ofisi ya rais - mwalimu wa kiswahili

13
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA MKOA WA DAR ES SALAAM MTIHANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA SITA 2020 KISWAHILI -2 Msimbo: 121/1 Muda: Saa 3.00 ljumaa, 04 Disemba, 2020 Asubuhi MAELEKEZO 1. Karatasi hii ina maswali nane (8) katika sehemu A na B 1. 2. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali Sehemu A ina alama arobaini (40) na sehemu B ina alama sitini (60) 3. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani A. Andika nanmba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako 5. cha kujibia Mtihani huu una kurasa 3 zilizochapishwa

Upload: others

Post on 01-Jan-2022

20 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MKOA WA DAR ES SALAAM

MTIHANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA SITA 2020

KISWAHILI -2

Msimbo: 121/1

Muda: Saa 3.00 ljumaa, 04 Disemba, 2020 Asubuhi

MAELEKEZO

1. Karatasi hii ina maswali nane (8) katika sehemu A na B 1.

2. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali

Sehemu A ina alama arobaini (40) na sehemu B ina alama sitini (60) 3.

Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani A.

Andika nanmba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako 5. cha kujibia

Mtihani huu una kurasa 3 zilizochapishwa

Page 2: OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili

SEHEMU A: (ALAMA 40) Jibu maswali yote katika sehemu hii

"Hadithi ni utenzi wa fasihi simulizi wenye dhima kubwa kwa jamil" Fafanua bayana Fani ya 1.

Utenzi huu. (hoja tano)

2. Ushairi na ngonjera ni tanzu za fasihi simulizi zenye kufanana na kutofautiana. Bainisha

hoja tatu za kufanana na hona mbili za kutofautiana kwa tanzu hizo.

Fafanua mambo matano (5) muhimu yanayopaswa kuzingatia ili kuwepo kwa uhuru wa 3.

mwandishi wa kazi za kifasihi nchini Tanzania.

Bainisha kwa kutoa mifano dhahiri vipengele vya kisanaa vilivyotumika katika shairi 4.

lifuatalo. Walivyosema wahenga, sifa ya mke tabia

Si kule kuvaa kanga, kwa sura ukavutiya Utuni akijitenga, hadhi yake humpoteya

Sura njema sio pambo, sifa ya mke tabia

Kinompa taadhima, ukinaifu na haya,

Utifu na huruma, hata uhodari piya,

Kigezo cha mke mwema, sifa niliwatajiya,

Sura njema sio pambo, sifa ya mke tabia.

Pia awe mtulivu, asiwe kiruka njiya,

Ufedhuli na uovu, kama yake mazoweya,

Usijipe maumivu, ukiowa utaliya

Sura njema ni kipambo, sifa ya mke tabia.

Awe kama malaika, mzuri kupindukiya,

Tabia zikipotoka, si vizuri kusogeya,

Utakuja fedheheka, tahadhari nakwambiya

Sura njema ni kipambo, sifa ya mke tabia

2

Page 3: OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili

Sehemu B (Alama 60) Jibu maswali matatu (3) kutoka sehemu hii

Swali la tano (5) ni la lazima

ORODHA YA VITABU VYA SWALI LA 5-8

USHAIRI

Uchungu Tamu TheobaldA. Mvungi Fungate ya Uhuru Mohamed.S. Khatibu

Kimbunga Haji Gora Haji

Mapenzi Bora Shaaban Robert

RIWAYA

Kufikirika Shaaban Robert

Mfadhili Hussein Tuwa

Vuta Nkuvute Shafi Adam Shafi

Usiku utakapokwisha- Mbunda Msokile

TAMTHILIA

Kivuli kinaishi Saidi Mohamed

Kwenye ukingo wa Thim Ebrahim Hussein

Nguzo mama Penina Muhando

Morani Emanuel Mbogo

"Ushairi ni msingi mzuri sana wa kujenga jamii yenye maadili mema kwa vizazi nyote" 5. Thibitisha usemi huo kwa kutoa hoja nne kwa kila Diwani katika Diwani mbili ulizosoma.

6. Matumizi ya Taswira katika ushairi huonesha ukomavu na umahiri wa mwandishi. Onesha

ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja nne (4) kwa kila kitabu katika Diwani mbili ulizosoma

"Mtindo ni kipengele muhimu sana katika utanzi wa riwaya kwani hufanya kazi ya 7

mwandishi kufikisha ujumbe aliokusudia kwa jamii lengwa" Thibitisha usemi huu kwa

kutoa vipengele vinne kwa kila kitabu katika riwaya mbili ulizosoma.

Tamthiliya nyingi ni za machungu kutokana na ujumbe mzito unaobebwa kwa jami. 8. Fafanua dai hili kwa kutoa hoja nne zinazodhihirisha machungu kwa kila kitabu kati ya

tamthilia mbili ulizosoma.

3

Page 4: OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili
Page 5: OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili
Page 6: OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili
Page 7: OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili
Page 8: OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili
Page 9: OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili
Page 10: OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili
Page 11: OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili
Page 12: OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili
Page 13: OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili