imaan newspaper issue 33

Click here to load reader

Download Imaan Newspaper issue 33

Post on 23-Jan-2016

1.309 views

Category:

Documents

3 download

Embed Size (px)

DESCRIPTION

Imaan Newspaper 336 Muharram 1437, Jumatatu Oktoba 19 - 25, 2015

TRANSCRIPT

 • www.islamicftz.org6 muharram 1437, jumatatu oktoba 19 - 25, 2015

  huwatoa watu gizani

  Head office, Lumumba Street, Opp: Viwanja vya Mnazi Mmoja, P. O Box 779 Dar es Salaam, TanzaniaTell: 255 22 2182482/ 255 222184419, Fax: 255 22 2181424, E-mail: info@Binslum.com

  TIF yaTumIa mIl. 700 kuchImba vIsIma bagamoyo -uk 5

  Sheikh Alhad akosoa malumbano ajali ya Makka- uk 5

  aref Nahdi

  Sheikh Chembea

  Sheikh Ibrahim

  ayatollah ali khamenei

  Viongozi TiF wawaasa waTanzania:

  Marekani na Boko Haram

  Busara itumike kulinda amani

  ISSN 5618 - N0. 033 bEI: Sh800/- kSh80/- uSh1,200/-

  Sheikh Ponda asubiriwa kwa hamu

  Uk 7Uk 6

 • Uboreshaji wa matangazo ya tV imaan

  Kuanzia tarehe 10, Agost, 2015 kwa watumiaji wa receiver, TV Imaan itahama kutoka MPEG2 na kuwa MPEG4 (HD)Masafa ya satEllitE

  Satellite: IntelSat 906 Frequency: 4066.25 Symbol rate: 1613.475 FEC: 2/3 DVBS2 Vile vile unaweza kuangalia TV Imaan kwa njia ya mtandao (online) kupitia

  http:// www.ustream.tv/channel/radio-imaan-fm-2

  HaBari / Tangazo2 Na. mjI aLFajr Dhuhur aSr maGharIb ISha 9 KIGOMA 11:28 6:45 09:57 12:52 1:59 10 MWANZA 11:18 6:34 09:48 12:39 1:45 11 KAGERA 11:25 6:43 09:55 12:49 1:56 12 TABORA 11:16 6:34 09:45 12:41 1:48 13 SHINYANGA 11:17 6:33 09:46 12:39 1:46 14 SINGIDA 11:09 6:27 09:38 12:35 1:41 15 IRINGA 11:04 6:25 09:32 12:35 1:43

  Na. mjI aLFajr Dhuhur aSr maGharIb ISha 1 DAR ES SALAAM 10:49 6:08 09:18 12:17 1:23 2 ZANZIBAR 10:49 6:08 09:19 12:16 1:23 3 TANGA 10:55 6:12 09:24 12:19 1:26 4 MOROGORO 10:57 6:17 09:25 12:27 1:34 5 MTWARA 10:46 6:09 09:13 12:21 1:28 6 ARUSHA 11:05 6:21 09:35 12:27 1:33 7 DODOMA 11:03 6:21 09:32 12:29 1:36 8 MBEYA 11:13 6:33 09:40 12:43 1:50 oktoba 19 -25, 2015

  Na Kassim Lyimomorogoro

  TAASISI ya The Islamic Foundation (TIF) im-eziunganisha Shule ya Sekondari ya Imaan na Shule ya Sekondari ya Forest Hill ili kukuza viwango vya taaluma katika shule hizo.

  Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa TIF, Aref Nahdi wakati akizungumza na wazazi wa wanafunzi wa Shule ya Imaan katika ukumbi wa Shule ya Forest Hill.

  Nahdi alisema kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya Bodi ya Shule ya Forest Hill kuomba uon-gozi wa taasisi ya TIF kuingani-sha shule hiyo na Shule ya Imaan, ambazo zote zinamilikiwa na taa-sisi hiyo.

  Ni muda mrefu tumepokea maombi kutoka kwa Bodi ya Shule ya Forest Hill ya kuungani-sha shule hiyo na Shule ya Imaan, sasa leo tumewaita wazazi ili tu-waambie jambo hili ili nanyi mtoe maoni yenu, alisema Nah-di.

  Nahdi alisema kuwa watawa-punguzia wazazi wa Shule ya Im-aan gharama za vitu mbalimbali, ikiwemo ada pamoja na kutoa usafiri bure kwa wanafunzi wa bweni.

  Pia, tunampango wa kuten-geneza mabweni katika shule hii ya Forest kwani tuna eneo kubwa

  ambalo litasaidia kujengwa kwa mabweni hayo, Al isema Mwenyekiti huyo. Nae, Gavana wa Shule ya Imaan, Khamis Al-Jabr, amewataka wazazi kushiri-

  kiana na walimu katika kusima mia maadili, kutokana na mu-ungano wa shule hizo, ili kuima-risha maadili ya Kiislamu katika shule hizo Hali kadhalika, wazazi

  wa Shule ya Imaan wameponge-za hatua hiyo na kuongeza kuwa itasaidia kuboresha viwango vya ufaulu kwa wanafunzi wa shule hizo.

  shule za sekondari Forest Hill, imaan kuungana

  seLemaNi magaLi

  Taasisi ya The Islamic Founda-tion (TIF) imempeleka mwa-nafunzi Juma Kapilimbi kati-ka chuo cha kuhifadhisha Quran kiitwacho Tarteel Quran kili-chopo katika mji wa Azadvil mjini Jo-hansburg ikiwa ni jitihada za kumu-wezesha kijana huyo kuhifadhi kitabu kitukufu cha Allah. Akizungumza na gazeti Imaan, Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Sheikh Ally Ajirani alisema kijana huyo ni mwanafunzi ambaye alikuwa akilelewa katika kituo cha yatima kina-chofahamika kwa jina la Darul Imaan kilichopo Kola hili Mjini Morogoro .

  Sheikh Ajirani ameongeza kuwa ki-jana huyo atakuwa masomoni katika kipindi cha miaka miwili ambapo baada ya hapo anatarajiwa kurudi nchini ili kuendelea na masomo yake ya elimu ya mazingira katika shule ya Forest Hill ambayo pia inamilikiwa na TIF.

  Katika hatua nyingine, Sheikh Ajira-ni amebainisha kuwa licha ya kituo cha Darul Imaan, pia taasisi ya The Islamic Foundation inamiliki vituo vingine vi-wili ambavyo vimejikita katika kuwalea watoto yatima hapa nchini.

  TiF yafadhili yatima masomo afrika ya Kusini

  Shule za sekondari za Forest (pichani juu) na Imaan zilizopo mjini morogoro.

 • www.islamicftz.org

  6 MuHarraM 1437, juMaTaTu oKToBa 19 - 25, 2015

  3MaKala

  mussa imaNi sheha , ZaNZibar

  Kila binadamu ana mchango katika jamii na hakuna awezae kuishi bila ya msaada wa wengine. Tajiri humuhitaji maskini, mkulima humuhitaji mchuuzi, mfanya biashara nae huhitaji mazao ya mkulima. Abiria anahitaji chombo cha der-eva, na dereva hana kazi bila abiria. Mgonjwa na daktari, mwanafunzi na mwalimu; wote hawa hutegemeana.

  Yaani mshonano huu wa aja-bu unaonesha kila mtu ni mtu-mishi wa mwingine na watu hutegemeana ndio maisha yakawa. Quran inasema: Ni wake yeye (Allah) ufalme wa mbingu na ardhi na wala hakuji-fanyia mtoto na wala hana mshirika katika ufalme wake na ameumba kila kitu na kukiwekea vipimo vizuri (25:2)

  Kwa hivyo, ni vyema kwa kila mtu kumheshimu, kumjali na kumtumia mwingine kwa nafasi yake. Uislamu unasisitiza kum-tunza na kumtumia kila mtu ka-tika jamii kwa vile alivyo na kwa nafasi yake ili atoe mchango wake (nguvu, elimu, ufundi, fikra, ushauri, mali n.k.) alimradi maisha yarahisike na yawezekane ili kutimiza lengo la kuumbwa mwanadamu.

  Maustaadh katika jamiiMingoni mwa watu muhimu

  katika jamii ni wale tunaowaita ma ustaadh. Ingawa maana halisi ya neno ustaadh kwa lugha ya kiarabu ni mhadhiri wa Chuo Kikuu chochote kile kiwe cha Ki-islamu au cha maarifa ya dunia, hapa Tanzania neno ustaadh lina maana nyingi, pana na zinazoto-fautiana. Katika jamii ya kitan-zania, ustaadh ni yule afundishae dini, Quran, kiarabu na masomo mengine katika madrasa, msikitini au shule za Kiislamu, Mwalimu wa shule za kawaida ni nadra kuitwa ustaadh. Pia, mha-dhiri wa dini ya Kiislamu iwe kwa sura ya mijadala au nyingin-ezo nae huitwa ustaadh.

  Wakati mwingine Watanza-nia wametanua zaidi maana ya neno hilo kwa kumuita ustaadh hata mvaa kofia au kilemba, anayefuga ndevu au anayevaa kanzu fupi. Pia neno ustaadh limenasibishwa na mtu mstaara-bu, mkarimu, maridadi, mpole, apendae kusamehe anapoko-sewa, mwenye kuijali dini yake kwa kujitahidi kuyatekeleza kivi-tendo maagizo ya Mola wake na ambaye hujiepusha na makatazo yake.

  Mchango waoMaustaadh wakiwa ni sehe-

  mu ya jamii, wana umuhimu na mchango mkubwa katika mai-sha ya kila siku hasa katika jamii ambazo zina idadi kubwa ya Waislamu. Maustaadh ni tegem-eo kubwa la jamii katika kusima-

  mia dini na imani. Hufundisha watu, wakubwa na wadogo, wake kwa waume, katika muda wote usiku na mchana katika misikiti, vyuo na viwanja vya mi-hadhara ili jamii ijue, ijali na ishikamane na mafunzo ya dini yao. Kwa maana nyingine, hu-fundisha jinsi ya kujenga uhu-siano na Muumba wao ili wajue na kufikia lengo la kuumbwa kwao.

  Watu wengi katika jamii zetu, ikiwemo wakubwa, hawajui cho-chote juu ya dini. Baadhi hawajui sio tu namna ya utekelezaji wa majukumu yao bali hata maju-kumu yenyewe. Mama mmoja alipolinganiwa kuhusu swala al-isema: Kwani mwanamke nae anapaswa kuswali? Mimi nilid-hani swala ni kwa ajili ya wa-naume tu!

  Wengine wamefanya mengi kumkasirisha Allah Taala katika maisha yao kiasi hata hawawezi kuyataja mbele za watu. Wana-tafuta njia ya kutubu wao lakini hawajui waanzie wapi. Na hapo huwatafuta maustaadh ambao huwapokea, huwaongoza jinsi ya kutubia na kuwafundisha ibada mpaka wanakuwa sawa sawa.

  Maustaadh wamekuwa waki-wasaidia vijana wanaotaka ku-fanya mitihani ya taifa ya kidato pili, nne na cha sita katika somo la dini na kiarabu na vijana hao wamekuwa wakifaulu vizuri na kupata daraja zilizowawezesha kujiunga na masomo ya juu! Maustaadh wamekuwa wakiwa-saidia watahiniwa hao bila ku-choka na kwa moyo mkunjufu kwa njia zote za mawasiliano ikiwemo simu ili wafikie lengo.

  Kiuzoefu na kiutamaduni, wazee wengi Waislamu huwape-leka watoto wao madrasa waki-

  wa bado wadogo kupata mafunzo ya awali muhimu kwa ajili ya kuyakabili maisha yao hapa duniani na maustaadh hupokea watoto na vijana hao wa Kiis-lamu katika madrasa zao. Baadhi ya wa-toto hao huwa hawajaweza hata kutun-za usafi wa miili na nguo zao. Maus-taadh katika asasi zao hizo huwafundis-ha vijana Quran ambayo ni muongozo wa maisha kwa kuanza kuwatamkisha herufi kwa herufi, neno kwa neno mpa-ka wanaweza kusoma Quran.

  Maustaadh pia hufundisha vijana misingi ya uhusiano na mola wao kama vile swala, swaumu, dua na nyiradi, pamoja na jinsi ya kuamiliana na vi-umbe wenzao kwa huruma,upendo, ukweli, uaminifu, moyo wa kujitolea, kuwaheshimu wakubwa, kuwafanyia wema wazazi, ushujaa kupitia maisha (sira) ya Mtume wao. Athari ya mafunzo hayo huendelea hadi ukubwani.

  Kwa ujumla, madrasa ni vituo muhimu vya kuwafinyanga vijana, wak-iwa wadogo ili wawe wanajamii bora. Katika madrasa, utawaona watoto wa familia masikini na hata za waheshimi-wa viongozi na matajiri wakiamini kwamba watoto wao wasipopitia ma-drasa wakanyooshwa na maustaadh, watawasumbua sana hapo baadae. Wa-toto wengine wanakuwa wameshindika-na huko majumbani.

  Hebu niambie msomaji, kwa maju-kumu kama haya unamzingatia us-taadh kama nani katika jamii?

  Vile vile maustaadh hutatua mi-gogoro na ugomvi baina ya wanajamii, hasa wanandoa, baada ya kuombwa na wahusika au wazazi na mara nyingi Al-lah husaidia lengo kufikiwa. Jamii hu-wabebesha maustaadh jukumu hili zito kwa kuamini wana busara na wenye heshima kubwa mbele ya macho na nyoyo za wanajamii.

  Katika mkasa uliomkumba ustaadh wangu Abuu Hussein, akiwa amelala nyumbani kwake majira ya saa