wizara ya kilimo, mifugo, uvuvi na unyunyizaji (moalfi) · 4. mfumo wa vmgf utatumiwa na idara ya...
TRANSCRIPT
JAMHURI YA KENYA
WIZARA YA KILIMO, MIFUGO, UVUVI NA UNYUNYIZAJI
(MoALFI)
IDARA YA KITAIFA YA UVUVI, KILIMO CHA MAJINI NA UCHUMI
WA BAHARINI (SDFA-BE)
RASIMU YA MWISHO MFUMO WA MAKUNDI
YALIYOTENGWA NA KUTELEKEZWA (VMGF)
MRADI WA MAENDELEO YA KIJAMII NA KIUCHUMI WA
UVUVI WA BAHARINI KENYA (KEMFSED) WARSHA YA KUHALALISHA
MOMBASA
JUNI 19 - 20, 2019
Utangulizi
1. Mfumo huu wa Makundi ya Waliotengwa na Kutelekezwa (VMGF) umeandaliwa kwa ajili ya
Maendeleo ya Uchumi wa Jamii katika Uvuvi wa Baharini nchini Kenya (KEMFSED) na
utafadhiliwa na Benki ya Dunia. Umebuniwa kutokana na matokeo na mapendekezo ya utafiti
wa Kuchunguza Jamii ambao ulifanywa kwa ajili ya mradi huu katika Makundi ya
Waliotengwa na Kutelekezwa wanaoishi katika maeneo yaliyo karibu na kingo za maji katika
Pwani ya Kenya. Kwa sababu mikakati ya mradi unaopendekeza itatekelezwa katika maeneo
ambapo kuna Wenyeji (IP) ambao wanarejelewa kuwa Makundi ya Waliotengwa na
Kutelekezwa (VMG)1 nchini Kenya, sera ya ulinzi ya Benki ya Dunia (WB) ya OP/BP 4.10
imerejelewa na mfumo wa VMGF umetayarishwa ili kuongoza utekelezaji wa mradi huu.
2. Mradi wa KEMFSED unalenga kuimarisha uchumi na maisha ya wapwani kutokana na uvuvi
wa baharini na kilimo cha maji huku ikidumisha ubora wa mfumo husika wa ekolojia kupitia
utaratibu unaoshirikisha jamii. Imebuniwa kutokana mafunzo tuliyopata kupitia utekelezaji wa
Mradi wa Maendeleo ya Pwani ya Kenya (KCDP) ambao pia ulifadhiliwa na Benki ya Dunia
na mikakati mbalimbali iliyotekelezwa na jamii ambayo ililenga kuboresha maisha ya makundi
ya VMG katika kaunti za pwani ya Kenya.
Malengo ya Mfumo wa Makundi ya Waliotengwa na Kutelekezwa (VMGF)
3. Lengo la mfumo wa VMGF ni kuongoza muundo, mpangilio na utekelezaji wa mikakati ya
KEMFSED ambayo huenda ikaathiri makundi ya VMG katika maeneo yaliyopendekezwa
kwenye mradi. Mfumo wa VMGF unatokana na kifungu cha OP 4.10 cha Benki ya Dunia
pamoja na kanuni na sheria husika za Serikali ya Kenya. Kifungu cha OP 4.10 hurejelewa
wakati ambapo kuna uwezekano wa makundi ambayo yanatimiza vigezo vya kifungu cha
Benki ya Dunia cha OP 4.10 “yanayoishi au yana uhusiano wa pamoja na eneo ambako mradi
utafanyika.” Mfumo wa VMGF inajumuisha aina za shughuli na mikakati iliyopendekezwa;
athari nzuri na mbaya kwenye makundi ya VMG; mbinu za kuhakikisha mashauriano
yanayoeleweka, ya wazi na yanayopangwa mapema; mipango ya taasisi ya kukagua shughuli
zinazoendelezwa katika mradi na kukagua na kubaini uwepo wa makundi yaVMG katika eneo
la mradi; mbinu za kufuatilia na kuripoti, na kufahamisha makundi yaVMG kuhusu mbinu
hizo.
4. Mfumo wa VMGF utatumiwa na Idara ya Kitaifa ya Uvuvi na Uchumi wa Baharini, mashirika
ya kutekeleza mradi wa KEMFSED na Benki ya Dunia ili kuhakikisha kuwa vifungu vya Sera
ya Utendaji wa Benki ya Dunia (OP) 4.10 vinazingatiwa katika utekelezaji na usimamizi wa
mradi huu. Hatua hii itahakikisha kuwa athari mbaya zinatambuliwa kikamilifu na
kushughulikiwa, ilhali athari nzuri zinaendelezwa kwenye makundi ya VMG.
Vipengee vya Mradi
1 VMG ni jamii ambazo zinalengwa na mradi wa KEMFSED na zinatimiza masharti na vigezo vya Benki ya Dunia kwa mujibu wa kifungu cha OP 4.10 na vigezo vya Serikali ya Kenya (GoK) vya “jamii zilizotengwa” na za “wachache” kwa mujibu wa Katiba ya Kenya.
5. Vipengee vya Mradi vimebuniwa ili kuafikiana na Mfumo mpana wa Uchumi wa Baharini
nchini Kenya na mchakato unaoendelea wa ugatuzi. Vipengee vikuu na vidogo vilibainishwa
na kupangwa ili kuboresha malengo, utaratibu, ujumuishaji na usawazishaji wa dhana za
miundombinu pamoja na usaidizi wa kiufundi/programu, mafunzo na kukuza uwezo
wafanyakazi.
Mchoro 1: Nadharia ya Mabadiliko ya Mradi wa KEMFSED
Kipengee cha 1 – Kuboresha Uongozi na Usimamizi wa Uvuvi wa Baharini.
6. Hatua hi italenga kuboresha usimamizi wa uvuvi wa baharini katika maeneo yanayokaribia
kingo za maji nchini Kenya.
a) Kipengee kidogo cha 1.1: Kuboresha uongozi wa uvuvi na uchumi wa baharini. Kipengee
hiki kidogo kitalenga kuboresha uongozi na usimamizi wa uvuvi, kukagua sera za uvuvi
na sheria husika na kuimarisha mbinu za ufuatiliaji na uchunguzi wa mradi. Kipengee hiki
kidogo pia kitalenga utafiti unaotakikana ili kuimarisha usimamizi wa uvuvi baharini,
ikiwa ni pamoja na kutengenezwa kwa Mfumo wa Ufuatiliaji na Habari za Uvuvi (FIMS)
ambao ni thabiti na utarahisisha hatua ya kufikia habari ili kuboresha usimamizi wa
shughuli za uvuvi. Katika maeneo yakayobainishwa, uvuvi maalum utalengwa kupitia
mikakati mahususi kulingana na Mipango ya Kuboresha Uvuvi (FIP), ikiwa na nia ya
kubadilisha uvuvi huu ili uweze kusimamiwa vizuri kwa nia ya kuhakikisha manufaa ya
kudumu katika jamii husika. Mradi huu pia utasaidia kuendeleza Hatua ya Mipango za
Kitaifa za kukabili uvuvi wa papa, ndege na Uvuvi Haramu, Usioripotiwa na Usiodhibitiwa
(IUU).
b) Kipengee kidogo cha 1.2: Kuboresha usimamizi wa uvuvi unaokaribia ufuko. Kipengee
hiki kitaimarisha usimamizi wa shughuli za uvuvi zinazofanyika karibu na ufuko na
utekeleza wa Mipango ya Usimamizi wa Uvuvi (FMP). Kwa kushirikiana na FMP za
kitaifa kwa ajili ya uvuvi maalum, maeneo mapya Yaliyounganishwa na Kusimamiwa kwa
Pamoja (JCMA) yatabuniwa. Usimamizi wa maeneo yaliyopo utaimarishwa. Mradi huu
pia utaendeleza utekelezaji wa Maeneo Yanayosimamiwa kwa Pamoja (CMA) ikiwa ni
pamoja na utekelezaji wa mikakati ya Ufuatiliaji, Udhibiti na Uchunguzi (MCS) na utoaji
wa vifaa vinavyotakikana na usaidizi wa kiufundi kwa ajili ya MCS.
c) Kipengee kidogo cha 1.3: Uendelezaji wa miundombinu kwa ajili ya usimamizi wa uvuvi.
Kipengee hiki kidogo kinajumuisha uendelezaji wa miundombinu ambayo inalenga
kusaidia usimamizi wa uvuvi katika viwango vya kitaifa na kaunti. Hususan, inajumuisha
jengo la ofisi ya Huduma za Uvuvi Kenya (KeFS) mjini Nairobi na Kituo cha Kitaifa cha
Mafunzo na Rasilimali za Baharini katika Kaunti ya Kwale. Mifano ya miundombinu ya
uvuvi inajumuisha kuboresha viwango vya ofisi za uvuvi za kaunti na kupanua chuo cha
Mombasa Bandari Maritime Training College.
Kipengee cha 2 – Kuwezesha Uwekezaji wa Kudumu katika sekta ya Uvuvi wa Baharini na Kilimo
cha Majini
7. Hatua hii itabuni Huduma ya Maendeleo ya Biashara Ndogo Ndogo na za Wastani
(SME/SME-DS), zinazotoa huduma za kitaalamu kwa wajasiriamali, SME na makundi ya
serikali katika kaunti za pwani,. Pia itawezesha kuongezeka kwa faida inayotokana na uvuvi
na kilimo cha baharini kwa kuwekeza katika miundombinu ya umma kama vile barabara,
umeme na maji, inayohusiana na utaratibu wa kuboresha bidhaa na uwekezaji wa binafsi.
a) Kipengee Kidogo cha 2.1: SME-DS Katika Jamii za Pwani. Tutahusisha SME-DS
itakayojumuisha timu ya wataalamu wa SME wanaoshughulikia maendeleo,
watakaopatikana katika jamii za wavuvi zinazoishi katika pwani ya Kenya. Wataalamu
hawa wataendeleza huduma zao kwa Vitengo vya Usimamizi wa Fuo (BMU) na wenyeji
wa pwani wanaotaka kuanzisha au kukuza biashara inayohusiana na uvuvi. Pia, watatoa
usaidizi wa kiufundi unapotakikana, huduma za uchanganuzi, mafunzo kwa wafanyakazi
na kutoa ushauri mbalimbali. SME-DS itabaini pia matatizo au hatari za kimfumo ambazo
zinazuia kutelelezwa kwa miradi inayotarajiwa na itapendekeza hatua za kusuluhisha
zinazotakikana ili kuondoa au kupunguza athari za hatari hizo. Itajumuisha pia mafunzo na
maelekezo ya kufikia njia mpya na zilizopo za kupata mikopo. Kipengee hiki kidogo pia
kitasaidia SME ambazo zinataka kuanzisha huduma ili kuboresha na kufanya utaratibu wa
kutengeneza vyakula vya baharini uwe wazi zaidi. Zaidi ya hayo, mradi utatoa usaidizi wa
kiufundi ili kuongoza mchakato wa kuanzisha na kuendeshwa kwa Mamlaka ya Kenya ya
Soko la Samaki.
b) Kipengee Kidogo cha 2.2: Kuboresha Miundombinu Inayohusiana na Uvuvi na Kilimo
cha Majini kwa ajili ya kuendeleza Utaratibu wa Kutayarisha Bidhaa. Kipengee hiki kidogo
kitalenga mapengo yanayobainishwa na kaunti katika miundombinu ya umma (maji,
umeme, usafiri) ambayo inazuia nafasi za uwekezaji wa binafsi katika uvuvi wa mabahari
na Kilimo cha Baharini. Ili kuhakikisha kuwa uwekezaji wote utathibitishwa vizuri,
kuendeleza uwekezaji wa binafsi na kupunguza uwezo wa kuvua samaki kupita kiasi,
miundombinu yote ya umma inayohusiana na utaratibu wa kutayarisha bidhaa
inayopendekezwa na kaunti itatokana na mpangilio na ramani ya maendeleo ya
miundombinu ya Kilimo cha Baharini na uvuvi katika kaunti. Mabadiliko ya anga
yanayohusiana na hatari yatazingatiwa wakati wa kuanzisha uwekezaji wote wa
miundombinu.
Kipengee cha 3 – Riziki na Uimarishaji wa Jamii za Pwani. (Dola za Marekani milioni 30)
8. Kipengele hiki kitalenga kuimarisha maisha ya familia maskini katika jamii za pwani, kama
njia ya kijitegemea na pia kuwasaidia wavuvi kutii masharti ya usimamizi wa uvuvi. Mbinu ya
jumla inayolenga njia za ziada za kuendeleza maisha itafuatwa, kwa kiasi fulani kupitia
kuanzisha ushirikiano wa kimkakati na biashara za kifedha zilizopo au biashara mpya
zinazotumia mifumo ya kilimo ya kandarasi katika kilimo cha majini au kilimo cha kawaida
ili kuwasaidia watu wanaokuza bidhaa ndogo ndogo. Kwa njia ya jumla zaidi, miradi midogo
ya kujipatia riziki, inayotekelezwa na watu mahususi au makundi ya biashara ndogo ndogo,
itafadhiliwa kupitia utoaji wa ruzuku, usaidizi wa kiufundi na mafunzo ya ujuzi na ya biashara.
a) Kipengee Kidogo cha 3.1: Kuimarisha Hali ya Maisha ya Jamii za Pwani. Kipengee hiki
kidogo kinajumuisha ufadhili wa ruzuku unaosaidia watu wanaotimiza masharti kupitia
njia tatu zilizobainishwa: i) Ruzuku za kujipatia riziki kwa wakulima wa kiwango cha chini
wanaofanya miradi midogo, ambao wametimiza masharti; ii) Ruzuku kwa ajili ya miradi
midogo ya jamii na mazingira (mtaji asili); na iii) Ruzuku za kuongeza mtaji kwa makundi
ya akiba na mikopo vijijini (VSL).
b) Kipengee Kidogo cha 3.2: Huduma za Usaidizi katika Kuendeleza Uwezo wa
Wafanyakazi na Kuboresha Riziki. Vipengee hivi vidogo ambavyo vitatekelezwa na
kaunti mahususi, vitatoa aina mbalimbali za huduma za usaidizi na kukuza uwezo wa
wafanyakazi katika makundi yanayolengwa ambayo yanatarajiwa kuanzisha shughuli
zinazotekelezwa chini ya kipengee kidogo cha 3.1 ikiwa ni pamoja na: i) Kutoa Huduma
na Usaidizi wa Kiufundi (TA) ili kutambua na huduma ili kubaini watakaopokea ruzuku
na kusaidia katika maandalizi, usimamizi na uchunguzi wa miradi midogo; ii) Kutoa
mafunzo ya ujuzi na biashara kwa watakaopokea ruzuku na wafanyabiashara wengine
wadogo wadogo; iii) Mpango wa Akiba na Mikopo Vijijini (VSL); na iv) Ufadhili wa
masomo rasmi, mafunzo ya kiufundi na elimu ya shule.
Kipengee cha 4 – Usimamizi wa Mradi.
9. Kipengee hiki cha 4 kitatoa usaidizi waziada wa kifedha katika usimamizi wa miradi katika
viwango vya kitaifa na kaunti ili kuhakikisha usimamizi na utekelezaji unaofaa wa shughuli za
miradi. Hususan, itasaidia kuchunguza na kusimamia mradi ikiwa ni pamoja na kuwezesha
Kamati ya Kitaifa ya Kuendeleza Miradi (NPSC) na Kamati ya Kutoa Ushauri wa Kiufundi
kwenye Mradi (PTAC); kuanzisha na kuendeleza Kitengo cha Usimamizi wa Mradi (PCU)
katika kiwango cha kitaifa na Vitengo vya Kutekeleza Mradi (PIU) katika kiwango cha kaunti,
ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa, usimamizi udhamini, ikijumuisha uhasibu na ukaguzi wa
hesabu za ndani/nje; mifumo ya kuhakikisha na kudhibiti ubora, usimamizi wa ulinzi wa jamii
na mazingira; na ukaguzi wa kiufundi kadri inavyotakikana. Kipengee hiki pia kitatoa ufadhili
wa kutayarisha na kutekeleza mikakati ya mawasiliano na utekelezaji wa mfumo wa
Kutathmini na Kufuatilia. Mfumo wa Kutathmini na Kufuatilia (M&E), ambao unahitaji
kutekelezwa ili kurekodi data kuhusu hatua za kifedha na hali halisi, utendaji wa shirika la
utekelezaji na mashirika mengine ya kutoa huduma, na matokeo yatakayopatikana kwa njia za
matumizi na mafanikio. Vile vile, itasaidia ubunifu wa Mbinu za Kushughulikia Malamiko na
kuhakikisha kuwa wananchi wanashirikishwa.
Eneo la Mradi
10. Mradi huu utatekelezwa katika sehemu tano zinazokaribia kingo za maji katika kaunti za
Kwale, Mombasa, Kilifi, Lamu na Tana River; kwenye kaunti ndogo za Matuga, Kinango,
Msambweni, Lunga Lunga, Kilifi Kusini, Kilifi Kaskazini, Malindi, Magarini, Lamu
Magharibi, Lamu Mashariki, Tana Delta/Garsen, Changamwe, Nyali, Kisauni, Jomvu, Likoni,
Mvita.
11. Mahali kwenye mradi ambapo jamii ya VMG inaishi na ambapo kifungu cha sera ya Benki ya
Dunia cha OP.4.10 kitarejelewa wakati wa mradi ikijumuisha; Wadi ya Pongwe/Kikokeni
(Visiwa vya mukwiro na wasini na kijiji cha Tswaka) katika kaunti ndogo ya Lunga Lunga,
wadi ya Ramisi katika kaunti ndogo ya Msambweni na Samburu/Chengoni, Kasemeni, wadi
za Mackinon Road katika kaunti ndogo ya Kinango zote zinapatikana katika kaunti ya Kwale;
Dabaso na wadi ya Watamu katika kaunti ya ndogo ya Kilifi Kaskazini, Maarafa, wadi za
Gongoni na Adu katika kaunti ndogo ya Magarini zote zinapatikana katika kaunti ya Kilifi;
wadi za Kiunga na Basuba katika kaunti ndogo ya Lamu Mashariki na wadi za Hindi,
Mkunumbi, Witu na Mkomani katika kaunti ndogo ya Lamu Magharibi katika kaunti la Lamu
na Kipini katika kaunri ndogo ya Garsen/Tana Delta, kaunti ya Tana River. Vikundi vya VMG
ambavyo vilijumuishwa katika uchunguzi huu vilikuwa; Wakifundi, Wavumba, Watshwaka,
Washiratzi, Watha katika Kwale (kaunti ndogo ya Kinango) na kaunti ya Kilifi; Aweer/Boni
na Saanye katika kaunti ya Lamu na Wasaanye wanaoishi katika wadi ya Kipini katika kaunti
ndogo ya Tana Delta, kaunti ya Tana River.
Miradi Midogo ambayo inaweza kufadhiliwa chini ya mradi wa KEMFSED kulingana na vipengele
vya Mradi
12. Kipengee cha 1 – Usimamizi na udhibiti wa uvuvi wa baharini na rasilimali za majini ambao
unalenga kuimarisha udhibiti wa kilimo cha majini na uvuvi wa baharini ili kuzuia matukio ya
kuvua samaki kupitia kiasi na kudumisha au kuboresha ongezeko la bidhaa na kukuza hadhi
ya mfumo wa ekolojia husika. Kipengee kidogo cha 1 kitalenga kusimamia na kuimarisha
taasisi ili kuhakikisha kuwa rasilimali za kilimo cha majini na uvuvi zinalindwa katika
muktadha wa kutekeleza mfumo wa uchumi wa baharini. kipengee kidogo cha 2 kitalenga
uimarishaji wa Mifumo ya Mawasiliano ya Uvuvi (FIS) ili kuhakikisha upatikanaji wa habari
za sekta zote kwa ajili ya kuwasiliana kuhusu umuhimu wa sekta ya kilimo cha majini na uvuvi
katika kuleta maendeleo kwenye maeneo yote ya pwani. Kipengee kidogo cha 3 kitalenga
kuboresha usimamizi wa uvuvi wa kiwango kidogo kidogo unaofanyika ufuoni. Kipengee
kidogo cha 4 kitalenga kuboresha usimamizi wa uvuvi unaofanyika maeneo yaliyo mbali na
ufuo. Utekelezaji wa Mipango ya Kuboresha Uvuvi (FIP) na usaidizi wa kubadilisha sekta ya
uvuvi ili kuboresha usimamizi, utazingatia jinsi makundi ya VMG yatakavyoathiriwa na
mabadiliko katika usimamizi ambayo yanaweza kujumuisha uanzishaji wa kanuni, masharti
na miundo mipya ambayo znaweza kuathiri kabisa kushiriki kwa makundi ya VMG katika
shughuli za uvuvi kutokana na kiwango cha chini cha elimu, matatizo ya hesabu na kiwango
kidogo cha kujishirikisha katika shughuli za uchumi wa uvuvi, ingawa kuna uwezo wa
kuboresha jinsi wanavyoweza kushirikishwa katika uvuvi karibu na ufuo unaofanywa na
wanaume wa VMG na shughuli za kuboresha hatua za wanawake kutayarisha samaki, kama
vile biashara za mama karanga, kung'oa mwani na shughuli za burudani kwenye ufuo.
Mojawapo ya miundo hii ya usimamizi ni Kuanzisha Maeneo Yaliyounganishwa na
Kusimamiwa kwa Pamoja (JCMA) ambayo yanajumuisha wenyeji kupitia mpango wa
kupendelea wenyeji. Mashauriano yatafanyika ili kutathmini uwezekano wa athari ya miundo
mipya iliyotekelezwa ya udhibiti wa uvuvi kwenye jamii za VMG. Mbinu za kujumuisha
makundi ya VMG pamoja na wenyeji katika miundo ya udhibiti zitajadiliwa kupitia mikutano
ya mashauriano na kukubaliwa na pande zote kabla ya kutekeleza miundo mipya au kuimarisha
miundo iliyopo ya udhibiti ambayo inafaa ili kutimiza malengo ya mradi wa KEMFSED. Zaidi
ya hayo, tutaangazia zaidi miundo iliyopendekezwa ambayo inalenga kuboresha usimamizi wa
uvuvi wa kiwango kidogo au unaofanyika karibu na ufuo kwa sababu hii ndiyo shughuli ya
uvuvi inayofanywa na makundi ya VMG katika pwani ya Kenya.
13. Kipengee cha 2 – Kuendeleza uwekezaji katika uvuvi wa baharini na kilimo cha majini ili
kuwezesha utumiaji bora na kuongeza thamani kwa rasilimali kwa kuongeza kiasi cha
uwekezaji katika sekta ya kilimo cha majini na uvuvi wa baharini. Kipengee kidogo cha 1
kitalenga kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji wa sekta ya binafsi katika uvuvi na
kilimo cha majini kupitia Huduma za Maendeleo ya Biashara za Wastani na Ndogo Ndogo
(SME/SME-DS). SME-DS zitatoa huduma za kitaalamu kwa wajasiriamali, SME na makundi
ya serikali katika kaunti za pwani. Kutakuwepo na wataalam wa kuendeleza huduma za
Vitengo vya Usimamizi wa Ufuo (BMU) na wenyeji wa pwani wanaotaka kuendeleza au
kukuza biashara zinazohusiana na uvuvi. Pia, watatoa usaidizi wa kiufundi unapotakikana
kupitia juhudi za kuboresha ujuzi wa wafanyakazi, ambazo zitajumuisha huduma za mafunzo.
Utekelezaji wa shughuli katika kipengee hiki kidogo utaanza kwa kutathmini kiwango cha
uwakilishaji wa makundi ya VMG, kwa wanaume au wanawake katika BMU. Uendelezaji wa
uwekezaji katika uvuvi wa baharini utahitaji pia juhudi za kuboresha ujuzi wa wafanyakazi
kwa lengo la kubadilisha mitazamo ya jamii za VMG ili kuchukulia shughuli za uvuvi kama
uwekezaji huku wakitarajia kupata faida ikilinganishwa na mtazamo wa sasa wa jamii ambapo
shughuli za uvuvi katika fuo za pwani zinafanywa na jamii za VMG kama njia ya kupata riziki
tu. SME-DS itabaini pia matatizo au hatari za kimfumo ambazo zinazuia kutelelezwa kwa
miradi inayotarajiwa na itapendekeza hatua za kusuluhisha zinazotakikana ili kuondoa au
kupunguza athari za hatari hizo. Tutachukua tahadhari ili kuhakikisha kuwa tathmini za
matatizo au hatari za kimfumo za kuzuia utekelezaji wa mradi inafanyika katika njia inayofaa
tamaduni ya wanajamii wa VMG bila kupoteza utambulisho wao wa kitamaduni. Itajumuisha
pia mafunzo na maelekezo ya kufikia njia mpya na zilizopo za kupata mikopo. Kipengee hiki
kidogo pia kitasaidia SME ambazo zinataka kuanzisha huduma ili kuboresha na kufanya
utaratibu wa kutengeneza vyakula vya baharini uwe wazi zaidi. Zaidi ya hayo, mradi utatoa
usaidizi wa kiufundi ili kuongoza mchakato wa kuanzisha na kuendeshwa kwa Mamlaka ya
Kenya ya Soko la Samaki. Ufikiaji wa soko la samaki chini ya Mamlaka ya Soko la Samaki
nchini Kenya na masharti ya utaratubu wa utayarishaji katika ufikiaji kama huo yatakuwa
sehemu ya kanuni chini ya hatua ya kupendelea wenyeji ili kuwezesha jamii za VMG kufikia
huduma. Shughuli za SME-DS zitategemea SME zilizobainishwa, ambazo jamii za VMG
zinafanya jinsi itakavyobainishwa katika utafiti wa Kuchunguza Jamii za VMG kama vile
kujihusisha katika biashara za kiwango kidogo katika maeneo kuweka samaki na maeneo
yenye samaki wengi, shughuli za watalii kutokana na vijana, biashara ya korosho na nazi na
shughuli za kilimo cha mwani.
14. Kipengee kidogo cha 2 kitaboresha miundombinu inayohusiana na uvuvi na Kilimo cha
Baharini ili kuwezesha uongezaji wa thamani ya bidhaa. Kaunti hii ndogo italenga mapengo
yaliyobainishwa na kaunti katika miundombinu ya msingi ya umma kama vile maji, umeme
na usafirishaji, ambayo inazuia nafasi za uwekezaji wa binafsi katika uvuvi na Kilimo cha
Baharini. Miundombinu yote ya umma inayohusiana na michakato ya kuongeza thamani ya
bidhaa, itakayopendekezwa na kaunti itatokana na mpango na ramani ya maendeleo ya
miundombinu ya uvuvi na Kilimo cha Baharini katika kaunti. Hii itaunganishwa na Mipango
ya Maendeleo Iliyojumuishwa katika Kaunti (CIDP) maeneo ya kaunti zinazolengwa
yanayokaribia kingo za maji. Juhudi zitatekelezwa ili kuhakikisha mipango na mipangilio ya
maendeleo ya uvuvi na Kilimo cha Baharini inajumuisha kwa njia ya wazi maeneo/wadi
ambazo VMG wanaishi. La muhimu pia ni kuendeleza miundombinu ya maji ili iwafae kwa
njia ya wazi wanajamii wa VMG, katika mpango uliojumuishwa kupitia hatua za kupendelea
wenyeji. Jamii za VMG zililalamika wakati wa utafiti wa kuchunguza jamii, kwamba kulikuwa
na miradi ya maji ambayo ilipitia maeneo yao lakini hawakufaidika kutokana na miradi hiyo
kwa kufungua maeneo ya kuuza maji ili kuhudumia jamii za VMG jinsi ilivyofanyika katika
jamii jirani za Mijikenda.
15. Kipengee cha 3 – Kuboresha Riziki inayotokana na Kilimo cha Majini na Uvuvi wa Baharini
kwa jamii zinazoishi pwani, ambayo inalenga kupitia mbinu ya jumla, kuleta manufaa ya
kiuchumi na kijamii ambayo jamii za pwani zitapata kupitia utumiaji wa kudumu wa rasilimali
za baharini. Uendelezaji wa njia za ziada za kupata riziki kupitia mchakato wa kubuni ushirika
wa kimkakati na biashara mpya za kifedha au au zilizopo, kwa kutumia mifumo ya kilimo cha
kandarasi cha majini au kilimo cha kawaida ambacho kinawafaidi wakulima wadogo wadogo,
itakuwa sehemu ya shughuli za kipengee hiki. Juhudi za wazi zitafanyika ili kuwezesha jamii
za VMG zishiriki na zipate manufaa kutokana na miradi midogo ya kupata riziki inayofanywa
na makundi mahususi ya VMG au makundi madogo ya biashara kupitia uanachama kwenye
VMG. Katika hali ambapo usaidizi kama huo unatolewa kwa vikundi vya biashara kupitia
uanachama kwenye VMG pamoja na wanachama wa kikundi kikubwa cha wenyeji, mbinu za
ndani zitabainishwa katika uanachama wa kikundi uliojumuishwa ili kuhakikisha kuwa VMG
zilizo ndani ya vikundi zinanufaika kupitia utoaji wa ruzuku, usaidizi wa kiufundi na mafunzo
ya ujuzi na biashara, pamoja na wanachama wengine wa kundi. Hatua muhimu ya utekelezaji
katika kipengee hiki itakuwa kurekodi kwa njia ya wazi kuwepo kwa mpango wa Akiba na
Mikopo Vijijini (VSL) miongoni mwa VMG na ufaafu wa kupata manufaa kutokana na
shughuli za kipengee cha tatu cha mradi wa KEMFSED. Ili kufanikisha mbinu inayojumuisha
jamii kupata maendeleo yanayotarajiwa chini ya mradi wa KEMFSED, tutabuni kigezo
ambapo VSL au makundi ya Jamii yanayotuma ombi, yanapaswa kuonyesha kuwepo kwa
wanachama wa VMG miongoni mwa wanachama wengine wa jamii. Tunastahili kuwa makini
kuzuia ujumuishaji wa wanachama wa jamii jirani wanaojifanya kuwa wawakilishi wa VMG
na kutenga wawakilishi halisi wa VMG kwenye vikundi vinavyozingatiwa kupata ruzuku na
kuboresha uwezo wa wafanyakazi. Kigezo cha kuchagua VMG katika mashirika makubwa ya
jamii kitabuniwa kupitia mchakato wa mashauriano wakati wa kubuni VMGP na kujumuisha
VMGP katika mpango wa utekelezaji wa miradi mikubwa ya KEMFSED.
16. Kipengele cha 4 –Kipengee hiki kinalenga usimamizi wa mradi ambao unajumuisha uzinduzi
na utekelezaji wa kamati ya mradi, wadhamini na ulinzi wa jamii na mazingira na ufuatiliaji
na kutathmini mradi. Utekelezaji unaofaa wa ulinzi wa kijamii na kimazingira unaobuniwa na
KEMFSED utahakikisha kushirikishwa na kujumuishwa kwa jamii ya VMG katika shughuli
za mradi.
17. Kutokana na matokeo ya utafiti wa kuchunguza jamii na ukaguzi wa mpango wa utekelezaji
wa mradi wa KEMFSED, kuna uwezekano wa kupendekeza miradi kadhaa midogo. Kuna
uwezekano kuwa miradi hii midogo inaweza kupendekezwa ili kufathiliwa chini ya vipengee
vitatu vya mradi wa KEMFSED ambavyo vinajumuisha; Udhibiti Bora wa Uvuvi na Uchumi
wa Baharini, Kuboresha Usimamizi wa Uvuvi Karibu na Fuo, Kuendeleza Miundombinu ya
Usimamizi wa Uvuvi chini ya kipengee cha kwanza. Miradi midogo inayoweza kubuniwa
chini ya kipengee hiki italenga kuzuia matendo ya kuvua samaki kupita kiasi, uvuvi haramu
na shughuli za uvuvi ambazo haziripotiwi katika Fuo za Bahari ya Hindi.
18. Baadhi ya shughuli za miradi midogo ambazo zitapendekezwa chini ya kipengee hiki kidogo
zinaweza kujumuisha; kuzuia matendo ya kuvua samaki kupita kiasi, kudumisha uzalishaji wa
samaki na kuboresha mfumo husika wa ekolojia. VMG zinaweza kunufaika kutokana shughuli
za kuvua samaki kupita kiasi kupita shughuli za ‘mama karanga’. Kuna jamii za VMG ambazo
zinahusika na uhifadhi wa msitu wa mikoko ambayo inatambulika kuwa maeneo muhimu ya
kudumisha ukuzaji wa samaki na mfumo wa ekolojia ya bahari. Juhudi za kuboresha uwezo
wa wafanyakazi zinazolenga kuimarisha shughuli za miradi midogo chini ya kipengee hiki
kidogo zinaweza kufanywa katika lugha ya Kiswahili ambayo inaeleweka na jamii zote za
VMG. Zaidi ya hayo, shughuli nyingine za miradi iliyo chini ya kipengee hiki zinaweza
kujumuisha kuimarisha usimamizi wa uvuvi unaodumu na utumiaji wa rasilimali za baharini
na inaweza kuhusisha uimarishaji wa taasisi za usimamizi na kubuni masharti mapya au
kuendeleza masharti yaliyopo yanayohusu shughuli za uvuvi ambayo hayawezi kuathiri riziki
ya watu mahususi wanaotumia boti za kuvuta nyavu, neti au mikuki na pia jamii nzima ambayo
inategemea uvuvi kwa jumla. Hii itajumuisha shughuli za jamii za VMG ambao ni mama
karanga wanaofanya biashara ya samaki katika maeneo ya kuweka samaki, zinazotegemea
kiwango cha samaki waliovuliwa. Kuna uwezekano kuwa shughuli za mradi mdogo
zitajumuisha kuboresha/kupanua miundombinu ili kuboresha usimamizi wa uvuvi kando na
maeneo ya kuweka samaki, maeneo yenye samaki wengi kama vile Shimoni, kupanua na
kuwezesha BMU ili kuboresha shughuli za usimamizi wa uvuvi. Kuna BMU ambazo
zinajumuisha VMG wengi ambako watu wa VMG hizo ndio wengi katika jamii. Hii ni hali
halisi katika BMU walio katika Visiwa vya Mukwiro na Wasini pia BMU wa Bodo na Munje
katika kaunti ya Kwale ambazo zina Washiratzi wengi. Hata hivyo, kuna ubaguzi na utengaji
wa jamii za VMG katika maeneo mengine kama vile BMU ya Kilifi ambapo jamii za VMG
zinaishi pamoja na jamii za Mijikenda, Wabajuni na Wapemba.
19. Utafiti wa kuchunguza jamii ya VMG ulionyesha kuwa kutokana na hali ya utengaji, jamii za
VMG hazifikii taasisi za mikopo, hazina makundi ya kujitegemea yaliyosajiliwa au Mashirika
ya Jamii (CBO) na kuwa baadhi ya mashirika ya jamii ambayo yalianzishwa hapo awali
yalianguka kutokana na usimamizi mbaya na ukosefu wa soko kwa bidhaa zao kama vile
mwani. Vijana katika jamii za VMG ambao wanajihusisha katika shughuli za utalii wamesajili
makundi ya vijana ambayo yanajumuisha wahudumu wa mashua (aghalabu ni wanaume) na
wanawake kufanya shughuli za burudani kwenye ufuo. Utafiti wa kuchunguza jamii
ulionyesha kuwa wanapata changamoto za kufikia huduma za mikopo na kuna umuhimu wa
kuboresha uwezo wa wafanyakazi ili waweze kushindana na watu wengine wanaojihusisha na
shughuli za kuendeleza utalii, zinazowapa riziki.
20. Baadhi ya miradi midogo katika kipengee cha 2 inaweza kujumuisha kuendeleza shughuli za
kilimo cha majini na Kilimo cha Baharini kupitia miundombinu bora, kuendeleza biashara
Ndogo Ndogo na za Wastani (SME) kwa kutoa mikopo, ushauri au kuboresha uwezo wa
wafanyakazi watakaopata mikopo. Jamii za VMG zitalengwa na shughuli hizi katika mradi.
21. Kipengee cha 3 cha KEMFSED kinalenga kuwezesha jamii za pwani na kuwapa njia za
kudumu za kupata riziki kupitia huduma za usaidizi na riziki kwa Jamii za Pwani zinazolenga
kuimarisha riziki na kuboresha uwezo wa wafanyakazi. Baadhi ya shughuli za miradi
zitakazofanyika chini ya kipengele hiki ni pamoja na; kutoa ufadhili wa elimu, kutoa zawadi
za kifedha na za kiufundi kama njia za ziada za kupata riziki na kupanua nyenzo za mapato na
kuendeleza utalii wa Baharini na Pwani. Hizi zinaweza kujumuisha kuendeleza shughuli za
kilimo, kuwapa vijana mafunzo ili kupata riziki kupitia shughuli za kitalii na kufufua baadhi
ya viwanda vilivyokuwa vimeanguka kama vile kiwanda cha korosho na kuboresha njia za
mapato yanayotokana na ukulima wa nazi. Pia itasaidia makundi ya jamii ili yapande miti kama
njia mbadala ya kukuza mikoko. Kwa mfano, miongoni mwa Washiratzi, kuna Shirika la Jamii
la Misitu (CFA) ambalo linahifadhi misitu na juhudi hizi zinastahili kuigwa katika jamii
nyingine za VMG ili zihifadhi mikoko. Wakifundi na Wavumba tayari wanajihusisha katika
shughuli za kitalii licha ya kupata changamoto kadhaa ambazo zinawazuia kutekeleza uwezo
wao kikamilifu. Kutakuwepo na juhudi za kusaidia njia hizi mbadala za kupata riziki kupitia
ubunifu wa mipango ya hatua kujumuishwa kwa jamii za VMG ambazo zinategemea mipango
ya jumla ya utekelezaji wa mradi wa KEMFSED.
Mipango ya Utekelezaji
22. Mradi wa KEMFSED utatekelezwa na Idara ya Taifa ya Uvuvi na Uchumi wa Baharini kama
shirika kuu, kwa ushirikiano na idara mbalimbali za serikali kama vile za mimea, Mifugo,
usimamizi wa uvuvi, Hazina ya Kitaifa, Idara ya Kitaifa ya Mazingira na Misitu, mwenyekiti
wa kamati ya idara za serikali katika Sekta ya Kilimo, Kitengo cha Mfumo wa Usimamizi wa
Fuo za Bahari ya Pwani, Shirika la Pwani la Wakulima wa Samaki na Shirika la Kenya la
Watayarishaji na Wauzaji wa Samaki katika Nchi za Kigeni (AFIPEK) katika ngazi ya kitaifa;
Serikali za kaunti husika katika fuo za pwani zitakuwa mashirika ya utekelezaji wa mradi
katika kiwango cha serikali za kaunti. Zitatoa mbinu za ufuatiliaji na utekelezaji katika
kiwango cha kaunti. Chini ya viwango vya kaunti vya utekelezaji na viwango vya usimamizi,
kutakuwa na viwango vya jamii vya miundo ya utekelezaji ambavyo vitajumuisha hasa
Mashirika ya Maendeleo Yanayosimamiwa na Jamii. Miundo ya utekelezaji katika kiwango
cha jamii itakuwa na kamati ndogo. Kutakuwepo na mashauriano mengine baada ya
Mashauriano yanayoeleweka, ya wazi na yanayopangwa mapema (FPIC) yanayofanywa
katika jamii za VMG kuhusu mipango ya utekelezaji WA mradi wa KEMFSED na kutambua
mikakati ya kutekeleza mradi jumuishi ambao unazingatia sifa za kipekee za uchumi na jamii
za VMG kabla ya kufanya mikutano ya mashauriano ya utekelezaji wa jamii yote.
Methodolojia
23. Data ilikusanywa kwa wakati mmoja ili kufahamisha SA na VMGF kwa kutumia njia za
msingi na za upili. Data ya upili ilipatikana kupitia kusoma vitabu, ilhali data ya msingi
ilikusanywa kupitia mashauriano na wadau, kuhoji wataalamu (KII), majadiliano
yanayoangazia makundi (FGD) na kutembea nyanjani.
Mifumo ya Sheria, Sera na Taasisi
24. Katiba ya Kenya (CoK) 2010 inatambua haki za tamaduni uchumi na uchumi wa jamii za
wananchi wote jinsi ilivyoashiriwa katika Kifungu cha 56 kinachohusu Makundi ya
waliotengwa na ya wachache. Kifungu hiki kinabainisha kuwa “taifa litaanzisha mipango ya
kupendelea wenyeji ambayo itahakikisha kuwa makundi ya waliotengwa na ya wachache
yanashiriki na kuwakilishwa katika uongozi na sehemu nyingine za maisha, b) yanapewa
nafasi maalum katika nyanja za uchumi na elimu, c) yanapewa nafasi maalum za kazi, d)
yanaendeleza matendo, lugha na shughuli za kitamaduni, na e) yanapata huduma nzuri za maji,
matibabu na miundombinu. Kifungu cha 260 kinatambua makundi yaliyotengwa na
yaliyotelekezwa. Kinatambua jamii za VMG kuwa jamii za wachache ambao wametengwa
kupitia matendo ya kihistoria. Inakataza ubaguzi wa makundi yaliyotengwa kupitia dhana
kuwa jamii hizo zina watu wachache au sababu nyinginezo, haijaweza kushiriki kikamilifu
katika shughuli za uchumi na jamii nchini Kenya kwa jumla. Pia, inatambua jamii ambazo
zimedumisha utambulisho na tamaduni zao za kipekee, hatua inayozizuia kushiriki katika
shughuli za maendeleo ya kiuchumi katika nchi ikiwa ni pamoja na usasi na utafutaji wa
vyakula mwituni, miongoni mwa nyingine. Utambuaji wa makundi haya ya VMG unapaswa
kuchangia katika uhifadhi wa utambulisho wao na kuwawezesha washirikishwe katika
maendeleo na makundi mengine, ikiwa ni pamoja na shughuli za kisiasa.
Hali za Uchumi wa Jamii za Kaunti za KEMFSED
25. VMG ilibaini ukosefu wa zana za uvuvi unaofanyika katikati mwa bahari, ukosefu wa ujuzi
wa uvuvi, kukosa kuwakilishwa katika miradi ya jamii ikiwa ni pamoja na uanachama katika
Vitengo vya Usimamizi wa Fuo kwa sababu zinashindwa katika kura na makundi yenye watu
wengi. Makundi ya Waliotengwa na Waliotelekezwa (VMG) yana matatizo ya mashamba na
wanaishi kama maskwota.
26. Vijana katika makundi ya VMG wameanzisha njia za kutengeneza mapato kupitia miradi
ambayo inajumuisha uhifadhi wa mazingira (upanzi wa miti na kuhifadhi mikoko), kuosha
magari, huduma za burudani kwenye ufuo na shughuli za mashua zinazolenga watalii.
27. Wanawake miongoni mwa makundi ya VMG wamejikita katika shughuli za ukulima wa
mwani, ushonaji na ‘mama karanga’ (kukaanga samaki) kuwa njia ya kutengeneza mapato
pamoja na ukulima wa vyakula ambao unategemea mvua.
28. SA ilitambua kuwa makundi mengi ya VMG yanapungua katika idadi au yanaacha tamaduni
zao ili kufuata tamaduni za wengi; kwa mfano, lugha ya Kisaanye inapotea na inajumuishwa
katika tamaduni na lugha ya Kibajuni. Watha wamejipanga ili kulinda utamaduni wao, kutetea
haki zao na kuhamasisha jamii zao ili kuendeleza mipango ya maendeleo.
29. Kuna kiwango cha chini cha elimu miongoni mwa jamii za VMG katika Pwani ya Kenya.
Kiwango cha chini cha elimu kinatokana na ukosefu wa pesa za kulipa karo ya watoto kwa
sababu ya viwango vikubwa vya umaskini. Ukosefu wa elimu rasmi unaoendeleza hali ya
kutengwa na jamii jirani.
Athari Zinazoweza Kutokea Kulingana na Vipengee
Kipengee cha 1: Kuboresha Udhibiti na Usimamizi wa Uvuvi wa Baharini.
30. Makundi ya VMG yatafaidika haswa kutokana na uimarishaji wa taasisi kama vile BMU
kupitia kuboresha uwakilishaji wake katika miundo ya usimamizi wa uvuvi kwenye maeneo
ya pwani. Kuzuia shughuli za kuvua samaki kupita kiasi na kudumisha uzalishaji wa samaki
pamoja na mfumo wa ekolojia ulioimairishwa utachangia kuongezeka kwa idadi ya samaki
wanaovuliwa na kuongezeka kwa mapato ya makundi ya VMG.
31. Nafasi za kazi zitaongezeka kupitia watu kujiari au kuajiriwa iwapo shughuli za uvuvi
zitasimamiwa vizuri.
Kipengee cha 2: Kuwezesha Uwekezaji wa Kudumu katika sekata ya Uvuvi wa Baharini na Kilimo cha
Majini
32. VMG zitanufaika kutokana na mipango ya kuendeleza kilimo cha majini kama njia mbadala
za kutengeneza pesa kupitia mpango wa mradi wa KEMFSED wa kujadili vikwazo
vinavyozuia uwekezaji katika shughuli za kudumu za uvuvi.
33. Baadhi ya VMG katika utafiti wa kuchunguza jamii walisema kuwa waliacha kujihusisha
katika kilimo cha mwani kwa sababu walikosa soko la bidhaa zao. Uboreshaji wa mazingira
ya biashara kupitia shughuli za mradi wa KEMFSED utaimarisha ufikiaji wa soko kwa
wakulima wa mwani na kuendeleza shughuli za kilimo cha majini katika jamii za VMG.
Kipengee cha 3: Riziki na Uimarishaji wa Jamii za Pwani
34. Utafiti wa kuchunguza jamii uliofanywa na KEMFSED umeonyesha kuwa jamii za VMG
zilizo katika eneo la mradi zinakosa uwezo wa kiufundi (ujuzi unaotakikana katika shughuli
za uvuvi bora) na uwezo wa kifedha (vifaa vya uvuvi) ambazo zinaweza kuwasaidia wapate
riziki ya kudumu kutokana na rasilimali za baharini. Zaidi ya hayo, utafiti wa kuchunguza
jamii umeonyesha umuhimu wa kuwa na mabadiliko ya mitazamo ya jamii za VMG kuwa
uvuvi unaweza kutumika kama shughuli za kibiashara lakini si kwa matumizi ya nyumbani
pekee. Pia VMG walielezea kuwa watoto wao hawawezi kupata ufadhili wa kielimu au pesa
zilizotengewa jamii ambako wanaishi kutokana na ubaguzi. Watanufaika kutokana na shughuli
za mradi wa KEMFSED zinazolenga kuimarisha uwezo wa jamii kupata ujuzi wa biashara na
kupata usaidizi wa ruzuku na kifedha. Mipango kama hiyo ya kuboresha uwezo wa
wafanyakazi itakuza ujuzi wao katika uvuvi na biashara ikiwa ni pamoja na kubadilisha
mitazamo kuhusu shughuli za uvuvi.
35. Utoaji wa huduma za mikopo na ufadhili wa elimu utaboresha viwango vya elimu kwa watoto
katika jamii za VMG kwa kuwafanya kuendelea na masomo.
36. Utafiti wa kuchunguza jamii ulionyesha kuwa kuna mashirika yaliyopo ya Jamii ambayo
yamesajiliwa ama hayajasajiliwa ambayo yanatoa mikopo kwa jamii za VMG. Pia kuna
ushahidi wa mashirika ya jamii ambayo yalianguka katika maeneo ya jamii za VMG. Makundi
ya VMG yatapata fursa ya kufufua mashirika yaliyoanguka au kuimarisha mashirika ya jamii
yaliyopo kupitia njia za kupata fedha na mikopo.
37. Kuboresha shughuli za uchumi na utumiaji wa kudumu wa rasilimali za bahari kupitia mpango
jumuishi utaendeleza utangamano katika jamii miongoni mwa makundi ya VMG na jamii
kubwa jirani ili yaishi kwa amani.
Athari Mbaya Zinazoweza Kutokea
38. Utafiti wa kuchunguza jamii ulionyesha kuwa kuna wanawake – ‘mama karanga’ ambao
wanapata samaki kutoka kwa wavuvi wa kiume wanaotoka baharini ili wazikarange na
wawauzie wenyeji katika maeneo ambayo samaki zinaletwa kutoka Bahari ya Hindi ya pwani
mwa Kenya. Hiki ni kitega uchumi kikuu ambacho ni maarufu kwa wanawake maskini na
wanaoweza kutelekezwa ambao pia wanatafuta riziki kwa familia zao katika Pwani mwa
Kenya. Usasishaji na uboreshaji wa maeneo ya kuwekwa samaki, unaweza kuanzisha kodi na
masharti mapya ya usafi. Hali hii inaweza kuwafurusha mama karanga kwenye biashara zao
na kuathiri riziki ya jamii za VMG ambazo tayari ni maskini. Kama njia ya kuzuia hili, kupitia
mpango wa makazi mapya, njia za ziada za kupata riziki zitaanzishwa katika mradi huu kuwa
njia za kufidia hasara yoyote inayotokana na uchumi.
39. Utafiti huu ulionyesha zaidi kuwa kuna vijana ambao wanabeba wasafiri kwa mashua kati ya
visiwa kama vile jamii za Wakifundi na Wavumba katika Visiwa vya Mukwiro na Wasini
katika bandari ya kuweka samaki ya Shimoni. Vijana hawa wanaoendesha mashua
wanasafirisha watu kutoka na kuenda barani na kituo cha afya ambacho wenyeji wanategemea
kiko Msambweni –Msambweni Sub-District Hospital. Vijana walihofia kuwa uboreshaji wa
bandari ya Shimoni, uwezekano wa kuzuia usafiri na uanzishaji wa vyombo vikubwa vya
majini, zinaweza kufanya wakose kazi. Pia kulikuwa na hofu kuwa njia ya kufikia kituo cha
afya cha Msambweni itakuwa vigumu iwapo bandari itaboreshwa na mashua ndogo kuzuiliwa
kufanya kazi kwenye visiwa. Pia, usasishaji wa bandari ya Shimoni unaweza kusababisha
uhamiaji wa wahudumu wengi walioelimika wanaoendesha mashua, ambao wanajimudu
katika lugha za kigeni kama vile Kihispani, Kifansa na Kijerumani, walio na vyeti vya
Mawasiliano ya Kompyuta ambao unatakikana ili kuhudumu katika sekta ya utalii, hali
ambayo itawaathiri wenyeji Wavumba na Wakifundi wanaoendesha mashua na hawajui lugha
hizi za kigeni.
40. Shughuli za mradi wa KEMFSED zitaathiri vibaya Makundi ya Waliotengwa na Kutelekezwa
(VMG) iwapo shughuli za mradi zitasababisha uharibifu wa miti au maeneo ya kidini kama
vile makaburi au maeneo ya kuabudu. Jamii za VMG ziliteta kwamba hakutakuwa na
mashauriano iwapo shughuli za mradi zitaharibu misitu na maeneo ya kidini.
Mipango ya Kufuatilia na Kuripoti
41. Ripoti za maendeleo ya kila robo ya mwaka zitaandaliwa na mashirika yanayotekeleza mradi
kuanzia mifumo ya kiwango cha jamii, kaunti na mifumo ya kiwango cha kitaifa, kama
masharti ya ripoti ya jumla ya Ufuatiliaji na Tathmini ili kufafanua maandalizi na utekelezaji
wa VMGP na malalamiko yaliyopatikana na kusuluhishwa. Ripoti hii itawasilishwa kwa Benki
ya Dunia kupitia shirika linaloongoza utekelezaji – idara ya Uvuvi na Uchumi wa Baharini.
Mifumo ya Kufuatilia na Kutathmini Mradi
42. Hatua zifuatazo zimependekezwa kuwa mbinu za kubuni mfumo bora wa kutathmini na
kufuatilia mradi:
Kuhamasisha na kufunza jamii kuhusu usanifu, uandalizi na utekelezaji wa mradi.
Mafunzo haya yanayolenga jamii yanapaswa kushirikisha wadau wote katika viwango vya
jamii na vinajumuisha; viongozi wa jamii, viongozi wa madini na utamaduni, vijana
(wakibainishwa kulingana na jinsia), wanawake na makundi mengine husika katika jamii
Kubuni mbinu ya kuhakikisha kuwa kuna mfumo wa kutoa maoni kwa wakati unaofaa,
ambao unaweza kudumisha kuangaziwa kwa shughuli za mradi. Mbinu hii itakayobuniwa
wakati wa mashauriano ya jamii inapaswa kuwa na mbinu ya kindani ya kuwawezesha
wawakilishi wa jamii kutoa ripoti maendeleo kwa jamii pana. Aidha, njia zinazofaa na
zilizokubaliwa za mawasiliano katika jamii zinatakiwa kubuniwa ili kuimarisha shughuli
za kutathmini na kufuatilia mradi.
Timu inayofaa ya kufuatilia na kutathmini mradi inapaswa kuwepo na itajumuisha
wawakilishi waliochaguliwa wa jamii ya VMG kuwa miongoni mwa wawakilisha kutoka
kwa jamii jirani, wawakilishi wa serikali ya kaunti na wawakilishi wa kamati ya utekelezaji
wa mradi wa KEMFSED.
Mbinu inapaswa kubuniwa ili kujumuisha wawakilishi waliochaguliwa wa vijana,
walemavu na wanawake katika timu ya kutathmini na kufuatilia mradi.
Viashiria vya Kutathmini na Kufuatilia Mradi wa KEMFSED/VMGF
43. Jedwali lililo hapa chini linaonyesha viashiria vya kufuatilia na kutathmini jinsi KEMFSED
itakavyoathiri jamii ya VMG.
Ufuatiliaji na Tathmini
Viashiria vya KEMFSED
Mradi
Kiashiria Wajibu Vyanzo vya Data
Juhudi za kuboresha
uwezo wa wafanyakazi
katika SME, ujuzi wa
uvuvi,
Kuendesha mashua,
usalama baharini na
shughuli za utalii
zinazohusika, Kilimo cha
Baharini
Na kilimo cha majini
Idadi ya wanachama wa
VMG waliopata mafunzo
ya biashara, kuvua,
kuendesha mashua
Na ujuzi wa usalama wa
baharini, Kilimo cha
Baharini na kilimo cha
majini.
Usimamizi wa
Uvuvi na Idara
ya Kitaifa ya
Uvuvi na
Uchumi wa
Baharini
Warsha za mafunzo
Kuipa jamii mapema
Vifaa vya uvuvi vya kisasa
(neti, boti n.k)
Idadi ya wanachama wa
VMG ambao wamepata
boti na neti bora za uvuvi,
nk
Usimamizi wa
Uvuvi na Idara
ya Kitaifa ya
Uvuvi na
Uchumi wa
Baharini
Fomu za maombi ya
bidhaa
zinazonunuliwa
Kuimarisha ufikiaji wa
huduma za ufadhili wa
kifedha na usaidizi wa
ruzuku
Idadi ya wanachama wa
VMG ambao wamenufaika
kutokana na usaidizi wa
ruzuku/kifedha
Usimamizi wa
Uvuvi na Idara
ya Kitaifa ya
Uvuvi na
Uchumi wa
Baharini
Rekodi ya
walionufaika kupata
usaidizi wa kifedha
na ruzuku
Ushauri kwa walionufaika
kutokana na usaidizi wa
ruzuku na fedha
Usaidizi
Idadi ya VMG
walionufaika kutokana na
usaidizi wa ruzuku na
fedha ambao wamefunzwa
kuhusu SME
Usimamizi wa
Uvuvi na Idara
ya Kitaifa ya
Uvuvi na
Uchumi wa
Baharini
Orodha za
mahudhurio na ripoti
za mafunzo
Ufadhili wa elimu Idadi ya wanajamii wa
VMG ambao wamenufaika
kutokana na ufadhili wa
elimu katika viwango
mbalimbali
Usimamizi wa
Uvuvi na Idara
ya Kitaifa ya
Uvuvi na
Uchumi wa
Baharini
Rekodi za
walionufaika
kutokana na ufadhili
wa elimu katika
vikundi mbalimbali
Ufuatiliaji wa utendaji wa
BMU
Wawakilishi wa wanajamii
wa VMG katika BMU
ambapo BMU hiyo
inapatikana katika
jamii/mfumo wa
wanajamii wa VMG
Usimamizi wa
Uvuvi na Idara
ya Kitaifa ya
Uvuvi na
Uchumi wa
Baharini
Ripoti za Kufuatilia
na Kutathmini Mradi
Kuboresha uwezo wa
Wafanyakazi katika BMU
Idadi ya wawakilishi wa
VMG ambao
wameshiriki/kuhudhuria
vipindi vya kuboresha
uwezo wa wafanyakazi
katika BMU
Usimamizi wa
Uvuvi na Idara
ya Kitaifa ya
Uvuvi na
Uchumi wa
Baharini
Orodha za
mahudhurio na ripoti
za mafunzo
Usajili na utoaji leseni wa
mashua za uvuvi
Idadi ya mashua za uvuvi
zinazomilikiwa na VMG
ambazo zimesajiliwa na
Usimamizi wa
Uvuvi na Idara
ya Kitaifa ya
Ripoti za Kufuatilia
na Kutathmini Mradi
kupewa leseni ili
zihudumu katika BMU
Uvuvi na
Uchumi wa
Baharini
Uwezeshaji wa jinsia ili
kupata riziki ya ziada
Shughuli
Ulinganishaji wa idadi ya
wanawake na wanaume
katika VMG ambao
wamewezeshwa kuendesha
SME, wamesaidiwa
kufanya kilimo,
Usimamizi wa
Uvuvi na Idara
ya Kitaifa ya
Uvuvi na
Uchumi wa
Baharini
Ripoti za Kufuatilia
na Kutathmini Mradi
Uendelezaji wa shughuli za
kudumu za mfumo wa
ekolojia
Idadi ya shughuli za
kuhifadhi mazingira katika
jamii (mikoko, njia
mbadala ya kupanda miti
nk) ambazo zimeanzishwa
na kujumuisha uongozi wa
VMG miongoni mwa
wanachama wengine
katika jamii pana
Usimamizi wa
Uvuvi na Idara
ya Kitaifa ya
Uvuvi na
Uchumi wa
Baharini
Ripoti za Kufuatilia
na Kutathmini Mradi
Mikutano ya uhamasishaji
wa jamii ya kusaidia jamii
pana ya VMG
Idadi ya mikutanao ya
uhamasishaji ya kusaidia
jamii pana iliyofanywa
miongoni
mwa/kuhudhuriwa na
jamii za VMG
Usimamizi wa
Uvuvi na Idara
ya Kitaifa ya
Uvuvi na
Uchumi wa
Baharini
Rekodi za mikutano
za jamii
Mbinu ya Kushughulikia Malalamiko
44. Kila mwanachama wa VMG katika eneo la mradi alikuwa na mbinu thabiti za zinazoongozwa
na tamaduni/mila kulingana na mfumo wa Baraza la Wazee ambao waliashiria kuwa njia
waliyopendelea kusuluhisha mizozo wakati wa kutekeleza VMGP. Kulingana na jamii nyingi,
mwanajamii yeyote ambaye anakataa kukubali unamuzi wa “mahakama” za kimataduni
amelaaniwa na wazee na jamii na yuko tayari kusuluhisha mzozo kupitia njia za mahakama na
kisheria. Kanuni hii itatumika kama njia ya kusuluhisha mizozo katika mradi huu.
45. Wakati wa mashauriano, wanachama mbalimbali wa VMG walielezea kuwa wangependa
kusuluhisha mizozo na malalamiko kupitia miundo ambayo wamewakilishwa kikamilifu na
isiyoathiriwa zaidi na jamii kuu. Walipendekeza kiwango cha chini zaidi, yaani kiwango cha
jamii, kwa kutumia mifumo ya kiusimamizi na ya kitamaduni ya wazee wa vijiji kadri
iwezekanavyo. Walitilia shaka viwango vya juu vya Kusuluhisha Mizozo kwa kuwa
hawajawakilishwa na hawakuamini mifumo ambayo inasimamiwa na watu waliosoma sana.
Mipango ya Kuidhinisha na Kuvumbua
Kuidhinisha
46. Rasimu hii ya VMGF itapitia hatua mbalimbali za uidhinishaji katika Idara ya Kitaifa ya
Uvuvi, Kilimo cha Majini na Kilimo cha Baharini, timu ya utekelezaji wa mradi wa
KEMFSED na timu ya Ulinzi wa Benki ya Dunia katika nchi na kanda.
Uvumbuzi
47. Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya ya CoK, 2010 na sera ya Benki ya Dunia ya Kuvumbua kwa
Umma, 2011, uwazi na uwajibikaji ni mambo muhimu katika mchakato wa maendeleo
yanayolenga kupunguza umaskini. Kwa hivyo, uvumbuzi katika umma wa VMGF utachukua
mtindo wa: (i) shughuli ambazo mradi unafadhili; (ii) jinsi rasilimali zimegawanywa na
kutumiwa; (iii) maendeleo katika utekelezaji wa mradi; na mwisho, (iv) mafunzo ambayo
yametokana na mradi ili yashirikiwe miongoni mwa wadau na wahusika wa mradi.
48. Njia inayofaa ya kuvumbua maelezo haya itabainishwa mara kwa mara, japo kupitia
mashauriano tulifahamu kuwa mabaraza ya umma (mikutano ya jumla ya jamii), wadi, utawala
wa eneo, miundo inayofaa ya kiwango cha kaunti na kaunti ndogo na ofisi za chifu
ingependelewa kwa VMG. Uvumbuzi hasa katika kiwango cha jamii, hasa kupitia mabaraza
ya jumla utafanyika katika Kiswahili, lugha ambayo inatumiwa zaidi na jamii ya VMG.
Muhtasari utafaa katika hali hii. Ripoti kamili inapaswa kuvumbuliwa kwenye makao makuu
ya Kaunti na Kaunti ndogo. Mwisho, VMGF imechapishwa kwenye tovuti za washirika
wanaotekeleza mradi, haswa zile za idara ya Kitaifa ya Uvuvi na Uchumi wa Baharini na pia
Tovuti za Nje za Kimataifa.
Muhtasari wa Mapendekezo, Majukumu na Wajibu wa KEMFSED
Mapendekezo
49. Ili kushirikisha VMG zaidi, kuna umuhimu wa kujumuisha jamii katika hatua zote za mradi.
Wakati wa utekelezaji, ujumuishaji wa VMG na uhusiano wao na jamii nyingine, pamoja na
athari za mradi katika masilahi yao yanapaswa kufuatiliwa kikamilifu.
a) Shughuli zinazofaa za uhamasishaji na uwasilishaji zinapaswa kuratibiwa kupitia hatua
mbalimbali zinazotumika za mawasiliano, kuwa sehemu ya mbinu za utoaji huduma (yaani
ulengaji, malipo, G&CM nk.). Inatarajiwa kuwa hali hii itaendelea katika awamu zote za
huduma ya KEMFSED, na kutekelezwa zaidi wakati wa KEMFSED.
b) Mikakati na zana za mawasiliano itajumuisha mabaraza ya jumla ya jamii, redio, SMS,
vipeperushi, matangazo kupitia megafoni nk. Hususan, Mikakati ya Uhamasishaji kwa
Wanaonufaika kupitia ujumbe maalum wa VMG itatumika ili kuhakikisha ujumuishaji wa
VMG na itatoa mbinu zinazofaa za kuhakikisha kuwa VMG wamefikiwa na kuwa habari
inatolewa kwa njia ambazo zinaeleweka kwa urahisi. Huenda hatua hii itahitaji kulenga
makundi mbalimbali ya VMG, kulingana na mahali waliko, lugha, kiwango cha elimu,
kujumuishwa katika jamii pana na elimu ya uraia.
c) Kuandika idadi na aina ya malalamiko ambayo yamewasilishwa kuhusu mradi na hatua
ambazo zimechukuliwa na kuhakikisha kuwa njia zinazofaa zimebuniwa na kutekelezwa.
d) Kukusanya data ya malalamiko na maoni ya wanaonufaika mara kwa mara ili kuhakikisha
kuwa maeneo yanayolengwa ambayo jamii ya wachache ipo yanafikiwa na malalamiko
yanayojirudia yanapelelezwa ili kupata njia za kuyasuluhisha.
e) Kuhakikisha kuwa vizuizi vya ujumuishaji (kama vile ugumu wa kupata Vitambulisho na
Huduma Namba) vinashughulikiwa kwa wanajamii husika, ikiwa ni pamoja na VMG.
f) Ufahamu na rekodi bora za lugha, tamaduni na kizazi cha Wasaanye itatakikana ili
kuchunguza Wasaanye ambao watanufaika kutokana na mradi wa KEMFSED na miradi
ya baadaye ya Benki ya Dunia inayolenga jamii Zilizotengwa na Zinazotelekezwa
g) Kuna umuhimu wa mawasiliano ya ziada katika jamii ili kubainisha maeneo mengine
ambako inatarajiwa kuwa shughuli za mradi wa KEMFSED zinaweza kuathiri misitu ya
kidini na sehemu za VMG.
50. Kuna umuhimu wa kuhamasisha na kuwapa mafunzo wadau wote kuhusu utambulisho na
ujumuishaji unaofaa wa aina mbalimbali za VMG. Kwa hivyo, mashirika yanayotekeleza
KEMFSED yanapaswa kukagua hifadhidata iliyopo ya VMG kwa kila kaunti ya KEMFSED.
Zaidi ya hayo, maafisa wa mpango wanapaswa kuhamasishwa kuhusu hali za ukasumba, na
jinsi ya kujumuisha makundi kama hayo katika KEMFSED. Hatua hii itasaidia kuelewa sifa
na maeneo ya VMG na kuwahamasisha maafisa kuhusu VMG ili waweze kuwasiliana nao na
kuwalenga vizuri. Ili kuongeza uhusiano na VMG, kuna haja ya kuhimiza ushirikiano kati ya
idara za serikali za uvuvi na uchumi wa baharini na washirika wa utekelezaji na mashirika
mengine ya jamii na ya serikali ambayo yanafanya kazi na VMG.
51. Elimu ya uraia na mafunzo kwa jamii yanapaswa kufanywa ili kuimarisha weledi na haki za
kila mtu, ikiwa ni pamoja na VMG. Mafunzo kuhusu haki yanaweza kufanywa kama sehemu
ya mpango wa kuhamasiaha wanaonufaika katika jamii na wote wanaonufaishwa na
KEMFSED.
52. Wakati wa kuwasiliana na VMG, hakikisha kuwa njia na mbinu zinazofaa za mawasiliano
zinatumiwa na kutambuliwa na wanajamii wa VMG wenyewe. Huenda vituo vya redio vya
FM visifikiwe au kueleweka na kila mtu. Kwa hivyo, unaweza kupiga simu, kutuma ujumbe
kwa wawakilishi na viongozi na kufanya mikutano ya mabaraza ya moja kwa moja.
53. Wakati unalenga makundi ya wachache, jumuisha makundi ya wachache wakati wa kupanga
ili wakuunge mkono na uendeleze utangamano unaofaa. Hakikisha kuwa makundi ya
wanawake na vijana yanashauriwa vizuri kuhusu njia bora ya kuyahusisha na mapendekezo
yao ili mradi utimize malengo yake.
54. Mashirika ya utekelezaji yanapaswa kuandaa VMGP kwa kila shughuli ya KEMFSED iwapo
VMG watatambuliwa kuwepo katika eneo la shughuli na kuchukuliwa kuwa wameathiriwa na
shughuli na itaongozwa na sheria ya Benki ya Dunia ya OP4.10, Annex B. Hususan, VMGP
itatayarishwa kwa ajili ya jaribio la mikakati ya kiuchumi, kwa kuwa athari kwenye VMG
inatarajiwa iwe kubwa zaidi katika shughuli hizi. Hata hivyo, VMGP pia itaandaliwa katika
shughuli hizo nyingine mbili (utoaji wa pesa na upanuaji wa neti za usalama), panapofaa,
kutokana na utambuaji wa VMG katika maeneo ya mradi. Idhini ya Benki ya Dunia kwa
VMGP itatakikana kabla ya utekelezaji.
Majukumu na Wajibu
Mashirika ya Utekelezaji wa KEMFSED
55. Mashirika ya utekelezaji wa KEMFSED katika Kaunti yatakuwa na wajibu wa:
i. Kubaini makundi ya VMG katika kaunti zao, ikiwa ni pamoja na mahali waliko na jinsi ya
kuwafikia;
ii. Kuendeleza VMGP ili kutambua athari kubwa, kubuni njia za kusuluhisha na kutoa mwelekeo
kuhusu jinsi njia hizo za kusuluhisha zitafadhiliwa na kufuatiliwa.
iii. Kuchunguza athari za mradi na ufanisi wa njia zilizopendekezwa za kusuluhisha matatizo
yanayotokana na VMG husika. Wakati wa kutekeleza shughuli za mradi, athari na hatari za jamii,
hali za makundi ya VMG yaliyoathiriwa na uwezo wa mashirika ya utekelezaji kutoka kiwango
cha kitaifa na kaunti, unapaswa kuchunguzwa.
iv. Kuchunguza utoshelezaji wa utaratibu wa mashauriano na usaidizi mpana wa VMG zilizoathiriwa
katika mradi. Hii itajumuisha utekelezaji wa VMGP, kushughulikia matatizo ya utekelezaji na
kurekodi mambo waliyojifunza yanayohusu VMG na utumiaji wa VMGF/VMGP.
Benki ya Dunia
i. Kuidhinisha VMGF kwa KEMFSED.
ii. Kupokea VMGP zote zilizoandaliwa, kuzikagua na Kuziidhinisha au vinginevyo, kabla ya
kutekeleza shughuli za KEMFSED.
iii. Wakati wa kutekeleza, itathmini na kufuatilia nyanjani, inavyohitajika.
iv. Kusaidia katika kuboresha uwezo wa wafanyakazi kadri inavyotakikana.