shuhuda za kweli fb

4
Page 1 of 4 SHUHUDA ZA KWELI Tumepokea barua pepe kutoka kwa waliosoma na kuathirika na kitabu chetu kinachoitwa “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” na sasa kimefasiriwa kwa Kiswahili na kujulikana kwa jina “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno”. Waliotuandikia barua pepe ni watu tusiowajua kabla na hatujawaomba watuandikie ila tu wameathirika na kitabu na wakaamua watuandikie barua. Hii itakuwa kiashirio chema cha athari, umuhimu na Taufiq ya hiki kitabu. Hawa ni wachache tu ya wale walioathirika na wakaamua kutuma barua pepe. Na Allah anajua wangapi wameathirika na hawakauona umuhimu wa kuonesha taathira iliyowapata kupitia njia hiyo. Soma baadhi ya shuhuda hizi hapa: Mwanamke (Mzungu) afanyae kazi katika kituo cha kijeshi cha Marekani huko katika ncha ya Kaskazini mwa Dunia (North Pole). “Assalaam alaykum kaka, mimi ni dada ninayefanya kazi katika kituo cha kijeshi cha Marekani huko ncha ya kaskazini mwa dunia (North Pole). Nilitumia muda wa mwezi mtukufu wa Ramadhan nikiwa Nairobi na nikapata bahati ya kununua kitabu chako “Wao Ima Ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” kutoka msikiti mkubwa wa Jamia. Maasha-Allah! Ni kitabu chenye uzuri ulioje! Namuomba Allah [s.a] akulipe kwa juhudi zako. Nimenunua nakala ya ziada kwa ajili ya rafiki yangu pia.” [J’nne, 18 Sep 2012, Saa 11:24 jioni]. Katika barua pepe nyengine, aliandika; “Nimenunua toleo jipya la 2012 na nikaanza kumuelezea rafiki yangu wa karibu huko London kuhusu uzuri na umuhimu wa kitabu hiki na ameweka nia ya kukiagizia vile vile.” [Ijumaa, 12 Okt 2012, saa 12: 21 maghrib]. Asie-Muislam akisomea PhD ya umisheni, Afrika ya Kusini. “Najisikia faraja kukuandikia Bw. Salim Boss. Jina langu ni …. Mwanafunzi wa PhD ya umisheni katika Chuo Kikuu cha North West, Afrika ya Kusini. Nilikuwa nafanya utafiti wangu huko Eldoret-Kenya na nikatokea kukipitia kitabu chako “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno.” Kwa muda mchache, nikaweza kuona mada nyingi zenye umuhimu na zinazovutia zilizoongelewa katika kitabu hiko. Japokuwa sikuweza kusoma kitabu hiki kwa sababu zisizoepukika. Kwa bahati, niliweza kupata anuani yako ya barua pepe kutoka nyuma ya kitabu. Na hii ndio sababu ya kukuandikia barua hii, kukuomba vipi naweza pata nakala yangu iliyofanana na ile. Kwa sasa nafanya kazi kote, Eldoret na Nairobi, Kenya na ningeshukuru kama ukinielekeza mahala pa kuweza kukinunua kabla sijarudi zangu Afrika ya Kusini. Nasubiria jibu lako haraka.” [J’tatu, Juni 20, 2011 saa 3:54 usiku] Dada wa Kiiislam kutoka Mombasa “Asslaaalm alaykum Warahamatullah Wabarakaatuh kaka Salim Omar, Barakallahu fiiqah kwa ukusanyaji wako “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno”. Nimekipitia na maasha-Allah ningependa kupata nakala yangu kwani hiki nilikipata kwa ndugu aliyopewa kama zawadi, tafadhali nielekeze wapi naweza pata nakala yangu, hii ni hazina inayoweza kuleta mabadiliko makubwa kwa watu wengi,…” [J’tatu, Nov 26, 2012, saa 4 na nusu Usiku]

Upload: salim-omar

Post on 07-Nov-2015

155 views

Category:

Documents


3 download

DESCRIPTION

Katika hii PDF utasoma shuhuda za watu tofauti tofauti kutoka nchi tofauti kuhusu vile kitabu cha "Waerevu Mno au Wajinga Mno" kilivyowaathiri.

TRANSCRIPT

  • Page1of4

    SHUHUDA ZA KWELI Tumepokea barua pepe kutoka kwa waliosoma na kuathirika na kitabu chetu kinachoitwa They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant na sasa kimefasiriwa kwa Kiswahili na kujulikana kwa jina Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno. Waliotuandikia barua pepe ni watu tusiowajua kabla na hatujawaomba watuandikie ila tu wameathirika na kitabu na wakaamua watuandikie barua. Hii itakuwa kiashirio chema cha athari, umuhimu na Taufiq ya hiki kitabu. Hawa ni wachache tu ya wale walioathirika na wakaamua kutuma barua pepe. Na Allah anajua wangapi wameathirika na hawakauona umuhimu wa kuonesha taathira iliyowapata kupitia njia hiyo. Soma baadhi ya shuhuda hizi hapa:

    Mwanamke (Mzungu) afanyae kazi katika kituo cha kijeshi cha Marekani huko katika ncha ya Kaskazini mwa Dunia (North Pole).

    Assalaam alaykum kaka, mimi ni dada ninayefanya kazi katika kituo cha kijeshi cha Marekani huko ncha ya kaskazini mwa dunia (North Pole). Nilitumia muda wa mwezi mtukufu wa Ramadhan nikiwa Nairobi na nikapata bahati ya kununua kitabu chako Wao Ima Ni Waerevu Mno au Wajinga Mno kutoka msikiti mkubwa wa Jamia. Maasha-Allah! Ni kitabu chenye uzuri ulioje! Namuomba Allah [s.a] akulipe kwa juhudi zako. Nimenunua nakala ya ziada kwa ajili ya rafiki yangu pia. [Jnne, 18 Sep 2012, Saa 11:24 jioni].

    Katika barua pepe nyengine, aliandika;

    Nimenunua toleo jipya la 2012 na nikaanza kumuelezea rafiki yangu wa karibu huko London kuhusu uzuri na umuhimu wa kitabu hiki na ameweka nia ya kukiagizia vile vile. [Ijumaa, 12 Okt 2012, saa 12: 21 maghrib].

    Asie-Muislam akisomea PhD ya umisheni, Afrika ya Kusini.

    Najisikia faraja kukuandikia Bw. Salim Boss. Jina langu ni . Mwanafunzi wa PhD ya umisheni katika Chuo Kikuu cha North West, Afrika ya Kusini. Nilikuwa nafanya utafiti wangu huko Eldoret-Kenya na nikatokea kukipitia kitabu chako Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno. Kwa muda mchache, nikaweza kuona mada nyingi zenye umuhimu na zinazovutia zilizoongelewa katika kitabu hiko. Japokuwa sikuweza kusoma kitabu hiki kwa sababu zisizoepukika. Kwa bahati, niliweza kupata anuani yako ya barua pepe kutoka nyuma ya kitabu. Na hii ndio sababu ya kukuandikia barua hii, kukuomba vipi naweza pata nakala yangu iliyofanana na ile. Kwa sasa nafanya kazi kote, Eldoret na Nairobi, Kenya na ningeshukuru kama ukinielekeza mahala pa kuweza kukinunua kabla sijarudi zangu Afrika ya Kusini. Nasubiria jibu lako haraka. [Jtatu, Juni 20, 2011 saa 3:54 usiku]

    Dada wa Kiiislam kutoka Mombasa

    Asslaaalm alaykum Warahamatullah Wabarakaatuh kaka Salim Omar, Barakallahu fiiqah kwa ukusanyaji wako Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno. Nimekipitia na maasha-Allah ningependa kupata nakala yangu kwani hiki nilikipata kwa ndugu aliyopewa kama zawadi, tafadhali nielekeze wapi naweza pata nakala yangu, hii ni hazina inayoweza kuleta mabadiliko makubwa kwa watu wengi, [Jtatu, Nov 26, 2012, saa 4 na nusu Usiku]

  • Page2of4

    Dada wa Kiislamu anaesoma Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kenya.

    Assalaam Aleikum Salim. Naomba barua hii ikufikie ukiwa katika afya njema inshaAllah. MashaAllah, Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno ni kitabu kizuri mno, nina uchache wa maneno kuelezea uzuri wake. Ila jua ni kitabu kizuri kwa Muislamu yeyote yule, hasa hasa kwa vijana. nikiwa mwanafunzi wa chuo, nilikihitaji kweli kitabu hiki. Kinakufanya ujihisi u-mbora/ujifakhirir kwa kuwa (dada wa) Kiislam. Unajua kwanini kitabu hiki kina utofauti na vitabu vingi nilivyowahi soma? Kwa sababu kitabu hiki kinaelezea maisha yetu halisi, vitu vinavyotokea kwa sasa na sio vitu vilivyotokea karne zilizopita. Unatumia watu maarufu ambao vijana wanawatambua na kwa kuongezea, kitabu kinavutia kwa rangi zake!!!! Namuomba Mwenyezi abariki kazi ya mikono yako na akuongoze katika njia iliyo sawa kama unavyotuongoza sisi tuliobakia ambao ni waja wake., amiin! Nakisubiri kwa hamu kitabu kinachofuata Between Mars and Venus (Baina Sayari ya Mas na Zuhura). Kwa sasa nitaendelea kusoma na kukisoma Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno. [Jtatu, Nov 28, 2011 saa 1:59 jioni]

    Mmarekani kutoka New Jersey, U.S.A

    Umefanya kazi nzuri!!! [Alhamis, Mei 19, 2011 saa 9:13 alasiri]; Inabidi ukiuze kitabu chako kupitia amazon.com, watu watavinunua tena sana!!! [Juni 22, 2011]

    Mwanaume kutoka Harare, Zimbabwe.

    Assalaam Alaikum kaka Salim Boss, nakuandikia kutoka Harare, Zimbabwe. Nimepatiwa leo nakala ya kitabu chako kipya kuhusu Uislam na visa vya waliosilimu (Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno). Mimi ni Msomali, niliezaliwa katika familia ya Kisomali na ya Kiislamu, lakini inabidi nikiri ukweli tu kuwa, nimetokwa na machozi zaidi ya mara moja wakati nakisoma kitabu chako. Weledi uliyotumia kuandikia kitabu hiki ni mzuri mno usio na dosari. Umeweza kuvuka utamaduni uliozoeleka wa kuandika vitabu vya dawah, ambayo huwa haina mifano hai. Utumizi wa visa vya kweli vya watu maarufu, unajirudia mara nyingi katika masikio ya wale wanaowajua. Nakutumia ujumbe huu, kukueleza kuwa, kitabu hiki sio tu kinawavuta wasio-Waislamu katika Uislam bali pia kinatia nguvu nyoyo na akili za walio Waislam katika dini hii nzuri. Kinampa mtu imani zaidi na kinamhakikishia usahihi wa ujumbe wa Allah ambao umeshakuwa kaa la moto kuubeba katika maeneo mengi duniani. Shukran Jazeelan na naomba uniambie wapi naweza nunua hiki kitau chako kwa wingi sana ili niweze wapatia watu wengine kwani nataka kuwaalika katika ukweli. [Jpili, Aprili 22, 2012 saa 11:38 jioni]

    Mhitimu wa shule ya sekondari ya Kenya.

    Assalaam aleykumhii ni kutokana na kitabu chako kama nilivyoeleza hapo juu. Mimi ni , nimehitimu elimu yangu ya sekondari kupitia Kenya High School hivi punde. Nimekuwa nikisoma kitabu chako kwa muda sasa, sijakimaliza chote kutoka jalada la mwanzo mpaka la mwisho, lakini nishapitia sehemu kubwa ya kitabu, na nimekirudia mara kadhaa. Napata ile hali ya kusoma kitu na kujiuliza hivi ilikuwaje, na kisha kwenda kupitia tena na tena. Wallah, kitabu kile kinashangazasi cha kawaidachatoka sayari nyenginesijui niseme nini Wallahikimenifanya nitafakari, na sio tu kutafakari bali kutafakari kwa kina. Unajua tumegundua kuwa kuzaliwa katika Uislam bado haimaanishi ndio unajua kila kitu kuhusu Uislam, na hawa Waislam wapya kila siku wanakufanya ufikirinimeufanyia nini Uislam kwa kweli?...wewe umweza kusema, na nakiri kitabu kimebadili maisha yangu...kwa hali ya juuna naamini kimefanya hivyo kwa wengi zaidi.Subhaanallah! Sijui tunaweza tumia njia gani kukisaidia kitabu chako kiwafikie wengi zaidi, najua wengi watakuwa bado hawajakijua, na kama tukiweza kukifikisha kwa watu, kitaleta mabadiliko makubwa,makubwa mno. Kinasema mambo watu wanayoyahitaji, unajua tunapaswa kufungua macho yetu na hiki kitabu kwa kweli ni kifungua machonimekitangaza katika akaunti yangu ya Facebook na naamini kutakuwa na watu watakaothirika. Shukran sana. [Alhamis, Nov 17, 2011 saa 1:52 asubuhi]

  • Page3of4

    Mtu kutoka jimbo la Maiduguri Borno, Nigeria.

    Shukrani zote zinamstahiki Allah. Naomba Allah [s.a] aendelee kukubariki na kukulinda wewe na familia yako, kukulipa hapa duniani na akhera kwa kutengeneza kitabu hiki kizuri inshaallah. Kimenivutia sana na huwa nakisoma kila siku kwa kuongeza imani yangu kama Muislam, na uhakika ni kitabu kitachoongeza imani yako kama Muislam. Nitaendelea kukisoma na nitajitahidi kupata nakala zaidi kwa ajili ya jamaa na rafiki zangu hata kwa wasio-Waislam ambao naamini watasalimu amri kwake inshaAllah. [Jmosi, Des 17, 2011 saa 11:09 usiku]

    Jamaa kutoka Mombasa, Kenya.

    Kwa bahati tu nilijikwaa katika kitabu chako Wao ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno na sikusita kusema kama ni muunganiko wa hazina nyingi, MaashaAllah. Siku zote nimekuwa na ndoto za kutengeneza kazi kama hiyo lakini amini sikufikiria kwa kiwango ambacho wewe umefikia. Inaonekana umetumia rasilimali zako nyingi kufanyia utafiti, kukusanya na kuchapisha kitabu kama hiki ambavyo ni vichache mno. Namuomba Allah akulipe zaidi kwa jitihada zakoamiin [Jtatu, 12 Machi 2012 saa 5:28 asubuhi]

    Jamaa wa Goa, India

    Assalaam Alaykum kaka, shukran kwa juhudi zako kubwa ambazo umezifanya katika kitabu Wao Ima Ni Waerevu Mno au Wajinga Mno. Ningependa kupata nakala mbili za kitabu hiki kwa ajili ya kuwaita watu katika Uislam. Unaweza nieleza kiasi gani natakiwa kulipa ili kuvipata pamoja na usafirishaji kuja huku Goa-India? Na itachukua muda gani kufika hapa? [Jtano, 7 Machi, 2012, saa 7:35 mchana]

    Mwanaume kutoka Kilifi, Kenya.

    Nimesoma kazi yako Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno. Kinavutia sana na kinahamasisha sana. Kusema kweli, nimekipenda [Ijumaa, Feb 10, 2012 saa 11: 39 jioni]

    Mwanafunzi wa Utakwimu Bima kutoka Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta, Kenya.

    Assalaam Alaikum kaka katika Uislam. Je kuna ujira wa jambo zuri zaidi ya uzuri? Allah akulipe kwa kufanikisha utafiti huo mkubwa na kukusanya katika kitabu kimoja bomba.itakuwa sadakatul jaariya kwako.mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta nikichukua shahada ya Utakwimu bima (Bsc, Actuarial Science)Nimekinunua kitabu chako majuma mawili yaliyopita na nimekimaliza jana. Nilihamasishwa kukinunua kwa vile napenda sana kusoma visa vya walio maarufu duniani na wakasilimu. Kitabu kimeweka wazi ukweli mgumu ambao watu wengi (hata Waislamu walio wengi) hawapendi kuuona au kuufikiriaNajaribu kufanyia kazi dini yangu nje na ndani ya chuo, na huwa napenda kujadiliana na wenzangu darasani na hata baadhi ya wahadhiri ambao nimewagundua wanapenda kujiuliza kuhusu Uislam, kuhusu dini na zaidi kwenye taa ambayo wewe (Salim boss) umeweka wazi katika kitabu: kuutafuta ukweli hata kama inabadilisha misimamo yako iliyojikita muda mrefu. (Alhamis, Okt 13, 2011, Saa 11:55 jioni)

  • Page4of4

    Jamaa kutoka Nairobi, Kenya.

    Kwa sasa nasoma kitabu kiitwacho Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno cha Salim Boss, ambacho nakiona kinavutia sana na kilichojaa tafiti nyingi kufikia hatua hadi nataka kukutana na huyo mtunzi. [Jnne, Mei 31, saa 4:25 asubuhi]

    Mwanaume kutoka mahala pasipojulikana

    Haloo, u hali gani? Wakati nikiwa napita katika kipindi cha kutojitambua cha maisha yangu, nikakutana na kitabu chako, na nikakipenda. Nimeamua kununua nakala 5 na kuwapatia marafiki zangu wa Kikiristo na wale wasio utendea haki Uislam wao ili na wao waione taa ya maisha kwa sababu nikiwa napita katika kipindi hiki kigumu cha maisha, kitabu hiki kimenisaidia kufanya mambo yawe bora na naomba uniombee na mimi niweze kuwa mbora zaidi. [Jpili, Mei 15, 2011 saa 5:49 asubuhi]

    Dada kutoka Nairobi.

    Assalaam alaikum, Rehma za Allah ziwe kwa Waislam, amiin. Nimekisoma kitabu chako na nikawa na furaha sana kwa kujifunza mengi. Jazaakkallah [Jtano, Aprili 13, 2011 saa 8:40 usiku]

    Ujumbe rasmi kutoka kikundi cha Madaiyah wa kujadiliana na Wakristo (Comparative religion Dawah Group) la Uganda.

    Assalaam alaikum bwana Salim Boss. Kitabu chako ni kizuri mno, Allah [s.a] akulipe kheri na kukiwezesha kibadilishe maisha ya wengiDhumuni la barua hii ni kwa pia kuomba nakala za kitabu hiki murua kwa ajili ya wana-Uganda. Niko na nia ya kuvisambaza bure kwa vyuo vikuu na shule za sekondari na Taasisi nyenginezo hasa hasa kwa wasio-Waislam. Tunatumai juhudi zetu za Dawah zitaongezwa nguvu sana kwa kufikisha ujumbe huu wa Uislam. Wako katika huduma za Kiislam [Jtatu, Machi 14, 2011 saa 4:58 usiku].

    Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Mount Kenya

    Assalaam alaikum, akhi mimi ni mwanafunzi wa MKU University na baada ya kukisoma kitabu, inabidi nikupe hongera MAASHALLAH WA JAZAKAALLAHU KHEYR. Wasio-waislam wanahitaji vitabu kama hivyo, kazi zenye kutia msukumo, ili waweze kumjua Allah [s.a] na Mtume wake {s.a.w}. Natumai kukutana na wewe siku moja inshaalAllah, naishi Mombasa. [Jtano Aprili 6, 2011 saa 11:32 jioni].

    Mwanamke kutoka Ugiriki

    Ni kitabu kizuri Mashaallah! Je inajuzu kukitangaza katika blogi yangu? Allah akulipe kila la kheir, jazaaka Allah [27 Julai 2010]

    Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na kwake Yeye naelekea. [Q 11:88]