mofolojia ya kiswahili · web viewkatika lugha ya kiswahili viambishi ni vingi. na kama...
TRANSCRIPT
Mofolojia ya Kiswahili 2018
OSW 233 MOFOLOJIA YA KISWAHILI (NUKUU)
MUHADHARA WA KWANZA 1: MOFOLOJIA
Fasili ya MofolojiaMofolojia ni taaluma ya isimu inayoshughuliki muundo wa maneno. Ni taaluma inayoshughulikia vipashio vya lugha na mpangilio wake katika uundaji wa maneno.
Mofolojia : ni utanzu mmojawapo katika tanzu za isimu
Tanzu hizo za isimu ni:
1. Mofolojia2. Fonolojia3. Sintaksia4. Semantiki na5. Pragmatiki
Uhusiano wa Mofolojia na matawi mengine ya isimu Mofolojia na fonolojia
Vipashio vya kifonolojia (fonimu) ndivyo vitumikavyo kuunda vipashio vya kimofolojia (mofimu). Mfano soda limeundwa kwa fonimu /s/, /o/, /d/, /a/ na bibi limeundwa kwa fonimu /b/, /i/, /b/, /i/
Kanuni za kifonolojia huweza kutumika kuelezea maumbo ya kimofolojia ambayo yanaathiriana. Mfano: mofimu ya umoja katika ngeli ya kwanza inajitokeza kama m- ikifuatiwa na konsonanti ila hujitokeza kama mw- ikifuatiwa na irabu (m + ti = mti, mu + eupe = mweupe).
Mofolojia na sintaksia
Vipashio vya kimofolojia (mofimu/neno) huunda daraja ya sintaksia. Mfano: sentensi walitusafirisha imeundwa na mofimu wa-li-tu-safiri-sh-a
Mabadiliko ya umbo la mofimu/neno huathiri muundo wa sentensi nzima (mf. umoja na wingi).
(i) Mtoto mefu mweusi anakuja(ii)Watoto warefu weusi wanakuja
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 1
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Mofolojia na semantiki
Semantiki ni taaluma ya maana. Mofimu ni kipashio cha lugha chenye maana mfano; neno kisu lina mofimu mbili ambazo ni ki- umoja na – su ya mzizi. Ukizigawanya zaidi mofimu hizi utapata k-i-s-u; ambazo ni sauti/herufi zisizo na maana na si mofimu. Hivyo mofimu si umbo ni maana – ikiwa ni ya kisarufi au ya kileksika.
Mofolojia hujishughulisha na uundaji wa maneno katika lugha husika; msingi wa neno ni maana. Hivyo mpangilio wa mofimu usioleta maana katika lugha husika hauwezi kutambuliwa kama neno. Mfano. palingunywi ni mfuatano wa fonimu uliozingatia taratibu za lugha ya Kiswahili lakini si neno la Kiswahili kwa sababu halina maana katika lugha hiyo.
Mambo ya kuzingatia katika taaluma ya mofolojia
Uundaji wa maneno
Hapa tunaangalia vijenzi vya neno husika. Kwa mfano neno limeundwa na mofimu huru pekee kama papai, mofimu huru na mofimu tegemezi kama mpapai (m + papai) au mofimu tegemezi tupu kama mtu (m + tu).
Katika uundaji wa maneno tunaangalia vilevile njia mbalimbali za uundaji wa maneno katika lugha ya Kiswahili kama vile kutohoa, uambatishaji, urudufu, uhulutishaji, uambishaji, n.k.
NJIA ZA UUNDAJI WA MANENO /ISTILAHI/ MSAMIATIUundaji wa maneno ni mchakato unaowezesha lugha kujiongezea msamiati ili kukidhi haja ya mawasiliano na kuendana na mabadiliko yanayotokea kila siku.
Maneno ya lugha ya Kiswahili hayaundwi kiholela bali hufuata taratibu na kanuni zinazokubalika kitaalamu.
Njia zitumikazo kuunda maneno ni kama zifuatazo:
Unyambuaji
Njia hii inatumia mzizi mmoja wa neno na kuzalisha maneno mapya kwa kupachika viambishi nyambuaji.
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 2
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Mfano
soma
Somo
Kisomo
Msomi
Msomaji
lima
Mkulima
Kilimo
Mlimaji
Uambatishaji/mwambatano
Hii ni njia ya kuunda maneno mapya kwa kuambatanisha maneno mawili.
Mfano
Mwana+chama - Mwanachama
Askari+kanzu – Askarikanzu Bwana+shamba - Bwanashamba
Urudufishaji / Uradidi
Hii ni mbinu ya kurudiarudia neno au sehemu ya neno na kuunda neno jipya ambalo huwa na maana tofauti na maneno yanayorudiwarudiwa.
Mfano
(a) Pole : polepole
(b) Sawa : sawasawa
(c) Haraka : harakaharaka
Akronimu/ufupishajiMaeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 3
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Ufupishaji ni njia mojawapo ya kuunda maneno mapya, ufupishaji huweza kufanyika kwa namna mbili ambazo ni.
Kufupisha kwa kuchukua herufi za mwanzo MfanoCWT (Chama cha Walimu Tanzania) VVU (Virusi Vya Ukimwi)
Kufupisha kwa kuchukua silabi za mwanzo za maneno yanayofupishwa
Mfano
BAKITA (Baraza la Kiswahili la Taifa)
TUKI (Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili)
TATAKI (Taasisi ya Taaluma za Kiswahili)
Uhulutishaji
Ni njia ya kuunda maneno mapya kwa kuchukua vijisehemu vya neno pasipo kufuata kanuni yoyote.
Mfano:
Mnyama mfu – nyamafuChakula cha jioni – chajioHati za kukataza – hatazaMtu asiye kwao - msikwao
Utohoaji
Ni uchukuaji wa maneno toka lugha moja na kuyatumia kwenye lugha nyingine baada ya kuyarekebisha kimatamshi na kimaandishi ili yaendane na sarufi ya lugha inayotohoa.
Mfano
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 4
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Neno Lugha asilia Kiswahili
Shirt Kiingereza Shati
Schule Kijerumani Shule
Bakura Kiarabu Bakora
Benjera Kireno Bendera
Matching guys Kiingereza Machinga
KuchukuaHii ni mbinu ya kuongenza maneno kwa kuyachukua toka lugha yake ya asili na kuyatumia kama yalivyo katika lugha inayotohoa. Uchukuaji hufanyika kwa lugha zinazoendana kisarufi kama Kiswahili na lugha za kibantu.
MfanoKitivo — kisambaa /kipareIkulu - kinyamweziKigoda - kizaramo
Kubadili mpangilio wa fonimu
Mfano
Lima – mila – imla - mali
Kufananisha umbo /sauti /tabia
MfanoKufananisha umbo Kifaru-(mnyama faru)Mkono wa tembo-(mkonga wa tembo)Kidole tumbo-(umbo la kidole)Kufananisha TabiaUbeberu-(beberu la mbuzi)Ukupe-(mdudu kupe)
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 5
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Kufananisha SautiPikipiki (mlio wa pikipiki)Mtutu (mlio wa bunduki)Nyau (mlio wa paka)Kuku - kokoriko (mlio wa kuku)
Njia ya udondoshaji
Mfanomkwe wake - mkwewe mwana wake - mwanawe ndugu yake – nduguye
Kuzingatia matumizi ya kitu
MfanoBanio - (kubana) Chanio - (kuchana) Fyekeo - (kufyeka)Kutarjumi/kutafsiriMfano;Fluid – (ugiligili)Acquired immunal deficiency syndrome - Upungufu wa kinga mwiliniHuman immunal virus – virusi vya ukimwiAnti-rentro-virus - dawa za kufubaza makali ya ukimwi
Makundi na mahusiano ya maneno
Taaluma ya mofolojia inaangalia pia makundi ya aina za maneno kama vile nomino, kitenzi, kivumishi, kielezi, n.k. na wakati huohuo huchunguza uhusiano uliopo baina ya makundi hayo ya maneno. Kwa mfano kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya nomino na kivumishi au baina ya kitenzi na kielezi wakati ambapo hakuna uhusiano huo baina ya kitenzi na kivumishi au baina ya nomino na kielezi. Aidha, hakuna uhusiano wowote wa kisarufi baina ya vihisishi na maneno mengine yaliyomo katika tungo.
Kanuni za uundaji wa maneno
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 6
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Uundaji wa maneno hufuata kanuni mbalimbali za kimofolojia na za kimofofonolojia. Miongoni mwa kanuni zinazotawala katika kuunda maneno ni kama vile uyeyushaji, ukaakaishaji, odondoshaji, uingizaji, tangamano la irabu, mvutano wa irabu, n.k.
Hivyo mwanaisimu yeyote anayejishughulisha na uwanja huu wa mofolojia lazima ayajue na kuyazingatia kwa kina mambo haya.
MUHADHARA WA 2 : MOFU NA MOFIMU
MOFU
Fasili ya mofuMofu ni kipashio cha kimofolojia kiwakilishacho mofimu.kutokana na maana hii twaweza kusema mofu ni kiwakilishi na mofimu ndiyo iwakilishwayo na mofu.
Mofu ni umbo linalositiri mofimu. Hivyo mofu ni umbo tu linalodhihirika kimatamshi kama fonimu/sauti na kimaandishi kama herufi.
Aina za mofuMara nyingi mofu huainishwa kwa kutumia vigezo vikuu viwili. Kigezo cha kwanza ni kwa mujibu wa maana iwakilishwayo na mofu na kigezo cha pili ni kwa mujibu wa muundo/mofolojia ya mofu yenyewe. Kwa kutumia kigezo cha maana iwakilishwayo na mofu tunapata mofu huru, mofu funge na mofu tata.
Mofu huruNi yale maumbo yanayobeba maana zinazojitosheleza/kamili. Katika Kiswahili mizizi ya maneno mengi huwa ni mofu huru kwa mfano nomino (baba, kalamu, Magomeni, n.k.), vivumishi (safi, imara, bora, dhaifu, n.k.), viwakilishi (sisi, wewe, wao, n.k.), vielezi (leo, haraka, taratibu, n.k.) viunganishi (na, halafu, lakini).
Mofu Funge/tegemeziNi maumbo ambayo husitiri maana zisizojitosheleza. Mofu funge huhitaji kufungamana na mofu nyengine ili kuzalisha umbo lenye maana kamili. Kwa mfano; maumbo a, li, tu, lish, na a ni maumbo ambayo hatuwezi kujua maana zake hadi pale maumbo hayo yatakapounganishwa na kuwa umbo
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 7
Mofolojia ya Kiswahili 2018
moja alitulisha. Hapa sasa tunaweza kufafanua maana zilizofichwa ndani ya maumbo haya ambazo ni:-
Mofu Maana (mofimu)a- Nafsi (ya tatu)
Idadi (umoja)Neli (ya kwanza A-WA)
-li- MtendaWakati (uliopita)
-tu- Nafsi (ya kwanza)Idadi (wingi)
-l- Mzizi-ish- Usababishi/utendeshi-a Dhamira arifu
Mofu tataNi mofu ambazo hubeba maana zaidi ya moja. Mfano neno ‘atanipikia’ lina mofu sita (a-ta-ni-pik-i-a), mofu i- (ya pili kutoka kulia) inawakilisha mofimu/inabeba maana ya utendea ambayo ndiyo chanzo cha utata; kwani yaweza kueleweka kama:
Kupika kwa niaba yangu Kupika kwa ajili yangu
Kigezo cha mofolojia ya mofu tunapata mofu kapa na mofu changamano.
Mofu kapaNi mofu zisizodhihirika kimatamshi wala kimaandishi ila athari zake zipo na zinaeleweka kwa wamilisi wa lugha husika. Mofu hizi huwakilishwa kwa alama Ɵ. Mfano;Umoja wingiu-funguo ƟfunguoƟjani ma-janiƟsimu Ɵsimu
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 8
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Mofu changamanoMofu changamano ni mofu ambazo huundwa kwa kuweka pamoja angalau mofu huru mbili au mofu funge na mofu huru na kuunda neno lenye kuleta maana kamili, kwa mfano:Mofu huru + Mofu huru- {fundi} + {chuma} = fundichuma. - {gari} + {moshi} = garimoshi.
Mofu funge + Mofu huru-{mw} + {ana} + nchi = mwananchi. {ki} + {ona} + mbali = kionambali.
MOFIMUMofimu ni kipashio dhahania cha lugha ambacho husitiriwa na mofu. Hivyo tunapozungumzia mofimu tunaangalia zaidi maana ambayo ni dhahania na siyo umbo. Kwa mantiki hii kigezo kikubwa cha kubainisha/kutambua mofimu ni maana.
Aina za mofimu
Mofimu huruNi mofimu inayojitosheleza kimaana bila ya kuongezwa kiambishi cha aina yoyote. Ina uwezo wa kusimama pekee kama neno. Mfano; Maryam, paka, simu, papai, n.k.
Mofimu tegemeziNi aina ya mofimu ambazo hazijitoshelezi kimaana. Mofimu hizi hukamilika kimaana zinapoongezwa mofimu nyengine. Haziwezi kusimama pekee kama neno. Mfano; ki-tabu, m-tu, mu-ana-funz-i, n.k.
Matatizo ya utengaji/ubainishaji wa mofimu Tatizo la kwanza ni kukosekana kwa umbo dhahiri la mofimu
Mfano: θ+chungwa : ma+chungwa
θ+bega : ma+begaθ+jiwe : ma+we
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 9
Mofolojia ya Kiswahili 2018
θ+shati : ma+shati
Katika mifano hiyo mofimu za umoja ni //θ// na za wingi ni //ma//
Tatizo la pili ni kukosekana maneno asilia yanayozalisha maneno unde.
Mfano:
Fupi – fupika –fupishaRefu - refuka –refusha
*Kau – kauka – kausha
Mifano hiyo ina maneno asilia na maneno unde. Maneno (fupi na refu) ni maneno asilia ya maneno unde fupisha na refusha. Lakini (kau) sio neno asili la neno (kauka na kausha) kwa sababu neno hilo (kau) halikubaliki kwa maneno ya namna hiyo.
Tatizo la tatu ni ugumu wa kutenganisha mofimu katika maneno mwambatano.
Mfano:
Mwanajeshi
Mu-ana-jeshi
Mw-ana-jeshi
Mw-an-a-jeshi
Mw-anajeshi
Maneno mwambatano yanaundwa kwa mzizi zaidi ya mmoja hivyo huwa ni vigumu kubaini mofimu ni zipi na mizizi ni ipi.
KANUNI ZA KUTENGANISHA MOFIMU
Kanuni ya kwanza; zingatia maumbo yenye maana sawa. Maumbo hayo huweza kufanana au kuhitilafiana kiumbo lakini hutokea katika mazingira yaleyale.
Mfano
a) atakupiga
b) atampiga
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 10
Mofolojia ya Kiswahili 2018
ata-ku-pig-a
a-ta-m-pig-a
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 11
Mofolojia ya Kiswahili 2018
c) alikupiga -li-ku-pig-a
d) utanipiga -ta-ni-pig-a
e) utatupiga -ta-tu-pig-a
f) mlijipiga -li-ji-pig-a
Mofimu
1. mofimu nafsi --------- (a)-3-umoja
--------- (u)-2-umoja
---------- (m)-2-wingi
---------- (tu)-1-wingi
2. mofimu njeo ------------- (ta)-ijayo
------------- (li)-iliyopita
-------------- (na)-iliyopo
3. yambwa ---------------- (ku)-wewe
--------- (m)-yeye
---------- (ni)-mimi
----------- (ji)-binafsi
Kanuni ya pili; Hapa kinachozingatiwa ni maumbo yenye maana moja lakini yasiyo na umbo sawa la kimofolojia.
Mfano;
a) mtumwab) mvulanac) mjakazid) mwenzie) mwanadamu
watumwawavulanawajakaziwenziwanadamu
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 12
Mofolojia ya Kiswahili 2018
mofimumofimu za idadi
//umoja//---------m/-k-------- mw/-i
//wingi//--------- wa/-k---------- w/-I
Kanuni ya tatu; Kanuni hii inadai kuwa alomofu moja au zaidi zimo katika mtawanyo mkamilishano ambapo moja ikitokea basi ya pili haitokei. Yambwa na yambiwa haziwezi kutokea katika mazingira yale yale.
Mfano
Baba alinimpigia mimi simu
Sisi tuliwamuona nyinyi
Yeye alimwakuta wao
(m) na (mu)
(wa) na (w)Zimo katika mtawanyo mkamilishano au mgawanyo wa kiutowano
Kanuni ya nne; Umbo moja na zaidi huweza kuwa katika mpishano huru kama maumbo hayo yana maana moja na yametokea katika mazingira yaleyale.Mfanongombe badala ya ng’ombe khabari badala ya habari lafiki badala ya Rafiki ntoto badala ya mtoto
Kanuni ya tano; inadai kuwa maumbo yenye maana tofauti ni mofimu na maumbo tofauti yenye maana sawa ni alomofu.
MUHADHARA WA 3 : ALOMOFUMaeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 13
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Fasili ya alomofu
Alomofu ni maumbo mbalimbali yanayowakilisha dhana moja ya kisarufi. Alomofu ni maumbo mbalimbali ya mofimu moja.
Alomofu hufafanuliwa kama maumbo zaidi ya moja (mbalimbali) ya mofimu moja.
Mazingira ya utokeaji wa alomofu
Alomofu hazitokei kibahati nasibu tu. Mara nyingi utokeaji wa alomofu fulani unategemea kupatikana kwa mazingira mahususi. Mazingira hayo yanaweza kuelezeka kifonolojia, kileksika na kisarufi.
Mazingira ya kifonolojia
Kuna baadhi ya alomofu utokeaji wake hutegemea kuwepo au kutokuwepo kwa sauti/fonimu fulani. Kwa mfano; mofimu iwakilishayo umoja katika ngeli ya KI-VI hujitokeza kwa umbo la ki- ikifuatiwa na konsonanti lakini mofimu hiyo hiyo huwakilishwa na umbo la ch- ikifuatwa na irabu.
Mfano:
Ki +tabu = kitabu, ki+buyu = kibuyu, ki+sima = kisima
Ki+umba = chumba, ki+ama =chama, ki+etu = chetu, ki+ekundu = chekundu
Mazingira ya kileksika (kikamusi/kimaana)
Alomofu pia hujitokeza kutokana na mazingira ya kileksika. Tofauti na mazingira ya kifonolojia ambayo aghalabu hutabirika mazingira ya kileksika hayatabiriki na hutegemea zaidi neno husika.
Mfano:
Mtume ---------mitume
Waziri---------mawaziri
Kiongozi ----viongozi
Malaika --------malaika
Mganga --------waganga
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 14
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Kwa kuzingatia mazingira ya kileksika ya mifano hapo juu tunaweza kusema kuwa mofu ya umoja //m// inaweza kujitokeza kama //m//, /θ/ na /ki/ wakati mofu ya wingi //wa// inajitokeza kama //mi//, //ma//, //vi// na // θ //.
Mazingira ya kisarufi
Wakati mwengine alomofu hutokea kwa sababu za kisarufi. Mfano mzuri unapatikana katika mofimu za njeo. Mabadiliko ya wakati unaohusishwa na tendo husababisha kupatikana kwa maumbo mbalimbali yawakilishayo njeo. Angalia mifano ifuatayo:
A B
Anaandika - haandiki
Aliandika - hakuandika
Ataandika - hataandika
Ameandika - hajaandika
Kutokana na mifano hii maumbo yanayowakilisha njeo katika kifungu A ni //na//, /li//, //ta// na //me// yanayoashiria wakati uliopo, wakati uliopita (muda mrefu) na wakati uliopita (muda mfupi) hali yakinishi na katika kifungu B ni //i//, //ku//, //ta// na //ja// yanayowakilisha nyakati hizohizo katika ukanushi.
Aina za alomofu
Alomofu za njeo : ----- -na-, -li-, -me-, -ta-, -ku-, -ja- (anasoma, alisoma, amesoma, atasoma, hakusoma, hajasoma).
Alomofu za nafsi : ni, tu, u, m, a, wa (ninasoma, tunasoma, unasoma, mnasoma, anasoma, wanasoma).
Alomofu za wingi : mi-, vi, wa-, ma-, n.k. (miti, vijiko, watoto, majembe)
Alomofu za umoja : ki-, m-, u-, li-, n.k. (kibanda, mkeka, ukuta, limeoza)
Alomofu za usababishi/utendeshi : ish, esh, z, fy, vy, sh (katisha, somesha, liza, ogofya, levya, safisha)
Alomofu za ukanushi : si, ha, (hu-) (siandiki, haandiki, h(a)uandiki)
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 15
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Alomofu za urejeshi : ye, cho, po, vyo, ko, n.k. (aliyeondoka, kilichozama, nilipokosa, ulivyokurupuka, walikokimbilia)
Alomofu za masharti : ki, nge, ngeli, ngali, ngeli, kama, endapo (akija, angekuja, angalikuja, kama atakuja, endapo atakuja)
MUHADHARA WA 4 : KIAMBISHI
Fasili ya kiambishi
Kiambishi ni mofu iongezwayo kwenye mzizi wa neno na kuwakilisha maana ya kisarufi.
Aina za viambishi
Aghalabu viambishi huainishwa kwa kutegemea mahali ambapo viambishi hivyo huwekwa katika neno. Hivyo kwa ujumla tunapata aina kuu tatu za viambishi ambazo ni; viambishi awali, viambishi ndani/kati na viambishi tamati.
Viambishi awaliNi viambishi ambavyo huwekwa kabla ya mzizi wa neno. Mfano; neno tunakuja……tu-na-ku ni viambishi awali vilivyowekwa kabla ya mzizi wa neno –j- . mifano mingine ni hatulimi, wanasoma, n.k.
Viambishi ndani/katiHivi ni viambishi ambavyo huwekwa katikati ya mzizi wa neno. Hakuna mfano wa neno la Kiswahili lenye kiambishi ndani kwa sababu lugha ya Kiswahili haina muundo huo. Mifano tunaweza kuipata katika lugha nyingine kama vile lugha ya Kibari kutoka Sudani ya kusini. Katika lugha hii mofimu ya idadi huoneshwa kwa kutumia viambishi ndani. Mfano;Popon ------------------------ shimo (umoja)Popojin ---------------------- mashimo (wingi) –ji ni kiambishi ndani cha wingi.Bun ----------------------------- kitabu (umoja)Bukan ------------------------ vitabu (wingi) –ka- ni kiambishi ndani cha wingi.
Viambishi tamatiNi aina ya viambishi ambavyo huwekwa baada ya mzizi wa neno. Mfano
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 16
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Chumbani ------------------ chumba (mzizi) + -ni (kiambishi tamati)Somo ------------------------som (mzizi) + -o (kiambishi tamati)Pikisha --------------------- pik (mzizi) + ish + -a (viambishi tamati)Kutokana na maelezo na mifano ya hapo juu tunaona kuwa lugha ya Kiswahili ina aina mbili tu za viambishi; viambishi awali na viambishi tamati. Jambo la kuzingatia ni kwamba viambishi vya aina zote huweza kujitokeza katika neno moja la Kiswahili. Kwa mfano hatujawapigisheni- maumbo yaliyokolezwa wino kabla ya mzizi –pig- ni viambishi awali na yale yaliyo baada ya mzizi ni viambishi tamati. Vilevile tunaona kuwa viambishi ni maumbo tegemezi yanayofanya kazi ya kuleta maana yanapounganishwa na mzizi tu. Na pia tumegusia kuwa viambishi huwakilisha maana za kisarufi tu.
Mpangilio wa viambishiKatika lugha ya Kiswahili viambishi ni vingi. Na kama ilivyogusiwa hapo juu kuwa vinaweza kujitokeza kwa pamoja katika neno moja ili kutoa maana fulani ya kisarufi. Hivyo basi ni lazima kuwe na utaratibu maalumu wa kuvipanga viambishi katika mzizi wa neno ili neno litoe maana na taarifa iliyokusudiwa. Katika sehemu hii tutaonesha mpangilio wa viambishi katika maneno ya lugha ya Kiswahili. Tutaangalia zaidi kitenzi na nomino.
Mpangilio wa viambishi awali katika kitenzi Kwa kawaida kitenzi huanza na kiambishi nafsi, mfano a-cheka Kiambishi nafsi hufuatiwa na kiambishi cha wakati mfano alicheka Kiambishi cha wakati hufuatiwa na kiambishi rejeshi mfano
aliyecheka Kiambishi rejeshi hufuatiwa na kiambishi yambwa/yambiwa mfano
aliyemcheka.
Mpangilio wa viambishi tamati katika kitenziKama ilivyoelezwa awali kuwa viambishi tamati ni vile vinavyokaa baada ya mzizi wa neno. Aghalabu viambishi tamati huwa ni vya mnyambuliko na hutokea kimoja tu katika neno. Mfano; Wanapigwa – utendwa.Wanapigana – kutendana
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 17
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Wanapigika – kutendekaWanapigisha – kutendeshaWanapigiana – kutendeana, n.k.Hata hivyo, iwapo kitenzi kitakuwa na viambishi tamati zaidi basi mzizi huo huwa ni mzizi wa mnyambuliko na aghalabu unakuwa umeundwa kwa kiini cha neno na mofimu ya kutendana (mf. pigan). Ikiwa mzizi una kiambishi cha kutendana //an//, baadaye huja kiambishi cha kutendesha //sh,ish,esh// n.k. na kisha hufuata kiambishi cha utendeka //ik, ek// au kiambishi cha utendwa //w// (hutegemea na taarifa inayotolewa) na kumalizia na kiambishi –a kinachokamilisha maana. Chunguza utaratibu huu katika maneno yafuatayo:
TuliowapiganishaTumepiganishikaTumepiganishwa
Mifano iliyotolewa hapo juu ni ya vitenzi yakinifu tu. Hata hivyo, ni vyema ieleweke kuwa utaratibu huu hufanya kazi hata katika hali ya ukanushi isipokuwa kiambishi cha ukanushi si, ha (hu) hutokea mwanzoni kabisa kabla ya kile cha nafsi. Mfano.Utapika ---------------- h(a)utapika (wakati ujao)Tumepigana ---------- hatujapigana (wakati uliopita – muda mfupi)Walitufurahisha --------- hawakutufurahisha (wakati uliopita)Hata hivy, hali huwa tofauti kidogo kwa upande wa wakati uliopo kwani kiambishi cha wakati na hudondoshwa na umbo la kitenzi humalisika kwa irabu i badala ya a kama ilivyozoeleka. Kuna wataalamu wanaodai kuwa hii irabu ya mwisho i ndicho kiambishi cha wakati uliopo katika ukanushi.Mfano:
Tunasoma – hatusomi (*hatunasoma)Ninapika – sipiki (*sinapika)
Mpangilio wa viambishi katika nomino
Aghalabu nomino huweza kuandamana na viambishi vya aina tatu tu. Viambishi hivyo ni bya idadi (umoja na wingi), ukubwa na udogo. Mfano;
Mtoto (m ya umoja) kitoto (ki ya udogo) jitoto (ji ya ukubwa) kijitoto (ki ya umoja na udogo na ji ya udogo).
Watoto – vitoto- mitoto – mijitoto – vijitotoMaeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 18
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Wakati mwingine hutokea nomino ikabeba viambishi vya aina mbili kwa pamoja. Katika hali hiyo kiambishi cha idadi hutangulia na ndipo kikaja kiambishi cha ukubwa/udogo kama ilivyo katika mifano hapo juu.
Viambishi nominishi: ni vile ambavyo vinapoambikwa katika neno lisilokuwa nomino hulifanya neno hilo kuwa nomino.
Mfano
Ji > mchoraji, mtangazaji, uimbaji, muuaji, upimaji, n.k. Zi> Upekuzi, uchaguzi, ufafanuzi i > Ushindi, uchunguzi, ubishi, msomi O > Somo, upendo, mkopo fu > udanganyifu, usahaulifu, uchangamfu, usumbufu
kama ilivyoelezwa katika mifano hapo juu, utokeaji wa viambishi hivi aghalabu huambatana na utokeaji wa viambishi awali vya nomino vinavyodokeza idadi, udogo au ukubwa wa nomino (m/wa, ki/vi, u, ma, n.k.)
viambishi elezi: ni vile ambavyo vinapoambikwa katika neno lisilokuwa kielezi hulifanya neno hilo kuwa kielezi.
Mfano
ni > sokoni, barabarani, darasani, n.k ki > kijeuri, kiume, kikatili vi > vizuri, vibaya
MUHADHARA WA 5 : MZIZI
Fasili ya mzizi
Mzizi ni neno au sehemu ya neno ambayo hubeba taarifa ya msingi na haibadilikibadiliki.
Sifa bainifu za mzizi
Mzizi hubeba taarifa ya kileksika Mzizi haubadilikibadiliki Mzizi ni mofu muhimu kuliko mofu zote katika neno Mzizi hauwezi kuachwa wakati wote neno linapotumika
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 19
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Aina za mzizi
Mzizi huru: ni mzizi usiopokea kiambishi cha aina yoyote. Mfano; mama, sawa, chungwa, n.k.
Mzizi funge: ni mzizi unaoandamana na viambishi ili kukamilisha maana mfano; kisu, mti, n.k. –su na –ti ni mfano wa mizizi ya maneno ambayo maana zake hupatikana baada ya kufungamanishwa na viambishi.
Mzizi asilia: ni mzizi unaotokana na kiini cha neno. Mfano wa mzizi asilia ni andik- katika neno andika, kat- katika neno kata, n.k.
Mzizi wa mnyambuliko: ni mzizi unaotokana na mzizi asilia pamoja na viambishi. Kwa mfano andikish- ni mzizi wa mnyambuliko unaoweza kuzalisha maneno kama andikisha, andikishwa, andikishana, andikishia, n.k. na pigan- ni mzizi wa mnyambuliko unaoweza kuzalisha maneno kama vile pigana, oigania, piganiwa, piganisha, n.k
Miundo ya mzizi
Neno zima: mf. sungura, mbuzi, kopo, bibi Konsonanti pekee: mf. –p- katika nipe, -f- katika kifo Irabu pekee: mf. –u- katika usiniue, o- katika wameoana Silabi moja: mf. –ki katika kiti, to- katika toa, li-katika lia Silabi moja au zaidi pamoja na sehemu tu ya silabi nyingine : mf. som-
katika soma, kat-katika kata, andik-katika andika, tafut-katika tafuta. Silabi zaidi ya moja : mf. kimbi- katika kimbia, fafanu-katika ufafanuzi.
MUHADHARA WA 6 : NENO
Fasili ya neno
Neno ni kipashio cha kiisimu kinachoundwa na mofimu moja au zaidi na kutoa maana fulani katika lugha husika. Maana hiyo yaweza kuwa ya kisarufi au ya kileksika.
Aina za maneno
Maneno hugawanywa katika aina zake kwa vigezo viwili ambavyo ni: kigezo cha muundo na kigezo cha kazi.
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 20
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Aina za maneno kimuundo
Neno sahili : ni neno linaloundwa kwa mzizi huru mmoja (mf. mama, wewe, maji, hewa, n.k)
Neno ambatani : ni neno linaloundwa kwa mizizi miwili. Yawezekana ikawa ni mzizi funge na mzizi huru au mizizi huru miwili (mf. mwanaanga, mwanahewa, bwanashamba)
Neno changamano : ni neno linaloundwa kwa mzizi funge pamoja na viambishi mbalimbali (mf. mapigo, mwendeshaji, n.k.)
Aina za maneno kikazi/kiuamilifu
Kwa kutumia kigezo cha kazi/uamilifu tunapata aina zifuatazo za maneno:-
Nomino (N) Kiwakilishi (w) Kivumishi (V) Kitenzi (T) Kielezi (E) Kihusishi (H) Kiunganishi (U) Kihisishi/Kiingizi (I)
TAARIFA ZINAZOPATIKANA KATIKA NENO
Taarifa ya kifonolojiaNi kujua fonimu zilizotumika kuunda neno hilo. Mf. neno /paka/ limeundwa na fonimu /p/, /a/ na /k/
Taarifa ya kimofolojiaNi kujua mofimu zinazounda neno hilo. Mf. neno /paka/ limeundwa kwa mofimu moja huru na neno /mtu/ limeundwa na mofimu tegemezi mbili m-na -tu
Taarifa ya kisintaksiaNi kujua aina ya neno kulingana na uamilifu wake katika tungo. Mf;(a) Kitu chema hakidumu (b) chema hakidumu
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 21
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Neno chema katika (a) ni kivumishi na neno chema katika (b) ni kiwakilishi. Tunajua aina ya neno kwa kuangalia kazi na nafasi yake katika tungo.
Taarifa ya kisemantikiNi kujua maana ya neno. Ili mkusanyiko wa silabi ukubalike kuwa ni neno lazima uwe na maana katika lugha husika; hivyo mkusanyiko usioleta maana si neno. Mf; paletihoju ni mkusanyiko wa silabi usioleta maana katika lugha ya Kiswahili na hivyo hili si neno la Kiswahili.
Neno na leksimuImeelezwa katika fasili ya neno kwamba neno lazima liwe na maana ya kisarufi au ya kileksika/kikamusi. Neno lenye maana kileksika huweza kusimama peke yake kama kidahizo katika kamusi. Hivyo basi tunaweza kusema leksimu ni kipashio cha kidhahania ambacho ni cha msingi katika msamiati wa lugha na hubeba dhana ya kwanza ya neno. Ni maneno yenye maana za kileksika ambayo huwa vidahizo katika kamusi. Mfano;Doa ji/ma – 1. Alama au tone ambalo lina rangi tofauti na mwili wa kitu 2. Aibu, dosari, ila, kasoro.Maneno yenye maana za kisarufi ambayo hayawezi kutumika kama kidahizo katika kamusi yanabaki kuwa maneno tu lakini si leksimu.NENO NA MOFIMUNeno ni mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa au kuandikwa na kuleta maana fulani katika lugha. Mkusanyiko huo wa silabi unaweza kuwa ishara ya maana ya kileksa au maana kisarufi.Mofimu kwa upande mwingine ni kipashio cha kiisimu chenye maana ya kileksika au kisarufi. Maneno huweza kuwa na mofimu moja au zaidi lakini si lazima wakati wote iwe neno.LEKSIMU NA MOFIMULeksimu ni kipashio kidogo cha msamiati kinachoweza kusimama peke yake katika kamusi kama kidahizo. Mofimu inaweza kusimama peke yake hasa ikiwa mofimu huru.
MUHADHARA WA 7: NENO (Aina za Maneno – Nomino)Nomino: ni maneno ambayo hutaja majina ya watu, vitu, mahali, vyeo, dhana na hata tendo.
Aina za nominoNomino za pekee
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 22
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Nomino za kawaidaNomino za dhahaniaNomino za jumla
Dhima ya nominoKiima cha sentensi: Juma analimaYambwa : Juma amenunua kitabuYambiwa : Juma amemnunulia Ali kitabuKijalizo : Juma ndiye kiongozi wetu
MUHADHARA WA 8 : NGELI ZA NOMINO (Mkabala wa Kimofolojia)
Fasili ya ngeli
Ni uwekaji wa nomino katika makundi mbalimbali kulingana na vigezo maalumu. Vigezo hivyo vyaweza kuwa vya kimofolojia, kisintaksia n.k. kutokana na vigezo hivyo ndipo tunapopata migawanyo tofauti ya ngeli; kama mgawanyo wa ngeli kimapokeo na mgawanyo wa ngeli kimamboleo/kisasa.
Mgawanyo wa ngeli za nomino kimapokeo
Huu ni uainishaji wa ngeli kwa kutumia kigezo cha mofolojia ya nomino. Tunapotumia kigezo hiki kugawa nomino za Kiswahili katika ngeli tunazingatia zaidi viambishi awali vya idadi – umoja na wingi ambavyo ni vya kawaida katika nomino hizo – si viambishi vyenye kuonesha dhana ya ukubwa na udogo. Kwa kigezo hiki tunapata makundi yafuatayo ya ngeli:-
a) Ngeli ya M(U) – WA (Mtu-watu, mtoto-watoto)b) Ngeli ya M-Mi (mti-miti, mkono-mikono)c) Ngeli ya JI-MA (jicho-macho, jiwe-mawe)d) Ngeli ya KI-VI (kinu-vinu, kiwete-viwete)e) Ngeli ya U-N (ulimi-ndimi, ufa-nyufa)f) Ngeli ya U-MA (uamuzi-maamuzi, upishi-mapishi)g) Ngeli ya U-Ɵ (upawa- Ɵpawa, ukucha- Ɵkucha)h) Ngeli ya Ɵ-MA (Ɵchungwa-machungwa, Ɵjani-majani)i) Ngeli ya Ɵ- Ɵ (Ɵnyumba- Ɵnyumba, Ɵnguo- Ɵnguo)
UBORA WA KIGEZO CHA KIMOFOLOJIA
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 23
Mofolojia ya Kiswahili 2018
a) Uwezekano wa kuzigawa nomino nyingi za Kiswahili ni mkubwa kwa kuwa nyingi zimegawanyika katika maumbo hayo ya umoja na wingi.
b) Ni kigezo muhimu kwani kinajikita zaidi katika nomino na kivumishi chake peke yake hakigusi aina nyingine ya neno tofauti na kigezo cha kisintaksia ambacho hugusa hadi kitenzi.
c) Huwasaidia wanasarufi linganishi kuonesha uhusiano wa lugha za kikoa kimoja.
d) Kilisaidia kuondokana na uainishaji ngeli kwa kutegemea tofauti za kibayolojia.
e) Kinasaidia kutambua mofolojia ya nomino kama ni huru au changamano.
UDHAIFU WA KIGEZO CHA KIMOFOLOJIA
a) Kuna viambishi katika ngeli tofauti vinavyofanana. Mfano Kiambishi M- kinajitokeza katika ngeli ya 1 na 3 na MA- inajitokeza katika ngeli ya 8 na 13.
b) Kuna nomino nyingine ambazo hazijidhihirishi katika umoja na wingi. Mfano ngeli ya 8 na 9.
c) Nomino zenye hadhi tofauti kuwekwa kwenye ngeli moja mf. (kiwete,kinu), (sikio,tawi).
d) Kuna matumizi ya vigezo viwili kwa pamoja, kigezo cha maumbo ya idadi na kigezo cha sifa za nomino.
e) Idadi ya ngeli ni kubwa na hivyo humfanya msomaji kupata tabu ya kuzikariri.
f) Wanamapokeo wamegawanyika pasipo sababu za msingi, kuna wenye ngeli 18, 16 na 9.
MUHADHARA WA 9 : MGAWANYO WA NGELI ZA NOMINO KIMAMBOLEO
Huu ni uainishaji wa ngeli kwa kutumia kigezo cha sintaksia ya nomino. Uainishaji huu huzingatia uhusiano wa nomino na maneno mengine katika tungo kwa kuangalia viambishi vya upatanishi wa kisarufi vinavyojitokeza mwanzoni mwa maneno yanayoandamana na nomino katika tungo. Viambishi hivyo huathiriwa na umbo la nomino inayozungumzwa katika tungo husika. Kwa kutumia kigezo hiki tunapata makundi yafuatayo ya ngeli:-
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 24
Mofolojia ya Kiswahili 2018
a) Ngeli ya YU-A/WA: mtoto yuasoma/mtoto anasoma-watoto wanasoma
b) Ngeli ya U-I: mkoba umechanika-mikoba imechanika
c) Ngali ya LI-YA: debe linauzwa-madebe yanauzwa
d) Ngeli ya KI-VI: kiatu kimetupwa-viatu vimetupwa
e) Ngeli ya I-ZI: ndizi imeiva-ndizi zimeiva
f) Ngeli ya U: ushawishi umemponza-ufisadi umekithiri
g) Ngeli ya U-YA: ugonjwa umetukatisha tamaa-magonjwa yametukatisha tamaa
h) Ngeli ya U-ZI: ungo umeharibika-nyungo zimeharibika
i) Ngeli ya YA: maji yanamwagika, mafuta yamekwisha
j) Ngeli ya I: chai imenywewa
k) Ngeli ya KU: kulima kunakondesha, kula kwake kutamdhuru
l) Ngeli ya PA-MU-KU: kiwanjani petu panafaa, nyumba munagiza, kule kunatisha
UBORA WA MTAZAMO WA KISASA
Kigezo cha kisintaksia kinachotumiwa katika mtazamo wa kisasa kugawa ngeli kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi kina ubora wake kama ifuatavyo:
Kimepunguza makundi mengi ya ngeli za nomino
Ni rahisi kuzikariri kwani ni chache.
Kila nomino huweza kuingia katika ngeli yake kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi.
Nomino hupangwa katika ngeli zake kulingana na sifa na hadhi yake.
Husaidia kubaini umoja na wingi wa nomino zisizo na maumbo dhahiri ya idadi.
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 25
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Kigezo hiki kimepunguza kujirudiarudia kwa ngeli.
Husaidia kubainisha uhusiano wa nomino na maneno mengine katika tungo.
Husaidia kuonesha urejeshi wa vitenzi na nomino zake.
UDHAIFU WA MTAZAMO WA KISASA
Bado kuna ngeli za nomino zinazojirudia mf. Ngeli ya 2,6 na 7 umoja zinatumia u.
Ngeli ya kwanza umoja ina viambishi viwili (Yu/A)
Bado kuna nomino zenye kuleta mgogoro katika ngeli mf. Makala, Jambazi, marashi.
Pamoja na umoja na wingi kutawala, kigezo cha sifa ya nomino hujitokeza ili kuepuka kuchanganya majina yenye sifa na hadhi tofauti mf. Kinyonga hukubali zaidi ngeli ya (KI-VI) lakini huwekwa katika ngeli ya kwanza kwa sifa ya kiumbe hai.
Kigezo hiki hakijaweza kuonesha mofolojia ya nomino.
MUHADHARA WA 10: VIWAKILISHI
Fasili ya viwakilishi
Viwakilishi ni maneno yanayosimama badala ya nomino au kikundi nomino.
Muundo wa viwakilishi
Kwa ujumla viwakilishi hujitokeza katika miundo miwili. Kiwakilishi huweza kuwa huru au kiambata. Kiwakilishi huru ni kile kinachosimama pekee kikiwa neno kamili kama vile mimi, yeye, nani, nini, n.k. kwa upande wa kiwakilishi kiambata ni kiwakilishi ambacho huambatanishwa mwanzoni mwa kitenzi.
Aina za viwakilishi
1. Viwaklishi vya sifa : kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza
2. Viwakilishi vya idadi: wawil wameokolewa, mmoja hajulikani alipo.
3. Viwakilishi vioneshi: yule habebeki, huyu nampenda
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 26
Mofolojia ya Kiswahili 2018
4. Viwakilishi viulizi: ipi unaitaka? Lipi limekuudhi?
5. Viwakilishi vimilikishi: wangu ni mweusi, wao amezidi mno
6. Viwakilishi nafsi: mimi sijali, nyinyi mnacheza
Nafasi ya kiwakilishi: kiwakilishi hutokea badala ya nomino/huchukua nafasi ya nomino pale ambapo nomino haipo.
MUHADHARA WA 11 : VIVUMISHI
Fasili ya kivumishi
Vivumishi ni maneno ambayo huandamana na nomino ili kuongeza sifa au taarifa muhimu kwa nomino (huifanya nomino ivume).
Muundo wa vivumishi
Kwa kutumia kigezo cha kimuundo kuna aina mbili za vivumishi ambazo ni:
Vivumishi vinavyoambishwa mf; dogo, refu, chungu, zuri, n.k
Vivumishi vinaweza kuambishwa kulingana na upatanishi wa kisarufi wa nomino inayovumishwa. Hivyo tunaweza kupata tungo kama ki+dogo, wa+refu, m+chungu, vi+zuri, n.k
Vivumishi visivyoambishwa-aghalabu vivumishi vya aina hii hutokana na maneno yenye asili ya lugha ya Kiarabu mf; Jamali,dhaifu,n.k
Aina za vivumishi
Vivumishi vya sifa: hivi ni aina ya vivumishi vinavyotoa sifa ya nomino. Mfano kitambaa kizuri, mti mrefu, mwanafunzi mvivu, mtandio mweupe. Jambo la kuzingatia hapa si lazima ile sifa iwe njema hata sifa mbaya pia ni kivumishi.
Vivumishi vya idadi: hivi ni vivumishi vinavyoonesha idadi ya vitu mbalimbali. Mfano watoto wawili, nyumba moja.
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 27
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Vivumishi vya idadi vinaweza kujitokeza katika aina tatu ndogondogo.
- Vivumihi vya aina hii hutoa taarifa kuhusu idadi ya nomino ambazo kiwango chake kimetajwa.
- Vivumishi vya idadi vinavyoweza kuvumisha nomino kwa kutaja idadi ya nomino hizo kiujumla jumla bila kudhihirisha idadi halisi.
- Vivumishi vya idadi ambavyo huonesha nafasi iliyochukuliwa na nomino fulani katika orodha.
Vivumishi vya kuonesha:vivumishi vya aina hii huonesha mahali au upande kitu kilipo. Vivumishi vya aina hii hujengwa na mzizi {h} kwa vitu vilivyopo karibu na mzizi {le} kwa vitu vilivyo mbali. mfano kijana huyu, kuku wale
Vivumishi vya pekee: vivumishi hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila kimojwapo huwa na maana maalumu. Pia kila kimojawapo huchukua upatanisho wake wa kisarufi kulingana na ngeli ya nomino ambayo kinaivumisha. Mizizi ya vivumishi hivi ni ote, o-ote, enye, enyewe, ingine, ingineo. Mfano chakula chochote, wakati wowote
Vivumishi viulizi: hivi ni vivumishi ambavyo hufafanua nomino kwa kuuliza habari zake. Mfano nguo ipi? Msichana yupi?watu wangapi?
Vivumishi vya jina kwa jina: ni vivumishi ambavyo jina huvumisha jina lililotangulia katika mfuatano. mfano mwalimu Majaliwa, Mzee kipofu
Vivumishi vimilikishi: ni vivumishi vinavyoonesha kuwa kitu fulani kina milikiwa na mtu au kitu kingine mfano: mali yangu, paka wako, nchi yetu
MODULI 4: VITENZI, VIELIZI NA VIUNGANISHI
VITENZI (T)
Vitenzi ni maneno yanayosimamia kitendo. Kila kitenzi huwa na shina la kitenzi (sehemu ndogo zaidi ya kitenzi ambayo ndiyo huwakilisha tendo hilo). Shina la kitenzi huambatanishwa na viambishi ili kutoa maana iliyokusudiwa
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 28
Mofolojia ya Kiswahili 2018
kama vile mtendaji, mtendewa, wakati kitendo kinafanyika na pia kauli ya kitenzi hicho.
Aina za Vitenzi
Vitenzi Halisi
Vitenzi Visaidizi + Vitenzi Vikuu
Vitenzi Vishirikishi
Vitenzi Sambamba
Vitenzi Halisi
Hivi ni vitenzi vinavyorejelea kitendo moja kwa moja. Vitenzi halisi vinapoambatanishwa na vitenzi vidogo katika sentensi, huitwa vitenzi vikuu.
k.m: soma, kula, sikiza
Waziri Mwasimba aliwasili jana kutoka ng'ambo.
Kawia atapikia wageni.
Funga mlango wa dirisha.
Vitenzi Visaidizi
Vitenzi visaidizi hutangulia vitenzi halisi (vitenzi vikuu) katika sentensi ili kuleta maana inayokusudiwa kulingana na wakati au hali.
k.m: -kuwa, -ngali,
Jua lilikuwa limewaka sana.
Bi Safina angali analala
Vitenzi Vishirikishi
Vitenzi vishirikishi hutumika kuelezea hali iliyopo au mazingira. Kuna aina mbili za vitenzi vishirikishi:
a) Vitenzi Vishirikishi Vipungufu - havichukua viambishi vyovyote.
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 29
Mofolojia ya Kiswahili 2018
k.m: ni, si, yu
Kaka yako ni mjanja sana.
Huyo si mtoto wangu!
Paka wake yu hapa.
b) Vitenzi Vishirikishi Vikamilifu - huchukua viambishi vya nafsi au ngeli. Vitenzi hivi vinaweza kusimama peke yake au vinaweza kufuatiliwa na vitenzi vikuu.
k.m: ndiye, ndio, ndipo
Sanita ndiye mkurugenzi wa kampuni
Huku ndiko kulikoibiwa
Muundo wa Vitenzi
Kwa kuzingatia muundo wa vitenzi, tunaweza kuweka vitenzi katika aina zifuatazo:
1. Vitenzi vya Silabi Moja
2. Vitenzi vya Kigeni
3. Vitenzi vya Kibantu
Vitenzi vya Silabi Moja
Hivi ni vitenzi vyenye silabi moja pekee. Ili kuleta maana kamili, vitenzi hivi huambatanishwa na kiungo KU- katika kauli ya kutenda. Kama vitenzi vingine, vitenzi vya silabi moja vinaweza kunyambuliwa.
k.m: soma, kula, sikiza
1. -cha - kucha - jua linapochomoza asubuhi k.m kumekucha
2. -fa - kufa - kuacha kupumua, kupoteza uhai k.m amekufa
3. -ja- kuja - fika mahali hapa k.m nimekuja
4. -la- kula - kutia chakula mdomoni k.m anakulaMaeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 30
Mofolojia ya Kiswahili 2018
5. -nya- kunya - kutoa mabaki ya chakula toka tumboni k.m mtoto amekunya
6. -nywa- kunywa - kutia kinywaji kama vile maji au maziwa mdomoni k.m ninakunywa uji
7. -pa- kupa - kumkabithi/kumpatia mtu kitu k.m amenipa pesa
8. -pwa- kupwa - kujaa hadi pomoni - k.m kisima kimekupwa maji
9. -twa- kutwa - jua linapozama magharibi na usiku kuingia k.m kumekutwa
10.-wa- kuwa - kutokea katika hali au mahali fulani k.m alikuwa
Vitenzi vya Kigeni
Hivi ni vitenzi vyenye asili kutoka kwa lugha nyingine badala ya Kibantu. Baadhi ya lugha hizo ni Kiarabu, Kizungu, Kireno, Kihispania n.k. Vitenzi hivi havifuatilii muundo wa kawaida wa vitenzi vya Kiswahili ambavyo huishia kwa sauti -a. Badala yake, vitenzi hivi huishia kwa sauti nyingine kama vile -e, i, -o, na u
k.m: haribu, tubu, shukuru, salimu, thamini, amini, samehe, baleghe
Vitenzi vya Kibantu
Hivi ni vitenzi vyenye asili ya Kibantu na ambavyo huishia kwa sauti -a. Kitengo hiki hujumuisha asilimia kubwa zaidi ya vitenzi vya Kiswahili
k.m: simama, shika, tembea, beba, soma, lia
VIELEZI (E)
Vielezi ni maneno yanayotoa habari zaidi kuhusu kitendo kilivyofanyika. Pia vielezi hutoa habari zaidi kuhusu hali, vivumishi au vielezi vingine.
Aina za Vielezi
Vielezi vya Mahali
Vielezi vya mahali hutoa habari kuhusu mahali ambapo kitendo kilifanyika. Aghalabu vielezi hivi huundwa kwa kutumia jina la mahali au kwa kuongeza kiungo -NI mwishoni mwa neno linaloashiria mahali.
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 31
Mofolojia ya Kiswahili 2018
k.m: nyumbani, kazini, shuleni
Mtoto huyo hajatulia nyumbani tangu alipotoka Mombasa.
Msipitie sokoni mkienda kanisani.
Vielezi vya Wakati
Huelezea zaidi kuhusu wakati kitendo kipofanyika
k.m: jioni, jana, asubuhi, saa saba, mwaka juzi
Mzee Kasorogani amesema kwamba ataoga mwaka ujao
Musa alilazimishwa kuchimba mtaro saa sita usiku
Kisaka na Musa watakutana kesho
Vielezi vya Idadi
Vielezi vya idadi hutulezea kitendo kilifanyika mara ngapi
a) Idadi Kamili
Vielezi vya Idadi Kamili hutaja idadi kamili ya mara ngapi kitendo kilifanyika.
k.m: mara mbili, siku mbili kwa juma, mara kumi
Gibi alimzaba kofi mara tatu na kisha akakimbia.
Daktari alimwagiza mama huyo achukue dawa mara tatu kwa siku na arudi hospitalini siku mbili kwa mwezi
b) Idadi Isiyodhihirika
Vielezi vya Idadi Isiyodhirika huelezea kiasi ambacho kitendo kilifanyika bila kutaja kiasi kamili
k.m: chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani
Mwizi wa kuku alipigwa mara kadhaa kabla ya kuokolewa na polisi.
Yeye hunipigia simu mara kwa mara
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 32
Mofolojia ya Kiswahili 2018
VIelezi Vya Namna
Huelezea jinsi au namna kitendo kinavyofanyika. Kitendo kinaweza kufanyika kwa namna mbalimbali. Hivyo basi kuna aina mbalimbali za vielezi vya namna:
a) Vielezi vya Namna Halisi
Hutufahamisha jinsi kitendo kinavyofanyika kwa kutumia maneno halisi (bila kuambatanishwa na maneno mengine au viambishi vingine).
k.m: vizuri, ovyo, haraka
Kioo cha bibi harusi kilianguka na kuharibika vibaya
Mama alipika chakula upesi
Amepigwa kalamu kwa kufanya kazi kiholela
b) Vielezi vya Namna Hali
Hutufahamisha hali ambayo kitendo kilifanyika. Vielezi hivi hujihusisha na tabia ya kitu/mtendaji wa kitendo
k.m: kwa furaha, kwa makini,
Bibi harusi aliingia kanisani kwa madaha
Mtoto alilia kwa maumivu mengi
c) Vielezi vya Namna Kitumizi/Ala
Hutoa habari kuhusu kifaa, ala au mbinu iliyotumiwa kufanya kitendo fulani
k.m: kwa kisu, kwa jembe, kwa meno, kwa moto, kwa maji
Mkulima aliangusha mti mkubwa kwa shoka
Mzee huyo alimpiga mke wake kwa bakora kabla ya kuchoma nguo zake kwa makaa
d) Vielezi Vikariri
Husisitiza kitendo kinavyofanyika kwa kutaja kielezi kinachorejelewa mara mbili mfululizo.
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 33
Mofolojia ya Kiswahili 2018
k.m: haraka haraka, ovyo ovyo, juu juu
Polisi walipoingia, wezi walitawanyika haraka haraka.
Wanafunzi wengi hufanya kazi yao ovyo ovyo
e) Vielezi vya Ki-Mfanano
Vielezi mfanano hutumia KI-mfanano kuelezea kitendo kinavyofanyika kwa kulinganisha.
k.m: kitoto, kiungwana,
Babake huongea kiungwana.
Harida hutembea kijeshi
f) Vielezi Viigizi
Vielezi hivi huigiza sauti au mlio wa kitu, kitendo kitendo kilipofanyika kwa kutumia tanakali za sauti
k.m: tuli, chubwi, tifu, chururu
Mwanafunzi alitulia tuli mwalimu alipomzaba kofi pa!
Kaswimu aliangusha simu changaraweni tifu na kujitumbukiza majini chubwi
g) Vielezi vya Vielezi
Vielezi hivi hutumika kuelezea kielezi kingine. Hivyo basi, hutanguliwa na kielezi badala ya kitendo
k.m: sana, kabisa, hasa, mno
Mamake Kajino alitembea polepole sana.
Chungu kilivunjika vibaya kabisa
h) Vielezi vya Vivumishi
Hutoa habari zaidi kuhusu kivumishi
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 34
Mofolojia ya Kiswahili 2018
k.m: sana, kabisa, hasa, mno
Yeye ni mrefu sana
Mtoto wake ana tabia nzuri mno
VIUNGANISHI (U)
Viunganishi ni maneno yanayoutumika kuunganisha, kulinganisha au kuonesha uhusiano wa dhana mbili au zaidi.
Aina za Viunganishi
Zifuatazo ni aina mbalimbali za viunganishi kulingana na matumizi yake
Kuonesha Umilikaji
A-Unganifu Kiatu cha Mzee Sakarani kimepasuka.
KWA (umilikaji wa mahali)
Mbinguni kwa kuna makao mengi.
Kujumuisha
na Baba, mama na watoto huunda familia kamili.
pamoja na Mwizi aliiba runinga pamoja na redio
fauka ya, licha ya
Fauka ya mapigo yote, Kafa alikatakatwa kwa kisu.
zaidi ya, juu ya
Unataka nini tena zaidi ya mema yote niliyokutendea?
pia, vilevile Alimpiga mkewe na bintiye vilevile
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 35
Mofolojia ya Kiswahili 2018
mbali na Mbali na hayo nitakujengea nyumba ya kifahari.
aidha Keti akitoka shuleni atapika. Aidha atampelekea nyanya sukuma wiki.
wala (kukanusha)
Kutofautisha
lakini, ila Ongea nayeilausimwambie mipango yetu.
bila Tasha aliondoka bila kusema lolote.
bali Sitawaacha kama mayatima bali nitawatumia msaidizi.
kinyume na, tofauti na
Jana kulinyesha kinyume na utabiri wa hali ya hewa.
ingawa, ingawaje
Nitamtembelea ingawa sijui nitamwambia nini.
japo, ijapokuwa Nakuomba upokee nilichokileta japo ni kidogo sana.
ilhali Fungo zimepotea ilhali zilikuwa zimewekwa vizuri.
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 36
Mofolojia ya Kiswahili 2018
minghairi ya Waliendelea kutenda dhambi minghairi ya kuhubiriwa kanisani.
dhidi ya Vita dhidi ya gonjwa hilo vingali vinaendelea.
Kuonesha Sababu
ili Hanna aliumizwa ili asikumbuke aliyoyaona.
kwa, kwa vile
Emili alinyamaza kwa vile kugombana na rafikize.
kwa maana, kwa kuwa
Aria alipigwa na butwaa kwa maana mpenzi wake aligeuka kuwa mwalimu wake.
kwani Melisa alijificha kwani hakutaka kuonekana na Spensa.
kwa minanjili ya
Chali alitembea mwendo huo wote kwa minanjili ya kuongea na Katosha.
maadam Wanawake katika familia hiyo hawali maini maadam mama mkongwe alilaani maini katika familia hiyo.
madhali Madhali sote tuko hapa, tunaweza kuanzisha mkutano mapema
Kuonesha Matokeo
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 37
Mofolojia ya Kiswahili 2018
basi, hivyo basi
Umekula ng'ombe mzima, hivyo basi huna budi kumalizia mkia.
kwa hivyo Alipatikana na makosa ya kumnajisi bintiye, kwa hivyo akahukumiwa miaka kumi gerezani.
ndiposa Mama Kelele alipenda kuongea sana, ndiposa wakamkata midomo.
Kulinganisha
kama, sawa na
Kunywa pombe ni kama kujichimbia kaburi mwenyewe.
kulingana na Mwalimu Makunza hafanyi kazi kulingana na maadili ya shuleni.
kuliko, zaidi ya
Talia ni mfupi kuliko Nuru
vile Mganga Daimoni hutibu vile alivyofunzwa na Mganga Kuzimu.
Kuonesha Kitu kimoja kama sehemu ya kingine
kati ya Vitatu kati ya vitabu hivi vimepigwa marufuku.
miongoni mwa
Miongoni mwa walioachiliwa, ni Ngiri na Mende.
baadhi ya Baadhi ya wasichana kutoka Vikwazoni
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 38
Mofolojia ya Kiswahili 2018
hawaheshimu miili yao.
mojawapo Mojawapo ya maembe uliyochuma yameoza.
Kuonesha Kitu kufanyika baada ya kingine
kisha Soma mfano huu kisha usome sentensi ifuatayo.
halafu Alichukua kisu halafu akatokomea gizani.
Kuonesha Kitu kufanyika badala ya kingine
badala ya Mapepo yalimchukua Shakawa badala ya bintiye
kwa niaba ya Mama Roga alitoa hotuba kwa niaba ya mumewe.
Kuonesha Uwezekano
labda, pengine Sina pesa leo, labda uje kesho.
ama, au Ama Anita au Katosha anaweza kuja.
huenda Huenda kesho ikifika, Mungu atende miujiza.
Kuonesha Masharti
bora, muradi Sitakuuliza bora tu usichelewe.
ikiwa, iwapo Ikiwa huna jambo muhimu la kusema, nyamaza.
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 39
Mofolojia ya Kiswahili 2018
VIHISISHI, VIHUSISHI NA NJIA ZA KUUNDA MANENO
Vihisishi: ni sauti, neno au kikundi cha maneno kinachotamkwa na mwanadamu kuashiria hisia tofauti kama vie furaha, huzuni, mshituko, n.k. mfano wa vihisishi ni kama Mungu wangu!, mama wee! Mtume simama!
Kwa kawaida vihisishi ni maneno ambayo huwa hayana uhusiano wa kisarufi na aina nyingine za maneno katika tungo. Hivyo vihisishi hujitegemea na kujitosheleza.
Kimuundo vihisishi haviambishwi na wala havina kanuni maalumu ya mfuatano.
Vilevile kwa vihisishi vyenye muundo wa kikundi hauwezi kubadilisha neno moja kwa lingine hata kama yana hadhi sawa.
Kwa mfano hatuwezi kusema
*miungu yangu! (badala ya Mungu wangu!)
*baba wee! (badala ya mama wee!)
Aina za vihisishi/viingizi
Viingizi vinaweza kugawanywa kwa kutumia vigezo vya kisemantiki.
Mkabala huu unatumika kugawa viingizi kulingana na maana zinazowakilishwa na viingizi vyenyewe.
Maana hizo ni hisia zinazobebwa na viingizi hivyo. Kutokana na hisia hizo tunaweza kuvigawanya katika makundi ya maana zinazohusiana kwa karibu. Kwa mtazamo huo, viingizi vinaweza kugawanywa katika makundi matatu makuu ambayo ni:
(a) Viingizi vinavyoonesha mhemko au hisia kali:
Viingizi hivi ni vile vinavyowakilisha hisia tofauti anazokuwa nazo mzungumzaji ambazo zinaweza kuwa nzuri au mbaya. Kundi hili la kwanza linaweza kugawanywa katika sehemu ndogo nne kutokana na hisia mbalimbali alizonazo mzungumzaji zinazowakilishwa na aina hii ya viingizi ni kama ifuatavyo:
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 40
Mofolojia ya Kiswahili 2018
(i) Viingizi vya furaha – hivi ni vile vinavyoonesha hali ya furaha aliyonayo mzungumzaji, kwa mfano, oyaa!, oyee!, huree!, n.k.
(ii)Viingizi vya huzuni – hivi ni vile vinavyoonesha hali ya masikitiko au huzuni iliyompata mzungumzaji, kwa mfano, pole!, maskini! Jamani!, n.k.
(iii)Viingizi vya mshangao – hivi ni vile vinavyoonesha hali ya mshangao uliompata mzungumzaji, kama vile. Eti!, salale!, ajabu!, kumbe!, n.k.
(iv) Viingizi vya mshituko – hivi ni vile vinavyoonesha hali ya mshituko uliompata mzungumzaji, kwa mfano loo!, amaa!, aisee!, n.k
(b)Viingizi vya maamrisho au msisitizo wa jambo au tukio:
Viingizi vya namna hii huonesha amri anayotoa mzungumzaji, kama vile haraka!, hima!, njoo!, nenda!, n.k.
(c) Viingizi vya maadili : hivi ni vile vinavyoonesha hisia zinazohusiana na maadili mbalimbali, yawe mema au mabaya. Aina hii ya viingizi inaweza kugawanywa katika makundi yafuatayo:
(i) Viingizi vya mwitiko – hivi ni vile ambavyo vinaonesha hisia za mwitiko anaokuwa nao mzungumzaji akiwa ameitwa au anapokabiliana na jambo katika mazungumzo, kwa mfano abee!, bee!, rabeka!, naam!, n.k.
(ii)Viingizi vya ombi – hivi ni vile ambavyo vinaonesha hisia za ombi kwa mfano, aha!, enhe!, simile!, astaghafirullah!, hodi!, n.k.
(iii)Viingizi vya bezo – hivi ni vile ambavyo vinaonesha hisia za bezo na dharau ya mzungumzaji, kwa mfano aka!, zii!, sasa!, n.k.
(iv) Viingizi vya kutakia heri – hivi ni vile vinavyowasilisha hisia za mzungumzaji za kutakia heri na kupongezana, kama vile: inshaallah!, ahsante!, hongera!, n.k.
(v)Viingizi vya kukiri jambo – hivi ni vile vinavyowasilisha hisia za kukiri, kwa mfano; laity! Haya! Taib!, n.k.
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 41
Mofolojia ya Kiswahili 2018
(vi) Viingizi vya kiapo – hivi ni vile ambavyo vinaonesha hisia za kuapa ili kuonesha mzungumzaji wa jambo fulani atalitenda au kukana kutenda jambo, kwa mfano; wallah!
(vii) Viingizi vya salamu – hivi ni vile vinavyotumika kutoa salamu za mzungumzaji kwa mtu mwingine wanapokutana watu wawili au zaidi, kwa mfano; shikamoo! Marhaba! Hujambo!, n.k.
Kwa kawaida viingizi havina uhusiano wa kimuundo na maneno mengine katika sentensi.
Huweza kuondolewa katika sentensi bila ya kuathiri muundo wa sentensi husika. Hata hivyo, viingizi huipa sentensi dhamira/hali fulani.
VIHUSISHI
Ni maneno yanayojitokeza baada ya nomino na kufanya kazi ya kuhusisha dhana tofauti. Umbo kuu/muhimu la kihusishi ni a-unganifu. Imeitwa a-unganifu kutokana na namna maumbile yake ya utendaji kazi yalivyo – kwamba ni lazima iunganishwe na mofu zinazowakilisha aina ya ngeli inayohusika mfano;
- Mtoto wa mama – wa-inahusisha mtoto na mama (ngei ya A-WA)
- Kiti cha mbao – cha – inahusisha kiti na mbao (ngeli ya KI-VI)
- Jiko la umeme – la – inahusisha jiko na umeme (ngeli ya (LI-YA)
Vilevile, kuna umbo na na kwa ambayo pia hutumika kama vihusishi ingawa yapo pia katika kundi la viunganishi mfano;
- Ameondoka na mkoba wako
- Ameangukiwa na jiwe
- Amejikata kwa kisu
- Tutasafiri kwa ndege, n.k.
Katika kujifunza aina za maneno ni muhimu kuelewa kuwa umbo la neno halitoshi kutambulisha aina ya neno. Unaweza ukagundua kuwa neno moja linajitokeza katika makundi tofauti; kwa mfano neno vizuri linaweza kuwa kiwakilishi, kivumishi au kielezi pia, neno kulala linaweza kuwa nomino au kitenzi.
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 42
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Halikadhalika neno Juma linaweza kuwa nomino au kivumishi. Hivyo ambo la msingi ni kuangalia kazi na nafasi ambayo neno hilo huchukua katika tungo.
UUNDAJI WA MANENO (NJIA ZA UUNDAJI WA MANENO)
Uundaji wa maneno ni mchakato unaowezesha lugha kujiongezea msamiati ili kukidhi haja ya mawasiliano na kuendana na mabadiliko yanayotokea kila siku.
Maneno ya lugha ya Kiswahili hayaundwi kiholela bali hufuata taratibu na kanuni zinazokubalika kitaalamu.
Njia zitumikazo kuunda maneno ni kama zifuatazo:
Unyambuaji
Njia hii inatumia mzizi mmoja wa neno na kuzalisha maneno mapya kwa kupachika viambishi nyambuaji
Mfano
Soma
Somo
Kisomo
Msomi
Msomaji
Lima
Mkulima
Kilimo
Mlimaji
Uambatishaji/mwambatano
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 43
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Hii ni njia ya kuunda maneno mapya kwa kuambatanisha maneno mawili.
Mfano
Mwana+chama - Mwanachama
Askari+kanzu - Askarikanzu
Bwana+shamba – Bwanashamba
Urudufishaji / Uradidi
Hii ni mbinu ya kurudiarudia neno au sehemu ya neno na kuunda neno jipya ambalo huwa na maana tofauti na maneno yanayorudiwarudiwa.
Mfano
(d) Pole : polepole
(e) Sawa : sawasawa
(f) Haraka : harakaharaka
Akronimu/ufupishaji
Ufupishaji ni njia mojawapo ya kuundia maneno mapya,ufupishaji huweza kufanyika kwa namna mbili ambazo ni.
Kufupisha kwa kuchukua herufi za mwanzo Mfano
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 44
Mofolojia ya Kiswahili 2018
CWT (Chama cha Walimu Tanzania) VVU (Virusi Vya Ukimwi)
Kufupisha kwa kuchukua silabi za mwanzo za maneno yanayo fupishwa
Mfano
BAKITA (Baraza la Kiswahili la Taifa)
TUKI (Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili)
TATAKI (Taasisi ya Taaluma za Kiswahili)
Uhulutishaji
Ni njia ya kuunda maneno mapya kwa kuchukua vijisehemu vya neno pasipo kufuata kanuni yoyote.
Mfano
Mnyama mfu – nyamafu
chakula cha jioni – chajio
hati za kukataza – hataza
Mtu asiye kwao - msikwao
Utohoaji
Ni uchukuaji wa maneno toka lugha moja na kuyatumia kwenye lugha nyingine baada ya kuyarekebisha kimatamshi na kimaandishi ili yaendane na sarufi ya lugha inayotohoa.
Mfano
Neno Lugha asilia Kiswahili
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 45
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Shirt Kiingereza Shati
Schule Kijerumani Shule
Bakura Kiarabu Bakora
Benjera Kireno Bendera
Matching Kiingereza machinga
guys
Kuchukua
Hii ni mbinu ya kuongenza maneno kwa kuyachukua toka lugha yake na kuyatumia kama yalivyo. Uchukuaji hufanyika kwa lugha zinazoendana kisarufi kama Kiswahili na lugha za kibantu.
Mfano
Kitivo — kisambaa /kipare
Ikulu - kinyamwezi
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 46
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Kigoda - kizaramo
Kubadili mpangilio wa fonimu
Mfano
Lima – mila – imla - mali
Kufananisha umbo /sauti /tabia
Mfano
Kufananisha umbo
- kifaru-(mnyama faru)
- mkono wa tembo-(mkonga wa tembo)
- kidole tumbo-(umbo la kidole)
Kufananisha Tabia
Ubeberu-(beberu la mbuzi)
Ukupe-(mdudu kupe)
Kufananisha Sauti
Pikipiki (mlio wa pikipiki)
Mtutu (mlio wa bunduki)
Nyau (mlio wa paka)
Kuku - kokoriko (mlio wa kuku)
Njia ya udondoshaji
Mfano
mkwe wake - mkwewe Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 47
Mofolojia ya Kiswahili 2018
mwana wake - mwanawe
ndugu yake – nduguye
Kuzingatia matumizi ya kitu
Mfano
Banio - (kubana)
Chanio - (kuchana)
Fyekeo - (kufyeka)
Kutarjumi/kutafsiri
Mfano;
Fluid – (ugiligili)
Acquired immunal deficiency syndrome (Upungufu wa kinga mwilini)
Human immunal virus – (virusi vya ukimwi)
Anti-rentro-virus - (dawa za kufubaza makali ya ukimwi)
DHANA YA MOFOFONOLOJIA NA MOFOSINTAKSIA
Maana ya Mofofonolojia
Ni taaluma inayoshughulikia uchanganuzi na uainishaji wa vipengele vya kifonolojia vinavyoathiri maumbo ya mofimu katika mfuatano wake.
Mofofonolojia huzalisha kanuni ambazo zinaelezea mazingira ya utokeaji wa mofu na alomofu zake.
Kanuni hizi huelezea maathiriano ya kifonolojia yanayoathiri mofolojia ya maneno na jinsi badiliko la kimofofonolojia la neno linavyoelezeka kikanuni.
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 48
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Kanuni hizi husaidia kujua jinsi maneno yanavyobadilika toka muundo ndani wa neno hadi muundo nje wa neno.
Kanuni za kimofofonolojia hutawaliwa na sifa zifuatazo
1. Kanuni za kifonolojia hazina vighairi mfano; hakuna vighairi katika kanuni ya kifonolojia isemayo mkazo katika Kiswahili huwekwa silabi ya pili kutoka mwishoni mwa neno.
2. Kanuni za kimofofonolojia huwa na vighairi vingi; Kanuni hii huhusu lugha mahususi na hutumika katika baadhi ya mofimu tu kwa mfano katika mofu ya utendea.
mfano
piga> pigia
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 49
Mofolojia ya Kiswahili 2018
panga> pangia
funga> fungia
tenga> tengea
choma> chomea
//utendea//----->i/-mz+[a,i,u]
------->e/-mz+[e,o]
AINA ZA KANUNI ZA KIMOFOFONOLOJIA
1.Kanuni ya usilimisho
Kanuni hii inahusu maathiriano ya mofimu zinazofuatana. Maathiriano hayo huzifanya mofimu zifanane zaidi kuliko zikiwa pekee.
Mfano(1)
a) n+goma----->{ngoma}
b) n+dizi------>{ndizi}
c) n+buzi----->{mbuzi}Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 50
Mofolojia ya Kiswahili 2018
d) n+bingu----->{mbingu}
n------>m/-k
Huu ni usilimisho wa nazali inayofuatwa na konsonanti
a) n+refu----->{ndefu}
b) n+limi---->{ndimi}
r------>d/n-
l------->d/n-
Huo ni usilimisho wa konsonanti inayotanguliwa na nazali(N)
2.Ukaakaishaji
Haya ni maathiriano ambayo sauti isiyo ya kaakaa gumu hulazimishwa kuwa sauti ya kaakaa gumu.
Mfano
a) ki+ama------->chama
b) ki+ombo------->chombo
c) ki+uma-------->chuma
d) ki+eo------>cheo
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 51
Mofolojia ya Kiswahili 2018
3. Udondoshaji
Mofimu hudondoshwa kutokana na mfuatano wa mofimu unaoleta maathiriano Mfano
a) wanasoma –hawasomi
b) anasoma-hasomi
c) nilikunywa-sikunywa //njeo// -------> θ/-ukanushi
4. Tangamano la irabu
Ni utaratibu wa irabu moja kukubali kuandamana na irabu nyingine katika mazingira maalumu. Kwa kawaida irabu iliyo katika mzizi huathiri utokeaji wa irabu ya mnyambuliko. Hivyo ikiwa irabu ya mzizi ni a,i au u irabu ya mnyambuliko huwa i na ikiwa irabu ya mzizi ni e au o basi irabu ya mnyambuliko huwa e.
Mfano
Panga ----- pangia
Funga …. Fungia
Piga ……pigia
Choma …..chomea
Sema …… semea
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 52
Mofolojia ya Kiswahili 2018
5. Mvutano wa irabu
Ni hali inayojitokeza wakati irabu ya juu na irabu ya chini zinapofuatana katika neno. Irabu hizo huvutana na kusababisha kutokea kwa irabu isiyo ya juu wala chini. Mfano,
ma+ino = meno
wa+ingi = wengi
ma+ingine = mengine
6. Uyeyushaji
Ni kitendo cha kubadili irabu kuwa nusu –irabu au kiyeyusho. Hali hii hutokea wakati irabu mbili zinapokutana mfano; irabu – u hubadilika na kuwa kiyeyusho /w/ inapokaribiana na a au i (mu+alimu=mwalimu, mu+imbaji = mwimbaji) na irabu -i- hubadilika na kuwa kiyeyusho /y/ inapokaribiana na irabu a, o au u (vi+ama= vyama, vi+ombo = vyombo, vi+uma = vyuma)
7. Vighairi
Ni mofimu au maneno yanayokiuka kanuni za kawaida za lugha husika. Mfano;
Kiatu………… viatu
Kisu……………visu
Choo ………….vyoo
Chama ………..vyama
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 53
Mofolojia ya Kiswahili 2018
Nomino choo, vyoo, chama, vyama ni vighairi kwa sababu yanaingia ngeli ya KI-VI lakini hayabebi viambishi husika mwanzoni.
D11/9/2018HANA YA MOFOSINTAKSIA
Ni taaluma inayoshughulikia uchanganuzi na uainishaji wa vipengele vya kisintaksia vinavyoathiri maumbo ya mofimu katika mfuatano wake.
Vipengele vya kisintaksia vinavyoathiri mofolojia ni:
(a) Umoja na wingi: maneno mengi ya Kiswahili huwa na maumbo tofauti yanapokuwa katika hali ya umoja na yanapokuwa katika hali ya wingi.
Mfano
Umoja Wingi
Kidole vidole
Ungo nyungo
Jicho macho
Kwa kuangalia mifano ya hapo juu tunaona kuwa wingi wa kitu kinachotajwa ni kilekile, mabadiliko ya maumbo hutokea kuingana na idadi ya kitajwa. Maneno mengi tu ya Kiswahili huwa na tabia hii lakini sio yote. Hii ina maana kwamba baadhi ya maneno hubaki kama yalivyo (hayabadiliki) ikiwa yapo katika umoja au katika wingi. Mfano wa maneno hayo ni sabuni, njia, nguo, nyumba, zawadi, n.k.
(b)Njeo: katika Kiswahili kuna viambishi mbalimbali vinavyotumiwa kuwakilisha njeo. Hivyo basi, kadiri mzungumzaji anavyofikiria dhana
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 54
Mofolojia ya Kiswahili 2018
ya wakati fulani katika mazungumzo yake ndipo umbo la neno linapobadilika kulingana na wakati huo. Mfano; analima,atalima,amelima,alilima (na – wakati uliopo, ta – wakati ujao, me – wakati uliopita timilifu, li – wakati uliopita)
(c) Ukanushi : dhana ingine ya kisintaksia inayosababisha umbo la neno kubadilika ni ukanushi. Angalia mifano ifuatayo:
A B
Uyakinishi Ukanushi
Anapika ……………. hapiki
Amepika …………… hajapika
Alipika …………….. hakupika
Atapika …………….. hatapika
Mifano hiyo inaonesha kwamba kutokana na kuwepo kwa mofimu ha ya ukanushi katika maneno ya jozi B maumbo yanayowakilisha wakati yamebadilika. Umbo na la wakati uliopo halionekani katika nafasi yake badala yake kuna umbo i mwishoni mwa kitenzi, wakati uliopita (muda mfupi) unawakilishwa na ja badala ya me na wakati uliopita unawakilishwa na ku badala ya li. Umbo linalowakilisha wakati ujao pekee ndilo lisiloathiriwa na mabadiliko haya.
(d)
Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 55