sera ya maji ya taifa

20
Sera ya Maji ya Taifa Warsha ya Waandishi wa Habari ARM Hotel – Novemba 08 – 09, 2010

Upload: darajatz

Post on 23-Jan-2015

1.646 views

Category:

News & Politics


6 download

DESCRIPTION

 

TRANSCRIPT

Page 1: Sera ya maji ya taifa

Sera ya Maji ya TaifaWarsha ya Waandishi wa Habari

ARM Hotel – Novemba 08 – 09, 2010

Page 2: Sera ya maji ya taifa

YaliyomoSera ya maji 1991Mapitio ya sera ya maji ya 1991Sera ya maji ya mwaka 2002Malengo ya seraMuundo wa seraHuduma za maji vijijiniMasuala ya kiseraWatekelezaji wa sera ni nani

Page 3: Sera ya maji ya taifa

Sera ya Maji ya 1991

Sera ya kwanza ya maji Tanzania

Lengo: Maji safi na salama kwa wote ifikapo 2002

Serikali ndio mwekezaji, mwendeshaji na msimamizi wa miradi na mtunzaji wa rasilimali

Page 4: Sera ya maji ya taifa

Mapitio ya Sera ya Maji 1991Yalianza mwaka 1996Sababu – Mapungufu ya sera ya 1991

Hali halisi ya upatikanaji maji na uendelevu 50% wanapata maji, 30% vituo vya maji havifanyi

kaziKutoshirikisha kikamilifu wadau hususan

wananchiKutoipa umuhimu sekta binafsi ktk utoaji

hudumaMapungufu katika mfumo wa kitaasisi na

kisheria

Page 5: Sera ya maji ya taifa

Sera ya Maji ya 2002 Imetokana na mapitio ya sera ya mwaka 1991Imeandaliwa kushirikisha wadau wote

muhimuImeundwa kuzingatia malengo ya dira ya

taifa 2025 na MKUKUTAImeweka mfumo madhubuti na endelevu wa

kusimamia rasilimali za majiPia taratibu za kisheria na muundo wa

kitaasisi wa kutekeleza sera

Page 6: Sera ya maji ya taifa

Malengo ya SeraKushirikisha walengwa kubuni, kupanga,

kujenga, kuendesha, kufanya matengenezo na kuchangia gharama za huduma

Utunzaji na usimamizi endelevu wa rasilimali za maji kwa kushirikisha wadau wote

Kupunguza majukumu ya utekelezaji kwa serikali – ili kusimamia, kuratibu, kushauri, kuwezesha na kutoa miongozo

Page 7: Sera ya maji ya taifa

Muundo wa SeraSera ina sehemu kuu tatu

i. Usimamizi wa rasilimali za maji- kuweka na kuendeleza mfumo endelevu na

madhubuti wa kusimamia rasilimali maji

ii. Utoaji wa huduma ya maji vijijini- Kuboresha afya za wananchi wa vijijini, kuchangia

kupunguza umasikini kwa kutoa huduma endelevu ya maji safi, salama na ya kutosha

iii. Utoaji wa huduma ya majisafi na majitaka mijini

- Kuweka mfumo endelevu wa kutoa huduma kwa bei nafuu ili makundi yote yafaidike

Page 8: Sera ya maji ya taifa

Huduma ya Maji Vijijini

Mikakati itakayotumika katikautekelezaji wa sera ili kufikia

madhumuni yasera kwa maeneo ya vijijini

Page 9: Sera ya maji ya taifa

MadhumuniUpatikanaji wa huduma endelevu kwa gharama iliyo ndani ya

uwezo wa wananchi vijijini.

Kuweka bayana majukumu na wajibu wa wadau mbalimbali.

Kuweka mkazo wananchi kulipia sehemu ya gharama za ujenzi wa miradi, gharama zote za uendeshaji na matengenezo ya miradi yao

Kubadili utaratibu ili wananchi wabuni, waanzishe na kuendesha miradi yao wenyewe.

Kuhamasisha Sekta Binafsi kushiriki katika kugharamia, kujenga, kuendesha na kutoa huduma ya maji vijijini.

Kuboresha afya ya jamii kwa kuunganisha mipango ya utoaji wa huduma ya maji, usafi wa mazingira na elimu ya afya.

Page 10: Sera ya maji ya taifa

Misingi ya SeraMaji ni hitaji la msingi na haki ya kila mtuMatumizi ya maji kwa ajili ya binadamu ni

muhimu kwanzaMaeneo yenye uhaba kupewa kipaumbele cha

miradiMaji ni bidhaa ya kiuchumiKulinda na kuhifadhi vyanzo vya majiHuduma endelevu

Page 11: Sera ya maji ya taifa

Masuala ya kiseraUshiriki wa jamii

Kumiliki miradi ya maji, kuchagua teknolojia, kubuni, usanifu, ujenzi wa miradi, uendeshaji na matengenezo ya miradi

Kushirikisha sekta binafsi kutoa huduma ya maji vijijini

Serikali kuwa mdhibiti, mwezeshaji na mratibu wa maji vijijini

Jinsia zote kushiriki kikamilifu katika miradi ya maji

Page 12: Sera ya maji ya taifa

Masuala ya kisera....Kiwango cha chini cha utoaji huduma vijijini

Lita 25 za maji safi na salama kwa mtu kwa siku Vituo vya maji viwe umbali usiozidi mita 400 Kila kituo kuhudumia watu 250

Udhibiti wa utoaji huduma za maji vijijiniWananchi kugharamia miradi ya maji vijijiniWananchi kuendesha miradi yao ya maji

kisheriaKuwa na mfumo mzuri wa ufuatiliaji na

tathmini ya miradi ya maji

Page 13: Sera ya maji ya taifa
Page 14: Sera ya maji ya taifa

Ni nani watekelezaji wa sera ya maji?1. Wananchi

Ndio watekelezaji wakuu. Wanapaswa

Kubuni, kumiliki, kusimamia na kuiendesha miradi yao ya maji. Kulipia gharama za uendeshaji, matengenezo, ukarabati na

upanuzi wa miradiya majiKulinda vyanzo vya maji na maeneo yanayozunguka vyanzo

hivyo. Kuhakikisha kuwa kuna uwiano mzuri kati ya teknolojia

iliyochaguliwa na kiwango cha huduma na upatikanaji wa maji kwa upande mmoja, na uwezo wa kiuchumi wa watumiaji maji wenyewe kwa upande mwingine.

Kutambua kuwa wanawake ni miongoni mwa wahusika wakuu katika utoaji wa huduma ya maji vijijini.

Page 15: Sera ya maji ya taifa
Page 16: Sera ya maji ya taifa

Ni nani watekelezaji wa sera ya maji.......

2. Serikali za MitaaJukumu kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya

maji safi na salama.Hivyo ni wasimamizi na wawezeshaji wa jamii. Majukumu

yao ni;• Kusimamia na kufuatilia upatikanaji wa maji.• Kusimamia vyombo vya watumia maji na kuhakikisha jamii

inakusanya fedha kwa ajili ya marekebisho ya miradi ya maji• Kuhakikisha miundombinu ya maji inalindwa, na kufanyiwa

matengenezo• Kutoa msaada wa kitaalamu tatizo linapotokea• Kuwezesha wanajamii kupata vipuri pale ambapo

vinahitajika

Page 17: Sera ya maji ya taifa
Page 18: Sera ya maji ya taifa

Ni nani watekelezaji wa sera ya maji?....

3. Wizara ya Maji na UmwagiliajiNi wasimamizi wakuu wa seraMajukumu yao ni

kuandaa sera na mipangokuratibu, kusimamia na kutoa miongozokuziwezesha halmashauri za wilaya, kukagua

na kutathimini utekelezaji wa miradi ya maji

Page 19: Sera ya maji ya taifa

Ni nani watekelezaji wa sera ya maji?.....4. Mashirika binafsi na Vyombo vya habari

Kuhakikisha sera zinawanufaisha wananchiKusambaza taarifa za kisera, mipango na bajetiKutoa elimu kwa ummaKuhamasisha ushiriki wa wananchiKuwajengea uwezo wananchi ili;

Kushiriki katika utekelezaji wa sera Kufuatilia utekelezaji wa sera Kutathmini utekelezaji wa sera

Page 20: Sera ya maji ya taifa

Asanteni

Maswali na maoni

Karibuni