annuur 1211a.pdf

Click here to load reader

Upload: zanzibariyetu

Post on 26-Jan-2016

1.612 views

Category:

Documents


23 download

TRANSCRIPT

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1211 RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA , JANUARI 8 - 14, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected]

    Soma Uk. 20

    Mh. Magufuli anaturudisha kule kwa Sheikh Takadiri

    Kamkaribisha Mufti Ikulu, lakiniTuna ya kujifunza kwa Mwinyi, MteiJK yalimkuta. Prof. Chachage akajibu

    Dkt. Ali Mohamed Shein MAALIM Seif Sharif Hamad

    RAIS John Pombe Magufuli.

    Maimamu wataka Dk. Shein aheshimu kura za wananchi

    Wasema hakuna Shura baada ya ShuraMapinduzi si kupindua Uchaguzi-KarumeHuo ni usaliti kwa Mapinduzi yenyewe

    Kweli, hofu ya ugaidi huwafanya watu kuwa wajinga kupindukia

    Putin kidume. Awaumbua wenye IS

    MUFT Sheikh Abubakar Zubeir MZEE Edwin Mtei. (Uk. 9)

    Soma Uk. 10

    Kesi ya Sheikh Msellemdanadana zaendelea

    ANNUUR NEW.indd 1 1/7/2016 3:17:00 PM

  • 2 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

    Jee Unajua?

    MASUALA1.Itaje Sura inayotaja juu ya matunda mawili? Jawabu : Attin.2.Jina kamili la Imam Shafi. Jawabu : Muhama Idrissa.3.Sura ipi ya Quran inayomalizia kwa majina ya Mitume wawili? Jawabu : Suratul Al Alaa.4.Alipohama Mtume Muhammad (SAW) Makka kwenda Madina alimtaka sahaba yupi alale kwenye kitanda chake? Jawabu : Ali Abi Talib.5.Suratul Faatiha ina aya ngapi? Jawabu : 7.6.Ashuraa ipo katika mwezi gani wa Kiislamu? Jawabu : Muharam.7.Mtume Hud (AS) alitumwa kwa Umma upi? Jawabu : Ad.8.Mtume Saleh alitumwa kwa Umma upi? Jawabu : Thamood.9.Mtume Mussa alifwatana na Mtume gani kwenda kukabiliana na Firauni? Jawabu : Haroon.10.Jina la ngamia Mtume Muhammad (SAW) alimpanda alipoingia Madina? Jawabu : Kaswah

    JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 33

    CHEMSHA BONGO: 34Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.

    MASUALA1.Jina la kitabu cha Hadithi kilichokusanywa na Imam Malik kinaitwa: Muwatta, Bukhari, Riyadh Salihina.2.Sahaba yupi aliotajwa kwa jina katika Quran? 3.Taja jina la mava ambalo wamezikwa Masahaba na ambalo hadi sasa wanazikwa watu.4.Taja jina kati ya wake wa Mtume Muhammad (SAW) aliokuwa na umri mdogo na alikuwa sio mjane.5.Mtume Muhammad (SAW) alipohajiri kwenda Madina alikuwa na umri gani?6.Mtume Muhammad (SAW) alipohajiri kwenda Madina aliishi Madina kwa miaka mingapi kabla ya kufariki?7. Shahidi wa mwanzo kuuwawa katika Uislamu alikuwa ni: Syd Hamza, Bibi Sumayah au Bilali (RA).8.Mtumwa wa mwazno kusilimu?9. Taurat aliteremshiwa Mtume gani?10.Nimrood aliishi katika zama za Mtume yupi?

    1.Uwanja wa ndege wa Paro uliopo Bhutan ni mmoja kati ya viwanja vya ndege vilivyo hatari duniani, pale inapotaka kutuwa ndege abiria hupewa dawa ya kutopata kushtuka. Marubani 8 tu ambao huruhusiwa kuendesha ndege katika kiwanja hicho, hairuhusiwi ndege kutuwa katika kiwanja hicho nyakati za usiku. Uwanja wa ndege huu upo baina ya nyumba na milima: http://www.curiosityaroused.com/world/12-most-dangerous-airports-to-avoid/2.Nchini Canada pesa ijuliknayo Penny imekuwa haitumiwi tena pesa iliyodumu kutumiwa kwa miaka 154, maamuzi hayo yamekuja kutokana na gharama kubwa inayopatikana katika utengenezwaji wake: http://www.curiosityaroused.com/culture/what-are-pennies-made-of/3.Inakadiriwa kuwa watu wengi duniani wana simu za mkononi kuliko kuwa na vyoo majumbani mwao, aidha inasadikiwa thuluthi ya skuli zote ziliopo duniani huwa hazina vyoo: http://water.org/water-crisis/water-sanitation-facts/4.Kila siku hufa watoto 500 duniani kote kwa kukosa maji safi na salama: http://waterfortheworld.net/index.php?id=125.Makadirio yanaonyesha kuwa dunia hii tuliopo asilimia 72 imezungukwa na maji na kati ya asimia hio ya maji ni asilimia 97 ni maji ya chumvi. http://www.livescience.com/29673-how-much-water-on-earth.html6.Watu Bilioni moja maji safi na salama kwao ni ndoto: http://thewaterproject.org/water_scarcity7.Maji hayana mipaka, inakisiwa kuwa kuna nchi 148 zinagawanya maji na nchi nyengine : http://www.unwater.org/water-cooperation-2013/water-cooperation/facts-and-figures/en/8.Ziwa Victoria lina kilomita za mraba 69,485 km2 ni ziwa la 3 kwa ukubwa duniani : http://10mosttoday.com/10-largest-lakes-in-the-world/9.Yajuwe maziwa yalio makubwa duniani ikiwa Afrika imo kwenye listi hio kuwa na maziwa mengi makubwa : http://www.factmonster.com/ipka/A0001777.htmlMto Nile ndio ulio na masafa marefu ukiwa na kilomita 6,695 ukianzia kutokea Afrika Mashariki : http://www.primaryhomeworkhelp.co.uk/rivers/longest.htm

    A T T I N B A Q A R A A A A

    M U H A M A D I D R I S S A

    S U R A T U L A L A L A A K

    A L I A B I T A L I B 7 8 9

    M U H A R A M A A D U M A R

    T H A M O O D A I S H A A A

    H A R O O N S A F I A A A A

    T H A M O O D J A B A L I I

    K A S W A H H I J R A A H T

    M U S S A K U S A I B A N U

    M A N S B D E Z S L D M I Z

    U L O A I A B A H U A U S A

    W A U L B R R I U T U S S I

    A M H E I S A D A K D S S D

    T U I H S A H I I U M A A H

    T B D T U H I Z B S H M A A

    A A R H M A M Z Y A U W I R

    53 A I A A M A A E Y D E S I

    54 I S M Y Z A H M I U Z H T

    10 E A D H A D N E I Y I A H

    HAKIKA shukrani zote zinamstahikia Allah.

    T u n a m h i m i d i , tunaomba msaada Kwake, na tunaomba maghfira. Tunaomba hifadhi kwake Allah kutokana na maovu ya nafsi zetu, na makosa ya matendo yetu. Yeyote Allah Anayemuongoza, hakuna wa kumpotosha, na yeyote Allah Anayempotosha, hakuna wa kumuongoa. N i n a s h u h u d i a p i a kwamba hakuna yeyote anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah, na ninashuhudia kwamba M u h a m m a d ( S w a l l a Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) ni mjumbe na Mtume Wake.

    Amesema Allah (SWT):Enyi mlioamini !

    Mcheni Allaah kama i p a s a v y o k u m c h a ; wala msife isipokuwa m m e k w i s h a k u w a Wais lamu kami l i . (Suratul Al-Imraan: 102).

    Enyi watu! Mcheni Mola wenu Ambaye amekuumbeni katika nafsi (asli) moja. Na Akamuumba mkewe katika nafsi ile ile.

    Na Akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka katika wawili hao. Na mcheni Allaah ambaye kwaye mnaombana. Na (mwatazame) jamaa.

    Hakika ni Mlinzi juu yenu (anayaona kila mnayoyafanya). (Suratul An-Nisaa: 1)

    E n y i m l i o a m i n i ! M u o g o p e n i A l l a a h na semeni maneno ya haki. Atakutengenezeeni vizuri vitendo vyenu na Atakusameheni madhambi yenu; na anayemtii Allaah na Mtume Wake, bila shaka amefanikiwa mafanikio makubwa. (suratul Al-Ahzaab: 70-71).

    Amesema Allah (s.w): Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa. (Suurat Al 'Imran 3: 104).

    Na amesema Allah (s.w):Na saidianeni katika

    wema na uchamungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyez i Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. (Suurat Al- Maida 5: 2).

    Muislamu kama yeye binafsi hawezi kuibadili jamii bila kusubiana na watu wengine wenye lengo kama lake.

    Kazi ya harakati ya

    Darsa Duara-1Daawah (Ulinganizi) ili kuweza kuubadili Umma ni kazi tukufu ya kuweza kuuongoza Umma kwa kuokoa kutoka kwenye minyororo ya utumwa wa mfumo wa maisha ya Kitwaaghuut ambao ni giza la dhuluma, ufisadi, utapeli, hadaa, Shirki, nk.

    Na kupelekea kuweza kuishi maisha ya uadilifu, haki, insafu, utulivu na amani ya kweli ya hapa ulimwenguni na kesho Akhera.

    Hali hiyo itaufanya Umma wa Kiislamu kuweza kufikia lengo, Dhima na Jukumu lakuletwa kwao hapa ulimwenguni na Allah (s.w.).

    Dalili: Amesema Allah (s.w.): Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa wale walioamini . Huwatoa gizani na kuwaingiza katika mwangaza. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashet'ani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, na humo watadumu. (Surat Al- Baqara 2: 257).

    Amesema Allah (s.w.):Na pale Mola wako

    Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka kat ika a rdhi Kha l i fa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema:

    Hakika Mimi nayajua msiyo yajua. (Surat Al- Baqara 2: 30).

    Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki, ili aitukuze juu yadini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi. (Suratul Al Fat-h'I 48: 28).

    A m e s e m a A l l a h ( s . w . ) : S i k u w a u m b a majini na watu ila waniabudu Mimi. (Surat Adh-dhaariyaat 51: 56).

    Na amesema Al lah (s.w.):Na kwa hakika k wa k i l a u m m a t u l i u t u m i a M t u m e kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi

    kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu.

    Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha. (Suurat An Nahl 16: 36).

    Kwa hivyo, kazi ya Harakati za kutaka kuubalidi Umma ili uweza kuishi Kiislamu ni kazi Tukufu. Ni kwamba ina kanuni, miiko, sheria, tararibu na muongozo w a k e . E n d a p o k i t u kimoja kati ya hivyo kitakosewa, kuvunjwa, na au kukeukwa itakuwa Harakati pasipo na tija.

    Moja ya kanuni hizo ni kufanya kazi kamaummah. S i kazi ya kila mtu kivyake. Na katika silka aliyoumbwa nayo mwanadamu ni kwamba hawezi kufanya Harakati zake zozote iwe ni za kimaisha au za kijamii bila kufungamana na watu wengine; kwani watu hao wanakuwa ni msaada kwake wa kuweza kufikia malengo yake kwa Tawfiq ya Allah (s.w.).

    Dalili: Amesema Allah (s.w.): Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea.

    Na atakaye fanya urafiki na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, basi hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kushinda. (Suurat Al-Maida 5: 55-6).

    Swali la msingi sasa hapa linakuwa hao walioamini na ambao wapo tayari kufanya kazi ya Allah kwa ikhlas, wanapatikanaje?

    U k i w a w e w e m t u b i n a f s i w a k u f a n y a kazi ya kupigania Dini, unawapataje wenzako ambao nao watakuwa na ikhlas, wa kufanya nao kazi?

    (Abu Saumu, Kombo Hassani Kidumbu- E-Mail: [email protected], 0714 720 965 Mahali: Mikanjuni,Tanga.)

    ANNUUR NEW.indd 2 1/7/2016 3:17:01 PM

  • 3 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016Habari

    Inaendelea Uk. 8

    Maimamu wataka Dk. Shein aheshimu kura za wananchiHAKUNA Shura baada ya Shura, bali kutekeleza yaliyoamuliwa katika Shura.

    Huo ndio msimamo wa Jumuiya ya Maimamu ( JUMAZA) na Taasisi nyingine za Kiislamu Zanzibar.

    K wa m t i z a m o h u o wa Kifiqihi ya Kiislamu katika uongozi, JUMAZA wanasema kuwa hakuna u c h a g u z i b a a d a y a uchaguzi kwa sababu wananchi walishafanya maamuzi.

    W a k a s e m a k u w a k i n a c h o t a k i w a n i kukamilisha utekelezaji wa maamuzi ya wananchi, na sio kuwapuuza na kuyatupilia kwa mbali na kuja na uchaguzi mpya.

    Kwa upande mwingine, i m e e l e z w a k u w a madhumini ya Mapinduzi haikuwa kuiweka CCM madarakani milele bali kurejesha madaraka kwa wananchi.

    Wa n a o r e j e a k a t i k a madhumuni ya mapinduzi

    Na Mwandishi Wetu

    na kutaka yaheshimiwe wanasema kuwa, ni jambo la kusikitisha na ambalo halikuwa linategemewa kuwa CCM watatumia nguvu kutaka kubaki madarakani kwa mtindo wa kuvuruga katiba na kuendeleza ubaguzi.

    JUMAZA katika tamko

    lao la tarehe 6 Januari mwaka huu wamesema kuwa hawaoni kuwa ni busara kurejewa kwa Uchaguzi uliofanyika kwa ufanisi na kukamilika.

    Aidha walirejea historia ya nyuma na kuonyesha jinsi ghilba za marudio ya uchaguzi zilivyoleta

    machafuko na hata kufa watu.

    Walitoa pia mifano ya nchi kadhaa za Kiafrika a m b a p o d e m o k r a s i a ya kuheshimu kura wa wananchi ilivurugwa.

    Wakitoa maoni yao juu ya zilizodaiwa kuwa dosari ambazo ndio zinatajwa

    kuwa ndio sababu ya Jecha kufuta uchaguzi, walisema kwamba kama kweli hoja ni dosari hizo, basi utumike utaratibu wa kisheria ambao ni kurudiwa uchaguzi kwa majimbo tu yenye dosari.

    J U M A Z A inashangazwa sana na hatua ya kufuta Uchaguzi huu iliyochukuliwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jecha Salim Jecha. JUMAZA inauliza kwanini wakati tulipokuwa na kasoro kubwa zaidi katika chaguzi za mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010 Uchaguzi haukufutwa na kutakiwa kurejewa tena iwe Uchaguzi wa mwaka 2015 tu? Na jee, kama uchaguzi utakaorejewa nao ukawa na kasoro zitakazolalamikiwa, utafutwa tena? Tutafanya chaguzi ngapi kwa mtindo huu?

    Hoja hii ya JUMAZA ndiyo pia inayotolewa na Mwanasheria Fatma Karume akisema kuwa k a m a k u n a m a h a l i

    Uchaguzi wa nini wakati serikali haitolewi kwa karatasi za kura?

    Moja kwa Sita bado kitendawili tataHuenda kikawafumbua macho wengiJussa hajasema kweli. Anapiga siasa

    U C H A G U Z I w a n i n i wakati kilichosababisha Jecha kutangaza kufuta uchaguzi, ni msimamo wa wahafidhina wa CCM kwamba maadhali SMZ ilipatikana kwa mapinduzi, haiwezi kutolewa kwa vikaratasi vya kura.

    Hayo ni maoni ya baadhi ya Wazanzibari kufuatia kauli ya Makamo wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar, Balozi Seif Idi, na CCM Zanzibar wakiwatangazia wana-CCM na wananchi wa Zanzibar kuwa wajiandae kwa marudio ya uchaguzi.

    Hivi karibuni uongozi wa CCM Zanzibar umetoa kauli ukishadidia kuwa lazima kuwepo uchaguzi wa marudio na kwamba chama hicho kipo tayari na hivyo kuwataka wanachama wake kujiandaa ili kupata ushindi wa kishindo.

    H a t a h i v y o , h o j a z a Wazanzibari walio katika vyama vya upinzani ni kuwa unaodaiwa kuwa mkwamo wa kisiasa haupo, na kama upo unatokana na CCM kugoma kukubali matokeo ya uchaguzi ambapo dhahiri kilishindwa.

    Na hiyo ni kutokana na msimamo wao wa kihafidhina kwamba hawawezi kutoa nchi kwa vikaratasi.

    Kama huo ndio msimamo, yanini kupoteza pesa kurejea

    Na Mwandishi Maalum

    uchaguzi ambapo matokeo yanajulikana kwamba lazima CCM itangazwe mshindi na isipotangazwa, uchaguzi unaharibiwa? Alisema na kuuliza bwana mmoja wa maskani iliyo jirani na ofisi za CUF Mtendeni.

    Kama ul ivyofanyika ubabe kufuta uchaguzi chini ya mtutu wa bunduki kwa staili ya umafia, wafanye hivyo hivyo kumtangaza mtu wao wa CCM wanayemtaka, wasiharibu kodi za wananchi na muda wao kuendesha

    kiini macho cha uchaguzi. Aliongeza.

    Wakati hayo yakijiri, Rais Mstaafu, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, aliye katika jopo la wazee na Marais wastaafu wa n a o d a i wa k u wa n a mazungumzo na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad katika j i t ihada za kuikwamua Zanzibar katika unaodaiwa kuwa mkwamo wa kisiasa, amejikuta akikabiliwa na tuhuma akidaiwa kuwa haitakii mema Zanzibar, bali kuangalia masilahi binafsi na ya CCM.

    Hiyo ni kutokana na kauli zake za hivi karibuni ambazo zinadaiwa kuwa zinayaweka masilahi ya Zanzibar na Wazanzibari mbali kabisa.

    Hiyo ni pamoja na ile kauli yake akihutubia hadhara ya sherehe za Maulid ya Mtume Muhammad (SAW) akisema

    Zanzibar ni raha tupu, huku wakiwataka Wazanzibari wasitafute mambo mengine, badala yake waitazame Syria inavyovurugwa kwa vurugu.

    Kauli hiyo imetafsiriwa na wengi kwamba ni kushadidia watu kubaki na CCM na Serikali yake na kwamba kujali kura za wananchi walizopiga katika uchaguzi uliopita, ndio kutafuta ya Syria.

    Wengi wanashangaa, kwa Mzee Mwinyi kuona kuwa suala la kupuuza kura za wananchi na kufuta uchaguzi uliogharimu mabilioni ya kodi za wananchi ni matatizo madogo madogo ambayo hayazuii Zanzibar kuwa raha tupu!

    Kama uzee ni dawa, basi uzee wa mwenzetu huyu, umekuwa sumu inayouwa Wazanzibari na Zanzibar kama nchi, alisema mzee mmoja.

    Wakati huo huo, ki le k i t e n d a w i l i c h a M o j a kwa Sita, bado kimekuwa kikiwatatiza wengi.

    Hoja inayotolewa ni kuwa inakuwaje jambo la chama likawa la mtu mmoja.

    Pekee anakwenda katika mazungumzo utadhani anawakilisha kampuni binafsi.

    Kadiri ninavyowatizama h a wa C U F , wa n a n i t i a wasiwasi. Suala la matokeo ya uchaguzi sio la mtu, sio

    Inaendelea Uk. 8

    DKT. Ali Mohamed Shein (kulia), Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) akisalimiana na Balozi Seif Idd. Katikati yao ni Mhe. Pandu Amiri Kificho.

    Alhaji Ali Hassan Mwinyi Mhe. Ismail Jusa Ludu

    ANNUUR NEW.indd 3 1/7/2016 3:17:09 PM

  • 4 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016Tahariri/HabariAN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

    M I S A M A H A y a kodi isiyoleta tija i n a y o t o l e w a n a serikali kwa taasisi, m a k a m p u n i n a wa f a n ya b i a s h a r a w a k u b w a k w a ujumla, ni jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa m u d a m r e f u n a wananchi, wabunge na wanahatakati wa kijamii hapa nchini.

    K i l a m w a k a wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Ta n z a n i a h u p i t i a n a k u c h a n g a n u a kwa makini bajeti ya Serikali. Lakini misamaha ya kodi kwa upande mwingine, haipati nafasi sawia ya kupitiwa vizuri Bungeni, hivyo kuwa vigumu kufahamika bayana ni kiwango gani cha misamaha k inachoto lewa na imesababisha hasara kiasi gani kwa serikali, au imewasaida vipi wananchi.

    Hata hivyo mwaka 2009/10 peke yake, i l i b a i n i k a k u w a asilimia 2.3 ya pato la taifa au TZS 695 bi l ion i z i l i to lewa kama misamaha ya kodi . Ukubwa wa kiwango cha fedha kinachohusishwa na misamaha kiliibua m a s w a l i k u h u s u makusudi ya motisha hizi na iwapo kiwango kinachotumika kinafaa kutolewa.

    Kwa kuwa misamaha ya kodi ilionekana k u w a m i k u b w a m n o k w a n c h i ambayo inakabiliwa na changamoto ya kukusanya fedha za

    Misamaha ya kodi taasisi za Dini:Lengo lake nini na nani anafaidika?

    kutosha kugharamia bajeti yake, mwaka 2 0 0 9 S e r i k a l i ya awamu ya nne ya Rais mstaafu Jakaya Mrisho K i k we t e , i l i e l e z a B u n g e n i k wa m b a imefuta misamaha ya kodi kwa mashirika na taasisi za dini hapa nchini kama moja ya hatua ya kuongeza mapato.

    Ser ika l i i l i e leza kwamba hatua yake hiyo, i l i tokana na kubaini kukithiri kwa matumizi mabaya ya misamaha ya kodi inayotolewa katika taasisi hizo za kidini.

    Tulishuhudia hoja hiyo ikiibua mvutano m k u b w a k a t i y a serikali na viongozi wa dini ambao ndio w a n a o s i m a m i a m a s h i r i k a n a taasisi hizo za dini zinazosamehewa kodi.

    Viongozi mbalimbali wa d i n i h a s a wa Kikristo, walijitokeza kupinga kwa nguvu hatua hiyo ya serikali ambapo tulishuhudia wakilazimika kuweka kambi Dodoma, ili kushinikiza kuzuiwa hoja hiyo ya kufutwa misamaha Bungeni. Kweli, shinikizo lao lilifaulu na hatimaye hoja ile ilikwama.

    Serikali ikarejesha misamaha kwa sharti la kuwataka viongozi hao kuwa waadilifu k w a m i s a m a h a w a n a y o p e w a n a serikali.

    Tunafamu kwamba l e n g o l a s e r i k a l i kuweka misamaha ya kodi kwa taasisi n a m a s h i r i k a ya d i n i , l i l i k u wa n i

    k u y a w e z e s h a mashirika na taasisi hizo kuisaidia serikali k u t o a h u d u m a nafuu za kijamii kwa wananchi kama vile kutumika kugharimia afya, maji na elimu nk.

    L a k i n i p a m o j a n a k u w e p o k w a misamaha hiyo, bado huduma za kijamii katika taasisi hizo zimeendelea kuwa za ghali kama ilivyo katika taasisi za binafsi. Hakuna nafuu yeyote inayopatakina hadi sasa. Ada katika shule zao ni sawa au zaidi ya shule za binafsi na serikali. Gharama za huduma za matibabu katika hospitali zao hazina tofauti na zile za binafsi . Ndipo linapokuja swali, nini sababu ya misamaha hii na ni nani anafaidika na misamaha hii?

    Tunaamini kabisa kwamba, fursa hii ya ser ika l i kutoa misamaha ya kodi kwa taasisi na mashirika ya dini, ilikuwa ni kwa lengo la kuisaidia ser ikal i kuf ikisha huduma nafuu kwa Mtanzania. Kwamba m a s h i r i k a h a y o yaweze kupata uwezo wa kutoa huduma kwa wananchi kwa gharama nafuu. Lakini hali imekuwa sivyo.

    Kimsingi, kwa jinsi hali ilivyo sasa ya huduma za kijamii zinazotolewa katika taasisi hizi za dini, hakuna tena sababu ya kuwepo misamaha ya kodi, maana lengo limekiukwa.

    Wanaofaidika na misamaha hii bila shaka ni hao hao v iongozi wa din i n a m a r a f i k i z a o , lakini sio waumini w a l a w a n a n c h i wanaozunguka taasisi husika.

    K w a m a a n a nyingine, tuna imani k w a m b a s e r i k a l i i n a t a m b u a k u wa f u r s a wa l i y o i t o a ,

    i n a w a n u f a i s h a w a c h a c h e , t e n a wenye uwezo badala ya kunufaisha wengi ambao ni makabwela.

    N d i o m a a n a wa l i p o c h u n g u z a , w a k a n g u n d u a udha ifu, wakafuta msamaha huo kwa kuwa kihalisia ulikuwa hauna maana kwa mwananchi na kwa hivyo hauna madhara ukiondolewa.

    Tukiacha suala la misamaha ya kodi, bado kuna nafuuu nyingine wanayopata mashirika na taasisi za kidini hasa katika sekta ya Afya. Kwa muda mrefu serikali i m e k u w a i k i t o a ruzuku katika vituo vya afya na hospitali za taasisi za kidini, i l i kuweza ku toa huduma ya afya kwa wananchi.

    Pamoja na kutolewa ruzuku hizo, bado tunaona hospita l i hizo zikiendeshwa k i b i a s h a r a z a i d i huku huduma zake z ik iendelea kuwa za gharama kubwa iki l inganishwa na hospitali za serikali, a m b a z o n a z o h u e n d e s h wa k wa fedha za serikali.

    Tunaona kuna haja ya serikali kufikiri upya kuhusu misamaha ya kodi kwa taasisi zetu za dini.

    Tunaona siku hizi v iongozi wa din i wakiiba sadaka za waumini. Wakitajirika, wakijenga mahekalu y a o b i n a f s i k w a sadaka, wakinunua magari ya thamani kwa matumizi yao binafsi kwa sadaka n a k wa k u t u m i a fursa za misamaha y a k o d i w a l i y o nayo. Wanajenga na kuendesha shule zao binafsi kwa mgongo wa taasisi za kidini, wakipata misamaha ya kodi lakini huduma zikiwa juu zaidi kwa Mtanzania.

    W e n g i

    wameshindwa kuwa waadilifu kiasi cha kuaminiwa kutumia fursa ya misamaha wa kodi kutoka serikalini ili kuihudumia jamii. Tunaona hata serikali inapogusa eneo hilo la kuondoa misamaha, v i o n g o z i h a w a hungaka na kuwa wakali kama mbogo, l a k i n i w a n a k i r i kwamba kuna udhaifu japo waona dawa sio serikali kufuta misamaha hiyo.

    Wengi wanaficha u h a l i s i a w a o , wakihadaa kwamba i n a c h o t a k i w a kufanya serikali ni kuwatafuta wakosaji n a k u wa c h u k u l i a hatua, lakini si kufuta misamaha ya kodi!.

    Leo tukiambiwa taas is i za dini n i miongoni mwa zile kampuni zinazotakiwa kuwasilisha nyaraka kwa ajili ya kuhakiki k a m a z i n a l i p a ushuru wa Bandari uliosababisha serikali kupoteza kiasi cha shilingi bil ioni 48 haishangazi.

    Ta ya r i t u m e o n a k a t i k a o r o d h a iliyotolewa na TPA Jumatano ya Desemba 30, 2015 ambapo taasisi na mashirika haya ya dini, tena makubwa na yanayoaminiwa yakiwemo.

    D a l i l i k a m a h i i i n a d h i h i r i s h a wazi kwamba hata hiyo misamaha ya kodi haiwezi kuwa inatumika vizuri hata baada ya kutolewa onyo na serikali 2009.

    Ni ushauri wetu kwa serikali kwamba, kwa hali tuliyofikia ambapo mashirika ya dini yamekuwa yakifanya biashara kama taasisi au kampuni nyingine za kibiashara, iangalie upya kipengele hiki cha misamaha ya kodi.

    Vinginevyo kuwe na utaratibu madhubuti wa kuhakikisha kuwa malengo ya misamaha hiyo yanafikiwa.

    ANNUUR NEW.indd 4 1/7/2016 3:17:09 PM

  • 5 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016Habari za Kimataifa

    KAMATI ya Uchunguzi ya Baraza la Wawakilishi la Marekani imelitaka Shirika la Usalama wa Taifa NSA, kutoa taarifa kuhusu ripoti kwamba shirika hilo lilinasa mawasiliano kati ya maafisa wa Waisrael na wabunge wa Marekani.

    Katika barua iliyotumwa kwa Mkurugenzi wa NSA Michael Rogers, Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi Jason Chaffetz na Mwenyekiti wa Kamati Ndogo Ron DeSantis, walisema habari iliyotokea katika toleo la Jumanne la jarida la Wall Street, iliibua maswali kuhusu utaratibu unaofuatwa na wafanyakazi wa NSA katika kuanisha iwapo mawasiliano yaliyonaswa yanawahusisha wabunge wa Bunge la Marekani Congress.

    Jarida hilo likiwanukuu maafisa wa sasa na wa zamani wa serikali ya Marekani, lilisema NSA ilikuwa ikimlenga Waziri Mkuu wa Israel Benjamin

    WAKATI mzozo nchini Burundi ukiendela kupanuka zaidi, tayari kuna harufu ya kuibuka mzozo mbaya wa ukabila huku Rais Pierre Nkurunziza akiwa ameshatishia kukabiliana na wanajeshi wa kusimamia amani wa Umoja wa Afrika.

    Rais Nkurunziza amesema kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika ambacho kimependekezwa kwenda kulinda amani nchini humo, kitakiuka katiba ya Burundi ambayo inapinga uingiliaji wowote iwapo kuna serikali inayofanya kazi na hakuna vita kati ya pande mbili.

    Rais huyo amesema Burundi itachukulia hatua hiyo ya kupelekewa vikosi vuya Afrika nchini kwake kuwa ya uvamizi na ikiwa wanajeshi wa kigeni wataingia nchini humo, atawakabili.

    Tayari kuna taarifa kwamba Rais Nkurunziza, ambaye anatoka kabila la Hutu anaonekana kuwatenga maafisa kijeshi wa Kitutsi, ambao utiifu wao unatiliwa shaka.

    Baadhi ya Watusti wamedaiwa kuanza pia kuliasi jeshi na tayari Kanali mmoja ametangaza kuunda kundi jipya la waasi wiki iliyopita.

    Kuasi kwa Luteni Kanali Edouard Nshimirima, kumeeneza uvumi kuwa wanajeshi wengine Watusti watamfuata na kusababisha kuzidi kwa mzozo huo na umwagikaji mkubwa wa damu.

    Serikali ya Burundi imeilaumu Rwanda ambayo ina makabila sawa na Burundi na inayoongozwa na Rais Mtutsi Paul Kagame kwa kusajili na kutoa mafunzo kwa waasi wanaompinga Nkurunziza, madai ambayo serikali ya Rwanda imeyakanusha.

    Bado ulimwengu unakumbuka kwamba zaidi ya watu 800,000 kutoka kabila la Watsusi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawawa nchini Rwanda wakati wa mauwaji wa halaiki 1994.

    MWIGIZAJI maarufu wa filamu za Hollywood nchini Marekani Samuel Jackson, amesema hivi sasa waumini wa dini ya Kiislamu nchini humo wanabaguliwa kama wanavyobaguliwa watu Weusi.

    Samuel Jackson aliyasema hayo hivi karibuni kwamba waumini wa dini ya Kiislamu nchini Marekani kwa sasa wamekuwa kama watu Weusi kwa kubaguliwa na wanaonekana hivi sasa kuwa ni Weusi wapya wa Kimarekani, ambapo hufanyiwa dhulma na kudharauliwa na daima hawapewi haki zao za msingi.

    Aidha mwigizaji huyo aliashiria matukio ya kigaidi ya hivi karibuni yaliyotokea Paris

    Waislamu wanabaguliwa kama watu weusi Marekani

    na California, kuwa matukio hayo yalikuwa ndio ufunguo wa kushadidia hali hiyo ya ubaguzi na kuwanyanyapaa Waislamu.

    Alimalizia maelezo yake kwa kusema kuwa baada ya matukio hayo nchini Marekani na Ufaransa, siku hadi siku kumekuwa kukitokea suala la kuvamiwa Misikiti na kuichoma moto, kuwanyanyapaa Waislamu katika mataifa hayo na mataifa mengine katika bara la Amerika na Ulaya. ABNA. SAMUEL Jackson

    Bunge Marekani laishtukia NSA kwa kudukuwa mawasiliano yake

    MKURUGENZI wa NSA Michael Rogers.

    Netanyahu na maafisa wengine wa Israel, baada ya kuanzisha kampeni yao katika Bunge la Marekani kujaribu kukwamisha makubaliano ya nyuklia ya Iran.

    Sambamba na kunasa mawasiliano ya maafisa wa serikali ya Israel, uchunguzi huo ulinasa pia taarifa za ndani kuhusu juhudi zao za uraghibishi, ikiwa ni pamoja na baadhi ya mazungumzo yao na wabunge wa Congress na makundi ya Wayahudi wa Marekani, liliripoti

    jarida hilo.Barua kutoka kwa

    Chaffetz na DeSantis, wote kutoka chama cha Republicans, ilimtaka Rogers kuwapatia taarifa juu ya utaratibu wa shirika hilo kuamua iwapo mawasiliano ya wabunge yamenaswa katika udukuzi wa NSA, na kwa kiasi gani wafanyakazi wa shirika hilo wamekuwa wakitoa taarifa hizo kwa mashirika mengine ya Marekani pamoja na Ikulu (White House).

    Kamati hiyo pia iliitaka NSA iipe maelezo mafupi kuhusu wafanyakazi wake. Jarida la Wall Street liliripoti kuwa NSA ilifuata muongozo unaozitaka ripoti zake za uchunguzi kuondoa majina yoyote ya Wamarekani, wakiwemo wabunge waliotajwa katika mawasiliano ya Waisrael yalionaswa.

    Ripoti ya Jarida hilo ilisema hata baada ya Rais Barack Obama kutangaza miaka miwili iliyopita kuwa angeweka ukomo kwenye kuyachunguza

    mataifa washirika, NSA iliendelea kumchunguza Waziri Mkuu wa Israel Banjamini Netanyahu, pamoja na maafisa wa ngazi za juu nchini humo.

    White House ilikataa kuzungumzia shughuli zozote mahususi za kijasusi zilizofanywa na Marekani. Lakini maafisa wa White House walisema Marekani haifanyi uchunguzi nje ya nchi, mpaka pawepo na sababu ya usalama wa taifa inayoisukuma kufanya hivyo na kusisitiza kuwa, kanuni hiyo inatumika kwa viongozi wa dunia na raia wa kawaida.

    Na katika juhudi za kuonyesha kuwa uhusiano wa kiulinzi kati ya Marekani na Israel haujaathiriwa na ripoti hizo, maafisa walibainisha kuwa maafisa wa Marekani walisafiri kwenda Israel mwezi huu kuanzisha tena mazungumzo ya makubaliano mapya ya miaka 10 kuhusu msaada wa kijeshi wa Marekani. DW.

    Nkurunziza kurejesha mchezo wa hatari Burundi

    RAIS Pierre Nkurunziza.

    ANNUUR NEW.indd 5 1/7/2016 3:17:11 PM

  • 6 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016Hoja ya Juma Kilaghai

    KAMA una tabia ya kufuatilia mambo unaweza ukawa umegundua kuwa hivi sasa watu wengi hawana kumbukumbu vizuri. Kinachotisha zaidi ni kwamba kundi kubwa la hawa watu ni vijana chini ya umri wa miaka thelathini. Nasema hali hii inatisha zaidi kwa sababu kimazoea inaaminika kuwa kupungukiwa na kumbukumbu ni zao la uharibifu wa seli za ubongo na mishipa ya fahamu unaosababishwa na umri kusonga mbele.

    Kwa hiyo ni kitu gani kinaendelea? Ni kitu gani kinasababisha vijana ambao kinadharia bado bongo zao na mishipa ya fahamu ni safi nao wakumbwe na tatizo ambalo chimbuko lake ni uchakavu? Kuna tafiti zimebainisha kuwa moja ya sababu kubwa sana za hali hii ni maisha ya kisasa ambayo yamesababisha kundi kubwa la kemikali hatari kutumika katika maisha ya kila siku. Kemikali hizi zinatajwa kama ni sumu kwa seli za ubongo pamoja na zile za mishipa ya fahamu. Baadhi ya kemikali hizi ni madini ya alminium; madini ya fluorine; na dawa za kupunguza lehemu (cholesterol) mwilini zinazoitwa statins.

    Maisha ya kisasa yameongeza wingi wa madini ya alminium tunayoingiza kwenye miili yetu kwa kiasi kikubwa sana. Ongezeko hili ni kupitia maji ya kunywa, hususan yale yanayosambazwa na mamlaka za maji na yale ya chupa; dawa mbalimbali, hususan kundi kubwa ya zile za kuzimua tindikali tumboni (antiacids); vipodozi vya kuzuia jasho kwenye makwapa na kuzuia harufu ya kikwapa (antiperspirants and deodorants); na mabaki yanayoingia kwenye chakula kilichopikwa na kuhifadhiwa na vyombo vilivyotengenezwa kwa madini alminium.

    Tafiti zingine zimebainisha kuwa

    Ulimwengu wa kemikali na madhara yakeNi kitu gani kinaendelea? Kumbukumbu inazidi kuwa bidhaa adimu!

    moja ya sababu nyingine kubwa za watu kupoteza kumbukumbu ni madini ya fluoride. Mara nyingi madini ya fluoride huingia kwenye miili yetu kupitia matumizi ya chai; dawa za mswaki; maji ya kunywa; na baadhi ya madawa ya kifamasia,

    (rosuvastatin); Zocor (simvastatin) and Vytorin (simvastatin/ezetimibe). Kufuatia tafiti kadhaa zilizohusisha makundi makubwa ya watumiaji, hatimaye mnamo mwezi wa 2, mwaka 2012 taasisi ya chakula na dawa ya Marekani, FDA, ilitoa orodha yenye maonyo

    ghrelin kuwepo. Hii ina maana kuwa unapokuwa muda wote katika hali ya kushiba seli zako za ubongo zinazochakaa hazifanyiwi ukarabati. Upotevu wa seli nyingi za ubongo kutokana na kutofanyika ukarabati inaweza pia kuwa chanzo kimojawapo cha upotevu

    hususan viua vijasumu vikali vya kundi la fluoroquinolones. Kutokana na ubaya wa fluoride, baadhi ya serikali za nchi za Ulaya kama Sweden, Norway, Denmark, Ujerumani, Italia, Ubelgiji, Austria, Ufaransa, and Uholanzi zimepiga marufuku bidhaa zenye madini hayo katika nchi zao.

    Kumekuwa na mvutano wa muda mrefu kuhusu dawa za kupunguza lehemu (cholesterol) mwilini zinazoitwa statins. Baadhi ya watafiti wamekuwa wakizihusisha dawa hizi na madhara mengi ya kiafya ikiwa ni pamoja na watumiaji kupoteza kumbukumbu. Baadhi ya dawa hizi ni Lipitor (atorvastatin); Crestor

    mapya kwa watumiaji wa dawa hizi kwamba zilikuwa zinaongeza uwezekano wa mtumiaji kupata kisukari cha ukubwani na kuugua ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu.

    Shibe iliyopindukia nayo inaweza kuwa tatizo jingine. Shibe iliyopindukia ni ile inayohusisha kifungua kinywa cha kutosha, chakula cha mchana cha kutosha na chakula cha usiku cha kutosha siku saba kwa juma. Tafiti zimebaini kuwa kuna homoni inazalishwa na mwili pale mtu anapokuwa na njaa inayoitwa ghrelin. Tafiti hizi zimebaini pia kuwa ukarabati wa seli za ubongo haufanyiki bila ya hii homoni ya

    wa kumbukumbu.Kutopata muda wa

    kutosha wa kupumzika, hususan wakati wa usiku, ni chanzo kingine kikubwa cha kumbukumbu dhaifu. Kwa baadhi ya viumbe, mwanadamu akiwemo, usiku (kwa maana ya kuingia giza) ni muda mahsusi kwa ajili ya kupumzika. Viumbe hawa ni wale ambao hawaoni gizani. Ni dhahiri kuwa tofauti na mababu zetu, hivi sasa tumepunguza sana muda wa kupumzika usiku kutokana na msaada wa mataa, hususan yale yanayotumia umeme.

    Kwa viumbe ambao hawakuumbwa kuhangaika usiku, lakini wanafanya hivyo kwa msaada wa

    mwanga wa taa, bila ya shaka wanadhuru afya zao kwa kiwango kikubwa. Sababu kubwa ni kwamba kuna homoni zinafanya kazi gizani tu, na pale giza linapokosekana, homoni hizi hazizalishwi na kwa maana hiyo faida zinazooanishwa na hizo homoni hazipatikani. Moja ya homoni hizi ni ile inayojulikana kama Human Growth Hormon (HGH). Homoni hii huhusika na uwezeshaji wa seli za mwili - ikiwa ni pamoja na ubongo - kukua, pamoja na ukarabati wake. Bila homoni hii mwili hauwezi kuwa na misuli iliyojengeka na mifupa iliyojaza vizuri. Aidha homoni hii hutusaidia kupunguza kiwango cha mafuta kinachohifadhiwa mwilini, huimarisha uwezo na hamu yetu ya kufanya tendo la ndoa, na huufanya mwili kuwa na nguvu kwa ujumla. Hata hivyo tafiti zimebaini kuwa njia nyingine zinazoweza kutusaidia kuvuna homoni hii ni kwa kufunga (kuacha kula) na kufanya mazoezi.

    Msongo ni tatizo lingine kubwa sana linaloweza kuchangia ongezeko la tatizo la kumbukumbu hafifu. Msongo pamoja na athari zingine hupelekea mtu akakosa usingizi. Kama tulivyoona bila usingizi mwili wako hauwezi kuzalisha HGH, na bila hii homoni uwezekano wa seli zako za ubongo kuzalishwa kwa kiwango kinachotakiwa na kukua inavyotakiwa unakuwa mdogo.

    Ubongo wako ni raslimali muhimu sana ambayo inatakiwa ilindwe kwa kila hali. Chukua hatua muafaka kuhakikisha unalifikia lengo hilo. Moja ya hatua hizi ni kuondosha au kupunguza matumizi ya vitu vyote vinavyotuhumiwa kuharibu ubongo pamoja na mishipa ya fahamu.

    ANNUUR NEW.indd 6 1/7/2016 3:17:13 PM

  • 7 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016MakalaSHUKRAN zote njema ni zake Allah Taala, Mola Mlezi wa ulimwengu wote. Rehema na amani zimwendee mtume Muhammad (Swallalahu Alayh Wassalam), sahaba zake, aali zake na wote waliofuata sunnah yake mpaka siku ya Qiyaamah.

    Ni takriban miaka thelathini na sita sasa tangu kutokea kwa vita ya Tanzania na Uganda, almaarufu vita vya Kagera. Ni vita ambavyo vilipiganwa kati ya mwaka 1978-1979. Kutokana na utata uliopatikana kufuatia vita hivyo na ambao mpaka leo wengi wetu hawajui vema ni nani aliyeanzisha vita ile, nimeamua nieleze kwa uchache kuhusu vita hivyo. Tusafiri pamoja na makala ya Inocent Kasyate, ya Julai 26, 2009, ambayo nimeifanyia marekebisho kidogo ya lugha, kwa kuongeza na kupunguza bila kuharibu maudhui yenyewe.Nani Aliyeanzisha Vita Hivyo?Je, ni Iddi Amini au Tanzania?

    Kila mwaka nchi yetu imekuwa ikisherehekea kumbukumbu ya mashujaa wa vita ya Kagera. Ni tukio linalokumbushia juu ya ushiriki wa nchi ya Tanzania katika vita pekee kubwa iliyoigharimu nchi yetu kwa kiwango kikubwa kabisa. Hebu kwanza tuangalie mtizamo wa nje ya Tanzania juu ya chanzo cha vita ile:

    Miaka thelathini na sita iliyopita, serikali ya kijeshi ya Uganda ikiongozwa na Iddi Amin ilipinduliwa na muungano wa majeshi ya wakombozi ambao walikuwa ni waasi waliokuwa wakiishi nchini Kenya na Tanzania katika miaka ya sabini

    Vita vya Kagera

    RAIS wa zamani wa Uganda Iddi Amin.wakisaidiwa na jeshi la Uganda. Kupinduliwa kwa serikali ya Iddi Amini kulileta hatima ya uongozi wa mtu ambaye ni miongoni mwa madikteta waliowahi kutokea katika historia ya Afrika. Makala hii inataka kuchokonoa kutoka kwa wanaokumbuka kama kweli vita hii ilisababishwa na Iddi Amini ama kuna sababu zingine za msingi zilizojificha nyuma ya pazia?

    Swali la kujiuliza juu ya vita ya Kagera ya mwaka 1978 79 ama Tanzania na Uganda ni je vita hii ilisababishwa na nini? Hisia na imani za watu wengi kuanzia kwenye vitabu, majarida na magazeti, na hata wavuti mbalimbali duniani ni kuwa Iddi Amini ndiye alikuwa mtu mbaya ambaye aliamua kutuma majeshi yake kuivamia Tanzania bila sababu yeyote, na ndipo Tanzania ikajibiza mashambulizi. Kuna imani nyingine kuwa hapo tarehe 19/04/1978 ilitokea ajali ya gari ambayo

    ilimuua Makamu wa Rais wa Amini, ndugu Mustapha Adrisi; kutokana na ajali hiyo watu waliamini kuwa ajali hiyo ilipangwa na ilileta hali ya wasiwasi mkubwa katika jeshi la Uganda. Hali hii ilimfanya Amini aamue kuivamia Tanzania ili kuhamisha mawazo ya maafisa wa jeshi na hata akili za wananchi wa Uganda. Hili linathibitishwa na taarifa iliyowahi kutolewa na Rais Milton Obote ambaye alipinduliwa na Iddi Amin ambaye alisema kuwa: Kuna ushahidi wa kutosha kuwa uvamizi wa Amini dhidi ya Tanzania ulikuwa ni hatua za makusudi za Amini kujinasua kutokana na kushindwa kwa Amini kulidhibiti jeshi lake.

    Tatizo moja kubwa ambalo limejitokeza kila tunapojaribu kuelezea kuhusu historia ya Uganda wakati wa utawala wa Iddi Amini, ni ile kukosekana kwa mtizamo wenye usawa na kuachana na mitizamo iliyojaa uzandiki (stereotyping)

    juu ya Iddi Amini. Ni wazi kizazi cha leo kinamjua Iddi Amini kama mtawala dhalimu kabisa na hili limeachiwa likaenea dunia nzima bila utafiti wa kina. Na ili tuweze kujua nini hasa ni ukweli wa hali halisi wa vita ya Kagera, ni lazima tuitizame hali ya Uganda kati ya mwaka 1977 na 1978 kabla ya vita kutokea.

    Kwa mujibu wa Compton Encyclopedia Yearbook, 1979, inasema kuwa mwaka 1977 Uganda ilipata mafanikio makubwa kiuchumi hasa kutokana na bei kubwa ya zao la kahawa kwenye soko la Dunia. Ukiacha mafanikio hayo, kitabu hicho kinaendelea kusema kuwa mafanikio hayo kiuchumi yaliambatana na kuundwa kwa vikundi vya waasi nje na ndani ya nchi vyote vikitaka kumpindua Iddi Amini ambaye naye aliponea chupuchupu kuuawa mara nne. Kuponea huku kuuawa kulisababishwa na uimara ulioambatana na unyama wa

    wanausalama wa Iddi Amini na pia heshima kwa amiri jeshi mkuu. Kutokana na uongozi wa Amini kuwa wa kibabe hasa ikizingatiwa alikuwa tayari ana maadui wengi, vyombo vya habari vya magharibi vilikuwa havina uhusiano mzuri na Iddi Amini hasa ikizingatiwa ugonjwa wa kutu ya kahawa (frost) kule Brazili uliwezesha mauzo ya kahawa ya Uganda kuleta mafanikio katika uchumi hivyo hakujali sana nchi za magharibi.

    Tarehe 28/07/2006, kupitia kituo cha redio cha STAR FM, mtangazaji Semwanga Kisolo alikumbusha wasikilizaji kuwa kipindi cha Iddi Amini alihakikisha mishahara ya wafanyakazi wa umma ilikuwa inalipwa si zaidi ya tarehe ishirini na tano na kama ingelichelewa Iddi Amini mwenyewe alikuwa akitoa karipio kali kwa wanaohusika. Anaeleza kuwa Amini alikuwa mtu anayejali muda kuwahi kazini na katika matukio muhimu ya kitaifa na alisisitiza wafanyakazi pia wajaliwe ili waweze kuwahi na kutimiza majukumu yao. Anasema kuwa wakati wa serikali ya Iddi Amini, majeshi yote, polisi, magereza, jeshi la anga, na usalama wa Taifa na hata maafisa wa kati katika utumishi wa umma, waliishi maisha ya kujitosheleza (comfortable): kama kumudu kusomesha watoto katika shule nzuri, kuendesha magari mapya katika idara mbalimbali za serikali. Magari hayo yalikuwa kama Fiat Mirafiori, Honda Civic, na Honda Accord. Kwa ufupi kipindi cha utawala wa Iddi Amini sarafu ya Uganda

    Inaendelea Uk. 16

    ANNUUR NEW.indd 7 1/7/2016 3:17:13 PM

  • 8 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016Habari

    Maimamu wataka Dk. Shein aheshimu kura za wananchiInatoka Uk. 3palikuwa na dosari, basi hapo ndipo pafanyike marudio na hayo ndiyo matakwa ya sheria ya uchaguzi.

    N i n i k i m e t o k e a mwaka huu? Kama dosari zilijitokeza Pemba kama wanavyodai kwa nini urudiwe Unguja? Kwa nini hawataki kutumia uamuzi wa mwaka 2000 wa kurudia maeneo yenye dosari tu?

    Alisema Fatma Karume akiho j iwa na baadhi ya vyombo vya habari ambapo alinukuu kauli ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akisisitiza kuwa matakwa ya sheria ni kurudia uchaguzi maeneo yenye dosari, sio kufuta uchaguzi.

    Katika mahojiano hayo Fatma Karume alisema kuwa anajihisi kusalitiwa kwani CCM wamegeuza m a p i n d u z i k u wa n i wao kupora madaraka

    ya wananchi na kuleta ukoloni wa watu Weusi dhidi ya watu Weusi jambo linalowapora Wazanzibari haki yao ya msingi ya kumchagua kiongozi wanayemtaka.

    W a k a t i h u o h u o , M a i m a m u Zanzibar wameelezea k u t o k u r i d h i s h w a kwao na yanayodaiwa k u w a m a z u n g u m z o yanayofanyika Ikulu Z a n z i b a r k u t a f u t a muafaka.

    Wamesema, kwanza m a z u n g u m z o h a y o yametawaliwa na usiri mkubwa na kwamba mpaka sasa hakijulikani kinachozungumzwa.

    Lakini pia wakasema kwamba mazungumzo yamechukua muda mrefu huku hao hao wa upande wa CCM wanaoshiriki m a z u n g u m z o h a y o , wakitoka wanatoa kauli z a c h u k i , u c h o c h e z i na kuwakatisha tamaa

    wananchi.Wananchi wa Zanzibar

    t u l i p a t a m a t u m a i n i tulipoona kuwa viongozi w a k u u w a k i s i a s a wanakutana kuzungumzia hali ya kisiasa nchini, tuliamini kuwa katika vikao hivyo Viongozi hawa wenye kuheshimika

    wakitawaliwa na busara, h e k i m a , u a d i l i f u n a wakiweka mbele maslahi ya taifa badala ya vyama vyao, basi muda si mrefu tungepata ufumbuzi wa mgogoro huu.

    I l i s e m a t a a r i f a ya JUMAZA il iyosomwa na Katibu wake Sheikh M u h i d d i n Z u b e r n a kuongeza kuwa, bahati mbaya ni vikao 8 sasa vimeshafanyika tokea kikao cha mwanzo cha tarehe 9 Novemba, 2015 (lakini) hakuonekani kuwa matumaini yale wananchi waliyoyajenga kwao kuwa yatatimia.

    Lakini zaidi anasema kuwa pamoja na vikao hivo kuchukua muda mrefu sana na kufanyika kwa siri kubwa, baadhi ya wajumbe wanaoshiriki m a z u n g u m z o h a y o wamekuwa wakitoa kauli zinazoshabikia msimamo wa u p a n d e m m o j a hali inayowatoa imani

    wananchi juu ya kuwepo kwa nia njema katika mazungumzo hayo.

    Na kwa maana hiyo JUMAZA wanasema kuwa, wananchi wana wasiwasi i wa p o m a z u n g u m z o hayo yanaweza kuivusha Zanzibar salama katika mkwamo huu wa kisiasa.

    A w a l i J U M A Z A walieleza kuwa hali inazidi kuwa mbaya Zanzibar hasa kiuchumi huku watu wakiwa hawajui nini mustakbali wa maisha yao na nchi kwa ujumla.

    W a m e s e m a , w a o wa l i k u wa n i k a t i k a waangalizi wa uchaguzi, na kama zilivyosema taarifa za waangalizi wengine wa ndani na wale wa nje, hakukuwa na dosari za kiwango cha kuhalalisha kufutwa uchaguzi.

    Na ndio maana tangazo la Jecha la kufuta uchaguzi limezua balaa ambalo haijukani litaishia wapi.

    RAIS Mstaafu, Benjamin William Mkapa.

    Uchaguzi wa nini wakati serikali haitolewi kwa karatasi za kura?

    Inatoka Uk. 3la Katibu Mkuu wa Chama au mgombea pekee, ni la chama. Lakini kila nikitizama kinachoitwa mazungumzo, ni mtu mmoja Vs Sita wa upande wa pil i , ambao tafsiri yake ni kuwa hao CUF wenyewe kamwe hawatajua kinachozungumzwa!

    Alisema Mzee mmoja na kusisitiza kuwa hajawahi k u o n a w a l a k u s i k i a mahali popote duniani a m b a p o m g o g o r o w a kisiasa unatatuliwa kwa kufanywa mazungumzo ya sura ya jambo binafsi na bila kuzingatia uwiano wa ushiriki wa pande mbili husika katika mgogoro.

    H a d i s a s a , z a i d i ya habari za kuambiwa, CUF, hawajui kwa uhakika nini Maalim aliongea na Rais Mstaafu Kikwete wala alichoongea na Rais JPM au anachozungumza na wazee Marais wastaafu.

    CCM ikitangaza kujiandaa na uchaguzi wa marudio, kuna wasiwasi kuwa hilo n d i l o a m b a l o M a a l i m a m e k u b a l i a n a n a R a i s Magufuli walipokutana Ikulu jijini Dar es Salaam.

    Ukiangalia mfuatano wa matukio baina ya kikao cha Rais na Kamati ya CCM, Zanzibar na kutolewa tamko la kurudiwa uchaguzi, lakini pia ukisikiliza msisitizo wa CCM, Zanzibar kwamba eti nao hawamkubali Jecha na Tume yake, kuna wasiwasi kwamba hapa kuna mchezo.

    A l i s e m a m c h a m b u z i

    mmoja akisisitiza kuwa haoni ni kwa namna gani CCM wangekuwa na ujasiri wa kutangaza marudio ya Uchaguzi Mkuu bila ya kupata ushirikiano na viongozi wa CUF.

    Sioni namna ambavyo CCM wanaweza kuibuka na kutangaza habari za marudio ya uchaguzi iwapo katika vikao vyao na CUF wanauona msimamo thabiti usio yumba

    wa aliyekuwa mgombea urais kupitia CUF kupinga jambo hilo. Alisema.

    Katika hali kama hiyo amesema kuwa hata ile kauli ya Jussa kwamba CUF ipo imara na itasimamia kura za wananchi, inaonekana ni kupiga porojo tu na danganya toto.

    Taarifa ya chama hicho iliyotolewa na Ismail Jussa kufuatia kauli ya viongozi wa

    CCM juu ya uchaguzi mkuu imesema kwamba, CUF inawahakikishia Wazanzibari k wa m b a h a i t o t e t e r e k a na itasimamia kwa dhati maamuzi yao waliyoyafanya kwa njia za kidemokrasia kupitia Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na italinda chaguo lao la Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani wao.

    Hata hivyo, imeelezwa

    kuwa kitendawili cha Moja kwa Sita na nguvu mpya ya CCM katika hali ya kujiamini kutangaza uwepo wa uchaguzi, inatoa picha tofauti.

    Ni ishara kuwa Moja imemezwa na Sita, huku CUF na UKAWA wakiwa kizani juu ya kinachojadiliwa baina ya Maalim, Dr. Shein, Balozi Seif na wazee watatu walio makada wa CCM.

    Pengine ni kutokana na utata na wasiwasi uliopo juu ya kinachoendelea baina ya Maalim Seif na makada hao wa CCM, Mzee Hassan Nassor Moyo amesema kuwa kamwe hatamuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ikiwa ataridhia kurudiwa Uchaguzi Mkuu Zanzibar.

    Mzee Moyo amesema hayo akijenga hoja kuwa dunia nzima inajua kuwa Uchaguzi ulifanyika vizuri na kwamba mshindi anajulikana.

    A l i s e m a , k u i t i s h a Uchaguzi Mkuu mwingine, n i dhulma, dhambi na kutowatendea haki wananchi waliopiga kura zao.

    Akiungana na Mzee Moyo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya amesema kuwa msimamo wa CUF ni kwamba hawatakubali uchaguzi urudiwe.

    Alisema Baraza Kuu la Uongozi Taifa, ambalo ndio chombo cha mwisho kutoa uamuzi, limeshatoa uamuzi na msimamo kwamba hakuna kurudiwa uchaguzi, bali kilichopo ni kukamilishwa utangazaji wa matokeo.

    MZEE Hassan Nassor MoyoNaibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya

    ANNUUR NEW.indd 8 1/7/2016 3:17:14 PM

  • 9 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016Makala

    R A I S J o h n P o m b e M a g u f u l i ( J P M ) a m e j i t a h i d i kutengeneza mazingira ya k u a m i n i wa n a ameaminika.

    Kila kona ni slogan za Rais Magufuli. Kila mtu anamuunga mkono Mh. Rais Magufuli.

    Kamual ika Muf t i Zuber wa BAKWATA akamsifia sana.

    Kipi tena mnataka Wais lamu za id i ya heshma aliyopewa Mufti kukaribishwa Ikulu?

    AWA L I y a y o t e naomba nitangulie kusema na mapema k u wa ya we z e k a n a wakatokea watakao t o f a u t i a n a n a m i n a p e n g i n e h a t a kunishambulia. Hii ni kwasababu kila mmoja ana haki ya kuwa na mtazamo wake na hata ujasiri wa kufumbia m a c h o d h u l m a p a l e i n a p o f a n y wa kwasababu dhulma hiyo haimgusi yeye wala familia yake.

    Wakati tunaelekea kupata uhuru mwishoni mwa miaka ya 1960, wengi tunakumbuka k u l i k u w a n a mgawanyiko miongoni mwa wapigania uhuru. M g a w a n y i k o h u u ulipelekea kuwa na vyama viwili, TANU n a A M N U T . J a p o AMNUT haikuwa na nguvu sana kiasi cha kuitikisa TANU, bado ukweli unabaki kuwa yalikuwepo makundi mawili tofauti. Moja katika mtazamo wa A M N U T i l i k u w a k w a m b a , i l i k u w a n i m a p e m a k w a Tanganyika kupewa uhuru, kwakuwa kwa hali ilivyokuwa kwa wa k a t i u l e , TA N U kupewa uhuru ilikuwa kuwapa nafasi Wakristo wanufaike na kufaidika na uhuru peke yao huku Waislamu wapigania uhuru wakiishia kuwa raia wa daraja la tatu. Kwa maoni yao, ilikuwa n i bora kuche lewa kupata uhuru ili kupata muda wa kusawazisha tofauti zilizokuwepo, hasa za kielimu, baina ya wananchi wa dini kuu mbili, Uislamu na Ukristo.

    Mh. Magufuli anaturudisha kule kwa Sheikh Takadiri

    Katika kujibu hoja hiyo, msimamo wa M wa l i m u N y e r e r e u l i k u w a k w a m b a , mkoloni yu le yu le a l i y e wa k a n d a m i z a Waislamu wakabaki nyuma, hawezi kutatua tatizo hilo. Badala yake, ni jukumu la Viongozi katika Tanganyika huru kushughulikia tatizo hilo. Kisiasa, ni wazi hoja ya Mwalimu Nyerere i l ikuwa na maana , na hivyo Waislamu wengi wakamuunga mkono. Kutokana na jinsi Mwalimu Nyerere alivocheza karata zake za kisiasa katika kupigania uhuru na hata baada ya kupatikana uhuru, ilimjengea imani kwa Waislamu na wananchi kwa ujumla.

    Kutokana na Imani hiyo, na hasa Waislamu, ilikuwa ni vigumu kwa m t u k u m n y o o s h e a kidole kuwa hatendi haki. Na akithubutu, a t a s h a m b u l i wa n a k u t e n g wa . N i k wa n a m n a h i i S h e i k h Suleiman Takadir alipata misukosuko na hata kutengwa na Waislamu wenzake. Matokeo yake, malalamiko na madai ya ubaguzi na hujuma dhidi ya Waislamu wakati wa

    serikali ya Awamu ya Kwanza, imebakia kuwa historia chungu kwa Umma wa Kiislamu nchini Tanzania. Kama alivyojisemea Remmy O n g a l a , i m e k u w a ni kilio cha samaki, machozi yamekwenda na maji. Hakuna hata anayesikia na kujali kilio cha Waislamu katika walioshikilia mpini.

    Wakati wa kamapeni, M h . J o h n P o m b e Magufuli mara kadhaa a l i s i s i t i z a k u w a hatowabagua watu kwa rangi zao, kwa makabila yao wala kwa dini zao. Hii ilileta faraja kuwa Mh. Magufuli ataleta usawa na haki katika serikali yake. Hata hivyo, Rais John Pombe Magufuli (JPM) nae ameingia kwa gia ileile. Amejitahidi kutengeneza mazingira y a k u a m i n i w a n a a m e a m i n i k a . K i l a kona ni slogan za Rais Magufuli . Kila mtu anamuunga mkono Mh. Rais Magufuli. Sasa katika mazingira haya na katika kuzingatia historia na uzoefu wa m a m b o wa k a t i wa Mwalimu Nyerere, kuna haja ya kuwa makini. K a t i k a m a z i n g i r a haya yanayoendelea

    k u j i u m b a , i w a p o atatokea wa kulalamika kwamba kuna hujuma dhidi ya kundi fulani, iwe la kidini au kikabila, watu watamshangaa. Na ni hivi majuzi tu kakutana na Mufti Zuber wa BAKWATA naye akamsifia sana. Kipi tena cha kuthibitisha kuwa Rais ni mtenda haki, asiye bagua watu zaidi ya heshma aliyopewa Mufti kukaribishwa Ikulu?

    M a r a b a a d a y a k u a p i s h w a k u w a Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Magufuli alianza kwa hotuba kali sana wakat i ak i l iz indua Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hotuba ile ilileta hamasa ya hali ya juu sana na hata kuamsha ari ya uungwaji mkono kutoka kwa Watanzania wa ngazi ya kati na chini. Kilichofuatia ni kuanza na operation aliyoiita operation ya kutumbua majipu! Operation hii ilifanyika kwa kuanzia bandari na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Msisimko na shangwe za uungwaji mkono zilisikika kila kona ya Tanzania. Haikuchukua

    m u d a , a k a a n z a kuonekana kama mtu aliyekuja kulikomboa ta i fa le tu Naam, m a z i n g i r a ya k a wa wazi kufanya atakalo na hakuna mtu wa kulalama wala kudadisi. Kwanini? Kwasababu ameaminiwa kuwa yeye anafanya kwa maslahi ya taifa. Yeyote atakaye nyoosha kidole kudadisi au kuhoji, anaonekana mtu wa a jabu tena anataka kukwamisha harakati za kizalendo.

    Ubaya wa mazingira kama haya ni kuwa huenda watu wakawa w a z i t o k u m s a i d i a Mheshimiwa Rais pale wanapohisi kwamba mambo hayaendi sawa. Wingu la umaarufu na kuungwa mkono l i t a w a z u i y a w a t u kuwa wakweli kwa R a i s k w a k u h o f i a ya s i j e ya k a wa k u t a yaliyomkuta Sheikh Sule iman Takadir i . Lakini kwa Mheshimiwa Rais naye, kwa kusikia nyimbo na ngonjera za sifa tu na kuungwa m k o n o , a n a w e z a a s i p a t e f u r s a y a kutizama pale penye dosari ndogo ndogo ambapo pangehitaji marekebisho.

    B i n a f s i n a a m i n i kwamba, haitakuwa t u n a m s a i d i a Mheshimiwa Rais JPM iwapo hatutasema pale tunapoona kuwa mambo hayaendi sawa kama ilivyo dhamira njema ya Rais. Mheshimiwa Rais JPM ni binadamu na katika ari na hamasa ya kulitumikia taifa a n a we z a k u j i k wa a h a p a n a p a l e . N a hivyo ni wajibu wetu kumsaidia Rais wetu kipenzi. Na hapa mimi nitazungumzia yale ambayo nadhani hata katika mazungumzo yake na Mufti Zuberi hawakuyagusa.

    Uteuzi wa Baraza la Mawaziri

    Uteuzi wa Baraza la Mawaziri, kwangu mimi, umeacha maswali mengi kuliko majibu. J a p o i n a s h a n g a z a Wais lamu kupigwa

    Inaendelea Uk. 15

    RAIS Dk. John Magufuli (kulia) akiwa na Muft wa BAKWATA Sheikh Abubakar Zuberi.

    ANNUUR NEW.indd 9 1/7/2016 3:17:18 PM

  • 10 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016Makala

    UKIENDA Zanzibar ukifika pale bandarini Dar es Salaam, utakutana na kijana kashika kipaza sauti akiwahimiza abiria kwamba saa zao, simu, mikanda ya suruali , sarafu na vitu vya chuma, waweke ndani ya mabegi yao, tayari kwa ukaguzi. Kwa nini wanafanya hivyo? Hofu ya ugaidi n d i y o i m e t u f i k i s h a hapo. Baada ya hofu, watu hawana tena muda wa kujiuliza, zoezi lile linamzuiya vipi gaidi?

    Kiasi wiki tatu zilizopita zilisambaa habari katika vyombo vya habari vya Kenya na vya kimataifa juu kilichodaiwa ushujaa na uzalendo wa akina m a m a wa K i i s l a m u a m b a o w a l i c h u k u a hatua za kuwanusuru abiria wenzao Wakristo. Kinachoelezwa ni kuwa basi lililokuwa likisafiri kutoka Nairobi kwenda Mandera, lilivamiwa na magaidi wa Al-Shabaab wapatao 15. Wakaingia ndani ya basi wakiwa na bunduki nzito AK-4 7 . Wa k a a n z a z o e z i l a k u w a t e n g a n i s h a Waislamu na Wakristo ili wawauwe Wakristo. Hata hivyo, akina mama Waislamu wakavua hijabu zao na kuwapa Wakristo wavae, kwa hiyo zoezi la kuwatambua Wakristo likakwama Al-Shabaab wakakimbia.

    Ni katika taarifa ya habari, katika televisheni zetu, unamkuta mtangazaji anatangaza habari hizo kwa mkazo akiwaaminisha wasikilizaji na watazamaji kuwa hizo ni habari za kweli kabisa! Ile akili ndogo tu ya mtu kujiuliza, h ivi hao akinamama w a k i v u a h i j a b u n a kuwapa Wakristo wavae, Al-Shabaab walikuwa hawaoni? Kitisho cha ugaidi kimewaondolea hata kile kiwango cha chini kabisa cha kufikiri na kutumia akili.

    Kuna l i l e tukio la Paris ambapo ilidaiwa kuwa magaidi walilipua mabomu katika uwanja wa mpira. Unatizama taarifa ya habari au unasoma gazeti, imewekwa picha ya mashabiki wapo uwanjani, wengine wanaongea na simu wakicheka, wengine wamekaa wanasogoa. Ilimuradi hakuna ishara yoyote ya taharuki. Lakini mwandishi anakuambia kuwa hawa ni mashabiki wanaosubiri kuokolewa

    Kweli, hofu ya ugaidi huwafanya watu kuwa wajinga kupindukia

    Putin kidume. Awaumbua wenye ISWaanza kukimbia. Agenda kukwama

    Na Omar Msangi

    na polisi wa uokozi baada ya magaidi kupiga bomu! Hivi kweli pale uwanja wa taifa wakati wa mechi l i r ipuke bomu, yupo mtu atasubiri waje polisi kumuokoa? Lakini yote hayo, wala watu hawana tena muda wa kufikiri. Ngoma ya kitisho cha ugaidi iliyopigwa kwa muda mrefu, ishawatia ujinga uliokusudiwa.

    N a m k u m b u k a mwal imu wangu wa inorganic chemistry Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1984, Profesa Saxena akisema kuwa yeye alikuwa hatoi mtihani mgumu maana akitaka wanafunzi wake wote wafaulu. Kwa hiyo mtihani wake anaokupa unahitajia kutumia asilimia 10 tu ya akili yako, kufaulu. Sasa, ukifeli ujue kuwa sio kosa lake. Jilaumu mwenyewe kwa kushindwa kutumia japo sehemu moja tu ya kumi ya akili yako. Inavyoonekana katika hili la kitisho cha ugaidi, tumef ik ishwa mbal i . Vichwa havifanyi kazi tena.

    Aliwahi kusema Josef Stalin kuwa-The easiest way to gain control of a population is to carry out acts of terror."- Akimaanisha kwamba njia nyepesi ya kuwadhibiti

    watu na kuwapelekesha unavyotaka, ni kuwapa k i p i g o c h a u g a i d i , kuwaundia ugaidi. Kwa nini? Kwa sababu, Fear of Terror Makes People Stupid ikiwa na maana kuwa kitisho cha ugaidi huwatia watu ujinga. Kinawaondolea kufikiri na kutumia akili zao. Na ndio maana Rais Franklin Roosevelt katika hotuba yake ya kwanza kwa wananchi wa Marekani alisema kuwa kama kuna jambo la kuogopa, basi ni hofu yenyewe.

    Kwa bahati mbaya katika ulimwengu tunaokwenda nao wa utandawazi na ubeberu wa ma-neocons, wanaotengeneza hofu na kitisho cha ugaidi ni vyombo vya dola ili kukidhi matakwa na agenda za mabeberu. K a t i k a v i wa n g o v ya kimataifa, wametegeneza kitisho cha ugaidi wa S a d d a m H u s s e i n n a A l - Q a i d a w a k a p a t a sababu ya kuzipiga na kuzisambaratisha Iraq na Afghanistan. Wakaunda kitisho cha Gadhafi kuwa anauwa watu wake, na sasa cha Bashar Assad. Libya ishasambaratishwa, Syria ipo chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).

    Ili uone kitisho cha

    u g a i d i k i n a v y o t i a watu ujinga, tizama IS wanavyopambwa kwamba wana nguvu za kutisha na jeshi lisilowezekana. Kwa zaidi ya miaka miwili Marekani na washirika w a k e w a n a j i t a h i d i kuwaangamiza, lakini wapi! Bado wana nguvu na uwezo wa kupenya hadi Par is wakapiga na wakaondoka b i la kukamatwa! Na watu wanaamini. Wala mtu hajiulizi, kama ni kweli h a o I S wa n a n g u v u kiasi hicho, hizo silaha wanapata wapi?

    Marekani, Uingereza n a w a s h i r i k a w a o , wanadai kupeleka ndege za kivita kuwapiga IS kwa miaka miwili sasa, IS wanadunda tu. Na watu wanaamini kuwa Marekani na washirika wake wamewashindwa IS. Ukiwaambia kuwa Marekani inafanya usanii, haiwapigi IS kwa sababu ni vijana wake, wanaona kama unafanya masikhara.

    Lakini sasa imefika mahali, Vladimir Putin kafanya kweli. Alianza kwa kutoa kauli kwamba ule mtindo wa mtu mmoja (Marekani) kuwaburuza walimwengu wote na k u wa f a n ya we n g i n e wajinga, ufikie mwisho.

    Kisha akaingia Syria akawa anawapiga kikweli IS. Hivi sasa IS wanasambaratika. Wanakimbia wanatoka nje ya Syria na Iraq. Miji inakombolewa. Kitendo cha IS kukimbilia nje ya Syria maana yake ni kuwa wengi wao walikuwa sio waasi wananchi wa Syria. Walikuwa mamluki waliopenyezwa nchini humo.

    Russia Vindicated by Terrorist Surrenders in Syria, ndivyo anavyochambua m w a n d i s h i F i n i a n C u n n i n g h a m , a k i m a a n i s h a k u w a i l e kwamba magaidi hivi sasa wanabwaga manyanga, kunaisafisha Urusi . Lakini wakati huo huo, inawaanika mabeberu wa Marekani na Ulaya kwamba ni w a o n g o . Wa l i k u w a hawapigi IS kwa sababu ni mamluki wao. Wao ndio waliwatengeneza na wao ndio walikuwa wakiwapa silaha kupitia Uturuki huku wakiwamiminia mapesa, tena baadae kupitia uuzaji wa mafuta yaliyokuwa yakichimbwa katika maeneo yaliyokuwa yakishikiliwa na vijana wao IS.

    Ilichofanya Urusi ni kukata mzizi wa fitna. Kwanza ni kushambulia na kuangamiza malori ya mafuta kutoka kwa magaidi kwenda nchi za NATO. Pili, kushambulia m a g a r i y a l i y o k u w a yakiwapelekea si laha I S . B a a d a ya k u o n a wamezidiwa, hivi sasa IS wanaomba waruhusiwe kuondoka chini ya mpango utakaosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba M w e k u n d u ( U n i t e d Nations and International Committee for the Red Cross.) BBC wakiripoti juu ya kubadilika kwa hali katika uwanja wa mapambano wanasema, Syria fighters evacuation from Zabadani under way. Hata hivyo h a w a k o m i k u p i g a propaganda. Kwanza w a n a k w e p a k u t a j a kwamba hali hiyo imekuja kutokana na kipigo kutoka Urusi. Pili hawataji kuwa wanaobwaga manyanga ni magaidi wa IS, al-Nusra Front na Jaish al-Islam wakiongozwa na kamanda Zahran Alloush, aliyeuliwa na majeshi ya Urusi. Huyu anatajwa kuwa ndiye akipokea silaha na vifaa vingine kupitia Saudi Arabia

    Inaendelea Uk. 10

    RAIS Barack Obama wa Marekani (kushoto) akiwa na Rais Vladimir Putin wa Urusi.

    ANNUUR NEW.indd 10 1/7/2016 3:17:19 PM

  • 11 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 201611 AN-NUURMakala

    Kweli, hofu ya ugaidi huwafanya watu kuwa wajinga kupindukia

    Inatoka Uk. 10na Qatar. Mwandishi F in ian Cunningham, a k i z i c h a m b u a S a u d i Arabia na Qatar katika mchezo huu wa ugaidi anasema: Saudi Arabia and Qatar, serves as a conduit for American CIA weapons to the more known terrorist outlets.

    Hili BBC wamekwepa kulisema badala yake wanaeleza kana kwamba, wanaokimbia ni wapinzani wa kawaida wa Bashar, Voice of America (VOA) wakimpa Zahran Alloush, cheo cha rebel leader.

    U k i j a k a t i k a n c h i zetu, ujinga ni ule ule, tena wenye maangamizi makubwa kwa nchi. Hivi sasa Kenya, vipo vikosi maalum ambavyo hupokea amri na maelekezo kutoka makachero wa nchi za U l a ya , M a r e k a n i n a Israel (Western Security Agencies), sio kutoka kwa Amiri Jeshi Mkuu wa nchi wala kwa wakuu wa vyombo vya usalama vya nchi hiyo. (Tazama: Inside Kenyas Death Squads) . Kwa ujumla kutokana na propaganda ya kitisho cha ugaidi, serikali zetu z imef ik ishwa mahal i pa kuamini kwamba hatupo salama mpaka tupate ulinzi kutoka kwa mabeberu. Na kwa sababu h i y o , t u n a wa r u h u s u kuweka kambi zao za kijeshi (military bases) na kuwa na kauli juu ya majeshi yetu. Zipo nchi hivi sasa wanajeshi wao wamekuwa kama mgambo wa kuwabebea m i k o b a m a k a m a n d a wa jeshi la Marekani. K u p i t i a k i t i s h o c h a ugaidi, tunapumbazwa, t u n a p u m b a z i k a , tunafanikisha agenda ya beberu kusambaza makucha yake ya kijeshi duniani (Network of Military Bases) kufikia lengo lake la World Hegemony.

    Tunachopata nini? Nchi huru inafikishwa mahali inakuwa koloni kasorobo. Haina sauti hata juu ya rasilimali zake. Haiwezi kuamua ifanye biashara na nani katika madini yake na mafuta/gesi yake. Na wenyewe hawafichi. Wanasema wazi kwamba wanacholenga kat ika kusambaza makucha yao ya kijeshi ni namna mbili. Kwanza kudhibiti uchumi wa dunia na masoko yake ya fedha. Pili, kudhibiti na kukomba rasilimali zote muhimu. Lakini kwa ujinga tuliokwishatiwa kutokana na kitisho cha

    ugaidi, tunawakaribisha kwa mikono miwili kwa hoja kuwa wanatusaidia kupambana na ugaidi. Ndio wataalamu wetu wa kutufundisha na kutuelekeza namna ya kukabiliana na Al-Qaida na Al-Shabaab!

    Lakini baya zaidi, i l i u g a i d i u k o l e e , mta le tewa ugaid i ambao utaporomosha na kuondoa Amani m l i y o k u w a n a y o . M a t u k i o k a m a y a Westgate, Garrisa na Mandera, lazima yaje mara kwa mara i l i kukumbushwa kuwa magaid i wapo . Na kwa bahat i mbaya, w a l a h a m t a j u a nani anawapiga au

    anawachezea akili kwa sababu kwa u j inga mliokwishatiwa, kazi yenu itakuwa kuimba Al-Shabaab, Al-Qaida, Boko Harm na majina kama hayo. Lakini pia utawala bora, wa sheria na haki, utaondoka. Watu watahujumiwa, watateswa, watauliwa bila kujali sheria na haki za b inadamu. Maana katika harakati z a k u p a m b a n a n a ugaidi, afisa wa polisi amepewa kibali cha kupiga risasi kwanza, m e n g i n e b a a d a e . Anaripoti yule Afisa wa GSU Recce Company (Kenya) akisema kuwa wanawakamata watu k a t i k a b a r ( k i l a b u

    ya pombe, hotelini, mtaani au majumbani) wanawafikisha polisi, lakini hawawasajili , bali huwapeleka porini na kuwapiga r isasi (Elimination Programme). Ndio maana katika ile documentary ya Aljazeera wakapewa jina la Death Squad.

    Ninaandika haya nikizingatia kuwa kuna Watanzania wenzetu wamo mikononi mwa v y o m b o v y a d o l a kwa muda mrefu sasa wakikabiliwa na tuhuma za ugaidi. Watuhumiwa h a w a u n a w e z a k u w a g a w a k a t i k a makundi mawili. Wapo ambao inawezekana hawana hatia kabisa. Ni wahanga ama wa njama za makusudi a u w a m e a n g u k i a katika bahati mbaya ya mtego wa panya. Lakini yawezekana wapo ambao kulikuwa na sababu za msingi za kuwatilia shaka na pengine walishafanya au walikuwa mbioni kufanya mambo ya hatari. Hawa nao ni wahanga tu wa mpango mzima wa maadui. Wametumbukia kwa

    u j i n g a , h a t a k a m a walikuwa wakilipwa au walighilibika kiimani, bado ni katika ujinga tu.

    Ili twende vizuri na tuwe salama kinchi, nadhani la muhimu na kuzingatia hapa ni kuwa katika kuwashughulikia watuhumiwa hawa, t u s i j e t u k a j i k u t a tukiongozwa na ujinga ule ule uliopandikizwa na kitisho cha ugaidi.

    Wiki iliyopita kulikuwa na mjadala mzuri sana k a t i k a A z a m T W O , ukatolewa mfano wa Nigeria: Kwamba polisi wanasema wamegundua m a h a l i B o k o H a r a m w a n a p o t e n g e n e z a mabomu (kiwanda cha silaha). Sasa mtu unajiuliza, nchi gani hiyo duniani ambapo watatokea waasi/magaidi, wajenge kiwanda cha silaha katikati ya mji (au hata ikiwa pembezoni), waingize mali ghafi za kutengeneza mabomu, mpaka wanayatumia mabomu hayo kuuwa watu, serikali na vyombo vyake vya usalama havina habari?

    Sasa huu ndio ujinga ninao zungumzia. Kwamba kama tutajiaminisha (kwa ujinga) kwamba kuna watu wanaweza kumiliki AK-47 na mabomu, wanazunguka n a y o m i t a a n i , h u k u serikali haina habari, basi kwa usalama wa nchi, sisi tutakuwa ndio magaidi wabaya zaidi kuliko tunaowatuhumu kwa ugaidi.

    Kamanda Suleiman Kova akitangaza kustaafu amesema kuwa katika m a t u k i o a m b a y o hatayasahau, ni pamoja na la Sitakishari. Na kweli, lile sio la kusahaulika mpaka kiteguliwe kile kitendawili cha maburungutu ya noti zinazomeremeta (ndio kwanza zinatoka Benki Kuu) zikiwa hazijaguswa kabisa kutumika, lakini Afande Kova akatuambia zimechimbuliwa chini a r i d h i n i ! Z i l i k u w a zimefukiwa shimoni na magaidi/majambazi!

    Lazima ifike mahali t u j i u l i z e , m a b e b e r u wanapiga ngoma ya kitisho cha ugaidi watutie ujinga ili wafanikishe ya kwao. Sisi tunapoitikia, tukapiga zumari na kucheza ngoma hii, tunatarajia kupata nini kama nchi?

    MWANDISHI Finian Cunningham

    WANANCHI wa Nigeria wakiandamana kushinikiza serikali ya nchi yao iharakishe kurejeshwa kwa mabinti zao wanaodaiwa kutekwa na kundi la Boko Haram.

    ANNUUR NEW.indd 11 1/7/2016 3:17:20 PM

  • 12 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 201612 Safu ya Ben Rijal

    KAMA tilivyosoma katika makala iliopita kuwa Sheikh Abdalla Saleh Farsy alikuwa ni alim, alikuwa hakusita kujisomea ili kuweza kupanua mawazo na kujiongezea elimu. Katika makala hii ya pili itamuangalia zaidi Sheikh Abdalla Saleh Farsy katika kazi zake alizozifanya na namna alivyopokewa katika jamii kazi zake ikiwa pamoja na tafsiri ya Quran na vitabu mbalimbali alivyoviandika. Nyingi ya kazi zake hazikuwa na haki miliki na wengine wamezigeuza kuzifanya kuwa ni kazi zao. Kuna juhudi hivi sasa inayofanywa na Jumuia moja ya Kiislamu kuweza kuzikusanya kazi zake zote alizozifanya kati ya zile alizozichapisha na zile ambazo hakuzichapisha.

    SHEIKH Abdalla Saleh Farsy.

    KATIKA makala za nyuma niliandika juu ya wahubiri wa Kikristo waliokuwa wanaletwa katika ukanda wa Afrika ya Mashariki ikiwa wengi wao walikuwa wajuzi wa kuielewa Quran na walikuwa wanakizungumza Kiarabu kwahio walikuwa wanaifanya kazi yao ya uhubiri kwa kuelewa vipi kukabiliana na Waislamu wengi hasa wale ambao walikuwa wakazi wa mwambao.

    Quran ya mwanzo kwa lugha ya Kiswahili iliandikiwa mwaka wa 1923 na Padri Dale ambaye alifanya kazi nzito ya kutafsiri Quran kwa Kiswahili ambayo Kiswahili chake kilikuwa cha watu wa Pwani. Tafsiri hiyo ilikuwa na kurasa 542 na kurasa zisopungua 142 ikiwa ni Sharhi (maelezo ya ufafanuzi) Quran hii hasa ililengwa kwa wahubiri wa Kikiristo walioajiriwa na University Mission to Central Africa (UMCA), iliyoanzishwa mwaka 1873. Wahubiri hao wakiitumia na kuwashtua Masheikhe namna walivyokuwa wanaielezea, hio ikawa ndio Quran iliopo kwa Kiswahili.

    Tafsiri hii ya Padre Dale ililenga zaidi kuikingia kifua Ukiristo na sherhe yake ilikuwa imezama sana kuwa nje ya ukweli wa Kiislamu. Kutokana na hayo, ikaonekana kuwa kuna haja haraka kabisa kupatikana kwa tafsiri

    Masheikhe wetu: Sheikh Abdalla Saleh Farsy-10 Sehemu ya Pili

    ya Kiswahili ambayo imeandikwa na Waislamu wenyewe. Hapo ndipo Sheikh Mubarak bin Ahmed akiwa kiongozi mkuu wa Makadiani wa Afrika ya Mashariki akaanza kuandaa matayarisho ya uandikaji wa Tafsiri ya Quran kwa Kiswahili na katika mwaka wa 1942. Tafsiri hio ikapelekwa kwa mchapishaji na kuhakikiwa katika kamati ya lugha ya Kiswahili iliokuwa ikijulikana kwa jina la Inter-Territorial Swahili Language ili iweze kukubalika na kusomeka kirahisi na Waswahili. Kamati hiyo ilithibitisha kuwa lugha iliotumika ni lugha ya Kiswahili bulbul na inakubalika kisha tafsiri hiyo ikapelekwa kwa viongozi mbalimbali wa Makadiani wa Afrika ya Mashariki na kukubaliwa kuwa lugha iliyotumika inakidhi haja.

    Sheikh Amri Abeid malenga wa lugha ya Kiswahili maarufu wakati huo katika Tanganyika na ukanda wa Afrika ya Mashariki, aliokuja kuheshimika na kupewa jina uwanja

    wa mpira wa Arusha kwa jina lake Sheikh Amri Abeid Stadium. Sheikh Amri Abeid akiwa muumini wa madhehebu ya Makadiani alipewa mafunzo ya dehehebu hilo ambalo liliasiwa nchini India, alifanyiwa mpango wa kwenda kupata taaluma ya ndani ya madhehebu hio na alikwenda nchini Pakistan kati ya mwaka wa 1954 hadi 1956 huko alipikwa vya kutosha. Wakati Sheikh Amri Abeid anakwenda Pakistan, Makadiyani walikuwa tayari wameshatoa nakala ya Quran ya Kiswahili ambayo inakingana na mwenendo wa kuwa Mtume Muhammad (SAW) ndio Khatim yaani mwisho wa Mitume wote. Sheikh Amri Abeid alikuja kuwa mtetezi mkubwa wa tafsiri hii na wafuasi wa madhehebu ya Suni kuemewa na kuonekana kuwa kuna haja ya kutengenezwa tafsiri ambayo itakidhi haja ya watu wa madhehehbu hio ikiwa idadi yao ni wengi katika ukanda wa Afrika Mashariki kama yalivyokuwa madhebu

    ya Malik kuwa na wafuasi wengi katika Afrika ya Kaskazini.

    Nchini Kenya tafsiri ya Quran iliyoegemea madhehebu ya Sunni ilikuwa inatafsiriwa kwa khatua na Sheikh Al-Amin Ali Mazrui, lakini haikuwa kamili na ndipo Sheikhe Abdalla Saleh Farsy akaanza kuitafsiri Quran kwa Kiswahili katika mwaka wa 1956 kwa kuirejeza tafsiri ya Makadiyani. Mmoja kati ya wanafunzi wake Sheikh Abdalla Saleh Farsy, marehemu Shariff Abdulwahab Alawy ambaye nilipata fursa ya kujadiliyana naye katika nyakati mbalimbali, alinambia kuwa Sheikh Abdalla Saleh aliwateua wanafunzi wake watano akiwa yeye mmoja kati ya hao na kuwapa kazi ya kila baada ya darsa kutalii nao na kutafsiri baadhi ya aya kuzitafsiri naye Sheikh Abdalla alikuwa kila aendapo alikuwa na kitabu chake maalumu ambacho alikuwa ananukulu na kufanya tafsiri. Alikuwa na mkoba wake maalumu ambao humo ulikuwa mfano wa maktaba, kwani wakati wote alikuwa na rejea (references) mbalimbali zilizoshikamana na Uislamu na tarekhe yake. Kwahivyo alianza kazi hii kwa juhudi kubwa sana na alikuwa akiwasiliana na watu mbalimbali ikiwa Kenya, Pakistan na maeneo mengineo. Kazi yake iliweza kukamilika ilipofika mwaka wa 1961 alikuwa tayari kishakamilisha juzuu 12 na kuweza kuchapishwa. Sheikh Abdalla alipata moyo kuona kazi yake kuwa sasa imo kwenye mikono ya Waislamu na kueleweka maelezo ya kina ya Quran na kuonyesha yale mapunguku ya

    Makadiyani. Sheikhe alikuwa na upungufu wa kifedha lakini juu ya kuwa na upungufu wa kifedha wa kumwezesha kuichapisha kopi yake ya kwanza lakini hayo hayakumsitisha kuiendeleza kazi yake hio na ilipofika mwaka wa 1969 chini ya udhamini wa Islamic Foundation ya Kenya ilitoka tafsiri hio kwa mara ya kwanza maarufu ambayo Sultan wa Qatar alisaidia pakubwa kifedha kuweza kuchapishwa nakala ya mwanzo (first edition) na kutolewa nakala 4,000 kugaiwa bure na nakala 3,000 zikawa zinauzwa kwa shilling 3,000.

    Islamic Foundation ya Nairobi yenye kuunga mkono Jamaat al Islam ya Pakistan, ndiyo iliyosimamia upigwaji wa chapa kwa mara ya mwanzo Tafsiri ya Sheikh Abdullah Saleh Farsy, na kumpatia tafsiri hiyo gwiji mwanaharakati wa Pakistan Sayyid Abdul Ala Maududi ambaye baada ya kufanyiwa tafsiri na kufahamu yalioandikwa, akaikubali tafsiri ya Qurani Takatifu ya Sheikh Abdalla na kwa upande wake Sheikh Abdullah Saleh Farsy akaitegemea tafsiri ya Maududi inayoitwa 'Qur'an Fahmi Ke Bunyadi Usul' (Msingi wa kuifahamu Qur-aan), na Syd Maududi akaombwa utangulizi wa tafsiri yake hio Tafhim Al-Qur-aan itumike kwenye utangulizi wa Qurani Takatifu ya Sheikh Abdalla hapo ikawa Waswahili wamepata tafsiri iliokamilika. Sambamba na tafsiri hii ipo tafsiri ya Kiswahili ilioandkiwa na Mzanzibari mwengine Sheikh Ali Muhsin Barwany kwa jina la Al Muntakhab Qurani Takatifu (quranitukufu.net).

    ANNUUR NEW.indd 12 1/7/2016 3:17:21 PM

  • 13 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016Safu ya Ben Rijal

    SAFARI hii makala hii itajaribu kuangaza utupwaji wa t a k a n a m b i n u z a kutumika. Taka zinakuwa mazonge kwetu kutokana na kushindwa kujuwa namna ya kuzitupa. Tuzitupe vipi na tuzitupe wapi?

    Jiulize wewe unaosoma makala hii unazitupaje taka ulizonazo ikiwa kutoka unapoishi, kiwandani kazini au popote pale. Jee, unazitupa popote pale utapoona kuna u p e n y u u t a k u we z e s h a kutupa taka, au unazitupa katika msingi (mtaro) wa maji, au unazitupa katika maeneo ya skuli ambapo baada ya masomo huwa h a k u n a u s i m a m i z i a u unazitupa pembeni mwa jirani yako au unazitupa palipotengwa taka tuzitupe, au unazifukia au unazichoma moto?

    Kama ningeweza kupata watu 100 wakawa wakweli kunambia wanavyozitupa t a k a , n a a m i n i j a wa b u nitayoipata zaidi ya asilimia 9 0 w a t a n i p a j a w a b u is ior idhisha. Uki j iul iza kwanini ikawa hivyo? Moja kati ya jawabu nikuwa ni dharau na watu kuona mji, nchi, makazi yao sio lolote lile na wao kutokuwa na wajibu wa usafi kwa kuwa wapo wahusika wanaowajibika kusafisha wakiwa wanalipwa na serikali. Fikra hizi ni potofu zinahitajika kupatiwa ufumbuzi kwa haraka kabisa ili dhana nzima ile ya yale Yawe Endelevu ipatikane.

    W a t u w a n a f i k r a mbalimbali fikra walizonazo zinatafautiana na fikra za binadamu kuna wakat i zinahitajika kutafautiana na kuna wakati zinahitajika ziwe za aina mmoja. Kwenye uvumbuzi hapa ndipo fikra za mwanadamu zinatafautiana na kutafaut iana kwake kunapelekea binadamu kufanya tafiti na kuweza kuja na mambo yenye manufaa. Lakini kuna sehemu fikra za wanadamu hazitakiwi kutafautiana na ukitaka kutafautiana na fikra za pamoja huwa ni majanga. Kwa mfano kupiga chanjo ya Polio, jambo hili ni lazima wala hakuna kutafautiana na utapo jifanya hutaki ni janga litakalo kukabili kwa mtoto atakaye kuja kuzaliwa, tumeyaona haya Nigeria. Sasa sisi tukiwa kama ni wananchi tumo katika taifa letu kuna haja kabisa fikra zetu ziwe zenye kukubaliana kwa yale yalio lazima tuwe tunakwenda sambamba kwa uslama na maendeleo yetu.

    Tunatupa taka kila kukicha na tunazlizalisha kila siku ikiwa kitu hicho kila siku unakizalisha kisha inabidi ukitupe itakulazimu uwe na mbinu yakinifu zilizokuwa mujarab kufanya hivyo. Huko nyuma tushasema namna ya kuzigawa hizo taka na kuzitupa, sasa l a k u j i u l i z a w a h u s i k a

    Yawe endelevu-3

    Aina ya Tanuri ya kuchomea taka

    Tanuri la kileo la kuchomea taka

    Gari la kukusanya taka.wametutengea mwahali muwafaka pakutupia taka zetu? Wapanga Miji na Vijiji ni sehemu muhimu kwetu kutupangia maeneo makhsusi ambayo tutakuwa tunatupa taka zetu kisha Manispaa zetu kuwa na mipango madhubuti ya ukusanyaji na kuzipeleka katika jaa kubwa la utupwaji wa taka.

    Mara nyengine huwa tunashindwa kuwalaumu wananchi kwa kuwa mtu anapoishi hajui akazitupe wapi taka ndio anapoona popote pale pametupwa taka nayeye ataona ni sawa kufanya hivyo. Jee hio ni sababu ya kujihalalisha hayo tunayoyafanya kuwa ni sawa? Inaweza ikawa ndio lakini nitasema sio, muhimu kupatafuta pale palipotengwa na kutakiwa mtu kuzitupa

    taka anazozizalisha. Ninapoishi mie kulikuwa

    na jaa kubwa ambalo taka zote za Manispaa zikitupwa hapo, lakini mji ulipotanuka na kukua imebidi jaa hilo liondoshwe lisogezwe nje ya mji kidogo na huko l i l iposogezwa kutokana na kutotumika utaalamu wa kuzitupa taka, matokeo yake katika kipindi kifupi eneo hilo lilijaa kwa kuwa gari la Manispaa linachukua hizo taka na kisha kuzitupa kwenye shimo ambalo lilipata kuchimbwa mawe, gari la Manispaa linabeba taka kisha huja gari la kuzifukia na kumwagwa mchanga na nyengine huchomwa moto. Hapo utajiuliza dunia ndivyo inavyozidhibiti taka kwa mtindo huo? Haya nayazungumzia eneo la kisiwa cha Unguja lakini

    utapotembea katika maeneo mengi ya Afrika Mashariki mambo ndio hayo kwa hayo hayatafautiani.

    Utupwaji wa TakaKatika kutupa taka kuna

    njia tatu kuu zinatakiwa z i z i n g a t i w e n a z o n i : Kuzikwa kwa taka (Landfill), Kuzichoma taka kwenye tanuri (Incineration) na njia nyengine ni Kurejezwa kwa taka (Recycling).

    Utupaji wa taka kwa kufukia kunahitajia kutengwa eneo maalumu na kisha kuhakikishwe kuwa taka zinazokwenda kumwagwa na kutupwa ni kuwa tayari zimeshabaguliwa. Kisha kuandaliwe mtindo wa jaa la kimambo leo (sanitary landfill).

    N i v i p i j a a h i l o linavyokuwa? Katika mwaka wa 1935 mtido huo uliasisiwa nchini Marekani katika mji wa Fresno, California na hadi sasa asilimia 58 ya taka zote za Marekani zinatumia mtindo huo, ikiwa taka zinafukiwa kwa kiwango kikubwa lakini sio kwa njia ya kupopoa lakini kwa taratibu maalumu ikiwa zinafukiwa kisha wataalamu wanaangalia na kufwatilia kinachoendelea.

    K i n a c h o f a n y i k a n i huchimbwa shimo kubwa au kati ya mashimo yalioachwa kisha huchimbiwa na Plastiki kubwa ikiwa na upana wa kiasi centimeter 120, baada ya taka kuingizwa humo kisha udongo huekewa juu, na kuhakikishwa kuwa maji hayaingii wala hayapenyi kutoka kwenye hilo shimo na kupenya kwenye ardhi (Leacheates). Ufukiaji huu unapokuwa tayari huwa kila tabaka hujazwa taka na udongo na kazi hi i i k a wa i n a e n d e l e a k i l a siku zikipinduka na huku taka zinaoza, shimo hilo linapokuwa limejaa hujazwa juu udongo bila ya kuongeza chochote. Sasa eneo hilo ambalo lilifanyiwa kazi hio linakuja mwisho kugeuzwa kuwa sehemu ya bustani na kuwa eneo la burdani, na maeneo hayo tunayo mengi ima yalichimbwa mawe, kifusi, jasi ambayo tunaweza k u j a k u ya g e u z a k u wa maeneo ya thamani baada ya kuwa maeneo yaliotupwa yasio na faida.

    Mpango huu wa majaa ya kileo unagharama kwa kiasi fulani lakini unajiuliza washauri na wataalamu wanashauri nini katika utupwaji wa hizi taka kwa jaa hili la kimambo leo? Vijana wanasoma somo la Environmental Engineering wamefuzu vizuri masomo yao wameajiriwa na wapo na hamu kuja mbele na kuonyesha uwezo wao katika elimu walioisoma ila balaa iliopo ni kuwa kuna vinganganizi wazee kama mie kiumri lakini sio mie wasiotaka fikra za vijana na kubakia na fikra mgando (Stagnant) na vijana hao huvunjwa moyo kisha huja wakafunga miko na kusema

    potelea mbali wacha twende tutafika. Nchi kama Japan mfanyakazi anayobuni chochote kile iwe uvumbuzi au jambo litaleta faida kwa nchi sio hupandishwa cheo tu, bali hutunzwa fedha tele. Ndipo unapoona Japan kila kukicha ipo inapiga maendeleo wakati maeneo ya kwetu kila kijana akija na kuleta mageuzi, huwa ndio adui katika kazi, mjuaji, anataka kuja kuhar ibu mambo, hayo yaliotengenea ndio yepi tukiuliza hayana jawabu.

    Kuna njia ya uchomaji wa taka (Incineration) inagawa njia hii kwa miaka hii kwenye mabadiliko ya tabia nchi na kuongezeka kwa joto duniani imekuwa haishauriwi sana, lakini bado inahitajika hasa kwa sisi nchi zanaozendelea kwani taka kama zinazotoka katika mahospitali yetu zinahitaj iwa kuchomwa kitaalamu kwenye matanuri. Nchi inahitajia aidha iwe na matanur i maa lumu ya kuchomea taka katika kupunguza mzigo wa taka, na yasiiwe yamezagaa. Kwenye mshadhari wa mahoteli (Chains of hotel) kunahitajia kuwe na Tanuri moja la kuchomea taka kwa hoteli zote zilizokuwepo hapo aidha na taka kutoka majumbani nazo zikapelekwa hapo kwa kuchomwa. Kwanini, kwanini tunabaki kama hivi ikawa taka kwetu mzigo? Kwanini, kwanini? Jawabu sote tunazo kuwa tunashindwa kuvipa vipaombele yalio takiwa kupewa umuhimu. Saa nyengine gari za Prado 4 hayo yanayoitwa Mashangingi zinajenga Tanuri safi kabisa la kileo. Lakini wapangaji wapo kufikiria manunuzi ya magari ya fakhari kwa taifa kisha watanue, watatanua mpaka lini?

    Kuzirejeza taka (recycle) hii nayo ni njia ya kupunguza mzigo wa taka, utaona kwa hapa Zanzibar hamna mtambo hata mmoja wa hakika wa kuzirejeza taka na kwa Tanzania bara ipo kwa mikoa michache ambaye inahesabika yenye taratibu ya mashine za kuzirejeza taka tupo duniani au tupo kwenye Kusadikika nchi alioielezea Shaabni Robert?

    Awamu ya 5 ya Serikali ya Muungano inachanga moto kubwa ya kufanya na moja ni hili la taka na lazima lipewe umuhimu kwa kiwamngo cha juu, hasa ukizingatia nchi inataka kuelekea kwenye kipato cha kati, na kufikia huko taka tujuwe zitazidi kuzalishwa na kukiwa hakuna taratibu za kuzidhibiti ifahamike ni kuelekea kuchangia uchafu n a m a r a d h i k u e n e z wa yanayotokana na uchafu. Hivi miji yetu mingi ipo na usalama duni wa afya kwa watu na kupunguza hata wanaotamani kuja kutembelea nchi yetu na nchi zetu za Kiafrika kwa jumla kuingia na khofu.

    Namalizia makala hii kwa kusema Jee taka zimekuwa kitanzi kwetu?

    ANNUUR NEW.indd 13 1/7/2016 3:17:22 PM

  • 14 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 8 - 14, 2016MAKALA/MASHAIRINa Shaban Rajab

    SIKU hizi matukio ya watumishi wa majumbani (yaya) kuwatesa watoto yameonekana kuwa ni mengi na kuwagusa watu wengi. Yawezekana m a t u k i o n a n a m n a hii yamekuwepo kwa kipindi k i refu s iku z a n y u m a l a k i n i yalikuwa hayafamiki au kugundulika. Na hata yakigundulika taarifa z a k e z i l i i s h i a e n e o lilipotokea tukio husika.

    Lakini kutokana na kasi ya kukua sayansi na teknolojia ya mawasiliano, wingi wa vyombo vya habari vya kielekroniki kama mitandao ya kijamii na televisheni na internet, siku hizi matukio haya yamekuwa yakigundulika mapema na kufahamika kwa haraka sana. Matukio haya ya utesaji watoto mbali na kuzua hisia za hofu na hasira miongoni m w a j a m i i , l a k i n i yamewafanya wazazi, hasa kina mama kufikiria upya ni nani wa kumuajiri kuwa yaya.

    Kwa kuwa fami l ia nyingi wazazi hawashindi nyumbani, yameripotiwa m a t u k i o y a y a y a kuwatwesa watoto katika madimbwi ya maji, yaya kumweka mtoto kwenye jokofu na yeye kutoweka, wakati mwingine yaya kumweka mtoto mchanga hata kwenye jiko la oven. Aidha yameshuhudia matukio mengi ya watoto k u n y i m w a c h a k u l a , kupigwa, kutelekezwa nyumbani bila uangalizi h u k u y a y a a k i k a t a mitaa. Matukio ya wizi ndio hayaelezeki. Hayo ni baadhi tu ya madhila ambayo hufanywa na watumishi wa majumbani kwa watoto wakati wazazi wao hawapo nyumbani.

    Zipo sababu nyingi ambazo zinaweza kuwa c h a n z o c h a k u we p o kwa ufedhuli huu kwa watoto. Pande zote mbili, mwajiri na mwajiriwa zimekuwa na kasoro katika mahusiano yao. Upande mmoja unaweza kuwa sahihi na upande wa pili ukawa na matatizo kulingana na mazingira ya pande husika.

    Kwa mfano kwa upande wa Mayaya, mojawapo ya kasoro au udhaifu unaoweza kuwa sababu ya malezo mabaya ya watoto inaweza kuwa historia ya maisha pamoja na malezi aliyopitia yaya katika makuzi yake.

    Yaya wengine wametoka katika familia zenye malezi yasiyokuwa na madili.

    Uhusiano wa mwajiri na YayaHupunguza matukio ya kuteswa watoto

    MMOJA wa wasichana wanaofanya kazi za ndani. (Picha kwa hisani ya Mtandao)

    Wengine wapitia malezi ya uteswaji na unyanyaswaji k ias i cha kuath i r ika kisaikolojia kiasi kwamba, hawaoni shida kutumia mazoea waliyolelewa, kulelea watoto wa waajiri wao kwa style waliyokulia wao. Na hata wanapopata ajira, aliyempa ajira hiyo ya uyaya naye asihangaike kujua kama aliyemwajiri ana ufahamu wa mambo yote ya msingi ya ulezi wa watoto na kutunza nyumba.

    Hata hivyo kulingana na washauari wa masuala ya kifamilia, kwa kiasi k i k u b w a m a d h i l a haya kwa watoto mara nyingi husababishwa na uhusiano mbaya kati mayaya na waajiri wao, kuanzia kitabia na ki-utu. Baadhi ya familia (baba na mama) hasa akina mama, wamejenga mazoea kwamba, yaya ni binadamu asiye na thamani muhimu ndani ya familia. Hakuna fikra ya utambuzi kwamba yaya ndiye mlezi wa watoto, mtunza nyumba na wakati mwingine ni mtunza siri za ndani. Waajiri wengi hawawapi Mayaya muda wa kupumzika hata kidogo, kauli kwao mara zote, ni ya kufoka na kukemea badala ya kufundisha na kuelekeza. Nyumba nyingi waajiri hawako tayari kukaa meza moja ya chakula na Yaya, wakala pamoja kama familia. Hawawezi kuangal ia televisheni pamoja na Yaya wala kuzungumza mazungumzo ya kawaida na yaya.

    Katika familia za namna

    hii, utu kwa yaya ni kitu adimu sana. Kuna hisia za ubwana na utwana. Yaya hana nafasi ya kuwa huru kushauri kutoa maoni au kushitakia jambo. Anakula jikoni, anakaa jikoni, kukaa sebuleni kwa bwana iwe ni wito au shughuli maalum.

    Katika familia hizi, yaya akivunja kikombe au glasi ni kama amenunua kesi ya mauaji. Atakaripiwa, atatukanwa matusi ya kila namna, kejeli, dharau na wakati mwingine kipigo kitakuwa juu yake. Lakini hatma ya yote lazima a takatwa u j i ra wake kiduchu, kufidia uharibifu uliotokea.

    Katika familia nyingi, siku za sikukuu wazazi watawanunulia watoto wao zawadi mbalimbali, ikiwani pamoja na nguo, v i a t u , k u t e m b e z w a sehemu za burudani nk. Katika hesabu hii, yaya hayupo wala hana sikukuu. Kisa analipwa mshahara hivyo ajipe raha mwenyewe asitegemee hisani ya familia.

    Wapo baadhi ya Mayaya hata wakiuguliwa, kufiwa au kuumwa, wakiomba mapumziko au kusafiri kujumuika na familia zao kwenye matatizo, asilani ruhusa haitatoka la, akizidi kukera ataondoka na ndio kujifukuzisha utwana wake.

    Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa, wana familia wengi wanawaona watumishi wa kazi za ndani kama watu wenye dhiki kali na hata ajira wanayopewa na mabwana ni kama kupewa ihsani tu

    wasiyostahili.Watoto anaweza kuwa

    watundu sana , k ias i k wa m b a a n a ye wa l e a anaweza kuwa na kipimo cha adhabu ya kiungwana m r a d i a s i w a u m i z e a u k u wa d h u r u , i l i k u w a j e n g e a h o f u wasirudie makosa. Lakini wengi hawawezi kufanya hivyo hata kama watoto watamkosea. Atanyamaza hadi afikishe ujumbe kwa mama mwenye nyumba. Lakini alishuhudia mtoto anayemlea amefanya kosa na kweli linahitaji kumchapa kidogo au kumfinya kama mwana familia na hata wazazi wakirudi akawaeleza kisa chote. Katika mahusiano mabovu ya namna hii, ndio maana tunashuhudia kuna matukio mengi ya kuteswa watoto, ambao hawana makosa. Watoto w a n a d h u l u m i w a n a k u k o s a m s a a d a k wa sababu ya umri wao mdogo.

    I m e f i k a b a a d h i ya wazazi hasa wale wenye uwezo, kuanza kutumia teknolojia ili kuhakikisha usalama wa watoto wao wa n a p o k u wa n j e ya nyumba, badala ya kujenga magusiano ya kiutu baina ya pande mbili hizo.

    "Nik iwa na uwezo nitaweka kamera kwa nyumba yangu. Kwa sababu kama umeweka kamera ukiwa kazini hautakuwa na wasiwasi. Anazungumza mzazi mmoja wa huko Uganda.

    Lakini mshauri wa mambo ya jamii Bi. Anne Nafula anaona kwamba kuweka mi tambo ya kamera sio suluhu la kutosha kwa masuala

    kama haya. "Lazima mwajiri aelewe

    k wa m b a m f a n ya k a z i nyumbani sio mfanyakazi tu, anafaa amuweke karibu kama mmoja wa ukoo au jamii ili ajione ni sehemuya familia na amwangalilie mtoto kwa njia nzuri, l a k i n i u k i m c h u k u l i a kwamba hana thamani katika nyumba yako, basi atafanya vile anavyopenda" Alibainishamtaalam huyo.

    Aidha kulingana na ripoti za vyombo vya habari ni wazi matukio ya yaya kuolewa au kupata watoto na waajiri wao yameongezeka.

    Haya ni matokeo ya wazazi kuthamini zaidi kazi na kutumia muda w o t e k a z i n i k u l i k o mahusiano ya kifamilia. Bi. Nafula analaumu baadhi ya wanawake walioolewa kwa kutelekeza majukumu yao na kumwaachia yaya kufanya shughuli zote za nyumba hata z i le zinazochochea mahusiano ya mume na mke.

    M a j u k u m u yanayostahili kufanywa na mke wa nyumba, yanapatiwa msichana wa k a z i . Wa n a wa k e wengi wameshindwa na majukumu yao hata ya kulea watoto, hata kuangalia waume zao. Na weng