‘active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/active for future_na...

50
‘Active for future’ na mradi/mpango wa vijana Mwongozo kwa Wataalamu wa maswala ya vijana PROGRAMU YA ERASMUS+ HATUA YA PILI:USHIRIKIANO KATIKA UJUZI NA USHIRIKISHANAJI WA MBINU BORA KATIKA KUWAJENGEA UWEZO VIJANA Nambari ya mradi: 565821-EPP-1-2015-1-SI-EPPKA2-CBY-ACPALA

Upload: others

Post on 13-Oct-2020

1 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

‘Active for future’ na mradi/mpango wa

vijana Mwongozo kwa Wataalamu wa

maswala ya vijana

PROGRAMU YA ERASMUS+

HATUA YA PILI:USHIRIKIANO KATIKA UJUZI NA USHIRIKISHANAJI WA

MBINU BORA KATIKA KUWAJENGEA UWEZO VIJANA

Nambari ya mradi: 565821-EPP-1-2015-1-SI-EPPKA2-CBY-ACPALA

Page 2: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

2

Mradi huu umefadhiliwa kwa msaada kutoka Umoja wa nchi za Ulaya (EU). Chapisho hili linaonyesha maoni tu ya mwandishi, na Umoja wa nchi za Ulaya hauwezi kuwajibika kwa ma-tumizi yoyote, ambayo yanaweza kufanyika kutokana na habari zilizomo ndani ya chapisho hili.

All information: www.activeforfuture.net

Izvirni naslov: Active for future with youth initiatives - Methodology for youth workers

Active for future’ na mradi/mpango wa vijana Mwongozo kwa Wataalamu wa maswala ya vijana

Authors: Sonja Majcen and Katja Kolenc

Design: Katja Kolenc

Translation: Happiness Hangaika

Celje, 2017

Elektronska izdaja.

Založnik: Celjski mladinski center, javni zavod za mladinsko kulturo, izobraževanje, informiranje in šport, Maribor-

ska 2, 3000 Celje, Slovenija

__________________________

Kataložni zapis o publikaciji (CIP) pripravili v Narodni in univerzitetni knjižnici v Ljubljani

COBISS.SI-ID=291174656

ISBN 978-961-92953-9-7 (pdf)

Page 3: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

3

Yaliyomo

Badala ya utangulizi ....................................................................................... 4

Muongozo ...................................................................................................... 7

Kuhusu mradi wa Active for future............................................................... 10

Mpango/mradi wa wijana ............................................................................ 15

Hatua za kufuata katika kutambua mpango/mradi wa vijana ....................... 19

Muundo wa mradi/mpango wa vijana ......................................................... 22

Ujuzi na umahiri ........................................................................................... 31

Kuelekea katika ajira .................................................................................... 34

Mradi huu umenifanyia nini? ....................................................................... 36

Mifano ya miradi bora ambayo imeandaliwa katika kipindi cha utekelezaji wa

Active for future ........................................................................................... 38

Fasihi……..…………………………………………………………………………………………………..49

Page 4: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

4

BADALA YA UTANGULIZI

Naam hiki ni kilele cha mwaka kwangu.Habari! jina langu ni Muthoni Kirumba (unaweza

kuniita unique MK ). Daima Nilikuwa ninaomba kwa ajili ya kuifikia hatua hii katika

maisha yangu,na kila nilipopata wasaa niliomba sala ya Yabesi, 1 mambo ya nyakati 4;10

ambayo inasema ‘Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba

ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja

nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu!- Naye Mungu akamjalia

Yebesi (unique MK)hayo aliyoyaomba'.Angalia naamini Mungu ni Mungu Mkuu

mwenye kuleta mabadiliko, Siku moja nilipigiwa simu nisiyoitegemea na kile

nilichokisikia toka upande wa pili wa simu ilikuwa kukamilika kwa ndoto yangu ; VACK-

Volunteer Action for Change Kenya ilikuwa ikichagua washiriki ambao wangeiwakilisha

Kenya katika semina ya kimataifa ya vijana nchini Slovenia.Nilifurahi kuwa miongoni

mwa waliochaguliwa kwani sikuwahi kwenda Ulaya kabla.Umoja wa ulaya ndio uliokuwa

unafadhili mradi huu ulio chini ya programu ya Erasmus +, ambao ulitoa fursa kwa

lengo la kutoa maarifa,ujuzi na uwezo ambao ungeweza kukuza uelewa na uwezo kwa

vijana .Ambapo washiriki sita kutoka kila nchi katika nchi sita ambazo ni

Romania,Bulgaria,Slovania,Uganda ,Tanzania na kenya walitakiwa kukutana Slovenia

kwa muda wa juma moja kwa ajili ya mradi ambao ulihusisha kubadilishana mawazo na

utamaduni ambao utasaidia kuongeza ushirikiano,maarifa na ujuzi utakaoleta

changamoto katika mazingira ya biashara na kuongeza ubunifu na uguduzi katika

viwango mbalimbali. Hii ilikuwa ni kwa lengo la kutuwezesha kuja na ufumbuzi

utakaosaidia kuboresha jamii zetu na taifa kwa ujumla na kuufanya ulimwengu kuwa

mahala salama zaidi, pia tulitarajia kwamba uwezo wetu katika mambo mbalimbali

ungeongezeka zaidi.

Page 5: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

5

Mchakato wote wa kujifunza ulikuwa ni wa kuvutia sana kwani tulikuwa na mijadala

mbalimbalii ,pia tulikuwa na shughuli nyingine za nje ambapo tuliweza kutembela ma-

kumbusho ya Celje Castle, ziwa la Smartinsko Jezero na kutembelea jiji na baadae tu-

liweza kutoa maoni yetu. Tulitamani pia kupata wasaa wa kutembelea mji mkuu wa Lju-

bljana lakini pengine tutafanya hivyo kwa wakati ujao. Slovenia ni nchi yenye utulivu,

Celje ni mji mzuri sana ... ungependa kabisa kurudi huko. NILIKUPENDA SANA..... . Miku-

tano kama hii hutengeneza na kukuza ushirikiano. Tulikuwa na usiku wa kushangaza

ambapo washiriki kutoka nchi za Ulaya walipaswa kuonesha utamaduni wao (chakula,

ngoma n.k) na usiku wa Kiafrika pia ambapo waafrika walipaswa kuonesha utamaduni

wao.. Kwa hiyo kwenye usiku wa kiafrika, tulipika, tulivaa, tulicheza, tuliongea mambo

megi na kupiga picha nyingi ,watu wote walivutiwa na utamaduni wetu . kwa ujumla

kufika Ulaya imekuwa ni sehemu ya kuweza kutubadlisha sote tulioshiriki. Ni-

mesukumwa na kuvutiwa kiasi kwamba nitaendeleza mazungumzo haya kupitia mitan-

dao ya kijamii ambapo unaweza kufuatilia kwa kuandika hivi: #talentconversation ......

tafadhali tuendeee kushirikian katika mazungumzo haya.

Nilipofika nyumbani nilikuwa na haraka ya kusambaza picha na kwa bahati mbaya nilipo-

teza kadi ndogo ya kuhifadhia kumbukumbuku za picha ila naamini nitaipata tena

mapema. Ingawa nilisikitika sana lakini pia lilikuwa somo kwangu somo ambalo nin-

gependa na nyie mjifunze kwamba siku nyingine ni vizuri kuhifadhi picha na taarifa nyin-

gine muhimu kaika sehemu mbalimbali kama vile kwenye mitandao ya kijamii au njia

nyingine za kuhifadhi kumbukumbuku kwa njia ya mtandao ili hata kadi za kuhifadhia

kumbukumbuku zinapopotea bado uaweza kupata kumbukumbu zako katika mtan-

dao.Hata hivyo bado tuna picha nyingi japokuwa haziwezi kuwa nyingi za kutos-

ha.Tuliona vitu vingi vizuri madukani lakini hatukuweza kununua kwa wakati.Mara nyin-

gine unapoona vitu vizuri ni bora kuvinunua hapohapo kwa sababu unaweza ukakosa

kabisa fursa ya kuvinunua tena kwa wakati mwingine.

Page 6: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

6

Kwa namna yoyote ile, tulikutana na watu wa kuvutia, tulikuwa na shughuli za kuvutia,

kumbukumbu nyingi nzuri na za kufurahisha huku tukisubiria kutekeleza kile tulichojifun-

za,si kwa faida yetu bali kwa ajili ya vijana ambao ni asilimia kubwa katika idadi ya watu

kwenye jamii zetu.Na sasa tumeboresha zaidi kwa kuwa na mtandao na ushirikiano

kutoka katika nchi sita.Hivyo tegemea kusikia shughuli za kuvutia, hadithi za kuvutia na

miradi mingine kupitia hapa www.maya.co.ke .....tutaendelea kukujuza.......endelea ku-

tufuatilia.

Kwa ujumla,mimi binafsi nina furaha,nipo katika mitaa ya Nairobi nikitabasamu peke

yangu kila ninapokumbuka mambo na vitu vizuri nilivyoviona katika mji wa Celje kama

vile upendo,utulivu na urithi uliopo.Nimekuwa nikitabasamu muda

wote,nikikaa,nikitembea na nikiwa nafanya shughuli mbalimbali kiasi kwamba watu

wanajiuliza nini chanzo cha furaha yangu,Naam chanzo cha furahaha yangu kinatoka

katika kina kirefu cha chemchem,huko Ulaya.....nafikiri nimezama katika mapenzi.

Inatosha kwa sasa, Wako mtiifu,Muthoni Kirumba. Kwa kutazama picha zaidi unaweza

kunifuatilia kwenye Facebook kwa jina la Muthoni Kirumba na kwa jina la –soni-k kati-

ka ukurasa wangu rasmi wa instagram.Tafadhali fuatilia pia mayakenya kwenye uku-

rasa instagram,twitter: mayakenya7 na ukurasa wa facobook unaoitwa Market

&Advertise youAfrika..Barikiwa.)

Muthoni Kirumba (Kenya), mshiriki , Semina ya kimataifa ya vijana-Celje, Slovenia.

Page 7: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

7

MUONGOZO

Muongozo kwa wataalamu wa maswala ya vijana ambao hufanya kazi na vijana na hu-toa msaada kwa vijana katika utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali ya vija-na,muongozo huu umeandaliwa na mradi wa Active For Future. Mradi unaofadhiliwa na Erasmus + ,wenye lengo la kuimarisha uwezo wa taasisi zinazofanya kazi na vijana , am-bao umewawezesha washiriki kutoka nchi za Ulaya na Afrika kupata mbinu au muongozo kwa ajili ya wafanyakazi vijana ambao wanapaswa kuwa vielelezo na kusaidia kukamilisha mipango ya vijana. Kushabihiana katika shughuli mbalimbali ambazo ni shughuli za washiriki wa mradi kama vile(shughuli halali zinazofanywa na vijana mi-taani,kilimo,ufundi,sanaa pamoja na kazi za kujitolea) zimetusaidia kutambua kuwa mbinu tulizoziandaa kupitia huu mradi zinaweza kufanya kazi katika mazingira mbalim-bali na maeneo tofauti.

Kila mtaalamu wa maswala ya vijana atakaetumia muongozo huu , mwishoni ataomb-wa kueleza uzoefu wake katika kutumia muongozo huu kwa mifano dhahiri, namna gani ameweza fanya kazi na vijana katika mazingira mbalimbali na maeneo mbalimbali ya ulimwengu.

Miradi ya vijana ni mwanzo bora wa kuimarisha ustadi wa vijana katika utambuzi wa mawazo, ambapo vijana wanapanga, wanatekeleza na kutathmini miradi iliyopo katika mazingira yao, hivyo msukumo wa utekelezaji na ushirikiano ni mkubwa na unatoa nafasi nzuri ya mfumo usio rasmi wa kujifunza, kupata na kuimarisha ujuzi na ustadi.

Page 8: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

8

Jukumu la wataalamu wa maswala ya vijana ni kutoa msaada na ushauri katika utekelezaji wa mipango au miradi ya vijana. Hivyo mradi unakuwa unatekelezwa na vija-na kwa msaada wa wataalamu wa maswala ya vijana, hususani katika ushauri, mipango na usimamizi wa fedha . Kwa njia hii wataalamu wa maswala ya vijana huwapa vijana ufumbuzi na ujuzi wa kuandaa pendekezo la mradi, njia za kupata ufadhili kwa ajili ya mradi huo, njia za habari na mawasiliano kwaajili ya mradi huo; msaada wa kitaalamu kulingana na maudhui ya mawazo yao; njia za kutangaza na kukuza mradi, ushirikiano, utekelezaji wa kiufundi , kusitisha na kutathmini miradi.

Ufuatiliaji kabla na baada ya utekelezaji wa mpango/mradi wa vijana ni muhimu kwa wataalamu wa maswala ya vijana kwasababu njia hii inasaidia kuweza kupima matokeo ya mipango/miradi ya vijana.

Page 9: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

9

Kupitia uzoefu wa utekelezaji wa mradi wa Active For Future, unaojumuisha mbinu mba-limbali na njia za kufuatilia mipango/miradi, tumeweza kuona mengi ambayo vijana wanapitia katika miradi yao.Hivyo tumeandaa hatua za kujifunza na kufanya kazi na vija-na,ambazo vijana wanatakiwa wazifuate kuanzia kwenye mipango yao hadi watakapofi-ka hatua ya kuanza utekelezaji wa kazi zao za mwanzo.

Chapisho hili ni muongozo kwa wataalamu wa maswala ya vijana, mashirika ya vijana, mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa na muongozo huu , ambayo yanahusika na ushiriki wa vijana na kusaidia utekelezaji wa mipango/miradi kwa ajili ya vijana. Muongozo huu unakuletea hatua za utekelezaji wa mipango ya vijana, kama ambavyo uzoefu uliopatikana kupitia mradi wa Active for future.

Sonja Majcen

Page 10: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

10

KUHUSU MRADI WA ACTIVE FOR FUTURE

Lengo:

Mfumo usio rasmi wa upatikanaji wa ujuzi na maarifa ambayo waajiri wanatarajia kuya-pata kutoka kwa vijana wanaotafuta kazi umekuwa ukipata umaarufu na thamani kubwa katika kuchangia utaalamu pamoja na maendeleo , na mfumo huu ni muhimu sa-na kwa vijana katika kutafuta na kupata ujuzi.

Mradi wa Active For Future umelenga kuwajenga watalaamu wa maswala ya vijana ujuzi,maarifa na uwezo wa kuongeza uzalishaji na kuongeza fursa za ajira, na kuwapa zana mpya zinazoweza kutumika katika shughuli zao za kila siku pia kuboresha mazingi-ra ya kukuza ajira kwa vijana.

Page 11: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

11

Malengo ya mradi:

1. Kuanzisha ushirikiano na kufanya utafiti juu ya hali ya ajira kwa vijana katika nchi shiriki, kwa lengo la kubadilishana uzoefu,kupata mbinu mpya za kupambana na swala la ukosefu wa ajira wa vijana

2. Kuyajengea uwezo mashirika ya vijana na wataalamu wa maswala ya vijana katika kuhakikisha malengo ya vijana yanafikiwa na jinsi ya kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana kupitia jitihada za vijana (kufanya kazi katika vikundi vidogo katika maeneo yao)

3. Kutoa mafunzo kwa wataalamu wa maswala ya vijana 12 kuhusiana na ajira kwa vijana na mipango/miradi ya vijana na kuwapa ujuzi na maarifa ya kuendesha shughuli za vikundi katika maeneo yao(ambayo watapata mafunzo hayo kupitia mafunzo ya kimataifa ya wataalamu wa maswala ya vijana)

4. Kuandaa muongozo kwa wataalamu wa maswala ya vijana ambao unaweza kutumi-ka katika nchi zote shiriki pamoja na mashirika yote ya vijana ambayo yanashirikiana na washirika wa mradi wa Active for future

5. Kuongeza ustadi wa vijana watakapokua wakifanya kazi kwa vitendo kupitia mi-pango/miradi ambayo itatekelezwa katika jamii zao - ustadi utaopatikana wakati wa utekelezaji wa shughuli hizo utaongeza nafasi yao katika kupata ajira

6. Kutekeleza miradi nane ya vijana katika maeneo yao ambayo itaonyesha njia na mbinu bora ambazo zitajumuishwa katika muongozo utakaoandaliwa.

Page 12: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

12

7. Kuendeleza na kuanzisha mtandao wa washirika ambao watabadilishana ujuzi na ku-shirikishana uzoefu na watatumia muongozo utakaoandaliwa kama zana ya kujifunzia katika shughuli zao za kila siku 8. Kuimarisha mtandao wa mashirika ya vijana na kupata mtazamo mpya jinsi ya kuka-biliana na ukosefu wa ajira wa vijana (Katika kipindi chote cha mradi). Muda wa mradi: 1.10.2015-30.9.2017 (miezi 24)

Page 13: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

13

Duration of the project: 1.10.2015-30.9.2017 (24 months)

Project partners:

Uganda Youth Skills Training Organization (UYSTO) – Kampala, Uganda

Volunteer Action for Change Kenya – Nairobi, Kenya

National Management School – Sofia, Bulgaria

Celjski Mladinski Center – Celje, Slovenia

Romanian Youth Forum – Bucharest, Romania

Amsha Institute of Rural Entrepreneurship – Dar es Salaam, Tanzania

Washirika wa mradi:

Uganda Youth Skills Training Organization (UYSTO) – Kampala, Uganda

Volunteer Action for Change Kenya – Nairobi, Kenija

National Management School – Sofia, Bolgarija

Celjski Mladinski Center – Celje, Slovenija

Romanian Youth Forum – Bucharest, Romunija

Amsha Institute of Rural Entrepreneurship – Dar es Salaam, Tanzanija

Page 14: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

14

Page 15: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

15

MPANGO/MRADI WA VIJANA

Mpango/mradi wa vijana ni nini? Ni mojawapo ya njia inayoshughulika au kutatua changamoto za vijana, iliyoanzishwa na kusimamiwa na vijana. Mpango wa vijana huwezesha idadi kubwa ya vijana kuwa wagunduzi katika maisha yao ya kila siku na kuweza kuzungumza juu ya mahitaji yao ya ndani, maslahi na masuala mbalimbali ya ulimwengu.

Mpango wa vijana unawalenga vijana na mashirika ya vijana, hivyo wazee wanaweza kuingizwa kama washauri, wahadhiri au walimu katika kuwezesha mshikamano na ushirikiano. Katika utekelezaji wa mipango/miradi ya Vijana, Vijana wanapata msaada kutoka kwa wataalamu wa maswla ya vijana ambao huwaongoza katika mchakato mzi-ma wa utekelezaji wa mpango wa vijana. Mipango ya Vijana inaweza kutekelezwa kwa namna mbalimbali, bila gharama na kwa kujitolea.

Page 16: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

16

Mpango wa vijana ni mchakato wa kujifunza, ambapo vijana hupata ujuzi mpya na maarifa na uhamasikaji ambao baadaye husaidia kuongeza fursa za ajira kwa vijana. Kupitia mradi wa Active For Future ,Vijana wamejifunza ujuzi wa kuandika kazi za mradi na kuandaa mipango, ubunifu wa mawazo,; Usisamizi wa fedha za mipango/miradi ; Usimamizi wa miradi, Usimamizi wa rasilimali watu, kazii; Ujuzi wa masoko au uende-lezaji ,ujuzi unaohusiana na teknolojia ya habari na mawasiliano - ICT (kubuni vipeperu-shi na mabango, shughuli za uhamasishaji kwa kutumia mitandao ya kijamii i, mawasili-ano ya kisasa, ..).

Jukumu la mtaalamu wa maswala ya vijana, sio tu kushauri na kutatua matatizo wakati / ikiwa yatatokea ndani ya mpango/mradi wa vijana,bali kuwajengea uwezo vijana kwa namna ambayo wataweza kupata matokeo chanya wakati wa ya mchakato wa utekelezaji wa mpango wao.

Page 17: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

17

Kabla ya utekelezaji wa mradi wa vijana,mtaalamu wa maswala ya vijana ajadili pamo-ja na kuamua kwa pamoja na vijana uwezekano wa kutekeleza mpango/mradi katika mazingira mahususi. Inahitajika wazo litoshelezwe,ijulikane kama kuna idadi ya kutosha ya vijana ambao watashiriki,ni rasilimali zipi za kifedha zitakazohitajika,miundo mbinu inayohitajika,uwezo wa kitaalamu wa kufanya kazi,vyanzo vya fedha vilivyopo,wakati unaofaa kutekeleza mradi na malengo yanayotakiwa kufikiwa.

Kwa wataalamu wa maswala ya vijana katika sehemu hii ni muhimu sana kuchukua juku-mu kwa kiwango cha kile wanachama wa mpango wa vijana wanaotaka au wanahitaji, HAIRUHUSIWI kuingilia maudhui ya mpango wa vijana na isipokuwa katika kujenga mawasiliano sawa (ufadhili unakaribishwa).

Mipango ya vijana inatofautiana sana katika maudhui na dhamira pamoja na mpangilio wa shughuli zinazofanywa.

Page 18: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

18

Aina ya mipango/miradi inatofautiana kulingana na asili ya maudhui, inaweza kupatika-na kutoka kwa makundi yasiyo rasmi,watu binafsi,makundi ya vijana na hata wataalamu wa maswala ya vijana.Maudhui haya yanatofautiana kulingana na mahitaji ya vijana katika mazingira husika.Hvyo miradi ya vijana huweza kuwa inayohusiana na utamadu-ni,utunzaji wa mazingira,kilimo, pamoja na ujasiliamali........Baadhi ya mipango /miradi ya vijana ambayo iilifanyika ndani ya mradi wa active for future imeambatanishwa kati-ka chapisho hili.

Mipango/miradi ya vijana ni njia bora ya kuimarisha ujuzi wa ujasiriamali na kwa miaka kadhaa imeonesha kuwa na matokeo chanya katika kuongeza kiwango cha ajira kwa vija-na. Vijana ambao hawajawahi kushiriki katika mipango/miradi yoyote wameunganishwa pamoja na kuweza kupata au kuongeza ujuzi ambao unahitajika kwa ajili ya ushindani katika soko la ajira.

Page 19: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

19

HATUA ZA KUFUATA KATIKA KUTAMBUA MPAN-

GO/MRADI WA VIJANA

Awali, ni muhimu Kutambua maudhui ya mpango wa vijana ambapo katika hatua hii wataalamu wa maswala ya vijana, watakuwa tu kama waelekezi na si kama waamuzi wa maudhui ya mradi huo.Jambo la muhimu katika utekelezaji huu ni kupata ujuzi na mafunzo rasmi na kupitia majaribio . Jukumu la mtaalamu wa maswala ya vijana ni kufu-atilia mchakato mzima wa kujifunza kutokea mwanzo.

Fursa zinazotolewa kwa vijana katika utekelezaji wa mipango/miradi ya vijana hasa zi-nahusiana na kupata na kuimarisha:

Ujuzi wa utambuzi;

Ujuzi wa kijamii na;

Kuanzisha na kukuza mahusiano (ujuzi wa mawasiliano, majadiliano ya vikundi, kusikiliza kwa makini ,kujenga hoja na usimamizi wa watu, ....);

Ujuzi juu ya makundi tofauti ya watu (uwazi kwa wengine,utofauti, kuendeleza mshikamano, heshima kwa misingi ya kidemokrasia ya haki za binadamu na usawa, ..);

Ujuzi wa kisayansi na kimkakati (kujaza fomu, kuzingatia muda , kupanga na utekelezaji wa shughuli mbalimbali ...);

Ujuzi wa kisiasa (kuendeleza mazungumzo na watoa maamuzi).

Page 20: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

20

Hatua muhimu katika utekelezaji wa Mpango/Mradi wa vijana : upangaji , utekelezaji , tathmini, ufuatiliaji na tathimini ya matokeo.

1. UPANGAJI(MIPANGO)

Katika mchakato wa kupanga vijana huandaa mradi, mpango wa shughuli, gharama za uendeshaji , rasilimali hitajika na mgawanyo wa kazi ndani ya kikundi.

2. UTEKELEZAJI

Awamu ya utekelezaji inahusisha kutekeleza shughuli zilizopangwa mwanzoni wakati wa kubuni wazo hii ni pamoja na kuheshimu makubaliano ambayo yamefanyika ndani ya kikundi pamoja na wadau wengine na mwisho kufuatilia mchakato mzima pamoja nna matokeo.

3. TATHMINI

Sehemu ya tathmini inahusisha kufuatilia na kutathmini maendeleo ya mradi mzima, na si mwishoni tu mwa mradi.

Page 21: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

21

Tathmini inatuwezesha kufuatilia hatua zote za mradi/ mpango wa vijana pamoja na kufuatilia na kushirikishana uzoefu katika kujifunza na kujifunza kwa pamoja.

4. UFUATILIAJI WA SHUGHULI NA UBORESHAJI

Pamoja na kuhitimisha mradi/mpango wa vijana, ni muhimu elimu, ujuzi na maarifa kuendelea kutumika au kuboreshwa.wataalamu wa maswala ya vijana wahimize vijana kuangalia uwezekano wa kupata kazi zaidi,kuboresha,kutumia au kuhamisha ujuzi uli-opatikana.

5. MATOKEO

Kila shughulI katika mpango/mradi wa vijana ina matokeo ya moja kwa moja,au yasiyo ya moja kwa moja. Jukumu la mtaalamu wa maswala ya vijana ni kufanya kazi na vijana wanaofanya au kushiriki katika mpango/mradi huo kuchunguza kwa pamoja matokeo ya shughuli moja moja katika mazingira ambayo mradi unatekelezwa.

Page 22: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

22

MUUNDO WA MRADI/MPANGO WA VIJANA

Kabla ya hatua ya kupanga juu ya Mradi/mpango wa vijana ,baadhi ya vipengele vya mradi huo vinatakiwa kufanyiwa kazi kwa kiwango ambacho mpango mzima wa mradi utaweza kujulikana , malengo yake, athari, matokeo, shughuli, washiriki na makadirio ya gharama.

Muundo wa mradi/mpango wa vijana unatakiwa kuweza kujibu maswali yafuatayo:

1. Mosi, ni muhimu kufafanua mazingira ya mradi na motisha:

Kwa nini wazo hili ni muhimu kwa vijana?

Kwa nini walitaka kulitekeleza?

Je, mazingira ya mradi ni yapi?

Je, vijana ambao watashiriki katika mpango huo watapata motisha gani?

2. Kisha ni muhimu kufafanua wazi malengo na maazimio ya mradi:

Lengo ni nini na malengo ya mradi wa vijana ni yapi?

Malengo yapi vijana wanataka kuyafikia na ni kwa nini?

Ni mabadiliko gani ambayo mradi huu utaleta kwa vijana na kwa njia gani?

Page 23: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

23

3. Hatua inayofuata ni kutambua wanufaika:

Nani watafaidika na mradi huo?

Ni nani watu ambao mradi huu utawagusa moja kwa moja na ni faida gani watapa-ta?

Je! Vijana watafaidika kutokana na mradi huo?

Nini matarajio yao?, kuna vitu watajifunza?

4. Katika utekelezaji shughuli zote zinapangwa vizuri, ambapo pia ni muhimu kuwe na maandalizi:

Ni shughuli gani zinazopaswa kufanywa ili kujiandaa kwa utekelezaji wa mradi na kufikia malengo?

Page 24: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

24

5. Ushiriki wa wanakikundi:

Ni kwa jinsi gani kila mwanakikundi wa kikundi cha vijana atawajibika na kutekele-za wazo la mradi?

Je, wanakikundi wote wanaweza kuchangia katika kujenga na kuendeleza mawazo?

Je, kuna kiongozi katika kikundi?

Ni majukumu gani yaliyopo ndani ya kikundi na ni njia gani za mawasiliano zitakazotumiwa na kikundi katika kipindi chote cha mradi huo?

6. Kila mpango /mradi wa vijana unakua na matokeo fulani (chanya au hasi) katika maz-ingira ambapo mradi/mpango unafanyika, hivyo ni muhimu kuyatambua mazingira hayo:

Je, ni mawakala au taasisi zipi ambazo zimehusishwa katika mpango/mradi huo na zipo tayari kusaidia katika utekelezaji wake?

Je, ni muhimu kwa kina nani kushiriki katika mradi huo na matokeo yake yakawe-za kuonekana kwa jamii nzima?

Wakati wa kupanga maswala yanayohusu mradi/mpango wa viijana , ni muhimu kuzingatia ufafanuzi sahihi wa shughuli, ambapo muda wa kuanza na kumalizika kwa utekelezaji wa mradi unakuwa unafahamika vizuri. Shughuli zinazofanyika ni lazima zipelekee kutimia kwa lengo ambalo limewekwa katika hatua za mwanzo za kuandaa mradi/mpango, Pia ni lazima yajumuishwe maeneo yote ambayo yatahusika katika utendaji/utekelezaji. Ni muhimu kuyafahamu majukumu ya kila mshiriki na wajibu wake katika utekelezaji wa shughuli za mtu mmoja mmoja. Hii inasaidia kukuza uwezo wa kila mmoja na pia wanajifunza kuheshimu wajibu walionao katika kazi, vikundi na mazingi-ra ya jamii ambayo wanafanya nayo kazi na zaidi ya hayo inawaongezea ujuzi wa uongozI.

Page 25: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

25

Wakati wa kupanga kuhusiana na bajeti ya mradi wa vijana, ni busara kwa vijana waka-kaa pamoja na kuangalia gharama zitakazotakiwa katika utekelezaji wa mradi/mpango, yaani ni rasilimali zipi zinahitajika katika utekelezaji wa mpango/mradi. Katika mipango/miradi ya vijana huwa kunakuwa na gharama tofauti ambazo zinaweza kugawanywa kulingana na shughuli moja moja hivyo inawezekana kupanga ni wakati gani gharama hizo zitahitajika kutumika, gharama hizo zinaweza kuwa gharama za vifaa, gharama za huduma za nje n.k kwa kila shughuli.

Jukumu la vijana ni kutathmini mradi mara kwa mara, kuamua namna ambayo watatath-mini mchakato na matokeo ili kufikia lengo ambalo walianza nalo toka mwanzo. Katika tathmini hatupaswi kusahau kwamba ni muhimu kutathmini kazi ya kikundi na matokeo ya mradi katika jamii inayotuzunguka.

Page 26: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

26

Mwisho wa mradi/mpango wa vijana si pale tu mradi unapokamilika, bali katika kipin-di cha utekelezaji na ufuatiliaji huwa unajitokeza uwezekano wa kuboresha , hii huwa ni matokeo ya mchango wa vijana ambao wanahusika kwa namna moja au nyingine na mradi huo,pia vijana huwa wanaweza kuamua ni hatua gani muhimu za kuchukua ili mradi/ au sehemu ya mradi kuweza kuendelea hata pale mradi unapokuwa umekamili-ka.Mradi unapokuwa umekamilika vijana huwa wanakabiliana na changamoto mbalim-bali kuhusiana na namna ambayo wataweza kuuboreha mradi, kuanzisha miradi mipya na kuhusu matarajio yao juu ya kuendelea kwa ushirikiano wao katika miradi ijayo.

Page 27: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

27

Kila mtaalamu wa maswala ya vijana ambaye anashiriki kama mshauri katika mpango/mradi wa vijana, kwa kushirikiana na vijana anahitaji kutambua kiwango cha ushiriki wake ambacho hakitaathiri katika kujenga mawazo na utekelezaji wa mradi . Mfan-yakazi wa vijana kwa kushirikiana na vijana wanapaswa kuamua njia ya mawasiliano, jinsi ya kutoa ripoti na msaada mwingine ambao vijana watauhitaji.

Kwa ujumla, mfanyakazi wa vijana anaongoza vijana kujibu maswali yafuatayo wakati wa kuandaa mradi wao:

NINI – kuelezea malengo na shughuli za mradi.

KWANINI - nini kusudi na sababu kutekeleza mradi/mpango.

KWAAJIII YA NANI ?- mradi unamlenga nani?

NANI?- Ni nani anaunda kundi letu kwaajili ya utekelezaji wa mradi na washirika wetu ni kina nani.

KWA JINSI GANI?- Njia gani zitatumika kutekeleza mradi huo na kufikia malengo yake.

WAPI?- Kuamua eneo la mradi huo.

LINI? - Kupanga muda wa kila shughuli na muda wa kumalizika kwake.

Changamoto tunayokabiliana nayo katika utekelezaji wa miradi/mipango ya vijana, ni ufafanuzi wa malengo, utambuzi wa rasilimali, mienendo ya kikundi ,uongozi pamoja na usimamizI.

Page 28: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

28

Jukumu la mtaalamu wa maswala ya vijana katika mchakato wote kuanzia kwenye mi-pango,utekelezaji,ufuatiliaji,uboreshaji na tathmini ni kuhakikisha kwamba anafuatilia vizuri mchakato wa kujifunza kwa vijana wanaoshiriki wa mradi.Ni lazima kutambua kwamba ubora na ufanisi wa mpango/ mradi wa vijana hautachukuliwa kama ambavyo imeainishwa katika malengo ya mradi ,bali kama hatua ya ukuaji binafsi na kuongeza uzoefu kupitia mchakato mzima wa kujifunza ambao unajumuisha watu kufanya ka-zi,kujitambua ,mawasiliano,utatuzi wa matatizo na uhuru katika maamuzi binafsi.Chini ya mpango/mradi wa vijana, vijana wanaweza kujifunza mambo mbalimbali kama kudumisha ushiriki, kuimarisha maendeleo binafsi na kushiriki vizuri katika shughuli za maendeleo binafsi na ya jamii kwa ujumla.

Page 29: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

29

Mpango/mradi wa vijana unatoa nafasi ya kuwaunganisha vijana wenye mawazo ya kufanana katika mfumo wa kufanya shughuli na kutekeleza miradi yao katika vikundi visivyo rasmi na vilivyo rasmi i(kama ushirika).

Katika hatua ya utekelezaji wa miradi chini ya ushirika mtaalamu wa maswala ya vijana anatakiwa kufanya kazi kama vile ambavyo zimepangwa katika huo ushirika.Tofauti na ilivyo katika mipango ya kawaida ya vijana, miradi inayotekelezwa chini ya ushirika hu-wapa vijana ngazi ya juu ya utaalamu na kuwaongezea uwezo mkubwa wa utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Page 30: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

30

Washirika katika mradi wa Active For Future kupitia uzoefu wao wa utekelezaji wa mira-di ya vijana katika ushirika,wameweza kuandaa muongozo wenye vipengele vifuatavyo:

1. Kuamua matarajio halisi na malengo;kwakupitia miradi mbalimbali vijana wanaweza wakajifunza kama malengo ya mradi yanaendana na malengo yao binafsi.

2. Kukubali wajibu; katika kutekeleza mradi vijana wanakabiliwa na changamoto ya kuku-bali wajibu(mfano kuwa kiongozi katika semina ya vijana).Hapa panahitaji mazungumzo ya kina kati ya vijana na mtaalamu wa maswala ya vijana.

3. Uelewa wa uwezo walionao na chaguzi zilizopo;vijana wanapata fursa nyingi za ushiri-ki lakini wanakabiliwa na changamoto ya vipaumbele vyao kama vitaendana na malengo ya wadau,hapa yanatakiwa maamuzi muhimu kuhusu mwelekeo wa utendaji wa kazi.

4. Uelewa wa jitihada na fursa za kiuchumi; vijana hujifunza thamani ya kazi zao wenyewe,uwekezaji katika muda na suala la kuboresha kazi zao,hapa hujitokeza maswali ya ndani juu ya utendaji wenye tija.

5. Kutatua matatizo ni mojawapo ya jambo la muhimu katika utekelezaji wa miradi . Vija-na kuweza kuyaelewa matatizo kunaweza kusaidia katika kuendeleza kazi za vijana au kusitisha kazi zinazoendelea . hapa msaada wa mfanyakazi wa vijana huitajika zaidi.

Page 31: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

31

UJUZI NA UMAHIRI

»Umahiri unafasiliwa na bunge la ulaya kama 'muunganiko wa maarifa,ujuzi pamoja na mtazamo katika muktadha husika'.umahiri wa msingi ni ule am bao mtu anauhitaji kwaajili ya maendeleo binafsi,uraia hai,ushirikishwaji pamoja na kuweza kupata ajira.umahiri unahamishika,unajumuisha na unaunganisha na kutengeneza msingi wa mafunzo endelevu «.

(Key competence for life long learningin the program Youth in Action, Ljubljana: Movit NA Mladina, 2009).

Page 32: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

32

Kwa mujibu wa fasili hiyo., umahiri umegawanyika katika sehemu nane:

1. Mawasiliano kwa kutumia lugha mama

2. Mawasiliano kwa kutumia lugha za kigeni

3. Uwezo katika hisabati na ujuzi wa msingi katika sayansi na teknolojia

4. Uwezo wa kidigitali

5. Uwezo wa kuweza kujifunza

6. Umahiri katika Ustawi wa kijamii na kiraia

7. Jitihada binafsi na kujituma

8. Utambuzi tamaduni na uwezo wa kujieleza

Key competences for lifelong learning in the program Youth in action, Ljubljana: Movit NA Mladina, 2009).

»Umahiri huu ni muhimu kwa ajili ya utendaji bora katika maisha ya mtu binafsi,kazi na kujifunza kusiko na kikomo.» Key competences for lifelong learning in the program Youth in action,

Ljubljana: Movit NA Mladina, 2009).

Wakati wa kupanga, kutekeleza na kutathmini ya mpango/mradi wa vijana, vijana wana-takiwa kuimarisha umahiri wao kama ilivyoorodheshwa hapo juu ili kuongeza ujuzi wao katika mambo ya kijamii.(kwa kiwango cha kuyakabili majukumu ili kujenga tabia ya mtu kuweza kujitegemea na kusimama mwenyewe )na kupata ujuzi wa hali ya juu katika mambo ya usimamizi wa shirika.

Page 33: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

33

Watalaamu wa maswala ya vijana wanaweza kufuatilia mchakato wa kujifunza na mato-keo ya kujifunza katika mpango/mradi wa vijana wakishirikiana na Youthpass (www.youthpass.eu). Youthpass ni chombo kilicholenga kuimarisha uwezo wa kupata ajira,kuakisi ukuaji binafsi katika mchakato wa kujifunza usio rasmi na kuhamasisha kujulikana na kutambulika kwa kazi za vijana kwa jamii.

Mtaalamu wa maswala ya vijana kwa kutumia mbinu tofauti anaweza kufuatilia kwa ukaribu mchakato usio rasmi wa kujifunza kwa kila mshiriki wa mradi/mpango wa vija-na na wote kwa pamoja wanaweza kufuatilia matokeo katika mchakato wa kujifunza.

Page 34: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

34

KUELEKEA KATIKA AJIRA

Kupitia mpango/mradi wa vijana, vijana wanapata na kuendeleza ujuzi ,maarifa,wanakuza mtandao pamoja na ushirikiano,wanaweza kuongeza uwezo wao katika ujasiriamali na uwezekano wa kujiajiri na kupambana na ushindani katika soko la ajira.Kupitia mchakato huu,vijana wanakuwa na uwezo wa kuthaminisha ujuzi,maarifa na uwezo walionao na kuanza kufikiri juu ya matumizi bora na umuhimu wa uwezo,ujuzi na maarifa waliyonayo.

Katika mpango/mradi wa vijana tunapaswa kutofautisha mambo muhimu mawili ya kuji-funza:

Mchakato wa kujifunza ambao huleta matokeo ya kujifunza kupitia utekelezaji wa mipango ya vijana na

Ujuzi unaotolewa katika mazingira ya mipango/miradi ya vijana na lengo la mipan-go/miradi ya vijana.

Page 35: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

35

Kujifunza kupitia mpango/mradi wa vijana inawakilisha mojawapo ya nguzo muhimu. Sababu muhimu ya kuwashirikisha wataalamu wa maswala ya vijana katika mpango/mradi wa vijana ni kuongeza uelewa kwa vijana juu ya umuhimu wa maendeleo ya usta-di tofauti kupitia elimu rasmi na isiyo rasmi.

Vijana wanaweza kuanzisha mambo wanayoyatamani wao wenyewe na kutoa miongozo ya maendeleo juu ya njia zao za kujiajiri kupitia miradi ya vijana , wanaweza kujua kwam-ba wana uwezo wa kuunda kazi zao kupitia mipango/miradi au kujifunza na kupata ujuzi ambao unahitajika kulingana na uchumi wa wakati huo.

Page 36: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

36

MRADI HUU UMENIFANYIA NINI?

Mugabi Enock William (Uganda), mshiriki katika programu ya kutaniko la vijana-Celje: »Ukijaribu kuangalia kama jana tu lakini uzoefu na kumbukumbu tulizozipata katika mji wa Celje zilikuwa ni za pekee. Wanasema huwezi kujua ulichokuwa unakosa mpaka utakapokipata. Kwa msaada wa Erasmus + kupitia mradi wake wa Active for Future,nchi sita zikiwemo Uganda, Tanzania, Kenya, Slovenia nchi mwenyeji-Slovenia, Romania na Bulgaria zimekutana pamoja mjini Celje.«

Urška Pavlovič (Slovenia), mtaalamu wa maswala ya vijana: »Katika mradi wa Active for Future nchini Kenya Nilijifunza zaidi kuliko nilivyotarajia. Ninahisi kama sasa ninajua zaidi kuhusu kufanya kazi na vijana na jinsi ya kuwaongoza ili kufanikisha mipango yao kwa ufanisi. Nilijifunza mengi zaidi juu yangu binafsi kwani tulikuwa katika utamaduni mwingine uliochanganyikana na tamaduni zingine hivyo kufanya mchakato wa kujifunza kuwa mzuri zaidi. Ninashukuru sana kwa fursa hii ambapo nilikutana na watu wengi wap-ya ambao tulitengeneza kumbukumbu za maisha.«

Todor Raykov – mgeni rasmi kwenye shughuli za kikundi za A4F, Sofia, Bulgaria: »Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa timu nzima ya mradi wa Active For Furure kwa kunikaribisha kama mgeni rasmi katika warsha za vikundi vya vijana huko Bulgaria, Katika mada iliyolenga kuleta ufanisi katika kupata fedha za mradi. Malengo ya mpan-go huu wa mafunzo yanashawishi na kuhamasisha sana, nilikuwa na furaha kuunga mkono jitihada hizi katika kusambaza ujuzi na uzoefu mzuri ambao unaweza kusaidia kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana katika nchi shiriki.«

Page 37: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

37

Enock Musasizi (Uganda) - mshiriki katika CeljeYouth Exchange: »Tulifanya shughuli nyingi lakini bora zaidi ilikuwa n utafiti kuhusu Celje. Ilikuwa namna mpya ya kujifunza kwa sababu wakati mwingi mwalimu anakupa habari habari kwa ufupi lakini fursa ikipatikana unafanya utafiti huo wewe mwenyewe na hiyo inasaidia kuongeza ufahamu na uwezo wa mtu kuwasiliana na watu tofauti.Asante kwa ujuzi na maarifa pamoja na kutunganisha watu kutoka asili tofauti.«

Page 38: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

38

MIFANO YA MIRADI BORA AMBAYO IMEANDALI-

WA KATIKA KIPINDI CHA UTEKELEZAJI WA

MRADI WA ACTIVE FOR FUTURE

MRADI WA SKILLSHARE (BULGARIA)

Skillshare ni mradi/mpango wa vijana ambao Ulianzishwa wakati wa mafunzo ya siku 4 yaliyofanyika huko Sofia chini ya Mradi wa Active for future (Programu ya Erasmus + ya kuwajengea uwezo vijana). Wakati wa mafunzo, kulikuwa na mihadhara na semina zili-zotoa muongozo katika kuandaa mpango/mradi , na baadae mpango/mradi huu wa vija-na ulipatikana kutokana na mjadala na kazi ya kikundi ya vijana 10 kutoka Sofia.. Mpan-go/mradi wa vijana wa skillshare unalenga kuboresha mazingira ya maisha ya wazee katika mji wa Sofia kwa kujenga mfumo wa ushirikiano wa pamoja kati ya wazee na vija-na.

Bulgaria ni nchi ya Umoja wa Ulaya yenye kiwango cha juu zaidi cha wazee walio katika hatari ya umaskini, na kutengwa kijamii. Tatizo kubwa linalozungumzwa na mradi huu ni kiwango cha chini cha maisha na umaskini kwa wazee nchini. Wazee wengi hawawezi kupata kazi ambayo inaweza kuwasaidia kiuchumi, ingawa wana uwezo wa kutoa na kuutumia ujuzi wao lakini hawana soko la kufanya hivyo.Asilimia kubwa ya wazee nchini Bulgaria wana sifa na stadi maalumu za kufanya kazi wakati Kwa upande mwingine, kuna asilimia kubwa ya vijana ambao wanatafuta msaada binafsi ili kupata ujuzi fulani au maarifa.

Page 39: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

39

SkillShare - "Shirikisha ujuzi wako" ni mpango ambao unalenga kujenga uhusiano kati ya wazee wenye ujuzi maalum na vijana ambao ujuzi huu utawasaidia. Lengo ni kuwasaidia wazee wanaoishi kwa pensheni kidogo na kutengwa na jamii, huku wana ujuzi maalum na / au ujuzi kutokana na uzoefu wa kitaalamu wa miaka mingi kwa kuunda uhusiano kati yao na vijana ambao wangeweza kununua huu Ujuzi. Maono ya mradi wa SkillShare ni kujenga jamii ambayo vizazi tofauti vitapata manufaa.

KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAZAO BAADA YA MAVUNO KWA KU-

WAUNGANISHA WAKULIMA WADOGO NA MASOKO (TANZANIA)

Upotevu wa mazao baada ya mavuno umeleta changamoto kubwa katika Kuimarisha mnyororo wa thamani. Ripoti iliyotolewa mapema mwaka huu na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) la Umoja wa Mataifa iligundua kuwa karibu theluthi moja ya chakula kili-chozalishwa duniani kwa ajili ya matumizi ya binadamu ambayo ni sawa na tani milioni 1.4 hupotea kila mwaka. Na zaidi ni upotevu wa virutubisho vinavyotokana na mboga mboga, matunda, samaki, nyama na maziwa - ambapo karibu asilimia 50 hupotea kila mwaka. Karibu nusu ya hasara hiyo hutokea baada ya chakula kuwa kimeshavunwa am-bapo husababisha sio tu mapato ya chini Kwa wakulima wadogo bali pia huuzwa bei kubwa kwa watumiaji, hii ni kutokana kukosekana kwa njia bora za uhifadhi na soko la kuaminika. Mpango huu wa vijana utahamasisha matumizi ya vifaa vya uhifadhi vya asili vil-ivyoboreshwa na kufikisha mazao ya wakulima sokoni kwa wakati .Lengo la Kuanzisha vifaa vilivyoboreshwa vya kuhifadhia chakula katika kilimo ni kupunguza upotevu baada ya mavuno. Msingi wa ugunduzi huu ni kuwasaidia wakulima wadogo kupata mapato bora kwa kuhifadhi na kuuza bidhaa zinazozalishwa katika soko la kuaminika zikiwa na ubora wake.

Page 40: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

40

Lengo ni kuongeza kiwango cha kawaida cha mapato kwa wakulima wadogo katika mnyorororo wa thamani kwa kuwapatia vifaa vilivyoboreshwa vya kuhifadhia na ku-waunganisha na soko la kuaminika. Mpango huu unatarajiwa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 100 ifikapo mwaka 2019, ambapo matarajio ni wafanyakazi zaidi ya 100 rasmi na 300 wasio rasmi. Kwa kiasi kikubwa mpango utapunguza uchafuzi wa mazingira unaosaba-bishwa na taka za chakula. ambapo kwa sasa jumla ya tani milioni 1.2 ya chakulakwa mwaka hugeuka kuwa taka na kuchafua miji hasa katika maeneo ya masoko. Hivyo tutapunguza uharibifu wa chakula kwa kutumia vifaa vilivyoboreshwa vya kuhifadhia vyakula, ili kuepuka taka ambazo hazihitajiki na kupunguza upotevu wa chakula. Mradi utawasaidia wakulima kwa kuongeza mapato yao. Tunatarajia kuongeza mapato kuwa dola za Marekani 3,124 kwa kila mkulima (kutoka dola za kimarekani 540 kwa mwaka) katika miaka 6 ijayo Hili itatokana na kuongezeka kwa mauzo ya mazao yao kwenye soko la kuaminika. Pia tutasaidia kupunguza changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana nchini Tanzania.

Page 41: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

41

MRADI WA ROAD TO EMPLOYMENT (SLOVENIA)

Kwa kuwa vijana hasa ni watu wasiokuwa na uzoefu wa kutosha katika mambo ya kijamii hivyo kuna haja ya kuwaelimisha zaidi katika kipengele hicho. Hivi sasa, programu ya Erasmus + inawezesha vijana kupata uzoefu na kuongeza ujuzi kupitia mfumo wa kuji-funza usio rasmi, na mojawapo ya suluhisho ni kuandaa semina ya vijana, ambapo washiriki wataweza kubadilishana uzoefu na wataweza kuanzisha mfumo wa ku-badilishana mbinu bora katika usaili wa kupata kazi.. Lengo lla programu ya kutaniko la vijana ni kuwaandaa vijana katika usahili wa kupata ajira zao za kwanza kiasi kwamba watakuwa na uhakika na nafasi kubwa ya kupata ajira. Washiriki wa mradi watashiri-kishwa katika maandalizi ya mradi wenyewe, tangu mwanzo hadi mwisho ambapo uta-wawezesha kujifunza kuhusu usimamizi wa mradi, usimamizi wa fedha na mengineyo. Matokeo yanayotarajiwa katika mradi huo ni kuandaa vijana kwa usaili wao wa kwanza wa kazi, kuboresha stadi zao za kijamii ili ziwe bora, kuwajulisha kuhusu mambo wanayohitaji kuyajua kabla ya kufanya usaili na kuwaelimisha juu ya hali ya soko la ajira kwa sasa.

Page 42: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

42

MRADI WA CAFÉ: NA OFF (SLOVENIA) Wazo ni kufungua mgahawa ambayo kila siku utatoa huduma ya elimu na utamaduni wa watu wenye ulemavu wa kusikia. Mgahawa utawaajiri watu wenye shida za kusikia ambao wanaonekana kuwa na nafasi ndogo za kupata ajira. Madhumuni ya mradi ni kuiunganisha dunia ya watu wanaosikia na wale wenye ulemavu wa kusikia pia kuwafundisha lugha ya ishara watu wanaosikia. Lengo la mradi ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na mapato ya mara kwa mara kwa watu wenye ulemavu wa kusikia ambao hawana nafasi ya kupata ajira katika soko la ajira. Matokeo yanayotarajiwa na huu mradi ni kuongeza ufahamu kwa umma juu ya maisha ya watu wenye ulemavu na matatizo ya kusikia.

Page 43: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

43

MRADI WA WOODEN TOYS (SLOVENIA)

Wazo la kutengeneza na kuuza midoli ya mbao tumelipata toka utotoni.Mali ghafi za kutengenezea midoli ya mbao inaweza kukusanywa kwa urahisi kwenye viwanda vya mbao ambapo hupatikana bure na ni nzuri kwa kutengenezea vitu vidogo vidogo..Mara ya kwanza tutaanza kwa kutengeneza midoli ya watoto wadogo lakini tutaendelea kupanua soko kwa kutengeneza midoli ya mazoezi kwa ajili ya watoto wa umri tofauti tofauti, Matokeo tunayotarajia kupata ni kutengeneza midoli inayotokana na vitu vya asili ambayo ni salama na rafiki kwa mazingira.

Page 44: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

44

S. Y. D. A. R. C – SAVE YOUTH DRUG ABUSE REHABILITATION CENTER (UGANDA)

Maono ya mpango huo ni kutengeneza jamii ya vijana itakayokuwa huru kutoka kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kwa kuhakikisha huduma bora za matibabu kwa watu waloathirika na kuzuia matumizi ya madawa ya kulevya ili kuhakikisha tunapata raia vi-jana wachapakazii, hadi sasa inakadiriwa vijana 140 wanaohudumiwa kwenye hospitali ya akili kutokana na athari za matumizi mabaya ya madawa ya kulevya wengi wao ni vijana kati ya umri wa miaka 18 na 25 na hii imesemekana kuwa ni wachache ambao wamaweza kufika hospitali.Hii inaonesha kuwa hali ni mbaya zaidi katika rika hilo.

Kwa upande mwingine asilimia 22% ya wanafunzi waliopo shuleni wanaaminika kujihu-sisha na matumizi ya madawa ya kulevya (pombe, bangi na kadhalika),wakiwa ni kundi linaloathirika zaidi wanahitaji kuzuiwa,kushauriwa na kuhudumiwa kwa kupewa tiba . Hatua za SYDARC zitashughulikia moja kwa moja changamoto hizi kwa vijana wa Ugan-da. Tatizo hili linazungumzwa katika vyombo vya habari, majumbani na hata katika bunge bunge, lakini jitihada kidogo zimefanywa juu ya suala hili. Mpango/mradi huu utaimarisha ushauri nasaha ,mahusiano na ushirikiano katika maeneo yaliyoathiriwa. SYDARC inalenga kupunguza uwezekano wa vijana na watu wazima kushiriki katika ta-bia za hatari kwa kutoa ushauri na muongozo shuleni, nyumbani na katika Maeneo ya kazi kwa kushiriki na kuwawezesha watu na familia.

Page 45: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

45

UGA CRISPS (UGANDA) Lengo la mpango ni kuanzisha kampuni ya vitafunwa vyenye ubora Afrika Mashariki. Maono ni kwamba timu iliyojumuishwa katika mpango huo itaazisha na kuendeleza huduma ya kutengeneza vitafunwa vyenye ubora wa hali ya juu kwa watu wa Afrika mashariki.Hii itafanywa kwa kutoa mafunzo kwa vijana yanayohusiana na ujuzi pamoja na jinsi ya kuendesha biashara ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vija-na.Malengo ya mpango huu ni kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu,kuajiri vijana katika idara za usimamizi na uzalishaji,kuwafundisha vijana katika maandalizi ya vitafun-wa,kukudhi mahitajiya vitafunwa kwa watu wa Afrika Mashariki hasa katika kipindi hiki cha jumuiya ya Afrika Mashariki,kutoa mafunzo ya kiufundi kuhusiana na biashara na hatimaye kutatua tatizo la ajira kwa vijana.

Page 46: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

46

CAREER CENTRE: CA–HUB (KENYA)

Lengo ni kuanzisha kituo cha kutoa elimu na mafunzo ili kuweza kukabiliana na soko la ajirai. Hii itaunganisha wataalamu wote na wale wanaotaka kuendeleza ujuzi wao. Lengo ni kuimarisha ujuzi kuhusiana na soko la ajira kwa vijana ambao wataweza kupata fursa ya ajira baada ya kuhitimu shule na kutengeneza chanzo cha mapato ambapo nao wa-taweza kuwapa ajira vijana wengine. Kituo hicho kitakuwa kiunganishi kati ya vijana na waajiri wanaopata elimu hivyo kupunguza muda unaopotea katika kutafuta ajira. Mato-keo ya mpango yatakuwa ni: kuongeza uelewa kwa vijana juu ya kazi zilizopo na jinsi ambavyo zinaweza kuwa muhimu katika soko laajirai.Kuwahamasisha vijana kupitia kipindi cha mpito ambapo wataendelezwa katika ujuzi na uzoefu kwa kushirikiana na wanajamii ili kujiandaa kwa hatua zinazofuata katika maisha.Uhusiano ambao unaimar-ishwa kati ya ujuzi ambao mtu anao na mahitaji ya soko. Kupunguza utegemezi katika jamii kwani watu wengi watashiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii.

Page 47: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

47

Page 48: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

48

YEB MUSIC ACADEMY (UGANDA) Youth Evolution Bamivule (YEB Music Academy) ni shirika lisilo la Serikali nchini Uganda ambalo hutoa ujuzi wa kitaaluma kwa vijana ambao wanataka kujiendeleza katika muziki kama ajira yao. Hii ni kwa kutambua, kuwezesha, kukuza na kuimarisha muziki kwa vija-na wote kwa kuwajengea uwezo mzuri na kazi za kutosha katika sekta ya muziki nchini Uganda. Malengo ya mpango wa kuanzisha shirika ni: kuwawezesha vijana kuelekea kazi zao maarufu za muziki. Kutambua na kukuza vipaji maarufu ya muziki; Ili kutengeneza msingi wa rasilimali watu na ushindani kwa sekta maarufu ya muziki; Kutengeneza kiun-ganishi cha kazi kati ya taasisi na makampuni ya nje ya muziki.

Page 49: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

49

Fasihi

Lebič, Tadej in Sonja Majcen. (2013). Od mladinske pobude do prve zaposlitve. Cel-je: Celjski mladinski center, javni zavod za mladinsko kulturo, izobraževanje, in-formiranje in šport.

Zavod MOVIT NA MLADINA. 2009. Ključne kompetence za vseživljenjsko učenje v programu Mladi v akciji. Ljubljana: Zavod MOVIT NA MLADINA.

Page 50: ‘Active for future’ na mradi/mpango wacms.nbschool.eu/files/Active for future_na mradi_mpango... · 2017. 8. 29. · mashirika kwa ajili ya vijana na mashirika mengine yatakayopendezewa

50

Celjski mladinski center, javni zavod za mladinsko kulturo, izobraževanje, informiranje in šport Mariborska 2, SI—3000 Celje T +386 (0)3 490 87 40 E [email protected] W www.mc-celje.si