makubaliano mapya ya ulaya kuhusu maendeleo · jukwaa kuu la utendaji, ambapo maelewano ya pamoja...
TRANSCRIPT
SN 3109/17 YML/ik 1
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
MAKUBALIANO MAPYA YA ULAYA KUHUSU MAENDELEO
‘ULIMWENGU WETU, HESHIMA YETU, MUSTAKABALI WETU’
1. Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu1 (Ajenda ya 2030), iliyokubaliwa na Umoja wa
Mataifa mnamo Septemba 2015, ni suluhisho la jamii ya kimataifa la changamoto na mitindo
ya ulimwengu mzima kuhusiana na maendeleo endelevu. Huku Malengo ya Maendeleo
Endelevu (SDG) yakiwa ni kiini chake, Ajenda ya 2030 ni utaratibu wa kisiasa wenye kuleta
mabadiliko na wenye nia ya kumaliza umaskini na kutimiza maendeleo endelevu
ulimwenguni kote. Inasawazisha vipengele vya kiuchumi, kijamii, na kimazingira vya
maendeleo endelevu, ikiwa ni pamoja na masuala makuu ya utawala na jamii zenye amani na
ujumuishwaji, na kutambua uhusiano muhimu uliopo baina ya maazimio na malengo yake. Ni
lazima itekelezwe kikamilifu na sio kwa kuchagua vipengele fulani tu. Ajenda ya 2030
inaazimia kutomuacha yeyote nyuma na inalenga kuwafikia kwanza walio nyuma sana
kimaendeleo.
2. Mabadiliko kutoka kwa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG) hadi Malengo ya
Maendeleo Endelevu yanaonyesha badiliko la mtazamo wa maendeleo ya ulimwengu mzima.
Mtazamo huu, ambao unazingatia maendeleo endelevu na haki za binadamu, unaambatana
kikamilifu na maadili na kanuni za Umoja wa Ulaya. Ajenda ya 2030 na Malengo yake 17 ya
Maendeleo Endelevu yanawahusu wote na yanatumika kwa nchi zote katika viwango vyote
vya maendeleo, kulingana na umiliki wa kitaifa na majukumu ya pamoja. Ushirikiano wa
wadau mbalimbali ni muhimu katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu.
3. Ajenda ya Utendaji ya Addis Ababa2 (AAAA), kama sehemu muhimu ya Ajenda ya 2030,
inatoa mtazamo mpya wa utekelezaji kupitia matumizi yanayofaa ya mbinu za kifedha na
zisizo za kifedha, kwa kuziweka hatua za ndani ya nchi na sera bora katika mstari wa mbele.
Aidha, Ajenda ya 2030 inasaidiwa na Utaratibu wa Sendai kuhusu Upunguzaji wa Hatari za
Janga3, na Mkataba wa Paris kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa
4, ambao unatoa utaratibu
wa kisheria na kuleta mwelekeo mpya katika juhudi za ulimwengu mzima za kupambana na
mabadiliko ya hali ya hewa. Utekelezaji wa ahadi hizi lazima uzingatie utaratibu wa
1 A/RES/70/1
2 A/RES/69/313
3 A/RES/69/283
4 FCCC/CP/2015/L.9/REV.1
SN 3109/17 YML/ik 2
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
ulimwengu mzima unaotilia maanani sheria, huku ushirikiano baina nchi ya mbalimbali
ukiwa ndio kanuni yake kuu na msingi wake ukiwa ni Umoja wa Mataifa.
4. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wamejituma ili kuhakikisha kuwa watu wote
wanaishi maisha yenye heshima yanayopatanisha maendeleo na ufanisi wa kiuchumi, jamii
zenye amani, ujumuishi wa kijamii na uwajibikaji kwa mazingira. Kwa kufanya hivyo, juhudi
zitaelekezwa katika kumaliza umaskini, kupunguza udhaifu na kushughulikia ukosefu wa
usawa ili kuhakikisha hakuna mtu yeyote anayeachwa nyuma. Kwa kuchangia katika
kutimiza Ajenda ya 2030, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watakuza pia Ulaya
thabiti, endelevu, jumuishi, salama, na yenye ustawi zaidi.
5. Makubaliano haya ya Ulaya kuhusu Maendeleo yanatoa utekelezaji wa Ajenda ya 2030 kwa
ushirikiano na nchi zote zinazoendelea, huku yakizingatia utaratibu uliotolewa na Mkataba wa
Lisbon. Aidha, Mkakati wa Ulimwengu wote wa Sera ya Umoja wa Ulaya ya Masuala ya
Kigeni na ya Usalama (Mkakati wa Ulimwengu wote) unatoa dira ya jumla ya ushirikiano
unaojumuisha watu wote, wenye kuaminika, na wenye mwitikio duniani.
6. Madhumuni ya Makubaliano haya ni kutoa utaratibu wa mtazamo wa pamoja wa sera ya
maendeleo ambao utatumika na taasisi za Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake huku
wakiheshimu majukumu na uwezo tofauti wa kila mmoja wao. Yataelekeza hatua ya taasisi za
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama katika ushirikiano wao na mataifa yanayoendelea.
Hatua za Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake zitakuwa zenye kuhimizwa na wote na
zilizoratibiwa ili kuhakikisha wanakamilishana na zinaleta matokeo mazuri.
SN 3109/17 YML/ik 3
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
1. SULUHU LA UMOJA WA MATAIFA KWA AJENDA YA 2030
1.1. Utendaji thabiti na unaofaa zaidi wa Umoja wa Ulaya katika ulimwengu
unaobadilika
7. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake lazima watoe suluhu kwa changamoto na fursa
zinazokumba ulimwengu mzima kwa kuambatana na Ajenda ya 2030. Watatekeleza Ajenda
ya 2030 katika sera zote za ndani na za nje kwa njia ya utendeti na kimkakati, wakijumuisha
vipengele tatuvya maen deleo endelevu kwa namna yenye usawa na ushikamano, na
wakishughulikia uhusiano baina ya Malengo ya Maendeleo Endelevu na vile vile matokeo
mapana ya vitendo vyao vya ndani ya nchi katika kiwango cha kimataifa na cha ulimwengu
wote. Utekelezaji (wa Ajenda ya 2030) utaratibiwa kwa karibu na utekelezaji wa Mkataba wa
Paris kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa na mikataba mingine ya kimataifa, ikiwa ni pamoja
na Ajenda ya Jiji Lipya5.
8. Ndani ya utaratibu huu jumuishi, mtazamo wenye ushikamano na uratibu wa vitendo vya nje
ya nchi vya Umoja wa Ulaya utakuwa muhimu katika utekelezaji wenye ufanisi wa agenda ya
2030 ulimwenguni kote. Ukiwa na muundo wake wa kitaasisi na nyenzo za kisiasa
zinazopeanwa chini ya Mkataba wa Lisbon, Umoja wa Ulaya umejitayarisha vilivyo ili
kupambana na changamoto na fursa za ulimwengu wote pahali zinapotokea.
9. Mkakati wa Ulimwengu wote wa Umoja wa Ulaya unatoa dira ya ushirikiano wa Umoja wa
Ulaya duniani, kupitia sera kadhaa. Unaangazia jukumu muhimu ya Ajenda ya 2030, ambayo
ina uwezo wa kuchochea mabadiliko yanayohitajika ili kuunga mkono kanuni za Umoja wa
Ulaya na malengo ya vitendo vya nje ya nchi vya Umoja wa Ulaya. Malengo ya Maendeleo
Endelevu yatakuwa ni kipengele jumuishi cha kazi yote ya kutekeleza Mkakati wa
Ulimwengu wote wa Umoja wa Ulaya. Makubaliano haya yatachangia katika maafanikio ya
vipaumbele vya vitendo vya nje ya nchi vya Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na kupitia
kuunga mkono uthabiti katika viwango vyote. Kwa kufanya hivyo, Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama wake watakuza mtazamo wa uthabiti wenye vipengele tofauti na wenye nguvu,
ili kukabiliana na udhaifu unaoweza kusababisha hatari mbali mbali zinazohusiana.
5 A/RES/71/256
SN 3109/17 YML/ik 4
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
1.2. Suluhu ya maendeleo
1 0 . Makubaliano haya ndiyo msingi wa sera ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa, ambayo ni
sehemu ya jumla ya suluhu ya Umoja wa Ulaya kwa ajenda ya 2030. Lengo kuu la sera ya
maendeleo ya Umoja wa Ulaya, kama lilivyoainishwa katika Kifungu cha 208 cha Mkataba
wa Utendakazi wa Umoja wa Ulaya, ni kupunguza, na mwishowe, kumaliza umaskini. Umoja
wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watatumia kanuni ya ushikamano wa sera kwa ajili ya
maendeleo (PCD), na watazingatia malengo ya ushirikiano wa maendeleo katika sera zake
zote za ndani na nje ya nchi watakazozitekeleza na ambazo zinaweza kuathiri nchi
zinazoendelea. Ushikamano wa sera kwa ajili ya maendeleo (PCD) ni sehemu kuu ya
mchango wa Umoja wa Ulaya katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu.
1 1 . Sera ya maendeleo ya Umoja wa Ulaya pia inafuatilia malengo ya vitendo vya nje ya Umoja
wa Ulaya, hasa yale yaliyoainishwa katika Kifungu cha 21(2)(d) cha Mkataba kuhusu Umoja
wa Ulaya (TEU) wa kukuza maendeleo endelevu ya kiuchumi, kijamii na kimazingira ya nchi
zinazoendelea, lengo kuu likiwa ni kumaliza umaskini. Kuambatana na malengo yaliyoko
kwenye Kifungu cha 21(2) cha Mkataba kuhusu Umoja wa Ulaya, sera ya maendeleo pia
huchangia katika, miongoni mwa mengine, kuunga mkono demokrasia, utawala wa sheria na
haki za binadamu, kudumisha amani na kuzuia migogoro, kuboresha hali ya mazingira na
usimamizi endelevu wa rasilimali asilia za ulimwengu wote, kusaidia watu, nchi na maeneo
kukabiliana na majanga asilia na yale yanayosababishwa na vitendo vya binadamu, na
kuendeleza mfumo wa kimataifa unaotegemea ushirikiano thabiti zaidi baina ya nchi
mbalimbali na utawala mzuri wa ulimwengu wote. Kwa hivyo, Mkataba huu utachangia pia
katika hitaji la kuhakikisha uthabiti baina ya nyanja tofauti za vitendo vya nje ya Umoja wa
Ulaya, na baina ya nyanja hizi na sera zake zingine.
1 2 . Jambo kuu katika utimizaji wa malengo haya ya pamoja ni Umoja wa Ulaya kufanya kazi
kwa pamoja. Kwa hivyo, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wanajitolea kufanya
kazi vyema zaidi kwa moja. Ushikamano mkubwa zaidi unahitajika baina ya Nchi
Wanachama na taasisi za Umoja wa Ulaya. Ushirikiano wenye ushikamano na uthabiti
utapelekea kuwepo na uaminifu, uhalali, uwajibikaji, thamani iliyoongezwa, ushawishi na
athari zuri zaidi katika ulimwengu. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake lazima
waungane katika utofauti wao, kwa kutumia mitazamo na uzoefu mbalimbali, wakitilia
maanani faida za ulinganifu wa kila mmoja.
SN 3109/17 YML/ik 5
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
1.3. Kanuni na maadili yanayoongoza hatua ya maendeleo
13. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake hutenda kazi kulingana na kanuni za vitendo vya
nje ya Umoja wa Ulaya zilizoainishwa katika Kifungu cha 21(1) cha Mkataba kuhusu Umoja
wa Ulaya: demokrasia, utawala wa sheria, hali ya haki za binadamu kuwa za watu wote na
kutogawanyika kwa haki hizo na aina tofauti za uhuru ambazo ni msingi, udumishaji wa
heshima ya binadamu, kanuni za usawa na umoja, na udumishaji wa kanuni za Mkataba wa
Umoja wa Mataifa na sheria ya kimataifa. Maadili haya ya watu wote na utawala mzuri ni
kiini cha Ajenda ya 2030.
14. Majadiliano ya kisiasa ni njia muhimu ya kuendeleza kanuni za maendeleo na pia yana
kipengele cha uzuiaji kinacholenga kuhakikisha kuwa maadili ya Umoja wa Ulaya
yanadumishwa. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watajumuisha udumishaji wa
haki za binadamu, demokrasia, utawala wa sheria na usawa wa kijinsia katika majadiliano ya
kisiasa. Mazungumzo haya yatafanyika ndani na nje ya serikali washirika na yatakuwa
jukwaa kuu la utendaji, ambapo maelewano ya pamoja yataendelezwa, maendeleo
yatarekebishwa mara kwa mara na hatua za usaidizi zinazofaa kutambuliwa.
15. Usawa wa kijinsia ni msingi wa maadili ya Umoja wa Ulaya na umejumuishwa katika
utaratibu wake wa kisiasa na kisheria. Una umuhimu katika kutimiza Malengo ya Maendeleo
Endelevu na yanahusika katika Ajenda yote ya 2030. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama
wake wataendeleza haki za wanawake na wasichana, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa
wanawake na wasichana na ulinzi wao kama jambo la kupewa kipaumbele katika nyanja zote
za utendaji.
16. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watatekeleza mtazamo wa ushirikiano wa
maendeleo unaozingatia haki, na wenye kujumuisha haki zote za binadamu. Wataendeleza
ujumuishwaji na ushirikishwaji, kutobagua, usawa na usawa, uwazi na uwajibikaji. Umoja wa
Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendelea kuwa na jukumu kubwa katika kuhakikisha
kuwa hakuna yeyote anayeachwa nyuma, mahali popote wanapoishi watu, na bila kuzingatia
kabila, jinsia, umri, ulemavu, dini au imani, mvuto wa kijinsia na utambulisho wa kijinsia,
hali ya uhamiaji na mambo mengine. Mtazamo huu unajumuisha kushughulikia aina
mbalimbali za ubaguzi unaoukumbana na watu walio katika hali ya udhaifu na vikundi
vilivyotengwa.
SN 3109/17 YML/ik 6
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
17. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wanathamini kushiriki kwa mashirika ya asasi za
jamii (CSO) katika maendeleo na wanahimiza sehemu zote za jamii kushiriki kiamilifu.
Wanatambua majukumu mbalimbali ya mashirika ya asasi za jamii kama waendelezaji wa
demokrasia, walinzi wa wenye haki na utawala wa sheria, haki ya kijamii na haki za
binadamu. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza nafasi ya asasi za jamii
na kuboresha uungaji mkono wao wa kujenga uwezo wa mashirika ya asasi za kijamii, ili
kuimarisha mchango wao katika mchakato wa maendeleo na kuendeleza mazungumzo ya
kisiasa, kijamii na kiuchumi.
18. Ufanisi wa maendeleo ni muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu na ni lazima
yajumuishwe katika miundo yote ya ushirikiano wa maendeleo. Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama wake watatumia kanuni za ufanisi wa maendeleo zilizokubaliwa katika
Muungano wa Ulimwengu mzima wa Ushirikiano Fanifu wa Mendeleo (GPEDC) wakati wa
Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Busan kuhusu Usanifu wa Msaada mnamo mwaka wa 2011 na
uliosasishwa wakati wa Mkutano wa Ngazi ya Juu uliofanyika Nairobi mnamo mwaka wa
2016: ambazo ni, umiliki wa vipaumbele vya maendeleo kwa mataifa yanayoendelea,
uangaziaji wa matokeo, miungano jumuishi ya maendeleo, uwazi na uwajibikaji wa pande
zote husika.
2. UTARATIBU WA UTENDAJI
19. Utekelezaji wa Ajenda ya 2030 unahitaji mikakati mipana ya kitaifa ya maendeleo endelevu
inayozingatia Malengo ya Maendeleo Endelevu na uhusiano wao. Wakati wa kupanga na
kutekeleza ushirikiano wa kimaendeleo, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
watazingatia hasa uhusiano wa aina hiyo na vitendo jumuishi ambavyo vinaweza kuleta
manufaa ya pamoja na kufikia malengo mengi kwa njia yenye ushikamano. Katika muktadha
huu, hatua zinazochukuliwa na Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake zitaonyesha
dhamira kuu za Ajenda ya 2030: Watu, Sayari, Maendeleo, Amani na Ushirikiano.
SN 3109/17 YML/ik 7
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
20. Huku wakitambua kwamba lazima Ajenda ya 2030 itekelezwe kwa ukamilifu, na sio kwa
kuchagua vipengele fulani, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watashughulikia
vipengele tofauti jumuishi ili kufikia maendeleo endelevu na kuongeza kasi ya mabadiliko,
kama vile: vijana; usawa wa kijinsia; uhamiaji na uhamaji; nishati endelevu na mabadiliko ya
hali ya hewa; uwekezaji na biashara; utawala mzuri, demokrasia, utawala wa sheria na haki za
binadamu; ushirikiano bunifu na nchi zinazoendelea zilizosonga mbele zaidi; na kukusanya na
kutumia rasilimali za ndani ya nchi.
2.1. Watu – Maendeleo na heshima ya kibinadamu
21. Ukuaji na mabadiliko ya kidemografia duniani, pamoja na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii
na kimazingira, unatoa fursa kwa, na wakati huo huo, kuibua changamoto kwa maendeleo
endelevu. Idadi ya watu ulimwenguni inatarajiwa kuongezeka kwa kiasi cha bilioni 2.4
ifikiapo mwaka wa 2050, ambapo watu bilioni 1.3 watakuwa wanaishi Afrika. Kushughulikia
mahitaji ya kielimu ya watoto na vijana ni muhimu sana katika kuendeleza uraia uliowajibika,
kuendeleza jamii endelevu na zenye maendeleo na kutia nguvu ajira ya vijana.
22. Kumaliza umaskini, kupambana na ubaguzi na ukosefu wa usawa na kutomuacha yeyote
nyuma vyote viko katika kiini cha sera ya ushirikiano wa kimaendeleo ya Umoja wa Ulaya.
Umaskini una sifa mbalimbali na unahusiana na vipengele vya kiuchumi, kijamii,
kimazingira, kitamaduni na kisiasa. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watajituma
kumaliza njaa na aina zote za utapiamlo na vile vile kuendeleza ufikivu wa huduma za afya
kwa watu wote, ufikivu wa elimu na mafunzo bora kwa wote, ulinzi unaotosha na endelevu
wa jamii na ajira zuri kwa wote katika mazingira safi. Maendeleo katika nyanja hizi yatatoa
msingi thabiti zaidi wa maendeleo endelevu. Umoja wa Ulaya unasisitiza tena ahadi yake ya
kugawa asilimia 20 ya Usaidizi wake Rasmi wa Maendeleo (ODA) ili kugharamia
ujumuishwaji wa kijamii na maendeleo ya binadamu.
23. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataunga mkono nchi washirika katika kutimiza
majukumu yao ya kuimarisha sera za kitaifa na utawala ili kuziwezesha kutoa huduma
muhimu na kutimiza haki za kibinadamu kwa njia endelevu.
SN 3109/17 YML/ik 8
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
24. Ukosefu wa chakula chenye virutubishi vinavyotosha na utapiamlo ni vikwazo vikuu vya
maendeleo na mzingo wa maisha, kwa sababu unasababisha upungufu wa kuelewa, unashusha
uwezo wa watoto shuleni na kusababisha afya mbaya na upungufu wa uzalishaji wa
kiuchumi. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watajizatiti ili kuhakikisha watu wote
wanaweza kupata chakula salama, kinachotosha, na chenye virutubishi vinavyofaa. Watu
walio katika hali zenye hatari zaidi watazingatiwa kwa karibu sana, wakiwemo watoto wa
chini ya miaka tano, wasichana wa makamo na wanawake hasa walio na mimba na
wanaonyonyesha. Watafanya juhudi zilizoratibiwa, kwa haraka, na zinazojumuisha sekta
mbalimbali ili kumaliza njaa, kuongeza uwezo wa uzalishaji wa chakula ndani ya nchi na
kwenye eneo, kuhakikisha kuna chakula cha kutosha na chenye virutubishi na kuboresha
uthabiti wa walio hatarini zaidi, hasa katika nchi zenye majanga yaliyoendelea kwa muda
mrefu au yanayotokea mara kwa mara. Wataendelea kuwekeza katika maendeleo ya watoto
wachanga kwa kushughulikia aina zote za utapiamlo, ikiwa ni pamoja na kutokua kwa urefu
na uzito kwa watoto kupitia usaidizi wa huduma za kimsingi katika afya, virutubishi, usafi wa
maji na wa mwili, na ulinzi wa kijamii.
25. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watasaidia jamii zilizo maskini zaidi kuboresha
ufikiaji wa ardhi, chakula, maji, na nishati safi, ya bei nafuu na endelevu, huku wakiepuka
madhara yoyote mabaya kwa mazingira. Wataendeleza miradi ya sera na kuunga mkono nchi
washirika katika kupanga na kutekeleza mtazamo jumuishi ili kushughulikia kikamilifu
uhusiano unaofaa zaidi kati ya ardhi, chakula, maji na kawi.
26. Ongezeko kubwa la mahitaji ya maji na uhaba wa maji katika miongo inayofuata, litapelekea
changamoto kuu hasa katika ujirekebishaji kufuatia mabadiliko ya hali ya hewa. Ufikiaji wa
maji safi ya kunywa kwa watu wote, usafi wa mazingira na wa mwili vinahitajika ili kuwepo
na afya na uzima, ukuaji na uzalishaji. Rasilimali za maji zinaweza kuathiriwa hasa na
uharibifu wa mazingira, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa, yanayotishia kilimo
na uwepo wa chakula cha kutosha. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataunga
mkono usimamizi wa maji endelevu na jumuishi na pia matumizi bora ya maji na utumiaji wa
majichafu kwa mara ya pili baada ya kuisafisha ikiwa ni pamoja na kupitia mtazamo wa
kimkakati zaidi wa maendeleo na ujumuishi wa kanda.
SN 3109/17 YML/ik 9
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
27. Afya ni muhimu kwa maisha ya watu na ni kipengele kikuu cha ukuaji na maendeleo
endelevu na wenye usawa, ikiwa ni pamoja na umalizaji wa umaskini. Umoja wa Ulaya na
Nchi Wanachama wake wanasisitiza tena ahadi yao ya kulinda na kuendeleza haki ya kila
mmoja ya kufurahia afya ya mwili na ya akili ya hali ya juu zaidi iwezekenavyo ili
kuendeleza heshima ya binadamu, uzima na maendeleo. Wataendelea kuunga mkono nchi
washirika katika juhudi zao za kujenga mifumo ya afya ambayo ni imara, bora, na thabiti,
kwa kutoa ufikiaji sawa wa huduma za afya na kuhakikisha wote wanapata huduma za afya.
Kwa madhumuni haya, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watasaidia nchi
zinazoendelea katika kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa sekta ya afya, kuwaajiri,
kuwasambaza nyanjani na kuwapa mafunzo zaidi katika taaluma zao. Wataendeleza
uwekezaji katika na uwezeshaji wa wafanyakazi wa kijamii walio katika mstari wa mbele
ambao huwa na jukumu muhimu sana la kuhakikisha sehemu zilizo mbali sana mashambani,
zisizo na huduma za kutosha, zenye umaskini na zinazokubwa na migogoro zinapata huduma
za afya. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendelea kuwekeza katika kuzuia na
kupambana na magonjwa ya kuambukiza, kama vile VVU/Ukimwi, kifua kikuu, malaria na
homa ya manjano na watasaidia kuhakikisha kuwa watu wote wanaweza kupata dawa na
chanjo muhimu kwa bei nafuu. Wataendeleza utafiti na uwekezaji katika, na uundaji wa
teknolojia mpya za afya. Watachukua hatua ili kupambana na hatari za afya za ulimwengu
mzima, kama vile majanga na viini sugu, kupitia mtazamo wa afya ya umma. Watafanya kazi
ili kupunguza vifo vya watoto wachanga na kina mama wajawazito/wanaonyonyesha,
kuendeleza afya ya akili na kushughulikia ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza
katika nchi washirika pamoja na kutatua uchafuzi wa mazingira wa kemikali na hewa chafu.
Kwa sababu ya uhusiano mbalimbali uliopo, wataunga mkono nchi washirika katika
kuendeleza mtazamo wa “afya katika sera zote”.
28. Kuhakikisha watu wote wanapata elimu bora kunahitajika ili vijana wawe wanaweza
kuajiriwa na kuwepo na maendeleo yanayodumu. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
wataunga mkono mafunzo jumuishi na ya kujitolea ili kujiendeleza kibinafsi au kitaaluma na
elimu bora yenye usawa, hasa katika masomo ya watoto wadogo na wale walio katika shule
ya msingi. Vile vile wataendeleza elimu katika kiwango cha sekondari na cha ngazi ya juu,
mafunzo ya kiufundi na taaluma na pia mafunzo ya kazini na ya ngumbaru, ikiwa ni pamoja
na katika hali za dharura au janga. Fursa za elimu na mafunzo kwa wasichana na wanawake
zitapewa kipaumbele. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataongeza juhudi zao za
kuhakikisha kila mmoja ana ufahamu, ustadi, uwezo na haki wanazohitaji kufurahia maisha
yenye heshima, kushiriki kikamilifu katika jamii kama watu wazima wanaowajibika na
SN 3109/17 YML/ik 10
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
wanaoweza kufanya kazi, na kuchangia katika uzima wa jamii zao kiuchumi, kimazingira, na
kijamii.
29. Mahitaji, haki, na maazimio ya watoto yanafaa kutiliwa maanani. Hatua zenye manufaa
makubwa zaidi kiuchumi na kijamii ni pamoja na miradi mipana ya uendelezaji wa watoto
wachanga. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataongeza juhudi zao za kutoa
mazingira salama na yanayokuza watoto kama kiungo muhimu cha kuongeza idadi ya vijana
wanaoweza kufikia uwezo wao kamili. Aidha, wanatambua kwamba kila mtoto anafaa kuwa
na maisha matulivu ya utotoni na elimu bora, ikiwa ni pamoja na nyakati za dharura na hali za
majanga ili kuzuia hatari ya kuwepo na ‘kizazi kilichopotea’. Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama wake watafanya kazi na nchi washirika ili kuboresha ulinzi wa watoto na
kushiriki kwao katika maamuzi yanayowahusu.
30. Kuambatana na kanuni ya kutomuacha yeyote nyuma, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama
wake watawapa kipaumbele maalum wale walio katika hali za udhaifu, hatari na zilizotengwa
wakiwemo watoto, wazee, watu wenye ulemavu, wasagaji, shoga, wanaovutiwa na jinsia zote
mbili, wasenge, na wenye sifa za jinsia mbili, pamoja na watu asilia. Hii itajumuisha hatua za
kuwalenga, kuwalinda na kuwasaidia vizuri zaidi ili kuwapa fursa sawa na kuhakikisha
hakuna ubaguzi.
31. Takriban watu bilioni moja ulimwenguni kote wana ulemavu, huku asilimia 80 yao wakiishi
katika nchi zinazoendelea. Watu wenye ulemavu aghalabu huwa ndio maskini zaidi katika
jamii wanazoishi, na hukumbana na viwango vya juu zaidi vya unyanyapaa na ubaguzi.
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watazingatia mahitaji mahususi ya watu wenye
ulemavu katika ushirikiano wao wa maendeleo. Kuambatana na Kanuni ya Umoja wa Mataifa
ya Haki za Watu wenye Ulemavu, wataendeleza zaidi haki za watu wenye ulemavu na
kuchukua hatua thabiti za kuhakikisha wanajumuishwa kikamilifu katika jamii na wanashiriki
kwa usawa katika soko la ajira.
32. Kuanzisha ajira bora na zinazotosha kwa vijana kutaendelea kuwa changamoto kuu. Sera
zinazowalenga vijana na uwekezaji unaowafaa zinahitajika ili kuendeleza haki za vijana,
kuwawezesha kushiriki katika maisha ya kijamii, kiraia na kiuchumi, na kuhakikisha
wanachangia kikamilifu katika ukuaji na maendeleo endelevu. Vijana wanapaswa kushiriki
pia katika michakato ya kidemokrasia na kujitwika majukumu ya uongozi.
SN 3109/17 YML/ik 11
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
Vijana
Vijana ni wahusika wakuu wa kuchochea maendeleo na mabadiliko na hivyo basi wana mchango
muhimu katika Ajenda ya 2030, ikiwa ni pamoja na kupitia uwezo wao wa kubuni. Kutoshughulikia
mahitaji yao ya kielimu, ajira, kijamii na kisiasa kutarudisha nyuma ufikiaji wa Malengo ya
Maendeleo Endelevu na kuwaacha wakiwa katika hatari ya kutumbukia katika uhalifu na itikadi
kali hasa katika hali za migogoro.
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataangazia hatua halisi za kutimiza mahitaji ya
vijana, hasa wanawake wachanga na wasichana, kwa kuongeza fursa bora za ajira na ujasiriamali,
zinazoungwa mkono na sera zinazofaa katika elimu, mafunzo ya taaluma, uendelezaji wa ustadi, na
ufikiaji wa teknolojia na huduma za kidijitali. Hili litalenga kutumia uwezo wa ubunifu wa kidijitali
na kuleta fursa za kunufaika na maendeleo ya kiteknolojia. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama
wake watalenga pia kuimarisha haki za vijana na uwezeshaji wao wa kujihusisha na masuala ya
umma ikiwa ni pamoja na kuendeleza kushiriki kwao katika mambo ya uchumi wa mitaa, jamii, na
kufanya maamuzi hasa kupitia mashirika ya vijana.
33. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendelea kutimiza wajibu wao chini ya
Kanuni ya Kumaliza Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake. Wataendeleza zaidi ulinzi na
utimizaji wa haki za wanawake na wasichana na kufanya kazi pamoja na washirika ili
kumaliza aina zote za unyanyasaji na ubaguzi kwa misingi ya jinsia, ikiwa ni pamoja tabia
zenye kulet madhara mabaya kama vile ndoa za kulazimishwa, za mapema, na zile za baina
ya watoto wenye umri mdogo, na ukeketaji. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
watachukua hatua na kuimarisha mazungumzo kuhusu sera ili kuwawezesha wanawake na
wasichana, kuendeleza jukumu lao muhimu kama wahusika wakuu wa kuchochea maendeleo
na mabadiliko na kuongeza hatua zinazolenga kuleta usawa wa kijinsia. Hii itajumuisha
kuendeleza haki zao za kiuchumi na kijamii na uwezeshaji, uimarishaji wa sauti zao na
ushirikishwaji wao katika maisha ya kijamii, kiuchumi, kisiasa, na kiraia, wakihakikisha
uadilifu wao kimwili na kiakili, na kubadili mitindo ya taasisi za Umoja wa Ulaya na nchi
Wanachama wake ili kutimiza ahadi zao. Kuendeleza ufikiaji sawa wa ajira yenye faida kwa
wanawake, kazi zuri, malipo sawa na huduma za kifedha kutanufaisha watu wote katika jamii.
SN 3109/17 YML/ik 12
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
34. Umoja wa Ulaya unazidi kujitolea kuendeleza, kulinda, na kutimiza haki zote za binadamu na
kutekeleza Mpango wa Utendaji wa Beijing na Programu ya Utendaji ya Kongamano la
Kimataifa kuhusu Idadi ya Watu na Maendeleo (ICPD) kwa ukamilifu na kwa njia inayofaa
na matokeo ya kongamano zao za kutathmini na unazidi kujitolea kuendeleza haki na afya ya
uzazi na ya jinsia (SRHR), katika muktadha huu. Ikitilia hayo maanani, Umoja wa Ulaya
unasisitiza tena kujitolea kwake katika kuendeleza, kulinda, na kutimiza haki ya kila mtu ya
kudhibiti kikamilifu, na kuamua kwa hiari na kwa kuwajibika katika masuala yanayohusiana
na ujinsia wao na afya ya jinsia na uzazi, bila ubaguzi, matumizi ya nguvu na unyanyasaji.
Zaidi, Umoja wa Ulaya unasisitiza haja ya watu wote kufikia taarifa na elimu kamili ya afya
ya ngono na uzazi zilizo bora na za bei nafuu, ikiwa ni pamoja na elimu kamili ya masuala ya
kijinsia, na huduma za afya.
SN 3109/17 YML/ik 13
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
Usawa wa Kijinsia
Usawa baina ya wanawake na wanaume wa umri wote ni muhimu sana kwa maendeleo endelevu.
Una athari zinazoongeza uwezo wa kutimiza umalizaji wa umaskini na ni muhimu katika
kuchochea maendeleo ya jamii za kidemokrasia kwa misingi ya haki za binadamu, haki ya kijamii
na uendelevu. Aidha, usawa wa kijinsia unachangia katika ongezeko la ustawi, uthabiti na matokeo
mazuri katika nyanja za afya na elimu. Umoja wa Ulaya na nchi Wanachama wake wanatambua
wanawake na wasichana kuwa wahusika wakuu wa kuchochea maendeleo na mabadiliko, ikiwa ni
pamoja na mchango wao katika kudumisha amani na kusuluhisha migogoro na utoaji wa usaidizi
wa kibinadamu.
Hata hivyo, bado kuna wanawake na wasichana wengi wanaozidi kunyimwa haki, rasilimali na
nafasi ya kusikika. Ukosefu wa usawa wa kijinsia una uhusiano na aina zingine za kutojumuishwa.
Kuendeleza ukuzaji wa hadhi ya wanawake na wasichana na usawa wa kijinsia kunahitaji kufanya
kazi na wavulana, wanaume, wasichana na wanawake ili kuelewa haki, usawa, na majukumu katika
jamii. Hii inajumumisha pia kufanya kazi na wadau wakuu katika jamii kama vile waalimu,
viongozi wa dini na wale wa jamii ili kumaliza ubaguzi dhidi ya wasichana na wanawake.
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watahakikisha kuwa mtazamo wa jinsia
umejumuishwa kwa utaratibu katika sera zote kama mchango mkuu wa utimizaji wa Malengo ya
Maendeleo Enedelevu. Watazidisha juhudi zao za kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa
wanawake kwa kukuza zaidi ushirikiano wa wadau mbalimbali, kuimarisha uwezo wa uundaji wa
bajeti inayozingatia masuala ya jinsia, upangaji, na kuhakikisha ushirikishwaji amilifu wa
wanawake na mashirika ya wanawake katika kufanya maamuzi.
SN 3109/17 YML/ik 14
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
35. Utamaduni ni chombo kinachowezesha maendeleo na ni kiungo muhimu cha maendeleo na
unaweza kuwezesha ujumuishwaji wa kijamii, uhuru wa kujieleza, kujenga utambulisho,
uwezeshaji wa raia na uzuiaji wa migogoro huku ukiimarisha ukuaji wa uchumi. Wakisisitiza
kuwa Umoja wa Ulaya unaongozwa na ufikiaji kwa wote, kutogawanyika, uwepo wa
uhusiano na hali ya utegemeano wa haki zote za binadamu, Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama wake wataendeleza mazungumzo ya ushirikiano baina ya tamaduni mbalimbali,
utofauti wa tamaduni na watalinda urithi wa kitamaduni, kutia nguvu viwanda vya bidhaa na
huduma za kitamaduni na ubunifu na wataunga mkono sera za kitamaduni ambapo hizi
zitasaidia kutimiza maendeleo endelevu huku zikizingatia hali za mahali pale.
36. Umoja wa Ulaya na nchi Wanachama wake watachukua hatua ili kupunguza ukosefu wa
usawa wa matokeo na kuendeleza fursa sawa kwa watu wote. Kwa kufanya hivyo, watasaidia
moja kwa mojawatu walio maskini na dhaifu zaidi katika jamii na watasaidia pia kuendeleza
ukuaji ulio jumuishi na endelevu zaidi na ambao hauathiri uwezo wa vizazi vijavyo wa
kukidhi mahitaji yao. Ukuaji wa uchumi hudumu na hunufaisha zaidi walio maskini sana
ikiwa utakuwa jumuishi. Ili kukabiliana na ongezeko la ukosefu wa usawa wa kiuchumi na
kijamii, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataunga mkono mipango ya maendeleo
ya kitaifa inayoleta matokeo na athari zuri zaidi za kijamii. Watafanya kazi pamoja na nchi
washirika ili kuendeleza sera za umma zinazonuia kuongeza kodi inayotozwa kuambatana na
ongezeko la kiasi kinachotozwa na ugavi wa kodi hiyo kwa miradi ya jamii, na zinazozingatia
ugavi wa faida za ukuaji, utengenezaji wa mali na utoaji wa kazi zuri na uboreshaji wa ufikiaji
wa vipengele vya uzalishaji, kama vile ardhi, fedha, na rasilimali watu.
37. Ili kukabiliana na ukosefu wa usawa, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataunga
mkono pia mifumo ya ulinzi wa jamii iliyo bora na endelevu ili kuhakikisha mapato ya
msingi, kuzuia kurudi tena kwenye umaskini uliokidhiri na kujenga ustahimilivu.
Watatathmini mambo yanayoamua uwepo wa, na mitindo ya, ukosefu wa usawa wa kiuchumi
na kijamii na wataimarisha nyenzo na mitazamo yao ili kuifanya bora zaidi katika
kushughulikia ukosefu wa usawa. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watajumuisha
upunguzaji wa ukosefu wa usawa katika ushirikiano wao wa maendeleo na kuunga mkono
mitindo bunifu ya kijamii.
SN 3109/17 YML/ik 15
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
38. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataimarisha uthabiti, hasa kwa watu walio
hatarini, wakati wanapokumbwa na hali za hatari za kimazingira na kiuchumi, majanga asilia
na yale yanayosababishwa na vitendo vya binadamu, migogoro na hatari za ulimwengu wote
kwa afya. Watajumuisha kwa utaratibu ustahilivu katika hatua zao, wakihakikisha kuwa watu
binafsi, jamii, taasisi na nchi zinaweza kujitayarishia vyema, kustahimili, kujirekebisha, na
kupata afueni haraka kufuatia mikazo na mishtuko bila kuathiri uwezekano wa maendeleo ya
kudumu. Hii itafanyika pia katika kipindi cha kuleta afueni baada ya janga kutokea,
urekebishaji na urudishaji wa hali ya kabla ya janga. Ni lazima kudumisha ushirikiano wa
karibu na vitendo vya kukamilishana baina ya wadau wa maendeleo na watoaji msaada kwa
binadamu, unaotegemea uchanganuzi wa pamoja wa hatari na udhaifu.
39. Uhamaji ni swali tata, linalodumu na kuathiri ulimwengu mzima, na hivyo linahitaji
ushughulikiaji kupitia sera iliyoundwa kwa uangalivu, usawa, na inayozingatia ushahidi
ambao utatilia maanani ustadi wa kila taifa, na hasa ambao hautaathiri haki ya Nchi
Wanachama chini ya Kifungu cha 79(5) cha Mkataba wa Utendakazi wa Umoja wa Ulaya
(TFEU) ya kuamua kiasi cha raia wanaokubalika kuhamia Umoja wa Ulaya kutoka katika
mataifa yanayoendelea wakitafutta ajira. Kusimamia vyema uhamaji na utembeaji wa watu
kunaweza kuchangia katika ukuaji jumuishi na maendeleo endelevu. Uhamaji na utembeaji
wa kiwango cha kawaida unaweza kuleta faida kupitia uhamisho wa maarifa, ustadi na uwezo
wa uzalishaji kwa wahamiaji wao wenyewe, familia zao na kwa nchi wanazotoka na zile
wanazoelekea. Wakati huo huo, uhamaji wa kiwango kisicho cha kawaida unaweza kuibua
changamoto na kuleta madhara mabaya kwa nchi wanazotoka wahamiaji, wanazopitia, na
wanazoelekea. Uhamaji umekuwa suala lenye msukumo zaidi kwa nchi zinazoendelea na hata
zile zilizoendelea. Katika hali zingine, watu ambao ni wahamiaji wananyimwa haki zao za
kibinadamu na ufikiaji wa afya na elimu, na wana hatari ya kuwa waathiriwa wa utumwa na
usafirishaji wa binadamu usio halali. Ushirikiano imara utasaidia kuwezesha uhamaji na
utembeaji wa watu ulio salama, wenye mpangilio, na wa kiwango cha kawaida, ikiwa ni
pamoja utekelezaji wa sera za uhamaji zilizopangwa na kusimamiwa vizuri.
SN 3109/17 YML/ik 16
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
40. Kushughulikia uhamaji kuna uhusiano na nyanja zote za sera, ikiwa ni pamoja na maendeleo,
utawala mzuri, usalama, haki za binadamu, ajira, afya, elimu, kilimo, chakula cha kutosha,
ulinzi wa kijamii na mazingira, na vile vile mabadiliko ya hali ya hewa. Kupitia mtazamo wa
Utaratibu wa Ushirikiano, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watashughulikia kwa
utendeti hali mbalimbali za uhamaji na uhamishwaji wa kushurutishwa, ikiwa ni pamoja na
upitishaji na usafirishaji haramu wa binadamu, usimamizi wa mipaka, utumaji pesa kutoka
nchi za nje, utatuzi wa vyanzo vikuu, ulinzi wa kimataifa na urudishwaji wa watu wasiohitaji
ulinzi, kukubali wahamiaji na kuwajumuisha tena katika jamii, kwa msingi wa uwajibikaji wa
pande zote husika na uzingatiaji kamili wa majukumu ya haki na msaada kwa kibinadamu.
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watazingatia mtazamo ulioratibiwa, unaozingatia
masuala yote husika, na wenye muundo zaidi, wakifaidi kutokana na umoja wa nguvu zao na
wakitumia faida inayohitajika kwa kutumia sera, nyenzo na mbinu zote husika za Umoja wa
Ulaya, ikiwa ni pamoja na maendeleo na biashara. Kupitia juhudi hizi zilizoimarishwa, Umoja
wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataunga mkono kwa uamilifu utekelezaji zaidi wa
Mpango pamoja wa Utendaji wa Valleta wa mwaka wa 2015 na ufafanuzi wa Makubaliano ya
Ulimwengu kuhusu Uhamaji na Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa, kama ulivyoitishwa na
Maazimio ya New York ya mwaka wa 2016 ya Wakimbizi na Wahamiaji.
41. Kupitia sera ya maendeleo, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watashughulikia
vyanzo vikuu vya uhamaji wa kiwango kisicho cha kawaida na, pamoja na mengine,
watachangia katika ujumuishwaji endelevu wa wahamiaji katika nchi zinazowapokea na
kusaidia kuhakikisha wahamiaji wanaorudi katika nchi zao za asili au walizopitia
wanafanikiwa kuingiliana na jamii na uchumi wa nchi hizi. Hii itajumuisha kuendeleza
uwekezaji, biashara na ubunifu katika nchi washirika ili kuongeza ukuaji na fursa za
ajiraikiwa ni pamoja na kupitia ushirikiano na watu walio katika mataifa ya kigeni, kusaidia
mifumo ya jamii na uchumi, na vile vile kufanya kazi pamoja na washirika wa sekta ya
kibinafsi na wengineo ili kupunguza gharama ya kutuma pesa kutoka nchi za nje na
kuendeleza utumaji wa pesa kwa haraka, kwa bei nafuu na salama zaidi katika nchi
zinapotoka na zinapopokelewa, na hivyo kufaidi na uwezo wake wa kuleta maendeleo.
SN 3109/17 YML/ik 17
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
Utembeaji na uhamaji
Ajenda ya 2030 inatambua kwa uwazi mchango mzuri wa uhamiaji na utembeaji kwa ukuaji
jumuishi na maendeleo endelevu. Wahamiaji ni viungo wakuu wakuendeleza uchumi wa
ulimwengu, hasa kupitia pesa wanazotuma nchi walizotoka. Kushughulikia uhamiaji katika miundo
yake yote, uwe ni wa kiwango cha kawaida au kisicho cha kawaida, kunahitaji suluhu, sera na
taratibu za kisheria za muda mfupi na za kudumu zinazojumisha sekta mbalimbali, ili kukidhi
mahitaji ya wahamiaji na watu wa nchi walipopokelewa na kuhakikisha usalama wao. Inakubalika
kuwa kuna changamoto nyingi katika nchi zinazoendelea. Kuhusiana na suala hilo, hatua muhimu
ziliafikiwa katika Mkutano wa Valleta uliofanyika Novemba 2015, ambapo mpango wa utendaji
wenye matumaini makubwa ulikubaliwa.
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataongeza juhudi za kushughulikia vyanzo vikuu vya
uhamiaji usio wa kiwango cha kawaida na uhamishwaji wa kulazimishwa, na kuendeleza usimamizi
bora wa uhamaji katika nchi washirika katika miundo yake yote. Wataendelea kujumuisha uhamaji
kama sehemu muhimu ya mazungumzo ya sera ya masuala ya kigeni ya Umoja wa Ulaya, ikiwa ni
pamoja na kupitia ufafanuzi wa ushughulikiaji unaoambatana na hali na ushirikiano ulioimarisha
kwa njia ya uwazi na ya kidemokrasia.
42. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza heshima na ustahimilivu wa watu
walioondolewa makwao kwa muda mrefu na ujumuishwaji wao katika masuala ya kiuchumi
na maisha ya kijamii ya nchi na jamii walipopokelewa, wakitambua kuwa uwezo wa watu
waliohamishwa makwao ni rasilimali yenye muhimu inayoweza kuhamishwa, yenye thamani
kwa ustahimilivu wao na katika kujenga maisha yao tena, na vile vile kama mchango kwa
jamii zilizowapokelea. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watatumia mtazamo
unaozingatia haki, wakitilia maanani kwa karibu wanawake, wato ambao wanaambatana na
wasioambatana na watu wazi, na watu walio hatarini. Watalinda mifumo ya kijamii ya
kudumu, wakijumuisha watu waliohamishwa makwao kwa muda mrefu katika mipango
mipana ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na kupitia ufikiaji wa elimu na kazi zuri.
SN 3109/17 YML/ik 18
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
2.2. Sayari - Kulinda mazingira, kusimamia rasilimali asilia na kukabiliana na
mabadiliko ya hali ya hewa
43. Uzima wa binadamu na jamii zenye ustahimilivu hutegemea mazingira bora na mifumo ya
mazingira inayofanya kazi vizuri. Uharibifu wa mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa, hali
mbaya zaidi za hewa, na majanga asilia au yanayosababishwa na vitendo vya biandamu
yanaweza kurudisha nyuma faida zinazoletwa na maendeleo na ustawi wa uchumi, hasa kwa
watu maskini. Hii inaweza kuongeza hali za udhaifu na mahitaji, na kuhatarisha amani na
uthabiti na kusababisha uhamaji wa kiasi kikubwa. Kando na vitendo vya kujitolea,
uzingatiaji wa mazingira unahitaji kujumuishwa katika sekta zote za ushirikiano wa
maendeleo, ikiwa ni pamoja na kupitia hatua za uzuiaji. Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama wake wataendeleza matumizi mazuri na utumiaji na uzalishaji endelevu,
ikiwemo usimamizi endelevu wa kemikali na uchafu, wakiwa na nia ya kutenganisha ukuaji
wa kiuchumi kutoka kwa uharibifu wa mazingira na kuwezesha kugeuka kuelekea uchumi wa
mzunguko. Sekta ya kibinafsi inayowajibika na kufanyisha kazi kwa utaratibu kwa kanuni ya
“mchafuzi atalipa” pia kutachangia pakubwa kwa ufanisi. Watasaidia kujenga uwezo wa
udumishaji uendelevu wa mazingira, malengo ya mabadiliko ya hali ya hewa na uendelezaji
wa ukuaji unaohifadhi mazingira katika mikakati ya maendeleo ya kitaifa na ya mitaa.
Isitoshe, watatumia vizuri zaidi sayansi, teknolojia na ubunifu ili kuendeleza uendelevu wa
kimazingira, na kuunga mkono washirika wao watumie data na habari za kina zinazopatikana
kupitia mipango ya uangalizi ya Ulaya na ya Dunia ya kimataifa ili kuunga mkono matumizi
yaliyo na msingi wa uthibitisho na yanayotilia maanani hali ya mazingira.
SN 3109/17 YML/ik 19
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
44. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataunga mkono udumishaji na usimamizi
endelevu wa rasilimali zote asili, na udumishaji na matumizi endelevu ya bayoanuwai na
mazingira, ikiwemo misitu, sehemu za pwani, mabonde ya maji ya mto, na mifumo mingine
ya mazingira, ili kutoa huduma za mifumo ya mazingira. Kuambatana na ahadi za kimataifa,
watapambana na ukataji miti haramu na biashara inayohusiana nayo, uharibifu wa ardhi na
vichaka, ueneaji wa jangwa, ukame, na kupotea kwa aina mbalimbali za viumbe.
Wataendeleza faida za pamoja zinazotokana na usimamizi endelevu, ikiwemo kuwezesha
ustahimilivu na uzoeaji wa hali ya hewa. Wataboresha ujumuishwaji wa uendelevu katika
sekta zote za ushirikiano na kuinua hadhi ya masuala ya mazingira katika mazungumzo na
washirika wao. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza matumizi ya
uhasibu wa mali rasilimali asilia. Wataunga mkono utawala bora na ukuzaji wa uwezeshaji
wa usimamizi endelevu wa rasilimali asilia, ikiwemo uzuiaji wa matumizi haramu ya misitu.
Wataendeleza pia ushirikishwaji wa wadau wa eneo husika na uzingatiaji wa haki za wote,
wakiwemo watu wenyeji na jamii za eneo hilo. Watatua uwindaji haramu wa wanyama pori,
biashara haramu ya wanyama pori na mbao, na utumiaji usio halali wa rasilimali zingine
asilia. Ili kuwa na bahari zuri na zenye uzalishaji, wataendeleza ulinzi na urejeshaji wa
mifumo ya mazingira ya baharini kwa hali ya kawaida, usimamizi endelevu wa rasilimali za
baharini na kilimo endelevu cha samaki, ikiwemo kupitia usimamiza bora wa bahari na
uendelezaji wa uchumi wa bidhaa zitokazo kwa maji.
SN 3109/17 YML/ik 20
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
45. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watajumuisha mazingira na mabadiliko ya hali
ya hewa katika mikakati yao yote ya ushirikiano wa maendeleo, ikiwemo kwa kuendeleza
usawa unaofaa baina ya kupunguza athari na uwezo wa kubadilika kulingana na hali.
Watatekeleza Ajenda ya 2030 na Makubaliano ya Paris kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa
kupitia matendo yaliyoratibiwa na yenye ushikamano, na watatumia vyema zaidi umoja wa
nguvu zao. Wataunga mkono mikakati ya kitaifa, ikiwemo upangaji na mipangilio ya
serikali yote, inayoendeleza ustahimilivu, kupunguza hatari ya hali ya hewa na kuchangia
katika kupunguza uchafuzi wa hewa, kuambatana na utekelezaji wa Michango
Inayoamuliwa na Taifa (NDC), wakizingatia changamoto zinazozikumba nchi
zinazoendelea, hasa Nchi Zenye Maendeleo Kidogo Zaidi (LDC) na Nchi Zinazoendelea
ambazo ni Visiwa Vidogo (SIDS). Watachangia katika kuibua watetezi wa hali ya hewa wa
sehemu zile na kusambaza na kuboresha kiukamilifu miradi inayofuata mitindo bora zaidi,
ikiwemo kwa kuunga mkono mipangilio inayowahusisha wadau mbalimbali. Hali ya
Mkataba wa Paris unaobana kisheria na hitaji la kutayarisha Michango Inayoamuliwa na
Taifa (NDC) kunaweza pia kuchochea upangaji wa maendeleo wa kitaifa katika muktadha
wa Ajenda ya 2030.
SN 3109/17 YML/ik 21
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
Nishati endelevu na mabadiliko ya hali ya hewa
Nishati ni kiungo muhimu sana kinachowezesha maendeleo na ni msingi kwa suluhu za sayari
endelevu. Nchi zinazoendelea zinahitaji nishati ili kuendeleza ukuaji jumuishi na na kuboresha
zaidi hali za maisha. Uwekezaji katika nishati endelevu unaweza kuhakikisha na kuongeza
ufikiaji wa maji safi, upishi usiochafua mazingira, elimu na huduma za afya, na unaweza pia
kuleta ajira na kusaidia biashara za eneo lile kwa njia isiyodhuru mazingira.
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza malengo matatu yanayoingiliana:
kutatua ukosefu wa ufikiaji wa nishati; kuongeza matumizi bora ya nishati na uzalishaji wa
nishati inayodumu ili kufikia usawa endelevu baina ya uzalishaji na matumizi ya nishati; na
kuchangia katika juhudi za ulimwengu za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa
kuambatana na Mkataba wa Paris na Michango husika Inayoamuliwa na Taifa (NDC)
iliyowasilishwa na Wanachama. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watapambana na
ukosefu wa nishati kwa kuchangia katika ufikiaji kwa wote wa huduma za nishati ambazo ni za
bei nafuu, za kisasa, zinazoweza kutegemewa na endelevu, wakiangazia zaidi katika nishati
inayodumu na matumizi bora ya nishati. Nishati inayodumu na isiyochafua mazingira inaweza
kutolewa kupitia suluhu zinazoongozwa na jamii, zilizo kando na mifumo ya kawaida ya
usambazaji wa nishati au kutoka kwa mifumo midogo ya usambazaji wa nishati, na hivyo
kuwezesha ufikiaji wa nishati katika sehemu za vijijini.
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza umalizaji wa ruzuku za mafuta
yatokanayo na kaboni na ambayo yana athari mbaya kwa mazingira, masoko ua nishati ambayo
ni thabiti na wazi na utekelezaji wa mifumo ya usambazaji wa nishati ambayo inatumia
teknolojia za kisasa na za kidijitaji ili kusimamia nishati endelevu. Mkakati huu ulioboreshwa
utakuwa sambamba na hatua ya Umoja wa Ulaya inayoambatana na uongozi wake ulimwenguni
wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na kusaidia mataifa yanayoendelea kukabiliana
na mabadiliko ya hali ya hewa na mchakato wa kuanzisha uchumi ulio na uchafuzi mdogo wa
hewa na wenye ustahimilivu wa hali ya hewa.
SN 3109/17 YML/ik 22
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
46. Kiasi cha uwekezaji wa kifedha unaohitajika kuhakikisha watu wote wanafikia huduma za
nishati salama na isiyochafua mazingira kinahitaji ushirikiano na wadau wengi. Umoja wa
Ulaya na Nchi Wanachama wake wataongeza ushirikiano wao na wadau wote husika,
ikiwemo sekta ya kibinafsi, katika usimamizi wa mahitaji ya nishati, matumizi bora ya
nishati, uzalishaji wa nishati ya kudumu na uundaji na uhamishaji wa teknolojia isiyoathiri
mazingira. Wataunga mkono uboreshaji wa taratibu za udhibiti zinazofaa kwa sekta ya nishati
yenye ushindani na iliyo endelevu na kufaidi kutokana na fedha kutoka kwa watu/mashirika
binafsi. Watakusanya fedha za ziada, ikiwemo kutoka kwa sekta ya kibinafsi na kupitia miradi
na nyenzo bunifu za ugharamiaji. Kuunga mkono Afrika na ujirani wa Umoja wa Ulaya
katika haya mabadiliko ya nishati kutakuwa sehemu ya utaratibu wenye uwezeshaji kwa
Muungano wa Nishati wa Umoja wa Ulaya.
2.3. Ustawi - Ukuaji na ajira jumuishi na endelevu
47. Kutoa nafasi za kazi, hasa kwa wanawake na vijana ni muhimu kwa ukuaji jumuishi na
endelevu. Ustawi na ukuaji unaowashirikisha wote unachangia katika maslahi na heshima ya
binadamu. Ukuaji endelevu wenye ujumuishi hujenga ustahimilivu wa kudumu katika nchi
washirika, kwa kutoa fursa za makundi ya watu walio dhaifu na wale walio hatarini zaidi,
kushiriki katika, na kunufaika na, mali na utoaji wa nafasi za ajira zuri. Umoja wa Ulaya na
Nchi Wanachama wake wataendeleza mabadiliko ya kiuchumi yanayotoa nafasi za ajira zuri,
yanayoongeza uwezo wa uzalishaji, na kuzalisha mapato yanayotosha kugharamia huduma za
umma na ulinzi wa jamii, yanayokuza mifumo ya thamani endelevu na uundaji wa bidhaa
na/au utoaji wa huduma tofauti tofauti, ikwemo ujenzi wa viwanda endelevu. Hii ni pamoja
na kuendeleza mitindo endelevu ya matumizi na uzalishaji katika uchumi wa mzunguko,
ikiwemo kuendeleza utumiaji tena wa vitu visivyo na kemikali, matumizi bora ya rasilimali,
na mabadiliko kuelekea utumiaji wa nishati yenye madhara madogo kwa mazingira na
uchumi unaostahimili athari za mabadiliko ya hali ya hewa.
SN 3109/17 YML/ik 23
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
48. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wanatambua jukumu la mashirika madogo zaidi,
madogo kiasi na ya wastani (MSME) kama wawezeshaji wa maendeleo endelevu, na vile vile
kama wadau muhimu katika kukabiliana na umaskini. Mashirika madogo zaidi, madogo kiasi
na ya wastani (MSME) ni wadau wakuu wanaowezesha ukuaji, ajira, ubunifu na maendeleo
ya kijamii. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataunga mkono hatua zinazohusisha
vitendo na zilizo bunifu kupitia sera ya maendeleo ili kuongeza kushiriki kwa mashirika
madogo zaidi, madogo kiasi na ya wastani (MSME) katika kutekeleza hatua halisi uwanjani
na kufungulia uwezo wao wa kuleta maendeleo. Watawezesha ufikiaji wa taarifa muhimu
kwa mashirika madogo zaidi, madogo kiasi na ya wastani (MSME), katika Umoja wa Ulaya
na nchi washirika, na watayajumuisha katika mifumo ya usambazaji na ya thamani, huku
wakishughulikia upungufu wa fedha za ugharamiaji katika mashirika madogo zaidi, madogo
kiasi na ya wastani (MSME). Watahimiza ushirikiano na mazungumzo baina ya biashara
mbalimbali kati ya mashirika madogo zaidi, madogo kiasi na ya wastani (MSME) yaliyo
kwenye Umoja wa Ulaya na katika nchi washirika au maeneo.
Uwekezaji na biashara
Uwekezaji endelevu wa umma na binafsi ni kiungo muhimu kinaoendesha maendeleo endelevu.
Unasaidia kufanya uchumi uwe wa namna mbalimbali, kukuza ukuaji na kuleta nafasi zuri za kazi,
kutengeneza bidhaa na kutoa huduma bunifu, kuunganisha uchumi za nchi na mifumo ya thamani
ya maeneo na ya ulimwengu, kuendeleza ujumuishwaji na biashara ya eneo, na kukidhi mahitaji ya
jamii. Ajenda ya 2030 na Ajenda ya Vitendo ya Addis Ababa hutoa utaratibu ambapo uwekezaji
uliowajibika unaweza kuchangia kwa maendeleo endelevu katika miundo yake yote.
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watachukua hatua ili kuinua uwekezaji kwa kuleta
pamoja ufadhili wa maendeleo endelevu, usaidizi wa kiufundi ili kuendeleza miradi endelevu na
kuvutia wawekezaji, na hatua za kusaidia kuboresha usimamizi wa uchumi na mazingira ya
biashara, kukabiliana na ufisadi na kushirikisha sekta ya kibinafsi. Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama wake watachangia pia kwa kuinua uwekezaji wa binafsi na umma katika uchumi
unaotumia nishati yenye madhara madogo kwa mazingira, na unaostahimili mabadiliko ya hali ya
hewa.
Mbinu moja ya kutimiza hatua hizo itakuwa Mpango wa wa Ulaya wa Uwekezaji katika Nchi za
Nje, ambao utajumuisha hakikisho la kupunguza hali ya hatari za kuwekeza katika nchi
zinazoendelea na hivyo kunufaika kutokana na fedha za zaida, hasa kutoka kwa sekta ya kibinafsi.
Utachangia katika kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu, na hivyo kusaidia kukabiliana na
vyanzo vikuu vya uhamiaji usio wa kiwango cha kawaida.
SN 3109/17 YML/ik 24
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
Kupitia sera yake ya biashara, Umoja wa Ulaya pia utaendelea kuhakikisha kwamba nchi
zinazoendelea, hasa zile zilizo dhaifu sana, zinapata faida za ukuaji jumuishi na maendeleo
endelevu kutokana na ushirikishwaji ulioboreshwa katika ushirikiano wa eneo na katika mfumo wa
biashara baina ya nchi mbalimbali.
49. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watasaidia kukuza mazingira yanayofaa kwa
biashara katika nchi zinazoendelea, yanayozingatia viwango na kanuni za kimataifa za haki za
binadamu. Watachangia katika kuboresha hali za shughuli jumuishi za uchumi kwa
keundeleza sera na taratibu za udhibiti zilizo endelevu zaidi, haki za biandamu, vikiwemo
viwango vikuu vya kazi na mahitaji ya ukaguzi, mazingira yanayofaa zaidi kwa biashara,
mifumo mipya ya biashara na uwezo mkubwa zaidi wa serikali. Wataendeleza ufikiaji mpana
wa huduma za kifedha na za mikopo midogo, ikiwemo kwa wanawake, maskini na kwa
mashirika ya biashara yaliyo madogo sana, madogo kiasi na ya wastani (MSME).
Wataendeleza pia miradi ya sekta ya kibinafsi na mashirika ya jamii, miungano ya mashirika,
wajasiriamali wanawake na vijana, ili kuinua utoaji wa huduma kwa eneo husika na vile vile
mifumo ya biashara iliyo jumuishi na isiyodhuru mazingira. Wataendeleza ununuzi enedelevu
na wazi wa bidhaa na huduma na serikali ili kuunga mkono maendeleo endelevu na
kuwezesha ufikiaji wa mashirika ya biashara yaliyo madogo sana, madogo kiasi na ya wastani
(MSME) wa fedha za serikali za kununua bidhaa na huduma kutoka kwa sekta ya kibinafsi.
Uwekezaji wa sekta ya umma katika utafiti na ubunifu na ushirikiano katika sayansi na
teknolojia unaweza pia kuwa ufunguo wa uwekezaji wa sekta ya kibinafsi na kusaidia
kuendesha ukuaji endelevu na jumuishi katika nchi zinazoendelea.
50. Fedha chafu, ufisadi, utumaji na upokeaji haramu wa pesa, na ukwepaji na uepukaji wa kulipa
kodi yote yanazidi kurudisha nyuma maendeleo endelevu, huku yakiathiri sana hasa nchi
zinazoendelea. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watafanya kazi pamoja na nchi
washirika ili kuendeleza utozaji ushuru unaoongezeka kulingana na kiwango cha mapato,
hatua za kupambana na ufisadi na sera za ugavi wa mapato ya nchi kwa miradi inayofaidi
umma, na kukabiliana na utumaji na upokeaji haramu wa pesa ili kuendeleza ufikiaji wa
huduma bora za msingi kwa watu wote.
51. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataleta pamoja ustadi na rasilimali za sekta ya
kibinafsi na Msaada wa Biashara, sera na nyenzo za biashara, na diplomasia ya kiuchumi
zenye kuunga mkono maendeleo. Wataendeleza Msaada wa Biashara ili kuunga mkono
utekelezaji wa Ajenda ya 2030 na kushughulikia vyema mahitaji ya biashara na uwezo wa
SN 3109/17 YML/ik 25
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
uzalishaji wa nchi zinazoendelea. Mahitaji ya nchi zenye maendeleo madogo zaidi (LDC) na
nchi zinazoendelea zisizokuwa na bandari (LLDC), ambazo uwezeshaji wa biashara na
miundo msingi ya biashara ni mambo muhimu yanaoendesha maendeleo, na Nchi
Zinazoendelea ambazo ni Visiwa Vidogo (SIDS), zinafaa kutiliwa maanani.
52. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza na kuwezesha biashara na
uwekezaji katika nchi zinazoendelea ili kuunga mkono maendeleo endelevu. Umoja wa Ulaya
utazidi kuendeleza biashara na ushirikiano wa maeneo kama viendeshaji vikuu vya ukuaji na
upunguzaji wa umaskini katika nchi zinazoendelea. Kupitia utekelezaji wa mkakati wa
“Biashara kwa Wote”, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataunga mkono
washirika wao wa biashara, ikiwemo kupitia makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi, ili
kujumuisha maendeleo endelevu katika viwango vyote vya sera ya biashara. Kuambatana
ahadi za makubaliano ya Ushikamano wa Sera kwa ajili ya Maendeleo (PCD), usaidizi wa
maendeleo utatumika pale unapofaa ili kuhakikisha kwamba masharti yaliyoko kwenye
mikataba ya biashara yanayohusiana na biashara na maendeleo endelevu yanatekelezwa na
kutumika ipasavyo. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watendeleza ukuaji endelevu
wa uchumi na kusaidia nchi zinazoendelea kuanza kutumia mifumo ya ukuaji inayozingatia
uhaba wa rasilimali na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Hii ni pamoja na
maendeleo uendelevu katika mifumo ya thamani na viwango vya mazingira na jamii.
53. Sekta ya kibinafsi inaweza kuchangia katika utekelezaji wa Ajenda ya 2030. Umoja wa Ulaya
na Nchi Wanachama wake, kwa uratibu wa karibu na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya,
wataendeleza ukusanyaji wa rasilimali binafsi kwa ajili ya maendeleo, huku wakiendeleza
uwajibikaji katika sekta ya kibinafsi, katika nyanja zenye uwezo mkubwa wa mabadiliko ya
maendeleo endelevu. Hii ni pamoja na kilimo endelevu, nishati salama na isiyo na madhara
kwa mazingira, usimamizi jumuishi wa wa rasilimali za maji, miundo msingi thabiti, afya,
utalii endelevu, uchumi usioathiri mazingira na wa mzunguko, mawasiliano na teknolojia ya
kidijitali.
SN 3109/17 YML/ik 26
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
54. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watafanya kazi na sekta ya kibinafsi, yakiwemo
mashirika ya waajiri na wafanyakazi, ili kuendeleza mitazamo yenye uwajibikaji, endelevu na
bora, ikiwemo kupitia mazungumzo katika kijamii. Utumiaji wa kiwango cha juu cha mifumo
na mitindo ya biashara yenye uwajibikaji na ujumuishwaji kwa kampuni tofauti za Umoja wa
Ulaya zenye mifumo ya usambazaji katika nchi zinazoendelea, kwa ushirikiano wa karibu na
wadau wa umma na binafsi, na kuendeleza biashara yenye usawa, uwazi na inayozingatia
maadili, ikiwa ni pamoja na wazalishaji wadogo katika nchi zinazoendelea, unaweza
kuchangia pakubwa katika utekelezaji wa Ajenda ya 2030. Viwango na wajibu wa haki za
binadamu unaokubalika kimataifa kuhusu maendeleo endelevu, uwazi, na uwajibikaji wa
mashirika kwa jamii vinahitaji kujumuishwa katika mifumo ya biashara, ikiwemo kwa
ushirikiano na mchanganyiko wa sekta za umma na binafsi, kupitia mbinu tofauti, kama vile
kushiriki mitindo bora zaidi. Hii ni pamoja na kuhakikisha usimamizi na matumizi endelevu
ya rasilimali asilia kama vile madini na mbao. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
watazidi kuunga mkono mitindo ya biashara yenye uwajibikaji na usimamizi wa mifumo ya
usambazaji unaowajibika, kuheshimu haki za muda wa ajira na kuunganisha haki za
binadamu na za kazi, uadilifu katika masuala ya fedha na viwango vya mazingira na ufikiaji.
Watafanya kazi ili kuzuia ukiukaji wa haki za binadamu na kuendeleza Kanuni za Umoja wa
Mataifa Zinazoongoza Biashara na Haki za Binadamu. Wataendeleza viwango vya kazi
ambavyo vinahakikisha hali zuri za kufanyia kazi na mishahara bora kwa wafanyakazi, hasa
vile vinavyopeanwa na Shirika la Wafanyakazi Ulimwenguni, katika sekta rasmi na isiyo
rasmi, ikiwemo kwa kuunga mkono mabadiliko kutoka kwa uchumi usio rasmi kuelekea ulio
rasmi na kwa kukabiliana na ajira ya watoto.
SN 3109/17 YML/ik 27
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
55. Kilimo endelevu, pamoja na uvuvi na kilimo cha samaki endelevu, kinaendelea kuwa
kiendeshaji kikuu cha umalizaji wa umaskini na maendeleo endelevu na ni muhimu kwa
kumaliza njaa na kuhakikisha uwepo wa chakula cha kutosha. Thuluthi mbili za watu walio
maskini ulimwenguni kote hutegemea kilimo ili kujikimu kimaisha na nchi kadhaa
zinazoendelea zinasalia kutegemea sana biashara ya bidhaa chache. Usaidizi kwa wakulima
wadogo wadogo, wakiwemo wakulima wa familia na wachugaji mifugo, unaendelea kuwa
wenye umuhimu mkubwa, na unachangia katika kuhakikisha kuna chakula cha kutosha na
katika kupambana na mmomonyoko wa udongo na kupotea kwa bayoanuwai, huku ukitoa
ajira. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataunga mkono uboreshaji wa utawala
unaohusiana na usimamizi endelevu wa misitu, usimamizi wa sehemu za malisho ya mifugo
wenye ushirikishwaji, ufikiaji sawa wa uwezo wa kumiliki ardhi, hasa kwa wanawake,
kuzingatia haki za watu wanaoishi sehemu husika na za watu wenyeji wa sehemu hiyo,
ikiwemo matumizi ya ardhi kwa njia za kitamaduni na ufikiaji wa maji. Wataendeleza
uundaji wa mashirika na vyama vya ushirika vya wakulima ili kushughulikia, pamoja na
mambo mengine, uzalishaji bora wa mashamba ya familia, haki za matumizi ya ardhi mifumo
ya mbegu za wakulima ya zamani. Watachangia katika kuongeza ubora wa hali za usafi wa
mwili na wa mazao ya miti. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watalenga
kuendeleza masoko ya kilimo na mifumo ya thamani katika nchi washirika ambayo inafaidi
maskini na kuhimiza viwanda vya kilimo kutoa ajira na thamani inayoongezewa. Hii
itajumuisha kuunga mkono ujumuishwaji wa vijana na uwezeshaji wa wanawake, na
kuendeleza utafiti na ubunifu. Uwekezaji katika kilimo endelevu na katika sekta ya kilimo cha
chakula vinahitajika ili kuleta mifumo tofauti tofauti ya uzalishaji wa sehemu na eneo husika,
kuzuia utapiamlo, kuleta ongezeko la uzalishaji na kutoa nafasi za kazi zuri, bila kuathiri
mazingira. Kuna haja ya uwekezaji mwingi wa sekta ya umma na binafsi katika kilimo
endelevu kwa nchi nyingi zinazoendelea, hasa barani Afrika. Uwekezaji na madailiko haya
sera lazima yawe na uwajibikaji na ujumuishwaji, na yawafaidi watu wanaoishi katika
sehemu husika.
SN 3109/17 YML/ik 28
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
56. Itabidi mifumo endelevu ya kilimo na chakula, ikiwemo uvuvi endelevu, itatue mahitaji ya
idadi inayoongezeka ya watu ulimwenguni huku ikilinda mazingira. Umoja wa Ulaya na nchi
Wanachama wake wataunga mkono mitindo na vitendo vya ukulima unaotilia maanani
michakato ya mazingira na viumbe ili kupunguza hasara ya kupoteza chakula baada ya
kuvuna na uharibifu wa chakula, na vile vile kulinda udongo, kuhifadhi rasilimali za maji,
kusimamisha na kuzuia ukataji miti, kupanda miti tena ili kukuza misitu, na kudumisha
bayoanuwai na mazingira bora. Uwezo wa kilimo endelevu na udongo wa kupunguza utoaji
wa gesi zinazosababisha ongezeko la kiwango cha joto duniani ni lazima utumiwe, na
ustahimilivu wa athari za mabadiliko ya hali ya hewa unapaswa kuboreshwa. Umoja wa
Ulaya na Nchi Wanachama wake watendeleza uvuvi endelevu na mitindo ya kilimo cha
samaki, na kuunga mkono hatua za kukabiliana na uvuvi haramu, uchafuzi wa bahari na athari
za mabadiliko ya hali ya hewa.
57. Umoja wa Ulaya na nchi Wanachama wake watazidi kuunga mkono teknolojia za habari na
mawasiliano katika nchi zinazoendelea kama viungo vikuu vya kuwezesha ukuaji jumuishi na
maendeleo endelevu. Teknolojia za kidijitali zinatumika katika nchi zinazoendelea kwa
kiwango cha juu mno. Hata hivyo, ukosefu wa uunganisho unaendelea kuwa kikwazo kikuu
cha maendeleo katika nyingi ya nchi zinazoendelea, hasa kwenye sehemu za vijijini na zile
zilizo mbali sana, hususan barani Afrika. Aidha, ukosefu wa ushindani mara nyingi unaweza
kufanya teknolojia za kidijitali kuwa ghali na vigumu kupatikana kwa watu wengi. Umoja wa
Ulaya na Nchi Wanachama wake watafanya kazi ili kujumuisha suluhu za kidijitali katika
maendeleo na kuendeleza matumizi ya teknolojia za kidijitali katika nyanja tofauti muhimu
(kama vile utawala kwa mifumo kielektroniki, kilimo, elimu, usimamizi wa maji, afya, na
kawi). Wataunga mkono mazingira yanayowezesha uchumi wa kidijitali kwa kuboresha
uunganisho wa bure, wazi, na salama, na kuondoa vikwazo ili kudhihirisha uwezo wake
kamili wa kuleta maendeleo endelevu. Wataunga mkono ujasiriamali wa kidijitali, yakiwemo
mashirika madogo sana, madogo kiasi na ya wastani ya biashara (MSME), ili kuendeleza
maudhui yanayofaa kwa sehemu husika na kuendeleza ubunifu na utoaji wa nafasi za kazi
zuri. Wataunga mkono ufahamu na ustadi wa teknolojia ya dijitali ili kuwezesha watu, hasa
wanawake na watu walio kwenye sehemu za hatari na zilizotengwa, kuendeleza ujumuishwaji
kwa jamii na kuwezesha kushiriki katika utawala wa kidemokrasia na uchumi wa kidijitali.
SN 3109/17 YML/ik 29
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
58. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataunga mkono usanifu, ujenzi na uendeshaji
wa miundo msingi na mijengo bora ambayo inatumia vizuri rasilimali na nishati. Wataunga
mkono uundaji wa mitandao ya usafirishaji na uchukuzi, iliyo endelevu, yenye uchafuzi
mdogo kwa mazingira, na yenye uunganishi na miundo misingi ingine thabiti na isiyodhuru
mazingira, kama vile mitandao ya kawi, mifumo ya maji na mifumo ya kusimamia takataka,
ili kuendeleza ufikiaji sawa na wa bei nafuu kwa watu wote, ukuaji, biashara na uwekezaji.
Watajumuisha kwa utaratibu malengo ya kupunguza utoaji wa gesi zinazoongeza kiwango
cha joto katika miradi ya miundo msingi.
59. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wanasisitiza haja ya uzingatiaji kamili wa viwango
vya kimataifa vya mazingira na usalama wa nyuklia katika nchi washirika.
60. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watafanya juhudi za kuinua uwezo wa miji kama
vitovu vya ukuaji na ubunifu endelevu na jumuishi, wakizingatia jamii zao pana zilizo vijijini
na maendeleo ya eneo yenye usawa. Wataendeleza maendeleo ya miji jumuishi na endelevu
ili kukabilifu na ukosefu wa usawa, wakiangazia wale wenye mahitaji zaidi, wakiwemo watu
wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda na vitongoji duni. Wataunga mkono washirika ili
kuboresha utoaji wa huduma msingi na ufikiaji sawa wa chakula cha kutosha na makazi
mazuri, ya bei nafuu, na yanayopatikana, na kuboresha hali ya maisha ya idadi ya watu
inayoongezeka na ambayo inaishi kwenye miji. Kuambatana na Ajenda ya Miji Mpya ya
Umoja wa Mataifa, wataendeleza upangaji wa matumizi endelevu ya ardhi, usimamizi sawa
wa masoko ya ardhi, usafirishaji endelevu kwenye miji na miji salama, ya kisasa inayotumia
fursa za teknolojia za kidijitali. Watendeleza sera za maeneo na miji zilizo jumuishi, zenye
usawa, na ujumuishwaji, na uratibu wa viwango mbalimbali vya serikali, wakikuza uhusiano
imara baina ya sehemu za vijijini na mijini. Watajenga ustahimilivu wa miji kwa misukosuko
na kutumia fursa za uchumi wenye madhara madogo kwa mazingira na unaostahimili
mabadiliko ya hali ya hewa.
SN 3109/17 YML/ik 30
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
2.4. Amani – jamii zenye amani na jumuishi, demokrasia, taasisi bora na zenye
uwajibikaji, utawala wa sheria na haki za kibinadamu kwa wote
61. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza maadili ya demokrasia ya watu
wote, utawala bora, utawala wa sheria na haki za kibinadamu kwa wote, kwa sababu ni
masharti yanayopaswa kutimizwa ili kuwepo na maendeleo endelevu na uthabiti, katika
viwango mbalimbali vya ushirikiano na vya nyenzo katika hali na nchi zote, ikiwemo kupitia
hatua ya maendeleo. Wataunga mkono juhudi za ndani ya nchi, zinazoafikiana na mahitaji na
muktadha wa kila jamii ili kujenga nchi za kidemkorasia, zinazoweza kustahimili athari za
misukosuko ya nje na ya ndani ya nchi na kushughulikia sababu zinazoendesha udhaifu wa
jamii, ikiwemo ukosefu wa usawa.
Utawala mzuri, demokrasia, utawala wa sheria na haki za biandamu
Utawala mzuri, demokrasia, utawala wa sheria ni muhimu kwa maendeleo endelevu. Utawala wa
sheria unahitajika ili kulinda haki zote za kimsingi. Taasisi na mifumo bora ya utawala na ambayo
inashughulikia mahitaji ya umma hutoa huduma muhimu na huendeleza ukuaji jumuishi, huku
michakato ya kisiasa ikihakikisha kuwa raia wanaweza kuwataka maofisa wa umma wawajibike
katika viwango vyote.
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza taasisi zinazowajibika na wazi,
zikiwemo bunge za taifa, na kukuza ushirikishwaji katika kufanya maamuzi na ufikiaji wa taarifa
kwa umma. Wataendeleza mahakama huru na zisizoegemea upande wowote, na kuunga mkono
utoaji wa haki yenye usawa, ikiwemo ufikiaji wa usaidizi wa kisheria. Wataunga mkono uwezeshaji
wa taasisi thabiti na utawala wa viwango mbalimbali, kwa kushirikisha watu walio kwenye hali za
udhaifu na wale wa makundi madogo katika jamii kupitia ushirikiano baina ya serikali za kitaifa,
serikali ndogo za kitaifa, na zile za mitaa na kwa kutumia uwezo wa suluhu za kidijitali. Wataunga
mkono miradi ya kukabiliana na ufisadi na kuleta uwazi na uwajibikaji zaidi katika ufadhili
unaotokana na fedha za umma na katika utoaji wa huduma za umma.
SN 3109/17 YML/ik 31
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
62. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataunga mkono nafasi wazi na yenye
uwezeshaji kwa asasi za kijamii, mitazamo jumuishi na uwazi katika kufanya maamuzi katika
viwango vyote. Watazidi kuunga mkono chaguzi jumuishi, wazi, na za kuaminika kwa kutoa
usaidizi kwa muda unaofaa katika wakati wote wa mzunguko wa uchaguzi, na vile vile
kuendeleza vyama vya kisiasa vya kidemokrasia na vinavyowajibika na ushirikishwaji amilifu
wa raia katika mchakato wote wa uchaguzi. Ujumbe Huru wa Uangalizi wa Uchaguzi wa
Umoja wa Ulaya ni mbinu muhimu ya kuafikia lengo hili. Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama wake wataunga mkono na kuendeleza utawala wa kidemokrasia unaohakikisha
uhuru wa mambo muhimu unadumishwa, kama vile uhuru wa kuwa na dhana, wa dini au
imani, uhuru wa kukusanyika na kushirikiana, ikiwemo kwa watu wa makundi yaliyotengwa,
na ambao unazingatia haki za binadamu za watu wote, haijalishi kama ni za kiraia, kisiasa,
kiuchumi, kijamii au kiutamaduni. Watatetea uhuru wa kujieleza na wa kuwa na maoni na
kutoa usaidizi kwa vyombo vya habari vilivyo huru na vyenye kuheshimu maoni ya watu
tofauti na vinavyotoa habari bora kulingana na ukweli na data.
63. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watakuza mifumo ya mahakama iliyo bora, wazi,
huru, na inayaowajibika na kuendeleza ufikiaji wa haki kwa wote - hasa maskini na watu
walio hatarini. Hii inajumuisha juhudi za kukabiliana na uhalifu, ukiwemo uhalifu na vurugu
mijini, na juhudi za kupambana na makundi ya uhalifu yanayotoka mataifa mbalimbali
yanayohusiana na uuzaji na usafirishaji haramu wa silaha, madawa ya kulevya na binadamu.
64. Umaskini, migogoro, udhaifu na uhamishwaji wa lazima zina uhusiano mkubwa na ni lazima
pia zishughulikiwe kwa utendeti na kwa ushikamano kama sehemu ya uunganisho baina ya
msaada wa kibinadamu na maendeleo. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
watashughulikia vyanzo vyao vikuu katika viwango vyote, ikwemo kutengwa, ukosefu wa
usawa, ukosefu wa chakula cha kutosha, ukiukaji wa haki za binadamu na dhuluma, uepukaji
wa adhabu na ukosefu wa utawala wa sheria, ukiwemo pia uharibifu wa mazingira na
mabadiliko ya hali ya hewa.
SN 3109/17 YML/ik 32
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
65. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watatumia ushirikiano wa maendeleo kama
sehemu ya sera na nyenzo mbalimbali za kuzuia, kusimamia na kusaidia kutatua migogoro na
hali za hatari, kuepukana na mahitaji ya kibinadamu na kuleta amani ya kudumu na utawala
bora. Ushirikiano wa maendeleo unaangazia sana umalizaji wa aina zote za umaskini, na
juhudi zote zitaelekezwa katikakutimiza lengo hilo. Wataendeleza mfumo pana wa kutatua
migogoro na hali za hatari kupitia matumizi bora ya mikakati ya mpwito na ya mfumo wa
kutoa tahadhari ya mapema wa Umoja wa Ulaya, wakiangazia udhaifu, usalama wa binadamu
na kutambua uunganisho uliopo baina ya maendeleo endelevu, hatua ya msaada wa
kibinadamu, amani na usalama.
66. Udumishaji wa amani na ujenzi wa nchi ni muhimu kwa maendeleo endelevu na vinafaa
kufanyika katika viwango vyote, kuanzia ulimwengu mzima hadi kwa eneo husika, na katika
hatua zote za mchakato wa mgogoro, kuanzia tahadhari ya mapema na uzuiaji hadi kwa
kushughulikia hatari na kuleta hali ya utulivu. Katika muktadha wa ushirkiano wa maendeleo,
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wanaweza pia kushirikiana na sekta ya kibinafsi
ili kuzipa uwezo wa kuhakikisha uafikiaji wa malengo ya maendeleo endelevu, hasa utimizaji
wa jamii jumuishi na zenye amani. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza
suluhu za wote kwa changamoto za usalama na maendeleo, ikiwemo kupitia kuunga mkono
utawala wa kidemokrasia wa sekta ya kibinafsi, ufanisi wake katika kutoa usalama kwa
binadamu, na kukuza uwezeshaji. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wanatambua
haja ya kuzuia na kupambana na uenezaji wa itikadi kali za kidini unaosababisha vitendo
vibaya vya dhuluma, ikiwemo kupitia kukuza maelewano na majadiliano baina ya dini
mbalimbali. Wataendelea kuunga mkono kanuni ya wajibu wa kulinda na uzuiaji wa vitendo
vya ukatili. Katika muktadha huu, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watendelea
kukuza ushirikiano wao na Umoja wa Mataifa na washirika wa kitaifa na wa kanda.
67. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watachangia kwa Mabadiliko ya Sekta ya Ulinzi,
ambayo yanaweza kuchangia kuleta udhibiti bora wa kidemokrasia na uwajibikaji, uboreshaji
wa usalama wa binadamu, maendeleo endelevu na umalizaji wa umaskini. Mabadiliko ya
sekta ya ulinzi ni lazima yaambatane na mahitaji ya nchi washirika na izingatie umiliki wa
kitaifa ulio wazi na unaodumu.
SN 3109/17 YML/ik 33
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
68. Nchi zilizo kwenye hali za udhaifu au zinazoathiriwa na migogoro zinahitaji kushughulikiwa
kwa makini na kuendeleza ushirikiano wa kimataifa ili kufikia maendeleo endelevu. Malengo
ya kudumisha amani na kujenga nchi ni muhimu ili kukuza uwezo wa nchi wa kuunganisha
kikamilifu masuala ya kiuchumi, kijamii na kimazingira na yale ya usalama ma maendeleo.
Katika usaidizi wao wa kimaendeleo, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
watazingatia hasa nchi zilizo dhaifu na zinazoathiriwa na migogoro na watasaidia wale walio
wadhaifu zaidi. Kwa kuendeleza na kulinda haki za binadamu, demokrasia, utawala wa
kisheria na utawala bora, watajituma ili kuchangia katika uthabiti na usalama na vile vile
katika ustahimilivu. Watajumuisha ufahamu wa masuala ya migogoro katika kazi zao zote, ili
kuwe na matokeo mengi na mazuri katika juhudi za kuleta amani. Wataendeleza uwazi,
uwajibikai na ufikiaji wa haki, kwa kuwashirikisha wadau wote katika michakato ya uzuiaji
wa migogoro, udumishaji na upatikanaji wa amani. Wataunga mkono haki ya mpwito kupitia
hatua zinazohusiana na muktadha husika na ambazo zinaendeleza ukweli, haki, fidia na
uhakikisho wa kutotokea tena. Uimarishaji unahitaji kuziba pengo lililopo kati ya usuluhishaji
wa mgogoro na michakato ya kudumu ya mabadiliko, na kukuza uaminifu baina ya serikali na
raia, ikiwemo kupitia kuboresha utoaji wa huduma. Katika muktadha huu, Umoja wa Ulaya
na Nchi Wanachama wake wataimarisha ushirikiano na washirika wa kanda wanaostahili.
Ufanisi wa juhudi za uingiliaji kati zinazohusiana na amani na ulinzi hutegemea hasa
ushirikiano na wadau wa eneo husika na umiliki wao wa mchakato huo. Kujifunza kutokana
na nchi zingine zenye udhaifu na zinazokumbwa na migogoro pia kunaweza kusaidia. Umoja
wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watashughulikia mambo yote yanayohusiana na uzuiaji
na utatuaji wa dhuluma ya kimapenzi na yenye msingi wa kijinsia wakati wa migogoro na
baada ya migogoro kutokea, usuluhishaji wa migogoro, kuleta afueni na utulivu, na kukuza
amani inayodumu.
SN 3109/17 YML/ik 34
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
69. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watatekeleza hatua ya usaidizi wa kibinadamu na
ushirikiano katika maendeleo kwa njia yenye ushikamano na kukamilishana zaidi,
wakichangia kwa uamilifu katika kujenga ustahimilivu wa watu binafsi, jumuiya, jamii na
nchi, wakishughulikia umaskini uliokidhiri, kuzuia na kukabiliana na hali za hatari,
wakipunguza udhaifu wa kila wakati na kujenga uwezo wa kujitegemea. Suluhu za kudumu
zinahitaji mitazamo inayowashirikisha wadau mbalimbali, uingiliaji kati katika viwango
tofauti na dira ya muda mrefu. Hii inamaanisha kuimarisha uhusiano baina ya utoaji wa
msaada wa kutuliza, na wa kurekebisha na maendeleo, ikiwemo kupitia ubadilishanaji mpana
wa taarifa, uratibu wa wafadhili na uchanganuzi wa pamoja wa mapengo, hatari na udhaifu,
na dira ya pamoja ya mikakati ya kupewa kipaumbele, mapema iwezekanavyo. Umoja wa
Ulaya na Nchi Wanachama wake watahakikisha uhusishwaji wa mapema na ushirikiano wa
karibu baina ya wadau wa kisiasa na wa maendeleo kuanzia mwanzo hadi tamati na kufuata
juhudi za uingiliaji kati za wadau wanaotoa msaada wa kibinadamu wakati wa dharura na
wanaoleta afueni ya mapema majanga yanapotokea. Hii itafanyika kwa njia ambayo
inadumisha kanuni za msaada kwa binadamu kulingana na sheria ya kimataifa ya msaada kwa
binadamu.
70. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataongeza juhudi zao za kukuza ustahimilivu
na uwezo wa kujirekebisha kulingana na mabadilika, kuambatana na, pamoja na mengine,
Utaratibu wa Sendai wa Upunguzaji wa Hatari za Janga wa 2015-2030 na Mkataba wa Paris
kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa. Kusaidia watu na jamii ili wawe wamejitarisha vilivyo,
kupunguza uwezekano wao wa kukumbwa na hatari na udhaifu, na kuimarisha uthabiti wa
kustahimili na kurudia hali ya kawaida baada ya mishtuko na majanga ni muhimu katika
kupunguza madhara zaidi na kuepuka kupoteza maisha na riziki. Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama watajumuisha utathmini wa hatari na uchanganuzi wa pengo katika programu
zao za ushirikiano wa mendeleo. Wataendelea pia kukuza uwezo wa kujitayarisha kwa hatari
kwa afya zinazoweza kutokea kati ya mipaka mbalimbali, kulingana na Kanuni za Kimataifa
za Afya, hasa kupitia kutoa uwezeshaji wa mifumo ya afya ya kitaifa na ya kanda na
uboreshaji wa kushiriki taarifa. Wakijifunza kutokana na hali za hatari za afya ya ulimwengu,
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watazidi kuendeleza miradi inayoshirikisha sekta
mablimbali katika viwango vya kimataifa, kanda, na vya eneo husika na watafanya
uimarishaji wa mifumo ya afya ya kiwango kimoja kuwa msingi wa mipangilio ya maendeleo
ya sekta ya afya.
SN 3109/17 YML/ik 35
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
71. Uhamaji, maendeleo endelevu na uthabiti yana uhusiano mkubwa. Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama wake wamejitolea kuratibu hatua za kushughulikia vyanzo vikuu vya uhamiaji
usio wa kawaida na uhamishwaji wa kulazimishwa, kama vile migogoro, udhaifu wa nchi,
ukosefu wa usalama na kutengwa, umaskini, ukosefu wa chakula cha kutosha, ukosefu wa
usawa na ubaguzi, uharibifu wa mazingira, ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa.
Wataendeleza haki za binadamu na heshima ya watu, ujenzi wa demokrasia, utawala bora na
utawala wa sheria, ujumuishwaji kwa jamii na utangamano, fursa za kiuchumi zenye kazi zuri
na kupitia biashara zinazozingatia watu, na nafasi ya sera za asasi za jamii. Watakabiliana na
usafirishaji usio halali wa wahamiaji na biashara haramu ya kusafirisha watu, ambavyo
ndivyo vyanzo vya ukosefu wa uthabiti. Ni muhimu kukukuza ushirikiano imara na nchi
ambazo wahamiaji hutoka, kupitia, na kuelekea, kwa kutumia sera za kudumu na za muda
mrefu zinazoshughulikia hali mbalimbali za changamoto hii.
3 USHIRIKIANO – UMOJA WA ULAYA KAMA NGUZO YA UTEKELEZAJI
WA AJENDA YA 2030
72. Huku ikitambua kwamba kila nchi ina wajibu mkuu wa maendeleo yake ya kiuchumi na
kijamii, Ajenda ya 2030 ni lazima itekelezwe na nchi zote na wadau wote kwa ushirikiano.
Tasnia ya maendeleo inazidi kupanuka, na kuwajumuisha wadau wengi zaidi na wapya.
Bunge, vyama vya kisiasa, mamlaka za maeneo na mitaa, taasisi za uchunguzi, mashirika ya
kutoa msaada, vyama vya ushirika, sekta ya kibinafsi na asasi za jamii waote wamekuwa
washirika wakuu katika kuwafikia watu walio dhaifu na waliotengwa zaidi. Uendelezaji na
ulinzi wa nafasi ambapo wadau hawa wanaweza kufanya kazi kwa usalama ni muhimu ili
kufikia maendeleo endelevu.
SN 3109/17 YML/ik 36
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
3.1. Kufanya kazi vyema zaidi kwa kushirikiana
73. Ili kushughulikia changamoto za ulimwengu, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
wataboresha zaidi jinsi wanavyoshirikiana, ikiwemo kwa kufanya kazi vyema zaidi kwa
pamoja, wakizingatia faida zinazotokana na uwezo wa kila mwanachama. Hii ni pamoja na
kuboresha ufanisi na matokeo mazuri kupitia uratibu na utangamano zaidi, kwa kutumia
kanuni za ufanisi wa maendeleo na kwa kufanikisha ushirikiano katika maendeleo kama
sehemu moja ya hatua ya jumla ya ndani na nje ya nchi ya kuendeleza utekelezaji wa Ajenda
ya 2030. Ili kufanikiwa zaidi katika kuendeleza malengo haya, na kuambatana na azimio kuu
la kumaliza umaskini, sera ya maendeleo ya Umoja wa Ulaya inapaswa kuwa na uwezo wa
kubadilika na iwe inayoweza kushughulikia mahitaji, hali za hatari na masuala muhimu
yanayobadilika kila siku.
74. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataratibu na kuendeleza misimamo ya pamoja
kuhusu masuala yanayohusiana na sera ya maendeleo katika viwango vya kimataifa. Hii
itaboresha jumla ya ushawishi wa Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake na itachangia
katika majadiliano yenye ufanisi baina ya nchi mbalimbali.
75. Katika kiwango cha nchi, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wataboresha Mipangilio ya
Pamoja katika ushirikiano katika maendeleo ili kuongeza matokeo yao ya jumla kwa kuleta
pamoja rasilimali na uwezo wao. Mipangilio ya Pamoja inapaswa kuendelezwa na
kuimarishwa, na kuwa ya kujitolea kwa hiari, iwe inayoweza kubadilika kwa urahisi, yenye
jumuishi, na inayozingatia muktadha wa nchi, na vile vile inayotoa nafasi ya kubadilisha hati
za mipangilio za Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama na mahali pake kuchukuliwa na hati
za Mipangilio ya Pamoja za Umoja wa Ulaya. Ushirikiano wa nchi washirika,ugavi na umiliki
ni muhimu kwa mchakato huu. Mipangilio ya Pamoja ni lazima iongozwe na mkakati wa
maendeleo wa nchi mshirika na iambatane na vipaumbele vya maendeleo vya nchi mshirika.
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama watafanya kazi pamoja ili kuunda hatua za kimkakati
za ushughulikiaji zinazotegemea maarifa ya pamoja, thamani iliyoongezwa, mafunzo na
uchanganuzi wapamoja wa muktadha wa nchi, ikiwemo umaskini na uendelevu, na uhusiano
wa jumla wa nchi na Umoja wa Ulaya. Kwa kufanya hivyo, watazingatia nyenzo
zinazopatikana za ufadhili wa maendeleo, kulingana na Ajenda ya Utendaji ya Addis Ababa.
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wataendeleza uratibu ulioboreshwa na nguvu za
pamoja katika nchi zenye udhaifu na zinazoathiriwa na migogoro, ikiwemo kupitia michakato
SN 3109/17 YML/ik 37
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
ya Mipangilio ya Pamoja na uchanganuzi wa pamoja wa migogoro. Watachangia pia katika
Makubaliano Mapya ya Ushirikiano katika Nchi zenye Udhaifu.
76. Kuongezeka kwa matumizi ya masuluhisho ya pamoja ya Umoja wa Ulaya unaotokana na
Mipangilio ya Pamoja ya Umoja wa Ulaya kunaweza kuhakikisha kuna matokeo mazuri zaidi
kwa Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake kunaonekana zaidi katika maeneo husika.
Mtazamo huu utasaidia kukusanya rasilimali, kupunguza mgawanyiko na kuzidisha wa
maafanikio. Uangalizi wa pamoja na taratibu za matokeo zitakuwa viungo vikuu vya
ushughulikiaji wa pamoja wa kudumisha kasi, vya kutoa taarifa muhimu katika majadiliano
na kuimarisha uwajibikaji wa pande zote husika. Mipangilio ya Pamoja ni lazima iwe wazi
kwa wafadhili na wadau wengine wa kimataifa wanaohusika jambo iwapo hili
limetathminiwa na Umoja wa Ulaya na wawakilishi wa Nchi Wanachama na kuonekana
linafaa.
77. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watafanya juhudi za kusaidia nchi washirika
kupitia utekelezaji wa pamoja wakati panafaa. Utekelezaji wa pamoja ni njia ya keundeleza
usaidizi wa Umoja wa Ulaya wenye ushikamano, ufanisi na ulioratibiwa kulingana na
malengo ya pamoja katika sekta teule au katika mada maalum kwenye sekta mbalimbali na
yanayolingana na hali za nchi tofauti. Utekelezaji wa pamoja utafuata uchanganuzi wa
pamoja, utazingatia rasilimali zinazopatikana na utaangaliwa na kutathminiwa kwa pamoja.
Utekelezaji wa pamoja unaweza kufanyika katika kiwango cha kitaifa, eneo, au ulimwengu na
unaweza kuunganishwa na nyanja zingine za hatua za nje ya nje kama inavyofaa.
78. Utekelezaji wa pamoja utakuwa jumuishi na wazi kwa washirika wote wa Umoja wa Ulaya
wanaokubali na kuchangia kwa dira ya pamoja, wakiwemo mawakala wa Nchi Wanachama
na taasisi zao zinazofadhili maendeleo, sekta ya kibinafsi, asasi za jamii na wanazuoni. Iwapo
utathmini utaonyesha kuwa ni muhimu, serikali zingine zenye mtazamo sawa zinaweza
kujumuishwa, na vile vile Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa na ya kanda
na taasisi za kifedha. Utekelezaji wa pamoja unaweza kuhusisha mbinu tofauti za ufadhili,
kama vile ufadhili wa pamoja, ushirikiano kupitia wajumbe, na vile vile mbinu za utekelezaji
zisizo za kifedha, na unapaswa kufuata faida zinazoletwa na uwezo wa wadau mbalimbali na
kushiriki kwa mitindo bora zaidi. Katika muktadha huu, Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama wakewatendelea kujifunza kutokana na na kushiriki katika matukio ya Nchi
Wanachama wote, ikiwemo matukio ya mpito.
SN 3109/17 YML/ik 38
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
79. Kuunda mipango ya maendeleo kulingana na eneo au mada kutafuatilia utaratibu wa miaka
mingi. Katika ushirikiano wao katika maendeleo, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
watatumia mbinu tofauti na zinazokamilishana (kama vile usaidizi katika miradi, usaidizi wa
programu ya sekta, usaidizi wa sekta na wa bajeti ya jumla) na njia za utoaji wa msaada
(ushirikiano baina ya miji, usaidizi wa kiufundi na ukuzaji wa uwezeshaji), kulingana na
mbinu itayofaa zaidi kwa kila nchi kwa kuzingatia uwezo, mahitaji, na utendakazi wa nchi, na
vile vile kulingana na hali maalum.
80. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake, inapofaa, watatafuta fursa za kukusanya
rasilimali na kufanya maamuzi ya haraka na yanayoweza kubadilishwa na utekelezaji ili
kuleta matokeo, ufanisi, na kuonekana zaidi kwa ushirikiano wa maendeleo wa Umoja wa
Ulaya wa kutimiza malengo ya maendeleo endelevu (SDG), kupitia miradi, hasa Hazina za
Amana za Umoja wa Ulaya zinazotumika wakati wa dharura, baada ya dharura au matendo
yenye azimio moja, ambayo yanaweza kutoa fursa za utendaji wa pamoja wenye ufanisi wa
Umoja wa Ulaya, Nchi Wanachama na washirika wengine wa maendeleo. Wanafaa kuleta
ufanisi wa usimamizi na thamani nyongeza na wanapaswa kuwa na ujumuishi kwa
kuwashirikisha wafadhili wote, wakiwemo wafadhili wadogo. Tume itahakikisha uwazi kwa
kutoa, kati ya mengine, taarifa za mara kwa mara kwa Bunge na Baraza la Ulaya, na kupitia
kuhusika kwao kunaofaa katika miundo muhimu ya utawala, kulingana na sheria husika ya
Umoja wa Ulaya. Hazina za Amana zitatumia kanuni mbalimbali za ufanisi wa maendeleo na
zitaambatana na vipaumbele vya kudumu vya maendeleo, mikakati ya kitaifa na ya nchi ya
Umoja wa Ulaya na nyenzo na programu zingine muhimu.
SN 3109/17 YML/ik 39
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
81. Kazi iliyoratibiwa na Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake kuhusu usaidizi wa bajeti
itasaidia kuendeleza juhudi za utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu katika nchi
washirika, kuboresha usimamizi wa uchumi mkubwa na wa fedha za umma, na kuboresha
mazingira ya biashara. Usaidizi wa bajeti, unapoweza kutumika na pamoja na wale walio
tayari kushiriki, utasaidia kuimarisha ushirikiano, mazungumzo ya kisiasa, umiliki wa nchi na
uwajibikaji wa pande zote husika na nchi zinazoendelea, kulingana na kanuni, malengo na
maslahi ya pamoja na kufuatia hali za kisiasa, kiuchumi na kijamii katika nchi washirika.
Usaidizi wa bajeti utatumiwa kuambatana na kanuni za ufanisi wa maendeleo na ambapo hali
ni sawa na mifumo ya udhibiti wa utawala imetekelezwa, na utakuwa pamoja na ukuzaji wa
uwezo, uhamisho wa ujuzi na utaalamu. Hivyo utakuwa nyongeza kwa juhudi za nchi
zinazoendelea za kukusanya mapato mengi zaidi na kutumia vyema kwa kuunga mkono
maendeleo endelevu, na kuendeleza ukuaji jumuishi na utoaji wa nafasi za ajira, umalizaji wa
umaskini, upunguzaji wa ukosefu wa usawa na jamii zenye amani. Usaidizi wa bajeti
unaweza pia kuchangia katika kutatua vyanzo vya udhaifu na katika kuendeleza udhaifu na
ujenzi wa nchi katika mataifa yenye hali za udhaifu au yenye serikali za mpwito.
82. Mchanganyiko wa hiba na mikopo, kama njia ya kufaidi kutokana na fedha za ziada
zinazotoka kwa sekta ya kibinafsi, ni mbinu nyingine muhimu ya kutekeleza Ajenda ya 2030.
Mchanganyiko unajumuisha maeneo yote ya ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na nchi za nje
katika sekta zikiwemo kawi, miundo msingi ya uchukuzi na maji, usaidizi kwa mashirika ya
madogo na ya kadiri ya biashara, sekta za kijamii na mazingira. Ushirikiano imara zaidi na
sekta ya kibinafsi utahitajika, kwa kutumia nyenzo za kifedha ili kuvutia ufadhili kutoka kwa
sekta ya kibinafsi kwa ajili ya maendeleo endelevu, ikiwemo kwa lengo la kukabiliana na
mabadiliko ya hali ya hewa. Huku ukihakikisha nyongeza ya usaidizi kwa mapato, na
kuangazia umuhimu wa maendeleo, mchanganyiko utatumiwa kuboresha ufanisi na
kushughulikia kutofauli kwa masoko huku ukipunguza kudhoofika kwa masoko. Shughuli za
mchanganyiko wa ufadhili zitaendeleza uwajibikaji wa mashirika ya kibiashara kwa jamii,
ikiwemo kupitia utekelezaji wa miongozo, kanuni na nyenzo muhimu zinazokubalika
kimataifa. Mchanganyiko wa ufadhili ni sehemu kuu ya Mpango wa Ulaya wa Uwekezaji wa
Nje ya Nchi. Ushirikiano wa karibu na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na taasisi zingine
za kifedha za Nchi Wanachama kutakuwa sifa kuu ya shughuli za kuchanganya ufadhili za
Umoja wa Ulaya. Taasisi zingine za kifedha za kimataifa zitashirikishwa pia.
SN 3109/17 YML/ik 40
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
3.2. Kukuza miungano ya wadau mbalimbali iliyo imara, na jumuishi zaidi
83. Miungano imara ndio msingi wa mtazamo wa Umoja wa Ulaya kwa utekelezaji wa malengo
ya mendeleo endelevu. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watafanya kazi kwa
ushirikiano wa karibu zaidi na wadau wengine wote wanaohusika ili kuendeleza utekelezaji
wa Ajenda ya 2030 na kuimarisha uwezo wao wa umiliki wa demokrasia. Bunge na vyama
vya kisiasa na vile vile mamlaka za eneo na za mitaa ni lazima zitimize wajibu wao
kikamilifu, ikiwemo wajibu wa kuchunguza, pamoja na serikali za kitaifa, na ni lazima
zishiriki kwa uamilifu katika michakato ya kufanya maamuzi. Hii ni pamoja na jukumu
muhimu la bunge za kitaifa na za kanda katika uundaji wa sheria, uidhinishaji bajeti na kwa
kuhakikisha serikali zinawajibika.
84. Serikali za kitaifa zina wajibu mkuu wa utekelezaji wa Ajenda ya 2030. Kwa kushirikiana na
nchi washirika, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watasisitiza upya umiliki wa
nchi, ushirikiano na majadilano, ili kuchangia katika ufanisi zaidi. Watatoa msaada kwa
upangaji mpana na jumuishi katika nchi zinazoendelea na unaofuata mikakati ya maendeleo
ya kitaifa na ya taifa dogo, programu na bajeti. Wataendeleza mazungumzo wazi ya serikali
na wadau wote katika awamu za kufanya maamuzi, kupanga, kutekeleza na kutathmini.
Michakato ya aina hiyo itasaidia serikali za kitaifa kukadiria mbinu za utekelezaji
zinazopatikana, kutambua mapengo na kuchagua nyanja zinazofaa kwa maendeleo na
ushirikiano mwingine katika ngazi ya kimataifa.
85. Baadhi ya malengo ya msingi yatakuwa ni kukuza uwezo wa nchi zinazoendelea wa
kutekeleza Ajenda ya 2030 katika ngazi za eneo, kanda, na kitaifa, ili kuendeleza mazingira
ya sera yanayofaa, hasa kwa jamii zilizotengwa zaidi, na kuunga mkono kujifunza na
kushiriki ujuzi. Hii itajumuisha pia kuunga mkono ukusanyaji na matumizi bora ya fedha za
umma za nchi, ambao ndio chanzo kikubwa na imara zaidi cha ugharamiaji wa maendeleo
endelevu. Itajumuisha pia kuenldeza mifumo ya Serikali ya kieletroniki ili kusaidia katika
ukusanyaji bora wa kodi na uwazi katika matumizi ya fedha za umma. Umoja wa Ulaya na
Nchi Wanachama wake wataunga mkono ukuzaji wa uwezo katika taratibu za uangalizi
zinazomilikiwa na taifa, ukusanyaji, ugawanyaji na uchanganuzi bora wa data kupitia nyenzo
za uangalizi za kidijitali na ushikamano wa sera kwa ajili ya maendeleo endelevu.
SN 3109/17 YML/ik 41
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
86. Utimizaji wa mengi ya malengo ya maendeleo endelevu unategemea sana uhusishwaji amilifu
wa mamlaka za mitaa na za eneo. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataunga
mkono mabadiliko yenye nia ya kuleta uwazi, uwajibikaji na ugatuzi, inapofaa, ili
kuziwezesha mamlaka za eneo na za mitaa kuwa na utawala bora na matokea mema ya
maendeleo, na kushughulikia vyema ukosefu wa usawa ndani ya nchi. Wataunga mkono
michakato ya kusaidia watu kushirikiana vyema na serikali katika ngazi zote za kupanga na
kutekeleza sera, na wataimarisha ushirikiano wao na mamlaka za mitaa na zingine za kiwango
kidogo cha taifa, ikiwemo kupitia ushirikiano uliogatuliwa.
87. Utekelezaji fanifu wa Ajenda ya 2030 unahitaji pia kuendeleza miungano imara zaidi kando
na ile ya serikali. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watapanua miungano na sekta
ya kibinafsi, asasi za jamii, ikiwemo miungano ya wafanyakazi na mashirika ya waajiri,
mashirika ya kimataifa na ya kanda, wanazuoni, watu wanaoishi/kufanya kazi katika nchi za
nje na wadau wengine husika. Wataendelea kuunga mkono ukuzaji wa uwezo wa wadau
hawa, ili kuwapa nafasi ya kutimiza wajibu wao wa kuunda, kutekeleza, kuangalia na
kutathmini mikakati ya maendeleo endelevu.
88. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watazidisha ushirikiano wao na mashirika ya
kiraia katika kuunga mkono maendeleo endelevu. Wataendeleza nafasi na mazingirira ya
mashirika ya kiraia yanayowawezesha kuendeleza shughuli zao, kwa ushirikishwaji kamili wa
umma, ili kuwapa nafasi ya kutimiza wajibu wao kama watetezi huru, watekelezaji na
waendeshaji wa maendeleo, katika kutoa elimu ya maendeleo na uhamasishaji na katika
kuangalia na kuhakikisha mamlaka zinawajabika ipasavyo. Wataunga mkono kujitolea kwa
mashirika ya kiraia kwa ushirikiano katika maendeleo wenye ufanisi, uwazi, uwajibikaji na
unaonuia kuleta matokeo mazuri.
89. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watatambua jukumu kuu la sekta ya kibinafsi
kama injini ya maendeleo endelevu ya kudumu na haja ya kushirikiana nayo kupitia
mazungumzo yenye utaratibu na malengo ya pamoja ya maendeleo. Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama wake wataendeleza mipangilio halisi ya ushirikiano ambayo inashirikisha
wengine, ina uwazi, na inayotoa nafasi kwa biashara, raia na wadau wengine kushiriki.
Wataunga mkono shughuli za biashara zilizo endelevu na zenye maadili mema na kuunda
vichochezi vya uwekezaji wa sekta ya kibinafsi katika maendeleo endelevu ya ulimwengu.
SN 3109/17 YML/ik 42
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
90. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataimarisha ushirikiano wao na mashirika ya
kimataifa, ukiwemo mfumo wa Umoja wa Mataifa, Hazina ya Fedha ya Kimataifa, Kundi la
Benki ya Ulimwengu, benki za maendeleo za kanda, G7, G20, Shirika la Ushirikiano wa
Kiuchumi na Maendeleo (OECD) na taasisi zingine za kanda na za kimataifa. Watawahimiza
kuambatanisha upangaji wao wa kimkakati na shughuli za uendeshaji na Ajenda ya 2030 na
kukuza usaidizi ulioratibiwa na unaofaidi pande zote katika utekelezaji wake, kulingana
kikamilifu na mikakati ya kitaifa ya maendeleo endelevu. Ili kuboresha ufanisi wa Umoja wa
Mataifa na mfumo wake wa maendeleo, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
wataendeleza mabadiliko na nguvu za pamoja ndani ya Umoja wa Mataifa, katika ngazi ya
Ofisi kuu na pia katika kiwango cha nchi, wakiwa na nia ya kuufanya mfumo wa Umoja wa
Mataifa kuwa wa ‘kufanya kazi kwa pamoja’. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
wataendeleza kushiriki kwa nchi zinazoendelea katika usimamizi wa mashirika ya kimataifa.
3.3 Kuambatanisha ushirikiano katika maendeleo na uwezo na mahitaji
91. Ushirikiano katika maendeleo utaendelea kufuata muktadha wa nchi au eneo, kulingana na
mahitaji, mikakati, vipaumbele na rasilimali za washirika wenyewe. Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama wake watashirikiana na nchi zinazoendelea kwa njia tofauti zaidi na kwa jinsi
inayozingatia muktadha husika. Miungano inapaswa kujumuisha ushirikiano katika
maendeleo na usaidizi wa kifedha, lakini pia ujumuishe ndani mikakati, sera na nyenzo
mbalimbali, ili ushughulikie ongezeko la hali tofauti za nchi zinazoendelea.
SN 3109/17 YML/ik 43
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
92. Huku ukiheshimu vipaumbele vya kila Nchi Mwanachama, ushirikiano katika maendeleo wa
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake utalenga pale ambapo kuna haja kubwa zaidi na
ambapo unaweza kuleta matokeo mazuri zaidi, hasa katika Nchi Zilizo na Maendeleo
Machache zaidi na katika hali za udhaifu na migogoro. Nchi hizi, ambazo nyingi hupatika
barani Afrika, zina idadi kubwa na inayozidi kuongezeka ya watu maskini zaidi ulimwenguni
na zina uwezo wa chini mno wa mapato na udhaifu mkubwa katika mbinu za kutimiza
malengo ya maendeleo endelevu. Watazidi kutegemea pakubwa fedha za jamii ya kimataifa
za kufadhili huduma za umma katika siku zijazo. Misaada ya kimataifa ya fedha za umma
ambayo ina masharti nafuu, hasa hiba, ni lazima ielekezwe kwa nchi ambazo zina mahitaji
sana, zikiwemo zile zilizo katika hali ya udhaifu. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
watazingatia changamoto mahususi za nchi ambazo zinapanda ngazi kutoka kiwango cha
mapato ya chini hadi kile cha mapato ya kadiri.
93. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watajihusisha na ushirikiano wa maendeleo,
mazungumzo kuhusu sera na kuungana na Nchi zenye Mapato ya Kadiri (MIC) katika
maendeleo endelevu, umalizaji wa umaskini, hatari za wahamiaji zinazoendelea kwa muda
mrefu na maslahi mengine ya pamoja. Wataleta pamoja ushirikiano wa kisiasa, kiulinzi,
kiuchumi, kisayansi, kiufundi, kiteknolojia na kifedha, kama inavyofaa. Mazungumzo kuhusu
sera na mabadiliko kwa umma yatatilia maanani sifa tofauti za Nchi zenye Mapato ya Kadiri,
yaendeleze maslahi ya pande zote husika na kutambua vipaumbele vya pamoja, miungano na
kanuni za ushirikiano. Wataunga mkono utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu,
ambayo yanatoa utaratibu wa pamoja na jumuishi wa ushirikiano, na kushughulikia pia mali
na changamoto za umma wa ulimwengu.
SN 3109/17 YML/ik 44
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
94. Nchi nyingi zenye Mapato ya Kadiri zina idadi kubwa ya watu wanaoishi katika umaskini
ndani ya mipaka yao na mara nyingi huwa na viwango vya juu vya ukosefu wa usawa na
kutengwa katika jamii. Suala kuu la kuangazia katika ushirikiano na Nchi zenye Mapato ya
Kadiri litakuwa ni kuhakikisha kwamba hakuna yeyote anayeachwa nyuma, kwa kukabiliana
na umaskini na vile vile vizuizi rasmi na visivyo rasmi vya ujumuishwaji katika jamii kupitia
utengenezaji na ugavi sawa wa mali. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
watashughulikia pia haja ya kuongeza kasi na kuunga mkono uendelezaji wa mifumo
endelevu ya matumizi na uzalishaji, upunguzaji wa takataka, usimamizi wa kemikali wenye
uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
watafanya kazi ili kushiriki utaalamu na kuwezesha uhamisho wa teknolojia na ubadilishanaji
wa mitindo bora, ikiwemo kupitia kuanzisha ulingo wa biashara kwa Mashirika Madogo
zaidi, Madogo Kiasi, na ya Kadiri, kuhimiza uwekezaji wenye uwajibikaji na mabadiliko
katika masuala ya fedha, na badala yake kutumia nishati mbadala, usimamizi endelevu wa
rasilimali asilia na uendelezaji wa utawala bora, utawala wa sheria na haki za binadamu.
95. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataanzisha pia ushirikiano bunifu na nchi
zinazoendelea zilizo juu zaidi kimaendeleo, ikiwemo na zaidi ya ushirikiano wa kifedha, kwa
sababu nchi hizi zinahitaji mbinu chache za usaidizi zenye masharti nafuu au hata hazina haja
ya mbinu hizo. Nchi hizi ni muhimu katika utekelezaji wa Ajenda ya 2030 na kwa maana
uchumi wao ni muhimu, athari zake kwa mali na changamoto za umma wa ulimwengu,
yakiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, zinazidi kuongezeka pakubwa.
SN 3109/17 YML/ik 45
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
Ushirikiano bunifu na nchi zinazoendelea na zilizo juu zaidi kimaendeleo
Nchi zinazoendelea na zilizo juu zaidi kimaendeleo zina athari na ushawishi muhimu ndani ya
maeneo yao, zikiwemo kama vyanzo vya uthabiti wa eneo. Ushirikiano wao na nchi zingine
zinazoendelea unazidi kuongezeka kwa kasi sana na ni sehemu kubwa ya mgao wa ushirikiano wa
kimataifa.
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataanzisha miungano mipya na nchi zinazoendelea na
zilizo juu zaidi kimaendeleo ili kuendeleza utekelezaji wa Ajenda ya 2030 kupitia ushirikiano wa
aina mbalimbali. Msingi wa miungano hii ni mazungumzo kuhusu sera na mabadiliko kwa umma.
Mazungumzo kuhusu sera yataendeleza maslahi ya pande zote husika na kutambua vipaumbele vya
pamoja, miungano na kanuni za ushirikiano katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu,
ambayo yanatoa utaratibu wa pamoja na jumuishi wa ushirikiano. Miungano hii mipya itaendeleza
ubadilishanaji wa mitindo bora zaidi, usaidizi wa kiufundi na kushiriki ujuzi. Aidha, Umoja wa
Ulaya na Nchi Wanachama wake watafanya kazi na nchi hizi ili kuendeleza ushirikiano baina ya
nchi zinazoendelea, na baina ya nchi zinazoendelea zikisaidiwa na nchi iliyoendelea/zilizoendelea
kulingana na kanuni za ufanisi wa maendeleo.
96. Mikataba, taratibu, mikakati, miungano na sera za kanda zinazohusiana na nchi zote
zinazoendelea zitaongozwa na Makubaliano haya na zatafuata malengo, kanuni na maadili ya
pamoja. Wataendeleza utekelezaji wa Ajenda ya 2030 katika ngazi ya kanda na nchi
washirika, zikiwemo zile zilizo Afrika, Karibia na Pasifiki, na vile vile zilizoko Amerika ya
Kusini na Asia.
97. Makubaliano haya yataongoza hatua za Umoja wa Ulaya katika nchi zinazoendelea za
maeneo jirani kwa ushikamano na kuambatana na Sera ya Ujirani ya Ulaya. Umoja wa Ulaya
na Nchi Wanachama wake watatumia nyenzo mbalimbali katika ujirani wao, kuambatana na
hatua zingine za Umoja wa Ulaya chini ya Ajenda ya 2030.
SN 3109/17 YML/ik 46
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
4. KUIMARISHA MBINU ZA KUBORESHA MATOKEO YA HATUA
ZINAZOCHUKULIWA NA UMOJA WA ULAYA
4.1. Kuleta pamoja na kutumia ipasavyo mbinu zote za utekelezaji
98. Ili kuonyesha utaratibu uliowekwa katika Ajenda ya Utendaji ya Addis Ababa (AAAA) na
Ajenda ya 2030, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake ni lazima wabadilishe mtazamo
wao ili kuleta pamoja na kutumia vizuri mbinu zote za utekelezaji, ikiwemo kupitia mifumo
bunifu ya ufadhili. Hii inahitaji kuangazia upya kuanzisha mazingira ya sera yanayowezesha
na kufaa katika ngazi zote. Hii ni pamoja na kukusanya na kutumia ipasavyo fedha za umma
za ndani ya nchi na za kimataifa, kuleta pamoja sekta ya kibinafsi ya ndani ya nchi na ya
kimataifa, kuimarisha uwezo wa nchi washirika wa kuleta mabadiliko, kuchochea biashara na
uwekezaji, kukuza sayansi, teknolojia na ubunifu, na hata kushughulikia changamoto na
kufaidi kutokana na matokeo mazuri ya uhamaji.
99. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watafanya kazi na nchi washirika ili kuendeleza
mazingira mazuri ya sera kwa ajili ya utekelezaji wa Ajenda ya 2030. Wataunga mkono
uwezo wa nchi wa kuunda na kutekeleza sera jumuishi za kitaifa za maendeleo endelevu na
taratibu za matokeo na vile vile kuongeza uwajibikaji na ushughulikiaji wa maslahi ya raia.
Wataendeleza sera zinazounganisha hatua za umma na za sekta ya kibinafsi zinaounga mkono
maendeleo na mazingira yanayowezesha ukuaji jumuishi na endelevu na ugavi wake kwa njia
ya usawa kupitia bajeti za kitaifa. Watapanga ushirikiano wao katika maendeleo wakizingatia
uimarishaji wa uwezo wa kila nchi wa kutekeleza Ajenda ya 2030 na kutimiza mahitaji na
maazimio ya raia wake.
100. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataangazia zaidi kuzalisha rasilimali za ziada
kwa ajili ya maendeleo endelevu katika nchi washirika. Hii itajumuisha kuendeleza
ukusanyaji wa rasilimali za ndani ya nchi, kuendeleza mazingira ya kuongeza ufadhili kutoka
kwa sekta ya kibinafsi ya ndani ya nchi, kuimarisha biashara ya kimataifa kama injini ya
maendeleo na kukabiliana na vyanzo na matumizi haramu wa fedha zisizotozwa ushuru.
SN 3109/17 YML/ik 47
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
Kukusanya na kutumia rasilimali za nchi
Kuboresha ukusanyaji wa rasilimali za ndani ya nchi ni muhimu kwa juhudi zote za serikali za
kufikia ukuaji jumuishi, umalizaji wa umaskini na maendeleo endelevu. Unaongeza uhakika na
uthabiti wa ugharamiaji wa maendeleo endelevu na kupunguza utegemeaji wa msaada. Pamoja na
usimamizi bora wa matumizi ya umma, ukusanyaji wa rasilimali za nchi unatoa mali na huduma za
umma mahali zinapohitajika, nahivyo kuimarisha kandarasi ya kijamii baina ya serikali na raia.
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza ukusanyaji na matumizi fanifu na bora
ya rasilimali, ikiwemo kupitia mipango kama vile mtazamo wa ‘Kusanya Zaidi, Tumia Vyema
Zaidi’. Watakabilianana wanaokwepa na kuhepa kulipa ushuru, vyanzo na utumiaji haramu wa
pesa, na ubora, ufanisi na usawa wa mifumo ya ukusanyaji ushuru na wa ufadhili wa ulinzi wa
kijamii. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake pia wataunga mkono Mpango wa Ushuru wa
Addis (Addis Tax Initiative) na kazi ya Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo
(OECD)/G20 ya kushughulikia tatizo la kampuni zinazohamisha faida zao kwa nchi zisizotoza
ushuru wa juu/zenye shughuli chahce za biashara, ikiwemo utoaji ripoti wa kila nchi na
ubadilishanaji wa taarifa za ushuru, ili kuhakikisha kwamba kampuni zinalipa ushuru unaolingana
na faida na shughuli zao za kibiashara. Wataunga mkono kushiriki kwa nchi zinazoendelea katika
usimamizi wa ushuru wa ulimwengu na majadiliano muhimu ya kimataifa na michakato ya kuweka
viwango, ikiwemo katika Jukwaa la Ulimwengu kuhusu Uwazi na Ubadilishanaji wa Taarifa kwa
Madhumuni ya Ushuru na majadiliano ya G20/Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo
(OECD). Wanajitolea kuendeleza ushikamano baina ya sera zao za ushuru na athari zake kwa nchi
zinazoendelea.
SN 3109/17 YML/ik 48
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
101. Mapato ya nchi yanayotokana na ulipaji ushuru ni muhimu katika kutekeleza Ajenda ya 2030
katika nchi zote. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watongeza usaidizi kwa nchi
zinazoendelea katika juhudi zao za kuimarisha ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa ulipaji
wa madeni na gharama za umma, za kuanzisha mifumo ya ushuru, kuongeza ubora na ufanifu
wa matumizi ya umma na kumaliza ruzuku za mafuta ya petroli yenye madhara kwa
mazingira. Usaidizi Rasmi wa Maendeleo una jukumu muhimu katika kupiga jeki juhudi za
nchi – hasa zile ambazo ni maskini na dhaifu zaidi – za kukusanya rasilimali zilizoko ndani ya
nchi. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wanaweza kuchangia katika kuboresha
ufanisi wa uwekezaji wa umma katika nchi washirika kwa kuunga mkono mifumo ya uthabiti
wa uchumi mkubwa na wa kifedha, sera na mabadiliko bora ya sekta, taratibu pana za bajeti
za baada ya kila mwaka na nusu muhula na mifumo ya usimamizi unaofaa wa fedha za umma,
ikiwemo ununuzi wazi na endelevu.
102. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake ni wakarimu katika kutoa msaada wa ushirikiano
kwenye maendeleo, na wametoa zaidi ya nusu ya Usaidizi Rasmi wa Maendeleo kote
ulimwenguni katika miaka ya hivi majuzi. Ingawa Usaidizi Rasmi wa Maendeleo ni wa
kiwango kidogo kwa ujumla kwa nchi zinazoendelea, ni chanzo kikuu cha fedha kwa nchi
zilizo maskini zaidi na Nchi zenye Maendeleo Machache Zaidi, ambazo hazina uwezo wa
kupata fedha kutoka vyanzo vingine. Usaidizi Rasmi wa Maendeleo unaweza kunufaika pia
na mbinu zingine za utekelezaji, hasa ufadhili wa umma wa ndani ya nchi na uwekezaji wa
sekta ya kibinafsi, na hata pia sayansi, teknolojia na ubunifu.
103. Umoja wa Ulaya kwa pamoja umejitolea kutoa asilimia 0.7 ya Jumla ya Mapato ya ya Taifa
(GNI) kama Usaidizi Rasmi wa Maendeleo kuambatana na ratiba ya Ajenda ya 2030. Ili
kuelekeza rasilimali pale ambapo zinahitajika zaidi, hasa Nchi zenye Maendeleo Machache
Zaidi na zile zilizo kwenye hali za udhaifu na migogoro, Umoja wa Ulaya umehapa kutimiza
kwa pamoja lengo la asilimia 0.15-0.20 ya Usaidizi Rasmi wa Maendeleo/Jumla ya Mapato
ya Taifa kwa Nchi zenye Maendeleo Machache Zaidi katika kipindi kifupi, na kufikisha
asilimia 0.20 ya Usaidizi Rasmi wa Maendeleo/Jumla ya Mapato ya Taifa kwa Nchi zenye
Maendeleo Machache Zaidi kuambatana na ratiba ya Ajenda ya 2030. Umoja wa Ulaya na
Nchi Wanachama wake pia wanatambua changamoto mahususi zinazozikumba nchi za
Afrika. Kwa hili, Umoja wa Ulaya unasisitiza umuhimu wa kuelekeza Usaidizi Rasmi wa
Maendeleo kwa bara hilo huku ukiheshimu vipaumbele vya kila Nchi Mwanachama katika
usaidizi wa maendeleo. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wanatilia mkazo ahadi
zao za Usaidizi Rasmi wa Maendeleo za kila mmoja na za pamoja na watachukua hatua halisi
SN 3109/17 YML/ik 49
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
na zinazoweza kuthibitishwa kutimiza ahadi hizi. Wataendelea kuangalia maendeleo na kutoa
ripoti kila mwaka ili kutoa nafasi ya uwazi na uwajibikaji kwa umma.
104. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake pia wataendelea kuimarisha ukusanyaji wa fedha
za kugharamia miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kama sehemu ya juhudi
za ulimwengu, hasa kwa kutoa uungaji mkono imara kwa juhudi za kupunguza visababishi na
athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika nchi zinazoendelea, kulingana na masharti chini
ya Utaratibu wa Kanuni kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa wa Umoja wa Mataifa na
Mkataba wa Paris. Wanatambua haja ya kuongeza juhudi na ufadhili wa kukabiliana na athari
za mabadiliko ya hali ya hewa na upunguzaji wa ongezeko la hali joto duniani, ikiwemo
kupitia sera zao za ushirikiano na nchi za nje ya Umoja wa Ulaya na ushirikiano katika
maendeleo. Watajizatiti kuimarisha na kuongeza faida za pamoja za hali ya hewa katika
programu za ushirikiano wa maendeleo. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
wamejitolea kukusanya mgao wao wa lengo la nchi zilizoendelea la kukusanya kwa pamoja
Dolaza Marekani bilioni 100 kila mwaka ifikapo mwaka wa 2020 na hadi mwaka wa 2025 za
kukabiliana na visababishi na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, kutoka kwa vyanzo,
nyenzo na mbinu tofauti. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza
mazungumzo ya masuala ya siasa ili kuboresha ahadi kutoka kwa wafadhili wengine.
105. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watazidi kuhakikisha kuwa Usaidizi Rasmi wa
Maendeleo una lengo linalofaa na unatumika kimkakati na kwa ushikamano kulingana na
mbinu zingine za utekelezaji kutoka kwa vyanzo vyote. Kwa muktadha huu, Umoja wa Ulaya
utashirikisha mipangilio ya kupima vyema aina zote za ufadhili wa maendeleo, kama vile
hatua inayopendekezwa ya Jumla ya Usaidizi Rasmi kwa Maendeleo Endelevu ya Shirika la
Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo.
106. Ushirikiano wa maendeleo utasaidia nchi washirika kuleta ukuaji jumuishi kupitia kushiriki
katika biashara ya kimataifa, na vile vile kuimarisha mchango wa sera ya biashara ya Umoja
wa Ulaya kwa maendeleo endelevu. Ushirikiano wa maendeleo utasaidia kuimarisha
ujumuishwaji na utekelezaji wa sura zinazohusu biashara na maendeleo endelevu katika
mikataba ya biashara, upendeleo zaidi wa ufikiaji wa soko la Umoja wa Ulaya kwa nchi zilizo
dhaifu na uungaji mkono wa biashara ya haki na inayoongozwa na maadili mema, na
kuanzisha zaidi sera za kuhakikisha usimamizi wenye uwajibikaji wa mifumo ya usambazaji.
Hii inajumuisha pia kuunga mkono utekelezaji wa Mikataba ya Ushirikiano wa Kiuchumi na
Mikataba ya Biashara Huru na nchi zinazoendelea, na pia upendeleo wa ufikiaji wa soko la
SN 3109/17 YML/ik 50
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
Umoja wa Ulaya bila kutozwa kodi au kuwekewa vikazo unaopewa Nchi zenye Maendeleo
Machache Zaidi kupitia utaratibu wa Kila Kitu isipokuwa Silaha. Kuratibu programu za
msaada na ushirikiano katika sehemu hizi utatoa nafasi ya Umoja wa Ulaya kutumia fursa na
kunufaika na uhusiano wa karibu wa kibiashara ili kuendeleza agenda yake inayofuata kanuni
kwa washirika wake wa biashara.
107. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza matumizi ya mbinu zingine za
utekelezaji, ikiwemo sayansi, teknolojia na ubunifu. Watanuia kutumia vyema zaidi fursa
zitokanazo na sayansi, teknolojia na ubunifu ili kutafuta suluhu mpya kwa changamoto za
ulimwengu, wakizingatia kazi ya Mfumo wa Uwezeshaji wa Teknolojia, Benki ya Teknolojia
ya Nchi zenye Maendeleo Machache Zaidi na mashirika mengine muhimu. Watazidi
kuwekeza katika utafiti na maendeleo katika na kwa nchi zinazoendelea, ikiwemo kwa
uboreshaji wa mifumo ya ubunifu ya kitaifa. Watalenga kuimarisha matokeo yanayopimika
kuhusu hatua za kueleke kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu kupitia mfumo wa Utafiti
na Ubunifu Unaowajibika, ikiwemo ufikiaji wazi wa matokeo na data ya utafiti wa miradi
inayofadhiliwa na umma na elimu kwa ajili ya sayansi.
4.2. Ushikamano wa sera ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu (SDG)
108. Maendeleo endelevu ni msingi wa mradi wa Umoja wa Ulaya na umejikita katika Mikataba,
ikiwemo ya ushirikiano wake na mataifa ya nje ya Umoja wa Ulaya. Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama wake wamejitolea kuleta maendeleo yanayotimiza mahitaji ya sasa bila
kuhatarisha uwezo wa vizazi vijavyo wa kukidhi mahitaji yao. Kuhakikisha ushikamano wa
sera kwa maendeleo endelevu kama ilivyo katika Ajenda ya 2030 kunahitaji kuzingatia athari
ya sera zote kuhusu maendeleo endelevu katika ngazi zote – kitaifa, ndani ya Umoja wa
Ulaya, katika nchi zingine na katika kiwango cha ulimwengu mzima.
109. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wanasisitiza tena kujitolea kwao kwa
Mshikamano wa Sera kwa ajili ya Maendeleo (PCD), ambao unahitaji kuzingatia malengo ya
ushirikiano wa maendeleo katika sera zinazoweza kuathiri nchi zinazoendelea. Hiki ni
kipengele muhimu cha mkakati wa kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu na mchango
muhimu katika lengo pana la Mshikamano wa Sera kwa ajili ya Maendeleo Endelevu
(PCSD). Ajenda ya 2030 inatoa msukumo kwa Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
kuunda na kutekeleza sera zinazohusisha na kuathiri pande zote.
SN 3109/17 YML/ik 51
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
110. Makubaliano haya yataongoza juhudi za kutekeleza Mshikamano wa Sera kwa ajili ya
Maendeleo katika sera na nyanja zote zinazojumuishwa katika Ajenda ya 2030, yakitafuta
nguvu za pamoja, hasa kwa biashara, fedha, mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa, uwepo
wa chakula cha kutosha, uhamaji na ulinzi. Masuala ya kukabiliana na fedha zenye chanzo
haramu na zisitozwa ushuru, ukwepaji wa kulipa ushuru, na uendelezaji wa biashara na
uwekezaji unaowajibika yataangaziwa kwa karibu.
111. Kupata matokeo kwa mfumo wa wote wa maendeleo endelevu katika tasnia ya ushirikiano wa
maendeleo ni jukumu la pamoja la wadau wote. Maendeleo endelevu yanahitaji mtazamo wa
sera wa jumla na unaoshirikisha sekta mbalimbali, na bila shaka ni suala la utawala
linalohitaji kuendeleza kwa ushirikiano na wadau wote na katika ngazi zote. Hivyo basi,
Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza mitazamo ya serikali zima na
kuhakikisha juhudi za uangalizi na uratibu wa kisiasa katika viwango vyote kwa ajili ya
utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Ili kuunga mkono vizuri uundaji wa sera na
uamuzi, watahakikisha msingi wa uthibitisho wa sera unaleta matokeo kwa nchi
zinazoendelea kupitia mashauriano, ushirikiano na wadau, utathmini wa utabiri wa matokeo
na ukadiriaji wa matokeo ya miradi mikuu ya sera. Hatua za Umoja wa Ulaya zinazoendelea
zenye nia ya kuleta uendelevu katika mifumo ya ulimwengu ya usamabazaji, kama vile katika
sekta za mbao na nguo, zinazonyesha faida ya ziada ya kuendeleza mfumo wa ushikamano.
Miradi ya utekelezaji wa sera, inapofaa, inapaswa kuonyesha jinsi inavyochangia kwa
maendeleo endelevu katika nchi zinazoendelea. Hii ni muhimu pia kwa Umoja wa Ulaya na
Nchi Wanachama wake ili kuboresha utoaji ripoti na uangalizi wao wa Mshikamano wa Sera
kwa ajili ya Maendeleo
112. Kwa kuwa Ajenda ya 2030 inawahusisha watu wote, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama
wake watahimiza pia nchi zingine zitathmini athari za sera zao wenyewe katika kutimiza
Malengo ya Maendeleo Endelevu, ikiwemo katika nchi zinazoendelea. Aidha, Umoja wa
Ulaya na Nchi Wanachama wake wataimarisha mazungumzo na nchi washirika kuhusu
mshikamano wa sera na kusaidia nchi washirika katika juhudi zao za kutekeleza taratibu za
kuwezesha mshikamano wa sera kwa ajili ya maendeleo endelevu. Wataongoza katika
kuendeleza mshikamano wa sera katika ngazi za kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa na
G20, kama sehemu ya uungaji mkono wa jumla kwa Ajenda ya 2030 katika ushirikiano wao
na nchi zingine zisizo za Ulaya.
SN 3109/17 YML/ik 52
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
4.3 Ufanisi wa maendeleo
113. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watasisitiza kujitolea kwao katika kutumia
kanuni kuu za ufanisi wa maendeleo kama zilivyokubaliwa huko Busan mnamo mwaka wa
2011 na kusasishwa katika Kongamano la Ngazi ya Juu la Nairobi mnamo mwaka wa 2016.
Wanajitolea kuimarisha uangaziaji wa matokea, kuboresha uwazi na uwajibikaji wa pande
zote husika, kuboresha umiliki wa nchi na kuendeleza miungano jumuishi ya maendeleo.
Wanatambua haja ya rasilimali zote za maendeleo na washirika wote kufanya kazi pamoja
kwa ufanisi ili kuleta matokeo endelevu na kuhakikisha hakuna yeyote anayeachwa nyuma
kimaendeleo. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza kazi hii kwa
wahusika wote, ikiwemo katika muktadha wa Muungano wa Ulimwengu mzima kwa ajili ya
Ufanisi wa Ushirikiano wa Maendeleo (GPEDC). Ushirikiano wao wa maendeleo
utaendelezwa kwa kushirikiana kwa karibu na washirika wengine na kwa kuwa wazi
kikamilifu kwa raia walio Ulaya na wale wa nchi zinazoendelea.
114. Kanuni za ufanisi wa maendeleo zinatumika kwa aina zote za ushirikiano wa maendeleo. Hii
inajumuisha fedha za umma za kimataifa, kama vile Usaidizi Rasmi wa Maendeleo na
ushirikiano baina ya nchi zinazoendelea na baina ya nchi zinazoendelea wakihusisha ufadhili
kutoka kwa nchi zilizoendelea, mikopo yenye masharti nafuu na isiyokuwa na masharti nafuu,
na shughuli za wadau wa asasi za jamii, sekta ya kibinafsi na wakfu wa wahisani. Umoja wa
Ulaya na Nchi Wanachama wake wanatarajia washirika wote wa maendeleo wajumuishe
kanuni hizi katika shughuli zao wenyewe, kuambatana na hali husika.
115. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watazidi kutetea uwazi, ambao unapaswa
kuendelea kutekelezwa katika rasilimali mbalimbali za maendeleo. Wataanzisha nyenzo za
kuwasilisha na kutumia ipasavyo data ya ya ushirikiano katika maendeleo. Watasaidia nchi
washirika kuunganisha rasilimali za maendele na matokeo, kwa kuunganisha vyema zaidi
michakato ya uandalizi na uundaji bajeti ili kuboresha michakato na viwango vya uwajibikaji.
SN 3109/17 YML/ik 53
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
116. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendeleza na kuangalia zaidi matumizi ya
mifumo ya nchi katika mbinu za usaidizi, ambapo ubora unaruhusu, ikiwemo katika kiwango
cha chini kabisa, ili kusaidia kuboresha umiliki wa demokrasia na ufanisi wa taasisi katika
ngazi ya kitaifa na ngazi dogo ya taifa. Watatathmini kwa pamoja ufanisi wa mifumo ya nchi
washirika, ili kuhakikisha ina utaratibu wenye ujuzi na ulioratibiwa. Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama wake watajibidiisha kutoa usaidizi usio na masharti ya mahali pa kununua bidhaa
au huduma na kuhimiza wote wanaoshirikiana katika maendeleo, zikiwemo nchi za uchumi
unaoibuka, kufanya vivyo hivyo. Wanalenga kuweka wazi zaidi maana ya usaidizi usio na
masharti ya mahali pa kununua bidhaa au huduma ili kuhakikisha kwamba watoaji wa
kimataifa usaidizi wa kifedha, wakiwemo washirika wa maendeleo wanaoibukia, wanatoa
masharti ya msaada wao vilevile.
5. KUFUATILIA AHADI ZETU
117. Kuhusiana na ushirikiano wa maendeleo, Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
wamejitolea kikamilifu kufuata mfumo pana, wazi, na wenye uwajibikaji wa kuangalia na
kutathmini kusudi la utekelezaji wa Ajenda ya 2030. Hii inajumuisha uwajibikaji kwa raia wa
Umoja wa Ulaya, ikiwemo kupitia bunge za Ulaya na za kitaifa.
118. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake wataendelea kubadili mifumo yao ya utoaji ripoti
katika tasnia ya ushirikiano wa maendeleo ili iambatane na michakato na viashiria vya
ufuatiliaji vya Ajenda ya 2030. Wataimarisha ubora na upatikanaji wa data kuhusu shughuli
za ushirikiano wa maendeleo, katika Ajenda yote ya 2030. Watafanya kazi kuhakikisha utoaji
ripoti una ulinganifu na kuambatana zaidi na ule wa mikataba mingine ya kimataifa.
119. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watajumuisha Ajenda ya 2030 na kuunga mkono
matumizi ya viashiria vya Malengo ya Maendeleo Endelevu ili kupima matokeo ya
maendeleo katika kiwango cha nchi. Hasa, viashiria vya Malengo ya Maendeleo Endelevu
vinaweza kukuza na kuwezesha mfumo wa pamoja wa Umoja wa Ulaya unaonuia kuleta
matokeo na unapoendelea utoaji ripoti ya matokeo yaliyosawazishwa katika kiwango cha nchi
mshirika, zikiwemo taratibu za matokeo katika kiwango cha nchi mshirika, iwapo zipo.
SN 3109/17 YML/ik 54
DG C 1 USAMBAZAJI
KWA UMMA
UMEDHIBITIWA
SW
120. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watatoa ripoti ya pamoja ya mukhtasari wa
Makubaliano kuhusu Maendeleo ikiwemo matokeo ya hatua zao za kuunga mkono Ajenda ya
2030 katika nchi zinazoendelea, kama mchango wa Umoja wa Ulaya ukiripoti kwa Jukwaa la
Kisiasa la Ngazi ya Juu la Umoja wa Mataifa (HLPF), unapokutana katika ngazi ya Viongozi
wa Nchi kila baada ya miaka minne. Ripoti hii itatumia na kufuata ripoti zingine muhimu za
Umoja wa Ulaya, ikiwemo kutoa ripoti kuhusu matokeo, Usaidizi Rasmi wa Maendeleo,
uwajibikaji katika ufadhili wa maendeleo, Ushikamano wa Sera kwa ajili ya Maendeleo, na
uangalizi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika muktadha wa Umoja wa Ulaya.
121. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake watainua uwezo wa kitakwimu wa nchi
zinazoendelea, ikiwemo kupitia kuimarisha uwezo wa uzalishaji na uchanganuzi wa data, ili
kuongoza sera na katika kufanya maamuzi. Data hii inapaswa kugawanywa inapowezekana
kulingana na mapato, jinsia, umri na mambo mengine, na kutoa taarifa kuhusu makundi
yaliyotengwa, dhaifu na ambayo ni vigumu kuafikia, utawala jumuishi na masuala mengine,
kuambatana na mtazamo unaozingatia haki wa Umoja wa Ulaya. Itajumuisha pia uwekezaji
katika taasisi imara zaidi za takwimu katika kiwango kidogo cha kitaifa, kiwango cha kitaifa
na cha eneo, na matumizi ya teknolojia na vyanzo vipya vya data. Umoja wa Ulaya na Nchi
Wanachama wake watahimiza nchi zao washirika kujumuisha michango ya jamii
zilizotengwa katika kuangalia malengo ya maendeleo endelevu na kuendeleza mbinu hali za
kufikia lengo hili.
122. Aidha, elimu na uhamasishwaji kuhusu maendeleo inaweza kuchangia pakubwa katika kuinua
viwango vya ushirikiano miongoni mwa umma na katika kushughulikia Malengo ya
Maendeleo Endelevu katika ngazi ya kitaifa na ulimwengu, na hivyo kuchangia katika uraia
wa ulimwengu mzima.
123. Utathmini wa katikati ya muhula wa utekelezaji wa Makubaliano haya utafanyika ifikapo
mwaka wa 2024. Itaainisha jinsi Makubaliano haya yametumika na yapi yametimiza katika
kuunga mkono utekelezaji wa Ajenda ya 2030. Umoja wa Ulaya na Nchi Wanachama wake
watapima maendeleo kwa utaratibu na kubadili vitendo vyao ili kuhakikisha ushirikiano wao
katika maendeleo, ikiwemo kupitia uhusiano wake na nyanja za sera husika, unaendelea
kuunga mkono utekelezaji wa Ajenda ya 2030 katika nchi zinazoendelea.