rozari takatifu

28
Kiswahili Rosary Prayers Rozari Takatifu Ya Kibiblia Ya Bikira Maria Mtakatifu Nia ya Rozali Kuombea wale wote wanaotafuta kazi na wale wote wanaotafuta wachumba. Basi katika mwezi huu wa Rozari kwa maombezi ya Bikira Maria amwombe Mwenyezi Mungu akakutane na nia zao. Wanaotafuta kazi na wanaotafuta wachumba nia zao zikamilike. Ishara Ya Msalaba Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina! Nasadiki Nasadiki kwa Mungu baba Mwenyezi, Muumba wa Mbingu na dunia na Kwa Yesu Kristu mwanaye wa pekee Bwana wetu, Aliye tungwa kwa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, Akateswa kwa mamlaka ya Ponsio Pilato,Akasulubiwa, akafa, akazikwa akashukia kuzimu, siku ya tatu akafufuka katika wafu, Akapaa mbinguni, Amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; Toka huko atakuja tena kwa atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu Katoliki ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili na uzima wa milele AMINA. Baba Yetu Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina. Salamu Maria

Upload: eligius-ndunguru

Post on 09-Aug-2015

1.352 views

Category:

Documents

72 download

TRANSCRIPT

Page 1: Rozari takatifu

 Kiswahili Rosary Prayers

Rozari Takatifu Ya Kibiblia Ya Bikira Maria Mtakatifu

Nia ya Rozali

Kuombea wale wote wanaotafuta kazi na wale wote wanaotafuta wachumba. Basi katika mwezi huu wa Rozari kwa maombezi ya Bikira Maria amwombe Mwenyezi Mungu akakutane na nia zao. Wanaotafuta kazi na wanaotafuta wachumba nia zao zikamilike.

  Ishara Ya Msalaba  Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina!

Nasadiki Nasadiki kwa Mungu baba Mwenyezi,Muumba wa Mbingu na dunia na Kwa Yesu Kristu mwanaye wa pekee Bwana wetu, Aliye tungwa kwa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, Akateswa kwa mamlaka ya Ponsio Pilato,Akasulubiwa, akafa, akazikwa akashukia kuzimu, siku ya tatu akafufuka katika wafu, Akapaa mbinguni, Amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; Toka huko atakuja tena kwa atakuja kuwahukumu wazima na wafu.Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu Katoliki ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili na uzima wa milele AMINA.

Baba Yetu Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe.Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.Utupe leo mkate wetu wa kila siku.Utusamehe makosa yetu,kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.Usitutie katika kishawishi,lakini utuopoe maovuni.Amina.

Salamu Maria

Mungu Baba atuzidishie Imani, Salamu, Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe,umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu,mzao wa tumbo lako amebarikiwa.Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu.

Page 2: Rozari takatifu

Amina.

Mungu Mwana utuongezee Matumaini Salamu, Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe,umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu,mzao wa tumbo lako amebarikiwa.Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu.Amina.

Mungu Roho Mtakatifu utuwashie moto wa mapendo moyoni Mwetu . Salamu, Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe,umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu,mzao wa tumbo lako amebarikiwa.Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu.Amina.

Atukuzwe Baba Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.Kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele.Amina.

Ee Yesu mwema Ee Yesu wangu, utusamee dhambi zetu, utukinge na moto wa milele, ongoza roho zote Mbinguni hasa za wale wanao hitaji zaidi Huruma yako.

Damu ya kristu iziokoe roho zinazoteseka tohorani, ijalie nuru ya uzima wa milele. Amina.

Matendo ya Rozari ya Uchungu. Fungu la kwanza.Yesu anatoka jasho la damu. Akasema ABBa yaani Baba yote yanawezekana kwako. Niondolee kikombe hiki.walakini siyo kama nitakavyo mimi Tunaombea wagonjwa wanaoteseka ili uwape nguvu kufanya mapenzi yako Baba.

Baba Yetu Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe.Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.Utupe leo mkate wetu wa kila siku.Utusamehe makosa yetu,kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.Usitutie katika kishawishi,lakini utuopoe maovuni.Amina.

Page 3: Rozari takatifu

Salamu, Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe,umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu,mzao wa tumbo lako amebarikiwa.Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu.Amina. X 10.

Atukuzwe Baba Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.Kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele.Amina.

Ee Yesu mwema Ee Yesu wangu, utusamee dhambi zetu, utukinge na moto wa milele, ongoza roho zote Mbinguni hasa za wale wanao hitaji zaidi Huruma yako.

Damu ya KristuDamu ya kristu iziokoe roho zinazoteseka tohorani, izijalie nuru ya uzima wa milele. Amina.

Matendo ya Uchungu Fungu la PiliYesu anapigwa mijeledi. Pilato akawambia kwani ana ubaya gani ameutendaAskari wakamchukuwa ndani ya behewa wakamvisha vazi la zambarau. Pilato akamwambia kweili ana ubaya gani alioutenda? Akafunguliwa Barnaba.

Baba Yetu Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe.Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.Utupe leo mkate wetu wa kila siku.Utusamehe makosa yetu,kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.Usitutie katika kishawishi,lakini utuopoe maovuni.Amina.

Salamu, Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe,umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu,mzao wa tumbo lako amebarikiwa.Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu.Amina. X 10.

Page 4: Rozari takatifu

Atukuzwe Baba Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.Kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele.Amina. Tuwasifu mileleEe Yesu mwema Ee Yesu wangu, utusamee dhambi zetu, utukinge na moto wa milele, ongoza roho zote Mbinguni hasa za wale wanao hitaji zaidi Huruma yako.

Damu ya KristuDamu ya kristu iziokoe roho zinazoteseka tohorani, izijalie nuru ya uzima wa milele. Amina.

Matendo ya Uchungu Fungu la TatuYesu anatiwa miiba kichwani. Tufanye tuwapende wale wote wanaotuchukia.Baba Yetu Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe.Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.Utupe leo mkate wetu wa kila siku.Utusamehe makosa yetu,kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.Usitutie katika kishawishi,lakini utuopoe maovuni.Amina.

Salamu, Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe,umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu,mzao wa tumbo lako amebarikiwa.Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu.Amina. X 10.Atukuzwe Baba Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.Kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele.Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni hasa wale wanaohitaji zaidi ya huruma yako.AMINA.Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef.

Damu ya Kristu

Page 5: Rozari takatifu

Damu ya kristu iziokoe roho zinazoteseka tohorani, izijalie nuru ya uzima wa milele. Amina.

Matendo ya Uchungu Fungu la Nne.

Yesu anachukuwa msalaba. Yesu akabeba msalaba wake hadi povu la kichwa. Akasulubishwa katikati ya wawili. Wakamvika vazi la rangi ya zambarau. Wapatanishe familia, ukoo na mataifa yanayogombana.

Baba Yetu Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe.Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.Utupe leo mkate wetu wa kila siku.Utusamehe makosa yetu,kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.Usitutie katika kishawishi,lakini utuopoe maovuni.Amina.

Salamu, Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe,umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu,mzao wa tumbo lako amebarikiwa.Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu.Amina. X 10.Atukuzwe Baba Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.Kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele.Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni hasa za wale wanaohitaji zaidi ya huruma yako.AMINA.Damu ya KristuDamu ya kristu iziokoe roho zinazoteseka tohorani, izijalie nuru ya uzima wa milele. Amina.

Matendo ya Uchungu Fungu la Tano.Yesu anakufa msabani.

Basi Yesu aliinama kichwa akakata roho. Akamsulubisha huko pamoja huku wawili Ee Kwa njia ya pekee tuwaombee wale wanaokufa ili wafike mbinguni.

Page 6: Rozari takatifu

Baba Yetu Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe.Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.Utupe leo mkate wetu wa kila siku.Utusamehe makosa yetu,kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.Usitutie katika kishawishi,lakini utuopoe maovuni.Amina.

Salamu, Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe,umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu,mzao wa tumbo lako amebarikiwa.Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu.Amina. X 10.Atukuzwe Baba Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.Kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele.Amina. Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef.Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni hasa za wale wanaohitaji zaidi ya huruma yako.AMINA.Damu ya KristuDamu ya kristu iziokoe roho zinazoteseka tohorani, izijalie nuru ya uzima wa milele. Amina.

Litania ya Bikira MariaChuo cha sala.Ukurasa 257.Memorare

Moyo Mtakatifu wa YesuTunakimbilia ulinziKwa ajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.

MAFUMBO YA ROZARIMafumbo Matendo ya Furaha,Jumatatu na Jumamosi

Malaika anampasha habari Maria, kwamba atakuwa Mama wa Mkombozi

Page 7: Rozari takatifu

Malaika akamwambia, “Usiogope Mariamu, kwa maana umepata neema; utazaa mwana na jina lake utamwita Yesu …….Mariamu akasema “Tazama mimi ni kijakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema” (Luk. 1:30 – 31.38)

Tuombe!Ee Bwana, tujalie Imani kukubali mapenzi yako daima bila kusitasita. Tunawaombea pia wale wote ambao hawakujui, lakini wanakutafuta kwa moyo mnyoofu.Tuwasifu milele – Yesu Maria na na Yosefu….x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteswa tohoroni, izijalie mwanga wa milele, Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.

Baba yetu x1Salamu Maria x10

2.Bikira Maria anakwenda kumtembelea Elizabeti.Basi, Maria akaondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya mlimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda, akaingia nyumbani kwa Zakaria, akamwamkia Elizabeti. Ikawa Elizabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake, Elizabeti akajazwa Roho Mtakatifu. (Luk. 1:39 – 41).

Ee Bwana ijaze miyo yetu furaha na shukrani kwa kuwa umetuita kuwa watoto wako. Kwa njia ya kipekee tunawaombea wakatukumeni na wale wote ambao kwa mafundisho yao, wanwaongoza wanwaongoza kwako.

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.

Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

3.Yesu anazaliwa Bethethemu

Page 8: Rozari takatifu

Ikawa katika kukaa huko, siku zake za kumzaa mwanawe kifungua mimba. Akamvisha nguo za kitoto, akamlaza katika hori la ng’ombe kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni (Luk. 2:6-7)

Tuombe!Ee Bwana, Amani yako na ibaki mioyoni mwetu daima tunapojaribu kukupendeza na kuishi kwa ajili ya utukufu wako. Tunaiombea nchi yetu na wote wenye madaraka na watumishi wa umma, ili waweze kufanya kazi kwa amaini, haki na kwa manufaa ya wote.

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.

Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

Yesu anatolewa hekaluniKisha zilipotimia siku za kutakasika kwao kama ilivyo torati ya Musa, Walikwenda naye mpaka Yerusalemu wamweke kwa Bwana, Kama ilvoandikwa katika sharia ya Bwana. Kila mtoto mwanaume aliyekifungua mimba kwa mamaye, na aitwe Mtakatifu wa Bwana (Luk. 2:22 – 23)

Tuombe!Ee Bwana tusaidie tuyatolee maisha yetu yote kwako mwili na roho, kazi na mapumziko, furaha na uchungu. Tunawaombea pia mapadri wetu, ili kwa njia ya sala zao, mahubiri, ni kwa njia ya maisha yao, waweza kutuongoza kwako.

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

5.Maria na Yusufu wanamkuta Yesu Hekaluni

Page 9: Rozari takatifu

Na walipomwona walishangaa, na Mama yake akamwambia, “Mwanangu” mbona umetutendea hivi? Tazama; Baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni. Akawaambia; kwa nini kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu? (Luk2:48-49).

Tuombe!Ee Bwana tufundishe kuheshimiana na kuchukuliana kwa upendo, kwa sababu unaishi ndani yetu. Tunaziombea familia zetu, na familia zote, ili wazazi na watoto waishi katika upendo na kuheshimiana.

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

Mafumbo (Matendo) ya Uchungu,Jumanne na Ijumaa

Yesu anatoka Jasho la Damu.Akasema Aba, Baba, yote yawezekana kwako, uniondolee kikombe hiki, walani si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe (Mk 14:36)

Tuombe!Ee Bwana, tunakuomba usitutie katika majaribu, bali utujalie nguvu ya kuvishinda vishawishi vyote, kuwaombea wadhaifu, wagonjwa na wanaoteseka, ili uwape nguvu ya kufanya mapenzi yako.

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

Yesu anapigwa mijeledi

Page 10: Rozari takatifu

Pilato akawambia kwani ana ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele. “Msulubishe Msulubishe”. Pilato akipenda kuwaridhisha makutano, akawafungulia Baraba, akamtoa Yesu, baada ya kumpiga mijeledi, ili asulubiwe. Mk15:14-15)

Tuombe!Ee Bwana, wakati tunapokosewa haki, tunapodharauliwa na kutendewa ubaya bila sababu tusaidie kuyakumbuka mateso yako. Tunawaombea haki wote wanaonyanyaswa, waliofungwa na kuteswa, kwa ajili ya Amani zao za kidini,kijamii na kisiasa.

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

Yesu anavikwa taji la miiba KichwaniNao askari wakamcukua ndani ya behewa, ndiyo Praitorio (yaani myumba ya uliwali). Wakakusanya askari kikosi kizima. Wakamvika vazi la rangi ya Zambarau. Wakasokota taji la miiba, wakamtia kichwani (Mk 15: 16-17)

Tuombe!Ee Bwana, tunakuomba uondoe ndani ya mioyoni yetu hisia zote za chuki, na kulipiza kisasi. Tufanye tuwapende na kuwasamehe wote wanaotutia uchungu. Tunaomba uwajalie roho ya upatanisho wanandoa waliotalikana, familia zinazogombana, jamii na makabila yanayobaguliwa, na mataifa yanayopigana.Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

Yesu anabeba Msalaba

Page 11: Rozari takatifu

Basi, ndipo walipomtia mikononi mwo ili asulubiwe, nao wakampokea Yesu.Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake mpaka mahali paitwapo, Fuvu la kichwa na kwa kiebrania (Golgotha) Wakamsulubisha huko, na wengine wawili pamoja naye, mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati. (Yah> 19:17 – 18).

Tuombe!Ee Bwana, tujalie neema ya kudumu na kuwa mwaminifu kila mwisho. Tunawaombea wakosefu wote waliokuasi. Tupatie sote neema ya kutubu, ili tuweze kuubeba msalaba wetu na kumfuata mwanao.Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

Yesu anakufa MsalabaniBasi, Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema(Yametimia) akainama kichwa akaisalimau roho yake.(Yoh. 19:30)

Tuombe!Ee Bwna, kwa maombi ya Mama yako Mtakatifu aliyesimama chini ya Msalaba, tunakuomba uwe nasi sasa, na saa ya kufa kwetu. Kwa njia ya pekee, tunawaombea wote wanaokufa, ili waweze kufika mbinguni.

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

Mafumbo (Matendo) ya Utukufu,Jumatano na Jumapili

1. Yesu anafufuka

Page 12: Rozari takatifu

Watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumeta meta, nao walipoingia na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, nao waliwaambia, kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu? Hayupo hapa amefufuka. Kumbukeni alivyosema alipokuwapo Galilaya, Imempasa mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi na kusulubishwa, na kufufuka siku ya tatu (Luk24:4- 7)

Tuombe!

Bwana mfufuka chanzo cha maisha ya kweli, tusaidie tuishi ubatizo wetu kwa kukataa dhambi, na kuishi ndani yako. Tunawaombea watu wote wasiokujua bado uwapatie maisha mapya na Zaidi ya Imani kwa nguvu ya ufufuko wako.

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10

Atukuzwe Baba……x1

Yesu anapaa Mbinguni“Nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na Uyahudi wote, na Samaria, na hata miisho ya dunia” akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa; Wingu likampokea kutoka machoni pao(Mdo. 1:8-9)

Tuombe Ee Bwana, katika sakramenti ya kipaimara umetuita kuwa mashahidi wako, tufanye tuwe mitume wa wamisionari wa kweli wa ujumbe wako wa upendo. Na utujalie ongezeko la miito ya kimisionari katka kanisa letu.

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

Page 13: Rozari takatifu

2. Roho Mtakatifu anawashukia MitumeKukaja ghafla toka mbinguni uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi, kuwatokea ndimi zilizogawanyika kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kunenea kwa lugha nyingine, kama Roho aliyowajalia kutamka Mdo (2:1-4)

Tuombe!

Bwana mfufuka, tunakuomba uijaze mioyo yetu Roho wako, ili kaika familia zetu, jumuiya zetu, na katika kanisa zima, tuishi Pamoja kwa Amani na upendo. Tujalie umoja hasa miongoni mwa Wakristo ili tuweze kuvishinda vishawishi vya majivuno na kuwahukumu wengine, na hivyo tupate kweli kushuhudia nguvu yako ya wokovu.

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

3. Bikira Maria Anapalizwa Mbinguni

Na ishara kuu ilionekana Mbinguni, mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji la nyota kumi na mbili. (Ufu. 12- 1)

Tuombe!Ee Bwana, katika matatizo yote ya ulimwengu huu unaopita, tunakuomba uijaze mioyo yetu tamaa kubwa ya kufika katika makao yetu ya mbinguni. Tunaombea watu wote waliofariki, hasa jamaa na marafiki zetu, ili waweze kupata huruma yako na kupumzika pamoja na Mama yetu wa Mbinguni katika ufalme wako.

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Page 14: Rozari takatifu

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10

Atukuzwe Baba……x1

4. Bikira Maria anavikwa Taji MbinguniYeye ashindaye nitampa kuketi pamoja katika kiti change cha enzi (Ufu: 3:21)

Tuombe!Ee Bwana ijaze mioyo yetu iweze kuelekea katika ufalme wako na kuigeuza kuendana na mapenzi yako. Tujalie haki na Amani duniani, ili sote tuweze kuishi katika matazamio ya ujio wa ufalme wako. Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

Mafumbo ya MwangaAlhamisi

1. Ubatizo wa Yesu Mtoni Yordani

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho zote watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

Yesu anageuza maji huko Kana

Page 15: Rozari takatifu

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

3. Yesu anatangaza Habari njema kwa ajili ya Ufalme wa Mbinguni

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

4. Yesu anageuka sura

Page 16: Rozari takatifu

5. Yesu anaweka Ekaristi takatifu

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

LITANIA YA BIKIRA MARIA

Litania ya Bikira MariaBwana, utuhurumie, - Bwana utuhurumie.Kristu, utuhurumie, - kristu, utuhurumieBwana, utuhurumie, - Bwana utuhurumie.Bwana wa Mbinguni, Mungu utuhurumie.Mwana mkombozi wa dunia, Mungu, utuhurumie.Mwana, Mkombozi wa dunia, Mungu, utuhurumie.Roho, Mtakatifu, Mungu, utuhurumie.Roho Mtakatifu, Mungu, utuhurumie.Utatu Mtakatifu, Mungu mmoja, utuhurumie.Maria Mtakatifu, Utuombee.Mzazi Mtakatifu wa Mungu,Bikira Mtakatifu, wa Mabikira.Mama wa Kristu.Mama wa neema wa Mungu.Mama Mtakatifu kabisa.Mama mwenye usafi wa moyo.Mama mwenye ubikira.Mama usiye na dhambi.Mama mpendevu.Mama mstaajabivu.Mama wa shauri jema.Mama wa Muumba.Mama wa Mkombozi.Bikira mwenye utaratibu kamili.Bikira mwenye heshima.Bikira mwenye sifa.Bikira mwenye enzi kuu.sababu ya furaha yetu,Chombo bora cha ibada,Waridi lenye fumbo,

Page 17: Rozari takatifu

Mnara wa Daudi,Mnara wa pembe,Nyumba ya dhahabu,Chombo cha agano,Mlango wa Mbingu,Nyota ya asubuhi,Salaamu ya wagonjwa,Kimbilio la wakosefu,Mtuliza wa enye huzuni,Msaada wa wakristu,Malkia wa malaika,Malkia wa mababu,Malkia wa manabii,Malkia wa mitume,Malkia wa mashahidi,Malkia wa waungama ,Malkia wa mabikira,Malkia wa watakatifu wote,Malkia uliyeumbwa pasipo dhambi ya asili,Malkia uliyepokelewa mbinguni,Malkia wa rozari takatifu,Malkia wa Amani,Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,utusamehe, Bwana.Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,utusikilize, Bwana.Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,utuhurumie.

K. Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu.W, Tujalie ahadi za Kristu.

Tuombe: Ee Bwana Mungu, tujalie sisi watumishi wako kuwa na uzima waroho na wa mwili siku zote, twakuomba kwa ajili ya maombezi matukufu ya Bikira daima, tuopolewe katika masikitiko ya sasa, tupate furaha za milele. Kwa Kristu, Bwana wetu. W. Amina.

Tuombe!

Ee bwana, twakuomba utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote, na kwa maombezi ya matukufu ya Maria Mtakatifu Bikira daima tuopolewe katika masikitiko ya sasa, tupate furaha za milele. Kwa Kristu, Bwana wetu. W. Amina.

MemorareUkumbuke, ee Bikira maria mpole mno, / toka zamani za kale haikusikiwa, / kwamba ulimwacha mtu aliyefuata ulinzi wako, /akiomba msaada wako, / akitaka maombezi yako. / Kwa matumaini hayo ninakimbilia kwako, /Bikira wa mabikira, /ninakuja kwako, /ninasimama mbele yako /nikilalalamika miye

Page 18: Rozari takatifu

mkosefu: /Mama wa wa neon la Mungu, /usikatae maneno yangu, / bali uyasikilize uyatimize. Amina.

Moyo Mtakatifu wa Yesu, UtuombeeMoyo Mtakatifu wa YesuMoyo Mtakatifu wa YesuWatakatifu wote wa Mungu, Mtuombee.

Tunakimbilia ulinziKwa ajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.

Mafumbo ya MwangaAlhamisi

1. Ubatizo wa Yesu Mtoni YordaniWakati huo Yesu kaja kutoka Galilayo mpaka Yordani kwa Yohane ili abatizwe….Naye Yesu alipokwisha kubatizwa, mara akapanda kutoka majini na tazama, Mbingu zikamfumukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama ua akija juu yake. Na tazama sauti toka Mbinguni ikisema “Huyu ni mwanangu mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” (Mt 3:13,16- 17)

Tuombe!

Ee Mungu, kwa fadhila zako, kwa maji na Roho Mtakatifu, tunazaliwa katika maisha ya uzima wa milele. Tunakusihi kwa wema wako, uendelee kuzimimina Baraka zako juu yetu; na kutufanya kuwa wanafamilia wa Taifa lako Takatifu. Amina.

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

Yesu anageuza maji huko Kana

Na siku ya tatu, palikuwa na harusi huko Kana, mji wa Galilayo; naye Mama yake Yesu alikuwepo, Yesu naya alikuwa na pamoja wanafunzi wake, Hata divai ilipo watindikia mama yake Yesu akamwambia, Hawana divai, naye

Page 19: Rozari takatifu

Yesu akageuza maji kuwa divai.” Naye mkuu wa meza akaonja yale maji yaliyopata kuwa divai….. Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kanani ya Galilayo, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. Yoh. 2:1-3, 9,11).

Tuombe!Ee Bwana, tunakuomba ujalie upendo, ukiimarishwa na neema ya sakramenti ya ndoa, uweze kushinda udhaifu na majaribu yoteyanayozikumba familia zetu wakati mwingine. Kwa maombezi ya familia Takatifu ya Nazareti, Ilijalie kanisa liweze kutekeleza utume wake kwa fanaka duniani kote, ndani ya familia, na kwa njia ya familia. Amina(Papa Paulo Yohane Paulo wa Pili)

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

3. Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu

Hata baada ya Yohane kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya akihubiri habari njema ya Mungu, akisema, “Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribi, tubuni na kuiamini Injili. (Mk. 1:14-15)

Tuombe!

Tuwaombee watu wote wanaume kwa wanawake, wa kila kabila na taifa, ili wammtambue Mungu mmoja, aliye Baba wa wote, kwa mshikamano wa undugu, waweze kuutafuta ufalme wake ambao ni Amani na furaha katika Roho Mtakatifu. Amina.

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1

Page 20: Rozari takatifu

Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

4. Yesu anageuka sura

Baada ya maneno hayo, yapata siku nane, aliwatwaa Petro na Yakobo, akapanda milimani ili kuomba. (Ikawa katika kuomba kwake, sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta, sauti ikatoka katika wingu, ikisema “huyu ni mwanangu, mteule wangu, msikilizeni yeye. (Luk.9:28-35)

Tuombe!

Ee Bwana tunakuomba uinue nyoyo zetu juu ya udanganyifu wa vitu tuvionavyo, uoga na wivu, ubinafsi na uchoyo, mila na mitindo mibovu na kuzituliza kwenye ukweli wako wa milele,ili tuweze ili tuweze kuishi kwa furaha, tukitumaini kwa Imani kwamba umwokozi wetu,mfalme na rafiki yetu, hapa duniani na katika uzima ujao. Amina

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

5. Yesu anaweka Ekaristi takatifuNao walipokuwa wakila, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa akisema, “twaeni; huu ndio mwili wangu” akatwaa na kikombe, akashukuru akawapa wakakinywea wote. Akawaambia, hii ndiyo damu yangu ya agano, kwa ajili ya wengi. Amini nawaambia ninyi: sitakunywa tena kabisa mzao wa mizabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya katika ufalme wa Mungu. (Mk. 14:22-25)

Tuombe!

“Upende kutufanya, Ee Bwana, tustahili kuwatumikia ndugu zetu, wanaume kwa wanawake, duniani kote, ambao wanaishi na kufa katika umasikini na njaa. Leo hii mkate wao wa kila siku, na kwa upendo wetu, wajalie Amani na furaha” (Mama Teresa wa Calcuta).

Page 21: Rozari takatifu

Tuwasifu milele – Yesu, Maria na Yosefu…x1Damu ya Kristu – iziokoe Roho zinazoteshwa rohoni, izilijazie mwanga wa milele. Amina.

Ee Yesu mwema utusamehe dhambi zetu,utukinge na moto wa milele, ongoza roho za watu wote ili wote wafike mbinguni, hasa wale wanaohitaji zaidi huruma yako.AMINA.Baba yetu x1Salamu Maria x10Atukuzwe Baba……x1

LITANIA YA BIKIRA MARIA

Litania ya Bikira MariaBwana, utuhurumie, - Bwana utuhurumie.Kristu, utuhurumie, - kristu, utuhurumieBwana, utuhurumie, - Bwana utuhurumie.Bwana wa Mbinguni, Mungu utuhurumie.Mwana mkombozi wa dunia, Mungu, utuhurumie.Mwana, Mkombozi wa dunia, Mungu, utuhurumie.Roho, Mtakatifu, Mungu, utuhurumie.Roho Mtakatifu, Mungu, utuhurumie.Utatu Mtakatifu, Mungu mmoja, utuhurumie.Maria Mtakatifu, Utuombee.Mzazi Mtakatifu wa Mungu,Bikira Mtakatifu, wa Mabikira.Mama wa Kristu.Mama wa neema wa Mungu.Mama Mtakatifu kabisa.Mama mwenye usafi wa moyo.Mama mwenye ubikira.Mama usiye na dhambi.Mama mpendevu.Mama mstaajabivu.Mama wa shauri jema.Mama wa Muumba.Mama wa Mkombozi.Bikira mwenye utaratibu kamili.Bikira mwenye heshima.Bikira mwenye sifa.Bikira mwenye enzi kuu.sababu ya furaha yetu,Chombo bora cha ibada,Waridi lenye fumbo,Mnara wa Daudi,Mnara wa pembe,Nyumba ya dhahabu,

Page 22: Rozari takatifu

Chombo cha agano,Mlango wa Mbingu,Nyota ya asubuhi,Salaamu ya wagonjwa,Kimbilio la wakosefu,Mtuliza wa enye huzuni,Msaada wa wakristu,Malkia wa malaika,Malkia wa mababu,Malkia wa manabii,Malkia wa mitume,Malkia wa mashahidi,Malkia wa waungama ,Malkia wa mabikira,Malkia wa watakatifu wote,Malkia uliyeumbwa pasipo dhambi ya asili,Malkia uliyepokelewa mbinguni,Malkia wa rozari takatifu,Malkia wa Amani,Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,utusamehe, Bwana.Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,utusikilize, Bwana.Mwana kondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,utuhurumie.

K. Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu.W, Tujalie ahadi za Kristu.

Tuombe: Ee Bwana Mungu, tujalie sisi watumishi wako kuwa na uzima waroho na wa mwili siku zote, twakuomba kwa ajili ya maombezi matukufu ya Bikira daima, tuopolewe katika masikitiko ya sasa, tupate furaha za milele. Kwa Kristu, Bwana wetu. W. Amina.

Tuombe!

Ee bwana, twakuomba utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote, na kwa maombezi ya matukufu ya Maria Mtakatifu Bikira daima tuopolewe katika masikitiko ya sasa, tupate furaha za milele. Kwa Kristu, Bwana wetu. W. Amina.

MemorareUkumbuke, ee Bikira maria mpole mno, / toka zamani za kale haikusikiwa, / kwamba ulimwacha mtu aliyefuata ulinzi wako, /akiomba msaada wako, / akitaka maombezi yako. / Kwa matumaini hayo ninakimbilia kwako, /Bikira wa mabikira, /ninakuja kwako, /ninasimama mbele yako /nikilalalamika miye mkosefu: /Mama wa wa neon la Mungu, /usikatae maneno yangu, / bali uyasikilize uyatimize. Amina.

Page 23: Rozari takatifu

Moyo Mtakatifu wa Yesu, UtuombeeMoyo Mtakatifu wa YesuMoyo Mtakatifu wa YesuWatakatifu wote wa Mungu, Mtuombee.

Salamu Malkia

Tunaukimbilia