private forestry programme...eneo la kikundi cha wakulima wa miti kwa kuzingatia mpango wa matumizi...

27
United Republic of Tanzania MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM Forestry and Beekeeping MWONGOZO WA KUTOA MOTISHA KWA WAKULIMA WA MITI KIBIASHARA UNAOTEKELEZWA NA MRADI WA PANDA MITI KIBIASHARA KWA KIPINDI CHA 2017/18 TREE GROWING INCENTIVE SCHEME GUIDELINES FOR 2017/18 PRIVATE FORESTRY PROGRAMME

Upload: others

Post on 24-Jan-2021

2 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • United Republic of TanzaniaMINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM

    Forestry and Beekeeping

    MWONGOZO WA KUTOA MOTISHA KWA WAKULIMA WA MITI KIBIASHARA UNAOTEKELEZWA NA MRADI WA PANDA MITI

    KIBIASHARA KWA KIPINDI CHA 2017/18

    TREE GROWING INCENTIVE SCHEME GUIDELINES FOR 2017/18

    PRIVATE FORESTRY PROGRAMME

  • PANDA MITI KIBIASHARA PRIVATE FORESTRY PROGRAMME (PFP)

    MWONGOZO WA KUTOA MOTISHA KWA WAKULIMA WA MITI KIBIASHARA UNAOTEKELEZWA NA MRADI WA PANDA MITI KIBIASHARA KWA KIPINDI CHA 2017/18

    Septemba 2017

  • YALIYOMO

    1. MAELEZO YA AWALI 1

    2. UGAWAJI NA USAMBAZAJI WA MICHE YA MITI 2

    2.1 Ugawaji wa miche ya mikaratusi na mipaina 2 2.2 Usambaji wa miche ya msaji 3 2.3 Vigezo vya kitalaam vinavyozingatiwa katika usambazaji na

    ugawaji wa miche kwa vikundi vya wakulima wa miti kibiashara 3

    3. UTOAJI FEDHA KWA AJILI YA PALIZI CHINI YA MPANGO WA KUTOA MOTISHA KWA WAKULIMA WA MITI KIBIASHARA 6

    3.1 Motisha ya kifedha kwa wakulima wenye mashamba ya mipaina na mikaratusi 6

    3.2 Motisha ya kifedha kwa wakulima wenye mashamba ya miti ya msaji 6

    4. TARATIBU ZA MAOMBI YA RUZUKU NA UTOAJI WA IDHINI YA MALIPO 8

    ORODHA YA VIAMBATISHO

    Kiambatisho Na. 1 Fomu ya maombi ya ruzuku ya miche ya mipaina na milingoti chini ya mpango wa motisha kwa wakulima wa kupanda miti kibiashara 9

  • 1

    1. MAELEZO YA AWALI

    Mradi wa Panda Miti Kibiashara ni mradi unaotekelezwa kwa pamoja na Wizara ya Mali Asili na Utalii, Tanzania na Serikali ya Finland. Lengo la mradi wa Panda Miti Kibiashara ni kuendeleza ustawishaji wa miti kibiashara na viwanda vya timbao vitakavyokuwa endelevu wa kuwawezesha wananchi kujipatia riziki halali, na hivyo kuongeza uchumi katika Nyanda za Juu Kusini. Mradi umeratibiwa ili uweze ku-tekelezwa kwa kipindi kirefu kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka wa 2030.

    Mradi unatekeleza mpango wa kuvisaidia vikundi vya wakulima wa miti kibiashara (TGIS) kwa kuvipatia motisha mbalimbali. Vikundi hivyo vimechaguliwa kutoka vijiji vya mikoa ya Njombe, Ruvuma, Iringa, na Morogoro. Mpango huu unaelekeza namna mradi utakavyotekelezwa kati ya Julai hadi Juni 2018. Mpango wa kutoa motisha kwa wakulima wa miti unalenga kuimarisha sekta binafsi ya misitu kupitia kwa wakulima wadogo. Katika kipindi cha mwaka 2017/18 mradi unatoa miche na fedha ya palizi chini ya mpango wa kuvisaidia vikundi vya wakulima wa miti.

    Mradi wa Panda Miti Kibiashara umetoa masharti ya upatikanaji wa ruzuku katika utekelezaji wa mpango huo wa utoaji motisha kwa vijiji vilivyoteuliwa ambayo ni:

    a) Kutoharibu misitu ya asili, mito na vijito, ardhi oevu, nyasi za ardhi oevu na maeneo yenye umuhimu mkubwa kisayansi na kiutamaduni.

    b) Mashamba yenye sifa stahiki ndiyo yatakayoteuliwa. Upandaji miti hau-taruhusiwa kufanyika kwenye mashamba yanayopata mvua chini ya watani wa mm 1,000 kwa mwaka.

    c) Waombaji wa ruzuku wajiandae kutekeleza kazi zote za uanzishwaji na utunzaji wa mashamaba ya miti kwa kuzingatia maelekezo ya mradi. Pia wakubali kuyakinga mashamba yao dhidi ya moto kichaa, magonjwa na wadudu waha-ribifu.

    d) Waombaji wasiwe ni wale wa kipindi kilichopita ambao walizembea kutunza mashamba waliyo yaanzisha baada ya kupata ruzuku

    Uongozi wa Mradi wa Panda miti Kibiashara na Vyama vya wakulima wa miti kibiasha-ra wanayo haki ya kusitisha kumsaidia mkulima binafsi na vyama vya upandaji miti kibiashara vitakavyo zembea kutekeleza kwa ufanisi masharti yaliyotolewa.

    Mradi wa Panda Miti Kibiashara na wafanyakazi wake hawana maslahi ya kiuchumi katika mashamba ya miti yanayostawishwa kutokana na ruzuku zinazotolewa. Isitoshe wafanya kazi na uongozi wa mradi hawana haki ya kuanzisha mashamba binafsi ya miti kwa ruzuku hizo. Uongozi wa mradi unayo haki ya kuzungukia mashamba yote ya miti yaliyostawishwa kwa nia ya kuchukua vipimo na kufanya ukaguzi wa kazi zote zilizofanyika ili kuhakiki kama majukumu ya wafanyakazi yanatimizwa ipasavyo, k.m utoaji wa huduma ya ugani kwa wakulima.

  • 2

    2. UGAWAJI NA USAMBAZAJI WA MICHE YA MITI

    2.1 Ugawaji wa miche ya mikaratusi na mipaina

    Mradi huwagawia walengwa miche yenye ubora wa hali ya juu ya jamii ya mikaratusi na mipaina katika vijiji vilivyoteuiwa. Miche hufikishwa shambani au kwenye barabara iliyo karibu na shamba ili kuepuka gharama kubwa za usafirishaji hadi shambani.

    Katika msimu wa mwaka 2017/18, mradi unasaidia wanachama kupanda miche hiyo kwenye shamba la wanachama lililotengwa kwa kuzingatia mpango bora wa matumizi ya ardhi wa kijiji kinacho husika. Pia shule za msingi na sekondari zinastahili kupewa kiwango kidogo cha msaada wa kupanda miti kwa lengo la kutoa elimu ya miti . Jedwali Na.1 linaonyesha makundi yanaostahili kupata ruzuku ya miche na kiwango cha ruzuku wanachostahili kupewa.

    Jedwali Na. 1 Gharama ya miche ya mipaina na mikaratusi kwa vikundi binafsi katika vijiji vinavyofadhiliwa na mradi wa Panda Miti Kibiashara

    Ukubwa wa shamba

    (ha)

    Idadi ya miche

    Gharama ya miche

    Mwanachama anayepanda kwenye eneo la kikundi cha wakulima wa miti kwa kuzingatia mpango wa

    matumizi bora ya ardhi

    Shule za Msingi na Sekondari*

    0.0–0.8 ≤ 890 Miche hutolewa bure Miche hutolewa bure

    0.8–5.0 891–5,555 50% ya gharama ya miche

    itolewapo bustanini Hakuna msaada unaotolewa

    ≥ 5.0 ≥ 5,556 Gharama yote

    * Kwa ajili ya kuelimisha

    Masharti na mipaka iliyoweka ya usambazaji na ugawaji wa miche ya mikaratusi na mipaina ambayo inaambatana na mpango wa kutoa motisha kwa wakulima wa miti ni kama ifuatavyo:

    i. Vikundi ndivyo vitabeba dhamana ya usambazaji na ugawaji wa miche. Na vikundi ndivyo vitapaswa kulipwa gharama zote za usambazaji na ugawaji wa miche.

    ii. Taasisi nyinginezo, zikiwemo za dini na mashirika yasiyo ya kiserikali hayakidhi kupata msaada huo, isipokuwa shule za elimu ya msingi na sekondari, hata kama ni miongoni mwa wanachama wa vikundi vya wakulima wa miti yaani TGA.

    iii. Shule za msingi na sekondari wanaweza kupanda katika ardhi zao binafsi kwa kigezo cha awali kinachoainisha kwamba afisa ugani wa PFP – Panda Miti Kibiashara atakuwa amekagua na amethibitisha eneo la kupandwa kabla ya kuidhinishwa kwa maombi.

    iv. Mradi wa Upandaji Miti Kibiashara unao wajibu wa kukagua ubora na ustawi wa miche iliyosambazwa. Hivyo mkulima/ taasisi yoyote iliyopendekezwa kupewa ruzuku hupaswa kuwaruhusu watendaji wa Mradi kufika mashambani mwao kufanya ukaguzi.

    v. Makao makuu ya mradi yaombwe ushauri, kuhusiana na maombi yoyote yenye utata.

  • 3

    2.2 Usambaji wa miche ya msaji

    Katika msimu wa 2017/16 Mradi utasambaza na kugawa miche ya Msaji kwa ajili ya mashamba yaliyotengwa katika Wilaya ya Nyasa. Ili kunufaika kiuchumi kutokana na ustawishaji wa miti ya msaji, inapaswa mashamba ya msaji yatunzwe kwa umakini wa hali ya juu ikilinganishwa na yanavvotunzwa mashamba ya mipaina na mikaratusi. Mradi utahakikisha wagani wanawaelekeza wakulima vizuri namna ya kupata matokeo chanya kutokana na ustawishaji wa mashamba ya msaji. Hivyo watakaonufaika na mgao wa miche ya msaji ni wanachama tu wa kilimo cha miti walio katika ukanda wa kupandwa miti ya msaji na watakaokuwa ndani ya eneo lililotengwa kwa kilimo cha msaji kama inavoainishwa na mpango bora wa matumizi ya ardhi. Kila mwanachama ataruhusiwa kumiliki si zaidi ya hekta 0.8 sawa na ekari mbili ya miti ya msaji kwa kila ombi (Jedwali Na. 2).

    Jedwali Na. 2 Gharama ya miche ya msaji, Wilaya ya Nyasa, katika zoni inayofaa kustawisha miti ya msaji

    Ukubwa wa shamba

    (ha)

    Idadi ya miche

    Gharama ya miche

    Mwanachama anayepanda kwenye eneo la kikundi cha wakulima wa miti kwa kuzingatia mpango wa

    matumizi bora ya ardhi

    Shule za Elimu ya Msingi na Sekondari*

    0.0–0.8 ≤ 890 Miche hutolewa bure 0.0–0.8

    * Kwa ajili ya kuelimisha

    Masharti na mipaka iliyoweka ya usambazaji na ugawaji wa miche ya msajii am-bayo inaambatana na mpango wa kutoa motisha kwa wakulima wa miti:

    i. Kiwango cha msaada kinachokubalika kwa mwombaji mmoja ni hekta 0.8 (au jumla ya miche 890), bila kujali idadi ya maombi yaliyowasilishwa na mwombaji ama idadi ya mashamba aliyoombea.

    ii. Taasisi nyingine, zikiwemo za dini na mashirika yasiyo ya kiserikali hayakidhi kupata msaada huo, isipokuwa shule za elimu ya msingi na sekondari

    iii. Shule za elimu ya msingi na sekondari zinaweza kupanda katika ardhi binafsi kwa kuzingatia kigezo cha awali ya kwamba Afisa ugani wa mradi amekagua na kujiridhisha eneo husika lilipo kabla ya hatua za uidhinishwaji wa maombi.

    iv. Mradi wa Upandaji Miti Kibiashara unao wajibu wa kukagua ubora na ukuaji wa miche iliyosambazwa. Hivyo mkulima/ taasisi yoyote iliyopendekezwa kupewa msaada hupaswa kuwaruhusu watendaji wa Mradi kufika mashambani mwao kufanya ukaguzi.

    v. Makao makuu ya mradi yashaurishwe kila wakati, kuhusiana na maombi yoyote yenye utata.

    2.3 Vigezo vya kitalaam vinavyozingatiwa katika usambazaji na ugawaji wa miche

    kwa vikundi vya wakulima wa miti kibiashara

    Mkulima yeyote anayetuma maombi ya ruzuku ya kupata miche kupitia vikundi binafsi katika vijiji vinavyofadhiliwa na mradi wa Panda Miti Kibiashara atakuwa amejifunga kutekeleza mpango wa uanzishaji na utunzaji wa mashamba ya miti kwa kuzingatia vigezo na viwango vilivyowekwa na Mradi wa Panda Miti Kibiashara, kwa ukamilifu.

    Ufuatiliaji wa utekelezaji wa vigezo na viwango utafanyika kwa kuyatembelea na kuyakagua mashamba. Mradi wa Panda Miti Kibiashara unayo haki ya kusitisha misaada iliyotolewa endapo wakulima au vyama vya wakulima wa kupanda miti kibi-ashara vitashindwa kutimiza vigezo na viwango vilivyowekwa. Viwango na vigezo vinavyokubalika vimeonyeshwa katika Jedwali Na. 3 na Na.4. Masharti yote ni kwa ajili ya miche ya mipaina, mikaratusi na msaji pia.

  • 4

    Jedwali Na. 3 Vigezo na viwango vya kitalaam kwa ajili ya kusafisha mashamba na usambazaji miche chini ya mpango wa motisha kwa wakulima wa miti

    Shughuli Viwango vinavyokubalika Visivyokubalika

    Vigezo: • Utayarishaji wa shamba uwe umekamilika ifikapo Disemba 31

    • Miche itasambazwa na Mradi kati ya Januari 1 hadi Machi 31

    Uchaguaji wa shamba

    • Shamba linalofaa kufuatana na mahitaji ya spishi zitakazopandwa

    • Misitu ya asili isiondolewe

    • Vipande vya mabaki ya misitu ya asili viachwa bila kuguswa na katikati ya vipande hivyo paachwe ili misitu hiyi istawi na kuungana

    • Ardhi oevu

    • Kando ya mito

    • Maeneo yenye bioanuwa kwa wingi k.m. misitu ya asili na mbuga

    • Mita 60 kutoka kwenye kanda za kinga ya maeneo ya mito na maeneo oevu

    Usafishaji wa shamba, uwekaji alama na uchimbaji mashimo

    • Taka za matawi shambani zondolewe na kukatwakatwa katika vipande vya urefu usiozidi mita 1

    • Vigingi vinavyosalia view chini ya sm 20

    • Kipimo cha kupanda mipaina, mikatausi na msaji iwe ni mita 3 kwa mita 3

    • Palizi kwa njia ya visahani ifanyike kuzingatia sm 50 kuzunguka shimo la kupanda mche

    • Mashimo yawe katikati ya eneo lilisafishwa

    • Upana na kina cha shimo kiwe na urefu wa sm 25

    • Mashimo yote yawe katika mistari iliyonyooka

    • Kufyeka maeneo yaliyokatazwa kadri yalivyotajwa hapo juu

    • Kusambaza taka katika hifadhi

  • 5

    Jedwali Na. 4 Vigezo na viwango vya kitalaam vya kuanzisha mashamba ya miti na usambazaji wa miche chini ya mpango wa kutoa motisha kwa wakulima wa miti

    Shughuli Viwango vinavyokubalika Visivyokubalika

    Vigezo: • Kupanda na kurudishia miche iliyokufa kuwe kumekamilika ifikapo Machi 31. Kwa kuwa kazi hii ni wajibu wa mkulima binafsi, hakuna motisha itakayotolewa

    Miche ya kupanda

    • Miche itasambazwa kutoka kwenye vitalu vinavyotambuliwa na kuthibitishwa na Mradi wa Panda Miti Kibiashara

    • Miche iwe yenye afya na ya kuvutia

    • Miche yenye ugonjwa, iliyokufa, iliyoambukizwa na mogonjwa na iliyoshambuliwa na wadudu waharibifu

    • Miche iliyopauka rangi

    • Shina lillovunjika

    • Mizizi iliyoharibiwa

    Upandaji na kurudishia miche iliyokufa

    • Miche yote ipandwe kwa kisimamishwa wima shimoni

    • Mashimo yarudishiwe udongo hadi kufikia kimo cha kola ya mche

    • Urudishiaji wa miche iliyokufa ufanyike katika kipindi cha mwezi mmoja wa kipindi cha upandaji

    • Viriba vya plastiki vikusanye pamoja na kuondolewa kutoka sehemu iliyopandwa miti

    • Kuwepo kwa viriba vya plastiki shamabani au kwenye mashimo ya kupanda mche

    • Kuwepo kwa mawe na majabali kuuzunguka mmea

    • Kuwepo kwa Magugu sm 50 kuzunguka mmea

    • Mkusanyiko wa udongo kuzunguka mti

    • Viriba vya plastiki kuachwa shambani

  • 6

    3. UTOAJI FEDHA KWA AJILI YA PALIZI CHINI YA MPANGO WA KUTOA MOTISHA KWA WAKULIMA WA MITI KIBIASHARA

    3.1 Motisha ya kifedha kwa wakulima wenye mashamba ya mipaina na mikaratusi

    Wakulima walioanzisha mashamba ya miti ya mipaina na mikaratusi kwa kuzingatia kustawisha mashamba hayo katika maeneo yaliyopimwa chini ya mpango wa matumizi bora ya ardhi ya vijiji, na kwa msaada wa wanachama wa kupanda miti kibiashara, wana haki ya kupewa ruzuku kwa ajili ya kupalilia mashamba yao. Ruzuku hiyo hutolewa kwa ajili ya palizi mbili kwa mwaka, katika misimu miwili mfululizo (ikiwa ni pamoja na msimu wa kwanza wa upandaji miche).

    Awali ya yote, wahusika wa Mradi wa Panda Miti Kibiashara watatembelea mashamba hayo na kufanya ukaguzi wa jinsi masharti ya upaliliaji yalivyozingatiwa kwa vigezo vyote (Jedwali Na 5).

    Utaratibu wa kutoa malipo wamtaka mkulima awe amekamilisha palizi zote mbili na uponaji wa miche iliyopandwa uwe uliofikia kiwango cha juu cha kitaalamu. Endapo wakaguzi wa mashamba wataridhia, basi mkulima atalipwa Tshs. 45,000/ kwa hekta moja, kupitia uongozi wa juu wa chama cha wakulima wa miti kibiashara.

    Jedwali Na. 5 Vigezo na viwango vya kitalaam vya kutoa motisha kifedha kwa ajili ya mashamba ya miti ya Mipaina na Mikaratusi

    Shughuli Viwango vinavyokubalika Visivyokubalika

    Vigezo: • Palizi kwa njia ya visahani na kufyeka majani iwe imekamilika ifikapo Mei 15

    Palizi kwa njia ya visahani

    • Magugu yote yanayozunguka mmea kwa kiwango cha kipenyo cha sm 50, huondolewa

    • Miti kuharibiwa

    Palizi kwa kufyeka nyasi

    • Magugu mabichi yakatwe hadi kufikia kimo cha cm 30 toaka usawa wa ardhi

    • Kuharibiwa kwa miti

    Huduma kwa ujumla

    • Uponaji wa miche iliyopandwa ifikie asilimia 80%, unapofanyika ukaguzi mwisho wa msimu wa mvua

    • Uponaji wa miche chini ya 80%

    3.2 Motisha ya kifedha kwa wakulima wenye mashamba ya miti ya msaji

    Wakulima ambao wameanzisha mashamba ya miti katika zoni maalum ya ustawi wa miti ya msaji Wilayani Nyasa, wanastahili kupewa ruzuku maalum ya kifedha kwa ajili ya palizi ya mashamba chini ya mpango wa kutoa motisha kwa wakulima wa kupanda miti kibiashara. Wakulima wa miti ya msaji hupewa ruzuku kubwa zaidi kuliko waku-lima wa miti ya mikaratusi na mipaina. Wao hulipwa mara mbili kukidhi palizi ya mara mbili kwa mwaka kwa mashamba mapya. Uongozi wa mradi wa Panda Miti Kibiashara huanza kufanya ukaguzi wa mashamba na kupima utekelezaji na uzingatiaji wa masharti yaliyo ainishwa katika Jedwali Na.6

    Utaratibu wa kutoa malipo wamtaka mkulima awe amekamilisha palizi zote mbili na uponaji wa miche iliyopandwa uwe wa kiwango cha kitaalamu cha hali ya juu. Endapo wakaguzi wa mashamba wataridhia, basi mkulima atalipwa Tshs. 45,000/ kwa hekta moja kwa palizi ya kwanza, na kwa palizi ya pili atalipwa kiasi hicho hicho cha Tshs. 45,000 na kufanya jumla ya Tshs. 90,000/- Malipo yatafanyika kwa awamu mbili kupitia uongozi wa juu wa chama cha wakulima wa miti kibiashara.

  • 7

    Jedwali Na. 6 Vigezo na viwango vya kitalaam vya kutoa motisha kifedha kwa ajili ya mashamba ya miti ya msaji

    Shughuli Viwango vinavyokubalika Visivyokubalika

    Vigezo: • Palizi ya kwanza kwa njia ya visahani iwe imefanyika kabla ya wiki 5 baada ya kupanda

    • Palizi ya pili kwa njia ya visahani na kufyeka majani iwe imekamilika ifikapo Mei 15

    Palizi kwa njia ya visahani

    • Magugu yote yanayozunguka mmea kwa kiwango cha kipenyo cha sm 50, huondolewa

    • Miti kuharibiwa

    Palizi kwa kufyeka nyasi

    • Magugu mabichi yakatwe hadi kufikia kimo cha cm 30 toaka usawa wa ardhi

    • Kuharibiwa kwa miti

    Huduma kwa ujumla

    • Uponaji wa miche iliyopandwa ifikie asilimia 80%, unapofanyika ukaguzi mwisho wa msimu wa mvua

    • Uponaji wa miche chini ya 80%

  • 8

    4. TARATIBU ZA MAOMBI YA RUZUKU NA UTOAJI WA IDHINI YA MALIPO

    Maombi ya ruzuku chini ya mpango wa kutoa motisha kwa wakulima wa miti hufanyi-ka kwa kupitia chama cha wakulima wa miti kibiashara kijijini. Chama cha wapanda miti kibiashara wanao utaratibu wa kuchuja maombi ya ruzuku kwa wakulima amabo unazingatia:

    1. Kulitazama shamba na kuhakiki kama lakidhi vigezo vyote vilivyoainishwa katika Jedwali Na. 3 (mashamba nje ya mpango wa matumizi bora ya ardhi hukaguliwa kipekee);

    2. Kuthibisha umri wa mwombaji ruzuku kama katimiza miaka 18;

    3. Kuchunguza wakulima waliopewa msaada, wakashindwa kuanzisha au kutunza mashamba yao katika msimu uliopita;

    4. Kuandaa takwimu muhimu: kuhusu maombi yaliyofanyika, ikiwa ni pamoja na:

    a. Ukubwa wa shamba na aina ya spishi itakayo pandwa (kwa kutofautisha maombi yaliyokubaliwa na yaliyokataliwa)

    b. Idadi ya waombaji kwa jinsi ya kike, kiume na shule (kwa kugawa waliokubaliwa na walio kataliwa)

    c. Jumla kuu ya ukubwa wa mashamba na idadi ya waliotuma maombi

    5. Kuwasilisha maombi yote kwa Afisa ugani wa Mradi wa Panda Miti Kibiashara ili ayapitie na kuyaridhia kwa niaba ya Uongozi wa Mradi.

    Ni wajibu wa Afisa Ugani kuhakikisha na kujiridhisha kuwa utaratibu mzima wa uteuzi umefuatwa na kuzingatiwa kwa ukamilifu kabisa.

    Maumuzi ya uteuzi wa mwisho utafanywa na kamati maalum itakayoteuliwa na Uongozi wa Mradi wa Panda Miti Kibiashara.

  • 9

    Kiambatisho Na. 1 Fomu ya maombi ya ruzuku ya miche ya mipaina na milingoti chini ya mpango wa motisha kwa wakulima wa kupanda miti kibiashara

    Annex 1 Application form for TGIS seedling support (pine and eucalyptus)

  • _________________________________________________________________________________ Fomu hii HAIUZWI. Tafadhali toa taarifa. Ikiwa kuna mtu anataka kukuuzia, tafadhali wasiliana na afisa misitu uenezi wa PMK wa eneo lako / This form is not for sale. If someone tries to sell you this form,

    please contact the Private Forestry Programme Extension Officer in your area

    FOMU YA MAOMBI YA RUZUKU / APPLICATION FOR TREE GROWING SUPPORT

    Taarifa Muhimu / Basic information:

    1. Aina ya Mwombaji / Type of applicant:

    1. Mtu binafsi / Private: 2. Familia / Family: 3. Shule / School:

    2. A. Mwombaji biafsi na kaya / For private and family applicants:

    1. Jina la kwanza / First name: _____________________

    2. Jina la kati / Middle name: _____________________

    3. Jina la mwisho / Last name: _____________________

    4. Jinsia ya mwombaji mkuu / Gender: a. Kiume / Male: b. Kike / Female:

    5. Mwaka wa kuzaliwa / Year of birth: _____________

    6. Aina ya utambulisho (chagua moja) / Person identified from (select one):

    a. Kadi ya kura / Voting card: , namba / number: __________________

    b. Leseni ya udereva / Driving licence: , namba / number: __________________

    c. Hati ya kusafiria / Passport: , namba / number: __________________

    d. Ushuhuda kutoka kiongozi wa kijiji kwa ajili ya utambulisho kama vyote hapo juu havipatikani / Village leader’s certification of the identification of the applicant:

    Jina na Sahihi ya Mtendaji Kijiji Jina na Sahihi ya Mfadhaliwa

    __________________________ __________________________

    2. B. Shule / For School applicants:

    1. Jina kamili la shule / Full name of the School:

    ______________________________________________

    2. Namba ya usajili ya shule / School identification number: ______________________

    3. Namba ya simu / Phone number: ______________________

    4. Mahali shamba lilipo / Location of farm

    1. Kijiji / Village: ______________________

    2. Kata / Ward: ______________________

    3. Wilaya / District: ______________________

    5. Mwombaji mkuu ni mwanachama wa chama cha wakulima wa miti (TGA) / Are you a TGA member? a. Ndiyo / Yes: b. Hapana / No:

    6. Ulishawahi kupata ruzuku ya miche kutoka PFP kabla? / Have you received TGIS support from the PFP before: a. Ndiyo / Yes: b. Hapana / No:

    TO BE FILLED BY EXTENSION OFFICER: If yes, fill in the PFP beneficiary ID: ________________________

    Tarehe / Date __________________

  • _________________________________________________________________________________ Fomu hii HAIUZWI. Tafadhali toa taarifa. Ikiwa kuna mtu anataka kukuuzia, tafadhali wasiliana na afisa misitu uenezi wa PMK wa eneo lako / This form is not for sale. If someone tries to sell you this form,

    please contact the Private Forestry Programme Extension Officer in your area

    Taarifa za uombaji wa ruzuku ya miche / TGIS application information:

    Msimu wa 2017/18 miche ya ruzuku itatolewa kama ifuatavyo / During season 2017/18, the PFP provides support to TGA members planting as per VLUP as follows:

    1) Miche ya bila malipo kwa eneo mpka ekari mbili / Free seedlings up to 0.8 ha

    2) Miche ya Zaidi ya ekari mbili hadi ekari kumi na mbili na nusu italipiwa nusu ya bei ya kwa kila mche / 50% seedling price between 0.8 ha and 5 ha

    3) Zaidi ya ekari kumi na mbili na nusu miche italipiwa bei kamili / Full seedling price after 5 ha

    Shule za msingi na sekondari zinaweza kupata ruzuku ya miche kwa hekta 0.8 tu na sio zaidi ya hapo / Primary and secondary schools are entitled to free seedlings up to 0.8 ha but no further support.

    7. Eneo lililoombewa ruzuku (Unaweza kuomba mpaka maeneo matuatu katika fomu moja) / Plots applied to be planted (you can apply up to three plots with a single application):

    a. Plot 1: Aina ya miti (chagua moja) / Species (select one):

    i. Misindano / Pine , hekta / hectares ________ ha

    ii. Mikaratusi / Milingoti / Eucalyptus , hekta / hectares ________ ha

    Je, shamba lipo kwenye eneo lililo ainishwa kwa upandaji miti na mpango wa kijiji wa ma-tumizi bora ya ardhi? / Is the plot located within common land designated for tree planting in VLUP? Ndiyo / Yes: Hapana / No:

    b. Plot 2: Aina ya miti (chagua moja) / Species (select one):

    i. Misindano / Pine , hekta / hectares ________ ha

    ii. Mikaratusi / Milingoti / Eucalyptus , hekta / hectares ________ ha

    Je, shamba lipo kwenye eneo lililo ainishwa kwa upandaji miti na mpango wa kijiji wa ma-tumizi bora ya ardhi? / Is the plot located within common land designated for tree planting in VLUP? Ndiyo / Yes: Hapana / No:

    c. Plot 3: Aina ya miti (chagua moja) / Species (select one):

    i. Misindano / Pine , hekta / hectares ________ ha

    ii. Mikaratusi / Milingoti / Eucalyptus , hekta / hectares ________ ha

    Je, shamba lipo kwenye eneo lililo ainishwa kwa upandaji miti na mpango wa kijiji wa ma-tumizi bora ya ardhi? / Is the plot located within common land designated for tree planting in VLUP? Ndiyo / Yes: Hapana / No:

    Ekari moja ni sawa na 0.40 ya hektari / Please notice that 1 acre = 0.40 hectares

    8. Upeo wa shughuli na utalaam unaohitajika / Technical requirements:

    Mwombaji anaridhia kuwa eneo linalopandwa miti linakidhi vigezo vya kitaalamu vya upandaji wa miti. Afisa misitu uenezi wa PMK atahakiki maeneo pendekezwa kwa upandaji kama yana-kidhi vigezo kabla ya kupata ruzuku/motisha. / The applicant certifies that the planted area fulfils the following technical requirements for tree plantations. PFP Extension Officers will verify that the proposed areas fulfil the requirement and the support is subject to fulfilment.

    a) Utayari wa kupanda miche iliyothibitishwa na Programu ya Panda Miti Kibiashara. / Use of PFP-provided seedlings.

    b) Kiwango cha chini cha mvua shambani kwa mwaka kinafikia 1,000 mm. / Mean annual rainfall min 1,000 mm.

  • _________________________________________________________________________________ Fomu hii HAIUZWI. Tafadhali toa taarifa. Ikiwa kuna mtu anataka kukuuzia, tafadhali wasiliana na afisa misitu uenezi wa PMK wa eneo lako / This form is not for sale. If someone tries to sell you this form,

    please contact the Private Forestry Programme Extension Officer in your area

    c) Shamba litastawishwa umbali unaokubalika kisheria kutoka kwenye kingo za mito na she-ria nyingine za kuhifadhi mazingira zitazingatiwa. / Sites need to be located at least 60 m away from river beds, and other ecologically or socially vulnerable areas.

    d) Eneo lisiwe lenye misitu na miti ya asili au maeneo yenye bionuwai muhimu kimazingira / Sites shall not require conversion of any natural or semi-natural ecosystem, such as na-tive woodland or edaphic grassland.

    e) Maeneo ya shamba yanamikiliwa halali kisheria na hakuna mgogoro wowote. / Sites are not disputed and the applicant is the legal user of the site.

    f) Mwombaji anakubali na kuahidi kutimiza masharti ya mradi kuhusu utunzaji wa mas-hamba ya miti na pale masharti yanapokiukwa PFP wanaweza kuacha kutoa ruzuku. / The applicant will commit to conduct all plantation establishment and maintenance work as stated by the PFP minimum requirements, and agrees to be responsible for the ade-quate protection of the plantations. PFP retains the right to withdraw support from tree growers who demonstrate negligence concerning these commitments.

    g) Muombaji atakuwa tayari kushiriki katika zoezi la upimaji wa shamba lake lolote ambalo amepokea ruzuku ya miche kupitia mpango wa motisha kwa wakulima wa miti / The ap-plicant will commit in allowing PFP field checks on any plantations established with seed-lings received through the TGIS seedling support.

    Sahihi / Signatures:

    Uthibistisho wa mwombaji kuwa vigezo vya kitaalamu vimetimizwa na kuwa taarifa za kiuchumi - jamii ni za kweli / Certification by Applicant that the technical requirements are fulfilled and that the given socio-economic information is correct (if applicable):

    Sahihi na tarehe / Signature and date: __________________________________________

    Sahihi ya Mtendaji wa kijiji, au mwakilishi wake, au mwakilishi wa kamati ya ardhi ya kijiji ili kuthibitisha umiliki kisheria wa ardhi ya mwombaji. / Signature of the Village Chief or Representative or document signed by representative of Village Land Committee as proof of legal ownership of the land by the applicant.

    Sahihi na tarehe / Signature and date: __________________________________________

    Jina na Cheo (Inapowezekana) / Name and title: ___________________________________

    Imepokelewa na kuhakikiwa na mwakilishi wa PMK / Received and checked by a PFP representative:

    Sahihi na tarehe / Signature and date: __________________________________________

    Jina na Cheo (Inapowezekana) / Name and title: ___________________________________

  • _________________________________________________________________________________ Fomu hii HAIUZWI. Tafadhali toa taarifa. Ikiwa kuna mtu anataka kukuuzia, tafadhali wasiliana na afisa misitu uenezi wa PMK wa eneo lako / This form is not for sale. If someone tries to sell you this form,

    please contact the Private Forestry Programme Extension Officer in your area

    Aina hii ni kwa mtu binafsi na familia tu: Taarifa za kiuchumi-jamii za kaya kwa waombaji wapya tu / Private and family type only: Household socio-economic information for new TGIS applicants only

    1. Idadi ya watu katika kaya wenye miaka {0-18} / How many household members are 18-years-old or younger?

    1. Sita na zaidi translation / Six or more 2. Tano / Five 3. Nne / Four 4. Tatu / Three 5. Mbili / Two 6. Moja / One 7. Hakuna/ None

    2. Watoto wenye umri kati ya miaka 6–18 wanasoma shule? / Are all household members ages 6 to 18 currently in school?

    1. Hapana / No 2. Ndiyo / Yes 3. Hakuna watoto wa miaka 6 hadi 18 / No members ages 6 to 18

    3. Vifaa vilivyotumika kujengea kuta za Nyumba ya kuishi / What is the main building material used for the walls of the main building?

    1. Matofali ya kuchoma / Baked bricks 2. Miti na tope, nyasi, matofali mabichi au mengine? / Poles and mud, grass, sun-dried

    bricks, or other 3. Mawe matofali ya sementi au mbao? / Stones, cement bricks, or timber

    4. Nyumba imeezekwa kwa vifaa gani? / What is the main building material used for the roof of the main building?

    1. Nyasi, makuti,matope ,majani au nyinginezo / Grass/leaves, mud and leaves, or other

    2. Mabati vigae zege au asbesto / Iron sheets, tiles, concrete, or asbestos 5. Unatumia nishati gani kwa kupikia / What is the main fuel used for cooking?

    1. Kuni, mkaa wa mawe, mionzi ya jua gasi asilia,mabaki ya mazao au samadi ya mif-ugo / Firewood, coal, solar, gas (biogas), wood or farm residuals, or animal residuals

    2. Mkaa,mafuta ya taa,gesi ya viwandani / Charcoal, paraffin, gas (industrial), electricity, generator/private source, or other

    6. Je Kaya yako ina runinga (TV) yoyote / Does your household have any televisions? 1. Hapana / No 2. Ndiyo / Yes

    7. Je kaya yako ina redio au redio kaseti ama vifaa vya kusikilizia nyimbo / Does your household have any radios, cassette/tape recorders, or hi-fi systems?

    1. Hapana / No 2. Ndiyo / Yes

    8. Kaya yako inamiliki taa ya mafuta? {kandili} / Does your household own any lanterns? 1. Hapana / No 2. Ndiyo / Yes

    9. Je kaya yako ina meza yoyote? / Does your household have any tables? 1. Hapana / No 2. Ndiyo / Yes

    10. Je kaya yako imelima mazao yoyote katika kipindi cha miezi kumi na mbili iliyopita, unamiliki ngombe kondoo/mbuzi ,mtamba, vidume, ndama au maksai? / If the household cultivated any crops in the last 12 months, does it currently own any bulls, cows, steers, heifers, male calves, female calves, or oxen?

    1. Hakuna mazao na ngombe / No crops, and no cattle 2. Hakuna mazao ila kuna ng’ombe / No crops, but cattle 3. Kuna mazao lakini hakuna ng’ombe / Crops, but no cattle 4. Kuna mazao na ngombe / Crops, and cattle

  • PANDA MITI KIBIASHARA PRIVATE FORESTRY PROGRAMME (PFP)

    PFP TREE GROWING INCENTIVE SCHEME GUIDELINES FOR 2017/18

    September 2017

  • TABLE OF CONTENTS

    1. BACKGROUND 1

    2. TGIS SEEDLING SUPPLY 2

    2.1 TGIS seedling supply for pine and eucalyptus 2 2.2 TGIS seedling supply for teak 2 2.3 Technical requirements for TGIS seedling supply provision 3

    3. TGIS CASH INCENTIVES FOR WEEDING 5

    3.1 Cash incentive for pine and eucalyptus 5 3.2 Cash incentive for teak 5

    4. TGIS APPLICATION AND APPROVAL PROCESS 7

  • 1

    1. BACKGROUND

    The Private Forestry Programme (PFP) is a bilateral development cooperation pro-gramme, implemented together by the Ministry of Natural Resources and Tourism of Tanzania and the Government of Finland. The purpose of the PFP is to help develop commercial tree growing and forest industries as sustainable livelihoods and hence in-crease wealth in the Southern Highlands. It is designed to be a long intervention, run-ning from 2014 to 2030.

    PFP implements a tree growers’ incentive scheme (TGIS) to support tree growing in selected villages of Ruvuma, Njombe, Iringa and Morogoro Regions; and these guide-lines describe how it is to operate between July 2017 and June 2018.

    The TGIS is intended to strengthen private plantation forestry by smallholder tree grow-ers. In 2017/18, the PFP provides TGIS seedling support and TGIS cash incentive for weeding.

    As a precondition for providing any TGIS support in the selected villages, the PFP re-quires the following:

    a) Natural forests, watercourses, wetlands, edaphic grasslands, and areas of sci-entific and/or cultural value are not disturbed.

    b) Only the most viable of sites are selected. No planting is supported in areas that have less than an average of 1,000 mm of rainfall per year.

    c) Applicants commit to conduct all plantation establishment and maintenance work as stated by the PFP minimum requirements and agree to be responsible for the adequate protection of the plantations.

    d) Applicants must not have failed to look after plantations established previously under TGIS support.

    The PFP and Tree Grower Associations (TGAs) retain the right to withdraw all support from individual tree growers and TGAs who demonstrate negligence concerning these commitments.

    The PFP and PFP staff do not take any financial interest in the plantations that are supported. Neither PFP nor PFP staff have any rights to produce from the supported plantations. The PFP does retain the right to access any supported plantations for in-spection and measurements, in order to be able to follow up the results and provide adequate support and extension services to the plantation owners.

  • 2

    2. TGIS SEEDLING SUPPLY

    2.1 TGIS seedling supply for pine and eucalyptus

    PFP makes high quality pine and eucalyptus seedlings available in specified quantities to eligible recipients in the programme-supported villages. Wherever it is reasonably possible, the PFP delivers the seedlings from the nursery supplier to an accessible road-head near the planting site without extra charges for the service.

    In 2017/18, the PFP supports planting by TGA members on common land designated for the purpose in VLUP. In addition, primary and secondary schools are eligible for limited support for planting for educational purposes. Table 1 specifies the groups that are eligible for TGIS seedling supply and the extent of support they are entitled to.

    Table 1 Pine and eucalyptus seedling charges in PFP-supported villages

    Area

    (ha)

    No. of seedlings

    Charge for pine and eucalyptus seedlings

    TGA member planting on land designated to TGA in the VLUP

    Primary and secondary schools*

    0.0–0.8 ≤ 890 Free Free

    0.8–5.0 891–5,555 50% of nursery gate cost No support

    ≥ 5.0 ≥ 5,556 Full nursery gate cost

    * For educational purposes

    Furthermore, the following guidelines and limitations apply:

    i. TGAs handle the seedling distribution. All charges for seedlings are to be paid for the delivering TGA.

    ii. Apart from primary and secondary schools, any other institutions (including non-governmental organisations and faith based organisations such as churches) do not qualify for the TGIS seedling supply, even if they are members of TGA.

    iii. Primary and secondary schools may plant on their private land, under the pre-condition that PFP Extension Officer inspects and verifies the planting site on location prior to application approval.

    iv. The PFP performs plantation quality and growth checks to monitor and follow up the support delivery. Hence, any beneficiary who has received TGIS seedling support shall agree to grant the PFP personnel access to their established wood-lot for the PFP survey purposes.

    v. The PFP main office is always to be consulted in any unclear application cases.

    2.2 TGIS seedling supply for teak

    In season 2017/18, the PFP delivers TGIS seedling supply for teak to be planted in a designated area within Nyasa District. In order to be economically viable, teak growing requires intensive woodlot management when compared to pine and eucalyptus, and the PFP needs to ensure especially effective extension service delivery to help growers reach good results. Hence, the TGIS seedling supply for teak is limited to TGA members planting on the VLUP-designated Teak Zone area only, with a maximum total area of 0.8 ha per applicant (Table 2).

    Table 2 Teak seedling charges within the Nyasa District Teak Zone

    Area

    (ha)

    No. of seedlings

    Charge for teak seedlings

    TGA member planting on land designated to TGA in the VLUP

    Primary and secondary schools*

    0.0–0.8 ≤ 890 Free Free

    * For educational purposes

  • 3

    Furthermore, the following guidelines and limitations apply:

    i. The total maximum support allowed per a single applicant is 0.8 ha (or 890 seed-lings), regardless of the number of applications submitted by the applicant or the number of woodlots applied.

    ii. Apart from primary and secondary schools, any other institutions (including non-governmental organisations and faith based organisations such as churches) do not qualify for the TGIS seedling supply, even if they are members of TGA.

    iii. Primary and secondary schools may plant on their private land, under the pre-condition that PFP Extension Officer inspects and verifies the planting site on location prior to application approval.

    iv. The PFP performs plantation quality and growth checks to monitor and follow up the support delivery. Hence, any beneficiary who has received TGIS seedling support shall agree to grant the PFP personnel access to their established wood-lot for the PFP survey purposes.

    v. The PFP main office is always to be consulted in any unclear application cases.

    2.3 Technical requirements for TGIS seedling supply provision

    By applying TGIS seedling supply support, the applicant commits to performing woodlot establishment and management up to the PFP technical standards for commercial plan-tations.

    The technical performance will be monitored by the PFP through field visits. The PFP retains the right to pull out further support from individual tree growers and TGAs that do not fulfil the technical standards.

    The acceptable technical standards and the respective milestones for TGIS seedling supply provision are listed in Table 3 and Table 4. These apply for pine and eucalyptus as well as teak.

    Table 3 Milestones and technical standards for site preparation under TGIS seedling supply

    Activity Acceptable standard Not acceptable

    Milestones: • Land preparation to be completed by 31 December

    • Seedlings to be provided by PFP between 1 January – 31 March

    Site Selection • Suitable site according to the site re-quirement of the species

    • No clearing of native woodland

    • In cases with some patches of natural forest remnants, these are to be left un-disturbed whilst they can be planted around. Corridors should be left un-planted to retain connectivity between forest remnant patches.

    • Wetlands

    • Riverine areas

    • High biodiversity ar-eas e.g. natural for-ests and native grass-lands

    • Any area within 60 m buffer zone to riverine areas and wetlands

    Land clearing, Marking and pitting

    • Waste material in the plot to be de-branched and crosscut to max 1 m length

    • Residual stumps to be lower than 20 cm

    • The spacing of 3 x 3 m to be applied for pine, eucalyptus and teak

    • Circular weeding within 50 cm radius around the marked pitting spot

    • The pit to be dug in the centre of the cleared area

    • Clearing of unac-ceptable land types as listed above

    • Spread of slashing into conservation ar-eas

  • 4

    Activity Acceptable standard Not acceptable

    • The pit to be 25 cm deep and 25 cm wide

    • All pits to be in a straight line

    Table 4 Milestones and technical standards for plantation establishment under TGIS seedling supply

    Activity Acceptable standard Not acceptable

    Milestones: • Planting and blanking to be completed by 31 March. No incentive at this stage because this is the tree grower’s responsibility

    Planting mate-rial

    • Seedlings to be from PFP-approved nurseries

    • Seedlings/stumps to be healthy and ac-tively growing plants

    • Diseases, dead, dying and pest infested seedlings

    • Discoloured seedlings

    • Broken stem

    • Damaged roots

    Planting and blanking / beating up

    • Seedlings to be planted upright in the centre of the pit

    • Planting pit to be filled so that soil is 2 cm above root collar or cutting point

    • Blanking to be done within 1 month of planting

    • Empty polytubes to be collected and re-moved from the planting site

    • Polythene tube in planting pit or field

    • Rocks or stones around the plant

    • Weeds within 50 cm from the plant

    • Soil heaped around the plant

    • Polytubes left to the site

  • 5

    3. TGIS CASH INCENTIVES FOR WEEDING

    3.1 Cash incentive for pine and eucalyptus

    Pine and eucalyptus woodlots that have been established under TGIS seedling supply support by TGA members on land designated in VLUP are eligible for cash incentive for weeding. The cash incentive is to cover two different weeding operations once per year for the first two growing seasons (including the year of establishment).

    The PFP will commence a field survey to visit these woodlots and assess whether the technical requirements for the two different types of weeding are acceptably fulfilled (Table 5). The payment requires that the both types of weeding have been completed up to technical standards in the woodlot by the time of survey and that the overall sur-vival rate is sufficiently high. If approved, the area-based cash support will subsequently be paid to the woodlot owner by the TGA Apex Body.

    The TGIS cash support for pine and eucalyptus woodlots is TZS 45,000 per ha.

    Table 5 Milestones and technical standards for TGIS cash incentive for pine and eucalyptus plantations

    Activity Acceptable standard Not acceptable

    Milestones: • Circle weeding and slash weeding to be completed by 15 May

    Circle weeding • All weeds within 50 cm radius around the tree to be removed

    • Damage done to trees

    Slash weeding • All living weeds to be cut lower than 30 cm high

    • Damage done to trees

    Overall maintenance

    • Survival rate of 80% or better during end of rainy season survival check

    • Survival rate lower than 80%

    3.2 Cash incentive for teak

    Teak woodlots that have been established under TGIS seedling supply support in the Nyasa District Teak Zone are eligible for enhanced cash incentive for weeding. The cash incentive for teak is a more intensive version of the standard cash incentive for pine and eucalyptus.

    The cash incentive for teak is to cover two different weeding operations twice per year for the newly planted teak woodlots.

    The PFP will commence two field surveys during the season to visit these woodlots and assess whether the technical requirements for the two different types of weeding are acceptably fulfilled (Table 6). The payment requires that the both types of weeding have been completed in the woodlot up to technical standards by the time of survey and that the overall survival rate is sufficiently high. If approved, the area-based cash support will subsequently be paid to the woodlot owner by the TGA Apex Body.

    The TGIS cash support for teak woodlots is TZS 45,000 per ha per round of weedings. Hence the maximum total to be paid per season is TZS 90,000 per ha in two payment batches.

  • 6

    Table 6 Milestones and technical standards for TGIS cash incentive for teak plantations

    Activity Acceptable standard Not acceptable

    Milestones: • First round of circle weeding and slash weeding to be completed 5 weeks after the planting date

    • Second round of circle weeding and slash weeding to be com-pleted by 15 May

    Circle weeding • All weeds within 50 cm radius around the tree to be removed

    • Damage done to trees

    Slash weeding • All living weeds to be cut lower than 30 cm high

    • Damage done to trees

    Overall maintenance

    • Survival rate of 80% or better during end of rainy season survival check

    • Survival rate lower than 80%

  • 7

    4. TGIS APPLICATION AND APPROVAL PROCESS

    Applications for TGIS support should be made to the local TGA.

    The TGA together with the facilitator will screen the applications and recommend ap-proval or disapproval for each individual each application. The TGA screening process should include:

    1. Observing the area allocated for planting on location and verifying it meets all technical criteria specified in Table 3 (planting sites on school private land are to be visited individually);

    2. Verifying that each applicant is over 18 years of age;

    3. Screening out applications from people who have failed establishing or main-taining previous PFP-supported plantations;

    4. Drafting basic statistics of the applications, including:

    a. Area applied by species (disaggregation of approved and disapproved applications)

    b. Number of male applicants, female applicants and school applicants (disaggregation of approved and disapproved applications)

    c. Total aggregate figures for the applied area and number of applicants;

    5. Submitting the applications for PFP Extension Officer to screen on behalf of the PFP.

    PFP Extension Officer is to observe the process on location and verify that it has been carried out and completed properly.

    The final decision on the approval of the applications is to be made by a special com-mittee designated by the PFP.

  • TGIS English &Swahili .pdf (p.1)TGIS Guideline ENG. MergedTGIS English MergedTGIS INCENTIVE SCHEME

    TGIS_Guidelines_2017-18_Swahili-English.pdf (p.2-26)TGIS_guidelines_2017-18_Revised_Swahili_2017_09_27.pdf (p.1-15)TGIS_guidelines_2017-18_no-annex_2017_09_27.pdf (p.16-25)

    Back cover.pdf (p.27)