mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka 2019/20 - … wa maendeleo wa taifa 2019.20.pdf ·...
TRANSCRIPT
i
MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA
KWA MWAKA 2019/20
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20 ii
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20 iii
YALIYOMO
SURA YA KWANZA ..................................................................................................... 1
UTANGULIZI ................................................................................................................ 1
1.1. Rejea ................................................................................................................ 1
1.2. Maeneo ya Kipaumbele .................................................................................... 1
1.3. Dhima ya Mpango ............................................................................................. 2
1.4. Mawanda yaliyoongoza Mpango ....................................................................... 2
1.5. Ushirikishwaji wa Wadau .................................................................................. 2
1.6. Matokeo ya Utekelezaji wa Mpango 2019/20 .................................................... 3
1.7. Mpangilio wa Kitabu .......................................................................................... 3
SURA YA PILI .............................................................................................................. 4
HALI YA UCHUMI ........................................................................................................ 4
2.1. Utangulizi .......................................................................................................... 4
2.2. Mapitio ya Hali ya Uchumi................................................................................. 4
2.2.1. Uchumi wa Dunia .................................................................................. 4
2.2.1.1. Uchumi wa Nchi Zilizoendelea ................................................ 4
2.2.1.2. Uchumi wa Nchi Zinazoibukia na Zinazoendelea .................... 5
2.2.2. Uchumi wa Afrika na Kanda ................................................................. 5
2.2.2.1. Uchumi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki .................... 6
2.2.3. Uchumi wa Taifa ................................................................................... 6
2.2.3.1 Pato la Taifa na Ukuaji wa Uchumi ............................................ 6
2.2.3.2 Wastani wa Pato la kila Mtu ....................................................... 7
2.2.3.3 Mwenendo wa Mfumuko wa Bei Nchini ...................................... 8
2.2.3.4 Sekta ya Nje .............................................................................. 9
2.2.3.5 Sekta ya Fedha........................................................................ 10
2.2.3.6 Deni la Serikali ......................................................................... 12
2.3 Idadi ya Watu na Mabadiliko ya Maisha .......................................................... 13
2.3.1 Ongezeko la Idadi ya Watu ................................................................. 13
2.3.2 Mwenendo wa Viashiria vya Umaskini ................................................. 13
2.3.2.1 Umiliki wa Mali Zinazodumu..................................................... 14
2.3.2.2 Hali ya Upatikanaji wa Chakula Nchini ..................................... 15
2.3.2.3 Misaada kwa Kaya/Familia Maskini ......................................... 15
2.3.2.4 Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge
Tanzania .................................................................................. 15
SURA YA TATU ......................................................................................................... 17
MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO ............................................................... 17
3.1. Utangulizi ........................................................................................................ 17
3.2. Utekelezaji wa Bajeti na Mpango wa Maendeleo 2018/19 .............................. 17
3.2.1. Utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo .................................................... 17
3.2.2. Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ................................................... 17
3.2.2.1. Miradi ya Kielelezo ................................................................ 17
3.2.2.2. Kukuza Uchumi na Ujenzi wa Msingi wa Uchumi wa Viwanda
21
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20 iv
3.2.2.3. Kufungamanisha Maendeleo ya Viwanda na Maendeleo ya
Watu ........................................................................................ 33
3.2.2.4. Mazingira Wezeshi kwa Uendeshaji Biashara na Uwekezaji . 50
3.2.2.5. Kuimarisha Usimamizi wa Utekelezaji wa Mpango ................ 65
3.2.2.6. Maeneo Mengine Muhimu kwa Ukuaji wa Uchumi na Ustawi
na Taifa ................................................................................... 67
3.2.3. Miradi Iliyofuatiliwa katika Mwaka 2018/19 .......................................... 71
SURA YA NNE ........................................................................................................... 81
MIRADI NA SHUGHULI ZA KIPAUMBELE KWA MWAKA 2019/20 ........................... 81
4.1. Utangulizi ........................................................................................................ 81
4.2. Misingi na Shabaha za Ukuaji wa Uchumi ...................................................... 81
4.2.1. Misingi ya Mpango kwa Mwaka 2019/20 ............................................. 81
4.2.2. Shabaha za Ukuaji wa Uchumi ............................................................ 81
4.3. Miradi na Shughuli Zitakazotekelezwa ........................................................... 82
4.3.1. Miradi ya Kielelezo .............................................................................. 82
4.3.2. Kukuza Uchumi na Ujenzi wa Msingi wa Uchumi wa Viwanda ............ 84
4.3.2.1. Uzalishaji Viwandani ............................................................. 84
4.3.2.2. Utafiti wa Teknolojia na Bidhaa za Viwandani ....................... 85
4.3.2.3. Kilimo .................................................................................... 86
4.3.2.4. Mifugo ................................................................................... 91
4.3.2.5. Uvuvi..................................................................................... 92
4.3.2.6. Maliasili na Misitu .................................................................. 93
4.3.2.7. Madini ................................................................................... 94
4.3.3. Miradi ya Kufungamanisha Maendeleo ya Viwanda na Maendeleo ya
Watu.................................................................................................... 95
4.3.3.1. Elimu, Sayansi na Teknolojia ................................................ 95
4.3.3.2. Afya na Maendeleo ya Jamii ............................................... 102
4.3.3.3. Maji na Usafi wa Mazingira ................................................. 105
4.3.3.4. Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ................................ 106
4.3.3.5. Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ............................... 107
4.3.3.6. Hifadhi ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi ................ 107
4.3.4. Mazingira Wezeshi kwa Uendeshaji Biashara na Uwekezaji ............. 108
4.3.4.1. Miundombinu ...................................................................... 108
4.3.4.2. Ardhi na Maeneo ya Uwekezaji na Biashara ....................... 119
4.3.4.3. Huduma za Fedha .............................................................. 120
4.3.4.4. Utalii, Biashara na Masoko ................................................. 120
4.3.5. Kuimarisha Usimamizi na Utekelezaji wa Mpango ............................. 121
4.3.6. Maeneo Mengine Muhimu kwa Ukuaji wa Uchumi na Ustawi wa Taifa
.......................................................................................................... 123
4.3.6.1. Diplomasia ya Kiuchumi ...................................................... 123
4.3.6.2. Kuimarisha Ushiriki wa Sekta Binafsi .................................. 124
4.3.6.3. Mchango wa Mashirika na Taasisi za Umma ...................... 125
SURA YA TANO ....................................................................................................... 126
UGHARAMIAJI WA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA 2019/20 .................... 126
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20 v
5.1. Utangulizi ...................................................................................................... 126
5.2. Gharama za Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20 .............. 126
5.3. Vyanzo vya Mapato kwa Mwaka 2019/20 ..................................................... 126
5.3.1 Vyanzo vya Mapato ya Ndani ............................................................ 127
5.3.2 Vyanzo vya Mapato ya Nje ................................................................ 127
5.3.3 Uwekezaji wa Moja kwa Moja kutoka Nje ya Nchi ( FDI) .................. 127
5.3.4 Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ................................... 128
5.3.5 Vyanzo Bunifu ................................................................................... 128
SURA YA SITA......................................................................................................... 129
UFUATILIAJI, TATHMINI NA UTOAJI WA TAARIFA ................................................ 129
6.1. Utangulizi ...................................................................................................... 129
6.2. Malengo ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Mpango .............................................. 129
6.3. Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Mpango ................................................ 129
6.4. Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, 2016/17
– 2020/21 ...................................................................................................... 130
6.5. Mkakati wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Mpango wa Mwaka 2019/20 ............... 130
6.6. Utoaji Taarifa ................................................................................................ 130
6.7. Mgawanyo wa Majukumu katika Ufuatiliaji na Tathmini ya Mpango .............. 131
SURA YA SABA ....................................................................................................... 132
VIHATARISHI VYA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA KINGA ................................. 132
7.1. Utangulizi ...................................................................................................... 132
7.2. Vihatarishi vya Ndani na Mikakati ya Kukabiliana Navyo .............................. 132
7.3. Vihatarishi vya Nje na Mikakati ya Kukabiliana Navyo .................................. 133
KIAMBATISHO I:UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA
MWAKA 2018/19 .......................................................................................... 136
1
SURA YA KWANZA
UTANGULIZI
1.1. Rejea
Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2019/20 ni wa nne katika mfululizo wa mipango ya
kila mwaka ya kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano
2016/17 – 2020/21. Dhima ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano ni
Kujenga Uchumi wa Viwanda ili Kuchochea Mageuzi ya Uchumi na Maendeleo ya
Watu. Hivyo, Mpango huu unatekeleza vipaumbele vilivyoainishwa katika Mpango
wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambavyo ni: (i) Kujenga viwanda vya
kukuza uchumi na kuweka msingi wa uchumi wa viwanda; (ii) Kufungamanisha
ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu; (iii) Kuboresha mazingira wezeshi kwa
uendeshaji wa biashara na uwekezaji; na (iv) Kuimarisha usimamizi wa utekelezaji
wa Mpango.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2019/20 umezingatia Mkakati wa Utekelezaji wa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21. Mkakati huo
unaainisha hatua za utekelezaji na vigezo vya kupima ufanisi wa utekelezaji wa
miradi kwa mwaka husika; hatua za kuchukuliwa kuwezesha upatikanaji wa fedha;
mfumo wa usimamizi, ufuatiliaji na tathmini; na mfumo wa mawasiliano kwa nia ya
kuleta ufanisi katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa
Miaka Mitano. Aidha, Mkakati huo unatumika kama rejea kwa taasisi katika
kubainisha vipaumbele na hatua za utekelezaji katika Mpango na Bajeti kwa mwaka
husika. Vile vile, Mpango huu umejumuisha miradi mbalimbali ya kielelezo ikiwemo:
Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Standard Gauge; Kufua Umeme wa Maji Mto
Rufiji (MW 2,115); Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania; Ujenzi wa Bomba la
Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania); Kusomesha Kwa
Wingi Katika Fani Na Ujuzi Adimu na Maalum; na Uanzishwaji wa Kanda Maalum za
Kiuchumi.
1.2. Maeneo ya Kipaumbele
Vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2019/20 vinatokana na maeneo
manne ya kipaumbele ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17
– 2020/21 ambapo katika eneo la ukuzaji uchumi msisitizo umewekwa katika
viwanda vya uzalishaji wa bidhaa kwa kutumia malighafi kutoka nchini (pamba hadi
nguo, ngozi na bidhaa zake, dawa na vifaa tiba), Kilimo, Maliasili na Utalii, Madini,
Biashara na Uwekezaji. Katika eneo la maendeleo ya watu msisititizo umewekwa
katika Elimu, Afya, Maji, Utawala Bora, Mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi na
Ulinzi na Usalama. Katika eneo la kuboresha mazingira wezeshi kwa uendeshaji wa
biashara na uwekezaji msisitizo umewekwa katika kuboresha mazingira ya kufanya
biashara, miundombinu ya usafirishaji; ukuaji wa miji na majiji; Nishati; na Sayansi,
Teknolojia na Ubunifu. Katika eneo la kuimarisha utekelezaji wa mpango msisitizo
umewekwa katika kuboresha Ufuatiliaji na Tathmini; kuimarisha uandaaji wa miradi;
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 2
na kuimarisha upatikanaji na usimamizi wa rasilimali.
Miradi itakayotekelezwa katika maeneo hayo manne ya kipaumbele kwa mwaka
2019/20 imeainishwa katika sura ya nne ya kitabu. Katika maeneo haya manne ipo
miradi iliyopewa hadhi ya kuwa ya kielelezo ambayo utekelezaji wake unapewa
msukumo wa kipekee ili kusaidia kufikiwa kwa malengo ya Mpango.
1.3. Dhima ya Mpango
Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2019/20 umebeba dhima ya “Kujenga Uchumi wa
Viwanda ili Kuchochea Mageuzi ya Uchumi na Maendeleo ya Watu”
iliyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 –
2020/21 ambayo inajumuisha misingi ya mikakati yote miwili ya mageuzi ya kiuchumi
na kupunguza umaskini.
Serikali imeweka msukumo katika kuboresha mazingira wezeshi ili kuvutia
wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Kwa kuwa sekta binafsi ndio mhimili mkubwa
wa ukuaji wa uchumi hususan katika ujenzi wa viwanda, Serikali imeweka mfumo wa
kisera, kitaasisi na kisheria pamoja na kanuni zake ili kuweka mazingira wezeshi ya
kuongeza ushiriki wa Sekta Binafsi katika kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo.
1.4. Mawanda yaliyoongoza Mpango
Mawanda yaliyoongoza uandaaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2019/20 ni
azma ya kufikia malengo na mahitaji ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Mpango
wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21 na Mkakati wa
Utekelezaji wa mpango huo; Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya
Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015; na sera na malengo ya kisekta. Vile vile, Mpango
umezingatia makubaliano ya Kikanda (EAC, SADC na Agenda ya Maendeleo ya
Afrika ya mwaka 2063) na ya kimataifa kama vile Malengo ya Maendeleo Endelevu
ya mwaka 2030. Aidha, Mpango umezingatia mapitio ya hali ya uchumi kitaifa,
kikanda na kimataifa kwa mwaka 2018 na mwelekeo kwa mwaka 2019, na hali halisi
ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2018/19 na changamoto za
utekelezaji zilizojitokeza.
1.5. Ushirikishwaji wa Wadau
Uandaaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2019/20 umeshirikisha wadau
mbalimbali ambao ni Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na
Mashirika ya Umma na Sekta Binafsi. Aidha, Waheshimiwa Wabunge
walishirikishwa wakati wa maandalizi ya Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa
Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2019/20. Washirika wa Maendeleo walishirikishwa
kupitia majadiliano ya kufikia maeneo ya ushirikiano, ufadhili wa miradi mahsusi na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 3
misaada ya kisekta.
1.6. Matokeo ya Utekelezaji wa Mpango 2019/20
Utekelezaji wa Mpango huu utachochea azma ya Serikali ya ujenzi wa uchumi wa
viwanda na maendeleo ya watu. Matokeo yanayotarajiwa ni pamoja na: kuongeza
kasi ya ukuaji wa uchumi na utengamavu wa viashiria vya uchumi jumla; kuimarisha
utoaji wa huduma za jamii zikijumuisha huduma za maji, elimu, afya na umeme
vijijini; kuimarika kwa biashara na uwekezaji; na kuongezeka kwa ajira na kipato cha
wananchi na hatimaye kupungua kwa kiwango cha umaskini nchini.
1.7. Mpangilio wa Kitabu
Kitabu cha Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2019/20 kimepangwa katika sura saba
(7): Sura ya kwanza ni utangulizi; Sura ya pili inaainisha mapitio ya hali ya uchumi;
Sura ya tatu inahusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2018/19; Sura
ya nne inaainisha maeneo ya kipaumbele kwa mwaka 2019/20; Sura ya tano
inaelezea ugharamiaji wa Mpango; Sura ya sita inaainisha mfumo na utaratibu wa
ufuatiliaji, tathmini na utoaji taarifa za utekelezaji wa Mpango; na Sura ya saba
inabainisha vihatarishi vya utekelezaji wa Mpango na hatua za kukabiliana navyo.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 4
SURA YA PILI
HALI YA UCHUMI
2.1. Utangulizi
Sura hii inatoa muhtasari wa mapitio ya hali ya uchumi kwa mwaka 2018. Mapitio
haya yanajenga msingi wa Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2019/20. Viashiria
vilivyochambuliwa ni pamoja na Pato la Taifa, mwenendo wa mfumuko wa bei,
mwenendo wa sekta ya nje, mwenendo wa sekta ya fedha, hali ya umaskini na
mabadiliko ya idadi ya watu.
2.2. Mapitio ya Hali ya Uchumi
2.2.1. Uchumi wa Dunia
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ya Aprili 2019, Uchumi
wa dunia kwa mwaka 2018 ulikua kwa asilimia 3.6 ikilinganishwa na ukuaji wa
asilimia 3.8 mwaka 2017. Kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi kulitokana na
kushuka kwa ukuaji wa uchumi kwa nchi zilizoendelea na zinazoendelea
kulikotokana na sababu mbalimbali zikiwemo: kupungua kwa mahitaji ya bidhaa na
huduma kutoka nje; hali ya wasiwasi kuhusu kujitoa kwa Uingereza katika Jumuiya
ya Ulaya (Brexit); kushuka kwa kasi ya uwekezaji; msuguano wa kibiashara baina ya
China na Marekani, kudorora kwa soko la fedha kwa nchi za Argentina na Uturuki,
na mvutano wa kisiasa Mashariki ya Kati. Matarajio ni kuwa kasi ya ukuaji wa
uchumi wa dunia itapungua kidogo kufikia wastani wa asilimia 3.3 mwaka 2019
kutokana na kupungua kwa ukuaji wa nchi zilizoendelea, na hatimaye kuongezeka
kufikia wastani wa asilimia 3.6 mwaka 2020.
Mfumuko wa bei wa dunia uliongezeka na kufikia wastani wa asilimia 3.8 kutoka
wastani wa asilimia 3.1 mwaka 2017. Ongezeko hilo lilitokana na kupungua kwa
uzalishaji viwandani hususan, katika nchi zinazoendelea, majanga ya asili na
kulegezwa kwa sera za bajeti na fedha kwa baadhi ya nchi.
2.2.1.1. Uchumi wa Nchi Zilizoendelea
Mwaka 2018, ukuaji wa uchumi kwa nchi zilizoendelea ulipungua kufikia wastani wa
asilimia 2.2 kutoka asilimia 2.4 mwaka 2017. Hii ilitokana na kupungua kwa kasi ya
ukuaji katika ukanda wa Ulaya kutokana na: kupungua kwa shughuli za biashara na
walaji; kuongezeka kwa riba na kupungua kwa uwekezaji kutokana na sera za bajeti
za baadhi ya nchi wanachama kama vile Italia; na mchakato wa nchi ya Uingereza
kujitoa katika umoja wa Ulaya iliyopunguza uwekezaji na mauzo nje. Matarajio ni
ukuaji wa nchi zilizoendelea kuendelea kupungua kufikia wastani wa asilimia 1.8
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 5
mwaka 2019 na asilimia 1.7 mwaka 2020 kutokana na hatua za kuongezeka kwa
ushuru wa bidhaa katika nchi za Marekani na China, kutotabirika kwa matokeo ya
hatua za Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya na matokeo yake katika
uwekezaji na mitaji pamoja na kupungua kwa hatua za kibajeti za kusisimua uchumi
kwa nchi ya Marekani.
2.2.1.2. Uchumi wa Nchi Zinazoibukia na Zinazoendelea
Uchumi wa nchi zinazoibukia na zinazoendelea ulikua kwa wastani wa asilimia 4.5
mwaka 2018. Matarajio ni kuwa kasi ya ukuaji kwa nchi zinazoibukia na
zinazoendelea itapungua kufikia wastani wa asilimia 4.4 mwaka 2019 kutokana na
kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa China na mdororo wa uchumi kwa nchi
za Uturuki na Iran. Kwa mwaka 2020, matarajio ni kuimarika kwa kasi ya ukuaji
kufikia asilimia 4.8 kutokana na matarajio ya kuimarika kwa uchumi kufuatia
marekebisho ya sera za kiuchumi na kupungua kwa mivutano ya kibiashara na
kiuchumi kati ya Marekani na nchi hizo. Jedwali Na. 2.1 linaonesha mwenendo wa
ukuaji wa Pato la Dunia kwa mwaka 2017 na 2018 na matarajio kwa mwaka 2019 na
2020.
Jedwali 2.1: Ukuaji wa Pato Halisi la Dunia 2017 - 2018 na Matarajio 2019 –
2020
Kundi/Mwaka
Ukuaji Halisi (Asilimia) Matarajio (Asilimia)
2017 2018 2019 2020
Dunia 3.8 3.6 3.3 3.6
Nchi Zilizoendelea 2.4 2.2 1.8 1.7
Nchi Zinazoibukia na Zinazoendelea 4.8 4.5 4.4 4.8
Nchi Zinazoibukia Barani Asia 6.6 6.4 6.3 6.3
Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara 2.9 3.0 3.5 3.7
Chanzo: Shirika la Fedha la Kimataifa, Aprili 2019
2.2.2. Uchumi wa Afrika na Kanda
Wastani wa kasi ya ukuaji wa uchumi kwa upande wa nchi za Afrika, Kusini mwa
Jangwa la Sahara uliongezeka hadi asilimia 3.0 mwaka 2018 ikilinganishwa na
asilimia 2.9 mwaka 2017. Ukuaji huu ulitokana na kupanda kwa bei za bidhaa na
marekebisho ya sera za kiuchumi. Matarajio ni kuimarika kwa uchumi wa nchi za
Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara kufikia asilimia 3.5 mwaka 2019 na asilimia
3.7 mwaka 2020 kutokana na matarajio ya kuimarika kwa ukuaji wa nchi za Nigeria
na Angola pamoja na uzalishaji wa mafuta.
Wakati huo huo, mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara
ulipungua na kufikia wastani wa asilimia 8.5 kutoka wastani wa asilimia 11.0 mwaka
2017. Hali hii ilitokana na kuimarika kwa sera za fedha ikiwemo viwango imara vya
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 6
kubadilisha fedha na kuimarika kwa sera za matumizi.
2.2.2.1. Uchumi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Katika mwaka 2018, uchumi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ulikua kwa
wastani wa asilimia 5.6 ikilinganishwa na ukuaji wa wastani wa asilimia 4.8 mwaka
2017. Ukuaji huu ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na kuimarika kwa mavuno ya kilimo
yaliyoimarisha kiwango cha utoshelevu wa chakula pamoja na utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo ya kikanda na katika mataifa wanachama. Jedwali Na. 2.2
linaonesha mwenendo wa ukuaji halisi wa Pato la Taifa kwa Nchi za Afrika Mashariki
kuanzia mwaka 2015 hadi 2018 na matarajio ya mwaka 2019 hadi 2020.
Jedwali 2.2: Ukuaji Halisi wa Pato la Taifa kwa Nchi za Afrika Mashariki; 2015 –
2018 na Matarajio ya Ukuaji 2019 na 2020
Nchi/Mwaka Ukuaji Halisi (Asilimia) Matarajio (Asilimia)
2015 2016 2017 2018 2019 2020
Tanzania 6.2 6.9 6.8 7.0 7.1 7.3
Kenya 5.6 6.0 4.8 6.0 5.8 5.9
Uganda 4.8 4.9 4.5 6.2 6.3 6.2
Rwanda 6.9 6.0 6.1 8.6 7.8 8.1
Burundi -4.0 -0.5 2.0 0.1 0.4 0.5
Wastani 3.9 4.7 4.8 5.6 5.5 5.6
Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)
2.2.3. Uchumi wa Taifa
2.2.3.1 Pato la Taifa na Ukuaji wa Uchumi
Katika mwaka 2018, Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu ilifanya maboresho ya
takwimu za Pato la Taifa kwa kutumia mwaka 2015 kama mwaka wa kizio kutoka
mwaka wa kizio wa 2007. Maboresho hayo yalifanyika ili kuzingatia mabadiliko
yaliyotokea kwenye uchumi kutokana na mageuzi ya kiuchumi, kijamii na
kiteknolojia. Kutokana na maboresho hayo, yapo mabadiliko kadhaa yaliyojitokeza
ikiwemo mfumo na ukubwa wa Pato la Taifa; viwango vya ukuaji na mchango wa
sekta mbalimbali katika Pato la Taifa; na uwiano wa viashiria mbalimbali kwa Pato la
Taifa.
Kwa mujibu wa takwimu za Pato la Taifa kwa kutumia mwaka wa kizio wa 2015,
Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 7.0 mwaka 2018 ikilinganishwa na
ukuaji wa asilimia 6.8 mwaka 2017. Shughuli za kiuchumi zilizokuwa na ukuaji
mkubwa ni pamoja na: sanaa na burudani (asilimia 13.7); ujenzi (asilimia 12.9);
usafirishaji na uhifadhi mizigo (asilimia 11.8); na shughuli za kitaaluma, sayansi na
ufundi (asilimia 9.9). Sekta ya kilimo inayoajiri zaidi ya asilimia 65 ya watanzania
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 7
ilikua kwa wastani wa asilimia 5.3 ambapo shughuli za kilimo cha mazao zilikua kwa
asilimia 5.0, mifugo asilimia 4.9, misitu asilimia 4.9, uvuvi asilimia 9.2 na huduma
saidizi katika shughuli za kilimo asilimia 5.1. Kielelezo Na. 2.1 kinaonesha
mwenendo wa ukuaji wa Pato la Taifa kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2018.
Kielelezo Na.2.1: Mwenendo wa Ukuaji wa Pato Halisi la Taifa katika Mwaka
2013 hadi 2018
Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu
2.2.3.2 Wastani wa Pato la kila Mtu
Mwaka 2018 Pato la Taifa kwa bei za miaka husika lilikuwa shilingi milioni
129,364,353 ikilinganishwa na shilingi milioni 118,744,498 mwaka 2017. Aidha,
mwaka 2018, Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa na watu 52,619,314 ambapo Pato la
wastani la kila mtu lilifikia Shilingi 2,458,496 ikilinganishwa na Shilingi 2,327,395
mwaka 2017 sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 5.6. Kiasi hicho cha Pato la
wastani kwa kila mtu kwa mwaka 2018 ni sawa na dola za Marekani 1,090
ikilinganishwa na dola za Marekani 1,044 mwaka 2017, sawa na ongezeko la
asilimia 4.4. Kielelezo Na. 2.2 kinaonesha mwenendo wa wastani wa Pato la kila
mtu kwa mwaka 2014 hadi 2018.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 8
Kielelezo Na 2.2: Mwenendo wa Wastani wa Pato la Kila Mtu (2014 - 2018)
Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu
2.2.3.3 Mwenendo wa Mfumuko wa Bei Nchini
Katika mwaka 2018 na robo ya kwanza ya mwaka 2019, mwenendo wa mfumuko
wa bei nchini uliendelea kuwa tulivu katika wigo wa tarakimu moja kutokana na
kuimarika kwa hali ya upatikanaji wa chakula nchini na nchi jirani. Katika kipindi
hicho, mfumuko wa bei ulipungua kutoka wastani wa asilimia 4.0 Januari 2018 na
kufikia asilimia 3.4 Juni 2018 na kuendelea kupungua zaidi kufikia asilimia 3.2 Aprili
2019. Mwenendo wa mfumuko wa bei za chakula ulipungua kutoka wastani wa
asilimia 9.6 Januari 2018 kufikia asilimia 2.3 Januari 2019 na kuongezeka kidogo
kufikia asilimia 2.7 Aprili 2019. Aidha, mfumuko wa bei za nishati uliongezeka kutoka
wastani wa asilimia 10.5 Januari 2018 hadi asilimia 15.7 Januari 2019, na hatimaye
kupungua kidogo kufikia wastani wa asilimia 13.2 Aprili 2019.
Kielelezo Na. 2.3: Mwenendo wa Mfumuko wa Bei (Aprili 2017 – Aprili 2019).
0.0
5.0
10.0
15.0
20.0
25.0
Asilimia
Mfumuko wa Bei Mfumuko wa Bei za Chakula Mfumuko wa Bei za Nishati
Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 9
Hivyo, katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2018 wastani wa mfumuko wa bei
ulikuwa asilimia 3.5 ikilinganishwa na asilimia 5.3 kipindi kama hicho mwaka 2017.
Vile vile, katika kipindi hicho wastani wa mfumuko wa bei za vyakula ulikuwa asilimia
3.7 ikilinganishwa na asilimia 9.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2017 na wastani
wa mfumuko wa bei za nishati ulikuwa asilimia 17.3 ikilinganishwa na wastani wa
asilimia 10.5 mwaka 2017. Ongezeko la mfumuko wa bei za nishati lilitokana na
kupanda kwa bei za nishati hususan mafuta katika soko la Dunia.
Mfumuko wa Bei kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Nchi Jirani
Mwenendo wa mfumuko wa bei katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2018 katika
nchi za ukanda wa Afrika Mashariki umeendelea kuwa tulivu katika wigo wa tarakimu
moja. Katika kipindi hicho, wastani wa mfumuko wa bei kwa Tanzania ulikuwa
asilimia 3.5, Kenya asilimia 4.7, Uganda asilimia 2.6 na Zambia asilimia 7.5.
Mwenendo huu ulitokana na hali nzuri ya hewa iliyochangia ongezeo la mavuno ya
mazao ya chakula katika ukanda huo na utekelezaji wa sera za fedha na bajeti. Hadi
Aprili 2019, mfumuko wa bei kwa Tanzania ulifikia asilimia 3.2, Kenya asilimia 6.6,
Uganda asilimia 3.5 na Zambia asilimia 7.7.
Jedwali Na. 2.3: Mfumuko wa Bei katika Nchi za Afrika Mashariki na Nchi Jirani
kwa Mwaka 2018
Jan Feb March Apr May Jun July Aug Sept Oct Nov Dec
Tanzania 4.0 4.1 3.9 3.8 3.6 3.4 3.3 3.3 3.4 3.2 3.0 3.3 3.5 5.3
Kenya 4.8 4.5 4.2 3.7 4.0 4.3 4.4 4.0 5.7 5.5 5.6 5.7 4.7 8.0
Uganda 3.0 2.1 2.0 1.8 1.7 2.1 3.1 3.8 3.7 3.0 3.0 2.2 2.6 5.2
Zambia 6 6.1 7.1 7.4 7.8 7.4 7.8 8.1 7.9 8.3 7.8 7.9 7.5 6.6
Rwanda 0.1 -1.3 -1.4 -0.1 1.8 1.4 0.6 0.6 -1.1 -3.4 -1.0 0.1 -0.3 8.3
Burundi 6 -1.3 -2.6 -1.7 -1.0 -0.4 -0.8 -2.3 -5.6 -8.4 -7.3 - -2.3 16.1
Wastani
Jan-Dec
2018
Wastani
Jan-Dec
2017
Mwaka 2018
Nchi/Mwezi
Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Taarifa za Nchi Husika.
2.2.3.4 Sekta ya Nje
(a) Urari wa Malipo
Katika kipindi cha mwaka ulioishia Aprili 2019, urari wa jumla wa malipo ulikuwa na
nakisi ya dola za Marekani milioni 1,089.2 ikilinganishwa na ziada ya dola za
Marekani milioni 299.2 katika kipindi kama hicho mwaka 2018. Hali hii ilisababishwa
kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa nakisi kwenye akaunti ya bidhaa, huduma,
kipato cha msingi na cha pili ambapo nakisi iliongezeka kwa dola za Marekani milioni
423.1 na kufikia dola za Marekani milioni 2,132.6 mwezi Aprili 2019.
Thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi katika kipindi cha Julai 2018
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 10
hadi Aprili 2019 ilifikia dola za Marekani milioni 7,210.6 ikilinganishwa na dola za
Marekani milioni 7,291.9 katika kipindi kama hicho mwaka 2018. Thamani ya bidhaa
na huduma zilizoagizwa kutoka nje ya nchi zilifika dola za Marekani milioni 9,024.9
ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 8,464.6 katika kipindi kama hicho mwaka
2018, sawa na ongezeko la asilimia 6.6. Ongezeko hili, kwa kiasi kubwa, lilitokana
na uagizaji mkubwa wa vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya reli, viwanja vya ndege,
bandari na barabara. Thamani ya uagizaji wa mafuta nayo iliongezeka hususan
kutokana na kupanda kwa bei katika soko la dunia. Aidha, uagizaji wa bidhaa za
chakula ulipungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kuongezeka kwa mavuno kipindi
cha msimu wa mwaka 2018/19. Kwa upande wa huduma, thamani ya malipo
kwenda nje ya nchi ilipungua na kufikia dola za Marekani milioni 1,709.3 mwezi Aprili
2019 ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 1,848.5 Aprili 2018 kutokana na
kupungua kwa malipo ya huduma za safari.
(b) Akiba ya Fedha za Kigeni
Akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha na kuendelea kukidhi
mahitaji ya kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi, na pia kuongeza imani kwa
wawekezaji katika uchumi. Akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Marekani milioni
4,395.2 Aprili 2019, kiasi ambacho kinatosha uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka
nje ya nchi kwa kipindi cha takriban miezi 4.3. Kiwango hiki ni zaidi ya lengo la nchi
la kuwa na akiba ya kutosha kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi kwa muda wa
miezi 4.0.
2.2.3.5 Sekta ya Fedha
(a) Ujazi wa Fedha na Karadha
Hadi Aprili 2019, ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) uliongezeka hadi shilingi
bilioni 25,629.1 kutoka shilingi bilioni 24,433.8 katika kipindi kama hicho mwaka
2018, sawa na ongezeko la asilimia 4.9. Ukuaji huu ulikuwa sawia na mahitaji ya
uchumi kutokana na kuongezeka kwa kasi ya mzunguko wa fedha kufuatia
ongezeko la matumizi ya mifumo ya kielektroniki ya malipo ambayo imechochea
kupungua hitaji la kubeba sarafu.
(b) Mwenendo wa Sekta ya Benki
Sekta ya benki imeendelea kuwa imara, salama na yenye mtaji na ukwasi wa
kutosha zaidi ya kiwango kinachotakiwa kisheria. Hadi Aprili 2019, uwiano wa mtaji
wa msingi na rasilimali za benki ulikuwa asilimia 16.96 ikilinganishwa na asilimia
18.52 Aprili 2018, ukiwa juu ya kiwango cha chini kinachohitajika kisheria cha
asilimia 10.
Kiwango cha mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu ikilinganishwa na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 11
kiwango cha amana zinazoweza kuhitajika katika muda mfupi (liquid assets to
demand liabilities) kilifikia asilimia 33.60 Aprili 2019 ikilinganishwa na asilimia 39.11
na kukidhi kiwango cha chini kinachohitajika kisheria cha asilimia 20. Kwa upande
wa kiwango cha mikopo chechefu katika mabenki na taasisi za fedha, imeendelea
kupungua na kufikia asilimia 11.10 Aprili 2019 ikilinganishwa na asilimia 11.59 Aprili
2018. Aidha, Serikali kupitia Benki Kuu inaendelea na jitihada za kuhakikisha mikopo
chechefu inapungua ikiwa ni pamoja na kuhimiza na kuwezesha matumizi ya mfumo
wa upashanaji taarifa za wakopaji (credit reference system).
(c) Mwenendo wa Mikopo kwa Sekta Binafsi
Mikopo kwa sekta binafsi iliendelea kuimarika kufuatia utekelezaji wa sera ya fedha
ili kuongeza ukwasi kwenye uchumi pamoja na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na
Serikali kupitia Benki kuu katika kuchochea ongezeko la mikopo kwa sekta binafsi
ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo ya muda mfupi kwa benki za biashara, kushusha
riba ya mikopo kwa mabenki (discount rate) mwezi Agosti 2018 kutoka asilimia 9.0
hadi asilimia 7.0 pamoja na kununua fedha za kigeni kutoka katika benki za biashara
na taasisi za serikali. Kufuatia hatua hizo, ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi
umeendelea kuimarika na kufikia asilimia 10.6 Aprili 2019 ikilinganishwa na asilimia
0.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2018. Sehemu kubwa ya mikopo kwa sekta
binafsi imeendelea kuelekezwa katika shughuli binafsi/kaya ambazo zilipata wastani
wa asilimia 28.8 ya mikopo yote ikifuatiwa na shughuli za biashara zilizokuwa na
wastani wa asilimia 18.5 na shughuli za uzalishaji viwandani asilimia 11.3.
(d) Mwenendo wa Viwango vya Riba
Hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali kupitia Benki Kuu katika kuongeza
ukwasi kwenye uchumi zimechangia kwa kiasi kikubwa utulivu wa bei na riba katika
masoko ya fedha na benki za biashara. Katika kipindi cha Julai 2018 hadi Aprili
2019, riba ya siku moja katika soko la fedha baina ya benki za biashara (overnight
interbank cash market interest rate) imeendelea kuwa tulivu katika wastani wa
asilimia 3.18 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.67 katika kipindi kama hicho
mwaka 2017/18. Riba za dhamana za Serikali zilifikia wastani wa asilimia 8.07 katika
kipindi cha Julai 2018 hadi Aprili 2019 ikilinganishwa asilimia 7.75 katika kipindi
kama hicho mwaka 2017/18. Vile vile, riba za mikopo inayotolewa na benki za
biashara zilishuka na kufikia wastani wa asilimia 17.15 katika kipindi cha Julai 2018
hadi Aprili 2019 kutoka wastani wa asilimia 17.93 katika kipindi kama hicho mwaka
2017/18. Aidha, riba za amana za muda maalum zilifikia wastani wa asilimia 7.65
katika kipindi cha Julai 2018 hadi Aprili 2019 ikilinganishwa na wastani wa asilimia
9.51 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2017/18.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 12
(e) Mwenendo wa Thamani ya Shilingi
Mwenendo wa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani
umeendelea kuwa tulivu ambapo katika kipindi kinachoishia Aprili 2019, dola moja
ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa shilingi 2,300.9 ikilinganishwa na shilingi
2,270.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2018. Mwenendo huu ulitokana na
utekelezaji madhubuti wa sera ya fedha, usimamizi thabiti wa mapato na matumizi
ya Serikali, matumizi ya gesi asilia badala ya mafuta katika kuzalisha umeme na
baadhi ya viwanda nchini kuzalisha bidhaa ambazo awali zilikua zikiagizwa kwa
wingi kutoka nje ikiwemo vigae na marumaru. Kielelezo Na. 2.4 kinaonesha
mwenendo wa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani kwa kipindi husika.
Kielelezo Na. 2.4: Mwenendo wa Thamani ya Shilingi Dhidi ya Dola ya Marekani
Chanzo: Benki Kuu ya Tanzania
2.2.3.6 Deni la Serikali
Hadi Aprili 2019, deni la Serikali lilifikia shilingi bilioni 51,036.42 ikinganishwa na
shilingi bilioni 49,866.17 Aprili 2018. Kati ya kiasi hicho, deni la ndani lilifikia shilingi
bilioni 13,251.66 na deni la nje shilingi bilioni 37,784.76. Ongezeko la deni lilitokana
na kupokelewa kwa mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya
maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, madaraja ya juu na miradi ya barabara.
Aidha, kwa mujibu wa tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanywa Desemba 2018,
inaonesha kuwa nchi ina uwezo wa kukopa ndani na nje, na kulipa mikopo hiyo bila
kuwa na athari hasi kwenye ukuaji wa uchumi na msukosuko wa kifedha. Aidha,
katika kuhakikisha kuwa deni linaendelea kuwa himilivu, Serikali itaendelea kukopa
kutoka kwenye vyanzo nafuu na kuhakikisha mikopo inaelekezwa kwenye miradi
ambayo itachochea kasi ya ukuaji wa uchumi.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 13
2.3 Idadi ya Watu na Mabadiliko ya Maisha
2.3.1 Ongezeko la Idadi ya Watu
Idadi ya watu nchini imeendelea kuongezeka kwa wastani wa asilimia 3.1. Kwa
mujibu wa taarifa ya makadirio ya idadi ya watu ya Februari 2018, Tanzania Bara ina
watu 52,619,314 kwa mwaka 2018, ikijumuisha wanaume 25,741,567 na wanawake
26,877,747. Katika idadi hiyo, watoto wenye umri kati ya miaka 0 - 14 ni 22,998,096
(asilimia 43.7), miaka 15 - 64 ambao ndiyo nguvu kazi ni 27,957,929 (asilimia 53.1)
na miaka 65 na zaidi ni 1,663,289 (asilimia 3.1). Ongezeko la idadi ya watu linatoa
fursa ya ongezeko la nguvu kazi ya kutosha kwa ajili ya ujenzi wa uchumi, ajira na
kipato. Kwa upande mwingine, ongezeko hilo linatoa changamoto ya upatikanaji wa
ajira huduma za msingi za kijamii kama vile afya, elimu, maji, lishe na nishati. Aidha,
taarifa hiyo inaonesha kuwa umri wa kuishi kwa Tanzania bara umeongezeka kutoka
wastani wa miaka 62.2 mwaka 2013 hadi wastani wa miaka 64.9 mwaka 2018 na
unakadiriwa kuwa miaka 65.4 mwaka 2019.
Serikali inaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa ongezeko la idadi ya watu
linaendana na ongezeko la uzalishaji na ukuzaji tija katika uchumi. Juhudi hizo ni
pamoja na kuendelea kuimarisha huduma mbalimbali za jamii zikiwemo:
elimumsingi; mafunzo na huduma za afya; fursa za ajira; upatikanaji wa maji safi na
salama; miundombinu ya barabara; nishati; na uboreshaji wa nyumba na makazi.
2.3.2 Mwenendo wa Viashiria vya Umaskini
Mwenendo wa vishiria vya umaskini umeendelea kuwa wa kuridhisha ambapo,
Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa mwaka 2017/18 unaonesha kuwa
idadi ya watanzania waishio chini ya mstari wa umaskini wa mahitaji ya msingi na
mahitaji ya chakula umeendelea kupungua. Umaskini wa mahitaji ya msingi
umepungua kutoka asilimia 28.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia 26.4 mwaka 2017/18
ambapo, kwa maeneo ya vijijini umepungua kutoka asilimia 33.2 mwaka 2011/12
hadi asilimia 31.3 mwaka 2017/18 na kwa maeneo ya mijini umepungua kutoka
asilimia 21.7 mwaka 2011/12 hadi asilimia 15.8 mwaka 2017/18.
Vile vile, umaskini wa chakula umeendelea kupungua kufikia asilimia 8.0 mwaka
2017/18 ikilinganishwa na asilimia 9.7 mwaka 2011/12, ambapo kwa maeneo ya
vijijini umepungua kutoka asilimia 11.3 (2011/12) hadi asilimia 9.7 (2017/18) na kwa
upande wa mijini ulipungua kutoka asilimia 8.7 (2011/12) hadi asilimia 4.4 (2017/18).
Kielelezo Na. 2.5 kinaonesha mwenendo wa hali ya umaskini nchini.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 14
Kielelezo Na. 2.5: Mwenendo wa Hali ya Umaskini Nchini
2.3.2.1 Umiliki wa Mali Zinazodumu
Umiliki wa mali zinazodumu kama vile simu za mkononi, friji, pikipiki, magari, redio,
baiskeli na ardhi hutumika katika kutathmini hali ya umaskini katika ngazi ya kaya.
Tafiti mbalimbali zilizofanyika kati ya mwaka 2012 na 2017 zinaonesha kuwa idadi
ya kaya zinazomiliki simu za mkononi, pikipiki na baiskeli zimeongezeka kati ya
mwaka 2016 na 2017 ikiashiria kuwa kipato cha kaya kimeongezeka. Katika kipindi
hicho idadi ya kaya zinazomiliki simu za mkononi zimeongezeka kutoka asilimia 78.1
hadi asilimia 81.3, pikipiki kutoka asilimia 7.3 hadi asilimia 11.0 na baiskeli kutoka
asilimia 29.6 hadi asilimia 38.7.
Vile vile, kwa mujibu wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa mwaka
2007 na mwaka 2012 idadi ya watu wanaomiliki ardhi imeongeza kutoka asilimia
72.6 mwaka 2007 na kufikia asilimia 87.7 mwaka 2012. Jedwali Na. 2.4 linaonesha
kiwango cha umiliki wa samani/mali za kudumu kati ya mwaka 2012, 2016 na
mwaka 2017.
Jedwali Na. 2.4: Umiliki wa Mali Zinazodumu (Durable Goods)
Mwaka 2012 2016 2017
Simu za mkononi 63.4 78.1 81.3
Runinga 15.1 23.6 22.7
Pikipiki 4.9 7.3 11.0
Jokofu 3.1 8.3 7.4
Magari 2.5 2.1 2.8
Redio 61.4 56.5 49.1
Baiskeli 39.8 29.6 38.7
Ardhi 87.7 - -
Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 15
2.3.2.2 Hali ya Upatikanaji wa Chakula Nchini
Hali ya uzalishaji na upatikanaji wa mazao ya chakula nchini imeendelea kuimarika.
Tathmini ya uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2017/18 na hali ya
upatikanaji wa chakula kwa mwaka 2018/19 inaonesha kuwa uzalishaji wa mazao ya
chakula ulifikia tani 16,981,974. Kati ya kiasi hicho, tani 9,537,857 ni za mazao ya
nafaka na tani 7,354,117 ni za mazao yasiyo nafaka. Aidha mahitaji ya chakula kwa
mwaka 2018/19 ni tani 13,569,285 ambapo tani 8,627,273 ni mazao ya nafaka na
tani 4,942,012 ni mazao yasiyo nafaka. Mahitaji haya yakilinganishwa na uzalishaji
yanaonesha kuwa nchi ina ziada ya chakula ya tani 3,322,689 za mazao yote ya
chakula ambapo tani 910,584 ni za mazao ya nafaka na tani 2,412,105 ni za mazao
yasiyo nafaka. Kwa kuzingatia kigezo cha upimaji wa kiwango cha utoshelevu Taifa
lina kiwango cha utoshelevu wa chakula cha asilimia 124 kwa kipindi cha mwaka
2018/19 ikilinganishwa na asilimia 120 kwa mwaka 2017/18.
2.3.2.3 Misaada kwa Kaya/Familia Maskini
Serikali imeendelea na juhudi za kupambana na umaskini kupitia mpango wa
Kunusuru Kaya Masikini kwa lengo la kupunguza ukali wa maisha. Katika mwaka
2018, idadi ya kaya zilizoandikishwa zilikuwa 1,118,752 zikiwa na wanufaika
5,259,503 ambapo jumla ya Shilingi bilioni 931.7 zililipwa kwa kaya hizo kwa
Tanzania Bara na Zanzibar ikilinganishwa na Shilingi billioni 668.3 zilizolipwa kwa
kaya 1,100,000 zenye wanufaika milioni 5.1 mwaka 2017. Katika kipindi hicho, jumla
ya kaya maskini zilizotambuliwa zilikuwa 1,363,448 zikiwa na wanufaika 5,726,101.
Kwa upande wa ajira kupitia mradi wa ajira za muda, jumla ya Shilingi bilioni 119.085
zililipwa, ambapo kati ya hizo Shilingi bilioni 83.293 zililipwa kwa kaya za wanufaika
kama ujira wa kazi hizo.
2.3.2.4 Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge
Tanzania
Serikali imeendelea na hatua mbalimbali za kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali
za Mitaa katika urasimishaji wa rasilimali ardhi na biashara mijini na vijijini kupitia
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania
(MKURABITA). Katika mwaka 2018/19, vilianzishwa vituo saba (7) vya urasimishaji
na uendelezaji biashara (One Stop Business Formalization Centers) katika
Halmashauri za Wilaya za Bariadi, Urambo, Njombe, manispaa za Morogoro,
Singida na Mtwara pamoja na jiji la Tanga. Kufuatia uanzishwaji wa vituo hivyo,
wafanyabiashara 7,943 wamepatiwa mafunzo ya urasimishaji, uendeshaji na
uendelezaji biashara. Matokeo yaliyopatikana ni kama ifuatavyo:
(i) Wafanyabiashara 3,967 wamesajili majina ya biashara na kampuni saba (7)
zimeanzishwa katika halmashauri za Wilaya za Bariadi na Urambo kwa ajili ya
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 16
uendeshaji biashara na kuanzisha viwanda;
(ii) Kuongezeka kwa makusanyo ya ada za leseni za biashara kutoka shilingi
21,353,520 mwezi Julai 2018 hadi shilingi 42,166,780 Desemba 2018 katika
Wilaya ya Bariadi na kutoka shilingi 20,964,670 mwezi Februari 2018 hadi
shilingi 42,965,320 kwa Wilaya ya Urambo. Aidha, makusanyo katika
Manispaa ya Morogoro yameongezeka kutoka shilingi 568,814,883 mwaka
2017 hadi shilingi 654,370,575 mwaka 2018 kutokana na huduma za Kituo
cha biashara;
(iii) Kuongezeka kwa usajili wa majina ya biashara katika halmashauri ya Wilaya
ya Bariadi kutoka asilimia 3.3 Julai 2018 hadi asilimia 17.1 Desemba 2018 na
katika Halmashauri ya wilaya ya Urambo, usajili umengezeka kutoka asilimia
3.3 Februari 2018 hadi asilimia tano (5) Desemba 2018;
(iv) Kuongezeka kwa biashara zenye mitaji ya zaidi ya Shilingi 3,000,000 kutoka
asilimia 3.3 Julai 2018 hadi asilimia 26.0 Desemba 2018 katika halmashauri
ya mji wa Bariadi na katika wilaya ya Urambo kutoka asilimia nne (4) Februari
2018 hadi asilimia 10 Desemba 2018;
(v) Kuongezeka kwa wafanyakazi wenye mikataba ya ajira kutoka silimia 1.1
Julai 2018 hadi asilimia tisa (9) Desemba 2018 katika halmashauri ya mji wa
Bariadi na kutoka asilimia 1.5 Februari 2018 hadi asilimia 19 Desemba 2018
katika Wilaya ya Urambo;
(vi) Kuongezeka kwa ulipaji kodi kutoka asilimia 29.4 Julai 2018 hadi asilimia 68.9
Desemba 2018 katika halmashauri ya mji wa Bariadi na kutoka asilimia 19.4
Februari 2018 hadi asilimia 95 Desemba 2018 katika wilaya ya Urambo; na
(vii) Kuongezeka kwa wafanyabiashara wenye akaunti za benki kutoka asilimia
59.2 Julai 2018 hadi asilimia 63.7 Desemba 2018 katika halmashauri ya mji
wa Bariadi na kutoka asilimia 70 Februari 2018 hadi asilimia 82 Desemba
2018 katika halmashauri ya wilaya ya Urambo.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 17
SURA YA TATU
MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO
3.1. Utangulizi
Sura hii inawasilisha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka
2018/19, kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo,
changamoto zilizojitokeza na hatua zinazochukuliwa kukabiliana na changamoto
hizo.
3.2. Utekelezaji wa Bajeti na Mpango wa Maendeleo 2018/19
3.2.1. Utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo
Katika mwaka 2018/19, Serikali ilitenga Shilingi trilioni 12.01 kwa ajili ya miradi ya
maendeleo, zikijumuisha Shilingi trilioni 9.88 fedha za ndani na Shilingi trilioni 2.13
fedha za nje. Hadi Aprili 2019, jumla ya Shilingi trilioni 5.44 zilitolewa kwa ajili ya
kugharamia miradi ya maendeleo. Kati ya kiasi kilichotolewa, Shilingi trilioni 4.89 ni
fedha za ndani na Shilingi bilioni 547 ni fedha za nje. Kiasi hiki hakijumuishi fedha
zilizopelekwa moja kwa moja na Washirika wa Maendeleo kwenye miradi ya
maendeleo. Sehemu kubwa ya fedha za maendeleo zilielekezwa katika utekelezaji
wa miradi ya kufua umeme kwa kutumia nguvu ya maji Mto Rufiji (Shilingi bilioni
723.598), elimumsingi bila ada na mikopo ya elimu ya juu (Shilingi bilioni 616.9),
usambazaji wa umeme vijijini kupitia REA (Shilingi bilioni 269.314) na ununuzi na
uendeshaji wa ndege (Shilingi bilioni 238.82).
3.2.2. Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
3.2.2.1. Miradi ya Kielelezo
(a) Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Standard Gauge
Ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro (km 300) unaendelea ambapo
utekelezaji umefikia asilimia 48.9. Shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na: kutandika
km 30 za reli; ujenzi wa makalavati asilimia 55; ujenzi wa madaraja asilimia 42;
ujenzi wa daraja refu katikati ya Jiji la Dar es Salaam lenye urefu wa km 2.54 ambao
umekamilika kwa asilimia 63; na ukataji wa miinuko na ujazaji wa mabonde
umekamilika kwa asilimia 66. Kazi zinazoendelea ni pamoja na uwekaji wa nguzo
za mfumo wa umeme kwa ajili ya kuendeshea treni; na ujenzi wa stesheni za Dar es
Salaam, Pugu na Soga unaendelea.
Katika kipande cha Morogoro – Makutupora (km 422), utekelezaji wa mradi
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 18
umefikia asilimia 7.12 ambapo kazi zinazoendelea ni pamoja na: uthamini na uhakiki
wa mali za wananchi watakaopisha mradi; ukataji wa miinuko na ujazaji wa
mabonde; usanifu wa njia na ujenzi wa kambi za Kilosa na Ihumwa. Aidha, kazi ya
utafutaji fedha kwa sehemu za Makutupora – Tabora (km 295), Tabora – Isaka
(km 133) na Isaka – Mwanza (km 250) zinaendelea ambapo wawekezaji mbalimbali
wameonesha nia ya kufanikisha upatikanaji wa fedha na kushiriki katika ujenzi wa
vipande hivyo. Vile vile, Isaka – Rusumo (km 371), mapitio ya upembuzi yakinifu na
usanifu wa awali yamekamilika. Tabora – Kigoma, Kaliua – Mpanda na Uvinza –
Msongati (Burundi), upembuzi yakinifu unaendelea.
Shughuli zingine za utekelezaji wa mradi ni pamoja na: kusainiwa kwa mkataba wa
miezi 11 kuanzia Desemba 2018 kati ya Serikali kupitia TRC na TANESCO na
Kampuni ya Larsen & Tourbo (L&T) Construction kwa ajili ya ujenzi wa mfumo wa
umeme wa SGR ambapo kazi hiyo imeanza; kuendelea na taratibu za ununuzi wa
mabehewa, injini na mitambo itakayotumika kutoa huduma ya usafiri kwenye reli ya
Standard Gauge.
(b) Uboreshaji wa Shirika la Ndege Tanzania
Hatua iliyofikiwa ni: kupokelewa kwa ndege moja aina ya Boeing 787-8 Dreamliner
na mbili aina ya Airbus A220-300; kulipa sehemu ya gharama za ununuzi wa ndege
mbili aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na Bombadier Dash 8 Q400 zinazotarajiwa
kuwasili nchini kabla ya mwishoni mwa mwaka 2019; na malipo ya bima, gharama
za uendeshaji wa ndege, mafunzo ya marubani (51), wahandisi (14) na wahudumu
(66) pamoja na madeni ya Shirika la Ndege Tanzania. Aidha, shughuli nyingine
zilizofanyika ni pamoja na kuanza kwa ukarabati wa Karakana ya Matengenezo ya
Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
(c) Kufua Umeme wa Maji Bonde la Mto Rufiji - MW 2,115
Hatua iliyofikiwa ni: Kupatikana kwa mkandarasi wa mradi wa kufua umeme
utokanao na nguvu ya maji katika Mto Rufiji ambaye ni Kampuni ya Ubia kati ya
Arab Contractors na Elsewedy Electric S.A.E kutoka Misri ambapo mkataba wa
ujenzi umesainiwa na mkandarasi alikabidhiwa eneo la mradi mwezi Februari 2019
na kuanza utekelezaji wa kazi za awali. Kazi zilizokamilika ni: ujenzi wa
miundombinu wezeshi ikijumuisha njia ya kusafirisha umeme wa MW 8 yenye
msongo wa kV 33 kutoka Msamvu, Morogoro hadi eneo la mradi yenye urefu wa
kilomita 170; barabara za kiwango cha changarawe za Ubena Zomozi na Kibiti –
Mloka hadi eneo la mradi; mifumo ya maji; mawasiliano ya simu; na nyumba za
kuishi Mkandarasi. Vile vile, kulingana na mahitaji ya umeme wakati wa ujenzi,
TANESCO imeanza ujenzi wa njia ya pili ya umeme msongo wa kV 33 kutoka kituo
cha kupoza umeme cha Gongo la Mboto kupitia Kisarawe hadi eneo la mradi
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 19
urefu wa kilomita 245 itakayosafirisha umeme wa MW 22.
(d) Kituo cha Biashara na Huduma Kurasini
Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa: uthamini wa nyumba tatu ambazo awali
hazikufanyiwa uthamini; na mpango wa uendelelezaji wa eneo la mradi.
(e) Uanzishwaji wa Kanda Maalum za Kiuchumi
(i) Eneo Maalum la Uwekezaji Bagamoyo: Kazi zilizotekelezwa ni: kukamilika
kwa mpango kabambe wa kuendeleza eneo la hekta 175 lililotengwa kwa ajili
ya ujenzi wa kituo cha Teknolojia. Aidha, makampuni 12 yamepewa leseni
kwa ajili ya kujenga viwanda katika eneo la Bagamoyo SEZ.
(ii) Eneo Maalum la Uwekezaji Kigoma: Kazi zilizotekelezwa ni: kukamilika kwa
upembuzi yakinifu na Mpango Kabambe wa uendelezaji wa eneo (Master
Plan) na ugawaji wa viwanja kwa ajili ya kupewa wawekezaji; kuendeleza
miundombinu kwa kufungua barabara zenye jumla ya km 28.46 na kuweka
alama za mipaka 106; kupatikana kwa wawekezaji watatu ambao ni Next Gen
Solowazi Limited, Third Man Limited na SGC Investment Limited
watakaowekeza kwenye ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa jua,
ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki (asali) na ujenzi wa
kiwanda cha kuchakata zao la michikichi na ghala kwa mtiririko huo.
(iii) Eneo Maalum la Uwekezaji Mtwara: Kazi zilizotekelezwa ni: usanifu na
ujenzi wa barabara yenye urefu wa km 2.7 kufika eneo la mradi; na kuendelea
na maandalizi kwa ajili ya kuanza mradi ambapo mikataba ya utekelezaji kati
ya EPZA na waendelezaji wa miundombinu wezeshi (TARURA na
MTUWASA) inahakikiwa na Serikali ili makabidhiano ya rasilimali fedha
yafanyike.
(f) Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia – Lindi
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilisha Tathmini ya Athari za Mazingira na Kijamii - ESIA;
kukamilisha mpango wa uhamishaji wananchi watakaopisha mradi; kuanza kwa
majadiliano ya kimkataba (Host Government Agreement – HGA) baina ya Serikali na
wawekezaji na kuandaliwa kwa moduli ya kiuchumi (economic model) ya mradi.
(g) Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga
(Tanzania)
Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na majadiliano ya mkataba kati ya kampuni ya mradi
na Nchi Hodhi (Host Government Agereement – HGA); kuendelea na maandalizi ya
majadiliano ya Mkataba wa Ubia (Shareholding Agreement – SHA); na kukamilika
kwa tathmini ya fidia kwa maeneo ya kipaumbele (main camps and coating yard) na
eneo lote la mkuza.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 20
(h) Shamba la Miwa na Kiwanda cha Sukari Mkulazi I
Kazi zilizofanyika katika mradi huu ni pamoja na: kupatikana kwa kibali cha kutumia
maji ya mto Ruvu; kukamilika kwa michoro kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la maji
lenye ukubwa wa mita za ujazo milioni 15 na maandalizi ya eneo kwa ajili ya ujenzi
wa kiwanda. Aidha, mzabuni wa kutengeneza na kufunga mitambo ya kiwanda
amepatikana.
(i) Shamba la Miwa na Kiwanda cha Sukari Mbigiri – Mkulazi II
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa upembuzi yakinifu wa eneo la mradi; kuendelea
na ujenzi wa majengo ya kiwanda cha sukari; kuboresha miundombinu ya barabara
na majengo; na kupatikana kwa mzabuni wa kutengeneza na kufunga mitambo ya
kiwanda. Aidha, shamba lenye ukubwa wa hekta 1,158 kati ya hekta 3,500
limelimwa ambapo hekta 880 zimepandwa miwa.
(j) Kuongeza Rasilimali Watu Wenye Ujuzi Adimu na Maalumu kwa
Maendeleo ya Viwanda na Watu
(i) Wizara ya Nishati: hatua liyofikiwa ni kugharamiwa: mafunzo kwa vijana 24
katika fani za mafuta na gesi kwa ngazi za shahada ya uzamivu (3), shahada
ya Uzamili (19), na shahada ya kwanza (2); mafunzo muda mrefu kwa
watumishi 8 wa TPDC na mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi 50 wa
Wizara ya Nishati, PURA, EWURA, TRA na Timu ya Majadiliano ya mradi wa
LNG kuhusu usimamizi na uendeshaji wa miradi ya mafuta na gesi;
(ii) Wizara ya Madini: hatua liyofikiwa ni kupatiwa mafunzo ya muda mfupi na
mrefu watumishi 41 katika fani za Jiolojia, Jemolojia, Uhandisi migodi, na
utunzaji wa kumbukumbu na utafutaji wa madini. Kati ya hao, watumishi 14
wamehudhuria mafunzo ya muda mrefu katika ngazi ya Astahahada (1),
Shahada ya kwanza (1), Shahada ya uzamili (9), na Shahada ya uzamivu (3)
na watumishi 27 wamehudhuria mafunzo ya muda mfupi katika fani husika.
(iii) Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto: hatua
liyofikiwa ni kugharamiwa madaktari 311 kuendelea na masomo ya kibingwa
kna kuratibu mafunzo kwa wanafunzi 50 kupitia ufadhili kutoka Serikali ya
China kwenda China kusoma masomo ya udatari.
(iv) Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia: hatua liyofikiwa ni kuendelea
kudhamini mafunzo kwa wanafunzi madaktari 158 katika fani za ubobezi kwa
magonjwa ya damu na utoaji damu (1), Magonjwa ya utumbo na ini (2),
upasuaji wa utumbo na ini (3), Magonjwa ya figo (1), magonjwa ya kifua (1),
udaktari bingwa (102), ufamisia (6), uuguzi (14), afya ya jamii na mazingira,
menejimenti na taarifa za afya (28).
(v) Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili – MUHAS: hatua
liyofikiwa ni kuhitimu kwa wataalam 15 katika fani ya udaktari bingwa maalum
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 21
(Master of Science Super-specialty) kwa magonjwa ya: Moyo (4), ubongo na
mishipa ya fahamu (3), damu na utoaji damu (1), utumbo na ini (4), figo (2),
na njia ya mkojo (1). Vile vile, madaktari bingwa 131 wamehitimu mafunzo
katika fani mbalimbali zikiwemo udaktari bingwa katika huduma za usingizi,
magonjwa ya dharura na mahututi, mifupa na mivunjiko, watoto, radiologia,
upasuaji na njia ya mkojo. Kuhitimu kwa wataalam wengine 102 wasaidizi wa
madaktari bingwa katika Nyanja za sayansi ya uuguzi wa afya ya akili,
magonjwa mahututi na ajali, ukunga na afya ya akinamama, ufamasia, afya
ya jamii na mazingira, na sayansi ya menejimenti ya taarifa za afya. Aidha,
chuo kwa kushirikiana na Ubalozi wa China kimepeleka wataalam 18 nje ya
nchi kusomea ubingwa na ubobezi katika fani za upandikizaji figo, ini na
uboho (bone marrow).
(vi) Hospitali ya Mloganzila: hatua liyofikiwa ni kugharamiwa mafunzo kwa
watumishi 37 katika fani mbalimbali za kibingwa (NmeD) ambao wanaendelea
na masomo katika Chuo cha Muhimbili (MUHAS) na Bugando. Vile vile,
hospitali kwa kushirikiana na Serikali za China na Korea ya Kusini imepeleka
wataalam sita (6) katika nchi hizo kwa ajili ya mafunzo mbalimbali.
3.2.2.2. Kukuza Uchumi na Ujenzi wa Msingi wa Uchumi wa Viwanda
A. Uzalishaji Viwandani
(a) Kiwanda cha Kuunganisha Matrekta – TAMCO, Kibaha
Ujenzi wa Kiwanda kipya cha kuunganisha Matrekta unaendelea ambapo utekelezaji
umefikia asilimia 40. Vile vile, jumla ya matrekta 822 kati ya 2,400 aina ya URSUS
yameingizwa nchini kutoka Poland yakiwa katika vipande (semi knocked down). Kati
ya matrekta 822 yaliyoingizwa, Matrekta 571 yameunganishwa na matrekta 399
yameuzwa.
(b) Kuendeleza Kongane ya Viwanda TAMCO – Kibaha
Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kuandaa Mpango Kabambe (detailed Master Plan)
wa eneo la ekari 201.6 ili kuvutia uwekezaji. Eneo la ekari 77.41 limetengwa kwa ajili
ya Viwanda vya nguo na mavazi, ekari 60.23 zimetengwa kwa ajili ya viwanda vya
kuunganisha magari na mitambo na ekari 43.04 limetengwa kwa ajili ya Sekta ya
Viwanda vya Dawa za Binadamu na Vifaa Tiba. Kazi zingine ni pamoja na:
kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu
waenezao ugonjwa wa malaria, kiwanda cha kuzalisha vifaa tiba na kiwanda cha
vifungashio; kuendelea na ujenzi wa kiwanda cha chanjo za wanyama; kukamilika
kwa upembuzi yakinifu kwa ajili ya viwanda vya nguo na mavazi; na kuendelea na
ujenzi wa kiwanda cha betri za magari cha China Boda; ujenzi wa barabara yenye
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 22
urefu wa mita 400 kuelekea kiwanda cha viuadudu (biolarvicides plant) imekamilika;
na ujenzi wa barabara yenye urefu wa mita 580 ya kuingia eneo la viwanda
unaendelea ambapo utekelezaji umefika asilimia 80. Vile vile, majadiliano kati ya
NDC na TANESCO yanaendelea kwa ajili ya kujenga kituo kidogo cha kupozea
umeme (substation) katika eneo la Viwanda la TAMCO. Majadiliano ya ujenzi wa
Kiwanda cha Kutengeneza Sindano (syringes) kitakachojengwa na Kampuni ya El-
Dawlia Limited yanaendelea.
(c) Mradi wa Magadi Soda - Bonde la Engaruka
Kazi zilizotekelezwa ni: kukamilika kwa upimaji wa ardhi ya mradi pamoja na
uthaminishaji wa mali za wananchi; kukamilisha michoro ya matumizi ya ardhi; na
kuendelea kutangaza mradi kwa wawekezaji mbalimbali ili kumpata mwekezaji wa
kushirikiana na Serikali kupitia NDC.
(d) Kiwanda cha Matairi General Tyre – Arusha
Kazi zilizotekelezwa ni: kukamilika kwa utafiti wa namna bora ya kufufua kiwanda;
kukamilika kwa makabidhiano ya kiwanda ambapo Ofisi ya Msajili wa Hazina
imekabidhi kiwanda hicho kwa NDC; na kukamilika kwa uthamini wa mali za
kiwanda.
B. Utafiti wa Teknolojia na Bidhaa za Viwandani
(a) Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini - CAMARTEC
Kazi zilizotekelezwa ni: kutengeneza zana mbalimbali na kubuni teknolojia mpya
kwa ajili ya kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa. Zana hizo ni pamoja na
mashine 64 zikiwemo za kupandia mbegu za pamba, kusaga karanga, kukausha
mbogamboga na kukata majani; kubuni na kutengeneza trela lenye uwezo wa
kubeba mizigo ya tani mbili kwa matumizi ya trekta za URSUS; kujengwa kwa
mitambo 55 ya biogas; na kukamilika kwa tafiti tatu zinazohusiana na matumizi ya
nishati jadidifu ya biogas na kufanya utafiti wa mahitaji ya zana za kilimo (technology
needs assessment) katika mikoa 14 ya Tanzania Bara ambayo ni Kilimanjaro,
Arusha, Manyara, Singida, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Geita, Kigoma, Dodoma,
Iringa, Njombe, Lindi na Mbeya. Matokeo yameonesha uhitaji mkubwa wa teknolojia
na zana za kisasa za kupandia mazao, kupalilia, kupura na kupepeta mazao ya
nafaka.
Shughuli nyingine zilizofanyika ni kuendelea na utafiti wa Camartec Fas Trucktor
(CFT) trekta kwa kuzingatia changamoto zinazobainika wakati wa majaribio ya trekta
hizo; na kubuni na kuunda zana mbalimbali zikiwemo: kipandio cha mbegu
kinachovutwa na trekta aina ya CFT; mashine za kupura mazao; mashine ya
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 23
kufunga majani ya malisho ya mifugo; mashine ya kutenganisha makapi ya mbegu
za mchikichi; mashine ya kutengeneza chakula cha kuku kwa mfumo wa punje; na
jembe la kulainisha udongo (harrow) linalokotwa na punda.
(b) Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania – TIRDO
Shughuli zilizotekelezwa ni: kukamilika kwa asilimia 80 ya ukarabati wa jengo la
maabara ya mafuta na gesi asilia; kukamilika kwa michoro na makadirio ya gharama
za ukarabati wa maabara ya makaa ya mawe na kuendelea kukamilisha taratibu za
kumpata mkandarasi wa ujenzi. Aidha, Shirika linakamilisha taratibu za uhakiki wa
maabara ya mazingira baada ya kutuma maombi ya uhakiki kwa Mamlaka ya
Uhakiki Kusini mwa Afrika - SADCAS na kuelekezwa kurekebisha baadhi ya nyaraka
kabla ya ukaguzi.
(c) Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo – TEMDO
Kazi zilizofanyika ni: kubuni mashine ya kutengeneza tofali zinazozuia upotevu wa
joto (refractory bricks); majokofu makubwa; kiteketezi taka kidogo kinachobebeka
kwa ajili ya zahanati na maabara za afya; mtambo wa kusindika na kusafisha mafuta
ya kula na mtambo wa kuzalisha umeme kutokana na nguvu ya maji na ufungaji wa
mitambo wa kuzalisha umeme (kW 20) kutokana na nguvu za upepo na jua katika
Kituo cha Olduvai Gorge – Ngorongoro.
(d) Uendelezaji wa Viwanda Vidogo – SIDO
Shughuli zilizofanyika ni kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya viwanda
(barabara, mifumo ya maji na umeme) na ujenzi wa majengo ya viwanda (12) katika
Mikoa ya Dodoma, Geita, Kagera, Manyara, na Mtwara na ujenzi wa ofisi za SIDO
za kutolea huduma katika Mikoa mipya ya Geita, Simiyu na Katavi; kuboresha kituo
cha teknolojia cha Lindi kwa kununua mitambo mipya ya kubangua korosho;
kuimarisha vituo vya teknolojia vya Shinyanga na Kigoma ili viwe katika nafasi nzuri
ya kutengeneza teknolojia za kuchakata zao la chikichi pamoja na mazao mengine;
kuongeza majengo ya viwanda katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma, na Kigoma;
kutambua, kuanzisha na kusambaza teknolojia mpya 40 za ubanguaji korosho,
usindikaji na ufungashaji wa vyakula, utengenezaji wa vifaa vya ujenzi hususan
tofali, utengenezaji wa chokaa na chaki, ukamuaji wa mafuta ya kula kutokana na
michikichi na usindikaji wa ngozi kwa kutumia njia za asili.
C. Kilimo
(a) Kilimo cha Mpunga
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa ghala la kuhifadhia mpunga lenye
uwezo wa kuhifadhi tani 1,500 pamoja na ukarabati na ujenzi wa barabara
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 24
zinazounganisha ghala na skimu ya umwagiliaji ya Mwendamtitu Wilayani Mbarali;
kutoa mafunzo ya kilimo shadidi cha mpunga kwa Maafisa Ugani na Mafundi Sanifu
wa Umwagiliaji 109 na wakulima 5,647 kutoka skimu za umwagiliaji 40 katika
Halmashauri za Ulanga, Mvomero, Kilombero, Morogoro Vijijini, Kilosa na Malinyi;
kuendeshwa kwa mashamba darasa yapatayo 1,331; na mbegu mpya za mpunga
11 zimetambulishwa kwa wakulima kupitia mashamba ya mfano ambapo wakulima
walichagua aina mbili ambazo ni TXD 306 (SARO 5) na NERICA 7. Aidha, katika
kuthibiti ubora wa mbegu za mpunga, Taasisi ya Uthibiti wa Ubora wa Mbegu
Tanzania - TOSCI imefanya ukaguzi wa mashamba yaliyoandikishwa kuzalisha
mbegu, imehakiki kiasi cha mbegu zilizozalishwa kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo
- TARI, Taasisi ya uzalishaji wa mbegu Tanzania - ASA na kutoka kwa wakulima
waliozalisha mbegu zenye ubora wa kuazimiwa.
(b) Kilimo cha Mahindi
Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea kuboresha uzalishaji wa mahindi kwa kuhamasisha
matumizi ya mbegu bora na mbolea, ambapo jumla ya tani 17,525.65 za mbegu
bora za mahindi zilipatikana na kusambazwa kwa wakulima; kutolewa elimu kuhusu
udhibiti wa viwavijeshi vamizi kwa wakulima 2,080 wa mahindi kutoka mikoa ya
Singida (385), Shinyanga (425), Simiyu (495), Tabora (530) na Morogoro (245).
Aidha, katika kuongeza thamani ya zao la mahindi Bodi ya Nafaka na Mazao
Mchanganyiko ilinunua tani 7,230 za mahindi na kusagisha tani 1,003. Vile vile,
uzalishaji wa mahindi kwa misimu minne iliyopita ni: 6,148,699 kwa mwaka 2015;
6,680,758 kwa mwaka 2016; tani 6,273,150 kwa mwaka 2017; na tani 6,300,000
kwa mwaka 2018.
(c) Kilimo cha Miwa
Hatua iliyofikiwa ni: kukarabatiwa kwa kilometa 33.5 za miundombinu ya barabara
zilizopo kwenye mashamba ya wakulima wadogo wa miwa katika maeneo ya
Kilombero, Mtibwa na Kagera; kusajiliwa kwa wakulima 6,125 kupitia mfumo wa
kielektroniki katika mashamba ya Kilombero (5,899) na Mtibwa (226); kuanzishwa
kwa Vyama vya Ushirika vya wakulima; kukarabatiwa kwa kilometa 33.5 za barabara
za mashamba ya wakulima katika wilaya za Kilombero na Misenyi; kujengwa kwa
miundombinu ya umwagiliaji katika kijiji cha Msolwa Ujamaa kwa ajili ya wakulima
wadogo 146 wanaomiliki ekari 250; kujengwa kwa tuta la kukinga maji lenye urefu
wa km 10.6 katika bonde la Ruembe (Kilosa) na wakulima wa miwa 316 kutoka
katika mashamba ya Kilombero, Mtibwa na Kagera wamepatiwa mafunzo ya mbinu
bora za kilimo bora cha miwa, biashara, uongozi, ushawishi na utetezi; kutolewa kwa
viuatilifu vya kudhibiti wadudu waharibifu na visumbufu kwa wakulima wadogo wa
Mkoa wa Manyara.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 25
(d) Kilimo cha Chai
Hatua iliyofikiwa ni: kuzalishwa kwa miche bora 7,130,000 kupitia sekta binafsi na
umma. Kati ya miche hiyo, miche 3,100,000 imesambazwa kwa wakulima wa Wilaya
za Njombe, Ludewa, Tarime, Rungwe na Mufindi kwa ajili ya kujaza mapengo na
kufungua mashamba mapya; kutolewa mafunzo kuhusu uanzishaji na utunzaji wa
bustani za miche bora ya chai, upandaji chai mashambani, uchumaji wa majani
mabichi ya chai na matumizi sahihi ya pembejeo kupitia shamba darasa kwa
wakulima wadogo wa chai 15,000 na maafisa ugani saba (7) katika mkoa wa
Njombe; kuzalishwa kwa tani 19,412.16 sawa na asilimia 52.5 ya lengo la kuzalisha
tani 37,000; na kuongezeka kwa mauzo ya chai kavu kufikia tani 5,500 ongezeko
ambalo limetokana na kuimarishwa kwa viwanda vya Rift Valley – Dar es Salaam na
BK Tea Blenders – Kagera.
(e) Kilimo cha Kahawa
Hatua iliyofikiwa ni: kuzalishwa kwa miche 6,494,930 kwa ajili ya kupandwa katika
kanda za uzalishaji wa kahawa, ambapo miche 1,780,430 imezalishwa na Bodi ya
Kahawa na miche 4,714,500 imezalishwa na Taasisi ya Utafiti wa Zao la Kahawa -
TaCRI katika vituo vya Lyamungo - Moshi, Ugano - Mbinga, Mbimba - Mbozi,
Maruku – Bukoba, Mwayaya - Buhigwe na Sirari - Tarime.
(f) Kilimo cha Pamba
Hatua iliyofikiwa ni: kutolewa kwa mafunzo ya kanuni bora za kilimo cha pamba,
ikiwemo utambuzi wa visumbufu, viuatilifu na matumizi sahihi ya viuatilifu kwa
washiriki 2,036 wakiwemo maafisa ugani, wakulima, na maafisa ushirika kutoka
mikoa ya Tabora, Mwanza, Mara, Shinyanga, Katavi, Kigoma, Singida, Kagera,
Geita, Simiyu, Iringa, Dodoma, Manyara, Kilimanjaro, Morogoro, Pwani na Tanga;
kusambazwa kwa tani 21,535.62 za mbegu bora za pamba aina ya UKM08 kwa
wakulima nchini ambapo ongezeko la usambazaji limetokana na mwamko wa
wakulima kulima zao la pamba. Vile vile, jumla ya ekapaki 3,326,990 za viuatilifu
zimesambazwa katika Halmashauri 41 za mikoa ya Kigoma, Katavi, Singida,
Dodoma, Kagera, Mara, Tabora, Geita, Mwanza, Shinyanga na Simiyu. Aidha, Bodi
ya Pamba inaendelea kuratibu usambazaji wa viuatilifu kupitia kampuni binafsi.
(g) Kilimo cha Tumbaku
Hatua iliyofikiwa ni: kusambazwa kwa kilo 588 za mbegu zinazotosheleza hekta
39,191 kwa wakulima 53,903 kwenye vyama vya ushirika 258 katika mikoa ya
Kigoma, Katavi, Ruvuma, Mbeya, Tabora, Shinyanga, Geita na Iringa. Mbegu hizo
zinatarajiwa kuzalisha tani 54,868 za tumbaku; kuzalishwa kwa tani 16,460 za
tumbaku sawa na asilimia 30 ya lengo la kuzalisha tani 54,868; kuboreshwa kwa
mabani 23,960 ya kukaushia tumbaku sawa na asilimia 42.5 ya lengo la kuboresha
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 26
mabani 56,398; kuoteshwa kwa miche 13,657,493 kwa ajili ya kutunza mazingira na
kusajiliwa kwa vituo 60,000 vya kufungia na kuchambua tumbaku.
(h) Upatikanaji wa Pembejeo
Hatua iliyofikiwa ni: kununuliwa kwa lita 269,000 na kilo 3,000 za viuatilifu kwa ajili ya
kukabiliana na dharura ya milipuko ya visumbufu vya mazao vikiwemo Kwelea
kwelea, Panya, Nzige wekundu na Viwavijeshi vamizi; usambazaji wa mbolea katika
mikoa 26 ya Tanzania Bara ulikuwa tani 492,394.18 sawa na asilimia 95.77 ya
mahitaji ya tani 514,138 katika msimu wa mwaka 2018/19; na maghala 11 yenye
uwezo wa kuhifadhi tani 65,500 za mbolea yamejengwa katika maeneo ya
Sumbawanga, Mbozi, Makambako, Njombe, Iringa, Morogoro, Moshi DC, Himo, Hai,
Usa River na Kisongo. Vilevile, upatikanaji wa salfa ya unga umefikia tani 31,500 na
viuatilifu vya maji lita 520,000 ambapo tani 3,325.850 na lita 248,207 zimesambazwa
kwa wakulima. Aidha, upatikanaji wa mbegu bora umefikia tani 49,040.66 ambapo
kati ya kiasi hicho, tani 38,507.87 zimezalishwa hapa nchini, tani 8,361.46
zimeagizwa kutoka nje ya nchi na tani 2,171.33 ni baki ya msimu wa 2017/18. Kati
ya mbegu zilizozalishwa hapa nchini, asilimia 96.5 zimetokana na sekta binafsi na
asilimia 3.5 zimetokana na uzalishaji wa sekta ya umma. Katika kipindi hicho miche
1,507 ya miwa, vipando 121,805 vya muhogo na vikonyo 520,000 vya viazi lishe
vilizalishwa.
(i) Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Umwagiliaji
Shughuli zilizofanyika ni: kuanza kufanya mapitio ya usanifu wa ukarabati wa
miundombinu ya skimu za umwagiliaji za Kigugu - Mvomero (hekta 200), Mvumi -
Kilosa (hekta 249), Msolwa Ujamaa (hekta 675) na Njage - Kilombero (hekta 325),
ukarabati wa barabara za kuingia katika skimu ya Mvumi yenye urefu wa kilomita 8
na Njage kilomita 7 na usanifu wa shamba la mbegu la Kilangali (hekta 400); na
kutolewa mafunzo kwa wajumbe 311 kutoka skimu za umwagiliaji za Njage, Msolwa
Ujamaa, Mvumi, Kigugu na Mbogo Komtonga ya kuimarisha na kuendesha umoja.
Vile vile, Skimu za umwagiliaji 129 zimekarabatiwa katika Halmashauri 68 nchini
pamoja na ununuzi wa mitambo ya ujenzi.
(j) Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo
Hatua iliyofikiwa: Wanafunzi 2,389 wamedahiliwa katika vyuo 14 vya mafunzo ya
Kilimo ambapo wanafunzi 2,051 wamepewa ufadhili na Serikali na 338 wamejilipia,
kati yao wanafunzi 1,537 ni wa ngazi ya Astashahada na wanafunzi 852 ni wa ngazi
ya Stashahada katika Vyuo vya Ilonga, Mlingano, Mtwara, Tumbi, Ukiriguru, Uyole,
HORTI Tengeru, Mubondo, Maruku, KATC Moshi, Igurusi, KATRIN, Chuo cha
Sukari Kidatu na Inyala. Aidha, Wanafunzi 338 wanajilipia ambapo 239 ni kwa ngazi
ya Astashahada na 99 ni Stashahada. Aidha, zabuni ya kukarabati vyuo vitatu (3)
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 27
vya mafunzo ya Kilimo vya Inyara, Mlingano na Mubondo imetangazwa na imefikia
hatua ya tathmini ya kumpata mkandarasi.
(k) Tafiti za Kilimo
Hatua iliyofikiwa ni: kugunduliwa kwa mbegu bora mpya aina 4 za mbegu bora za
mahindi (WE5135, WE7118, WE5141 na WE7133) zenye uwezo wa kustahimili
ukame, kutoa mavuno kwa wastani wa tani 5.8 kwa hekta, na ukizani wa magonjwa
ya majani ya mahindi (maize leaf necrosis), michuruzi na ukungu. Mbegu hizo
zitatumika kuzalisha mbegu za msingi kuanzia msimu wa 2019/2020; kuzalishwa
kwa mbegu za korosho kilo 47,484 katika kituo cha Utafiti Naliendele, ambazo
zitatumika kuzalisha miche 6,647,760 ambayo itatosheleza ekari 391,045.19. Mbegu
hizo zimesambazwa katika mikoa 20 na uzalishaji wa miche bora ya unaendelea
ambapo hadi Machi 2019 miche 52,839 imezalishwa na kusambazwa kwa wakulima
katika mikoa ya Mtwara (7,273), Lindi (30,612), Pwani (11,792), Ruvuma (2,680),
Dar es Salaam (82), Dodoma (200), na Singida (200); na kuendelea na ukarabati wa
miundombinu ya vituo vitatu (3) vya utafiti (ARI-Ukiriguru, ARI- Tumbi, ARI -
Ilonga).
(l) Maghala na Kuboresha Hifadhi ya Taifa ya Chakula
Hatua iliyofikiwa ni: ujenzi wa vihenge vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 190,000 na
maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 60,000 unaendelea katika mikoa ya
Ruvuma (Songea), Njombe (Makambako), Songwe (Mbozi), Rukwa (Sumbawanga),
Katavi (Mpanda), Shinyanga, Manyara (Babati) na Dodoma; na kununuliwa kwa tani
46,236.035 za mahindi sawa na asilimia 163.95 ya lengo la ununuzi.
(m) Kusimamia Matumizi Endelevu ya Ardhi ya Kilimo na Maji
Shughuli zilizofanyika ni; kuendelea na utekelezaji wa mradi wa matumizi endelevu
ya ardhi katika lindimaji za mito ya Ruvu na Zigi iliyo katika mikoa ya Morogoro na
Tanga; kutoa mafunzo kuhusu hifadhi ya udongo na maji mashambani kwa Maafisa
ugani 40 kutoka wilaya za Muheza, Korogwe na Mkinga; na kuandaliwa kwa shamba
darasa lenye teknolojia za kuhifadhi udongo na maji mashambani katika kijiji cha
Mbomole (Muheza).
(n) Kuimarisha Maendeleo ya Ushirika
Hatua iliyofikiwa ni: kufanyika kwa ukaguzi wa nje kwa vyama 2,296 vya ushirika;
kutatua migogoro katika vyama vya Ushirika vya RCG AMCOS dhidi ya MIWA
AMCOS, UWABINDOCHA dhidi ya Manispaa ya Morogoro, Mshikamano SACCOS
na Kapolo AMCOS dhidi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo - TADB na migogoro
mingine inaendelea kushughulikiwa; kuendelea kuhimiza matumizi ya Mfumo wa
Stakabadhi Ghalani katika vyama vya ushirika ambapo vyama vya mazao ya
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 28
Korosho, Ufuta, Kakao na Mahindi vimeunganishwa kwenye mfumo. Aidha,
uhamasishaji unaendelea ili kuunganisha vyama vya mazao ya Dengu na kutekeleza
dhana ya kilimo cha mkataba kwa kununua mahindi kupitia vyama vya ushirika
kwenye mikoa ya Iringa na Ruvuma kwa bei shindani.
D. Mifugo
(a) Miundombinu ya Uzalishaji na Masoko
Shughuli zilizotekelezwa ni: kujenga na kukarabati minada ya mpakani kwa kujenga
ukuta na jengo la ofisi ya mnada wa Kirumi (Butiama) ambalo litakuwa na huduma
za kibenki; kuendelea na ujenzi wa sakafu ya mnada uliopo Longido, kuendelea na
ujenzi wa kituo cha polisi na uzio katika mnada Buhigwe, na kuendelea na ujenzi wa
uzio katika minada ya Kasesya na Nyamatala, kuendelea kuimarishwa kwa vituo vya
kanda vya uhimilishaji nchini, ambapo kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC)
kilichopo Usa River (Arusha) kimepatiwa kichambuzi cha mbegu (semen analyzer-
CASA) na madume bora matatu (3) aina ya Boran, ununuzi wa mitungi 71 ya
kuhifadhi kimiminika cha naitrojeni (lita 35) pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalam
389 wa uhimilishaji.
(b) Vituo vya Utafiti, Mafunzo na Ugani wa Mifugo
Kazi zilizotekelezwa ni: kukarabatiwa kwa mabweni manne na kiwanda kidogo cha
kusindika maziwa katika Kampasi ya Tengeru; kudahili wanachuo 2,536 katika
mwaka wa masomo 2018/19; kutoa elimu kwa Maafisa Ugani wa wafugaji 19,839 ili
kuhamasisha ufugaji wa kisasa na kibiashara na kuongeza uzalishaji na ubora wa
malighafi zitokanazo na mifugo ili kukidhi mahitaji ya viwanda vinavyoendelea
kujengwa nchini.
Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TARILI) imefanya tafiti nane (8) vituoni na
kwa wafugaji katika mikoa 16 ambapo matokeo yake yatawezesha ng‟ombe jike
kuzalisha viinitete nane (8) mpaka 450 kwa mwaka kwa ajili ya uhimilishaji na
uhawilishaji. Vile vile, kuongeza kasi ya uzalishaji wa mitamba na madume kwa ajili
ya maziwa na nyama (ndama 50 kwa mwaka kwa ng‟ombe mmoja). Aidha, TARILI
imetoa elimu kwa wafugaji 8,347 na kusambaza teknolojia ya kuzalisha maziwa kwa
wingi kwa Halmashauri 41 nchini na kuwafikia wadau 23,659 wakiwemo wataalam
wa ugani 127, wanafunzi 346 wa vyuo vya LITA, SUA, Visele na MATI.
(c) Usimamizi wa Ardhi, Maji na Upatikanaji wa Malisho
Kazi zilizotekelezwa: kukamilisha ujenzi wa bwawa la Mbagala (Songwe), lambo
katika Kijiji cha Chamakweza (Bagamoyo) na visima virefu katika Vijiji vya Mpapa
(Manyoni) na Nsolanga-Ismani (Iringa); na kuendelea na ukarabati wa bwawa la
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 29
Nyakanga (Butiama) na lambo katika Kijiji cha Wami-Dakawa (Mvomero). Ujenzi na
ukarabati huo umewezesha kuongeza idadi ya mabwawa/malambo kufikia 1,384 na
visima virefu 103.
Vile vile, hekta 350,576.05 zimetengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo katika vituo
vya kupumzishia mifugo, Ranchi za Taifa, mashamba ya TARILI na Mashamba ya
Kuzalisha Mifugo (LMUs). Aidha, hekta 199,827.3 zimetengwa katika Halmashauri
tano za Tunduru, Mpanda, Biharamulo, Muleba na Kyerwa kwa ajili ya malisho ya
mifugo ili kupunguza migogoro ya wafugaji na watumiaji wa ardhi wengine nchini.
(d) Tiba na Udhibiti wa Magonjwa ya Mifugo
Shughuli zilizotekelezwa ni: ukarabati wa majosho 151 katika Mamlaka za Serikali za
Mitaa katika Mikoa 21; na kuhamasisha matumizi ya dawa za kuogesha mifugo na
kutoa chanjo na viuatilifu vya mifugo kwa kufanya michovyo 40,352,228 ya Ng‟ombe,
Mbuzi na Kondoo. Aidha jumla ya lita 8,823.53 za dawa za kuogesha mifugo aina ya
Paranex zimenunuliwa na kuzigawa katika majosho 1,486 yanayofanya kazi katika
Mikoa 24, kuzalishwa kwa dozi 39,548,000 za chanjo kwa magonjwa ya Mdondo,
Kimeta na Chambavu na kusambazwa kupitia vituo saba vya Wakala ya Maabara ya
Veterinari Tanzania katika kanda.
E. Uvuvi
(a) TAFICO
Shuguli zilizotekelezwa ili kufufua TAFICO ni: utambuzi wa mali za shirika ambapo
mpaka sasa mali zenye thamani ya shilingi bilioni 118 zimetambuliwa; na kuzindua
Menejimenti ya kusimamia shirika, kuandaa na kuutekeleza mkakati wa kufufua
TAFICO.
(b) Kusimamia na Kuendeleza Uwekezaji katika Sekta ya Uvuvi
Shughuli zilizotekelezwa ni: kuwezeshwa kwa vikundi 50 vya Usimamizi wa
Rasilimali za Uvuvi (BMUs) katika Wilaya za Pangani (12), Mkinga (14), Jiji la Tanga
(5), Bagamoyo (9) na Lindi Vijijini (10); kusambazwa kwa majiko banifu 100 katika
Vijiji/Mialo ya uvuvi 16 katika Mkoa wa Kigoma na kutoa mafunzo wa wachakataji wa
samaki 640 katika Vijiji 16 ili kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi katika Ziwa
Tanganyika; na kuwezeshwa vikundi vya ushirika vya wavuvi kwa kupatiwa fedha na
vifaa katika maeneo ya Igombe-Mwanza, Ikumbaitale-Chato, Nkasi (Ziwa
Tanganyika), Migoli-Mtera na vikundi vya ufugaji samaki Peramiho (Ruvuma).
(c) Bandari ya Uvuvi
Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na upembuzi yakinifu unaofanywa na Mtaalam Elekezi
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 30
(kampuni za Sering Ingegneria ya Italia na Doch Tanzania Limited) katika ujenzi wa
bandari ya uvuvi ambayo itajengwa kati ya Mtwara, Kilwa, Tanga na Pwani.
(d) Kuimarisha Tafiti, Huduma za Ugani na Mafunzo ya Uvuvi
Hatua iliyofikiwa ni: kufanyika kwa utafiti wa kuangalia wingi wa samaki Ziwa Victoria
kwa kutumia Teknolojia ya Hydro-acoustic survey; kuimarisha upatikanaji wa
takwimu za uvuvi kwa kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa takwimu kwa njia ya
kielektroniki ikiwemo matumizi ya simu za viganjani ujulikanao kama e-CAS
(electronic Catch Assessment Survey) ambao kwa majaribio jumla ya simu 108
zimetolewa kwa maafisa Uvuvi kutoka Halmashauri zenye maeneo ya Uvuvi katika
Ziwa Victoria, Ukanda wa Bahari ya Hindi na Ziwa Tanganyika.
Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania – TAFIRI kwa kushirikiana na Mamlaka ya
Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu imetoa mafunzo ya mbinu za ukaguzi, uhakiki wa
njia na vifaa vya kupimia na usimamizi wa maabara kwa watalaam tisa (9) wa
Maabara ya Uvuvi-Nyegezi; kuendelea na utafiti wa vifaa vya kuvutia samaki FADs
(Fish Aggregaring Devices) katika maeneo ya Bagamoyo na Nungwi Zanzibar;
kuendelea na utafiti wa kujua wingi wa biolojia ya Kambamiti katika Pwani ya
Tanzania; kuendelea na utafiti wa kupata samaki wazazi (brood stock); na kudahili
wanafunzi 1,088 katika masomo ya ngazi za Astashahada na Stashahada kwenye
Kampasi za Mbegani, Nyegezi na Kigoma. Aidha, Wakala wa Elimu na Mafunzo ya
Uvuvi (FETA) imetoa mafunzo kwa wananchi 1,300 kuhusu mbinu za kuvua na
ukuzaji wa viumbe.
(e) Ufugaji Samaki
Shughuli zilizofanyika ni: ujenzi wa kituo Nyamirembe (Chato) ili kuongeza uzalishaji
wa vifaranga; kufanywa kwa makadirio na mchanganuo wa gharama za ujenzi na
ukarabati wa miundombinu ya vituo vya Ruhila (Songea), Mwamapuli (Igunga) na
Kingolwira (Morogoro); na kuendelea kuboresha kituo cha Machui (Tanga) ikiwa ni
pamoja na kukiunganisha na umeme wa Tanesco; Shughuli zingine zilizotekelezwa
ni kuandaa Mpango wa Kitaifa wa Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji- NADSP,
kuzalishwa vifaranga 17,301,076 katika vituo vya Serikali na Sekta binafsi; kuwekwa
vizimba (fish cage) 408 katika Ziwa Victoria (346); Ziwa Tanganyika (9) na malambo
(53) ili kuongeza matumizi ya teknolojia stahiki katika kuzalisha viumbe maji.
(f) Kuimarisha na Kuendeleza Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi na Mazingira
Shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na: kuanzishwa kwa Kanda Kuu tatu za
usimamizi na udhibiti wa rasilimali za uvuvi katika Ukanda wa Ziwa Viktoria,
Tanganyika na Ukanda wa Pwani na kanda ndogo mbili za Ukerewe na Sengerema;
kuimarisha vituo 27 vilivyopo vya usimamizi wa rasilimali za uvuvi nchini; kusimamia
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 31
hifadhi za bahari na maeneo tengefu kwa kufanya doria zenye sikukazi 677 katika
maeneo yote 18 yaliyohifadhiwa; na kufanya doria na operesheni mbalimbali zenye
sikukazi 10,914 ili kuimarisha usimamizi na udhibiti wa uvuvi na biashara haramu ya
mazao ya uvuvi. Aidha kaguzi 3,155 za kuhakiki ubora na usalama wa mazao ya
uvuvi zilifanyika mipakani, viwanja vya ndege na bandari.
F. Maliasili na Misitu
(a) Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Ikolojia ya Ardhi Oevu ya Bonde la Mto
Kilombero na Mto Rufiji
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa ofisi ya Maliasili katika Wilaya ya
Ulanga; kukamilika kwa Ujenzi wa vituo viwili vya Askari wa Wanyamapori katika
Wilaya ya Ulanga; kuanzishwa vikundi vinne (4) vya uvuvi katika Mto Kilombero na
kuviwezesha kutekeleza majukumu yake; kurejesha maeneo yaliyoharibika
kimazingira katika hali yake ya awali; kutoa elimu kwa jamii kuhusu usimamizi na
matumizi bora ya ardhi; kufanya mapitio ya Mipango ya usimamizi na uvunaji wa
misitu katika Wilaya ya Ulanga; kujenga na kununua vifaa vya ofisi mbili (2) za
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ngorongoro, Utete na Rufiji
(JUHIWANGUMWA) na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ifakara, Lupiro na
Mang‟ula (ILUMA) – Kilombero.
(b) Mradi wa Kuimarisha Mapori Tengefu na Vitendo vya Kupambana na
Ujangili Nchini
Hatua iliyofikiwa ni: kutangazwa kwa misitu mitano (5) ya Hifadhi ya Mazingira Asilia
ya Chome, Magamba, Mkingu, Minziro na Udzungwa Scarp kwenye Gazeti la
Serikali; na ukarabati wa nyumba za watumishi katika hifadhi za Chome, Mlima
Rungwe, Mkingu na Minziro ambapo ukarabati umefikia asilimia 90.
(c) Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Maliasili
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa utafiti wa fursa za utalii katika Wilaya ya
Ngorongoro; kuandaa mpango mkakati na miongozo ya kuwezesha Mamlaka ya
Usimamizi wa Wanyamapori kujiendesha; kutoa mizinga ya nyuki (115) kwa
wananchi wa Wilaya za Serengeti (80) na Ngorongoro (35) ili kuwezesha wananchi
kiuchumi na kuendeleza uhifadhi; kupatiwa ufumbuzi wa mgogoro wa mipaka kati ya
vijiji vya Hekwe na Magatini na Hifadhi ya Serengeti; kutoa mafunzo kwa wananchi
wa Wilaya ya Serengeti kuhusu namna ya kujilinda na wanyamapori wakali na
waharibifu; kukamilishwa kwa Mpango wa Usimamizi wa Pori Tengefu la Kijereshi;
kuimarishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) kwa kununuliwa
magari na vifaa vya TEHAMA; kukamilishwa kwa Mwongozo wa Uwindaji wa Simba;
na kujengea uwezo Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji na Kata ambapo jumla ya wajumbe
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 32
240 wamepatiwa mafunzo.
(d) Mradi wa Kusaidia Uendelezaji wa Misitu Binafsi na Mnyororo wa
Thamani
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa tafiti tano (5) kuhusu ushiriki wa sekta binafsi
katika upandaji miti; na kupandwa kwa miche 5,500 aina ya misindano katika Wilaya
za Nyasa, Songea, Makete, Ludewa, Mufindi na Njombe.
G. Madini
(a) Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini
Shughuli zilizotekelezwa ni: kukamilisha uandaaji wa Mwongozo wa Mpango wa
Utunzaji wa Mazingira kwa wachimbaji wadogo; ununuzi wa mtambo wa
kuchorongea miamba ambao utatoa huduma kwa wachimbaji wadogo kwa bei nafuu
kupitia Shirika la Madini la Taifa - STAMICO; kutoa mafunzo ya matumizi ya mtambo
wa uchorongaji miamba kwa wataalam na wachimbaji wadogo kuhusu masuala ya
utafiti wa madini kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini - GST na STAMICO;
kuandaa Mpango wa Kibiashara na Mpango Mkakati wa Kituo cha Jemolojia
Tanzania; kukamilika kwa ujenzi wa ukuta wa ofisi ya madini Moshi na ukarabati wa
ofisi ya madini Nachingwea; kukamilika kwa ujenzi wa mgodi wa mfano na ufungwaji
wa mtambo kwa ajili ya uchenjuaji wa madini ya dhahabu kwa wachimbaji wadogo
katika eneo la Lwamgasa, Geita; na kuendelea na ufungwaji wa mitambo ya
uchenjuaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Katente, Geita na Itumbi, Mbeya.
Shughuli nyingine zilizofanyika ni: ujenzi wa vituo Saba (7) vya umahiri (Centre of
Excellency) katika maeneo ya Bariadi, Bukoba, Musoma, Handeni, Mpanda, Chunya
na Songea ambapo kati ya hivyo, vituo vya Bariadi, Musoma, Bukoba na Handeni
vimekamilika; kumpata mkandarasi wa kujenga mitambo itakayofanikisha uongezaji
thamani wa madini (smelter and refinery); kuboresha miundombinu ya Chuo cha
Madini katika Kampasi ya Dodoma na Nzega; kukamilika kwa ujenzi wa jengo la
wafanyabiashara wa madini (Brokers house) na kuendelea na ujenzi wa kituo cha
pamoja (one stop centre) katika eneo la Mirerani. Vilevile, Serikali imeanzisha
mfumo wa masoko ya madini katika mikoa yote yenye madini ya metali na vito.
(b) Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini,
Mafuta na Gesi Asilia - TEITI
Shughuli zilizotekelezwa ni: kukamilika kwa mfumo wa kieletroniki wa kuhifadhi
takwimu za rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia (Dashboard) na kuelimisha
wananchi kuhusu takwimu hizo; kutoa mafunzo kuhusu uwekaji wazi wa majina ya
wamiliki wa hisa katika kampuni za madini, mafuta na gesi asilia; na kukamilisha
marekebisho ya Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 33
Gesi asilia ya mwaka, 2015 na Kanuni kwa ajili ya kutekeleza sheria hiyo.
(c) Mradi wa Dhahabu wa Buhemba
Shughuli zilizotekelezwa ni: kukamilika kwa ununuzi wa mtambo wa kuzalisha
dhahabu kwa kuchakata mabaki ya dhahabu; kufanya shughuli za awali na
uchorongaji katika eneo la mashapo ya mwamba mgumu kwenye mgodi; na
kukamilika kwa upembuzi yakinifu katika mabaki ya dhahabu yaliyoachwa kipindi
cha nyuma ambapo umebaini kuwapo kwa takribani tani 796,400 za mabaki ya
mchanga wa dhahabu yenye wastani wa kilo 852 za dhahabu.
3.2.2.3. Kufungamanisha Maendeleo ya Viwanda na Maendeleo ya Watu
A. Elimu, Sayansi na Teknolojia
(a) Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari
(i) Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (Programu ya Lipa Kulingana
na Matokeo – EP4R)
Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa miundombinu katika shule 504 (msingi
219 na sekondari 285) katika mikoa yote Tanzania Bara ambao unahusisha
madarasa 938, mabweni 210, vyoo 2,141, nyumba 39 (2 in 1), mabwalo 76 na
huduma za maji katika shule 10; kuendelea na ujenzi wa shule 4 mpya za msingi
katika Halmashauri za Dodoma Jiji, Masasi Mji, Buhigwe na Chato; kukamilika kwa
ujenzi wa shule ya Sekondari Maalum Patandi kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji
maalum yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 640 ambao unahusisha madarasa
nane (8), jengo la utawala, bwalo na jiko, chumba cha maabara, chumba cha
TEHAMA, maktaba na bweni moja; kugharamiwa mafunzo wanataaluma 68 kutoka
vyuo vikuu vya Umma katika ngazi za shahada za uzamili (66) na uzamivu (2);
kuendelea na maandalizi ya ukarabati wa vyuo vinane (8) vya ualimu vya Bustani,
Vikindu, Mtwara Kawaida, Mtwara Ufundi, Singa chini, Monduli, Bunda na Katoke;
na kununuliwa kwa magari 20 kwa ajili ya vyuo vya Ualimu.
(ii) Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu ya Msingi (MMEM) –
Kuimarisha Mafunzo ya Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK)
Hatua iliyofikiwa ni: kutolewa mafunzo kwa walimu wa nyongeza 402 wa Elimu
Maalum yaliyotolewa katika Vyuo vya Ualimu vya Morogoro, Butimba (Mwanza) na
Patandi (Arusha) ambapo walimu walipatiwa stadi za kufundishia za KKK kwa
wanafunzi wasioona na wasiosikia wa Darasa la I - IV kwa kutumia mtaala mpya;
kukamilika kwa mafunzo kwa walimu wa nyongeza 1,598 wanaofundisha darasa la I
na II yaliyotolewa katika vyuo vya ualimu vya Morogoro na Butimba ambapo walimu
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 34
walipatiwa stadi za ufundishaji na ujifunzaji wa Stadi za KKK kwa kuzingatia mtaala
mpya; kufanyika ufuatiliaji wa pamoja wa Programu katika sampuli ya Mikoa 5
ambao ulihusisha Halmashauri za wilaya za Liwale, Mafia, Magu, Manyoni na
Monduli na kushirikisha Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, OR-TAMISEMI,
pamoja na Washirika wa Maendeleo ya Elimu, na wajumbe kutoka Taasisi zisizo za
Serikali zinazohusika na masuala ya Elimu; na kuhamasisha ushiriki wa jamii katika
kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa stadi za KKK kupitia mtandao wa elimu (TEN
– MET) .
(iii) Mradi wa Huduma ya Maji, Elimu ya Afya na Usafi wa Mazingira Shuleni
– SWASH
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa tathmini ya kitaifa ya Huduma ya Maji, Elimu ya
Afya ya usafi wa mazingira shuleni iliofanyika katika shule za msingi na sekondari
2,228 Tanzania Bara na 156 Zanzibar ambayo ililenga kubaini hali halisi ya
miundombinu ya vyoo, maji na usafi wa mazingira nchini ili kuweka mikakati ya
kitaifa ya kuiboresha; na kukamilika kwa mafunzo ya mwongozo wa huduma ya maji,
elimu ya afya na usafi wa mazingira shuleni kwa wathibiti ubora wa shule wa
Halmashauri 63 za mikoa ya Njombe, Ruvuma, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi,
Arusha, Dodoma, Tanga na Kilimanjaro kwa lengo la kuwajengea uwezo wathibiti
ubora wa shule katika kufuatilia, kutathmini na kutoa ushauri kuhusu huduma ya
maji, usafi wa mazingira na ujenzi wa miundombinu ya vyoo shuleni.
(b) Mamlaka ya Elimu Tanzania - TEA
Ujenzi na Ukarabati wa Shule za Sekondari: Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa
asilimia 60 ya ujenzi wa mabweni 12 katika shule 11 za sekondari; kuendelea na
ujenzi wa nyumba 60 za walimu katika shule 15 za sekondari; na kuendelea na
ujenzi wa madarasa 252 katika shule 84 za msingi.
(c) Elimu ya Ufundi na Ualimu
(i) Ujenzi na Ukarabati wa Vyuo vya Ufundi Stadi
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya
cha Namtumbo; kukamilika kwa ujenzi wa karakana ya kisasa ya useremala katika
Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Dodoma; kukamilika kwa ujenzi
wa karakana za useremala, umeme wa magari na jengo la utawala katika chuo cha
Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Morogoro – Kihonda; kukamilika kwa ujenzi
wa karakana ya ushonaji katika chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa
Pwani; kuendelea na ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Chato
ambapo utekelezaji umefikia asilimia 48; kujengwa kwa miundombinu ya maji,
umeme na barabara katika eneo la ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Mkoa wa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 35
Kagera; kuendelea na ujenzi wa mabweni mawili (2) na nyumba mbili (2) za
wafanyakazi katika chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Makete; kuendelea na
ukamilishaji wa majengo na ununuzi wa vifaa kwa ajili ya kuanzisha vyuo vya
Ufundi Stadi katika wilaya za Ileje, Nkasi, Urambo, Newala, Muleba, Kasulu DC,
Itilima, Ngorongoro na Babati na kuendelea na ukarabati na upanuzi wa Chuo cha
Ufundi Stadi cha Wilaya ya Karagwe.
(ii) Kuimarisha Elimu ya Ufundi, Mafunzo ya Ufundi Stadi na Elimu ya
Ualimu
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa utafiti wa kubaini mahitaji ya ujuzi na utaalam
katika sekta za Viwanda, Utalii na Ukarimu; kukamilika kwa maandalizi ya kuanza
ujenzi na ukarabati katika vyuo vya Ualimu 6 vya Dakawa, Mpwapwa, Kleruu,
Marangu, Tabora na Butimba; kuendelea na ujenzi katika vyuo vya Ufundi Stadi na
Huduma (RVTSCs) vya mikoa ya Geita, Simiyu na Rukwa; na kuendelea na ujenzi
wa mabweni mawili (2) katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro.
(iii) Chuo cha Ufundi Arusha
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ufungaji wa mashine mpya katika karakana tano
(5); kukamilika kwa asilimia 95 ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya Kikuletwa;
kukamilika kwa asilimia 85 ya ujenzi wa kituo cha kupima mitambo midogo ya kufua
umeme kutokana na nguvu ya maji; kuendelea na ujenzi wa kituo kipya cha
Kikuletwa cha kufua umeme wa MW 1.7 ambapo utekelezaji umefikia asilimia 70;
kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa miundombinu ya kituo cha Oljoro kwa ajili
ya mafunzo kwa vitendo ya kilimo cha umwagiliaji; na kununuliwa kwa kompyuta
100, meza 100 na viti 200; kuendelea na ujenzi wa jengo la ghorofa tatu (3)
linalojumuisha maabara, madarasa, ofisi na stoo; na kugharamia mafunzo ya muda
mrefu kwa watumishi 40 ambapo watumishi 15 (shahada ya uzamivu), watumishi 22
(shahada ya uzamili) na watumishi 3 (shahada ya kwanza).
(iv) Kuendeleza Elimu ya Ualimu
Hatua iliyofikiwa ni: kununuliwa kwa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa vitendo
kwa ajili ya vyuo 35 vya Serikali; kununuliwa kwa kompyuta za mezani 300 na
projector 100 kwa ajili ya kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na
ujifunzaji na kusambazwa katika vyuo vya Ualimu 18; kukamilika kwa miongozo 22
ya mafunzo kazini kwa wakufunzi kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa kufundisha
masomo mbalimbali; kuendelea na maandalizi ya kuunganisha vyuo vya Ualimu
katika Mkongo wa Taifa; kuanza kwa ujenzi wa chuo cha Ualimu Kabanga; kupatiwa
mafunzo kazini Walimu 398 (Shule za Msingi 200 na Walimu wa Sekondari 198) wa
Hisabati; kukamilika kwa maandalizi ya mafunzo kwa menejimenti za vyuo vya
Ualimu vya Serikali; na kuendelea kununua vifaa vya wakufunzi na wanafunzi ili
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 36
kuboresha ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
(d) Ukarabati wa Vyuo vya Ualimu
Hatua iliyofikiwa ni:
(i) Chuo cha Ualimu Mpuguso: kukamilika kwa ujenzi na ukarabati awamu ya
kwanza ambao umehusisha nyumba tatu za ghorofa kwa ajili ya familia 12 za
walimu, nyumba moja (1) ya mwalimu isiyo ya ghorofa; nyumba 2 za ghorofa
kwa ajili ya mabweni ya wanafunzi 304; na ukarabati wa nyumba moja (1) ya
mwalimu. Ujenzi wa Awamu ya pili umefikia hatua ya umaliziaji ambao
umehusisha majengo mawili (2) ya ghorofa yenye vyumba 16 vya madarasa,
maktaba, jengo la mihadhara, maabara na ukarabati wa mabweni;
(ii) Chuo cha Ualimu Shinyanga: kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ujenzi
na ukarabati ambao umehusisha nyumba 1 ya ghorofa ya walimu kwa ajili ya
familia 4, nyumba 1 ya ghorofa kwa ajili ya mabweni ya wanafunzi 152 na
ukarabati wa nyumba nne (4) za walimu na mabweni mawili (2), na vyoo vya
wanafunzi. Ujenzi wa awamu ya pili umefikia hatua ya uezekaji na
ukamilishaji ambao umehusisha nyumba 2 za ghorofa zenye vyumba 16 vya
madarasa, bweni moja (1) la ghorofa kwa wanafunzi 152, maktaba na jengo
la mihadhara na ukarabati wa mabweni mawili (2) na bwalo la chakula;
(iii) Chuo cha Ualimu Kitangali: ujenzi kwa awamu ya kwanza na ya pili upo
katika hatua za mwisho za ukamilishaji ambapo awamu ya kwanza
inahusisha nyumba 10 za walimu, nyumba 1 ya Mkuu wa Chuo, na jengo la
mikutano. Awamu ya pili inahusisha ujenzi wa nyumba 2 za ghorofa zenye
vyumba 16 vya madarasa, maktaba, jengo la mihadhara, na majengo 2 ya
ghorofa ya mabweni kwa wanafunzi 304; na
(iv) Chuo cha Ualimu Ndala: kuendelea na ujenzi wa awamu ya kwanza ambayo
ipo katika hatua za msingi na unahusisha, ujenzi wa nyumba 2 za ghorofa za
mabweni kwa wanafunzi 304, nyumba 2 za ghorofa za madarasa zenye
vyumba 16, jengo la mihadhara, maktaba, na maabara. Awamu ya pili ya
mradi ambapo utekelezaji upo katika hatua za umaliziaji na unahusisha
nyumba 5 za kawaida za walimu; nyumba 2 za ghorofa za walimu kwa ajili ya
familia 8; na ukarabati wa mabweni mawili (2) pamoja na vyoo vya wanafunzi.
(v) Kuimarisha Taasisi ya Elimu Tanzania
Hatua iliyofikiwa ni: kuandikwa kwa vitabu vya kiada vya masomo ya Historia na
Jiografia ngazi ya sekondari (O-level) na masomo ya Sayansi na Kiswahili ngazi ya
sekondari (A-level) kwa kutumia mtaala wa mwaka 2005; kukamilika kwa uandishi,
uchapaji na usambazaji wa aina nane (8) za vitabu vya kiada kwa Darasa la Tano
kwa masomo ya Hisabati, Kiingereza, Uraia na Maadili, Maarifa ya Jamii, Stadi za
Kazi, Sayansi na Teknolojia na Kifaransa kwa kuzingatia mtaala wa mwaka 2015;
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 37
kusambazwa kwa nakala 2,933,791 za vitabu hivyo kwa uwiano wa kitabu kimoja
kwa wanafunzi watatu (1:3) katika Halmashauri za Mikoa mitano ya Geita, Mwanza,
Kigoma, Arusha na Kilimanjaro; kusambazwa nakala 281,148 za Kiongozi cha
Mwalimu kwa masomo hayo katika Halmashauri za Mikoa yote Tanzania Bara;
kukamilika kwa uandishi, uchapaji na usambazaji wa nakala 391,949 za vitabu vya
somo la Kiingereza kwa Kidato cha Kwanza na cha Pili kwa uwiano wa kitabu kimoja
kwa wanafunzi watatu (1:3); na kuandaliwa kwa vitabu vya kiada rafiki kwa
wanafunzi wenye uoni hafifu na wasioona wa Darasa la Tatu na la Nne ambavyo
vimeandaliwa katika mfumo wa maandishi makubwa (large print), nukta nundu
(braille) na mchoro mguso ambapo usambazaji unaendelea.
Hatua nyingine ni pamoja na: kuandikwa kwa Kiongozi cha Mwalimu kwa masomo
matano (5) ambayo ni Kuhesabu, Kuandika, Kusoma, Afya na Mazingira, na Sanaa
na Michezo kwa Darasa la Kwanza na la Pili na aina saba (7) za Kiongozi cha
Mwalimu kwa Darasa la Tatu; kusambazwa nakala 6,286,476 za vitabu vya kiada
kwa Darasa la Nne (uwiano wa 1:1) vya masomo ya Hisabati, Kiingereza, Uraia na
Maadili, Maarifa ya Jamii, Stadi za Kazi, Sayansi na Teknolojia na Kifaransa katika
Halmashauri za mikoa yote Tanzania Bara; na kusambazwa nakala 7,835,697 za
vitabu aina 25 vya Hadithi kwa Darasa la Kwanza na la Pili (uwiano wa 1:3) katika
Halmashauri za mikoa yote Tanzania Bara.
(e) Elimu ya Juu
(i) Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu
Hatua iliyofikiwa ni: kutolewa mikopo ya Shilingi bilioni 424.76 kwa wanafunzi
122,754 ambapo wanafunzi 41,234 ni wa mwaka wa kwanza na 81,520
wanaoendelea na masomo; kukusanywa kwa mikopo iliyoiva ya thamani ya shilingi
bilioni 128.07 sawa na asilimia 81.2 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 157.7;
kutambuliwa kwa wadaiwa wapya 14,627 na kupatiwa hati za madai sawa na
asilimia 47 ya lengo la kutambua wadaiwa wapya 31,000; na ukaguzi umefanyika
kwa waajiri 2,698 kati ya lengo la waajiri 3,426.
(ii) Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa
(MUCE)
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa ukumbi wa mihadhara wenye uwezo
wa kuchukua wanafunzi 1,209 kwa wakati mmoja na ofisi 14 zenye uwezo wa
kuchukua wahadhiri 28; na kuendelea na ujenzi wa maabara za Sayansi zenye
uwezo wa kukaa wanafunzi 240 kwa wakati mmoja.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 38
(iii) Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam
(DUCE)
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa uwekaji wa miundombinu ya TEHAMA katika
shule za mazoezi; kununuliwa kwa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa ajili ya
wanafunzi wenye mahitaji maalum; na kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa
jengo la utawala na ofisi za wafanyakazi na utafiti ambapo utekelezaji upo katika
hatua za ukamilishaji.
(iv) Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mwl. Julius Nyerere cha Kilimo na Teknolojia
Hatua iliyofikiwa ni: kuendesha mafunzo kwa wakulima 455 juu ya mbinu bora za
kilimo; kulimwa mazao mbalimbali katika shamba darasa la ekari 7; na kugharamiwa
mafunzo watumishi wanne (4) katika shahada ya uzamili kupitia mradi wa
CREATES.
(v) Ukarabati na Ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ukarabati wa mabweni sita (6); kuendelea na
ujenzi wa jengo la utawala na madarasa katika kampasi ya Mbeya ambapo
utekelezaji umefikia asilimia 70; na kuendelea na ujenzi wa hosteli nne (4) katika
Kampasi Kuu ya Morogoro zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,024.
(vi) Ujenzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Ardhi
Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa Jengo la Ardhi lenye
nafasi ya ofisi 125 na madarasa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,980.
(vii) Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili
Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa kituo mahiri cha Magonjwa ya Moyo
Awamu ya Kwanza katika Kampasi ya Mloganzila ambao upo katika hatua za
mwisho za ukamilishaji; kukamilika kwa mpango wa uzalishaji mali wa hospitali ya
kufundishia na taaluma - Mloganzila; na kuanzishwa mifumo 6 ya kimtandao ya
uendeshaji wa Chuo ambayo imeunganishwa na mfumo wa kuratibu ufundishaji na
ujifunzaji – eLearning.
(viii) Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa michoro ya jengo la maktaba lenye uwezo wa
kuchukua wanafunzi 2,500 kwa wakati mmoja; na kukarabatiwa kwa kafeteria na
eneo la mapokezi katika kituo cha Mikutano cha Ushirika.
(ix) Upanuzi na Ukarabati wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl. Nyerere
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa jengo la mihadhara lenye uwezo wa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 39
kuchukua wanafunzi 324 kwa wakati mmoja; na kukamilika kwa michoro na
makadirio ya gharama za ujenzi wa maktaba katika kampasi ya Kivukoni na hosteli
katika kampasi ya Zanzibar.
(x) Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela - Arusha
Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na utekelezaji wa miradi ya utafiti 33 inayojumuisha
utafiti wa ugonjwa wa kimeta kwa wanyama pori na wanaofugwa, utafiti wa kuondoa
sumu kuvu katika nafaka (Aflatoxin) na utafiti katika zao la ndizi ili kupata miche bora
inayohimili magonjwa ya kitropiki.
(xi) Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaaam - DIT
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ukarabati wa jengo la madarasa mawili yenye
uwezo wa kuchukua wanafunzi 50 kila moja katika Kampasi ya Myunga; na
kununuliwa kwa asilimia 40 ya vifaa vya upanuzi wa jengo la maktaba.
(xii) Upanuzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa michoro ya ramani ya jengo la vyumba viwili (2)
vya madarasa vyenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 600 kwa wakati mmoja;
kukamilika kwa ukarabati wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika
kampasi ya Rukwa; na kukamilika kwa asilimia 69 ya ujenzi wa jengo la maktaba
awamu ya kwanza lenye uwezo wa kuchukua wananfunzi 2,500 kwa wakati mmoja.
(xiii) Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - SUA
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ukarabati wa mabweni matano (5) ya wananfunzi
yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 222 katika Kampasi ya Solomon Mahlangu na
mabweni mawili (2) ya Nicholaus Kuhanga yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi
924 katika Kampasi Kuu; kukamilika kwa ukarabati wa hosteli moja (1) iliyopo katika
Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza kwa ajili ya wanafunzi wa kigeni yenye uwezo wa
kuchukua wanafunzi 16 kwa wakati mmoja; kukamilika kwa ukarabati wa Hospitali ya
Rufaa ya Taifa ya Wanyama iliyopo katika ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za
Afya; na kuendelea na ujenzi wa maabara mtambuka yenye uwezo wa kuchukua
wanafunzi 1,600 kwa wakati mmoja ambapo utekelezaji wa awamu ya kwanza
umefikia asilimia 50.
(xiv) Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa Maktaba ya Kimataifa yenye uwezo wa
kuchukua wanafunzi 2,100 kwa wakati mmoja, ukumbi wa mikutano unaochukua
watu 580 na Kituo cha Utamaduni wa Kichina chenye ofisi 5 na madarasa 10 yenye
uwezo wa kuchukua wananfunzi 550 kwa wakati mmoja; na kununuliwa kwa vitabu
6,927 na mashubaka (bookshelf) kwa ajili ya kuhifadhi vitabu katika maktaba
iliyojengwa.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 40
(f) Ujuzi na Utafiti
(i) Kukuza Stadi za Kazi kwa ajili ya Shughuli za Kuzalisha na Kukuza
Uchumi
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ukarabati na ujenzi wa
vyuo 20 vya Maendeleo ya Wananchi; kukamilika ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa
kike katika Chuo Kikuu Ardhi (ARU); kutolewa kwa mafunzo kwa vijana 650 kutoka
kaya maskini katika taasisi mbalimbali za mafunzo kulingana na mahitaji yao na
vipaumbele vya Taifa; kuanzishwa mabaraza ya kisekta ya kusimamia maarifa kwa
kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF); kutolewa mafunzo kuhusu malipo
kwa mfumo wa kielektroniki kwa wahasibu kutoka vyuo 54 vya Maendeleo ya
Wananchi, vyuo 35 vya Ualimu na makao makuu ya Wizara, wakaguzi 16 wa ndani,
na wataalam 8 wa TEHAMA kutoka Wizarani (MoEST), NACTE, HESLB, VETA, na
TCU; na kutolewa mafunzo kwa watumishi 304 katika nyanja za huduma kwa
wateja, utunzaji nyaraka, maadili katika Utumishi wa Umma.
(ii) Mfuko wa Utafiti na Maendeleo wa COSTECH
Hatua iliyofikiwa ni: kutolewa mafunzo kwa washiriki 20 wakiwemo wasimamizi wa
masuala ya Bioteknolojia katika taasisi na wizara mbalimbali; kuendelea kufadhili na
kusimamia miradi ya utafiti katika maeneo ya kipaumbele kwa sekta za Viwanda,
TEHAMA, Kilimo, Afya, Mazingira na Maliasili; kuwezeshwa kifedha wabunifu 30
kuendeleza ubunifu wao; kuendelea na ujenzi na ukarabati wa maabara za utafiti
katika tafiti za utafiti wa mifugo Tanga (TALIRI – Tanga), Uyole (TALIRI – Uyole), na
Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI – Sota, Musoma); kugharamiwa kwa miradi
mipya minane (8) ya ukarabati wa miundombinu ya utafiti katika taasisi sita (6) za
utafiti (NIMR, SUA, HORTI, TALIRI – Mpwapwa, MUHAS, na TVI); kugharamiwa
kwa miradi minne (4) ya utafiti iliyotekelezwa na TAFIRI, STAMICO na TIRDO.
(iii) Ujenzi wa Maabara ya Mionzi ya Nguvu za Atomiki
Hatua iliyofikiwa ni: kukaguliwa kwa migodi sita (6) ya chini ya ardhi (underground
mines) ambayo ni Geita Gold Mine, North Mara Gold Mine, Bulyankulu Gold Mine,
Tanzanite One Limited, Stamigold Company Limited, na Buzwagi Gold Mine na
kubaini kuwa ipo salama na haina madhara kwa mazingira na wafanyakazi;
kukaguliwa na kuhakikiwa kwa vituo 590 vya vyanzo vya mionzi; kusajiliwa kwa vituo
vipya 101 kwa ajili ya kuanza kutumia vyanzo vya mionzi; kupimwa viwango vya
mionzi kwa wafanyakazi 1,663 kwenye vituo 376; kupimwa kwa sampuli 12,628 na
kutoa vibali 12,628; kufunguliwa kwa ofisi ya Kanda ya Ziwa - Mwanza na ofisi
ndogo saba (7) maeneo ya Kigoma, Pemba, Mtwara (Mtambaswala na Kalambo),
Kagera (Kabanga), Songwe (Kasumulu) , Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA)
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 41
hivyo TAEC kuwa na ofisi 22 nchini; na kununuliwa kwa vifaa 17 vya kudhibiti ubora
wa machine za tiba ya mionzi na matumizi salama ya mionzi kwa ajili ya ofisi za
mipakani.
(g) Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi
Upanuzi na Ukarabati wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi
Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na ukarabati wa awamu ya kwanza wa Vyuo vya
Maendeleo ya Wananchi 20 vya Rubondo, Gera, Munguri, Chisalu, Newala, Kilwa
Masoko, Ikwiriri, Mtawanya, Handeni, Mto wa Mbu, Urambo, Kasulu, Tarime, Ilula,
Muhukuru, Sofi, Chilala, Kiwanda, Malampaka na Karumo ambapo ukarabati upo
katika hatua za ukamilishaji.
B. Afya na Maendeleo ya Jamii
Afya
(a) Mradi wa Kupunguza Vifo vya akina Mama Vinavyotokana na Uzazi:
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa marekebisho katika Wodi ya Wazazi na ufungaji
vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora – Kitete na kujenga
kichomea taka, kuweka mifumo ya gesi na vifaa tiba; kukamilika kwa ujenzi na
marekebisho ya Wodi za Wazazi katika Vituo vya Afya vya Kitunda na Mazinge
katika Wilaya ya Sikonge; na kukamilika kwa ujenzi na marekebisho katika Chuo cha
Maafisa Tabibu Tabora ikiwemo kukamilisha mfumo wa umeme.
(b) Mradi wa Kuboresha Hospitali za Rufaa za Mikoa
Hatua iliyofikiwa ni:
(i) Simiyu: Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje na kuanza kutoa
huduma; ujenzi wa msingi wa jengo la uchunguzi na jengo la mama na mtoto
umekamilika ambapo hatua inayofuata ni usimakaji wa nguzo kwa ajili ujenzi
wa sakafu ya pili; na kununuliwa kwa mashine 1 ya x-ray kwa ajili ya
kuboresha huduma za uchunguzi wa magonjwa; na kuendelea na ujenzi wa
jengo la kutolea huduma za uzazi.
(ii) Geita: Ujenzi wa majengo ya kutolea huduma za wagonjwa wa nje, mgahawa
na sehemu ya kufulia upo kwenye hatua za mwisho kukamilika na ujenzi wa
jengo ya upasuaji na jengo la mionzi uko katika hatua za awali; na upatikanaji
wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 91.
(iii) Njombe: Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje; kununuliwa
kwa mashine 1 ya X-ray kwa ajili ya kuboresha huduma za uchunguzi wa
magonjwa; kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za uzazi; na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 42
upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 97.
(iv) Katavi: Kuendelea na ujenzi wa jengo la wazazi, jengo la uchunguzi na jengo
la utawala ambapo ujenzi umefikia hatua ya msingi; na kununuliwa kwa
mashine 1 ya X-ray kwa ajili ya kuboresha huduma za uchunguzi wa
magonjwa; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 96.
(v) Shinyanga: kukamilika kwa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje na utawala;
kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za uzazi; na upatikanaji wa
dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 97.
(vi) Kwangwa (Mara): Kukamilika kwa Jengo la wagonjwa wa nje, jengo la
wazazi, jengo la uchunguzi na wodi za kulaza wagonjwa.
(vii) Manyara: Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje na utawala umefikia hatua ya
upauaji na hatua inayofuata ni kuweka samani, vifaa na vifaa tiba; na
upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 94.
(viii) Sekou Toure (Mwanza): Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za
uzazi; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 97.
(ix) Mwananyamala (Dar es Salaam): Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea
huduma za uzazi; kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za
dharura na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 97.
(x) Mawenzi (Kilimanjaro): Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za
uzazi; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 75.
(xi) Sokoine (Lindi): Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za
dharura; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 97.
(xii) Amana (Dar es Salaam): Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma
za dharura; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia
99.
(xiii) Temeke (Dar es Salaam): Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma
za dharura; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia
95.
(xiv) Kagera: Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za dharura; na
upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 99.
(c) Ujenzi wa Hospitali za Halmashauri na Vituo vya Afya: Hatua iliyofikiwa ni:
kuendelea na ujenzi wa hospitali za Halmashauri (67); kuendelea na ujenzi na
ukarabati wa vituo vya kutolea huduma za afya 352 (zikiwemo Hospitali 9, Vituo vya
Afya 304 na Zahanati 39); na kuendelea na ujenzi na ukarabati wa nyumba 301 za
watumishi.
(d) Mradi wa Ununuzi na Usambazaji wa Dawa: Hatua iliyofikiwa ni kununuliwa
kwa dawa, vifaa tiba na vitendanishi na kusambazwa katika vituo vya umma vya
kutolea huduma nchini ambapo upatikanaji wa dawa muhimu aina 30 katika vituo
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 43
vya kutolea huduma za afya umefikia asilimia 94.4; kusambazwa lita 239,020 za
viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi vya mbu katika Halmashauri zote nchini;
kununuliwa mashine za X-ray 11 za Kidigitali ambazo zimesambazwa katika
hospitali za Ruvuma, Chato, Morogoro, Simiyu, Magu, Singida, Nzega, Njombe,
Bukoba, Amana na Katavi; kununuliwa vifaa na vifaa tiba na kusambazwa katika
vituo vya afya 318; kununuliwa na kusambazwa mashine 8 za X-ray na viti 20 kwa
ajili ya kutolea huduma ya kinywa; na kununuliwa kwa Digital X-rays 28 na LED
Microscope 389 ambazo zimesambazwa katika mikoa ya Iringa, Kilimanjaro, Mara,
Mbeya, Ruvuma, Tanga, Rukwa, Njombe, Songwe na Dar es Salaam.
Vile vile, mfumo wa Mshitiri umeanzishwa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara
unaoviwezesha vituo vya kutolea huduma za afya kupata mahitaji ya vifaa, vifaa tiba,
dawa na vitendanishi toka kwa wauzaji binafsi walioteuliwa pindi mahitaji
yanapokosekana katika Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na kutolewa mafunzo kwa
Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri na
wataalam ngazi ya Wizara pamoja na watoa huduma ya afya 103 ngazi ya Taifa,
431 ngazi ya Mkoa, 540 Hospitali za Halmashauri na wafanyabiashara 142 kuhusu
matumizi ya mfumo huo.
(e) Hospitali ya Rufaa Mbeya: Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa
jengo la vifaa vya uchunguzi wa mionzi; kukamilika kwa upanuzi wa eneo la
mapokezi na jengo la huduma za uzazi na mtoto katika kitengo cha wazazi Meta;
kuendelea na upanuzi wa jengo la kutolea huduma; na kununuliwa kwa CT-Scan
mpya.
(f) Hospitali ya Rufaa ya Magonjwa ya Kifua Kikuu – Kibong’oto: Hatua
iliyofikiwa ni kununuliwa kwa mashine nne (4) za uchunguzi wa madhara yatokanayo
na dawa; na kununuliwa kwa mashine 1 ya ultrasound kwa ajili ya uchunguzi wa
magonjwa.
(g) Hospitali ya Rufaa Bugando: Hatua iliyofikiwa ni kununuliwa kwa mashine
ya tiba ya mionzi aina ya Brachytherapy na kukamilika kwa ujenzi wa maabara ya
kisasa ya uchunguzi wa magonjwa kupitia vinasaba.
(h) Mradi wa Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza: Hatua iliyofikiwa ni
kununuliwa na kusambazwa kwa chanjo hadi kufikia kiwango cha uchanjaji cha
asilimia 98 ya lengo kwa watoto chini ya mwaka mmoja. Chanjo hizo ni pamoja na:
dozi 3,000,000 za BCC kwa ajili ya kuwakinga watoto wachanga na ugonjwa wa
kifua kikuu; dozi 3,400,000 (bOPV) za kuzuia ugonjwa wa kupooza, dozi 3,000,000
(TT) za kuzuia ugonjwa wa pepopunda kwa mama wajawazito; dozi 5,453,400
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 44
(PCV-13) za kuwakinga watoto dhidi ya nimonia na homa ya uti wa mgongo; dozi
2,155,500 (Rota) za kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa kuhara; dozi 950,500 za
HPV kwa ajili ya kuwakinga wasichana dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi; dozi
1,598,850 za chanjo ya sindano (IPV) kwa ajili ya kuzuia ugonjwa wa kupooza kwa
watoto; na dozi 3,012,000 za Penta kwa ajili ya kuzuia magonjwa ya dondakoo,
kifaduro, kupooza, homa ya ini, na homa ya uti wa mgongo.
(i) Hospitali ya Taifa ya Muhimbili: Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa
ukarabati wa jengo la uchunguzi maalum wa watoto wagonjwa walio mahututi
pamoja na ufungaji wa vifaa tiba na kuunganishwa mfumo wa taarifa wa hospitali na
mfumo wa Malipo wa Serikali GePG.
(j) Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI): Hatua iliyofikiwa ni kununuliwa darubini
ya kisasa kwa ajili ya kufanya upasuaji wa mishipa ya fahamu na ubongo
(Neurosurgeries); kununuliwa kwa mtambo mpya na wa kisasa aina ya Chiller kwa
ajili ya kutawanya hewa kwenye vyumba vya upasuaji na Chumba cha Wagonjwa
Mahututi – ICU; kununuliwa kwa mashine tatu (3) za kisasa aina ya ERBA XL 600,
DYMIND DH 76 na COBAS e411 kwa ajili ya kupima sampuli za damu; kukamilika
kwa ujenzi wa vyumba vitatu vya upasuaji hivyo kuongeza idadi ya vyumba vya
upasuaji kutoka 6 hadi 9; kukamilika kwa upanuzi wa eneo kubwa la mapokezi ya
dharura; na kukamilika kwa ufungaji wa vifaa tiba mbalimbali vikiwemo MRI, CT
Scan, Digital X-Ray machine, Modern Ultrasound machine na vifaa vya wodini.
(k) Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ukarabati wa jengo la hospitali kwa ajili ya wodi
mpya ya watoto yenye vitanda 32 vya kuhudumia watoto wenye matatizo ya moyo;
na kuboreshwa kwa huduma za famasia kwa kutoa dawa muhimu kwa matibabu ya
moyo kwa asilimia 95.
Maendeleo ya Jamii
(a) Ukarabati na Ujenzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii
Kazi zilizotekelezwa ni kuendelea na ukarabati wa hosteli, kumbi za mihadhara,
madarasa, majengo ya utawala na nyumba za watumishi katika vyuo vya
Rungemba, Mlale, Misungwi, Monduli, Ruaha, Buhare na Uyole; na kukamilika kwa
ujenzi wa fensi katika Chuo cha Rungemba na ukarabati wa karakana katika Chuo
cha Mabughai.
(b) Uwezeshaji Wanawake
Shughuli zilizofanyika ni: kutolewa kwa mikopo ya Shilingi bilioni 2.05 kwa
wanawake wajasiriamali 3,035 kupitia Dirisha la Wanawake katika Benki ya TPB;
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 45
kutolewa kwa mikopo ya uwezeshaji wanawake, Shilingi bilioni 11.128 inayotokana
na asilimia 4 ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa vikundi 4,898 vyenye
wanawake wajasiriamali 44,210; kuwezeshwa kwa vikundi 583 vya wanawake
vyenye wanawake wajasiriamali 11,833 kutoka mikoa 15 kupata masoko ya huduma
na bidhaa wanazozalisha, uzoefu na teknolojia rahisi na rafiki kupitia maonesho ya
biashara ya kitaifa na kimataifa; na kutolewa kwa mafunzo kwa wanawake
wajasiriamali 444 kuhusu stadi za ujasiriamali, huduma ya hifadhi ya jamii, fursa za
kiuchumi, uboreshaji wa huduma na bidhaa wanazozalisha, teknolojia rahisi za
uzalishaji wa bidhaa na urasimishaji wa biashara.
(c) Maendeleo ya Awali ya Mtoto
Kuendelea kutolewa kwa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya watoto katika
maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa; kuongezeka kwa idadi ya watoto
waliopatiwa huduma ya simu bure (Na. 116) kutoka watoto 493 (2017/18) hadi
watoto 3,833 (2018/19); kutolewa mafunzo kuhusu malezi chanya kwa watoto
ambapo walishiriki wazazi na walezi 635 katika ngazi ya familia kutoka halmashauri
132; kuanzishwa kwa vikundi vya malezi 1,184 katika halmashauri 15 za mikoa 7;
kusajiliwa kwa vituo 146 vya kulelea watoto walio chini ya miaka mitano (Day Care
Centres) ambapo watoto 149,093 (Ke 76,094 na Me 72,999) waliandikishwa;
kutolewa kwa mafunzo kuhusu Programu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali
ya Mtoto kwa walezi 970 katika vituo vya kulelela watoto mchana kutoka Arusha,
Temeke, Ubungo, na Ilala; na kuundwa kwa kamati za ulinzi na usalama wa mtoto
na mwanamke katika mikoa 26, Halmashauri 184, kata 2,490 kati ya 4,420 na Vijiji
7,900 kati ya 16,626.
(d) Kuwezesha Huduma za Ustawi wa Jamii
Shughuli zilizofanyika ni: kutambuliwa kwa watoto 389,012 waishio katika mazingira
hatarishi hivyo kufikisha idadi ya watoto 1,495,049; kutolewa kwa kadi za bima ya
afya kwa watoto 900 wanaoishi katika makao ya watoto; kuendelea kusajili makao
ya watoto ambapo leseni 64 za usajili zilitolewa; kuwezeshwa upatikanaji wa
huduma za msingi za malazi, chakula, mavazi, matibabu na elimu kwa watoto
13,420 (Ke 6,651 na Me 6,769) waishio katika makao ya watoto yanayomilikiwa na
Serikali na taasisi binafsi; kutolewa kwa huduma za chakula, malazi, mavazi,
matibabu na elimu kwa watoto 467 (Ke 49 na Me 418) katika mahabusu 5 za watoto
walio katika mkinzano na sheria; kuendelea kutekeleza programu ya marekebisho ya
tabia kwa watoto walio katika mkinzano wa kisheria ambapo watoto 64 (Ke 7 na Me
57) walichepushwa kutoka katika mfumo rasmi wa haki jinai; na kuendelea kutoa
huduma za malezi ya kambo na kuasili watoto ambapo watoto 70 (Ke 36 na Me 34)
walipata huduma hizo.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 46
Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni kutambuliwa kwa wazee 750,622 kwa ajili ya
kupatiwa vitambulisho vya matibabu bure ambapo wazee 247,705 wamepatiwa kadi
za matibabu bure; kuendelea kutolewa huduma za msingi za chakula, malazi,
mavazi na matibabu kwa wazee wasiojiweza 510 (Ke 234 na Me 276) katika makazi
17 ya wazee; na kutambuliwa kwa watu wenye ulemavu 405,426 na kupatiwa
huduma za afya.
(e) Mpango wa Uimarishaji wa Mifumo ya Taarifa za Ustawi wa Jamii
Shughuli zilizofanyika ni kuweka mfumo wa kieletroniki wa ukusanyaji na utunzaji
taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi na wale waishio na kufanya kazi
mitaani katika Halmashauri 147 kati ya 184; na kununuliwa na kusambazwa kwa
kompyuta, mashine za kurudufu na modemu 101 kwenye Mikoa 23 na Halmashauri
73 kwa ajili ya matumizi ya mfumo wa kieletroniki wa Taarifa za Ustawi wa Jamii.
(f) Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
Shughuli zilizofanyika ni: kuboreshwa kwa mfuko ili kuruhusu watumiaji kupata
huduma za matibabu ya rufaa hadi katika hospitali za rufaa za Mikoa; na kukamilika
na kuanza kutumika kwa kanzidata ya utunzaji wa taarifa za wanachama nchi nzima.
C. Maji na Usafi wa Mazingira
(a) Kuboresha Huduma za Maji Dar es Salaam
Hatua iliyofikiwa ni: ukamilishaji wa ujenzi wa matenki na ulazaji wa mabomba ya
kusambaza maji katika jiji la Dar es salaam na maeneo ya Bagamoyo, Kibaha na
Mlandizi ambayo yanapata huduma ya maji kutoka miradi ya Ruvu Juu na Chini; na
kupatikana kwa mkandarasi kwa ajili ya ununuzi na ufungaji wa dira za maji pamoja
na vifaa vya uboreshaji wa huduma za maji.
(b) Mradi wa Maji wa Kimbiji na Mpera
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa visima 19 kati ya 20 vilivyopangwa kuchimbwa
katika eneo la Kimbiji na Mpera; na kuanza maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya
kusambaza huduma ya maji kwa wananchi kutoka katika visima vitano vya awali vya
Kimbiji.
(c) Maji kutoka Ziwa Victoria
Hatua iliyofikiwa ni: ujenzi wa miundombinu ya maji katika miji ya Tabora, Igunga,
Uyui na Nzega pamoja na vijiji 89 vilivyo pembezoni mwa bomba Kuu umefikia
asilimia 68.5; na kazi ya ulazaji wa bomba la kusambazia maji katika miji ya Isaka,
Tinde na Kagongwa imekamilika kwa asilimia 87.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 47
(d) Miradi ya Maji ya Kitaifa
Hatua iliyofikiwa ni kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya maji hususan katika
ulazaji wa mambomba, upanuzi na ukarabati katika maeneo yanayohudumiwa na
miradi ya kitaifa ambapo: Mradi wa Chalinze (Pwani) utekelezaji umefikia asilimia
79.5 ikihusisha pamoja na kazi nyingine ujenzi wa matanki, upanuzi wa mtandao wa
mabomba na upanuzi wa kidakio; mradi wa Wanging‟ombe (Njombe) ambao
umefikia asilimia 85 za ukarabati na kuwezesha kukamilika kwa matanki 44 ya
kuhifadhi maji na mabirika 59 ya kunyweshea mifugo pamoja na kuendelea
kumalizia ukarabati wa chanzo cha Mbukwa. Aidha, miradi ya Mugango - Kiabakari
(Mara) na Handeni Trunk Main usanifu wa kina umekamilika na taratibu za
kuwapata makandarasi wa ujenzi zinaendelea.
(e) Mradi wa Maji Masasi – Nachingwea
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ukarabati wa mradi ambapo wananchi 24,077
katika baadhi ya maeneo wameanza kusambaziwa maji; na kuanza ujenzi wa
mtambo wa kutibu na kusafisha maji kwa ajili ya kuwapatia wananchi huduma ya
maji safi na salama katika eneo lote la mradi.
(f) Kuboresha Huduma za Maji Vijijini
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa miradi 198 na kufanya jumla ya miradi yote
iliyokamilika kufikia 1,659 ambapo vituo vya kuchotea maji vimeongezeka kufikia
131,370 na kuhudumia wananchi 25,359,290; miradi 653 ya maji vijijini inaendelea
kutekelezwa ikiwa katika hatua mbalimbali katika Halmashauri nchini. Kwa upande
wa mradi wa Same – Mwanga - Korogwe ukamilishaji wa miundombinu ya msingi
unaendelea ambapo bomba kuu la kusafirisha maji, kitekeo cha maji, mtambo wa
kusafisha maji na matanki ya kuhifadhi maji, maabara na eneo la kuhifadhia dawa za
kutibu maji vimekamilika. Kazi zinazoendelea ni usambazaji wa maji kati miji ya
Same ambapo umefikia asilimia 55 na Mwanga asilimia 15.
(g) Kuboresha Huduma za Maji Mijini
(i) Upatikanaji wa huduma za maji Jijini Dar es Salaam umefikia asilimia 85,
katika mikoa mingine asilimia 80, miji midogo asilimia 64 na vijijini asilimia
64.8;
(ii) Ujenzi wa miradi ya maji katika miji mikuu ya mikoa mipya umeendelea
kutekelezwa na kufikia hatua zifuatazo: Geita (umekamilika), Njombe (asilimia
95); na Songwe (asilimia 90);
(iii) Ukamilishaji wa miradi ya maji katika Miji ya Wilaya na Miji midogo ya
Misungwi, Lamadi, Magu, Longido, Orkesumet unaendelea pamoja na miradi
ya matokeo ya haraka (quickwins) katika miji 57; na
(iv) Mradi wa uondoaji majitaka Jijini Dar es Salaam katika eneo la Jangwani na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 48
Mbezi Beach unaendelea ambapo Mtaalamu Mshauri atakayesimamia kazi
hiyo amepatikana. Aidha, ulipaji wa fidia katika eneo la Kurasini umekamilika
na taratibu za kuanza kazi ya upembuzi yakinifu zinaendelea.
(h) Kuimarisha Maabara na Bodi za Maji za Mabonde
Ofisi za maji za mabonde na maabara za maji zimeendelea kuimarishwa kwa
kujengwa na kukarabatiwa kama ifuatavyo: Ruvuma na Pwani ya Kusini (asilimia
90), Ziwa Nyasa (asilimia 50), Ziwa Rukwa (asilimia 65), Bonde la Kanda ya Kati
(asilimia 95) na ujenzi wa ofisi ndogo za katika Bonde la Rufiji katika maeneo ya
Mkoji na Kimani (asilimia 65). Ujenzi na ukarabati wa Maabara ya Maji ya Dar es
Salaam umefikia asilimia 99. Vile vile, vifaa vya upimaji wa rasilimali za maji
vimetolewa kwa mabonde ya Mto Rufiji na Wami Ruvu kwa ajili ya kuongeza tija
katika mabonde hayo.
D. Vijana na Ajira
(a) Programu ya Kitaifa ya Kukuza Ujuzi
Hatua iliyofikia katika kutekeleza Programu hiyo ni kama ifuatavyo:
(i) Kutolewa kwa mafunzo ya kilimo cha kitalu nyumba kwa vijana 18,800 kwa
lengo la kuwapatia vijana ujuzi stahiki ili waweze kujiajiri na kuajiriwa;
(ii) Kutolewa mafunzo kwa vijana 10,443 ya kurasimisha ujuzi uliopatikana kwa
mfumo usio rasmi kwa fani za ufundi wa magari, useremala, uashi, upishi,
huduma za vyakula na vinywaji, ufundi umeme, uchomeleaji, ufundi bomba,
uchorongaji vipuri na ushonaji nguo kupitia vyuo vya ufundi VETA wanapata
mafunzo; na
(iii) Kutolewa kwa mafunzo ya vitendo kwa wahitimu 136 wa elimu ya juu kupitia
viwanda na kampuni mbalimbali ya umma na sekta binafsi.
(b) Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
Hatua iliyofikiwa ni: kutolewa kwa mikopo nafuu yenye thamani ya Shilingi bilioni 4.2
kwa vikundi vya vijana 755, vyenye wanachama 3,661 katika Halmashauri 128 za
Tanzania Bara; kuanzishwa kwa SACCOS 127 za Vijana kati ya 184 zinazotarajiwa
kuanzishwa hadi kufikia mwaka 2020; kutolewa kwa mashine 4 za kutengeneza
matofali na mtaji wa Shilingi 500,000 kwa kila halmashauri kwenye halmashauri 168
nchini. Aidha, vijana 6,720 wamepata ajira ya moja kwa moja na vijana 1,905
wamepata ajira zilizotokana na utekelezaji wa programu ya utengenezaji wa matofali
ya bei nafuu.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 49
E. Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
(a) Upanuzi wa Usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
Kazi zilizotekelezwa ni: kuendelea kupanua usikivu wa redio ambapo umeongezeka
kutoka wilaya 87 mwaka 2017 hadi wilaya 102 Machi 2019; kukamilika kwa usanifu
wa Jengo la Makao Makuu ya TBC Jijini Dodoma litakalo husisha jengo la
Utangazaji na Utawala; uanzishaji wa Chaneli ya Tanzania Safari inayotangaza
vivutio vya utalii; kuanzishwa kwa mifumo ya kielekroniki hususan tovuti na
programu tumizi (protu au App); na kuratibiwa kwa jumla ya vipindi 17 vya
TUNATEKELEZA, vipindi hivyo vilihusisha Wizara 16 na Mikoa miwili (2).
(b) Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika
Shughuli zilizotekelezwa ni: kuendelea kukarabati jengo lililokuwa likitumiwa na Ofisi
iliyokuwa ya Kamati ya Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika;
kuorodheshwa kwa maeneo 255 ya ukombozi wa Bara la Afrika pamoja na
kukusanywa kwa vifaa mbalimbali 6,782 vya historia; uanzishaji wa tovuti ya
Programu, kazi inayotarajiwa kuanza ni uingizaji wa taarifa mbalimbali za Programu
na uanzishaji wa sheria ya kulinda vifaa na maeneo yanayosimamiwa na Programu.
(c) Ujenzi wa Eneo Changamani la Michezo – Dar es Salaam na Dodoma
Shughuli zilizotekelezwa ni: Dar es Salaam: kuendelea kwa ukarabati katika Uwanja
wa Taifa ambapo vyumba vya wachezaji kubadilishia nguo pamoja na kukamilika
kwa chumba cha “Antidopping”; kuendelea kwa ukarabati wa chumba cha waandishi
wa habari; ujenzi wa paa la watu Maalum (VVIP); kuwekwa kwa nyasi bandia kwa
ajili ya Uwanja wa Uhuru; Dodoma: kuendelea kwa maandalizi ya ujenzi wa Uwanja
wa Michezo wa Dodoma kwa kubainisha barabara kwa kuwekwa vibao na nguzo za
tahadhari dhidi ya wavamizi; na kukamilika kwa upembuzi yakinifu, “topographical
survey”, tathmini ya mazingira, “geotechnical Survey” na maandalizi ya mchoro wa
uwanja.
(d) Chuo cha Michezo cha Malya
Kazi zilizotekelezwa ni: kudahiliwa kwa wanafunzi 141; kununuliwa kwa matenki sita
(6) ya kuhifadhia maji yenye ujazo wa lita 5,000 kila moja, hatua ambayo
imeimarisha upatikanaji wa maji chuoni hapo.
F. Hifadhi ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
(a) Usimamizi Endelevu wa Matumizi ya Ardhi ya Bonde la Nyasa
Hatua iliyofikiwa ni: kufundisha wawezeshaji 20 kwa Wilaya za Makete, Kyela,
Mbinga, Nyasa na Ludewa zinazotekeleza mradi; uanzishwaji wa vikundi vitatu vya
wakulima katika wilaya zinazotekeleza mradi; kukamilika kwa Mpango wa Matumizi
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 50
bora ya ardhi katika vijiji 15 katika wilaya zinazotekeleza mradi; uandaaji wa vitalu
vya miche ya miti na uanzishwaji wa mashamba darasa katika Wilaya za Ludewa,
Kyela na Mbinga; na ununuzi wa vifaa vitakavyotumika wakati wa utekelezaji wa
mradi.
(b) Mradi wa Kuwezesha Mfuko wa Mazingira
Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na maandalizi ya marekebisho ya Sheria ya
Mazingira ya mwaka 2004 ili kuwezesha Mfuko wa Mazingira kufanya kazi kwa
ufanisi.
(c) Mradi wa Kukabiliana na Changamoto za Kimazingira-Pwani ya Dar es
Salaam Kutokana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi
Kupanda hekari 40 za miti ya mikoko katika wilaya ya Temeke katika maeneo ya
Tundwi, Songani na Pembemnazi; kukamilika kwa ujenzi wa mifereji ya maji
iliyoharibiwa na mafuriko; na kuendelea na tathmini ya uwezo wa kuhimili mabadiliko
ya tabianchi kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
3.2.2.4. Mazingira Wezeshi kwa Uendeshaji Biashara na Uwekezaji
A. Miundombinu
(a) Reli
(i) Mfuko wa Maendeleo ya Reli
Hatua iliyofikiwa ni: kupokelewa kwa Shilingi bilioni 123.2 katika Mfuko wa Reli
ambapo Shilingi bilioni 38 zilitumika kama sehemu ya malipo ya awali kwa ajili ya
ujenzi wa reli ya kati kwa standard gauge ya kutoka Dar es salaam hadi Morogoro.
Aidha, jumla ya Shilingi bilioni 59.6 zilitumka kununua vichwa 11 vya treni kwa ajili
ya njia kuu.
(ii) Ukarabati wa Njia Kuu ya Reli
Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ukarabati wa reli kwa sehemu ya Dar es Salaam –
Isaka (km 970); kuboresha eneo la kupakia/kupakua mizigo katika Bandari ya Dar es
Salaam; na kukarabati vituo vya kuhudumia mizigo vya Ilala na Isaka.
(iii) Ufufuaji wa Njia ya Reli ya Tanga – Arusha (km 439)
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ukarabati wa kipande cha Tanga – Mombo (km
129) ambacho kimeanza kufanya kazi ya kusafirisha mizigo; kipande cha Mombo –
Same (km 124) kipo katika hatua za mwisho kukamilika ambapo ukarabati wa njia
ya reli umekamilika na kazi inayoendelea kwa kipande hiki ni ujenzi wa madaraja 7;
na kuendelea na ukarabati wa kipande cha Same – Arusha (km 186). Kwa ujumla
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 51
ukarabati wa Reli ya Tanga – Arusha (439) umefikia asilimia 80.
(iv) Ukarabati wa Mabehewa
Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ukarabati wa mabehewa 15.
(v) Usafiri wa Reli Jijini Dar es Salaam
Hatua iliyofikiwa ni: kuimarika kwa usafirishaji kwa njia ya treni katika jiji la Dar es
Salaam ambapo abiria 1,524,381 walisafirishwa kati ya stesheni za Dar es Salaam
na Mwakanga kupitia reli ya TAZARA; na abiria 5,431,037 walisafirishwa kati ya
Stesheni – Ubungo – Pugu.
(b) Barabara na Madaraja
Barabara za Lami Zinazofungua Fursa za Kiuchumi
(i) Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupilo - Mahenge /Malinyi - Londo -
Lumecha/Songea (km 499): hatua iliyofikiwa ni kuendelea na ujenzi kwa
sehemu ya Kidatu – Ifakara (km 66.9).
(ii) Barabara ya Tabora - Ipole - Koga - Mpanda (km 370): hatua iliyofikiwa ni
kujengwa kwa barabara sehemu za Tabora – Sikonge (km 30) ambapo
utekelezaji umekamilika; na kuendelea na utekelezaji katika sehemu za
Usesula - Komanga (km 115.5) ambapo ujenzi umefikia asilimia 12.91,
Komanga – Kasinde (km 112.8) asilimia 18.26, na Kasinde – Mpanda (km
111.7) asilimia 15.94.
(iii) Barabara ya Makutano - Natta – Mugumu (km 125)/Loliondo - Mto wa
Mbu (km 213): hatua iliyofikiwa ni: kufika asilimia 74 ya ujenzi katika
barabara ya Makutano - Natta – Mugumu (km 125) sehemu ya Makutano -
Sanzate (km 50) na kuendelea na hatua za kumpata mkandarasi wa ujenzi
kwa sehemu ya Sanzate - Natta - Mugumu (km 85). Aidha, ujenzi wa
barabara ya Mto wa Mbu - Loliondo sehemu ya Wasso - Sale Junction (km
49) unaendelea ambapo utekelezaji umefikia asilimia 25.15.
(iv) Barabara ya Manyoni - Itigi – Tabora (km 259.7): hatua iliyofikiwa ni:
kukamilika kwa ujenzi wa sehemu ya Tabora – Nyahua (km 85) na Manyoni -
Itigi - Chaya (km 89.35); na kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Nyahua –
Chaya (km 85.4) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 26.
(v) Barabara ya Itoni – Ludewa - Manda (km 211): hatua iliyofikiwa ni
kuendelea kwa ujenzi wa kiwango cha lami na zege katika sehemu ya Lusitu
– Mawengi (km 50) ambapo utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 20.14.
(vi) Barabara ya Handeni - Kibereshi – Kibaya - Singida (km 460): hatua
iliyofikiwa ni kukamilika kwa usanifu wa kina.
(vii) Barabara ya Dodoma – Mtera - Iringa (km 260): Mradi umekamilika. Kazi
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 52
inayoendelea kwa mchepuo wa barabara ya Iringa (Iringa Bypass km 7.3) ni
kuanza taratibu za kumpata mkandarasi.
(viii) Barabara ya Dodoma – Babati (km 243.80): Mradi umekamilika. Kazi
inayoendelea ni taratibu za kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya kazi ya
upembuzi na usanifu wa kina wa barabara ya mchepuo wa Babati (Babati
Bypass – km 12).
(ix) Barabara ya Mbeya - Makongolosi - Rungwa – Itigi - Mkiwa (km 171.9):
hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa sehemu za Chunya –
Makongolosi (km 43) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 20.6.
(x) Barabara ya Kigoma - Kidahwe - Uvinza – Kaliua - Tabora (km 389.7):
hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya
Urambo - Kaliua (km 28) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 35; na kuanza
maandalizi ya kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami
sehemu za Uvinza - Malagarasi (km 51.1) na Kazilambwa - Chagu (km 36).
(xi) Barabara ya Mtwara - Masasi - Songea - Mbamba Bay (km 1,470.9): hatua
iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi kwa sehemu ya Mbinga - Mbamba Bay (km
66) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 8.2 na sehemu ya Mtwara – Mnivata
(km 50) asilimia 42.7. Aidha, Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa
barabara ya Masasi - Nachingwea – Nanganga (km 96). Vile vile, kazi za
upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara ya Nanganga - Ruangwa
- Nachingwea (km 107) zimekamilika. Kwa barabara ya Likuyufusi - Mkenda
(km 122.5), maandalizi ya nyaraka za zabuni yanaendelea na kwa barabara
ya Kitui - Lituhi (km 90) mkataba wa ujenzi umesainiwa. Kwa sehemu ya
Mnivata - Masasi (km 160), taratibu za utafutaji fedha zinaendelea. Kwa
upande wa barabara ya Nachingwea - Liwale (km 130), mkataba kwa ajili ya
kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umesainiwa.
Barabara Zinazounganisha Tanzania na Nchi Jirani
(i) Barabara ya Sumbawanga - Matai - Kasanga Port (km 112): hatua
iliyofikiwa ni: kufikia asilimia 80.5 kwa kazi ya ujenzi kwa sehemu
Sumbawanga - Matai - Kasanga Port (km 112); na kuendelea na taratibu za
manunuzi za kumpata mkandarasi wa ujenzi kwa sehemu ya Matai - Kasesya
(km 50).
(ii) Barabara ya Marangu - Tarakea - Rongai - Kamwanga /Bomang’ombe -
Sanya Juu (km 330.31): hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa barabara ya
Arusha - Moshi - Holili (sehemu ya Sakina - Tengeru na mchepuo wa Arusha
– km 56.51) na kuendelea na ujenzi kwa sehemu za Sanya Juu - Elerai (km
32.2) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 92. Aidha, mikataba ya ujenzi
imesainiwa na maandalizi ya ujenzi yameanza kwa barabara za Kwa Sadala -
Masama - Machame Junction (km 16), Kiboroloni - Kikarara - Tsuduni - Kidia
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 53
(km 10.8), na km 2.6 katika barabara ya Kijenge - Usa River (km 14). Vile vile,
maandalizi ya upanuzi wa sehemu ya Tengeru - Moshi - Himo (km 105)
pamoja na ujenzi wa mizani ya Himo yamefikia hatua ya mwisho kabla ya
kutangaza zabuni za ujenzi.
(iii) Barabara ya Isaka - Lusahunga (km 533): hatua iliyofikiwa ni: kukamilika
kwa ukarabati wa barabara ya Isaka – Ushirombo (km 132); kufikia asilimia
74.8 ya kazi ya ukarabati kwa sehemu ya Ushirombo – Lusahunga (km 110);
kufikia asilimia 60 ya ujenzi wa kituo cha Pamoja cha Ukaguzi (One Stop
Inspection Station – OSIS) cha Nyakanazi; kukamilika kwa usanifu wa kina
wa barabara za Lusahunga - Rusumo (km 91) na Nyakasanza - Kobero (km
59) ili zijengwe upya kwa kiwango cha lami. Vile vile, upembuzi yakinifu na
usanifu wa kina wa barabara za Nyakahura - Kumubuga - Murusagamba na
Kumubuga - Rulenge - Kabanga Nickel zenye jumla ya urefu wa km 141
unaendelea.
(iv) Barabara ya Sumbawanga - Mpanda - Nyakanazi (km 517.4): hatua
iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa barabara ya Mpanda - Mishamo (km
100) sehemu ya Mpanda - Ifukutwa - Vikonge (km 35) ambapo utekelezaji
umefikia asilimia 66.3. Kwa upande wa barabara ya Namanyere - Katongoro -
New Kipili Port (km 64), upembuzi yakinifu na usanifu wa kina unaendelea.
(v) Barabara ya Nyanguge - Musoma, na Michepuo ya Usagara - Kisesa na
Bulamba - Kisorya (km 495.9): hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ukarabati
wa barabara ya Makutano - Sirari (km 83) na upanuzi wa barabara ya
kuelekea uwanja wa ndege wa Mwanza (km 12); kuendelea na ujenzi wa
barabara ya Nansio - Kisorya - Bunda - Nyamuswa sehemu ya Kisorya -
Bulamba (km 51) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 55; kuendelea na
taratibu za kuwapata makandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya
Musoma - Makojo - Busekela (km 92) na ukarabati wa sehemu ya Nyanguge -
Simiyu/Mara Border (km 100.4). Kwa upande wa barabara ya Nyamuswa -
Bunda - Bulamba (km 55), mapitio ya usanifu wa kina yanaendelea.
(vi) Barabara ya Mwigumbi - Maswa - Bariadi - Lamadi (km 171.8): hatua
iliyofikiwa ni kuendelea kwa ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya Maswa -
Bariadi (km 49.7) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 40.
(vii) Barabara ya Kidahwe - Kasulu – Kibondo - Nyakanazi (km 413): hatua
iliyofikiwa ni: kuendelea na ujezi wa barabara sehemu za Kidahwe - Kasulu
(km 63) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 70 na Nyakanazi - Kibondo (km
50) asilimia 60; kukamilika kwa usanifu wa kina na kutangazwa zabuni kwa
ajili ya ujenzi wa barabara ya Kabingo – Kibondo – Kasulu – Manyovu (km
260); na kuendelea na taratibu za kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa
barabara sehemu ya njia panda ya Nduta - Kibondo Mjini (km 25.6).
(viii) Barabara ya Usagara - Geita - Buzirayombo – Kyamyorwa (km 230):
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 54
hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa barabara za Bwanga -
Biharamulo (km 67); na kukamilika kwa nyaraka za zabuni kwa ajili ya
kumpata mkandarasi wa ujenzi wa barabara za Geita - Bulyanhulu Junction
(km 58.3) na Bulyanhulu Junction - Kahama (km 61.7).
Barabara za Mikoa
Hatua iliyofikiwa ni kujengwa kwa km 12.43 za barabara za mikoa kwa kiwango cha
lami na kukarabati km 128.5 za barabara za mikoa kwa kiwango cha changarawe.
Barabara za Kupunguza Msongamano Jijini Dar es Salaam (km 169.66)
Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa barabara ya Kimara Korogwe - Maji
Chumvi (km 6), Tegeta Kibaoni - Wazo Hill – Goba – Mbezi Mwisho (km 20) sehemu
ya Madale - Goba (km 5), Banana - Kitunda - Kivule - Msongola (km 14.7) sehemu
ya Kitunda - Kivule (km 3.2) na Maji Chumvi – Chang‟ombe – Barakuda (km 2.5),
kuendelea na taratibu za manunuzi za kumpata mkandarasi wa kujenga barabara za
Kibamba - Kisopwa – Kwembe – Makondeko (km 14.66) sehemu ya Mloganzila -
Kisopwa (km 1), Mwai Kibaki (km 9.1), Kawe Round about - Garden Road Junction
(km 2.9), Kongowe - Mji Mwema - Kivukoni (km 25.1) na kukamilika kwa usanifu wa
kina kwa barabara ya Mji Mwema – Kimbiji (km 27).
Kuhusu mradi wa upanuzi wa barabara ya Kimara – Kibaha (km 19.2) kuwa njia
nane, ujenzi unaendelea.
Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka
Awamu ya Kwanza ya mradi huu ilikamilika Desemba, 2015 ambapo ulihusisha
ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) katika barabara za
Kimara – Kivukoni, Magomeni – Morocco na Fire – Kariakoo yenye jumla ya
kilometa 20.9. Hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huu kwa awamu
zinazofuata ni:
(i) Awamu ya Pili: kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi utakaohusisha ujenzi wa
miundombinu katika barabara za Kilwa, Kawawa, Sokoine, Gerezani, Bandari
na Chang‟ombe zenye urefu wa kilometa 20.3 kwa ufadhili wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika – AfDB. Wananchi na taasisi 90 kati ya 105 wamelipwa
fidia ya shillingi bilion 28.52 kati ya shilingi bilioni 34.19;
(ii) Awamu ya Tatu: Mradi upo katika hatua ya mapitio ya usanifu wa kina na
maandalizi ya nyaraka za zabuni. Mradi utahusisha barabara za Azikiwe na
Maktaba, Bibi Titi, Uhuru na Nyerere hadi Gongo la Mboto na kituo kikuu cha
mabasi Kariakoo, Shaurimoyo na Uhuru kupitia Buguruni hadi TAZARA zenye
jumla ya urefu wa barabara hizo ni kilometa 23.6. Shughuli nyingine
zilizofanyika ni uthamini na uhakiki wa madai ya wananchi watakaopisha
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 55
mradi; Serikali kutoa eneo la Gongo la Mboto kwa ajili ya ujenzi wa karakana
ya mabasi (bus depot), eneo la ndani la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya kujenga kituo cha mabasi ili kuunganisha
uwanja na huduma za mabasi hayo, na eneo la kujenga kituo mlisho eneo la
Banana. Mradi huu upo chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia; na
(iii) Awamu ya Nne: Mradi upo katika hatua ya ununuzi wa mhandisi mshauri wa
kufanya usanifu. Mradi utahusisha barabara za Ali Hassan Mwinyi na
Bagamoyo hadi Tegeta pamoja na barabara ya Sam Nujoma (Ubungo -
Mwenge) zenye jumla ya km 25.9.
Ujenzi wa Barabara za Juu (Flyover) Jijini Dar es Salaam
Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya juu (flyover) katika
makutano ya TAZARA (Mfugale flyover); kuendelea na ujenzi kwa mradi wa
Interchange katika makutano ya Ubungo ambapo utekelezaji umefikia asilimia 28;
kuendelea na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara za juu kwenye
makutano ya barabara maeneo ya Fire (Morogoro/United Nations), Magomeni
(Morogoro/ Kawawa), Mwenge (Sam Nujoma/New Bagamoyo Road),
Tabata/Mandela, Morocco (Ali Hassan Mwinyi/Kinondoni), Buguruni
(Mandela/Uhuru), Kinondoni (Kinondoni/ Ali Hassan Mwinyi) na Selander (Ali
Hassan Mwinyi/ United Nations).
Barabara za Vijijini na Mijini
Shughuli zilizofanyika kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) ni:
kuendelea na matengenezo ya kawaida ya barabara za lami, changarawe na
udongo ambapo kilomita 5,565.3 za barabara zimekamilika pamoja na ujenzi na
ukarabati wa madaraja 167, makalavati makubwa 27, drift 59 na mifereji ya maji
yenye urefu wa mita 51,347. Kupitia Programu ya Uboreshaji wa Barabara Vijijini
chini ya ufadhili wa DfID barabara zenye urefu wa kilomita 151 zimejengwa kwa
kiwango cha changarawe pamoja na madaraja 3 na makalavati makubwa 42 katika
Halmashauri za Wilaya za Iramba, Kyela, Kyerwa, Rungwe, Bahi, Gairo, Kishapu,
Babati, Mpwapwa, Magu, Busokelo, Bariadi, Kondoa, Kisarawe, Kibiti, Ushetu,
Songwe, na Halmashauri ya Jiji la Dodoma; vile vile, halmashauri ya Manispaa ya
Iringa inaendelea na ukamilishaji wa daraja la Tagamenda na halmashauri ya Wilaya
ya Kilombero imekamilisha ujenzi wa barabara ya Chita hadi Melela. Kupitia
Programu ya Road Transport Sector Policy Support Programme-RTSPSP II (chini ya
ufadhili wa Umoja wa Ulaya) kilometa 219.6 za barabara zimejengwa (kilomita 21.3
kwa kiwango cha lami na kilomita 198.3 kwa kiwango cha changarawe) katika
Halmashauri za Wilaya za Chamwino, Kilolo, Kondoa, Kisarawe, Songea, Mbinga,
Mwanga, Mbulu, Kongwa, Mbogwe, Busokelo, Kalambo, Iringa, Ludewa, Hanang,
Kiteto, na Manispaa ya Temeke. Pia kilomita 152.1 za barabara zimejengwa kwa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 56
kiwango cha changarawe katika Halmashauri za Wilaya za Kongwa, Kiteto,
Mvomero na Kilombero kupitia Programu ya Feed the Future inayofadhiliwa na
Serikali na USAID.
Ujenzi wa Madaraja
(i) Ujenzi wa Madaraja Makubwa
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa daraja la Mlalakuwa (Dar es
Salaam), Momba (Rukwa), Sibiti (Singida), na Lukuledi (Lindi); kuendelea na
ujenzi wa madaraja ya Mara (Mara) asilimia 85, Ruhuhu (Ruvuma) asilimia
75, na Mangara (Manyara) asilimia 48; kuanza ujenzi wa Daraja Jipya la
Selander na barabara unganishi zenye urefu wa km 5.2; kuanza maandalizi
ya ujenzi wa madaraja ya New Wami (Pwani), Msingi (Singida), Sukuma
(Mwanza), Simiyu (barabara ya Simiyu – Mwanza), Kigongo/ Busisi
(Mwanza), Mkundi (Morogoro), Mtera (Dodoma) na Malagarasi Chini
(Kigoma) pamoja na ununuzi wa vyuma vya madaraja ya dharura yapo katika
hatua mbalimbali za utekelezaji.
(ii) Daraja la Nyerere na Barabara Unganishi (km 6.9): hatua iliyofikiwa ni
kuendelea na ujenzi wa barabara unganishi za Kigamboni (Daraja la Nyerere)
– Vijibweni (km 1.5) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 92. Aidha,
upembuzi yakinifu na usanifu wa kina unaendelea kwa barabara za Tungi –
Kibada (km 3.8) na Kibada – Mjimwema (km 1.6).
(c) Usafiri Majini
(i) Ujenzi wa Maegesho ya Vivuko: hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa upanuzi
wa jengo la abiria katika maegesho ya Kigamboni na maegesho ya Bwina
katika kivuko cha Chato - Nkomeae; kuendeea na ujenzi wa jengo la abiria na
ofisi ya kivuko cha Lindi – Kitunda ambapo utekelezaji umefikia asilimia 80; na
kuanza maandalizi ya ujenzi wa maegesho ya Nyamisati – Mafia.
(ii) Ununuzi wa Vivuko Vipya: hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa
kivuko kipya cha Kigongo - Busisi, na kupatikana kwa mkandarasi ambaye
ameanza maandalizi ya ujenzi wa kivuko kipya cha Nyamisati - Mafia.
(iii) Ukarabati wa Vivuko: hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ukarabati wa kivuko
cha MV Pangani II; na kuendelea kukarabati vivuko vya MV Sengerema
ambapo utekelezaji umefikia asilimia 40, MV Kigamboni asilimia 40, na MV
Utete asilimia 90. Aidha, taratibu za kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa MV
Misungwi zimekamilika.
(iv) Ununuzi na Ukarabati wa Meli katika Maziwa Makuu: Hatua iliyofikiwa ni
kuendelea na ujenzi wa meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na
tani 400 za mizigo katika ziwa Victoria; ujenzi wa chelezo; ukarabati wa meli
ya MV Victoria na MV Butiama. Aidha, makandarasi kwa ajili ya ukarabati wa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 57
meli za MV. Umoja na MV. Serengeti zilizopo katika ziwa Victoria
wamepatikana.
Kwa upande wa Ziwa Tanganyika, Kampuni ya Meli - MSCL inatekeleza
ujenzi wa meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400, ambapo
uandaaji wa mikataba kwa ajili ya ujenzi wa meli hiyo pamoja na ukarabati wa
meli ya MV Liemba umekamilika.
Aidha, ujenzi wa meli moja mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na
mizigo tani 200 katika Ziwa Nyasa unaendelea ambapo utekelezaji umefikia
asilimia 86. Vile vile, ujenzi wa matishari mawili katika Ziwa Nyasa
umekamilika.
(d) Bandari
(i) Bandari ya Dar es Salaam: Hatua zilizofikiwa ni: kukamilika kwa upanuzi wa
Gati Na.1 na kuanza kutumika; kuanza kwa upanuzi wa Gati Na. 2
sambamba na kuongeza kina chake; na ujenzi wa Gati la kupakia na kupakua
magari (Ro-Ro) unaendelea na upo katika hatua ya ujenzi wa sakafu ngumu
ya gati. Kwa ujumla uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam umefikia asilimia
50.
(ii) Bandari ya Tanga: Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ukarabati wa maegesho
ya meli na sehemu ya kupakulia shehena; na kukamilika kwa ukarabati wa
miundombinu ya barabara kuelekea lango Na. 2. Aidha, ukarabati wa
maegesho umefikia asilimia 86.
(iii) Bandari ya Mtwara: Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa gati lenye
urefu wa mita 300 la kuhudumia shehena mchanganyiko ambapo kwa ujumla
utekelezaji umefikia asilimia 50.
(iv) Bandari Kavu katika eneo la Ruvu: Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa
ujazaji wa kokoto katika eneo lenye ukubwa wa hekta 20.8; na kuendelea na
ujenzi wa reli ya kuunganisha bandari kavu na reli ya kati ambapo utekelezaji
umefikia asilimia 70.
(v) Bandari za Maziwa Makuu: Ziwa Victoria: kuendelea na ujenzi wa gati za
Nyamirembe - Chato na Magarine ambapo utekelezaji umefikia asilimia 30 na
asilimia 54 kwa mtiririko huo. Ziwa Tanganyika: ujenzi wa gati la
Kalya/Sibwesa unaendelea ambapo utekelezaji umefikia asilimia 93. Aidha,
upembuzi yakinifu wa ujenzi wa gati la Karema, imekamilika. Ziwa Nyasa:
kuendelea na ujenzi wa gati la Ndumbi.
(e) Usafiri wa Anga
(i) Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere: Hatua iliyofikiwa ni:
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 58
kukamilika kwa ujenzi wa jengo jipya la abiria (Terminal III); na kuendelea kwa
kazi ya kuunganishwa umeme wa gridi ya Taifa.
(ii) Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro: Hatua iliyofikiwa ni:
kukamilisha maeneo ambayo hayakujumuishwa katika ukarabati uliofanyika
awali ambapo shughuli zinazoendelea ni taratibu za manunuzi za kumpata
Mhandisi Mshauri wa kufanya usanifu wa kina wa ukarabati wa barabara ya
kuruka na kutua ndege.
(iii) Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato: Hatua iliyofikiwa ni:
kuendelea kwa usanifu wa kina na kuanza maandalizi ya ujenzi; na kulipa
fidia kwa mali zitakazoathiriwa na utekelezaji wa mradi.
(iv) Kiwanja cha Ndege cha Mwanza: Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na upanuzi
wa maegesho ya ndege; ujenzi wa jengo la mizigo, uzio wa kiwanja pamoja
na maegesho ya ndege za mizigo; ujenzi wa jengo la kuongozea ndege, kituo
cha umeme, maegesho ya magari, kufunga taa za kuongozea ndege; ujenzi
wa mfumo wa kuondoa maji ya mvua kiwanjani; na kuendelea na maandalizi
ya ujenzi wa jengo jipya la abiria.
(v) Viwanja vya ndege vya Mtwara: Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na kazi ya
ukarabati wa barabara ya kutua na kuruka ndege, viungio, maegesho ya
ndege, jengo la abiria, jengo la kuongezea ndege, barabara ya kuingia
kiwanjani, maegesho ya magari, ufungaji wa taa na mitambo ya kuongozea
ndege pamoja na uzio.
(vi) Viwanja vya Ndege vya Kigoma, Tabora, Sumbawanga na Shinyanga:
Hatua iliyofikiwa ni: kupatikana kwa wahandisi washauri na kuendelea na
taratibu za manunuzi za kumpata mkandarasi atakayetekeleza mradi wa
kuboresha viwanja hivyo.
(vii) Viwanja vya Ndege vya Mikoa: Katika viwanja vya Dodoma, Geita, Iringa,
Ruvuma, Lindi, Tanga, Mara, Simiyu na Lake Manyara: hatua iliyofikiwa ni
kukamilika kwa maandalizi kwa ajili ya kuanza ujenzi na ukarabati wa viwanja.
(viii) Ufungaji wa rada nne za kuongozea ndege za kiraia JNIA, KIA Mwanza
na Songwe: Hatua iliyofikiwa ni: JNIA: Kukamilika kwa miundombinu ya rada;
ufungaji wa mtambo unaendelea na umefikia asilimia 90; na majaribio ya
mtambo wa rada yanaendelea. Mwanza: ujenzi wa miundombinu ya rada
unaendelea ambapo utekelezaji umefikia asilimia 50; na kuanza kwa ufungaji
wa rada. KIA: ujenzi wa miundombinu ya rada umefikia asilimia 90. Songwe:
mtambo umewasili nchini.
(ix) Ununuzi wa Rada ya tatu (3) ya Hali ya Hewa: Hatua iliyofikiwa ni:
kusainiwa kwa mkataba wa ununuzi wa rada ya hali ya hewa na kufanya
malipo ya awali. Aidha, eneo kwa ajili ya kufunga rada limepatikana huko
Mikindani, Mtwara na malipo ya fidia kwa wananchi waliopisha eneo la mradi
yamefanyika.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 59
(f) Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(i) Mfumo wa Anuani za Makazi na Postikodi: Hatua iliyofikiwa ni: kuanza
kuweka nguzo zenye majina ya barabara/mitaa, namba za vibao vya nyumba
na kuanza maandalizi ya kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu matumizi ya
mfumo katika kata 48 za halmashauri za majiji ya Dodoma, Mwanza na
Tanga, manispaa za Ilemela, Shinyanga, Morogoro na Moshi, wilaya za
Chamwino, Chato na Bahi na miji ya Geita na Kibaha; kuendelea na taratibu
za manunuzi kwa ajili ya kuweka miundombinu ya mfumo katika mji wa
Serikali na kuweka vibao vyenye namba za nyumba katika halmashauri 12 za
majiji ya Dodoma, Mwanza na Tanga, manispaa za Ilemela, Shinyanga,
Morogoro na Moshi, wilaya za Chamwino, Chato na Bahi na miji ya Geita na
Kibaha.
(ii) Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano: Hatua iliyofikiwa ni:
kukamilika kwa ujenzi wa vituo sita (6) vya kutolea huduma za Mkongo wa
Taifa katika maeneo ya Tukuyu, Kibaha, Kahama, Ifakara, Kidatu na Mafinga;
kukamilika kwa taratibu za kumpata mshauri mwelekezi wa kusanifu majengo
ya vituo vya data katika maeneo ya Doma na Zanzibar; maunganisho ya vifaa
vya „video conference‟ kwa „sites‟ 12 zilizounganishwa katika mkongo wa
Taifa na mtandao wa TTCL kwa mikoa yote 26 ya Tanzania bara na
Zanzibar yamekamilika na vituo hivyo vinafanya kazi.
(iii) Ujenzi wa Kituo cha Kutengeneza Vifaa vya TEHAMA: kuandaliwa kwa
andiko la uanzishaji wa kituo cha kutengeneza programu za kompyuta
pamoja na Softcenter Operationalization Guide kwa ajili ya hatua za
utekelezaji.
(g) Nishati
Miradi ya Kufua Umeme
(i) Mradi wa Kinyerezi I Extension – MW 185: Hatua iliyofikiwa ni: kuanza
kufungwa kwa mitambo minne (4) katika eneo la mradi; kukamilika kwa
upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kinyerezi I kV 220; na kuendelea
na upanuzi wa njia ya msongo wa kV 132 kutoka Kinyerezi I hadi kituo cha
kupoza umeme cha Gongo la Mboto.
(ii) Mradi wa Kufua Umeme wa Rusumo MW 80: Hatua iliyofikiwa ni:
kukamilika kwa ujenzi wa barabara za kuingia eneo la mradi; kukamilika kwa
ujenzi wa kikinga maji; kukamilika kwa ujenzi wa nyumba za watumishi wa
mradi; na kukamilika kwa uchimbaji wa eneo la kufunga mitambo.
(iii) Mradi wa Kufua Umeme Mtwara MW 300 kwa kutumia Gesi Asilia: Hatua
iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu wa kituo cha kuzalisha umeme
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 60
na miundombinu wezeshi ya maji, barabara na gesi asilia.
(iv) Mradi wa Kakono - MW 87: Hatua iliyofikiwa ni: kukamilisha utafiti wa
kijiolojia na haidrolojia; kukamilisha usanifu wa awali wa mradi; kufanya
maandalizi ya zabuni kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa ujenzi; kuhuisha
tathmini ya athari za mazingira na kijamii na kukamilisha mpango wa
kuhamisha wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi.
(v) Umeme wa Jotoardhi – Ngozi (Mbeya): Hatua iliyofikiwa ni: kuajiriwa kwa
Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kuandaa mpango na kusimamia uchorongaji;
kuendelea na taratibu za ununuzi wa mtambo wa uchorongaji wa visima vya
utafiti; na maandalizi ya upimaji na uthamini wa ardhi hitajika kwa ajili ya
uchorongaji.
Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme
(i) Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 Makambako –
Songea: Hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa njia ya kusafirisha umeme yenye
urefu wa km 250 pamoja na vituo vitatu vya kupoza umeme vya Makambako,
Madaba na Songea. Aidha, kupitia mradi huu mikoa ya Njombe na Ruvuma
iliunganishwa rasmi katika Gridi ya Taifa. Kazi zinazoendelea ni kusambaza
umeme kwenye vijiji ambapo ujenzi wa miundombinu ya usambazaji umeme
katika vijiji 112 kati ya 122 imekamilika.
(ii) Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 - North West Grid
(Iringa - Mbeya - Sumbawanga - Mpanda - Kigoma - Nyakanazi): Hatua
iliyofikiwa ni: kuendelea na uthamini wa mali kwa wananchi watakaopisha
mradi pamoja na taratibu za kumpata mkandarasi wa mradi kwa sehemu ya
Iringa - Mbeya - Tunduma - Sumbawanga (km 624); kupatikana kwa Mtaalam
Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi, uthamini wa mali zitakazoathiriwa na
kupata eneo la kujenga kituo cha kupoza umeme Kidahwe mkoani Kigoma
kwa sehemu ya Nyakanazi - Kigoma (km 280); na kuendelea na majadiliano
kati Serikali na wafadhili kwa sehemu ya Sumbawanga - Mpanda - Kigoma
(km 480).
(iii) Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 Geita – Nyakanazi
(North West Grid): Hatua iliyofikiwa ni: kupatikana kwa mkandarasi;
kukamilika kwa uhakiki wa mali za wananchi watakaopisha mradi na kuanza
kulipa fidia.
(iv) Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa Kv 400 Singida – Arusha -
Namanga: Hatua iliyofikiwa ni: kulipa fidia na kuanza shughuli za ujenzi wa
mradi;
(v) Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 Bulyanhulu – Geita:
Hatua iliyofikiwa ni: kupatikana kwa mkandarasi wa ujenzi wa njia ya
kusafirisha umeme; kuanza ujenzi wa kituo cha kupoza umeme; kupatikana
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 61
kwa mkandarasi wa usambazaji umeme vijijini; na kulipa fidia kwa wananchi
wanaopisha mradi.
(vi) Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA –
III): Hatua iliyofikiwa ni: kuunganishwa umeme katika vijiji 5,109 ambapo,
taasisi za elimu 3,165, maeneo ya biashara 3,451, pampu za maji 210, taasisi
za afya 1,211 na nyumba za ibada 984 zimefikishiwa umeme
B. Ardhi na Maeneo ya Uwekezaji na Biashara
(a) Programu ya Umilikishaji wa Ardhi
Hatua iliyofikiwa ni: kupimwa kwa vipande vya ardhi na kuandaa Hati za hakimiliki ya
Kimila(CCROs) katika vijiji 109 vya Wilaya ya Kilombero (56), Ulanga (37) na Malinyi
(16); Kuhakikiwa na kupimwa kwa jumla ya vipande vya ardhi 178,980 kwa ajili ya
kuandaa Hati za Hakimiliki ya Kimila katika wilaya za Kilombero (61,530), Ulanga
(65,143) na Malinyi (52,307); kuandaliwa kwa jumla ya hati za hakimiliki ya Kimila
118,538 katika wilaya za Kilombero (56,680), Ulanga (37,353) na malinyi (24,501);
Kuandaliwa kwa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 79 katika wilaya Kilombero
(41), Ulanga (23) na Malinyi (15) na kuandaliwa kwa mipango ya kina ya makazi ya
vijiji 66 katika wilaya za Kilombero (28), Ulanga (20) na Malinyi (18); Kuendelea na
ujenzi wa ofisi za ardhi za Wilaya ya Kilombero, Ulanga na Malinyi uliofikia asilimia
50; na kuwezeshwa kwa vijiji 44 kukamilisha ujenzi wa masijala za ardhi katika
Wilaya za Kilombero (18), Ulanga (14) na Malinyi (12).
(b) Programu ya Kupanga na Kupima Ardhi
Hatua iliyofikiwa ni: Rasimu ya Mpango Kabambe wa jiji la Dodoma (Dodoma Master
Plan) imeandaliwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI. Mpango huu
umeanisha matumizi mbalimbali ya ardhi yakiwemo ujenzi wa ofisi za Serikali eneo
la Ihumwa, jijini Dodoma; Rasimu ya Mpango Kabambe wa jiji la Dar es Salaam
imekamilika kwa sasa uko katika hatua ya kusikilizwa na wadau; na Shilingi bilioni
6.28 za ndani zimetolewa kwa ajili ya upangaji, upimaji na umilikishaji ardhi katika
Halmashauri 24.
(c) Mradi wa Kuimarisha Mipaka ya Kimataifa
Hatua iliyofikiwa ni: Mpaka wa Tanzania na Kenya: Kikao cha majadiliano cha
ngazi ya Wataalam (JTC) kimefanyika. Kikao hicho kilichofanyika nchini Kenya
kimeandaa mpangokazi wa kazi zilizobaki katika km 238 na kuendelea na
uimarishaji wa awamu inayofuata ya km 110; Maandalizi ya kufanya kazi ya
mahesabu na uchakataji wa alama (pillars) na picha za anga (Aerial Triangulation)
yamekamilika; na Kukagua kazi ya uwekaji wa alama za mipaka (pillars) zilizowekwa
katika kipande cha mpaka cha km 172; Mpaka wa Tanzania na Uganda:
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 62
Kukamilika kwa maandalizi ya kuendelea na uimarishaji wa km 149; na Mpaka wa
Tanzania na Zambia: Maandalizi ya kuendelea na uimarishaji wa km 120 za nchi
kavu na 56 za kwenye maji yamekamilika.
(d) Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi
Hatua iliyofikiwa ni: Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi umeanzishwa kwa lengo
la kuboresha utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka za ardhi kwa njia ya kielektroniki,
kurahisisha utendaji kazi, kuharakisha mchakato wa utoaji milki na kuongeza mapato
ya Serikali. Mfumo huu umeanza kufanya kazi katika ofisi za Ardhi za Kanda ya Dar
es Salaam na ofisi za Ardhi za Manispaa ya Kinondoni na Ubungo kwa kubadilisha
kumbukumbu za ardhi zikiwemo ramani na hatimilki za ardhi zilizokuwa katika
mfumo wa analogia kuwa dijitali.
(e) Mradi wa Mikopo ya Nyumba
Hatua iliyofikiwa ni: Kupitia Mradi wa Mikopo ya Nyumba unaosimamiwa na Benki
Kuu ya Tanzania, Idadi ya mabenki na taasisi za fedha zinazotoa mikopo ya nyumba
zimeongezeka na kufikia 31. Jumla ya wananchi 4,174 wamenufaika na mikopo
inayotolewa na benki na taasisi hizo za fedha. Aidha, Mfuko wa Mikopo Midogo
Midogo ya Nyumba ulio chini ya Benki Kuu umeongezewa mtaji wa dola za Marekani
milioni 18 ambapo taasisi za fedha tano (5) zimepatiwa mtaji wa shilingi bilioni 13.87
kwa ajili ya kukopesha wananchi wa kipato cha chini kwa masharti nafuu. Vifaa vya
upimaji vya kisasa vyenye jumla ya shilingi bilioni 3 vimenunuliwa na kupelekwa
kwenye Kanda kwa ajili ya matumizi kwenye Halmashauri husika.
C. Huduma za Fedha
(a) Benki ya Maendeleo TIB
Hatua iliyofikiwa ni: Benki ya Maendeleo ya Tanzania ya TIB – DFI imefanikiwa
kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 634.58; kuongezeka kwa mapato ya
benki kufikia shilingi bilioni 46.41; kupatikana kwa faida ya shilingi milioni 499.88; na
kukusanywa kwa marejesho ya mkopo yenye thamani ya shilingi bilioni 62.72. aidha,
kwa upande wa TIB Corparate Bank – TIB shughuli zilizotekelezwa ni: kutolewa kwa
mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 6.1 kwa ajili ya ununuzi wa Pamba; shilingi
bilioni 6.9 kwa ajili ya ununuzi wa kahawa; na kuidhinishwa kwa mikopo yenye
thamani ya shilingi 68.7 kwa sekta mbalimbali za uchumi.
(b) Benki ya Maendeleo ya Kilimo - TADB
Shughuli zilizotekelezwa ni: kutolewa kwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni
73.9 na kufanya jumla ya mikopo iliyotolewa kwa wakulima kufika shilingi bilioni
113.07. Mikopo hii imewanufaisha wakulima 1,266,374 wa mahindi, mpunga,
mtama, alizeti, michikichi, korosho, kahawa, pamba, miwa, matunda na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 63
mbogamboga, ufugaji wa ng‟ombe wa maziwa na nyama, kuku, samaki, na nyuki wa
asali katika mikoa mbalimbali nchini. Kati ya mikopo iliyotolewa, kiasi cha shilingi
bilioni 10.9 zilitolewa kwa ajili ya kuendeleza miradi kumi na tatu (13) ya viwanda
vya uchakataji wa mazao; shilingi bilioni 10.4 kwa ajili ya miradi ya umwagiliaji; na
shilingi bilioni 3,4 kwa ajili ya kilimo cha kisasa cha zao la pamba na mpunga. Benki
imeendelea kutoa mafunzo ya ujasiriamali ambapo jumla ya wakulima wadogo 7,519
walipatiwa mafunzo. Aidha, benki inasimamia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima
Wadogo (Smallholder Farmers Credit Guarantee Scheme - SCGS) ambapo mfuko
wa SCGS umetoa udhamini uliowezesha mabenki ya biashara kutoa mikopo ya
jumla ya shilingi bilioni 5.2 kwa wakulima wadogo 925.
D. Utalii, Biashara na Masoko
(a) Utalii
(i) Sekta Ndogo ya Utalii: shughuli zilizotekelezwa ni: utambulisho wa vivutio
vya utalii vilivyopo Tanzania (Tanzania Destination Branding) ambao una kauli mbiu
ya ‘Tanzania Unforgettable’; uanzishwaji wa chaneli maalumu ya Tanzania Safari
kwa ajili ya kutangaza utalii nchini inayoratibiwa na TBC; uanzishwaji wa
maadhimisho ya kuenzi utamaduni wa Mtanzania (Tanzania Heritage Month)
yaliyofanyika katika mikoa minne (Dodoma, Arusha, Manyara, na Dar es salaam) ya
Tanzania Bara na Zanzibar; na uanzishwaji wa safari za basi la kitalii katika Jiji la
Dar es salaam. Aidha, serikali imefanya maonesho katika nchi 13 za Uingereza,
Ujerumani, Ufaransa, Rwanda, Kenya, Kanada, China, Uholanzi, India, Hispania,
Ubeligiji, Israeli na Falme za Kiarabu. Kupitia maonesho hayo idadi ya watalii
walioingia nchini imeongezeka kutoka 1,327,143 mwaka 2017 hadi kufikia watalii
1,505,702 mwaka 2018.
Serikali imeendelea kuboresha miundombinu wezeshi kwa ajili ya kuendeleza utalii
ambapo jumla ya ofisi sita na vituo 15 vya ulinzi vimejengwa katika hifadhi za
mazingira asilia za Chome, Magamba, Mlima Rungwe, Mkingu, Minziro, na
Udzungwa Scarp. Aidha, barabara zenye urefu wa kilometa 89.6 na njia za
kutembea watalii zenye urefu wa kilometa 102.6 zimesafishwa katika misitu hiyo.
Vilevile, ujenzi wa ngazi yenye mita 183 kuelekea kwenye maporomoko ya Kalambo
umefanyika. Pia, kambi 11 za kupumzikia wageni zimesafishwa katika misitu saba
ya hifadhi za asilia za Mlima Hanang, Rungwe, Udzungwa, Uluguru, Kimboza,
Rondo na Kilombero.
(ii) Mradi wa Uendelezaji wa Utalii katika Ukanda wa Kusini – REGROW:
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ununuzi wa vifaa na samani kwa ajili ya ofisi za
mradi; kutolewa kwa ushauri elekezi kuhusu mazao ya utalii katika jamii na utafiti
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 64
kuhusu hali ya kijamii na kiuchumi katika jamii zinazozunguka maeneo
yaliyohifadhiwa katika ukanda wa kusini; na kukamilika kwa zoezi la ufuatiliaji
maeneo ya Mbarali na Pori la Akiba la Selous.
(b) Biashara
(i) Mradi wa Kukuza Shughuli za Kibiashara katika Jumuiya ya Maendeleo
ya Nchi za Kusini mwa Afrika – SADC
Shughuli zilizotekelezwa ni: ununuzi wa mashine maalam ya kupima mafuta ya kula;
vifaa vya maabara kwa ajili ya Shirika la Viwango Tanzania - TBS; vifaa vya
maabara kwa ajili ya Wizara ya Kilimo; na kuandaliwa kwa kitabu cha Mwongozo wa
Mauzo Nje.
(ii) Uboreshaji wa Mazingira ya Kufanyia Biashara Nchini: hatua iliyofikiwa ni
kuondolewa kwa vikwazo mbalimbali vya biashara ikiwemo vya kikodi ambapo jumla
ya tozo 1,010 katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi zimeondolewa na 4
kupunguzwa.
Shughuli nyingine zilizotekelezwa ni: kupatiwa mafunzo kwa wajasiriamali 6,336 ya
kuwajengea uwezo wa kuongeza thamani katika sekta za kilimo, uzalishaji, ujenzi na
madini katika kanda tatu za Arusha (Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida na
Tanga), Morogoro (Dodoma, Iringa, Mbeya, Morogoro na Songwe) na Mtwara (Dar
es Salaam, Lindi, Mtwara na Pwani); uhamasishaji wa matumizi ya mfumo wa
stakabadhi ghalani; utoaji elimu kwa wafanyabiashara kuhusu fursa na taratibu za
kufanya biashara, uimarishaji wa mifumo ya taarifa pamoja na ukusanyaji wa taarifa
za masoko na utafiti; na kuondolewa kwa vikwazo 45 visivyo vya kibiashara kati ya
62. Aidha, mfumo wa upatikanaji wa huduma kwa njia ya kieletroniki mahali pamoja
(Eletronic One Stop Shop) umewezesha kusajiliwa kwa kampuni 6,918, majina ya
biashara 11,382 na leseni za viwanda 166.
(c) Masoko
Hatua iliyofikiwa ni: kuendelea kusimamia mfumo wa stakabadhi ghalani kwa mazao
ya korosho, mahindi na mpunga katika maghala yaliyosajiliwa; na kutengwa kwa
maeneo ya masoko ya mipakani katika mikoa ya Kagera, Mara, Mtwara, Ruvuma,
Kigoma, Rukwa, Mbeya, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 65
3.2.2.5. Kuimarisha Usimamizi wa Utekelezaji wa Mpango
A. Utawala Bora na Utawala wa Sheria
(a) Kuharakisha Azma ya Serikali Kuu Kuhamia Dodoma
Hatua iliyofikiwa ni: kuhamishwa kwa jumla ya watumishi 8,883 wa Wizara na
Taasisi za Serikali kwenda Makao Makuu ya Serikali, Dodoma; kukamilisha ujenzi
wa majengo ya Ofisi za Serikali katika mji wa Serikali; kukabidhiwa hati 64 za umiliki
wa viwanja kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini kwa ajili ya ujenzi wa
Ofisi za balozi; kupitishwa kwa Sheria ya kulitangaza jiji la Dodoma kuwa Makao
Makuu ya Nchi; kuongeza kasi ya upimaji wa maeneo ili kuhakikisha uendelezaji
unazingatia sheria ya mipango miji; kuendelea na ujenzi wa barabara za lami na
changarawe katika maeneo ya Dodoma ikiwemo Mji wa Serikali; na kuendelea
kufanya mapitio ya Mpango Kabambe wa jiji la Dodoma ili kuandaa Mpango
Kabambe ambao utakidhi na kuendana na uendelezaji wa Makao Makuu ya nchi.
(b) Mfuko wa Bunge
Hatua iliyofikiwa ni: Kuendelea na ujenzi wa nyumba ya makazi ya Katibu wa Bunge
– Dodoma; Kufanyika kwa ukarabati wa majengo ya Bunge ikiwa ni pamoja na
usimikaji wa lift paa katika jengo la Utawala; kufanyika kwa malipo ya awali kwa ajili
ya kuwezesha ununuzi wa mitambo ya usalama kwenye ukumbi wa Bunge;
Kuwajengea uwezo Wabunge na watumishi kupitia mafunzo mbalimbali ili
kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.
(c) Utoaji Haki na Huduma za Kisheria
Hatua iliyofikiwa ni: kujenga mifumo ya kielektroniki ya kusajili na kuratibu mashauri
yanayosajiliwa Mahakamani, Mfumo wa kusajili na kuratibu shughuli za mawakili na
Mfumo wa utambuzi wa mahitaji ya mahakama (court mapping); Ujenzi wa majengo
ya mahakama kuu katika mikoa ya Kigoma na Mara; Ukarabati wa nyumba tatu za
majaji katika mkoa wa Mtwara; ujenzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi katika Mkoa
wa Manyara; Ujenzi wa mahakama 5 za Wilaya (Kilwa, Ruangwa, Bukombe, Geita
na Chato); Kuendelea kwa ujenzi wa Mahakama 4 za Hakimu Mkazi na Mahakama
11 za wilaya; Kuanzishwa kwa mahakama maalum zinazotembea na kuweza
kusogeza huduma za mahakama karibu na wananchi hususan walio katika sehemu
zisizo na huduma ya mahakama; naKununuliwa kwa magari mawili yatakayotumika
kutoa huduma katika mikoa ya Dar es Salaam, Wilaya ya Kindondoni (Bunju),
Wilaya ya Ilala (Chanika), Wilaya ya Temeke (Buza) na Wilaya ya Ubungo
(Kibamba); na Mkoa wa Mwanza, Wilaya ya Ilemela (Nyegezi) katika awamu ya
kwanza ya majaribio.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 66
(d) UNICEF Support to Multisectoral
Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: Kuimarisha shughuli za usajili wa vizazi, vifo,
ndoa, talaka na watoto wa kuasili ikiwa ni haki ya msingi ya utambuzi wa binadamu
na upatikanaji wa takwimu kwa ajili ya maendeleo; kusajiliwa kwa vizazi 1,271,372;
vifo 28,285; ndoa 26,953; talaka 122 na hati 28 za watoto wa kuasili; kuongezeka
kiwango cha usajili kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kutoka asilimia 13,
kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 38 kwa mwaka
2018/2019; na kuendelea na usimamizi wa mirathi, usajili wa bodi za wadhamini,
uandishi na uhifadhi wa wosia ambapo wosia 38 zimeandikwa na kuhifidhiwa katika
kipindi cha 2018/2019.
(e) Access to Justice and Human Rights
Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kuendelea kubuni na kutekeleza mikakati kadhaa
kwa kutunga na kurekebisha sheria pamoja na kanuni zake; kuendesha tafiti za
kisheria; kutoa elimu kwa umma kuhusu haki za binadamu na za kiraia; kupokea na
kufanyia uchunguzi malalamiko ya wananchi yanayohusu ukiukwaji wa Haki za
Binadamu na misingi ya Utawala Bora; kutengeneza mfumo jumuishi wa kukusanya,
kuchambua na kuhifadhi takwimu muhimu zinazohusu sekta ndogo ya haki jinai
ambao umejadiliwa na kutolewa maoni na wadau mbalimbali, kwa sasa unaendelea
kufanyiwa majaribio; kuandaliwa kwa Mpango Kazi wa Pili wa Kitaifa wa Haki za
Binadamu kwa kipindi cha mwaka 2018/19 hadi 2022/23 kulinda, kukuza na
kuhifadhi haki za Binadamu wakati Serikali inapotekeleza majukumu yake;
kutungwa kwa Sheria ya Msaada wa Kisheria ya mwaka 2017 na kanuni zake na
kupitishwa kwa Mkakati wa Kitaifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa
mwaka 2017 hadi 2021 wenye lengo la kuhakikisha kuwa haki za wanawake, watoto
na watu wenye ulemavu zinalindwa na kudumishwa; na kutolewa kwa muongozo
unaoelekeza mashauri yote yanayohusu wanawake, watoto, wazee na watu wenye
ulemavu kumalizika ndani ya muda mfupi usiozidi miezi sita.
(f) Vitambulisho vya Taifa
Hatua iliyofikiwa ni: kusajili na kutambua raia wa Tanzania, wageni wakaazi pamoja
na wakimbizi wapatao 19,648,857 wenye umri wa Miaka 18 sawa na lengo la
asilimia 82 la kusajili wananchi wapatao milioni 24,295,468; vitambulisho 4,850,724
vimechapishwa ambapo viambulisho 4,503,769 vimetolewa kwa wananchi;
kuunganishwa kwa Ofisi ya Wilaya ya Mbinga na Busega na mtandao wa
mawasilianao na makao na makao makuu kupitia Mkongo wa Taifa chini ya Shirika
la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na hivyo kufikisha ofisi 119 nchi nzima; kutolewa
kwa vitambuliso 1,000,000 kwa wajasiriamali wadogo; na kuunganishwa kwa jumla
ya taasisi 45 za serikali na binafsi katika mfumo wa usajili na utambuzi.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 67
(g) Mradi wa Mfuko wa Mahakama
(i) Kukamilika kwa michoro ya ujenzi na tathmini ya gharama kwa ajili ya Makao
Makuu ya Mahakama ya Tanzania - Dodoma katika eneo la NCC, Kitalu D
Kiwanja Na. 1. Aidha, michoro hiyo na tahthmini ya gharama vimewasilishwa
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kupata idhini ya kuanza ujenzi;
(ii) Ujenzi wa majengo ya Mahakama Kuu upo katika hatua za mwisho
kukamilika ambapo Kigoma na Mara umefikia asilimia 80;
(iii) Ujenzi wa Mahakama za Wilaya za Bukombe, Bunda, Chato, Kasulu, Kilindi,
Kondoa, Sikonge, Rungwe, Loliondo, Kilwa na Ruangwa umekamilika;
(iv) Katika kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za kisheria
kazi zilizofanyika ni kukamilika kwa uboreshaji wa mfumo wa ukusanyaji wa
takwimu (Judicial Statistical Dashbord System). Mfumo huu unatumika kusajili
mashauri, kuingiza taarifa muhimu za Wadaawa ikiwa ni pamoja na kutuma
taarifa kwa ujumbe mfupi (sms) kwa wadaawa kuhusu mwenendo wa
mashauri yao;
(v) Watumishi 183 (wanaume 113 na wanawake 70) walipata mafunzo katika
kada mbalimbali kupitia program ya Maboresho ya Huduma za Mahakama.
(vi) Kujenga mifumo ya kielektroniki katika kusajili na kuendesha mashauri
Mahakamani; na
(vii) Kuanza rasmi kutumika kwa mfumo wa kielektroniki wa uendeshaji wa
mashauri ulioboreshwa unaojulikana kama JSDS 2 katika Mahakama za
ngazi ya Wilaya hadi Mahakama ya Rufani.
3.2.2.6. Maeneo Mengine Muhimu kwa Ukuaji wa Uchumi na Ustawi na Taifa
A. Kuimarisha Ushiriki wa Sekta Binafsi
(a) Mradi wa Kuimarisha Ushindani wa Sekta Binafsi – Ardhi
Hatua iliyofikiwa ni kuendelea na: kukamilika kwa ujenzi wa ofisi ndogo mfumo wa
Intergrated Land Management Information System (ILMIS) katika halmashauri
nchini; ununuzi wa vifaa vya TEHAMA; na utoaji nyaraka za kielektroniki za ardhi.
(b) Viwanda
Sekta imeendelea kushiriki katika ujenzi wa viwanda ambapo katika kipindi cha 2015
hadi 2018, jumla ya viwanda 3,530 vilijengwa na kuanza uzalishaji. Kati ya hivyo
viwanda ambavyo vimeajiri watu zaidi ya 50 viko 61. Aidha, Serikali imeendelea
kuchukua hatua katika kuimarisha ushindani wa sekta binafsi ambapo mafanikio
yaliyopatikana ni pamoja na kukamilika/kuendelea kwa ujenzi wa viwanda
vinavyomilikiwa na sekta binafsi na mashirika ya umma ambavyo ni pamoja na:
(i) Kiwanda cha Lakairo Pipi Industries (Mwanza) ambacho kinajumuisha
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 68
viwanda vitatu vya kuzalisha Pipi na Jojo; Steel wool; na vifungashio
(magunia). Kiwanda kimetoa ajira 120 za kudumu na 250 za muda mfupi na
kina uwezo wa kuzalisha tani 3.5 za magunia na tani 2 steel wool kwa siku.
(ii) Kiwanda cha usindikaji matunda cha Sayona Fruits Ltd (Pwani). Kiwanda
kilizinduliwa Julai 2018 na kuanza uzalishaji katika hatua za majairibio kwa
kusindika juisi ya embe na kutengeneza nyanya za pakti. Uwezo wa kiwanda
ni kusindika tani 3 za matunda kwa siku na kimetoa ajira 400 za kudumu.
(iii) Kiwanda cha kuzalisha vilainishi cha Lake Oil Lubricants (Dar es Salaam):
Kiwanda kilizinduliwa Septemba 2018, kina uwezo wa kuzalisha vilainishi lita
300 kwa siku na kimetoa ajira 76 za kudumu.
(iv) Kiwanda cha Kubangua Korosho cha Terra Cashew Processing Ltd (Pwani):
kiwanda kilizinduliwa Agosti 2018 na kina uwezo wa kubangua tani 9 za
korosho kwa siku. Aidha, kiwanda kimetoa ajira za kudumu 27 na ajira za
muda mfupi 126.
(v) Kiwanda cha kuzalisha Gypsum board cha San Hao Co.Ltd (Pwani): kiwanda
kilianza uzalishaji mwaka 2018 na kimetoa ajira za kududmu zaidi ya 60.
(vi) Kiwanda cha kutengeneza maji safi ya kunywa cha Hill Packaging Limited
(Pwani): kiwanda kilizinduliwa Septemba 2018 na kimetoa ajira za kudumu
378 na za muda mfupi 96.
(vii) Kiwanda cha kutengeneza sabuni ya unga na detergents cha Keds (T)
Company Ltd - Keds Washing Powder Detergents (Pwani): kiwanda kina
uwezo wa kutoa ajira zaidi ya 100 za kudumu.
(viii) Kiwanda cha Galaxy Food and Beverage Limited (Jijini Arusha). Kiwanda
kinasindika maziwa lita 75,000 kwa siku na kimeajiri jumla ya wafanyakazi 30.
Gharama za uwekezaji wa kiwanda hicho ni Dola za Marekani milioni 2.5
sawa na shilingi bilioni 5.7. Kiwanda hicho kimeanza uzalishaji wa maziwa
aina ya Kilimanjaro fresh kwa kiwango cha UHT.
(ix) Upanuzi wa kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi cha Gereza la Karanga ili
kuongeza uzalishaji wake kutoka jozi 150 hadi kufikia jozi 400 za viatu kwa
siku. Uboreshaji huu umekamilika.
(x) Viwanda vinavyojengwa ndani ya Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo
(Bagamoyo – SEZ):
(xi) Kiwanda cha Africa Dragon Enterprises Limited kinachozalishaji vifaa vya
ujenzi (Color coated steel coils). Kiwanda hiki kimeanza uzalishaji.
Viwanda vingine vilivyo katika hatua mbalimbali za ujenzi ni pamoja na:
(i) Kiwanda cha kusindika zao la muhogo cha Fjs African Starch Development
Ltd (Pwani): kiwanda kinatarajia kutoa ajira zaidi ya 180 pindi kitakapoanza
uzalishaji.
(ii) Ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuzalisha chanjo za mifugo cha Hester
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 69
Bioscience Africa Limited - Kibaha. Kiwanda kitazalisha aina 27 za chanjo
zinazoagizwa kutoka nje ya nchi kwa sasa. Gharama za uwekezaji wa
kiwanda ni Dola za Marekani milioni 18 sawa na Shilingi bilioni 41.
(iii) Kiwanda cha TAN CHOICE (Kibaha – Pwani). Kiwanda kina uwezo wa
kuchinja na kuchakata ng‟ombe 1000 na mbuzi/kondoo 4,500 kwa siku.
Uwekezaji wa kiwanda ni Dola za Marekani milioni 5.5 sawa na shilingi bilioni
12.5. Kiwanda kinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 500.
(iv) Kiwanda cha Elia Food and Overseas Ltd (Longido). Kiwanda kina uwezo wa
kuchakata ng‟ombe 400 na mbuzi/kondoo 2000 kwa siku. Ujenzi wa kiwanda
unagharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 5 sawa na Shilingi bilioni 11.3.
Kiwanda kinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 200.
(v) Viwanda vinavyojengwa ndani ya Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo
(Bagamoyo – SEZ) ni kama ifuatavyo:
Kiwanda cha Seif For Tobacco Trade Limited kinachotarajia kuzalisha
bidhaa za Tumbaku pamoja na Sigara. Kiwanda hiki kipo katika hatua za
ujenzi.
Kiwanda cha Fujian Hexingwang Industry Company Limited
kinachotarajiwa kuzalisha vifaa vya ujenzi na kipo katika hatua ya ujenzi.
Kiwanda cha Siparcoci International Limited kitakachojishughulisha na
uzalishaji wa vipodozi (cosmetics) na kipo katika hatua za ujenzi.
Kiwanda cha uzalishaji wa vifaa vya ujenzi cha Hua Teng Metallurgical
Company Limited.
Kiwanda cha uzalishaji wa vifungashio (packaging materials) cha Wegmar
Packing Limited.
Kiwanda cha uzalishaji wa Juisi cha Jambo Food Products Limited.
Kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za ngozi (Leather and Leather products)
cha Phiss Tannery Limited.
Kiwanda cha uzalishaji wa mifuko ya saruji (cement bags) cha Tube
Limited.
Kiwanda cha kuchakata taka za kibiologia (biological waste management)
cha Ramky Tanzania Limited.
Kiwanda cha kuchakata bidhaa za nyama cha Tanfroz Limited kilichopo.
B. Miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi
Serikali imeendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusiana na uibuaji wa
miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ambapo imechangia
kuongezeka kwa miradi ya ubia. Aidha, Sheria ya PPP imefanyiwa marekebisho
ambayo yamesasadia kuleta mafanikio mbalimbali yakiwemo kundaliwa kwa Rasimu
ya mwongozo wa manunuzi wa miradi ya PPP; kuandaliwa kwa Rasimu ya Kanuni
za PPP za mwaka 2019 ya Sheria iliyorekebishwa; na kuwezesha Serikali za Mitaa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 70
kutekeleza miradi ya PPP. Vile vile, miradi mikubwa ya PPP iliyo katika hatua
mbalimbali za utekelezaji ni pamoja na:
(a) Mradi wa ujenzi wa reli ya Tanga – Arusha - Musoma pamoja na matawi
ya Engaruka na Minjingu kwa standard gauge: kukamilika kwa upembuzi
yakinifu na usanifu wa awali wa ujenzi wa reli na matawi yake; kupatikana
kwa Mshauri wa uwekezaji ambaye ataandaa upembuzi yakinifu Aidha,
majadiliano baina ya Serikali na Mshauri wa Uwekezaji yanaendelea;
(b) Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Mtwara – Mbamba Bay na Matawi ya
Mchuchuma na Liganga kwa Standard Gauge: Hatua iliyofikiwa ni
kusainiwa kwa mkataba baina ya Serikali na Mshauri wa Mwelekezi ambaye
anaendelea kufanya upembuzi yakinifu wa mradi ili kupata wawekezaji kwa
utaratibu wa ubia;
(c) Mradi wa Dawa Muhimu na Vifaa Tiba unaotekelezwa na Bohari kuu ya
madawa (MSD) katika Pwani, Mwanza na Mbeya: hatua iliyofikiwa ni
kukamilika kwa upembuzi yakinifu na kuendelea na utaratibu wa kumpata
mbia; na
(d) Mradi wa Kusambaza Gesi Asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi
na Mtwara: hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa upembuzi yakinifu wa awali.
(e) Miradi miwili ya Ujenzi wa Hoteli ya Nyota Nne na Kituo cha Biashara katika
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julias Nyerere; kukamilika kwa
upembuzi yakinifu wa awali
(f) Miradi miwili ya ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya
Biashara Kampasi ya Dar es Salaam na Dodoma; hatua iliyofikiwa ni
kukamilika kwa andiko la awali
(g) Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Saratani Tanzania wa Taasisi ya
Ocean Road utakojengwa Mloganzila, Kibaha; kukamilika kwa andiko la
awali.
C. Mchango wa Serikali katika Kuimarisha Ushiriki wa Sekta Binafsi
Uhamasishaji wa ushiriki wa sekta binafsi katika utekelezaji wa Mpango wa
Maendeleo umefanikisha kusajiliwa kwa jumla ya miradi mipya 145 yenye thamani
ya dola za Marekani bilioni 1.84 na kuzalisha ajira mpya 15,491 kupitia Kituo cha
Uwekezaji – TIC. Kati ya miradi hiyo, miradi 104 sawa na asilimia 72 inamilikiwa na
wawekezaji wa ndani. Pamoja na mafanikio hayo, mikakati mbalimbali imeandaliwa
ili kuimarisha ushiriki wa sekta hiyo katika uwekezaji wa moja kwa moja au kwa
utaratibu wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Mikakati hiyo ni:
kuandaliwa kwa Mwongozo wa Kuboresha Mazingira ya Biashara; kuendelea na
ukamilishaji rasimu ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Sekta Binafsi; kuendelea
kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ikijumuisha barabara, nishati ya
umeme, viwanja vya ndege, mawasiliano, reli na maji; kuendelea kutoa vivutio vya
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 71
kipekee na vivutio vya kikodi kuvutia sekta binafsi kuwekeza katika maeneo ya
kipaumbele; kuendelea kuboresha majadiliano kati ya Serikali, sekta binafsi na
wawekezaji; kuendelea na maboresho ya kimifumo na kitaasisi; na kurekebishwa
kwa Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili kuondoa changamoto
za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia utaratibu wa ubia.
D. Uwekezaji wa Mashirika na Taasisi za Umma
Serikali imeendelea kusimamia uwekezaji wa Taasisi na Mashirika ya Umma
ambapo uwekezaji wa mtaji umekua kwa asilimia 13.7 kutoka Shilingi billioni
48,530.72 kwa mwaka 2016/17 hadi Shilingi bilioni 55,178.3 kwa mwaka 2017/18
kwa Taasisi na Mashirika ya Umma yaliyopo nchini; Uwekezaji wa Serikali katika
Taasisi za Nje umekua kwa asilimia 9.63 kutoka Shilingi bilioni 529.8 kwa mwaka
2016/17 hadi Shilingi bilioni 580.8 kwa mwaka 2017/18; hivyo kuongeza kwa mapato
yatokanayo na Taasisi na Mashirika ya Umma.
Vile vile, katika kuwachukulia hatua wawekezaji waliokiuka masharti ya mikataba ya
mauziano Serikali imerejesha jumla ya viwanda 12 ambavyo havifanyi kazi. Viwanda
26 vimepewa taarifa ya kusudio la kuvirejesha katika umiliki wa Serikali baada ya
kukiuka masharti ya mkataba. Aidha, Serikali imeendelea na jitihada za kutafuta
wawekezaji mahiri ili viwanda vilivyorejeshwa Serikalini viweze kuendelezwa.
Sambamba na hatua hiyo, Serikali imeandaa “Information Memorandum” (Company
Profile) ili kutoa taswira halisi ya viwanda na fursa zilizopo. Aidha, viwanda vya Utegi
Dairy Farm, kiwanda cha Chai Mponde na Lindi Cashew nuts vimepata wawekezaji.
3.2.3. Miradi Iliyofuatiliwa katika Mwaka 2018/19
A. Hatua za Utekelezaji
Mwaka 2018/19, Serikali ilifuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
inayotekelezwa na sekta ya Umma na Binafsi. Jumla ya miradi 102 ilifuatiliwa katika
sekta za Maji, Uchukuzi, Sheria, Madini, Ujenzi, Uvuvi, Nishati, Viwanda, Afya,
Kilimo, na Elimu katika mikoa ya Simiyu, Mara, Kigoma, Kagera, Rukwa, Mtwara,
Dar es Salaam, Lindi, Pwani, Ruvuma, Morogoro, Njombe na Katavi. Baadhi ya
miradi ya maendeleo iliyofuatiliwa ni kama ifuatavyo:
(a) Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa - Simiyu
Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Simiyu
ulianza Novemba 2015 na kukamilika Mei 2018. Huduma zinazotolewa na Hospitali
kwa sasa ni pamoja na: huduma za wagonjwa wa nje; huduma za dharura; huduma
za ustawi wa jamii; huduma za maabara kwa vipimo vya kawaida ikiwemo malaria,
wingi wa damu, sukari na VVU. Serikali inaendelea na ujenzi wa: jengo la uchunguzi
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 72
litakalokuwa na huduma za mionzi; Maabara; na kichomea taka hatarishi za
hospitali.
Mwonekano wa Jengo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
(b) Ujenzi wa Bomba la Maji Lagangabilili – Itilima - Simiyu
Utekelezaji wa mradi ulianza Juni 2017 na umekamilika kwa asilimia 98 ambapo
shughuli zilizofanyika ni: ujenzi wa tenki la juu la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita
225,000, vituo 21 vya kuchotea maji; kulaza bomba kuu lenye jumla ya mita 1,760
linalopeleka maji kwenye tenki; kulaza mtandao wa bomba za kusambaza maji
zenye jumla ya urefu wa mita 29,000; kununua na kufunga pampu moja ya
kusukuma maji kwenye chanzo cha kisima kirefu; na ujenzi wa njia ya umeme ili
kuunganisha umeme katika kituo cha pampu ya kisima kirefu chenye uwezo wa
kuzalisha maji lita 18,000 kwa saa (sawa na lita 432,000 kwa siku). Mradi
unahudumia wananchi wapatao 2,212.
(c) Ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi – Maswa – Bariadi – Lamadi sehemu
ya Maswa – Bariadi (km 49.7) - Simiyu
Mradi wa ujenzi wa Barabara ya Maswa – Bariadi yenye urefu wa km 49.7 kwa
kiwango cha lami ni sehemu ya ujenzi wa Barabara inayoanzia Mwigumbi – Maswa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 73
– Bariadi – Lamadi yenye urefu wa km 171.8. Utekelezaji wa mradi ulianza Oktoba
2017 na unatarajiwa kukamilika Oktoba 2019. Mradi unatekelezwa na Kampuni ya
CHICO ya China na Mhandisi Msimamizi ni Kampuni ya DOCH Ltd ya Tanzania.
Utekelezaji wa mradi unaendelea ambapo hatua iliyofikiwa ni: ujenzi wa pipe culvert
57, box culvert 10 kati ya 12; na kuendelea na ujenzi wa madaraja makubwa 2 katika
mito ya Simiyu na Banya.
(d) Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya - Serengeti (Mara)
Mradi unalenga kusogeza huduma muhimu za afya bora kwa wananchi wa
Serengeti na maeneo jirani. Aidha, hospitali hii itatoa huduma kwa watalii
wanaotembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti. Mradi unahusisha ujenzi wa
majengo ya wagonjwa wa nje, mama na mtoto, magonjwa yasiyopewa kipaumbele,
na wodi za wanaume na wanawake. Shughuli zinazoendelea kwa sasa ni
ukamilishaji wa OPD, MCH na eneo la kupumzika wagonjwa na wasindikizaji wakati
wa kusubiri matibabu.
Taswira ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti-Mara
(e) Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini – Katavi
Mradi unahusisha ujenzi wa jengo la ofisi ya kituo cha umahiri lenye ghorofa moja
(1). Mkandarasi wa mradi ni SUMA JKT. Kituo hiki kitakapokamilika kitasimamia
shughuli za madini zikijumuisha kutoa mfunzo kwa wajasiriamali wadogo wa madini,
kuongeza thamani rasilimali za madini na kuwa ofisi ya madini ya kanda ya nyanda
za juu Kusini. Ujenzi wa mradi ulianza Agosti 2018 na unatarajiwa kukamilika
Februari 2019.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 74
(f) Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya –
Kampasi ya Rukwa
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya Kampasi ya Rukwa kilianzishwa
mwaka 2015 katika majengo ya iliyokuwa kambi ya Mkandarasi wa ujenzi wa
barabara ya Tunduma – Sumbawanga. Kampasi ya Rukwa kwa sasa ina eneo la
ekari 120. Lengo la mradi ni kuinua mikoa ya nyanda za juu Kusini (Songwe, Rukwa
na Katavi) na mikoa mingine kitaaluma na kuchochea matumizi ya teknolojia
zitakazobuniwa na watafiti katika kusaidia maendeleo ya kilimo na viwanda.
Ukarabati wa chuo ulianza Juni 2018 na upo katika hatua za ukamilishaji.
(g) Ujenzi wa Jengo la Mahakama Kuu – Kigoma
Utekelezaji wa mradi ulianza Oktoba 2017 na unatarajia kukamilika Aprili 2019.
Mradi unalenga kuanzisha masijala ya mahakama kuu katika Mkoa wa Kigoma,
ambayo itajumuisha Masijala ndogo ya Mahakama ya Rufani. Mradi huu utasaidia
kutatua changamoto ya wananchi kufuata huduma za mahakama kuu na ya rufani
mkoani Tabora umbali wa kilometa 426. Utekelezaji wa mradi unaendelea kulingana
na mpango kazi, ambapo ujenzi wa jengo umekamilika; na kazi za umaliziaji
zinaendelea. Kwa ujumla utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 80.
(h) Eneo Maalumu la Uwekezaji Kigoma - KiSEZ
Utekelezaji wa mradi ulianza mwaka 2008/09 kwa matarajio ya kukamilika mwaka
2019/20. Jukumu kubwa la Serikali katika mradi wa KiSEZ ni kuvutia wawekezaji
kwa kuweka mazingira wezeshi kwa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha eneo la
mradi, kupima eneo na kuweka mipaka rasmi. Kufuatia makubaliano yaliyopo ya
mradi, Serikali ya Mkoa wa Kigoma ikishirikiana na Sekta Binafsi ndio itagharamia
ujenzi wa miundombinu wezeshi ya eneo la mradi kwa kuweka nishati muhimu kama
umeme, maji safi na mfumo wa majitaka.
Mradi wa KiSEZ una eneo la ukubwa wa hekari 691 lililopimwa, lina master Plan
nyenye viwanja vyenye hati 401 vyenye ukubwa wa kuanzia mita za mraba 10,000.
Viwanja hivyo vimetengwa maalumu kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya
uzalishaji/uchakataji, kufungasha na maghala ya kuhifadhia bidhaa; kujenga nyumba
za makazi; ujenzi wa taasisi kama vyuo, hospitali, shule; shughuli za biashara kama
benki, hoteli, maduka makubwa; viwanja vya michezo, bustani za kupumzika na
kumbi; na huduma za usafiri za bandari, mabasi na malori ya mizigo. Hatua
iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huu ni kupatikana wawekezaji ambao ni SGC
Investment Ltd, Next Gen Solowazi Ltd na Third Man Ltd na wameanza uwekezaji.
(i) Kiwanda cha Kahawa – Instant Coffee cha Amimza – Kagera
Mradi unahusisha kiwanda cha kukoboa kahawa na kuweka madaraja, kukaanga na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 75
kusaga na kuzalisha instant coffee. Kiwanda kilianza uzalishaji mwaka 1998 na
kinamilikiwa na mwekezaji binafsi kampuni ya AMIMZA. Lengo la kiwanda ni
kukoboa, kutengeneza instant coffee na kuzalisha aina mbalimbali za kahawa zenye
ubora zaidi na zilizoongezwa thamani. Kutokana na ubora, kahawa nyingi
inayozalishwa na kiwanda hiki huuzwa nje ya nchi. Aidha, kiwanda kina mpango wa
kuanza kuzalisha kahawa ya chengachenga ambayo hutumia teknolojia mpya katika
uzalishaji wa kahawa.
Uwepo wa kiwanda umenufaisha wananchi wanaokizunguka kupitia miradi
inayotekelezwa na kiwanda kama vile umeme, maji na barabara. Aidha, kiwanda
kimetoa ajira takriban 150.
Eneo la Kiwanda cha Kukoboa Kahawa cha AMIMZA kilichopo Mkoani Kagera.
(j) Ujenzi wa Shule ya Sekondari Nyakato - Bukoba Vijijini – Kagera
Mradi unajengwa na Serikali kutokana na majengo yalikuwepo awali kuathiriwa na
tetemeko la ardhi lililotokea katika mkoa wa Kagera Oktoba 2017. Hatua ya
utekelezaji iliyofikiwa ni kukamilika kwa miundombinu ya madarasa 12, Jengo la
Utawala, mabweni 9 ya wanafunzi, maabara 2, nyumba za walimu na chumba cha
kupumzika wagonjwa.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 76
Jengo la Utawala katika Shule ya Sekondari Nyakato.
(k) Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji Rusumo MW 80 – Kagera
Mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo MW 80 unatekelezwa kwa kuzingatia
makubaliano ya Serikali za nchi za Burundi, Rwanda na Tanzania yaliyoingiwa
mwaka 2013. Lengo la mradi ni kuzalisha umeme wa MW 80 na kila nchi kupata MW
26.6 mradi utakapokamilika. Mradi unasimamiwa na taasisi ya Nile Equatorial Lakes
Subsidiary Action Program Co-ordination Unit (NELSAP-CU) kupitia Kampuni ya
Rusumo Power Ltd (RPCL). Mradi unahusisha, ujenzi wa bwawa la maji na
miundombinu yake, mitambo ya kuzalisha umeme na kituo cha kupoza/kuchochea
umeme.
Hatua iliyofikiwa ni: kukamilika kwa ujenzi wa kambi ya kudumu ya wafanyakazi;
kuendelea na ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa mradi ambapo nyumba mbili (2)
kati ya tano (5) za wafanyakazi zimekamilika; kukamilika kwa ujenzi wa
miundombinu ya barabara za kuingia eneo la mradi; kuanza kazi ya kuchimba
handaki la kupitisha maji; kukamilika kwa asilimia 65 ya uchimbaji wa eneo la
kufunga mitambo; kukamilika kwa ujenzi wa kikinga maji; kuendelea na ujenzi wa
bwawa la kuhifadhia maji, njia za kupitisha maji na kuchimba eneo la kufunga
mitambo.
(l) Mradi wa Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili – Kampasi ya Mloganzila
Mradi unahusisha ujenzi wa jengo la ghorofa 4 la kutolea huduma zikiwemo mafunzo
ya kitabibu na ubobezi wa maradhi ya Moyo (cardiovascular) na maeneo ya
kufundishia kozi zinginezo. Mradi unasimamiwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 77
Shirikishi cha Muhimbili.
Utekelezaji wa mradi ulianza Februari 2018 na umefikia asilimia 65. Shughuli
zilizotekelezwa ni pamoja na: kukamilika kwa ujenzi wa jengo; kuendelea na
umaliziaji; na ufungwaji wa mifumo mbalimbali ya maji, umeme, TEHAMA na
usalama. Kukamilika kwa mradi huu kutasaidia kuongezeka kwa wigo wa kitaaluma
kutokana na mafunzo mbalimbali yatakayopatikana. Aidha, mapato yataongezeka
kutoka kwa wanafunzi wa nchi mbalimbali watakaopata mafunzo chuoni.
Mwonekano wa Jengo la Hospitali ya Mloganzila kwa sasa
Baadhi ya vifaa (Vitanda) katika mradi wa Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili – Mloganzila
(m) Upanuzi wa Barabara ya Morogoro sehemu ya Kimara - Kibaha (km 19.2)
kuwa Njia Nane pamoja na Ujenzi wa Madaraja ya Kibamba, Kiluvya na
Mpiji
Upanuzi wa barabara ya Morogoro sehemu ya Kimara – Kibaha (km 19) unalenga
kupunguza msongamano wa magari na ajali za barabarani. Upanuzi huu unahusisha
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 78
ujenzi wa barabara kwa njia nane. Mkataba wa ujenzi ulisainiwa Julai, 2018 na
unatarajiwa kukamilika Januari, 2021.
Utekelezaji wa mradi unaendelea kulingana na mpango kazi ambapo shughuli
zilizotekelezwa ni pamoja na: usanifu wa kina wa km 19.2; usanifu wa madaraja
yote; ujenzi wa nguzo za misingi ya madaraja; kusafisha eneo la barabara km 11;
ujenzi wa kuta kwa kujaza udongo aina ya G3 na G7 kwa km 7; ujenzi wa makalavati
madogo 36 umekamilika na kalavati kubwa moja eneo la Kibanda cha mkaa
umefikia asilimia 75; ujenzi wa piles cap upande wa kulia daraja la Kibamba
umekamilika na ujenzi wa abutment unaendelea.
(n) Ujenzi wa Barabara ya Mtwara - Newala – Masasi (km 210), Sehemu ya
Mtwara - Mnivata (km 50)
Barabara ya Mtwara - Mnivata ni sehemu ya barabara ya Mtwara - Masasi kupitia
Wilaya za Tandahimba na Newala ukiwa na lengo la kuunganisha mikoa ya Mtwara,
Ruvuma na nchi jirani za Malawi na Msumbiji. Ujenzi wa mradi ulianza Aprili 2017 na
unatarajiwa kukamilika Agosti 2019. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 65.
Barabara hii itarahisisha usafiri wa wananchi pamoja na mazao katika maeneo
yanayopitiwa na mradi huu katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma; na
kuchochea maendeleo kwa kuvutia wawekezaji katika rasilimali zinazopatikana
katika eneo hilo hususan katika kilimo cha korosho na viwanda vitakavyosaidia
kuongeza thamani ya mazao yanayopatikana katika eneo hilo.
Kipande cha barabara ya Mtwara- Mviwata katika eneo la mlima Simba (kushoto) na kulia ni eneo la
Mnivata kikijengwa kwa kiwango cha lami.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 79
(o) Mradi wa Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi Chakula – Songea
Mradi huu unatekelezwa katika mikoa (8) ambayo ni Ruvuma, Njombe, Songwe,
Rukwa, Katavi, Shinyanga, Dodoma na Manyara. Katika mkoa wa Ruvuma, mradi
unagharimu dola za Marekani milioni 10.17 (Shilingi bilioni 23.4) ambapo unahusisha
ujenzi wa vihenge kumi na viwili (12) vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 45,000; ujenzi
wa maghala mawili (2) yenye uwezo wa kuhifadhi tani 10,000; ujenzi wa stoo ya
vifaa; ujenzi wa stoo ya viuatilifu; ujenzi wa ofisi; ujenzi wa maabara; ujenzi wa uzio;
ujenzi wa barabara za ndani na miundombinu ya kutoa maji; ununuzi wa vifaa vya
maabara na stoo pamoja na mafunzo ya kujenga uwezo kwa watumishi. Utekelezaji
wa mradi ulianza Juni 2018 na unatarajiwa kukamilika Desemba 2019.
Utekelezaji wa mradi unaendelea ambapo uingizaji wa vifaa vya vihenge na ujenzi
wa misingi ya vihenge 12 umekamilika. Mradi huu utakapokamilika unatarajiwa
kupunguza matumizi ya magunia, pallet na viuatilifu.
B. Changamoto za Utekelezaji wa Miradi
Changamoto za Jumla Zilizobainishwa katika Miradi Iliyofuatiliwa
(a) Kukosekana kwa umeme wa uhakika katika baadhi ya viwanda
kumesababisha hasara na kushindwa kupanua uwekezaji;
(b) baadhi ya makandarasi kuwa na uwezo mdogo wa kukamilisha kazi ipasavyo;
(c) Mawasiliano hafifu baina ya wadau wa miradi hususan watekelezaji, waratibu
na wasimamizi;
(d) Kutopatikana fedha kwa wakati imeathiri utekelezaji wa miradi kulingana na
ratiba na kuongeza gharama;
(e) Uchakavu wa miundombinu na mitambo katika baadhi ya miradi
umesababisha miradi kuzalisha chini ya kiwango kinachotakiwa; na
(f) Maandalizi hafifu ya upembuzi yakinifu na utafiti wa athari za mazingira kwa
baadhi ya miradi imeathiri utekelezaji wa miradi.
Hatua za Kukabiliana na Changamoto
(a) Kuongeza uzalishaji na usamabazaji wa umeme kwenye maeneo ya mradi;
(b) Kuimarisha mfumo wa utoaji wa zabuni ili zitolewe kwa watu wenye sifa na
kupunguza tatizo la wakandarasi kutokuzingatia muda wa utekelezaji;
(c) Kuimarisha uratibu na mawasiliano baina ya taaisisi zinazotekeleza mradi na
wadau wengine kama ilivyobainishwa katika Mkakati wa Mawasiliano wa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21;
(d) Kuboresha mifumo ya kuongeza mapato kwa kupanua wigo wa kodi, mikopo
ya masharti nafuu, kumarisha mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa
mapato na kuongeza ushirikishwaji wa sekta binafsi;
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 80
(e) Kuboresha miundombinu na mitambo iliyochakaa kwa kufanya matengenezo,
ukarabati na ununuzi wa mitambo mipya; na
(f) Kutoa mafunzo ya uandaaji wa miradi ya maendeleo kwa wataalam wa
Wizara, Idara Zinazojitegemea na Taasisi za Serikali kama ilivyoelezwa katika
Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma (PIM – OM).
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 81
SURA YA NNE
MIRADI NA SHUGHULI ZA KIPAUMBELE KWA MWAKA 2019/20
4.1. Utangulizi
Sura hii inaelezea miradi na shughuli za kipaumbele kwa mwaka 2019/20 ambazo ni
muendelezo wa utekelezaji wa miradi iliyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa
Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21. Aidha, miradi na shughuli hizo
zimezingatia mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka
2018/19, Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa
Mwaka 2015, Mkakati wa Utekelezaji wa Mpango wa Miaka Mitano na Mapendekezo
ya Mpango yaliyoidhinishwa na Bunge, Novemba 2018.
4.2. Misingi na Shabaha za Ukuaji wa Uchumi
4.2.1. Misingi ya Mpango kwa Mwaka 2019/20
Misingi iliyozingatiwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20 ni
kama ifuatavyo:
(a) Amani, usalama, na utulivu wa ndani na nchi jirani vitaendelea kuimarishwa
na kudumishwa;
(b) Viashiria vya uchumi jumla na maendeleo ya jamii kama vile Pato la Taifa,
biashara ya nje, ujazi wa fedha, mapato na matumizi na viashiria vya huduma
za jamii vitaendelea kuimarika;
(c) Sera za fedha zitaendelea kuimarishwa ili ziendane na sera za bajeti
zitakazosaidia kupunguza mfumuko wa bei;
(d) Kuendelea kuimarika na kutengemaa kwa uchumi wa dunia;
(e) Bei za mafuta katika soko la dunia zitaendelea kuwa nzuri; na
(f) Kuwepo kwa hali nzuri ya hewa nchini na katika nchi jirani.
4.2.2. Shabaha za Ukuaji wa Uchumi
Shabaha kuu za uchumi ni kama ifuatavyo:
(a) Kukua kwa Pato Halisi la Taifa kufikia asilimia 7.1 mwaka 2019 ikilinganishwa
na ukuaji wa asilimia 7.0 mwaka 2018;
(b) Kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa unabaki
kwenye wigo wa tarakimu moja kati ya asilimia 3.0 hadi asilimia 4.5;
(c) Mapato ya kodi kufikia asilimia 13.1 ya Pato la Taifa mwaka 2019/20 kutoka
matarajio ya asilimia 12.1 mwaka 2018/19;
(d) Matumizi ya Serikali yanatarajiwa kuwa asilimia 22.7 ya Pato la Taifa mwaka
2019/20; na
(e) Nakisi ya bajeti (ikijumuisha misaada) kuwa asilimia 2.3 mwaka 2019/20.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 82
4.3. Miradi na Shughuli Zitakazotekelezwa
4.3.1. Miradi ya Kielelezo
(a) Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Standard Gauge
Shilingi bilioni 2,476.0 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi
huo. Katika fedha hizo shilingi bilioni 2,446.0 ni kwa ajili ya kuendelea na ujenzi kwa
sehemu ya Dar es Salaam – Makutopora (km 722), shilingi bilioni 10 kwa ajili ya
maandalizi ya ujenzi wa Isaka – Rusumo (km 371) na shilingi bilioni 20 ni kwa ajili ya
maandalizi ya ujenzi kwa sehemu ya Makutopora – Tabora – Isaka - Mwanza (km
676).
(b) Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania - ATCL
Shilingi bilioni 500.0 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kumalizia malipo ya
ununuzi wa ndege moja aina ya Boeing 787 - 8 Dreamliner na moja mpya aina ya
Bombardier Dash 8 Q400; malipo ya awali ya ununuzi ya ndege mbili aina ya Airbus
A220 – 300; ununuzi wa ndege moja aina ya Bombardier Dash 8 Q400 na injini ya
akiba kwa ndege aina ya Bombardier Dash 8 Q400; kuendelea kuboresha karakana
ya matengenezo ya ndege iliyopo KIA; na kulipa madeni yaliyohakikiwa pamoja na
gharama za kuanzia kwa ndege mpya zitakazopokelewa katika kipindi hicho.
(c) Mradi wa Kufua Umeme wa Maji Bonde la Mto Rufiji - MW 2,115
Shilingi bilioni 1,443 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi
ambapo kazi zitakazofanyika ni pamoja na kuanza ujenzi wa bwawa, kuanza ujenzi
wa njia za kupitisha maji; na kukamilisha ujenzi wa njia ya pili ya umeme msongo wa
kV 33 kutoka Gongo la Mboto.
(d) Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia - Lindi
Shilingi bilioni 6.7 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi ambapo
kazi zitakazofanyika ni pamoja na kukamilisha majadiliano ya mradi na kulipa fidia
kwa wananchi watakaopisha mradi.
(e) Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga
(Tanzania)
Shilingi bilioni 7 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha majadiliano ya
mkataba wa Ubia (SHA) kati ya nchi washirika na kampuni zilizowekeza katika mradi
pamoja na kulipa fidia wakazi watakaohamishwa kupisha eneo la mkuza litakapopita
bomba.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 83
(f) Shamba na Kiwanda cha Sukari Mkulazi
Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na uandaaji wa shamba na kupanda
miwa; kununua na kufunga mitambo pamoja na kuanza uzalishaji wa sukari; na
kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja.
(g) Mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma
Shilingi milioni 670 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kulipia leseni za
uchimbaji wa makaa ya mawe; kulipa fidia ya mali za wananchi watakaopisha eneo
la mradi baada ya tathmini kukamilika; na kuratibu na kufuatilia kazi za mradi;
kusimamia ujenzi wa mgodi wa makaa ya mawe na msongo wa umeme wa
Mchuchuma – Liganga.
(h) Kiwanda cha Kufua Chuma cha Liganga
Shilingi milioni 490 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kulipia leseni za
mashapo; kulipa fidia ya mali za wananchi watakaopisha eneo la mradi baada ya
tathmini kukamilika; kusimamia ujenzi wa mgodi wa chuma na kiwanda cha chuma;
na kusimamia ujenzi wa miundombinu wezeshi, kuratibu na kufuatilia kazi za mradi.
(i) Uanzishwaji wa Kanda Maalum za Kiuchumi
Kipaumbele kimewekwa katika kuharakisha utekelezaji wa kanda zilizoainishwa
katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano kama miradi ya kielelezo
ambapo jumla ya Shilingi bilioni 8.5 zimetengwa. Shughuli zitakazotekelezwa ni:-
(i) Eneo Maalum la Uwekezaji Bagamoyo: Kufanya usanifu wa kina na ujenzi
wa miundombinu wezeshi katika eneo la kituo cha Teknolojia Bagamoyo;
kufanya upembuzi yakinifu, usanifu wa kina na ujenzi wa miundombinu ya
ndani kwa eneo lililolipwa fidia pamoja na kukamilisha majadiliano na
maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa Bagamoyo; kukamilisha hatua zote za
utwaaji wa Ardhi na kufanya upimaji wa eneo ili kupata hati miliki ya eneo
lililokwisha lipiwa fidia.
(ii) Kituo cha Biashara na Huduma Kurasini: Kukamilisha hatua zote za
utwaaji ardhi ili kupata hati; kufanya upembuzi yakinifu; kuandaa mpango wa
matumizi ya ardhi (masterplan) kufanya usanifu wa kina na ujenzi wa
miundombinu ya ndani; kuweka uzio eneo la mradi; kununua gari la mradi
pamoja na kulipia gharama za mashauri elekezi.
(j) Kuongeza Rasilimali Watu Wenye Ujuzi Adimu na Maalumu kwa
Maendeleo ya Viwanda na Watu
Katika mwaka 2019/20, Serikali kupitia Wizara ya Nishati itagharamia mafunzo kwa
wanafunzi 20 katika fani za mafuta na gesi. Vile vile, Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi Muhimbili - MUHAS kitaendelea kutoa mafunzo kwa wataalam
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 84
katika fani za afya hususan udaktari bingwa kwa ngazi za uzamili na uzamivu katika
nyanja zote za magonjwa ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu,
upandikizaji figo, ini na uboho (bone marrow), tiba za ndani za moyo, figo na ini, na
uhudumiaji wa wagonjwa wa dharura na mahututi (Emergency medicine and critical
care). Aidha, MUHAS imepanga kudahili wanafunzi wapya 500 katika fani za afya ya
binadamu ambapo wafanyakazi 300 wa sekta ya afya kutoka hospitali na taasisi za
Serikali watapewa kipaumbele.
4.3.2. Kukuza Uchumi na Ujenzi wa Msingi wa Uchumi wa Viwanda
4.3.2.1. Uzalishaji Viwandani
(a) Kiwanda cha Kuunganisha Matrekta – TAMCO, Kibaha
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni: kuendelea na maboresho ya kiwanda; ujenzi
wa kiwanda kipya cha kuunganisha matrekta na kusimamia shughuli za kufanya
matengenezo ya matrekta nchini na kusimamia na kulipia gharama za uingizaji
matrekta na zana zake bandarini na kuyapeleka eneo la mradi ambapo Shilingi
bilioni 3.0 fedha za ndani zimetengwa.
(b) Eneo la Kongane za Viwanda – TAMCO, Kibaha
Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa miundombinu wezeshi katika
eneo la mradi na kuendelea kutangaza eneo kwa wawekezaji ambapo Shilingi bilioni
4.5 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya shughuli hizo.
(c) Mradi wa Magadi Soda - Bonde la Engaruka
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni: kufanya upembuzi yakinifu; kujenga
miundombinu wezeshi katika eneo la mradi; kufanya tathmini ya athari za
kimazingira na kijamii; kufanya utafiti wa upatikanaji wa maji kwa ajili ya mradi wa
wananchi; kufanya upembuzi yakinifu wa barabara za ndani na za kufikia eneo la
mradi; na kulipia leseni za uchimbaji. Shilingi bilioni 5.0 fedha za ndani zimetengwa
kwa ajili ya kutekeleza shughuli hizo.
(d) Kufufua Kiwanda cha General Tyre – Arusha
Shughuli zitakazotekelezwa ni kufanya upembuzi yakinifu na kutayarisha financial
model kuendelea na uendelezaji wa mashamba ya mpira na kuboresha teknolojia ya
uchakataji wa utomvu ili kupata malighafi ya kutengeneza matairi. Shilingi bilioni 1.5
zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu.
(e) Maeneo Mengine Maalum ya Uwekezaji
(i) Maeneo Maalum ya Mtwara, Tanga, Kigoma, Manyara, Bunda, Dodoma.
Kigamboni, Ruvuma, na Manyoni. Shughuli zitakazotekelezwa ni:
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 85
Kuendeleza miundombinu ya ndani ya mradi awamu ya kwanza na ujenzi wa
jengo la One Stop Centre kwenye maeneo ya Mtwara Free Port Zone, Tanga,
Kigoma, Manyara, na Bunda; kukamilisha hatua zote za utwaaji ardhi na
kufanya upimaji wa maeneo ili kupata hati miliki ya maeneo
yaliyokwishalipiwa fidia. Maeneo hayo ni Bunda, Tanga, Manyara, Ruvuma,
na Manyoni; kufanya upembuzi yakinifu; kuandaa Masterplan; na kufanya
usanifu wa kina wa miundombinu kwa maeneo ya Kigamboni, Bunda, Tanga,
Manyara na Dodoma ambapo jumla ya shilingi bilioni 3.0 fedha za ndani
zimetengwa.
(ii) Eneo Maalum la Uwekezaji Benjamin William Mkapa. Shughuli
zitakazotekelezwa ni: kuweka mfumo wa kisasa wa ulinzi kuzunguka eneo
lote la mradi ambapo Shilingi millioni 500 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili
ya shughuli hizo.
(iii) Kongane ya Viwanda vya Ngozi – Dodoma (Zuzu). Shughuli
zitakazotekelezwa ni: kuandaa Mpango Kabambe; kuandaa layout plan na
usanifu wa kina; kufanya upembuzi yakinifu; kufanya tathmini ya athari ya
mazingira na kuandaa Mpango wa Biashara; na ujenzi wa baadhi ya majengo
ya kufanyia shughuli za viwanda.
4.3.2.2. Utafiti wa Teknolojia na Bidhaa za Viwandani
(a) Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini - CAMARTEC
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni kuendelea kufanya utafiti wa mahitaji ya
teknolojia za kilimo na teknolojia zinazohitajika vijijini na kujua hali ya matumizi ya
teknolojia hizo katika maeneo mingine ambayo utafiti huo bado haujafanyika;
kufanya utafiti na kuunda teknolojia zinazolenga kuongeza tija katika shughuli za
kilimo vijijini; kuunda na kuzalisha sampuli kifani za teknolojia za kilimo na teknolojia
nyingine zinazotumika vijijini; kuhamasisha utengenezaji wa mashine za kilimo, zana
za kilimo na teknolojia nyingine za ufundi vijijini; na kuendelea kuimarisha
miundombinu ya kituo ili kuweza kufanya utafiti kwa ufanisi zaidi ambapo Shilingi
bilioni 2.0 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya shughuli hizo.
(b) Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania - TIRDO
Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuanzisha na kukidhi vigezo vya kupata ithibati kwa
maabara ya mafuta na gesi asilia, makaa ya mawe na maabara ya vipimo vya
chuma ngumu; kuhuisha teknolojia ya kutumia sensor kufuatilia uzalishaji viwandani
kwa wajasiriamali; kukamilisha vigezo vya upatikanaji wa ithibati na kuboresha
maabara ya chakula, mazingira, kemia, na maabara ya vifaa vya kihandisi ili ziweze
kufikia viwango vya kimataifa; na kukamilisha Jengo la Utawala na kutoa mafunzo
kwa wadau mbalimbali wa sekta ya ngozi kuhusu utunzaji wa mazingira. Shilingi
bilioni 4.0 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya shughuli hizo.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 86
(c) Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo – TEMDO
Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na uboreshaji wa karakana na ofisi ya
usanifu pamoja na miundombinu ya Taasisi kwa ujumla; kubuni na kuendeleza
utengenezaji wa mtambo wa kuweka baridi; kubuni na kuendeleza chasili ya
kusindika chai; kubuni na kuendeleza chasili cha mtambo mdogo wa kutengeneza
brikwiti kutokana na vumbi la makaa ya mawe; kubuni na kuendeleza chasili cha
mtambo wa kukausha mazao ya kilimo; kuhawilisha teknolojia na kuhamasisha
uzalishaji wa kibiashara wa mitambo iliyobuniwa; kutoa huduma za kiufundi kwa
viwanda; kujenga miundombinu ya kiatamizi cha teknolojia na biashara; kuanzisha
na kuwezesha mpango wa kusambaza viwanda nchini kwa utaratibu wa kiwanda
kimoja kila wilaya; na kuanza ujenzi wa ofisi Dodoma. Fedha zilizotengwa ni Shilingi
bilioni 2.0 fedha za ndani kwa ajili ya shughuli hizo.
(d) Uendelezaji wa Viwanda Vidogo – SIDO
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni kuboresha miundombinu wezeshi ya
barabara, maji, umeme, uzio, mfumo wa maji taka na TEHAMA katika mikoa ya
Tabora, Kigoma, Iringa, Mwanza, Morogoro, Lindi, Mtwara, na Kagera; kujenga
majengo ya viwanda katika mikoa ya Pwani, Ruvuma, Katavi, Mwanza, Tabora na
Morogoro; kuongeza mtaji kwa ajili ya kutunisha Mfuko wa Maendeleo ya
Wajasiriamali – NEDF ambao unatoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati
kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo. Shilingi bilioni 6.0 fedha za
ndani zimetengwa kwa ajili ya shughuli hizo.
4.3.2.3. Kilimo
Shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja na:
(a) Kilimo cha Kahawa
Kuongeza uzalishaji wa kahawa kutoka tani 65,000 hadi tani 80,000 kwa kuzalisha
na kusambaza miche bora ya kahawa 10,000,000 katika wilaya 42 zinazolima
kahawa; kutoa mafunzo kwa wakulima 4,000, maafisa ugani 500 na wakulima
viongozi 300; kufanya maboresho ya maabara ya kuonjea kahawa na ununuzi wa
mtambo wa kukaanga kahawa; kuanza kuendesha minada ya kahawa katika kanda
nne za uzalishaji wa kahawa ambazo ni Bukoba - Kagera, Songwe - Mbeya, Mbinga
- Ruvuma, Moshi - Kilimanjaro na kuendesha kampeni ya kufufua mashamba ya
zamani na upandaji wa miche mipya. Shughuli hizo zimetengewa Shilingi bilioni 1.4
fedha za ndani.
(b) Kilimo cha Pamba
Kununua, kuchakata na kusambaza tani 18,000 za mbegu za pamba zilizoondolewa
manyoya kwa ajili ya kupanda; kuongeza upatikanaji wa mbegu kutoka tani 22,000
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 87
hadi 40,000; kutoa elimu kwa wakulima kuhusu matumizi sahihi ya viuadudu na
vinyunyizi; kuwasajili wakulima 500,000 wa pamba kidigitali; kutengeneza,
kusambaza na kuhamasisha matumizi ya teknolojia rahisi katika uzalishaji wa
pamba; kuwezesha ufuatiliaji na ukusanyaji wa takwimu za uzalishaji na uchakataji;
kuwezesha usimamiaji wa shughuli za mfuko wa kuendeleza zao la pamba; kununua
na kusambaza ekapaki 10,000,000 za viuadudu vya pamba kwa wakulima; kutoa
mafunzo kwa wadau wa pamba kuhusu kanuni za kilimo bora cha pamba na
kuwezesha shughuli za maendeleo na utafiti katika taasisi za utafiti (Ukiriguru na
Ilonga). Shughuli hizo zimetengewa Shilingi bilioni 1.2 fedha za ndani.
(c) Kilimo cha Chai
Kuanzisha na kutunza mashamba mama 45 katika halmashauri za wilaya saba
(Njombe, Mufindi, Kilolo, Ludewa, Tarime, Bumbuli na Korogwe) kwa kutumia mbegu
bora (clones) za chai kutoka TRIT; kufufua kiwanda cha chai Mponde (Ludewa)
kuzalisha miche bora ya chai 2,500,000 kwa ajili ya wakulima wadogo wa chai katika
halmashauri za wilaya tano (Tarime, Bumbuli, Korogwe, Mufindi na Bukoba); na
kuwezesha usafirishaji na upandaji wa miche bora ya chai 650,000 kutoka vitaluni
kwenda mashambani katika wilaya za Tarime na Mufindi. Shughuli hizo
zimetengewa Shilingi bilioni 1.1 fedha za ndani.
(d) Kilimo cha Mpunga
Kuendesha mashamba ya mfano 1,200 ya kilimo shadidi cha mpunga kutoka skimu
za umwagiliaji 40; kutoa mafunzo kwa wakulima, viongozi na maafisa ugani;
kuendesha siku ya mkulima kwa wakulima 280 kutoka skimu 10 zilizofanya vizuri.
Shughuli hizo zimetengewa Shilingi bilioni 2.8 fedha za nje.
(e) Kilimo cha Tumbaku
Kutengeneza kanzi data ya usajili na kusajili wakulima wa tumbaku wapatao 60,000
kutoka vyama vyote vya msingi vya ushirika; kukagua na kusajili vituo vya
kuchambulia na kufungia tumbaku vipatavyo 1,972 na vya kuuzia 790; kufanya
tathmini ya wingi na ubora wa zao shambani ili kubaini idadi ya kaya na wakulima
walioshiriki kilimo, eneo lililopandwa tumbaku, uzalishaji na ubora tarajiwa katika
vyama vyote; kuendesha mafunzo kwa wataalam wa masoko wa zao la tumbaku;
kuendesha tafiti za zao la tumbaku ili kupata mbegu bora; kuelimisha wakulima
kupanda na kutunza miti na kuboresha mabani kuwa majiko banifu katika wilaya 25
katika vyama 298 na kukagua uzingatiaji wa taratibu za hifadhi ya mazingira na
matumizi ya mabani yenye majiko sanifu na banifu katika vyama 298 kwenye wilaya
25 ambapo Shilingi bilioni 1.4 fedha za ndani zimetengwa.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 88
(f) Kilimo cha Miwa
Kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu mbinu bora za kilimo cha miwa kupitia
mashamba darasa yaliyopo Kilombero, Mtibwa, Kagera, Mbigiri, Bagamoyo, Geita,
Chamwino, Manyara - Kiru Valley, Singida, Ikungi, Katavi, Kalambo na Songea;
kuwezesha upatikanaji wa ardhi ya uwekezaji katika maeneo yaliyoainishwa kwa ajili
ya uwekezaji wa miradi mipya ya sukari, katika maeneo ya Kasulu, Kibondo, Rufiji,
Geita, Kilombero, Karagwe, Pangani, Bagamoyo na Morogoro; kuanzisha ekari 100
za vitalu vya mbegu za miwa katika maeneo ya miradi ya kati na midogo katika
halmashauri za wilaya za Geita, Chamwino, Mpanda, Nsimbo na Mlele; na ukarabati
wa mitambo ya kiwanda kidogo cha sukari Lumuma ambapo Shilingi bilioni 6.1 fedha
za ndani zimetengwa.
(g) Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Umwagiliaji
Kukamilisha ujenzi wa mabwawa ya Lwanyo, Kongogo na Nyisanzi; kujenga
miundombinu mipya ya umwagiliaji katika skimu za Lupilo (Ulanga), Bugwema
(Musoma), Mara, Ngono, Nyisanzi na Kongogo; kujenga mabwawa mapya ya
Borenga (Bonde la Mara), Kalebe (Bonde la Ngono) na Luiche-Kigoma; kukarabati
miundombinu ya skimu za umwagiliaji za Kigugu-Mvomero, Mvumi-Kilosa, Msolwa
Ujamaa na Njage-Kilombero; ukarabati wa miundombinu 88 ya umwagiliaji katika
shamba la Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) Kilangali pamoja na barabara za
kuingia katika skimu za Mvumi (km 8) na Njage (km 7); kukamilisha upembuzi
yakinifu kwa skimu ya Luiche (Ujiji Kigoma) na Ibanda (Sengerema/Geita); kufanya
upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika skimu nne (4) za Mwamkulu (Mpanda),
Mkombozi (Iringa), Msia (Mbozi) na Luhafwe (Tanganyika); na kukamilisha ukarabati
na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika skimu za Lwanyo, Kirya, Igenge,
Endagaw (Hanang‟), Rudewa (Kilosa) na Nyamitita (Serengeti). Jumla ya Shilingi
bilioni 13.0 fedha za ndani na Shilingi bilioni 15.3 fedha za nje zimetengwa.
(h) Ujenzi wa Maghala na Kuboresha Hifadhi ya Taifa ya Chakula
Kukamilisha ujenzi wa maghala matano (5) yenye uwezo wa kuhifadhi tani 60,000
na vihenge nane (8) vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 190,000 za nafaka; kufanya
upembuzi yakinifu na usanifu wa maghala matano (5) kwa ajili ya kuhifadhi mahindi
katika Halmashauri za Wilaya za Buchosa (1), Mkalama (1), Kasulu (1), Itilima (1) na
Ileje (1); ujenzi wa maghala matano (5) yenye uwezo wa kuhifadhi tani 6,700 za
mpunga katika skimu tano (5) za umwagiliaji za Njale (1,700), Msolwa Ujamaa
(1,700), Kigugu (1,000), Mvumi (1,300) na Mbogokomtonga (1,000) katika mkoa wa
Morogoro; ukarabati wa kituo cha udhibiti wa magonjwa ya kibaolojia (Kibaha);
kusindika tani 29,000 za mahindi ili kuzalisha tani 17,400 za unga wa mahindi na tani
4,350 za pumba za mahindi kwa ajili ya chakula cha mifugo; kusindika tani 15,000 za
alizeti ili kuzalisha lita 3,461,000 za mafuta na tani 10,350 za mashudu ya alizeti; na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 89
kukoboa tani 27,000 za mpunga zitakazozalisha tani 8,100 za mchele na tani 4,000
za pumba, ambapo Shilingi bilioni 40.83 fedha za ndani na Shilingi bilioni 1.4 fedha
za nje zimetengwa.
(i) Upatikanaji wa Mbegu na Pembejeo za Kilimo
Kuzalisha mbegu za alizeti tani 200, pamba tani 200, miche ya michikichi milioni 5
na miche ya korosho milioni 1; kukarabati vituo 36 vya Afya ya mimea na vituo 8 vya
ukaguzi wa mazao; kuagiza na kusambaza tani 625,000 za mbolea; kukarabati
ghala moja (1) lenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 za mbolea katika wilaya ya
Tabora; kuanza ujenzi wa kiwanda cha kuchanganya mbolea kwa uwiano katika
mkoa wa Dar es Salaam; kununua na kusambaza lita 300,000 na kilo 3,000 za
viuatilifu; ukarabati na ununuzi wa vifaa katika maabara mbili (2) za kupimia viuatilifu
ili zipate ithibati ya kimataifa; kutoa mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya viuatilifu na
uhifadhi wa taka zake kwa wakulima na maafisa ugani 1,200 katika kanda za
Mashariki, Kaskazini, Kati na Magharibi; kuanzisha kituo kimoja (1) cha zana za
kilimo kwa ajili ya kutoa huduma za kiufundi kwa lengo kusogeza huduma karibu na
wakulima katika kanda ya ziwa ambapo Shilingi bilioni 12.9 fedha za ndani
zimetengwa.
(j) Utafiti wa Kilimo
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni:kutafiti na kusambaza aina 15 za mbegu bora
za mazao ya nafaka, mizizi, mbegu za mafuta, mikunde na mazao ya bustani;
kukamilisha majaribio ya mbegu mpya za NARITAs Hybrid zenye kustahimili
magonjwa katika mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya na Kagera; kugundua na kusambaza
teknolojia bora 20 za agronomia, teknolojia tano (5) za kupunguza harubu katika
kilimo na usindikaji; na kujenga kinu cha kubangua korosho chenye uwezo wa
kubangua tani 1,800 kwa mwaka na kusindika tani 1,000 za mvinyo na sharubati,
ambapo Shilingi bilioni 1.2 fedha za ndani zimetengwa.
(k) Miundombinu ya Utafiti wa Kilimo
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni: kukarabati ofisi za vituo vitatu (3) vya utafiti
vya Ukiriguru, Ilonga, na Tumbi na kuvipatia vifaa muhimu; kuboresha miundombinu
ya umwagiliaji katika vituo vya utafiti vya Ilonga, Naliendele, Ukiriguru na
miundombinu ya uhifadhi wa mbegu katika vituo vya Uyole, Ilonga na Seliani;
kujenga Makao Makuu ya TARI pamoja na kituo cha Biosayansi yatakayokuwa
Chamwino Dodoma; kufanyia ukarabati vituo 16 vya utafiti ikiwemo ofisi, nyumba 40
za wafanyakazi pamoja na maabara 3 ili kuviwezesha kufanya ufatiti wake kwa
ufanisi; kufanyia ukarabati wa miundombinu ya kituo cha ukusanyaji na utunzaji
nasabu za mimea (NPGRC) na kuongeza vitendea kazi; kuboresha mashamba
matano (5) ya kuzalisha mbegu na maghala ya kuhifadhia mbegu; kujenga na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 90
kukarabati miundombinu 9 ya umwagiliaji ili kuwezesha uzalishaji wa mbegu
ambapo Shilingi bilioni 8.35 za fedha za ndani zimetengwa.
(l) Uzalishaji wa Mbegu Bora za Mazao
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni: kuzalisha na kusambaza mbegu bora za
awali tani 200, za msingi tani 1,000, na mbegu zilizothibitishwa tani 3,000 za mazao
ya aina ya nafaka, mikunde, mboga mboga, mafuta na miche milioni 20 ya mazao ya
mizizi; kuzalisha tani 2,000 za mbegu za Alizeti na kuzisambaza kwa wakulima;
kuboresha miundombinu ya umwagiliaji kwa mashamba ya Arusha, Mwere,
Bugagana na Dabaga; kuboresha na kujenga maghala ya kuhifadhia mbegu za
kilimo kwa shamba la Msimba na Kilangali; na kufanya tathmini ya afya ya udongo
katika mashamba 8 ambapo Shilingi bilioni 6.3 fedha za ndani zimetengwa.
(m) Huduma za Upimaji wa Matabaka na Ubora wa Udongo
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni: kupima matabaka ya udongo katika vijiji
vinavyozunguka mashamba makubwa ya kimkakati ya Lukulilo Muhoro na Tawi
pamoja na mashamba ya miwa ya Pangani, Kitengule na Bagamoyo; kuimarisha
upimaji wa matabaka ya udongo katika mikoa ya kanda ya kati (Singida na Dodoma)
ili kuwa na uhakika wa matumizi ya mbolea katika mazao ya mafuta (Karanga na
alizeti); na kufanya tathmini ya udongo kwenye ardhi ya kilimo katika halmashauri za
wilaya za Singida na Morogoro ambapo Shilingi milioni 300 fedha za ndani
zimetengwa.
(n) Huduma za Ushauri kuhusu Utafiti, Mafunzo na Usambazaji Taarifa za
Kilimo na Sayansi Shirikishi
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni: kuandaa mashamba ya mfano 50 kwa
teknolojia ya mazao mbalimbali; kutoa machapisho 1,000 ya aina 20 za teknolojia za
mazao ya nafaka, mizizi, mikunde, pamba, na mboga mboga na kuzisambaza kwa
wakulima; kuandaa kanzidata ya kielektroniki ya teknolojia zote zilizozalishwa na
vituo vya utafiti na kuziunganisha na simu za mkononi za wakulima ili wapate taarifa
kwa urahisi; na kutoa elimu kwa wakulima 2,000 na wagani 200 katika utumiaji wa
teknolojia mpya ikiwa ni pamoja na matumizi ya mbegu bora, udhibiti wa magonjwa
na matumizi ya madawa ambapo Shilingi milioni 500 fedha za ndani zimetengwa.
(o) Mkakati wa uzalishaji wa zao la Mchikichi
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni; TARI kwa kushirikiana na ASA, Jeshi la
Kujenga Taifa, Magereza, Sekretarieti za Mikoa na Sekta Binafsi itazalisha miche ya
michikichi 5,000,000; kuboresha miundombinu ya umwagiliaji katika shamba la
Bugaga (Kasulu); na kujenga kituo kipya cha TARI Kihinga kwa ajili ya utafiti wa zao
la michikichi ambapo shilingi bilioni 2.1 fedha za ndani zimetengwa.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 91
4.3.2.4. Mifugo
(a) Kuimarisha Vituo vya Uhimilishaji Kitaifa na Kikanda
Shilingi bilioni 3.4 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kununua mtambo mpya
wa Naitrojeni wenye uwezo wa kuzalisha lita kumi (10) za kimiminika baridi cha
hewa ya Naitrojeni kwa saa moja; kununua mitungi 70 ya kuhifadhi kimiminika baridi
cha hewa ya Naitrojeni yenye ujazo wa lita 35 kwa kila mtungi na kuisambaza
kwenye halmashauri 70; kununua mtungi wa kuhifadhi kimiminika cha hewa baridi ya
Naitrojeni wenye ujazo wa lita 200 kwa ajili ya kituo cha NAIC Arusha; kununua
chupa 75,000 za homoni; kutoa elimu ya uhimilishaji kwa wahimilishaji 600 kutoka
mikoa ya Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida, Simiyu, Shinyanga, Tabora, Kigoma,
Katavi, Mwanza na Geita na kununua darubini 2 kwa ajili ya vituo viwili vya
uhimilishaji vya mikoa ya Pwani na Dodoma.
(b) Kuimarisha Huduma za Utafiti, Ugani na Mafunzo kwa Maafisa Ugani wa
Mifugo
Shilingi milioni 200 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kuwezesha TALIRI
kuhaulisha teknolojia ya kiinitete kwa wafugaji; kukarabati miundombinu ya taasisi 7
za utafiti (Mpwapwa, West Kilimanjaro, Tanga, Naliendele, Mabuki, Uyole na
Kongwa) na kujenga kituo cha mfano cha kukusanyia maziwa, maeneo ya Mkuranga
(Pwani).
(c) Kuongeza Thamani Bidhaa za Mifugo na Kuimarisha Ukusanyaji wa
Maduhuli na Udhibiti wa Biashara ya Magendo ya Mifugo
Shilingi milioni 500 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kuzalisha ng‟ombe
4,791, mbuzi/kondoo 1,399 na kuzalisha na kuuza nyama tani 323.6; kuhamasisha
ufugaji wa kisasa ukiwemo wa ranchi na unenepeshaji wa mifugo ili kufikia ng‟ombe
550,000 kwa mwaka; kusimamia uingizaji holela wa mazao na pembejeo za mifugo
kutoka nje; kuendesha doria maalum za usimamizi wa ukusanyaji maduhuli na
kuzuia biashara ya magendo ya mifugo na mazao yake kwenye minada ya mifugo
ya mipakani; na kufanya ukarabati wa miundombinu ya masoko/minada ya mifugo.
(d) Kutenga Maeneo ya Malisho na Upatikanaji wa Maji
Shilingi milioni 95 fedha za ndani zimetengwa kwa ajiili ya: uendelezaji wa
miundombinu ya majosho na malisho; kuendelea kutenga na kupima maeneo ya
malisho na kuandaa miongozo ya utumiaji na usimamizi wa maeneo hayo;
kusimamia na kudhibiti ubora wa vyakula vya mifugo kwa kufanya ukaguzi wa
viwanda, maeneo ya kuuzia na kutoa mafunzo kwa wakaguzi na watengenezaji;
kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora za malisho kwa kuimarisha na
kupanua mashamba saba (7) ya Serikali; kuchimba na kujenga visima 50 katika
maeneo mbalimbali nchini; na ukarabati wa malambo sita (6) katika mikoa ya
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 92
Manyara, Pwani, Simiyu, Arusha, Geita na Tabora.
(e) Kuimarisha Tiba na Udhibiti wa Magonjwa ya Mifugo
Shilingi bilioni 1 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kujenga uwezo Kiwanda
cha Chanjo za Mifugo cha Serikali kilichopo Kibaha ili kiweze kuzalisha aina saba (7)
za chanjo za magonjwa; kuwezesha Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania
kuzalisha dozi milioni 111 za chanzo za mifugo ikiwa ni pamoja na dozi milioni 100
za chanjo ya Mdondo ya TEMEVAC 12, milioni 5 za CBPP, milioni 3 za Kimeta na
milioni 3 za Chambavu; na kuanza majaribio ya kuzalisha chanjo dhidi ya ugonjwa
Sotoka ya Mbuzi na Kondoo (CCPP), dhidi ya Kichaa cha Mbwa na Mapele ya
Ngozi.
4.3.2.5. Uvuvi
(a) Kuimarisha Shughuli za Utafiti, Huduma za Ugani na Mafunzo ya Uvuvi
Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni: kufanya utafiti wa samaki wapya wa kufugwa;
kufanya utafiti wa vyakula vya samaki na kuongeza ubora wa mbegu za samaki wa
kufugwa na mwani; na kufanya tafiti za kujua wingi wa rasilimali za uvuvi zilizo katika
ukanda wa Uchumi wa Bahari Kuu.
(b) Kuongeza Upatikanaji wa Vifaranga vya Samaki
Shilingi milioni 405 fedha za ndani zimetengewa kwa ajili ya: kuwezesha Vituo vitatu
(3) vya samaki wa maji baridi vya Ruhila, Kingolwira na Mwamapuli na kujenga kituo
kimoja (1) cha Nyamirembe ili kuzalisha vifaranga milioni 15 vya samaki; kuboresha
matumizi ya teknolojia za uzalishaji, kuchakata na kuongeza thamani ya mazao ya
viumbe vya majini; na kuunda kanda 3 za ufugaji wa vizimba katika Ziwa Victoria na
kanda 2 za ukuzaji viumbe wa maji bahari katika mikoa ya Pwani na Mtwara.
(c) Kuimarisha na Kuendeleza Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi na Mazingira
Shilingi bilioni 1.4 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kuimarisha vituo vya ulinzi
wa rasilimali za uvuvi vilivyopo na kuanzisha kanda na vituo katika maeneo ya maji
na nchi kavu; kufanya doria za kawaida za kudhibiti uvuvi na biashara haramu;
kufanya operesheni za kila robo ya mwaka za kudhibiti Uvuvi haramu na uharibifu
wa mazingira.
(d) Kusimamia na Kuhamasisha Uwekezaji katika Uvuvi na Viwanda vya
Kuchakata Mazao ya Uvuvi
Shilingi milioni 242.2 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kuimarisha vituo vya
ubora na uthibiti wa mazao ya uvuvi na kuanzisha vituo vipya vitatu vya Singida,
Kisesya na Murusagamba; kufanya kaguzi 7,200 za ubora wa samaki na mazao
yake wakati wa kusafirisha nje ya nchi; kufanya kaguzi 120 za kina kwenye viwanda
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 93
vinavyochakata samaki, maghala ya kuhifadhi mazao ya uvuvi, mialo na masoko ya
samaki; kuimarisha maabara za samaki za Nyegezi (Mwanza) na ya viuatilifu Dar es
Salaam kwa kuzipatia vitendea kazi, watumishi na mafunzo kwa Wataalam; na
kufanya chunguzi za kimaabara kwa sampuli 4,800 za minofu ya samaki, maji,
udongo, masalia ya madawa ya mimea, asidi, alikali na madini tembo ili kuhakiki
usalama wa mazao ya uvuvi.
(e) Kuimarisha Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi katika Ukanda wa Uchumi
wa Bahari na Bahari Kuu
Shilingi bilioni 1 fedha za ndani na Shilingi bilioni 4.2 fedha za nje zimetengwa kwa
ajili ya: kukamilisha upembuzi yakinifu na kuanza ujenzi wa Bandari ya Uvuvi;
kuboresha mfumo wa ufuatiliaji wa meli za uvuvi wa Baharini; kununua meli ya doria
kwa ajili ya kufanya operesheni mbalimbali kwenye Ukanda wa Uchumi wa Bahari
kuu; na kununua meli mbili (2) za uvuvi za long line na Purse seine.
(f) Kuimarisha Miundombinu na Kukuza Biashara ya Mazao ya Uvuvi
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni kukarabati mialo ya kupokelea samaki na
masoko ya samaki (Mialo) ya Sota, Marehe, Kigangama, Kahunda, Ikumbaitale,
Bwai, Nyamisati, Igombe, Ihale, Mafia, Kilwa, Kirumba na Feri.
(g) Kuboresha Upatikanaji wa Taarifa Sahihi za Uvuvi
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni: kufanya sensa ya uvuvi katika maeneo ya
Ziwa Tanganyika na Nyasa na kusimamia ukusanyaji, uchakataji, utunzaji na
usambazaji wa takwimu za uvuvi.
4.3.2.6. Maliasili na Misitu
(a) Mradi wa Kujenga Uwezo katika Mapori ya Akiba
Shilingi milioni 500 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kukarabati nyumba 58 za
watumishi katika mapori ya akiba 27; kuboresha miundombinu ya barabara, viwanja
vya ndege na ofisi katika mapori ya akiba; na kuwajengea uwezo askari
wanyamapori katika kulinda na kusimamia rasilimali za wanyamapori.
(b) Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Maliasili
Shilingi bilioni 13.9 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya: kusaidia halmashauri za
Ngorongoro na Serengeti katika masuala ya Sera, Sheria na taratibu zinazohusu
mgawanyo wa faida zitokanazo na uhifadhi wa maliasili; na kuzijengea uwezo
halmashauri za Ngorongoro na Serengeti katika kutatua migogoro inayotokana na
mwingiliano kati ya wanyamapori na wananchi.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 94
(c) Mradi wa Usimamizi wa Maliasili kwa ajili ya Maendeleo ya Kiuchumi
Shilingi bilioni 4.1 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya: kukamilisha mipango ya
usimamizi wa misitu ya hifadhi ya vijiji 33 vya mradi; kusimamia utekelezaji wa
mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji 36 na kutoa hati miliki za kimila;
kuandaa mpango wa uendelezaji wa matokeo ya mradi, uwekezaji na mambo ya
kujifunza yaliyotokea kwenye kila uwanda; na kujenga uwezo kwa wataalam ngazi
ya kijiji kusimamia shughuli za mradi.
(d) Mradi wa Kuimarisha Mtandao wa Misitu Asilia kwa ajili ya Kuhifadhi
Bioanuai Tanzania
Shilingi bilioni 4.3 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya: kuweka alama za kudumu
kuzunguka misitu yote ya mazingira asilia; na kuwezesha halmashauri za Wilaya na
Vijiji vinavyozunguka misitu ya mazingira asilia kufanya doria za mara kwa mara kwa
kuvipatia vifaa.
(e) Programu ya Misitu na Uendelezaji wa Mnyororo wa Thamani wa Mazao
ya Misitu
Shilingi bilioni 4.7 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya: kuandaa mipango ya
matumizi bora ya ardhi na mipango ya usimamizi wa misitu ya hifadhi ya vijiji katika
wilaya nane (8) za mikoa ya Tanga, Lindi Mtwara na Ruvuma; kutoa elimu kwa
Kamati za Maliasili za vijiji, sekta binafsi kuhusu umuhimu wa rasilimali na namna ya
kuongeza thamani mazao ya misitu; kutoa elimu na uraghibishi kwa Kamati za
Maliasili za vijiji, watumishi wa halmashauri na Asasi zisizo za Serikali; na
kuwezesha Kamati za Mazingira za vijiji katika kufanya doria mbalimbali kwenye
misitu ya hifadhi ya vijiji kwa kuvipatia vifaa.
(f) Mradi wa Kujenga Uwezo katika Misitu na Nyuki
Shilingi milioni 200 fedha za ndani na Shilingi milioni 220 fedha za nje zimetengwa
kwa ajili ya: kuboresha miundombinu katika Chuo cha Misitu Olmotonyi na Chuo cha
Viwanda vya Mazao ya Misitu; ujenzi wa jengo la utawala la Chuo cha Ufugaji Nyuki
- Tabora; kuendeleza shughuli za utafiti; na kukamilisha maabara ya asali katika
Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).
4.3.2.7. Madini
(a) Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini,
Mafuta na Gesi Asilia - TEITI
Shilingi bilioni 1.04 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kuelimisha umma
kuhusu matumizi ya takwimu za taarifa za TEITI katika kuhoji ufanisi wa ukusanyaji
na mapato yanayotokana na rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia; na kuanzisha
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 95
rejista ya taarifa na majina ya watu wanaomiliki hisa katika kampuni za madini,
mafuta na gesi asilia.
(b) Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini
Shilingi bilioni 6.0 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kuwezesha shughuli za
utafiti wa madini ili kuongeza taarifa za kijilojia na kuvutia uwekezaji; kuhamasisha
uongezaji thamani madini nchini; kufanya mapitio na kuandaa mkakati wa Sera ya
madini ya Mwaka 2009; uendelezaji wa wachimbaji wadogo nchini; usimamizi wa
masuala ya mazingira, afya na usalama migodini; uendelezaji wa masoko ya madini;
na ufuatiliaji na tathmini ya sekta ya madini.
(c) Mradi wa Kuendeleza Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira wa Kuzalisha
Umeme MW 200
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni: kuendelea na uchimbaji na kuanza uoshaji
wa makaa ya mawe ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya uchimbaji na mtambo
wa kuoshea makaa hayo kwa ajili ya kuyaongezea thamani; kuanza uzalishaji wa
nishati mbadala (coal briquette) kwa ajili ya matumizi ya nyumbani; na uzalishaji wa
tani laki 1.6 za makaa ya mawe.
4.3.3. Miradi ya Kufungamanisha Maendeleo ya Viwanda na Maendeleo ya
Watu
4.3.3.1. Elimu, Sayansi na Teknolojia
A. Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari
(a) Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo katika Elimu: Shilingi bilioni 94.6
fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya: kununua magari 65 kwa ajili ya kuimarisha
uthibiti ubora wa shule; kujenga ofisi 55 za wathibiti ubora wa shule; kununua magari
10 kwa ajili ya Vyuo vya Ualimu; kutoa motisha kwa shule 400 za msingi na
sekondari zilizoongeza kiwango cha ufaulu katika mitihani ya Taifa ya Darasa la
Saba na Kidato cha Nne 2018; kutoa motisha kwa halmashauri 184 kutokana na
utekelezaji wa vigezo vilivyokubalika kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo;
kununua magari matano (5) na malori mawili (2) kwa ajili ya Baraza la Mitihani la
Taifa; na ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya mfano mkoani Dodoma kwa ajili ya
kidato cha 1 – 6.
(b) Ukarabati wa Vyuo vya Ualimu: Shilingi bilioni 7.29 fedha za ndani
zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi na ukarabati wa vyuo vinne (4) vya
Ualimu vya Shinyanga, Mpuguso, Ndala na Kitangali.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 96
(c) Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu ya Msingi (MMEM)-KKK
Shilingi bilioni 20.44 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya: kuandaa, kuchapisha na
kusambaza vitabu vya mwanafunzi na kiongozi cha mwalimu kwa masomo yote vya
darasa la VI na VII; kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa programu;
kugharamia matengenezo ya magari ya wathibiti ubora wa shule kwa ajili ya kazi za
ufuatiliaji wa utekelezaji wa Kiunzi cha uthibiti ubora wa shule; kuwezesha
uendeshaji na uratibu wa Programu ya LANES na ukaguzi wa ndani na nje;
kuwajengea uwezo waratibu wa Vituo vya Walimu; na kununua na kusambaza vifaa
vya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
(d) Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari: Shilingi bilioni 30.81 fedha za
nje zimetengwa kwa ajili ya: kutoa mafunzo kazini kwa walimu 10,000 wa Sayansi,
Hisabati, na Lugha; kununua vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa shule 500 za
sekondari; uchapaji na usambazaji wa nakala milioni 6 za vitabu vya Hisabati,
Sayansi na Lugha; ununuzi wa mashine za uchapaji kwa ajili ya Taasisi ya Elimu
Tanzania; kuandaa moduli za elimu jumuishi pamoja na mwongozo wa mafunzo;
kuandaa kiunzi cha utoaji tuzo kwa walimu mahiri pamoja na uchapaji wa vyeti;
kununua kompyuta, printa na projekta kwa shule za sekondari 700 na kutoa mafunzo
ya TEHAMA kwa walimu 1,000; kununua vifaa vya upimaji kwa wanafunzi wa
sekondari wenye mahitaji maalum; na kuandaa mkakati wa upatikanaji wa walimu
wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
(e) Programu ya Huduma ya Maji, Elimu ya Afya na Usafi wa Mazingira
Shuleni: Shilingi bilioni 6.94 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya: ujenzi wa
miundombinu ya maji na vyoo katika shule za msingi 200; na kuendelea kutoa
mafunzo kuhusu utumiaji wa mwongozo wa programu kwa wathibiti ubora wa shule
na waratibu wa programu katika ngazi ya halmashauri.
(f) Mamlaka ya Elimu Tanzania - TEA: Shilingi bilioni 12 fedha za ndani
zimetengwa kwa ajili ya: ujenzi wa nyumba 20 za walimu wa sekondari katika
maeneo yasiyofikika kwa urahisi; ujenzi wa madarasa 75 katika shule za Msingi na
Sekondari zenye uhaba mkubwa wa madarasa; ujenzi wa mabweni 16 ya wanafunzi
wa kike katika shule za sekondari; ujenzi wa vyoo katika shule 10 zenye upungufu
mkubwa; ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na uboreshaji wa
miundombinu katika vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu 2 vya Zanzibar; kukamilisha
ukarabati wa majengo katika shule kongwe 4 za Sekondari za Serikali (Mwenge,
Msalato, Nganza na Mzumbe); ukarabati wa shule za msingi 5 katika jiji la Dodoma;
na ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia na ujenzi wa miundombinu kwa
ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa shule 10 za msingi na sekondari.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 97
B. Elimu ya Ufundi na Ualimu
(a) Ujenzi na Ukarabati wa Vyuo vya Ufundi Stadi: Shilingi bilioni 54 fedha za
ndani na Shilingi bilioni 18.85 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya: kujenga
karakana tano (5) katika vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi katika mikoa ya Lindi (1),
Pwani (1), Manyara (2) na ujenzi wa karakana ya “Mechatronics” katika chuo cha
TEHAMA-Kipawa, Dar es Salaam; kujenga jengo la utawala, uzio na kufanya
marekebisho katika bweni moja na madarasa mawili katika Chuo cha Ufundi cha
Arusha (ATC); kujenga bweni la wasichana lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 200
katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Mkoa wa Mbeya; kujenga karakana ya
mitambo mizito katika Chuo cha Ufundi Stadi cha Mwanza; kujenga nyumba 10 za
watumishi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Ulyankulu; ununuzi wa
nyumba 10 za watumishi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Manyara;
kujenga karakana katika Chuo cha Ualimu wa Mafunzo ya Ufundi Stadi Morogoro
(MVTTC); na kununua vifaa vya kisasa kwa Vyuo vitatu vya Ufundi Stadi vya
TEHAMA Kipawa-Dar es Salaam, Mtwara na Lindi.
(b) Kuimarisha Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Elimu ya
Ualimu: Shilingi bilioni 5.5 fedha za ndani na Shilingi bilioni 1.79 fedha za nje
zimetengwa kwa ajili ya: kuendelea na ujenzi wa vyuo vya Ufundi Stadi na huduma
vya mikoa ya Geita na Rukwa; kujenga mabweni mawili (2) katika chuo cha Ualimu
wa Ufundi Stadi cha Morogoro; kuendelea na ujenzi wa jengo la ghorofa nne (4) kwa
ajili ya madarasa, maabara, ugavi na ofisi za walimu katika Chuo cha Ufundi
Arusha; kujenga mabweni mawili (2) yenye uwezo wa kulaza wanachuo 576, jengo
la ghorofa 2 lenye madarasa 6 na ukumbi wa mikutano wenye uwezo wa kuchukua
watu 1,500, na jengo la jiko katika Chuo cha Ualimu Dakawa; kujenga nyumba nne
(4) za walimu katika Chuo cha Ualimu Marangu; kujenga bweni la ghorofa moja (1),
nyumba nane (8) za walimu na kukarabati jengo la utawala katika Chuo cha Ualimu
Butimba; kujenga maabara ya ghorofa moja (1), bweni la ghorofa moja (1) kwa ajili
ya wanafunzi 576 katika Chuo cha Ualimu Tabora; kujenga bwalo la chakula, bweni
la ghorofa moja (1) la wanafunzi wa kike 176, maabara ya ghorofa moja (1) na
nyumba mbili (2) za walimu katika Chuo cha Ualimu Mpwapwa; kununua na kufunga
vifaa kwa ajili ya programu ya vito na usonara katika Chuo cha Ufundi Arusha; na
kununua na kufunga vifaa vya Biomedical katika maabara ya uhandisi ya ujenzi na
umwagiliaji katika Chuo cha Ufundi Arusha.
(c) Chuo cha Ufundi Arusha: Shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa kwa
ajili ya: kujenga bweni moja (1) la wanafunzi wa kike lenye uwezo wa kulaza
wanafunzi 250; kuendelea na utafiti wa kuzalisha umeme Wilayani Mbulu chini ya
ufadhili wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA); na kujenga maktaba yenye uwezo wa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 98
kuchukua jumla ya wanafunzi 1,000 na bweni la wasichana lenye uwezo wa kulaza
wanafunzi 250.
(d) Kuimarisha Mafunzo ya Elimu ya Ualimu: Shilingi bilioni 20.3 fedha za nje
zimetengwa kwa ajili ya: kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa vyuo 35
vya ualimu; kununua vitabu vya rejea vya kielektroniki kwa ajili ya vyuo vya ualimu
35 na kusambaza vifaa vya TEHAMA; kutoa mafunzo ya TEHAMA na teknolojia
saidizi kwa wakufunzi /walimu 150 wenye mahitaji maalum; kuboresha miundombinu
ya TEHAMA katika vyuo vya ualimu na kuviunganisha na Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano; kuendelea na ujenzi wa Chuo cha Ualimu cha Kabanga; kutoa
mafunzo kwa wawezeshaji 300 wa kitaifa kuhusu mtaala wa umahiri; kutoa mafunzo
ya programu ya wakufunzi wa chuo kwa wakufunzi 1,300 wa vyuo vya ualimu; kutoa
mafunzo ya Hisabati kwa walimu waliopo kazini katika halmashauri 20 zenye ufaulu
hafifu; kuanzisha vituo vya kitaalam vya Hisabati na kuandaa vifaa vya mafunzo kwa
somo la Hisabati; na kutoa mafunzo kwa walimu 500 (350 Msingi na 150 Sekondari)
kuhusu lugha ya alama na mbinu sahihi za ufundishaji kwa wanafunzi viziwi.
(e) Kuimarisha Taasisi ya Elimu Tanzania: Shilingi bilioni 10 fedha za ndani
zimetengwa kwa ajili ya: kuandika muhtasari wa lugha ya Kichina kidato cha Tano
na Sita ambayo inafundishwa katika shule za Sekondari 16; kuandaa mtaala na
muhtasari wa somo la Kiswahili kwa shule za msingi na sekondari za nchi za Afrika
ya Kusini na nchi nyingine zitakazowasilisha maombi; kuhuisha mtaala wa elimu ya
sekondari ili uzingatie mahitaji ya wanafunzi viziwi; kuendelea na uandishi wa vitabu
vya kiada kwa Darasa la VI, VII, Kidato cha I - VI na moduli kwa Elimu ya Ualimu
pamoja na kuandaa maudhui ya kielektroniki; kuchapa vitabu vya kiada vya Darasa
la VI - VII, Kidato cha I – VI na vitabu vya Elimu ya Ualimu; kurusha hewani vipindi
vya Taasisi ya Elimu Tanzania vyenye kubeba maudhui ya kielektroniki kwa lengo la
kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu; kutoa mafunzo kazini kwa walimu
wa shule za msingi (darasa la V – VII) kwa mtaala ulioboreshwa; na kuendelea
kuandika vitabu vya hadithi kwa ajili ya shule za msingi.
C. Elimu ya Juu
(a) Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu: Shughuli zilizopangwa
kutekelezwa ni: kutoa mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 450 kwa wanafunzi
128,285 ambapo wanafunzi 45,485 ni wa mwaka wa kwanza; kukusanya Shilingi
bilioni 221.5 kutoka kwa wanufaika ambao mikopo yao imeiva; kuanzisha na
kuimarisha ofisi mbili (2) za kanda katika mikoa ya Mbeya na Mtwara; kuendeleza
utekelezaji wa mkakati wa uboreshaji wa mifumo ya TEHAMA ili kuunganisha
mifumo ya Bodi ya Mikopo na ya wadau wengine; na kutekeleza kampeni za
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 99
uelimishaji kuhusu huduma zinazotolewa na Bodi ya Mikopo, vigezo, utaratibu,
wajibu wa wanufaika na waajiri katika urejeshaji wa mikopo.
(b) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam: Shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani na
Shilingi milioni 500 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya: kukamilisha awamu ya
kwanza na kuanza awamu ya pili ya ujenzi wa kituo cha wanafunzi; kuanza ujenzi
wa Ndaki ya Tiba za Afya – Mbeya; kufanya upanuzi wa hosteli za Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli kwa ghorofa mbili zaidi; kukamilisha ujenzi wa jengo jipya la Kituo
cha Afya cha Chuo; kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo la Shule Kuu ya
Uchumi na ukarabati wa nyumba za walimu; kukarabati mabweni ya wanafunzi,
barabara za ndani; na kuanza ujenzi wa jengo la ofisi na vyumba vya madarasa
katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari pamoja na ujenzi wa jengo la Taasisi ya
Sayansi za Bahari lililopo Buyuni Zanzibar.
(c) Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa -
MUCE: Shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kujenga hosteli
mbili (2) zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 kila moja na maktaba yenye
uwezo wa kuchukuwa wanafunzi 1,000 kwa wakati mmoja; na kuimarisha kitengo
cha masomo ya uzamili, utafiti na huduma kwa jamii.
(d) Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam -
DUCE: Shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kuendelea na
awamu ya pili ya ujenzi wa jengo la utawala; na kununua vifaa vya ufundishaji na
ujifunzaji wa wanafunzi 57 wenye mahitaji maalum pamoja na vifaa vya utafiti kwa
wanataaluma.
Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mwl. Julius Nyerere cha Kilimo na Teknolojia:
Shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: ukarabati wa
miundombinu katika Kampasi ya Oswald Mang‟ombe; na kukamilisha upatikanaji wa
hati ya maeneo ya chuo hususan, Kisangura - Mugumu katika Wilaya ya Serengeti
na Kinesi-Wilaya ya Rorya.
(e) Ukarabati na Ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe: Shilingi bilioni 1.0 fedha za
ndani zimetengwa kwa ajili ya kuweka samani katika hosteli za wanafunzi Kampasi
Kuu eneo la Maekani.
(f) Ujenzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Ardhi: Shilingi milioni 500 fedha za
ndani zimetengwa kwa ajili ya: kukamilisha ujenzi wa jengo la Ardhi pamoja na
kuweka samani, maabara itakayokuwa na matumizi zaidi ya moja, mabweni ya
wanafunzi, ukumbi wa mihadhara, mifumo ya maji taka, na miundombinu ya
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 100
TEHAMA; kukarabati karakana, madarasa, hosteli ya wanafunzi, bwalo la chakula
na nyumba za watumishi; kuanza ujenzi wa jengo la usanifu majengo, kuandaa
michoro ya ujenzi wa karakana, bwalo la chakula na kituo cha Afya; na kununua
magari matatu (3), genereta moja (1), samani na vifaa vya TEHAMA.
(g) Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili: Shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani na Shilingi bilioni 1.57 fedha za nje
zimetengwa kwa ajili ya: kukamilisha ujenzi wa kituo cha umahiri wa magonjwa ya
moyo na mishipa ya damu katika Kampasi ya Mloganzila; na kukarabati kituo cha
kufundishia na tafiti cha Bagamoyo.
(h) Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi: Shilingi bilioni
1.0 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kujenga maktaba yenye uwezo wa
kuchukua wanafunzi 2,500 kwa wakati mmoja; na kujenga hosteli za wanafunzi.
(i) Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela – Arusha:
Shilingi bilioni 1.0 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya: kuanza ujenzi wa hosteli
yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 kwa wakati mmoja; na kutekeleza miradi
33 ya kitafiti na ubunifu kwa kufadhili wanafunzi na kulipa gharama za kiutafiti kwa
wanafunzi na wanataaluma.
(j) Mradi wa Jengo la kufundishia Katika Chuo cha Teknolojia Dar es
Salaam: Shilingi milioni 500 fedha za ndani na Shilingi bilioni 11.47 fedha za nje
zimetengwa kwa ajili ya: kukamilisha upanuzi wa jengo la maktaba kwa kutumia
mapato ya ndani lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 kwa wakati mmoja;
kuweka samani za ndani na miundombinu ya TEHAMA katika jengo la DIT Teaching
Tower; na kuendelea kutafuta maeneo ya ardhi kwa ajili ya kuanzisha kampasi mpya
mikoa ya Pwani na Jijini Dodoma.
(k) Upanuzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya: Shilingi bilioni
1.0 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kuendelea kukamilisha ujenzi wa jengo
la maktaba lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,500 kwa wakati mmoja; kuanza
ujenzi wa jengo la ukumbi wa mihadhara lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 300
kwa wakati mmoja; kuendelea kukarabati miundombinu ya majengo ya madarasa,
hosteli na nyumba za watumishi; kufanya tathmini ya mali za wananchi katika eneo
la Kitalu Na. 2 lenye hekta 511 (Mbeya Vijijini) litakalotumika kwa ajili ya upanuzi wa
chuo; na kufanya tathimini ya mali za wananchi katika eneo ambalo limeainishwa
kuongezwa katika kampasi ya Rukwa ili kufikia hekta 500.
(l) Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo: shughuli
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 101
zilizopangwa kutekelezwa ni: kujenga kumbi mbili (2) za mihadhara zenye uwezo wa
kuchukua wanafunzi 1,000 kila mmoja, ukumbi mmoja (1) wa mikutano wenye
uwezo wa kuchukua watu 1,000 na madarasa manne (4) yenye uwezo wa kuchukua
watu 50 kila moja; kuendelea na ujenzi wa hosteli moja (1) Kampasi ya Solomon
Mahlangu, yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 700; kujenga maabara mtambuka
katika kampasi kuu; na kukarabati miundombinu iliyochakaa ikijumuisha vyumba 17
vya kufundishia, mabweni sita (6), nyumba 30 za watumishi na barabara za ndani
zenye urefu wa kilomita 10 katika Kampasi Kuu na Solomon Mahlangu; ofisi na
madarasa Kampasi ya Tunduru na Kampasi kuu na Solomon Mahlangu ambapo
Shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kugharamia shughuli hizo.
D. Ujuzi na Utafiti
Kukuza Stadi za Kazi na Ujuzi kwa Ajili ya Shughuli za Kuzalisha na Kukuza
Uchumi: Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni: kuendelea na utekelezaji wa Mfuko
wa Kukuza Stadi za Kazi kwa kutoa ruzuku kwa ushindani kwa taasisi za mafunzo;
kuanza ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi (VETA) katika halmashauri za Ruangwa,
Kongwa, Kasulu TC na Nyasa; kukarabati vyuo vya maendeleo ya wananchi na
kuvinunulia vifaa vya kufundishia na kujifunzia; kuendelea na ukarabati wa vyuo 14
vya Maendeleo ya Wananchi; kutoa mafunzo ya uanagenzi katika vyuo vya Ufundi
Stadi na Elimu ya Ufundi; kuendelea na ujenzi wa chuo cha ufundi Dodoma chenye
uwezo wa kudahili wanafunzi 5,000 kwa wakati mmoja ambapo Shilingi bilioni 56.55
fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kugharamia shughuli hizo.
(a) Mfuko wa Utafiti na Maendeleo wa COSTECH: Shughuli zilizopangwa
kutekelezwa ni: kugharamia miradi mipya 8 ya utafiti kulingana na vipaumbele vya
utafiti vya Taifa; kuboresha mifumo ya ubunifu na kuwaendeleza wabunifu nchini ili
waweze kujiajiri; kubiasharisha matokeo ya utafiti nchini ili ziweze kutumika na kuleta
tija kwa maendeleo ya nchi; kuandaa mfumo wa uhawilishaji wa teknolojia kupitia
uwekezaji wa nje, pamoja na uhakiki wa teknolojia zinazoibukia; kuboresha mfumo
wa udhibiti na utoaji vibali vya utafiti nchini; na kuendesha mafunzo, semina,
mijadala, na mikutano mbalimbali kuhusiana na Sayansi, Teknolojia na Ubunifu
ambapo Shilingi bilioni 3.0 fedha za ndani na Shilingi bilioni 3.57 fedha za nje
zimetengwa kwa ajili ya kugharamia shughuli hizo.
(b) Maabara ya Mionzi ya Nguvu za Atomiki - Arusha: shughuli
zitakazotekelezwa ni: kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa maabara ya Tume;
kuanza ujenzi wa maabara za kanda ya Zanzibar na mikoa ya Dar es Salaam na
Mwanza; kukamilisha upembuzi yakinifu wa mradi wa kutengeneza madawa ya
kuchunguza na kutibu saratani pamoja na kinu cha tafiti za kinyuklia; kupima kiasi
cha mionzi katika sampuli 16,357 za vyakula na mbolea; kuimarisha upimaji wa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 102
mionzi kwenye mazingira katika vituo 50 ambapo Shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani
zimetengwa kwa ajili ya kugharamia shughuli hizo.
E. Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi
(a) Upanuzi na Ukarabati wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi: Shughuli
zitakazotekelezwa ni: kujenga na kukarabati miundombinu katika vyuo 34 vya
maendeleo ya wananchi na ununuzi wa vifaa vipya vya kisasa vya kufundishia na
kujifunzia ambapo Shilingi bilioni 4.0 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya
kugharamia shughuli hizo.
4.3.3.2. Afya na Maendeleo ya Jamii
A. Afya
(a) Mradi wa Kupunguza Vifo vya akina Mama Vinavyotokana na Uzazi:
Shughuli zilizopangwa ni: ujenzi wa vituo 12 vya damu salama katika mikoa 12;
upanuzi wa wodi za wazazi na kutenga vyumba vya wagonjwa mahututi
wanaotokana na uzazi katika Hospitali za Rufaa za Mikoa mitano (5); na ukarabati
na ujenzi wa wodi maalum kwa ajili ya watoto wachanga katika Hospitali za Rufaa za
Mikoa 7 ambapo Shilingi bilioni 5 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya shughuli
hizo.
(b) Mradi wa Kuboresha Hospitali za Rufaa: Shughuli zilizopangwa
kutekelezwa ni: kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za tiba, kufanya
ukarabati na upanuzi wa miundombinu, kuanzisha na kuboresha vitengo vya
dharura, wagonjwa mahututi, maeneo ya kutakasia vifaa, upasuaji na Mama na
Mtoto katika Hospitali za Rufaa za mikoa; kuendelea na ujenzi wa hospitali mpya za
mikoa katika mikoa ya Katavi, Njombe, Geita, Simiyu, Songwe na Mara ambapo
shilingi bilioni 12 fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.29 fedha za nje zimetengwa kwa
ajili ya shughuli hizo.
(c) Mradi wa Ununuzi na Usambazaji wa Dawa: Shughuli zitakazotekelezwa ni:
kuendelea kununua na kusambaza dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika
vituo vya umma vya kutolea huduma za afya ambapo Shilingi bilioni 200 fedha za
ndani zimetengwa kwa ajili ya kugharamia shughuli hizo.
(d) Taasisi ya Saratani Ocean Road: Shughuli zilizopangwa ni: kuendelea
kuimarisha huduma za kinga, uchunguzi, mafunzo na tiba ya saratani; na kuanza
ujenzi wa wodi mpya ya kulaza wagonjwa wa saratani ambapo Shilingi bilioni 10
fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kugharamia shughuli hizo.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 103
(e) Taasisi ya Tiba ya Moyo Jakaya Kikwete: Shughuli zilizopangwa
kutekelezwa ni: kununua vifaa tiba ili kuimarisha huduma za (Cathetarization
Laboratory) upasuaji moyo ambapo shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani zimetengwa
kwa ajili ya kugharamia shughuli hizo.
(f) Hospitali ya Rufaa Kibong'oto: Shughuli zitakazotekelezwa ni kununua
mashine ya CT - SCAN kwa ajili ya uchunguzi wa kifua kikuu na kujenga mtambo wa
kuzalisha hewa ya Oxygen ambapo Shilingi bilioni 1.9 fedha za ndani zimetengwa
kwa ajili ya kugharamia shughuli hizo.
(g) Hospitali ya Rufaa Bugando: Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na
awamu ya pili ya Mradi wa Saratani kwa kujenga wodi ya kulaza wagonjwa wa
Saratani, ambapo Shilingi bilioni 1.7 fedha za ndani zimetengwa.
(h) Hospitali ya Taifa Muhimbili: Shughuli itakayotekelezwa ni kuendelea na
ujenzi wa jengo la kutolea huduma za wagonjwa wanaojigharamia (private ward)
ambapo Shilingi bilioni 4 fedha za ndani zimetengwa.
(i) Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI): Shughuli zilizopangwa ni: kuwaongezea
ujuzi watalaam wa upasuaji; kununua vifaa tiba vya kisasa; na kuendelea kurejesha
mkopo wa ujenzi kutoka Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo Shilingi bilioni 5
fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kugharamia shughuli hizo.
(j) Udhibiti Magonjwa ya Kuambukiza: Shughuli zitakazotekelezwa ni:
kununua na kusambaza chanjo kulingana na mahitaji ya nchi kwa ajili ya kuwakinga
watoto chini ya mwaka mmoja; na kuimarisha huduma za kudhibiti magonjwa ya
kuambukiza ambapo Shilingi bilioni 30 fedha za ndani na Shilingi bilioni 96.93 fedha
za nje zimetengwa kwa ajili ya kugharamia shughuli hizo.
(k) Ujenzi wa Hospitali za Wilaya na vituo vya Afya: Shughuli
zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi wa hospitali za wilaya (67) na kuendelea
na upanuzi na ukarabati wa vituo vya afya ili kuviongezea ubora ikiwemo uwezo wa
kufanya upasuaji wa akina mama wenye uhitaji ili kupunguza vifo vya akina mama
na watoto vitokanavyo na uzazi.
B. Maendeleo ya Jamii
(a) Ujenzi na Ukarabati wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii: Shughuli
itakayotekelezwa ni ukarabati wa miundombinu katika vyuo vya maendeleo ya jamii
vya Mlale, Rungemba, Uyole na Misungwi ambapo Shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani
zimetengwa.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 104
(b) Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi: Shughuli zitakazotekelezwa ni:
kukamilisha kanzidata ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake; kuwezesha
upatikanaji wa teknolojia sahihi za uzalishaji, uchakataji, masoko na vifungashio kwa
wanawake wajasiriamali; na kuratibu na kuhamasisha utoaji wa mikopo yenye
masharti nafuu kwa wanawake ambapo Shilingi bilioni 1.12 fedha za nje
zimetengwa. Aidha, Shilingi bilioni 62.25 zimetengwa kwa ajili ya utoaji wa mikopo
nafuu kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu katika
Halmashauri zote nchini.
(c) Maendeleo ya Awali ya Mtoto: Shughuli zitakazotekelezwa ni: kutokomeza
ukatili dhidi ya watoto katika mikoa yote nchini; kutoa elimu ya malezi chanya kwa
jamii ili kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na watoto; kuanzisha vikundi vya
malezi chanya kwa watoto; na kuratibu uanzishwaji na uendeshaji wa mabaraza ya
watoto katika mikoa na halmashauri ambapo Shilingi milioni 191.3 fedha za nje
zimetengwa kwa ajili ya kugharamia shughuli hizo.
(d) Kuwezesha Huduma za Ustawi wa Jamii: Shughuli zitakazotekelezwa ni:
kuboresha miundombinu katika makazi ya wazee, mahabusu za watoto na makao ya
watoto; kuwezesha upatikanaji wa vitambulisho vya matibabu kwa wazee;
kuwezesha huduma za msingi kwa watoto walio katika mazingira hatarishi, walio
katika mkinzano na sheria waliopo katika makao ya Taifa ya Watoto Kurasini, Shule
ya Maadilisho ya Irambo, na watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani; kuwezesha
huduma za msingi kwa wazee wasiojiweza walio katika makazi 17 ya wazee; kutoa
usuluhishi wa migogoro ya ndoa katika familia; kuwezesha upatikanaji wa huduma
ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto katika vituo vya kulelea watoto
wadogo mchana; kuwezesha huduma za malezi ya kambo na kuasili kwa watoto
walio katika mazingira hatarishi; na kusajili makao ya watoto walio katika mazingira
hatarishi ambapo Shilingi milioni 444.67 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya
kugharamia shughuli hizo.
(e) Uimarishaji wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia Katika taasisi
za Maendeleo na Ustawi wa Jamii: Shughuli zitakazotekelezwa ni: kujenga na
kukarabati majengo na miundombinu katika vyuo vya maendeleo ya jamii, Taasisi ya
Maendeleo ya Jamii Tengeru, Taasisi ya Ustawi wa Jamii na Chuo cha Ustawi wa
Jamii Kisangara ambapo Shilingi bilioni 1 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya
kugharamia shughuli hizo.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 105
4.3.3.3. Maji na Usafi wa Mazingira
(a) Kuboresha Huduma za Maji Dar es Salaam: Shughuli zitakazotekelezwa ni:
kuanza ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji kwa visima vitano vilivyopo
Kimbiji; kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya mfumo wa majitaka katika Jiji la
Dar es Salaam; kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji na
matenki; na kukarabati miundombinu chakavu ya usambazaji maji ili kupunguza
upotevu wa maji ambapo Shilingi bilioni 18.5 fedha za ndani na bilioni 45.0 fedha za
nje zimetengwa kwa ajili ya kugharamia shughuli hizo.
(b) Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria: Shughuli zitakazotekelezwa ni:
kukamilisha ujenzi wa mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria hadi miji ya Tabora, Igunga,
Nzega, Uyui na vijiji 110 vilivyo pembezoni mwa bomba kuu; kukamilisha ujenzi wa
miundombinu ya maji katika miji ya Isaka na Kagongwa; na kuanza ujenzi wa mradi
wa kupeleka maji kutoka Ziwa Victoria kwenda miji ya Busega, Bariadi, Lagangabilili
na Mwanhuzi ambapo kiasi cha Shilingi bilioni 7.8 fedha za ndani zimetengwa kwa
ajili ya kugharamia shughuli hizo.
(c) Miradi ya Maji ya Kitaifa: Shughuli zitakazotekelezwa ni kufanya usanifu,
kukamilisha ujenzi wa vituo vya kusambaza maji, upanuzi na ukarabati wa
miundombinu ya maji katika maeneo yanayohudumiwa na miradi ya kitaifa ya
Makonde (Mtwara), Maswa (Simiyu), Wanging‟ombe (Njombe), Chalinze (Pwani),
Ujenzi wa mradi wa Mugango/Kiabakari – Butiama (Mara) ikijumuisha vijiji vilivyo
pembezoni mwa bomba kuu la mradi pamoja na mradi wa Handeni Trunk Main.
(d) Mradi wa Maji Masasi – Nachingwea: Shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani
zimetengwa kwa ajili ya kuboresha huduma za maji kwenye eneo linalohudumiwa na
mradi na kukamilisha malipo ya ujenzi wa mtambo wa kutibu na kusafisha maji.
(e) Kuboresha Huduma za Maji Vijijini: Shughuli zitakazotekelezwa ni:
kukamilisha miradi inayoendelea katika Halmashauri mbalimbali na kuanza ujenzi
wa miradi mipya ambayo usanifu wake umekamilika; kuendelea na mpango wa
kuimarisha uendelevu wa huduma za maji vijijini kupitia mfumo wa malipo kwa
matokeo; kuboresha miundombinu ya maji iliyochakaa kwa kufanya upanuzi na
ukarabati; kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa miradi kandokando ya Maziwa
Makuu na Mito Mikubwa ili kuhudumia wakazi wengi zaidi; na kujenga miundombinu
ya kusambaza maji kutoka kwenye visima vilivyochimbwa na kukarabati mabwawa
na miradi isiyofanya kazi katika Halmashauri ambapo Shilingi bilioni 202.4 fedha za
ndani na shilingi bilioni 59.1 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kugharamia
shughuli hizo.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 106
(f) Mradi wa Maji Same - Mwanga – Korogwe: Shilingi bilioni 11.2 fedha za
ndani na Shilingi bilioni 18 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi
wa miundombinu ya kuzalisha maji, ulazaji wa bomba kuu la kusafirisha maji,
mtambo wa kusafishia maji na matenki; na kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya
usambazaji wa maji katika mji wa Mwanga.
(g) Kuboresha Huduma za Maji Mijini: Shilingi bilioni 20.8 fedha za ndani na
Shilingi bilioni 35.0 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya: ujenzi, upanuzi na
ukarabati wa miundombinu ya maji katika miji midogo, miji mikuu ya wilaya
itakayofanikisha uunganishwaji wateja wapya na ujenzi wa magati ya maji;
kuboresha huduma ya maji safi na majitaka katika Jiji la Dodoma na mji wa Serikali;
na kuendelea na ujenzi wa mradi wa majisafi na usafi wa mazingira katika Jiji la
Arusha, mji wa Geita, manispaa ya Lindi na Kigoma; na kuendelea na upanuzi wa
miradi ya maji katika miji mikuu ya mikoa mipya.
(h) Kusimamia na Kuendeleza Rasilimali za Maji Nchini: Shughuli
zitakazotekelezwa ni pamoja na: ujenzi wa mabwawa makubwa ya Kidunda
(Morogoro), Farkwa (Dodoma), Ndembera (Iringa) na Dongo (Manyara); kuandaa
na kutekeleza mipango ya utunzaji wa vyanzo vya maji katika mabonde ya maji
nchini; kukusanya taarifa za rasilimali za maji na kuandaa mahitaji ya mfumo wa
kielektroniki wa rasilimali za maji; kufanya tafiti katika maeneo 91 yanayofaa
kuchimbwa visima katika mabonde ya Ruvuma na Pwani ya Kusini, Ziwa Victoria,
Rufiji na Bonde la Kati; na kuandaa mipango shirikishi ya usimamizi na uendelezaji
wa rasilimali za maji katika mabonde ya maji ambapo jumla ya shilingi bilioni 10
fedha za ndani na Shilingi bilioni 25 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya
kugharamia shughuli hizo.
(i) Kuimarisha Huduma za ubora wa Maabara za Maji: Shughuli
zitakazotekelezwa ni: kukamilisha ujenzi wa maabara katika mikoa ya Singida,
Rukwa, Mbeya, Mtwara, Shinyanga, Songea na Dar es Salaam; ujenzi wa maabara
ya maji Bukoba; kuanza ujenzi wa maabara ya maji Morogoro; kuendelea kutekeleza
mipango ya usalama wa maji yanayosambazwa mijini na vijijini ambapo jumla ya
sampuli 4,713 za maji safi zilichunguzwa kati ya sampuli 10,000 zilizokusanywa; na
kuimarisha Maabara za Maji na Kituo cha Utafiti cha Ngurdoto kwa kuzijengea
uwezo ili ziendelee kutoa takwimu sahihi za ubora wa maji.
4.3.3.4. Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
(a) Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini: Shilingi bilioni 18 fedha za ndani
zimetengwa kwa ajili ya: kukuza ujuzi na stadi za kazi katika viwanda, kilimo,
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 107
biashara, utalii, usafirishaji, TEHAMA, madini, mafuta na gesi; kutoa mafunzo ya
vitendo kazini kwa vijana 10,500 wanaohitimu katika ngazi mbalimbali za elimu;
kutoa mafunzo ya kuongeza tija na ufanisi mahali pa kazi na ujuzi wa kujiajiri kwa
vijana walio kwenye sekta isiyo rasmi; na kurasimisha ujuzi uliopatikana nje ya
mfumo rasmi wa mafunzo.
(b) Mfuko wa Maendeleo ya Vijana: Shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani
zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza utolewaji wa mitaji na mikopo yenye masharti
nafuu kwa vijana kupitia SACCOS katika mamlaka za Serikali za mitaa nchini.
(c) Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF): Shilingi bilioni 2 fedha za ndani
zimetengwa kwa ajili ya: kutekeleza miradi ya ajira za muda kupitia shughuli za
kijamii; na kuhawilisha fedha kunusuru kaya maskini Tanzania Bara na Zanzibar.
4.3.3.5. Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
(a) Upanuzi wa Usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuimarisha Chaneli y Utalii kwa kununua vifaa na
mitambo vikiwemo kamera za kawaida, kamera maalum magari na vifaa vingine
muhimu kwa ajili ya kuandaa vipindi maalum vya utalii ndani ya hifadhi na maeneo
ya vivutio; ununuzi wa mitambo ya studio na utangazaji na masoko ili kupata watalii
wengi kutoka ndani na nje ya nchi. Vile vile, kuendelea na ujenzi wa jengo la
utangazaji makao makuu ya Serikali jijini Dodoma; ujenzi na ukarabati wa studio za
redio (TBC Taifa, TBC FM na TBC International); ununuzi wa vifaa vya utangazaji
pamoja na mitambo ya kurushia matangazo mubashara; kuboresha mifumo ya
TEHAMA ya utangazaji wa redio na televisheni kwa kuunganisha katika Mkongo wa
Taifa ili kuongeza ufanisi katika urushaji wa matangazo; ununuzi wa magari ya
kurushia matangazo ya moja kwa moja kwa ajili ya matangazo ya redio na
televisheni ambapo Shilingi bilioni 5.0 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya
kugharamia shughuli hizo.
(b) Habari kwa Umma
Shughuli zitakazotekelezwa ni:kuhabarisha Umma kuhusu utekelezaji wa sera na
kazi za serikali; kuhabarisha umma kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za
Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais; na kuandaa mfumo wa
mtandao wa utoaji wa leseni za machapisho, vitambulisho vya waandishi wa habari
na picha za viongozi na matukio mbalimbali ya Serikali ambapo shilingi bilioni 1.0
fedha za ndani zimetengwa.
4.3.3.6. Hifadhi ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendeleza uhifadhi endelevu wa bonde la Ziwa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 108
Nyasa; kuimarisha Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Mazingira; kujenga uwezo wa
taasisi kusimamia na kupunguza athari za mazingira kwa jamii za vijijini katika
sehemu zenye ukame; kuimarisha mifumo ya ikolojia ili kuhimili athari za mabadiliko
ya tabianchi; kuongoa maeneo ya ikolojia yaliyoharibika na kuhifadhi baianuai; na
kujenga uwezo wa kitaifa wa kutekeleza Sheria ya Mazingira. Shilingi bilioni 18.2
fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kugharamia shughuli hizo.
4.3.4. Mazingira Wezeshi kwa Uendeshaji Biashara na Uwekezaji
4.3.4.1. Miundombinu
A. Reli
(a) Mfuko wa Maendeleo ya Reli: Shilingi bilioni 255.7 fedha za ndani
zimetengwa kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa reli kwa standard gauge, kuboresha
miundombinu ya reli iliyopo, ununuzi wa injini na mabehewa ya mizigo na abiria na
upembuzi yakinifu kwa sehemu za Kaliua – Mpanda – Karema, Tabora – Kagoma,
Tanga – Arusha – Musoma na Mtwara – Mbamba Bay na matawi ya Mchuchuma na
Liganga.
(b) Kuboresha miundombinu ya reli iliyopo kutoka Dar es Salaam hadi
Isaka: Shilingi bilioni 216.0 zimetengwa kwa ajili ya: ujenzi/ukarabati wa madaraja
na makalvati katika eneo la Dar es Salaam - Itigi (Km 626); ukarabati wa njia ya reli
kutoka Itigi - Isaka (Km 344); huduma za ushauri; ujenzi wa njia za kupishana katika
stesheni za Ilala na Isaka; na ununuzi wa vifaa na mitambo (track recording car, injini
(3), mabehewa ya mizigo (44), train control system, train modelling software na
management accounting Information Software).
(c) Ujenzi wa Reli ya jijini Dar es Salaam (DSM Commuter Trains): shughuli
zitakazotekelezwa ni kukamilisha upembuzi yakinifu wa usanifu wa awali wa ujenzi
wa reli ya mjini (DSM Commuter Trains). Hii inajumuisha kuanza kazi ya kumtafuta
Mshauri wa Uwekezaji wa kuandaa andiko la kutafuta wawekezaji.
(d) Kuboresha Miundombinu ya Reli ya TAZARA: Shughuli zitakazotekelezwa
ni: kukarabati vichwa sita (6) na mabehewa 221; kununua mtambo wa kuimarisha
njia (Tamping Machine); kununua mitambo ya kusaidia upasuaji wa kokoto na
kutengeneza mataruma ya zege katika mgodi wa Kongolo; kujenga njia mbili za reli
zenye jumla ya urefu wa mita 600 na jukwaa la kupandia abiria katika kituo cha
dharura cha Matabwe; kufanya upembuzi yakinifu wa matawi mapya ya reli za
kutoka bandari mpya ya Bagamoyo hadi kituo cha reli Mzenga - TAZARA na mgodi
wa makaa ya mawe Magamba hadi Mlowo (kilomita 20).
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 109
B. Barabara na Madaraja
(a) Barabara Zinazofungua Fursa za Kiuchumi
(i) Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupilo - Mahenge /Malinyi - Londo -
Lumecha/Songea (km 499): Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na
ujenzi sehemu ya Kidatu – Ifakara (km 68); na kuanza taratibu za ujenzi
sehemu ya Ifakara – Kihansi – Mlimba – Taweta/Madeke (km 220.22) na
Ifakara – Lupiro - Mahenge /Malinyi - Londo - Lumecha/Songea (km 396)
ambapo shilingi milioni 515 fedha za ndani na shilingi bilioni 11.6 fedha za nje
zimetengwa.
(ii) Barabara ya Tabora - Ipole - Koga - Mpanda (km 370): Shughuli
zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara sehemu za Usesula -
Komanga (km 115), Komanga – Kasinde (km 120) na Kasinde – Mpanda (km
118) ambapo Shilingi bilioni 1.9 fedha za ndani na shilingi bilioni 59.7 fedha
za nje zimetengwa.
(iii) Barabara ya Makutano - Natta – Mugumu (km 125) na Loliondo - Mto wa
Mbu (km 213): Shilingi bilioni 7.1 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya:
kuendelea na ujenzi wa sehemu za Makutano - Sanzate (km 50) na Waso -
Sale Junction (km 50); na kuanza ujenzi sehemu ya Sanzante – Natta (km
40), Natta – Mugumu (km 45), Karatu – Mbulu – Hydom – Sibiti River –
Lalago –Maswa (km 389) sehemu ya Mbulu – Hydom (km 50).
(iv) Barabara ya Manyoni - Itigi – Tabora (km 259.7): Shughuli
zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi sehemu ya Nyahua – Chaya (km
85.4) ambapo shilingi milioni 600 fedha za ndani na shilingi bilioni 10.7 fedha
za nje zimetengwa.
(v) Barabara ya Itoni – Ludewa - Manda (km 211): Shughuli zitakazotekelezwa
ni kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Lusitu – Mawenge (km 50) kwa
kiwango cha zege ambapo shilingi bilioni 4.3 zimetengwa.
(vi) Barabara ya Handeni - Kibereshi – Kibaya - Singida (km 460): Shughuli
zitakazotekelezwa ni kuanza ujenzi sehemu ya Handeni – Kiberashi (km 50)
ambapo shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa.
(vii) Barabara ya Dodoma – Iringa (km 267.1): Shughuli zitakazotekelezwa ni
kuanza ujenzi wa barabara ya mchepuo wa Iringa (Iringa Bypass km 7.3)
ambapo shilingi milioni 950 fedha za ndani zimetengwa.
(viii) Barabara ya Dodoma – Babati (km 243.80): Shughuli zitakazotekelezwa ni
kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara
ya mchepuo wa Babati (Babati Bypass km 12) ambapo shilingi milioni 70
fedha za ndani na shilingi milioni 980 fedha za nje zimetengwa.
(ix) Barabara ya Mbeya - Makongolosi - Rungwa – Itigi - Mkiwa (km 171.9):
Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi sehemu ya Chunya –
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 110
Makongolosi (km 43); na kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya
Mkiwa – Itigi - Noranga (km 56.9) na Mbalizi – Makongolosi (km 50) ambapo
shilingi bilioni 6.1 fedha za ndani zimetengwa.
(x) Barabara ya Kigoma - Kidahwe - Uvinza – Kaliua - Tabora (km 389.7):
Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi sehemu ya Urambo –
Kaliua (km 28); kuanza ujenzi sehemu ya Uvinza - Malagarasi (km 51.1) na
sehemu ya Kazilambwa - Chagu (km 36) ambapo shilingi bilioni 3.1 fedha za
ndani na shilingi bilioni 5.5 fedha za nje zimetengwa.
(xi) Barabara ya Mtwara – Mingoyo – Masasi – Songea – Mbamba Bay (km
1,470.9): Shilingi bilioni 11.3 fedha za ndani na shilingi bilioni 19.1 fedha za
nje zimetengwa kwa ajili ya: kuendelea na ujenzi wa barabara za Mbinga -
Mbamba Bay (km 66) na Masasi – Newala – Mnivata (sehemu ya Mtwara –
Mnivata km 50); kuanza ujenzi wa barabara za Masasi – Nachingwea (km
50), Mtwara – Newala – Masasi (sehemu ya Mnivata – Tandahimba km 50),
Likuyufusi – Mkenda (km 122.5) na Kitai – Lituhi (km 90); kuanza maandalizi
ya ujenzi wa barabara ya Nanganga – Ruangwa – Nachingwea (km 100),
ukarabati wa barabara ya Mtwara – Mingoyo - Masasi (km 200); na kufanya
upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara ya Nachingwea – Liwale
(km 130).
(xii) Barabara ya Bagamoyo – Makurunge – Saadani - Tanga (km 246):
Shilingi bilioni 3.2 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kuendelea na
ujenzi sehemu za TAMCO – Vikawe – Mapinga (km 24), Kisarawe –
Maneromango (km 54); kuanza ujenzi sehemu ya Tanga – Pangani (km 50);
kuendelea na maandalizi ya upanuzi wa sehemu ya Tegeta – Bagamoyo (km
46.9), Mbegani – Bagamoyo (km 7.2) na kuanza maandalizi ya ujenzi wa
barabara ya Makofia – Mlandizi (km 36.7).
(b) Barabara Zinazounganisha Tanzania na Nchi Jirani
(i) Barabara ya Sumbawanga – Matai - Kasanga Port (km 112): Shughuli
zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi sehemu iliyobaki kati ya Matai –
Kasanga Port (km 32) na kuanza ujenzi wa barabara ya Matai – Kasesya (km
50) ambapo shilingi bilioni 8.1 fedha za ndani zimetengwa.
(ii) Barabara ya Marangu - Tarakea - Rongai - Kamwanga /Bomang’ombe -
Sanya Juu (km 330.31): Shilingi bilioni 3.5 fedha za ndani na shilingi bilioni
29.7 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya: kuendelea na ujenzi wa barabara
za Kwasadala – Masama – Machame Junction (km 16), Kiboroloni – Kikarara
– Tsuduni - Kidia (km 10.8), Kijenge – Usa River (Nelson Mandela AIST: km
14); kuanza mandalizi ya ujenzi wa barabara ya Mianzini – Ngaramtoni (km
18), upanuzi wa barabara ya Arusha – Moshi – Himo – Holili (sehemu ya
Tengeru – Moshi – Himo (km 105) na ujenzi wa mizani ya Himo.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 111
(iii) Barabara ya Isaka - Lusahunga (km 533): Shilingi bilioni 4.4 fedha za ndani
na shilingi bilioni 6.3 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya: kuendelea na
ukarabati sehemu ya Ushirombo - Lusahunga (km 110), ujenzi wa kituo cha
Pamoja cha Ukaguzi (One Stop Inspection Station - OSIS) cha Nyakanazi;
kuanza ukarabati wa barabara ya Lusahunga – Rusumo (km 92); na
kuendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya
Nyakahura – Kumubuga – Murusagamba/ Rulenge – Murugarama na
barabara ya Rulenge – Kabanga nickel (km 141).
(iv) Barabara ya Sumbawanga - Mpanda – Nyakanazi (km 517.4): Shilingi
bilioni 8 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kuendelea na ujenzi wa
barabara ya Mpanda - Mishamo (km 100) sehemu ya Mpanda – Ifukutwa –
Vikonge (km 35); kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu za
Kibaoni – Sitalike (km 71), Kizi – Lyambalyamfipa - Sitalike (km 86.31);
kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Vikonge – Magunga – Uvinza
(km 159); na kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa sehemu ya
Namanyere – Katongoro - New Kipili Port (km 64.8).
(v) Barabara ya Nyanguge – Musoma, na Michepuo ya Usagara – Kisesa na
Bulamba – Kisorya (km 495.9): Shilingi bilioni 6.4 fedha za ndani
zimetengwa kwa ajili ya: kufunga taa za barabarani katika mradi wa upanuzi
wa barabara ya kwenda uwanja wa ndege wa Mwanza (km 12); kuendelea na
ujenzi barabara ya Nansio – Kisorya – Bunda - Nyamuswa (sehemu ya
Kisorya – Bulamba km 51); kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami kwa
barabara ya Nyamuswa – Bunda - Bulamba (km 55), Musoma – Makojo –
Busekela (km 92); na kuendelea na maandalizi ya ukarabati wa barabara za
Nyanguge – Simiyu/Mara Boarder (km 100.4) na Makutano – Sirari (km 83).
(vi) Barabara ya Mwigumbi – Maswa - Bariadi – Lamadi (km 171.8): Shughuli
zitakazotekelezwa ni: kuendelea na ujenzi sehemu ya Maswa - Bariadi (km
49.7); kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara za Kolandoto – Mwanhuzi
(km 10), Lalago – Ng‟oboko – Mwanhuzi (km 74) na Isabdula (Magu) –
Bukwimba – Ngudu – Ng‟hungumalwa (km 10) ambapo shilingi bilioni 4.8
fedha za ndani zimetengwa.
(vii) Barabara ya Kidahwe - Kasulu – Kibondo - Nyakanazi (km 413): Shilingi
bilioni 9.2 fedha za ndani na shilingi bilioni 15 fedha za nje zimetengwa kwa
ajili ya: kuendelea na ujenzi sehemu za Kidahwe – Kasulu (km 63) na
Nyakanazi – Kakonko/Kabingo (km 50); kuanza ujenzi sehemu ya Kakonko
(Kabingo) – Kibondo – Kasulu – Manyovu (km 260) na barabara ya Nduta
Junction – Kibondo mjini (km 25.6).
(viii) Kidahwe (Kigoma) – Ilunde – Malagarasi – Kaliua (km 188). Shughuli
zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi sehemu ya Urambo – Kaliua (km
28) na kuanza ujenzi sehemu za Uvinza – Malagarasi (km 51.1) na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 112
Kazilambwa – Chagu (km 36) ambapo shilingi bilioni 3.1 fedha za ndani na
shilingi bilioni 5.5 fedha za nje zimetengwa.
(ix) Barabara ya Usagara - Geita - Buzirayombo – Kyamyorwa (km 230):
Shilingi bilioni 5.2 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza shughuli
zilizopangwa ambazo ni kuanza ujenzi wa barabara za Geita - Bulyanhulu
Juntion (km 58.3), Bulyanhulu Junction - Kahama (km 61.7) na kuanza
maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Nyamirembe Port – Katoke (km 50).
(c) Barabara za Mikoa
Shilingi bilioni 40 zimetengwa kwa ajili ya kujenga km 40.81 za barabara za mikoa
kwa kiwango cha lami, kukarabati km 486.07 kwa kiwango cha changarawe na
kujenga madaraja 12.
(d) Barabara za Kupunguza Msongamano Jijini Dar es Salaam (km 169.66)
Shilingi bilioni 33.1 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya: kuanza ujenzi wa km 4
kwenye barabara ya Kibamba – Kisopwa – Kwembe - Makondeko (km 14.66),
Banana – Kitunda – Kivule – Msongola (km14.7), Mji Mwema – Kimbiji – Pemba
Mnazi (km 30), Goba – Makongo (km 4), na Wazo Hill – Madale (km 9) na kuanza
maandalizi ya upanuzi wa barabara za Mwai Kibaki (km 9) na Kongowe – Mji
Mwema – Kivukoni (km 25.1).
(e) Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka
Shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani na shilingi 27.3 fedha za nje zimetengwa kwa ajili
ya kuanza ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam
kwa awamu ya pili (km 20.3) na kuendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina
wa barabara zilizopangwa awamu ya tatu (km 23.6) na ya nne (km 25.6).
(f) Ujenzi wa Barabara za Juu (Flyover) Jijini Dar es Salaam
Shughuli zitakazotekelzwa ni: kuendelea na ujenzi wa Ubungo Interchange;
kuendelea na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kuanza
ujenzi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara katika maeneo ya Fire,
Morocco, Mwenge, Magomeni Tabata/Mandela, Buguruni, makutano ya barabara
Kinondoni/Ali Hassan Mwinyi na Selander (Ali Hassan Mwinyi/UN Road Junction);
na kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa Mabey Flyovers katika jiji la Dar es
Salaam, Dodoma na Mwanza ambapo Shilingi bilioni 1.7 fedha za ndani na Shilingi
bilioni 20.3 fedha za nje zimetengwa.
(g) Barabara ya Dodoma University na Barabara ya Mzunguko wa Dodoma
Shilingi bilioni 9 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa
barabara za Ihumwa - Chuo Kikuu cha Dodoma (km 12), barabara za Ikulu
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 113
(Chamwino), kuanza ujenzi wa barabara ya mzunguko ya Nala – Veyula – Ihumwa –
Matumbulu – Nala (km 104) na barabara ya Kongwa Junction – Ng‟ambi –
Mpwapwa – Gulwe – Kibakwe (km 98).
(h) Barabara za Vijijini na Mijini
Shilingi bilioni 224.94 fedha za ndani zimetengwa kupitia TARURA kwa ajili ya
kufanya matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilometa 21,525.04,
matengenezo ya makalvati madogo 2,403, madaraja 113, makalvati makubwa 273
na mifereji yenye urefu wa mita 82,627.81. Vile vile, shilingi bilioni 22.44 zimetengwa
kupitia Mfuko wa Barabara kwa ajili ya ujenzi wa kilomita 15.1 za barabara za lami,
ukarabati wa kilomita 185.7 za barabara za changarawe na ujenzi wa madaraja 23.
(i) Ujenzi wa Madaraja
(i) Ujenzi wa Madaraja Makubwa: Shilingi bilioni 12.5 fedha za ndani na shilingi
milioni 890 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya: kuendelea na ujenzi wa
daraja la Ruhuhu (Ruvuma), daraja jipya la Wami (Pwani), daraja la Magara
(Manyara), daraja la Kitengule (Kagera), na barabara unganishi katika daraja
la Sibiti; kuanza ujenzi wa daraja la Kigongo/Busisi (Mwanza), daraja la
Sukuma (Mwanza) na daraja la Msingi (Singida); kuanza maandalizi ya ujenzi
wa daraja la Mkenda (Ruvuma), daraja la Simiyu (Mwanza), na daraja la
Mzinga (Dar es salaam); kuanza maandalizi ya ukarabati wa daraja la Kirumi
(Mara); kufanya usanifu na kuanza ujenzi wa daraja la Godegode (Dodoma);
kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa daraja la Mtera (Dodoma),
daraja la Mkundi (Morogoro), daraja la Malagarasi Chini (Kigoma), daraja la
Ugalla (Katavi), na daraja la Mitomoni (Ruvuma); na ununuzi wa vipuri vya
daraja la dharura (emmergency Steel Bridge Parts).
(ii) Daraja jipya la Selander (Dar es Salaam): Shughuli zitakazotekelezwa ni
kuendelea na ujenzi wa daraja (km 1.03) na barabara unganishi zenye jumla
ya urefu wa km 5.2 ambapo shilingi milioni 310 fedha za ndani na shilingi
bilioni 10.7 fedha za nje zimetengwa.
(iii) Daraja la Nyerere na Barabara Unganishi (km 6.9): Shughuli
zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa barabara unganishi za
Kigamboni (Daraja la Nyerere) – Vijibweni (km 1.5), kuanza ujenzi wa
barabara ya Kibada – Mwasonga – Tundwisongani Jct/ Tundwisongani –
Kimbiji (km 41) na kuendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa
barabara ya Tungi – Kibada (km 3.8) ambapo shilingi bilioni 60.7 fedha za
ndani zimetengwa.
C. Usafiri Majini
(a) Ujenzi wa Maegesho ya Vivuko: Shilingi bilioni 1.6 fedha za ndani
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 114
zimetengwa kwa ajili ya: kuendelea na kazi ya upanuzi wa maegesho ya
Kigamboni; ujenzi wa maegesho ya Bukondo na Zumacheli katika kivuko cha
Chato – Nkome; ujenzi wa maegesho ya Nyamisati; ujenzi wa maegesho ya
kivuko cha Lindi – Kitunda; na ukarabati wa maegesho ya Bugolora – Ukara,
Rugezi – Kisorya, Kilambo - Namoto na Utete - Mkongo.
(b) Ununuzi wa Vivuko Vipya: shughuli zitakazotekelezwa ni kukamilisha malipo
ya ununuzi wa kivuko kipya cha Magogoni – Kigamboni na kivuko kipya cha
Nyamisati – Mafia, kivuko kipya cha Bugolora – Ukara, boti moja (1) ya uokozi
kwa ajili ya usafiri wa majini kati ya Lindi na Kitunda, boti nne (4) kwa ajili ya
kisiwa cha Ukerewe (Ilugwa, Nafuba, na Ghana) na Magogoni – Kigamboni
ambapo shilingi bilioni 5.9 fedha za ndani zimetengwa.
(c) Ukarabati wa Vivuko: shughuli zitakazotekelezwa ni kukarabati vivuko vya
MV Sengerema, MV Kigamboni na MV Misungwi, MV Kome II, MV Ujenzi, MV
KIU, MV Mara, MV Musoma, MV Tegemeo ambapo shilingi bilioni 2.1 fedha
za ndani zimetengwa.
(d) Ununuzi na Ukarabati wa Meli katika Maziwa Makuu: Shilingi bilioni 70.0
zimetengwa kwa ajili ya: kuendelea na ujenzi wa meli mpya yenye uwezo wa
kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo katika ziwa Victoria; Ujenzi wa meli
mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 3,000 za mizigo kila moja katika
Ziwa Victoria; ujenzi wa chelezo; ukarabati wa meli ya MV Victoria, MV
Umoja, MV Serengeti, MT Ukerewe na MV Butiama katika Ziwa Victoria; na
ujenzi wa meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za
mizigo pamoja na ukarabati wa Meli ya MV. Liemba katika Ziwa Tanganyika.
D. Bandari
(a) Maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam: Shughuli za zitakazotekelezwa ni
pamoja na kuendelea na kazi ya kuboresha Gati Na. 2 hadi 7; kuendelea na
ujenzi wa Gati la kupakua na kupakia magari (Ro-Ro); na kuongeza kina na
upana wa lango la kuingilia na kutokea meli pamoja na sehemu ya kugeuzia
meli.
(b) Bandari ya Tanga: Shughuli zitakazotekelezwa ni kuimarisha sakafu ngumu
na kuongeza kina cha gati Na. 1-2.
(c) Bandari ya Mtwara Shughuli za zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa
gati moja (multi purpose terminal) lenye urefu wa mita 300.
(d) Bandari Kavu Ruvu: Shughuli za zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi
wa bandari kavu katika eneo la Ruvu.
(e) Bandari za Maziwa Makuu: kuendelea na ujenzi na ukarabati wa magati
katika Ziwa Victoria (Nkome, Nyamirembe, Magarine, Lushamba na
Mwigobero), Ziwa Tanganyika (Lagosa, Kalya – Sibwesa, Kasanga,
Kagunga, Ujiji, Kabwe, ujenzi wa Bandari ya Karema na chelezo katika
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 115
Bandari ya Kigoma) na Ziwa Nyasa (Kiwira, Ndumbi na Itungi) pamoja na
miundombinu ya usalama.
E. Usafiri wa Anga
(a) Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria katika Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere
Shilingi bilioni 4 fedha za ndani na shilingi bilioni 9.7 fedha za nje zimetengwa
kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo jipya la abiria (Terminal III),
kuuganisha umeme wa gridi ya Taifa kwenye jengo hilo na kufanya usanifu
wa kina kwa ajili ya upanuzi na ukarabati jengo la pili la abiria (Terminal
Building II). Aidha, shilingi bilioni 26.0 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya
uendeshaji na kuweka miundombinu katika jengo la Tatu la Abiria (Terminal
III).
(b) Chuo cha Taifa cha Usafirishaji
Shughuli zitakazotekelezwa ni: ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa
vifaa/nyenzo za kufundishia wahandisi ikijumuisha ujenzi wa karakana ya
ndege ya mafunzo - uwanja wa ndege wa Kilimanjaro; ununuzi wa ndege
mbili (2) za mafunzo; ununuzi wa cabin crew equipment; ununuzi wa
vifaa/nyenzo za kufundishia mafunzo ya anga; na ujenzi wa majengo ya
utawala, madarasa, karakana, nyumba za watumishi na mabweni katika
Uwanja wa Ndege Kilimanjaro.
(c) Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Kilimanjaro: Shughuli zilizopangwa ni
kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na kuanza maandalizi ya
kukarabati barabara za kuruka na kutua ndege, kufunga taa za kuongoza
ndege na kukarabati eneo la kuegesha magari ambapo shilingi milioni 100
fedha za ndani zimetengwa.
(d) Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato: Shughuli
zilizopangwa ni: kufanya mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na
kuanza kulipa fidia kwa mali za wananchi watakaopisha eneo la mradi
ambapo shilingi bilioni 3.1 fedha za ndani na shilingi bilioni 8.5 fedha za nje
zimetengwa.
(e) Kiwanja cha Ndege Mwanza: Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni: ujenzi
wa jengo jipya la abiria, uzio wa kiwanja, mfumo wa maji safi, mfumo wa
kuondoa maji taka na maji ya mvua kiwanjani, maegesho ya magari na
kufunga taa za kuongozea ndege ambapo shilingi bilioni 5.1 fedha za ndani
na shilingi bilioni 3 fedha a nje zimetengwa.
(f) Kiwanja cha Ndege Kigoma: Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni kujenga
jengo la abiria na miundombinu yake ikijumuisha maegesho ya ndege,
maegesho ya magari na barabara za kuingia na kutoka kiwanjani; ufungaji wa
taa na mitambo ya kuongozea ndege; ujenzi wa uzio wa kiwanja, jengo la
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 116
kuongozea ndege, na jengo la uangalizi wa hali ya hewa ambapo shilingi
milioni 120 fedha za ndani na shilingi milioni 570 fedha za nje zimetengwa.
(g) Kiwanja cha Ndege Tabora: Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa
jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege, maegesho ya magari, barabara za
kuingia na kutoka kiwanjani na jengo la uangalizi wa hali ya hewa ambapo
shilingi milioni 902 fedha za ndani na shilingi bilioni 5.2 fedha za nje
zimetengwa.
(h) Kiwanja cha Ndege Mtwara: Shughuli zilizopangwa ni kuendelea na
ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege, viungio, maegesho ya
ndege, kufunga taa za kuongozea ndege, maegesho ya magari na barabara
za kuingia na kutoka kiwanjani ambapo shilingi bilioni 4.5 fedha za ndani
zimetengwa.
(i) Kiwanja cha Ndege Sumbawanga: Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni:
ujenzi wa barabara ya kutua na kuruka ndege, viungio, maegesho ya ndege,
jengo la abiria, jengo la kuongoza ndege, jengo la uangalizi wa hali ya hewa,
maegesho ya magari na barabara za kuingia na kutoka kiwanjani ambapo
shilingi milioni 100 fedha za ndani na shilingi bilioni 7.2 fedha za nje
zimetengwa.
(j) Kiwanja cha Ndege Shinyanga: Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni:
ujenzi wa barabara ya kutua na kuruka ndege, viungio, maegesho ya ndege,
jengo la abiria, jengo la kuongoza ndege, jengo la uangalizi wa hali ya hewa,
maegesho ya magari na barabara za kuingia na kutoka kiwanjani, ufungaji wa
taa na mitambo ya kuongozea ndege pamoja na uzio wa kiwanja ambapo
shilingi milioni 100 fedha za ndani na shilingi bilioni 8.8 fedha za nje
zimetengwa.
(k) Uendelezaji wa Viwanja vya Ndege vya Mikoa: Shilingi bilioni 16.9 fedha za
ndani na shilingi bilioni 19.4 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza
shughuli zilizopangwa ambazo ni ujenzi wa viwanja vya ndege katika mikoa
ya Geita na Simiyu; upanuzi wa viwanja vya ndege vya mikoa ya Iringa,
Ruvuma (Songea), Lindi, Lake Manyara, Tanga na Mara (Musoma);
kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi waliopisha mradi wa kiwanja cha
ndege Dodoma; na kuanza ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Moshi.
(l) Ufungaji wa rada za kuongozea ndege za kiraia: kuendelea na ufungaji wa
rada za kuongozea ndege za kiraia katika viwanja vya KIA, Mwanza na
Songwe na kuziendesha:
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 117
F. Nishati
(a) Miradi ya Kuzalisha Umeme
Miradi ifuatayo imepangwa kutekelezwa:
(i) Kinyerezi I Extension – MW 185 (Dar es Salaam): kukamilisha ufungaji wa
mitambo ambapo Shilingi bilioni 60.0 fedha za ndani zimetengwa;
(ii) Kufua Umeme Rusumo - MW 80 (Kagera): kujenga miundombinu ya
kukinga na kuingiza maji katika handaki; ujenzi wa kituo cha kuzalisha
umeme; ufungaji wa mitambo katika kituo cha kuzalisha umeme; ujenzi wa
kituo cha kupoza umeme; na kukamilisha miradi ya kijamii kwa wananchi
wanaozunguka eneo la mradi ambapo Shilingi bilioni 3 zimetengwa;
(iii) Mtwara Power Project (MW 300): kukamilisha uthamini na kulipa fidia kwa
wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi; kumpata Mtaalam Mshauri wa
kusimamia ujenzi wa mradi; na kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa mradi
ambapo shilingi bilioni 1.0 fedha za ndani na Shilingi bilioni 3.2 fedha za nje
zimetengwa;
(iv) Kakono - MW 87 (Kagera): kutwaa ardhi na kulipa fidia katika eneo la mradi;
na kutafuta Wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa mradi na njia ya kusafirisha
umeme ya msongo wa kV 220 ambapo Shilingi milioni 500 fedha za ndani na
Shilingi bilioni 2 fedha za nje zimetengwa;
(v) Malagarasi – MW 45 (Kigoma): kutwaa ardhi na kulipa fidia kwa wananchi
watakaopisha mradi; kumpata Mtaalam Mshauri na Wakandarasi kwa ajili ya
ujenzi wa mradi na njia ya umeme ya msongo wa kV 132 ambapo Shilingi
milioni 600 fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.4 zimetengwa;
(vi) Mradi wa Ruhudji - MW 358 (Njombe): kumpata Mtaalam Mshauri wa
kusimamia ujenzi wa mradi; na kumpata Mkandarasi wa kujenga mradi
ambapo Shilingi bilioni 10.0 fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.5 fedha za nje
zimetengwa; na
(vii) Umeme wa Jotoardhi – Ngozi (Mbeya): kuendelea na utaratibu wa ununuzi
wa mtambo wa kuchoronga visima vya utafiti ambapo Shilingi milioni 500
fedha za ndani na Shilingi bilioni 7.5 fedha za nje zimetengwa.
(b) Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni:
(i) Mradi wa Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 Makambako –
Songea: kuendelea kuunganisha wateja ikiwemo vijiji vya Lutikila, Ifinga na
Mbangamawe mkoani Ruvuma vilivyoongezeka pamoja na kukamilisha kazi
ya kufunga Reactor na Distribution Panels katika vituo vya kupoza umeme
vya Makambako, Madaba na Songea ambapo Shilingi bilioni 2 fedha za ndani
na Shilingi milioni 500 fedha za nje zimetengwa.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 118
(ii) Mradi wa Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 - North West Grid
Extension (Iringa – Mbeya - Sumbawanga – Mpanda - Kigoma –
Nyakanazi): kukamilisha uthamini na kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha
eneo la mradi; kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi
katika sehemu ya Iringa - Mbeya - Tunduma - Sumbawanga (km 624);
kuhakiki na kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi na kumpata
Mkandarasi wa ujenzi wa mradi katika sehemu ya Nyakanazi - Kigoma (km
280); kufanya tathmini ya mali za wananchi zitakazoathiriwa na mradi; na
kuandaa nyaraka za zabuni za kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia
mradi katika sehemu ya Sumbawanga - Mpanda - Kigoma (km 480) ambapo
shilingi bilioni 11.35 zimetengwa;
(iii) Mradi wa Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 North West Grid
Extension (Geita – Nyakanazi): ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka
Geita hadi Nyakanazi; ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi;
upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Geita kitakachojengwa kupitia
mradi wa Bulyanhulu – Geita; na usambazaji wa umeme katika vijiji 32
ambapo Shilingi Bilioni 1 imetengwa;
(iv) Mradi wa Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 Bulyanhulu – Geita:
kukamilisha ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kV 220; kukamilisha
ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme cha kV 220 Geita; upanuzi wa kituo
cha kupoza umeme cha kV 220 Bulyanhulu; kukamilisha ujenzi wa njia za
kusambaza umeme za msongo wa kV 33 na kV 0.4; na kuunganisha umeme
kwa wateja wapya 1,500 ambapo Shilingi bilioni 1.50 fedha za ndani na
Shilingi bilioni 2.60 fedha za nje zimetengwa;
(v) Mradi wa Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 Rufiji – Chalinze –
Dodoma: kukamilisha upembuzi yakinifu; kufanya uthamini wa mali za
wananchi watakaopisha mradi na kulipa fidia; kumpata Mtaalam Mshauri wa
kusimamia mradi; na kumpata Mkandarasi wa kujenga njia ya kusafirisha
umeme ambapo shilingi bilioni 8 fedha za ndani na Shilingi bilioni 3 fedha za
nje zimetengwa;
(vi) Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 kutoka
Chalinze – Segera, kV 400 Segera-Tanga, kV 220 Kibaha-Bagamoyo:
kufanya upembuzi yakinifu; na kuwapata wakandarasi wa ujenzi wa njia za
kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme ambapo Shilingi bilioni 3
zimetengwa;
(vii) Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 kutoka
Singida - Arusha – Namanga: kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha
umeme na vituo vya kupoza umeme ambapo shilingi bilioni 4 zimetengwa;
(viii) Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 400 Kinyerezi –
Chalinze: kukamilisha upembuzi yakinifu; kulipa fidia kwa wananchi
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 119
watakaopisha mradi; na kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha
umeme na kituo cha kupoza umeme ambapo Shilingi bilioni 15 zimetengwa;
(ix) Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini na Makao Makuu ya Wilaya: Shilingi
bilioni 423.10 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.
(c) Miradi ya Kusambaza Gesi Asilia Viwandani: ujenzi wa miundombinu ya
kuunganisha viwanda vya Shreeji Silicates Tanzania Limited, LN Future na Kings
Aluminium; na kujenga trunk-line kutoka Mwenge hadi Tegeta na kuunganisha
wateja mbalimbali wakiwemo Estim Construction, Chem &Cortex, Polypet, Interchik,
Giraffe Hotel, Jangwani Sea Breeze, Ramada Resort Hotel, Landmark Hotel,
Seascape Hotel na White Sands Hotel ambapo Shilingi bilioni 11.22 zimetengwa.
(d) Utafiti katika Vitalu vya Songo Songo Magharibi, 4/1B na Mnazi Bay
Kaskazini: kumpata Mshauri Mwelekezi wa kukusanya, kuchakata na kutathmini
taarifa za mitetemo ya 3D zenye ukubwa wa kilomita za mraba 693.1 kwa kitalu cha
4/1B na Mnazi Bay Kaskazini kwa maeneo ambayo hayajafanyiwa utafiti; kumpata
Mshauri Mwelekezi kwa ajili ya kutathmini athari za mazingira kwa kitalu cha 4/1B na
Mnazi Bay Kaskazini; na kufanya tafiti za kijiolojia na kijiofizikia, kumpata mbia wa
kimkakati wa kutekeleza mradi na kufanya maandalizi ya awali ya uchorongaji wa
kisima cha utafiti kwa upande wa Kitalu cha Songo Songo Magharibi ambapo
Shilingi milioni 905 zimetengwa.
4.3.4.2. Ardhi na Maeneo ya Uwekezaji na Biashara
(a) Progamu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi: shughuli
zitakazotekelezwa ni: Kuimarisha Mfuko wa Fidia; kuendelea kutekeleza Programu
ya Taifa ya Kurasimisha Makazi katika kanda zote na kuwapatia wananchi hatimilki
za makazi; kuhuisha Ramani za Msingi zenye uwiano wa 1:50,000 katika Jiji la
Dodoma; kupima na kuidhinisha viwanja 200,000; kutoa Hati za Kumiliki Ardhi
200,000 na Hatimiliki za Kimila 150,000; na kushirikiana na Tume ya Taifa ya
Matumizi ya Ardhi na Mamlaka za Upangaji kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi
kwenye “corridors” za Reli ya Dar-es-Salaam –Isaka na Bomba la Mafuta kuanzia
Mtukula hadi Chongoleani Tanga ifikapo Juni, 2020. Aidha, Shilingi bilioni 8.0 fedha
za ndani zimetengwa.
(b) Programu ya Umilikishaji wa Ardhi: shughuli zitakazotekelezwa ni:
kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ambapo vijiji 50 katika wilaya za Kilombero,
Ulanga na Malinyi (Morogoro); kupima vipande vya ardhi 150,000; kuhakiki na
kuandaa hati miliki za kimila 60,000 katika wilaya hizo; kuendelea na upimaji wa
viwanja 15,000 na kuwapatia wananchi hati miliki za kimila; kukamilisha ujenzi wa
ofisi za ardhi za Wilaya 3 za Ulanga, Malinyi na Kilombe; na kuandaa mipango
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 120
kabambe ya Ifakara, Mahenge na malinyi. Aidha, wizara inaandaa programu ya
utekelezaji katika maeneo mengine nchini ambapo shilingi bilioni 2 fedha za ndani
na shilingi bilioni 4.02 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli
hizi.
(c) Mradi wa Kuimarisha Mipaka ya Kimataifa: Shughuli zitakazotekelezwa ni:
Kuimarisha mipaka minne (4) ya kimataifa (Tanzania-Kenya; Tanzania-Zambia;
Tanzania – Burundi; Tanzania-DRC/Burundi/Zambia); Kuandaa kanzidata ya taarifa
ya mipaka ya kimataifa; Kukusanya na kutunza taarifa za upimaji majini Kupima
mipaka ya nchi katika maziwa na Ufuatiliaji wa utekelezaji wa mradi ambapo shilingi
bilioni 5.4 imetengwa kwa ajili hya kutekeleza shughuli hizo.
4.3.4.3. Huduma za Fedha
(a) Benki ya Maendeleo TIB
Shughuli zilizopangwa kutekelezwa ni: kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni
144.5 katika sekta za viwanda, maji, nishati, utalii, kilimo na miundombinu ya Serikali
za mitaa; kukuza mizania ya Benki kufikia kiasi cha Shilingi bilioni 872.9; kupunguza
kiwango cha mikopo chechefu kutoka asilimia 32 ya mwaka 2018 hadi asilimia 22.5
kwa mwaka 2019; na kuongeza faida kutoka Shilingi bilioni 8 mwaka 2018 hadi
Shilingi bilioni 9 mwaka 2019.
(b) Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Shughuli zitakazotekelezwa ni: kutoa mikopo kwa ajili ya miradi ya uchakataji
mazao, kilimo cha umwagiliaji, ujenzi wa maghala ya kisasa, miradi ya kilimo kwa
kutumia zana bora za kilimo (mechanized agriculture); kuanzisha vituo vya huduma
za zana za kilimo; na kutoa dhamana za mikopo ili kuchagiza mabenki na taasisi za
fedha kuongeza ukopeshaji kwa miradi ya kilimo kupitia Mfuko wa Dhamana kwa
Wakulima Wadogo (Smallholder Farmers Credit Guarantee Scheme - SCGS).
Aidha, Benki itaendelea kuwajengea uwezo wakulima wadogo kupitia mafunzo ya
mbinu bora za kilimo, usimamizi wa fedha, uendeshaji bora wa vikundi na vyama,
utunzaji wa kumbukumbu na utengenezaji wa miradi inayokidhi masharti ya mikopo
kutoka katika mabenki na taasisi za fedha.
4.3.4.4. Utalii, Biashara na Masoko
(a) Utalii
Shughuli zitakazotekelezwa ni: kutoa elimu katika kanda nne za utalii kuhusu kanuni,
sheria na miongozo ya uendelezaji biashara ya utalii; kuendelea kutangaza vivutio
vya malikale vya Caravan-Serai Bagamoyo, Kaburi (Mausoleum) la Mkwawa
Kalenga, Eneo la zana za kale za mawe Isimila, Tembe la Dr. Livingstone Ujiji na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 121
nyumba ya Mwl. Nyerere Magomeni; kuendelea kuboresha miundombinu wezeshi
ya utalii kwa kujenga barabara katika eneo la Ndutu na barabara za kushuka Kreta
kuu; ukarabati wa miundombinu ya vivutio sita vya malikale ambayo ni Michoro ya
Kolo (Kondoa), Magofu ya Kaole na Mji wa Zamani wa Bagamoyo, Tembe la
Livingstone (Tabora), Jengo la Zamani la Afya (Tabora) na Magofu ya Tongoni
(Tanga); kuendelea kuboresha huduma za utalii katika mapori ya akiba kwa kujenga
hosteli za kisasa sita katika mapori ya akiba ya Swagaswaga (1) na Selous (5) na
kambi 12 za kulala wageni katika mapori ya akiba Mpanga - Kipengere (1),
Swagaswaga (4), eneo la Matambwe, Selous (4), na Kijereshi (3).
Shughuli zitakazotekelezwa kupitia mradi wa Uendelezaji wa Utalii katika Ukanda wa
Kusini – REGROW ni kuanza maandalizi ya awali ya ujenzi wa babarara, viwanja
vya ndege, mabanda kwa ajili ya kupokea wageni katika hifadhi zilizo kusini mwa
Tanzania.
(b) Biashara na Masoko
(i) Mradi wa Kukuza Shughuli za Kibiashara katika Jumuiya ya Maendeleo
ya Nchi za Kusini mwa Afrika – SADC: Shughuli zitakazotekelezwa ni:
utekelezaji wa Sera ya Viwanda na Mpango Mkakati; uendelezaji wa
mnyororo wa thamani kwa zao la alizeti; uwezeshaji biashara na utafiti katika
biashara ya huduma.
(ii) Mradi wa EU – EAC wa kuboresha upatikanaji wa masoko: Shughuli
zitakazotekelezwa ni: kuboresha uzalishaji wa mazao ya chai, kahawa,
viungo, embe, parachichi pamoja na kuwawezesha wakulima na wafanya
biashara kuyafikia masoko ya Jumuiya ya Ulaya.
(iii) Kuboresha Mazingira ya Biashara: Shughuli zitakazotekelezwa ni:
kuendelea kushirikiana na kuhamasisha jumuiya ya wafanyabiashara juu ya
fursa za masoko ya upendeleo ambayo Tanzania inanufaika; kufanya
majadiliano ya kibiashara kati ya Tanzania na nchi nyingine, Kikanda na
Kimataifa kwa lengo la kupanua fursa za masoko na uwekezaji; kukamilisha
mapitio ya Sheria ya Anti-dumping and Countervailing Measures; na
kutekeleza Mkataba wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) kuhusu
uwezeshaji wa Biashara.
4.3.5. Kuimarisha Usimamizi na Utekelezaji wa Mpango
Utawala bora
(a) Azma ya Serikali Kuhamia Dodoma
Shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa mji wa Serikali na Jiji la
Dodoma kwa kuimarisha miundombinu ya masoko, huduma za jamii, barabara,
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 122
mfumo wa maji safi na maji taka.
(b) Utoaji Haki na Huduma za Kisheria
(i) Mradi wa E-Justice: Shughuli zitakazotekelezwa ni: kuziunganisha taasisi za
haki jinai katika mfumo mmoja wa kielektroniki ambapo Shilingi bilioni 1.0
fedha za ndani zimetengwa.
(ii) Mradi wa Kuimarisha Upatikanaji wa Haki za Kibinadamu: Shughuli
zitakazotekelezwa ni: kuimarisha mfumo wa upatikanaji haki za kisheria na
ulinzi wa haki za binadamu kwa wanawake na watu walio kwenye makundi
maalum ambapo shilingi milioni 802.4 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya
shughuli hizo.
(iii) Mradi wa Kuboresha Uwajibikaji: Shughuli zitakazotekelezwa ni: kusajili na
kutoa mafunzo kwa Watoa Msaada wa Kisheria (Paralegals); kuendesha wiki
ya Msaada wa Kisheria ambayo huadhimishwa nchini kote ambapo ushauri
wa kisheria kwa mtu mmoja mmoja utatolewa, elimu kupitia vijarida,
vipeperushi, na machapisho; kutoa huduma ya kisheria kwa wafungwa na
mahabusu katika magereza nchini; na kutoa msaada wa kisheria kwa
wanawake katika masuala mbalimbali hususan masuala ya umiliki wa ardhi.
(iv) Vitambulisho vya Taifa: Shughuli zitakazotekelezwa ni: usajili na utambuzi
wa wananchi, wageni wakazi na wakimbizi waliofikia umri wa miaka 18;
kuendelea na utoaji wa vitambulisho vya Taifa katika mikoa yote nchini;
kukamilisha mfumo wa mawasiliano katika wilaya 34 na makao makuu ya
wilaya; kuunganisha mfumo wa vitambulisho vya Taifa pamoja na mifumo ya
taasisi nyingine (40); kukamilisha sheria ya usajili na utambuzi wa watu;
kununua vifaa vya usajili na vitendea kazi kwa kila wilaya; na ujenzi wa ofisi
za makao makuu – Dodoma na ofisi za usajili katika wilaya 42 ambapo
Shilingi bilioni 10 zimetengwa kwa ajili ya shughuli hizo.
(c) Mfuko wa Mahakama
Jumla ya Shilingi bilioni 15.0 fedha za ndani na shilingi bilioni 7.2 fedha za nje
zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza shughuli za:
(i) Kuanza ujenzi wa majengo ya Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini
Dodoma;
(ii) Kuendelea na ujenzi wa mahakama nchini kote zikiwemo Mahakama Kuu
mbili (2) zinazoendelea kujengwa mkoani Kigoma na Mara na kuanza kujenga
nyingine katika mikoa ya Morogoro, Mwanza, Dodoma na Singida. Pia
Mahakama kujenga Mahakama za Wilaya 32 na Mahakama za Mwanzo 20
(iii) Kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za kisheria kwa
kufunga mfumo wa kielektroniki wa utunzaji wa kumbukumbu, usikilizaji wa
mashauri, ukusanyaji wa takwimu za mashauri na kutoa taarifa mbalimbali za
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 123
kimahakama;
(iv) Kujenga mfumo wa kieletroniki wa utoaji haki (e-justice) ili kuharakisha
usikilizaji wa mashauri na hivyo kupunguza msongamano wa mahabusu
magerezani; na
(v) Usimamizi wa kamati za maadili ya mawakili wa kujitegemea, udhibiti na
kuwaondoa kwenye orodha mawakili wanaokiuka maadili pamoja na
kujihusisha na vitendo vya kushawishi na kutoa rushwa.
(d) Mfuko wa Bunge
(i) Ukarabati wa Majengo ya Bunge: Shilingi bilioni 2.65 fedha za ndani
zimetengwa kwa ajili ya: kuanzisha Bunge mtandao na kituo cha kurusha
matangazo ya redio na televisheni ya Bunge; ukarabati wa majengo ya
Bunge; na ukarabati wa ukumbi wa Bunge.
(ii) Ujenzi wa Miundombinu ya Bunge: shughuli zitazotekelezwa ni ujenzi wa
nyumba za makazi ya viongozi wa Bunge (Katibu wa Bunge na Naibu Spika)
na Ununuzi na ufungaji wa mitambo ya usalama ambapo shilingi bilioni 2.35
fedha za ndani zimetengwa.
(iii) Mradi wa Maboresho ya Usimamizi wa Fedha Za Umma: Shilingi milioni
650 fedha za nje zimetengwa kwa ajili ya kujengea uwezo Idara ya Bajeti.
(iv) Mradi wa kulijengea uwezo Bunge: Kazi zilizopangwa ni Mafunzo ya
kuwajengea uwezo Wabunge na Watumishi ambapo shilingi billioni 1.96
fedha za nje zimetengwa.
(e) Usajili wa Vizazi na Vifo
Katika kusajili matukio muhimu ya binadamu, hususan vizazi na vifo Serikali
inaendelea kutekeleza mradi wa Usajili wa Watoto chini ya Miaka mitano.
4.3.6. Maeneo Mengine Muhimu kwa Ukuaji wa Uchumi na Ustawi wa Taifa
4.3.6.1. Diplomasia ya Kiuchumi
Shughuli zitakazotekelezwa ni: Kuendelea kusimamia na kuratibu Sera ya Mambo
ya Nje kwa kuweka msisitizo kwenye Diplomasia ya Uchumi kuelekea Tanzania ya
viwanda; Uboreshaji wa miundombinu ya Chuo cha Diplomasia ili kuendelea
kukifanya kuwa kitovu/kituo cha ufundishaji na utafiti wa Diplomasia ya uchumi
kitaifa na kikanda; kuvutia fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo ya
biashara pamoja na kutangaza vivutio vya utalii; Kufungua ubalozi mpya mmoja na
Konseli Kuu katika maeneo ya kimkakati ambayo yataiwezesha nchi yetu
kunufuaika na fursa za kiuchumi na biashara; na Kuendelea na ujenzi na ukarabati
wa majengo ya ofisi na nyumba za makazi ya watumishi katika balozi 15 ambazo ni
Ubalozi wa Tanzania Moroni, Comoro; Ubalozi wa Tanzania Washington D.C,
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 124
Marekani; Ubalozi wa Tanzania London, Uingereza; Ubalozi wa Tanzania Geneva,
Uswisi; Ubalozi wa Tanzania Lusaka, Zambia; Ubalozi wa Tanzania Pretoria, Afrika
Kusini; Ubalozi wa Tanzania Harare, Zimbwabe; Ubalozi wa Tanzania
Kigali,Rwanda; Ubalozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia; Ubalozi wa Tanzania
Beijing, China; Ubalozi wa Tanzania Berlin, Ujerumani; Ubalozi wa Tanzania Rome,
Italia; Ubalozi wa Tanzania New York, Marekani; Ubalozi wa Tanzania Lilongwe,
Malawi; na Ubalozi wa Tanzania Ottawa, Canada. Hatua hii itaipunguzia Serikali
gharama za kulipa pango za ofisi za balozi na na makazi ya watumishi. Katika
kutekeleza majukumu hayo jumla ya shilingi bilioni 4 zimetengwa.
4.3.6.2. Kuimarisha Ushiriki wa Sekta Binafsi
(a) Miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi - PPP
Miradi itakayotekelezwa ni:
(i) Mradi wa uzalishaji wa Dawa Muhimu na Vifaa Tiba katika mikoa ya
Pwani, Mwanza na Mbeya: kuwapata wabia wa ujenzi wa viwanda vitatu vya
uzalishaji wa dawa muhimu na vifaa tiba na kuanza ujenzi;
(ii) Mradi wa ujenzi wa vyuo kumi (10) vya Ufundi: kukamilisha mapitio ya
upembuzi yakinifu na kufanya upekuzi (due diligence) kwa mwekezaji
aliyewasilisha andiko;
(iii) Mradi wa Kusambaza Gesi Asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi
na Mtwara: kumpata Mtaalam Elekezi wa kufanya upembuzi yakinifu na
kuutangaza mradi kwa ajili ya kumpata Mbia;
(iv) Kujenga Hosteli za wanafunzi katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)
kampasi za Dar es Salaam na Dodoma: Kuendelea kuandaa taarifa ya
upembuzi yakinifu;
(v) Ujenzi wa Reli ya Mtwara – Mbamba Bay na matawi ya Mchuchuma na
Liganga kwa standard gauge: kuendelea na upembuzi yakinifu na
kutangaza zabuni ya kumpata Mbia;
(vi) Ujenzi wa Reli ya Tanga (Mwambani) - Arusha – Musoma) pamoja na
matawi ya Engaruka na Minjingu kwa standard gauge: kukamilisha
upembuzi yakinifu na kutangaza zabuni ya kumpata Mbia;
(vii) Ujenzi wa jengo la biashara commercial complex na hoteli ya nyota nne
katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA):
kukamilisha upembuzi yakinifu na kutafuta mbia;
(viii) Mradi wa Uendeshaji wa Huduma ya Usafiri jijini Dar es Salaam Awamu
ya Kwanza: Awamu ya I: kutafuta mbia wa kutoa huduma Service Providers
kuendesha huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka. Awamu ya II: kuendelea
na taratibu za kumpata "Transaction Advisor" wa kusaidia kuandaa Upembuzi
Yakinifu (Feasibility Study) na kusaidia kuwapata watoa huduma wa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 125
kuendesha Huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka. Awamu ya III na IV:
kuendelea na taratibu za kumpata "Transaction Advisor" wa kusaidia
kuaandaa Upembuzi Yakinifu Feasibility Study na kusaidia kupata watoa
huduma wa kuendesha Huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka; na
(ix) Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Saratani cha Taasisi ya Ocean Road
(Mloganzila): Kukamilisha upembuzi yakinifu.
(b) Mchango wa Serikali katika Kuimarisha Ushiriki wa Sekta Binafsi
Shughuli zitakazotekelezwa ni: kukamilisha Sera na Mkakati wa Maendeleo ya Sekta
Binafsi ya mwaka 2019; na kuboresha sera za masuala ya uchumi katika usimamizi
wa fedha, riba na kodi; kuendelea na utekelezaji wa Mwongozo wa Kuboresha
Mfumo wa Udhibiti wa Biashara; kuandaa kanuni na miongozo ya Sheria ya Ubia
kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi; na kuendelea kuwezesha upatikanaji wa
maeneo ya uwezeshaji yenye miundombinu ili kuvutia wawekezaji zaidi.
4.3.6.3. Mchango wa Mashirika na Taasisi za Umma
(a) Ujenzi wa Hospitali Rufaa ya Kanda ya Mtwara. Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya - NHIF kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto itaendeleza ujenzi wa hospitali ya rufaa ya kanda ya Kusini
Mtwara. Mradi huu kwa awamu ya kwanza unatarajiwa kugharimu Shilingi
billioni 30.
(b) Ufufuaji wa Kiwanda cha Chai cha Mponde - Lushoto (Tanga). Mfuko wa
PSSSF umefikia makubaliano na wanahisa wa Kiwanda cha Mponde juu ya
utayari wa kuingia ubia wa kufufua kiwanda. Gharama za mradi husika
zinatarajia kufikia Shilingi bilioni 10 na jumla ya wafanyakazi kati ya 30 na 40
wanatarajiwa kuajiriwa. Mradi utawanufaisha wakulima kati ya 250 mpaka 300
ambao watapata soko la majani ya Chai.
(c) Mpango wa NSSF kutoa Mikopo kwa Makampuni. Shirika linatarajia kutenga
Shilingi bilioni 20 kwa ajili ya kutoa mikopo yenye tija kwa taasisi mbalimbali na
mashirika ili kuwezesha kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa. Mikopo
hiyo inatarajia kutolewa hususan kwa kuendeleza viwanda ili kuungana na
juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kufikia uchumi wa kati.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 126
SURA YA TANO
UGHARAMIAJI WA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA 2019/20
5.1. Utangulizi
Sura hii inaeleza kwa kifupi ugharamiaji wa Mpango kwa kuzingatia vyanzo
mbalimbali vya mapato. Vyanzo hivyo ni mapato ya ndani, mikopo na misaada, ubia
kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, uwekezaji wa mashirika ya umma na vyanzo
bunifu vya kuongeza mapato ya Serikali. Ugharamiaji wa Mpango umezingatia
makadirio ya awali ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2019/20, Mkakati
wa Ugharamiaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano na Mwongozo
wa Ushirikiano wa Maendeleo - DCF.
5.2. Gharama za Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Mwaka 2019/20, makadirio ya fedha za maendeleo ni Shilingi bilioni 12,248.6 sawa
na asilimia 37 ya bajeti yote ikilinganishwa na Shilingi bilioni 12,007.3 zilizotengwa
mwaka 2018/19. Kati ya kiasi hicho, Shilingi bilioni 9,737.7 sawa na asilimia 79.5 ya
fedha za maendeleo ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2,510.9 sawa na asilimia
20.5 ya fedha za maendeleo ni fedha za nje. Kiasi hiki kinakidhi kiwango
kilichobainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano cha
kutenga fedha za maendeleo kati ya asilimia 30 hadi 40 ya bajeti yote.
Katika kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo, hatua mbalimbali zitachukuliwa na
Serikali ikijumuisha: kuendelea kuimarisha makusanyo ya mapato ya ndani hususan
kwa kuendelea kurasimisha sekta isiyo rasmi ikiwemo kugawa vitambulisho kwa
wajasiliamali wadogo na kutoa elimu kwa walipakodi; Kuhamasisha ulipaji wa kodi
kwa hiari kupitia vipindi mbalimbali vya elimu kwa umma; Kutekeleza mwongozo wa
ushirikiano baina ya Serikali na Washirika wa Maendeleo (Development Cooperation
Framework – DCF); Kuendelea kusisitiza nidhamu ya matumizi katika utekelezaji wa
bajeti kwa kuzingatia Sheria ya Bajeti Na. 11 ya Mwaka 2015; Kuanza kutumika kwa
Mfumo wa Kielekroniki wa Stampu za kodi (Electronic Tax Stamp - ETS); na
Kutekeleza Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Mapato ya Ndani (IDRAS); na
kuendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini (Blueprint
for Regulatory Reforms to Improve Business Environment for Tanzania).
5.3. Vyanzo vya Mapato kwa Mwaka 2019/20
Serikali inatarajia mapato ya ndani na nje ili kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa
mwaka 2019/20. Ili kuhakikisha mapato tarajiwa yanapatikana, Serikali itaendelea
kutekeleza Mkakati wa Ugharamiaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka
Mitano; kuboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji ili kuvutia uwekezaji
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 127
wa moja kwa moja kutoka ndani na nje ya nchi na uwekezaji kwenye miradi ya ubia
kati ya sekta ya umma na sekta binafsi. Aidha, Serikali itaimarisha ukusanyaji wa
mapato ya ndani; na kuanza mapema na kuongeza ufanisi katika majadiliano na
Washirika wa Mendeleo ili kuwezesha kupatikana kwa misaada na mikopo hiyo kwa
wakati.
5.3.1 Vyanzo vya Mapato ya Ndani
Serikali itaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuongeza ukusanyaji wa
mapato ya ndani yanayojumuisha mapato ya kodi, yasiyo ya kodi na mikopo ya
ndani. Mikakati hii ni pamoja na kutekeleza Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa
Mapato ya Ndani - IDRAS ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa makusanyo ya
kodi za ndani; kupanua wigo wa kodi kupitia utambuzi na usajili wa walipakodi
wapya na kuendelea na urasimishaji wa sekta isiyo rasmi; kuendelea kusisitiza
matumizi sahihi ya Mashine za Risiti za Kielektroniki - EFDs; kuimarisha Mfumo wa
Serikali wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato - GePG ili kuongeza ufanisi
katika ukusanyaji wa mapato; na kuimarisha mifumo ya usimamizi na ufuatiliaji
katika taasisi za Serikali ili kuhakikisha yanatekeleza majukumu yake kwa tija na
kutoa michango stahiki ya Mashirika kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Aidha, Serikali
itaendelea kufanya majadiliano na wawekezaji wa dhamana na hatifungani za
Serikali na kutekeleza mikakati ya kuwezesha Mifuko ya jamii kuwekeza katika soko
la ndani la fedha pamoja na kuendelea na uhamasishaji taasisi, wananchi na wadau
wengine kuwekeza katika soko la ndani la fedha.
5.3.2 Vyanzo vya Mapato ya Nje
Katika kuhakikisha mapato kutoka vyanzo vya nje yanapatikana, Serikali itaendelea
kuimarisha Ushirikiano na Washirika wa Maendeleo kwa kutekeleza mpango kazi wa
DCF; na kutumia fursa ya mikopo yenye masharti nafuu na ya kibiashara kwa
kuzingatia wigo wa uhimilivu wa deni la Taifa.
5.3.3 Uwekezaji wa Moja kwa Moja kutoka Nje ya Nchi ( FDI)
Uwekezaji huu unafanywa na Kampuni au taasisi za kimataifa katika sekta
mbalimbali za uchumi nchini zikiwemo zilizopewa msukumo katika Mpango wa
Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 - 2020/21. Sekta hizo ni pamoja na
viwanda, kilimo, maliasili, gesi, mafuta, madini, mawasiliano, ujenzi na utalii. Serikali
itaendelea kuweka mazingira bora na wezeshi ili kuongeza uwekezaji huo kulingana
na fursa zilizopo. Aidha, Serikali kupitia Kituo cha Taifa cha Uwekezaji - TIC
itaendelea kutangaza fursa za uwekezaji na kuandaa miongozo kwa ajili ya vivutio
vya wawekezaji katika miradi ya maendeleo ili kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja
pamoja na kupitia taratibu na Sheria za uwekezaji ili kuziboresha.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 128
5.3.4 Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi
Serikali itaendelea kutoa elimu kwa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa na mashirika na taasisi za umma kuhusiana na mbinu za uibuaji,
maandalizi na utekelezaji wa miradi ya PPP. Aidha, Serikali itaendelea kuimarisha
na kuuwezesha Mfuko wa Uwezeshaji wa miradi ya ubia (Facilitation Fund) ili
kugharamia pembuzi yakinifu kwa miradi ya PPP iliyoibuliwa katika taasisi au Wizara
ambazo zimeshindwa kulipa gharama za Wataalam Elekezi (Transaction Advisors).
5.3.5 Vyanzo Bunifu
(a) Mifuko ya Kimataifa ya Mabadiliko ya Tabia Nchi na Mazingira
Kwa upande wa fedha za mifuko mbalimbali ya kimataifa inayohusika na mabadiliko
ya tabianchi, mwaka 2019/20 Serikali inategemea kupata takribani Shilingi bilioni
15.99 fedha za nje ili kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo. Ili kuwezesha
upatikanaji wa fedha hizi Serikali itaendelea kuchukua hatua za kuandaa miradi
pamoja na kuendelea na mazungumzo na wafadhili ili kuwezesha upatikanaji wa
fedha kutoka mifuko mbalimbali inayohusiana na hifadhi na usimamizi wa mazingira
na mabadiliko ya tabianchi kama vile Least Developed Countries Fund (LDCF);
Global Environmental Facility (GEF); Adaptation Fund (AF); United National
Environmental Programme (UNEP) na Bank ya Maendeleo ya Afrika(AfDB). Vyanzo
hivi vitawezesha kuimarisha utekelezaji wa miradi ya mazingira. Aidha, Serikali
imewasilisha miradi kwa ajili ya kupata ufadhili kwenye mfuko wa Global
Environmental Facility (GEF) kwa kipindi cha miaka 5 (2019 – 2023) ambapo
Tanzania inatazamia kupata jumla ya dola za kimarekani milioni 24 kwenye
programu hiyo.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 129
SURA YA SITA
UFUATILIAJI, TATHMINI NA UTOAJI WA TAARIFA
6.1. Utangulizi
Sura hii inaeleza Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini; Mkakati wa Ufuatiliaji na Tathmini
ya Mpango 2019/20, ambao utatumika kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo
katika ngazi zote; Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa
Miaka Mitano na Mgawanyo wa Majukumu katika Ufuatiliaji na Tathmini ya Mpango.
6.2. Malengo ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Mpango
Katika kuhakikisha kuwa Mfumo wa ufuatiliaji na tathmini unatoa matokeo tarajiwa
kwa Mwaka 2019/20, Serikali itajikita katika:
(a) Kukamilisha mapitio ya muda wa kati (mid term review) ya utekelezaji wa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21;
(b) Kufuatilia miradi ya kimkakati ili kujiridhisha na malengo yaliyopangwa na
kuhakikisha kuwa utekelezaji umezingatia thamani ya matumizi ya fedha;
(c) Kuratibu na kuwezesha Wizara, Idara Zinazojitegemea, Taasisi na Wakala za
Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekta Binafsi na
wadau wengine kufuatilia mara kwa mara hatua iliyofikiwa katika utekelezaji
wa miradi ya kipaumbele ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa;
(d) Kuendelea kutoa tahadhari kwa changamoto zinazoweza kujitokeza na
kukwamisha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mkakati wa
Ufuatiliaji na Tathmini; na
(e) Kuendelea kutoa fursa ya kujifunza kwa wadau zikiwemo Wizara, Idara
Zinazojitegemea, Taasisi na Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa,
Mamlaka za Serikali za Mitaa na wadau wengine wa ufuatiliaji na tathmini
katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa.
6.3. Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Mpango
Katika mwaka 2019/20, Serikali itaendelea kutekeleza Mfumo wa Ufuatiliaji na
Tathmini kama ulivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka
Mitano ili kufuatilia mwenendo na kupima mafanikio au matokeo yaliyofikiwa katika
kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Aidha, Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini
utabaini mapungufu yatakayojitokeza katika utekelezaji ili kuyatafutia ufumbuzi.
Katika kuhakikisha kuwa malengo yaliyokusudiwa ya utekelezaji wa miradi ya
maendeleo yanafikiwa, mfumo huu utaainisha vipengele muhimu vya ufuatiliaji na
tathmini katika maeneo ya matumizi ya mfumo wa takwimu, udhibiti, ukaguzi,
mapitio, utafiti, pamoja na usimamizi. Aidha, mfumo huu utaendelea kutoa fursa ya
mafunzo ya uchambuzi na utoaji taarifa kwa wataalamu ili kuwezesha watoa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 130
maamuzi kupata taarifa zenye kuleta ufanisi katika utekelezaji wa Mpango. Vile vile,
mfumo utaendelea kutoa kipaumbele kwenye mgawanyo wa majukumu katika
ufuatiliaji, uratibu, tathmini na utoaji wa taarifa za utekelezaji pamoja na upatikanaji
wa taarifa za uhakika zitakazotumika kupima mafanikio kwa kutumia viashiria vya
kitakwimu na visivyo vya kitakwimu.
6.4. Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano,
2016/17 – 2020/21
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano unafanyiwa tathmini katika
awamu nne ambazo ni: Tathmini ya ndani ya mwaka, Mapitio ya Muda wa kati wa
utekelezaji, Tathmini ya mwisho wa Utekelezaji pamoja na Uchunguzi na Uchambuzi
wa kina wa Taarifa. Tathmini hizo zitabainisha mafanikio na changamoto halisi za
utekelezaji wa miradi pamoja na kutoa mapendekezo ya mabadiliko yanayohitajika ili
kuhakikisha malengo ya Mpango yanafikiwa kama yalivyopangwa. Aidha, Serikali
itaendelea na taratibu za kufanya tathmini ya Mpango kwa muda wa kati kupitia
Mtathmini Huru, zoezi linalotarajiwa kufanyika mwaka 2019.
6.5. Mkakati wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Mpango wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kuratibu ufuatiliaji na tathmini ya Mpango
kwa kushirikiana na Wizara, Idara Zinazojitegemea, Taasisi na Wakala za Serikali
zinazotekeleza miradi ya maendeleo. Katika kufanikisha utekelezaji wa
mapendekezo yatakayotolewa katika ufuatiliaji na tathmini hiyo, mfumo utakuwa
kama ifuatavyo:
(a) Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na wadau wa sekta za miradi
husika itafuatilia utekelezaji wa miradi kila robo mwaka;
(b) Wizara ya Fedha na Mipango itaitisha kikao na wadau kujadili changamoto
zilizobainishwa katika utekelezaji wa miradi na kukubaliana hatua za
kukabiliana nazo; na
(c) Kufuatilia utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika kukabiliana na
changamoto za utekelezaji wa miradi.
6.6. Utoaji Taarifa
Serikali itatumia Mkakati wa Mawasiliano wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka
Mitano katika utoaji taarifa kwa wananchi. Mkakati wa mawasiliano umelenga
kuhakikisha kuwa wananchi wanapata uelewa kuhusu Mpango na wajibu wao katika
kuutekeleza, mafanikio na changamoto za utekelezaji na mbinu zitakazotumika
katika kufikia malengo ya Mpango. Aidha, katika kutekeleza mkakati huo, mbinu
mbalimbali zitaendelea kutumika katika utoaji wa taarifa kwa umma ikiwemo
Maonesho ya Kimataifa (Saba Saba na Nane Nane), tovuti za Serikali, magazeti,
vipeperushi, vyombo vya habari (televisheni na radio) pamoja na vikao vya wadau.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 131
6.7. Mgawanyo wa Majukumu katika Ufuatiliaji na Tathmini ya Mpango
Katika kuhakikisha kuwa Mkakati wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Mpango
unatekelezwa, taasisi zifuatazo zitahusika:
(a) Wizara ya Fedha na Mipango
Wizara ya Fedha na Mipango itaratibu utekelezaji wa Ufuatiliaji na Tathmini ya
Mpango wa Maendeleo na ushiriki wa wadau. Vile vile, Wizara itahakikisha kuwa
rasilimali fedha zinapatikana kugharamia shughuli za ufuatiliaji na tathmini na
kufuatilia matumizi ya fedha kwa ajili ya uwajibikaji. Wizara ya Fedha na Mipango
itakuwa na wajibu wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya
mwaka na taarifa za ufuatiliaji wa miradi.
(b) Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Katika kukabiliana na uhaba wa wataalam wa ufuatiliaji na tathmini, Ofisi ya Rais -
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itakuwa na wajibu wa
kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali watu katika nyanja hiyo ya ufuatiliaji. Hii
itahusika pia na kuwajengea uwezo wataalam waliopo ili waweze kuchambua na
kutoa taarifa zenye ubora.
(c) Ofisi ya Rais – TAMISEMI
Ofisi ya Rais – TAMISEMI ina jukumu la kuratibu ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji
wa miradi ya maendeleo katika ngazi za Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za
Serikali za Mitaa. Aidha, Ofisi ya Rais, TAMISEMI itawajibika kuwasilisha Wizara ya
Fedha na Mipango taarifa za utekelezaji wa miradi.
(d) Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala wa Serikali
Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala wa Serikali zitatakiwa kuandaa na kutoa
taarifa za utekelezaji wa Mpango, ufuatiliaji na tathmini na hatua iliyofikiwa
ikilinganishwa na malengo yaliyopangwa. Hatua hii itasaidia Serikali kuhakikisha
kuwa fedha za umma zinatumika ipasavyo.
(e) Sekta Binafsi
Sekta Binafsi ni mdau muhimu katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa
Taifa wa Miaka Mitano na itahusika na utoaji taarifa sahihi kuhusu maeneo
watakayowekeza. Vile vile, watatoa taarifa zinazohusu wajibu wa Serikali katika
kusaidia sekta binafsi ikiwemo changamoto na ushauri.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 132
SURA YA SABA
VIHATARISHI VYA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA KINGA
7.1. Utangulizi
Vihatarishi ni uwezekano wa matukio mbalimbali yanayoweza kujitokeza na kuathiri
utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyoainishwa katika Mpango wa Taifa wa
maendeleo. Sura hii inaainisha viashiria vya vihatarishi na mikakati ya kukabiliana
navyo. Vihatarishi vimegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni
vihatarishi vya ndani na nje.
7.2. Vihatarishi vya Ndani na Mikakati ya Kukabiliana Navyo
Vihatarishi vya ndani ni uwezekano wa matukio yanayoweza kujitokeza ambayo
udhibiti wake upo ndani ya uwezo wa mamlaka ya nchi. Matukio hayo yakiachwa
yatokee yanaweza kuathiri utekelezaji wa Mpango. Matukio hayo ni pamoja na:
(a) Upungufu wa Rasilimali Fedha: kutofikiwa kwa malengo ya makusanyo ya
rasilimali fedha za kutosha na kwa wakati ni kihatarishi kinachopelekea
utekelezaji usioridhisha wa Mpango. Katika kukabiliana na kihatarishi hiki,
Serikali itatekeleza yafuatayo: kuendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato
ikiwa ni pamoja na kuharakisha urasimishaji wa sekta isiyo rasmi ili iweze
kuingizwa kwenye wigo wa kodi; kuimarisha nidhamu katika usimamizi wa
matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo; na utekelezaji wa Mwongozo wa
Ushirikiano wa Maendeleo – DCF.
(b) Ushiriki Mdogo wa Sekta Binafsi: mafanikio ya utekelezaji wa mpango
yanategemea ushiriki chanya wa sekta binafsi katika maeneo ya kipaumbele
ya Mpango. Ushiriki mdogo wa sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi ya
maendeleo ni kihatarishi kinachopelekea kutofikiwa kwa malengo ya Mpango.
Hatua za kukabiliana na kihatarishi hiki ni pamoja na: kuendelea kuboresha
mazingira wezeshi ya biashara ili kupunguza gharama za uwekezaji;
kuboresha huduma za kifedha ili kuwezesha sekta binafsi kukopa zaidi kwa
ajili ya uwekezaji; kuendeleza majadiliano ya mara kwa mara kati ya Serikali
na Sekta Binafsi ili kutatua changamoto za uwekezaji na kufanya biashara; na
kuvutia ushiriki wa sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi kwa utaratibu wa
ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP).
(c) Umiliki wa Ardhi na Usimamizi wa Migogoro: taratibu za umiliki wa ardhi
kwa ajili ya uwekezaji zinaweza kuchangia katika kuchelewesha utekelezaji
wa miradi kwa ufanisi hususan wakati wa ulipaji fidia. Katika kukabiliana na
kihatarishi hiki, Serikali itaendelea na usimamizi wa matumizi bora ya ardhi
kwa kuandaa na kuimarisha Mipango Miji ili kurahisisha utoaji wa huduma
mbalimbali za kijamii.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 133
(d) Ufuatiliaji na Tathmini usio wa kina: ufuatiliaji na tathmini usio wa kina
unaweza kuathiri utekelezaji wa mipango kwa kutoa taarifa zisizo sahihi za
utekelezaji na mafanikio ya utekelezaji wa mpango na hivyo kuweza
kusababisha matumizi mabaya ya rasilimali fedha. Serikali itaendelea
kuboresha mifumo ya tathmini na ufuatiliaji kwa kutoa mafunzo na kuimarisha
usimamizi wa matumizi ya fedha za umma.
(e) Uharibifu wa Mazingira: Shughuli za binadamu huweza kuathiri mazingira
na hivyo kusababisha uzalishaji duni katika uchumi. Serikali itaendelea
kuhamasisha matumizi sahihi ya teknolojia katika kutekeleza shughuli za
maeendeleo ili kupunguza athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira.
(f) Usalama Mtandaoni: matumizi mabaya ya teknolojia yanaweza kuathiri
utekelezaji wa mpango. Serikali itaendelea kuimarisha mfumo wa matumizi ya
mitandao kwa kila taasisi kuwa na anuani yenye usimamizi madhubuti pamoja
na kuendelea na utambuzi wa raia na utoaji wa vitambulisho vya Taifa na
anuani za makazi.
7.3. Vihatarishi vya Nje na Mikakati ya Kukabiliana Navyo
Vihatarishi vya nje ni uwezekano wa matukio yanayoweza kujitokeza ambayo utatuzi
wake upo nje ya uwezo wa Serikali wa moja kwa moja na hivyo kuathiri utekelezaji
wa Mpango. Vihatarishi hivyo ni pamoja na:
(a) Mtikisiko wa Kiuchumi Kikanda na Kimataifa. Mtikisiko wa kiuchumi
kikanda na kimataifa unapotokea husababisha kupungua kwa mahitaji ya
bidhaa na huduma katika masoko ya nje na hivyo kuchangia kupungua kwa
fedha za kigeni zitokanazo na uuzaji wa bidhaa nje na wawekezaji wa mitaji
ambao ni muhimu katika kugharamia miradi ya maendeleo. Mikakati ya
kukabiliana na kihatarishi hiki ni pamoja na: kuongeza mapato ya ndani na
kuharakisha urasimishaji wa sekta isiyo rasmi; na kuendelea na jitihada za
kupunguza utegemezi kwa kuwianisha mapato na matumizi;
(b) Matukio Asilia kama vile matetemeko, mafuriko na ukame huathiri uendelevu
wa rasilimali asili na ikolojia na hivyo kusababisha kupungua kwa uzalishaji.
Mikakati ya kukabiliana na kihatarishi hiki ni pamoja na: kuendelea kuimarisha
mifumo ya kutabiri majanga na kuchukua tahadhari pamoja na kutekeleza
miradi ya kuhimili athari za matukio asilia;
(c) Migogoro ya ndani na ya kimataifa inaweza kuathiri utekelezaji wa mpango
kutokana na kuwa matukio kama hayo yanabadili hali ya mshikamano na
soko pamoja na vyanzo vya fedha kwa ajili ya uwekezaji. Mkakati wa
kukabiliana na kihatarishi hiki ni pamoja na kuendelea kushiriki katika
majadiliano ili kuzuia matukio yanayoweza kuhatarisha amani kimataifa na
kikanda; na
(d) Mabadiliko ya Tabia Nchi: Mabadiliko ya hali ya hewa yasiyotabirika kama
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 134
mvua nyingi, ongezeko la joto duniani na ukame vinaweza kupunguza kasi ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo na shughuli za kiuchumi kutokana na
Tabia nchi iliyozoeleka kubadilika isivyotarajiwa na hivyo kuathiri baadhi ya
miradi. Mikakati ya kukabiliana na kihatarishi hiki ni pamoja na Serikali
kuendelea kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi katika utekelezaji wa baadhi ya
miradi kwa kuzingatia hali iliyopo ya tabia nchi na hivyo kuepusha hasara
zisizotarajiwa.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 135
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 136
KIAMBATISHO I
UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MWAKA 2018/19
137
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Miradi ya Kielelezo
Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Standard Gauge
Ujenzi wa reli kutoka Dar es salaam - Morogoro (km 300);
Ujenzi wa reli kutoka Morogoro - Makutupora (km 422); na
Ujenzi wa reli ya Isaka - Rusumo (km 371).
Ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro (km 300) unaendelea ambapo utekelezaji umefikia aslimia 48.9. Shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na: kutandika km 30 za reli; ujenzi wa makalvati asilimia 55; ujenzi wa madaraja asilimia 42; ujenzi wa daraja refu katikati ya Jiji la Dar es Salaam lenye urefu wa km 2.54 ambao umekamilika kwa asilia 63; ukataji wa miinuko na ujazaji wa mabonde umekamilika kwa asilimia 66. Kazi zinazoendelea ni pamoja na uwekaji wa nguzo za mfumo wa umeme kwa ajili ya kuendeshea treni; na ujenzi wa stesheni za Dar es Salaam, Pugu na Soga.
Katika kipande cha Morogoro – Makutupora (km 422),utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 7.12 ambapo kazi zinazoendelea ni pamoja na: uthamini na uhakiki wa wananchi watakaopisha mradi; ukataji wa miinuko na ujazaji wa mabonde; usanifu wa njia na ujenzi wa kambi za Kilosa na Ihumwa.
Kazi za utafutaji fedha kwa sehemu ya Makutupora – Tabora (km 295), Tabora – Isaka (km 133) na Isaka – Mwanza (km 250) zinaendelea ambapo wawekezaji mbalimbali wameonesha nia ya kufanikisha upatikanaji wa fedha na kushiriki katika ujenzi wa vipande hivyo. Aidha, Isaka – Rusumo (km 371), mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali yamekamilika. Tabora – Kigoma, Kaliua – Mpanda na Uvinza – Msongati (Burundi), upembuzi yakinifu unaendelea ambao unatarajiwa kukamilika Juni 2019.
Shughuli zingine za utekelezaji wa mradi ni pamoja na: kusainiwa kwa mkataba wa miezi 11 kuanzia Desemba 2018 kati ya Serikali kupitia TRC na TANESCO na Kampuni ya Larsen & TOURBO (L&T) Construction kwa ajili ya ujenzi wa mfumo wa umeme wa SGR ambapo kazi hiyo imeanza; kuendelea na taratibu za ununuzi wa mabehewa, injini na mitambo itakayotumika kutoa huduma ya usafiri kwenye reli ya Standard Gauge.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 138
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Uboreshaji wa Shirika la Ndege Tanzania
Ununuzi wa ndege moja aina ya Boeing 787 - 8 Dreamliner;
Ununuzi wa ndege moja mpya aina ya Bombadier Dash 8 Q400; na
Kulipa bima, gharama za uendeshaji wa ndege (start up cost), mafunzo ya marubani, wahandisi na wahudumu pamoja na ulipaji wa madeni.
kupokelewa kwa ndege 3 ambapo moja ni aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na mbili ni Airbus A220-300;
kulipa sehemu ya gharama za ununuzi wa ndege mbili aina ya Boeing 787-8 Dreamliner na Bombadier Dash 8 Q400 zinazotarajiwa kuwasili nchini kabla ya mwishoni mwa Mwaka 2019;
malipo ya bima, gharama za uendeshaji wa ndege, mafunzo ya marubani (51), wahandisi (14) na wahudumu (66) pamoja na madeni ya Shirika la Ndege Tanzania; na
kuanza kwa ukarabati wa Karakana ya Matengenezo ya Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Kufua Umeme wa Maji Bonde la Mto Rufiji - MW 2,115
Ujenzi wa kambi na ofisi za wafanyakazi;
Ujenzi wa bwawa (main dam and spillways); na
Ujenzi wa njia kuu za kupitisha maji (tunnels).
kupatikana kwa mkandarasi Kampuni ya Ubia kati ya Arab Contractors na Elsewedy Electric S.A.E kutoka Misri ambapo mkataba wa ujenzi umesainiwa;
Mkandarasi amekabidhiwa eneo la mradi Februari 2019 na kuanza kazi za awali za ujenzi;
Kukamilika kwa ujenzi na uwekaji wa miundombinu wezeshi ambayo ni pamoja njia ya kusafirisha umeme wa MW 8 yenye msongo wa kV 33 kutoka Msamvu, Morogoro hadi eneo la mradi yenye urefu wa kilomita 170; barabara za kiwango cha changarawe za Ubena – Zomozi na Kibiti – Mloka hadi eneo la mradi; mifumo ya maji; mawasiliano ya simu; na nyumba za kuishi Mkandarasi; na
Kuanza ujenzi wa njia ya pili ya umeme msongo wa kV 33 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Gongo la Mboto kupitia Kisarawe hadi eneo la mradi urefu wa kilomita 245 itakayosafirisha umeme wa MW 22.
Mradi wa makaa ya mawe Mchuchuma
Mradi wa Vanadium,
Kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha eneo la mradi;
Kusimamia ujenzi wa miundombinu wezeshi;
Kurejea mikataba ya kuendeleza mradi wa Mchuchuma na Liganga;
Kurejea sheria za kuendeleza mradi unganishi wa Mchuchuma na Liganga kwa kuzingatia Sheria za Madini ya Mwaka 2010 na Sheria Na. 6 na Na. 7 za mwaka 2017.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 139
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Titanium na chuma Liganga Kulipa tozo ya ardhi;
Kufanya utafiti wa faida za kiuchumi za mradi;
Kupitia upya vivutio kwa ajili ya uwekezaji;
Kuelimisha wananchi kuhusu faida za mradi katika Mkoa wa Njombe
Mradi wa kuendeleza kituo cha biashara na usafirishaji Kurasini
Kukamilisha malipo ya fidia kwa wakazi watatu (3) ambao nyumba zao hazikuthaminiwa awali
Kuwezesha utekelezaji wa mradi
Kukamilika kwa uthamini wa nyumba
Kukamilika kwa upimaji wa eneo;
Kuendelea na taratibu za kupata hati miliki ambazo zipo katika hatua za mwisho.
Uanzishwaji wa Kanda Maalum za Kiuchumi
Eneo Maalum la Uwekezaji Bagamoyo: kufanya usanifu wa kina na ujenzi wa miundombinu ya ndani katika eneo la kituo cha Teknolojia Bagamoyo; kuandaa nyaraka za kisheria kwa ajili ya mradi; na kukamilisha hatua za utwaaji wa Ardhi na kupima na kupata hatimiliki ya eneo lililokwishalipiwa fidia.
Eneo Maalum la Uwekezaji Kigoma: Kuratibu usanifu wa kina na ujenzi wa miundombinu ya ndani ya eneo la mradi; kupima viwanja na kupata Hatimiliki ya eneo; na kutangaza eneo kwa ajili ya kupata wawekezaji;
Eneo Maalum la Uwekezaji la Mtwara: usanifu na ujenzi wa barabara (access road) kufika eneo la mradi; na
Eneo maalum la Uwekezaji Ruvuma: kukamilisha ulipaji wa fidia; upembuzi
Eneo Maalum la Uwekezaji Bagamoyo: mpango kabambe wa kuendeleza eneo la hekta 175 lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Teknolojia umekamilika; makampuni mengine 12 yamepewa leseni kwa ajili ya kujenga viwanda katika eneo la Bagamoyo SEZ lililokwisha lipiwa fidia nje ya eneo la kujenga bandari;
Eneo Maalum la Uwekezaji Kigoma: kukamilika kwa upembuzi yakinifu na Mpango Kabambe wa uendelezaji wa eneo (Master Plan) na ugawaji wa viwanja kwa ajili ya kupewa wawekezaji; kuendeleza miundombinu kwa kufungua barabara zenye jumla ya km 28.46 na kuweka alama za mipaka 106; kupatikana kwa wawekezaji watatu ambao ni Next Gen Solowazi Limited, Third Man Limited na SGC Investment Limited watakaowekeza kwenye ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa jua, ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki (asali) na ujenzi wa kiwanda cha kuchakata zao la michikichi na ghala kwa mtiririko huo;
Eneo Maalum la Uwekezaji Mtwara: usanifu na ujenzi wa barabara kufika eneo la mradi; na kuendelea na maandalizi kwa ajili ya kuanza mradi ambapo mikataba ya utekelezaji kati ya EPZA na waendelezaji wa miundombinu wezeshi (TARURA na MTUWASA) inahakikiwa na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 140
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
yakinifu na kuandaa mpango kabambe; kupima na kupata hatimiliki ya eneo; na kutangaza eneo kwa ajili ya kupata wawekezaji.
Serikali ili makabidhiano ya rasilimali fedha yafanyike;
Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia – Lindi
kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha ujenzi wa mradi;
kuendelea na majadiliano ya HGA; na
kufanya usanifu wa Awali wa Kihandisi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha LNG.
Kukamilisha Tathmini ya Athari za Mazingira na Kijamii (ESIA);
Kukamilisha Mpango wa uhamishaji wananchi watakaopisha Mradi;
Kuanza kwa majadiliano ya kimkataba (Host Government Agreement – HGA) baina ya Serikali na wawekezaji; na
Kuandaliwa kwa moduli ya kiuchumi ya mradi.
Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania
Kukamilisha majadiliano ya Host Government Agreement (HGA) na Sharing Host Government Agreement (SHA)
Kukamilisha usanifu wa kina wa kihandisi
Kuwalipa fidia wananchi watakaopisha mradi
Kuendelea na majadiliano ya mkataba kati ya kampuni ya mradi na Nchi Hodhi (Host Government Agereement – HGA);
Kuendelea na maandalizi ya majadiliano ya Mkataba wa Ubia ambayo yanategemewa kukamilika mwezi Juni 2019; na
Kukamilika kwa tathmini ya fidia kwa maeneo ya kipaumbele na eneo lote la mkuza.
Miradi ya Kukuza Uchumi na Ujenzi wa Masingi wa Uchumi wa Viwanda
Uzalishaji Viwandani
Kuunganisha Matrekta, TAMCO, Kibaha
Kuratibu mauzo;
Kuratibu ujenzi wa viwanda vipya;
Kugharamia uingizaji wa vifaa bandarini na kuvipeleka kwenye eneo la mradi; na
Kusimamia uanzishwaji wa maeneo mengine nane ya kufanya matengenezo ya matrekta nchini na kulipa tozo ya ardhi
Matrekta 822 kati ya 2,400 yameingizwa nchini;
Matrekta 536 yameunganishwa; na
Matrekta 399 yameuzwa.
Kuendeleza Kongane ya Viwanda TAMCO – Kibaha
Kuratibu ujenzi wa mtandao wa barabara za ndani ya eneo la mradi;
Kujenga uzio kuzunguka eneo la mradi; na
Kusanifu na kujenga bwawa la maji taka
Uandaaji wa Mpango Kabambe (detailed Master Plan) wa eneo kwa ajili ya kuvutia uwekezaji. Eneo la ekari 43.04 limetengwa kwa ajili ya Sekta ya Viwanda vya Dawa za Binadamu na Vifaa Tiba. Kampuni ya Hester Biosciences imeanza kusafisha eneo la Ekari 8.95 kwa ajili ya kujenga Kiwanda cha kuzalisha chanjo za Mifugo; kuendelea na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 141
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
(oxidation ponds). ujenzi wa barabara yenye urefu wa Km 0.58 kwa kiwango cha lami;
majadiliano kati ya NDC na TANESCO yanaendelea kwa ajili ya kujenga kituo kidogo cha kupozea umeme (substation) katika eneo la Viwanda la TAMCO yanaendelea; na
NDC kuendelea na majadiliano ya ujenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Sindano (syringes) utakaotekelezwa na Kampuni ya El-Dawlia Limited.
Mradi wa Magadi Soda - Bonde la Engaruka
kuandaa taarifa ya kina ya upembuzi yakinifu ambayo inaweza kuvutia taasisi za fedha na kutangaza eneo kwa ajili ya kupata wawekezaji na
kulipa tozo ya ardhi ambapo shilingi milioni 200 fedha za ndani zimetengwa.
Kazi zilizotekelezwa ni: kukamilika kwa upimaji wa ardhi ya mradi pamoja na uthaminishaji wa mali za wananchi; kukamilisha michoro ya matumizi ya ardhi; na kuendelea kutangaza mradi kwa wawekezaji mbalimbali ili kumpata mwekezaji wa kushirikiana na Serikali kupitia NDC
Kiwanda cha Matairi General Tyre – Arusha
Kuandaa taarifa ya kina ya upembuzi yakinifu ambayo inaweza kuvutia taasisi za fedha
Kutangaza eneo kwa ajili ya kupata wawekezaji na
Kulipa tozo ya ardhi.
Kukamilika kwa utafiti wa namna bora ya kufufua kiwanda;
Kukamilika kwa makabidhiano ya kiwanda kati ya NDC na Ofisi ya Msajili wa Hazina; na
Kukamilika kwa uthamini wa mali za kiwanda
Maeneo mengine maalumu ya uwekezaji
Eneo Maalum la Uwekezaji Tanga
Eneo Maalum la Uwekezaji Bunda
Eneo Maalum la Uwekezaji Dodorelia
Eneo Maalum la Uwekezaji Benjamin William Mkapa
Eneo la viwanda Kigamboni
Kongano la Viwanda vya Ngozi – Dodoma:
kuendelea na taratibu za kutafuta wawekezaji watakaowekeza katika maeneo ya Tanga, Bunda, Kigamboni na Dodoma (Zuzu).
Utafiti wa Teknolojia na Bidhaa za Viwandani
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 142
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kituo cha zana za Kilimo na Ufundi Vijijini - CAMARTEC
Kuendeleza utafiti wa technolojia za zana za kilimo;
Kukuza wazalishaji wa ndani wanaojihusisha na zana za kilimo;
Kusimamia utekelezaji wa kanuni za majaribio na ukaguzi wa zana za kilimo na teknolojia za ufundi vijijini;
Kujenga miundombinu ya utafiti; na
Kuhakiki ubora wa zana za kilimo nchini
Kubuni mashine 64 zikiwemo za kupandia mbegu za pamba, kusaga karanga, kukausha mbogamboga na kukata majani;
Ujenzi wa mitambo 55 ya biogas;
Mafunzo na elimu ya utumiaji wa biogas yalitolewa; na
Kukamilika kwa tafiti tatu zinazohusiana na matumizi ya nishati mbadala ya biogas; na
kufanya utafiti wa mahitaji ya zana za kilimo (technology needs assessment) katika mikoa 14 ya Tanzania Bara ambayo ni Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Singida, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Geita, Kigoma, Dodoma, Iringa, Njombe, Lindi na Mbeya. Matokeo yameonyesha uhitaji mkubwa wa teknolojia za kupandia mazao za kupalilia, kupura na kupepeta mazao ya nafaka.
Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania – TIRDO
kubuni teknolojia itakayowezesha makaa ya mawe kutumika majumbani pamoja na kuendesha utafiti;
kuanzisha na kuhakiki maabara ya mafuta na gesi asilia na maabara ya vipimo vya chuma ngumu;
kukamilisha mchakato wa kuhakiki (Accreditation) na kuboresha maabara ya chakula, mazingira, kemia, na maabara ya vifaa vya kihandisi ili ziweze kufikia viwango vya kimataifa;
kuhuisha teknolojia ya kutumia sensor kufuatilia uzalishaji viwandani kwa wajasiriamali; na
kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa sekta ya ngozi kuhusu utunzaji wa mazingira
Shughuli zilizotekelezwa ni: kuendelea na ukarabati wa jengo la maabara ya mafuta na gesi asilia; kukamilika kwa michoro na makadirio ya gharama za ukarabati wa maabara ya makaa ya mawe na kuendelea kukamilisha taratibu za kumpata mkandarasi wa ujenzi. Aidha, Shirika linakamilisha taratibu za uhakiki wa maabara ya mazingira baada ya kutuma maombi ya uhakiki kwa Mamlaka ya Uhakiki Kusini mwa Afrika - SADCAS na kuelekezwa kurekebisha baadhi ya nyaraka kabla ya ukaguzi.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 143
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo – TEMDO
Kutoa huduma za kiufundi kwa viwanda;
Kujenga miundombinu ya kiatamizi cha teknolojia na biashara;
Kuendelea na uboreshaji wa karakana na ofisi ya usanifu pamoja na miundombinu ya taasisi kwa ujumla;
Kupitia upya sheria iliyoanzisha taasisi ya TEMDO;
Kubuni na kuendeleza chasili cha mtambo wa kukausha mazao ya kilimo;
Kubuni na kuendeleza chasili ya kusindika chai;
Kubuni na kuendeleza utengenezaji wa mtambo wa kuweka baridi (cold room);
Kubuni na kuendeleza chasili cha mtambo mdogo wa kutengeneza brikwiti kutokana na vumbi la makaa ya mawe;
Kufanya utafiti ili kubainisha mahitaji ya soko katika teknolojia na huduma za kitaalam;
Kuanzisha na kuwezesha mpango wa kusambaza viwanda nchini kwa utaratibu wa kiwanda kimoja kila wilaya (one district one factory - odof); na
Kuhawilisha teknolojia na kuhamasisha uzalishaji wa kibiashara wa mitambo iliyobuniwa.
Kubuni mashine ya kutengeneza tofali zinazozuia upotevu wa joto (refractory bricks);
Kubuni majokofu makubwa;
Kubuni kiteketezi taka kidogo kinachobebeka kwa ajili ya zahanati na maabara za afya;
Kubuni mtambo wa kusindika na kusafisha mafuta ya kula na mtambo wa kuzalisha umeme kutokana na nguvu ya maji na ufungaji wa mtambo wa kuzalisha umeme (kw 20) kutokana na nguvu za upepo na jua katika kituo cha Olduvai Gorge – Ngorongoro.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 144
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Uendelezaji wa Viwanda Vidogo – SIDO
Kujenga miundombinu ya viwanda katika mikoa ya Morogoro, Mara, Shinyanga, Lindi, Kagera, Ruvuma, Rukwa na Singida;
Kujenga majengo ya viwanda katika mikoa ya Morogoro, Kagera, Simiyu, Katavi na Njombe;
Kujenga ofisi tatu (3) za kutolea huduma katika mikoa ya Morogoro, Songwe na Katavi;
Kusaidia kuanzisha viwanda vidogo 1,320 chini ya mkakati wa ODOP;
Kuboresha vituo vya kuendeleza teknolojia vya Arusha, Mbeya na Shinyanga kwa kununua mashine za kisasa; na
Kununua mashine za teknolojia za kutengeneza vifungashio kwa ajili ya bidhaa za wajasiliamali
Kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya viwanda (barabara, mifumo ya maji na umeme)
Ujenzi wa majengo ya viwanda (12) katika Mikoa ya Dodoma, Geita, Kagera, Manyara, na Mtwara na
Ujenzi wa ofisi za SIDO za kutolea huduma katika Mikoa mipya ya Geita, Simiyu na Katavi pamoja na wilaya ya Chato;
Kuboresha kituo cha teknolojia cha Lindi kwa kununua mitambo mipya ya kubangua korosho; kuimarisha vituo vya teknolojia vya Shinyanga na Kigoma ili viwe katika nafasi nzuri ya kutengeneza teknolojia za kuchakata zao la Chikichi pamoja na mazao mengine; kuongeza majengo ya viwanda katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma, na Kigoma;
Kutambua, kuanzisha na kusambaza teknolojia mpya 40 za ubanguaji korosho usindikaji na ufungashaji wa vyakula, utengenezaji wa vifaa vya ujenzi hasa matofali, utengenezaji wa chokaa na chaki, ukamuaji wa mafuta ya kula kutokana na michikichi na usindikaji wa ngozikwa kutumia njia za asili.
KILIMO
Kilimo cha Mpunga
kuzalisha tani 10 za mbegu bora mama za mpunga;
kuhamasisha matumizi ya mbegu bora za mpunga;
kuboresha miundombinu ikiwemo barabara za mashambani;
ujenzi wa maghala pamoja na mitambo ya usindikaji;
upanuzi wa miundombinu ya umwagiliaji ambapo jumla ya hekta 8,182 zitajengwa na kukarabatiwa kote nchini.
kupatiwa mafunzo ya kilimo shadidi cha mpunga kwa Maafisa Ugani na Mafundi Sanifu wa Umwagiliaji 109 na wakulima 5,647 kutoka skimu za umwagiliaji 40;
kuendeshwa kwa mashamba darasa yapatayo 1,331; mbegu mpya za mpunga 11 aina ya TXD 306 (SARO 5), TXD 88, TXD 85, Tai, Kalalu na Komboka zinazofaa kwa kilimo cha mabondeni na NERICA 1, NERICA 2, NERICA 4 na NERICA 7 zinazofaa kwa kilimo cha nyanda za juu zilitambulishwa kwa wakulima na kuwezesha wakulima 3050 kuchagua aina 2 za mbegu walizopendelea zaidi ambazo ni TXD 306 (SARO 5) na NERICA 7.
katika kudhibiti ubora wa mbegu za mpunga, Taasisi ya Udhibiti wa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 145
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
kuendelea kutolewa kwa wakulima kwa mfumo wa shamba darasa ambao utamsaidia mkulima kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa tani 2.5 hadi kufikia tani 6.5 kwa hekta
Ubora wa Mbegu Tanzania - TOSCI imefanya ukaguzi wa mashamba yaliyoandikishwa kuzalisha mbegu. Kuhakikiwa kwa mbegu zilizozalishwa kutoka Taasisi ya Utafifiti wa Kilimo - TARI, Taasisi ya uzalishaji wa mbegu Tanzania - ASA na kutoka kwa wakulima waliozalisha mbegu zenye ubora wa kuazimiwa.
Kilimo cha Mahindi
kupeleka teknolojia za kilimo kwa wakulima; kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa wakati zikiwemo mbegu bora, mbolea na madawa;
kuwaelimisha wakulima kuhusu matumizi sahihi ya pembejeo; na
kuimarisha masoko ya zao la mahindi kwa kujenga miundombinu ya masoko hususan maghala kwa lengo la kupata bei nzuri na kuongeza thamani;
kuimarisha udhibiti wa visumbufu vya mimea na mazao pamoja na udhibiti wa magonjwa
kuendelea kuboresha uzalishaji wa mahindi kwa kuhamasisha matumizi ya mbegu bora na mbolea, ambapo jumla ya tani 17,525.65 za mbegu bora za mahindi zilipatikana na kusambazwa kwa wakulima
kutolewa elimu kuhusu udhibiti wa viwavijeshi vamizi kwa wakulima 2,080 wa mahindi kutoka mikoa ya Singida (385), Shinyanga (425), Simiyu (495), Tabora (530) na Morogoro (245).
Kuimarika kwa uzalishaji mahindi kwa misimu mitatu iliyopita ni: 5,908,000 kwa mwaka 2015; 6,149,000 kwa mwaka 2016; na tani 6,681,000 kwa mwaka 2017.
Serikali kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ilinunua tani 2,489.27 za mahindi na kusagisha tani 462.73 ambapo tani 344.78 za unga na tani 117.95 za pumba zilipatikana.
Mauzo ya unga na pumba yalikuwa tani 213.42 za unga zenye thamani ya Shilingi 135,805,550 na tani 6.1 za pumba zenye thamani ya Shilingi 1,531,000 katika mikoa ya Iringa, Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam.
Kilimo cha Miwa
kuimarisha miundombinu ya wakulima wadogo wa miwa katika maeneo mbalimbali nchini;
kuimarisha upatikanaji wa pembejeo ikiwa ni pamoja na mbolea na viuatilifu;
kuhamasisha uanzishwaji wa mashamba na viwanda vipya vya sukari na kuimarisha upatikanaji wa huduma za mafunzo na
kukarabatiwa kwa kilometa 33.5 za miundombinu ya barabara zilizopo kwenye mashamba ya wakulima wadogo wa miwa katika maeneo ya Kilombero, Mtibwa na Kagera;
kusajiliwa kwa wakulima 6,125 kupitia mfumo wa kielektroniki katika mashamba ya Kilombero (5,899) na Mtibwa;
kujengwa kwa miundombinu ya umwagiliaji katika kijiji cha Msolwa Ujamaa kwa ajili ya wakulima wadogo 146 wanaomiliki ekari 250;
kujengwa kwa tuta la kukinga maji lenye urefu wa km 10.6 katika
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 146
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
ugani; na
kuweka mazingira bora kwa ajili ya kuvutia uwekezaji katika viwanda vipya vya sukari nchini.
bonde la Ruembe (Kilosa);
wakulima 316 kutoka katika mashamba ya Kilombero, Mtibwa na Kagera wamepatiwa mafunzo ya mbinu bora za kilimo bora cha miwa, biashara, uongozi, ushawishi na utetezi; na
kutolewa kwa mafunzo ya kilimo bora cha miwa, kutolewa kwa viuatilifu vya kudhibiti wadudu waharibifu na visumbufu kwa wakulima wadogo wa Mkoa wa Manyara.
Kilimo cha Chai
kuzalisha miche bora ya chai inayohimili ukame;
Kufanya utafiti wa umwagiliaji wa gharama nafuu kwa wakulima wadogo wa chai;
Kuendelea kutoa elimu kwa wakulima wa chai juu ya kilimo bora;
Kuziba mapengo kwenye mashamba ambayo yana nafasi kubwa;
Kuwekeza kwenye umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wakati wa kiangazi;
kuimarisha matumizi ya vipando bora vya chai;
Kuongeza uwekezaji katika viwanda vya kusindika chai na kufufua mashamba ya chai yaliyotelekezwa.
Kuzalishwa kwa miche bora 7,139,000 kupitia sekta binafsi na umma. Kati ya miche hiyo, miche 3,100,000 imesambazwa kwa wakulima wa Wilaya za Njombe, Ludewa, Tarime, Rungwe na Mufindi kwa ajili ya kujaza mapengo na kufungua mashamba mapya;
kuzalishwa kwa tani 19,412.16 sawa na asilimia 52.5 ya lengo la kuzalisha tani 37,000;
kuongezeka kwa mauzo ya chai kavu kufikia tani 5,500 ongezeko ambalo limetokana na kuimarishwa kwa viwanda vya Rift Valley – Dar es Salaam na BK Tea Blenders – Kagera; na
kutolewa mafunzo kuhusu uanzishaji na utunzaji wa bustani za miche bora ya chai, upandaji chai mashambani, uchumaji wa majani mabichi ya chai na matumizi sahihi ya pembejeo kupitia shamba darasa kwa wakulima wadogo wa chai 15,000 na maafisa ugani saba (7) katika mkoa wa Njombe;
Kilimo cha Kahawa
kuongeza maeneo ya uzalishaji wa kahawa;
kuongeza uzalishaji na usambazaji wa miche ya kahawa ipatayo milioni 10 kwa wakulima na kuimarisha huduma za ugani na upatikanaji wa pembejeo
kuzalishwa kwa miche 6,494,930 kwa ajili ya kupandwa katika kanda za uzalishaji wa kahawa ambapo miche 1,780,430 imezalishwa na Bodi ya Kahawa na miche 4,714,500 imezalishwa na TaCRIkatika vituo vya Lyamungo - Moshi, Ugano - Mbinga, Mbimba - Mbozi, Maruku – Bukoba, Mwayaya - Buhigwe na Sirari - Tarime.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 147
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kilimo cha Pamba
kuongeza uzalishaji wa mbegu bora za pamba aina ya UKM08 ambapo zitazalishwa tani 40,000;
kutenga maeneo maalum ya kuzalisha mbegu bora;
kutoa elimu kwa wakulima juu ya kanuni bora za uzalishaji wa pamba ili kuongeza tija;
kutoa vitendea kazi vitakavyorahisisha utendaji na kuhamasisha uzalishaji katika mikoa ya Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Pwani na Iringa
Kusambazwa kwa tani 21,535.62 za mbegu bora za pamba aina ya UKM08 kwa wakulima nchini ambapo ongezeko la usambazaji limetokana na mwamko wa wakulima kulima zao la pamba;
ekapaki 3,326,990 za viuatilifu zimesambazwa katika Halmashauri 41 za mikoa ya Kigoma, Katavi, Singida, Dodoma, Kagera, Mara, Tabora, Geita, Mwanza, Shinyanga na Simiyu; na
kutolewa kwa mafunzo ya kanuni bora za kilimo cha pamba, ikiwemo utambuzi wa visumbufu, viuatilifu na matumizi sahihi ya viuatilifu kwa washiriki 2,036 wakiwemo maafisa ugani, wakulima, na maafisa ushirika kutoka mikoa ya Tabora, Mwanza, Mara, Shinyanga, Katavi, Kigoma, Singida, Kagera, Geita, Simiyu, Iringa, Dodoma, Manyara, Kilimanjaro, Morogoro, Pwani na Tanga;
Kilimo cha Tumbaku kutambua na kupanda aina mpya za tumbaku ambazo zinapendwa na wanunuzi wengi wakubwa katika soko la dunia;
kudhibiti na kusimamia ubora wa viuatilifu kabla ya kusambazwa kwa wakulima;
kuimarisha usimamizi wa masoko;
kuhamasisha wakulima zaidi kutumia kanuni bora za kilimo;
kuongeza uzalishaji wa zao la tumbaku ikiwa ni pamoja na kuimarisha kilimo cha mkataba; na
upatikanaji wa pembejeo kwa wakati na masoko ya uhakika
kusambazwa kilo 588 za mbegu kwa wakulima zinazotosheleza hekta 39,191 kwa wakulima 53,903 kwenye vyama vya ushirika 258 katika mikoa ya Kigoma, Katavi, Ruvuma, Mbeya, Tabora, Shinyanga, Geita na Iringa. Mbegu hizo zinatarajiwa kuzalisha tani 54,868 za tumbaku;
kuzalishwa kwa tani 16,460 za tumbaku sawa na asilimia 30 ya lengo la kuzalisha tani 54,868;
kuboreshwa kwa mabani 23,960 ya kukaushia tumbaku sawa na asilimia 42.5 ya lengo la kuboresha mabani 56,398; na
kuoteshwa kwa miche 13,657,493 kwa ajili ya kutunza mazingira na kusajiliwa kwa vituo 60,000 vya kufungia na kuchambua tumbaku.
Upatikanaji wa Pembejeo
kuweka mfumo endelevu wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya pembejeo za kilimo kwa kununua viuatilifu kwa ajili ya kudhibiti milipuko ya mimea na mazao;
kununuliwa kwa lita 269,000 na kilo 3,000 za viuatilifu vyeye thamani ya shilingi Bilioni tisa (9) kwa ajili ya kukabiliana na dharura ya milipuko ya visumbufu vya mazao vikiwemo Kwelea kwelea, Panya, Nzige wekundu, Viwavijeshi wa Afrika na Viwavijeshi vamizi.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 148
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
kuhamasisha ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhia mbolea;
kutoa mikopo ya mitambo ya mashambani (matrekta) 57; mikopo 34 kwa ajili ya pembejeo za kilimo na mifugo;
kutoa elimu kwa wafanyabiashara wa mbolea (Mawakala) kuhusu ununuzi wa mbolea kwa pamoja (bulk procurement) kutoka kwa wasambazaji wakubwa;
kutoa elimu kwa wakulima kuhusu umuhimu wa matumizi ya pembejeo;
kuhamasisha makampuni ya mbegu kuzalisha mbegu bora;
kupitisha, kuidhinisha na kutangaza aina mpya za mbegu; na
kuimarisha, kufuatilia na kutathmini upatikanaji na matumizi ya pembejeo za kilimo
Upatikanaji na usambazaji wa mbolea katika mikoa 26 ya Tanzania Bara hadi machi 2019 ulikuwa tani 492,394.18 sawa na asilimia 95.77 ya mahitaji ikilinganishwa na mahitaji ya tani 514,138 katika msimu wa mwaka 2018/19. Kati ya hizo, tani 380,307.35 ziliagizwa kutoka nje ya nchi na tani 112,086.83 ni baki ya msimu wa 2017/2018;
Kujenga maghala 11 yenye uwezo wa kuhifadhi tani 65,500 za mbolea katika maeneo ya Sumbawanga, Mbozi, Makambako, Njombe, Iringa, Morogoro, Moshi DC, Himo, Hai, Usa River na Kisongo.
Kupatikana kwa salfa ya unga tani 31,500 na viuatilifu vya maji lita 520,000 ambapo tani 3,325.850 na lita 248,207 zimesambazwa kwa wakulima.
Kupatikana kwa mbegu bora tani 49,040.66. Kati ya kiasi hicho, tani 38,507.87 zimezalishwa hapa nchini, tani 8,361.46 zimeagizwa kutoka nje ya nchi na tani 2,171.33 ni baki ya msimu wa 2017/2018. Kati ya mbegu zilizozalishwa hapa nchini, asilimia 96.5 zimetokana na sekta binafsi na asilimia 3.5 zimetokana na uzalishaji wa sekta ya umma.
Kuzalishwa kwa miche 1,507 ya miwa, vipando 121,805 vya muhogo na vikonyo 520,000 vya viazi lishe.
Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Umwagiliaji
kupitia usanifu wa Michoro, kufanya mchakato wa utoaji wa zabuni na kuanza ujenzi wa Miundombinu ya Umwagiliaji wa Skimu ya Ngono ikiwa ni pamoja na Bwawa la Kalebe;
kutoa mafunzo kwa wakufunzi (ToT) na kuanzisha mashamba darasa 158 (Mchele 28, Pamba 50, muhogo 30, mtama 30 & ndizi 20) kwa ajili ya kutoa mafunzo ya
kuanza kufanya mapitio (review) ya usanifu wa ukarabati wa miundombinu ya skimu za umwagiliaji za Kigugu - Mvomero (hekta 200), Mvumi - Kilosa (hekta 249), Msolwa Ujamaa (hekta 675) na Njage - Kilombero (hekta 325), ukarabati wa barabara za kuingia katika skimu ya Mvumi yenye urefu wa kilomita 8 na Njage kilomita 7 na usanifu wa shamba la mbegu la Kilangali (hekta 400);
Kuendelea na mazungumzo ya kumpata mtaalamu Elekezi kwa ajili ya kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira na Jamii na jumla ya wajumbe 311 kutoka skimu za umwagiliaji za Njage, Msolwa Ujamaa,
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 149
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
vitendo ya kilimo kwa wakulima viongozi na Maafisa Ugani katika Mikoa ya Geita, Simiyu, Mwanza, Mara, Kagera, Tabora, Shinyanga na Mikoa ya Pwani
Mvumi, Kigugu na Mbogo Komtonga wamepatiwa mafunzo ya kuimarisha na kuendesha umoja.
Kukarabatiwa kwa Skimu za Umwagiliaji za Wakulima Wadogo (SSIDP) 129 katika Halmashauri 68 nchini pamoja na ununuzi wa mitambo ya ujenzi.
Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo
kuimarisha vyuo vya mafunzo kuweza kudahili wanafunzi 2,300 wa mafunzo ya kilimo katika ngazi ya astashahada na stashahada;
kukarabati na kujenga miundombinu katika vyuo saba vya mafunzo ya kilimo ikiwemo ofisi, madarasa, mabweni, maabara, maktaba, nyumba za watumishi;
kuimarisha mashamba darasa; kukarabati na kutoa vitendea kazi kwenye vituo vitano vya wakulima; na
kuandaa mtaala wa stashada ya matumizi bora ya ardhi katika mfumo wa moduli; na kuhuisha mtaala wa stashada ya mboga, maua, na matunda
Wanafunzi 2,051 wamepewa ufadhili kwenye mafunzo ya kilimo, kati yao wanafunzi 1,298 ni wa ngazi ya Astashahada na wanafunzi 753 ni wa ngazi ya Stashahada katika Vyuo vya Ilonga, Mlingano, Mtwara, Tumbi, Ukiriguru, Uyole, HORTI Tengeru, Mubondo, Maruku, KATC Moshi, Igurusi, KATRIN, Chuo cha Sukari Kidatu na Inyala.
Wanafunzi 338 wanajilipia ambapo 239 ni kwa ngazi ya Astashahada na 99 ni Stashahada. Wanafunzi wa mwaka wa pili wa ngazi ya Stashahada ni 263 na ngazi ya Astashahada ni 763 ambao wanategemea kuhitimu masomo yao Juni 2019.
Tafiti za Kilimo
kutafiti mbegu bora zinazotoa mazao kwa wingi, na kustahimili mabadiliko ya tabia nchi na magonjwa;
kubuni na kusambaza teknolojia za kuchanganyia viinilishe kwa bidhaa zinazozalishwa viwandani;
kuboresha na kuimarisha miundombinu ya utafiti kwa kukarabati nyumba, ofisi na maabara katika vituo 7 vya utafiti;
Kuzalishwa kwa aina 4 za mbegu bora za mahindi (WE5135, WE7118, WE5141 na WE7133) zenye uwezo wa kustahimili ukame na uzalishaji mkubwa (kituo cha utafiti TARI - Ilonga);
Kuzalishwa kwa aina moja ya maharage (kituo cha utafiti Uyole);
Kuzalishwa kwa aina mbili za mbegu za mpunga zinazotoa mazao mengi (kituo cha utafiti cha Dakawa);
Kusambazwa kwa kilo 40,131 za mbegu za korosho kwa wazalishaji wa miche katika mikoa 20. Mbegu hizo zitazalisha miche 5,618,340 katika eneo la ekari 330,491;
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 150
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
kujenga makao makuu ya taasisi mpya ya utafiti wa kilimo nchini – TARI;
kufanya utafiti wa udongo katika maeneo mbalimbali ya kanda za ikolojia ili kuainisha tabaka za rutuba ya udongo; na
kuchora ramani kuonyesha tabaka hizo kwa maeneo kwa ajili ya kusaidia maamuzi katika uwekezaji wa mazao mbalimbali kwenye maeneo husika
Kuzalishwa na kusambazwa miche bora ya korosho 37,816 kwa wakulima wa mikoa ya Mtwara (7,155), Lindi (20,156), Pwani (6,950), Ruvuma (2,000), Tanga (1,120), Dodoma (135), Singida (200) na Dar Es Salaam (100); na
Kuendelea na ukarabati wa miundombinu ya vituo viwili vya utafiti (ARI - Makutopora na HORTI - Tengeru).
Maghala na Kuboresha Hifadhi ya Taifa ya Chakula
kujenga miundombinu 18 ya ukaushaji na hifadhi ya mazao ya mahindi na karanga katika Halmashauri za Wilaya za Sikonge, Chemba, Kondoa, Chamwino, Manispaa ya Dodoma na Kiteto ili kupunguza madhara ya sumu kuvu;
kujenga maghala 15 ya kimkakati na kukarabati maghala 33 katika mikoa ya Singida, Mwanza, Kigoma, Manyara, Simiyu, Tanga na Tabora;
kuimarisha mfumo wa upatikanaji wa taarifa za uzalishaji mazao ya chakula na hali ya chakula nchini;
kujenga maghala yenye uwezo wa kuhifadhi jumla ya tani 60,000 na vihenge vya kisasa (silos) vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 190,000 hivyo kuongeza uwezo wa Hifadhi ya Taifa ya chakula kufikia 501,000
Kununuliwa kwa tani 36,940.167 za mahindi sawa na asilimia 130.99 ya lengo la ununuzi. Kati ya kiasi kilichonunuliwa, tani 14,191.455 zimenunuliwa kupitia vituo vya ununuzi na tani 22,748.712 zimenunuliwa kupitia vikundi vya wakulima;
Ujenzi wa vihenge vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 190,000 na maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 60,000 unaendelea katika mikoa ya Ruvuma (Songea), Njombe (Makambako), Songwe (Mbozi), Rukwa (Sumbawanga), Katavi (Mpanda), Shinyanga, Manyara (Babati) na Dodoma.
Kuimarisha Maendeleo ya kuimarisha masuala ya utawala bora na Kufanyika kwa ukaguzi wa nje kwa vyama 2,296 vya ushirika;
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 151
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Ushirika
uwajibikaji katika vyama vya ushirika;
kujenga na kuimarisha uwezo wa kiuchumi na kiushindani katika vyama vya ushirika kwa kuhimiza na kusimamia mfumo wa stakabadhi ghalani;
kuratibu mikataba kati ya Bodi ya Mazao Mchanganyiko na vyama vya ushirika ili kuwezesha vyama kuuza mazao ya wakulima kwa bei yenye tija; na
Kuimarisha uwezo wa Tume ya Ushirika kutoa huduma kwa wadau.
kutatua migogoro katika vyama vya Ushirika vya RCG AMCOS dhidi ya MIWA AMCOS, UWABINDOCHA dhidi ya Manispaa ya Morogoro, Mshikamano SACCOS na Kapolo AMCOS dhidi ya TADB Bank na migogoro mingine inaendelea kushughulikiwa;
Kuendelea kuhimiza matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani katika vyama vya ushirika ambapo vyama vya mazao ya Korosho, Ufuta, Kakao na Mahindi vimeunganishwa kwenye mfumo.
Kuendelea uhamasishaji ili kuunganisha vyama vya mazao ya Dengu na kutekeleza dhana ya kilimo cha mkataba kwa kununua mahindi kupitia vyama vya ushirika kwenye mikoa ya Iringa na Ruvuma kwa bei shindani.
MIFUGO
Miundombinu ya Uzalishaji na Masoko
kukarabati minada mitatu (3) ya mifugo ya upili ya Murusagamba (Ngara), Mutukula (Missenyi) na Buhigwe (Buhigwe);
kujenga minada mipya miwili (2) ya mipakani ya Longido na Kirumi na kukarabati minada ya upili ya Nyamatala na Kasesya;
kuimarisha kituo cha Taifa cha uhimilishaji cha NAIC USA River, Arusha kwa kununua vitendea kazi kama vile semen analyzer (CASA), minibus, disc plough, pampu ya umwagiliaji, vifaa vya ofisi, kukarabati mabanda ya madume na kuendeleza malisho
kujenga na kukarabati minada ya mpakani kwa kujenga ukuta na jengo la ofisi ya mnada wa Kirumi (Butiama) ambalo litakuwa na huduma za kibenki; kuendelea na ujenzi wa sakafu ya mnada uliopo Longido, kuendelea na ujenzi wa kituo cha polisi na uzio katika mnada wa Buhigwe, na kuendelea na ujenzi wa uzio katika minada ya Kasesya na Nyamatala;
ukarabati wa mazizi katika mnada wa Kirumi umefanyika na ujenzi wa ofisi katika mnada wa Kirumi na ujenzi wa sakafu katika mnada wa Longido unaendelea. Pia, ujenzi wa uzio katika mnada wa Kasesya, Buhigwe na Nyamatala inaendelea;
kuendelea na tathmini ya ukarabati wa minada ya Nyamatala na Kasesya;
kuendelea kuimarishwa kwa vituo vya kanda vya uhimilishaji nchini, ambapo kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) kilichopo Usa River (Arusha) kimepatiwa kichambuzi cha mbegu (semen analyzer-CASA) na madume bora matatu (3) aina ya Boran, ununuzi wa mitungi 71 ya kuhifadhi kimiminika cha naitrojeni (lita 35) pamoja na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 152
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
kutoa mafunzo kwa wataalam 389 wa uhimilishaji.
Vituo vya Utafiti, Mafunzo na Ugani wa Mifugo
kuiwezesha Wakala wa vyuo vya mafunzo ya Mifugo - LITA kutoa mafunzo ngazi ya astashahada na stashahada kwa wanafunzi 2,700, kukarabati na kuimarisha uendeshaji wa vitengo vya uzalishaji katika Kampasi nane (8) za wakala
kuiwezesha TARILI kuhudumia mifugo 5000 (ng‟ombe, mbuzi, kondoo, kuku na punda) waliopo katika vituo saba nchini, kuibua, kutafiti na kusambaza ng‟ombe bora wa nyama 100 katika vituo vya Mpwapwa, Kongwa, Mabuki na West Kilimanjaro, kutafiti na kuzalisha mitamba bora 200 ya ng‟ombe wa maziwa katika vituo vinne vya utafiti na mitamba bora 400 ya ng‟ombe wa nyama katika vituo vitatu (3) vya utafiti na kuiwezesha TALIRI kutekeleza mradi wa kuboresha Mbari za Kuku wa Asili Afrika (Afrika Chicken Genetic Gain-ACGG) kwa ufadhili wa Taasisi ya Bill & Mellinda Gates Foundation ambao unatekelezwa kwa pamoja na nchi tatu za Ethiopia, Tanzania na Nigeria kwa miaka mitano (5)
Shughuli zilizotekelezwa ni: kufanyika kwa udahili wa wanachuo 2,536 kupitia Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (Livestock Training Agency – LITA). Aidha, wanafunzi 580 kutoka vyuo vya Serikali na 398 kutoka vyuo binafsi wanatarajia kuhitimu mafunzo ya Stashahada na Astashahada mwezi Juni, 2019.
Kupatia mafunzo wafugaji 156 katika Kampasi za Wakala juu ya uzalishaji bora wa mifugo na malisho.
Kukarabatiwa kwa mabweni manne (4) na Kiwanda kidogo cha Kusindika Maziwa katika Kampasi ya Tengeru. Aidha, jumla ya mitamba 15 ya maziwa yenye thamani ya Shilingi 22,000,000 imenunuliwa kwa ajili ya Kampasi ya Madaba ili kuongeza uzalishaji wa maziwa na mafunzo kupitia LITA kwa ushirikiano na Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Poland
kufanyika kwa tafiti nane vituoni na kwa wafugaji katika Mikoa ya Mbeya, Songwe, Niombe, Iringa, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mwanza, Simiyu, Dodoma, Pwani, Morogoro, Singida, Lindi, Mtwara na Kigoma 16 ambapo matokeo yake yatawezesha ng‟ombe jike kuzalisha viinitete nane (8) mpaka 450 kwa mwaka kwa ajili ya uhimilishaji na uhawilishaji (Mulitiple Ovulation and Embryo Transfer) na kuongeza kasi ya uzalishaji wa mitamba na madume kwa ajili ya maziwa na nyama (ndama 50 kwa mwaka kwa ng‟ombe mmoja) kupitia Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TARILI). Aidha TARILI wameendelea kutekeleza Mradi wa Kuboresha Mbari za Ng‟ombe wa Maziwa (African Dairy Genetic Gain, ADGG) ambapo kupitia mradi huo wafugaji 8,347 wamepata elimu na kutembelewa kila mwezi;
Kuongeza kasi ya uzalishaji wa mifugo nchini hasa mitamba na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 153
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
madume kwa ajili ya maziwa na nyama (ndama 50 kwa mwaka kwa ng‟ombe mmoja);
Kusambazwa kwa kuku 468 na mayai 720 kwa wafugaji 1,801 kupitia kupitia TALIRI kwa kushirikiana na mradi wa Kuboresha Mbari za Kuku (African Chicken Genetic Gain, ACGG);
Kuimarisha tafiti za kuainisha vinasaba vya kuongeza uzalishaji wa nyama katika mbuzi wa asili kwa kuimarisha maabara ya uhimilishaji wa mbuzi katika Kituo cha West Kilimanjaro kupitia TARILI kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo katika maeneo kame (International Centre for Agricultural Research in Dry land Areas, ICARDA)
Usimamizi wa Ardhi na Upatikanaji wa Malisho
Kuhamasisha na kuwezesha ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya maji;
Kuhakikisha uwepo na upatikanaji wa uhakika wa malisho na maji
kukamilisha ujenzi wa bwawa la Mbagala (Songwe), lambo katika Kijiji cha Chamakweza (Bagamoyo) na visima virefu katika Vijiji vya Mpapa(Manyoni) na Nsolanga-Ismani (Iringa);
kukamilisha ukarabati wa bwawa la Nyakanga (Butiama) na kuendelea na ukarabati wa lambo katika Kijiji cha Wami-Dakawa (Mvomero) na hivyo kufikia mabwawa/malambo 1,384 na visima virefu 103;
kutengwa kwa hekta 350,576.05 za maeneo kwa ajili ya malisho ya mifugo katika vituo vya kupumzishia mifugo, Ranchi za Taifa, mashamba ya TARILI na Mashamba ya Kuzalisha Mifugo (LMUs);
kutengwa kwa hekta 199,827.3 katika Halmashauri tano za Tunduru, Mpanda, Biharamulo, Muleba na Kyerwa kwa ajili ya malisho ya mifugo ili kupunguza migogoro ya wafugaji na watumiaji wa ardhi wengine nchini; kuzalisha marobota 550,919 ya nyasi za mifugo (hay);
kuzalishwa kwa tani 12.1 za mbegu bora za malisho, kustawishwa kwa hekta 730 za mbegu za nyasi na hekta 245 za mbegu za mikunde katika mashamba ya TALIRI, LMUs-Sao Hill na Mabuki.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 154
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Aidha mashamba darasa ya malisho 67 yamestawishwa katika Halmashauri 17 za Bunda, Butiama, Chato, Itilima, Lushoto, Maswa, Mbarali, Meatu, Mpanda, Morogoro, Mufindi, Muleba, Njombe, Nkasi, Nsimbo, Rungwe na Tunduru.
Tiba na Udhibiti wa Magonjwa ya Mifugo
kuhamasisha matumizi ya dawa za kuogesha mifugo na kutoa chanjo dhidi ya Ndigana Kali ili kudhibiti kupe na magonjwa wayaenezayo;
kuendelea kudhibiti Mbung‟o na Ndorobo kwa kununua vitendea kazi ili kutokomeza ugonjwa wa Malale na Ndigana kwa Binadamu na Mifugo katika Mikoa ya Katavi, Kigoma, Manyara, Rukwa na Tabora;
kuratibu upatikanaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Kimeta;
kuratibu upatikanaji na usambazaji wa chanjo ya Kichaa cha Mbwa na kutoa elimu kwa wananchi; na
kuendelea kutekeleza Mpango Mkakati wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa hatarishi yaambukizwayo kwa binadamu kupitia wanyama
kutolewa kwa michovyo 40,352,228, kati ya michovyo hiyo, ng‟ombe ni 22,400,170, Mbuzi ni 12,836,389 na Kondoo ni 5,115,669;
Kutolewa kwa dawa lita 8,823.53 aina ya Paranex (Alphacypermethrin) na kuzigawa katika majosho 1,486 yanayofanya kazi katika Mikoa 24;
kuzalishwa kwa dozi 39,548,00 za chanjo kwa magonjwa ya Mdondo, Kimeta na Chambavu na kusambazwa kupitia vituo saba vya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania katika kanda;
Kuchanjwa kwa ng‟ombe milioni 3.9 (9.6%), mbuzi milioni 2.3 (7.8%) na mbwa milioni 0.3 (7.5%) dhidi ya magonjwa mbalimbali;
kununuliwa kwa kifaa cha kupima ubora wa dawa ya kuogeshea mifugo (HPLC) ili kudhibiti ubora wa dawa za kuogeshea nchini kupitia TVLA;
kukarabati majosho 151 katika mikoa mbalimbali nchini;
kuundwa kwa kamati 847 za kusimamia majosho na kufungua akaunti za uendeshaji;
kuendelea kutekeleza Mikakati ya kutokomeza magonjwa yanayoambukiza binadamu kutoka kwa wanyama kwa dhana ya Afya Moja (Malale, Mafua Makali ya Ndege, Kimeta, Ugonjwa wa Kutupa Mimba, Ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa na Homa ya Bonde la Ufa) ambapo vituo vinane (8) vya Kanda vya Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo (ZVC) viliimarishwa kwa kuwezeshwa katika utendaji kazi wake;
Kukarabatiwa kwa kituo cha Sumbawanga; na
Kupewa vifaa vya kielekitroniki na kutolewa kwa mafunzo juu ya
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 155
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
ufuatiliaji wa magonjwa ya mifugo kwa wataalam 108 kutoka katika Wilaya 50.
UVUVI
Kusimamia na Kuendeleza Uwekezaji katika Sekta ya Uvuvi
kujenga na kukarabati miundombinu ya uvuvi ikiwemo vituo vitano (5) vya kudhibiti ubora;
kufufua Shirika la Uvuvi (TAFICO) kwa kukunua meli mbili (2) za uvuvi; na
kuimarisha mfumo wa usimamizi wa pamoja wa taarifa zinzohusu uvuvi kulingana na matakwa ya kikanda
kuendelea na taratibu wa kupata fedha ili kununua meli mbili za uvuvi;
kutafuta fedha za kukarabati majengo na miundombinu ya TAFICO inayojumuisha mitambo ya kuzalisha barafu, gati vyumba vya ubaridi na kuzuia mmomonyoko wa ardhi;
kuzindua Menejimenti ya kusimamia shirika, kuandaa na kuutekeleza mkakati wa kufufua TAFICO, na utambuzi wa mali za shirika ambapo mpaka sasa mali zenye thamani ya shilingi bilioni 118 zimetambuliwa.
kupatikana kwa fedha kwa ajili ununuzi wa Meli ya Uvuvi kwenye maji ya Kitaifa, ukarabati wa chumba na ununzi wa mtambo wa barafu na gari maalum la kubebea samaki;
kuwezeshwa kwa vikundi 50 vya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi (BMUs) katika Wilaya za Pangani (12), Mkinga (14), Jiji la Tanga (5), Bagamoyo (9) na Lindi Vijijini (10).
kutolewa kwa mafunzo kwa maafisa uvuvi 10 wa Halmashauri na watano (5) wa Serikali Kuu;
kusambazwa kwa majiko banifu 100 katika Vijiji/Mialo ya uvuvi 16 katika Mkoa wa Kigoma;
kutoa mafunzo kwa wachakataji wa samaki 640 katika Vijiji 16 ili kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi katika Ziwa Tanganyika; na
kuwezeshwa vikundi vya ushirika vya wavuvi vya Igombe-Mwanza, Ikumba Itale-Chato, Nkasi (Ziwa Tanganyika), Migoli-Mtera na vikundi vya ufugaji samaki Peramiho (Ruvuma) kwa kupatiwa fedha na vifaa
Bandari ya Uvuvi
kufanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa bandari ya uvuvi ambayo itajengwa kati ya Mtwara, Kilwa, Tanga na Pwani
Kuendelea kufanyika kwa upembuzi yakinifu unaofanywa na Mtaalam Elekezi (kampuni za Sering Ingegneria ya Italia na Doch Tanzania Limited ya hapa nchini) katika ujenzi wa bandari ya uvuvi ambayo
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 156
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
kutegemeana na taarifa ya upembuzi yakinifu ili kuiwezesha Serikali kusimamia uvuvi wa Bahari Kuu na kupata mapato zaidi yatokanayo na uvuvi ambapo meli zinazovua zitalazimika kutia nanga katika bandari hiyo
itajengwa kati ya Mtwara, Kilwa, Tanga na Pwani. Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi unategemea taarifa ya upembuzi yakinifu ambao utawezesha Serikali kusimamia uvuvi wa Bahari Kuu na kupata mapato zaidi yatokanayo na uvuvi, ambapo meli zinazovua zitalazimika kutia nanga katika bandari hiyo.
Kuimarisha Tafiti, Huduma za Ugani na Mafunzo ya uvuvi
kuongeza udahili wa wanafunzi wa Astashahada na Stashahada kutoka 1,072 hadi 1,500 kwa mwaka;
kutoa elimu na mafunzo ya uvuvi, uchakataji na ufugaji samaki kwa nadharia na vitendo;
Kununua na kukarabati mashine na mitambo ya kuwezesha utoaji wa elimu na mafunzo ya kisasa ya uvuvi na ufugaji wa samaki.
kufanyika kwa utafiti wa kuangalia wingi wa samaki Ziwa Victoria kwa kutumia Teknolojia ya Hydro-acoustic survey;
kuimarisha upatikanaji wa takwimu za uvuvi kwa kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa takwimu kwa njia ya kielektroniki ikiwemo matumizi ya simu za viganjani ujulikanao kama e-CAS (electronic Catch Assessment Survey) ambao kwa majaribio jumla ya simu 108 zimetolewa kwa maafisa Uvuvi kutoka Halmashauri zenye maeneo ya Uvuvi katika Ziwa Victoria, Ukanda wa Bahari ya Hindi na Ziwa Tanganyika;
kutolewa kwa mafunzo ya mbinu za ukaguzi, uhakiki wa njia na vifaa vya kupimia na usimamizi wa maabara kwa watalaam tisa (9)wa Maabara ya Uvuvi-Nyegezi;
kuendelea na utafiti wa vifaa vya kuvutia samaki FADs (Fish Aggregaring Devices) katika maeneo ya Bagamoyo na Nungwi Zanzibar;
kuendelea na utafiti wa kujua wingi wa biolojia ya Kambamiti katika Pwani ya Tanzania, kuendelea na utafiti wa kupata samaki wazazi (brood stock);
kudahili wanafunzi 1,088 katika masomo ya ngazi za Astashahada na Stashahada kwenye Kampasi za Mbegani, Nyegezi na Kigoma na kutoa mafunzo kwa wananchi 1,300 kuhusu mbinu za kuvua na ukuzaji wa viumbe kupitia Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA)
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 157
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Ufugaji Samaki
Kuimarisha na kuendeleza vituo vitano (5) vya ufugaji samaki wa maji baridi vya Ruhila (Songea), Mwamapuli (Tabora), Kingolwira (Morogoro), Nyengedi (Lindi) na Nyamirembe (Chato) kwa ajili ya kuzalisha vifaranga milioni 10.
Kuendeleza vituo viwili (2) vya ufugaji samaki wa maji bahari vya Machui (Tanga) na Mbegani (Pwani) kwa ajili ya kuzalisha vifaranga milioni 3;
kuzalisha na kupandikiza vifaranga vya samaki katika malambo na mabwawa ya asili na kwenye skimu za umwagiliaji miwa na mpunga katika vituo vya Bukoba, Kilimanjaro, Mwanza na Mara
kujenga kituo Nyamirembe (Chato) ili kuongeza uzalishaji wa vifaranga;
kufanywa kwa makadirio na mchanganuo wa gharama za ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo vya Ruhila (Songea), Mwamapuli (Igunga) na Kingolwira (Morogoro);
kuendelea kuboresha kituo cha Machui (Tanga) ikiwa ni pamoja na kukiunganisha na umeme wa Tanesco;
kuandaa Mpango wa Kitaifa wa Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji- NADSP;
kuzalishwa vifaranga 17,301,076 katika vituo vya Serikali na Sekta binafsi;
kuwekwa vizimba (fish cage) 408 katika Ziwa Victoria (346), Ziwa Tanganyika (9) na malambo (53) ili kuongeza matumizi ya teknolojia stahiki katika kuzalisha viumbe maji
Kuimarisha na Kuendeleza Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi na Mazingira
kufanya doria za anga na za baharini ili kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu katika Ukanda wa Kiuchumi wa bahari ya Tanzania; na
Kushirikiana na nchi wanachama wa kamisheni ya usimamizi wa Uvuvi wa Samaki aina ya Jodari katika Bahari ya Hindi.
kuanzishwa kwa Kanda Kuu tatu za usimamizi na udhibiti wa rasilimali za uvuvi katika Ukanda wa Ziwa Viktoria, Tanganyika na Ukanda wa Pwani na kunzishwa kwa kanda ndogo mbili za Ukerewe na Sengerema;
kuimarishwa vituo 27 vilivyopo vya usimamizi wa rasilimali za uvuvi kote nchini na kusimamia hifadhi za bahari na maeneo tengefu kwa kufanya doria zenye sikukazi 677 katika maeneo yote 18 yaliyohifadhiwa ambayo ni Hifadhi ya bahari tatu na Maeneo Tengefu 15;
kufanyika kwa doria na operesheni mbalimbali zenye sikukazi 10,914 ili kuimarisha usimamizi na udhibiti wa uvuvi na biashara haramu ya mazao ya uvuvi;
kufanyika kwa kaguzi 3,155 za kuhakiki ubora na usalama wa mazao ya uvuvi maeneo ya mipakani, viwanja vya ndege na bandari.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 158
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
MALIASILI NA MISITU
Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Ikolojia ya Ardhi Oevu ya Bonde la Mto Kilombero na Mto Rufiji
Usimamizi endelevu wa ikolojia ya ardhi oevu ya Bonde la Mto Kilombero na Mto Rufiji kwa kuboresha maisha ya watu na kuhakikisha kunakuwepo na uchumi endelevu; na
Kuimarisha uwezo wa usimamizi endelevu wa sera, sheria na miongozo mbalimbali ya ikolojia ya ardhi oevu ya bonde la Mto Kilombero na Mto Rufiji.
kukamilika kwa ujenzi wa ofisi ya Maliasili katika Wilaya ya Ulanga; kukamilika kwa Ujenzi wa vituo viwili vya Askari wa Wanyamapori katika Wilaya ya Ulanga;
kuanzishwa vikundi vinne (4) vya uvuvi katika Mto Kilombero na kuviwezesha kutekeleza majukumu yake;
kurejesha maeneo yaliyoharibika kimazingira katika hali yake ya awali (hábitat restoration);
kutoa elimu kwa jamii kuhusu usimamizi na matumizi bora ya ardhi;
kufanya mapitio ya Mipango ya usimamizi na uvunaji wa misitu katika Wilaya ya Ulanga; na
Kujenga na kununua vifaa vya ofisi mbili (2) za Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ngorongoro, Utete na Rufiji (JUHIWANGUMWA) na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Ifakara, Lupiro na Mang‟ula (ILUMA) – Kilombero.
Mradi wa Kuimarisha Misitu Asilia, Mapori Tengefu na Vitendo vya Kupambana na Ujangili Nchini
Kuboresha miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege, nyumba na watumishi katika mapori ya Chome, Magamba, Mkingu, Minziro, Udzungwa na Rungwe;
Kuboresha huduma za jamii zikiwemo maji na vituo vya afya kwa jamii zinazozunguka mapori ya akiba; na
Kuongeza uwezo wa askari wanyamapori.
Kutangazwa kwa misitu mitano (5) ya Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Chome, Magamba, Mkingu, Minziro na Udzungwa Scarp kwenye Gazeti la Serikali; na
Ukarabati wa nyumba za watumishi katika hifadhi za Chome, Mlima Rungwe, Mkingu na Minziro ambapo ukarabati umefikia asilimia 90.
Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Maliasili
Kuimarisha usimamizi na uhifadhi endelevu wa maliasili katika wilaya za Loliondo, Serengeti na Pori la Akiba Selous
Kukamilika kwa utafiti wa fursa za utalii katika wilaya ya Ngorongoro;
Kuandaa mpango mkakati na miongozo ya kuwezesha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori kujiendesha;
Kutoa mizinga ya nyuki (115) kwa wananchi wa Wilaya za Serengeti (80) na Ngorongoro (35) ili kuwezesha wananchi kiuchumi na kuendeleza uhifadhi;
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 159
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kupatiwa ufumbuzi wa mgogoro wa mipaka kati ya vijiji vya Hekwe na Magatini na Hifadhi ya Serengeti;
Kutoa mafunzo kwa wananchi wa Wilaya ya Serengeti kuhusu namna ya kujilinda na wanyamapori wakali na waharibifu;
Kukamilishwa kwa Mpango wa Usimamizi wa Pori Tengefu la Kijereshi; kuimarishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) kwa kununuliwa magari na vifaa vya TEHAMA;
Kukamilisha kwa Mwongozo wa Uwindaji wa Simba; na
Kujengea uwezo Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji na Kata ambapo jumla ya Wajumbe 240 wamepatiwa mafunzo.
Mradi wa Kusaidia Uendelezaji wa Misitu Binafsi na Mnyororo wa Thamani
kujenga mazingira wezeshi ya kuendeleza misitu binafsi;
kuwezesha utayarishaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi;
kuwezesha vikundi vinavyojishughulisha na kilimo cha miti kwa kutoa elimu ya shughuli mbadala za kiuchumi zaidi ya upandaji miti. Mradi huu utatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali za Tanzania na Finland; na
Kutawezesha vikundi 120 kupanda jumla ya hekta 4,000 za miti na kuendesha mafunzo katika kituo cha Mafinga ili kuwajengea wananchi uwezo wa kupanda na kuendeleza misitu
Kuwezesha maandalizi ya mradi mpya wa kuongeza thamani mazao ya Misitu (Forestry and Value Chain);
Kukamilika kwa tafiti tano (5) kuhusu ushiriki wa sekta binafsi katika upandaji miti; na
Kupandwa kwa miche 5,500 aina ya misindano katika wilaya za Nyasa, Songea, Makete, Ludewa, Mufindi na Njombe.
Mradi wa kuwezesha Wananchi Kunufaika na Rasilimali za Misitu kwa Maendeleo ya Kiuchumi
Kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi ili kunufaika na rasilimali za Maliasili na kuzingatia matumizi endelevu - Kigoma
Kutolewa kwa hati za umiliki wa ardhi kimila 901 zitakazowapa wananchi uwezo wa kupata mikopo ya kuanzisha miradi midogo;
Kuanzishwa kwa Misitu ya Hifadhi 40 kwenye vijiji 33 kwa Wilaya za Kasulu, Kibondo na Uvinza, Kakonko;
Kuanzishwa na kupatiwa mafunzo kwa vikundi vitano (5) vya wavuvi
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 160
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
na vikundi 94 vya Wajasiriamali; na
Kujumuisha masuala ya uhifadhi na uzalishaji mali kwenye mipango ya Vijiji 20 na Halmashauri za Wilaya 6 za Uvinza, Kigoma, Kasulu, Buhigwe, Kibondo na Kakonko.
MADINI
Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini
kuendelea na ukarabati wa ofisi za madini Bariadi, Bukoba, Melerani, Musoma, Songea, Mpanda, Handeni, Kigoma na Chunya;
kuendelea na ujenzi wa ofisi za STAMICO - Dodoma na jengo la elimu Chuo cha Madini Dodoma;
kujenga vituo saba (7) vya umahiri vya mafunzo katika Mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Lindi, Mara, Mbeya na Tanga;
kuboresha mfumo maalum wa kielektroniki wa utoaji leseni na ukusanyaji wa maduhuli (Flexi Cadastre);
kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini kwa kutoa mafunzo ya usanifu wa madini ya vito (lapidary) kwa Watanzania 36 kupitia Kituo cha Jiolojia Tanzania (TGC), kumpata mwekezaji katika ujenzi wa smelter na refinery ya madini ya metaliki na kukamilisha Muswada wa Sheria ya uongezaji thamani madini na kanuni zake (The Mineral Value Addition Act and Regulations); na
kutenga maeneo 11 kwa ajili ya
Kukamilisha uandaaji wa Mwongozo wa Mpango wa Utunzaji wa Mazingira kwa wachimbaji wadogo;
Kununua Mtambo wa kuchorongea miamba ambao utatoa huduma kwa wachimbaji wadogo kwa bei nafuu kupitia Shirika la Madini la Taifa - STAMICO;
Kufanya mafunzo ya matumizi ya mtambo wa uchorongaji miamba kwa wataalam na wachimbaji wadogo kuhusu masuala ya utafiti wa madini kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini - GST na STAMICO;
Kuandaa Mpango wa Kibiashara na Mpango Mkakati wa Kituo cha Jimolojia Tanzania;
Kukamilika kwa ujenzi wa ukuta wa ofisi ya madini Moshi na ukarabati wa ofisi ya madini Nachingwea;
Kukamilika kwa ujenzi wa mgodi wa mfano na ufungwaji wa mtambo kwa ajili ya uchenjuaji wa madini ya dhahabu kwa wachimbaji wadogo katika eneo la Lwamgasa, Geita;
Kuendelea na ufungwaji wa mitambo ya uchenjuaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Katente, Geita na Itumbi, Mbeya;
Ujenzi wa vituo Saba (7) vya umahiri katika maeneo ya Bariadi, Bukoba, Musoma, Handeni, Mpanda, Chunya na Songea ambapo kati ya hivyo, vituo vya Bariadi, Musoma, Bukoba na Handeni vimekamilika;
Kumpata mkandarasi wa kujenga mitambo itakayofanikisha uongezaji thamani wa madini (smelter and refinery);
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 161
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
wachimbaji wadogo Kuboresha miundombinu ya Chuo cha Madini katika Kampasi ya Dodoma na Nzega.
Ujenzi wa jengo la wafanyabiashara wa madini (Brokers house) katika eneo la Mirerani umekamilika na ujenzi wa kituo cha pamoja (one stop centre) unaendelea; na
Kuanzisha mfumo wa masoko ya madini katika mikoa yote yenye madini ya metali na vito.
Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia - TEITI
kukamilisha na kutoa kwa Umma taarifa ya malipo ya kodi kutoka kampuni za madini, mafuta na gesi asilia kwa mwaka 2016/17;
kuendelea kujenga uwezo wa wananchi kuhoji ufanisi katika ukusanyaji na matumizi ya mapato yatokanayo na rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia; na
kuanzisha rejista ya taarifa na majina ya watu wanaomiliki hisa katika kampuni za madini, mafuta na gesi asilia
Kukamilika kwa muhtasari wa takwimu zilizowekwa katika vielelezo kwa lugha ya kiswahili na kiingereza za taarifa ya TEITI ya Mwaka 2015/16 kwa ajili ya kufanya wepesi wa kufikisha matokeo ya taarifa za TEITI kwa wadau;
Kukamilika kwa mfumo wa kieletroniki wa kuhifadhi takwimu za rasilimali za madini mafuta na gesi asilia (Dashboard) na kuelimisha wananchi kuhusu takwimu hizo;
Kutoa mafunzo kuhusu uwekaji wazi wa majina ya wamiliki wa hisa katika kampuni za madini, mafuta na gesi asilia; na
Kukamilisha marekebisho ya Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi asilia ya mwaka, 2015 na Kanuni kwa ajili ya kutekeleza sheria hiyo.
Mradi wa Dhahabu wa Buhemba
kununua mtambo wa kuzalisha dhahabu kwa kuchakata mabaki ya dhahabu (Gold tailings) na kufanya shughuli za awali na uchorongaji katika eneo la mashapo ya mwamba mgumu (Hard rock recource)
Kukamilika kwa ununuzi wa mtambo wa kuzalisha dhahabu kwa kuchakata mabaki ya dhahabu;
Kufanya shughuli za awali na uchorongaji katika eneo la mashapo ya mwamba mgumu kwenye mgodi; na
Kukamilika kwa upembuzi yakinifu katika mabaki ya dhahabu yaliyoachwa kipindi cha nyuma ambapo umebaini kuwapo takribani tani 796,400 za mabaki ya mchanga wa dhahabu yenye wastani wa kilo 852 za dhahabu.
KUFUNGAMANISHA MAENDELEO YA VIWANDA NA MAENDELEO YA WATU
Elimu, Sayansi na Teknolojia
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 162
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo katika Elimu)
Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya uendeshaji wa programu;
Kutoa motisha kwa shule za msingi na sekondari zilizofanya vizuri na zilizoongeza kiwango cha ufaulu katika mitihani ya Taifa ya Darasa la Saba na Kidato cha Nne mwaka 2018;
Kujenga madarasa 2000 na miundombinu yake katika shule za msingi na sekondari;
Kujenga mabwalo katika shule 85 za sekondari zilizopanuliwa kwa ajili ya kudahili wanafunzi wa kidato cha tano;
Kununua vifaa vya maabara awamu ya II kwa shule 1,800 za sekondari za wananchi;
Kukarabati shule kongwe 25 za sekondari; ukarabati na upanuzi wa vyuo 8 vya ualimu (Bustani, Vikindu, Mtwara Kawaida, Mtwara Ufundi, Singachini, Monduli, Bunda, na Katoke); na
Kununua magari 20 kwa ajili ya vyuo vya ualimu
Kuendelea na ujenzi wa miundombinu katika shule 504 (msingi 219 na sekondari 285) katika mikoa yote Tanzania Bara ambao unahusisha madarasa 938, mabweni 210, vyoo 2,141, nyumba 39 (2 in 1), mabwalo 76 na huduma za maji katika shule 10;
Kuendelea na ujenzi wa shule 4 mpya za msingi katika Halmashauri za Dodoma Jiji, Masasi Mji, Buhigwe na Chato;
Kukamilika kwa ujenzi wa shule ya Sekondari Maalum Patandi kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 640 ambao unahusisha madarasa nane (8), jengo la utawala, bwalo na jiko, chumba cha maabara, chumba cha TEHAMA, maktaba na bweni moja;
Kugharamiwa mafunzo kwa wanataaluma 68 kutoka vyuo vikuu vya Umma katika ngazi za shahada za uzamili (66) na uzamivu (2);
Kuendelea na maandalizi ya ukarabati wa vyuo vinane (8) vya ualimu vya Bustani, Vikindu, Mtwara Kawaida, Mtwara Ufundi, Singa chini, Monduli, Bunda na Katoke; na magari 20 yamenunuliwa kwa ajili ya vyuo vya Ualimu; na
Uboreshaji wa miundombinu ya Elimu ya Sekondari: ujenzi wa madarasa 938, mabweni 210, matundu ya vyoo 2,141, nyumba za walimu 47, majengo ya utawala 13, maabara za sayansi 22, maktaba 39 mabwalo ya chakula 79 na visima 10 vya maji zinaendelea katika Halmashauri mbalimbali.
Ukarabati wa Vyuo vya Ualimu
Ujenzi na ukarabati wa vyuo 4 vya Ualimu vya Shinyanga, Mpuguso, Ndala na Kitangali
Chuo cha Ualimu Mpuguso: Kukamilika kwa ujenzi na ukarabati awamu ya kwanza ambao umehusisha nyumba tatu za ghorofa kwa ajili ya familia 12 za walimu, nyumba moja (1) ya mwalimu isiyo ya ghorofa; nyumba 2 za ghorofa kwa ajili ya mabweni ya wanafunzi 304; na ukarabati wa nyumba moja (1) ya mwalimu. Ujenzi wa Awamu ya pili umefikia hatua ya umaliziaji ambao umehusisha majengo mawili (2) ya ghorofa yenye vyumba 16 vya madarasa,
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 163
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
maktaba, jengo la mihadhara, maabara na ukarabati wa mabweni;
Chuo cha Ualimu Shinyanga: kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ujenzi na ukarabati ambao umehusisha nyumba 1 ya ghorofa ya walimu kwa ajili ya familia 4, nyumba 1 ya ghorofa kwa ajili ya mabweni ya wanafunzi 152 na ukarabati wa nyumba nne (4) za walimu na mabweni mawili (2), na vyoo vya wanafunzi. Ujenzi wa awamu ya pili umefikia hatua ya uezekaji na ukamilishaji ambao umehusisha nyumba 2 za ghorofa zenye vyumba 16 vya madarasa, bweni moja (1) la ghorofa kwa wanafunzi 152, maktaba na jengo la mihadhara na ukarabati wa mabweni mawili (2) na bwalo la chakula;
Chuo cha Ualimu Kitangali: ujenzi kwa awamu ya kwanza na ya pili upo katika hatua za mwisho za ukamilishaji ambapo awamu ya kwanza inahusisha nyumba 10 za walimu, nyumba 1 ya Mkuu wa Chuo, na jengo la mikutano. Awamu ya pili inahusisha ujenzi wa nyumba 2 za ghorofa zenye vyumba 16 vya madarasa, maktaba, jengo la mihadhara, na majengo 2 ya ghorofa ya mabweni kwa wanafunzi 304; na
Chuo cha Ualimu Ndala: kuendelea na ujenzi wa awamu ya kwanza ambayo ipo katika hatua za msingi na unahusisha, ujenzi wa nyumba 2 za ghorofa za mabweni kwa wanafunzi 304, nyumba 2 za ghorofa za madarasa zenye vyumba 16, jengo la mihadhara, maktaba, na maabara. Awamu ya pili ya mradi ambapo utekelezaji upo katika hatua za umaliziaji na unahusisha nyumba 5 za kawaida za walimu; nyumba 2 za ghorofa za walimu kwa ajili ya familia 8; na ukarabati wa mabweni mawili (2) pamoja na vyoo vya wanafunzi.
Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu ya Msingi (MMEM) –Kuimarisha Mafunzo ya Stadi za Kusoma, Kuandika na
Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mikakati ya Sekta ya Elimu;
Kufanya tathmini ya mwisho ya pamoja ya utekelezaji wa shughuli za programu za
Kutolewa mafunzo kwa walimu wa nyongeza 402 wa Elimu Maalum yaliyotolewa katika Vyuo vya Ualimu vya Morogoro, Butimba (Mwanza) na Patandi (Arusha) ambapo walimu walipatiwa stadi za kufundishia za KKK kwa wanafunzi wasioona na wasiosikia wa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 164
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kuhesabu (KKK) LANES na Sekta ya Elimu;
Kuimarisha kitengo cha tathmini na ufuatiliaji cha Wizara katika ukusanyaji wa takwimu za programu; na
Kununua na kusambaza vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum
Darasa la I - IV kwa kutumia mtaala mpya;
Kukamilika kwa mafunzo kwa walimu wa nyongeza 1,598 wanaofundisha darasa la I na II yaliyotolewa katika vyuo vya ualimu vya Morogoro na Butimba ambapo walimu walipatiwa stadi za ufundishaji na ujifunzaji wa Stadi za KKK kwa kuzingatia mtaala mpya;
Kufanyika ufuatiliaji wa pamoja wa Programu katika sampuli ya Mikoa 5 ambao ulihusisha Halmashauri za wilaya za Liwale, Mafia, Magu, Manyoni na Monduli na kushirikisha Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, OR-TAMISEMI, pamoja na Washirika wa Maendeleo ya Elimu, na wajumbe kutoka Taasisi zisizo za Serikali zinazohusika na masuala ya Elimu; na
Kuhamasisha ushiriki wa jamii katika kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji wa stadi za KKK kupitia mtandao wa elimu (TEN – MET)
Mradi wa Huduma ya Maji, Elimu ya Afya na Usafi wa Mazingira Shuleni – SWASH
Kujenga miundombinu ya maji na vyoo katika shule za msingi 500;
Kufanya uhakiki na ufuatiliaji wa miundombinu itakayojengwa kwa kuzingatia mwongozo wa SWASH kwa kushirikiana na wadau wa programu hiyo; na
Kutoa elimu kuhusu utumiaji wa mwongozo wa SWASH kwa wathibiti ubora wa shule na waratibu wa SWASH wa Halmashauri na Mikoa.
Kukamilika kwa tathmini ya kitaifa ya Huduma ya Maji, Elimu ya Afya ya usafi wa mazingira shuleni iliofanyika katika shule za msingi na sekondari 2,228 Tanzania Bara na 156 Zanzibar ambayo ililenga kubaini hali halisi ya miundombinu ya vyoo, maji na usafi wa mazingira nchini ili kuweka mikakati ya kitaifa ya kuiboresha; na
Kukamilika kwa mafunzo ya mwongozo wa huduma ya maji, elimu ya afya na usafi wa mazingira shuleni kwa wathibiti ubora wa shule wa Halmashauri 63 za mikoa ya Njombe, Ruvuma, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Arusha, Dodoma, Tanga na Kilimanjaro kwa lengo la kuwajengea uwezo wathibiti ubora wa shule katika kufuatilia, kutathmini na kutoa ushauri kuhusu huduma ya maji, usafi wa mazingira na ujenzi wa miundombinu ya vyoo shuleni.
Mamlaka ya Elimu Tanzania - TEA
Kujenga nyumba 15 za walimu katika shule za sekondari zilizo kwenye mazingira magumu na maeneo yasiyofikika kwa
Kukamilika kwa asilimia 60 ya ujenzi wa mabweni 12 katika shule 11 za sekondari;
Kuendelea na ujenzi wa nyumba 60 za walimu katika shule 15 za
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 165
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
urahisi;
Kujenga madarasa 300 kwenye shule za msingi 60 zenye uhitaji mkubwa;
Kujenga mabweni 10 ya wanafunzi wa kike katika shule za sekondari zilizo kwenye mazingira magumu kufikika; na
Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya miradi.
sekondari; na
Kuendelea na ujenzi wa madarasa 252 katika shule 84 za msingi.
Mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa Vyuo vya Ufundi Stadi
Kujenga chuo cha ufundi stadi cha Kagera;
Kujenga karakana 2 za ufundi wa zana za kilimo na ufundi wa uungaji vyuma katika chuo cha ufundi stadi Arusha;
Kuanza ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi katika Wilaya za Chunya, Kilindi, Nyasa na Ukerewe; kukamilisha ujenzi wa madarasa 2 na mabweni 2 katika chuo cha ufundi stadi cha Wilaya ya Makete;
Kuweka vifaa vya mafunzo kwenye karakana ya Useremala katika chuo cha ufundi stadi VETA Dodoma; na
Kuboresha teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika usimamizi wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETMIS)
Kukamilika kwa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya cha Namtumbo;
Kkamilika kwa ujenzi wa karakana ya kisasa ya useremala katika Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Dodoma;
Kukamilika kwa ujenzi wa karakana za useremala, umeme wa magari na jengo la utawala katika chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Morogoro – Kihonda;
Kukamilika kwa ujenzi wa karakana ya ushonaji katika chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Pwani;
Kuendelea na ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Chato ambapo utekelezaji umefikia asilimia 48;
Kujengwa kwa miundombinu ya maji, umeme na barabara katika eneo la ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Mkoa wa Kagera;
Kuendelea na ujenzi wa mabweni mawili (2) na nyumba mbili (2) za wafanyakazi katika chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Makete;
Kuendelea na ukamilishaji wa majengo na ununuzi wa vifaa kwa ajili ya kuanzisha vyuo vya Ufundi Stadi katika wilaya za Ileje, Nkasi, Urambo, Newala, Muleba, Kasulu DC, Itilima, Ngorongoro na Babati na kuendelea na ukarabati na upanuzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Karagwe.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 166
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kuimarisha Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Elimu ya Ualimu
Kukamilisha ujenzi wa chuo cha Ufundi Stadi cha Mkoa wa Njombe;
Kuanza ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vya mikoa ya Simiyu, Geita, na Rukwa; na
Kuanza ujenzi katika vyuo 6 vya Ualimu vya Dakawa, Mpwapwa, Kleruu, Marangu, Tabora na Butimba.
Kukamilika kwa utafiti wa kubaini mahitaji ya ujuzi na utaalam katika sekta za Viwanda, Utalii na Ukarimu;
Kukamilika kwa maandalizi ya kuanza ujenzi na ukarabati katika vyuo vya Ualimu 6 vya Dakawa, Mpwapwa, Kleruu, Marangu, Tabora na Butimba;
Kuendelea na ujenzi katika vyuo vya Ufundi Stadi na Huduma (RVTSCs) vya mikoa ya Geita, Simiyu na Rukwa; na
Kuendelea na ujenzi wa mabweni mawili (2) katika Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro.
Ukarabati na Upanuzi wa Chuo cha Ufundi Arusha
Kukamilisha ukarabati na ufungaji vifaa katika karakana 5 kwa ajili ya mafunzo ya uhandisi mitambo, useremala na uhandisi magari kwa vitendo;
Kujenga bweni 1 la wanafunzi wa kike lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 250 kwa mara moja;
Kujenga na kukarabati miundombinu ya madarasa, maabara na karakana katika vituo vya mafunzo vya Kikuletwa na Oljoro; na
Kukamilisha ufungaji wa mtandao wa internet katika majengo yote ya chuo kutoka katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuboresha utoaji mafunzo kupitia TEHAMA
Kukamilika kwa ufungaji wa mashine mpya katika karakana tano (5);
Kukamilika kwa asilimia 95 ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya Kikuletwa; kukamilika kwa asilimia 85 ya ujenzi wa kituo cha kupima mitambo midogo ya kufua umeme kutokana na nguvu ya maji;
Kuendelea na ujenzi wa kituo kipya cha Kikuletwa cha kufua umeme wa MW 1.7 ambapo utekelezaji umefikia asilimia 70;
Kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa miundombinu ya kituo cha Oljoro kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo ya kilimo cha umwagiliaji; na kununuliwa kwa kompyuta 100, meza 100 na viti 200;
Kuendelea na ujenzi wa jengo la ghorofa tatu (3) linalojumuisha maabara, madarasa, ofisi na stoo; na kugharamia mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi 40 ambapo watumishi 15 (shahada ya uzamivu), watumishi 22 (shahada ya uzamili) na watumishi 3 (shahada ya kwanza).
Kuendeleza Elimu ya Ualimu
Kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa vyuo 35 vya ualimu na vifaa vya Elimu Maalum kwa vyuo vya Patandi, Mtwara Ufundi na Mpwapwa;
Kununuliwa kwa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa vitendo kwa ajili ya vyuo 35 vya Serikali;
Kununuliwa kwa kompyuta za mezani 300 na projector 100 kwa ajili ya kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 167
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kuimarisha mifumo ya TEHAMA na kununua vifaa vya TEHAMA kwa vyuo vya ualimu na kuviunganisha na Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa;
Kuendelea na ujenzi wa chuo cha Ualimu Kabanga;
Kukarabati maktaba za vyuo 8 vya Ualimu (Bustani, Vikindu, Mtwara Kawaida, Mtwara Ufundi, Murutunguru, Monduli na Bunda);
Kutoa mafunzo ya TEHAMA kwa wanafunzi 821;
Kutoa mafunzo kazini kwa wakufunzi 323;
Kuandaa kanzidata ya mfumo wa mawasiliano na utoaji taarifa za Elimu ya Ualimu;
Kuwezesha programu ya Hisabati ya Korogwe na kutoa mafunzo kwa walimu 200 wa somo la Hisabati wa shule za msingi na sekondari;
Kutoa ufadhili kwa wahitimu 500 wa vyuo vikuu wa fani za sayansi, kilimo, na ufundi kusomea postgraduate diploma ya ualimu; na
Kutoa ufadhili kwa wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Patandi kujiendeleza katika ngazi ya Shahada ya Pili katika Elimu Maalum
na kusambazwa katika vyuo vya Ualimu 18;
Kukamilika kwa miongozo 22 ya mafunzo kazini kwa wakufunzi kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa kufundisha masomo mbalimbali;
Kuendelea na maandalizi ya kuunganisha vyuo vya Ualimu katika Mkongo wa Taifa;
Kuanza kwa ujenzi wa chuo cha Ualimu Kabanga;
Kupatiwa mafunzo kazini Walimu 398 (Shule za Msingi 200 na Walimu wa Sekondari 198) wa Hisabati;
Kukamilika kwa maandalizi ya mafunzo kwa menejimenti za vyuo vya Ualimu vya Serikali; na
Kuendelea kununua vifaa vya wakufunzi na wanafunzi ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Kuimarisha Taasisi ya Elimu Tanzania
kuboresha mtaala wa kidato cha kwanza hadi cha nne na mtaala wa Elimu ya Ualimu ngazi ya cheti na stashahada;
Kuandikwa kwa vitabu vya kiada vya masomo ya Historia na Jiografia ngazi ya sekondari (O-level) na masomo ya Sayansi na Kiswahili ngazi ya sekondari (A-level) kwa kutumia mtaala wa mwaka 2005;
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 168
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kuendelea na uandishi wa vitabu vya kiada kwa kidato cha kwanza hadi cha sita, na moduli/vibutu vya Elimu ya Ualimu na kuandaa maudhui ya kielektroniki kwa darasa la kwanza na la pili;
Kutoa mafunzo kazini kwa walimu wa elimu msingi kwa kutumia mtaala ulioboreshwa;
Kurusha hewani vipindi vya vikaragosi kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi wa elimu ya awali, darasa la kwanza na la pili kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK);
Kuandika vitabu vya hadithi vya shule za msingi, kufanya uhakiki na tathmini ya vitabu vya ziada na maudhui ya kielektroniki; na
Kuandika na kuchapa mtaala, mihtasari na moduli za mafunzo kwa ngazi ya Cheti na Stashahada ya Ualimu.
Kukamilika kwa uandishi, uchapaji na usambazaji wa aina nane (8) za vitabu vya kiada kwa Darasa la Tano kwa masomo ya Hisabati, Kiingereza, Uraia na Maadili, Maarifa ya Jamii, Stadi za Kazi, Sayansi na Teknolojia na Kifaransa kwa kuzingatia mtaala wa mwaka 2015;
Kusambazwa kwa nakala 2,933,791 za vitabu hivyo kwa uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi watatu (1:3) katika Halmashauri za Mikoa mitano ya Geita, Mwanza, Kigoma, Arusha na Kilimanjaro;
Kusambazwa nakala 281,148 za Kiongozi cha Mwalimu kwa masomo hayo katika Halmashauri za Mikoa yote Tanzania Bara;
Kukamilika kwa uandishi, uchapaji na usambazaji wa nakala 391,949 za vitabu vya somo la Kiingereza kwa Kidato cha Kwanza na cha Pili kwa uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi watatu (1:3);
Kuandaliwa kwa vitabu vya kiada rafiki kwa wanafunzi wenye uoni hafifu na wasioona wa Darasa la Tatu na la Nne ambavyo vimeandaliwa katika mfumo wa maandishi makubwa (large print), nukta nundu (braille) na mchoro mguso ambapo usambazaji unaendelea.
Kuandikwa kwa Kiongozi cha Mwalimu kwa masomo matano (5) ambayo ni Kuhesabu, Kuandika, Kusoma, Afya na Mazingira, na Sanaa na Michezo kwa Darasa la Kwanza na la Pili na aina saba (7) za Kiongozi cha Mwalimu kwa Darasa la Tatu;
Kusambazwa nakala 6,286,476 za vitabu vya kiada kwa Darasa la Nne (uwiano wa 1:1) vya masomo ya Hisabati, Kiingereza, Uraia na Maadili, Maarifa ya Jamii, Stadi za Kazi, Sayansi na Teknolojia na Kifaransa katika Halmashauri za mikoa yote Tanzania Bara; na
Kusambazwa nakala 7,835,697 za vitabu aina 25 vya Hadithi kwa Darasa la Kwanza na la Pili (uwiano wa 1:3) katika Halmashauri za mikoa yote Tanzania Bara.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 169
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu
Kutoa mikopo kwa wanafunzi 123,285 wa elimu ya juu wenye kukidhi vigezo. Kati ya hao, wanafunzi wa mwaka wa kwanza ni 40,544 na wanafunzi 82,741 wanaendelea na masomo.
Kutolewa mikopo ya Shilingi bilioni 424.76 kwa wanafunzi 122,754 ambapo wanafunzi 41,234 ni wa mwaka wa kwanza na 81,520 wanaoendelea na masomo;
Kukusanywa kwa mikopo iliyoiva ya thamani ya shilingi bilioni 128.07 sawa na asilimia 81.2 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 157.7;
Kutambuliwa kwa wadaiwa wapya 14,627 na kupatiwa hati za madai sawa na asilimia 47 ya lengo la kutambua wadaiwa wapya 31,000; na
Kukaguliwa kwa waajiri 2,698 kati ya lengo la waajiri 3,426.
Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE)
kukamilisha ujenzi wa maabara ya sayansi na kompyuta
Kukamilika kwa ujenzi wa ukumbi wa mihadhara wenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,209 kwa wakati mmoja na ofisi 14 zenye uwezo wa kuchukua wahadhiri 28; na
Kuendelea na ujenzi wa maabara za Sayansi zenye uwezo wa kukaa wanafunzi 240 kwa wakati mmoja.
Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)
Kujenga jengo la makazi ya wanataaluma watafiti; na
Kujenga madarasa na kuweka mifumo ya kiusalama na miundombinu ya TEHAMA.
Kukamilika kwa uwekaji wa miundombinu ya TEHAMA katika shule za mazoezi;
Kununuliwa kwa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum; na
Kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa jengo la utawala na ofisi za wafanyakazi na utafiti ambapo utekelezaji upo katika hatua za ukamilishaji.
Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mwl. Julius Nyerere cha Kilimo na Teknolojia
Kuandaa michoro na mpango wa matumizi ya ardhi; na
Kupima ardhi na kufuatilia upatikanaji wa hati miliki za ardhi ya chuo kwa Kampasi za Butiama,
Rorya, na Serengeti
Kuendesha mafunzo kwa wakulima 455 juu ya mbinu bora za kilimo;
Kulimwa mazao mbalimbali katika shamba darasa la ekari 7; na
Kugharamiwa mafunzo watumishi wanne (4) katika shahada ya uzamili kupitia mradi wa CREATES.
Ujenzi na Upanuzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe
kuendeleza ujenzi na kuweka samani kwenye jengo la madarasa na utawala katika Kampasi ya Mbeya.
Kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa Jengo la Ardhi lenye nafasi ya ofisi 125 na madarasa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,980.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 170
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu Ardhi
Kujenga jengo la Ardhi na kuliunganisha na mfumo wa maji;
Kuendelea na ujenzi wa maabara itakayokuwa na matumizi zaidi ya moja; na
Kukarabati karakana, nyumba za watumishi na madarasa.
Kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa Jengo la Ardhi lenye nafasi ya ofisi 125 na madarasa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,980.
Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.
Kukamilisha ujenzi wa Kituo Mahiri cha magonjwa ya moyo awamu ya kwanza katika kampasi ya Mloganzila.
Kuendelea na ujenzi wa kituo mahiri cha Magonjwa ya Moyo Awamu ya Kwanza katika Kampasi ya Mloganzila ambao upo katika hatua za mwisho za ukamilishaji;
Kukamilika kwa mpango wa uzalishaji mali wa hospitali ya kufundishia na taaluma - Mloganzila; na
Kuanzishwa mifumo 6 ya kimtandao ya uendeshaji wa Chuo ambayo imeunganishwa na mfumo wa kuratibu ufundishaji na ujifunzaji – eLearning.
Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
Kujenga maktaba yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,500 kwa wakati mmoja
Kukamilika kwa michoro ya jengo la maktaba lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,500 kwa wakati mmoja; na
Kukarabatiwa kwa kafeteria na eneo la mapokezi katika kituo cha Mikutano cha Ushirika.
Upanuzi na Ukarabati wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Kujenga jengo la maktaba lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,500 kwa wakati mmoja katika Kampasi ya Kivukoni; na
Kujenga bweni la wanafunzi katika Kampasi ya Zanzibar.
Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la mihadhara lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 324 kwa wakati mmoja; na
Kukamilika kwa michoro na makadirio ya gharama za ujenzi wa maktaba katika kampasi ya Kivukoni na hosteli katika kampasi ya Zanzibar.
Ujenzi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela – Arusha (NM - AIST)
Kuanza ujenzi wa hosteli yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 kwa wakati mmoja
Kuendelea na utekelezaji wa miradi ya utafiti 33 inayojumuisha utafiti wa ugonjwa wa kimeta kwa wanyama pori na wanaofugwa, utafiti wa kuondoa sumu kuvu katika nafaka (Aflatoxin) na utafiti katika zao la ndizi ili kupata miche bora inayohimili magonjwa ya kitropiki.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 171
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Jengo la Kufundishia Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaaam - DIT
Kuweka samani za ndani, miundombinu na vifaa vya TEHAMA katika jengo jipya la DIT Teaching Tower na
Kukamilisha upanuzi wa jengo la maktaba.
Kukamilika kwa ukarabati wa jengo la madarasa mawili yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 50 kila moja katika Kampasi ya Myunga; na
Kununuliwa kwa asilimia 40 ya vifaa vya upanuzi wa jengo la maktaba.
Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - SUA
Kujenga na kukarabati miundombinu ya chuo
Kukamilika kwa ukarabati wa mabweni matano (5) ya wananfunzi yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 222 katika Kampasi ya Solomon Mahlangu na mabweni mawili (2) ya Nicholaus Kuhanga yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 924 katika Kampasi Kuu;
Kukamilika kwa ukarabati wa hosteli moja (1) iliyopo katika Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza kwa ajili ya wanafunzi wa kigeni yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 16 kwa wakati mmoja; kukamilika kwa ukarabati wa Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Wanyama iliyopo katika ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za Afya; na kuendelea na ujenzi wa maabara mtambuka yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,600 kwa wakati mmoja ambapo utekelezaji wa awamu ya kwanza umefikia asilimia 50.
Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya
Kukamilisha ujenzi wa jengo la maktaba lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,500 kwa wakati mmoja
Kukamilika kwa michoro ya ramani ya jengo la vyumba viwili (2) vya madarasa vyenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 600 kwa wakati mmoja;
Kukamilika kwa ukarabati wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika kampasi ya Rukwa; na
Kukamilika kwa asilimia 69 ya ujenzi wa jengo la maktaba awamu ya kwanza lenye uwezo wa kuchukua wananfunzi 2,500 kwa wakati mmoja.
Upanuzi na Ukarabati wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Kampasi ya Dar es salaam
Upanuzi wa hosteli za Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Kukamilika kwa ujenzi wa Maktaba ya Kimataifa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,100 kwa wakati mmoja, ukumbi wa mikutano unaochukua watu 580 na Kituo cha Utamaduni wa Kichina chenye ofisi 5 na madarasa 10 yenye uwezo wa kuchukua wananfunzi 550 kwa wakati mmoja; na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 172
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kununuliwa kwa vitabu 6,927 na mashubaka (bookshelf) kwa ajili ya kuhifadhi vitabu katika maktaba iliyojengwa.
Kukuza Stadi za Kazi kwa Ajili ya Shughuli za Kuzalisha na Kukuza Uchumi
kuendelea na utekelezaji wa Mfuko wa Kukuza Stadi za Kazi kwa kutoa ruzuku kwa ushindani kwa vyuo vya ufundi nchini; kuendelea kutoa ruzuku za masomo ya ufundi kupitia Skimu za Vocha za Mafunzo (Trainee Voucher Scheme) kwa vijana 7000 wasio na uwezo wa kujiendeleza;
kuviwezesha vyuo 20 vya Maendeleo ya Wananchi kutoa mafunzo ya ufundi kwa kuvikarabati na kuvinunulia vifaa; kuzijengea uwezo taasisi za VETA, NACTE na TCU wa kusimamia ubora ya elimu ya ufundi na stadi za kazi; na
Kuimarisha vyuo vya VETA na Elimu ya Ufundi kwa kuvinunulia vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya Uanagenzi (Apprenticeship).
Kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ukarabati na ujenzi wa vyuo 20 vya Maendeleo ya Wananchi;
Kukamilika ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu Ardhi (ARU);
Kutolewa kwa mafunzo kwa vijana 650 kutoka kaya maskini katika taasisi mbalimbali za mafunzo kulingana na mahitaji yao na vipaumbele vya Taifa;
Kuanzishwa mabaraza ya kisekta ya kusimamia maarifa kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF);
Kutolewa mafunzo kuhusu malipo kwa mfumo wa kielektroniki kwa wahasibu kutoka vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi, vyuo 35 vya Ualimu na makao makuu ya Wizara, wakaguzi 16 wa ndani, na wataalam 8 wa TEHAMA kutoka Wizarani (MoEST), NACTE, HESLB, VETA, na TCU; na
Kutolewa mafunzo kwa watumishi 304 katika nyanja za huduma kwa wateja, utunzaji nyaraka, maadili katika Utumishi wa Umma.
Mfuko wa Utafiti na Maendeleo wa COSTECH
Kuanzisha na kuendeleza atamizi za ubunifu katika Halmashauri za miji ya Mbeya na Dodoma kwa lengo la kukuza ubunifu kwa vijana 50;
Kuwatambua wagunduzi na wabunifu nchini na kuwawezesha kuendeleza ubunifu na ugunduzi wao kupitia mfuko wa MTUSATE;
Kutolewa mafunzo kwa washiriki 20 wakiwemo wasimamizi wa masuala ya Bioteknolojia katika taasisi na wizara mbalimbali;
Kuendelea kufadhili na kusimamia miradi ya utafiti katika maeneo ya kipaumbele kwa sekta za Viwanda, TEHAMA, Kilimo, Afya, Mazingira na Maliasili;
Kuwezeshwa kifedha kwa wabunifu 30 kuendeleza ubunifu wao;
Kuendelea na ujenzi na ukarabati wa maabara za utafiti katika tafiti za utafiti wa mifugo Tanga (TALIRI – Tanga), Uyole (TALIRI – Uyole), na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 173
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kufadhili miradi 20 ya ubunifu;
Kuhamasisha matumizi ya teknolojia mpya kama Bioteknolojia, Nanoteknolojia, Mekatroniksi na Bigdata;
Kuandaa vipindi na makala 42 zinazohusu masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu (STU) na kuzisambaza kupitia radio na televisheni;
Kuanzisha na kuendeleza kumbi za ubunifu katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam kwa lengo la kuchochea uanzishwaji wa kampuni za kiteknolojia ili kukuza ubunifu na kuongeza ajira kwa vijana
Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI – Sota, Musoma);
Kugharamiwa kwa miradi mipya minane (8) ya ukarabati wa miundombinu ya utafiti katika taasisi sita (6) za utafiti (NIMR, SUA, HORTI, TALIRI – Mpwapwa, MUHAS, na TVI); na
Kugharamiwa kwa miradi minne (4) ya utafiti iliyotekelezwa na TAFIRI, STAMICO na TIRDO.
Ujenzi wa Maabara ya Mionzi ya Nguvu za Atomiki
Kuanza ujenzi wa maabara Awamu ya II; kuendelea na ukaguzi wa migodi 6 inayofanya kazi;
kuendelea kukagua vituo 150 vyenye vyanzo vya mionzi;
kuendelea kusajili vituo 1,045 vyenye vyanzo vya mionzi;
kufanya kaguzi katika vituo 120 vinavyotoa mionzi isiyoainishwa; na
kufungua ofisi za Tume ya Nguvu za Atomiki katika kanda ya kati mkoani Dodoma, kanda ya nyanda za juu kusini mkoani Mbeya, na kanda ya ziwa mkoani Mwanza
Kukaguliwa kwa migodi sita (6) ya chini ya ardhi (underground mines) ambayo ni Geita Gold Mine, North Mara Gold Mine, Bulyankulu Gold Mine, Tanzanite One Limited, Stamigold Company Limited, na Buzwagi Gold Mine na kubaini kuwa ipo salama na haina madhara kwa mazingira na wafanyakazi;
Kukaguliwa na kuhakikiwa kwa vituo 590 vya vyanzo vya mionzi; kusajiliwa kwa vituo vipya 101 kwa ajili ya kuanza kutumia vyanzo vya mionzi;
Kupimwa viwango vya mionzi kwa wafanyakazi 1,663 kwenye vituo 376;
Kupimwa kwa sampuli 12,628 na kutoa vibali 12,628;
Kufunguliwa kwa ofisi ya Kanda ya Ziwa - Mwanza na ofisi ndogo saba (7) maeneo ya Kigoma, Pemba, Mtwara (Mtambaswala na Kalambo), Kagera (Kabanga), Songwe (Kasumulu) , Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) hivyo TAEC kuwa na ofisi 22 nchini; na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 174
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kununuliwa kwa vifaa 17 vya kudhibiti ubora wa machine za tiba ya mionzi na matumizi salama ya mionzi kwa ajili ya ofisi za mipakani.
Upanuzi na Ukarabati wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi – FDCs
Kujenga na kukarabati miundombinu katika vyuo 28 vya maendeleo ya wananchi.
Kuendelea na ukarabati wa awamu ya kwanza wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 20 vya Rubondo, Gera, Munguri, Chisalu, Newala, Kilwa Masoko, Ikwiriri, Mtawanya, Handeni, Mto wa Mbu, Urambo, Kasulu, Tarime, Ilula, Muhukuru, Sofi, Chilala, Kiwanda, Malampaka na Karumo ambapo ukarabati upo katika hatua za ukamilishaji.
Afya na Maendeleo ya Jamii
Mradi wa Kupunguza Vifo vya akina Mama Vinavyotokana na Uzazi
Kujenga vituo 12 vya damu salama katika Mikoa 12;
Kukarabati na kujenga wodi maalum kwa ajili ya watoto wachanga (Neonatal Care Units) katika Hospitali za Rufaa za Mikoa 7; na
Kufanya upanuzi wa wodi za wazazi na kutenga vyumba vya wagonjwa mahututi wanaotokana na uzazi katika hospitali za Rufaa za mikoa 5.
Kukamilika kwa marekebisho katika Wodi ya Wazazi na ufungaji vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora – Kitete na kujenga kichomea taka, kuweka mifumo ya gesi na vifaa tiba;
Kukamilika kwa ujenzi na marekebisho ya Wodi za Wazazi katika Vituo vya Afya vya Kitunda na Mazinge katika Wilaya ya Sikonge; na
Kukamilika kwa ujenzi na marekebisho katika Chuo cha Maafisa Tabibu Tabora ikiwemo kukamilisha mfumo wa umeme.
Mradi wa Kuboresha Hospitali za Rufaa za Mikoa
Ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma za tiba katika Hospitali za Rufaa za Mikoa, kuanzishwa na kuboresha vitengo vya dharura (Emergency Units) katika Hospitali za Rufaa za mikoa, ujenzi wa hospitali mpya za mikoa katika mikoa ya Katavi, Njombe, Geita, Simiyu, Songwe na Mara.
Simiyu - Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje na kuanza kutoa huduma; ujenzi wa msingi wa jengo la uchunguzi na jengo la mama na mtoto umekamilika ambapo hatua inayofuata ni usimakaji wa nguzo kwa ajili ujenzi wa sakafu ya pili; na kununuliwa kwa mashine 1 ya x-ray kwa ajili ya kuboresha huduma za uchunguzi wa magonjwa; na kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za uzazi.
Geita – Ujenzi wa majengo ya kutolea huduma za wagonjwa wa nje, mgahawa na sehemu ya kufulia upo kwenye hatua za mwisho
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 175
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
kukamilika na ujenzi wa jengo ya upasuaji na jengo la mionzi uko katika hatua za awali; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 91.
Njombe – Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje; kununuliwa kwa mashine 1 ya X-ray kwa ajili ya kuboresha huduma za uchunguzi wa magonjwa; kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za uzazi; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 97.
Katavi – Kuendelea na ujenzi wa jengo la wazazi, jengo la uchunguzi na jengo la utawala ambapo ujenzi umefikia hatua ya msingi; na kununuliwa kwa mashine 1 ya X-ray kwa ajili ya kuboresha huduma za uchunguzi wa magonjwa; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 96.
Shinyanga – kukamilika kwa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje na utawala; kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za uzazi; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 97.
Kwangwa (Mara) – Kukamilika kwa Jengo la wagonjwa wa nje, jengo la wazazi, jengo la uchunguzi na wodi za kulaza wagonjwa.
Manyara – Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje na utawala umefikia hatua ya upauaji na hatua inayofuata ni kuweka samani, vifaa na vifaa tiba; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 94.
Sekou Toure (Mwanza) – Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za uzazi; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 97.
Mwananyamala (Dar es Salaam) – Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za uzazi; kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za dharura na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 97.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 176
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Mawenzi (Kilimanjaro) – Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za uzazi; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 75.
Sokoine (Lindi) – Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za dharura; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 97.
Amana (Dar es Salaam) – Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za dharura; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 99.
Temeke (Dar es Salaam) – Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za dharura; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 95.
Kagera – Kuendelea na ujenzi wa jengo la kutolea huduma za dharura; na upatikanaji wa dawa muhimu 30 umeimarika kufikia asilimia 99.
Ujenzi wa Hospitali za Halmashauri na Vituo vya Afya
Ujenzi na ukarabati wa Vituo vya Afya Nchini ili kuboresha huduma za afya msingi (Primary Health Care) na kupunguza msongamano Hospitali za Rufaa za Mikoa na Taifa
Kuendelea na ujenzi wa hospitali za Halmashauri (67);
Kuendelea na ujenzi na ukarabati wa vituo vya kutolea huduma za afya 352 (zikiwemo Hospitali 9, Vituo vya Afya 304 na Zahanati 39); na
Kuendelea na ujenzi na ukarabati wa nyumba 301.
Mradi wa Ununuzi na Usambazaji wa Dawa
Kununua na kusambaza Dawa, Chanjo, Vifaa, Vifaa Tiba na Vitendanishi kwa ajili ya Vituo vya Umma vya kutolea huduma za afya nchini.
Kununuliwa kwa dawa, vifaa tiba na vitendanishi na kusambazwa katika vituo vya umma vya kutolea huduma nchini ambapo upatikanaji wa dawa muhimu aina 30 katika vituo vya kutolea huduma za afya umefikia asilimia 94.4;
Kusambazwa lita 239,020 za viuadudu vya kuangamiza viluwiluwi vya mbu katika Halmashauri zote nchini;
Kununuliwa mashine za X-ray 11 za Kidigitali ambazo zimesambazwa katika hospitali za Ruvuma, Chato, Morogoro, Simiyu, Magu, Singida, Nzega, Njombe, Bukoba, Amana na Katavi;
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 177
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kununuliwa vifaa na vifaa tiba na kusambazwa katika vituo vya afya 318;
Kununuliwa na kusambazwa mashine 8 za X-ray na viti 20 kwa ajili ya kutolea huduma ya kinywa; na
Kununuliwa kwa Digital X-rays 28 na LED Microscope 389 ambazo zimesambazwa katika mikoa ya Iringa, Kilimanjaro, Mara, Mbeya, Ruvuma, Tanga, Rukwa, Njombe, Songwe na Dar es Salaam; na
Kuanzishwa kwa mfumo wa Mshitiri katika mikoa 26 ya Tanzania Bara unaoviwezesha vituo vya kutolea huduma za afya kupata mahitaji ya vifaa, vifaa tiba, dawa na vitendanishi toka kwa wauzaji binafsi walioteuliwa pindi mahitaji yanapokosekana katika Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na kutolewa mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri na wataalam ngazi ya Wizara pamoja na watoa huduma ya afya 103 ngazi ya Taifa, 431 ngazi ya Mkoa, 540 Hospitali za Halmashauri na wafanyabiashara 142 kuhusu matumizi ya mfumo huo.
Hospitali ya Rufaa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini – Mbeya
Kuendelea na ujenzi wa jengo la ghorofa la kusimikwa vifaa vya uchunguzi vya X – ray na kununua vifaa tiba
Kukamilika kwa ujenzi wa jengo la vifaa vya uchunguzi wa mionzi;
Kukamilika kwa upanuzi wa eneo la mapokezi na jengo la huduma za uzazi na mtoto katika kitengo cha wazazi Meta; na
Kuendelea na upanuzi wa jengo la kutolea huduma; na kununuliwa kwa CT-Scan mpya.
Hospitali ya Rufaa ya Magonjwa ya Kifua Kikuu – Kibong‟oto
Kujenga jengo na kununua mashine ya CT-SCAN kwa ajili ya uchunguzi wa kifua kikuu
Kujenga mtambo wa kuzalisha hewa ya oxygen
Kununuliwa kwa mashine nne (4) za uchunguzi wa madhara yatokanayo na dawa; na
Kununuliwa kwa mashine 1 ya ultrasound kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa.
Hospitali ya Rufaa Bugando
Kununua mashine ya CT-SCAN ili kuboresha huduma za uchunguzi
Kununuliwa kwa mashine ya tiba ya mionzi aina ya Brachytherapy; na
Kukamilika kwa ujenzi wa maabara ya kisasa ya uchunguzi wa magonjwa kupitia vinasaba.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 178
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Mradi wa Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza
Kuimarisha huduma za kupambana na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza pamoja na utoaji wa chanjo na kutoa mchango wa Serikali kwa shirika la GAVI
Kununuliwa na kusambazwa kwa chanjo hadi kufikia kiwango cha uchanjaji cha asilimia 98 ya lengo kwa watoto chini ya mwaka mmoja. Chanjo hizo ni pamoja na:
Dozi 3,000,000 za BCC kwa ajili ya kuwakinga watoto wachanga na ugonjwa wa kifua kikuu;
Dozi 3,400,000 (bOPV) za kuzuia ugonjwa wa kupooza;
Dozi 3,000,000 (TT) za kuzuia ugonjwa wa pepopunda kwa mama wajawazito; dozi 5,453,400 (PCV-13) za kuwakinga watoto dhidi ya nimonia na homa ya uti wa mgongo;
Dozi 2,155,500 (Rota) za kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa kuhara; dozi 950,500 za HPV kwa ajili ya kuwakinga wasichana dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi;
Dozi 1,598,850 za chanjo ya sindano (IPV) kwa ajili ya kuzuia ugonjwa wa kupooza kwa watoto; na
Dozi 3,012,000 za Penta kwa ajili ya kuzuia magonjwa ya dondakoo, kifaduro, kupooza, homa ya ini, na homa ya uti wa mgongo.
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili - MNH
Kuendelea na ujenzim wa jengo la kutolea huduma kwa wagonjwa wa kulipia
Kukamilika kwa ukarabati wa jengo la uchunguzi maalum wa watoto wagonjwa walio mahututi pamoja na ufungaji wa vifaa tiba na kuunganishwa mfumo wa taarifa wa hospitali na mfumo wa Malipo wa Serikali GePG.
Taasisi ya Mifupa Muhimbili - MOI
Kulipa mkopo wa ujenzi kutoka NHIF
Kununua mitambo, vifaa tiba na vipandikizi kwa ajili ya jengo jipya
Kununuliwa darubini ya kisasa kwa ajili ya kufanya upasuaji wa mishipa ya fahamu na ubongo (Neurosurgeries);
Kununuliwa kwa mtambo mpya na wa kisasa aina ya Chiller kwa ajili ya kutawanya hewa kwenye vyumba vya upasuaji na Chumba cha Wagonjwa Mahututi – ICU;
Kununuliwa kwa mashine tatu (3) za kisasa aina ya ERBA XL 600, DYMIND DH 76 na COBAS e411 kwa ajili ya kupima sampuli za damu;
Kukamilika kwa ujenzi wa vyumba vitatu vya upasuaji hivyo kuongeza
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 179
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
idadi ya vyumba vya upasuaji kutoka 6 hadi 9;
Kukamilika kwa upanuzi wa eneo kubwa la mapokezi ya dharura; na
Kukamilika kwa ufungaji wa vifaa tiba mbalimbali vikiwemo MRI, CT Scan, Digital X-Ray machine, Modern Ultrasound machine na vifaa vya wodini.
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete - JKCI
Kununua vifaa tiba Kukamilika kwa ukarabati wa jengo la hospitali kwa ajili ya wodi mpya ya watoto yenye vitanda 32 vya kuhudumia watoto wenye matatizo ya moyo; na
Kuboreshwa kwa huduma za famasia kwa kutoa dawa muhimu kwa matibabu ya moyo kwa asilimia 95.
Ukarabati na Ujenzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii
kukarabati majengo na miundombinu katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vya Mlale, Uyole na Misungwi
Kuendelea na ukarabati wa hosteli, kumbi za mihadhara, madarasa, majengo ya utawala na nyumba za watumishi katika vyuo vya Rungemba, Mlale, Misungwi, Monduli, Ruaha, Buhare na Uyole; na
Kukamilika kwa ujenzi wa fensi katika Chuo cha Rungemba na ukarabati wa karakana katika Chuo cha Mabughai.
Uwezeshaji Wanawake – UNDP
kufanya tathmini ya utendaji wa Dawati la Jinsia katika Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala;
kufanya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya jinsia katika sekta tano; kuanzisha kanzidata ya jinsia; na
kuandaa ripoti ya nchi kwa miaka miwili ya utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Kuondoa Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake
Kutolewa kwa mikopo ya Shilingi bilioni 2.05 kwa wanawake wajasiriamali 3,035 kupitia Dirisha la Wanawake katika Benki ya TPB;
Kutolewa kwa mikopo ya uwezeshaji wanawake, Shilingi bilioni 11.128 inayotokana na asilimia 4 ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa vikundi 4,898 vyenye wanawake wajasiriamali 44,210;
Kuwezeshwa kwa vikundi 583 vya wanawake vyenye wanawake wajasiriamali 11,833 kutoka mikoa 15 kupata masoko ya huduma na bidhaa wanazozalisha, uzoefu na teknolojia rahisi na rafiki kupitia maonesho ya biashara ya kitaifa na kimataifa; na
Kutolewa kwa mafunzo kwa wanawake wajasiriamali 444 kuhusu stadi za ujasiriamali, huduma ya hifadhi ya jamii, fursa za kiuchumi, uboreshaji wa huduma na bidhaa wanazozalisha, teknolojia rahisi za uzalishaji wa bidhaa na urasimishaji wa biashara.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 180
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Maendeleo ya Awali ya Mtoto
kuhamasisha uanzishwaji na uimarishaji wa vituo vya jamii vya maendeleo ya awali ya mtoto katika Halmashauri 186;
kuratibu uanzishwaji na utendaji wa mabaraza ya watoto katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara; na
kuwezesha programu za kuzuia ukatili dhidi ya watoto
Kuendelea kutolewa kwa elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya watoto katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa;
Kuongezeka kwa idadi ya watoto waliopatiwa huduma ya simu bure (Na. 116) kutoka watoto 493 (2017/18) hadi watoto 3,833 (2018/19);
Kutolewa mafunzo kuhusu malezi chanya kwa watoto ambapo walishiriki wazazi na walezi 635 katika ngazi ya familia kutoka halmashauri 132;
Kuanzishwa kwa vikundi vya malezi 1,184 katika halmashauri 15 za mikoa 7;
Kusajiliwa kwa vituo 146 vya kulelea watoto walio chini ya miaka mitano (Day Care Centres) ambapo watoto 149,093 (Ke 76,094 na Me 72,999) waliandikishwa;
Kutolewa kwa mafunzo kuhusu Programu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwa walezi 970 katika vituo vya kulelela watoto mchana kutoka Arusha, Temeke, Ubungo, na Ilala; na
Kuundwa kwa kamati za ulinzi na usalama wa mtoto na mwanamke katika mikoa 26, Halmashauri 184, kata 2,490 kati ya 4,420 na Vijiji 7,900 kati ya 16,626.
Kuwezesha Huduma za Ustawi wa Jamii
kuboresha majengo na miundombinu katika makazi ya Wazee na mahabusu za Watoto na kuimarisha shughuli za ulinzi wa mtoto nchini
Kutambuliwa kwa watoto 389,012 waishio katika mazingira hatarishi hivyo kufikisha idadi ya watoto 1,495,049;
Kutolewa kwa kadi za bima ya afya kwa watoto 900 wanaoishi katika makao ya watoto;
Kuendelea kusajili makao ya watoto ambapo leseni 64 za usajili zilitolewa;
Kuwezeshwa upatikanaji wa huduma za msingi za malazi, chakula, mavazi, matibabu na elimu kwa watoto 13,420 (Ke 6,651 na Me 6,769) waishio katika makao ya watoto yanayomilikiwa na Serikali na taasisi binafsi;
Kutolewa kwa huduma za chakula, malazi, mavazi, matibabu na elimu
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 181
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
kwa watoto 467 (Ke 49 na Me 418) katika mahabusu 5 za watoto walio katika mkinzano na sheria;
Kuendelea kutekeleza programu ya marekebisho ya tabia kwa watoto walio katika mkinzano wa kisheria ambapo watoto 64 (Ke 7 na Me 57) walichepushwa kutoka katika mfumo rasmi wa haki jinai; na
Kuendelea kutoa huduma za malezi ya kambo na kuasili watoto ambapo watoto 70 (Ke 36 na Me 34) walipata huduma hizo;
Kutambuliwa kwa wazee 750,622 kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya matibabu bure ambapo wazee 247,705 wamepatiwa kadi za matibabu bure;
Kuendelea kutolewa huduma za msingi za chakula, malazi, mavazi na matibabu kwa wazee wasiojiweza 510 (Ke 234 na Me 276) katika makazi 17 ya wazee; na
Kutambuliwa kwa watu wenye ulemavu 405,426 na kupatiwa huduma za afya.
Mpango wa Uimarishaji wa Mifumo ya Taarifa za Ustawi wa Jamii
Kuimarisha mfumo wa Taarifa za masuala ya Ustawi wa Jamii
Kuweka mfumo wa kieletroniki wa ukusanyaji na utunzaji taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi na wale waishio na kufanya kazi mitaani katika Halmashauri 147 kati ya 184; na
Kununuliwa na kusambazwa kwa kompyuta, mashine za kurudufu na modemu 101 kwenye Mikoa 23 na Halmashauri 73 kwa ajili ya matumizi ya mfumo wa kieletroniki wa Taarifa za Ustawi wa Jamii.
Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
Kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa kuongeza idadi ya watumiaji na upatikanaji huduma
Kuboreshwa kwa mfuko ili kuruhusu watumiaji kupata huduma za matibabu ya rufaa hadi katika hospitali za rufaa za Mikoa; na
Kukamilika na kuanza kutumika kwa kanzidata ya utunzaji wa taarifa za wanachama nchi nzima.
Maji na Usafi wa Mazingira
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 182
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
programu ya kuboresha usambazaji wa maji safi na usafi wa mazingira jiji la Dar es Salaam
Kujenga matenki na kulaza mabomba ya kusambaza maji kutoka mitambo ya Ruvu Chini na Ruvu Juu katika Jiji la Dar es Salaam na miji ya Kibaha, Bagamoyo na maeneo ya Mkuranga;
Kukarabati miundombinu ya usambazaji maji ili kupunguza upotevu wa maji katika jiji la Dar es Salaam;
Upanuzi wa mtambo wa bomba kuu la kusambaza maji na ujenzi wa matenki ya Kimara na ulipaji wa fidia kwa wakazi wanaopisha ujenzi huo; na
Kuanza ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya uondoaji maji taka katika Jiji la Dar es Salaam kwa kujenga mabwawa ya kutibia maji taka katika maeneo ya Mbezi Beach, Jangwani na Kurasini.
Kuendelea na ujenzi wa matenki na ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji ambapo utekelezaji umefikia asilimia 97 ya upanuzi wa mtandao wa maji katika jiji la Dar es salaam na maeneo ya Bagamoyo, Kibaha na Mlandizi ambayo yamesambaziwa maji kutoka miradi mikubwa ya Ruvu Juu na Chini.; na kupatikana kwa mkandarasi kwa ajili ya ununuzi na ufungaji wa dira za maji pamoja na vifaa vya uboreshaji wa huduma za maji.
Mradi wa maji wa Kimbiji na Mpera
Kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji kutoka visima vya Kimbiji na Mpera katika maeneo yanayohudumiwa na DAWASA ambayo hayana mtandao wa mabomba hususan Kigamboni, Temeke, Mbagala na Mkuranga
kukamilika kwa visima 19 kati ya 20 vilivyopangwa kuchimbwa katika eneo la Kimbiji na Mpera;
kuanza maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza huduma ya maji kwa wananchi kutoka katika visima vitano vya awali vya Kimbiji.
Maji kutoka Ziwa Victoria
Kujenga bomba kuu la maji kutoka ziwa Victoria kwenda miji ya Nzega, Igunga, Tabora na Sikonge; na
Kukamilisha usambazaji maji katika miji ya Tinde, Kagongwa, Isaka; Kwimba,
ujenzi wa miundombinu ya maji katika miji ya Tabora, Igunga, Uyui na Nzega pamoja na vijiji 89 vilivyo pembezoni mwa bomba Kuu umefikia asilimia 68.5;
kazi ya ulazaji wa bomba la kusambazia maji katika miji ya Isaka, Tinde na Kagongwa imekamilika kwa asilimia 87.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 183
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Malampaka, Sumve, Malya, Kishapu, Kolandoto na Maganzo
Miradi ya maji kitaifa kukamilisha upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya maji katika maeneo yanayohudumiwa na miradi ya kitaifa ya Makonde (Mtwara), Wanging‟ombe (Njombe), Chalinze (Pwani), Mugango-Kiabakari (Mara), na Handeni Trunk Main
kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya maji hususan katika ulazaji wa mambomba, upanuzi na ukarabati katika miradi ya kitaifa ya Chalinze (Pwani) utekelezaji umefikia asilimia 79.5 ikihusisha pamoja na kazi nyingine ujenzi wa matanki, upanuzi wa mtandao wa mabomba na upanuzi wa kidakio;
mradi wa Wanging‟ombe (Njombe) ambao umefikia asilimia 85 za ukarabati na kuwezesha kukamilika kwa matanki 44 ya kuhifadhi maji na mabirika 59 ya kunyweshea mifugo pamoja na kuendelea kumalizia ukarabati wa chanzo cha Mbukwa;
miradi ya Mugango - Kiabakari (Mara) na Handeni Trunk Main usanifu wa kina umekamilika na taratibu za kuwapata makandarasi wa ujenzi zinaendelea.
Mradi wa Maji Masasi – Nachingwea
Ujenzi wa mtambo wa kusafisha maji kukamilika kwa ukarabati wa mradi ambapo wananchi 24,077 katika baadhi ya maeneo wameanza kusambaziwa maji; na
kuanza ujenzi wa mtambo wa kutibu na kusafisha maji.
Kuboresha Huduma za Maji Vijijini
Kukamilisha ujenzi wa miradi inayoendelea kwa kila halmashauri na kuanza ujenzi wa miradi mipya katika halmashauri zote;
Kukarabati mradi wa maji wa Ntomoko; na
Kujenga miundombinu ya maji katika maeneo ya Dodoma, Singida, Shinyanga, Tabora, Arusha, Pwani, Manyara, Mtwara na Songwe;
Kujenga miundombinu ya kusambaza maji kutoka visima vilivyochimbwa na kukarabati mabwawa na miradi isiyofanya kazi katika
kukamilika kwa miradi 198 na kufanya jumla ya miradi yote iliyokamilika kufikia 1,659 ambapo vituo vya kuchotea maji vimeongezeka kufikia 131,370 na kuhudumia wananchi 25,359,290;
miradi 653 ya maji vijijini inaendelea kutekelezwa ikiwa katika hatua mbalimbali katika Halmashauri nchini;
mradi wa Same – Mwanga - Korogwe miundombinu ya msingi inaendelea ambapo bomba kuu la kusafirisha maji, kitekeo cha maji, mtambo wa kusafisha maji na matanki ya kuhifadhi maji, maabara na eneo la kuhifadhia dawa za kutibu maji vimekamilika.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 184
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
halmashauri; na
Kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya maji katika mradi wa Same - Mwanga na Korogwe.
Kuboresha Huduma za Maji Mijini
Upanuzi wa miundombinu iliyopo na kukamilisha shughuli zinazoendelea za miradi ya maji katika miji mikuu ya mikoa mipya ya Geita (Geita), Simiyu (Bariadi), Njombe (Njombe), Katavi (Mpanda) na Songwe (Vwawa); na
Ujenzi, upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya maji katika miji midogo, miji mikuu ya wilaya itakayowezesha kuunganisha wateja wapya 110,000; na
Kujenga magati ya maji 272.
Upatikanaji wa huduma za maji Jijini Dar es Salaam umefikia asilimia 85, katika mikoa mingine asilimia 80, miji midogo asilimia 64 na vijijini asilimia 64.8;
Ujenzi wa miradi ya maji katika miji mikuu ya mikoa mipya umeendelea kutekelezwa na kufikia hatua zifuatazo: Geita (umekamilika), Njombe (asilimia 95); na Songwe (asilimia 90);
Ukamilishaji wa miradi ya maji katika Miji ya Wilaya na Miji midogo ya Misungwi, Lamadi, Magu, Longido, Orkesumet unaendelea pamoja na miradi ya matokeo ya haraka (quickwins) katika miji 57; na
Mradi wa uondoaji majitaka Jijini Dar es Salaam katika eneo la Jangwani na Mbezi Beach unaendelea ambapo Mtaalamu Mshauri atakayesimamia kazi hiyo amepatikana. Aidha, ulipaji wa fidia katika eneo la Kurasini umekamilika na taratibu za kuanza kazi ya upembuzi yakinifu zinaendelea.
Kuimarisha Maabara na Bodi za Maji za Mabonde
Ujenzi na ukarabati wa maabara na ofisi za maji za mabonde
kuimarishwa kwa kujengwa na kukarabatiwa kwa Ofisi za maji za mabonde kama ifuatavyo: Ruvuma na Pwani ya Kusini (asilimia 90), Ziwa Nyasa (asilimia 50), Ziwa Rukwa (asilimia 65), Bonde la Kanda ya Kati (asilimia 95) na ujenzi wa ofisi ndogo za katika Bonde la Rufiji katika maeneo ya Mkoji na Kimani (asilimia 65);
Ujenzi na ukarabati wa Maabara ya Maji ya Dar es Salaam umefikia asilimia 99. Vile vile, vifaa vya upimaji wa rasilimali za maji vimetolewa kwa mabonde ya Mto Rufiji na Wami Ruvu kwa ajili ya kuongeza tija katika mabonde hayo.
VIJANA NA AJIRA
Programu ya Kukuza Ujuzi Kuimarisha nguvu kazi iliyo katika Soko la Kutolewa kwa mafunzo ya kilimo cha kitalu nyumba kwa vijana
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 185
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Nchini ajira kiujuzi ili kuwezesha kufikiwa kwa uchumi wa viwanda kwa kuongeza ufanisi na tija katika uzalishaji mali na utoaji wa huduma; na
Kuwezesha vijana kujiajiri au kuajirika katika soko la ndani na la nje na hivyo kufikia mahitaji ya nchi ya uchumi wa kipato cha kati
18,800 kwa lengo la kuwapatia vijana ujuzi stahiki ili waweze kujiajiri na kuajiriwa;
Kutolewa mafunzo kwa vijana 10,443 ya kurasimisha ujuzi uliopatikana kwa mfumo usio rasmi kwa fani za ufundi wa magari, useremala, uashi, upishi, huduma za vyakula na vinywaji, ufundi umeme, uchomeleaji, ufundi bomba, uchorongaji vipuri na ushonaji nguo kupitia vyuo vya ufundi VETA wanapata mafunzo; na
Kutolewa kwa mafunzo ya vitendo kwa wahitimu 136 wa elimu ya juu kupitia viwanda na kampuni mbalimbali ya umma na sekta binafsi
Mfuko Wa Maendeleo Ya Vijana
Kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu;
Kuimarisha utoaji wa Mikopo kwa Vijana mmoja mmoja au vikundi vya uzalishaji mali ili kukuza mitaji kwa ajili ya kuimarisha au kuanzisha miradi mipya ya kiuchumi inayowawezesha kupata kipato na hivyo kujitegemea kwa kujiajiri wenyewe.
Kutolewa kwa mikopo nafuu yenye thamani ya Shilingi bilioni 4.2 kwa vikundi vya vijana 755, vyenye wanachama 3,661 katika Halmashauri 128 za Tanzania Bara;
Kuanzishwa kwa SACCOS 127 za Vijana kati ya 184 zinazotarajiwa kuanzishwa hadi kufikia mwaka 2020;
Kutolewa kwa mashine 4 za kutengeneza matofali na mtaji wa Shilingi 500,000 kwa kila halmashauri kwenye halmashauri 168 nchini. Aidha, vijana 6,720 wamepata ajira ya moja kwa moja na vijana 1,905 wamepata ajira zilizotokana na utekelezaji wa programu ya utengenezaji wa matofali ya bei nafuu
HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
Upanuzi wa Usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
kuanza ujenzi wa jengo la utangazaji na utawala Makao Makuu Dodoma;
kuanzisha chaneli ya utalii kwa ajili ya kutangaza maliasili nchini; na
kununua magari 11 ya utangazaji, utafutaji na uandishi wa habari
kuendelea kupanua usikivu wa redio ambapo umeongezeka kutoka wilaya 87 mwaka 2017 hadi wilaya 102 Machi 2019;
kukamilika kwa usanifu wa Jengo la Makao Makuu ya TBC Jijini Dodoma litakalo husisha jengo la Utangazaji na Utawala;
uanzishaji wa Chaneli ya Tanzania Safari inayotangaza vivutio vya utalii; kuanzishwa kwa mifumo ya kielekroniki hususan tovuti na programu tumizi (protu au App); na
kuratibiwa kwa jumla ya vipindi 17 vya TUNATEKELEZA, vipindi hivyo vilihusisha Wizara 16 na Mikoa miwili (2).
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 186
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika
kuendelea na ukarabati wa Makao Makuu ya Programu na kufanya utafiti na kuhifadhi nyaraka kidijiti katika maeneo yaliyotumika katika harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika.
kuendelea kukarabati jengo lililokuwa likitumiwa na Ofisi iliyokuwa ya Kamati ya Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika;
kuorodheshwa kwa maeneo 255 ya ukombozi wa Bara la Afrika pamoja na kukusanywa kwa vifaa mbalimbali 6,782 vya historia;
Ujenzi wa Eneo Changamani la Michezo – Dar es Salaam na Dodoma
kuanza ujenzi wa uwanja wa ndani na jumba la maonesho la michezo Dar es Salaam na kuendelea na ujenzi wa kiwanja cha mpira wa miguu Dodoma.
Dar es Salaam: kuendelea kwa ukarabati katika Uwanja wa Taifa ambapo vyumba vya wachezaji kubadilishia nguo pamoja na kukamilika kwa chumba cha “Antidopping”; kuendelea kwa ukarabati wa chumba cha waandishi wa habari; ujenzi wa paa la watu Maalum (VVIP)
Dodoma: kuendelea kwa maandalizi ya ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Dodoma kwa kubainisha barabara kwa kuwekwa vibao na nguzo za tahadhari dhidi ya wavamizi; na kukamilika kwa upembuzi yakinifu, “topographical survey”, tathmini ya mazingira, “geotechnical Survey” na maandalizi ya mchoro wa uwanja.
Ujenzi wa Chuo cha Michezo cha Malya
kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi watakaohamishwa kupisha mradi na kujenga vituo vitatu vya shule za michezo
kudahiliwa kwa wanafunzi 141; kununuliwa kwa matenki sita (6) ya kuhifadhia maji yenye ujazo wa lita 5,000 kila moja.
HIFADHI YA MAZINGIRA NA MABADILIKO YA TABIANCHI
Usimamizi Endelevu wa Matumizi ya Ardhi ya Bonde Nyasa
kuendeleza uhifadhi endelevu wa bonde la Ziwa nyasa na Tanganyika; na
kujenga uwezo wa mifumo ya usimamizi endelevu wa ardhi na rasilimali asili.
Kufundisha wawezeshaji 20 kwa Wilaya za Makete, Kyela, Mbinga, Nyasa na Ludewa zinazotekeleza mradi;
Uanzishwaji wa vikundi vitatu vya wakulima katika wilaya zinazotekeleza mradi;
Kukamilika kwa Mpango wa Matumizi bora ya ardhi katika vijiji 15 katika wilaya zinazotekeleza mradi;
Uandaaji wa vitalu vya miche ya miti na uanzishwaji wa mashamba darasa katika Wilaya za Ludewa, Kyela na Mbinga; na
Ununuzi wa vifaa vitakavyotumika wakati wa utekelezaji wa mradi.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 187
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Mradi wa Kuwezesha Mfuko wa Mazingira
kuimarisha Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Mazingira;
Kuendelea na maandalizi ya marekebisho ya Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 ili kuwezesha Mfuko wa Mazingira kufanya kazi kwa ufanisi na ipo katika ngazi ya maamuzi.
Mradi wa Kukabiliana na Changamoto za Kimazingira-Pwani ya Dar es Salaam Kutokana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi
Kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya athari ya tabianchi katika Pwani ya Dar es Salaam
Kukamilika kwa ujenzi wa mifereji ya maji iliyoharibiwa na mafuriko yenye urefu wa mita 550;
Kupanda hekari 40 za miti ya mikoko katika wilaya ya Temeke katika maeneo ya Tundwi, Songani na Pembemnazi; na
Kuendelea kwa tathmini ya uwezo wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mradi wa Kujenga Uwezo wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi katika maeneo ya Pwani
Kuhimili kwa mabadiliko ya tabianchi kwa kujenga uwezo
Kukamilika kwa ujenzi wa ukuta wa kingo za bahari katika eneo la Pangani kwa mita 610
Kuendelea kwa ujenzi wa awamu ya pili eneo la urefu wa mita 340;
Kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa kuvuna maji ya mvua katika Shule ya Matipwili Bagamoyo;
Kukamilika kwa ujenzi wa matanki 10 katika wilaya ya Bagamoyo na kuendelea kwa usimikaji wa Pampu za kuvuta maji na uunganishwaji wa umeme; na
Usafishaji wa maeneo yaliyopandwa mikoko katika Delta ya Rufiji ili kupanda maeneo ambayo mikoko haikuota vizuri unaendelea kufanyika na hekari 120 kati ya 208 zimepandwa.
Miradi ya Ujenzi wa Mazingira Wezeshi kwa Uendeshaji Biashara na Uwekezaji
Miundombinu
Reli
Ukarabati wa Njia Kuu ya Reli
Kuondoa reli zote nyepesi na kuweka reli mpya zenye uzito wa ratili 80 kwa yadi kati ya Dar es Salaam na Isaka.
Ukarabati unaendelea ambapo:
Dar es Salaam – Isaka (970) utekelezaji umefikia asilimia 13. Ukarabti unatarajiwa kukamilika Juni 2020
Kuboresha eneo la kupakia/kupakua mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam na kukarabati vituo vya kuhudumia mizigo vya Ilala na Isaka
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 188
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Mfuko wa Maendeleo ya Reli
Ufufuaji wa reli ya Tanga – Arusha
Kununua vichwa vya treni
Kukarabati mabehewa 200
Kupokelewa kwa Shilingi bilioni 123.2 ambapo Shilingi bilioni 38 zilitumika kama sehemu ya malipo ya awali kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati kwa standard gauge ya kutoka Dar es salaam hadi Morogoro. Aidha, jumla ya Shilingi bilioni 59.6 zilitumka kununua vichwa 11 vya treni kwa ajili ya njia kuu.
Ufufuaji wa Njia ya Reli ya Tanga – Arusha (km 439)
Kufufua njia ya reli ya Tanga – Arusha (km 439)
Shilingi bilioni 2 zilitumika kwa ajili ya ufuafuaji wa njia ya reli ya Tanga – Arusha (km 439) ambapo hatua iliyofikiwa ni:
kukamilika kwa kipande cha Tanga – Mombo (km 129) ambacho kimeanza kufanya kazi ya kusafirisha mizigo;
kipande cha Mombo – Same (km 124) kipo katika hatua za mwisho kukamilika ambapo ukarabati wa njia ya reli umekamilika na kazi inayoendelea kwa kipande hiki ni ujenzi wa madaraja 7; na
Kuendelea na ukarabati wa kipande cha Same – Arusha (km 186) kwa kubadili reli na mataruma, kurejesha madaraja na makalvati, kukarabati stesheni, na kufungua mifereji ya maji ya mvua (Drainage system).
Kwa ujumla ukarabati wa Reli ya Tanga – Arusha (439) na umefikia asilimia 80 unatarajiwa kukamilika kabla ya Desemba, 2019.
Ukarabati wa Mabehewa Ukarabati wa mabehewa 200 Kuendelea na ukarabati wa mabehewa ambapo hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ukarabati wa mabehewa 15.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 189
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Ukarabati wa Miundombinu ya Reli ya TAZARA
Ukarabati na uimarishaji wa miundombinu ya njia kuu ya reli iliyopo; Kununua Traction Motor 90 kwa ajili ya injini 15 zitakazokarabatiwa;
Matengenezo na ukarabati wa vichwa vya teni vilivyopo, mitambo, mabehewa ya mizigo na ya abiria;
Ukarabati wa majengo ya karakana ya Dar es Salaam, mitambo, vifaa na mashine mbalimbali ikijumuisha karakana ya Mbeya, kiwanda cha kokoto na uzalishaji wa mataruma ya zege cha Kongolo;
ukarabati wa mabehewa 21 ya kusafirisha abiria katika treni za mjini Dar es Salaam na treni ya Udzungwa inayo hudumia kati ya stesheni za Mlimba – Kidatu - Makambako; na
kufanya upembuzi yakinifu wa kujenga mchepuko wa njia ya reli kati ya Mlowo na Magamba.
Kufanyika matengenezo makubwa ya njia kwenye sehemu zilizowekewa kazato la mwendokasi ya jumla ya kilometa 82.5;
Ukarabati wa mabehewa ya mizigo 85 na mahehewa ya abiria 4;
Kubailisha mataruma ya zege 12,827 na mataruma ya mbao 2,708;
Ununuzi wa vipuri vya Injini vinavyojulikana kwa jina la Traction Motor, na mitambo (Excavator, Dumper Track na Drill Rig) ya kusaidia uzalishaji wa kokoto na mataruma ya zege katika mgodi wa Kongolo. Vifaa hivyo vimeanza kuanza kuwasili kwa awamu ambapo mwezi Aprili 2019 Drill Rig imeshawasili;
Ununuzi wa vichwa vya treni vya njia kuu vine (4), Injini za Sogeza nne (4), mashine za uokoaji mbili (2), forklift sita (6), winchi nne (4), mabehewa ya abiria 18, mataruma ya mbao 30,000, viberenge vitano (5), saruji ya kutengenezea mataruma ya zege kwenye kiwanda cha kongoro,
BARABARA NA MADARAJA
Barabara za Lami Zinzofungua Fursa za Kiuchumi
Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupilo - Mahenge /Malinyi - Londo - Lumecha/Songea (km 499)
Kuendelea na ujenzi sehemu za Kidatu - Ifakara (km 66.9)
kuendelea na ujenzi kwa sehemu ya Kidatu – Ifakara (km 66.9).
Kwa upande wa sehemu ya Ifakara – Lupilo - Mahenge /Malinyi - Londo - Lumecha/Songea (km 396), Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi kwa kiwango cha lami.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 190
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Barabara ya Tabora - Ipole - Koga - Mpanda (km 370):.
Kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu za Tabora -Sikonge (km 30), Usesula - Komanga (km 115.5), Komanga – Kasinde (km 112.8) na Kasinde – Mpanda (km 111.7).
kujengwa kwa barabara kwa kiwango cha lami kwa sehemu za Tabora – Sikonge (km 30) ambapo utekelezaji umekamilika;
kuendelea na ujenzi katika maeneo ya Usesula- Komanga (km 115.5) ) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 12.91, Komanga – Kasinde (km 112.8) asilimia 18.26, na Kasinde – Mpanda (km 111.7) asilimia 15.94.
Barabara ya Makutano - Natta – Mugumu (km 125)/Loliondo - Mto wa Mbu (km 213):
Kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami katika barabara ya Makutano – Sanzate (km 50) na Waso - Sale Jct (km 50) na kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya Sanzante – Natta – Mugumu (km 85)
Kufikia asilimia 74 ya ujenzi katika barabara ya Makutano - Natta – Mugumu (km 125) sehemu ya Makutano - Sanzate (km 50);
Kuendelea na hatua za kumpata mkandarasi wa ujenzi kwa sehemu ya Senzate - Natta - Mugumu (km 85); na
Kuendelea kwa ujenzi wa barabara ya Mto wa Mbu – Loliondo sehemu ya Wasso - Sale Junction (km 49) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 25.15.
Barabara ya Manyoni - Itigi – Tabora (km 259.7).
Kulipa sehemu ya madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri wa ujenzi wa sehemu za Manyoni – Itigi – Chaya (km 89.35) na Tabora - Nyahua (km 85); kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Nyahua – Chaya (km 85.4)
Kukamilika kwa ujenzi wa sehemu ya Tabora – Nyahua (km 85) na Manyoni - Itigi - Chaya (km 89.35); na
Kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Nyahua – Chaya (km 85.4). ambapo utekelezaji umefikia asilimia 26.
Barabara ya Itoni – Ludewa - Manda (km 211):
Kuendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha zege sehemu ya Lusitu – Mawengi (km 50).
Kuendelea kwa ujenzi wa kiwango cha lami na zege katika sehemu ya Lusitu – Mawengi (km 50) ambapo utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 20.14.
Barabara ya Handeni - Kibereshi – Kibaya - Singida (km 460):
Kuanza ujenzi wa barabara ya Handeni - Kibereshi – Kibaya - Singida
Kukamilika kwa usanifu wa kina na kuanza taratibu za kutafuta fedha kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Barabara ya Dodoma – Mtera - Iringa (km 260):
Kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya michepuo ya Iringa (Iringa
Kukamilika kwa mradi wa barabara ya Dodoma –Mtera – Iringa;
Kuanza taratibu za kumpata mkandarasi na kutafuta fedha kwa ajili
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 191
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Bypass 7.3) ya ujenzi wa mchepuo wa barabara ya Iringa (Iringa Bypass km 7.3).
Barabara ya Dodoma – Babati (km 243.80):
Kulipa sehemu ya madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri wa ujenzi wa sehemu za Dodoma - Mayamaya (km 43.65), Mayamaya - Mela (km 99.35), Mela - Bonga (km 88.80) na
Kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya mchepuo wa Babati (Babati Bypass km 12).
Kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo ambayo makabidhiano yalifanyika Oktoba 2018; na
Kuendelea na taratibu za kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya kazi ya upembuzi na usanifu wa kina wa barabara ya mchepuo wa Babati (Babati Bypass – km 12).
Barabara ya Mbeya - Makongolosi - Rungwa – Itigi - Mkiwa (km 171.9)
Kulipa sehemu ya madai ya makandarasi na Mhandisi mshauri wa barabara wa sehemu ya Mbeya - Lwanjilo (km 36) na sehemu ya Lwanjilo – Chunya (km 36);
Kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Chunya – Makongolosi (km 43); na kuanza ujenzi wa sehemu ya Itigi - Mkiwa - Noranga (km 56)
Kuendelea na ujenzi wa sehemu za Chunya – Makongorosi (km 43) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 20.6; na
Kuendelea na taratibu za kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara sehemu ya Makongorosi – Rungwa - Itigi - Mkiwa (km 413).
Barabara ya Kigoma - Kidahwe - Uvinza – Kaliua - Tabora (km 389.7):
Kulipa sehemu ya malipo ya Makandarasi waliojenga miradi ya Daraja la Kikwete katika Mto wa Malagarasi na barabara za maingilio (km 48), barabara za Kidahwe – Uvinza (km 76.6), Ndono – Urambo (km 52), Tabora – Ndono (km 42) na Kaliua -Kazilambwa (km 56);
Kuendelea na ujenzi sehemu ya Urambo –Kaliua (km 28); na
Kuanza ujenzi wa kwa kiwango cha lami sehemu ya Uvinza - Malagarasi (km 51.1)
Kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya Urambo - Kaliua (km 28) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 35; na
Kuanza maandalizi ya kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu za Uvinza - Malagarasi (km 51.1) na Kazilambwa - Chagu (km 36).
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 192
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
na sehemu ya Kazilambwa - Chagu (km 42)
Barabara ya Mtwara - Mingoyo - Masasi - Songea - Mbamba Bay (km 1,470.9):
Kulipa sehemu ya mwisho ya madai ya Makandarasi na wahandisi washauri wa ujenzi wa sehemu za Tunduru - Matemanga (km 59), Matemanga - Kilimasera (km 68.2) na Kilimasera - Namtumbo (km 60);
Kuendelea na ujenzi wa barabara za Mbinga - Mbamba Bay (km 66); Mtwara – Mnivata (km 50); kufanya maandalizi ya ujenzi wa barabara za Masasi - Nachingwea (km 45), Nanganga – Ruangwa - Nachingwea (km 107), Likuyufusi –Mkenda (km 122.5), Kitui - Lituhi (km 90);
Ukarabati wa barabara ya Mtwara –Mingoyo – Masasi (km 200); na
Kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Nachingwea – Liwale (km 130)
Kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya Mbinga - Mbamba Bay (km 66) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 8.2 na Mtwara – Mnivata (km 50) asilimia 42.7;
Kuendelea na taratibu za kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Masasi - Nachingwea – Nanganga (km 96).;
Kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara ya Nanganga - Ruangwa - Nachingwea (km 107) ;
Kusainiwa mkataba wa ujenzi kwa barabara ya Kitui – Lituhi (km 90);
Kuendele na maandalizi ya nyaraka za zabuni za kumpata mkandarasi wa ujenzi wa barabara ya Likuyufusi - Mkenda (km 122.5)
Kuendelea na taratibu za kupata kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Mtwara - Mingoyo - Masasi (km 200); na
Kusainiwa mkataba wa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Nachingwea - Liwale (km 130).
Barabara Zinazounganisha Tanzania na Nchi Jirani
Barabara ya Sumbawanga - Matai - Kasanga Port (km 112):
Kujenga barabara ya Sumbawanga - Matai - Kasanga Port (km 112) na kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya Matai – Kasesya (km 50)
Kukamilisha asilimia 80.5 ya kazi ya ujenzi kwa sehemu ya Sumbawanga - Matai - Kasanga Port (km 112); na
Kuendelea na taratibu za manunuzi za kumpata mkandarasi wa ujenzi kwa sehemu ya Matai - Kasesya (km 50).
Barabara ya Marangu - Tarakea - Rongai -
Kulipa madeni ya mkandarasi na mhandisi mshauri wa barabara ya KIA - Mererani;
Kukamilika kwa barabara ya Arusha - Moshi - Holili (sehemu ya Sakina - Tengeru na mchepuo wa Arusha – km 56.51);
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 193
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kamwanga /Bomang‟ombe - Sanya Juu (km 330.31)
kuendelea na ujenzi wa barabara za Arusha – Moshi - Holili (sehemu ya Sakina-Tengeru na mchepuo wa Arusha – km 56.51) Sanya Juu – Kamwanga (sehemu ya Sanya Juu – Alerai, km 32), Kwa Sadala – Masama - Machame Junction (km 16), Kiboroloni – Kikarara – Tsuduni - Kidia (km 10.8), Kijenge - Usa River (km 20); na
Kuendelea na maandalizi ya upanuzi wa sehemu ya Tengeru – Moshi – Himo (km 105) pamoja na ujenzi wa mizani ya Himo
Kuendelea na ujenzi kwa sehemu za Sanya Juu - Elerai (km 32.2) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 92;
Kusainiwa mikataba na kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara za Kwa Sadala - Masama - Machame Junction (km 16), Kiboroloni - Kikarara - Tsuduni - Kidia (km 10.8), na km 2.6 katika barabara ya Kijenge - Usa River (km 14); na
Kuanza maandalizi ya nyaraka za zabuni kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa kazi ya upanuzi wa barabara sehemu ya Tengeru - Moshi - Himo (km 105) na ujenzi wa mizani ya Himo.
Barabara ya Isaka - Lusahunga (km 533)
Kulipa sehemu ya madai ya mkandarasi na mhandisi mshauri wa sehemu ya Isaka - Ushirombo (km 132);
Kuendelea na ukarabati sehemu ya Ushirombo - Lusahunga (km 110) na ujenzi wa kituo cha Pamoja cha Ukaguzi - OSIS cha Nyakanazi;
Kuanza ukarabati wa sehemu ya Lusahunga – Rusumo (km 91);na
Kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Nyakahura – Kumubuga - Murusagamba na Kumubuga – Rulele - Kabanga Nickel (km 141)
Kufikia asilimia 74.8 ya kazi ya ukarabati kwa kiwango cha lami sehemu ya Ushirombo – Lusahunga (km 110);
Kuendelea na ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Ukaguzi (One Stop Inspection Station – OSIS) cha Nyakanazi ambapo utekelezaji umefikia asilimia 60;
Kukamilika kwa usanifu wa kina wa barabara za Lusahunga - Rusumo (km 91) na Nyakasanza - Kobero (km 59) ili zijengwe upya kwa kiwango cha lami katika sehemu korofi za barabara hizi; na
Kuendelea na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara za Nyakahura - Kumubuga - Murusagamba na Kumubuga - Rulenge - Kabanga Nickel (km 141).
Barabara ya Sumbawanga - Mpanda - Nyakanazi (km 517.4):
Kulipa sehemu ya madai ya Makandarasi na Wahandisi washauri wa sehemu za Sumbawanga – Kanazi (km 75), Kanazi - Kizi – Kibaoni (km 76.60) na Sitalike – Mpanda (km 36);
Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Mpanda - Mishamo (km 100) sehemu ya Mpanda - Ifukutwa - Vikonge (km 35) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 66.3;
Kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya Kibaoni – Sitalike (km 71); na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 194
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Mpanda – Ifukutwa – Vikonge (km 30);
Kuanza maandalizi ya ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya Kibaoni – Sitalike (km 71) na Vikonge – Magunga – Uvinza (km 159);
Kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Namanyere – Katongoro - New Kipili Port (km 64.5)
Kuendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Namanyere - Katongoro - New Kipili Port (km 64).
Barabara ya Nyanguge - Musoma, na Michepuo ya Usagara - Kisesa na Bulamba - Kisorya (km 495.9):
Kulipa sehemu ya madai ya mkandarasi wa barabara ya Simiyu/Mara Border – Musoma (km 85.5); na Usagara – Kisesa (Mwanza Bypass km 17);
Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Nansio –Kisorya – Bunda - Nyamuswa (sehemu ya Kisorya – Bulamba (km 51); ukarabati wa barabara ya Makutano – Sirari (km 83)
Upanuzi wa barabara ya kwenda uwanja wa ndege wa Mwanza (km 12);
Kufanya mapitio ya usanifu wa kina kwa sehemu ya Nyamuswa – Bunda - Bulamba (km 55); na
Kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Musoma – Makojo – Busekela (km 92) na ukarabati wa sehemu ya Nyanguge - Simiyu/Mara Border (km 100.4).
Kukamilika kwa ukarabati wa barabara ya Makutano - Sirari (km 83) na upanuzi wa barabara ya kuelekea uwanja wa ndege wa Mwanza (km 12);
Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Nansio - Kisorya - Bunda - Nyamuswa sehemu ya Kisorya - Bulamba (km 51) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 55;
kuendelea na taratibu za kuwapata makandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya Musoma - Makojo - Busekela (km 92) na ukarabati wa sehemu ya Nyanguge - Simiyu/Mara Border (km 100.4); na
Kuendelea na mapitio ya usanifu wa kina kwa barabara ya Nyamuswa - Bunda - Bulamba (km 55).
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 195
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Barabara ya Mwigumbi - Maswa - Bariadi - Lamadi (km 171.8):
Kulipa sehemu ya madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri wa barabara ya Bariadi - Lamadi (km 71.8) na Mwigumbi - Maswa (km 50)
Kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya Maswa - Bariadi (km 49.7)
Kuendelea kwa ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya Maswa - Bariadi (km 49.7) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 40.
Barabara ya Kidahwe - Kasulu – Kibondo - Nyakanazi (km 413):
Kuendelea na ujenzi kwa sehemu za Kidahwe – Kasulu (km 63) na Nyakanazi – Kakonko (km 50);
Kuanza ujenzi sehemu ya Nduta – Kibondo – Kabingo (km 61.84) na barabara ya kupitia Kibondo mjini
Kuendelea na ujezi wa barabara sehemu za Kidahwe - Kasulu (km 63) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 70, na Nyakanazi - Kibondo (km 50) asilimia 60;
Kukamilika kwa usanifu wa kina na kutangazwa zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kabingo – Kibondo – Kasulu – Manyovu (km 260); na
Kuendelea na taratibu za kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa barabara sehemu ya njia panda ya Nduta - Kibondo mjini (km 25.6).
Barabara ya Usagara - Geita - Buzirayombo – Kyamyorwa (Km 230):
Kulipa sehemu ya malipo ya Makandarasi kwa sehemu ya Uyovu - Bwanga (km 43), kuendelea na ujenzi wa barabara ya Bwanga - Biharamulo (km 67); na
Kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Geita - Bulyanhulu Jet (km 58.3) na Bulyanhulu Jet - Kahama (km 61.7).
Kukamilika kwa ijenzi wa barabara za Bwanga - Biharamulo (km 67); na
Kukamilika kwa nyaraka za zabuni kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa ujenzi wa barabara za Geita - Bulyanhulu Junction (km 58.3) na Bulyanhulu Junction - Kahama (km 61.7).
Barabara za Mikoa
Ujenzi wa km 36.51 za barabara za mikoa kwa kiwango cha lami; na ukarabati wa km 606 .12 kwa kiwango cha changarawe
Kujenga km 12.43 za barabara za mikoa kwa kiwango cha lami na kukarabati km 128.5 za barabara za mikoa kwa kiwango cha changarawe.
Barabara za Kupunguza Msongamano jijini Dar es Salaam (km 169.66)
Kulipa sehemu ya madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri wa miradi ya: o Kimara - Kilungule – External (km 9) o Mbezi – Malambamawili – Kinyerezi -
Kuendelea na ujenzi wa barabara ya Kimara Korogwe - Maji chumvi (km 6), Tegeta Kibaoni - Wazo Hill – Goba – Mbezi Mwisho (km 20) sehemu ya Madale - Goba (km 5), Banana - Kitunda - Kivule - Msongola (km 14.7) sehemu ya Kitunda - Kivule (km 3.2) na Maji
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 196
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Banana (km 14) sehemu ya Kifuru – Malambamawili - Msigani (km 4)
o Tegeta – Kibaoni - Wazo Hill – Goba - Mbezi (Morogoro road) sehemu ya Mbezi Mwisho – Goba (km 7)
o Tangi Bovu - Goba (km 9), Kimara Baruti – Msewe - Changanyikeni (km 2.6)
o Kibamba – Kisopwa – Kwembe - Makondeko (km 14.66) sehemu ya Kibamba –Mlonganzila (km 4)
o Ardhi – Makongo - Goba (km 9) sehemu ya Goba - Makongo;
Kuendelea na ujenzi wa barabara za: o Kimara – Kilungule - External (km 9),
sehemu ya ya Kimara – Kilungule - Majichumvi (km 6);
o Mbezi – Malambamawili – Kinyerezi – Banana (km 14), sehemu ya Msigani (km 2); na
o Tegeta Kibaoni - Wazo Hill – Goba (km 13), sehemu ya Madale - Goba (km 5);
Kuendelea na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara ya Banana – Kitunda – Kivule - Msongola (km 14.7);
kuanza ujenzi wa barabara za Kibamba – Kisopwa – Kwembe – Makondeko (km 14.66), sehemu ya Mloganzila - Mloganzila Citizen (km 4); Maji Chumvi - Chang‟ombe – Barakuda (km 2.5) na Mji Mwema -
Chumvi – Chang‟ombe – Barakuda (km 2.5);
Kuendelea na taratibu za manunuzi za kumpata mkandarasi wa kujenga barabara za Kibamba - Kisopwa – Kwembe – Makondeko (km 14.66) sehemu ya Mloganzila - Kisopwa (km 1), Mwai Kibaki (km 9.1), Kawe Round about - Garden Road Junction (km 2.9), Kongowe - Mji Mwema - Kivukoni (km 25.1);
Kukamilika kwa usanifu wa kina kwa barabara ya Mji Mwema – Kimbiji (km 27); na
Kuendelea na upanuzi wa barabara ya Kimara – Kibaha (km 19.2) kuwa njia nane
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 197
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kimbiji; na
Kuanza upanuzi wa barabara ya Mwai Kibaki (km 9.1) na Kongowe - Mji Mwema - Kivukoni (km 25.1).
Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka.
Kuanza ujenzi wa miundombinu ya Mabasi yaendayo haraka awamu ya pili, ya tatu na nne
Awamu ya Kwanza: Kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi Desemba, 2015 ambapo ulihusisha ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) katika barabara za Kimara – Kivukoni, Magomeni – Morocco na Fire – Kariakoo yenye jumla ya kilometa 20.9
Awamu ya Pili: kukamilisha maandalizi ya kutekeleza mradi ambao utahusisha ujenzi wa miundombinu katika barabara za Kilwa, Kawawa, Sokoine, Gerezani, Bandari na Chang‟ombe zenye urefu wa kilometa 20.3; wananchi na taasisi 90 kati ya 105 wamelipwa fidia ya shillingi bilion 28.52 kati ya shilingi bilioni 34.19;
Awamu ya Tatu: Kuendelea na hatua za maandalizi ya utekelezaji ikiwemo uthamini na uhakiki wa madai ya wananchi watakaopisha mradi ambapo watu 78 wameshafanyiwa tathimini; pia Serikali imetoa eneo la Gongo la Mboto, eneo la ndani la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere (JNIA), na eneo la Banana karibu na Ofisi za tcaa kwa ajili ya utekelezaji mradi. Mradi utahusisha barabara za Azikiwe na Maktaba, Bibi Titi, Uhuru na Nyerere hadi Gongo la Mboto, na kituo kikuu cha mabasi Kariakoo, Shaurimoyo na Uhuru kupitia Buguruni hadi TAZARA zenye jumla ya urefu wa kilometa 23.6; na
Awamu ya Nne: Kuendelea na taratibu za manunuzi za kumpata mhandisi mshauri wa kufanya usanifu. Mradi utahusisha barabara za Ali Hassan Mwinyi na Bagamoyo hadi Tegeta pamoja na barabara ya Sam Nujoma (Ubungo - Mwenge) zenye jumla ya km 25.9. Mradi huu unatarajiwa kufadhiliwa na Benki ya Dunia.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 198
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Ujenzi wa Barabara za Juu (Flyover) jijini Dar es Salaam
Kuendelea na ujenzi wa „fly over‟ ya TAZARA na Interchange ya Ubungo;
Kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kuboresha makutano ya barabara katika maeneo ya KAMATA, Magomeni, Mwenge, Tabata/Mandela, Morocco, Buguruni makutano ya barabara za Kinondoni/Ally Hassan Mwinyi na Kenyata na Selander (AH Hassan Mwinyi/UN Road Jet) na
Kuanza maandalizi ya ujenzi wa Mabey Flyovers katika jiji la Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza
Kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya juu (flyover) katika makutano ya TAZARA (Mfugale flyover);
Kuendelea na ujenzi kwa mradi wa Interchange katika makutano ya Ubungo ambapo utekelezaji umefikia asilimia 28; na
Kuendelea na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara maeneo ya Fire (Morogoro/United Nations), Magomeni (Morogoro/Kawawa), Mwenge (Sam Nujoma/New Bagamoyo Road), Tabata/Mandela, Morocco (Ali Hassan Mwinyi/ Kinondoni), Buguruni (Mandela/ Uhuru), Kinondoni (Kinondoni/Ali Hassan Mwinyi) na Selander (Ali Hassan Mwinyi/ United Nations).
Barabara za Vijijini na Mijini
Ujenzi na ukarabati wa barabara za Mijini na Vijijini
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) kuendelea na matengenezo ya kawaida ya barabara za lami, changarawe na udongo ambapo kilomita 5,565.3 za barabara zimekamilika pamoja na ujenzi na ukarabati wa madaraja 167, Makalvati makubwa (Box Culverts) 27, drift 59 na mifereji ya maji yenye urefu wa mita 51,347;
Kukamilisha ujenzi wa kilomita 151 za barabara kwa kiwango cha changarawe pamoja na madaraja 3 na Makalvati makubwa 42 katika Halmashauri za Wilaya za Iramba, Kyela, Kyerwa, Rungwe, Bahi, Gairo, Kishapu, Bbati, Mpwapwa, Magu, Busokelo, Bariadi, Kondoa, Kisarawe, Kibiti, Ushetu, Songwe, na Halmashauri ya Jiji la Dodoma; pia Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inaendelea na ukamilishaji wa daraja la Tagamenda na Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero imekamilisha ujenzi wa barabara ya Chita hadi Melela. Miradi inatekelezwa chini ya Programu ya Uboreshaji wa Barabara Vijijini chini ya ufadhili wa DfID;
Kukamilisha ujenzi wa kilometa 219.6 za barabara zimejengwa
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 199
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
(kilomita 21.3 kwa kiwango cha lami na kilomita 198.3 kwa kiwango cha changarawe) katika Halmashauri za Wilaya za Chamwino, Kilolo, Kondoa, Kisarawe, Songea, Mbinga, Mwanga, Mbulu, Kongwa, Mbogwe, Busokelo, Kalambo, Iringa, Ludewa, Hanang, Kiteto, na Manispaa ya Temeke, kupitia Programu ya Road Transport Sector Policy Support Programme-RTSPPSP II (chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya); na
Ujenzi wa kilomita 152.1 za barabara kwa kiwango cha changarawe katika Halmashauri za Wilaya za Kongwa, Kiteto, Mvomero na Kilombero kupitia Programu ya Feed the Future inayofadhiliwa na Serikali na USAID
Ujenzi wa Madaraja
Ujenzi wa Madaraja Makubwa
Kulipa sehemu ya madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri wa ujenzi wa daraja la Magufuli (Morogoro), daraja la Kavuu (Katavi);
Kuanza ukarabati wa daraja la Kirumi (Mara);
Kuendelea na ujenzi wa madaraja ya Magara (Manyara), Sibiti (Singida), Ruhuhu (Ruvuma), Momba (Rukwa), Mlalakuwa (Dar es Salaam), Lukuledi (Lindi), Mara (Mara) na Mkenda (Ruvuma);
Kuanza ujenzi wa madaraja ya New Wami (Pwani), Selander (Dar es Salaam), Msingi (Singida), Sukuma (Mwanza), Simiyu (Mwanza);
Kuendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa daraja la Kigongo/Busisi
Kukamilika kwa ujezni wa Daraja la Mlalakuwa (Dar es Salaam), Momba (Rukwa), Sibiti (Singida), na Lukuledi;
Kuendelea na ujenzi wa madaraja ya Mara (Mara) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 85, Ruhuhu (Ruvuma) asilimia 75, na Mangara (Manyara) asilimia 48;
Kuanza ujenzi wa Daraja Jipya la Selander na barabara unganishi zenye urefu wa km 5.2;
Kuanza maandalizi ya ujenzi wa madaraja ya New Wami (Pwani), Msingi (Singida), Sukuma (Mwanza), Simiyu (barabara ya Simiyu – Mwanza), Kigogo/ Busisi(Mwanza), Mkundi (Morogoro), Mtera (Dodoma) na Malagarasi Chini (Kigoma);
Kuanza maandalizi ya ukarabati wa daraja la Kirumi (Mara); na
Kufikia hatua mbalimbali za utekelezaji katika manunuzi wa vyuma vya madaraja ya dharura.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 200
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
(Mwanza);
Kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa daraja la Mtera (Dodoma) na Malagarasi Chini (Kigoma)
Daraja la Nyerere na Barabara Unganishi (km 6.9):
Kuendelea na ujenzi wa barabara unganishi za Kigamboni (Daraja la Nyerere) – Vijibweni (km 1.5);
Kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara za Tungi – Kibada (km 3.8) na Kibada – Mjimwema (km 1.6)
Kuendelea na ujenzi wa barabara unganishi za Kigamboni (Daraja la Nyerere) – Vijibweni (km 1.5) ambapo utekelezaji umefikia asilimia 92.
Kuendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara za Tungi – Kibada (km 3.8) na Kibada – Mjimwema (km 1.6).
Usafiri Majini
Ujenzi wa Maegesho ya Vivuko
Upanuzi wa maegesho ya Kigamboni,
Ujenzi wa maegesho ya Bwina, Bukondo na Zumacheli katika kivuko cha Chato - Nkome,
Ujenzi wa maegesho ya Nyamisati - Mafia na
Ujenzi wa jengo la abiria na ofisi ya kivuko cha Lindi - Kitunda
Kukamilika kwa upanuzi wa jengo la abiria katika maegesho ya Kigamboni na maegesho ya Bwina katika kivuko cha Chato - Nkomeae;
Kuendeea na ujenzi wa jengo la abiria na ofisi ya kivuko cha Lindi – Kitunda ambapo utekelezaji umefikia asilimia 80; na
Kuanza maandalizi ya ujenzi wa maegesho ya Nyamisati – Mafia.
Ununuzi wa Vivuko Vipya Kukamilisha malipo ya ununuzi wa kivuko kipya cha Magogoni – Kigamboni;
Kuendelea na ujenzi wa vivuko vipya vya Kigongo - Busisi na Nyamisati - Mafia
Kukamilika kwa ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo – Busisi; na
Kupatikana kwa mkandarasi ambaye ameanza maandalizi ya ujenzi wa kivuko kipya cha Nyamisati - Mafia.
Ukarabati wa Vivuko Kukamilisha malipo ya kazi ya ukarabati wa kivuko MV Pangani II, MV Sengerema, MV Kigamboni na MV Misungwi
Kukamilika kwa ukarabati wa kivuko cha MV Pangani II;
Kuendelea kukarabati vivuko vya MV Sengerema ambapo utekelezaji umefikia asilimia 40, MV Kigamboni asilimia 40, na MV Utete asilimia 90; na
Kupatikana kwa Mkandarasi wa ujenzi wa MV Misungwi.
Ununuzi na Ukarabati wa Kuendelea na ujenzi wa meli mpya katika Kuendelea na Ujenzi wa meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 201
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Meli katika Maziwa Makuu ziwa Victoria na Tanganyika; na
Kuendelea na ukarabati wa meli za MV Victoria, MV Butiama, MV Liemba, MV Umoja, MV Serengeti na MV Songea
1,200 na tani 400 za mizigo katika ziwa Victoria; na ujenzi wa chelezo;
Ukarabati wa meli ya MV Victoria na MV Butiama unaendelea.
Makandarasi kwa ajili ya ukarabati wa meli za MV. Umoja na MV. Serengeti zilizopo katika ziwa Victoria wamepatikana na uandaaji wa mikataba kwa ajili ya ukarabati wa meli tajwa umekamilishwa na inatarajiwa kusaniniwa kabala ya Julai 2019;
Kwa upande wa Ziwa Tanganyika, Kampuni ya Meli - MSCL inatekeleza Ujenzi wa Meli Mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400, ambapo uandaaji wa mikataba kwa ajili ya ujenzi wa meli hiyo pamoja na ukarabati wa meli ya MV Liemba umekamilika na inatarajiwa kusaniniwa kabala ya Julai 2019;
Ujenzi wa meli moja mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na mizigo tani 200 unaendelea ambapo utekelezaji umefikia asilimia 86; na kukamilika kwa ujenzi wa matishari mawili katika Ziwa Nyasa.
Bandari
Bandari ya Dar es Salaam Kuendelea na kazi ya kuboresha Gati Na. 1 hadi 7; na kuongeza kina na upana wa lango la kuingilia na kutokea meli, pamoja na kuongeza kina cha sehemu ya kugeuzia meli
Kukamilika kwa ujenzi wa Gati Na.1 na kuanza kutumika;
Kuanza kwa ujenzi wa Gati Na. 2 sambamba na kuongeza kina chake; na
Ujenzi wa Gati la Ro-Ro unaendelea na upo katika hatua ya ujenzi wa sakafu ngumu ya gati.
Kwa ujumla uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam umefikia asilimia 50.
Bandari ya Tanga Kukamilisha kwa ukarabati na kuongeza kina cha Gati Namba 2, ukarabati wa barabara kuelekea lango Na. 2; na
Kukamilisha mapitio ya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa bandari ya Mwambani.
Kuendelea na ukarabati wa maegesho ya meli na sehemu ya kupakulia shehena; na
Kukamilika kwa ukarabati wa miundombinu ya barabara kuelekea lango Na. 2.
Ukarabati wa maegesho umefikia asilimia 86.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 202
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Bandari ya Mtwara Kuendelea na ujenzi wa gati moja lenye urefu wa mita 300,
kuboresha mfumo wa usalama,
kukarabati barabara na maegesho ya kuhudumia shehena,
kuboresha maegesho ya meli na
Kukarabati eneo la gati Na.3.
kuendelea na ujenzi wa gati la mita 300 la kuhudumia shehena mchanganyiko ambapo kwa ujumla utekelezaji umefikia asilimia 50.
Bandari ya Mbegani - Bagamoyo
Kuendelea na majadiliano na wawekezaji waliokuwepo
Majadiliano na wawekezaji waliokuwepo yaani Kampuni ya China Merchant Holdings Intenational Limited na State General Reserve Fund (SFRF) ya Serikali ya Oman yamesitishwa baada ya wawekezaji hao kuweka masharti yasiyokuwa na maslahi kwa Taifa. Aidha, majadiliano hayo yanaweza kuendelea iwapo wawekezaji hao wataondoa masharti hayo yasiyo na maslahi kwa Taifa.
Bandari za Maziwa Makuu Kukamilisha ujenzi na ukarabati wa magati katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa pamoja na miundombinu ya usalama.
Ziwa Victoria: kuendelea na ujenzi wa gati za Nyamirembe - Chato na Magarine ambapo utekelezaji umefikia asilimia 30 na asilimia 54 kwa mtiririko huo na ujenzi wa Bandari ya Lushamba umefikia aslimia 80.
Ziwa Tanganyika: kukamilika kwa asilimia 90 wa ujenzi wa gati la Kalya/Sibwesa na asilimia 25 katika gati la Lagosa.
Ziwa Nyasa: kuendela na ujenzi wa gati la Ndumbi. Aidha, ujenzi wa magati ya Mbamba Bay, Manda na Matema upo katika hatua za mwisho za manunuzi.
Bandari kavu katika eneo la Ruvu
Kuendelea na ujenzi wa bandari kavu katika eneo la Ruvu
Kukamilika kwa ujazaji wa kokoto katika eneo lenye ukubwa wa hekta 20.8; na
Kuendelea na ujenzi wa reli ya kuunganisha bandari kavu na reli ya kati iliyopo ambapo utekelezaji umefikia asilimia 70.
USAFIRI WA ANGA
Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius
Kuendelea na ujenzi wa jengo jipya la abiria (Terminal III);
Kukamilika kwa asilimia 96 ya ujenzi wa jengo jipya la abiria (Terminal III); na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 203
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Nyerere
Kuanza ukarabati wa jengo la pili la abiria na kulipa fidia kwa wananchi waliohamishwa kupisha utekelezaji wa mradi
Kuendelea na kazi ya kuunganishwa umeme wa gridi ya Taifa.
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro
Kufanya usanifu wa kina na kuanza ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege na ujenzi wa barabara ya kiungio,
Ufungaji wa taa za kuongozea ndege na ukarabati wa maegesho ya magari
Kukamilisha maeneo ambayo hayakujumuishwa katika ukarabati uliofanyika awali ambapo shughuli zinazoendelea ni taratibu za manunuzi za kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya usanifu wa kina wa ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege.
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato
Kuendelea na usanifu wa kina na kuanza maandalizi ya ujenzi,
Kulipa fidia kwa mali zitakazoathiriwa na utekelezaji wa mradi
Kuendelea na usanifu wa kina na kuanza maandalizi ya ujenzi; na
Kulipa fidia kwa mali zitakazoathiriwa na utekelezaji wa mradi.
Kiwanja cha ndege cha Mwanza
Kuanza ujenzi wa jengo jipya la abiria,
Kuendelea na upanuzi wa maegesho ya ndege, ujenzi wa jengo la mizigo, uzio wa kiwanja pamoja na maegesho ya ndege za mizigo,
Ujenzi wa jengo la kuongozea ndege, kituo cha umeme, maegesho ya magari, kufunga taa za kuongozea ndege na ujenzi wa mfumo wa kuondoa maji ya mvua kiwanjani
Kuendelea na upanuzi wa maegesho ya ndege, ujenzi wa jengo la mizigo, uzio wa kiwanja pamoja na maegesho ya ndege za mizigo;
Kuendelea na ujenzi wa jengo la kuongozea ndege, kituo cha umeme, maegesho ya magari, kufunga taa za kuongozea ndege; ujenzi wa mfumo wa kuondoa maji ya mvua kiwanjani; na
Kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la abiria.
Kiwanja cha ndege cha Mtwara
Kukarabati jengo ya abiria, maegesho ya ndege, kufunga taa na mitambo ya kuongozea ndege, ujenzi wa majengo ya kuongozea ndege, maegesho ya magari na barabara za kuingia na kutoka pamoja na uzio wa viwanja
Kuendelea na kazi ya ukarabati wa barabara ya kutua na kuruka ndege, viungio, maegesho ya ndege, jengo la abiria, jengo la kuongezea ndege, barabara ya kuingia kiwanjani, maegesho ya magari;
Ufungaji wa taa na mitambo ya kuongozea ndege; na
ujenzi wa uzio wa kiwanja.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 204
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kiwanja cha ndege cha Kigoma, Kiwanja cha ndege cha Tabora, Kiwanja cha ndege cha Sumbawanga Kiwanja cha ndege cha Shinyanga
Kujenga majengo ya abiria, maegesho ya ndege, kufunga wa taa na mitambo ya kuongozea ndege, ujenzi wa majengo ya kuongozea ndege, maegesho ya magari na barabara za kuingia na kutoka pamoja na uzio wa viwanja
Kupatikana kwa wahandisi washauri na kuendelea na taratibu za manunuzi za kumpata mkandarasi atakayetekeleza mradi wa kuboresha viwanja hivyo.
Viwanja vya Ndege vya Mikoa
Ujenzi wa viwanja vya ndege vya mikoa ya Geita, Iringa, Ruvuma, Lindi, Tanga, Mara, Simiyu pamoja na kiwanja cha Lake Manyara;
Kukarabati viwanja vingine vya mikoa; na
Kukarabati jengo la abiria pamoja na kukamilisha ulipaji wa fidia kwenye kiwanja cha ndege cha Dodoma
Kukamilika kwa maandalizi kwa ajili ya kuanza ujenzi na ukarabati wa viwanja.
Ufungaji wa rada nne za kuongozea ndege za kiraia
Ufungaji wa rada nne za kuongozea ndege za kiraia JNIA,KIA Mwanza na Songwe
JNIA Kukamilika kwa asilimia 100 ya miundombinu ya radar (jengo la mnara wa Rada, kibanda cha mlinzi na jengo la mitambo ya rada); Ufungaji wa mtambo unaendelea umefikia asilimia 90; na Majaribio ya mtambo wa rada yanaendelea.
Mwanza: Ujenzi wa miundombinu ya radar (jengo la mnara wa Rada, kibanda cha mlinzi na jengo la mitambo ya rada) unaendelea ambapo utekelezaji umefikia asilimia 50; na Mtambo umewasili katika kituo cha Mwanza na ufungaji umeanza Mei 2019.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 205
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
KIA: Ujenzi wa miundombinu ya radar (jengo la mnara wa Rada, kibanda cha mlinzi na jengo la mitambo ya rada) umefikia asilimia 90 na unatajiwa kukamilika Julai 2019.
Songwe: Majadiliano ya kupitisha michoro yanaendelea; Utekelezaji wa mradi utaanza mara michoro itakapokamilika na kuridhiwa; na Mtambo umewasil nchini na kazi ya ufungaji inatarajiwa kukamilika September 2019.
Ununuzi wa Rada ya tatu (3) ya Hali ya Hewa
Ununuzi wa Rada ya tatu (3) ya Hali ya Hewa itakayofungwa mkoa wa Mtwara
kusainiwa kwa mkataba wa ununuzi wa Rada ya Hali ya Hewa na kufanya malipo ya awali.
Eneo kwa ajili ya kufunga Rada limepatikana huko Mikindani, Mtwara na malipo ya fidia kwa wananchi waliopisha eneo la mradi yamefanyika.
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - TEHAMA
Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi
Kusimamia utekelezaji, uendeshaji na uendelezaji wa mradi ili kufikisha huduma za Mkongo hadi Makao Makuu ya Wilaya na watumiaji wa mwisho,
Ujenzi wa kituo cha data Dodoma na Zanzibar pamoja na ujenzi wa Miundombinu ya Mawasiliano ya Mitandao “Public Key Infrastucture”.
kuanza kuweka nguzo zenye majina ya barabara/mitaa, namba za vibao vya nyumba na kuanza maandalizi ya kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu matumizi ya Mfumo katika kata 48 za halmashauri za Majiji ya Dodoma, Mwanza na Tanga; manispaa za Ilemela, Shinyanga, Morogoro na Moshi; wilaya za Chamwino, Chato na Bahi; na miji ya Geita na Kibaha;
kukamilika kwa maandalizi ya mahitaji ya muundombinu katika mji wa Serikali - Dodoma;
kuendelea na taratibu za manunuzi kwa ajili ya kuweka miundombinu ya mfumo katika mji wa Serikali na kuweka vibao vyenye namba za nyumba katika halmashauri 12 za Majiji ya Dodoma, Mwanza na Tanga; Manispaa za Ilemela, Shinyanga, Morogoro na Moshi; Wilaya za Chamwino, Chato na Bahi; na Miji ya Geita na Kibaha.
Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano
Kuendelea kuratibu utekelezaji wa Mpango wa Anwani za Makazi na Postikodi katika miji yote Tanzania Bara na Zanzibar
kukamilika kwa ujenzi wa vituo vitatu (6) vya kutolea huduma za Mkongo wa Taifa katika maeneo ya Tukuyu, Kibaha, Kahama, Ifakara, Kidatu na Mafinga;
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 206
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
kukamilika kwa taratibu za kumpata mshauri mwelekezi wa kusanifu majengo ya vituo vya data Doma na Zanzibar; Maunganisho ya vifaa vya „video conference‟ kwa „sites‟ 12 zilizounganishwa katika mkongo wa Taifa na mtandao wa TTCL kwa mikoa yote 26 ya Tanzania bara na Zanzibar yamekamilika na vituo hivyo vinafanya kazi.
Taratibu za kupata mkandarasi wa kuunganisha halmashauri 17 kwenye mkongo wa Taifa zinaendelea. Aidha, taratibu za kupata mshauri mwelekezi kwa ujenzi wa Mkakati wa Kitaifa wa brodibendi unaendelea.
Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kutengeneza Vifaa vya TEHAMA
Kufanya upembuzi yakinifu wa mradi wa kituo cha kutengeneza vifaa vya TEHAMA kutokana na TEHAMA zinazofikia mwisho wa matumizi;
Kufanya maboresho ya kituo cha kutengeneza programu za TEHAMA; na
Kununua samani za kituo cha kutengenezea programu za kompyuta
kuandaliwa kwa hadidu za rejea kwa ajili ya kumpata Mshauri Elekezi wa kufanya upembuzi yakinifu;
kuandaliwa kwa andiko la uanzishaji wa kituo cha kutengeneza programu za kompyuta pamoja na Softcenter Operationalization Guide kwa ajili ya hatua za utekelezaji; na
kukamilika kwa maandalizi ya mchanganuo wa mahitaji kwa ajili ya ununuzi vifaa vya TEHAMA na samani za kituo cha kutengenezea programu za kompyuta. Mchanganuo wa mahitaji upo tayari kwa ajili ya kuanza mchakato wa manunuzi..
Nishati
Miradi ya Kuzalisha Umeme
Ujenzi wa Mradi wa Kinyerezi I Extension – MW 185
Ufungaji wa mitambo na kukamilisha ujenzi wa kituo cha kupozea umeme
Kukamilika kwa utengenezwaji wa mitambo yote minne (4) na kuanza kufungwa katika eneo la mradi; kukamilika kwa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kinyerezi I kV 220; na
Kuendelea na upanuzi wa njia ya msongo wa kV 132 kutoka Kinyerezi I hadi kituo cha kupoza umeme cha Gongo la Mboto.
Kufua Umeme wa Rusumo MW 80
Kuendelea na ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji;
Kukamilisha miundombinu ya barabara za kiungia eneo la mradi;
Kukamilika kwa ujenzi wa barabara za kuingia eneo la mradi;
Kukamilika kwa ujenzi wa kikinga maji; na
Kukamilika kwa uchimbaji wa eneo la kufunga mitambo.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 207
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kuendelea na ujenzi wa njia za kupitisha maji na eneo la kufunga mitambo; na
kukamilisha ujenzi wa kambi ya kudumu ya wafanyakazi
Kufua Umeme Mtwara MW 300 kwa kutumia Gesi Asilia
Kukamilisha upembuzi yakinifu;
Kumtafuta Mshauri Mwelekezi; na
Kuandaa nyaraka za zabuni kwa ajili ya kumpata Mkandarasi.
Kukamilika kwa upembuzi yakinifu wa kituo cha kuzalisha umeme na miundombinu wezeshi ya maji, barabara na gesi asilia
Mradi wa Kakono - MW 87 Ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi;
Kumpata Mtaalam Mshauri wa kufanya utafiti zaidi wa kijiolojia na haidrolojia; na
Kutayarisha zabuni kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa kituo na miundombinu ya kusafirisha umeme
Kukamilisha utafiti wa kijiolojia na haidrolojia; kukamilisha usanifu wa awali wa mradi;
Kufanya maandalizi ya zabuni kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa ujenzi;
Kuhuisha tathmini ya athari za mazingira na kijamii na kukamilisha mpango wa kuhamisha wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi
Mradi wa Umeme wa Jotoardhi – Ngozi (Mbeya)
Kuajiri mshauri mwelekezi wa kuandaa mpango kazi na kusimamia uchorongaji wa visima vya utafiti;
Kufanya tathimni ya ardhi hitajika na kulipa fidia;
Kuajiri mkandarasi wa uchorongaji; na
Ujenzi wa miundombinu ya barabara na maji.
Kuajiri Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kuandaa mpango na kusimamia uchorongaji; taratibu za ununuzi wa mtambo wa uchorongaji wa visima vya utafiti; na maandalizi ya upimaji na uthamini wa ardhi hitajika kwa ajili ya uchorongaji.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 208
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Miradi ya Nishati Vijijini kupitia REA
Kukamilisha usambazaji wa umeme vijijini Awamu ya II hususan katika mikoa ya Kilimanjaro na Singida;
Kusambaza umeme vijijini Awamu ya III ikijumuisha usambazaji umeme katika maeneo ambayo yameshafikiwa na miundombinu ya umeme,
Usambazaji umeme vijijini Awamu ya Tatu - mzunguko wa kwanza;
usambazaji umeme katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa mkuza wa njia ya msongo wa kv 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga,
Uendelezaji wa nishati jadidifu na usambazaji wa umeme katika vijiji
Kuunganishwa kwa vijiji 5,109, Taasisi za Elimu 3,165; Maeneo ya Biashara 3,451; Pampu za Maji 210; Taasisi za Afya 1,211 na Nyumba za Ibada 984
Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme
Kusafirisha Umeme ya Msongo wa kV 220 Makambako – Songea
Kukamilisha ujenzi wa vituo vya kupozea umeme; na
Ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kv 220; na
Kuunganisha wateja.
Kukamilika kwa njia ya kusafirisha umeme yenye urefu wa km 250 ya msongo wa kv 220 pamoja na vituo vitatu vya kupoza umeme vya Makambako, Madaba na Songea.
Kuunganishwa kwa mikoa ya Njombe na Ruvuma katika Gridi ya Taifa.
Kuendela kusambaza umeme kwenye vijiji ambapo ujenzi wa miundombinu ya usambazaji umeme katika vijiji 112 kati ya 122 umekamilika.
Kusafirisha Umeme ya Msongo wa kV 400 North West Grid Line (Iringa - Mbeya – Sumbawanga – Mpanda - Kigoma – Nyakanazi)
Ulipaji fidia kwa wananchi watakaopisha mradi, na
Kukamilisha majadiliano na wafadhili wa mradi kuwapata Wakandarasi na kuanza kwa utekelezaji wa mradi.
Kukamilisha taarifa ya awali ya upembuzi yakinifu kati ya Mbeya na Sumbawanga, kuanza uthamini wa mali kwa wananchi watakaopisha mradi pamoja na kuanza taratibu za kumpata mkandarasi wa mradi kwa sehemu ya Iringa - Mbeya - Tunduma - Sumbawanga (km 624);
Kumpata mtaalam mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi, uthamini wa mali zitakazoathiriwa na ujenzi wa mradi, na kupata eneo la
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 209
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
kujenga kituo cha kupoza umeme Kidahwe mkoani Kigoma kwa sehemu ya Nyakanazi - Kigoma (km 280); na
Kuendelea na majadiliano kati Serikali na wafadhali kwa sehemu ya Sumbawanga – Mpanda – Kigoma (km 480).
Njia ya Kusafirisha Umeme ya Msongo wa kV 220 North West Grid (Geita – Nyakanazi)
Kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi
Kukamilisha upatikanaji wa mkandarasi; na
Kukamilisha uhakiki wa mali za wananchi watakaopisha mradi na kuanza kulipa fidia.
Njia ya Kusafirisha Umeme ya Msongo wa kV 220 Bulyahulu – Geita
Utekelezaji wa mradi.
Kupatikana kwa mkandarasi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme;
Kuanza ujenzi wa kituo cha kupoza umeme;
Kupatikana kwa mkandarasi wa usambazaji umeme vijijini; na kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha mradi
Ardhi na Maeneo ya Uwekezaji na Biashara
Programu ya Umilikishaji wa Ardhi
Kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 35 katika wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro;
Kuandaa mipango-kina ya matumizi ya ardhi katika maeneo ya makazi ya vijiji 50;
Kupima vipande vya ardhi 120,000 na kuandaa hati miliki za kimila katika wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi;
Kutayarisha mipango kina ya vitovu vya makazi ya vijiji 30 (detailed planning of village centres) na kupima viwanja 15,000 na kuwapatia wananchi hati miliki za kimila za viwanja hivyo;
Kukamilisha ujenzi wa ofisi za ardhi za Wilaya 3 za Ulanga, Malinyi na Kilombero; na
kupimwa kwa vipande vya ardhi na kuandaa Hati za hakimiliki ya Kimila(CCROs) katika vijiji 109 vya Wilaya ya Kilombero (56), Ulanga (37) na Malinyi (16);
Kuhakikiwa na kupimwa kwa jumla ya vipande vya ardhi 178,980 kwa ajili ya kuandaa Hati za Hakimiliki ya Kimila katika wilaya za Kilombero (61,530), Ulanga (65,143) na Malinyi (52,307);
Kuandaliwa kwa jumla ya hati za hakimiliki ya Kimila 118,538 katika wilaya za Kilombero (56,680), Ulanga (37,353) na malinyi (24,501);
Kuandaliwa kwa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 79 katika wilaya Kilombero (41), Ulanga (23) na Malinyi (15);
Kuandaliwa kwa mipango ya kina ya makazi ya vijiji 66 katika wilaya za Kilombero (28), Ulanga (20) na Malinyi (18);
Kuendelea na ujenzi wa ofisi za ardhi za Wilaya ya Kilombero, Ulanga na Malinyi uliofikia asilimia 50; na
Kuwezeshwa kwa vijiji 44 kukamilisha ujenzi wa masijala za ardhi katika Wilaya za Kilombero (18), Ulanga (14) na Malinyi (12).
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 210
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kuhuisha Sera ya Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2000
Programu ya Kupanga na Kupima Ardhi
Kuimarisha Mfuko wa Fidia;
kutoa hatimiliki za kimila 500,000;
Kupima mipaka ya vijiji 500 pamoja na kuviandalia mipango ya matumizi ya ardhi
Kuandaliwa kwa rasimu ya Mpango Kabambe wa jiji la Dodoma (Dodoma Master Plan) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI. Mpango huu umeanisha matumizi mbalimbali ya ardhi yakiwemo ujenzi wa ofisi za Serikali eneo la Ihumwa, jijini Dodoma;
Kukamilika kwa rasimu ya Mpango Kabambe wa jiji la Dar es Salaam imekamilika kwa sasa uko katika hatua ya kusikilizwa na wadau; na
Kutolewa kwa shilingi bilioni 6.28 za ndani zimetolewa kwa ajili ya upangaji, upimaji na umilikishaji ardhi katika Halmashauri 24
Mradi wa Kuimarisha Mipaka ya Kimataifa
Kuimarisha mipaka 4 ya kimataifa kwa kusimika na kupima vigingi (Tanzania -Kenya; Tanzania - Zambia; Tanzania – Burundi; Tanzania - DRC/Burundi/ Zambia); na
Kujenga uwezo wa kitengo cha upimaji majini kwa kukusanya na kutunza taarifa za upimaji majini katika eneo la nje ya ukanda wa kiuchumi baharini
Mpaka wa Tanzania na Kenya
Kikao cha majadiliano cha ngazi ya Wataalam (JTC) kimefanyika. Kikao hicho kilichofanyika nchini Kenya kimeandaa mpangokazi wa kazi zilizobaki katika km 238 na kuendelea na uimarishaji wa awamu inayofuata ya km 110;
Kukamilika kwa maandalizi ya kufanya kazi ya mahesabu na uchakataji wa alama (pillars) na picha za anga (Aerial Triangulation); na
Kukagua kazi ya uwekaji wa alama za mipaka (pillars) zilizowekwa katika kipande cha mpaka cha km 172;
Mpaka wa Tanzania na Uganda: Kukamilika kwa maandalizi ya kuendelea na uimarishaji wa km 149; na Mpaka wa Tanzania na Zambia: Kukamilika kwa maandalizi ya kuendelea na uimarishaji wa km 120 za nchi kavu na 56 za kwenye maji yamekamilika.
Huduma za Fedha
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 211
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Benki ya Maendeleo TIB (TIB – DFI na TIB Corparate Bank – TIB)
Kuendelea kutoa mikopo ya muda wa kati na mrefu kwa wawekezaji katika sekta ya viwanda vinavyotumia rasilimali za ndani, miundombinu, Kilimo na kuongeza thamani kwenye madini;
Kuwezesha sekta za utoaji wa huduma hususan afya, elimu, upimaji viwanja; ujenzi wa hoteli na nyumba.
Kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 198.94; kukusanya riba ya shilingi bilioni 24.76; kuongeza amana (assets) kufika 842.93; na kukusanya mapato yasiyotokana na riba ya shilingi bilioni 14.26.
Kutolewa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 634.58;
Kuongezeka kwa mapato ya benki kufikia shilingi bilioni 46.41;
Kupatikana kwa faida ya shilingi milioni 499.88; na
Kukusanywa kwa marejesho ya mkopo yenye thamani ya shilingi bilioni 62.72. aidha,
Kutolewa kwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 6.1 kwa ajili ya ununuzi wa Pamba; shilingi bilioni 6.9 kwa ajili ya ununuzi wa kahawa; na kuidhinishwa kwa mikopo yenye thamani ya shilingi 68.7 kwa sekta mbalimbali za uchumi.
Benki ya Kilimo
kushirikiana kwa karibu na Tanzania Merchantile Exchange katika kuhakikisha wakulima wanaunganishwa na masoko ya uhakika;
kuanzisha ofisi za kanda ili kuwezesha kutoa mikopo nchi nzima na kuwa na usimamizi wa karibu;
kushirikiana na MIVARF kuwezesha taasisi mbalimbali za fedha kutoa mikopo katika sekta ya kilimo; na
kuendelea kutoa mafunzo kwa vikundi vya wakulima wadogo nchi nzima kwa awamu.
Kutolewa kwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 73.9 na kufanya jumla ya mikopo iliyotolewa kwa wakulima kufika shilingi bilioni 113.07;
Wakulima 1,266,374 wa mahindi, mpunga, mtama, alizeti, michikichi, korosho, kahawa, pamba, miwa, matunda na mbogamboga, ufugaji wa ng‟ombe wa maziwa na nyama, kuku, samaki, na nyuki wa asali katika mikoa wamefufaika na mikopo;
Kiasi cha shilingi bilioni 10.9 zilitolewa kwa ajili ya kuendeleza miradi kumi na tatu (13) ya viwanda vya uchakataji wa mazao;
Shilingi bilioni 10.4 kwa ajili ya miradi ya umwagiliaji;
Shilingi bilioni 3,4 kwa ajili ya kilimo cha kisasa cha zao la pamba na mpunga; na
kutolewa kwa mafunzo ya ujasiriamali ambapo jumla ya wakulima wadogo 7,519 walipatiwa mafunzo;
Mfuko wa SCGS umetoa udhamini uliowezesha mabenki ya biashara
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 212
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
kutoa mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 5.2 kwa wakulima wadogo 925.
Utalii, Biashara na Masoko
Utalii
Mradi wa Uendelezaji wa Utalii katika Ukanda wa Kusini – REGROW
kuboresha usimamizi na uhifadhi wa rasilimali za maliasili katika Ukanda wa Kusini wa Hifadhi za Taifa za wanyama za Ruaha, Udzungwa, Mikumi, na sehemu ya kaskazini ya mbuga ya Selous.
Kukamilika kwa ununuzi wa vifaa na samani kwa ajili ya ofisi za mradi;
Kutolewa kwa ushauri elekezi kuhusu mazao ya utalii katika jamii na utafiti kuhusu hali ya kijamii na kiuchumi katika jamii zinazozunguka maeneo yaliyohifadhiwa katika ukanda wa kusini; na
Kukamilika kwa zoezi la ufuatiliaji maeneo ya Mbarali na Pori la Akiba la Selous.
Sekta Ndogo ya Utalii kufanya ukaguzi wa Mawakala wa biashara za utalii katika kanda nne na kufanya tathmini na kutoa madaraja kwa huduma za malazi na chakula kwa daraja la nyota katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga na Mwanza.
Kuendelea kutoa elimu katika kanda nne za utalii kuhusu kanuni, sheria na miongozo ya uendelezaji biashara ya utalii na kubainisha vivutio vipya vya Utalii katika mikoa ya Simiyu, Geita, Kigoma, Kagera,Tanga na Manyara.
Utambulisho wa vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania (Tanzania Destination Branding) ambao una kauli mbiu ya „Tanzania Unforgettable‟;
Uanzishwaji wa chaneli maalumu ya Tanzania Safari kwa ajili ya kutangaza utalii nchini inayoratibiwa na TBC;
Uanzishwaji wa maadhimisho ya kuenzi utamaduni wa Mtanzania (Tanzania Heritage Month) yaliyofanyika katika mikoa minne (Dodoma, Arusha, Manyara, na Dar es salaam) ya Tanzania Bara na Zanzibar; na uanzishwaji wa safari za basi la kitalii katika Jiji la Dar es salaam;
Kufanyika kwa maonesho katika nchi 13 za Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Rwanda, Kenya, Kanada, China, Uholanzi, India, Hispania, Ubeligiji, Israeli na Falme za Kiarabu;
Kuongezeka kwa idadi ya watalii walioingia nchini kutoka 1,327,143 mwaka 2017 hadi kufikia watalii 1,505,702 mwaka 2018;
Kuboresha miundombinu wezeshi kwa ajili ya kuendeleza utalii ambapo jumla ya ofisi sita na vituo 15 vya ulinzi vimejengwa katika hifadhi za mazingira asilia za Chome, Magamba, Mlima Rungwe,
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 213
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Mkingu, Minziro, na Udzungwa Scarp;
Ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 89.6 na njia za kutembea watalii zenye urefu wa kilometa 102.6 zimesafishwa;
Ujenzi wa ngazi yenye mita 183 kuelekea kwenye maporomoko ya Kalambo umefanyika; na
Kambi 11 za kupumzikia wageni zimesafishwa katika misitu saba ya hifadhi za asilia za Mlima Hanang, Rungwe, Udzungwa, Uluguru, Kimboza, Rondo na Kilombero.
Biashara na Masoko
Mradi wa Kukuza Shughuli za Kibiashara katika Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika – SADC
kuboresha mazingira ya kufanyia biashara kwa kupitia na kupunguza vikwazo visivyo vya kikodi
Kununuliwa kwa mashine maalam ya kupima mafuta ya kula;
Kununuliwa kwa vifaa vya maabara kwa ajili ya Shirika la Viwango Tanzania - TBS;
Kununuliwa kwa vifaa vya maabara kwa ajili ya Wizara ya Kilimo; na
Kuandaliwa kwa kitabu cha Mwongozo wa Mauzo Nje.
Kuimarisha Usimamizi na Utekelezaji wa Mpango
Utawala Bora na Utawala wa Sheria
Kuharakisha Azma ya Serikali Kuu Kuhamia Dodoma
Programu ya Uboreshaji Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma: kuimarisha shughuli za Serikali Mtandao hususan miundombinu ya TEHAMA ili kuunganisha taasisi zilizopo Dodoma na Dar es Salaam; kujenga uwezo wa kitaasisi na kiutendaji; na kuboresha na kukuza matumizi ya TEHAMA katika utoaji huduma
Kuhamishwa kwa jumla ya watumishi 8,883 wa Wizara na Taasisi za Serikali kwenda Makao Makuu ya Serikali, Dodoma;
Kuendelea kwa taratibu za kuhakikiksha kuwa watumishi waliobaki wanahamia Dodoma
Kukamilisha kwa ujenzi wa majengo ya Ofisi za awali za Wizara 23 likiwemo Jengo la Mwanasheria Mkuu.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alikabidhi hati 64 za umiliki wa viwanja kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za kibalozi katika eneo hilo Julai, 2018.
Mfuko wa Bunge
Ujenzi wa Miundombinu ya Bunge: kuanza ujenzi wa nyumba ya makazi ya
Kuendelea na ujenzi wa nyumba ya makazi ya Katibu wa Bunge – Dodoma; Kufanyika kwa ukarabati wa majengo ya Bunge ikiwa ni
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 214
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Naibu Spika eneo la Kilimani - Dodoma na nyumba ya makazi ya Katibu wa Bunge – Dodoma, kuanzisha Bunge Mtandao na kituo cha kurusha matangazo ya redio na luninga ya Bunge ambapo shilingi bilioni 3.7 fedha za ndani zimetengwa.
Ukarabati wa Majengo ya Bunge: mradi unalenga kukarabati sehemu ya ndani ya Ukumbi Mpya wa Bunge, ukumbi wa Msekwa na majengo ya ofisi za Bunge ambapo shilingi bilioni 1.3 fedha za ndani zimetengwa.
pamoja na usimikaji wa lift paa katika jengo la Utawala; kufanyika kwa malipo ya awali kwa ajili ya kuwezesha ununuzi wa mitambo ya usalama kwenye ukumbi wa Bunge; Kuwajengea uwezo Wabunge na watumishi kupitia mafunzo mbalimbali ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.
Utoaji Haki na Huduma za Kisheria
kuanza ujenzi wa Ofisi tatu (3) za Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika mikoa;
kuimarisha mfumo wa uandishi na urekebu wa sheria;
kutoa mafunzo ya kitaaluma kwenye maeneo mapya ya uendeshaji wa mashauri ya jinai, usimamizi wa madai, usuluhishi, katiba na mikataba; na
ununuzi wa vitendea kazi kwa ajili ya ofisi za mikoa, wilaya na makao makuu
Kujenga mifumo ya kielektroniki ya kusajili na kuratibu mashauri yanayosajiliwa Mahakamani, Mfumo wa kusajili na kuratibu shughuli za mawakili na Mfumo wa utambuzi wa mahitaji ya mahakama (court mapping);
Ujenzi wa majengo ya mahakama kuu katika mikoa ya Kigoma na Mara;
Ukarabati wa nyumba tatu za majaji katika mkoa wa Mtwara; ujenzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi katika Mkoa wa Manyara;
Ujenzi wa mahakama 5 za Wilaya (Kilwa, Ruangwa, Bukombe, Geita na Chato);
Kuendelea kwa ujenzi wa Mahakama 4 za Hakimu Mkazi na Mahakama 11 za wilaya;
Kuanzishwa kwa mahakama maalum zinazotembea na kuweza kusogeza huduma za mahakama karibu na wananchi hususan walio katika sehemu zisizo na huduma ya mahakama; na
Kununuliwa kwa magari mawili yatakayotumika kutoa huduma katika mikoa ya Dar es Salaam, Wilaya ya Kindondoni (Bunju), Wilaya ya
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 215
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Ilala (Chanika), Wilaya ya Temeke (Buza) na Wilaya ya Ubungo (Kibamba); na Mkoa wa Mwanza, Wilaya ya Ilemela (Nyegezi) katika awamu ya kwanza ya majaribio.
Unicef Support to Multisectroral
Kuandaa mipango ya maendeleo inayojumuisha haki ya mtoto
Kuimarisha shughuli za usajili wa vizazi, vifo, ndoa, talaka na watoto wa kuasili ikiwa ni haki ya msingi ya utambuzi wa binadamu na upatikanaji wa takwimu kwa ajili ya maendeleo;
Kusajiliwa kwa vizazi 1,271,372; vifo 28,285; ndoa 26,953; talaka 122 na hati 28 za watoto wa kuasili;
Kuongezeka kiwango cha usajili kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kutoka asilimia 13, kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 38 kwa mwaka 2018/2019; na
Kuendelea na usimamizi wa mirathi, usajili wa bodi za wadhamini, uandishi na uhifadhi wa wosia ambapo wosia 38 zimeandikwa na kuhifidhiwa katika kipindi cha 2018/2019.
Access to Justice & Human Rights
Kuimarisha upatikanaji haki na ulinzi wa haki za binadamu nchini
Kuendelea kubuni na kutekeleza mikakati kadhaa kwa kutunga na kurekebisha sheria pamoja na kanuni zake;
Kuendesha tafiti za kisheria;
Kutoa elimu kwa umma kuhusu haki za binadamu na za kiraia;
Kupokea na kufanyia uchunguzi malalamiko ya wananchi yanayohusu ukiukwaji wa Haki za Binadamu na misingi ya Utawala Bora;
Kutengeneza mfumo jumuishi wa kukusanya, kuchambua na kuhifadhi takwimu muhimu zinazohusu sekta ndogo ya haki jinai ambao umejadiliwa na kutolewa maoni na wadau mbalimbali, kwa sasa unaendelea kufanyiwa majaribio;
Kuandaliwa kwa Mpango Kazi wa Pili wa Kitaifa wa Haki za Binadamu kwa kipindi cha mwaka 2018/19 hadi 2022/23 kulinda, kukuza na kuhifadhi haki za Binadamu wakati Serikali inapotekeleza majukumu yake;
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 216
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Kutungwa kwa Sheria ya Msaada wa Kisheria ya mwaka 2017 na kanuni zake na kupitishwa kwa Mkakati wa Kitaifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa mwaka 2017 hadi 2021 wenye lengo la kuhakikisha kuwa haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu zinalindwa na kudumishwa; na
Kutolewa kwa muongozo unaoelekeza mashauri yote yanayohusu wanawake, watoto, wazee na watu wenye ulemavu kumalizika ndani ya muda mfupi usiozidi miezi sita.
Vitambulisho vya Taifa uendelea na usajili na utambuzi wa watu nchi nzima ambapo wananchi, wageni wakazi na wakimbizi wapatao milioni 25 wanatarajiwa kusajiliwa na kutambuliwa;
kuendelea kuunganisha Mfumo wa Vitambulisho vya Taifa na Mifumo ya taasisi nyingine ili iweze kusomana kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma; na
kuunganisha mtandao wa mawasiliano kati ya ofisi za usajili za wilaya 33 na makao makuu
kusajili na kutambua raia wa Tanzania, wageni wakaazi pamoja na wakimbizi wapatao 19,648,857 wenye umri wa Miaka 18 sawa na lengo la asilimia 82 la kusajili wananchi wapatao milioni 24,295,468;
vitambulisho 4,850,724 vimechapishwa ambapo viambulisho 4,503,769 vimetolewa kwa wananchi;
kuunganishwa kwa Ofisi ya Wilaya ya Mbinga na Busega na mtandao wa mawasilianao na makao na makao makuu kupitia Mkongo wa Taifa chini ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).na hivyo kufikisha ofisi 119 nchi nzima;
kutolewa kwa vitambuliso 1,000,000 kwa wajasiriamali wadogo; kuunganishwa kwa jumla ya taasisi 45 za serikali na binafsi katika mfumo wa usajili na utambuzi.
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 217
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
Mradi wa Mfuko wa Mahakama
ujenzi wa majengo ya Makao Mkauu ya Mahakama ya Tanzania mjini Dododma;
kuendelea na ujenzi wa mahakama nchi nzima ikijumuisha Mhakama Kuu 2 zinazoendelea kujengwa katika mikoa ya Kigoma na Mara, na kuanza ujenzi katika mikoa ya Morogoro, Mwanza, Dodoma na Singida;
ujenzi wa mahakama za Wilaya 32 na Mhakama za Mwanzo 20;
kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za kisheria kwa kufunga mfumo wa kielektroniki wa utunzaji wa kumbukumbu, usikilizaji wa mashauri, ukusanyaji wa takwimu za mashauri na kutoa taarifa mbalimbali za kimahakama; na
kuwajengea uwezo watumishi ili kuendeleza vipaji vya ubunifu, kuimarisha weledi na kuongeza tija
Kukamilika kwa michoro ya ujenzi na tathmini ya gharama kwa ajili ya Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania - Dodoma katika eneo la NCC, Kitalu D Kiwanja Na. 1. Aidha, michoro hiyo na tahthmini ya gharama vimewasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kupata idhini ya kuanza ujenzi;
Ujenzi wa majengo ya Mahakama Kuu upo katika hatua za mwisho kukamilika ambapo Kigoma na Mara umefikia asilimia 80;
Ujenzi wa Mahakama za Wilaya za Bukombe, Bunda, Chato, Kasulu, Kilindi, Kondoa, Sikonge, Rungwe, Loliondo, Kilwa na Ruangwa umekamilika;
Katika kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za kisheria kazi zilizofanyika ni kukamilika kwa uboreshaji wa mfumo wa ukusanyaji wa takwimu (Judicial Statistical Dashbord System). Mfumo huu unatumika kusajili mashauri, kuingiza taarifa muhimu za Wadaawa ikiwa ni pamoja na kutuma taarifa kwa ujumbe mfupi (sms) kwa wadaawa kuhusu mwenendo wa mashauri yao;
Watumishi 183 (wanaume 113 na wanawake 70) walipata mafunzo katika kada mbalimbali kupitia program ya Maboresho ya Huduma za Mahakama;
Kujenga mifumo ya kielektroniki katika kusajili na kuendesha mashauri Mahakamani; na
Kuanza rasmi kutumika kwa mfumo wa kielektroniki wa uendeshaji wa mashauri ulioboreshwa unaojulikana kama JSDS 2 katika Mahakama za ngazi ya Wilaya hadi Mahakama ya Rufani.
Maeneo Mengine Muhimu kwa Ukuaji wa Uchumi na Ustawi na Taifa
Kuimarisha Ushiriki wa Sekta Binafsi
Mradi wa kuimarisha ushindani wa Sekta Binafsi – Ardhi
kujenga ofisi ndogo za kuhifadhia mfumo huo kwa awamu katika halmashauri;
kununua vifaa vya TEHAMA; na
ujenzi wa ofisi ndogo mfumo wa Intergrated Land Management Information System (ILMIS) katika halmashauri nchini;
ununuzi wa vifaa vya TEHAMA; na
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 218
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
kubadilisha nyaraka za ardhi kuwa za kielektroniki.
utoaji nyaraka za kielektroniki za ardhi.
Miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi
Mradi wa ujenzi wa reli ya Tanga – Arusha - Musoma pamoja na matawi ya Engaruka na Minjingu kwa Standard Gauge
kukamilisha mkataba wa kumpata Mshauri Elekezi atakaye andaa upembuzi yakinifu wa njia ya reli ya standard Gauge kati ya Arusha - Musoma, pamoja na matawi ya kwenda Engaruka na Minjingu
kuendelea na taratibu za kumwajiri Mshauri Elekezi.
kuandaa upembuzi yakinifu wa njia ya reli
Mradi wa ujenzi wa reli ya Mtwara – Mbamba Bay na matawi ya Mchuchuma na Liganga kwa Standard Gauge
kukamilisha kwa upembuzi yakinifu kuendelea kuandaa upembuzi yakinifu
kutafuta wawekezaji katika ujenzi wa reli kwa utaratibu wa PPP
Mradi wa Dawa Muhimu na Vifaa Tiba (Pwani, Mwanza na Mbeya)
kukamilisha kwa upembuzi yakinifu na kutafuta mbia
kukamilika kwa upembuzi yakinifu kuendelea na utaratibu wa kumpata mbia
Mradi wa Kusambaza Gesi Asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara:
kuwapata wabia kutoka sekta binafsi;
kufanya majadiliano ya uendeshaji na uwekezaji;
kuunda kampuni za pamoja za ubia; na
kuanza utekelezaji wa mradi.
Kukamilisha upembuzi yakinifu
Kumtafuta Mbia.
Ujenzi wa Vyuo kumi vya Ufundi
Kukamilisha uoembuzi yakinifu Kuendelea na ukamilishwaji wa upembuzi yakinifu
kupitia modeli ya fedha ili mradi uwe wa tija.
Miradi miwili ya Ujenzi wa Hotel ya Nyota Nne na Kituo cha Biashara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julias Nyerere ambayo
kukamilisha upembuzi yakinifu
kukamilisha taratibu za kuwapata wa bia
kuendelea kukamilisha upembuzi yakinifu
kuendelea na utaratibu wa kumpata mbia
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20
Wizara ya Fedha na Mipango 219
Jina la Mradi Malengo /Shughuli 2018/19 Shughuli Zilizotekelezwa 2018/19
itatekelezwa na Mamlaka ya Viwanja