· web view“kwa maelezo ya ki-kristo, dunia kwa mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na...

165
Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved. HUDUMA YA KIMATAIFA YA KUWAIMARISHA WACHUNGAJI THEOLOJIA YA KI-BIBLIA na Jonathan M. Menn B.A., University of Wisconsin-Madison, 1974 J.D., Cornell Law School, 1977 M.Div., Trinity Evangelical Divinity School, 2007 Equipping Church Leaders-East Africa 3701 N. Gillett St., Appleton, WI 54914 (920) 731-5523 [email protected] www.eclea.net December 2009; revised February 2011. Theolojia ya Ki-Biblia ni mkondo wa maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji wa nchi na mwanadamu katika Mwanzo, kupitia anguko la mwanadamu na matokeo yake, na historia ya ukombozi wa Mungu kwa mwanadamu, hata utimilifu wa mbingu mpya na nchi mpya katika Ufunuo. Biblia inaeleza ksimulizi

Upload: others

Post on 08-Jan-2020

102 views

Category:

Documents


19 download

TRANSCRIPT

Page 1:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

HUDUMA YA KIMATAIFA YA KUWAIMARISHA WACHUNGAJI

THEOLOJIA YA KI-BIBLIA

na

Jonathan M. Menn

B.A., University of Wisconsin-Madison, 1974J.D., Cornell Law School, 1977

M.Div., Trinity Evangelical Divinity School, 2007

Equipping Church Leaders-East Africa3701 N. Gillett St., Appleton, WI 54914

(920) [email protected]

www.eclea.net

December 2009; revised February 2011.

Theolojia ya Ki-Biblia ni mkondo wa maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji wa nchi na mwanadamu katika Mwanzo, kupitia anguko la mwanadamu na matokeo yake, na historia ya ukombozi wa Mungu kwa mwanadamu, hata utimilifu wa mbingu mpya na nchi mpya katika Ufunuo. Biblia inaeleza ksimulizi

inayofungamana, huku Yesu Kristo akiwa ndiye moyo wake. Theolojia ya Ki-Biblia huangalia dhana kuu ambazo zinazopitia katika Biblia nzima, zinazolenga juu ya uhusiano wa Mungu na mwanadamu. Pia huonyesha jinsi Kristo na kanisa ndio utimilizo wa maagano, ahadi, unabii, na taasisi zilizoanzishwa katika Agano la Kale.

Ramani za nyakati, na Dibaji zimeambatanishwa kama nyenzo za kusaidia.

Page 2:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

ORODHA YA YALIYOMO

THEOLOJIA YA KI-BIBLIA: UTANGULIZI…………………………………………………………..........................3

I. Tabia ya Theolojia ya Ki-Biblia …………………………………………………………………….............................3A. Maelezo ya Theolojia ya Ki-Biblia……………………………………………………………..….....…………………..3B. Fikira za Theolojia yaKi-Biblia ………………………………………………………………...….…………………..3

II. Mtazamo wa Mkondo wa simulizi na Dhana za Theolojia ya Ki-Biblia….……………………................................4A. Msingi wa mkondo wa simulizi za Biblia …………………………………………………………...…………………..4B. Dhana ya Theolojia ya Ki-Biblia …..………………………………………………………………..…………………..4

MSINGI WA SIMULIZI YA MKONDO WA BIBLIA ………………………………………….…...............................5

I. Uumbaji (Mwanzo 1-2)………………………………………………………..................................................................5A. Simulizi ya mkondo wa Biblia huanzia na Mungu (Mwa 1:1) ………………………………………...........................6B. Mungu aliumba kila kitu bila kutumia chochote …………………..………………………………..............................6C. Mungu alimuumba mwanadamu ili atawale viumbe vingine vyote (Mwa 1:26-28) …………………………………..6

II. Anguko la Mwanadamu Katika Dhambi na Matokeo Yake (Mwanzo 3-11:26)……………….…………………..7A. Uhusiano kati ya uwepo wa Mungu na dhambi …….……………………………………………….............................7B. Adamu naHawa watenda dhambi na kufukuzwa kutoka bustani ya Edeni (Mwanzo 3)……………………………...9C. Matokeo ya Anguko—kutoka kwa Kaini hadi Mnara wa Babeli (Mwanzo 4-11:26)…………….…………………..12

III. Tukio la Ukombozi—Mungu aita Watu Kwa Ajili Yake Mwenyewe (Mwa 11:27-Ufu 20)……………………..14A. Mwanzo mpya wa Mungu—Kutoka Ibrahimu hadi Yusufu (Mwa 11:27-50:26)…………………………………….14B. Kuanza kwa taifa la Israeli—Kutoka Misri kwenda nchi ya ahadi (Kutoka- Kumbu-kumbu)…................................16C. Israeli ndani ya hiyo nchi (Yoshua-1 Samueli 7)……………………………………………………..........................18D. Israeli kama ufalme ulioungana (1 Samueli 8-1 Wafalme 11; 1 Nyakati 1-2 Nyakati 9;

Zaburi-Wimbo ulio bora)…………………………………………………………………………………………18E. Israeli kama ufalme uliogawanyika (1 Wafalme 12-2 Wafalme 17; 2 Nyakati 10-31; Isaya na Mika

[utabiri kwa Israeli na Yuda]; Yoeli [utabiri kwa Yuda]; Hosea na Amosi [utabiri kwa Israeli]; Obadia [utabiri kwa Edomu]; Yona [utabiri kwa Ninawi])………….………………….19

F. Kuwepo, kushuka, na kuanguka, kwa ufalme wa Kusini (2 Wafalme 18-25; 2 Nyak 32-36:21; Isaya-Danieli; Nahumu-Zefania)………………………………………………………………………….……19

G. Kurejeshwa kwa ufalme wa Kusini (2 Nyak 36:22-Esta; Hagai-Malaki)…………………………………….……...21H. Kutimia kwa mpango wa Mungu wa ukombozi katika Yesu Kristo (Mathayo-Ufunuo 20)………………………...21I. Ufunuo wa Yesu wa Masiha wa kweli ufalme wa Mungu, na kanisa……………………………..……………….....22

IV. Mbingu Mpya na Nchi Mpya (Ufunuo 21-22)…………………………………………..……………………….…24

DHANA MBILI ZA KI-BIBLIA KUHUSU UHUSIANO WA MUNGU NA MWANADAMU.…………………....24

I. Hekalu na Nchi: Maskani ya Mungu na Mwanadamu……………………………………………………………...24A. Bustani ya Edeni (Mwanzo 2-3; ona pia Ezek 28:13-16)………………………………….………………………....25B. Hema ya kukutania (Kutoka 25-31, 35-40)……………………………………………………………...……………26C. Hekalu (2 Sam 7:1-17; 1 Waf 6; 8:1-11; 1 Nyak 17:1-15; 22:1-16; 28:1-29:9; 2 Nyak 3-5)……..............................27D. Maono ya Ezekiel ya Hekalu Jipya (Ezek 40-48)……………………………………………………………………..29E. Yesu ndiye hekalu la kweli……………………………………………………………………………….....................33F. Kama kiwakilishi cha Yesu kionekanacho duniani, kanisa ni “Hekalu” la Mungu duniani ………........................36G. Ufunuo wa Mbingu Mpya na Nchi Mpya (Ufunuo 21-22)………… ……………………………………………….38

II. Uhusiano wa Mungu na Watu Wake Kuhusu Ndoa……………………………………………………………......42A. Mwa 2:23-24 (mwanamke kuumbwa rasmi kwa ajili ya mwanaume;mwanaume kuwaacha babaye na

mamaye na kuunganishwa na mkewe na kuwa “mwili moja” naye) ni mfano unaoelezea uhusiano ambao Mungu anautaka kwa watu.…………………………..………………………………………………...42

B. Katika AK kiungo cha ndoa kati ya Mungu na watu wake kiliwekwa, lakini Israeli hakuwa mwaminifu.………..42C. Katika AK kiungo cha ndoa kati ya Mungu na watu wake kiliwekwa, lakini Israeli hakuwa mwaminifu……….41D. Katika Ufunuo, picha ya Ki-Biblia kuhusu uhusiano wa kindoa kati ya Mungu na watu wake huja

kutimilika katika Kristo, bibi arusi (Kanisa), na Nchi Mpya…………………………………………………..45

1

Page 3:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

KRISTO NA KANISA KAMA UTIMILIZO WA AK……………….……….……………………………………….46

I. Biblia Kimsingi ni Kumhusu Yesu Kristo—Yeye Ndiye Mtu Aliye Kiungo na Dhana Iunganishayo Yote.…....46A. Zinapotazamwa peke yao, simulizi za AK na nabii zake hazimtaji moja kwa moja Yesu Kristo, bali huwa na

Nguzo ya kusimamia, na hutumia lugha zinazolenga, na kumwelekea mlengwa wa kuibukia taifa la Israeli.…………………………………………………………………………………………………………....47

B. Yesu na waandishi wa AJ wote walitumia AK kumhusu Yesu na kwa Injili..……………………………………....47

II. Agano la Ibrahimu, la Daudi, na Jipya Yalielekea Kwake na Kutimilizwa Katika Kristo na Kanisa.………..48A. Agano la Ibrahimu limetimizwa katika Kristo na Kanisa…………………….………………..…………………….48B. Agano la Daudi limetimizwa katika Kristo na Kanisa…………………………………..…….……………………...51C. Agano Jipya limetimizwa katika Kristo na Kanisa………………………………………….………………………..55

III. Yesu Atimiza Maana na Kusudio la Israeli Kama Taifa, na Taasisi Zote za Israeli: Sikukuu zake; Mifumo ya Dhabihu; Ukuhani; Sheria, na Sabato…………………………………………………………...56

A. Yesu ndiye Israeli mpya, wa kweli, na mwaminifu…………………………………………………………………...57B. Yesu atabiriwa kuwa ndiye “Mtumishi wa Bwana.”………………………………………………………………….59 C. Katika Yesu, ahadi za AK za marejezo kwa Israeli zinatimizwa.……………………………………………………..60D. Yesu alitimiliza na kubadilisha siku kuu za Kiyahudi, mifumo ya dhabihu, na ukuhani……………………….….64E. Yesu alitimiza na kubadilisha Sheria ya AK na Sabato.……………………………………………………………...75

IV. Kwa vile Kanisa Liko “Katika Kristo,” Kanisa ndilo Israeli Mpya, wa Kweli na wa Kiroho.………………...80A. Neema ya kimwili na ya kiroho, uteuzi, na imani katika AK.….………………...…………………………………..80B. Aina mbili za uteuzi —wa kimwili na wa kiroho—huonyesha jinsi Maagano ya Ibrahimu, Musa na

Agano Jipya yanavyooana.……………………………………………………………………………………...80C. Aina mbili za uteuzi—ya kimwili na ya kiroho—huonyesha kwamba Israeli ya AK ilikuwa taifa la

kimwili ambalo “ni mabaki tu” yaliyookolewa kiroho.………………………………………………………...81D. Uhusiano kati ya Israeli ya AK na kanisa.……………………………………………………………………………82E. Yesu alilikataa taifa la Israeli kama chombo cha kuujengea ufalme wa Mungu, na kutoa jukumu hilo

kwa wafuasi wake mwenyewe, kanisa.……..…………………………………………………………………...84F. Kanisa ndio watu wapya, wa kweli, wa Mungu—Israeli wa kiroho………………………………………………….85G. Kanisa ni jumuisho la “Mtumishi wa Bwana,” kama vile Yesu kibinafsi alivyokuwa “Mtumishi wa

Bwana” (Isa 42:1-9; 49:1-6; 50:4-9; 52:13-53:12)……………………………………… ……………..88H. Kama Israeli mpya, wa kweli, kanisa linakabiliwa na mitihani ile ile ya uamini fu ambao Israeli ya AK

ya kimwili ilikumbana nayo……………………………………………………………………………………..89

NUKUU ZILIKOTOLEWA……………………………………………………………………………………………..89

DIBAJI 1— VIFUPISHO KWA UCHACHE VYA VITABU VYA BIBLIA ………………………………………..95DIBAJI 2— MIPANGILIO YA MUDA WA HISTORIA YA BIBLIA …………………………………………...…98DIBAJI 3— MPANGILIO WA MUDA WA WAFALME NA MANABII WA ISRAELI NA YUDA .…...............100DIBAJI 4— NABII ZA KIMASIHI CHACHE NA KUTIMIZWA KWAKE ...........................................................102DIBAJI 5— RAMANI ZA HIMAYA ZA ASHURU, BABELI, NA UAJEMI ………………...…………………....103DIBAJI 6— RAMANI YA HIMAYA YA RUMI & MAJIMBO YAKE……………………………………………104DIBAJI 7— RAMANI YA KANAANI: SEHEMU 12 ZA MAKABILA…………………………………………....104DIBAJI 8— RAMANI YA UFALME ULIOUNGANA WA ISRAELI…………………………………………….105DIBAJI 9— RAMANI YA FALME ZILIZOGAWANYIKANA ZA YUDA NA ISRAELI………………………105DIBAJI 10— RAMANI YA ISRAELI NYAKATI ZA AGANO JIPYA……………………………………………106

2

Page 4:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

THEOLOJIA YA KI-BIBLIA: UTANGULIZI

I. Tabia ya Theolojia ya Ki-Biblia.

A. Maelezo ya Theolojia ya Ki-Biblia.1. Theolojia ya Ki-Biblia (TK) ni masomo yahusuyo kuweka bayana mkondo wa simulizi za Biblia kuanzia mwanzoni (Mwanzo) hadi mwisho (Ufunuo). Ni “kutafuta unganiko la ndani la Biblia” (Bartholomew 2005: 84).2. Theolojia ya Ki-Biblia “Hufuatia hatua za ufunuo tangu neno la kwanza la Mungu kwa mwanadamu kupitia kupambanuliwa kwa utukufu kamili wa Kristo. Huchunguza hatua mbali mbali za historia ya Biblia na mahusiano kati yao. Kwa hiyo, hutoa msingi wa kuelewa jinsi vifungu vya sehemu moja ya Biblia vinavyohusiana na vifungu vingine vyote. Tafsiri iliyo safi ya Biblia hutegemeana na yapatikanayo katika [TK].” (Goldsworthy 1991: 32) 3. Kwa vile inajihusisha kuelezea kiunganisho cha ndani cha Biblia kwa namna yake yenyewe, ni “ya kujieleza na ya kihistoria kiasi kwamba tafsiri ya kitheolojia na theolojia ya ki-mfumo haiwezi kuwa hivyo” (Bartholomew 2005: 86).

B. Fikira za Theolojia ya Ki-Biblia.1. Biblia inaelezea simulizi inayoshikamana, na Yesu Kristo ndiye moyo wa simulizi hiyo ( Luka 24:25- 27, 44-47; Yoh 5:39 ). Kila kitabu cha Biblia kinachangia kitu fulani kwenye simulizi hiyo, na ujumla wa simulizi nzima hutoa mpangilio ambao kila kitabu kilichomo kinaweza kutafsiriwa vizuri zaidi.2. Ingawaje Biblia inaelezea simulizi iliyounganika, ufunuo wa Mungu ni hatua kwa hatua— hujifunua kila mahali katika Biblia yote. Kanuni kadhaa muhimu huibuka kutokana na kweli hizi.

a. Andiko halitalipinga Andiko. Vifungu viwili vinavyoonekana vinapingana, vitakuja kuonyesha havipingani pale vitakapochunguzwa kwa umakini zaidi. Kifungu kimoja kinaweza kurekebisha au kuongezea sifa ya kingine, lakini hakitakipinga.b. Yote mawili- hatua za ukombozi na “kusudi lote la Mungu” (Mdo 20:27) lazima yaangaliwe ili kuelewa kiusahihi kifungu chochote kile. Mafundisho ya “ufunuo wa hatua kwa hatua” hutueleza kwamba hatua za ukombozi lazima zizingatiwe wakati wa kutafakari kifungu chochote kile. Biblia ni muunganiko unaoelezea simulizi ya kisa kilichoungan. Hata hivyo, kweli za Biblia hazifunuliwi zote kwa mkupuo moja, bali hufunuliwa hatua kwa hatua. Maana kamili ya kifungu chochote husika au fundisho la Ki-Biblia laweza lisiwe wazi hadi Biblia nzima iwe imezingatiwa.c. Agano Jipya linavyolitafsiri Agano la Kale.

(1) Maandishi yoyote ya Ki-Biblia yanapaswa kusomwa ndani ya muundo wa maneno yaliyotumiwa (lugha na mfumo wa maandishi husika) na mazingira ya kihistoria yalipoandikwa mara ya kwanza. Agano Jipya limeandikwa kwa misingi ya Agano la Kale. Miktadha mingi ya Agano Jipya husimamia Agano la Kale. Uelewa wetu wa Agano Jipya hutajirishwa kwa kiwango kikubwa kwa kulielewa Agano la Kale. Wakati huo huo, hatupaswi kulisoma Agano la Kale kama kwamba Jipya halipo. Yote mawili yapo – kutokuendeleza na mwendelezo kati ya Agano la Kale na Agano Jipya. Agano Jipya hujengwa juu ya miktadha ya Agano la Kale, mara nyingi katika namna za kushangaza. Hilo ni kweli zaidi kuhusu jinsi Agano Jipya linavyohusisha unabii wa Agano la Kale. (2) Lazima tukumbuke kwamba sheria za Agano la Kale, sikukuu, na taratibu nyingine zimetimilizwa na kukamilishwa katika Kristo ( Math 5:17; Rum 10:4; 2 Wakor 3:12- 16; Wagal 3:23-4:7 ). Kwa namna nyingi, Israeli ya kimwili ya Agano la kale, sheria zake, sikukuu zake, na taratibu nyingine, zilikuwa “aina,” “vivuli,” au “mifano” ya uhalisi wa Agano Jipya (1 Wakor 10:1-6; Wakol 2:16-17; Waebr 8; 10:1). Kwa hiyo, tunapoiangalia picha nzima, hasa tunapotumia Maandiko, tunapaswa “kuyasoma Maandiko ya Agano la Kale kwa kupitia miwani ya Maandiko ya Agano Jipya” (Lehrer 2006: 177). Kama ilivyosemwa, “Hili Jipya, ni lile la Kale lililotimilika; la Kale ni Jipya lililofunuliwa.”

3

Page 5:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

II. Mtazamo wa Mkondo wa Simulizi na Dhana za Theolojia ya Ki-Biblia.

A. Msingi wa mkondo wa simulizi za Biblia.1. Katika mtazamo wa kawaida zaidi, Biblia ni simulizi ya uumbaji, historia, na hatima ya ulimwengu na mwanadamu, kama ielezwavyo kimsingi kwa mtazamo wa kitheolojia. Mungu aliumba ulimwengu wa kupendeza sana na wanadamu kuishi kwa furaha, na maisha yaliyotimilika katika ushirika na yeye. Kupitia dhambi zetu tulipoteza ushirika ule na kuleta uovu na uharibifu na mauti duniani. Hata hivyo, Mungu hakutuacha katika dhambi zetu na mauti. Kwa njia ya mpango mahususi uliohusisha kumwita Ibrahimu na taifa la Israeli, aliandaa njia kwa ajili ya kuja ndani ya mwanadamu kwaYesu Kristo ili kuleta msamaha wa dhambi na kurejesha ushirika na yeye. Anakuja tena, kumaliza dhambi kabisa na mauti pasipo kutuangamiza sisi. Atakwenda kutimiliza kurejeshwa kwetu na uhusiano wetu na yeye. Na pia ataifanya upya nchi, hata iwe ya utukufu zaidi ya ilivyoumbwa mara ya kwanza. Katika muundo huo, mkondo wa simulizi hii ungeonekana namna hii: uumbaji (Mwanzo 1-2)=>Anguko na madhara yake (Mwanzo 3-11:26)=>Ukombozi (Mwanzo 11:27-Ufunuo 20)=>Uumbaji mpya (Ufunuo 21-22). Mungu mwenyewe ndiye yote mawili -mtunzi wa simulizi na ndiye mhusika mkuu wake.2. Biblia ni ufunuo wa Mungu kuhusu jinsi alivyo na mpango wake (Injili) kwa mwanadamu.

a. Kiungo cha katikati cha ufunuo huo—yeye aliye kiungo mtendaji wa uumbaji, njia ya ukombozi, na chanzo na utimilifu wa uumbaji mpya—ni Yesu Kristo (ona 2 Wakor 1:20; Waef 1:9-10; Wafil 2:6-11; Waebr 1:1-3). b. Kwa hiyo, Agano la Kale ni maandalizi ya Injili, Injlili zile ni udhihirisho wa Injili; Matendo ya Mitume ni upanuzi wa Injlili; Nyaraka ni maelezo ya Injili; na Ufunuo ni utimilifu wa Injili.

3. Biblia ni simulizi ya uhusiano na mwanadamu, tangu uumbaji hadi uumbaji mpya . Wanenaji mbalimbali wameielezea simulizi kwa njia nyingine zinazotofautiana kidogo:

a. “Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi, hadi kuutwaa mwili, kusulubiwa, ufufuo na kupaa; na mwafaka ni hukumu ya mwisho, mbingu na jehanamu” (Sykes 1997: 14).b. “Theolojia ya Ki-Biblia ni Mungu kuuleta ufalme wake ambamo mahusiano yote yanakuwa yamerejeshwa kwenye ukamilifu” (Goldsworthy 1991: 76).c. “Watu wa Mungu, katika nafasi ya Mungu, chini ya utawala wa Mungu, wakiishi kwa njia ya ki-Mungu, katika uwepo mtakatifu na wa upendo wa Mungu, kama familia” (Cole 2006: n.p.).

B. Dhana za Theolojia ya Ki-Bibia.TK yaweza kukabiliwa kwa njia mbali mbali. Mtu moja aweza kuikabili TK kwa kujaribu kuelezea

mpangilio mzima wa mtiririko wa mkondo wa simulizi ya Biblia kiutaratibu kuanzia mwanzo hadi mwisho. Ndani ya mtiririko wa mkondo wa simulizi hiyo, dhana na miktadha muhimu hujitokeza mara kwa mara kila mahali katika Biblia, ambayo husaidia kukazia na “kuimarisha upya” mkondo wa simulizi nzima ya Biblia. mwishowe, dhana hizi, na Biblia yenyewe, huhusishwa, na huweza kutimilizwa, katika Yesu Kristo (ona Luka 24:25-27; Yohn 5:39, 46). Baadhi ya dhana muhimu zaidi na miktadha ni:

1. Ahadi na Kutimizwa. Mungu ni mwaminifu kutimiza ahadi zake. Lakini mara zote ahadi zake hutimizwa kwa njia za kushangaza. Utimilifu wa mwisho wa ahadi za Mungu hupatikana katika Yesu Kristo. Kama asemavyo Paulo katika Waef 1:9-10, “Akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo. Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia, naam, katika yeye huyo.”2. Agano la Mungu. Mungu alifanya Maagano kadhaa (mapatano maalum) kipindi chote cha historia ya Biblia. Maagano makuu ni: Agano la Nuhu (Mwa 8:20-9:17); Agano la Ibrahimu (Mwa 12:1-3; 13:14-17; 15:1-21; 17:1-21; na 22:15-18); Agano la Musa (Kutoka 19-24), pia hujulikana kama Agano la Kale (2 Wakor 3:14; Waeb 8:6, 13); Agano la Daudi (2 Sam 7:8-17; Zab 89:1-4); na Agano Jipya (Yer 31:31-34; 32:40; Ezek 36:22-28; 37:15-28; Luka 22:20; 1 Wakor 11:25; 2 Wakor 3:6; Waebr 8:6-13; 10:15-17). Kwa namna nyingi, mpango mzima wa Mungu wa ukombozi waweza kuonekana kama ni kutenda kazi kwa Agano la Ibrahimu. Kama simulizi ya ukombozi inavyoendelea, Maagano ya Ibrahimu, Musa, na Daudi, yote hupata utimilifu wake katika Agano Jipya, na Agano hilo hupata utimilifu wake katika Kristo na watu wake, na kanisa. 3. Aina husika-Aina-Kinyume; Kivuli- Kitu halisi. Kadiri mpango wa Mungu ulivyoendelea na wakati, kwanza alimwita Ibrahimu, kisha Isaka, kisha Yakobo, ambaye kupitia yeye alianzisha taifa la Israeli, kuwa chombo ambacho kwacho mpango wake ulifanyika uhalisi. Hata hivyo katika mtazamo wa

4

Page 6:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

kitheolojia na wa kiroho, mifano yote ya Agano la Kale au taasisi zake—kama vile Madhabahu na Hema, mifumo ya utoaji dhabihu. Sikukuu, Sheria, na Nchi ya Ahadi. Ufalme, Sayuni, Yerusalemu, na Israeli yenyewe—viliwakilisha “vielelezo” au “vivuli” vya kuonekana au vya kidunia, ambavyo vilielekeza kwenye Agano Jipya, na uhalisi wa kiroho wa siku za mbeleni (Wagal 4:21-31; Wakol 2:16-17; Waebr 8:5; 9:15-10:22; 12:18-24). Uhalisi wa kweli ambao aina na vivuli vya Agano la Kale (AK) vilielekeza, viko katika Kristo, kanisa, mbingu, Yerusalemu mpya, na mbingu mpya na nchi mpya.4. Mkondo wa Mungu wa Uhusiano: Mungu huanzisha na hutenda kwa neema yake, watu wake wanatakiwa kuonyesha mwitikio kwa imani.

a. Mungu siku zote ametafuta watu kwa ajili yake. Hivyo, kauli inayojirudia mara zote katika Biblia nzima (ikitumia maneno tofauti) ni, “Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu” (ona Mwa 17:8; Kut 6:7; 29:45; Walawi 26:12; Yer 7:23; 11:4; 24:7; 30:22; 31:1, 33; 32:38; Ezek 11:19-20; 14:10-11; 36:28; 37:23, 27; Hos 2:23; Zek 8:8; 13:9; 2 Wakor 6:16; Waebr 8:10; Uf 21:3). b. Mkondo unaojirudia mara kwa mara katika Biblia nzima kwa ajili ya watu kuwa na uhusiano mzuri na Mungu ni kwamba, Mungu huanzisha, na watu wake huonyesha mwitikio kwa imani (ambayo kimsingi humaanisha “kutumaini na kutii kutoka moyoni”).

(1) Mungu hutenda kwa neema kwa watu; hata katika kuhukumu na kuwaadhibu makosa huonyesha neema yake. Mungu alianza mchakato kwa kumuumba Adamu na Hawa na alizungumza nao katika bustani ya Edeni (Mwa 2:7, 15-25; 3:8). Baada ya Adamu na Hawa kuanguka dhambini, kwa neema Mungu alianzisha mpango wa ukombozi kwa kuahidi mwokozi (Mwa 3:15) na kutoa sadaka ya wanyama ili kuwavika mavazi (Mwa 3:21). Kwa neema, Mungu alimchagua Nuhu na familia yake waokolewe wakati alipoiangamiza dunia yote kwa Gharika Kuu, na Nuhu aliitikia kwa imani (Mwa 6:5-22). Mungu akamchagua Ibrahimu, aliyeitikia kwa imani (Mwa 12:1-5; 15:5-6). Kwa neema yake, Mungu alituma manabii wake kuwaonya Israeli juu ya maafa ya dhambi zake na kuwaita warudi kwenye uaminifu tena. Mwishowe, kwa neema yake, Mungu mwenyewe akafanyika mwili katika mwanadamu aitwaye Yesu Kristokuwaokoa watu wake na dhambi zao na kurejeza mahusiano mazuri kati ya Mungu na wanadamu.(2) Kwa vile wanadamu kiasili ni wadhambi, hawawezi “kustahili” au “kufanyia kazi” mbinu iwawezeshayo kuwa na mahusiano mazuri na Mungu ( Mdo 13:39; Wagal 2:16; 3:11; Waef 2:1-3, 12 ). Njia pekee ya watu kuwa na mahusiano mazuri na Mungu ni tu kama wataitikia kwa imani kile Mungu, kwa neema yake, alichokifanya kwa ajili yao. Kwa sababu hiyo, muktadha wa imani na uaminifu kwa Mungu—“mwenye haki ataishi kwa imani”—hujirudia kila mahali katika Biblia (Hab 2:4; War 1:17; Gal 3:11; Waebr 10:38; ona pia Yoh 6:27-29; 20:26-29; 1 Yoh 3:23). Bahati mbaya, mkondo umekuwa mara nyingi watu wengi hawaweki imani zao kwa Mungu, ingawaje daima wamekuwako “mabaki wachache waaminifu” ambao wamefanya hivyo (1 Waf 19:11-18; Rum 11:1-5; ona pia Luka 18:8).

MSINGI WA SIMULIZI YA MKONDO WA BIBLIA

I. Uumbaji (Mwanzo 1-2).“Uumbaji si swala tu la vyanzo, bali la kusudi na mahusiano” (Goldsworthy 1991: 92). Katika uumbaji,

twamwona Mungu kama chanzo cha kila kitu. Zaidi ya hapo, kama kila kitu kilivyoumbwa mwanzoni, twaona “kila kitu kuwa chema” (Mwa 1:31)—m.y., Mungu, mwanadamu, wanyama, mimea, na maumbile mengine yote kutimiza makusudi ya kuumbwa kwao katika mahusiano mazuri kila kimoja kwa kingine. “Wasomi wamegundua kwamba Sura za mwanzo za kitabu cha Mwanzo . . . zimeandaliwa ili kujibu swali la kwa nini mambo yako jinsi yalivyo. Seti moja ya maswali ambayo sura za mwanzo za kitabu cha Mwanzo ni, ‘Kwa nini wanadamu wako jinsi hii? Kwa nini wanadamu hutafuta maarifa zaidi? Kwa nini wanadamu hutafuta utawala mkubwa zaidi juu ya dunia? Kwa nini daima hujaribu kuvumbua vitu vipya, kutafuta matumizi mapya ya rasilimali za “asili”? Kwa nini wanadamu hupaka rangi, huchonga sanamu, huchora picha, hujenga majengo, hutunga nyimbo na mashairi? Kwa nini wanadamu mara kwa mara na kwa namna tofauti hujihusisha na utamaduni wa kisanii, sayansi, na teknolojia?’ Jawabu la Mwanzo 1 ni kwamba Mungu alimfanya mwanadamu awe hivyo. Mwanadamu ni mfano wa Mungu. Mungu ni Muumbaji na ni Mfalme. Kama mfano wake, mwanadamu hubuni na kutawala.” (Leithart n.d.: n.p.)

5

Page 7:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

A. Simulizi ya mkondo wa Biblia huanzia na Mungu (Mwa 1:1).1. Mungu pekee ni wa milele na anaishi kwa kujitegemea. Mungu si sehemu ya ulimwengu wala si kinyume chake pia. Kila kitu kilichopo kumwacha Mungu (vitu; malaika; wanadamu, nk) viliumbwa na Mungu, na humtegemea Mungu kwa kuwepo kwao (Mdo17:28; Wakol 1:17; Waebr 1:3). Ukweli huu huonyesha kwamba Mungu wa kweli, wa Ki-Biblia hafanani na “miungu” ya dini nyingine. Mungu si kama wazo la Mashariki (n.k., Wahindu; Wabudha) kwamba Mungu na maumbile yote ni kitu “kimoja” (m.y; muktadha wa muunganiko katika kimoja). Mungu pia si wa dini za kiutamaduni (zikiwamo zile za Mashariki ya Karibu ya kale wakati Biblia ilipoandikwa), ambazo huamini kwamba vitu vilivyokufa vina “roho”, na wanadamu wa kwanza walikuwa kwa sehemu moja ni wanadamu na sehemu nyingine miungu.2. Mungu peke yake anajitosheleza. Yuko Mungu moja tu, lakini ni mwenye hali isiyoelezeka kabisa, tofauti na kila kitu kingine. Kwa hiyo, ingawaje yuko Mungu moja tu, anaishi katika nafsi tatu (Utatu): Baba; Mwana; na Roho Mtakatifu. Hili ni muhimu. Kama Mungu angekuwa ni wa nafsi moja (kama dhana ya Allah wa Ki-Islam), na si Mungu wa Utatu, Mungu asingekuwa anajitosheleza: m.y., angekuwa anawajibika aviumbe viumbe vingine ili awe na uhusiano navyo. Hata hivyo, Mungu hakuhitaji aumbe chochote (ona Mdo 17:24-26)—tayari alishaumba ulimwengu, alishakuwa na upendo kamili wa kiuhusiano kati ya zile nafsi tatu za Utatu kabla hajaumba ulimwengu. Kwa hiyo, Biblia (tofauti na Qur’an) hutueleza kwamba “Mungu ni upendo” (1 Yoh 4:8).

B. Mungu aliumba kila kitu bila kutumia chochote.1. Ulimwengu haukuwa na kitu kilichokuweko kabla ambacho kwacho Mungu aliumbia nyota au mimea au wanyama. Badala yake, Mungu alifanya tu kutamka au kutangaza, na ulimwengu ukatokea pasipo kutumia chochote (Mwa 1:1, 3, 6-7, 9, 11, 14-16, 20-21, 24, 26-27). Sehemu nyingine, kote katika AK na AJ, Biblia inakazia kitu hicho hicho (ona Kut 20:11; 31:17; Zab 8:3-5; 33:6; Math 19:4; Yoh 1:3; Mdo 14:15; Rum 11:36; 1 Wakor 8:6; Wakol 1:16; Waebr 11:3; Ufu 4:11).1

2. Mwanadamu alikuwa ni tukio la kilele katika uumbaji wa Mungu. Ni wanadamu pekee wanasemekana kuwa wameumbwa “kwa mfano wa Mungu” (Mwa 1:26-27); Mungu akambariki mwanaume na mwanamke (Mwa 1:28); na Mungu akawaambia atakuwa na ushirika nao (Mwa 1:28-30; 2:16-17, 19; 3:8-9). Zaidi ya hapo, wakati kila siku baada ya kuumba vitu visivyo hai, mimea, au wanyama, Mungu aliuita uumbaji wake kuwa “mzuri (njema)” (Mwa 1:4, 10, 12, 18, 21, 25), baada ya kuumba wanadamu, Mungu akaona kwamba uumbaji ule ni “mwema sana” (Mwa 1:31). 3. Tukio la uumbaji la Mwa 2:4-25 ni sambamba au nyongeza ya tukio la kiuumbaji lililoko katika Mwa 1:1-2:3 . Tukio la Mwa 2:4-25 hurudi nyuma na kujazia undani wa yaliopo katika Mwa 1:26-27 kuhusiana na jinsi Mungu alivyoumba wanadamu. Wote wawili mwanaume na mwanamke walikuwa sehemu ya mpango wa Mungu tangu mwanzo (ona, Mwa 1:27), ingawaje Mungu alimuumba Adamu kwanza na kisha Hawa baadaye ili awe msaidizi na mwenzi wake (ona Mwa 2:18-25). Hii inaonyesha kwamba tabia na majukumu ya mwanaume na mwanamke kwa kiwango fulani ni nyongeza, siyo ya kubadilishana kabisa (ona 1 Wakor 11:3-15; Waef 5:28-32; 1 Tim 2:11-13), ingawaje ni kwa kiwango gani yanaweza kuwa hivyo bado yanajadiliwa.4. Wote wawili mwanaume na mwanamke wana mfano wa Mungu. Maana ya msingi ya “mtu” (Kiebrania, adam) ni neno la kiujumla “mwanadamu, watu,” ambalo hujumlisha wote wanaume na wanawake. Hilo linawekwa bayana katika Mwa 1:26, panaposema, “Na tumfanye mtu kwa mfano wetu . . . wakatawale.” Mwa 1:27 likieleza wazi kwamba wote wawili mwanaume na mwanamke wanahusika kiusawa, kwani panasema, “Mungu akaumba mtu [Adamu] kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” Zaidi, katika Mwa 1:28 Mungu akawabariki “hao” (mwanamume na mwanamke) kiusawa na Mungu alisema “nao”. Katika Mwa 1:29, wakati Mungu anasema “Nimewapa kila mche utoao mbegu,” hiyo “wa” ni uwingi, siyo umoja.

C. Mungu alimuumba mwanadamu ili atawale viumbe vingine vyote (Mwa 1:26-28).1. Adamu na Hawa wakiishi mbele za Mungu katika bustani ya Eden hutupatia mkondo wa ufalme wa Mungu. “Mkondo wa ufalme wa Mungu ni huu: Mungu huanzisha uumbaji ulio kamili ambao anaupenda na ambao yeye hutawala. Heshima kuu kabisa inatolewa kwa mwanadamu kama sehemu pekee ya uumbaji uliofanywa kwa mfano wa Mungu. Ufalme unamaanisha kwamba kila kitu kilichomo katika uumbaji kishirikiane vizuri, hiyo maana yake, kama Mungu alivyokusudia kiwe, kwa kingine chochote na kwa Mungu mwenyewe.” (Goldsworthy 1991: 99)

1 Whether the six days of creation referred to in Genesis 1 are literal or metaphorical is a matter of some debate. See, David G. Hagopian, ed., The Genesis Debate: Three Views on the Days of Creation (Mission Viejo, CA: Crux, 2001).

6

Page 8:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

2. Adamu na Hawa waliagizwa “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha dunia” ( Mwa 1:26- 28 ). Kwa vile wanadamu wameumbwa kiajabu “kwa mfano wa Mungu,” kwa kuenea duniani wakitii maagizo ya Mungu, watu wangekuwa wanaukuza utukufu wa Mungu, kwa kueneza sura yake, juu ya dunia yote. Hali hiyo ya “dhana ya wajibu wa kutawala” huendelea kuonyesha kwamba walitakiwa kupanua mipaka ya kijiografia ya Edeni hadi ienee dunia nzima. Kwa kupanua Edeni hadi kuenea dunia nzima, Adamu na Hawa na vizazi vyao wangekuwa wanaigeuza dunia kuwa kioo cha mbinguni: m.y; kuifanya dunia nzima kuwa paradiso imfaayo Mungu na mwanadamu, iliyojaa watu watakatifu. 3. Ni kwa kutegemea Neno la Mungu peke yake kwamwezesha mwanadamu kutimiliza ile dhana ya wajibu wa kutawala sawa-sawa. “Pale Adamu alipowapa majina wanyama, alianza mchakato wa uchunguzi, kupanga makundi, na maelezo toshelevu, ambayo ndiyo moyo wa uchunguzi wa maarifa ya kisayansi. Lakini hangeweza kamwe kufanikisha uhusiano wake mwenyewe kwa Mungu au hata kwa ulimwengu kwa kutegemea uchunguzi peke yake. Badala yake, lilikuwa ni Neno la Mungu lililokuja kwa Adamu kumwambia jinsi ya kuhusiana na Mungu na kwa ulimwengu. Ni Neno la Mungu linalomjulisha mwanadamu kwamba awe mwanasayansi na mwenye kuutunza kiupendo ulimwengu, badala ya kufanya uchawi na kuwa mtu mharibifu asukumwaye na kutaka madaraka katika dunia.” (Goldsworthy 1991: 99)

II. Anguko la Mwanadamu Katika Dhambi na Matokeo Yake (Mwanzo 3-11:26).

A. Uhusiano kati ya uwepo wa Mungu na dhambi.1. Mungu ndiye mkuu juu ya yote, na yuko kazini daima akitimiza mpango wake (ona Ayu 12:13-25; Isa 40:21-26; Mdo 4:27-28; Rum 9:14-24; Ufu 17:14-17 ). Hii inamaanisha kwamba, kwa namna fulani, Mungu ndiye mmiliki wa uovu, ingawa si kwa namna kwamba ndiye mwanzilishi wa ule uovu wa mwovu (ona Mwa 4:1-7; Isa 10:5-16; Hab 1:1-11; Mdo 2:22-24). Kwa maneno mengine, Mungu huruhusu na huachilia dhambi, si kwa ajili ya ule uovu wake au udhambi wa dhambi yenyewe, bali kwa makusudi ya matokeo yaliyo “ya busara, matakatifu, na yafaayo sana” (Edwards 1984, Freedom, §IX: 76; pia ona, Piper 2000: 107-31). Mungu hivyo husimama katika uhusiano ambao “siyo pacha” nyuma ya wema na uovu: pasipo kuvuruga enzi za ukuu wake, ule “uovu” wa mwovu siku zote hutokana na sababu zinazousababisha, ambapo wema siku zote hutokana na Mungu mwenyewe.2. Mtu mwingine anaweza kutazama swala la Mungu kuruhusu dhambi na uovu kutokea kwa mantiki ya uhusiano wa jua na giza na baridi. “Kuna tofauti kubwa kwa Mungu kuhusiana na hivyo, kwa ruhusa, yake katika tukio au tendo, ambalo, kwa jinsi lilivyo na sura yake, ni dhambi, (ingawaje tukio hilo bila shaka litafuatana na ruhusa yake,) na kwa yeye kuhusika katika hilo kwa kulizalisha na kuongoza tendo la dhambi; au katika ya yeye kuamuru kitu fulani kiwepo, kwa kutokukizuia, katika mazingira fulani, na kwa yeye kuwa mtendaji au mmiliki astahiliye, kwa kutumika kiuzuri au kiuwezeshwaji. . . . kama kulivyo na utofauti mkubwa kati ya jua kuwa chanzo cha ile nuru na ujoto wa anga, na uangavu wa dhahabu na almasi, kwa uwepo wake na athari njema za kuwepo kwake; na kwa kuhusiana na hiho hilo kunakuja giza na baridi kali, usiku, kwa mwenendo wake, itokeapo linazama kwenye miisho ya dunia. Mwenendo wa jua ni sababisho la aina ya matukio yanayofuatia baadaye; lakini silo sababu halisi, uwezeshwaji, au mzalishaji wa hayo; ingawaje lazima yatokee kutokana na mwenendo wake, katika mazingira hayo: hakuna tena tendo lolote la Ki-Uungu kuwa ndiyo sababu ya uovu wa mapenzi ya kianadamu. Kama jua lingekuwa ndiyo chemchemi ya mambo hayo, kama lilivyo chemchem ya nuru na joto: na kisha kitu chaweza kujadiliwa kutokana na tabia ya ubaridi na giza, kwa kulinganisha na sifa za jua; na pia inaweza kabisa kukubalika kwamba, jua lenyewe ni giza na baridi, na ya kuwa miali yake ni myeusi na yenye ukungu. Lakini kwa kufanyika sababu si kwa vinginevyo zaidi ya kutokuwepo kwake, hakuna kitu kama hicho kiwezacho kuhusishwa, isipokuwa kinyume chake; yawezekana kiusahihi kabisa ukadai, kwamba jua ni angavu na lenye joto kali, ikiwa baridi na giza ni matokeo ya kutokuwepo kwake; na kadiri matokeo haya yanavyounganishwa na kuwajibishwa zaidi mara kwa mara na kutokuwepo kwake, ndivyo inavyotia nguvu zaidi hoja kwamba jua ni chemchemi ya nuru na joto. Kwa hiyo, kama ambavyo dhambi si tunda litokanalo kwa jinsi yoyote ile na utendaji mwema au uvuvio mzuri wa Aliye Juu sana, bali, kinyume chake, hutokana na kuzuilia matendo yake na nguvu, na katika mazingira fulani, hufuatia ulazima wa athari ya utendaji wake; hili si hoja kusema kuwa yeye ni wa dhambi, au utendaji wake ni wa uovu, au una lolote la asili ya uovu; bali kinyume chake, ni kuwa Yeye, na utendaji wake, pamoja ni mzuri na wa utakatifu, na kwamba yeye ni chemchemi ya utakatifu wote. Itakuwa ni hoja ya kustaajabisha, tena sana, kusema wanadamu hawafanyi dhambi, isipokuwa tu pale Mungu anapowaachia wenyewe, na kulazimika kutenda dhambi afanyapo hivyo, kwamba Mungu lazima awe wa asili ya dhambi: ndivyo itakavyokuwa hoja ya kustaajabisha, kwani siku zote ni giza jua

7

Page 9:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

linapokuwa limezama, na kamwe hakuwi giza wakati jua likiwapo, hivyo basi, giza lote latokana na jua, na kwamba mduara wake na miale yake lazima iwe myeusi.” (Edwards 1984, Freedom, §IX: 77)3. Mungu anaweza kuagiza jambo kwa mapenzi yake ya siri (au “ki-mamlaka”) ambayo mapenzi yake yaliyofunuliwa (au “mtazamo” wake unakataza. “Mungu anao uwezo wa kuitazama dunia kwa vioo viwili. Anaweza kuiangalia kupitia kioo cha upeo mwembamba au kupitia kioo cha upeo mpana. Mungu atazamapo tukio lenye kuumiza au lililo ovu kupitia kioo cha upeo mwembamba, huona maafa au dhambi ilivyo yenyewe na huchukizwa na kuhuzunika. ‘Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye, asema Bwana Mungu’ (Ezek. 18:32). Lakini Mungu anapoliangalia tukio lenye kuumiza au lililo ovu kwa kupitia kioo chake chenye upeo mpana, huona maafa, au ile dhambi kuhusisha na kila kitu kilichosababisha na kitakachotokea kutokana nayo. Huona inavyounganika na mpangilio kuelekea umilele. Mpangilio huo, pamoja na sehemu zake zote (nzuri na mbaya) anazotaka ziwe (Zab 115:3).” (Piper 2000: 126) Kwa mfano, Ayubu alielewa kwamba mabaya yote yaliyompata kiuhalisia yalikuwa yamepangwa na kuruhusiwa na Mungu; kwa hiyo alimwelekezea kilio na kumbariki Mungu, ingawaje aliyesababisha moja kwa moja uovu ule alikuwa ni Shetani (Ayu 1:21-22). Mungu aliwatumia Waashuri kwa kuwaadhibu Waisraeli kwa dhambi yao, bali baadaye aliwaadhibu Waashuri kwa kiburi chao (Isa 10:5-19). 4. Uovu wote ambao Mungu anauruhusu na anauagiza hatima yake hutumika au kuleta wema mkubwa zaidi kwa uumbaji wenyewe. Paulo alisema “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.” (Rum 8:28). “Hakuna mantiki yoyote kufikiria, kwamba anaweza kukichukia kitu kama kilivyo, na kukiona tu kuwa kiovu, na bado ikawa ni mapenzi yake kitokee, akijua maafa yake yote. . . . Wanadamu hupenda dhambi kama dhambi, kwa hiyo ndio waanzilishi na watendaji wake: wanaipenda kama dhambi, na kwa makusudio mabaya na matokeo mabaya. Mungu hakusudii dhambi kama dhambi, au kwa kusudio la kitu chochote cha ubaya; ingawaje huwa ni furaha yake kuagiza mambo, ambayo, kwa kuyaruhusu, dhambi itakuja kutendeka, kwa makusudio ya uzuri au wema mkubwa zaidi, ambao kwa kutimia kwake yatakuwa ndio lengo. Kule kukubali kuachia mambo ili uovu uweze kutendeka, kama uovu: na kama ndivyo, basi hakuna sababu kwa nini asiweze kiuzuri tu kuuzuia uovu kama uovu, na kuuadhibu kama ulivyo.” (Edwards 1984, Freedom, §IX: 78-79; (pia ona, Piper 2000: 107-31; Edwards, Remarks, ch. 3: 525-43). Kwa mfano, Yusufu aliuzwa utumwani na ndugu zake lakini baadaye aliwaambia, “Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.” (Mwa 50:20). Huenda mfano mkubwa zaidi kuliko yote ni kusulubiwa kwa Kristo. Yuda, Herodi, Pilato, na watu wengine wasiomcha Mungu walimsaliti, kumlaani, na kumsulubisha Kristo asiyekuwa na dhambi, na bado alikuwa ndiye Mungu aliyeagiza tukio hilo lifanyike kama njia ya kuleta masamaha ya dhambi, mabadiliko ya maisha, na upatanisho wa mwanadamu kwa Mungu (Mdo 2:22-23; 4:27-28).5. Kwa vile Mungu ndiye wema mkuu zaidi ya wote uwezekanao kuweko, dhambi na uovu ni vya lazima ili hali zote za Uungu na tabia za Mungu ziweze kufunuliwa vizuri. “Ni jambo jema na zuri kabisa kwa utukufu wa Ki-Ungu kung’ara; na kwa sababu hiyo hiyo, ni vyema kwamba uangavu huo wa utukufu wa Mungu uwe kamili; yaani, sehemu zote za utukufu wake zing’are, kwamba uzuri wote uwe kimlingano unaangaza, kwamba mhusika awe na sura halisi ya Mungu. Si vyema kwamba utukufu moja udhihirishwe kupita kiasi, na mwingine usiwepo kabisa; maana hapo, kule kung’ara hakutaleta uhalisia. Kwa sababu hiyo hiyo si sahihi moja udhihirishwe kupita kiasi, na mwingine kidogo sana. Ni vyema sana ule uangavu wa Mungu utoe majibu ya unyofu wake wenyewe; kwamba ile enzi ya kiutukufu iwajibike kwa utukufu halisi na ulio muhimu, kwa sababu hiyo hiyo ni vyema na bora kabisa kwa Mungu kujitukuza mwenyewe kabisa. Kwa hiyo ni lazima, kwamba ukuu wa Mungu usioneneka, mamlaka yake na enzi yake ya kutisha, haki yake, na utakatifu, udhihirishwe. . . . Kama isingelikuwa ni vyema kwamba Mungu aagize na kuruhusu na kuiadhibu dhambi, kusingekuwa na udhihirisho wa utakatifu wa Mungu katika kuchukia dhambi, au katika kuonyesha lile alipendalo, katika upaji wake, katika uchaji mbele zake. Kusingekuwa na udhihirisho wowote wa neema ya Mungu au ucha Mungu wa kweli, kama kusingekuwa na dhambi za kusamehewa, hakuna maafa ya kuokolewa kwayo. . . . Huwa tunajali kidogo mno kiasi gani hisia ya wema inavyoinuliwa kutumia hisia ya uovu, kwa yote mawili – kihamasa na kiasili. Na kama ilivyo lazima kuwe na uovu, kwa sababu kuonekana kwa utukufu wa Mungu kusingelikuwepo na kusingekamilika, kama uovu usingalikuwepo, kwa hiyo uovu ni wa lazima, ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha furaha ya kiumbe, na kukamilika mawasiliano ya Mungu, ambayo kwayo aliuumba ulimwengu, kwa sababu furaha ya kiumbe hujumuishwa katika kumjua Mungu, na hisia ya upendo wake. Na ikiwa kumjua yeye kutakuwa hakujakamilika, furaha ya kiumbe lazima iwe haina uwiano kimlingano.” (Edwards 1986, Remarks, ch. 3: 528; ona pia, Piper 1997: n.p.;

8

Page 10:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Erlandson 1991: n.p.; Edwards 1984, The End: 94-121; Piper 2003a: 17-50; Piper 2003b:17-35)

B. Adamu na Hawa watenda dhambi na kufukuzwa kutoka bustani ya Edeni (Mwanzo 3).1. Biblia inaweka bayana kwamba Shetani “alianguka” kabla ya dhambi ya Adamu na Hawa, kwa vile Shetani ndiye aliyewajaribu Adamun a Hawa na kuwadanganya kuhusu sababu na matokeo ya kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya (fananisha, Mwa 2:16-17 na Mwa 3:1-4 ). Kwa hiyo, Yesu alimwita Shetani yote mawili, “muuaji tangu mwanzo” na “mwongo na baba wa huo” (Yoh 8:44-45).2. “Ujuzi wa mema na mabaya” ( Mwa 2:17 ) huwakilisha uhuru wa kimaadili na kujitawala.

a. Ule “mti wa ujuzi wa mema na mabaya” haukuwa mti wa kiuchawi ambao ulizaa ujuzi wa mema na mabaya kwa kila mtu aliyeula. “Inaelekea sana kwamba Mungu aliuandaa huo mti kama uwigo wa mpaka, kama njia ya kuonyesha tofauti kati ya mema na mabaya. Kwa maneno mengine, uchaguzi wa Adamu na Hawa haukuwa kati ya kutokujua na kujua mema na mabaya, bali katika kubakia wema na wenyewe kuwa wabaya. Sura ya mtihani ilikuwa kwamba lolote watakalolichagua, watakuja kujua mema na mabaya. Walikuwa viumbe vya kimaadili ambavyo vingejua yaliyo sahihi na yasiyo sahihi kwa kutumia mwitikio wao binafsi kwa Mungu.” (Goldsworthy 1991: 98) Kama wangefaulu mtihani huo, kule kumtegemea na kumtii Mungu kungeliuthibitisha wema wao, na wangelilijua hilo. Kama wangelishindwa mtihani huo, kutomtegemea na kutokumtii Mungu kungeliwageuza kuwa watu wenye uovu kwenye kiini kabisa cha uanadamu wao, na wangelilijua hilo pia. b. Katika vifungu Fulani vya AK (2 Sam 4:17; 1 Waf 3:9) maneno “mema na mabaya” huzungumzia kimsingi uwezo wa kuchukua hatua kisheria. Kwa hiyo, kilichokuwa kimekatazwa kwa mwanadamu kilikuwa ni ule uwezo wa kuamua nini kiwe kwa ajili ya manufaa yake na nini kisiwe hivyo. Mungu hakutoa maamuzi ya aina hiyo kwa mwanadamu, kwa sababu ni Mungu pekee ndiye ajuaye yote, mwenye hekima yote, na mwenye upendo wote. Kwa hiyo, ni Mungu pekee anaweza kufanya uamuzi sahihi na wenye upendo kwa ajili ya manufaa ya mwanadamu ya kweli, wakati wote. Mwanadamu atendapo katika hali ya kujitawala mwenyewe, hujiweka nafsi yake mwenyewe kuwa mhimili wa kati kwa miongozo yake ya kimaadili na hujiamulia nini chema na nini kibaya. Hivyo hujaribu kuwa “kama Mungu” (ona Mwa 3:5, 22). Hata hivyo, kwa vile mwanadamu hajui yote, hana hekima yote, na hana upendo wote, juhudi zake za kuwa kama Mungu ni dhahiri zitashindwa. Badala yake, ataishia kutenda zaidi kama “mungu wa dunia hii” (2 Wakor 4:4), na matokeo yanayofanana nayo.

3. Shetani alimwingia nyoka na kumdanganya Hawa ( Yoh 8:44; 2 Wakor 11:3; Ufu 12:9 ). Adamu alikuwapo pamoja naye na, yeye pasipo kudanganywa, alikubali kumfuata mkewe katika dhambi (Mwa 3:6; 1 Tim 2:14). Hilo laweza kuwa sababu kwa nini dhambi ya Adamu ni kubwa zaidi, na kwa nini matokeo yaliyowajia wanadamu wote baadaye husemekana kutokana na dhambi ya Adamu (ona Rum 5:12-14, 17-21; 1 Wakor 15:21-22).4. Mbinu ya Shetani ni kielelezo cha majaribu yanayotukabili.

a. Alimjia Hawa kwanza. Huo ulikuwa ni ujanja wa juhudi za kujaribu kumdanganya mtu ambaye hakupokea maagizo moja kwa moja kutoka kwa Mungu, na kumgonganisha mtu moja na mwingineb. Alilenga jambo pekee ambalo Mungu alikuwa amelikataza. Licha ya Mungu kutoa mahitaji yote kwa wingi mkuu, kwa kule kukazia kitu pekee ambacho hawakutakiwa kukifanya, Shetani ndipo kama matokeo yake alipandikiza wazo ambalo limepotoka au lililokengeuka kuhusu uhalisi katika akili zao.c. Alitafuta kuingiza mashaka kwenye kweli ya Neno la Mungu (3:1). Kwa kuuliza “ati Mungu [kweli] alisema, ‘msile matunda ya miti yote ya bustani?’” Shetani alitafuta kuingiza mashaka na kupandikiza kuchanganyikiwa kuhusu kile ambacho alikitaka Mungu. d. Alidanganya na kuligeuza Neno la Mungu (3:4). La kushangaza, ukweli mmoja ndio Shetani aliushambulia kuhusiana na ghadhabu ya Mungu na madhara ya dhambi. Kama ilivyokuwa kwa Adamu na Hawa, tunakabiliwa na uamuzi: nani tumwamini? Kwa mbinu za Shetani (na za kidunia), Neno la Mungu halikubaliwi tena kama kweli inayojieleza yenyewe, bali limefanywa kuwa ngazi ya neno la kiumbe. Yote mawili–Mungu na Neno lake huonekana kuwa na mamlaka ya chini zaidi ambayo lazima yapimwe na mamlaka iliyo juu zaidi. Kwa mara nyingine, ujanja wa nyoka: haupendekezi wanadamu wamwachie Mungu enzi yake mwenyewe, bali wao wenyewe tu waangalie na kutathmini madai ya Mungu kuhusu kweli. Matokeo ya mwisho yalikuwa sawa tu na kumweka Shetani awe Bwana, lakini hayo hufanyika pasipo mwanadamu kuelewa.” (Goldsworthy 1991: 104)

9

Page 11:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

e. Ailzijumuisha sifa za Mungu mwenyewe (3:5). Kimsingi, Shetani alikuwa anasema kwamba Mungu alikuwa hana upendo kwa kuwazuia Adamu na Hawa vitu vya kula, na alikuwa hana upendo kwa kuvitaka viumbe vyake kumtegemea yeye kwa maarifa ya mema na mabaya, badala ya kufanya maamuzi hayo wenyewe. f. Alichochea kiburi cha kianadamu. Shetani alimwahidi Hawa kwamba kwa kumuasi Mungu angelikuwa na uzima (“hakika hutakufa”), maarifa (“na macho yako yatafumbuka”), furaha kutokana na hali ya kuinuka (“utakuwa kama Mungu”), na ukuu wa kujitawa kimaadili (“kujua mema na mabaya”). Kinyume chake, hata hivyo, kwa Adamu na Hawa kufanya maamuzi kwa njia yao wenyewe (m.y., kujitawala kimaadili) ni sura ya kifo kwa sababu ni kutengwa mbali na Mungu. Kwa hiyo, kiini cha dhambi yao kilikuwa kutokuamini (m.y., kukosa imani na tumaini kwa Mungu, kunakodhihirishwa kwa kumtii Mungu). Hata tangu mwanzo, mpango wa Mungu ulikuwa kwamba watu wamwangalie yeye na kumtumaini yeye kwa ajili ya kweli kuhusu nini ni chema na nini kibaya, na kwa vipi tunatakiwa kuishi maisha yetu—m.y., “mwenye haki ataishi kwa imani” (Hab 2:4; Rum 1:17; Wgal 3:11; Waeb 10:38).

5. Dhambi ya Adamu na Hawa iliwadhuru si wao tu, bali kila mtu katika historia yote.a. Badala ya kuleta furaha na utoshelevu, Adamu na Hawa walileta hukumu, aibu, hofu, kufarakana na Mungu, uumbaji wote, wao kwa wao, na hatimaye mauti. (Mwa 3:7-19). Adamu na Hawa walitaka kujitawala (m.y., uhuru; kutengwa na Mungu), na wakapata hayo. Hata hivyo, kujitenga huko na Mungu ni sura ya kifo na mauti. Kutokana na kile walichokifanya, Adamu na Hawa kwanza walijikuta na aibu kuhusiana na hali yao ya kuwa uchi (Mwa 3:7-10). Hali yao ya kijinsia ingeliwakumbusha kwamba wao hawakuwa kama Mungu: hawakuwa na uwezo wa kuumba pasipo kutumia chochote (kama Mungu), bali tu waliweza kuzaa. “Hivyo hali yao ya ujinsia ilikuwa iwakumbushe [au ingepaswa iwakumbushe] juu ya uhuru wao na changamoto zake [au ingetoa changamoto] kwa fikira zao za uhuru na hali yao ya kuwa kama Mungu” (Goldsworthy 1991: 105).2 Kama matokeo ya mkondo ulioanzishwa bustanini, Mungu mara zote huwaachia watu waamue wenyewe njia zao na kisha kubeba madhara yao wenyewe (ona, Kut 16:1-20; Hes 11:18-20, 31-34; Rum 1:24, 26, 28). b. Adhabu ambayo Mungu aliiagiza (Mwa 3:16-19) kwa mwanaume (kazi inafanyika ngumut) na mwanamke kuzaa watoto kunakuwa kwa uchungu) zote zahusiana na uwajibikazi kimaisha kwa wanaume na wanawake. Zaidi ya hapo, Mwa 3:16b panaonyesha mwanzo wa mgongano wa kindoa na/au mvutano wa madaraka ya kindoa—tangu sasa na kuendelea, uhusiano kati ya waume na wake utakuwa una harufu ya dhambi (ona, k.m., kufuatia kwa mawazo mbali mbali yahusuyo namna ya mwingiliano kati ya “kutamani” na “kutawala” katika 3:16: Busenitz 1986: 203-12; Cassuto 1961: 165-66; Walton 2001: 227-28; Stitzinger 1981: 41-42; Foh 1974-75: 376-83).c. Dhambi ya Adamu huathiri uumbaji wote. “Uumbaji upo hapo kwa ajili ya manufaa yetu. Unyenyekevu ni uwakilishi wa uumbaji wote ili kwamba Mungu aushughulikie uumbaji kwa msingi wa anavyoshughulika na wanadamu. . . . Mwanadamu aangukapo kwa sababu ya dhambi, uumbaji hufanywa kuanguka pamoja naye.” (Goldsworthy 1991: 96) Zaidi ya hapo, Adamu hupata baadhi ya dawa zake: kama tu jinsi alivyoasi kinyume na utawala wa Mungu, sasa uumbaji wote, ambao anatakiwa kuutawala, utamwasi kinyume naye. “Laana ardhini kusema kweli ni laana kwa Adamu. Mfalme wa dunia sasa hana mtumishi anayemtii ardhini. Uhuru wa kula miti yote katika bustani unabadilishwa na kwa masumbufu kuifanya dunia itoe mkate unaolazimika kila siku. . . . Mwisho wa mwanadamu ni kuipa ardhi mbolea kwa yeye kuurudia mavumbi ambako alitokea.” (Ibid.: 106)d. Biblia huona watu wote kuwa kama moja na Adamu (“katika Adamu”), Adamu akitenda kama kichwa chetu au mwakilishi wetu (ona, Rum 5:12-19; 1 Wakor 15:21-22; nk., Waeb 7:9-10). Hatimaye, kama matokeo ya dhambi ya Adamu, kizazi chote cha mwanadamu kinapokea: “uhalali” wa kuwa na hatia dunia nzima, kunakoongoza kwenye kuharibika kimaadili dunia nzima (Zab 51:5; Yer 17:9; Rum 3:9; 7:14-25), kunakoongoza kwenye dhambi ya mtu moja moja dunia nzima (Rum 3:10-18, 23), kunakoongoza kwenye hatia ya mtu moja moja. Jinsi kamili ya namna ilivyokuwa na kwa nini na vizazi vya Adamu vimehesabiwa hatia na kuwa na uharibifu mkubwa kutokana na dhambi ya Adamu, ni swala la mjadala. Zifuatazo ni baadhi ya fikira zifikiriwazo:

(1) Biblia siku zote hutazama makundi ya watu kama mtu “moja aliyekamilika” (ona,

2 Baada ya Hawa “kutwaa na kula” (Mwa 3:6), Yesu kristo ilibidi aonje umasikini na mauti kabla ya maneno “twaa, kula” (Math 26:26) kufanyika maneno ya wokovu badala ya mauti .

10

Page 12:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Yosh 7:10-26; Rum 5:12-19; 1 Wakor 15:21-22 ). Hii ni sawa na kumtazama Adamu kama mbegu au mzizi wa mti, na uzao wake kama matawi na majani: Vyote ni mti moja; matawi na majani hupokea yote mawili - uzima na sura kutoka kwa ile mbegu na mzizi. Adamu, kama kichwa cha kizazi chote, huzalisha viumbe vilivyoanguka, vyenye uasi, kama vile yeye alivyifanya dhambi. Hali ya Adamu kama kichwa “huhusisha fursa za ndani zaidi kuliko ubaba wa kikawaida. Huhusisha utukuzaji wa kuelezea nini kinamaanisha kuwa mwanadamu [ona, Mwa 5:3; 1 Wakor 15:49]. . . . Ikiwa wahusika wanataka kuasi, je wasimamie wapi ili kufanya hilo? Sioni msingi wowote wa wao kusimamia, hakuna kitovu cha madai yao, uhuru wao binafsi hauko huru, mshabihiano wenye kujitegemea. Mungu ndiye aliyeuumba kama vile alivyowaumba, ndani na kupitia Adamu, kama sehemu ya sifa za Adamu.” (Blocher 1997: 130).(2) Kwa vile Adamu aliumbwa pasipo dhambi na alikuwa na kila fursa na mazingira yake binafsi, hakukuwa na mtu bora zaidi yake wa kuwakilisha wanadamu katika ujumla wao. Kama mwakilishi wetu, dhambi ya Adamu, na hivyo hata kukosa kwake, kuliwekezwa kwetu (sona, Johnson 1974: 298-316). Hali ilivyo ni kama taifa: “itokeapo mkuu wa nchi akitangaza vita na taifa jingine, watoto wote wanao zaliwa wakati huo wa vita huwa wako vitani na taifa jingine. Katika swala la Adamu, maafa hutenda kazi kwa kina cha ndani zaidi, kwa sababu mshikamano wetu wa ki-Adamu (yaani, uanadamu) ni muhimu zaidi na, kwa vile uhusiano ni kwa Mungu ‘ambaye tunaishi na kuenenda na kuwa na uhalisi ndani yake’.” (Blocher 1997: 129).(3) Ilikuwa lazima kabisa kwa Mungu kufanya kitu fulani kwa watu wote ili wawe na uharibifu kama matokeo ya dhambi ya Adamu. “Ni kutoa katika yaliyojitokeza, kama ilivyokuwa sahihi na lazima kwa kiwango cha juu sana afanye hivyo, kutoka kwa huyo mwanadamu mwasi, na kanuni zake za kiasili zikiwa zimeachwa zenyewe, kwatosha kumfanya awe mharibifu kabisa na aliyepindana kutenda dhambi kinyume na Mungu” (Edwards, 1984, Original Sin: 219).

e. Matokeo ya anguko, na utu wetu “katika Adamu,”ni kwamba kwa jinsi yetu wenyewe, pasipo Kristo, tunakuwa “wafu katika makosa na dhambi zetu” (Waef 2:1). Hii inamaanisha kwamba kuna upungufu kupita kiasi au uharibifu kuhusiana na kila mtu (pia huitwa nguvu ya dhambi ikaayo ndani) ambayo huathiri kila kitu ndani yetu, kuchanganya hata jinsi tunavyofikiri, kuwaza, kuongea, kutenda, kujisikia, na mahusiano na watu na kwa Mungu. Matokeo ya uharibifu huu ni kuwa, nje ya msaada wa Kristo, tunakuwa: hatuna uwezo kabisa kumjia Kristo na kumwamini yeye (Yoh 6:44, 65; Waef 2:8-9); hatuwezi kabisa hata kuuona ufalme wa Mungu (Yoh 3:3, 5); hatuwezi kabisa kujitoa kwa sheria ya Mungu na kumtii (Rum 8:6- 8); hatuwezi kabisa kuelewa kweli za kiroho kumhusu Mungu (1 Wakor 2:14); hatuwezi kabisa kumpendeza Mungu (Waeb 11:6); tunakuwa watumwa wa dhambi, dunia, mwili, na Ibilisi, hatuna kabisa uzima wowote ule, na tunapaswa ghadhabu ya Mungu na hukumu yake (Rum 6:16-17; Waef 2:1-3) (ona pia Edwards, 1984, Original Sin: 143-233; Owen 1979: passim).

6. Hata katika hukumu yake kwa Adamu na Hawa, Mungu alidhihirisha neema yake. a. Alitengeneza mavazi ya kuwatosha ya ngozi ya wanyama ili kuwavika Adamu na Hawa (Mwa 3:21). b. Ingawaje Mungu alimfukuza Adamu na Hawa kutoka bustanini (Mwa 3:22-24), hakuuondolea uwakili wao juu ya hii dunia (k.m., Mwa 2:15 na 3:23). Bila shaka, kufukuzwa kwao kutoka bustanini kulisaidia kukamilika kwa mpango wa Mungu wa mwanadamu kuijaza na kuimiliki dunia (Mwa 1:28). c. Katika Mwa 3:15 alitoa tamko la kwanza la mpango wake wa wokovu kwa dunia: “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.” Mtu fulani kati ya uzao wa mwanamke (amekuwa akitajwa kama mzao wa Ibrahimu [Kristo]) atatoa pigo la kichwa na kuleta ushindi kwa Shetani msalabani, wakati Shetani atamponda kisigino, au kumsababisha ateseke. Tamko hili limetekelezeka hatua kwa hatua katika Biblia nzima yote. Bila shaka, tamko hilo, likijumuishwa na swala kwamba Adamu na Hawa wasile kutoka katika mti wa uzima (Mwa 3:22), kuliwahakikishia kuwa wasingeweza kuishi milele wakiwa katika dhambi. Badala yake, kama Mungu alivyofunua hatua kwa hatua mpango wake, wale waishio kwa imani katika Kristo wataweza kula kutoka kwenye mti wa uzima katika nchi mpya milele katika haki (Ufu 22:2).

C. Matokeo ya Anguko—kutoka kwa Kaini hadi Mnara wa Babeli (Mwanzo 4-11:26).

11

Page 13:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

“Baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi, uzao uliowafuatia uliendelea kuitawala dunia. Tatizo halikuwa kama walikuwa hawatawali. Kinyume chake, Mwanzo 4 panaonyesha michango yao katika ubunifu wa muziki, ufuaji vyuma, ufugaji, ustadi wa ujenzi, na siasa (‘Kaini akajenga mji, mst. 17). Tatizo kuu la mwanadamu mwenye dhambi halijawahi kuwa kukataa kwake kuitawala dunia. Tatizo lake kuu ni kwamba huitawala dunia katika namna isiyomcha Mungu. Mwanadamu huyu wa asili ya ki-Adamu hutawala ili kujifanyia jina mwenyewe, siyo kwa kulitukuza jina la Bwana. Wanadamu wadhambi hujaribu kutawala wakati wao wenyewe ni watumwa wa dhambi na Shetani. Mungu aliwaumba Adamu na Hawa ili wajenge nakala ya ule Mji Wake hapa duniani. Wazao wao wakajenga mji uliopotoka wa Mwanadamu.” (Leithart n.d.: n.p.)

1. Kaini na uzao wake ( Mwa 4:1-24 ). a. Kwa Kaini twaona kuongezeka kwa dhambi: kukufuru3 (4:3); hasira (4:5); wivu, udanganyifu, na mauaji (4:7-8); uongo (4:9); kujitafutia binafsi na kujihurumia (4:13-14); kukengeuka kutoka kwa Mungu (4:14, 16). Kuongezeka kwa dhambi pia kunaonekana kwamba Kaini siyo tu hakumuua kila mtu, bali alimuua ndugu yake mwenyewe ambaye alikuwa mtu “mwenye haki” (Math 23:35; Waebr 11:4). Pia, hata hivyo, angalia neema ya Mungu kwa Kaini katika kumlinda ili asiuawe na ndugu zake wengine wa kike na wa kiume (Mwa 4:15).b. Uzao wa baadaye wa Kaini, Lameki (4:18-19, 23-24) apelekea uharibifu kimaadili kuwa kiwango cha chini kabisa: ana kiburi na majivuno; ageuza mgongo wake kwa mpango wa Mungu wa mke moja (Mwa 2:23-24; Math 19:3-6). Wake wengi siyo mpango sahihi wa Mungu. Katika Biblia kuwa na wake wengi mara zote kumeonekana kuwa siyo sahihi, na kuliongoza kuletesha matokeo mabaya. Kwa hiyo, haishangazi kwamba hata aliyeanzisha kuwa na wake zaidi ya moja, Lameki, ni mtu mkali aliyejipatia uhuru wake kamili kutoka kwa Mungu kwa kuua watu kwa visasi vya maswala madogo madogo na kudai haki ya Mungu ya kulipa kisasi (ona Kumb 32:35). Madai yake makali ya kutaka kulipa kisasi kwa wengine “mara sabini na saba” (Mwa 4:24) hupata mkondo mwenza katika kauli ya Kristo kuwa tunatakiwa kuwasamehe wengine “mara sabini na saba” (Math 18:21-22).

2. Tangu Seti hadi Nuhu ( Mwa 4:25-6:8 ). a. Moja ya sifa kuu za kitabu cha Mwanzo ni matumizi ya vichwa vinavyofanana katika kutambulisha simulizi na vizazi ambavyo hubadilishana katika Kitabu kizima. “Hivyo hutokea katika 2:4; 5:1; 6:9; 10:1; 11:10, 27; 25:12, 19; 36:1, 9; 37:2. Kitu kinachofanana kote katika vichwa hivi vyote ni neno la Kiebrania [Toledot—ambalo kikawaida hutafsiriwa kama “kizazi (vizazi); uzao; hesabu; orodha; kumbu-kumbu”]. . . . Hivyo vichwa [Toledot] hutenda kazi mbili. Kwanza, huwa kama vichwa vya sura katika vitabu vya kisasa. Baadhi yao hutambulisha sehemu kuu za simulizi, kuonyesha hatua mpya ya kukua kwa mpango. . . . [Pili, hivyo vichwa vya Toledot] hukazia mtazamo wa msomaji kwa mtu maalum na watoto wake aliowazaa. Humwezesha mwandishi wa Mwanzo kufuatilia mema ya mkondo mzima wa familia kuu pasipo kulazimika kufuatilia kwa kina maisha ya ndugu zao wengine.” (Alexander 1993: 258, 259)b. Kuanzia Mwa 4:25 mpango wa kitabu unageukia mkondo wa Seti. Kwa hiyo, hivyo Toledot vya Adamu, kuanzia Mwa 5:1 hukazia kwa Seti na kIsha kwa wazao fulani wa Seti. Biblia hufanya hilo kwa makusudi, kwa sababu watu inaowakazia ndio kitovu cha kuanikwa wazi kwa simulizi nzima.4

c. Hivyo Toledot vya Adamu pia ni muhimu kwa sababu nyingine:baada ya kutaja kizazi cha kila mtu na uzao wake muhimu, mara nyingi hurudia kwa kuhitimisha, “naye akafa” (Mwa 5:5,

3 Dhabihu ya Habili ilikuwa kwa imani (Waeb 11:4); Ile ya Kaini bila shaka haikuwa hivyo. Ni lazima, bila shaka, dhabihu ya Kaini ilikuwa ya “matendo,” m,y., juhudi za kumghairi Mungu. Zaidi ya hapo, dhabihu ya Habili ilikuwa ni malimbuko, kutambua kwamba kuongezeka kwa mifugo kwatoka kwa Bwana na kwamba yote ni mali ya Bwana. Dhabihu ya Habili pia ilikuwa ni wale walio bora kabisa katika mifugo (m.y., “sehemu iliyonona’). Ikimaanisha, bila shaka, ya kaini haikuwa malimbuko, bali ilikuwa tu baadhi ya“mazao ya nchi”—ni dhahiri, tofauti na dhabihu ya Habili, ni dhabihu bila kufikiri, iliyofanyika si kwa imani, na kwa kusudio bovu. Hivyo, 1 Yoh 3:12 huyaita matendo ya kaini (katika muktadha kuhusiana na dhabihu) “ovu” na ile ya Habili “ya haki.”4 Kuna mabishano kuhusiana kwamba ni nani waliokuwa “wana wa Mungu” na “binti za wanadamu” katika Mwa 6:2. Dhana nne kuu ni: 1. “Wana wa Mungu” = malaika walioanguka; “binti za wanadamu” = udunia; dhambi zao = ndoa kati ya ulimwengu usio wa kawaida na viumbe vya kidunia. 2. WWM = Mkondo wa Kiungu wa Sethi; BW = mkondo usio wa Kimungu wa Kaini; dhambi = ndoa kati ya watakatifu na wasio watakatifu. 3. WWM = watawala wa kiukoo; BM = wa kawaida; dhambi = ndoa ya mwenzi zaidi ya moja. 4. WWM = watawala wa kiukoo wenye pepo; BM = wa kawaida; dhambi = unganiko lisilo la ki-ungu. Ona kwamba katika dhana ya 1 na 4 hao WWM ni waovu; katika dhana ya 2 WWM ni wazuri.

12

Page 14:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

8, 11, 14, 17, 20, 27, 31). Hilo husisitiza madhara ya “laana” ambayo ilitokana na dhambi ya Adamu (ona Mwa 2:17; 3:19). Ingawaje watu kabla ya gharika kuu waliishi miaka mingi zaidi kuliko waishivyo leo, kila moja wao alikumbana na mauti kwa sababu kila moja alikuwa ni wa mfano na umbo la Adamu (Mwa 5:3)—m.y., ana dhambi ikaayo ndani. Tofauti moja ni Enoki (Mwa 5:21-24). Si kwamba Enoki hakuwa na dhambi ikaayo ndani (kama watu wengine walivyo, naye alikuwa vivyo). Isipokuwa, kule “kumtwaa” Enoki kulikuwa udhihirisho mwingine wa neema ya Mungu kwa sababu alikuwa “ametembea na Mungu” kama mcha Mungu.d. Hivyo Toledot za Adamu pia zindhihirisha kuporomoka kwa uanadamu kupitia dhambi. Huanzia na Adam katika hali ya baraka za Mungu (Mwa 5:1), na kumalizikia na huzuni ya Mungu kwamba alimfanya mwanadamu, na uamuzi wake wa kuisafisha dunia kuondosha wanadamu, kwa sababu “kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote” (Mwa 6:5-7). Hata hivyo, mtu moja, Nuhu, alipata neema machoni pa Mungu na kwa yeye likapatikana tumaini kwa wanadamu (Mwa 6:8).

3. Nuhu na Gharika ( Mwa 6:9-9:29 ). a. Sehemu hii ni moja yenye mlinganisho.Huanzia na hukumu ya Mungu kwa dunia (Mwa 6:11-13), lakini huishia kuweka agano na viumbe vyote vilivyo hai kwamba hataangamiza dunia kwa gharika (Mwa 8:21-9:17). Kwa upande mwingine, sehemu hii huanza na Nuhu kutajwa kama “mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu [ambaye] alikwenda pamoja na Mungu. Mwenye haki, mtu mkamilifu nyakati zake” (Mwa 6:9). Huishia na Nuhu kulewa na kumlaani Kanaani (Mwa 9:20-27).5 Alama moja ya sifa ya ukweli kuhusu Biblia ni kwamba haionei haya kuelezea dhambi hata za watu ambao ni mshuhuri sana.b. Simulizi ya gharika, inakwenda sambamba na simulizi za uumbaji wa awali, na huishia “uumbaji ” wa dunia: “Dunia inakaliwa na watu kwa kutenganisha ardhi na maji (Mwa. 8:1-3; pia Mwa. 1:9-10). Viumbe hai vinatolewa ili kuijaza upya dunia (Mwa. 8:17-19; pia Mwa. 1:20-22, 24-25). Siku na majira zarejezwa upya (Mwa. 8:22; pia Mwa. 1:14-18). Wanadamu wabarikiwa na Mungu (Mwa. 9:1; pia Mwa. 1:28a), wanaagizwa ‘Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.’ (Mwa. 9:1b, 7; pia Mwa. 1:28b), na kupewa mamlaka juu ya wanyama wote (Mwa. 9:2; pia Mwa. 1:28c). Mungu awapa wanadamu—walioumbwa kwa mfano wake (Mwa. 9:6; pia Mwa. 1:26-27)—chakula (Mwa. 9:3; pia Mwa. 1:29-30).” (Williamson 2007: 61) Hata hivyo, kuna tofauti moja muhimu kati ya dunia iliyofanywa upya baada ya gharika, na ile ya uumbvaji wa mwanzo: kuwepo kwa dhambi ya mwanadamu.

4. Agano alilolifanya Mungu na Nuhu (“Agano la Nuhu,” Mwa 8:21-9:17 ) ni agano la kwanza kutajwa wazi katika Biblia. 6 Katika Agano hili “Mungu alionyesha neema ya rehema zake kwa wanadamu wote, wote –waliokombolewa na wasiokombolewa. . . . Alidhihirisha kutokubali kwa dhambi ya mwanadamu kutopangua mpango wake aliouandaa katika Mwanzo 3:15, kutokubali kwa dhambi ya mwanadamu kutotangua agizo lililotolewa kabla ya anguko la ‘Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.’” (Busenitz 1999: 182). In Mwa 8:21 Mungu anautazama upungufu wa mwanadamu kama sababu ya rehema zake, kama vile mwanzoni aliuona kama sababu ya hukumu yake (Mwa 6:5-7). Isingalikuwa rehema na neema za Mungu katika kufanya upya agano lake na Nuhu, basi mwanadamu angelikuwa anaelekea kuangamia tena, kama vile ilivyotokea wakati wa gharika kuu. “Umuhimu wa kitheolojia wa Agano la Nuhu ni wa namna angalau mbili. Kwanza kabisa, ni msingi kwa ujasiri wetu wa sasa kwa Mungu kama mhimili. Ni Agano la Nuhu ndilo linalotupatia uhakika kwamba Mungu ataudhibiti utaratibu wa viumbe, licha ya machafuko na fujo zinazoendelea kutishia kulimeza. . . . [Pili] Agano la Nuhu linatoa mpangilio wa theolojia ya Ki-Biblia ambao ndani yake maagano yote ya ki-Ungu yanayofuatia yanatenda kazi.” (Williamson 2007: 67-68)5. Orodha ya mataifa ( Mwa 10:1-32 ) na Mnara wa Babeli ( Mwa 11:1-9 ).

a. Orodha ya mataifa (Mwa 10:1-32) huenda ilifuatia Mnara wa Babeli (Mwa 11:1-11:9) katika historia, kuanziai misemo ya awali na magawanyiko na kutawanyika kwa mataifa mbali

5 Kuna mjadala kuhusu nini Hamu alifanya pale “alipouona uchi wa babaye,” na kwa nini Nuhu alimlaani Kanaani (mwana wa Hamu), na si Hamu mwenyewe (Mwa 9:21-27). Kwa vile Mwanzo ni sehemu ya “Torati” (maelekezo), inaunganika na zile Amri Kumi, ikiwamo amri ya “kumheshimu baba yako na mama yako” (Kut 20:12; Kumb 5:16). Kwa hiyo, maelekezo yanayoelekea sana ni kuwa Hamu aliona uchi wa baba yake, na kupitia dhihaka katika hilo alimdharau baba yake. Nuhu alimlaani Kanaani ili kwamba baadaye amchukie baba yake mwenyewe.6 Agano la Ki-ungu la mwanadamu laweza kutafsiriwa kama “udhibiti mkuu wa uhakika wa uhusiano uliochagulika uliopo uhusishao ahadi au uwajibikaji ambao umetiwa muhuri wa kiapo” (Williamson 2007: 43; ona pia Klooster 1988: 149; Beckwith 1987: 96). Maagano makuu katika Biblia ni ya Nuhu, Ibrahimu, Musa, Daudi, na Agano Jipya.

13

Page 15:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

mbali kulingana na lugha zao. Mwandishi wa Mwanzo huenda aliweka habari hii kwanza kwa sababu ya kiuandishi: hufuatilia juu ya historia za Shemu, Hamu, na Yafeti kuanzia mwisho wa Mwanzo 9; huonyesha kwamba, kwa vile watu wote duniani ni wazao wa kutokea kwa Nuhu kupitia Shemu, Hamu, na Yafeti, watu wote ni wa “damu” moja na hatimaye kuwa wa familia moja; hufanya kazi kama utimilizo wa agizo la ki-Ungu katika Mwa 9:1, na huonyesha kwamba kutawanyika kwa mataifa kwaweza bila shaka kutathiminiwa kiuzuri tu kama hasi na pia chanya (m.y., hukumu ya Mungu katika Mwa 11:9).b. Mnara wa Babeli (Mwa 11:1-9) kwaonyesha upotofu wa watu ulieendelea kinyume na Mungu. Jukumu la awali alilotoa Mungu kwa mwanadamu lilikuwa “kuijaza dunia” (Mwa 1:28). Alirudia agizo hilo kwa Nuhu na wanawe katika Mwa 9:1. Hata hivyo, licha ya hukumu ya Mungu ya Gharika kuu, bado tena wanadamu wakamwasi Mungu kwa dhahiri: Watu wanaamua siyo kuijaza dunia, bali kukaa mahali pamoja. Zaidi ya hayo, wanataka kujenga mnara kufika mbinguni ili kuliinua jina lao wenyewe na kuwa kama Mungu (kwa mara nyingine, kama ile dhambi ya Adamu). Kusema ukweli, “uasi wa Babeli ulikuwa ni uharibifu mbaya zaidi kuliko ule uliosababisha gharika; ulikuwa wa dunia nzima na ulikuwa umepangika. Ule mji, na minara yake ikiwa imefika mbinguni ulikuwa ni mbegu ya yule nyoka kumwangusha Mungu Aliye hai kama mfalme.” (Klooster 1988: 147) Matokeo yake, Mungu“alizichafua lugha zao” na “akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote” (Mwa 11:7-8).7 Maelezo haya hudhihirisha kiwango cha udhambi wa mwanadamu. Kulingana na msimamo wa kiuandishi, humwachia msomaji kutafuta jawabu la mwanadamu kuendelea na dhambi na uasi kwa Mungu.

6. Vile Toledot vya Shemu ( Mwa 11:10-26 ). Baada ya Babeli, Biblia hukazia mkondo wa Shemu, ambao wote wawili- Nuhu na Mungu walivibariki. Toledot hizo hutupeleka kwa Ibrahimu, ambaye Mungu atamwita ambaye kwa kupitia yeye, Mungu atatekeleza mpango wake kukomboa na kuibariki dunia.

III. Tukio la Ukombozi— Mungu aita Watu Kwa Ajili Yake Mwenyewe (Mwa 11:27-Ufu 20

A. Mwanzo mpya wa Mungu—tangu Ibrahimu hadi Yusufu (Mwa 11:27-50:26).1. Katika sehemu hii ya historia ya Biblia, Mungu sasa anamchagua mtu moja (Ibrahimu) ili kuanza mpango wake maalum wa ukombozi wa dunia. “Licha ya uasi wa wanadamu, Mungu hauachi mpango wake kwa dunia yake. Kama miaka Elfu mbili kabla ya Yesu, Mungu anauanzisha mpango utakaoleta kuponywa tena kwa dunia. Mpango huu ulioahidiwa una sehemu mbili: kwanza, kutoka katika jmii hii ya watu walio waasi, Mungu atamchagua mtu moja [Ibrahimu]. Mungu atamfanya mtu huyu kuwa taifa kuu na kulipatia taifa hilo nchi na kuwabariki. Pili, Mungu atapanua uwigo wa baraka hizo kwa mataifa yote (Mwa 12:1-3; 18:18).

Sehemu iliyobakia ya kitabu hicho cha Mwanzo hufuatilia miinuko na mabonde ya ahadi hii yenye pande mbili. Ahadi inatolewa siyo tu kwa Ibrahimu bali hata kwa mwanaye Isaka (Mwa 26:3-4) na kwa mwana wa mwana wake Yakobo (Mwa 28:13-15). Hatari nyingi zinahatarisha ahadi ya mpango wa Mungu kadri unavyoendelea: utasa, na kutokuzaa,wafalme wa kigeni na maharimu, mikasa ya kimaumbile, kushambuliwa na watu wanaowazunguka, na kutokuamini kwa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, wenyewe. Kupitia hayo yote, anajionyesha mwenyewe kuwa ‘Mungu Mwenyenzi (Mwa 17:1; Kut. 6:3), Yeye aliye na uwezo wa kutekeleza mpango wake.

Akiwa anakaribia mwisho wa maisha yake, Yakobo anawasafirisha wana wake kumi na mbili na familia zao kwenda Misri ili kuziokoa na njaa. Kisa kinachotia mhimili cha mtoto wake wa kumi na moja, Yusufu, kinaonyesha uaminifu wa Mungu na udhibiti wake wa historia anapoweza kuhifadhi

7 Katika siku ya Pentekoste (Mdo2:1-11), Kiuhalisia, Mungu ageuza nyuma Babeli: “Mungu asababisha wawakilishi kutoka mataifa yale yaliyotawanyika kujumuika Yerusalemu ili waweze kupokea baraka za kuelewa lugha mbali mbali kana kwamba lugha hizo zote ni moja. . . . Kusudi la kuwa na uelewa uliounganika ni kudhihirisha nguvu za Roho wa siku za mbeleni katika kushuhudia kifo cha Yesu, ufufuo na kupaa kwenye kiti cha enzi kutawala kama mfalme wa enzi yote. Chini ya utawala wa Yesu na kupitia nguvu za Roho wake, wawakilishi wa mataifa walitakiwa ‘kutawanyika’ tyena na kutawala nguvu za uovu kwa kuijaza dunia uwepo wa Mungu . . . Namna halisi ambayo walitakiwa kufanya hilo, ilikuwa kwa ‘kuwa mashahidi’ kupitia nguvu za Roho katika neno na matendo kwa niaba ya Yesu Kristo (ona Mdo 1:8).” (Beale 2004: 202-03) Kwa hiyo, “Pentekoset ni hatua mwenza ya ukombozi kwa Babeli; ambapo, katika kutimiliza ahadi za agano zililotolewa kwa Ibrahimu, umoja mpya kupitia Roho Mtakatifu kwa misingi ya kazi iliyomalizika ya Yesu Kristo huunganisha waamini kutoka mataifa yote ya dunia. Bali vigezo vya neema kwa hukumu ya Babeli havikuwa vimefunuliwa kikamilifu kwa Ibrahimu wala kwa wale waliopewa mwanzoni kile kitabu cha Mwanzo.” (Klooster 1988: 147)

14

Page 16:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

watu ambao kupitia hao atauleta wokovu kwa dunia (Mwa 45:5; 50:20).” (Bartholomew and Goheen n.d.: 2)2. Mungu afanya Agano na Ibrahimu (“Agano la Ibrahimu,” Mwa 12:1-3; 13:14-17; 15:1-21; 17:1-21; 22:15-18 ), ambalo linathibitishwa kwa Isaka, mwana wa Ibrahimu ( Mwa 26:1-5, 24 ) na kwa Yakobo, mwana mdogo wa Isaka ( Mwa 28:3-4, 13-15; 35:11-12 ).

a. Agano la Ibrahimu kama lilivyoanzishwa awali, na kisha kuimarika kwa jinsi tofauti katika Mwanzo lina “kamba tatu za ki-ahadi” kimsingi: utekelezaji ki-uzao (m.y., ahadi zihusianazo na “uzao”); mipaka ya kitaifa (m.ya ahadi zinazohusiana na “nchi (ardhi)”); na baraka za dunia nzima ahadi zinazohusiana na baraka kwa watu wengine kupitia uzao wa Ibrahimu) (Williamson 2000: 100-01; pia ona, Kaiser 1978: 86; Essex 1999: 208; Reisinger 1998: 6; Williamson 2007: 82-90 [Williamson anaona maagano mawili yakifanywa na Ibrahimu, la kwanza katika Mwanzo 15 na la pili katika Mwanzo 17, hayo hutenda kazi pamoja kutimiza kusudio moja linalolengwa]). Wakati watu wa Babeli walitaka kufanya jina lao wenyewe liwe kuu (Mwa 11:4), kwa neema yake Mungu atalifanya jina la Ibrahimu kuu na kuibariki dunia kumpitia yeye. (Mwa 12:2-3). b. Agano hili linajikunjua na kutimilizika kila mahali kote katika AK na AJ (bila shaka, ni kweli, uhalisi wa kiroho na hatima ya utimilifu wake unakutikana tu katika AJ). Agano limetendeka kihistoria kwa kuundwa na kuinuka kwa taifa la Israeli. Hasa baada ya mgawanyiko wa taifa la Israeli na utumwa wake, kutimizwa kwa agano hilo kunatajwa na manabii wakiiita “siku ya Bwana” ijayo. Utimilifu wa mwisho na wa kweli wa Agano unapatikana katika Kristo, kupitia Roho Mtakatifu. Kwa namna nyingi, bila shaka, Agano la Ibrahimu ni uti wa mgongo wa theolojia na ni mchoro wa ramani ya Biblia yote inayobakia. “Kwa hiyo, wakati Yahwe anamkusudia kimsingi Ibrahimu na taifa litakalotokana na yeye, hatimaye kuna kuhusishwa kiupana zaidi: ‘jamaa zote za dunia’ (Mwa 12:3 ESV) ambazo, kupitia Ibrahimu, pia zitabarikiwa. Kwa maneno mengine, mipango ya Mungu kwa Israeli siku zote ilikuwa ikiendana na kusudio lake kuu, mipango kwa jamaa za dunia yote.” (Williamson 2007: 84)

3. Kwa kupitia Yakobo, taifa la Israeli litaanzishwa. Ingawaje Ibrahimu na mkewe Sara walikuwa wazee na hawakuweza kuwa na watoto wao wenyewe, Mungu kimuujiza akawawezesha kupata mimba na kumzaa mwana, Isaka (Mwa 18:1-15; 21:1-8). Hilo lilidhihirisha kwamba Mungu alikuwa anaendesha mambo, kuhakikisha kwamba mpango wake na Agano alilolifanya na Ibrahimu litatimizwa. Wakati mke wa Isaka aitwaye Rebeka alipokuwa na mimba ya watoto mapacha, Bwana alimwambia kwamba, kiuhalisi, mataifa mawili yalikuwa ndani yake na kwamba mwana mkubwa (Esau) atamtumika mdogo (Yakobo) (Mwa 25:21-26). Mungu baadaye alilibadilisha jina la Yakobo kuwa Israeli (Mwa 32:24-32; 35:9-12).8 Kutoka kwa Yakobo (Israeli) yalipatikana makabila kumi na mbili ya Israeli (Mwa 30:1-24; 35:16-18, 22-27; 41:50-52; 49:1-28). 4. Mungu awapeleka watu wake Misri. Wana wa Yakobo walianza kuishi maisha yasiyofaa kama walivyofanya Wakanaani waliokuwa wanakaa nao (Mwa 34:1-31; 35:22; 38:1-26). Kama hilo lingeendelea, kusingekuwa na Israeli tena. Kwa hiyo, Mungu aliwahifadhi hao wateule wake kwa kuwaondoa kutoka Kanaani kwenda Misri kwa njia ya dhambi ya kaka za Yusufu, na haki ya Yusufu. Mungu pia aliitumia dhambi ya Yuda na mkwewe Tamari kama sehemu ya mpango wake jumla wa ukombozi (ona Mwa 38:12-19; Rut 4:18; Math 1:3). Kisa kumhusu Yusufu (Mwa 37; 39-50) kimsingi kinaonyesha jinsi Israeli walivyoingia Misri, na jinsi Mungu alivyokuwa akishughulikia mpango wake alioutangaza miaka mamia kadhaa nyuma (Mwa 15:13-14) kwa Ibrahimu. Kuwepo kwa Israeli Misri kuliandaa jukwaa kwa ajili ya Mungu kufanya hatua inayofuata katika mpango kabambe wa Mungu, wa kuwatoa. 5. Mungu hutenda katika historia (kikawaida kupitia matukio na matendo ya watu ambayo huonekana kwetu kama “ya kawaida” tu, na wala siyo matukio yapitayo ukawaida) kuhakikisha kwamba mpango wake unatekelezwa. Matukio mengi hutishia kuzuia ahadi za Mungu kuonekama kwamba hazitatimizwa tena. “Umuhimu wa vitisho vizuiavyo kutimizwa hutegemea ukweli kwamba ahadi huelekeza jinsi ya utimilizwaji wake kuweza kufanyika tu kwa kazi isiyo ya kawaida ya Mungu. Si kitu kilicho katika uwezo wa mwanadamu, wala si swala la matukio ya kikawaida.” (Goldsworthy 1991: 121) 6. “Mkondo wa ukinyume” (m.y., Mungu kuchagua wa umri mdogo, walio wadhaifu, wageni) ili kutekeleza mipango yake, inajitokeza kila mahali katika Maandiko. Neema ya Mungu na maamuzi yake ya Ki-Ungu huonyeshwa kila mahali katika sehemu hii: k.m., Seti juu ya Kaini (Mwa 4:25); Isaka juu ya Ishmaili (Mwa 17:18-19; ona Rum 9:6-9); Yakobo juu ya Esau (Mwa 25:23; ona Rum 9:10-13);

8 Yakobo apigana mieleka na Mungu (Mwa 32:24-32) Mungu alipombadili jina Yakobo kuwa Israeli ni kivuli kiashiriacho cha taifa la Israeli kuendelea kupambana na Mungu historia yake yote (ona Hos 12:1-6).

15

Page 17:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Efraimu juu ya Manase (Mwa 48:8-21); Yuda juu ya ndugu zake wakubwa (Mwa 49:1-12). Hii inaonyesha kwamba Mungu hajali nguvu, umashuhuri, na utajiri ambao ulimwengu huwa unauthamini, lakini neema yake huchagua “wadogo kama hawa” (ona, Math 25:40, 45). Mungu hudhihirisha mkondo huu huu tena na tena: k.m., Musa juu ya Farao (Kut 2:1-14:31; Waeb 11:25-29); Israeli juu ya mataifa mengine (Kumb 7:7-8); Daudi juu ya ndugu zake wakubwa (1 Sam 16:1-13); Sulemani juu ya ndugu zake wakubwa (1 Waf 1:5-40; 1 Nyak 3:1-5); mwanamke mjane wa Sarepta juu ya wajane wa Israeli (1 Waf 17:9; ona Luka 4:25-26); Naaman Muashuri juu ya wakoma wa Israeli (2 Waf 5:1-14; ona, Luka 4:27). Yesu mwenyewe alikuwa mtu masikini na mtumwa wa wote (Math 20:25-28; Wafil 2:5-8). Kwa hiyo, anatuambia, “bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama yule atumikaye.” (Luka 22:26). Anasema, “Mtu atakaye kuwa wa kwanza, atakuwa wa mwisho kuliko wote” (Mark 9:35; ona pia Mark 10:42-44; Yoh 13:12-16). Anaongeza, “kwa kuwa aliye mdogo miongoni mwenu nyote, huyo ndiye mkubwa” (Luka 9:48). Anahitimisha, “Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.” (Math 18:4; ona pia, Mark 10:14-15).

B. Kuanza kwa taifa la Israeli—Kutoka Misri kwenda nchi ya ahadi (Kutoka-Kumbu-kumbu).1. Katika hatua hii kuu ya Mungu kwa tukio la ukombozi, Israeli lafanyika taifa, na kupata uhuru wake kutoka utumwani huko Misri, kama matokeo ya uaminifu wa Mungu kwa Agano alilomfanyia Ibrahimu, Isaka, na Yakobo ( Kut 2:24 ).

a. Kipindi cha miaka mia nne chapita kabla ya kurudia mwendelezo wa matukio. “Uzao wa Ibrahimu, sasa ujulikanao kama Israeli (jina ambalo Mungu ampatia Yakobo), unaongezeka idadi katika Misri. Bali mafanikio huleta matatizo ya aina yake yenyewe. Mfalme wa Misri aanza kuona jamii hii ndogo inayoongezeka kama tishio. Ili kuizima hatari inayojitokeza, Farao anawaingiza Israeli katika utumwa. Kitabu cha Kutoka kinaanzia wakati wa kilele cha kukandamizwa kwa Waisraeli katika Misri. Katika mazingira haya ya maumivu mazito na kongwa, Mungu anamchagua Musa kuwakomboa Waisraeli kutokana na utawala wa kikatili wa Misri ili Waisraeli waweze kurudi kwa Mungu. Katika mfululizo wa matukio ya kushangaza, mapigo kumi yanaleta hukumu ya Mungu kwa miungu ya Misri (Kut 12:12), na Israeli inaokolewa kimiujiza kutoka jeshi lenye nguvu la Misri pale walipokuwa wanavuka bahari ya Shamu. Mwishowe Israeli wanafika mahali ambapo wanakutana na Mungu—katika mlm. Sinai. Hapo, Mungu akutana na Israeli kwa jinsi ya kiajabu ya ngurumo na radi na moto. Kwa nini Mungu afanye yote haya kwa Israeli? Mungu anayo kazi kwa ajili yao kuifanya. Wanapaswa kuwa taifa na ufalme watakaotumika kama makuhani. Kazi yao ni kuwa kiungo cha baraka za Mungu kwa mataifa na kufanyika watu walio kielelezo kuwavuta watu wengine wote kwa Mungu (Kut 19:3-6). Huu ndio wito utakaoliunda taifa la Israeli kuanzia hapa na kuendelea: watapaswa kuwa mfano na kielelezo mbele za mataifa wakiufunua ule mpango mzuri wa awali wa Mungu wa muundo kwa maisha ya mwanadamu. Baada ya kuwapa kazi hii, Mungu anawapa sheria kuongoza maisha yao, na watu wa Israeli kuahidi kuishi kama watu wa Mungu walio waaminifu. Kisha Mungu anawaamuru kujenga maskani ambamo atakaa ndani yake. Kuanzia hapa na kuendelea, kila waendapo, Mungu ataishi akionekana kati kati yao.

Katika Mambo ya Walawi twaona jinsi Israeli wanavyopaswa kuishi katika ushirika na Mungu Mtakatifu. Kitabu cha Hesabu kinasimulia safari wa Israeli kutoka Sinai hadi Kanaani. Kwa bahati mbaya, kutokuamini kwa Israeli kunawagharimu kukaa miaka arobaini nyikani kabla ya kuingia Moabi, iliyo kando kabisa mwa nchi ya ahadi. Katika Kumbukumbu la Torati, kiongozi wa Israeli, Musa, anawaelekeza Israeli jinsi wanavyopaswa kuishi watakapoingia katika ile nchi ya ahadi. Israeli wanajiandaa kuingia nchi ya ahadi—wanaapizwa kuwa watu wa Mungu na kuwaonyesha mataifa yawazungukayo, kufahamu Mungu ni nani na hekima ya mpango wa uumbaji wake wa awali kwa maisha ya mwanadamu. Israeli wanavyojipanga tayari kwa kuingia, Musa anakufa na uongozi unahamia kwa Yoshua.” (Bartholomew and Goheen (n.d.: 2-3) b. Mazungumzo kati ya Mungu na Musa yanaongoza sehemu hii ya Maandiko. Tendo la Mungu kwa niaba ya Israeli kulingana na Agano la Ibrahimu (Kut 2:24).9 Kwa Mungu kujifunua mwenyewe kwa Musa —“NIKO AMBAYE NIKO” (Kut 3:14)—Mungu kimsingi alikuwa anamwambia Musa kwamba, “Mimi ni wa kipekee, na kuhusu Mimi ni nani, hueleweka

9 Wakati Mungu anafanya Agano na Ibrahimu, hata alimwambia kuwa uzao wa Ibrahimu utatumikishwa na kukandamizwa katika nchi ya kigeni kwa miaka 400, bali utatoka ukiwa na mali nyingi (Mwa 15:13-14).

16

Page 18:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

kutegemeana na nini nataka kukifanya” (ona, Kut 3:13-22).10 Sifa za Mungu na Tabia yake husimuliwa kwa dhati zaidi katika Kut 34:6-7. Musa mwenyewe anatawala katika AK, karibu 1/3 yake katika Kutoka. Licha ya mazungumzo ya karibu, ya binafsi, na ya kimuujiza aliyokuwa nayo Musa na Mungu kwa kipindi cha miaka 40, ilikuwa ni ukosefu wa Musa kutowakilisha tabia ya Mungu kikamilifu (wakati Musa alipopiga mwamba pale Meriba, badala ya kuuambia mwamba), ndiko kulikomzuia Musa asiwaingize kabisa Israeli katika nchi ya ahadi (Hes 20:8-13).

2. Kutoka kulikuwa ni tukio la kimaamuzi kwa Israeli ya AK. a. Kutoka kulikuwa ni tukio la kihistoria, la kimwili ambalo liliwakilisha ukweli wa kiroho utendao kazi kwa watu wote wa Mungu katika historia yote. “Kila mahali katika Agano la Kale, kumiliki nchi kunawakilishwa kama kivuli cha uhalisi wa kuishi kama watu wa Mungu katika ufalme wake. Lakini hakuelezwi mkondo ulio wazi kabisa wa njia ya lazima ambayo kwayo kila mtoto wa Mungu anauingilia ufalme. Kwa sababu hii, uzoefu wa kipekee na usiokosewa wa ukombozi kutoka nguvu nje ya ulimwengu huu ilitakiwa.” (Goldsworthy 1991: 130-31) Kutoka pia ni hatua ya mwanzo ya lazima kukamilisha ahadi ya utaifa uliomo katika Agano la Ibrahimu.b. Kutoka kulikuwa ni msingi wa Mungu kujifunua mwenyewe kwa Israeli. Mungu anasisitiza kutoka kabla na baada ya amri 10 (Kut 19:4-6; 20:2; Kumb 5:6, 15). Kwa umuhimu mkubwa, katika amri 10, neno la kwanza Mungu alisemalo kwa Israeli ni kuhusu neema yake katika kuwakomboa kutoka kifungoni. Ni baada tu ya hapo inakuja Sheria. Kutoka kulikuwa msingi kwa sikukuu ya Pasaka (Kut 12:1-27). Kulikuwa mara nyingi kukirejewa katika Zaburi (ona Zab 66; 77; 80; 81; 105; 106; 114; 135; 136). Kulitumiwa na manabii kuwaitia Waisraeli kurudi katika uaminifu wa kimaagano na Mungu, au kama onyo, au kutoka kwa Mungu (ona Isa 11:16; Yer 2:6; 7:22, 25; 11:4, 7; 16:14; 23:7; 32:21; 34:13; Hos 2:15; 11:1; 12:9, 13; 13:4; Amos 2:10; 3:1; 9:7; Mika 6:4; 7:15).

3. Agano la Mungu na Musa (“Agano la Musa [la Kale])” ( Kut 19-24; ona 2 Wakor 3:14; Waeb 8 ), na Sheria ya Musa ( Kut 20-23; Walawi 11-15; 18-20; 25:23-55; 27; Hes 5; 27:1-14; 36; Kumb 5; 12-13 ; 20-22; 24-25 ), mifumo ya dhabihu, hema ya kukutania, Sabato, sikukuu, ukuhani, sikukuu za kidini ambazo zilikuwa sehemu za ndani za Agano ( Kut 23; 25-31; 35-40; Walawi 1-9; 16-17; 21-25:22; Hes 3-4; 6-10; 15; 18-19; 28-30; 34-35; Kumb 14-19; 23; 26 ), zilielezea taifa la Israeli hadi Kristo alipokuja na kuzikamilisha.11 Kwa njia ya Agano la Musa, Mungu aliitenga Israeli kando na mataifa mengine. Agano la Musa lililipita Agano la Ibrahimu kwa kuhakikishia uhifadhi wa Israeli, taifa lililo kizazi cha Ibrahimu, katika nchi. Pia lilirekebisha jinsi taifa la kimwili la Israeli lilivyotakiwa kuishi ndani ya Agano la Ibrahimu katika nchi. (ona Walawi 26:42). Kwa sababu lilifanya kazi ile, Agano la Musa lilikuwa tofauti ki-umuhimu na lile Agano la Ibrahimu na maagano ya baadaye katika Biblia kwa vile lilisisitiza wajibu wa mwanadamu kwa Agano (Israeli) katika namna ambazo maagano mengine hayafanyi hivyo. “Tabia ya pande mbili inaakisiwa katika muundo wa masharti yake (m.y; ‘Kama mtatii . . . ndipo . . .’ TNIV; pia, ESV) ya Kutoka 19:5-6” (Williamson 2007: 96). Ndipo, baraka na laana za Mungu zilifungamanishwa kiuhalisia moja kwa moja kupitia kutii au kutokutii kwa Israeli zile Sheria za Musa (ona Walawi 26; Kumb 4; 6-9; 11; 27-29). Kupitia njia zile za kiuhalisia, Mungu alikuwa anakusudia kuwafundisha Israeli kanuni ya kiroho kuwa, “Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wenu, ni mtakatifu” (Walawi 19:2; “takatifu” limetajwa mara 152 katika Walawi). Zaidi ya hapo, Agano pamoja na taasisi zilizoundwa kama sehemu zake, liliunda kanuni ambazo watu wadhambi waliweza kumkaribia Mungu kwa njia ya mpatanishi peke yake. Musa alifanyika kama mpatanishi kati ya Mungu na Israeli kule nyikani. Pale Sinai, ukuhani ulianzishwa. Mfumo wake na muundo wa hema ya kukutania pia kimwelekeo ulionyesha mpaka kati ya watu wadhambi na Mungu aliye mtakatifu, ambao wangeweza tu kupatanishwa kupitia dhabihu na ofisi ya mpatanishi na ukuhani.

C. Israeli ndani ya hiyo nchi (Yoshua-1 Samueli 7).“Kitabu cha Yoshua kinatueleza jinsi Mungu anavyotimiza ahadi zake kwa Israeli ya kuwapa ile nchi.

10 La kuvutia, ibada ya Mungu mbinguni hulenga Mungu ni nani (utukufu wake; alivyo wa ajabu), na nini Mungu amefanya, anachofanya, na atakachofanya (uumbaji; wokovu; utawala wake; hukumu yake ijayo)—ona Isa 6:1-8; Ufu 4-5; 7:9-17; 11:15-19; 15; 19:1-6. Tabia ya Mungu na matendo yake pia ni kitovu cha ibada katika Zaburi kuu za kuabudu (ona Zab 8; 19; 24; 29; 33; 46-48; 63; 65-68; 76; 84; 87; 92; 93; 96-100; 103; 104; 111; 113; 115; 117; 135; 145-150).11 Musa alipokuwa anapokea zile Amri 10 kutoka kwa Mungu kwa mara ya kwanza, watu walianguka katika dhambi kuhusiana na vitu vile vile vilivyokatazwa na zile Amri 10 zenyewe (Kut 32:1-6). Toba ya Musa kwa Mungu kuwasamehe watu ulisimamia Agano la Ibrahimu (Kut 32:11-14). Matokeo yake, Mungu hakuwaangamiza watu, na akampa Musa Amri nyingine 10 (Kut 34).

17

Page 19:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Bwana anawaongoza Israeli kuiteka nchi na kuwahukumu mataifa maovu yakaayo ndani yake, na kisha anaigawanya nchi kwa zile kabila kumi na mbili. Kitabu kinaishia kwa Yoshua kuwasihi Israeli kudumu waaminifu kama watu wa Mungu. Waamuzi kinaanzia na kutokutii kwa Israeli: wanakataa kupambana na kutokuamini na kuachana na ibada za sanamu katika nchi (Waamuzi 1). Mungu aja na hukumu ya ki-agano na kuwaambia Israeli kuwa sasa itawabidi waishi kati ya Wakanaani (Waamuzi 2). Waamuzi husimulia kisa cha kusikitisha cha jinsi Israeli inavyogeuka kutoka kwa Mungu na kuendelea kugeukia ibada za Wakanaani na mitindo ya kuishi kwao. Mungu mwishowe anawaachia Wakanaani na watu wengine wanaowazunguka kuwatawala na kuwakandamiza mpaka Israeli walipomlilia ili kuwasaidia. Na akawajibu kwa rehema, akiwainulia viongozi wa kijeshi, waitwao waamuzi, ili kuwaokoa. Katika kila mduara wa uasi, hata hivyo, hali inakuwa mbaya zaidi. Kitabu kinaishia na visa viwili vinavyoonyesha uasi wa Israeli na Israeli kulia daima kutaka kuwa na mfalme ili awaokoe na uharibifu huu. (Waamuzi 21:25).” (Bartholomew and Goheen n.d.: 3)

D. Israeli kama ufalme ulioungana (1 Samweli 8-1 Wafalme 11; 1 Nyakati 1-2 Nyakati 9; Zaburi-Wimbo ulio bora).

“Samweli ndiye mwamuzi mkuu wa mwisho, na pia ni kuhani na nabii. Vitabu vya Samweli, vilivyotajwa jina lake, huzungumzia badiliko kubwa ndani ya taifa la Israeli. Israeli wanamtaka Mungu awape mfalme ili wawe kama mataifa mengine (1 Sam. 8:5, 19-20). Kwa hiyo Mungu anamtumia Samueli kumteua Sauli [miaka 1050-1010 KK], na kisha Daudi [1010-970 KK], kama wafalme wa kwanza juu ya watu wake. Sauli ni mfalme aliyeshindwa, lakini Daudi anamtumikia Mungu kama mfalme mwaminifu, akiyashinda mataifa ya kipagani yaliyowazunguka, na kuiimarisha sheria ya Mungu, na kuhamisha makao ya Mungu kuja Yerusalemu. Hapa, kwenye kiini cha taifa, uwepo wa Mungu ni ukumbusho wa kudumu kwa Israeli kwamba Mungu ndiye mfalme wao wa kweli. Sulemani [970-930 KK], mwana wa Daudi na aliyetawala baada yake, analijenga hekalu kama mahali pa kudumu zaidi pa Mungu kukaa na kusikia sifa na sala za watu wake. Licha ya kupewa hekima kuu sana kutoka kwa Mungu, kule kuoa kwa Sulemani wanawake wa kigeni, na tamaa za miradi iliyokuwa inamsukuma sana inamfanya ajulikane kama mtesaji.” (Bartholomew and Goheen n.d.: 3) Daudi ndiye kiungo cha kati cha ufalme ulioungana. Ufalme wake huonyesha sura ya ufalme wa ki-Masiha yenyewe.

1. Kulikuwa na wafalme watarajiwa ( Mwa 49:8-10; Kumb17:14-20 ) na wafalme kinyume ( Waamuzi 8:22-23; 1 Sam 8:1-18 ) hujitokeza katika historia ya Israeli kabla hawajampata mfalwe wao wa kwanza. Hata hivyo, watu hao walimtaka mfalme ili “sisi nasi tufanane na mataifa mengine yote” (1 Sam 8:20). “Hili kiuhakika ni kukataa muundo wa Agano na, kwa hiyo kuukataa utawala wa Mungu (1 Sam 8:4-8)” (Goldsworthy 1991: 165). Huenda, kwa vile siku zote alikusudia kuwatawala kupitia mfalme, Mungu aliwapa haja waliyoitaka.2. Mungu afanya agano na Daudi (“Agano la Daudi,” 2 Sam 7:8-17; 1 Nyak 17:3-15; ona 2 Sam 23:5; 2 Nyak 6:16; Zab 89:1-4, 28-29 ). Agano la Daudi linafanyika njia maalum ya Agano la Ibrahimu kuja kutimilizwa. Hata masharti yake yanagusia ahadi alizozifanya Mungu kwa Ibrahimu. Katika Agano hili (2 Sam 7) Mungu amwahidi Daudi: mst. 9—jina kuu (k.m. Mwa 12:2); mst. 10—mahali (k.m. Mwa 12:7; 13:14-17; 15:7, 18; 17:8); mst.11—utulivu kutoka kwa adui (k.m. Mwa 22:17); v. 12— “uzao” (k.m. Mwa 22:18); mist. 12-16—ufalme usio na mwisho na kiti cha enzi (k.m. Mwa 12:3; 13:15; 17:5-7). “Mwendelezo wa agano hili kwa lile agano la Ibrahimu kwaweza kuonekana katika mahitimisho yao. ‘Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu’ hujumuisha kusudio la Mungu katika agano na Ibrahimu na baada yake, na Israeli (Mwa 17:7-8; Walawi 26:12; Yer 7:23; 11:4; 30:22). Sasa ahadi kumhusu mwana wa Daudi, yeye atakayewakilisha wengi, yatolewa kama, ‘nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu’ (2 Sam 7:14). Kwa hiyo, mwana wa Daudi pia ni mwana wa Mungu, na nyumba yake, kiti chake cha enzi na ufalme vitadumu milele (2 Sam 7:16).” (Goldsworthy 1991: 167) Agano hili lilipata utimizwaji wake wa kwanza kwa mwana wa Daudi Sulemani, aliyelijenga hekalu katika Yerusalemu. Hata hivyo, licha ya “kutangulizwa kwa kivuli cha ‘baraka za mataifa’ wakati wa enzi za Daudi - Sulemani, ahadi hii ilisubiri utimizwaji wake wa mwisho. Historia ya kifalme ya Israeli inathibitisha kwa nini hilo liko hivyo. Licha ya wafalme wachache waliokuwa wanarejeza yaliyoharibika, hakuna hata moja wa uzao wa kifalme wa Daudi—kumchanganya na Daudi mwenyewe—aliyetekeleza kikamilifu mwongozo wa muhimu wa mahusiano ya Ki-ungu: mwenendo unaokubalika [ona 1 Waf 2:4; 6:12-13; 8:25; 9:4-9].” (Williamson 2007: 145) Mungu alikuwa ameahidi kubariki mataifa kupitia “uzao” wa Ibrahimu (Mwa 12:3; 22:18). Agano la Daudi huonyesha “ukoo wa kifalme ambamo ule “uzao” wa ushindi unaotarajiwa hatimaye utatokea. . . [lakini kwa sababu ya dhambi katika mlolongo wa Daudi] hatimaye ukategemea ufalme wa ki-Daudi ambaye atakuwa mzao wa Ibrahimu kwa kiwango kitimilifu kuliko vyote, na siyo tu kibayolojia (k.m. Zab. 72).” (Ibid.) Kwa hiyo, Agano la ki-Daudi lilionyesha mbele kumwelekea Yesu Kristo.

18

Page 20:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

3. Fasihi za kihekima ( Ayubu, Zaburi, Mithali, Mhubiri, Wimbo ulio bora ). Ayubu kwa undani kabisa hutumia dhana ya kiulimwengu ya maumivu na mateso yasiyo haki kama ngazi ya kushughulika na ukuu wa Mungu juu ya mateso ya wanadamu na imani zao kwa Mungu mwenyewe wakiwa katika mtwango wa mateso yenyewe. “Tenzi za sifa [za Daudi], toba, na maelekezo (Zaburi, si zote zilitolewa na Daudi) ni za wakati wake, hata hivyo ni za nyakati zote kwa maelekezi ya kiroho na hivyo ni kitovu cha theolojia ya Ki-Biblia. Vivyo hivyo, hekima (iliyotolewa waziwazi na Mungu: 1 Waf 3:12) ya mwanaye Sulemani husimama pia kwa uzito unaolingana kama kitovu cha mhimili wa kazi za theolojia ya Ki-Biblia, ziitwazo fasihi za Kihekima.” (Yarbrough 1996: 64) Fasihi za kihekima huhusika na kiu na njaa ya maarifa, ufahamu, na uhusiano na Mungu na watu wengineo hapa duniani ambayo yote kwa pamoja yamevurugikwa kwa dhambi.

E. Israeli kama ufalme uliogawanyika (1 Wafalme 12-2 Wafalme17; 2 Nyakati 10-31; Isaya na Mika [vilitabiri kwa Israeli na Yuda]; Yoeli [alitabiri kwa Yuda]; Hosea na Amosi [walitabiri kwa Israeli]; Obadia [Alitabiri kwa Edomu]; Yona [alitabiri kwa Ninawi]).

“Wakati wa utawala wa mwana [wa Sulemani] Rehoboamu, roho ile iliyokuwa inasonga [iliyoanzia kwaSulemani] ikaletesha kugawanyika kwa taifa. Mengi ya makabila yakagawanyikia Kaskazini (Israeli), na kuacha nyuma makabila machache ya Kusini [m.y., Yuda na Benjamini, kujumlisha na baadhi ya watu kutokea makabila ya Kaskazini] (Yuda) [930 KK].

Tangu mwaka huo na kuendelea, sehemu hizo mbili zikawa na wafalme wao binafsi. Vitabu vya 1& 2 Wafalme na 1 & 2 Nyakati huelezea simulizi zao. Simulizi hizo ni kuporomoka kwa uelekeo wa uasi ulioongozwa na wafalme waliokuwa si waaminifu. Badala ya kuwa kielelezo kwa mataifa, watu wa Mungu wanausukumia mbali uvumilivu wa Mungu hadi kufikia kufukuzwa mbali na nchi ile. Mungu akatafuta njia ya kusimamisha njia zao mbaya kwa kuwainulia manabii kuwaonya warudi tena kwenye toba. Eliya na Elisha ndio manabii wajitokezao sana katika 1 & 2 Wafalme. Kupitia manabii hawa, Mungu anaahidi kama Israeli watarejea kwake, Mungu atawapa neema na ataendelea kufanya kati kati yao. Pia anaonya kwamba ikiwa Israeli wataendelea kuasi, atawaletea hukumu na hatimaye kuwapeleka uhamishoni. Kadri hali ya Israeli ianvyoendelea kuwa mbovu zaidi ya kutoponyeka, manabii wanaahidi kuwa Mungu hajashindwa. Kusema ukweli, Anaahidi kwamba atawaletea mfalme baadaye ambaye atauleta ufalme wa amani na haki. Mfalme huyo aliyeahidiwa atawezesha kusudio la Mungu la uumbaji.

Maneno ya manabii hao yaangukia katika masikio yasiyosikia. Kwa hiyo, kwanza, raia wa ufalme wa Kaskazini (722 KK na raia wa ufalme wa Kusini (586 KK.) watekwa uhamishoni na falme zilizokuwa zina nguvu zilizotawala enzi hizo [Israeli kwa Waashuri na Yuda kwa Babeli].” (Bartholomew and Goheen n.d.: 3-4)

F. Kuweko, kushuka, na kuanguka, kwa ufalme wa Kusini (2 Wafalme 18-25; 2 Nyak 32-36:21; Isaya-Danieli; Nahumu-Zefania).

1. Makabila mawili ya Kusini (Yuda) waenda utumwani Babeli. Yuda walifuata nyayo mbaya za wenzao Israeli wa Kaskazini. Kwa hiyo, ikahusuriwa, Yerusalemu ukaharibiwa, na taifa likapelekwa uhamishoni Babeli. “Hali ya uhamisho inawafadhaisha sana Israeli. Nini kilitokea kwa ahadi za Mungu na makusudio yake? Je alizitupilia mbali kabisa? Wakati wa uhamisho huo, Mungu aliendelea kusema nao kupitia manabii kama vile Ezekieli, akielezea ubaya huo umewajia na kuwahakikishia kwamba watarudi tena kwao.” (Bartholomew and Goheen n.d.: 4)2. Kipindi chote cha historia ya Israeli, hasa wakati wa kipindi cha ufalme uliogawanyikana, na kisha kuendelea hadi wakati wa matengenezo ya ufalme wa Kusini, manabii walifanya sehemu muhimu ya kuwaitia watu warejee kwenye uaminifu kwa Mungu.

a. Manabii wa Mungu walitumia neno la Mungu wakati huo mgumu wa mahusiano ya kiagano kati ya Mungu na watu wake. Kazi kuu ya manabii wa AK haikuwa kutabiri mambo ya baadaye. Badala yake, manabii walinena nyakati hizo ngumu, na wote walikuwa na ujumbe na huduma iliyokuwa ina pande mbili kimsingi: (1) Wanawaonya watu wa Mungu juu ya maafa ya kutofuata njia za Mungu kwa tahadhari za matukio ya hukumu na (2) wanawaitia watu warudi kwenye uaminifu kwa Mungu kwa mausia ya matukio ya matumaini na wokovu. Manabii wote wa AK walihusika na kubadili mienendo ya tabia za watu. Ujumbe wao kiujumla ulikuwa, “Kama hamtafanya hivi, hukumu itawajia; kama mtamfuata Bwana, baraka zitawajia.” Ujumbe wao wa hukumu na wokovu ndio ulio na nguvu kwa vizazi vingi.b. Kihistoria, mtu anaweza kuona mabadiliko ya msisitizo wa kinabii baada ya utumwa wa Israeli kule Babeli. Kabla ya uhamisho, manabii walielekea kusisitiza ukaidi wa Israeli. Baada ya utumwa msisitizo ukahamia kwenye wajibu wa watu wa Mungu kujiandaa kwa kuujenga kikamilifu ufalme wa Mungu.

19

Page 21:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

3. Kabla ya uhamisho, manabii wakanena kuhusiana na dhana mbali mbali, zikiwamo: a. Safari mpya. Watu wa Mungu wataokolewa kutoka kwa wachungaji wasiofaa (Ezek 34). Wataokolewa kutoka uhamishoni (Isaya 40:1-5; 43:1-7, 15-21; 48:20-21; 49:24-26; 51:9-11; Yer 23:7-8). b. Watu wapya. Wakati mwingine hili huchukuliwa kama mabaki yenye uaminifu kwa Mungu (Isaya 10:20-23; 11:11-12; 14:1-4; 40:1-2; 46:3-4; 51:11; 61:4-7; Yer 23:1-8; 29:10-14; 30:10-11; 31:7-9; Ezek 34:1-6; 36:22-24; 37:15-22; Mik 2:12). Watu wa Mungu walioshindwa, walio uhamishoni, na waliogawanyikana watafanywa upya, watahuishwa, na kuunganishwa upya (Ezek 37). Mungu atayabariki mataifa (Isaya 2:2-4; 19:18-25; 49:5-6; 56:1-8; Mik 4:1-4; Zef 3:9; Zek 8:20-23). Isaya anaonekana kuwaelezea upya “watu wa Mungu” (tofauti na mipaka yao katika Agano la Musa; ona, Kumb 23:1-8): “Isaya anatangaza kwamba katika siku za mwisho, wakati Mungu atakapoidhihirisha haki, wale wazao wa kibayolojia au utofauti wa kimwili [m.y., ukoo] hautahusika tena kupangilia ushirika wake. Watu wageni “nao watajiunga kwa Bwana, kumtumikia kwake, kulipenda Jina la Bwana, na kwa watumishi wake” (56:7). . . . Kigezo cha kuwa hitimisho la matengenezo ya mwishoni ya YHWH na kuujenga ufalme wake si uzao wa kikabila, bali ni roho zilizotubu na moyo uliotubu [57:15] na mwitikio wa haki kwa mapenzi ya Mungu kwa watu wale ambao ni sehemu ya mabaki ya waliorehemiwa na Mungu. (58:7-14)—wale “wamkimbiliao” YHWH “ wataimiliki nchi na urithi wa mlima wangu mtakatifu” [57:13], wote “walio mbali na walio karibu” [57:19]. Hii ina maana kwamba katika unabii wa Isaya, vigezo kwa kuingia katika kundi teule la watu wa Mungu vimebadilika kwa namna kubwa kabisa: wakati YHWH anarejesha nchi, Wayahudi wote waliotubu na watu wa mataifa waliotubu watajumuishwa kuunda watu wa agano.” (Schnabel 2002: 41)c. Chombo kipya cha kutimiliza makusudi ya Mungu. Chombo kipya cha Mungu ni mtumishi wake aliye mpakwa mafuta (Isaya 42:1-9; 61:1-3). Chombo cha Mungu chaonekana kama mtumishi atesekaye (Isaya 42:1-9; 49:1-6; 50:4-9; 52:13-53:12). Aonekana kama “mwana wa mwanadamu” asiye wa kawaida (Dan 7:13-14). Ni Daudi mpya (Isa 9:2-7; 11:1-5; 16:5; Yer 23:1-6; Ezek 34:23-24; 37:24-25; Amosi 9:11). Eliya atakuja (Mal 4:5-6). d. Nchi mpya. Kutakuwako Sayuni mpya (Isaya 2; 11:6-9; 35:1-10; 54; 61:3-62:12; Ezek 34:11-16, 25-31; 36:35-38). Hata kutakuwako mbingu mpya na nchi mpya (Isaya 42:14-17; 65-66). e. “Agano Jipya” (Yer 31:31-34; 32:38-40; 50:4-5; Ezek 11:16-20; 36:24-32; 37:15-28).

(1) Ahadi ya “Agano Jipya” inaelezwa wazi katika AK katika Y er 31:31 , tu bali imefichika katika sehemu nyingine zaYeremia na Ezekieli. Iko dhahiri kutokana na Yer 31:32 kwamba Agano Jipya ni bora zaidi ya lile la Agano la Kale, la Musa. “Sehemu nyingi zinaunganisha uendelezo wa yale maagano ya Ki-Ungu: msisitizo wake kuhusu Torati [“sheria” au maagizo (Yer. 31:33; Ezek. 36:27; Isa. 42:1-4; 51:4-8); mkazo wake kwa ‘mzao ’wa Ibahimu (Yer. 31:36; Ezek. 36:37; Isa. 63:16), hasa kwa ‘uzao’ wake mteule (Yer. 33:15-26; Ezek. 37:24-25; Isa. 55:3); matumizi ya mpangilio wake, ‘Nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu’ (Yer. 31:33; Ezek. 37:23, 27; cf. Isa. 54:5-10).” (Williamson 2007: 180) (2) Agano Jipya halitakuwa kama Agano la Kale, la Musa ambalo Israeli walilivunja. Agano Jipya “linaingia kwa ndani” na “kubinafsisha” uhusiano kati ya Mungu na watu wake kwa namna ambazo hakuna maagano yoyote ya awali yaliyowahi kufikia. Huo “upya” wa Agano Jipya “kamwe usije ukapuuzwa; likachanganya viwango vya kifalme vinavyotoa mwangwi unaoonyesha kukatika kwa mwendelezo wa ukale (k.m. Yer. 31:32): kuondolewa kabisa kwa dhambi (Yer. 31:34; Ezek. 36: 29, 33); mabadiliko ya ndani ya moyo (Yer. 31:33; Ezek. 36:26); uhusiano wa ndani na Mungu (Yer. 31:34a; Ezek. 36:27I)” (Williamson 2007: 180). Hakuna dalili zozote za “u-masharti” uliokuwa umenenwa katika Agano la Musa. Bila shaka , dhambi haina uwezo tena wa kuathiri uhusiano wa ki-Ungu wa mwanadamu kwa sababu, chini ya Agano Jipya, Mungu afanya tamko kuu, “Nitausamehe uovu wao wala dhambi yao sitaikumbuka tena” (Yer 31:34). Kwa hiyo, “tofauti na Agano la Kale, hakutakuwa na uwezekano wa kuvunjika kwa Agano Jipya” (Ibid.: 157). Moyo huu mpya, hali ya kukaa ndani kwa sheria ya Mungu, uhusiano kibinafsi na Mungu, na msamaha kamili wa dhambi, utaletesha upeo mpya wa “ufahamu (m.y; utii wa imani) kwaYahweh, [ambao ndio] alama itambulishayo “jamii hii mpya ya watu wa Agano Jipya” (Ibid.). “Agano Jipya

20

Page 22:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

ni utimilifu wa kimajira wa maagano ambayo Mungu aliyafanya na mababu zetu, taifa la Israeli, na uzao wa kifalme wa Daudi. Ahadi za maagano yale ya awali hutimilizwa kikamilifu katika hili Agano Jipya, na ndani yake, ahadi hizi zinakuwa “za milele” kwa jinsi ya ukweli kuliko yote.” (Ibid.: 181)

f. Utawala mpya wa Mungu. Kutakuwa na uwepo mpya wa Mungu na hekalu jipya (Isa 12:6; Ezek 37:27-28; 40-48; Yoeli 3:16-17; Zeph 3:14-17). Mungu atamimina Roho wake kwa watu wake (Yoeli 2:28-32; Isa 32:9-20; Ezek 36:25-28). Wakati mwingine, Mungu mwenyewe anaelezewa kuwa anairudia tena Sayuni (Isa 26:21; 42:2-3, 9; 52:7-9; 66:15; Ezek 43:2-7; Zek 2:10; 8:3; 14:3-5; Mal 3:1).

4. Dhana hizi za kinabii hazikufanyika katika mfumo wa kushikamana kiujumuifu. Hata hivyo, zilitoa tumaini na matarajio. Mfanyizo wenyewe unapatikana katika Kristo, ambaye Paulo anasema, “Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin” (2 Wakor 1:20).

G. Matengenezo ya ufalme wa Kusini (2 Nyak 36:22-Esta; Hagai-Malaki).“Baada ya nusu muhula wa miaka ya utumwa, njia inafunguka kwa Israeli kurudi Yerusalemu [Mbiu ya

Koreshi, 538 KK—2 Nyak 36:22-23; Ezra 1:1-4]. Baadhi wanarudi; bali walio wengi wabaki. Muda upitavyo, chini ya uongozi wa Zerubabeli, Ezra, na Nehemia, Yerusalemu na hekalu, ulioteketezwa na walioivamia Yuda, wajengwa upya [536-516 KK]. Lakini Israeli, Yerusalemu, na hekalu ni vivuli tu vyao wenyewe.

Agano la Kale laishia tu kwa Israeli kuikalia upya ile nchi, lakini ni kukaa sehemu chache na huku wakikabiliwa na vitisho vikali. Wakaishi chini ya kivuli cha himaya zenye nguvu za nyakati zile. Wakiwa na ahadi za manabii wao zikiwa zinavuma masikioni mwao, wangojea siku ambayo Mungu atawakomboa na kuimaliza kazi yake hiyo ya ukombozi. Pazia linaposhushwa kwa hatua ya tatu, Israeli ilishindwa kutekeleza jukumu alilowapa Mungu pale Sinai, lakini kuna tumaini bado kwa sababu Mungu ametoa ahadi,” (Bartholomew and Goheen n.d.: 4)

1. Muda baada ya kurudi kutoka uhamishoni kule Babeli, uongozi unakuwa umo mikononi mwa uzao wa Daudi, mtu aitwaye Zerubabeli ( Ezra 2-5; Hagai 1-2; Math 1:13; Luka 3:27 ). Hata hivyo, simulizi za Ezra na Nehemia zaonyesha wazi kwamba taifa lililorejeshwa silo ufalme wa Mungu. Manabii wote baada ya uhamisho wanaonyesha kwamba kuna utukufu unaokuja mbeleni (Hag 2:6-9; Zek 8:20-23; 14:1-21; Mal 4:1-6). Katika hali ya kuvutia sana, AK linaishia kama “kitabu kisicho na mwisho.” Biblia ya Kiebrania huishia na 2 Nyak, ambayo huishia na tumaini la hekalu jipya na kurejea kutoka uhamishoni; mpangilio wa ki-Kristo wa AK unaishia na kitabu cha Malaki, kinachoishia na ahadi ya Mungu kumtuma Eliya na kuja kwa siku ya Bwana 2. Kati ya mwisho wa AK na kuanza kwa AJ pana nafasi ya miaka mia nne. “Kipindi hiki huitwa “Kipindi cha kati ya maagano”. Katika kipindi hiki, Israeli wanaendelea kuamini kuwa ndio watu waliochaguliwa na Mungu na ya kwamba Mungu atatenda katika siku za karibuni kuuleta ufalme wake. Chini ya ukandamizwaji wa Waperizi, Wayunani, na hasa Waashuri na Warumi, cheche ya matumaini iliyowaka katika mioyo ya wayahudi inapamba moto kuwa kali zaidi. Jinsi ufalme wa Mungu utakavyokuja, nani atauleta, na jinsi gani ya kuishi hadi utakapokuja—katika mambo haya kuna tofauti kubwa kati ya Mafarisayo, Masadukayo, Wazealoti, na Waesene. Bali Waisraeli wote wanakubali: kisa chao kinasubiria mwisho. Ufalme utakuja mara. Hivyo wanasubiri katika matumaini.” (Bartholomew and Goheen n.d.: 4-5)

H. Kutimizwa kwa mpango wa Mungu wa ukombozi ni Yesu Kristo (Mathayo-Ufunuo 20).1. Injili: AK lilivyotaraji, na kutimilizwa katika, Yesu. “Vizazi vya sehemu zote Mathayo na Luka hushudia undani wa uhusiano wa kuja kwa Yesu na kusudio la Mungu na utendaji wake katika matukio ya nyuma. Luka 1-2 huelezea matumaini ya Agano la Kale ya watu kama Zakaria, Elizabeti, Mariamu, Simeoni, na Ana kwani wote hao wanena kuhusu uhakika wa uaminifu wa Mungu kwa ahadi zake za Agano la Kale.

Katika Yesu wa Nazareti ukombozi wa Mungu na utimilifu unawadia. . . . Kwa zaidi ya miaka mitatu Yesu atembea kati ya nchi ya Galilaya, Yudea, na Samaria, na wilaya zinazokaribia. Anaweka mkazo maalum kwa kikundi cha watu kumi na mbili watakaoiendeleza kazi yake mara yeye akiondoka, lakini pia anatoa wito na maelekezo kwa watu walio (sehemu kubwa lakini sio Wayahudi pekee). Ujumbe wake unalenga Waisraeli asilia, lakini hutenda kazi kwa watu wote, hata wakati wa maisha yake. Mafundisho yake, yenye uvuvio wenye uzito, hauwezi kivyovyote kutenganishwa na uelewa wa uwakilisho wa uhusiano usio wa kawaida na Mungu. Alionekana akieleza kwamba yeye kinamna fulani yu sawa na Mungu. Mafundisho yake lazima yatazamwe katika nuru kwamba yeye alikuja kuleta ukombozi, siyo kwa ujuzi wa maarifa ayatoayo, bali kwa kumtumainia kibinafsi kwa kina cha dhabihu,

21

Page 23:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

na kifo kiokoacho akipitiacho (Marko 8:31; 10:32-34, 45). Injili nne zinaendana katika kuwakilisha kilele cha kuja kwa Yesu, si kwa miujiza yake, hekima, wala maadili yake, ingawaje ni makuu sana, bali ni katika kifo chake na ushindi wa ufufuo wake.

Huduma ya Yesu, basi, ndicho kilele cha utimilifu wa mpango wa Mungu aliouanzisha katika nyakati za Agano la kale. Wito wake kutubu na kutoa uzima mpya hutimiliza ofisi ya kinabii; kifo chake cha kidhabihu na wajibu wake wa usuluhishi unatimiliza jukumu la kuhani mkuu wa milele; jukumu alilo nalo sasa (Yohana 18:37) katika mkondo wa Daudi, humfanya yeye kuwa Mfalme wa wafalme, mwakilishi katika mwili wa Mungu juu ya vyote, wakati wote, na historia yote. Ukombozi wa kimasihi uliotabiriwa tangu zamani katika Edeni (Mwa 3:15) unakuja kujitokeza katika masihi Yesu.” (Yarbrough 1996: 64-65)2. Matendo ya Mitume na Nyaraka: Kuenea kwa kanisa. “Kitabu cha Matendo kinaanzia kwa mfumuko wa ghafla na wa nguvu wa ujio wa Roho Mtakatifu, ambaye kuja kwake kuliahidiwa na manabii na yeye mwenyewe (Mdo 2). Anakuja, kwa kusudi la kuleta uzima mpya wa ufalme wa Mungu kwa wote wageukao kutoka kwenye dhambi, waamninio kuwa upya umekuja katika Yesu, na kubatizwa kuwa jamii ya ufalme unaoibukia. Jamii hii mpya inajengwa na kujidhatiti kufanya yale ambayo Mungu anaahidi kuyatumia kurejeshea upya ndani mwao uzima wa ufufuo: Neno la Mungu, maombi, ushirika moja kwa mwingine, na Meza ya Bwana (Mdo 2:42). Wafanyapo hivyo, uzima wa ufalme wa Mungu hujionyesha zaidi na zaidi katika Yerusalemu, na kanisa huanza kukua. Kanisa lasambaa kutoka Yerusalemu hadi Yudea na hata Samaria. Kisha kituo kipya chaanzishwa kule Antiokia (Mdo 11:19-28). . . . Paulo anahusika kwa kiwango kikubwa zaidi katika kueneza habari njema katika himaya nzima ya Rumi. Hapo kwanza alikuwa adui mbaya wa kanisa, lakini kukutana kwake na Yesu kiajabu kukambadilisha kuwa mmishinari aliyeongoza kuelekea ulimwengu wa wasio Wayahudi. Katika safari tatu tofauti alisafiri katika himaya yote ya Rumi akianzisha makanisa. Akaandika nyaraka kumi na tatu, kwa makanisa hayo mapya kuyatia moyo na kuwaelekeza kuhusu jinsi ya kuwa wafuasi wa Yesu aliyefufuka. Nyaraka hizi, pamoja na nyingine, hatimaye zinakusanywa katika Agano Jipya. Kila moja ya nyaraka hizi huendelea leo, katika karne ya Ishirini na moja, kutoa maelekezo muhimu kuhusu nini cha kuamini kuhusiana na habari njema, na jinsi ya kuishi kwa uaminifu chini ya utawala wa Mungu katika maisha yetu ya kila siku.” (Bartholomew and Goheen n.d.: 6)

I. Ufunuo wa Yesu kuhusu hali halisi ya Masihi, Ufalme wa Mungu, na kanisa.Ingawaje Yesu ndiye ufunuo wa mwisho na mkamilifu wa Mungu, ambaye anatimiliza unabii wa AK na

matarajio yake, “anatimiliza hayo kwa njia ya kushangaza kiasi kwamba hakuna yeyote ambaye angeweza kutabiri kikamilifu jinsi ambavyo angeuleta ufalme huo” (Goldsworthy 1991: 203). Zile Injili, Matendo ya Mitume, na Nyaraka zadhihirisha njia isiyo ya kawaida ya Yesu ya hali halisi ya masihi, Ufalme wa Mungu, na kanisa.

1. Yesu Masihi. Wayahudi walio wengi walimtarajia Masihi kuwa wa uelekeo wa kisiasa zaidi ambaye angewafukuzia mbali Warumi na kuijenga Yerusalemu na hekalu kiufahari kama ndiyo makao ya dunia mpya. Yesu hakukidhi matarajio yao wala ufafanuzi wa viongozi wa Kiyahudi. Aliunda miundo ya mikondo mipya kutokana na AK kwa njia ambazo hazikuweko katika mifumo ya awali. Alifunua kwamba yeye ndiye Mungu katika mwili. (Yoh 1:1-14; 10:30; 14:6-11; Wafil 2:5-7; Wakol 1:16-17; 2:9; Tit 2:13; Waeb 1:8), na bado alikuwa ni mwanadamu kamili—Adamu wa mwisho, uzao wa Ibrahimu, mwana wa Daudi, nabii wa kweli (Math 21:9; Luka 14:16-24; Rum 1:3; 5:19; 1 Wakor 15:22, 45; Wagal 3:16; Wakol 1:15). Madai yake kuwa ni Mungu, na kule kuchukua jukumu la kuwa hekalu la Mungu yeye mwenyewe (ona Yoh 2:13-22; 7:37), kuliwafanya viongozi wa Kiyahudi wamchukie sana. Sababu ni kwamba, katika dini za Mashariki, “Mungu” alikuwa ni kama “nguvu ya uhai” ambayo iliingilia kila mtu na kila kitu. Katika dini za ki-Magharibi na za imani pana, kulikuwa na “miungu” mingi iliyokuwa ikijibadili kuwa umbo la mwanadamu mara kwa mara. Kwa mwanadamu katika mtazamo huo kujidai kuwa na uungu, kusingekosa kuungwa mkono kabisa. Uyahudi ulikuwa tofauti. Ulikuwa na mtazamo makini wa “kiuvuvio” kuhusu Mungu: Mungu alikuwa ni muumba, mbali na kando na viumbe vyake. Kwa mwanadamu kudai kwamba ni Mungu katika muktadha wa Yesu kwa Uyahudi wa karne ya kwanza, kulikuwa yote mawili: hakuingii kichwani na ni kukufuru. Bila shaka, kwa zaidi ya mara moja, viongozi wa Kiyahudi hawakuyaelewa madai ya Yesu na hata kutaka kumpiga kwa mawe hadi afe kwa kukufuru. (ona Walawi 24:10-16; Math 9:2-3; 26:63-66; Marko 2:5-7; 14:61-64; Luka 22:70-71; Yoh 5:17-18; 8:58-59; 10:30-33; 19:7). 2. Hali ya kiroho ya ufalme wa Mungu. Hali halisi ya ufalme ni tofauti na matarajio ya Wayahudi na hata ya wanafunzi wa Yesu mwenyewe (mwanzoni). Walikuwa wanatarajia kufunuliwa kwa mfumo wa kidunia wa Israeli na nguvu zake (ona Mdo 1:6). Badala yake, Yesu akalikabidhi kanisa lake kama

22

Page 24:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

wakili mwenye kuonekana wa ufalme hapa duniani (Math 16:18-19). Alimwambia Pilato, “Ufalme wangu si wa dunia hii” (Yoh 18:36). Kabla yake alikuwa amewaambia Mafarisayo, “Ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza; wala hawatasema, ‘Tazama, upo huku!’ au, ‘kule!’ kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu” (Luka 17:20-21). Zaidi ya hayo, ufalme hauna mipaka ya Uyahudi wala nchi ya Palestina. Badala yake, umejumuisha kiupana sana. Unajumuisha Wayahudi na Mataifa kwa kiwango (Mdo 10-11; Waef 2:11-22), na hujumuisha dunia nzima (Math 28:18-20; Mdo 1:8; Ufu 5:9; 7:9). Mdo 1:8 ni kielelezo cha kuenezea kanisa.3. Sehemu ya kipengele cha“tayari/bado” kwa Ufalme wa Mungu. “Ambacho hakikueleweka vizuri, kinamna fulani, ama na manabii wa Agano la Kale, au na wanafunzi wa kwanza kabisa wa Agano Jipya, kilikuwa, utata wa kuwa tayari au kuwa bado kwa majira ya Ki-Masihi” (Yarbrough 1996: 65). Wakati Yesu alipoyatoa mapepo aliwaambia Mafarisayo, “Ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia” (Luka 11:20). Yesu amepewa mamlaka yote mbinguni na duniani, na hata sasa anatawala kutoka “kiti cha enzi cha Daudi” mbinguni (Math 28:18; Mdo 2:29-36; Waef 1:18-23). Bado tunaona dhambi na uovu, na sehemu kubwa ya dunia inampinga Kristo na utawala wake. Ukinzani huu unaopishana unaoelezwa kama hali ya “tayari/bado” ya ufalme wa Mungu: m.y., ingawaje ufalme wa Mungu na utawala wa Kristo umeshaanzishwa na kutambulishwa, kimsingi (hali ya “tayari” ya ufalme), bado haijadhihirika kikamilifu, bali wanasubiri utimilifu wote wa utukufu ujao (hali ya “bado” ya ufalme).12 Hili huonekana kwa njia nyingi:

a. Kila mahali katika AJ, waandishi huzungumzia kuhusu “vipindi viwili”: “zama hizi,” na “zama zijazo.” “zama hizi” zina mambo kama kuoana na mambo ambayo ni ya kitambo (k.m., Marko 10:30; Luka 20:34; Rum 12:2), uovu (Wagal 1:4; Waef 2:2), na hekima ya kidunia (1 Wakor 1:20; 2:6-8). Kwa upande mwingine, “zama zijazo” zinatawaliwa na maisha ya ufufuo na kutokufa (k.m., Marko 10:30; 1 Wakor 15:50), kutokuoa au kutokuolewa (Luka 20:35), na kutokuwepo na uovu (1 Wakor 6:9-10; Wagal 5:21; Waef 5:5) (Riddlebarger 2003: 82-83). Kuja kwa mara ya kwanza kwa Kristo kulikuja pamoja na uanzishwaji wa zama zijazo katika Kristo na kati ya wale walio wake. Matokeo yake, vipindi vile viwili vinaingiliana. Kwa vile utawala wa Kristo umeshaanza (Waeb 2:9; Waef 1:21), kwa namna fulani zama zijazo pia zimeshaanza. Kama jinsi nyakati hizi ndizo nyakati za uumbaji wa kale, na nyakati zijazo ni nyakati za uumbaji mpya, kinamna fulani uumbaji umeshaanzishwa (2 Wakor. 5:17; Wagal 6:15). Kama matokeo ya kuja kwa Yesu kwa mara ya kwanza, nyakati hizi ziko katika “siku zake za mwisho” (ona Mdo 2:17; Waeb 1:2; Yak 5:3; 1 Pet 1:20; 1 Yoh 2:18; Yuda 18). “Nyakati hizi” zitakoma na “nyakati zijazo” zitafikia kilele cha utimilifu wa utukufu wake wakati wa Kuja kwa mara ya pili kwa Kristo (ona Math 24:3; Tito 2:12-13).b. Kuingiliana kwa nyakati hizo mbili, na “kuingia ” kwa nyakati zijazo katika nyakati hizi, kwaelezea kwa nini Biblia mara kwa mara hutaja “hatua mbili”za wokovu. “Kuhesabiwa haki (War 5:1; Math 12:37), kuitwa wana (War 8:14-16 na mst. 23 wa sura hiyo hiyo na pia Wagal 4:4-6 na Waef. 4:30), na ukombozi (Waef1:7 na 4:30) pamoja na uhalisi mwingi wa Kibiblia uhusianao na wokovu waweza kunenwa kwa namna zote mbili; kama uhalisi uliopita na baraka zijazo. Hii iko hivyo kwa sababu zama zijazo ambazo huleta wokovu hujikunjua zenyewe katika hatua mbili. Kuna mwingiliano wa zama hizi na zama zijazo.” (Waldron n.d.: n.p.) Vivyo hivyo, baadhi ya mifano ya Yesu, kama mfano wa ngano na magugu (Math 13:24-30, 36-43) na mfano wa juya (Math 13:47-50), huzungumzia juu ya tabia pacha ya ufalme.Ufalme upo sasa, lakini bado haujatimilizika kikamilifu. Kwa sasa, wema na uovu upo pamoja, lakini kutakuja wakati wa mavuno na wakati wa kutenganishwa wema mbali na uovu. 1 Wakor 15:20-28 panaonyesha kitu hicho hicho: kama vile kuja kwa Masihi kama mpanzi na kisha kama mvunaji katika Math 13 kwaonyesha kuanzishwa na kutimilizwa kwa ufalme, kwa hiyo ufufuo wa Kristo kama malimbuko ya kwanza na kisha ufufuo wa wale walio wa Kristo wakati wa kuja kwake (1 Wakor 15:23) kwaonyesha ufunguzi na utimilifu wa ufalme.

4. Ufalme wa Mungu huja kwa kuhubiri na kuishi maisha ya Injili chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Kama vile Yesu alivyowakilisha utimilifu usiotarajiwa wa Masihi na ule ufalme ulivyokuwa kiuthabiti, hivyo akatambulisha uelekeo mpya wa matarajio ya AK kuhusu Roho wa Mungu na utawala mpya wa Mungu: atakuwa mbali na mwili, bali yu ndani ya wafuasi wake katika Roho (Yoh 14-16; Mdo 1-2). Yesu alianza huduma yake ya hadharani kwa kuunganisha ufalme na Injili: “Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni na kuiamini Injili” (Marko 1:15). Kwa kifo, ufufuo, na kupaa kwa Yesu, nguvu kamili ya Injili sasa inapatikana. Mdo 2:38 huelezea nini kinatokea wakati mtu yeyote

12 The “already/not yet” schema has been discussed by many commentators. See, e.g., Hoekema 1979: 13-22; Venema 2000: 12-32; Vos 1979: 38 (helpful diagram).

23

Page 25:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

aisikiapo Injili na kuiamini: dhambi zake husamehewa na hupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Katika kuwajibu wanafunzi wake kuhusiana na lini ataurejesha ufalme kwa Israeli (Mdo 1:6-8), Yesu kwa kujibu akajibu: “Ufalme unarejeshwa hivi sasa, lakini si kwa jinsi walivyokuwa wanautarajia. Huja kwa njia ya kuhubiri Injili chini ya uvuvio wa Roho Mtakatifu. Nguvu ya ufalme haiegemei utendaji wa Roho Mtakatifu peke yake, wala hauegemei kwa Neno la Mungu peke yake, badala yake hutegemea yote mawili kutenda kazi pamoja. Yesu hivyo anatoa tafsiri kamili ya unabii wa Agano la Kale kuhusiana na siku ya wokovu.” (Goldsworthy 1991: 212) 5. Kanisa kwa sasa ni sura ya ufalme ujao. Kristo alilifanya kanisa lake kama udhihirisho wa mwili wake hapa duniani baada ya yeye kupaa kurejea kwa Baba (Math 16:18; ona 1 Wakor 12:12-28). Kristo alilituma kanisa “Kama vile Baba alivyonituma mimi,mimi nami nawapeleka ninyi” (Yoh 20:21), na “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi, na tazama,mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari” (Math 28:19-20). Nyaraka za AJ huliagiza kanisa “kushikilia kwa dhati katika uelewa wetu kwamba kuwepo kote kwa Ukristo ni utekelezaji wa Injili kwa kila sehemu ya maisha yetu. Tunaanza na Kristo kama uumbaji mpya kwa ajili yetu, na kuendelea kuelekea lengo, ambalo ni kumfanania yeye katika utimilifu wa uumbaji mpya.” (Goldsworthy 1991: 233) “Kanisa linachukua kazi ya Israeli ya kuwa kielelezo cha kusudi la Mungu kwa maisha ya mwanadamu (Kut. 19:3-6; pia. 1 Petr. 2:9-12). Kanisa linatakiwa kuendeleza utume wa ufalme ambao Yesu aliuanzisha kati ya Wayahudi, ufalme ulioanzishwa sasa kati ya watu wote wa duniani. Kanisa leo linaongozwa na simulizi za kanisa katika Matendo ya Mitume kadiri linavyokabiliwa na miktadha mipya na iliyo tofauti kabisa ya utume wake. Utume wa watu wa Mungu ni kuelewesha habari njema za Ufalme. Hili ndilo linalofanya wakati iliopo sasa maana yake. Na kwa vile utawala wa Yesu unaenea dunia nzima, utume wa watu wa Mungu pia ni mpana kama uumbaji. Matokeo yake, watu wa Mungu wanapaswa kuishi maisha yanayosema, Hivi ndivyo dunia itakavyokuwa siku fulani Yesu atakaporudi!’” (Bartholomew and Goheen n.d.: 6-7)

IV. Mbingu Mpya na Nchi Mpya (Ufunuo 21-22).“Kitabu cha mwisho katika Biblia ni Ufunuo. Katika kitabu kile Yohana anasogezwa kwenye kiti cha

enzi ili kuona jinsi mambo yalivyo kiuhalisia. Anaonyeshwa kwamba, haijalishi tukio gani linatokeza kuwa kinyume, Yesu ambaye kanisa linamfuata, ndiye atawalaye matukio ya duniani. Anaelekeza simulizi yake kuelekea kwenye ule mwisho uliokusudiwa. Katika mwisho ule, dunia ya kwanza iliyotawaliwa na uovu, maumivu, mateso, na mauti itatupiliwa mbali. Mungu kwa mara nyingine atakaa kati ya watu kama alivyofanya mwanzoni. Atafuta mbali machozi. Hakutakuwa tena mauti, kuugua, maumivu, mateso, wala uovu. Tukiwa na furaha, wale tuliofuatia simulizi hii tutarajiao kuisikia sauti ya Mungu mwenyewe: ‘Nami nayafanya yote kuwa mapya!’ (Ufu. 21:5) Picha ya kuvutia ionekanayo katika sura za mwisho za Ufunuo huelekeza macho ya msomaji kwenye mwisho wa historian a kwa urejezaji wa uumbaji wote wa Mungu. Anawaalika wote wenye kiu kuja hata sasa kunywa maji ya uzima lakini anawaonya wale wote wanaobakia nje ya ufalme. Biblia huishia na ahadi iliyorudiwa mara tatu—‘Naja upesi (Ufu. 22:7, 12, 20). Nasi twatoa mwitikio wa mwangwi wa mwandishi wa Ufunuo: ‘Amin! Na uje Bwana Yesu.’” (Bartholomew and Goheen n.d.: 7).

DHANA MBILI ZA KIBIBLIA KUHUSU UHUSIANO WA MUNGU NA WANADAMU

I. Hekalu na Nchi: Mahali pa Makao ya Mungu na Wanadamu.Simulizi ya mahusiano ya Mungu na wanadamu huanzia na Mungu kumuumba mwanadamu na

kumweka katika bustani (Mwa 1-3). Inaishia na maono ya “mbingu mpya na nchi mpya” (Ufu 21:1), ambayo Ufu 21:2-3, 10-2:3 kisha mara huelezewa kama “mji ulio kama bustani, katika umbo la hekalu” (Beale 2004: 23). “Uhusiano wa nguvu kati ya Mwanzo 1-3 na Ufunuo 20-22 hupendekeza kwamba vifungu hivi hujenga nguzo ya simulizi ya Biblia nzima” (Alexander 2008: 10). Kati ya Mwanzo 1-3 na Ufunuo 21-22 tunamwona Mungu akikaa na mwanadamu kwanza katika bustani, kisha katika hema, hekalu, katika Yesu Kristo, ndani ya watu wake (kanisa), na hatimaye katika mbingu mpya na nchi mpya (Yerusalemu mpya). Makao hayo yote yana mambo mengi yanayofanana na kuhusiana, ambayo yanaisokota simulizi ya Biblia yote pamoja. Yanaonyesha kwamba Biblia huelezea kufunuliwa kwa mpango uliojumuishwa wa Mungu kukaa na wanadamu katika nchi.

A. Bustani ya Edeni (Mwanzo 2-3; ona pia Ezek 28:13-16).1. Bustani ya Edeni ilikuwa na vitu kadhaa ambavyo ni dalili ya mahali patakatifu, hasa vya mahekalu matakatifu ya Mungu au mahali pa kukaa Mungu.

a. Bustani ilikuwa mahali pa kipekee pa uwepo wa Mungu (Mwa 3:8).

24

Page 26:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

b. Bustani ilikuwa ni mahali palipoinuka, huenda ni mlimani (ona Ezek 28:14, 16), kwani kutoka hapo palitokea mto (Mwa 2:10).c. Bustani hiyo ilijulikana kwa dhahabu na mawe ya thamani, zaidi ya mimea yake mingi (Mwa 2:11-17; 3:22; ona, Ezek 28:13).d. Kama walivyoumbwa mwanzoni, Adamu na Hawa walikuwa watakatifu (m.y., pasipo dhambi).e. Katika Mwa 2:15, Mungu amweka Adamu katika bustani “ili ailime na kuitunza.” Neno la Kiebrania la “kulima” ni abad (ambalo pia humaanisha “kazi” na “kutumikia”). Neno la Kiebrania la “kutunza” ni shamar (ambalo pia humaanisha “hifadhi” na “linda”). Maneno hayo “yanapatikana tena kwa pamoja katika vitabu vitano vya mwanzo katika majukumu ya Walawi ndani ya madhabahu (k.m. Hes. 3:7-8; 8:26; 18:5-6)” (Alexander 2008: 22-23).f. Edeni iliingiliwa kutokea Mashariki na ililindwa na makerubi (Mwa 3:24). “Kulinda” katika 3:24 ni neno lile lile (shamar) kama “kutunza” katika 2:15. “Kazi ya kulinda ya Makerubi huenda haikuhusisha kulima bustani, bali kuilinda na dhambi na uchafu, ambalo linaonyesha kuwa ndilo jukumu la Adamu lililonenwa katika Mwanzo 2:15 yaelekea ilihusu zaidi ya kuilima ardhi, bali pia “kulinda” mahali patakatifu” (Beale 2004: 70).

2. Upande moja wa jukumu la Adamu na Hawa katika bustani halijatajwa moja kwa moja, lakini laweza kudhaniwa: walitakiwa kuipanua mipaka ya kijiografia ya Edeni hadi ienee dunia nzima. Hilo linafuatia ahadi kutokana na baraka za Mungu na maagizo yake kwa Adamu na Hawa “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha.” (Mwa 1:26-28). Wanadamu wameumbwa kipekee “kwa mfano wa Mungu” (Mwa 1:26-27). Kwa kuenea duniani katika hali ya utii agizo la Mungu, watu wangelikuwa wanaukuza utukufu wa Mungu, kwa kueneza sura yake, duniani kote. “Wakati Mwanzo 2 hufanya tu kuanzisha hatua hiyo, matokeo ya muda mrefu ni ujenzi wa hekalu- mji unaotarajiwa ambamo Mungu na wanadamu watakaa pamoja vizuri kabisa. . . . kwani Mungu anapenda kuifanya dunia nzima makao yake kwa kuijaza na watu watakatifu.” (Alexander 2008: 25-26, 29). 3. Historia baada ya Adam na Hawa kufukuzwa katika bustani ya Edeni inaonyesha yote mawili, mwendelezo wa mwanadamu kuasi kinyume na mpango wa Mungu, lakini pia mpango mwendelezo wa Mungu juu ya dunia yote kama mahali pake pa kukaa palipojazwa na watu watakatifu.

a. Nuhu na Gharika kuu (Mwa 6-9). Wanadamu walikuwa watiifu kwa agizo la “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.” Hata hivyo, hawakuwa wanaeneza sawa sawa sura ya Mungu duniani mwote, na hawakuwa “wanalinda” au “kuitunza” kwa njia za Ki-Mungu, kwa sababu “BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote” (Mwa 6:5). Kwa hiyo, Mungu akaitumia Gharika kuu kuisafisha dunia na uovu wote wa dhambi ambazo wanadamu walizileta juu yake. Pamoja na hayo, Mungu alimpa ahadi Nuhu na wajibu ambao alimpatia mwanzoniAdamu: “Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.’” (Mwa 9:1; ona pia 9:7). b. Mnara wa Babeli (Mwa 11:1-9). Uasi wa wanadamu ukachukua mtindo mpya. Watu wakakataa kueneza sura ya Mungu duniani mwote, badala yake wakataka kukaa mahali pamoja, na kujifanyia jina lao kuu, na (kama ilivyokuwa wakati wa Anguko) wafike hadi mbinguni kwa njia yao wenyewe (Mwa 11:4). Kwa hiyo, Mungu akawalazimisha watu wasambae duniani mwote (Mwa 11:8).c. Mungu alimchagua mtu moja, Ibrahimu, na kuahidi kulifanya jina lake kuu, kumbariki na kuwa pamoja naye, na kuzibariki jamaa zote za dunia kupitia yeye (Mwa 12:1-3; 17:1-8; 22:15-18). Mungu aliendeleza baraka na ahadi hizo kwa wana wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo (Israeli) (Mwa 26:1-5; 28:1-4; 35:9-12).d. Kujengwa kwa madhabahu na sehemu za kuabudia za Nuhu, Ibrahimu, Isaka, na Yakobo (Mwa 8:20; 12:7-8; 13:4, 18; 22:9; 26:25; 33:20; 35:1, 3, 7). Wao ni kama wasafiri wagunduzi au wahamiaji ambao “hupandisha bendera” kwa ajili ya Mungu na “kuikamata nchi” ambapo Mungu baadaye atakuja kufanya makao ya kudumu. Madhabahu hizo na mahali pa kuabudia, hutanguliza kivuli cha hema ya kukutania na hekalu.

B. Hema ya kukutania (Kutoka 25-31, 35-40).1. Hema ya kukutania ilikuwa ni hema maalum iliyotumiwa na Waisraeli kama mahali maalum pa kuabudia wakati wa mwanzo katika historia yao. Muundo wa Hema hiyo ya kukutania ulitolewa na Mungu kwa Musa juu ya mlima Sinai ambapo pia Mungu alimpa Musa zile amri 10 na sheria nyinginezo. (Mwa 25-30).

25

Page 27:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

a. Muundo na vitu vilivyomo huwakilisha Mungu kuwepo na watu wake. “Kadiri mtu alivyokaribia Mahali Patakatifu [au, “Patakatifu pa Patakatifu”] hali ya mazingira iliongezeka hatua kwa hatua kuwa takatifu zaidi. Hii inaonyeshwa katika uhusiano kati ya umbali kusogelea Mahali Patakatifu Sana na uthamani wa vitu vilivyotumiwa kujengea pia (k.m. mapazia; vyuma). Kwa hiyo vitu vilivyotumika kujengea kimsingi huwakilisha ukweli kwamba Mungu aliye Mtakatifu aliketi kati kati ya watu wake.” (Williamson 2007: 104)b. Ukumbi wa nje. Ile Hema ya kukutania ilikuwa na ukumbi wa nje wenye uzio uliouzunguka unaokaribia urefu wa futi 150 kwa upana wa futi 75 (Kut 27:9-19). Ukumbi huo wa nje ulikuwa na madhabahu ya shaba kwa ajili ya kutolea sadaka ya wanyama (Kut 27:1-8) na birika la shaba ambapo makuhani walinawa kabla ya kuingia ndani ya Hema ya kukutania (Kut 30:17-21).c. Hema ya kukutania yenyewe. Hema ya kukutania yenyewe ilikuwa ni hema lenye urefu wa kukaribia futi 45 kwa futi 15 upana wake; ilikuwa na sehemu kuu mbili: ukumbi wa nje, uliojulikana kama Mahali Patakatifu, na ukumbi wa ndani, ujulikanao kama Patakatifu pa Patakatifu (Kut 26:33).

(1) Ukumbi wa Nje (“Patakatifu”). Huo ulikuwa na madhabahu ambapo uvumba ulifukizwa kwa kuchomwa (Kut 30:1-10); kinara cha dhahabu chenye matawi ya mishumaa saba (Kut 25:31-40); na meza ya wonyesho, kuonyesha uwepo wa Mungu (Kut 25:23-30).(2) Chumba cha ndani (“Patakatifu pa Patakatifu”). Hicho kilikuwa kimetenganishwa na Patakatifu kwa kitambaa au pazia (Kut 26:31-37). Patakatifu pa Patakatifu palikuwa na “sanduku la agano” (Kut 25:10-15), ambalo pia liliitwa “sanduku la ushuhuda” kwa sababu ndani yake kuliwekwa jiwe lile lenye zile amri 10 zimeandikwa (m.y., “ushuhuda”) (Kut 25:16, 22; 40:20; Kumb 10:1-5; 1 Waf 8:9; 2 Nyak 5:10). Juu ya sanduku la agano, kulikuwa na kifuniko kiitwacho “kiti cha rehema” kilichofanywa kwa dhahabu, na makerubi wawili wa dhahabu waliogeukiana (Kut 25:17-22). Kilichowekwa mbele ya sanduku la agano, ni kopo la mana (Kut 16:31-36), sehemu ya manukato ya Musa (Kut 30:36), fimbo ya Haruni iliyochipuza matawi (Hes 17:8-11); na nakala ya kitabu cha sheria iliyoandikwa na Musa alipomwamuru Yoshua kuwaingiza Israeli katika nchi ya ahadi (Kumbt 31:24-26) (pia ona Waeb 9:3-4).

2. Wakati Israeli waalipokuwa wakisafiri nyikani, ile Hema ilisafirishwa pamoja nao kutoka mahali pamoja kwenda kwingine ( Kut 40:36-38 ). Wakati Waisraeli walipofanya kambi nyikani, ile Hema iliwekwa kati kati yao, huku yale makabila yao yakiwa yamepangika kwa utaratibu fulani rasmi kwenye zile pande nne za ile hema (Hes 2). Walawi walikuwa ni wasimamizi wa ile Hema na mapambizo yake yote, nao walipanga kuizunguka pande zote (Hes 1:47-54; 4). 3. Baada ya kuiteka Kanaani, ile Hema ilipelekwa Shilo, ilikokaa wakati wa vipindi vya waamuzi ( Yosh 5:10-11; 18:1 ). Baadaye, Hema ikakaa huko Nobu (1 Sam 21:1-6), na Gibeoni (1 Waf 3:4). Hekalu lilipokamilika, Sulemani akaihamishia ile Hema Yerusalemu (1 Waf 8:4), ambapo kinamna fulani ikawa haina kazi tena.4. Kama ilivyokuwa bustani ya Edeni, ile Hema ya kukutania ilikuwa na vitu kadhaa iliyoifanyiza kuwa maalum na tatatifu kama mahali pa kukaa Mungu.

a. Hema ya kukutania ilikuwa mahali maalum pa Mungu kukaa duniani. “Hema ya kukutania” yenyewe humaanisha “kukaa” au “mahali pa kukaa.” Zaidi ya hapo, lile wingu la utukufu wa Mungu ( “Shekina”) liliijaza Hema ya kukutania na lilikaa hapo (Kut 40:34-38; Hes 9:15-23). Musa alikutana na Mungu mara kwa mara katika Hema ya kukutania, iliyoitwa “Hema ya kukutania” (Kut 25:22; 27:21; 28:43; 29:4; 40:2; Wal 1:1; 3:2; Hes 1:1; 2:2). b. Sanduku la agano liliwekwa Patakatifu pa Patakatifu (Kut 25:33), liliwakilisha uhalisi, usioonekana, wa kimbingu. Sanduku la agano liliitwa “mahali pa kuwekea miguu” ya Mungu (1 Nyak 28:2; ona pia, Zab 99:5; 132:7). Hilo linaonyesha kwamba kiti cha enzi cha kweli cha Mungu kiko mbinguni, na hakiishii kwenye hema ya kukutania , bali pia huunganisha mbinguni na duniani au, hukileta kiti cha enzi kutoka mbinguni hadi duniani.c. Makerubi walikuwepo kwenye kile kiti cha rehema juu ya sanduku la agano (Kut 25:18-22). Wale ni vielelezo vinavyowakilisha viumbe vya kimbingu vilindavyo kiti cha kweli cha enzi cha (ona Isa 6:1-6; Ezek 10:1-22; Uf 4:5-9).d. Ni makuhani waliojitakasa tu, walio watakatifu wa kabila la Lawi waliruhusiwa “kutumikia na kulinda katika hema ya kukutania (Kut 29; Hes 3:5-10; 8:1-26; 18:5-6). Mavazi ya kuhani mkuu yalikuwa na dhahabu na vito vya thamani (Kut 28:6-30). Baadaye, ni kuhani mkuu tu

26

Page 28:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

ndiye aliyeruhusiwa kuingia Patakatifu pa Patakatifu, ni mara moja tu kwa mwaka katika siku ya utakaso, kufuatia desturi maalum iliyoagizwa, ili kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi za taifa mbele ya Mungu (Walawi 16).

5. Hema ya kukutania ilikuwa na vitu vingi vilivyokumbushia Bustani ya Edeni.a. Hema ya kukutania na mapambo yake ilifanyishwa kwa kiasi kukubwa kwa dhahabu na fedha (kiti cha rehema na kitako cha mishumaa, kila kimoja kilifanywa kwa dhahabu safi) (Kut 25:17-18, 31; 38:24-28).b. Mahali pa kuingilia Hema ya kukutania palikuwa upande wa Mashariki (Kut 38:13-19).c. Hicho kinara chenye matawi saba ya kuwekea mishumaa kilifanania mti, labda mti wa uzima (Kut 25:31-37).d. Kerubi anakumbushia kerubi ambaye Mungu alimweka “kuilinda njia kuuendea mti wa uzima” (Mwa 3:24).e. Maelekezo ya kuitengeneza Hema ya kukutania na mavazi ya kuhani yalitolewa kwa Musa mlimani (Kut 24:18-25:1, 40).

6. Muundo wa Hema ya kukutania huenda ukaonyesha kuwa ni kiwakilishi cha ulimwengu “kuonyesha wazo kwamba dunia yote iwe ni mahali pa Mungu kukaa” (Alexander 2008: 42).

a. Utengenezaji wa Hema ya kukutania ulihusiana na Sabato (Kut 31:12-17; 35:1-3). Njia sita za maelekezo ya Mungu kwa Musa (Kut 25:1; 30:11, 17, 22, 34; 31:1) sambamba na siku sita za uumbaji katika bustani ya Edeni Mwa 1:1-2:3. Lugha ya Ki-Biblia kuhusiana na uumbaji huenda sambamba na Hema ya kukutania (k.m., Zab 104:2—“Umezitandika mbingu kama pazia”). b. Mwanahistoria wa Kiyahudi wa karne ya kwanza Josephus anaandika kwamba muundo wa Hema ya kukutania ulikuwa “ni mfananio wa mfumo wa dunia,” wenye pazia moja “lililopambwa na aina zote za maua ambayo dunia inaotesha,” na mapazia mengine “yalioneka kutotofautiana kabisa na rangi ya anga” (Josephus, Ant.: 3.123, 126, 132). Anaongeza kwamba rangi ya mapazia ilijulisha hasa “vitu vinne” (hewa, dunia, moto, maji), kama zilivyofanya rangi na mchanganyiko wa mavazi ya kuhani (Ibid.: 3.179-87).c. Mwishowe, Hema ya kukutania (na baadaye hekalu) ilikuwa ni “kivuli” au “nakala” ya mbingu yenyewe (Waeb 8:1-5; 9:23-24). Kwa hiyo, utimilifu kamili utakuja wakati Yerusalemu mpya utakaposhushwa kutoka mbinguni kuja duniani na makao ya Mungu yatakuwa pamoja na watu wake (Ufu 21:1-3, 10-11).

C. Hekalu (2 Sam 7:1-17; 1 Waf 6; 8:1-11; 1 Nyak 17:1-15; 22:1-16; 28:1-29:9; 2 Nyak 3-5).1. Hekalu liliundwa kwa makusudi ya kuwa makao ya kudumu ya Mungu duniani, na kwa namna nyingi huendana sambamba na Bustani ya Edeni na Hema ya kukutania.

a. Hekalu lile lililofanyika kitovu cha Uyahudi wa kale, lilikuwa mojawapo ya majengo mashuhuri sana katika ulimwengu ule wa kale, lilikuwa mahali pekee pa kutolea dhabihu (1 Waf 3:2; 1 Nyak 28:1-29:22).b. Wingu la uwepo wa Mungu lililijaza Hekalu kama jinsi lilivyoijaza Hema ya kukutania (1 Waf 8:10-11; 2 Nyak 5:11-14; 7:1-2).c. Jengo zima lilikuwa limemiminiwa dhahabu, na kuwekewa mapambo ya mawe ya thamani (1 Waf 6:20-35; 1 Nyak 29:1-8; 2 Nyak 3:4-10).d. Sehemu ya ndani ya Hekalu ilifuatia mkondo wa Hema ya kukutania, likiwa na Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu (1 Waf 6:16-20; 2 Nyak 3:3-8). Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu palitenganishwa kwa pazia kubwa (2 Nyak 3:14). e. Patakatifu pa Patakatifu palikuwa pembetatu mraba kamili: mikono 20x20x20 (kukaribia futi 30x30x30) kwa ukubwa (1 Waf 6:20; 2 Nyak 3:8). Palikuwa pametandikwa na dhahabu safi (1 Waf 6:20; 2 Nyak 3:8). Katika Patakatifu pa Patakatifu, palikuwa na makerubi wawili, waliofunikwa na dhahabu, ambao mabawa yao yaligusa kuta na kukutania kati kati (1 Waf 6:23-28; 2 Nyak 3:10-13). Sanduku la Agano liliwekwa Patakatifu pa Patakatifu (1 Waf 8:1-9; 2 Nyak 5:1-10).f. Kila mahali katika Hekalu na mapambizo yake, palikuwa na michoro ya ki-bustani ya kerubi, mwerezi, na maua (1 Waf 6:18, 29, 32, 35; 7:24-26, 49-50). Mayungi na makomamanga yalipamba juu ya nguzo (1 Waf 7:15-22, 42; 2 Nyak 3:15-16).g. Hekalu lilijengwa juu ya mlima Moria (“Sayuni”), ambapo Mungu alikuwa amemwambia Ibrahimu amtolee Isaka (Mwa 22:2; 2 Nyak 3:1). Sehemu ya Yerusalemu ambayo ilikuwa ngome kuu ya Wayebu (waliokalia hapo mwanzo huo Yerusalemu) iliitwa Sayuni. Daudi

27

Page 29:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

aliuteka na akauita “Mji wa Daudi” (2 Sam 5:6-9; 1 Waf 8:1). Kuhamishiwa kwa Sanduku la Agano kuja Hekaluni kulisababisha Hekalu, Mlima wa Hekalu, na hata mji mzima wa Yerusalemu kuitwa Sayuni (ona, Zab 2:6; 76:1-2). Kwa hiyo, kwa namna maalum Hekalu, na, kiujumla zaidi, Yerusalemu na Mlima Sayuni, palikuwa ni mahali pa kukaa Mungu (Zab 48:1-3, 12-14; 78:68; 84:1-7; 87:1-7; 132:13-14).h. Mlango mkuu wa Hekalu ulikuwa lango la Mashariki, lililoitwa “Mlango Mzuri” (Edersheim 1988: 47; ona Mdo 3:2, 10). i. “Kama mahali pa kukaa pa Mungu duniani, mji wa hekalu wa Yerusalemu ni kielelezo kidogo cha kile akitakacho Mungu kwa dunia nzima” (Alexander 2008: 45).

(1) Zab 78:69 inasema, “Akajenga patakatifu pake kama vilele, kama dunia aliyoiweka imara milele.” Hili linaonyesha kwamba Hekalu la AK lilikuwa kielelezo kidogo cha mbingu nzima na dunia. Waeb 8:1-10:1 pia huonyesha kwamba Hema ya kukutania na Hekalu vilikuwa “vivuli” au “nakala” ya vitu halisi vilivyoko mbinguni. (2) Wengine walihusisha utukufu wa dhahabu katika Hekalu na uwepo wa Mungu (ona Josephus, Ant.: 3.187). Hilo laweza kueleza sababu ya Sulemani kuleta kiasi kikubwa cha dhahabu Yerusalemu (2 Nyak 1:15). Hilo pia laweza kudhihirisha kwamba mji ule mzima umekuwa mahali pa kukaa Mungu.(3) Kuwepo kwa Hekalu katika Yerusalemu kwaweza kuhusishwa na nchi ya Israeli kufananishwa na Bustani ya Edeni (ona Mwa 13:10; Isa 51:3; Ezek 36:35; Yoeli 2:3).(4) Mwanahistoria Myahudi wa karne ya kwanza Josephus aliona siri kubwa katika pazia la Hekalu (alikuwa akiandika kuhusiana na Hekalu lililokuwepo wakati wa Yesu, lakini hilo lilikuwa limetegemea muundo wa hekalu uliotolewa na Sulemani). Pazia kubwa “lilikuwa aina ya umbo la ulimwengu . . . Pazia hili lilikuwa pia limenakshiwa pande zote kiustaajabu wa kimbingu, isipokuwa zile alama [kumi na mbili], zikiwakilisha viumbe hai” (Josephus, Wars: 5.212-14; ona Kut 26:31; 2 Nyak 3:14).

2. Hekalu liliharibiwa na Babeli 586 KK ( 2 Waf 25:1-21; 2 Nyak 36:11-21; Yer 32:28-44; Maom; Zab 79 ).

a. Israeli (m.y., Yuda baada ya kugawanyika kwa Israeli kuwa falme mbili) hawakuwa waaminifu kwa Mungu au kwa lile agano. Kwa hiyo, Mungu alituma manabii walioonya kwamba, kama ufalme huo hautatubu, utapinduliwa, Yerusalemu kuharibiwa, na taifa kuchukuliwa uhamishoni huko Babeli kwa miaka 70 (ona Isa 1:21-5:30; 28:14-30:17; 39:1-8; yer 2-29; Eze 4-16:52; 23; Mika 1-3; Hab 1-2; Zef 1; 3:1-11). b. Kabla Babeli kuharibu Hekalu, wingu la utukufu wa Mungu na uwepo wake uliondoka Hekaluni (Ezek 9:3; 10:1-19; 11:22-23).c. Ni jambo la kushangaza sana kwamba Mungu aliwatumia Babeli kuangamiza Yerusalemu na Hekalu, kwa sababu katika Mwa 11:1-9 “Babeli” ulikuwa kinyume kabisa na mpango wa Mungu (Kwa Kiebrania “Babeli” na “Babiloni” ni kitu kimoja).

3. Baada ya uhamisho huko Babiloni, lile Hekalu lilijengwa upya na Zerubabeli mwaka 515 KK ( Ezra 3-6; Hag 1-2; Zek 2-4 ); Hekalu lile lilijengwa upya tena chini ya mfalme Herodi Mkuu kuanzia mwaka 20 BC.

a. Hekalu lilijengwa upya na Herodi ndilo lililokuwepo wakati wa Yesu alipokuwa hapa duniani.b. Vipimo vya ndani na muundo wa hekalu (m.y., Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu), pia na mapazia, vilifuata mkondo wa Sulemani. Hata hivyo, Herodi alipanua ukubwa wa Hekalu kiujumla. Lilikuwa mikono 100 (karibu futi 150) kwenda juu. Herodi pia aliongeza sana upana wa kumbi za hekalu (zilizokuwa nje ya jengo lenyewe) (Josephus, Wars: 5.184-221). c. Ingawaje Hekalu lenyewe lilijengwa upya, lilikosa kipengele chake muhimu: Uwepo wa Mungu. Biblia kamwe haisemi utukufu wa Mungu uliwahi kulijaza Hekalu jipya lililojengwa kama lilivyokuwa limeijaza Hema ya kukutania na Hekalu la Sulemani. Kitabu fafanuzi cha Jewish Encyclopedia chasema, “Kulingana na “Babylonian Talmud “(Yoma 22b), Hekalu la pili [lile la Zerubabeli] lilipungua vitu vitano ambavyo vilikuwamo katika Hekalu la Sulemani, ambavyo ni, Sanduku la Agano, moto mtakatifu, Shekina, Roho Mtakatifu, na Urimu na Thumimu” (Jewish Encyclopedia, “Temple, the Second,” 2002: n.p.). Katika hekalu la Herodi “Patakatifu pa Patakatifu palikuwa patupu kabisa” (Jewish Encyclopedia, “Temple of Herod,” 2002: n.p.).d. Hekalu la Herodi liliharibiwa kabisa na Warumi mwaka 70 BK, sawa kabisa na Yesu alivyosema itakuwa (Math 24:1-2, 15-22; Mark 13:1-2, 14-20; Luka 21:20-24).

28

Page 30:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

D. Maono ya Ezekieli ya Hekalu Jipya (Ezek 40-48).Wakati Israeli walipokuwa uhamishoni Babiloni, Ezekieli aliona maono ya hekalu Jipya na Yerusalemu

Mpya.1. Hekalu aliloliona Ezekieli katika maono yake lilikuwa tofauti na Hekalu jingine lolote la kimwili.

a. Hekalu la Ezekieli lilikuwa la mraba, mikono 500 (kukaribia maili 1) ukubwa wake (Ezek 42:15-20; ona, Ezek 40:5; ona pia Ezek 48:30-35 ambamo mwanena urefu wa mikono 4500 upande moja). Huo unakaribia kabisa mipaka ya Yerusalemu ya kale yenyewe nyakati za Hekalu la pili (Beale 2004: 341). Maelezo ya Ezekieli kiujumla hutaja urefu na mapana, siyo kimo, isipokuwa nguzo za pembeni za mikono 60 (Ezek 40:14). b. Hekalu la Ezekieli inapungukiwa vipengele muhimu kutoka ile Hema ya kukutania na hekalu la Sulemani. Hakutajwi mabirika ya shaba, minara ya mishumaa ya dhahabu, meza ya mikate ya wonyesho madhabahu ya kuvukizia manukato, pazia la kutenganisha Patakatifu pa Patakatifu, Sanduku la Agano, Makerubi, mafuta ya upako, au kuhani mkuu.c. Kama sehemu ya maono, Mungu alimwambia Ezekieli kwamba nchi ya Israeli itagawanyishwa kati ya makabila kwa njia tofauti kabisa. Palikuwa pawe na mikondo 13 sambamba ya nchi ya upana unaowiana, ikipita kutoka mashariki kwenda magharibi kati ya bahari ya Shamu na mto Yordani, kumi na mbili kwa ajili ya makabila na moja kwa ajili ya Bwana (Ezek 45:1-8; 47:13-48:29).d. Utukufu wa Bwana utalijaza Helaku na Mungu atakaa na watu wake milele (Ezek 43:1-9).

2. Kwa kiwango kwamba Hekalu la Ezekieli na uwepo wa Mungu vilikusudiwa kuchukua nafasi ya Hekalu la Sulemani, ndivyo vilikuwa vigezo kwa Israeli kutubu na kumtii Mungu kikamilifu, ambavyo Israeli haikuvitekeleza.

a. Masharti ya Mungu yalihusisha siyo tu kutubu na utii (Ezek 43:6-12; 45:9-12), bali mgawanyiko wa nchi kwa ajili ya Bwana, makuhani, Walawi, makabila, na Mataifa (Ezek 45:1-8; 47:13-48:29). b. Watu hawakutubu wala kumtii Bwana (ona Ezra 10; Hag 1:1-11). Hekalu ambalo hatimaye walilijenga chini ya uongozi wa Zerubabeli halikujengwa kulingana na maono ya Ezekieli, na wala halikufanana kwa utukufu kama Hekalu la Sulemani (Ezra 3:8-13: Hag 2:1-3). Zaidi ya hapo, hata baada ya Hekalu kukamilika, Israeli na ukuhani wake haikutubia dhambi zao na njia zao za uasi (Malaki 1-4)

3. Kutokutubu kwa Israeli na ukweli kwamba Hekalu la Ezekieli halikujengwa kihalisia kabla ya kuja kwa Yesu, kwaonyesha kwamba kusudi kamili la maono ya Ezekieli lilikuwa kuonyesha kiishara uhalisia wa kimbingu ambao, kusema ukweli, ulianzishwa rasmi katika Kristo na kanisa na utafikia utimilifu wake katika mbingu mpya na nchi mpya. “Ukweli muhimu wa Hekalu la Ezekieli umefanyika ukweli tofauti na jengo la mawe. Hilo laweza kuonekana kama kugeuka kimshangao katika kuutimiza unabii, lakini kwa Stephano na nabii Isaya, tunapaswa tujue kwamba ‘Ila Yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizofanywa kwa mikono’ (Mdo 7:48). Mungu hukaa ndani ya Yesu na sisi (Yoh 14:23), na uhalisi wa Hekalu la Ezekieli upo duniani kote. . . . Wakati utimilifu unatokea, taasisi ambazo zilikuwa ni mfano na aina ya uhalisia ule hazihitajiki tena. Hupangiliwa na uhalisia ambao vilikuwa vinawakilisha. Mwili wa Yesu ni hekalu jipya kwa sababu Yesu ni yote mawili, mahali ya utakaso na mahali pa uwepo wa Mungu. . . . Yesu hakuja kugeuza ramani ya mchoro wa jengo la Ezekieli kuwa hekalu kubwa la kushangaza kuliko yote yaliyowahi kutengenezwa kwa mikono ya wanadamu. Kwamba ati Masihi alitakiwa kufanya hivyo ndiko kutokumwelewa kulikofanywa na maadui wa Yesu, kutokumwelewa kulikofanywa pia na wanafunzi wake mwenyewe hadi kufufuka kulipofungua akili zao. Hekalu la Ezekieli la utukufu ni Yesu, ukweli uliofunuliwa katika mwili, ukatangazika katika mafundisho ya Yesu, na kuweza kueleweka kwa ufufuo wake [Yoh 2:21-22].” (Holwerda 1995: 74-75)4. Yesu alianzisha utimilifu wa maono ya hekalu la Ezekieli ya hekalu jipya ndani yake mwenyewe na watu wake (kanisa lake).

a. Maono ya Ezekieli yalionyesha “utukufu wa Bwana” kulijaza Hekalu, na kukaa kati kati ya watu wake milele (Ezek 43:1-9; ona pia, Ezek 37:26). Yohana anatumia lugha kumhusu Yesu yenye maana kama ya Ezekieli: “Naye Neno alifanyika mwili, akaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli” (Yoh 1:14; ona pia, Luka 9:32; Yoh 2:11; 2 Pet 1:16-18). Yesu alisema kwamba, kupitia Roho Mtakatifu, atakaa ndani ya watu wake naye atakuwa pamoja nasi siku zote (Math 28:20; Yoh 14:16-17; Waeb 13:5). Utimizwaji wa ahadi hiyo ulianzia ile siku ya Pentekoste wakati wanafunzi wake walipojazwa na Roho Mtakatifu (Mdo 2:1-21).

29

Page 31:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

b. Maono ya Ezekieli pia yalionyesha mto wa uzima-ukitoka nje kutokea chini ya Hekalu (Ezek 47:1-12). Kwa vile Yesu ndiye Hekalu la kweli la Mungu, ndiye chanzo cha kweli cha maji yaletayo uzima. Katika Yohana 4:10-14 alimwambia mwanamke wa Kisamaria kwamba yeye ndiye chanzo cha “maji ya uzima” ya milele. Katika Yohana 7:37-39 Yesu alisema, akizungumzia kuhusu kumtoa Roho Mtakatifu wake, “Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, ‘mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.’” Kwa vile hakuna mstari wa AK unaosema wazi wazi, “mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake,” “inaelekea kwamba sehemu nyingi za kuchukulia maandiko yanayohusiana zinakuja kichwani. Hivyo vingekuwa ni vifungu vya maandiko ambavyo vingekuwa na umuhimu wa kwanza kwa maana ya sikukuu na vilisomwa wakati huo: kinachoongoza kati ya hivyo ni rekodi ya kipawa cha maji yaliyotokea kwenye mwanba kule jangwani, Kut: 17:1-6 (k.m. pia Zab78:15-16; 105:40-41), kububujika kwa mto wa uzima kutoka hekaluni katika ufalme wa Mungu, Ezek 47:1-11, na maji yanayobubujika katika zama mpya kutoka Yerusalemu kwenda bahari za mashariki na magharibi, Zek 14:8.” (Beasley-Murray 1999: 116) Kwa maneno mengine, Yesu anaunganisha hekalu la siku zijazo na Ezekieli na yeye mwenyewe kama hekalu jipya. Hivyo basi, maji yanabubujika, siyo kutokea hekalu la kuonekana katika Yerusalemu, bali kutoka kwa Yesu mwenyewe. Kanisa ndio mkondo kwa maji yatoayo uzima ambayo chanzo chake ni Yesu.

5. Yerusalemu mpya ( Ufu 21:1-22:5 ), siyo jengo la kujengwa kimwili duniani siku za baadaye, ni kutimia kwa Hekalu la Ezekieli ( Ezek 40-48 ) na ni uhalisi wa kweli ambao maono ya Ezekieli yalielekeza.

a. Katika Ezek 40:2 Ezekieli alichukuliwa kwenye “mlima mrefu sana” ambako aliona “kitu kama mji.” Hakuna “milima mirefu sana ndani wala kuzunguka Yerusalemu iliyopo. Zaidi ya hayo, ule ukweli kwamba aliona kitu “kama” mji pia huonyesha kwamba Ezekieli anaingia katika “ulimwengu wa jiografia ya kimbingu na nchi ambayo inaendana na mazingira ya siku zijazo” (Beale 2004: 336). Hilo linathibitishwa na Ufu 21:10 ambalo linaenda sambamba na lugha ya Ezekieli katika kuelezea Yerusalemu mpya. Kifungu kile kinasema malaika “Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu.”b. Katika maono ya Ezekieli vyote viwili, hekalu na mji huelezwa kuwa mraba (Ezek 42:15-20; 48:15-20). Kuuhusisha mji wa Ezekieli na Yerusalemu mpya kunathibitishwa katika Ufu 21:16 ambapo huuelezea Yerusalemu mpya kama “uliojengwa kwa mraba.” Neno la Kiyunani kimsingi ni “pande nne mraba” (tetragōnos). “AK la Kiyunani la Ezek 45:1-5 na 41:21 hutumia neno hilo hilo kwa lile hekalu lote” (Beale 2004: 348n.37). c. Kipengele muhimu kwa maono ya Ezekieli ni kuwa Mungu yupo na atakaa kati ya watu wake milele. Kusema ukweli, kitabu cha Ezekieli huishia kwa kauli, “jina la mji huo tangu siku hiyo litakuwa, ‘BWANA yupo hapa’.” (Ezek 48:35). Hilo linatimilizwa katika Yerusalemu mpya ya Ufunuo 21-22.

(1) Katika 2 Wakor 6:16-7:1 Paulo alihusisha ahadi za Walawi 26:11-12, 2 Sam 7:14, na Ezek 37:27 , na akaonyesha jinsi utimizwaji wa ahadi hizo ulivyoanzishwa katika kanisa. Maono ya mwisho ya Ezekieli hujenga na kutimiza kile alichokisema awali katika Ezek 37:26-28. Kama ambavyo kifungu hicho kilisema mara mbili kwamba Mungu “na patakatifu pangu nitapaweka kati kati yao milele,” kwa hiyo Ezek 43:7-9 asema mara mbili “nitakaa kati yao milele” Katika AK la Kiyunani, mzizi wa “kukaa” wa Ezek 43:7 ni “hema ya kukutania.” Ufu 21:3 kwaonyesha kwamba Yerusalemu Mpya ndiyo kutimizwa kwa unabii wote, kuchanganya na maono ya Ezekieli, katika kutoa mwangwi wa Ezek 43:7, 9 na kusema mara mbili, “patakatifu pa Mungu ni kati kati yao” na“Naye atakaa kati kati yao.” Kwa nyongeza, mara tatu katika Ufu 21:3 panasema kwamba Mungu atakuwa “pamoja“ na watu wake. (2) Vivyo hivyo, Ezek 43:7 husema, “Hapa ni mahali pangu pa kiti cha enzi.” Ufu 22:1, 3 kote husema kwamba “Kiti cha enzi cha Mungu na Mwana Kondoo” kitakuwa katika Yerusalemu Mpya. (3) Mitume na makabila ya Israeli yanatajwa kama sehemu kamili ya Yerusalemu Mpya yenyewe: mitume ndio msingi ( Ufu 21:14 ); zile kabila kumi na mbili ndiyo milango ( Ufu 21:12-13 ). Siyo tu kwamba Hekalu la Ezekieli na Yerusalemu Mpya vina muundo moja, vyote viwili vina milango kumi na mbili katika mpangilio ule ule: mitatu kaskazini; mitatu mashariki; mitatu mashariki; mitatu magharibi (linganisha Ezek

30

Page 32:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

48:31-34 na Ufu 21:12-13). “Mwingiliano kati ya mitume na kabila za Israeli kama sehemu ya jengo la mji-hekalu lililotabiriwa katika Ezekieli 40-48 huthibitisha zaidi uamuzi wetu . . . kwamba kanisa la Kikristo la jamii za watu mbali mbali litakuwa ni kundi lililokombolewa ambalo, pamoja na Kristo, kutatimiza unabii wa Ezekieli juu ya hekalu litakalokuwepo na mji. Hili ni sambamba na vifungu vya AJ ambavyo jumuia zote za agano huunda hekalu la kiroho ambapo uwelo wa Mungu hukaa ndni yake (1 Wakor.3:16-17; 6:19; 2 Wakor 6:16; Waef. 2:21-22; 1 Pet. 2:5).” (Beale 1999a: 1070)(4) Hekalu la Ezekieli liko kati kati ya kila kitu. Katika Yerusalemu mpya hakuna jengo la kuonekana pale, “Kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana Kondoo ndio hekalu lake” (Ufu 21:22). Kwa hiyo, hekalu la kweli—Mungu na Kondoo—ndilo sasa kitovu. “Uwiano kati ya Mungu na Mwana Kondoo na hekalu unakaribia sana sura ya maono ya Ezekieli, ambayo ni uwepo wa kiutukufu wa Mungu wenyewe (k.m., 48:35, ‘jina la mji’ ni ‘Bwana yupo hapa). Kila kitu ambacho hekalu la kale la Israeli lilielekeza, kutanuka kwa uwepo wa Mungu, kumetimizwa katika Ufunuo 21:1-22:5, na kutimizwa huko kumetarajiwa ndani ya Ezekieli 40-48 yenyewe.” (Beale 2004: 348)

d. Ezek 47:1-12 huelezea mto unaopita kutoka hekaluni ambao unaponya na kutoa uzima. Ufu 22:1-2 hutumia picha ile ile na huitumia kwa Yerusalemu Mpya. Kufananishwa kwa mto katika maono ya Ezekieli na mto katika Yerusalemu Mpya unaambatanishwa katika Ezek 47:7, 12 ambapo panasema kwamba palikuwa na miti upande huu na upande huu wa mto. Hilo linaenda sambamba na Ufu 22:2 ambayo pia husema kwamba mti wa uzima ulikuwa “upande huu na upande huu wa mto.” Katika matukio yote mawili miti ilisemwa kuzaa matunda (Ezek 47:12; Ufu 22:2). Zaidi ya hapo, katika matukio yote, majani ya miti hiyo ni “ya uponyaji” (Ezek 47:12; Ufu 22:2).e. Hekalu la Ezekieli lingekuwa tu kiuhalisi kwa wale walioacha machukizo na dhambi zao wenyewe (Ezek 43:6-9). Ufu 21:27 vivyo hivyo husema kwamba “hakuna kilicho kichafu, wala yeye afanyaye machukizo” atakayekuwa katika Yerusalemu Mpya. Hilo linaonyesha kwamba, Hekalu la Ezekieli litakuwa tu linazungumzia watu walio “katika Kristo”. Kama vile Kristo alivyouanzisha ufalme wake na kusameme dhambi wakati wa kuja kwake kwa mara ya kwanza, ndivyo Yerusalemu Mpya huunda utimilifu wa ufalme wa Kristo, ambamo dhambi zimeondolewa milele.

6. Vipengele fulani vya maono ya Ezekieli yaonyesha kwamba, siku zote ilikusudiwa kuwa kielelezo cha mambo ya kimbingu, na siyo ya kimwili, kwa asili yake.

a. Utangulizi katika Ezek 40:1-2 una vipengele vitatu: (1) panatajwa tarehe maalum ambayo tukio lilitokea; (2) maneno“mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu”; na (3) maneno kwamba aliona “maono.” Sehemu nyingine pekee katika Ezekieli penye mtindo wa utambulisho wenye vipengele hivyo vitatu kwa pamoja hupatikana katika Ezek 1:1-3 na 8:1-3. Katika sehemu zote hizo mbili, maono ambayo Ezekieli aliona yalikuwa ya hekalu la kimbingu (m.y., mahali pa kukaa Mungu mbinguni), siyo ya kidunia. Hekalu la kimbingu liko wazi kabisa katika Ezek 1:1-28, ambapo mkazo unakuwa kabisa mbinguni. Katika Ezek 8:1-11:23 maono ni ya uwepo wa mbingu ambayo yanahusishwa na uwepo wa Mungu duniani na watu wake. Ezekieli aliona utukufu wa Mungu (8:4), ambao ulikuwepo katika siku za Hekalu la Sulemani. Hata hivyo, Ezekieli baadaye aliona machukizo yaliyokuwa yakifanyika katika hekalu la duniani. (9:3). Kisha picha ikageukia hekalu la mbinguni (10:1-22), na utukufu wa Mungu unamalizia kuondoka kwake katika hekalu la duniani (10:4; 11:22-23). Uwepo wa Mungu bado upo kwa wale waaminifu walioko uhamishoni Babeli (11:16), ambao ndio hekalu la kweli la duniani, ingawaje jengo la duniani lilikuwa limeharibiwa na watu wa Babeli.b. Katika maono ya Ezekieli, mto lazima uwe ni ishara na si wa ulimwengu huu kwa sababu hata kama hakuna matawi yaliyotajwa, maji huendelea kuwa marefu zaidi, kutoka chemchemi kuwa mto ambao hauwezi kuuvuka (47:2-5). Zaidi, tofauti na mto wa kidunia wa asili; hufanya maji ya chumvi yawe safi, badala ya kinyume chake (47:6-12).c. Ingawa Ezekieli aliandika kwa kutumia lugha na picha ya kuwafanya wasomaji wake wamwelewe, katika nuru ya kuja kwa Kristo, Hekalu la Ezekieli lisingeweza kuwakilisha kivyovyote jengo la kuonekana, litakalojengwa siku za mbeleni.

(1) Katika maono yake yote, Ezekieli anaelezea dhabihu za wanyama ambazo zinasemekana kuwa na kusudi la “kutakasa” na kutendea kazi ( Ezek 43:13-27; 45:15- 25 ). Dhabihu kama hizo zisingeweza kuwa za kutakasa kiukweli, kwani hizo zingegeuza historia ya ukombozi na kukataa uwezo na utoshelevu wa dhabihu ya mara

31

Page 33:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

moja na isiyorudiwa tena aliyojitoa Kristo mwenyewe, kinyume na Waeb 9:11-10:22. Hilo pia lingerudisha ile hali ya “vivuli” badala ya vitu kamili na halisi (ona Wakol 2:16-17; Waeb 8:1-10:22). (2) Kuchukulia “kiuhalisia” (m.y., kimwilini) picha ya Ezekieli ya Yerusalemu kama kitovu cha ibada za dunia ( Ezek 47-48 ), ambapo wasio–Waisraeli wanakuwa wametengwa kutoka katika hekalu ( Ezek 44:6-9 ), vivyo hivyo hugeuza kabisa kile ambacho Kristo amekifanya. Yesu aliondoa uhitaji wa kulazimika kuifanya ibada mahali fulani palipo maalum (Yoh 4:21, 23), na aliondoa utofauti kati ya Wayahudi na Mataifa katika watu wa Mungu (1 Wakor 12:13; Wagal 3:28; Waef 2:11-22; Wakol 3:11; Ufu 5:9; 7:9).13

(3) Kusema kwamba dhabihu ni “kumbu-kumbu” tu ya dhabihu ya Kristo, kunamaanisha pia hakuna sababu kulichukua hekalu lenyewe “kimwili” (m.y., kama jengo lililojengwa). Zaidi ya hapo, kutazama dhabihu zilizotajwa na Ezekieli kama “kumbu-kumbu” pia ni kumshushia heshima Kristo kwani kumbu-kumbu pekee aliyoiagiza Kristo mwenyewe “ya kukumbuka” kazi ya ukombozi aliyoifanya ilikuwa ni Meza ya Bwana, siyo kurudi kwenye dhabihu za AK (Luka 22:14-20; 1 Wakor 11:23-26).

7. Matokeo yake, swala la tafsiri ya maono ya Ezekieli ni swala laufunuo wa hatua kwa hatua. a. Lugha ya kinabii na ufunuo wa hatua kwa hatua. “Ezekiel 40-48 ni maono ya kimaumbo ya hekalu halisi la mbinguni ambalo litashushwa na kuimarishwa duniani katika hali ya kutokuwa na jengo katika siku zijazo. . . . Ezekieli angeweza pia kuwa ametabiria hekalu la nyakati za mwisho kupitia viwakilisho vya hekalu la kuonekana ambalo Waisraeli wakati huo wangelielewa. Kwa maana hiyo, anaweka picha ya hekalu lisilo lenyewe ili kutoa mwangaza kwa sehemu kwamba hilo litakuwa hekalu la aina tofauti. Ufunuo wa kihatua wa Agano Jipya huweka wazi kiasi gani hekalu la siku zijazo linapaswa liwe: halikuwa, kusema ukweli, liwe jengo bali liwe limetimilizwa kwa Masihi kukaa kati ya watu wake.” (Beale 2004: 353, 359) b. AJ linavyotafsiri AK. “Wengi wangeona upana wa maono ya Hekalu ya Ezekieli (Sura za 40-48) kama kutia moyo imani kuwa kutakuwa na Hekalu la siku za mwisho linaloendana na maelezo ya kinabii ya Ezekieli. Hata hivyo, mwanatheolojia wa ki-Biblia hawezi kuuendea unabii huo pasipo kugundua namna ambayo unabii huu unaeleweka na waandishi wa Agano Jipya. Picha ya Ezekieli ya mto unaopita kutoka katika Hekalu (Ezek. 47:1 n.k.) hujirudia mara mbili katika Agano Jipya. Katika Yohana 7:37-9 ‘mito ya maji ya uzima’ hububujika kutoka kwa Yesu mwenyewe; wakati huo huo katika Ufunuo ‘mto wa maji ya uzima’ hupita katikati ya Yerusalemu Mpya (Ufu. 22:1n.k.). Waandishi hawa wawili kwa kuelewa kabisa wamechota kutokana na unabii wa Ezekieli na kuutumia kwa Yesu na Yerusalemu ya kimbingu. Matokeo yake, hawakuwa kinamna fulani wakitegemea unabii wa Ezekieli utakuja kutimizwa siku za mbeleni kwa kuona Hekalu lililojengwa. Badala yake unabii huu ukafanyika namna angavu ya kunenea kwa njia ya picha kile ambacho Mungu sasa alikuwa amekitimiza katika, na kupitia kwaYesu. Kinyume chake basi, kwa hiyo, ingawaje maono ya Ezekieli yalikazia sana kuhusu Hekalu, yalikuja kutimilizika katika ule mji ambamo mlikuwa ‘hamna Hekalu kwa sababu ‘Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana Kondoo, ndio Hekalu lake’ (Ufu. 21:22).” (Walker 1996: 313)

E. Yesu ndiye Hekalu la kweli.1. Yesu, siyo Hekalu, alikuwa mahali maalum pa Mungu kukaa duniani.

a. Yesu aliitwa “Imanueli” ambalo linamaanisha “Mungu pamoja nasi” (Math 1:23).

13 Mwonekano wa muundo wa maono ya Ezekieli huonyeshwa katika taharii mahususi ya Bob Pickle, iitwayo “Mji wa Ezekieli: Akifanya hesabu ya mduara wa dunia,” (Pickle 2004: n.p.). Pickle huutazama mji ule na nchi ile ilivyotolewa kwa Ezekieli kama kielelezo cha nchi mpya. Anasema, “Tukiikuza ramani ya Ezekieli [m.y., vipande 13 vya nchi viliyopewa kwa makabila na kwa Bwana] hadi mji wa Ezekieli unakuwa ukubwa wa Yerusalemu mpya ya Ufunuo, basi ramani ya Ezekieli huizunguka Dunia. Vipimo vya mji wa Ezekieli kwa Yerusalemu mpya ya Ufunuo ni sawa na ramani ya Ezekieli kwa mduara wa dunia.” Mahesabu yake yanasimamia fikira kadhaa: (1) Hutumia mianzi 4500 kwa kila upande wa mji wa Ezekieli (Ezek 48:30-35); (2) Seehmu zote 13 za nchi (Ezek 45:1-8; 47:13-48:29) zina upana sawa 25,000 mianzi (kwa jumla ya mianzi 325,000); (3) Ukubwa wa yerusalemu Mpya (Ufu 21:16) ni 3000 dhiraa kila upande, kwa jumla ya dhiraa 12,000, siyo dhiraa 12,000 kila upande (Ya Kiyunani husema kuwa vipimo vilikuwa dhiraa “12,000” na kwamba “marefu yake ni sawa na mapana yake”); (4) Kila kiwanja cha Kirumi ni karibu futi 606-607 kwa urefu. Ingawaje wazo la Pickle sicho kinachoshindaniwa hapa, inashangaza, na hutambua kwamba kile alichokiona Ezekieli kilikuwa, kiundani zaidi, kichukuliwe kiishara, badala ya jengo au mji wa kimwili wa kweli utakaojengwa siku za mbeleni..

32

Page 34:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

b. Yohana 1:14 panasema “Naye Neno alifanyika mwili, naye akakaa kwetu.” Neno “akakaa” ni neno na kitenzi la “hema” au “hema ya kukutania” (hivyo kimsingi panamaanisha kwamba, yeye “alifanyika hema ya kukutania” kati yetu). c. Kama vile Mungu alijaza Hema ya kukutania na Hekalu (Kut 40:34-38; Hes 9:15-23; 1 Waf 8:10-11; 2 Nyak 5:11-14; 7:1-2), Hivyo Roho Mtakatifu alishuka hadharani juu ya Yesu na kumjaza (Math 3:16-17; Mark 1:10-11; Luka 3:21-22; Yoh 1:32-34). Yesu alikuwa yote mawili – anaongozwa na Roho na amejazwa na Roho (Math 4:1; Mark 1:12; Luka 1:15; 4:1). Tofauti na Mungu kuliacha Hekalu, Roho Mtakatifu alibakia na Yesu (Yoh 1:32-33) hadi Yesu alipomwachilia akiwa pale juu msalabani (Luka 23:46). Roho humtukuza Yesu (Yoh 16:14). Yesu ana uwezo wa kumtuma Roho Mtakatifu kukaa ndani ya wafuasi wake (Yoh 14:16, 26; 15:26; 16:7).

2. Yesu alitimiza jukumu la Hekalu katika namna iliyo kuu zaidi kuliko wakati wowote ambapo zile desturi za ki-hekalu zilikuwa zinafanyika.

a. Yesu alikuwa na uwezo usio wa kawaida kusamehe dhambi za watu zenyewe, pasipokuwa na haja ya kutoa dhabihu zozote au pasipo kushiriki katika desturi zozote za ki-hekalu za AK (ona Math 9:2-6; Mark 2:1-12; Luka 5:17-25; 7:40-50; Yoh 8:1-11). Kusema ukweli, kupitia dhabihu moja aliyojitoa mwenyewe, Yesu huondoa dhambi moja kwa moja kwa ajili ya watu wote wa “kila lugha na kabila na jamaa na taifa” (Ufu 5:9; ona Waeb 9-10). Dhabihu na desturi zilizokuwa zikifanywa Hekaluni zilifunika dhambi za Israeli tu, nazo zilifunikwa kwa kitambo tu.b. Katika Warumi 9:4-5 Paulo anatangaza kwamba Yesu anao ubora zaidi ya baraka na ahadi bora kupita zote nyingine za Israeli, zikiwamo ibada za hekalu. Katika War 9:4 “ibada” (hē latreia) “inaelekea kuwa ni ‘huduma ya Hekalu (Ndivyo NASB, NASB isemavyo) au ‘ibada ya hekalu (NEB, NIV), ambayo hufaa zaidi ya zile tafsiri za juu juu ‘kuabudu’ ya RSV, NAB, na NRSV” (Sweeney 2003: 608n.16). Kwa hiyo, Yesu siyo tu kwamba alikuwa dhabihu iliyokamilika kwa dhambi, bali pia ni kuhani mkuu aliyekamilika katika hekalu la kweli (Waeb 2:17; 4:14-5:10; 7:1-8:6; 10:11-22).

3. Yesu alidhihirisha ubora na mamlaka yake zaidi ya Hekalu.a. Katika Math 12:6 Yesu alisema, “Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu.” Yesu ni “mkuu kuliko hekalu” kwa sababu hekalu lilikuwa ni jengo tu lililofanywa na wanadamu, ambalo lilimwelekea Mungu na ulimwengu ulioumbwa. Kwa upande mwingine, Yesu ni Mungu mwenyewe, na ndiye anahusika na yote mawili –aliumba na pia kuushikilia ulimwengu (Waeb 1:1-3). “Hekalu la Israeli la mwanzoni, lililojengwa lilikuwa ni kivuli tu kilichotangulia cha Kristo na watu wake kama hekalu. Kwani, kumbuka, kazi ya kwanza ya hekalu ilikuwa ni mahali ambapo uwepo wa utukufu wa Mungu ulidhihirika duniani kwa watu wake. Sasa kwa vile Yesu ameshakuja kama Mungu katika mwili, yeye sasa ni mahali ambapo uwepo wa Mungu unadhihirika katika dunia.” (Beale 2004: 276).b. Katika Yoh 1:51 Yesu alisema, “mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.” Hilo ndilo linaendana na Mwa 28:12, ambapo madhabahu ndogo ya Yakobo ilikumbusha unganiko la mbingu na duniani. Lile lilikuwa ni utangulizi wa hekalu, ambapo uwepo wa Mungu mbinguni ulikuwa umeunganishwa duniani. Yesu, katika kujitaja mwenyewe kama ngazi ya Mwa 28 ni njia nyingine ya kudai kwamba yeye, na siyo hekalu la Yerusalemu, ndiye kiungo cha msingi kati ya mbingu na duniani.c. Katika Yoh 4:21-26 Yesu alirudia kuthibitisha kuwa yeye ndiye aliyeleta ibada ya kweli ya Mungu, na siyo hekalu la Yerusalemu. Kwa kusema “Hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu” (Yoh 4:21), Yesu alikuwa anasema kwamba, mifumo yote ya dhabihu ya AK lote ya kuabudu ilikuwa inavuliwa. Kuanzia sasa na kuendelea, kuabudu kwa kweli kwaweza kutendeka popote duniani ili mradi mtu awe na Yesu, na hatazuiwa na desturi zilizokuwa zinafanyika katika Hekalu.

4. Yesu alilihukumu Hekalu.a. Yesu aliwafukuza wabadilishao fedha kutoka Hekaluni (Math 21:12-13; Mark 11:15-18; Luka 19:45-46; Yoh 2:13-16. Katika kufanya hivyo, Yesu alinukuu kutoka Isa 56:7 (“nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala”), ambayo ni sehemu ya unabii (Isa 56:3-8) kwamba Mungu atawaita Mataifa kuja kwake katika “hekalu” lake (“mlima mtakatifu”). Pia alinukuu kutoka Yer 7:11 (“pango la wanyang’anyi”), ambalo ni sehemu ya neno kutoka kwa Bwana (Yer 7:1-11) kwamba Mungu ameona jinsi Israeli isivyotenda kwa haki, imewakandamiza wageni na

33

Page 35:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

wasio na msaada, na wamemwaga damu isiyo na hatia, na wameiendea miungu migeni. Hoja ya Yesu ni kuwa, kama vile Mungu alivyolikataa Hekalu la kwanza katka mwaka 586 KK kwa sababu lilikuwa limenajisika, hivyo Hekalu lililokuwa limejengwa Yerusalemu lilitakiwa kubadilishwa na “Hekalu” kuu zaidi kwa sababu lilikuwa lina uharibifu na lilikuwa halitekelezi jukumu lake lililokusudiwa. b. Katika sheria za AK, mlemavu, kipofu, kiwete walikuwa hawaruhusiwi kutumika katika Hekalu (Walawi 21:16-24). Wakati Yesu alipowatupa nje wale wabadilishao fedha, “vipofu na viwete wakamwendea mle hekaluni, akawaponya” (Math 21:14). Hilo kwa mara nyingine, linaonyesha kwamba Yesu alikuwa anatimiliza unabii wa Isa 56:3-8, katika kusafisha njia kwa ajili ya hekalu la kweli, kwa vile unabii ule ulikuwa umeonyesha kwamba walemavu wataweza kuabudu pamoja na Mataifa. c. Kuwatupa nje wabadilishao fedha kwaweza kuwa kulisimamisha kwa kitambo utoaji wa dhabihu kwa kuzifunga taratibu ambazo wanyama walikuwa wanaletwa na kutolewa sadaka. Ikiwa hali ni hivyo, pia ingeonyesha kwamba kusudi la Hekalu la kutoa dhabihu kwa msamaha lilikuwa linapita zake.

5. Yesu alitabiri kuharibiwa kwa Hekalu.a. Katika Math 21:18-22 (Mark 11:12-14, 20-24) Yesu aliulaani mtini. Mtini unadhihirisha wazi wazi kukataliwa kwa Israeli na Mungu (kama ilivyokuwa katika Yer 8:11-13 ambako inachimbukia). Kiini kwa kukataliwa kwa Israeli ni kukataliwa kwa hekalu. Hilo linaendana na kauli ya Yesu kuhusu kuung’oa “mlima huu” ukatupwe baharini. “Mlima” wenyewe huenda alimaanisha ule mlima wa hekalu, kwani ule ndio uliokuwa mlima wa muhimu zaidi katika Yerusalemu na lile Hekalu siku zote lilitajwa kuendana na ule mlima lililokuwapo.b. Katika Math 21:33-46 (Mark 12:1-12; Luka 20:9-19) Yesu aliwakataa Israeli na Hekalu katika mfano ule wa mwenye shamba na shamba la Mizabibu. Mfano ule unatokea Isa 5:1-7. Maandishi ya kale ya Waaramaiki na Wayahudi huweka ngazi moja Shamba la mizabibu, mzabibu mwema, au mnara pamoja na Hekalu (Beale 2004: 183). Sura ya Hekalu huunganisha fikira za kilimo na ujenzi katika mfano huo. Kutaja kwa Yesu swala la “jiwe walilolikataa waashi, hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni” (Math 21:42, akinukuu kutoka Zab 118:22) humaanisha kwamba “kukataliwa kwa Yesu kama ‘jiwe kuu la pembeni’ la Hekalu . . . ni sawa na kumkataa Yesu kama hekalu la kweli” (Ibid.: 184). Waandishi wa baadaye wa AJ wazi wazi wanamtambua Yesu kama ndiye “jiwe kuu la pembeni” ambalo juu yake, Hekalu la kweli (kanisa) linajengwa (Mdo 4:10-11; Waef 2:20-22; 1 Petr 2:4-8 [ambapo pananukuu Zab 118:22]).c. Ingawaje Yesu alithibitisha hekalu kuwa ndipo mahali kimsingi pa Mungu kukaa duniani (Math 23:21), katika uelekeo huo huo aliliita “nyumba yenu ,” na kusema kwamba “mmeachiwa hali ya ukiwa” (Math 23:38). Kauli hizo zaonyesha kwamba, kwa sababu ya dhambi za Israeli na kutokutii kwa Mungu—kulitangulia-hali ya kumkataa Yesu kama Masihi wao—hekalu halikuwa tena linatimiza wajibu wake. Kwa hiyo, halikuwa tena Hekalu “la Mungu”, na lingeharibiwa.d. Yesu alisema bayana kwamba Yerusalemu na Hekalu vitaharibiwa (Math 24:1-2; Mark 13:1-2; Luka 21:20-24; ona pia Math 26:61; Mark 14:58; Mdo 6:13-14). Katika vifungu hivi vyote Yesu alihusisha kuharibiwa kwa hekalu; na Ufalme wake na ujio wake.

6. Mwili wa yesu, hasa katika kufufuka kwake, hutambuliwa kama Hekalu jipya, la kweli. a. Yesu kibayana kabisa aliuita mwili wake “hekalu.” Alifananisha kuharibiwa kwa Hekalu lile la kidunia katika Yerusalemu na kufufuka kwa mwili wake mwenyewe (Mark 14:58; Yoh 2:18-22; ona pia Math 26:60-61; 27:40; Mark 14:57-58; 15:29).b. Tukio katika Mark 14:57-58 la Yesu wakati anakamatwa. Pale panasema kwamba baadhi walitoa “ushahidi wa uongo” kinyume na Yesu wakisema, “Sisi tulimsikia akisema, ‘Nitalivunja hekalu hili lililofanyika kwa mikono, na katika siku tatu nitajenga jingine lisilofanywa kwa mikono.’” Uongo wa ushuhuda “huenda ukawa unalalia zaidi katika mashitaka kwamba Yesu mwenyewe ataliharibu hekalu la Yerusalemu” (Walker 1996: 10). Maneno “lililofanyika kwa mikono . . . lisilofanywa kwa mikono” hulinganisha Hekalu la Yerusalemu na Yesu: “Maelezo ya Hekalu la Yerusalemu kuwa ‘lililofanyika kwa mikono (cheiropoiētos) ni namna yenye nguvu ya kushusha umuhimu wake. Hii ilikuwa njia ya kupondea sanamu za kipagani (k.m. Zab. 15:4; pia Isa. 46:6); kulisimulia Hekalu kwa mtindo kama huu kulikuwa ni kukashifu kuletako hasira kali sana. Hata hivyo, katika muktadha huu, hoja ya msemo inalalia zaidi katika mlinganisho na maelezo ya Hekalu mbadala ‘lisilofanywa kwa mikono’

34

Page 36:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

(acheiropoiētos). Hekalu la Yerusalemu lilikuwa limetolewa na Mungu, lakini Yesu alitabiri kuonekana kwa aina mpya ya Hekalu, linalotokana na Mungu—katika kulinganisha na hekalu la kujengwa ambalo lingeonekana kuwa ni la kianadamu, ‘lililofanyika kwa mikono.” (Ibid.)c. Waeb 8:1-2 Moja kwa moja huunganisha ufufuo wa Kristo na hema ya kukutania. Kifungu hicho huzungumzia kuhusu Kristo “akisha kuketi kwenye kiti chake . . . katika hema ya kweli, ambayo Bwana aliibuni, si mwanadamu” (ona pia Waeb 9:11). Kwa hiyo, hekalu katika Yerusalemu “lilikuwa utambuzi usiokamilika wa kianadamu wa unabii [2 Sam 7:11-13] kwamba mzao wa Daudi atalijenga hekalu, na ambalo limekuja kutimilizwa kwa kiwango kikubwa zaidi katika ufufuo wa Kristo” (Beale 2004: 237).

7. Yesu aliposulubiw a “pazia la hekalu lilipasuka vipande viwili toka juu hadi chini” ( Math 27:51; Mark 15:38; Luka 23:45 ). Kupasuka kwa pazia ni alama ya kuharibiwa kwa Hekalu na njia iliyo wazi waliyo nayo watu sasa kwa Mungu kupitia kwa Yesu. Kama matokeo ya dhabihu ya Yesu, sasa tunao “ujasiri wa kupaingia patakatifu . . . kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia” (Waeb 10:19-20). Katika Kristo, hakuna mtu anayetakiwa (au kuweza) kumkaribia Mungu kwa kupitia mfumo wa Agano la Kale au kwa sheria za Musa ambazo Yesu alizikomesha.8. Yesu ni uhalisi wa kweli ambao Hemaya kukutania na Hekalu katika Yerusalemu viliwakilishwa kama kivuli ( Waeb 4:14-5:10; 7:1-10:22 ). Muhimu zaidi, Waeb kamwe haizungumzii rasmi “hekalu,” bali mara zote ni “hema ya kukutania.” Walker anaonyesha sababu yake: “Mwandishi wa Waebrania, hata hivyo, hakutaka kuingiza michepuo yoyote katika Hekalu la kileo lililoko, lakini zaidi, hufanya hoja njema zaidi kuhusiana na dhana yenyewe ya Hekalu. Kwa kuweka msisitizo kwenye ‘hema’ kule nyikani, angeweza kujenga hoja kwamba mfumo wa kuabudu wa Hema ya kukutania, hata katika kutazamwa kama mfumo ulio bora na safi chini ya Musa (kabla dhambi ya mwanadamu yeyote haijageuza jicho la mbinguni), ulikuwa umetangazwa kuwa haifai na Mungu kupitia Yesu. Kukosoa kwake Hekalu lililokuwepo hakukufungamana na maswala yoyote ya kisiasa au kukataa kwake mwenyewe, bali zaidi na makusudi ya Mungu ya umilele.” (Walker 1996: 207-08) Yesu ni uhalisi wa mwisho. Mfumo wote wa AK wa Ki-hekalu hauna kazi tena.

a. Waeb 4:14-5:10; 7:1-10:22 panamwonyesha Kristo kama yote mawili- kuhani mkuu na Hema / Hekalu. Hili lina umuhimu ufuatao: “Kristo ni kuhani-mfalme ambaye kufufuka kwake kulikuwa ni mwanzo wa hekalu la zama zijazo na ambaye kupaa kwake mbinguni kulimaanisha kwamba kiiini cha mvutano cha hekalu kimehamishwa kutoka duniani kwenda mbinguni, na kitabakia huko wakati uliopo. Kristo kama kuhani mkuu anaendelea kutawala na kuhudumia ndani ya hekalu la jumba la kifalme la mbinguni.” (Beale 2004: 299) b. Waeb 8:1-10:22 hujenga hoja kwamba madhabahu ya kweli ni ya mbinguni na ile ya kuwakilishwa ni ile ya duniani. “Waeb 9:8-9 pia huizungumzia ‘hema ’ ile ya zamani (iliyo njema, mahali patakatifu) kama ‘alama’ au ‘mfano’ wa hema ya siku zijazo (k.m., katika 9:11) ili kuthibitisha kwamba ile hema ya zamani haikuwa ndiyo yenyewe” (Beale 2004: 295).c. Waeb 9:11 panasema kwamba Kristo aliingia “kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu.” 9:12 panaongezea kwamba alipaingia “kupitia damu yake mwenyewe.” Kwa hiyo, “hema” ya kweli, ya kimbingu ilijijumuisha na Kristo mwenyewe (m.y., na “damu yake”).d. Waeb 10:19-20 panasema rasmi kwamba “pazia” [ndani ya Hekalu] ni “Mwili wake.” AK lilikuwa linamnyoshea Kristo kila mahali. “Katika Kristo kuna kuelewa. Siyo hasa kwamba Kristo anatimiliza kile ambacho Hekalu linamaanisha; badala yake Kristo ndiyo maana yenyewe ya kwa nini hekalu lilikuwapo. . . . Kristo ndiye hekalu la kweli, nuru ya utukufu wa kweli, mana ya kweli, divai ya kweli. Kuja kwa kweli yenyewe huwekesha kando ile ya uwakilisho. Pazia la hekalu lililofanywa kwa mikono limeharibiwa, kwani ule uwakilisho wake umeharibiwa.” (Clowney 1972-73: 177, 183)

F. Kama uwakilishi uonekanao wa Kristo duniani, kanisa ni “Hekalu” la Mungu duniani.1. Kanisa kwa ujumla, na waamini binafsi, huitwa “Hekalu la Mungu.”

a. Kanisa huitwa “mwili moja wa Kristo,” na waamini binafsi “viungo” vya mwili ule (Rum 12:4-5; 1 Wakor 10:17; 12:12-27; Waef 1:22-23; 2:16; 4:4, 12; 5:30; Wakol 1:18; 3:15). Kwa hiyo, kama vile Kristo alivyouita mwili wake Hekalu, hivyo kanisa ni Hekalu. Katika 2 Wakor 5:1 Paulo hutumia lugha zote mbili “hekalu” na “hema”, kwa kuiita miili yetu, kimsingi, “makao ya hema yetu ya kidunia”b. Kanisa kiujumla huitwa wazi wazi Hekalu la Mungu (ona 1 Wakor 3:9, 16-17; 2 Wakor

35

Page 37:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

6:16-7:1; Waef 2:21; 1 Petr 2:5; Ufu 3:12; ona pia, Ufu 13:6 ambapo kanisa huitwa “Maskani yake”). “Maneno ‘hekalu la Mungu’ huonekana mara kumi zaidi katika Agano Jipya licha ya 2 Wathes [Math 26:61; 1 Wakor 3:16, 17a, 17b; 2 Wakor 6:16a, 16b; Ufu 3:12; 7:15; 11:1, 19], na, isipokuwa mara moja tu, daima huwa yanazungumzia kanisa. Ni mara moja tu huzungumzia hekalu lile lenyewe la Israeli lililopita au lijalo. Katika Mathayo 26:61 Yesu anukuliwa akisema, ‘Naweza kulivunja hekalu la Mungu na kulijenga kwa siku tatu.’ . . . Hekalu la kujengeka (la mikono) linatajwa ili kuonyesha kubadilishana kwa historia ya ki-ukombozi kuingia hekalu la siku za mwisho. Mathayo analiona hekalu lililojengwa likiharibiwa na kujengwa upya katika mwili wa ufufuo wa Yesu. . . . hekalu la zamani la Israeli lilikuwa, si chochote isipokuwa kivuli kitanguliacho cha Kristo na watu wake kama hekalu. Kwani, kumbuka, kusudio la msingi la hekalu lilikuwa ni mahali uwepo wa utukufu wa Mungu ulidhihirishwa duniani kwa watu wake. Sasa mradi Yesu ameshakuja kama Mungu katika mwili, Yeye sasa ni mahali ambapo uwepo wa Mungu unadhihirika duniani.” (Beale 2004: 275-76) Kwa umuhimu wa pekee, katika 1-2 Wakor “Paulo aliweza kuwaita waamini miaka ile ya 50 BK wakati Hekalu la Yerusalemu lilikuwa bado linasimama, kama hekalu la Mungu linalokaliwa na Roho” (Sweeney 2003: 629).14 Kwa hiyo, katika macho ya Mungu lile Hekalu la Yerusalemu tayari lilikuwa limeshabadilishwa, hata kabla halijahribiwa kiuhalisi na Warumi mwaka 70 BK. Katika 2 Wakor 6:16-7:1, baada ya kulinganisha kanisa na hekalu, 7:1 Paulo anahitimisha kwa kusema, “Kwa kuwa, tuna ahadi hizo.” Ahadi hizo ambazo anazinukuu katika 2 Wakor 6:16-18 ni pamoja na Walawi 26:11-12, 2 Sam 7:14, na Ezek 37:27, ambapo Mungu anaahidi kujenga nyumba na kukifanya imara kiti cha enzi cha Daudi milele na kuwa baba yake, na kuimarisha madhabahu yake na mahali pake pa kukaa milele na watu wake. Kwa kuhusisha ahadi hizo katika muktadha wa kuliita kanisa “hekalu la Mungu aliye hai” (2 Wakor 6:16) Paulo anasema, “Kuonekana kwa kiwango kitimilifu zaidi cha Ahadi ya Mungu, uwepo wa milele na wa kudumu wa Mungu, kuwasogeza watu wake kwake mwenyewe, na Yeye kwa watu wake milele:hizi ndizo ahadi ambazo zimetimilizwa katika kanisa—sisi ni hekalu la Mungu aliye hai” (Clowney 1972-73: 186). c. Kwa kuwa kanisa ni Hekalu lililo hai, lisilofanywa kwa mikono, kama ambavyo kila moja wetu ni “kiungo” cha “mwili” wa Kristo, kwa hiyo tunaitwa “mawe” mmejengwa muwe nyumba ya Roho” (1 Petr 2:5). Kwa njia hiyo hiyo, Waef 2:21-22 huzungumzia kuhusu kanisa kama hekalu ambalo “linajengwa,” lina“kua,” na ni “makazi ya Mungu katika Roho.” d. Waamini moja moja huitwa Hekalu (1 Wakor 6:19). Ni kwa kuunganika na Kristo tu ndipo mtu anaelezwa kuwa ni Hekalu.

2. Kanisa ni makazi maalum ya Mungu duniani. Kama ambavyo Hema ya kukutania na Hekalu lile la mwanzoni, kanisa limejazwa na uwepo wa Mungu (Math 18:20; 28:20; Yoh 14:17, 23; 20:22; Mdo 1:8; 2:1-11, 38-39; 4:31; 8:14-17; 10:44-47; Waef 3:19; 5:18; 1 Wakor 3:16; 6:19). Musa aliomba, “Ingekuwa heri kama watu wote wa BWANA wangekuwa manabii, na kama BWANA angewatia roho yake!” (Hes 11:29). Kuanzia siku ya Pentekoste, Bwana amelifanya hilo. Siyo tena Roho au karama zinawahusu wachache, lakini sasa katika kanisa Mungu amemimina Roho wake juu ya watu wake wote, bila kujali umri, jinsia, au rangi (Mdo 2:14-18). Petro hata anatumia mabaki ya lugha ya utukufu wa Mungu wa Shekina kujaza Hema ya kukutania ya AK na Hekalu pale asemapo, “Roho wa utukufu, na wa Mungu anawakalia” (1 Petr 4:14). Katika Hekalu jipya la kweli, Mungu siyo tu anakaa kati ya watu wake, bali sasa anakaa ndani ya watu wake. Zaidi ya hayo, Roho “huwatia muhuri” watu wake, tofauti na ilivyokuwa katika AK (Waef 1:13-14).Kwa hiyo, Mungu kamwe hataliacha Hekalu lake jipya, la kweli, lililo kanisa, tofauti na ilivyokuwa kwa Hekalu la zamani (Math 18:20; 28:20; Rum 8:33-39). 3. Kanisa lilipokea “moto” wa Mungu wakati wa kuanza kwake, kama ilivyotokea kwa hemaya kukutania, na Hekalu la Sulemani.

a. Wakati Haruni alipowekwa wakfu awe kuhani mkuu na kutoa dhabihu juu ya madhabahu katika Hema ya kukutania, moto ulishuka kutoka kwa juu kwa Bwana, na kuteketeza zile sadaka na sehemu zenye mafuta madhabahuni” (Walawi 9:24). Wakati Sulemani alipoweka wakfu lile Hekalu la kwanza, “moto ulishuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, na utukufu wa Bwana ukaijaza nyumba.” (2 Nyak 7:1). Huo utukufu wa Shekina wa Bwana uliiacha Hekalu kabla ya uvamizi wa Babeli (Ezek 9:3; 10:1-19; 11:22-23). Hakutajwi tena kwa ama Shekina kurudi upya, au moto kutoka mbinguni wakati Hekalu jipya lilipotengenezwa na Zerubabel baada ya uhamisho (ona Ezra 3-6; Hagai 1-2; Zek 2-4). b. Kutajwa kunakofuatia kwa “moto” ni wakati Yohana mbatizaji aliposema kwamba Yesu

14 “Tarehe za 1 Wak katika Mwango wa Hamsini wa karne ya kwanza haujadiliwi sana” (Sweeney 2003: 629n.116).36

Page 38:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

“atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto” (Math 3:11; Luka 3:16). Hilo lilitokea Siku ya Pentekoste ambapo “Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.” (Mdo 2:2-4) La muhimu zaidi, wakati ambapo sadaka za kuteketezwa katika Hema na Hekalu ziliteketea kwa ule moto, moto haukuwateketeza wanafunzi katika Siku ile ya Pentekoste, kwa sababu tunapaswa tuwe “dhabihu iliyo hai, takatifu” (Rum 12:1).

4. Ingawa Hema na hekalu chini ya Agano la Kale vilifanywa na wanadamu, Hekalu jipya, la kweli la kanisa, na waamini moja moja, ndio kimsingi sehemu ya mbinguni na roho— “lililojengwa na Mungu, lisilofanywa kwa mikono” ( 2 Wakor 5:1-5; ona pia, Mdo 7:44-50 ). Ufunuo 11 hulitazama kanisa katika Hekalu la mbinguni na uhalisi wenyewe, ingawaje kwa sasa lipo katika kukutana na magumu hapa duniani. Ufu 11:1-2 panazungumzia kuchukua vipimo vya “Hekalu la Mungu.” Hilo linaleta picha kutoka Ufu 3:12 ambapo Yesu anasema, “Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa.” Ufu 11:4 hutaja “vinara,” ambavyo hapo mwanzo vilikuwa vimeelezwa katika Ufu 1:20 kuwa ni makanisa. Ufu 11:4, ambapo hujadili “vinara viwili” na “mizeituni miwili” pia huleta picha kutokea Zekariah 4. Katika kifungu kile, “kinara” kilielezwa kuwakilisha Hekalu ambalo lilikuwa limeanza (ona, Zek 4:2, 4-10) na “mizeituni” ilielezwa kuwa ni wawili “walioteuliwa” (huenda ni Yoshua kuhani mkuu na Zerubabeli mfalme, ambao ndio lile Hekalu lilijengwa upya chini yao baada ya uhamisho kutokea Babeli) (ona, Zek 4:3, 11-14). Hali hii ya majukumu mawili ya kanisa kama kuhani na wafalme huthibitishwa katika Ufu 1:6; 5:10, na 20:6. Ufu 13:6 huendelea kuonyesha zaidi kwamba, kama ilivyo katika Ufu 11:7-10 ambapo waamini wanaweza kuuawa kimwili duniani, hata hivyo, makazi yao ya kweli, hema yao ya kweli, ni mbinguni. Ufu11:19 panaeleza kwamba “Hekalu la Mungu” “liko mbinguni.” Kwa jinsi iyo hiyo ni Waef 2:6 panaposema kwamba Kristo “akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu.”5. Ingawaje katika Hema na Hekalu la AK, ni makuhani peke yao waliweza kuingia lile jengo; katika Hekalu jipya, la kweli la kanisa, waamini wote ni wafalme na makuhani watakatifu ( 1 Petr 2:5, 9; Ufu 1:6; 5:10 ). Katika AK, kuhani alipaswa atimize sifa kuu mbili: ilikuwa lazima awe wa kabila la Yuda, na hakutakiwa awe na dosari yoyote mwilini mwake (Walawi 21:16-24; Hes 4:1-4; 8:23-26; 1 Nyak 23:24-32). “Wale waliokuwa wametimiza hizo sifa mbili walivalishwa vazi jeupe, na majina yao yaliandikwa vizuri” (Edersheim 1988: 95). Hili linajitokeza katika Ufu 3:5 likiwazungumzia waamini: “Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima.” Zaidi ya hapo, kile kitambaa cha kifuani cha makuhani “kilifanyizwa kwa ‘kitani’ au, kwa usahihi zaidi, ‘byssus,’ kile kitambaa cheupe sana cha pamba king’aracho kutoka Misri” (Ibid.: 97). Vivyo hivyo, Ufu 19:8 panasema kwamba bibi arusi wa Kristo (kanisa) amevikwa “kitani safi [Kiyunani = bussinos], king’aracho, kisafi; kwa kitani safi [bussinos] ambayo ni matendo ya haki ya watakatifu.”

a. Kuhani wetu mkuu ni Yesu Kristo, aingiaye pasipo mipaka, na ambaye yuko, aliye hekalu la kweli la mbinguni la Mungu (Waeb 4:14-5:10; 7:1-10:25).b. Tofauti na hema na hekalu la mikono, sisi nasi twaingia pasipo mipaka kwa Mungu, Baba yetu, kupitia Yesu Kristo (Math 27:51; Waeb 10:19-22). c. “Dhabihu” tunazozitoa katika Hekalu jipya, la kweli, ni miili yetu na maisha yetu (Rum 12:1), sifa zetu na shukurani (Waeb 13:15), utoaji wa fedha zetu kuiendeleza Injili na kuwasaidia masikini na wahitaji (2 Wakor 9:1, 12-13; Wafil 4:18), na “dhabihu za rohoni” za maisha yetu ya uaminifu katika utumishi kwa Kristo na kwa wanadamu wenzetu katika Jina lake (Rum 15:16; Waeb 13:16; Yak 1:27; 1 Petr 2:5).d. Kwa vile waamini wote ni “makuhani” katika Hekalu hili jipya, la kweli, la Mungu, tunatakiwa tuwe watakatifu katika mienendo yetu yote ya maisha yetu, kama vile wale makuhani wa AK walivyotakiwa kuwa watakatifu (1 Wakor 3:17; 6:12-20; 2 Wakor 6:14-7:1; Yak 1:27).

6. Kama lilivyokuwa Hekalu la AK, kanisa kama Hekalu jipya, la kweli la Mungu, lina sifa za kuwa na dhahabu, fedha, na mawe yake ya thamani. Katika 1 Wakor 3:10-12 Paulo, katika kumzungumzia Kristo na matendo ya imani, azungumzia kuhusu “msingi,” na kisha kujenga juu yake kwa “dhahabu, fedha, mawe ya thamani.” Sehemu nyingine pekee katika Maandiko ambayo “msingi” wa jengo unajengwa kwa “dhahabu,” “fedha,” na “mawe ya thamani” ambapo “pamejengwa” hivyo ni Hekalu la Sulemani (1 Waf 5:17-6:36). Kwa vile Hekalu hili jipya, la kweli, ni Hekalu lililo hai, basi dhahabu,

37

Page 39:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

fedha, na mawe ya thamani ni matendo ambayo tunayatenda katika maisha haya kujengea ufalme na kuwasaidia masikini na wahitaji (1 Wakor 3:9-17).7. Kanisa ni chombo cha Mungu kutimiza mpango wa Mungu kuifanya dunia iwe maskani iliyojazwa na watu watakatifu ( Math 28:18-20; Mdo 1:8; Ufu 5:9; 7:9 ). Hilo lilikuwa kusudio la awali la Mungu katika Bustani ya Edeni na liliigizwa kwa mfumo wa muundo Hema ya kukutania na Hekalu katika Yerusalemu. Kadiri kanisa linavyokuwa aminifu kwa utume wake wa “enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu” (Math 28:19), mpango huo unadhihirika zaidi na zaidi duniani. Kuenea ulimwenguni kote kwa utume wa Kristo kunaonekana kwa njia mbili:

a. Hakuna mipaka ya Kijiografia kwa ufalme wa Kristo. Hema na Hekalu la Yerusalemu vilikuwa na mipaka ya kimazingira kwa mahali yalipokuwepo. Ilibidi watu waje hapo ili kumwaabudu Mungu katika Hekalu. Hata hivyo, katika Yohana 4:21, 23 Yesu alisema, “Saa inakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. . . . Lakini saa inakuja, nayo saa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli.” Katika Kristo, Mungu amekuja kwa watu wake zaidi kuliko kinyume chake. Kwa hiyo, Yesu alisema, “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao” (Math 18:20).b. Hakuna mipaka ya kibaguzi kwa rangi, jamii, au ya kikabila kwa ufalme wa Kristo. Katika Agano la Kale Israeli ndio “wateule” wa Mungu (Kumb 7:6). Chini ya Agano la Kale, Wayahudi na Mataifa walikuwa mbali mbali. Katika Hekalu lile la mikono kulikuwa na ukuta kabisa wa kuwatenganisha Wayahudi na Mataifa. Pia kulikuwa na maeneo yaliyotengwa kwa wanaume na wanawake, makuhani na watu wa kawaida. Katika hekalu jipya, la kweli, la kanisa, mgawanyiko kati ya Wayahudi na Mataifa umeondolewa. Wote kama “mtu mmoja” kanisa “linakua kuwa hekalu takatifu katika Mungu” (Waef 2:11-22; ona pia Rum 3:22; Wagal 2:11-14). Katika Kristo, bila kujali jinsia ya mtu, jamii uliyotokea, hali ya kiuchumi, lugha, au sifa nyingine za kimwili (1 Wakor 12:13; Wagal 3:28; Wakol 3:11; Ufu 5:9; 7:9).

8. Mateso ya kanisa ni sehemu ya hukumu ya Mungu kwa “Hekalu” yake mwenyewe ( 1 Petr 4:12-17 ). Katika 1 Petr 4:14 Petro alitumia lugha inayokumbushia utukufu wa Mungu wa Shekina ulioshuka katika Hema na Hekalu la AK pale alipoelezea “Roho wa utukufu na wa Mungu” kukaa juu ya kanisa. Matamshi hayo yalinenwa katika muktadha wa “kuudhiwa,” “kujaribiwa,” “mateso,” na “kuchukiwa” (1 Petr 4:12-16). Petro anahitimisha, “Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika [nyumba] ya Mungu” (1 Petr 4:17). Neno la Kiyunani analolitumia ni oikos, ambalo linaweza kutafsiriwa ama “nyumba ya kukaa” au “nyumba.” Katika 1 Petr 2:5 neno hilo hilo wazi wazi huzungumzia kanisa kama “nyumba ya roho” mpya (hekalu) la Mungu. Ingawa tafsiri nyingi huiita “nyumba ya kukaa” katika 1 Petr 4:17, maelezo nyuma ya kifungu huonyesha kwamba tafsiri njema zaidi hapa ingelikuwa ni “nyumba,” kama “hekalu”: “Picha inaundwa kutoka kauli mbili za vifungu vya AK ambazo huzungumzia kazi ya hukumu ya Mungu kuanzia Hekalu la Yerusalemu (Ezek. 9; Mal. 3:1-5). Petro sasa anachukua mafundisho haya ya kimaandiko na kuyatumia bila kusita kwa Kanisa. Jamii ya Kikristo hivyo hurithi siyo tu fursa njema, bali pia wajibu uhusikao wa Hekalu la Yerusalemu (mahali pa kwanza kushuhudia hukumu ya Mungu). Huu ulikuwa ni mfano ulio wazi wa jinsi Kanisa linavyotakiwa kukwepa majivuno na siku zote kutumia dhana ya ki-Biblia ya hukumu kwanza kabisa juu yake lenyewe. Siku zote ilionyesha wazi kwamba Kanisa lilikuwa na haki kujiona lenyewe kama mrithi wa kweli wa uhalisi huu wa AK. Wakristo walikuwa ni Hekalu jipya.” (Walker 1996: 311; ona pia Johnson 1986: 285-94)

G. Ufunuo wa Mbingu Mpya na Nchi Mpya (Ufunuo 21-22).1. Yerusalemu Mpya ni utimilifu wa mpango wa milele wa Mungu wa kukaa katika mahali patakatifu pamoja na watu watakatifu, ambao walitangulizwa kama kivuli na Bustani, Hema ya kukutania, na Hekalu.

a. Jumuisho la Yerusalemu Mpya ni Patakatifu pa Patakatifu.(1) Kama ilivyokuwa Patakatifu pa Patakatifu (1 Waf 6:16-20; 2 Nyak 3:8), mji huo ni mraba wa pembe nne kamili (Ufu 21:16). (2) Kama ilivyokuwa Patakatifu pa Patakatifu palitandikwa na dhahabu safi (1 Waf 6:16-20; 2 Nyak 3:8), “mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi” (Ufu 21:18).(3) Kama ilivyokuwa Patakatifu pa Patakatifu ulivyokuwa mahali maalum pa uwepo wa Mungu na utukufu wake, mji huu sasa ni mahali pa uwepo wa Mungu na utukufu wake (Ufu 21:22-23; 22:1, 3-5).

38

Page 40:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

(4) Kwa hiyo, ni Patakatifu pa Patakatifu tu, siyo sehemu nyingine za Hekalu la Israeli (m.y., Mahali patakatifu na ukumbi wa nje), panapatikana katika Ufunuo 21. Sababu ni uwepo maalum wa Mungu, ambao kwanza uliishia Patakatifu pa Patakatifu, sasa unaenea uumbaji wake wote mpya .

b. Yerusalemu mpya hutimiliza na kuzidi vyote viwili Patakatifu pa Patakatifu na hata kanisa la sasa kuhusiana hasa na ukaribu wa Mungu.

(1) Ni Adamu na Hawa peke yao katika Edeni, na ni makuhani wakuu peke yao walioweza kuingia Patakatifu pa Patakatifu. Katika Yerusalemu Mpya, watu wote wa Mungu hawana dhambi na wako Patakatifu pa Patakatifu ya Yerusalemu Mpya, na watamtumikia Bwana na kutawala milele na milele (Ufu 21:7-8, 27; 22:3-5). (2) Katika Siku ya Utakaso—siku pekee ambapo kuhani mkuu aliweza kuingia Patakatifu pa Patakatifu—kuhani mkuu alitakiwa achome uvumba ambao ulisababisha wingu kubwa lililojaza kiti cha rehema ili kwamba asiweze kuuona uso wa uwepo wa utukufu wa Mungu, ama sivyo angelikufa ( Walawi 16:13; ona Kut 33:20 ). Katika Yerusalemu Mpya watu wote wa Mungu wata“uona uso wake” (Ufu 22:4).(3) Hata katika kanisa lilivyo sasa, ni kuhani wetu mkuu, Yesu Kristo, aliye na uwepo usio na mipaka katika hema ya kweli ya mbinguni ya Mungu ( Waeb 4:14-5:10; 7:1- 10:25 ). Sasa tunao mlango wazi kwa Mungu usio na mipaka Baba yetu, kupitia Yesu Kristo (Math 27:51; Waeb 10:19-22). Katika Yerusalemu Mpya siyo tu tuna mlango wazi kwa Mungu, bali siku zote tunakuwa katika uwepo wake moja kwa moja (ufu 21:3-4, 22-23; 22:3-5).

c. Katika Ufu 3:12 Yesu aliahidi, “yeye ashindaye, nitamfanya nguzo katika hekalu la Mungu wangu.” Kifungu hicho “hakizungumzii mahekalu ya kipagani au hekalu la Sulemani katika Yerusalemu (1 Waf 7:15-21; 2 Nyak 3:15-17) bali kuhusu Yerusalemu Mpya ushukao kutoka mbinguni. Hii maana yake ni kwamba watakatifu wanatunukiwa heshima hiyo ndani ya hekalu hilo la kimbingu, ambalo kusema ukweli si chochote pungufu ya uwepo wa Mungu wenyewe. . . . Kwa kifupi, maneno ‘hekalu’ lazima yatafsiriwe kiumbo. Mungu anakusudia kutunuku watu wake katika uwepo wake mtakatifu.” (Kistemaker 2000: 434)

2. Sifa nyingine za Yerusalemu Mpya huonyesha kwamba hutimiliza miktadha mingine ambayo ile Bustani, Hema ya kukutania, na Hekalu vilitanguliza kivuli chake.

a. Kama ambavyo Mungu mwenyewe“akapanda bustani” ya Edeni (Mwa 2:8), na kutoa maelekezo ya Hema ya kukutania na ya Hekalu ambayo yaliendana na uhalisia wa kimbinguni, sasa Yerusalemu Mpya “ukishuka chini kuja kwenye nchi mpya iliyofanywa upya] kutokea mbinguni kwa Mungu” (Ufu 21:10; ona pia Rum 8:18-21).b. Kama ilivyokuwa Edeni, Hema ya kukutania, na Hekalu zilivyokuwa zimesifika kwa dhahabu na mawe ya thamani, ndivyo Yerusalemu Mpya inasimulika kwa dhahabu zake na mawe yake ya thamani (Ufu 21:18-22).c. Kama vile Edeni, Hema ya kukutania, na Hekalu zilivyokuwa zimesifika kwa mimea yake (au mwonekano wa kibustani kwa jinsi ya mimea), ndivyo Yerusalemu Mpya inasifika kwa miti yake ya matunda (Ufu 22:2). d. Kama ambavyo Bustani ilikuwa na mti wa uzima, ndivyo Yerusalemu Mpya una mti wa uzima (Ufu 22:2).e. Kama vile Edeni na Hekalu la Ezekieli zilivyokuwa mwanzo wa mto, ndivyo Yerusalemu Mpya una “mto wa maji ya uzima wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo” (Ufu 21:6; 22:1).f. Kama ambavyo kuhani mkuu katika Hema ya kukutania na Hekalu walivaa bamba lililochorwa na kuandikwa “Mtakatifu kwa Bwana” katika paji la uso wake (Kut 28:36-38), ndivyo katika Yerusalemu Mpya watu wote wa Mungu watakuwa na“jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao” (Ufu 22:4). g. Kama vile hakukuwa na mauti, majonzi, wala maumivu, katika Bustani ya Edeni kabla ya Anguko katika dhambi, ndivyo Yerusalemu Mpya hakuna tena, mauti, au machungu, wala maumivu (Ufu 21:4; 22:3).h. Kama vile Mungu “alivyotembea katika bustani” (Mwa 3:8), na kupajaza Patakatifu pa Patakatifu katika Hema ya kukutania na hekalu na uwepo wake, ndivyo itakavyokuwa Yerusalemu Mpya. “Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao” (Ufu 21:3).

39

Page 41:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

3. Ufunuo 21 huonyesha kwamba “Yerusalemu Mpya” NI “nchi mpya.” Yohana anaanza kwa kuelezea “mbingu mpya na nchi mpya” (Ufu 21:1), lakini kisha mara huelezea “mji mtakatifu, Yerusalemu Mpya” (Ufu 21:2-3; 10-22:5). Mkazo wa Yohana kutoka Ufu 21:2 na kuendelea, ni katika mji, na si kwa chochote nje ya huo au kuongeza kingine zaidi ya huo. Kuhusian kwa Yerusalemu Mpya na nchi mpya huunganishwa zaidi kwa yafuatayo:

a. Mkondo wa “kuona-kusikia” unaoonekana katika Ufu, ambapo, kile Yohana aonacho hutafsiriwa baadaye kwa kile asikiacho (au kinyume chake), unaonyesha kwamba Yerusalemu Mpya ni sawa na mbingu mpya na nchi mpya.

(1) Katika Ufu 21:1 Yohana aliona “mbingu mpya na nchi mpya.” Hilo lilifuatiwa na maono yake ya “mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu” ( 21:2 ). Katika 21:3 Yohana kisha “akasikia sauti kubwa” isemayo “Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao.” Kile kinachoonekana kutokea ni kuwa, maono ya pili (21:2) yanatafsiri ya kwanza, na kile kinachosikiwa kuhusiana na maskani mapya (21:3) hutafsiri wazi wazi zaidi mistari yote miwili—m.y., mbingu mpya na nchi mpya za 21:1 hushabihiana na Yerusalemu mpya ya 21:2, na zote mbili zinashabihiana na maskani mapya ya 21:3.(2) Mkondo huo huo wa mrandano ulitokea katika Ufu 5:1-10 . Katika kifungu hicho, Yohana aliona kitabu. Kisha akamsikia mojawapo wa wazee akisema kuwa “Simba aliye wa kabila la Yuda” amestahili kukifungua kitabu (5:5). Hata hivyo, kitu kinachofuatia ambacho Yohana aliona hakikuwa simba, bali “Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa,” (5:6). Alikuwa ni Mwana-kondoo aliyekichukua kitabu na ndiye aliyestahili kukifungua (5:7-10). Kwa hiyo, Mwana-Kondoo ni sawa na Simba (na zote hizo ni picha za Yesu Kristo).

b. “Kiti cha enzi cha Mungu,” ambacho sehemu nyingine katika Biblia hutajwa kuwa kiko mbinguni, sasa chanenw akuwa kiko katikati ya watu wa Mungu katika Yerusalemu Mpya. Kila mahali katika Biblia, “kiti cha enzi cha Mungu” husemekana kuwa kiko mbinguni (ona 1 Waf 22:19; 2 Nyak 18:18; Zab 103:19; Isa 6:1; 66:1; Math 5:34; 23:22; Mdo 7:49; Waeb 8:1; Ufu 4:2-10; 5:1-13; 6:16; 7:9-15; 8:3; 12:5; 14:3-5; 16:17; 19:4-5; 20:11). Katika Ufu 22:1-3 Kiti cha enzi cha Mungu chasemwa kiko katika Yerusalemu Mpya. Kwa hiyo, Yerusalemu Mpya yaonekana kama ni sawa na mbingu mpya na nchi mpya.c. Ufu 21:27 panasema kuwa “Na ndani yake [mji huo] hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge wala yeye afanyaye machukizo na uongo.” Kwa jinsi hiyo hiyo ni Ufu 22:15 ambapo panasema kwamba “Huko nje [ ya mji] wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.” Mistari hiyo huenda inamaanisha kwamba hakuna mtu yeyote aliye mdhambi anaruhusiwa kuingia mbingu mpya na nchi mpya, kwa sababu Ufu 21:8 hutumia lugha ile ile, na kusema “Bali waongo, na wasioamini, na wachukizao, wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”d. Ufu 21:27 pia husema kwamba “bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.” Wataweza kuingia katika mji huo. Hilo pia humaanisha ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo wataweza kuingia mbingu mpa na nchi mpya, kwa sababu Ufu 20:15 panasema kwamba, “Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.”e. Ule usawa wa“mbingu mpya na nchi mpya” na “Yerusalemu Mpya” katika Ufunuo 21 unaonyeshwa kwa usambamba wa matumizi ya maneno haya ya Isaya 65-66. “Ufunuo 21:1-2 hufuatisha mkondo wa Isaya 65:17-18. Kwa vile Isaya 65:17 hujitokeza wazi wazi katika Ufunuo 21:1, ni dhahiri kuelewa kuwa Yerusalemu Mpya wa Ufu 21:2 pia hutoa mwangwi wa Isaya 65:18 na ni sawa na ‘mbingu mpya na nchi mpya’ za Ufunuo 21:1! . . . Matokeo yake, uumbaji mpya na Yerusalemu mpya si kitu kingine isipokuwa maskani ya Mungu, hekalu la kweli la Mungu la uwepo wake maalum linaloonyeshwa kila mahali katika sura ya 21. (Beale 2004: 368) Mahali pekee katika AK ambapo “mbingu mpya na nchi mpya” hutajwa ni katika Isa 65:17 na 66:22. Katika Isaya 65-66 “Yerusalemu” huonekana kuwa sawa na “mbingu mpya na nchi mpya,” kwa sababu zifuatazo:

(1) Isa 65:17-18 huonyesha kuweka usawa kati ya “mbingu mpya na nchi mpya” na “Yerusalemu.” Isa 65:17 panasema, “Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya; na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni.” Isa 65:18 kisha mara husema, “Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo; maana,

40

Page 42:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

tazama, naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha.” Vivyo hivyo, mpangilio wa lugha ya “tazama, naumba” umetumiwa kwa yote mawili mbingu mpya na nchi mpya” na “Yerusalemu” katika 65:17-18. Sehemu ya kwanza ya 65:18 (“Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo;”) huzungumzia kile ambacho Mungu “anaumba,” ambacho tayari kimeshatajwa katika 65:17 kuwa ndiyo “mbingu mpya na nchi mpya,” lakini 65:18 kisha tena husimulia kile ambacho Mungu “anakiumba” kama“Yerusalemu.”Katika 65:18 Mungu hata husema “furahini, mkashangilie” kwa kile akiumbacho (m.y., kile ambacho amekwisha kukieleza kama “mbingu mpya na nchi mpya”), lakini kisha husema “Yerusalemu” imeumbwa kwa ajili ya “kufurahia” na watu wake “kushangilia.”(2) Isa 65:19-66:24 huonekana kuoanisha “mbingu na nchi” na “Yerusalemu.” 65:19-25 hutanguliwa kwa kuutaja “Yerusalemu,” bali kisha huzungumzia mazingira ambayo bila shaka yatakuwepo katika “mbingu mpya na nchi mpya.” 66:1-2 huzungumzia “mbingu” na “nchi” kutumia lugha ya “hekalu” (m.y., “Mbingu ni kiti changu cha enzi na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu”) na huonekana kuhusisha nyuma na kile ambacho kilishasemwa kuhusu “Yerusalemu,” tangu 66:1 huanzia na “Kwa hiyo” na 66:2 panasema“Maana mkono wangu ndio uliofanya hivyo vyote.” Zaidi, 66:3-21 huhusisha kile ambacho Mungu amekwisha kukizungumzia kuhusu “mbingu” na “nchi,” bali hujadili mazingira gani yatakuwepo ya utoaji wa dhabihu za ki-Hekalu na Yerusalemu. Isa 66:22 ndipo kisha huzungumzia kuhusu “mbingu mpya na nchi mpya,” lakini huhusisha hilo nyuma na kile ambacho tayari kimekwisha kusemwa kuhusiana na Yerusalemu kwa kuanzisha mstari kwa neno“Kwa maana.” Hatimaye, katika Isa 66:23 Mungu anaendelea mbele akitumia lugha ya “ki-Hekalu”, na kusema “Wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu.” Hilo linaonyesha tukio kutendeka mahali maalum kama vile hekalu katika Yerusalemu. Kwa hiyo, ‘mbingu mpya na nchi mpya” huomyesha kuwa sawa na“Yerusalemu,” na hata na hekalu la Yerusalemu.

f. Ule usawa kati ya“mbingu mpya na nchi mpya” na “Yerusalemu mpya unaonyeshwa na lengo la Mungu kila mahali katika historia ya Biblia: kujaza kila sehemu ya uumbaji wake na uwepo wake. Kuanzia Bustanini pale Edeni, Mungu alikuwa na shauku ya kuifanya dunian yote makzi yake, na kwamba angekuwa na ushirika na watu wake watakatifu. Kwa sababu ya dhambi, utukufu wa Mungu haukuweza kukaa kabisa katika uumbaji wa awali. Kwa hiyo, ingawaje alitembea katika Bustani na Adamu na Hawa (Mwa 3:8), kutokana na dhambi zao, aliwaondoa kutoka katika Bustani ile (Mwa 3:24). Kisha Mungu taratibu akaufunua uwepo wake maalum duniani kati kati ya watu wake katika hema ya kukutania na katika hekalu la Sulemani, ambayo yanaweza kuwa ni vielelezo vya mbinguni na nchi, na vilifanya kazi kama “mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni” (Waeb 8:5; ona pia Zab 78:69; Waeb 8:1-10:1). Kisha akaanzisha hatua ya mwisho ya uwepo wake katika mwanadamu Yesu Kristo. Kupitia kukaa kwa Roho Mtakatifu ndani ya watu wake, kanisa, uwepo wake sasa umeenea dunia nzima. Ule wakati wa “vivuli” vya mahekalu yaliyofanywa kwa mikono ya wanadamu umekwisha, na wakati wa hekalu jipya, la kweli—uwepo wake halisi katika Kristo na kanisa—umewadia. Hata hivyo, ingawaje uhalisi wa kweli wa kiroho ambao Maskani ya AK na hekalu umeshaanzishiwa, bado haujatimilika. Kutimilika huko kutatokea wakati Kristo ataporudi duniani. Atakapofanya hivyo, uumbaji wote utakombolewa (Rum 8:15-25). Wakati dhambi itakuwa imeodnolewa milele kutoka katika uumbaji huo, dunia nzima (“mbingu mpya na nchi mpya”) zitakuwa bustani/mji/hekalu mfano wa Edeni —mahali mahususi palipokamilika kwa uwepo wa utukufu wa Mungu. Kwa hiyo, uumbaji wote utakuwa Patakatifu pa Patakatifu papana sana (Ufu21:16). Hakutahitajika tena uhitaji wa kuuweka utukufu maalum wa Mungu katika jengo la mikono, badala yake Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo wenyewe wataujaza, siyo sehemu ya uumbaji, ulimwengu wote (Ufu 21:22).

II. Uhusiano wa Mungu na Watu Wake Katika Maswala ya Ndoa.

A. Mwa 2:23-24 (mwanamke kuumbwa rasmi kwa ajili ya mwanaume;mwanaume kuwaacha babaye na mamaye na kuunganishwa na mkewe na kuwa “mwili moja” naye) ni mfano unaoelezea uhusiano ambao Mungu anautaka kwa watu.

1. Adamu na Hawa mwanzoni walitembea kwa umoja na mshikamano kati yao kila moja na kwa

41

Page 43:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Mungu katika Bustani ya Edeni. Dhambi (Mwanzo 3) iliharibu uhusiano mzuri na mshikamano kati ya watu na Mungu.2. Mpango wa Mungu wa ukombozi, kama ambavyo unafunulika katika Biblia nzima, umeandaliwa kurejesha unganiko la ndoa lililo kamili, lenye mshikamano kati ya Mungu na watu wake. Kwa hiyo, Yesu “alimwacha Baba yake” (Mwa 2:24; ona Wafil 2:6-8), ili kurejesha unganiko kamili kati ya Mungu na watu wake katika mahusiano kati ya Kristo na bibi–arusi wake, Kanisa.

B. Katika AK kiungo cha ndoa kati ya Mungu na watu wake kiliwekwa, lakini Israeli hakuwa mwaminifu. 1. Uhusiano wa Israeli na Mungu ukawa umefunikwa na tabia hasa za “kufanya uzinzi kwa miungu mingine.” Kufanya uzinzi” na miungu mingine ni “kufanya uhusiano nao, kujitoa kwao ili kuitii na kuifanyia ibada yao, kuenenda kwa njia zao na kufuata mashauri yao. . . . sura hiyo iko katika muundo wa tendo la ndoa . . . kwa sababu sehemu kubwa yenye udhibiti ni ya kindoa” (Ortland 1996: 32).2. Kuanzia mwanzo wake kupitia kipindi cha ufalme uliounganika, Israeli walikuwa si waaminifu.

a. Katika Kut 34:11-16, mara baada ya Israeli kufanya ibada ya sanamu kwa ndama wa dhahabu wakati Musa alipokuwa anapokea zile amri 10 kutoka kwa Mungu, Mungu alizitaja ibada za kipagani kama “kivutio cha ukahaba chenye urahisi mkubwa wa kueneza ushawishi wake kwa wengine” (Ortland 1996: 32). Kusema ukweli, wakati Musa alipokuwa anapokea zile amri 10 kutoka kwa Mungu kwa mara ile ya kwanza, watu walianguka katika dhambi kulingana na mambo yale yale ambayo yalikuwa yanakatazwa na zile amri 10 zenyewe. (Kut 32:1-6). Hiyo ni kama mtu kufanya uzinzi usiku huo huo wa kufungia ndoa!b. Katika Walawi 17:3-7 na 20:4-6, Mungu alipowapatia Israeli Sheria za Walawi, aliwaonya tena watu kuhusu uovu na hatari ya kuifuata miungu ya uongo, akiita “kufanya uzinifu.” Katika Walawi 20:6 aliongeza mapana ya maonyo zidi ya kuabudu miungu mingine, na hata kuingia katika tabia za kuagua na utambuzi kupitia wanadamu wengine. Kwa hiyo, “kuwaendea wapunga pepo na wale wachezeshao mizimu pia hujumuishwa katika ukahaba, kwa sababu kama ilivyo katika kuabudu sanamu, kueleza moyo kwenye utendaji wa hao ni kukataa uwezo wa Yahwe, mwenye uweza wote” (Ortland 1996: 37).c. Katika Hes 15:38-40 watu waliwasikiliza wale wapelelezi10 badala ya kumsikiliza Yoshua na Kalebu. Mungu tena anaonyesha tabia ya “kufanya uzinzi” kwa kuchanganya “njia zote za kushibisha mioyo na tamaa za macho . . . akihusisha bila kuweka mipaka vishawishi vyote ambavyo vinaweza kufikirika, vinavyopokeleka na kuburudishwa kupitia njia za fahamu” (Ortland 1996: 39).d. Katika Kumb 31:14-21 Musa alimwinua Yoshua kama atakayemrithi baada yake. Mungu alimwonya Musa kwamba, hata pale kabla hawajaingia katika ile nchi, watu walikuwa na msukumo mkubwa wa uzinzi katika nchi waliyokuwa wamaiendea, na upotofu wa kiasi hicho utawaletea “matatizo na mabaya mengi.”e. Katika Waam 2:16-17; 8:22-35, nyakati za vipindi vya waamuzi watu tena na tena walisahau matendo ya Mungu ya ukombozi na hawakusikiliza waamuzi ambao Mungu aliwainulia. Badala yake, mara waliigeukia miungu ya maadui zao ambao Mungu alikuwa amewashindia! Ukweli kuwa “mara” waligeukia mbali na Mungu kuelekea miungu ya sanamu kunaonyesha undani wao ambao ni kuvutiwa na miungu ya Wakanaani na mtazamo wao wa kutomjali Yahwe. Hakika, kwa Gideoni, walidiriki hata kutengeneza sanamu ya naivera ya Gideoni (Waam 8:27). Hilo bila shaka liliwazoelea watu akilini kiasi kwamba“mara Gideoni alipokufa” kwa mara nyingine “wakarudia uzinzi” kwa miungu mungine (Waam 8:33). f. Katika Nyaraka za Hekima (m.y., Zab 50:18; Mith 6:26-32; 7:1-27; 30:20) uasherati na uzinzi huwekwa katika kundi la ujinga, dhambi, na mauti. Mambo hayo hummwondosha mtu katika agano na Mungu.

3. Wakati wa kipindi cha ufalme uliogawanyikana, Mungu alikemea yote mawili- kutokuwa na uaminifu kwa Israeli na Yuda.

a. Ufalme wa Kaskazini (Israeli). Mungu kimsingi alimtuma nabii Hosea (kwenye mwaka 750 KK) ambaye siyo tu alionya Israeli isiandamie miungu mingine, bali alitakiwa atende kiuhalisia ile hali ya Mungu kuikataa tabia ya Israeli kuabudu sanamu kwa yeye mwenyewe kumwoa malaya au kahaba (Hosea 1-2). Mungu aliikataa nchi ile nzima kwa “nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana” (Hos 1:2). Licha ya uzinzi wa Israeli kinyume na Mungu, na adhabu ambayo ataileta, hata hivyo alijiridi kwa uaminifu mkuu na upendo wake mwingi kwake, akausia ili watubu, na kuwawekea matumaini ya kurejezwa katika siku zake za baadaye. (Hos 2:1-3, 14-23; 11:1-11; 14:1-9). Nabii Mika (miaka ya 750-686 KK), alipinga zaidi tabia

42

Page 44:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

ya uzinzi wa Israeli ambao aliulinganisha na ukahaba, na ambao ungewaletea maangamizo makuu (Mika 1:1-7).

(1) Jambo la msingi ambalo Israeli walikabiliana nalo. “Katika hili utoshelevu wote wa Yahwe, huenda kukiwa na swali labda liko namna hii: Ni wapi maisha, katika utajiri wake wote na utoshelevu wake, hutokea? Je hutokea kwa Yahwe peke yake, au kutoka kwa Yahwe pamoja na wengineyo? Kama yanatokea kwa Yahwe peke yake, basi ndipo hapo mtu atamgeukia yeye na kumtii yeye tu kwa maisha hayo. Lakini kama yanatokea kwa Yahwe pamoja na kwingineko, basi hapo mtu atatanua uwanda wa mategemeo, kwa sababu Yahwe peke yake hatoshi.” (Ortland 1996: 49)(2) Aina mbali mbali za uzinzi wa Israeli ni pamoja na umwagaji wa damu za wasio na hatia, hii iliigwa na dersturi za kidini za Wakanaani, kujitosheleza kiuchumi, kutowajali masikini, na kutafuta usalama wa kisiasa katika siasa za mlengo wa “reali-politiki” (kufungamana na Misri na Ashuru) badala ya utii kwa Mungu ( Hos 4:1-10:15; 1:12-13:16 ). Reali-politiki (m.y., msingi wa siasa unaotokana na kuzingatia uwezo wa nguvu na mambo ya kimatendo kuliko kanuni au maadili) ni “ukahaba Kwa Mungu” kwa sababu huonyesha ushahidi wa “hali ya msimamo wa kujitoa kuwaegemea wengine katika namna ya ‘lolote liwalo’ . Uzinzi wa kiroho huhusisha zaidi ya makosa ya kidini; popote itokeapo kwamba Mungu hategemewi kikamilifu na kutiiwa ipasavyo; kuchanganya na mazingira ya kisiasa, watu wake hukataa utoshelevu wa uangalizi na ulinzi wake, kwa hiyo wanajiamulia wenyewe, kwa mipango yao wenyewe.” (Ortland 1996: 52) Kusema ukweli, kama Hos 2:4-5, 13 panavyotuambia, tofauti na makahaba wengine, ambao wateja wao huwa wanawafuata wenyewe, Israeli iliamua kwa nguvu zake zote kuwafuatia “wapenzi” wake wengine na kumsahau Mungu. Hata hivyo, vitu pekee ambavyo wapenzi wake wapya walimpatia vilikuwa ni vya kidunia [kwa kiwango kikubwa ni kama kile kikitwacho “injili ya mafanikio”], kuliko mambo ya juu zaidi ambayo Mungu peke yake (ambaye pia ni mmiliki pekee wa vitu vyote vya duniani) anaweza kuvitoa.(3) Kama matokeo ya ukahaba wa Israeli, Mungu aligeuza vitu vile vya kimwili na mishikamano ya kisiasa iliyojikita nayo ( Hos 2:6-13 ), na kuwasababisha Waashuri kuharibu Ufalme wa Kaskazini na kuwabebakatika utummwa ( Hos 6:4-10:15; 12:1- 13:16 ). Kuharibiwa kwa Israeli kulikamilika mwaka 721 KK.

b. Ufalme wa Kusini (Yuda). Mungu alituma manabii kadhaa, waliojulikana sana (kufuatana na mtiririko walivyoandikwa): Isaya (miaka 740-700 KK), Yeremia (miaka 626-586 KK), na Ezekieli (mwaka 593-571 KK). Kila moja wa manabii hawa aliikosoa Yuda kwa uzinzi wake wa kiroho kwa nyingi za sababu zile zile ambazo Ufalme wa Kaskazini ilikosolewa.

(1) Isaya alijumuisha uzinzi wa Yuda na ukosefu wa haki, dhuluma zake, kupenda mali, na kutojali masikini na wahitaji ( Isa 1:21-23 ). Katika Isa 57:1-13, nabii anasema kwamba matendo kama hayo yanaonyesha kwamba, ingawaje wanaweza kujidai kwamba wao ni “wana wa Ibrahimu,” watu wafanyao mambo kama hayo kwa hakika ni wa baba na mama mwingine. Ni “wana wa mwanamke mchawi, uzao wa mzinzi na kahaba” (Isa 57:3). Lugha hiyo inafanana sana na lugha aliyoitumia Yesu kinyume na Mafarisayo katika Yohana 8:34-47.(2) Yeremia 2-3 imejaa picha za ndoa na maswala la ki-tendo la ndoa kuelezea hali ya kutokuwa na uaminifu ya Yuda kwa Mungu. Mungu anakumbushia uaminifu wake kwa Yuda (Yer 2:1-7). Hata hivyo, kama ilivyokuwa kweli kwa Ufalme wa kaskazini wa Israeli, Yuda ikamsahau Bwana, na kuandamia wote wawili Misri na Ashuru, na kuelezwa kuwa anatafuta tena wapenzi wake wengine zaidi (Yer 2:7-3:10). (3) Kama ilivyokuwa kwa Ufalme wa Kaskazini, Ufalme wa Kusini ulivamiwa, Yerusalemu ikaharibiwa, na watu wakachukuliwa utumwani huko Babeli kati ya miaka 606-586 KK. Pamoja na hayo, hata kati kati ya maonyo kwa Yuda kuhusu kile kinachowajia, Mungu bado aliwasihi watubu (Yer 3:11-23).(4) Wakati wa kipindi cha uhamisho huko Babeli Ezekieli aliandika ili “uujulishe Yerusalemu machukizo yake” ( Ezek 16:2 ). Katika Ezekieli 16 Nabii anabainisha kwamba Mungu alimtoa Yuda kutoka sifuri, akampatia kila kitu, lakini malipo yake yakawa “ukamwaga mambo yako ya kikahaba juu ya kila mtu aliyepita” (Ezek 16:15). Ukahaba huo ni pamoja na kuabudu sanamu, kushikamana na mataifa ya kigeni kama vile Misri, Waashuru, na Babeli, ukosefu wa kimaadili ki-ndoa, kutowasaidia masikini

43

Page 45:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

na wahitaji licha ya kuwa na utele wa kiuchumi (Ezek 16:16-59). Ezekieli 23 hulinganisha ufalme wa Kaskazini na wa Kusini, na kuzikosoa kwa uzinzi wa kuabudu sanamu, muunganiko na mataifa ya kigeni yasiyoamini, na hali ya udunia. Kama matokeo, Mungu anasema, “Hivyo nitaukomesha uasherati katika nch hiii, ili wanawake wote wafundishwe wasifanye mambo ya uasherati wenu. Nao watawalipa ninyi malipo ya uasherati wenu, nanyi mtachukua dhambi za vinyago vyenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.” (Ezek 23:48-49)

C. Katika AJ jina la wahusika wa ndoa huwekwa bayana kati ya Kristo na Kanisa.1. Wote wawili, Yohana mbatizaji na Kristo mwenyewe humtambua Yesu kama “bwana arusi” ( Yoh 3:28-30; Math 9:14-15 [ Mark 2:18-20; Luka 5:33-35 ]). Picha ya AK ya Yahwe kuwa mume wa watu wake inatumika katika AJ kwa Yesu mwenyewe. 2. Hata kama Yesu ndiye bwana arusi, na watu wake wanapaswa kushangilia wakati akiwapo pamoja nao, utimilifu wa sherehe za arusi utacheleweshwa wakati atakapoondolewa kwao ( Math 9:14-15 [ Mark 2:18-20; Luka 5:33-35 ]). Hilo linatia nguvu ule muktadha au dhana ya “bado kitambo kidogo” ya ufalme wa Mungu, ambao tayari upo kwa kuja kwake Yesu kwa mara ile ya kwanza, bali bado kutimilika kikamilifu hadi Kurudi kwa mara ya pili. Yesu pia alitarajiwa kukataliwa na watu wa Mungu wa AK, Israeli. Kwa hiyo, anafungua milango ya sherehe ya arusi kwa watu wa mataifa yote (ona, Math 22:1-14; 25:1-13). 3. Nyaraka za AJ hufanya dhana ya “ndoa” bayana kabisa, kidhahiri ikitaja kwamba ni kanisa, na kuongeza nguvu uhusiano na Mwa 2:24.

a. Katika 2 Wakor 11:1-3 Paulo huelezea uhusiano wa kanisa na Kristo kama “nadhiri kwa mume moja.” Kisha anaonyesha kwamba, Adamu ni “mfano” wa Kristo (Rum 5:14; 1 Wakor 15:22, 45-47), na anahusisha na kanisa (2 Wakor 11:3). “Katika Kristo, waamini wanakuwa wako katika Edeni mpya,” na kama vile “hakukuwa na ndoa kabla ya Adamu na Hawa, [vivyo hivyo] hakuna iliyo kuu zaidi baada ya ile ya Kristo na kanisa lake” (Ortland 1996: 152).b. Katika Waef 5:29-32 Paulo hufanya uhusiano kati ya Kristo na kanisa kama kielelezo sawia cha uhusiano kati ya mume na mkewe. Waef 5:32 huhusisha bayana ndoa kwa “kristo na kanisa.” Waef 5:30-31 huweka sambamba moja kwa moja na Mwa 2:23-24: (1) “sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu” (Mwa 2:23); “kwa kuwa tu viungo vya mwili wake” (Waef 5:30). (2) “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake . . . nao watakuwa mwili moja” (Mwa 2:24); “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake . . . na hao wawili watakuwa mwili moja” (Waef 5:31). Kwa maneno mengine: “Kisababisho na mwongozo mkuu zaidi kwa wanandoa Wakristo ni maono ya Kristo na kanisa lake katika upendo wa pamoja. . . . Kuunganika kwetu na Kristo kama mwili wake, huturejesha kwenye neema za undani kama ilivyo kwa unganiko la ki-ndani la ndoa litendavyo na kukidhiwa, kama si rahisi, kwa wanandoa wa ki-Kristo. Ndoa ya kanisa kwa Kristo ni yote mawili, ilipata umbo katika Adamu na Hawa; na huwapatia wanadoa wa ki-Kristo uwajibikaji binafsi wa kuhakikisha umoja wa kindoa kwa kiwango cha ndani sana. . . . Kitovu cha ujumbe katika mstari huo, basi, ni kwamba ndoa ya ki-Kristo katika uaminifu kwa ile maana ya “mwili moja” huwekesha kimwili uhalisi wa upendo wa kujitolea katika Kristo kuunganishwa ki-ndoa na wanadamu waliojitoa kwa furaha katika kanisa. . . . Mume aliye Mkristo humpenda mkewe kwa kumpatia dhabihu za kila siku za muda wa maisha yake, ili kwamba huyo mkewe aweze kung’ara zaidi kama mwanamke wa Ki-Mungu. Naye, kwa upande wake, huthibitisha na kuonyesha mwitikio kwa vitendo ajitoleavyo mumewe kwake. Kupitia yote hayo, siri ya Injili hufunuliwa.” (Ortland 1996: 155-58)

4. Yesu na waandishi wa AJ hulinganisha kumkataa Yesu na “uzinzi.”a. Yesu alilinganisha kule kumkataa yeye na uzinzi (Math 12:38-39; 16:1-4; Mark 8:38). b. Yak 4:4 huendeleza ile dhana au muktadha wa uzinzi wa kiroho zaidi ya ibada za sanamu au matendo yake kwa kuwaita watu “wazinzi” ambao “wanaipenda dunia,” au hata wana“tamani kuwa na urafiki na dunia.”

(1) Tamaa kama hiyo ya “kuipenda dunia” siyo tu ni kushindwa kidogo, bali “ni kinyume mbele za Mungu,” na “humfanya [mtu] adui wa Mungu.” Ukweli kwamba kuipenda dunia hujumuishwa kuwa ni uzinzi wa kiroho kinyume na Mungu huonekana katika ukweli kwamba Ufu 17:5 huita mifumo ya kidunia “Babeli Mkuu, Mama wa Makahaba na machukizo ya dunia.” (2) Sababu kwa nini urafiki wa kuipenda dunia ni uadui na Mungu hufuatia moja kwa

44

Page 46:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

moja kutokana na mlinganisho wa imani na ndoa: ni kama mke wa ndoa ambaye anahangaika kwa kuwaandamia wanaume wengine badala ya mume wake. “

Yakobo siyo tu anataka kuwalinda wasomaji wake kutokana na mikondo ya mienendo ya tabia za kidunia; anawausia waondokane na shauku ya kukubaliwa na dunia kwa kuelezea swala hilo wazi kabisa, kwa uzito na kwa vizuri kabisa kiasi kwamba hakuna mtu yeyote apendaye kuwa rafiki wa Mungu akajiruhusu kuvutwa na dunia, mfano wa akina Dema, katika mivuto na misisimko yake. . . . Ingawaje tukio lilivyo Ki-Biblia halisukumwi kwa kasi na andiko hili la Agano Jipya, mtu hata hivyo atajikuta anahisi tayari anaingizwa katika hali ya ukahaba wa rohoni ulio wa kina zaidi, wa binafsi zaidi, na utafutao zaidi, ambao unapatikana kwenye mzizi wa udhihirisho unaoonekana nje. Pale ugonjwa huu wa ndani ufikiapo hatima ya kuponyeka, basi sura kamilifu itafikiwa. (Ortland 1996: 142-43)

b. 1 Wakor 6:15-20 huelezea umuhinu wa ndani wa upotofu halisi wa kimwili, wa mambo ya zinaa. Mtu “aliyeungwa na kahaba ni mwili moja naye” huyo kahaba (mst. 16), lakini mtu “aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye” Bwana (mst. 17). Kwa kutumia mpangilio huo huo wa maneno katika mistari yote miwili, Paulo anatuelezea ni machukizo kiasi gani ya kiroho dhambi ya zinaa ilivyo. Wakristo wameunganika na Kristo ki-undani sana kwa unganiko la (“roho moja m.y, Kristo, kwa kupitia Roho Mtakatifu, kiuhalisia anakaa katika miili yetu (mst. 19), na “sisi tu viungo vya mwili wake” (Waef 5:30). Kwa kutenda dhambi ya zinaa, mwamini anaunda unganiko kutoa lidude la ajabu kati ya Kristo na kahaba. Badala yake, tunapaswa “kumtukuza Mungu katika miili yetu” (mst. 20) kwa “itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana” (Rum 12:1). Kile tukifanyiayo miili yetu hudhihirisha tunawaza nini kuhusu Kristo.

D. Katika Ufunuo, picha ya Ki-Biblia kuhusu uhusiano wa kindoa kati ya Mungu na watu wake huja kutimilika katika Kristo, bibi arusi (Kanisa), na Nchi Mpya.

1. Katika Ufu19:5-9 hiyo “karamu ya arusi ya Mwana Kondoo” inafanyika. Katika zama hizi hapa duniani, tuna kile tukiitacho “tayari” ya ufalme, bali husubiria “bado kidogo” ya utimilifu. Wakati Kristo atarudi tena, tutaona kutimilika kwa Ufalme. Ile furaha ya “karamu ya Mwana Kondoo” na bibi arusi wake hutofautiana na“karamu ya Mungu iliyo kuu,” ambayo itamhusisha kila moja anayempinga Kristo (Ufu19:17-21). Wote wanaoalikwa kwenye “karamu ya Mwana Kondoo” ni “wabarikiwa” (Ufu 19:9). Kwa upande mwingine, kule kwenye “karamu ya Mungu iliyo kuu” ndege wana“kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa. . . [hadi] Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao” (Ufu 19:18, 21).2. Ufunuo hutofautisha uaminifu wa bibi arusi wa Kristo na makahaba wa dunia.

a. Jinsi walivyovaa. Bibi arusi alivaa “kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu” (Ufu 19:8). Bwana arusi amemtakasa kwa“kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa” (Waef 5:26-27). Kwa upande mwingine, “Mama wa makahaba mwenyewe amevaa mavazi ya ukahaba, “alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake” (Ufu 17:4; 18:16). b. Nini kinatokea kwao. Mpangilio wa maneno wa Ufu 17:1 na 21:9 ni sambamba. Kama yalivyo mavazi ya kahaba mkuu wa dunia na bibi arusi wa Kristo yalikuwa yanatofautiana, ndivyo katika 17:1 huyo kahaba anahukumiwa na kuangamizwa, lakini katika 21:9 bibi arusi wa Mwana Kondoo anatukuzwa.

3. Katika Ufu 21:1-11 uhusiano wa kudumu na uliokamilika wa kindoa kati ya Kristo na Bibi arusi, Kanisa, waelezwa.

a. Katika kumalizia maono yake, Yohana anamwona Bibi arusi wa Kristo kama “mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu, wenye utukufu wa Mungu” (Ufu 21:10-11). “Makazi ya Mungu na wanadamu katika umbo la mji huweza . . . kuonyesha unganiko la kijumuiya lililo kamilifu la waliokombolewa wenyewe kwa wenyewe kama hitimisho la Mungu na jawabu la milele kwa matatizo yanayoendelea kwa muda mrefu katika historia ya wanadamu. ” (Ortland 1996: 166n.73).b. Yerusalemu Mpya hufananishwa “kama bibi-arusi aliyekwisha kupanbwa kwa mumewe”

45

Page 47:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

(Ufu 21:2). Katika Ufu 19:7-8 bibi arusi ni watakatifu (m.y., kanisa). Kule kuoanishwa kwa Bibi arusi na Yerusalemu Mpya huwekwa bayana katika Ufu 21:9 ambapo malaika asema, “Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo kisha katika mst. 10 mara husema, “Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu.” Kwa hiyo, Yerusalemu Mpya huonekana kushabihiana kiukaribu na watu wa Mungu kiasi kwamba huenda ukawa ndio kielelezo cha uhusiano wa watu wa Mungu na Mungu kwao. Ufunuo bila shaka ni kitabu cha ufasaha mkubwa. Maelezo yake ya Yerusalemu Mpya yako zaidi “kibinafsi kuliko kimtazamo wa uchunguzi wa muundo wa mji kijiografia toka juu.” (Gundry 1987: 256). Matokeo yake, kama ambavyo Yesu na kanisa ni Hekalu jipya, la kweli, ndivyo Yerusalemu Mpya huzungumzia zaidi kuhusu watu wa Mungu na uhusiano nao, kuliko maelezo ya Jiografia mpya ambayo yatakuwepo baada ya Kristo kurudi tena.

KRISTO NA KANISA KAMA UTIMILIZO WA AK

I. Biblia Kimsingi ni Kumhusu Yesu Kristo—Yeye Ndiye Mtu Aliye Kiungo na Dhana Iunganishayo Yote.“Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Je! haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katia utukufu wake? Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.” (Luka 24:25-27)

“Mwayachunguza maandiko, kwa sababu ninyi mnadhani mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. . . . Kwa maana kama mngalimwamini Musa,mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu.” (Yohana 5:39-40, 46)

“Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo. . . . Naam, na manabii wote tangu Samweli na wale waliokuja baada yake, wote walionena, walihuburi habari za siku hizi.” (Matendo 3:18, 24)

“Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.” (Matendo 10:43)

“Basi kwa kuwa nimeupata msaada utokao kwa Mungu nimesimama hata leo hivi nikiwashuhudia wadogo kwa wakubwa, wala sisemi neno ila yale ambayo manabii na Musa waliyasema, kwamba yatakuwa; ya kwamba Kristo hana budi kuteswa na ya kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika wafu atatangaza habari za nuru kwa watu wake na kwa watu wa Mataifa.” (Matendo 26:22-23)

“Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta- tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo. Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia.” (1 Petr 1:10-12)

A. Zinapotazamwa peke yao, simulizi za AK na nabii zake hazimtaji moja kwa moja Yesu Kristo, bali huwa na nguzo ya kusimamia, na hutumia lugha zinazolenga, na kumwelekea mlengwa wa kuibukia taifa la Israeli.

1. Ukweli kwamba Yesu ndiye kilele cha ujumbe katika AK chaonyesha kwamba AK halijisimamii lenyewe. Twaweza kufikia uelewa kwa kiwango cha kihistoria kuhusiana na matukio ya AK, na twaweza hata kufikia pia uelewa fulani wa kitheolojia kuhusiana na kutokutimizwa kwa ahadi fulani za Mungu kwa watu wake katika AK. Hata hivyo, “haiwezekani kutoka katika AK peke yake kuelewa kipimo kamili cha matendo ya Mungu na ahadi zake zilizoandikwa” (Goldsworthy 1991: 54).2. Sababu ya kwa nini AK peke yake halileti maana yake toshelevu, ambayo ndiyo msingi halisia; ni mafundisho ya ufunuo wa hatua kwa hatua (ona Waeb 1:1-3 ). “Ufunuo wa hatua kwa hatua maana yake ni kwamba ufunuo wa Mungu haukutolewa wote kwa mkupuo pale mwanzoni, bali ulifunuliwa kwa

46

Page 48:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

hatua, hadi nuru kamili ya kweli ilipofunuliwa katika Yesu Kristo. Ufunuo huu ulio kama kiini cha ahadi za Mungu na kutimizika kwake. . . . [Yesu] ndiye ufunuo wa mwisho na uliokamilika kuliko wote wa jinsi zile ahadi zinavyokuwa. Hii maana yake ni muundo na kilichomo ndani ya utimilizo huo hupita kwa mbali muundo na kilichomo kwenye ahadi hizo zenyewe.” (Goldsworthy 1991: 64, 65)3. Maagano ya AK, taasisi, matukio, na taifa la Israeli lenyewe, vilinyoshesa kidole kwa kweli za kiroho za AJ. “Katika Maagano ya zama za AK twaona kweli za kiroho zikiwa zinatolewa katika hali ya muundo wa picha. Mungu alipofunua haja ya mwanadamu ya utakaso, alitumia mifano na vivuli vya mifumo ya kuonekana ya dhabihu ikiwamo maelfu ya makuhani na wanyama wa kuteketezwa. Wakati Mungu alipofunua ahadi ya watu wake kukaa pamoja naye, alifanya hivyo katika mifano na vivuli vya nchi iliyo Mashariki ya Kati na majengo yaliyofanywa kwa matofali na nzege. Hii ndiyo njia Mungu aliyofunulia mpango wake katika zama za AK. Kwa hiyo, wakati Mungu alipowatumia manabii kuelezea utimilifu wa kiroho wa mpango wa Mungu katika zama za Agano Jipya, Mungu aliamua kutumia lugha ya mifano na vivuli. Alikuwa akielezea Agano Jipya katika lugha ya Agano la Kale. Alielekeza kwenye lengo la kiroho la mpango wa Mungu katika njia iangazayo zaidi na iliyo wazi kuliko zote ambazo mifano na vivuli vya kuonekana vya awali vingeweza kufikiwa.” (Lehrer 2006: 85)

B. Yesu na waandishi wa AJ wote walitumia AK kumhusu Yesu na kwa Injili.1. Yesu alilitumia AK kwake mwenyewe. “Kwa ukweli huu [m.y., kwamba alikuwa ndiye mhusika wa AK] ushuhuda mkali kuliko wote ni wa Bwana wetu mwenyewe. Akiwa katika mabishano na Wayahudi, aliwaambia, “Mwayachunguza maandiko, kwa sababu ninyi mnadhani mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia” (Yohana 5:39). Na katika muktadha huo huo aliendelea kusema, ‘Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu’ (Yohana 5:46). Siyo hivyo tu, daima aliyataja Maandiko kuwa yalikuwa yanamlenga yeye. Kwa mfano, katika Mathayo 21:42-46, aliuhitimisha mfano wa bwana mwenye nyumba, kwa kuiombolezea Israeli kwa kumkataa Masihi wao kwa kuihusisha na yeye mwenyewe Zab 118:22, 23, ‘Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waandishi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?’ Vivyo hivyo baada ya ile Meza ya Bwana, alisema kwa wanafunzi wake, ‘Mtakunguwazwa ninyi nyote kwa ajili yangu usiku huu; kwa kuwa imeandikwa nitampiga mchungaji, na kondoo watatawanyika’ (Marko 14:27), na hivyo akajionyesha mwenyewe kuwa ndiye mlengwa wa ile Zekaria 13:7.” (Gaebelein 1958: 393)2. Mitume walitumia AK kwa Yesu. “Ukweli kwamba mitume wanamfuata Bwana wetu Yesu katika kumuona kama kitovu cha Maandiko hudhihirika kutokana na jumbe zao zilizoandikwa katika Matendo ya Mitume. Siku ile ya Pentekoste, Petro alitumia Zab 16:8–11 na Zab 110:1 kama msingi wa kumtangaza Kristo aliyefufuka (Mdo 2:25-36); na katika ujumbe wake wa pili alimtaja yeye kama nabii ambaye Musa aliandika habari zake katika Kumbukumbu 18:15, 18, 19 (Mdo 3:20-22). Wakati Yule towashi wa Ki- Ethiopia alipomuuliza mhubiri Filipo maana ya Isaya 53, Filipo ‘akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri Habari Njema za Yesu’ (Mdo 8:30-35). Huko Antiokia katika Pisidia Paulo alimhubiri Kristo (Mdo 13:32-37) kutoka Zab 2, Isaya 55 na Zab 16. Na kwamba mahubiri yake yalisimamia kwa Yesu kama kitovu katika Maandiko yote hudhihirishwa kutokana na maelezo ya mbinu yake katika Matendo 17:2, 3, yanayoarifu kuwa ‘Na Pauo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu, akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo.’ Kama ilivyo kwa huduma hii pana zaidi ya makanisa ambapo pana uwepo wa machafuzi makubwa ya watu wa Mataifa, ujumbe huo huo wa Kristo katika Agano la Kale ni sehemu ya kiini na nguzo ya nyaraka za Paulo.

Kilichokuwa kweli kwa Paulo kilikuwa kwa hivyo wengine pia. Hivyo twasoma kwamba Myahudi wa Aleksandria, Apollo, alipoelekezwa na wanafunzi wa Paulo, Akila na Prisila, ‘Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa mbele ya watu wote akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.’ (Mdo 18:24-28). Petro katika nyaraka zake, Yohana katika nyaraka zake, mwandishi wa Waebrania; Yakobo na Yuda na Ufunuo—zote zina mwegemeo wa shina la Kristo. Bila shaka, usemi katika Ufunuo 19:10, ‘Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii,’ unahusisha siyo tu vitabu vya kinabii, bali kwa Biblia yote kiujumla.” (Gaebelein 1958: 393-94) Chati ifuatayo yaonyesha kushabihiana kwa jumbe za Petro na Paulo za kwanza kabisa katika Matendo ya Mitume:

Injili1. AK limetimizwa2. Katika mwanadamu na kazi za Yesu3. Aliyekufa

Petro (Mdo 2)2:16-21, 25-31, 34-362:222:23

Paulo (Mdo 13)13:16-23, 32-3913:23-2613:27-29

47

Page 49:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

4. Na kufufuka5. Naye ametukuzwa6. Katika yeye kuna masamaha ya dhambi 7. Kwa hiyo . . .

2:24, 322:33, 362:382:38-40

13:30-31, 34-3713:3413:38-3913:40-41

3. Injili ya Yesu Kristo in msingi wake, na iliahidiwa katika, AK. Rum 1:1-4 huzungumzia “ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu; 3 yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili, 4 na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu.” Goldsworthy anaelezea hili: “Kwanza, ni Injili ya Mungu. . . . haishughulikii kimsingi haja zetu kama tunavyozielewa—nitawezaje kuishi maisha bora zaidi, kushinda mambo yanayonilemea, kufanya maisha yangu yawe na maana zaidi—ingawaje yaweza kuhusishwa na hayo. Injili ni njia ya Mungu ya kushughulika na ‘tatizo’ lake la jinsi yeye, aliye mtakatifu na Mungu wa haki, anaweza kumhesabia haki na kumkubali mdhambi. . . .

Pili, ni injili ya Agano la Kale. Sehemu muhimu ya theolojia ya ki-Biblia ni kujaribu kuelewa jinsi ahadi zilizotolewa katika Agano la Kale zinavyotimizika kiuhalisia katika hili Jipya. Kwa maneno mengine, matumizi ya Ki-Kristo ya Agano la Kale yanaongozwa na jinsi tunavyoona ujumbe wake unavyohusiana na Kristo na, kupitia yeye, kuja kwetu. . . .

Tatu, kuna mada inayoeleweka ya injili. Inamhusu Mwana kwa namna ambayo haimhusu Baba, au Roho Mtakatifu, au mwamini. . . . yeye siyo tu ni Mungu Mwana, nafsi ya pili ya Utatu wa Uungu. Yeye ni Yesu wa Nazareti ambaye ni uzao wa Daudi Mfalme wa Israeli. . . .

Nne, kuna ukweli wa kati wa injili, ambao ni ufufuo wa Yesu kutoka kwa wafu. Paulo anasema kwamba ufufuo ndio ulimtambulisha Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu. . . . Kufufuka kimwili kwa Yesu kunatawala uelewa Agano Jipya wa injili. . . . Ufufuo ni kitovu kwa sababu hujijenga juu ya kifo chake na kwa sababu unasimama kama mwanzo mpya wa jamii ya uanadamu. . . . Kwa hiyo, tunazaliwa upya kwa ufufuo wa Kristo (1 Pet 1:3). Kwa kupitia ufufuo wake tunaingia katika upya wa uzima (Rum 6:4-11).” (Goldsworthy 1991: 81-82, 229)

II. Agano la Ibrahimu, la Daudi, na Jipya Yalielekea Kwake na Kutimilizwa Katika Kristo na Kanisa.

A. Agano la Ibrahimu limetimizwa katika Kristo na kanisa.“Agano la Mungu na Ibrahimu linaweka msingi kwa historia nzima inayofuatia ya ukombozi

iliyoandikwa katika Maandiko” (Holwerda 1995: 32). Lilikuwa “ni hatua ya kwanza kutimiliza utabiri uliofanyika katika Mwanzo 3:15 kuhusiana na Uzao Maalum kuja kufa msalabani katika kutekeleza kusudio la kimbingu lisilobadilika la neema” (Reisinger 1998: 25). Kwa njia moja au nyingine, maagano mengine huota kutokana na Agano la Ibrahimu. Hoja ya Waeb 6:13-8:2 ni kwamba Yesu pia ni mkuu zaidi kwa Ibrahimu, na ndiye mdhamini wa agano lillilo bora zaidi.

1. Katika Agano la brahimu ( Mwa 12:1-3; 13:14-17; 15:1-21; 17:1-21; 22:15-18 ) kuna kamba tatu “za vifundo vya ahadi”: a. uzao unaohusika (m.y., ahadi kuhusu“mzao”); b. himaya ya utaifa (m.y., ahadi zinazohusiana na “nchi”); na. baraka ki-dunia nzima (ahadi za baraka kwa watu wengine kupitia/ au ndani ya uzao wa Ibrahimu) (Williamson 2000: 100-01; ona pia Kaiser 1978: 86; Essex 1999: 208; Reisinger 1998: 6).2. Muundo wa agano la Mungu ulibadilika kadiri alivyoendelea kushughulika na Ibrahimu. Mungu mwanzoni aliahidi kumfanya Ibrahimu “taifa kuu” (Mwa 12:2), lakini baadaye akapanua hilo na kumfanya baba wa “mataifa mengi” (Mwa 17:5). Ile “nchi,” aliyoahidiwa mwanzoni kabisa (Mwa 12:1), ilielezwa kuwa ni ile ambayo macho yake yaliweza kuona (Mwa 13:14-15), kisha ikapewa mipaka ya kijiografia (Mwa 15:18-21; 17:8), na hatimaye ikajumuishwa katika maneno yaliyonena kwamba “uzao wako utamiliki mlango wa adui zao [kihalisia., adui ‘yake’]” (Mwa 22:17). Wakati huo huo, Mungu alifinya ule “uzao” ambao kwamba aliimarisha agano lake: siyo wazao wote wa viuno vya Ibrahimu walijumuishwa, bali mkondo wa kupitia Isaka tu (Mwa 17:18-21). Kila mahali kupitia uzao ule “mataifa yote ya dunia watajibarikia” (Mwa 22:18). 3. Agano la Ibrahimu liliundwa kwa kusudi la kuenea zaidi ya utimilizo wa Israeli “ya kuonekana” ya AK.

a. Israeli ya AK ilikuwa utimilizo wa “kuonekana” wa Agano la Ibrahimu. Kuhusiana na ahadi za “uzao”, Kut 1:6-13; Hes 23:10; Kumb 1:10 zinaonyesha utaratibu wa kupanuka kwa Waisraeli. Kumb 1:10 panasema BWANA, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi, nanyi, angalieni, mmekuwa leo mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi.” Vivyo hivyo, ahadi ya “nchi” ilitimizwa angalau mara mbili (katika siku za Yoshua [Yosh 21:43-45] na hata wakati wa kutawala kwa Sulemani [1 Waf 4:20-21]). Kuhusiana na ahadi za “baraka”, katika 1 Waf

48

Page 50:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

10:1-13; 2 Nyak 9:1-12 Malkia wa Sheba alishuhudia baraka nyingi ambazo Sulemani alizileta kwa Israeli na kwa kila moja aliyezisikia hekima zake. Kwa hiyo, Sulemani akatamka katika 1 Waf 8:56, “halikukosa kupatikana neno lolote katika ahadi yake njema, aliyoahidi kwa mkono wake Musa” (ona pia Yosh 21:45; 23:14).b. Licha ya kutimizika kwake kwa awali katika Israeli ya AK, AK huonyesha vipengele vya kutokukamilishwa vya Agano la Ibrahimu. Kuhusiana na ahadi ya “uzao”, Kumb 30:4-5; Yer 23:3; Ezek 36:10-11 “huelekeza ahadi ya ongezeko la kihesabu kwa kipindi baada ya uhamisho na kukihusisha nacho na baraka zitarajiwazo katika katika zama za Agano Jipya” (Williamson 2000: 112). Kuhusiana na ahadi za “nchi”, kurudishwa kwa Kanaani kulitokana na utii wa Israeli. AK linaonyesha picha ya mkondo wa utimilifu kwa sehemu, kufuatiwa na kutomiliki na kisha kumiliki kutakakofuatia. Kwa hiyo, muktadha wa nchi haukufikia ukamilifu wake sawa sawa nyakati za AK. Kuhusiana na ahadi ya “kubarikiwa dunia nzima”, Isa 42:6; Isa 49:6 humwelekea mtumishi wa Mungu ambaye, hapo baadaye, atakuwa “nuru ya mataifa.” “Ukiachia uwezekano wa “Kipindi cha Dhahabu”, cha Sulemani, ‘baraka kwa mataifa’ zilibakia kuwa ni tumaini lisilojulikana kwa kipindi chote kilichozingirwa na Agano la Kale. Bila shaka katika Fasihi za Kinabii, dhana kama hiyo ilitazamika kama zama zijazo.” (Williamson 2000: 115) Ujasiri kwamba Mungu angetimiza ahadi zake kwa Ibrahimu uliivusha Israeli wakati walipokabiliwa na hukumu ya Mungu (Isa 41:8-16; Mika 7:18-20). Yer 33:23-26 huunganisha kutimizwa kwa Agano la Ibrahimu na Bwana kumleta mfalme wake katika kutimiliza Hes 24:17 na 2 Sam 7:16, tukio ambalo lingetokea siku za baadaye.

4. AJ “huzifaya kuwa za kiroho” ahadi zote za Ibrahimu. Kulingana na AJ, kutimizwa kwa Agano la Ibrahimu kunapatikana kwa kuja, kuteswa, na kufufuka kwa Yesu Kristo.

a. Ahadi ya “uzao”. Katika AJ, hiyo ahadi ya “uzao” huhusiana kimsingi na Kristo kama ndiye “uzao” wa kweli wa Ibrahimu, na kisha kwa wale wote ambao wako “katika Kristo” kwa imani (kanisa).

(1) Yesu ndiye “mzao” wa kweli wa Ibrahimu. Rehema za Mungu, na agano lake na Ibrahimu, zinazotajwa katika Yer 33:26, huonekana kwa Mariamu katika Luka 1:54-55 kuhusiana na kuja kwa Yesu. Zakaria, baba yake Yohana mbatizaji, naye pia alikumbushia kuja kwa Kristo, na hata yule mtangulizi wake Yohana, kama kutimiliza agano lake na Ibrahimu (Luka 1:67-79). Luka 2:32 hufanyia kazi Isa 42:6; 49:6 kwa Yesu. Yesu mwenyewe alisisitiza kwamba Agano la Ibrahimu hatimaye lilikuja kuwa la kiroho, na ya kwamba yeye ndiye aliyelitimiliza (ona Yoh 8:31-58). Katika Wagal 3:16 Paulo kwa bayana kabisa anaelekeza kuwa ahadi ilifanywa kwa Ibrahimu “na kwa mzao wake.” Anasisitiza kwamba hilo neno “mzao” ni mmoja, na humlenga Kristo. (2) Wote “walio katika Kristo” kwa imani ni watoto wa kweli wa Ibrahimu. Hoja hii muhimu huungwa mkono na watu wote muhimu wa AJ.

(A) Yohana Mbatizaji. Yohana Mbatizaji aliubeza uzaliwa wa kimwili wa Ibrahimu kwa kusema, “msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto” (Math 3:9; Luke 3:8). (B) Yesu Kristo. Yesu alitofautisha kati ya uzao wa kimwili wa Ibrahimu (ambao sio kule kutimizwa kwa kweli kwa Agano la Ibrahimu), na wazao wa kiroho wa Ibrahimu (ambao ndio kutimizika kwa kweli kwa Agano la Ibrahimu). Alionyesha hilo tangu Wayahudi walipokuwa watumwa wa dhambi, hawakuwa tena wana wa kweli wa Ibrahimu (Yoh 8:33-36). Kama wangelikuwa kweli wana wa Ibrahimu wangelitenda matendo ya Ibrahimu, lakini kule kutaka kumuua yeye kulikuwa uthibitisho kwamba wao sio. Kwa hiyo, wao sio wana wa Ibrahimu, bali wa Ibilisi (Yoh 8:39-41, 44). Alihoji ikiwa Mungu angelikuwa baba yao, basi wangelimpenda Yesu na kulisikia neno lake (Yoh 8:42). (C) Mtume Petro. Katika Mdo 3:25-26 Petro anataja rasmi kwamba ni waamini katika Kristo “Ninyi mmekuwa watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu.” (D) Mtume Paulo. Paulo anatoa mwangwi kile alichosema Yesu katika Yoh 8:34-44 kuhusiana na ni akina nani ambao ni wana halisi wa Ibrahimu. Ahadi kwa Ibrahimu hutimizwa kwa wale wenye imani katika Kristo. Katika Rum 4:11-18 anaonyesha kwamba ahadi kwa Ibrahimu ilifanyika “si kwa sheria bali

49

Page 51:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

kwa haki aliyohesabiwa kwa imani.” Anawekea uzito katika Rum 9:6-8 ambapo anadhihirisha kwamba “Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli,” na “si waatoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao.” Hoja ya Wagalatia 3-4 kiujumla ni kuwa Kristo na Kanisa ndio utimilifu wa Agano la Ibrahimu. “Huyu mtu Ibrahimu ni wa umuhimu wa kipekee katika hoja za Paulo kuanzia [Wagal 3:6] na kuendelea—‘Mtazameni Ibrahimu (mst. 6)—ambaye anarudia kumtaja tena na tena katika kifungu chote cha sura za 3 (mst. 6, 7, 8, 9, 14, 16, 18, 29). Lakini ni muhimu kuelewa kwamba wale mababu zetu walichipuka tu na kuwa njia ya kuongozea kwa utimizwaji wa Agano la Ibrahimu, Yesu Kristo., Mwana wa Mungu (3:16, 26). Hasa kabisa, kile Paulo anachokiwakilisha katika kifungu hiki ni kutafsiri kiueleko wa mhimili wa Kristo na kitovu kuwa Kristo katika Agano la Ibrahimu. . . . Kwa kifupi, Paulo anatafsiri upya Agano la Ibrahimu, ambapo kipaumbele ni kuwa mali ya Kristo, na wote walio katika yeye, Wayahudi na Mataifa pia, wote wanayo sifa ya kuitwa mzao wa Ibrahimu.” (Burke 2006: 112, 114n.33) Kwa hiyo, katika Wagal 3:29 Paulo anabainisha, “ikiwa wewe ni wa Kristo, wewe u mwana wa Ibrahimu, warithi sawa na ahadi.” Hilo halitokani na uzao wa kimwili, bali kwa njia ya imani (Wagal 3:7-9, 14). Kama vile Mungu alivyomwahihi Ibrahimu kuwa uzao wake utakuwa mwingi “kama nyota za mbinguni na kama mchanga ulioko pwani” (Mwa 22:17), hivyo hilo limekuja kutimizika kwa kanisa la Kristo (m.y., uzao wa kweli wa Ibrahimu wa kiroho), ambao una watu “wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa” duniani (Ufu 5:9; 7:9).

b. Ahadi ya “nchi”: (1) Katika AJ “nchi” imepanuka kuwa ulimwengu mzima. Kwa vile kanisa la Kristo limeundwa na watu wa kila “kabila na lugha na jamaa na taifa” (Ufu 5:9; 7:9), Rum 4:13 hupanua zaidi hiyo ahadi ya “nchi” kumhusisha Ibrahimu na uzao wake kama “warithi wa ulimwengu.” Wakati Paulo ananukuu agizo la “Waheshimu baba yako na mama yako . . . upate heri, ukae siku nyingi katika dunia” (Waef 6:2-3), hapo “anarekebisha muundo wa Agano la Kale wa ahadi kwa kuyaacha maneno yasemayo, ‘ambayo Bwana Mungu wako akupatia,’ maneno yaliyokuwa yanazungumai nchi ya Kanaani (Kumb 5:16). Kwa kuacha pale palipokuwa pamelengwa, Paulo anatamka kwamba sasa katika Kristo ahadi inahusu kila nchi . . . Kile kilichokuwa mwanzoni ni ahadi ya baraka kwa watu wa Mungu katika nchi maalum iitwayo Kanaani, iliyotolewa na Mungu kama zawadi, sasa imeahidiwa kwa watu wa Mungu waishio popote duniani, ambayo ilitolewa na Mungu kama zawadi.” (Holwerda 1995: 102)(2) AJ huitafsiri upya ile Kanaani ya AK (ambayo iliahidiwa kwa Ibrahimu) kama mtu wa “nchi” ya kweli: m.y., mji wa ki-mbingu, Yerusalemu Mpya ( Waeb 11:8-16; Ufu 21-22 ). Picha ya AK ya “mlima wa Mungu” (ona, k.m., Isa 56:7) ilikuwa “kivuli” au “nakala,” kutumia lugha ya picha au ya vitu vya kuonekana, kuonyesha maisha makuu zaidi na uhalisi wa kiroho wa Kristo mwenyewe (Wakol 2:16-17; Waeb 8:1-10:22). Katika Kristo, sisi“hamkufikia mlima uwezao kuguswa, . . . bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu ya mbinguni” (Waeb 12:18, 22; 13:14). Waeb 11:8-16 pia huweka bayana zaidi kuwa Ibrahimu mwenyewe hakuwa anatafuta nchi ya duniani ya kuonekana, bali wa kiroho: “Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu” (Waeb 11:10); na “Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni” (Waeb 11:16). Paulo aliweka hoja hiyo hiyo katika Wagal 4:21-31, aliposema kwamba mlima ule wa Sinai na Yerusalemu ya kidunia vilikuwa kiuhalisia kwenye utumwa, bali “Yerusalemu ya juu” ni huru, na “ni mama yetu.” Muhimu zaidi, “Paulo, siyo tu alihusisha mstari waYerusalemu ya kimbingu wa Agano la Kale (Isa. 54:1 in Wagal. 4:27) ambao hapo awali ulikuwa unahusu Yerusalemu ya kidunia; pia alikataa kabisa kuwa huo uliotangulia ulihusiana kivyovyote na ‘Yerusalemu ya juu’ (Walker 1996: 131). Vivyo hivyo, katika Math 5:14 Yesu alipozungumzia kuhusu “mji ulio mlimani,” maneno yake huenda yalikuwa “yanagusia unabii wa AK kuhusu wakati ambapo Yerusalemu au mlima wa nyumba ya Bwana, au Sayuni, utainuliwa juu, na mataifa wakiukimbilia” (Carson 1984: 139-40). Hakuna neno la uthabiti (“ule”) kabla ya “mji,” kwa hiyo

50

Page 52:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

kunenewa kwake hapo hakulengi uthabiti maalum, bali “kama kuna uthabiti, panasisitiza wanafunzi wa Yesu ndio wafanyao mlengo hasa wa watu wa Mungu, lengo thabiti la ufalme uliokamilishwa, na njia ya ushuhuda kwa ulimwengu—dhana zote hutokana na fikira za Mathayo” (Ibid.: 140).(3) AJ huendelea kutafsiri zaidi hiyo ahadi ya “nchi” kuhusisha roho ya mwamini au raha ya wokovu. Moyo wa ahadi ya nchi ulikuwa “raha” ya Israeli kutokana na adui zake wote, na kukidhiwa haja zake kamilifu kwa mahitaji yote (ona Kumb 12:9-11; 25:19; Yosh 1:23; Zab 95:10-11). “Maana ya kimsingi ya ahadi katika Mwanzo 17:8 [kuhusiana na nchi] ingelikuwa kiukweli imetuingiza sisi kuelewa kwamba kutahiriwa bado ni sharti kwa watu wa Mungu (Mwanzo 17:9-14). Bali Paulo alishinda ubishi kuhusiana na mtazamo huo katika Wagalatia na katika baraza la Yerusalemu (Matendo 15)!” (Travis 1982: 134) matokeo yake, Waeb 3:7-4:11 hubadilisha maana ya ahadi ya “nchi” iliyotolewa katika Agano la Ibrahimu, na kuilinganisha na raha yetu ya wokovu. Kuhusiana na ahadi ya nchi, Waeb 3:7-11, 15, 4:3, 5, 7 panaponukuu kutoka Zab 95:7-11, panaoibukia kutoka Hes 14:23 na Kumb 1:34-35, ambapo “kuingia katika raha ya Mungu” kunalinganishwa na nchi ya ahadi ya Kanaani. Hata hivyo, Waeb 3:11; 4:3, 5 pia palinukuu sehemu ile ya Zab 95:11`panaposema, “hawataingia katika raha yangu.” Waeb 4:9-11 huhitimisha kwa kusema kwamba kuna raha ambayo tunapaswa tuitamani kuiingia. “Maandiko haya [m.y., Waeb 3:7-4:11] yaelekea kupingana moja kwa moja [na Yosh 21:43-45] hadi tuelewe ni aina gani ya raha) na nchi humaanishwa katika Waebrania sura ya 3 na 4. Kizazi cha jangwani katika kitabu cha Kutoka hakikuruhusiwa ‘kuingia katika raha ya Mungu,’ ikimaanisha kwamba hawakuruhusiwa kuingia katika Nchi ya Ahadi. Hilo linaeleweshwa katika Waebrania 3 kumaanisha kuwa hawakuupokea wokovu. Yoshua, hata hivyo, aliwaingiza Waisraeli katika Nchi ya Ahadi na wakapewa raha kutokana na adui zao wa kimwili! Lakini mwandishi wa Waebrania anaelekeza kupitiliza utimilifu wa kimwili kuhusiana na nchi ya kidunia na raha yake mbali na vita kuingia katika raha ya kiroho. Ahadi ya Kanaani kama umiliki wa kudumu hatimaye na mwishowe unatimilizwa kwa umiliki wa wokovu wetu wa milele.” (Lehrer 2006: 36)

c. Ahadi ya“baraka”. “Kupitia Yesu, Mungu amefanya sawa sawa na alivyomwahidi Ibrahimu (Mwa 12:3) na baadaye akaipanua kupitia manabii; yaani, kupanua baraka kwa mataifa yote ya dunia” (Williamson 2007: 190). Katika Matendo 3:25-26 Pettro anukuu ahadi ya “baraka” iliyotolewa kwa Ibrahimu katika Mwa 22:18 na kuiweka kwa wote waliookolewa kwa imani katika Kristo, akitamka, “Ninyi mmekuwa watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa. Mungu, akisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.” Katika Wagal 3:8-9, 14 Paulo ananukuu ile ahadi ya “baraka” ya Mwa 12:3, bali aeleza kwamba “Baraka za Ibrahimu” ni kuhesabiwa haki katika imani ambako kunapatikana tu “katika Kristo Yesu.” Kwa hiyo, kama ilivyo kwa ahadi za “uzao” na ya “nchi”, hiyo “baraka” ilikusudiwa daima kutimilizika, siyo katika njia ya “kimwili”, bali kiroho katika Kristo.

B. Agano la Daudi linatimilizwa katika Kristo na kanisa.2 Sam 7:1-17 pana “Agano la Daudi” ambapo Mungu aliahidi kumwinua mzao wa Daudi baada yake na

“kukifanya imara kiti cha enzi cha ufalme wake milele” (2 Sam 7:12-13, 16). Agano la Daudi lilirekebisha Agano la Ibrahimu, na kuelekeza, kwa sehemu, jinsi Mungu atakavyotimiza ahadi yake kwa Ibrahimu. Matokeo yake, maagano hayo mawili yanashikamana. Hilo lilionekana katika Yer 33:23-26, ambapo panaunganisha utimizwaji wa maagano ya Ibrahimu na Daudi. Kusema ukweli, matamshi ya Mariamu (Luka 1:46-55) na unabii wa Zakaria (Luka 1:67-79), “huyaweka maagano ya Daudi na Ibrahimu kuwa kitu kimoja. . . . Na katika uelewa wa hatua kwa hatua wa nyaraka zinavyojieleza, wasomaji wanatambua kwamba ahadi ya Gabrieli kuhusu Yesu katika kiti cha enzi cha Daudi husimamia juu ya ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu” (Brawley 1995: 20). “Matukio muhimu mawili, juu ya yote, yanaonekana kama maandalizi ya kuja kwa Yesu. Hizi ni ahadi za maagano ya Ibrahimu, Isaka na Yakobo, na utawala wa Daudi. Watu watatu, Ibrahimu, Daudi, na Yesu, hufunganisha makusudio ya wokovu na matendo ya Mungu katika kazi moja kuu ya wokovu. Historia nzima ya Israeli hatimaye hunasika katika ufunuo wa ukombozi wa Mungu, ambao kilele chake ni Yesu Kristo.” (Goldsworthy 1991: 56)

1. Kizazi cha Yesu’ na kuzaliwa kwake kunaonyesha kwamba anatimiliza lile Agano la Daudi.

51

Page 53:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

a. Hata kabla Yesu hajazaliwa, malaika Gabrieli aliendeleza kutoka 2 Sam 7:12-13 na Isa 9:6-7, na kusema kwamba Yesu angelitimiza lile Agano la Daudi, pale alipomwambia Mariamu kwamba Yesu “Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho” (Luka 1:31-33). Kwa hiyo, Mathayo anaanza Injili yake kwa kumwelezea Yesu kama “mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu” (Math 1:1).15 Msemo “mwana wa Daudi” ni lugha ya kimasihi (ona, Math 22:42; Mark 12:35). Wengine waliotambua nguvu za Yesu na utofauti wake walitumia maneno “mwana wa Daudi” kwake (Math 9:27; 12:23; 15:22; 20:30-31; 21:9; Mark 10:47-48; Luka 18:38-39). Yesu alitumia maneno hayo kwake mwenyewe (Mark 12:35-37). b. Kulingana na 2 Sam 7:14 (“mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu”) maneno “Mwana wa Mungu” yalikuwa maneno ya kimasihi kuonyesha mfalme aliyeahidiwa wa kutokea kwa Daudi. Kwa hiyo, ili kuonyesha kutimizwa kwa Agano la Daudi, Yesu mara nyingi huitwa “Mwana wa Daudi” (Math 4:3, 6; 8:29; 26:63; 27:40, 54; Mark 1:1; 3:11; 15:39; Luka 1:35; 3:38; 4:3, 9, 41; Yoh 1:34, 49; 11:27; 20:31; Mdo 8:37; 9:20; Rum 1:4; 2 Wakor 1:19; Wagal 2:20; Waef 4:13; Waeb 4:14; 6:6; 7:3; 10:29; 1 Yoh 3:8; 4:15; 5:5, 10, 12, 13, 20). Yesu pia alijiita mwenyewe “Mwana wa Mungu” (Math 26:63-64; 27:43; Mark 14:61-62; Luka 22:70; Yoh 3:18; 5:25; 10:36; 11:4; 19:7; Ufu 2:18). c. Uhusiano wa Yesu na Yohana Mbatizaji ulitimiza unabii, na pia Agano la Daudi. Isa 40:3-11 naMal 3:1 panasema Bwana atamtuma mjumbe wake kabla Bwana hajaja kwa watu wake na kwenye hekalu lake. Zakaria (baba yake Yohana Mbatizaji) alithibitisha hilo kwa kusema kwamba Mungu “ametusimamishia penbe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake” (Luka 1:69, akimzungumzia Yesu). Kisha katika Luka 1:76, alinukuu kutoka Mal 3:1 katika kumzungumzia Yohana Mbatizaji (“ Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake Aliye juu. Kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake”). Yohana Mbatizaji mwenyewe alinukuu kutoka Isa 40:3-5 na Mal 3:1 kabla ya Yesu kubatizwa (Math 3:3; Mark 1:2-3; Luka 3:4-6; Yoh 1:23). Yesu mwenyewe anathibitisha kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ndiye“mjumbe” aliyetajwa katika unabii wa Mal 3:1 (ona Math 11:7-10; Luka 7:24-27). Kwa hiyo, Yohana Mbatizaji na Yesu walitimiza unabii wa Isa 40:3-11 na Mal 3:1. Zaidi ya hayo, kama vile Mal 4:5 palivyosema kwamba Mungu angelimleta Eliya nabii, hivyo Yohana Mbatizaji anaonekana kuwa na roho ya Eliya kuandaa watu kwa ajili ya kuja kwa Bwana (Math 11:14; 17:10-13; Mark 9:11-13; Luka 1:13-17, 76). d. Katika kutimizwa kwa unabii wa Mika (Mika 5:2; Math 2:1-6; Yoh 7:42) Yesu alizaliwa Bethlehemu, ambako alitokea Daudi (Ruth 4:11, 22; 1 Sam 16:1-13). Luka anataarifu kwa umakini kwamba Yusufu (baba yake mlezi) alikuwa “wa nyumba na ukoo wa Daudi,” na ya kuwa Bethlehemu, ambako Yesu alizaliwa, ulikuwa “mji wa Daudi” (Luka 2:4).

2. AJ huonyesha maisha ya Yesu kama yale ya mfalme aliyeahidiwa wa kiti cha Daudi. Katika Isa 11:1-10 nabii alitabiri kwamba, “basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda. Na Roho ya Bwana itakaa juu yake.” Yer 23:5 panasema kwamba “chipukizi la haki” ambalo Bwana “atamchipushia Daudi” lita “tawala kama mfalme” (ona pia, Yer 30:9). Waandishi wa AJ wanasisitiza ukweli kwamba Yesu alikuwa “mzao wa Daudi” (Yoh7:42; Mdo13:22-23; Rum 1:3; 2 Tim 2:8). Yesu mwenyewe anathibitisha yote mawili – mamlaka yake ya Ki-Daudi na ukoo wake (Ufu 3:7; 5:5; 22:16). Katika Rum 15:12 Paulo anukuu Isa 11:10 na kuihusisha kwa Yesu Kristo na kusanyiko la Mataifa kuwa kanisa. Nafasi ya Yesu kama mfalme aliyetabiriwa wa ukoo wa Daudi kwa Israeli huonekana katika kila hatua ya maisha yake duniani, na sasa katika utukufu wake wa ki-ufufuo.

a. Maisha ya Yesu ya mwanzo. Mamajusi waliokuja kutokea Mashariki baada ya Yesu kuzaliwa walilielewa hilo kutokana na kusoma AK (ona Math 2:1-6). Swali lao lilikuwa, “Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia” (Math 2:2). b. Kubatizwa kwa Yesu na kubadilika sura. Math 3:16 na Yoh 1:32 zote huhusisha Isa 11:2 kwa Yesu wakati wa kubatizwa kwake ambapo Yohana Mbatizaji aliona “Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake.” Wakati wa kubatizwa kwa Yesu na kubadilika sura kwake, tamko la Baba yake lilikuwa, “Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu, anayependezwa

15 “Wengi wameonelea kwamba mgawanyo wa Mathayo wa vizazi vya Yesu kuwa katika mafungu matatu-matatu ya vizazi kumi na nne (1:17) huweza pia kudokeza tabiza zake za Udaudi kwa vile thamani ya kihesabu ya jina la Daudi kwa Kiebrania (herufi d, w, na d) ni kumi na nne (d = 4, w = 6)” (Holwerda 1995: 33n.10).

52

Page 54:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

nawe” (Math 3:17; Mark 1:11; Luka 3:22), huleta mwangwi Zab 2:7. Zaburi 2 ni Zaburi ya kimasihi, na “mistari inayotangulia mara tu kabla ya Zaburi ile ilikuwa inahusiana na dhana ya ufalme wa Daudi katika Yerusalemu” (Walker 1996: 2). Katika Mdo13:32-33 Paulo ahusisha kibayana Zab 2:7 kwa Yesu kuhusiana na ufufuo. Kama vile Daudi alivyopakwa mafuta na Samweli kabla hajatambuliwa kama mfalme wa kweli wa Israeli, ndivyo ubatizo wa “Yesu’ ulivyokuwa utawazo wake kama mfalme wa kweli wa ukoo wa Daudi juu ya Yerusalemu. . . . Wakati Marko baadaye anaelezea kuja kiukweli kwa Yesu alipoingia Yerusalemu, dhana hizi hujitokeza juu—za Yesu kama ‘Mfalme’ wa kweli wa ukoo wa Daudi (10:47-48; 11:10; 12:35) na kama ‘Bwana’ (11:3).” (Ibid.) Mwonekano huo huo wa Yesu, Eliya [yaani Yule Eliya mwenyewe, siyo Yohana Mbatizaji], na kupaka mafuta kwa Baba “huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye” uliokuwepo wakati wa kubatizwa kwa Yesu, hujitokeza pia wakati wa kubadilika sura yake (Math 17:1-13; Mark 9:1-13; Luka 9:28-36). c. Mwanzo wa huduma ya Yesu. Mtu wa Nathanaeli wa kwanza kukutana na Yesu alisema, “Rabi, wewe u Mwana wa Mungu; ndiwe Mfalme wa Israeli” (Yoh 1:49).d. Huduma ya Yesu katika Galilaya. Yesu alipoanza huduma yake katika Galilaya, Math 4:14-16 anaiweka hiyo katika nuru ya kutimizwa kwa unabii, kwa kunukuu Isa 9:1-2 (“nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali . . . wameona nuru kuu”). “Mathayo anatamka muunganiko wa aina mbili kati ya unabii huu na Yesu. Kwanza, unabii unaahidi nuru na wokovu kwa watu waishio katika Galilaya. Pili, Muktadha wa Isaya 9: m.y; ahadi kwamba wokovu utapatikana kwa Mwana wa Daudi aliyeahidiwa, atakayeufanya imara ufalme wa milele. Kwa hiyo kwamba Yesu alihudumu Galilaya siyo kwamba inabainishwa kwa sababu za Kijiografia, bali ni ufunuo kuwa wivu wa Yahwe sasa uko kazini katika historia kuimarisha utawala wa usawa na wa haki ulioahidiwa wa Daudi (Isaya 9:6f.).” (Holwerda 1995: 49)e. Kuingia kwa Yesu Yerusalemu kwa mara ya mwisho. Sef 3:8-20 ni tamko la hukumu na wokovu. Huishia na jumuiya mpya (“mabaki ya Israeli”—Sef 3:12-13) na “mfalme wa Israeli, maana yeye Bwana, yu kati kati yako” (Sef 3:14-17). Ataleta amani na furaha “katika mlima wangu mtakatifu” (Sef 3:11, 18-20). Zek 9:8-17 hutoa tamko linalofanana la wokovu kwa Israeli. Mfalme aelezwa kama “anakuja kwako . . . mnyenyekevu, na amepanda punda, naam, mwana-punda, mtoto wa punda (Zek 9:9). Yesu alipoingia Yerusalemu mara ya mwisho, Injili zote nne zilitafsiri kuwa ni ujio wa mfalme aliyetabiriwa wa kiti cha Daudi (Math 21:1-11; Mark 11:1-11; Luka 19:28-40; Yoh 12:12-16). Mark 11:10 husema bayana, “Umebarikiwa na ufalme ujao.” Mathayo na Yohana huchanganya nukuu za kutoka Isa 62:11, Sef 3:16, na Zek 9:9 kuthibitisha kwamba Yesu atimiza unabii wa mfalme wa Israeli kuingia Yerusalemu (Math 21:1-5; Yoh 12:12-16).f. Kuteswa kwa Yesu na kifo chake. Yesu mwenyewe alithibitisha kwamba alikuwa “mfalme wa Wayahudi” (Math 27:11; Mark 15:2; Luka 23:3). Katika Yoh 18:33-37, hata hivyo, akiwa katika kuthibitisha kwamba ndiye, hakika, mfalme, Yesu pia alionyesha kwamba aina ya ufalme wake haukuwa wa kuonekana, wa hapa duniani ambao watu walio wengi walikuwa wakiutarajia. Alipokuwa anasulubiwa, kibao kiliwekwa juu yake kikimtangaza kwamba yeye alikuwa “Mfalme wa Wayahudi” (Math 27:37; Mark 15:26; Luka 23:38; Yoh 19:19-20; ona pia, Math 27:42; Mark 15:32; Luka 23:37; Yoh 19:21-22). g. Ufufuo wa Yesu. Katika Mdo 2:29-36 Petro alinukuu Agano la Daudi “Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake [Daudi] atamketisha mmoja katika kiti chake cha enzi” (Mdo 2:30; k.v. Zab 132:11), na pia alinukuu Zab 16:10 kwamba Mungu “hatamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu” (Mdo 2:27, 31). Kisha akasema unabii huo haukuwa unamzungumzia Daudi, kwa sababu “alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo” (Mdo 2:29). Badala yake, unabii huo “yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake” (Mdo 2:31). Zaidi ya hayo, ahadi zote za milele, baraka, na rehema zilizoonyeshwa kwa Daudi zilijumuishwa kwa maneno ya Isaya “rehema za Daudi zilizo imara” (Isa 55:3). Ahadi muhimu na baraka kwa Daudi zilikuwa “Na nyumba yako na, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako, nacho kiti chako kitafanywa imara milele” (2 Sam 7:16). Katika Mdo13:34 Paulo anukuu LXX [m.y., tafsiri ya Biblia ya Kiyunani; pia kujulikana kama “Septuagint”] ya Isa 55:3 na husema kwamba ahadi za “baraka za hakika na takatifu za Daudi” zimetimizwa katika ufufuo wa Yesu. Kwa hiyo, ufufuo wa Kristo kutoka kwa wafu ni njia ya Mungu kutimiza ahadi zake kuimarisha kiti cha enzi cha Daudi milele.

3. Yesu alithibitisha mwenyewe kama “mwana mkuu” wa Daudi zaidi ya mara moja.a. Wakati wanafunzi wa Yesu walipotwaa masuke ya ngano siku ya Sabato (Math 12:1-8; Mark

53

Page 55:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

2:23-28; Luka 6:1-5). Wakati wanafunzi wa Yesu wanashutumiwa na Mafarisayo kuhusu kuivunja Sabato kwa kuvunja masuke ya ngano walipokuwa wakipita katika mashamba, Yesu akagusia 1 Sam 21:1-6, ambapo Daudi na wafuasi wake walipokula “mikate ya wonyesho” iliyowekwa wakfu kutoka Hema ya kukutania. Yesu aliona kule kukosea kwa kitendo cha Daudi (ambapo“haipaswi mtu mwingine kuila isipokuwa makuhani peke yao”). Hoja ya Yesu siyo kwamba kitendo cha Daudi kinaondoa hatia ya kile wanafunzi walichokifanya (“haipendekezwi kwamba mfano wa Daudi utoe kibali kwa kila Mwisraeli mwenye njaa kula mkate wa wonyesho, au kuvuna masuke ya ngano siku ya Sabato” [Beare 1960: 134]). Wala pia haendekezi vipaumbele vya haja za watu vitangulizwe zaidi ya sheria inavyotaka (katika tukio hili, hadai kuwa wale wanafunzi walikuwa wana njaa ya kufa au kinamna walikuwa na uhitaji). Wala hasemi pia kimsingi kwamba Maandiko huruhusu huruma kubwa zaidi kuliko Mafarisayo. Bila shaka, Yesu anatangaza ki-masihi: “Mtazamo wa kuridhisha zaidi waweza kupatikana pale msisitizo wa muktadha ulio katika mstari unatambuliwa: 1. Simulizi zote tatu huonyesha kwa nguvu, kwa mifano ya kiutata, uhusiano wa Daudi na wafuasi wake; 2. Simulizi zote tatu huhitimisha kwa madai ya uelekeo wa mamlka ya mwelekeo wa ki-Kristo juu ya Sabato; na 3. Mathayo anaongeza mara moja baada ya kuzingatia 1 Samuel 21 uzingativu bayana wa kielelezo cha AK [m.y., Math 12:5-6]. Vikichukuliwa pamoja, vipengele hivi huashiria kwamba hoja ya msingi ni kuweka mfananisho wa uhusiano kati ya Daudi na Yesu: ikiwa Daudi, pamoja na wafuasi wake, anayo haki ya kuivunja sheria, ‘mwana mkuu ’ wa Daudi na wafuasi wake wanayo haki iliyo kuu zaidi.” (Moo 1984: 8; ona pia, Beare 1960: 134)b. Baada ya Kuingia Kwa Shangwe Yerusalemu, wakati Yesu ananhojiana na Mafarisayo (Math 22:41-46; Mark 12:35-37; Luka 20:41-44). Yesu aliwauliwa Mafarisayo walikuwa waonaje kuhusu Kristo: “Yeye ni Mwana wa nani?” Walimjibu kuwa yeye ni “mwana wa Daudi.” Kristo, kisha wakanukuu Zab110:1 ambayo husema, “neno la BWANA kwa Bwana wangu.” Kisha tena akasema, “Ikiwa Daudi [aliyeiandika Zaburi] amwita yeye ‘Bwana,’ inakuwaje basi huyo awe mwanawe?” Yesu alikuwa anajielekezea kwake mwenyewe kama Masihi, “mwana mkuu” wa Daudi, na ya kuwa alikuwa ni Mungu. Waandishi wa AJ walielewa kile ambacho Yesu alikuwa anakisema. Zab 110:1 kwa sababu mstari wa msingi katika AJ (kuna nukuu au vihusisho 21 vinavyolenga mstari huo katika maandiko mengi ya AJ). Umuhimu wa hili kwa waandishi wa mwanzo wa Ukristo, hasa tukichukulia muktadha wao binafsi wa ufinyu wa kifikara wa Kiyahudi ulikwa mkubwa. “[Zab110:1] je pasingeweza, kwa mfano, kusomeka kiharaka kumaanisha kuwa Masihi anapewa nafasi ya heshima kama mtu apendwaye tu tofauti na kiti cha enzi cha Uungu, ambapo anaketi pasipo kazi akingojea ufunguzi wa utawala duniani. Hivi ndivyo baadhi ya walimu baadaye walivyolielewa. Inaonyesha dhahiri, hata hivyo, kwamba Wakristo wa mwanzo walielewa tofauti: kama kumweka Yesu katika nafasi ya kiti cha enzi cha Uungu chenyewe, wakiutumia utawala wa Mungu juu ya vitu vyote.” (Bauckham 1998: 29)

4. Hivi sasa Yesu amepaa , na anakalia, na anatawala kutoka, hicho “kiti cha enzi cha Daudi.” Kabla hajazaliwa, malaika Gabrieli alimwahidi Mariamu kuwa Bwana Mungu angempa Yesu “kiti cha enzi cha Daudi, baba yake; na ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho” (Luka 1:32-33). Baada ya kufufuka kwake, Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa, “Nimepewa mamlaka yote mbiguni na duniani” (Math 28:18). Ilikuwa ni katika kupaa kwake, hata hivyo, ndipo kipengele cha mwisho cha Agano la Daudi kilitimizwa— “mzao” wa kweli wa Daudi, Mwana wa Mungu alikaa juu ya “kiti cha enzi cha Daudi” ambapo anatawala sasa kwa mamlaka yote (ona, Mark 16:19; Luka 22:69; Waef 1:20-23; Wakol 3:1; Waeb 1:3; 1 Petr 3:21-22; Ufu 1:5; 3:21). Katika siku ya Pentekoste, Petro alielezea wazi wazi jinsi Yesu alivyotimiza Agano la Daudi kwa kufufuka na kupaa kwake (Mdo 2:22-36). Petro alihusisha, kwa kunukuu na kuhusisha, 2 Samweli 7 na Zaburi 16:8-11, 110:1, na 132:11, kuoanisha na, “Kukaa katika kiti cha enzi cha Daudi kunaoanishwa na kuketi mkono wa kuume wa Mungu. Kwa maneno mengine, Kufufuka na kupaa kwa Yesu kwenda mkono wa kuume wa Mungu kwawekwa bayana na Petro kama ni kutimilizwa kwa Agano la Daudi” (Bock 1992: 49).

C. Agano Jipya latimilizwa katika Kristo na kanisa.Yer 31:31-34 paliahidi Agano Jipya “kwa nyumba ya Israeil na nyumba ya Yuda.” Agano Jipya

litakuwa ni Agano la milele ambalo Mungu ataandika sheria zake katika mioyo ya watu wake; watu wake watamjua Bwana; naye atawasamehe dhambi zao na kutozikumbuka tena (ona pia Yer 32:38-40; 50:4-5; Ezek 11:16-20; 36:24-32; 37:15-28).

54

Page 56:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

1. Katika Karamu ya Mwisho, Yesu aliweka bayana kuwa alikuwa anaweka Agano Jipya kwa damu yake ( Luka 22:20; ona 1 Wakor 11:25 ). “Kuoanisha kwa hayo mawili, msamaha uliotarajiwa na Yeremia (Math. 26:28; Yer. 31:34) na damu inavyohusishwa na kuimarishwa kwa Agano la Kwanza na Musa (Luka 22:20; Kut. 24:7) huongeza uzito kwamba Yesu alielewa kifo chake kuwa ni kuanzisha Agano Jipya” (Williamson 2007: 184). Agano lilithibitishwa na kuhitimishwa msalabani (Waeb 9:12-17). Lilithibitishwa wakati Yesu alipofufuka kutoka kwa wafu, kisha akapaa mbinguni na kuketi katika kiti cha enzi na Baba (Waeb 10:11-18). 2. Ingawaje katika muundo wake wa awali lilipotolewa kwa Yeremia, Agano Jipya lilikuwa kwa “nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda,” kama ilivyo kweli kwa Maagano ya Ibrahimu na Daudi, AJ huthibitisha kuwa Agano Jipya hutimilizwa katika Kristo na kanisa, na siyo kwa (ma)taifa ya kimwili ya Israeli na Yuda.

a. Yesu alipoanzisha Agano Jipya wakati wa Karamu ya Mwisho, kuhusisha na “hilo” Agano Jipya kungeweza tu kuhusishwa na Agano Jipya lililoahidiwa na Yeremia, kwa sababu Yer 31:31 ni mahali pekee ambapo maneno “Agano Jipya” yalitumiwa katika Maandiko kabla ya Yesu kulitaja wakati wa Karamu ya Mwisho. Kwa hiyo, Agano Jipya hufanya kazi kwa wale wote walio waamini katika Kristo (m.y., kanisa), awe Myahudi au Mataifa (kama Paulo awekavyo wazi anaponukuu maneno ya Yesu kwa sehemu kubwa akilenga kanisa la Wamataifa katika Korintho 1 Wakor 11:25).16 b. Waebrania 8-10 moja kwa moja hulihusisha Agano Jipya na Kristo na kanisa. Waeb 8:8-12, nukuu ndefu kuliko zote ya AK katika AJ hunukuu Agano Jipya la Yer 31:31-34 lote (kuchanganya mahusiano na “nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda”). Sehemu iliyobakia ya Waebr 8-10 huhusisha Agano Jipya kwa kanisa. Hunukuliwa tena katika Waeb 10:16-17. Waeb 10:15-18 huhusisha Agano Jipya “kwetu” [m.y., Wakristo; kanisa]. Waeb 8:6, 9:15, na 12:24 zote hueleza kwamba Kristo ndiye mpatanishi wa Agano Jipya. Ukweli kwamba yeye “ndiye” (wakati wa sasa) mpatanishi huonyesha kwamba Agano Jipya liko kazini sasa. Waeb 9:12-17 huonyesha kwamba damu ya Kristo ilithibitisha na kukamilisha Agano Jipya. Waeb 8:13 huonyesha kwamba Agano Jipya limefanya Agano la kwanza (m.y., la Kale, au Agano la Musa [ona Waeb 8:9]) liwe kuu kuu. Waeb 10:9 vivyo hivyo husema kwamba, “aondoa la kwanza, ili makusudi alisimamishe la pili.” Hoja nzima ya Waebr 8-10 ni kwamba Agano la Musa, hekalu, ukuhani, sheria, na mfumo mzima wa dhabihu za Israeli, zilikuwa tu ni “ishara” (Waeb 9:9), au “nakala” (Waeb 9:23-24), au “kivuli” (Waeb 10:1; ona pia, Wakol 2:16-17) cha “agano lililo bora zaidi” lililofanywa kwa “ahadi zilizo bora zaidi” (Waeb 8:6): m.y., uhalisi wa kweli na wa kudumu upatikanao katika Kristo na Agano Jipya. c. Paulo analihusisha Agano Jipya kwa kanisa. Katika 2 Wakor 3:5-6 (iliyoandikwa kwa kiasi kikubwa kwa kanisa la Mataifa la Korintho) Paulo anasema kuwa “Mungu . . . ametufanya sisi . . . watumishi wa Agano Jipya.” Hoja nzima ya 2 Wakor 3 hutofautisha Agano la Musa na Agano Jipya: (1) Ni utofauti kati ya andishi na Roho (2 Wakor 3:3, 6, 17-18). (2) La kwanza ni huduma ya mauti na hukumu; la pili ni uzima, matumaini, uhuru, na Roho (2 Wakor 3:6-9, 12, 17). (3) Ni utofauti kati ya kitu kilichoandikwa juu ya mawe na kuandikwa juu ya mioyo ya wanadamu (2 Wakor 3:2-3, 7). (4) Kila moja lina utukufu wake, lakini lile la pili lina utukufu mkuu zaidi usio na kifani (2 Wakor 3:7-11, 18). (5) La kwanza linatoweka, bali la pili ladumu milele (2 Wakor 3:7, 11, 13). (6) La kwanza lina pazia, lakini katika lile la pili, pazia limeondolewa (2 Wakor 3:13-16, 18). Matokeo yake, ni Agano Jipya peke yake linatupa ujasiri na kutubadilisha kuwa katika kumfanania Kristo (2 Wakor 3:2-3, 12, 18). Vivyo hivyo, Katika 2 Wakor 4:3-6 Paulo “analiita ‘Agano Jipya’ kuwa ni Injili ya Yesu Kristo (2 Wakor. 4:3-6), na jumuiya ya Wakristo kuwa ndio ambao baraka za Agano Jipya zimetolewa kwao (2 Wakor. 3:3; cf. Yer. 31:32-33; Ezek. 11:19; 36:26-27). . . . Bila shaka, mistari hii hutoa bubujiko la uzima, ukombozi na “huduma ya Roho” ya utukufu zaidi (2 Wakor. 3:8) inayoendana na ‘watumishi wa Agano Jipya (2 Wakor. 3:6).” (Williamson 2007: 192, 192n.33) Katika Wagal 4:21-31 “Wake za Ibrahimu, Hajiri na Sara, wanatafsiriwa kuwakilisha maagano mawili tofauti. La kwanza katika hayo (liwakilishwalo na Hajiri) hujulikana kama Agano la Musa (‘kutoka mlima Sinai . . . katika Uarabuni’ Wagal. 4:24-25 ESV). Agano la pili (linalowakilishwa na Sara),

16 Kusema ukweli, mtu anaweza kusema kwamba Agano Jipya lilianzishwa na Israeli na Yuda kwa maana kwamba wanafunzi wote waliokuwepo wakati wa Karamu ya Mwisho walikuwa Waisraeli. NHata hivyo, AJ laweka bayana kabisa kwamba Agano Jipya huhusisha Wakristo wote (m.y., kanisa), pasipo kujali ni Wayahudi au Mataifa. Kwa vile ni Agano Jipya peke yake linalosamehe dhambi (m.y., kupitia Kristo), Agano Jipya ni njia pekee ambayo Israeli wanaweza kuokolewa (ona Rum 11:26-27).

55

Page 57:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

ingawaje haitajwi wazi, ni dhahiri huhusishwa na mlima Sayuni na ahadi za Agano Jipya (Wagal. 4:26-27; pia. Isa. 54:1). Kwa hiyo Hajirii huwakilisha agano la utumwa (kwa sheria), liendanalo na ‘Yerusalemu ya sasa (Wagal. 4:25 ESV), ambapo Sara anawakilisha agano la uhuru na ahadi iunganikayo na ‘Yerusalemu ya juu’ (Wagal. 4:26 ESV).” (Ibid.: 199)

3. Katika Ezek 36:25-27 Mungu aliahidi “kunyunyizia maji safi juu yenu, nanyi mtakuwa safi,” na akasema, “nami nitawapa ninyi moyo mpya nami nitatia roho mpya ndani yenu; nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapeni moyo wa nyama,” na “nitatia Roho yangu ndani yenu.”

a. Musa aliomba, “ingekuwa heri kama watu wote wa BWANA wangekuwa manabii, na kama BWANA angewatia roho yake!” (Hes 11:29). katika AK, Roho wa Mungu aliwajia watu wa aina fulani tu, kikawaida ni wale walio katika nafasi za kidini au mamlaka ya kisiasa, ili kufanya majukumu fulani (ona Kut 31:3; Hes 11:16-29; Waam 3:10; 6:34; 14: 6, 19; 1 Sam 10:1-11; 16:13-14; 19:20-24). b. Waeb 10:22 huibua Ezek 36:25 kwa kunena kuwa“hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya; tumeoshwa miili kwa maji safi.” 2 Wakor 3:3 pia huibua Ezek 36:26 pale Paulo asemapo, “mmedhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.” Yesu aliahidi kutuma Roho wake ambaye “atakuwa nanyi hata milele” naye “atakaa nayi” (Yohana 14:16-17). Kuanzia siku ya Pentekoste amelitekeleza hilo. Hakuna tena kwamba Roho wake wala vipawa vyake kuwa kwa wachache tu , bali sasa katika Agano Jipya Mungu amemwaga Roho wake kwa watu wake wote, bila kujali umri, jinsia, au jamii ya watu (Mdo 2:14-18; ona pia Rum 8:9; 1 Wakor 3:16; 6:19). Sasa, “wale wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” (Rum 8:14). Roho “hutia arabuni” watu wake, tofauti na wakati wa AK (Waef 1:13-14). “Paulo anaendelea zaidi kueleza kwamba Roho sasa huwawezesha watu wa Mungu kutekeleza yale ambayo Sheria haikuweza kuyakamilisha: ‘ili kwamba maagizo ya haki katika sheria yapate kutimilizwa kikamilifu ndani yetu’ (Rum. 8:4)” (Burke 2006: 133-34). Kwa hiyo, “Agano la Kale lililoanzishwa mlima Sinai limesimamishwa na Agano Jipya lililotabiriwa katika Agano la Kale na nabii Yeremia na Ezekieli. . . . Mkondo huu wa kiujumla (kubadilisha Agano la Kale na Jipya) kama tulivyoona, hutajwa katika Wagalatia na Warumi kuwa ndiko zama za kale za Sheria (Wagal. 3/Rum. 7) na zama mpya ya Roho (Wagal. 4/Rum. 8). Mabadiliko ya maagano yalikuwa ni lazima kwa sababu hakuna mtu yeyote aliyeweza kutimiza kikamilifu maagizo yote ya Agano la Kale, ukweli ambao Israeli waliuthibitisha mara kwa mara kitaifa na hata kwa mtu moja moja binafsi.” (Ibid.: 132)

4. Kwa vile ni Agano Jipya pekee litoalo msamaha wa dhambi, na ni katika Kristo peke yake dhambi za watu zinasamehewa, msamaha wa dhambi ndio msingi wa Injili. Agano Jipya ni Agano pekee kati ya yote ya Mungu ambalo linatoa mwanya wa kusamehewa dhambi. Hilo hukamilishwa na Kristo, “Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya dunia” (Yohana 1:29; ona pia Math 1:21; Mdo 5:31; 1 Yoh 3:5). Matokeo yake, kutangaza masamaha ya dhambi katika Kristo ndiko msingi wa Injili (ona, Luka 24:44-49; Mdo 2:38; 10:43; 13:38-39; 26:15-18).

III. Yesu Atimiza Maana na Kusudio la Israeli Kama Taifa, na Taasisi Zote za Israeli: Sikukuu zake; Mifumo ya Dhabihu; Ukuhani; Sheria, na Sabato.

Taifa la Israeli la Agano la Kale, na Sheria zake zote, sikukuu zake, na taasisi zake, zilikuwa “ni aina,” “ishara,” “vivuli,” “nakala,” au “mifano” ya uhalisi wa AJ uliotimilizwa katika Kristo na kanisa lake (Math 5:17; 1 Wakor 10:1-6; 2 Wakor 3:12-16; Wagal 3:23-4:7, 21-31; Wakol 2:16-17; Waeb 1:1-2; 8:1-10:22).

A. Yesu ndiye Israeli mpya, wa kweli, aliye mwaminifu.“Ikiwa Yesu ndiye ambaye kwa yeye ahadi ya [Ibrahimu] inatimilizwa, basi anaweza akadai kuwa

ndiye mzao wa kweli wa Ibrahimu, na ndivyo alivyopaswa awe mzao wa Ibrahimu. Yesu basi, ndiye Israeli wa kweli, yeye afanyaye kila kitu ambacho Israeli alitakiwa kukifanya na ndiye kila kitu ambacho Israeli alitakiwa awe.” (Holwerda 1995: 33) Yesu anaendeleza pale wote wawili, Adamu na Israeli waliposhindwa. Kwa hiyo, yeye peke yake afanya uwezekano wa utu mpya. Hili linaonekana kwa njia kadhaa.

1. Yesu arandana na historia ya Israeli. a. Yesu na Kutoka. Math 2:15 hunukuu Hos 11:1, “Kutoka Misri nalimwita Mwanangu,” na kuihusisha na Yesu. Mungu hapo kwanza alimwita Israeli “mwanangu” wakati ule wa Kutoka (Kut 4:22—“Israeli ni mwanangu, mzaliwa wangu wa kwanza”). Mathayo sasa anatuonyesha

56

Page 58:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

jinsi historia ya Israeli ya AK inavyojirudia kwa Yesu. Yesu kimsingi anatenda upya Kutoka kuanzia Misri katika Math 2:19-21. Hos 11:1-11 sehemu zote huelezea kutoka kwa Israeli na hudokeza kutoka kwa mara ya pili kwa sababu ya kutokutii kwa Israeli baada ya kutoka kwa mara ya kwanza kupangua mpango wa Mungu kuumba watu watakatifu. Ingawaje lile taifa la kimwili lilirudi katika nchi baada ya uhamisho Babeli, lilibaki chini ya mamlaka ya tawala za kigeni, na “taifa takatifu” kamwe halikupatikana kiukweli. Kwa kuihusisha Hos 11:1 na Yesu, “Mathayo anatamka siyo tu kwamba ndiye Israeli, Mwana mpendwa wa Mungu, bali pia kutoka kulikotarajiwa muda mrefu kumeanza.” (Holwerda 1995: 40). b. Kubatizwa kwa Yesu pia ni marudio ya tendo la kuvuka kwa Bahari ya Shamu na mto Yordani (ambao ndio aliobatiziwa nao), na kuiingia nchi (Kut 14:13-22; Yosh 3:14-17; ona Math 3:13-17; Mark 1:9-11; Luka 3:21-22; Yoh 1:31-34).c. Yesu ni Mwana wa kweli wa Mungu. Kama vile Hos 11:1 iimwita Israeli “mwanangu,” Baba anathibitisha kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu wa kweli wakati wa kubatizwa kwa Yesu (na pale alipobadilika sura yake), ambapo alimwita Yesu “mwanangu mpendwa wangu” (ubatizo—Math 3:17; Mark 1:11; Luka 3:22; kubadilika sura—Math 17:5; Mark 9:7; Luka 9:35; ona pia Math 4:3; 14:33; Mark 3:11; Luka 1:35; Yoh 1:34, 49; Mdo 9:20; Wagal 2:22, kwa Yesu kama “Mwana wa Mungu”). d. Yesu akiwa nyikani. Siku arobaini za Yesu nyikani (Math 4:1-2) ni kifupisho cha miaka arobaini ambayo Israeli ilitumia katika nyika. Majaribu aliyokutana nayo Yesu kule nyikani (Math 4:1-11; Luka 4:1-13) huendana sambamba na majaribu ya Israeli kule nyikani. “Katika jaribu la kwanza, na majibu ya Yesu kuna mambo kadhaa ya kuvutia na ya muhimu yanayoshabihiana yanayojikita katika dhana inayofanana ya uana wa wote wawili, Yesu na taifa la Israeli. Wote ni ‘wana’ (Kumb. 8:5; pia. Math. 4:3, 6); wote ‘wanaongozwa’ (Kumb. 8:2; pia. Math. 4:1); wote wanapelekwa jangwani/ nyikani (Kumb. 8:2; pia. Math. 4:1); na wote wawili wanaona njaa (Kumb. 8:3; pia. Math. 4:2).” (Burke 2006: 173-74n.55) Pale Israeli ilipokuwa haikuridhishwa na mana iliyotolewa na Mungu (Hes 11:1-6), Yesu alijaribiwa kubadili mawe yawe mkate (Math 4:3; Luka 4:3). Baadaye, baada ya kulisha watu 5000, Yesu alijifananisha mwenyewe rasmi na mana ambayo Israeli walikula kule jangwani kwa kusema, “Mimi ndimi mkate ushukao kutoka mbinguni” (Yoh 6:1-14, 41, 48-58). Pale Israeli walipomjaribu Mungu kule Masa na Meriba wakitaka uthibitisho wa uwepo wake na nguvu zake (Kut 17:1-7), Yesu alijaribiwa kuruka kutoka juu ya Hekalu kumlazimisha Mungu asimamie ahadi zake (Math 4:5-6; Luka 4:9-11). Israeli walipomwacha Mungu na kuiabudu sanamu ya ndama (Kut 32:1-6), na baadaye kuabudu Baali (Hos 2:1-13), Yesu alijaribiwa kumpigia magoti na kumwabudu Shetani (Math 4:8-9; Luka 4:5-7). Zaidi ya hapo, Yesu alikutana na majaribu kwa kunukuu kwa makusudi kabisa kutoka kwa ufupisho wa historia ya Musa ya wana wa Israeli kule nyikani (Kumb 8:3; 6:13, 16). e. Mathayo hunukuu Yer 31:15 (“Sauti imesikiwa Rama . . . Raheli akiwalilia watoto wake”) na kulihusisha kwa Yesu (Math 2:17-18). Rama ni mahali ambapo mateka wa Yuda walikusanywa katika minyororo kupelekwa uhamishoni Babeli (ona, Yer 40:1). Umuhimu wa Mathayo kutumia “Rahei kuwalilia” ni kama ifuatavyo: “Raheli, mama mpendwa wa Israeli, alikuwa ameshakufa karne kadhaa nyuma na alizikwa njiani kutoka Betheli kwenda Bethlehemu-Efrati, siyo mbali kutoka Rama. Israeli walivyokuwa wakisafiri kwenda uhamishoni, nabii ‘amsikia’ Raheli akiomboleza na kuwalilia watoto wake. Bali Bwana amwagiza Raheli aache kulia kwa sababu ‘kuna tumaini kwa siku zako za mbeleni’ na watoto wake watarudi tena (31:16-17). Israeli walirudi kutoka uhamishoni, bali makandamizo kutoka kwa adui yaliendelea pasipo kukoma. Kwa hiyo, Mathayo, kama Yeremia, amsikia Raheli akiendelea kulia juu ya upotevu wa watoto wake: Kwa Herodi kuwachinja watoto, makandamizo na uharibifu kwa Israeli bado waendelezwa. Tumaini lililoahidiwa kwa Raheli halikuwa limedhihirika kikamilifu. Mathayo ananukuu Yeremia 31:15 siyo tu kujenga uendelevu wa maombolezo ya Israeli, bali pia kutoa ishara ya kutimizwa kwa tumaini la Israeli lililomo katika muktadha wake. Yesu aponyoka na uchinjwaji ule, na ndani yake kuna utimizwaji wa tumaini la Israeli. Kwa vile sasa Yesu ndiye Israeli, uzao wa kweli wa Ibrahimu na Mwana wa kweli wa Mungu, ahadi ya Mungu kwa Raheli ya jamaa kurejeshwa iko njiani kutimilizwa. Ahadi iliyoahidiwa kwa ajili ya siku zijazo sasa inaonekana. Yesu aondoa kongwa la historia ya Israeli na katika hilo kuirejesha Israeli.” (Holwerda 1995: 42)

2. AJ lamwonyesha Yesu kama Musa mpya aliye mkuu zaidi, awafunguaye watu wake siyo tu kutoka katika vifungo vya kimwili, bali kutoka katika utumwa wa kiroho wa dhambi na mauti ( Yoh 1:29; Rum

57

Page 59:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

6:3-23 ). a. Musa alikuwa kitangulizi cha Masihi. Musa alitabiri kwamba Mungu atamwinua nabii mwingine kama yeye. Yesu alitimiliza unabii ule (ona Kumb 18:15, 18-19; Yoh 1:45; 6:14; Mdo 3:20-23). b. Kuna usambamba ulio wazi kabisa kati ya juhudi za Farao na Herodi kuua watoto wa Waebrania (Kut 1:16; Math 2:16). Wote wawili, Musa na Yesu walitoroshewa nchi nyingine (Kut 2:15; Math 2:13-15). Katika matukio yote mawili walitahadharishwa kimiujiza lini warudi, wale waliokuwa wanataka kuwaua walikuwa wameshakufa (Kut 4:19-20; Math 2:19-21). c. Musa aliupiga mwamba jangwani, na kuwapa watu maji (Kut 17:6; Hes 20:11; Zab78:15). Katika 1 Wakor 10:4, Paulo anasema kwamba Waisraeli kiukweli “walikunywa kutoka kwenye mwamba wa . . . na mwamba huo ulikuwa Kristo.” Bila shaka, Yesu anasema kwamba hutoa “maji yaliyo hai” ya uzima wa milele (Yoh 4:10-14; 7:36-39).d. Kama ambavyo Mungu alimpa Musa Sheria juu ya mlima (Kut 19:20), vivyo Yesu alitoa sheria yake mlimani (Math 5:1-2).e. Kama ambavyo uso wa Musa ulivyoangaza alipokuwa anashuka kutoka mlima Sinai baada ya kupokea amri zile kumi kwa mara ya pili (Kut 34:29), ndivyo uso wa Yesu na mavazi yake yaling’ara juu ya mlima ule aliobadilikia sura (Math 17:2; Mark 9:2-3; Luka 9:29). Luka anaarifu kuwa katika mlima wa kubadilikia sura, Yesu, Musa, na Eliya walikuwa wakizungumzia kuhusu “kutoka” kwa Yesu mwenyewe [neno la Kiyunani lililotafsiriwa “kuondoka”] (Luka 9:30-31). f. Kama alivyokuwa Musa ni mpatanishi kati ya Mungu na Israeli (Kut 20:19; Kumb 5:5; Wagal 3:19), ndivyo alivyo Yesu “mpatanishi moja kati ya Mungu na wanadamu” (1 Tim 2:5). g. Katika ile Karamu ya mwishoYesu alisema “Hii ni damu yangu ya Agano” (Math 26:28; Mark 14:24). Hayo yanatoa mwangwi wa maneno ya Musa katika Kut 24:8. h. Yesu alifananisha kifo chake na tukio la Musa: “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa” (Yoh 3:14; ona Hes 21:9). i. Licha ya mrandano huo, Yesu haitwi kamwe moja kwa moja kuwa ni Musa wa pili; badala yake, kuna kipengele cha mlinganisho ambacho Yesu anaonekana kwa kiwango kuwa mkuu zaidi kuliko Musa. Kwa hiyo, “Sheria ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu” (Yoh 1:17). Katika kujifananisha mwenyewe na mana waliyokula Waisraeli kule jangwani, Yesu alisema, “Amin, amin, nawaambieni, siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni” (Yoh 6:32). Ile mana ilikuwa ya kuonekana kwa macho na ni ya kitambo tu. Mkate ambao Yesu anautoa (yeye mwenyewe hutoa uzima wa milele kwa yeyote aulaye (Yoh 6:48-58). Vivyo hivyo, Waeb humweleza Kristo kama Musa, lakini aliye mkuu zaidi kuliko Musa (Waeb 3:1-6): Kristo “anastahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya nyumba” (Waeb 3:3); ambapo “Musa alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi . . . Kristo alikuwa mwaminifu kama Mwana juu ya nyumba yote ya Mungu” (Waeb 3:5-6).

3. Yesu alijiita mwenyewe “mzabibu wa kweli” ( Yoh 15:1 ). “Katika Agano la Kale, mzabibu ni ishara ya kawaida kuwakilisha Israeli, watu wa Agano na Mungu (Zab. 80:9-16; pia 5:1-7; 27:2 vivyo Yer. 2:21; 12:10 vivyo.; Ezk. 15:1-8; 17:1-21; 19:10-14; Ho. 10:1-2). Kitu kikuu zaidi ni ukweli kwamba wakati wowote Israeli ile ya zamani ilipotajwa kama umbo la mmea huo, huwa ni wakati mzabibu umeshindwa kuzaa matunda mazuri ambayo yanasisitizwa, pamoja na vitisho vya hukumu ya Mungu kwa taifa. Sasa, kinyume na kushindwa huko, Yesu anadai, ‘mimi ni mzabibu wa kweli’m.y; yeye ambaye Israeli walielekezwa kwake, kitu kimoja kiletacho matunda mazuri. . . . mzabibu . . . wa kweli, ndipo basi, si watu wasaliti, bali Yesu mwenyewe, na wale ambao wamehusishwa ndani yake. Muktadha ungethibitisha hasa kuwaeleza Wayahudi wenye msimamo: kama wanataka kufurahia hali ya kuwa mzabibu mteule wa Mungu,wanapaswa kuwa na msimamo ulio sahihi na Yesu.” (Carson 1991: 513-14)

B. Yesu atabiriwa kuwa ndiye “Mtumishi wa Bwana.” Katika Isaya vifungu vinne hujulikana kama “Nyimbo za Mtumishi”: Isa 42:1-9; 49:1-6 [au, 13]; 50:4-

58

Page 60:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

9; 52:13-53:12.17 Kutambulikana rasmi kwa “Mtumishi” ni neno linalochanganya sana. Wakati mwingine huonekana kama lenye uwingi kiujumla (m.y., Waisraeli wote, Israeli “kamilifu”, au mabaki ya Israeli walio waaminifu) (ona, Isa 41:8-9; 44:1-2; 45:4). Hata hivyo, nyimbo zote za Mtumishi pia huelezea tabia za kibinafsi ambazo humtofautisha Mtumishi, mbali na taifa la Israeli lenyewe, hasa Wimbo wa tatu na wa nne ambazo humwelezea “Mtumishi atesekaye.” Kama asimuliwavyo na Isaya: huyo Mtumishi ana Roho wa Mungu juu yake (42:1); ataleta wokovu kwa Israeli na kwa Mataifa, na ni “nuru ya mataifa” (42:6; 49:6); apigwa na kuumizwa (50:6; 52:14, 53:4-5, 7, 10); adharauliwa na kutupiliwa mbali (53:3); licha ya mateso hafungui kinywa chake (42:2; 53:7); anakufa kama dhabihu, akizichukua dhambi za walio wengi (53:4-6, 8-12). Yesu aliishi yote mawili, kama Mtumishi na kujitaja mwenyewe kama Mtumishi (Math 20:28; Mark 10:45; Luka 22:27; Yoh 13:5-16). Waandishi wa AJ humtaja Yesu kama “Mtumishi” (Mdo 3:13, 26; 4:27. 30; Wafil 2:7), na hasa hunukuu na kutumia vifungu vya Mtumishi kwa Yesu kama utimilizo wa unabii.

1. Wimbo wa Kwanza wa Mtumishi— Isa 42:1-9. a. Math 12:17-21 hunukuu Isa 42:1-4, kwa utofauti kidogo, na kuueleza kwa Yesu kama utimilizo wa unabii. b. Isa 42:1 husema kwamba Mungu “apendezwa” katika Mtumishi wake “nimeweka Roho yangu juu yake.” Wakati wa ubatizo wake na wakati wa kubadilika sura, Baba alisema kwamba alikuwa“amependezwa sana” na Yesu (ubatizo—Math 3:17; Mark 1:11; Luka 3:22 kugeuka sura—Math 17:5). Wakati wa kubatizwa kwake, Roho alikuja “juu” yake (Math 3:16; Mark 1:10; Luka 3:22; Yoh 1:32). Yesu mwenyewe, alinukuu kutoka Isa 61:1 kuwa“Roho ya Bwana I juu yangu,” katika kutimiza Maandiko (Luka 4:18, 21).

2. Wimbo wa Pili wa Mtumishi— Isa 49:1-6 [au, 49:1-13]. a. Isa 49:1 panasema, “toka tumbo la mama yangu [Bwana] a menitaja jina langu.” Kabla Yesu hajazaliwa malaika Gabriel alimwambia Mariamu kwamba, “Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu” (Luka 1:31; pia ona, Math 1:21-23).b. Isa 49:2 panasema, “naye anifanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali.” Ufu 1:16; 2:12; na 19:15 zote hutaja neno kali kutoka katika kinywa cha Kristo aliyefufuka.c. Isa 49:6 panasema, “nitakufanya uwe nuru ya mataifa.” Wakati yesu alipoletwa hekaluni ili kutahiriwa, Roho Mtakatifu alimjia Simeoni aliyempokea Yesu mkononi mwake, na kisha akanukuu au akiunganishia lile la Isa 9:2; 42:6; 49:6 kumhusisha Yesu, kusema, “Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa” (Luka 2:32). Yesu mwenyewe alijiunganisha na kifungu hicho aliposema kwamba “Mimi ndimi nuru ya ulimwengu” (Yoh 8:12; 9:5; 12:46). Isa 49:6 ilinukuliwa pia na Paulo na Barnaba katika Mdo 13:47 kuwa imetimizwa kwa wokovu kwa Mataifa katika kuiitikia Injili. d. Isa 49:5-6 panaonekana kuonyesha mkondo wa mpangilio wa marejesho ya Israeli kwanza, ili kwamba wokovu upate kufikilia miisho ya dunia. Katika ujumbe wa Petro wa Mdo 3:11-26, anahitimisha kwa kusema, “Mungu, akisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake” (Mdo 3:26). “Kutumia neno‘kwanza’ (prōton) kwaonyesha mkondo wa mpangilio ulioonyeshwa katika Isaya 49:5-6, ambapo Mtumishi wa Bwana anatumiwa ‘kurejesha makabila ya Yakobo ili wawe ‘nuru ya Mataifa’ na kuuleta wokovu wa Mungu ‘kwa miisho ya dunia (kama Mdo 1:6; 13:46-48; 26:16-18). Kwa maneno mengine, ‘Wimbo wa Mtumishi huo muhimu, unaofunua njia ambayo Mungu ataitumia katika kutimiliza ahadi yake kwa Ibrahimu, waonyesha kuwa katika hatua yake ya changamoto ya mwisho ya ujumbe wa Petro.” (Peterson 2009: 185)e. Isa 49:8 panasema, “Wakati uliokubalika nimekujibu, na siku ya wokovu nimekusaidia.” Paulo anukuu hilo katika 2 Wakor 6:2 na analitumia hilo kuonyesha neema ya Mungu ya wokovu katika Kristo.

3. Wimbo wa Tatu wa mtumishi— Isa 50:4-9. Isa 50:6 panaeleza kuwa Mtumishi anapigwa, kudharauliwa, na kutemewa mate. Katika Mark 10:33-34 Yesu aliunganisha kwa Isa 50:6 kuelezea kile

17 “Wimbo wa kwanza wa Mtumishi hujulikana kidesturi Isa. 42:1-4. Hata hivyo, mistari ifuatayo (mst. 5-9) waonyesha kupakua huduma ya Mtumishi. K.m. Isa. 49:7-13, ambapo pia hupakua kazi ya Mtumishi baada ya kumtambulisha upya Mtumishi katika mst. 1-6. Wengi huuelewa wimbo wa pili kuishia katika mst. 6, kumtambulisha mhusika wa ‘wewe’ katika vifungu 7-8 kama Israeli. Kwa maana hii mwito wa Mtumishi kama ‘agano la watu waendelezwa kupitia jamii iliyorejezwa na agano. . . . Hata hivyo, mistari ifuatayo (mst. 7-13) yaelekea kusimulia kazi ya Mtumishi . . . na ‘watu’ huelekea kuzungumzia Israeli. Hivyo, hakuna sababu isukumayo ya kuitambua Israeli, kama ndiye mtuishi, kama ‘watu wa agano’ katika Isa. 49:8.” (Williamson 2007: 159n.44)

59

Page 61:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

kitakachotokea kwake atakapofika Yerusalemu. Kabla hajasulubiwa, mambo hayo yote matatu (m.y., kupigwa, kudharauliwa, kutemewa mate) yalitokea kwa Yesu (Math 27:26-31; Mark 15:15-20; Luka 22:63-65; 23:11; Yoh 18:22; 19:1-3).4. Wimbo wa Nne wa Mtumishi— Isa 52:13-52:12.

a. Katika Rum 15:18-21 Paulo anukuu kutoka Isa 52:15 akiihusisha na mahubiri ya Injilili ya Kristo katika Yerusalemu na sehemu nyingine nyingi, kwa wote wawili, Wayahudi na Mataifa.b. Katika Yoh 12:37-38 Yohana anukuu kutoka Isa 53:1 kama imetimizwa pale watu walipokuwa hawamwamini Yesu hata baada ya kufanya ishara nyingi mbele yao. c. Katika Math 8:14-17, baada ya Yesu kuwaponya wagonjwa na kuwatoa pepo wachafu wengi kutoka kwa watu, Mathayo anukuu Isa 53:4 na kusema imetimizwa. d. Katika 1 Peter 2:21-24 Petro anukuu katika Isa 53:9, na akaibua kutoka Isa 53:4-7, kusema yametimizwa na Yesu (ona pia, Rum 4:25).e. Katika Mdo 8:26-35 Filipo alimwambia towashi wa Kushi kuwa Isa 53:7-8 iliandikwa kumhusu Yesu. f. Katika Luka 22:37 Yesu mwenyewe anukuu kutoka Isa 53:12 kumhusisha yeye mwenyewe katika kutimiza unabii (ona pia Mark 15:28).g. Zaidi ya nukuu hizo na udhahiri huo ulio wazi, AJ huonyesha maunganisho mengi kuhusiana na Wimbo wa Nne wa Mtumishi kumhusisha Yesu. Wafil 2:9 huibukia kutokana na Isa 52:13; Math 26:38 huibukia kutoka Isa 53:3, 12; Yoh 1:29; 1 Wakor 15:3; 2 Wakor 5:21; Waeb 9:28 zote huibukia kutokana na Isa 53:4-6, 8-12; Math 26:62-63; 27:12-14; Mark 14:60-61; 15:3-5; Luka 23:9; Yoh 19:9 zote huibukia kutoka Isa 53:7; Math 27:57-60 huibukia kutoka Isa 53:9.

C. Katika Yesu, ahadi za AK za marejezo kwa Israeli zinatimizwa. Manabii (k.m., Isaya 60-62; Yeremia 30-33; Ezekieli 34-37) walitabiri marejesho ya Israeli chini ya

uongozi wa mfalme aliyepakwa mafuta na Mungu, atakayetawala kutokea Yerusalemu, au mlima Sayuni. Hilo lilikuwa bado linategemewa na watu wa nyakati za Yesu (ona Luka 2:25, 38; 19:11; 24:21; Mdo1:6). Katika Yesu, unabii huo unatimizwa (Luka 1:68), bali ni katika namna isiyotarajiwa: Sayuni mpya, Israeli iliyorejezwa, haitambulikani kwa kutaja mahali fulani au hali ya utaifa fulani, bali katika kuwa ndani ya Kristo na watu wake.

1. Jesus’ ministry was intimately linked with the restoration or redemption of Israel. Yesu alipoletwa hekaluni ili kutahiriwa, nabii mke Ana “alianza kunena Kumhusu [m.y; Yesu] na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu” (Luka 2:38).2. Math 4:13-17 hutafsiri upya unabii kuuunganisha na Yesu. “Mathayo anaunganisha maelezo yake ya mafundisho ya kwanza yaYesu huko Galilaya na hoja kuwa ile safari yake kwenda ‘Kapernaumu kwa njia ya bahari . . . nchi ya Zabuloni na Naftali hutimiliza unabii wa Isaya 9:1-2: ‘nchi ya Zabuloni, nchi ya Naftali, njiani kwa njia ya bahari, ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya Mataifa—watu waliokaa gizani wameiona nuru kuu, na kwa wale waliokaa katika uwanda na kivuli cha mauti nuru imekuja kuonekana’ (Math 4:13-16). Muktadha wa mwanzoni kabisa unazungumzia juu ya watu waliovunjika moyo, walioshindwa na jeshi la Waashuri na kupelekwa utumwani (2 Waf 15:29; 1 Nyak 5:26), ambao walipewa ahadi ya kupewa mwana kutoka nyumba ya Daudi atakayeleta wokovu. Mathayo anaona unabii huu ulitimizwa katika huduma ya Yesu: anautafsiri uharibifu na machafuko ya kisiasa kama giza za kimaadili na la kiroho, na anatafsiri tangazo la Yesu la kuja kwa ufalme wa Mungu (Math 4:17) kama kutimizwa kwa ukombozi wa ‘njia ya bahari, ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya Mataifa’ (Isa 9:1).” (Schnabel 2002: 43)3. Yesu alimdhihirisha Yohana Mbatizaji kama ndiye Eliya, ambaye “anakuja na kuyatengeneza mambo yote” ( Math 17:11-13 ). Kumtambua huko “kuliweka wazi lililotarajiwa kwa vizazi na vizazi la ‘kutengenezwa’ sasa lilikuwa katika mchakato wa kutimizwa—bali kinyume chake ni kwa kupitia ‘mateso’ ya Mwana wa Adamu” (Walker 1996: 43).4. Yesu aliwachagua wanafunzi 12 ( Math 10:1-2; Mark 3:13-19; Luka 6:12-26 ), ambalo linatokana na makabila 12 na huonyesha matengenezo au marejesho ya Israeli. “Yesu kuwaita wanafunzi kumi na wawili (Mark 3:13-19; Luka 6:12-26; Math 10:1-2) ni kwa muhimu sana: ikiwa Yesu alijiona mwenyewe kama Masihi, wale wanafunzi kumi na wawili wanawakilisha madai yake kuwa huduma yake inaanzisha matengenezo ya siku zijazo ya makabila kumi na mbili ya Israeli” (Schnabel 2002: 45). (ona pia kifungu IV.F.4., hapo chini.)5. Kuhusiana na uhamisho, manabii mara kwa mara wanena kuwa Mungu “awakusanya” tena mabaki ya Israeli ( Zab 147:2; Isa 11:12; 27:12; 49:5; 56:8; Yer 6:9; 31:10; Ezek 11:17; 28:25; 34:13; 37:21;

60

Page 62:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

38:8; 39:28; Hos 1:11; Mik 2:12; 4:6; Zef 3:18-20; Zek 10:8, 10 ). Yesu alidai “kuwakusanya” Israeli (Math 3:12; 12:30; 13:30, 47-48; 18:20; 22:10; 23:37; 24:31; Mark 13:27; Luka 3:17; 11:23; 13:34). Zaidi ya hayo, “Yesu ajinenapo mwenyewe kuwa mchungaji mwenye kundi la kondoo (Yohana 10:11), huibua hilo kutokana na hazina kubwa ya desturi ya Israeli inayolitaja Israeli kama kundi la YHWH, kuhusisha na YHWH (Zab 23) au viongozi wa Israeli (Ezek 34) kama wachungaji” (Schnabel 2002: 44). Vivyo hivyo, Yesu aliinenea imani ya akida wa Kirumi (Mataifa) “Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli! Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni; bali wana wa ufalme watutupwa katika giza la nje.” (Math 8:10-12). “Kitu cha kuvutia hapa ni kwamba maelezo ya hao watu watokao ‘kutoka mashariki na magharibi’ hutokana na vifungu kama vile Isaya 43:5f. na Zab 107:3 vilivyozungumzia Wayahudi kurudi kutoka uhamishoni. Zaidi basi hapa Yesu anahusisha na Mataifa, kujumuishwa na watu wa Mungu. Hali maalum ya Wayahudi kama watu wa Mungu ilikoma. Nafasi ya kuwa sehemu ya watu hao ipo wazi kwa wote—Wayahudi na Mataifa wote sawa—walio na imani katika Yesu.” (Travis 1982: 129)7. Baada ya kufufuka kwake, Yesu aliweka wazi kuwa “kuwatengeneza au kuwarejesha Israeli” kulikuwa ni kuwarejesha kiroho kutokana na watu wote kuigeukia imani kwake, siyo matengenezo au marejesho ya kimwili au ya kisiasa ya Israeli kama taifa. Jibu la Yesu kwa wanafunzi wake akiwa njiani kuelekea Emau (Luka 24:21, 25-27). Mara baada ya kufufuka kwake, Yesu alikutana na wawili kati ya wanafunzi wake wakielekea Emau. Hawakumtambua, lakini walisema“walikuwa wanatumaini kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli” (Luka 24:21).

a. Yesu aliwakemea hao wanafunzi wawili. Katika kuwajibu hao wanafunzi, Yesu aliwakemea, akisema, “Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Je! haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katia utukufu wake?” (Luka 24:25-26). “Ni dhahiri Yesu ameikomboa au kuirejesha Israeli, bali kwa njia kinyume na walivyotarajia. Katika kumtazamia Masihi wa kisiasa ambaye angeelekeza katika ‘marejezo’ ya kisiasa, walikuwa wamezielewa vibaya kabisa zile nabii za Agano la Kale. Walikuwa waone marejesho ya Israeli yakiwa yametimilika baada ya kufufuka kwa Yesu.” (Walker 1996: 285) b. Umuhimu wa “siku ya tatu.” Wale wanafunzi wawili walikuwa wamegundua kuwa “leo ni siku tatu tangu mambo haya yatendeke” (Luka 24:21). Katika Luka 24:46 Yesu anataja kwamba kufufuka kwake“siku ya tatu” kulikuwa “kumeandikwa” katika AK. “Sasa ni katika mstari gani anazungumzia? Wakati inawezekana kuwa hilo linaibukia kisa cha Yona, maelezo yanayoendana zaidi yako katika Hosea 6:2 (‘Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua’). Ikiwa ndivyo, Yesu ameuchukua mstari ambao mwanzoni ulihusika na merejezo ya uamsho wa Israeli na kuutumia badala yake kwake mwenyewe kama Masihi wa Israeli. . . . Kama Dodd alivyohitimisha kiusahihi kabisa: ‘Ufufuo wa Kristo ni ufufuo wa Israeli waliounenea manabii.” (Walker 1996: 285)

8. Agizo Kuu ( Math 28:18-20 ). a. Mazingira ya AK. Zab 2:6-8 ilitabiria Israeli iliyorejeshwa, yenye kiti cha enzi cha kifalme cha ki-Masihi juu ya mlima Sayuni, “mlima mtakatifu,” wa Mungu kama “Mwana,” wa Mungu pamoja na mataifa na “miisho ya dunia” iliyotolewa kwake kama umiliki wake (ona pia Zab 48:1-2). Katika unabii wa AK, Mungu alionyeshwa kukaa na watu wake juu ya mlima Sayuni (Zab 26; ona, Zab 9:11; 43:3; 68:16; 76:1-2; Isa 8:18; Yoeli 3:17; Zek 8:3). Mataifa yangefanya kuja Sayuni ili kupata uwepo wa Mungu na baraka zake (ona, Isa 2:2-3; 25:6-7; 56:6-8; Mika 4:1-2; Zek 8:20-23).b. Yesu alipitia upya Zab 2:6-8 na nabii zinazofanana nayo kwa ajili yake mwenyewe, watu wake (kanisa), na kuenea kwa Injili. Yesu “Mwana” (Zab 2:7; Math 28:19; pia Mdo13:33, ambapo Paulo aihusisha Zab 2:7 na Yesu) ambaye ana “mamlaka yote mbinguni na duniani” kama mfalme wa Ki-Masihi (Zab 2:6; Math 28:18). Yesu aliye Bwana anatamka kwa wanafunzi wake (Zab 2:7; Math 28:18-20). Tamko lake vivyo hivyo linahusu “mataifa yote” (Zab 2:8; Math 28:19). Hata hivyo, badala ya watu kuja kwa “mlima mtakatifu,” wa Mungu, Yesu awaambia watu wake kwenda huko nje kwa watu wote na mahali pote kulifundisha Neno la Bwana. Hatuna haja ya kwenda mahali maalum ili kuwa na Bwana (ona Yoh 4:21-23). Badala yake, anatuhakikishia kwamba “Mimi nipo pamoja nanyi sikuzote hata ukamilifu wa dahari” (Math 28:20; pia Math 1:23—“Nao watamwita jina lake Imanueli, yaani ‘Mungu pamoja nasi’”). Ufalme mpya, Sayuni mpya ndipo alipo mfalme. Siyo tema mahali fulani pa kijiografia, bali ni pa kiroho. Ni kila mahali ambapo watu wa Kristo wapo (ona Yoh 4:21-24; Waeb 12:22-24). Kristo ameibadilisha Sayuni kuwa kitovu cha shughuli za Mungu kwa watu

61

Page 63:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

wake, na katika Kristo matumaini yote yanayohusiana na Sayuni yametimizwa. 9. Mwitikio wa Yesu kwa wanafunzi wake kuhusu swali lihusulo kurudishiwa ufalme katika Mdo 1:6- 8 . Kabla ya Pentekoste na kupokea nguvu za Roho Mtakatifu, hata wanafunzi wa Yesu hawakuelewa jinsi Yesu alivyoelezea upya “kurudishiwa au kurejezwa kwa ufalme wa Israeli” kulihusu nini. Walikuwa bado wanafikiria mambo ya kijiografia na ya kisiasa, siyo ya rohoni. Walikuwa wanafikiria tu kwamba Masihi atarejeza taifa dogo, siyo kukomboa dunia nzima. Hata hivyo, katika kuwajibu swali lao kuhusu “kuurudisha ufalme kwa Israeli” Yesu anafafanua kile alichokisema katika “Agizo Kuu,” na kulipangilia katika namna ya wazo tofauti na lile la “ufalme wa Israeli uliorejezwa” lilivyo kihalisia:

a. Tafsiri mpya ya “kurudishiwa ufalme.” Ingawaje sehemu ya kwanza ya ‘muda wa matukio’ ya (‘kurudishiwa’ huku ungelifanyika, bali siyo sasa),” sehemu ya pili ya jibu lake (m.y., kuanzia Mdo 1:8), kwaonyesha nini Yesu anachokizungumzia hasa ni muktadha mpya na wa tofauti wa “kurudishiwa ufalme”: “Mazingira yaliyoko katika Luka 24 hupendekeza kwamba Yesu alikosoa muktadha wao wa ‘kurudishiwa’. Anathibitisha upya matarajio, ila anarekebisha uelewa wao. Msisitizo wake uko kwenye ‘ufalme wa Mungu’ (mst. 3), siyo ufalme wa kisiasa wa Israeli; Roho atatolewa (mst. 4-5), siyo kwa ajili ya ‘kurudishiwa ufalme wa Israeli’, bali kuwawezesha kushuhudia zaidi kabisa ya mipaka ya Israeli. . . Katika Luka 24 wanafunzi walialikwa kuona kazi ya Yesu ya ukombozi kwa kutazama nyuma katika kusulubiwa kwake, sasa wanaalikwa kutazama mbele kwenye utume wa agizo lao ‘hadi mwisho wa nchi’ (Mdo 1:8). ‘Kukombolewa kwa Israeli’ ni swala la vipengele viwili—lililoanzishwa kupitia kifo cha Yesu na kufufuka kwake, bali lilitekelezwa kupitia agizo kuu la wanafunzi. . . . Israeli ilikuwa inarejeshwa kupitia ufufuo wa Masihi na kipawa kilichofuatia cha Roho. Jinsi Israeli itakavyoonyesha ukuu wake juu ya dunia hautakuwa kutokana na uhuru wa kisiasa, bali zaidi kupitia utawala na mamlaka wa Masihi wa Israeli. Mbinu iliyochaguliwa ya utawala wa Masihi huyu ilikuwa kupitia Mitume kuitangaza Injili dunia nzima kuwaleta watu wapate ‘kuitii imani’ (kama. War. 1:5). Mtazamo wa Yesu, sasa kama mwanzo, haukuwa wa ‘ufalme wa Israeli’ wa kisiasa, bali zaidi kwa ajili ya ‘ufalme wa Mungu’ (Mdo 1:3).” (Walker 1996:96, 292) b. Tafsiri ya Yesu ya “kurudishiwa ufalme” huonyesha umuhimu wa tafsiri mpya ya “Israeli.” Yesu hakuyakatalia matarajio ya wanafunzi wake kuhusu “kurudishiwa.” Badala yake, “aliutafsiri kwa maana ya Roho mtakatifu na kutimilizwa kwa unabii kuhusu kurejeshwa kwa Israeli kama jumuiya–mtumishi, iliyoitwa kuwa ‘shahidi’ wa Mungu kwa mataifa (Isa. 43:10, 12 na 44:8). Matengenezo ya nyakati za mwisho yataanzia na kumiminwa kwa Roho aliyeahidiwa na kuuleta wokovu wa Mungu, kwanza kwa Israeli na kisha ‘hadi mwisho wa nchi’ (Isa. 49:6; cf. Isa. 42:6-7). Yatakamilika hapo Yesu atakaporudi (kama [Mdo] 1:11; 3:20-21). Kupitia ushuhuda wa wanafunzi wa Yesu, ‘ufalme’ ungerejeshwa kwa Israeli, siyo kwa maana ya kitaifa wala kisiasa, wala si katika ukamili na mwonekano wa mwisho uliosimuliwa katika unabii wa Biblia (kama [Mdo] 3:19-26).” (Peterson 2009: 109-10)c. “Hadi mwisho wa nchi” pia ilitafsiri upya unabii. Hitimisho la jibu la Yesu, kwamba wanafunzi wake waende “hadi miisho ya nchi” (Mdo1:8, Biblia ya NIV), hukumbushia Utume Mkuu, na kutoa mwangwi Zab 2:8, ambao unasema kwamba “mwisho wa nchi” umetolewa kwa wafalme wa Ki-Mashihi kama mali yake. “Kwa Yesu kuwaagiza wanafunzi wake waende kwa mataifa yote ‘hadi miisho ya nchi,’ maono ya kinabii ya mataifa yakiijia Yerusalemu (Isa 2:2-5, Mik 4:1-5; Zek 8:20-23) umebadilishwa kwa wamishinari wa Kiyahudi kuwaendea mataifa yote. Mwelekeo uliotarajiwa kutokea pembezoni kuja kati kati unaongozwa kwa upya kwa maana ya utume wa kutokea katikati (Yerusalemu, ambapo Yesu alikufa na akafufuka kutoka kwa wafu) kuelekea pembezoni (mwisho wa nchi).” (Schnabel 2002: 47)

10. Hali ya kiroho ya matengenezo ya Israeli ilithibitishwa katika Baraza la Yerusalemu katika Mdo 15. Ingawaje Daudi alikuwa ameahidiwa ufalme usio na mwisho, Israeli ilikuwa imegawanyikana, kisha kupelekwa uhamishoni. Mungu, kupitia nabii Amosi, aliahidi marejesho au matengenezo: “Siku hiyo nitaiinua tena maskani ya Daudi iliyoanguka,” na baada yake mataifa ya kigeni yatamtafuta au kumgeukia Bwana. (Amos 9:11-12).

a. Kuanzia Mdo 10, Mungu alimwonyesha Petro kwamba hakuna taifa, kabila, au jamii ya watu watakaoitwa “najisi.” Matokeo yake, idadi kubwa ya Wamataifa walianza kuokolewa, bali hawakuwa wanatahiriwa au kuishi kulingana na Sheria ya Kiyahudi. Swala la kuwa je Wamataifa wanapaswa kuwa chini ya sheria na desturi za Wayahudi za AK lilikuwa ndilo swala la mjadala katika Baraza la Yerusalemu katika Mdo 15. Baraza liliamua kwamba Mataifa hawakulazimika kuzifuata sheria na desturi za AK. b. Katika kufikia uamuzi huu, katika Mdo 15:15-18 mtume Yakobo alinukuu kutoka Amosi

62

Page 64:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

9:11-12 (kwa tafsiri ya LXX), bali alianza na kuhitimisha AK lake kwa kunukuu maneno kutoka Hos 3:5, Yer 12:15, na Isa 45:21. Mistari hiyo huweka nukuu kuu kutoka Amosi katika muktadha wa kuokolewa kwa Mataifa katika zama za Masihi. Yakobo anahitimisha kwamba kujumuishwa kwa Mataifa katika kanisa ndiko kujengwa upya “maskani ya Daudi” (m.y., kurejeshwa kwa Israeli). Kusema ukweli, kuja kwa imani kwa Mataifa kwaonyesha kwamba “maskani ya Daudi” tayari ilishajengwa, kwa vile “muktadha waonyesha ni lazima kuwepo na ‘marejesho’ kabla Mataifa hawajaingia ndani (‘Nitalirejesha, ili kwamba . . . Mataifa). Kwa Yakobo kulitumia hilo kwathibitisha uthamani wa utume kwa Mataifa lazima uonyeshe kukubali kuwa Israeli tayari ilisharejeshwa.” (Walker 1996: 97). c. Kama ilivyokuwa kweli kwa ahadi kwa Ibrahimu ya “nchi,” kanisa la nmwanzo“lilifanyisha ukiroho” unabii wa AK wa Amosi kuhusisha kanisa, siyo kwa hekalu jipya la kuonekana au ufalme wa kisiasa wa Israeli. “Katika kuchagua mstari wa kuthibitisha uhalali wa kuingizwa Mataifa, Yakobo aliuchagua moja uliochochea uhakiki wa kazi ya Mungu kati ya Mataifa ungeweza tu kuanza baada ya yeye kufanya kitu kwa niaba ya watu wake (‘hema la Daudi lililoanguka’). Matokeo ya dhahiri ni kuwa mfululizo huu wa (kurejeshwa kwa, kukifuatiwa na ‘kujumuishwa kwa mataifa’) kulikuwa kivyake sahihi kabisa. Kilichokuwa kimekosewa ni ile tafsiri ya Israeli kuhusu ‘kurejeshwa au kurudishwa’. . . . uamuzi wa Yakobo ulikubalika, kuonyesha kwamba mitume hatimaye waliweka kando imani yoyote iliyotangulia kuwa kurejeshwa kwa Israeli kulihusu uhuru wa kisiasa au kwa watu wake kuja kama moja katika imani katika Kristo.” (Walker 1996: 293-94)d. Uamuzi wa Baraza la Yerusalemu uliofichika katika Isa 49:6. Isa 49:6 ni mojawapo ya vifungu vya “mtumishi” vya Isaya. Huunganisha marejesho ya Israeli na mwito wa Mungu kwa Mataifa: “Anasema, ‘Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.” Kama ilivyokuwa kwa Amosi 9:11-12, hao “Mataifa’ kufikiwa na Injili kulikuwa ishara kwamba majira yaliyosubiriwa kwa muda mrefu ya kurejezwa kwa Israeli yalikuwa yamewadia” (Walker 1996: 98). Paulo na Barnaba walinukuu sehemu ya pili ya Isa 49:6 katika Mdo 13:47. Bila shaka walikuwa wanaelewa kiungo kati ya “kurejezwa kwa Israeli” na wokovu wa Mataifa. Nukuu kutoka Isa 49:6 ilisababisha shangwe, kulitukuza Neno la Bwana, na wokovu kati ya Mataifa (ona, Mdo13:48-49). Kusema kweli, hali hiyo ndiyo ilikuwa nyuma ya mazingira ya Baraza la Yerusalemu, tangu na wote wawili Paulo na Barnaba walipoeleza kila kitu Mungu alichokifanya kupitia wao kwa lile Baraza (Mdo 15:2-4, 12).

11. Paulo alilielezea kanisa kama “marejesho ya Israeli.”a. Katika Rum 9:4-5 Paulo humtazama Yesu kama kilele, na aliye mkuu zaidi kwa, baraka zote za utajiri wa Israeli: kufanyika kuwa wana, utukufu, maagano, sheria, ibada ya hekalu, ahadi, na mababa. Kwa hiyo, “kutangaza kwa Yesu kuhusu kuja kwa ufalme wa Mungu kuliandamana na tafsiri mpya ya ufalme kumaanisha nini, pamoja na viambatanisho vya utambulisho wa Israeli ama kutokuwepo (kutahiri, Sabato, vyakula) au (taifa, nchi, Sheria, Hekalu) vilivyobadilishwa. Israeli iliyorejeshwa iliyoahidiwa ilitafsiriwa upya kwa maana ya kujitoa kwa Yesu kulikoni vigezo vya kale vya Uisraeli: mkazo siyo katika Hekalu, au sheria, au nchi, bali katika ujumbe wa kuja kwa ufalme wa Mungu katika huduma katika mwanadamuYesu.” (Schnabel 2002: 42-43)b. Paulo alitafsiri upya “kurejeshwa kwa Israeli” kama tukio la kiroho. Isa 49:8 panazungumzia kuhusu Bwana kukusaidia “Wewe” (mtumishi wake) “kuirejeza nchi.” Paulo anukuu nusu ya kwanza ya mstari wa 2 Wakor 6:2, si kuhusisha marejesho yoyote ya kimwili ya nchi au ufalme wa Israeli, bali kuhusiana na kuwa balozi wa Kristo na kupokea neema ya Mungu. Mahali pengine abainisha kuwa Ibrahimu ni baba wa wote waaminio, na wote walio katika Kristo ni wana wa Ibrahimu (War 4:11; Wagal 3:29). Ule utofauti wa kale kati ya Wayahudi na Mataifa, “walio nje” na “walio ndani,” umeondolewa katika Kristo (1 Wakor 5:12; Wagal 3:28; Waef 2:14-19; Wakol 3:11; 1 Wathes 4:12). “Kwa hiyo, wakati Paulo asemapo kuwa sasa ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu imetimizwa kikamilifu katika Kristo, kuchanganya hasa na kupanuliwa kwa Baraka za Mungu kwa Mataifa, na pale asemapo kwamba kuhusishwa huko hufanyika kwa jamii ya wale waaminio katika Kristo, hueleza kuridhika kwake kwamba kanisa, linaloambatanisha Wakristo waaminio Wakiyahudi na [Mataifa], huwakilisha siku za mbeleni za marejezo ya Israeli” (Schnabel 2002: 54) Vivyo hivyo, katika Mdo 13:32-34, 38-39 Paulo aliweka usawa “baraka kamilifu za Daudi” na ufufuo

63

Page 65:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

wa Yesu. “Ahadi na baraka hizi, zaidi ya hapo, hutafsrika kuwa, siyo ufalme wa mbeleni wa Wayahudi kwa miaka elfu, bali msamaha wa dhambi na wokovu. Ahadi zilizofanywa kwa Israeli, bila shaka, zinatimizwa katika kanisa la Agano Jipya.” (Hoekema 1979: 197)c. Viongozi wa Kiyahudi walielewa kwamba Paulo alikuwa akihubiri maana mpya ya “merejesho ya Israeli.” Baada ya kukamatwa kwake Paulo alishuhudia kwamba “sasa ninasimama hapa nihukumiwe kwa ajili ya tumaini la ahadi baba zetu waliyopewa na Mungu” (Mdo 26:6). Alipopelekwa Rumi aliserma, “kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli” (Mdo 28:20). Ni dhahiri kuwa uelewa wa Paulo kuhusu “tumaini la Israeli” ulikuwa tofauti sana, na ulipingana kabisa, nauelewa wa viongozi wa Kiyahudi. Viongozi wa Kiyahudi walidhihirisha kuwa na uelewa wa kimwilini wa matumaini ya Israeli—m.y., Israeli kurejezwa kama taifa ufalme muhimu wa kisiasa, wenye mipaka dhahiri kati ya Wayahudi na Mataifa, na wenye kushikamana na Sheria za AK za Kiyahudi na lile Hekalu. Ikiwa Paulo alikuwa na uelewa wa unabii wa AK kuhusiana na matumaini ya Iraeli ya kurejezwa, angelikuwa amekubalika, hasa kwa vile alikuwa ni msomi mwenye elimu kubwa (Mdo22:3; 23:6; 26:5; Wafil 3:5). Badala yake, Paulo alihubiri “tumaini” tofauti,” liitwalo Kristo, ile “sheria ya Kristo,” watu wapya wa Mungu waliojumuisha Wayahudi na Mataifawalio mmoja “katika Kristo,” na “tumaini la marejezo” (Mdo 17:1-7; 23:6; 24:14-15; 26:6-23). Hilo ndilo lililowafanya Wayahudi wajaribu kumuua, na kusababisha kukamatwa kwa Paulo (Mdo21:28-33; Mdo 22:17-22).

12. Waandishi wa AJ walielewa kwamba Yesu alipitia unabii wote wa AK. Waeb 12:18, 22 panasema kwamba katika Yesu “hamkufikilia mlima uwezao kuguswa . . . ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu ya mbinguni,” (ona pia Wagal 4:21-31). Wakati AK lilikuwa bado lina nguvu, hata wakati wa huduma ya Yesu alipokuwa duniani, Yerusalemu uliitwa “Mji mtakatifu” (Isa 48:2; Dan 9:24; Neh 11:1, 18; Math 4:4; 27:53). Hata hivyo, “baada ya kipindi hicho, maneno ‘mji mtakatifu’ hayaonekani tena, kwani Mungu alitwaa makao siyo katika Yerusalemu, bali katika kanisa; na siku ya Pentekoste, Roho Mtakatifu alijaza siyo hekalu wala Yerusalemu, bali mitume na watu wote waliotubu na kubatizwa (Mdo 2:1-4, 38-39). Muundo huu ulithibitishwa katika Ufunuo ambapo Yohana anauelezea Yerusalemu mpya kama mji mtakatifu (21:2, 10; 22:19). Anaeleza kwamba huu ndio ‘mji wa watakatifu na mji mzuri wa kupendeza (20:9) ambao Yesu anauita ‘mji wa Mungu wangu’ (3:12). Mji mtakatifu ni Yerusalemu ya kiroho ya watakatifu.” (Kistemaker 2000: 437)

D. Yesu alitimiliza na kubadilisha siku kuu za Kiyahudi, mifumo ya dhabihu, na ukuhani. 1. Kalenda ya AK ya Israeli.

a. Israeli ya AK ilitumia kalenda ya jua; kila siku mpya ilianza na kuishia kuzama kwa jua (ona, Mwa 1:1, 8, 19, 23, 31). Kwa vile kalenda ya jua ilikuwa ni siku 360 (12X30), mara nyingi sana waliwajibika kuongeza “mwezi mrefu.” Israeli ya AK pia ilikuwa na kalenda ya kawaida na kalenda ya wakfu. Mwezi wa kwanza wa kalenda ya kawaida (Tishri, unaoshabihiana na Septemba-Octoba) ulikuwa mwezi wa saba wa kalenda ya wakfu (Abibu [au, baada ya uhamisho, uliitwa Nisani], unaoshabihiana na March-Aprili), na kinyume chake. Siku ya kwanza ya mwaka mpya (1 Tishri) huitwa Rosh Ha-Shanah (“kichwa cha mwaka”), na ilijulikana kwa alama ya Sikukuu ya Mabaragumu. Kila juma liliishia na siku ya Sabato, wakati Waisraeli walipotakiwa kupumzika na kutofanya kazi yoyote (Mwa 2:2-3; Kut 16:22-23; 20:9-11; 23:12; 31:13-17; 34:21). Sabato ilipoisha wakati wa jua kuzama , juma jipya lilianza. b. Israeli pia walikuwa na“Mwaka wa Sabato” na “mwaka wa Jubilee.” Mwaka wa Sabato ulikuwa kila baada ya miaka saba. Katika mwaka huo: nchi ilitakiwa kutolimwa (Kut23:10-11); madeni yote (isipokuwa yaliyotokana na wageni) yalitakiwa kusamehewa (Kumb 15:1-11); watumwa wa Kiebrania waliachiliwa (Kut 21:1-6; Kumb 15:12-18). Mwaka wa Jubulee ulikuwa kila baada ya miaka 50. Wakati huo: madeni yaliachiliwa; watumwa wa Kiebrania walitakiwa kuachiliwa huru; na kila eneo la ardhi lilitakiwa kurudishwa kwa mwenye shamba (Wal 25:8-55). Biblia inaonyesha kwamba sababu mojawapo ya uhamisho kupelekwa Babeli ilikuwa kushindwa kwa Israeli kuzishika sheria hizi za Sabato za nchi (ona, Wal 26:34-35; 2 Nyak 36:20-21; Yer 25:11-12; 29:10).

2. Israeli ya AK ilikuwa na makundi matatu ya dhabihu au sadaka. Yote yalihusu kutoa sadaka za wanyama isipokuwa sadaka za nafaka na vinywaji (lakini pia huandamana na dhabuhu za kuteketeza za amani).

a. Dhabihu za Kujitengeneza (m.y., kutuliza ghadhabu ya Mungu).(1) Sadaka za dhambi ( Wal 4:1-5:13; 6:24-30; 8:14-17; 16:3-22 ): Kufanya upatanisho

64

Page 66:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

kwa ajili ya dhambi mahali ambapo malipizi yalikuwa hayawezekani. (2) Sadaka za Ukengeufu/Makosa ( Wal 5:14-6:7; 7:1-8; Hes 5:5-10 ): Dhabihu maalum kwa ajili ya upatanisho wa dhambi iliweza kufanyika kunufaisha upande ulioathirika (upande uliokosea ulilipa kwa waliokosewa kiasi chote, au kuongezea na nyongeza ya 20%).

b. Dhabihu ya Kujitoa (m.y., kuweka wakfu na/au kuonyesha adhama kwaMungu).(1) Sadaka za Kuteketezwa ( Walawi 1:1-17; 6:8-13; 8:18-21; 16:24 ): Kujiweka wakfu mwenyewe au jengo kwa Mungu, au kuonyesha adhama kwa dhabihu nyinginezo. (2) Sadaka za Unga ( Walawi 2:1-16; 6:14-23; 7:9-10 ): Shukurani na kuhitajia ulinzi na kujitakia mema kwa Mungu. (3) Sadaka za Vinywaji ( Walawi 23:37; Hes 15:1-10 ): Kwa ajili ya kujitoa.

c. Sadaka ya Amani (m.y., kujenga uhusiano wa ndani zaidi na Mungu) (Walawi 3:1-17; 7:11-34; 19:5-8; 22:18-30).

(1) Sukurani ( Walawi 7:12-15; 22:29-30 ): Kwa ajili ya kumshukuru Mungu au ushirika na Mungu, au kwa ajili ya baraka zisizotetegemewa ambazo tayari zimekuja.(2) Sadaka ya Nadhiri ( Walawi 7:16-18; 22:18-25 ): Kwa ajili ya baraka au ukombozi uliokwisha kupatikana ambapo nadhiri ilikuwa imewekwa kusindika dua hiyo.(3) Sadaka ya Hiari ( Walawi 7:16-18; 22:18-26 ): Kuelezea shukurani ya kiujumla na upendo kwa Mungu pasipo sababu ya baraka fulani.

d. Mfumo wa dhabihu wa Walawi haukuwa mpango kamili wa mwisho ambao ungeweza kuondosha dhambi yote. Mifumo ya dhabihu hiyo ilikuwa inahusika haswa na dhambi zisizokusudiwa, kukosa uangalifu, ajali, na kutokutimiza yapasayo, zikiwamo kutokuendana na desturi na mienendo isiyofaayo inayoharibu umiliki wa haki wa mali. “Dhambi zisizozuilika,” zikiwamo zile zinazopaswa hukumu ya kifo, hazikuweza kupatanishwa kwa desturi za kidhabihu (ona Hes 15:30-31). Dhambi kama hizo za kumkosea Bwana na kuasi maagizo yake zingeweza kusamehewa na Mungu mwenyewe kwa misingi tu ya neema isiyo na ukomo wa kustahili kwa mwitikio wa imani na toba (ona Zab 32, 51), au kutakasika kusubiriwako katika siku ya Upatanisho.

3. Israeli ya AK ilikuwa na Sikukuu, sherehe, au siku takatifu saba kuu, katika seti mbili: Sikukuu za Kuinuka na Sikukuu za Kuanguka. Wanaume wa Kiebrani walitakiwa kuhudhuria mbele za Bwana mahali palipoteuliwa (m.y., Yerusalemu, baada ya kutekwa nchi na kujengwa hekalu) mara tatu kwa mwaka, katika Sikukuu ya Mikate isiyotiwa chachu (Pasaka); Sikukuu za Majuma; Na Sikukuu za Vibanda (Kut 23:14-17; 34:23-24; Kumb 16:16).

a. Sikukuu za Kuinuka zilianzia mwezi wa kwanza wa Kalenda ya wakfu (Abibu/Nisani [March-Aprili]):

(1) Pasaka (14 Abibu/Nisani): Ilikuwa ukumbusho wa kutolewa kutoka utumwa wa Misri (m.y., Malaika wa Mungu wa mauti “aliwaruka” Waisraeli). Mwana kondoo alichinjwa, damu yake ikanyunyizwa katika miimo na vizingiti vya juu vya milango ya nyumba, na kisha ikaandaliwa na kuliwa na familia hiyo (Kut 12:1-13, 21-27; Walawi 23:5; Hes 28:16; Kumb 16:1-8).18 (2) Mkate Usiotiwa chachu (15-22 Abibu/Nisani): Uliendana na Pasaka (ona Math 26:17; Mark 14:12; Luka 22:1),19 Ni kukumbusha kuondoka kwa haraka kutoka Misri. Makusanyiko matakatifu ya Abibu 15 na 22 yalitajwa kuwa Sabato. Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi zilifanyika. Mkate usiotiwa chachu uliliwa katika juma hilo (Kut 12:14-20; 34:18; Walawi 23:6-8; Hes 28:17-25). (3) Malimbuko ya Mazao (Abibu/Nisani16): Ilisherehekea malimbuko ya kwanza ya Shayiri. Mganda wa malimbuko ya shayiri ulishikwa na mkono wa kuhani na kupungwa hewani na kisha sadaka ya kuteketezwa ikafanyika (Kut 34:26; Wal 23:10-14).(4) Sikukuu za Juma (pia huitwa Sikuu za Mavuno); Siku ya Malimbuko; na Pentekoste) (Sivani 6 [May-Juni]): Ilisherehekea malimbuko ya mavuno ya ngano, na jinsi Bwana alivyowatoa Waisraeli kutoka utumwani. Ilitendeka siku 50 baada ya

18 After Israel left Egypt and entered the promised land, modifications from the “Egyptian” manner of observing Passover were made, including no longer sprinkling the blood on the lintel and doorposts (Edersheim 1988: 212-18).

19 “From their close connection [Passover and Unleavened Bread] are generally treated as one, both in the Old and in the New Testament” (Edersheim 1988: 208).

65

Page 67:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Malimbuko (ndiyo sababu ya kuitwa Pentekoste [“ya Hamsini”], Mdo 2:1; 20:16; 1 Wakor 16:8). Kusanyiko takatifu lililotajwa kama Sabato, sadaka za kutikisa, kuteketeza, dhambi, na amani zilifanyika (Kut 23:16; 34:21-24; Walawi 23:15-21; Hes 28:26-31; Kumb 16:9-12).

b. Sikukuu za Kuanguka zilianzia mwezi wa kwanza wa Kalenda ya Kawaida (Tishri [Septemba-Octoba]):

(5) Sikukuu ya Mabaragumu ( Rosh Ha-Shanah ) (Tishri 1): Ilisherehekewa mwanzo wa mwezi wa saba (Mwaka Mpya wa kawaida), na ilitahadharisha kuhusu siku ijayo ya Upatanisho, siku tisa baadaye. Tukio takatifu, mabaragumu yalipulizwa, na kufanya sadaka za kuteketeza, unga, na za dhambi (Walawi 23:23-25; Hes 29:1-6). (6) Siku ya Upatanisho ( Yom Kippur ) (Tishri 10): Ni siku takatifu kuliko zote katika mwaka. Dhambi za watu zilifunikwa na kutakaswa kwa mwaka ule. Kusanyiko takatifu, sadaka za kuteketezwa, za unga, na za dhambi zilitolewa. Baada ya kufanya matoleo kwa ajili yake mwenyewe, kuhani mkuu aliruhusiwa kuingia patakatifu pa patakatifu ndani ya hekalu na kunyunyizia damu katika kiti cha rehema kama upatanisho kwa dhambi za watu. Hatua za utakaso zilihusisha mbuzi wawili: moja aliuawa na damu yake kunyunyiziwa katika kiti cha rehema; mwingine (yule wa “Aazazeli”) alikuwa amebeba dhambi za Israeli zilizotamkiwa juu yake na kisha kupelekwa nyikani (Walawi 16:1-34; 23:27-32; Num 29:7-11). (7) Sikukuu ya Vibanda (Makao) (pia huitwa Sikukuu ya Makusanyiko) (Tishri 15-22): Ilikumbushia kutangatanga nyikani na kusherehekea kukamilishwa kwa mavuno. Makusanyiko matakatifu siku ya 15 na 22 Tishri yaliyoitwa Sabato. Sadaka za kuteketeza, unga, na dhambi zilifanyika. Washiriki walitakiwa kukaa katika makao ya kitambo kifupi tu na kufurahia kwa shangwe na makuti ya matawi ya mitende (Kut 23:16; 34:22; Wal 23:33-43; Hes 29:12-38; Kumb 16:13-15).

4. Yesu alitimiliza sikukuu na hizo shereke zote. Wakol 2:16-17 panaonyesha kwamba sikukuu zote za AK zilikuwa“kivuli” na kutimizwa katika Kristo, ambaye ndiye “kitu halisi.” Sadaka zilihitajika kama sehemu ya sikukuu na sherehe. Kwa vile Kristo ndiye aliyekuwa, dhabihu ya kudumu iliyotimiza dhabihu ya mifumo ile yote, basi alitimiliza sikukuu zote na sherehe zile. Kama Kristo hakutimiza zile sikukuu na sherehe nyingine za AK, basi tungelikuwa bado tunatakiwa kuzitimiza, kwa sababu zilisemekana“sharti zitunzwe” (m.y., zilipaswa zidumishwe “milele”) (ona Kut 12:14; Walawi 23:14, 21, 31, 41). Ukweli kwamba kanisa halijazitunza hizo, huonyesha kwamba limetambua kuwa sikukuu zote zilielekezwa kwa Kristo, na matakwa yahusikayo yametimilizika katika Kristo. Twazitimiza sikukuu hizo milele “katika Kristo,” na hivyo hatuhitaji tena kuzitenda kwa namna za ki-nje kama zinavyotakiwa katika Sheria za Agano la Kale za Musa. Jinsi Yesu alivyotimiza kila mojawapo ya sikukuu na sherehe hizo inaelezwa hapo chini.5. Yesu alitimiza Pasaka na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu.

a. AJ linamhusisha Yesu na Mwana kondoo wa Pasaka. Mwanzoni mwa huduma ya Yesu hadharani, Yohana Mbatizaji alimtambua Yesu na kumwita “Mwana kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (Yoh 1:29, 36). Kwa kumtaja hivyo, Yohana alikuwa anaunganisha Pasaka (ambayo inahitaji kuwepo na dhabihu ya kondoo) na siku ya Upatanisho (ambayo dhambi za Israeli zilifunikwa). Kumhusisha Yesu na mwana kondoo wa dhabihu kunathibitishwa tena katika 1 Petr 1:19; Ufu 5:6, 8. Yesu alisulubiwa wakati wa Pasaka wakati ambao mwana kondoo wa Pasaka alichinjwa (Luka 22:1; Yoh 19:14, 31). AJ linasema kwamba Pasaka ilikuwa ni unabii wa dhabihu ya Kristo. Yoh 19:36 hunukuu Kut 12:46 na Hes 9:12 (ambapo hueleza dhahiri kwamba mifupa ya kondoo wa Pasaka haipaswi kuvunjwa) na husema, “mambo haya [m.y., wale maaskari kutoivunja miguu ya Kristo kama walivyoifanyia miguu ya watu wengine waliosulubiwa pamoja na Yesu] yalikuja kutimiliza Maandiko, ‘hakuna mfupa wake utakaovunjwa.’” 1 Wakor 5:7 pia husema, “Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani Kristo.” b. Katika Karamu ya Mwisho Yesu alianzisha Sikukuu ya Pasaka/Sherehe ya Mkate usiochachwa—Meza ya Bwana (Math 26:20-29; Mark 14:12-25; Luka 22:1-22; Yoh 13:1-2; 1 Wakor 11:23-32). Bretscher (1954: 199-209) anaorodhesha tofauti 11 kati ya Pasaka ile ya awali /Mkate usiotiwa chachu na Meza ya Bwana:

(1) Kila Sikukuu ilianzishwa kwa agizo la Mungu (Kut 12:1; 1 Wakor 11:23).(2) Kila Sikukuu ilihusisha kutoa sadaka ya mwana kondoo (Kut 12:3; 1 Wakor 5:7).(3) Katika kila Sikukuu, mwana kondoo alitakiwa awe hana ulemavu (Kut 12:5; 1 Petr

66

Page 68:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

1:19).(4) Katika kila Sikukuu, hakuna mfupa wowote wa mwana kondoo ulitakiwa kuvunjwa (Kut 12:46; Yoh 19:31-36). (5) Katika kila Sikukuu kulikuwa na kuliwa nyama ya mwana kondoo aliyetolewa dhabihu na mhusika ambaye hunufaika moja kwa moja na dhabihu (Kut 12:47; Yoh 6:52-57; 1 Wakor 10:18; Math 26:26; Mark 14:22; Luka 22:17-19; 1 Wakor 11:24).(6) Katika kila Sikukuu, ile damu iliyomwagika inafanya kazi kubwa sana kama kiini cha sherehe hiyo. Katika Pasaka, ile damu ya mwana kondoo ilipaswa kunyunyizwa juu ya miimo na vizingiti vya milango (Kut 12:7, 22); Katika Meza ya Bwana, damu inafanyika sehemu ya sherehe yenyewe (Math 26:27-29; Mark 14:23-25; Luka 22:17-20; 1 Wakor 11:25-26).(7) Kwa kila Sikukuu Mungu huhusisha ahadi ya Mungu. Katika Pasaka Mungu aliahidi kuwaokoa watu wake na pigo la mauti la wazaliwa wa kwanza (Kut 12:13, 23). Katika Meza ya Bwana Kristo anaahidi msamaha wa dhambi(Math 26:28; ona, Mark 14:24; Luka 22:20). Meza ya Bwana basi ni sikukuu yenye nguvu na uwezo zaidi, kwa sababu haiishii kuokoa miili ya wahusika ya kimwili tu, bali huokoa miili na roho za wahusika (ona Math 10:28).(8) Sikukuu zote mbili zimetolewa kama kumbu kumbu, Zisherehekewe vizazi na vizazi. Pasaka hukumbusha Waisraeli juu ya ukombozi wao kutoka Misri (Kut 12:14, 24-27). Meza ya Bwana hukumbusha Kristo ambaye, kwa kifo chake, “huchukua dhambi ya ulimwengu” (1 Wakor 11:25-26).(9) Sikukuu zote mbili huhusisha umuhimu wa imani. Utii wa Israeli kwa Mungu wakati wa Pasaka ulionyesha imani yao na tumaini katika kile alichokisema (Kut 12:27-28), na ndipo alipowaokoa kutoka katika mauti. Katika Meza ya Bwana, washiriki lazima wajiangalie wenyewe na kushiriki Meza hiyo katika namna inayostahili; kushindwa kufanya hivyo husababisha hukumu, hata mauti (1 Wakor 11:27-32).(10) Damu halisi huwa msingi wa kila Sikukuu, bali hiyo damu inayoweka msingi wa Meza ya Bwana ina thamani na uwezo wa ndani, usio na mwisho ambapo ile damu inayoweka msingi katika Pasaka haikuwa hivyo. Hiyo damu ya mwana kondoo katika Pasaka ilikuwa ni “alama” kwamba Mungu angeiona wakati malaika wake wa mauti anapopita kati ya Misri, lakini haikuwa na nguvu za ndani za kuwaokoa watu ndani yake (Kut 12:13). Kwa upande mwingine, damu ya Kristo ambayo inaweka msingi Meza ya Bwana ni damu halisi ya Mwana wa Mungu, ambayo peke yake kiukamilifu inaweza na inatosha “kuchukua dhambi ya ulimwengu” (Math 26:28). Kwa hiyo, Yesu aliweza kusema, “Hili . . . ni Agano jipya katika damu yangu” (Luka 22:20), siyo tu kwamba damu yake ilikuwa “alama” ya agano jipya. (11) Sikukuu zote mbili ni tenganifu. Pasaka ilikuwa kwa ajili ya Waebrania peke yao, wasio Waisraeli walitakiwa watahiriwe kwanza ili waweze kushirikishwa (Kut 12:43-45). Meza ya Bwana ni kwa ajili ya mwili wa Kristo (1 Wakor 10:16-17, 20-21).

c. Umuhimu wa Yesu kuanzisha Pasaka “mpya” katika Yerusalemu. “Hii kiukamilifu ilimaanisha kuwa hata katika Yerusalemu watu wa Israeli walikuwa bado wako Misri na katika ‘utumwa’. Kama hili litaonekana kama si la kuaminika, kuna uhusiano, kwamba [Marko] anatumia neno la Kiyunani [eksagō] kuelezea Yesu ‘kutolewa’ nje ya mji ili kusulubiwa (15:20)—neno ambalo sehemu nyingine katika Agano Jipya hutumiwa mara kwa mara kuelezea ‘kuongoza katika kutoka’ kwa wana wa Israeli kutoka Misri chini ya Musa [ona Mdo 7:36, 40; 13:17; Waeb 8:9].” (Walker 1996: 14) Ni tu kwa kupitia kifo cha kujitoa cha Yesu ndipo Israeli, na yeyote mwingine “aulaye mwili wake na kuinywa damu yake,” huwekwa huru kutoka utumwani—ndicho Yesu na AJ lote lililobakia hufundisha (ona Yoh 8:31-36; Rum 6:1-23; Waeb 2:14-15).

6. Yesu aliitimiza ile siku ya Upatanisho, ule mfumo mzima, na ukuhani.a. AJ laonyesha kwamba kifo cha Yesu juu msalabani kilitimiliza dhabihu za kimsingi za Walawi. “Wazo la kimsingi la dhabihu katika Agano la Kale ni la utendaji wa mabadilishano, ambalo pia huhusika katika mambo mengine pia—utakaso na ukombozi, adhabu kali na msamaha” (Edersheim 1988: 107). Hivyo basi, kilicho chini ya dhabihu zote za damu kilikuwa mbadala wa maisha ya asiye na hatia (yule mnyama atolewaye sadaka) kwa ajili ya yule mwenye hatia. Kristo alitimiliza msingi mzima wa mfumo wa sadaka au dhabihu kwa sababu ni yeye pekee aliyekuwa na uwezo kutenda kama dhabihu mbadala wetu kwa vile ni yeye peke

67

Page 69:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

yake aliyekuwa hana dhambi (Isa 53:4-12; Luka 23:41, 47; Mdo3:14-15; 2 Wakor 5:21; Waeb 4:15; 7:26; 1 Petr 2:21-24; 1 Yoh 3:5).

(1) Kristo alitimiliza muktadha wa dhabihu za matengenezo (ona Isa 53:4-8, 10; Rum 8:1-4; 2 Wakor 5:18-21; Waeb 9:11-28; 10:11-12; 13:10-15).(2) Kristo alitimiza muktadha wa dhabihu za uwekaji wakfu (ona Math 26:39; Marko 14:36; Luka 22:42; Yoh 4:34; 5:17-20, 30; 6:38; 8:28-29; 10:18; 12:49-50; 14:10, 24, 31; 17:1-26). (3) Kristo alitimiliza muktadha wa dhabihu za amani (ona Yoh 14:27; 16:33; Rum 5:1-11; Waef 2:13-18; Wakol 1:18-20).

b. AJ huunganisha Pasaka, siku ya Upatanisho, na mfumo mzima wa dhabihu, na kusema kwamba kifo cha Yesu juu ya msalaba kilitimiliza na kuleta mbadala wa zote. Katika Rum 3:25 kifo cha Yesu kilitajwa kama “upatanisho” au “dhabihu ya upayanisho.” Hilo ni neno lile lile la Kiyunani litumiwalo kwa ajili ya “kiti cha rehema” kilichofunika sanduku la agano katika patakatifu pa patakatifu (Kut 25:17), na ilihusishwa haswa na Siku ya Upatanisho. “Hili linapounganishwa na Paulo alivyolitumia sehemu nyinginezo kuhusu ‘damu’ ya Kristo [ona Rum 3:25; 5:9; 1 Wakor 11:25; Waef 1:7; 2:13; Wakol 1:14, 20] na maelezo haya ya Kristo kama ‘kondoo wetu wa pasaka’ (1 Wakor 5:7), ni dhahiri kwamba Paulo aliiona kazi ya Kristo kama iliyounganishwa kikamilifu na sikuu kuu mbili zihusianazo na Hekalu: Pasaka na Yom Kippur [“Siku ya Utakaso”]. Pamoja na umuhimu mkubwa wa nguvu ya kiutendaji wake, hata hivyo, Paulo atakuwa ameona Msalaba kama kutimilizwa kwa desturi hizi za Hekalu—siyo tu kama kitu ambacho kimesaidia kuwakamilishia jambo tu. Kifo cha Yesu chaonekana katika namna ya upekee, na ni dhahiri kuwa kinaleta mbadala wa kile ambacho vinginevyo kingelikuwa ndiyo majukumu ya Hekalu na sadaka au dhabihu zake.” (Walker 1996: 123) c. Siku ya Upatanisho ilikuwa ni “mfano” ulioomwelekea Kristo juu ya msalaba.

(1) Tofauti kati ya damu za wanyama na damu ya Kristo . Walawi 16-17 husisitiza umuhimu wa damu ya dabihu ili kuleta upatanisho wa dhambi. Kumwagika damu ya dhabihu kulikuwa lazima kwa ajili ya kuhani mkuu ili awe na damu aliyoihitaji kuja nayo patakatifu pa patakatifu na kuinyunyizia juu ya kiti cha rehema. Waebrania 7-10 panaonyesha kuwa kujitoa kwa Kristo msalabani kulikuwa ndicho Siku ya Upatanisho ulichokilenga. “Msalaba ulimaanisha kungeliweza kuwa na ‘kitu cha kutolewa’ ili kwamba Kristo aweze kutenda kama kuhani (8:3).” (Nelson 2003: 254) Damu yake Yesu mwenyewe kiumbali kabisa ilipitiliza thamani ya damu za wanyama. “Ile hati ya awali ilikuwa dhaifu kwa sababu ilitumia damu za wanyama na ilitakiwa kurudiwa tena na tena (10:1-4); Tendo la kikuhani la Kristo lilitendeka mara moja tu na lilihusisha damu yake mwenyewe kama dhabihu yake (7:27; 9:25-26). Zaidi ya hapo, ilitendeka katika anga za kimbingu za uhalisi wa kweli (9:24 tofauti na 10:1). Kukamisha kwa Kristo ni kielelezo cha mwisho cha ukweli wa Kimaandiko kwamba utakaso lazima ukamilike kwa utaratibu wa kutumia damu (9:13-14, 21-23). Lakini damu yake ina uwezo zaidi kwa vile kimsingi ilikuwa ya kwake mwenyewe, matokeo ya utii wake mwenyewe uliofanyika kupitia ‘roho ya milele’ na hivyo basi ni kinyume kabisa cha kitu chochote cha kuonekana au cha muda mfupi (9:12). Uwezo wa kukomboa na kutakasa wa damu hii ni wa ndani na wa milele zaidi kuliko ule wa ki-nje na wa kitambo kifupi (9:12-14; cf. 10:1-4).” (Ibid.: 256) (2) Utofauti kati ya mahali patakatifu alipoingia kuhani na mahali patakatifu alipoingia Kristo. Kipengele muhimu cha Siku ya Upatanisho kilikuwa ni kuhani mkuu kuingia patakatifu pa patakatifu ili kuonana na uwepo wa Mungu, nyuma ya pazia, na kuitumia damu ya sadaka kunyunyiza juu ya kiti cha rehema kuvitakasa vitu vitakatifu na taifa kutokana na uharibifu na dhambi (Walawi 16:2-19). Kinyume chake, kwa kupitia ufufuo wake na kupaa kwake Kristo aliziingia “mbingu zenyewe” (Waeb 9:24; pia ona, Heb 4:14; 8:1-2), katika “ndani, mlimo nyuma ya pazia” (Waeb 6:19-20, RSV). Kwa hiyo, Kristo hutenda yote mawili, kama mhanga na kama kuhani mkuu : kama mhanga damu yake ilikuwa kamilifu kwa sababu aliishi maisha yasiyo na hatia na hakuwa na dhambi (9:12-14; Waeb 10:4-10); kama kuhani mkuu alikuwa pia kamilifu kwa sababu hakuhitajika kutoa dhabihu kwa ajili yake mwenyewe (Waeb 7:26-27; 9:7).(3) Tofauti kati ya nyikani ambapo mbuzi wa Azazeli alipelekwa na kutenganishwa kwa Kristo na Baba. “Jukumu la mbuzi wa Azazeli ni maalum kwa ajili ya Siku ya Upatanisho, ikiwakilisha (ndani kabisa ya mahali pasipotakaswa) kwa dhambi za

68

Page 70:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Israeli. Kwa hiyo damu ya mbuzi moja inaletwa Mahali Patakatifu sana, ambapo mbuzi wa Azazeli anaachiliwa kwenda mbali na Mungu (nyikani).” (Williamson 2007: 110) Katika umilele wote, Yesu alikuwa amepata upendo, na ushirika mkamilifu na Baba. Hata hivyo, juu ya msalaba Yesu alibeba dhambi zetu (Isa 53:4-5), na “Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa [na] amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai” (Isa 53:8). “Katika Mathayo 10:28 Yesu anasema kuwa hakuna uangamivu wa kimwili unaoweza kufanana na uangamivu wa roho katika jehanamu, wa kuukosa uso wa Mungu. Lakini hicho ndicho haswa kilichotokea kwa Yesu alipokuwa msalabani—alikuwa ameachwa na Baba (Mathayo 27:46). . . . Alipolia kuwa Baba yake amemwacha, alikuwa anaionja jehanamu yenyewe. Lakini kumbuka—ikiwa deni letu la dhambi ni kuu sana kwamba halilipiwi pale, bali jehanamu yetu yaendelea milele, basi tuseme nini kutokana na kile alichosema Yesu aliposema gharama kulipia deni letu ‘imekwisha’ (Yoh 19:30) baada ya siku tatu tu? Twajifunza kuwa kile alichojisikia akiwa juu ya msalaba kilikuwa kibaya zaidi na chenye kina zaidi kuliko jehanamu zetu zote tulizokuwa tunastahili zikichanganywa pamoja.” (Keller n.d.: n.p.) Mbuzi wa Azazeli aliyeachiliwa anaendana kwa usambamba na Yesu kuachilika kutoka uwepo wa Baba .

d. Yesu ametimiza na kupitiliza ukuhani wote wa AK. Waeb 7:28 husema, “Maana torati yawaweka wanadamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hata milele.” Kwa vile Mwana“amekamilika hata milele,” ukuhani wa AK ulio mdhaifu” umeondolewa milele. Zaidi ya hayo, Yesu alikuwa “ametoka katika Yuda, kabila ambalo Musa hakunena neno lo lote juu yake katika mambo ya ukuhani.” (Waeb 7:14). Kulingana na Sheria ya AK, Haruni na Walawi walitakiwa wawe makuhani wa Mungu“milele” (Hes 18:1-8, 11, 19-23; 1 Nyak 15:2; 23:13). Hata hivyo, katika Agano Jipya, hayo yote yamebadilika. Yesu ni kuhani “kwa mfano wa Melkizedeki, … kwa mfano wa Haruni” (Waeb 7:11; ona pia 5:6). Ukweli kwamba Yesu anaitwa yote mawili “kuhani” na “kuhani mkuu” huonyesha kwamba mfumo mzima wa AK na ukuhani wake umebadilishwa kwa sababu, kulingana na sheria za AK,Yesu asingeweza kuwa kuhani hata kidogo, kwa vile hakuwa mzaliwa wa ukoo wa Haruni wala kabila la Walawi, bali kutoka kabila la Yuda (Waeb 8:4; ona Math 1:2-3; Luka 3:33-34). Kwa hiyo, “Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike” (Waeb 7:12).e. Waebrania hutofautisha mfumo mzima wa desturi za dhabihu, ukuhani wa Israeli na Kristo.

(1) Dhabihu za AK zinatofautishwa na Kristo. “Mwandishi wa [Waebrania] huukosoa mfumo mzima wa dhabihu wa Israeli akiuona hauna nguvu (7:11, 18-19; 10:4), na ni wa kurudiwa-rudiwa pasipo mwisho (7:23; 10:1), si wa kudumu (8:13; 9:9-10), na ulio na rangi za dhambi za makuhani waliozitoa (5:3; 7:27; 9:3). . . . Waebrania hukosoa mifumo ya kale ya dhabihu ili kutoa nuru, kwa mlinganisho, ubora wa dhabihu iliyo ‘bora’ inayofuatia (9:23) ambayo inafanya ‘agano lililo bora zaidi’ (7:22) inayosimamia ‘ahadi zilizo bora zaidi’ (8:26) lililofanywana kristo kama kuhani mkuu zaidi. (7:1, 15, 26-27).” (Nelson 2003: 251) (2) Mlinganisho katika Waebrania hauishii kwenye ile Siku ya Upatanisho ya kila mwaka. Badala yake unahusisha mfumo mzima wa dhabihu za Israeli na ukuhani wake. “Damu iliyonyunyizwa ilikuwa pia sura ya desturi ambayo kwayo Musa alianzisha agano katika Kutoka 24:3-8. Ile damu ambayo Musa aliinyunyizia kwa watu na madhabahu iliwaunganisha Mungu na Israeli kimaagano. Vivyo hivyo, Yesu alianzisha agano jipya kupitia kifo na damu yake mwenyewe iliyonyunyizwa (9:15; 12:24). Waebrania 9:18-22 hupanua zaidi kile Maandiko yalichoandika kuhusiana na Musa—Musa hunyunyizia Kitabu cha Sheria, hema ya kukutania, na vyombo vyake—na hutimiza desturi kadhaa na mambo kutokea desturi zihusiananazo na ng’ombe jike mwekundu (Hes 19:9, 18, 20) sufu nyekundu (Walawi 14:2-6). Kitengo hicho cha utaratibu huonyesha kuwa kitendo cha ukuhani wa Yesu kilitimiliza na kupitiliza kiukamilifa mifumo yote ya kidhabihu ya awali.” (Nelson 2003: 256-57) (3) Waeb 13:10-14 huonyesha kwamba kuendelea kuabudu kwa mtindo wa AK katika Hekalu la kuonekana na kumwabudu Yesu hayaendani sambamba. “Yesu alianzisha mfumo mpya wa Hekalu jipya (uliowakilishwa na alama ya ‘madhabahu’) uliosimama tofauti kabisa na mfumo wa Hekalu liendanalo na ‘hema’. Kusema ukweli, mifumo hiyo miwili ilikuwa haiendi pamoja: wale waliohusika na mfumo wa awali walikuwa wametengeka kabisa kutoka katika mfumo huu mpya (‘wale wanaosimamia katika

69

Page 71:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

hema hawana haki ya kula’: v. 10); kwa maana halisi; wale wanaoamini katika Yesu nao walipaswa vivyo kujihesabu wenyewe kuwa wametengeka kutoka katika mfumo wa awali (‘na tumwendee nje ya kambi’: mst. 13). . . . Hii hulazimisha namna mpya ya uelewa. Kifo cha Yesu kilitokea ‘nje ya lango la mji’ (v. 12), siyo (kama ilivyo kwa wanyama wa dhabihu) ndani ya ‘patakatifu’ (mst. 11). Kwa hiyo,uchaguzi ulihitajika —ama wa kumwendea Yesu ‘nje ya kambi (mst. 13) ama kubakia, kama ilivyokuwa, ndani ya mji na kukazia kwenye lile Hekalu. Kwa kutumia lugha mbadala ya ‘kijiografia’, ambapo moyo wa uthabiti wa mtu ulijikita kuhusiana na mlima wa Hekalu au na ‘mahali pa fuvu’? Utofauti kati ya hayo mawili ulikuwa dhahiri. Njia mpya ya kumkaribia Mungu ilikuwa imeanzishwa; uchaguzi lazima ufanyike.” (Walker 1996: 206-07)(4) Hatima na ukamilifu wa Upatanisho wa Yesu—na kwa hiyo uondolewaji kabisa wa kudumu wa mfumo mzima wa dhabihu na ukuhani wa AK—unaonekana katika ukweli kuwa “aliketi mkono wa kuume wa Mungu” katika patakatifu pa patakatifu pa kweli pa kimbingu ( Waeb 1:3; 10:12, 14, ona Zab 110:1; Marko 16:19; Luka 22:69; Rum 8:34; Waef 1:20-21; Wakol 3:1; 1 Petr 3:21-22 ). “Kwa vile ibada ya dhabihu iliwakilisha hali ya kusimama mbele za Mungu au madhabahu (10:11; Kumb 10:8; 18:7), hali ya utofauti wa kuketi huonyesha ukomo wa tendo la dhabihu ya Kristo (10:12). Hata hivyo, wakati huo huo, kupewa enzi kwake mkono wa kuume wa Mungu humpatia nafasi kuweza kuingia na cheo kwa ajili ya maombezi yanayoendelea, na yenye nguvu.” (Nelson 2003: 257) (5) Dhabihu ya Kristo msalabani, na ufufuo na kupaa kwake, kulipitiliza kwa mbali mifumo yote ya Israeli na ukuhani wake, kuchanganya ukuhani mkuu siku ile ya Upatanisho, ambavyo ungeweza.

(A) Ule mfumo wa kale wa dhabihu ulihitaji dhabihu na makuhani mbali mbali (Waeb 7:23; 9:25; 10:1, 11). Ukuhani wa Yesu ni wa kudumu, naye alihitajika kutoa dhabihu moja tu kwa ajili ya watu wote kwa ajili ya wakati wote (Waeb 7:24, 27; 9:12, 25-28; 10:10-14). (B) Ule mfumo wa kale wa dhabihu haukuweza kuwabadilisha watu kwa ndani au kuwakamilisha. Kwa dhabihu yake, Kristo anatimiza hilo (Waeb 7:11; 9:9-10; 10:1-2, 14-16). (C) Ile siku ya kale ya ilitumika kama “ukumbusho” wa dhambi kila mwaka. Kupitia dhabihu ya Kristo, Baba asema“Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa” (Waeb 10:3, 16-18). (D) Kristo alitekeleza kile ambacho hakuna kuhani wa duniani angeweza kukifanya. Alipaa hadi mbingu zenyewe, ambako anaendelea kuwaombea watu wake milele kwa Baba (Waeb 7:24-25), na siyo tu kama kuhani bali kuhani mkuu (Waeb 4:14-15; 7:26; 8:1-2). (E) Kwa kifo, ufufuo, na kupaa kwa Kristo, sasa kila mwamini huwezeshwa kufanya kile ambacho makuhani wa AK peke yao walikuwa wanakifanya. Katika AK ni makuhani tu ndio walioweza kuingia patakatifu katika Hekalu. Yesu aliwawezesha watu wote “kwa ujasiri kabisa kuingia patakatifu pa Mungu kwa njia ya damu ya damu ya Yesu” wakati wowote (Waeb 10:19-22; 4:16).

7. Yesu alitimiza ile Sikukuu ya Malimbuko na ya Majuma. “Malimbuko” ilisherehekea malimbuko ya mavuno ya shayiri, na ilikuwa ni sehemu ya juma zima la Pasaka/sherehe za Mkate usiotiwa chachu (Kut 34:26; Walawi 23:10-14). Pia ilijulisha siku ya kwanza ya kipindi cha siku 50 zilizoishia katika Sikukuu ya Majuma (hivyo, Majuma pia yaliitwa “Pentekoste”) (Walawi 23:15-16). Majuma ilisherehekea Malimbuko ya mavuno ya shayiri. Kwa hiyo, Majuma pia yaliitwa Sikukuu ya Mavuno (Kut 23:16; 34:22), na siku ya kwanza ya Sikukuu hiyo iliitwa “siku ya malimbuko” (Hes 28:26). Sikukuu zote mbili zilikuwa ni kusherehekea uwingi au utele ambao Mungu alikuwa amewapa hilo taifa, ambapo “malimbuko yake” ndiyo yalikuwa yanatolewa.

a. Kama vile Yesu katika kifo chake alikuwa Pasaka wetu, vivyo katika ufufuo wake amekuwa Malimbuko yetu. Katika1 Wakor 15:20, 23 Kristo huitwa wazi wazi“malimbuko” kwa ajili ya wote walio katika Kristo. Kwa hiyo, tutafufuka kama jinsi ambavo yeye amefufuka kutoka kwa wafu (1 Wakor 15:20-58).b. Kutumwa kwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste (“siku ya malimbuko”) kulitimiza Sikukuu

70

Page 72:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

ya Majuma. Kristo alifufuka kutoka kwa wafu Jumapili asubuhi sana baada ya Sabato ya Pasaka (m.y., katika “Malimbuko” Walawi 23:15-16; Math 28:1-6; Marko 16:1-6; Luka 24:1-6; Yoh 20:1-2). Alionekana kwa siku 40 kwa makundi mbali mbali ya watu (Mdo1:3). Kisha akapaa mbinguni, ila aliwaambia wanafunzi wake kungojea Yerusalemu ile ahadi ya Baba ya kuwabatiza kwa Roho Mtakatifu (Mdo 1:4-5). Siku kumi baadaye (m.y., siku 50 baada ya kufufuka) “siku ya Pentekoste ilipowadia” Roho Mtakatifu aliwashukia na kuwajaza wanafunzi wa Yesu (Mdo 2:1-4). Kwa kumtuma Roho Mtakatifu, Kristo alitimiza maana na kusudio la kiroho la kweli la Sikukuu ya Majuma. Kama zilivyo ishara, nakala, na vivuli vingi sana vya AK, malimbuko ya kuonekana ya kimwili haswa yalielekeza na kuwa na maana na utimilizo wa kiroho (k.m., Luka 11:13).c. Katika Rum 8:23 Paulo anasema kuwa tunayo “malimbuko ya Roho.” Alitambua kwamba, kama ilivyo kwa malimbuko ya mavuno ya shayiri na ngano, sasa tuna mwanzo wa malimbuko ya Roho. Malimbuko ni matoleo ya mavuno kamili, ambayo twaweza kuyatarajia kwa ujasiri na kuyatumainia. Bali mavuno kamili bado hayajakamilika. Kwa hiyo, Paul o alihitimisha Rum 8:23 kwa kusema kuwa sisi “tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.” Hilo litatokea wakati wa kuja kwa mara ya pili kwa Kristo tutakapobadilishwa na kutukuzwa, na kuipokea miili mipya (1 Wakor 15:35-49).

8. Yesu alitimiza Sikukuu ya Mabaragumu. Sikukuu ya Mabaragumu ilikuwa ya kwanza kati ya Sikukuu tatu za Maanguko (sambamba na Siku ya Upatanisho na Sikukuu ya Vibanda ). Ilitangaza mwaka mpya wa kawaida, na kutarajia kwa siku ijayo ya Upatanisho (Wal 23:23-25; hes 29:1-6).

a. Watu wengi wanafikiria kuwa Mabaragumu huhusiana tu na kuja kwa mara ya pili kwa Kristo. Vifungu kadhaa huonyesha kwamba kuja kwa mara ya pili na ufufuo wa wafu kutatanguliwa na “mabaragumu” ya malaika (ona Math 24:31; 1 Wakor 15:52; 1 Wathes 4:16). Watu wengine husema kuwa Mabaragumu (maparapanda) kinamna fulani huhusiana na “hukumu ya mabaragumu” ya Ufu 8:1-9:21; 11:15-19. Hata hivyo, maoni yote mawili hupuuza hoja muhimu sana.b. Sikukuu ya Mabaragumu huenda isihusiane na kuja kwa mara ya pili kwa Kristo au “hukumu ya mabaragumu,” bali ilikuwa imetimizwa katika ujio wa kwanza wa Kristo. Angalau sababu tatu zinathibitisha hilo:

(1) Jukumu la msingi la Baragumu lilikuwa kutangaza majira ya kugeuka kiwakati—mwanzo wa mwaka mpya. Ujio wa kwanza wa Yesu ulitimiza hilo.

(A) Yesu mwenyewe ki-udhahiri kabisa alitamka hilo katika Luka 4:18-19 aliponukuu kutoka Isa 61:1-2 kwamba alikuwa ametumwa “kuutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika.” Katika Luka 4:21 kisha akanena, “leo Maandiko haya yametimia masikioni mwenu.” (B) Ukweli kwamba ujio wa Kristo wa mara ya kwanza unaweka alama mpya ya muda wa historia ya maisha ya mwanadamu unathibitishwa kutokana na ukweli kuwa kuja kwake kulianzisha kuanza kwa“siku za mwisho” ambazo sasa ziko, na zitaendelea hadi kurudi kwake tena (ona Mdo 2:16-17; Waeb 1:2; Yak 5:1-3; 1 Petr 1:20; 1 Yoh 2:18). 2 Wakor 5:17 huendelea kuthibitisha “upya” anaouleta Kristo asemapo, “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya [au, “uumbaji mpya”]; ya kale yamepita, tazama! yamekuwa mapya.”(C) Kuja kwa mara ya kwanza kwa Kristo kumebadilisha wakati kutoka KK (“Kabla ya Kristo”) kuja BK (ambayo hutokana na maneno ya Kilatini AD“anno domini”—“Katika mwaka wa Bwana”).20

(2) Mabaragumu yanahusiana kwa ukaribu na Siku ya Upatanisho, ambayo Yesu aliitimiza. “Kwa waalimu, Rosh Ha-Shanah ilikuwa ni siku kubwa sana ya hukumu, ikiashiria kuingia kipindi cha kujihoji kilichofikia kilele Siku ya ambayo Sikukuu ya Mabaragumu ilielekeza, bila shaka pia alitimiza sikukuu ya Mabaragumu.(3) Yesu alitimiza sababu ya desturi ya Kiyahudi ya kupuliza shofar (“pembe ya kondoo dume”) katika Sikukuu ya Mabaragumu. Katika mwaka 942 BK, mwalimu mashuhuri wa Babeli, Saadi Gaon, aliorodhesha sababu 10 kwa nini Wayahudi walipuliza shofar wakati wa Sikukuu ya Mabaragumu (Jacobs 1959: 44-48). Zote hizo,

20 Hata wale wasiotumia nembo za KK na BK—bali hutumia vifupisho vya “Zama za Jumuiya”, “BCE” na “CE”—kimsingi wanakiri uwezo wa kubadilisha majira wa ujio wa kwanza wa Kristo. Tarehe ziko sawa kama tarehe za KK na BK, bali wale watumiao vifupisho vya BCE na CE hawataki kukiri kwamba Yesu ndiye, kusema ukweli, ni Bwana.

71

Page 73:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

moja kwa moja, au si moja kwa moja, zinamhusu Kristo:(A) Mungu anatangazwa kuwa Mfalme wakati wa Mwaka mpya. Kristo ni Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana, na ana mamlaka yote (Math 28:18; Mdo 2:36; Waef 1:20-22; Wafil 2:9-11; Wakol 2:9-10; 1 Petr 3:22; Ufu 17:14; 19:16). Wakati wa kusulubiwa kwake, kibao kiliwekwa kichwani pake msalabani kisemacho Yesu ni “mfalme wa Wayahudi” (Math 27:37; Marko 15:26; Luka 23:28; Yoh 19:19).(B) Rosh Ha-Shanah ni mwanzo wa Siku kumi za matengenezo. Kristo alitimiza Siku ya Upatanisho, ambazo zile siku kumi za Matengenezo zilielekezwa.(C) Torati ilitolewa juu ya Sinai iliyoandamana na sauti ya shofar. Kristo ndiye mtoa sheria mpya, aliye mkuu zaidi kuliko Musa (Math 5:1-48). (D) Manabii huelezea mshangao wao kwa zile sauti za shofar. Yesu ni nabii kama Musa, aliyeahidiwa na Mungu (ona Kumb 18:15, 18-19; Yoh 1:45; 6:14; Mdo 3:20-23).(E) Hekalu katika Yerusalemu liliharibiwa katikati ya milio ya mabaragumu, katika mwaka mpya Wayahudi hutazamia marejezo ya utukufu wa kwanza. Yesu alitimiza na kurejeza yote mawili, Hekalu na taifa lenyewe.(F) Katika Mwanzo 22 kondoo alitolewa badala ya Isaka. Simulizi nzima ya kisa cha Ibrahimu na Isaka ilionyesha ki-mapema kusulubiwa kwa Yesu. Kama ilivyokuwa kwamba Isaka alikuwa ndiye mwana “pekee wa Ibrahimu m.y., mwana [si wa kawaida]” (Mwa 22:2), ndivyo alivyokuwa Kristo “Mwana wa pekee” (Yoh 3:16). Kama vile kuni za kutolea dhabihu zilivyowekwa juu ya Isaka (Mwa 22:6), ndivyo Yesu alifanywa abebe msalaba wake mwenyewe (Yoh 19:17). Kama vile Ibrahimu alivyosema kuwa “Mungu atajipatia mwana- kondoo” (Mwa 22:8) kwa hiyo sadaka, ndivyo Mungu alivyomtoa Yesu, “Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya dunia” (Yoh 1:29; ona pia Ufu 5:6). Kama vile Isaka alivyokuwa mtii kwa mapenzi ya baba yake, hata kufikia mauti, ndivyo Yesu alivyokuwa kwa mapenzi ya Baba yake, hata mauti (Math 26:39; Wafil 2:8). Kama vile Isaka alivyokuwa “mfu” kwa Ibrahimu ndani ya zile siku tatu wakiwa njiani (Mwan 22:4), ndivyo Yesu alikuwa kaburini kwa siku tatu (Math 12:40; Luka 24:21). Kama vile Ibrahimu aliamini kuwa angelimfufua Isaka kutoka kwa wafu (Waeb 11:19 ndivyo Yesu kimsingi alivyofufuka (Math 28:1-6; Marko 16:1-13; Luka 24:1-6; Yoh 20:1-28). Waeb 11:19 (Biblia ya NASB) hata husema kwamba Ibrahimu alimpata tena Isaka “kama mfano.”(G) Amosi 3:6 watu wasiogope?” Hisia za udhati, adhama , na heshima ya maisha na kwake yeye Aliyeutoa huamshika vizuri kwa hiyo sauti ya tarumbeta. Yesu hushikilia maisha yetu, na ni “Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake” (Waeb 1:3).(H) Sefania 1:16 huinenea siku ya hukumu kama ni “siku ya tarumbeta na ya kamsa.” Ni Kristo atakayetoa hukumu ya wote wawili; walio hai na waliokufa (Math 7:22-23; Yoh 5:22; Mdo 10:42; 17:31; Rum 14:10; 2 Wakor 5:10; 2 Tim 4:1; Yuda 14-15; Ufu 19:11). Katika uhalisia kabisa, hukumu ile imeshatokea kutokana na mwitikio wa watu kwa Yesu (Yoh 3:17-19), Ingawaje hukumu hiyo itahitimishwa wakati wa kuja kwake kwa mara ya pili (Math 13:24-30, 36-43, 47-50; 16:27; 25:31-46; Yoh 12:48; Rum 2:1-16; 1 Wakor 4:5; 2 Wathes 1:6-10; Ufu 22:12).(I) Isa 27:13 huzungumzia matarumbeta yatasikiwa wakati wa kutangaza kuja kwa Masihi kuwatoa wateule wa Israeli kurudi katika nchi. Yesu ndiye Masihi (Yoh 4:25-26). Ameleta Israeli mpya, ya kweli katika “nchi” ya raha ya wokovu wao.(J) Tarumbeta itasikiwa wakati wa kufufuka. Yesu ndiye ufufuo na ni uzima (Yoh 11:25). Ufufuo wa Yesu mwenyewe umeshatokea. Huo ndio “malimbuko” ya ufufuo wote (1 Wakor 15:22) utakaotokea “wakati wa tarumbeta ya mwisho” (1 Wakor 15:51-52).

9. Yesu alitimiza Sikukuu ya Vibanda. Sikukuu ya Vibanda (Mahema) ilikuwa ndiyo ya mwisho kati ya

72

Page 74:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Sikukuu za Israeli. Ilichukua juma moja, na ilikumbusha kutanga-tanga kwao nyikani. Pia ilisherehekea kumalizika kwa mavuno ya Anguko. Ili kukumbuka kutanga-tanga kwao nyikani, ilibidi watu watengeneze makao ya muda na kuyakalia kwa muda mfupi (mahema) wakati wa juma la hiyo Sikukuu (Kut 23:16-17; 34:22-23; Walawi 23:33-43; Hes 29:12-38; Kumb 16:13-15).

a. Kama ilivyokuwa kwenye Sikukuu ya Tarumbeta, watu wengi hufikiria kuwa Mahema yanahusiana tu na kuja kwa mara ya pili kwa Kristo. Watu hao wenye fikira maalum daima huitazama Zek 14:16 ili kuunga mkono imani kwamba Kristo atakapokuja tena atarejesha upya desturi za mifumo ya sadaka za Kiyahudi na zile Sikukuu, ikiwamo Sikukuu ya Vibanda katika mji halisi wa Yerusalemu (ona kifungu c., hapo chini, kwa ajili ya umuhimu wa kweli wa Zek 14:16).b. Kama ilivyo kwa Sikukuu nyinginezo, Vibanda ilitimizwa na Kristo katika kuja kwake mara ya kwanza.

(1) Yoh 1:14 husema kuwa “Neno [m.y., Yesu] alifanyika mwili naye akakaa kwetu.” neno “akakaa” ni neno la kitenzi ( skēnoō ) la neno “hema au vibanda” ( skēnē ). Kwa hiyo, Biblia ya NASB ina angalizo kwa Yoh 1:14 lisemalo, “au alifanya kibanda; m.y; aliishi kwa kitambo.” Kama vile vibanda ambavyo watu walivitengeneza havikuwa vya fahari au majengo ya kuvutia, hakukuwa na chochote katika kuonekana kwa Yesu hapa duniani ambacho kingetuvutia sisi kwake (Isa 53:2).(2) Vibanda viliwakumbusha ukombozi wa Mungu kwa Israeli kutoka utumwani kule Misri na kutanga-tanga kwao jangwani wakiwa njiani kuelekea nchi ya ahadi ( Walawi 23:42-43 ). Yesu ndiye Musa mpya na aliye mkuu zaidi, awakomboaye watu siyo kutoka kwenye vifungo vya kimwili tu, bali kutoka katika vifungo vya kiroho vya dhambi na mauti, ili kwamba “nasi tuenende katika upya wa uzima ” (Yoh 1:29; Rum 6:3-23). Yesu alijaribiwa na Shetani kule nyikani, kama vile Israeli walivyojaribiwa (Math 4:1-11; Luka 4:1-13). Hata hivyo, tofauti na Israeli, Yesu hakushindwa na hayo majaribu. Alipojaribiwa, Yesu alimjibu Shetani hata kwa kukusudia kabisa kunukuu kutoka katika ujumbe wa Musa wa historia ya Israeli wakiwa nyikani (Kumb 8:3; 6:13, 16). Kwa hiyo, katika maisha yake Yesu alitimiza kila kitu ambacho Hema ilikuwa “mfano” wake. (3) Kipindi Yesu alipoishi duniani, kiini cha sherehe za Sikukuu za Vibanda katika Yerusalemu kilikuwa ni sherehe ya “kumimina maji” ambapo makuhani walimwaga maji na divai kwa Bwana Hekaluni (Carson 1991: 321-22; Hillyer 1970: 46-48). “Sherehe hizi za Sikukuu ya Vibanda zilihusika katika fikira za Wayahudi kwa yote mawili , kwa Bwana kuwapatia maji kule jangwani na kwa Bwana kuwamwagia Roho katika siku za mwisho. Kumwaga wakati wa Sikukuu ya Vibanda huonyesha kialama kipindi cha Ki-Masihi ambacho maji kutoka mwamba mtakatifu ungebubujikia dunia nzima.” (Carson 1991: 322) Ni katika muktadha huo—pale Hekaluni katika Sikukuu ya Vibanda yenyewe (Yoh 7:2, 37)—ikawa Yesu “akasimama, akapaza sauti yake, akisema, ‘mtu akiona kiu, na aje kwangu na anywe. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.’” Maana ya matamshi hayo ya Yesu ni wazi: yuko katika kutimiliza Sikukuu ya Vibanda iliyotarajiwa. Kama Isaya aliweza kuwaalika wenye kiu ili wanywe katika maji (Isaya 55:1), Yesu atangaza kuwa yeye ndiye mwenye uwezo wa kutoa hayo maji” (Carson 1991: 322-23).(4) Wakati Yesu anaishi duniani, sherehe nyingine ilifanyika katika Hekalu kusherehekea Sikukuu ya Vibanda: taa nne kubwa ziliwashwa, na usiku watu walisherehekea wakishika mienge inayowaka moto; mwanga kutokea Hekaluni uliangaza kutia nuru Yerusalemu yote (Carson 1991: 337; Hillyer 1970: 49-50). Ni katika muktadha huo ndipo Yesu alisema, “Mimi ndimi nuru ya ulimwengu; yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima” (Yoh 8:12).21 Kwa mara nyingine, Yesu alikuwa anasema kuwa Sikukuu ya Vibanda ilikuwa imetimilizwa ndani yake (ona pia Yoh 3:19-21; 1 Yoh 1:5-7).

c. Kwa vile ilihusiana na kumalizika kwa mavuno (m.y., “Sikukuu ya Mavuno”), Sikukuu ya Vibanda pia ilichukua maana nyingine kwa siku za mbeleni. Huenda kuhusiana na maji yake na kuhsiana kwake na mavuno Zekaria 14 ilisomwa siku ya kwanza

21 Maandishi ya AJ ya awali zaidi hayana Yoh 7:53-8:11. Badala yake, Yoh 8:12 hufuatia mara baada ya Yoh 7:52. Kwa hiyo, muktadha wa 8:12 huonyesha kuhusiana na Sikukuu ya Vibanda (Carson 1991: 333-37).

73

Page 75:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

ya sikukuu (Carson 1991: 322; Balfour 1995: 376). Vibanda “Ilitazamia mbeleni kwenye mavuno ya furaha, wakati ujumbe wa Israeli duniani unapaswa ukamilike kwa kukusanya mataifa yote ya dunia kwa Bwana, kama ilivyotabiriwa na nabii Zekaria (14:16)” (Hillyer 1970: 40).

(1) Kauli ya Yesu katika Yoh7:37-38 kuhusiana na “maji yaliyo hai” huelekea kuibuka kutokana na mistari kadhaa ya AK. Hiyo ni pamoja na: maji kutoka ule mwamba jangwani, Kut 17:1-6, mto wa maji ya uzima katika Hekalu la Ezekieli, Ezek 47:1-11, na maji yabubujikayo katika ukingo mpya kutoka Yerusalemu kwenda bahari za ,Mashariki na Magharibi, Zek 14:8 (ona pia Zab 78:15-16; 105:40-41) (Balfour 1995: 368-78). Kwa kujitaja mwenyewe kuwa ndiye mwamba, hekalu jipya, Yerusalemu mpya, na maji yaliyo hai, Yesu alikuwa akionyesha kuwa maandiko hayo ya AK yanatimilizwa sasa: Zama mpya zijazo zimeanza. (2) Yesu ndiye mkazo wa kukusanyika huko. Uhusiano kati ya Vibanda na mavuno na kumalizika kwa ujumbe wa Israeli wa siku zijazo wa kukusanyika kwa mataifa kwa (Zek 14:16-21) hutimilizika katika Yesu. Yesu ndiye Israeli mpya, wa kweli. Yoh 11:52 huweka bayana kwamba Yesu awakusanya watu wake (ona pia Yoh 10:16; Ufu 5:9; 7:9). Hata hivyo, kusanyiko lake halihusishi kurudishiwa mahali kijiografia kwa Israeli au Yerusalemu. Yesu alisema kwamba kuinuliwa kwake kifoni juu ya msalaba (siyo kuja kwake kwa mara ya pili) ndiko “kutawavuta watu wote kuja kwake” (Yoh 12:32). “Yesu, siyo ‘nchi iliyoahidiwa’, ndilo mkazo wa hili ‘kusanyiko’ lililotarajiwa kwa muda mrefu” (Walker 1996: 189). Kwa hiyo, Zek 14:16 hawazii kuuendea mji wa kidunia ili kumwabudu Bwana (ona Yoh 4:21-24). Ingawaje unabii wa Zekaria (kama zilivyo nabii nyingine za AK) hutumia lugha na alama za AK za Israeli ya kimwili (ambayo watu wa wakati ule waliweza kuielewa), kiuhalisia humwelekea Kristo mwenyewe, Yerusalemu ya mbinguni, mji usiojengwa kwa mikono, “ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu” (Waeb 11:8-10; 12:18-24).(3) Namna ya Mavuno. Mavuno ni watu “kutoka kila kabila na lugha na jamii na taifa” la dunia (Math 9:36; Luka 10:1; Ufu 5:9; 7:9). Yesu ameanzisha mavuno sasa. Alisema mashamba “yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno” (Yoh 4:35). Pia alisema, “mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.” (Math 9:37-38; Luka 10:2) Katika ule “utume Mkuu” (Math 28:18-20) aliwatuma wafuasi wake kwenda duniani kote na kuwafanya wanafunzi. Watu sasa wanakuja kwenye ufalme wake, au wanamkataa. Kwa hiyo, waamini ni vyote viwili; wafanyakazi katika shamba la mavuno na ni “malimbuko” ya mavuno (Yak 1:18; Ufu 14:4). Waamini sasa tunaishi katika mahema yao ya muda, tukingojea miili ya kudumu, iliyotukuzwa, ya milele (ona, 2 Wakor 5:1-4; 2 Petr 1:14). Katika mfano wake wa ngano na magugu, Yesu alisema kwamba “mavuno ni mwisho wa nyakati” (Math 13:24-30, 36-43). Yesu atakapokuja tena, zama za makao ya muda zitakoma, mavuno yatakamilika, na hukumu itafunua ni nani ni ngano na akina nani magugu.

E. Yesu alitimiza na kubadilisha Sheria ya AK na Sabato.1. Sheria ya AK ilikuwa sehemu ya Agano la Musa la (Kale). Agano la Musa na Sheria (ikiwamo Sabato) vilikusudiwa kulirekebisha taifa la Israeli katika nchi. Hivyo basi, baraka za Mungu na laana zake zilifungashiwa katika jinsi ya kimwili moja kwa moja kulingana na Israeli kutii ama kutokutii sheria hizo za Musa (ona Walawi 26; Kumb 4; 6-9; 11; 27-29). Ingawaje Sheria yenyewe ilikuwa takatifu, ya kiroho, na njema (Rum 7:12, 14, 16), haikuandaliwa au haikuweza kuingiza uzima (Wagal 3:21). Haikuweza kuwahesabia haki watu (Rum 3:21; Wagal 3:11). Haikuwa msingi wa haki (Wagal 3:21). Kama Sheria ingelikuwa ni jinsi ya kupata uzima, basi Kristo asingehitajika kuja (ona Wagal 3:11-13, 19-24; 4:4-5). Sheria ya Musa ilianzishwa kwa sababu ya dhambi za watu (Wagal 3:19). Ilifunua dhambi za watu (Rum 3:19-20; 7:7-12). Pia ilichochea na hata kuongeza dhambi (Rum 4:15; 5:13-14, 20; 7:5; 1 Wakor 15:56). Iliwafunga watu chini ya dhambi (Rum 7:6, 23; 8:2-3; Wagal 3:23; 5:1; Col 2:14). Ilileta mauti na kuwahukumu watu kwa ajili ya tabia yao ya dhambi (Rum 7:5, 9-11; 2 Wakor 3:7-9). Ilithitika kuwa “kongwa ambalo baba zetu, wala sisi wenyewe hatukuliweza” (Mdo 15:10). 2. Sheria ya AK iliundwa kuwa na utendaji wa kitambo kidogo tu uliowandaa watu wa ajili ya Kristo

74

Page 76:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

( Wagal 3:15-4:31; ona pia, Rum 7:24-25 ). a. Kulingana na Agano lililotangulia la Ibrahimu, Sheria ya AK ilikuwa ya kitambo tu hadi kuja kwa Kristo. Katika Wagal 3:1-19 Paulo ajadili mahusiano ya Agano la Ibrahimu, Agano la Musa na Sheria, na Kristo. “Katika 3.1-14 Paulo anahoji kuwa si wale walio ‘wa matendo ya Sheria’ bali wale ‘wa imani’ ndio ‘wana wa Ibrahimu’ (3.1-5, 7). Kwani ilikuwa ni kwa misingi ya imani kwamba Ibrahimu mwenyewe alihesabiwa haki (mst. 6) na kwamba Mungu alitangaza kwamba mataifa pia wanaweza kuhesabiwa haki (mist. 8-9). . . . Paulo anaendelea katika 3.15-18 kujadili uhusiano wa kitambo wa ahadi na sheria, akijadili kwamba ahadi za Mungu kwa Ibrahimu na kwa ‘mzao’ wake (Kristo) isingeliweza kujumuishwa au kuongezwa katika agano litakalofuata kwa sababu agano hilo lifuatalo halitegemei ahadi . Urithi katika ‘mzao’ basi ni kwa ahadi na siyo kwa sheria. . . . Hivyo Sheria ni ya kitambo tu, iliyoanzishwa hadi kuja kwa huyo mzao (mst. 19b).” (Belleville 1986: 56) b. Sheria ya AK ilitenda kama “kiongozi” (mwelekezi) cha “wana wa kando” hadi uana ulipokuja na Kristo. Mwelekezi (Kiyunani = paidagōgos) “alikuwa mtumwa wa ndani katika kaya, ambaye kazi zake zilikuwa kuangalia shughuli za watoto katika familia hiyo kutokea utoto wao hadi kupevuka kwao. . . Matokeo yake, maisha ya mtoto huyo chini ya paidagōgos yalikuwa yanaangaliwa sana. Yalikuwa hayana kipimo cha uhuru.” (Belleville 1986: 59, 60) Katika Wagal 3:22-4:11 Paulo anajadili kwamba Sheria ilikuwa“mwelekezi” (2:24-25), yaani “kiongozi na mwalimu” (Wagal 4:2), iliyokuwa na kifungo kwa“mrithi” (Wagal 4:1-3). “Umbo lililosukwa kikamilifu la hoja hii na mkondo mpana wa msisimko katika mistari hii huelekeza kwenye kazi moja ya Sheria. Kazi hii ni ya mwangalizi ambaye hurekebisha na kusimamia watu wa Mungu kwa kipindi cha uduni wa kiroho. Kama zilivyo kanuni za awali za ulimwengu [Wagal 4:3, 9], Sheria huagiza shughuli za kila siku za watenda kazi wake hadi uana kamili unapofikiwa. Iliwekwa kama ya kitambo kidogo, lakini iliyo njia ya lazima iliyotolewa kwa kanuni ya utendaji wa dhanbi, na hutumika kama kanuni ya kiutendaji ya dhambi na kuwa kama ‘kichocheo’ kwa watu wapendao kutenda dhambi, kuleta nuru mapenzi kamili ya Mungu kama msingi kwa ajili ya uwajibikaji wa agano. Kwa kuja kwa imani katika Kristo, kazi ya Sheria kama kiongozi na mlinzi hukoma na Roho huwa ndiyo kanuni ya ndani iongozayo.” (Belleville 1986: 70)22 Wagal 3:23 na 3:25 huonyesha utofauti wake: “Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria,” bali “Lakini iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi.” Hiyo “imani” inapatikana katika Yesu Kristo (3:24).

3. Sheria ya AK ilikuwa na kazi ya nabii iliyotimizwa na kukomea kwa Yesu. Katika Luka 16:16 (“Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa,”) Yesu alitangaza badiliko la msingi sana kuhusu Sheria ya AK (ona pia Math 11:13 panaposema kwamba Sheria ilikuwa na kazi ya nabii iliyoishia na Yohana). Yesu alikuwa anasema kwamba “Kipindi ambacho watu walihusiana na Mungu chini ya mazingira yake [m.y., AK] kimeishia kwa Yohana . . . AK zima hutazamwa kama sehemu ya kwanza ya uelewa wa historia kuhusu ‘utimizwaji wa unabii’” (Moo 1984: 23). Kwa sababu Sheria ya Musa (na AK kiujumla) vilikuwa na kazi ya unabii ulioelekeza kwa Yesu na mafundisho yake, yale yanayotabiri kwa jinsi yake kitambo na “huchukulika na kuleta maana yake katika kutimilizwa kwa unabii” (Carson 1984: 146).4. Yesu alisema, “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, Yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie” ( Math 5:17-18 ).

a. “Sheria au Manabii” huzungumzia AK lote. “Yesu anataabika kuhusisha mafundisho yake na mahali katika historia ya ukombozi na Maandiko ya AK. Kwa maana ‘Sheria au Manabii’ hapa humaanisha: Maandiko. Kiunganishi ‘au’ huweka wazi kuwa kati ya hayo lisipuuzwe lolote. Wayahudi wa siku za Yesu walikuwa wanayaona Maandiko kuwa ‘Sheria na Manabii’ (7:12; 11:13; 22:40; Luka 16:16; Yoh 1:45; Mdo 13:15; 28:23; Rum 3:21); ‘Sheria. . . , Manabii, na Zaburi (Luka 24:44); au ‘Sheria’peke yake (5:18; Yoh 10:34; 12:34; 15:25; 1 Wakor 14:21); Wakati huo haikuwepo migawanyiko ya majina ya vifungu.” (Carson 1984: 142)b. Neno “kutimiza” (n., plēroō) kikawaida humaanisha “kufikisha kwenye lengo lililokusudiwa” (Hays 2001: 29). Katika Injili ya Mathayo, ambayo ndiyo muktadha wa 5:17, kiasi kikubwa cha matumizi ya neno plēroō “kiudhahiri kabisa huzungumzia kutimizwa kwa

22 Kwa kutumia “sisi” katika 4:3, Paulo alikuwa anajijumuisha mwenyewe Wakristo Wagalatia, na pia alikuwa anaonyesha kuwa Sheria ya Musa ilikuwa mojawapo kati ya vitu viletavyo utumwa ulimwenguni. Wagalatia walivyokuwa kabla ya kuwa Wakristo, ni Wapagani, Wamataifa- walikuwa wamekuwa “utumwani katika ibada zao za sanamu sawa kama vile Wayahudi walivyokuwa katika katika kongwa kutumikia Sheria,” na wote walihitaji sana wokovu (Burke 2006: 86-87).

75

Page 77:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

unabii katika maisha na shauku ya Kristo” (Meier 1976: 80). Wakati Yesu aliposema kwamba alikuja ili “kutimiliza” Sheria, alikuwa anasema kwamba Sheria na Manabii walikuwa wanamlenga yeye. Walikuwa hawakukamilika ki-wenyewe, bali walitarajia mafundisho yake. Yeye na mfundisho yake alikamilisha na kutimiza kile walichokidokezea, walichokuwa wanakilenga, na kukianza. Kazi ya Yesu juu ya msalaba ililetesha kusudio na mtindo wa kushikamanisha wa Sheria ya AK (ya Musa) kufikia ukomo. Pia ona, Rum 10:4 (“Kristo ni mwisho [au, lengo] la sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki”).c. “Yote yalitimizwa” (Math 5:18) pale msalabani na katika ufufuo. Kifo cha Yesu na ufufuo wake ni mahali pa kubadilikia kati ya zama za kale na mpya. Katika Math 5:18 mstari “18 d[“hadi yote yatimizwe”] hutafsiri upya lugha ya kiufunuo ya 18b [“mbingu na nchi zitapita”] kwa maana ya kutimizwa unabii wote katika Kristo (ifikiayo kilele katika kifo na ufufuo wake). Kwa kifupi, 18d husema kwamba 18b hutendeka katika kufa-ufufuo wa Yesu, ambako ndiko utimizo wa unabii wa AK; kinyume na 18b isemayo kuwa 18d ni tukio la ya kiufunuo linaloashiria zama mpya. Maeneo hayo mawili yana uhusiano unaorandana.” (Meier 1976: 64-65) Kwa hiyo, maneno ya mwisho ya Yesu akiwa msalabani, kabla tu ya kukata roho, yalikuwa “Imekwisha!” (Yoh 19:30).d. Katika kufa na kufufuka kwake, Yesu aliipa maana na kuipitiliza Sheria ya AK. “Yesu alikufa kwa kusulubiwa na hivyo, kulingana na Sheria, akafanyika laana kwa Mungu [ona, Kumb 21:23, iliyonukuliwa katika Wagal 3:13]. Lakini kugeuzwa imani kwa Paulo kulimsababisha aelewe kuwa sasa Mungu alikuwa amemhesabia haki Yesu kwa kumfufua kutoka kwa wafu. Hivyo basi, Yesu (au kiusahihi zaidi, tendo la Mungu katika Kristo) likaileteshea maana ile sheria iliyokuwa inayomwona Yeye kuwa amelaanika na sasa ikawa inatenda kazi kwa njia nyingine mpya; sasa alikuwa Yesu, na siyo Sheria au agano la Musa, aliyefanyika kiini cha kazi ya Mungu ya wokovu kwa wote wawili Wayahudi na Mataifa.” (DeLacey 1982: 161)

5. Yesu alionyesha na kudhihirisha mamlaka yake juu ya Sabato na Sheria yote ya AK. a. Yesu alisema kwamba yeye ni “Bwana wa Sabato” (Math 12:6; Mark 2:28; Luka 6:5). Mafarisayo walidai kwamba Yesu alikuwa na makosa ya kuivunja Sabato kwa sababu walikata vichwa vya ngano siku ya Sabato. Yesu aliwajibu kuwa “wanafunzi hawana hatia yoyote kwa sababu [Yeye] kama Mwana wa Adamu ni Bwana wa Sabato” (Carson 1982: 67). By akisema kwamba, Yesua alikuwa akionyesha “ukuu wake juu ya Sabato na, matokeo yake, ana mamlaka ya kuibadili au kuigeuza Sheria ya Sabato” (Moo 1984: 17). Alitoa madai ya jinsi hiyo hiyo akidai kuwa sawa na Mungu katika Yoh 5:17-18 wakati alipomponya mtu siku ya Sabato na kumwambia “jitwike godoro lako na uende,” ikiwa ni kinyume na taratibu za Sabato. Hivyo basi, madai ya Yesu kuwa ni “Bwana wa sabato” hayahusiani tu na mwenendo wake mwenyewe, bali pia huathiri mwenendo wa wengine (m.y., yaliruhusu mtu kubeba godoro lake ambapo ilikuwa hairuhusiwi). Madai yake kuwa Bwana wa Sabato “siyo tu ni madai ya Ki-Masihi wa viwango vikuu, bali huinua uwezekano wa mabadiliko ya baadaye au tafsiri mpya ya Sabato, kwa usahihi jinsi ile ile kama ubora wake uliotabiriwa juu ya Hekalu [Math 12:6] huinua uwezekano fulani kuhusu desturi za sheria ” (Carson 1982: 66). Kwa vile Sheria ya Sabato ilikuwa sehemu ya zile Amri 10, “mamlaka ya Yesu kama mtimizaji wa Sheria husimama hata juu ya Amri kumi za Mungu (Moo 1984: 29). b. Yesu alifundisha kwa mamlaka yake mwenyewe, si kwa kutegemea sheria za vinywa wala za desturi, wala hata Sheria iliyoandikwa ya AK (Math 7:28-29; 13:54; Marko 1:21-22; Luka 4:31-32; Yoh 7:46). Kauli zake, “Mmesikia imenenwa . . . Bali nawaambia” (Math 5:21-22, 27-28, 31-32, 33-34, 38-39, 43-44), siyo tu zilikuwa zinachambua Sheria za AK, au kuonyesha “maana zake za kweli,” au hata kutegemea kuzikuza. Badala yake, “ile ‘Mimi nawaambia’ husisitiza mkazo mpya na wa kushangaza kuhusu mamlaka ya huyu Yesu wa Nazareti, mamlaka ambayo huenda mbali zaidi ya mpangilio mpya wa maneno ya Sheria ya AK” (Moo 1988: 205). Bila shaka, “Mamlaka ya Yesu mwenyewe huenda mbali zaidi kidhahiri kupita chimbuko lolote la wastani la mistari anayoinukuu; wala ukuu wake aunenao haupati kitako tegemezi sehemu yoyote katika Agano la Kale” (Ibid.). Alithibitisha mamlaka yake kwa miujiza na ishara alizozifanya (Math 9:2-8; Marko 2:1-12; Luka 5:18-26).c. Yesu kwa wazi kabisa alivunja na kuihukumu “Sheria ya kinywa.” Wayahudi waliamini kuwa “sheria ya kinywa” (Halakah) ilikuwa imetolewa juu ya mlima Sinai pamoja na Sheria iliyoandikwa (Torah). Sheria ya kinywa ilikubalika kama yenye mamlaka, hata kama mamlaka yake haikuendana na ile iliyoandikwa (Carson 1982: 76; Moo 1984: 18). Maisha ya Yesu yalionyesha utofauti wa wazi kati ya sheria iliyoandikwa na sheria ya kinywa. “Hakuna mfano

76

Page 78:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

wowote usio na ubishi wa mafundisho ya sheria iliyoandikwa – Torati mbayo Yeye mwenyewe aliipinga au kwenda kinyume nayo” (Carson 1982: 79). Kwa upande mwingine, “kiujumla, anaikataa Sheria ya Kinywa kwa nmna ya dhahiri, pasipo kubembeleza na pasipo kupiga chenga, hasa inapopingana na matumizi Yake ya Agano la Kale, au na Mafundisho ya Ufalme” (Ibid.: 76). Mifano ya mashambulizi ya Yesu, au kuivunja, Sheria ya kinywa ni kama vile: “Korban” (fedha zilizotolewa Hekaluni) (Math 15:5-12; Marko 7:9-13); uponyaji usio wa dharura siku ya Sabato (Math 12:9-14; Luka 13:10-17; Yoh 5:1-17); kula na mikono isiyosafishwa (Math 15:1-3; Marko 7:1-9).

6. Yesu aliishi chini ya Agano la Kale, bali alikuwa mjumbe wa Agano Jipya.a. Yesu alizaliwa chini ya Sheria na aliitunza vizuri sana. Yesu alikuwa “amezaliwa chini ya Sheria” (Wagal 4:4). Alitimiza maagizo yote ya Agano la Kale na Sheria (ona Isa 53:9; Luka 23:40-41; Yoh 8:46; Waeb 4:15). Yesu hakushitakiwa kwa kuivunja Sheria wakati wa kukamatwa kwake (ona Math 26:57-68; Marko 14:53-65; Luka 22:66-71; Yoh18:19-24).b. Ingawaje Yesu mwenyewe aliishi chini ya Agano la Kale, mafundisho yake yaligonga moyo wa Sheria ya Musa na kuingiza Agano Jipya.

(1) Kuishi kwa Yesu na mafundisho yake kulitokea katika muktadha wa Israeli ya AK, lakini kulitarajia zama za Agano Jipya. “Wakati wa huduma yake ya hadharani, Yesu alijizuia mwenyewe kwa kanuni kwenye nchi na watu wa Israeli, ingawaje kulikuwa na matamshi machache ya kinabii yaliyodhihirisha nini kitatokea baada ya kufa na kufufuka kwake. Katika hili, wakati wa huduma yake ya hadharani, Yesu alitangaza utiifu wake mkali kwa Sheria ya Musa. . . . baada ya kufa na kufufuka kwake, Bwana anaondosha mipaka hiyo ya ki-nchi na watu walioshikamana na huduma yake ya hadharani. Pamoja na hayo, agizo lake kufanya wanafunzi wa mataifa yote na kuwabatiza bila shaka huendana na agizo la kutahiriwa na kuhimiza utiifu kwa Sheria ya Musa iliyotokeza huduma yake ya hadharani. Katika haya yote kuna fikira ya kihalisia, ya ndani. Huduma iliyoishia kwa nchi na watu wa Israeli isingeweza kutendeka kwa jinsi nyingine isipokuwa kwa kutii Sheria ya Musa, kama vile utume usio na mipaka kwa Mataifa usingeweza kueleweka—achia mbali kufanikiwa—pasipo kuzingatia maelekezo kama vile kutahiriwa.” (Meier 1976: 29-30)(2) Yesu alifundisha kanuni ambazo ziligonga moyo wa Sheria ya Musa. Katika Marko 7:14-23 Yesu aliingiza kanuni (“hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, [bali] vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu”) Hiyo ilikuwa “imekusudiwa kubadilisha kiasi kikubwa cha sheria za mababa” (Moo 1984: 28). Baada ya ufufuo, wanafunzi walielewa umuhimu wote wa kile alichokisema Yesu. Marko 7:19 panasema kuwa, kutokana na kanuni ile, Yesu “alivitakasa vyakula vyote” (ona pia Mdo 10:9-16; Rum 14:1-17; 1 Wakor 8:1-9:4; 10:23-30). Kwa hiyo alipindua kiwili-wili kizima cha sheria za vyakula za AK. Zaidi ya hapo, ikiwa kanisa, kulingana na agizo la Yesu katika Math 28:19, “litatumia ubatizo badala ya kutahiriwa kama hati ya kianzishio muhimu kwa ajili ya hao wanaoingizwa, basi kiukweli hatutaweza kuzungumzia . . . Kristo au . . . kanisa kama watiifu kiusahihi wa Sheria ya Musa . . . katika kipindi baada ya ufufuo. Kwa Uyahudi wa Ki-Rabi, kutii kwa uaminifu Sheria ya Musa kulikoweka kando kikanuni kutahiriwa kulikuwa kunaenda kinyume na utaratibu.” (Meier 1976: 29) (3) Mafundisho halisi ya Yesu kuhusu Sheria yalibadilisha au yaliondosha nguvu za Sheria ya Musa. “Yesu waziwazi na kwa mamlaka alirekebisha [akikataza kuachana, Math 5:31-32], aliongeza nguvu [mpende adui yako kama umpendavyo jirani yako, Math 5:43-44], pangua [viapo, Math 5:33-37; ulipaji kisasi (“jicho kwa jicho”), Math 38-42], au kuwekwa uzito zaidi zaidi [uuaji ni pamoja na chuki, Math 5:21-22; uzinzi ni pamoja na tamaa, Math 5:27-28], sehemu mbali mbali za Agano la Kale. . . . mafundisho ya Yesu yemye mamlaka hutarajia mabadiliko, ambayo kiukweli hayaji hadi ufunuo.” (Carson 1982: 79)

7. Wakristo hawafungwi na Sheria za Musa, Sabato, au Sheria zozote za AK, bali wako chini ya “Sheria ya Kristo.”

a. Ama Yesu alisimamisha Sheria yote ya AK, au Sheria yote ya AK bado inatenda kazi hata sasa. Wakristo hawawezi “kuchukua na kuokoteza” sheria zipi za AK bado zinatenda kazi moja kwa moja leo na zipi hazitendi kazi. Yesu alisema “Yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie” (Math 5:18). Aliposema hayo, “Yesu hakuwa anatamka

77

Page 79:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

kwamba Sheria milele itawabana waamini wa Agano Jipya. Kama hilo lingelikuwa ndivyo, Wakristo leo wangelitakiwa kuzitunza sheria za utoaji sadaka na zile sheria za sherehe pamoja na maadili yake, na hilo lingelipingana kabisa na sehemu nyinginezo za Agano Jipya” (Hays 2001: 29). Kwa hiyo, kuhusiana na kutahiriwa, Paulo alisema kwamba kwa mtu kurudi tena nyuma na kujiweka chini ya mamlaka ya kipande kimoja cha sheria yaAK kunamaanisha kuwa huyo mtu basi anatakiwa kuitii Sheria yote ya Agano la Kale: “Katika uungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa. Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno. Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote. Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.” (Wagal 5:1-4)b. Matokeo ya zama za ukombozi (m.y., kutoka Agano la Kale hadi kuja kwa Kristo) ni kuwa hakuna amri ya Musa inayotenda kazi moja kwa moja kwa waamini. Kwa vile Yesu alisema “Yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.” (Math 5:18), sheria moja ilipobadilishwa, sheria nzima ya AK ilifanyika vivyo. Kwa hiyo, pale Kristo aliposema “alivitakasa vyakula vyote” (Marko7:19), na Mungu alimwambia Petro “Vilivyotakazwa na Mungu, usiviite wewe najisi.” (Mdo 10:14), hilo lilimaanisha yote yalikuwa yamekamilishwa: Sheria yote ya AK ilikuwa imetimizwa na haiendelei tena moja-kwa moja kutenda kazi kwa Wakristo. Vivyo hivyo, ulazima wa AK wa kutahiriwa—ulioenda hadi kwenye moyo wa Agano la Kale—umeondolewa (1 Wakor 7: 18-19; Wagal 5:1-2, 11-12; 6:13-15; Wafil 3:2-3). Agano la Kale lote ni “nje ya wakati” (ona Waeb 8:13). Waef 2:14-15 panasema, “ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo.” Kilichotofautisha kati ya Wayahudi na Mataifa kikawa“kimevunjika” na “kuondolewa” katika Kristo. Wakol 2:13-14 panasema,“akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu” ika“futwa,” “ikaondolewa kando ya njia” na “akaigongomelea msalabani.” Waeb 7:11-12 panasema kwamba kuja kwa Kristo kulileta ukuhani mpya, na “Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike.” Wagal 3:13 panasema, “Kristo alitukomboa katika laana ya torati.” Waeb 10:9 paongeza, “Aondoa la kwanza [Agano la zamani la Musa], ili kusudi alisimamishe la pili [Agano Jipya].” Rum 6:14 panasema, “dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.” Hoja ya Paulo ni kuwa, “Mkristo anaishi katika uhuru mpya kutoka katika nguvu za dhambi, kwa sababu haendelei tena kuishi chini ya utawala ambao Sheria ya Musa iliiongeza nguvu ya dhambi. . . . Kutokuwa chini ya sheria, kisha, pamoja na kutokuwa moja kwa moja chini ya maagizo ya Sheria ya Musa.” (Moo 1988: 212) Katika Rum 7:1-6 Paulo anajadili kwamba “torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai” (7:1). Hata hivyo, kuhusu sisi,“ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo” (7:4). Kwa hiyo, “Bali sasa tumefuguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko.” (7:6). Hoja ya Wagal 4:21-31 ni kuwa, “agano la Musa kama agano ni tengefu kwa ajili ya Wayahudi tu (“Yerusalemu ya sasa,” 4:25); Utendaji mpya wa Mungu, wenye Wayahudi na Mataifa kuwa sawa, umeliweka hilo kando” (DeLacey 1982: 163). c. Yesu ndiye mtafsiri wa kweli wa AK, na ni chanzo kikamilifu cha mafundisho yenye mamlaka. Wakati Yesu aliposema kuwa hakuja “kuitangua, bali kuitimiliza” hiyo “Sheria au Manabii” (m.y., AK) (Math 5:17) alikuwa anasema kwamba “mamlaka halisi ya AK iliyomo lazima ieleweke kupitia nafsi na mafundisho yake yeye ambaye inamwelekezea na ambaye aliitimiliza kwa utoshelevu mkubwa sana” (Carson 1984: 144). Kwa hiyo, “Yesu alivyo kwa Musa, ni kama kipepeo alivyo kwa kiwavi. . . . Katika Kristo, Musa hufikia kupevuka na kutokeza katika ukomavu kamili. Sheria ya Musa inayo maana, bali ni pale tu inapotujia kwa mikono ya Bwana Yesu. Wakristo leo wanatakiwa kuendelea kusoma – sheria ya Musa, na kwa manufaa makuu, ila wanaposoma hiyo wanapaswa kuwa wamevaa miwani yao ya Ukristo” (Wells and Zaspel 2002: 157). Kwa maneno mengine, Sheria ya AK, na Manabii “zimeboreshwa kwa mbali na mtimilizaji wa mbeleni wa hiyo Sheria na Manabii, Yesu aliye Masihi. Yesu, katika maneno yake na matendo yake, ndiye kawaida ya maadili kwa Wakristo. . . . Mwana wa Mungu peke yake aweza kuwafundisha wana kunamaanisha nini kuyafanya mapenzi ya Baba wa mbinguni (km. [Math] 5:43-48 and 11:25-30). Kwa Mkristo, nafsi ya Yesu, ambaye ndiye Mungu pamoja nasi, kimsingi huchukua nafasi ya Torati kama kiini cha maisha ya Ukristo (km. [Math] 18:20, ni pamoja na 1:23 na 28:20).” (Meier 1976: 88)d. Badala ya kutawaliwa na AK, Wakristo sasa wanatawaliwa na Agano Jipya—hiyo “sheria ya

78

Page 80:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Kristo” (Luka 22:20; 1 Wakor 11:25; 2 Wakor 3:6; Waeb 8:8-13; 9:15). Hiyo “sheria ya Kristo” siyo tu mafundisho ya Yesu, bali pia ya waandishi wa AJ (ona, k.m., Yoh 14:24-26; 16:12-15; 17:8, 18-20; 1 Wakor 14:37; Wagal 1:11-12; Waef 2:20; 1 Wathes 2:13; 2 Wathes 2:15; 3:6, 14; Waeb 2:3; Ufu 1:11). Sheria ya Kristo inachanganya “yote mawili kanuni za kiujumla na maagizo maalum —zaidi kabisa ya maagizo ya upendo” (Moo 1984: 30). Yesu pekee huleta “uzima” (Yoh 3:36; 4:14; 5:24; 6:40, 68: 10:10; 11:25; 14:6; 20:31). Alisema kuwa ikiwa “tutakaa” au “kudumu katika” neno lake, ndipo “mtaijua kweli,nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yoh 8:31-32). Neno lake hutubadilisha kutoka “ndani kuja nje” kufikia hali ya kumfanania Kristo mwenyewe (ona Rum 8:29; 12:2). Sheria ya AK kamwe haikuweza kufanya kile Yesu na sheria ya Kristo huweza kufanya (ona pia Mdo 15:10-11).

8. Wakristo wa mwanzo walitambua umuhimu wa ukomo wa Agano la Kale kwa kubadilisha uelewa wao wa Sabato, na kutoendelea “kuishikilia au kuheshimu siku ya saba” kama siku ya pumziko na kuabudia.

a. AJ hubadili umuhimu wa Sabato. “Ile amri ya Nne ya [Kut 20:8-11; Kumb 5:12-15] hueleza wazi wazi ile siku ya saba, siyo tu ni kanuni ‘moja kati ya saba’” (Moo 1984: 48n.204). Sabato ilikuwa inahusiana kipekee na Israeli (ona Kut 16:22-30; 31:12-17; Neh 9:13-14). Ilikuwa ni alama ya AK (Kut 31:16-17). Amri ya nne (kuhusiana na Sabato) ilikuwa na pande mbili: Mungu kuingia katika raha kupumzika baada ya kazi ya uumbaji (Kut 20:11); na kutolewa kutoka Misri (Kumb 5:15). Waeb 3:7-4:11 hubadilisha maana ya Sabato, na huoanisha na pumziko letu la wokovu. Waeb 4:4, 8 huoanisha yote mawili pande mbili za Sabato na “raha ya Sabato” ya Agano Jipya. Ingawaje kukamilika kwa pumziko au raha yetu bado kunabakia kwa siku zijazo (Waeb 4:11), Waeb 4:3, 10 panaeleza kwamba wale walio katika Kristo“huingia katika raha” au “wameingia katika raha Yake.” Kwa maneno mengine: “Raya ya Mungu huingiwa kwa kuamnini (4:3). Kwa hiyo watu wa Mungu wa Agano Jipya huondokana na utekelezaji wa kuisimamia Sabato, kulingana na mwandishi, kwa kusimamia imani. . . . Kwa hiyo Sabato ya kweli, iliyokuja na Kristo, siyo raha ya kuonekana kwa macho, ya kimwili, bali huonekana ikiwa imejumuishwa katika wokovu ambao Mungu ameutoa. . . . . Kwa ufupi, pumziko la kimwili la Sabato ya Agano la Kale limefanyika wokovu wa Sabato ya kweli. Waamini katika Kristo wanaweza sasa kuishi katika Sabato ya Mungu ambayo imekwisha kupambazuka. Kazi ya Yesu ya kuikamilisha hiyo imekuwa kuu zaidi kuliko Sabato ya Agano la Kale (Yoh 5:17) na ndivyo pia katika kuifanya kazi ya Mungu anayotaka watu waifanye—Kumwamini yule ambaye ametumwa na Mungu (Yoh 6:28, 29). Kusema ukweli, kuitunza Sabato kunakotakiwa sasa ni kukoma kutegemea nguvu za matendo yako mwenyewe (Waeb. 4:9, 10). . . . Kristo huleta uhalisia wa kiroho; kazi yake hutimiliza kusudio ya Sabato, na pamoja na Kristo huja lile ambalo lilisababisha kuwepo kwa Sabato. Uhalisi wa pumziko la wokovu hupita ubora wa alama au ishara. Vifungu vya Injili huonyesha kwamba Sabato ya Agano la Kale na pumziko liendanalo nayo huweza kuelezea uhalisia ambao umekuja na Kristo, wakati Waebrania huonyesha kwa nyongeza kuwa huweza kutumiwa kuelezea uhalisia wa kimbingu ambao utakuja na Kristo.” (Lincoln 1982: 213, 215) Wakati Agano la Kale lilipokuwa limewekwa kando sababu ya Agano Jipya, ndivyo ilivyokuwa kwa alama ya Agano la Kale. Kwa hiyo, chini ya Agano Jipya, Sabato na sherehe za Kiyahudi hazifanyi kazi tena (Rum 14:5; Wagal 4:8-11; Wakol 2:15-17).b. Kutimizwa kwa Sabato katika Kristo kunamaanisha kwamba Jumapili siyo tu ni“Sabato ya Ki-Kristo” siku ya pumziko iliyo sawa na Jumamosi ile ya Sabato ya Kiyahudi. Katika Baraza la Yerusalemu (Mdo15) hoja kuu ilikuwa kama “ni lazima kutahiri [waamini wa Mataifa walio wapya] na kuwawajibisha kuishika Sheria ya Musa” (Mdo 15:5). Jibu lilikuwa la kuwasha masikio “Hapana!” Kuishika Sabato (au hata “siku ya Sabato” mbadala kwa Mataifa ) hakukutakiwa kwa mwamini Mmataifa kwa tamko la kimitume la Mdo15. Baada ya muda, Wakristo wakaanza kukutanika kwa ajili ya kuabudu siku ya Jumapili. Wakristo “hawakuamriwa” kuabudu Jumapili. Wako huru kuabudu siku yoyote ya juma. Hata hivyo, Ibada ya Kikristo Jumapili (‘Siku ya Bwana”) ina sababu za msingi za kuabudu za Kikristo tofauti na kule kuabudu katika Sabato ya Kiyahudi: “kwa vile Ufufuo wa Kristo unatimiliza pumziko au raha iliyomaanishwa na Sabato ya Agano la Kale, kiunganishi chaweza kuonekana kati ya siku ya saba na siku ya kwanza ambayo Wakristo hukumbuka Ufufuo. Kiunganishi hicho hakisemi lolote kuhusu ‘Siku ya Wakristo ya pumziko au raha’ . . . [Hicho] kiunganishi kati ya hii siku ya kwanza ya Sabato ya Agano la Kale hakikuonekana kwa maana ya siku ya pumziko la kimwili bali ni kwa maana ya kusherehekea pumziko la kweli la Sabato ya kweli ya

79

Page 81:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

wokovu ulioletwa na Kristo ambaye waamini walimwabudu na ambaye kwaye walikuwa na ushirika. Ushahidi kutoka mtazamo wa waandishi wa Agano Jipya kuhusu raha ya Sabato waonyesha kutoelekeza uhakiki wa kuwa na pumziko la kimwili la Agano la Kale kwa Siku ya Bwana ya Agano Jipya..” (Lincoln 1982: 205, 215-16)

IV. Kwa vile Kanisa Liko “Katika Kristo,” Kanisa ndilo Israeli Mpya, wa Kweli na wa Kiroho.

A. Neema ya kimwili na ya kiroho, uteuzi, na imani katika AK. 1. Muktadha wa “neema,” “uteuzi,” na “imani” uko kazini katika AK, kama ulivyo katika AJ. “Dhana muhimu za Ki-Biblia zimeviringana katika historia ya Ibrahimu na agano. Ya kwanza ni neema. Kama ilivyokuwa kwa Nuhu, hakuna chochote maalum kuhusu Ibrahimu ambacho kinastahili wema wa Mungu katika kumwitia kwenye baraka hizi. . . . Dhana ya pili, ambayo huenda pamoja na neema, ni uteuzi. Popote pale Mungu atendapo wema kwa ajili ya watu wake, hutenda kinyume na kile wakitumikiacho kama wadhambi walio waasi, na kutenda huko ndiko neema. Uteuzi unamaanisha kuwa Mungu huwachagua baadhi na siyo wengine kulingana na neema yake. . . . Dhana ya tatu ni imani kama njia ya urejezwaji kwa Mungu. Imani ya Ibrahimu bila shaka si kamilifu, isiyokuwa imara daima, na wakati mwingine huelekea katika kutokuamini (Mwa 15:2-3). Hata hivyo nyakati ambazo ni za muhimu sana humwamini Mungu katika Neno lake na kuziamini ahadi zake. La msingi si nguvu au uimara au ukamilifu wa imani ya Ibrahimu, bali nguvu na ukamilifu wa Mungu amtumainiye. . . . Na kwa vile Ibrahimu hana ustahili wowote wa jinsi alivyoahidiwa, lazima ionekane kama ni kipawa au zawadi kamili na isiyostahili. Hiyo ndiyo maana anahesabiwa mwenye haki mbele za Mungu kwa kule kuamini tu (Mwa 15:6).” (Goldsworthy 1991: 122-23)2. AK lafunua kuwa Mungu“huteua” au “huchagua” kwa njia mbili tofauti: kimwili na kiroho. Kumb 7:6 husema kuwa, “Mungu wako, amekuchagua [Israeli] kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.” Hata hivyo, kuchaguliwa kwa maana ya kuwekwa kando kama taifa teule (m.y., “kuchaguliwa kimwili”) si sawa na kuokolewa milele (m.y., “kuteuliwa kiroho”). Ni waamini tu ndio Mungu amewabariki“kwa baraka zote za rohoni, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo” (Waef 1:3-4; ona pia, Rum 8:29-30; 9:8-24; 2 Wathes 2:13; 2 Tim 1:9). Kwa kifupi: “Israeli ni taifa teule, bali ufunuo unaokuja mbeleni waonyesha kwamba uteuzi huu wa mwilini huendana bega kwa bega na uteuzi wa kiroho kwa uzima wa milele. Si Waisraeli wote ni Waisraeli, mtume Paulo baadaye alihitimisha (Rum 9:6). Kujihusisha kwa Mungu nalo kama taifa itabidi utenganishwe na kujishughulisha kwake na watu binafsi kwa ajili ya wokovu wa milele. Nyanja hizi mbili za uteuzi zitatenganishwa pia kutoka uchaguzi wa watu fulani ambao Mungu anaweka umakini wake zaidi kwa ajili ya kusudio lake maalum.” (Goldsworthy 1991: 126) Hata katika AK njia ya Mungu ya wokovu wa milele wa kiroho ilikuwa tu kwa njia ya neema kupitia imani, siyo tu swala la kutii ki-nje Sheria ya Musa (Mwa 15:6; Kumb 10:16; 30:6; Hos 6:6; Hab 2:4; Rum 1:16-17; 4:13-24; 9:27-33; 11:17-23; Waeb 11:1-12:2).

B. Aina mbili za uteuzi —wa kimwili na wa kiroho—huonyesha jinsi Maagano ya Ibrahimu, Musa na Agano Jipya yanavyooana.

“Agano la Ibrahimu lina yote mawili, Agano la Kale [m.y., la Musa] na Agano Jipya. Maana yake, Agano la Kale na Jipya ni utimilizwaji wa kimwili na wa kiroho wa agano la Ibrahimu. Agano alilolifanya Mungu na Ibrahimu hufunua mpango wa Mungu kuwaokoa watu na kuwaleta katika nchi yake. Chini ya Agano la Kale, Mungu kimwili awaokoa watu wa Israeli (uzao wa kimwili wa Ibrahimu) kutoka kwa Wamisri na kuwaleta kwenye Nchi ya Ahadi, Palestina. Katika Agano Jipya, Mungu huwaokoa watu wake kiroho (uzao wa kiroho wa Ibrahimu) kutoka dhambi na maangamizo na kuwaleta kwenye nchi ya kiroho (raha ya wokovu sasa na kule mbinguni). . . . Kulingana na hili, katika zama za Agano la Kale twaona kweli za kiroho zikihusishwa katika hali ya taswira ya picha. Wakati Mungu alipofunua haja ya mwanadamu ya utakaso, alitumia mifano na vivuli vya mifumo na vivuli vingi vya utoaji sadaka vikihusisha makuhani maelfu na wanyama mbali mbali wa kufugwa. Mungu alipofunua uhitaji wa watu wake kukaa naye, alifanya hivyo kwa mifano na vivuli vya nchi katika Mashariki ya Kati na katika jengo lililofanywa la mawe na udongo. Hii ndiyo namna Mungu alivyofunua mpango wake katika zama za Agano la Kale. Hivyo, Mungu alipowatumia manabii kuelezea kutimilizwa kiroho kwa mpango wa Mungu katika zama za Agano Jipya, Mungu aliamua kutumia lugha ya mifano na vivuli. Alikuwa analielezea Aagano Jipya katika lugha ya Agano la Kale. Alielekeza kwenye lengo la kiroho la mpango wa Mungu katika namna angavu na iliyo wazi kuliko zote ambazo mifano na vivuli vya kimwili vingeliwezesha.” (Lehrer 2006: 29, 85)

80

Page 82:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

C. Aina mbili za uteuzi—ya kimwili na ya kiroho—huonyesha kwamba Israeli ya AK ilikuwa taifa la kimwili ambalo “ni mabaki tu” yaliyookolewa kiroho.

1. Ingawaje Mungu aliwachagua Israeli ( Kumb7:6-8 ), akawakomboa Israeli kutoka utumwani ( Kut 13- 15 ), akawapa Israeli nchi yao wenyewe ( Yosh 1-21 ), na kuingia katika maagano na Israeli ( Mwa 12:1- 3; 13:14-17; 15:1-21; 17:1-21; 22:15-18 ; Kut 19-24; 2 Sam 7:8-17; 1 Nyak 17:3-15 ), kipindi chote katika historia yake ya taifa kiujumla walikuwa kwa kiwango kikubwa ni watu wasioamini (ona, Neh 9:1-37; Mdo 7:1-53 ). Kote kuwili, katika AK na AJ huandikwa kuwa historia ya Israeli iliandamana na kutokuamini na kukosa uaminifu kwa Mungu.

a. Wakati Musa alipokuwa juu ya mlima Sinai akipokea amri zile 10. Taifa likaanza kuabudu ndama wa dhahabu. Hivyo Mungu akataka kuwaangamiza wote (Kut 32). b. Walipokaribia kabisa Nchi ya Ahadi. 10 kati ya wapelelezi 12 walirudisha habari kuwa hawapaswi kuiingia nchi ile, na jamii kubwa ya watu wakamwasi Bwana. Hivyo Mungu akawasababisha watange-tange nyikani kwa miaka 40, ambapo ni Yoshua na Kalebu ndio walioruhusiwa katika kizazi kizima kuingia nchi hiyo (Hes 13-14).c. Baada ya kuingia katika nchi hiyo, wakati wa uongozi wa Waamuzi. Watu mara kwa mara waliabudu miungu mingine na “kufanya uovu mbele za macho ya Bwana” (Waam 2:11-13; 3:5-7, 12; 4:1; 6:1; 10:6; 13:1; 17:6; 21:25).d. Israeli wataka mfalme wao wenyewe. Madai hayo yalikuwa ni kumkataa Mungu, ili kwamba wapate kuwa kama mataifa mengine (1 Sam 8:1-9).e. Kabla ya uhamisho kwenda Babeli. Mungu alinena kupitia manabii, na kuifupisha historia ya Israeli kwa kusema,“Nami nitawatupa mabaki ya urithi wangu, na kuwatia mikononi mwa adui zao, nao watakuwa nyara na mateka kwa adui zao wote; kwa sababu wamenitenda yaliyo mabaya machoni pangu, na kunikasirisha tangu siku ile walipotoka baba zao katika nchi ya Misri, hata leo hivi” (2 Waf 21:14-15).f. Baada ya taifa kurudi kutoka uhamishoni huko Babeli. Dhambi za Israeli ziliendelea, zikiwamo kuoana na wapagani (Neh 13:23-26; Mal 2:11-15); kushindwa kutoa zaka au kuacha kuitii Sheria (Neh 13:10-14; Mal 2:10; 3:8-10; 4:4); kutojali Sabato (Neh 13:15-22; Mal 2:8-9); makuhani wasiofaa (Neh 13:7-9; Mal 1:7-14; 2:1-9); na uovu wote kiujumla (Neh 5:1-13; Mal 3:5). g. Mkondo wa Israeli wa kutokuamini, kutokutii, na kumkataa Mungu uliendelea hata baada ya wakati wa Yesu. Yesu “alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea“(Yoh 1:11). Mfano wa Yesu kuhusu mtu mwenye ardhi na shamba la mzabibu (Math 21:22-46; Mark 12:1-12; Luka 20:9-19) ulifupisha historia ya Israeli kuwakataa manabii wa Mungu na kumkataa Mwana wa Mungu. Waeb 3:7-4:9 huhitimisha kuwa Israeli hawakuweza kuingia kamwe katika “raha” ya Mungu kwa sababu ya kutokuamini. Stefano alihitimisha historia ya Israeli kama mateso ya manabii, usaliti uuaji wa Kristo, na kutokuitii sheria (Mdo 7:51-53). Katika Mdo 28:23-27 Paulo anukuu Isa 6:9-10 kuhusiana na upofu wa Israeli na hali ya uziwi kuhusiana na Israeli kumkataa Yesu.

2. Katika Rum 9:6-7 Paulo anaeleza, “maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli; wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu.” “Kuliko kutofautisha kati ya Israeli na kanisa, Biblia huweka utofauti muhimu ndani ya Israeli wenyewe—mgawanyiko kati ya mabaki, walio waaminifu kwa Mungu, na wale wasiozingatia, ambao, kulingana na Yesu, wanaitwa wana wa Shetani (Yoh 8:44)” (Grenz 1992: 125). Rum 9-11 hujishughulisha na swala kama Mungu ameivunja sheria yake na Maagano kwa Israeli: “Mungu hajawahi, na kamwe hatafanya hivyo, akashindwa kushika agano lolote Alilolifanya. ‘Hata hivyo,’ Paulo atamka, ‘Mungu hajawahi kuahidi baraka zozote za kiroho kwa yeyote kwa misingi ya kuzaliwa kimwili.’ Huu ndio moyo wa jambo lote! Maneno ya Paulo hutenda kazi kwa kila mtoto wa Kiyahudi aliyezaliwa katika taifa la Israeli, na maneno yake pia hutenda kazi kwa mtoto aliyezaliwa kutoka kwa wazazi wa Ki-Kristo leo. Ikiwa kanuni hii itaeleweka na kutumiwa mara kwa mara hakutakuwa kamwe na kuzungumzia ‘taifa la agano’ (Israeli ya kimwili) au ‘watoto wa agano’ (watoto wa kimwili wa Waamini). Kila ahadi moja- moja ya Mungu ambayo huleta baraka za kiroho kwa mtu yeyote huhitaji kila mtu binafsi kuamini ahadi husika. Israeli hawakuweza kurithi baraka za ahadi zilizoahidiwa kwa sababu ‘hawakuzitafuta kwa imani’ (Warumi 9:32). . . . Kiuhalisia kabisa, Paulo anasema kuwa ‘siyo Waisraeli wote walio Waisraeli akimaanisha kiuhalisia utofauti kati ya watu wenye fursa maalum na watu ambao kiukweli wanayo neema [iokoayo]. Kila Mwisraeli alifurahia fursa kubwa kwa sababu ya kuzaliwa kwake kimwili (Rum 3:1-3), bali hakuna Mwisraeli (au yeyote mwingine) aliyekuwa na hali yoyote maalum kiroho au kupokea baraka zozote za

81

Page 83:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

kiroho nje ya toba yake binafsi na imani. . . . Hoja yake halisi katika mfano huo ni ‘Israeli kuwa ndani ya Israeli’ ni swala la kuchaguliwa kiungu (Rum 9:11) na wito rasmi (Rum 9:24), na hakuna uhusiano uwao wote na mkondo wa ukoo wa kuzaliwa. . . . Ni muhimu kuelewa kwamba [katika Rum 9:6-13] Paulo haelezi na kuthibitisha mafundisho ya namna za uteuzi kwa kulinganisha ‘mtoto wa agano’ (uzao wa Ibrahimu) na mtoto ‘asiye wa agano’ (Mmataifa), bali analinganisha watoto wawili wa ‘agano’. Na si watoto wa agano wa kawaida; ni wajukuu mapacha wa Ibrahimu mwenyewe na pia ni wana wa kweli wa Isaka aaminiye. . . . Paulo anawatumia watoto mapacha katika mfano wake kudhihirisha pasipo maswali yoyote kuwa kurithi ahadi za kweli zozote za Mungu hakuhusiani lolote na kuitwa ‘mtoto wa agano,’ wala kuwa ‘ni walioitwa na kuwekewa muhuri’ na alama za agano—hata lile agano la kutahiri lililoletwa na Mungu mwenyewe lililowekwa kwa Ibrahimu, mwanaye Isaka, na wajukuu mapacha wake. . . . Katika mfano huo, Paulo anatuambia kiukamilifu kile anachomaanisha kwa ‘si Waisraeli wote ni Waisraeli.’ Hakuna chochote ambacho Mungu alikiahidi au alichofanyia agano kwa taifa la Israeli kilikuwa na arabuni, kwa kila hali iwayo yote, kwamba wao, au watoto wao, watapokea baraka za kiroho. Walikuwa na fursa, bali hawakuwa na uhakiki wa hizo baraka.” (Reisinger 1998: 47-48)

D. Uhusiano kati ya Israeli ya AK na kanisa.Kanisa ni yote mawili, ni jipya na, kwa jinsi nyingine, si jipya. “Agano Jipya kusema ukweli halisemi

sana kuhusu watakatifu wa Agano la Kale kuingizwa katika kanisa, bali kwa waamini Mataifa wa zama za Agano Jipya kuingizwa kwa Israeli” (Bell 1967: 102).

1. Kanisa si jipya kwa maana kuwa kanisa ni “mabaki ya Israeli” ( Rum 9:27; 11:1-7 ), na huwakilisha mpanuko mkubwa sana ulimwenguni kote wa “mabaki ya Israeli” (ona Math 13:31-32, 47-48; 16:18; Waeb 11:40; ufu 5:9; 7:9 ). Kanisa ni “matunda ya Israeli,” m.y., “mwendelezo na mpanuko wa Israeli kama watu wa Mungu, walioundwa na wote wawili-wateule wa Kiyahudi na Mataifa ambao, kwa pamoja, huunda ‘Israeli wa Mungu’ (Wagal. 6:16)” (Williamson 2007: 191). Kama ambavyo Rum 9:6-7 huonyesha kwamba kuna tofauti muhimu kati ya Israeli ya kimwili na kanisa, pia huonyesha kwamba kuna uwiano muhimu na mwendelezo kati ya Israeli “ya kiroho” (“Waisraeli kati ya Waisraeli”) na kanisa. Uwiano na mwendelezo huo huonekana katika muktadha wa mabaki “maaminifu” ambayo Paulo anawawakilishia katika mfano wake wa “mzeituni” katika Rum 11:17-24: “Mzeituni unawakilisha mabaki ya Israeli. Wazo hili linaungwa mkono kwa nguvu kwa muktadha wa kifungu. Nyuma ya hapo, Paulo aliitaja Israeli ya kweli (9:6 mabaki ya Israeli (9:27, 11:5), uteule wa Israeli (11:7). . . . Ikiwa Paulo angeliubana mfano wa mzeituni wake kuweka watu wa Kiyahudi tu, mabaki ya Israeli wangeweza kuwa kitu tofauti na Kanisa, kisichoungika, au kitu kilichowekwa ndani ya Kanisa. Kwa vile Waamini wa Mataifa wamepandikizwa katika mzeituni, hata hivyo [Rum 11:17], ni wazi kuwa mabaki ya Israeli hawaishii kwa Wayahudi wa kimwili tu, bali sana sana, huhusisha watu wale wale waliokombolewa walio washirika wa Kanisa.” (Gay 2002: n.p.) “Ukweli kwamba Kanisa ni mabaki ya Israeli huthibitishwa kwa jina la nyumba ya milele ya waamini (Yerusalemu mpya), kwa milango ya nyumba ile (majina ya kabila kumi na mbili za Israeli), kwa nguzo za nyumba ile (mitume kumi na mbili wa Yesu), na kwa Yule aketiye katika kiti cha enzi cha nyumba ile (Yesu, Mfalme wa Israeli, yeye mwenyewe na Waisraeli).

Kwa vile Kanisa ni mabaki ya Israeli, Paulo—bila shaka mshirika wa Kanisa—aliweza kusema kwamba kwa vile alikuwa mwamini wa Yesu, alikuwa mabaki ya Israeli (Warumi 11:1-5). Kwa vile Kanisa ni mabaki ya Israeli, Paulo aliweza kusema kwamba waamini wa Mataifa katika Yesu wamepandikizwa katika mabaki ya Israeli (Warumi 11:17). Kwa vile Kanisa ni mabaki ya Israeli, wote wawili Paulo na Petro waliweza kusema kwamba Wayahudi ambao hawakumpokea Yesu wangekatiliwa mbali kutoka Israeli (Warumi 11:17; Matendo :23). Kwa vile Kanisa ni mabaki ya Israeli, Paulo aliweza kusema kwamba waamini wa Mataifa hawaendelei tena “kutengwa uraia wa kuwa Waisraeli” na si “wageni tena kwa ahadi za maagano” (Waefeso 2:12). Kwa vile Kanisa ni mabaki ya Israeli, Paulo aliweza kusema kwamba waamini wa Mataifa “si wageni wala wapitaji, bali ni wenyeji na raia pamoja na watu wa Mungu, na washirika wa nyumba ya Mungu” (Ephesians 2:19).” (Gay 2002: n.p.) Mifano ifuatayo miwili yaonyesha hili ilivyo:

a. “Jumuiya za Israeli” (Waef 2:11-22). Mataifa hunenwa kuwa“wametengwa na jumuiya” na “wageni kwenye maagano” (2:12). Hata hivyo, 2:19 husema kuwa “katika Kristo” Mataifa “si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamija na watakatifu [Wa-kiyahudi], watu wa nyumbani mwake Mungu.” Kifungu hicho kiko wazi kuwa: “Mataifa waaminio, washirika wa kanisa, wamehesabiwa kama wenyeji kwa jumuiya ya Israeli, ambako walikuwa wapitaji hapo kwanza, na hivyo hushiriki maagano yaliyofanywa na Mungu na Israeli nyakati za Agano la Kale. Hakuna shaka kuwa jumuiya hii imepitia badiliko, lakini uendelevu wake unabakia.”

82

Page 84:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

(Bell 1967: 105)b. Mzeituni (Rum 11:1-24). Picha ya mzeituni hutokea Yer 11:16 na Hos 14:5-6. Rum 11:1-6 huanza kwa kuonyesha kile ambacho Mungu amekitunza kama ahadi yake kwa Israeli kupitia mabaki maaminifu (ambayo Paulo, mshirika wa kanisa) ni mshiriki wake. Paulo ndipo afananisha Israeli na Mzeituni mwema: “Mungu ameondoa baadhi ya matawi ya huu Mzeituni sababu ya kutokumwamini Mwana wake, Masihi wao. Wakati huo huo, ameyachukua matawi kutoka mzeituni mwitu, na kuyapandikiza kati ya matawi ya Mzeituni mwema. Bali haya matawi mapya yaliyopandikizwa hayapaswi kujisifu kwa sababu ya nafasi yao, yakijivuna juu ya Wayahudi waliokatiliwa nje. Matawi ya Kiyahudi yalikatwa kwa sababu ya kutokuamini kwao. Matawi ya Mataifa yalipandikizwa kwa sababu ya kuamini kwao. Kama Mataifa hawa wataishia katika kutokuamini, nao pia watakatiliwa nje. Nafasi katika Mzeituni mwema ni kwa njia ya imani peke yake.” (Bear 1940-41: 152) “Inapaswa ieleweke kwamba Wayahudi waaminio, wawakilishao matawi mema ya kiasilia, hayakuhamishwa. Hayakupelekwa kwenye mti mwingine, nk. Walikuwa ni Wakristo wa Mataifa ndio waliofanyika sehemu ya mzeituni mwema ambao tayari ulishakuwepo (Israeli) na ambao wanashirikiana na matawi yaliyopo tayari ya kiasilia (Wayahudi) . . . . Warumi 11, katika hali ya mwingiliano mzuri na vifungu vingine vya Paulo kama vile Waefeso 2 na Agano Jipya kiujumla, hufundisha kwamba ahadi za Mungu kwa Israeli hazikukusudiwa kwa uzao wa kimwili kiujumla, bali kwa Waisraeli waaminio tu, mabaki ya Israeli, waliowakilishwa nyakati za Paulo na yeye mwenyewe na Wayahudi wengine waaminio, na kwamba ahadi hizi sasa zinawafikia Mataifa waaminio ambao, kwa kuingizwa ndani ya Israeli ya kale (kupandikizwa kwenye Mzeituni mwema), wanashiriki pamoja na Wayahudi waaminio; kwa pamoja kufanya Israeli ya Kiroho na/au kanisa la Kristo.” (Bell 1967: 116, 118)

2. Kanisa ni jipya kwa maana Yesu alisema, “wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda” ( Math 16:18). Kauli hiyo ya Yesu iko katika wakati ujao (“nitalijenga”) ambayo huonyesha kwamba lilikuwa kitu kipya, cha kujengwa. Kanisa ni jipya kwa angalau sababu mbili:

a. Kanisa lina msingi wa kifo na ufufuo wa Kristo. “Kanisa ni jipya ukichukulia hasa kwa vile ni kusanyiko la Masihi ambalo atalijenga kwa misingi ya kifo cha mateso na ufufuo Wake. Vivyo hivyo, Musa aliyewatoa “eklesia” [Kiyunani kwa ajili ya “kusanyiko”; ona, Mdo 7:38] (Waisraeli) nje ya Misri kimwili, Masihi angelitoa kusanyiko lake kutoka katika dunia kiroho, kuunda kusanyiko la kiroho linalochanganya wote Wayahudi na Mataifa.” (Gay 2002: n.p.) b. Kanisa ndilo maskani ya Roho Mtakatifu akaaye ndani yake. “Kanisa pia ni jipya kulingana na ahadi ya maskani ya Agano Jipya ya Roho atakayekaa ndani (Ezekieli 36:24-26; Yeremia 31:31-33). Siri hiyo ya Kanisa ilikuwa kwamba, wasio Wayahudi pia wangelipokea Roho na kuingizwa katika mwili huo huo (pamoja na Wayahudi waaminio) kupitia Roho (Matendo 10:45, 15:8; Waefeso 2:19-3:6). Hii ilikuwa ni siri kwa sababu katika Agano Jipya ujio wa Roho ulikuwa umeahidiwa tu kwa nyumba ya Yuda (Yeremia 31:31), siyo kwa Mataifa. Kwa hiyo, ilikuwa imefichika katika Agano la Kale, kinamna fulani, kama vile katika agano lililotolewa kwa Ibrahimu, ambaye uzao wake (Masihi) atakuwa baraka kwa mataifa yote.” (Gay 2002: n.p.)

E. Yesu alilikataa taifa la Israeli kama chombo cha kuujengea ufalme wa Mungu, na kutoa jukumu hilo kwa wafuasi wake mwenyewe, kanisa.

Injili humweka Yesu kama ndiye baraka za maagano. Hata hivyo, katika Injili “pia kuna dhana kinyume: utimilizo wa laana za maagano (hukumu) kwa Israeli isiyoamini (Math. 8:12; 13:12-14; 21:43; 23:37-39; pia. Luka 16:19-31). Ili kuweza kurithi baraka za agano, kulitakiwa zaidi ya mkondo wa ukoo wa uzaliwa (Math. 3:9)!” (Williamson 2007: 185)

1. Katika maelezo yake kuhusu mfano wa mpanzi ( Math 13:10-17 ) Yesu alitofautisha hali ya kutokusikia, pia na upofu wa Israeli; na wanafunzi wake mwenyewe. Kwanza, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.” (Math 13:11). Pili, Ingawaje Israeli ilikuwa na siri nyingi za ufalme katika Sheria na Mnabii, hawakuzielewa, na kuamua kuandamia ufalme wa kimwili ulio wa kisiasa. Matokeo, Yesu akasema, “lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa” (Math 13:12). Tatu, “Yesu alitamka hukumu ya kiroho kwa Israeli kwa kunukuu Isa 6:9-10” (Beale 2008: 163) inayosema kuwa Israeli “Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa [na] kutazama mtatazama, wala hamtaona. Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, na kwa masikio yao hawasikii vema na macho yao wameyafumba,

83

Page 85:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya” (Math 13:14-15; pia ona, Marko 4:12; Luka 8:10; Yoh 12:39-40). Anahitimisha kwa kutofautisha wanafunzi wake na upofu na ukiziwi wa Israeli, kwa kusema, “heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia. Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie” (Math 13:16-17). 2. AJ hutumia Isa 6:9-10 kama unabii kinyume na Israeli kwa kumkataa Yesu. Kama ilivyotolewa mwanzoni, Isa 6:9-10 ilikuwa sehemu ya utume wa kinabii kwa Isaya uliofanyika katika maisha yake mwenyewe, bali Yesu anauita “unabii” ambao “unatimia” (Math 13:14). Katika Isa 6:9-10 Israeli ilikuwa inahukumiwa kwa kuabudu sanamu. Katika siku za Yesu, Israeli bado walikuwa na hatia ya kuabudu sanamu, isipokuwa sanamu yenyewe ilikuwa tofauti: ilibadili desturi za kianadamu badala ya upendo wa Mungu (ona Isa 29:9-13; Ezek 14:4, 7; Math 15:7-9; 23:29-33; Marko 7:6-13), na ilitafuta kujipa haki yake yenyewe badala ya haki ya Mungu (Rum 10:3). Dhambi ya Israeli ilikuwa mbaya zaidi kuliko ya vizazi vilivyotangulia, kwani walimkataa Mungu mwenyewe aliyekuja duniani katika nafsi ya Yesu. “Katika Isaya 6:11 nabii anauliza ‘ni hata lini hukumu ya upofu wa kiroho na ukiziwi huo utadumu, na jawabu likawa utaendelea hata kwa mabaki wataookoka utumwa wa Babeli na watakaokuwa katika nchi ya ahadi baada ya kutekwa kule. Inaeleweka kwamba Yesu aliwaona umati wa Waisraeli wasioamini katika siku zake mwenyewe wakati wa uendelevu wa mabaki wasioamini na walio vipofu. Kwa maana hiyo, inaeleweka pia kwa nini aliona kwamba Isaya 6:9-10 ulikuwa ni unabii wa hali ya kiroho ya Wayahudi katika siku za Isaya na pia wa siku zake mwenyewe.” (Beale 2008: 165) Katika Yohana 12:40 mtume Yohana anukuu Isa 6:10 akihusisha na upofu wa Israeli “kwa kutomwamini Yeye [Yesu]” (Yoh 12:37). Yohana hata aongezea kuwa, “mambo haya Isaya aliyasema kwa sababu aliuona utukufu Wake, na akatajaa habari zake [m.y., Yesu].” Katika Mdo 28:23-28 Paulo anukuu Isa 6:9-10 akiihusisha na Israeli kumkataa Yesu, na kuiona kama sababu ya Mungu kuuleta wokovu kwa Mataifa.3. Yesu alionyesha ishara ya kulikataa taifa la Israeli, alipoulaani mtini ( Math 21:18-22; Mark 11: 12- 14, 20-24 ). Kuulani mtini kulikuwa ni “mfano uliotolewa kimatendo.” Mtini ulikuwa ishara ya taifa la Israeli (Hos 9:10; Nah 3:12; Zek 3:10). Katika kuulaani mtini, Yesu alikuwa akilaani ile hali ya “kujionyesha” ki-nje ya kidini inayopungukiwa tunda la kweli, la kiroho. Hata hivyo, alikuwa akifanya zaidi ya hapo. Yer 5:17, 8:13, Hos 2:12; Amos 4:9, na Mik 7:1-6 zote huzungumzia kuhusu hukumu kwa mtini kama sehemu ya hukumu ya Mungu juu ya Israeli. “Kifungu kinachoelekea kuja kichwani kutokana na kisa hiki ni Mika 7: 1-6, ambapo mshangao wa nabii kuhusu upotofu wa Yuda waelezwa kama kushindwa kwake kupata ‘tunda lake la kwanza la mtini ambalo amelitamani kwa njaa.’ Kufuatia kauli ya dhahiri kwamba Yesu alikuwa na njaa katika mst. 18, kule kuyakosa matunda ya mtini yaliyotarajiwa ya kula hunena kwa nguvu kuu jinsi maoni ya kinabii yanavyotimizwa katika kushindwa kwa Yerusalemu iliyokuwapo na hekalu lake” (France 2007: 793) Yesu aliunganisha kulaani kwake mtini na maneno, “Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele” (Math 21:19). Kwa kauli ile, Yesu hakuwa tu anakemea unafiki wa kidini (kwani wanafiki wanaweza angalau wakatubu na kubadilika). Badala yake, alikuwa akidhihirisha kwamba taifa kiujumla kama chombo cha kueneza Ufalme wa Mungu lilikuwa limekataliwa kabisa na kutupwa nje. Vivyo hivyo, baada ya kuwashambulia Mafarisayo, Yesu alisema, “Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang’olewa.” (Math 15:13).4. Katika mfano wa mwenye shamba na mzeituni,Yesu alifanya yote mawili; aliwakaripia viongozi wa Israeli na kusema “Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake” ( Math 21:33-46; ona pia Mark 12:1-11; Luka 20:9-18 ). “Katika muktadha mpana zaidi wa Mathayo, kisa cha wale wenye talanta waovu hutenda kazi kama mfano wa pili, kati ya mitatu ambayo kwa mfululizo huelezea kuhukumiwa kwa Israeli (21:28-32), tamshi (21:33-46), na utekelezaji (22:1-14)” (Beale and Carson 2007: 74). Mfano huu huchotwa kutoka Isa 5:1-7 ambapo “shamba la mzabibu la Bwana wa majeshi ni nyumba ya Israeli” (Isa 5:7). Yote mawili; kulaani kwa Yesu ule mtini na hukumu yake kwa Israeli katika mfano huu kulihusiana na tunda: wa kwanza ulikuwa kunyume kabisa—“ Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele” (Math 21:19); wa pili ulielekea kwenye upande bora—“ Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake” (Math 21:43). Hitimisho la Yesu (21:43) anatumia neno lisilo la uwingi ethnos (“watu” au “taifa”). Hilo ni sawa na kauli ya baadaye ya Paulo, “siyo wote Israeli walio uzao wa Israeli” (Rum 9:6). Kwa maneno mengine, “Kutaja kwingine kwa ‘taifa’ badala ya ‘ninyi’ katika mkataba wa shamba la mzabibu kwatuchukua hadi moyo wa swala lenyewe la [nani aliye] Israeli wa kweli ahusikaye katika kifungu hiki chote cha Injili” (France 2007: 808). Hitimisho la

84

Page 86:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Yesu ni la ndani sana. “Kuweka kando huku kwa fursa ya Israeli kama watu maalum wa Mungu na kuwapenda zaidi watu wengine, waitwao kanisa. . . si tukio duni la kimapinduzi. Neno lisilo la uwingi [ethnos], limaanishalo ‘watu’ au ‘taifa,’ ni dhahiri huibukia kwenye utume uliofuatia kwa Mataifa, [ethnoi], neno la uwingi la neno hilo hilo.” (Hagner 1995: 623) 5. Ufupishi wa Takwimu za Biblia. “Hakuna kifungu kimoja cha wazi cha AJ kinachotaja marejezo ya Israeli kama taifa la kisiasa au kutabiri utawala wa kidunia wa Kristo kabla ya kurudi kwake mara ya mwisho. Hakuna unaotaja kukamilika kwa utukufu kama ufalme wa kidunia utawalao juu ya taifa la Israeli lililorejezwa. Ukimya wa Roho unatisha. . . . Wakati upande uchunguzao wa shilingi ya AJ ukiwa na alama nzito kuwa hakuna kifungu kamili kifundishacho kurejezwa kwa utaifa wa Israeli, upande wa chini yake una alama za ukweli mgumu usemao kuwa taifa la Israeli na Sheria zake limebadilishwa kabisa kwa kanisa na Agano Jipya. Pasipo mahangaiko Math 15:13 na Marko 12:1-9, Bwana wetu alitamka katika vifungu hivi kwamba taifa la Kiyahudi halina nafasi tena kama watu maalum wa Mungu; nafasi hiyo imechukuliwa na jumuiya ya Ki-Kristo; inayotimiliza makusudi ya Mungu kwa Israeli. (Waltke 1988: 273, 274-75).

F. Kanisa ndilo watu wapya, wa kweli, wa Mungu—Israeli ya Kiroho.1. Kanisa liko “katika” waamini, na waamini wako “katika Kristo.” Kama Kristo alivyo Israeli mpya, wa kweli, aliye mwaminifu, ndivyo walivyo waliounganishwa na Kristo kwa imani.

a. Kristo yuko “ndani ya” waamini (Yoh 14:20; 17:23; Rum 8:10; Wagal 2:20; Waef 3:17; Col 1:27; 1 Yoh 3:24; Ufu 3:20).b. Waamini wako “ndani ya Kristo” (k.m Rum 8:1; 12:5; 16: 6, 7, 9-10; 1 Wakor 1:2, 30; 4:10, 15; 15:18, 22; 2 Cor 1:21; 5:17; 12:2; Gal 1:22; 3:28; 6:15; Waef 1:3; 2:6, 10; Wafil 1:1; Col 1:2; 1 Wathes 2:14; 4:16; 1 Tim 3:13; 2 Tim 3:12; Filem 23; 1 Petr 5:14).c. Waamini wameunganishwa na Kristo katika kusulubiwa na kufuka kwake (Wagal 2:20; Waef 2:5-6).d. Kanisa linaitwa “mwili wa Kristo,” moja, na waamini moja- moja ni “viungo” vya mwili (Rum 12:4-5; 1 Wakor 10:17; 12:12-27; Waef 1:22-23; 2:16; 4:4, 12; 5:30; Wakol 1:18; 3:15). e. Yesu alilituma kanisa lake liende kwa misingi ile ile kama Baba yake alivyomtuma (Math 16:19; 28:18-20; Yoh 17:18; 20:21, 23).

2. AJ huchukua mawazo makuu ya AK na maana zake zilizoelezea Israeli, na kuzihusisha na kanisa. a. Jamii iliyoteuliwa, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki yake Mungu. Waef 1:4-5; Wakol 3:12; Tit 2:14; 1 Petr 2:5, 9; linganisha Kut 19:5-6; Kumb 4:20; 7:6-7; 14:2; Isa 43:20-21.b. Watu wake Mungu. Rum 9:22-26; I Petr 2:10; linganisha Hos 1:10; 2:23. Katika Rum 9:24-26 Paulo siyo tu anukuu Hosea, bali kibayana asema kwamba (aliyekuwa akizungumzia kuhusu Israeli) anena kutuhusu “sisi” (m.y., kanisa).c. Wana au watoto wa Mungu. Rum 8:14, 16; 9:26; Wagal 3:26; 1 Yoh 3:1-2; linganisha Kut 4:22; Kumb 14:1.d. Uzao (wazao) wa Ibrahimu. Rum 4:13-16; Wagal 3:29; linganisha Zab 105:6-7.e. “Mimi nitakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu wangu.” 2 Wakor 6:16; Waeb 8:10; Ufu 21:3; linganisha Mwa 17:8; Kut 6:7; 29:45; Walawi 26:12; Yer 7:23; 11:4; 24:7; 30:22; 31:1, 33; 32:38; Ezek 11:19-20; 14:10-11; 36:28; 37:23, 27; Hos 2:23; Zek 8:8; 13:9. f. Mke wa Mungu. Waef 5:25-32; Ufu 21:9-14; linganisha Isa 54:4-7.g. Nyumba ya Mungu. Waef2:19; 1 Tim 3:15; linganisha Hes 12:7.h. Kundi la Mungu. Luka 12:32; Yoh 10:15-16; 1 Petr 5:2-3; linganisha Ezek 34:12-16.i. Shamba la Mungu. 1 Wakor 3:9; linganisha Yer 12:10.j. Matumizi ya neno la Kiyunani “ekklēsia” kwa ajili ya kanisa. “neno la Kiebrania qāhāl, ambalo mara nyingi limefanyishwa ekklēsia katika “Septuagint” (Tafsiri ya Kiyunani ya Biblia ya Kiebrania), huhusisha Israeli katika Agano la Kale. Kutoa mifano michache, twaona qāhāl lilitumiwa kwa ajili ya kusanyiko au ushirika wa Israeli katika Kutoka 12:6, Hesabu 14:5, Kumb 5:22, Yoshua 8:35, Ezra 2:64, na Yoeli 2:16. Kwa vile “Septuagint” ilikuwa Biblia ya mitume, kutumia kwao neno ekklēsia, ambalo ni sawa na neno la “Septuagint” lenye maana ya qāhāl, kwa ajili ya kanisa la Agano Jipya huonyesha wazi wazi mwendelezo kati ya kanisa na Israeli ya Agano la Kale.” (Hoekema 1979: 215)k. Tohara (ya kweli). Rum 2:28-29; Wafil 3:3; wakol 2:11; linganisha Mwa 17:9-15; Kumb 30:6; Mdo 7:51; Waef 2:11; Wafil 3:2.

85

Page 87:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

l. Mzeituni. Rum 11:17-24; linganisha Yer 11:16; Hos 14:6.m. Mzabibu wa Mungu. Yoh 15:1-5; linganisha Hos 10:1.n. “Israeli wa Mungu.” Wagal 6:16. Msemo huu huonekana hapa peke yake katika AJ. Anayelengwa hapo ni jambo la kujadiliwa: kanisa kiujumla; Wakristo wa Kiyahudi; “Waisraeli wote” wataokolewa (wanaonenwa katika Rum 11:26 [neno lenyewe ni la kimjadala]); au huenda Wayahudi kama Wayahudi. Kupitia hoja za Paulo kila mahali katika Wagalatia, wazo analotoa hapa kama baraka kwa Wayahudi wasioamini kwa kweli haliendani kabisa. Wengine husema kwamba, maneno hayo yanazungumzia Wayahudi waaminio. Hata hivyo, kwa mantiki ya muktadha wa Wagalatia yote kiujumla, “Israeli wa Mungu” huenda inazungumzia kanisa lote (m.y., waamini Wayahudi na Mataifa). “Kilichopo katika Kristo, Paulo anatoa hoja, ni msalaba na uumbaji mpya, siyo tohara. . . . Ikiwa maneno hayo yanamaanisha watu wa Kiyahudi, au hata Wakristo Wakiyahudi, atakuwa moja kwa moja anajipinga mwenyewe. . . . Haiwezi kukubalika kwamba Israeli wa Mungu imaanishe watu wa kweli wa Mungu (tofauti na dini ya Kiyahudi) wajitukuzao katika msalaba na kuhesabu kuzaliwa kupya kama tendo la wokovu la Mungu na siyo tohara.” (Ramm 1970: 263-64) Zaidi ya hapo, “kwa vile ujumbe mkuu [katika Wagalatia] ni ule wa kuondokana na utofauti wa utaifa kati ya watu wa Mungu (3,7-8,26-29; 4,26-31; 5,2-12), ingeonyesha kutoelekea kwamba angehitimisha waraka wake kwa kuzungumzia wale walio katika kanisa kulingana na misingi ya jamii. Wazo hili halielekei kabisa hasa kwenye 6,11-18, kama hitimisho la waraka, limekusudiwa na Paulo kujumuisha dhana zake kuu.” (Beale 1999b: 205; ona pia LaRondelle 1983: 108-14; Cole 1989: 235-37; McKnight 1995: 302-04; Longenecker 1990: 297-99)

3. AJ huchukua alama na unabii wa AK unazohusu Israeli, na kuuhusisha na Kanisa.a. Tohara. Tohara ilikuwa ni alama ya agano alilofanya Mungu na Ibrahimu (Mwa 17:9-14). Alama hiyo ya ki-nje, yenye kuonekana kiuhalisia ilikuwa inalenga hali ya ndani, ya kiroho—“tohara ya moyo” (ona Kumb 10:16; 30:6; Yer 4:4). AJ linasema, “bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani; na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko. Ambayo sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu” (Rum 2:29). Wafil 3:3 huongeza, “Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatutamani mwili.” Vivyo hivyo, Wakol 2:11 panasema, “Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo.”b. Agano jipya. Agano Jipya, kama lilivyotolewa mwanzoni, liliahidiwa kwa “nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda” (Yer 31:31). Hata hivyo, wakati wa Karamu ya Mwisho Yesu aliweka bayana kuwa alikuwa anaweka Agano Jipya kwa damu yake (Luka 22:20; ona, 1 Wakor 11:25). Waebr 8-10 yote huhusisha Agano Jipya kwa Kanisa. Waeb 8:8 hunukuu Yer 31:31 (ikiwamo nukuu ya “nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda”). Waeb 8:6, 9:15, na 12:24 zote hueleza kwamba Kristo ni mpatanishi wa Agano Jipya. Ukweli kwamba “ni” (kitenzi cha sasa) mpatanishi huonyesha kwamba Agano Jipya sasa liko kazini. Waeb 9:12-17 huonyesha kwamba damu ya Kristo ilithibitisha na kukamilisha agano hilo. Waeb 10:15-18 rasmi hutumia maneno ya Agano “kwetu” [m.y., Wakristo; kanisa]. Katika 2 Rum 3:5-6 (palipoandikwa kwa sehemu kubwa kwa ajili ya kanisa la Wamataifa la Korintho) Paulo anasema kuwa “Mungu . . . alitufanya sisi . . . watumishi wa Agano Jipya.”c. Maono ya Ezekieli ya mifupa mikavu na fimbo mbili (Ezekieli 37). Maono yaliyotolewa kwa Ezekieli ya mifupa mikavu ikipata uhai (Ezek 37:1-14) ilitokea wakati ufalme wa Yuda ulikuwa uhamishoni Babeli. “Mifupa ile ni nyumba yote ya Israeli” (Ezek 37:11). Unabii uliahidi, “nitafunua makaburi yenu, na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni katika nchi ya Israeli . . . Nami nitatia roho yangu ndani yenu” (Ezek 37:12, 14). Maono ya fimbo mbili (Ezek 37:15-28), zilizowakilisha nyumba ya Yuda na nyumba ya Israeli, pia ilitokea wakati ule. Katika unabii huo, Mungu aliahidi “kufanya fimbo iwe moja . . . nami nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi hiyo . . . Na mtumishi wangu Daudi atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji moja; . . . tena nitafanya agano la amani pamoja nao; litakuwa agano la milele pamoja nao . . . nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu” (Ezek 37:19, 22, 24, 26-27). Ingawaje Israeli ilirudi katika nchi yao kutoka Babeli baada ya utumwa wa miaka 70, ule unabii wa “mifupa mikavu” ulilenga kwenye utimizwaji wa kiroho, siyo wa kimwili, muda wote, wakati wa maono ya Ezekiel, taifa halikuwa limekufa kimwilini, bali lilikuwa linaishi, ingawaje “ndani ya kaburi” katika Babeli. Waefeso 2 huweka sambamba kikamilifu Ezekieli 37. Robert Suh (2007: 723-24) aonyesha hivi:

Ezekieli 37 37:1-10—Kufufua mifupa iliyokufa

Waefeso 2 2:1-7—Kuwafufua wadhambi waliokuwa wafu katika dhambi zao

86

Page 88:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

37:11-14—Maelezo37:15-23—Kuunganika kwa Yuda na Israeli37:24-28—Kuutazamia Kujengwa maskani mapya katika utawala moja wa Daudi

2:8-10—Maelezo 2:11-18—Kuunganisha Wayahudi na Mataifa2:19-22—Kuutazamia ufalme wa mwisho kuandaliwa kwa maskani mapya chini ya utawala wa Kristo

Jinsi Paulo anavyougeuza unabii huu huendana na sehemu yote ya AJ inavyosema, ambapo ahadi kwa Israeli na Yuda zimehamia kwa kanisa, ambalo lina Wayahudi na Mataifa (ona Rum 9:22-33; Waeb 8:8-13). d. Unabii wa Yoeli wa kumimina Roho (Yoeli 2:28-32). Katika unabii wa Yoeli, Mungu aliahidi “nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili” (Yoeli 2:28). Kulingana na muundo wa unabii, Mungu alikuwa azungumzia Israeli peke yao (Yoeli 2:27; 3:1-2). Katika siku ya Pentekoste, hata hivyo, Petro alinukuu unabii ule na kusema kabisa kwamba ulikuwa umetimia kwa kuwamwagia Roho Mtakatifu waaminio katika Yesu Kristo, uliowawezesha kunena kwa lugha nyingine (Mdo 2:14-21). Yoeli 2:32 pia huzungumzia wale wa“mlima Sayuni na Yerusalemu” ambao “waliitia jina la Bwana” watapona hukumu ya Mungu. Rum 10:13 hunukuu Yoeli 2:32 na kuuhusisha na Yesu na mahubiri ya Injili.e. Unabii wa Amosi wa “kujenga upya maskani ya Daudi” (Amosi 9:11-12). Muktadha wa unabii wa Amosi ulikuwa marejesho ya Israeli kufuatia hukumu ya Mungu na kutekwa kwa Israeli (Amos 9:7-10, 13-15). Katika Baraza la Yerusalemu Mdo 15 swala lilikuwa ikiwa Mataifa wanaomgeukia Yesu Kristo, wanalazimika kutii Sheria za Musa na kutahiriwa. Kwa kuelewa kwamba hawakutakiwa kufanya hivyo, katika Mdo 15:13-19 mtume Yakobo anukuu Amosi 9:11-12 na kusema kuwa unabii huo, haukuhusiana lolote na marejesho ya Israeli, au kujenga upya kimwili kiti cha enzi cha Daudi, au Maskani ya Israeli, bali badala yake kulitimizwa kwa Mataifa kufanyika sehemu ya Kanisa. “Taswira ya kujengwa upya hema iliyoanguka ya Daudi huenda sambamba kwa ukaribu na taswira za zama za kimasihi zilizoelezwa katika Isa 11:1. Shina la Yese litachipuka. Litakuwa ishara kwa watu. Mataifa wataitafuta ishara hiyo. [Vivyo hivo] hema ya Daudi inapaswa kurejezwa ili mabaki ya watu wapate kumtafuta Bwana.” (Robertson 1988: 105) Kusema ukweli, “Mataifa sasa wanalo jina la Mungu kwa ajili yao, kuonyeshako kwamba ‘hema ya Daudi’ tayari imesharejezwa” (Ibid.: 107).

4. Yesu kuliweka kanisa kwenye msingi wa wanafunzi 12/mitume12 huonyesha kwamba alikuwa anajenga Israeli mpya, ya kiroho.

a. JesusYesu kuwachagua wanafunzi 12 /mitume12 (Math 10:1-2; Marko 3:13-19; Luka 6:12-26) ni ishara ya kabila 12 za Israeli. Kimsingi kabisa, hakujiweka mwenyewe tu kama miongoni mwa wale 12. Badala yake, yeye alikuwa ndiye kichwa.b. Mitume wenyewe walielewa umuhimu wa “12”:

(1) Katika Mdo 1:12-26 walifikia uamuzi kwamba ilikuwa ni lazima kuijaza nafasi ya Yuda Iskarioti kama mtume. (2) Ingawaje Paulo alikuwa mtume (ona, k.m., Rum 1:1; 1 Wakor 1:1; 9:1 ), AJ (na Paulo mwenyewe) huelewa utofauti kati utume wa Paulo na “wale kumi na mbili” (ona Mdo 6:2; 1 Wakor 15:5, 8 ). Hilo laweza kuhusiana na ukweli kwamba huduma ya Paulo kimsingi ilikuwa kwa Mataifa (ona, Mdo 9:15; 13:46; 18:6; Wagal 1:16; 2:7), ambapo Petro, kiongozi dhahiri na mnenaji wa wale kumi na mbili, kimsingi alikuwa mtume kwa Wayahudi (ona Wagal 2:7-8). (3) Yakobo aanza waraka wake “kwa kabila kumi na mbili waliotawanyika” ( Yak 1:1 ). Waraka ule ni dhahiri umeandikwa kwa Wakristo (ona, Yak 2:1). “Katika kutumia maneno [ai dōdeka phulai; “kabila kumi na mbili”], mwandishi awaangalia wale wanaolengwa kwenye waraka huo kama Israeli wa kweli. Kanisa pasipo shaka yoyote limepokea cheo hicho, kwani ilikuwa kazi ya Masihi kuwarejesha upya kabila kumi na mbili (Yer. 3:18; Ezek. 37:19-24; Zab. 17:28), na Wakristo walijitambua wenyewe kama warithi wa kweli wa imani ya (Warumi 4; 1 Wakor. 10:18; Wagal. 4:21-31; Wafil. 3:3).” (Davids 1982: 63)

c. Katika Math 19:27-28 Yesu anasema kwamba, “katika ulimwengu mpya, [au wa kufanywa upya vitu vyote] atakapoketi Mwana Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.” (ona pia Luka 22:29-30). Kuhusiana na “Mwana wa Mungu” kunaibukia kutoka Dan 7:13. “Katika Danieli 7 ni Israeli ‘watakatifu wa aliye juu sana’ [Dan 7:22, 27] waupokeao ufalme na kutawala juu ya mataifa, ambapo Yesu asema kwamba ni wale wanafunzi kumi na wawili wataohukumu kabila kumi na mbili za Israeli. Kuhama huku kwaashiria jukumu la wanafunzi kwa hali ya kiroho na

87

Page 89:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

kwa hatima ya mbeleni ya Israeli.” (Schnabel 2002: 45) Zaidi ya hapo, Yesu kuwahusisha wale kumi na mbili kuwahukumu Israeli “huenda kukahusiana na wale Kumi na mbili kushiriki katika kuhukumu watu wasioamini wa Israeli kumhusu Yesu kuliko kwa aina fulani ya utawala wa kikatiba wa jamii ya Israeli iliyorejezwa . Lugha ni ya kiishara tu, bali uishara huo unalenga jumuiya ya aina fulani inayofanania kabila kumi na mbili za Israeli. Yesu asema kwa namna ya nguvu kabisa iwezekanavyo kwamba Israeli ile ya kale inakuja kuhukumiwa, na kwamba hukumu hiyo itakuwa mikononi mwa walioitwa naye kama wanafunzi wake wa karibu. Matokeo ni kwamba kutakuwa na kile tuwezacho kukiita Israeli mpya.” (Marshall 1992: 123)d. Kwenye milango Kumi na mbili ya Yerusalemu Mpya yameandikwa “majina kumi na mbili ya kabila za Israeli” (Ufu 21:12), na ukuta wa mji wa Yerusalemu Mpya ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi “majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.” (Ufu 21:14). “Wale wamwaminio huyu Yesu bila woga wote ndio uendelevu wa kweli wa ‘watu wa Mungu’. Milango kumi na mbili ya Yerusalemu Mpya imeandikwa kufuatana na ‘kabila kumi na mbili za Israeli’, bali misingi kumi na miwili ya mji imeandikwa kufuatana na ‘mitume kumi na wawili wa Mwana-kondoo’ (21:12-14). Yohana ahimiza muunganiko kati ya Israeli ya Agano la Kale na wafuasi wa Yesu na mitume wake. Badala ya kuiachilia kando ‘Israeli’ ya kale, kuna kuhusishwa kukubwa kwa hali yake.” (Walker 1996: 239)

G. Kanisa ni jumuisho la “Mtumishi wa Bwana,” kama vile Yesu kibinafsi alivyokuwa “Mtumishi wa Bwana” (Isa 42:1-9; 49:1-6; 50:4-9; 52:13-53:12).

Yesu alihusisha viashiria vya “Mtumishi” kwa kanisa.1. “Nimeweka Roho yangu juu yake” ( Isa 42:1 ). Yesu aliahidi kumtuma Roho Mtakatifu kwa kanisa lake (Yoh 14:16-17, 26; 15:26; 16:7-14). Katika Yoh 20:22 (katika kile ambacho huenda kilikuwa “mfano kimatendo”), “aliwavuvia na kuwaambia, ‘Pokeeni Roho Mtakatifu.’” Katika Mdo 1:8 Yesu aliahidi kwamba “mtapokea nguvu akisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu.” Hilo lilitokea Siku ya Pentekoste (Mdo 2:1-4). Sasa, “ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu [kanisa] . . . Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” (Rum 8:11, 14).2. “Mtumishi wa Bwana” aliitwa “mtumishi” ( Isa 42:1; 49:3, 5-6; 52:13 ). Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi” (Math 20:25-28; ona pia Math 23:11; Mark 9:35; 10:42-45; Luka 22:25-27). Katika Yoh 13:5-17 Yesu alitenda kazi ya mtumwa alipowaosha wanafunzi wake miguu. Aliwaambia wanafunzi wake, “Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama vile mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo . . . [kwa sababu] mtumwa si mkuu kuliko bwana wake” (Yoh 13:15-16).3. “Nitakutoa uwe nuru ya [au, kwa] wamataifa [au, mataifa]” ( Isa 49:6 ). Katika Math 5:14 Yesu aliwambia wanafunzi wake, “Ninyi ni nuru ya ulimwengu.” Katika Mdo 13:47 Paulo anukuu Isa 42:6; 49:6, “upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia,” kuunganisha na utume wake mwenyewe kuwafikia Mataifa na Injili ya Yesu Kristo.4. Mtumishi wa Bwana akataliwa, apigwa na kuteswa ( Isa 50:6; 52:14, 53:1, 4-5, 7, 10 ). Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi pia” (Yoh 15:20). Hilo limethibitika kuwa kweli kipindi chote cha historia ya kanisa, kuanzia mara baada ya Yesu kufa na kurudi akipaa kwa Baba (ona, Mdo 4:1-22; 5:17-32; 8:3; 11:19; 12:1-5; 14:19-22; 16:19-24; 21:27-36; 2 Wakor 4:8-9; 11:23-33; 2 Tim 3:12). Paulo pia ahusisha “wimbo wa Mtumishi” wa nne kwa kanisa kwa kunukuu Isa 53:1 (“Bwana, ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta?”) Katika Rum 10:16, ili kuonyesha kwamba si kila mtu aliyesikia Injili aliamini.

H. Kama Israeli mpya, wa kweli, kanisa linakabiliwa na mitihani ile ile ya uamini fu ambao Israeli ya AK ya kimwili ilikumbana nayo.

“Kwa kukaza macho kwa Yesu kama utimilizo wa mahusiano ya kiagano, AJ linaweza kufumbua mvutano wa AK kati ya ‘wema na ukali wa Mungu’, kama awekavyo Paulo katika Warumi 11:22. Israeli ilikutana na yote mawili: wema wa Mungu kwani walifanyika ‘Israeli’ kabisa, na pia ukali wake kwa maana kwamba walibakia ‘Yakobo’asiyekombolewa. Na sasa, Kwa vile ni Yesu, kuliko kanisa,

88

Page 90:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

atimilizaye mahusiano ya kiagano, kanisa linakabiliwa na uhitaji ule ule wa maadili kama ilivyofanya Israeli, ‘Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu’ (Wakol. 3:5, tafsiri ya mwandishi). Paulo anajua kwamba dhambi ya kuabudu sanamu iliyowalemea Israeli ni swala linalonyemelea kanisa pia, lililojificha, siku zote, kujikuta limechoka, na halina upendo kwa Mungu. Wakristo huishi wakiwa na mvutano kati ya Israeli na Yakobo ndani yao wenyewe hadi ukombozi wa mwisho utakapowasili (Rum. 8:23, etc.).” (Motyer 2000: 596)

NUKUU ZILIKOTOLEWAAlexander, T. D. 1993. “Genealogies, Seed and the Compositional Unity of Genesis.” Tyndale Bulletin 44: 255-70.

Accessed 26 December 2009 at: http://www.biblicalstudies.org.uk/pdf/tb/genealogies_alexander.pdf

. 2008. From Eden to the New Jerusalem: Exploring God’s plan for life on earth. Nottingham, England: InterVarsity.

Balfour, Glenn. 1995. “The Jewishness of John’s Use of the Scriptures in John 6:31 and 7:37-38.” Tyndale Bulletin 46: 357-80. Accessed 26 December 2009 at: http://www.tyndalehouse.com/tynbul/library/TynBull_1995_46_2_08_Balfour_John6_7.pdf

Bartholomew, Craig. 2005. “Biblical Theology.” In Dictionary for Theological Interpretation of the Bible, ed. Kevin Vanhoozer, 84-90. Grand Rapids, MI: Baker Academic.

Bartholomew, Craig, and Michael Goheen. Not dated. “The Story-Line of the Bible.” Accessed 26 December 2009 at: http://www.biblicaltheology.ca/blue_files/The%20Story-Line%20of%20the%20Bible.pdf

Bauckham, Richard. 1998. God Crucified: Monotheism and Christology in the New Testament. Grand Rapids, MI: Eerdmans.

Beale, G. K. 1999a. The Book of Revelation: A Commentary on the Greek Text (NIGTC). Grand Rapids, MI: Eerdmans.

. 1999b. “Peace and Mercy Upon the Israel of God: The Old Testament Background of Galatians 6,16b.” Biblica 80: 204-23. Accessed 15 February 2011 at: http://www.bsw.org/Biblica/Vol-80-1999/Peace-And-Mercy-Upon-The-Israel-Of-God-The-Old-Testament-Background-Of-Galatians-6-16b/320/

. 2004. The Temple and the Church’s Mission: A Biblical Theology of the Dwelling Place of God (NSBT 17). Downers Grove, IL: InterVarsity.

. 2008. We Become What We Worship: A Biblical Theology of Idolatry. Downers Grove, IL: IVP Academic.

Beale, G. K., and D. A. Carson. 2007. Commentary on the New Testament Use of the Old Testament. Grand Rapids, MI: Baker Academic.

Beare, Francis. 1960. “The Sabbath was Made for Man?” Journal for Biblical Literature 79: 130-36.Beasley-Murray, George. 1999. John, 2nd ed. (WBC 36). Nashville, TN: Thomas Nelson.

Beckwith, Roger. 1987. “The Unity and Diversity of God’s Covenants.” Tyndale Bulletin 38: 93-118. Accessed 26 December 2009 at: http://www.tyndalehouse.com/TynBul/Library/TynBull_1987_38_04_Beckwith_GodsCovenant.pdf

Bell, William Everett, Jr. 1967. “A Critical Evaluation of the Pretribulation Rapture Doctrine in Christian Eschatology.” Ph.D. diss., New York University.

Belleville, Linda. 1986. “‘Under Law’: Structural Analysis and the Pauline Concept of Law in Galatians 3:21-4:11.” Journal for the Study of the New Testament 26: 53-78.

Blocher, Henri. 1997. Original Sin: Illuminating the Riddle. Leicester, England: Apollos.

Blomberg, Craig. 2007. “Matthew.” In Commentary on the New Testament Use of the Old Testament, ed. G. K. Beale and D. A. Carson, 1-109. Grand Rapids, MI: Baker Academic.

89

Page 91:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Bock, Darrell. “The Reign of the Lord Jesus Christ.” In Dispensationalism, Israel and the Church, ed. Craig Blaising and Darrell Bock, 37-67. Grand Rapids, MI: Zondervan, 1992.

Brawley, Robert. “For Blessing All Families of the Earth: Covenant Traditions in Luke-Acts,” Currents in Theology and Mission 22 (February 1995): 18-26.

Bretscher, Paul. 1954. “The Covenant of Blood.” Concordia Theological Monthly 25:199-209.

Burke, Trevor. 2006. Adopted into God’s Family: Exploring a Pauline Metaphor (NSBT 22). Nottingham, England: Apollos.

Busenitz, Irvin. 1986. “Woman’s Desire for Man: Genesis 3:16 Reconsidered.” Grace Theological Journal 7: 203-12. Accessed 26 December 2009 at: http://faculty.gordon.edu/hu/bi/Ted_Hildebrandt/OTeSources/01-Genesis/Text/Articles-Books/Busenitz-Gen3-GTJ.pdf

. 1999. “Introduction to the Biblical Covenants: The Noahic Covenant and the Priestly Covenant.” The Masters Seminary Journal 10: 173-89. Accessed 26 December 2009 at: http://www.tms.edu/tmsj/tmsj10m.pdf

Carson, D. A. 1982. “Jesus and the Sabbath in the Four Gospels.” In From Sabbath to Lord’s Day: A Biblical, Historical and Theological Investigation, ed. D. A. Carson, 57-97. Grand Rapids, MI: Zondervan.

. 1984. “Matthew.” In Expositor’s Bible Commentary, vol. 8, ed. Frank Gaebelein, 1-599. Grand Rapids, MI: Zondervan.

. 1991. The Gospel According to John (PNTC). Grand Rapids, MI: Eerdmans.

Cassuto, Umberto. 1961. A Commentary on the Book of Genesis, Part I. Translated by Israel Abrahams. Jerusalem: Magnes.

Clowney, Edmund. 1972-73. “The Final Temple.” Westminster Theological Journal 35: 156-89. Accessed 26 December 2009 at: http://www.beginningwithmoses.org/articles/finaltemple.htm

Cole, Graham. 2006. IG 500, unpublished class notes. Deerfield, IL: Trinity Evangelical Divinity School.

Cole, R. A. 1989. The Letter of Paul to the Galatians, 2nd ed. Leicester, England: Inter-Varsity.

Davids, Peter. 1982. The Epistle of James (NIGTC). Grand Rapids, MI: Eerdmans.

DeLacey, D. R. 1982. “The Sabbath/Sunday Question and the Law in the Pauline Corpus.” In From Sabbath to Lord’s Day: A Biblical, Historical and Theological Investigation, ed. D. A. Carson, 159-95. Grand Rapids, MI: Zondervan.

Edersheim, Alfred. 1988. The Temple. Grand Rapids, MI: Eerdmans.

Edwards, Jonathan. 1984 (reprint). The Works of Jonathan Edwards. Vol. 1, A Careful and Strict Inquiry into the Prevailing Notions of the Freedom of Will; Dissertation on the End for which God Created the World; The Great Christian Doctrine of Original Sin Defended; A History of the Work of Redemption. Carlisle, PA: The Banner of Truth Trust. Accessed 26 December 2009 at: http://www.ccel.org/ccel/edwards/works1.html

. 1986 (reprint). The Works of Jonathan Edwards. Vol. 2, Remarks on Important Theological Controversies. Carlisle, PA: The Banner of Truth Trust. Accessed 26 December 2009 at: http://www.ccel.org/ccel/edwards/works2.toc.html

Epistle of Barnabas. c.70-131. In The Apostolic Fathers, 2nd ed., 1989, ed. Michael Holmes, translated by J. B. Lightfoot and J. R. Harmer, 159-88. Grand Rapids, MI: Baker. Accessed 5 Mach 2012 at: http://www.ccel.org/ccel/schaff/anf01/Page_137.html

Erlandson, Doug. 1991. “A New Perspective on the Problem of Evil.” Accessed 26 December 2009 at: http://www.reformed.org/webfiles/antithesis/index.html?mainframe=/webfiles/antithesis/v2n2/ant_v2n2_evil.html

Essex, Keith. 1999. “The Abrahamic Covenant.” The Master’s Seminary Journal 10: 191-212. Accessed 26 December 2009 at: http://www.ondoctrine.com/2ess0001.pdf

90

Page 92:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Foh, Susan. 1974-75. “What is the Woman’s Desire?” Westminster Theological Journal 37: 376-83. Accessed 26 December 2009 at: http://faculty.gordon.edu/hu/bi/Ted_Hildebrandt/OTeSources/01-Genesis/Text/Articles-Books/Foh-WomansDesire-WTJ.pdf

Ford, Desmond. 1979. The Abomination of Desolation in Biblical Eschatology. Washington, DC: University Press of America.

France, R. T. 1975. “Old Testament Prophecy and the Future of Israel: A Study of the Teaching of Jesus.” Tyndale Bulletin 26:53-78. Accessed 11 January 2012 at: http://www.tyndale.cam.ac.uk/index.php?page=frame&add=http://www.tyndalehouse.com/TynBul/Library/00_TyndaleBulletin_ByAuthor.htm

. 2007. The Gospel of Matthew (NICNT). Grand Rapids, MI: Eerdmans.

Gaebelein, Frank. 1958. “The Unity of the Bible.” In Revelation and the Bible: Contemporary Evangelical Thought, ed. Carl F. H. Henry, 389-401. Grand Rapids, MI: Baker. Accessed 26 December 2009 at: http://www.biblicalstudies.org.uk/pdf/rev-henry/24_unity_gaebelein.pdf

Gay, John. 2002. “Remnant Theology: Different Perspectives on the Church and Israel.” No pages. Accessed 26 December 2009 at: http://www.leaderu.com/theology/remnanttheo.html

Gentry, Peter. 2010. “Daniel’s Seventy Weeks and the New Exodus.” Southern Baptist Journal of Theology 14: 26-44. Accessed 1 August 2011 at: http://www.sbts.edu/resources/files/2010/05/sbjt_v14_n1_gentry.pdf

Gleason, Randall. 2002. “The Eschatology of the Warning in Hebrews 10:26-31.” Tyndale Bulletin 53: 97-120. Accessed 2 March 2012 at: http://www.tyndalehouse.com/tynbul/library/TynBull_2002_53_1_06_Gleason_Hebrews10Warning.pdf

Goldsworthy, Graeme. 1991. According to Plan: The Unfolding Revelation of God in the Bible. Downers Grove, IL: InterVarsity.

. 2000. Preaching the Whole Bible as Christian Scripture. Grand Rapids, MI: Eerdmans.

Grenz, Stanley. 1992. The Millennial Maze. Downers Grove, IL: InterVarsity.

Gundry, Robert. 1987. “The New Jerusalem: People as Place, Not Place for People.” Novum Testamentum 29: 254-64.

Hagopian, David G., ed. 2001. The Genesis Debate: Three Views on the Days of Creation. Mission Viejo, CA: Crux.

Hagner, Donald. 1990. Hebrews (NIBC). Peabody, MA: Hendrickson.

. 1995. Matthew 14-28 (WBC 33B). Dallas, TX: Word.

Hamstra, Sam. 1998. “An Idealist View of Revelation.” In Four Views on the Book of Revelation, 95-131. Grand Rapids, MI: Zodervan.

Hauerwas, Stanley. 2006. Matthew (BTCB). Grand Rapids, MI: Brazos.

Hillyer, Norman. 1970. “First Peter and the Feast of Tabernacles,” Tyndale Bulletin 21: 39-70. Accessed 26 December 2009 at: http://www.tyndalehouse.com/tynbul/library/TynBull_1970_21_02_Hillyer_1PeterFeastTabernacles.pdf

Hoekema, Anthony. 1979. The Bible and the Future. Grand Rapids, MI: Eerdmans.

Holwerda, David. 1995. Jesus and Israel: One Covenant or Two? Grand Rapids, MI: Eerdmans.

Hughes, Philip. 1977. A Commentary on the Epistle to the Hebrews. Grand Rapids, MI: Eerdmans.

Jacobs, Louis, 1959. A Guide to Rosh Ha-Shanah. London: Jewish Chronicle.

Jewish Encyclopedia. 2002. “Temple of Herod.” Accessed 26 December 2009 at:http://www.jewishencyclopedia.com/view.jsp?artid=123&letter=T

. 2002. “Temple, the Second.” Accessed 26 December 2009 at:

91

Page 93:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

http://www.jewishencyclopedia.com/view.jsp?artid=128&letter=T

Johnson, Dennis. 1986. “Fire in God’s House: Imagery from Malachi 3 in Peter’s Theology of Suffering (1 Pet. 4:12-19).” Journal of the Evangelical Theological Society 29: 285-94. Accessed 12 January 2012 at: http://www.etsjets.org/files/JETS-PDFs/29/29-3/29-3-pp285-294_JETS.pdf

. 2007. Him We Proclaim: Preaching Christ from All the Scriptures. Phillipsburg, NJ: P&R.

Johnson, S. Lewis. 1974. “Romans 5:12—An Exercise in Exegesis and Theology.” In New Dimensions in New Testament Study, ed. Richard Longenecker and Merrill Tenney, 298-316. Grand Rapids, MI: Zondervan.

Josephus. 1987. The Works of Josephus Complete and Unabridged. Translated by William Whiston. Peabody, MA: Hendrickson.

Kaiser, Walter. 1978. Toward an Old Testament Theology. Grand Rapids, MI: Zondervan.

Keller, Timothy. 2008. The Reason for God. New York: Dutton.

. Not dated. “The Importance of Hell.” Accessed 26 December 2009 at: http://www.redeemer.com/news_and_events/articles/the_importance_of_hell.html

Kistemaker, Simon. “The Temple in the Apocalypse.” Journal of the Evangelical Theological Society 43: 433-41.

Klooster, Fred. 1988. “The Biblical Method of Salvation: A Case for Continuity.” In Continuity and Discontinuity: Perspectives on the Relationship Between the Old and New Testaments, ed. John Feinberg, 132-60. Westchester, IL: Crossway.

LaRondelle, Hans. 1983. The Israel of God in Prophecy: Principles of Prophetic Interpretation. Berrien Springs, MI: Andrews University Press.

Lehrer, Steve. 2006. New Covenant Theology: Questions Answered. Steve Lehrer.

Leithart, Peter. Not dated. “The Kingdom of God.” Accessed 26 December 2009 at: http://www.beginningwithmoses.org/articles/leithartkingdomofgod.htm

Lincoln, A. T. 1982. “Sabbath, Rest, and Eschatology in the New Testament.” In From Sabbath to Lord’s Day:A Biblical, Historical and Theological Investigation, ed. D. A. Carson, 197-220. Grand Rapids, MI: Zondervan.

Longenecker, Richard. 1990. Galatians (WBC 41). Nashville, TN: Thomas Nelson.

Marshall, I. H. 1992. “Church.” In Dictionary of Jesus and the Gospels, ed. Joel Green, Scot McKnight, and I. Howard Marshall, 122-25. Downers Grove, IL: InterVarsity.

McKnight, Scot. 1995. Galatians (NIVAC). Grand Rapids, MI: Zondervan.

Meier, John. 1976. Law and History in Matthew’s Gospel (AnBib 71). Rome: Biblical Institute.

Moo, Douglas. 1984. “Jesus and the Authority of the Mosaic Law.” Journal for the Study of the New Testament 20: 3-49.

. 1988. “The Law of Moses or the Law of Christ.” In Continuity and Discontinuity: Perspectives on the Relationship Between the Old and New Testaments, ed. John Feinberg, 203-18. Westchester, IL: Crossway.

Moo, Jonathan. 2009. “The Sea that is No More: Rev 21:1 and the Function of Sea Imagery in the Apocalypse of John.” Novum Testamentum 51: 148-67.

Motyer, Stephen. 2000. “Israel (Nation).” In New Dictionary of Biblical Theology, ed. T. Desmond Alexander and Brian Rosner, 581-87. Leicester, England: Inter-Varsity.

Nelson, Richard. 2003. “‘He Offered Himself’: Sacrifice in Hebrews.” Interpretation 57: 251-65.

O’Brien, Peter. 2010. The Letter to the Hebrews (PNTC). Grand Rapids, MI: Eerdmans.

92

Page 94:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Ortlund, Raymond. 1996. God’s Unfaithful Wife: A Biblical Theology of Spiritual Adultery (NSBT 2). Downers Grove, IL: InterVarsity.

Osborne, Grant. 2010. Matthew (ZECNT). Grand Rapids, MI: Zondervan.

Owen, John. 1979. Indwelling Sin in Believers. Grand Rapids, MI: Baker. Accessed 26 December 2009 at: http://www.godrules.net/library/owen/131-295owen_f4.htm

Pao, David, and Eckhard Schnabel. 2007. “Luke.” In Commentary on the New Testament Use of the Old Testament, ed. G. K. Beale and D. A. Carson, 251-414. Grand Rapids, MI: Baker Academic.

Peterson, David. 1979. “The Prophecy of the New Covenant in the Argument of Hebrews.” Reformed Theological Review 38: 74-81.

. 2009. The Acts of the Apostles (Pillar). Grand Rapids, MI: Eerdmans.

Pickle, Bob. 2004. “Ezekiel’s City: Calculating the Circumference of the Earth.” Accessed 26 December 2009 at: http://www.pickle-publishing.com/papers/ezekiels-city-circumference-of-the-earth.htm

Piper, John. 1998. “Is God Less Glorious Because He Ordained that Evil Be?” Accessed 26 December 2009 at: http://www.desiringgod.org/ResourceLibrary/ConferenceMessages/ByDate/1998/1476_Is_God_Less_Glorious_Because_He_Ordained_that_Evil_Be/

. 2000. “Are There Two Wills In God?” In Still Sovereign, ed. Thomas R. Schreiner and Bruce A. Ware, 107-31. Grand Rapids, MI: Baker. Accessed 26 December 2009 at: http://www.desiring god.org/ResourceLibrary/Articles/ByDate/1995/1580_Are_There_Two_Wills_in_God/

. 2003a. Desiring God. Colorado Springs, CO: Multnomah.

. 2003b. Let the Nations be Glad!, 2nd ed. Grand Rapids, MI: Baker Academic.

Plummer, Alfred. 1942 (reprint). A Critical and Exegetical Commentary on the Gospel According to St. Luke (ICC), 5th ed. Edinburgh: T&T Clark.

Poythress, Vern. 1991. The Shadow of Christ in the Law of Moses. Brentwood, TN: Wolgemuth & Hyatt.

Ramm, Bernard. Protestant Biblical Interpretation, 3rd ed. Grand Rapids, MI: Baker.

Reisinger, John. 1998. Abraham’s Four Seeds. Frederick, MD: New Covenant Media. Accessed 26 December 2009 at: http://www.worldwithoutend.info/bbc/books/NC/abrahams_seed/toc.htm

Riddlebarger, Kim. 2003. A Case for Amillennialism. Grand Rapids, MI: Baker.

Robertson, O. Palmer. 1988. “Hermeneutics of Continuity.” In Continuity and Discontinuity: Perspectives on the Relationship Between the Old and New Testaments, ed. John Feinberg, 89-108. Westchester, IL: Crossway.

Schnabel, Eckhard. 2002. “Israel, the People of God, and the Nation.” Journal of the Evangelical Theological Society 45: 35-57.

Stitzinger, Michael. 1981. “Genesis 1-3 and the Male/Female Role Relationship.” Grace Theological Journal 22: 41-42. Accessed 26 December 2009 at: http://faculty.gordon.edu/hu/bi/Ted_Hildebrandt/OTeSources/01-Genesis/Text/Articles-Books/Stitzinger-Gen-1-3-GTJ-1981.htm

Suh, Robert. 2007. “The Use of Ezekiel 37 in Ephesians 2.” Journal of the Evangelical Theological Society 50: 715-33.

Sweeney, James. 2003. “Jesus, Paul, and the Temple: An Exploration of Some Patterns of Continuity.” Journal of the Evangelical Theological Society 46: 605-31. Accessed 11 March 2012 at: http://www.etsjets.org/files/JETS-PDFs/46/46-4/46-4-pp605-631_JETS.pdf

Sykes, Stephen. 1997. The Story of Atonement. London: Darton, Longman & Todd, Ltd.

Talbot, Mark. 2005. “All the Good that is Ours in Christ: Seeing God’s Gracious Hand in the Hurts Others Do to Us.” 93

Page 95:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Audio message. Accessed 5 March 2012 at: http://www.desiringgod.org/resource-library/conference-messages/all-the-good-that-is-ours-in-christ-seeing-gods-gracious-hand-in-the-hurts-others-do-to-us

Travis, Stephen. 1982. I Believe in the Second Coming of Jesus. Grand Rapids, MI: Eerdmans.

Venema, Cornelis. 2000. The Promise of the Future. Carlisle, PA: Banner of Truth.

Vos, Geerhardus. 1979 (reprint). The Pauline Eschatology. Grand Rapids, MI: Baker.

Waldron, Samuel. Not dated. “Structural Considerations.” In Lecture Notes on Eschatology. Accessed 26 December 2009 at: http://www.vor.org/truth/rbst/escatology03.html

Walker, P. W. L. 1996. Jesus and the Holy City: New Testament Perspectives on Jerusalem. Grand Rapids, MI: Eerdmans.

Waltke, Bruce. 1988. “Kingdom Promises as Spiritual.” In Continuity and Discontinuity: Perspectives on the Relationship Between the Old and New Testaments, ed. John Feinberg, 263-87. Westchester, IL: Crossway.

Walton, John. 2001. Genesis (NIVAC). Grand Rapids, MI: Zondervan.

Wells, Tom, and Fred Zaspel. 2002. New Covenant Theology. Frederick, MD: New Covenant Media.

Williamson, Paul. 2000. “Abraham, Israel and the Church.” Evangelical Quarterly 72: 99-118. Accessed 26 December 2009 at: http://www.beginningwithmoses.org/articles/abrahamisraelchurch.htm

. 2007. Sealed with an Oath: Covenant in God’s Unfolding Purpose (NSBT 23). Nottingham, England: Apollos.

Wright. N. T. 1996. Jesus and the Victory of God. Minneapolis, MN: Fortress.

Yarbrough, Robert. 1996. “Biblical Theology.” In Evangelical Dictionary of Biblical Theology, ed. Walter Elwell, 61-66. Grand Rapids, MI: Baker. Accessed 26 December 2009 at: http://www.biblestudytools.com/dictionaries/bakers-evangelical-dictionary/biblical-theology.html

DIBAJI 1—VIFUPISHO KWA UCHACHE VYA VITABU VYA BIBLIA http://www.bible-history.com/resource/r_books.htm

Vitabu vya Biblia na Muhtasari Mfupi, by Rusty Russell

Vitabu vya Agano la Kale – Jumla Vitabu 39

Vitabu vya Mwanzoni – Vitabu 5 Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu, Kumbu kumbu la Torati

Vitabu vya Historia - Vitabu12 Yoshua, Waamuzi, Ruthu, 1 Samueli, 2 Samueli, 1 Wafalme, 2 Wafalme, 1 Nyakati, 2 Nyakati, Ezra,

Nehemia, Esta.

Ushairi - Vitabu 5 Ayubu, Zaburi, Mithali, Mhubiri, Wimbo ulio Bora

Vitabu vya Kinabii – Vitabu 17 94

Page 96:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Manabii wakuu - Isaya, Yeremia, Maombolezo, Ezekieli, DanieliManabii Wadogo - Hosea, Yoeli, Amosi, Obadia, Yona, Mika,  Nahumu, Habaki, Zefania, Hagai, Zekaria, Malaki

Vitabu vya Mwanzoni – vitabu 5 1. Mwanzo – Msingi wa taifa la Waebrania. Uumbaji, Anguko, Gharika kuu, Kuenea kwa mataifa, Ibrahimu, Isaka, Yakobo, na Yusufu. Utumwa katika Misri. 2. Kutoka- Agano na taifa la Waebrania. Kwa miaka 400 bado wanakuwa watumwa, Musa, mapigo10, Pasaka, Kutoka Misri, Kuvuka bahari ya Shamu, Mlima Sinai na Sheria za maadili, Kijamii, na Sherehe .3. Walawi – Sheria za taifa la Waebrania. Maelekezo ya mifumo ya utoaji sadaka na ukuhani. Maagizo kuhusu usafi wa kimaadili. 4. Hesabu – Safari kwenda Nchi ya Ahadi. Bado katika mlima Sinai, watu waunda sanamu ya ndama wa dhahabu, adhabu yao, miaka 40 ya kutanga-tanga jangwani yaanza. 5. Kumbu kumbu - Kukumbushwa Agano . Mazungumzo ya Musa na Mungu kuhusu tendo la Mungu kwa Israeli. Sheria kuhusu Desturi, Sherehe, Jamii, na za Maadili, na Kupitisha Agano.

Vitabu vya Historia - vitabu12 1. Yoshua – Utekaji wa Kanaani. Nusu ya kwanza ya Yoshua huelezea miaka 7 ya kuiteka Nchi ya Ahadi. Nusu ya mwisho hushughulikia ugawanyaji wa ile nchi kwa kabila 12. 2. Waamuzi – Miaka 300 ya kwanza katika nchi. Kipindi cha Waamuzi. Wengi wao walikuwa wabaya sana. Waisraeli hawakuwaondosha wenyeji wote wa Kanaani na wakaanza kushiriki ibada zao za sanamu. Mizunguko7 ya makandamizo ya wageni, toba, na ukombozi. mwishowe, watu washindwa kujifunza somo lao. 3. Ruthu – Mwanzo wa familia ya kimasihi ya Daudi. Boazi Mkombozi wa kiukoo, amkomboa Ruthu, Mmoabi. Anena kuhusu haki, upendo, na uaminifu kwa Bwana.

Vitabu vinavyofuatia 6 hufuatilia wakati kutokea Samuel hadi Kutekwa kwao4. 1Samweli – Ufalme ulivyojengeka. Samweli awabeba kutoka Waamuzi hadi kwa Mfalme Sauli. 5. 2 Samweli – Utawala wa Daudi. Daudi kama mfalme, uzinzi, na uuaji.6. 2 Wafalme- Kugawanyika kwa Ufalme. Sulemani, Israeli yawa yenye nguvu na maarufu. Sulemani afa kwenye mwaka 931 KK, kisha mgawanyiko wa makabila: 10 ya Kaskazini (Israeli) na 2 Kusini (Yuda). 7. 2 Wafalme – Historia ya Ufalme uliogawanyikana. Wafalme wote 19 wa Israeli walikuwa wabaya; kwa hiyo, wakachukuliwa mateka Ashuru (722 KK). Katika Yuda, 8 kati ya watawala 20 walikuwa wakimtafuta Bwana, waliobakia walikuwa katika ibada ya sanamu. Kutekwa na Babeli (586 KK)8. 1 Nyakati – Utawala wa mfalme Daudi. Marudio ya historia ya Israeli hadi kutekwa na Waashuri na Babeli . 9. 2 Nyakati – Historia ya Ufalme wa Kusini wa Yuda. Historia ya maisha ya Sulemani, kujengwa kwa Hekalu, na historia ya Yuda.

Vitabu vinavyofuatia 3 hushughulika na kurejezwa kwa Israeli 10. Ezra – Kurudi kutoka uhamishoni. Koreshi aliruhusu Wayahudi walio wengi kurudi katika nchi yao ya Israeli. Zerubabeli aliwaongoza watu (539 KK). Ezra alirudi baadaye akiwa na Wayahudi wengi zaidi (458 KK) wakajenga Hekalu la pili.11. Nehemia – Kuijenga upya Yerusalemu. Kujenga kuta za Yerusalemu. Nehemia alipata kibali kutoka kwa Artashasta, mfalme wa Uajemi, kujenga upya ukuta (444 KK). Uamsho mkuu katika nchi.12. Estha – Ukombozi kutokana na Uangamizi mkuu. Historia kutoka sura ya 6 na 7 za Ezra. Artashasta, Malkia Esta, Modekai na Hamani. Mpango wa kuua watu wa Kiyahudi.

Vitabu vya Ushairi - vitabu 5 1. Ayubu – Tatizo la Uovu na Mateso. Mtu wa haki ajaribiwa na Mungu. Undani wa ukamilifu wa Mungu. 2. Zaburi – Kitabu cha Taifa la Israeli cha Nyimbo za tenzi. Zaburi za Daudi, mtu asiye mkamilifu, bali aliyekuwa na moyo wa Mungu. Ina sehemu 5. Kuabudu katika wimbo. Maswala mengi yahusishwa. 3. Mithali – Hekima za Sulemani. Hekima ya kiutendaji katika maswala ya kila siku. 4. Mhubiri – Ubatili wa Mambo ya Kidunia. Yote ni ubatili. Hekima ya mwanadamu ni udanganyifu. 5. Wimbo Ulio Bora – Utukufu wa Upendo wa Ndoa. Wimbo kati ya Sulemani na bibi arusi wake Mshulami wakionyesha upendo kati ya mwanaume na mwanamke.

Vitabu vya Kinabii – vitabu 17

Manabii Wakuu – vitabu 5 1. Isaya – Nabii wa Kimasihi. Aangalia dhambi ya Yuda na kutangaza hukumu ya Mungu. Hezekia. Yeye Ajaye. Marejesho na baraka. 2. Yeremia – Mwito wa mwisho kwa Toba ya Israeli. Kuitwa na Mungu kuomboleza kwa watu kutubu na kutangaza habari za hukumu kwa Yuda, ambayo ilikuja kutimia. Mpango wa Mungu kwa Agano Jipya lililojengwa kwa misingi ya ahadi zilizo bora zaidi.

95

Page 97:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

3. Maombolezo – Sikitiko juu ya Kuachwa kwa Yerusalemu. Mashairi 5 ya maombolezo. Maelezo ya kushindwa na kuanguka kwa Yerusalemu. 4. Ezekieli - "Nao Watajua Kuwa Mimi Ndimi Bwana.” Alihudumu kwa Wayahudi wakiwa uhamishoni Babeli. Maelezo ya nyakati za mwisho. 5. Danieli – Nabii Atabiriye Himaya Katika Babeli. Maono mengi ya siku zijazo akitabiri kabla ya nyakati himaya ambazo zitatawala dunia, zikiwamo Babeli, kisha Ashuri, Uyunani, kisha Rumi na hatimaye siku za baadaye za Himaya ya Rumi.

Manabii Wadogo - vitabu 12 1. Hosea – Siku za mbeleni za Israeli. Simulizi ya Hosea na mkewe asiyekuwa mwaminifu, Gomeri. Huwakilisha upendo wa Mungu na uaminifu wake, na uzinifu wa kiroho wa Israeli. Israeli itahukumiwa na kurejezwa. 2. Yoeli – Utabiri wa zama za Roho Mtakatifu. Atangaza siku za mbeleni za kutisha akitumia picha ya nzige. Hukumu itakuja, lakini baraka zitafuatia. 3. Amosi- Hatima ya Utawala wa Daudi (Mfano wa Masihi). Alionya Israeli kuhusu hukumu inayokuja. Israeli yakataa onyo la Mungu. 4. Obadia – Uharibifu wa Edomu. Tangazo kinyume na Edomu, taifa lililo jirani na Israeli lililoshangilia juu ya hukumu ya Yerusalemu. Unabii juu ya hukumu yao ijayo.5. Yona – Kazi ya rehema kwa Ninawi. Yona atangaza hukumu ijayo juu ya Ninawi. Bali wao walitubu na hukumu ikaondolewa. 6. Mika – Masihi atazaliwa katika Bethlehemu (Nyumba ya Mkate). Maelezo ya uharibifu mkubwa wa kimaadili katika viwango vyote vya Israeli. Mungu atahukumu lakini atasamehe na kurejeza. Bethlehemu patakuwa ni mahali pa kuzaliwa Masihi. 7. Nahumu – Kuangamizwa kwa Ninawi. Ninawi ukaingia katika kujisahau (karibia miaka 125 baada ya Yona) na utaangamizwa. Yote yakatendeka. 8. Habakuki- Mwenye Haki Ataishi kwa Imani. Karibu na mwisho wa ufalme wa Yuda, Habakuki amuuliza Mungu kwa nini Mungu hashughuliki na dhambi za Yuda. Mungu asema atawatumia Wababeli. Habakuki amuuliza Mungu awezaje kulitumia taifa lililo ovu zaidi hata kupita Yuda. 9. Zefania – Kuja kwa Lugha iliyo Safi. Dhana inajengwa ya Siku ya Bwana na hukumu Yake na baraka zijazo. Yuda haitatubu, isipokuwa mabaki tu, watakaorejezwa. 10. Hagai – Kujengwa upya kwa hekalu. Watu walishindwa kumweka Mungu namba ya kwanza, kwa kujenga nyumba zao kabla ya kumaliza hekalu la Mungu. Kwa hiyo, hawakupata mafanikio. 11. Zekaria – Anahimiza kujengwa upya hekalu. Zekaria anawahimiza Wayahudi kulimaliza Hekalu. Unabii mwingi wa Ki-Masihi. 12. Malaki – Ujumbe wa mwisho wa watu Wasiotii. Watu wa Mungu wanakuwa wazembe kwa majukumu yao kwa Mungu. Wanazidi kwenda mbali na Mungu. Kukubaliana na upotofu wa kimaadili. Kutangaza hukumu ijayo.

Vitabu vya Agano Jipya – Jumla Vitabu 27

Vitabu vya Historia – Vitabu 5  Mathayo, Marko, Luka, Yohana, Matendo

Nyaraka za Paulo – Vitabu 13 Warumi, 1 Wakorintho, 2 Wakorintho, Wgalatia, Waefeso, Wafilipi, Wakolosai, 1 Wathesalonike, 2 Wathesalonike. 1

Timotheo, 2 Timotheo, Tito, Filemoni

Nyaraka Zisizo za paulo – Vitabu 9 Hebrews, James, 1 Peter, 2 Peter, 1 John, 2 John, 3 John, Jude, Revelation

Vitabu vya Historia – Vitabu 5 1. Mathayo – Yesu Mfalme (Simba). Humwonyesha Yesu kama Masihi. Kizazi cha Yesu kupitia Yusufu kutokeza uzao wa kifalme kuanzia kwa Daudi. Kutimizwa kwa unabii wa AK. 2. Marko – Yesu Mtumishi atesekaye kwa ajili ya wanadamu (Ndama). Humwonyesha Yesu kama Mtumishi. 1/3 ya Injili hiyo hushughulika na lile juma la mwisho la Maisha Yake. 3. Luka – Yesu mwanadamu kamilifu (Mtu). Humwakilisha Yesu kama Mwana wa Adamu kutafuta na kuokoa kilichopotea. Ukoo wa Yesu kupitia Mariamu hurudi nyuma hadi kwa Adamu (wanadamu wote). Injili pana zaidi ya zote. Mwana wa Adamu (tabia ya mwanadamu). 4. Yohana – Yesu Mungu -mtu aliyekuja kutoka juu (Tai). Humwakilisha Yesu kama Mungu aliyetwaa mwili (Mungu katika mwili), Kristo, atendaye miujiza na Maneno ya Mungu ili kwamba mpate kuamini. Mwana wa Mungu (Jina la Mungu). 5. Matendo – Kuundwa kwa Kanisa. Maelezo ya historia ya tukio kuanzia kupaa kwa Yesu hadi safari za Paulo za utume wa upandaji wa makanisa.

Nyaraka za Paulo – Vitabu 13

96

Page 98:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

1. Warumi – Sura ya kazi za Kristo. Mpangilio wa uchambuzi wa kuhesabiwa haki, kutakaswa, na kutukuzwa. Huchambua mpango wa Mungu kwa Wayahudi na Mataifa. 2. 1 Wakorintho – Mapungufu Mbali mbali ya Kanisa. Waraka huu hushughulika na makundi na marekebisho yatokanayo na kukosa uadilifu, kutokufuata utaratibu, na kudhalilisha Meza ya Bwana. Pia hutaja sanamu, ndoa, na ufufuo. 3. 2 Wakorintho – Uthibitisho wa Utume wa Paulo. Utetezi wa Paulo wa nafasi yake ya Mtume. 4. Wagalatia – Kwa Neema, Kamwe si Kwa Sherria. Paulo akosoa makosa yatokanayo na kusimamia sheria na huzingatia mahali papaswapo pa neema katika maisha ya Mkristo. 5. Waefeso – Umoja wa Kanisa. Nafasi ya mwamini katika Kristo na maelezo ya vita vya Kiroho. 6. Wafilipi – Waraka wa Ki-utume. Paulo azungumzia kuhusu kuwekwa kwake gerezani, upendo wake kwa Wafilipi. Anawahimiza waishi maisha ya utauwa na kuwaonya kuachana na sheria. 7. Wakolosai – Uungu wa Yesu. Paulo anakazia kuhusika kwa Yesu katika uumbaji, ukombozi, na uungu. 8. 1 Wathesalonike – Ujio wa pili wa Yesu. Huduma ya Paulo kwa Wathesalonike. Mafundisho kuhusu usafi na kutaja kurudi kwa mara ya pili kwa Kristo. 9. 2 Wathesalonike – Ujio wa pili wa Yesu. Maelezo zaidi kuhusu Siku ya Bwana. 10. 1 Timotheo – Kiini cha Kanisa. Maelekezo kwa Timotheo kuhusu uongozi sahihi na kushughuliia walimu wa uongo, na majukumu ya wanawake, maombi, na uhitajio wa wazee na mashemasi. 11. 2 Timotheo – Maneno ya mwisho ya Paulo. Waraka wa kumtia moyo Timotheo awe hodari. 12. Tito – Makanisa ya Krete. Paulo alimwacha Tito Krete kuangalia makanisa pale. Yanayotakiwa kwa wazee. 13. Filemoni – Kuongoka kwa Mtumwa aliyetoroka. Waraka kwa mwenye kummiliki mtumwa aliyetoroka. Paulo anamsihi Filemoni amsamehe Onesimo.

Nyaraka Zisizo za Paulo – Vitabu 9 1. Waebrania – Yesu Mpatanishi wa Agano Jipya. Waraka kwa Wakristo Waebrania waliokuwa katika hatari ya kurudi kwenye imani ya Uyahudi. Hudhihirisha ukuu wa Yesu kuliko mfumo wa AK. Hutaja ukuhani wa Melkizedeki. (Waebrania huenda uliandikwa na Paulo.  Kuna mjadala mkubwa juu ya mwandishi wa Waebrania).2. Yakobo – Mtu huokolewa kwa Matendo, IKIWA Mungu anatenda kazi kupitia yeye. Ushauri wa kimatendo wa kuishi maisha ya Kikristo ukithibitisha kujizalisha. Unahimiza kujichunguza mwenyewe kama kuna mabadiliko ya maisha mapya. 3. 1 Petro – Kwa Kanisa Lipitialo Mateso. Petro aliandika waraka huu kutia moyo watakaousoma kuhusiana na mateso yao na kunyenyekea katika hayo. Hutaja ubatizo. 4. 2 Petro – Utabiri wa Kujisahau. Hushughulika na mtu kwa ngazi ya undani, ikionya kuhusu walimu wa uongo, na kuitaja siku ya Bwana. 5. 1 Yohana – Upendo wa Mungu. Yohana huelezea ushirika wa kweli wa mwamini kwa mwamini mwingine na kwa Mungu. Humwelezea Mungu kama nuru na upendo. Huhimiza mwenendo mtakatifu kwa Wakristo mbele za Bwana. Huzungumzia sana upendo wa Kikristo.6. 2 Yohana – Huonya kuhusu waalimu wa uongo. Pongezi kwa kuenenda katika Kristo na kukumbushia juu ya kuenenda katika upendo wa Mungu.7. 3 Yohana – Kemeo kwa Wasaidizi wa aina fulani. Yohana amshukuru Gayo kwa wema wake kwa watu wa Mungu na kumkemea Diotrefe. 8. Yuda – Mashindano Ya Kweli Ya Imani Kinyume na Ulegevu. Kuwaanika waalimu wa uongo na kutumia makosa ya AK kuonyesha hukumu juu yao. Kuishindania Imani. 9. Ufunuo – Mmiliki wa Haki (Mrithi) Akija na Nyaraka za Kisheria Kudai Mali Aliyoinunua . Maono yaliyojaa mwonekano wa vitu halisi wa siku za uasi utakaokuja mbeleni, hukumu, na kufikia kilele kwa mambo yote. Hatua nyingi za mchakato wa Kisheria za Wayahudi zilizotajwa kuhusiana na haki ya ukombozi na adhabu zihusuzo mali kurudishwa kwa mkombozi mhusika kama ionekanavyo katika kitabu cha Yeremia na Ruthu.

DIBAJI 2—MIPANGILIO YA MUDA WA HISTORIA YA BIBLIA http://www.konig.org/timeline.htm, copyright ©1999-2009 George Konig

Mipangilio ya Muda wa Historia ya Biblia, na George Konig na Ray Konig, www.konig.orgHapo chini ni orodha ya matukio ya kihistoria ambayo ni muhimu kwa kujifunza Biblia na utabiri wake. Utafiti wa historia hii ya mpangilio wa muda wa Biblia ulifanywa na George Konig na Ray Konig, waandishi wa kitabu, Nabii 100. Wasomi hutofautiana kuhusu tarehe hizo zinazolenga matukio hayo ya kale. Tarehe zinazoonyeshwa hapo chini ni za kukadiria tu.

2100 KK (kama miaka 4100 iliyopita)—Mungu amwahidi Ibrahimu wazao wengi. Ibrahimu aliishi kunako 2100 KK katika ile iitwayo kwa sasa Iraki. Mungu alimwambia kuondoka kwenda Kanaani, ambayo baadaye ikawa Israeli. Tofauti na watu wengi, Ibrahimu alimwamini Mungu moja aliye wa kweli. Mungu akampa thawabu kwa hiyo imani yake, akimfanya yeye kuwa baba wa taifa kuu (Israeli), na kuwa babu mzazi wa Masihi (Yesu Kristo).

2000 KK (kama miaka 4000 iliyopita)—Yakobo (Israeli) azaliwa. Yakobo, mwana wa Isaka, aliyekuwa mwana wa Ibrahimu, azaliwa Kanaani. Jina la Yakobo labadilishwa kuwa Israeli. (Kanaani baadaye yabadilishwwa jina na kuitwa Israeli, kutokana na Yakobo). Ana wana 12, ambaye kwa hao Kabila 12 za Israeli zinaitwa.

97

Page 99:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

1900 KK (kama miaka 3900 iliyopita)—Yusufu aliuzwa utumwani. Yusufu, moja wa wana 12 wa Yakobo (Israeli), auzwa utumwani na ndugu zake, wanaomwonea wivu. Yusufu aishia Misri, ambako ainuka kuwa na mamlaka, kuwa msaidizi maalum wa karibu wa Farao. Baba yake na ndugu zake baadaye waondoka kanaani kwa sababu ya ukame, na kuhamia Misri. Wanakuja kuokolewa kutoka maafani na Yusufu.

1446 KK (kama 3400 iliyopita)—Kutoka kwaanza. Waebrania, au Waisraeli (uzao wa Yakobo), wanakuwa utumwani kwa miaka 400 katika Misri hadi Musa awaongoza kutoka Misri. Wanatanga-tanga jangwani kwa miaka 40. Musa, ndipo awafikisha kwenye mpaka wa Kanaani, nchi ambayo Mungu alikuwa ameiahidia mwanzoni kwa baba yao mkuu Ibrahimu.

1406 KK (kama miaka 3400 iliyopita)—Israeli yaanza kujiimarisha yenyewe kama nchi inayojisimamia. Baada ya Musa kufa, Yoshua awaongoza Waisraeli katika Kanaani na kuanza kuiteka nchi, kuanzisha taifa kamili la Israeli kwa mara ya kwanza katika historia.

1400 KK (kama 3400 iliyopita)—Israeli inatawaliwa na waamuzi, siyo wafalme. Kuanzia kama 1400 KK hadi kwenye 1050 KK, Israeli haikutawaliwa na wafalme. Watu wafikiria kuwa Mungu ndiye mfalme wao, badala ya wafalme wa kidunia, Israeli inaongozwa na waamuzi wanaotatua migongano.

1050 KK (kama3000 iliyopita)—Sauli anakuwa mfalme wa kwanza wa Israeli. Baada ya karibu miaka 350 ya kutawaliwa na waamuzi, watu wa Israeli wanadai kuwa na mfalme, kama nchi za ujirani. Kwa kimtaka mfalme, watu wanageuza imani zao kutoka kwa Mungu kama mfalme wao. Sauli anakuwa mfalme na anatawala kwa karibu miaka 40.

1010 KK (kama 3000 iliyopita)—Daudi anakuwa mfalme wa Israeli. Daudi anafanyika mfalme wa Israeli kwenye mwaka 1010 KK na anatawala kwa mikaka 40. Daudi, tofauti na Sauli, anafuata maagizo ya Mungu. Afanya makosa, bali atubu kwa uovu huo. Atafuta kumpendeza Mungu. Apanua mipaka ya Israeli na atawala hata maeneo mengine yanayomzunguka.

970 KK (kama miaka 3000 iliyopita)—Sulemani anakuwa mfalme, ajenga Hekalu. Sulemani, mwana wa Daudi, awa mfalme kwenye mwaka 970 KK. Naye pia atawala kwa karibu miaka 40. Sulemani ajenga Hekalu kwa kumheshimu Mungu. Kazi inamalizika kwenye mwaka 960 KK. Bali, Sulemani hatimaye ageuka mbali na Mungu na kuabudu miungu ya uongo.

926 KK (kama miaka 2900 iliyopita)—Israeli yafanyika ufalme uliogawanyikana. Mara tu baada ya utawala wa Sulemani, Israeli inafanyika ufalme uliogawanyikana. Ufalme wa kusini, uitwao Yuda, unachanganya mji wa Yerusalemu na Hekalu. Utawala wa kaskazini uliendelea kuitwa Israeli. Hizo mbili mara nyingi zilipigana vita .

721 KK (kama miaka 2700 iliyopita)—Waashuri wateka utawala wa kaskazini wa Israeli. Himaya ya Ashuru yateka utawala wa kaskazini wa Israeli kwenye mwaka 721 KK. Waashuri wawatesa na kuwaua wengi. Wawaamuru Waisraeli wengi (Kabila 10 kati ya 12 za Israeli) kuondoka nchi ya Israeli na kuwaingiza wageni.

612 KK (kama miaka 2600 iliyopita)—Babeli yateka Ninawi (Himaya ya Waashuri). Mji mkuu wa himaya ya Waashuri - Ninawi – washambuliwa kwa majeshi ya ushirika ya Wababeli na wengineo. Kama ilivyoelezwa kwa nabii Nahumu katika Biblia, Ninawi ulikuwa uangamizwe kwa sababu ya Waashuri kuwatendea vibaya Israeli na watu wengine. 605 KK (kama miaka 2600 iliyopita)—Babeli yatwaa madaraka juu ya Yuda. Ufalme mpya wa Babeli chini ya utawala wa mfalme Nebukadreza, waanza kuilazimisha Yuda kusalimu amri kwake. Nebukadreza awachukua Wayahudi wengi kama mateka kulazimisha utii wa Yuda.

597 KK (kama miaka 2600 iliyopita)—Babeli yashambulia Yuda. Jeshi la Babeli lashambulia Yuda na kuwachukua Wayahudi wengi zaidi kama mateka kwenda Babeli. Ezekieli, moja wa mateka, afanyika nabii wa Mungu. Ezekieli aeleza kwamba Mungu anaruhusu Babeli kuiadhibu Yuda kwa sababu watu wamekuwa si waaminifu kwa Mungu.

586 KK (kama miaka 2600 iliyopita)—Babeli yaangamiza Yerusalemu na Hekalu. Babeli yashambulia Yuda tena. Safari hii, Wababeli waangamiza Yerusalemu na Hekalu ambalo Sulemani alikuwa amelijenga. Wayahudi wengi zaidi wachukuliwa mateka huko Babeli.

586 KK hadi 573 KK (kama miaka 2600 iliyopita)—Mfalme Nebukadreza ashambulia Tiro iliyo bara. Babeli yaanza mashambulizi ya miaka 13 kuteka mji wa bara wa Foeniki wa Tiro.

539 KK (kama miaka 2500 iliyopita)—Siro Mkuu ateka Babeli. Baada ya kifo cha Nebukadreza, Himaya kongwe ya Babeli yaanza kupoteza nguvu. Siro Mkuu ateka Babeli 539 KK, na kusitawisha Himaya ya Uajemi ya Kati.

538 KK (kama miaka 2500 iliyopita)—Siro Awaachilia Wayahudi kutoka Uteka wa Babeli. Baada ya kuteka Babeli,

98

Page 100:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Siro awapa uhuru wao kuondoka Babeli na kurudi Yuda. Ufalme wa Siro watawala juu ya Yuda na sehemu nyingi za Mashariki ya Kati, lakini Siro awapa watu uhuru zaidi wa desturi na wa kidini kuliko ulivyofanya ule wa Himaya Kongwe ya Babeli ya kwanza.

536 KK (kama miaka 2500 iliyopita)—Kazi yaanza kulijenga upya Hekalu. Baadhi ya Wayahudi wa Babeli warudi Yuda na kuanza kazi kwenye mwaka 536 KK kujenga upya Hekalu, ambalo lilikuwa limeharibiwa na Babeli kwenye mwaka 586 KK.

516 KK (kama miaka 2500 iliyopita)—Hekalu la pili lawekwa wakfu. Hekalu limejengwa la kuabudia, miaka 70 baada ya Wababeli kuliharibu mwaka wa 586 KK.

333 KK (kama miaka 2300 iliyopita)—Wayunani waanza kutawala juu ya Israeli. Wayunani, chini ya uongozi wa Alekisanda Mkuu, wawashinda majeshi ya Waajemi katika Makedonia mwaka 333 KK. Hii yaashiria kuanguka kwa Himaya ya Uajemi ya Kati na kuinuka kwa Himaya ya Uyunani.

332 KK (kama miaka 2300 iliyopita)—Alekisanda ateka Tiro (Himaya ya Foeniki). Alekisanda afanya vita kinyume na ngome za kisiwani za mji wa Foeniki wa Tiro. Achukua taka-taka kutoka huko bara ya Tiro na kujenga njia ya ya kuingilia kisiwani. Majeshi ya Alekisanda ndipo yateka ngome ya kisiwani, na kuimaliza Himaya ya Foeniki.

250 KK (kama miaka 2300 iliyopita)—Agano la Kale latafsiriwa kuja Kiyunani. Mtawala wa Uyunani awaagiza Wayahudi kutafsiri sehemu zote au sehemu fulani ya Agano la Kale kuja lugha ya Kiyunani. Tafsiri hiyo inaitwa “Septuagint”.

175 KK (kama miaka 2200 iliyopita)—Mtawala wa Uyunani Antiokusi Epifanesi awatesa Wayahudi. Mtawala wa Uyunani Antiokusi Epifanesi atawala Ashuri kuanzia kwenye mwaka 175 KK hadi kwenye mwaka 164 KK. Atawala juu ya Yuda na ajaribu kuharibu dini ya Kiyahudi. Pia alidhalilisha Hekalu.

164 KK to 63 KK (kama miaka 2200 iliyopita)—Wayahudi wanapata uhuru. Makabii, kundi la watu waliopigania uhuru wa Wayahudi, wapanga uasi kinyume na Uyunani na kustawisha mkondo wa kifalme wa Hasmonia, na pia enzi za mkondo wa kiutawala kwa sehemu zote za nchi ya Israelia kwa karibu miaka 100, kuanzia kunako mwaka 164 KK hadi 63 KK.

63 KK (kama miaka 2100 iliyopita)—Warumi wateka nchi ya Israeli. Baada ya kifo cha Alekisanda Mkuu, himaya ya Uyunani ikagawanyika na kuwa dhaifu zaidi. Kipindi hiki, Himaya ya Warumi ikawa inaongezeka nguvu zaidi na zaidi. Generali wa Kirumi aitwaye Pompi ateka madaraka juu ya Israeli.

Kama miaka 5 KK (kama miaka 2000 iliyopita)—Yesu azaliwa Bethlehemu. Yesu azaliwa katika mji wa Bethlehemu. Mtume Mathayo baadaye athibitishwa kwamba kuzaliwa kwa Yesu kulitimiliza unabii uliotolewa na nabii Mika, kama mika 700 kabla yake. (Ona Mika 5:2).

Kama miaka 25 BK (kama miaka 2000 iliyopita)—Yesu Aanza Huduma Yake. Yesu anakaribia umri wa miaka 30 anapoanza huduma yake. Ahubiri wokovu , atoa unabii, na kutenda miujiza . Ataja kwamba Yeye ndiye Masihi (Kristo) aliyetabiriwa na manbii wa Agano la Kale. Yesu aahidi wokovu na uzima wa milele kwa wale wamwaminio yeye (Ona Yohana 3:16, kama mfano). [ANGALIZO: Watu walio wengi hutaja mwanzo wa huduma ya Yesu hadharani kuwa ni mwaka 26 au 27 BK—Jonathan Menn]

Kama miaka 28 AD (kama miaka2000 iliyopita)—Yesu asulubiwa na kufufuka. Yesu ashitakiwa mashitaka ya uongo na kupelekwa kwa Pontio Pilato, mtawala wa Kirumi katika jimbo la Israeli, ili akasulubiwe. Yesu baadaye afufuka, kumaanisha arudi tena kwenye uhai, na wafuasi wake waanza kutangaza habari zake kwa wengine, kufanya Ukristo kuenea kwa haraka sana kila mahali katika ulimwengu wa Kirumi na hatimaye kuwa ndiyo dini ya kwanza kuenea duniani kote. [ANGALIZO: Watu walio wengi hutaja kusulubiwa kuwa ni mwaka 30 BK au 33 BK—Jonathan Menn]

70 AD (kama miaka 1900 iliyopita)—Warumi waangamiza Yerusalemu na Hekalu. Katika mwaka 70 BK, Jeshi la Kirumi, chini ya Tito, laangamiza Yerusalemu na Hekalu, kupoozesha maasi ya Israeli. Kulingana na mwana-historia Josefasi, karibu Wayahudi milioni 1.1 waliuawa. Wengine walichukuliwa kama watumwa.

Karne ya Kwanza AD (kama miaka 1900 iliyopita)—Biblia inakamilika. Wakati wa karne ya kwanza ya zama hizi, Agano Jipya, ambalo huelezea maisha na mafundisho ya Yesu Kristo, lakamilika. Maandiko ya Biblia (Agano la Kale na Agano Jipya) yafikia hatima yake. Huanzia nyakati za Musa, karibu miaka 3400 iliyopita. Yesu anakuwa, na anabakia, mada ya mwisho ya Biblia.

DIBAJI 3—MPANGILIO WA MUDA WA WAFALME NA MANABII WA ISRAELI NA YUDA

99

Page 101:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

Kulingana na K. Lawson Younger, 2006, OT 716—Vitabu vya Historia: Mpangilio wa Wafalme na Manabii wa Waebrania, jumbe zisizochapishwa. Deerfield, IL: Trinity Evangelical Divinity School, na New American Standard Bible, zilizoandikwa upya, 1999, “Watawala wa Israeli na Yuda” orodha, 336-37. Mwaka wa Kukadiriwa United Kingdom (Israel) Nabii1050 Sauli, miaka 40 (1050-1010): 1 Sam 9:15-35;

28:1-25; 31:1-13; 1 Nyak 10:1-141010 Daudi, miaka 40 (1010-970): 1 Sam 16:1-13;

2 Sam 1:1-1Waf 2:11; 1 Nyak 11:1-22:19970 Sulemani, miaka 40 (970-930): 1 Waf 1:11-11:43

1 Nyak 23:1-2 Nyak 9:31Ufalme Uliogawanyikana

Yuda (Ufalme wa Kus) Israeli (Ufalme wa Kask)930 Rehoboamu, miaka 17 (930-913): Yeroboamu I, mwaka 22 (930-

1 Waf 12:1-24; 14:21-31 909): 1 Waf 12:25-14:20913 Abijamu, 3 (913-910), mwaka wa 18

wa Yeroboamu: 1 Waf 15:1-8; 2 Nyak13:1-14:1

910 Asa, miaka 41 (910-869), mwaka wa 20 waYeroboamu: 1 Waf 15:9-24; 2 Nyak 14:1-16:14

909 Nadabu, miaka 2 (909-908), mwaka wa 2 wa Asa: 1 Waf 15:25-31

908 Baasha, miaka 24 (908-886), mwaka wa 3 wa Asa: 1 Waf 15:32-16:7; 2 Nyak 16:1-6

886 Ela, miaka 2 (886-885), mwaka wa 26 wa Asa: 1 Waf 16:8-14

885 Zimri, siku 7 (885), mwaka wa 27 wa Asa: 1 Waf 16:15-20Tibni, miaka 5 (885-880), huingiliana na Omri: 1 Waf 16:21-22Omri, miaka 12 (885-874), mwaka wa 27 wa Asa: 1 Waf 16:23-28

874 Ahabu, miaka 22 (874-853), mwaka wa 38 Eliya (870-850): wa Asa: 1 Waf 16:29-22:40 1 Waf 17-2 Waf

2:12, kwa Israeli872 Yehoshafati, miaka 25 (872-848) (alianza

kama mtawala mwenza na Asa; kutawala kamili kulianza 869): 1 Waf 22:41-50

853 Ahazia, miaka 2 (853-852), mwaka wa 17 wa Yehoshafati: 1 Waf 22:51-2 Waf 1:18

852 Yoramu, miaka 12 (852-841), mwaka wa 18 Elisha (850-800?):wa Yehoshafati: 2 Waf 1:17; 3:1-8:15 2 Waf 2:1-8:15;

13:14-21, kwa Israeli

848 Yehoramu, miaka 8 (848-841), mwaka wa 5 Obadia (848-841), hadiwa Yoramu: 2 Waf 8:16-24 Edomu

841 Ahazia, mwaka 1 (841), mwaka wa 11wa Yehu, miaka 28 (841-814): Yoramu: 2 Waf 9:29 2 Waf 9:30-10:36Atalia, miaka 7 (Malkia) (841-835): 2 Waf 11:1-21

835 Yoashi, miaka 40 (835-796), mwaka wa 7 Yoeli (830-815), hadiWa Yehu: 2 Waf 12:1-21; 2 Nyak 24: Yuda1-27

814 Yehoahazi, miaka 17 (814-798), mwaka wa 23 wa Yoashi: 2 Waf 13:1-9

798 Yehoashi, miaka 16 (798-782), mwaka wa 37 wa Yoashi: 2 Waf 13:10-25

796 Amazia, miaka 29 (796-767), Huingiliana na Uzia (Azaria), mwaka wa 2 wa Yehoashi: 2 Waf 14:1-22

793 Yeroboamu II, miaka 41 (793-753) (alianza kutawala kama mwenza na Yehoashi;

100

Page 102:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

kutawala kamili kulianza 782), mwaka wa 15 wa Amazia: 2 Waf 14:23-29

792 Uzia (Azaria), miaka 52 (792-740) (alianza Yona (782-746): 2 Wafkutawala kama mwenza na Amaziah; 14:25, kwa NinawiUtawala kamili 767), mwaka wa 27 wa (Ashuru)Jeroboam II: 2 Waf 15:1-7; 2 Nyak 26:1-23

Amosi (c. 765-755), kwaIsraeliHosea (c. 755-714), kwa Israeli

753 Zekaria, miezi 6 (753), mwaka wa 38 wa Uzia: 2 Waf 15:8-12

752 Shalumu, mwezi 1 (752), mwaka wa 39wa Uzia: 2 Waf 15:13-15Menahemu, miaka10 (752-742) (alitawala Samaria), mwaka wa 39 waUzia: 2 Waf 15:16-22 Peka, miaka 20 (752-732) (alitawala Gileadi; utawala kamili ulianza 740), 52 wa Uzia: 2 Waf 15:27-31

742 Pekahiah, miaka 2 (alitawala Samaria),Mwaka wa 50 wa Uzia: 2 Waf 15:23-26

740 Yothamu, miaka 16 (750-732) (alianzia Mika (740-700?), hadikama mtawala mwenza wa Uzia; utawala Yudakamili ulianza 740), mwaka wa 2 wa Peka: Isaya (739-691?), hadi 2 Waf 15:32-38 Yuda

735 Ahazi, miaka 16 (735-715, miaka 16 baada yamwaka wa mwisho wa Yothamu, 732), mwaka wa 17 wa Peka

732 Hoshea, miaka 9 (732-722): 2 Waf15:30; 17:1-41.

722 Israeli yaangukia kwa Waashuri na kuhamishwa.715 Hezekia, miaka 29 (715-686): 2 Waf 18:1-20:21686 Manase, miaka 55 (697-642) (alianza kama mtawala mwenza wa Hezekia; Nahumu (649-625?)

Utawala kamili ualianza 686): 2 Waf 21:1-18642 Amoni, miaka 2 (642-640): 2 Waf 21: 19-26640 Yosia, miaka 31 (640-609): 2 Waf 22:1-23:30 Zefania (635-625)

Yeremia (627-575)Habakuki (620?-610?)

609 Yehoahazi, miezi 3 (609): 2 Waf 23:31-33Yehoiakimu, miaka 11 (609-598): 2 Waf 23:34-24:7

605 Uhamisho wa 1 kwenda Babeli Danieli (605-536)598 Yekonia, miezi 3 (598-597): 2 Waf 24:8-17597 Uhamisho wa 2 kwenda Babeli

Zedekia, miaka 11 (597-586): 2 Waf 24:18-25:26 Ezekieli (597-581)586 Yerusalemu yaanguka kwa Babeli. Hekalu kuharibiwa. Miaka 70 ya utumwa

Babeli yaanza Babloni kuanza: 2 Waf 25:1-30; 2 Nyak 36:11-21539 Kuanguka kwa Babeli kwa Uajemi—(Belshaza, 539-530): Dan 5:1-31538 Tamko la Belshaza kuruhusu kurudishwa kwa watumwa na kujenga upya

Hekalu katika Yerusalemu: 2 Nyak 36:22-23; Ezra 1:1-4; 6:1-5.529 Kambisisi II (Mtawala wa Uajemi, 529-523)522 Dario I (Mtawala wa Uajemi, 522-486)520 Tangazo la Dario I kuruhusu kumalizia Hekalu: Ezra 6:6-12 Hagai (520-505)

Zekaria (520-487)515 Hekalu lawekwa wakfu upya Yerusalemu486 Kseso (Ahasuero) (Mtawala wa uajemi, 486-465)—Esta (Malkia)464 Artashasta I (Mtawala wa Uajemi, 464-424)458 Tangazo la Artashasta I kulikamilisha Hekalu huko Yerusalemu: Ezra 7:11-26445 Tangazo laf Artashasta I kuruhusu kujengwa upya ukuta wa Yerusalemu:

Neh 2:1-6424 Dario II (Mtawala wa Uajemi, 424-404) Malaki (420)404 Artashasta II (Mtawala wa Uajemi, 404-358)

101

Page 103:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

335 Dario III (Mtawala wa Uajemi, 335-331)331 Uajemi yaanguka kwa Aleksanda Mkuu.

DIBAJI 4—NABII ZA KIMASIHI CHACHE NA KUTIMIZWA KWAKE

Unabii Chanzo Katika AK Utimizwaji Katika AJ1. Kuzaliwa kwa uzao wa mwanamke Mwa 3:15 Math 1:20; Wagal 4:4 2. Kuzaliwa na bikira Isa 7:14 Math 1:18, 24-25; Luka 1:26-353. Uzao wa Ibrahimu Mwan 22:18 Math 1:1; Wagal 3:164. Kutokea kwa Isaka Mwan 21:12 Math 1:2; Luka 3:23, 34 5. Kutokea kwa Yakobo Hes 24:17 Math 1:2; Luka 3:23, 34 6. Kabila la Yuda Mwan 49:10 Math 1:2; Luka 3:23, 33; Heb 7:147. Kutoka kwa Yese Isa 11:1, 10 Math 1:6; Luka 3:23, 32 8. Kutoka kwa Daudi Yer 23:5; Ps 132:11 Math 1:1; 9:27; Luka 3:23, 31 9. Kuzaliwa bethlehemu Mik 5:2 Math 2:1-8; Luka 2:4-7; Yoh 7:4210. Kuweko kwake hata kabla Mik 5:2 Yoh 1:1-2; 8:58; 17:5; Wakol 1:1711. Kutangulia kwa mjumbe Isa 40:3; Mal 3:1 Math 3:1-3; 11:10; Luka 1:17; Yoh 1:2312. Ataitwa Bwana Zab 110:1 Math 22:43-4513. Ataitwa Imanueli Isa 7:14 Math 1:2314. Atakuwa nabii Kumb 18:15, 18-19 Math 21:11; Luka 7:16; Yoh 4:19; 6:14; 7:4015. Atakuwa kuhani Zab 110:4 Waeb 3:1; 5:5-616. Atatoa hukumu ` Isa 33:22 Yoh 5:30; 2 Tim 4:117. Atakuwa mfalme Zab 2:6; Zech 9:9 Math 21:5; 27:37; Yoh 18:33-3718. Anaitwa Mwana wa Mungu Zab2:7 Math 3:17; 16:16; 17:5; Luka 1:3219. Yeye ni nuru ya mataifa Isa 42:6; 49:6 Luka 2:32; Yoh 1:9; 8:12; 9:5; 12:4620. Roho Mtakatifu kukaa juu yake Isa 11:2; 42:1; 61:1 Math 3:16; Marko 1:10; Luka 4:1821. Wivu wa Bwana Zab 69:9 Yoh 2:15-1722. Huduma kuanza Galilaya Isa 9:1 Math 4:12-1723. Atenda miujiza Isa 35:5-6; 53:4 Math 8:14-17; 9:32-35; 11:4-5; Marko 7:33-3524. Afundisha kwa mifano Zab 78:2 Math 13:34-3525. Aingia Yerusalemu juu ya punda Zek 9:9 Math 21:6-11; Luka 35-3726. Aingia Hekaluni Mal 3:1 Math 21:1227. Kuhubiri masikini Isa 61:1 Math 11:5; Luka 4:18-2128. Kukataliwa na watu wake Zab 118:22; Isa 28:16 Math 21:42; Yoh 1:11; 7:48; 1 Petr 2:6-729. Kukataliwa na watu wa familia yake Zab 69:8 Marko 3:21; Yoh 7:530. Kuchukiwa bila sababu Zab 69:4; Isa 49:7 Yoh 15:2531. Kusalitiwa na rafiki Zab 41:9; 55:12-14 Math 10:4; 26:47-50; 13:21-27; Luka 22:19-2332. Kusalitiwa kwa vipande 30 vya fedha Zek 11:12 Math 26:15; 27:333. Fedha kutupwa katika nyumba ya

Mungu Zek 11:13 Math 27:534. Fedha kutolewa kwa shamba la

mfinyanzi Zek 11:13 Math 27:6-1035. Kuachwa na wanafunzi wake Zek 13:7 Math 26:31. 69-74; Marko 14:27, 5036. Kimya mbele za washitaki wake Isa 53:7 Math 27:12; Mdo 8:32-3537. Kupigwa na kutemewa mate Isa 50:6; 53:5 Math 26:67; 27:26; Marko 10:33-3438. Kudhihakiwa Zab 22:7-8 Math 27:31; Luka 22:63-6539. Mikono na miguu kutobolewa Zab 22:16; Zech 12:10 Luka 23:33; Yoh 20:25-2740. Kuteswa kwa dhambi za wengine Isa 53:5-6, 8, 10-12 Rum 4:25; 1 Wakor 15:341. Kufa pamoja na wakosaji Isa 53:12 Math 27:38; Marko 15:27-28; Luka 22:3742. Kuwaombea wafanya makosa Isa 53:12 Luka 23:3443. Kura kupigwa kwa ajili ya nguo zake Zab 22:18 Yoh 19:23-2444. Marafiki kukaa mbali naye Zab 38:11 Math 27:55-56; Marko 15:40; Luka 23:4945. Watu kutikisa vichwa vyao Zab 22:7 Math 27:3946. Watu kumwangalia Zab 22:17 Luka 23:3547. Augua kiu Zab 22:15; 69:21 Yoh 19:2848. Kupewa siki chungu Zab 69:21 Yoh19:28-29; Math 27:3449. Kulia kwa kuachwa na Mungu Zab 22:1 Math 27:4650. Kukabidhi roho yake kwa Mungu Zab 31:5 Luka 23:4651. Mifupa yake haikuvunjika Zab 34:20 Yoh 19:3352. Ubavu wake kutobolewa Zek 12:10 Yoh 19:34-3753. Moyo kuvunjwa Zab 22:14; 69:20 Yoh 19:3454. Giza juu ya nchi Amos 8:9 Math 27:4555. Kuzikwa katika kaburi la mtu tajiri Isa 53:9 Math 27:57-60

102

Page 104:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

56. Mwili haukuoza Zab 16:10 Yoh 20:1-18; Mdo 2:31; 13:35-3757. Kuketi mkono wa kuume wa Mungu Zab 110:1 Marko 16:19; Mdo 2:34-35; Waeb 1:3

DIBAJI 5—RAMANI ZA HIMAYA ZA ASHURU, BABELI, NA UAJEMI http://www.bible.ca/maps/maps-near-east-500BC.htm

DIBAJI 6—RAMANI YA HIMAYA YA RUMI & MAJIMBO YAKEhttp://www.bible.ca/maps/maps-roman-empire-peak-116AD.jpg

103

Page 105:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

DIBAJI 7—RAMANI YA KANAANI: SEHEMU 12 ZA MAKABILAhttp://www.bible-history.com/geography/maps/map_canaan_tribal_portions.html

DIBAJI 8—RAMANI YA UFALME ULIOUNGANA WA ISRAELIhttp://www.bible.ca/maps/maps-united-kingdom.htm

104

Page 106:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

DIBAJI 9—RAMANI YA FALME ZILIZOGAWANYIKANA ZA YUDA NA ISRAELIhttp://www.bible.ca/maps/maps-divided-kingdom.htm

DIBAJI 10—RAMANI YA ISRAELI NYAKATI ZA AGANO JIPYAhttp://www.bible-history.com/maps/palestine_nt_times.html

105

Page 107:  · Web view“Kwa maelezo ya Ki-Kristo, dunia kwa Mungu ni muundo, na dhana ni wokovu wa dunia na mwanadamu aliyeanguka; vipengele vyake ni maelezo ya Biblia, kuanzia uumbaji, uteuzi,

Copyright © 2009-2011 by Jonathan Menn. All rights reserved.

106