waerevu mno brochure

2
Jishindie Mabilioni kupitia hiki Kitabu Wanaofahamu Kiengereza waliki- soma na kufaidika mno. Lugha ya kwanza ya kitabu ni Kiengereza kwa jina. “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” am- bacho sasa kimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno”. KINUNUE UWE TAJIRI a Tshs. 20,000 Kshs. 1,060 $12 US Bei ya Kitabu Imechapishwa kwa Jalada: Ni Tshs 20,000 Usikinunue kwa zaidi ya hizo [email protected] [email protected] +255 685 661 331 +255 712 216 745 Website: www.extremelysmart.org Blog: www.muerevumno.wordpress.com www.facebook.com/muerevumno Kitabu kina kurasa 672, zote zimechapishwa kwa rangi.

Upload: salim-omar

Post on 16-Apr-2016

160 views

Category:

Documents


14 download

DESCRIPTION

Alichoshuhudia Mwandishi.

TRANSCRIPT

Jishindie Mabilioni kupitia hiki KitabuWanaofahamu Kiengereza waliki-soma na kufaidika mno. Lugha ya kwanza ya kitabu ni Kiengereza kwa jina. “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” am-bacho sasa kimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno”.

KINUNUE UWE TAJIRI

~ Xenia Younes, Mtaalamu wa mitandao, Mgiriki na Meneja wa mahesabu katika kampuni binafsi, Uingereza.

~ Sabine Kuesshauer,Mwanafunzi wa shahada ya pili, kitengo cha Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Leipzig, Ujermani.

“Kitabu hiki ni muungano wa maandiko yali- yopangiliwa kwa taaluma ya hali ya juu, kikiwa kimesheheni nukuu kibao za kweli, picha na kina rundo la vitabu vilivyo muhimu kuvipitia kwa wote Waislamu na Wasio-Waislamu. Vile vile kuna riwaya ambazo si tu zina visa vyenye mvuto bali vimejaa kweli tupu.”

~ Wambui Nyamathwe Kabage, Mwanasheria wa mahakama kuu ya Kenya. Ana shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Sydney.

~ Billow Kerrow,Aliyekuwa waziri kivuli wa fedha na mbunge, Kenya.

“Ni kitabu kinachovutia sana, kili- chojaa tafiti na ni chepesi kuele- weka. Mwandishi wake yuko wazi, mkweli, aliyepangilia hoja zake katika utaratibu na lugha nzuri. Nimefurahia vichekesho vya mwandishi.

“Kwa kitabu hiki, watu kweli wataweza kufikiri”

“Salim Boss ameweza! Hiki kitabu kinaweza kubadilisha fikra zako kuhusu Uislamu.”

www.extremelysmart.org

www.extremelysmart.org

9 789966 162816

ISBN 978-9966-1628-1-6

WAEREVU MNOAUWAJINGA MNO

Wao Ima niKitabu kitawafanya watu

wajishuku kama walikuwa waerevu hapo awali. Kinaweka wazi suala hili la watu

wengi kusilimu na kuwazungumzia baadhi yao walio mashuhuri. Wale waliodhani kuwa Uislamu

ni dini ya Waarabu, Waswahili, Wasomali au waAsia watashtushwa kuona watu wa hadhi, haiba na rangi zote

wanamiminika kuikumbatia dini hii inayodharauliwa, inayoeleweka vibaya zaidi duniani, inayonasibishwa na

ugaidi na inayozungumzwa zaidi katika vyombo vya habari na kwengineko.

Kitabu pia kinatoa tahadhari ya ujio wa utawala wa Uislamu ambao ni tishio kwa mabepari duniani. Tushaanza kusikia waandishi wakitabiri bara la Ulaya (Europe) kuwa Eurabia (bara la Waarabu au Kiislamu); adhana zikisikika katika majiji ya nchi za Magharibi; Sharia za Kiislamu (Shariah Law) zikianza kutumika katika serikali zisizo za dini; mfumo wa uchumi unaoendana na tamaduni za Kiislamu kufuatwa kama kuibuka kwa mabenki ya Kiislamu; mwaka 2007, jina ‘Muhammad’ limeshika nafasi ya pili katika majina waliyogaiwa watoto wengi waliozaliwa Uingereza; la kufurahisha zaidi “Hussein” analala ikulu ya Marekani; na kama alivyosema Prof. Ali Mazrui katika utabiri wake “… kwa miaka 40 ijayo hatimaye tutakuwa na rais wa Marekani Muislamu”; hotuba ya raisi Obama alipotawazishwa rasmi: “Kwa Waislamu, tunahitaji kujipanga upya, kwa kutimiziana maslahi na kuheshimiana.”; na kuna vita vya mila (clash of civilizations) vinavyotarajiwa kutokea; tunaona hata kuku wenye chapa ya Halal katika maduka na migawaha….na mengineyo mengi. Je hatuoni kuwa Shariah ya Kiislamu

kama mfumo mpya wa maisha unaanza kututawala?

Isisahaulike kuwa Sir George Bernard Shaw alitabiri: “Kama kuna dini nyengine itapata

fursa ya kutawala Uingereza na hata Ulaya nzima ndani ya kipindi cha miaka

100 inayokuja basi utakuwa bila shaka ni Uislam.”

Wao Im

a niW

AEREVU MNO

au W

AJINGA MNO

Maisha yako yanaweza kubadilika

Wao Ima niWaerevu Mno au Wajinga Mno

Ujumbe wa mtunzi ni kujaribu kuwafanya watu watumie uwerevu wao wa kufikiri

na si kukubali tu imani zinazolazimishwa kwao kutoka kwa wazazi, viongozi wao wa dini, na mazingira. Anajitahidi kuwaeleza watu kuepuka ule uvivu wa kiakili hivyo, kutumia kanuni ya ‘Jitahidi-Kufikiria-Mwenyewe’ na sio ile ya ‘Kuna-Ambaye-Anaweza-Kunisaidia-Kufikiria-Nahofia-Kuchoka-Nikifanya-Mwenyewe’!?

Kitabu hiki kinaelezea watu mashuhuri waliosilimu pamoja na sababu zao za kufanya hivyo. Kwa kutumia nukuu ya William Wordsworth: “Njooni kwenye taa ya vitu, acha uasili uwe mwalimu wako”, mwandishi kwa uhodari na ustadi wa hali ya juu ametumia uasili kufungua vifungo vyote vya kidini viliyo vichwani mwa watu.

Kwa vile kitabu kilivyoandaliwa katika njia nyepesi ya kusoma, ikiambatanishwa na michoro, picha halisi za watu, na maelezo yaliyo pangiliwa vizuri, masimulizi ya kweli, na rejea zinazoweza kuthibitishwa, mtunzi ameweza bila utata wowote kuonesha nukta yake ya msingi kwa wasomaji.

Kitabu kimeangazia vile binadamu amechoka na maisha ya kisanii ya kutengenezwa na mwanadamu na sasa yuko katika pirika zisizokwisha kutafuta sanaa ya maisha iliyoandaliwa na Mungu. Kitabu kinaonesha jamii, ukweli usiopingika wa waume kwa wanawake sasa wanavyoingia katika Uislam kwa kasi ya ajabu. Pia kinaainisha ukweli wa kuwa Uislam ndio dini inayokua kwa kasi kuliko zote ulimwenguni.

(Inaendelea katika upindo wa nyuma)

www.extremelysmart.org

(Imeendelezwa kutoka upindo wa mbele)

Mwandishi anatumai wasomaji watajiuliza hili suali muhimu: Kwanini hawa waingie katika

Uislam?........ na baadae kutafuta majibu yake.

Takribani miaka 1430 iliyopita Muhammad, Mtume wa Uislam alisema:

“Huu ujumbe (Uislam) utafika kila sehemu ambapo usiku na mchana vinafika (jua linachomoza na kuzama), na Mungu hata acha hata nyumba moja iliyojengwa kwa udongo, tofali, au turubai (yaani si jiji wala kijiji) , ila ataifikisha dini yake katika nyumba hiyo.”

Muhammad pia alisema:

“Bila shaka Mwenyezi Mungu amenionesha mashariki na magharibi mwa dunia, na nikaona mamlaka ya ummah (taifa) wangu yakitawala kote nilipoona”.

Salim Omar, alizaliwa pwani ya Kenya, amehitimu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi mwaka 2006, kwa digrii ya Sayansi ya Siasa na Sosiolojia. Mtu wa sanaa wa kuzaliwa, kipaji alichopewa na Mungu kinachomuwezesha kuona mambo ambayo watu wengine wa kawaida hawaoni. Sanaa ya rangi (kuchora/fine art) ni moja ya shughuli anazopendelea. Kitabu chake kijacho kiitwacho “Between Mars and Venus” (Baina Sayari ya Mas na Zuhura)” kinafikiriwa kuja kuleta mapinduzi ya

kifikra na mabadiliko makubwa ya kihistoria.

“Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. ” [Yeremia 29:13]

Tshs. 20,000

Kshs. 1,060

$12 US

Bei ya Kitabu Imechapishwa kwa Jalada: Ni Tshs 20,000

Usikinunue kwa zaidi ya hizo

[email protected][email protected]

+255 685 661 331+255 712 216 745Website:

www.extremelysmart.orgBlog: www.muerevumno.wordpress.com

www.facebook.com/muerevumno

Kitabu kina kurasa 672, zote zimechapishwa kwa rangi.

Kitabu Kimebadili Maisha ya Wengi

Wamekisoma na Wakasilimu

ALICHOSHUHUDIA MWANDISHINimepokea barua pepe nyingi mno kutoka kwa watu wakinielezea athari zilizowatokea baada ya kusoma kitabu hiki. Mathalan, dada mmoja anaesoma Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya alisema, “Kitabu hiki kinakufanya ujihisi una hadhi kubwa na ufahari (proud) kwa kuwa Muislamu wa kike.” Mhitimu wa elimu ya sekondari (dada wa Kiislamu) alikiri, “Kitabu kimeyabadilisha maisha yangu…tena sana....” Wengine wameweka bayana, baada ya kukisoma kitabu wameweza kupata nguvu ya kuachana na mambo ya haraam. Mwengine kutoka Nigeria kani-tumia barua pepe akieleza kitabu kilivyoongeza imani yake kama Muislam. Akasema: “…Nina uhakika ni kitabu kitakachokuongezea imani yako hata kama wewe ni Muislam, na nitaendelea kukisoma zaidi na zaidi na nitatafuta nakala zaidi kwa ajili ya kukisambaza kwa jamaa na marafiki…” Mtu mwengine kutoka Zimbabwe alikiri kupitia barua pepe akinielezea, “Nimebubujikwa machozi zaidi ya mara moja wakati nakisoma kitabu chako hiki.” Na , amini usiamini, kitabu kimefika hadi North Pole kwani kuna dada mmoja Mmarekani, anaefanya kazi na kituo cha jeshi cha Marekani (US military base) huko North Pole (Ncha ya Kaskazini), ambaye alinitumia barua kunielezea vile kitabu kilimfurahisha mpaka akanunua viwili ili ampelekee mwenzake huko. Dada mmoja kutoka nchi ya Brunei, Darussalam ambaye ni Meneja, Kitengo cha Mahesabu (Account Services), Citibank ya Brunei alinunua kitabu kwa mtandao na hivi ndivyo alivyoniandikia: “Mpendwa Salim Boss...wewe ni genius (umeruzukiwa kipaji cha akili), wewe ni mmoja kati ya mamilioni ambao Allah amewabariki katika ummah huu. MashaAllah. kitabu chako ni kizuri sana kwa kizazi cha sasa. Ni kazi iliyotumia akili ya hali ya juu, Waislam na wasio-Waislam, nikiwemo mimi mwenyewe, wataongozwa kwenda kwenye njia ya kweli, kuelekea katika kitabu cha Allah, Qur’an tukufu....Nitampatia zawadi nakala moja Prof. Syukri, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Sayansi (University of Science, Malaysia.)”

Alhamdulillah, hiki ni kitabu kilichouzika sana. Mmarekani mmoja kutokea New Jersey, alinunua nakala 17 peke yake kupitia mtandaoni ili akigawe kwa wasiokuwa Waislamu. Wanunuzi wa hiki kitabu wanatoka nchi tofauti kama vile United Arab Emirates, Oman, Malaysia, Nigeria, Marekani, na nchi nyenginezo. Taasisi moja ya Ki-islamu ilinunua nakala nyingi na kuzisambaza kwa wafungwa mbalimbali katika magereza ya Kenya. Wengine walinunua kwa madazeni vitumike kwa Da’awah. Muislamu mmoja kutoka India aliomba apewe matayarisho ya kitabu ya kikompyuta (print files) atumie kutengeneza nakala nyingi, ili azigawe kwa wasio-Waislam huko India. Nimepokea maombi ya kutafsiri kitabu kwa lugha za Kifaransa, Kireno, Kiswahili na hata kwa lugha ya Kisomali. Zaidi ya watu 20 000, kutoka nchi 151 tofauti, (wengi zaidi kutoma Marekani) wametembelea website yetu ya kitabu katika mtandao. Cha kushangaza zaidi, nakala za vitabu zilipotuishia, alitokea Muislam (jina kapuni) na kujitolea kiasi kisichopungua Shilingi milioni 30 za Kitanzania kusaidia utengenezaji wa nakala nyengine 5,000 za vitabu. Kitabu pia kimeuzika na bado kinauzika kupitia mtandao wa www.amazon.com kwa wale wenye kifaa cha Kindle.

Kwa taufeeq ya Allah, kitabu hiki kimeleta maajabu kiasi ya kwamba asiyekuwa Muislam kila akikisoma (kwa agha-labu) anasilimu. Na asiyesilimu huheshimu Uislamu. Kwa mfano, Mchina mmoja kwa jina Paris Fuhua Wang ambaye ni Afisa mauzo, Heng Yuan Manufacturing Co., Limited, Guangzhou, China na Mhitimu, Chuo Kikuu cha HAFLRU, Heilong jiang, China. Alikipitia kitabu na kusema yafuatayo: “Mimi sio Muislam ila baada ya kukisoma kitabu hiki, sasa nawaheshimu Waislamu. Natamani siku moja nikutane na mtunzi. Kitabu hiki kimeni-funza mengi.” Alhamdulilah, baadhi ya Watanzania wamesilimu tu baada ya kukisoma. Mmoja kutoka Bukoba aliwasiliana nasi na kusema kuwa, bado yuko katikati ya kitabu na ameamua kusilimu hata kabla hajakimaliza. Hivi karibuni tu (May 2014), Muislamu mmoja kutoka Mbaghala aliwasilimisha watu watatu kupitia hiki kitabu. Na Waislamu wanaokisoma, huzidi imani na kuwa na msimamo kwa dini.

Pata picha John amekipokea kitabu hiki kwa kusababishwa na wewe. Akakisoma na kuuvumbua ukweli wa Uislam na akasilimu. Kutokana na hadithi sahihi, tendo lolote la ibada litakalofanywa na John, thawabu yake it-aingizwa kwenye akaunti yako ya matendo mema pia. Swala ya John itakuwa yako; visimamo vya John usiku kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (Qiyaamu-llail) vitakuwa vyako; thawabu ya John katika ibada yake ya dua itakuwa ni ya kwako pia; thawabu zake katika kufunga hazitakuacha kando; na pale Allah akimtunuku John kwa kutabasamu, wewe utahusika na kupata zako vilevile; ikiwa hiyo haitoshi, John akifunga safari kwa ajili ya kufanya Hijja, utapata thawabu zake za Hijja! Sasa fikiria mlundikano wa thawabu utakaokuwa wako pale tu utaposababisha wasio-Waislam 500 kukipata kitabu hiki na 200 kati yao wakaingia katika Uislam!!! Utakuwa tajiri mno. Ikiwa, kwa uchache, utanunua nakala 3 uwape jirani zako watatu wasiokuwa Waislamu, na mmoja asilimu, utapata thawabu nyingi. Je ikiwa ni kumi wamesilimu, ni mabilioni mangapi ya thawabu utakuwa umejishindia! Mola atupe tawfeeq ya kufikisha dini yake kwa walimwengu. Shukran. Salim Boss (Mwandishi). {July 2014}

Na hata kama wewe ni mwana-biashara, ukikisoma kitabu utapata fikra za kufaidika kiuchumi au kutengenza hela kupitia biashara zinazolenga uwingi wa Waislamu na Wanaosilimu. Ila, bora zaidi ni kutafuta mamilioni ya thawabu kwa kusilimisha watu kupitia hiki kitabu cha Da’awah.