamika kwamba tumekuwa na sheria za ardhi ambazo si kamilifu. Hata hivyo tatizo la watu kufurushwa nchini Kenya halijatokana na ukosefu wa sheria za ardhi pekee.

Sababu tatu za kimsingi za watu kuhamishwa nchini Kenya zinajumuisha: (1) Migogoro dhidi ya haki za kumiliki ardhi (2) Watu kukataa kulipa gharama ya juu ya kukodi nyumba au ardhi (3) Maendeleo ya miji .

HISTORIA YA KIKATIBA KUHUSU TARATIBU ZA UHAMISHO KATIKA MABADILIKO YA SHERIA ZA ARDHI

Lengo kuu la kutoa mwongozo kuhusu kufursha watu ni kutambua kwamba,kila mtu ana haki inayohitaji kuheshimiwa na kulindwa. Kadhalika kila mtu ana haki ya kupata makaazi katika mazingira safi.

Katiba ya Kenya chini ya muswada wa haki,imelinda haki za watu kupata makaazi katika mazingira safi. Ibara ya 10 ya maadili na kanuni za kitaifa kuhusu utawala imejumuisha jukumu la kulinda hadhi na haki za ya binadamu pamoja na haki za kimsingi zinazomlinda kutokana na ubaguzi na jamii zilizotengwa. Ibara ya 21inatoa jukumu kwa serikali ya kitaifa na idara zake kuweka mikakati ya sera na sheria mwafaka kuafikia malengo ya kuimarisha haki za kiuchumi na jamii, Kifungu cha 28 cha katiba kinatoa mwongozo kuhusu kulinda hadhi ya binadamu.

Kifungu hicho kinatoa taratibu zinazotoa mwongozo kuambatana na marekebisho ya sheria za ardhi. Sheria hii imeundwa katika wakati mwafaka ili kuelekeza jinsi ya kuendesha hatua ya kufurusha watu,wengi ambao wameachwa bila makao kutokana na dhulma. Sheria hii italinda jamii hasa zile zilizotengwa katika taratibu za uhamisho .

Sheria hii inatoa mwongozo maksusi kwamba uhamisho wowote utafanywa kuambatana na sheria iliyopo na taratibu zifuatazo.

Page 6: Maelezo Kuhusu Hakijamii. · nchini Kenya halijatokana na ukosefu wa sheria za ardhi pekee. Sababu tatu za kimsingi za watu kuhamishwa nchini Kenya zinajumuisha: (1) Migogoro dhidi

Mwongozo wa hali halisia2

Taratibu za lazima wakati wa kufurusha watu

(i) Wale watakaotekeleza hatua ya kufurusha watu wawe na vitambulisho vya kuwatambua

(ii) Idhini maalum iwasilishwe kabla hatua ya kufurusha watu au kuwahamisha

(iii) Maafisa wakuu serikalini au wawakilishi wanatakiwa kuwepo wakati wa kufurusha watu .

(iv) Hatua ya kuhamisha watu itekelezwe kuambatana na taratibu za kulinda haki za maisha ya watu na usalama wao

(v) Makundi maalum ya watu kama vile wanawake, watoto, wazee na watu walemavu yalindwe wakati wa kufurusha watu.

(vi) Mikakati ya kulinda mali ya watu na kuzuia uharibifu ifuatwe. (vii) Mikakati iundwe kuzuia uharibifu wa mali au mali inayosalia wakati

watu wanapofurushwa. (viii) Kuheshimu kanuni zinazodhibiti kufursha watu kwa kutumia

nguvu,kufuata mwongozo wowote wa kitaifa au kimataifa , unaoambatana na sheria za utekelezaji kuambatana na matakwa ya kuhifadhi haki za binadamu.

(ix) Watu walioathiriwa na hatua ya kuwafurusha wapewe nafasi ya kubomoa, kuokoa na kubeba mali yao.

Page 7: Maelezo Kuhusu Hakijamii. · nchini Kenya halijatokana na ukosefu wa sheria za ardhi pekee. Sababu tatu za kimsingi za watu kuhamishwa nchini Kenya zinajumuisha: (1) Migogoro dhidi

Mwongozo wa hali halisia 3

Uhamisho katika ardhi ya umma

Ardhi ya uma imetambuliwa katika katiba ya Kenya 2010 kifungu cha 62 (1)1 kama:

i) Ardhi inayotambuliwa kama ardhi ya serikali kutokana na sheria ya bunge iliyoidhinishwa wakati wa kupitishiwa kwa katiba mpya ya mwaka 2010;.

ii) Ardhi inayomilikiwa kisheria, inayotumiwa au ni makaazi ya idara za serikali isipokuwa ardhi ya serikali iliyokodishwa katika mkataba wa makubaliano ya kibinafsi ya kukodi ardhi.

iii) Kuhamishwa kwa ardhi kwa mikono ya serikali kupitia mauzo, kuregeshwa kwa miliki ya serikali au kubadilisha matumizi.

iv) Ardhi ambayo haimilikiwi na mtu binafsi au jamii kisheria. v) Arhdi ambayo mrithi wake hajatambuliwa kisheria; vi) Mali asili na madini ya mafuta kama yalivyotambulika kisheria. vii) Misitu ya serikali kando na misitu iliyotambuliwa chini ya kifungo cha

63 (2)(d)(i) , Hifadhi za misitu ya serikali,maeneo ya maji,mbuga za wanyama,hifadhi za serikali za wanyama na maeneo yote yaliolindwa.

viii) Barabara zote na njia zilizobuniwa kupitia sheria ya bunge.ix) Mito yote na maeneo ya maji kama inavyotambuliwa katika sheria ya

bunge.x) Ardhi ambayo haijatengwa kama ya kibinafsi au ya jamii chini ya katiba.

Tume ya kitaifa ya ardhi ina jukumu la kufanya maamuzi kuhusu kufurushwa kwa watu katika ardhi ya umma kuambatana na taratibu zifuatazo: i) Kupitia notisi ya gazeti la serikali miezi mitatu kabla tarehe ya

kuwafurusha :ii) Notisi katika gazette la kitaifa linalosambazwa kote nchini miezi mitatu

kabla tarehe ya kuwafurusha watu;iii) Kutolewa tangazo la radio kwa lugha ya jamii husika miezi mitatu kabla

ya tarehe ya kuwafurusha .

1 katiba ya Kenya 2010, http://www.icla.up.ac.za/images/constitutions/kenya_constitution.pdf ilitumika 6 machi 2017.

Page 8: Maelezo Kuhusu Hakijamii. · nchini Kenya halijatokana na ukosefu wa sheria za ardhi pekee. Sababu tatu za kimsingi za watu kuhamishwa nchini Kenya zinajumuisha: (1) Migogoro dhidi

Mwongozo wa hali halisia4

Uhamisho wa watu katika ardhi ya jamiiJe ardhi ya jamii ni ipi?

i) Ardhi ambayo imesajiliwa katika jina la kundi wakilishi chini ya sheria yeyote;

ii) Ardhi iliyohamishwa kwa jamii maalum kupitia taratibu za kisheria; iii) Ardhi yeyote iliyotangazwa kuwa ardhi ya jamii kupitia sheria ya bunge;iv) pia Ardhi ambayo:

a) Inamilikiwa kisheria,kusimamiwa na kutumiwa na jamii kama ardhi ya misitu,malisho au maeneo takatifu

b) Ardhi iliyorithiwa kutoka kwa mababu na ardhi inayomilikiwa na jamii za wawindaji au;

c) Ardhi iliyosimamiwa kisheria kwa amana na serikali ya kaunti , kando na ardhi ya umma inayoshikiliwa kwa amana na serikali ya kaunti.

Kuna taswira mbili kutokana na masuala haya:i) Notisi ya uhamisho wa watu katika ardhi ya jamii ambayo haijasajiliwa ii) Notisi ya uhamisho wa watu katika ardhi iliyosajiliwa.

Page 9: Maelezo Kuhusu Hakijamii. · nchini Kenya halijatokana na ukosefu wa sheria za ardhi pekee. Sababu tatu za kimsingi za watu kuhamishwa nchini Kenya zinajumuisha: (1) Migogoro dhidi

Mwongozo wa hali halisia 5

Taratibu za kuhamisha watu katika ardhi isiyo sajiliwa

Ardhi ya jamii ambayo haijasajiliwa husimamiwa kwa amana na serikali ya kaunti.

Ikiwa kutakua na maamuzi ya kufurusha watu,waziri wa seriali ya kaunti katika kamati ya ardhi ana jukumu la kuwafahamisha waathiriwa kuhusu hatua hiyo

Taratibu za kuhamisha watu katika ardhi iliyosajiliwa

Katika ardhi ya jamii iliyosajiliwa,anayesimamia kufurusha watu ni waziri wa serikali ya kaunti katika kamati ya ardhi, atatakiwa kufuata taratibu zifuatazo: i) Kupitia notisi ya gazeti la serikali miezi mitatu kabla ya kufurushwa. ii) Kuweka notisi katika gazette linalosamabzwa kote nchini miezi mitatu

iliyopitaiii) Tangazo la radio kwa lugha ya jamii miezi mitatu kabla kufurusha watu .

Taratibu za kuhamisha watu katika ardhi ya kibinafsi

Ikiwa mmiliki wa shamba la kibinafsi amekata kauli kwamba mtu au kundi la watu wanaishi katika ardhi yake bila ruhusa,mmiliki au msimamizi anatakiwa kutoa notisi kwa mtu au kundi la watu miezi mitatu kabla ya kuwafurusha. Hatua za kufurusha watu zifuatazo lazima zifuatwe;

Page 10: Maelezo Kuhusu Hakijamii. · nchini Kenya halijatokana na ukosefu wa sheria za ardhi pekee. Sababu tatu za kimsingi za watu kuhamishwa nchini Kenya zinajumuisha: (1) Migogoro dhidi

i) Notisi iandikwe kwa lugha ya kiswahili na kingereza. ii) Ikiwa waathiriwa ni wengi, notisi ichapishwe katika magazeti mawili

yanayosambazwa kitaifa na kuchapishwa katika maeneo tano katika ardhi hiyo ya kibinafsi.

iii) Notisi ieleze jinsi watakavyoshughulikia mijengo na mazao yeyote yaliyoko shambani na masuala yoyote kuambatana na kesi hiyo.

iv) Chapa ya notisi iwasilishwe kwa naibu kamishna wa kaunti anayesimamia eneo hilo pamoja na afisa mkuu wa polisi wa eneo hilo.

Jinsi ya kushughulikia mali iliyosalia baada ya watu kufurushwa

Afisa mwenye ujuzi kutoka afisi ya tume ya ardhi(NLC),serikali ya kaunti au mmiliki wa eneo binafsi au ardhi anahitajika baada ya siku saba, kufuatia hatua ya kufurusha watu,kuondoa mali yeyote kwa njia ya mnada kwenye ardhi binafsi au ya jamii.

Hitimisho

Kwa jumla, mwongozo wa kufurusha watu unaojumuisha sheria zilizorekebishwa za ardhi,umeundwa katika wakati mwafaka kuzuia dhulma dhidi ya waathiriwa. Kadhalika utapunguza uharibifu wa mali na kutoa suluhisho kwa mtu yeyote aliyeathiriwa kuelekea mahakamani kudai haki.

� Mtu yeyote ambaye amepokea notisi ya kufurushwa anaweza kutafuta haki mahakamani dhidi ya notisi hiyo. Mahakama kuambatana na mamlaka yake itaamua ikiwa mwathiriwa atalipwa fidia au njia mbadala ya kumpa afueni.

Mwongozo wa hali halisia6

Page 11: Maelezo Kuhusu Hakijamii. · nchini Kenya halijatokana na ukosefu wa sheria za ardhi pekee. Sababu tatu za kimsingi za watu kuhamishwa nchini Kenya zinajumuisha: (1) Migogoro dhidi

NOTES

Page 12: Maelezo Kuhusu Hakijamii. · nchini Kenya halijatokana na ukosefu wa sheria za ardhi pekee. Sababu tatu za kimsingi za watu kuhamishwa nchini Kenya zinajumuisha: (1) Migogoro dhidi

Mwongozo wa hali halisia8

MWONGOZO WA HALI HALISIA

TARATIBU ZA KUFURUSHA WATUKUAMBATANA NA SHERIA ZA ARDHI 2016

Maelezo Kuhusu Hakijamii.

Kuhusu Haki jamii

Hakii jamaii ni shirika lisilo la kiserikali linalotetea haki za binadamu na lililoasisiwa mwaka wa 2004. Hakii Jamii hushugulikia jamii zilizotengwa kutetea haki zao za uchumi na jamii ili kuimarisha uwezo wao wa kukidhi maisha yao. Dhamira yetu ni kuhakikisha ulinzi na uimarishaji wa haki za kila mtu.

Shirika hili lililosajiliwa kama shirika lisilo la kiserikali na chini ya sheria ya ya kushirikisha mashirika yasio ya kiserikali; linaongozwa na mkurugenzi ambaye husimamiwa na bodi ya wakurugeni. With a secretariat in Nairobi, Hakijamii has strategic community partners in Nairobi, Kisumu, Kitale, Eldoret, Garissa, Kakamega, Kisii, Migori, Homa Bay, Turkana, Lamu and Mombasa

Economic and Social Rights Centre (Hakijamii)53 Park Building, Along Ring Rd, off Ngong Rd

Sanduku la Posta: 11356 - 00100, Nairobi, KenyaSimu ya Rununu: +254 726 527876 +254 020 528 3496

Barua Pepe: [email protected] | Tovuti: www.hakijamii.com

© 2017. Haki zote zimehifadhiwa