ercec.sc.keercec.sc.ke/.../f4/sarufi-na-matumizi-ya-lugha-f1-4.docx · web viewbaada ya kutaja jina...
Post on 20-Oct-2020
8 Views
Preview:
TRANSCRIPT
SARUFI
NOMINO
Nomino ni maneno yanayotumiwa kutajia mtu, kitu, hali au mahali maalum. Inafahamika kuwa kuna aina sita za nomino mathalan;
AINA ZA NOMINO
(a) Nomino za pekee
Hizi ni nomino ambazo huanza kwa herufi kubwa. Hasa hutaja vitu mahsusi kama vile, milima, nchi, watu, mito, maziwa n.k.
Mifano ya katika sentensi
i) MtoNzoiahufurika wakati wamasika.
ii) Fatuma ameenda sokoni sasa hivi.
iii) Nairobi ndio mji mkuu wa Kenya.
iv) Ziwa Bogoria hupatikana katika eneo la Bonde la Ufa
(b) Nomino za kawaida
Hizi ni nomino ambazo hazianzi kwa herufi kubwa ila tu zinapotumika mwanzoni mwa sentensi k.m.
i) Wanafunzi walishirikishwa kupanda miti mwaka huu.
ii) Wanaiunzi watazuru ikulu ya raisi hiyo kesho.
iii) Wananchi hupaswa kutii sheria za nchi kila mara.
(c) Nomini za dhania
Hizi ni nomino ambazo zinahusu vitu au mambo ya kufikirika tu pasi mguso wowote lakini matokeo yake ndio
huonekanak.m
i) Ukosefiiwachakulaulisababishamaala mengi nchini.
ii) UovualioutendaulMfanyalmfikishwakotini.
iii) Uhuni wake ulimfanyakuogopewa sana katika karia.
iv) Uvivu husababishawa na wanafunzi kufeli katika mitihani.
(d) Nomino za makundi/Jamii
Nomino hizi hasa huhusisha nomino zinazopatikana katika makundi
Mifano katika sentenzi
i) Kikosichamajeshi kilipelekwa mlima Elgon kulcabiliana na waasi.
ii) Zizi lang'ombe litajengwaupyabaadayakuharibiwanamafiariko.
iii) Moto uliwaka kwa kasi katika kichaka cha miti.
iv) Kambi ya wanajeshi ilivunj wa mlima Elgon baada ya kuwana waasi wote.
(e) Nomino za wingi
Hizi huwa ni nomino ambazo hupatikana tu katika wingi^na huwa haziwezi kuhesabika
Waziri aliwahakikishia wanafiinzi kuwa wakifanya vizuri katika mtihani ya kitaifa atawapa maziwa mengi
i) Nyumba ilipoanza kuvuja maji yalijaa chumbani.
(f) Nomino za kitenzi Una
Hizi ni nomino ambazo huundwa kutokana na vitenzi. Huundwa kwa kuambishwa. Kiambishi 'ku' kwenye mzizi kitenzi
Mifano katika sentensi
i) Kusoma kwake kuliwafurahisKa wasikilizaji.
ii) Mwanafunzi aliyependa kucheza darasani amefukunza ndakini.
iii) Wanafunziwalikasirishwanakuchekakwabawabu.
iii) KulimakwaBw.Bidii,kuliwafurahisha watalii
VITENZI
Vitenzi ni maneno yanayoeleza mambo yanayofanywa pia hujulikana kama kiarifa. k.m.
i) Mwanafunzi anacheza uwanjani.
ii) Baba anaandika vizuri
iii)Jumaa liadhibiwa sana na mwalimu.
AINA YA VITENZI
a) Vitenzi Halisi
Hivi ni vielezi ambavyo huelezea kuhusu mambo yanayotendwa. Hasa huwa na viambishi awali na tampmati. Viambishi vihi aghalabu huwakilisha nafsi, wakati, kitendwa lyambwa, mzizi na kimalizio, kwa mfano Anakimbia
A - nafsi
na - wakati
kimbi-mzizi
a - kimalizio
b) Vitenzi vikuu
Hivi ndivyo vitenzi ambavyo hubeba maana kuu ya kitendo pasi kuchukua viambishi awali natemati kama ilivyo"
katika vitenzi halisi.
Aghalabu vitenzi hivi hufungamanishwa na kiambishi cku'kwa mfano
Cheza Lima Ondoka
kula soma safiri
lia amka lala
piga
Mifano katika sentensi
i) Wanafunzi waliamua kusoma kwa bidii.
ii) Baba amehitimisha safari yake.
iii) Mtoto alitaka kula samaki jana jioni.
iv) Jua kali anapenda kuimba nyimbo za mapenzi.
c) Vitenzi visaidizi
Vitenzi hivi hujiri tu kwa kutumika painoja na vitenzi vikuu katika sentensi kwa vile vitenzi hivi haviwezi
kujisimamia huwa vinachukua viambishi awali na pia hutokea kabla ya vitenzi vikuu au vitenzi halisi. Kwa mfano;
i) Juma atakuwa akisoma kila asubuhi kabla ya kuelekea shuleni.
ii) Babu amekwenda kucheza bao.
iii) Wanafunzi wa shule yet hawajawahi kuzuru mbuga la wanvama pori.
Wanajeshi watu wanataka kununua vifaru vya kulinda usalama. ,
(d) Vitenzi Vishirikishi
Vitenzi hivi hasa huwa ni vya ainambili. Hasahutumiwakuashiriaishitighalaainati. Mathalanimaziagira, hulka,
Hali n.k.
Kwa mfano;
Vitenzi vishirikishi huwa ni vya ainambili;
a) WenzivishirikisMvikamMifo .
b) vitenzi vishirikishi vipungufii
a) Vitenzi vishirikishi vikamilifu
Katika aina hii ya vitenzi vishirikishi. Vitenzi hivi hasa huchukua viambishi vya wakati; uliopita-Li
timlifu - me
ujao - ta
na nafsi, Ni - Tu, U - M, a - wa
Matumizi katika sentensi
i) Nyanya hakumaliza kula mkate alionunuliwa na mjuukuu wake.
if) Hamisi hakwenda kwa mwalimu mkuu.
iii) Yohana hakufanya kazi ya mwalimu.
iv) Babaalikuwaanalima.
Zoezi
Tambua vitenzi vishirikishi vikamilifu katika sentensi zifuatazo
i) Amekwisha sema hayo mara nyingi.
ii) Baba amekwenda kuletwa.
iii) Atakuja kesho asubuhi.
iv) juma hakuweza kusafiri ulaya.
v) Yeye anataka kuimba leo.
b) Vitenzi vishirikishi vipungufu
Vitenzi hivi hujisimamiapasi kuchukua viambishi vyangeli nafsi au wakati, Kwa mfano; Ngali ii si tu
ndi . ngali japo
i) Katibu cha mwalimu kombo ndicho kizuri cha kudurusu
ii) Juma ndiye mtangazaji bora mwaka huu.
iii) Mwalimu wetu angali hajatuzwa zawadi.
iv) Nuru ya fasihi ni kitabu kizuri cha kudurusu.
v) Ogala si kocha mzuri kama Kimanzi.
e) Vitenzi Sambamba
Hivi ni vitenzi ambavyo hutumiwa viwili au zaidi kwa pamoj a iii kutoa maana moja kwa ukamftifb. Yamkini vitenzi visaidizi. Vitenzi hivi vyote vinapotumika huwa vimechukua viarnbishi vya wakati kwa mfano;
i) Wanafunzi waliweza kuona wanyamapori wengi.
ii) Hatujaenda kumwona mgonj wa hospitalini.
iii) Yusufu aliweza kuftindisha kabla ya kustaafu.
iv) Mama hai aenda kumtembelea tanRu atoke marekani.
v) Atapaswa kusoma makala hayo aliyoyandika. .
AINA ZA MANENO
Sentensi huwa zimeundwa kwa aina mbalimbali ya maneno. Maneno haya yote huwa yametengewa herufi maalum ill yaweze kutofautishwa. Maneno haya ni; , ^
Nomino - N
Kitenzi - T
Kiwakilishi- W
Kivumishi - V
Kielezi - E
Kiunganishi- U
Kihusishi - H
Kihisihi - I
Nomino –
Huwa ni jina litumiwalo kumtajamtu, kitu, jambo fulani, mahali fulani, vitu tofauti tofauti n.k. Kwa mfano; Juma, Nairobi, Mto Nzoia, Ijumaa, Krismasi, Agosti n.k.
Kitenzi - Ni neno linalotoa taarifa kuhusu kitendo kilichofanyika, Kwa mfano;
i) Timu va Harambee ililakiwa kwa shangwe.
ii) Sisi tunacheza mpira.
iii) Kijakazi alipika wali asubuhi
Kivumishi –
Huwa ni neno linalotoa habari zaidi kuhusu nomino. Neno hili hujiri baada ya nomino k.m.
i) Kijana yule ni mtundu sana.
ii) Wanaiunziwerevuwatafiizwakesho.
iii) Mwalimu mwenvewe ndive alivemfukuza.
iv) Wananchi wengi walimpigia kura.
Kiwakilishi (W)
Ni maneno au ni viambishi vibadala vya nomino ambavyo huchukua mahala pa nomino, kwa mfano;
i) Nytnvi mtafukuzwa nyumbani leo.
ii) Atawindawanyamamwituleo.
iii) Nani amecheka?
Kiunganishi (u)
Huunganisha hasa fungu la maneno au neno iii kuleta gezo mbalimbali katika sentensi. Kwa mfano; au, na, lakini, ilhali, fauka ya, licha ya, sembuze, ijapo, ijapokuwa n.k.
Kielezi (e)
Haya ni maneno ambayo hufafanua zaidi kuhusu vivumishi, vitenzi au vielezi virjgine, kwa mfano;
i) Baba alilima sanajana. –
ii) Rashidalituzwazawadinzuri.
iii) Magaidi walilipuliwavibaya.
Kihisishi/kishangao/kiingizi (I)
Haya ni maneno ambayo huonyesha mshutuko, kuduwaza au kustaajabu kuhusu ufldhuli au wema wa mja. Kwa mfano;
i) Lo! Sikujua kuwa jirani ni mwizi
ii) Masalaale! Nani yule?
iii) Ah! Wacha niondoke sasa hivi
Kihusishi (H)
Haya ni maneno yanayoonyesha uhusiano baina ya vitu mbali mbali.
Kwamfano:
i) Baba alitembea kando ya barabrara.
ii) Mama aliweka maziwa ndani ya kabati.
iii) Monika aliweka mzigo wake chini ya meza.
MATUMIZI YA LUGHA
Kiimbo
Jinsi sauti inavyopanda na kushuka mtu anapoongea.
Huibua maana halisi ya maneno yanayosemwa kama ifuatavyo:
Sentensi za taarifa
Mtoto anaandika barua.
Sentensi za maswali
Mtoto anaandika barua?
Sentensi za mshangao
Mtoto anaandika barua!
Sentensi za amri
Kachezeeni nje!
Sentensi za rai/ombi
Nisaidie/eni.
Zoezi
Eleza maana ya kiimbo kwa kutoa mifano.
Tambua sentensi zifuatazo ni za aina gani kutokana na kiimbo.
Watu wanakula nyoka?
Watu wanakula nyoka.
Watu wanakula nyoka.
Tafadhali nisaidie.
Silabi
Tamko moja katika neno/herufi moja au zaidi ambazo hutamkwa pamoja.
Miundo Miwili ya Silabi za Kiswahili
Silabi wazi
Huishia kwa irabu k.m. o-a, (I) i-ga (KI), mbu-zi (KKI) na u-ngwa (KKKI)
Silabi funge
Huishia kwa konsonanti k.m. m-tu (K)
Zoezi
Ukitoa mifano, fafanua miundo miwili ya silabi za Kiswahili.
Tenganisha silabi katika maneno yafuatayo:
inkisari
baiskeli.
Shadda/Mkazo
Mkazo unaowekwa kwenye silabi fulani ya neno ikiwa imetamkwa kwa msisitizo.
Alama ya ritifaa hutumiwa kutambulisha shadda.
Huwekwa kwenye silabi ya pili kutoka ya mwisho, kwenye vitenzi vishirikishi vya silabi moja au kubadilisha maana ya neno.
ka’lamu, I’mba, thu’mni, ‘leta, n.k.
Kitabu ‘ki mezani.
Bara’bara (njia), ba’rabara (sawasawa), wala’kini (lakini), wa’lakini (kasoro/dosari/ila)
Zoezi
Weka shada katika maneno haya:
imba
baba
Onyesha kwa kupiga mstari iliko shada katika maneno yafuatayo:
malaika
nge
Sauti za Kiswahili
Kuna makundi mawili ya sauti za kiswahili:
Irabu
Sauti ambazo hutamkwa kwa ulaini bila hewa kuzuiliwa katika ala za sauti.
Konsonanti
Sauti ambazo wakati wa kutamkwa hewa huzuiliwa katika ala za sauti.
Aina za Ala za Sauti
Ala tuli
Ambazo hazisogei mtu akitamka k.m. meno, ufizi, kaa kaa gumu, kaa kaa laini na koo/koromeo.
Ala sogezi
Ambazo husogea mtu akitamka k.m. midomo na ulimi.
Matamshi/Uainishaji wa Irabu
a ni ya katikati na chini kinywani na midomo ikiwa imeviringa.
e ni ya mbele na kati kinywani na midomo ikiwa imetandazwa.
i ni ya mbele na juu kinywani na midomo ikiwa imetandazwa.
o ni ya nyuma na kati kinywani na midomo ikiwa imeviringa.
u ni ya nyuma na juu kinywani na midomo ikiwa imeviringa.
Zoezi
Taja makundi mawili ya sauti za Kiswahili.
Yatofautishe makundi ya sauti za Kiswahili uliyotaja katika (a)
Toa mifano miwili miwili ya irabu ambazo hutamkwa:
midomo ikiwa imeviringa
midomo ikiwa imetandazwa
Eleza jinsi irabu /e/ inavyotamkwa.
Taja aina mbili za ala za kutamkia na utoe mfano mfano mmoja mmoja.
Matamshi/Uainishaji wa Konsonanti
MAHALI
AINA
MIDOMO
MDOMO
MENO
MENO
UFIZI
KAAKAA
GUMU
KAAKAA
LAINI
KOROMEO
VIPASUO (H)
(GH)
p
b
t
d
k
g
VIPASUO (GH)
KWAMIZO (H)
ch
j
NAZALI (GH)
(VING’ONG’O)
m
n
ny
ng'
VIKWAMIZO (H)
(VIKWARUZO)(GH)
f
v
th
dh
s
z
sh
gh
h
KITAMBAZA
l
KIMADENDE
r
NUSU IRABU
VIYEYUSHO
w
y
Huainishwa kulingana na inapotamkiwa, kuwepo au kutokuwepo kwa mtetemeko katika nyuzi za sauti na jinsi hewa inavyozuiliwa katika ala k.m. /p/ ni ya midomo, kipasuo na sighuna.
Vipasuo
Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa, huzuiliwa kabisa na kuachiliwa kwa ghafla na mpasuko mdogo kutokea.
Vikwamizo/Vikwaruzo
Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa hupitishwa katikati ya ala kwa kukwamizwa.
Vipasuo kwamizo/kwaruzo
Konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa nje kwa nguvu, huzuiliwa kabisa halafu mwanya mdogo huachwa hewa ipite kwa kukwamizwa.
Nazali/Ving’ong’o
Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa kuna kiasi cha hewa huachiliwa na kupitia puani
Kitambaza
Konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa kwa nguvu, kuzuiliwa na kuachiliwa ipite kando ya ulimi
Kimadende
Konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa, kuzuiliwa na kuachiliwa na kusababisha ncha ya ulimi kupigapiga ufizi mfululizo.
Nusu irabu/Viyeyusho
Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa hupitishwa katikati ya ala kwa ulaini kama katika utamkaji wa irabu.
Zoezi
Tambua kikwamizo cha kaakaa laini na kiyeyusho cha midomo.
Tambua konsonanti ambazo si za orodha hii na ueleze kwa nini: /m/, /n/, /ny/,/ng’/, /f/, /b/
Tofautisha konsonanti /p/ na /dh/.
Taja konsonanti mbilimbili ambazo hujulikana kama:
viyeyusho
vikwaruzo
Aina za Maneno
Nomino (N)
Neno linalotaja kiumbe, kitu, hali, mahali, tendo, dhana, n.k.
Aina
Nomino za Pekee
Ambazo hutaja kitu kwa kutumia jina lake/ambazo hutambulisha upekee wa kitu hicho.
Mwanzoni huandikwa kwa herufi kubwa.
majina ya watu k.m. Kamau
mahali k.m. Mombasa
siku k.m. Alhamisi
miezi k.m. Disemba
miaka k.m. 1930
milima k.m. Kilimanjaro
Mito k.m. Tana
maziwa k.m. Victoria
bahari k.m. Hindi
Mabara k.m. Africa
Nomono za Kawaida/Jumla
Majina ya jumla ya viumbe/vitu vinavyoonyesha umbile la jinsi moja k.m. mtu, gari, kalamu, n.k.
Nomino za Jamii
Majina ya makundi ya viumbe au vitu k.m. bunge, jamii, halaiki, bunda n.k.
Nomino za Wingi
Majina ya vitu vitokeavyo kwa wingi japo kimsingi hazina umoja au wingi k.m. maji, mate, maziwa, mahubiri, marashi, mchanga, ngeu, poda, unga, n.k.
Nomino za Dhahania
Majina ya viumbe au mambo ya kudhani/yasiyoweza kugusika k.m. k.m ujinga, werevu, malaika, shetani, amani, imani, roho, wazo, dhana, n.k.
Nomino za Vitenzi Jina
Vitenzi vyenye kiambishi awali ku ambavyo huweza pia kutumika kama nomino k.m. Kucheza kwake kunaudhi.
Zoezi
Sahihisha jedwali lifuatalo
nomino
aina
Juma
kisu
maziwa
bunda
amani
kuomba
wingi
dhahania
pekee
kitenzi jina
kawaida/jumla
wingi
Bainisha nomino katika sentensi ifuatayo
Kuendesha baiskeli kwa kasi kulimfanya Hasani aangushe bunda la noti alilokuwa anaenda kununulia mchanga.
Sentensi ya Kiswahili
Sentensi ni fungu la maneno linalojitosheleza kimaana linalotumiwa katika mawasiliano.
Sifa
Huwa na ujumbe uliokamilika.
Huwa na mpangilio maalum wa maneno.
Huwa na muundo wa kiima na kiarifu.
Aina
Sentensi Sahili
Sentensi rahisi au nyepesi.
Sifa
Huwa fupi.
Huwa na kitenzi kimoja pekee.
Huwasilisha dhana moja.
Yaweza kuwa ya neno moja au zaidi.
Yaweza kuwa na kiima kilichododoshwa.
Wataenda.
Watoto wawili wanaelekea uwanjani.
Gachiku ni msichana mtiifu.
Sentensi Ambatano
Inayoundwa kwa kuunganisha sentensi sahili mbili.
Sifa
Huwa na vishazi huru viwili.
Huwa na kiunganishi.
Huwa na vitenzi viwili au zaidi.
Hutoa zaidi ya wazo moja.
Yaweza kuwa na viima vilivyododoshwa.
Mwanafunzi alipita mtihani ingawa hakuwa anasoma kwa bidii.
Maria aliendelea kupika kwa utaratibu huku akiimba wimbo.
Sentensi Changamano
Ambayo huwa na kishazi tegemezi kilichochopekwa ndani.
Sifa
Huwa na kishazi tegemezi chenye kitenzi kinachovumisha nomino kwa kuirejelea.
Huwa na kishazi huru kimoja au zaidi.
Huwa na virejeshi (amba na O) au –enye.
Tunda alilonunua jana limeoza.
Mwizi aliiba pesa zilizokuwa kabatini.
Kundi Nomino (KN) na Kundi Tenzi (KT)
Kundi Nomino ni sehemu katika sentensi inayoarifu kuhusu nomino na hutokea mwanzoni mwa sentensi.
Kundi tenzi ni sehemu katika sentensi inayoarifu kuhusu kitenzi na hutokea mwishoni mwa sentensi.
Virai
Vikundi vya maneno vitumiwavyo na binadamu visivyo na maana kamili.
Tungo zinayoundwa kwa maneno aghalabu mawili au zaidi yanayoashiria kitu kimoja na inayojengwa juu ya neno kuu.
Aina
Kirai Nomino (Kn)
Kirai Kitenzi
T
T+E
T+N
T+N+T
TS+T
t+N
t+V+E
Kirai Kivumishi(Kv)
V+E
V+U+V+E
V+V+U+V+E
V+N+V+E
Kirai kielezi (Ke)/Chagizo
E
E+E
E+E+E…
Kirai Kihusishi (Kh)
H+N
H+N+V
H+N+V+E
Zoezi
Bainisha virai katika sentensi ifuatayo
Mzazi na watoto wawili werevu sana waliwasili shuleni leo asubuhi kabla ya mwalimu.
Vishazi
Kundi la maneno lenye kiima na kiarifu likiwa ndani ya sentensi kuu.
Aina
Vishazi Huru
Vifungu vya maneno katika sentensi ambavyo hutoa maana kamili.
Vishazi Tegemezi
Vifungu vya maneno katika sentensi ambavyo havitoi maana kamili.
Aina
Vishazi tegemezi vya viunganishi k.m. Alimwadhibu ingawa hakuwa na makosa.
Vishazi tegemezi vya virejeshi k.m. Polisi walimpata mtoto aliyekuwa amepotea.
Vishazi Viambatani
Vinavyoundwa kwa vishazi huru viwili vikiwa vimeunganishwa k.m. Baba analala na mama anapika.
Zoezi
Bainisha Vishazi Katika Sentensi Zifuatazo
Mwalimu amewasili.
Amina ambaye ni daktari atakuja.
Ametajirika japo hakupata elimu.
Mwalimu anafundisha na wanafunzi wanaandika.
Tumeanzisha shirika ili tunyanyue hali zetu.
Unaweza kuamua kunyamaza au kujitetea.
Shamirisho/Yambwa
Aina
Shamirisho Kipozi/Yambwa Tendwa
Nomino inayoathiriwa na kitenzi.
Shamirisho Kitondo/Yambwa Tendewa
Nomino inayotendewa kitendo.
Shamirisho Ala/Yambwa Kitumizi
Chombo kinatumiwa kufanyia kitendo fulani.
Mifano
Mama alimpikia baba chakula kwa sufuria.
Baba alipikiwa chakula na mama kwa sufuria.
Sufuria ilitumiwa na mama kumpikia baba chakula.
Chakula (Shamirisho Kipozi/Yambwa Tendwa)
Baba (Shamirisho Kitondo/Yambwa atendewa)
Sufuria (Shamirisho Ala/Yambwa Kitumizi)
Ngeli za Nomino
Makundi ya nomino katika lugha ya Kiswahili yenye sifa zinazofanana kisarufi.
A-WA
Huwa na majina ya watu, vilema, viumbe, vyeo na viumbe vya kiroho, n.k.
Huchukua miundo kama vile M-WA, M-MI, KI-VI, n.k.
mtu-watu,
mkulima-wakulima
mtume-mitume
mkizi-mikizi
kiwete-viwete
kibyongo-vibyongo
nabii-manabii
kuku-kuku
Waziri-Mawaziri
U-I
Huwa na majina ya mimea, sehemu za mwili, vifaa, matendo, maumbile, n.k.
Huchukua muundo wa M-MI.
Mchungwa-michungwa
Mkoko-mikoko
mkono-mikono
mfupa-mifupa
msumari-misumari
mgomo-migomo
mwendo-myendo
msukosuko-misukosuko
mlima-milima
mwamba-myamba
U-YA
Huwa na majina ya hali, matendo, n.k.
Huchukua muundo wa U-MA.
Ugonjwa-magonjwa
upana-mapana
uasi-maasi
uchungu-machungu
ulezi-malezi
uovu-maovu
uhusiano-mahusiano
YA-YA
Huchukua muundo wa MA-MA.
Huwa na nomino zipatikanazo kwa wingi.
Hazibadiliki katika umoja na wingi.
manukato
mauti
maziwa
marashi
mahubiri
majira
maradhi
maafa
mazingira
KI-VI
Ni majina ya vifaa, sehemu za mwili, vitu, udogo, lugha, n.k.
Huchukua miundo KI-VI na CH-VY.
kisu-visu
kitabu-vitabu
chakula-vyakula
chanda-vyanda
kijitu-vijitu
kigombe-vigombe
kiguu-viguu
kidovu-vidovu
LI-YA
Huwa na majina ya sehemu za mwili, dhana, vifaa, ukubwa, n.k.
Huchukua muundo wa JI-MA, JI-ME, JA-MA, JE-MA n.k.
jicho-macho
jina-majina
jitu-majitu
goma-magoma
jambo-mambo
janga-majanga
jembe-majembe
jeneza-majeneza
wazo-mawazo
tunda-matunda
jua-majua
ziwa-maziwa
ua-maua
I-I
Huwa na nomino dhahania na vitu visivyoweza kuhesabika.
Hazibadiliki katika umoja na wingi.
sukari
amani
chai
mvua
Imani
chumvi
subira
imani
amani
furaha
I-ZI
Huhusisha nomino dhahania na vitu.
Hazibadiliki katika umoja na wingi.
nyumba
baiskeli
karatasi
redio
meza
dini
dawa
ndizi
jozi
U-ZI
Huchukua miundo W-NY, U-NY, U-F, n.k.
wayo-nyayo
wakati-nyakati
uso-nyuso
ufa-nyufa
ufunguo-funguo
ufagio-fagio
wembe-nyembe
uwanja-nyanja
ujumbe-jumbe
ukoo-koo
waraka-nyaraka
waya-nyaya
U-U
Huwa na nomino za dhahania na vitu visivyoweza kuhesabika.
Hazibadiliki kimaumbo.
Huchukua U au W.
Ujinga
Ulafi
Ulaji
Werevu
Unga
Uji
Ugali
udongo
KU
Nomino zinazoundwa kutokana na vitenzi k.m. kuomba kwake kumemsaidia.
PAKUMU
Ngeli ya mahali.
Huwa na nomino moja ‘mahali’.
PA (mahali karibu au panapodhihirika) k.m. Kitabu kipo pale.
KU (mahali mbali au kusikodhihirika) k.m. Mahali kule kunafaa.
MU (ndani ya) k.m. Mahali mle mna siafu.
Zoezi
Tunga sentensi ukitumia nomino kutoka katika ngeli ya U-ZI.
Andika kwa wingi. Makaribisho aliyopewa yalimfurahisha.
Andika katika ukubwa wingi: Paka mweupe amenaswa mguuni.
Andika katika wingi wa hali ya udogo: Mtu aliumwa na mbwa.
Huku ukitoa mifano, fafanua miundo mitatu ya majina katika ngeli ya LI-YA.
Tambua ngeli/viwakilishi ngeli vya nomino zifuatazo:
chakula
shairi
mtwana
Uundaji wa maneno
Nomino kutokana na mzizi wa kitenzi
danganya-kudanganya, mdanganyifu,udanganyifu
soma-kusoma, masomo,msomi,usomaji
unda-kuunda, muundaji,uundaji,muundo
funika-kufunika, kifuniko, mfunikaji, ufunikaji
Kitenzi kutokana na mzizi wa nomino
mlo-kula
mlevi-kulewa, kulevuka
mwimbaji-kuimba
fikra-kufikiri
malezi-kulea
fumbo-kufumba, kufumbua
Nomino kutokana na mzizi wa nomino
mwimbaji-kuimba, wimbo, uimbaji, kiimbo
mchezo-kucheza, uchezaji, mchezaji
ulaghai-kulaghai, mlaghai
hesabu-kuhesabu,uhesabu
mdhalimu- kudhulumu, dhuluma, udhalimu
Nomino kutokana na mzizi wa kivumishi
-refu-mrefu, urefu, urefushaji
-baya-mbaya, ubaya
-zuri-mzuri, uzuri
-kali-mkali, ukali
-eupe-mweupe,weupe
Kivumishi kutokana na mzizi wa nomino
ujinga -jinga
werevu -erevu
mzuri -zuri
mpumbavu -pumbavu
mpyoro -pyoro
Kitenzi kutokana na mzizi wa kivumishi
haramu-kuharamisha, kuharamika
halali-kuhalalisha, kuhalalika
-fupi-kufupisha, kufupika
bora-kuboresha, kuboreka
-refu-kurefusha, kurefuka
sahihi-kusahihisha, kusahihika
-sikivu-kusikia
-danganyifu-kudanganya
Kivumishi kutokana na mzizi wa kitenzi
dunisha - duni
Haramisha - haramu
fupisha -fupi
sahilisha -sahili
tukuka -tukufu
fahamu -fahamivu
teua -teule
nyamaza -nyamavu
ongoka -ongofu
sahihisha -sahihi
danganya -danganyifu
Kitenzi kutokana na kielezi
haraka-harakisha
zaidi-zidisha
bidii-bidiisha
hima-himiza
Zoezi
Unda neno ulilopewa katika mabano kutokana na maneno yafuatayo:
zingatia (kivumishi)
sahili (kitenzi)
taliki (nomino)
Unda nomino kutokana na mizizi ya maneno yafuatayo kisha utunge sentensi.
-kali
lia
Vitenzi
Kitenzi ni neno linaloeleza kuhusu jambo linalofanywa.
Aina za Vitenzi
Kitenzi halisi
Kinachofahamisha tendo halisi.
Hutokea peke yake k.m. Boke anacheza mpira.
Kitenzi kikuu (T)
Kinachoeleza tendo kuu katika sentensi.
Hutokea pamoja na kitenzi kisaidizi k.m. Baba anataka kulala.
Kitenzi Kisaidizi (Ts)
Kinachosaidia kitenzi kikuu
Maneno yanayoweza kutumiwa kama vitenzi visaidizi
ngali
kuwa
taka
pasa
bidi
huenda
kuja
weza
kwisha
stahili
wahi
maliza
Vitenzi Sambamba
Vinavyofuatana moja kwa moja/vinavyotokea kwa mfululizo.
Hutumika kutoa maelezo kuhusu tendo moja maalum kwa uwazi zaidi.
Wachezaji huenda wanaweza kushinda mchezo wa leo.
Vitenzi Vishirikishi (t)
Vinavyoshirikisha vitu kihali, kitabia au kimazingira.
Aina
Vitenzi Vishirikishi Vikamilifu
Ambavyo huchukua viambishi.
Mama alikuwa mgonjwa/jikoni/muuguzi.
Aisha angali kitandani/mkaidi/ mwanafunzi.
Vitenzi Vishirikishi Vipunguvu
Ambavyo havichukui viambishi
kuyakinisha
kukanusha
ni/niko
ndiko
yuko
li/liko
si/siko
siko
hayuko
hali/haliko
Viwakilishi (W) na Vivumishi (V)
Viwakilishi ni viambishi au maneno yanayotumiwa badala ya nomino.
Vivumishi ni maneno yanayotoa habari zaidi kuhusu nomino.
VIVUMISHI
VIWAKILISHI
Viulizi
Viulizi
Maneno ya kuulizia.
Mizizi ni –pi, -ngapi na gani.
Amechukua kitabu kipi?(V. kiulizi)
Kipi kimepotea? (W. Kiulizi)
Amenunuliwa mangapi?
Gani imefungwa?
a-unganifu
a-unganifu
Maneno yanayoundwa kwa viwakilishi ngeli na kiishio a.
Hutoa maana ya umilikaji
Mtoto wa shangazi amelala. (V. a-unganifu)
Wa Juma analia. (W. a-unganifu)
Cha mlevi huliwa na mgema.
Vimilikishi
Vimilikishi
Hutoa maana ya umilikaji.
Mizizi
nafsi
kuyakinisha
kukanusha
1
2
3
-angu
-ako
-ake
-etu
-enu
-ao
Kiatu changu kimepotea. (V. kimilikishi).
Usichukue chake. (W. kimilikishi)
Sifa
Sifa
Maneno ya kusifu au kueleza jinsi nomino ilivyo k.m. -fupi, -baya, -kali, -dogo, n.k.
Mti mrefu umeanguka. (V. sifa)
Alichukua cheupe. (W. Sifa)
Vionyeshi/viashiria
Vionyeshi/viashiria
Maneno ya kuonyesha nomino ilipo.
Huwa za karibu, wastani na mbali k.m. hili, hilo, lile.
Kiatu hiki kimechafuka. (V. kionyeshi/kiashiria)
Hii ni ya nani? (W. kionyeshi/kiashiria)
Viashiria visisitizi
Viashiria visisitizi
Maneno ya kutilia mkazo nomino yakizingatia ilipo.
Huwa ya karibu, wastani na mbali.
Huundwa kwa kutumia kiwakilishi ngeli katika kionyeshi cha kwanza k.m. kiki hiki-vivi-hivi, lili hili-yaya haya, n.k.
Chumvi ii hii ilimwagika. (V. kisisitizi)
Kuku huku ndiko kulinyesha. (W. kisisitizi)
Virejeshi
Virejeshi
Hurejelea nomino au kukumbusha kuihusu.
Huwa amba- na -o- rejeshi.
Mtoto ambaye analala ni wake.
Watoto wanaolala ni wao. (V. kirejeshi)
Mnyama ambaye huwindwa ni nguruwe.
Mnyama awindwaye ni nguruwe.
Ambaye aliniibia ninamjua.
Aliyeniibia ninamjua.
Ambaye hula nyasi ni ng’ombe.
Alaye nyasi ni ng’ombe.
Idadi
idadi
Hutaja idadi ya nomino
Aina
Idadi halisi (iliyo dhahiri) k.m. -moja, sita, n.k.
Idadi ya jumla (isiyo dhahiri) k.m. -chache, -kadha –ingi, n.k.
Mwalimu mmoja na wanafunzi sita wameenda. (V-idadi halisi)
Vitabu vichache vimechukuliwa na watoto kadha. (V. idadi ya jumla)
Nipe kumi na kimoja. (V. idadi halisi).
Amechukua machache tu. (V. idadi ya jumla)
Pekee
Pekee
Hutoa taarifa zaidi kuhusu nomino kwa njia ya pekee.
–enye (umilikaji)
Msichana mwenye maringo ni yule. (V. Pekee)
–enyewe (halisi au kusisitiza)
Barua yenyewe niliipeleka posta.
–ote (bila kubakisha)
Chakula chote kimeliwa.
-o-ote (bila kubagua)
Mtu yeyote anaweza kuugua.
-ingine (sehemu ya baadhi ya vitu)
Mikufu mingine imeibwa.
-ingine-o (mbali na/zaidi ya)
Nyuzi nyinginezo zilikatika.
Mwenye macho haambiwi tazama. (W.pekee)
Yenyewe yaliiva jana.
Kiliharibika chote.
Popote paliposafishwa pamechafuka.
Ametorokea kwingine.
Nyingineyo niliweka katika chakula.
Nomino/majina
W
Nomino/majina ambayo hutumika kama vivumishi
Mtu mzee hutembea kwa mkongojo. (V. jina/nomino)
W
Ngeli
Viwakilishi ngeli ambavyo huwakilisha nomino k.m. Liliiva jana-Yaliiva jana.
W
Nafsi
Maneno au viambishi vinavyotajia nafsi.
Aina
Nafsi huru
Maneno ya kutajia nafsi.
nafsi
umoja
wingi
1
2
3
Mimi
Wewe
yeye
Sisi
Nyinyi
wao
Yeye ni mtiifu. (W. nafsi huru)
Nafsi tegemezi/viambata
Viambishi ambavyo hutaja nafsi.
nafsi
umoja
wingi
1
2
3
ni
u
a
tu
m
wa
Walisahau kumwambia. (W. nafsi tegemezi)
Vielezi (E)
Viambishi au maneno yanayoeleza zaidi kuhusu kivumishi, kitenzi au kielezi kingine.
Yeye ni mweupe sana/ajabu/kwelikweli/kupindukia/pepepe.
Alikula pole pole sana.
Aina
Vielezi vya Namna/Jinsi
Ambavyo hueleza vile jambo lilifanyika.
Aina
Vielezi namna mfanano
Vinavyoeleza vile jambo lilifanyika kwa kufananisha na nomino au vivumishi.
Huchukua viambishi KI na VI.
Anakula kifisi.
Tulifanya kazi vizuri.
Vielezi namna viigizi
Maneno ambayo kiasili ni vielezi k.m. sana, haraka, ghafla, mno, kabisa, pole, barabara n.k.
Mwenda pole hajikwai.
Vielezi namna hali
Hueleza hali ya tendo.
Alilelewa kwa shida.
Alilewa chakari
Vielezi namna vikariri
Huelezea vile jambo lilifanyika kwa kurudiwarudiwa
Alinijibu kimzahamzaha.
Tembea polepole.
Yeye hufanya kazi yake hivi hivi/ovyo ovyo
Mbwa alibweka bwe! Bwe! Bwe!
Vielezi namna ala
Walimpiga Stephano mawe/kwa mawe.
Vielezi Namna Viigizi
Hueleza vile kitendo kilitendeka kwa kutumia tanakali.
Mbuni alianguka majini chubwi!
Vielezi vya Idadi/Kiasi
Maneno ambayo hutaja kitendo kimetendeka mara ngapi.
Aina
Vielezi vya idadi halisi
Tulivamiwa mara moja.
Vielezi vya idadi ya jumla
Alitoroka mara kadha/nyingi/chache.
Vielezi vya mahali
Hutaja mahali kitendo kilitendekea.
Aina
Vielezi vya mahali vya maneno kamili
Ndege ilipofika Nairobi, ilitua chini.
Vielezi vya mahali vya aina ya viambishi
Ni viambishi po, ko, mo na ni.
Alipolala palikuwa na siafu.
Wanacheza uwanjani.
Vielezi vya wakati
Hutaja kitendo kililifanyika wakati gani.
Aina
Vielezi vya wakati vya maneno kamili
Rais atawasili kesho/mwaka ujao.
Kielezi cha wakati cha kiambishi (po ya wakati)
Nililala nilipofika nyumbani
Viunganishi (U)
Neno au fungu la maneno la kuunganishia.
Aina
Vya kujumuisha pamoja
na
aidha (pia)
isitoshe
kadhalika (pia))
tena
mbali na
fauka ya (zaidi ya)
Vya kukatiza ili kupambanua
walakini (lakini)
bali (lakini)
ijapokuwa (hata kama)
ingawa (hata kama)
Vya kuonyesha kinyume cha mambo
ilhali
licha ya
Kuonyesha masharti
budi (lazima)
lazima
sharti
ikiwa (kama)
bidi
Vya sababu
kwa
kwa sababu
maadamu (kwa kuwa)
madhali (kwa kuwa)
kwa vile/maana
kwa ajili/minajili ya
mintaarafu (kutokana na)
Vya kuonyesha Chaguo
au
ama
wala
Viunganishi vingine na maana zake
ila (isipokuwa)
laiti (kama)
lau (kama)
mradi (bora)
angalau (bora zaidi)
bighairi (bila ya kujali) k.m.Minghairi vitu vilivyo kwenye kabati vinginevyo unaweza kuvichukua.
seuze/sembuse (kulinganisha ili kuonyesha tofauti)
labda (pengine)
Vihusishi (H)
Maneno yanayoonyesha uhusiano.
Aina
Mahali
juu ya, miongoni mwa, katika, mpaka, hadi
Wakati
kabla ya, baada ya, tangu, hadi, mpaka
Sababu
kwa, kwani, kwa sababu, mintaarafu ya
Ala
Alimkata kwa kisu.
A-unganifu
Simu ya rununu inalia.
Jumba la mikutano limeandaliwa.
Kiatu cha ngozi hudumu.
Kikome cha plastiki ni duni.
Ulinganisho
Zaidi ya, kuliko, kuzidi, kushinda.
Kiwango
Zaidi ya, kati ya, takriban, karibu
Vya hali
Mithili ya, kwa niaba ya
Vihisishi (I)
Maneno yanayotoa hisia za moyoni.
furaha
Hoyee! Haleluya! Alhamdulilahi!
hasira
Kefle! Ah! He!
majuto
Kumbe! Jamani! Ole wangu! Laiti
huzuni/huruma
Pole! Ole! Maskini!
kuitikia
Bee! Labela! Naam! Ehee! Ahaa!
mshangao/mshtuko
Eti! Salaale! Ajabu! Msalia mtume! Lahaula!
kubeza
Mawe! Ngo! Mmm! Mwangalie!
kusisitiza
Hata
kutakia heri
inshallah
Mwingiliano wa Maneno
Hali ya maneno kuwa na matumizi tofauti mifano:
W kuwa V
Huyu analia.
Mtoto huyu analia.
V kuwa W
Vikombe vizuri vitavunjika.
Vizuri vitaliwa.
V kuwa N
Mti mrefu haupandiki.
Mrefu alikufa jana jioni.
V kuwa E
Viatu vibaya vitachomwa.
Uliifanya kazi vibaya.
Mtu mjinga ni huyu.
Anaongea kijinga.
N kuwa V
Tajiri alimdharau Razaro.
Mtu tajiri huheshimiwa.
N kuwa E
Nairobi ni mji mkuu.
Amewasili Nairobi.
Kitoto kinalia.
Unaongea kitoto.
Haraka haina baraka.
Fanya haraka tuondoke hapa.
Sindano ya babu imepotea
Alidungwa sindano/kwa sindano na daktari.
E kuwa N
Niliwasili jana.
Jana yangu haikuwa nzuri.
T kuwa N
Nataka kulala sasa.
Kulala kwake kunaudhi.
N kuwa U
Ila yake imemwathiri sana.
Watu wote ila yeye walikwenda.
Kichwa changu kina walakini.
Nimekula walakini sijashiba.
E kuwa I
Mwenda pole hajikwai.
Pole! Usijali utapona.
Amepaka rangi sawasawa.
Sawasawa! Siku moja tutakutana.
H kuwa E
Paka amepanda juu ya mti.
Ameingia katika choo.
T kuwa E
Mtoto akilia atatapika.
Aliingia akilia.
N kuwa I
Gege anacheza ala yake ya muziki.
Ala! Waniwekea uchafu katika chakula?
Mofimu
Kipashio kidogo zaidi katika lugha kisichoweza kuvunjwavunjwa zaidi bila kupoteza maana yake.
Aina
Mofimu huru
Neno lisiloweza kugawanywa katika vipande mbalimbali na linalojisimamia na kuwa na maana kamili.
Kuku, baba, mama, sana, labda, jana n.k.
Mofimu tegemezi
Isiyoweza kujisimamia na kujitosheleza kisarufi, mifano:
Mzizi (Sehemu ya neno inayobeba maana kuu na isiyoweza kubadilishwa)
m-tu, samahe-k-a, n.k.
Nafsi
Tumesahau
Ngeli
Lilianguka.
Yalianguka.
Kikanushi
Sikumpiga
Halijaoza.
Huli.
Njeo/wakati
Liliiva.
Analia.
Tutaimba.
Alipoenda.
Hali
Me, nge, ngali, hu, ki, ka, n.k.
Mahali
Alipoingia.
Alikoingia.
Alimoingia.
Virejeshi
Lililonunuliwa.
Alijikata.
Mtendwa/watendwa/kitendwa/vitendwa/shamirisho
Alichikichukua.
Kilichowaua.
Mnyambuliko/kauli
Alimpigia.
Alimlilia
Alinikosea.
Alimtolea.
Kiishio
a, e, i, u
Viambishi
Viungo vyenye maana vinavyofungamanishwa na mziziwa neno ili kulipa maana mbalimbali.
Aina
Viambishi Awali
Ambavyo hutokea kabla ya mzizi.
A-li-ye-ku-kata-a
Viambishi Tamati
Ambavyo hutokea baada ya mzizi k.m. ki-pig-ishw-a-cho
Mnyambuliko wa Vitenzi
Kunyambua kitenzi ni kukiongeza viambishi tamati ili kukipa maana tofauti.
Aina za minyambuliko/kauli za vitenzi
Kutenda
Hali ya kawaida ya kitenzi.
Kutendatenda
Hali ya kitenzi kurudiwa.
Kutendea
Kwa niaba ya
Badala ya
Sababu
Kuonyesha kitumizi
Mwendo wa kitu kuelekea kingine
Kutendwa
Huonyesha nomino iliyoathiriwa na kitenzi.
Kutendewa
Humaanisha kitendo kimetendwa na mtu badala au kwa niaba ya mtu mwingine.
Kutendana
Unamtenda mtu jambo naye anakutenda jambo lilo hilo.
Kutendeana
Unamtendea mtu jambo naye anakutendea jambo lilo hilo.
Kutendeka
Uwezekano wa kitendo kufanyika
Kutendesha
Mtu au kitu kusababisha kufanyika kwa kitendo.
Kutendeshea
Kusababisha kitendo kitendeke kwa niaba ya mwingine.
Kutendeshwa
Kusababishwa kufanya jambo.
Kutendeshewa
Mtu kusababishwa kitendo kitendeke kwa niaba yake.
Kutendeshana
Kusababisha kitendo kitendeke kwa mtu naye anasababisha kitendo kicho hicho kitendeke kwako.
Kutendesheana
Kusababisha kitendo kitendeke kwa niaba ya mtu naye anasababisha kitendo kicho hicho kitendeke kwa niaba yako.
Kutendesheka
Kitendo fulani kinaweza kusaababishwa.
Kutendama
Kuwa katika hali fulani bila ya mabadiliko.
lala-lalama
ficha-fichama
shika-shikama
ganda-gandama
chuta-chutama
funga-fungama
kwaa-kwama
unga-ungama
andaa-andama
saki-sakama
Kutendata
Hali ya mgusano au kushikanisha vitu viwili.
paka-pakata
fumba-fumbata
kokoa-kokota
okoa-okota
kama-kamata
Kutendua
Hali ya kiyume
choma-chomoa
funga-fungua
Kutenduka
Kuweza kufanyika kwa hali ya kinyume.
chomoka
funguka
Vinyume vya vitenzi
komea-komoa
bariki-laani
patana-kosana
angika-angua
mwaga-zoa
ziba-zibua
tatiza-tatua
funika-funua
tega-tegua
tawanya-kusanya
ugua-pona
nasa-nasua
kwamiza-kwamua
kosa-kosoa
pakia-pakua
twika-tua
paa-tua
cheka-lia
anika-anua
simama-keti
fukia-fukua
inama-inuka
funga-fungua
furahi-huzunika
kumbuka-sahau
oa-taliki
choka-pumzika
uliza- jibu
jenga-bomoa
ishi-kufa/hama
kufa-kufufuka/ishi
lewa-levuka
anza-maliza/isha
saza/bakiza-maliza
meza-tapika/tema
ingia-toka
dharau-heshimu
kweya-teremka
panda-shuka
sifu-kashifu
chimba-fukia
chafua-safisha
cheka-lia
panda-shuka
babaika-tulia
pokea-aga
zama-elea
vaa-vua
kitenzi
tendea
tendwa
tendewa
tendana
tendeka
tendeana
tendesha
tendeshea
tendesheka
cha
ogopa
chia
chwa
chiwa
chiana
chika
chiana
chisha
chishia
chishika
cha
pambazuka
chea
0
chewa
0
0
0
chesha
cheshea
chesheka
chwa
jua kuanza kutua
chwea
0
chwewa
chweka
0
0
chwesha
chweshea
chwesheka
fa
tokwa na uhai
fia
0
fiwa
fika
0
fiana
fisha
fishia
fishika
gwa
anguka
gwia
0
gwiwa
0
0
gwiana
gwisha
gwishia
gwishika
ja
sogea karibu
jia
0
jiwa
jika
0
jiana
jisha
jishia
jishika
la
tia chakula kinywani na kumeza
lia
liwa
liwa
lika
lana
liana
lisha
lishia
lishika
nya
enda haja kubwa
anguka matone
nyea
nyewa
nyewa
nyeka
0
nyeana
nyesha
nyeshea
nyesheka
nywa
tia kitu majimaji kinywani na kukimeza
nywea
nywewa
nywewa
nyweka
0
nyweana
nywesha
nyweshea
nywesheka
pa
kabidhi
pea
0
pewa
peka
pana
peana
pesha
peshea
pesheka
pwa
maji toka ufuoni hadi mbali ya bahari
pwea
0
pwewa
pweka
0
0
pwesha
pweshea
pwesheka
ta
taga
tia
o
tiwa
tika
0
0
tisha
tishia
tishika
wa
tokea
wia
0
wiwa
wika
wana
wiana
wisha
wishia
wishika
Matumizi ya Maneno na Viambishi Maalum
Maneno Maalum
ila
isipokuwa
Watu wote ila yeye wameenda.
kasoro
Hakuna kizuri kisicho na ila.
labda (pengine/shaka)
Haonekani siku hizi labda amepata uhamisho.
ikiwa
(kama/shaka)
Tutamkuta nyumbani ikiwa amepewa likizo.
masharti
Mgonjwa atapona ikiwa atakunywa dawa ipasavyo.
walakini
dosari
Ghorofa limebomolewa kwa sababu lilikuwa na walakini.
lakini/bali
Nimekula walakini sijashiba.
ingawa/ingawaje (hata kama)
Nilijilaza kitandani ingawa sikuwa na usingizi.
ijapokuwa/japo (hata kama)
Usicheze na nyoka ijapokuwa ni mdogo.
jinsi
njia/utaratibu wa kufanyia jambo
Sijui jinsi ugali unavyopikwa.
aina/namna/sampuli
Siwezi kula chakula jinsi hii.
kulingana na/kama
Alikuja jinsi alivyoniahidi.
kwa
mahali
Ameenda kwa Juma.
jinsi
Alisoma kwa bidii.
sehemu ya kitu kisima/akisami
Amepata alama moja kwa tano katika mtihani.
pamoja na
Harusi ilihudhuliwa na wazee kwa vijana na tulikula wali kwa nyama.
kuonyesha kitu kilitumiwa kama kifaa
Alikata mkate kwa kisu.
sababu
Aliugua kwa kunywa maji machafu.
kuunganisha vipashio viwili
Leo ndiwe utapika kwa hivyo tayarisha viazi.
muda/kipindi
Alilia kwa nusu sana.
kufanya jambo bila kupoteza wakati
Baada ya kula, tulienda moja kwa moja kulala.
kivumishi cha a-unganifu cha ngeli ya KU
Kucheka kwa Maria kunaudhi.
umiliki wa mahali
Twende nyumbani kwangu.
na
kiunganishi
Mama na baba wanalima.
umilikaji
Kamau ana kitabu kizuri.
wakati uliopo
Anaandika barua.
kauli/mnyambuliko
Kamau na Juma wanapigana.
kuonyesha tofauti
Kiatu hiki ni tofauti na kile.
mtenzi
Alipigwa na mwalimu.
kuonyesha ufupisho wa nafsi
Alisaidiwa nao.
Zoezi
Eleza matumizi ya na katika sentensi zifuatazo:
Baba na mama wanapigana kwani ana tabia ya kulewa.
Mtoto aliteswa na mama yake kwa kuwa tofauti na wengine nami kikamkanya.
wala (kukanusha)
Sikumtusi wala kumpiga.
Viambishi Maalum
me/ja (hali timilifu/kitendo kutendeka na si muda mrefu uliopia)
Mama amewasili.
Mama hajawasili.
hu
mazoea/jambo hutokea kila wakati
Yeye hulala mapema.
kikanushi
Hukutibiwa vizuri.
li
wakati uliopita
Alitupatia zawadi.
ngeli
Tunda limeiva.
kitenzi kishirikishi kipungufu
Jembe li ghalani.
ni
nafsi ya kwanza umoja
Niliwasili jana.
mahali
Twende kanisani.
kitenzi kishirikishi kipungufu
Yeye ni daktari.
wingi
Tokeni nje.
ndi- (kitenzi kishirikishi kipungufu)
Yeye ndiye aliniibia pesa.
ji
udogo
Kijitu kimeanguka.
ukubwa
Jibwa limebweka.
kirejeshi
Alijipalia makaa.
nafsi ya pili
Jichukulie upendacho.
kiambishi tamati cha kuunda nomino.
Mwimbaji alituzwa.
Ki
kitendo ki katika hali ya kuendelea
Tulikuwa tukila alipoingia.
masharti/kitendo kinategemea kingine
Utapita mtihani ukijitahidi.
udogo
Kitoto kinalia.
ngeli
Kitabu kimechukuliwa.
kitenzi kishirikishi kipungufu
chakula ki mezani.
kielezi namna mfanano.
Yeye hula kifisi.
kitendo hakifanyiki kamwe
Chai hii hainyweki.
ku
kikanushi cha wakati uliopita
Hakumpiga kwa jiwe.
nafsi ya pili umoja.
Alikupigia simu jana.
mahali
Huku kumesafishwa.
ngeli
Kuugua kumemnyenyekesha.
mwanzo wa kitenzi
Ameenda kusafisha nyumba.
ka
mfuatano wa matukio
Tulikula chakula, tukanywa chai kisha tukalala.
vichwa vya habari
Mwizi kapigwa mawe
kutoa amri
Kachezeeni nje!
kitendo fulani ni tokeo la kingine
Tulisoma kwa bidii tukapita mtihani.
kutoa nasaha/shauri
Kamwombe babako msamaha.
a
Hali isiyodhihirika ya wakati uliopo
Watoto wacheza uwanjani.
vichwa vya habari
Waziri aaibishwa na wananchi.
kitendo kinaendelea
Twaenda sokoni.
nafsi ya tatu umoja
Yeye aliudhika sana.
ngeli
Mbuzi yule atachinjwa kesho.
kiishio
Mtoto amekula vizuri.
nge/ngali (masharti yanayowezekana au yasiyowezekana)
Ningekuwa na pesa, ningenunua kiatu.
Laiti ningalijua nisingaliingia katika hilo basi.
po
wakati
maalum
Yeye anapolala hukoroma.
Wowote/mazoea
Mwalimu aingiapo wanafunzi husimama.
mahali
Paliposafishwa pamechafuka.
masharti
Mtoto aamkapo, mpe uji.
kikanushi cha ki ya masharti
Akila.-asipokula.
Viakifishi
Alama za usemi(“”)
Usemi halisi
“Njoo kesho,” mama akamwambia.
Lugha ngeni
“Ninunulie jarida la ‘Parents’”, babake akamwambia.
Vipindi, filamu, makala
“Vioja Mahakamani”
Semi
“kumwaga zigo”
Dukuduku (…)
maneno yameachwa ya kutangulia, kati au ya mwisho. Yaweza kuachwa kwa kuwa makali
Nyani haoni…
kukatizwa usemi/kauli
AMINA: Mama ni…
MAMA: Kwanza watoka wapi usiku huu?
maneno yanaendelea
Alimwambia ajihadhari anapovuka barabara…
Koma/mkato/kipumuo( , )
pumziko fupi katika senyensi
Tulipofika sokoni, tulinunua mboga.
kuorodhesha
Alinunua mboga, samaki, nyanya na viazi.
kuonyesha mwanzo au mwisho wa usemi halisi
“Njoo kesho,”mama akamwambia.
kuandika anwani
Shule ya upili Gatwe, S.L.P 160, Kerugoya.
baada ya kutaja jina la mtu anayepewa habari
Daktari, ningependa kukuona.
kutenganisha sentensi zenye masharti
Usipofanya kazi, usile.
kuandika tarehe
Alizaliwa mwezi wa Julai, tarehe 18, 1999.
kuandika tarakimu zinazozidi elfu
1,000, 13,000, n.k.
Ritifaa/kibainishi( ’ )
herufi imeachwa
wal’otutuma
shadda/mkazo
`iba, ka`lamu
katika sauti ya king’ong’o
Ng`ombe amekufa.
Kufupisha
Tu’shasafisha nguo.
katika kuandika miaka yenye namba izilizoachwa
`73-`99.
Mshazari/mkwaju(/)
Tarehe
Alizaliwa tarehe 5/6/1998.
kuonyesha kumbukumbu
KUMB 1/2009
kuonyesha visawe
Nenda katika shule/skuli.
Kuonyesha au
Wanawake/wanaume wataajiriwa.
Kistari kifupi( - )
kuandika tarehe
5/6/2006
kuonyesha silabi, viambishi au mofimu
sa-la-mu na imb-a.
kuonyesha neno linaendelea katika mstari unaofuata.
Usitenganishe sauti za silabi.
Kuonyesha mzizi wa neno
-ma,-bwa
kuonyesha kudumishwa kwa sauti
Lo-o-o-o!
Hadi/ kipindi cha tukio fulani
1999-2008.
Kutenganisha usemi na msemaji
Huo ni upumbavu-Kibaki
Kistari kirefu()
kutenganisha usemi na msemaji
kuonyesha mabadiliko ya ghafla
Wanafaunzi ni wajinga-samahani, simaanishi wote.
kutangulia maelezo ya ziada
Walisaidia nchi za Afrika Mashariki- Kenya, Uganda na Tanzania kwa msaada
Mstari( )
kusisitiza
Jibu maswali mawili pekee.
kuonyesha aina za maneno
Mtoto wangu analala (V. kimilikishi).
kuonyesha vitabu, majarida na magazeti
Chemchemi za Kiswahili, “True Love”, n.k.
kuandika anwani/kichwa
Mwanafunzi Adhibiwa/Kaadhibiwa Vikali
Kikomo/kitone/nukta (.)
mwishoni mwa sentensi.
kuandika tarehe
2.3.2013
kuonyesha ufupisho wa maneno
Dkt.,Bw.,Bi.,C.C.M
kuonyesha takwimu
4.5, 86.27, n.k.
kutenga shilingi na senti
6.50-shilingi sita na senti hamsini
juu ya herufi j na I
Nusu/semi koloni/nukta na kituo (:)
kugawa sentensi mbili zinazoweza kujisimamia bila ya viunganishi
Wasichana walifuata maagizo waliyopewa; wafulana waliyagomea.
kama kipumziko katika sentensi ndefu
Alipochunguza ile hati aliyokabidhiwa na wale wafanya biashara aliona kuwa si nzuri; akaamua kujitenga nayo.
Vifungo/mabano/paradesi( )
kuzingira nambari au herufi katika orodha
(i),(a)
kuonyesha maelezo ya vitendo vya msemaji katika mazungumzo, mahojiano au tamthilia
MAMA :( Akiinama.) Hebu njoo haraka.
kutoa maelezo zaidi
Ema (kifungua mimba changu) chaja leo kutoka marekani.
kuonyesha visawe
Mamba (ngwena) huliwa.
Herufi kubwa(H)
mwanzoni mwa sentensi.
kuandika anwani
S.L.P 1000, Bura.
mwanzoni mwa usemi halisi
“Twendeni zetu,” akatwambia.
baada ya kiulizi (?) na hisi (!)
Lo! Ulienda? Hebu niambie yaliyojiri.
mwanzoni mwa nomino za pekee
Musa
ufupisho wa maneno
C.C.M (Chama cha Mapinduzi)
mwanzoni mwa majina ya vitabu, majarida, magazeti, vipindi, filamu, n.k.
kuandika sifa inayotokana na jina la pekee
Kiganda, Kikristu.
Koloni/ Nukta mbili ( : )
kuorodhesha
Ukitaka kuandaa samosa, unahitaji vitu hivi: unga, nyama, chumvi, mafuta na kitunguu
kutangulia usemi halisi
Alimwangalia kisha akamtupia: “mshenzi.”
kuandika mazungumo, mahojiano au tamthilia
MAMA :( Akiinuka.) Umechelewa wapi?
kutenganisha dakika na sekunde
9.25:05
kutangulia maelezo fulani
Alipofungua mlango alishtuka: mizoga ya punda ilikuwa imetapakaa nje.
Hisi/mshangao (!)
kuamrisha
Kachezeeni nje!
Kamau! Unafanya nini?
baada ya vihisishi
Masalaale! Pesa zangu zote zimeibwa.
baada ya sentensi iliyo mshangao
Gari langu limeibwa!
kusisitiza
Kesho msichelewe kuwasili shuleni!
kudharau/kubeza
Mwangalie! Kichwa kama jiwe.
baada ya tanakali
Mate yalimdondoka ndo! Ndo! Ndo!
Kiulizo (?)
mwishoni mwa sentensi iliyo swali
mwishoni mwa methali zenye muudo wa swali
Pilipili usiyoila yakuwashiani?
kuonyesha shaka
Kenyatta alizaliwa mwaka wa 1945(?)
kuonyesha mwaka wa kuchapishwa kwa kitabu haujulikani
Mlacha J (?) Tujijue Ipasavyo
Herufi nzito (h)
kusisitiza
Jibu maswali manne pekee.
kuonyesha wakati/njeo au hali
Nilicheza,Nimelima
kuonyesha umoja na wingi
mtoto-watoto
kuonyesha aina ya neno katika sentensi
Mtoto wake amelala (kivumishi)
Herufi za mlazo/italiki(h)
kuonyesha aina ya kiambishi au mofimu
Ki-li-cho-ib-w-a (kirejeshi).
kusisitiza
Jibu maswali mawili.
kuonyesha jina la kitabu
Nyota ya Rehema
kuonyesha maneno ya kigeni
Napenda mukimo.
kuonyesha maelezo ya vitendo vya mhusika katika mazungumzo, mahojiano na tamthilia
AMINA: (Akiinuka) Mama ameenda kwa Farashuu.
Kinyota(*)
kuonyesha neno limeendelezwa vibaya
*kitaabu
kuonyesha sentensi haina mpangilio sahihi wa maneno
*Kisu cha hiki ni nani?
kuonyesha tanbihi (maelezo ya neno yanapatikana chini mwa ukurasa)
idhibati*
kuonyesha sentensi ina makosa kisarufi
*Kuku hii ni ya nani?
Usemi Halisi
Maneno halisi kama yanavyotamkwa na msemaji.
Huandikwa bila kugeuza chochote.
Huanzia kwa herufi kubwa.
Hunukuliwa kwa alama za usemi ambazo huandikwa zikiwa mbili mbili na moja moja katika dondoo ndogo k.m. “Mwambie ‘ugua pole’ ukimuona,” baba aliniambia.
Koma hutumiwa mwanzoni au mwishoni mwake.
Msemaji mpya anapoanza kusema, unapaswa kufungua aya mpya k.m.
Alimuuliza, “Huendi kwa nini?”
“Sikupewa ruhusa,” alijibu Zahara.
Baada ya (?) na (!) na (.) maneno huanzia kwa herufi kubwa k.m. Lo! Unatoka wapi saa hii? Aliniuliza.
Usemi wa Taarifa
Ripoti kuhusu mambo yaliyosemwa na mtu mwingine.
Si lazima maneno yatokee yalivyosemwa. Yanaweza kubadilishwa mradi ujumbe ubakie ule ule.
Alama za mtajo, kiulizi na hisi hazitumiki.
Maneno “kwamba’ na ‘kuwa’ hutumiwa.
Baadhi ya maneno na viambishi hubadilika k.m.
usemi halisi
usemi wa taarifa
-angu
-etu
-enu
-ako
wiki ijayo
kesho
leo
sasa
huyu
hii
ta/ki
ni
na
jana
Lo!
?
-ake
-ao
-ao
-ake
wiki iliyofuata
siku iliyofuata
siku hiyo
wakati huo
huyo
hiyo
nge
a
li
siku iliyotangulia
alishangaa
alitaka kujua
VITATE T/D
Tata
hali ya kutoeleweka
sentensi hii ni tata.
fundo katika uzi
uzi umeingia tata/umetata.
Dada
ndugu wa kike
Tua
shuka kutoka angani
ndege ilitua uwanjani.
weka chini k.v. mzigo
Dua
maombi kwa Mungu
omba dua
piga dua –apiza/laani
Toa
ondoa kitu ndani ya kinginea
kinyume cha jumlisha
Doa
alama yenye rangi tofauti na mwili wa kitu
dosari/ila/walakini
Ndoa
arusi/makubaliano rasmi ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mke na mume/chuo
Tundu
uwazi mdogo wa mviringo kwenye kitu k.v. sindano
kitu maalum cha kuwekea ndege kilichotengenezwa kwa mabati, matete n.k.
Dundu
mdudu anayebeba uchafu
rundo la vitu /mtumba
Tuma
peleka kitu k.v. barua kwa njia ya posta
agiza mtu kufanya jambo
Duma
mnyama mkubwa mwenye umbo kama la paka
kamata, hasa katika vita
K/G
Kuku
aina ya ndege anayefugwa nyumbani
Gugu
mmea unaoota mahali usipotakiwa
mmea wa mwituni mfano wa unyasi
Kuni
vipande vya mti vya kukokea moto
Guni
shairi la arudhi lililokosa kutosheleza kanuni moja au zaidi ya uandishi
Kuna
kwaruza kwa kucha /kitu chenye menomeno
Guna
toa sauti ya kuonyesha kukataa, kutoridhika, au kuchukia jambo.
Kenge
mnyama kama mjusi mdogo
Genge
kundi la watu
pango/shimo
Kesi
daawa/mashtaka yanayosikilizwa mahakamani
Gesi
hewa inayotumiwa kupikia au kutiwa katika vinywaji
hewa ambayo haigeuki na kuwa majimaji katika joto la kawaida
CH/J
Changa
toa kitu ili kukusanya kwa kusudi fulani
siokomaa
chanja/pasua vipande vipande vidogo vidogo k.v. kuni
Janga
hatari/balaa
Chema
kizuri
Jema
zuri
Chini
kwenye ardhi/sakafu
Jini
shetani/ mtu muovu
Choka
pungukiwa na nguvu baada ya kufanya kazi
Joka
nyoka mkubwa sana
Chungu
chombo kinachofinyangwa cha kupikia
kinyume cha tamu
idadi kubwa (chungu nzima)
mdudu mdogo wa jamii ya siafu
Chambo
kinachowekwa kwenye mtego kunasia wanyama,samaki n.k.
Jambo
habari,tukio shughuli
Kucha
elekea asubuhi
ogopa
Kuja
hali ya kusogea karibu
Chuma
pata mali
madini magumu yanayotumiwa kujengea na kuundia vitu
tungua matunda au maua kutoka mtini
Juma
wiki
jina la mtu
Chenga
hepa kwa hila
mchele uliovunjikavunjika(mchele wa chenga)
Jenga
aka nyumba
fanya madhubuti/imarisha
Mchi
mti wa kupondea kwenye kinu
Mji
makazi ya watu wengi kulikojengwa nyumba nyingi
mahali kaburini anapowekwa mauti
sehemu ya kati ya chupa ya mwanamke mja mzito inayounganisha mtoto na mwili wa mama
Kichana
kitu cha kuchania nywele
Kijana
mtu wa makamo mwenye nguvu/mtoto wa kiume kabla ya kubaleghe
F/V
Faa
kusaidia
kuwa vizuri
Vaa
eneza kitu katika mwili ili kufunika sehemu fulani
Fua
safisha nguo
tengeneza kitu kutokana na madini
toa maji katika chombo
fua maji
Hakufua dafu. (hakufaulu)
Vua
pata samaki kwa kutumia wavu, mshipi, ndoana n.k.
ondoa nguo mwilini
nusuru, okoa, ponya
vua macho (tazama)
Fika
wasili mahali
bila shaka/kabisa
Vika
valisha
Fuka
toa moshi bila kuwaka
uji wowote mwepesi (uji fuka)
Vuka
enda upande wa pili
Fuma
piga kwa mkuki
ona kwa ghafla bila kutazamia mtu anayetenda jambo ovu
tengeneza kitu kwa kusokota nyuzi,ukindu n.k
Vuma
julikana kwa watu wengi k.v. habari, mtu n.k.
toa sauti nzito k.v. simba,.upepo mkali,.ngoma n.k.
Afya
hali nzuri ya mwili/siha
Avya
toa mamba
tumia ovyoovyo mali, pesa, n.k.
Fito
vipande vya miti au chuma vya kujengea nyumba
Vito
mawe ya thamani
Fuja
tumia vibaya
haribu mali, nguo ,chakula n.k.
Vuja
pita kwa kitu mahali penye upenyo
Gunia hili linavuja.
Vunja
fanya kitu kigumu kuwa vipande vipande
badilisha pesa ziwe ndogondogo
enda kinyume na kanuni
Futa
pangusa
chomoa kisu
toa maji nje ya chombo/fua maji
Vuta
fanya kufuata/burura
ingiza hewa au moshi mapafuni
Wafu
waliokufa
Wavu
utando wa nyuzi wa kufulia samaki,kutegea wanyama,kuweka golini/kimiani n.k
CH/SH
Chaka
mahali penye miti iliyosongamana
msimu wa kaskasi/joto na ukavu wa ardhi
Shaka
wasiwasi
tuhumuma
Chali
lala mgongo juu kichwa chini
mtu anayechekesha watu kwa kuwatolea mkasa
Shali
kitambaa cha begani cha shehe
Shari
balaa (pata shari)
Chati
mchoro unaotoa maelezo Fulani
Shati
vazi la juu la mwili lenye mikono
Sharti
lazima
Choka
pungukiwa na nguvu baada ya kufanya jambo kwa muda mrefu
Shoka
kifaa cha kukatia na kupasulia miti
Chombo
ala ya kufanyia kazi
Shombo
harufu mbaya ya samaki
Chokoa
tia kitu chenye ncha kwenye tundu au shimo ili kutoa kitu k.m chokoa meno
Shokoa
kazi ya kulazimishwa (fanyishwa shokoa)
shamba lililolimwa na kuachwa kumea nyasi
TH /DH
Thamini
tia maanani, heshimu
Dhamini
toa pesa maakamani ili mshtakiwa asitiwe korokoroni
Thamani
kima
Dhamana
malipo ya kortini
Thibiti
kuwa ya kweli/kuaminika
Habari imethibiti.
Dhibiti
tia mkononi
Nikidhibiti pesa zangu kutoka kwake nitanunua baiskeli.
weka chini ya mamlaka
Ridhi
kubali
pendezwa na jambo
Rithi
miliki kitu kutoka kwa mtu aliyekufa ama uliye na uhusiano naye
pata jambo au ujuzi kutoka kwa mtu mwingine
A/H
Apa
tamka jina aghalabu la Mungu kuthibitisha jambo Fulani
Hapa
mahali karibu
Ama
au
Hama
toka mahali fulani ili kwenda mahali pengine kuishi (gura)
Adimu
-a shida kupatikana,nadra
Hadimu
-mtumishi (mahadimu)
Ajali
jambo la madhara au hatari
Hajali
kinyume cha jali
Auni
saidia
Launi
rangi
L/R
Lahani
tuni
Rahani
chumba maalum katika nyumba au chombo cha kuwekea vitu
Lea
tunza mtoto
Rea
ghadhibika
Lemba
nyanganya kwa hila,punja
Remba
pamba, rembesha
Fahali
ng`ombe dume
Fahari
-a kujivuniwa kwa watu
Mahali
sehemu ambapo mtu au kitu huweza kukaa
Mahari
mali au fedha inayotolewa na mwanamme kupewa wazazi wa mwanamke anayetaka kumuoa
S /SH
Saba
namba inayoonyesha idadi
Shaba
madini yenye rangi ya manjano
Saka
tafuta,winda
Shaka
wasiwasi
tuhuma
kutokuwa na hakika
Suka
tikisa kitu
pitisha kitu kama nywele baina ya zenyewe kupata mfumo fulani
Shuka
enda chini kutoka juu ya kitu
kitambaa cha kujifunga kiunoni
Soga
mazungumzo ya kupitisha wakati
Shoga
jina waitanalo wanawake marafiki
msenge
Sababu
kinachofanya jambo kutokea,chanzo
Shababu
kijana
J/NJ
Jaa
tosha
tapakaa kila mahali
mahali pa kutupia taka
Njaa
hali ya tumbo kutaka kupata chakula
ukosefu mkubwa wa chakula
Chema
kizuri
Jema
zuri
Njema
nzuri
Jia
sogelea karibu
Njia
barabara
namna au jinsi ya kufanya jambo
Jozi
vitu viwili vinavyofanana vilivyo pamoja
Njozi
maono yatokeayo usingizini;ruia
Jana
siku kabla ya leo,mwaka kabla ya huu
buu la nyuki-kama kiluwiwi cha nzi
Njana-samaki mwenye rangi nyekundu
D/ND
Dege
eropleni kubwa
ndege mkubwa
ugonjwa wa watoto unaosababishwa na homa kali
Ndege
mnyama aghalabu anayeruka kwa mabawa
eropleni inayosafiri angani
ndege mbaya/mzuri (bahati nzuri/mbaya)
Duni
kitu chenye thamani ya chini
Nduni
ajabu/lisilo la kawaida
B/MB
Basi
gari la abiria
kisha
Mbasi
rafiki
Buni
gundua
unda
tunga
Mbuni
ndege asiyeweza kuruka lakini huenda mbio sana
mkahawa au mti uzaao kahawa
Bali
lakini
sijali wala sibali (kusisitiza kutojali)
Mbali
si karibu
tofauti
Mbari
ukoo
Bega
sehemu ya mwili juu ya mkono na chini ya shingo
Mbega
nyani
manyoya ya ndege wanayojifunga wachezaji ngoma (jifunga mbega)
Iba
chukua kitu cha mtu mwingine bila ruhusa
Imba
tamka maneno kwa sauti ya mziki
G/NG
Gawa
tenga katika sehemu mbalimbali
aina ya ndege wa usiku;kirukanjia
Ngawa
mnyama afananaye na paka
Guu
mguu mkubwa sana
Nguu
kilele cha mlima
nguru_aina ya samaki
Goma
kataa kufanya jambo mpaka masharti fulani yatimizwe
ngoma kubwa sana
duwi (aina ya samaki)
Ngoma
ala ya mziki inayotengenezwa kwa kuwambwa ngozi kwenye mzinga (piga ngoma)
mchezo wa kufuata mdundo wa ngoma (cheza ngoma)
Koma
alama ya kituo
acha kufanya jambo
P/B
Pata
kuwa na jambo, hali au kitu
kuwa kali
Kinolewacho hupata.
Bata
ndege mwenye vidole vilivyotandwa aghalabu akaaye majini
Papa
samaki mkubwa
Baba
mzazi wa kiume
Pana
kinyume cha –embamba
Bana
finya
Bango
uwazi ulio ardhini,mtini au jabalini
Bango
kipande cha karatasi ngumu kama kadi
bati linalozuia matope juu ya gurudumu la gari au baiskeli
Pacha
watoto wanaozaliwa kutokana na mamba moja
Bacha
tundu kwenye ukuta; shubaka(closet)
Paja
sehemu ya mguu kati ya goti na nyonga
Pania
kazana ili kufanya jambo lililokusudiwa
Bania
zuia kitu bila ya kutaka kukitumia (bania pesa)
Pima
tafuta urefu, uzito n.k.
Bima
mkataba na shirika wa kulipa pesa ili kupata fidia mtu anapofikwa na hasara
Punda
mnyama
Bunda
fungu la karatasi,noti,ngozi n.k
Panda
enda juu
kifaa cha kurushia vijiwe; manati
baragumu
tia mbegu ardhini ili zimee
Banda
jengo kubwa la kuwekea vitu au wanyama
Pasi
fuzu/faulu
hati inayomruhusu mtu kusafiri nje ya nchi/pasipoti
chombo cha kunyooshea nguo
Basi
gari kubwa la abiria
Mbasi
rafiki
T/D
Tamu
enye ladha ya kuridhisha mdomo
Damu
maji mekundu yanayozunguka mwilini
ukoo
Taka
kuwa na haja ya jambo fulani
uchafu
Daka
pokea kwa mikono kilichorushwa
tunda bichi (nazi daka/danga)
Tokeza
fanya kuonekana
Dokeza
toa habari za siri kwa uchache
Tai
ndege mkubwa mwenye makucha marefu alaye mizoga (vulture)
kitambaa kinachovaliwa kwenye ukosi wa shati
Dai
taka kupewa kilicho chako
habari inayosemwa na haijathibitishwa
K/G
Kamba
uzi mnene
samaki mdogo
mnyama wa baharini mwenye miguu mingi ambaye huliwa
kata kamba (kimbia)
Gamba
ngozi kama pembe ya kasa, samaki ,kasa au kobe(scales)
Konga
kuwa mzee
kusanya vitu au watu mahali pamoja (kongamano)
meza maji kidogo ili kupunguza kiu (konga roho)
Gonga
kutanisha kitu kimoja na kingine kwa kuvipiganisha
Koti
vazi zito livaliwalo juu ya nguo
Korti
mahakama
Goti
kiungo cha mguu kinachounganisha paja na muundi
Mfugo
mnyama anayefugwa nyumbani kwa ajili ya kuliwa au biashara
Mfuko
kitu cha kitambaa cha kutilia vitu
Tegua
fanya mtego usifanye kazi
ondoa chombo kama chungu mekoni
fanya kiungo cha mwili kifyatuke
Tekua
angusha kwa kusukuma
ng`oa kwa nguvu k.v. mmea
Mkuu
kiongozi
wenye hadhi kubwa
Mguu
kiungo cha binadamu au mnyama cha kusimamia au kutembelea
Oka
tia ndani ya tanuu kitu ili kiive au kikauke k.v unga uliokandwa au matofali
Oga
safisha mwili
enye hofu
Pika
weka kitu k.v. chakula sufuriani juu ya moto ili kiive
Piga
kutanisha vitu kwa nguvu
piga chafya, maji, hodi n.k.
Ukali
hali ya kutokuwa mpole
hali ya uchungu (ladha)
Ugali
chakula kinachopikwa kwa unga wa mahindi na kusongwa na maji moto hadi yakauke
MASWALI YA SARUFI
C1
(a) Akifisha kifungu kifuatacho
"Baba Wafua, ona barua iliyotoka kwa mwanao. Hata hati haisomeki" "Lo" baba watoto akamaka. Hii barua kweli imetoka kwa mwanangu Wafua. "Waniuliza mimi?" mama akamjibu "Tazama maandishi na anwani basi. Shule ya Msingi ya Burungani S.L.P 128 Vuga" (alama 5)
(b) (i) Andika sentensi ifutayo kwa wingi
Uwanja mwingineo umechimbuliwa kuongezea ule wazamani (alama 1)
(ii) Unda jina kutokana na kivumishi hiki
Refu (alama 1)
(iii) Tunga sentensi moj a ukitumia-ki-yamsahrti (alama 1)
(c) (i) Tunga sentensi tano kuonyesha matumizi matano tofautiyaneno ,
KWA (alama5)
(ii) Tumiaviunganishivifuatavyokatika sentensi
I)Mighairi ya
IIMaadam (alama 2)
(d) Sentensi ifuatavyo ina maanambilitofauti. Zieleze
Huyu amekuja kutuliza (alama 2)
(e) Tofautisha maana
(i) Ningekuwa na uwezo ningesafiri kwenda ng'ambo
(ii) Ningalikuwanauwezoningalisarikikwendang'ambo (alama2)
(f)Ainisha sehemu zote sarufi katika sentensi ifuatayo
Ninaondoka
(g) Unda jina moja kutokana na majina yoyote mawiliyaKiswahilisanifti (alamal)
C2
(a) SahiWshamakosayaliyomokatika sentensi hizi mbili zifuatazo
(i) Bei za vitu zimepanda juu sana siku hizi
(ii) Weka mizigo kwa gari (alama2)
(b) Elezamaanaya sentensi hizi
(i)mikono yao imeshikana
(ii)mikono yao imeshikamana (alama2)
(c) Andika sentensi zifuatazo ukitumia kinyume cha neon lililoandikwa kwa herufi za mlazo;
(i) Usijaribu kupaaza sauti unapoimba (alamal)
(ii) Huyu ni mtu mwenye busara (alamal)
(iii) Binadamu hawezi kumuumbua mwenzake (alama 1 )
(d) Akifisha kifungu kifioatacho:
Bwana mwenyekiti mgeni wetu wa leo wazazi waalimu wote hata wanafunzi leo ni siku muhimu je mngependa niwafahamishe msaada tuliopokea kutoka kwa wizara ya elimu
(alama 4)
(e) Tunasema: Mtoto huyu mzuri anapendeza
Ukitumia majina yafuatayo kamilisha sentensi ukifuata mfano ulio hapo juu
(i) Ngome (alamal)
(ii) Mitume (alamal)
(iii) Heshima
(iv) Ng'ombe (alamal)
(v) Vilema (alamal)
(h) Kutokana na vitenzi tunaweza kuunda maj ina, na pia kutokana na maj ina tunaweza kuunda vitenzi. Mfano:
Jina Kiteado
Mwuzaji uza
Muzo uza
Wimbo imba
Sasa kamilisha:
Jina Kitendo
(i) Mnada _________ (n) Kikomo _________
(iii) ___________ ruhusu
(iv) ____________ ashiki
(v) ___________ husudu (alama5)
(i) Andika katika msemo halisi
Mvulana, alimwambia baba yake kuwa alitaka kwenda sokoni (alama 2)
(n) Andika katika msemo wataarifa
Nitakuwa nikija hapa kila siku kukuona",Kamau alimwambia shangazi yake '
Eleza matumizi ya' Po' katika sentensi hii Nilipofika nilirnwona pale alipokuwa amesimama
(alama 2)
(k)Mtu akicheza mchezo mahali fulani tunaweza kusema alicheza hapo ukifuata mfano huu, tumia vitenzi vilivyoko l^tika mabano lojkamilisha:
(i) Alihapo (la)
(ii) Alihapo (fa)
(iii) Alihapo (oa)
C3
Jibu maswali yafutayo kulingana na maagizo
(a) Andika katika msemo wa taarifa
Mzazi 'lieshonatokaufikenyumba Mtoto:
"Nitajaribu, lakini mwalimu alisema tutafanya mtihani jioni (alama4)
(b) Badiisha katika udogo kisha uukanushe udogo huo
(i)Guu lake limepona baada ya kuumwa na jibwa la jijini (alama2)
(ii)Nyumba yenyewe ilijengwa bondeni karibu na mto (alama2)
(c) Andika katika kauli ya kutendesha
(i)Nataka upike chakula hiki vizuri(alamal)
(ii)Toa ushuru forodhani(alamal)
(d) Sahihisha bila kubadilisha maana ;
(i)Usikuje hapa kwetu kwani sitakuwamo (alamal)
(ii) Basi la shule limeharibika moshi nyingi inatokea dirishani na maji inatiririka ovyo
(alamal)
(e) Eila kubadilisha maana andika sentensi zifuatazo ukitumia kirejeleo cha ngeli kifaacho
(i)Nyumba alishinda farasi kukimbia (alamal)
(ii)Milango yote yajifunga ovyo nenda ukafunge (alamal)
(iii)Hamisiamekatanyasivizuri (alamal)
(iv)Jiwe lile liliangukia matunda (alamal)
(f) Eleza matumizi manne tofautiya - na - (alama 4)
(g) Eleza maana mbili mbili zinazotakana na sentensi zifuatazo
(i)Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka (alama 2)
(ii)Juma alifagia chakula (alamal)
(iii)sisikii vizuri (alama2)
(h) Tunga sentensi ya neno moja ambayo ina visehemu vifuatavyo vya sarufi
-kiima,
-Wakati
-kirejeleo
- Kiwakilishi kitendwa
-Kitenzi (alama 5)
(i) Bila kunyambua andika maneno mawili ambayo yanatokana na shina moja na neno:
Imani
C4
1. (a) Akifisha kifungu hiki:
nilipomwendea aliniangalia kisha akaniambia siamini kuwa ni wewe uliyeandika barua(alama3)
(b) Onyesha viunganishi vingine badala ya vile vilivyotumiwa katika sentensi hizi:
Watu wanne walipeperushwajuu kwajuu na upepo mkali(alama 4)
(c) Tumia viunganishi vingine badataya vile vilivyotumiwa katika sentensi hizi:
(i) Anayetafuta hachoki hata akichoka keshapata (alama 1)
(ii)Ngojeeni hadi washiriki wote wafike (alama 1)
(d) Tumia kiulizio –pi-kukamilisha:
(i)Nimitume........... ........... aliowataja? (alama 1)
(ii) Ni kiziwi ..................... aliyemwona akipita? (alama 1)
(e) Tunatumia viashiria vya kuthibitisha kwa mfano:-
Kitabu kiki hiki
Sasa kamilisha:
Ni mbwa ................. aliyekula chakula cha mtoto (alama 1)
(f) Andika upya sentensi ifutayo ukitumia kirejeshi (kihusiano cha ngeli cha mwisho
Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia anayetii wakuu wake. (alama 2)
(g) Jaza viambishi vifaavyo katika sentensi zifuatazo:
(i) Ukuta..........enyewe uria hyiifa nyingi lakini fundi....ote anaweza kuukarabati (alama2)
(ii)Maji yalizoa changarawe....ote na vitu....ingine....o ufuoni mwa bahari
C5
A. (a) Jaza kiambishi kifaacho:
Ume_______ona kalamu nyekundu zili____potea?(alama 2)
(b) Andika kwa umoja:
Tumewaondoleeni matatizo yenu yafaa mtushukuru (alama 2)
(c) Nyambua vitenzi vifiiavyo ili kupata majina (nomino) mawili tofauti:
(i) Kumbuka.........................................................
(ii) Shona...............................................................
(m) Cheka.............................................................
(d) Ondoa - amba-bila kubadilisha maana:
(i) Kuimba ambako kulisifika siku nyingi sasa kunatia shaka (alama 1)
(ii)Mibuni ambayo hupandwa wakati wa mvua hustawi (alama 1)
(e) Sahihisha:
Siku hizi mahitaji imezidi na pesa haitoshi (alama 1)
(f) Akifisha:
Sijaona kitabu kizuri kama hiki utaniazima siku ngapi Bashiri alimwuliza Sijaona
(alama4)
(g) Eleza maana mbili za sentenzi:
Jua nisemalo ni muhimu kwetu (alama2)
(h) Kiambishi-U-hutambulisha majinayangeliyaU (umoja), Hatahivyobaadhiya
majina haya huchukua viambishi tofauti katika wingi. Orodhesha maj ina matano kama hayo, kisha . uonyeshe viambishi hivyo tofauti vya ngeli (katika umoja na wingi)(alama 5)
C6
A. (a) Eleza tofauti iliyopo katika jozi hii ya sentensi
Alimpatia soda na chupa
Alimpatia soda kwa chupa (alama2)
(b) Kamiliska jedwali ukifuatia mfano uliopewa
Wimbo Mwimbaji Uimbaji
Jengo ........................ ..............
Pendo ........................ …..........
(c) Taja vielezi vinavyopatikana katika sentensi hizi; kiska eleza nl vielei4 vya aika gain(alama4)
(i) Aliamka alfajiri
(ii) Mtu huyu ni hodari sana
(d) Andika kwa usemi kalisi
Yohana alisema kwamba nj iani kulikuwa kumenyesha sana ndio sababu tulichikwa.(alama2)
(e)Tunga sentensi moja mojaukkttmia alama zifuatazo za udkifishaji
(alam 4)
(i) ritifaa
(ii) parandesi
(iii) ckikuduku
(iv) mshangao
(f) Tunga sentensi ukionyesha niatumizi ya vitenzi vya silabi moja katika jinsi ya kutendesha ukitumia silabi hizi ... (alam 3)
(i)-la
(ii) nywa
(iii) fa
(g) Taja na ubainishe aina za viwakilishi katika sentensi zifuatazo (alama 4)
(i) He minazi yangu niliyopalilia inakua vizuri
(ii) Mimi niriataka kumwona mwanariadha aliyepata nishani ya dhahabu
(h) Andika kwa wingi:
(i) Uta wake nimrefunamkubwa sana
(ii)Merikebu itakayofika kesho itang'oa nanga keshokutwa
(i) Andika upya sentenzi zifiiatazo ukitumia neno amba (alama 2)
(i)Kijiti kilichovinjika kiliimwumiza Anmina mguuni
(ii) Barua zitakazoandikwa na baba kesho zitatumwa mwaka uj ao
(j) Sahihisha sentensi hizi: (alama 2)
(i) Bahasha ilionunuliwa jana ni kubwa na mzuri
(ii) Mananasi hizi zinauzwa ghali kwa sababu zimeiva vizuri sana
C7
(a) Kwa kutumia kirejeshi kifaacho9 rekebisha sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti
Yulendiyeinkwasiambayealiyeniisurika (alama 2)
(b) Andika umoja wa sentensi hizi:
(i) Kwato za wanyama hutufaidi
(ii)Mnabdca vyeti vya kuwasaidia?
(c) Andika ukubwa wa
Mwizi aliiba kikapu na ng'ombe
(d) Tunga sentensi sahihi ukidhihinsha wingi wa majina yafuatayo
(i) Ukanda
(ii)Uzee
(e) Sahihisha sentensizifuatazo bila kugeuza maana
(i) Kikombechenyekimevunjikantkipya
(ii) Nimepeanakilabukwamwalimumkuu (alamal)
(f) Tunaweza kusema katika chumba au
(i)…………………………………………………………..
(ii)…………………………………………………………..
(g) Andika sentensi zifuatazo katika halt ya kutendewa
(i) Yuleng'ombealizaandamanikubwajana
(ii) Mavu hawa wamemsumbua Nyatogo kwa muda mrefu
(h) Kwa kurejelea ngeli za mahali, andika sentensi tatu ukionyesha matumiziya kila moja(alama 3)
(i) Andika sentenm za mseto kutokana na mbilifupi uizopewa
(i) Mwanafunzi amesoma kwa bidii. Mwanafunzi anataka kupita mtihani
(alamal)
(ii) Leonimerucknyumbani. Sipendelei kuishi hapa - (alama 2)
(j) Geuza sentensi hizi kutoka msemo wa taarifa hadi msemo halisi
(i) Mamaalisemanichukuenafakayetunikauzesokoni(alama2)
(ii)Mwalimualiombaaletewevitabuvyake kutoka darasani (alama 2)
(k) Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii.
Wenzake wamelipwa pesa zao, yeye bado amelala (alama 2)
C8
(a) Eleza matumizi matatuyaKIna utunge sentensi moja kwa kila mojawapo.
(alama 6)
(b) Tambulisha viwakilishi nafsi katika sentensi zifuatazo, halafu u/igeuze sentensi
hizokwawingi .
(i) Nilisomakitabuchake
(ii) Umekuwa mwadilifu kupindukia
(iii) Alishinda nishani ya dhahabu(alama 6)
(c) Akifisha sentensi hit -
Watu wengi warnezoea kusema ajali bwana basi yakaishia hapo lakini kufanya
hivyo ni sawa. (alama 3)
(d) Andika sentensi hizi kwa umola (alama 2)
(i) Mafuta haya yanachuruzika sana
(ii) Miinuko ile ndiyo mwanzo wa milima ya Chungu
(e) Sahihisha sentensi zifuatazo: (alama 2)
(i) Kile kitabu kilipasuka ni changu
(ii)Mtotomwenyeameangukaninduguyangu
(f) Kanusha:
(i)Matawi ya mti ambayo yalikauka yalikatwa (alama 2)
(ii) Matofali haya yanatumiwa kwa ujenzi wa nyumba
(g) Andika sentensi hizi upya ukitumia -o-te-
(i) Chakula kikibaki hutupiliwa mbali(alama 2)
(ii) Kila nyumba unayoingia unapata watoto wawili
h)Yapange majina yafuatayo katika ngeli zake
(i) Neno.............................................
(ii) Kiongozi..........................................
(iii) Mate.............................................(alama 3)
j)Ukizingatia neno lililo katika mabano, andika sentensi hizi katika haliya kutendeka(alama 2)
(i) Daraja hili(vuka)tu wa kati wakiangazi
(ii) Kitabu hicho (soma) ijapokuwa sura zingine hazimo
(j) Tunga sentensi ukionyesha matumiziya:
(i) -enye(alama 2)
(ii) -enyewe
C9
(a) Tumia viashiria vya kutilia mkazo katika sentensi zifutazo
(i) Kibogoyo................ Ndiye anayehitaj i meno ya dhahabu
(ii) Vyakula.................. mvipikavyo nyinyi, nasi twavipika
(b) Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika haliya umoja
(i)Huku kuimba kwenu kuzuri kutawapendeza wageni
(ii)Hii miche ni mizuri sana, itatufaa (alama 2)
(c) Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumiaviunganisliivifaavyo
(i)Chakula hiki hakina mchuzi. Hakina chumvi (alama 1)
(ii) Romeo aliamka. Alitazama saa yake Akaia kiamsha kinywa mbio mbio
(alama 2)
(d) Ziandike upya sentensi zifuatazo kwa kufaata maagizo uliyopewa
(i) Nimemleta paka ili aue panya wote wanaotusumbua hapa kwetu nyumbani
(anza: Panya......) (alama2)
(ii) Mbwa ambaye aliripotiwa kuwa ameibwa amepatikana katika bwawa la maji (anza Katika bwawa.....) (alama 2)
(e) Andikakwamsemohalisi sentensi. Tajiri alishangaa kuwa niliweza kuubeba mzigo huo peke yangu (alama 2)
(f) Piga mstari vivumishi katika sentensi hizi
(i) Sina nguo yoyote niwezayo kuvaa (alama 1)
(ii) Mtoto mwenyewe ataileta kalamu (alama 1)
(g) Andika vitenzi vinavyotokana na majina haya;
(i)mfuasi
(ii)kifaa
(iii)mharibu (alama 3)
(h) Kanusha
(i)Ungemwuliza vizuri angekujibu bila wasiwasi (alama 1)
(ii) Andika kinyume
Mjomba alichomeka upanga kwenye ala - (alama 2)
(i) Eleza maana nne tofauti za sentensi hii
Alinunuliwa samaki na mtoto wake (alama 4)
(j) Eleza tofauti bainaya sentensi hizi
(i) Ningekuwa na pesa ningenunua shamba
(a) Ningalikuwa na pesa ningalinunua shamba (alama 2)
B.
(a) kamilisha tashbihi zifuatazo
(i) Baidika kama
(ii) Mzima kama
(b) Tumia tanakali za sauti zifuatazo kukamilisha sentensi hizi;
(i)Sauti ya waimbaji haikusikika tena, ilikuwa imedidima...... wageni walipoflka katika jukwaa
(ii) Simba ni mnyama hodari sana, akimkamata swara humrarua (alama 2)
(c) Tunga sentensi mbili tofauti zinazo bainisha maana tofauti kati ya: (i) Nduni (ii) Duni (alama 4),
(d) (i)Mdudu anayetengeneza utandu huitwa (alama 1)
(ii) Mdudu mwenye mkia uliopinda nchani ambao una sumu ni
(alama 1)
(e) Andika inethali mojainayotokananamaelezoyafuatayo Asiye na uwezo ataendelea kuwa bila uwezo hata akifanya bidii namna gain (alama 2)
C1O
(a) Andika udogo na ukubwa wa jina ngoma
(i)____________
(ii)………………
(b) (i) Eleza namna mbili za matumizi ya alama ifutayo ya uakifishi (;)
(ii) Tunga sentensi mbili tofauti zinazoonyesha matumizi hayo.
(c)Tofautishamaanaza sentensi zifuatazo:
(i) Kazi yote ni muhimu
(ii) Kazi yoyote nimuhimu
(d) Tunga sentensi mbilimbili kuonyesha matumizi mawili tofauti ya:
Ka (i) ………………………..
(ii)………………………
Ndivyo (i)…………………………
(ii)…………………………
(e) Tunga sentensi kuonyesha matumizi sahihiyaviunganishihivi
(i) ingawaje ______________________
(ii)ilhali _________________________
(f) Tambulisha kielelezi, kivumishi na mnyambuliko wa kitenzi katika sentensi ifuatayo: Msichana mrembo alikuja upesi akimkimbilia dadake.
(g) Andika kifungu hiki kutoka usemi wa taarifa hadi usemi halisi(alama 2)
Watoto waliambiwa na mama yao watakaporudi nyumbani waoge, wale, hala III waanze kusoma moja kwa moja badala ya kuharibu wakati wao kwa kutazama vipindi vya runinga. Aliwakumbusha kuwa wanaofanya maonyesho kwenye runinga tayari wamefuzu shuleni na wameaj iriwa kazi.
(h) (i) Taja vihusishi vitatu vinavyorejelea mahali, wakati na kiwango(alama3)
(ii) Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya kila kihusishi
(i) Andika sentensi zifuatazo upya kwa kufuata maagizo
(i) Alicheza kwa bidii akawafurahisha wengi waliohudhuria tamasha hizo Anza kwa: Kucheza
(ii) Karamu hiyo ilifana sana, kila mtu alikula chakula akatosheka Anza kwa: Chakula
(j) Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia vitenzi hivi vya silabi moja
(i) Pa ________________
(ii)La
(k) Unda vitenzi kutokana na maj ina haya:
(i) Mtukufu ______________
(ii) Mchumba
C11
(a)Bainisha aina ya vivumishi katika sentensi hii
Nyiimba yangu rd maridadi
(b)Kamilishajedwali
Kufanya kufanyia kufanywa
Kula _____
Kuunga______ ______
(c)Eleza matumizi ya kwa katika sentensi hii
Aliimba kwa sauti tamu
(d)Andika kwa wingi
Pahala hapa ni pake
(e)Eleza mtumizi ya na katika sentensi:
Halima na Asha wanasaidiana
(f)Huku ukitoa mifano, fafanua miundo mitatu ya majina katika ngeli ya LI-YA
(g)Onyesha (i) Kielezi (ii) Kitenzi katika sentensi: Mvua ilinyeshamfululizo
(h)Kanusha sentensi hii:
Tumechukua nguo chache kuuza
(i)Tumia-ndi-pamojanaviashiria vyangelikujazamapengo cw-
(i) Wewe _____ninayekutafiita
(ii) Nyinyi______mnaoongoza
(j)Andika sentensi hiiupya kwa kufuatamaagizo
(i) Nilikuwa nimejitayarisha vizuri kwa hivyo sikuona ugumu wowote katika
safari yangu
Anza: Safari............. (alama2)
(k)Geuza vitenzi hivi viwe majina
(i)Shukuru
(ii)Enda
(1)Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii.
Mamake Juma na Mariamu walitutembelea
C12
a) Tunga sentensi inayodhihirisha matumizi ya ngeli ya I -1
b) Changanua sentensi ifiiatayoukitumiamchoro wa matawi: Mkulima mzembe amepata hasara
c) Onyesha viambishi awali na tamati katika kitenzi: Alimchezea
d) Taja sauti mbili zinazo tamki wa midomoni
e) Kanusha sentensi ifiiatayo: Ningaiikuwa napesa ningalinunua nyumba.
f) Kitenzi Fumbata kiko katika hali( kauli) ya Tendata, Fanyata.
g) Tunga sentensi ukitumiakielelezi cha:
i)Wakati
ii)Mahali
h) Andika sentensi zifuatazo kulingana na maagizo uliyopewa.
i) Mhunzi mrefu alisliinda tuzo (anza kwa: Tuzo.....)
ii) Mwanaftinzi huyu anasoma Idf aransa (Anza kwa Idashiria kisisitizi)
i) Sente
top related