ufunuowayohana - ebible.org · ufunuowayohana2:3 3 ufunuowayohana2:13 najua kwamba huwezi...

40
UFUNUO WA YOHANA 1:1 1 UFUNUO WA YOHANA 1:10 UFUNUO WA YOHANA 1 Hizi ni habari za mambo ambayo yalifunuliwa na Yesu Kristo. Mungu alimpa Kristo ufunuo huu ili awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo yanapaswa kutukia kari- buni. Kristo alimtuma malaika wake amjulishe Yohane, mtumishi wake, mambo hayo, 2 naye Yohane, ameyasema yote aliyoyaona. Na hii ndio taarifa yake kuhusu ujumbe wa Mungu na ukweli uliofunuliwa na Yesu Kristo. 3 Heri yake mtu anayesoma kitabu hiki; heri yao wale wanaosik- iliza maneno ya ujumbe huu wa kinabii na kushika yaliyoandikwa humu, maana wakati umekaribia ambapo mambo haya yatatukia. 4 Mimi Yohane nayaandikia makanisa yaliyoko mkoani Asia. Nawatakieni neema na amani kutoka kwake yeye aliyeko, aliyekuwako na anayekuja; na kutoka kwa roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi, 5 na kutoka kwa Yesu Kristo, shahidi mwaminifu, wa kwanza kufufuliwa kutoka wafu, na am- baye ni mtawala wa wafalme wa dunia. Yeye anatupenda, na kwa damu yake ametufungua kutoka vifungo vya dhambi zetu, 6 akatufanya sisi kuwa ufalme wa makuhani, tumtumikie Mungu, Baba yake. Kwake Yesu Kristo uwe utukufu na nguvu, milele na milele! Amina. 7 Tazama! Anakuja katika mawingu! Kila mtu atamwona, hata wale waliomchoma. Makabila yote duniani yataomboleza juu yake. Naam! Amina. 8 “Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu Mwenye Uwezo, aliyeko, aliyekuwako na anayekuja. 9 Mimi ni Yohane, ndugu yenu; na kwa kuun- gana na Kristo nashiriki pamoja nanyi katika kustahimili mateso yanayowapata wale walio wa Utawala wake. Mimi nilikuwa kisiwani Patmo kwa sababu ya kuhubiri ujumbe wa Mungu na ukweli wa Yesu. 10 Basi, wakati mmoja, siku

Upload: buihanh

Post on 02-Mar-2019

468 views

Category:

Documents


3 download

TRANSCRIPT

Page 1: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 1:1 1 UFUNUOWA YOHANA 1:10

UFUNUOWA YOHANA1Hizi ni habari za mambo ambayo yalifunuliwa na Yesu

Kristo. Mungu alimpa Kristo ufunuo huu ili awaonyeshewatumishi wakemambo ambayo yanapaswa kutukia kari-buni. Kristo alimtuma malaika wake amjulishe Yohane,mtumishi wake, mambo hayo, 2naye Yohane, ameyasemayote aliyoyaona. Na hii ndio taarifa yake kuhusu ujumbewa Mungu na ukweli uliofunuliwa na Yesu Kristo. 3 Heriyake mtu anayesoma kitabu hiki; heri yao wale wanaosik-iliza maneno ya ujumbe huu wa kinabii na kushikayaliyoandikwa humu, maana wakati umekaribia ambapomambo haya yatatukia. 4 Mimi Yohane nayaandikiamakanisa yaliyoko mkoani Asia. Nawatakieni neemana amani kutoka kwake yeye aliyeko, aliyekuwako naanayekuja; na kutoka kwa roho saba walio mbele ya kitichake cha enzi, 5 na kutoka kwa Yesu Kristo, shahidimwaminifu, wa kwanza kufufuliwa kutoka wafu, na am-baye ni mtawala wa wafalme wa dunia. Yeye anatupenda,na kwa damu yake ametufungua kutoka vifungo vyadhambi zetu, 6 akatufanya sisi kuwa ufalme wamakuhani,tumtumikie Mungu, Baba yake. Kwake Yesu Kristo uweutukufu na nguvu, milele na milele! Amina. 7 Tazama!Anakuja katika mawingu! Kila mtu atamwona, hata walewaliomchoma. Makabila yote duniani yataomboleza juuyake. Naam! Amina. 8 “Mimi ni Alfa na Omega,” asemaBwana Mungu Mwenye Uwezo, aliyeko, aliyekuwako naanayekuja. 9Mimi ni Yohane, ndugu yenu; na kwa kuun-gana na Kristo nashiriki pamoja nanyi katika kustahimilimateso yanayowapata wale walio wa Utawala wake. Miminilikuwa kisiwani Patmo kwa sababu ya kuhubiri ujumbewa Mungu na ukweli wa Yesu. 10Basi, wakati mmoja, siku

Page 2: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 1:11 2 UFUNUOWA YOHANA 2:2ya Bwana, nilikumbwa na Roho, nikasikia nyuma yangusauti kubwa kama sauti ya tarumbeta. 11 Nayo ilisema,“Andika katika kitabu yote unayoyaona, ukipeleke kwamakanisa haya saba: Efeso, Smurna, Pergamoni, Thuatira,Sarde, Filadelfia na Laodikea.” 12 Basi, nikageuka nim-wone huyo aliyesema nami, nikaona vinara vya taa sabavya dhahabu, 13 na katikati yake kulikuwa na kitu kamamtu, naye alikuwa amevaa kanzu ndefu na ukanda wadhahabu kifuani. 14 Nywele zake zilikuwa nyeupe kamapamba safi, kama theluji; macho yake yalimetameta kamamoto; 15 miguu yake iling'aa kama shaba iliyosafishwakatika tanuru ya moto na kusuguliwa, na sauti yakeilikuwa, kama sauti ya poromoko la maji. 16Katika mkonowakewa kulia, alikuwa na nyota saba, na kinywanimwakemlitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake uling'aakama jua kali. 17 Basi, nilipomwona tu, nilianguka mbeleya miguu yake kama maiti. Lakini yeye akaweka mkonowakewa kulia juu yangu, akasema, “Usiogope! Mimi niwakwanza nawamwisho. 18Mimi ni yeye aliye hai! Nilikuwanimekufa, lakini, tazama, sasa ni mzima milele na milele.Ninazo funguo za kifo na Kuzimu. 19 Basi, sasa andikamambo haya unayoyaona, mambo yanayotukia sasa nayale yatakayotukia baadaye. 20 Siri ya nyota zile sabaulizoziona katika mkono wangu wa kulia, na siri ya vilevinara saba vya taa hii: zile nyota saba ni malaika wamakanisa; na vile vinara saba vya taa ni makanisa saba.

21 “Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika hivi: “Huu

ndio ujumbe kutoka kwake yeye ashikaye nyota sabakatika mkono wake wa kulia, na ambaye hutembeakatikati ya vinara saba vya taa vya dhahabu. 2 Najuamambo yako yote; najua bidii yako na uvumilivu wako.

Page 3: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 2:3 3 UFUNUOWA YOHANA 2:13Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, nakwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitumena kumbe sio, ukagundua kwamba ni waongo. 3 Weweunayo saburi, umestahimili taabu nyingi kwa ajili yajina langu, wala hukuvunjika moyo. 4 Lakini ninayohoja moja juu yako: wewe hunipendi tena sasa kamapale awali. 5 Basi, pakumbuke pale ulipokuwa kabla yakuanguka, ukayaache madhambi yako, na kufanya kamaulivyofanya pale awali. La sivyo, naja kwako na kukiondoakinara chako mahali pake. 6 Lakini nakusifu juu ya kitukimoja: wewe unayachukia wanayoyatenda Wanikolaikama ninavyoyachukia mimi. 7 “Aliye na masikio, basi,na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Walewanaoshinda nitawapa haki ya kula matunda ya mtiwa uzima ulioko ndani ya bustani ya Mungu. 8 “Kwamalaika wa kanisa la Smurna andika hivi: “Huu ndioujumbe kutoka kwake yeye wa kwanza na wa mwisho,ambaye alikufa na akaishi tena. 9Najua taabu zako; najuapia umaskini wako, ingawaje kwa kweli wewe ni tajiri;najua kashfa walizokufanyia wale wanaojiita Wayahudilakini si Wayahudi wa kweli, bali ni kundi lake Shetani.10 Usiogope hata kidogo yale ambayo itakulazimu kute-seka. Sikiliza! Ibilisi anataka kuwajaribu kwa kuwatiabaadhi yenu gerezani; nanyi mtapata dhiki kwa mudawa siku kumi. Muwe waaminifu hata mpaka kufa, naminitawapeni taji ya uzima. 11 “Aliye na masikio, basi,na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Walewanaoshinda hawataumizwa na kifo cha pili. 12 “Kwamalaika wa kanisa la Pergamoni andika hivi: “Huu ndioujumbe wake yeye aliye na upanga mkali wenye kuwili.13 Najua unakoishi: Wewe unaishi kwenye makao makuuya Shetani! Lakini bado unashikilia jina langu; hukuikanaimani yako kwangu hata siku zile Antipa shahidi wangu

Page 4: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 2:14 4 UFUNUOWA YOHANA 2:24mwaminifu, alipouawa pale mahali anapoishi Shetani.14 Lakini ninayo machache dhidi yako: baadhi yenuni wafuasi wa Balaamu aliyemfundisha Balaki kuwategawana wa Israeli wale vyakula vilivyotambikiwa sanamuza kufanya uzinzi. 15 Vivyo hivyo, wako pia mion-goni mwenu watu wanaofuata mafundisho ya Wanikolai.16 Basi, achana na madhambi yako. La sivyo, nitakujakwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga utokaokinywani mwangu. 17 “Aliye na masikio, basi, na asikieyale Roho anayoyaambia makanisa! “Wale wanaoshindanitawapa ile mana iliyofichika. Nitawapa pia jiwe jeupelililoandikwa jina jipya ambalo hakuna mtu aliyelijuaisipokuwa tu wale wanaolipokea. 18 “Kwa malaika wakanisa la Thuatira andika hivi: “Huu ndio ujumbe waMwana wa Mungu, ambaye macho yake yametametakamamoto, na miguu yake inang'aa kama shaba iliyosug-uliwa. 19 Najua mambo yako yote. Najua upendo wako,imani yako, utumishi wako na uvumilivu wako. Weweunafanya vizuri zaidi sasa kuliko pale awali. 20Lakini ninahoja moja juu yako: wewe unamvumilia yule mwanamkeYezabeli anayejiita nabii wa Mungu. Yeye huwafundishana kuwapotoshawatumishiwanguwafanye uzinzi na kulavyakula vilivyotambikiwa sanamu. 21Nimempa muda wakutubu dhambi zake, lakini hataki kuachana na uzinziwake. 22 Sikiliza! Sasa namtupa kitandani ambapo yeyepamoja na wote waliofanya uzinzi naye watapatwa namateso makali. Naam, nitafanya hivyo, kama wasipotubumatendo yaomabaya waliyotenda naye. 23Tena nitawauawafuasi wake, ili makanisa yote yatambue kwamba mimindiye ninayechunguza mioyo na fikira za watu. 24 “Lakinininyi wengine mlioko huko Thuatira ambao hamfuatimafundisho yake Yezabeli, na ambao hamkujifunza kilewanachokiita Siri ya Shetani, nawaambieni kwamba

Page 5: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 2:25 5 UFUNUOWA YOHANA 3:8sitawapeni mzigo mwingine. 25 Lazima mzingatie yalemliyo nayo sasa mpaka nitakapokuja. 26 “Wanaoshinda,na wale watakaozingatia mpaka mwisho kutenda ninay-otaka, nitawapa mamlaka juu ya mataifa. 27 Naam,nitawapa uwezo uleule nilioupokea kwa Baba: yaani,watayatawala mataifa kwa fimbo ya chuma na kuyavun-javunja kama chombo cha udongo. 28 Tena nitawapanyota ya asubuhi. 29 “Aliye na masikio, basi, na ayasikieyale Roho anayoyaambia makanisa!

31 “Kwa malaika wa kanisa la Sarde andika hivi: “Huu

ndio ujumbe kutoka kwake yeye aliye na roho saba zaMungu na nyota saba. Nayajua mambo yako yote; najuaunajulikana kuwa na uhai kumbe umekufa! 2 Amka!Imarisha chochote chema kilichokubakia kabla nachohakijatoweka kabisa. Maana, mpaka sasa, sijayaona ma-tendo yako kuwa ni makamilifu mbele ya Mungu wangu.3 Kumbuka, basi, yale uliyofundishwa na jinsi ulivyoy-asikia, uyatii na ubadili nia yako mbaya. Usipokeshanitakujia ghafla kama mwizi, na wala hutaijua saa ni-takapokujia. 4 Lakini wako wachache huko Sarde ambaohawakuyachafua mavazi yao. Hao wanastahili kutembeapamoja nami wakiwa wamevaa mavazi meupe. 5 “Walewanaoshinda, watavikwa mavazi meupe kama hao. Namisitayafuta majina yao kutoka katika kitabu cha uzima;tena nitawakiri kwamba ni wangu mbele ya Baba yanguna mbele ya malaika wake. 6 “Aliye na masikio, basi,na ayasikie yale Roho anayoyaambia makanisa! 7 “Kwamalaika wa kanisa la Filadelfia andika hivi: “Huu ndioujumbe kutoka kwake yeye aliye mtakatifu na wa kweli,ambaye anao ule ufunguo wa Daudi, na ambaye hufunguana hakuna mtu awezaye kufungua. 8 Nayajua mamboyako yote! Sasa, nimefungua mbele yako mlango ambao

Page 6: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 3:9 6 UFUNUOWA YOHANA 3:18hakuna mtu awezaye kuufunga; najua kwamba ingawahuna nguvu sana, hata hivyo, umezishika amri zangu,umelitii neno langu wala hukulikana jina langu. 9Sikiliza!Nitawapeleka kwako watu wa kundi lake Shetani, watuambao hujisema kuwa ni Wayahudi, kumbe ni wadan-ganyifu. Naam, nitawapeleka kwako na kuwafanyawapige magoti mbele yako wapate kujua kwamba kwelinakupenda wewe. 10 Kwa kuwa wewe umezingatia agizolangu la kuwa na uvumilivu, nami pia nitakutegemezasalama wakati ule wa dhiki inayoujia ulimwengu mzimakuwajaribu wote wanaoishi duniani. 11Naja kwako upesi!Linda, basi, ulicho nacho sasa, ili usije ukanyang'anywanamtu yeyote taji yako ya ushindi. 12 “Wale wanaoshindanitawafanyawaweminara katikaHekalu laMunguwangu,na hawatatoka humo kamwe. Pia nitaandika juu yaojina la Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu,yaani Yerusalemu mpya, mji ambao utashuka kutoka juumbinguni kwa Mungu wangu. Tena nitaandika juu yaojina langu jipya. 13 “Aliye na masikio, basi, na ayasikieyale Roho anayoyaambia makanisa! 14 “Kwa malaikawa kanisa la Laodikea andika hivi: “Huu ndio ujumbekutoka kwake yeye aitwaye Amina. Yeye ni shahidimwaminifu na wa kweli, ambaye ni chanzo cha viumbevyote alivyoumba Mungu. 15 Nayajua mambo yako yote!Najua kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhaliungekuwa kimojawapo: baridi au moto. 16 Basi, kwakuwa hali yako ni vuguvugu, si baridi wala si moto,nitakutapika! 17 Wewe unajisema, Mimi ni tajiri; ni-najitosheleza, sina haja ya kitu chochote. Kumbe, hu-jui kwamba wewe ni mnyonge, unahitaji kuhurumiwa,maskini, kipofu tena uko uchi! 18 Nakushauri ununuekwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto upate kuwatajiri kweli. Tena afadhali ununue pia vazi jeupe, uvae na

Page 7: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 3:19 7 UFUNUOWA YOHANA 4:6kufunika aibu ya uchi wako. Nunua pia mafuta ukapakemachoni pako upate kuona. 19 Mimi ndiye mwenyekumwonya na kumrudi yeyote ninayempenda. Kwa hiyokaza moyo, achana na dhambi zako. 20 Sikiliza! Miminasimama mlangoni na kubisha hodi. Mtu akisikia sautiyangu na kufungua mlango, nitaingia nyumbani kwakena kula chakula pamoja naye, naye atakula pamoja nami.21 “Wale wanaoshinda nitawaketisha pamoja nami juuya kiti changu cha enzi, kama vile mimi mwenyewenilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu juu ya kitichake cha enzi. 22 “Aliye na masikio, basi, na ayasikie yaleRoho anayoyaambia makanisa!”

41 Baada ya hayo nilitazama nikaona mlango umefun-

guliwa mbinguni. Na ile sauti niliyoisikia pale awaliambayo ilikuwa kama sauti ya tarumbeta, ikasema, “Njoohapa juu nami nitakuonyesha mambo yatakayotukiabaadaye.” 2 Mara nikachukuliwa na Roho. Kumbe,huko mbinguni kuna kiti cha enzi na juu yake ameketimmoja. 3 Huyo aliyeketi juu yake alikuwa kama almasina jiwe zuri jekundu. Upinde wa mvua ulikuwa unang'aakama zumaridi na ulikizunguka kiti cha enzi pande zote.4 Kulikuwa na duara la viti ishirini na vinne kukizungukakiti cha enzi, na juu ya viti hivyo wazee ishirini na wannewalikuwa wameketi wamevaa mavazi meupe na taji zadhahabu vichwani. 5Umeme, sauti na ngurumo, vilikuwavinatoka kwenye hicho kiti cha enzi. Taa saba za motozilikuwa zinawaka mbele ya hicho kiti cha enzi. Taa hizoni roho saba za Mungu. 6Mbele ya kiti cha enzi kulikuwana kitu kama bahari ya kioo, angavu kama jiwe linga'aalosana. Katika pande zote za hicho kiti cha enzi na kuk-izunguka, kilikuwa na viumbe hai vinne. Viumbe hivyo

Page 8: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 4:7 8 UFUNUOWA YOHANA 5:6vilikuwa vimejaa macho mbele na nyuma. 7 Kiumbe chakwanza kulikuwa kama simba, cha pili kama ng'ombe, chatatu kilikuwana sura kamamtu, na channe kilikuwakamatai anayeruka. 8Viumbe hivyo vinne vilikuwa na mabawasita kila kimoja, na vilikuwa vimejaa macho, ndani na nje.Usiku na mchana, bila kupumzika huimba: “Mtakatifu,mtakatifu, mtakatifu ni Bwana, Mungu Mwenye Uwezo,aliyekuwako, aliyeko na anayekuja!” 9 Kila mara viumbevinne vilipoimba nyimbo za kumtukuza, kumheshimu nakumshukuru huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzi, ambayeanaishi milele na milele, 10wale wazee ishirini na wannehujiangusha mbele ya huyo aliyeketi juu ya kiti cha enzina kumwabudu huyo ambaye anaishi milele na milele;na huziweka taji zao mbele ya kiti cha enzi wakisema:11 “Wewe ni Bwana na Mungu wetu, unastahili utukufuna heshima na nguvu; maana wewe uliumba vitu vyote,na kwamatakwa yako kila kitu kimepewa uhai na uzima.”

51 Kisha katika mkono wa kulia wa huyo aliyeketi juu

ya kiti cha enzi, nikaona kitabu; nacho kilikuwa kime-andikwa ndani na nje na kufungwa na mihuri saba.2 Tena nikamwona malaika mwenye nguvu akitangazakwa sauti kubwa: “Nani anayestahili kuvunja hiyo mihurina kukifungua kitabu hicho?” 3 Lakini hakupatikanamtu yeyote mbinguni, wala duniani, wala chini Kuzimu,aliyeweza kukifungua hicho kitabu au kukitazama ndani.4 Basi, mimi nikalia sana kwa sababu hakupatikana mtualiyestahili kukifungua, au kukitazama ndani. 5 Kishammoja wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama!Simba wa kabila la Yuda, mjukuu maarufu wa Daudi,ameshinda. Yeye anaweza kuivunja mihuri yake saba nakukifungua hicho kitabu.” 6 Kisha nikaona pale katikati

Page 9: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 5:7 9 UFUNUOWA YOHANA 6:1ya kiti cha enzi Mwana kondoo amesimama, akizun-gukwa kila upande na vile viumbe hai vinne, na walewazee. Huyo Mwanakondoo alionekana kana kwambaamechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho sabaambayo ni roho saba za Mungu zilizokuwa zimepelekwakila mahali duniani. 7Mwanakondoo akaenda, akakitwaahicho kitabu kutoka mkono wa kulia wa yule aliyeketi juuya kiti cha enzi. 8Mara tu alipokwisha twaa hicho kitabu,vile viumbe hai vinne pamoja na wale wazee ishirini nawanne walianguka kifudifudi mbele ya Mwanakondoo.Kila mmoja, alikuwa na kinubi na bakuli za dhahabuzilizojaa ubani, ambao ni sala za watu wa Mungu. 9 Basi,wakaimba wimbo huu mpya: “Wewe unastahili kukitwaahicho kitabu na kuivunja mihuri yake. Kwa sababu weweumechinjwa, na kwa damu yako umemnunulia Munguwatu kutoka katika kila kabila, lugha, jamaa na taifa.10Wewe umewafanya wawe ufalme wa makuhani wamtu-mikie Mungu wetu nao watatawala duniani.” 11 Kishanikatazama, nikasikia sauti ya malaika wengi sana, idadiisiyohesabika, maelfu na maelfu. Walikuwa wamekaakuzunguka kiti cha enzi, vile viumbe hai vinne na walewazee; 12 wakasema kwa sauti kuu: “Mwanakondooaliyechinjwa anastahili kupokea uwezo, utajiri, hekima,nguvu, utukufu na sifa.” 13Nikasikia viumbe vyote mbin-guni, duniani, chini kuzimuni na baharini—viumbe vyoteulimwenguni—vikisema: “Kwake yeye aketiye katika kiticha enzi, na kwa Mwanakondoo, iwe sifa na heshima nautukufu na enzi milele na milele.” 14 Na vile viumbevinne hai vikasema, “Amina!” Nawalewazeewakaangukakifudifudi, wakaabudu.

61 Kisha nikamwona Mwanakondoo anavunja mhuri

mmojawapo wa ile mihuri saba. Nikasikia kimoja cha vile

Page 10: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 6:2 10 UFUNUOWA YOHANA 6:11viumbe hai vinne kikisema kwa sauti kama ya ngurumo,“Njoo!” 2Mimi nikatazama, na kumbe palikuwa na farasimmoja mweupe hapo. Na mpanda farasi wake alikuwa naupinde, akapewa na taji. Basi, akatoka kamamshindi aen-delee kushinda. 3 Kisha, Mwanakondoo akavunja mhuriwa pili. Nikamsikia yule kiumbe hai wa pili akisema,“Njoo!” 4 Nami nikatazama na kumbe palikuwapofarasi mwingine hapo, mwekundu. Mpanda farasi wakealikabidhiwa jukumu la kuondoa amani duniani, watuwauane, akapewa upanga mkubwa. 5 Kisha Mwanakon-doo akavunja mhuri wa tatu. Nikamsikia yule kiumbehai wa tatu akisema, “Njoo!” Nikatazama na kumbepalikuwapo farasi mmoja hapo, mweusi. Mpanda farasiwake alikuwa na vipimo viwili vya kupimia uzitomkononimwake. 6 Nikasikia kitu kama sauti itokayo kwa vileviumbe hai vinne. Nayo ilisema, “Kibaba kimoja cha ungawa ngano wa kiasi cha fedha dinari moja, na vibaba vitatuvya shayiri kwa dinari moja. Lakini usiharibu mafutawala divai!” 7 Kisha Mwanakondoo akavunja mhuri wanne. Nikamsikia yule kiumbe hai wa nne akisema, “Njoo!”8 Nami nikatazama, na kumbe alikuwapo farasi mmojahapo, rangi yake kijivu. Na jina la mpanda farasi wakelilikuwa kifo, na Kuzimu alimfuata nyuma. Hao walipewamamlaka juu ya robo moja ya dunia, wawaue watu kwaupanga, njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia.9 Kisha Mwanakondoo akavunja mhuri wa tano. Nikaonapale chini ya madhabahu ya kufukizia ubani roho za walewaliouawa kwa sababu ya ujumbe wa Mungu, na kwasababu ya ushuhuda waliotoa. 10 Basi, wakalia kwa sautikubwa: “Ee Bwana, uliyemtakatifu namwaminifu, mpakalini utakawia kulipiza kisasi kwa wakazi wote wa duniakwa ajili ya kuuawa kwetu?” 11 Wakapewa kila mmojavazi refu jeupe, wakaambiwa wazidi kusubiri kwa muda

Page 11: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 6:12 11 UFUNUOWA YOHANA 7:5mfupi, mpaka itakapotimia idadi ya watumishi wenzaona ndugu ambao watawaua kama wao wenyewe walivy-ouawa. 12 Kisha nikatazama, na wakati Mwanakondooalipouvunja mhuri wa sita, kukawa na tetemeko kubwala ardhi; jua likawa jeusi kama gunia; mwezi wote ukawamwekundu kama damu; 13 nazo nyota za mbingu zikaan-guka juu ya ardhi kama matunda ya mtini yasiyokomaayaangukavyo wakati mti wake unapotikiswa na upepomkali. 14 Anga likatoweka kama vile karatasi inavyokun-jwakunjwa; milima yote na visima vyote vikaondolewamahali pake. 15 Kisha wafalme wa duniani, wakuu,majemadari, matajiri, wenye nguvu, kila mtumwa namtu huru, wakajificha mapangoni na kwenye majabalimilimani. 16 Wakaiambia hiyo milima na hayo majabali,“Tuangukieni, mkatufiche mbali na yeye aketiye juu yakiti cha enzi, na mbali na ghadhabu ya Mwanakondoo!17 Maana siku maalum ya ghadhabu yao imefika. Naniawezaye kuikabili?”

71 Baada ya hayo nikawaona malaika wanne wamesi-

mama katika pembe nne za dunia wakishika pepo nneza dunia ili upepo usivume hata kidogo: wala katikanchi, wala baharini, wala kwenye miti. 2 Kisha nikam-wona malaika mwingine akipanda juu kutoka masharikiakiwa na mhuri wa Mungu aliye hai. Akapaaza sauti nakuwaambia hao malaika wanne waliokabidhiwa jukumula kuiharibu nchi na bahari, 3 “Msiharibu nchi, walabahari, wala miti, mpaka tutakapokwisha wapiga mhuriwatumishi wa Mungu wetu katika paji la uso.” 4 Kishanikasikia idadi ya hao waliopigwa mhuri: Watu mia mojaarobaini na nne elfu wa makabila yote ya watu wa Israeli.5Kabila la Yuda walikuwa watu kumi na mbili elfu; kabilala Reubeni, kumi na mbili elfu, kabila la Gadi, kumi

Page 12: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 7:6 12 UFUNUOWA YOHANA 7:17na mbili elfu; 6 Kabila la Asheri, kumi na mbili elfu;kabila la Naftali, kumi na mbili elfu; kabila la Manase,kumi na mbili elfu; 7 kabila la Simeoni, kumi na mbilielfu, kabila la Lawi, kumi na mbili elfu, kabila la Isakari,kumi na mbili elfu; 8 kabila la Zabuloni, kumi na mbilielfu; kabila la Yosefu, kumi na mbili elfu, na kabila laBenyamini, kumi na mbili elfu. 9 Kisha nikatazama,nikaona umati mkubwa wa watu wasiohesabika: watu wakila taifa, ukoo, jamaa na lugha. Nao walikuwa wamesi-mama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo,wakiwa wamevaa mavazi meupe na kushika matawi yamitende mikononi mwao. 10 Wakapaaza sauti: “Ukom-bozi wetu watoka kwa Mungu wetu aketiye juu ya kiticha enzi, na kutoka kwa Mwanakondoo!” 11 Malaikawote wakasimama kukizunguka kiti cha enzi, wazee navile viumbe hai vinne. Wakaanguka kifudifudi mbeleya kiti cha enzi, wakamwabudu Mungu, 12 wakisema,“Amina! Sifa, utukufu, hekima, shukrani, heshima,uwezo na nguvu viwe kwa Mungu wetu, milele na milele!Amina!” 13 Mmoja wa hao wazee akaniuliza, “Hawawaliovaa mavazi meupe ni watu gani? Na wametokawapi?” 14 Nami nikamjibu, “Mheshimiwa, wewe wa-jua!” Naye akaniambia, “Hawa ni wale waliopita salamakatika ule udhalimumkuu. Waliyaosha mavazi yao katikadamu ya Mwanakondoo, yakawa meupe kabisa. 15 Ndiyomaana wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Humtu-mikia Mungu mchana na usiku katika Hekalu lake; nayeaketiye juu ya kiti cha enzi atatandaza hema lake juu yaokuwalinda. 16Hawataona tena njaa wala kiu; jua wala jotokali halitawachoma tena, 17 kwa sababu Mwanakondooaliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungaji wao,naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji ya uzima.Naye Mungu atayafuta machozi yote machoni mwao.”

Page 13: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 8:1 13 UFUNUOWA YOHANA 8:128

1NaMwanakondoo alipouvunjamhuriwa saba, kukawakimya mbinguni kwa muda wa nusu saa. 2 Kishanikawaona wale malaika saba wanaosimama mbele yaMungu wamepewa tarumbeta saba. 3Malaika mwingineakafika, akiwa anachukua chetezo cha dhahabu, akasi-mama mbele ya madhabahu ya kufukizia ubani. Nayeakapewa ubani mwingi autoe sadaka pamoja na sala zawatu wote wa Mungu, juu ya madhabahu ya dhahabuiliyo mbele ya kiti cha enzi. 4Moshi wa ubani ukapandajuu, pamoja na sala za watu wa Mungu, kutoka mikononimwake huyo malaika aliyekuwa mbele ya Mungu. 5Kishamalaika akakichukua hicho chetezo, akakijaza moto wamadhabahuni akakitupa duniani. Kukawa na ngurumo,sauti, umeme na tetemeko la ardhi. 6 Kisha wale malaikasaba wenye tarumbeta saba wakajiweka tayari kupigambiu ya mgambo. 7 Malaika wa kwanza akapiga tarum-beta yake. Mchanganyiko wa mvua ya mawe na moto,pamoja na damu, ukamwagwa juu ya nchi. Theluthi mojaya nchi ikaungua, theluthi moja ya miti ikaungua, namajani yotemabichi yakaungua. 8Malaika wa pili akapigatarumbeta yake. Na kitu kama mlima mkubwa unaowakamoto ukatupwa baharini. Theluthi moja ya bahari ikawadamu, 9 theluthi moja ya viumbe vya baharini vikafa natheluthi moja ya meli zikaharibiwa. 10 Kisha malaika watatu akapiga tarumbeta yake. Na nyota kubwa ikiwakakama bonge la moto, ikaanguka kutoka mbinguni, nakutua juu ya theluthimoja yamito na chemchemi zamaji.11 (Nyota hiyo inaitwa “Uchungu.”) Basi, theluthi mojaya maji yakawa machungu; watu wengi wakafa kutokanana maji hayo, kwa sababu yaligeuka kuwa machungu.12 Kisha malaika wa nne akapiga tarumbeta yake. Ndipotheluthi moja ya jua, ya mwezi na ya nyota ikapata pigo;

Page 14: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 8:13 14UFUNUOWA YOHANA 9:10hatamwangaza ukapoteza theluthi moja yamng'ao wake.Theluthi moja yamchana ikakosamwanga, hali kadhalikana theluthi moja ya usiku. 13 Kisha nikatazama, nikasikiatai akiruka juu kabisa angani anasema kwa sauti kubwa,“Ole, ole, ole kwa wanaoishi duniani wakati malaikawatatu waliobaki watakapopiga tarumbeta zao!”

91Kisha malaika wa tano akapiga tarumbeta yake. Nami

nikaona nyota iliyokuwa imeanguka juu ya nchi kutokambinguni. Nayo ikapewa ufunguo wa shimo la Kuzimu.2 Basi, nyota hiyo ikafungua shimo la Kuzimu, kukatokamoshi wa tanuru kubwa. Jua na anga vikatiwa gizakwa moshi huo wa Kuzimu. 3 Nzige wakatoka katikamoshi huo, wakaingia duniani wakapewa nguvu kamaya ng'e. 4 Wakaamrishwa wasiharibu nyasi za nchiwala majani wala miti yoyote, bali wawaharibu waletu ambao hawakupigwa mhuri wa Mungu katika pajila uso. 5 Nzige hao hawakuruhusiwa kuwaua watu, ilakuwatesa tu kwa muda wa miezi mitano. Maumivuwatakayosababisha ni kama maumivu yanayompata mtuwakati anapoumwa na ng'e. 6Muda huo watu watatafutakifo lakini hawatakipata; watatamani kufa lakini kifokitawakimbia. 7 Kwa kuonekana, nzige hao walikuwakama farasi waliowekwa tayari kwa vita. Juu ya vichwavyao walikuwa na taji zilizo kama za dhahabu, na nyusozao zilikuwa kama za binadamu. 8 Nywele zao zilikuwakama nywele za wanawake, na meno yao yalikuwa kamameno ya simba. 9 Vifua vyao vilikuwa vimefunikwa kitukama ngao ya chuma. Sauti ya mabawa yao ilikuwa kamasauti yamsafarawamagari ya farasi wengi wanaokimbiliavitani. 10 Walikuwa na mikia na miiba kama ng'e, nakwa mikia hiyo, walikuwa na nguvu ya kuwadhuru watu

Page 15: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 9:11 15UFUNUOWA YOHANA 9:21kwa muda wa miezi mitano. 11 Tena wanaye mfalmeanayewatawala, naye ndiye malaika wa kuzimu; jina lakekwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kigiriki ni Apolioni,yaani mwangamizi. 12 Maafa ya kwanza yamepita; badomengine mawili yanafuata. 13 Kisha malaika wa sitaakapiga tarumbeta yake. Nami nikasikia sauti mojakutoka katika pembe nne za madhabahu ya dhahabuiliyokuwa mbele ya Mungu. 14 Sauti hiyo ikamwambiahuyo malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafunguliemalaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Eu-frate!” 15Naye akawafungulia malaika hao wanne ambaowalikuwa wametayarishwa kwa ajili ya saa hiyo ya sikuya mwezi huo, wa mwaka huohuo, kuua theluthi moja yawanaadamu. 16 Nilisikia idadi ya majeshi wapanda farasiilikuwa milioni mia mbili. 17 Hivi ndivyo nilivyowaonahao farasi na wapanda farasi katika hiyo njozi: Walikuwana ngao vifuani zilizokuwa moto mtupu, zenye rangiya samawati na njano kama kiberiti. Vichwa vya haofarasi vilikuwa kama vya simba; na moto, moshi, nakiberiti vilikuwa vinatoka kinywani mwao. 18 Theluthimoja ya wanaadamu waliuawa kwa mabaa hayo matatuyaani, moto, moshi na kiberiti, yaliyokuwa yanatokakatika vinywa vyao; 19maana nguvu ya farasi hao ilikuwavinywani mwao na katika mikia yao. Mikia yao ilikuwa navichwa kama nyoka, na waliitumia hiyo kuwadhuru watu.20Wanaadamuwengine waliobaki ambao hawakuuawa namabaa hayo, hawakugeuka na kuviacha vitu walivyokuwawametengeneza kwa mikono yao wenyewe; bali wakaen-delea kuabudu pepo, sanamu za dhahabu, fedha, shaba,mawe na miti, vitu ambavyo haviwezi kuona, kusikiawala kutembea. 21Wala hawakutubu na kuacha kufanyamauaji, uchawi, uzinzi, na wizi.

Page 16: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 10:116UFUNUOWA YOHANA 10:1010

1 Kisha nikamwona malaika mwingine mwenye nguvuakishuka kutoka mbinguni. Alikuwa amevikwa wingu,na upinde wa mvua kichwani mwake. Uso wake ulikuwakama jua, na miguu yake ilikuwa kama moto. 2Mikononimwake alishika kitabu kidogo kimefunguliwa. Aliwekamguu wake wa kulia juu ya bahari, na wa kushotojuu ya nchi kavu, 3 na kuita kwa sauti kubwa kamaya mngurumo wa simba. Alipopaaza sauti, ngurumosaba ziliitikia kwa kishindo. 4 Na hizo ngurumo sabaziliposema, mimi nikataka kuandika. Lakini nikasikiasauti kutoka mbinguni: “Maneno ya ngurumo hizo sabani siri; usiyaandike!” 5 Kisha yule malaika niliyemwonaakisimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu akainuamkono wake wa kulia juu mbinguni, 6 akaapa kwa jinala Mungu aishiye milele na milele, Mungu aliyeumbambingu na vyote vilivyomo, bahari na vyote vilivyomo,dunia na vyote vilivyomo. Akasema, “Wakati wa kusubirizaidi umekwisha! 7 Lakini wakati ule malaika wa sabaatakapotoa sauti yake, wakati atakapopiga tarumbetayake, Mungu atakamilisha mpango wake wa siri kamaalivyowatangazia watumishi wake manabii.” 8 Kisha ilesauti niliyokuwa nimeisikia kutoka mbinguni pale awaliikasema nami tena: “Nenda ukakichukue kile kitabu kili-chofunguliwa, kilicho mkononi mwa malaika asimamayejuu ya bahari na juu ya nchi kavu.” 9 Basi, nikamwen-dea huyo malaika, nikamwambia anipe hicho kitabukidogo. Naye akaniambia, “Kichukue, ukile; kinywanimwako kitakuwa kitamu kama asali, lakini tumboni ki-takuwa kichungu!” 10 Basi, nikakichukua kitabu hichokidogo kutoka mkononi mwa huyo malaika, nikakila;nacho kilikuwa kitamu kinywani mwangu kama asali,lakini nilipokimeza kikawa kichungu tumboni mwangu.

Page 17: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWAYOHANA10:1117UFUNUOWAYOHANA11:1011 Kisha nikaambiwa, “Inakubidi tena kutangaza ujumbewa Mungu kuhusu watu wengi, mataifa, watu wa lughanyingi na wafalme!”

111 Kisha nikapewa mwanzi uliokuwa kama kijiti cha

kupimia, nikaambiwa, “Inuka, ukalipime Hekalu laMungu, madhabahu ya kufukizia ubani, na ukawah-esabu watu wanaoabudu ndani ya Hekalu. 2 Lakiniuache ukumbi ulio nje ya Hekalu; usiupime, maanahuo umekabidhiwa watu wa mataifa mengine, am-bao wataukanyanga mji Mtakatifu kwa muda wa mieziarobaini na miwili. 3Nami nitawatuma mashahidi wanguwawili ili watangaze ujumbe wa Mungu kwa muda huowa siku elfu moja mia mbili na sitini wakiwa wamevaamavazi ya magunia.” 4 Hao mashahidi wawili ni mitimiwili ya Mizeituni na taa mbili zinazosimama mbele yaBwana wa dunia. 5Kama mtu akijaribu kuwadhuru, motohutoka kinywani mwao na kuwaangamiza adui zao; nakila mtu atakayejaribu kuwadhuru atakufa namna hiyo.6Hao wanayo mamlaka ya kufunga anga, mvua isinyeshewakati wanapotangaza ujumbe wa Mungu. Tena wanayomamlaka ya kuzigeuza chemchemi zote za maji ziwedamu, na ya kusababisha maafa ya kila namna dunianikilamarawapendavyo. 7Lakini wakishamaliza kutangazaujumbe huo, mnyama atokaye shimoni kuzimu atapigananao, atawashinda na kuwaua. 8Maiti zao zitabaki katikabarabara za mji mkuu ambapo Bwana wao alisulubiwa;jina la kupanga la mji huo ni Sodoma au Misri. 9 Watuwa kila kabila, lugha, taifa na rangi wataziangalia maitihizo kwa muda wa siku tatu na nusu, na hawataruhusuzizikwe. 10 Watu waishio duniani watafurahia kifo chahao wawili. Watafanya sherehe na kupelekeana zawadimaana manabii hawa wawili walikuwa wamewasumbua

Page 18: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 11:1118UFUNUOWA YOHANA 12:1mno watu wa dunia. 11 Lakini baada ya zile siku tatuna nusu pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu iliwaingia,nao wakasimama; wote waliowaona wakaingiwa na hofukuu. 12 Kisha hao manabii wawili wakasikia sauti kubwakutoka mbinguni ikiwaambia, “Njoni hapa juu!” Naowakapanda juu mbinguni katika wingu, maadui waowakiwa wanawatazama. 13 Wakati huohuo, kukatokeatetemeko kubwa la ardhi, sehemu moja ya kumi ya ardhiikaharibiwa. Watu elfu saba wakauawa kwa tetemekohilo la ardhi. Watu waliosalia wakaogopa sana, wakam-tukuza Mungu wa mbinguni. 14 Maafa ya pili yamepita;lakini tazama! Maafa ya tatu yanafuata hima. 15 Kishamalaika wa saba akapiga tarumbeta yake. Na sautikuu zikasikika mbinguni zikisema, “Sasa utawala juu yaulimwengu ni wa Bwana wetu na Kristo wake. Nayeatatawala milele na milele!” 16 Kisha wale wazee ishirinina wanne walioketi mbele ya Mungu katika viti vyaovya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,17wakisema: “Bwana Mungu Mwenye uwezo, uliyeko nauliyekuwako! Tunakushukuru, maana umetumia nguvuyako kuu ukaanza kutawala! 18 Watu wa mataifa wali-waka hasira, maana wakati wa ghadhabu yako umefika,wakati wa kuwahukumu wafu. Ndio wakati wa kuwatuzawatumishi wako manabii, watu wako na wote wanaoli-tukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wakuwaangamiza wale wanaoangamiza dunia.” 19 Hekalula Mungu mbinguni likafunguliwa, na Sanduku la Aganolake likaonekana Hekaluni mwake. Kisha kukatokeaumeme, sauti, ngurumo, tetemeko la ardhi, na mvuakubwa ya mawe.

121 Kisha ishara kubwa ikaonekana mbinguni. Palikuwa

hapomwanamke aliyevikwa jua, namwezi chini yamiguu

Page 19: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 12:219UFUNUOWA YOHANA 12:12yake, na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake!2 Alikuwa mja mzito, na akapaaza sauti kwa maumivuna uchungu wa kujifungua mtoto. 3 Ishara nyingineikatokea mbinguni: joka kubwa jekundu na lenye pembekumi na vichwa saba; na kila kichwa kilikuwa na taji.4 Joka hilo liliburuta kwa mkia wake theluthi moja yanyota za anga na kuzitupa duniani. Nalo lilisimamambele ya huyomama aliyekuwa karibu kujifunguamtoto,tayari kabisa kummeza mtoto, mara tu atakapozaliwa.5Kisha mama huyo akajifungua mtoto wa kiume, ambayeatayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Lakinimtoto akanyakuliwana kupelekwa kwaMunguna kwenyekiti chake cha enzi. 6 Huyo mama akakimbilia jangwani,ambako Mungu alikuwa amemtayarishia mahali pa us-alama ambapo angehifadhiwa kwa muda wa siku elfumoja mia mbili na sitini. 7Kisha kukazuka vita mbinguni:Mikaeli na malaika wake walipigana na hilo joka, nalolikawashambulia pamoja na malaika wake. 8 Lakini jokahilo halikuweza kuwashinda, na hatimaye hapakuwa tenana nafasi mbinguni kwa ajili yake na malaika wake. 9Basi,joka hilo kuu likatupwa nje. Joka hilo ndiye yule nyokawakale ambaye huitwa pia Ibilisi au Shetani. Ndiye anayeu-danganya ulimwengu wote. Naam, alitupwa duniani, namalaika wake wote pamoja naye. 10 Kisha nikasikia sautikubwa kutoka mbinguni ikisema: “Sasa ukombozi utokaokwa Mungu umefika! Nguvu na Utawala wa Mungu wetuumedhihirika. Na Kristo wake ameonyesha mamlakayake! Maana yule mdhalimu wa ndugu zetu, aliyesimamambele ya Mungu akiwashtaki usiku na mchana, sasaametupwa nje. 11 Ndugu zetu wameshinda kwa damu yaMwanakondoo na kwa nguvu ya ukweli walioutangaza;maana hawakuyathamini maisha yao kuwa kitu sana,wakawa tayari kufa. 12 Kwa sababu hiyo, furahini enyi

Page 20: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 12:1320UFUNUOWA YOHANA 13:4mbingu na vyote vilivyomo ndani yenu. Lakini, olewenu nchi na bahari, maana Ibilisi amewajieni akiwana ghadhabu kuu, kwa sababu anajua kwamba siku zakezilizobakia ni chache.” 13 Joka lilipotambua kwambalimetupwa chini duniani, likaanza kumwinda yule mamaaliyekuwa amejifungua mtoto wa kiume. 14 Lakini mamahuyo akapewa mabawa mawili ya tai apate kuruka mbalisana na hilo joka, mpaka mahali, pake jangwani ambapoangehifadhiwa salama kwa muda wa miaka mitatu nanusu. 15 Basi, joka likatapika maji mengi kama mto,yakamfuata huyo mama nyuma ili yamchukue. 16 Lakininchi ikamsaidia huyo mama: ikajifunua kama mdomo nakuyameza maji hayo yaliyotoka kinywani mwa hilo joka.17Basi, jokahilo likamkasirikia huyomama, likajiondokea,likaenda kupigana na wazawa wengine wa huyo mama,yaaniwotewanaotii amri zaMunguna kuuzingatia ukweliwa Yesu.

131 (G12-18) Na likajisimamia ukingoni mwa bahari.

(G13-1) Kisha nikaona mnyama mmoja akitoka baharini.Alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na kila pembeilikuwa na taji. Jina la kashfa lilikuwa limeandikwa juuya vichwa hivyo. 2 Mnyama huyo niliyemwona alikuwakama chui; miguu yake ilikuwa kama ya dubu, na kinywachake kama cha simba. Lile joka likampa huyo mnyamanguvu yake, kiti chake cha enzi na uwezo mkuu. 3Kichwakimojawapo cha huyo mnyama kilionekana kama kilik-wisha jeruhiwa vibaya sana, lakini jeraha hilo lilikuwalimepona. Dunia nzima ilishangazwa na huyomnyama nakumfuata. 4Watu wote wakaliabudu lile joka kwa sababulilimpa huyo mnyama uwezo wake. Wakamwabudupia huyo mnyama wakisema, “Nani aliye kama huyu

Page 21: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 13:521UFUNUOWA YOHANA 13:16mnyama? Ni nani awezaye kupigana naye?” 5Kisha huyomnyama akaruhusiwa kusema maneno ya kujigamba nakumkufuru Mungu; akaruhusiwa kuwa na mamlaka kwamuda wa miezi arobaini na miwili. 6 Basi, akaanzakumtukana Mungu, kulitukana jina lake, makao yake, nawote wakaao mbinguni. 7 Aliruhusiwa kuwapiga vita nakuwashinda watu wa Mungu. Alipewa mamlaka juu yawatu wa kila kabila, ukoo, lugha na taifa. 8Wote waishioduniani watamwabudu isipokuwa tu wale ambao majinayao yameandikwa tangu mwanzo wa ulimwengu katikakitabu chauzima chaMwanakondoo aliyechinjwa. 9“Aliyena masikio, na asikie! 10 Waliokusudiwa kuchukuliwamateka lazima watatekwa; waliokusudiwa kuuawa kwaupanga lazima watauawa kwa upanga. Kutokana nahayo ni lazima watu wa Mungu wawe na uvumilivu naimani.” 11 Kisha nikamwona mnyama mwingine anatokaardhini. Alikuwa na pembembili kama pembe za kondoo,na aliongea kama joka. 12 Alikuwa na mamlaka kamilikutoka kwa yule mnyama wa kwanza, na akautumiauwezo huo mbele ya huyo mnyama. Akailazimisha duniayote na wote waliomo humo kumwabudu huyo mnyamawa kwanza ambaye alikuwa na jeraha la kifo lililokuwalimepona. 13 Basi, huyu mnyama wa pili akafanya miu-jiza mikubwa hata akasababisha moto kutoka mbinguniushuke duniani mbele ya watu. 14 Aliwapotosha wakaziwa dunia kwa miujiza hiyo aliyojaliwa kutenda mbele yamnyamawa kwanza. Aliwaambia wakazi wa dunia waten-geneze sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwaamejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi tena. 15 Kishaalijaliwa kuipulizia uhai hiyo sanamu ya yule mnyamawa kwanza, hata ikaweza kuongea na kuwaua watu woteambaohawakuiabudu. 16Aliwalazimishawote, wadogonawakubwa, matajiri na maskini, watu huru na watumwa,

Page 22: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 13:1722UFUNUOWA YOHANA 14:7watiwe alama juu ya mikono yao ya kulia au juu ya paji zanyuso zao. 17 Akapiga marufuku mtu yeyote kununua aukuuza kitu isipokuwa tu mtu aliyetiwa alama hiyo, yaanijina la yule mnyama au tarakimu ya jina hilo. 18 Hapa nilazima kutumia ujasiri! Mwenye akili anaweza kufafanuamaana ya tarakimu ya mnyama huyo, maana ni tarakimuyenye maana ya mtu fulani. Tarakimu hiyo ni mia sitasitini na sita.

141 Kisha nikaona mlima Sioni, na Mwanakondoo ames-

imama juu yake; pamoja naye walikuwa watu mia mojaarobaini na nne elfu ambao juu ya paji za nyuso zaowalikuwa wameandikwa jina la Mwanakondoo na jina laBaba yake. 2 Basi, nikasikia sauti kutoka mbinguni, sautiiliyokuwa kama sauti ya maji mengi na kama sauti yangurumo kubwa. Sauti niliyosikia ilikuwa kama sautiya wachezaji muziki wakipiga vinubi vyao. 3 Walikuwawanaimba wimbo mpya mbele ya kiti cha enzi na mbeleya wale viumbe hai wanne na wale wazee. Hakunamtu aliyeweza kujifunza wimbo huo isipokuwa hao watumia moja arobaini na nne elfu waliokombolewa duniani.4 Watu hao ndio wale waliojiweka safi kwa kutoonanakimwili na wanawake, nao ni mabikira. Wao humfu-ata Mwanakondoo kokote aendako. Wamekombolewakutoka miongoni mwa binadamu wengine, wakawa wakwanza kutolewa kwa Mungu na kwa Mwanakondoo.5 Hawakupata kamwe kuwa waongo; hawana hatia yoy-ote. 6 Kisha nikamwona malaika mwingine anaruka juuangani akiwa na Habari Njema ya milele ya Mungu,aitangaze kwa watu wote waishio duniani, kwa mataifayote, makabila yote, watu wa lugha zote na rangi zote.7 Akasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kum-tukuza! Maana saa imefika ya kutoa hukumu yake.

Page 23: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 14:823UFUNUOWA YOHANA 14:16Mwabuduni yeye aliyeumba mbingu na nchi, bahari nachemchemi za maji.” 8 Malaika wa pili alimfuata huyowa kwanza akisema, “Ameanguka! Naam, Babulonimkuu ameanguka! Babuloni ambaye aliwapa mataifayote wainywe divai yake —divai kali ya uzinzi wake!”9 Na malaika wa tatu aliwafuata hao wawili akisemakwa sauti kubwa, “Yeyote anayemwabudu yule mnyamana sanamu yake na kukubali kutiwa alama yake juuya paji la uso wake au juu ya mkono wake, 10 yeyemwenyewe atakunywa divai ya ghadhabu ya Mungu,ambayo imemiminwa katika kikombe cha ghadhabu yakebila kuchanganywa na maji. Mtu huyo atateseka ndaniya moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu nambele ya Mwanakondoo. 11 Moshi wa moto unaowatesakupanda juu milele na milele. Watu hao waliomwabuduhuyo mnyama na sanamu yake, na kutiwa alama ya jinalake, hawatakuwa na nafuu yoyote usiku na mchana.”12 Kutokana na hayo, ni lazima watu wa Mungu, yaaniwatu wanaotii amri ya Mungu na kumwamini Yesu, wawena uvumilivu. 13 Kisha nikasikia sauti kutoka mbinguniikisema, “Andika! Heri watu ambao tangu sasa wanakufawakiwa wameungana na Bwana.” Naye Roho asema,“Naam! Watapumzika kutoka taabu zao; maana matundaya jasho lao yatawafuata.” 14Kisha nikatazama, na kumbepalikuwapo wingu jeupe hapo. Na juu ya wingu hilokulikuwa na kiumbe kama mtu. Alikuwa amevaa taji yadhahabu kichwani, na kushika mundu mkononi mwake.15Kishamalaikamwingine akatokaHekaluni, na kwa sautikubwa akamwambia yule aliyekuwa amekaa juu yawingu,“Tafadhali, tumia mundu wako ukavune mavuno, maanawakati wa mavuno umefika; mavuno ya dunia yameiva.”16 Basi, yule aliyekuwa amekaa juu ya wingu akautupamundu wake duniani, na mavuno ya dunia yakavunwa.

Page 24: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 14:1724UFUNUOWA YOHANA 15:617 Kisha malaika mwingine akatoka katika Hekalu mbin-guni akiwa na mundu wenye makali. 18 Kisha malaikamwingine msimamizi wa moto, akatoka madhabahuniakamwambia kwa sauti kubwa yule malaika mwenyemundu wenye makali, “Nawe tia huo mundu wako mkali,ukakate vichala vya mizabibu ya dunia, maana zabibuzake zimeiva!” 19 Basi, malaika huyo akautupa munduwake duniani, akakata zabibu za dunia, akazitia ndaniya chombo kikubwa cha kukamulia zabibu, chombo chaghadhabu ya Mungu. 20 Zabibu zikakamuliwa ndani yahilo shinikizo lililoko nje ya mji, na damu ikatoka katikashinikizo hilo mtiririko mrefu kiasi cha mita mia tatu nakina chake kiasi cha mita mia mbili.

151Kisha nikaona ishara nyinginembinguni, kubwa na ya

kushangaza. Palikuwa hapo malaika saba wenye mabaamakubwa saba ya mwisho. Kwa mabaa hayo makubwasaba, ghadhabu ya Mungu imekamilishwa. 2 Kishanikaona kitu kama bahari ya kioo, imechanganywa namoto. Nikawaona pia wale watu waliomshinda yulemnyama na sanamu yake na ambaye jina lake lilitajwakwa ile tarakimu. Watu hao walikuwa wamesimamakando ya hiyo bahari ya kioo, wakiwa na vinubi walivy-opewa na Mungu. 3 Walikuwa wakiimba wimbo waMose, mtumishi wa Mungu, na wimbo waMwanakondoo:“Bwana Mungu Mwenye Uwezo, matendo yako ni makuumno! Ewe Mfalme wa mataifa, njia zako ni za haki na zakweli! 4 Bwana, ni nani asiyekucha wewe? Nani asiyeli-tukuza jina lako? Wewe peke yako ni Mtakatifu. Mataifayote yatakujia na kukuabudu maana matendo yako yahaki yameonekana na wote.” 5 Baada ya hayo nikaonaHekalu limefunguliwa mbinguni, na ndani yake hemaionyeshayo kuwapo kwaMungu. 6Basi, walemalaika saba

Page 25: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 15:7 25UFUNUOWA YOHANA 16:9wenye mabaa saba wakatoka humo Hekaluni, wakiwawamevaa nguo za kitani safi zenye kung'aa, na kandaza dhahabu vifuani mwao. 7 Kisha, mmojawapo wa vileviumbe vinne akawapa hao malaika saba mabakuli yadhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu, aishiye milele namilele. 8Hekalu likajaa moshi uliosababishwa na utukufuna nguvu ya Mungu, na hakuna mtu aliyeweza kuingiaHekalunimpakamwishowamabaamakubwa saba yawalemalaika saba.

161Kisha nikasikia sauti kubwa kutokaHekaluni ikiwaam-

bia wale malaika saba, “Nendeni mkamwage mabakulihayo saba ya ghadhabu ya Mungu duniani.” 2 Basi,malaika wa kwanza akaenda akamwaga bakuli lake juuya nchi. Mara madonda mabaya na ya kuumiza sanayakawapata wote waliokuwa na alama ya yule mnyama,na wale walioiabudu sanamu yake. 3 Kisha malaika wapili akamwaga bakuli lake baharini. Nayo bahari ikawadamu tupu kama damu ya mtu aliyekufa, na viumbevyote hai baharini vikafa. 4 Malaika wa tatu akamwagabakuli lake katika mito na chemchemi za maji, navyo vik-ageuka damu. 5 Nikamsikia malaika msimamizi wa majiakisema, “Ewe mtakatifu, Uliyeko na uliyekuwako! Weweni mwenye haki katika hukumu hii uliyotoa. 6 Maanawaliimwaga damu ya watu wako na ya manabii, naweumewapa damu wainywe; wamestahili hivyo!” 7 Kishanikasikia sauti madhabahuni ikisema, “Naam, BwanaMungu Mwenye Uwezo! Hukumu zako ni za kweli nahaki!” 8 Kisha malaika wa nne akamwaga bakuli lakejuu ya jua. Jua likapewa nguvu ya kuwachoma watukwa moto wake. 9 Basi, watu wakaunguzwa vibaya sana;wakamtukana Mungu aliye na uwezo juu ya mabaa hayo

Page 26: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWAYOHANA16:1026UFUNUOWAYOHANA16:21makubwa. Lakini hawakuziacha dhambi zao na kum-tukuza Mungu. 10 Kisha malaika wa tano akamwagabakuli lake juu ya makao makuu ya yule mnyama. Gizalikauvamia utawala wake, watu wakauma ndimi zao kwasababu za maumivu, 11 wakamtukana Mungu wa mbin-guni kwa sababu yamaumivu yao namadonda yao. Lakinihawakuyaacha matendo yao mabaya. 12 Kisha malaikawa sita akamwaga bakuli lake juu ya mto mkubwa uitwaoEufrate. Maji yake yakakauka, na hivyo njia ilitengenezwakwa ajili ya wafalme wa mashariki. 13Kisha nikaona pepowabaya watatu walio kama vyura, wakitoka kinywanimwa yule joka, kinywani mwa yule mnyama, na kinywanimwa yule nabii wa uongo. 14 Hawa ndio roho za pepowafanyao miujiza. Ndio wanaokwenda kwa wafalme waulimwengu wote na kuwakusanya pamoja kwa ajili yavita kuu Siku ile ya Mungu Mwenye Uwezo. 15 “Sikiliza!Mimi naja kama mwizi! Heri mtu akeshaye na kuvaanguo zake ili asije akaenda uchi huko na huko mbele yawatu.” 16 Basi, roho hao wakawakusanya hao wafalmemahali paitwapo kwa Kiebrania Harmagedoni. 17 Kishamalaika wa saba akamwaga bakuli lake hewani. Sautikubwa ikasikika kutoka kwenye kiti cha enzi, Hekaluni,ikisema, “Mwisho umefika!” 18Kukatokea umeme, kelele,ngurumo na tetemeko kubwa la ardhi ambalo halijapatakutokea tangu Mungu alipomuumba mtu. 19 Mji ulemkuu ukapasuliwa sehemu tatu, nayo miji ya mataifaikateketea. Babuloni, mji mkuu, haukusahauliwa naMungu. Aliunywesha kikombe cha divai ya ghadhabuyake kuu. 20 Visiwa vyote vikatoweka, nayo milimahaikuonekena tena. 21 Mvua ya mawe makubwa yenyeuzitowa kama kilo hamsini kilamoja, ikawanyesheawatu.NaowakamtukanaMungu kwa sababu yamapigo yamvuahiyo ya mawe. Naam, pigo la mvua hiyo ya mawe lilikuwa

Page 27: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 17:1 27UFUNUOWA YOHANA 17:8kubwa mno.

171 Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na bakuli

akaja, akaniambia, “Njoo, mimi nitakuonyesha adhabualiyopewa yule mzinzi mkuu, mji ule uliojengwa juuya maji mengi. 2 Wafalme wa dunia wamefanya uzinzipamoja naye; na wakazi wa dunia wamelewa divai yauzinzi wake.” 3 Kisha, Roho akanikumba, akaniongozampaka jangwani. Huko nikamwona mwanamke ameketijuu ya mnyama mwekundu. Mnyama huyo alikuwaameandikwa kila mahali majina ya makufuru; alikuwa navichwa saba na pembe kumi. 4Mwanamke huyo alikuwaamevaa vazi la rangi ya zambarau na nyekundu; alikuwaamejipamba kwa dhahabu, mawe ya thamani na lulu.Mkononi mwake alishika kikombe cha dhahabu ambachokilikuwa kimejaa machukizo na mambo machafu yanay-oonyesha uzinzi wake. 5 Alikuwa ameandikwa juu ya pajila uso wake jina la fumbo “Babuloni mkuu, mama wawazinzi na wa mambo yote ya kuchukiza sana duniani.”6 Nikamwona huyo mwanamke amelewa damu ya watuwa Mungu, na damu ya watu waliouawa kwa sababuya kumtangaza Yesu. Nilipomwona nilishangaa mno.7 Lakini malaika akaniambia, “Kwa nini unashangaa?Mimi nitakuambiamaana iliyofichika yamwanamkehuyuna mnyama huyo amchukuaye ambaye ana vichwa sabana pembe kumi. 8Huyomnyama uliyemwona alikuwa haihapo awali, lakini sasa amekufa. Hata hivyo, karibu sanaatapanda kutoka shimoni kuzimu, lakini ataangamizwa.Wanaoishi duniani watashangaa; naam, watu wote am-bao majina yao hayakupata kuandikwa katika kitabu chauzima tangu mwanzo wa ulimwengu, watashangaa kum-wona huyo mnyama ambaye hapo awali, aliishi, kisha

Page 28: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 17:9 28UFUNUOWA YOHANA 18:1akafa na sasa anatokea tena! 9 “Hapa panahitaji ak-ili na hekima! Hivyo vichwa saba ni vilima saba, nahuyo mwanamke anaketi juu yake. Vichwa hivyo piani wafalme saba. 10 Kati ya hao wafalme saba, watanowamekwisha angamia, mmoja anatawala bado, na yulemwingine bado hajafika; na atakapofika atabaki kwamuda mfupi. 11 Huyo mnyama ambaye alikuwa anaishihapo awali lakini sasa haishi tena ni mfalme wa nane,naye pia ni miongoni mwa hao saba, na anakwenda zakekuharibiwa. 12 “Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalmeambao bado hawajaanza kutawala. Lakini watapewamamlaka ya kutawala kwa muda wa saa moja pamojana yule mnyama. 13 Shabaha ya hawa kumi ni moja,na watampa yule mnyama nguvu na mamlaka yao yote.14 Watapigana na Mwanakondoo, lakini Mwanakondoopamoja na wale aliowaita na kuwachagua, ambao niwaaminifu, atawashinda kwa sababu yeye ni Bwana wamabwana naMfalmewawafalme.” 15Malaika akaniambiapia, “Yale maji uliyoyaona pale alipokaa yule mzinzi, nimataifa, watu wa kila rangi na lugha. 16 Pembe zilekumi ulizoziona na yule mnyama watamchukia huyomzinzi. Watachukua kila kitu alicho nacho na kumwachauchi; watakula nyama yake na kumteketeza kwa moto.17Maana Mungu ametia mioyoni mwao nia ya kutekelezashabaha yake, yaani kwa kukubaliana wao kwa waona kumpa huyo mnyama mamlaka yao ya kutawala,mpaka hapo neno la Mungu litakapotimia. 18 “Na yulemwanamkeuliyemwonandio ulemjimkuuunaowatawalawafalme wa dunia.”

181 Baada ya hayo, nilimwona malaika mwingine ak-

ishuka kutoka mbinguni. Alikuwa na uwezo mkuu,

Page 29: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 18:229UFUNUOWA YOHANA 18:12na dunia ikamulikwa na mng'ao wake. 2 Basi, aka-paaza sauti kwa nguvu akisema, “Umeanguka; Bab-uloni mkuu umeanguka! Sasa umekuwa makao yamashetani na pepo wachafu; umekuwa makao ya ndegewachafu na wa kuchukiza mno. 3 Maana mataifa yoteyalileweshwa kwa divai kali ya uzinzi wake, nao wafalmewa dunia wamefanya uzinzi naye. Nao wafanyabiasharawa dunia wametajirika kutokana na anasa zake zisizona kipimo.” 4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutokambinguni ikisema, “Watu wangu, ondokeni kwake, ilimsishirikiane naye katika dhambi zake, msije mkaipataadhabu yake. 5 Kwa maana dhambi zake zimekuwanyingi mno, zimelundikana mpaka mbinguni, na Munguameyakumbuka maovu yake. 6 Mtendeeni kama alivy-owatendea ninyi; mlipeni mara mbili kwa yale aliyoya-tenda. Jazeni kikombe chake kwa kinywaji kikali marambili zaidi ya kile alichowapeni. 7 Mpeni mateso nauchungu kadiri ya kujigamba kwake, na kuishi kwakekwa anasa. Maana anajisemea moyoni: Ninaketi hapa;mimi ni malkia. Mimi si mjane, wala sitapatwa nauchungu! 8 Kwa sababu hiyo mabaa yake yatampatakwa siku moja: ugonjwa, huzuni na njaa. Atachomwamoto, maana Bwana Mungu mwenye kumhukumu niMwenye Uwezo.” 9Wafalme wa Dunia waliofanya uzinzinaye na kuishi naye maisha ya anasa wataomboleza nakulia wakati watakapoonamoshi wamji huo unaoteketea.10Wanasimama kwambali kwa sababu ya kuogopamatesoyake, na kusema, “Ole! Ole kwako Babuloni, mji maarufuna wenye nguvu! Kwa muda wa saa moja tu adhabuyako imekupata.” 11 Wafanyabiashara wa dunia wataliana kumfanyia matanga, maana hakuna mtu anayenunuatena bidhaa zao; 12 hakuna tena wa kununua dhahabuyao, fedha, mawe ya thamani na lulu, kitani na nguo za

Page 30: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWAYOHANA18:1330UFUNUOWAYOHANA18:22rangi ya zambarau, hariri na nguo nyekundu; vyombovya kila aina ya miti ya pekee, vyombo vya pembe zandovu, vya miti ya thamani kubwa, vya shaba, chumana marmari; 13 mdalasini, viungo, ubani, manemane,udi, divai, mafuta, unga na ngano, ng'ombe na kondoo,farasi na magari ya kukokotwa, watumwa wao na hatamaisha ya watu. 14 Wafanyabiashara wanamwambia:“Faida yote uliyotazamia imetoweka, na utajiri na faharivimekuponyoka; hutaweza kuvipata tena!” 15 Wafanyabiashara waliotajirika kutokana na mji huo, watasimamambali kwa sababu ya hofu ya mateso yake, watalalamikana kuomboleza, 16wakisema, “Ole! Ole kwamji huumkuu.Ulizoea kuvalia nguo za kitani, za rangi ya zambarau nanyekundu, na kujipamba kwa dhahabu, mawe ya thamanina lulu! 17Kwa saa moja tu utajiri wako umetoweka!” Ha-lafu manahodha wote na wasafiri wao, wanamaji na wotewanaofanya kazi baharini, walisimama kwa mbali, 18 nawalipouona moshi wa moto ule uliouteketeza, wakaliakwa sauti: “Hakujapata kuwakomji kamamji huumkuu!”19 Wakajimwagia vumbi juu ya vichwa vyao wakilia kwasauti na kuomboleza: “Ole! Ole kwako mji mkuu! Ni mjiambamo wote wenye meli zisafirizo baharini walitajirikakutokana na utajiri wake. Kwa muda wa saa moja tuumepoteza kila kitu!” 20 Furahi ee mbingu, kwa sababuya uharibifu wake. Furahini watu wa Mungu, mitume namanabii! Kwa maana Mungu ameuhukumu kwa sababuya mambo uliyowatenda ninyi! 21 Kisha malaika mmojamwenye nguvu sana akainua jiwe mfano wa jiwe kubwala kusagia, akalitupa baharini akisema, “Ndivyo, Babuloniatakavyotupwa na kupotea kabisa. 22 Sauti za vinubi zamuziki, sauti za wapiga filimbi na tarumbeta hazitasikikatena ndani yako. Hakuna fundi wa namna yoyote ileatakayepatikana tena ndani yako; wala sauti ya jiwe la

Page 31: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 18:2331UFUNUOWA YOHANA 19:9kusagia haitasikika tena ndani yako. 23 Mwanga wa taahautaonekana tena ndani yako; sauti za bwana arusi nabibi arusi hazitasikika tena ndani yako. Wafanyabiasharawako walikuwa wakuu duniani, na kwa uchawi wakomataifa yote yalipotoshwa!” 24Mji huo uliadhibiwa kwanihumo mlipatikana damu ya manabii, damu ya watu waMungu na damu ya watu wote waliouawa duniani.

191 Baada ya hayo nikasikia kitu kama sauti kubwa ya

umati wa watu wengi mbinguni ikisema, “Haleluya!Ukombozi, utukufu na nguvu ni mali yake Munguwetu! 2 Maana hukumu yake ni ya kweli na ya haki.Amemhukumu yule mzinzi mkuu ambaye alikuwaameipotosha dunia kwa uzinzi wake. Amemwadhibukwa sababu ya kumwaga damu ya watumishi wake!”3 Wakasema, “Asifiwe Mungu! Moshi wa motounaoteketezamji huoutapanda juumilele namilele!” 4Nawale wazee ishirini na wanne, na vile viumbe hai vinne,wakajitupa chini, wakamwabudu Mungu aliyeketi juu yakiti cha enzi wakisema, “Amina! Asifiwe Mungu!” 5 Kishakukatokea sauti kwenye kiti cha enzi: “Msifuni Munguenyi watumishi wake wote, nyote mnaomcha, wadogokwawakubwa.” 6Kisha nikasikia kitu kama sauti ya umatimkubwa wa watu na sauti ya maji mengi na ya ngurumokubwa, ikisema, “Haleluya! Maana Bwana Mungu wetuMwenye Uwezo ni Mfalme! 7 Tufurahi na kushangilia;tumtukuze, kwani wakati wa arusi ya Mwanakondooumefika, na bibi arusi yuko tayari. 8 Amepewa uwezowa kujivalia nguo ya kitani safi, iliyotakata na yenyekung'aa!” (Nguo hiyo ya kitani safi ni matendo mema yawatu wa Mungu.) 9 Kisha malaika akaniambia, “Andikahaya: Heri wale walioalikwa kwenye karamu ya arusi ya

Page 32: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWAYOHANA19:1032UFUNUOWAYOHANA19:19Mwanakondoo!” Tena akaniambia, “Hayo ni maneno yakweli ya Mungu.” 10 Basi, mimi nikaanguka kifudifudimbele ya miguu yake nikataka kumwabudu. Lakiniyeye akaniambia, “Acha! Mimi ni mtumishi tu kamawewe na ndugu zako; sote tunauzingatia ukweli ulealioufunua Yesu. Mwabudu Mungu! Maana ukwelialioufunua Yesu ndio unaowaangazia manabii.” 11 Kishanikaona mbingu zimefunguliwa; na huko alikuwakofarasi mmoja mweupe, na mpanda farasi wake aliitwa“Mwaminifu” na “Kweli”. Huyo huhukumu na kupiganakwa ajili ya haki. 12 Macho yake ni kama mwali wamoto, na alikuwa amevaa taji nyingi kichwani. Alikuwaameandikwa jina ambalo hakuna mtu alijuaye isipokuwatu yeye mwenyewe. 13 Alikuwa amevaa vazi lililokuwalimelowekwa katika damu. Na jina lake huyo ni “Nenola Mungu.” 14 Majeshi ya mbinguni yalimfuata yakiwayamepanda farasiweupenawalikuwawamevaamavazi yakitani, meupe na safi. 15 Upanga mkali hutoka kinywanimwake, na kwa upanga huo atawashinda mataifa. Yeyendiye atakayetawala kwa fimbo ya chuma na kuikamuadivai katika chombo cha kukamulia zabibu za ghadhabukuu ya Mungu Mwenye Uwezo. 16 Juu ya vazi lake, na juuya mguu wake, alikuwa ameandikwa jina: “Mfalme wawafalme na Bwana wa mabwana.” 17 Kisha nikamwonamalaika mmoja amesimama katika jua. Akapaaza sautina kuwaambia ndege wote waliokuwa wanaruka juuangani, “Njoni! Kusanyikeni pamoja kwa karamu kuuya Mungu. 18 Njoni mkaitafune miili ya wafalme, yamajemadari, ya watu wenye nguvu, ya farasi na wapandafarasi wao; njoni mkaitafune miili ya watu wote: waliohuru na watumwa, wadogo na wakubwa.” 19 Kishanikaona yule mnyama pamoja na mfalme wa dunia naaskari wao wamekusanyika pamoja kusudi wapigane na

Page 33: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 19:2033UFUNUOWA YOHANA 20:6yule aliyekuwa ameketi juu ya farasi, pamoja na jeshilake. 20 Lakini huyo mnyama akachukuliwa mateka,pamoja na nabii wa uongo aliyekuwa akifanya miujizambele yake. (Kwa miujiza hiyo, alikuwa amewapotoshawale waliokuwa na chapa ya huyo mnyama, na ambaowalikuwa wameiabudu sanamu yake.) Huyo mnyamapamoja na huyo nabii walitupwa wote wawili, wakiwawazimawazima, ndani ya ziwa linalowaka moto wakiberiti. 21 Majeshi yao yaliuawa kwa upanga uliotokakinywani mwa yule anayepanda farasi. Ndege wotewakajishibisha kwa nyama zao.

201 Kisha nikamwona malaika mmoja anashuka kutoka

mbinguni akiwa na ufunguo wa kuzimu na mnyororomkubwa mkononi mwake. 2 Akalikamata lile joka —nyoka wa kale, yaani Ibilisi au Shetani—akalifunga kwamuda wa miaka elfu moja. 3 Malaika akalitupa Kuz-imu, akaufunga mlango wa kuingilia huko na kuutiamhuri ili lisiweze tena kuyapotosha mataifa mpaka hapomiaka elfu moja itakapotimia. Lakini baada ya miakahiyo ni lazima lifunguliwe tena, lakini kwa muda mfupitu. 4 Kisha nikaona viti vya enzi na watu walioketi juuyake; watu hao walipewa mamlaka ya hukumu. Nil-iona pia roho za wale waliokuwa wamenyongwa kwasababu ya kumtangaza Yesu na kwa sababu ya nenola Mungu. Hawa hawakumwabudu yule mnyama nasanamu yake, wala hawakupigwa alama yake juu ya pajiza nyuso zao, au juu ya mikono yao. Walipata tena uhai,wakatawala pamoja na Kristo kwa muda wa miaka elfumoja. 5 (Wale wengine waliokufa hawakupata uhai mpakamiaka elfu moja itimie.) Huu ndio ufufuo wa kwanza.6 Wameneemeka sana, tena heri yao wote wanaoshiriki

Page 34: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 20:7 34UFUNUOWA YOHANA 21:1ufufuo huuwa kwanza. Kifo cha pili hakitakuwa na nguvujuu yao; watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nawatatawala pamoja naye kwa miaka elfu moja. 7 Wakatimiaka elfu mia moja itakapotimia, Shetani atafunguliwakutoka gerezani mwake. 8 Basi, atatoka nje, ataanzakuyapotosha mataifa yote yaliyotawanyika kila mahaliduniani, yaani Gogu na Magogu. Shetani atawakusanyapamoja kwa ajili ya vita; nao watakuwa wengi kamamchanga wa pwani. 9 Walitawanyika katika nchi yote,wakaizunguka kambi ya watu wa Mungu na mji waMungu aupendao. Lakini moto ulishuka kutoka mbin-guni, ukawaangamiza. 10 Ibilisi, aliyekuwa anawapotosha,akatupwa ndani ya ziwa linalowakamoto wa kiberiti, wal-imo yule mnyama na yule nabii wa uongo, nao watateswamchana na usiku, milele na milele. 11 Kisha nikaonakiti cha enzi kikubwa cheupe, na yule aketiye juu yake.Dunia na mbingu vikatoweka mbele ya macho yake, nahavikuonekana tena. 12 Kisha nikawaona watu wakubwanawadogo, wamesimamambele ya kiti cha enzi, na vitabuvikafunguliwa. Halafu kitabu kingine, yaani kitabu chauzima, kikafunguliwa pia. Wafu wakahukumiwa kadiriya matendo yao, kama ilivyoandikwa ndani ya vitabuhivyo. 13Bahari ikawatoa nje wafu waliokuwa ndani yake;kifo na kuzimu vikawatoa nje wafu waliokuwa ndani yao.Kila mmoja akahukumiwa kufuatana na matendo yake.14Kisha kifo na kuzimu vikatupwa ndani ya ziwa la moto.Ziwa hili la moto ndicho kifo cha pili. 15Mtu yeyote am-baye jina lake halikupatikana limeandikwa katika kitabucha uzima, alitupwa katika ziwa la moto.

211 Kisha nikaona mbingu mpya na dunia mpya. Mbingu

ile ya kwanza na dunia ile ya kwanza vilikuwa vime-

Page 35: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 21:235UFUNUOWA YOHANA 21:12toweka, nayo bahari pia haikuweko tena. 2 Nikaonamji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwaMungu mbinguni. Ulikuwa umetayarishwa vizuri kamabibi arusi aliyepambwa tayari kukutana na mumewe.3 Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka katika kiti chaenzi ikisema, “Tazama! Mungu amefanya makao yakekati ya watu. Atakaa kati yao, nao watakuwa watuwake, naye atakuwa Mungu wao. 4 Yeye atayafuta ma-chozi yao yote; maana hakutakuwako tena na kifo, walauchungu, wala kilio, wala maumivu; maana ile hali yakale imepita!” 5 Kisha yule aliyeketi juu ya kiti chaenzi akasema, “Tazama, nafanya yote mapya.” Tenaakaniambia, “Andika hili, maana maneno haya ni yakuaminika na ya kweli!” 6 Kisha akaniambia, “Yame-timia! Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho.Aliye na kiu nitampa kinywaji cha bure kutoka katikachemchemi ya maji ya uzima. 7 Yeyote atakayeshindaatapokea hiki, nami nitakuwaMunguwake, naye atakuwamwanangu. 8 Lakini watu waoga, wasioamini, wapotovu,wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, na waongowote, mahali pao patakuwa ndani ya lile ziwa linalowakamoto na kiberiti; hicho ndicho kifo cha pili.” 9 Kishammoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakulisaba yaliyokuwa yamejaamabaa saba yamwisho, akaja nakuniambia, “Njoo! Mimi nitakuonyesha bibi arusi, mkeweMwanakondoo!” 10 Basi, Roho akanikumba, naye malaikaakanipeleka juu ya mlima mrefu sana. Akanionyeshamji mtakatifu, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni,11 uking'aa kwa utukufu wa Mungu. Mwangaza wakeulikuwa kama wa jiwe la thamani kubwa kama yaspi,angavu kamakioo. 12Ulikuwanaukutamrefunamkubwa,wenye milango kumi na miwili, na malaika wanangojeakumi na wawili. Majina ya wangoja milango kumi na

Page 36: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWAYOHANA21:1336UFUNUOWAYOHANA21:24mawili ya Israeli yalikuwa yameandikwa juu ya milangohiyo. 13 Kila upande ulikuwa na milango mitatu: upandewa mashariki, milango mitatu, kaskazini milango mitatu,kusini milango mitatu na magharibi milango mitatu.14 Kuta za mji huo zilikuwa zimejengwa juu ya mawe yamsingi kumi na mawili, na juu ya mawe hayo yalikuwayameandikwa majina na mitume kumi na wawili waMwanakondoo. 15 Basi, yule malaika aliyekuwa anasemanami alikuwa na kijiti cha dhahabu cha kupimia, kwa ajiliya kuupima huo mji, milango yake na kuta zake. 16 Mjiwenyewe ulikuwa wa mraba, upana na urefu wake sawa.Basi, malaika akaupima mji huo kwa kijiti chake: ulikuwana urefu, upana na urefu wa kwenda juu, kama kilomitaelfu mbili na mia nne. 17 Kisha akaupima ukuta wakepia; nao ulikuwa mita sitini kwa kipimo cha macho chakibinadamu ambacho malaika alitumia. 18 Ukuta huoulikuwa umejengwa kwa mawe mekundu ya thamani,na mji wenyewe ulikuwa umejengwa kwa dhahabu safi,angavu kama kioo. 19Mawe ya msingi wa ukuta huo ya-likuwa yamepambwa kwa kila aina ya mawe ya thamani.Jiwe la kwanza lamsingi lilikuwa jiwe la thamani jekundu,la pili yakuti samawati, la tatu kalkedoni, la nne zamaradi,20 la tano sardoniki, la sita akiki, la saba krisolito, lanane zabarijadi, la tisa topazi, la kumi krisopraso, lakumi na moja yasinto, na la kumi na mbili amethisto.21 Na ile milango kumi na miwili ilikuwa lulu kumi nambili; kila mlango ulikuwa umetengenezwa kwa lulumoja. Barabara kuu ya mji ilikuwa imetengenezwa kwadhahabu safi, angavu kama kioo. 22 Sikuona hekalu katikamji huo, maana Bwana Mungu Mwenye Uwezo na yuleMwanakondoo ndio Hekalu lake. 23 Mji huo hauhitajijua wala mwezi kuangazia, maana utukufu wa Munguhuuangazia, na taa yake ni yule Mwanakondoo. 24 Watu

Page 37: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWA YOHANA 21:2537UFUNUOWA YOHANA 22:9wamataifa watatembea katikamwangawake, na wafalmewa dunia watauletea utajiri wao. 25 Milango ya mji huoitakuwa wazi mchana wote; maana hakutakuwa na usikuhumo. 26 Fahari na utajiri wa watu wa mataifa utaletwahumo ndani. 27 Lakini hakuna chochote kilicho najisikitakachoingia humo; wala mtu yeyote atendaye mamboya kuchukiza au ya uongo hataingia humo. Ni wale tuwalioandikwa katika kitabu cha uzima chaMwanakondoondio watakaoingia ndani.

221 Kisha malaika akanionyesha mto wa maji ya uzima

maangavu kama kioo yakitoka kwenye kiti cha enzi chaMungu na Mwanakondoo. 2 Mto huo ulitiririka kupitiakatikati ya barabara kuu ya mji. Kandokando ya mto huokulikuwa na mti wa uzima unaozaa matunda mara kumina mbili kwa mwaka, yaani kila mwezi; na majani yakeni dawa ya kuwaponya watu wa mataifa. 3 Hapana kituchochote kilicholaaniwa kitakachokuwa katika mji huo.Kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwanakondoo kitakuwakatika mji huo, na watumishi wake watamwabudu.4Watauona uso wake, na jina lake litaandikwa juu ya pajiza nyuso zao. 5Usiku hautakuwako tena, wala hawatahi-taji mwanga wa taa au wa jua, maana Bwana Munguatawaangazia, nao watatawala milele na milele. 6 Kishamalaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kweli na yakuaminika. BwanaMungu ambaye huwapamanabii Rohowake, alimtuma malaika wake awaonyeshe watumishiwake mambo ambayo lazima yatukie punde. 7 “Sikiliza!Naja upesi. Heri yake anayeyazingatia maneno ya unabiiyaliyo katika kitabu hiki.” 8 Mimi Yohane, niliyaonana kusikia mambo haya. Nilipokwisha sikia na kuonanikajitupa chini mbele ya miguu ya huyo malaika aliye-nionyesha mambo hayo, nikataka kumwabudu. 9 Lakini

Page 38: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWAYOHANA22:1038UFUNUOWAYOHANA22:20yeye akaniambia, “Acha! Mimi ni mtumishi tu kamawewe na ndugu zako manabii na wote wanaoyatii maa-gizo yaliyomo katika kitabu hiki. Mwabudu Mungu!”10 Tena akaniambia, “Usiyafiche kama siri maneno yaunabii yaliyomo katika kitabu hiki, maana wakati wakutimizwa kwake umekaribia. 11 Kwa sasa anayetendamabaya na aendelee kutenda mabaya, na aliye mchafuaendelee kuwa mchafu. Mwenye kutenda mema na azidikutenda mema, na aliye mtakatifu na azidi kuwa mtakat-ifu.” 12 “Sikiliza!” Asema Yesu, “Naja upesi, pamojana tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendoyake. 13 Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho,wa kwanza na wa mwisho.” 14 Heri yao wale wanaooshamavazi yao, kwani watakuwa na haki ya kula tunda la mtiwa uzima, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milangoyake. 15 Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudusanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaanje ya mji. 16 “Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wanguawathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi nimzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu yaasubuhi!” 17 Roho na Bibiarusi waseme, “Njoo!” Kilamtu asikiaye hili, na aseme, “Njoo!” Kisha, yeyotealiye na kiu na aje; anayetaka maji ya uzima na apokeebila malipo yoyote. 18 Mimi Yohane nawapa onyo wotewanaosikia maneno ya unabii yaliyomo katika kitabuhiki: mtu yeyote akiongeza chochote katika mambohaya, Mungu atamwongezea mabaa yaliyoandikwa katikakitabu hiki. 19Namtu yeyote akipunguza chochote katikamaneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, Munguatamnyang'anya sehemu yake katika ulemti wa uzima, nasehemu yake katika mji mtakatifu, ambavyo vimeelezwakatika kitabu hiki. 20Naye anayetoa ushahidi wake juu yamambo haya asema: “Naam! Naja upesi.” Amina. Na iwe

Page 39: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

UFUNUOWAYOHANA22:2139UFUNUOWAYOHANA22:21hivyo! Njoo Bwana Yesu! 21Nawatakieni nyote neema yaBwana Yesu. Amen.

Page 40: UFUNUOWAYOHANA - ebible.org · UFUNUOWAYOHANA2:3 3 UFUNUOWAYOHANA2:13 Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume nakumbesio, ukagunduakwambaniwaongo

40Biblia Takatifu

Portions of the New Testament in the Swahili Language of Kenya,Mozambique, Somalia, and Tanzania, translation by Dr. Johann

Ludvig Krapf completed in 1850Public DomainLanguage: Kiswahili (Swahili)Dialect: KimvitaTranslation by: Dr. Johann Ludvig Krapf

2014-08-25UpdateseBible.orgPDF generated using Haiola and XeLaTeX on 17 Nov 2018 from source files dated 12Nov 201862071dc0-70e6-5b86-b569-c1b45e7771bd