toleo namba 8 julai-desemba 2018 - tanzania · 2018. 10. 30. · malipo ya mishahara ya serikali...

16
Toleo Namba 8 Julai-Desemba 2018 Hutolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini , Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Barabara ya Mkalama, S.L.P 670, 40404,Dodoma, Barua Pepe:[email protected] Tovuti:www.utumishi.go.tz Taarifa ya mwisho ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi yabaini Watumishi 14,409 kuwa na vyeti vya kughushi UK.5 “Tangu tumeingia madarakani mwaka 2015, tumepata mafanikio makubwa katika kubadilisha taswira ya Utumishi wa Umma. Tulianza na zoezi la kuhakiki Watumishi wa Umma ili kuhakikisha kwamba Watumishi wa Umma wanakuwa wale wenye sifa stahiki. Tumefanikiwa kuondoa Watumishi hewa 19,708 na watumishi wenye vyeti vya kughushi 14,152. Haya ni mafanikio makubwa ambayo yametuwezesha kuokoa mabilioni ya shilingi, lakini pia tumeweza kubaki na watumishi wenye sifa ya kufanya kazi” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. News

Upload: others

Post on 25-Jan-2021

2 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • Toleo Namba 8 Julai-Desemba 2018

    Hutolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,

    Barabara ya Mkalama, S.L.P 670, 40404,Dodoma,Barua Pepe:[email protected]

    Tovuti:www.utumishi.go.tz

    Taarifa ya mwisho ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi yabaini Watumishi 14,409 kuwa na vyeti vya kughushi UK.5

    “Tangu tumeingia madarakani mwaka 2015, tumepata mafanikio makubwa katika kubadilisha taswira ya Utumishi wa Umma. Tulianza na zoezi la kuhakiki Watumishi wa Umma ili kuhakikisha kwamba Watumishi wa Umma wanakuwa wale wenye sifa stahiki. Tumefanikiwa kuondoa Watumishi hewa 19,708 na watumishi wenye vyeti vya kughushi

    14,152. Haya ni mafanikio makubwa ambayo yametuwezesha kuokoa mabilioni ya shilingi, lakini pia tumeweza kubaki na watumishi wenye sifa ya kufanya kazi”

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

    News

  • YALIYOMO

    1. Serikali yadhamiria kupambana na rushwa................................................3-5

    2.Taarifa ya mwisho ya zoezi la uhakiki...............................................5-6

    3. Katibu Mkuu atoa huduma sehemu ya mapokezi...............................................7

    4.Watumishi wa Umma wahimizwa kuwajibika...........................................8-9

    5. WHC waagizwa kujenga katika mikoa mipya...............................................9-10

    6.Serikali yawarejesha kazini watendaji wa vijiji................................................11-12

    7.UTUMISHI yatekeleza mwongozo wa huduma kwa watumishi wenye ulemavu...............................................12

    8.Serikali yawataka waratibu wa masuala ya VVU, Ukimwi na magonjwa yasiyoambukiza mahala pa kazi kutekeleza wajibu wao....................................................13

    9. Serikali yawataka waajiri nchini kuandaa mapema taarifa sahihi za watumishi.............................................14

    10.Watumishi wa Umma watakiwa kuzingatia kwa vitendo tamko la ahadi ya uadilifu ili kutekeleza majukumu yao kikamilifu.............................................15

    CHUMBA CHA HABARI

    Bodi ya Uhariri:

    Dkt. Laurean J. Ndumbaro Bi. Dorothy A. Mwaluko Bi. Mary L. Mwakapenda Bw. James K. Mwanamyoto Bi. Happiness S. Shayo

    Dira

    Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora (OR-MUUUB) kuwa Taasisi

    itakayowezesha kuwa na Utumishi wa Umma uliotukuka kwa kutoa

    huduma bora kwa Umma na hivyo kuchangia katika kukuza uchumi,

    kupunguza umaskini na kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania

    ifikapo mwaka 2025.

    Dhamira

    Kuhakikisha kuwa utumishi wa umma nchini unasimamiwa vizuri na kwa ufanisi kupitia usimamizi

    wa rasilimaliwatu, mifumo na miundo ya kiutumishi

    Uk.

  • Serikali yadhamiria kupambana na rushwa kwa kutoa huduma kupitia mifumo ya TEHAMA ya utoaji huduma kwa umma aziri Mkuu wa Jamhuri

    ya Muungano wa Tanza-nia, Mhe. Kassim

    Majaliwa (Mb) amesema S e r i k a l i imedhamiria kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa kwa kutoa huduma bora kupitia mifumo ya TEHAMA ya utoaji huduma kwa umma.

    Mhe. Majaliwa alisema hayo katika kilele cha maadhi-misho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2018, yaliyo-fanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Square jijini Dodoma.

    Mhe. Majaliwa, alibainisha kuwa, kwa sasa serikali imepiga hatua katika mapambano dhidi ya rushwa, kwani kupitia TEHAMA huduma zinatolewa bila rushwa wala bughudha yoyote kwa wananchi.

    Mhe. Majaliwa aliipongeza Wakala ya Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kutoa huduma kwa wakati kupitia Mfumo wa Usajili wa Vizazi na Vifo kwa wananchi waliofuata huduma wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

    Mhe. Majaliwa aliongeza kuwa,

    mapambano dhidi ya rushwa ni utekelezaji wa malengo ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika na malengo ya maendeleo ende-

    levu kama inavyojiainisha katika kauli mbiu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2018 inayosema “Mapam-bano dhidi ya Rushwa kwa kush-irikisha wadau na kujenga uon-gozi bora ili kufikia Malengo ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika na Malengo ya Maendeleo Ende-levu”.

    Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2018, ni ya kipekee kwani yalienda sam-bamba na uzinduzi wa mifumo tisa ya TEHAMA ya serikali ya utoaji huduma kwa umma.

    Mifumo iliyozinduliwa ni Mfumo wa Usajili, Vizazi na Vifo, Mfumo wa Taarifa za Kitabibu, Mfumo wa Taarifa za Ununuzi, Mfumo wa

    Kumbukumbu za Kielektroniki, Mfumo wa Ofisi Mtandao, Mfumo wa Taarifa za Kulipia Mishahara ya Watumishi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki, Mfumo wa Malipo wa Serikali, Mfumo wa Utoaji Huduma za Serikali Kupitia Simu za Mikononi na Mfumo wa Vibali vya Kusafiri nje ya nchi kwa watumishi wa umma kwa safari binafsi au za kikazi kwa mtu binafsi au kikundi.

    Waziri Mkuu aliwashukuru wadau wote wa maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia kwa ushirikiano wanaoutoa kwa serikali hasa katika utengenezaji wa mifumo hiyo.

    Aliongeza kuwa, Serikali inaende-lea kuboresha huduma ikiwa ni utekelezaji wa ahadi alizozitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuwezesha wananchi kupata huduma kwa wakati hususani maeneo ya viji-jini na kuwataka wananchi kuen-delea kuwa na imani na serikali yao.

    Alitoa wito kwa wasimamizi wa mifumo hiyo na watumiaji kuil-inda ili iweze kuwa na tija na isitumike vinginevyo na kuwak-waza wananchi.

    Akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wananchi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Meneji-menti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) alisema Ofisi yake, iliamua kihitimisha wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2018 kwa kuzindua mifumo ya TEHAMA ya serikali ili kuwezesha kutoa huduma kwa umma kwa haraka na bila usum-bufu.

    Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mifumo ya TEHAMA ya Serikali ya utoaji huduma kwa umma, siku ya kilele cha Maadhimisho

    ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2018 katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Square jijini

    Dodoma.

    3

  • Mhe. Mkuchika alisema kwa muda mrefu, serikali imeendelea kuboresha huduma kupitia TEHAMA kwa kuzingatia mipango ya taifa ya maendeleo ikiwamo Dira ya Taifa ya mwaka 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano wa mwaka 2011/12 hadi 2015/16 na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala.

    Aliongeza kuwa, katika vipindi tofauti, serikali imefanikiwa kuwa na mifumo mbalimbali ya TEHAMA iliyojengwa na wataalam wa ndani na wakandarasi. “Jambo la kujivunia ni kuwa sehemu kubwa ya mifumo hiyo imetengenezwa na wataalam wa ndani hivyo ni vema kuwaendeleza wataalam hawa wa TEHAMA katika kila taasisi za seri-kali ili kutoa huduma bora zaidi.” Mhe. Mkuchika alisisitiza

    Naye Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro aliwataka watumishi wa umma nchini kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magu-fuli kwa kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma, mambo ambayo aliyasisitiza wakati akizindua Bunge la Jam-huri ya Muungano wa Tanzania.

    Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza-nia, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akikabidhi cheti cha kuzaliwa kwa Shukran George kwa niaba ya mtoto wake Magreth Msomba, siku ya kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2018 katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Square jijini Dodoma.

    Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akisalimiana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Lau-rean Ndumbaro siku ya kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2018 katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Square jijini Dodoma.

    4

  • Taarifa ya mwisho ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma yabaini watumishi 14,409 kuwa na vyeti vya kughushi na

    watumishi 1,907 kutowasilisha vyeti kwa ajili ya kuhakikiwa

    umla ya watumishi wa umma 14,409 wame-bainika kuwa na vyeti vya kughushi na watu-mishi 1,907 kutowasilisha vyeti kwa ajili ya kuhakikiwa licha ya Serikali kutoa muda wa kutosha kwa watumishi hao kuwasilisha vyeti

    vyao Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa ajili ya uhakiki.

    Taarifa hiyo ilitolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dkt. Charles Msonde wakati akiwasilisha taarifa ya sita na ya mwisho ya zoezi la uhakiki wa vyeti vya Watumishi wa Umma vya ufaulu wa kidato cha Nne, cha Sita na Ualimu kwa Katibu Mkuu-UTUMISHI Dkt. Laurean Ndumbaro.Dkt. Msonde alisema katika awamu ya sita jumla ya watumishi 5,696 walihakikiwa vyeti vyao, kati ya hao, watumishi 5,404 sawa na asilimia 94.82 wali-

    bainika kuwa na vyeti halali na watumishi 295 sawa na asilimia 5.518 walibainika kuwa na vyeti vya kughushi.

    Aidha, Dkt. Msonde alifafanua kuwa, jumla ya watumishi wa umma 511,789 walihakikiwa katika awamu zote sita za uhakiki, kati ya hao watumishi 494,554 sawa na asilimia 96.71 vyeti vyao vilibainika kuwa ni halali, watumishi 14,409 sawa na asilimia 2.82 walibainika kuwa na vyeti vya kughushi na watu-mishi 1,907 hawakuwasilisha vyeti vyao kwa ajili ya kuhakikiwa.

    Dkt. Msonde alisema, ofisi yake imebaini watumishi 71 ambao majina yao halisi waliyoajiriwa nayo ni tofauti na majina yaliyomo katika vyeti walivyotumia kujipatia ajira katika Utumishi wa Umma

    Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akibofya kitufe kuzindua Mifumo ya TEHAMA ya Serikali ya utoaji huduma kwa umma, siku ya kilele cha

    Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2018 katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Square jijini Dodoma.

    5

  • na kuongeza kuwa wahusika walihojiwa na kutoa sababu mbalimbali zilizopelekea utofauti wa majina yao ikiwemo sababu ya kubadili dini, hivyo ameli-wasilisha kwa Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa ajili ya hatua stahiki.Baada ya kupokea taarifa hiyo, Katibu Mkuu-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro alisema anaamini kuwa waajiri wameshawaondoa katika Orodha ya Malipo ya Mishahara ya Serikali (payroll) watumishi wote waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi kuan-zia awamu ya kwanza hadi ya tano ya uhakiki, isipokuwa waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi katika awamu ya sita.

    Kuhusu watumishi 1,907 ambao hawajawasilisha vyeti vyao kwa ajili ya kuhakikiwa, Dkt. Ndumbaro alisema Mhe. Rais au Mamlaka yoyote inayotambulika kisheria katika Utumishi wa Umma inapotoa maele-kezo au maagizo na wanaotakiwa kutekeleza wasipo-tekeleza wanakuwa wametenda kosa kwa mujibu wa Kanuni, Sheria na Taratibu za Utumishi wa Umma. Kutokana na kosa hilo Dkt. Ndumbaro aliwaagiza waajiri kuwachukulia hatua watumishi hao.

    Aidha, Dkt. Ndumbaro aliwashukuru wananchi na Watumishi wa Umma ambao walitoa taarifa za uwepo wa watumishi wenye vyeti vya kughushi Serikalini na kuwaomba kuendelea kutoa taarifa za watumishi wengine wasio na sifa kupitia namba yake ya simu ya

    kiganjani 0754 261 965 ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais za kuwa na watumishi wa umma wenye sifa stahiki.

    Dkt. Ndumbaro alitoa maelekezo kwa Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kufanya ukaguzi wa majadala ya watumishi walio chini ya ofisi zao ili kujiridhisha kama watumishi waliobakia wana sifa stahiki na kusisitiza kuwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itafanya ukaguzi wa kushtukiza katika baadhi ya Ofisi na Taasisi za Umma ili kujiridhisha na namna zoezi la uhakiki lilivyofanyika kwa Waajiri wote katika Utumishi wa Umma.

    Pamoja na maelekezo hayo, Dkt. Ndumbaro alieleza kuwa Serikali inaandaa utaratibu wa kuhakiki vyeti vya Taaluma vinayotolewa na vyuo vya elimu ya Juu vya

    ndani na nje ya Nchi. Aidha, Watumishi walisoma vyuo vya nje ya nchi, watapaswa kuviwasilisha Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania – TCU ili vihakikiwe kujiridhi-sha na uhalali wa vyeti husika.

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akikabidhiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dkt. Charles Msonde nakala ya taarifa ya sita na ya mwisho ya zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma.

    Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanza-nia (NECTA) Dkt. Charles Msonde (kulia) akiwasilisha taarifa ya mwisho ya zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro.

    6

  • Katibu Mkuu - Utumishi atoa huduma sehemu ya mapokezi kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma, 2018

    atibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utu-mishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ame-hudumia wadau eneo la mapokezi ya ofisi

    yake, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2018.

    Dkt. Ndumbaro, alitekeleza kwa vitendo maagizo aliyoyatoa kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi za Seri-kali, kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kujikita katika eneo la utoaji huduma ili kupata fursa ya kubaini changamoto na kufanya tathmini ya ubora wa huduma zinazotolewa kwa umma kwa lengo la kuziboresha.

    Dkt. Ndumbaro alisema, Watendaji Wakuu wanapaswa kuwa mstari wa mbele kutoa huduma kwa wadau ili kuhamasisha Watumishi wa Umma nchini kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia weledi.

    Dkt. Ndumbaro alifafanua kuwa, katika Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2018, Wakuu wa Idara na

    Vitengo katika ofisi yake, walishiriki kutoa huduma sehemu ya mapokezi kwa kupokezana ili kuwa mfano bora kwa watumishi wengine kutekeleza wajibu wao ipasavyo.

    Aidha, wadau waliofika kupata huduma Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora kwa nyakati tofauti, walisema wamefurahishwa na kitendo cha kuhudu-miwa na Katibu Mkuu-Utumishi sehemu ya mapokezi na walisisitiza kuwa huu ni mfano mzuri wa kuigwa na Wakuu wengine wa Taasisi za Serikali.

    Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma huadhi-mishwa kila mwaka kuanzia tarehe 16-23 Juni. Kauli Mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni; “Mapam-bano dhidi ya Rushwa kwa kushirikisha wadau na kujenga uongozi bora ili kufikia Malengo ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika na Malengo ya Maendeleo Endelevu.”

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa huduma kwa mdau eneo la mapokezi ya ofisi yake, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka, 2018.

    7

  • Watumishi wa umma wahimizwa kuwajibika katika mapambano dhidi ya rushwa ili kuhakikisha taifa linafikia uchumi wa viwanda

    atumishi wa umma nchini wame-kumbushwa na kuhimizwa

    kutekeleza wajibu wao ipasavyo katika mapambano dhidi ya rushwa

    i l i kuliwezesha taifa kufikia lengo la uchumi wa viwanda.Msisitizo huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati akizungumza na watumishi wa umma na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya rushwa katika Siku Maalum ya Mapambano dhidi ya Rushwa, iliyo-adhimishwa kwenye Maonesho ya 42 ya Kima-taifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.

    Mhe. Mkuchika alisema, Serikali imeweka sera na mikakati madhubuti ya kupambana na rushwa, hivyo ni jukumu la kila mtumishi kuwa-jibika ipasavyo badala ya kuwa kikwazo katika utekelezaji wake.

    Mhe. Mkuchika amezihimiza taasisi za Serikali kuhakikisha zinatoa mwaliko kwa TAKURURU katika mikutano yao ili mada za elimu ya rushwa ziwasilishwe kwa watumishi na kuon-geza kuwa anamshukuru Mhe. Waziri Mkuu kwa kutoa maelekezo kwa taasisi zote za umma kuwaalika TAKUKURU kutoa elimu kuhusu rushwa katika mikutano mikubwa ya taasisi za umma yenye lengo la kuboresha utendaji.

    Mhe. Mkuchika aliainisha kuwa, watanzania wengi wakielewa athari za rushwa hawatajihu-sisha na vitendo vya rushwa na hatimaye nchi itakuwa mahala salama pa kuishi na kupiga hatua katika maendeleo ya kiuchumi.

    Aidha, Mhe. Mkuchika aliwataka wadau wote nchini kushiriki katika kuitokomeza rushwa nchini kwani Serikali haina uwezo wa kumaliza tatizo la rushwa bila kushirikiana na wadau na wananchi. Naye, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya (Mb) alisema, rushwa imelichelewesha taifa kupiga hatua ya maendeleo kiuchumi hususani katika sekta ya viwanda na kuongeza kuwa imeua baadhi ya viwanda vilivyokuwa vimeanzishwa na kukwamisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

    Mhe. Manyanya alisisitiza kuwa, ni jukumu la kila

    mtu kwa kushirikiana na TAKUKURU kupiga vita rushwa ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ndiye anayeongoza vita hii kwa lengo la kuinua uchumi wa taifa.

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na watumishi wa umma na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya rushwa katika Siku Maalum ya Mapambano dhidi ya Rushwa, iliyoadhimishwa kwenye Maonesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akibadilishana mawazo na mmoja wa wadau wa maendeleo katika Siku Maalum ya Mapam-bano dhidi ya Rushwa, iliyoadhimishwa kwenye Maone-sho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.

    8

  • Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola alisema kwa mara ya kwanza katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam mwaka huu, ilitengwa siku maalum ya mapambano dhidi ya rushwa, lengo likiwa ni kusam-baza ujumbe wa elimu ya rushwa kwa wadau wa sekta ya viwanda na biashara pamoja na wananchi wote ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto ya rushwa nchini.

    Bw. Mlowola aliahidi kuwa TAKUKURU itaendelea

    kujenga mahusiano na mshikamano na wadau wote na hatimaye kwa pamoja kujiwekea mikakati ende-levu ya kushirikiana katika kuzuia na kupambana na rushwa.

    Sanjali na hilo, Bw. Mlowola aliwashukuru TANTRADE kwa kutambua uzito wa tatizo la rushwa na kutenga siku maalumu ya kuwezesha ushiriki wa TAKUKURU kutoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwenye Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam.

    Watumishi Housing Company waagizwa kutoa kipaumbele cha ujenzi wa nyumba katika mikoa na halmashauri mpya

    nchini

    erikali imeia-giza Bodi na Menejimenti

    ya Watumishi Housing Company kutoa kipaumbele cha ujenzi wa nyumba za kuishi watumishi wa umma na viongozi katika mikoa mipya na halmashauri mpya nchini kwani maeneo hayo yanakabiliwa na uhaba wa nyumba za kuishi watumi-shi. Agizo hilo lime-tolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Meneji-menti ya Utu-mishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) alipo-t e m b e l e a baadhi ya miradi inayo-tekelezwa na W a t u m i s h i Housing Company iliyopo jijini Dar es Salaam.

    Moja ya mradi wa ujenzi wa nyumba unatekelezwa na Watumishi Housing Company (WHC) eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam.

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumi-shi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na Mkurugenzi wa Watumishi Housing Com-pany (WHC) Dkt. Fred Msemwa kuhusu utekelezaji wa mradi ya ujenzi wa nyumba katika eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam.

    9

  • Mhe. Mkuchika alisisitiza Watumi-shi Housing Company kuweka mpango wa kuanzisha miradi ya ujenzi wa nyumba katika maeneo hayo mapya akitoa mfano wa Geita, Simiyu, Chemba na Nyang’wale ili kuwawezesha watumishi katika maeneo hayo kupata makazi bora na hatimaye kutoa huduma bora kwa wananchi kama ilivyokusudiwa na Serikali.

    Mhe. Mkuchika aliipongeza Watu-mishi Housing Company kwa

    k u j e n g a nyumba za polisi saba w i l a y a n i

    Nyang’wale na k u w a t a k a kuwasiliana na halmashaur i nchini ili k u p a t i w a viwanja na k u j e n g e w a miundo mbinu ya barabara, maji na umeme kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za

    gharama nafuu.

    “Serikali ya Awamu ya Tano inajali na kuz-ingatia thamani ya fedha inayotumika katika miradi

    mbalimbali ya maendeleo nchini, hivyo mnatakiwa kusimamia ubora na viwango katika miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi nchini ili iendane na thamani ya fedha iliyo-tumika” Mhe. Mkuchika alisisitiza.

    Naye, Mkurugenzi wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa alisema katika Mradi wa nyumba za Gezaulole, kiwango cha chini cha gharama ya nyumba ni shilingi milioni 38 kwa nyumba ya chumba kimoja hadi viwili na nyumba ya vyumba vitatu gharama yake inaanzia shilingi milioni 49 za kitanzania.Watumishi Housing Company ni kampuni ya uwekezaji iliyo-anzishwa mwaka 2014 ikiwa na

    majukumu makuu ya kujenga nyumba kwa ajili ya wafanyakazi katika sekta za umma, sekta binafsi, wanachama wa mifuko ya hifadhi za pamoja na kuhamasisha uwekezaji wa pamoja katika milki.

    Tangu kuanzishwa kwake, Watu-mishi Housing Company imefani-kiwa kujenga nyumba 950 katika mikoa 19 nchini.

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mku-chika akitembelea mradi wa ujenzi wa nyumba wa Gezaulole wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea miradi inayo-tekelezwa na Watumishi Housing Company (WHC) jijini Dar es Salaam.

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb)akisalimiana na mmoja wa wakandarasi wa kigeni wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea miradi ya ujenzi wa nyumba inayotekelezwa na Watu-mishi Housing Company (WHC) jijini Dar es Salaam.

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizung-umza na watendaji (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea miradi ya ujenzi wa nyumba inayotekelezwa na Watumishi Housing Company (WHC) jijini Dar es Salaam.

    10

  • erikali imewarejesha kazini Watendaji wa Vijiji na Mitaa walioajiriwa kabla ya tarehe 20 Mei, 2004 ulipoanza kutumika Waraka wa Utumishi

    (Establishment Circular) Na. 1 wa Mwaka 2004 na watumishi 1,370 waliolegezewa masharti ya muundo na Mkuu wa Utumishi wa Umma kupitia barua ya Katibu Mkuu-Utumishi ya tarehe 30 Juni, 2011 yenye Kumb. Na.CCB.271/431/01/P/13, watumishi hawa walioondolewa kwenye Mfumo wa Malipo ya Msha-hara kwa kukosa sifa ya cheti cha kufaulu mtihani wa elimu ya Kidato cha Nne.

    Uamuzi huo ulitolewa na Serikali wakati wa kipindi cha Bunge kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb).

    Mhe. Mkuchika alisema licha ya Serikali kutoa maele-kezo sahihi mara kwa mara kuhusu utekelezaji wa zoezi la uhakiki wa sifa za watumishi wa umma nchini, lakini kumejitokeza malalamiko ya kutoz-ingatiwa kwa maelelekezo hayo wakati wa utekelezaji wa zoezi hili.

    Mhe. Mkuchika alifa-fanua kuwa, Ofisi yake imepokea malalalamiko kutoka kwa Watumishi walioathirika pamoja na Vyama vya Wafan-yakazi na kuongeza kuwa, Serikali ime-pokea Ushauri na Maoni kutoka kwa Waheshi-miwa Wabunge katika Mkutano wa Bunge ulio-kuwa ukiendelea, hivyo iliamua na kuagiza kurejeshwa kazini watumishi hao.

    Aidha, Mhe. Mkuchika alielekeza watumishi hao walipwe mishahara yao kwa kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa kazini na waendelee na ajira zao hadi watakaposta-afu kwa mujibu wa

    Sheria.

    Pia, Mhe. Mkuchika aliriarifu Bunge kuwa, Uamuzi huo hauwahusu Watumishi wa makundi yafuatayo;

    i. Watumishi waliowasilisha vyeti vya kughushi katika kumbukumbu za ajira yao.

    ii. Watumishi waliokuwepo katika ajira kabla ya tarehe 20 Mei, 2004 ambao katika kumbukumbu zao rasmi kama vile taarifa binafsi (Personal Records), fomu za tathmini ya utendaji kazi (OPRAS) walijaza taarifa za uwongo kwamba wanayo elimu ya kidato cha nne lakini wakashindwa kuthibitisha kwa kuwasilisha vielelezo vya sifa hizo kwa mujibu wa Miundo yao ya Utumishi.

    iii. Watumishi wote waliioajiriwa baada ya tarehe 20 Mei, 2004 wakiwa hawana sifa ya kufaulu mtihani wa kidato cha nne kwa kuwa walijipatia ajira kinyume cha maelekezo ya Serikali.Sanjari na maelekezo hayo, Mhe. Mkuchika alisema, Watendaji Wakuu na Wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi wote walioshiriki kuwaajiri Watumishi

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akitoa taarifa Bungeni kuhusu uamuzi wa Serikali wa kuwarejesha kazini Watendaji wa Vijiji na Mitaa walioajiriwa kabla ya tarehe 20 Mei, 2014 na watumishi 1,370 waliolegezewa masharti ya muundo na Mkuu wa Utumishi wa Umma.

    Serikali yawarejesha kazini watendaji wa vijiji na mitaa walioajiriwa kabla ya tarehe 20 Mei, 2004 na watumishi 1,370 waliolegezewa

    masharti ya muundo na mkuu wa utumishi wa umma

    11

  • Watumishi wasiokuwa na sifa ya kufaulu mtihani wa kidato cha nne katika Utumishi wa Umma baada ya tarehe 20 Mei, 2004 watachukuliwa hatua za kinid-hamu kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.Mhe. Mkuchika alitoa tahadhali kwa Watendaji Wakuu na Maafisa wote wanaosimamia zoezi la kuwarejesha watumishi hao, kuwa kwa namna yoyote ile wakishiriki kuhujumu zoezi hili kwa kuon-doa au kuharibu kumbukumbu za Watumishi, Serikali itawachukulia hatua za kinidhamu na za Kijinai ikibidi.

    Awali, Serikali ilitoa maelekezo kupitia barua ya Katibu Mkuu - Utumishi yenye Kumb.Na. CFC.26/205/01”Q”/61 ya tarehe 10 Julai, 2017 ikiwataka Waajiri kusimamisha mishahara ya watu-

    mishi waliaojiriwa baada ya tarehe 20 Mei, 2004 wakiwa hawana sifa ya kufaulu mtihani wa elimu ya kidato cha nne hadi watakapowasilisha vyeti husika. Katika zoezi hilo, jumla ya Watumishi 7,382 (Watendaji wa Vijiji - 3,817, Watendaji wa Mitaa - 51, Watendaji wa Kata - 253, Madereva wa Magari - 330, Kada za Afya - 1,060 na Kada nyinginezo - 1,871) walisimamishiwa mishahara na waajiri wao.

    Hata hivyo, idadi hii ya watumishi 7,382 ilichanganya Watumishi ambao hawakuwa na sifa, Watumishi waliokuwepo kabla ya tarehe 20 Mei, 2004 pamoja na wale waliolegezewa masharti ya Muundo na Mkuu wa Utumishi wa Umma yaani Katibu Mkuu Kiongozi kupitia barua ya Katibu Mkuu-Utumishi yenye Kumb. Na. CCB.271/431/01/P/13 ya tarehe 30 Juni, 2011.

    Ofisi ya Rais-Utumishi yatekeleza mwongozo wa huduma kwa watumishi wa umma wenye ulemavu

    fisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetekeleza Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma Wenye

    Ulemavu kwa kuhakikisha mtumishi wake mwenye uhitaji anapatiwa nyenzo ya kumwezesha kutekeleza majukumu yake ya kazi.

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro akikabidhi nyenzo hiyo, ambayo ni pikipiki ya gurudumu tatu (Bajaji) kwa Bw. Abbas Mpunga (Mtakwimu) alisema, mwajiri pamoja na watumishi wa ofisi yake ndio waliofanikisha kupatikana kwa Bajaji hiyo.

    Dkt. Ndumbaro alisema chombo hicho ni moja ya motisha kwa mtumishi mahala pa kazi na kuwapongeza watumishi wa ofisi yake kwa kushiriki kikamilifu kufanikisha tukio hilo.

    Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inatambua umuhimu wa suala la kuboresha mazingira ya kazi na ajira kwa watumishi wa umma wenye ulemavu, na ilitoa Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma Wenye Ulemavu wa mwaka 2008.

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utu-mishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akikata utepe kabla kumkabidhi Bajaji mmoja wa mtumi-

    shi wake Bw. Abbas Mpunga.

    Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumi-shi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akikabidhi

    nyaraka za umiliki wa Bajaji kwa Bw. Abbas Mpunga.

    12

  • Serikali yawataka waratibu wa masuala ya VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukizwa (MSY) mahala pa kazi

    kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia weledierikali ime-wataka Waratibu wanaos imamia

    masuala ya VVU, UKIMWI na Magonjwa Ya s i y oambuk i zwa (MSY) katika taasisi za umma kutekeleza wajibu wao ili kupata takwimu sahihi za watumishi wanaoishi na VVU, UKIMWI na wenye Magonjwa Ya s i y oambuk i zwa (MSY) kwa lengo la k u r a h i s i s h a utekelezaji wa mpango wa kupam-bana na magonjwa hayo yanayoathiri utendaji kazi wa watumishi kwa kiasi kikubwa.

    Wito huo ulitolewa mjini Morogoro na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha Waratibu wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukizwa (MSY) mahala pa kazi kutoka katika wizara mbalimbali nchini. Bi. Mwaluko alisema, kukosekana kwa taarifa sahihi za watumishi wenye maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI, kumekwamisha mpango thabiti wa Serikali wa kukabiliana na changamoto ya maambukizi mapya kwa Watumishi wa Umma nchini.

    Aidha, Bi. Mwaluko alihoji uhalisia wa takwimu zilizopo sasa za watumishi wa umma 1852 waliobainika kuishi na VVU/UKIMWI iwapo zinatoa taswira halisi ya tatizo lililopo.

    Bi. Mwaluko alitoa angalizo kwa waratibu kusimamia vizuri suala la afya za watumishi kwani lina athari

    kubwa kiutendaji l is iposimamiwa vema. Naye, Katibu wa Kamati Tendaji ya Kitaifa ambaye pia ni Afisa Mwi-tikio wa taasisi za Umma kutoka TACAIDS, Dkt. Ameir Hafidh, alisema kuwa Serikali imeweka mkakati wa k u h a k i k i s h a ifikapo mwaka 2020 asilimia tisini ya wanaoishi na VVU/UKIMWI watakuwa wam-etambua hali zao na kuanza kutu-

    mia dawa za kupunguza makali kwa usahihi.

    Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akifungua kikao kazi cha siku mbili cha Waratibu wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoam-bukizwa (MSY) mahala pa kazi kutoka katika wizara mbalimbali nchini yaliyofanyika mjini Morogoro

    Baadhi ya Waratibu wanaosimamia masuala ya VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukizwa (MSY) katika taasisi za umma wakim-sikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) alipokuwa akifungua kikao kazi cha Waratibu hao mjini Morogoro.

    13

  • Serikali yawataka waajiri nchini kuandaa mapema taarifa sahihi za watumishi ili wanapostaafu wapate mafao kwa wakati

    erikali imewataka waajiri nchini kuhakikisha kwamba, nyaraka na taarifa zinazom-

    husu mtumishi wa umma zinaandaliwa, kutunzwa vizuri, kuhuis-hwa na kuhakikiwa mara kwa mara kwa lengo la kumuwezesha mtumishi anapostaafu kupata mafao yake kwa wakati.

    Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb), alipokuwa akizung-umza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma.

    Mhe. Mkuchika, aliwaelekeza Wakuu wa Idara za Usimamizi wa Rasilimaliwatu, kuhakikisha wanakuwa na Tange zilizo hai wakati wote na kuweka utaratibu mahsusi wa kushughulikia masuala ya Watumishi wanaokaribia kusta-

    afu kwa mujibu wa matakwa ya Sheria, Kanuni, Taratibu na M i o n g o z o inayotolewa na Serikali.

    “Ni jukumu la mwajiri kum-saidia mstaafu k u k a m i l i s h a taratibu za k u f u a t i l i a mafao yake badala ya k u m u a c h a a k i h a n g a i k a bila usaidizi wowote mkum-buke kuwa

    wengi wa wastaafu hao wanatoka maeneo ya mbali” Mhe. Alisisitiza.

    Mhe. Mkuchika alibainisha kuw-

    kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wastaafu kuche-leweshewa mafao yao kutokana na baadhi ya wadau wa mchakato huo kutotekeleza wajibu wao ipasavyo na matokeo yake kusa-

    babisha usumbufu kwa watumishi wastaafu kutolipwa mafao yao kwa wakati.

    “Serikali imeona changamoto hiyo na ndio maana hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tan-zania, ameidhinisha mabadiliko ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii iliyopit-ishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inaunganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili kuwa na mifuko miwili ambayo itarahisisha usimamizi wa mafao ya watumishi wastaafu wa sekta ya umma na binafsi” Mhe. Mkuchika alisema.

    Mhe. Mkuchika alisisitiza kuwa, Serikali imedhamiria kutatua changamoto ya kucheleweshwa kwa mafao ya wastaafu, hivyo, haitakuwa tayari kumvumilia mdau yeyote atakayezembea kuwahudumia wastaafu.

    Aidha, Mhe. Mkuchika aliwataka watumishi wa umma wanaotara-jia kustaafu kutoa taarifa kwa waajiri wao kuhusu nia yao ya kustaafu angalau miezi 6 kabla ya tarehe ya kustaafu ili kum-wezesha mwajiri kuandaa utara-tibu wa mafao yao.

    Mhe. Mkuchika aliwasisitiza watumishi wa umma nchini, kila mmoja kwa nafasi yake kutimiza wajibu wake kikamilifu ili kuon-doa kero kwa watumishi wasta-afu pindi wanapofuatilia mafao yao.

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mafao ya wastaafu katika ukumbi wa Habari wa Bunge jijini Dodoma.

    Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utu-mishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) katika ukumbi wa Habari wa Bunge jijini Dodoma.

    14

  • Watumishi wa umma watakiwa kuzingatia kwa vitendo tamko la ahadi ya uadilifu ili kutekeleza majukumu yao kikamilifu

    atumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi

    wa Umma, Ofisi ya Rais-Utumishi na

    Utawala Bora wametakiwa kuwa-jibika kikamilifu kwa kuzingatia maadili ya utendaji kazi kwa mujibu wa tamko la kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma walilolitoa ili kutii takwa la kisheria.

    Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Bw. Mathew Kirama wakati akiendesha zoezi la kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa Idara yake.

    Bw. Kirama alisema, mtumishi wa umma anao wajibu wa kutoa tamko la ahadi ya uadilifu ili kuonyesha utayari wa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Kanuni, Sheria, Taratibu na Mion-gozo iliyopo katika Utumishi wa Umma.

    Bw. Kirama alifafanua kuwa, Mkuu wa Utumishi wa Umma kupitia Waraka Na. 2 wa mwaka 2015, anamtaka kila mtumishi wa umma kutoa ahadi ya uadilifu ili kuonyesha ni kwa kiasi gani mtu-mishi huyo yuko tayari kuwa-jibika na kutoa huduma kwa wadau kwa kuzingatia maadili ya utendaji kazi katika utumishi wa umma.

    Watumishi wa umma mnatakiwa kutoa huduma bora kwa kuzingati weledi, uaminifu kwa serikali na wananchi kwa ujumla na mki-fanya hivyo mtaendelea kujenga taswira nzuri ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

    Nao watumishi waliotoa Tamko la Ahadi ya Uadilifu, waliahidi kutoa huduma bora kwa usawa kwa watu wote na kutofanya ubaguzi kwa misingi ya dini, siasa, kabila, udugu, ukanda, jinsia, urafiki au hali ya mtu na kuhudumia umma na watumishi wen-gine kwa heshima.

    Aidha, watumishi hao waliahidi kuwa waza-lendo kwa nchi yao na kuwa watiifu kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanza-nia ikiwa ni pamoja na kulinda na kutumia rasilimali za umma kwa manufaa ya umma.

    Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Watumi-shi wa Umma ni la kisheria na linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na.

    8 ya mwaka 2002, Kanuni za Utu-mishi wa Umma za mwaka 2003 na Kanuni za Maadili ya Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma za

    mwaka 2005.

    Watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora wakitoa Tamko la Ahadi ya Uadilifu mbele ya Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Bw. Mathew Kirama.

    Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Bw. Mathew Kirama akimkabidhi Afisa Utumishi Mkuu Bi. Felister Shuli, nakala ya Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa Umma, baada ya Mtumishi huyo kutoa Tamko la Kiapo cha Uadilifu.

    15

  • “Ni jukumu la mwajiri kumsaidia mstaafu kukamilisha taratibu za kufuatilia mafao yake badala ya kumuacha akihangaika

    bila usaidizi wowote mkumbuke kuwa wengi wa wastaafu hao wanatoka maeneo ya mbali” Mhe. George Mkuchika

    publicservicemanagement.blogspot.com

    https://www.facebook.com/utumishiweek

    https://twitter.com/utumishiweek?lang=en

    O�si ya Rais Utumishi