tra saccos limited ya chama .pdfiii) kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya chama. 10...

42
CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO CHA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA TRA SACCOS LIMITED MASHARTI YA CHAMA (BY-LAWS) (Marekebisho ya Mwaka 2012) S. L. P 63225 DAR-ES-SALAA

Upload: others

Post on 18-Feb-2020

27 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO

CHA

MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA

TRA SACCOS LIMITED

MASHARTI YA CHAMA

(BY-LAWS)

(Marekebisho ya Mwaka 2012)

S. L. P 63225

DAR-ES-SALAA

Page 2: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

I

YALIYOMO Tafsiri ya Maneno ……………………………….. i Sehemu ya Kwanza 1.0 Jina la Chama na utambulisho wake ……… 1 Sehemu ya Pili 2.0 Madhumuni ya Chama ……………………… 2 Sehemu ya Tatu Uanachama 2.0 Kutakua na aina zifuatazo za Uanachama .. 4 3.1 Sifa za Mwanachama ……………………….. 4 3.2 Utaratibu wa Kujiunga ………………………. 5 3.3 Haki na Wajibu wa Mwanachama …………. 6 3.3.1 Haki za Mwanachama ………………….. 6 3.3.2 Wajibu wa Mwanachama ………………. 7 3.4 Kukoma Uanachama ……………………….. 8 3.5 Kusimamishwa/Kufukuzwa Uanachama …. 9 Sehemu ya Nne Kazi za Chama ………………………………….. 11 Sehemu ya Tano Uongozi na Usimamizi wa Chama 5.1 Mkutano Mkuu wa Wanachama ………….. 12 5.2 Bodi ya Chama …………………………….. 12 5.3 Mwenyekiti wa Chama …………………….. 15 5.4 Meneja/Katibu ………………………………. 16 5.5 Kamati ya Usimamizi ………………………. 18 5.6 Uchaguzi wa Bodi na Kamati ya Usimamizi 18 5.7 Sifa za Mgombea …………………………… 19 5.8 Utaratibu wa kuwapata wagombea ……….. 20

Page 3: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

II

5.9 Muda wa Uongozi ………………………….. 21 5.10 Kuacha Uongozi ……………………….. 22 Sehemu ya Sita Mikutano ya Chama 6.1 Mkutano Mkuu wa Mwaka ………………… 24 6.2 Mkutano wa Kawaida ……………………… 25 6.3 Mkutano Maalumu …………………………. 26 6.4 Taarifa ya Mikutano ……………………….. 27 6.5 Mahudhurio …………………………………. 27 6.6 Mkutano wa Tawi …………………………… 28 6.7 Dondoo za Mkutano Mkuu ………………… 29 Sehemu ya Saba Mali na Fedha za Chama 7.1 Mali za Chama …………………………….. 30 7.2 Umiliki ………………………………………. 30 7.3 Fedha ………………………………………. 30 7.4 Utunzaji wa fedha …………………………. 31 Sehemu ya Nane Mwongozo wa Mkopo 8.1 Mahitaji ya jumla …………………………… 32 8.2 Mikopo isiyolipika na ifutwayo ……………. 32 8.3 Taarifa ya mikopo …………………………. 33 Sehemu ya Tisa Mgao wa Ziada 9.1 Matengo ……………………………………. 35 Sehemu ya Kumi Kufutwa kwa Chama 10.1 Utaratibu wa kukifuta Chama …………… 36

Page 4: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

III

TAFSIRI YA MANENO

Tafsiri ifuatayo ya maana na maneno itatumika katika

Masharti haya na kwa kutilia maanani tafsiri ya maneno

kama yalivyoelekezwa kwenye Sheria ya Vyama vya

Ushirika ya mwaka 2003, isipokuwa pale

itakavyosemwa vinginevyo;

“Bodi” inamaanisha Wajumbe saba waliochaguliwa na

Mkutano Mkuu kusimamia uendeshaji wa shughuli za

kila siku za Chama.

“Chama” inamaanisha Chama cha Akiba na Mikopo

cha Mamlaka ya Mapato Tanzania.

“Daftari la Wanachama” inamaanisha orodha ya

Wanachama kama inavyotolewa kutoka kwenye mfumo

wa Komputa.

“Gawio” inamaanisha kiwango kinacholipwa kwa

Wanachama kwa kuwekeza pindi faida inapopatikana.

“Fedha” inamaanisha Shilingi za Kitanzania.

“Fungamano” inamaanisha hitaji ambalo Wanachama

wote wanataka/wanahitaji.

“Mkutano Mkuu” inamaanisha Mkutano wa

Wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo cha

Mamlaka ya Mapato Tanzania kama ilivyoainishwa

kwenye Sheria ya Ushirika Namba 20 ya mwaka 2003

na Kanuni zake za mwaka 2004.

Page 5: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

IV

“Mwanachama” inamaanisha mtu yeyote

atakayekubaliwa na bodi, pamoja na Wanachama wa

Chama cha Akiba na Mikopo cha Mamlaka ya Mapato

Tanzania kuwa Mwanachama na ambaye atakuwa

ametii Katiba na Masharti ya Chama.

“Ruzuku” inamaanisha fedha/mali inayotolewa na

wadau mbalimbali ndani na nje ya Nchi.

“Sheria” inamaanisha sheria ya Vyama vya Ushirika

ya mwaka 2003 (namba 20).

“Tawi” inamaanisha mikoa yote ya Tanzania kama

itambulikavyo na Mamlaka ya Mapato.

“Tozo” inamaanisha malipo yatolewayo na

Mwanachama kama adhabu kwa kutorejesha au

kuchelewesha mkopo.

“Wafanyakazi” inamaanisha watu walioajiriwa na Bodi,

wanaofanya kazi katika Chama cha Akiba na Mikopo

cha Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa niaba ya bodi.

Page 6: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

1

SEHEMU YA KWANZA

1.0 Jina la Chama na utambulisho wake

a) Jina la Chama “TRA SAVINGS AND

CREDIT COOPERATIVE SOCIETY

LIMITED”.

b) Anuani ya chama

S.L.P 63225, Dar-es-Salaam, Simu namba

+255 2864556 0712–494312/ 0752– 494312/

0684 - 557070

c) Tarehe ya kuandikishwa : 19.07.2006

d) Nambari ya Kuandikishwa: DSR 894.

e) Idadi ya Wanachama waliodhamini 9.

f) Eneo la shughuli za Chama litakuwa:

Tanzania.

g) Makao makuu ya Chama yatakuwa: Ghorofa

ya Tano, Jengo la Mariam, Mtaa wa

Shaurimoyo, Ilala.

h) Fungamanisho:MFANYAKAZI MWAJIRIWA/

MSTAAFU/ALIYEACHA KAZI KATIKA

MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA.

i) Kifupi cha jina itakuwa ni TRA SACCOS

LIMITED.

Page 7: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

2

SEHEMU YA PILI

2.0 Madhumuni ya Chama.

Madhumuni ya Chama yatakuwa ni kuinua, kustawisha

na kuboresha hali ya Wanachama wake katika kukidhi

mahitaji mbalimbali ya Kiuchumi na Kijamii kwa kufuata

taratibu za Kidemokrasia, Misingi, Sheria za Vyama vya

Ushirika na Kanuni zake na Masharti ya Chama pamoja

na;

a) Kupokea Hisa, Akiba na Amana kutoka kwa

Wanachama.

b) Kushawishi Wanachama kuweka Akiba na

kununua Hisa kwa kuweka riba juu ya Akiba.

c) Kutoa bidhaa mbalimbali za fedha (financial

products) kwa Wanachama ili waweze kushiriki

zaidi kuimarisha mitaji ya Chama na mitaji yao

binafsi na kuleta mvuto kwa wasio Wanachama

kujiunga na Chama.

d) Kutoa Elimu inayolenga kushawishi na kujenga

tabia ya kuweka Akiba na Amana kwa

Wanachama wake na kuepuka matumizi ya

fedha yasiyo ya lazima miongoni mwa

Wanachama.

e) Kujenga tabia ya kujitegemea kwa Wanachama

wake.

Page 8: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

3

f) Kujenga tabia ya uaminifu kati ya Wanachama

wake.

g) Kusaidia maendeleo ya jamii.

h) Kushawishi Watu na Vikundi mbalimbali kujiunga

na Chama.

Page 9: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

4

SEHEMU YA TATU

UANACHAMA

3.0 Kutakuwa na aina zifuatazo za Uanachama

a) Wanachama wote waliojiandikisha wakati wa

kuomba kuandikishwa kwa Chama katika daftari

la Chama (Waanzilishi).

b) Wanachama wapya, waliojiunga baada ya

kutimiza masharti ya Chama ambao ni waajiriwa

wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

c) Mwanachama ambaye ameamua kuendeleza

Uanachama katika Chama baada ya kustaafu,

kuacha au kuachishwa kazi katika Mamlaka ya

Mapato Tanzania na kuendelea kutoa michango

yake ya kila mwezi.

d) Vikundi vilivyomo ndani ya Mamlaka ya Mapato

Tanzania ambavyo vimesajiliwa kisheria.

3.1 Sifa za Mwanachama.

a) Awe ametimiza umri wa miaka 18.

b) Awe na akili timamu.

c) Awe wa kuaminika na kufahamika na

wanachama wenzake.

d) Awe Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato

Tanzania

Page 10: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

5

aliyeajiriwa/aliyestaafu/aliyeacha/kuachishwa

kazi.

e) Awe tayari kushiriki kikamilifu katika shughuli

zote za Chama.

f) Asiwe na shughuli binafsi zinazofanana na

shughuli za Chama.

g) Awe amelipa kiingilio na kununua kima cha chini

cha Hisa.

h) Awe tayari kufuata sheria ya Vyama vya Ushirika

Na. 20 ya Mwaka 2003 na Marekebisho yake

pamoja na Kanuni za Ushirika za Mwaka 2004

na Masharti ya Chama.

3.2 Utaratibu wa Kujiunga

a) Mwombaji atatakiwa ajaze Fomu ya maombi ya

Uanachama inayopatikana ofisini na kutuima

kwa Mwenyekiti.

b) Mwombaji atakubaliwa kuwa Mwanachama

baada ya kupitishwa na wingi wa kura za

Wajumbe wa Bodi waliohudhuria Kikao, lakini

hatakuwa Mwanachama hadi atakapolipa ada ya

kiingilio na kununua kiwango cha chini cha Hisa

kilichokubaliwa na Wanachama.

c) Mwanachama akishathibitishwa na Mkutano

Mkuu jina lake litaorodheshwa kwenye daftari la

Uanachama.

Page 11: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

6

3.3 Haki na Wajibu wa Mwanachama

3.3.1 Haki za Mwanachama

a) Kupiga na kupigiwa kura kuwa Kiongozi.

b) Kuhudhuria Mikutano ya Chama.

c) Kusikilizwa na kutoa maoni.

d) Kuomba kuitisha Mkutano Mkuu kwa mujibu wa

Masharti ya Chama na Sheria ya Ushirika Na. 20

ya Mwaka 2003 pamoja na Kanuni zake za

Mwaka 2004.

e) Kushiriki katika shughuli zote za Chama.

f) Kuweka na kutoa Amana, Akiba na Hisa zake

kwa kufuata kanuni za Chama.

g) Kupatiwa Mikopo kwa ajili ya kuongeza tija na

maendeleo ya kijamii.

h) Kuwa Mdhamini wa Mkopo wa Mwanachama

mwingine.

i) Kusoma taarifa za Mikutano ya Chama, Mizania,

Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, katika

ofisi ya Chama katika nyakati za saa za kazi.

j) Kujitoa Uanachama.

k) Kukata rufaa.

Page 12: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

7

l) Kumiliki kiasi chochote cha Hisa, ilimradi tu

hataruhusiwa kumiliki zaidi ya asimilia 20 ya

Hisa zote za Chama.

m) Kupatiwa Cheti cha Hisa mara baada ya

kununua Hisa zinazokubalika na Chama.

n) Kuchagua Mrithi.

3.3.2 Wajibu wa Mwanachama

a) Kutii Sheria za Chama, Kanuni na Miongozo

yake kama ilivyokubaliwa na Wanachama wote.

b) Kulipa ada ya kiingilio, kununua Hisa na kulipa

ada zozote zitakazokuwa zimeamuliwa na

Wanachama kwenye Mkutano Mkuu.

c) Kushiriki katika shughuli za kiuchumi za Chama

kama zilivyoainishwa kwenye Sera za Chama.

d) Kuhudhuria Mikutano ya Chama.

e) Kuchagua Viongozi wa Chama.

f) Kutii maamuzi ya Mkutano Mkuu.

g) Kulinda na kutunza Mali za Chama.

h) Kudhamini Chama pale inapohitajika.

i) Kubeba dhamana ikiwa janga lolote litatokea.

Dhamana hiyo kikomo chake ni kiasi cha Hisa

alizonazo kwenye Chama.

Page 13: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

8

j) Kuchagua Warithi wao.

k) Kulipa madeni aliyonayo ndani ya Chama kwa

wakati uliopangwa.

l) Kulipa mkopo alioudhamini endapo mkopaji

atashindwa kulipa mkopo wake bila sababu za

msingi.

m) Kuwa na angalau kiwango cha chini cha Hisa

kwa mujibu wa Masharti ya Chama.

n) Kuweka Akiba mara kwa mara.

o) Kutoa taarifa kwenye Uongozi wa Chama iwapo

Mtumishi au Kiongozi anatoa huduma kwa

upendeleo, au anatoa au kupokea rushwa.

3.4 Kukoma Uanachama

Mwanachama atakoma Uanachama kutokana na

miongoni mwa sababu zifuatazo;

a) Kifo.

b) Akiwa na Ugonjwa wa Akili uliothibitika.

c) Akipatikana na hatia ya jinai ambayo

itasababisha afungwe jela.

d) Kutohudhuria Mikutano ya Chama mara tatu

mfululizo bila sababu za msingi.

Page 14: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

9

e) Kufukuzwa Uanachama na theluthi mbili (2/3) ya

Wanachama waliohudhuria katika Mkutano

Mkuu wa Chama baada ya kupewa nafasi ya

kujitetea.

f) Kujiuzulu kwa Hiari yake.

g) Kwa sababu zozote zilizomo kwenye Kanuni za

Ushirika za Mwaka 2004 kifungu cha 25.

3.5 Kusimamishwa/Kufukuzwa Uanachama

a) Kwa mujibu wa Masharti ya Chama, Bodi ya

Chama itawasilisha kwenye Mkutano Mkuu

majina ya Wanachama ambao kwa nyakati

tofauti wataonekana kutenda makosa ambayo

yanaenda kinyume na Kanuni na Taratibu za

Chama kama ifuatavyo;

i) Kutoheshimu na kutotekeleza maamuzi

ya Mikutano Mikuu na vikao vya Bodi ya

Chama.

ii) Kutolipa Hisa na ada mbalimbali za

Chama baada ya kupewa muda

uliokubaliwa na Mkutano.

iii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na

kutozingatia maadili ya Chama.

Page 15: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

10

iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za

Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

Kanuni na Sera za Chama.

v) Kubainika kutoa au kupokea rushwa

katika utekelezaji wa shughuli za Chama.

vi) Wizi.

vii) Sababu zozote zilizomo katika kifungu

cha 26 cha Kanuni za Ushirika za Mwaka

2004.

b) Kusimamishwa au kufukuzwa kwa Mwanachama

kutafanywa na Mkutano Mkuu ambapo

Wanachama waliohudhuria wasiopungua theluthi

mbili (2/3) watatoa uamuzi huo baada ya

mhusika kutoa utetezi wake.

Mwanachama aliyejiuzulu au kufukuzwa

Uanachama anaweza kujiunga tena kwa kuomba

upya na taratibu za kujiunga na Chama

zitazingatiwa.

Page 16: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

11

SEHEMU YA NNE

KAZI ZA CHAMA

4.1. Kuandikisha Wanachama.

4.1.1. Kuandaa taarifa zifuatazo na kuzituma kwa

Mkaguzi wa nje ndani ya miezi mitatu (3) baada

ya kufunga mwaka wa fedha kwa mujibu wa

Sheria na Kanuni za Ushirika;

a) Hesabu zinazoonyesha mapato na matumizi.

b) Hesabu za mtiririko wa fedha.

c) Urari wa Chama.

4.2. Kuweka wazi taarifa za Hesabu za Chama kila

mwaka kwa Mwanachama yeyote atakayekuwa

anahitaji kupata taarifa juu ya utendaji wa Chama

katika muda wa saa za kazi.

Page 17: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

12

SEHEMU YA TANO

UONGOZI NA USIMAMIZI WA CHAMA

5.1 Mkutano Mkuu wa Wanachama

Kutakuwa na Mkutano Mkuu wa Wanachama wote

ambao ndicho chombo cha juu cha maamuzi juu ya

utendaji wa shughuli za Chama. Kwa mujibu wa

Sheria ya Ushirika ya Mwaka 2003 na Kanuni zake

za Mwaka 2004, Mkutano Mkuu utachagua Bodi ya

Chama yenye Wajumbe wasiopungua watano na

wasiozidi tisa ili kuendesha na kusimamia shughuli

za kila siku za Chama.

5.2 Bodi ya Chama

Kutakuwa na Bodi yenye wajumbe saba (7). Bodi

itachagua Wajumbe watatu miongoni mwao kuwa

Wajumbe wa Kamati ya Mikopo.

Kazi za Bodi:

a) Kusimamia shughuli za Chama kidemokrasia

kwa kutilia maanani mipango na njia za

kushirikiana baina ya Wanachama.

b) Kufanikisha mahitaji ya kiuchumi na kijamii

ya Wanachama.

c) Kutoa elimu ya Ushirika kwa Wanachama.

Page 18: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

13

d) Kuandaa miongozo sahihi ya fedha za

Chama zitakazosaidia kuwepo na taarifa

sahihi za mahesabu ya Chama.

e) Kuandaa Sera muhimu za Chama, kama vile

Sera ya Mikopo na kuwasilisha kwenye

Mkutano Mkuu kwa ajili ya kuidhinishwa.

f) Kuhakikisha hesabu za Chama zinaandaliwa

na kupitiwa na Mkaguzi wa Nje kwa mujibu

wa Sheria ya Ushirika, Kanuni za Ushirika na

Masharti ya Chama.

g) Kuwasilisha kwenye Mkutano Mkuu wa

Chama hesabu zilizokaguliwa na Mkaguzi

wa Nje.

h) Kuandaa makisio ya mapato na matumizi ya

Chama kwa mwaka unaofuata na

kuwasilisha kwenye Mkutano Mkuu kwa ajili

ya kuidhinishwa.

i) Kuwezesha ukaguzi wa vitabu kwa wakaguzi

wa ndani na nje kama walivyoidhinishwa na

Mkutano Mkuu na kwa mujibu wa Sheria ya

Ushirika.

j) Kuhakikisha mikopo inaainisha dhumuni la

mkopo husika.

Page 19: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

14

k) Kuhakikisha Sera za Chama na Mikataba

inatolewa kwa kuzingatia shughuli za

Chama.

l) Kuandaa mikataba na miongozo ya kazi na

masuala yahusuyo Wafanyakazi.

m) Kuajiri Meneja/Katibu na Wafanyakazi

wengine wa Chama kwa mikataba endelevu

ya kila baada ya miaka mitatu.

n) Kumsimamisha Mjumbe yeyote wa Bodi

asiyetii matakwa ya Sheria na Masharti

akisubiri maamuzi ya Mkutano Mkuu.

o) Kuhakikisha ufunguzi na kuendesha akaunti

ya Chama.

p) Kutunza kitabu cha Rejista ya Wanachama.

q) Kutunza kitabu cha Rejista ya mahudhurio ya

Wajumbe wa Bodi

r) Kutunza dondoo za Mikutano ya Chama.

s) Kuandaa mipango endelevu ya Chama,

mpango wa biashara na kuhakikisha

utekelezaji wake kwa kipindi husika.

t) Kuandaa miongozo ya uongozi wa ndani ya

Chama na namna ya kutoa ripoti.

Page 20: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

15

u) Kuhakikisha ina uwezo wa kujua kazi za kila

siku za Meneja/Katibu na Wafanyakazi pia

kusimamia akaunti ya chama.

v) Kusaini cheki za Chama.

5.3 Mwenyekiti wa Chama

Mwenyekiti wa Chama atakuwa na majukumu

yafuatayo:

a) Kuwa msemaji Mkuu wa Chama.

b) Kuongoza Mikutano Mikuu ya Chama

(isipokuwa Mkutano Mkuu Maalum

ulioitishwa na Mrajisi na Kamati ya

Usimamizi).

c) Kuongoza vikao vya Bodi.

d) Kuweka sahihi pamoja na Katibu kwenye

Mikataba kwa niaba ya Chama kwa

kuzingatia matakwa ya Sheria na Kanuni za

Vyama vya Ushirika.

e) Kuwakilisha Chama katika Taasisi/Asasi

mbalimbali ndani na nje ya Nchi.

Page 21: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

16

5.4 Meneja/Katibu

Kutakuwepo Meneja ambaye ataajiriwa na Bodi na

atakuwa na kazi zifuatazo:

a) Kusaidia Majukumu ya Mwenyekiti.

b) Kusimamia kazi za kila siku za Chama

zinazofanywa na Wafanyakazi wengine.

c) Kuandaa malipo ya Mishahara ya

Wafanyakazi na kuwasilisha kwa Bodi kwa

ajili ya kuidhinishwa.

d) Kutoa taarifa za utendaji wa shughuli za

Chama kwa Bodi.

e) Kuandaa au kuhakikisha inaandaliwa taarifa

ya maendeleo ya Chama, hesabu za Chama

za kila mwezi na taarifa nyinginezo muhimu

ambazo zitasaidia Bodi kulinganisha makisio

ya mwaka na matumizi yaliyotumika na pia

kutoa maamuzi sahihi.

f) Kuandaa Hesabu za chama za mwisho wa

mwaka na kuziwakilisha kwa Bodi pamoja na

kwa Mkaguzi wa Nje.

g) Kuhakikisha vitabu vinaandikwa kwa usahihi

na kuhakikisha mali za kudumu zinarekodiwa

kwenye vitabu husika.

Page 22: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

17

h) Kuhusika na upokeaji wa Hisa kwa

Wanachama na kutoa Cheti cha Umiliki

i) Kutunza vizuri mali za Chama.

j) Kuwa Katibu wa Mikutano yote ya Chama.

k) Kutunza kitabu cha majina ya Wanachama

na taarifa zao muhimu.

l) Kusaini nyaraka na mikataba ya Chama kwa

niaba ya Chama.

m) Kuandaa mpango mkakati wa Chama na

kuwasilisha kwa Bodi ya Chama kwa ajili ya

kuidhinishwa.

n) Kusimamia utekelezaji wa mpango mkakati

ulioidhinishwa na Mkutano Mkuu.

o) Kutoa mapendekezo ya marekebisho ya

Masharti na Sera za Chama.

p) Kutunza taarifa za Wanachama na

Wafanyakazi wa Chama.

q) Kufanya kazi nyingine zozote kama itakavyo

amuliwa na Bodi.

Page 23: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

18

5.5 Kamati ya Usimamizi

Kutakuwa na Kamati ya Usimamizi yenye wajumbe

watatu (3) ambao hawatokani na Wajumbe wa Bodi

ya Chama.

Kazi za Kamati ya Usimamizi:

a) Kuhakikiksha kwamba, Bodi, Kamati na

Wafanyakazi wa Chama wanafuata Sheria,

Masharti na Sera za Chama.

b) Kuhakikisha hesabu za Chama na vitabu

vingine vya Chama ikihusisha vitabu vya

Wanachama na Daftari la Wanachama

vinatunzwa vizuri.

c) Kupokea na kupitia taarifa za Mkaguzi wa

Ndani.

d) Kutoa ushauri kwa Bodi na Wafanyakazi wa

Chama, juu ya utekelezaji bora wa shughuli

za Chama na kutoa taarifa kwenye Mkutano

Mkuu wa Chama.

5.6 Uchaguzi wa Bodi na Kamati ya Usimamizi

a) Uchaguzi wa Bodi utafanyika kwa mujibu wa

kifungu cha 63 (1-6) cha Sheria ya Vyama

vya Ushirika Na.20 ya mwaka 2003 na

Page 24: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

19

Kanuni za Vyama vya Ushirika za Mwaka

2004 kifungu cha 78.

b) Kila Mwanachama kwenye Mkutano Mkuu

atakuwa na haki ya kupiga kura moja kwa

kila nafasi ya uongozi.

5.7 Sifa za Mgombea

Mwanachama anayetaka kugombea uongozi katika

Chama itabidi azingatie maadili ya Uongozi kwa mujibu

wa kifungu Na.125 cha Sheria ya Vyama vya Ushirika

Na.20 ya Mwaka 2003.

Sifa za kugombea:

a) Awe na upeo na elimu ya kutosha kuweza

kuongoza Chama kulingana na mabadiliko ya

hali ya uchumi wa nchi.

b) Awe ni mfuatiliaji wa shughuli za Chama kwa

kutekeleza wajibu wake katika Chama na kwa

kuzingatia Sheria ya Vyama vya Ushirika,

Kanuni na Masharti ya Chama.

c) Awe ni mtu mwenye ari ya kutoa mchango wake

wenye nia ya kuendeleza Chama endapo

atachaguliwa kuwa Kiongozi.

d) Awe na ufahamu wa shughuli za Ushirika.

Page 25: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

20

e) Awe mwaminifu na si mpenda kupokea wala

kutoa rushwa.

f) Awe ni mtu ambaye hajawahi kuenguliwa katika

uongozi katika Chama chochote cha Ushirika

kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.

g) Awe Mwanachama hai kwa kulipa kiingilio na

Hisa zote zinazotakiwa kwa mujibu wa Masharti

ya Chama.

h) Awe anashiriki kikamilifu katika shughuli za

Chama.

i) Awe ni Mwanachama katika kipindi

kisichopungua mwaka mmoja.

5.8 Utaratibu wa kuwapata Wagombea wa Uongozi

wa Chama

Itakapofika wakati wa uchaguzi Mrajis (Registrar) wa

Vyama vya Ushirika nchini atateua Afisa wa uchaguzi

kusimamia uchaguzi wa viongozi wa Chama kulingana

na maadili ya uongozi kwa mujibu wa kifungu Na.125

cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Na.20 ya mwaka

2003.

Page 26: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

21

Mwenyekiti wa Chama atatoa tangazo la kufanyika

uchaguzi ambalo litabandikwa katika mbao za

matangazo zilizopo kwenye ofisi za Chama na katika

Matawi yote ya Chama. Tangazo hilo litaeleza tarehe ya

uchaguzi, nafasi zinazogombewa, sifa za Wagombea

katika kila nafasi, tarehe ya kuchukua na kurudisha

fomu za maombi na mahali pa kurudisha fomu hizo

baada ya kujazwa.

5.9 Muda wa Uongozi

a) Muda wa Uongozi utakuwa ni miaka tisa (9)

tu.

b) Kama kutatokea nafasi wazi ya uongozi

kabla ya kumalizika muda huo wa miaka tisa

(9) Bodi itateua Mwanachama mwenye sifa

kujaza nafasi hiyo hadi Mkutano Mkuu

utakapothibitisha uteuzi huo kuwa

madarakani katika kipindi kitakachokuwa

kimebakia.

c) Kila baada ya miaka mitatu theluthi moja

(1/3) ya wajumbe wa Bodi itapigiwa kura ya

kuondoka madarakani, mwaka wa sita nusu

(1/2) ya wajumbe ambao walibaki itapigiwa

Page 27: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

22

kura ya kuondoka madarakani. Wajumbe

walioondoka madarakani hawataruhusiwa

kugombea hadi miaka mitatu ipite. Katika

mwaka wa tisa nusu (1/2) itakayobakia

itapigiwa kura ya kuondoka madarakani na

hawataruhusiwa kugombea hadi miaka

mitatu kupita. Kuondoka kwa Wajumbe hao

kutaruhusu kufanyika uchaguzi wa kuziba

nafasi zao, hii ni kwa mujibu wa kifungu cha

63(1-6) cha Sheria Na.20 ya mwaka 2003.

5.10 Mjumbe wa Bodi na Kamati ya Usimamizi

ataacha kuwa Mjumbe wa Bodi/Kamati iwapo:

a) Litatokea tukio lolote lililo orodheshwa kwenye

vifungu 3.3 na 3.4 vya Masharti ya Chama.

b) Atafanya biashara inayofanywa na Chama.

c) Atafukuzwa na Mkutano Mkuu kwa vitendo vya

kwenda kinyume na maadili ya uongozi baada

ya kupewa nafasi ya kujitetea.

d) Atajiuzulu kwa hiari kwa kutoa taarifa ya siku

zisizopungua thelathini.

e) Atashindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo bila

ya sababu inayokubaliwa na Bodi.

Page 28: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

23

f) Atastaafu baada ya muda wa Uongozi

kukamilika kwa mujibu wa Sheria.

Page 29: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

24

SEHEMU YA SITA

MIKUTANO YA CHAMA

Kutakuwa na aina zifuatazo za Mikutano:

a) Mkutano Mkuu wa Mwaka.

b) Mkutano wa Kawaida.

c) Mkutano Maalum.

d) Mkutano wa Tawi.

6.1 Mkutano Mkuu wa Mwaka

a) Maamuzi ya Chama, yatakuwa yanaamuliwa

kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama.

Mkutano mkuu wa Mwaka wa Wanachama

utafanyika ndani ya siku thelathini (30) tangu

baada ya kupokea taarifa ya Ukaguzi wa Chama

toka kwa Mkaguzi wa nje lakini si zaidi ya siku

mia na themanini (180) baada ya mwaka wa

fedha kuisha, Mwanachama yeyote aliyetimiza

matakwa ya Masharti ya Chama na Katiba ya

Chama ana haki ya kuhudhuria.

b) Yatakayo zungumzwa kwenye Mkutano Mkuu ni

pamoja na:

i. Kupokea na kukubali taarifa ya Hesabu

za Chama, ripoti ya Viongozi na Kamati

ya Usimamizi na taarifa nyingine zozote

muhimu.

ii. Kuidhinisha gawio endapo kuna ziada.

Page 30: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

25

iii. Kuidhinisha posho kwa Watendaji ambao

hawalipwi mshahara kwa Mujibu wa

Sheria.

iv. Kupokea na kuidhinisha makisio ya

Mapato na Matumizi ya Mwaka wa fedha

unaofuata.

v. Kupokea na kuidhinisha Mpango Mkakati

wa Chama na utekelezaji wake.

vi. Kuidhinisha shughuli zozote ambazo

Bodi ya Chama inadhani zinahitaji

maamuzi ya Wanachama wote.

6.2 Mkutano wa Kawaida

a) Chama kitakuwa na Mkutano wa Kawaida mara

moja kwa Mwaka, na itakuwa kati ya Mwezi

Septemba na Desemba.

b) Yatakayozungumzwa kwenye Mkutano wa

Kawaida ni pamoja na:

i. Kupendekeza Wajumbe wa Bodi kama

ambavyo Sheria na Kanuni za Vyama

vya Ushirika zinavyoelekeza na pia

kuchagua Kamati ya Usimamizi ya

Wajumbe 3 ambao sio Wajumbe wa

Bodi.

Page 31: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

26

ii. Kurekebisha Katiba, Masharti na Sera

pale inapohitajika.

iii. Kuchagua, kufukuza au kumwondoa

Mjumbe yeyote wa Bodi.

iv. Kuidhinisha manunuzi au mauzo ya Mali

zinazohamishika na zisizohamishika za

Chama.

v. Kupitia na kukubali Mpango Mkakati wa

Chama.

vi. Kuidhinisha Mikataba na Makubaliano.

c) Bila kuangalia vipengele (a) na (b) hapo juu,

mambo yatakayozungumzwa kwenye Mkutano

wa Kawaida yanaweza kuzungumzwa kwenye

Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama kama

yalivyoelekezwa kifungu 6.1 (b).

6.3 Mkutano Maalumu

a) Mkutano Maalumu unaweza kufanyika pale

ambapo angalau moja ya tatu ya Wanachama

kwa maandishi wataomba kufanya Mkutano

Maalumu wa Chama na lazima watume nakala

kwa Mrajis wa Ushirika.

b) Mrajis au yoyote atakayechaguliwa na Mrajis

anaweza kuongoza Mkutano Maalumu wa

Page 32: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

27

Wanachama, sehemu na muda ambao Mrajis

atapanga.

c) Mkutano Maalumu utakuwa na agenda maalum

moja.

6.4 Taarifa ya Mikutano

a) Taarifa ya Maandishi ya angalau siku ishirini na

moja (21) itatolewa kwa Mkutano Mkuu wa

Mwaka na Mkutano wa Kawaida na taarifa ya

siku saba (7) itatolewa kwa Mkutano Maalum wa

Chama kwa njia ya matangazo, barua au

vinginevyo.

b) Taarifa itaelezea madhumuni ya Mkutano na

agenda za Mkutano zitatumwa kwa kila

Mwanachama.

c) Kushindwa kupata taarifa kwa wakati muafaka

kwa Mwanachama haitakuwa kigezo cha yeye

kuharibu yatakayo zungumzwa kwenye

Mkutano.

6.5 Mahudhurio

a) Mahudhurio yanayohitajika kwa ajili ya Mikutano

ya Wanachama ni asilimia hamsini (50%) ya

Wanachama au Wanachama 50 wa Chama, kwa

idadi yeyote iliyondogo.

Page 33: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

28

b) Kama mahudhurio hayatafikiwa Kwa Mikutano

ya Wanachama basi Mkutano huo utaahirishwa

kwa siku saba (7). Kama Mkutano utaahirishwa

na baada ya siku saba kama mahudhurio

hayatatimia basi Mkutano huo utafutwa.

c) Mkutano Maalumu unaoongozwa na Mrajis

utafanyika kwa idadi yoyote ya Wanachama

watakaohudhuria na maamuzi yatakayofikiwa

yatachukuliwa kuwa maamuzi ya Wanachama

wote.

d) Mwenyekiti wa Chama ataendesha Mikutano

yote ya Chama, iwapo Mwenyekiti hayupo,

Makamu wake ataendesha Mikutano na iwapo

wote hawapo kwa muda wa dakika 30,

Mwanachama yeyote katika waliohudhuria

atachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa muda na

ataongoza Mkutano huo.

6.6 Mkutano wa Tawi

6.6.1 Kutakuwa na Mikutano minne ya Tawi (Kila robo

mwaka) ambao utahudhuriwa na Wanachama wote wa

Tawi husika.

Mambo yafuatayo yatajadiliwa kwenye Mkutano wa

Tawi:

a) Kupokea na kupitia taarifa za Bodi ya Chama na

Maazimio ya Mkutano Mkuu kwa utekelezaji.

Page 34: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

29

b) Kutoa maoni na kuwasilisha mapendekezo

mbalimbali yanayohusu shughuli za Chama

katika Tawi na kuyapeleka kwenye Bodi ya

Chama ili yajadiliwe kwenye Mikutano Mikuu ya

Chama.

c) Kuchagua Viongozi wa Tawi iwapo waliopo

muda wao umekwisha/wamehama na uchaguzi

huo utasimamiwa na Mwenyekiti wa Chama au

Mjumbe wa Bodi ya Chama.

d) Viongozi wa Tawi wataongoza kwa kipindi cha

miaka miwili.

6.6.2 Taarifa za Mikutano ya Tawi zitatolewa siku 14

kabla ya Mkutano.

6.7 Dondoo za Mkutano Mkuu

a) Mambo yote yatakayozungumzwa na kuamuliwa

kwenye Mkutano Mkuu yataandikwa na

kuhifadhiwa kwenye kitabu maalumu mara

baada ya kuidhinishwa kwenye Mkutano

unaofuata na Mwenyekiti pamoja na Katibu.

b) Nakala ya dondoo baada ya kuidhinishwa

zitatumwa kwa Mrajis.

Page 35: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

30

SEHEMU YA SABA

MALI NA FEDHA ZA CHAMA

7.1 Mali za Chama

Mali za Chama zitahusisha mali zote

zinazohamishika na zisizohamishika za Chama

ambazo Chama itazinunua kila inapohitaji.

7.2 Umiliki

Mali za kudumu na nyinginezo za Chama

zitamilikiwa na Chama.

7.3 Fedha

Fedha za Chama zitahusisha:

a) Ada ya viingilio, na uuzwaji wa vitabu.

b) Uuzaji wa Hisa.

c) Akiba na Amana.

d) Ruzuku.

e) Tozo za adhabu.

f) Faida.

g) Bima ya mkopo.

h) Njia nyinginezo halali ambazo Bodi itaona

zinafaa.

Page 36: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

31

7.4 Utunzaji wa fedha.

Fedha zote za Chama zitatunzwa katika Benki

itakayo amuliwa na Bodi ya Chama kwa niaba ya

Chama .

7.5 Mwaka wa fedha.

Mwaka wa fedha wa Chama utakuwa kuanzia

Januari 1 mpaka Disemba 31 kila mwaka.

7.6 Upokeaji wa fedha.

Karani/Mtunza Hazina wa Chama ndiye

atakayekuwa na mamlaka ya kupokea na kutoa

risiti za Chama kwa kusimamiwa na ofisa wa

fedha/Mhasibu na Meneja.

Page 37: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

32

SEHEMU YA NANE

MWONGOZO WA MKOPO

8.1 Mahitaji ya Jumla ya Mwongozo wa Mkopo

Sera ya Mikopo inaainisha njia zote za namna ya

kutoa na urejeshwaji wa Mikopo, na yafuatayo

yatazingatiwa:

a) Hakuna Mwanachama atakayepatiwa mkopo

mpaka pale atakapokua amenunua Hisa

zinazohitajika na kwa msingi wa Masharti ya

Chama.

b) Hakuna Mkopo utakaotolewa zaidi ya mara

tatu ya AKIBA/AMANA za Mwanachama.

c) Ukomo wa juu wa kukopa kwa Mwanachama

na Chama, vitapangwa kwenye Mkutano

Mkuu wa Chama.

d) Faida na adhabu juu ya Mkopo itakuwa kama

ambavyo imeamuliwa na Mkutano Mkuu na

ambavyo sera ya Chama inaonyesha.

e) Muda wa juu wa kurejesha Mkopo

utaamuliwa na Mkutano Mkuu na ambavyo

Sera za Chama zinavyoonyesha.

8.2 Mikopo isiyolipika na ifutwayo.

a) Endapo mkopo au kiasi cha mkopo utakuwa

haujalipwa kwa siku zaidi ya tisini (90) kama

ambavyo ilikuwa imekubaliwa kwenye fomu

ya marejesho, Chama kitafuta mkopo kwa

Akiba na Amana za muhusika zilizowekwa

Page 38: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

33

kama dhamana na itaendelea kukusanya

mali yoyote iliyowekwa kama dhamana.

b) Endapo kiasi chochote kitakuwa hakijalipwa

kwa zaidi ya mwaka mmoja, mkopo huo

utafutwa kwa kupunguza akaunti ya madeni

mabaya/hatari.

c) Malipo yeyote yatakayopatikana baada ya

mkopo kufutwa, yatapokelewa kama faida ya

ziada na itapelekwa kwenye tengo la lazima.

d) Chama kitatenga matengo ya mikopo

iliyocheleweshwa kama ifuatavyo:

i. Siku 0 – 30 mkopo uliocheleweshwa =

1% ya mkopo na ufuatiliaji wa hali ya juu.

ii. Siku 31 – 180 mkopo uliocheleweshwa =

30% ya kiasi cha mkopo unaodaiwa.

iii. Siku 181 – 365 mkopo uliocheleweshwa

= 50% ya kiasi cha mkopo unaodaiwa.

iv. Zaidi ya siku 365 = 100% ya mkopo

unaodaiwa.

Mkopo unaodaiwa kwenye tengo hili utapatikana

kwa kutoa kiasi chote cha mkopo unaodaiwa

kwa Akiba na Amana zilizowekwa na

Mwanachama kama dhamana ya mkopo huo.

Page 39: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

34

8.3 Taarifa ya mikopo

Chama kitaandaa na kutoa taarifa za shughuli za

mikopo. Taarifa hiyo itahusisha pamoja na

mambo mengine:

a) Jina la Mwanachama.

b) Tarehe mkopo ulipochukuliwa.

c) Kiasi alichokopa na kiasi anachodaiwa.

d) Namna ya marejesho na riba juu yake.

e) Kiasi ambacho kinadaiwa/kilichopitisha muda

wa marejesho.

f) Majina ya Wadhamini na Dhamana

zilizowekwa.

Taarifa itakaguliwa na kusainiwa na

Katibu/Meneja na kuidhinishwa na Kamati ya

Mikopo.

Page 40: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

35

SEHEMU YA TISA

MGAO WA ZIADA

9.1 Matengo

Ziada itakayopatikana mara baada ya Taarifa ya

fedha za Chama kupitiwa na Mkaguzi wa nje na

kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Chama, salio

la ziada litagawanywa kama ifuatavyo:

a) 20% ya ziada itapelekwa kwenye tengo la

lazima.

b) 15% ya ziada itapelekwa kwenye tengo la

madeni mabaya ilimradi tengo hilo lisizidi

asilimia 15% ya madeni yote za Chama.

c) 15% ya ziada itapelekwa kwenye tengo la

kukombolea Hisa ilimradi tengo hilo lisizidi

asilimia 15% ya Hisa zote za Chama.

d) 10% ya ziada itapelekwa kwenye tengo la

Elimu ya Ushirika na mafunzo mbalimbali.

e) Kiasi kinachobaki kitagawiwa kama ambavyo

Mkutano Mkuu utakavyoamua.

Page 41: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

36

SEHEMU YA KUMI

KUFUTWA KWA CHAMA.

10.1 Utaratibu ufuatao utatumika kukifuta Chama:

a) Chama kinaweza kufutwa kwa maombi ya

zaidi ya robo tatu ya Wanachama kwenye

Mkutano Maalumu ulioitishwa kwa ajili ya

hitaji hilo na dondoo za Mkutano huo

zitatumwa kwa Mrajis na Wanachama.

b) Baada ya kukamilisha njia za kufuta

uandikishwaji wa Chama, Mrajis atatoa

taarifa ikiwataka wale wote wanaokidai

Chama watoe taarifa kwake au kwa Mfilisi wa

Chama ndani ya mwezi mmoja.

c) Mufilisi atachukua jukumu la kumiliki vitabu

vya Chama ili kuweza kukifuta Chama.

d) Mufilisi ataendelea kushughulikia kuwajua

wanaokidai na wanaodaiwa na Chama tangu

suala la kufuta uandikishwaji wa Chama

uanze na pia atahakikisha anafahamu kiasi

walichochangia Wanachama waliopo na

waliopita katika mtaji wa Chama.

e) Mufilisi atatoa taarifa kwa Mrajis kama

ambavyo Mrajis atataka ikionesha hatua

aliyofikia katika kukifuta Chama.

f) Kiasi chochote cha fedha kitakachopatikana

katika shughuli ya kukifuta Chama kitawekwa

Benki ambayo Mrajis ataamua.

g) Mufilisi baada ya kukusanya madeni ya

Chama na kutoa matumizi ya kukifuta

Page 42: TRA SACCOS LIMITED ya chama .pdfiii) Kuwa mgomvi,mwenye matusi na kutozingatia maadili ya Chama. 10 iv) Kushindwa kufuata Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya Chama,

37

Chama na kujua kiasi walichochangia

Wanachama wa zamani na waliopo katika

mtaji wa Chama na mara baada ya kulipa

wanaokidai Chama, atakifuta Chama na

kuwakilisha taarifa kwa Mrajis.

h) Mrajis atapanga muda wa Mufilisi

kukamilisha kazi.