moduli namba 2 uandaaji sahihi wa - forestry development...

19

Upload: others

Post on 19-Feb-2021

3 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • MODULI NAMBA 2

    Uandaaji sahihi wa kitalu cha miche

    MKULI

    MA WA MITI

  • ShukuraniKIJITABU HIKI KIMEANDALIWA KWA AJILI YA KUFIKISHA MAUDHUI YA TAALUMA YA NAMNA YA KUANZISHA NA KUENDELEZA BUSTANI YA MITI KWA MKULIMA MDOGO NA MKUBWA PIA.

    KIMEANDALIWA KWA MICHORO ZAIDI ILI KUMRAHISISHIA MSOMAJI KUJARIBU KILA KITU KWA USAHIHI ZAIDI. MARA BAADA YA KUKAMILIKA, KIMEPITISHWA KWA WADAU MBALIMBALI NA WATAALAMU WA MISITU ILI KUTOA UZOEFU NA UTAALAMU WAO ILI KUBORESHA UTOAJI WA MAFUNZO SAHIHI YA UANZISHWAJI NA UENDELEZAJI WA BUSTANI YA MITI HAPA TANZANIA.

    NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA TAASISI YA UENDELEZAJI WA MISITU TANZANIA HUSUSANI KITENGO CHA huduma kwa wakulima wa miti KWA KUWEZESHA KAZI HII KUKAMILIKA.

    PIA NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA WAFADHILI WA TAASISI HII AMBAO NI GATSBY NA dfid KWA KUWEZESHA KUFADHILI UANDAAJI WA KIJITABU HIKI.

    MWISHO, NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA BWANA JOSEPH MAKANZA KWA KUCHORA MICHORO na kusanifu KIJARIDA HIKI NA PIA SHUKURANI ZA PEKEE KWA BWANA HAMISI MALINGA NA GEORG STRUNDEN KWA USHAURI WA KITAALAMU KUHUSIANA NA MICHORO NA MAUDHUI yA KITABU HIKI.

    1

    Utangulizi

    Watafiti na wataalam wa misitu wanaamini kuwa watanzania wengi wamehamasika na wanapenda kilimo cha miti ya mbao.

    Moduli hii inatoa maelekezo ya namna ya kuzalisha miche bora itokanayo na kupanda mbegu bora, inatoa mafunzo ya namna ya upandaji mzuri wa mbegu na uanzishaji mzuri wa mashamba ya miti.

    Inatoa mwongozo kwa wenye bustani za miti ili nao watoe mafunzo ya namna ya upandaji mzuri kwa wanunuzi wa miche. Hatua zilizoelezewa humu zinahusisha uandaaji kwa mbegu za Milingoti na Paina pia.

    Moduli hii itatueleza kisa cha MACHOKODO aliyenufaika kwa Kilimo cha Miti baada ya kujifunza na kutumia utaalam alioupata kutokana na mafunzo kujitengenezea faida na kubadili Maisha yake.

  • 1. MAANDALIZI YA KUWATIKA MBEGU

    2

    HAKIKISHA UNATUMIA MBEGU BORA KWA KUWA ZITAKUPA UKUAJI WA HARAKA NA KUKUPA KIPATO KWA MUDA MFUPI. BUSTANI NZURI BILA MBEGU BORA HAINA FAIDA KABISA.

    Unapotaka kuwatika MBEGU Chagua eneo ambalo linafaa kwa kutengeneza tuta la kusia mbegu ambalo lina mteremko, jua kidogo NA ULINZI KUHAKIKISHA MICHE AIHARIBIWI

    Pima eneo ambalo ni msitatili KWa futikamba.

    Pima kama futi 4 kwa futi 10 au zaidi kulingana na miche unayotaka kuzalisha.

  • JUU YAKE WEKA KAMA INCHI 2”-3” ZA MCHANGA WA KAWAIDA...MCHANGA JUU YA TUTA LA KUOTESHEA HUSAIDIA KATIKA UOTAJI WA MBEGU NA HURAHISISHA UNG’OAJI WA MICHE WAKATI WA KUHAMISHA MICHE KWENDA KWENYE VIRIBA

    Weka sawa udongo kwa kutumia rake na kupigapiga udongo ili ulainike. Pia toa mawe, magugu na vijiti kwenye hilo tuta lenye sura ya kitanda

    3

    Lima kwa kuinua tuta lenye urefu tajwa AU PIGILIA MABANZI NA JAZA UDONGO. Sawazisha kwa kutumia jEMBE AU mpini wa jembe au ubao ili kupata tuta lililo na sura ya kitanda.

  • EPUKA MAKOSA/ZINGATIA

    UsiwekE Mbolea ya samadi kwenye tuta la kuoteshea mbegu....Samadi huwa na vimelea wengi ambao huweza kuathiri uotaji wa mbegu. Samadi husababisha kuwepo na wadudu kama minyoo, funza na wadudu wengi ambao hukata mizizi ya miche na wadudu wengine hula mbegu kabla ya kuota na kusababisha hasara kubwa sana

    Weka mchanga juu ya tuta ili kurahisisha Uotaji wa miche...

    MCHANGA HUSAIDIA MBEGU KUOTA HARAKA, PIA HUSAIDIA UNAPOHAMISHIA KWENYE VIRIBA MCHANGA HUACHIA MICHE BILA KUNG’ANG’ANIA

    4

    INCHI 2-3 zA mchanga

    udongo

  • 2. KUSIA MBEGU KWENYE TUTA

    Mbegu za milingoti (Eucalyptus) ni ndogo ndogo sana, changanya mbegu na mchanga Kipimo 1 cha MLINGOTI na vipimo 3 vya mchanga kisha sambaza juu ya tuta

    Kwa mbegu za Paina chora vistari kwenye tuta na kuzimwaga bila kuchanganya na mchanga funika na mchanga kidogo.

    Mwagilia maji taratibu bila kusababisha udongo kutepeta kwa maji.

    Funika kwa nyasi KAVU kwa muda wa wiki moja (2) hadi tatu (3).... NYASI HUONGEZA JOTO KWA UDONGO NA KUSISIMUA UOTAJI WA HARAKA NA NYASI ZIONDOLEWE BAADA YA KUONA MAJANI MAWILI YAKIWA YAMEANZA KUTOKA KWA MBEGU ( KUOTA)

    mbegu mchanga

    5

  • Mwagilia mara mbili kwa siku vizuri, asubuhi na jioni.

    kumwagilia maji mpaka udongo unatepeta KUNAWEZA kusababisha ugonjwa wa ukungu (Fangasi), wadudu waharibifu kama minyoo, funza na panzi....

    Ukiona dalili zozote za magonjwa ya miche bustanini pata ushauri wa Mtaalamu wa Misitu ili akueleze ni dawa gani waweza kutumia

    ASUBUHI JIONI

    6

    baada ya wiki 3 Funika kwa nyasi kwa paa la mwinamo...

    KAMA ENEO LA BUSTANI LINA JUA KALI SANA FUNIKA MICHE KWA NYASI

    EPUKA MAKOSA/ZINGATIA

    usifanye hivi namna hivi

  • udongo wa msitunivipimo 3

    udongo wa mfinyanzi.vipimo 3

    mchanga.kipimo 1

    Udongo wa kujaza

    kwenye viriba.

    3. KUCHANGANYA UDONGO WA KUJAZA KWENYE VIRIBA

    Kwa Milingoti Weka:-

    7

    Kipimo: lori, tOLORI, beseni, DEBE

    Kwa Paina Weka :-

    udongo wa msituniVIPIMO 3

    udongo wa mfinyanzi.VIPIMO 3

    mchanga.KIPIMO 1

    Udongo wa kujaza

    kwenye viriba.UDONGO TOKA MSITU WA PAINA (MYCORRHIZA)

    KIPIMO 1

    Kipimo: lori, tOLORI, beseni, DEBE

  • Sasa unaweza kujaza Udongo kujaza kwenye viriba...

    KABLA YA KUANZA KUJAZA UDONGO KWENYE VIRIBA, NYUNYIZA MAJI UDONGO, UCHANGANYE UDONGO VIZURI, INGIZA VIDOLE VIWILI NDANI YA KIRIBA, JAZA UDONGO, SHINDILIA VIZURI KISHA PANGA KWENYE MISTARI. UKUBWA WA VIRIBA NI INCHI 3-4 KIPENYO NA UREFU NI INCHI 3

    8

    EPUKA MAKOSA/ZINGATIA

    Chekecha udongo ili kuondoa mizizi na takataka nyingine halafu changanya vizuri kabla ya kujaza kwenye viriba

    DOKEZO KUHUSU VIRIBA

    KILO MOJA YA PLASTIC NI SAWA NA VIRIBA TUPU 600 VYA INCHI 3 KWA 4. MCHANGANYO WA UDONGO TOLOLI MOJA NI SAWA NA VIRIBA 470

  • Ili kuhamisha miche Anzia kwenye kona YA TUTA KWA KUnyanyua udongo kwa kijiti, kisha ingiza mkono chini na inua mche au miche kadhaa mkononi.

    4. KUHAMISHIA MICHE KWENYE VIRIBA

    IWEKE MICHE HIYO KWENYE CHOMBO KAMA BAKULI IKIWA NA MAJI NA ANZA KUPANDIKIZA MICHE MMOJA KWA KILA KIRIBA

    9

    ...hamisha mche kutoka katika tuta la kusia mbegu kwenda kwenye viriba...

  • Panga viriba vilivyo na miche kwenye mstari eneo ambalo ni safi kama uwanja.

    MWAGILIA MICHE HIYO MARA MBILI KWA SIKU. MWAGILIA KILA SIKU ASUBUHI NA MAPEMA NA JIONI...TUMIA CHOMBO CHENYE MATUNDU MADOGO KUEPUSHA KUDHURU MICHE

    10

    Wakati wa Kuhamisha miche shika kwenye vijani viwili (coteledons) na usishike kwenye SHINA AU mizizi. Kwa kushika kwenye mizizi kunaweza kusababisha kufa kwa mche kwani... vidole huwa na chumvichumvi na mafuta ambavyo huDHURU mche.

    IKIWA UMECHELEWA KUOTESHA MICHE UNAWEZA KUONGEZA UKUAJI HARAKA BUSTANINI KWA KUPIGA MBOLEA YA NPK YA MAJIMAJI INAYOITWA BUSTA PAMOJA NA KUPIGA DAWA YA KUUA WADUDU WAHARIBIFU WA MICHE

  • EPUKA MAKOSA/ZINGATIA

    Epuka MIZIZI ILIYOJIKUNJA KAMA HERUFI (J)...TOBOA SHIMO LA KUTOSHA KWA KIJITI NA SI KWA KIDOLE, chomeka mchE halafu vuta juu kidogo ili mzizi usipinde

    11

    ...EPUKA KUMWAGILIWA MAJI MENGI SANA MPAKA MICHE INAZAMISHWA KWENYE MAJI

  • 5.KUPUNGUZA/KUKATA MIZIZIKata mizizi kila unapoona inaanza kuingia ardhini KWA KUtumia kisu kikali au waya....Au hamisha miche kila baada ya wiki mbili

    Hiki ni kitendo cha kuikomaza miche kwa kupunguza kiwango cha umwagiliaji maji ili ianze kuzoea hali ya shambani itakakopandwa

    6. KUIKOMAZA MICHE

    12

    mizizi haijakatwa

    mizizi imekatwa

    ng’oa magugu kwenye viriba

  • BAADA YA MIEZI SITA MICHE YAKO ITAKUWA TAYARI KWA KUPANDWA SHAMBANI AU KUUZA KWA MTEJA

    ...urefu unaofaa kwa kupandwa milingoti ni Sentimeta 20-25 na Mipaina ni sentimeta 10-15

    SABABU YA KUIKOMAZA MICHE NI KWA AJILI YA KUIANDAA MICHE KWA MAZINGIRA MAGUMU YA SHAMBANI NA PIA HII HUFANYIKA KWA MICHE ILIYOBAKI MPANDO WA MWAKA HUO NA KUSUBIRI HADI MPANDO WA MWAKA MWINGINE...

    KAMA NINATAKA KUANZISHA KITALU CHA KIBIASHARA MAMBO GANI YA KUZINGATIA?

    ZINGATIA ENEO LA BUSTANI LIWE NA CHOO, STOO, OFISI, MAJI YA KUNYWA. PIA TUNZA KUMBUKUMBU ZOTE ZA UZALISHAJI NA MAUZO.

    13

  • 14

    7. GHARAMA ZA KUKUZA NA KUUZA MICHE

    dr ULALO WA FAIDA NA HASARA CR

    MTAJI/ MAPATO MATUMIZI/ GHARAMA

    Mtaji wa fedha (Saccos) 5,000 Kununua reki 700

    Nyongeza ya mtaji 100,000 Kulipa vibarua 40,000

    Kununua viriba 14,000

    Kununua mbegu 50,000

    Mauzo ya miche 200,000 Kununua jembe 2,000

    Mauzo ya miche 50,000 Vibao vya kwenye matuta 500

    Mauzo ya miche 20,000 Kutengeneza bango 1,000

    Kununua makeni 3,000

    Kununua madawa 3,000

    Tofauti ( faida) 254,500

    JUMLA 375,000 JUMLA 375,000

    *angalizo: tarakimu zilizoandikwa hapa ni mfano tu.

    Ukiona matumizi ni makubwa kuliko MAPATO Ujue umefanya biashara kwa HASARA

    Ukiona Mtaji au mapato ni Makubwa kuliko matumizi ujue kuwa umefanya biashara kwa FAIDA. Jumlishia pembeni kwanza kisha jumla iliyo kubwa kati ya kulia na kushoto ndiyo iandikwe kwenye jumla kuu. Kisha kama kushoto ndio kudogo andika TOFAUTI HASARA au kama kulia ndio kudogo Zaidi hivyo juu ya jumla kuu andika TOFAUTI FAIDA

    kisha andika hiyo tofauti ili UWEKE UWIANO/ BALANSI.

  • 15

    Vigezo vya mahali sahihi pa kuweka bustani

    1. Mahali panapofikika vizuri kwa gari2. Mahali ambapo nguvukazi inaweza patikana

    kiurahisi3. Mahali ambapo pana maji ya uhakika4. Mahali ambapo hapana mteremko mkali5. Mahali ambapo rasilimali muhimu kama udongo

    vinapatikana mapema.6. maji kwa ajili ya umwagiliaji

    Mbegu bora maana yake nini?

    Ni mbegu zilizotokea kutoka kwenye miti iliyopandwa maalumu kwa ajili ya kuzalisha mbegu na kwamba Chavusha ( Poleni) hutoka katika uzao ambao ni bora na hufanywa kwa mikono ya wataalamu au wadudu toka katika miti ( Baba) yenye uzao mzuri.

    Vitu vya muhimu kuwepo katika bustani ya kibiashara

    1. Pawepo choo kwa ajili ya wafanyakazi na wageni2. Pawepo ofisi na stoo kwa ajili ya nyaraka na

    vifaa vya bustani3. Weka wigo kwa ajili ya kulinda miche yako4. Maji safi kwa ajili ya kunywa wafanyakazi na

    wageni bustanini5. Bango kwa ajili ya kutangaza biashara yako

    (Biashara matangazo)

  • Jedwali la Kalenda ya shughuli za bustani za miti

    SHUGHULI MUDA WA MWAKA

    1. Kuchagua eneo la kuweka bustani Mei

    2. Kuagiza/ kununua mbegu za Mipaina Mei na Juni

    3. Kuandaa bustani ya mipaina Juni

    4. Kukusanya udongo kwa ajili ya bustani Juni

    5. Kutengeneza tuta la kusia mbegu Juni

    6. Kuchanganya udongo kwa ajili ya

    kuweka kwenye viriba Juni/ Julai

    7. Kujaza udongo kwenye viriba Julai

    8. Kuhamisha miche kwenye viriba Julai

    9. Umwagiliaji wa miche iliyoko

    kwenye viriba Julai- Desemba

    10. Kuandaa bustani ya Milingoti Septemba

    11. Kutengeneza tuta la kusia

    mbegu za Milingoti Septemba

    12. Kuchanganya udongo kwa Septemba/

    ajili ya Milingoti Oktoba

    13. Kuhamisha miche kwenye viriba Oktoba

    14. Umwagiliaji wa miche iliyoko Oktoba/

    kwenye viriba Novemba

    15. Kung’oa magugu kwenye miche

    ya Milingoti na Mipaina Novemba

    16. Kukata Mizizi kwenye Mipaina

    na Milingoti Novemba

    17. Kukomaza miche Mipaina na Novemba/

    Milingoti Desemba

    18. Kupanda mashambani/ kuuza Desemba-

    Mipaina na Milingoti Februari

    16

  • FORESTRY DEVELOPMENT TRUSTUENDELEZAJ I M IS ITU TANZANIA

    2 0 B A L O Z I R O A D , G A N G I L O N G A , I R I N G A , P O B O X 2

    t : + 2 5 5 2 6 2 7 0 0 5 5 0 | I N F O @ F O R E S T RY- T R U S T. O R G