9.ombi la imani (1) - koinonia-education.com file9.ombi la imani (2) • kubali imani yako iungane...

10
9.OMBI LA IMANI (1) Mt 21:22 Yesu anasema; 22 Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. Hapo hoja zote za kutoamini zinajikusanja kusudi ziondoe maana ya ahadi hii wazi na jepesi. Tunahitaji kuwa na fikra inayonyenyekea chini ya neno na kulitii neno la Mungu 2Kor 10:5 Wana wa Israeli walikuwa na tatizo hilo hilo

Upload: others

Post on 25-Sep-2019

12 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

9.OMBI LA IMANI (1)

• Mt 21:22 Yesu anasema; 22Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.

• Hapo hoja zote za kutoamini zinajikusanja kusudi ziondoe maana ya ahadi hii wazi na jepesi.

• Tunahitaji kuwa na fikra inayonyenyekea chini ya neno na kulitii neno la Mungu 2Kor 10:5

• Wana wa Israeli walikuwa na tatizo hilo hilo

9.OMBI LA IMANI (2)

• KUBALI IMANI YAKO IUNGANE NA AHADI ZA MUNGU • Wana wa Israeli walikuwa wamepewa ahadi kutoka kwa Mungu, Mungu

aliwaahidi kila kitu! Lakini wao walishindwa kuunganisha ahadi na imani, kwa sababu hiyo ahadi zilishindwa kuzaa matunda.

• Hata kwetu sisi, dawa ni ile ile, ahadi inahitaji kupatiwa imani (dawa) kusudi ianze kutoa matunda.

• Katika Mt 21:22 , Yoh 16:24, Yoh 15:7. Mk 11:22-24. Yesu anasema kwaba YOTE muombalo mtapewa.

• Haweki kiwango

• Ahadi inahusu kila eneo la maisha yako, maana agano linakuhusu wewe mzima mzima

• Yesu aliweka sharti moja tu ya kutuwezesha kupokea ahadi zake zote, IMANI

• Na ni Yesu mwenyewe anayesema hayo maneno.

• Yesu anaposema ”lote linawezekana kwa anaye amini” Mk9:23 ni kwa makusudi ya kutupatia moyo. Anapenda kuamsha hamu ndani yetu ya kuona miujza ya baba yetu

9.OMBI LA IMANI (3)

• IMANI SI MADAI NI MSAADA • Watu wengi wanaona mafundisho juu ya kuwa na imani inaleta madai , lakini

sivyo ilivyo. Tukiwa na imani ndani ya maisha yetu inakuwa msaada kwetu.

• Yesu anatusaidia kuamini, kusudi imani yetu iwe kama inavyoelezewa katika Ebr 11:1

• kwa sababu twamjua tunayemwamini 2Tim 1:12b.

• Maajabu yangestahili kuwa ”kawaida yetu” maana tumeumbwa kwa ajili ya ulimwengu wa maajabu.

• Tukijifunza maisha ya kiimani inakuwa kama kuendesha basikeli au kutembea, unafanya hata bila kufikiria inajipa tu.

• Lakini ulipokuwa mtoto ulilazimika kujifunza kutembea, hakuna aliyetuambia tulipoanguka ” mwanangu huhitaji kujifunza kutembea, Mungu anakupenda vile ulivyo”. Badala yake mzazi atamtia moyo mtoto wake, na ndani ya mtoto pia kuna hamu inayowasukuma hadi wanapoweza.

9.OMBI LA IMANI (4)

• WOTE WANAOMWAMINI MUNGU WAMEPEWA ROHO WA IMANI • 2Kor 4:13 Roho anatutia moyo, anatupa nguvu na kutusaidia. Roho anahitaji

vitenda kazi, na vitendakazi hivyo ni Neno la Mungu na hamu kwako.

• Wakati neno linapandwa ndani ya miyoyo yetu, na tunapoanza kupata hamu sawa na neno Roho anakuja kutusaidia Rum 8:26a

• Utajikuta unakuwa na uwepesi wa kuona kwa macho ya kiroho, badala ya macho ya kawaida. Tunaona ahaidi za Mungu na yanakuwa kweli yetu katika imani.

• Yak 1:5-8 inasema;

• Kama umepungukiwa, mwombe Mungu afidie, lakini omba kwa imani bila hivyo hupati kitu

• Mashaka yanaondoa majibu ya maombi yetu, kimsingi mashaka ni ujeuri unaompinga Mungu na uweza wake.

• Mashaka ni imani hasi, ni imani inayokubaliana mazingira.

• Unapoweza kuamini na kuishi ”kiroho” unalindwa na yule mwovu 1Yoh 5:18.

9.OMBI LA IMANI (5)

• USIKUBALI MAZINGIRA YA KUONGOZE AU KUKUTAWALA • Wengi wanatawaliwa na mazingira

• Mambo yakienda vizuri na watu wanapowakubali maisha ni mazuri.

• Wakipingwa wanakosa raha

• Wanaishi kufuatana na mazingira, Mungu hapendi maisha yetu yawe kama tanga au bendera. Anapenda uwe na msingi wako imara katika Kristo. Nanga yako isingoke ukatupwa tupwa na mawimbi bila mpango wala msimamo.

• Ukiwa na msingi wako kwake utaweza kufikia malengo Yake ya maisha yako, mazingira yanapoyumba wewe hutikisiki. Ukiishi hivyo maisha yako yanakuwa bora zaidi na utajikuta unawezea kutyafaidi sana.

9.OMBI LA IMANI (6)

• OMBI LA IMANI • Ombi la imani linajenga juu ya ufahamu waku kuhusu mapenzi ya Mungu.

• Kama hujui mapenzi ya Mungu huwezi kuomba kwa imni

• Kupata kujua mapenzi yake inafanyika kwa kusoma Neno lake na kushirikiana naye, kukaa mbele za uso wake.

• Wakati umeshafahamu mapenzi yake unaweza kuomba ombi la imani, kwa sababu unajua analolitaka. Na Biblia inasema kwamba anawapa thawabu wote wamtafutao.

• Ebr 11:6. 6Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

9.OMBI LA IMANI (7)

• OMBI LA KUKABIDHI NA OMBI LA IMANI. • Ombi la kukabidhi unatumia wakati bado mapenzi ya Mungu hayajadhihirika

kwako. Unaomba mapenzi yako yatimike, na pia unaomba akuonyeshe mapenzi Yake.

• Utakapofahamu mapenzi yake sasa unamjia lakini si kwa kumweleza shida bali kwa sababu unaamini mapenzi yake.

• Kwa hiyo imani yako na ufahamu wako juu ya utatuzi ndiyo utakayokuongoza.

• Rum 10:11-13 10Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. 11Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. 12Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; 13kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.

9.OMBI LA IMANI (8)

• MWACHIE MUNGU AWE MUNGU • Unapofahamu mapenzi ya Mungu unaomba mambo yatatuliwe kwa njia

yake.

• Usijali sana jinsi anavyotatua jambo, hiyo si tatizo lako, ni tatizo lake.

• Unaomba kwa imani na unatulia kwa imani

• Lini, wapi, kwa njia gani na kupitia nani unamwachia Mungu kuamua.

• Usijaribu kumsaidia Mungu kujibu maombi yako

• Mungu anakujali

• 1Petr 5:7 7huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

• Fil 4:5-7 5Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. 6Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

9.OMBI LA IMANI (9)

• TUNAHITAJI KUONA MAJIBU YA MAOMBI YETU KWA MACHO YA IMANI. • Mk 11:24

• Wakati gani basi ni wakati mwafaka kuamini kua tumejibiwa?

• Wakati tumepewa?

• Wakati tunapopata hisia nzuri juu ya hilo jambo?

• Wakati mwafaka ni wakati unapoomba, amini kwamba umejibiwa, anza kumshukuru Mungu.

• Mt 7:11

• Mungu si mbahili! Anapenda hata zaidi yako utoshelezwe

• Unapoomba ombi la imani, neno linaanz kufanya kazi, jibu liko njiani na unaweza kuanza kushukuru…

• 1Yoh 5:14-15 Inasema;

9.OMBI LA IMANI (10)

• ANZA KUTAMKA UTATUZI BADALA YA MATATIZO! • Anza kutamka jibu, si umepewa (ukiamini). Kuomba omba omba omba

mwisho ombi lako linakuwa kinyume na imani kwa sababu inaonekana hujaamini. (umeomba bila kujua mapenzi ya Mungu.

• tunaweza kusema kwamba ”unahitaji kumwomba Mungu mara moja tu, baadaye ni kuanza kushukuru” (kama unafahamu mapenzi yake)

• Lakini kuna wakati tunahitaji ”kupitisha ombi letu kwenye anga ya kiroho” kwa sababu imecheleweshwa.

• Tunatangaza ahadi yetu toka kwa Mungu na hiy inafungua njia.

• Ebr 4:16 16Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.