mkutano wa uwaba na tanroads dar es salaam 24 mei 2006

19
Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Upload: charla-stone

Post on 18-Dec-2015

236 views

Category:

Documents


8 download

TRANSCRIPT

Page 1: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Mkutano wa UWABA

na TANROADS Dar es Salaam

24 Mei 2006

Page 2: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Yaliyomo

1) Utabulisho wa UWABA

2) Umuhimu wa njia za baisikeli

3) Hali ya barabara za Dar es Salaam kwa wapanda baisikeli

4) Mapendekezo yetu

5) Vipi tunaweza kushirikiana kati ya UWABA na TANROADS

Page 3: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

1) Utambulisho wa UWABA

Umma wa Wapanda Baisikeli Dar es Salaam

Wanachama 50, wote wapanda baisikeli

Tumeanzisha januari 2006Tumesajili na serikali

Tovuti: www.geocities.com/UwabaDar

Page 4: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Utambulisho wa UWABA

Malengo yetu:Kushirikiana na serikali kutafuta mazingira mazuri na usalama kwa wapanda baisikeli Dar es Salaam

Kufuatilia haki za wapanda baisikeli

Kuelimisha wapanda baisikeli kuhusu matumizi mazuri ya barabara

Kuhamasisha watu kupanda baisikeli

Page 5: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

2) Faida za baisikeli

zinaondoa msongamano wa magari

zinalinda mazingira

zinakuza uchumi

zinaboresha afya

Page 6: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Umuhimu wa njia za baisikeliKupunguza msongamano wa magari Wanafunzi kufika shuleni mapemaKurahisisha watu kufika kazini na kufanya biashara Kurahisisha kusafirisha bidhaaKurahisisha kuuza bidhaa (matunda, icecream) Watu wa siyojiweza - walemavu, wagonjwa, wazeeMazoezi na michezo

Page 7: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Umuhimu wa njia za baisikeli

37% za safari za Dar es Salaam ni kwa miguu au baisikeli Mwaka 1994 wapanda baisikeli 24 na watembea kwa miguu 63 wamekufa na ajali Dar es Salaam, siku hizi zaidiTulipouliza kwa nini watu hawapandi baisikeli, 60% za majibu yalihusu usalamaUsalama unahusu sheria za barabarani, polisi na udereva lakini miundombinu ni muhimu zaidi

Page 8: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

3) Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Morogoro Road

Kuna njia moja kwa wapanda baisikeli na watembea kwa miguu Mijini – ni nyembamba, misingi ya barabara inasababisha waendesha baisikeli kushuka mara kwa mara.Fire – teksi zinapaki njianiJangwani – karavat – lazima kushuka baisikeli mara nyingi kila upande.Manzese na Ubungo wafanyabiashara wanaziba njia kabisa.

Page 9: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Kawawa Road

Njia moja baisikeli na watembea kwa miguu Njia inapita mbele ya vituo vya mabasi siyo nyuma - ngumu kwa baisikeli kupita katika watu wengi wanaosubiri. Kati ya Kigogo na Msimbazi njia ni embamba sana baisikeli haiwezi kupita Teksi na lori zinanapaki njiani mfano Kona ya BoraKinondoni kuna wafanyabiashara wengi njiani wanaziba njia Magomeni kuna nguzo zinaziba magari kuingia njiani - hii ni nzuri Nyerere Road mpaka Kilwa Road, hakuna njia ya baisikeli wala watembea kwa miguuEneo la Keko, barabara ni nyembamba na watu wengi barabarani

Page 10: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Nyerere Road

Mijini –misingi, baisikeli inatumia njia ya magari

Kariakoo-Ilala njia nzuri sana upande mmoja, kuliko upande mwingine

Njia inapita nyuma ya kituo darajani - nzuri

Njia ya baisikeli lami ni tofauti na eneo la watembea kwa miguu lakini hakuna alama

Njia imeharibika sana karibu na Shoprite

Page 11: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Nelson Mandela RoadSehemu nyingine kuna njia ya baisikeli na watu, sehemu nyingine hakuna kabisa (kama kati ya gereji na Mabibo External) Sehemu nyingine njia ni ya vumbi, mashimo mengi, tupu na michanga mingi. Tabata shimo kubwa inalazimika kushuka. Sehemu nyingi lori zinapaki njiani kama Vingunguti, Gereji, Mabibo External Taxi zinapaki njiani – External na River side.Corner Bar malori yamegeuza gereji njiani.Tabata njia ni embamba sana baisikeli haiwezi kupita na mtembea kwa miguu Riverside ngumu kupita kituo cha dala dala Matawi ya miti yapo chini inazuia kuona pande zote za barabara-ajali ni nyingiKaribu na Ubungo kuna wafanyabiashara wengi njiani

Page 12: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Kilwa Road, Mbande

Hakuna njia ya baisikeli kabisa na wapanda baisikeli wengi

Barabara ya magari nyembamba sana – magari hayawapi nafasi wapanda baisikeli

Mbande hakuna njia ya baisikeli kabisa

Mbande hakuna vituo vya mabasi maalumu

Page 13: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Ali Hassan Mwinyi

Njia moja- baisikeli na watembea kwa miguu Vituo vya mabasi vya Aga Khan, Palm Beach watu wengi, ngumu kupita Palm Beach teksi zinapaki njiani Salanda Bridge, Kinondoni Road, Kenyatta Rd - misingiLami imeharibika sana kati ya Salandar Bridge na Ubalozi wa Ufaransa Njia nzuri kati ya Ubalozi na Best Bite Kati ya Best Bite na Morocco magari mengi yanapaki njiani yanaziba njia kabisaKutoka Morocco mpaka Regent ni pazuri ila ni nyembamba sanaKutoka Regent mpaka Tegeta hakuna njia za baisikeli wala waenda kwa miguu.Eneo la Sayansi taxi zinapaki njiani.

Page 14: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Sam Nujoma Road

Hakuna njia ya baisikeli wala watembea kwa miguu, hata sehemu ya vumbi ni mbovuDarajani baisikeli haiwezi kupita njia ya pembeni kwa ajili ya nguzo, daraja mbovu na nyembambaHakuna vituo vya mabasi maalum, mabasi yanaziba njia yanaposimama

Page 15: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – New Bagamoyo Road

Kati ya Mwenge na Lugalo kuna njia upanda moja ila darajani kuna nguzo nyembamba sana baisikeli haiwezi kupita

Lugalo – Wazo: hakuna njia ya baisikeli wala waenda kwa miguu, barabara nyembamba

Page 16: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Hali ya barabara kwa wapanda baisikeli – Old Bagamoyo Road

Hakuna njia ya baisikeli wala watembea kwa miguu

Shoppers Plaza kuna msongamano sana wa watu na hakuna kituo cha mabasi maalum, nguma kupita

Barabara ya magari ni nyembamba magari yanapita baisikeli kwa karibu

Madaraja membamba

Maeneo ya Kawe watu wengi kituoni, ngumu kupita

Page 17: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

4) Mapendekezo yetu

Njia hasa kwa baisikeli, njia hasa kwa watembea kwa miguu, sehemu maalum kwa wafanya biashara bila kuziba njia Linda njia ya baisikeli kutoka magari – mfano karavat, kerbs, nguzo – epuka magari kuendesha na kupaki kwenye njia ya baisikeliNjia na nguzo ziwe pana ya kutosha kwa guta na kwa baisikeli kupitanaNjiani uwezo wa kupita bila kushuka na kupanda tena (misingi njiani, mashimo makubwa, karavat njiani)

Page 18: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

Mapendekezo yetu

Njia ipite nyuma ya vituo vya dala dala Alama kuonyesha njia ya baisikeli iko wapi Drainage kuepuka maji mengi njianiMataa na reflectorsSehemu za kuvuka barabara kwa watembea kwa miguu na wapanda baisikeli (U-turn, zebra)Kama nafasi ipo, miti inayoleta kivuli bila kuziba njia

Page 19: Mkutano wa UWABA na TANROADS Dar es Salaam 24 Mei 2006

5) Ushirikiano

UWABA tunapenda kushirikiana na TANROADS. Tunaweza kuwasaidia: Kufanya savei za barabaraKutoa maoni wakati wa kupanga, kujenga na kurekebisha barabaraKutoa feedback kuhusu hali za barabaraKuhamasisha watu kutumia barabara vizuri

Tunapenda kuendelea kuwasiliana na kutana na TANROADS Dar es Salaam