dear brothers and sisters in christ, hamjambo: it is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa...

16
1

Upload: others

Post on 30-Mar-2020

7 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

1

Page 2: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

2

Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo:

It is truly a great honor as chairman of The Kenya Catholic Community in America (KCCA) and all its affiliate Jumuiya Ndogo

Ndogo, that I take this opportunity to welcome you all to this magnificent celebration, our 8th Annual Cultural Gathering, that

brings us all together to thank our God for the many precious gifts He has graced us with in our everyday lives. This year’s event

is special because it is the first time KCCA is holding its Annual Swahili Mass and festivities here in the Pacific Northwest and in

this great Jesuits institution, Bellermine Preparatory School.

We wish to welcome Most Rev. Philip Arnold Anyolo, Archbishop of the Archdiocese of Kisumu, Kenya, our main celebrant

today; our concelebrant priests, the clergy, deacons, religious Sisters, and all religious men and women here today. We welcome

all the civic leaders here with us today and the entire congregation for coming in solidarity.

We sincerely thank Most Rev. J. Peter Sartain, Archbishop of Seattle, for welcoming us to the Archdiocese of Seattle. Deacon Carl

Chilo and all those at the Archdiocese who helped us navigate the protocols to make this event possible. Thank you. Our

appreciation goes out to Rev. Ray Cleveland Pastor of Holy Spirit Church Kent, for embracing our Kenyan Catholic Community

to his parish, a parish the KCC in the greater Seattle area call home. A home we have all come to celebrate and praise God as

brothers and sisters in Christ. Thank you KCC Seattle for the devotion and dedication in making this event a success.

The Mission of the Kenyan Catholic Community in America as an organization is, to promote and support Small Christian

Communities “Jumuiya Ndogo Ndogo” in the diaspora (USA); to strengthen our faith and families by nurturing spiritual

wellbeing, peaceful and just communities by supporting and/or coordinating activities that serve Kenyan Catholics in the United

States to live their faith in solidarity with their brothers and sisters.

This is one of the many events that KCCA organizes to evangelize and grow our spirituality and Catholic faith. Please be part of

the team and let’s walk together in following our Lord’s footsteps.

Sincerely yours in Christ

George N. Marucha MBA , CMA

KCCA Chairman

www.kcca2012.org

Page 3: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

3

All Stand for Entrance and Opening prayers

ENTRANCE SONG/KUINGIA: NJOONI TUIMBE Holy Spirit Parish Jumuiya – Kent, WA

Njoni tuimbe, Njoni tuucheze, njoni tufurahi mbele zake Bwana.

Piga makofi, piga vigelegele, mshangilieni Bwana leo asubuhi x2

1. Sauti ya kwanza semeni alleluya, Sauti ya pili tumsifu Yesu Kristu,

Sauti ya tatu na ile ya nne, waseme pamoja, milele amina.

2. Wamama wote pigeni vigelegele, Wababa wote vinanda vipigwa sana,

Pigeni filimbi ngoma na kayamba, watoto wadogo wote changamkeni

3. Mataifa yote njoni mbele za Bwana, makabila yote simameni tuimbe

Nyanyukeni wote pigeni makofi, shangwe na nderemo vifijo machazo

4. Bahari na vitu vyote viijazavyo, milima mito na miti shangilieni,

Ndege wa angani na warukeruke, wanyama kondeni furahini sana.

ENTRANCE SONG/KUINGIA TWENDE SOTE NYUMBANI Holy Spirit Parish Jumuiya – Kent, WA

[Twende sote nyumbani mwake, Bwana Mungu [aee]

Twende sote nyumbani mwake aliyetuumba] x2

1. Yeye ndiye nguvu yetu - Bwana Mungu (aee) Twende sote nyumbani mwake aliyetuumba

Yeye Bwana wa majeshi -

2. Ndiye Mungu wa Yakobo - Bwana Mungu (aee) Twende sote nyumbani mwake aliyetuumba

Yeye mfalme wa wafalme -

3. Yeye mfalme wa dunia - Bwana Mungu (aee) Twende sote nyumbani mwake aliyetuumba

Ndiye mfalme wa mbinguni -

4. Yeye Mungu wa wokovu - Bwana Mungu (aee) Twende sote nyumbani mwake aliyetuumba

Yeye ndiye mwamba wetu -

5. Ni hakimu wa dunia - Bwana Mungu (aee) Twende sote nyumbani mwake aliyetuumba

Jina lake litukuzwe -

6. Ndiye Mungu mtakatifu - Bwana Mungu (aee) Twende sote nyumbani mwake aliyetuumba

Pendo lake la milele -

KYRIE - MISA AMECEA: BWANA UTUHURUMIE Holy Spirit Parish Jumuiya – Kent, WA

[S/A] - Bwana utuhurumie [ee Bwana]

All - Bwana utuhurumie x2

Page 4: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

4

[T/B] - Kristu utuhurumie [ee Kristu]

All - Kristu utuhurumie x2

[S/A] - Bwana utuhurumie [ee Bwana]

All - Bwana utuhurumie x2

GLORIA – MISA AMECEA: UTUKUFU KWA MUNGU Holy Spirit Parish Jumuiya – Kent, WA

1. [Tenor] - Utukufu kwa Mungu juu mbinguni

[All] - Na amani kote duniani,

[kwa watu] wenye mapenzi mema.

Tunakusifu Baba Tunakuheshimu,

Twakuabudu sisi Tunakutuza [x2]

2. Twakushukuru Mungu kwa ‘tukufu

Wako mkuu ewe Mungu mfalme,

[Ee Baba] wa mbingu Baba yetu

3. Bwana wetu Mwokozi Yesu Kristu

Mwana wa pekee wake Mungu,

[Uliye] Mwanakondoo wa Mungu

4. Unayeziondoa dhambi zote

Za dunia utuhurumie

[Pokea] pokea ombi letu

5. Wewe unayeketi kuume

Kwake Baba utuhurumie

[Sikia] sikia ombi letu

6. Kwani pekee yako ndiwe Bwana

Pekee yako mkuu na mkombozi

[Pekee] pekee Yesu Kristu

7. Kwa umoja wa Roho Mtakatifu

Ndani yake Baba watukuzwa

[Ee Yesu] milele na milele

LECTIONARY PROCESSION/MASOMO: NENO TOKA KWA BWANA Boston Jumuiya – MA

[Ni neno toka kwa Bwana linakuja,

Ni neno toka kwa Bwana linakuja] X2

Lisikie neno, neno lake Bwana

Ni neno toka kwa Bwana linakuja

Page 5: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

5

1. Injili toka kwa Bwana inakuja . . .

2. Ushindi toka Bwana unakuja . . .

3. Baraka toka kwa Bwana zinakuja . . .

4. Hekima toka kwa Bwana inakuja .

All Remain Seated For Readings

Somo la Kwanza (Ufunuo11: 19a; 12.1-6a) Minnesota Jumuiya

Mwanamke anayeonglewa katika ufunuo huu ni mfano wa Kanisa; joka ni mfano wa shetani; na mtoto wa

mwanamke ndiye masiya. Vita kati ya joka na mwanamke ni mapigano kati ya nguvu za shetani na Kanisa.

Liturjia hulinganisha Mama Maria na Kanisa sababu ya kufaulu kumshinda shetani kwa nguvu za Kristo.

Somo Katika Ufunuo wa Yohana

Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake.

Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi na mvua ya mawe nyingi sana. Na ishara kuu

ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa

chake taji ya nyota kumi na mbili. Naye alikuwa an mimba, akilia, hali ana uchungu na kuumwa katika kuzaa.

Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, aliyekuwa na vichwa saba na pembe

kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na

kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo,

amle mtoto wake. Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya

chuma. Na mtoto wake akanyabuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi. Yule mwanamke

akakimbia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na

mia mbili na sitini. Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa

Mungu wetu, na mamlaka ya Kristu wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye

awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.

Hilo ndilo neno la Mungu: W. Tumshukuru Mungu

Responsorial Psalm/Wimbo wa Katikati (Zab. 45:10,11, 12,16 K. 10) Boston Jumuiya

1. Binti za wafalme wamo / Miongoni mwa akina bibi wako wastaahiki.

Mkono wako wa kuume amesimama malkia, /Amevaa dhahabu ya Ofiri.

Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, / Uwasahau watu wako na nyumba ya Baba yako. (K)

(K) Mkono wako wa kuume amesimama malkia, amevaa dhahabu ya Ofiri.

2. Naye mfalme atautamani uzuri wako, / Maana ndiye Bwana wako, nawe umsujudie.

Watapelekwa kwa furaha na shangwe, / Na kuingia katika nyumba ya mfalme. (K)

Somo la Pili (1 Wakorintho 15:20-27) St. Patrick’s, NJ Jumuiya

Somo latueleza kwamba Yesu amemshinda shetani na ubaya wake, yaani dhambi na mauti. Ushindi huu

umedhirishwa katika ufufuko wake Kristo, na utadhirishwa zaidi nyakati za mwisho katika ufufuko wa miili ya

watu. Tunda lingine la ushindi wa Kristo ni kupalizwa Bikira Maria mbinguni.

Somo katika waraka wa kwanza wa Mtume Paulo kwa Wakorintho.

Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na

kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo

Page 6: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

6

wote watanuishwa. Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja.

Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote,

na nguvu. Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho

atakayebatilishwa ni mauti.

Hilo ndilo neno la Mungu: W. Tumshukuru Mungu

All Stand For Gospel Acclamation

GOSPEL ACCLAMATION/INJILI: Alleluia Wasafiri Jumuiya - MD

Aleluiya!....Aleluiya aaa Aleluiya aaa Aleluiya!

yelele yelele Aleluiya! x2

Maria amepalizwa mbinguni majeshi yote ya malaika wanafurahi.

Aleluiya!....Aleluiya aaa Aleluiya aaa Aleluiya!

yelele yelele Aleluiya! x2

GOSPEL READING: Lk 1:39-56

HOMILY: All Seated For Homily

CREED/NASADIKI - MISA KARIOBANGI: NASADIKI KWA MUNGU Boston Jumuiya – MA

1. Nasadiki kwa Mungu mmoja - Ninasadiki

Ndiye Baba yetu mwenyezi - “

Mwumba mbingu pia dunia - “

Nasadiki kwa Yesu Kristu - “

Nasadiki nasadiki –ninasadiki

Nasadiki nasadiki –ninasadiki

2. Mwana wa pekee wa Mungu - Ninasadiki

Mwenye kuzaliwa kwa Baba - “

Akapata mwili kwa Roho - “

Kazaliwa naye Bikira - “

3. Kisha yeye kasulubiwa - Ninasadiki

Kwa amri ya Ponsio Pilato - “

Kwa ajili yetu kateswa - “

Akafa na akazikwa - “

4. Kafufuka katika wafu - Ninasadiki

Kapaa juu Mbinguni - “

Ameketi kuume kwake - “

Mungu Baba yetu Mwenyezi - “

Page 7: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

7

5. Ndipo atakapotokea - Ninasadiki

Kuhukumu wazima na wafu - “

Kwake Roho Mtakatifu - “

Kwa Kanisa la Katoliki - “

6. Ushirika wa watakatifu - Ninasadiki

Ondoleo la dhambi zetu - “

Nangojea ufufuko wa miili - “

Na uzima wa milele - “

All Stand For Prayers Of The Faithful/Sala za Waumini

Response: Ee Bwana twakuomba utusikie

All Seated For Offertory

OFFERTORY/SADAKA: TOENI SADAKA Washington DC Jumuiya

Toeni Sadaka - Toeni Sadaka, Toeni Sadaka

Kwa Upendo wa Mungu toa x2.

1. Ulicho nacho - kwa upendo wa Mungu toa

Sadaka yako - kwa upendo wa Mungu toa

2. Utajiri wako - kwa upendi wa Mungu toa

Umaskini wako - “

3. Uzee wako - kwa upendo wa Mungu toa

Ujana wako - “

4. Na mali yako - kwa upendo wa Mungu toa

Akiba yako - “

5. Maisha yako - kwa upendo wa Mungu toa

Na pesa zako - “

6. Furaha yako - kwa upendo wa Mungu toa

Ukarimu wako - “

7. Na nafsi yako - kwa upendo wa Mungu toa

Ujasiri wako - “

8. Matendo yako - kwa upendo wa Mungu toa

Mapendo yako - “

9. Na fedha zako - kwa upendo wa Mungu toa

Shukrani zako - “

OFFERTORY/SADAKA: VIUZENI VYOTE Delaware Jumuiya

Viuzeni vyote mlivyo navyo, Nendeni, mkavitoe sadaka ×2

Kwa kuwa yote mliyo nayo yametoka kwa Mungu,

Hazina yetu iko mbinguni×2

Page 8: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

8

1. Mazao ya mashamba, leteni kwake Mungu

Kazi ya mikono yetu.. Leteni kwake Mungu...

Mmepewa bure, naye Mungu, leteni vyote, kwake Mungu.

2. Mali mliyo nayo... _Leteni kwake Mungu_.....

Fedha za mifuko yenu.... _Leteni kwake Mungu_....

Mmepewa bure , naye Mungu, Leteni vyote kwake Mungu..×2

3. Vyote mlivyo navyo.. _Leteni kwake Mungu_ ....

Ijapo vidogo vilivyo... _Leteni kwake Mungu_

Mmepewa bure, naye Mungu, leteni vyote kwake Mungu ×2

OFFERTORY/SADAKA: NJOONI WATU WOTE St. Gabriel & St. Lwanga Jumuiya – PA

1. Njooni watu wote tutoe (tutoe] - njoni tutoe sadaka x2

2. Kila mtu aanze kutoa (kutoa] - njoni tutoe sadaka x2

3. Toa sehemuyo ya kumi (ya kumi] - njoni tutoe sadaka x2

4. Asante yako urudishe (rudishe] - njoni tutoe sadaka x2

5. Utoe kwa moyo karimu (karimu] - njoni tutoe sadaka x2

6. Ndiyo siri yako na Mungu (na Mungu] - njoni tutoe sadaka x2

7. Ulicho nacho anajua (najua] - njoni tutoe sadaka x2

8. Uonyeshe mapendo yako (ndo yako] - njoni tutoe sadaka x2

9. Nafsi yako nzima tolea (tolea] - njoni tutoe sadaka x2

OFFERTORY/SADAKA: BEBA MIKONONI Worcester Jumuiya – MA

1. Tusimame ndugu [leo] twende kwake Bwana

Usisite ndugu [yangu] amka twende hima x2

Beba mikononi [Mwako] uliojaliwa

Peleka kwa Bwana [Mungu] upate Baraka

2. Peleka kwa moyo [ule] moyo wa mapendo [Kweli]

Peleka kwa Bwana [yale] uliojaliwa x2

3. Sadaka ya fedha [kweli] fedha za mifuko [ndugu]

Amka upeleke [leo] Mezani kwa Bwana x2

4. Mavuno, mifugo [yote] ni mali ya Bwana [kweli]

Tupeleke kwake [leo] atazipokea x2

5. Mkate divai [vyote] tupeleke kwake [leo]

Tupate Baraka [tele] mbele zake Bwana x2

6. Twende ndugu twende [hima] mbele zake Mungu

Tupeleke nafsi [nasi] zote kwake Bwana x2

PRESENTATION OF GIFTS/MATOLEO: UPOKEE SADAKA YETU Boston Jumuiya – MA

1. Upokee sadaka yetu, twakutolea Baba

Upokee navyo vipaji, twakutolea Baba

Page 9: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

9

Pokea Baba zawadi x2 twakutolea Baba

2. Upokee mkate wetu -

Upokee divai yetu

3. Upokee mazao yetu-

Upokee na fedha zetu –

4. Nasi pia ni mali yako -

Tunatubu makosa yetu –

5. Upokee mioyo yetu -

Upokee na nafsi zetu –

6. Haya yote ni mali yako-

Uyapokee kwa huruma –

7. Uviunge vipaji vyetu -

Na sadaka yake mwanao –

8. Usifiwe ewe mtukufu -

Kwa sadaka yake na yetu –

9. Utuhurumie wakosefu -

Tuletee baraka yako -

PRESENTATION OF GIFTS/MATOLEO: SADAKA NALETA Holy Spirit Parish, Kent-WA Jumuiya

Naja kwako nipoke ingawa mimi ni mdhambi X2

1. Naja mbele yako ewe Bwana Mungu huku nimejawa na dhambi;

Bwana usiniache uniwie radhi mbele yako Bwana natubu.

2. Sadaka naleta ingawa sifai lakini ee Bwana pokea;

Mkate divai yote naileta mbele yako Bwana pokea.

3. Shetani muovu amenizingira pembe zote Bwana nalia;

Usiku silali ninahangaika Bwana wangu mwema nipokee.

4. Nipe nguvu Bwana nishinde shetani niishi na wewe daima;

Nikutumikie siku zangu zote nikin’gara kama theluji.

SANCTUS/MTAKATIFU -MISA AMECEA: Holy Spirit Parish, Kent-WA Jumuiya

[Tenor]: Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu - wa Majeshi

[Sop]: Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi

[Sop/Alto]: Mbingu na dunia zimeja zimejaa

Mbingu na-a dunia zimeja Utukufu wako x2

Ho-sanna juu, hosanna juu, ho-osanna juu hosanna juu mbinguni x2

Page 10: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

10

[Tenor]: Mbarikiwa – ‘naye kuja x2

Mbarikiwa

Mbarikiwa anayekuja kwa jina jina lake Bwana x2

All Kneel For Consecration

BREAKING OF THE BREAD: Wasafiri Jumuiya - MD

Mwili wake na sadaka nategemea daima yote chini yakiisha Mwokozi atanitosha

Damu yake na sadaka nategemea daima yote chini yakiisha Mwokozi atanitosha

MEMORIAL ACCLAMATION/FUMBO LA IMANI: Wasafiri Jumuiya - MD

Hili ni fumbo la Imani

Kristu alikufa, Kristu alifufuka,

[Kristu atarudi tena] ×2

GREATER AMEN: Wasafiri Jumuiya – MD

Aaamina Aamina/ Aaamina Aaamina

Aamina Aamina/ Aamina Aamina

All Stand and Recite Our Father - Baba yetu uliye mbinguni ………

SIGN OF PEACE/KUPEANA AMANI: Tupeane Amani St. Patrick’s & St. Agatha - NJ

1. Mungu wetu ni wa Amani [Mungu wetu ni wa amani x3]

Kanitoa wapi kaniweka wapi

Kanitoa chini kaniweka kati

Kanitoa kati kaniweka juu

Mungu wetu ni wa Amani

2. Mungu wetu ni wa upendo, baraka, faraja,

LAMB OF GOD/ MWANA KONDOO: Worcester Jumuiya - MA

[Mwana kondoo wa Mungu tuhurumie leo x2]

Tuhurumie x4

Mwana kondoo wa Mungu tuhurumie leo.

[Mwana kondoo wa Mungu tuhurumie leo x2]

Tuhurumie x4

Mwana kondoo wa Mungu tuhurumie leo.

Page 11: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

11

[Mwana kondoo wa Mungu tujalie amani x2]

Tujalie x4

Mwana kondoo wa Mungu tujalie amani

All Kneel

COMMUNION/KUPOKEA: MWILI WA BWANA YESU California Jumuiya - CA

1. Mwili wa Bwana Yesu, chakula cha Mbingu

Ni chakula cha Roho, chenye uzima

Hima uwe nasi ee Bwana Yesu

Ukatushibishe chakula bora

[Ni chakula cha Roho, chenye uzima x2]

2. Yesu alituambia, Yeye ni chakula

Ni chakula cha Roho, chenye uzima

Sote twaamini, ni mwili wake

Pia twaamini ni damu yake

[Ni chakula cha Roho, chenye uzima x2]

3. Yesu alituambia, kuwa tumpokee

Ni chakula cha Roho, chenye uzima

Ee Bwana mkombozi tunakuomba

Kwa chakula hiki tuinamie

[Ni chakula cha roho, chenye uzima x2]

4. Hii ndiyo karamu, aliyotuachia

Ni chakula cha Roho, chenye uzima

Alaye mwili na kunywa damu

Ana uzima wa siku zote

[Ni chakula cha roho, chenye uzima x2]

COMMUNION/KUPOKEA: BWANA ATUALIKA KARAMUNI MWAKE St Patrick’s & St. Agatha - NJ

Bwana atualika karamuni mwake x2

Tule mwili wake damu yake Bwana tunywe

(tupate uzima) uzima wa milele x2

1. Ameandaa mkate, chakula cha kiroho, ashirikiaye ana uzima wa milele.

Ameandaa divai, kinywaji cha kiroho, ashirikiaye ana uzima wa milele.

2. Tule mkate huu, ni mwili wake Yesu, tupate neema, neema ya milele.

Tunywe divai hii, ni damu yake Yesu, tupate uzima uzima wa milele

3. Atulisha mwili wake, atunywesha damu yake, karamu yake Bwana ni pendo la milele.

Atupenda kwa rehema, atupenda kwa neema, pendo lake mwana kondoo ni pendo la milele.

Page 12: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

12

4. Twashukuru Bwana Yesu, kwa chakula chako bora, chashibisha Roho twasema asante.

Kwa mfano wako bora, kwa kuja ndani yetu. Kutupa neema twasema asante.

COMMUNION/KUPOKEA: AULAYE MWILI WANGU Washington DC Jumuiya

Aulaye mwili wangu, na kuinywa damu yangu, [Asema Bwana]

hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake x2

1. Aulaye mwili wangu, na kuinywa damu yangu, ana uzima wa milele

2. Njoni enyi wenye njaa, njooni enyi wenye kiu, Njoni kwangu niwashibishe

3. Aniaminiye mimi, na kushika nisemavyo, Nitamfufua siku ya mwisho

4. Mlapo chakula hiki, mnywapo kinywaji hiki, Mwatangaza kifo cha Bwana.

COMMUNION/KUPOKEA: POKEA MOYO WANGU St. Gabriel & St. Lwanga – PA

Pokea moyo wangu ee Mungu wangu

Niweze kukupenda kwa pendo lako

Unipe moyo wako, ewe Yesu mkombozi wangu

Shinda kwangu, nami daima kwako

1. Onjeni muone kwamba Bwana yu mwema

Na heri yule mtu anayetumaini Yesu Kristu

2. Katika nguvu za giza katutoa

Na kutukaribisha katika ufalme wa upendo

3. Habari njema alituhubiria na kutufungulia

Akatangaza mwaka wa neema

4. Mchungaji wangu mkuu ndiye Bwana Yesu,

Sikosi kitu kamwe kuniongoza kwenye njia nyofu

THANKSGIVING/SHUKRANI: MOYO WANGU WAMTUKUZA BWANA California Jumuiya

[Moyo] Moyo wangu wamtukuza Bwana

[Roho] Roho yangu inafurahi x2

1. Kwa kuwa amemwangalia, kwa huruma mtumishi wake, hivyo tangu sasa watu wote, wataniita

mwenye heri

2. Kwa sababu Mwenyezi Mungu, amenifanyia makuu, jina lake ni takatifu

3. Huruma yake ni kwa wote, wote wale wanaomcha kizazi hata na kizazi,

4. Huyatenda mambo makuu, kwa nguvu za mkono wake, wenye kiburi uwatawanya,

5. Hushusha wote wenye vyeo, kutoka vitini vya enzi, nao wale wanyenyekevu, wote hao huwainua

Page 13: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

13

6. Huwashibisha wenye njaa, na matajiri huwaacha, waende mikono mitupu,

7. Hulilinda taifa lake, teule la mtumishi wake, akikumbuka huruma yake.

8. Kama alivyowaahidia, babu zetu kuwaahidia, Ibrahimu na uzao wake.

9. Atukuzwe Baba na Mwana, naye Roho Mtakatifu, leo kesho hata milele, kwa shangwe milele Amina

All Stand For Final Blessings

FINAL BLESSING:

RECESSIONAL/MWISHO: NI NANI MAMA WA KANISA Worcester Jumuiya – MA

1. Ni nani mama wa kanisa - Bikira Maria

Ni nani mama wa Jumuiya - Bikira Maria

Alimkanyanga shetani, Akamyang'anya uwezo -- Bikira Maria x2

2. Ni nani mama wa watoto - Bikira Maria

Ni nani mama wa vijana - Bikira Maria

3. Ni nani mama wa mama - Bikira Maria

Ni nani mama wa wazee - Bikira Maria

4. Ni nani mama wa watu wote - Bikira Maria

Ni nani mama wa nchi zote - Bikira Maria.

RECESSIONAL/MWISHO: JINA MARIA NI JINA TUKUFU Holy Spirit Parish Jumuiya – Kent, WA

Jina Maria - Ni Jina tukufu

Lafurahisha - Linatutuliza

Malaika mbinguni wanaliimba, usiku na mchana wanaliimba

[Wakisema “Ave! Ave Maria”

Ni jina tukufu: Jina la Maria Ee, ee ee …. X2]

1. Maria Mama wa Mungu tuombee, [tuombee kwa mwanao Yesu x2]

2. Jina lako siku zote lapendeza, [wewe uliye mnara wa Daudi x2]

3. Jina lako siku zote lapendeza [wewe uliye Malkia wa Mbinguni x2]

4. Twaliimba jina lako siku zote [jina Maria linatufurahisha x2]

Page 14: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

14

Page 15: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

15

Page 16: Dear Brothers and Sisters in Christ, Hamjambo: It is …...ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota

16