waraka 1 - koinonia-education.com › wp-content › uploads › 2018 › 11 › 12.-waraka-1.pdfwao...

8
WARAKA 1 NYARAKA (barua) maandiko yana uhusiano gani ? Kwani barua (waraka) inahitaji kutafsiriwa ? Mbona yanaeleweka wazi ! Mfano Rum 3:23 ” wote wamefanya dhambi..” , Rum 6:23 ”Mshahara wa dhambi ni mauti”, Ef 2:8 ” Kwa maana mmeokolewa kwa neema, ...” Ni kweli kwamba baadhi ya mistari ni rahisi kuelewa, lakini pia kuna mistari migumu ambayo inatupa shida kidogo. Kwa mfano: 1Kor 7:25f; Paulo anatoa mashauri ya kibinafsi..... maneno yake kweli yana uzito kama ya Mungu ? Wengi wasinge mpa ndugu Paulo uzito huo, ni maneno machungu kidogo yanayopinga kuunda familia kuwa hali bora. 1Kor 5; Je kuna maana yeyote kumtenga mkristo wakati anaweza kuanzisha dhehebu yake mara akipenda ? 1Kor 12-14; Inahusu vipawa, wengine wanadai kwamba nguvu za vipawa zimepitwa na wakati.. 1Kor 11:2-16; Inahusu wanawake kujifunika kichwa wakati wanapoomba na kutabiri, ou swala inayosema waombe na kutabiri katika ibada...? Tukianza kuchunguza tunaona kunauwezekano wa kuleta tafsiri mbali mbali, na kwamba kuna matatizo katika kuelewa jinsi ya kufuatilia na kuelewa maandiko kama haya. Pia shida inazidi wakati tunapoona umuhimu wa kuelewa ujumbe ya barua kama 1Kor. Maana ni barua yenye mafundisho mengi ya muhimu kwa kila mkristo. 1Kor itakua mfano wetu tunapojifunza juu ya kusoma waraka za Agano Jipya

Upload: others

Post on 26-Jan-2021

14 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • WARAKA 1• NYARAKA (barua) maandiko yana uhusiano gani ? • Kwani barua (waraka) inahitaji kutafsiriwa ?

    • Mbona yanaeleweka wazi ! Mfano Rum 3:23 ” wote wamefanya dhambi..” , Rum 6:23 ”Mshahara wa dhambi ni mauti”, Ef 2:8 ” Kwa maana mmeokolewa kwa neema, ...”

    • Ni kweli kwamba baadhi ya mistari ni rahisi kuelewa, lakini pia kuna mistari migumu ambayo inatupa shida kidogo. Kwa mfano:

    • 1Kor 7:25f; Paulo anatoa mashauri ya kibinafsi..... maneno yake kweli yana uzito kama ya Mungu ? Wengi wasinge mpa ndugu Paulo uzito huo, ni maneno machungu kidogo yanayopinga kuunda familia kuwa hali bora.

    • 1Kor 5; Je kuna maana yeyote kumtenga mkristo wakati anaweza kuanzisha dhehebu yake mara akipenda ?

    • 1Kor 12-14; Inahusu vipawa, wengine wanadai kwamba nguvu za vipawa zimepitwa na wakati..

    • 1Kor 11:2-16; Inahusu wanawake kujifunika kichwa wakati wanapoomba na kutabiri, ou swala inayosema waombe na kutabiri katika ibada...?

    • Tukianza kuchunguza tunaona kunauwezekano wa kuleta tafsiri mbali mbali, na kwamba kuna matatizo katika kuelewa jinsi ya kufuatilia na kuelewa maandiko kama haya. Pia shida inazidi wakati tunapoona umuhimu wa kuelewa ujumbe ya barua kama 1Kor. Maana ni barua yenye mafundisho mengi ya muhimu kwa kila mkristo.

    • 1Kor itakua mfano wetu tunapojifunza juu ya kusoma waraka za Agano Jipya

  • WARAKA 2• Maumbile za nyaraka za Biblia

    • Kwanza ni muhimu kutambua kwamba nyaraka zimetofautiana kiuandishi. • Zipo za mtu binafsi, za watu wengi, zinazohusu wote . Zote zimetokana na

    dharura au shida fulani. Labda tu Waraka kwa Filemoni, Waraka wa Yakobo na labda pia Warumi (Waroma). Ziliandikwa katika karne ya kwanza.

    • Jambo hili ya kwamba zimeandikwa katika miaka hiyo, mbali na wakati wetu, zimejaa theologia na pia zimeandikwa kutokana na sababu maalum inatupa shida kidogo wakati tunaposoma.

    • Wanaposhughulikia shida fulani inawezekana muandishi anashochea au kuongeza kidogo kusudi aweze kueleweka kwao wenye kupata hiyo barua. Wao walisaidiwa ila sisi tunashindwa kuelewa maana tunashindwa kujitambua katika shida zao.

    • Mkristo wa kawaida anaweza kujisikia hahusiki na maswala mbali mbali yanayotiwa uzito katika maandiko.

    • Nyaraka zimejaa theologia lakini siyo ”vitabu vya sheria” bali yanahusika na matatizo yaliyokuwepo katika mazingira yale. Kwa hiyo utakuta barua moja inahusu hili, nyingine lile na kuna wakati ni kama zinapingana kwa namna fulani.

  • WARAKA 3

    • Mazingira ya wakati ule (Mazingira ya Kihistoria) 1 • Tunapoanza kufanya kazi katika barua fulani kwanza tunahitaji ku

    ”reconstruct” (kuunda mazingira ya pale ya kihistoria) hali iliyo kuwepo. Maswali ambayo yanafaa ”kuuliza” maandiko.

    • Kuna sababu gani iliyomsababisha Paulo kuwaandikia wakristo wa Korinth ?

    • Habari zao alikua amezipataje ?

    • Alikua na uhusiano gani na Wakorintho ? • Uhusiano wao ulikuaje katika historia ? (Yaani miaka yanyuma) • Anatoa picha gani juu ya wapokeaji wa barua ? • Tunamuonaje Paulo ?

  • WARAKA 4• Mazingira ya wakati ule (Mazingira ya Kihistoria) 2 • Maswali hayo yatapata majibu kwa njia gani ?

    • Kamusi ya Biblia, au commentary inayohusu andiko hili. Vitabu vya historia. Ni kujaribu kufanya utafiti mzuri katika vitabu kusudi kuelewa mazingira ya mahali pale na wakati ule.

    • Tukifanya hivyo tutapata kufahamu kwamba Korinth ilikua mji mkubwa, palikua na watu kabila mbali mbali. Dini na thehebu nyingi zilikuwepo. Wafanyabiashara walikua wengi sana. Ilikua mji yenye mawasiliano mazuri na miji mengine. Hayo yote yanatusaidia kufahamu ”The historical situation ya wakati ule.

    • Hayo yote yanatusaidia katika kufahamu kwa nini anaandika kwa jinsi anavyoandika. • Pia ni vizuri kusoma barua yenyewe kwa mfululizo. Hata mara mbili - tatu. Kumbuka

    kutenga mda wa kutosha kwa zoezi hii. Zoezi hili linataka kukupatia picha ya barua yote. Hatuchambui sana bali tunaisoma ”juu juu”.

    • Rudia kusoma tena, sasa uchukue nots ambayo itakusaidia katika kufahamu mahali na hali ya pale. Kumbuka kuelekeza nots yako kwenye mistari. ”referenses”

    • Unaposoma ”uende na maswali” • 1. Kuna nini kinayohusu; wayahudi au wayunani, matajiri au maskini, wanamatatizo gani,

    wana mtazamo gani ? • 2. Vipi Paulo yukoje, anawaonaje ? • 3. Tunapata kujua sababu zake za kuandika barua hii ? • 4. Kuna ”structure” mpangilio unaojitokeza katika barua ?

  • WARAKA 5• Mazingira ya wakati ule (Mazingira ya Kihistoria) 3 • Pia unaposoma unaweza kusoma kwakutafuta majibu ya maswali. Katika 1Kor majibu yanaweza kua kama yafuatavyo:

    • 1.Waumini waliyowengi wakati huo katika mji wa Korintho ni wayunani. Lakini pia wayahudi wachache wapo. (6:9-11; 8:10; 12:13) Wanapenda sana Hekima na ufahamu (1:18-2:25; 4:10; 8:1-13) Wanakiburi na wanajidai (4:18; 5:2,6) Hata Paulo ”wanamhukumu”(4:1-5; 9:1-18) Hiyo hata wakiwa na matatizo mengi ya ndani ya kikundichao.

    • 2.Paulo yoko katika hali mbali mbali, anawashawishi (4:8-21; 5:2; 6:1-8) Anawasihi (4:14-17; 16:10-11) Anawaonya (6:18-20; 16:12-14)

    • 3.Sababu za kuandika barua ni nyingi. Paulo amepata barua ya watu wa Kloe (1:10-12) katika 5:1 anasema amepata taarifa na katika 7:1 anasema sasa tushughulikie muliyoyaandika. Pia alikuwa amepata barua kotoka kanisa la pale. Inaonekana anajibu maswali yao kwa mpangilio, maswali ambayo amepata katika barua zao. (7:25; 8:1; 12.1; 16:1; 16:12) Katika 16:17 tunalikuta jina la Stefana, Fortunato na Akaio. Na katika mstari wa 16 imeandikwa kwamba wamtii Stefana. Hapo inalekea kuwa kwamba hao walikua viongozi wa kanisa la pale. (Kugundua mambo kama hayo si rahisi sana , usijisikie vibaya kama umepitiwa. Kazi ni kurudia, rudia, rudia maara nyingi halafu kusoma kwa makini sana)

  • WARAKA 6• 4.Halafu inarahisisha tukiweza kukichambua ”kitabu” chetu katika vipindi (vipengele) hapo inatusaidia

    kuangalia kila kipande kwa peke yake. Tunapochambua tunachabua kidoga halafu tuna zidi kukichambua kwa hatua (Angalia uchambuzi wa Johanna katika Survey) Tukigawa 1Kor katka vipande viwili tungeweza kugawa kwenye sura ya 7:1 kwa sababu hapo ndipo anaanza kujibu masawali ya wakristo wa Korintho. Hapo tungaepata ”part 1” sura ya 1-6 ”part 2” 7-16. Halafu tunachambua katika sehemu ndogo ndogo pia njia moja ni kama yafuatavyo:

    • Salamu na shukrani 1:1-9 • Tatizo la kugawanyika kwa waumini wa Korintho 1:10-4:21 • Tatizo la yule bwana aliye lala na mke wa babaye. 5:1-13 • Tatizo la kushatikiana 6:1-11 • Tatizo la kuzinaa 6:12-20

    • Juu ya kuishi bibi na bwana katika ndoa 7:1-24 • Juu ya wasiyooa na kuolewa 7:25-40 • Juu ya vyakula vilivyotolewa kama sadaka kwa miungu 8:1-11:1 • Juu ya mwanamke kujifunika kichwa kanisani 11:2-16 • Juu ya kudharahu ushirika mtakatifu 11:17-34 • Juu ya vipawa vya Roho 12-14 • Juu ya kufufuka kimwili 15:1-58 • Juu ya mchango 16:1-11 • Juu ya kurejea kwa Apolo 16:12 • Salamu na maonyo (vielekezo) 16:13-24

  • WARAKA 7• Maandiko yenye matatizo • Sehemu hizo (1kor 1-4 na Fil 1:27-2:13) siyo maandiko yenye matatizo

    sana, majibu ya maswali yetu tutayapata na pia tutaweza kupata mafundisho fulani. Lakini kunavisehemu vingine ambavyo si rahisi kama hizo. Mfano: ”Kwa ajili ya malaika” 1Kor 11:10 au ”jibatize kwa ajili ya waliyokufa” 1Kor 15:29 au Kristo anapowahubiri ”mapepo katika ufungwa wao” (1Petr 3:19) au ”mwana wa uharibifu” (2Thess 2:3). Tufanyeje sehemu ngumu za namna hiyo ?

    • 1. Tatizo ya fungu inaweza kuwepo sababu siyo sisi tuliyoandikiwa mara ya kwanza. Waliyopokea hayo maandiko walikuwa na ufahamu tofauti na sisi, huenda walipewa mafundisho ”kwa mdomo” iliyowasaidia kufahamu mafundisho ya maandishi. Hayo mafundisho sisi hatunayo (2Thess 2:5-6). Tonaposhindwa kujibiwa maswali yetu ”tusiunde *doctrins”. Inawezekana tutalazimishwa kukubali kwamba ”Maneno yata funuliwa kwa wakati wake” na wakati huo haujawa bado. Tusitoe majibu wakati msingi ni wa wasiwasi. ”Tusiunde” *doctrins yenye msingi wa kuyumba.

  • WARAKA 8• 2. Saa nyingine tunashindwa kuelewa vyote, lakini ”point” ya mwandishi

    tunaielewa. Kwa mfano: 1Kor 15:29 Fungo hii haihusiki na tatizo la ”kubatizwa kwa ajili ya waliyokufa” . Inahusu jinsi waliyoamini juu ya ufufuo. Inaonekana waliyumba sana katika msimamo wao. Maana walidai kwamba ufufuo umeshafanyika katikati yao, yaani wamekua watu wa kiroho, lakini hata hivyo ufufuo huo. Ni kwamba upande mmoja wanasema imeshafanyika lakini upande mwingine wana jaribu kuandaa kwa ufufuo utakaokuja....

    • 3. Katika fungo hii tunaona kwamba Paulo anasema kwamba”Baadhi ya waumini walijibatiza kwa ajili ya waliyokwisha kufariki” Hasemi kwamba ni mbaya au nzuri anaeleza tu. Hatuwezi kupata ufumbuzi zaidi ya kitendo hiki . Wala kufanya doctrin juu ya mambo haya hatuwezi kwa msingi huo tu. Ingawa Paulo hapa hapingi kitendo hiki kunasehemu nyingine katika Biblia inayoweza kutuelekeza juu ya swali hi.

    • 4. Wakati maandiko yanakuwa magumu kiasi hiki ni vizuri kutafuta commentary nzuri ya sehemu hii. Hapo utaweza kusoma juu ya njia mbali mbali za kuelewa andiko lenyewe halafu mwenyewe utaweza kuangalia uzito wa ufahamu unaelekea wapi. Lakini wakati tafsiri ya andiko fulani inatengana katika tafsiri mbali mbali hatuwezi kufikia msimamo kamili. Itabidi tukubali kwamba ni makisio na inabidi tuwe wanyenyekevu katika kutetea msimamo wetu.